Simulizi : Msichana Ndotoni Mwangu
Sehemu Ya Tatu (3)
KILIKUWA chumba chenye ukubwa usiopungua mita za mraba hamsini, kilijazwa samani nyingi zenye thamani kubwa, ukutani kukiwa na picha kubwa ya
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mwanaume akiwa na watoto wawili mapacha. Mwanaume kwenye picha hiyo ndiye aliyekuwa ndani ya chumba hicho akiwa ameketi nyuma ya meza kubwa,
akiiangalia picha kubwa iliyokuwa mbele yake kwa umakini, ghafla akatabasamu.
“Siwezi kuamini kama hawa watoto wako mikononi mwangu!” aliwaza Victor Federov.
Moyo wake ulikuwa umejaa furaha kubwa kupindukia, ujio wa Dorice na Dorica ambao hivi sasa waliitwa Mariya na Marina ulifanyika kwa wakati muafaka.
Kitu pekee kilichomsumbua akilini mwake ni kwa namna gani angeweza kuificha siri hiyo isivuje, kwani aliwahusisha watu wengi katika zoezi la utekaji na
alielewa duniani hapakuwa na siri ya watu wawili, lazima siku moja kama si Ditrov basi watu aliokuwa nao, mmoja lazima angefungua mdomo na kuueleza
ulimwengu namna watoto wake walivyopatikana. Mawazo hayo yalimfanya auchukue mkono wa simu uliokuwa kando yake na kuanza kupiga namba ya Ditrov.
“Ndio mkuu.”
“Uko wapi?”
“Ofisini kwangu.”
“Naomba uje haraka.”
“Sawa.”
Simu ikakatika.
Dakika tano baadaye mlango wa ofisi yake ukagongwa na Ditrov akaingia na kuketi mbele ya meza ya Victor. Mwili wake ulikuwa umeongezeka zaidi sababu ya
mazoezi, fedha nyingi aliyolipwa katika zoezi la kuwateka Dorice na Dorica ilikuwa imebadilisha kabisa maisha yake, sasa hakuhangaikia mambo madogo
madogo tena, mara nyingi baada ya kazi alitumia muda mwingi kwenye jengo la mazoezi.
“Ndio bosi nimeitika wito.”
“Ahsante, suala langu sio kubwa, nataka kukuuliza kama watu wote ulioshirikiana nao kwenye operesheni hii unawafahamu!”
“Sana, ni rafiki zangu.”
“Wakati wowote unaweza kuwapata?”
“Bila shida.”
“Sasa sikiliza.”
“Ndiyo.”
“Duniani hakuna siri ya watu …?”
“Wawili.”
“Ningependa kuona watu hawa wote wanakufa.”
“Mh!”
“Mbona umeguna? Nitalipa dola laki tano.”
“Kweli?”
“Bila shaka.”
“Kama dola laki tano zipo, mimi naweza kufanya hivyo kazi bila matatizo. Ni kiasi cha kutafuta Blood Pressure Uplifter, ambayo wakishainywea kwenye chai au
kinywaji chochote, shinikizo la damu litapanda na watakufa mmoja baada ya mwingine.”
“Unaweza kufanya hivyo?”
“Bila matatizo, ndiyo kazi yangu.”
“Hiyo dawa utaipata wapi?”
“Ninayo.”
“Kabisa?”
“Tangu enzi za KGB,” Ditrov aliongea akimaanisha Shirika la Ujasusi la Urusi ambalo aliwahi kulifanyia kazi miaka mingi kabla.
“Basi kama ni hivyo, tekeleza.”
“Fedha yangu?”
“Ukimaliza kazi njoo unione.”
“Ahsante.”
Ditrov akaondoka kichwani mwake akifikiria dola laki tano ambazo angelipwa akimaliza kazi ya kuwaua watu wote alioshirikiana nao kwenye zoezi la utekaji,
alielewa ingekuwa kazi rahisi sababu wote walimwamini. Alichokifanya kuanzia siku hiyo ni kuwa anawaita mmoja baada ya mwingine na kumpakia ndani ya
gari lake hadi ufukweni mwa bahari kwa ahadi kwamba walikuwa wanakwenda kupunga upepo, huko aliitoa dawa hiyo na kumchanganyia mlengwa kwenye
kinywaji, dakika chache baada ya kunywa hali ilibadilika, Ditrov akambeba ndani ya gari, njiani alikufa.
Alichokifanya ni kutumia boti maalum aliyopewa na Victor Federov kuubeba mwili huo mpaka katikati ya bahari ambako aliufunga jiwe na kuuzamisha hadi
kwenye kina cha maji, akiamini huko usingeonekana milele. Alifanya hivyo mpaka akawamaliza wote, akimpa taarifa Victor Federov juu ya maendeleo.
“Hongera sana, njoo ofisini leo usiku kama saa saba hivi uchukue hundi yako.”
“Nakuja bosi.”
Katika muda huo huo aliopangiwa, ofisi ikiwa haina mtu, Ditrov alipandisha ngazi mpaka ofisini kwa Victor Federov ambako alipokelewa kama shujaa, akaketi
kusubiri hundi yake, Victor alipofungua droo, badala ya kutoka na kitabu cha hundi, mkono ulitoka ukiwa na bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti.
“Nilikuambia duniani hakuna siri ya watu wangapi?”
“Wawili.”
“Inabidi Ditrov ufe ili nibaki peke yangu.”
“Hapana mzee nisamehe.”
“Paa! Paa! Paa!”
***
Kitanda kilikuwa kinacheza kama vile ni cha spiringi, ingawa kilitengenezwa kwa mbao imara za mninga, Phillip alikuwa kazini akijituma impasavyo
mwanaume aliyekuwa akitafuta sifa. Alitaka kumwonyesha Lina kwamba uzuri wake haukuwa umbile la sura tu, bali hata kwenye ukanda wa sita kwa sita
alikuwa ni mtaalam haswa.
Lina alikuwa akilia, si kwa maumivu bali kwa raha aliyokuwa akiipata. Ilikuwa imepita miaka mingi tangu akutane mara ya mwisho na mwanaume kimwili,
moto uliomteketeza uliondoka na uzuri wake wote, hivyo hakuna mwanaume aliyevutiwa naye labda kwa wale walioangalia maumbile, maana mtaji peke yake
aliokuwa nao ulikuwa ni hips zilizochomoza kama vilele vya mlima Meru!
Miili yao ilikuwa imelowa kwa jasho ingawa kulikuwa na kiyoyozi chumbani kilichoonyesha joto lilikuwa sentigredi kumi na nane. Mashuka yote yalikuwa
yamelowa, kijana Phillip akiwajibika, kwake kitendo cha ngono kilikuwa ni njia ya kumsahaulisha yaliyokuwa yakimsumbua akilini mwake, aliichukulia ni
kama faraja.
“Ahsante!” Lina alitamka maneno hayo Phillip alipojitupa kando yake.
“Karibu.”
“Sijawahi.”
“Hujawahi nini?”
“Kukutana na mtu wa aina yako, umezidi kunitia uchizi.”
“Nakupenda Lina.”
“Nakupenda pia Phillip, miaka yote, kama uliyoyasema ni kweli, basi mapenzi yangu kwako ndiyo yalinisababishia hata huu ulemavu.”
“Ndio maana niko na wewe, ndio njia pekee ya kukulipa kwa kile ulichopoteza kwa ajili yangu.”
Wakakumbatiana, Lina akiwa tayari kuanza tena lakini Phillip alimshauri wapumzike. Nusu saa baadaye ndipo walipoendelea mpaka usiku wa manane, kiasi
kwamba Phillip hakuweza kuondoka tena, huo ndio ukawa mwanzo wa kuishi ndani ya nyumba hiyo akifarijiana na Lina ambaye kwake Phillip alikuwa kila kitu.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Miezi sita ikapita na taarifa za uhusiano wao zikaenea kila mahali, wazazi wa Genevieve wakafurahishwa na jambo hilo wakiamini Phillip angesahau maumivu
aliyokuwa nayo.
“Kuna jambo nataka kukueleza.”
“Jambo gani?” Lina aliuliza.
“Nimefikia uamuzi wa kukuoa, wewe peke yako ndiye unaweza kunisahaulisha vifo vya mke na watoto wangu,” alisema Phillip.
Hakuwa na habari kabisa juu ya kilichotokea, kwamba watoto wake hawakuwa marehemu bali walitekwa na vijana wa Victor Federov.
“Unasema kweli Phillip?”
“Kweli kabisa.”
“Nipo tayari.”
“Lakini kuna kitu kimoja tu nataka kukueleza, kama utakubaliana nacho basi tutafunga ndoa yetu ili tuishi kwa furaha, kikikushinda basi tena maana mimi sina
la kufanya, ni maumbile na sitaki kurudia tena kufanya kitendo nilichokifanya huko nyuma.”
“Kitu gani hicho unachotaka kunieleza, usizunguke, niambie tu.”
“Bila shaka nimewahi kukueleza kwamba nina uwezo wa kutoa mbegu za kiume lakini hazina uwezo wa kurutubisha yai la mwanamke, hii ina maana kama
tukioana hatutakuwa na uwezo wa kuwa na motto. Je, hilo ni kikwazo kwako?”
“Hapana hata kidogo, cha muhimu kwangu ni kuwa na mtu anayenipenda, watoto ni majaliwa ya Mungu.”
“Ahsante Lina,” Phillip aliongea akimvuta na kumkumbatia, kilichofuata baada ya hapo ni sauti zao kuendelea kushuka huku wakinong’ona, neno I love you,
likisikika mara nyingi, ghafla ukimya ukasikika na milio ya “Jwig!Jwig!Jwig!” ikasikika! Kilikuwa ni kitanda kikipiga kelele. Phillip alikuwa kazini akifanya kila
alichoamini alikuwa na utaalam nacho ingawa hakuwa na uwezo wa kupata mtoto.
Siku iliyofuata kazini Lina alikuwa na jambo moja tu, kuwataarifu rafiki na wafanyakazi wenzake juu ya kilichokuwa kikifuata maishani mwake. Kila mtu
akawa na hamu ya kumwona Phillip, aliyejitolea kumuoa Lina. Siku ya siku ikafika, Phillip akatambulishwa kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa jijini Dar es
Salaam kwenye tafrija ndogo iliyofanyika katika Hoteli ya
Johannesburg, ambayo pia Phillip aliitumia kumvisha Lina pete ya uchumba.
Kamati ikaundwa na utaratibu wa michango kama ilivyozoeleka nchini Tanzania ukafuata. Kiasi kikubwa cha fedha kikakusanywa na hatimaye harusi kubwa
tena ya kifahari iliyosimamiwa na familia ya Lina pamoja na familia ya Genevieve na ndugu wa Phillip ikafanyika, ndoto ya Lina kuolewa na Phillip ikatimia.
Wakaanza kuishi pamoja kama mke na mume, katika maisha yaliyojaa furaha, huzuni zote zilizokuwa zimewafunika zikaondoka ingawa Phillip hakuisahau
familia yake. Kila Jumapili ilikuwa ni lazima asindikizwe na mke wake wakiwa njiani kuelekea kanisani hadi makaburini ambako alisali akimkumbuka mke
wake Genevieve na watoto wao Dorice na Dorica.
Hakuwa hata na hisia kidogo kwamba watoto wake walikuwa upande wa pili wa dunia, nchini Urusi wakiishi na baba yao wa kuwazaa, pia wakiwa hawana
kumbukumbu ya mahali walikotokea baada ya kumbukumbu zote kufutwa kichwani kwa sindano za dawa iitwayo Memory Eraser.
***
Ditrov alikuwa amelala sakafuni, risasi mbili zikiwa zimepenya mwilini. Kulikuwa na dalili zote kwamba alikuwa amekufa na Victor akiamini siri yake ya
kuwatorosha Dorice na Dorica kutoka Tanzania isingevuja, alisogeza mfuko mkubwa wa nailoni aliokuwa ameuandaa kwa ajili ya kazi hiyo na kuanza
kumwingiza ndani yake huku mwili wake wote ukitetemeka.
Alikuwa na uhakika asilimia mia moja hakuna mtu angegundua kilichokuwa kikiendelea, taratibu akausogeza mfuko kando na kuanza kuisafisha sakafu mpaka
alipohakikisha imetakata bila doa lolote la damu, akaunyanyua tena mfuko na kuupeleka mpaka kwenye lifti. Alipoingia ndani akabonyeza alama iliyoandikwa G,
ili kuiamuru lifti ishuke moja kwa moja mpaka chini kulikokuwa na maegesho ya magari.
“Afande! Afande! Afande!” aliita alipotoka kwenye lifti bila kuuchukua mwili wa Ditrov, alitaka kuhakikisha hakuna mtu eneo hilo, ukimya ulimthibitishia
kwamba aidha askari alikuwa amelala au alikuwa amepandisha juu kwa walinzi wenzake.
Akarejea kwenye lifti na kufungua, akaubeba mwili mpaka kwenye gari na kufungua buti kisha kuuingiza ndani na kufunika. Kwa kasi akazunguka upande wa
dereva na kufungua mlango, akawasha na kuondoka kwa kasi, sehemu ya kutokea askari walimsimamisha lakini walipogundua ni bosi wao hawakuwa na swali.
“Nahitaji jiwe, kamba ninayo,” aliwaza akiendesha gari kuelekea nyumbani kwake.
Nyumba yake ilijengwa ufukweni kabisa na alimiliki boti iendayo kasi, hiyo ndiyo alipanga kuitumia kwa ajili ya kazi iliyokuwa mbele yake. Bahati nzuri
hakuwa na mlinzi, alitumia mbwa na nyaya za umeme, hivyo alichofanya baada ya kuingia ndani ya ngome yake kabla hajafungua buti na kuutoa mwili wa Ditrov
ni kutafuta jiwe kubwa na kushuka nalo hadi ufukweni, akalifunga vizuri na kamba.
Bila kupoteza wakati akaja kwenye gari, akafungua buti na kuutoa mwili wa Ditrov ukiwa kwenye mfuko wa nailoni usiovujisha damu na kuubeba begani huku
akikimbia nao ufukweni.
Akaangaza macho yake huku na kule bila kuona mtu yeyote zaidi ya mbwa wake waliokuwa wakibweka, kilichosikika dakika chache baadaye ni muungurumo
wa boti ikikata maji kuelekea katikati ya bahari.
Dakika ishirini hivi baadaye, alizima injini na boti kusimama. Giza lilikuwa nene kila upande, hivyo hakumhofia mtu yeyote, haraka akalikamata jiwe na kulitupa
majini kisha kuusukuma mfuko, taratibu ukaingia majini na kuanza kuzama.
Huo ukawa mwisho wa Ditrov. Badala ya kusikitika, Victor Federov alitabasamu na kuwasha boti yake kisha kuondoka kwa kasi kurejea nyumbani ambako
aliegesha na kuingia ndani bila mtu yeyote kugundua.
Hakupata usingizi hata kidogo mpaka kulipopambazuka asubuhi,akajiandaa kwa ajili ya kwenda kazini ambako alifanya kazi kama kawaida, saa nne na nusu
alimpigia simu katibu muhtasi wake na kumwomba amwitie Ditrov.
“Hajaonekana tangu asubuhi bosi.”
“Haiwezekani, mtafuteni haraka sana nina kazi ya kufanya naye.”
“Sawa bosi.”
***
“Jina lako unaitwa nani?”
“Marina!”
“Na mwenzako?”
“Mariya.”
“Ninyi ni mapacha?”
“Ndiyo.”
“Baba yenu ni nani?”
“Victor Federov.”
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ahaaa! Kumbe ni ninyi?”
“Ndiyo.”
“Karibuni sana Moscow International School.”
“Ahsante.”
Victor Federov aliwapenda sana watoto wake, kuthibitisha jambo hilo alihakikisha wanapata elimu bora. Alikuwa na fedha nyingi, utajiri wake ulitisha hata
kama angetumia fedha zake kwa fujo kiasi gani, haikuwa rahisi kuzimaliza hivyo aliona ni bora kusomesha watoto wake kwenye shule nzuri ili wapate elimu
bora itakayowasaidia kuendesha miradi yake vizuri baada ya yeye kuondoka duniani.
Shule aliyoona inawafaa ni Moscow International School, ambayo kwa mwaka kila mtoto alilipiwa milioni ishirini na tano. Watoto walimfurahia baba yao,
hawakuwa na kumbukumbu yoyote tena juu ya Tanzania wala Phillip na Genevieve.
VICTOR Fedorov alipohakikisha kwamba sasa alikuwa amemaliza zoezi zima la mauaji, alirejea nyumbani kwake na kuingia moja kwa moja chumbani kwake
ambako alijitupa kitandani, hakika alijiona mshindi kwa kazi aliyokuwa ameifanya na sasa siri juu ya watoto ilikuwa imebaki kuwa yake peke yake.
Hakupata usingizi hata kidogo mpaka kulipopambazuka asubuhi, akajiandaa kwa ajili ya kwenda kazini ambako alifanya kazi kama kawaida, saa nne na nusu
alimpigia katibu muhtasi wake na kumwomba amwitie Ditrov.
“Hajaonekana tangu asubuhi bosi.”
“Haiwezekani, mtafuteni haraka sana nina kazi ya kufanya naye.”
“Sawa bosi,” katibu muhtasi alijibu.
Kwa muda wa nusu saa katibu muhtasi aliendelea kumtafuta Ditrov kwa namba zote alizozifahamu lakini hakupatikana, yeye pia akaingiwa na hofu, kwani
haikuwa kawaida ya Ditrov kutofika kazini bila sababu yoyote na hakuwahi hata mara moja kuzima simu zake za mkononi.
“Lazima atakuwa na matatizo huyu,” aliwaza katibu muhtasi akinyanyua simu ili amtaarifu bosi wake.
“Ngrii! Ngrii! Ngrii!” simu ilisikika upande wa pili ikiita.
“Ndiyo.”
“Bosi mpaka sasa sijafanikiwa kumpata Ditrov.”
“Umepiga simu yake ya mkononi?”
“Ndiyo, bosi, tena zote mbili.”
“Sasa atakuwa wapi huyu?”
“Kwa kweli hata mimi inanishangaza.”
“Jaribu kwa mara ya mwisho kumtafuta nitahitaji majibu kama bado atakuwa hapatikani basi taarifa itolewe polisi, sawa?”
“Nitafanya hivyo,” alijibu katibu muhtasi na kukata simu.
***
Wakaanza kuishi pamoja kama mke na mume, katika maisha yaliyojaa furaha, huzuni zote zilizokuwa zimewafunika zikaondoka ingawa Phillip hakuisahau
familia yake, kila siku ya Jumapili ilikuwa ni lazima asindikizwe na mke wake wakiwa njiani kuelekea kanisani hadi makaburini ambako alisali akimkumbuka
mke wake Genevieve na watoto wao Dorice na Dorica.
Wiki moja baada ya kufunga ndoa maisha yakiwa ya furaha Lina alitakiwa kurejea kazini, hivyo alilazimika kumpa Phillip taarifa juu ya habari hiyo.
“Mpenzi!”
“Ndiyo,” Phillip aliitika
“Kesho nitaanza kazi.”
“Vyema mke wangu mimi nitakuwepo tu hapa nyumbani.”
“Nyumbani?”
“Ndiyo.”
“Ok! Nahitaji kufahamu ulisomea nini?”
“Nilisomea mambo ya sheria.”
“Unao uzoefu wa kutosha?”
“Kabisa.”
“Basi nitakutafutia kazi nahitaji utoke nyumbani ili usiwe mpweke.”
“Mwaa! Mwaa!” Phillip alimbusu Lina mfululizo.
“Ahsante nakupenda Phillip, hakika nitakufanya kuwa mwanaume mwenye furaha siku zote.”
“Nitafurahi sana Lina, nakuwa mpweke zaidi pale ninapokumbuka familia yangu, hakika niliipenda lakini naona yalikuwa mapenzi ya Mungu wote wakaniacha,
naamini ujio wako kwangu utanirejeshea furaha iliyopotea miaka mingi kabla.”
“Hakika nakupenda amini,” Lina aliongea huku akimkumbatia Phillip wote kwa pamoja wakajifunika shuka na kulala. Kwao usiku ulionekana kuwa mfupi,
hakuna aliyekuwa akitamani kumwacha mwenzake kitandani lakini kwa Lina ilikuwa ni lazima afanye hivyo kutokana na kazi yake. Hivyo alijilazimisha na
kuamka kitandani kisha kuingia bafuni kuoga na kujiandaa tayari kwa kwenda kazini.
“Nitarejea muda si mrefu, nikuletee nini mpenzi?”
“Mh! Mh!” Phillip aliguna.
“Sema basi nikuletee kitu gani?”
“Nakuhitaji wewe,” alisema Phillip akimvuta Lina na kumpiga busu huku akimtakia siku njema.
Taratibu akatoka chumbani na kufunga mlango nyuma yake huku akimwacha Phillip kitandani.
****
Kwa muda wa saa tatu katibu muhtasi aliendelea kujaribu simu ya Ditrov bila majibu yoyote na hata alipojaribu kutuma mtu nyumba kwake na sehemu
mbalimbali ambazo alifahamu angeweza kuwepo, bado hakupatikana.
“Ni vyema nikamtaarifu bosi juu ya Ditrov kwamba hapatikani,” aliwaza akinyanyua simu na sekunde mbili tu baadaye sauti nzito ikasikika upande wa pili.
“Ndiyo.”
“Bosi sijafanikiwa kumpata.”
“Unasema?”
“Ditrov hapatikani tumejaribu kufuatilia sehemu mbalimbali ambazo mara nyingi hupenda kutembelea, majibu yanayotolewa ni yaleyale kwamba hajaonekana.”
“Mh! Piga simu polisi kisha utoe taarifa, inawezekana ametekwa au kuuawa na watu fulani, unanisikia?”
“Ndiyo.”
“Nahitaji kufahamu majibu ya polisi mara moja na kama inawezekana msako mkali ufanyike, nataka Ditrov apatikane haraka iwezekanavyo,” alisema Victor
Fedorov kwa hasira kali na kukata simu.
“Haa! Haaa! Haaa!” Victor Fedorov alicheka huku akinyanyuka kitini taratibu akasogelea picha kubwa iliyokuwa ukutani kisha kuibusu.
“Merina! Mariya! Nitawapenda mpaka kufa siko tayari kuwapoteza kwa gharama yoyote ile, ndiyo maana nimeamua kumuua Ditrov ili kuficha siri hii. Mwaa!
Mwaa!” Victor Fedorov aliongea akiikodolea macho picha hiyo.
ILI asigundulike kwa mauaji ya Ditrov anampigia simu katibu muhtasi wake akimtaka amtaarifu Ditrov kwamba alikuwa akimhitaji ofisini kwake kwa kazi
maalum. Ditrov anatafutwa kwa muda bila mafanikio.
Katibu muhtasi anamrejeshea majibu kwamba mpaka wakati huo bado Ditrov alikuwa hajapatikana sehemu yoyote ile.
Uamuzi pekee wa Victor Fedorov aliyekuwa akifahamu wazi mauaji aliyoyafanya, anaamuru taarifa hizo zitolewe kwa jeshi la polisi ili msako maalum ufanyike
haraka na Ditrov apatikane.
Ili kuficha siri ya mauaji ya Ditrov, Victor Fedorov anaudanganya umma wa Urusi kwamba naye pia yuko tayari kufanya kila kinachowezekana ili mradi tu
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ditrov apatikane, hivyo ameamua kwenda makao makuu ya polisi na kuzungumza na mkuu wao ili kama jeshi hilo lingehitaji msaada wowote kutoka kwake
basi wasisite kumweleza.
Baada ya maongezi hayo wote wawili waliagana na Victor Fedorov akatoka nje ya ofisi moja kwa moja akaliendea gari lake na kupanda kisha kuwasha na
kuondoka kwa kasi ya ajabu, kwa kumwangalia alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa kwa upotevu wa Ditrov lakini ukweli ni kwamba aliidanganya dunia,
aliufahamu ukweli wote na mpaka wakati huo alishaamini kwamba Ditrov alikuwa marehemu hivyo isingekuwa rahisi kupatikana tena.
Jeshi la polisi nchini Urusi lilidhamiria kufanya kila kilichowezekana ambapo Ditrov alitafutwa kila pembe, Urusi ikabinuliwa nje ndani, vyombo vya habari,
zikiwemo televisheni, vikirusha matangazo na kuonyesha picha ya Ditrov kwamba alikuwa amepotea katika njia ya kutatanisha na alikuwa akitafutwa kwa udi na
uvumba na yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwake awe mzima au marehemu basi angelipwa kiasi kikubwa cha fedha.
Watu nchini humo wakanyanyuka, wakaingia katika msako, Ditrov alikuwa akisakwa, kiasi kikubwa cha fedha alichokitangaza Victor Fedorov kiliwachanganya
watu wengi.Wakati msako huo ukiendelea, Victor Fedorov alikuwa akifuatilia kila kitu kwa karibu, aliwaona watu wote kuwa wajinga kwake, kwani ukweli ni
kwamba mpaka wakati huo Ditrov hakuwa tena hai, hicho ndicho alichoamini, hivyo hata zawadi aliyokuwa ameitangaza kwa umma alifahamu wazi kwamba
isingekwenda kwa mtu yeyote yule.
“Hata kitokee nini hawawezi kumpata niko tayari kufanya kila kitu watakachohitaji ili mradi tu kuuficha ukweli huu, sipo tayari, duniani hakuna siri ya watu
wawili, hivyo kifo cha Ditrov kimefanya siri kubaki kwangu peke yangu, Mungu atanisamehe,” aliwaza akiangalia tangazo lililomwonyesha Ditrov likipita
kwenye televisheni kubwa iliyokuwa ofisini kwake.
Mpaka wakati huo jeshi la polisi lilishafanikiwa kukagua hospitali zote nchini Urusi na kupata kibali cha kuingia katika vyumba vya kuhifadhia maiti kumsaka
mtu huyo lakini bado hakupatikana sehemu yoyote, nao pia wakaanza kupoteza matumaini kwani upotevu wa mtu huyo ulisababisha kusimamisha kazi zao
nyingi sana kutokana na Victor Fedorov kuwa na nguvu na ushawishi mkubwa sana ndani ya nchi hiyo.
Wiki ya kwanza ikapita msako ukiendelea kwa nguvu zote, wiki ya pili nayo ikapita hatimaye mwezi bila Ditrov kupatikana sehemu yoyote. Jeshi likashindwa
kuelewa ni wapi alikokuwa mtu huyo.
“Ngrii!Ngrii!Ngrii!” mlio simu ukasikika ndani ya ofisi ya Mkuu wa Polisi.
“Ndiyo.”
“Sawa mkuu, hakuna shida hata sisi wenyewe tumeona ni vyema tukapumzika ili tujipange tena upya kutafuta njia nyingine, zoezi hili limekuwa gumu sana
kwetu,” aliongea Mkuu wa Polisi ofisini kwake.
Victor Fedorov aliyekuwa upande wa pili wa simu ndiye aliyekuwa akiongea na mkuu huyo wa polisi akimpa ushauri wa juu ya zoezi hilo kwamba sasa lilikuwa
limeshindikana hivyo watafute mbinu nyingine zitakazowezesha kupatikana kwa Ditrov.
Mkuu wa polisi alikubaliana na Victor na kusitisha zoezi hilo akiwa haelewi kabisa upande wa pili wa myu huyo, akaunga mkono hoja na kukata simu.
“Sasa nina hakika Ditrov atakuwa amekufa, laiti kama angepona angeshajitokeza ninavyomfahamu mimi ni mtu hatari sana huyu, hawezi kuwa hai akaendelea
kujificha ni lazima angetoka na kuuelezea umma kila kitu,” aliwaza Victor Fedorov akiwa ndani ya ofisi yake.
***
Kitendo cha Lina kuongea na bosi wake na kumweleza kwamba katika ofisi yao alihitajika mwanasheria anayefahamu vyema sheria, kilikuwa ni kama bahati ya
mtende, akatembea taratibu na kurejea ndani ya ofisi yake, huku machozi ya furaha yakimtoka, alishindwa kuelewa ni bahati gani iliyokuwa ikimtokea, machozi
ya furaha yakaendelea kumtoka.
“Ahsante baba, Mungu kweli unatenda, hatimaye Phillip naye amepata kazi?” alijiuliza.
Kwa siku nzima, muda kwa Lina ulikwenda taratibu, saa zilikuwa hazisogei hamu yake kubwa ikiwa ni kurejea nyumbani na kumweleza Phillip juu ya habari
aliyokuwa ameipata.
“Phillip atafurahi sana kusikia habari hii,” aliwaza.
Akiwa ofisini kwake akakivuta kiti na kuketi, sauti nyingi zikimwijia kichwani mwake, tangu siku aliyokutana na Phillip jinsi alivyomweleza kwamba bado
alikuwa akimpenda na hatimaye kufunga ndoa na sasa alikuwa mke wa mwanaume aliyempenda kwa moyo wake wote.
“Ni kweli Phillip amefiwa na mke na watoto wake, lakini ilikuwepo sababu jambo hilo litokee ili mimi niweze kumpata, masikini Genevieve watoto wake
Dorice na Dorica nauahidi moyo wangu kumpa Phillip furaha yote mpaka mwisho wa maisha yetu, hakika ninampenda kwa dhati,” alijisemea Lina kwa sauti ya
chini chini.
Muda wa kurejea nyumbani ulipofika, hakuwa na sababu ya kuendelea kukaa ofisini, haja ya moyo wake ilikuwa ni kufika nyumbani na kumkuta mume wake
mpendwa Phillip ili amweleze habari njema aliyokuwa nayo.
Huku akitembea kwa madaha, mkononi akiwa amening’iniza funguo akalisogelea gari lake akaingia ndani na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi, mawazo
yake yote yakiwa kwa Phillip.
“Ninampenda, nafahamu wazi hata yeye ananipenda hanidanganyi hata kidogo, nitafanya kila kitu kuhakikisha simpotezi, mwanaume niliyempenda akanifanya
nikapata matatizo mengi maishani mwangu ndiye aliyeko ndani ya nyumba yangu sasa tena akiwa mume wangu!” aliongea Lina huku akizidi kukanyaga mafuta.
Kwa mwendo wa saa moja na dakika kadhaa tayari alikuwa nje ya lango la nyumba yake, bila kuchelewa akapiga honi na lango likafunguliwa, akapita moja kwa
moja ndani bila kusema kitu chochote na mlinzi wake.
“Mh!” mlinzi aliguna akishuhudia gari likizidi kutokomea. Kilikuwa ni kitendo cha ajabu sana kwani mazoea aliyokwishajijengea ilikuwa ni lazima asimamishe
gari na kumtania kidogo lakini siku hiyo haikuwa hivyo kwa Lina ilionekana kuwa tofauti.
“Pengine anaumwa au kuna nini kimempata? Si kawaida ya bosi wangu kuwa hivyo lazima takuwa na walakini. Ngoja nisogee karibu nione,” aliongea mlinzi
akisogea kwa mwendo wa pole.
“Bosi!” aliita.
“Bee!” Lina akaitika akitembea kwa kasi kuelekea lango la kuingilia ndani ya nyumba yake.
“Nini tatizo si kawaida yako kuwa hivyo unaumwa?”
“Mh!” alijibu akiingia ndani.
Mlinzi huyo alibaki hapo akiwa haelewi ni kitu gani kilikuwa kimempata bosi wake huyo, haraka akapata wazo kichwani mwake akaamua kuzunguka upande wa
pili wa nyumba ambako dirisha la chumba cha bosi lilikuwepo huko.
“Ngoja nisimame hapa kama kuna tatizo nitajua kupitia hapa,” aliongea mlinzi akisogea kwa kunyata dirishani.
“Darling! Darling! Uko wapi? Tafadhali njoo, nakuhitaji haraka sana!” sauti ya Lina ilisikika.
“Yes baby!” (Ndio mpenzi) sauti ya Phillip ikasikika kwa chini kutoka chumbani.
“Bado umelala?” Lina aliuliza.
“Ndiyo!” Phillip akajibu.
Kwa mwendo wa haraka h Lina akatembea kuelekea chumbani akafungua mlango na kuingia, Phillip bado alikuwa kitandani akiwa amelala na shuka likiwa
limemfunika mpaka kichwani.
“No! Unaumwa?” Lina aliuliza.
“Mh!” Phillip alijibu akitingisha kichwa.
Bila kuchelewa Lina akalivuta shuka na kulitupa pembeni, Phillip akaonekana na alipomwangalia vyema usoni aligundua alikuwa akilia kwani macho yake
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
yalivimba kupita kiasi.
“What happened?” (Nini tatizo?)
“Familia yangu, mke na watoto wangu wapendwa!” alijibu Phillip kwikwi ya kulia ikizidi kumkaba.
“Sikiliza mume wangu hebu niambie unachohitaji tufanye nini ili upate furaha iliyopotea, niambie niko tayari kutoka moyoni mimi siipendi hali hii!”
“Watoto! Nahitaji kupata mtoto angalau mmoja,” aliongea Phillip akilia kwa uchungu.
Maneno hayo pekee yalimfanya Lina aelewe ni kiasi gani Phillip alikuwa katika upweke bila kuchelewa akaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine na kuzitupa
pembeni kisha kukisogelea kitanda na kupanda juu yake akamvuta Phillip na kumkumbatia, mabusu mfululizo yakishuka juu ya mwili wa Phillip na neno I love
you, likisikika.
Mlinzi akiwa amesimama nje ya dirisha bila kuelewa ni kitu gani kilikuwa kikitokea alisikia sauti nyingine.
“Jwig!Jwig!Jwig!” kitanda kikipiga kelele.
“Mh!” mlinzi aliguna akiondoka eneo hilo.
KITENDO cha Lina kuongea na bosi wake na kumweleza kwamba katika ofisi yao alihitajika mwanasheria anayefahamu vyema sheria, kilikuwa ni kama bahati
ya mtende, baada ya kumaliza maongezi Lina anatembea na kurejea ndani ya ofisi yake, huku machozi ya furaha yakimtoka, anashindwa kuelewa ni bahati gani
iliyokuwa ikimtokea.
Muda wa kurejea nyumbani unapofika, ni wakati huo ndiyo haswa aliokuwa akiusubiri kwa hamu kubwa, ili akamweleza Phillip habari njema aliyokuwa
ameipata.Moja kwa moja anatembea kutoka nje ya ofisi yake kisha kulielekea gari lake aina ya Land Cruiser, anafungua mlango na kuingia ndani yake kisha
kuliwasha na kuliondoka kwa mwendo wa kasi mawazo yake yote yakiwa kwa Phillip.
Kwa mwendo wa saa moja na dakika kadhaa tayari alikuwa nje ya lango la nyumba yake bila kuchelewa akapiga honi na lango likafunguliwa, akapita moja kwa
moja ndani bila kusema kitu chochote na mlinzi wake, hali ambayo ilimshtua sana mlinzi huyo, kwani haikuwa kawaida ya Lina kufanya hivyo ilikuwa ni lazima
amtanie kidogo kisha kuelekea kwenye maegesho.
Hofu inamwingia mlinzi, hivyo kumlazimu kumfuata kujua ni kitu gani kilikuwa kimempata bosi wake, ananyata mpaka karibu na dirisha la chumba na
kusikiliza, anasikia maongezi kidogo na baada ya muda sauti ya kitanda inasikika, anaguna na kuondoka eneo hilo.
Upande wa pili wa hadithi hii tunamwona tajiri Victor Fedorov akiwa kifua mbele katika msako wa Ditrov, anaitumia nafasi hiyo kuficha uovu kwani ukweli
wote anaufahamu. Zoezi hilo linaendelea kwa muda mrefu bila mafanikio, hatimaye jeshi la polisi linasimamisha msako ili kutafuta njia mbadala ya kumpata
Ditrov. Taarifa hizo ndizo zinamfanya Victor Fedorov ajione mshindi.
Kwa muda wa saa mbili mfululizo, Phillip na Lina walikuwa kitandani kila mmoja akimwonyesha mwenzake ufundi wake wote kuhakikisha anapata furaha
aliyoitarajia. Si Phillip wala Lina wote wawili walikuwa katika ulimwengu mwingine wakisahau shida na matatizo yote yaliyokuwa yamepita katika maisha yao.
“Phillip” Lina aliita.
“Naam mke wangu”
“Leo nahitaji uniambie ni kitu gani nitakufanyia ili uwe na furaha, sihitaji kuona machozi yako kila wakati, yananisikitisha mno!”
“Unajua nini?”
“Mh!” Lina aliguna.
“Lina.” Phillip aliita huku macho yake yakimuangalia Lina.
“Bee.”
“Nahitaji mtoto hata mmoja tu”
“Hicho tu?”
“Hakika ndicho.”
“Phillip ni jambo la kuzungumza tu na si kuliweka kichwani mwako.”
“Nitazungumza nini Lina ili hali unafahamu wazi kwamba sina uwezo wa kuzaa!”
“Najua lakini kwangu hilo si tatizo.”
“Kwangu ni tatizo mpenzi, nahitaji mtoto hata mmoja tu ambaye ataniita baba nami nitamwita mwanangu.”
“Mh!” Lina akaguna tena huku akionyesha kusikitishwa na maneno ya Phillip.
Kwa muda wote wapenzi hao walikaa kimya kila mmoja akifikiri ni jinsi gani wangeweza kupata watoto, kwa Lina halikuwa swali gumu kwani yeye alikuwa ni
mzima kwa kila kitu tatizo pekee lilikuwa kwa Phillip ambaye mbegu zake hazikuwa na uwezo wa kurutubisha yai la mwanamke hivyo hata kama wangefanya
tendo la ndoa kwa muda wa zaidi ya miaka kumi bado uwezekano wa kupata mtoto usingekuwepo.
“Phillip!” Lina aliita akimgusa mumewe begani.
“Nakusikia.”
“Twende tukaoge kisha tujadiliane kuhusu jambo hili.”
“Sawa.” Alijibu Phillip wakinyanyuka kutoka kitandani wakajikongoja hadi bafuni na kuanza kuoga.
Kwa muda wa dakika kumi nzima waliutumia kuoga bafuni huko Lina akiongea mambo mengi kuhusu mapenzi, nia yake kubwa ikiwa ni kumfanya Phillip
aondokane na msongo wa mawazo uliokuwepo kichwani mwake. Hatimaye wakamaliza na kurejea tena chumbani ambako Lina alimkaribisha Phillip kwenye
kiti maalum kisha yeye akaelekea sebuleni ambako alifungua jokofu akatoa boksi la juisi, akachukuwa glasi mbili na kurejea chumbani.
Kwa mwendo wa madaha huku akiwa ndani ya taulo dogo la rangi nyeupe, Lina alitembea mpaka karibu kabisa na Phillip, akaweka vitu alivyokuwa navyo
mezani kisha kumsogelea Phillip na kumbusu mfululizo.
“Mwaa!Mwaaa!Mwaaa!”
“Ahsante,” alijibu Phillip kwa sauti ya chini.
Akiwa hapo, Lina alifungua boksi na kuanza kumimina juisi kwenye glasi moja baada ya nyingine na kumkaribisha Phillip huku akinyanyua glasi na kuipeleka
mdomoni mwake kisha kuirejesha tena kwa Phillip kama ishara ya kuonyesha pendo zito alilokuwa nalo juu yake.
“Nakupenda.”
“Mimi pia nakupenda Lina.”
“Ahsante, lakini pia nina habari njema sana kwako.”
“Kuhusu mtoto?” Phillip aliuliza.
“Mh! Hapana lakini ni njema.”
“Tafadhali nieleze usikawie.”
“Mh! Mh!” Lina aliguna mfululizo.
“Hebu shika mapigo ya moyo wangu yanasubiri habari hiyo kwa hamu kubwa, tafadhali nieleze kabla sija…” Phillip aliongea lakini kabla hajafika mwisho wa
sentensi yake Lina akanyoosha mkono wake na kuziba mdomo wa Phillip.
“Kunywa juisi kwanza nitakueleza si habari mbaya ni njema sana wewe mwenyewe hakika utafurahi.”
“Kweli?”
“Kabisa.”
Taratibu wakaendelea kunywa juisi huku mikono ya Lina ikipita huku na kule mwilini mwa Phillip huku maongezi matamu kati yao yakiendelea.
Hakika wawili hao walipendana kwa dhati, hawakuwa tayari kukumbuka historia zao za nyuma na hata ilipotokea jambo hilo likajirudia vichwani mwao basi
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
waliona ilikuwepo haja ya kupuuza mawazo hayo na kuendelea na starehe.
Muda ukazidi kusonga bila Lina kufungua mdomo wake kumweleza Phillip kitu chochote, moyoni akitafakari ni jinsi gani habari hiyo ingepokelewa kwani
alifahamu wazi kwa Phillip kupata kazi ingekuwa njia moja wapo ya kumwondoa katika msongo wa mawazo aliokuwa nao na hilo lingekuwa limekwisha na
jambo ambalo lingebaki kuwa kitendawili katika maisha yao, watoto ambao kwa Lina japo alikuwa mwanamke kamili hakuona umuhimu wowote alichohitaji
yeye kwa wakati huo ni kuwa na mwanaume aliyempenda kwa dhati na si kingine.
“Tafadhali Lina hebu nitoe katika mateso haya, nahitaji kufahamu ni kitu gani unataka kunieleza.”
“Hakuna jambo baya mpenzi wangu ni habari juu ya kazi”
“Kazi?”
“Ndiyo.”
“Imefanya nini?”
“Amini tayari umepata kazi”
“Mungu wangu! Unasema kweli Lina?”
“Ni kweli na si ndoto, Phillip tayari umeishika kazi mikononi mwako.”
“Wapi na lini?”
“Hivi sasa ninavyozungumza na wewe kesho asubuhi na mapema tutaongozana, kitu cha muhimu ni vyeti vyako vyote.”
“Sehemu gani?”
“Ofisini kwetu, Phillip ni bahati iliyoje, leo nilipoingia tu ofisini bosi wangu akaniita na kunieleza kwamba shirika letu lilihitaji mtu anayefahamu vyema sheria,
akili yangu ikakumbuka kwamba hata wewe ulisoma sheria na uliimudu vyema kazi hiyo.”
“Lina ahsante kwa mara nyingine, nimeamini unanipenda nami ninakupenda pia, moyoni mwangu naanza kuamini kabisa kwamba Mungu alikuwa nayo sababu
ya mambo yaliyotokea nyuma ya kupoteza mke na watoto wangu wote akifahamu wazi kwamba nitakutana na mwanamke mwingine atakayenipenda kama
Genevieve, Mungu azilaze roho za wapendwa wangu hawa mahali pema peponi amina,” alisema Phillip machozi yakimtiririka, wakati hayo yakiendelea Phillip
alihisi ni ndoto lakini alipofungua macho vizuri na kumwona Lina mbele yake akiwa katika sura ya kutabasamu, akanyoosha mikono na kumwelekea ambapo
bila kuchelewa Lina akajichomeka katikati ya mikono hiyo wakakumbatiana na kuanza kulia.
***
Wiki moja baadaye Victor Fedorov akiwa ofisini kwake akiamini kabisa kwamba kila kitu kilikuwa kimekwenda kama alivyotaka, anashtushwa na taarifa ya
habari kwenye televisheni.
“Mh ni kitu gani hiki?” anajiuliza akisogea karibu kabisa ili kusikiliza kwa ukaribu.
Mamia ya watu nchini Urusi walikuwa wakiandamana kupiga hoja ya jeshi la polisi kuhusu msako wa Ditrov, kwa ilivyoonekana wengi walikuwa wameumizwa
na jambo hilo na walichokihitaji kwa wakati huo ni kufahamu ukweli juu ya mauaji hayo, wakisisitiza na kulaani kwa nguvu zote uamuzi huo, wananchi wengi
wakidai kwamba nyuma ya pazia kulikuwa na siri nzito kwani kabla Ditrov hajapotea tayari washirika wake wote alioshirikiana nao katika kazi waliaminika kufa
tena vifo vya kutatanisha.
“Mh! Ni lazima niwafunge midomo, wataniletea matatizo hawa, sihitaji dunia ifahamu kwamba ninahusika na vifo hivi, nataka iendelee kubaki siri tena siri
kubwa, sasa ni wakati wa kuonyesha jeuri ya fedha zaidi ili kulifanya jeshi la polisi likae kimya milele,” aliongea Victor akinyanyua mkono wa simu.
“Hello!” akaita Victor Fedorov kwa sauti nzito.
“Ndiyo,” sauti upande wa pili ikajibu.
“Ah! Naweza kuongea na mkuu wenu, tafadhali?” aliuliza na ukimya wa ajabu ukatokea kwake akiwa bado ameshikilia mkono wa simu.
Akili yake yote ilisharuka, hakuelewa ni nini kingefuata baada ya hapo kwani kwa jinsi wananchi walivyokuwa wamekasirishwa na mauaji yaliyotokea, waliapa
kufanya chochote ili mradi tu wapate ukweli juu ya vifo vya ndugu zao.
Walikuwa tayari kufa lakini jeshi la polisi litoe tamko ambalo lingewaridhisha wote.
Pamoja na kiyoyozi kikali kilichokuwa ndani ya ofisi yake asubuhi hiyo Victor Fedorov alikuwa akitiririkwa na jasho mwili mzima akifahamu wazi kwamba
kama ingetokea siri yake ikagundulika basi angepoteza kila kitu alichokuwa nacho, si utajiri tu hata watoto wake na heshima aliyokuwa amejijengea kwa muda
mrefu.
Akiwa hapo taswira za watoto wake pacha, Mariya na Marina zikamwijia kichwani mwake, ni watoto hao ndiyo walisababisha afanye mauaji yaliyotokea ili
kuficha siri.
“Naitwa Victor Fedorov, nahitaji kuonana na wewe tena ikiwezekana leo hii, ni muhimu sana, kuna taarifa nimeiona ofisi kwangu sasa hivi juu ya wananchi
wanavyoandamana imeniumiza sana napenda nami niungane nao kufanya msako huo kwani nimepoteza mtu muhimu sana katika kazi zangu,” alisema
akipigapiga meza kuonyesha msisitizo.
“Karibu!” mkuu wa jeshi alijibu upande wa pili wa simu.
“Ok! Nitafika hapo ofisini kwako muda si mrefu, ni vyema tukapata muda wa faragha kwa mazungumzo yetu na ningeomba asiwepo mtu mwingine yeyote
wakati wa maongezi hayo.”
“Sawa hilo litafanyika,” sauti upande wa pili ikajibu na hapohapo simu ikakatwa.
Mkuu wa jeshi la polisi hakuelewa siri iliyokuwa ikimsumbua Victor Fedorov, alimwamini kwa asilimia mia moja kwamba naye alikuwa ameumizwa na mauaji
hayo ndiyo maana alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha msako unafanyika kwa namna yoyote ile.
Victor Fedorov akasimama kutoka kitini mwake na kutembea mpaka mbele ya kioo kikubwa kilichokuwa ndani ya ofisi yake, hapo akaweka tai yake vyema na
kuangalia uso wake na kwa kutumia kitambaa kidogo alichokuwa nacho akajifuta uso wake kisha kuchukua miwani ya rangi nyeusi akaivaa.
Kwa alivyoonekana, alidhamiria kuficha siri ya mauaji lakini msaada mkubwa ungetoka kwa jeshi hilo la polisi na kitu pekee ambacho angefanya ni kutumia
fedha tu ili mambo yaende kimya na hatimaye kupotea kabisa.
Akatoka nje ya ofisi yake na kumuaga katibu muhtasi wake kisha kutembea mpaka sehemu alipoegesha gari lake na kupanda, mwendo alioondoka nao eneo hilo
ulimshangaza kila mmoja aliyemwona kwani haikuwa kawaida yake.
“Mh!” mmoja wa wafanyakazi wake akaguna.
“Leo kuna tatizo hapa si kawaida ya bosi, hata miwani ulishawahi kumwona ameivaa?” mwingine alidakia.
“Mimi naona kupotea kwa Ditrov kumesababisha matatizo makubwa sana, alikuwa ni mtu wake wa karibu sana.”
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nakuunga mkono, hali hiyo imemchanganya kabisa bosi wetu,” yalikuwa ni maongezi ya wafanyakazi wawili waliokuwa nje ya ofisi wakimshuhudia Victor
Fedorov akitokomea.
Dakika kumi baadaye alishafika makao makuu ya jeshi la polisi Urusi, akaegesha gari na kushuka na kuanza kutembea kuelekea ndani ya ofisi, huku akiwa
mwenye wasiwasi mwingi.
Aliangaza huku na kule na kuingia ndani ambako alipokelewa na kukaribishwa moja kwa moja kwenye ofisi ya mkuu wa jeshi.
“Habari za muda?”
“Njema tu, pole na kazi.”
“Ah, tumeshazoea sisi, ndiyo kazi zetu.”
“Kuna jambo moja tu kwa sasa,” alisema Victor kwa kujiamini.
“Sawa kabisa.”
Mkuu wa jeshi akakaa vyema ili kumsikiliza Victor Fedorov.
“Kuna kitu gani kinaendelea mpaka sasa juu ya msako wa Ditrov?” Victor Fedorov aliuliza akivua miwani yake.
“Mh! Kama tulivyokubaliana, kwamba tusitishe zoezi mpaka tujipange upya halafu tuendelee lakini cha kushangaza wananchi wameanza kuingia mitaani
kupinga uamuzi huo huku wakisisitiza msako uendelee tena kwa nguvu zote, wengi wakidai kwamba kabla ya kupotea kwa Ditrov washirika wake wote
waliuawa tena vifo vya kutatanisha.
“Kwa hiyo ninyi kama jeshi mmeamua nini?”
“Tuendelee na msako…” alisema mkuu wa jeshi lakini kabla hajamaliza sentensi yake kelele za ajabu zikasika kutoka nje ya jengo.
“Ndiyo, tunataka uchunguzi uendelee, tunataka kufahamu ndugu zetu wako wapi, tunajua kuna mtu mkubwa anayefanya mauaji hayo, pengine kwa sababu zake
binafsi au kuficha siri fulani…Tunamtaka huyo atafutwe na ahukumiwe!” sauti zilisikika zikizidi kusogelea karibu kabisa.
“Choma hiyo! Choma jengo bila kuogopa, hakuna kurudi nyuma tunahitaji kufahamu ukweli tumechoshwa na jeshi kila wakati kutudanganya tu, chomaaaaa!”
sauti zilisikika zikisogea kuelekea makao makuu ya Jeshi la Polisi la Urusi.
“Mungu wangu!” mkuu wa jeshi alisema.
“Nini tena?”
“Wananchi hatimaye wameamua kuja mpaka huku, hili jambo siyo dogo hata kidogo ni lazima msako uendelee haraka sana,” alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi la
Urusi huku akinyanyua simu. Lakini kabla hajabonyeza namba mlango wa chumba chake ukafunguliwa kwa nguvu na askari mmoja akaonekana.
“Mkuu kuna matatizo.”
“Kimetokea nini?”
“Wananchi!”
“Wanafanya nini?”
“Wameamua kujitokeza kupambana na polisi eti wanadai kwamba kuna siri kubwa tunayoifahamu kuhusu mauaji yanayotokea.”
“Kwahiyo?”
“Wanaonekana wana hasira sana, tena wameshachoma vituo vya polisi karibu mji mzima na sasa wameingia hapa makao makuu.”
“Hebu nitoke kuongea nao.”
“Mkuu hapana, hutaweza! Wanaonekana kuwa na hasira nyingi sana.”
“Ni lazima kifanyike kitu hapa kunusuru usalama wetu na mali za nchi.”
“Kipi?”
“Mabomu ya machozi kuwatanya kwa nguvu sehemu zote ambazo wameandamana, umesikia?”
“Ndiyo mkuu,” alijibu askari huyo akitoka mbio kuelekea nje ambako alishuhudia maelfu ya watu wakizidi kusonga mbele kulielekea lango kuu ili waingie
ndani na kufanya walichokitarajia.
Askari huyo alipotupa macho mbele ili kuangalia vizuri, alishuhudia maaskari wengi wakiwa chini.
Lilionekana kuwa jambo la kutisha wananchi walikuwa wamedhamiria kwa nguvu zote kuingia mitaani si kufanya fujo bali kulitia hekaheka jeshi la polisi ili
liweze kuendelea na msako wake badala ya kukaa kimya.
“Hatimaye mwisho wangu umekuwa mbaya!” Victor Fedorov aliongea kwa sauti huku akinyanyuka kitini.
“Unasema?” mkuu wa jeshi aliuliza.
“Mh!” Victor Fedorov aliguna, na tayari alishaukamata mlango wa chumba akaufungua na kutoka nje huku akikimbia.
Walikuwa ni watoto wazuri, hakuna mtu aliyewaona watoto hao na kusita kutoa sifa midomoni mwao, japo walikuwa wadogo lakini uzuri wao ulionekana
waziwazi na watu wengi kusema kwamba wakikuwa wangekuwa tishio kwa wanaume wengi nchini Urusi.
Ni watoto hao Pacha Mariya na Merina ndiyo walikuwa wakileta machafuko nchini Urusi bila wao wenyewe kufahamu siri nzito ilikuwa imefichwa, wakilelewa
vyema na kusoma katika shule ya gharama huku wakihudumiwa kwa kila kitu walichohitaji wakiandaliwa kuja kuwa warithi wa mali za baba yao.
Kila aliyewaona watoto hao hakusita kujiuliza maswali juu yao, kwani walimfahamu vyema Victor Fedorov na historia ya maisha yake alishawahi kuoa
wanawake kadhaa na kuachana nao bila kuzaa nao watoto lakini ghafla watoto wawili wakaibuka na watu kuelezwa kwamba walikuwa ni watoto wake.
“Mh! watoto wazuri sana!”
“Ni kweli”
“Ni wa nani?”
“Victor Fedorov”
“Huyu tajiri hapa Urusi?”
“Haswa ndiye.”
“Amezaa lini na wapi?”
”Kwa kweli hilo swali hata mimi sifahamu ila wenyewe watoto ukiwauliza wanasema Victor Fedorov ndiye baba yao.”
“Mh! Haya ukiwaangalia wamefanana naye lakini walikuwa wapi na mama yao ni nani?”
“Mambo ya Ngoswe mwachie Ngoswe mwenyewe,” walikuwa ni walimu wawili wakiongea wakati watoto hao wakipita mbele yao.
***
Taarifa aliyokuwa ameipata Phillip kutoka kwa Lina ilimpa furaha ya ajabu mno, hakika hakuwaza wala kutegemea tena kwamba baada ya kifo cha mke na
watoto wake wapendwa angerejea katika hali ya kawaida kwani alishapoteza matumaini na hakuwa na furaha tena lakini kukutana na Lina kulirejesha furaha
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
iliyopotea miaka mingi huko nyuma.
“Ahsante mke wangu ninakupenda.”
“Nakupenda pia Phillip.” Lina alijibu macho yake yote yakimwangalia Phillip.
“Hakika sina cha kukuzawadia laiti kama ningeweza…”aliongea Phillip lakini sentensi yake ikakatishwa na busu la Lina ambalo lilitua moja kwa moja mdomoni
mwake.
“Najua unachotaka kusema.”
“Mh! Nini?”
“Unataka kuzungumza juu ya mtoto.”
“Ni kweli kabisa mke wangu sina uwezo wa kuzaa.”
“Tutapata mtoto.”
“Kwa njia gani?”
“Hata kama tutalazimika kutumia fedha zote tulizonazo lakini tupate mtoto!”
“Kivipi Lina?”
“Nitakueleza siku nyingine leo tupumzike kwa ajili ya kesho nitahitaji utafute vyeti vyako vyote na kuviweka pamoja tayari kwa kazi kesho.”
“Kesho?”
“Ndiyo!”
“Mh!” Phillip aliguna.
“Kwa nini unaguna?”
“Kesho sijajiandaa kabisa mke wangu.”
“Nasema kesho ni lazima tuondoke wote hapa nyumbani kwenda ofisini.”
“Sawa tuombe uzima,” alijibu Phillip na wote wakajitupa kitandani taratibu wakiwa hapo waliongea hiki na kile hatimaye wakapitiwa na usingizi.
***
Baaada tu ya kutoka ofisini kwa mkuu wa jeshi la polisi, Victor Fedorov huku akipishana na watu wengi njiani alifanikiwa kulifikia gari lake na kuingia ndani,
akaliwasha na kuondoka hapo kwa kasi ya ajabu kichwani mwake akiwaza kitu kimoja tu watoto wake.
Ni kweli alifahamu wazi kwamba wakati huo walikuwa shuleni lakini hakuelewa walikuwa katika hali gani kwani kwa jinsi hali ilivyoonekana mambo yalikuwa
yameharibika kabisa.
“Watoto wangu,”alitamka Victor Fedorov.
Shule waliyosoma Mariya na Merina haikuwa umbali mrefu sana kutoka mahali Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Urusi yalipokuwa hivyo wasiwasi wake ukazidi
kuongezeka maradufu.
“Kwa jinsi hali ilivyo lazima niwafuate watoto wangu,” aliwaza Victor Fedorov akiendesha gari kwa kasi kuelekea huko, kichwani akamkumbuka Ditrov na
unyama aliomfanyia, akaziona pia taswira za watoto wake Mariya na Merina wakimfurahia machozi ya uchungu yakamtoka lakini akajipa moyo na kusonga
mbele kuelekea shuleni kwa watoto wake.
Kwa mwendo wa dakika kumi nzima aliendesha gari hatimaye akafanikiwa kufika eneo la shule akiwa hapo akashangazwa na ukimya wa ajabu uliokuwepo,
hapakuonekana dalili ya walimu wala wanafunzi.
Haraka bila kuchelewa Victor Fedorov akaegesha gari lake na kushuka huku akiangaza macho huku na kule.
“Kimetokea nini hapa?” akajiuliza mwenyewe akitembea kwa kasi kuelekea majengo ya ofisi za walimu huko nako hakukuta mtu.
“Mungu wangu watoto wangu, haiwezekani,” aliongea Victor Fedorov akiingia mlango mmoja baada ya mwingine kukagua.
Shule ilikuwa kimya kabisa, hapakuonekana mtu yeyote eneo hilo zaidi ya karatasi zilizokuwa zikipepea juu kutoka ndani ya majengo kwenda nje. Moyo wake
ukamwenda mbio, jasho jingi likamtoka na alipojaribu kupaza sauti yake na kuita majina ya watoto wake halikupatikana jibu lolote.
“Nimekwisha!”alisema Victor Fedorov akiporomoka chini kama mzigo.
Oleg Malenko alikuwa ni mwanaume wa Kirusi, alizaliwa na kukulia nchi Urusi miaka mingi iliyopita, alikuwa ni baba wa watoto wawili na mke mmoja, jina
lake lilifahamika kwa wengi kutokana na kazi zake za uvuvi kwani aliendesha maisha yake kwa kazi hiyo.
Alikuwa ameifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka isiyopungua kumi na tano na bado, pamoja na umri wake mkubwa. aliendelea kuifanya kwani ndiyo kazi pekee
iliyoendesha maisha yake na familia yake.
Alfajiri ya siku hiyo kama ilivyokuwa kawaida yake, alitoka nyumbani kwake mapema kuliko kawaida akimuaga mke na watoto wake kwamba alikuwa akielekea
kazini kwake jambo ambalo liliishangaza sana familia yake lakini hawakutilia mashaka hali hiyo kwani walimfahamu vyema.
Hakuishi maeneo ya mbali sana kutoka ufukweni ambako ndiko aliegesha mtumbwi wake mdogo, hivyo kwa muda wa dakika kumi tu tayari alishafika eneo la
ufukweni, huku akiwa na taa ndogo mkononi mwake aliangaza macho yake huku na kule akijaribu kuangalia kama kulikuwa na mtu mwingine eneo hilo lakini
hakuona kitu.
Kwa ujasiri alitembea na kuusogelea mtumbwi wake kwa kutumia taa ndogo aliyokuwa nayo mkononi ambapo aliangaza ndani ya mtumbwi huo kuangalia kama
kulikuwa salama. Bila kuchelewa akaiweka taa ndogo aliyokuwa nayo mikononi mwake na kuanza kuusukuma mtumbwi huo kuelekea majini, tayari kwa
kuanza kazi.
Alfajiri ya siku hiyo bahari ilionekana kuwa kimya kabisa, hapakuwa na purukushani kama ilivyokuwa kila siku, hivyo kuwa na uhakika kabisa kwamba angevua
samaki wengi kwa sababu hakukuwa na watu wengine.
Kwa mwendo wa dakika kumi nzima aliendelea kupiga kasia akisonga mbele zaidi, lengo lake likiwa ni kufika mahali ambako aliamini samaki wengi zaidi
walipatikana lakini ghafla mbele yake aliona kitu cha ajabu ambacho hakukitarajia, moyo wake ukamwenda mbio pamoja na kwamba kwa wakati huo nchini
Urusi kulikuwa na hali nzuri ya hewa, lakini Oleg alitiririkwa na jasho jingi si kwa sababu ya kazi aliyokuwa ameifanya bali kwa kitu kilichokuwa mbele yake.
“Mungu wangu ni papa!”alijiuliza akinyanyua taa yake ndogo na kumulika eneo hilo.
Akayatoa macho yake yote kuangalia mbele lakini kwa sababu ya mwanga mdogo uliokuwepo hakuweza kuona vyema, woga ukazidi kumwingia na wazo pekee
lililomwijia kichwani mwake ni kugeuza mtumbwi wake haraka na kurejea alikotoka, jambo ambalo hakuwa na uhakika nalo kama angefanikiwa.
Akiwa hapo alishuhudia mtumbwi wake ukiyumbishwa huku na kule, tayari alijua alikuwa katika hatari.
“Leo ninakufa, sidhani kama nitasalimika, ” alijisemea Oleg huku machozi yakimbubujika.
***
Usiku ulionekana kuwa mrefu mno kwa Phillip, mawazo na akili zake zote zikiwa kwenye kazi ambayo Lina alikuwa amemuahidi. Moyoni akamshukuru Mungu
kwa mara nyingi kwa kumwona na kumchagua yeye, ni kweli alikuwa katika majonzi mazito lakini alikuwa amepewa njia nyingine tena.
“Jambo moja tu sasa litakalonisumbua ni jinsi gani nitapata tena watoto? Nahitaji watoto ambao watakuwa warithi wa mali zangu hapo baadaye,”aliwaza
kichwani mwake akivuta shuka na kujifunika.
Asubuhi ya siku hiyo yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuamka kitandani, taratibu bila kumwamsha Lina alitoka ndani ya chumba na kuelekea jikoni ambako
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
aliandaa kila kitu kwa ajili ya kifungua kinywa na kurejea chumbani ambako alifungua kabati akatoa nguo na kunyoosha tayari kwa maandalizi ya kwenda kazini.
“Darling?” (Mpenzi)
“Yes baby.” (Ndiyo mpenzi)
“Amka! Amka ukaoge sasa,” akasema Phillip kwa sauti ya kunong’ona.
“Mh!” Lina aliguna akijinyosha kitandani.
“Muda umefika?”
“Zamani sana mke wangu.”
Taratibu akafunua shuka na kunyosha mkono kuchukua simu yake ambayo haikuwa mbali, akatupa macho yake hapo na kugundua kwamba muda ulikuwa
umewadia na alitakiwa kufanya haraka ili wasichelewe.
Taratibu akashusha miguu yake kitandani huku akiwa katika hali ya usingizi, Phillip akamshika mkono na kumuongoza moja kwa moja mpaka bafuni ambako
walioga na kutoka.
“Utavaa nini leo?”
“Mimi?”
“Ndiyo.”
“Nguo tayari nimeshanyoosha.”
“Unasema kweli?”
“Hakika, nimeamka kitambo kidogo.”
Lina akasogea na kumbusu Phillip usoni ikiwa ni ishara ya kumshukuru, hakika watu hawa walikuwa katika penzi motomoto, kila mmoja akifanya mambo
mazuri kwa mwenzake kadiri alivyoweza.
Kwa pamoja wakavaa na kutoka chumbani kuelekea sebuleni ambako nako mambo yalizidi kumshangaza Lina kwani tayari chai ilishatengwa mezani, kazi yake
ilikuwa ni kusogea na kunywa.
“Leo umenifanyia mchezo wa ajabu sana mume wangu.”
“Kwa sababu nakupenda kupita kawaida.”
“Najua, nami pia ninakupenda sana Phillip.”
Kwa pamoja wakasogea mezani na kuketi hapo, wakanywa chai na walipomaliza Lina akachukua ufunguo wa gari lake aina ya Land Cruiser na kumkabidhi
Phillip.
“Wewe leo ndiye dereva.”
“Mh! Una uhakika?”
“Kabisa gari hilo ni lako sasa.”
“Na wewe je?”
“Nitapata lingine muda si mrefu.”
“Ahsante kwa kunipenda mke wangu.”
“Usijali.”
Huku mkono wa Phillip ukiwa kiunoni mwa Lina, taratibu wakitembea kuelekea eneo gari lilipoegeshwa, Phillip akabonyeza kitufe fulani kwenye ufunguo na
milango ikafunguka kisha kushika mlango mmoja wa mbele akaufungua na taratibu akamkaribisha Lina ambaye aliingia na kuketi huku akitabasamu.
Phillip naye akaelekea upande wa pili kwa dereva na kuingia ndani yake, akawasha gari kisha kutoka nje ya lango huku akipunga mkono kwa mlinzi ambaye naye
aliachia tabasamu.
***
Baada ya kutangaziwa hali ya machafuko nchini Urusi uamuzi pekee uliofikiwa na uongozi wa shule ni kufunga shule kwa muda, mkutano ukaitishiwa na
wanafunzi kupewa taarifa kwamba uongozi wa shule ulikuwa umeamua kusitisha masomo kwa muda kutokana na hali ilivyokuwa na kuwataka wanafunzi
warejee majumbani mwao mpaka hali itakapotulia.
Uamuzi huo pekee uliwafanya Mariya na Merina kutoa machozi, hawakuwa na uhakika kama wangeweza kufika nyumbani kwao salama bila matatizo yoyote,
isitoshe walizoea kuletwa shuleni na kufuatwa na sasa walikuwa wakirejea nyumbani wenyewe bila dereva.
“Mariya!” Merina aliita.
“Bee!”
“Twende huku.”
“Mimi sitaki nitakaa hapahapa kungojea gari la nyumbani.”
“Haliji sasa hivi na hali inazidi kuwa mbaya twende!”alisema Merina akimvuta Mariya ambaye muda wote alikuwa akilia.
Kwa pamoja huku kukiwa na purukushani nyingi, wakafanikiwa kutoka nje ya lango la shule wakiwa hawaelewi ni wapi waelekee.
“Merina! Mariya!” wakasikia majina yao yakitajwa.
Wakatupa macho yao kugeuka ili waangalie ni wapi sauti hiyo ilitoka na alikuwa ni nani aliyewatamka kwa majina.
“Mh! Unamjua?” Merina aliuliza.
“Hapana!”
“Lakini anatufahamu mbona ametuita kwa majina?”
“Hebu twende tukamsikilize pengine ametumwa na baba aje kutuchukua!”
“Mimi naogopa!” Mariya alijibu huku akisita.
Mbele yao alionekana mwanaume mrefu, mwili wake ulikuwa umejazia, na kwa kumwangalia harakaharaka alionekana kuwa ni mtu wa mazoezi. Kichwani
alivaa kofia kubwa, machoni alikuwa na miwani ya rangi nyeusi. Huku wakitetemeka kwa hofu, wakasogea karibu kabisa na mwanaume huyo.
“Mariya! Merina!” akaita tena.
“Bee!” wakaitika huku wakitetemeka kwa hofu.
“Safi dili limekamilika,”alijibu mwanaume huyo na kwa haraka akawakamata kwa nguvu na kuanza kuwavuta kuelekea sehemu ambayo hawakuifahamu.
Wakionekana wenye furaha mara kadhaa wakipigana mabusu bila kujali kwamba walikuwa barabarani, Phillip aliendesha gari na hatimaye kwa muda wa nusu
saa wakafika ofisini.
Ni Phillip aliyekuwa wa kwanza kushuka garini na kuzunguka tena upande wa Lina kisha kufungua mlango na kumshika mkono akimkaribisha.
“Ahsante”
“Mwaaa!”Phillip aliachia busu.
Kitendo hicho kilishuhudiwa na watu wengi waliokuwa wamefika ofisini muda huo. Hakika mapenzi yao yalipendeza.
“Si Lina yule?”
“Ndiye.”
“Na yule?”
“Mume wake.”
“Mh! Makubwa haya.”
“Kwa nini?”
“Si umeona mwenyewe,” yalikuwa ni maongezi ya wasichana wawili waliofanya kazi ofisi moja na Lina.
Kwa pamoja wakatembea njiani wakipishana na watu kadhaa na kuwasalimia na Lina alifanya utambulisho kidogo na kuendelea mbele.
“Ngo!Ngo!Ngo!” Sauti ya mlango ukigongwa ilisikika.
“Ndiyo.” Sauti kutoka ndani ikajibu.
Taratibu Lina akashika kitasa na kusukuma mlango kuingia ndani. Macho yake yakagongana moja kwa moja na bosi wake aliyekuwa ameketi nyuma ya meza
kubwa ofisini kwake asubuhi hiyo.
“Karibu sana Lina.”
“Ahsante,” alijibu Lina na alipofungua mlango vizuri alionekana kuongozana na mtu mwingine.
“Karibuni sana,” aliongea bosi huyo akijiweka vyema kitini huku macho yake yakimwangalia Phillip.
***
“Watoto hawa watanipa kile ninachokitafuta,” aliwaza mwanaume huyo akizidi kuwavuta watoto Mariya na Merina kuelekea sehemu ambayo hawakuifahamu.
Badru Divostroc alikuwa ni mwanaume katili aliyeogopwa na watu wengi nchini Urusi kwa vitendo vyake vya kimafia, kutokana na ukatili wake huo watu
wengi nchini humo wakambandika jina la Kuntakinte.
Kwake yeye kupata alichokihitaji halikuwa tatizo, hakuogopa kumwaga damu za watu ili mradi tu atimize alichokikusudia.
Kwa muda mrefu alifuatilia kwa ukaribu habari za tajiri Fedorov alitaka kumfahamu lakini hakupata mwanya huo, hivyo taarifa za Mariya na Merina ambao
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
walikuwa ni watoto wa Victor Fedorov kuingia nchini Urusi kulimpa furaha ya ajabu.
Baada ya kufuatilia kwa kina na kugundua kwamba Victor Fedorov aliwapenda watoto wake kuliko kitu kingine, aliamua kuwafuatilia kwa ukaribu akichunguza
shule waliyosoma na ni gari lililowapeleka na kuwafuata kuwarudisha nyumbani.
Kwa muda wa mwezi mzima alifanya kazi hiyo hatimaye akafanikiwa kugundua njia zote na namna watoto hao walivyopelekwa shuleni na kufuatwa
wakionekana kuwa katika ulinzi madhubuti.
Ni machafuko yaliyokuwa yakitokea nchini Urusi kwa wakati huo kwake yeye aliona ni kama bahati kwani nia yake ya kufanya utekaji nyara wa watoto wa tajiri
kama Victor Fedorov kungempa alichokikusudia.
“Leo nitajaribu kufanya utekaji nitatumia akili zangu zote kuwapata watoto wa Fedorov halafu…,”aliwaza huku akinyanyuka kitandani.
Akiwa chumbani kwake akaisogelea televisheni yake na kuiwasha macho yake yakakutana moja kwa moja na habari za maandamano makubwa ya wananchi
nchini Urusi waliokuwa wakipinga matokeo ya jeshi la polisi baada ya kusitisha msako wa kumsaka Ditrov, wananchi walikuwa wakiandamana mitaani wengi
wakishinikiza msako uendelee.
“Hureee! Hureee utajiri huo mikononi mwangu,”alipiga kelele akirukaruka chumbani mwake.
Taarifa hiyo iliamsha vyema hisia zake, kwani kwa muda mrefu alikuwa amefanya kila alichoweza kupata utajiri aliokuwa nao Victor Fedorov lakini
hakufanikiwa, sasa ulikuwa umekaribia kuingia mikononi mwake.
Haraka bila kuchelewa akavuta suruali yake aina ya jeans, fulana pamoja na koti kubwa akavaa, akageuka tena upande mwingine akavuta soksi za mikononi na
kuzivaa kisha kofia kubwa pamoja na miwani ya rangi nyeusi akakisogelea kioo kilichokuwa chumbani kwake na kujiangalia na kutikisa kichwa kwa jinsi
alivyobadilika.
Taratibu akanyanyua gorodo na kuchukua bastola yake ndogo na kuipachika kiunoni.
“Hakuna mtu atakayeweza kunitambua kwamba mimi ndiye Badru…,’aliongea akifungua mlango ili atoke nje.
Akitembea kwa kujiamini moja kwa moja akaliendea gari lake aina ya Noah akaingia na kuliwasha, mawazo yake yote yakiwa juu ya watoto wa Victor Fedorov,
aliamini kama angefanikiwa kuwapata watoto hao na kuwateka hakika angepata malipo makubwa kutoka kwa tajiri huyo.
Kwa mwendo wa dakika kumi nzima aliendesha gari hatimaye akafanikiwa kufika shule waliyosoma watoto hao. Akaliegesha gari lake mbali kidogo na shule
kisha kushuka na kutembea njiani akipishana na watu wengi wakikimbia huku na kule.
“Wale pale,”aliongea akisogea karibu kisha kuanza kuwaita kwa majina.
“Wewe ni nani?”
“Hakuna haja ya kunifahamu, twendeni huku.” Sauti ya mwanaume huyo ikajibu akiwavuta watoto hao.
“Mariya” Merina aliita huku akilia.
“Bee.”
“Huyu ni nani na tunakwenda wapi?” Merina aliuliza swali jingine tayari wote wawili walikuwa wakilia huku wakijaribu kujitoa mikononi mwa mwanaume
huyo.
Kwa nguvu zake zote aliwavuta watoto hao mpaka wakalifikia gari ambalo lilikuwa limeegeshwa nje kidogo ya eneo la shule akafungua mlango na kuwatupia
ndani yake, akaangaza macho huku na kule kuangalia kama kulikuwa na mtu yeyote karibu eneo hilo, wengi walionekana wakikimbia kunusuru maisha yao.
“Ninachohitaji hivi sasa ni fedha, Victor Fedorov ni lazima atoe fedha kuwaokoa watoto wake vinginevyo nitawaua,” Badru aliwaza kisha aliwasha gari na
kuliondoa kwa kasi.
Mshtuko aliokuwa ameupata hakika ulikuwa hauelezeki, kupotea kwa watoto wake wawili? Lilikuwa ni swali ambalo halikuwa na jibu kichwani mwake, kwa
dakika tano nzima aliendelea kubaki chini akiwa haelewi ni kitu gani angefanya ili kuwapata watoto wake Mariya na Merina.
Machozi yakamtiririka, alipojaribu tena kupaza sauti yake akiwaita kwa majina bado hakusikia sauti yoyote zaidi ya mwangwi uliopenya moja kwa moja
masikioni mwake. Victor Fedorov akajiona ni mwanaume mwenye mkosi maishani mwake.
Akiwa haelewi ni kitu gani afanye, alijikongoja na kunyanyuka chini bado akiendelea kuangaza macho yake huku na kule pengine kuona kama walikuwa
wamejificha mahali na baada ya kumwona wangejitokeza awachukue na kwenda nao nyumbani. Haikuwa kama alivyowaza, bado Merina na Mariya
hawakuonekana sehemu yoyote ile ndani ya shule. Jasho jingi likimtiririka, alijikongoja na kulifikia gari lake akafungua mlango na kuingia ndani kisha
akaliwasha na kutoka eneo hilo la shule.
“Watakuwa wapi hawa? Nini kimewapata watoto wangu,” alijiuliza maswali mfululizo bila kupata majibu.
Nje ya lango la shule bado vurugu iliendelea kuongezeka, watu wengi wakionekana kukimbia huku na kule kuokoa maisha yao, akakodoa macho yake yote
kuangaza kila upande akiwatafuta watoto wake lakini bado hakuwaona, lakini akiwa hapo akajipa moyo na kuamini kwamba huenda walimu waliamua
kuwarudisha nyumbani kwa sababu ya machafuko yaliyokuwa yametokea siku hiyo.
“Nakwenda nyumbani watakuwa huko nina uhakika,” aliwaza akikanyaga mafuta kusonga mbele.
Victor Fedorov aliishi nje kidogo ya jiji, hivyo ilimchukua muda wa dakika arobaini kufika kwenye makazi yake, kichwani mwake akiwa na mawazo mengi juu
ya usalama wa watoto wake ambao mpaka wakati huo hakufahamu kabisa ni wapi walipokuwa na kama walikuwa hai au wamekufa.
“Piii!Piiii!” ilikuwa ni honi nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake.
Mara moja bila kuchelewa mlinzi alilifungua lango, akaingia ndani ya ngome ambapo aliliegesha gari lake kisha akashuka haraka.
Akazungusha macho yake huku na kule ndani ya ngome yake lakini hakuona kitu, hata alipojaribu kuangalia gari ambalo mara kadhaa liliwapeleka shule watoto
wake na kuwafuata, nalo pia halikuonekana sehemu yake.
“Watoto wamerudi?” aliuliza kwa sauti ya ukali.
“Hapana bosi.”
“Unasema kweli?”
“Nina hakika.”
“Zhukov naye yuko wapi?”
“Sijamwona.”
“Mungu wangu watoto wangu!” alisema Victor Fedorov akichomoa simu yake ya mkononi mfukoni, akaonekana akibonyeza namba kadhaa kisha kuiweka
sikioni na kusikiliza. Akiwa hapo mlinzi akamshuhudia bosi wake akitoka mbio kuelekea ndani bila kusema chochote, alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa
kabisa.
Aliingia ndani na dakika mbili baadaye alitoka nje mkononi akiwa na bastola, na bila kusema chochote akaamuru lango kuu lifunguliwe, akaingia ndani ya gari
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kisha kuliwasha na kutoka mbio kama vile alikuwa katika mashindano.
“Nitaua! Nasema nitaua sina mchezo mbele ya watoto wangu,” alisema peke yake ndani ya gari.
Huku akiwa katika mwendo wa kasi, Victor Fedorov aliendelea kuangaza macho yake huku na kule pembezoni mwa barabara lakini bado hakuwaona watoto
wake. Alikuwa ameamua kuingia mwenyewe barabarani akiwasaka kwa udi na uvumba watoto wake Mariya na Merina ambao mpaka wakati huo hakujua
walikuwa wapi na kitu gani kilikuwa kimewapata. Kwa saa saba mfululizo aliendelea kuwasaka huku akijaribu kuwasiliana na watu mbalimbali kwa msaada,
lakini bado hawakupatikana sehemu yoyote.
Hatimaye akaamua kuingia katika hospitali moja baada ya nyingine akiuliza kama kulikuwa na majeruhi yeyote au watu waliofariki, lakini bado jibu liliendelea
kubaki palepale; hakukuwa na kitu cha aina hiyo.
“Fyuuu!”akashusha pumzi kwa nguvu. Victor Fedorov hakuwa tayari kuwapoteza watoto wake alikuwa tayari kutumia kila kitu alichokuwa nacho lakini si
kuwakosa maishani mwake, hakika aliwapenda kupita kawaida katika maisha yake yote yaliyobaki duniani, aliamini hakuwa na ndugu mwingine zaidi ya watoto
hao.
Siku hiyo ikapita kukiwa hakuna dalili zozote za kuwapata watoto wake na hata alipojaribu kurejea nyumbani na kuangalia bado walikuwa hawajaonekana,
akiwa hapo akamkumbuka Ditrov na kuamini kwamba pengine asingemuua angekuwa msaada mkubwa katika kupatikana kwa watoto wake.
“Ditrov angekua hai hakika ninaamini watoto wangu wangepatikana,” aliwaza akijifuta machozi.
Kwa siku tatu mfululizo bado watoto waliendelea kusakwa huku na kule nchini Urusi pamoja na machafuko yaliyokuwepo, nchi hiyo ilibinuliwa nje ndani,
msaada mkubwa ukifanywa na polisi lakini bado hawakupatikana.
Hatimaye siku ya nne asubuhi Victor Fedorov akiwa ameshakata tamaa juu ya kuwapata watoto wake, wazo likamjia kichwani mwake kwamba ajaribu
kutangaza katika vyombo vya habari juu ya kupotea kwa watoto.
Huku akiwa mwenye mawazo mengi akakubaliana na wazo hilo.
“Nitakwenda kwenye televisheni ya taifa na kutangaza pengine kuna mtu amewaona sehemu fulani,” aliwaza akilini mwake.
Ndani ya nyumba yake hakukulika wala kukakalika, mawazo na akili yote ilielekea kwa watoto wake. Hivyo asubuhi hiyo alitoka nyumbani kwake na jambo
moja tu; tangazo.
Akaingia ndani ya gari lake na kuliwasha bila kusema chochote akamwonyesha mlinzi ishara na lango likafunguliwa, taratibu akaanza kutoka nje, lakini kabla
hajafika mbali mbele yake aliona kitu ambacho hakikuwa cha kawaida.
“Mh ni kitu gani kile?” alijiuliza akizima gari lake na kushuka kukielekea kitu hicho moyoni mwake akiwa na wasiwasi mwingi.
JASHO jingi lilikuwa kitiririka mwilini mwake, akatembea taratibu kukielekea kitu kilichokuwa mbele yake hatua chache tu tayari akawa amekifikia, alipotupa
macho yake vyema kuangalia aligundua ilikuwa ni bahasha kubwa nyeupe na juu yake iliandikwa kwa maandishi ya rangi nyekundu akasimama kwa muda
akijaribu kusoma ni kitu gani kiliandikwa juu yake.
“Victor Fedorov!” Moyo wake ukazidi kumwenda mbio, kitendo cha kukuta bahasha hiyo nje ya lango lake hakikuwa cha kawaida tena na jina lake kwa
maandishi ya rangi nyekundu? Likawa ni swali jingine kichwani mwake akazidi kuchanganyikiwa.
Bila kupoteza wakati akiwa haelewi ni kitu gani kingetokea akapiga moyo konde na kuinama kuikota bahasha hiyo na kwa ujasiri wa hali ya juu haraka
akaifungua ndani na kutoa kipande kidogo cha karatasi nacho pia kiliandikwa kwa rangi nyekundu.
“Anayeua kwa upanga naye hufa kwa upanga” Kilisomeka kipande hicho cha karatasi.
Victor Fedorov akiwa haamini maneno aliyokutana nayo ndani ya karatasi hiyo akapikicha macho yake tena na kurudia bado yaliendelea kusomeka hivyo hivyo
kama mwanzo.
“Mungu wangu!” Akasema kimoyomoyo akiketi chini na kuendelea kusoma zaidi.
“Ninachohitaji kwako ni fedha, ili uweze kuwapata watoto wako Merina na Mariya kama unawahitaji wakiwa hai. Ninatoa muda wa saa ishirini na nne tu
kuanzia sasa vinginevyo watakuwa marehemu, nakuhakikishia watakufa kifo kibaya kwa kuwakata kiungo kimoja baada ya kingine hadi umauti uwafike.
Kumbuka kama unawapenda watoto wako ni vyema ukafanya kila unachoweza ili uweze kuwapata na usijaribu kutumia jeshi la polisi kwa usalama zaidi.
Mara tu utakapokuwa tayari nitapenda unitaarifu kwa namba hizo hapo chini ili tukubaliane, sawa?
Tahadhari mimi ni mtu hatari sana, ukigeuka nyuma utaniona , kushoto, kulia na mbele pia nipo hivyo kabla hujafanya maamuzi yoyote tumia busara zako zote
vinginevyo utajuta…
Kwa heri.” Ilisema sehemu ya barua hiyo.
“Ni Ditrov.”Alinong’ona.
Victor Fedorov akahisi vitu kama maji maji vikitiririka ndani ya suruali yake, hakika hakuamini alichokisoma kichwani mwake taswira ya Ditrov ikamjia akahisi
pengine mtu huyo hakufa kama alivyofahamu.
“Noooo!” Akapaza sauti.
Akatupa macho yake pande zote nne bila kuona kitu akayerejesha tena kwenye saa yake ya mkononi akasoma akagundua amebakiza saa kumi na tisa tu muda
aliokuwa amepewa na mtu aliyedai kuwa na watoto wake uwadie vinginevyo wangekufa.
“Mariya! Merina!” Akaita akikimbia kuelekea ndani ya nyumba yake, bila kukumbuka gari alilokuwa ameliegesha pembeni kidogo.
Moja kwa moja akagonga lango na mlinzi kulifungua bila kusema chochote akazama ndani akikimbia huku akilia.
“Kuna nini tena?” Mlinzi aliuliza lakini hakujibiwa kitu chochote.
Tayari Victor Fedorov alishazama ndani, kitu cha kwanza bila kupoteza wakati akaisogelea simu akainyanyua ili apige namba aliyokuwa ameisoma kwenye
kipande cha barua kilichokuwa mkononi mwake.
Huku machozi yakimbubujika akakikunjua kipande hicho na kuanza kuzisoma namba na kubonyeza moja baada ya nyingine kisha kuweka mkono wa simu
sikioni akisikiliza upande wa pili.
Takribani dakika tatu nzima simu hiyo iliita bila kupokelewa akili yake ikazidi kuvurugika akiwa haelewi ni kitu gani angefanya upande mmoja wa akili yake
ukimwambia atoe taarifa hiyo kwa Jeshi la Polisi na mwingine ukimwambia kufanya hivyo ni kuwapoteza watoto wake wapendwa Mariya na Merina kwani
alishapewa onyo juu ya jambo hilo.
“Hapana ngoja niwe mvumilivu nitawapata tu, isije kuwa ni Ditrov hana huruma mtu huyu anachokisema kinakuwa kweli, atawaua watoto wangu!” Alijiuliza
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
maswali mengi mfululizo bila kupata majibu.
Dakika tano nzima baadaye alikuwa tena katika simu akibonyeza namba zile zile na kusikiliza ghafla akasikia sauti nzito upande wa pili ikapokea.
“Ah!Ah!” Kigugumizi kikamshika pamoja na ukatili wake wote Victor Fedorov hapo alikuwa hana ujanja tena, alikuwa tayari kupoteza kila kitu alichokuwa
nacho lakini si watoto wake, aliwapenda kupita maelezo.
“Niko tayari...sawa…ndiyo…hapana…usiwaue…nitakupa hata kama ni utajiri wangu wote….Mungu wangu…niambie unapatikana wapi…nimekuelewa
sitafanya hivyo… niambie unataka kiasi gani?” Yalikuwa ni maongezi katika simu na mtu mwingine upande wa pili ambaye hakuonekana na baada ya maongezi
hayo simu ikakatwa.
Akiwa amepigwa na butwaa, taswira za watoto wake Mariya na Merina zikamjia, masikioni mwake akasikia sauti zao wakimwita na kumwomba asiwaache
wafe, Victor Fedorov akalia kama mtoto mdogo.
SURA yake ilikuwa imebadilika kabisa, macho yakabadilika na kuwa ya rangi nyekundu, mwili wake ukaanza kutetemeka kama mtu aliyekuwa na homa kali,
Victor Fedorov akauona utajiri wote aliokuwa nao haukuwa na maana kwake kama tu angewakosa watoto wake ambao kwa hakika alikuwa ametumia kiasi
kikubwa cha fedha ili kuwapata na sasa walikuwa katika hatari nyingine ya kifo kama tu asingetimiza jambo alilotakiwa kulifanya ndani ya saa chache alizopewa.
Kwa muda wa dakika tano aliendelea kutafakari na hakuelewa ni kwa nini mtekaji huyo alifanya tendo hilo, akavuta kumbukumbu zake nyuma akijaribu
kufikiria watu wote aliowahi kuwakosea na kuwadhulumu lakini hakuna alichokumbuka.
Mara kadhaa taswira ya Ditrov ilimjia lakini akatupilia mbali mawazo juu ya mtu huyo na kuamini kwamba tayari alishakufa.
“Nilimuua ili kuficha siri sikuwa na tatizo jingine kabla!” alisema akitembea kukielekea kiti kilichokuwa mbele yake. Huku jasho jingi likimtiririka,
akakisogelea kiti na kuketi, moyoni mwake akiwa na hofu juu ya watoto wake.
“Nitatoa kiasi chochote cha fedha atakachohitaji mtu huyo ili mradi tu niwapate watoto wangu!” aliwaza akijifuta machozi.
Alipotupa macho yake kwenye saa yake ya mkononi hofu ikazidi kumwingia, mbele yake kulikuwa na saa kumi tu zilizobaki katika saa ishirini na nne alizopewa
na muuaji.
Haraka akanyanyuka kitini na kusogelea tena simu akapiga namba zilezile alizobonyeza mwanzo kisha kuiweka simu sikioni, alikuwa hapo kuzungumza na mtu
huyo ataje kiasi hicho cha fedha na sehemu ambapo angezikuta na yeye kupata watoto wake wakiwa salama.
***
Ilikuwa ni familia yenye furaha kupita kawaida, kila mtu aliyewaona aliona wivu, hakika walivutia, walikuwa na kila sababu ya kuitwa mke na mume. Lakini
pamoja na mambo yote hayo kutawala maishani mwao, jambo moja tu lilikuwa likiwasumbua ni wapi wangepata mtoto.
Kwa mwanamke halikuwa tatizo sana, kazi kubwa ilikuwa kwa mwanaume ambaye alitumia muda mwingi kufikiria namna gani angeitwa baba kama ilivyowahi
kutokea miaka mingi kabla.
“Darling” (mpenzi), Phillip aliita siku moja asubuhi.
“Yes baby!” (Ndiyo mpenzi)
“Ni miaka minne sasa tupo kwenye ndoa lakini mimi sina uwezo wa kuzaa nataka tuliongelee jambo hili ili tufikie muafaka juu ya nini cha kufanya, napenda
niitwe baba hata kama mtoto huyo atakuwa si wa kwangu,” alisema Phillip.
“Unamaanisha nini Phillip?”
“Sina nia mbaya, ila nataka nikupe nafasi ya wewe kuzaa kwa sababu huna tatizo lolote.”
“Mh!” Lina akaguna.
“Ni ukweli mke wangu nakupenda sana lakini nitakupenda zaidi utakapofanikiwa kuniletea mtoto.”
“Phillip mbona sikuelewi, mtoto atoke wapi? Ni kweli mimi sina tatizo lakini nitampata wapi mtoto ili hali wewe ndiye mume wangu na tayari una tatizo?”
“Tafuta mwanaume yeyote ambaye atakuwa tayari kuzaa na wewe Lina halafu mimi nitalea mtoto huyo!” alisema Phillip akilengwalengwa na machozi.
Ilikuwa ni kauli ngumu sana kuitamka mdomoni hasa kwa mwanaume aliyempenda mke wake kupita maelezo, lakini haikukwepeka kwa sababu walihitaji mtoto
ndani ya nyumba ambaye angekuwa mrithi wa mali zote walizokuwa nazo.
Lina akamwangalia Phillip kwa muda, hakuwa tayari kuamini kauli aliyoisikia mdomoni mwa Phillip, kwani katika muda wote walioishi pamoja ndani ya
nyumba Phillip alionyesha kumpenda na mara kadhaa akimwomba kuwa mwaminifu katika mapenzi yao.
“Phillip!” Lina aliita.
“Yes honey” (ndiyo mpenzi) aliitikia Phillip huku macho yake yakimwangalia Lina kwa huruma.
“Unamaanisha unachosema?”
“Hakika, wala sina utani juu ya hilo.”
“Ni kwa nini umefikia hapo, hivi kweli unanipenda?”
“Nakupenda kupita maelezo wewe mwenyewe unafahamu.”
“Sasa?”
“Nataka kuitwa baba.”
“Phillip hutaumia kugundua kwamba mkeo unayempenda kwa dhati amekutana na mwanaume mwingine kisha kupata ujauzito?”
“Nimekaa na kufikiria kwa muda mrefu si kwamba sitaumia, ninachohitaji ni wewe kufanya kila unachoweza upate ujauzito halafu mimi nitautunza mpaka
utakapojifungua mke wangu.”
“Phillip kumbe hunipendi,” alisema Lina akibubujikwa na machozi.
Phillip akanyanyuka kitini na kusogea karibu kabisa na kiti alichoketi Lina kisha kumkumbatia wote kwa pamoja wakaanza kulia.
“Uamuzi wangu si mbaya, ninachohitaji wewe uwe na furaha mke wangu matatizo yangu mimi yasikufanye ukakosa kuitwa mama maishani mwako,” aliongea
huku akimpigapiga Lina mgongoni.
“Phillip hivi utajisikiaje kuona mimi ni mjamzito halafu si wa kwako?”
“Kwa sababu nimetoa idhini mimi mwenyewe sitaumia, ninachotaka ni wewe uitwe mama na mimi baba basi.”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni ngumu Phillip, mimi siwezi kulisaliti penzi letu acha tubaki hivihivi bila mtoto naamini Mungu alikuwa na makusudi juu ya hilo.”
“Unasema?” aliuliza Phillip akinyanyuka kitini, alikuwa hatanii bali alimaanisha alichokuwa akikisema. Haja ya moyo wake ilikuwa ni kuitwa baba bila kujali ni
wapi mtoto huyo angepatikana.
“Phillip.” Lina akaita huku akijaribu kumfuata.
“Lina nataka mtoto!”
“Phillip haiwezekani mimi siko tayari kusaliti penzi letu.”
“Unanipenda?” Phillip aliuliza kwa kujiamini.
“Nakupenda sana mume wangu.”
“Basi nataka mtoto!” aliongea Phillip huku akitembea kuondoka eneo hilo.
“Mungu wangu! Ni papa?”alijiuliza huku akinyanyua taa yake ndogo na kumulika eneo hilo huku akitetemeka kwa hofu.
Akayatoa macho yake yote kuangalia mbele lakini kwa sababu ya mwanga mdogo uliokuwepo hakuweza kuona vyema. Woga ukazidi kumwingia na wazo pekee
lililomjia kichwani kwa wakati ule lilikuwa ni kugeuza mtumbwi wake haraka na kurejea alikotoka, jambo ambalo hakuwa na uhakika nalo kama lingesaidia
kuokoa maisha yake.
Akiwa hapo alishuhudia mtumbwi wake ukiyumbishwa huku na kule, akajua tayari amejiingiza kwenye hatari.
“Leo ninakufa huku nikijiona,” alisema Oleg Malenko huku machozi yakimbubujika kwa wingi mashavuni. Hofu kuu ilikuwa imemkumba na hakuna
alichokuwa anakisubiri zaidi ya kifo, tena cha kuliwa na papa.
Aliifanya kazi ya uvuvi kwa kipindi kirefu lakini hata siku moja hakuwahi kukutana na dhahama kama ile. Zaidi alifanya kusimuliwa na wavuvi wenzake
kwamba watu wengi hufa baharini, hasa wavuvi baada ya mitubwi yao kuvamiwa na kupinduliwa na samaki wakubwa.
Kwa Oleg Malenko siku hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia tukio hilo, akaamini kabisa kwamba kifo kilikuwa kimemkaribia. Taswira za mke
na watoto wake zikawa zinapita kwa kasi kichwani mwake kama filamu ya kusisimua, machozi ya uchungu yakawa yanamtoka.
Akiwa katika mawazo hayo, haraka alipata wazo la kupiga kasia kwa nguvu na kugeuza mtubwi wake kwa kasi kurejea upande aliokuwa mara ya kwanza lakini
tayari alishachelewa, akahisi mtumbwi ukivutwa kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu.
“Nakufaa! Nakufaa!” alisema kwa lugha ya Kirusi akiomba msaada.
***
Muda mfupi baada ya kuzamishwa baharini akiwa amefungwa jiwe kubwa mwilini mwake ili asipate nafasi ya kujiokoa kwa lengo la kupoteza ushahidi, Ditrov
alirejewa na fahamu baada ya kupigwa na baridi kali. Alijaribu kufurukuta kwa kupiga mbizi ili kujiokoa lakini hakufanikiwa.
Alipotumia nguvu za ziada alizokuwa nazo mwilini mwake, bado aliendelea kutapatapa na sasa akawa anavutwa kuelekea chini ya bahari na lile jiwe kubwa
alilokuwa amefunganishwa mwilini. Akiwa katikati ya hali ya kupoteza fahamu na uzima, alikumbuka picha ya tukio zima lililotokea ofisini kwa bosi wake,
Victor Fedorov hadi wakati ule. Alikumbuka jinsi alivyofyatuliwa risasi bila huruma ambazo zilipenya kwenye mwili wake na kumsababishia maumivu makali.
Akiwa katika hali hiyo kwa takribani dakika kumi nzima, aliendelea kujivuta huku na kule ndani ya maji ili kujiokoa lakini zoezi hilo lilionekana kuwa gumu
kwake. Akawa anazidi kuzama! Ditrov alizidiwa nguvu na maji, akaanza kukata tamaa lakini upande mwingine wa akili yake alikuwa na matumaini makubwa ya
kusalimika na kifo.
“Ma…ji!” alitamka kwa tabu akiwa bado anatapatapa, moyoni akasikia sauti ikimwambia kuwa hapaswi kukata tama kwani kufanya hivyo kungemaanisha kifo
chake.
“Sitaki ku…fa!” akatamka tena kwa tabu.
Hali yake ilizidi kuwa mbaya, uwezekano wa kutoka baharini akiwa salama ukazidi kupungua kutokana na maumivu aliyokuwa anayahisi baada ya risasi
kuupenya mwili wake na kusababisha atokwe na damu nyingi. Pamoja na kuwa jabali, Ditrov hakuwa na uhakika kama angesalimika lakini bado hakukata tamaa.
Ghafla akiwa katika hali ya kukata tama, alikumbuka kitu. Wakati anaingia ofisini kwa Victor Fedorov, ndani ya mfuko mmoja katika suruali yake alikuwa na
kisu kidogo cha kukunja, akaamini huenda kingemsaidia kuokoa uhai wake.
Kwa nguvu zake zote alijitahidi kuingiza mkono mfukoni lakini hakufanikiwa, akajaribu tena upande mwingine wa suruali yake na kukumbana na maumivu
makali.
Licha ya maumivu hayo alijaribu tena kuusogeza mkono wake zaidi mpaka akaufikia mfuko wa suruali, kwa taabu kubwa akafanikiwa kugusa kitu kigumu na
kuamini kwamba kilikuwa chenyewe.
Akiwa katika hali ya kutapatapa akafanikiwa kuupenyeza mkono mfukoni na kuchomoa kisu, kwa taabu kubwa akakishika vyema na kujaribu kuikata kamba ili
ajinusuru na umauti uliokuwa ukiinyemelea roho yake.
Hakuwa tayari kukutana na kifo. Ni kweli alifahamu wazi kwamba kila binadamu angeonja mauti lakini hakuwa tayari kufa kikatili kiasi hicho.
“Nitajaribu mpaka mwisho, ikishindikana basi,”aliwaza akilini mwake.
Kwa nguvu kidogo alizokuwa nazo alikishika vyema kisu kidogo alichokuwa nacho mkononi, licha ya maumivu makali aliyokuwa nayo upande wake wa kulia,
aliikamata vyema kamba aliyokuwa amefungwa shingoni na kuanza kuikata.
“Krii!Krii!Krii!” aliendelea kusugua kisu katika kamba ili ikatike na kumwacha huru. Kwa takribani dakika tano nzima aliendelea kung’ang’ana na kisu lakini
zoezi hilo lilionekana kumshinda. Akaanza kuhisi fahamu zikipotea na nguvu kidogo alizobakiwa nazo zikamwishia. Licha ya hayo yote, bado hakuchoka, alitaka
kuendelea kujaribu.
***.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ngrii!Ngrii!Ngri” Ulikuwa ni mlio wa simu ndani ya nyumba ya Victor Fedorov. Aliinuka taratibu huku akitetemeka na kuisogelea simu hiyo ili aipokee akiwa
haelewi ni nani alikuwa akipiga.
“Ndiyo,” akajibu huku akitetemeka.
“Muda unazidi kuyoyoma! Ninachohitaji kutoka kwako ni kiasi cha dola milioni 290 ili niweze kuwaachia watoto wako. Ningependa fedha hizo nizipate ndani
ya Msitu wa Beloomut, kusini mwa Jiji la Moscow kwa usalama zaidi.
“Msitu wa Beloomut?” aliuliza lakini kabla hajapata jibu kutoka upande wa pili wa simu, alisikia sauti za watoto wake wakimwita.
“Daaaady!” (Babaaaa!) kilio kikali kilifuatia nyuma yake, Fedorov akazidi kuchanganyikiwa akili.
HALI yake ilikuwa mbaya hakuwa na uwezo wa kutoka baharini akiwa salama, risasi zilizoupenya mwili wake zilifanya amwage damu nyingi. Pamoja na kuwa
jabali, Ditrov hakuwa na uhakika kama angesalimika.
Ghafla akiwa katika hali ya kukata tamaa akakumbuka kitu wakati anaingia ofisini kwa Victor Fedorov, mfuko mmoja katika suruali yake alikuwa na kisu
kidogo cha kukunja akaamini huenda kisu hicho kingemsaidia kwa asilimia zote.
Kwa nguvu zake zote akajitahidi kuingiza mkono mfukoni lakini hakufanikiwa akajaribu tena upande mwingine wa suruali yake na kukumbana na maumivu
makali lakini pamoja na maumivu hayo akajaribu kuusogeza mkono wake zaidi mpaka kuufikia mfuko wa suruali. Kwa taabu kubwa akafanikiwa kukuta kitu
kigumu na kuamini kwamba kilikuwa chenyewe.
Akiwa katika hali ya kutapatapa akafanikiwa kuupenyeza mkono mfukoni na kukichomoa kisu kwa taabu kubwa, akakishika vyema na kujaribu kuikata kamba ili
ajinusuru na umauti uliokuwa ukiinyemelea roho yake.
Hakuwa tayari kukutana na kifo, ni kweli alifahamu wazi kwamba kila binadamu angeonja mauti lakini hakuwa tayari kufa kwa ukatili kiasi hicho, hivyo alitaka
kujiokoa.
Upande mwingine wa hadithi hii tunamwona Victor Fedorov na sharti alilopewa la kuzipeleka fedha hizo kwenye msitu wa Beloomut. Je, atafanikiwa
“Tafuta mwanaume yeyote ambaye atakuwa tayari kuzaa na wewe Lina halafu mimi nitalea mtoto huyo,” maneno hayo yalijirudia kichwani mwa Lina.
Hali ya hewa ikabadilika ghafla furaha yote iliyokuwepo ndani ya nyumba ikapotea, Phillip akiwaza jambo moja tu mtoto, hata Lina alipojaribu kumpa ushauri
bado hakusikiliza.
“Phillip mimi siko tayari,” alisema Lina.
“Unamaanisha nini?”
“Siko tayari kusaliti penzi letu sababu kubwa ikiwa ni mtoto.”
“Mimi ndiyo mumeo nimeshasema tafadhali fanyia kazi maneno yangu.”
“Hapana, kwa hilo nimekataa.”
“Lina unanipenda kweli?”
“Asilimia mia moja.”
“Basi fanya ninachotaka.”
Lina hakujibu kitu akainamisha kichwa chake chini huku kwikwi ya kulia ikimkaba, hakuwa tayari kukubaliana na maneno ya mumewe, kwake yeye mapenzi
yangekuwepo tu hata bila kupata mtoto. Ni kweli yeye binafsi alikuwa mzima, tatizo lilikuwa kwa mume wake lakini tangu mwanzo alishakubaliana nalo.
Akiwa katika mawazo hayo akamshuhudia Phillip akitoka sebuleni na kuelekea chumbani huko hakuchukua muda mrefu sana akamwona tena akitoka mkononi
akiwa na funguo za gari.
“Phillip!” Lina aliita lakini hakuitikiwa badala yake akashuhudia macho makali ya Phillip yakimwangalia, yalionyesha dalili zote kwamba alikuwa na hasira kali.
Akamshuhudia akifungua mlango na kutoka nje bila kusema neno lolote.
Uchungu wa ajabu ukaugubika moyo wa Lina, hakuwahi kushuhudia katika kipindi chote cha miaka minne alichoishi na Phillip kama mke na mume kwamba
siku moja ingegeuka na kuwa shubiri.
Machozi ya uchungu yakamtiririka mashavuni mwake.
“Mtoto! Mtoto analeta matatizo katika penzi letu,” alisema Lina akinyanyuka kitini kuelekea nje huko nako akamshuhudia Phillip akiwasha gari na kutokomea
kwenda sehemu ambayo haikujulikana.
***
Msitu wa Beloomut ulikuwa ni wa hatari sana, kila mtu nchini Urusi aliuogopa, wengi wakaupachika jina la msitu wa ajabu kwa matukio mbalimbali ya kutisha
yaliyowahi kutokea ndani yake.
Iliaminika kwamba mpaka wakati huo zaidi ya Warusi elfu moja walishakufa baada ya kuingia ndani ya msitu huo na wengi wao miili yao haikuonekana kabisa.
Ni matukio hayo ya kutisha ndiyo yaliyosababisha serikali ya nchi hiyo kuingilia kati na kuutangaza msitu huo kwamba ulikuwa tishio na watu kupewa onyo
kwamba asitokee mtu yeyote kwenda eneo hilo.
“Msitu wa Beloomut?” lilikuwa ni swali likipita kichwani mwa Victor Fedorov, pamoja na kuwa mwanaume wa shoka, jina hilo lilimtia wasiwasi, akavuta
kumbukumbu zake mara kadhaa juu ya matukio mabaya yaliyowahi kutokea katika msitu huo, akaangua kilio.
Kwa Victor Fedorov kiasi cha fedha alichotakiwa kukipeleka kwenye msitu huo hakikuwa tatizo, utajiri wake ulitisha lakini kitu kimoja tu kilimsumbua akilini
mwake, ni majanga mengi juu ya msitu huo, hakuwa tayari kwenda kufa lakini aliwahitaji sana watoto wake na ili awapate ni lazima apeleke fedha hizo sehemu
aliyoelekezwa.
“Niko tayari kutoa kiasi hicho cha fedha lakini je, nitanusurika? Watoto wangu watakuwa hai?” bado aliendelea kujiuliza kichwani mwake. Pamoja na maswali
yote hayo bado taswira za Merina na Mariya ziliendelea kuzunguka ndani ya akili yake, hakuwa tayari kuwapoteza, hao ndiyo ndugu pekee aliokuwa nao.
“Nitafanya kila ninachoweza kuwakomboa watoto wangu hata ikitokea mimi mwenyewe nikafa lakini wao wapone,” aliwaza.
Akili yake ikaonekana kusimama, kwa mara ya kwanza akamkumbuka Ditrov, kwa wakati huo alionekana kuwa ni mtu muhimu sana kwake, aliamini kabisa
kwamba mtu huyo angekuwepo maishani mwake kila kitu kingekwenda kama alivyotaka kwani fedha zilikuwa kila kitu katika maisha yake.
“Sitaki kujutia kifo cha Ditrov, nitapambana kiume,” alisema kwa sauti ya kunong’ona.
Akiwa na hofu, taratibu alianza kutembea kuelekea chumbani ambako alifungua mlango na kuingia ndani akanyoosha moja kwa moja mpaka kwenye moja ya
makabati makubwa na kufungua. Pamoja na utajiri wote aliokuwa nao, Victor Fedorov aliweka kiasi kikubwa cha fedha ndani ya nyumba ili kukwepa usumbufu
wa kwenda benki mara kwa mara.
Huku machozi yakimbubujika, akanyoosha mkono na kuvuta moja ya mifuko iliyoonekana ndani ya kabati hilo na kuutoa nje, fedha nyingi zikaonekana na bila
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kupoteza muda akaanza kuchukua bunda moja moja na kuyahesabu.
“Nitafanya kila kinachowezekana kuwapata watoto wangu hata akitaka nusu ya utajiri wangu nitampa lakini …” hakumalizia sentensi hiyo mara mlio wa simu
ndani ya nyumba yake ukasikika.
***
Kwa muda wa saa nne mfululizo Lina aliendelea kumsubiri Phillip lakini hakuonekana, hata alipopiga simu yake ya mkononi haikupatikana. Lina
akachanganyikiwa, hakuelewa ni wapi alikuwa na kitu gani kilimpata kwani hali aliyoondoka nayo nyumbani siku hiyo haikuwa ya kawaida.
“Mungu nisaidie arejee nyumbani akiwa mzima, nitaendelea kusubiri kama saa moja mbele asipotokea nitakwenda kutoa taarifa polisi, pengine amejinyo…”
alisema Lina na sentensi yake kukatizwa na honi ya gari nje ya lango la nyumba yao iliposikika.
Haraka akasimama kitini ili achungulie nje, akamshuhudia mlinzi akilisogelea lango lakini badala ya kufungua akachungulia, hofu ikazidi kumwingia.
“Ngoja niende mwenyewe,” alijisemea Lina akitembea kutoka nje kuelekea langoni na bila kusema chochote akauliza swali moja tu kwa mlinzi huyo.
“Ni Phillip?”
“Hapana ni mgeni tu.””Mgeni? Hebu nimwone,” alisema naye pia akachungulia.
Ilikuwa ni sura ngeni kabisa kati yao, alipoliangalia gari pia hakulifahamu, taratibu akasogea na kumsabahi kijana aliyesimama nje ya gari.
“Ndiyo kaka nikusaidie?”
“Samahani sijui hapa ndiyo kwa Phillip?”
“Ndiyo!”alijibu Lina akionekana mwenye wasiwasi mwingi.
“Amenituma barua hii hapa,” alisema kijana huyo akinyoosha mkono kumwelekea Lina ili amkabidhi bahasha ndogo iliyokuwa mikononi mwake.
HUKU akitetemeka aliunyoosha mkono na kupokea barua hiyo macho yake yote yakimwangalia kijana aliyemkabidhi, alitaka kumsoma vyema na kumwelewa
alitoka wapi na alitumwa na nani.
“Ahsante kaka sijui naweza kukuuliza jambo?”
“Uliza tu dada yangu.”
“Naweza kufahamu barua hii imetoka wapi na kwa nani?”
“Mh, kwa kweli sifahamu mimi nimetumwa tu kuileta hapa.”
“Uliambiwa umpe nani?”
“Mke wake Phillip?”
Tayari mashavu ya Lina yalishajaa machozi, kichwani mwake alielewa kabisa kwamba barua hiyo ilitoka kwa Phillip hivyo alitaka kuthibitisha jambo hilo.
Baada ya maongezi hayo kijana huyo aliingia ndani ya gari lake na kuliwasha kisha kuondoka.
Taratibu huku mapigo ya moyo yakimwenda mbio, Lina alijikaza na kutembea kuingia ndani lakini hakufika mbali sana akaketi chini. Haraka akaanza kuchana
bahasha ili asome barua iliyokuwa ndani.
Mke wangu mpendwa,Kwanza kabisa amini kwamba ninakupenda kwa dhati Mungu ni shahidi juu ya hili, nimeamua kuondoka hapo nyumbani kutokana na
hasira iliyokuwa ndani yangu. Lengo langu kwako si baya ni zuri, sihitaji kitu kingine kutoka kwako zaidi ya mtoto, napenda unizalie mtoto mmoja tu nami
niitwe baba. Jambo nililokueleza mwanzo sikukosea, nilitamka nikiwa na akili zangu timamu. Lina naamini unanipenda ndiyo maana ukaamua kunipokea mimi
na matatizo yangu yote. Tafadhali fanya kila unachoweza ili lengo letu litimie.
Najua itakuwia vigumu kuamini maneno yangu lakini kipande hiki cha barua ni ushahidi tosha kwamba siwezi kukuruka hata kitokee nini, nakupenda mke
wangu.
Ni kweli inauma sana lakini hakuna jinsi fanya unavyoweza tafuta mwanaume ambaye wewe mwenyewe utamridhia na uhakikishe unapata ujauzito wake, mimi
binafsi sihitaji kumfahamu hata kidogo ninachohitaji ni wewe kupata ujauzito basi.
Najua kichwani mwako utakuwa na maswali mengi ambayo hayatapata majibu lakini huo ndiyo uamuzi wangu, Lina uvumilivu umefikia mwisho. Tafadhali mke
wangu niamini niko tayari tena kwa moyo mkunjufu, nahitaji mtoto.
Kama utakuwa tayari kukubaliana na jambo hili na mimi mumeo, basi nipigie simu na kunijulisha nami nitakuwa tayari kurejea nyumbani tuendelee kuishi kama
awali.
Sisi wewe tu unayelia machozi hata mimi mwenyewe nakiri kutoka ndani ya moyo wangu huku nilipo sina raha hata kidogo akili yangu yote ikiwa kwako mke
wangu mpenzi.
Tafadhali chukua hatua fanya maamuzi sahihi kisha utanijulisha.
Nakupenda.
Ilimaliza barua hiyo.
Kwikwi ya kulia ikamkaba Lina, hakuwa tayari kuamini maneno yaliyokuwa ndani ya barua hiyo, taswira ya Phillip ikamjia kichwani mwake mfululizo, siku
zote aliamini kwamba Phillip alikuwa ni mwanaume wa maisha yake lakini sasa kulikuwa na dalili zote kwamba penzi lao lilikuwa likielekea mwisho.
“Nampenda sana Phillip lakini kwa hili sipo tayari,” alisema Lina huku akijifuta machozi, haraka akanyanyuka na kukimbilia ndani.
Ulikuwa ni mtihani mwingine tena katika maisha yake. Hakuwahi kusikia wala kuona mwanaume aliyeweza kumtoa mkewe kwa mwanaume mwingine ili
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wafanye tendo la ndoa lengo hasa likiwa ni kupata ujauzito.
“Mh! Phillip hivi amepatwa na nini? Kwangu mimi mtoto si kitu, ninachojali ni mapenzi ya dhati, kwa nini asikubaliane na mimi? Mungu wangu tafadhali okoa
jahazi hili lisizame, mimi siko tayari kufanya hivi anavyotaka.” Aliongea Lina machozi yakimbubujika.
Hatimaye usiku ukaingia bila kumwona Phillip akirejea nyumbani hapo ndipo akaamini kwamba mwanaume huyo alikuwa akimaanisha alichokisema.
“Nitamsubiri mpaka asubuhi niangalie kama kweli hatarudi basi nitajua cha kufanya.”
Usiku mzima hakupata hata lepe la usingizi, muda wote akimfikiria Phillip na mtihani aliokuwa amempa. Upande mwingine wa akili yake ulimwambia kwamba
huenda mtu huyo alikuwa akimpima imani lakini upande mwingine ulimweleza wazi kwamba Phillip hakutania. Hatimaye mapambazuko yakawadia, Phillip
akiwa bado hajarejea nyumbani, akayaamini maneno yake.
Siku nzima Lina alishinda ndani, aliamua kupiga simu kazini kwake na kuwaeleza kwamba siku hiyo asingeweza kudhuhuria kwani alikuwa mgonjwa hivyo
alihitaji kupumzika ili kuangalia afya yake. Aliamua kuuficha ukweli kwa kudanganya hivyo ili tu asipate bughudha, huku akiwa na mawazo mengi kichwani
mwake Lina bila kula kitu chohote alirejea kitandani kwake na kulala usingizi.
Saa zikazidi kusonga, hatimaye mchana ukaingia, akiwa hapo akapata wazo la kuamua kumpigia mmoja wa marafiki zake ofisini ili aongee naye na kumuuliza
kama alishamuona Phillip ofisini siku hiyo. Akaisogelea simu kisha kubonyeza namba kadhaa na kuiweka sikioni.
“Habari?” alisikika akisalimia mtu upande wa pili wa simu ambaye hakuonekana akatulia kidogo na kisha kujibu.
“Oh! Leo naumwa rafiki siko sawa, nauliza jambo moja tu vipi leo umemwona shemejio?” akatulia tena.
“Yupo, basi nilitaka tu kujua kama amekuja maana anaweza kusema amekwenda kazini kumbe kapita kona,” alidanganya kisha wakaagana na simu kukatwa.
“Yaani Phillip! Phillip ananitenda hivi? Ameshindwa kurejea nyumbani lakini ameweza kwenda kazini? Lazima atakuwa na mwanamke sehemu fulani.
Amepata wapi nguo za kuvaa? Kwa inavyoonekana Phillip hatanii anamaanisha anachokisema…lakini mimi siwezi kufanya anavyotaka…mh! Naona penzi letu
limefikia mwisho,” aliwaza Lina. Lakini ghafla akarejesha akili yake nyuma na kukumbuka mmoja wa marafiki zake katika ofisi yake alivyokuwa akimsifia
Phillip, alionekana kumpenda kama si kumtamani.
“Inawezekana Magreth amenigeuka? Mara kadhaa amekuwa akimsifia sana Phillip, pengine ndiko huko alikokwenda? Hapana nitafanya uchunguzi kwanza.”
Wiki nzima ikakatika bila Phillip kurejea nyumbani, hali hiyo ikazidi kumtia Lina kizungumkuti, ni hapo ndipo alipoamua kumpigia simu Phillip na kumweleza
kwamba anamwomba arejee nyumbani ili wafanye mazumgumzo.
“Tafadhali mume wangu naomba urudi nyumbani tuzungumze,” alisema Lina huku akilia.
“Je, umekubaliana na mimi?” aliuliza Phillip.
Kwa muda alikaa kimya akijaribu kutafakari ni jibu gani angempa mume wake ili akubali na kurejea nyumbani, hakuwa na jinsi alimhitaji mno. Huyo ndiye
alikuwa mwanaume wa maisha yake, hakika alimpenda Phillip kwa dhati.
“Ni…ko…taya…ri,” alitamka Lina huku akilia.
–
BAADA tu ya kufanikiwa kuikata kamba na kutumia nguvu kidogo alizokuwa nazo huku damu nyingi zikimwagika sehemu ya bega la kushoto, alijaribu kupiga
mbizi, lengo lake likiwa ni kujiokoa, kichwani mwake hakuwa na matumaini yoyote pamoja na kwamba alishapitia mambo mengi ya Kimafia lakini hilo kwake
lilionekana kuwa gumu.
Kadiri alivyoendelea kupiga mbizi ndivyo fahamu nazo zilivyozidi kupotea taratibu, nguvu zikaonekana kumwishia, akazama mara ya kwanza na kuibuka juu
akijaribu kupunga mikono hewani kuona kama angepata msaada wowote lakini haikuwa hivyo, akazama mara ya pili na kuibuka huku akimeza maji mengi
akaanza kukata tamaa ya kuiona dunia akiwa hai.
Ni wimbi hilo ndilo lililotingisha mtumbwi wa Oleg Malenko na kumfanya kuamini kwamba sasa kifo chake kilikuwa kimekaribia kwa kuliwa na samaki
mkubwa, kichwani mwake hakuelewa kabisa kwamba alikuwa ni mtu aliyekuwa akitapatapa baharini ili kujiokoa.
“Hapana nitahakikisha najiokoa, sipo tayari kuliwa na samaki hapa baharini,” alisema akiweka vizuri mtumbwi wake lakini ghafla alipotupa macho yake vizuri
eneo hilo huku mapigo yake ya moyo yakimwenda mbio, alishuhudia mikono ya mtu ikichomoza kutoka ndani ya maji.
“Mh! Mbona naona mikono?” alijiuliza akimulika eneo hilo kwa taa yake ndogo aliyokuwa akiitumia katika shughuli zake za uvuvi. Macho yake hayakukosea ni
kweli alikuwa ni mtu ambaye hakuelewa alikuwa mzima au mfu, kwa macho alionekana tayari alishakufa.
“Inawezekana amekufa lakini nitajuaje? Ni lazima nimguse kwa kasia ili nione pengine anaweza kuwa amezimia tu,” aliwaza.
Ghafla akiwa katika mawazo hayo alishuhudia mtu huyo akizama na kuibuka juu akitapatapa kama mtu aliyekuwa akikata roho kisha kutulia kimya, mwili wake
ukaelea juu ya maji. Haraka bila kuchelewa, Oleg, kwa kutumia kasia alilokuwa nalo mkononi mwake, akalikamata vyema na kusogea karibu kabisa na mwili wa
mtu huyo ambaye kwa kumwangalia mara moja alionekana kuwa amekufa.
Akiwa na hofu, akamgusa mtu huyo kwa kutumia kasia.
“Uko hai kweli wewe? Masikini wamekuua?” alijiuliza Oleg kwa Kirusi akizidi kumgeuza mtu huyo ambaye bado alionekana kutulia.
***
“Tafadhali mume wangu naomba urudi nyumbani njoo tuzungumze,” alisema Lina huku akilia.
“Je, umekubaliana na mimi?” aliuliza Phillip.
Kwa muda alikaa kimya akijaribu kutafakari ni jibu gani angempa mume wake ili akubali na kurejea nyumbani, hakuwa na jinsi alimhitaji mno, huyo ndiye
alikuwa mwanaume wa maisha yake hakika alimpenda Phillip kwa dhati.
“Ni…ko…taya…ri,” alitamka Lina huku akilia.
Akiwa hapo ghafla akasikia simu upande wa pili ikikatwa bila kupewa jibu lolote.
“Amekata simu?” alijiuliza huku akijifuta machozi.
Ulikuwa ni mtihani mgumu kweli kwa Lina lakini alitakiwa kuufanya na kufaulu kama tu alimhitaji Phillip maishani mwake, huku akilia akarejea moja kwa
moja na kuketi kwenye kiti, tayari ilishatimu saa kumi na mbili za jioni na mawazo yake yote yakiwa kwa Phillip ambaye mpaka wakati huo hakuelewa kama
angerejea nyumbani au la kwani hakuwa ametoa jibu lolote.
“Piii! Piii! Piii!” ilikuwa ni honi nje ya lango la nyumba yao.
“Naomba Mungu awe yeye, niongee naye na kumbembeleza ili anielewe mimi siko tayari kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa yetu,” alijisemea Lina.
Mawazo yake hayakukosea ni kweli alikuwa ni Phillip, Lina akanyanyuka kitini na kuusogelea mlango kisha kuufungua akimkaribisha ndani.
“Karibu mume wangu.”
“Mwaa!” lilikuwa ni busu lililotua moja kwa moja usoni mwa Lina kutoka kwa Phillip. Akiwa haamini alichokishuhudia kwa macho yake machozi ya uchungu
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
yakamtoka Lina.
“Tafadhali usilie mke wangu yote haya yanatokea kwa sababu moja tu, mtoto!”
“Phillip, maisha bila mtoto hayaendi?”
“Yatakwenda lakini mtoto ni lazima Lina, sikia nimekuja kwa suala moja tu,” alisema Phillip safari hii akionekana mpole.
“Ndiyo.”
“Lina ninakupa mwezi mmoja tu nipate matokeo ya mjadala wetu vinginevyo utanikosa kabisa katika maisha yako,” alisema Phillip akionyesha umakini wa hali
ya juu.
“Phillip hapana, bado nakupenda, nakuhitaji mume wangu.”
“Basi kama hivyo ndivyo fanya ninachotaka.”
“Nitafanya unachokitaka mume wangu lakini na nani?”
“Hilo suala nakuachia wewe mimi nimetoa ruhusa fanya unachoweza Lina wewe ni mwanamke tumia akili zako.”
“Mh!” Lina aliguna tayari Phillip alishanyanyuka kwenye kiti na kumwacha hapo peke yake akatembea kuuelekea mlango wa chumba chao, akaufungua na
kuingia ndani. Lina akamwaga machozi, ni kweli alikuwa amefanikiwa kumrejesha Phillip nyumbani lakini hakuwa tayari kukabiliana na mtihani uliokuwa
mbele yake kwani alishatumia akili zake zote kumshawishi kuondokana na mawazo hayo lakini ilionekana kushindikana, haja ya Phillip ilikuwa ni mtoto basi.
***
“Nitamuokoa hata kama atakuwa amekufa nitamzika kwa heshima zote, hastahili kuachwa kama mzoga!” alisema Oleg.
Moyo wake uliingia huruma na aliumia zaidi alipomwangalia mtu huyo akielea majini mwili wake ukiwa mtupu bila nguo.
“Ni kwa nini watu wanafanya ukatili wa aina hii? Alikosa nini huyu mpaka kustahili adhabu hii? Mungu nisaidie!” alisema mfululizo, muda wote huo akiendelea
kumtingisha mtu huyo kwa kutumia kasia.
Dakika tano nzima aliendelea kumtingisha bila mtu huyo kujigeuza wala kujitingisha hapo ndipo akaamini kwamba tayari alishakufa hivyo kufikia uamuzi wa
kumtoa ndani ya maji ili ampeleke ufukweni na huko angetafuta sehemu na kumzika kwa heshima zote.
Huku akitetemeka na jasho jingi kumtoka, Oleg Malenko alijitahidi kwa nguvu zake zote kumtoa mtu huyo ndani ya maji na kumpandisha juu ya mtumbwi wake
tayari kwa kurejea nchi kavu. Aliamini akifika huko ndiyo angefahamu ukweli wote kama alikuwa hai au amekufa.
“Kama atakuwa amekufa basi itakuwa ni bahati mbaya, nitamzika,” aliwaza huku akimgusa mtu huyo shingoni mwake. Baada tu ya kumpandisha ndani ya
mtumbwi, bila kuchelewa akaugeuza haraka na kuanza kupiga kasia kurejea nchi kavu. Haikumchukua muda, akawa tayari amewasili ufukweni, akaegesha vizuri
mtumbwi wake na kushuka, mikononi mwake akiwa amembeba mtu huyo.
Alipohakikisha kwamba tayari ameshayaacha maji kwa umbali mrefu, kwa haraka alimshusha chini na kumlaza, akainama na kuanza kusikiliza mapigo ya moyo.
Kwa takribani dakika tatu nzima alikuwa akisikiliza lakini hakusikia kitu, kichwani mwake akaamini kabisa kwamba mtu huyo hakuwa hai.
“Nitachimba shimo pale haraka haraka na kumfukia hapo,” aliongea kwa kunong’ona. Akaangaza macho yake huku na kule kuangalia kama kulikuwa na mtu
yeyote eneo lile lakini hakufanikiwa kuona kitu.
“Huu ndiyo muda, nikichelewa tu watu wakaniona watajua mimi ndiye nimemuua kumbe nasaidia tu,” akiwa katika mawazo hayo ghafla alisikia mtu akikohoa
mfululizo.
“Khoo!Khoo!Khoooo!” Oleg Malenko alishtuka na kugeuka kuangalia, lakini hakuona mtu, alipogeuka tena upande mwingine sauti ya kikohozi ikasikika, safari
hii kwa nguvu.
Haraka akatupa macho yake kumwangalia mwanaume aliyekuwa amelala chini, huyo ndiye aliyekuwa akikohoa mfululizo. Bila kuchelewa akasogea karibu ili
asikie vizuri, hakukosea alikuwa ni yeye.
“Mh! Amekohoa? Hajafa huyu, ngoja nimpe huduma ya kwanza niangalie itakuwajea,” alisema huku akimgeuza mtu huyo na kumlaza kifudifudi. Akapiga
magoti juu ya mgongo wake na kumkandamiza ili kumsaidia kutoa maji yaliyokuwa tumboni mwake.
Hakukosea, alichokuwa akikifanya kilikuwa ni sawa kabisa. Kwa takribani dakika tatu nzima aliendelea kumkandamiza mgongoni, maji mengi yakawa
yanamtoka hadi alipohakikisha maji aliyoyameza mtu huyo yamekwisha. Akamgeuza na kumlaza kiubavu huku akijaribu kuongea naye.
“Wewe ni nani? Umetoka wapi? Imekuwaje ukawa hapa?” aliuliza mfululizo lakini hakupata jibu kutoka kwa mtu huyo ambaye alilala kimya ardhini
akitetemeka.
“Tafadhali niambie nini kimekupata?” aliendelea kuuliza huku akimchunguza vyema mtu huyo.
“Di…t…ro…” aliongea kwa shida lakini kabla hajamaliza sentensi yake, Oleg Malenko akashuhudia mtu huyo akirusha mikono na miguu kisha kutulia kimya.
“Mh! Hizi damu zinatoka wapi?” alijiuliza huku akimfunua upande huo. Macho yake yakakutana na jeraha kubwa.
“Hili ni jeraha la risasi ambalo limesababisha kuvuja kwa damu nyingi kiasi hiki, lazima nifanye kitu kuokoa maisha ya mtu huyu,” alisema huku akijaribu
kumnyanyua sehemu aliyokuwa amelala.
Wazo pekee likamjia kichwani mwake kwamba ni lazima mtu huyo apate matibabu haraka hospitalini lakini hakujua atampeleka hospitali gani.
Hiyo ilikuwa ni kwa sababu ya machafuko makubwa yaliyoikumba nchi ya Urusi. Aliendelea kujiuliza ni hospitali gani angempeleka mtu huyo na kupokelewa
bila maelezo ya kutosha! Akahisi hiyo ingekuwa hatari nyingine kwake. Alihisi anaweza kuingia kwenye kesi ambayo asingeweza kujinasua kama mtu huyo
angekuwa amekufa.
“Hapana, sitampeleka hospitali. Nitampeleka nyumbani kwangu, naamini hajafa. Huko nitampa matibabu mpaka apone kabisa, hapo atakuwa tayari kunieleza
ukweli wa nini kilichompata,” alisema Oleg Malenko. Tayari mapambazuko yalishaanza kuchomoza.
***
Mapenzi yote yaliyokuwa katikati yao yalionekana kupotea, furaha ndani ya nyumba ikageuka na kuwa shubiri. Phillip akisisitiza jambo moja tu, mtoto! Kwa
muda wa wiki nzima, Lina aliendelea kumbembeleza na kumsihi Phillip aachane na jambo lililokuwepo kichwani mwake na badala yake wale na kufurahia
maisha.
“Lina, hakika hujaweza kunishauri juu ya hili. Fanya ninachotaka halafu tutaelewana,” alisema Phillip huku akigeuka upande mwingine wa kitanda, akavuta
shuka na kujifunika gubigubi. Hata Lina alipojaribu kumuita, bado hakujibu wala kugeuka. Kwa mara nyingine tena moyo wa Lina ukauma kupita kawaida,
akanyanyuka kitandani, akafungua mlango wa chumba na kutoka nje huku akilia.
Wakati akitembea kuelekea sebuleni ghafla wazo likamjia kichwani mwake. Akalikumbuka jina Daniel, kijana mtanashati kweli kweli ambaye kwa muda mrefu
alikuwa akimfuatilia Lina akimtaka kimapenzi. Mara zote aliambulia majibu ya karaha na pengine yaliyouchoma moyo wake kama mkuki wa moto.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Daniel! Sijui atakuwa wapi kwa sasa? Na sijui kama bado atakuwa hajaoa! Je, nitaanzia wapi kumweleza kwamba nampenda ilhali nilishamuumiza moyo?
Lakini nitajaribu, sipendi kumpoteza Phillip. Naamini huyu ndiye mwanaume wa maisha yangu yote,” alisema Lina, akakisogelea kiti na kuketi juu yake kwa
muda. Aliendelea kutafakari juu ya tatizo lililokuwa ndani ya nyumba yake, alitakiwa afanye kitu fulani ili kuinusuru ndoa yake. Tayari mashavu yake
yalishalowa kwa machozi.
“Kesho asubuhi nitamtafuta Daniel, najua atashangaa lakini sina jinsi, huyu pekee ndiye atakayewe…” alisema lakini kabla hajamaliza sentensi yake, kwikwi ya
kulia ikamkaba tena.
“Daniel! Sijui atakuwa wapi kwa sasa? Na sijui kama bado atakuwa hajaoa? Je, nitaanzia wapi kumweleza kwamba nampenda ili hali nilishamuumiza moyo?
Lakini nitajaribu, sipendi kumpoteza Phillip, naamini huyu ndiye mwanaume wa maisha yangu yote,” alisema Lina akakisogelea kiti na kuketi juu yake, kwa
muda aliendelea kutafakari juu ya tatizo lililokuwa ndani ya nyumba yake, alitakiwa afanye kitu fulani ili kuinusuru ndoa yake. Tayari mashavu yake yalishalowa
kwa machozi.
“Kesho asubuhi nitamtafuta Daniel najua atashangaa lakini sina jinsi, huyu pekee ndiye atawe…” aliwaza lakini kabla hajamaliza sentensi yake kwikwi ya kulia
ikamkaba tena.
Hakika hakuelewa maisha yake yangekuwa vipi kama tu asingeweza kukubaliana na Phillip, mumewe, ambaye mpaka wakati huo hawakuwa na maelewano
mazuri ndani ya nyumba. Aliendelea kubaki eneo hilo bila kurejea chumbani hapo, kazi ikawa moja tu kulia mpaka usingizi ulipomchukua ambapo alizinduliwa
na sauti ya mlango ukifunguliwa na aliponyanyua uso kuangalia alimwona Phillip akitembea kumsogelea.
Bila kusema kitu alimshuhudia akimwinamia na kumbusu kisha kumpigapiga mgongoni.
“Lina!”
“Yes darling!” alijibu huku machozi yakimbubujika, akili yake ikarejea kwenye mazungumzo yote yaliyofanyika jana yake.
“Naamini umeshapata jibu la tatizo linalotusumbua.”
Bila kujibu chochote akiwa hapo akanyanyua uso wake na kumwangalia Phillip machoni.
“Unalia nini?” lilikuwa ni swali kutoka kwa Phillip baada ya kumwangalia vyema Lina usoni aligundua macho yake yalikuwa yamevimba kupita kawaida.
“Hakika huo ndio msimamo wangu mke wangu, ni kweli inauma lakini sina jinsi.”
“Yupo mtu ambaye nimemfikiria jana usiku, huyu nadhani anaweza kunisaidia.”
“Ni vyema ukafanya hivyo mara moja lakini tu awe ni mtu unayemwamini sana na nisingependa afahamu siri iliyoko kati yetu, cha muhimu ni wewe kujiweka
sawa ili kupata ujauzito basi mambo mengine tutajua mbele ya safari. Sawa mke wangu?”
“Sa…wa,” alijibu lina huku akilia.
Bila kusema kitu Phillip akanyanyuka kitini kisha kumnyanyua Lina wote wawili wakaingia chumbani ili kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini, lakini mambo
hayakuwa hivyo.
Baada tu ya kuingia ndani huku wote wawili wakiwa kimya Phillip alimnyanyua Lina na kumrushia kitandani naye akifuata kwa nyuma bila kuchelewa, akaanza
kumvua nguo moja baada ya nyingine kisha akabaki mtupu kama alivyozaliwa.
“Lina nakupenda,” ilikuwa ni sauti ya Phillip ikipita masikioni mwa Lina.
“Una..se…ma..kwe..li?” aliuliza lina kwa sauti ya kutetemeka.
“Asilimia mia moja mke wangu mambo yote haya yanatokea si kwa sababu mimi nakuchukia hapana…” alisema Phillip akilivuta shuka na wote wawili
wakajifunika gubigubi.
Kilichofuata baada ya hapo hakiandikiki kwani ilikuwa ni kama vile watu wakiimba mapambio na wengine kuitikia, mara chache sana sauti ya Lina ilisikika
lakini ilimezwa na mabusu mfululizo yaliyotoka kinywani mwa Phillip. Saa mbili baadaye wote wawili walikuwa hoi bin taaban jasho jingi likiwatiririka.
“Nimeamua kufanya hivi kwa sababu nataka uamini kwamba ninakupenda kwa dhati na si kitu kingine, sawa?” Phillip alisema.
“Ahsante!” alijibu Lina akimwangalia Phillip kwa jicho la huruma.
“Hebu nieleze ni nani huyo unayemfikiria?” Phillip aliuliza kwa upole.
“Yupo kijana mmoja anaitwa Daniel huyu tulisoma naye huko nyuma na alinipenda sana.”
“Je, unamwamini?”
“Asilimia zote labda itokee tu kwamba ameoa kwa sasa?”
“Hata kama ameoa tunachohitaji sisi ni yeye kukupa mamba, basi, mambo mengine yote atuachie sisi wenyewe.”
“Nipe muda nimtafute kisha nitakujulisha.”
“Ahsante mke wangu sasa naamini kweli unanipenda.”
“Nakupenda pia Phillip, yote haya nafanya ili kulinda penzi letu, sipendi kukupoteza, wewe ni wangu mpaka mwisho.”
“Najua jambo hilo ila kitu kimoja tu nikuombe.”
“Ni nini hicho?”
“Nihakikishie kwamba baada tu ya kufahamu kwamba umepata mimba hutarejea tena kwa Daniel.”
“Siwezi kufanya hivyo Phillip unanifahamu vyema, jambo hili linatokea kwa sababu wewe ndiye umetaka.”
“Basi nakuamini fanya kila unachoweza umpate kisha utanijulisha kila hatua, sawa?”
“Nitafanya hivyo,” alisema Lina na wote wawili wakanyanyuka na kuingia bafuni kuoga ili wajiandae tayari kuelekea kazini.
Dakika tano baadaye tayari wote wawili walishakuwa tayari wakatoka mpaka nje ambako walisalimiana na mlinzi kisha wakaingia ndani ya gari, Phillip akiketi
kwenye usukani, safari kuelekea ofisini ikaanza, njiani wakiongea mambo mengi kuhusu maisha na mapenzi yao na furaha ilionekana kurejea tena katika
mapenzi yao.
Kutokana na msongamano wa magari siku hiyo walilazimika kutumia saa moja mpaka kufika ofisini kwao, wakafika na kuegesha gari lao kisha kushuka. Phillip
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akazunguka mpaka sehemu alipokuwa amesimama Lina na kumshika mkono, kwa pamoja wakatembea kuingia ndani ya ofisi. Yalikuwa ni mazoea ya Phillip
kumsindikiza Lina mpaka anahakikisha ameingia ndani ya ofisi yake ndipo yeye atoke na kuelekea ofisini kwake.
Taratibu huku wakionyesha nyuso za tabasamu walitembea mpaka kuufikia mlango wa ofisi ya Lina, akafungua ili aingie ndani lakini kabla hajafanya hivyo
akavutwa kwa nyuma.
“Darling!” ilikuwa ni sauti ya Phillip.
“Yes.” (Ndiyo.)
“Nimesahau kitu.”
“Kitu gani?”
Bila kusema kitu chochote akamsogelea Lina na kuanza kumbusu mfululizo bila kujali watu waliokuwa wakipita eneo hilo.
“Ahsante…” alisema Lina akitabasamu.
“Tafadhali kumbuka kumtafuta Daniel” alisema Phillip kwa sauti ya kunong’ona.
***
“Vrooom!Vrooom!” ilikuwa ni sauti ya kitu kikiburuzwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kwa sababu hakutaka jambo hilo ligundulike na mtu mwingine, aliamua kuuficha ukweli huo kwa kumburuza mtu huyo na kwenda kumweka pembezoni mwa
mitumbwi mibovu amwache hapo na yeye atembee kurejea mpaka sehemu ambako aliamini angepata usafiri na amchukue tayari kwa kumpelekea nyumbani
kwake ambako angefanya kila kilichowezekana kuokoa uhai wa mtu huyo.
“Nikipata tu usafiri na kuongea na dereva anisaidie kumfikisha mtu huyu nyumbani itakuwa safi, nitamlipa kiasi atakachotaka lakini afiche siri hii,” aliwaza Oleg
Malenko.
Haraka bila kupoteza muda alipohakikisha kwamba amemweka mtu huyo sehemu salama, alitoka haraka na kuangaza macho yake huku na kule na alipohakikisha
kwamba hapakuwa na mtu, akaanza kutembea kuondoka eneo hilo.
“Nitamsaidia mpaka mwisho bila kuchoka kwa kumwangalia, anaonekana ni mtu mwema, naomba Mungu asije kuwa mtu mbaya,” alijisemea akizidi kusonga
mbele.
Dakika tano tu tayari alishatokeza barabarani, akaongoza moja kwa moja mpaka mahali ambako teksi zilisimama hapo kungoja wateja, akaisogelea moja na
kuanza kuongea na dereva, kwa dakika tatu nzima walifanya mazungumzo na kuonekana kukubaliana, haraka akazunguka upande wa pili na kupanda kisha gari
hilo kuondoka eneo hilo.
“Nitakuonyesha sehemu ya kusimama kisha kuomba msaada wako ili tumchukue haraka kumpandisha ndani ya gari.”
“Hakuna shida,” alijibu dereva huyo kwa lugha ya Kirusi.
Haikuchukua muda tayari wakawasili eneo la tukio, Oleg Malenko akawa mtu wa kwanza kushuka ndani ya gari na kuanza kumwongoza mwenzake lakini kabla
hawajamfikia, macho yake yalishuhudia jambo ambalo halikuwa la kawaida.
“Mh!” aliguna.
HARAKA bila kupoteza muda anaangalia huku na kule na kuhakikisha kwamba alimweka mtu huyo sehemu salama. Oleg Malenko anatoka mbio eneo hilo
kuelekea barabarani kichwani mwake akiwa na wazo moja tu, kutafuta gari ambalo lingemsaidia kumfikisha mtu huyo nyumbani kwake na huko angepata
matibabu na kupona.
“Nitamsaidia mpaka mwisho bila kuchoka, kwa kumwangalia anaonekana ni mtu mwema naomba Mungu asije kuwa mtu mbaya.” Aliongea akizidi kusonga
mbele.
Dakika tano tu tayari alishatokeza barabarani, akaongoza moja kwa moja mpaka mahali ambako teksi zilisimama kwa ajili ya kungoja wateja, akaisogelea moja
na kuanza kuongea na dereva, kwa dakika tatu nzima walifanya mazungumzo na kuonekana kukubaliana, haraka akazunguka upande wa pili na kupanda kisha
gari kuondoka eneo hilo.
Haikuchukua muda wakawasili eneo la tukio, Oleg Malenko akawa mtu wa kwanza kushuka ndani ya gari na kuanza kumwongoza mwenzake lakini kabla
hawajamfikia macho yake yalishuhudia jambo ambalo halikuwa la kawaida.Je, nini kinaendelea?
Upande wa pili wa hadithi hii tunamwona Lina akifikiria jinsi ya kumpata kijana Daniel ambaye angeongea naye na kumshawishi wafanye tendo la ndoa na
kupata ujauzito, ni mtihani mgumu lakini alitakiwa kuufanya ili kumlinda mwanaume aliyempenda kwa dhati.
“Tafadhali kumbuka kumtafuta Daniel,” aliongea Phillip kwa sauti ya kunong’ona.
Ni maneno hayo yaliyofanya kumbukumbu za Lina kurejea upya kichwani mwake, moyo wake ukaenda mapigo ya haraka haraka kama vile mtu aliyekuwa
akikimbia mbio ndefu.
“Mungu nisaidie kufanya jambo hili.” Alinong’ona akizama ndani ya ofisi yake. Taratibu akakisogelea kiti kikubwa kilichokuwa nyuma ya meza kubwa na kuketi
huku jasho likimtiririka.
“Sina namna ni lazima nimtafute Daniel tu ili kulinda penzi langu kwa Phillip.” Aliwaza.
Kwa muda wa dakika tano nzima alikaa kimya akijaribu kutafakari nini cha kufanya lakini bado hakupata jibu na upande mmoja wa akili yake ulimwambia
kwamba kama asingethubutu kufanya jambo hilo hakika angemkosa Phillip maisha yake yote.
Akiwa hapo huku machozi yakimbubujika, Lina akavuta moja ya droo iliyokuwa karibu na meza aliyoketi, akaanza kuchambua karatasi moja baada ya nyingine
akitafuta mahali ambako aliamini angeweza kupata maelezo ya namna ya kumpata Daniel.
Alipitia karatasi moja baada ya nyingine na kwa bahati nzuri akafanikiwa kupata moja ya barua ambazo Daniel aliwahi kumwandikia miaka mingi.
“Nimeipata.” Aliongea akiichomoa karatasi hiyo na kuishika vyema mikononi mwake ili asome.
Taswira ya Daniel ikamjia kichwani mwake, akamwona jinsi alivyokuwa ni kweli alistahili kuitwa mwanaume wa shoka kwani alikuwa na kila sababu ya
kupewa tunu hiyo, alikuwa ni kijana mrefu, rangi yake ya ngozi pia ilivutia na midomo yake ilikuwa minene na zaidi ya yote, Daniel alikuwa na kifua kipana
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kilichofanya kila mwanamke aliyemwona amtamani kimapenzi. Hakika alisisimua.
“Anazo sifa zote lakini mimi …” Lina aliongea, hata kabla hajamalizia sentensi yake mlango wa ofisi yake ukagongwa.
***
“Mh!” Oleg Malengo aliguna akijaribu kuangaza macho yake huku na kule kama vile alikuwa akiangalia kitu fulani.
“Kuna nini?” Dereva wa teksi naye akauliza akionesha wasiwasi mwingi.
Bila kujibu swali alilokuwa ameulizwa alitembea haraka kusonga mbele hakika alionekana kama mtu aliyekuwa akisaka kitu ambacho hakikuonekana.
“Kimetokea nini? Mbona alikuwa hapa?” Alijiuliza.
Kwa ujasiri mkubwa akasogea mpaka mahali alipokuwa amemwacha mwanaume aliyemwokoa ndani ya maji lakini hakumwona, alichokuwa amekishuhudia
kwa macho yake yote mawili ni alama za mburuzo ulioonekana ardhini.
“Ameondoka.” Aliongea.
“Nani?”
“Yule niliyekueleza kwamba nahitaji unisaidie?”
“Lakini si ulisema ana hali mbaya?”
“Ni kweli nashangaa pengine amepata nguvu.”
“Sidhani hebu kumbuka vizuri ni hapa kweli ulipomwacha?”
“Hakika ni hapa alama zake zi hizi hapa.”
“Mh.” Dereva teksi naye akaguna hakuelewa ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea.
Kabla ya Oleg Malenko kwenda kutafuta usafiri alipokuwa akimweka mwanaume huyo vyema eneo aliloamini kuwa ni salama na kuondoka kuelekea barabarani
kwa ajili ya kutafuta usafiri jambo la ajabu lilitokea, upepo mkali ukiambatana na ubaridi mkali ulipiga eneo la ufukweni na upepo huo ndiyo uliosababisha
mwanaume aliyekuwa katika hali ya kutojitambua aanze kutapatapa kutafuta msaada, hatimaye kujikuta amejiburuza na kuelekea nyuma ya mitubwi mibovu
iliyokuwa karibu yake.
“Kama kweli una uhakika basi atakuwepo hapa hapa hebu tufuatilie alama za miburuzo kuangalia ilipoishia.” Aliongea dereva teksi huyo na moja kwa moja
wakaanza kuufuatilia miburuzo hiyo.
“Umepita hapa.” Aliongea Oleg Malenko.
Akili ya dereva teksi ilikuwa imefanya kazi sawasawa, ni kweli kabisa alikuwa hawajakosea wazo lake la kufuata miburuzo iliyokuwa ikionekana ardhini
lilisaidia na hatua chache tu kutoka mahali waliposimama waliona miguu ya mtu.
“Hii ni miguu ya mtu.”
“Ni kweli, hebu tuone,” Oleg Malenko aliongea.
Haraka haraka bila kuchelewa wakazunguka na kuanza kumwangalia mtu huyo usoni, alikuwa ni yule yule aliyekuwa amemwacha muda mfupi uliopita,
akamgeuza na kumlaza chali mdomoni alionekana kutokwa na mapovu mengi.
“Mh! Yuko hai kweli huyo?” Dereva teksi aliuliza.
“Sijui hata mimi nashangaa, nilipomwacha muda mfupi hakuwa hivi alikuwa amepoteza tu fahamu.”
“Sasa amefikaje hapa na ni kitu gani kimempata mpaka kufikia hatua hii?”
“Sina jibu ila nisaidie tu tumwondoe hapa.”
“Kwenda wapi, anaonekana tayari ameshakufa huyu.”
Oleg Malenko akainamna na kumshika mwanaume huyo sehemu ya shingo yake kuangalia kama moyo yake yalikuwa yakipiga au la!
“Bado hajafa nasikia mapigo yake yakipiga lakini kwa mbali.”
“Ushauri wangu ni bora umwache afe tu hapa kwani hakuna mtu atakayegundua.”
“Tafadhali nisaidie hata kama atakufa, basi afie ndani ya nyumba yangu wakati nikijaribu kumsaidia.” Aliongea Oleg Malenko kwa sauti ya upole.
“Sawa nitakusaidia wewe tenga tu fedha yangu.” Aliongea dereva huyo kwa lugha ya Kirusi.
Wote kwa pamoja wakainamna na kumnyanyua mwanaume aliyekuwa amelala chini na kuanza kutembea kuelekea sehemu walipokuwa wameegesha gari hapo
wakamlaza tena chini na dereva kufungua mlango kisha wakamwinua na kumweka kwenye kiti cha nyuma, wote wakaingia ndani ya gari na safari kuelekea
nyumbani kwa Oleg Malenko ikaanza, njia nzima alikuwa akimfikiria mgonjwa aliyekuwa naye, alitaka apone ili amsimulie ni kitu gani kilichompata.
“Naomba Mungu amsaidie asife, apone.” Aliwaza kichwani mwake gari likizidi kuchanja mbuga.
Baada ya mwendo wa nusu saa walishawasili nyumbani kwa Oleg Malenko, yeye akawa mtu wa kwanza kufungua mlango na kushuka bila kusema kitu
akamwomba tena dereva wa gari aliyekuja naye amsaidie kumshusha mgonjwa, haraka wakafanya hivyo na kumwingiza mgonjwa ndani ya nyumba.
“Ahsante sana rafiki.” Aliongea Oleg Malenko akimkabidhi dereva huyo kiasi cha fedha kama malipo yake na kumshukuru.
***
“Ngo!Ngo!Ngo!” Sauti ya mlango ikasikika na kumshtua Lina kutoka katika mawazo aliyokuwa nayo. Haraka bila kuchelewa hata kabla hajaitika akaifungua
droo na kuitumbukiza barua hiyo haraka alipohakikisha kwamba alikuwa sawa akamkaribisha mtu aliyekuwa mlangoni.
“Ndiyo karibu.” Aliongea kwa sauti ya upole.
Mlango ukafunguliwa na mwanaume mmoja akaonekana akiingia.
“Oh! Karibu sana bosi.” Aliongea Lina akionyesha tabasamu usoni mwake.
“Natumaini hujambo, nimekuja kwa jambo moja tu hapa.”
“Ndiyo bosi.”
“Ah! Mwezi ujao kutakuwa na safari ya kwenda Ujerumani na itatuhusisha mimi na wewe ni vyema ukawa na ufahamu na jambo hilo.”
Badala ya kujibu Lina akainamisha kichwa chake chini, si kwamba hakuifurahia safari hiyo, la hasha! Kichwa chake kilijaa mawazo mengi juu ya ndoa yake na
kitu pekee alichokuwa akikihitaji ni kulinda penzi lake kwa Phillip basi.
“Lina!” Sauti ikasikika.
“Bee”
“Kuna nini kinaendelea kichwani mwako? Hauko sawa kabisa.”
“Hapana bosi niko sawa niko tayari kwa safari hakuna shida.” Alijibu Lina kwa sauti ya chini.
Wakaagana, kisha bosi akafungua mlango na kutoka nje akimwacha Lina ndani ya ofisi peke yake.
Huku akitetemeka taratibu akanyoosha tena mkono wake na kufungua droo ambayo ndani yake ilikuwepo barua iliyokuwa na maelezo yote jinsi ya kumpata
Danniel akaichukua na kuanza kubonyeza.
“Ngrii! Ngrii! Ngriii,”Simu ilikuwa ikiita upande wa pili.
KWA moyo mmoja Oleg Malenko ameamua kumsaidia mtu huyo mpaka mwisho, moyoni mwake akiamini kwamba hakuwa na hatia na alikuwa ametendewa
ubaya na mtu fulani. Hakufahamu upande wa pili wa mtu huyo kwamba alikuwa katili kupindukia. Anaamini akipona atamweleza ukweli wa nini kilichompata
mpaka kufikia hapo?
Baada ya kumuuguza kwa wiki nzima huku kukiwa hakuna matumaini yoyote ya mwanaume huyo kunyanyuka kitandani, hatimaye uamuzi pekee anaoufikia ni
kutoka na kwenda kumtafuta daktari ambaye angemtibu mgonjwa huyo akiwa hapo hapo nyumbani na kumlipa kiasi chochote cha fedha atakachohitaji. Akiwa na
wazo hilo, asubuhi moja mwanaume huyo anaonekana kurejewa na fahamu zake, jambo linaloleta furaha kubwa moyoni mwake.
Upande wa pili wa hadithi hii tunamwona Lina akiwa na mawazo mengi juu ya mgogoro mkubwa ulioingia katika penzi lake. Mwanamke huyu anadhamiria
kuhakikisha analilinda penzi lake japo moyoni anayo maumivu na sasa yuko ndani ya ofisi yake. Wazo pekee linalozunguka kichwani mwake ni kumtafuta kijana
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Daniel ambaye huko nyuma aliwahi kumpenda kimapenzi lakini akamkataa. Anaamini kwa asilimia mia moja kwamba huyo pekee ndiye anayeweza kukidhi
shida aliyonayo.
Mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio mithili ya mtu aliyekuwa amekimbia umbali mrefu, jasho jingi pia lilikuwa likitiririka mwilini mwake, hofu
nyingi ikaugubika mtima wake. Lina hakuwa na uhakika kama kweli angempata Daniel na kukubaliana na mazungumzo aliyotaka kumweleza.
Kwa sekunde tano nzima mkono wa simu uliendelea kubaki sikioni mwake akisikiliza simu hiyo.
“Mh! Imeita kwa muda mrefu inaonekana hakuna majibu, au pengine nimekosea namba?” alijiuliza akisogeza karibu kipande cha barua ambacho ndicho haswa
kilikuwa na maelezo yote ya kumpata Daniel. Hakukosea namba aliyokuwa amebonyeza muda mfupi kabla, ndizo hizohizo zilizokuwa kwenye barua hiyo.
“Ngoja nijaribu tena pengine yuko mbali na simu,” alisema Lina mkono wa simu ukiwa sikioni mwake.
Mara kadhaa alijaribu lakini bado hakupata majibu, akaanza kuingiwa na wasiwasi kwamba huenda Daniel alishabadilisha namba hiyo ya simu muda mrefu na
hakufahamu kama jambo hilo lingekuwa kweli angempata wapi mwanaume huyo.
“Nitajaribu tena baada ya nusu saa nione itakuwaje, ” alisema Lina akiweka mkono wa simu chini.
***
Baada tu ya dereva teksi kulipwa fedha zake na kuondoka eneo hilo Oleg Malenko bila kutoa utambulisho wowote kwa familia yake alimwita mke wake na
kumwomba wasaidiane kumwingiza mwanaume huyo ndani kisha mambo mengine yangefuata baadaye.
“Ni nani huyu?” aliuliza mke wake baada ya kumwingiza mwanaume huyo ndani ya nyumba.
“Nitakueleza kila kitu baadaye, kitu pekee ninachohitaji hapa ni kujaribu kuokoa maisha ya mwanaume huyu.”
“Amepatwa na kitu gani?”
“Hata mimi mwenyewe sifahamu nimemkuta akiwa katika hali hii ya kuzimia ndani ya bahari wakati nikifanya kazi yangu ya uvuvi.”
“Mh! Ni mzima kweli huyu?”
“Ni mzima.”
“Mbona haonyeshi kupumua?”
“Hebu,” alisema Oleg Malenko akiweka mkono wake juu ya kifua cha mwanaume huyo.
Kwa muda wa sekunde tatu nzima aliweka mkono wake na kwa mbali alisikia mapigo ya moyo ya mtu huyo.
“Anapumua lakini kwa mbali.”
“Mume wangu ni vyema tukampeleka hospitali hapa hatutaweza kumsaidia.”
“Hapana hili litakuwa ni suala jingine binafsi sipo tayari kumpeleka huko nitamsaidia tu hapahapa.”
“Una uhakika?”
“Asilimia mia moja.”
Baada ya mabishano ya muda mrefu hatimaye Oleg Malenko akaomba apewe nafasi ya kubaki ndani ya chumba na mgojwa tu, alihitaji kumchunguza vyema.
Haraka akamgeuza mtu huyo na kumvua shati alilokuwa amelivaa akashuhudia jeraha kubwa begani kwake, kwa kuliangalia tu aligundua ilikuwa ni risasi
iliyopenya eneo hilo.
“Hii ni risasi ilipenya hapa, sijui ilitoka au ilibaki ndani?” alijiuliza akiangalia akigeuza upande wa pili wa bega ili kuangalia.
“Ah! Ilitoboa na kupenya moja kwa moja, nahisi kabisa jeraha hili ndilo limesababisha yeye kupoteza fahamu kwani inavyoonekana amemwagika damu nyingi
sana.”
Bila kusema kitu chochote akatoka ndani ya chumba na kuingia chumba kingine huko akatoka mkononi akiwa ameshikilia chupa ndogo pamoja na pamba na
kuzama tena chumbani.
“Nitamsaidia kama itashindikana basi nitatafuta daktari na kumlipa ili amsaidie,” aliwaza akiketi kitandani pembeni mwa mgonjwa.
Siku ya kwanza ikapita mtu huyo akiwa bado kitandani bila kujitambua, siku pili hatimaye wiki kukiwa hakuna matumaini yoyote ya yeye kurejewa na fahamu
zake .
“Mh! Kesho asubuhi nitadamka kwenda kuongea na daktari wangu nione atanisaidia vipi,” aliwaza Oleg Malenko akisogea karibu na kitanda.
“Mh! Mh! Taf…adha…li nio..koe,” sauti ndogo ilisikika ikitamka maneno hayo kwa taabu.
“Ameongea?” alisema Oleg Malenko akisogea karibu ili asikilize vyema.
“Tafa…dhali okoa mai…sha yangu si..taki kufa…” aliongea mwanaume huyo akijaribu kunyanyuka kitandani ili aketi.
“Mungu ni mkubwa!” aliongea Oleg akizidi kushangaa kwani kwa muda wa wiki nzima alishajaribu kufanya kilichowezekana akiwa ameiweka kazi yake ya
uvuvi pembeni ili kuokoa maisha ya mtu huyo lakini ilionekana kushindikana hivyo kwake kilichokuwa kikitokea asubuhi hiyo ulikuwa ni muujiza.
***
Nusu saa baadaye Lina alikuwa katika simu akibonyeza namba zilezile na kuweka mkono wa simu sikioni na kusikiliza, haikuchukua muda mrefu sana upande
wa pili simu ikapokelewa na sauti nzito.
“Yes, hallow!” iliita sauti hiyo na kupenya moja kwa moja sikioni mwa Lina.
“Ndiyo,” akajibu.
“Nikusaidie tafadhali.”
“Mh! Samahani.”
“Bila samahani dada endelea.”
“Naweza kuongea na Danny?”
Ukimya wa ajabu ukatokea kati yao.
“Hallow!” akaita huku akitetemeka.
“Unasema unataka kuongea na nani?”
“Danny,” alijibu Lina kwa kujiamini.
“Ndiye huyu anayeongea…sijui nani mwenzangu?” sauti hiyo iliuliza.
“Naitwa Lina…wewe kweli ni Danny?”
“Dada tafadhali acha utani, nenda moja kwa moja kwenye pointi sema unamhitaji nani,” aliongea mwanaume huyo safari hii kwa ukali.
“Naomba uniamini mimi naitwa Lina.”
“Lina?”
“Ndiyo, Danny tafadhali amini,” aliongea Lina safari hii kwikwi ya kulia ikionekana kumkaba.
“ Hebu nieleze kweli wewe ni Lina yuleyule ninayemfahamu!”
“Hakika mimi ndiye.”
“Mh!” Daniel aliguna hakuwa tayari kuamini alichokuwa amesikia upande wa pili wa simu alizidi kushangaa zaidi kwani ilishapita miaka mingi sana tangu awe
amemtoa Lina mawazoni mwake na kuamua kuendelea na mambo mengine maishani mwake hivyo kitendo cha kupokea simu asubuhi hiyo kilizidi
kumchanganya akili.
“Daniel! Daniel! Najua utakuwa umeshangaa sana kusikia jina langu lakini ukweli mimi ni Lina yule yule wa chuoni mwanamke uliyempenda kupindukia
tafadhali amini kwamba ndiye huyohuyo amekutafuta kwa njia ya simu…” aliongea Lina.
“Nini kimetokea Lina? Hivi sasa wewe ni mke wa mtu kama sijakosea, nilipata habari za wewe kuolewa kutoka kwa watu wanaokufahamu vyema tena nasikia
umeolewa na mtu maarufu sana hapa mjini…” aliongea Daniel.
“Hilo si muhimu kwako ninachohitaji kutoka kwako ni namna gani nitakupata nahitaji sana kuzungumza na wewe ni muhimu Daniel.”
“Leo inawezekana?”
“Itakuwa safi sana tafadhali naomba nikukute Lamada Hotel ukiweza chukua kabisa chumba nitakuja kurudisha fedha yako, sawa…” aliuliza Lina.
“Sa…wa,” sauti ya Daniel ilijibu ikitetemeka hata yeye mwenyewe hakuwa tayari kuamini kilichokuwa kikitokea kwa wakati huo iweje mwanamke
aliyemsumbua kwa miaka mingi akimtaka mapenzi na kumtolea nje leo hii ampigie simu akimsisitiza kuonana, kibaya zaidi hotelini tena ndani ya chumba
hakika hakuwa tayari kuamini aliiona hiyo kama ndoto ya alinacha.
Huku akiwa na huzuni kubwa moyoni mwake ananyanyua simu na kumpigia Daniel, anajaribu kumuingia na hatimaye anafanikiwa. Wanakubaliana kukutana
ndani ya Hoteli ya Lamada, tena ndani kabisa ya chumba. Ni habari za kushangaza kwa Daniel, haamini kinachotokea lakini hivyo ndivyo ilivyo.
Tafa…dhali okoa mai…sha yangu si..taki kufa…,” alisema mwanaume huyo akijaribu kunyanyuka kitandani ili aketi lakini zoezi hilo lilionekana kuwa gumu
kwake kutokana na jinsi hali yake ilivyokuwa.
Oleg Malenko, huku akitia huruma alimsogelea mwanaume huyo na kuanza kumsaidia ili anyanyuke na kuketi. Zoezi hilo lilipokamilika naye pia akaungana
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
naye kitandani lakini kabla hajaanza kusema kitu chochote, mwanaume huyo huku akitetemeka aliomba maji ya kunywa.
“Nisai…die ma…ji ya ku…nywa…,” alisema kwa tabu.
Haraka bila kuchelewa akanyanyuka na kuisogea meza ndogo iliyokuwepo ndani ya chumba kile, akachukua kikombe kikubwa kilichokuwa juu yake ambacho
ndani yake kulionekana kuwa na maji.
“Haya hapa.”
Huku akitetemeka mwanaume huyo akajitahidi kukipeleka kikombe hicho mdomoni na kuanza kunywa maji yaliyokuwemo ndani, haikuchukua hata sekunde
tatu, yakawa yamekwisha.
‘Inawezekana ana njaa huyu,’ aliwaza moyoni mwake huku akipokea kikombe na kukiweka mahali pake.
Bila kusema kitu chochote, Oleg Malenko akausogelea mlango na kufungua. Akachungulia na kuita jina la mkewe, bila kuchelewa mkewe alifika, ikasikika sauti
ya Oleg Malenko ikimwomba asaidie kupiga uji haraka kisha aulete chumbani mle kwa ajili ya mgonjwa.
“Kwani ameamka?”
“Ameamka lakini sijaweza kuongea naye, kwa anavyoonekana anahitaji kupata kitu kidogo cha kula.”
“Afadhali! Mungu ni mwema jamani, nilishakata tamaa.”
“Tafadhali nisaidie sasa hivi.”
“Sawa,” alisema mwanamke huyo na hatua za mtu aliyekuwa akitembea kuondoka eneo hilo zikasikika. Oleg Malenko akarejea ndani ya chumba na kufunga
mlango nyuma yake.
“Naweza kukuuliza maswali machache?” alisema huku akisogea karibu kabisa na kitanda alicholala mgonjwa.
Kwa ishara ya kichwa mwanaume huyo akaonesha kukubaliana na jambo alilolisikia kutoka kwa mwenyeji wake.
“Wewe ni nani vile?” aliuliza tena lengo likiwa ni kupata uhakika wa jina alilolisikia mwanzo.
“Ditrov!” alijibu kwa sauti ya kunong’ona.
”Ah! Kumbe ni sawa kabisa na jina ulilolitamka mwanzo kabla hujapoteza fahamu, pole.”
“Ahsante.”
“Nini kilitokea mpaka ukawa kwenye hali hii?”
Ditrov bila kujibu kitu chochote aliinamisha kichwa chake chini na kuanza kulia, aliishuhudia picha nzima ya tukio lote alilotendwa na Federov.
“Mbona unalia?”
“Nisaidie nipone, nitakueleza kila kitu. Ni habari ndefu kidogo lakini yenye machungu mengi,” alisema Ditrov huku akibubujikwa na machozi.
“Nitakusaidia na nina uhakika uta...” alisema Oleg Malenko lakini kabla hajamalizia sentensi yake, mlango wa chumba walichokuwemo ndani yake ukasikika
ukigongwa.
“Ngo!Ngo!Ngo.”
***
Muda mfupi baada ya kukata simu ya Daniel, Lina alinyoosha mkono wake tena na kunyanyua mkono wa simu akaonekana akibonyeza namba kadhaa na kuiweka
simu sikioni.
“Hallow,” aliita na bila kuchelewa sauti nzito ikijibu upande wa pili wa simu ikasikika.
“Phillip?” aliuliza.
“Yes darling.” (Ndio mpenzi) Ilikuwa ni sauti kutoka upande mwingine wa simu.
“Nimempata! Nimefanikiwa kuongea naye na tumekubaliana kukutana leo jioni Lamada Hoteli kwa mazungumzo zaidi,” alisema Lina na muda wote huo tayari
machozi yalishalowanisha mashavu yake.
“Lina?” Phillip akiwa upande wa pili wa simu aliita.
“Be…e” aliitikia kwa sauti ya kutetemeka. Ni sauti hiyo ndiyo iliyomfanya
Phillip ashtuke na kugundua kwamba Lina alikuwa akilia.
“Nakuja hapo sasa hivi,” alisema Phillip na kuikata simu. Bila kuchelewa haraka akanyanyuka kitini na kuufungua mlango wa ofisi yake. Akatoka bila kusema
kitu chochote, safari ya kuelekea ofisini kwa Lina ikaanza. Haikumchukua muda, baada ya dakika tatu tu akawa amewasili eneo hilo na kugonga mlango.
Aligonga kwa muda lakini hakupata jibu, hatimaye akaamua kuusukuma na kuzama ndani.
“Lina!” aliita baada ya kutupa macho yake mbele na kumwona Lina akiwa amejiinamia tena akionekana kulia.
“Nini kimetokea tena? Kwa nini unalia?” aliuliza mfululizo.
Akiwa hapo akamshuhudia Lina akinyanyuka na kumsogelea kisha kumkumbatia.
“Phillip ninakwenda kufanya jambo ulilohitaji ili kulinda ndoa yetu, siko tayari kukupoteza mume wangu, naamini wewe ni wangu mpaka kifo… lakini ukweli
kutoka ndani ya moyo wangu nasikia moto ukiwaka na kunipa maumivu makali. Nashindwa kuelewa ni kwa nini…” alisema Lina na kabla hajafika mwisho wa
sentensi yake wakasikia hatua za mtu akisogea karibu kabisa na mlango wa ofisi ya Lina.
Haraka Lina akamwachia Phillip na kujifuta machozi kisha kuzunguka upande wa pili ambako alikivuta kiti chake na kuketi. Hawakukosea, hatua walizozisikia
zilikielekea eneo hilo zilikuwa ni za bosi wake Lina ambaye aliondoka hapo muda mfupi uliopita.
Akabisha mlango na kukaribishwa kuingia ndani. Naye alishangazwa na hali aliyomwona nayo Lina.
“Lina nini kimetokea? Unaumwa?” aliuliza kwa sauti ya upole.
“Hajisikii vizuri ndiyo maana na mimi niko hapa, nataka kumpeleka hospitali,” Phillip alidakia.
“Basi ni vyema ukafanya hivyo, nitaongea naye kesho kwani nilikuwa na habari njema za kumpa,” alisema bosi huyo na kutoka huku akifunga mlango nyuma
yake.
Alipotoka, kwa haraka Phillip akanyanyuka kitini na kumsaidia Lina kuweka ofisi katika hali ya usafi. Mambo yalipokamilika akamwomba amsaidie kubeba
mkoba wake, wakatoka ofisini na kuelekea sehemu ambako waliegesha gari lao, wakapanda na kuondoka eneo lile.
Njia nzima Lina alikuwa akilia. Hakuweza kuvumilia, mara kadhaa alimuuliza Phillip maswali na kujibiwa lakini hakuwa tayari kukubaliana na majibu hayo.
“Sikia mke wangu, nakupenda sana na ili kukuhakikishia nitakupeleka mwenyewe mpaka hotelini na mimi nitakusubiri mpaka mwisho, umenielewa?” aliuliza
Phillip akimpigapiga Lina mgongoni.
“Fyuuu!” badala ya kujibu Lina akashusha pumzi.
Phillip akazidi kukanyaga mafuta na nusu saa baadaye tayari walishafika nyumbani hapo wakashuka na kuingia ndani. Kwa muda wote huo, Lina alikuwa kimya
kabisa, hakusema kitu chochote. Phillip akamshika mkono na wote kwa pamoja wakaingia chumbani, hawakutoka tena mpaka saa tano baadaye, wote wawili
wakiwa wamevalia vizuri.
Walitoka nje ya nyumba yao na kuingia tena ndani ya gari, safari kuelekea hotelini Lamada ikaanza. Njia nzima Phillip alijaribu kuongea na Lina akimsihi na
kumbembeleza kuondokana na wasiwasi aliokuwa nao.
“Lina tunaingia hotelini sasa, tafadhali hebu jifute machozi, nisingependa jambo hili ligundulike na watu wengi.”
“Siwezi mume wangu, moyo unaniuma sana. Phillip unanifanya nianze kujilaumu ni kwa nini nilikubali kuolewa na wewe, hivi kweli umedhamiria?” aliuliza
Lina.
“Fanya kwa ajili yangu Lina nakuahidi kukupenda mpaka mwisho. Nitakaa hapa hapa nilipokushusha, ukitoka utanikuta nakusubiri, sawa mke wangu?” alisema
Phillip huku akimbusu mfululizo.
Taratibu Lina akashuka kwenye gari na kujiweka sawa kisha kumwangalia Phillip kwa macho ya huruma. Bila kusema kitu chochote akaanza kutembea
kuondoka eneo hilo.
NDANI ya chumba wanaongea mengi juu ya maisha na jinsi walivyokuwa wamepotezana kwa muda mrefu. Daniel anasisitiza kwamba bado anampenda Lina
pamoja na mambo yote yaliyotokea maishani mwao. Muda wote huo Lina alikuwa akibubujikwa na machozi, mara kadhaa taswira ya mume wake Phillip ilimjia
kichwani mwake na sauti ikamsisitiza juu ya kuhakikisha anafanya tendo la ndoa ili hatimaye apate ujauzito.
Ni mambo hayo ndiyo yaliyomfanya Lina azidi kulia, kitu ambacho kilimshangaza sana Daniel. Alitumia muda mwingi kumbembeleza Lina ili anyamaze lakini
ilionekana kuwa ngumu.
Kwa muda wa saa zima walikuwa chumbani, kazi ikiwa moja tu ya kumbembeleza Lina ili anyamaze ndiyo waendelee na mambo mengine. Hata alipopewa
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
chakula alikataa bila kusema sababu, hatimaye Daniel uvumilivu nao unamshinda. Uchu wa kufanya tendo la ndoa na Lina unamkamata, anaona huo ndiyo muda
muafaka kwake.
Taratibu bila kusema kitu chochote baada ya kuwa ameshambembeleza kwa muda mrefu, anasogea karibu na Lina kisha anamnyanyua na kumlaza kitandani
huku akimpiga mabusu mfululizo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment