Simulizi : Msichana Ndotoni Mwangu
Sehemu Ya Nne (4)
HALI ya Ditrov ilikuwa ikiendelea vyema, akipata kila aina ya msaada kutoka kwa Oleg Malenko. Jeraha lake lilishapata nafuu kubwa na mwili wake ulionekana
kurejea katika hali yake ya kawaida. Pamoja na yote hayo bado hakuwa tayari kueleza ukweli kwamba alitokea wapi na ni kitu gani kilisababisha akatoswa
baharini.
“Nashukuru Mungu unaendelea vizuri, nadhani sasa tunaweza kuongea kidogo kuhusu wewe,” Oleg Malenko alisema.
“Sipo tayari kueleza chochote, kikubwa ninachokuomba ndugu yangu unitunzie siri ya mimi kuwepo hapa katika nyumba yako. Muda si mrefu nitaondoka ili
kukuepushia matatizo.”
“Matatizo yapi?”
“Ni historia ndefu sana kuhusu mkasa ulionipata. Ninachokushukuru sana ni kuokoa maisha yangu.”
“Hakuna shida,” alisema Oleg lakini tayari kichwani mwake alishaweka viulizo ni kwa nini mtu aliyekuwa ndani ya nyumba yake hakutaka kueleza ukweli wa
nini kilichompata na zaidi ya yote alitaka jambo hilo lifanywe siri.
Hivyo ndivyo maisha yalivyokwenda, Ditrov akawa ni mtu wa ndani muda wote akihitaji kubaki peke yake, jambo ambalo lilizidi kuitia shaka familia ya Oleg
Malenko. Wiki ya kwanza ikakatika, hali yake ikazidi kuwa imara na wiki ya pili ilipofika katikati akaamua kuvunja ukimya. Alimwita Oleg Malenko ili
waongee.
“Hivi sasa wewe ni kama ndugu yangu kwani umeokoa maisha yangu. Nakushukuru sana lakini naomba msaada mmoja tu kutoka kwako.”
“Sema tu ndugu yangu nitakusaidia.”
“Nahitaji fedha kidogo kwa ajili ya nauli.”
“Kwenda wapi?”
“Nataka kurejea nyumbani,” alidanganya.
“Hakuna shida, nipo tayari kukusaidia. Sijui unahitaji lini?”
“Ikiwezekana kesho asubuhi ili niondoke hapa,” alisema Ditrov akionesha shaka machoni mwake.
***
“Nakupenda mpenzi wangu, ni muda mrefu nimengoja jambo hili litokee hatimaye leo hii limewadia. Nieleze ni kitu gani kimesababisha unitafute Lina, huu
kwangu ni muujiza,” alisema Daniel akizidi kumwagia Lina mabusu mfululizo.
“Mh!” Aliguna huku kwikwi ya kulia ikizidi kumkaba.
“Lina,” Daniel aliita..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tafadhali toa ushirikiano, kwa nini unalia?”
“Hakuna kitu, nipo sawa.”
“Si kweli! Kama upo sawa hayo machozi ni ya nini sasa?”
“Una…ju…a nini?”
Daniel akatulia kidogo ili asikilize ni kitu gani Lina alitaka kumweleza.
“Nimefurahi kukutana na wewe Daniel, ni muda mrefu umepita eeh?” Aliuliza Lina akimpigapiga Daniel mgongoni. Mawazo na akili zake zote hazikuwa ndani
ya chumba hicho, mara kadhaa taswira ya mumewe Phillip ilimjia kichwani mwake na hiyo ndiyo iliyomfanya abubujikwe na machozi muda wote.
***
Nje ya hoteli, Phillip bado aliendelea kubaki hapo akimsubiri mkewe Lina, mapigo yake ya moyo yalikwenda mbio hakuelewa ni kitu gani kingekuwa kimetokea
ndani ya chumba kwani tangu mwanzo Lina alishaonesha dalili kwamba hakupenda kufanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine isipokuwa yeye tu.
“Atakuwa amefanikiwa, ni muda mrefu tangu aingie huko,” aliwaza Phillip.
Akaendelea kujiambia mwenyewe kwamba kusingekuwa na tatizo lolote, akatupa macho yake kwenye saa yake ya mkononi na kugundua kuwa tayari ilishatimu
saa tatu na nusu za usiku. Mpaka wakati huo hakuwa na taarifa yoyote ya Lina.
“Akichelewa zaidi nitampigia simu,” aliwaza Phillip akitoka ndani ya gari na kutembeatembea kulizunguka gari lake. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda
kasi kwani hakufikiria kwamba Lina angechukua muda mrefu kiasi kile.
***
Ndani ya chumba, Daniel aliendelea kuongea mambo mengi juu ya maisha yake baada ya kuachana na Lina. Aliweka wazi zaidi na kumweleza kwamba tayari
alishaoa na alikuwa na mtoto mmoja lakini akajiapiza kutoka ndani ya moyo wake kwamba alilazimika kuoa kwani umri ulikuwa ukienda. Akamwambia
hakuwahi kumpenda mwanamke mwingine kama ilivyotokea kwa Lina.
“Daniel unasema kweli?”
“Huo ndiyo ukweli wangu, hutaniamini lakini…”
“Usiseme hivyo bwana.”
“Lina ukweli nilikupenda na nitaendelea kukupenda maisha yangu yote, hapa nilipo nahisi nipo ndotoni pengine nitaaamka muda si mrefu.”
“Daniel uko na mimi wala si ndoto.”
“Umefikiria nini mpaka kuamua kunitafuta Lina?”
“Maisha yamesababisha hivyo, wahenga walisema milima haikutani lakini binadamu tunakutana, ndiyo kama hivi.”
“Ahsante kwa kunikumbuka na kuniingiza tena ndani ya moyo wako.”
Ukimya wa ajabu ukatokea kati yao, ghafla Daniel akaanza kumpapasa Lina sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimpa maneno matamu yaliyoambatana na
mabusu.
“Leo sitarudi nyumbani, nitalala hapa na wewe. Nataka nikuoneshe ni jinsi gani ninavyokupenda Lina. Nataka ujue kwamba mimi ndiye Daniel wa ukweli,
niambie unataka nifanye nini?” alisema Daniel huku akizidi kumpapasa mwilini.
Tayari hamu ya mapenzi ilishawaingia, kila mmoja alikuwa akihemka, si Daniel wala Lina wote walikuwa taabani.
“I lov..e yo…u ba…by...”(Nakupenda mpenzi) ilikuwa ni sauti nzito ya Daniel ambayo ilipenya na kwenda moja kwa moja kwenye sikio la Lina aliyekuwa
amelala kimya bila kusema kitu chochote. Bila kupata kibali chochote kutoka kwa Lina, Daniel akaanza kumvua viatu na kuvitupa chini, taratibu akapanda juu
na kuanza kumfungua vishikizo vya blauzi aliyokuwa amevaa.
“Leo ndiyo leo nataka kuweka historia ya mapenzi kwako,” alisema Daniel. Tayari macho yake yalishabadilika rangi na kuwa mekundu.
“Daniel!” Lina aliita.
“Yes baby.”
“Twende taratibu, usiwe na haraka.”
“Nashindwa kuvumilia, nilikusubiri kwa muda mrefu.”
“Hapana,” alisema Lina akijaribu kuitoa mikono ya Daniel kifuani kwake.
“Basi naomba nitoe tu hii halafu...” alisema Daniel tayari alishamaliza vishikizo vyote vya blauzi.
“Oh! My God!”(Oh! Mungu wangu!) alisema kimoyomoyo, hakuwa tayari kuamini alichokishuhudia juu ya kifua cha Lina. Chuchu ndogo zilizosimama vizuri
zilizidi kumpagawisha Daniel, akawa anapumua kwa kasi kubwa.
DITROV amepata nafuu na sasa ameomba msaada kutoka kwa Oleg Malenko ili aondoke sehemu hiyo mara moja na bila kujiuliza kwa kina Oleg anaahidi
kumpa msaada huo ingawa hajui anataka kuelekea wapi.
Upande wa pili, Lina na Daniel tayari wapo juu ya kitanda. Daniel anaonekana kuwa na hali mbaya zaidi kwani ana hamu kubwa ya kufanya tendo la ndoa na
Lina, mwanamke aliyempenda kwa moyo wake wote lakini akashindwa kulifaidi penzi lake baada ya kumkataa. Nafasi ile ya kuwa wawili tu na Lina chumbani
aliiona kama bahati ya mtende kuota jangwani, akazidi kuchanganyikiwa kwani alikuwa akilihitaji mno penzi lake.
Baada ya mazungumzo marefu, akitumia muda mwingi kumbembeleza Lina aliyekuwa akilia, hatimaye Daniel anafanikiwa kufungua vishikizo vya blauzi ya
Lina na kuziona chuchu ndogo zikiwa zimesimama kifuani. Kitendo kile kilifanya hamu yake ya kufanya mapenzi izidi kupamba moto, bila kusema kitu akaruka
kutoka kitandani na kuanza kuchojoa nguo moja baada ya nyingine huku mhemko ndani yake ukizidi kuongezeka kadiri saa zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele.
Bila kusema kitu chochote, anarejea tena kitandani na kulala huku mikono yake ikizunguka juu ya mwili wa Lina ambaye alitulia kimya kitandani, wakiwa hapo
mabusu ya mahaba yanamiminika mfululizo juu ya mwili wa Lina.
Nje ya hoteli, uvumilivu umeanza kumshinda Phillip kwani ameshasubiri kwa muda mrefu bila kumwona mkewe akitoka, akaanza kuhisi huenda kuna kitu
kibaya kimempata. Anajiambia moyoni kuwa aendelee kusubiri kidogo na kama hatatokea basi ataingia ndani ya hoteli kumtafuta.
“Mbona anazidi kuchelewa? Au kapatwa na tatizo kubwa? Nahisi hayupo sawa, kwa nini harejei?” Phillip alijiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu.
Alikuwa akizungukazunguka pale nje kama mtu aliyepoteza kitu. Mara kwa mara alikuwa akiingia ndani ya gari na kushuka, akiwa haelewi nini anachokitafuta.
Akili yake ilikuwa haitulii kabisa.
Wivu na hofu vilikuwa vikimshambulia kwa wakati mmoja. Kuna wakati alihisi huenda Lina amenogewa na penzi alilopewa na mwanaume aliyeenda kukutana
naye kiasi cha kujisahau. Akili nyingine ilimtuma kuwa huenda ameamua kuondoka na huyo mwanaume ingawa alishindwa kuelewa wamepitia wapi kwani
muda wote yeye alikuwa pale nje.
Hofu nayo haikumuacha, alihisi huenda amekumbana na kitu kibaya ambacho kimemdhuru na ndiyo maana hatoki mapema kama walivyokubaliana.
Mambo yote yalikuwa yakipita akilini mwake kama mkanda wa sinema. Japokuwa ni yeye ndiye aliyetoa wazo lile, kwa upande mwingine alijikuta akijutia
uamuzi wake lakini kwa kuwa alikuwa na shida ya mtoto, ilibidi avumilie.
Phillip aliendelea kujizungusha huku na kule huku akiangalia saa yake karibu kila baada ya dakika moja. Aliona muda unaenda taratibu sana, akatamani
angekuwa na nguvu za ziada za kuweza kuona kilichokuwa kinaendelea kwa Lina.
“Zikipita dakika kumi kama bado hajatoka, itabidi niende mapokezi kuuliza, ikishindikana nitaenda mpaka kwenye chumba alichoingia,” alisema Phillip huku
kichwa chake kikichemka kwa mawazo.
Muda ulizidi kuyoyoma bila Lina kutoka, hali iliyozidi kumuweka Phillip kwenye wakati mgumu. Aliendelea kuhesabu sekunde, dakika na saa hatimaye
uvumilivu ukamshinda. Kijasho chembamba kilikuwa kikimtiririka, akafunga mlango wa gari na kuanza kupiga hatua za taratibu kuelekea mapokezi huku
akiendelea kujiuliza maswali mengi ambayo yote yalikosa majibu.
***
Baada ya kupata nafuu kwa msaada mkubwa wa Oleg Malenko, Ditrov alijiandaa kuondoka huku mawazo mengi yakipita ndani ya kichwa chake. Mazingira
yaliyomfanya akaokolewa na Oleg Malenko yalimfanya atambue kuwa Mungu yupo kwani alishakata tamaa ya kuendelea kuishi. Alikuwa akijiuliza mara kwa
mara kwamba alimkosea nini bosi wake, Victor Federov mpaka kufikia hatua ya kumpiga risasi na kwenda kumtosa baharini, tena akiwa amefungwa na jiwe
kubwa shingoni.
Kila alipokuwa anakumbuka jinsi alivyonusurika kufa, mwili wote ulikuwa ukimsisimka. Baada ya kuagana na mwenyeji wake pamoja na familia yake, Ditrov
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alianza safari ya kuondoka ndani ya nyumba ya Oleg Malenko, akiwa haelewi anaelekea wapi. Alitembea taratibu mpaka alipotoka nje, akageuka nyuma na
kuwapungia mkono Oleg Malenko na familia yake kwa ishara ya kuwaaga.
Wakamsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kwenye upeo wa macho yao. Alikuwa anatembea huku kichwa chake amekiinamisha chini akiwa hataki mtu
yeyote amtambue. Alikuwa akikwepa macho ya watu kwani aliamini wengi wao walikuwa wanamfahamu.
“Mimi ni mwanaume bwana! Kama Mungu amenisimamia nimenusurika na mauti, hawezi kushindwa kuniongoza mahali pa kwenda wakati najiandaa kulipa
kisasi.
Nitatafuta sehemu yoyote ambapo nitajihifadhi wakati nafikiria jinsi ya kurudi kulipa kisasi, lazima nimfunze adabu Victor Federov. Tena kazi itakuwa rahisi
kwani anaamini nimeshakufa, hajui kuwa Mungu ambaye nilishaacha hata kumuabudu miaka mingi iliyopita amenipigania na naendelea kupumua,” alisema
Ditrov wakati akizidi kuchanja mbuga kuelekea mahali asikokujua.
Kumbukumbu za kuhuzunisha ziliendelea kuzunguka ndani ya kichwa chake, akajikuta akishindwa kuyazuia machozi kumtoka, hasa alipokumbuka maisha
aliyokuwa anaishi kabla ya kutokewa na balaa lile na kuponea chupuchupu kufa.
Taswira ya maisha aliyokuwa anaishi, japokuwa yalikuwa yanategemea kufanya shughuli haramu mara chache, ilikuwa ikipita akilini mwake na kumfanya
ashindwe kukubaliana na hali halisi.
Maisha mazuri aliyoishi, tena ya kifahari yalimfanya asiamini kuwa wakati ule alikuwa akitangatanga mahali asipopajua na kuishi kama mkimbizi. Maisha ya
kujificha kama digidigi hakuyazoea lakini sasa ndiyo alitakiwa ayaishi wakati anajiandaa kulipa kisasi akikwepa kugundulika kabla hajatimiza alichokipanga.
Alitembea kwa muda mrefu mpaka akaanza kuhisi uchovu. Ukizingatia kuwa afya yake ilikuwa bado haijatengamaa, nguvu zilimwisha kirahisi. Akaamua
kutafuta mahali pa kupumzika huku akiendelea kujiuliza kichwani mwake ni wapi angekwenda na kupata fedha za kumsaidia kukimu shida zake mbele ya safari.
Alipiga moyo konde na kuamini kuwa hakuna linaloshindikana chini ya jua.
“Najua nitapata shida sana lakini haya yote yatapita. Nitaanzia chini kabisa lakini naamini ipo siku nitapata fedha ambazo zitanifanya nirudi tena kwenye daraja la
maisha ya kifahari kama ilivyokuwa mwanzo, nikila na kunywa hadi kusaza,” alijisemea Ditrov wakati akiinuka na kuendelea na safari yake baada ya kupumzika
kwa muda.
Kichwani mwake hakuwa na ramani ya mahali anapokwenda lakini aliamini atafika tu mahali palipotulia ambapo ndipo yatakapokuwa makazi yake ya muda
wakati akijiandaa kulipa kisasi.
***
“Lina,” Daniel aliita.
“Abee,” aliitikia kwa sauti ya chini.
“Kweli unanipenda?”
“Ndiyo!”
“Kama kweli unanipenda tafadhali niache niwe huru juu ya mwili wako. Naomba unipe nafasi ya mimi kufanya ninachotaka, usinishike mikono na kunizuia,
niache nifurahie mapenzi yako,” alisema Daniel kwa sauti ya kubembeleza kuonesha kuwa hamu yake ilikuwa imefika juu kabisa.
Lina hakuwa mwepesi wa kukubali Daniel afanye kila alichokitaka kwenye mwili wake. Mara kwa mara alikuwa akiushika mkono wake na kumzuia kumpapasa
maungoni mwake, jambo ambalo lilizidi kumpa Daniel wakati mgumu.
“Yaani shida ya mtoto ndiyo inifanye nifanye jambo nisilolitaka, roho inaniuma sana,” alijisemea kimoyomoyo Lina huku dhamira yake ikigoma kabisa
kumruhusu Daniel afaidi penzi lake. Daniel hakukata tamaa, aliendelea kumbembeleza Lina kwa maneno matamu huku akitumia ujanja kuupapasa mwili wake.
Cha ajabu, kwa muda wote huo Lina alikuwa akibubujikwa na machozi kama yupo msibani, jambo lililomfanaya Daniel abaki njia panda. Alijiuliza kwa nini
Lina analia kiasi kile wakati ni yeye ndiye aliyempigia simu na wakakubaliana kukutana pale.
“Lina mpenzi wangu, naomba nipe haki yangu tafadhali, nionee huruma mwenzio nateseka,” Daniel alisema kwa sauti iliyokuwa inatetemeka baada ya kuzidiwa
na haja ya mwili wake kulifurahia penzi la Lina.
Alipoona hamjibu kitu bali anaendelea kulia, aliinuka kidogo na kujaribu kuivua sketi fupi aliyokuwa ameivaa Lina. Lina alishtuka na kuanza kumzuia, wakawa
wanavutana pale kitandani.
“Usitumie nguvu Daniel, niache nitavua mwenyewe,” alijitetea Lina lakini Daniel hakutaka kumuelewa. Akaikamata vizuri na kuivua kwa nguvu, Lina akabakia
na nguo ya ndani pekee.
“Duu! Leo sijui itakuwaje, si mchezo,” Daniel alijisemea kimoyomoyo wakati akimuangalia Lina aliyekuwa amebakiwa na ‘kufuli’ nyeupe iliyozidi kupandisha
mashetani ya Daniel.
“Nipe nafasi mpenzi wangu, mwenyewe utafurahi,” alisema Daniel huku akipeleka mikono yake kujaribu kulitoa kufuli la Lina.
“Subiri Daniel, nitakupa nafasi lakini usiwe na papara, subiri kidogo,” alijitetea Lina huku akibana miguu yake na kumzuia Daniel.
“Hakuna shida, nitasubiri hata ukisema mpaka usiku wa manane. Nakuhakikishia kuwa shughuli nitakayokupa leo, mwenyewe utanitafuta tena.”
Lina alifumba macho na kumruhusu Daniel apitishe mikono yake kiunoni, akawa anampapasa kimahaba huku akimpiga mabusu mwili mzima. Alipoona Lina
amejisahau, alishika pindo za kufuli lake na kuanza kuliteremsha kwa kushtukiza. Lina aliwahi kumzuia, lakini likiwa tayari limeshashuka mpaka karibu na
magoti. Daniel aliendelea kusumbuana naye, hatimaye akafanikiwa na wote wakabaki kama walivyoletwa duniani
Uwiii!” Daniel alisema kimoyomoyo, macho yake hayakuwa tayari kuamini kile alichokuwa akikishuhudia mbele ya macho yake, uzuri wa Lina haukuwa na
maelezo, akili ya Daniel ikazidi kuchanganyika zaidi aliposhusha macho yake na kuangalia mapaja ya Lina.
“Mungu wangu! Ninaota au?” alijiuliza.
“Huoti Daniel unachokiona ndicho.”
“Lina!”
“Yes.”
“Hakika wewe ni mwanamke mrembo,” aliongea Daniel na tayari mikono yake ilikuwa ikipita huku na kule juu ya mapaja ya Lina huku akihemuka, akimeza
mate mfululizo.
Akamnyanyua Lina na kumlaza kifudifudi mikono yake yote miwili ikiendelea kucheza juu ya mwili wake laini.
“Hakika wewe ni mwanamke mtamu.”
“Whaaat?” (Nini?)
“Naaminisha wewe ni mzuri sana.”
“Kama wewe Danny.”
“Sidhani,” alisema akishusha mdomo wake na kuanza kumng’ata ng’ata Lina jambo hilo likazidi kuwasha moto zaidi kwa Lina.
“Mh! Mh! Baby, taratibu usiwe na shaka leo ni siku yako.”
“Nahisi kuchelewa Lina tafadhali nipe.”
“Ah! tucheze kwanza kidogo muda ukifika nitakupa.”
“Shiiii! Mh! Uwiii! Yalaaa!” alilalama Daniel.
Kwa muda wa saa mbili mfululizo waliendelea kucheza juu ya kitanda huku kila mmoja akionekana kukolezwa na mwenzake, mara kadhaa Daniel alimgeuza
Lina akijaribu kumlaza chali lakini Lina alikataa akimweleza wazi kwamba muda muafaka ulikuwa bado haujafika.
Kwa kuwaangalia wote wawili walikuwa hoi kwa mapenzi kila mmoja akiguna na kuongea maneno yake huku wakiendelea kushikana hapa na pale.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Lina inatosha tafadhali ni…pe,” aliongea Daniel lakini hakumaliza sentensi yake tayari mdomo wake ukafunikwa na kiganja cha Lina.
“Shiii! Hebu jikaze bwa....” aliongea Lina lakini naye alionekana kuwa hoi kupita kawaida.
Kwa sauti ya upole huku akionyesha tabasamu akamwomba Daniel naye alale ili aweze kumfanyia alichotaka kufanya, bila hiyana taratibu mwanaume akashuka
kitandani na kulala akimpa Lina nafasi ya kufanya alichokusudia
“Mh!Mh!Mhhhhh” ilikuwa ni miguno kutoka kwa Daniel.
“Vipi?” Lina aliuliza.
“Imetosha, naomba unipe ki…do..go,” aliongea.
“Niachie nafasi kidogo nikupe raha Daniel ambayo nina hakika hutaisahau maishani mwako.”
Ulimi wa Lina ulikuwa ukipita ndani ya sikio la Daniel.
Ni tukio hilo ndilo lililofamfanya Daniel akajikunja kitandani kama jogoo, raha aliyokuwa ameisikia ilikuwa haielezeki hata kidogo, ni kweli alishakutana na
wanawake wengi maishani mwake lakini kwa Lina ilionekana kuwa kiboko.
“Lina niko tayari kuachana na mke wangu nikuoe wewe, unasemaje?”
“Danny! Hebu acha utani unamaanisha unachokisema?”
“Niko tayari hakika sitanii.”
“Unaweza kumwacha sasa hivi tena kwa kumpigia simu?”
“Haijalishi.”
Daniel alikuwa amechanganyikiwa kabisa, akili zake ziligeuka na alikuwa tayari kufanya kila kitu ambacho Lina angemwambia ili mradi tu aendelee kupata raha
aliyokuwa anaipata siku hiyo, kichwani mwake akisahau kabisa kwamba alikuwa ni baba wa watoto wawili waliomtegemea kwa kila kitu duniani.
***
Akiwa ndani ya gari lake usingizini, ubaridi mkali wa kiyoyozi ndiyo uliomshitua na kumfanya afungue macho na kuangaza huku na kule ndani ya gari na
kugundua kwamba alikuwa peke yake bado, haraka akanyoosha mkono wake na kuwasha redio ndani ya gari na sauti ikasikika ikitangaza kwamba muda huo
ndiyo ilikuwa ikitimu saa sita kamili usiku.
“Mungu wangu mpaka saa hizi? Amepatwa na kitu gani huyu mwanamke?”
aliongea Phillip akishuka ndani ya gari.
Akiwa hapo akaangaza huku na kule bila kuona kitu chochote, taratibu akazima gari na kuchomoa funguo kisha kufunga mlango.
“Lina amenisaliti hawezi kukaa ndani ya hoteli kwa muda mrefu kiasi hicho mkataba wangu mimi na yeye ni kuhakikisha anakutana na mwanaume huyo na
kufanya naye tendo la ndoa baada ya hapo basi atoke na tuondoke, kwa nini amechukua muda mrefu kiasi hiki? Inawezekana amepewa mambo mazuri mpaka
amenisahau?” aliongea Phillip akionyesha hasira nyingi.
Hofu ilishaugubika moyo wake, akiwa haelewi ni kitu gani angekwenda kushuhudia huko, Phillip alianza kutembea kichwani mwake akijiuliza maswali mengi
na mara kadhaa akianza kujilaumu kwa kitendo chake cha kumshawishi mkewe kwenda kukutana na mwanaume mwingine ili tu wafanye tendo la ndoa na kupata
ujauzito ambao angeulea na kuutunza mpaka mtoto atakapozaliwa. Moyo wake ukauma.
“Hivi kweli anaweza kuwa ameondoka na kuniacha mimi nikiwa hapa? Lina, sidhani lakini akili za mwanamke anazijua mwenyewe pengine ameamua kufanya
kweli ili kunikomoa kwani hakuwa tayari kufanya jambo hilo, mimi ndiye nimemlazimisha.”
Lawama nyingi akazielekeza kwake na kujiona ni mwanaume mjinga kiasi gani kwa kitendo cha kuruhusu mkewe kwenda kufanya ngono na mwanaume
mwingine, hakika alifahamu wazi kwamba kama dunia ingefahamu jambo hilo basi ingekuwa ni aibu mpaka siku anaingia kaburini.
Huku akiwa na wasiwasi mwingi moyoni mwake taratibu akaanza kutembea, lengo lake likiwa kuelekea eneo la mapokezi ambako angeingia na kuuliza.
“Najua nitakutana na maswali mengi sana hasa ukizingatia kwamba ni usiku
mkubwa lakini nitajibu moja baada ya jingine nikijifanya mimi ni dereva wake niliyekuwa nikimsubiri hapo nje,” aliendelea kuwaza akitembea taratibu.
Kwa fedha kidogo alizokuwa nazo, akiwa haelewi kabisa nini ingekuwa hatima ya safari yake hiyo, Ditrov alijipa moyo na kujiapiza kwamba ni lazima
angefanya kila kinachowezekana kusukuma maisha yake kwenda mbele lakini zaidi ya yote akili yake ilifikiria juu ya kulipa kisasi kwa Victor Fedorov. Alijiapiza
kuwa hata kama ingechukua miaka mingapi ni lazima jambo hilo litokee, hakufahamu lingetokea vipi lakini aliamini hivyo.
Hasira ya maisha mapya ilikuwa imemkaa Ditrov kupita maelezo, alitaka kurejea kwenye hali yake ya awali na kuwa Ditrov yuleyule wa zamani, bila mtu yeyote
kufahamu kwamba hakufa. Alipanga kujichimbia mahali na kuishi kwa siri kubwa akitafuta mbinu za kulipa kisasi kwa mtu aliyeamini kwamba alikuwa ni adui
yake.
“Yupo mtu mmoja tu nchini Urusi anayeweza kufanya kazi ninayotaka afanye. Nikitulia kidogo nitamfuta,” aliwaza siku moja akiwa ndani ya chumba chake
kidogo kilichokuwa nje kabisa ya mji.
Kwa muda wa wiki mbili mfululizo aliendelea kutafakari juu ya nani angeweza kufanya zoezi ambalo alilihitaji, hatimaye kumbukumbu zake zikamrejesha moja
kwa moja kwa kijana mmoja aliyeishi nchini Urusi ambaye aliamini kabisa kwamba angeweza kufanya kile alichokitaka.
Baada ya kuchunguza kwa muda mrefu, alimkumbuka kijana mmoja katili ambaye aliamini kabisa angeweza kufanya kazi ngumu iliyokuwa mbele yake. Mara
kadhaa alikumbuka matukio ya kutisha ambayo aliwahi kufanya kipindi cha nyuma.
“Nitampa kazi hii lakini sitaki afanye mauaji yoyote, kama ni kisasi nitalipa mimi mwenyewe,” aliwaza Ditrov.
Kazi yake ikabaki kuwa moja tu, kutafuta simu ambayo angeitumia kuwasiliana na kijana huyo ili ampe kazi hiyo mara moja.
“Kesho nitahakikisha napata simu kwa ajili ya mawasiliano,” alisema Ditrov akijaribu kuzungusha akili yake huku na kule. Akiwa hapo akaingiza mkono katika
moja ya mfuko wake wa suruali akijaribu kukagua kama angepata akiba yoyote ambayo ingeweza kumsaidia kupiga simu.
“Yes, hii itatosha kwa kazi hiyo,” alisema huku akitoka ndani. Nyumba aliyokuwa anaishi ilikuwa ndogo na iliyochakaa kupita kawaida. Hapakuwa na jirani
yeyote maeneo hayo na ilivyoonekana, nyumba ile ilikuwa imetelekezwa kwa muda mrefu. Hapo ndipo Ditrov alipoweka makazi yake, akiishi peke yake.
Licha ya mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, Ditrov aliamua kutoka ili kwenda kutafuta mahali ambapo angepata simu na kupiga nchini Urusi ili aweze kuongea
na mtu ambaye aliamini angemsaidia shida yake. Taratibu akatoka na kuanza kutembea, kichwani mwake akiwaza mambo mengi huku akitupa lawama nyingi
kwa Victor Fedorov kwamba bila yeye maisha yake yasingekuwa kama yalivyo. Alipofikiria hivyo, moyo wake ukazidi kumuuma.
“Mimi ni mwanaume, naamini nitashinda hata kama gharama yake itakuwa kubwa kiasi gani, lazima nishinde tu,” alisema huku akitokomea kwenda mbele.
Kwa muda wa saa nzima Ditrov alitembea bila kukutana na mtu yeyote zaidi ya magari machache yaliyoonekana kupita eneo hilo kwa kasi huku baadhi ya watu
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
waliokuwa ndani yake wakimshangaa.
“Mh! Kwa nini watu wananishangaa kiasi hiki, inawezekana eneo hili ni hatari?” alijiuliza huku akisonga mbele. Hatimaye nusu saa baadaye alifanikiwa kufika
katika mji mdogo ambao hata hakuufahamu jina lake. Akaona maduka kadhaa, huku akiwa na wasiwasi mkubwa akatembea na kusogea katika moja ya maduka
yaliyokuwepo eneo hilo. Bado watu walionekana kumshangaa kwani alionekana kuwa mgeni kwa kila kitu.
“Habari yako?” alimsabahi muuza duka.
“Salama nikusaidie nini?”
“Naweza kupata wapi huduma ya simu hapa?”
“Hata hapa unaweza kuipata,” alijibu mzee aliyekuwepo dukani hapo na bila kusema kitu chochote Ditrov akainamisha kichwa chini kama mtu aliyekuwa
anakumbuka kitu fulani, alipoinuka aliomba kalamu na karatasi kisha akaanza kuandika namba kwenye kipande cha karatasi.
”Hii hapa.”
Mzee mwenye duka akanyoosha mkono na kuipokea karatasi hiyo kisha bila kuchelewa akabonyeza namba alizopewa. Haikupita hata sekunde mbili, simu
ikasikika ikiita upande wa pili.
“Ngrii!Ngrii!Ngrii!” Haraka akakabidhi mkono wa simu kwa mteja wake.
“Mimi ni Ditrov, sikufa kama watu wengi nchini Urusi wanavyofahamu, nilinusurika na nina kazi moja nzito ambayo nitataka uifanye kwa uaminifu mkubwa.
Nakupa muda wa siku tatu tu iwe imekamilika, umenielewa?” Aliongea Ditrov kwa ukali, kitendo kilichofanya watu wote waliokuwepo eneo hilo kupigwa na
butwaa.
“Mungu wangu kumbe hukufa? Nini kilitokea mpaka ukawa hai? Dunia nzima inafahamu kwamba wewe na washirika wako wote mlishakufa?” Sauti ya upande
wa pili ilisikika ikiuliza.
“Ni historia ndefu kidogo lakini kwa ufupi nipo hai.”
“Nisikilize vizuri, tena kwa makini usije ukafanya kosa kabisa.”
“Nipo tayari.”
“Nahitaji kupata fedha ndani ya siku tatu, hakikisha unafanikiwa vinginevyo hata wewe maisha yako yatakuwa hatarini,” alisema Ditrov kwa msisitizo.
“Bosi nitazipata wapi? Tafadhali nipe maelekezo ya kufanikisha zoezi hilo.”
“Wewe ni Mafia nz umeshafanya michezo mingi hatari, hilo kwako halitakushinda. Kumbuka nimekuwa bosi wako kwa muda mrefu hivyo nafahamu wazi siri
zote na naamini unajua nini cha kufanya.”
“Mh!”
“Kumbuka nahitaji fedha hizo ndani ya siku tatu, nitakupigia simu baada ya siku mbili kujua umefikia wapi, sawa?” alisema Ditrov na alipomaliza alimkabidhi
mkono wa simu muuza duka, akatajiwa gharama ya huduma ile na kulipa.
“Nitahakikisha napata ninachokitaka,” aliongea Ditrov akitokomea kuingia mashambani.
Ditrov alikuwa amedhamiria na alitaka kutimiza alichokitamka kutoka mdomoni mwake pamoja na kwamba alifahamu wazi kwamba pengine zoezi hilo
lingeweza kutoa hata uhai wa mtu lakini kwake jambo hilo lilionekana kuwa dogo.
Taratibu huku akionekana mwenye wasiwasi mwingi alianza kutembea na kutokomea kuingia zaidi mashambani ambako ndiko hasa kulikuwa na makazi yake,
kichwani mwake akimfikiria Victor Fedorov na unyama aliomfanyia, hakika aliapa kumchukia mtu huyo maisha yake yote na aliuahidi moyo wake kufanya kila
kilichowezekana mpaka afanikiwe kulipa kisasi hata kama ingechukua miaka mingapi lakini aliamini jambo hilo lingetokea.
Kichwani mwake alidhamiria kabisa kulipa kisasi, lakini bila fedha? Jambo hilo lisingewezakana, alitaka kuwa na fedha hata kama kidogo tu ambazo
zingempatia gari, simu na hata wafuasi wachache ambao angewatumia kumwinda mbaya wake huyo kila sehemu mpaka mwisho na hatimaye kumpata.
“Nikifanikiwa nitatoka huku mashambani na kutafuta makazi mazuri kisha kuanza mchakato wa nini cha kufanya,” aliwaza.
Siku ya kwanza ikapita akiwa bado yuko mashambani na chakula chake kikubwa kikawa ni matunda tu na maji kidogo yaliyopatikana eneo hilo.
Hali yake iliendelea kutengemaa kadiri siku zilivyokwenda mbele, mara kadhaa akiikumbuka familia ya Oleg Malenko na kuishukuru kwa msaada wote
iliyompatia.
Akauahidi moyo wake siku moja kurudi kulipa fadhila kwa mema aliyotendewa na familia hiyo.
“Ipo siku nitarudi naomba niwakute hai, najua watanidadisi sana lakini nitarudi na kuwapa shukrani zangu, wameokoa maisha yangu wale, sijui isingekuwa Oleg
ingekuwaje kwani nilishakata tamaa nikiamini kwamba sasa ninakufa maji na maiti yangu kuliwa na samaki wakubwa baharini, hivyo hakuna mtu ambaye
angefahamu nini kilitokea katika maisha yangu,” aliwaza.
Siku ya pili asubuhi Ditrov alitoka tena kuelekea mji mdogo kwa lengo moja tu la kupiga simu kwa mtu aliyekuwa amempa kazi, alitaka kufahamu aliendeleaje
na kumkumbusha kwamba ilikuwa imebaki siku moja tu mbele ili kukamilisha mpango mzima na kumtaka asifanye mchezo na suala hilo vinginevyo angekiona
cha moto.
Muda wote akitembea hakudiriki hata mara moja kuinua uso wake na kama alifanya hivyo ni mara moja tu na kuendelea na safari yake, hatimaye akafika kwenye
mji mdogo sehemu ileile aliyowahi kupiga simu kwa mara ya kwanza na kutoa namba kisha kuomba msaada wa kupigiwa simu.
Sekunde tatu tu baadaye alikuwa katika simu akiongea na mtu upande wa pili huku akionyesha msisitizo na kwa sababu aliongea kwa lugha ya Kirusi hakuwepo
mtu eneo hilo aliyeweza kuelewa ni kitu gani aliongea, wengi walimtazama kwa macho na kugundua kwamba alikuwa na tatizo fulani kwani macho yake
yalionekana mekundu muda wote alipokuwa akiongea na simu.
“Sikia kwa makini nitakuwepo tena hapa muda kama huu kukupigia ili nikupe maelezo jinsi ya kunipata mara utakapofanikiwa kuchukua huo mzigo, sawa?”
aliongea na kuuliza.
“Sitaki uue lakini kama itatokea nitakupa ruhusa ya kujeruhi tu na si vinginevyo, nadhani unanielewa vyema sina mchezo na kazi yangu hasa pale ninapotaka kitu
ni lazima nikipate…”aliongea Ditrov huku akitetemeka, alionekana kama mtu aliyekuwa na homa kali.
Haraka akarudisha mkono wa simu huku akiuliza kiasi cha fedha anachodaiwa, bila kuchelewa akaingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi hicho akalipa na taratibu
akaanza kuondoka eneo hilo.
“Mh!” Mtu aliyempa huduma ya simu dukani aliguna, alionekana kumshangaa Ditrov kupita kawaida, kwanza kwa jinsi alivyokuwa na sura yake ilitisha.
Mwili wake mkubwa uliojazia vyema ni jambo lililosababisha kuingiwa na wasiwasi na kuamini kabisa kwamba mtu huyo hakuwa wa kawaida alikuwa na kitu
alichokuwa akikitafuta.
“Inawezekana akawa ni jambazi huyu,” aliongea macho yake yakimwangalia Ditrov kwa makini.
“Nimesikia akisema kesho atarejea tena hapa dukani kwa ajili ya kupiga simu nitamwangalia tena na kama nitakuwa sijamwelewa vyema nitatoa taarifa polisi
haraka ili waje kumkamata na kwenda kumhoji zaidi.”
***
Ndani ya chumba kila mtu alikuwa hoi kupita maelezo, kila mmoja akionekana kumhitaji mwenzake kwa hali na mali.
Mara kadhaa Daniel alipojaribu kupeleka mkono wake kwa lengo la kushika chuchu za Lina ili azitumbukize mdomoni mwake, jambo hilo lilionekana kuwa
gumu kwani Lina alimsukuma pembeni akimtaka kusubiri kwanza.
“Lakini kuna tatizo gani mpenzi wangu mimi nakuhitaji sana.”
“Najua lakini mimi siko tayari bado kidogo.””Unataka nikufanyie nini ili unipe nafasi Lina?”
“Mh! Haya inatosha njoo basi.”
Daniel akasogea karibu zaidi na Lina alipotupa macho yake kumwangalia usoni aligundua jambo fulani, macho yake yalikuwa mekundu kupita maelezo na mwili
wake ulionekana kutetemeka.”
“Daniel,” aliita.
“Yes, Lina.”
“Nipe kidogo halafu tupumzike, hali yangu kwa jinsi ilivyo hainiruhusu kuendelea zaidi ya hapa naweza kufa kama si kuzimia.”
“Na wewe una haraka kama nini sijui!”
“Nakuambia ukweli usiponipa naweza kufa muda si mrefu, nipe kidogo,” alibembeleza Daniel akionyesha umakini wa hali ya juu.
Maneno hayo yakapenya moja kwa moja masikioni mwa Lina na kumfanya amwonee huruma Daniel kupita kawaida, kwa sauti ya upole akamnong’oneza Daniel
sikioni mwake na kumweleza kwamba sasa alikuwa amekubali kufanya kitu alichokitaka.
“Ahsante Lina, nataka uamini kitu kimoja tu.”
“Kipi hicho?” aliuliza Lina kwa sauti ya mahaba.
“Nakupenda sana mpaka sasa siamini kama umenikubali lakini nitaamini zaidi pale tu utakaporuhusu tukafanya tendo la ndoa.”
Lina alikuwa kimya kitandani bila kujibu chochote huku machozi yakimbubujika, taswira ya mumewe Phillip ilionekana mbele yake ikimhimiza juu ya kukubali
kufanya tendo hilo na Daniel.
Ni hali hiyo ndiyo ilimfanya Daniel aamini kwamba sasa Lina alikuwa tayari kwa kila kitu bila kujiuliza mara mbili akamsogeza Lina karibu yake kisha kumlaza
vizuri kitandani tayari kwa kazi moja tu kutimiza shughuli moja ya kumpa Lina raha ambayo kamwe hataisahau maishani mwake.
“Lala vizuri basi mpenzi wangu tuanze...” aliongea Daniel kwa sauti ya kukatikakatika.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SIKU ya pili asubuhi, Ditrov alitoka tena kuelekea kwenye ule mji mdogo kwa lengo moja tu la kupiga simu kwa mtu aliyekuwa amempa kazi. Alitaka
kufahamu amefikia wapi na kumkumbusha kwamba ilikuwa imebaki siku moja tu mbele ili kukamilisha mpango mzima. Alipanga kurudia kumsisitiza na
kumtaka asifanye mchezo na suala hilo vinginevyo angekiona cha moto.
Muda wote wakati akitembea, hakudiriki hata mara moja kuinua uso wake na kama alifanya hivyo, aliangalia sehemu ambayo haina watu na kuendelea na safari
yake. Hatimaye akafika kwenye ule mji mdogo, sehemu ileile aliyopigia simu kwa mara ya kwanza, akatoa namba kisha kuomba msaada wa kupigiwa simu.
Sekunde tatu tu baadaye, tayari alikuwa katika simu akiongea na mtu upande wa pili huku akionesha msisitizo. Kwa sababu aliongea kwa lugha ya Kirusi,
hakuwepo mtu eneo hilo aliyeweza kuelewa ni kitu gani alichokuwa anaongea. Wengi walimtazama kwa macho yaliyojaa viulizo na kuhisi kwamba alikuwa na
matatizo makubwa kwani macho yake yalikuwa mekundu muda wote wakati akiongea na simu.
Upande wa pili, Lina na Daniel wapo ndani ya chumba, kila mmoja akiwa hoi kupita maelezo. Daniel ndiyo alikuwa na wakati mgumu zaidi kwani alionekana
kumhitaji mwenzake kwa hali na mali. Mara kadhaa Daniel alipojaribu kupeleka mkono wake kwa lengo la kushika chuchu za Lina ili azitumbukize mdomoni
mwake, Lina alikuwa akimsukumia pembeni na kumtaka asubiri kwanza.
Ghafla, Daniel anashuhudia machozi yakitiririka mashavuni mwa Lina, jambo ambalo analiona kama nafasi pekeee ya kutimiza alichokitaka, akamlaza vyema
Lina kitandani tayari kwa kazi huku akijifanya kumbembeleza.
KWAKE fedha hazikuwa na maana kuliko maisha ya watoto wake, Mariya na Merina ambao walikuwa kwenye hatari kubwa. Akiwa na hofu nyingi baada ya
kumaliza kuweka kiasi cha fedha alichotakiwa kwenye begi, Victor Federov alilikamata sawasawa na kuanza kutembea kutoka nje ya chumba kuelekea sebuleni.
Alipofika alipitiliza mpaka nje na kuingia ndani ya gari kisha kuliwasha, akiwa tayari kwa safari ya kuelekea Msitu wa Beloomut ambako alitakiwa kupeleka
fedha hizo kama masharti ya kukabidhiwa watoto wake wakiwa hai.
“No way out, I have to do this for my daughters,” (Hakuna jinsi, ni lazima nifanye hivi kwa ajili ya wanangu) Aliongea Victor Fedorov akiwa ndani ya gari lake.
Lakini kabla hajaingia ndani yake alikumbuka kitu kimoja muhimu sana kwa wakati huo, bastola ambayo aliamini kabisa ingeweza kumsaidia kama tu
angekutana na hatari yoyote katika safari yake, akalitupa begi la fedha ndani ya gari na yeye kutoka mbio kuelekea ndani ambako haikumchukua hata dakika tatu
tayari akawa amesharejea na kuingia ndani ya gari tayari kwa safari ndefu.
Moyoni mwake alikuwa na machungu makubwa, muda mwingi machozi yalikuwa yakimbumbujika. Hakuona tena thamani ya tajiri wake.
“This is the worst day in my entire life” (Hii ni siku mbaya zaidi katika maisha yangu yote) alizidi kuwaza Fedorov.
“Piiii! Piiii! Piii!” Ilikuwa ni honi ya gari akipiga kuomba msaada wa kufunguliwa lango na mlinzi ili atoke. Kwa kasi ya ajabu akaliendesha gari mpaka langoni
na kabla hajatoka alisimama na kuongea jambo fulani na mlinzi wake kisha akapandisha kioo na kuondoka.
Njia nzima aliliendesha gari akiwa ni mwingi wa mawazo kwanza maisha ya watoto wake na pili uhai wake yeye mwenyewe hakufahamu kabisa mtu
aliyekwenda kukutana naye alikuwa vipi na ni kwanini alisisitiza fedha hizo zipelekwe katika msitu wa Beloomut ambao kwa hakika historia yake haikuwa
njema.
“Acha niende cha muhimu ni kupata watoto wangu kama ni hizi fedha nitapata tu nyingine…”Aliwaza akizidi kukanyaga mafuta na gari kusonga mbele.
Mbele yake yalikuwa zilikuwa zimebaki saa saba tu ambazo zingefanya kutimia kwa saa ishirini na nne ambazo alikuwa amepewa na mtekaji wa watoto wake
hivyo kuchelewa kwake kungesababisha maradha makubwa na hata kusababisha kupoteza maisha ya Merina na Mariya.
Akiwa katika mwendo wa kasi akatupa macho yake kwenye saa yake ya mkono na kugundua kwamba alitakiwa kufanya kila alichoweza kuhakikisha saa hizo
zinamkuta akiwa tayari ndani ya msitu wa Beloomut ili kunusuru maisha ya watoto wake. Akaongeza mwendo wa kasi zaidi na kufanya kila aliyekutana naye
barabarani kushangaa na pengine kudhani kwamba alikuwa ni mwizi wa gari aliyekuwa ameiba sehemu fulani.
Kwa Victor Federov mwendo ulionekana kuwa mrefu kila alipotupa macho yake kwenye saa yake aligundua muda ulikuwa ukizidi kusonga kama vile kulikuwa
na mtu akihimiza kikimbiza saa mawazo mengi yakazidi kuufunika moyo wake akajikuta ameanza kukata tamaa juu ya kuwapata watoto wake wakiwa hai.
“Oh my God, do something for my daughters, they are the only kids I have” (Oh..Mungu wangu, tenda jambo flani kwa wanangu, ni watoto pekee nilionao)
alijikuta akitamka maneno hayo kwa nguvu japo hajawahi kukanyaga kanisani wala msikitini katika historia ya maisha yake.
“Kama sitawakuta wakiwa hai hata mimi sitaona sababu ya kuendelea kuishi nitajipiga risasi ili nife.” Aliwaza machozi yakzidui kuuchakaza uso wake.
***
Hasira kali zilikuwa zimempanda kupita maelezo akisahau kabisa kwamba chanzo cha mambo yote hayo ilikuwa ni yeye kumruhusu mkewe kwenda kufanya
tendo la ndoa na mwanaume mwingine ili tu ashike ujauzito ambao angeulea na kuutunza mpaka mtoto atakapozaliwa.
Phillip alitoka ndani ya gari lake na kufunga mlango nyuma yake bila kujiuliza mara mbili kwamba kitendo alichotaka kwenda kufanya ndani ya hoteli hiyo
kilikuwa cha aibu kuwa alitembea moja kwa moja na kuingia mapokezi.
“Habari yako dada?” Aliuliza kwa sauti ya juu.
“Salama tu nikusaidie?”
“Ah! Mh! Ah!”
“Kaka nakusikiliza nimekuuliza nikusaidie?”
“Ndio.”
“Sijui naweza kufahamu jambo fulani hapa?”
“Unaweza na hiyo ndiyo kazi yangu sema tu.”
“Nauliza…nauliza…”Aliongea akirudiarudia.
“Mh!” Msichana wa mapokezi aliguna yeye pia hakumwelewa Phillip alihitaji nini na kibaya zaidi tayari usiku ulikuwa umeshaingia.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Taratibu bila kusema kitu chochote huku macho yake yote yakimwangalia kwa makini alinyanyua simu na kupiga namba kadhaa hapo kisha kusikiliza.
“Hallow…ndio…tafadhali naomba ulinzi hapa mapokezi… kuna mtu ameingia hapa hata simuelewi…sijui anataka nini…nimeongea naye simuelewi kabisa…
inavyoonena kama vile amechanganyikiwa kidogo…tafadhali njoo mara moja… nina hofu kubwa sana…” Aliongea kwa sauti ya chini lakini bado Phillip
aliendelea kusimama eneo hilo bila kusema kitu chochote alionekana kama mtu aliyepigwa na butwaa.
Hazikupita hata sekunde tatu tayari watu wawili walioonekana kuwa walinzi waliingia mikononi mwao wakiwa wameshika bunduki. Kwa haraka wakatembea
mpaka sehemu ambako alisimama Phillip na kumsabahi.
“Sijui unahitaji nini ndugu yetu hapa?”
“Mh!”
“Tafadhali ongea vinginevyo tutavunja miguu yako sasa hivi.”
“Kwa kosa gani sasa?”
“Hii si sehemu ya kusimama tu kibaya zaidi ni usiku sasa, unahitaji nini tukusaidie?” Mlinzi mmoja aliongea huku akifoka tayari alishaiweka vyema bunduki
kulenga miguu ya Phillip.
“Tafadhali msinidhuru niko hapa kuhitaji msaada mmoja tu.”
“Ndio tunaotaka kukusaidia.”
“Nauliza….nauliza dada mmoja anaitwa…Lina.”
“Lina?”
“Ndio.”
“Hebu niangalie kwenye kitabu cha wageni wangu leo.” Haraka dada wa mapokezi akavuta daftari kubwa na kuanza kufunua ukurasa mmoja baada ya mwingine
akiangalia jina hilo.”
“Hatuna jina la mtu huyo leo labda kama ana jina jingine.”
“Hapana anaitwa Lina ndilo jina lake.”
Phillip akabaki mdomo wazi hakuwa na namna nyingine ya kueleza kwani jambo lililokuwa likifanyika ndani ya hoteli hiyo chumbani lilikuwa ni siri kubwa bila
kutarajia machozi yakaanza kumbubujika.
“Mungu baba, niondolee kikombe hiki kinazidi kuwa cha moto zaidi” aliwaza Phillip akiwa amejiinamia.
Huku akionekana mwenye wasiwasi mwingi machoni mwake, aliendesha gari mara kadhaa akigeuza shingo yake huku na kule kuangalia usalama kwani
alifahamu wazi kwamba sifa za msitu huo nchini Urusi zilitisha kupita maelezo, njia nzima aliendesha gari bila kukutana na mtu yeyote na kwa ilivyoonekana
hapakuwepo kiumbe hai kilichoishi ndani ya msitu huo.
Moyoni mwake hakuwa na uhakika kama angeweza kutoka ndani ya msitu huo akiwa salama lakini zaidi ya yote ni watoto wake Mariya na Merina hao ndiyo
walikuwa kila kitu na alitaka afanye kila alichoweza kuhakikisha anawapata wakiwa hai.
“Ikitokea nikifa halitakuwa tatizo sana lakini watoto wangu wapone, najua wataweza kuendesha maisha kwa utajiri nilionao, ninashukuru kwamba nimeandika
kila kitu kwa wakili wangu…”aliongea.
Victor Fedorov alifanikiwa kuingia ndani ya msitu na kuegesha gari lake sehemu moja iliyoonekana kuwa wazi, hapo akajiweka sawa akiangalia usalama wake,
taratibu bila kujiuliza mara mbili akalikamata vyema begi lililokuwa na fedha ndani yake kisha akaichomeka bastola yake kiunoni na kushuka garini.
Akatupa macho yake huku na kule bila kuona kitu chochote, akiwa katika hali hiyo milio ya risasi ikasikika.
“Puuu! Puuu! Puuu!”
“Mungu wangu… hiyo ni milio ya risasi…isijekuwa…” aliongea akijaribu kuzungusha macho yake huku na kule na katika kuangalia vyema macho yake
yakakutana na kitu cha ajabu mbele yake, mtu aliyevalia nguo nyeusi na uso wake ukiwa umefunikwa na kuacha sehemu ya macho tu.
Mtu huyo alisimama pembeni kidogo mahali Victor Fedorov alipokuwa ameegesha gari.
“Haaa! Haaa! Haaa” mtu huyo alicheka kwa sauti ya kebehi.
Akitetemeka, akatembea akisogea kuelekea mahali aliposimama mwanaume huyo lakini kabla hajamfikia karibu sauti nyingine ikasikika.
“Victor Fedorov?” mwanaume huyo aliuliza.
“Ndiyo.”
“Vyema umefika muda muafaka kabisa.”
“Watoto wangu wako wapi?”
“Usiwe na haraka watoto wapo lakini nataka kufahamu jambo moja; je umefika hapa na nani?”
“Peke yangu kabisa hakuna mtu…”
“Una uhakika?”
“Asilimia mia moja.”
“Kumbuka kama unaye mtu mwingine kwenye gari lako jambo hilo litamaanisha hatari kubwa pengine kupoteza watoto wote.”
“Ninachokizungumza ni ukweli mtupu, tafadhali chukua fedha hizi hapa kisha unipatie watoto wangu,” aliongea Victor Fedorov machozi yakimbubujika.
Pamoja na ukatili wake wote hapo alikuwa amefunga breki, hakuwa na namna nyingine yoyote ya kufanya zaidi ya kukubali kila alichokuwa ameelezwa ili mradi
tu awapate watoto wake Mariya na Merina.
“Daddyyyyy.” (baba.) Sauti hiyo ilipenya moja kwa moja masikioni mwa Victor Fedorov.
Haraka akageuza shingo yake huku na kule kuangalia ni wapi sauti hiyo ilitokea lakini hakufanikiwa kuona kitu chochote, alirudisha macho yake kumwangalia
mwanaume aliyekuwa mbele yake.
“Najua wazi huwezi kukosa silaha ni vyema ukaiweka chini haraka.”
Bila kusema kitu chochote akaichomoa bastola yake na kuitupa chini huku akiendelea kumsihi mwanaume huyo kumweleza ni wapi walipokuwa watoto wake.
“Weka pia begi hilo hapo chini na urudi nyuma mita tano!” aliamuru mwanaume huyo.
Taratibu, Victor Fedorov alitii kila alichoelezwa, akaliweka begi chini na kuanza kurudi kinyumenyume, macho yake yote yakimwangalia mwanaume huyo
ambaye hakuonekana sura kwani kichwa chake kilifunikwa na kitu kama soksi iliyoacha nafasi ndogo sehemu ya macho tu.
Wasiwasi mwingi ukamfunika na kumfanya ashindwe kuelewa ni kitu gani kingetokea mbele yake baada ya muda mfupi kwani kama ni silaha tayari
alishaikabidhi kwa adui aliyekuwa mbele yake.
“Mh!”aliguna huku akiendelea kurudi nyuma akahisi vitu vyepesi vikipenya kutoka ndani ya suruali yake kuelekea chini.
***
Baada ya mhudumu wa mapokezi kusoma kitabu cha wageni kwa muda akitafuta jina la Lina bila mafanikio, aliinua macho yake na kumwangalia Phillip ambaye
naye alionekana kulengwalengwa na machozi akimweleza wazi kwamba jina hilo halikuwepo ndani ya kitabu chake labda kama mgeni wake huyo alikuwa na jina
jingine alilolitumia.
“Hapana jina lake ni hilo hilo la Lina.”
“Kaka halipo tafadhali niamini na uondoke,” aliongea dada wa mapokezi akitoa ishara kwa walinzi waliokuwepo eneo hilo.
Akiwa katika hali ya kupigwa na butwaa upande mmoja wa akili yake ulimwambia aondoke na kurejea nyumbani huko angeendelea kumsubiri mkewe mpaka
atakaporejea lakini upande mwingine wa akili yake ulimwambia atoke nje ya hoteli hiyo na kuingia ndani ya gari lake akae hapo kusubiri mpaka mwisho.
“Mzee nadhani umepata maelezo yanayotosha kabisa kukufanya uelewe, tafadhali tunaomba nafasi hapa.”
Bila kujibu chochote Phillip akainua macho yake na kuwaangalia watu hao, moyo wake ulijaa siri nzito kupindukia lakini hakuwa na uwezo wa kumshirikisha
mtu mwingine kwani jambo lililokuwa likifanyika ndani ya hoteli hiyo usiku huo lilikuwa ni siri kubwa.
Machozi yakambubujika, taratibu akaanza kutembea kuelekea nje, moyoni mwake akijilaumu kwa kumtoa mkewe sadaka kwa mwanaume mwingine, akilini
mwake akiamini kabisa kwamba Lina alikuwa ameamua kumkimbia.
“Najutia maamuzi yangu haya isingekuwa mimi yote haya yasingetokea, Lina atakuwa ameamua kunitenda kama kisasi,” aliongea Phillip akiukaribia mlango ili
atoke nje
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Haraka bila kujiuliza mara mbili akazikamata kamba na kuanza kufungua moja baada ya nyingine kisha kumnyanyua mtoto wake na kuanza kukimbia naye
kuelekea garini, machozi ya furaha yalikuwa yakimbubujika.
“Hata ule mzigo mwingine atakuwa ni Mariya anahitaji pia msaada wangu, namshukuru Mungu amenirejeshea watoto wangu pamoja na kwamba afya ya Merina
ni mbaya lakini nashukuru yuko hai.”
Haraka akamlaza Merina garini kisha kutoka mbio kuelekea sehemu ambayo mzigo mwingine ulisukumwa kutoka garini akilini mwake aliamini kabisa kwamba
huyo angekuwa ni mtoto wake Mariya.
“Mbona haonyeshi dalili yoyote kwamba ni mzima?” aliwaza akipiga magoti chini huku akiita jina la Mariya, ni kweli alikuwa yeye na alipotupa macho yake na
kumwangalia vyema aligundua hakuwa na fahamu yoyote alionekana kupoteza fahamu kama siyo kukutwa na umauti.
“Mariya! Mariya!” aliita akigusa sehemu ya kifua kuangalia mapigo yake ya moyo.
“Hapana! Hapana Mariya usife mwanangu bado nakuhitaji, amka uungane na mwenzako Merina yule palee,” aliongea mfululizo akizidi kumtingisha Mariya
aliyekuwa amelala chini kimya bila kufungua macho wala kujitingisha.
Upande wa pili wa hadithi hii tunamwona Phillip akiwa ndani ya hoteli lakini ameshindwa kujieleza na matokeo yake anatolewa nje ya hoteli akitakiwa aondoke
eneo hilo haraka kabla hajapatwa na jambo baya, taratibu anatoka huku machozi yakimbubujika na kichwani mwake anapata picha kwamba huenda Lina alikuwa
ameamua kumsaliti au kulipa kisasi kwani kitendo cha kufanya ngono na mwanaume mwingine Lina hakukubaliana nacho pengine hicho ndicho kilisababisha
kumwacha kwenye mataa akiwa nje ya hoteli.
“Hapana! Hapana Mariya usife mwanangu bado nakuhitaji amka uungane na mwenzako Merina yule palee,” aliongea mfululizo akizidi kumtingisha Mariya
aliyekuwa amelala chini kimya bila kufungua macho wala kujitingisha.
Hali ilionekana kuwa mbaya, Victor Fedorov alizidi kumtingisha mwanaye ili aamke lakini haikuwa hivyo, Mariya alikuwa amelala ardhini kimya kabisa,
akatupa macho yake huku na kule kama vile mtu aliyekuwa akitafuta kitu fulani vile, giza nalo lilianza kutanda katika msitu huo.
“Ni lazima niondoke hapa haraka sana kabla giza halijaingia zaidi,” aliwaza akimnyanyua mtoto wake Mariya na kuanza kukimbia kuelekea kwenye gari lake.
Haraka akamketisha na alipohakikisha kila kitu kilikuwa sawa akaingia ndani ya gari na kukaa kwenye usukani huku akiwa na hofu, akawasha na kukanyaga
mafuta, lengo likiwa kuondoka eneo hilo.
Akiwa ndani ya gari baada ya kutoka nje ya msitu huo alisimamisha gari na kuanza kumwita tena Mariya ambaye bado alikuwa ametulia kimya.
“Mariya! Mariya! Nini kimekupata mwanangu?” aliuliza.
“Daddy!” Merina aliita huku akitetemeka, yeye pia afya yake haikuwa nzuri, walidhoofika sana, miili yao ilikuwa michafu kupindukia hata nywele zao
zilionekana kujisokota.
“Yes, tafadhali nieleze ni kitu gani kimempata nduguyo?” aliuliza hamu yake kubwa ikiwa ni kufahamu tatizo lililotokea huko nyuma kabla hawajafika eneo
hilo.
Merina hakujibu kitu chochote, zaidi aliishia kuangua kilio kilichozidi kumtia wasiwasi baba yao akashindwa kuendelea na safari na kuliegesha gari pembeni
kwanza ili azungumze na Merina ambaye alionyesha nafuu kidogo kuliko mwenzake Mariya.
“Baba tafadhali endesha gari ukichelewa kidogo tu hata mimi nitakuwa kama Mari…”aliongea Merina na kabla hajamalizia sentensi yake naye pia akatulia kimya
kitini.
Victor Fedorov akazidi kuchanganyikiwa zaidi akashindwa afanye kitu gani kwani kila kitu kilichokuwa kikimtokea katika maisha yake kwa wakati huo
kilionekana kuwa kama ndoto, alishatoa fedha nyingi ili kuokoa maisha ya watoto wake lakini ni hao sasa waliokuwa katika hali ya kufa kwani wote
walionekana kupoteza fahamu, moyo ukamuuma sana akajutia uamuzi wake wa kuwateka watoto hao kutoka nchini Tanzania na kuwaleta nchini Urusi na sasa
walikuwa wakifa bila hatia yoyote.
“Ubinafsi umeniponza pengine Mungu ananipa pigo hili ili nitubu kwa dhambi niliyoifanya ya kuwateka watoto hawa, lakini si ni uzao wangu huu? Hapana,
nasema hapana siko tayari nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu wote kuhakikisha maisha yao yanarejea tena naamini watakuwa hawajafa bali wamezimia tu…”
aliwaza huku akizidi kukanyaga mafuta.
Akili yake yote ilishahama na kwenda moja kwa moja kuokoa maisha ya watoto wake, alitaka afike nyumbani haraka na kutafuta daktari ambaye angeweza
kufanya kila atakachoweza kuokoa maisha ya watoto hao pacha, hata kama safari hii ingegharimu utajiri wake wote aliokuwa nao, Victor Fedorov alikuwa
tayari.
Kwa muda wa saa tatu bado alikuwa barabarani, mara kadhaa akisimama na kuwaangalia watoto wake ili kujua hali zao, bado zilikuwa zilezile
hawakuzungumza chochote zaidi ya kutulia kimya vitini.
Saa sita baadaye huku akimwagika jasho mwili mzima tayari alishawasili nje ya lango la nyumba yake, akapiga honi na mara moja lango likaonekana
likifunguliwa na gari kuzama ndani, bila kusema kitu chochote na mlinzi wake akaliendesha gari mpaka sehemu ya maegesho, akasimama na kushuka haraka
garini kisha akafungua milango ya nyuma.
“Mlinzi!”aliita kwa sauti ya juu na mara moja akakimbia na kusimama mbele ya gari lake.
“Tafadhali nisaidie kubeba mtoto mmoja haraka kwenda ndani,” aliamuru tayari mikononi mwake alishambeba Mariya.
Mlinzi hakuchelewa, alimbeba Merina wakaanza kukimbia kuelekea ndani.
***
Huku machozi yakimbubujika, moyoni mwake akiumia, Phillip alianza kutembea kuuelekea mlango wa mapokezi ili atoke nje na kuondoka eneo hilo kama
alivyoamriwa.
Walinzi wawili wenye silaha walikuwepo nyuma yake kumsindikiza, wao pia walionyesha kuchukizwa sana na kitendo alichokuwa amekifanya Phillip eneo lao
la kazi hivyo hawakuwa na utani walitaka kulinda vyema kibarua chao.
“Tembea haraka bwana tena tunakusihi uondoke eneo hili haraka sana kabla hatujakuchakaza…umesikia bwana mdogo…tembea…” aliongea askari mmoja
akimsukuma kwenda mbele. Machozi yakambubujika kwa mara nyingine tena hakuwa tayari kuondoka hotelini hapo na kumwacha mkewe Lina ambaye aliamini
kabisa kwamba bado alikuwepo ndani.
Wakati mlinzi wa mwisho anatoka na kufunga mlango nyuma yake sauti kali ikasikika ndani ya hoteli hiyo mwanamke akilia kuomba msaada na kishindo cha
mtu akikimbia kuelekea eneo la mapokezi kikasikika.
“Uwiii! Nisaidieni! Tafadhali niokoeni jamani! Anani…”
“Mh!” wote wakaguna.
“Sauti kama ya Lina! Ni sauti ya mk…” aliongea Phillip mfululizo na kushindwa kumalizia sentensi yake, wote wakaonekana wakikimbia mbio kurejea ndani ya
hoteli.
Hapana! Hapana Mariya usife mwanangu bado nakuhitaji amka uungane na mwenzako Merina yule palee,” aliongea mfululizo akizidi kumtingisha Mariya
aliyekuwa amelala chini kimya bila kufungua macho wala kujitingisha.
Hali ilionekana kuwa mbaya, Victor Fedorov alizidi kumtingisha mwanaye ili aamke lakini haikuwa hivyo, Mariya alikuwa amelala ardhini kimya kabisa,
akatupa macho yake huku na kule kama vile mtu aliyekuwa akitafuta kitu fulani vile, giza nalo lilianza kutanda katika msitu huo.
“Ni lazima niondoke hapa haraka sana kabla giza halijaingia zaidi,” aliwaza akimnyanyua mtoto wake Mariya na kuanza kukimbia kuelekea kwenye gari lake.
Haraka akamketisha na alipohakikisha kila kitu kilikuwa sawa akaingia ndani ya gari na kukaa kwenye usukani huku akiwa na hofu, akawasha na kukanyaga
mafuta, lengo likiwa kuondoka eneo hilo.
Akiwa ndani ya gari baada ya kutoka nje ya msitu huo alisimamisha gari na kuanza kumwita tena Mariya ambaye bado alikuwa ametulia kimya.
“Mariya! Mariya! Nini kimekupata mwanangu?” aliuliza.
“Daddy!” Merina aliita huku akitetemeka, yeye pia afya yake haikuwa nzuri, walidhoofika sana, miili yao ilikuwa michafu kupindukia hata nywele zao
zilionekana kujisokota.
“Yes, tafadhali nieleze ni kitu gani kimempata nduguyo?” aliuliza hamu yake kubwa ikiwa ni kufahamu tatizo lililotokea huko nyuma kabla hawajafika eneo
hilo.
Merina hakujibu kitu chochote, zaidi aliishia kuangua kilio kilichozidi kumtia wasiwasi baba yao akashindwa kuendelea na safari na kuliegesha gari pembeni
kwanza ili azungumze na Merina ambaye alionyesha nafuu kidogo kuliko mwenzake Mariya.
“Baba tafadhali endesha gari ukichelewa kidogo tu hata mimi nitakuwa kama Mari…”aliongea Merina na kabla hajamalizia sentensi yake naye pia akatulia kimya
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kitini.
Victor Fedorov akazidi kuchanganyikiwa zaidi akashindwa afanye kitu gani kwani kila kitu kilichokuwa kikimtokea katika maisha yake kwa wakati huo
kilionekana kuwa kama ndoto, alishatoa fedha nyingi ili kuokoa maisha ya watoto wake lakini ni hao sasa waliokuwa katika hali ya kufa kwani wote
walionekana kupoteza fahamu, moyo ukamuuma sana akajutia uamuzi wake wa kuwateka watoto hao kutoka nchini Tanzania na kuwaleta nchini Urusi na sasa
walikuwa wakifa bila hatia yoyote.
“Ubinafsi umeniponza pengine Mungu ananipa pigo hili ili nitubu kwa dhambi niliyoifanya ya kuwateka watoto hawa, lakini si ni uzao wangu huu? Hapana,
nasema hapana siko tayari nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu wote kuhakikisha maisha yao yanarejea tena naamini watakuwa hawajafa bali wamezimia tu…”
aliwaza huku akizidi kukanyaga mafuta.
Akili yake yote ilishahama na kwenda moja kwa moja kuokoa maisha ya watoto wake, alitaka afike nyumbani haraka na kutafuta daktari ambaye angeweza
kufanya kila atakachoweza kuokoa maisha ya watoto hao pacha, hata kama safari hii ingegharimu utajiri wake wote aliokuwa nao, Victor Fedorov alikuwa
tayari.
Kwa muda wa saa tatu bado alikuwa barabarani, mara kadhaa akisimama na kuwaangalia watoto wake ili kujua hali zao, bado zilikuwa zilezile
hawakuzungumza chochote zaidi ya kutulia kimya vitini.
Saa sita baadaye huku akimwagika jasho mwili mzima tayari alishawasili nje ya lango la nyumba yake, akapiga honi na mara moja lango likaonekana
likifunguliwa na gari kuzama ndani, bila kusema kitu chochote na mlinzi wake akaliendesha gari mpaka sehemu ya maegesho, akasimama na kushuka haraka
garini kisha akafungua milango ya nyuma.
“Mlinzi!”aliita kwa sauti ya juu na mara moja akakimbia na kusimama mbele ya gari lake.
“Tafadhali nisaidie kubeba mtoto mmoja haraka kwenda ndani,” aliamuru tayari mikononi mwake alishambeba Mariya.
Mlinzi hakuchelewa, alimbeba Merina wakaanza kukimbia kuelekea ndani.
***
Huku machozi yakimbubujika, moyoni mwake akiumia, Phillip alianza kutembea kuuelekea mlango wa mapokezi ili atoke nje na kuondoka eneo hilo kama
alivyoamriwa.
Walinzi wawili wenye silaha walikuwepo nyuma yake kumsindikiza, wao pia walionyesha kuchukizwa sana na kitendo alichokuwa amekifanya Phillip eneo lao
la kazi hivyo hawakuwa na utani walitaka kulinda vyema kibarua chao.
“Tembea haraka bwana tena tunakusihi uondoke eneo hili haraka sana kabla hatujakuchakaza…umesikia bwana mdogo…tembea…” aliongea askari mmoja
akimsukuma kwenda mbele. Machozi yakambubujika kwa mara nyingine tena hakuwa tayari kuondoka hotelini hapo na kumwacha mkewe Lina ambaye aliamini
kabisa kwamba bado alikuwepo ndani.
Wakati mlinzi wa mwisho anatoka na kufunga mlango nyuma yake sauti kali ikasikika ndani ya hoteli hiyo mwanamke akilia kuomba msaada na kishindo cha
mtu akikimbia kuelekea eneo la mapokezi kikasikika.
“Uwiii! Nisaidieni! Tafadhali niokoeni jamani! Anani…”
“Mh!” wote wakaguna.
“Sauti kama ya Lina! Ni sauti ya mk…” aliongea Phillip mfululizo na kushindwa kumalizia sentensi yake, wote wakaonekana wakikimbia mbio kurejea ndani ya
hoteli.
Mariya! Merina! ” Victor Fedorov aliita akizidi kuwatingisha watoto wake lakini bado hakuwepo hata mmoja aliyeweza kujibu neno lolote.
“Mlinzi hebu niletee maji haraka,” aliamuru, na bila kujibu kitu chochote, mlinzi alitoka mbio na sekunde tatu tu baadaye alirejea na maji kwenye bakuli kubwa.
Haraka akalipokea na kuanza kuwamwagia akiamini kwamba kufanya hivyo kungeweza kuwarejesha katika hali zao za kawaida lakini hilo halikutokea, akiwa
hapo machozi yakambubujika, akaiona kabisa picha ya kubaki peke yake duniani na utajiri aliokuwa nao.
Victor Fedorov akaikataa picha hiyo na kuendelea kuwatingisha tena na tena akiwaita watoto wake kwa majina.
Watoto wake walikuwa wamebadilika kwa kiasi kikubwa, afya zao zilikuwa mbaya kupita maelezo, walikuwa wamebadilika kwa kila kitu kuanzia mavazi
mpaka nywele, hali hiyo ndiyo iliyozidi kumtia wasiwasi Fedorov. Akiwa hapo ghafla akili yake ikamweleza kwamba kama alihitaji watoto wake wapone na
kurejea katika hali zao za kawaida ni lazima atamfute daktari ambaye angewasaidia.
“Jambo moja linaweza kufanyika kwa sasa?”
“Jambo gani mkuu.”
”Daktari, ni lazima nipate daktari ambaye atakuja hapa kuwaangalia nitamlipa kiasi chochote kile cha fedha ilimradi tu aokoe maisha ya watoto wangu,” aliongea
kwa majonzi, na taratibu akanyanyuka na kuisogelea simu lakini kabla hajaifikia alimsikia mlinzi akiguna.
Bila kujiuliza mara mbili akatoka mbio kuelekea eneo hilo, alichokishuhudia hapo kilimtoa machozi; Mariya na Merina walilala chini huku mapovu mengi
yakitoka midomoni mwao pia walionekana kutupa mikono na miguu kama vile walikuwa wakikata roho. Victor Federov akalia kama mtoto mdogo.
“Bosi hebu njoo uone mbona wanatoka mapovu!”
“Mapovu?” aliuliza akikimbia kurejea eneo hilo. Ni kweli Mariya na Merina walikuwa wakitiririkwa na mapovu kutoka midomoni mwao.
“Mungu wangu ni kitu gani hiki? watoto wangu wamepewa…”
“Wamepewa nini bosi wangu?”
“Wamepewa sumu hawa haya mapovu ni ya nini? Watoto wangu wanakufa wakati nikiwa tayari nimeshapoteza fedha nyingi, tafadhali msiniache, naomba
msiniache nitabaki na nani katika dunia hii? Fedha na mali si kitu kama sina ndugu wala mtoto yeyote? Mungu nisaidie,” aliongea mfululizo.
Akiwa hapo, Victor Fedorov akionyesha kukata tamaa kabisa, mawazo yake yote yakampeleka kwa jambazi aliyemwona ndani ya msitu wa Beloomut
akamshuhudia akikimbia na begi lililojaa fedha nyingi ndani yake na kutokomea.
“Kama ni fedha nilimpatia, kwa nini ameua watoto wangu? Kwa nini amewatesa viumbe wasio na hatia? Utajiri wangu umekwenda, na watoto pia wananiacha,
nimekosea nini kwa Mungu? Pengine jambo hili linatokea kwangu kama adhabu kwa makosa niliyoyafanya huko nyuma? Hapana! Nashindwa kuelewa…”
aliongea mfululizo akiwa pembeni mwa watoto wake ambao mpaka wakati huo walishatulia kimya, mapovu hayakutoka tena midomoni mwao na miguu na
mikono yao ilikuwa imetulia kimya.
“Yametimia!” hivyo ndivyo alivyosema Victor Fedorov na kuangua kilio kikali ndani ya nyumba, mlinzi akasogea karibu yake na kumbembeleza.
“Haiko haja ya kuishi! Bora nife niuungane na familia yangu? Watoto wangu wa kwanza walikufa kifo kibaya wakati wakicheza mchezo wa kuteleza katika
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
barafu na hawa nao …”
Kwikwi ya kulia ikamkaba ni kweli taswira za watoto wake wawili pamoja na mkewe waliokuwa wamekufa miaka mingi kabla, ilimjia kichwani mwake
akajiona ni mtu mwenye mkosi duniani hata thamani ya utajiri aliokuwa nao hakuiona, akatamani kuungana na familia yake.
“Nitakufa! Si muda mrefu kuanzia sasa nitaungana na familia yangu…Mungu wangu…kwa nini yote haya…kwa nini mimi? Nimekosa nini?” alizidi kujilaumu.
Akionyesha kukata tamaa kabisa, akasogeza mkono wake wa kulia na kuupeleka moja kwa moja upande wa shingo ya Mariya ili kupima mapigo yake ya moyo
ambapo yalionekana kutulia akageuka tena upande wa pili na kugusa mapigo ya Merina nayo yalionekana kuwa kimya kabisa.
Bila kusema tena neno lolote akatembea na kwenda kuketi juu ya kiti huku jasho jingi likimtoka na mwili wake ukitetemeka.
“Bosi mimi naona tuwapeleke hospitali huko tutapata mtaalamu ambaye atasema neno.”
“Lipi zaidi?”
“Mimi nashauri tufanye hivyo pengine wamezimia tu.”
“Nina hakika wamekufa, watoto wangu, wameniacha lakini naamini kabisa nyuma ya mchezo huu yupo mtu fulani sijui ni nani ila yupo, mbona nimetimiza
masharti yote? Nimetoa fedha nyingi sana kuwakomboa lakini amenilipa ubaya?” aliongea muda wote huo akiwa ameketi akionyesha kukata tamaa juu ya
maisha yake na mbele yake alifikiria kitu kimoja tu; kifo basi.
***
Baada tu ya kutoka ndani ya lango kuu la hoteli ya Lamada, Lina akiwa amejifunika shuka alikimbia na kuvuka upande wa pili wa barabara, watu wachache
waliokuwepo eneo hilo wakimshangaa, lakini hakujali alidhamiria kuondoka hapo na kutokomea, huku akilia akasogelea moja ya teksi.
“Wewe ni mtu au mzimu?” aliuliza dereva teksi aliyekuwa ndani ya gari, haraka akaufungua mlango na kutoka nje tayari kukimbia kwani mara kadhaa historia
katika eneo hilo ilionyesha kwamba mizimu ilikuja hapo kutoka makaburi ya jirani hivyo kutokea kwa mtu huyo tena akiwa katika shuka nyeupe
kulimwogopesha.
“Kaka usikimbie tafadhali naomba msaada wako mimi ni mwanadamu wa kawaida.”
“Mh! Hapana usinidanganye tena ona unaongea sauti ya mwanamke, kwa jina la Yesu toka mbele ya macho yangu!”
“Mimi si mzi…” aliongea Lina lakini kijana huyo hakuwa tayari kumsikiliza bado aliendelea kurudi kinyumenyume akijiandaa kukimbia ili kuondoka eneo hilo.
“Ona! Mimi ni mwanadamu!” aliongea akijaribu kufunua shuka alilojifunika.
“Mungu wangu! Nakufa jamani, jini hili tena yuko…” alipaza sauti na kufanya teksi nyingine zote zilizokuwa jirani madereva wake wawashe magari yao na
kuondoka eneo hilo kwa kasi.
Kwa uwezo wake wote alijaribu kujitetea kuwafanya watu waliokuwepo eneo hilo wamwone kwamba alikuwa ni mwanamke wa kawaida lakini ilionekana
kushindikana, teksi zote zikaondoka eneo hilo na kubaki moja tu ambayo dereva wake aliondoka na kuacha gari peke yake eneo hilo.
“Nitafanya nini sasa?” alijiuliza huku akilia, alitaka kufanya kila kilichowezekana kuondoka eneo hilo kurejea nyumbani kwake, ndani ya moyo wake kulijaa
hasira kali juu ya Phillip, hakika hakumpenda tena na aliapa kumchukia maisha yake yote yaliyobaki.
“Phillip amenidhalilisha kupita maelezo, sipo tayari tena kuendelea kuwa naye! Yaani hivi? Mimi kabisa? Mh! Siyo Lina nadhani ni mzimu wake?” alijiuliza
akizidi kusonga mbele, kichwani mwake hakuwa na picha ni wapi alikuwa akielekea lakini alitaka tu kuondoka eneo hilo.
“Naamini nitapata tu njia ya kuondoka hapa kabla hakujapambazuka,” aliwaza.
***
“Ngrii! Ngrii!Ngriii!” Ulikuwa ni mlio wa simu, mlinzi wa Victor Fedorov baada ya kuona kwamba bosi wake alikuwa amekata tamaa aliamua kutumia uwezo
aliokuwa nao, akasogea karibu na simu na kubonyeza namba kadhaa kitengo cha hatari akiomba gari la wagonjwa.
“Naweza kupata gari la wagonjwa haraka sana?”
Upande wa pili ulijibu.
“Ni nyumbani kwa Victor Fedorov nadhani ni mtu anayefahamika sana hapa kwetu, tafadhali fanyeni haraka kuna wagonjwa hapa…” aliongea kwa msisitizo.
“Hakuna haja tayari wamesha…” aliongea Victor Fedorov huku akilia.
“Hapana bosi sisi si madaktari ngoja tuwapeleke hospitali pengine huko tunaweza kupata ufumbuzi wa tatizo.”
“Kweli?”
“Ni kweli kabisa.”
“Mariya! Merina kweli mmeondoka na kuniacha wanangu? Maisha bila ninyi si kitu, nilijaribu kwa nguvu na uwezo wangu wote kuwapata lakini sasa
mmeondoka wana…”
Wakiwa hapo haikuchukua hata muda wa dakika tano tayari king’ora kikasikika nje ya lango la kuingilia ndani ya nyumba ya Fedorov, mlinzi akakimbia haraka
kwenda kufungua geti, moja kwa moja gari likazama ndani na watu wawili wakiwa wamevalia nguo za rangi ya bluu wakashuka.
“Yuko wapi huyo mgonjwa?”
“Siyo mgonjwa ni wagonjwa wako wawili?”
“Wawili?”
“Ndiyo.”
“Wako wapi?”
“Huku! Twendeni huku nikawaonyeshe,” mlinzi aliongea akitangulia mbele huku akikimbia.
Wote watatu wakazama ndani ambako mlinzi aliwaonyesha wagonjwa na kumtambulisha Victor Fedorov kwamba ndiye baba wa watoto hao na bila kusema kitu
watu hao wakainama na kuanza kuwachunguza watoto hao wakishika sehemu mbalimbali za miili yao kuwaangalia na mwisho kabisa wakachukua kipimo
maalum cha kusikiliza mapigo yao ya moyo.
Muda wote huo wakihangaika, Victor Fedorov alikuwa pembeni yao naye pia akionyesha wasiwasi mwingi.
“Wako hai?” aliuliza.
“Mh! Mh!” waliguna kwa pamoja huku wakinyanyua macho yao kumwangalia Fedorov, naye akayasoma vyema na kuelewa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.
“Tafadhali nielezeni ukweli msinifiche jambo kuna kitu hapa.”
“Mzee! Matumaini haya…” hawakumalizia sentensi yao wakamshuhudia Victor Fedorov akishuka chini na moja kwa moja akawainamia watoto wake na kuanza
kuwabusu mfululizo huku akilia.
Lina aliendelea kutembea barabarani huku akilia akili yake haikuonekana kufanya kazi kwani kila kitu alichokifikiria kuwa msaada kwake kilionekana
kukwamwa kabisa.
“Ni lazima niondoke hapa kabla hakujapambazuka.” Aliongea akizidi kusonga mbele.
Huku akijilaumu moyoni mwake kwa mambo yote yaliyomtokea, aliamini bila kukutana na Phillip na kumpenda kisha kufunga ndoa naye hayo yote
yasingempata, akazitupa lawama zote kwa mwanaume huyo na kumchukia kabisa.
Jambo moja liliendelea kupita kichwani mwake ni kwamba, mara tu akifanikiwa kufika nyumbani ni kuchukua kila kilichokuwa cha kwake kisha kumwachia
Phillip nyumba na yeye kwenda kutafuta sehemu nyingine ambako angeishi maisha yake.
“Nitaondoka, nitamwachia Phillip nyumba, kwa kitendo hiki siko tayari kumsamehe amenidhalilisha sana,” bado Lina aliendelea kujilaumu.
***
Phillip aliyekuwa ndani ya hoteli pamoja na walinzi wawili waliushuhudia mchezo mzima jinsi ulivyokuwa ukiendelea lakini hakuthubutu kufungua mdomo
wake kueleza jambo lolote.
Kufanya kwake hivyo ingekuwa ni kujipalia makaa ya moto kwani mwanamke aliyetoka mbio ndani ya chumba akiwa na shuka tu mwilini mwake ni mkewe na
kibaya zaidi mwanaume alikuwa akimfuata kwa nyuma huku akimwita ili arejee wamalizie shughuli iliyokuwa mbele yao, ilikuwa ni fedheha ya kutosha kwake.
“Sijui anakwenda wapi? Masikini mke wangu… nisamehe halikuwa kusudio langu kutenda haya,” aliwaza huku akikimbia kuelekea lango kuu la kutokea
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hotelini ili ashuhudie ni wapi Lina alikuwa akielekea.
Kabla hajatoka nje ya lango akalikumbuka gari lake, akaamua kurejea ili alichukue na kuondoka nalo kumfuatilia Lina, jambo hilo lilifanyika kwa haraka,
alipolifikia bila kusema kitu akaingia ndani ya gart hilo na kuliwasha haraka akakanyaga mafuta na likatii amri ba kutoka nje ya hoteli hiyo.
Aliwashuhudia walinzi wawili aliokuwanao wakiwa na mtu mwingine wa tatu na alipotupa macho yake kumwangalia mtu yule alimtambua kuwa ni mwanaume
aliyekuwa na Lina ndani ya hoteli, alikuwa akiangua kilio huku akiongea maneno ambayo Phillip hakuyasikia vyema.
“Nitamtafuta Lina mpaka nimpate nimwombe msamaha mke wangu najua ananipenda na atanisamehe,” aliongea akikunja usukuni na kutokeza barabarani.
Moyo wake ulijawa hofu na kujitupia lawama nyingine lakini alijipa moyo baada ya kuamini kwamba jambo lililokuwa limetokea siku hiyo lilikuwa ni kati ya
makubaliano yake na mkewe Lina.
Hakuwa na ufahamu kabisa wa kile kilichotokea ndani ya chumba cha hoteli ile mpaka mfarakano ukatokea, hakufahamu kabisa kwamba Lina hakuwa tayari
kufanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine, kwake yeye aliamini kwamba kufanya hivyo kungeidhalilisha ndoa yake kama si kuisaliti.
Phillip akaliendesha gari taratibu huku akitupa macho yake huku na kule kuangalia kama angeweza kumwona Lina eneo hilo lakini hakufanikiwa.
Baada ya mwendo mrefu alitupa macho upande wa pili wa barabara na kufanikiwa kulishuhudia kundi kubwa la watu walioonekana kubishana kitu fulani, wazo
la kuwafuata watu wale kujaribu kuwauliza likamwingia kichwani mwake.
Philip akaliendesha gari na kuelekea upande wa pili wa barabara na kupaki pembeni kisha kulizima kabisa, akashukua ndani na kuwasogelea watu wale
waliokuwa wamekusanyika kila mmoja akiongea lake.
“Habari za saa hizi jamani?” Aliuliza kwa sauti ya kiume.
“Salama!”
“Naomba kuuliza.”
“Uliza tu tunakusikiliza.”
“Sijui mmefanikiwa kumwona mwanamke mmoja akipita hapa?”
“Mwanamke?”
“Ndiyo”
“Mh! Yule si mwanamke ni mzimu.”
“Mzimu?”
“Ndiyo, tena umevaa shuka nyeupe, umekimbilia kuleeee,” alisema mtu mmoja huku akinyosha kidole kuelekeza upande alipoelekea Lina.
“Wapi?”
“Wee kaka huo mzimu unaoulizia umekwenda kule.”
Maumivu makali yakauchomoa moyo wake, yalikuwa kama vile mshale wa moto, Phillip akaonekana kama mtu aliyenyeshewa na mvua, bila kujibu chochote
taratibu akaingia tena ndani ya gari lake na kuanza kuondoka eneo lile bila kuuliza tena swali kwa mtu yeyote.
Watu waliokuwepo katika kundi lili wakazidi kumshangaa.
***
“Mzee hakuna haja ya kulia nashauri tuwapeleke watoto hospitalini.”
“Kufanya nini wakati wameshakufa?” Victor Fedorov aliuliza huku machozi yakimbubujika.
“Hakuna aliyesema wamekufa hawa ila…”
“Ila nini? Mbona mnazidi kunichanganya ninyi?”
“Bosi tufuate ushauri wa watalaam,” mlinzi wa Victor aliongea akimpigapiga bosi wake sehemu za mabegani.
“Sawa lakini matumaini hayapo, watoto wangu wameniacha mkiwa, Mariya na Merina wameondok…” Victor Fedorov aliangua kilio huku kwikwi ikimkaba.
Kwa Victor Fedorov tajiri ambaye alivuma kupita maelezo ilionekana kama ndoto, hakuwa tayari kuamini kwamba alibaki peke yake duniani huku akiwa ametoa
karibu nusu ya utajiri wake wote kuwakomboa watoto wake Mariya na Merina lakini sasa nao walikuwa wamemwacha mkiwa katika dunia ambayo hakika
hakufahamu nini ingekuwa hatima yake.
Utajiri wake wote aliokuwa nao sasa ulikuwa hauna maana tena.
“Ngoja twende hospitali nitajua kila kitu huko,” aliwaza kichwani mwake huku akishuhudia watoto wake wakibebwa mmoja baada ya mwingine na kuingizwa
ndani ya gari la wagonjwa.
“Mzee kwa sababu nafasi yetu ni finyu tungeomba uendeshe gari lako ukitufuata kwa nyuma”
“Hakuna shida”
Victor Fedorov akafanya hivyo lakini akamwomba mlinzi wake waongozane wote kwani hakuwa katika hali nzuri. Baada ya kuhakikisha kwamba kila kitu
kilikuwa sawa nyumbani hapo wakafunga milango na wote kutoka.
Gari la wagonjwa lilikuwa mbele yao huku likipiga king’ora cha kuashiria hatari na wao wakiwa nyuma huku Fedorov akionekana kuzama katika lindi la
mawazo.
Victor Fedorov aliendesha gari sambamba kabisa na gari la wagonjwa hakutaka kuliacha hata hatua moja, hamu yake kubwa ilikuwa ni kufika hospitalini na
kuona watoto wake wakifanyiwa uchunguzi maalum ambao aliamini ungerejesha majibu yakatayomfanya arejee tena katika dunia, kwani tayari alishajihesabu
kwamba alikuwa ni marehemu mtarajiwa kama tu angeelezwa kwamba watoto wake Mariya na Merina hawakuwa na maisha tena.
“Hapana! Sitaki wafe, nataka waishi, Mungu naomba unisaidie jambo hili, nawapenda mno watoto wangu kama kweli watakuwa wamefariki basi na mimi
nitakufa, hakika watazikwa siku moja na mimi,” aliongea kwa sauti iliyomshtua mlinzi wake ambaye muda wote huo naye alikjuwa akiwafikiria watoto hao.
“Hawatakufa,” mlinzi alijibu akimwangalia Fedorov.
“Vruuu! Vruuu!” Sauti ilisikika
“Vruuu! Vruuu!” sauti ilisikika.
Kelele za matairi ya gari yakisugua barabara zilisikika, dereva wa gari alikuwa akijitahidi kadiri ya uwezo wake kukanyaga breki ili kunusuru maisha ya mtu
aliyekuwa akikatiza barabarani asubuhi hiyo.
“Mungu wangu! ” Victor Fedorov aliongea macho yake yote yakimwangalia mtu huyo, hasira ya ajabu ilikuwa imemshika lakini alipokumbuka kwamba
alitakiwa kuondoka eneo hilo haraka kuliwahi gari la wagonjwa lililobeba watoto wake hakuongea neno jingine zaidi, akaliwasha gari na kuondoka eneo hilo
haraka.
“Pole sana bosi,” mlinzi aliongea.
“Ni balaa hilo limeshapita zake.”
“Dah! Sijui alikuwa haoni?”
“Siyo kuona tu hata king’ora hakukisikia?”
“Msamehe, pengine mawazo ya maisha yamemchanganya.”
“Ni kweli kabisa nimeshamsamehe, ndiyo maana sikufanya chochote zaidi ya kumwangalia tu,” aliongea Fedorov akikanyaga mafuta kulifuata gari lililobeba
watoto wake ambalo halikuwa umbali mrefu sana na gari lake.
Kwa mwendo wa dakika kumi nzima aliendelea kulifuata gari la wagonjwa kwa nyuma, hofu yake ikizidi kuongezeka juu ya hali ya watoto wake, na mawazo
mengi yaliufunika mtima wake. Ni mlinzi ndiye aliyekuwa pembeni yake kumfariji na kumweleza kwamba kila kitu kingekwenda sawa na hakusita kumweleza
wazi kwamba watoto hao hawakufa bali walikuwa katika hali ya kuzimia na muda si mrefu baada tu ya kuonana na madaktari wangepata nafuu na wote kurejea
nyumbani.“Ahsante ndugu yangu, sipendi kushuhudia vifo vya watoto wangu kwani hao ndiyo ndugu pekee niliobakiza duniani, kama ikitokea wakaniacha basi
na mimi sitaweza tena kuendelea kuishi dunia ya peke yangu, nitawafuata.”
Maneno hayo yalipita moja kwa moja masikioni mwa mlinzi na akili yake ikauona utajiri wa Victor Fedorov mikononi mwake kwani kama ingetokea watoto
wale wakawa wamefariki dunia na Victor Fedorov kujiua kama alivyokuwa akisema basi utajiri wote ungekuwa wake, aliliamini jambo hilo kwa asilimia mia
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
moja.
“Akijiua kweli basi nitakuwa mrithi wake, kwani hana ndugu huyu na kama mwenyewe alivyokiri kwa kinywa chake, utajiri huo utakuwa mikononi mwangu, ”
aliongea.
Ni sauti ya Fedorov iliyomshtua na kumtoa katika dimbwi hilo la mawazo.
“Je,uko wapi mbona umenyamaza ghafla, umepatwa na nini?”
“Ah! Bosi unajua ninakuonea huruma sana…lakini zaidi afya ya watoto…”
“Watakufa?” alidakia tena Fedorov.
“Mh! Kwa kweli sijui chochote mpaka sasa ngoja tufike hospitali kwanza,” aliongea mlinzi huyo akimwangalia bosi wake kwa jicho la tamaa ya utajiri.
“Ongea neno wewe sasa si mlinzi tu bali ndugu yangu.”
“Unasema?”
“Wewe ni ndugu yangu bwana,” kauli hiyo ikazidi kumchanganya zaidi ubongo wake.
“Mh! Au amenigudua? Kwa nini ameniambia kitu ninachokifikiria?” alijiuliza kimoyomoyo na haikuchukua muda mrefu sana, tayari wakawa wameshafika
hospitalini ambapo haraka wote wawili baada ya kuegesha gari sehemu ya maegesho wakashuka na kuanza kukimbilia eneo la mapokezi ambako gari la
wagonjwa lilionekana.
“Wakikaribia eneo hilo wakashuhudia machela mbili zikisukumwa kutoka ndani na kusogezwa karibu kabisa na mlango wa gari kisha kufunguliwa na watoto
wawili wakatolewa na kuweka juu yake.
“Tafadhali fanyeni haraka sana tujitahidi kuokoa maisha ya wagonjwa hawa,” ilikuwa ni sauti ya daktari aliyekuwepo ndani ya gari la wagonjwa.
Wakati zoezi hilo likiendelea Victor Fedorov alishafika eneo hilo na kushuhudia machela zikisukumwa kwa kasi ya ajabu kuingizwa ndani ambako naye
alizifuata kwa nyuma akiwa na mlinzi wake.
“Na ninyi mnakwenda wapi huku?” ilikuwa ni sauti ya mwanaume aliyesimama eneo hilo akionekana kuwa mlinzi.
“Watoto wangu, hawa ni watoto wangu.”
“Watoto wako?”
“Ndiyo,” alijibu akikimbia kuelekea mbele.
“Na wewe ni nani?”
“Huyo hapo ni bosi wangu mimi ni mlinzi wake.”
“Wewe unaweza kubaki hapa acha mhusika afuate nyuma, sawa?” aliuliza akimzuia mlinzi aliyekuwa ameongozana na Fedorov.
Akashuhudia Fedorov na wauguzi waliokuwa wakisukuma machela wakitokomea na kumwacha hapo peke yake akiwa hajui nini cha kufanya.
***
“Lina! Lina! Linaaaa!” ilikuwa ni sauti ya Phillip akiita jina la mke wake.
Ni sauti hiyo ndiyo iliyopenya moja kwa kwa moja masikioni mwa Lina na kumfanya ageuke kuangalia ilitokea wapi, taratibu huku akibubujikwa na machozi
akageuza shingo yake na kuangalia nyuma pamoja na kwamba kulikuwa na giza lakini aliweza kuona taa za gari zikija nyuma yake kwa kasi kubwa, akasimama.
”Tafadhali simama, simama tuongee mke wangu.”
“Mh! Sauti ya Phillip hiyo,” aliongea.
Akiwa hapo akashuhudia gari likisimama mbele yake na mwanaume akachomoka ndani yake akikimbia kumfuata.
“Nisamehe mke wangu ishara ya magoti kwako ni kuonyesha kwamba nimekukosea,” aliongea Phillip akipiga magoti mbele ya Lina.
Machozi yakambubujika Lina, hasira ilikuwa imemkaba zaidi alipomshuhudia mwanaume aliyempenda kupita kiasi akiwa mbele yake kumwomba msamaha na
ni huyu ndiye aliyekuwa amesababisha kutokea kwa sakata lote hilo ndani ya hoteli ya Lamada.
“Umenidhalilisha Phillip.”
“Nisamehe ndiyo maana niko chini ya miguu yako.”
“Phillip! Phillip nyanyuka uondoke sita…” aliongea Lina akijitoa mikononi mwa Phillip ambaye muda wote huo bado alikuwa chini amepiga magoti.
Kwa nguvu zake zote Lina alijaribu kujitoa kwa Phillip lakini haikuwezekana, wote wawili wakajikuta wakigalagala chini.
Phillip bado aliendelea kumwomba Lina msamaha akimsihi akubaliane na ombi lake pia akubali kuingia ndani ya gari waondoke kwenda nyumbani, huko
wangemaliza tofauti zao zote.
“Sitaki! Sitaki nasema sitaki mbona hutaki kunielewa, kwa kitendo hiki kilichotokea leo siko tayari kukusamehe.”
“Nisamehe mke wangu mimi mwenyewe ninaumia moyo.”
“Phillip uumie wewe? Nakuambia umenidhalilisha na si mimi tu hata Daniel, sidhani kama atakuwa tayari kunisamehe kwa ninavyomfahamu, huko aliko
anapanga jinsi ya kulipa kisasi kwangu, masikini wa Mungu haikuwa dhamira yangu kufanya yaliyotokea ni wewe ndiye umeni…” aliongea Lina na kushindwa
kumalizia sentensi yake kwani kwikwi ya kulia ikamkaba zaidi.
Phillip akautumia udhaifu huo wa Lina na kumbeba juujuu kama mtoto kisha kumwingiza ndani ya gari yeye pia kukimbilia upande wa pili na kuingia kisha
kuliwasha na kuondoka eneo hilo kwa kasi ya ajabu, watu wote waliokuwepo eneo hilo wakishangaa kwa kitendo hicho.
***
“Kazi uliyonituma mzee nimemaliza na mzigo ni huu hapa,” ilisikika sauti ndani ya chumba kidogo ndani yake, mwanga hafifu wa taa ulionekana na mzee mfupi
akiwa ameketi pembezoni kabisa mwa chumba hicho akaonekana.
“Haraka wapelekeni chumba cha wagonjwa mahututi,” ilikuwa ni sauti ya mwanaume aliyekuwa kwenye korido ambaye kwa kumwangalia tu ilitosha kugundua
kwamba ni daktari.
Bila kusema kitu chochote, machela zote mbili zikaanza kusukumwa kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi huku Victor Fedorov naye akifuata kwa
nyuma. Akili yake haikuonekana kufanya kazi kwa mateso aliyokuwa akiyashuhudia mbele yake, aliiona dunia haina maana kwake.
“Nisaidie jamani watoto wangu wasife, hawa ndiyo ndugu pekee niliobakiza duniani, bila hawa hata utajiri wote nilionao mimi si kitu, niko tayari kutoa kiasi
chochote cha fedha lakini ilimradi watoto wangu waokolewe…” alisema mfululizo.
Hakuwepo mtu hata mmoja aliyeweza kuongea kwa wakati huo, si wauguzi wala madaktari, wote walikuwa na hofu kubwa juu ya maisha ya watoto hao.
Hatimaye dakika tatu tu baadaye machela mbili ziliwasili nje ya wodi kubwa, Victor Fedorov akashuhudia maneno ICU juu ya mlango wa wodi hiyo.
”Oh! My God!”(Oh! Mungu wangu!) alisema.
“Shaka ondoa mzee, wanaingia kwenye chumba cha usalama, kila kitu kitakuwa sawa,” alisema muuguzi mmoja huku akimwangalia Fedorov kwa macho ya
huruma.
“Watapona kweli?”
“Mh! Watapona.”
“Mbona umeonesha kusita dada?”
“Tuombe Mungu kwani mpaka sasa hatufahamu vyema tatizo linalowasumbua.”
Wakiwa hapo, mlango ukafunguliwa na machela zote mbili zikaingizwa ndani na kumwacha Fedorov peke yake nje akiwa haelewi nini cha kufanya, akawa analia
huku akizungusha macho yake huku na kule. Pembeni kabisa ya wodi aliuona msingi, pamoja na kwamba juu yake paliandikwa kuwa si ruhusa kukaa yeye
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alinyoosha moja kwa moja na kwenda kuketi juu yake.
“Nitakaa hapahapa nikisubiri matokeo, siwezi kwenda mbali, moyo wangu umegubikwa na hofu kupindukia… masikini Mariya na Merina! Nimejitahidi kuokoa
maisha yenu wanangu lakini naona Mungu hakupanga jambo hili, hakupanga muendelee kubaki na mimi baba yenu! Bora ningewaacha tu Tanzania pengine yote
haya yasingetokea… lakini hapana ninyi ni sehemu ya damu yangu, isingekuwa rahisi kufanya hivyo,” Fedorov alikuwa akijisemea huku picha ya jinsi alivyotoa
mbegu zake za kiume na kuziuza kwa familia ya Phillip na Genevieve ikijirudia kichwani mwake. Alikumbuka pia fedha nyingi alizotoa kwa ajili ya malipo kwa
Ditrov ya kuwateka watoto hao kutoka mikononi mwa Phillip na kuwaleta nchini Urusi, hakutaka kuamini kuwa sasa walikuwa katika hali mbaya kiasi kile.
Akiwa katika dimbwi hilo la mawazo, ghafla akasikia mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi ukifunguliwa na wauguzi wawili wakatoka mbio wakikimbia.
Alipojaribu kuwafuata ili aongee nao na kufahamu hali za watoto wake, walimzuia na kumweleza kwamba walikuwa na haraka sana hivyo aendelee kusubiri
eneo hilo mpaka watakaporejea.
“Hatuwezi kukusikiliza, kuna jambo muhimu sana linatakiwa kufanyika sasa hivi.”
“Nataka kujua hali za wanangu… nisaidieni jamani… akili yangu haifanyi kazi vizuri,” alisema mfululizo lakini tayari wauguzi hao walishaondoka na
kumwacha hapo.
Haikuchukua hata dakika tano, kwa mbali akawashuhudia tena wauguzi wale wakirejea, lakini safari hii wakisukuma vitu viwili kama mitungi mikubwa. Akili
yake ikafanya kazi haraka na kugundua kwamba ilikuwa ni mitungi yenye hewa safi ya Oksijeni.
“Hii si mitungi ya gesi kweli?”alijiuliza huku akikodoa macho kuangalia.
Hakukosea, ilikuwa ni mitungi ya hewa ya oksijeni ikisukumwa kuingizwa ndani ya wodi ya wagonjwa mahututi, Fedorov akalia kwa uchungu.
“Hali imekuwa mbaya mpaka wanawekewa hii?” aliuliza huku machozi yakibubujika mashavuni mwake. Kwa hali aliyoiona alizidi kukata tamaa ya kuwaona
tena watoto wake wakiwa hai kwani mara kadhaa wagonjwa wengi waliowekewa hewa hivyo hawakuishi muda mrefu.
“Ni kweli lakini yakupasa uwe mvumilivu, utaelezwa kila kitu kinachoendelea baadaye…” walisema wauguzi wale na kusukuma mitungi hiyo kuingia ndani ya
wodi.
Fedorov akalisikia jasho jembamba likitiririka mwilini mwake taratibu huku akiwa hajui nini cha kufanya, akajikongoja na kusogea pembeni huku moyoni
mwake akiwaza jambo moja tu, kubaki hapo mpaka mwisho.
“Sitaondoka, nitakaa hapa kusubiri,” alisema.
***
“Puuuh!”
Ulikuwa ni mlio wa kitu kikirushwa juu ya meza.
Mzee mfupi mwenye mwili uliojazia kisawasawa, huku akitabasamu alinyanyuka kwenye kiti na kusogea karibu na meza ambayo juu yake ilikuwa na mzigo.
“Umeifanya vyema kazi hii,” alisema huku akipadisha suruali yake vizuri.
“Bila shaka mzee, hakuna tatizo juu ya hilo?”
“Una uhakika na maelezo yako kijana?” Sauti nzito ya mzee huyo ikasikika tena, safari hii akimzunguka kijana huyo kila upande na kukagua mifuko yote ya
suruali yake akimtaka kusalimisha silaha yoyote aliyokuwa nayo juu ya meza.
Bila kusema kitu chochote, kijana yule, huku akionesha kujiamini aliweka silaha zote mezani na alipomaliza aliachia kicheko.
“Kwa nini unacheka?” aliuliza.
“Bosi, inavyoonekana huniamini hata kidogo.”
“Uaminifu wangu umesafiri mbali sana na sidhani kama utarejea leo kwa mchezo mbaya niliofanyiwa huko nyuma, sipo tayari kumwamini mtu yeyote tena
maishani mwangu, labda roho yangu tu. Teh!Teh! Teh!” alimaliza mzee huyo kwa kicheko cha kejeli.
“Hata mimi kijana wako?”
“Nilichosema ndiyo hicho,”alisema huku akiendelea kuzungukazunguka ndani ya chumba hicho.
“Sawa nimekuelewa bosi wangu, ni vyema ukanipatia mgao wangu na mimi niondoke kuendelea na masuala mengine.”
“Naweza kuuliza tena?”
“Bila shaka?”
“Hukuua wala kujeruhi?”
“La hasha!”
“Watoto wote wawili wapo salama?” aliuliza mzee huyo akikodoa macho kumwangalia kijana aliyesimama mbele yake.
“Mh!”
“Unaguna nini?”
“Nauliza tena wako salama?”
“Baada ya kupata mzigo huu niliwarusha kutoka ndani ya gari langu mpaka chini, mmoja baada ya mwingine na mimi kuondoka eneo hilo haraka bila kuangalia
nyuma... lakini pia…” kigugumizi cha ghafla kikamshika kijana huyo na kushindwa kumalizia sentensi yake.
“Lakini nini? Umewaua?”aliuliza mzee huyo, safari hii kwa ukali.
“Hawajafa ila hali zao ni mba…ya sijui kama wataiona ke…sho?”
“Kwa nini?”
“Niliwa…” alisema kijana huyo huku akitetemeka.
“Unasema?” lilikuwa ni swali kutoka kwa mzee aliyekuwepo ndani ya chumba, bila huruma akaikamata vyema bastola iliyokuwa juu ya meza, akainyoosha na
kulielekea paji la uso wa kijana aliyesimama mbele yake.
KWA muda wa saa tatu mfululizo bado aliendelea kusimama nje ya chumba cha wagonjwa mahututi, macho yake yote yakielekezwa kwenye mlango huo ili
kuona mtu ambaye angetoka na yeye kuweza kumuuliza nini kiliendelea kwa watoto wake Mariya na Merina.
Victor Fedorov alikuwa ni mwanaume wa shoka lakini sasa alianza kuonyesha udhaifu wake kwani mpaka wakati huo tayari alishakata tamaa, moyo wake
ulimuuma kupita kiasi, akasikiliza sauti ndani yake ikimlaumu kwa kitendo chake cha kuwateka watoto hao kutoka Tanzania na kuwaleta nchini Urusi na sasa
walikuwa wakifa bila hatia.
Saa nne ilipogonga akaushuhudia mlango wa chumba hicho ukifunguliwa na kushuhudia machela ikisukumwa kutoka ndani ya wodi kwenda nje, juu yake
ikionekana kulazwa mtu aliyefunikwa na shuka la kijani kuanzia kichwani mpaka miguuni, hofu kwamba tayari kulikuwa na tatizo ikaugubika moyo wake.
“Mh!” aliguna akikimbia kuisogelea.
“Unakwenda wapi?” sauti ya muuguzi ilisikika ikimuuliza.
“Nataka nione hapo,” aliongea akinyoosha kidole chake cha shahada kuelekea ilipokuwa machela.
“Kaka samahani sana sheria yetu ya kazi hairuhusu kufanya hivyo,” muuguzi huyo alijibu na tayari walishaanza kusukuma tena machela kuondoka eneo hilo,
Victor Fedorov naye akifuata nyuma huku akilia.
“Dada tafadhali niruhusu nimwone huyo aliyelala hapo nataka nijue tu pengine ni mwanangu.”
“Mwanao?”
“Ndiyo!”
“Lakini hatuna ruhusa ya kufanya hivyo, kaka yangu, utanifanya nifukuzwe kazi.”
“Nionee huruma.”
“Hapana,” alijibu muuguzi huyo na kwa kasi ya ajabu akaisukuma machela kuondoka eneo hilo kuelekea chumba cha kuhifadhia maiti, Victor Fedorov akaangua
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kilio na kushuhudia machela hiyo ikizama ndani.
Akaamini kwamba hakika mmoja wa watoto wake tayari alikuwa ameaga dunia.
***
“Nataka kuondoka na nitakuachia kila kitu ndani ya nyumba hii.”
“Uende wapi mke wangu wewe ndiye wangu wa maisha.”
“Nimeshachoka huwezi kunidhalilisha kiasi hicho halafu ukadai kwamba unanipenda.”
“Chukua maneno yangu na uyafanyie kazi, wewe mwenyewe unafahamu ni jinsi gani ninavyokupenda.”
“Mh! Unaniona mimi mjinga? Hivi unafikiri mimi mtoto, unanichapa halafu unanibembeleza kwa pipi?” aliuliza Lina akizidi kukusanya nguo zake na kuzitupia
ndani ya sanduku.
“Haiko haja ya wewe kuondoka, hapa ni kwako acha mimi niondoke.”
Tayari Lina alishanyanyua sanduku akatembea na kuusogelea mlango wa chumba chao na kuufungua ili atoke nje.
“Hapana mpenzi, tafadhali nisemehe hamu ya kuitwa baba ndiyo ilinifikisha hapo.”
“Basi mtafute mwanamke mwingine ambaye atakubali kufanya unayotaka.”
Ukimya wa ajabu ukatokea kati yao Phillip aliyekuwa amepiga magoti chini akakimbia na kulikamata sanduku la Lina huku akimsihi asifanye maamuzi kama
hayo, lakini zoezi hilo lilionekana kushindikana na kujikuta akiambulia teke kutoka kwa mwanamke huyo.
Hasira ya Lina ilionekana wazi, si kwamba kweli hakumpenda Phillip bali alimpenda kwa dhati lakini hakuwa tayari kukutana kimwili na mwanaume mwingine
ili kupata ujauzito hivyo kitendo cha Phillip kulazimisha jambo hilo ndicho kilisababisha machafuko hayo kutokea ndani ya nyumba yao.
“Umenidhalilisha sana ni wapi nitaficha uso wangu pale nitakapokutana na Daniel? Hivi huoni umenijengea uadui mkubwa sana? Kwa hilo siko tayari
kukusamehe Phillip, mimi naondoka tutaonana tena kama si hapa duniani basi akhera,” aliongea Lina kwa sauti ya upole huku akifungua mlango wa sebuleni na
kutoka nje.
“Nakupenda mke wangu, ni shetani aliingilia kati penzi letu na kunipa akili isiyofaa.”
“Eti shetani, usimsingizie bure huyo shetani ni wewe mwenyewe.”
“Basi nakubali mke wangu nisamehe, tafadhali rudisha penzi lako kwangu tuanze upya, tukipanga ni namna gani tufanye ili tupate angalau mtoto mmoja.”
“Phillip sahau jambo hilo halipo tena,” aliongea Lina akiingia ndani ya gari tayari kuondoka eneo hilo.
“Hatanii, nikimwacha akaondoka nitamkosa nami sipo tayari,” aliongea Phillip na haraka akili ikamjia kichwani mwake, ili kumzuia Lina ni lazima aende na
kulala mbele ya lango la kutokea.
Haraka akatoka mbio na kwenda kujitupa katikati ya lango kuu la nyumba hiyo na kutulia kimya.
Wakati yote hayo yakitokea Lina akiwa ndani ya gari lake akaliwasha na kuanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu bila kuangalia. Kilichofuatia ni sauti ya mayowe
iliyopigwa na mlinzi wa nyumba yao.
“Mungu wangu utauaaa! Utauaaa!” ni sauti hiyo ndiyo iliyomfanya Lina afunge breki za gari kwa nguvu na kushuka kuangalia ni kitu gani kilikuwa kimetokea.
“Phillip unafanya nini? Unataka nikugonge halafu nipate kesi?”
“ Bora iwe hivyo kuliko kuondoka.”
“Sikia wewe ni mtu mzima sasa tafadhali ondoka ili mimi nipite.”
“Sitaondoka hapa mpaka utakaponipa msamaha wako.”
“Unasema?”
“Lina umesikia nini, nasema sina haja ya kurudia.”
“Unacheza na mimi, wewe hufahamu kwamba siku zote ulikuwa ukiishi na mwanamke Mafia? Leo utanifahamu mimi ni nani? Naapa nitaondoka kwa nguvu
wala sitanii...sasa kaa hapo ushuhudie ninavyoondoka. Pumbavu mkubwa wewe.”
***
“Kwa nini?”
“Niliwa…” alisema kijana huyo huku akitetemeka.
“Unasema?” lilikuwa ni swali kutoka kwa mzee aliyekuwepo ndani ya chumba, bila huruma akaikamata vyema bastola iliyokuwa juu ya meza, akainyosha na
kulielekea paji la uso wa kijana aliyesimama mbele yake. Kwa alivyomfahamu mzee huyo hakika alikuwa hatanii alimaanisha alichokifanya, hofu ikaugubika
moyo wake, akiwa haelewi nini cha kufanya akasikia kitu kama mkojo kikipenya kutoka ndani ya suruali yake.
“Nisemehe mzee wangu.”
“Nataka kufahamu ni kitu gani kiliendelea kwa watoto.”
“Hawajafa, nina hakika watakuwa hai japo hali zao sielewi zinaendeleaje?”
“Uliwapa nini?”
“Mh!” kijana aliguna.
“Husemi? Sasa nitakuonyesha mimi ni nani.”
“Hapana! Nipe muda nitakueleza.”
Mzee aliyekuwa ameiweka bastola kwenye paji la kijana aliyesimama mbele yake, taratibu huku akitabasamu akaishusha bastola hiyo chini.
“Fyuuuu!” kijana alishusha pumzi.
“Ninakupa dakika mbili tu kuanzia sasa uwe tayari kueleza kilichowapata watoto vinginevyo leo utani…” aliongea mzee huyo akiiweka vyema bastola yake.
Dakika mbili zikakatika bila kijana huyo kufungua mdomo kusema neno lolote, jambo hilo ndilo lililomtia hasira mzee aliyekuwa amesimama ndani ya chumba
hicho kidogo, akasogea karibu kabisa na kuiweka tena bastola juu ya paji la kijana huyo na haikuchukua hata sekunde mbili mlio wa bastola ukasika.
“Paa! Paaa!” kicheko kikafuatia nyuma yake.
MAMBO yanazidi kwenda mrama kwa Phillip ambaye kwa nguvu zake zote amejitahidi kumwomba mkewe Lina msamaha ili amsamehe na kuendelea na maisha
lakini inaonekana kushindikana. Lina ameingia ndani ya chumba na kukusanya nguo zake kisha kuziweka ndani ya sanduku, anamwambia Phillip kwamba
anaondoka mahali hapo na kumwachia kila kitu.
Jambo hilo linaonekana kuwa gumu kwa mwanaume huyo, akiwa hapo anamshuhudia Lina akitoka kuelekea nje, naye anamfuata kwa nyuma huku akiendelea
kumsihi na kumwomba radhi kwa yote yaliyotokea. Anaingia ndani ya gari na kuliwasha kisha kuliendesha kuelekea langoni bila kufahamu kwamba tayari Phillip
amefika eneo hilo na kulala usawa wa lango hilo, lengo kubwa likiwa ni kumzuia asiondoke.
Upande wa pili wa hadithi hii, tunamwona mwanaume mmoja ndani ya chumba akiwa na kijana, baada ya maongezi ya muda mrefu mtafaruku unatokea na mzee
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
huyo anataka kufahamu ni kitu gani kiliwapata watoto wawili pacha ambao walitekwa na kijana huyo kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa baba yao tajiri,
Victor Fedorov.
“Ninakupa dakika mbili tu kuanzia sasa uwe tayari kueleza kilichowapata watoto, vinginevyo leo utani…” alisema mzee huyo huku akiiweka vyema bastola
yake.
Dakika mbili zikakatika bila kijana huyo kufungua mdomo wake kusema neno lolote. Ni jambo hilo ndilo lililomtia hasira mzee aliyekuwa amesimama ndani ya
chumba hicho kidogo, akasogea karibu kabisa na kuiweka tena bastola juu ya paji la uso la kijana huyo, haikupita hata sekunde mbili, mlio wa bastola ukasika
ndani ya chumba.
“Paa! Paaa!” kicheko kikafuatia nyuma yake.
“Unacheza na mimi wewe, hivi hufahamu kwamba siku zote ulikuwa ukiishi na mwanamke Mafia? Leo utanifahamu mimi ni nani? Naapa nitaondoka kwa
nguvu zangu, wala sitanii! Kaa hapohapo ushuhudie ninavyoondoka. Pumbavu mkubwa wewe,” alisema Lina huku akitembea kwa kasi kulielekea gari na
kuingia ndani yake.
“Bora unikanyage nife lakini sipo tayari kukuacha uondoke, nakupenda sana Lina, mambo yote haya yaliyotokea ni Shetani tu.
“Eti Shetani? Shetani ni wewe mwenyewe, hebu ondoka mimi nipite.”
Phillip aliendelea kulala chini huku akilia, hakuwa tayari kushuhudia mwanamke aliyempenda akiondoka mbele ya macho yake. Ghafla akiwa hapo, taswira ya
Genevieve mkewe ikamjia, watoto wake wawili, Dorice na Dorica nao pia wakapita kichwani mwake kama sinema kali, machozi yakazidi kumbubujika.
“Bora nife niwafuate …” alisema Phillip, safari hii kwa sauti.
“Bosi kuna kitu gani kimetokea? Mbona mnanichanganya?” mlinzi aliuliza.
“Haya mambo hayakuhusu, ni vyema ukaachana nayo na wewe kuendelea na shughuli zako.”
“Lakini mimi ni mmoja wa watu wa familia hii?”
“Ondoka kafanye kazi, husikii?” aliuliza Phillip safari hii kwa ukali.
Taratibu bila kusema kitu, alianza kutembea kuondoka eneo hilo na kusogea pembeni ambako aliendelea kutupa macho yake na kumwona Phillip akiwa bado
hajabadilisha uamuzi wake wa kuendelea kulala eneo lilelile.
“Akifanya mchezo huyu mwanamke atamkanyaga kweli, kwa inavyoonekana wana ugomvi mkubwa sana hawa, lakini ni wa nini?
Mbona walitoka wote? Lakini mwanamke amerudi akiwa amejifunika shuka mwilini mwake? Mh! Hakyanani vile, kuna kitu kikubwa hapa kimetokea…” mlinzi
aliendelea kuwaza kichwani mwake, yeye pia alishaanza kuhofia kibarua chake, alifahamu wazi kuwa kama kweli Lina aongeondoka, basi ajira yake ingekuwa
matatani.
Akalishuhudia gari likija kwa kasi ya ajabu kuelekea eneo hilo, alipoangalia vizuri kuona kama bosi wake Phillip alikuwa ameondoka, alishangaa kumuona
akiwa bado amelala eneo lilelile bila kusogea.
***
Machela iliyokuwa ikisukumwa na kuingizwa chumba cha maiti ilimtia hofu sana Victor Fedorov, kichwani mwake hakuwa na picha kamili ya nini kingefuata
baada ya hapo, mawazo mengi yakaufunika ubongo wake.
“Sijui itakuwa nini? Lakini ngoja nirudi kule wodini, najua nitapata jibu kamili,” alisema mzee huyo na kuanza kutoka mbio kuondoka eneo hilo.
Kwa dakika tatu nzima, aliendelea kukimbia hatimaye akakifikia chumba cha wagonjwa mahututi, akaweka kambi hapo kusubiri mtu ambaye angetoka eneo hilo
na kumweleza ukweli juu ya afya za watoto wake na nini kilitokea.
Kwa takribani dakika tano nzima, aliendelea kuketi eneo hilo, ghafla macho yake yakaushuhudia mlango wa chumba hicho ukifunguliwa na mtu aliyevalia koti
jeupe akatokeza nje.
“Ni daktari,”alisema.
Mwanaume huyo akatembea kuelekea eneo alilokuwa ameketi Victor Fedorov na kumsabahi kisha kuanza kumuuliza maswali machache.
“Kama sijakosea nadhani wewe ndiye baba wa watoto wale wawili?’
“Eh! Ndiyo kabisa.”
“Naweza kufahamu umekuja na nani?”
“Mimi?”
“Ndiyo mzee.”
“Mh! Mh! Kwani kuna kitu gani daktari?”
“Ni vyema nikafahamu, umekuja hapa na nani?”
Swali hilo likaingia moja kwa moja masikioni mwa Fedorov na kwenda kugonga sehemu fulani ya ubongo wake. Akiwa hapo akanyanyua macho na
kumwangalia daktari ambaye bado aliendelea kusimama pembeni akimwangalia.
“Daktari?” aliita.
“Ndiyo mzee.”
“Nieleze ukweli, nini kimetokea ndani ya chumba hicho kwani muda mfupi uliopita nikiwa hapa nimeshuhudia machela ikipitishwa hapa kuelekea chumba cha
kuhifadhia maiti na juu yake kwa nilivyoona kuna mtu…”
“Si kazi yako hiyo mzee, hebu nijibu swali langu.”
Victor Fedorov hakujibu tena kitu, akainamisha kichwa chake chini, hakuwa tayari kusikia kwamba mmoja kati ya watoto wake alikuwa ameaga dunia.
“Tafadhali naomba kufahamu kuna ujumbe muhimu nataka kuutoa kwenu.”
“Ninaye mlinzi wangu kule mapokezi.”
“Tunaweza kuongozana?”
“Hakuna shida,” alijibu Fedorov akitetemeka.
Bila kuongea tena kitu chochote na daktari huyo, taratibu akaanza kutembea akimfuata nyuma. Hofu yake ikazidi kuongezeka kwani kitendo cha kuulizwa
kwamba alikuja na nani hospitalini hapo kilizidi kumtia hofu, mambo mengi yakazunguka kichwani mwake bila kujua cha kufanya.
“Nitapokea majibu yoyote nitakayopewa lakini si ya vifo vya watoto wangu.”
Akiwa katika mawazo hayo ni sauti ya daktari ndiyo iliyomshtua, alikuwa akimuuliza yu wapi mtu aliyeambatana naye.
“He! Kumbe tumefika mapokezi?”aliuliza.
“Mzee akili yako iko wapi?” Daktari alimuuliza huku akimpigapiga mgongoni.
“Yule paleee!”alinyoosha kidole chake cha shahada kuelekeza eneo alilokuwa ameketi kijana mmoja, haraka wote wawili wakatembea na kufika eneo hilo.
“Habari yako?”
“Nzuri tu.”
“Nadhani wewe ni mmoja kati ya watu waliokuja na mzee huyu hapa kwetu.”
“Ndiyo, ni bosi wangu huyu.”
“Ni vyema tukaongozana wote mpaka ofisini kwangu, ningependa kuongea na ninyi kuhusu watoto waliofikishwa hapa asubuhi hii.”
“Nini kimetokea? Hali zao zikoje? Wame…” Victor Fedorov aliuliza maswali mfululizo na alipotupa macho yake kumwangalia daktari aliyesimama mbele
yake, aligundua kitu fulani katika macho yake.
***
“Piiii!Piiiii!Piiiii!” ilikuwa ni honi ya gari ikipiga kuomba kupishwa eneo hilo lakini mtu aliyeonekana kulala chini bado hakushtuka wala kujitingisha.
“Mungu wangu! Mama yangu weee! Ayaaaa! Tayari ameua...” ilikuwa ni sauti ya mlinzi wa Lina akiwa pembezoni kabisa mwa kibanda kidogo karibu kabisa na
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
lango la kutokea.
“Nakufaaaaa!” Ndiyo sauti pekee iliyosikika.
UNAUA! Unaua! Mama yangu weee! Dah!”
Ni sauti hiyo ndiyo iliyopenya moja kwa moja masikioni mwa Lina akiwa ndani ya gari lake huku akionekana kuwa mwenye hasira nyingi, hakuwa na habari
kabisa kwamba wakati anamweleza Phillip kuhusu kuondoka eneo hilo hakufanya hivyo, aliendelea kubaki palepale.
“Whaat?”(Nini?) alijiuliza baada ya kugeuka na kumwona mlinzi wake akishika mikono kichwani huku akikimbia kuelekea langoni.
Akiwa ndani ya gari huku akiwa haelewi nini cha kufanya, alimshuhudia mlinzi akiruka kutoka kwenye kibanda chake na kuruka kuelekea mbele ya gari lake.
Bila kujiuliza akashuka haraka na kuugana na mlinzi wake, akamshuhudia Phillip akiwa chini ya gari. Alipomwangalia vizuri aligundua alikuwa akilia.
“Niue! Nasema niue siko tayari kukuruhusu uondoke hapa na kuniacha peke yangu.”
Maneno yale yakapenya tena moja kwa moja masikioni mwa Lina, naye akaangua kilio kama mtoto mdogo, akainama na kupiga magoti huku akimbembeleza
Phillip atoke chini ya uvungu wa gari ili waongee.
“Unasema kweli?”
“Hakika nakuambia.”
“Huwezi kunidanganya?”
“Mimi? Nakupenda sana Phillip,” aliongea Lina akimshika Phillip mkono kumsaidia kutoka chini ya uvungu wa gari.
Kwa takribani dakika tano nzima Phillip aliendelea kulala chini ya gari hata Lina alipombembeleza bado hakuwa tayari kuamini maneno yake, alichukulia kama
yalikuwa ni gia ya kumtoa yeye ili apate nafasi ya kuondoka na kumwacha salama bila majeraha.
Baada ya Lina kuona ameshindwa kumtoa Phillip, aliamua kumtumia mlinzi ambaye alikuwepo eneo hilo akatumia ushawishi wake wote ili kumtoa Phillip
lakini naye hakufanikiwa.
“Lina!” Phillip aliita.
“Ukitaka nitoke hapa nipatie funguo za gari.”
“Hicho tu?”
“Ukifanya hivyo naweza kutoka.”
“Basi chukua huu hapa,” Lina alijibu akinyoosha mkono uliokuwa na funguo kumwelekea Phillip ambaye aliunyakua kwa nguvu kama vile mwewe anyakuavyo
kifaranga cha kuku akiwa haamini kinachotokea, akachomoza na kuketi kitako pembeni kidogo tu mwa Lina.
“Nisamehe mke wangu.”
“Nimekusamehe toka zamani sana twende ndani,” aliongea Lina akimshika Phillip mkono na kumnyanyua kutoka chini na wote wakaongozana kwenda
chumbani kwao.
Walipoingia tu, Lina hakuwa na mazungumzo mengine zaidi akamkamata Phillip kwa nguvu zake zote na kuanza kumvua nguo moja baada ya nyingine huku
akimmiminia mabusu motomoto na alipomaliza akazikamata pia nguo zake na kuzitupa pembeni wote wawili wakabaki kama walivyozaliwa na kazi ikawa ni
moja tu.
Ndani ya chumba ni sauti pekee ya miguno na mihemo ya mahaba iliyosikika kila mmoja akionyesha ufundi wake kwa mwenzake, mara kadhaa Phillip
akiendelea kumwomba mkewe msamaha kwa mambo yote yaliyotokea na kumweleza wazi kwamba alimpenda kwa dhati.
“Je, ulifanikiwa kufanya tendo la ndoa na yule mwanaume?”
“Mh!” Lina aliguna.
“Nieleze mpenzi wangu ili nitoe dukuduku lililoko ndani ya moyo wangu.”
“Kwa nini unauliza hivyo? Na kama je ilitokea nikafanya hivyo utaniacha?”
Lilikuwa ni swali gumu kutoka kwa Lina kwenda kwa Phillip ambaye alikuwa kimya juu ya kitanda mikono yake ikiendelea kuupapasa mwili wa Lina.
Kwa muda wa saa nne mfululizo bado walikuwa juu ya kitanda wakibadilisha staili kutoka moja kwenda nyingine ili mradi kila mmoja wao alikuwa akisikia
raha.
“Mpenzi hebu tupumzike kidogo mwili hauna nguvu kabisa.”
“Unasema?” Phillip aliuliza.
“Nimecho…kaaa,” aliongea Lina akitetemeka.
“Bado nataka leo nikuonyesha ufundi wangu wote, nadhani utaamini maneno yangu kwamba ninakupenda.”
“Ashhhhh! Ashhhhh! Hapa…na,” Lina alizidi kulalama kitandani.
Kwa jinsi zoezi lilivyokuwa kwa Lina ilionekana ni pata shika nguo kuchanika, Phillip hakuwa tayari kumwachia Lina kwani alipania kumuonesha ufundi wake
wote.
***
Victor Fedorov alisimama ndani ya chumba cha daktari akitetemeka mwili mzima, hakuelewa mpaka wakati huo ni ujumbe gani ambao daktari alikuwa akienda
kuutoa kwao, hofu ya kwamba mmoja kati ya watoto wake alikuwa ameaga dunia hakuwa tayari kuupokea.
“Daktari hebu nenda moja kwa moja kwenye ujumbe wako.”
“Tafadhali naomba mketi kwanza.”
“Haipo haja, tueleze tu tukiwa wima.”
“Mh! Unajua ninyi sasa ni watu wazima yawapasa kukubali na kuelewa nini kinaendelea mpaka sasa,” Daktari aliongea na kutulia kidogo kisha kuendelea.
“Kikubwa kilichonifanya niwaite ndani ya chumba hiki ni juu ya hali za watoto wenu ambao mpaka saa wako chumba cha wagonjwa mahututi wakipatiwa
matibabu lakini…”
“Fyuuuuu!” Victor Fedorov alishusha pumzi.
“Kutokana na hali zao kuwa mbaya na sisi kama madaktari tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu wote kuokoa maisha yao lakini hali inaonekana kuwa tete hivyo
basi, ni vyema nikawashauri kuwahamisha kwenda katika hospitali kubwa zaidi pengine huko mnaweza kufanikiwa.”
“Daktari kwani wanawasumbuliwa na kitu gani?”
“Kwa inavyoonekana kama siyo njaa basi watakuwa wamepewa sumu.”
“Sumu?”
“Inavyoonekana.”
“Mungu wangu walitenda ubaya gani watoto hawa mpaka kustahili adhabu hiyo?” Mlinzi wa Victor Fedorov aliuliza.
“Nadhani sasa si wakati wa kuuliza hayo ni vyema mkafanya utaratibu na kuwahamisha haraka iwezekanavyo,” alimaliza daktari huyo huku macho yake
yakimwangalia Victor Fedorov ambaye muda wote alinyamaza kimya akionekana mwenye mawazo mengi kichwani.
***
Central Clinical Hospital ndiyo ilikuwa hospitali iliyokuwa na sifa kila kona ya nchi ya Urusi na ilisifika zaidi kwa watendaji wake wa kazi, kuanzia madaktari,
wauguzi na watu wengine wote waliofanya kazi ndani ya hospitali hiyo. Huko ndiko daktari aliyekuwa akiwahudumia watoto wa Victor Fedorov alishauri
wapelekwe kwani aliamini kwamba kufika katika hospitali hiyo kungeweza kunusuru maisha ya watoto hao.
“Huko mtapata kila kilicho kizuri, madaktari, wauguzi na hata huduma ili mradi tu uwe na fedha.”
“Ahsante,” alijibu Victor Fedorov akimfuata daktari kwa nyuma mawazo yake yote yakahama kutoka eneo hilo na kwenda moja kwa moja kwa watoto wake, hao
ndiyo walikuwa ni kila kitu kwake.
Maandalizi yakafanyika haraka, gari maalumu la wagonjwa likaandaliwa na watoto wakatolewa chumba cha wagonjwa mahututi huku mashine ya hewa ya
oksijeni ikiwa imefungwa kwa kila mmoja wao, hakika kwa kuwaangalia iliumiza sana, walilala kimya kitandani bila kujitambua.
Victor Fedorov akashindwa kuvumilia, akamwaga machozi mfululizo.
“Haraka wapelekeni chumba cha daktari,” muuguzi aliyekuwa ameongozana na watoto wa tajiri Victor Fedorov kutoka katika hospitali ya awali kwenda Central
Clinical Hospital alisema baada tu ya machela mbili zilizowabeba watoto wake kuteremshwa kutoka garini.
Kwa jinsi hali ilivyokuwa, watoto hao walihitajika kuingia moja kwa moja kwenye chumba cha daktari bila kusubiri utaratibu mwingine. Haikuchukua hata
sekunde tano wakawa tayari wamewasili ndani ya chumba cha daktari.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nini tatizo?”
“Wagonjwa sana.”
“Naweza kufahamu nini kinawasumbua?”
Ukimya wa ajabu ukatokea, hakuna mtu aliyeweza kueleza kilichokuwa kikiwasumbua watoto hao wawili.
“Mzazi wao yupo wapi?” daktari aliuliza.
“Mimi hapa,” alijibu Fedorov kwa sauti kubwa.
“Sogea karibu.”
Huku akionesha uso uliojawa na mashaka, Fedorov alisogea karibu kabisa na daktari.
“Ndiyo, hali hii imeanza lini?”
“Ni muda wa wiki sasa daktari lakini leo hali imebadilika zaidi.”
Daktari aliyekuwepo ndani ya chumba kile alianza kumpima mtoto mmoja baada ya mwingine, mara kadhaa alitingisha kichwa chake na zoezi hilo lilipokamilika
akawa anaandika maelezo fulani ndani ya mafaili ya wagonjwa. Alipomaliza alimwita muuguzi akimtaka awapeleke watoto hao kwenye wodi ya wagonjwa
mahututi, zoezi hilo likafanyika mara moja.
“Daktari, watoto wangu watapona?” Fedorov aliuliza huku macho yake yote yakimwangalia daktari huyo.
“Mh!”
“Tafadhali nijibu.”
“Ah! Unajua? Lakini watapona.”
“Umeonesha hofu sana, nini kinaendelea?” Fedorov aliuliza safari hii kwa sauti ya upole. Akili yake haikufanya kazi vizuri, alihisi kama anakaribia kuwa
mwendawazimu.
“Usijali, wapo katika mikono salama, watapona tu hawa,” daktari alijaribu kumpa moyo Fedorov ambaye kwa kumwangalia tu ungeweza kugundua ni kwa kiasi
gani yupo kwenye mateso na maumivu makali.
Machela mbili zilisukumwa moja kwa moja mpaka chumba cha wagonjwa mahututi, daktari akawa anafuata kwa nyuma.
“Watoeni juu ya mechela na kuwalaza kwenye vitanda,” ilikuwa ni sauti ya daktari akiwapa maelekezo manesi.
Haraka zoezi hilo likafanyika, watoto wote wawili wakalazwa juu ya vitanda vyao na daktari akaanza kufanya uchunguzi kwa kila mmoja akitafuta tatizo.
Kwa muda wa takribani saa tatu na nusu, bado alikuwa akiendelea kuchunguza afya za watoto hao, vipimo kadhaa vikachukuliwa na kupelekwa maabara.
Nje ya wodi, Fedorov aliendelea kusimama, hamu yake kubwa ikiwa ni kupata taarifa kutoka ndani ya wodi, jasho jembamba lilikuwa likitiririka mwilini
mwake.
“Mh! Mungu wasaidie wanangu, naamini hapa ndipo mahali ambapo watarejewa na fahamu zao na maisha yao kuendelea tena hata kama itanigharimu kia…”
alisema lakini kabla hajamalizia sentensi yake, macho yake yalishuhudia mlango wa wodi ya wagonjwa mahututi ukifunguliwa, yule daktari aliyewapokea wale
watoto akatokeza.
Kwa mbali akanyoosha mkono wake kwa ishara na kumwita Fedorov.
“Niambie daktari, umegundua tatizo gani?”
“Mh, baada ya kufanya uchunguzi wa kina tumegundua tatizo.
“Ahsante, ahsante sana daktari na Mungu akubariki. Je, mmegundua nini tatizo?”
“Uchunguzi tuliofanya umebaini kuwa watoto wako walipigwa na kitu kizito kichwani au walianguka kutoka umbali mrefu kwani kuna baadhi ya mishipa
imepasuka na kufanya damu kuvilia kwa ndani. Hilo ndiyo hasa tatizo kubwa linalowasumbua.”
Sentensi hiyo ilipenya moja kwa moja masikioni mwa Fedorov, kumbukumbu ya namna watoto wake walivyorushwa kutoka garini na kudondoka chini kama
mizigo ikamjia kichwani mwake kama sinema.
“Mzee! Mzee tafadhali ongea na mimi.”
“Mh! Inawezekana kabisa daktari lakini hilo si la muhimu sana kwangu, ninachotaka ni kuokoa maisha ya wanangu, basi.”
“Hivi ninavyoongea na wewe tayari wanaandaliwa ili kuingizwa chumba cha upasuaji tukajaribu kutoa hiyo damu iliyovilia.”
“Daktari watapona?” lilikuwa ni swali jingine kutoka kwa Fedorov, tayari daktari alishaanza kuondoka eneo hilo kurejea ndani ya chumba cha upasuaji.
“Tuombe Mungu lakini pia tutahitaji utie saini sehemu fulani ya fomu zetu ili kukubaliana na suala la wanao kufanyiwa upasuaji.”
“Nipo tayari daktari,” alijibu Fedorov huku mapigo yake ya moyo yakibadilika kwa kasi.
***
Mapumziko ndani ya chumba yalifanyika kwa dakika tano tu baada ya Lina kulia na kumbembeleza sana Phillip akidai kuwa amechoka. Baada ya dakika tano
kuisha kazi ilianza upya. Phillip alitaka kuonesha kwamba alikuwa ni mwanaume wa kuotea mbali, hakika hakutaka kumpa Lina nafasi hata kidogo, jambo
lililozidi kummaliza nguvu.
“Mpenzi kwa leo inatosha, tafadhali nisikilize mimi ni wako tutafanya…”
“Mwaaa!Mwaaa!” Phillip alimmwagia Lina mabusu mfululizo.
Shughuli ilikuwa pevu kwani wawili hao walicheza ‘rigwaride’ kwa saa tano, Lina akionekana kuwa taabani. Hata sauti nayo ilishakatika kwa kulalama.
“Nakupenda Lina ndiyo maana nafanya yote haya.”
“Mi…mi…pi..a” alijibu Lina.
“Nataka kuona nini mwisho wake.”
“Uta..niu.a…utani..ua.”
“Nataka kukupa raha ambayo nina hakika hukuwahi kuipata, leo ndiyo leo…” Phillip alizidi kujitapa huku akimpa Lina mambo, aliendelea kufanya hivyo mpaka
saa saba zilipokatika, akakubali kushuka na kumwacha Lina huru baada ya kuridhika kabisa. Lina alilala kimya kitandani, macho na miguno ndiyo vitu pekee
vilivyomfanya Phillip aamini kuwa bado alikuwa hai.
“Ahhhhh!” Phillip alishusha pumzi ndefu, akasogea pembeni mwa Lina na kuketi kitako huku akimwangalia kwa jicho la husuda.
“Nakupenda sana Phillip.”
“Nakupenda pia Lina.”
“Ahsante kwa mapenzi matamu, kweli leo nimekuaminia.”
“Ha!Ha!Haaa!” Phillip alicheka huku akijifuta jasho kwa taulo lililokuwa pembeni.
“Kweli sikutanii, hapa nilipo nipo hoi bin taaban sijiwezi kabisa.”
“Ahsante mke wangu.”
“Phillip,” Lina aliita kwa sauti ya upole.
“Yes baby,” Phillip akajibu.
“Ninalo wazo kichwani mwangu.”
“Unataka kuniacha tena?”
NDANI ya chumba cha upasuaji kulikuwa na hekaheka, madaktari wasiopungua watano wakiambatana na wauguzi waliingia na walionekana kuwa na hamu
kubwa ya kutaka kuokoa maisha ya watoto wawili pacha waliolala kitandani bila kujitambua pamoja na kwamba walikuwa wagonjwa, uzuri wao ulionekana
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wazi. Si madaktari wala wauguzi waliokuwa na tumaini juu ya watoto hao, lakini walitaka kujaribu.
“Watoto waandaliwe kwa ajili ya upasuaji.”
“Tayari daktari.”
“Basi hakikisheni kabla ya yote mashine za hewa ya oksijeni zifungwe ili kuwapatia hewa safi haraka sana,” ilikuwa ni sauti ya daktari mmoja aliyekuwa karibu
na kitanda cha mtoto mmoja.
“Sawa daktari tunafanya hivyo.”
“Wengine wagawanyike waende kwenye mashine nyingine haraka.”
“Hakuna shida.”
Haikuchukua hata sekunde mbili tayari watoto hao midomoni mwao zilishafungwa mashine hizo ili kuwasaidia kupata hewa safi.
Mambo yote hayo yalifanyika chini ya uangalizi maalum wa madaktari wao ambao ndiyo walioshika usukani wa kuendesha kila kitu ndani ya wodi na baada ya
kuhakikisha kwamba maandalizi yalitosha nao pia walijiweka sawa kwa kazi.
Vifaa vyote muhimu vilisogezwa karibu, hakika kwa kuviangalia vifaa hivyo, kwa mtu mwenye akili timamu lazima ungeingia woga.
“Ni vyema tukaanza kazi sasa, ni lazima tufanye kila kinachowezekana kuokoa maisha ya watoto hawa, ni wazuri mno kufa…sawa jamani?”
“Hakuna shida daktari lakini pia bila kumshirikisha Mungu hakuna kitakachokwenda sawa,” aliongea muuguzi mmoja aliyekuwa pembeni, naye pia alionekana
kuwaonea huruma watoto hao.
Zoezi likaanza, visu na mikasi ikipita huku na kule ni jambo hilo pekee ndilo lililoonyesha kwamba watu ndani ya chumba hicho walikuwa bize kupindukia. Saa
ya kwanza ikapita hatimaye ya tatu bado madaktari wakihangaikia kutoa damu iliyokuwa imevujia ndani ya ubongo wa watoto hao.
***
Nje ya wodi mambo kwa Victor Fedorov yalikuwa magumu, muda wote alikuwa akizungukazunguka huku na kule bila kutulia sehemu moja, alitaka kufahamu
ni kitu gani kiliendelea ndani ya chumba, hivyo muda wote macho yake hayakubanduka kwenye mlango wa chumba cha upasuaji.
Kwa saa tano aliendelea kubaki hapo, mwisho akaanza kukata tamaa kwani hakuwepo muuguzi wala daktari aliyetoka wodini.
“Kinaendelea nini humo?” aliuliza na sauti hiyo ikapenya moja kwa moja masikioni mwa mlinzi wake, huyo ndiye aliyekuwa hapo kumfariji.
“Bosi tuwe wavumilivu nahisi kazi ni kubwa.”
“Mh! Hapana moyo wangu unahisi hatari.”
“Kama ipi?”
“Sidhani kama watoto wangu watapona tena, hakika hawataamka.”
“Hapana lakini wewe siyo Mungu, hebu tumwachie yeye kila kitu anaweza,” mlinzi wake alizidi kumtia moyo na kumfariji wakati wote.
“Uwii! Mamaaa! Wananguuuu jamani…” Fedorov aliangua kilio, uvumilivu ulionekana kumshinda kabisa.
Saa saba baadaye bado hawakuona mtu, hofu ikawafunika mioyoni mwao nao pia wakashindwa kuelewa ni kitu kilikuwa kimetokea ndani ya chumba kwani
isingekuwa rahisi mpaka wakati huo asitokee mtu yeyote.
“Pengine wamepitia mlango mwingine,” aliongea Fedorov.
“Hapana mlango ni huu mmoja na kama kuna tatizo ni lazima watupe taarifa sisi wahusika.”
“Pengine wanaogopa au hawajui wataanzia wapi.”
“Bosi si rahisi, ni lazima watueleze tena bila kificho.”
“Basi tusubiri tuone,” aliongea Fedorov, tayari alishanyamaza kulia kwani maneno aliyopewa na kushauriwa na mlinzi wake yalionekana kuingia kichwani
mwake.
Wakiwa katika hali ya kupigwa butwaa, wakashuhudia mlango wa chumba cha upasuaji ukifunguliwa na machela ikitolewa na nyingine ikifuata kwa nyuma,
Victor Fedorov akaamini kwamba hao walikuwa ni watoto wake.
“Hao hapo,” alisema kwa sauti huku akisogea karibu kuhakikisha kama alichokuwa akikiona kilikuwa sawa au ni ndoto za mchana.
Akionekana mwenye mawazo mengi na wasiwasi, akatembea kwa unyonge na kusogea karibu lakini muuguzi aliyesukuma machela hiyo alionyesha wazi
kupingana na kitendo cha Fedorov kusogea karibu huku akimweleza wazi kwamba awe mvumilivu na muda si mrefu atapewa ruhusa ya kuwaona watoto wake.
“Wanaendeleaje?” aliuliza tena.
“Majibu yote kaka utayapata kwa madaktari.”
“Wako wapi sasa?”
“Subiri kidogo utawaona,” aliongea muuguzi akizidi kusonga mbele.
Ni kweli alichokuwa ameelezwa na muuguzi, alipogeuza shingo yake kuangalia nyuma alishuhudia jopo kubwa la madaktari na wauguzi wakitoka,
alipowaangalia vyema aligundua simanzi lililokuwa mioyoni mwao, naye bila kusita alisimama na kuwasubiri wafike karibu na mahali alipokuwa ili awaulize.
“Daktari, hebu nielezeni juu ya hali za watoto wangu.”
“Mh! Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa damu iliyokuwa imeganda ndani ya kichwa na kazi imekuwa ngumu sana ndiyo maana tumechukua muda wa
saa saba, tunatumaini zoezi letu litafanikiwa kwa asilimia kubwa.”
“Watapona?” aliuliza Fedorov.
“Kazi yetu sisi ilikuwa ni kuondoa tatizo ambalo tumefanikiwa, mengine tumwachie Mungu…ah! Sijui unaweza kuja ofisi mara moja?” daktari alisema.
“Bila shaka,” alijibu Fedorov akiungana na madaktari kuelekea ofisini kwa ajili ya kupata maelezo zaidi.
Taratibu wakatembea na kuufikia mlango ambao ndiyo ulikuwa chumba cha daktari, akakaribishwa na kuingia huko na akaonyeshwa kiti ili aketi kwa
mazungumzo zaidi.
“Kwanza pole sana mzee wetu.””Ahsanteni poleni na ninyi.”
“Ah! Sisi ni kazi yetu kuhakikisha tunafanya kila kinachowezekana kuokoa maisha ya wagonjwa,” daktari mmoja alijibu akimwangalia Fedorov ambaye aliketi
pembeni, macho yake yakionesha wasiwasi mkubwa.
“Hawa mbele yako ni madaktari waliohusika na upasuaji wa watoto wako.”
“Ndiyo.”
“Kazi tumemaliza tunachosubiri sasa ni kuona kama tutakuwa tumefanikiwa.”
“Nahitaji kufahamu kama tu wataamka,” Fedorov aliuliza.
“Kuamka wataamka lakini ni baada ya saa ishirini na nne kuanzia sasa, yakupasa uwe mvulivu,” aliongea daktari mwingine.
“Saa ishirini na nne?” aliuliza kwa sauti.
“SAA ishirini na nne?” Aliuliza kwa sauti.
Muda wa saa ishirini na nne ulionekana kama miaka mitatu au minne kwa Fedorov, asingeweza kuvumilia kukaa mbali na watoto wake ambao kwake ndiyo
walikuwa ndugu pekee duniani.
“Daktari tafadhali naomba kwa ruhusa yako niwaone japo kidogo.”
“Mh! Kwa sheria za kidaktari haturuhusu mtu kufanya hivyo, yakupasa uwe mvumilivu mpaka baada ya saa hizo.”
“Lakini sitaweza, natamani kuwaona watoto wangu,”aliongea tena huku akibubujikwa machozi.
“Dk. Nyoshi mpatie ruhusa awaone japo kidogo tu pengine ataridhika.”
“Lakini daktari wewe mwenyewe unafahamu utaratibu wetu.”
“Najua ila nimemwonea sana huruma mzee huyu.”
“Sawa,”alijibu daktari huyo akinyanyuka kwenye kiti.
Taratibu mlango ukafunguliwa na daktari akaanza kumwongoza Fedorov kuelekea chumba cha wagonjwa mahututi.
“Daktari naweza kukuuliza tena?”
“Uliza tu hakuna shaka.”
“Nataka kujua kama watoto wangu watapona.”
“Kama nilivyokueleza mwanzo, kazi yetu sisi kama madaktari tumeifanya vizuri hiyo sehemu nyingine tumemwachia Mungu atende.”
“Fyuuu!” Fedorov akashusha pumzi kwa nguvu.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakaufikia mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi, mapigo ya moyo wa Fedorov yakaenda mbio mithili ya mtu aliyekimbia mita ndefu, walipomaliza
kufanya taratibu zote wakaingia ndani.
Baada tu ya kuingia, macho ya Fedorov yakapiga moja kwa moja juu ya vitanda viwili vikiwa vimezungukwa na mashine ya hewa ya oksijeni, machozi
yakambubujika.
“Mungu wangu!”Ndiyo sauti pekee iliyosikika.
“Kuna nini?” Daktari akauliza.
“Mariya! Merina,” alitamka majina ya watoto wake akisogea taratibu kuelekea kwenye vitanda hivyo huku macho yake yakishuhudia vichwa vya watoto hao
vikiwa vimefungwa bandeji na kuachwa sehemu ndogo sana upande wa macho.
“Daktari mbona kama wamevimba vichwa?”
“Ni kweli kabisa lakini vitarejea katika hali yake ya kawaida kadiri muda unavyozidi kusonga.”
“Mh!” Fedorov akaguna kuonyesha kuumizwa na hali hiyo.
Kwa takribani dakika tano waliendelea kubaki ndani ya chumba hicho, Fedorov akizunguka kitanda kimoja na kurudi kingine na mara kadhaa akitamka;
“Mungu, wasaidie watoto wangu napenda kuona wanapona…sitaki wafe nataka waishi…naomba unisaidie…”aliongea kwa sauti ya chini.
***
“Phillip,” Lina aliita kwa sauti ya upole.
“Yes baby,” Phillip akajibu.
“Ninalo wazo kichwani mwangu.”
Phillip akageuka na kuketi vizuri macho yake yote yakimwangalia mwanamke aliyekuwa amelala kitandani, hofu ikaonekana kuufunika moyo wake akitaka
kufahamu ni kitu gani hasa Lina alitaka kumweleza.
“Unataka kuniacha?” Akauliza.
“Haa!Haaa!Haaa!” Lina akacheka.
“Ninakuomba usije ukanieleza kitu cha kuumiza mtima wangu.”
“Phillip hivi unadhani ni rahisi hivyo?”
“Nini?”
“Kukuacha, nikuhakikishe siwezi si kwa sababu ya penzi ulilonipa leo la hasha lakini toka ndani ya moyo wangu ninakupenda na siko tayari kukukosa katika
maisha yangu.”
“Mh! Nieleze basi,” aliongea Phillip, tayari macho yake yalishabadilika na kuwa mekundu.
Lina akajivuta kutoka kitandani na kuketi karibu, akamuangalia na kuachia kuachia tabasamu.
“Kwanza naomba nikutoe wasiwasi mume wangu, ukweli ninachokueleza hapa ndiyo ukichukue na kukifanya kuwa ukweli, sikuwahi na wala sikufanya mapenzi
na Daniel si kwamba sikuweza ila nakuheshimu sana…”
“Ukweli?”
“Hakika.”
“Tukiwa katika harakati hizo nilikurupuka kutoka juu ya kitanda na kukimbia ndiyo maana nilitoka na shuka tu.”
“Mwaa! Nakupenda Lina.”
“Natumai nitakuwa nimekutoa wasiwasi juu ya hilo.”
“Ni kweli kabisa lakini umeniambia unalo wazo.”
“Mh! Unajua…nitapenda uuangane na mimi katika hilo.”
“Lina niondoe jakamoyo nililonalo.”
“Nataka tukubaliane ili tushirikiane kulifanya pamoja.”
“Nimeshakueleza niko tayari kwa lolote,”aliongea Phillip kwa kujiamini.
“Phillip nimefikiria sana juu ya mtoto, wazo pekee nililonalo nimeona tutafute mtoto wa kuasili.”
“Mh!”
“Kwa sababu ya tatizo ulilonalo ili mimi na wewe tuendelee kuishi na kupendana mpaka mwisho wa uhai wetu ni bora tuasili mtoto mmoja tu.”
“Unamaanisha unachokisema.”
“Hakika nimefikia hapo ili kulinda penzi letu.”
“Lina!” Phillip aliita.
“Na iwe hivyo.”
“Jinsia gani?” Phillip aliuliza.
“Chagua wewe.”
“Hapana.”
“Mimi binafsi napenda mtoto wa kike sijui wewe?”
“Hata mimi,” Lina alijibu na kumpiga Phillip mabusu mfululizo.
Takribani sekunde tano, Phillip alibaki kimya akizungusha akili yake, hakuwa tayari kukubaliana na maneno aliyoyasikia kutoka kwa mkewe Lina.
“Lina nimeamini kwamba kweli unanipenda, ahsante mke wangu ninaungana na wewe asilimia zote na ninakuahidi kulitunza penzi letu hadi mwisho Mungu
akiwa mlinzi wetu, sipendi na wala sitaki kukuudhi tena...” alimaliza Phillip akiachia mabusu mfululizo.
Ghafla kama mshale uliofyatuliwa, akamkamata Lina na kumlaza tena kitandani na wote kujifunika shuka gubigubi, kilichofuata baada ya hapo kilikuwa
hakielezeki wala hakiandikiki gazetini.
Zoezi hilo lilipokamilika Phillip akamshukuru Lina akimweleza wazi kwamba angeshirikiana naye bega kwa bega kukamilisha mkakati wao wa kupata mtoto wa
kumuasili.
“Kesho tutaanza taratibu zote, nataka ndani ya mwezi huu tupate mtoto wetu ambaye tutamlea vyema nasi tuingie katika ulimwengu wa kuitwa baba na mama.”
“Ahsante mke wangu, ahsante kwa kunipenda.”
“Nakupenda pia.”
MAMBO hayakwenda sawa kama madaktari na wauguzi walivyotarajia, saa zikazidi kusonga mbele, hatimaye saa sabini na nne zikakatika, watoto wa Fedorov
wakiwa bado hawajapata fahamu, hofu ikawafunika madaktari na wauguzi ambao muda wote walizunguka vitanda vya watoto hao mara kadhaa wakisikiliza
mapigo yao ya moyo kama yalikwenda sawa.
“Mh!” Daktari aliguna.
“Kuna nini daktari?”
“Mbona…hebu tena,” aliongea daktari akisikiliza mapigo ya moyo kwa ukaribu zaidi.
Mapigo ya moyo ya watoto hao wawili ambao walilala kitandani bila kujitambua hayakusikika sawia jambo ambalo hakika lilizidi kuwachanganya madaktari
wote ndani ya chumba, hofu ikatawala kwani kama kungetokea jambo lolote baya juu ya watoto hao walifahamu wazi kwamba wangekuwa na kesi ya kujibu.
“Wauguzi wawili wakae karibu na vitanda vya watoto hawa na wapime mapigo ya moyo kila baada ya dakika kadhaa, sawa!” aliongea daktari mmoja aliyekuwa
pembeni na jambo hilo likafanyika haraka.
“Mzazi wao bado yuko hapo nje?”
“Ndiyo tena yuko katika hali ya kuchanganyikiwa sana.”
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Najua lakini pia ni lazima apate taarifa na kufahamu ni kitu gani kinaendelea ndani ya wodi ili kama kuna tatizo litatokea basi awe amejiandaa,” daktari aliongea
akionyesha msisitizo.
“Daktari kwa nini unasema hivyo?” muuguzi aliuliza.
“Mh! Hakika sijawahi kufanya upasuaji halafu mtu akachelewa kutoka usingizini, huwa inachukua saa ishirini na nne tu kuamka lakini hii ni kiboko.”
“Kama sisi tumekata tamaa je, huyo mzazi wake itakuwaje?”
“Ndiyo maana nashauri mzazi huyo apewe taarifa ya kila kitu,” daktari alizidi kusisitiza.
Muafaka ukawa umefikiwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi, wauguzi na madaktari wakakubaliana kwamba ingekuwa vyema akafahamu maendeleo ya
watoto wake ili kama kungetokea tatizo lolote awe amejiandaa.
Lilionekana kuwa zoezi gumu lakini ilikuwa ni lazima wampe mzee huyo taarifa zote kuhusu watoto wake. Daktari mmoja akatoka wodini kwa kujiamini
kabisa akatembea na kumsogelea Federov aliyekuwa nje ya wodi akiwa amesimama pembeni tu karibu na mlango, kwa kumwangalia tu alionekana kuchoka na
kukata tamaa.
“Habari za leo mzee wangu?” Alimsabahi.
“Mh! Niambie habari za afya ya watoto wangu,” Federov badala ya kuitikia salamu moja kwa moja akatupa swali kwa daktari.
“Yakupasa ujikaze kiume, hali za watoto bado hazijategema na mpaka sasa hawajaamka.”
“Lakini mlisema wataamka baada ya saa ishirini na nne lakini zimeshapita kitambo.”
“Ni kweli kama madaktari na upasuaji tuliofanya tulifikiria jambo hilo lakini halijatokea, nasi pia hali hii inatuchanganya.”
“Daktari nataka kufahamu watoto wangu wataamka tena?” Aliuliza machozi yakimbubujika.
“Tunajitahidi kufanya jambo hilo…lakini…” kigugumizi kikamshika daktari na hakuweza kuimalizia sentensi yake akamshuhudia mzee huyo akiporomoka chini
kama mzigo.
“Mzee! Mzee,” daktari alimwita lakini tayari alishachelewa Victor Fedorov alishafika chini.
***
Mapenzi mazito yalikuwa yameshamiri kati yao, kila mmoja akimjali mwenzake kwa hali na mali akihakikisha hafanyi kosa kumuumiza mwingine, baada tu ya
kupewa msamaha na Lina hakutaka tena kurudi nyuma alikubaliana na mkewe ili tu kulinda penzi lake hivyo wazo alilotoa Lina la kuasili mtoto likapita moja
kwa moja na kukubalika, kazi moja tu ilibaki mbele yao ya kufanya taratibu zote ili kumpata mtoto huyo.
“Kesho tutaanza taratibu zote, nataka ndani ya mwezi huu tupate mtoto wetu ambaye tutamlea vyema nasi tuingie katika ulimwengu wa kuitwa baba na mama.”
“Ahsante mke wangu, ahsante kwa kunipenda.”
“Nakupenda pia.”
Kwa fedha walizokuwa nazo waliamini jambo hilo lisingekuwa gumu kwao hivyo utaratibu ukawekwa na siku iliyofuata tu asubuhi walidamka mapema na
kwenda moja kwa moja kwenye kituo cha watoto yatima cha Msimbazi Centre ambako walifanikiwa kuongea na sista mkuu wa kituo na akalipokea wazo lao
kwa mikono miwili na kufurahia sana lakini akawaeleza wazi kwamba kulikuwepo na taratibu za kufuata ili kumpata mtoto waliyemtaka.
Akawaweka wazi kwamba ilikuwepo fomu maalum ambayo walitakiwa kuisoma na kukubaliana nayo kisha kuijaza ambayo ilieleza kila kitu ikiwa na masharti
ambayo walitakiwa kukubaliana nayo na kikubwa zaidi ni kula kiapo kwa wakili ambaye angetafutwa.
“Tuko tayari mama hatuna shida,” walijibu kwa pamoja.
“Wakili anatakiwa kulipwa sijui mnafahamu jambo hilo?” sista mkuu aliuliza.
“Fedha ipo sista hakuna shida.”
“Basi hakuna tatizo naomba mnipe muda kwa siku ya leo niandae utaratibu wote kisha kesho asubuhi mnaweza kurejea tena hapa na kumaliza zoezi hilo nanyi
kuondoka na mtoto mtakayemchagua.”
“Ahsante sana,” Lina aliongea.
“Nina swali moja kwenu, mtoto mtayemwasili mngependa awe na umri gani?” Sista aliuliza.
“Kama atapatikana mtoto mchanga kabisa huyo atatufaa.”
“Mh! Mtaweza?”
“Tutaweza tunapenda tumlee wenyewe na akue akifahamu kwamba sisi ndiyo wazazi wake na si vinginevyo,” Phillip aliongea akionyesha msisitizo.
“Basi, nendeni na kesho mrejee hapa mapema sana mtakuta nimeshatayarisha kila kitu,” alimaliza sista mkuu na kunyanyuka kwenye kiti.
Phillip na Lina wakatoka ndani ya ofisi ya sista mkuu wakionyesha tabasamu, furaha ilikuwa imetawala mioyo yao wakifurahia kupata mtoto ambaye kwao
wangemlea vyema katika hekima, katika maisha yao Lina angeitwa mama na Phillip angeitwa baba.
“Ahsante Mungu hili nalo litafanyika nasi tutakuwa na heshima katika huu ulimwengu…nitampenda sana mtoto huyo nakuhakikishia sitamuumiza na zaidi ya
yote nitampa kila lililo jema…,” aliongea Phillip mfululizo Lina akimwangalia.
“Kesho asubuhi mimi nitakuwa wa kwanza kuamka nitakuamsha wewe.”
“Wewe nani alale mimi silali ng’o! Nitakesha, natamani sana kumpata huyo mtoto.”
“Mimi pia mume wangu niko pamoja nawe, mwaa! mwaa,” Lina aliongea na kuachia mabusu mfululizo kwa Phillip.
Wakatembea na kulifikia gari kisha wakaingia ndani yake, safari kuelekea kazini ikaanza, njiani wakiongea mengi kuhusu mpango wa kesho na kila mmoja
akionyesha furaha ya ajabu.
“KWANZA naomba nikutoe wasiwasi mume wangu, ninachokueleza hapa ndicho ukichukue na kukifanya kuwa ukweli.
Sikuwahi na wala sitafanya mapenzi na Daniel, si kwamba sikuweza ila ni kwa sababu nakuheshimu sana…”
“Lina nimeamini kwamba kweli unanipenda, ahsante sana mke wangu. Naungana na wewe kwa asilimia zote, nakuahidi kulitunza penzi letu hadi mwisho wa
maisha yetu, ninaomba Mungu awe mlinzi wetu, sipendi na wala sitaki kukuudhi tena,” alimaliza Phillip huku akimuachia mabusu mfululizo.
Ghafla, kama mshale uliofyatuliwa, Phillip anamkamata Lina na kumnyanyua juu, anamlaza tena kitandani na wote wanajifunika shuka gubigubi, kinachofuata
baada ya hapo hakielezeki.
Wanakubaliana kuwa siku inayofuata wafanye taratibu zote na kuzikamilisha ili wampate mtoto wa kuasili. Walikuwa na hamu kubwa ya kuitwa baba na mama.
Baada ya kufikia muafaka wa kuasili mtoto ambaye wangemlea vyema na kumtunza katika maadili ya Kitanzania.
Wanaendelea kucheza kitandani mpaka usingizi unawapitia.
Upande wa pili, watoto wa tajiri mkubwa nchini Urusi, Victor Fedorov wapo hospitali na bado hali zao ni tete.
Wanakaa kwa zaidi ya saa sabini na mbili bila kuzinduka. Hali hiyo inamtia shaka baba yao, Fedorov na haamini kama wanaweza kutoka ndani ya chumba cha
wagonjwa mahututi wakiwa hai.
“HA! ” Ilisikika sauti ya mtu akiguna ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi ambako watoto wawili mapacha, Mariya na Merina walikuwa wamelazwa.
“Kuna nini tena?” mwingine aliuliza.
“Ameamka huyu! Ameamka.”
“Mungu wangu! Kweli jamani.”
Jopo lote la madaktari pamoja na wauguzi waliokuwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi walisogea karibu na kitanda.
“Chafya!”
“Mh! Kweli, hakyanani vile pacha mmoja ameamka na kupiga chafya.”
“Kweli Mungu mkubwa,” alisema mmoja wa madaktari.
“Kwa jinsi hali inavyoendelea, hata huyu mwingine ataamka muda si mrefu.”
“Ona! Amefumbua na macho.”
“Kweli,” daktari mwingine alijibu na wote wakatabasamu.
Dalili iliyokuwa imeoneshwa na pacha mmoja ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi, ilimfurahisha kila mtu. Hofu iliyokuwa imeanza kutanda katika mioyo
yao ikaondoka na matumaini mapya yakafufuka.
Hakuwepo hata mtu mmoja aliyetaka historia mbaya juu ya upasuaji huo wa watoto iandikwe.
“Hebu tuendelee kusubiri, tukiangalia nini kitaendelea kwa huyu pacha mwingine, naye ataamka muda si mrefu.”
Maongezi yaliendelea ndani ya chumba hicho kila mmoja akisema lake juu ya upasuaji huo. Saa ya kwanza ikapita, matumaini ya pacha mwingine kuzinduka
yakawa yanazidi kuongezeka, waliamini kwamba muda si mrefu naye angeamka.
“Daktari ni vyema tukatoa taarifa kwa mzazi wake juu ya nini kinaendelea humu ndani,” alisema muuguzi mmoja..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hakuna shida anaweza kupata kibali cha kuingia na kujionea mwenyewe.”
Muuguzi mwingine akatembea na kufungua mlango wa kutokea ndani ya chumba hicho, akatokeza nje na kwa ishara akamwita mzee aliyekuwa ameketi chini
pembeni ya mlango wa kutokea ndani ya chumba hicho kwa ishara.
“Samahani kidogo tunakuomba,” sauti ya muuguzi ilipenya katika masikio ya mzee yule ambaye alikua ametawaliwa na uso wa huruma.
“Mh! Nini tena watoto wangu wameamka?” alihoji huku akinyanyuka.
“Tafadhali tunakuomba mara moja.”
Taratibu bila kusema kitu tena mzee yule akatembea na kuufikia mlango kisha kuuliza tena swali kama alilouliza mwanzo.
“Muuguzi nini kimetokea?”
“Hakuna matatizo kuna habari njema kwako.”
“Oh! Habari njema? Watoto wameamka?” Aliuliza.
“Mh! Ni mmoja lakini mwingine bado.”
“Hapana, kwa nini iwe hivyo?”
“Utapata maelezo yote ndani ya chumba hiki, tafadhali ingia ndani na ufuate taratibu zetu,” muuguzi alisema na kuanza kumwongoza Fedorov kwenye chumba
maalum.
Mbele kidogo Fedorov akapewa maelezo kisha kuvishwa nguo maalum ambazo ilizivaa na kuingia ndani ya chumba hicho.
Baada ya zoezi hilo kukamilika alianza kumfuata muuguzi ambaye alimwongoza moja kwa moja mpaka kwenye wodi ambayo alishuhudia umati wa wauguzi na
madaktari ukiwa pembeni ya vitanda kila mmoja akionesha furaha.
“Pole sana mzee wetu,”
“Mh!” badala ya kujibu Fedorov aliguna tu na taratibu akasogea katika moja ya vitanda ambavyo juu yake ndipo walipolala watoto wake Mariya na Merina.
“Mmoja wa pacha amepata fahamu zake japo bado hajaweza kusema kitu.”
“Yupi?”
“Huyo hapo.”
“Mariya!” Fedorov akamwita kwa sauti na kusogea karibu zaidi akiwa hapo akashuhudia mtoto huyo akifumbua macho kwa tabu kisha kuyafumba, machozi ya
furaha yakamtoka akainama na kumbusu kwenye paji lake la uso huku akiongea.
“Nakupenda sana mwanangu nataka wote mtoke turejee nyumbani kuendelea na maisha, sipendi mniache, wewe umeamka lakini Merina bado…ahsante Mungu
kwa kujibu sala zangu, sijui ningekuwa mgeni wa nani katika dunia hii, ahsanteni pia madaktari kwa kazi nzuri.”
“Usijali kikubwa tunachoomba ni huyu mwenzake naye aamke,”
“Tii! Tiii!” mlio ndani ya chumba ukasikika na kuwafanya watu wote wageuke kuangalia upande ulipotokea mlio huo.
Ilikuwa ni mashine ya hewa ya oksijeni iliyokuwa imefungwa kwa mtoto Merina ikionekana kusimama.
“Mungu wangu mashine inataka kusimama...”
***
“Ahsante mke wangu, ahsante kwa kunipenda.”
“Ahsante nawe pia.”
Safari ya kuelekea ofisini ikaanza furaha ya Phillip ikionekana wazi na mara kadhaa alikuwa akimgeukia Lina na kumweleza wazi kwamba alimpenda kupita
maelezo.
Nusu saa tu baadaye waliingia ofisini na kila mmoja kuingia mzigoni lakini vichwa vyao vilionekana kufikiria juu ya kesho yake, kwani walitaka kumaliza
mambo hayo haraka sana.
“Rafiki leo unaonekana una furaha sana, hebu niambie unafurahia kitu gani?” Rafiki mmoja wa Lina aliuliza.
“Maisha, hakuna kitu kingine, pia nimempata mume anayenipenda kwa dhati.”
“Mh! Mshukuru Mungu wako, mimi natamani kupata mume kama wako.”
“Wee huko unakoelekea siko, usije ukaja…” aliongea Lina lakini kabla ya kumalizia sentensi yake rafiki yake akaingilia kati.
“Ahaa! Rafiki siwezi bwana, Phillip ni shemeji yangu na atabaki kuwa hivyo maisha.”
“Unanitia mashaka, unamsifia mno…haa!Haaa,” Lina aliongea na kuachia tabasamu lililoambatana na kicheko.
Aliyekuwa ndani ya ofisi ya Lina alikuwa ni rafiki yake wa siku nyingi waliyesoma naye chuo Kikuu na hatimaye walijikuta pamoja tena katika ofisi moja lakini
kila mmoja akiwa kwenye kitengo chake.
Walipendana na kuheshimiana kwa kila kitu na huyo ndiye aliyekuwa msiri wake mkubwa, halikuwepo jambo lililoendelea kati yake na Phillip na rafiki huyo
asilifahamu.
“Mimi natoka nilikuja kukusalimu tu kwani ni muda sijakutia machoni.”
“Ahsante,” alijibu Lina kwa kutabasamu.
Saa zikazidi kusogea na hatimaye muda wa kutoka ukawadia, Lina akakusanya kila kilichokuwa chake, kabla ya kutoka ndani ya ofisi akanyanyua simu yake na
kubonyeza namba kadhaa, baada ya muda akaonekana akizungumza na mtu upande wa pili.
“Darling muda wa kuondoka umefika, nakuja kukupitia hapo sasa hivi, twende nyumbani tukampumzike,” alisema na kukata simu kisha akaanza kutembea
kutoka ndani ya ofisi yake.
Baada ya sekunde tatu tu alishafika nje ya mlango wa ofisi ya mumewe, akaugonga mlango.
“Karibu,” sauti iliskika wakati alipokamata kitasa cha mlango na kufungua mlango, macho yake yakatua kwa Phillip aliyekuwa ameketi ofisini kwake akionesha
tabasamu.
“Twende nyumbani tukampumzike kesho tunatakiwa kuwahi mapema sana kituo cha Msimbazi kukamilisha kazi.., sawa?” alisema Lina akionesha kumsisitiza
Phillip ambaye hakuwa na hiyana, akakusanya vitu vyake kisha akanyanyuka na kutoka nje kuelekea nyumbani.
Kwao usiku ulionekana kwenda taratibu mno, saa zikisonga pole pole lakini hatimaye asubuhi ikafika na wote wakajiandaa kwa safari, Phillip akiwa ndiye
dereva.
Saa moja na nusu walifika katika kituo cha Msimbazi na kuelekea kwenye ofisi ya sista mkuu aliyewapokea na kuwakaribisha ndani ya ofisi ambako walikuta
taratibu zote zimeshaandaliwa na mwanasheria aliyekuwa akiwasubiri.
Baada tu ya utambulisho mfupi sista mkuu akawaomba waanze utaratibu ili kwenda na wakati, wakapewa fomu maalum Phillip na mkewe wakaisoma vyema na
kuielewa kisha wakatakiwa kuijaza kwa ufasaha.
Kwa takribani dakika kumi nzima walifanya zoezi hilo na walipolikamilisha wakairejesha tena kwa sista mkuu ambaye akawauliza kama wameyakubali masharti
yote yaliyoandikwa ndani ya fomu hiyo.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tunakubaliana na yote yaliyoandikwa humo na tuko tayari kumtunza na kumlea mtoto tutakayemchukua hapa kwa nguvu na juhudi zetu zote, tunahakikisha
atapata maisha anayostahili.”
“Basi ni wakati wa ninyi kula kiapo mbele ya mwanasheria wetu.”
“Sawa sista,” walijibu kwa pamoja na baada ya muda wakala kiapo na zoezi hilo lilipokamilika sista mkuu akauliza walihitaji mtoto wa jinsia gani na umri
wake.
“Kuanzia miezi mitatu na awe wa jinsia ya kike.”
Sista hakuongeza tena neno lingine, akawataka wamfuate, akawaongoza mpaka kwenye chumba kimoja kilichokuwa karibu kabisa na ofisi yake.
Akawakaribisha na kuwaingiza ndani ambako kulikuwa na watoto wadogo wakiwa wamelala kwenye vitanda na wafanyakazi wachache wakiwa hapo
kuwaangalia.
Hapo walitakiwa kuchagua mtoto mmoja tu ambaye ndiye wangemchukua na kwenda kumtunza mpaka mwisho wa uhai wake, wakafumbua macho yao yote
kuwaangalia watoto hao ambao kwa kweli walikuwa wazuri mno.
“Mnachagua mmoja tu,” sista mkuu aliongea akitabasamu.
“Mh! Watoto wote wazuri sijui tuchukue yupi kati yao,” Lina alimuuliza Phillip.
“Huyu hapa anafanana na sisi,” alisema Lina.
“Sawa…sista huyu ndiye tuliyemchagua,”
aliongeza Phillip akimnyanyua mtoto mzuri aliyekuwa amelala kitandani, alikuwa ni mdogo lakini uzuri wake ulionekana wazi
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment