Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

MSICHANA NDOTONI MWANGU - 5

 





    Simulizi : Msichana Ndotoni Mwangu

    Sehemu Ya Tano (5)



    -

    MAMBO hayakuwa kama walivyotarajia kwamba baada ya saa kadhaa mtoto huyo angeamka na kuungana na mwenzake, saa ya kwanza ikapita na sasa ilikuwa



    ikielekea ya pili, Victor Fedorov uvumilivu ukaanza kumshinda akajikuta akimwaga machozi kama mtoto mdogo, kazi ya wauguzi ndani ya chumba ikawa ni



    kumtuliza wakimtaka awe mvumilivu.

    “Lakini ni muda mrefu sana mbona mwenzake amesharejewa na fahamu?” aliuliza akisogea karibu kabisa na kitanda cha pacha ambaye hakuonyesha dalili



    yoyote ya kuamka.

    “Ataamka, kuwa mvumilivu.”



    “Mbona kama ni upasuaji umefanyika kwa saa sawa iweje yule aamke na huyu bado?” bado aliendelea kuuliza maswali mfululizo.

    “Tafadhali tunaomba sasa mzee utupishe tuendelee na matibabu yetu tutakuwa tukikujulisha kila kitu kadiri muda unavyokwenda tunaomba uende nje,” aliongea



    daktari mmoja, muuguzi aliyekuwa karibu na Fedorov akamshika mkono na kumwongoza kutoka nje naye pia akijaribu kuongea maneno ya kumpa faraja.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee huyo akatoka akilia, mawazo na akili zake zote zilikuwa juu ya mtoto wake huyo ambaye hakuonyesha matumaini, akatembea hatua ya kwanza na ya pili



    kisha akageuka nyuma kuangalia mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi.

    “Sitakwenda popote nitakaa hapahapa mpaka mwisho nataka kujua nini kinaendelea,” aliongea Fedorov akiketi chini, akiwa hapo haikupita hata sekunde tatu



    mlinzi wake naye akaungana naye, pia akijaribu kumfariji mzee huyo lakini zoezi hilo lilionekana kuwa gumu.



    “Naumia, moyo wangu una wasiwasi mkubwa sana juu ya mtoto wangu…sijui kama ataamka…lakini kama kuna kitu kibaya kwa nini wanifiche? Nataka



    wanieleze ukweli ili nijiandae kwa tatizo linalokuja,” aliongea akibubujikwa machozi.

    “Hapana bosi hawezi kufa, Mungu mkubwa anatenda.”

    “Najua hilo lakini kwa sasa nimekata…….”

    “Hutakiwi kukata tamaa unachotakiwa kufanya hivi sasa ni kuamini kwamba naye pia ataamka, mimi ninaamini kwamba yuko katika mikono ya madaktari



    bingwa atapona tu.”

    “Mh! Labda hebu tuone,”aliongea Fedorov akijifuta machozi.



    ***

    “Mnachagua mmoja tu,” sista mkuu aliongea akitabasamu.

    “Mh! Watoto wote wazuri sijui tuchukue yupi kati yao,” Lina alimuuliza Phillip.

    “Huyu hapa anafanana na sisi.”

    “Sawa…sista huyu ndiye tuliyemchagua.”



    Mabusu mfululizo yakatua kwenye paji la mtoto waliyemchukua, alikuwa ni mtoto wa jinsi ya kike, pamoja na kuwa mtoto mdogo uzuri wake ulionekana wazi,



    rangi ya ngozi yake ilifanana kabisa na ya Phillip, furaha ya ajabu ikatawala, hakuwepo hata mtu mmoja kati yao aliyeamini kwamba sasa wangekuwa wakiitwa



    baba na mama wa mtoto waliyemuasili kutoka katika Kituo cha Msimbazi.

    “Tutamlea na kumtunza mpaka mwisho wa uhai wetu tukimpatia kila aina ya mahitaji,” Phillip aliongea akimwangalia sista mkuu.

    “Ombi letu kwenu ninyi ni hili hapa,” sista aliongea.

    “Ndiyo sista tunakusiliza.”



    “Tutakuwa tukihitaji kumtembelea mtoto huyu kila baada ya mwezi mmoja kujua na kufahamu anaendeleaje, hiyo ni moja ya sheria zetu mpaka atakapofikisha



    umri wa miaka kumi na nane ambapo tutakuwa huru kumwacha aendelee na maisha yake kwani atakuwa ni mtu mzima.”

    “Hilo halina shaka sista na kama inawezekana tunaweza tu kuongozana mpaka nyumbani.”

    “Nitawapa mtu ambaye mtaongozana naye mpaka huko kwa ajili ya kupafahamu na kama kutatokea mabadiliko yoyote yawe ya kuhama nyumba au kwenda nje



    ya nchi ni vyema mkatujulisha mapema, sawa?” sista mkuu aliuliza.



    “Tumesikia,” Phillip na Lina walijibu kwa pamoja na kuanza kutoka nje ya chumba kuelekea ofisini kwa sista mkuu ambako wangekamilisha taratibu zote kisha



    kuondoka na mtoto waliyekuwa naye.

    Taratibu maalum zikafanyika ikiwa ni pamoja na kupigwa picha na kutia saini kwenye makubaliano yote yaliyofanyika ofisini kisha wakakabidhiwa mtoto na



    sista mmoja ambaye wangeongozana naye mpaka mahali wanapoishi. Wakatoka na kumshukuru sista kisha kutembea kuelekea sehemu waliyokuwa wameegesha



    gari, Phillip ndiye alikuwa dereva na Lina aliketi kiti cha nyuma akiwa amempakata mtoto.



    Gari liliendeshwa na kwa muda wa saa moja tu walifika nyumbani kwa Phillip na Lina wakamkaribisha sista waliyeongozana naye wakimweleza wazi kwamba



    hapo ndipo palikuwa nyumbani kwao ambako mtoto waliyekuwa wamemwasili angeishi maisha yake yote akitunzwa na kulelewa vyema.

    “Karibu sana sista hapa ndipo nyumbani kwetu ambako mtoto huyu atalelewa na kuishi, akitunzwa kwa hali na mali.”

    “Mh! Ahsanteni sana nafurahi kupafahamu tutakuwa tukija kila mwezi kumtembelea ili kujua maendeleo yake.”

    “Karibuni sana.”



    Dakika kumi na tano baadaye sista aliyeongozana na Phillip na Lina aliaga na kuondoka akiahidi kurejea tena baada ya mwezi mmoja kujua hali ya mtoto huyo.



    Wakamsindikiza kisha akaondoka.

    Kwa siku nzima walishinda ndani ya nyumba wakipanga mipango yote na jinsi ya kumlea na kumtunza mtoto huyo. Lina akatoa wazo kwamba ni vyema



    wangemtafuta mfanyakazi wa ndani ambaye angekuwa tayari kumlea mtoto huyo na wao wangemlipa mshahara ambao angeutaka.



    “Ni lazima atafutwe mtu wa kumlea mtoto huyu kwa upendo wote,” Lina aliongea.

    “Kabisa, lakini nashauri awe mtu mzima kidogo.”

    “Jinsi ya kumpata sasa ndiyo tatizo, sijui tuanzie wapi?”

    “Hebu subiri kidogo,” Phillip aliongea akinyanyuka kitini kuelekea chumbani.







    PHILLIP alitembea moja kwa moja na kuelekea mlango wa chumba chao akaingia na haikumchukua hata sekunde tatu tayari akawa amerejea akamsogelea Lina



    aliyekuwa ameketi bado sebuleni akimsubiri.

    “Soma hapa,” shika hiki kipande cha gazeti halafu nitakuonyesha kitu.

    Lina bila kusema kitu akionyesha kushangazwa na mumewe akanyoosha mkono wake na kupokea kipande hicho kisha kutulia akisikiliza maelekezo.



    “Ndani ya kipande hicho kuna tangazo la kampuni inayowatafutia watu wafanyakazi wa majumbani.”

    “Mh! Wewe ulikitoa wapi na ulijuaje kama tunaweza kutafuta mfanyakazi siku moja?” Lina aliuliza akiachia tabasamu.

    “Si unajua tena sisi watu wenye upako huwa tunaona vitu mapema sana kabla…,” aliongea Phillip akimwangalia Lina na kuachia tabasamu.

    Lina akakodoa macho yake na kuanza kusoma kipande hicho cha gazeti, ghafla akakutana na tangazo hilo akalisoma kwa umakini wa hali ya juu mpaka mwisho



    na kukutana na namba za simu kwa ajili ya mawasiliano kama tu mtu angehitaji mfanyakazi.



    “Mh! Hili liko safi tena wako wa aina mbili kike na kiume sijui yupi mume wangu?” Aliuliza Lina.

    “Wewe acha utani wako mwanaume wa nini hapa ndani ataweza kulea kweli?”

    “Anaweza kwani si sheria na masharti tu.”

    “Hapana tutafute wa kike,” aliongea Phillip akijilaza kwenye sofa.



    Lina akanyoosha mkono wake na kuchukua simu yake ya mkononi kisha kuanza kubonyeza namba kadhaa na kuweka simu sikioni, haikumchukua hata sekunde



    mbili tayari upande wa pili ukasikika.

    “Ndiyo naitwa Lina napiga simu kutoka hapa hapa Dar es Salaam, nimesoma tangazo lenu na nahitaji kupata mfanyakazi wa ndani ambaye umri wake ni mkubwa

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kidogo atakayeweza kulea vyema mtoto mdogo,” alimaliza Lina.

    “Hakuna shida dada yupo anapatikana sijui unamhitaji kwa lini?”



    “Hata leo ikiwezekana.”

    “Basi ni vyema ukatueleza wewe unapatikana wapi nasi tutakuja moja kwa moja nyumbani kwako na watu wawili kisha wewe utamchagua mmoja,”

    “Sawa.”

    Zoezi hili likawa limekamilika Lina akatoa maelekezo ya jinsi ya kufika nyumbani kwao na watu hao wakakubaliana naye na kumweleza wazi kwamba baada tu



    ya nusu saa wangefika nyumbani hapo.



    “Unajua nini mke wangu?”

    “Mh!”

    “Ubongo wangu unazunguka kuhusu majibu ambayo tutawapa watu wakitaka kufahamu juu ya huyu mtoto wetu tuliyemwasili?”

    “Mume wangu siku zote huwa watu hawakosi cha kusema wataongea na kujiuliza maswali mengi sana juu ya mtoto wetu lakini mwisho watanyamaza, hili



    litabaki kuwa jambo la familia na si vinginevyo.”



    “Mwaa! Mwaa! Mwanamke una akili sana wewe,” Phillip aliachia mabusu mfululizo kwenda kwa Lina ambaye naye aliyapokea kwa bashasha huku akinyanyuka



    na kutembea kwa madaha kuelekea sebuleni kumwangalia mtoto mchanga aliyekuwa amelala.

    “Bado amelala huyu,” sauti ya Lina ilisikika kutoka chumbani.

    “Basi njoo tuendelee kuongea hapa tukisubiri wageni.”

    “Sawa nakuja lakini mume wangu jambo moja hatujalifanya bado.”



    “Lipi hilo?” Phillip aliuliza kwa kutahamaki.

    “Hatujampa jina mtoto wetu.”

    “Hebu anza wewe kutoa la kwako,” Phillip alimwambia Lina.

    “Wewe kama baba wa familia unatakiwa useme na mimi nitafuata.”



    “Kutoka ndani ya moyo wangu mimi napenda sana mtoto huyu aitwe Genevieve.”

    “Saaaafi!” Lina aliongea kwa sauti.

    Hiyo pekee ilitosha kabisa kuonyesha kwamba jina hilo lilikuwa limepita moja kwa moja bila kipingamizi kwa pamoja wakanyanyuka na kukimbilia chumbani



    alikolazwa mtoto.



    ***

    “Nashauri huyu mtoto afanyiwe CT-Scan kuangalia tena upya mfumo mzima wa kichwa chake huenda kuna tatizo ambalo halikuonekana wakati wa upasuaji wa



    mwanzo,” aliongea daktari mmoja ndani ya chumba baada ya kuona kwamba hali ilikuwa si nzuri kwani saa nyingi zilishapita na tumaini la kurejewa na fahamu



    kwa mtoto mwingine halikuwepo.

    “Huo ni uamuzi mzuri.”

    Haraka akapandishwa katika machela na kuanza kusukumwa kuelekea kwenye chumba ambacho kipimo hicho kingefanyika na kutoa picha kamili ya tatizo



    ambalo lingeonekana.



    Mchakato mzima ukafanyika haraka picha ikachukuliwa na majibu hayakuchukua muda mrefu sana yakarejeshwa tena kwa madaktari ambao waliisoma vyema



    ripoti hiyo.

    “Mungu wangu!”

    “Nini tena?”

    “Mh! Haya majibu nakosea au nasoma sawa?”

    “Ni sawa kabisa daktari hivyo ndivyo yalivyo.”



    “Kwa hiyo?”

    “Hatuna jinsi ni lazima tufanye tena upasuaji ili kumsaidia huyu mtoto vinginevyo atakufa.”

    “Kwani kilitokea nini mpaka kuacha bonge hili la damu?”

    “Huu si wakati wa kulaumiana ni wakati wa kuokoa maisha ya mtoto huyu jamani mimi nashauri maandalizi yafanyike haraka sana na kazi ianze mara moja.”

    “Mzazi wake je?”



    “Ni lazima apewe taarifa na akubali jambo hili vinginevyo atampoteza mtoto wake.”

    “Sawa aitwe na kuelezwa kila kitu.”

    Muuguzi mmoja akatoka mbio na kumwita Fedorov akimtaka aingie ndani ya chumba ili kuongea na madaktari dakika moja tu baadaye watu wawili wakaingia



    ndani alikuwa ni muuguzi na Fedorov bila kupoteza muda daktari mmoja akamweleza wazi kwamba ililazimu mtoto wake arejeshwe tena chumba cha upasuaji



    haraka ili kuokoa maisha yake kwani picha iliyochukuliwa ilionyesha wazi kwamba kulikuwepo tatizo na kama tu wangezidi kumchelewesha basi asingeamka



    milele.



    “Mungu wa…ngu…sa…fari hii..hatapo…” Fedorov aliongea kwa sauti ya kukatikatika huku machozi yakumbubujika, macho yake yakashuhudia machela



    ikisukumwa haraka kutoka nje ya wodi hiyo kuelekea chumba cha upasuaji.











    MTOTO aliyeingia katika maisha ya Phillip na Lina na kupewa jina la Genevieve alikuwa ameleta furaha kubwa sana katika ndoa hiyo, kwani walimpenda kupita



    kawaida wakihakikisha wanampatia kila kilichohitajika katika maisha yake.

    “Genevieve, hatimaye jina hili limerudi tena katika maisha yangu,” alitamka Phillip kwa sauti ya juu.

    “Naam, hilo ndilo litakuwa jina lake.”



    “Ahsante Lina hii itakuwa kumbukumbu kwa mpenzi mke wangu ambaye aliondoka duniani nikiwa bado nampenda, mtoto huyu ameziba kabisa pengo lake.”

    “Ninafurahi pamoja na wewe mume wangu, siku zote haja ya moyo wangu ni kukuona unayo furaha kama hii,” Lina aliongea akitabasamu.

    “Nitampenda mtoto huyu mpaka kufa.”

    “Naungana na wewe lakini ninalo swali moja kwako Phillip.”



    “Endelea.”

    “Nataka kujua kama utanipenda kwa dhati kama ilivyokuwa mwanzo.”

    “Lina! Hakika nakuhakishia kutoka moyoni mwangu kwamba ninakupenda mno.”

    “Ahsante kwa penzi lako Phillip, hebu twende chumbani mara moja,” aliongea Lina huku akimwangalia mumewe na kuachia tabasamu. Ni Lina aliyekuwa wa



    kwanza kusimama na kumsogelea mumewe kisha kumshika mkono na kumnyanyua kutoka kitini wote wakaanza kutembea kuelekea chumbani.



    Kilichoendelea ndani ya chumba hakika kilikuwa hakielezeki wala kuandikika gazetini, kwani miguno na mihemo ya kila aina iliendelea kwa muda wa saa nne



    mfululizo, kilichowashtua hapo ilikuwa ni sauti ya honi ya gari nje ya lango lao, kwa sababu walifahamu kwamba mlinzi alikuwepo kwa kazi hiyo wao



    waliendelea na shughuli zao.

    “Lina sasa inatosha bwana.”



    “Hapana, mimi bado sijachoka.”

    “Wewe mtoto ataa…” aliongea Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake wakasikia sauti ya mlango ukigongwa.

    “Bosi! Bosi kuna wageni hapa,” sauti ya mlinzi ilisikika.

    “Nenda wewe mimi mpaka nikaoge.”



    “Sawa hakuna shida mke wangu,” Phillip aliongea huku akisogelea bukta yake iliyokuwa pembeni kisha akaiweka mwilini na taratibu akafungua mlango na



    kutembea kuelekea sebuleni ambako alifungua mlango na kukutana na sura ngeni za watu watatu na mtu wa nne akiwa mlinzi.

    “Karibuni,” aliongea.

    “Ahsante sana, nadhani hatujakosea, hapa ndiyo nyumbani kwa Phillip.”

    “Ni kweli kabisa karibuni sana.”.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Oke, sisi ni wale watu mliotupigia simu muda mchache uliopita mkihitaji mfanyakazi tuko hapa.”

    Wakaingia ndani na mlinzi kurejea sehemu yake ya kazi, haikuchukua hata sekunde tatu Lina naye akaungana nao sebuleni, mazumgumzo maalum yakaanza na



    hatimaye wakatakiwa kuchagua mtu mmoja kati ya wawili waliokuwepo hapo.

    “Sisi tunamchagua huyu hapa,” waliongea karibu kwa pamoja.



    “Hakuna shida hata sisi tulipendekeza huyuhuyu.”

    “Karibu sana mama sijui unaitwa nani?”

    “Naitwa Magdalena Simon, mwenyeji wa Rukwa na nimezaliwa miaka arobaini na saba iliyopita.”

    “Mh !” Phillip na Lina wakaguna, mwanamke huyo alikuwa ni mtu mzima si kwa mtoto mdogo tu bali hata kwao.

    “Mama utaweza kazi ya kulea mtoto kweli? Na je wewe katika maisha yako ulibahatika kupata mtoto?” Lina aliuliza akikodoa macho kumwangalia mwanamke



    huyo.



    “Mh! Mh! Hapana !” mwanamke huyo alijibu na walipomwangalia vyema usoni mwake waligundua alikuwa akibubujikwa machozi.

    “Basi mama sisi tunakupokea kwa mikono miwili ukae nasi na ulee mtoto wetu umpe mapenzi yote.”

    “Ahsante.”



    Makubaliano yakafanyika wakatakiwa kulipa kiasi cha fedha ambacho ndicho mwanamke huyo alitolewa kwao na wakamshukuru mtu aliyemleta mfanyakazi



    huyo huku akiwaeleza wazi kwamba angekuwa karibu nao kwa kila kitu kuhakikisha hapatokei tatizo lolote. Wakaaga na kuondoka.



    Wakampokea bibi Magdalena na kumwonyesha mambo yote yaliyomstahili ndani ya nyumba hiyo ikiwa ni pamoja na chumba ambacho angekitumia muda wote



    ambao angeishi hapo. Baada ya zoezi hilo wakamtaka aingie jikoni kuandaa chakula cha jioni hiyo ikiwa ni kama jaribio la kwanza kisha wao wakarejea



    chumbani.

    ***

    Upasuaji wa pili ulikuwa umefanyika kwa ufanisi wa hali ya juu na madaktari wakihakikisha halijirudii tena tatizo kama lililotokea mwanzo wakiomba Mungu



    mtoto huyo mzuri anyanyuke na kuendelea na maisha.

    “Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa, sasa atolewe humu na kurudishwa chumba cha wagonjwa mahututi.”



    “Sawa daktari,” wauguzi waliitikia, na bila kuchelewa machela ikaanza kusukumwa kutoka nje ya chumba ambako walimkuta Fedorov akiwa amesimama.

    “Oh! My God !” aliongea mzee huyo kwa sauti ya juu baada ya kuona bandeji iliyotapakaa damu ikiwa imefungwa kuzunguka kichwa cha mtoto wake.

    Machela ikapitishwa na wauguzi ambao hawakuongea kitu chochote zaidi ya neno moja tu.



    “Pole sana mzee.”

    “Ataamka baada ya saa ngapi?”

    “Saa kumi na mbili kuanzia sasa.”

    “Mh!” Fedorov aliguna hakika kwa kumwangalia tu mzee huyo ungegundua tu kwamba tayari alishachoka moyoni na tumaini lote lilishapotea katika maisha



    yake, mpaka kufikia hapo kwa umri aliokuwa nao hakuwahi kukutana na changamoto kubwa kama hiyo.



    Machela ikasukumwa na kuingizwa chumba cha wagonjwa mahututi pembeni tu ya pacha mwenzake ambaye kwa wakati huo tayari alishaanza kufungua macho



    na kuuliza maswali kadhaa japo kwa taabu akitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea.

    Victor Fedorov akatakiwa kusubiri nje ya chumba hicho kwa muda mwingine wa saa kumi na mbili.je nini kitaendelea? tukutane kesho kama kawa mwaaaaaaast



    gudnite all







    UPASUAJI wa pili ulikuwa umefanyika kwa ufanisi wa hali ya juu na madaktari wakihakikisha halijirudi tena tatizo kama lililotokea mwanzo, wakiomba



    Mungu mtoto huyo mzuri anyanyuke na kuendelea na maisha.

    “Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sasa atolewe humu na kurudishwa chumba cha wagonjwa mahututi.”

    “Sawa daktari,” wauguzi waliongea na bila kuchelewa machela ikaanza kusukumwa kutoka nje ya chumba ambako walimkuta Fedorov akiwa amesimama.



    “Oh! My God,” aliongea mzee huyo kwa sauti ya juu baada ya kuona bandeji iliyotapakaa damu ikiwa imefungwa kuzungukwa kichwa cha mtoto wake.

    Machela ikapitishwa na wauguzi ambao hawakuongea kitu chochote zaidi ya neno moja tu.

    “Pole sana mzee.”

    “Ataamka baada ya saa ngapi?”



    “Saa kumi na mbili kuanza sasa.”

    “Mh!” Fedorov aliguna hakika kwa kumwangalia tu mzee huyo ungegundua kwamba tayari alishachoka moyo na tumaini lote lilishapotea katika maisha yake



    mpaka kufikia hapo kwa umri aliokuwa nao hakuwahi kukutana na changamoto kubwa kama hiyo.



    Machela ikasukumwa na kuingizwa chumba cha wagonjwa mahututi pembeni tu ya pacha mwenzake ambaye yeye kwa wakati huo tayari alishaanza kufungua



    macho na kuuliza maswali kadhaa japo kwa taabu akitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea.

    Victor Fedorov akatakiwa kusubiri nje ya chumba hicho kwa muda mwingine wa saa kumi na mbili.





    “Paa! Paa! Paaa!” Ulikuwa ni mlio wa bastola ndani ya chumba kidogo chenye mwanga hafifu na mzee mfupi aliyejazia misuli akiwa amesimama mbele ya



    kijana mmoja akionekana mwenye hasira kali.

    “Usiniu…naomba uni…”

    “Unasema?”

    “Tafadhali mzee wangu kama ni huo mgawo wangu basi mimi nakuachia zote lakini wewe pia ufikirie maisha yangu.”



    “Ha! Haaaa!” Sauti ya kicheko kikali ikasikika tena mzee aliyesimama mbele ya kijana huyo huku akiwa amenyoosha bastola akashuka mkono wake na kuanza



    kutembea kumfuata mahali alipokuwa.

    “Simama,” alitamka kwa sauti ya ukali.

    “Mh!”

    “Ina manaa hujaelewa, nasema simama upesi.”



    Kijana yule bila kusema tena kitu akaanza kujivuta kutoka sakafuni na aliposimama tu wima vitu kama maji maji vilionekana kuchuruzika kutoka ndani ya



    suruali yake kwenda chini.

    “Hee! Umejikojolea?”

    “Nisamehe mzee wangu si kusudio langu ni bahati mbaya.”

    “Unaumwa?”

    “Hapana ni woga tu.”.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Lakini wewe ni mtoto wa kiume unatakiwa kuwa shupavu.”

    “Mh!” Kijana huyo alibaki akiguna tu huku akiwa amekodoa macho yote kumwangalia mzee huyo.

    Kwa ishara akaongozwa ili kusogelea meza ambayo juu yake ilikuwa na begi.

    “Fungua,” mzee huyo aliamuru.



    Taratibu kijana akalisogelea begi na kuanza kulifungua huku akionyesha hofu nyingi machoni mwake. Kwa sekunde tatu tu tayari alishamaliza kulifungua na



    idadi kubwa ya noti ikaonekana ndani yake.

    “Tayari mzee,” aliongea kwa sauti ya upole.

    “Sawa kabisa, sasa nisikilize vyema tena kwa umakini mkubwa,”

    “Ndiyo mzee.”



    “Kwa kuwa umeonyesha kufanya kazi vyema na mimi tena kwa ujasiri wa hali ya juu nikiamini kabisa kwamba hakukuwa na madhara yoyote yaliyotokea juu ya



    watoto, basi nakupa mgawo huu, uende ukaanze maisha na kumbuka mtu aliyesimama mbele yako si mtu mzuri hata kidogo, upande wake wa pili unatisha



    sitasita kutoa uhai wako pale utakapokuwa umenisaliti au kufanya jambo tofauti na kiapo chetu, mambo yote yaliyotokea ndani ya chumba hiki ilikuwa ni



    kukupima imani, nilitaka kujua jinsi unavyoweza kuhimili vishindo.”

    “Ndiyo mzee.”



    “Una hakika watoto wako salama? Nisingependa kusikia watoto wamekufa kwani hawana hatia hata kidogo, mwenye hatia ni baba yao ambaye nitashughulika



    naye mwenyewe.”

    “Mh! Mzee sina uhakika ila watakuwa wazima.”

    “Haya kamata hii halafu utokomee nisikuone mbele ya macho yangu,”aliongea mzee huyo akimkabidhi kijana maburungutu ya noti yasiyopungua kumi.



    Akazungusha macho yake huku na kule ndani ya chumba hicho na kufanikiwa kuona mfuko mmoja mchafumchafu, huo ndiyo aliutumia kuweka fedha zake zote



    alizokabidhiwa muda mfupi uliopita akamshukuru mzee huyo na kuanza kutembea kuelekea nje.



    “Kumbuka hutakiwi kusema kitu chochote juu ya maisha yangu, sawa?”

    “Sawa mzee hakuna shida.”

    “Tumia fedha hizo kuendeleza maisha yako, hivi sasa wewe ni mtu mzima.”

    “Ahsante mzee wangu nami pia nakutakia maisha mema, utakapokuwa na shida usisite kunitafuta...,” aliongea kijana huyo akitokomea.



    Hivyo ndivyo Ditrov alivyoagana na kijana huyo kisha kwa kujiamini kabisa akatembea kulisogelea begi lililokuwa juu ya meza akalinyanyua na kumwaga fedha



    zote juu ya meza.

    “Yap! Federov alikuwa hajui anacheza na mtu wa aina gani, hajui kwamba sisi tulishatangulia zamani, sasa asubiri kisasi changu ni lazima nitamtenda ubaya…,”



    aliongea Ditrov kwa kujiamini.



    ***

    Upasuaji ndani ya chumba ulifanyika kwa umakini mkubwa na hatimaye wakafanikiwa kulitoa bonge la damu lililokuwa limengandamiza ubongo wa mtoto



    Merina, wakarudisha kila kitu katika sehemu yake na wakamtoa kumpeleka chumba cha wagonjwa mahututi huku akiwa amefungiwa mashine ya hewa ya



    oksijeni ili kumsaidia kuvuta hewa safi.

    Muda wote huo Fedorov bado alikuwa nje ya mlango wa chumba hicho akizunguka huku na kule.



    “Ametoka!” alitamka baada tu ya kuona machela ikisukumwa kutoka ndani ya chumba cha upasuaji kutolewa nje.

    “Mzee tumefanikiwa kuondoa damu iliyoonekana na tunaamini sasa mtoto ataendelea vizuri lakini yahitaji saa kumi na mbili tena kupata fahamu zake,” aliongea



    daktari na machela ikasukumwa moja kwa moja chumba cha wagonjwa mahututi Fedovor akitakiwa kusubiri mpaka muda huo ufike na angepewa taarifa zote.



    Nje ya chumba hakutulia kabisa, alitaka kufahamu kila kitu kilichoendelea ndani ya wodi mara kadhaa akitupa macho kwenye saa yake ya mkononi kuangalia



    wakati hatimaye mpaka wakati huo saa kumi na mbili zilishapita hivyo mbele yake alikuwa na saa mbili tu muda alioelezwa na madaktari ufike na mtoto wake



    Merina kurejewa na fahamu. Macho yake yaliendelea kushuhudia wauguzi na madaktari wakitoka na kuingia kama vile walipeana zamu ndani ya chumba huku



    naye hofu ikimgubika likiwa limebaki saa moja tu mbele yake.



    ***

    “Baba! Baba!” Aliita kwa sauti iliyosikika ndani ya chumba.

    “Mh!” muuguzi ndani ya wodi aliguna kuonyesha mshangao wa ajabu kwani kitendo alichokishuhudia hakikuwa cha kawaida mtoto Mariya alikuwa



    amenyanyuka na kuketi kitako kitandani.

    “Amemwita baba yake,” waliongea wakisogea karibu na kitanda alichokuwa mtoto huyo.”

    “Unajisikiaje?” walimuuliza.



    “Merina! Merina”

    “Unaitwa nani?”

    “Namtaka baba yangu…Merina uko wapi?” aliongea mtoto huyo huku akinyanyua mikono yake na kushika kichwa chake akakutana na bendeji kubwa, hiyo



    ndiyo ilimfanya azidi kulia.

    “Baaaaba!” akapaza sauti.







    “Namtaka baba yangu…Merina uko wapi?” aliongea mtoto huyo huku akinyanyua mikono yake na kushika kichwa chake akakutana na bendeji kubwa, hiyo



    ndiyo iliyomfanya azidi kulia zaidi.

    “Baaaaba!” akapaza sauti.

    “Hebu mwiteni baba yake aje hapa haraka, hatakiwi kuongea muda mrefu kutokana na hali yake,” daktari aliongea kwa msisitizo na muuguzi akaonekana akitoka



    nje huku akikimbia.



    “Mzee tafadhali tunakuomba ndani ya chumba.”

    “Mh! Tatizo jingine tena,” aliongea tajiri Federov akinyanyuka kutoka chini alipokuwa ameketi, taratibu akatembea na kuingia ndani ya chumba ambako



    aliongozwa moja kwa moja mpaka mahali watoto wake pacha walipokuwa wamelala juu ya vitanda.

    Kwa macho yake akamshuhudia Mariya akiwa ameketi juu ya kitanda na alipotokeza tu mtoto huyo akaita tena kwa sauti ya juu.

    “Babaaa!”



    “Mwanangu, umeamka?”

    “Sogea karibu yangu baba.”

    Fedorov akasogea kisha akainamisha kichwa chake karibu kabisa na mwanaye, hapo akaachia mabusu mfululizo huku naye akilia.

    “Nini kimetokea baba? Kwa nini niko hapa? Merina, je, yuko wapi?”

    “Mh!” Watu wote ndani ya chumba waliguna. Hakukuwa na jibu kamili la kumpa Mariya kwamba pacha mwenzake alikuwa mgonjwa taabani muda mfupi



    uliopita.



    “Nataka kumwona Merina,” Mariya alizidi kusisitiza huku akizungusha kichwa chake huku na kule ndani ya chumba kama vile alikuwa akitafuta kitu fulani.

    Kwa nusu saa nzima walikuwa wamejaribu kumnyamazisha Mariya lakini ilionekana kushindikana, ni hapo ndipo daktari aliposhauri mtoto huyo aelezwe



    ukweli kwani kutokana na afya yake hakutakiwa kupata msongo wa mawazo ili kunusuru matatizo mengine yasitokee kwenye upasuaji wake wa kichwa.

    “Merina,” Fedorov aliita..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Mh!”

    “Merina yule pale, yeye bado hajaamka.”

    “Hajaamka? Kwa nini kalala mpaka sasa?”

    “La hasha si usingizi wa kawaida bali anaumwa.”

    “Anaumwa nini?” Aliuliza huku akizungusha mikono yake kushika sehemu ya kichwa.

    “Mwanangu hata wewe ni mgonjwa na hapa tulipo tupo hospitalini kwa muda sasa.”



    “Ina maana tunaumwa wote?”

    “Huo ndiyo ukweli.”

    “Basi nataka niende kumwona, si mmesema ndiye yule pale,” aliongea Mariya akielekeza kidole upande aliokuwa ameonyeshwa.

    Daktari aliyekuwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi akatakiwa kutoa ushauri kwani ili mtoto huyo anyamaze, ilikuwa ni lazima asogezwe mpaka karibu



    na kitanda cha pacha wake.

    “Kwa sababu kitanda kina magudurumu kisogezwe taratibu kwa uangalifu mkubwa mpaka pale ili akamwone mwenzake, nadhani baada ya jambo hilo ataacha



    kulia.”



    Ushauri uliotolewa na daktari ukafuatwa, taratibu kitanda kikaanza kusukumwa kuelekea eneo ambako kulikuwa na kitanda kingine ambacho juu yake alilala



    Merina akiwa hajitambui kabisa.

    “Huyu hapa Merina.”

    “Maskini wa Mungu kilitokea nini baba?”

    “Mlipata ajali mbaya, hiyo ndiyo iliyosababisha ninyi nyote kuwa hapa mkiwa mmeumia vibaya.”



    “Ajali! Baba!” Aliongea Mariya lakini kabla hajaenda mbali zaidi tukio zima la jinsi walivyotekwa na mwanaume wasiyemfahamu kisha kuwafungia mahali



    ambako walipata mateso wakiwa hawana chakula wala maji liliingia kichwani mwa Mariya kama sinema.

    “Baba na yule aliyetufunga vitambaa na kutupakiza ndani ya gari kisha kuturusha kama…” kwikwi ya kulia ikamkaba, alikumbuka kila kitu kilichotokea siku



    nyingi nyuma.

    “Nyamaza kulia mwanangu hayo yote yalishapita cha muhimu ni afya zenu.”



    “Lakini baba mbona mimi nimeamka na Merina bado, kwa nini?”

    “Huyu alipatwa na tatizo ambalo ilibidi afanyiwe tena upasuaji kwa mara ya pili lakini ataamka muda si mrefu.”

    “Napenda iwe hivyo, sipendi kumkosa nampenda mno,” aliongea Mariya akionyesha msisitizo.

    Baada ya mazungumzo hayo walimsihi arejeshwe sehemu alikokuwa lakini alionekana kugoma akisisitiza kubaki eneo hilohilo mpaka mwenzake aamke ili



    aongee naye.



    “Nitakaa hapahapa mpaka aamke, nataka kuongea naye, najua anasikia ila kujibu tu ndiyo tatizo…Merina! Merina tafadhali amka mimi Mariya nakuita…



    nakupenda sana, pia baba yuko hapa naye anataka kuona umeamka ili uongee nasi tunakumi…,” aliongea mtoto huyo kwa uchungu jambo lililowafanya wauguzi



    na madaktari waliokuwepo ndani ya chumba nao walengwe na machozi.

    Wakiwa katika mawazo hayo ghafla jambo lisilokuwa la kawaida likatokea.

    “Mh! Mh!” Ilikuwa ni sauti ya mguno kutoka kwa Merina, tayari zilishatimia saa kumi na mbili tangu atoke chumba cha upasuaji, watu wote wakaonekana



    kupigwa butwaa.







    MIAKA mitatu baadaye furaha ikiendelea kutawala ndani ya familia ya Phillip na mkewe Lina, mtoto Genevieve akiendelea kukua vyema mara kadhaa



    wawakilishi kutoka kituo cha Msimbazi cha kulelea watoto walikwenda nyumbani kwa Phillip kufuatilia maisha aliyoishi mtoto huyo, walionyesha furaha na



    kumshukuru Mungu kwani alipata mapenzi yote ya baba na mama.

    “Hakika Genevieve amekuwa binti mkubwa sasa.”



    “Sisi pia tunamshukuru Mungu kwa afya na baraka anazompa mtoto huyu.”

    “Amina,” aliongea Sista Maryjoyce.

    “Lakini pia anasoma shule nzuri sana mtoto wetu.”

    “Ah! Inaitwaje?”



    “Inaitwa FEZA huko ndiko tumeona inafaa na tunashukuru hata walimu pia wanatupa ushirikiano mzuri sana.”

    “Hakika mtoto huyu alikuwa anasubiri ujio wenu katika kituo chetu, hebu mwone nadhani anajua jinsi mnavyompenda.”

    “Hata sisi tunaona hivyo, tunaomba tu tuendelee kumwona akikua vyema.”

    “Hizo ni baraka za kila mzazi mwenye watoto.”



    Waliongea mengi huku wakiburudika kwa vinywaji, masista hawakusita kutoa sifa zao kwa familia ya Phillip wakimwombea kwa Mungu azidi kuwa na moyo



    huo mpaka mwisho. Baada ya mazungumzo hayo kwa sababu saa zilikuwa zimesonga sana wakaomba ruhusa ya kuondoka kurejea kwenye makazi yao,



    wakakubaliwa na kuondoka.

    Genevieve hakuwa mbali na mahali walipokuwa wameketi hivyo alipoona tu watu wakinyanyuka vitini alifahamu wazi kwamba walikuwa wakiondoka kitendo



    ambacho hakukipenda hivyo kuangua kilio.

    “Usilie mtoto mzuri tunakupenda tutakuja tena kukutembelea siku nyingine, sawa?” Sista MaryJoyce aliongea akimbembeleza Genevieve.



    ***

    Mapenzi yote ya Phillip yakatoka kwa Lina na kuhamia kwa Genevieve, alitumia muda mwingi kukaa na mtoto huyo kuliko ilivyokuwa kwa mkewe jambo



    ambalo lilianza kuleta matatizo kwani Lina pia akitaka apate nafasi kwa mumewe.

    “Mume nami pia nahitaji mapenzi yako unanishangaza sana kutwa kucha wewe na mtoto tu… huna tena muda wa kuwa nami,” Lina aliongea siku moja wakiwa



    wameketi bustanini nje ya nyumba yao.



    “Lina yaani unasikia wivu hata kwa mtoto wetu? Mke wangu jamani si hivyo kumbuka ni mtoto huyu huyu aliyekuwa akitugombanisha mimi na wewe, tafadhali



    mpatie naye nafasi mbona mimi silalamiki pale unapomchukua na kutoka naye?”

    “Ah! Unajua nini?”

    “Mh!”

    “Naona kama umenisahau sana, maana kila ukitoka na kurudi mkononi umebeba zawadi zake tu mimi ah!”



    “Haa!Haa!Haaa! Lina huo ni wivu tu mke wangu achana nao hebu tushirikiane kumlea mtoto wetu bwana, Mungu ametubariki ametupa mtoto mzuri kweli

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kweli huyu akikua atakuwa tishio, nitashikia watu bastola.”

    “Mh! Haya ngoja tuone itakuwaje, mwaa!mwaa!” Lina aliongea akisogea karibu na Phillip kisha kumwachia mabusu kwenye paji lake la uso.

    “Ahsante! Mwaaa, hebu twende ndani kwanza mara moja” Phillip naye akajibu kwa busu huku akimtaka Lina waingie ndani.

    “Kufanya nini?”



    “Nasema hivi twende ndani.”

    “Mtoto je?”

    “Atabaki na Magdalena hana shida.”

    “Na wewe,” Lina aliyemfahamu Phillip kupita maelezo aliongea kwani mara kadhaa alipomtaka kwenda ndani basi lazima kulikuwa na jambo.

    “Hivi wewe umenielewa nakuhitaji ndani haraka sana,” Phillip aliongea akionyesha msisitizo na tayari alishaanza kupiga hatua kuondoka eneo hilo.



    Lina bila ubishi naye akaanza kufuata nyuma akiwa na mtoto alipoingia tu sebuleni akamkabidhi mtoto kwa Magdalena kisha naye kufuata nyayo kuingia



    chumbani.

    “Funga mlango kwa funguo,” alitamka Phillip.

    “Unataka kunipiga?”

    “La hasha mwanamke huwa hapigwi kwa ngumi na mateka, anapigwa kwa kipande cha khanga lakini wewe sitakupiga hivyo nita…” Phillip aliongea huku



    akimvuta Lina na kumtupia juu ya kitanda.



    ***

    Miezi mitatu baadaye tayari afya za watoto wawili pacha Mariya na Merina zilikuwa zikindelea vizuri hatimaye wakawa wameruhusiwa kurejea nyumbani



    wakitakiwa kuhudhuria kliniki zao kila baada ya mwezi mmoja ili kuwaangalia kwa ukaribu.

    “Ahsanteni madaktari na Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya watoto wangu, sijui ningekuwa mgeni wa nani hapa duniani bila ya kuwa na watoto,



    utajiri wangu wote usingekuwa na maana, hakika ninawapenda sana wanangu,” aliongea Fedorov akichomoa burungutu la fedha na kuwapa madaktari pamoja na



    wauguzi kama ahsante kwa jinsi walivyojitoa kwake.



    “Ah! Mzee hakuna haja sisi ndiyo kazi yetu bwana.”

    “Najua ndiyo kazi yenu lakini hii si rushwa nawapa soda tu jamani ndugu zangu, tafadhali pokeeni vinginevyo nitajisikia vibaya sana.”

    Mabishano yakawa yametokea kwa muda wa dakika tano nzima, wakipiga hatua hiyo ya Federov kutoa fedha mfukoni mwake na kuwapatia lakini aliposihi na



    kubembeleza sana hatimaye walizipokea na kumshukuru.



    Utaratibu maalum ukafanyika na watoto wakachukuliwa kupelekwa nyumbani ambako furaha iliendelea, akawapokea tena na kuwakaribisha wao pia walikuwa



    na furaha lakini zaidi ya yote walitaka kufahamu ni kitu gani kilisababisha mpaka wakawa katika hali ile.

    “Wanangu ni historia ndefu sana sioni kama kuna haja ya kuwasimulia…nadhani mtaumia na nisingependa jambo hilo litokee tena, kwa ushauri wa madaktari



    hamtakiwi kupata kitu kitakachowafanya mfikirie sana.”

    “Basi baba hakuna shida lakini tunalo ombi moja kwako.”



    “Ombi gani tena?”

    “Tunataka kuendelea na shule ikiwezekana hata kesho.”

    “Hakuna shida mpumzike kwa muda wa wiki moja hivi halafu wiki inayofuata mtaanza tena shule.”

    “Ahsante baba tunakupenda sana,” waliongea Mariya na Merina kisha kunyanyuka vitini na kumsogelea baba yao, wakamkumbatia na kuanza kububujikwa



    machozi.







    MIAKA kumi na tano baadaye.

    Maisha nyumbani kwa tajiri Victor Fedorov yaliendelea, Mariya na Merina walisahau kabisa mambo yote yaliyotokea maishani mwao.

    Kilichotawala katika familia hiyo kilikuwa ni upendo, furaha na amani. Fedorov alihakikisha anafanya kila kitu kuwapa furaha watoto wake.

    Akiwa ameketi na Mariya na Merina, aliwaeleza kwamba maisha hayakuwa rahisi kama walivyofikiria hivyo kuwataka wasome kwa bidii ili nao wapate kitu



    ambacho kitaongoza maisha yao.



    “Nataka msome tena kwa bidii nami nitawaunga mkono kwa kila jambo, sawa wanangu?”

    “Ndiyo baba nasi hatutakuangusha.”

    Watoto hao kwa sababu walimpenda sana baba yao walijitahidi kufanya kila kilichokuwa kizuri ili wasimtie aibu, kwani walipata kila kitu walichohitaji.

    Hakika walijivunia kuwa na baba kama Fedorov bila kufahamu kwamba nyuma yake hakuwa mtu mzuri, alikuwa mtu hatari aliyeogopwa na kila mtu.



    “Nitahakikisha watoto hawa hawagundui jambo lolote linalohusu maisha yao na yangu,” aliongea Fedorov akisogelea kabati kubwa lililokuwa ndani ya chumba



    na kulifungua, taratibu akionekana mwenye wasiwasi mwingi akachomoa kitu kama faili na kuketi kitako juu ya kitanda.

    Kwa umakini wa hali ya juu akaanza kusoma karatasi moja baada ya nyingine. Lilikuwa ni faili lenye siri kubwa ambayo aliamini kabisa kwamba hakuwepo mtu



    yeyote aliyefahamu siri hiyo.

    “Maskini wa Mungu,” aliongea akigeuza shingo yake huku na kule na alipohakikisha kwamba hapakuwa na mtu aliyemwona akasogea tena mpaka kabatini na



    kulirejesha faili na kufunga mlango.



    “Nitahakikisha hakuna mtu hata mmoja atakayefahamu umafia nilioucheza, itabaki kuwa siri yangu tu.”

    Maneno aliyokuwa ameapa Fedorov yalimaanisha alichokisema lakini yeye kama mwanadamu hakufahamu kabisa kwamba maisha yake yalikuwa mikononi mwa



    Mwenyezi Mungu. Alikuwa amefanikiwa kuficha siri kwa kuua watu wote waliofahamu umafia alioutenda.

    Ndani ya faili alilolihifadhi kabatini, kuliandikwa kila kitu jinsi alivyofanikiwa kuteka watoto wawili yaani Mariya na Merina kutoka Tanzania na kuwafikisha



    nchini Urusi huku akihakikisha wanafutwa kumbukumbu zote na kuwafanya wamtambue yeye kama baba yao, jambo ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa



    lakini pia mauaji ya Ditrov na wenzake ili kuficha mpango mzima wa utekaji nyara.



    Pia kulikuwa na wosia mzito juu ya mali na fedha zote alizokuwa nazo akiagiza kama litatokea lolote basi huo ndiyo urithi kwa watoto wake hao.



    Alipohakikisha kila kitu kimekwenda sawa, akapanda kitandani na kujilaza.

    ***

    Kilichokuwa kinasikika ndani ya chumba kwa wakati huo ni kelele za kitanda tu, kwa zaidi ya saa tatu mfululizo Phillip na mkewe Lina walikuwa wakiwajibika



    ipasavyo.

    “Leo ndiyo leo asemaye kesho ni mwongo, Lina ukweli nakupenda kutoka ndani ya moyo wangu na furaha hiyo imeongezeka zaidi baada ya mtoto wetu



    Genevieve kuingia ndani ya familia yetu…mwaaa”.



    “Ahsante Phillip nami pia ninakupenda kuliko maelezo ndiyo maana sikuwaza kukusaliti hata mara moja, ingawa nilikuwa na uwezo huo.”

    “Mh! Usiseme hivyo mke wangu ni shetani tu, nilitamani kuitwa baba.”

    “Nami nililifahamu jambo hilo mapema ndiyo maana nikapata wazo la kuasili mtoto na kweli umekubali na sasa tunaye Genevieve.”

    “Nitampenda mtoto huyu mpaka mwisho, sipo tayari kuona akiteseka wakati nikiwa hai, sasa ni wakati wa mimi na wewe kufanya kazi kwa bidii ili mtoto aishi



    maisha ya kifalme baadaye au?”



    “Umesema kweli mu…” Lina alishindwa kumalizi sentensi yake, kigugumizi kikaonekana kumkamata.

    Waliendelea kubaki ndani ya chumba kwa muda mwingine wa saa mbili na kutimiza saa tano kamili.

    “Mume wangu sasa inatosha ni vyema tukatoka kwenda kumwangalia mtoto wetu ametumisi sana jamani.”

    “Umesema kweli kabisa lakini ni lazima nasi tupate nafasi kama hii.”

    “Ahsante nimeamini kwamba kweli unanipenda.”.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Saaana!” Phillip aliongea akinyanyuka kitandani kuelekea bafuni kuoga.

    Hayo ndiyo yakawa maisha yao wakifurahia mtoto aliyeingia ndani ya familia yao, wote wakiamini kwamba ameleta upya furaha katika nyumba yao, kila mmoja



    akiahidi kumpenda na kumtunza kwa hali na mali lakini mapenzi ya Phillip yalionekana wazi kwa sababu mtoto huyo alipewa jina la marehemu mke wake.

    “Hatimaye Genevieve amerudi tena katika maisha yangu…,” aliwaza kichwani mwake akitoka ndani ya chumba kuelekea sebuleni.

    “Phillip nimekumbuka jambo moja.”



    “Lipi tena hilo?”

    “Kesho ni siku ya kutembelea makaburi ya ndugu zetu kuangalia na kuyaweka safi, sijui unakumbuka?”

    “Mh! Ahsante sana kwa kunikumbusha, ndiyo maana Mungu amenipa mwanamke kama wewe, hakika unajali.”

    Ilikuwa ni kama desturi kwa Phillip kutembelea makaburi ya mke na watoto wake kufanya ibada kisha kufanya usafi ikiwa ni ishara mojawapo ya kuwaenzi.



    ***

    Tayari Mariya na Merina walishatimiza umri wa miaka kumi na nane na walihitimu elimu yao ya chuo kikuu, walitamani sana kufanya kazi lakini msimamo wa



    baba yao ulihitaji waendelee kusoma zaidi ili waje kuongoza makampuni aliyokuwa nayo, hivyo walitakiwa kupumzika kidogo kisha kuendelea na masomo ya



    juu zaidi.

    “Nataka muendelee kusoma zaidi ninyi ndiyo warithi wangu, mtapumzika kidogo halafu mtaendelea na masomo sijui mnataka kwenda nchi gani kwa



    mapumziko?”



    “Mh! Baba tunataka tukae hapahapa na wewe, hatuwezi kwenda mbali na upeo wa macho yako.”

    “Basi sawa na ni zawadi gani mnapenda?”

    “Mh! Gari aina ya Ferrari.”



    “Wow! Wazo hilo ndilo lilikuwa akilini mwangu, nilitaka kuwafanya miongoni mwa mastaa mjulikane ulimwengu mzima kama mimi ninavyojulikana.”

    “Ahsante baba kwa mapenzi unayotuonyesha, hakika unatupenda.







    TAYARI ilikuwa imeshatimia miaka kumi huku mtoto Geneveive akikua vyema na akiendelea na masomo yake katika shule ya Feza, mapenzi mema aliyopewa



    na wazazi wake wawili yalimfanya ajisikie mwenye furaha sana.

    Phillip na Lina walimtunza na kumfanyia kila lililo jema wakihakikisha hapungukiwi na kitu chochote maishani mwake.

    “Phillip ni vyema sasa tukamweleza mtoto huyu siri ambayo tumeiweka ndani ya mioyo yetu kwa muda mrefu.”

    “Lina!” Phillip alimwita mkewe kwa mshangao.



    “Ni lazima siku moja aje kuufahamu ukweli mume wangu.”

    “Najua hilo lakini si sasa, bado umri wake ni mdogo, anahitaji kukua zaidi.”

    “Mh! Haya kumbuka lakini sisi ni binadamu lolote linaweza kutokea.”

    “Lina tafadhali achana na fikra potofu,” aliongea Phillip huku akimwita Genevieve asogee karibu yake.

    Alihakikisha mtoto huyo anapata mapenzi ya dhati kutoka kwake na mkewe, hakuwa tayari kuona mtoto huyo akiumia wala kuumizwa na mtu mwingine.



    “Nakupenda sana mwanangu.”

    “Ahsante baba yangu nakupenda pia.”

    “Genevieve mimi pia ninakupenda,” aliongea Lina akiachia tabasamu mdomoni mwake.

    Hayo ndiyo yakawa maisha yao ndani ya nyumba, kuonesha mapenzi ya dhati kwa vitendo na maneno kwa Genevieve huku wakiitunza siri ya kwamba hawakuwa



    wazazi wake wa kumzaa bali walimuasili kutoka katika kituo cha watoto Yatima cha Msimbazi.



    Waliendelea kubaki sebuleni kwa mazungumzo wakiongea na kufurahi pamoja, mara kadhaa wakimsisitiza mtoto Genevieve umuhimu wa shule, wakimtaka



    asome kwa bidii kwani elimu ndiyo ulikuwa urithi wake mkubwa katika maisha yake ya baadaye.

    “Chakula tayari karibuni mezani,” ilikuwa ni sauti ya mfanyakazi wa ndani, Magdalena akiwakaribisha mezani kwa ajili ya chakula, wakamshukuru na kusogea



    mezani.



    Saa mbili baadaye walishapumzika vya kutosha na mmoja baada ya mwingine wakaaga na kuingia ndani ya vyumba vyao kupumzika kwa ajili ya siku iliyofuata,



    Lina na Phillip nao wakiingia ndani ya chumba chao.

    “Mke wangu kusema ukweli ninakupenda sana.”

    “Mimi pia nakupenda Phillip sikuwahi kumpenda mwanaume mwingine maishani mwangu kama ilivyokuwa kwako.”

    “Ahsante kwa kunipenda lakini ninataka kukueleza kitu kimoja.”



    “Kitu gani?”

    “Ninapokuwa na wewe hivi huwa sichoki kufanya tendo la ndoa na wewe, nakuhitaji kila wakati mke wangu…mh! Unajua nini?...hebu sogea hapa…” aliongea



    Phillip kwa sauti ya kutetemeka huku akimvuta Lina upande aliokuwa ameketi yeye.

    “Mh! Mh! Bwa…na” aliongea Lina kwa sauti ya chini chini huku akisogea kumfuata mumewe.



    ***

    Mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa watoto wake alihakikisha wanayafaidi maisha yote mazuri, akiwapa kila kitu muhimu maishani, hivyo, baada ya



    maongezi yao kukamilika na watoto kuhitaji zawadi ya gari kama ambavyo baba yao alivyowauliza aliahidi kuwatafuta gari hilo ndani ya saa ishirini na nne tu.



    Saa sita zikakatika watoto Mariya na Merina wakimsubiri baba yao kwa hamu kubwa, ghafla wakasikia sauti ya honi nje ya lango la kuingia ndani ya nyumba



    yao, haraka wakanyanyuka kwenye viti kuelekea langoni ambako mlinzi alishafungua kuruhusu gari kuingia.

    “Gosh!” walijikuta wakitamka maneno hayo.

    Mbele ya macho yao yalishuhudia gari aina ya Ferrari ambalo walilihitaji ndani yake kukiwa na mwanaume mmoja aliyejazia misuli, akaliendesha na kuliingia



    ndani kisha kuliegesha sehemu maalum na kushuka.



    “Naitwa Ford niko hapa kwa maelezo ya bosi Fedorov,” aliongea mwanaume huyo.

    Mariya na Merina hawakujibu kitu chochote macho yao yalikuwa bize yakishangaa huku na kule kuangalia gari hilo, wakiongea wenyewe katika mioyo yao na



    kujijibu.

    “Hallow” aliita mwanaume huyo.



    “Subiri kwanza kaka tutaongea baadaye.

    Kwa muda wa nusu saa nzima waliendelea kulishangaa gari lililokuwa ndani ya ngome yao, wakijiuliza maswali mbalimbali na waliporidhika walimsogelea



    mwanaume aliyekuwa pembeni na kuongea naye akajitambulisha tena kwa mara ya pili kwao.

    “Ahaa! Karibu sana.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mimi naitwa Mariya na huyu anaitwa Merina ni watoto wa Victor Fedorov.”

    “Vizuri nimetumwa na bosi wangu kuja hapa nyumbani si kuleta tu gari hili bali pia mimi ndiye nitakuwa dereva wenu kwa muda.”

    “Oh! Ahsante baba yuko wapi?”

    “Atakuja muda si mrefu mimi nimetangulia.



    Wakiwa katika maongezi hayo haikuchukua hata dakika tano, honi nyingine ikasikika nje ya lango la kuingilia ndani ya nyumba, mlinzi akaongekana akifungua



    lango na gari ya Fedorov kuingia ndani huku akipiga honi nyingi kuashiria furaha, akaliendesha gari mpaka sehemu ya maegesho akaliegesha na kushuka na



    watoto wake wote wawili wakamkimbilia na kumkumbatia huku wakimbusu kwa wingi katika mashavu yake.



    “I love you daddy,”(tunakupenda baba) walitamka maneno hayo wakimwangalia baba yao kwa macho ya upole.

    “I love you too,”(Nawapenda pia) Fedorov alijibu huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake.

    “Baba kwa nini unalia?”

    “Mh! Hapana”



    “Tafadhali tueleze nini kimekupata huko ulikotoka?”

    “Hakuna kitu wanangu ila…”

    “Bosi! Bosi! Nini kimetokea nini huko utokako?”

    Victor Fedorov hakuwa na jibu la kutoa kwa wakati huo akasogea taratibu na kuketi pembeni ya msingi uliokuwepo hapo kwikwi za kulia zikamkamata.







    “NAITWA Ford niko hapa kwa maelezo ya bosi Fedorov,” aliongea mwanaume huyo.

    Mariya na Merina wakati hawakujibu kitu chochote macho yao yalikuwa bize yakishangaa huku na kule kuangalia gari hilo wakiongea wenyewe na kujijibu.

    “Hallow!” aliita mwanaume huyo.

    “Subiri kwanza kaka tutaongea baadaye,” alijibu Merina.



    Kwa muda wa nusu saa nzima waliendelea kushangaa gari lililokuwa ndani ya ngome yao wakijiuliza maswali mbalimbali na waliporidhika walimsogelea



    mwanaume aliyekuwa pembeni na kuongea naye akajitambulisha tena kwa mara ya pili.

    “Ahaa! Karibu sana. Mimi naitwa Mariya na huyu anaitwa Merina ni watoto wa Victor Fedorov.”

    “Vizuri nimetumwa na bosi wangu kuja hapa nyumbani si kuleta tu gari hili bali pia mimi ndiye nitakuwa dereva wenu kwa muda..”

    “Oh! Ahsante, baba yuko wapi?”



    “Atakuja muda si mrefu mimi nimetangulia.”

    Wakiwa katika maongezi hayo haikuchukua hata dakika tano honi nyingine ikasikika nje ya lango la kuingikua ndani ya nyumba mlinzi akaonekana akifungua



    lango na gari la Fedorov kuingia ndani huku akipiga honi nyingi na kuashiria furaha, akaliendesha mpaka sehemu ya maegesho, akaegesha na kushuka na watoto



    wake wote wawili wakamkimbilia na kumkumbatia huku wakimpiga mabusu mengi.

    “We love you daddy!” (Tunakupenda baba) walitamka maneno hayo wakimwangalia baba yao kwa macho ya upole.

    “I love you too!” (Nawapenda pia) Fedorov alijibu huku machozi yakitiririka mashavuni mwake.



    “Baba kwa nini unalia?”

    “Mh! Hapana.”

    “Tafadhali tueleze nini kimekupata huko ulikotoka?”

    “Hakuna kitu wanangu ila…”



    “Bosi! Bosi! Nini kimetokea huko utokako?”

    Victor Fedorov hakuwa na jibu la kutoa kwa wakati huo, akasogea taratibu na kuketi pembeni mwa msingi uliokuwepo hapo, kwikwi ya kulia ikamkamata.





    “TAFADHALI tueleze nini tatizo?”

    “Mh!”

    “Baba kwa nini unatuweka roho juu?”

    “Naomba nitamke wazi leo…” kwikwi ya kulia ikamkamata tena Fedorov na kuangua kilio kama mtoto mdogo.

    Kwa takribani dakika tano nzima waliendelea kubaki eneo hilo wakiwa wameshikwa na butwaa wakiwa hawaelewi ni kitu gani kilikuwa kimetokea huko



    alikokuwa kabla ya kufika nyumbani.



    Walipohakikisha ametulia hawakuchoka kuendelea kumuuliza tena.

    “Mnajua nini?”

    “Eh!”

    “Ninawapenda sana wanangu historia yenu inanikumbusha maisha ya nyuma ambayo yanaumiza kupita maelezo.”

    “Baba lakini ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Unamkumbuka mama yetu?”

    “Mh!”



    “Unakumbuka nini?”

    “Jinsi nilivyowalea mpaka kufikia hapa nikiwa sina msaada wowote.”

    “Lakini baba hata sisi tunakupenda kupita maelezo.”

    “Najua wanangu nami nawapenda pia.”

    “Ahsante kwa zawadi nzuri ya gari.”



    “Ni wajibu wangu kufanya hivyo kwenu kama wanangu na huyu hapa mbele yetu ndiye atakuwa dereva wenu mpaka mtakapokuwa mmefuzu vyema udereva,



    atawapeleka kokote mtakapotaka na kuhakikisha anawapa ulinzi wa kutosha.”

    “Ahsante baba,” walijibu Mariya na Merina wakitabasamu.

    “Leo nitaomba tujumuike wote kwa chakula cha jioni ili kukamilisha furaha yetu wanangu na kesho ninafikiria kufanya matembezi kidogo kwenye mchezo wa



    kuteleza kwenye barafu.”

    “Babaaa!”



    “Ni kweli kabisa kwa sasa ni msimu mzuri wa kwenda huko nitaondoka na nitarejea baada ya wiki tatu.”

    “Twende wote.”

    “Hapana acha mimi niende kwanza nikirudi mara nyingine nitawachukua wote.”

    “Sawa baba tutashukuru.”

    Wakaingia ndani na kujiandaa kwa ajili ya kutoka kwenda kula chakula cha jioni kama familia wakifurahia maisha na mapenzi makubwa waliyoyapata kutoka



    kwa baba yao. Kwa muda wa saa nzima walikuwa chumbani wakijiandaa na waliporidhika walitoka.

    “Wow!” sauti ya Fedorov ilisikika baada tu ya kuwaona watoto wake wakitoka chumbani.



    “Heheee!” walicheka.

    “Mmempendeza sana wanangu hakika ninyi ni mabinti wazuri sana.”

    “Ahsante baba.”

    Wakatembea kwa mwendo wa madaha na kulielekea gari lao aina ya Ferarri na kuingia ndani ambapo Fedorov naye akaingia kwenye gari lake, yeye ndiye akawa



    mtu wa kwanza kutoka ndani, gari walilopanda watoto wake likifuata kwa nyuma.

    Kwa mwendo wa nusu saa hivi walikuwa barabarani hatimaye wakafika kwenye mgahawa maarufu wa Kalinin. Fedorov akawa wa kwanza kushuka ndani ya gari



    na kubaki kusubiri watoto pamoja na dereva washuke ili waingie wote kwa pamoja.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akionekana wenye furaha, akawakumbatia watoto wake na kuanza kutembea kuingia ndani ya mgahawa, wote wakionekana wenye furaha kupita maelezo. Kwa



    umaarufu na utajiri aliokuwa nao mzee huyo nchini Urusi alipewa heshima kubwa sana, alipokelewa kwa furaha na wafanyakazi karibu wote katika mgahawa



    huo na akaongozwa kupelekwa sehemu maalum kabisa akikaribishwa mara nyingi.

    “Leo nimekuja na watoto wangu, huyu hapa anaitwa Mariya na huyu ni Merina, huyu mwingine ni dereva wao anaitwa Ford,” aliongea Fedorov kwa kujiamini



    kabisa.



    “Karibuni sana ndugu zetu.”

    Menu yenye orodha ya chakula na vinywaji ikawekwa mezani na mhudumu akiwataka wachague kitu ambacho wangependa kula na kunywa siku hiyo na



    wakionekana wenye furaha, kila mmoja aliagiza alichotamani kula.

    Wakala na kunywa wakifurahi pamoja na baada ya hapo walilipa na kuondoka na kuingia maduka mbalimbali kununua vitu walivyohitaji na kurejea nyumbani.



    “Usiku mwema wanangu!”

    “Kwako pia baba!”

    Wakaingia ndani ya vyumba vyao na kulala na siku iliyofuata Fedorov ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuamka ili ajiandae kwa safari ambayo ingemchukua



    muda wa wiki mbili mfululizo akiwaacha watoto wake peke yao nyumbani, akatoka chumbani akiwa tayari na mizigo yake kisha kugonga mlango wa chumba



    cha watoto wake huku akiwaita majina akiwaaga na akiwatakia kila lililo jema na kutoa maelekezo ya mahali ambako wangechukua fedha za matumizi kwa



    muda wote ambao hangekuwepo.



    Kwa pamoja wakamrukia baba yao na kumkumbatia wakimtakia safari njema na kumtaka awahi kurejea nyumbani kwani kwa muda ambao hatakuwepo



    watakuwa wapweke sana.

    “Nitarejea muda si mrefu, mwaa ninawapenda sana,” aliongea lakini watoto wake walipomwangalia vyema usoni mwake waligundua alikuwa akibubujikwa na



    machozi na walipomuuliza ni kwa nini alipatwa na hali hiyo Fedorov hakujibu kitu zaidi ya kuanza kutembea kuelekea nje ya nyumba yake akiwa na begi kubwa



    mgongoni mwake.



    ***

    “Phillip! Phillip!” Lina aliita mfululizo

    “Naam!”

    “Ah! Najisikia vibaya.”

    “Kidogo tu mke wangu sita…”

    “Mh! Siyo hivyo mwenzio najisikia kizunguzungu.”



    “Kizunguzungu?” aliuliza kwa mshangao.

    “Ndiyo, nipe…”

    “Lina acha basi utani wako unanicha…”

    “Hapana Phillip naumwa mbona naona giza!”

    “Eh!”



    “Nipe maji ya kunywa fanya haraka kabla sija…” aliongea Lina lakini kabla hajamalizia sentensi yake ukimya wa ajabu ukatokea na Phillip alipojaribu kumwita



    na kumtingisha hakupata ushirikiano wowote zaidi ya yote alimshuhudia Lina akilegea kama mlenda.

    “Mungu wangu! Kimetokea nini?” alijiuliza akimlaza Lina vyema kitandani na yeye kushuka kitandani.

    Phillip akalisogelea taulo lililokuwa pembeni na kujifunga kiunoni, jasho jingi likimtiririka.







    Nipe maji ya kunywa fanya haraka kabla sija…,” aliongea Lina lakini kabla hajamalizia sentensi yake ukimya wa ajabu ukatokea na Phillip alipojaribu kumwita



    na kumtingisha hakupata ushirikiano wowote, zaidi ya yote alimshuhudia Lina akilegea kama mlenda.

    “Mungu wangu! Kimetokea nini?” alijiuliza akimlaza Lina vyema kitandani na yeye kushuka haraka kitandani, haraka akachukua taulo lililokuwa pembeni na



    kufunga kiunoni jasho jingi likimtiririka. Kitu kilichokuwa kikitokea mbele yake kilionekana kuwa ni ndoto kama siyo muujiza, akakizunguka chumba huku na



    kule akifikiria cha kufanya.



    “Lina! Lina mke wangu kimetokea nini?” aliita Phillip lakini hakupata jibu lolote kutoka kwa mkewe aliyekuwa kitandani akiwa ametulia kimya.

    “Hapa ni hospitali tu, hakuna kingine cha kufanya,” aliongea Phillip.

    Akiwa amechanganyikiwa alivaa shati kisha kumvalisha Lina, akausogelea mlango na kuufungua huku akiita jina la Bibi Magdalena ili aje kumsaidia.



    “Njoo haraka! Tafadhali njoo upesi,” alisisitiza Phillip.

    Haraka bila kuchelewa, Bibi Magdalena aliingia chumbani kwa Phillip na kumkuta Lina akiwa amelala kimya kitandani huku mumewe akizunguka huku na kule.

    “Nini kimetokea bosi wangu?”

    “Lina amenyamaza ghafla,” Phillip alimjibu Bibi Magdalena.

    “Umempiga?”



    “Huu si muda muafaka wa kuuliza hivyo tusaidieni nimpeleke hospitali,” Phillip alimwambia Bibi Magdalena.

    “Sawa bosi.”

    Haraka Phillip akamnyanyua Lina, Bibi Magdalena akitangulia mbele kufungua mlango, walipofika kwenye gari lililofunguliwa mlango, walimuingiza Lina na



    kumlaza siti ya nyuma kisha Phillip akazunguka upande wa pili na kuingia.

    Kabla hajaondoka, alimuaga Bibi Magdalena na kumwambia akifika hospitali atamfahamisha kilichomsibu mkewe.



    “Haya kila la kheri,” alijibu Bibi Magdalena akitembea kurejea ndani, furaha yote iliyokuwepo muda mchache uliopita ilikuwa imetoweka.

    “Sijui kapatwa na nini?” alijiuliza bibi huyo akiingia ndani.

    Kwa muda wa saa tatu na nusu Phillip bado alikuwa hajarejea, wasiwasi ukaugubika moyo wa Bibi Magdalana akitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea huko



    alikokuwa Phillip na mkewe Lina ambaye alikuwa mgonjwa taaban.



    Saa zilipozidi kusonga mtoto Geneveve alianza kumsumbua Bibi Magdalena akitaka kujua wazazi wake walikuwa wapi.

    Bila kujibu kitu chochote yeye mwenyewe akiwa na wasiwasi mwingi moyoni mwake alimtuliza mtoto Theresia na kumtaka atulie kwani wazazi wake



    wangerejea muda si mrefu, akatoka nje na kuelekea kwa mlinzi na kumweleza wazi wasiwasi aliokuwa nao.

    “Hebu tusubiri kidogo pengine wako njiani.”

    “Mh! Ni muda sana mtoto naye ananisumbua sijui wamepatwa na kitu gani, eh haya ni matatizo mengine tena!” aliongea bibi huyo akionyesha kulengwalengwa



    na machozi.



    Ghafla wakiwa katika maongezi hayo, honi ikasikika nje ya lango la kuingilia ndani ya nyumba yao.

    “Si hao!” aliongea mlinzi akilisogelea lango na kufungua, hakuwa amekosea gari la bosi wake lilikuwa limesimama nje ya lango hilo..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taratibu bila kusema kitu akionekana mwenye mawazo mengi kichwani mwake, Phillip akaendesha gari mpaka sehemu ya maegesho. Alipoangalia kwenye



    kibaraza cha nyumba yake, akamshuhudia mtoto wake Genevieve akikimbia kumfuata.



    “Dady why are you crying?”(Baba kwa nini unalia?)

    “It’s too painful,”(Inauma sana)

    “What?”(Nini?)

    Kwikwi ya kulia ikamkaba Phillip, akajikuta akilia mbele ya mtoto wake kitu kilichozidi kumchanganya zaidi Genevieve, naye bila kutegemea akaanza kuangulia



    kilio.



    ***

    Fedorov alitembea hatua mbili na kugeuka nyuma kuwaangalia watoto wake, hakuonekana kuwa na furaha kama ilivyokuwa siku zote aliposafiri kwenda mbali.

    Alipolifikia gari lake, akafungua sehemu ya kuweka mizigo akaweka begi na vifaa alivyokuwa navyo ndani kisha akawaita tena watoto wake;

    “Mariya, Merina.”



    “Bee,” waliitika wakikimbia kumfuata na walipomfikia karibu waligundua baba yao alikuwa tofauti kabisa.

    “Lakini unaonekana hauko sawa?” Merina aliuliza.

    “Unajua nini?”

    “Mh!”

    “Ninasikia sauti ndani ya moyo wake ikiniambia kwamba nisiwaache.”

    “Basi twende wote baba!”



    “Hapana nataka mbaki nyumbani nami niende kwenye mchezo huo nitarejea tu niombeeni wanangu,” aliongea Fedorov huku akiwakumbatia watoto wake.

    “Lakini umesema moyo wako hautaki kwenda huko?”

    “Hivyo ndivyo ninavyosikia ila acheni niende.”

    “Mh!” Mariya aliguna yeye pia alihisi kitu fulani ndani ya moyo wake lakini akajaribu kupingana na hisia hizo ili kumfanya baba yake arejee katika hali yake ya



    kawaida.



    “Nawapenda sana wanangu mbaki salama, nitarejea baada ya wiki mbili, mnapenda niwaletee nini nikirudi?”

    “Mh! Mh!”

    “Semeni basi!” aliongea Fedorov akifungua mlango ili aingie garini.

    “Tuletee zawadi ya saa.”

    “Hilo tu?”

    “Mh!” Waliitikia kwa kuguna huku wakitingisha vichwa vyao kuonyesha ishara ya kukubali.



    Fedorov akaingia ndani ya gari na kuliwasha kisha taratibu huku akiwaangalia watoto wake akaliendesha gari hadi langoni ambako mlinzi alifungua kisha



    akatoka ndani.

    “See you then,”(Tutaonana) ndiyo maneno pekee aliyoongea akitokomea.

    Wiki ya kwanza ikakatika hatimaye ikaja ya pili Mariya na Merina wakiwa tayari kumsubiri baba yao bila matarajio, walipojaribu kufanya mawasiliano naye kwa



    njia ya simu ya upepo bado Fedorov hakupatikana wakaanza kuingiwa na wasiwasi kwani halikuwa jambo la kawaida na kibaya zaidi safari hiyo aliondoka peke



    yake bila ya mlinzi.

    “Hivi unafikiri baba atakuwa wapi mpaka sasa?”



    “Kwa kweli sijui ila tusubiri tuone pengine yuko njiani.”

    “Mh! Nahisi hatari fulani ndani ya moyo wangu…,” aliongea Merina kwa sauti ya upole.

    Hatimaye wakiwa katika kusubiri wiki ya tatu ikaanza kuyoyoma bila baba yao kutokea, wakaingiwa na hofu na kuamua kutoa taarifa za kupotea kwa baba yao



    katika vituo mbalimbali vya televisheni na redio lakini hata baada ya matangazo kutolewa mzee huyo hakuonekana.







    MWEZI mmoja ulikuwa umekatika tayari watoto Mariya na Merina wakiwa katika kusubiri, mioyo yao ikiwa na huzuni kubwa kupita maelezo, ni mlinzi wa



    nyumbani kwao na dereva aliyewaendesha ndiyo waliotoa faraja kwa watoto hao wakiwapa moyo kwamba ipo siku Fedorov angerejea na huko alikokuwa



    hakukuwa na tatizo lolote kwani kama lingekuwepo mpaka wakati huo wangeshapewa taarifa.

    “Msiwe na hofu atarejea tu, huyu mtu ni mfanyabishara pengine ameshatoka huko na kuelekea nchi nyingine.”

    “Lakini bila kusema kitu chochote?” Merina alihoji.



    “Inawezekana anajua hakuna kitu kibaya.”

    “Hapana mimi ninawaeleza wazi kabisa ipo sauti ndani ya moyo wangu inanieleza jambo fulani la hatari, lazima kuna tatizo,” Mariya aliongea akibubujikwa na



    machozi.

    “Usilie nyamaza baba atarejea tu tena si muda mrefu.”

    “Mimi nashauri tutoe taarifa polisi.”



    ”Juu ya nini?”

    “Upoteaji wa baba yetu, mimi ninawaambia lazima atakuwa kwenye matatizo makubwa sana kama siyo kifo.”

    “Mh!” Wote wakaguna kwa mshangao.

    Baada ya maongezi hayo kwisha kila mmoja akionekana kuwa na msongo wa mawazo kichwani mwake, Mariya na Merina walinyanyuka na kuingia ndani ya



    chumba ambamo kwa takribani nusu saa nzima waliendelea kubaki huku wakiwaacha mlinzi na dereva waliokuwa wameketi bustanini wakiendelea kujiuliza



    maswali na ghafla wakiwa hapo wakawashuhudia tena watoto hao wakirejea.



    “Dereva tafadhali tupeleke.”

    “Wapi?”

    “Kituo cha polisi.”

    “Lakini tumepatana tuvute subira kidogo pengine yuko njiani anarejea.”

    “Hapana tumeamua twende tu polisi.”

    “Mh! Haya twendeni niwapeleke.”



    “Naweza kuongozana nanyi?” mlinzi aliuliza.

    “Hapana wewe baki tu hapa nyumbani tutarejea muda si mrefu.”

    “Sawa.”

    Wakatoka wakiongozana na dereva mpaka kwenye maegesho ya gari kisha wote wakafungua milango na kuingia ndani, Mariya na Merina wakiwa wameketi kiti



    cha nyuma na mara kadhaa wakiongea jambo fulani kwa kunong’ona.



    Gari likaendeshwa mpaka sehemu kulikokuwa na kituo cha polisi, hapo wakashuka na kuingia moja kwa moja ndani wakimtaka dereva aendelee kusubiri eneo



    lilelile.

    Wote wawili wakatembea na kuingia ndani ya kituo na kupokelewa na askari waliokuwa eneo hilo, kwa sababu ya umaarufu wao moja kwa moja wakaongozwa



    kuingia kwenye chumba maalum ambako walimkuta polisi akiwa ameketi akawakaribisha na kuwataka waeleze shida yao.

    “Ahsante sana,” aliongea Merina ambaye kwa kumwangalia tu machoni mwake ungegundua alikuwa akilia.

    “Kuna tatizo gani?” Polisi aliuliza.



    “Ni mwezi sasa umepita hatujui baba yetu yuko wapi?”

    “Tajiri Fedorov?”

    “Hujakosea,” Mariya alijibu.

    “Mh!” Polisi naye akaguna kuonyesha mshtuko, kwani historia ya mzee huyo ilifahamika nchini kote na kwa umafia wake aliogopwa na kila mtu.

    “Tunahitaji kutoa taarifa hii kwenu ili msako ufanyike haraka sana na kufahamu ni wapi alipo baba yetu, juu ya malipo hakuna shida ilimradi tu apatikane.”



    “Hata akiwa amekufa?”

    “Tunahitaji maiti yake.”

    “Basi hakuna shida tutafungua faili ambalo tutaandika malalamiko yenu kisha tutaanza msako na mnachotakiwa kufanya ni ninyi kutangaza kwenye vyombo vya



    habari vyote.”

    “Hakuna shida tutaifanya kazi hiyo, tunachotaka sisi ni kumpata baba yetu basi!” walijibu watoto hao kwa kujiamini.



    Baada ya kuhakikisha kwamba taarifa hiyo ilikuwa imefika jeshi la polisi, waliaga na kutoka nje wakitembea kuelekea lilipokuwa gari lao, wakapanda na dereva

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    bila kusema kitu chochote akaliendesha moja kwa moja kuelekea nyumbani.

    Jambo moja lilitawala vichwa vyao: ni wapi baba yao alikuwa na kama alikuwa amekufa maisha yao yangekuwaje baada ya hapo?

    “Merina tunatakiwa tuanze kutangaza mara moja kwenye vyombo vya habari bila kuchelewa.”

    “Kazi hii tutampatia huyu dereva azunguke kwenye vyombo vyote vya habari hata kama watahitaji fedha lakini watoe tangazo hili.”

    “Hakuna shida.”



    Nusu saa tu baadaye gari lilishafika nyumbani kwa tajiri Fedorov, lango likafunguliwa na dereva kuingiza gari ndani wakashuka na kumsabahi mlinzi wao na



    hawakusema tena kitu chochote wakatokomea na kuingia ndani.

    Watoto hao waliendelea kubaki ndani ya chumba kwa zaidi ya saa tatu wakiongea mambo mbalimbali, hata mlango wa chumba chao ulipogongwa wakitakiwa



    kwenda kula waliendelea kugoma wakitoa agizo kwamba watu wengine waendelee nao wangejumuika baadaye.

    Hata walipoitwa tena baada ya saa sita waliendelea kubaki chumbani na safari hii hawakusikika wakijibu kitu chochote zaidi ya ukimya tu.

    “Mh! Wanafanya nini hawa?”



    “Sijui hata wakiitwa hawaitiki.”

    “Wasije kuwa wamechukua maamuzi mabaya.”

    “Haiwezekani hebu tuchungulie dirishani.”

    Mlinzi na dereva wakazunguka nyuma ya nyumba na kuelekea sehemu dirisha la chumba cha watoto hao lilipokuwa na walipojaribu kutupa macho yao ndani



    yalikutana na pazia zito likiwa limefunikwa kwenye dirisha hilo.

    ***

    “Genevieve?” Phillip aliita kwa sauti ya upole.

    “Bee baba!”

    “Si kwamba napenda kulia mwanangu lakini…” kwikwi ya kulia ikamkaba tena Phillip akaangua kilio mbele ya mtoto wake.

    “Tafadhali nyamaza na utueleze tatizo, nini kimetokea huko?” Magdalena aliyekuwa mfanyakazi wa ndani nyumbani kwa Phillip aliongea.





    “Hali ya Lina ni mbaya sijui kama…” aliongea Phillip na kabla hajamalizia sentensi yake mlio wa simu ikiita ukasikika, taratibu akaingiza mkono wake mfukoni



    na kuichomoa haraka kisha akatupa macho kwenye kioo cha simu ili asome jina.

    “Hospitali!” Alitamka Phillip kwa sauti ya juu.









    MSAKO nchini Urusi ulikuwa mkali kweli kweli polisi wakifanya kazi usiku na mchana kumsaka tajiri mkubwa nchini humo, Victor `Fedorov ambaye



    alitoweka katika mazingira ya kutatanisha, makundi kwa makundi yalikuwa yakigawanyika ambapo watu wengine walielekea sehemu ambako tajiri huyo



    alikwenda kwenye mchezo wa kuteleza katika barafu.



    “Mkuu tumefika mpaka hapa lakini hakuna mtu wala hakuna taarifa yoyote ile inayoonyesha kwamba kuna uhai wa mtu na kwa mujibu wa mazingira



    hatukushudia kitu chochote kinachoonyesha uwepo wa mwanadamu,” ilikuwa ni sauti ya polisi mmoja katika kundi la polisi wasiopungua kumi waliotumwa



    kwenda kufanya uchunguzi eneo ambalo ndilo hasa Fedorov aliaga kwenda huko.

    “Kitu gani kingine kimefanyika?”



    “Tumejaribu kwa uwezo wetu wote kuangalia pengine hata nyayo na nguo ili kuridhika na upelelezi wetu lakini hatujafanikiwa kuona kitu.”

    “Basi ni vyema mkarejea na kufanya mkakati mwingine.”

    “Sawa mkuu.”

    Simu ya upepo ikakatika na polisi wakajiandaa na kupanda ndani ya helikopta kisha kurejea jijini kwa mkakati mwingine.



    ***

    Ndani ya chumba Mariya na Merina walikuwa wakipanga mkakati wa jinsi ya kumpata baba yao ambaye mpaka wakati huo hawakufahamu ni wapi alipokuwa na



    kama alikuwa mzima au la! Machozi na vilio vilitawala kila mmoja akionekana kumfariji mwenzake.

    “Baba atakuwa amekufa.”

    “Hapana usiseme hivyo.”



    “Nahisi hivyo si kawaida yake hata simu tu?”

    “Mh! Unasema kweli kwa jinsi anavyotupenda haiwezekani hata kidogo.”

    “Ngoja tuone uchunguzi wa polisi utasema nini?”

    “Hapana Merina ni muda mrefu sana…yapata miezi mitatu sasa lazina kuna tatizo mimi ninakuambia...”



    Mariya aliyekuwa ameketi kimya kitandani bila kujibu kitu machozi yakaonekana yakimbubujika, kichwani mwake hakupata picha kama kweli baba yao



    mpendwa angekuwa amekufa maisha bila yeye yangekuwaje? Ilikuwa ni picha ya kuumiza sana hakumfahamu mtu mwingine zaidi ya mlinzi na dereva



    waliyekuwa naye wakati huo.

    “Kama ikitokea mzee asionekane nini kitatokea katika maisha yetu?”

    “Kwa kweli sijui na hatukuwahi kumfahamu ndugu mwingine yeyote na kama sijakosea baba alitueleza kwamba mama yetu alifariki miaka mingi sana hivyo



    yeye ndiye alikuwa kila kitu.”



    “Sawa kabisa, kitu alichokuwa amekiongea Mariya kilikuwa ni ukweli, hawakufahamu ni kitu gani kingeendelea kwao, maisha yangekuwaje na ndugu wengine



    wangewafahamu vipi kwani Fedorov hakutaka kuwaeleza ukweli.

    “Lakini lazima kuna sehemu baba atakuwa ameandika kitu fulani hivi kweli hana ndugu?”

    “Wewe hivi unamjua vizuri baba?”

    “Namjua hebu…,” aliongea Merina akinyanyuka kitandani na kuanza kutembea kuelekea mlangoni akitoa ishara ya kumwita Mariya.

    “Twende huku.”



    “Wapi?”

    “Wewe twende tu utaona ninachotaka kwenda kufanya.”

    Baada tu ya kutoka ndani ya chumba chao wote wawili wakapiga hatua tatu kusonga mbele ambako macho yao yalikutana na mlango wa kioo hicho ndicho



    kilikuwa chumba cha baba yao.

    “Tuingie huku chumbani.”

    “Kufanya nini wakati ni chumba cha baba?”



    ‘Wewe nifuate mimi acha ubishi wako.”Haraka bila kujiuliza mara mbili wakaufungua mlango na kuzama ndani Mariya akionyesha hofu kubwa.

    Kwa saa tatu mfululizo waliendelea kubaki ndani ya chumba cha mzee wao wakifanya upekuzi kila kona kusoma na kutafuta mahali ambako wangegundua



    kuwepo kwa nyaraka zozote za siri ambazo zingewazesha kupata angalau ndugu mmoja upande wa baba au mama yao. Lakini bado hawakufanikiwa mwisho nao



    wakaanza kukata tamaa kabisa lakini ghafla wakiwa hapo wakakumbuka kwamba walifanya upekuzi kila mahali na walikuwa wamesahau sehemu moja tu ndani



    ya chumba hicho kabati kubwa lililokuwa pembeni kabisa mwa chumba.



    “Bado hili kabati hapa.”

    “Ehhe kweli tulisahau.”

    Wote wakakimbia kulielekea kabati hilo na kufungua mlango mmoja baada ya mwingine kupekua ndani wakitoa nyaraka moja baada ya nyingine na kuzisoma



    lakini bado hawakuona sehemu yoyote ambayo iliandikwa kuonyesha kama Federov alikuwa nani na alitokea wapi akiwa na ndugu wangapi.



    “Mh! Mimi mwenzako nimechoka.”

    “Basi pumzika mimi niendelee lazima tupate kitu humu ndani ya hili kabati vinginevyo sitatoka hapa,” aliongea Merina akiangusha vitu kutoka ndani ya kabati



    bila kujali.

    “Mh!” Merina aliguna.



    “Nini?”

    “Hili kabrasha ni la nini?”

    “Hebu? Tena la rangi nyekundu?”

    “Fungua ndani tuone,” Mariya aliongea na taratibu akasogea karibu kushuhudia ni kitu gani kingeonekana ndani yake.







    Walikuwa wawili tu ndani ya chumba lakini kila mmoja alionekana kuwa na hofu, walitaka kufahamu ni kitu gani kilikuwa ndani ya kabrasha hilo na kibaya



    zaidi lilikuwa la rangi nyekundu na juu yake maneno “Nyaraka muhimu” yalisomeka.

    “Mh! Kwa nini maneno hayo?”

    “Hata mimi sijui ila ngoja tufungue tuone.”

    “Mimi naogopa sana.”

    “Acha woga tunachotaka kufahamu sisi ni ndugu wa baba au upande wa mama yetu ambaye hatukuwahi kumfahamu.”

    “Haya fungua,” Mariya alizidi kusisitiza.

    Wakatembea na kuketi juu ya kitanda hapo wakiwa tayari kufungua kabrasha hilo na kwa ujasiri wa hali ya juu walilifungua na kuliacha wazi, kitu cha kwanza

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    walichokishuhudia kilikuwa ni vyeti vilivyofungwa vizuri na vilivyoonyesha majina yao.

    “Majina yetu haya.”

    “Mh!” pacha mmoja aliguna na kuonyesha mshangao.

    Wakaendelea mbele zaidi kufunua katarasi nyingine, hapo walikutana na wosia mzito wa Victor Federov ukieleza kwamba yeye alikuwa nani na alitokea wapi,



    alizaliwa miaka mingapi iliyopita, haukuishia hapo ukaendelea mbele zaidi akitaja mali zote alizokuwa nazo na kiasi chote cha fedha alizokuwa nazo katika



    benki mbalimbali nchini Urusi, majengo makubwamakubwa na miradi mbalimbali na alitaka vitu hivyo vyote chini ya mwanasheria aliyekuwepo ndani ya wosia



    huo kama siku ikitokea akafa basi utajiri wote huo uende kwa watoto wake.

    Maneno yale yalichoma mioyo ya watoto hao, machozi mfululizo yakawabubujika wakilia na kuomboleza kwani mpaka wakati huo pamoja na kwamba



    walishatoa taarifa katika vyombo vya habari na taarifa nyingine kuzipeleka kwenye vyombo vya habari wakimtafuta baba yao kwa udi na uvumba, alikuwa bado



    hajapatikana.

    “Nahisi hatari fulani.”

    “Mimi pia naungana na wewe.”

    “Ni kwa nini baba aliamua kuandika kitu kama hiki? Je, alifahamu kwamba atakufa muda si mrefu? Na huyu mwanasheria ni nani?” walijiuliza maswali



    mfululizo.

    Huzuni ilikuwa imewagubika lakini pamoja na yote hayo bado hawakutaka kuacha kusoma nyaraka zote zilizokuwa ndani ya kabrasha hilo wakitaka kufahamu



    zaidi siri zilizokuwa ndani.

    “Historia kamili ya watoto Mariya na Merina ilipoanzia mpaka hapa walipo leo, jinsi walivyopatikana na nani hasa alikuwa ni mama yao mzazi” maneno hayo



    yalisomeka kwenye moja ya karatasi ndani ya kabrasha.

    “Mh!” wakaguna.

    Wakaendelea mbele zaidi na kukutana na jina Genevieve huyo ndiye alikuwa mama yao wa kuwazaa lakini mwanamke huyo aliolewa na mwanaume aliyeitwa



    Phillip na waliishi nchini Tanzania.

    Maswali mengi yaliendelea kuzunguka ndani ya vichwa vyao wakitaka kufahamu ukweli wa historia yao lakini kwa wakati huo hakuwepo mtu ambaye



    angewaeleza ukweli, mtu pekee waliyemtengemea alikuwa ni Victor Fedorov.

    “Baba anajua ukweli wote na sasa hayupo, hebu tuendelee mbele zaidi tutajua tu,” aliongea Merina akionyesha msisitizo.

    Kadiri walivyozidi kusonga mbele ndivyo mambo mengi makubwa yalivyoibuka na kuzidi kuwaacha midomo wazi bila kupata ufafanuzi wowote.

    “Mama yetu aliitwa Genevieve?”

    “Historia inaonyesha tulipatikana kwa kupandikizwa katika chupa?”

    Bado watoto hao waliendelea kujiuliza maswali mengi kichwani mwao huku huzuni ikigubika ndani ya mioyo yao, hakika walikuwa wamesoma kitu ambacho



    mpaka wanafikisha umri wa miaka kumi na nane hawakufahamu ukweli wa jambo lolote zaidi sana Fedorov ndiye alikuwa kila kitu.

    “Ni lazima tuzungumze na huyu mwanasheria pengine anaweza kutusaidia zaidi.”

    “Umeongea jambo la maana sana.”

    “Lakini kabla ya yote tusubiri kwanza tuone taarifa za polisi zitasemaje kuhusu baba yetu.”

    Hivyo ndivyo walivyokubaliana na waliamua kusubiri kwa muda mpaka miezi sita baadaye lakini bado Fedorov alikuwa hajapatikana nao pia wakaamini kabisa



    kwamba huenda baba yao alikufa katika mchezo wa barafu na maiti yake kufukiwa na theluji.

    Wakiwa wenye majonzi mioyoni mwao, walipanga kukutana na mwanasheria ambaye alikuwa kwenye nyaraka za Fedorov ili kuongea na kufahamu ukweli wa



    mambo yote.

    Waliamini huyo angeweza kuwasaidia kwa mambo yote muhimu na kufahamu zaidi utajiri wa baba yao, ni kweli wakafanikiwa kuonana naye na kuongea naye



    akawaambia alikuwa ameshtushwa na habari za kupotea kwa Fedorov lakini akawaahidi kwamba angefuatilia kwa karibu majibu ya polisi na angekuwa nao bega



    kwa bega.

    “Tunakushukuru kwa kila kitu lakini jambo moja tunaomba kutoka kwako.”

    “Hakuna shida.”

    “Pamoja na kwamba hivi sasa sisi ni watu wazima lakini tunahitaji uendelee kuwa mshauri na msimamizi wa mali za baba yetu.”

    “Niko tayari,” mwanasheria huyo aliongea kwa kujiamini.

    Wote kwa pamoja wakasimama na kumshika mkono huku wakimtaka kuwa karibu yao na kushirikiana naye kwa kila jambo, wakamshukuru na kuondoka



    kurejea nyumbani.

    “Wiki ijayo lazima tufunge safari kuelekea Tanzania tukamwone huyo anayedaiwa kuwa mama yetu,” Mariya aliongea na Merina akamuunga mkono.

    Maandalizi maalum yakafanyika na utaratibu ulipokamilika Mariya na Merina wakasafiri kuja Afrika ya Mashariki nchini Tanzania, hamu yote ikiwa ni



    kuwafahamu watu wawili Phillip na mkewe Genevieve, pamoja na kugundua ukweli wote wa jinsi walivyopatikana, walitamani kuwaona watu hao wakiamini



    kabisa kwamba walikuwa ni watu muhimu mno katika maisha yao.

    ***

    “Haraka mpelekeni chumba cha wagonjwa mahututi na afungiwe mashine ya hewa ya oksijeni imsadie kupumua,” ilikuwa ni sauti ya daktari mmoja ndani ya



    wodi aliyekuwa akimhudumia Lina.

    “Kimetokea nini?”

    “Hali yake imebadilika ghafla, kwa inavyoonekana ana tatizo kubwa ndani ya kichwa chake ambalo linamsumbua.”

    “Mungu wangu na mume wake ameondoka sasa hivi kwenda nyumbani,” muuguzi aliongea.

    “Kama ana simu apigiwe haraka sana arudi hapa mara moja,” daktari alizidi kusisitiza.

    Muuguzi akachukua faili lililokuwa na kumbukumbu za Lina, hapo akakutana na namba ya mumewe Phillip, haraka bila kuchelewa akakimbia mpaka mapokezi



    ambako aliomba msaada wa kupigiwa namba hiyo.

    Haikuchukua hata dakika mbili tayari namba hiyo ikawa imeita.

    “Hallow, ndiyo hapa ni hospitali tunahitaji urejee haraka sana, hali ya mke wako ni mbaya na hivi sasa ninavyoongea na wewe tunajiandaa kumpeleka chumba



    cha wagonjwa mahututi…,” aliongea muuguzi huyo na simu ikakatika.



    Je, nini kitaendelea?mzigo unaendelea km kawa! love u all mwaaa!!!!





    “Haraka mpelekeni chumba cha wagonjwa mahututi na afungiwe mashine ya hewa ya oksijeni imsaidie kupumua,” ilikuwa ni sauti ya daktari mmoja ndani ya



    wodi aliyekuwa akimhudumia Lina.

    “Kimetokea nini?”

    “Hali yake imebadilika ghafla kwa inavyoonekana ana tatizo kubwa ndani ya kichwa chake ambalo linamsumbua.”

    “Mungu wangu na mume wake ameondoka sasa hivi kwenda nyumbani,” muuguzi aliongea.

    “Kama ana simu apigiwe haraka sana arudi hapa mara moja,” daktari alizidi kusisitiza.

    Muuguzi akachukua faili lililokuwa na kumbukumbu za Lina hapo akakutana na namba ya mumewe Phillip, haraka bila kuchelewa akakimbia mpaka mapokezi



    ambako aliomba msaada wa kupigiwa namba hiyo.

    Haikuchukua hata dakika mbili tayari namba hiyo ikawa imeita.

    “Hallow, ndiyo hapa ni hospitali tunahitaji urejee haraka sana hali ya mke wako ni mbaya na hivi sasa ninavyoongea na wewe tunajiandaa kumpeleka chumba cha



    wagonjwa mahututi…,” aliongea muuguzi huyo na simu ikakatika.

    “Wiki ijayo safari kuelekea Tanzania ni lazima, tukamwone huyo anayedaiwa kuwa mama yetu,” Mariya aliongea na Merina akamuunga mkono.

    Maandalizi maalum yakafanyika na utaratibu ulipokamilika Mariya na Merina wakasafiri kuja Afrika ya Mashariki nchini Tanzania, hamu yote ikiwa ni



    kuwafahamu watu wawili, Phillip na mkewe Genevieve pamoja na kugungua ukweli wote wa jinsi walivyopatikana, walitamani kuwaona watu hao wakiamini



    kabisa kwamba walikuwa ni muhimu mno katika maisha yao.





    Taarifa walizokuwa wamezisoma Mariya na Merina kwenye kabrasha la siri la baba yao, hakika lilikuwa limewatia simanzi kubwa ndani ya mioyo yao, pamoja

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    na kwamba waliufahamu ukweli wote lakini watoto hao walihitaji kumwona mama yao na mtu mwingine aliyekuwa ametajwa ndani ya nyaraka hizo



    aliyejulikana kama Phillip, walitamani kufika nchini Tanzania kwa gharama yoyote ile ilimradi tu wakutane na watu hao.





    Maandalizi yakafanyika haraka chini ya Mwanasheria wao wa familia ambaye ndiye alisimamia kila kitu na safari nzima ya watoto hao akihakikisha kwa fedha



    zilizokuwepo wangeweza kusafiri salama na kurejea salama bila matatizo yoyote yale.

    “Mariya lakini huyu ndiye baba yetu mzazi,”

    “Ni kweli kabisa hilo sina shaka nalo tatizo moja tu linakuja ni kwa nini baba hakuwa mkweli kwetu?”





    “Pengine alifahamu tukipata habari hizo tutaumia kwani kwa maelezo yaliyotolewa ni kwamba baba aliuza mbegu zake za kiume kwa familia ya Phillip ambazo



    zilipandikizwa kwa mwanamke aliyeitwa Genevieve huyo ndiye mama yetu lakini pia Phillip ni mtu muhimu kwetu ni kama baba ni lazima twende haraka,



    nakumbuka kuna wakati baba aliwahi kutueleza kwamba mama yetu alikufa, hivi inawezekana kweli?”

    “Inawezekana hawezi kusema uongo kama huo,”





    “Twende mambo mengine yote tutayajua huko huko?”

    “Tutafanya nini ili kuwafahamu watu hao?” Mariya alimuuliza Merina.

    “Tutatumia vyombo vya habari kutangaza na ikiwezekana kuzungumza kabisa na vyombo hivyo,” Merina alijibu.

    “Kivipi?”Mariya alihoji.





    “Fedha ni kila kitu kwetu,” Merina aliongea kwa kujiamini.

    Hivyo ndivyo walivyomaliza mazungumzo yao na kuanza kujitayarisha kwenda Afrika wakiwa hawaelewi kabisa ni wapi baba yao alipokuwa na alipatwa na kitu



    gani lakini walilazimika kufanya hivyo kwa sababu ya nyaraka za siri walizozisoma. Mioyo yao iliuma mara kadhaa walipomkumbuka baba yao, ucheshi,utani na



    mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwao hakika kwa wakati huo vilikuwa vimekosekana.





    “Mimi naona ni bora tukaondoka na huyu mwanasheria wetu ili akasaidie mchakato huu.”

    “Mh! Wazo zuri sana hebu tumpigie simu naye afanye maandalizi ili kesho jioni tuweze kuondoka.”



    Wakafanya kama walivyokubaliana simu ikapigwa na mwanasheria kupewa taarifa kwamba safari iliyokuwepo mbele yao ililazimu kuongozana nao kwa



    gharama yoyote.

    Hivyo ndivyo walivyofanya siku iliyofuata safari ikaanza, hamu yao kubwa ikiwa ni kuwafahamu watu hao wawili, Phillip na Genevieve, walitamani kuongea



    nao ili kufahamu ukweli juu ya nini kilichotokea.





    Safari yao ilisadikiwa kuchukua saa nane mpaka kufika nchini Tanzania ambako wangefanya utaratibu maalum wa kuwapata walengwa ambao walikuwa ni



    Phillip na Genevieve.

    ***

    Simu iliyokuwa imeingia kwa Phillip ikimtaarifu kwamba alitakiwa kufika hospitalini mara moja ilikuwa imemchanganya kupita maelezo, akiwa hapo alihisi



    hatari na kuiona taa nyekundu ikiwaka ndani ya kichwa chake.





    “Lina! Lina atakuwa amezidiwa,” hivyo ndivyo alivyoongea huku akitweta na bila kuchelewa aliwaaga bibi Magdalena na mtoto wake Genevieve waliokuwa



    pembeni yake akiwaambia wazi kwamba alitakiwa kurejea hospitalini haraka sana.

    “Twende wote baba,” Genevieve aliongea.

    “Hapa…,” alijibu Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake bibi Magdalena aliingilia.

    “Ni lazima tuongozane nasi tufahamu nini kimetokea huko, hatuko tayari kubaki hapa nyumbani, sawa?”

    “Mh! Unajua.”





    “Phillip hakuna haja ya mabishano hapo Genevieve hebu twende…,” bibi Magdalena aliongea akimvuta Genevieve kuelekea kwenye gari.

    Wote wakaingia ndani na Phillip akiwa ndiye dereva alionekana kuwa mtu mwenye msongo mwingi wa mawazo lakini hayo ndiyo yalikuwa maisha hakuwa na



    mtu mwingine wa kumsaidia tatizo lililokuwa mbele yake, kwa kasi ya ajabu akaliendesha gari hatimaye akafanikiwa kufika hospitali ndani ya dakika kumi na



    tano tu.





    Haraka akaegesha gari sehemu maalum na kushuka mbio bila kusema chochote kuelekea chumba ambacho ndicho hasa Lina alilazwa, Genevieve na Magdalena



    wakimfuata kwa nyuma nao pia wakionekana wenye wasiwasi mwingi.





    Dakika tano tu baadaye alifanikiwa kufika kwenye wodi hiyo lakini alishangazwa na ukimya uliokuwepo eneo hilo, bila kuuliza wala kusubiri akausukuma



    mlango na kuzama ndani, kitanda kilikuwa kitupu.

    “Nini kimetokea?” alijiuliza na ghafla akiwa katika kujiuliza muuguzi aliingia ndani ya wodi hiyo.

    “Dada! Dada!” aliita mfululizo.

    “Ndiyo kaka yangu nakusikiliza.”

    “Nauliza mgonjwa aliyekuwa amelazwa hapa muda mchache tu, anaitwa Lina.”





    “Lina?”

    “Ndiyo.”

    “Mh!” badala ya kujibu muuguzi aliguna.

    “Kwa nini unaguna dada?” aliuliza Phillip akimwangalia muuguzi machoni na kugundua kitu tofauti.

    “Ah! Hebu subiri kidogo.”

    “Dada mbona sikuelewi tafadhali nieleze nini kimetokea hapa?” Phillip aliuliza akionyesha msisitizo.





    “Kaka hali ya mgonjwa imebadilika ghafla kwa ujumla ni mbaya…,” aliongea muuguzi huyo lakini hakumaliza sentensi yake mlango ukafunguliwa kwa nguvu.

    “Monica!” ilikuwa ni sauti ya kiume ikiita ndani ya wodi.

    “Bee!” aliitika muuguzi huyo.

    “Unagonja nini tunasubiri hilo faili haraka?”





    “Sawa daktari lakini kuna huyu kaka hapa anauliza kuhusu mgonjwa Lina.”

    “Hebu nifuateni nyuma haraka,” daktari huyo aliongea na wote wakaanza kutoka mbio kumfuata kwa nyuma.

    Hawakupiga hata hatua kumi mbele ya mlango uliokuwa umeandikwa ICU walishuhudia machela ikitolewa kwa mwendo wa kasi kupelekwa sehemu ambayo



    hawakuielewa, Phillip alikuwa wa kwanza kutupa macho juu yake na kumwonga Lina akiwa amelala kimya mdomoni mwake akiwa amefungwa mashine ya



    oksijeni.

    “Mke wangu!” aliongea kwa sauti ya juu.





    “Hali yake ni mbaya tunajaribu kuokoa maisha yake imetulazimu kumpeleka chumba cha upasuaji haraka sana…” aliongea daktari huku machela ikisukumwa



    kuingizwa ndani ya chumba cha upasuaji, Phillip, Genevieve pamoja na Magdalena wakitakiwa kubaki hapo kusubiri.







    Baada ya Lina kuingizwa chumba cha wagonjwa mahututi, uchunguzi maalum uliendelea na Phillip ndiye aliyetakiwa kutoa historia ya mkewe kwani kwa



    wakati huo hakuwa akijitambua. Akawa tayari kueleza kila kitu kilichomtokea mkewe ikiwepo ajali ya moto aliyoipata baada ya gari lake kuwaka moto.

    Katika kufanya uchunguzi kuwa rahisi, jopo la madaktari likaanza kazi, na ni hapo ndipo walipogundua kwamba jeraha la moto alilolipata Lina lilileta madhara



    makubwa sana kwa ndani, madhara ambayo hayakufahamika mapema hivyo walitaka kujaribu kumsaidia kwa kumfanyia upasuaji ili kuondoa tatizo



    lililoonekana ndani ya kichwa.

    Wakiwa katika hali ya kusubiri kuona kama angerejewa na fahamu zake ili kukamilisha vyema uchunguzi wao, hali ya Lina ilibadilika ghafla, ni hapo ndipo



    walipolazimika kumkimbiza chumba cha upasuaji ili kuokoa maisha yake.

    “Hali yake ni mbaya tunajaribu kuokoa maisha yake imetulazimu kumpeleka chumba cha upasuaji haraka sana…,” aliongea daktari huku machela ikisukumwa



    kuingizwa ndani ya chumba cha upasuaji, Phillip, Genevieve pamoja na Magdalena wakitakiwa kubaki hapo kusubiri. Hayo yalikuwa maneno pekee aliyotamka



    daktari na kuingia ndani ya chumba.

    Walibaki nje ya chumba wakionyesha hofu kubwa, Phillip yeye alishindwa kujizuia akajikuta akitokwa na machozi.

    “Baba usilie mama atapona tu,” Genevieve aliongea akimpigapiga baba yake.

    “Najua atapona lakini…” kwikwi ya kulia ikamkamata Phillip binafsi ndani ya moyo wake kwani aliufahamu ukweli kwamba Lina alikuwa katika hali ya kufa



    kwani ripoti ya uchunguzi iliyokuwa imefanyika ilionyesha wazi kwamba alikuwa na tatizo kubwa ndani ya kichwa chake na tayari lilikuwa limechelewa kupata



    ufumbuzi.

    Kwa muda wa saa nne mfululizo waliendelea kusubiri, hamu yao kubwa ikiwa ni kufahamu ni kitu gani kiliendelea ndani ya chumba cha upasuaji, macho na



    masikio yao yote yalielekea kwenye mlango wa chumba kuangalia na kusikiliza.

    “Mbona wamechukua muda mrefu sana,” aliuliza Phillip.

    “Inawezekana bado wanafanya upasuaji.”

    “Mh!”

    “Hebu tuvute subira kidogo tuangalie,” Magdalena aliongea akijaribu kumpa Phillip moyo wa matumaini.Waliendelea kusubiri saa nyingine mbili na kufanya



    idadi ya saa kutimia sita lakini bado hawakuona muuguzi wala daktari akitoka ndani ya chumba hicho, wakaanza kukata tamaa na mioyo yao kuhisi kuna jambo

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    la hatari lilikuwa limetokea na taa nyekundu iliyoashiria hatari ikawa kichwani mwa Phillip.

    “Lazima kuna tatizo siyo rahisi,” aliongea Phillip akitembea kusogelea mlango wa chumba cha upasuaji, akapiga hatua tatu mbele lakini kabla hajanyanyua hatua



    ya nne mlango wa chumba hicho ukaonekana ukifunguliwa na mwanaume aliyevalia koti jeupe akatokeza, Phillip alipomwangalia alimgundua kwamba alikuwa



    ni daktari hivyo wakajikuta wakigonganisha macho na daktari akainama chini.

    Taratibu akionekana mwenye huzuni akamsogelea Phillip kisha akamsabahi na kumtaka kuongozana naye mpaka ofisini kwa maongezi zaidi.

    Ndani ya ofisi tu baada ya kuingia daktari hakutaka kupoteza muda zaidi alimtaka Phillip aketi kwenye kiti naye akaketi, ni hapo ndipo alipomweleza ukweli



    ambao alitakiwa kuufahamu.

    “Pole sana ndugu yetu, sisi kama madaktari pamoja na wauguzi tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu wote kuokoa maisha ya mke wako lakini imeshindi…”

    “Lina wangu amefariki?” Phillip alitamka kwa sauti akinyanyuka kitini.

    “Wewe ni mwanaume hebu jikaze kidogo kwani hayo ndiyo maisha yetu.”

    “Daktari! Daktari unamaanisha unachosema?”

    “Ni kweli tupu mkeo amefariki dunia akiwa juu ya kitanda cha upasuaji muda mfupi tu baada ya kupasua kichwa chake.”

    “Uwiii!Uwiiii!” Phillip alipiga mayowe akiwa hataki kuamini maneno aliyoyasikia kutoka kwa daktari kwamba mkewe mpendwa alikuwa ameaga dunia.

    “Huo ndiyo ukweli wote, tunasikitika sana lakini pia tunakupa pole.”

    Phillip hakujibu kitu tena akanyanyuka kwenye kiti akaufungua mlango na kutoka mbio kuelekea chumba cha upasuaji huku akilia kwa sauti ambayo ndiyo



    iliyowashtua Genevieve na Magdalana waliokuwa wameketi nje ya wodi wakimsubiri.

    “Lina hayupo nasi tena, ameondoka ametuacha” aliongea Phillip huku akilia.

    “Lina amefariki?”

    “Huo ndiyo ukweli hatutamwona tena,” wakiwa hapo wakashuhudia mlango ukifunguliwa na machela iliyoonekana kubeba mtu juu yake akiwa amefunikwa



    kwa shuka la rangi ya kijani kuanzia kichwani hadi miguu ikapitishwa mbele yao.

    “Mke wangu! Huyu ni mke wangu nataka nimwone, Lina wangu kweli umeniacha kama alivyoniacha Genevieve?” Phillip alilia kwa uchungu akitamka maneno



    ya kuumiza moyo. Wakiwa hapo huku wote wakilia wakashuhudia machela ikisukumwa na kupelekwa chumba cha maiti.

    Huku wakiwa na uchungu mioyoni mwao wakaondoka kurejea nyumbani ili kufanya taratibu nyingine, taarifa mbalimbali zikatolewa juu ya tukio hilo, simu



    nyingi zilipigwa na watu wengi walifika nyumbani kwa Phillip kumpa pole na kuomboleza, wengi wao wakiwa wafanyakazi waliofanya kazi na Lina ofisi moja.

    Siku tatu zikatolewa kwa maombolezo, watu wakilia wengi wakisikitikia kifo kilichomkuta Lina. Familia za Phillip na Lina zikajumuika pamoja hatimaye



    mazishi yakafanyika Phillip akitaka mkewe huyo azikwe pembeni tu mwa kaburi la mkewe wa kwanza na watoto wake. Jambo hilo likafanikiwa na Lina



    akazikwa akiwaacha watu wengi katika majonzi, kwa Phillip ikionekana kuwa kama ndoto lakini huo ndiyo ulikuwa ukweli.

    Ni wiki moja tu baada ya Phillip kumzika mkewe mambo yalianza kubadilika, mara kadhaa akionekana kama mtu aliyekuwa na tatizo la akili na alipoulizwa



    hakuwa na jibu la kutoa zaidi ya kububujikwa na machozi, kazini nako mambo hayakwenda sawa hivyo wakalazimika kumpa likizo ya muda akae nyumbani



    pengine akili yake ingetulia.

    Ni kama vile uamuzi huo walikuwa wameukosea, kwani Phillip badala ya kubadilika hali ndiyo ikazidi kuwa mbaya, akawa mlevi kupindukia na kuongea peke



    yake, jambo lililozidi kuishangaza familia yake.

    “Baba kwa nini umekuwa hivyo?” Genevieve aliuliza. Alikuwa ni mtoto mdogo lakini alikuwa na upeo wa kufahamu mazuri na mabaya.

    “Dunia hainitendei haki, ilichukua mke na watoto wangu wawili na sasa imegeuka na kumchukua Lina… ni bora na mimi niwafuate na kuungana nao, bora



    nife…nasem…” aliongea huku kwikwi ya kulia ikimkaba, haraka akanyanyuka kutoka kitini na kukimbia kuelekea chumbani.

    “Baba!Baba!” mtoto Genevieve alikimbia kumfuata baba yake lakini tayari alishachelewa aliposhika mlango ili ausukume kuingia ndani ulionekana kufungwa.







    Genevieve aliendelea kugonga mlango kwa muda bila baba yake kuitikia, naye pia akaanza kulia akimwita bibi Magdalena aje ili waungane kusaidia kumfanya



    Phillip afungue mlango. Kwa muda wa nusu saa nzima bado walisimama nje ya mlango wakimsihi Phillip afungue lakini hakufanya hivyo zaidi sauti ilisikika



    kutoka ndani ya chumba ikiwaeleza wazi kwamba alitaka kufanya uamuzi mgumu hivyo alihitaji nafasi.

    “Phillip lakini ni vyema ukatambua kwamba maisha baada ya kifo cha mkeo ni lazima yaendelee.”

    “Najua hilo tangu mwanzo lakini inauma, ni bora nikaungana nao.”

    “Usimkufuru Mungu na huyu mtoto?”

    “Mtoto? Ah! Atapata wasamaria wema wengine wa kumtunza.”

    “Baba! Baba!” Genevieve aliita na kwikwi ya kulia ikamkaba, hakuongea tena kitu akatoka mbio eneo hilo na kukimbilia ndani ya chumba kisha naye kujifungia.

    Ukawa ni mtihani kwa bibi Magdalena hakufahamu nini afanye kwani kila kitu kilionekana kwenda kombo, kwa muda aliendelea kusimama eneo hilo akitafakari



    nini cha kufanya hatimaye wazo likamjia ndani ya kichwa chake kwamba ni lazima Phillip akubali kushuka kwani hali ya Genevieve ilikuwa mbaya kutokana na



    sentensi aliyokuwa ameitamka muda mfupi uliopita.

    “Genevieve ameumizwa na kauli yako, hivyo amekimbia kuelekea chumbani, kwa ujumla ameumia.”

    “Unasema?”

    “Hivyo ndivyo, tafadhali nakusihi utoke na kumwendea ili kumbembeleza.”

    Ukimya wa ajabu ukatokea na sekunde tatu tu mlango wa chumba ukaonekana ukifunguliwa na Phillip kutokeza huku jasho jingi likitiririka mwilini mwake,



    hakusema kitu zaidi ya kukimbia kuelekea upande ambako ndiko chumba cha Genevieve kilikuwepo. Akausukuma mlango na kuingia ndani ya chumba na



    kilichosikika muda mfupi tu ndani ya chumba hicho ni kilio, wote wawili walikuwa wakilia.

    ***

    Ndani ya hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam ndimo Mariya, Merina na Mwanasheria wao walipokuwa wamefikia hapo ndipo pangekuwa nyumbani kwao



    kwa muda wote ambao wangekuwa Afrika, nchini Tanzania kusaka ukweli wa maisha ya baba yao Victor Federov kwa gharama yoyote ile.

    “Tutapumzika leo na kesho tutaanza mchakato, lazima kwanza tuitishe mkutano na waandishi wa habari lakini kabla ya hayo tunahitaji kukutana na mtu mmoja



    ambaye tutamfanya rafiki huyo ndiye atatusaidia.”

    “Mh! Naona kama ni zoezi gumu kidogo,” Mariya.

    “La hasha! Ni kitu rahisi nitampata mtu hapa hapa hotelini,” mwanasheria aliwaambia.

    “Haya ngoja tuone lakini pia uwe makini kwani hapa tupo ugenini,” Mariya alishauri.

    “Usiwe na shaka Mariya kila kitu kitakwenda sawia.”

    Baada ya mazungumzo hayo kukamilika pamoja na kwamba alikuwa ni mgeni kabisa, Morgan alitoka ndani ya hoteli hiyo kuangalia mazingira akitafuta ni



    namna gani angepata msaada ambao ungemsaidia kufanya kazi yake kwa urahisi, kwa kutumia lifti akashuka mpaka mapokezi hapo akawasabahi watu



    aliowakuta na ghafla kabla hajapiga hatua kutoka nje ya hoteli hiyo macho yake yakagongana na mtu aliyekuwa ameketi pembeni kabisa mwa hoteli hiyo



    mkononi akiwa na gazeti lililosomeka Uwazi, akapata hamu ya kusogea karibu yake ili aongee naye mambo kadhaa kwake hiyo akaiona kama bahati.

    “Habari?” alisabahi kwa lugha ya Kiingereza.

    “Nzuri tu,”

    “Ah! Naitwa Morgan natokea Urusi.”

    “Oh! Karibu mimi naitwa Erick Evarist naishi hapa hapa Tanzania,” Erick alijitambulisha.

    “Naweza kuungana na wewe hapa?”

    “Bila shaka karibu.”

    “Napenda kukufahamu zaidi.”

    “Ni mwandishi wa habari nafanya kazi zangu kwenye Kampuni ya Global Publishers.”

    “Oh! My God!” Morgan alipaza sauti na kuwafanya watu wote waliokuwa eneo hilo kuacha shughuli zao wakabaki kumshangaa. Erick naye akashindwa kuelewa



    ni kitu gani kilikuwa kinatokea eneo hilo.

    Kabla hajaendelea kusema chochote, Morgan akamwomba Erick wasogee pembeni ili waweze kuongea zaidi.

    “Hakuna shida,” Erick aliongea akimfuata mwanaume huyo na wote wakaketi kwenye viti vilivyokuwa hapo na mazungumzo maalum yakaanza, Morgan

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akimweleza wazi kwamba alifurahi kukutana naye na kazi iliyokuwa imemleta nchini Tanzania ni kutaka amsaidie kwa kila kitu na kama angehitaji kiasi



    chochote cha fedha angekuwa tayari kumpatia lakini tu amsaidie.

    Hakuficha kitu akaweka kila kitu wazi kwamba walikuja nchini hapo kutafuta ukweli wa mwanaume aliyeitwa Phillip na mkewe Genevieve na hawakuwa na



    msaada wowote.

    “Niko tayari kukusaidia.”

    “Kivipi?”

    “Nitakusaidia ufanye kitu kinachoitwa Press Conference, utakutana na waandishi wa habari ambao nitaongea nao kuwaeleza shida yako halafu utatakiwa kufanya



    kikao cha pamoja kisha kupiga picha ili kuandika habari hizo kwenye magazeti yetu, watu wakisoma naamini utapata ufumbuzi wa tatizo lako.”

    “Inaweza ikachukua muda gani kuanzia sasa?”

    “Kazi hiyo nitaifanya leo na kesho nitakupa majibu,”

    “Tutakutana wapi?”

    “Nitakuja hapa hapa hotelini lakini ni vyema ukanipatia namba yako ya simu ili iwe rahisi kuwasiliana na wewe.”

    “Ahsante rafiki, wewe kwangu ni kama malaika, chukua hii,” aliongea Morgan akichomoa kadi yake yenye namba za simu na kumkabidhi Erick ambaye



    aliipokea, wakaagana wakiahidiana kukutana tena kesho yake.

    Baada tu ya Erick kuondoka eneo hilo, Morgan alipandisha lifti haraka kwenda chumbani kwa akina Marina kuwaeleza kila kitu. Mariya na Marina walifurahi



    sana kupewa habari hizo njema.

    “Mungu yupo pamoja nasi, naona mwanzo umekuwa mzuri,” Mariya aliwaambia.

    “Tena tutakapofanikisha jambo hili itabidi tukamtolee shukurani ya pekee,” Marina aliunga mkono.

    Wakiwa pale hotelini, waliona saa zinachelewa ili kuifikia siku iliyofuata ambayo mwanasheria wao angekutana na Erick na kumpa utaratibu wa mkutano wao



    na waandishi wa habari ambao ungemaliza kazi iliyowaleta Tanzania.

    Kama walivyokuwa wamepanga kesho ikawadia, Morgan akiwa tayari kumsubiri Erick afike ili waendelee na mazungumzo yao na kuona walikuwa



    wamefanikiwa kwa kiasi gani kuhusu shughuli iliyokuwa mbele yao.

    Ilipotimu saa tatu kamili asuhubi, Erick aliwasilia hotelini hapo na mazungumzo yakafanyika na mwisho ukaonekana kuwa mzuri akimweleza wazi kwamba



    alishafanikiwa kukutana na baadhi ya waandishi na kuwaeleza habari hiyo na walipanga kukutana siku iliyofuata pale hotelini.

    Morgan akashukuru na kupeana ahadi ya kukutana na Erick siku iliyofuata kisha wakaagana.

    Muda huo huo alifanya utaratibu wa kupata kibali cha kufanya mkutano ndani ya hoteli hiyo, ambapo alipewa chumba kikubwa kilichotumika kwa shughuli



    hiyo.

    ***

    Hali ya Phillip ilikuwa imebadilika kabisa utanashati wote aliokuwa nao kipindi akiwa na mke wake ukawa umepotea, mahudhurio ya kazi nayo yalionekana



    kusuasua kitendo kilichofanya mpaka mabosi wake waaanze kuingiwa na wasiwasi.

    Nyumbani nako hali ilikuwa tofauti kwani muda mwingi aliutumia kulala na alipochoka alitoka bila kuaga na kuingia mtaani kunywa pombe ili kupoteza



    msongo wa mawazo.

    Phillip akawa ni mtu wa kukitamani kifo kuliko kitu kingine, haikuishia hapo akaanza tabia ya kutoka nyumbani na kwenda makaburini na alipofika huko



    alitafuta kaburi la mkewe Lina na kulala juu yake.

    Ni hali hiyo ndiyo iliyozidi kuichanganya zaidi familia yake nao pia wakaingiwa na wasiwasi na kuamini kwamba si muda mrefu Phillip angekuwa



    mwendawazimu, ndugu na jamaa wakakaa kikao kuangalia ni jinsi gani wanaweza kumsaidia na walipomuuliza, jibu lilikuwa moja tu.

    “Nataka kufa, basi.”





    MAISHA yalikuwa yamebadilika kabisa kwa Phillip ni kama vile dunia yake ilikuwa imegeuka na kuwa nje ndani, akapoteza kabisa mwelekeo wa maisha yake na



    kusahau kwamba alikuwa ana jukumu la kumlea mtoto mdogo Genevieve ambaye bado alihitaji ushauri wa wazazi wake japo tayari mmoja alishaaga dunia.

    Ushauri na ushawishi mkubwa wa ndugu, jamaa na marafiki haukusaidia kitu na hata walipoamua kutumia ofisi yake kumshauri bado hakubadilika ndiyo



    kwanza alizidisha ulevi na kutembea barabarani kutwa nzima akiongea na kutukana watu bila sababu.



    Phillip akawa ameharibikiwa kabisa, ofisi ikaamua kumwachisha kazi kwa nguvu lakini wakiahidi kumsaidia kama tu msaada wowote ungehitajika, nyumbani



    nako hali kwa mtoto ikawa mbaya hata shule akawa haendi tena kwa sababu hapakuwa na ada ili aweze kuendelea na masomo, hakika maisha yakawa magumu



    kupindukia.

    Lakini bado watu mbalimbali waliomfahamu Phillip hawakumwacha peke yake waliendelea kumshauri na kumpa moyo kwamba maisha yaliendelea na kamwe



    yasingesimama. Phillip akapokea ushauri wao ambao uliingia sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto kwani hakuweza kubadilika, zaidi sana vituko



    viliongezeka nao pia wakaanza kuchoka na kumwacha afanye alivyopenda.



    ***

    Ndani ya hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam chumba maalum kilikuwa kimeandaliwa tayari kwa mkutano mfupi ambao ungefanyika siku hiyo. Mariya na



    Merina ambao ndiyo waongeaji wakubwa, pembeni yao akiwepo mwanasheria aliyesimamia mambo yote zikiwemo mali za baba yao Victor Fedorov ambaye



    mpaka wakati huo hakufahamika kama alikuwa amekufa au la!

    Waandishi walikuwa ni wengi mno mikononi mwao wakiwa na kalamu zao na kamera ili kuchukua habari ambayo ingepelekwa katika vyombo vyote vya habari



    yaani magazeti, redio na televisheni.



    Mkutano ukawa umeanza, Mariya na Merina wakijitambulisha kwamba walikuwa akina nani na walitokea wapi na nini lilikuwa lengo lililowaleta nchini



    Tanzania, waliongea katika lugha ya Kirusi na Morgan akaitohoa katika lugha ya Kiingereza na baadaye Erick Evarist akatafsiri katika lugha ya Kiswahili.

    Wakisisitiza kwamba walihitaji kufahamu mahali ambako Phillip na mkewe Genevieve wangepatikana na kwa gharama yoyote ile wangekuwa tayari kutimiza



    hilo lakini tu wapate ushirikiano.



    Hivyo ndivyo mambo yalivyoendelea ndani ya hoteli hiyo kwenye chumba maalum, kwa muda wa saa nzima watoto hao waliendelea kuongea na waandishi wa



    habari wakiwaomba na kuwasihi kusaidia kuandika habari hizo ili hatimaye mtu anayetafutwa aweze kupatikana kwa urahisi.

    “Wanamtafuta nani?”

    “Wanasema wanatafuta familia ya Phillip na mkewe Genevieve.”

    “Mh!”



    “Kwa nini?”

    “Hata sisi hatujui ila wanasema kwamba Genevieve ndiye mama yao mzazi.”

    “Hawa watoto mbona siyo Watanzania?”

    “Unalosema ni kweli lakini hatuwezi kujua, sisi tufanye tu kazi yetu,” yalikuwa ni maongezi kati ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo



    wakijiuliza maswali mengi juu ya mkutano huo na watu waliouitisha.



    Baada ya habari kukamilika Mariya na Merina wakawashukuru waandishi huku wakiwashika mkono na kuwapatia bahasha ambayo ndani yake haikufahamika



    ilikuwa na nini na kuwatakia kila la kheri katika utendaji wa kazi zao na kuwaeleza wazi kwamba ili waweze kuwapata watu waliowahitaji, waliwategemea sana



    wao.

    Waandishi nao wakashukuru wakiahidi kufanya kila kilichowezekana habari hiyo ichapishwe katika magazeti na ikiwezekana kutangazwa katika vyombo vyote



    vya habari zikiwemo redio na televisheni.



    Baada ya waandishi kuondoka, wakarejea ndani ya vyumba vyao hamu yao kubwa ikabaki kusubiri nini magazeti yangeandika, ambapo macho na masikio yao



    yote yakaelekezwa huko.

    “Nafikiria kila kitu kitakwenda sawa, tusubiri kesho tuone,” Morgan aliongea.

    “Hata mimi nahisi hivyo ngoja tuone,” waliendelea kuongea wakijipa matumaini kwamba kila kitu kingekwenda sawa.

    Saa zikazidi kusonga mbele hatimaye kiza kikaingia, hapo wakaamua kula chakula cha usiku na kuingia kwenye vitanda vyao wakiwa na hamu ya kujua kesho



    yake kitatokea nini.



    ***

    Asubuhi ya siku iliyofuata Morgan alikuwa wa kwanza kutoka ndani ya chumba na bila kufanya kitu chochote akashuka kwa lifti mpaka mapokezi hapo



    akasabahi watu aliowakuta kisha kutoka nje ya hoteli kuelekea barabarani akitafuta mahali ambako angekutana na wauza magazeti na kununua ili kusoma kama



    habari yao ingekuwa imeandikwa siku hiyo.

    Ni kweli kabisa alichokuwa amekifikiria kichwani mwake hakikuwa uongo, mtu wa kwanza tu aliyekutana naye akiwa na magazeti mkononi akamwita na



    kuchukua moja ya magazeti aliyokuwa nayo, macho yake yakakutana na picha ya Mariya na Merina mbele yao kukiwa na vipaza sauti vingi, hakuelewa lugha ya



    Kiswahili lakini aliweza kuisoma picha.



    Akamwomba tena muuza magazeti ampatie magazeti mengine zaidi, nayo habari iliyosomeka ukurasa wa kwanza tu wa magazeti hayo ilikuwa ileile ya kwao,



    furaha ikamjaa moyoni mwake akajiona mshindi kati ya washindi na akalazimika kununua magazeti zaidi ya sita akalipa na kurejea ndani ya hoteli huku jasho



    likimtoka.

    Haraka akapandisha lifti na moja kwa moja akauendea mlango ambao ndani yake walilala Mariya na Merina akagonga kwa nguvu na kusubiri mlango

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ufunguliwe na akiwa hapo akashuhudia Mariya akichungulia baada ya kufungua mlango.



    “Magazeti haya hapa,” aliongea akinyoosha mkono kumpatia Mariya magazeti yote aliyokuwa nayo.

    Kwa macho yake yote mawili akashuhudia kurasa za mbele za magazeti hayo zikiwa na picha yao kubwa akacheka na kutabasamu na bila kusema neno akarejea



    ndani ya chumba chao huku akimwita Merina.

    “Merina! Merina, amka uone mwenyewe magazeti karibu yote yameandika habari yetu, kazi imekuwa rahisi sana kuliko tulivyotarajia…,” aliongea Mariya bila



    kuweka kituo.



    Furaha ilikuwa imetawala ndani ya chumba wakiamini kwamba muda si mrefu kila kitu kingekwenda sawa kama walivyofikiria, kwa pamoja wakakumbatiana na



    kupigana mabusu lakini ghafla wakiwa katika furaha yao hiyo taswira ya baba yao Victor Fedorov mwanaume aliyewapenda kupindukia ikawajia, ni kweli



    walikuwa na furaha ya kuufahamu ukweli mwingine uliokuwa umejificha lakini pia Fedorov alikuwa ndiye mzazi wao halisi pamoja na mambo yote mabaya



    aliyoyatenda bado walimpenda.

    “Sijui atakuwa wapi? Amepatwa na kitu gani? Inauma sana,” aliongea Merina huku akilia.



    ***

    Asubuhi ya siku iliyofuata baada tu ya Merina na Mariya kufanya mkutano jana yake na waandishi wa habari, Phillip alikuwa katika mitaa ya Posta akikatisha



    huku na kule bila kuelewa anakwenda wapi.

    Ghafla mbele yake akaiona meza ya magazeti na kuamua kutupa macho juu yake ili angalau asome kilichokuwa kimeandikwa siku hiyo, akasogea karibu kabisa



    na muuza magazeti kisha kumsabahi.

    “Habari za leo?”

    “Nzuri tu kaka karibu.”



    “Ahsante, naweza kupitishapitisha macho kidogo?”

    “Bila shaka lakini usiguse kama hutalinunua.”

    Akaitika kwa ishara ya kutingisha kichwa kisha akasogea karibu na meza hiyo na kutupa macho juu ya magazeti, ni habari ya kwanza tu katika gazeti la Uwazi



    ikamshtua.

    “Mh!”



    “Mbona umeguna kaka?”

    “Hii habari, inanihusu mimi kabisa na hao ni watoto wangu lakini walikufa.”

    “Wewe mzee chizi nini utakuwa hamnazo watoto wako? Wewe? Hebu ondoka hapa haraka kabla sijakuitia mgambo wa jiji.”

    “Dorice na Dorica,” alitamka kwa sauti ya juu.

    Nimekuambia ondoka haraka,” aliongea muuza magazeti huyo akimvuta Phillip kumwondoa eneo hilo.



    “Usinifanyie hivyo ndugu yangu nakuambia ukweli tafadhali nipe gazeti nione vizuri.”

    “Wazee wengine bwana sijui wachawi au wanatumwa kuwangia biashara za watu! Asubuhi hii, kama unataka gazeti si ununue lakini siyo ujipendekeze kwa



    watoto wa watu.”

    “Usinivu…,” aliongea Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake tayari akashuhudia vibao mfululizo vikipita mashavuni mwake.







    VIBAO mfululizo vilikuwa vimetua kwenye mashavu ya Phillip na kumpeleka chini akajikuta ameketi kitako bila kutarajia huku akilia na kujaribu kumweleza



    kijana yule ukweli kwamba habari iliyoandikwa ilimhusu yeye na watoto wake ambao hakika kwa wakati huo walikuwa ni marehemu.

    Ni kilio cha Phillip ndicho kilichokusanya watu eneo la tukio, wengi wakijaribu kudadisi ni kitu gani kilikuwa kimetokea asubuhi hiyo. Kijana wa magazeti



    akaanza kusimulia tukio zima, muda wote huo Phillip akiendelea kulia.



    Bahati nzuri asubuhi hiyo watu wengi walikuwa wakielekea makazini kwao, ni mfanyakazi mmoja aliyefanya kazi na Phillip alipita eneo hilo naye akitaka



    kuangalia nini lilikuwa tatizo. Akiwa hapo akatupa macho yake katikati ya umati wa watu akamwona mwanaume akiwa chini tena akilia.

    “Mh!” akaguna akisogea karibu ili kuhakikisha kitu alichokiona.

    “Phillip!” alitamka kwa sauti ya juu na kufanya watu wote kumwangalia yeye.



    “Namjua huyu ni shemeji yangu pia ni mfanyakazi mwenzangu, jamani amefanya nini tena? Halafu ana tatizo la akili kidogo toka amefiwa na mkewe amekuwa



    hivyo, hebu njoo,” msichana huyo aliongea.

    “Blandina sitaondoka hapa mpaka nipate gazeti.”

    “Gazeti?”

    “Ndiyo.”



    “Lina nini?”

    “Nimesoma kwa macho yangu habari kwamba Dorice na Dorica wako hapa Tanzania tena wananitafuta mimi na mama yao.”

    “Phillip!”

    “Hutaamini lakini huo ndiyo ukweli, wewe nunua usome kisha utanipatia na mimi.”



    Msichana huyo bila ubishi akafungua mkoba wake na kutoa noti ya shilingi mia tano kisha kununua gazeti la Nipashe haraka akatupa macho yake ukurasa wa



    mbele, yeye pia akashuhudia picha kubwa iliyoonyesha wasichana wawili na chini yake kulionekana habari iliyowahusu lakini pia ikimtaja Phillip kwa majina



    yote matatu na Genevieve ambaye kwa historia aliyokuwa ameipata alikuwa ni mke wa Phillip aliyefariki dunia miaka kadhaa iliyopita.

    “Naota au?”



    “Huoti unachokiona hapo ni kweli tupu, tafadhali nisaidie nahitaji kujua wako wapi niwafuate nikaongee nao niujue ukweli,” aliongea Phillip akinyanyuka



    kutoka chini.

    Watu wote waliokuwa eneo la tukio pamoja na kijana aliyekuwa akiuza magazeti wakaonekana kupigwa na butwaa kwani kwa wengi Phillip alionekana kichaa.

    “Twende,” aliongea msichana huyo akimshika Phillip mkono, wakatembea mpaka kwenye mgahawa mmoja hapo wakaketi na kwa umakini wa hali ya juu



    wakaanza kusoma habari hiyo mwanzo mpaka mwisho na kuelewa sehemu ambayo watoto hao walikuwa wamefikia.



    “Nisaidie ndugu yangu nahitaji kuonana nao leo hii.”

    “Hakuna shida ila watakubali? Unayo kumbukumbu gani itakayokufanya wakuamini kwamba wewe ni baba yao?”

    “Ninazo nyingi tu mojawapo ni picha zao za utotoni ziko nyumbani naweza kwenda kuzichukua.”

    “Basi twende tukajaribu,” msichana huyo akaamua kushirikiana na Phillip ili kumsaidia.



    Wakatembea mpaka kando kidogo na hapo akaita teksi ambayo iliwapeleka moja kwa moja nyumbani kwa Phillip ambako aliingia ndani na bila kusema kitu



    chochote akaingia chumbani kwake na kutoka na bahasha mkononi huku akikimbia akitoka tena nje na kuielekea teksi iliyokuwa ikimsubiri, akaingia ndani na



    dereva akaondoka kwa kasi ya ajabu moja kwa moja kuelekea katika hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam ambako wangejitambulisha na kuomba kuonana na



    Mariya na Merina.

    Njia nzima Phillip alikuwa akilia, hakuamini mambo yaliyokuwa yanamtokea maishani mwake na mara kadhaa akamwomba msichana aliyekuwa naye ajaribu



    kumfinya pengine angeamka kutoka usingizini.



    “Phillip shemeji yangu huoti hata kidogo yote yanayotokea ni kweli tupu, tatizo ni moja tu iweje watoto waliokuwa wamekufa na kuzikwa wawe hai? Hapo



    mimi nashindwa kabisa kuelewa na je, watakubali na kuamini kwamba wewe ndiye baba yao?”

    Swali hilo lilipenya moja kwa moja masikioni mwa Phillip na kwenda ndani kabisa ya kichwa chake, akaiona picha yote jinsi walivyohangaika mpaka kufikia



    kununua mbegu za mwanaume mwingine ambaye aliitwa Victor Fedorov, alipofika hapo machozi yakambubujika.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gari likaendeshwa na hatimaye nusu saa tu baadaye lilishawasili nje ya hoteli hiyo maarufu na wakalipa kisha kushuka kutembea kuelekea mapokezi ambako



    wangejitambulisha na kuomba kusaidiwa shida yao.

    Kwao zoezi halikuwa gumu walifanya kama walivyopanga na kufanikiwa kuonana na watoto hao wawili. Mapokezi simu ikapigwa moja kwa moja kwenye



    chumba alicholala Morgan na simu hiyo ikapokelewa.



    “Naongea kutoka mapokezi hapa kuna wageni wenu wawili.”

    “Wawili? Wa jinsia gani?”

    “Mwanamke na mwanaume.”

    “Mh! Sawa waeleze tutakuwa hapo baada ya dakika tano kuanzia sasa hivi.” Morgan alijibu na kukata simu na bila kuchelewa akatoka chumbani kwake kwenda



    kwa akina Marina hapo akawapa taarifa na kuwataka wajiandae kukutana na wageni waliokuwa wamefika pale kuwatafuta.



    “Pengine ndiyo hao tunaowatafuta.”

    “Umejuaje hebu tukawaone kwanza.”

    Haraka wakajiandaa na walipokuwa tayari wakatembea kuelekea sehemu kulikokuwa na mlango wenye lifti wote watatu wakashuka kuelekea chini wakitamani



    kuonana na watu hao.

    “Je, tutawaamini vipi kama kweli ndiyo wenyewe?” Morgan aliuliza.



    “Kabla ya yote tutahitaji kuwasikiliza kwanza wao na kama kuna kitu chochote kinachoonyesha kwamba wao ndiyo haswa walengwa wa safari yetu.”

    “Hilo nakubaliana na wewe,”Merina alidakia na tayari walishafika chini mlango wa lifti ukaonekana kufunguka na kutoka nje.



    Huku vichwani mwao wakijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu wakatokeza mapokezi na macho yao kukutana na watu wawili, mwanamke na mwanaume,



    ambao hawakuwafahamu kabisa lakini ghafla kabla hawajapiga hatua nyingine kwenda mbele zaidi wakashtushwa na sauti kubwa ndani ya chumba.

    “Dorice! Dorica! Si mliku…,” aliongea Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake akaanguka chini kama mzigo.







    GARI likaendeshwa na hatimaye nusu saa tu baadaye lilishawasili nje ya hoteli hiyo maarufu na wakalipa kisha kushuka kutembea kuelekea mapokezi ambako



    wangejitambulisha na kuomba kusaidiwa shida yao. Kwao zoezi halikuwa gumu, walifanya kama walivyopanga na kufanikiwa kuonana na watoto hao wawili.



    Katika eneo la mapokezi simu ikapigwa moja kwa moja kwenye chumba alicholala Morgan na simu hiyo ikapokelewa.

    “Naongea kutoka mapokezi, hapa kuna wageni wenu wawili.”



    “Wawili? Wa jinsi gani?”

    “Mwanamke na mwanaume.”

    “Mh! Sawa waeleze tutakuwa hapo baada ya dakika tano kuanzia sasa hivi.” Morgan alijibu na kukata simu na bila kuchelewa akatoka chumbani kwake kwenda



    kwa akina Marina hapo akawapa taarifa na kuwataka wajiandae kukutana na wageni waliokuwa wamekuja hapo kuwatafuta.



    “Pengine ndiyo hao tunaowatafuta.”

    “Umejuaje hebu tukawaone kwanza.”

    Haraka wakajiandaa na walipokuwa tayari wakatembea kuelekea sehemu kulikokuwa na mlango wenye lifti, wote watatu wakashuka kuelekea chini wakitamani



    kuonana na watu hao.



    “Je, tutawaamini vipi kama kweli ndiyo wenyewe?” Morgan aliuliza.

    “Kabla ya yote tutahitaji kuwasikiliza kwanza wao na kama kuna kitu chochote kinachoonyesha kwamba wao ndiyo haswa walengwa wa safari yetu tutafahamu



    huko.”

    “Hilo nakubaliana na wewe,” Merina alidakia na tayari walishafika chini mlango wa lifti ukaonekana kufunguka na kutoka nje.



    Huku vichwani mwao wakijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu wakatokeza mapokezi na macho yao kukutana na watu wawili, mwanamke na mwanaume,



    ambao hawakuwafahamu kabisa lakini ghafla kabla hawajapiga hatua nyingine kwenda mbele zaidi wakashtushwa na sauti kubwa ndani ya chumba.

    “Dorice! Dorica! Si mliku…” aliongea Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake akaanguka chini kama mzigo.



    ULIKUWA ni mshtuko mkubwa Phillip alipoanguka chini watu wote ndani ya chumba walianza kukimbizana huku na kule kutafuta msaada, Blandina aliyekuwa



    ameongozana na Phillip yeye pia alikuwa akilia huku akimwita Phillip.

    “Tafadhali usife, huu ndiyo wakati wa kuufahamu ukweli, amka nakuomba.”

    Lakini bado Phillip aliendelea kulala chini akiwa hajitambui.



    Haraka daktari aliyefanya kazi ndani ya hoteli kwa dharura akaitwa na mara moja akaanza kumpatia Phillip huduma ya kwanza ili kumnusuru na umauti ambao



    ulikuwa unamnyemelea.

    Kwa takribani nusu saa nzima daktari aliendelea kumpatia huduma ya kwanza Phillip mwisho naye akaanza kukata tamaa akieleza wazi kwamba ni vyema mtu



    huyo akapelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi.



    “Hospitali?”

    ”Ndiyo kwa jinsi hali ninavyoiona ni bora iwe hivyo.”

    “Mh!” Blandina akaguna lakini ghafla wakiwa katika kujadili wakashuhudia Phillip akifungua macho yake na kuangaza huku na kule ndani ya hoteli.

    Haraka kama vile alikuwa akiota akakurupuka kutoka chini na kusimama akionekana kutafuta kitu ambacho hakikuonekana kwa wengi.

    “Bahasha yangu! Nataka bahasha yangu nilikuwa nayo muda si mrefu.”



    “Hii hapa,” Blandina aliongea akinyoosha mkono kukabidhi bahasha kwa Phillip.

    “Nasema ukweli watoto hao hapo ni wa kwangu lakini sikuwahi kuwapa majina hayo ya Mariya na Merina waliitwa Dorica na Dorice!”

    “Lakini hawa ni Mariya na Merina si majina hayo unayosema wewe!”

    “Hakika ninawaeleza ni watoto wangu ushahidi wangu upo, ni picha nakumbuka vizuri sura zao na mama yao pia,” Phillip aliongea mfululizo.

    Morgan ambaye ndiye alikuwa mwanasheria aliyeongozana na akina Merina na Mariya akasogea karibu na Phillip ili kupata ushahidi wa picha kama Phillip



    mwenyewe alivyosema.



    “Naweza kuona picha hizo?” aliuliza.

    “Hizi hapa,” Phillip aliongea akifungua mfuko wa khaki na kuchomoa picha zilizokuwa ndani yake akazikabidhi kwa Morgan ambaye alianza kupitisha macho



    juu yake.

    “Mh!” akaguna, picha zilizokuwa mikononi mwake zilikuwa za watoto wawili waliokuwa wamesimama mbele yake yaani Merina na Mariya akashuhudia picha



    nyingine za watoto hao wakiwa na mama yao mzazi ambaye ndiye aliitwa Genevieve, yeye pia akapigwa na butwaa.



    Mariya na Merina nao pia wakasogea karibu na Morgan ili kushuhudia kilichokuwa kikiendelea, macho yao yakatua moja kwa moja katika picha zao na



    mwanamke mmoja akiwa pembeni yao, huyo ndiye alikuwa mama yao.

    “Anafanana na sisi kabisa kwa kila kitu,” waliongea kwa sauti.

    “Ni kweli yawezekana huyo ndiye tunayemtafuta.”

    “Je, yuko wapi mwanamke huyu?”



    “Genevieve alikufa!”

    “Unasema?”

    “Amini ninachowaambia, huo ndiyo ukweli wangu kama mnaweza kusadiki maneno yangu basi sadikini,” Phillip aliongea huku kwikwi ya kulia ikimkaba.

    Maswali yakawa mengi bila majibu, ni kweli walimtafuta mwanaume aliyeitwa Phillip na mkewe Genevieve lakini kilichozidi kuwashangaza zaidi ni kwamba



    iweje mwanaume huyo aseme kwamba walikufa na kuzikwa miaka mingi iliyopita ili hali wao walikuwa hai?



    Baada ya mvutano mrefu wakaomba chumba maalum ili waweze kuongea vizuri kuupata ukweli waliokuwa wakiutafuta Morgan akiwa ndiye kiongozi wa



    kikao, huko waliongea mengi Phillip akijaribu kueleza ukweli na ni kwa nini aliamini watoto hao walikufa. Akasimulia ajali ya gari kulipuliwa kwa bomu na



    watoto wote kufahamika walikufa.

    Ilikuwa ni historia chungu lakini ilibidi Merina na Mariya waikubali, wakataka kuonyeshwa makaburi ili wakashuhudie kwa macho yao, jambo ambalo halikuwa



    na tatizo. Historia nyingine iliyokuwa imewaumiza watoto hao ni taarifa kwamba mama yao alikufa muda mrefu lakini pia alizikwa pembeni mwa makaburi yao.



    “Hatuna muda wa kupoteza tunachohitaji sisi ni kuona hayo makaburi tena kama inawezekana sasa hivi,” Morgan aliongea.

    “Hakuna shida tunaweza kwenda,” Phillip aliongea kwa majonzi.

    Safari kuelekea makaburini ikaanza na kwa sababu walitumia usafiri wa kukodi haikuchukua muda wakawasili katika makaburi ambako walisemekana kuzikwa,

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakashuka wakiwa na hamu ya kufahamu historia ya kifo. Kwa sababu makaburi yao hayakuwa mbali sana haikuchukua muda kuyafikia ambapo wakashuhudia



    picha zikiwa katika fremu kwa pamoja wakaangua kilio.



    “Ni kwa nini haya yote? Mbona sisi tuko hai? Kuna nini kilitokea? Lazima ipo siri ambayo hatuwezi kuifahamu, na huyu ndiye mama yetu?” wakauliza.

    “Mnachokiona wanangu ndicho kilichotokea, sikuwahi kufahamu kwamba hamkufa, mimi pia nahisi ni mchezo ulichezwa naomba mnisamehe.”

    “Ukweli ni historia inayosikitisha sana lakini hatuna budi kuikubali pamoja na kuugundua ukweli huu wewe utabaki kuwa ba..ba..ye…tu!” waliongea watoto



    hao huku wakilia.



    Mioyo yao ilikuwa imeumia kupita kiasi kwa historia waliyokuwa wameipata lakini upande mwingine walionekana kufurahia kujua ukweli kwani



    walioufahamu kama ndiyo ukweli haukuwa sawa, Federov alikuwa ndiye baba yao halisi na mama yao alikuwa Genevieve lakini Phillip alihusishwa zaidi kwani



    ndiye aliyewalea wakiwa watoto wadogo baada ya kununua mbegu za kiume kutoka kwa Fedorov.

    “Tunakupenda sana,” waliongea wakitembea kuondoka eneo la makaburini kurejea hotelini ndani ya vichwa vyao wakiwaza na kuwazua mambo mengi bila



    kupata majibu, walihitaji kupata historia zaidi ili waamini kwa asilimia zote.



    “Lakini tunahitaji kupata historia ya ndani zaidi ili kukufahamu vizuri.”

    “Hakuna shida niko tayari kueleza kila kitu ambacho mtahitaji.”

    Wakati wakiongea hayo walishafika eneo la maegesho la hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam, wakashuka na kuingia ndani ili kuendelea na maongezi zaidi



    wakiwa tayari kumsikiliza Phillip.



    Walitaka kusikia kama Phillip angekuwa tayari kusema ukweli wake wote alioufahamu ili nao waoanishe na maelezo ambayo waliyasoma kutoka kwenye



    nyaraka za baba yao.

    “Historia nitakayosema inaumiza kupita maelezo lakini naomba muipokee kwa mikono miwili na kuichunguza hapo ndipo mtaugundua ukweli wote.”

    “Mh! Tuko tayari kukusikiliza.”



    “Mimi na mama yenu ambaye ni marehemu yaani Genevieve tulifunga ndoa miaka mingi iliyopita na maisha yetu yalikuwa ya raha mustarehe, jambo moja tu



    lilikosekana kwa bahati mbaya mimi sikuwa na mbegu za uzazi za kuweza kuzalisha mwanamke hivyo tukatafuta daktari ambaye tulimpata kama sikosei aliitwa



    Dk. Koher huyu alitusaidia sana na tukafanikiwa kupata mbegu za kununua kwa mwanaume mmoja aliyekuwa maskini akiishi mtaani, huyo aliitwa Victor



    Fedorov.



    Ukafanyika utaalam wa kitabibu na ninyi mkazaliwa, furaha ndani ya nyumba ikaongezeka huku tukiwalea vyema na kuwatunza mpaka mlipofikisha umri wa



    miaka mitano ndipo tukaamua kuwapeleka shule lakini siku moja asubuhi nikapata ujumbe kwamba gari iliyokuwa imewabeba ilitegeshwa bomu hivyo



    lingelipuka na watoto wote kufa.



    Nilijitahidi sana kunusuru maisha yenu lakini nilishachelewa, gari likalipuka na watoto wote ndani ya basi kuaminika kufa, tulilia na kuomboleza baadaye



    tukafanya mazishi ndiyo yale makaburi niliyowapeleka yakiwa na picha zenu juu. Akili yangu inavurugika zaidi iweje leo muwe hai tena katika nchi nyingine



    kabisa…,” aliongea Phillip muda wote huo akibubujikwa na machozi.

    “Usilie tafadhali nyamaza.”

    “Inanichanganya akili iweje muwe hai wakati mlishakufa tukawazika? Hapana hii ni ndoto pengine nitaamka na kukuta kila kitu kiko sawa, hebu nifinye.”







    PHILLIP hakuwa katika ndoto kama alivyokuwa akifikiria kwani mambo yote yaliyokuwa yakimtokea yalikuwa ya kweli japo historia iliumiza mioyo ya wengi.

    Vilio na machozi kwa Merina na Mariya havikukauka, walilia na kuomboleza kwa mambo mengi lakini kubwa zaidi ni lile la kuelezwa kwamba walikufa miaka



    mingi iliyopita kwa ajali ya bomu ambalo lilitegwa kwenye gari lao la shule na kuzikwa sehemu ambayo waliishuhudia kwa macho yao.



    “Ni nini kilitokea? Kuna nini baba alifanya? Huu lazima utakuwa ni mchezo,” Merina na Mariya walisema kwa lugha ya Kirusi.”

    Muafaka ukawa umefikiwa kwamba Phillip apewe muda wa kutafuta nyaraka zote muhimu za kumtambulisha kwamba yeye ndiye haswa alikuwa baba



    aliyewalea watoto hao. Akapata cheti cha ndoa na nyaraka nyingine kadhaa, pia baadhi ya ndugu nao wakasimama kusema ukweli mbele ya mwanasheria Morgan



    aliyepewa jukumu la kuongoza mambo yote yaliyotakiwa.



    Siku ya kwanza ikapita, ikaja siku ya pili na hatimaye wiki ikakatika wakiwa bado katika uchunguzi mzito. Vielelezo vingi vilipatikana na baadhi ya watu



    wakatoa ushahidi wao kuhusu Phillip.

    Jinsi watu wengi walivyotegemea ndivyo ilivyokuwa kwani baada ya uchunguzi wa kina, ukweli ulibainika. Phillip akaonekana kuwa mwenye haki pamoja na



    kwamba hakuwa baba wa kuwazaa watoto Mariya na Merina.

    “Nini kinaendelea kwa sasa?” Morgan aliuliza siku moja.



    “Nadhani mtu pekee wa kumtafuta kwa sasa ni Eric Evarist ili atusaidie tena tupate nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari.

    Jambo hilo likafanyika mara moja, mwandishi huyo akatafutwa na kupewa taarifa kamili. Siku mbili baadaye, kilifanyika kikao kingine ndani ya hoteli ileile



    waliyofikia.

    Waandishi wa habari wakafurika ndani ya chumba maalum tayari kwa kuchukua taarifa muhimu, macho na masikio vikawa makini kabisa kuhakikisha hawakosei



    kitu chochote.



    Hata waandishi wenyewe baada ya kusikia historia iliyokuwa imetolewa na mashahidi wa pande zote mbili, walishtushwa sana. Kilichowatatiza ni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kwamba,



    iweje watu waliozikwa siku nyingi wawe hai tena?

    “Ndugu zangu ninayo mambo matatu tu muhimu ya kuongea nanyi asubuhi ya leo lakini nianze kwa kuwaomba radhi kuchukua muda wenu mwingi kuja hapa



    kwetu,” aliongea Morgan na alipomaliza akapokelewa kwa shangwe, nderemo na makofi mengi ndani ya chumba.



    Mariya na Merina ndiyo walioanza kufungua mkutano huo, wakati wakiongea, Morgan ambaye ndiye alikuwa mwanasheria wao, alikuwa akitafsiri kwa lugha ya



    Kiingereza ambayo waliamini kabisa itaeleweka kwa watu wote. Walipomaliza, Phillip naye alikaribishwa kuongea na waandishi, akaeleza kila kitu bila kificho.



    Machoni mwa watu alionekana kama mwongo aliyetaka kujipatia fedha kutoka kwa watoto hao matajiri lakini Morgan alikanusha vikali uvumi huo, akasimama



    kumtetea Phillip kwa kipindi chote.

    “Hadanganyi, ni kweli ndiye baba halisi wa watoto hawa.”



    “Mh!”

    “Huo ndiyo ukweli?”

    “Lakini anasema wake walishakufa miaka mingi iliyopita kwa ajali, pengine wanafanana tu.”

    “Uchunguzi wa kina umefanyika na tumegundua kila kitu, kwa hilo naomba tukubaliane na tuungane na huyu ndugu yetu hapa,” Morgan alisema kwa kujiamini.



    Wakiwa hapo, waliongea mambo yote lakini jambo moja likabaki kuwa siri ya familia kwamba watoto hao walikuwa si mali ya Phillip kwani hakuwa na uwezo



    wa kumpa ujauzito mwanamke. Jambo hilo liliendelea kubaki siri ya familia ili kulinda heshima yake.

    Kwa muda wote huo, Phillip aliendelea kumwagika machoz. Si kwamba alikuwa akiliakwa majonzi bali furaha ya kukubaliwa na watoto wake wawili ambao



    kwa wakati huo walishabadili majina na kuitwa Merina na Mariya (Dorice na Dorica) ndiyo kitu kilichomliza.

    Wote kwa pamoja wakasimama na kukumbatiana, watoto pia walikuwa wakilia kwa furaha kwani walimpata mtu waliyekuwa wakimtafuta pamoja na kwamba



    Genevieve ambaye ndiye mama yao alishakufa.



    Kazi yote ikawa imeachwa mikononi mwa vyombo vya habari kutangaza ukweli kwa Watanzania kwamba mwanaume ambaye ndiye hasa alikuwa akitafutwa,



    alikuwa amepatikana na Mariya na Merina wakishirikiana na mwanasheria wao walikuwa wakiwashukuru watu wote waliofanikisha kupatikana kwa Phillip.



    Mariya na Merina walikuwa na hamu kubwa ya kuwafahamu ndugu wengine wa Phillip, ikabidi wasubiri vyombo vya habari vifanye kazi yao.



    Baada ya waandishi kuondoka, Phillip aliwaongoza Mariya, Merina na Morgan kuelekea nyumbani kwake ambako angekutana na familia yake, yaani mtoto wake



    Genevieve na bibi Magdalena ili kufahamiana zaidi, jambo ambalo lilichukua muda wa nusu saa hivi. Baada ya kufika nyumbani kwa Phillip, mapokezi



    yakafanyika kisha wakaungana na familia kufahamiana zaidi.

    Waliongea mengi huku furaha ikitawala, mara kadhaa Phillip alionesha mapenzi ya dhati kwa watoto wake kwa kuwapiga mabusu mfululizo kama ishara ya



    mapenzi ya dhati kwao. Baada ya kumaliza utambulisho huo, waliaga na kuondoka wakimtaka Phillip kufika hotelini asubuhi ya siku iliyofuata ili wazungumze



    zaidi.

    ***

    Magazeti yote ya siku iliyofuatia yaliandika habari ya kupatikana kwa Phillip, mwanaume aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba ambaye haswa ndiye alikuwa



    baba wa Merina na Mariya watoto wa Kirusi waliokuja nchini kuufahamu ukweli wa maisha yao.

    Vichwa vingi vya habari vilisomeka tofauti, wapo walioandika: “Baba wa watoto ajitokeza.” Mengine yakataka vipimo vya vinasaba (DNA) vifanyike ili kujua



    ukweli wa historia. “Watoto walioaminika kufa miaka mingi iliyopita wafufuka,” liliandika gazeti lingine. Kila gazeti liliandika lilivyotaka ilimradi kufanya



    biashara. Lakini wote hao hawakuufahamu upande wa pili wa shilingi kwamba nyuma yake kulikuwa na historia nyingine, tena ya kusikitisha ambayo ilikuwa



    ndani ya mioyo ya watoto wenyewe na Phillip.







    WATANZANIA wengi wakabaki midomo wazi baada ya kusoma habari hizo kwenye vyombo vya habari mbalimbali. Wengi wakijiuliza kuna kitu gani kilitokea



    mpaka dunia ikaamini kwamba watoto hao waliokuwa wakiuza magazeti kwa wakati huo walikuwa wamekufa kumbe walikuwa hai. Maswali hayo yote



    hayakuwa na majibu na yakaendelea kuwa kitendawili kwa wengi.

    Wakati dunia ikishangaa kwa upande wa Mariya, Merina na Phillip, kwao ilikuwa furaha kubwa, wakifurahia kuonana wakiwa hai, masikitiko makubwa



    yalitokea tu pale walipomkumbuka mama yao yaani Genevieve lakini wakajipa moyo na kuamini kwamba hiyo ndiyo dunia waliyoishi ndani yake, furaha kidogo



    na uchungu mwingi.



    Si watoto tu waliowaza siku iliyofuata hata Phillip naye hakupata hata lepe la usingizi, akifikiria kesho yake ingekuwaje, lakini alikabidhi kila kitu mikononi



    mwa Mungu ili yeye ndiye awe jaji wa kila jambo ambalo lingekwenda kutokea, lakini zaidi alitaka watoto hao wafahamu kwamba pamoja na kuwa hakuwa



    baba yao wa kuwazaa lakini aliwapenda kwa dhati kupita maelezo na shahidi pekee alikuwa ni Mungu na mama yao Genevieve ambaye kwa wakati huo alikuwa



    ni marehemu.



    Akaamka na kujiandaa na baada ya maandalizi hayo akatoka sebuleni na kuisabahi familia yake, hapo akaaga na kuondoka kuelekea hotelini akiahidi kurejea



    muda mfupi baadaye na kuwapa taarifa ni kitu gani kilizungumzwa. Njia nzima aliwaza na kuwazua bila kupata majibu, hatimaye nusu saa tu baadaye akawasili



    kwenye hoteli waliyokuwa wamefikia watoto wake, hapo akaingia moja kwa moja mapokezi na kuomba mawasiliano nao.



    “Niko hapa kuonana na watu watatu, Mariya, Merina na Morgan,” aliongea.

    “Sawa, karibu sana kaka taarifa zako ninazo kitambo sana.”

    “Ahsante,” alijibu Phillip akijivuta kuelekea kwenye kiti kilichokuwa maeneo hayo na kuketi kusubiri na haikuchukua muda akawaona watoto hao wakitokeza



    na kutembea kumwelekea huku wakionyesha uso wa tabasamu wakamsabahi na kumkaribisha kwenye chumba maalum ambacho kiliandaliwa.



    Wakaingia ndani na kuanza mazungumzo ambayo hakika Phillip mwenyewe hakuwa tayari kuyaamini mara zote alibubujikwa na machozi mfululizo. Morgan

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    aliyekuwa pembeni akiwa ndiye mkalimani akitafsiri jambo moja baada ya jingine na mwisho muafaka ukawa umefikiwa.

    “Kwa muda wa wiki nzima tumesubiri kuona kama kungejitokeza mtu mwingine na kudai kwamba sisi ni watoto wake lakini historia yako uliyotueleza



    inaendana kabisa na vielelezo vyetu.



    “Awali tulikuwa navyo hivyo tumelazimika kukuamini kwa asilimia zote ingawa ukweli wote uko wazi, hakika pamoja na mambo yote yaliyotokea maishani



    mwetu, wewe bado utabaki kuwa baba yetu.” “Tutakupenda mpaka mwisho na hivi tunavyoongea na wewe tayari tumeishaanza kufanya utaratibu maalum wa



    kuondoka na wewe, si wewe tu bali pia familia yako yote ili tukaishi wote kama ndugu.”

    “Ahsante, ahsanteni kwa kunijali wanangu hakika mnanipenda lakini kuna jambo moja linalosumbua ubongo wangu…,” aliongea Phillip lakini hakuweza



    kumalizia sentensi yake kwikwi ya kulia ikamkaba.



    “Ni kwa nini unalia?”

    “Mh! Unajua…”

    “Hebu nyamaza ueleze linalokusibu.”

    “Nalia furaha lakini pia swali moja linazunguka kichwani mwangu ni kwamba itakuwaje tukifika huko wakati ukweli wote mmeufahamu kwamba mimi si baba



    yenu?”

    “Wewe ndiye baba yetu hakika tunayo kila sababu ya kusimamia hilo hata ikiwezekana kwa mtutu wa bunduki.”

    “Mnasema kweli?”



    “Kweli kabisa!”

    “Na je vipi kuhusu Victor Fedorov ambaye ndiye mhusika wa kila kitu?””Tutakwenda kujua hukohuko kwani yapata kipindi kirefu sasa tangu ametoweka katika



    mazingira ya kutatanisha na hivi tunavyoongea nawe tumeliachia kazi jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kujua ni wapi alipo na kama yuko hai au la!” Mariya



    aliongea akimpigapiga Phillip mgongoni.



    Hatimaye muafaka ukafikiwa kwamba kwa kuwa Mariya , Merina na Morgan walikuwa wametoa muda wa wiki nzima kusubiri kuona kama kungetokea jambo



    lolote lakini halikuwepo, uamuzi pekee walioufikia ni kuondoka na Phillip na familia yake yote. Hivyo utaratibu ukaanza mara moja wakitakiwa kuwakilisha



    vielelezo vyao vyote muhimu ili kupata vibali vya kuondoka nchini.

    Hilo ndilo likawa jambo kubwa mbele yao, kwa Phillip yote hayo yakionekana kuwa ndoto akiamini kwamba ipo siku angeamka kutoka katika usingizi mzito



    aliokuwa amelala na kuona kila kitu kikiwa tofauti. Siku zikazidi kusonga mbele Morgan akishughulikia vibali vyote muhimu, hatimaye baada ya muda mrefu



    akafanikiwa kuvipata na furaha ikaendelea kutawala kati yao.



    “Nashukuru Mungu kila kitu kimekwenda sawa, kilichobaki mbele yetu ni safari tu nadhani ni bora tukafanya maandalizi haya haraka ili turejee nyumbani



    kuendelea na shughuli nyingine kubwa, zaidi ni ile tuliyoiacha ikiendelea kuhusu Victor Fedorov, ni lazima tufahamu nini kiliendelea baada ya sisi kuondoka,



    alipatikana akiwa hai au alifikwa na umauti?” aliongea Morgan akionyesha msisitizo na kuwafanya watu wote waliokuwepo hapo wakimsikiliza kumwaga



    machozi, kwani bado watoto Mariya na Merina walimhitaji baba yao kupita maelezo ili naye ashuhudie kilichokuwa kimetokea na kumkubali Phillip na familia



    yake yote kama mmoja wa familia yao.



    Kila kitu kikaenda kama walivyotarajia, Phillip akapewa nafsi ya kuaga ndugu, jamaa na rafiki zake akitakiwa kuwataarifu juu ya safari ambayo ilikuwa mbele



    yake naye akafanya hivyo bila kusita huku furaha ikiendelea kutawala katika moyo wake, kwa walio wengi walionekana kumpongeza na kufurahia tukio hilo



    lakini baadhi pia wakionekana kuumizwa kwa kumkosa kwani pamoja na matatizo yote aliyokuwa nayo alikuwa ni mtu wa watu.



    Siku mbili baadaye safari ilishawadia wote kwa pamoja wakiwa ndani ya gari la kukodi liliwachukua na moja kwa moja kuwapeleka uwanja wa ndege ambako



    wangefanya utaratibu na kuondoka kuelekea nchini Urusi kwenda kufaidi maisha.





    KWA Phillip, Genevieve na bibi Magdalena jambo lililokuwa likitokea mbele yao lilionekana kama ndoto na muda si mrefu wangezinduka kutoka katika



    uzingizi mzito. Lakini ukweli ulikuwa umebaki pale pale kwamba walikuwa safarini kuelekea nchini Urusi wakiambatana na wenyeji wao watatu yaani Merina,



    Mariya na Morgan ambaye alisimama kama mwanasheria wao.



    Ndege waliyokuwa wamepanda iliondoka uwanja wa ndege wa Dar es Salaam saa tisa na ilitarajiwa kutua nchini Gairo kwa mapumziko kidogo, hatimaye



    Moscow ilitakiwa kutua muda wa saa mbili asubuhi na hapo ndipo ingekuwa mwisho wa safari yao.

    Kama walivyokuwa wametarajia waliwasili saa mbili kamili za asubuhi, ndege ilipokanyaga tu ardhi ya nchi hiyo Mariya na Merina wakawa wa kwanza kushuka



    huku wakiwakaribisha Phillip na familia yake, muda wote huo furaha ilikuwa ikitawala kati yao walishasahau machungu yote na kilichokuwa mbele yao ni



    kuyafaidi maisha.



    “Karibuni sana nyumbani,” Morgan aliongea kwa lugha ya Kiingereza.

    “Tunashukuru sana,” Phillip alijibu akiachia tabasamu laini usoni mwake.

    Wakati Phillip akifurahia kuingia nchini urusi, kichwani mwa Mariya na Merina pamoja na kuwa na furaha walifikiria jambo moja tu, baba yao alikuwa wapi



    hivyo walipanga baada ya kufika tu kwenda kufuatilia taarifa za uchunguzi wa polisi ili kujua nini kilitokea baada ya wao kuikabidhi kazi ya kumsaka baba yao



    mikononi mwao.



    Wakaondoka ndani ya uwanja wa ndege moja kwa moja kuelekea nyumbani, huko wakapokelewa na wenyeji wao kisha wakawakaribisha Phillip na familia



    aliyoambatana nayo.

    Wakahakikisha kila kitu kinakwenda sawa na wageni walikuwa wamepata mahitaji yote muhimu wao wakaaga na kutoka kuelekea makao makuu ya polisi



    kufuatilia majibu ya uchunguzi, wakiongozana na Morgan.



    Gari likaendeshwa kwa kasi na baada ya nusu saa tu baadaye walishawasili kituoni hapo.

    Kwa umaarufu wao walikaribishwa moja kwa moja ndani na kuonana na mkuu wa polisi wakafanya mkutano mfupi wakitaka kujua nini kiliendelea na ripoti ya

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    polisi haikufichwa ilielezwa wazi kwamba tangu kupotea kwa Victor Fedorov yapata miezi sita, walikuwa wamefanya kila walichoweza na juhudi zote



    zilionekana kufikia ukingoni, wakapitiliza mbele zaidi na kusema kwamba huenda alikufa na kufunikwa na barafu nzito hivyo kumpoteza kabisa.



    Baada ya taarifa hiyo huzuni kubwa ikawafunika wao pia wakahisi kukata tamaa ya kumwona tena baba yao akiwa hai, lakini wakatamani kuona hata maiti yake



    tu waizike kwa heshima zote lakini hilo nalo lilikuwa limeshindikana, wakabaki njia panda wakisubiri muujiza. Huku wakionyesha masikitiko makubwa



    wakamshukuru mkuu wa polisi, wakamuaga na kurejea nyumbani.

    Mioyo yao iliuma kupita kiasi, mara kadhaa kumbukumbu za baba yao ziliwajia ndani ya vichwa vyao wakikumbuka wema, ucheshi na upendo mwingi



    aliowaonyesha na sasa alikuwa ametoweka kama upepo mbele ya macho yao.



    Ni mawazo hayo ndiyo yaliyosababisha watoto hao kububujikwa na machozi, hakika walikuwa wamepoteza mtu muhimu sana katika maisha yao na



    asingekuwepo wala kutokea mwingine ambaye angeweza kukidhi shida zao ni kweli alikuwa mkosaji lakini bado aliendelea kubaki kuwa ndiye baba halisi na



    kibaya zaidi na cha kuumiza, mama yao waliyefunga safari mpaka Afrika, nchini Tanzania kumfuata naye alishakufa miaka mingi iliyopita.



    Baada ya gari kufunga breki ndani ya jengo lao, haraka bila kuongea kitu watoto hao wakashuka mbio huku wakikimbia na kuingia ndani ambako nako walipita



    mbio sebuleni na kuingia chumbani kwao, jambo hilo liliwashangaza wengi na hata Phillip aliyewashuhudia alipojaribu kufuatilia hakupata jibu la kueleweka



    zaidi sana alisikia sauti ya vilio ikiambatana na kwikwi.



    “Morgan kimetokea nini huko mlikokwenda?”

    “Hali ni mbaya mpaka sasa hakuna taarifa yoyote muhimu juu ya Victor Fedorov na uchunguzi wa polisi umefikia kikomo jambo moja tu naweza kusema



    huenda alikufa na kufunikwa na barafu nzito, basi”

    “Mungu wangu!” Philllip aliongea kwa sauti ya juu.

    “Huo ndiyo ukweli japo unauma hatuna budi kuukubali,” Morgan aliongea naye machozi yalionekana kububujika kwenye mashavu yake.



    “Inauma,” Phillip alijibu.

    Morgan na Phillip waliendelea kubaki sebuleni kwa muda mrefu wakiongea mambo mengi kama kubadilishana mawazo hatimaye ushauri ukatoka kwamba



    Mariya na Merina waitwe ili waweze kuongea nao mambo fulani.



    “Hata mimi naunga mkono jambo hilo ni lazima tuwape maneno ya faraja, walikubali tukio hilo na kusubiri kama pengine atakuwa hakufa basi ipo siku



    atajitokeza na kuugana nao,” Phillip aliongea na sekunde tatu tu baadaye Mariya na Merina walishafika sebuleni na kuungana nao, hapo wakafanya mkutano



    mfupi wa majonzi wakijaribu kuwaeleza wazi kwamba hapakuwa na sababu ya kuhuzunika kwani kila jambo linalotokea katika maisha ya mwanadamu waamini



    kwamba lilikuwa na sababu.



    Wakionyesha majonzi makubwa, wakakubaliana na kilichotokea, zaidi sana Morgan aliwataka kufahamu haki zote za baba yao na yeye angekuwa nao bega kwa



    bega kuhakikisha hakuna kinachopotea.

    Maneno hayo yakawa yamerejesha furaha kwa watoto hao, wakageuka upande aliokuwa ameketi Phillip na kwa pamoja wakatamka maneno haya;



    “Umekuja kuchukua nafasi ya baba yetu, hakika wewe ndiye, kuanzia leo utachukua majukumu yote na kuifanya familia kuwa yenye furaha siku zote, tafadhali



    tunakuomba ukubali na kwa pamoja tunasema tunakupenda,” aliongea Merina kisha walisimama na kutembea kumwelekea Phillip.



    Walipomkaribia wakapiga magoti na kuanza kulia huku wakimweleza kwamba walimpenda sana.

    “Ninawepanda pia wanangu Mungu alikuwa nayo sababu niwashukuru pia nanyi kwa kunikubali kunipokea na kunilea, Mungu awabariki sana,” Phillip



    aliwaambia Merina na Mariya.

    Kwa pamoja wakakumbatiana na kuanza kulia, yalikuwa ni machozi ya furaha pamoja na kwamba walikuwa katika masikitiko makubwa ya kupotelewa na baba



    yao kipenzi.



    Baada ya muungano huo wote kwa pamoja walidhamiria kushikamana kama ndugu wakiapa kutimiza wajibu na kulinda heshima ya baba yao ambaye alikuwa



    ndiye muasisi wa utajiri wote waliokuwa nao.

    “Jambo la muhimu hivi sasa pamoja na yote tuliyoongea ni muhimu tukatangaza habari za kifo cha Victor Fedorov kwenye vyombo vya habari kwa muda



    usiopungua mwezi mmoja tuone nini matokeo yake,” Phillip alitoa wazo na wote wakalipokea kwa mikono miwili.



    Ilionekana kuwa safari nyingine ngumu lakini ilikuwa ni lazima waizoee nakuikubali ili maisha yaendelee kwani hivyo ndivyo dunia ilivyokuwa. Kwa



    pamojawakakubaliana na kusimama, tegemeo lao kubwa kwa wakati huo akiwa ni Phillip,ndiye alikuwa baba wa familia kipindi chote wakisubiri kuona nini



    kingetokeabaada ya kutangaza kwenye vyombo vya habari.

    “Tutakupenda mpaka mwisho na jambo pekee kwa hivi sasa ni vyema Genevieveakaanza shule haraka iwezekanavyo ili naye apate elimu kama sisi,”



    Mariyaaliongea siku moja wakiwa sebuleni.

    “Ni kweli kabisa ni lazima aanze shule mara moja, kesho nitakwenda kuongea namwalimu wa shule tuliyosoma.”

    “Ada je?”

    “Tutalipa hakuna shida huyu ni mdogo wetu ni lazima tutimize wajibu kwake.”

    “Ahsanteni wanangu Mungu awabariki sana,” Phillip aliongea huku akibubujikwa namachozi.

    Furaha ilikuwa imeizunguka nyumba ya Victor Fedorov, kazi zote zikiwa chini yausimamizi wa Phillip kama baba na Morgan ambaye alikuwa ndiye haswa



    mwanasheriawa miradi yote iliyomilikiwa na tajiri huyo.

    Siku nazo zikazidi kusonga mbele mambo yote yakiwa sawa kama walivyopanga,Genevieve akiwa tayari ameshaanza shule, Phillip, Mariya na



    Merinawakihakikisha miradi yote inakwenda sawa.

    Mwezi wa kwanza ukapita bado wakiwa katika kusubiri, taarifa mbalimbalizikiendelea kutolewa na vyombo vya habari wakati mwingine hata televishenikubwa



    nchini humo, lakini bado hakukuwa na majibu yoyote hatimaye nao wakaanzakukubaliana na madai ya polisi ya uchunguzi wao walioufanya kwa kina na



    kuaminikwamba huenda mzee huyo alikufa na kufunikwa na barafu nzito.

    “Pengine inawezekana kweli baba alikufa kitambo kama uchunguzi unavyosema.”

    “Hapana hebu tusubiri pengine anataka kutupima kama tumekua.”

    “Mariya hakyanani amini tu kwamba baba amefariki.”

    “Sijakataa, inawezekana ikawa hivyo ninachokiona mimi hebu tusubiri zaidi.”

    “Sawa,” Mariya aliitikia.

    Kwa muda wa miezi minne mfululizo bado waliendelea kusubiri huku wakiendelea nashughuli zao kama kawaida na ilipotimia mwezi wa tano wakaanza



    kuchoka nakukata tamaa kwani walikuwa wamefuatilia kwa karibu sana kila kitu kuchunguzakwa umakini wa hali ya juu na jibu walilokuwa wamelipata



    halikutofautiana napolisi. Huzuni na majonzi vikatawala upya wakikumbuka mema yote aliyowatendeababa yao enzi za uhai wake.

    Hatimaye ikatimu miezi sita wakiwa katika kusubiri mwisho wakafikia uamuzi wakuutangazia umma kwamba Victor Fedorov aliaminika kufa katika mchezo



    wakuteleza kwenye barafu.

    “Ni lazima sasa tutangaze kwamba Victor Fedorov alikufa.”

    “Tunaungana na wewe.”

    “Je, kama ikitokea siku moja akarudi?”

    “Hiyo itakuwa habari nyingine lakini sidhani kama jambo hili litatokea.”

    “Mh!”

    “Huo ndiyo ukweli, hakuna haja ya kuguna wala kujiuliza mara mbilimbili.”

    “Morgan kesho asubuhi mchakato huo uanze, sisi kama watoto wa marehemu tupatewasaa japo wa dakika kumi tu katika televisheni ya taifa kuuelezea umma



    juu yajambo hilo.”

    “Nakubaliana nanyi na kazi hiyo kesho asubuhi itafanyika.”

    Saa zikazidi kusonga mbele hatimaye kesho waliyoisubiri kwa hamu kubwa ikawadiana Morgan akafanya taratibu zote na kurejesha majibu kwa Mariya na



    Merinakwamba alishafanikiwa kuongea na televisheni hiyo kubwa. Maandalizi maalumyakafanyika hatimaye wakaiweka habari hiyo kweupe ikiliacha taifa la



    Urusikatika mshangao mkubwa na maumivu kutokana na ushirikiano wa mzee huyo kwajamii iliyomzunguka, umaarufu wa Victor Fedorov ulikuwa mkubwa



    hivyo kitendocha kutangazwa kwamba aliaminika kufa kiliwaumiza wengi.

    Majonzi, vilio na kuomboleza vikatawala nyumbani kwake, watu mbalimbali maarufuwakiongozwa na rais wa nchi hiyo walifika kutoa pole na rambirambi,

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wengi waowakitaka kujua historia kamili ya tukio. Sehemu maalum ilitengwa na kuwekapicha kubwa ya Fedorov huku chini yake kukiwa na maneno “?????



    ????”yakimaanisha “Shujaa ameondoka”.

    Kutokana na umaarufu wa tajiri huyo nchini Urusi, serikali ikatoa wiki nzima yamaombolezo ishara tosha kwamba alikuwa kipenzi cha watu wengi, hakuwepo



    mtuhata mmoja aliyefahamu upande wake wa pili kwamba alikuwa ni mtu hatarikupindukia.

    Ikiwa ni siku tatu tu tangu kufanyika kwa maombolezo ya Fedorov, kama familiawaliamua kwenda kutembelea eneo ambalo ndilo haswa lililoaminika



    kuchukuamaisha ya baba yao kipenzi ambapo mashada mengi yakawekwa eneo hilo pamoja napicha yake kama kumbukumbu pekee katika maisha yao na zoezi



    hilo lilipokamilikawakarejea nyumbani kuendelea na maombolezo.

    Siku ya nne asubuhi jambo la ajabu likatokea na kufanya watu wengi kupigwa nabutwaa, ni taarifa kwamba mwili wa mtu asiyefahamika ulikuwa umeonekana



    ndaniya shimo kubwa lililokuwa Mashariki ya Urusi na mtu mmoja aliyekuwa akifanyamchezo wa kuteleza katika barafu ndiye aliyegundua hilo na kuamua



    kutoa taarifapolisi ambao walifika mara moja eneo hilo.Gari maalum likatolewa likiwa napolisi ndani yake na likaenda moja kwa moja mpaka eneo husika ili



    kushuhudiatukio hilo, na ni kweli kabisa wao pia macho yao yaliona kama walivyokuwawameelezwa.

    Haraka taratibu za kuutoa mwili zikafanyika na kuufikisha katika hospitali kuunchini humo kwa utambuzi, watu wengi walifika na kuangalia kama



    wangewezakumfahamu.

    ***

    Akiwa mafichoni aliweza kufuatilia mambo yote ya tajiri huyo mkubwa lengo lakelikiwa ni kutaka kulipa kisasi kwa ubaya aliomtendea, hakuwepo mtu hata



    mmojaaliyefahamu kwamba Ditrov alikuwa hai sehemu fulani kama ilivyoaminika kwawengi alishakufa muda mrefu.

    “Nitakaa hapa huku nikifuatilia nijue jinsi ya kumpata huyu mpumbavu na kulipakisasi, safari hii atanijua mimi ni nani,” aliwaza Ditrov siku moja lakinighafla



    akazipata habari kwamba Victor alitoweka katika mazingira ya kutatanishana alikuwa akitafutwa bila mafanikio na kama familia walishaamua kuliweka



    jambohilo wazi kwamba alikufa.

    “Mh! Atakufaje kabla sijakutana naye? Lakini acha afe ili mimi niendelee kulamaisha na sasa nitarejea nyumbani,” alijisemea Ditrov. Akafanya maandalizi



    yasafari kurejea nyumbani nchini Urusi, huko ndiko alikofahamu ukweli kwambahakika mwanaume huyo alikuwa amekufa na mwili wake ulikuwa umeokotwa



    kwenyeshimo wakati wa mchezo wa kuteleza katika barafu na watoto wake walithibitishajambo hilo.

    “Maisha sasa mswano pamoja na ubaya wake Mungu ailaze roho yake mahali pemapeponi, Amina!” alimaliza Ditrov huku machozi yakimlengalenga.

    ***

    “Mimi naona tukafanye ukaguzi wa mwili huo,” Morgan aliongea ikiwa ni siku yanne tu.

    Bila ubishi wakaondoka nyumbani kuelekea hospitali kila mmoja akiwaza jambokichwani mwake, bila kupoteza muda moja kwa moja mpaka chumba cha



    kuhifadhiamaiti hapo wakajitambulisha na kuomba kuutambua mwili wa mwanaume aliyeonekanaakiwa amekufa.

    “Mh!” Merina ndiye aliyekuwa wa kwanza kukagua.

    “Kwa nini umeguna?”

    “Hapana siye baba, mbona amevimba kiasi hiki? Halafu amekuwa mweusikupindukia.”

    “Hebu?” Mariya akadakia naye bila kukawia akatupa macho yake kuangalia naghafla wakashuhudia kilio kikali ndani ya chumba.

    “Huyu ndiye!” ndilo neno pekee aliloweza kutamka Mariya na kufuatiwa na kwikwikali.

    “Unasema?” Phillip akauliza.

    “Hakika nawaambieni aliyelala hapo ni baba yetu!”

    Morgan akasogea karibu na kuangalia kwa umakini ni kweli alikuwa VictorFedorov, mwili wake ukiwa katika hali mbaya kutokana na kukaa katika barafu



    kwamuda mrefu.

    “Hii ni maiti ya Fedorov!”

    “Mna uhakika?”

    “Ulio kamilifu, hatujakosea hata kidogo, tungependa kupewa kibali cha kuuzikakwa heshima zote,” ndivyo alivyotamka huku akiukagua vyema mwili huo.



    Taratibu maalum zikafanyika wakitafuta vibali husika ili kupata ruhusa yakuuzika mwili huo kwa heshima zote na hatimaye uchunguzi ulipokamilika



    nakuridhika wakakabidhiwa mwili wa Fedorov ili wauzike.



    Jambo hilo liliamsha vilio upya watu wakalia na kuomboleza, wengi wakionekanakuzimia kwa tukio hilo lakini hatimaye mwili wa Fedorov ukashushwa



    kaburini kwaheshima zote, watu mbalimbali wakahudhuria msiba huo. Lilikuwa ni tukio lakuhuzunisha sana pengine kuliko yote yaliyowahi kutokea kwa



    wakati huo. Tajirimkubwa, Victor Fedorov akawa amezikwa.

    Kama familia, baada ya maziko wakatoa muda wa mwezi mzima kuombolezawakisimamisha shughuli zote kwa ajili ya maombolezo.

    Mwezi mmoja ulipomalizika wakiwa katika majonzi walianza tena kazi zao naPhillip akateuliwa kushika wadhifa wa Victor Fedorov, akipewa majukumu



    yotekama baba wa familia hiyo mpya.

    Furaha, upendo na amani vikitawala ndani na nje ya familia huku akipewa heshimazote kwa kila kitu. Maisha kwa Phillip yakanyanyuka tena baada ya



    kuwaameshaumizwa moyo mara kadhaa lakini akaonekana kusahau na kufurahia maishamapya akifuta maumivu yote aliyowahi kuyapata maishani mwake.

    “?? ????? ?? ?????? ???, ?? ? ????????? ? ??? ???? ?????????. ??? ??? ??????????? ?????? ????? ????? ...”

    (Tunakupenda si wewe tu bali pia Genevieve na bibi Magdalena. Kwetu sisi ninyini sehemu ya damu yetu...) waliongea Mariya na Merina kwa lugha ya Kirusi



    nawote kwa pamoja wakanyanyuka na kumsogelea Phillip wakammwagia mabusu mfululizohuku wakimkumbatia, ishara tosha kwamba walikuwa



    wamemkubali na kumpokea kamababa yao katika maisha yote yaliyobaki baada ya  VictorFedorov kufariki.



      ****    MWISHO    **

0 comments:

Post a Comment

Blog