Simulizi : Moyo Wa Kupenda
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wakati huo nilikuwa nipo kidato cha tatu, nakumbuka tulipofunga shule mwezi wa kumi na mbili, nilipokuwa naondoka shule nikiwa natembea kwa miguu, ilitokea Pikipiki aina ya Watco ikanigonga kwa nyuma nikaanguka chini huku nikisikia maumivu makali sana. Yule dereva wa pikipiki alikimbia hakusimama kabisa. Mara wakatokea wanafunzi wenzangu wengi lakini walikuwa wakinipita tu bila kunipa msaada wowote huku wakinikebehi kuwa najisikia sana hivyo na wao hawana msaada na mie. Mara wakatokea wale wavulana niliokuwa nawachongea shuleni walivyokuwa wakinitongoza. Mvulana mmoja aliekuwa anaitwa Jackson Mwapachu alikuwa akiletwa na kuchukuliwa na gari kila siku na dereva wao, ila sijui siku ile ilikuwaje hata akaja na gari shuleni yeye mwenyewe. Nikiwa pale chini nimekaa naugulia maumivu ya mguu, akatokea Jackson Mwapachu, akasimamisha gari kisha wale wavulana wengine wakanibeba na kunipakia nyuma ya gari ile Pick up Toyota Hilux, kisha na wale wanafunzi wakapanda ndani ya gari ile, mie nikawa nimelala nyuma ya gari ile Pick up, sikuwa najua napelekwa wapi, japo nilikuwa nadhani labda napelekwa nyumbani au labda Hospitali ya Bombo lakini badala yake ilikuwa ni tofauti na mawazo yangu!”
“Kwa kuwa nilikuwa nimelala chali nyuma ya gari ile ya wazi, sikuona wapi nilipokuwa nakwenda kwani nilikuwa naona mbingu tu kwa namna nilivyokuwa nimelala. Ila maumivu yalinizidi sana kiasi nikaanza kulia kwa maumivu ya mguu, lakini pia nikiwataka wanishushe ili nirejee nyumbani, lakini sikupewa jibu lolote ila gari ile iliendeshwa huku ikikatishwa kona kadhaa hadi ikafikia wakati nikahisi kuwa sasa tupo katika njia ya vumbi, kwani gari ile ilikuwa ikiruka ruka kwa mashimo hadi iliposimamishwa gari ile , nami nikashushwa chini na vijana wale waliokuwa takriban watano wane wakiwa niliokuwa nao kule nyuma, na mmoja ni dereva aliekuwa akiendesha gari ile niliekuwa namfahamu kwa jina lake akiitwa Jackson Mwapachu. Waliponiteremsha chini wakaniambia kuwa mimi nimewapigisha bakora sana shuleni kwa kujifanya mjanja, sasa leo shule imefungwa kwa mwezi mzima hivyo wamekuja kulipiza fimbo zao. Kilichotokea kwa kweli ilikuwa ni kata funua, mbata ngumi na kila kichapo kutoka kwa wale wanafunzi wenzangu, walinikamata pale chini wakanitoa nguo yangu ya ndani, kisha wakaanza kunitemea mate, katika uke wangu wakanikojolea wakanimwagia mchanga, wakinidhihaki kuwa hicho ninachokilingia wao hawana mpango nacho, na kwamba hakina ubora ukilinganisha na wanavyokutana navyo wao. Baada ya kunidhalilisha walivyopenda wakaondoka wakiniacha pale na maumivu makubwa sana. Kitu ninachomshukuru Mungu pale hawakuniingilia wala hawakunitia hata kidole katika sehemu zangu za siri, ila walinipiga nikasikia maumivu makali sana mwilini, ukichanganya nay ale maumivu ya pikipiki ndiyo ilikuwa kama kidonda kikachomwa msumari wa moto. Nililia kwa nguvu lakini sikupata msaada wowote kutoka kwa watu, kwani kule kulikuwa ni porini sana sikujuwa hata nilikuwa nipo sehemu gani!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rebeka alinyamaza kuzungumza, kwani alishikwa na kilio cha kwikwi, Mkuu wa kituo akamnyamazisha ili aendelee kuzungumza yale mambo yaliomsibu, nae akafuta machozi akaendelea kuelezea mkasa uliomsibu.
“Pale niliishiwa nguvu nikapoteza fahamu, ila nilipokuja kupata fahamu, nikashangaa sana kwani sikuwa pale nilipokuwa awali ila nilikuwa ndani ya nyumba. Tena ilikuwa ni katika nyumba ya udongo iliyokuwa na ukimya mwingi. Nikiwa nimelala katika kitanda cha kamba wakati huo kikiitwa T,T.(Teremka Tukaze) Ila sikuwa na nguvu kabisa, na ajabu sasa nikawa nahisi maumivu makali mbeleni katika Uke wangu, nilipopeleka mkono kupapasa, nikashika uvimbe na mkono wangu ukatapakaa damu, laahaula nilikuwa nimebakwa, nimetolewa uanamke wangu niliokuwa naulinda kwa muda mrefu kwa nguvu zote. Ila ndiyo hivyo sikuwa bikira tena, mbaya zaidi sikumfahamu hata Yule alieniingilia ni nani na kama nimeingiliwa na mtu mmoja au watu wengi. Tena sikuwa nafahamu afya zao, kusema kweli iliniuma sana, ila sikuwa na uwezo wa kufanya, nikajuwa nyumbani watakuwa wakinitafuta sana hata kufikia kuniwazia mambo mabaya lakini ningefanyaje sikuwa na lakufanya”
Rebeka alipofika hapo, akasimama kuzungumza akaanza kulia upya kwa masikitiko. Mkuu wa kituo alimtazama akanyamaza kimya akitaka kujua khatma ya mkasa ule ulivyokwenda lakini pia Rebeka amalize dukuduku lake moyoni. Baada ya kulia kwa muda akaendelea kueleza zaidi.
“Nilijizoazoa pale kitandani nikakaa kitako, lakini nilisikia maumivu makali sana. Mara nikiwa katika kujishauri cha kufanya nikaona mlango ukifunguliwa, nikakaa palepale chini huku woga ukiwa umenishika sana. Mara akaingia mama mmoja wa makamo aliekuwa amevaa kanga mbili, akiwa amefutika kitu ndani ya nguo zake. Nikamtazama kwa makini mama Yule akaninyooshea kidole mdomoni mwake, akiniashiria ninyamaze nisipige kelele. Nilikaa kimya huku woga ukiwa umetanda katika moyo wangu, akanambia kwa kunong’ona kuwa pale nilipo siyo mahala pazuri, kwani pale nilipo nilikuwa katika mji wa Pangani, na kwamba nimefanyiwa kitendo cha uzalimu na wanaume tena watu wazima, wenye akili zao timamu. Pale nimeweza kuingiliwa na wanaume kumi kwa pamoja, yeye amepewa taarifa zile na shemeji yake, mdogo wa mume wake, baada ya suruali yake kukutwa na damu mbeleni kwake, akaulizwa na kaka yake kwa nini ana damu mbele katika suruali yake, ndipo alipomjibu kaka yake kuwa kuna dada bikira aliekuwa ameokotwa, akiwa hana fahamu yupo katika nyumba ya mzee Hau ambae mwenyewe amekwenda Dagoni Saadani kuvua samaki. Ndipo Yule Mama akaja kuniona ali athibitishe. Aliponikuta ndipo akanitaka niondoke mahala pale , kwani watu wale wamekwenda kuambizana wanaweza kuja tena na kuniingilia tena. Mama Yule akanipa Khanga mbili kisha akanitoa katika nyumba ile nyenye Uwa wa makuti, akanisindikiza njia iliyokuwa katika viunga vya Minazi hadi barabarani, akaniuliza kwetu wapi nikamwambia akaniuliza pale nimefata nini, nikamueleza kila kitu kilichonitokea akanitaka niende kwetu, alinipa nauli likaja Basi lililokuwa linafanya safari zake Tanga mjini na Pangani, nikapanda gari ile na kurejea nyumbani. Nilipofika nyumbani nikakutana na Baba aliekuwa ameketi barazani kama vile aliekuwa na mawazo mengi dhidi yangu, aliponiona jinsi ninavyotembea hata nilipomfikia nikamuamkia lakini baba hakuitika, bali alimwita Mama kwa sauti kubwa. Mama alipoitika na kutoka nje akanikuta mie nipo pale nje ninalia akanishika mkono kuniingiza ndani, Baba alimpiga mama vibao mbele yangu, huku akimlaumu kuniendekeza kuwa nimekosa heshima kwa kulala nje ya nyumbani na kwamba nimeanza umalaya. Baba akanifukuza akiniambia niende kuishi hukohuko nilipokuwa nimelala jana.”
Rebeka alisimama kusema akameza mate, kisha akamtazama mkuu wa kituo aliekuwa kimya kabisa akimsikiliza maelezo yake yaliyokuwa yakiingia katika Recorder yakihifadhiwa. Rebeka akaendelea kueleza habari ile.
Baba akanifukuza niondoke nyumbani hakutaka kuniona tena, vinginevyo niende na mtu alienizuia kurudi nyumbani. Mama alipotaka kunisindikiza ili akajue kilichoendelea mwanae hadi ikawa sikulala nyumbani na kwa nini natembea kwa kuchechemea, Baba akamkataza mama kutoka na mimi akimwambia kama atavuka barabara tu, akiwa na mimi hiyo ndiyo itakuwa Talaka yake, kwani mie nishaanza umalaya, nishaanza kulala nje, hivyo akanitaka niende nilipolala jana au nimpeleke mtu niliekuwa nae, hadi ikawa sikulala nyumbani. Mama aliniachia mkono wangu akahami ndoa yake. Akaniambia bora nikamlete huyo niliekuwa nae jana pale kwa baba ili mambo yaishe, lakini ningempeleka nani mimi katika mazingira kama yale nilivyokuwa? Ikabidi nimuombe radhi baba kuwa sikuwa nimelala kwa mtu ila pia nimebakwa mie, lakini baba alinifukuza kama mwizi akanambia nisikanyage nyumbani kwake, Mama yangu na mimi wote tulimuomba radhi lakini sikuwa na msamaha kwa baba nikafukuzwa nyumbani, nikaingia mitaani.”
Rebeka hakika alikuwa akihuzunisha sana kwani alikuwa akifuta machozi machoni mwake, kwa baba yake kumfanyia ukatili pasi na kutaka kufahamu mambo yaliyomtokea yeye akaona maamuzi sahihi kwake ni kumfukuza nyumbani kwake, mama yake roho ilimuuma lakini hakuwa na lakufanya zaidi kwani baba yake alishika hatamu, kwani hakuwa na amri ila maamuzi yalikuwa kwa mzazi wa kiume.Ama ule mfumo dume basi pale ulikuwa ndiyo umelala.
Rebeka aliondoka nyumbani kwao akawa hana pa kwenda, kwani maisha aliyokuwa akiishi hakuwa na rafiki ambae angekwenda kumlalamia ili akapitishe japo siku chache kwake, hivyo hali ile ilimuuma sana, kwani hakuwa na nguo zaidi ya zile alizokuwa amevaa, hakuwa na pesa ya kula, njaa itakapomuuma, hakuwa na mahala pa kulala, usiku utakapoingia. Mawazo yale yalimuuma sana, kwani aliona ndoto zake za kusoma kwa bidii na kufika mbali zilikuwa zimetoweka kabisa, akaamua aende Kituo cha Pilisi pale Chumbageni ili kuelezea tatizo lake. Alipofika pale akaelezea kilichomsibu Pangani. Lakini alipoulizwa kama anapajua huko alipofanyiwa tukio lile, kwake ilikuwa ni vigumu sana kupafika tena. Lakini pia alipotakiwa kueleza kama akiwaona watu waliomfanyia tukio lile la kumbaka kama ataweza kuwatambua, akasema hawajuwi kwani tukio lile alifanyiwa akiwa amezirai. Bado akaulizwa kama anaweza kumpata Yule mama aliempeleka yeye njiani ili akaeleze kilichomsibu, pia akasema hamfahamu kwani sehemu yenyewe ilikuwa ni mbali sana. Polisi wakamwambia hawana namna ya kumsaidia ila wakampa RB kama ikitokezea kuwaona hao watu ambao yeye alishasema hawafahamu, akaambiwa aripoti taarifa ile kituo chochote kilichopo jirani nae pia wakampa na PF3 ili aende Hospitali kwa matibabu. Huo ukawa ndiyo mwisho wa Polisi msaada wao, kwani wangemkamata nani?! Ujinga alioufanya Rebka hakueleza namna alivyofikishwa mahala pale hadi akakutana na matatizo, bali yeye alisema tatizo moja kwa moja. Lakini hata kama angelisema watu waliomfikisha pale, aliona wale siyo waliombaka.
*******
Faudhia baada ya kufata gari yake alitafuta Lodge, akalipa akaingia kupitisha mapumziko kwa muda akitafakari kwa kina namna ya mustakabali wa maisha yake. Alifikiri sana akawaza na kuwazua, kuna wazo ambalo lilipita katika moyo wake ambalo hakutaka kulipuuza hata kidogo. Alilitafakari wazo lile kwa makini, akalitazama mwisho wake kama litakuwa na kheri akaona huo ndiyo uamuzi pekee wa busara kama atautumia katika maamuzi yake.
Moyo wake ulikuwa unapingana na maamuzi yale lakini baada ya muda wazo lile linarudi kwa kasi sana. Kila akijaribu kulipotezea lakini wazo lile linakaa tu, ndipo alipoamua kwenda hospitali kwa ajili ya kuwapelekea chakula lakini pia kuwapa uamuzi wake alioufikiria kwa kina.
Faudhia alitoka nje ya Lodge ile ikaenda kununua viazi na kuku mara mbili, vyote akaenda navyo hospitali akaingia wodini akampa mfuko mmoja Faridi, pia akaenda katika kitanda cha Rama akampa ule mfuko wa pili, akawakaribisha chakula. Rama hakuweza kula vizuri kwa mawazo mengi kwani alikuwa akihisi uchangamfu wa Faudhia katika muda ule, haukuwa kama wa awali, hivyo akahisi kuwa lazima kuna jambo.
Faridi alizitazama zile chipsi, akala chipsi mbili tatu akashindwa kuendelea kula zaidi, kwani na yeye hakumfahamu kabisa Faudhia muda ule kwa namna alivyokuwa amebadilika sana, hakuwa mchangamfu kabisa alikuwa ni mtu wa mawazo tele. Alimwita Faudhia akamwambia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Vipi unajisikia vibaya mbona upo hivyo?! Nakuona huna amani kabisa kulikoni, kama hujapata jibu muafaka nakutaka uache hadi kesho ndiyo utoe maamuzi yako kwangu, kwani nakuona huna amani kabisa.”
Faudhia alitabasamu kisha akamjibu faridi kuwa yupo sawa hana tatizo lolote, na yupo tayari kwa majibu. Faridi akahisi kwake majibu yale yanaweza yasimpendeze sana, hivyo akasubiri ili asikie hilo jibu lake ili atambue kama kusuka au kunyoa.
Wanaume wale wote kwa pamoja walikuwa mashaka yamewajaa mioyoni mwao, hivyo wote kama ungewapima mapigo yao ya moyo basi yangekuwa yapo juu kabisa. Ama kweli moyo wa kupenda una maajabu sana. Yaani pamoja wao wameumizwa na mwanamke mmoja, lakini bado pia wakati huu wanaumiza vichwa vyao kwa mwanamke mmoja.
Faudhia alimwambia Faridi kuwa asogee mwanzo wa kitanda ili atakapokuwa akizungumza aongee kwa wote watu wawili kwa pamoja wawe wakisikia kuliko kuongea na mtu mmoja mmoja. Faridi alifanya vile, Rebeka akamfata Rama yeye akamtaka akae mwisho wa kitanda chake ili awe yupo jirani na kitanda cha Faridi ili akizungumza awe anazungumza kwa watu wote. Rama akatii maagizo yale akasogea mwisho wa kitanda ili asikie maamuzi yake.
Baada ya wote kukaa kwa karibu, huku kila mmoja akiwa makini kusikiliza, ndipo Faudhia akasimama kati kati yao akatowa majibu ambayo yalimshangaza Faridi, lakini pia yakamshangaza na Rama vilevile.
“Nimekaa nikawaza nikafikiri kwa kina, na hatimae nikapata jibu sahihi kwa wakati sahihi, nimeamua kwamba kuanzia sasa sitakuwa na yeyote kati yenu. Nitabaki niishi peke yangu. Kwani nyie wote kila mmoja hapo alipo ni muathirika, hata kama Faridi ukipima sasa hivi hutoonekana kama ni muathirika ila naamini miezi mitatu baadae utakuwa ni mtu ambae vinaonekana virusi vyako. Halkadhalika Rama nawe tayari imeshathibitika kuwa ni muathirika, hivyo hatutaweza kuishi nami nikawa na amani. Kama ambavyo kwa Faridi nitakuwa na uoga huohuo ndiyo na kwako pia nitakuwa na woga pia, ndiyo maana ili niishi kwa amani ni bora niwe peke yangu. Kwa kuwa kuishi peke yangu ndiyo jawabu pekee na sahihi zaidi kwangu.”
Hali ikawa tete kwa Faridi, lakini ikawa tete zaidi kwa Rama.
Faudhia baada yakusema maneno yale, alitoka nje ya wodi ile moyo wake ukiwa unamuuma sana, asielewe kwa nini. Alikwenda nje hadi katika gari yake, akafungua mlango akaingia ndani huku donge likimjaa moyoni akaanza kulia kwa kwikwi. Alilia hadi mafua mepesi yakamtoka kisha akajiuliza kwa nini alie wakati aliyoyafanya ni maamuzi sahihi kabisa, maamuzi yakuokoa maisha yake, lakini pia maamuzi ya kuondosha chuki baina ya Rama na Mtalaka wake Faridi. Baada yakujiuliza sana hatimae akapata jawabu kuwa ni moyo wa kupenda ndiyo unaomsumbua.
Alifuta machozi, akaingia tena wodini ili akawaage kisha ashike njia ende zake lakini hali aliyoikuta wodini mle ilikuwa kama ni kwenye moto kisha akaweka mafuta ya petrol juu yake.
Kwani alimkuta Faridi amejiinamia akiwa hana la kufanya uso umemuwiva sana, lakini hakuthubutu kutoa chozi, ila alibadilika sana. Hali ikawa tete kwa Rama kwani alikuwa amejilaza kitandani kwake, akiwa amelala kifudifudi, viganja vya mikono yake, akiwa ameufunika uso wake akilia kwa kwikwi machozi yakipitiliza katika mikono yake na kudondokea katika shuka za kitanda kile. Faudhia alimfata Faridi akamshika bega lake kisha akamwambiakwa sauti ya upole.
“Faridi acha kuwaza sana, kwani hayo ni maamuzi ambayo leo nimekuwa nayo huwezi jua labda kesho yanaweza kubadilika, ila hadi sasa huo ndiyo msimamo wangu, ila sitaki nikufuru kwamba sitoweza kubadilisha maamuzi yangu hapana Mungu yeye ndiyo anaejua zaidi, ila kwa sasa rizika na hayo tu, kwani ningelikuwa nimekufa baada ya kunitenda nadhani ungeweza kuishi na mtu mwengine basi nakusihi usiwe mnyonge naomba unielewe.”
Baada yakusema maneno hayo Faudhia aliondoka akaenda katika kitanda cha Rama, akamshika mabegani kwake huku akimwita jina lake, Rama akageuka akamtazama usoni mwake, Faudhia nafsi yake ikazidiwa nguvu akajikuta yale machozi, na kilio kilichomtokea ndani ya gari kinakuja tena kwa kasi ya ajabu, akajizuwia asilie lakini alikuwa akishindana na moyo wake, kwani machozi yalipenya katika kingo zake yakatiririka mashavuni mwake. Rama hakutaka kumpa nafasi Faudhia yakuongea kwani alizungumza yeye maneno ambayo yalimuingia sana Faudhia katika moyo wake. Kwa uso wenye huzuni na wenye kutoa machozi, Rama akasema.
“Faudhia ninayaheshimu sana maamuzi yako, ingawa kwa kiasi kikubwa sana yameniumiza katika moyo wangu, uliokuwa umepata faraja na matarajio ya kuenziwa, kumbe ilikuwa nafikiri sivyo. Basi bora ungeniacha nikafa Fau kuliko kunipigania nisife kule pwani, kisha uje kunitelekeza huku umefufua maumivu yangu Faudhia, umekitonesha kidonda cha moyo wangu.”
“Rama lakini wewe ni muathirika utambue, na kwamba ningekaa kwa woga na wewe, pia kuna baadhi ya vitu ningeshindwa kujiachia na wewe, kama ingelikuwa na mimi nimeathirika kusingekuwa na pingamizi, lakini ndiyo hivyo Rama lisilo budi hutendwa. Naomba uyakubali maamuzi yangu na nakuombea Mungu akupe salama, ili uishi kwa muda mrefu zaidi, kwani mimi sitoweza kuishi katika mji huu tena, itabidi niende mikoani au visiwani nikaanze maisha mapya, ila pindi mwaka kwako nimeshapafahamu nikija Dar, basi nitakuja kukutembelea kukujulia hali.”
Faudhia wakati alipokuwa akisema maneno yale, machozi yalimzidi zaidi, akataka kutoka nje aondoke lakini Rama akamwita akamwambia;
“Faudhia nakushukuru sana kwa kila jambo ulilonitendea, lakini pia nakuomba msamaha ikiwa katika kukaa kwetu kwa muda mfupi kama nimekukwaza. Kwako nakili kuwa hujanikosea hata kidogo, hivyo nakuomba popote uendapo Mungu akikuruzuku mtoto wa kiume, narejea tena kauli yangu naomba umpe jina langu kama kumbukumbu, mie siwezi kuzalisha tena kwani maisha nishayakinai, hivyo ukisikia nimekufa, nitafuhi sana kama utakuja katika mazishi yangu, au kaburini kwangu ukaniombea dua, asante sana kwa heri yakuonana!”
Rama alinyamaza kuzungumza akalala kama alivyokuwa awali akalia hadi akapitiliza, kikohozi nacho kikaja kwa kasi akakohoa kwa sana, hatimae akawa kimya ahemi wala hasemi. Faudhia alimfata Dokta Neema Mnyampala aliekuwa akimuhudumia mgonjwa mwengine akamweleza kuhusu hali ya Rama, kisha yeye akatoka nje akaingia ndani ya gari yake huku akiwa amenuna na donge kubwa likiwa limemjaa moyoni mwake, akarudi pale Lodge alipochukuwa chumba siku ile, akaipitisha siku akiwa pale, huku akipanga na kupangua namna ya kuanza upya maisha yake yaliyoingia dosari.
Dokta Neema Mnyampala, alipofika katika kitanda cha Rama akamuona Rama akiwa katika hali mbaya sana, haraka Drip zikatundikwa akawekewa ili kuyanusuru maisha yake.
Faridi aliwaza na kuwazua uchungu mwingi ulimwiingia, katika moyo wake akamlaani Rebeka kwa kumshawishi amuache mkewe kwa Talaka tatu, halafu yeye akaamua amuibie na kutokomea mbele ya safari, kama hiyo ilikuwa haitoshi kumbe pia alikuwa ameathirika. Kwani alikaa na Faudhia akimuachia pesa hadi milioni mia moja, lakini pesa zake alizikuta zikiwa timamu kabisa bila yakupunguzwa hata senti tano.
Akiwa katika kutafakari huku hali yake ikiwa imeimarika, mara simu ya Faridi ikaanza kuita, Faridi aliipokea simu ile, akapewa ujumbe katika simu ile asioutarajia!
*******CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rebeka aliondoka pale kituo cha Polisi, ndoto za maisha yake zikiwa zimekatika zote. Akaingia katika mitaa huku tumbo likimtia adabu kwa njaa. Aliingia katika migahawa kuomba chukula, lakini alitimuliwa kama mbwa, hakupata msaada wowote ila baadhi ya wanaume walimdhihaki kuwa wakamuweke nyumbni kwao ili apike nakupakua akae kinyumba. Jambo hilo lilimuuma sana Rebeka. Alihanja katika mitaa akatanga na njia akaokota mabaki ya chakula katika mapipa ili aishi. Kivumbi kilikuwa usiku kwani alikuwa hana pakulala, kila alipojiegemeza katika vibaraza vya nyumba za watu ili kupata usingizi, alifukuzwa na wahuni wakitaka kumuingilia kwa nguvu. Rebeka hakuwa anafahamu chochote kuhusu kitu mapenzi maishani mwake.
Hali ya maisha yake Ilikuwa hivyo kwa kila siku ya Mungu, hadi siku moja katika kuupitisha usiku alikuwa amefika barabara ya ishirini na moja, kulikuwa kunakesha ngoma ya Baikoko, nae japo hakuwa mpenzi wa ngoma hiyo lakini ilimbidi akakeshe kwa kutizama ngoma hiyo ili asubuhi ifike awe usiku wake umepita, lakini pia ataweza kuzamia na kula chakula.
Ilipofika wakati wa mapumziko wasanii wa ngoma ile ya Baikoko wakatakiwa waende kula, ndipo na Rebeka alipojipenyeza katikati hadi katika chakula kile, akakaa na wadada wanaokatika katika ngoma ile. Wadada wale walimtazama, wakamwambia mbona anajifuja wakati ana uzuri namna ile, wakamuonea tunu umbo lake alivyo, wakampenda sana kiasi wakamshawishi ajiunge nao ili apate ajira ya kujikimu, kwani walimwambia kuwa yeye ni mzuri ila hana matunzo kama angepata matunzo angekuwa moto wa kuotea mbali! Rebeka kwa maisha aliyokuwa akiishi hakutaka kujiuliza mara mbili bali alikubaliana na ushauri wa wale wacheza ngoma ya Baikoko, ambao kimri alikuwa akifanana nao, ila yeye alikuwa ni mzuri wa sura na umbo ukilinganisha na wale wadada.
Rebeka kwa kuwa maisha yake yalikuwa hayana kichwa wala miguu, ikabidi awagande wale madada hadi asubuhi ngoma ile ilipomalizika na yeye akapanda gari na wasanii wale, akaenda nao masikani kwao Makorola. Alipokuwa kule angalau aliweza kupata kuoga na kula ingawa hakuipenda kazi ile yakucheza viuno mbele za watu, lakini angefanyaje hakuona kazi nyingine ya kufanya kutokana na uchache wa elimu yake, lakini pia hakuwa na mtaji wa kumfanya japo afanye biashara ndogondogo. Ikabidi mle katika kundi lile la wachezaji ngoma ile wamfundishe kukatika viuno, ili aweze kumudu kucheza ngoma ile yenye kutaka matao. Rebeka akajitahidi kujifunza hadi akawa ameweza, akaweza kunyonga kiuno taratibu, lakini pia akanyonga kiuno kwa kasi kutegemea na mipigo ya ngoma inavyokwenda.
Rebeka alifundishwa kula milaa (Mirungi) ili kupata handasi yakuondosha usingizi akiwa yupo katika maonesho, akawa akivaa khanga yake moja na nguo ya ndani tu, kisha akatike huku mdomoni akiwa amejaza lundo la mirungi katika mashavu yake. Ilikuwa kama ungebahatika kumuona Rebeka alivyokuwa akikatika, hakika hutotaka aache kucheza. Rebeka wanaume walimtunza pesa nyingi huku wakimuhonga aondoke nao akafanye nao mapenzi. Katika siku za mwanzo alikuwa akikataa, lakini wenzake walimshawishi ikawa na yeye anakwenda hadi akazowea.Ikawa kila wanapokwenda katika kucheza basi siku hiyo wanaume aliwapanga foleni, kwani alikatika katika hali ambayo, kila mkwale angetaka ende nae ndani ili akaone peke yake mambo yale.
Katika kikundi kile kilichokuwa kikimilikiwa na mama mmoja wa makamo aliekuwa akiitwa Mwanamkasi, yeye alitokea kumtunuku Rebeka kwa namna alivyokuwa hana maringo, hodari wa kazi pamoja na uzuri wake, wa sura na umbo lakini pia alikuwa siyo kiburi, alikuwa maridhia sana kwa watu wote. Mama Yule alikuwa akimnunulia nguo za thamani, akimpa pesa na kila mahitaji aliyokuwa akiyataka, lakini kumbe alikuwa na lake jambo. Siku moja alimwambia Rebeka asilale na wenzake bali akalale nae chumbani mwake, ndipo alipokwenda kulala nae siku hiyo Yule Mama Mwanamkasi, akamuomba Rebeka amfanyie usafi chini mbeleni kwake, akampa mashine yenye wembe, akatandika khanga kitandani kwake, Mwanamkasi akawa kama alivyozaliwa ili afanyiwe usafi na mwanawe mlezi.
Rebeka hakuona tatizo kumsafisha mama yake mlezi, lakini kadiri alivyokuwa akimnyoa, mama Yule alikuwa akiugulia kwa sauti za mahaba, Rebeka akashangaa alipomuuliza kama alikuwa akimuumiza katika kumnyoa kwake hadi anaugulia, Mwanamkasi akamwambia hapana anamnyoa vizuri sanaila anamtia ashki. Rebeka akaendelea kumnyoa taratibu hadi akamaliza.
Mwanamkasi akamshukuru Rebeka kwa kumsafisha vizuri, akamwambia haya bado zamu yako, Rebeka nae hakufanya ukaidi kwani hakika pori alikuwa nalo. Hivyo akataka kutoa Khanga yake ili atandike, lakini Mwanamkasi akamzuwia akaitandika Khanga yake nyingine pale walipotoa ile ya awali. Mwanamkasi akaanza kumnyoa taratibu huku akimpapasa, katika maeneo anayomnyoa akampandisha mzuka, hatimae Rebeka akawa jicho lake zito halifumbuki, Mwanamkasi alipomuona Rebeka amelegea kabisa kwa huduma ile, akaacha kumnyoa, akaanza kumpetipeti sehemu zake nyeti, alimshika kwa mikono, akatumia ulimi kufanya kinembe cha Rebeka kivimbe juu kwa kuandaliwa naam kikafanikiwa kuwa kikubwa kama moyo wa kuku! Rebeka alikuwa akipiga kelele za mahaba ambazo hakuwahi kuzipata kabla katika umri wake mdogo aliokuwa nao. Mwanamkasi aliendelea kumtia wazimu Rebeka hatimae akampandia juu,akakutanisha inembe chake na cha Rebeka kilichokuwa kimevimba kwa kunyonywa, akaanza kumsaga taratibu huku Rebeka akisikia raha ambayo hajawahi kuipata tangu azaliwe, raha ile ilipomdidi bila kuambiwa wala kuelekezwa Rebeka alijikuta akianza kuicheza Baikoko pale juu ya kitanda. Alicheza kwa ustadi mkubwa sana Mwanamkasi akawa anaongeza kasi, na Rebeka nae akawa anaongeza kasi ya kukatika na kusagana hatimae walikamatana kwa nguvu huku wakipiga kelele za mahaba, wakatua safari yao.
Rebeka alipopewa raha ile iliyokuwa haramu katika dini zote duniani, akanogewa sana ikawa kila siku anataka kuifanya, Mwanamkasi nae akazidi kumpenda Rebeka, ikawa hana anachotaka asimpe, pia ikawa anamuonea wivu hadi kwa wanaume waliokuwa wakimtaka Rebeka, ama kweli Shetani ana nguvu kubwa ya kutenda maasia.
Mwanamkasi alikuwa akiishi peke yake Mumewe alishafariki siku nyingi, ila alikuwa hataki wanaume yeye starehe yake ilikuwa ni kwa watoto wa kike, umri wake na vitendo vyake vilikuwa haviendani kabisa, Pamoja na umri wake lakini alikuwa mavazi yake akipendelea kuvaa, nguo za kiume na kofia za kapelo. Alikuwa akimfundisha kunywa pombe na kusaga mirungi Rebeka, hatimae akawiva akabobea, akawa hashikiki, hakamatiki hana burudani asiyoijuwa Baikoko ilikuwa akicheza hadi apende mwenyewe, kwani Mwanamkasi alikuwa akimzuwia kufanya hivyo, akichelea wanaume kumchukulia mpenzi wake.
Rebeka siku moja alitamani kwenda kuwaona wazazi wake, kwani siku zote alikuwa akiwadanganya wenzake kuwa wazazi wake hawapo pale Tanga mjini, alikuwa akiwaongopea kuwa wazazi wake walikuwa wakiishi Buyuni nje ya Mkoa ule wa Tanga.Lakini siku hiyo alimkumbuka sana mama yake, ikiwa ni muda wa mwaka mmoja umepita tangu aondoke nyumbani kwao, alijifungasha akambebea zawadi mama yake, akajisemea moyoni kuwa inambidi akamuone mama yake japo kwenda na kutoka, hata kama Baba yake, atamfukuza lakini atakuwa ameshamuona Mama yake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rebeka alijipamba vyema siku hiyo, akapiga pamba siyo kawaida hadi Mwanamkasi, ilikuwa nusura amkataze kwenda safari aliyoagwa ya kwenda Buyuni kuwaona wazazi wake, kumbe alikuwa akiongopewa kwani Rebeka alikuwa akienda Ngamiani. Aliogopa kumwambia kama wazazi wake wapo wanaishi mjini pengine angetaka kwenda kupajua, ndiyo kisa akamuongopea ile safari ya mbali ili asiweze kwenda.
Rebeka alitoka akapanda daladala ya Makorola inayokwenda Ngamiani sokoni pale karibu na stendi kuu akiwa amefungasha mizigo yake huku furaha kwa mzazi wake, ikiwa imemjaa tele moyoni mwake, kwani mzazi ni mzazi. Akiwa ndani ya gari alimkumbuka mama yake alivyotaka kwenda nae amsindikize ila baba yake alimkataza, akaikumbuka kauli ya Baba yake kwa mama yake kuwa akivuka tu barabara itakuwa ndiyo Talaka yake.
Rebeka alipiga moyo konde akaona safari hii, labda Baba yake atalegeza nguvu zake alizokuwa nazo awali, hasa baada yakutoonana kwa takribani mwaka mmoja. Aliombea ile gari iruke ili afike kwa mama yake, akawa anapanga moyoni mwake kuwa atakapomuona tu mama yake atamkimbilia atamrukia amdandie, acheke na afurahi. Alifikiri jinsi mama yake atakavyokuwa na furaha kubwa kwa kumuona mwanawe, akapanga namna atakavyomshangaza kwa zawadi zake. Hakika alipanga vitu vingi sana moyoni mwake, hivyo akasubiri afike tu ili akatimize yale aliyoyakusudia.
Gari ipofika Stendi kuu, ya mabasi Rebeka alikuwa wakwanza kuteremka, akajiweka vizuri nywele zake, akajipangusa vumbi kwa leso yake, akaanza kupiga hatua kuelekea nyumbani kwao ambapo hapakuwa mbali na kituo kile cha mabasi. Rebeka alitembea kwa mwendo wa pole ili asitoke jasho akaiharibu Fondishna yake na Angelface, aliyokuwa amejipamba vyema kabisa usoni mwake. Nguo zake alikuwa amezifusha Udi wa Mawaridi, pamoja na Mkadi na vihalua, hakika Rebeka alikuwa akionekana ni Halati hasa kwani kila aliepishana nae, aligeuka kumtazama. Rebeka alikuwa amependeza, amenenepa umbo lake zuri na nguo alizovaa za dashdash alikuwa anaonekana ni mke wa mtu mwenye pesa zake.
Rebeka alipokaribia nyumbani kwao, akashangaa sana kuona turubai kubwa limefungwa barazani kwao! Akajiuliza ilikuwa ni shughuli ya nani, lakini kadiri alivyokuwa akipiga hatua kuisogelea nyumba yao, ndivyo ilivyokuwa haimuingii akilini kuwa ile, ni shughuli kwani hakukuwa na shamrashamra zozote, wala sauti za music kutumbuiza mahala pale, lakini alipoutazama mlango wa nyumba yao, akaliona pazia likiwa limefungwa mlangoni, kuashiria kuwa kuna msiba!
Rebeka aliongeza hatua hadi pale mlangoni, akiwa ametaharuki akalifunua lile pazia akaingia ndani huku akiita;
“mama, mamaa, mamaaaaa!”
Lakini hakuweza kuitikiwa na Mama yake, badala yake majirani ndiyo waliangua kilio, wakililia msiba ule. Mama mmoja mtu mzima akamvuta Pembeni, akamwambia kwa upole.
“Pole mwanangu umeshakuwa Yatima, kwani Mama yako pamoja na Baba yako jana wamezikwa kutokana na ajali ya gari iliyotokea juzi, waligongwa na gari wakiwa wanakatiza Barabara pale Mabanda ya Papa, wakiwa wameshika usawa wa barabara ya Madina wakafariki Dunia pale pale hivyo huna Mama wala Baba mwanangu!”
Rebeka aliposikia maneno yale, moyo wake ulimuuma sana, alilia kwa uchungu mkubwa lakini baadhi ya waombolezaji walikuwa wakimtazama macho tu, kwani taarifa ya yeye kuwa ni mcheza ngoma ya Baikoko ilikuwa ishaenea, hivyo walimuona kama vile mtoto alielaanika, aliekosa razi za wazazi wake kwani ametoroka kwao na kwenda kwa bwana, hata alipoambiwa aondoke na wazazi wake akamlete mtu aliekuwa amemficha ndiyo akaenda kimoja hakutaka kurejea nyuma.
Watani walipomuona Rebeka analia kwa uchungu, walimnyamazisha kwa kumtania kuwa anyamaze yeye ndiye alieleta uchuro katika familia ile, kwa kuwatelekeza wazazi wake akaacha shule, akenda kuufanya uhuni mitaani. Kwa hiyo hakutakiwa kulia kwa msiba ule.
Maneno yale japokuwa yalikuwa yakisemwa na watani ambao wao hupewa pesa kwa kusema ujinga tu katika jambo la msiba linalomuumiza mtu, yaliuchoma moyo wa Rebeka, akaona chanzo cha matatizo yote hayo kutokea ni wanaume. Kwani wanaume ndiyo waliomfanya hadi akafukuzwa nyumbani kwao na kwenda kuangukia katika maisha ya kimalaya, yasiokuwa na chembe ya heshima katika jamii inayomzunguka. Rebeka akaapa kulipa kisasi kwa wanaume katika maisha yake kwa kuwekwa mbali na wazazi wake, kumfanya akatishe masomo yake pamoja na malengo yake ya kusoma kwa bidii ili aje kuwafaa wazazi wake, lakini badala yake amefitinishwa maisha yake na wazazi wake, amekatishwa kila kitu chake akazitazama zile zawadi alizokuwa nazo mkononi mwake, akazidi kulia kwa kulombokeza, kiasi aliwaliza watu wengi waliokuwa pale msibani.
“Mama umeondoka bila yakuniona mwanao, mama nilikuletea zawadi umezikataa mama, mama umeniacha peke yangu mie katika dunia hii, mama ulinisindikiza siku ile kumbe ndiyo ulikuwa ukiniaga, aaa mama yangu weee, mie sasa ndiyo nimekuwa sina kwetu tena, naishije mie mama, mie nilikuwa narudi nyumbani mama, maisha yakuishi mapamba nje sikuwa nayataka mamaaa, mama wanaume walionifanya hivi mamaaa, wamenitoza nguvu kwani wajua mara ngapi nimewaletea kesi zao kwenu, ooo mamaaaaaa”
Watu wazima waliokuwa pale na wao wakaangua kilio kwa maneno ya Rebeka, ikawa kama vile msiba ndiyo umetokea muda ule. Vilio vilishamiri Rebeka akaanguka chini akagalagala kwa uchungu huku akisema kwa masikitiko.
“Nisamehe baba yangu huko ulipo, mwanao nilikukosea mimi, japo halikuwa kosa langu. Baba hukutaka kunisikiliza ukanifukuza mwanao leo naishi kwa kudhalilishwa yote hiyo ni kwa maamuzi yako baba yangu, nimekula vyakula katika mapipa niliekuwa nakula chakula kizuri nyumbani, Baba kwa nini uliamua vile baba yangu, ungenisikiliza mwanao kisha ukanisaidia babaa, mimi ni mwanao usingeongeza maumivu katika maisha yangu babaa, wanaume wenzako wameniharibia kila kitu changu, baba na wewe ukanisaliti ukanifukuza, aaaa babaaa nisamehe, eee Mungu wasamehe wazazi wangu huko walipo, najua mioyo yao ilikuwa ikitembea na kusema juu yakuondoka kwangu, natambua nafsi zao zimejikunja, kwa kutokuona hata maiti zao. Mama sikuweza hata kukuosha mama yangu nimeshindwa kukuhifadhi mama, sikuona maiti zenu wazazi wangu. Kuanzia leo sitorudi tena Makorola basi sitaki tena maisha yale, ila naapa kwa nyumba hii, naapa katika msiba wa wazazi wangu wawili walionileta katika dunia hii, nitalipiza kisasi kwa wanaume, nitalipa lazima iwe isiwe!”
Rebeka alilia sana akapoteza nguvu, akazirai wakamkimbiza hospitali kwa matibabu zaidi. Alipokuja zinduka akawaambia watu waliokuwa wamempeleka hospitali pale Bombo, wampeleke katika Makaburi waliolazwa wazazi wake, majirani wale hawakumfanyia hiyana walimuongoza hadi katika makaburi waliolazwa wazazi wake, alipofika kule akayaona matuta mawili mapya ya wazazi wake, akaonesha kila moja alikuwa amelazwa nani uchungu ukaongezeka mara mbili ya mwanzoni, Rebeka akagalagala katika kaburi la mama yake, huku akilia kwa uchungu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mama umeniacha mama, mama umeondoka mama, nani atanidekeza katika Dunia hii mimi, mama Dunia hii nitasimangwa mama, watu watanichukia mama, mama rudi mama, Mungu ungenichukua mie ukamuacha mama yangu na baba wakaishi, ooo wazazi wangu.
*******
Mkuu wa kituo cha Polisi Magomeni alifuta machozi, kisha akamwambia Rebeka kwa utulivu. “Hakika umepitia majaribu makubwa sana, umepita katika mitihani mingi sana, lakini ulijuwaje kama wanaume wale kumi kama ndiyo waliokuambukiza virusi vya Ukimwi hata wewe, ukakusudia kuwaambukiza wanaume kumi ili ulipe kisasi chako?!”
“Siyo wanaume wale kumi kama ndiyo walioniambukiza Ukimwi, laa sina hakika na hilo ila kule kunifanya niwe mbali na wazazi wangu, hata wazazi wangu wakafariki Dunia nikiwa nipo mbali nao, ndiko kulikonifanya na mimi baada ya kupima virusi nikaonekana nimeathirika basi niwaambukize wanaume kwa idadi ile ambayo walionivunja uanamke wangu. Hivi niongeapo na wewe wale waliokuwa wanafunzi wenzangu, mara baada yakujigundua nimeathirika, niliwatafuta mmoja baada ya mmoja nikawashawishi kutembea nao nikiwaeleza kule kukataa kwa siku zile nilipokuwa shule nilikuwa ni motto sijaanza kutembea na wanaume, ila nimekuwa na kwa kuwa wao walikuwa wakinitaka sana na walipigwa kwa ajili yangu, nimeona niwape wote kila mtu kwa wakati wake wakakubali na hivi sasa tayari wapo kaburini, kwani kila mtu niliekuwa nimemuambukiza, sikuacha kumuachia ujumbe au cetin a dawa nilizokuwa nikitumia ili wafahamu kuwa na wao wafe kama walivyokufa wazazi wangu nikakosa kuwaona kwa sababu yao.”
Rebeka akaeleza kila kitu katika kuambukiza kwake wanaume virusi hadi kufikia idadi ya mtu wa tisa ambae ni dereva wa taxi misifa. Akieleza kwamba idadi hiyo ni tangu alipojigundua kuwa ni muathirika. Akaeleza pia aliondoka Tanga baada yakuwa akitafutwa na Mwanamkasi ili kwenda kufanya uchafu nae (kusagana), pamoja na wanawake wengine kadhaa waliokuwa wamesikia kuwa mwanamkasi anasagana na Rebeka na wao wakawa wanamtaka ili wacheze nae upuuzi ambao sasa anajuta kuufanya katika maisha yake.
Mkuu wa kituo aliingiza mkono wake katika droo ya kabati lake akatoa karatasi iliyoandikwa kwa mkono, akaiweka mbele ya uso wake akamuuliza kama anaufahamu ujumbe ule, Rebeka akatikisa kichwa kuwa anaufahamu ndiyo ujumbe aliomuachia Rama nyumbani kwake kabla hajemda kuolewa na Faridi.
Pia mkuu wa kituo akamuhoji kuwa haoni kuwa yeye ndiye chanzo cha kumfanya Faudhia aachike kwa Faridi.
“Mimi naweza kuwa chanzo, lakini kwa hahika mimi ndiyo niliotaka Faudhia aachike tena aachike Talaka tatu, kwani sikutaka Faudhia aingie katika kadhia hii yauathirika ndiyo maana nikatia shinikizo aachwe kwa Talaka zote tatu ili Faridi baada yakumuambukiza asiwe akaenda kumuambukiza mwanamke mwenzangu, ambae mwanamke ndiyo alioniokoa kule Pangani katika matatizo.”
Mkuu wa kituo alichukua kila kitu alichokuwa nacho Rebeka akakiweka katika Droo yake ya kabati, Rebeka akapelekwa Selo kusubiri hatua zaidi za kisheria dhidi yake. Raratibu zikafanywa ili kupewa taarifa mwenye mali aweze kwenda kituoni pale kwa ukaguzi wa pesa zake, na kusikiliza maamuzi ya mtendewa tukio, kama atataka kesi ile iende mahakamani au imalizwe palepale Polisi.
*******
Faridi alipokea simu yake akapewa ujumbe kutoka katika kituo cha Polisi Magomeni, akifahamishwa kukamatwa kwa Rebeka na kupelekwa katika kituo chao pale Polisi Magomeni akatakiwa afike haraka kituoni pale. Faridi alimueleza Dakitari kuhusu kujisikia vizuri, na kwamba alikuwa akitakiwa Polisi kufatilia pesa zake, Dakitari baada ya kuridhika na afya yake, akampa ruhusa yakutoka jioni ile, nae akaondoka katika Hospitali ile, amamuacha Rama bado akiwa anauguza majeraha ya moyo wa kupenda.
Faridi aliunganisha hadi kituo cha Polisi magomeni, akaonana na mkuu wa kituo akaelezwa kuhusu kuzitambua mali zake na kama anataka kufungua kesi ama hataki, Faridi akamjibu mkuu wa kituo kuwa anamtaka Rebeka aonane nae ili amuulize sababu za kufanya yale yote, ndipo atafanya maamuzi. Mkuu wa kituo aliwaamrisha askari wa zamu waliokuwa pale mapokezi, wampeleke Rebeka ofisini kwake. Mara Rebeka akiwa na askari wawili wa kike aliingizwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa kituo. Faridi alipomuona Rebeka alivyokuwa alimuhurumia ndani ya moyo wake, kwani alikuwa ni mnyonge sana, macho yake makubwa yalivimba kwa kilio, Faridi akamuuliza huku akimtazama usoni .
“Rebeka umefanya nini sasa Sikuelewi kabisa dhamira yako ilikuwa ni nini hadi ukaamua kutoroka na pesa zangu?!”
“Faridi hujui kilichonitokea ndiyo maana unasema hayo, nitoe hapa tukazungumze kwa kina kwani mie bado ni mke wako, Shamba la bwana Heri, na Mbuzi wa Bwana Heri, kama Mbuzi wamekula mazao katika shamba la mwenye mbuzi ubaya unatokea wapi, nahitaji nafasi kutoka kwako ili nikwambie kilichonisibu, kwani hata nilipoondoka pale haikumaanisha kuwa nilikukimbia. Hata ulipokuwa ukinipigia nimejaribu kupokea simu yako lakini chaji ikawa imekwisha ndiyo maana.”
Faridi akataka pesa zake kwa mkuu wa kituo akakabidhiwa. Alipoulizwa kama atafungua kesi ya wizi wa kuaminiwa dhidi ya Rebeka lakini Faridi akakataa katakata kufungua kesi kwani pesa zake alikuwa ameshazipata zote, hakuona haja yakupoteza wakati wake kwenda mahakamani, hasa wa wazifa aliokuwa nao.
Siku ya pili yake Rama alipewa ruhusa ya kwenda nyumbani baada ya hali yake kuonekana imeruhusu kidogo tofauti na awali ilivyokuwa hivyo akashauriwa na madikitari kuacha mawazo ya mara kwa mara kichwani kwake. Nae akakubaliana na wataalamu wa afya akashika njia kutafuta uelekeo wa kumfikisha nyumbani kwake Tabata Segerea.
Faudhia aliamka asubuhi pale Lodge, akajiandaa kwa kuoga na kupata kifungua kinywa, kisha akajipanga kwa safari kwani usiku alikuwa amewaza sana na akaamua auze duka lake kwanza ili akichanganya na pesa zake zilizokuwa Bank, aweze kupata mtaji wa kuendeshea maisha yake. Hivyo alikwenda Kariakoo katika jengo la Swahili Plazza, akapanda ghorofa ya kwanza akafika dukani kwake, akawatangazia wenye maduka wenzake azma yake ya kuuza duka lake ili asafiri. Wenzake kwanza walidhani anawacheza shere, lakini kadiri alivyokuwa akisisitiza wakatambua kuwa kweli hakuwa katika mzaha. Wakataka kujua Thamani ya duka lake kwani duka lile lilikuwa lipo katika kona, pia limesheheni urembo na linapokuwa wazi kina mama hujazana sana pale kwa ajili ya kupata vitu vya urembo. Kwa duka lilivyokuwa limejaza, mahali lilipo likiwa limeshalipiwa kodi ya miaka miwili na mkataba akiwa nao pale katika droo dukani kwake, iliwavutia wafanyabiashara kadhaa kutaka kulinunua duka lile. Kijana mmoja wa Kipemba alimtangazia kumpa shilingi Milioni kumi tasilimu palepale alipo, kama anataka kumuuzia yeye, lakini Faudhia akamwambia Mzigo uliopo dukani unathamani ya Tsh milioni tano, kodi kwa mwezi analipishwa shilingi Laki nane. Pale amelipiwa kodi ya miaka miwili ambayo ni Tsh milioni kumi na tisa na laki mbili, wakati yeye amekaa kwa muda wa miezi sita tu, hivyo bado mwaka mmoja na miezi sita mbele ambayo hiyo peke yake ni sawa na Tsh Milioni kumi na nne na laki nne, ukichanganya na mzigo wa milioni tano ni sawa na Milioni kumi na tisa na laki nne. kwa hivyo bei hiyo ipo chini sana kama kulipia pango tu, akamshauri aongeze walau nusu ya pesa ile, lakini Mpemba akasema ataongeza milioni moja tu basi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Faudhia akakataa kuuza kwa bei ya kutupa, ndipo alipotokea Mkinga akatoa Tsh milioni kumi na tano tasilimu, kiasi Faudhia hakurudi nyuma walikwenda kwa mwanasheria wakafanya Makubaliano ya mauziano, akatafutwa mmiliki wa jengo akafahamishwa mabadiliko yale, kwa kuwa yeye hakuwa na deni kwa Faudhia aliafiki mabadiliko yale, mikataba ikabadilishwa majina, wakaenda TRA napo wakabadilisha jina la mfanya biashara kutoka kwa Faudhia kwenda kwa Mkinga, gharama za mambo yale yote aliyafanya Mkinga, biashara ikesha, na Faudhia akashika njia hadi Bank akaziweka pesa zake, sasa akawa anajipanga rasmi kwa ajili ya safari. Akiwa katika kupanga mizigo yake ya safari, ndipo wazo kakwenda kuwaaga rasmi Rama na Faridi likamuingia katika moyo wake. Akaazimia aende akaagane nao ili aweze kusafiri. Alipita mjini akanunua simu nyingine, akaiweka Laini yake ya simu ambayo Dokta Neema Mnyampala alimpa siku ile akiwa anaondoka pale hospitali kwenda Polisi. Alipoiweka laini yake katika samu, mara ukaingia ujumbe katika simu yake, ujumbe ule baada yakuusoma ulimfanya asiyaamini macho yake makubwa kama anachokiona ni hakika!
Ulikuwa ni ujumbe wa kampuni ya simu, Mpesa ukisomeka ndani ya simu yake kuwa ameingiziwa Tsh milioni nne na mtalaka wake Faridi, lakini pia ukifatiwa na ujumbe mwingine ukimwambia kuwa nimekuangukia kwa pesa hizo, hivyo naomba kesho asubuhi uje ili tupange safari ya kupumzika Thailand, kwani najua kwa kiasi gani nimekukwaza, naomba utambue kuwa makosa ameumbiwa mwanaadamu.
Ujumbe ule ulimtia mshawasha sana Faudhia, akamkumbuka Faridi tangu siku ya kwanza wakati akimuoa kutoka kwao Same Kilimanjaro. Faudhia alikuwa katika wakati mgumu sana, kwani duka lake ameshauza ili akaishi katika mji mwengine asahau yale yaliyomsibu, lakini kwa pesa zile na safari ile aliifikiria kama ambayo ingeweza kumfanya aondoshe msongo wa mawazo, akafikiri mara mbili lakini akasikia nguvu ya ajabu kutoka katika moyo wake ukimpuuza kuhusu maamuzi yake ya kwenda kwa faridi. Nafsi yake ikamwambia kwamba kila likuepukalo lina kheri na wewe. Hakutaka kuipuuza kauli ile akaona dawa ya jambo lile ni yeye kuondoka bila kumuaga mtu yeyeto awaye pia abadili namba ya simu, ili asiwe anapata mawasiliano na wanaume wale kauli hiyo akaitilia mkazo, akaenda katika wauzaji line za simu akanunua laini ya mtandao mwengine tofauti na wa simu yake ya awali. Akaisajili namba yake mpya, mara moja akatoa pesa zile kwa wakala, akampigia simu shoga yake Issabela George, kuwa waonane akamuelekeza mahala alipo na kwa vile Issabela alivyokuwa akipenda umbea akaenda pale katika Lodge alipoelekezwa kwa haraka.
“Shoga yangu wewe ndiye msiri wangu, mimi mwenzako nimeshapata Talaka tatu ivi ninavyoongea na wewe. Hapa kesho mapema nainuka katika mji huu, hivyo utanitafuta katika namba hii.”
Faudhia alimpa kikaratasi alichokiandika namba yake mpya ya simu, akamkabidhi shoga yake mikononi mwake. Kisha akamtaka abakie na gari yake ili akifika huko aendako amtumie ile gari imfikie. Alimwambia kwa uchache masahibu yaliyompata tangu alipomwambia aangalie katika Wall ya Mumewe na akakutana na picha zilizoharibu maisha yake. Akamweleza kuwa amepanga kusafiri aende kuishi kwa muda kisiwani Mafia akatafute maisha. Issabela aliagana na shoga yake kwa unyonge mkubwa, akaondoka na gari ya faudhia kwa maelewano kuwa siku ya pili yake ampitie pale Lodge mapema ili amsindikize uwanja wa ndege. Mwisho wakaagana Issabela akaenda kwake na Faudhia akaenda kulala, lakini usingizi ulimfanyia khiyana, kwani ulimpaa hakupata hata lepe la usingizi.
Mawazo tele yalitanda kichwani mwake, aliwafikiria sana Rama na faridi, akatamani kujua khatma ya Rebeka kama amekamatwa au bado, lakini angemuuliza nani? Faudhia kichwa kilimuuma sana kwa kuwaza haya na yale, mara akastaajabu kusikia majogoo yanawika kuitambulisha alfajiri kuwa imeshaimgia, lakini Faudhia hakulala usingizi kabisa. Saa kumi na mbili kamili ya asubuhi, Issabela alifika kwa Faudhia akamgongea lakini hakupata tabu sana, kwani Faudhia aliitika kama vile ndiyo amepanda kitandani muda ule. Akajiandaa nakutoka akapelekwa uwanja wa ndege na hatimae akasafiri kwenda Mafia kuanza maisha mapya.
Dereva taxi misifa aliandika maelezo yake pale kituoni, akaachiwa kwa masharti kwamba ikiwa atahitajika ataitwa ili kuwa shahidi katika jambo lile huku akashauriwa baada ya miezi mitatu akapime afya yake kutambua kama ameambukizwa ama laa.
Mkuu wa kituo cha Polisi Magomeni alimpandisha mahakamani Rebeka kwa shitaka moja tu lakusambaza virusi kwa wanaume makusudi huku akijua kwamba yeye ni muathirika, kinyume na sheria ya kutokomeza Ukimwi inchini. Baada yakupanda na kusomewa shitaka Rebeka alikana shitaka lile akapelekwa Rumande katika gereza la wanawake Segerea kwa kukosa mtu wa kumdhamini, kesi yake ikapangwa kutajwa tena wiki mbili baadae. Baada ya wiki mbili Rebeka akapanda tena mahakamani ikatajwa tena kesi ile, huku upande wa mashitaka ukidai kuwa upelelezi bado haujakamilika. Rebeka alisota Gerezani hadi ikatimia miezi miwili kamili, ambapo kwa mujibu wa sheria upande wa mashitaka ulipaswa kukamilisha upelelezi wake lakini bado alipigwa kalenda kwa lugha ileile kuwa upelelezi bado haujakamilika hakuweza kusomewa Facts kuelezwa mashahidi wala ushahidi wa shitaka lile. Rebeka kwa kukaa kwake Jela akawa mzoefu wa mambo ya kesi akawa hana hofu tena, akajipanga hata siku hiyo iliyotimu miezi miwili upande wa mashitaka ulipoendelea kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika, akanyoosha kidole juu ili muheshimiwa Hakimu ampe ruhusa ya kuzungumza. Naam muheshimiwa baada yakuandika katika jalada lake, alimtazama Rebeka aliekuwa amenyoosha mkono na kidole juu, akampa nafasi azungumze nae akaitumia ipasavyo nafasi ile.
“Muheshimiwa hakimu, mimi sijui sheria sikusoma hivyo naomba nifahamishwe na mahakama yako tukufu, kwani upelelezi kwa mujibu wa sheria huwa unachukuwa mudi gani kukamilika na leo tangu nipandishwe katika mahakama yako ni muda gani?”
Muheshimiwa hakimu aliandika katika jalada lake, hoja ile kisha akamwambia muendesha mashitaka ajibu swali la mshitakiwa.Muendesha mashitaka akasimama nakujibu swali lile kwa mujibu wa sheria.
“Eee Muheshimiwa kwa mujibu wa sheria, upelelezi huchukua siku sitini kukamilika kwake, ikiwa ndani ya siku hizo sitini ikawa haujakamilika, basi upande wa mashitaka utaomba kibali kwa mkurugenzi wa mashitaka, ili kupewa ruhusa yakuendelea na upelelezi kwa muda wa siku sitini zingine”
Baada ya kujibu muendesha mashitaka akaa kitako katika bechi lake, pale katika mahakama ya wilaya ya Kinononi.
Muheshimiwa hakimu alipomtazama tena Rebeka akamuona ameinua tena mkono wake juu, akiomba ruhusa yakusema jambo, akamruhusu kuongea.
“Muheshimiwa nashukuru kwa kuniona na kunipa nafasi, upande wa mashitaka umeeleza wazi mbele ya mahakama yako tukufu kuwa upelelezi ni siku sitini, au waombe kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashitaka nchini, je nataka kujua kwa siku sitini zimeshafika, upande wa mashitaka wanacho hapo walipo kibali cha kuendelea kupeleleza kesi inayonikabili, kwani mie nipo gerezani muheshimiwa, sina ndugu wakunidhamini, na kama watu ninaodaiwa kuwaambukiza virusi vya Ukimwi makusudi wapo, wanashindwa nini kuwaleta mbele ya mahakama yako ili waeleze namna nilivyowaambukiza hivyo virusi?!”
Muheshimiwa hakimu aliandika tena katika jalada lake hoja ile, akamtazama mwendesha mashitaka na kumuuliza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“PP, unachokibali hapo ulipo kutoka kwa Mkurugenzi wa mashitaka?”
Muendesha mashitaka akajibu kuwa hana kibali ila ndiyo wanafanya taratibu ili waombe kibali, hivyo akaomba tarehe ili akija aje na kibali. Muheshimiwa hakimu aliandika majibu yale, akamtazama Rebeka akamuona ameinua tena mkono wake juu, akiomba nafasi ya kuzungumza.
“Amesema hana kibali ndiyo wanafanya mpango wa kupata kibali, kwani mshitakiwa unasemaje?”
Muheshimiwa hakimu alizungumza maneno yale huku akimtazama Rebeka usoni lakini pia akimpa nafasi ya kuzungumza.
“Muheshimiwa hakimu nafahamu kwamba wewe ndiyo mwenyekiti wa Mahakama, na upo hapa kwa ajili yakusimamia sheria, je sheria imesema kwamba ikifika miezi miwili kwa maana ya siku sitini, upelelezi ukiwa bado haujakamilika ifanyike mipango ya kuomba kibali au kuwepo na kibali cha kuendelea na upelelezi? Sasa ukiwapa nafasi ya kufanya mipango sasa hivi upande wa mashitaka utafute kibali huoni utakuwa umevunja sheria, kwani itakuwa imepita siku sitini kwa mujibu wa sheria na wewe bado ukaendelea kukubali kuahirisha shitaka langu, Muheshimiwa haki inayocheleweshwa ni sawa na haki inayonyimwa, naiomba mahakama yako tukufu initendee haki.”
Rebeka aliposema maneno yale machozi yalimlengalenga. Muheshimiwa hakimu aliandika kisha akasema.
“Kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai inchini CPA ya mwaka 1985, kifungu cha 225 namuachia huru mshitakiwa kwa sababu upande wa mashitaka umeshindwa kukamilisha upelelezi kwa muda wa kisheria, hivyo upande wa mashitaka mnaweza kukamilisha upelelezi wenu kama mnao kisha mtajua cha kufanya.”
Tatizo la kesi yenyewe ilivyokaa kuambukiza virusi jamii nyingi ya watanzania, wamekuwa hawapo tayari kufika mahakamani ili kutoa ushahidi wa kesi za aina hiyo, kwa kuogopa kuonekana wameathirika hivyo kesi nyingi zinazopelekwa mahakamani zimekuwa hazina ushahidi wa kuwatia hatiani washitakiwa.
Rebeka aliposikia maneno ya Muheshimiwa hakimu hakutaka kushangaa, aliondoka pale Kizimbani akatokomea mitaani huku akimshukuru Mungu kwa kumtoa jela akamrejesha tena uraiani. Akiwa anatembea akawa akitubu katika nafsi yake kuwa hataendelea tena na ile nia yake mbaya ya kuambukiza mtu wa kumi, hivyo akawa raia mwema aliekuwa ameingia Kanisani na kuungama dhambi zake akaomba msaada ili apewe sehemu ya kuishi, lakini pia akiwa ni muumini mzuri wa kanisa lake. Waumini walimchangia pesa, mama mmoja mjane akajitolea kukaa na Rebeka nyumbani kwake.
MIAKA MITATU BAADAE.
Faudhia alikuwa amenunua nyumba Mafia katika eneo la Kulungeni, jirani kabisa na uwanja wa ndege wa Mafia, siku hiyo akiwa amekaa dukani kwake nje asubuhi, mawazo ya Dar es salaam yalimjia sana, kila alipokuwa akiyaondosha mawazo yake lakini alishindwa, kwani mawazo au mvuto wa kwenda Dar es salaam ulikuwa ukimvuta sana. Aliishangaa hali ile akaona mbona muda wote aliokuwa Mafia tangu akiwa mgeni hadi sasa amekuwa mwenyeji, na amefunga ndoa na meneja wa uwanja wa ndege wa mafia mwaka mmoja uliopita, na sasa akiwa ametoka kuzaa mtoto wa kiume aliekuwa na umri wa miezi miwili. Ndipo sasa hamu yakutaka kufika katika mji wa Dar es salaam ikamjia kwa kasi sana. Aliwaza mambo mengi mno akaazimia kesho yake afunge safari. Mumewe aliporudi jioni alimuelezea kutaka kwenda mara moja Dsm kwenda kuwaona ndugu na jamaa zake, hivyo mumewe akampa ruhusa akamfanyia taratibu ya ndege na siku iliyofata Faudhia akaruka kwa ndege kuelekea Dsm.
Alipofika tu pale uwanja wa ndege alichukuwa taxi akamwambia dereva wa taxi ile ampeleke Tabata Segerea, akatajiwa bei akapelekwa. Alipofika pale akakuta watu wengi wamejaa katika nyumba aliyoikusudia nae akaenda kujumuika na watu wale, mara akasikia tangazo kutoka kwa mtu aliekuwa anazungumza.
“Ndugu zangu tunataka kusalia maiti, hivyo kama kawaida yetu ilivyo kama kuna mtu yeyote anaemdai Marehemu Rama, ajitokeze kwa wafiwa ili apewe taratibu yakulipwa deni lake, na kama yupo aliekuwa akidaiwa na marehemu basi awaone wahusika hapa ili amlipe marehemu. Pia leo baada yakuzika, kwa kuwa marehemu Rama alikuwa ameugua muda mrefu, basi jumapili tunaombwa sote kama tulivyo hivi tuje hapa ili kumuombea dua ndugu yetu”
Baada yakusema maneno yale maiti ilitolewa ndani kwa ajili ya kuswaliwa na hatimae kupelekwa katika kaburi lake.
Faudhia alilia sana mara aliposikia kuwa aliekufa katika mkusanyiko wa watu wale ni Rama, alilia huku akizungumza kwa masikitiko.
“Rama nimekuacha peke yako, hadi umekufa sikusikia kauli yako ya mwisho, Rama mtoto wangu nimempa jina lako kumbe jana ulikuwa ndiyo unaniita, nisamehe Rama haikuwa riziki mungu hakutaka tuishi pamoja, aaa Ramaaaaa!”
Faudhia alilia sana, mara akashikwa begani na mwanamama mmoja aliekuwa amemfata kutoka ndani, akataka kujua marehemu yupoje nae, akajitambulisha kuwa alikuwa ni rafiki yake tu, akamueleza kwa kifupi namna alivyokutana nae, Yule mama akamwambia; “Kumbe wewe ndiyo Faudhia?!” Tangu juzi Rama alikuwa akikutaja sana, lakini ameandika ujumbe ili ukija mwaka wowote upewe, yeye amefariki jana asubuhi, lakini kafa huku akilitaja jina lako kuwa anakufa bila kukuona.
Faudhia aliupokea ujumbe ule akaufungua palepale na kuusoma, ulikuwa umeandikwa kwa mkono.
Faudhia ndugu yangu, nakufa bila kukuona, moyo wangu umeshindwa kukusahau, hivyo mwaka wowote wa kupata ujumbe huu, nakuomba uwasamehe wale wote waliokukosea, mie nimemsamehe Rebeka, pia Nimemsamehe Faridi sina kinyongo nao tena, maradhi haya siponi, ikiwa utajaalia kupata mume mwema nakutakia uwe na Moyo wa kupenda kwa mumeo, lakini pia zingatia maneno haya. Moyo wa kupenda, usiwendekeze, utafilisika mali upoteze, jambo la khiyari lende likulize. Nakutakia maisha marefu, usisahau kuniletea mauwa kaburini kwangu, akupendae daima Rama.
Faudhia alilia sana kwa ujumbe ule wanaume waliporudi makaburini, akamuomba kijana mmoja ampeleke katika kaburi alilozikwa Rama, kijana Yule akakubali kumpeleka akakodi Bajaji akiwa na mtoto wake mikononi, akapitia pale Segerea mwisho katika duka la mauwa, akanunua mauwa akaelekea makaburini pale Segerea, alipofika pale Makaburini katika kaburi aliloelekezwa kuwa ndilo alilozikwa Rama,akapigwa na mshangao mkubwa, kwani alimuona mwanamke mmoja aliekondeana sana, akilia juu ya kabauri lile huku akiomba dua Mungu amsamehe marehemu Yule, Faudhia alipiga hatua hadi pale katika kaburi lile, nae akachuchumaa akaweka yale mashada ya mauwa juu ya kaburi lile, kisha akalia sana. Akiwa katika kulia mara Yule mwanamke dhaifu aliekondeana alimshika bega huku akimuita jina lake. Faudhia aligeuka kumtazama kwani ile sauti ilikuwa siyo ngeni masikioni mwake, naam alipigwa na butwaa kubwa sana. Alimuona Rebeka akiwa amekonda vibaya sana, ute mweupe ukiwa mdomoni mwake, vipele na vidoti vyeusi vikiwa vingi usoni mwake, kifuani kwake alikuwa ameuvaa msalaba mkubwa.
“Nisamehe Fudhia kwa kukuharibia ndoa yako, kwani bila mimi ungekuwa bado upo katika ndoa yako. Faridi amefariki mwaka jana, amejiuwa baada yakuona ameathirika, mie siku hizi nakaa huku Segerea kwa mama mmoja aliejitolea kunihifadhi nyumbani kwake, nakuomba msamaha sana kwa yote yaliopita, kwani na mimi kama unavyoniona muda wowote nitawafata wazazi wangu huko walipo, pamoja na Rama na faridi, kwani hii ni safari yetu sote.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Faudhia alimkumbatia Rebeka huku akimwambia. “Rama ameniachia wasia kuwa nikusamehe, hivyo mbele ya kaburi lake hapa natamka nimekusamehe sina kinyongo na wewe tangu leo Duniani na kesho Akhera.”
MWISHO
0 comments:
Post a Comment