Simulizi : Moyo Wa Kupenda
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mke wangu shaka ondoa kwani hadi sasa bila shaka atakuwa habari imeshamfikia huko alipo, kwani picha za harusi yetu, tayari nishazisambaza katika mitandao ya kijamii, ili aone ashikwe na uchungu aondoke, hivyo usiwe na wasiwasi hana muda mrefu ataondoka tu. Hapa tukimaliza saba yetu unaingia katika nyumba yako, kwani nishawapa kazi madalali wakutafutie nyumba nzuri, hivyo hilo niachie mie kwani pesa kwangu siyo tatizo, tatizo langu ni mtoto tu”
“Inamaana Dear na wewe siku zote toka ujana wako, hujawahi hata katika balehe yako kupata mtoto? Kwani ungemchukua ukakaa nae kuliko yule mchumia tumbo wako anashindwa kukupa mtoto basi japo angeshika mimba kisha iharibike angekutia tamaa yakupata mtoto, lakini hee hebu mpe talaka bwana aende zake.”
Mke na mume walikuwa wakizungumza wakiwa katika mapumziko baada ya mchakamchaka mkubwa, kwani ilikuwa ni mechi iliyokuwa na upinzani wa hali ya juu sana, kila mmoja akimuonesha mwenzie ufundi wake, ili mradi katika kupeana mapenzi mazito.
Walikuwa wapo katika hoteli ya Kempiski iliyokuwa pale mtaa wa Ohio wakiwa katika fungate, baada ya kufunga ndoa bomani Ilala katika ndoa iliyofungwa kila mmoja akiwa amesimama kidete katika dini yake, lakini wote kwa pamoja walisaini hati ya ndoa kuwa wanaoana katika ndoa ya wake wawili. Ndoa ile iliandaliwa kwa siri na ilitangazwa wiki moja kabla yakufungishwa ili kama kuna pingamizi basi liweze kutolewa, ndipo katika wiki hiyo kila mtu alizidisha mapenzi kwa mwenza wake, ili kusionekane tofauti yoyote na hatimae siku ya jumapili ilifungwa ndoa ile.
Kabla hajaenda kufunga ndoa, Rebeka alivuwa pete ya uchumba ya Rama akaiweka juu ya meza, ikiwa juu ya bahasha aliyoitumbukiza waraka ndani yake, akimuachia ujumbe mpenzi wake kuwa amevuwa uchumba, lakini pia anaondoka nchini, lakini pia ameathirika na virusi vya ukimwi. Kisha akashika njia na kumfata Faridi aliekuwa akimsubiri sehemu na kwa pamoja wakaenda Bomani kwa mujibu wa saa waliyopangiwa, na hatimae wakafanikiwa kufunga ndoa. Na sasa wapo katika fungate wakila Bata, wakijilia raha zao. Moyo wa mwanaume ukiwa katika furaha kubwa sana lakini ilikuwa ni tofauti katika moyo wa mwanamke. Kwani ndani ya moyo wake kulikuwa kumejaa dhihaka, udanganyifu na ulipizaji kisasi mkubwa pamoja na siri nzito.
Ama kweli moyo wa mtu ni fichio la siri, ama jambo usilolijuwa ni sawa na usiku wa kiza kinene.. F, na R , wakiwa katika chumba cha hoteli wakiburudika kwa mahaba mazito wakiponda raha. F, na R, wengine wakiwa hospitali kwa kuumizwa na F, na R. Dah yote ni kwa sababu ya Moyo wa kupenda.
“Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba mwanamke mmoja na mwanaume wamekutwa wamezirai ndani ya gari ndogo aina ya Toyota Halier wakiwa katika eneo la kuegeshea magari kwenye hotel ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam. Muda mfupi kabla Bendi ya Jahazi haijatowa burudani. Majina ya watu hao bado hayajajulikana mara moja. Mwandishi wetu aliekuwa katika eneo la tukio ameelekea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwa kupata taarifa zaidi. Kamanda wa polisi wa kanda ya Kinondoni, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Habari za awali ambazo bado hazijathibitishwa zinaeleza kuwa watu hao waliingia katika Hotel hiyo kwa minajili ya kwenda kumaliza wiki kwa kuburudika na muziki wa bendi ya jahazi iliyokuwa ikitumbuiza katika ukumbi huo. Kwa taarifa kamili ya tukio hilo, tujiunge na muandishi wetu aliekuwapo katika eneo la tukio”
Ilikuwa ni sauti ya mtangaji wa TBC 1 iliyokuwa ikitangaza habari za muda huo. Ikafatiwa na picha za video zililolionesha tukio zima la pale Traveltine Hotel. Yalionekana mahojiano ya yule mlinzi hadi, kuvunjwa kioo kwa gari ile, wakaonekana watu waliokuwa wamelaliana ndani ya gari mwanaume akiwa chini na mwanamke akiwa juu, zilioneshwa namba za gari ile, na hata ilivyokuwa ikiondoshwa na Polisi hadi kupotelea getini mwa Hoteli ile. Mwisho wa taarifa ile alionekana mtoa taarifa ile akihitimisha kwa kusema;
“Kutoka katika eneo la tukio hapa Traveltine hotel, mimi ni ripota wako Gama wa Gama wa TBC 1”
Faridi na Rebeka japo walikuwa wamelewa lakini waliweza kuiona habari ile kwa ufasaha, na Faridi alipoiona ile namba ya gari, mara moja aliitambuwa gari ile. Naam ni gari ya mkewe aliemnunulia yeye mwenyewe.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Faridi aliekuwa amelala na Rebeka kitandani akiwa kama alivyozaliwa, aliinuka akaa kitako. Macho yake yaliitazama ile Luninga kama vile ndiyo mara yake ya kwanza kuiona katika maisha yake. Moyo wake ukaongeza kasi ya mapigo yake, sintofahamu ikamjaa ndani ya moyo wake. Pombe ikamruka ikawa kama mtu aliekunywa maji, hakuwa na nishai tena katika kichwa chake wivu ulimjaa ukamtafuna, hasira zikampanda akatikisa kichwa chake kwa masikitiko.
Mkewe kwenda katika kumbi za burudani tena akiwa na mwanamme mwengine, roho yake ilimuuma sana akaona mkewe amemsaliti, na kama hivyo ndivyo basi atakuwa ameshafanya vile mara nyingi tu, kila baada ya yeye kusafiri. Ama kweli nyani haoni kundule!
Faridi alihisi kuwa mkewe amejuwa yeye yupo safari kama alivyomuhadaa, ndiyo akaamua aende kujirusha na mwanaume wake wa nje. Au ameamua kumlipizia kisasi kama atakuwa ameziona zile picha zake za harusi, baada ya yeye kuoa na kurusha zile picha za harusi yake katika mitandao ya kijamii. Ikawa hana hakika kama mkewe aliziona zile picha kisha na yeye akaamua kutoka na bwana wake au laa, lindi la mawazo likabarizi katika kichwa chake fungate ikaingia dosari.
Akasema na moyo wake kuwa Ikiwa swala la yeye kuoa mwanamke mwengine uwezo alikuwa nao, dini yake inamruhusu na sababu ya kuoa pia anayo, kwani furaha ya ndoa ni watoto. Sasa mkewe kwa nini aamue kushindana na yeye? Kwa nini anywe hadi anazirai ndani ya gari hadi kupigwa picha namna ile, tena akiwa amemlalia mwanaume kama vile. Basi amechemsha kwani sababu za talaka alizokuwa akizitafuta, sasa amezipata tena na ushahidi kabisa wa picha za video upo. Akatambua ifikapo muda mfupi ujao video ile ya mkewe itakuwa imeshapandishwa You Tube, Face Book na katika mitandao mingine ya kijamii.
Moyo wake ukasimama katika azma moja tu kumuwacha mkewe, kwani alishapata sababu za msingi zenye mashiko, kwanza mkewe siyo muaminifu, pili hazai ni Tasa. Tena kuna sababu gani asimpe talaka, nia ile ilisimama dede hakutaka kutafuta ushauri kwa mtu yoyote, akawaza namna tu ya kuiwasilisha talaka ile basi.
“Sweety sikuelewi unajuwa, kwani taarifa ile katika Tv imekuondosha kabisa mawazo yako vipi mpenzi kulikoni?”
“Mke wangu Rebeka, sasa nimeipata sababu ya talaka. Kwani taarifa iliyooneshwa katika Tv ile gari ni ya mke wangu, na hakika imeniuma sana yaani ameamua kutoka na mwanaume akenda kunywa hadi anazimia, hivi amekusudia kunidhalilisha siyo? Mimi ni mtu mkubwa ninaheshimika sana, watu nitawaeleza nini namna alivyonifanyia Faudhia?!”
“Haaaa makubwa haya, yaani yule mtu aliotangazwa hapa ndiyo mkeo mwenyewe? Bado hadi sasa hujaandika talaka ukampa, ningelikuwa mie ndiye weye saa hizi nishampa talaka japo kwenye simu! Kwani hana simu mkeo?!”
“Anayo simu”
“Sasa wasubiri nini humwandikii hiyo talaka, au umeshapewa limbwata Faridi na mkeo, jitu lisilozaa linasitiriwa kisha laenda fanya viroja, halafu aniharibia raha zangu mie.”
Rebeka alisema maneno hayo akiyatamka katika lafudhi ya kabila ya kidigo, kisha akainuka kitandani akiwa kama alivyozaliwa, akatembea kuzifata simu zao walizokuwa wamezizima wakaziweka ndani ya kabati ili kuepuka usumbufu wa watu kuwapigia pigia simu na meseji, pamoja na Whats App zisizo na faida yoyote katika jamii, kwani mtu mzima unarushiwa video ya katuni ya kutizama mwanao, na wewe unafurahia na ukaisambaza kwa wengine.
Rebeka alivyokuwa akitembea kwa mwendo wa haraka kuifata simu ya mumewe, Faridi aliyainuwa macho yake akamtazama maumbile yake kwa nyuma. Vyombo vilikuwa vikitikisika kama nyama ya kasa iliyokuwa kikaangoni. Faridi alitikisa kichwa na kujiona mshindi kuoa mwanamke yule, lakini pia akiwa hajutii kama atamuacha mkewe, kwani amefanya mabadiliko bora, ilikuwa kama kumtoa Zahoro Pazzi, kisha kumuingiza Cristian Ronaldo.
Rebeka alifika katika kabati akalifungua, akachukuwa simu ya mumewe akafunga kabati, akapiga hatua kurudi kitandanin kwa mumewe.
Faridi alimtazama mkewe alivyokuwa anatembea kumuelekea, maumbile yake yakakakamaa, Uume wake ukakataa kulala, ukaamka juu kama mwavuli uliokunjuliwa. Rebeka aliiona ile hali, alipomfikia mumewe alipiga magoti chini, akamkabidhi simu kisha mdomo wake ukauingiza ule uume uliokuwa umesimama, akaanza kuunyonya na kuuramba kama arambae askrimu ya koni.
Alifanya vile kwa ustadi mkubwa bila kumuuma meno, mikono yake akaipandisha kifuani kwa mumewe akawa anachezea bustani safi ya vinyweleo, na mara moja moja mikono ile ikazifikia chuchu ndogo za mumewe ikazipikicha taratibu, pasi na kuzipa maumivu.
Faridi aliipokea ile simu akaiwasha lakini alishindwa kuandika kitu chochote kile, akaiweka kitandani. Akainua kichwa chake juu ikawa kama mtu aliekuwa akitafuta kitu kilichokuwa juu ya dari ya hoteli ile. Mdomo wake alikuwa akiubana na kuuwachia, macho yake aliyafumba na kuyafumbua, mikono yake aliikaza kwa nguvu katika kitanda alipokuwa amekaa kitako, miguu yake ilikuwa haitulii pale chini, ilikuwa kama vile alipokuwa akikanyaga kulikuwa na kaa la moto, alikuwa akisikilizia ladha ya kunyonywa uume na mwanamke aliebobea katika kufanya majambo Rebeka binti John Makuka.
Rebeka alimkoleza mumewe hadi akamuona mapigo ya moyo wake pamoja na pumzi zinabadilika, akasimamisha zoezi lile akasimama wima akimtazama mumewe kwa macho yaliojaa pozi, macho yaliorembuliwa.
Faridi alikuwa yupo nchi jirani akikaribia kutua Tanzania, alipokatishwa akajikuta akiropokwa.
“Aaaaaaa dear ninyonye nimwage mpenzi unanikatili hivyo daah nilikuwa nataka kutua hapa”
Rebeka alitabasamu kicheko cha mahaba, akayatembeza macho yake makubwa yaliorembuliwa, huku mdomo wake ukiwa unapindishwa huku na kule, kisha kwa sauti ya mapozi, sauti tulivu yenye viwango akamwambia mumewe;
“Toa talaka tuendelee na raha zetu hivi huwezi kuandika andika kwanza itume nikupe mambo ambayo hujawahi kupewa maishani mwako!”
Faridi aliichukuwa simu yake akaingia sehemu ya kuandika ujumbe akaandika talaka.
Akiwa anaandika Rebeka alipiga magoti kwa mara nyingine akauchukuwa ule uume uliokuwa unaanza kusinzia, akauweka katikati ya matiti yake akawa anautia kasi kwa matiti a, k, a, manyonyo. Na ule uume ukarejea katika hali yake ya ushababi. Faridi alikuwa ni dume, ila siyo la mbegu.
“Andika talaka tatu mume wangu ili asikusumbue tena wala kukukalia eda huyo, kama hajuwi thamani yako mie ninaifahamu, usitake kumuandikia talaka moja wala mbili, maliza kabisa mume wangu”
Rebeka aliposema maneno yale aliuwamisha ule uume wa faridi kutoka kifuani kwake akauingiza tena mdomoni mwake shughuli ikawa inaendelea. Tena safari hii Rebeka alikuwa anacheza na tundu ndogo ya uume, alikuwa anavuta katika tundu ile mithili ya mtu anavyovuta mpira wa mafuta au maji katika bomba ili yaweze kuja na kutoka.
Tendo hilo lilimfanya Faridi asimame wima huku simu yake mkononi, maandishi yakirudiwarudiwa kuandikwa.
“Mpenzi ngoja kwanza nimalizane na huyu Tasa, lakini usiutoe mdomoni Honey, uwache upate joto huko, mie namalizia kuandika.”
Rebeka alisimamisha lile zoezi lakini akawa anapasha taratibu katika mwili wa mumewe kuhakikisha ule uume haupoi hata kidogo.
Faridi aliandika kwa haraka ile talaka, kisha kabla hajaituma akampa Rebeka aisome talaka ile.
Rebeka aliichukuwa ile simu kwa mkono mmoja, wa kulia na mkono wake wa shoto ukaukamata uume wa mumewe na kuendelea kuupasha, talaka ilikuwa ikisomeka hivi.
MIMI FARIDI KACHECHE, NIKIWA NA AKILI ZANGU TIMAMU, BILA KUSHAWISHIWA NA MTU MWENGINE YEYOTE YULE, NINAKUACHA FAUDHIA BADDY MNYONE TALAKA TATU. TALAKA SI MKE WANGU, KWA KOSA LA KUNIDHALILISHA NA KUNIFEDHEHESHA KATIKA JAMII. TALAKA HII INAANZA TAREHE YA LEO HII. KWA KUWA NIANDIKAPO TALAKA HII MUNGU ANANISHUHUDIA, BASI YEYE ANANITOSHA KUWA SHAHIDI WANGU.
“Hii imekaa vizuri mume wangu, itume sasa hivi kisha izime simu nikaihifadhi nije nikupe mambo ya ki Tanga mie, ushafika kisosora weye basi kama hujafika nataka nikufikishe nikutembeze Ngamiani, Mkwakwani, Sahare, Makorola ukiwa hapahapa chumbani upo?”
Faridi aliitikia kwa kichwa, huku akiandika namba ya mkewe Faudhia Baddy mnyone, na alipoipata akaitumia ile talaka. Ujumbe ule ukaenda ulipokusudiwa, na katika simu ya Faridi ukarudi ujumbe kuwa Derivared.
Rebeka alipousikia mlio wa simu umeingia, akaichukuwa simu ile kwa mumewe akaitazama ile simu akaona ujumbe uliokuwa ukiashiria kuwa umepokelewa katika namba iliyokuwa imehifadhiwa kwa jina la Sweet Fau. Akaizima ile simu akaiweka pembeni ya kitanda.
Rebeka alimpiga busu la paji la uso Faridi, kisha akampa ulimi akawa anamung’unya ulimi wa mumewe kama mtu alae peremende ya kifua, huku mikono yake ikiutalii mwili wa Faridi mgongoni, kiunoni, mbeleni, huku ikipanda juu kichwani. Mikono ile yenye vidole laini akavitumbukiza katika masikio akawa anapekecha taratibu bila haraka, bila kutumia nguvu. Faridi akazidi kupagawa akawa anatowa miguno ya ajabu migeni katika ulimwengu wa kawaida.
*******
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, ndani ya wodi namba moja Mwaisela kwa wagonjwa mahututi wasiojitambua, Dokta Neema Mnyampala akiwa katika vazi la koti jeupe la kitabibu, na kifaa cha kupimia alichokivaa shingoni mwake ambacho kitaalam kinaitwa STETHOSCOPE, alikivua kifaa kile na kuwapimia wagonjwa wawili wa jinsia tofauti, waliokuwa wamelazwa katika wodi ile ya Mwaisela katika vitanda tofauti. Ile Stethoscope aliiweka masikioni mwake na kifaa kingine kwa jina la kitaalamu kiitwacho SYPHIGMOMANOMETER au kama baadhi ya watu wengi wanaoshindwa kukiita katika jina lake halisi la SYPHIGMOMANOMETER hukitambuwa kama BLOOD PRESSURE MACHINE. Aliifunga katika mkono wa Rama wa kulia, akaikaza kisha akawa anapampu ile Syphigmomanometer akipima shinikizo la damu, alisikiliza katika masikio yake kwa ile mashine aliyoivaa, akapata jibu alilolitarajia, akaifungua ile mashine pale mkononi kwa Rama, kisha akaiweka ile mashine ya Stethoscope kifuani kwa Rama kujua kama mapafu yake yanapumua sawasawa katika mwenendo wake, akapata jibu.
Jibu alililolipata kwa Rama ndilo jibu alilolipata awali alipokuwa akimpima Faudhia. Alipata jibu kuwa wale wagonjwa mapigo yao ya moyo yalikuwa chini sana, hivyo walikosa nguvu ya kuzinduka haraka, kwani mioyo yao imepata maumivu makubwa sana.
Dokta Neema Mnyampala akawaagiza manesi waliokuwa pale pamoja nae, kuwatundikia wagonjwa wale wawili haraka Drip ya DEXTROSE/ SALINE hii ingeweza kuwarejeshea nguvu zao haraka na fahamu zao zingeweza kukumbuka matukio yote yaliyowafanya hadi kupelekea kupoteza fahamu. Mara watakapokuwa wameipata Drip ile.
Manesi wale waliokuwa wakimuhudumia Rama katika wodi ya Mwaisela, walimtundikia drip ile ikawa inaingia katika mwili wa Rama taratibu. Na manesi walewale ndiyo waliokuwa wakimuhudumia Faudhia, ambae pia walimtundikia drip aina ile ile ikawa inaingia taratibu.
Katika muda wa saa mbili tangu waanze kupatiwa huduma ile, wagonjwa wale walianza kupata fahamu na nguvu zao taratibu, wakawa wanaweza kuinua mkono na kupepesa macho huku na kule.
Dokta Neema Mnyampala alikuwa amewaeleza wale manesi wasiwalaze chali kabisa wagonjwa wale, kwa kuwa walihitajika kurejeshewa fahamu haraka, hivyo hata vitanda walivyolazwa wagonjwa wale vilikuwa juu kichwani vimeinuliwa kiasi wagonjwa wale wakawa kama waliokalishwa wakiwa wameegemea hivi, na kweli hali ile ya ulazwaji pamoja na zile drip zenye dawa za kutia nguvu mwili, ziliwasaidia sana wagonjwa wale kwani hata walipozimaliza drip zile walikuwa wapo vizuri kiasi lakini daktari Neema Mnyampala akashauri wagonjwa wale walazwe ili wapate kuangaliwa vyema maendeleo yao kwa karibu.
Rama alikuwa ameegama kitandani alipolazwa, mbele yake alikuwa anatizamana na Daktari Neema Mnyampala aliekuwa anampima mapigo yake ya moyo, mara kama mtu aliekurupuka akasema kwa sauti ya kinyonge.
“Yupo wapi Faudhia eee, amekwenda wapi Faudhia, niitieni Faudhia.”
Dokta Neema Mnyampala alimtazama kwa makini mgonjwa wake, akahisi kuwa huyo Faudhia labda ndiye yule mgonjwa wa wakike, kwani wagonjwa wale walipopelekwa pale hospitali na askari polisi, hawakuwa wakijulikana majina yao.
Dokta Neema Mnyampala akashangazwa pale alipomuuliza mgonjwa Yule na majibu aliyoyapata.
“Pole sana, Faudhia ni nani wako?”
“Sipo nae vyovyote ila namtaka mniitie kwani bado nampenda mchumba wangu Rebeka”
Dokta Neema Mnyampala alishangaa kwa kuwa hakuwa na taarifa za Rebeka kabisa, lakini mgonjwa huyu ametoka kumpima punde na amemuona anaendelea vyema lakini majibu aliyompa mbona kama ya mtu aliechanganyikiwa?
Alichukuwa karatasi na kalamu, akatumia mbinu za kitabibu kutaka kutambua kama mgonjwa wake amechanganyikiwa ama laa, akaanza kumsaili huku akiandika na kumtizama usoni. Alimuuliza jina lake, mahali anapoishi, kama anatambua pale alipo yupo wapi, nini kilichopelekea hadi awe pale wakati ule, Rama alimjibu kwa ufasaha kabisa pasi na chembe ya kuwa punguani.
Dokta Neema Mnyampala aliyaandika majibu yote ya Rama katika karatasi yake, kisha akamwambia Rama apumzike anakwenda kuongea na yule mgonjwa alieletwa nae pale, kabla dokta hajapiga hatua kuondoka Rama alimwita taratibu na kumwambia.
“Dokta naomba mnipime ukimwi tafadhali.”
Dokta Neema Mnyampala aligeuka kumtazama Rama, kisha akarejea kukaa pale kitandani akamuuliza Rama.
“Kwa nini unataka kupima Ukimwi?”
“Dokta hiyo ni habari ndefu sana ila naomba unipime na uniambie kweli majibu utakayoyapata, usinifiche chochote kwani nataka kujitambua afya yangu tu”
Dokta Mnyampala akamkubalia akainuka kwenda kuchukuwa vipimo, akarejea muda mfupi baadae akiwa na vifaa vyake. Alikuwa amevaa glove mikononi mwake, akawa na kisindano kidogo chakutobolea ambacho kitaalam kinaitwa PRICER. Akampaka spiriti iliyokuwa katika pamba kwenye kidole cha pili kutota kwenye kidole gumba cha mkono wa kulia, kisha akamtoboa kwa haraka katika kidole kile kwa ile Pricer, huku akimuomba samahani kwa kitendo kile cha kumtoboa. Damu yake akaikingia katika sehemu maalumu kwenye kifaa cha kupimia virusi vya ukimwi, kifaa kile kitaalam kinaitwa HIV 2 TEST.
Baada yakuingia matone kadhaa katika kifaa kile, dokta Neema Mnyampala, alikiweka kifaa kile juu ya kidroo kidogo kilichokuwa katika kitanda kile kikakaa sawasawa, akamu weka pamba nyingine yenye spiriti katika kidole kile kilichokuwa kikivuja damu, akamuachia pamba ile kidoleni kwake aishikilie.
Dokta Neema Mnyampala akaanza kumuuliza maswali kadhaa Rama kama alishawahi kupima Ukimwi, na Rama akamjibu kuwa hajawahi kupima Ukimwi. Akamuuliza swali lingine kama alishawahi kupata ajali katika siku za karibuni, Rama akajibu hajawahi kupata ajali.
Maswali yale Dokta Neema Mnyampala alikuwa akimuuliza Rama kwa lengo maalum nalo ni kukipa nafasi kile kifaa maalum cha kupimia maambukizi ya virusi vya Ukimwi HIV 2 TEST kiweze kufanya kazi yake sawasawa, naam katika muda usiozidi dakika tatu kifaa kile kilionesha majibu.
“Rama upo tayari kupokea majibu yako?”
Dokta Neema Mnyampala alimuuliza Rama huku akiwa anamtazama usoni.
“Naam nipo tayari Dokta na naomba usinifiche chochote katika majibu hayo ili nijijuwe.”
Rama alimjibu Dokta Neema mnyampala, huku akionekana ni mnyonge.
“Rama nikikwambia kuwa umzima hujaathirika utafanyaje, na ikitokezea kwa bahati mbaya ukawa umeathirika utafanyaje?”
Dokta Neema Mnyampala alimuuliza swali lile Rama huku akitazama kile kipimo ambacho sasa alikuwa amekichukuwa na kuwa nacho mkononi mwake.
“Aaa ikitokezea kama sijaathirika, nitamshukuru sana mungu kwa kuwa mzima, na ikiwa nimeathirika nitasikitika sana.”
Rama alimjibu Dokta Neema Mnyampala huku akiwa na wahaka wa hali ya juu sana, mapigo yake ya moyo yakikimbia kasi kuliko kawaida.
“Sawa Rama, kabla sijakwambia matokeo ya kipimo hiki, kwanza nataka ufahamu kuwa mtu akiwa anaishi na virusi, anakuwa bado hajawa mgonjwa wa Ukimwi hivyo anaweza kuishi kwa muda mrefu tu kama mtu mwengine yeyote ambae bado hajaathirika. Pia kuishi na virusi siyo kwamba ndiyo mtu atakufa laa hasha, kufa wanakufa watu wote hata wale ambao hawajaathirika pia wanakufa na ……..”
Dokta Neema Mnyampala alisimama kuzungumza, kwani alimjia nesi aliekuwa akimuhudumia Faudhia na kumwambia;
“Dokta unahitajika kule na mgonjwa”
“Ok nakuja muda si mrefu namaliza kuongea na mgonjwa”
Baada ya Yule nesi kutoka, Dokta Neema Mnyampala akaendelea kuzungumza na rama.
“Sasa Rama kipimo hiki kinavyopima ni baada ya kuiweka damu hapo nilipoiweka, ikiwa mtu bado hajaathirika, huwa unatokea mstari mmoja mwekundu, na kama ikiwa mtu ameathirika hujitokeza mistari miwili mekundu. Hivyo kipimo hiki kina mistari mekundu miwili, kuonesha umeathirika tayari.”
Rama aliyasikia maneno yale, moyo wake ukapigwa na ganzi, mate yakamkauka mdomoni mwake, mikono yake akashika kichwa chake akabaki amebung’aa asijue lakufanya.
“Pole sana Rama usiwe na mawazo, ikubali hali uliyonayo utaweza kuishi kwa matumaini, lakini kama hutaweza kuipokea hali uliyonayo sasa, utaweza kupata matatizo makubwa katika afya yako. Kuishi na virusi siyo kama ndiyo unaugua Ukimwi, wewe unaishi na virusi tu. Kipimo hiki kinaonesha kama umeathirika au laa, hivyo nakushauri uende katika kitengo chetu cha waathirika wanaoishi na virusi vya Ukimwi, ili ukapime CD4 zako ili waone kama umeathirika kwa kiwango gani, kama wakiona CD4 zako bado zipo juu basi hutaweza kula dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, watakupa ushauri jinsi ya kuweza kuishi na virusi vya Ukimwi. Ikiwa kama CD4 zako zitakuwa chini basi mara moja watakuorodhesha katika watu wanaokula dawa utaanza kula dawa. Na dawa zake ni bure serikali ndiyo inagharamia.”
Rama alikuwa akimsikiliza yule Dokta namna alivyokuwa akimueleza, lakini moyo wake haukuweza kupokea majibu yale, kwani alitamani iwe ndoto anaota isiwe kweli majibu yale. Kwani Rama alianza kumlaumu Faudhia katika nafsi yake kwa kupelekea yeye kutokutimiza azma yake kule katika ufukwe wa Coco. Bora angejiuwa kuliko madhila anayoyapata sasa. Alitikisa kichwa kwa masikitiko, akapiga ngumi katika mkono wake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Rebeka umesema kweli kuwa umeathirika sawa, lakini mbona hukuniambia mapema kabla? Sasa nateseka na mambo matatu, kwanza umenipa virusi, pili umenitoroka, tatu unaniuwa ilihali wewe ukiwa bado unafanya maambukizi kwa watu wengine kwa nini lakini, kwa nini unifanye hivi mimi? Kosa gani nililokutendea Rebeka la kulipwa Ugonjwa! Kipi ulichokitaka nikakunyima? Kwa nini lakini? Kwa nini Rebeka?! Umesema mimi ni mtu wa saba katika watu uliowauwa. Moyo wa kupenda leo unaniangamiza mimi, najuta majuto ya …..”
Rama hakumalizia kauli yake aliyokuwa akiongea peke yake, kwani machozi yalikuwa yakimtiririka mashavuni mwake, donge kubwa la uchungu lilimkaba kooni mwake, akajibwaga katika kitanda akajilaza kifudifudi, mikono yake akaufunika uso wake, akawa analia kwa kwi kwi.
“Jikaze Rama kubali matokeo, utajiumiza zaidi wewe ni mwanaume jikaze. Maji yakisha mwagika hayazoleki.”
Dokta Neema Mnyampala, alimwambia maneno yale kisha akaondoka katika kitanda cha Rama akaenda katika kitanda cha nane alichokuwa amelazwa Faudhia katika wodi ile namba moja pale Mwaisela.
“Dokta samahani sikuja na simu yangu hapa?”
Faudhia alimuuliza Dokta Neema Mnyampala, kwani kumbukumbu zilishamrejea muda na akakumbuka alikuwa na simu aliyokuwa ameitowa mlio, kwani huwa hapendi simu yake iite kwa mlio badala yake ameiweka katika mtindo wa kutetemesha.
“Kweli mgonjwa wangu sasa hivi upo vizuri sana kwani hadi simu yako umeikumbuka? Simu yako ipo kwani ulipoletwa hapa askari hawakujua kama ulikuwa na simu, hivyo mimi nilikupekuwa nikaiona simu yako nimekuhifadhia, lakini humu ni wodi ya wagonjwa wasiojitambua kama mlivyoletwa nyie, hivyo tunahitaji utulivu mkubwa sana, ikiwa unataka nikupe basi naomba uizime au uitoe mlio.”
Dokta Neema Mnyampala alimpa simu yake, kutoka katika mfuko wake wa koti la kitabibu alilolivaa.
Faudhia aliichukuwa simu yake ndogo yenye urefu wan chi nne kwa mbili aina ya SAMSUNG GT-S 5300 iliyokuwa ya Line moja, akamshukuru Dokta Neema Mnyampala kumtunzia simu yake akaitazama kama iliita au kupata ujumbe wowote.
Akiwa katika kuitazama simu yake mara ujumbe ukaingia katika simu yake. Hiyo ikiwa ni majira ya saa tano za usiku.
Faudhia alipoufungua ujumbe ule na kuusoma, hali ikawa tete.
Ilikuwa ni talaka tatu kutoka kwa Mumewe, hasira zikampanda, moyo ukamuuma sana, machozi yakamtoka akaibamiza chini sakafuni simu yake kwa hasira, kisha akaanza kulia huku akilombokeza kwa maneno.
“Faridi nimekukosa nini lakini hadi unanipa adhabu kubwa kama hii?! Nimekudhalilisha wapi mimi, siku zote nimetunza ndoa yangu nimejihifadhi, umekwenda kuoa umeona haitoshi hadi unanipa talaka tatu, ama kweli tenda wema wende zako haaah!”
Dokta Neema Mnyampala, alikuwa karibu na Faudhia akasogea karibu akaanza kuokota vipande vya simu ile iliyokuwa imetawanyika kila kitu sehemu yake, viliyosalimika na kuwa salama ni vitu vitatu tu ambavyo ni Betri, Memory card pamoja na Line yake lakini simu ilikuwa huwezi hata kuiunga ukapata japo mfano wa simu. Ama kweli hasira hasara.
Dokta Neema Mnyampala akamkabili Faudhia ili kutaka kujuwa kulikoni, hadi aivunje simu yake na kulia kwa uchungu namna vile, lakini hakupata majibu badala yake alipokea kilio kikubwa. Faudhia kila alipokuwa akiulizwa ndiyo alikuwa anazidi kupandishwa munkari, alichanganyikiwa vibaya sana. Alishuka kitandani akakaa sakafuni akajiona hatoshi, akaamua kugaragara sakafuni huku akilia kwa sauti, kama mtu aliekuwa amepatwa na mapepo wachafu kichwani mwake.
Ikawa huku Faudhia analia kwa sauti kwa kuachwa na mumewe talaka tatu, na kule Rama akawa analia kwa kwikwi kwa kuambukizwa virusi vya Ukimwi.
Dokta Neema Mnyampala akawaagiza manesi wamletee dawa ya usingizi aina ya VALIUM INJ ( DIAZEPAM ) ujazo wa 10MG (2ML) manesi wakaleta sindano yenye dawa hiyo ya usingizi aliyoelekeza Dokta Neema Mnyampala kisha manesi watatu wakamkamata Faudhia kwa nguvu, Dokta Neema akamchoma sindano ile katika mshipa, haikupita muda mrefu amani ikapatikana, Faudhia akawa katika usingizi mzito wa dawa.
Rama aliinuka kitandani akakaa kitako, mikono yake akiiweka katika mashavu, huku akiwa mwenye mawazo tele, donge likiwa limemkaba katika moyo wake. Aliwaza mengi sana akaona ndoto zake zote za maisha zimekatika kwa matatizo aliyoyapata, matatizo yaliyosababishwa na moyo wa kupenda. Kila kitu akakiona hovyo alishindwa kupokea majibu ya kuathirika, hatimae dhamira yake ya kujiuwa ikachipua upwa katika nafsi yake. Akaona hiyo ndiyo njia sahihi ya kuyakimbia matatizo, kwani hakutaka kuzolewa kinyesi chake, hakutaka kunyooshewa vidole na jamii, hakutaka kunyanyapaliwa, hakutaka kubaguliwa.
Rama akiwa katika mawazo tele Dokta Neema Mnyampala, akamgutusha alipokaa nae katika kitanda chake akamshika bega na kumwita jina lake. Rama aliinua uso wake uliokuwa umekunjika kwa hasira, umewiva kwa kilio, uso uliokata tamaa, akamtazama bila kusema neno lolote lile.
“Hebu niambie tafadhali kipi kinachokutia unyonge namna hiyo, wewe siyo wakwanza kuambukizwa virusi wapo mamia kwa maelfu ya waathirika wa virusi vya ukimwi duniani kote, wenzako wameikubali hali yao maisha yanakwenda na wanatimiza malengo yao. Kupata virusi siyo mwisho wa maisha, kama uhai unao unaweza kuishi miaka mingi tu mbele, bora kuishi kwa malengo tu ujitambue kuwa umeathirika, ufate masharti ya kula vyakula vyenye virutubisho, usifanye ngono zembe kabisa, kwani siyo uone kwamba umeshaathirika basi ndiyo ukatembee na kila mwanamke hapana kwani utakuwa unaongeza idadi ya maambukizi mapya katika mwili wako na kuzidi kuuchosha mwili wako. uhakikishe unafanya mazowezi, uepuke ulevi, epuka vinywaji vyenye Cafen na kila ambacho kitakupunguzia CD4 zako kwa haraka. Hivi nikuulize Rama, katika kunyongea huko unakonyongea utaweza kurudi kuwa huna virusi? Acha kabisa kuwaza sana hadi unapitiliza hili limekwisha kutokea usiwe unapoteza muda wako kuliwaza, sasa fikiri unaishije katika hali ulonayo sasa ndiyo njia pekee ya kukufanya uishi kwa furaha japo umeathirika?”
Maneno yale ya Dokta Neema Mnyampala yalimuingia Rama hadi ndani, yakauchoma moyo wake, kwa mbali yakampa faraja akaondosha mikono yake mashavuni mwake, akamtazama usoni Dokta Neema Mnyampala kwa makini kisha akatikisa kichwa chake juu chini, kuashiria kuafiki maneno yake.
Dokta Neema Mnyampala nae akatikisa kichwa chake kuonesha kukubali kwa kukubaliwa rai yake, akampa mkono wake Rama, nae Rama akaupokea mkono ule wa Dokta Neema Mnyampala na Dokta akamwambia;
“Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi”
Rama hatimae akatabasamu huku akisema;
“Nimekubali Dokta, hakika sasa nimeipata faraja katika moyo wangu”
Dokta Neema nae akatabasamu akamwambia;
“Anza maisha yako mapya kuanzia sasa, kwani maisha ya mwanaadamu ni mzunguko yanapanada na kushuka, yana mabonde na milima, amini huwezi kuishi maisha yasiyokuwa na changamoto”
Rama akatikisa kichwa kukubali maneno yale, akawa anarejea katika hali yake ya kawaida taratibu.
*******CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saa kumi na moja alfajiri Faudhia aliamka kutoka katika usingizi wa dawa, njaa ilikuwa akiisikia sana, hakuwa na nguvu katika mwili wake, alikuwa bado amelala japo hakulala usingizi, alikuwa akipepesa macho yake huku na kule, hatimae macho yake yakagota kwa mwanamme aliekuwa amemsimamia pale kitandani kwake.
Faudhia alimtazama kwa kumkazia macho mtu yule akainuka katika kitanda chake akakaa kitako, akawa anamtazama kwa makini.
“Pole sana Faudhia, hakika maisha yanabadilika mie yangu tayari yamebadilika na nimekubali hali niliyokuwa nayo, mwanzo nilitaka kujiuwa ukanikataza hakika umefanya jambo jema sana na ninakupongeza, umefanya jambo jema ni kwa sababu laiti kama ningelijiuwa basi yule mwanaharamu angeendelea kuuwa watu wengi sana bila kutambuliwa, sasa nataka kupambana nataka kuhakikisha Rebeka kwa kuambukiza watu virusi makusudi, aidha namuua kwa mkono wangu, au anafika katika mkono wa sheria ili sheria ichukue mkondo wake kwani dhamira yake ya kuniambukiza virusi ni kuniuwa, sasa na mimi sitomuacha auwe watu wengine zaidi ya mumeo, nitamtafuta popote alipo pale kwani picha zile ulizonionesha nimepatambua pale ni Bomani Ilala, hivyo bado yupo nchini malaya huyu”
Rama alimwambia Faudhia aliekuwa amebweteka kwa kujawa na msongo wa mawazo. Faudhia hatimae akasema.
“Rama nimepewa Talaka tatu na mume wangu, yaani nimeumia sana kwani mie nitakuwa mgeni wa nani japo biashara ninayo lakini ni yakupata pesa ndogondogo tu, nawezaje kupanga nyumba mimi kwa wakati huu, kwani yule bwana wakati amenioa nimemkuta na kila kitu chake, sasa naanzaje mie kudai vitu Faudhia mie? Hata kama nikiomba msada kwa ndugu na jamaa je nikipata nyumba ya kuishi nahamia na vitu vipi?”
“Pole sana kwa kuachwa Faudhia ila usilie sana, nakushauri pima kwanza ujue afya yako, inawezekana ukawa ni mzima mungu akawa amekuepusha na maambukizi ya virusi vya ukimwi na hatimae Ukimwi wenyewe, ndiyo maana umeachwa Talaka tatu kuepushwa kuambukizwa na mumeo ambae akiwa muathirika atakuambukiza na wewe kwani mungu ni wa ajabu sana anatenda kazi zake kwa hekima. kwani kila likuepukalo lina kheri na wewe. Mimi tayari nimeshajitambua kuwa Rebeka ameshaniambukiza tayari na ndiyo maana nataka nimsake hayawani huyu hadi nimtie mkononi mwangu kisha nimshikishe adabu”
“Ina maana umeshajijuwa kama na wewe umeathirika, haya je mie nitapona kweli yarabi?”
Rama akamwambia Faudhia kwa sauti ya upole iliyojaa msisitizo;
“Huna haja ya kuishi kwa mashaka wakati hapa tupo hosptitali pima uondoshe mashaka yako, pima ujitambue Faudhia.”
“Daah sasa hapo umenipa wazo zuri sana ngoja nipime na mimi nijuwe kama mzima au nimeshaumia”
Faudhia alipokubali rai ya Rama, akamwambia akamwiitie Dokta ili apime ajitambue, Rama akaiita kwa sauti kubwa Dokta, Dokta, na mara manesi na Dokta wakaingia kutoka katika chumba cha ofisi yao kwa haraka, wakidhani kuna tatizo kubwa.
Walipofika pale Rama akawaeleza wale wauguzi na Dokta Neema Mnyampala nia ya Faudhia kupima Ukimwi.
“Sasa wewe unaita kwa nguvu namna hiyo hadi unatushitua sie kumbe jambo lenyewe ni la kupima Ukimwi tu, siungesubiri hadi tunapopita kuwakagua ndiyo utuambie, Hivi hujui humu ndani hakutakiwi kelele? kama mmeshapata nafuu bora mruhusiwe muondoke kuliko kuwasumbua wagonjwa wa ukweli hapa waliokuwa hawajiwezi!”
Nesi mmoja aitwae Raya James aliekuwa ameegama kwa kusinzia, baada ya ule mtafaruku wa Faudhia uliokuwa siyo wa kitoto, alilalama kumlalamikia Rama aliewaita kwa kelele.
“Basi amesikia nesi, inawezekana hakufahamu kama humu hakutakiwi kupiga kelele kwani hii wodi ya wagonjwa mahututi.”
Dokta Neema Mnyampala alimwambia yule nesi, kisha akamwambia Rama akakae kitandani kwake, akamsogelea Faudhia katika kitanda chake, akaketi kitako akamwambia;
“Shoga vipi unataka kupima Virusi vya Ukimwi?”
Faudhia akaitikia kwa kichwa kuwa ndiyo anataka kupima. Faudhia alipokuwa na Rama alikuwa amekubali kuitambua afya yake, akapata ujasiri wa kupima lakini alipofika Daktari moyo wake ukafa ganzi kwa tendo la kupima, huku akijisemea ndani ya moyo wake kwamba je akiwa ameathirika itakuaje.
Dokta Neema Mnyampala, aliwaagiza manesi kumpelekea vifaa vya kupimia VVU manesi wakafanya hivyo na Faudhia akatobolewa katika kidole chake damu yake ikawekwa katika kifaa kile HIV 2 TEST na baada ya dakika tatu kipimo kile kikatowa jibu.
“Faudhia Shoga yangu, hivi ikiwa kama umeathirika utafanyaje, na ikiwa hukuathirika utafanyaje?”
Dokta Neema Mnyampala alimuuliza Faudhia aliekuwa amenyongea, moyo wake ulikuwa ukienda mbio kama saa mbovu.
“Dokta itategemea na majibu kwa kweli, kwanza hapa sina hali kabisa nasikia kiu ile mbaya koo limenikauka, wewe niambie tu Dokta kama nishaumia nijuwe”
Dokta Neema Mnyampala alimtazama Faudhia kwa kina akagundua hakuwa vizuri kisaikoloji, hivyo akamwambia kwa sauti ya upole.
“Shoga yangu naomba uwe tayari kuyapokea majibu yako, kipimo chako kinaonesha kuwa umenusurika na maambukizi, yaani upo salama hujaathirika ila nakushauri baada ya miezi mitatu upime tena ili uhakikishe kama bado upo mzima, pia nakushauri uendelee kujilinda.”
Faudhia aliruka juu kwa furaha akatua chini akawa anaweweseka kwa kule kuonekana mzima, kwani hakutegemea kabisa, akamshukuru Mungu kwa kumnusuru maambukizi akamsikitikia Mtalaka wake, pia akashukuru kuachwa kwani angeweza kuambukizwa.
“Asante Mungu wangu kwa kunilinda, nilikuwa najilinda kwa mume wangu, leo nimeumia kwa kuachwa kumbe umeninusuru na ugonjwa, ama kweli aliekuwamo hatoki, na asiekuwamo haingii”
Rama akiwa kitandani kwake alimuona Faudhia akifurahi, kwani yeye alitegemea asikie kilio cha kufa mtu lakini ikawa kinyume chake, moyo wake ukaingia simanzi kwa yeye kuathirika akashukuru mungu, akajilaza kitandani akiwa na nia moja tu sasa kumsaka Rebeba kwa Udi na Uvumba, ili atoe kinyongo chake, ili alipe kisasi kwa kuambukizwa virusi kwa makusudi mazima kisha kutorokwa.
*******
Saa moja asubuhi askari waliowapeleka kina Rama na Faudhia, walifika pale katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, wakaingia kwa dakitari wakapewa majibu ya maendeleo ya watu waliowapeleka pale usiku, wakapewa ruhusa yakuondoka nao.
Rama na Faudhia wakapandishwa katika gari ya Polisi wakapelekwa katika kituo cha Polisi Magomeni, kwa mahojiano zaidi.
Walipofikishwa kituoni Faudhia aliiona gari yake ikiwa imevunjwa kioo, akashangaa akawauliza wale maaskari;
“Nani alievunja gari yangu kioo?!”
Badala ya kujibiwa askari wa kike aliekuwa akimuongoza akamwambia;
“Wewe huko ndani kwa mkuu wa kituo huko utajua kila kitu”
Rama aliitazama ile gari nae akapigwa na bumbuwazi asijuwe kilichotokea hadi gari ile kupata dharuba namna ile.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakaongozwa hadi katika ofisi ya mkuu wa kituo, wale askari waliowapeleka wakatoa saluti kwa kiongozi wao na mmoja wa askari wale akamwambia mkuu wa kituo.
“Afande hawa ndiyo watu uliotaka kuonana nao, Daktari amethibitisha kwamba wapo salama kabisa.”
“Kazi nzuri vijana Sajenti kaa hapo nyie mnaweza kwenda.”
Mkuu wa kituo cha Polisi Magomeni aliwaambia askari waliokuwa wamewapeleka kina Rama kwake. Askari wale walipiga Saluti kwa mkuu wao wakatoka nje ya ofisi ile. Mkuu wa kituo cha Polisi Magomeni alikuwa akiwatazama Rama na Faudhia walioketishwa chini sakafuni kwa jicho kali sana, huku akiwa amenuna vibaya.
“Nyie majina yenu nayataka, kazi zenu na mnapoishi, mawasiliano yenu pamoja na uhusiano wenu.”
Mkuu wa kituo cha polisi Magomeni aliwauliza kina Rama maswali yale akiwa amenuna ile mbaya, huku akimpa karatasi na kalamu Sajenti Mbago Kizega aweze kuandika maelezo yao.
Kwa kawaida mkuu wa kituo huwa ahoji watuhumiwa au kuchukua maelezo yao kutokana na cheo chake na itifaki ya polisi ilivyo, ila kwa watuhumiwa hawa ilikuwa ni tofauti kwani vyombo vya habari vililiandika tukio lile sana, likaliandika vibaya jeshi la Polisi wakililaumu kwa kuharibu mali ya raia. Yaani watu wa habari kwao wao, habari haikuwa watu kuzirai ndani ya gari laa hasha, ila lile tendo la Polisi kuvunja kioo cha gari ya Faudhia kwao wao ndiyo ilikuwa habari njema ya kuuza magazeti yao! Habari iliyowafanya viongozi wa jeshi la Polisi kutaka undani wake.
Gazeti la Kiu ya Jibu katika siku ile ya Jumatatu, liliandika habari ile kwa kichwa cha habari POLISI WAHARIBU MALI YA RAIA, KUWATOWA WATU WALIOKUWA WAMELALA NDANI YA GARI YAO!. Mbali na kichwa cha habari hicho pia walitowa picha kubwa ya rangi ikimuonesha Constebo wa Polisi PC akivunja kioo cha gari kwa kitako cha bunduki. Pia magazeti mengine ya siku ile yaliandika habari hile, na hata katika taarifa za habari za Luninga za vituo vingi vilionesha tukio lile katika taarifa ya habari ya saa moja asubuhi.
Kutokana na jeshi la Polisi kuandikwa vibaya katika magazeti, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam alipimpigia simu Kamanda wa kanda ya Kinondoni ili apate taarifa ya watu wale na kwa nini watu waliokuwa wamelala ndani ya gari badala ya kutumika mbinu za kuufungua mlango bila kuuharibu askari wake wakaharibu mali ya raia, kwani waliokuwa ndani ya gari ile hawakuwa na silaha ya kuhatarisha amani. Sasa kwa nini nguvu kubwa imetumika namna vile tena mbaya zaidi kilifanyika kitendo kile mbele ya waandishi habari. Hivyo wakatakiwa askari wale waliohusikia katika tukio lile waandike maelezo kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu.
Kamanda wa Polisi kanda ya Kinondoni alikuwa hana data kamili ya tukio lile ingawa alipopigiwa simu usiku na wanahabari kuhusiana na tukio lile kama limetokea, yeye alimpigia simu mkuu wa kituo cha Polisi Magomeni kutaka uhakika wa tukio lile, nae akamthibitishia kutokea kwa tukio lile ila hakuweza kwa usiku ule kwa mazingira ya tukio lile lilivyotokea, kupata majina ya wahusika. Ndipo Kamanda wa Polisi kanda ya Kinondoni akamuagiza mkuu wa kituo cha polisi Magomeni ahakikishe hadi ikifika saa nne asubuhi siku ya jumatatu awe amempa taarifa kamili ya tukio lile na majina ya wahusika. Huku nae akithibitisha kutokea kwa tukio lile kwa waandishi habari.
Ndipo Mkuu wa kituo cha polisi Magomeni ilibidi awahoji Rama na Faudhia yeye mwenyewe ofisini kwake ili apate kujua mambo yale kwa undani zaidi na yeye atowe taarifa kwa wakubwa wake kwa ukamilifu juu ya tukio lile.
Rama na Faudhia walitowa maelezo yao kama walivyoulizwa na Mkuu wa kituo, na Sajenti Mbago Kizega aliyaandika maelezo yale.
“Sasa kama mnasema mlikuwa hamfahamiani kabla ya siku ya jana kuonana, itawezekanaje kuwa katika gari moja iliyofungwa vioo na kutiwa loki milango yake? Tambueni kuwa tumewahoji walinzi wa Traveltine Hotel, na wao wametuambia hadi muda wa gari yenu mlivyoingia Hotelini pale. Kwani katika utaratibu wao wa kazi, walinzi wale huwa wanaandika kila gari inayoingia katika Hoteli yao, huwa wanaandika namba ya gari pamoja na muda ulioingia gari katika hoteli ile.”
Mkuu wa kituo alikuwa akiwahoji Rama na Faudhia, akiwa hakubaliani na majibu yao kuwa wao siyo mahawara wala walikuwa hawajuwani kabla ya siku ile pale.
Kabla hawajajibu swali lile Sajenti Mbago Kizega alimpa kipande cha karatasi mkuu wake wa kituo alichokuwa amekiandika kitu, na mkuu wa kituo baada ya kukisoma kikaratasi kile akainua uso wake na kuwatazama kwa makini.
“Mnaweza kunieleza kwa nini mlipoteza fahamu? Na kama hamkuwa mkijuwana kwa nini mkutwe ndani ya gari pamoja tena mkiwa mmelaliana?”
Mkuu wa kituo aliwauliza swali lile huku, akiwatizama kwa zamu katika sura zao Rama na Faudhia.
Rama ilibidi aeleze mtiririko wa tukio zima lilivyotokea tangu kule ufukweni, matukio yaliyotokea hadi kuwakutanisha na Faudhia na hatimae kufika pale katika Hoteli ya Traveltine kwa mazungumzo, akazizungumzia waraka alioachiwa na Rebeka pamoja na picha za Rebeka na Mtalaka wa Faudhia, kuwa ndiyo zilizomfanya yeye apotelewe na fahamu hadi alipopata fahamu na kujikuta Hospitali.
Faudhia nae pia akaeleza kwa kirefu kila kitu kuhusu tukio lile hadi kufika ufukweni hadi kuwa Traveltine, na tukio lililotokea ndani ya gari kwa yeye kumuonesha picha za mumewe Rama, hali aliyoipata Rama ndani ya gari baada ya kuona picha ya mchumba wake, akamalizia na yeye kupoteza fahamu baada ya kuupata waraka katika mfuko wa nyuma wa Rama, uliokuwa unaelezea kuambukizwa kwa virusi.
Mkuu wa kituo alitikisa kichwa kupokea taarifa ile kisha akavuta droo la meza yake, akatowa bahasha ya khaki, iliyokuwa na vitu ndani yake akavimwaga juu ya meza. Zilikuwa picha nane leseni ya udereva ya Faudhia, kadi ya gari halisi, pamoja na waraka wa Rama.
Mkuu wa kituo alizisambaza pale mezani pake picha zile akawa anazitazama ili apate kuhoji. Rama alipoiona sura ya Rebeka katika picha zile uchungu ulimjaa sana, donge likamshika machozi yakawa yanamtiririka kama maji.
Mkuu wa kituo alimuona Rama alivyokuwa akitokwa na machozi, akamuuliza kwa upole.
“Umesema huyu mwanamke amekuambukiza virusi na anasambaza virusi hivyo kwa watu wengine, je una uthibitisho gani kuwa anafanya hivyo, na siyo wivu wako tu unaokupelekea kusema hivyo?”
Rama alimtazama mkuu wa kituo kwa jicho kali, kisha akasema huku akiwa amekasirika sana ndani ya moyo wake.
“Mimi natoka hospitali nimepima na kipimo kimenionesha kuwa nimeathirika na virusi vya Ukimwi, huyu Malaya huyu ameniambukiza mie na anasambaza virusi kwa watu wengine kwa nini?!”
Mkuu wa kituo alimtazama Rama namna alivyokuwa ameumia kwa kuona picha ya Rebeka, akafikiri kwa kina kisha akakata shauri.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huyu Rebeka anachokifanya ni kuambukiza watu zaidi, na hii nikupoteza nguvu kazi ya taifa huo pia nao ni uhalifu, inapaswa achukuliwe hatuwa mara moja na hakuna watu wanaoweza kutusaidia katika hili ila ni nyie watu wawili”
Rebeka akatikisa kichwa kuafikiana na jambo lile, na mkuu wa kituo akawataka Rama na Faudhia wampe namba za simu za Rebeka na Faridi.
Rama akataja namba za simu za Rebeka, na Faudhia akataja namba za simu za Faridi bin Kacheche mzaliwa wa Ujiji Kigoma.
Mkuu wa kituo kile cha polisi akaziandika namba zile katika simu yake kisha akaanza kuzipiga moja baada ya moja lakini zote zilileta jibu moja kuwa hazipatikani.
Mkuu wa kituo alijaribu tena na tena kuzipigia namba zile, lakini hazikuweza kupatikana. Hivyo akaahidi kumsaka Rebeka ili wakimkamata wakampime virusi vya Ukimwi kwa nguvu na ikiwa atagundulika kuwa ameathirika, basi awekwe katika mkono wa sheria, kwani ule waraka aliompa Rama utatumika kama uthibitisho wa yeye kusambaza makusudi virusi vya maambukizi ya maradhi ya Ukimwi.
“Sasa mama Faudhia, gari yako imevunjwa vioo na askari wetu katika kuwahami nyie mle ndani ya gari mlimokuwamo, mkiwa mmezirai. Tulifanya vile baada ya askari wetu kuwagongea sana ili muamke lakini ilishindikana. Hatukuwa na hakika kama mpo hai au mmekufa mle ndani ya gari. Ndipo askari wetu waliokuwa katika eneo la tukio wakaamua kuvunja kioo cha gari yako. Kwani hata humu ndani ya kadi hii ya gari unasomeka wewe kuwa ndiyo mmiliki wa gari lile. Kwa niaba ya jeshi la Polisi naomba radhi sana kwa uharibifu uliojitokeza”
Faudhia alinyamaza kimya akiwa ametulia tuli pale chini sakafuni, kisha kama mtu aliepata jibu akamuuliza yule mkuu wa kituo kwa utulivu mkubwa.
“Kabla sijazungumzia hilo gari nilitaka kufahamu. sie tumeletwa hapa na kukalishwa chini kwa kosa gani, ikiwa mimi ndiyo nimevunjiwa gari yangu kioo kisha nakalishwa chini kama muhalifu?”
Mkuu wa kituo sasa akiwa tofauti na awali walipokuwa wameingia kina Rama ofisini mle, muda huu alikuwa hana kisirani wala ukali, akamjibu Faudhia swali lake huku akimtazama moja kwa moja usoni.
“Hospitali hamkwenda kwa miguu yenu, mlipelekwa na sie, hivyo hamuwezi kutoka hospitali na kuondoka zenu tu kienyeji bila kujuwa kilichojiri, kwani kufikia muda huu ninaozungumza na nyie, taifa lote la Tanzania kila mtu alieangalia Luninga jana usiku, leo asubuhi pamoja na magazeti wameandika habari zenu, hivyo hata viongozi huko juu wamesoma na kutazama taarifa ile ndiyo maana hata nyie ikabidi niwahoji mimi mwenyewe na Sajenti hapo aandike maelezo yenu. Na kwa kuwa mlipokuja hapa kabla hamjanieleza hayo mliyonieleza, nyie mlikuwa ni wahalifu kwa sheria zetu muhalifu hawezi kuwekwa kitini ila anakaa chini.”
Maelezo yale ya mkuu wa kituo yaliwafanya Rama na Faudhia kutazamana usoni, kwani hawakuwa na habari kama tukio lao lilirushwa katika Luninga, Faudhia ikampambazukia akilini mwake kuwa ndiyo maana Mumewe alipompa Talaka, sababu ya Talaka aliandika ni kudhalilishwa katika jamii. Akatikisa kichwa kuashiria kuelewa kitu.
“Sawa Afande nimekuelewa sasa, ina maana hata kuletwa hapa kwako pia ilikuwa ni kuja kukabidhiwa mali yangu si ndiyo?”
Mkuu wa kituo alitikisa kichwa juu chini kukubaliana na maneno yale.
“Ok hicho kioo nitanunua kingine bora salama tu hivyo naomba basi mnikabidhi gari yangu ili niondoke nikajipange kwani hapa nilipo mie sijala tangu jana, nasikia vidonda tumboni vinataka kunianza hapa.”
Faudhia alimjibu mkuu wa kituo na mkuu wa kituo akamueleza faudhia.
“Kuna utaratibu wa makabidhiano hatukabidhi kienyeji, hivyo Sajeti Mbago nenda kafanye nae utaratibu wa makabidhiano umpe gari yake, hapa hawana kesi ila Rama wewe bado nataka kuzungumza na wewe kidogo katika namna ya kufanikisha kumpata Rebeka, hivyo muwache huyo mwenye gari akakabidhiwe gari yake, wewe utabaki kwa muda ili tukupe mikakati ya kuweza kuisaidia polisi katika kufanikisha jambo hilo.”
Baada ya kusema maneno yale, Sajenti Mbago Kizega alitowa saluti kwa mkuu wake akatoka nje ya ofisi ile akiwa pamoja na Faudhia.
Mkuu wa kituo alimwambia Rama ainuke pale chini na kuketi katika kiti alichokuwa amekalia Sajenti Mbago Kizega. akapanga mikakati na Rama, ya namna ya kufanikisha kumtia mikononi Rebeka, Rama akapewa namba ya simu ya mkuu wa kituo ili kuwezesha mawasiliano na mkuu wa kituo, pindi atakapomuona au kupata habari zake wawasiliane.
Mkuu wa kituo alichukuwa picha zile akatafuta moja kati ya picha zile, akawa na kazi nayo katika kuhakikisha wanamtia mikononi haraka iwezekanavyo Rebeka Bint John Makuka, mzaliwa wa Tanga mjini.
Dakika arubaini baadae Faudhia aligonga mlango katika ofisi ya mkuu wa kituo, akaingia ndani ya ofisi ile akamkuta mkuu wa kituo akiwa na Rama wakizungumza.
“Mkuu nashukuru nimeshapewa gari yangu, ila kadi yake unayo wewe ndiyo nimeifata kwako Leseni yangu pamoja na picha zangu.”
Faudhia alimwambia mkuu wa kituo, kile huku akiwa amesimama wima akamuona Rama ameketishwa katika kiti.
Mkuu wa kituo alimkabidhi vitu vyake Faudhia kasoro ile pisha ya Rebeka aliekuwa akionekana kwa mbele uso wake ukiwa na tabasamu baada ya kuveshwa pete na Faridi muda mchahe baada ya kutoka kufunga ndoa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rama na Faudhia walitoka pamoja ofisini kwa mkuu wa kituo wakiwa huru, wakaelekea katika gari yao na kabla hawajaingia kupanda ndani ya gari wakapigwa na butwaa!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment