Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

MSAFIRI SAFARINI - 2

 







    Simulizi : Msafiri Safarini

    Sehemu Ya Pili (2)







    Ulikuwa ni wimbo ulioimbwa kwa lugha niliyoifahamu na tafsiri ya wimbo huu katika lugha ya kiswahili ilikuwa ni:

    Sikuwa wa kuja hapa…

    Kuzaliwa kumenileta..

    Kuzaliwa kumeniletaa…x3

    Tulifika mpaka eneo la tukio na kushuhudia yaliyokuwa yakiendelea mahali pale. Tulishuhudia watu wakicheza ngoma pamoja na kuimba, wengine waliimba kwa fujo na wengine kwa mpangilio. Baadaye kidogo sauti za ngoma na nyimbo zilikoma na mara akasimama katikati mtu mmoja, aliangalia kushoto na kulia, akageuka nyuma na mbele kisha akaanza kuongea maneno niliyoyasikia sawia, maneno yalikuwa ni haya yafuatayo:

    “Watoto wa karne hii wanakikosa kile ambacho sisi tulikipata kale. Siamini na wala sitotaka kuamini kuwa huku ndiko kwenda na wakati. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wapo ambao wamenyimwa hata nafasi ya kuushuhudia ulimwengu baada ya mimba zao kuharibiwa kwa makusudi. Na hata waliopata nafasi ya kuushuhudia ulimwengu nao ni kama wametupwa kwenye bahari ya moto na kuachwa waungue polepole mpaka watakapoisha.

    Watoto wa siku hizi wameyakosa malezi boraambayo ni haki yao ya msingi. Labda ni kwa sababu wazazi na walezi wao wameshindwa kutambua umuhimu na faida za kumlea mtoto. Kwa kumlea mtoto; kwanza kabisa unajifunza hatua za ukuaji wa mtoto ikiwemo mabadiliko ya kitabia yasababishwayo na mazingira pamoja na mihemko ya mwili. Pili unampa mtoto fursa ya kukua katika malezi bora na baadaye kuufikia utu uzima sambamba na kutekeleza majukumu yake kama mtu kamili.

    Lakini cha kushangaza mwanadamu ambaye ndiye mlengwa wa mashairi amepagawa zaidi na midundo ya ngoma kuliko mashairi ambayo ndiyo huwa yamebeba ujumbe, na si ajabu kwa sasa mtu kuikumbuka zaidi midundo ya ngoma na kusahau kabisa maudhui ya shairi ambalo limeimbwa sambamba na midundo ya ngoma. Badilikeni!”

    Alimaliza yule kichaa na safari hii hakukaa chini, badala yake aliondoka kwa kupita kwenye nafasi iliyoachwa wazi kwa kila alivyozidi kupiga hatua kuelekea mbele.

    Wazazi na walezi wa siku hizi hawazijui hatua za ukuaji wa mtoto kama ilivyokuwa zamani, na watoto wa siku hizi hawakuzwi katika namna itakayowafanya wawe watu wema wenye kujijali wao na jamii nzima na kutekeleza majukumu yao kama watu wenye utu kamili”

    Baada ya kusema hayo yule mtu alikaa na milio ya ngoma ilifuatia sambamba na vigelegele. Wakati bado nikitafakari juu ya kilichokuwa kinatokea, nilishtukia naguswa begani na nilipogeuka nilimsikia Mzee akiniambia kuwa huyo ndiye kichaa kama watu wamwitavyo.

    Nilitikisa kichwa kwa kukipeleka juu na kisha kukirudisha chini mara kadhaa kisha nikarejea katika mkao wangu wa awali na wakati huo sauti za ngoma na vigelegele zilikoma kwa ghafla na yule kichaa akasimama tena na kuanza kusema maneno haya:

    “Kabla ya njia zote za kurithishana maarifa kuwepo, ushairi ulikita mizizi kama njia pekee ya kupeana maarifa toka kizazi hadi kizazi.

    Nyimbo zenye jumbe mbalimbali zilitungwa na baadaye mwanadamu akaongeza ubunifu kwa kuchanganya mashairi na midundo ya ngoma ambayo iliinogesha sanaa ya ushairi. Lengo la kuchanganya midundo ya ngoma na ushairi ilikuwa ni kuupa nguvu ushairi, baada ya kuwa imezaliwa ladha tofauti na ambayo ni mpya katika uga wa ushairi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Lakini cha kushangaza mwanadamu ambaye ndiye mlengwa wa mashairi amepagawa zaidi na midundo ya ngoma kuliko mashairi ambayo ndiyo huwa yamebeba ujumbe, na si ajabu kwa sasa mtu kuikumbuka zaidi midundo ya ngoma na kusahau kabisa maudhui ya shairi ambalo limeimbwa sambamba na midundo ya ngoma. Badilikeni!”



    Alimaliza yule kichaa na safari hii hakukaa chini, badala yake aliondoka kwa kupita kwenye nafasi iliyoachwa wazi kwa kila alivyozidi kupiga hatua kuelekea mbele. Midundo ya ngoma na vigelegele haikusikika kama ilivyokuwa hapo awali, nilipowatizama watu wote waliokuwa eneo lile walionekana wazi kuwa walikuwa wakitafakari jambo, nilipogeuka kumuona yule kichaa sikuweza kumuona tena. Nilipotaka kujaribu kumfuata alipoelekea nilishikwa mgongoni na nilipogeuka nyuma nilimkuta Mzee ambaye aliniashiria tuondoke. Sikuwa na pingamizi.



    Nilimfuata Mzee ambaye alikuwa mbele yangu akiongoza njia. Haikuchukua muda tayari tulikuwa nyumbani kwa Mzee. Njiani tulizungumza mengi kuhusu maisha na changamoto zake, misiba na furaha ambavyo vyote mlengwa ni mwanadamu.



    “Juhudi za kichaa katika kuipeleka jamii mahali inapotakiwa kuwa hazikuanza leo. Jambo la kushukuru kuhusiana na harakati zake, ni kule kuonyesha mafanikio ambayo hudhihirika kila uchao. Kila ahudhurishapo mawaidha yake wengi huguswa na kubadilika kwa namna aliyoikusudia.



    Na kama hali ikiendelea hivi, basi jamii nzima ya mahali hapa inaweza ikajikuta iko mahali panapofaa katika maisha. Wepesi katika jambo hili utakuja baada ya vichaa kuongezeka, ambao kwa pamoja watashiriki katika kutimiliza hili.”



    Alisema Mzee. Kabla ya kuingia ndani na kutoka na chupa mvinyo akiwa ameishikilia vema isipate nafasi ya kuanguka, akaja moja kwa moja mpaka nilipokuwa nimesimama na kunikabidhi kisha akaniambia:



    “Kuna gwiji wa hekima aliyewahi kuwapo katika upwa wa Afrika ya Mashariki, wakati Fulani kabla ya mauti yake na aliwahi kuandika hivi:

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Maisha hayapimwi kwa wingi miaka bali kwa ubora wa matendo. Maisha bora ni matokeo ya matendo bora na maisha duni ni matokeo ya matendo duni”



    hivyo mwanadamu hana budi kuwa na matamanio katika kutenda yaliyo bora kwa mafaa yake na jamii yake. Kichaa ni mfano bora kwa yale ayatendayo. Japokuwa changamoto ni nyingi lakini juhudi zake ziko bayana!



    Mzee alimeza funda la mate kidogo kisha akasema:

    “Chupa hiyo ina mvinyo wa kukutosha kwa miongo zaidi. Safari yako bado ni ndefu sana na huo ni ukweli usioweza kufichika! Imani yangu ni kuwa umeyafurahia mapumziko ukiwa pamoja nasi mahali hapa”



    Nilimtazama Mzee usoni, nikabaini kuwa uzee wake haukuwa kama ulivyokuwa awali kwani ulikuwa umeongezeka maradufu. Wakati nataka kusema neno, alinikatiza kwa kusema:



    Safari hii ni ndefu na yenye changamoto nyingi, milima na mabonde yaliyo mbele, si kama yale uliyoyapita huko nyuma, na misitu ya huko ni minene yenye giza totoro. Usitegemee kukuta njia japo wewe si msafiri wa kwanza. Wengi wamewahi kusafiri kuelekea huko. Matumaini ya vizazi vijavyo yako kwenye nyayo utakazoziacha wakati unapiga hatua. Watasafiri wakifuata nyayo zako kwa maana utawatengenezea njia.



    Wakati anamaliza kusema, upepo wa wastani ulivuma kutoka pande zote za dunia, kadri muda ulivyozidi kwenda mbele kasi ya upepo nayo iliongezeka. Upepo ulikusanya karatasi na nyasi na hatimaye kikawa kimbunga kilichokuwa na kasi ya kipekee. Ili kujiepusha na vumbi Mzee alijifunika shuka lake nami nikajikunyata. Kile kimbunga kilipotea ghafla na nilipofumbua macho sikumuona Mzee mbele yangu.



    Nikageuka kulia na kushoto lakini bado hakuonekana, na mazingira yale hayakuwa na muonekano kama ule wa awali, nilijikuta niko juu ya mlima wa mchanga usio na dalili ya kumea chochote.



    Ile chupa ya mvinyo ilikuwa imo mikononi mwangu na begi langu lilikua mgongoni. Sikuweza kujua kwa haraka nielekee upande gani, kwa sababu mazingira yote ya mahali pale yalionekana kuwa mageni machoni pangu. Nilikata shauri kuelekea macho yangu yalikokuwa yanatazama. Taratiibu nilianza kupiga hatua kuelekea mbele, lakini ungeniuliza ni wapi nisingeweza kukujibu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mchanga ulikuwa ni mwingi kiasi cha kuifanya miguu yangu kuwa mizito kila nilipojaribu kufanya mjongeo. Upepo uliokusanya mchanga uliifanya



    safari yangu kuwa ngumu kwa sababu mchanga ulikuwa ukiniingia machoni. Nilitembea umbali mrefu kwa taabu nyingi sana. Wingi wa mchanga ulionekana kupingana na hatua nilizopiga kuelekea mbele. Jambo lililonishangaza ni kuwa upepo ulikusanya mchanga na kuupeperusha utakako haukutosha kufukia nyayo nilizoziacha wakati natembea.



    Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, uchovu ulianza kuninyemelea, haikuchukua muda mrefu ukawa umenielemea kabisa na kunifanya nishindwe kunyanyua miguu yangu. Nikafungua chupa ya mvinyo na kuiweka mdomoni, haikuchukua muda mafundo yapatayo matano tayari yalikuwa yakivinjari tumboni mwangu. Nikaifunga chupa na kuiweka sawia ndani ya begi.



    Nilipotizama chini sikuweza kuona vizuri kwa sababu ya giza ambalo liliyazingira macho yangu. Nilijitahidi kunyanyua miguu yangu ili niweze kujongea mbele zaidi lakini nayo ilikuwa na uzito usiomithirika. Wakati naendeleza jitihada za kujinasua, mguu wa kushoto ulitoka ukifuatiwa na ule wa kulia, ghafla nilijizonga na kudondoka kifudifudi giza likatanda machoni pangu, na polepole sauti zote zilififia na kupotea kabisa. Sikujua tena kilichoendelea baada ya hapo.



    “Urahisi na ugumu tulio nao sasa upo tena baada ya maisha haya?”





    **************



    Upepo mkali ulikusanya mchanga na kuupeperusha utakako. Kwa taabu macho yalianza kuona na hatimaye nikaweza kuona bila shida kama ilivyokuwa



    hapo awali. Nilisimama na kuangaza kushoto na kulia nilipogeuka nyuma niliuona mlima wa mchanga uliokuwa na msitari mrefu toka kileleni mpaka nilipokuwa. Yawezekana nilipodondoka niliseleleka toka kwenye kilele cha mlima mpaka mahali hapa. Nilipotizama mbele dalili za mimea zilianza kuonekana japo mimea hiyo ilionekana kufubaa kwa kukosa maji. Nilijipangusa mchanga kisha nikaendelea na safari.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitembea umbali mrefu katika hali ya upweke na mashaka tele. Pote nilipopita palitawaliwa na ukimya usioweza kuelezeka kwa misamiati ya ulimwengu. Hapakuwa na dalili ya mdudu wala mnyama, hata majani yalikuwa ni kama yanapunga mkono wa kwaheri katika uso wa dunia. Nisingeweza kwenda mbele zaidi kama si matumaini yaliyotuama vema kwenye moyo wangu. Haya ndiyo yaliyonifanya nijione shujaa pekee aliyebaki chini ya jua, ambaye matumaini ya vizazi vijavyo yamo ndani mwangu.



    Chochote nilichoweza kukiona kwa wakati huo hakikuweza wala kuthubutu kunipa hofu wala mashaka. Hofu na mashaka yangu ilibaki juu ya vile nisivyoviona wala kuvijua. Maisha baada ya kifo yaliufikirisha ubongo wangu na bado majibu mwafaka ambayo yangesadifu maswali yangu hayakupatikana kwa urahisi.

    Nilijifikirisha tena na tena lakini jawabu halikuwa na mimi bado.



    “Hivi kama yapo maisha baada ya haya tuyaishiyo, hayo maisha ni ya namna gani?”



    “Urahisi na ugumu tulio nao sasa upo tena baada ya maisha haya?”

    Maisha tuliyo nayo sasa yamegubikwa na matabaka. Wapo wanaoishi katika hali ambayo huwafanya wengine kuwatamani namna waishivyo na maisha yao, ambao hupata chochote wakitakacho kwa pesa yao au kwa kile wanachomiliki. Ingawaje utajiri wao bado hauwafanyi kuweza kununua furaha au uhai.



    Lakini kwa pesa yao huifanya uongo kuwa kweli machoni pa watu japo ni kwa muda, kugeuza haramu kuwa halali. Japokuwa ubatili huo huwagandamiza wasio na sauti kwa ukosefu wa kipato, furaha ya matajiri hao dharimu bado haijapata kukamilika.



    Wapo pia ambao huishi maisha yasiyoweza kumtamanisha yeyote kuyaishi. Wao huishi kwa matumaini kuwa kuna siku wataondokana na hali hiyo ambayo ni chukizo hata kwao wenyewe. Katika jitihada za kuondokana na hali hiyo, wapo waliokata tamaa kwa imani kuwa ushindi hautokuwa pamoja nao hata kama watapambana bila kujipa likizo kwa siku zote za maisha yao. Katika kundi hili pia wamo wenye matumaini ya ushindi japo hawajishughulishi kwa kiwango cha kutosha, hawa huwa na imani na matumaini ya ushindi ambayo huishi ndani mwao hata wafikiapo hatua ya kuvuta pumzi ya mwisho chini ya jua.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika kundi hili pia hawakukosa ambao hupambana kwa kujishughulisha usiku na mchana tena kwa bidii isiyo kifani, pato lao lote huishia vinywani mwao na isibaki hata akiba kwa ajili ya kesho, na mara tu jogoo awikapo huamkia mihangaikoni ambako pato la siku hiyo huwa ni afadhali ya jana. Siku hupishana kwa mtindo huo huo, mpaka mwisho wa maisha yao chini ya jua. Kwa



    utofauti huo wa maisha baina ya mtu na mtu chini ya jua, maswali yanisumbuayo juu yake ni kuhusu maisha ambayo husemwa kuwa ndiyo yatakayofuata baada ya haya. Tangu kale imeaminika kuwa yapo makzi watakayokwenda watenda maovu na pia yapo makazi ambayo ni maalumu kwa watenda mema. Makazi hayo ya kufikirika huitwa jehanam kwa wale watenda maovu na peponi kwa ajili ya wale waliotenda mema katika kipindi chao cha maisha chini ya jua. Na kama hali iko hivyo, je watu kutoka tabaka mbalimbali zilizopo chini ya jua watapelekwa katika jehanam iliyo sawa na pepo iliyo sawa?



    Na kama hali iko hivyo nini maana ya shida na raha za dunia? Au kwa nini kuna umasikini na utajiri duniani? Kwa vile nionavyo; maisha ya masikini ni kama tanuu ya moto. Sasa kwa nini apelekwe tena jehanam iliyo sawa na yule tajiri?



    Fikra hizi zilitafuna muda bila ya mimi kujua na kwa wakati huo wote miguu yangu ilizidi kupiga hatua kuelekea mbele. Nilikuwa nimetembea mamia ya maili bila kutambua, japokuwa sikuwa na uhakika na huko niendako, lakini niliamini kuwa hatua za miguu yangu zilikuwa sahihi. Niliinua kichwa juu ili kulitazama jua nikabaini tayari lilikuwa limeshazama.



    Mwanga uliendelea kumezwa taratibu na giza ambalo halikuonekana kuwa hata na chembe ya huruma. Macho yalijitahidi kupingana na giza ili yaweze kuona mbele na mpaka wakati huu yalifanikiwa kuibuka na ushindi hafifu kwa kuiona miti ambayo ilikuwa mbele yangu.



    Uchovu uliokuwa ukinikabili uliifanya miti ionekane kama ilikuwa ikinikimbia, nilijikokota mpaka nilipoufikia mti uliokuwa mkono wangu wa kulia kati ya miti mitatu iliyokuwa mahali pale. Nilikaa kitako kwa lengo la kujipumzisha kwa usiku ule. Nilijiegemeza barabara kwenye mti ule kisha nikaichomoa chupa ya mvinyo kutoka ndani ya begi. Nikaifungua na kumimina matone kadhaa mdomoni mwangu, ambayo yaliteremka taratibu mpaka yalipofika tumboni, kabla ya kutokomea kwenye mishipa ya damu ambapo ilisafirishwa moja kwa moja kuelekea kwenye ubongo na kunifanya nianze kuchangamka ili hali nikiwa peke yangu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kileo kilichokuwa ndani ya ule mvinyo kilinisahaulisha uchungu wa safari ya maisha. Nilijikuta mwenye furaha japo ubatili wa furaha yangu ulizidi kubainika kila nilipojaribu kujifikirisha juu ya maisha, ukweli kuhusu maisha ulizidi kuitesa akili yangu kwa muda zaidi.

    Nilimimina mafundo zaidi ili mawazo juu ya maisha yaondoshwe kwa usingizi ambao ulinijia kwa harakaharaka kwa sababu ya ule mvinyo. Macho yalianza kuona kwa vituo na mara usingizi ulinichukua na kunipeleka nisikokujua.



    Kushoto na kulia palionekana kuwa na shimo, ambalo mwisho wake ulikuwa ni kitend awili kisicho na jibu, kwa sababu ya giza lilonifanya nisiweze kuona chochote shimoni mule. Sikuweza kujua umbali uliopo kutoka mahali nilipo mpaka kwenye kitako cha shimo lile. Ingawaje shauku ya kutaka kujua kilichomo ilikomeshwa mara moja na woga ulionizonga kila nilipojaribu kufikiria kilichomo shimoni.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog