IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI
*********************************************************************************
Simulizi : Kahaba Kutoka China
Sehemu Ya Kwanza (1)
‘Nisikilize Rose. Unataka niseme nini ili ujue kwamba nakupenda? Unataka nifanye nini ili ujue kwamba nakuhitaji? Au unataka nijiue? Au unataka usikie nimekimbizwa hospitali baada ya kunywa sumu ya panya kwa lengo la kujiua kwa sababu umenikataa? Naomba unionee huruma, naomba uone ni kwa jinsi gani umekuwa wa thamani kwangu. Naomba unielewe mrembo, ninakupenda sana’
‘Hivi Rose! Malkia wa moyo wangu hebu niambie nikwambie nini ili unielewe. Au mpaka niseme kwamba ninakupenda zaidi ya mama yangu? Au mpaka niseme kwamba ninakupenda zaidi ya ninavyojipenda? Hebu niambie nikwambie nini mtoto wa kike. Usifikiri kwamba nimekuona na kukutamani tu, nimekupenda toka moyoni mwangu na hata kama utakuwa tayari nifike hapo kwenu na kukutolea mahari ili nikuchukue jumla hebu niambie ili nije. Naomba unijibu, jibu lako zuri ndio litakuwa faraja ya moyo wangu usiku wa leo. Nakupenda mrembo’
Hizo zilikuwa meseji miongoni mwa meseji ambazo Rose alikuwa ametumiwa usiku wa siku hiyo, zilikuwa ni meseji ambazo zilitumwa na watu ambao walikuwa wameangukia katika penzi la msichana Rose ambaye kwao alionekana kuwa kama msumbufu. Kila siku Rose alikuwa msichana wa kupokea meseji kutoka kwa wavulana mbalimbali ambao walikuwa wakimtaka kimapenzi. Rose hakuonekana kuwa mwepesi kukubaliana nao, kwake, aliwaona wanaume kuwa wadanganyifu ambao walikuwa wakitaka kumchezea na kisha kumuacha katika mataa akilia.
Uzuri wake ndio ambao ulikuwa ukiwavutia wavulana wengi ambao walikuwa wakipanga mstari na kisha kumfuatilia Rose kila alipokuwa akienda nje ya nyumba yao. Alipokuwa akielekea dukani, alikuwa akipata wasindikizaji, alipokuwa akielekea sokoni napo alikuwa akipata wasidikizaji ambao kazi yao ilikuwa ni kumbebea kapu la mboga mpaka anafika nyumbani kwao.
Wavulana wa mtaa wa Magomeni Mapipa wakaonekana kuchanganyikiwa na uzuri wa Rose. Uso wake mwembamba, umbo lake la kimiss, hipsi zake ambazo zilikuwa zimetokeza kidogo kama za pundamilia unapomtazama kwa nyuma, tumbo lake lililoingia ndani pamoja na vijishimo viwili mashavuni vilivyokuwa vikionekana kila alipokuwa akicheka au kutabasamu ndivyo ambavyo vilikuwa vitu ambavyo viliwavutia wavulana wengi ambao walikuwa wakimwangalia.
Rose alionekana kama anafanya kusudi, kila alipokuwa akipita mbele ya wanaume, mwendo wake ulikuwa ni wa mapozi kana kwamba hakuwa akikanyaga ardhi hii ambayo watu walikuwa wakiitumia kuchimba vyoo, kila alipokuwa akipita karibu na wanaume, alikuwa akitoa tabasamu ambalo lilikuwa likiwavutia wavulana wengi kumwangalia kwa matamanio.
Rose hakuwa mwepesi hata kidogo, Rose hakuonekana kuwakubalia wanaume ambao walikuwa wakimwambia maneno mengi ya kimapenzi, kwao, Rose alionekana kuwa kama muuaji kwani hata kama ulikuwa ukiongea huku machozi yakikutoka, Rose hakukuonea huruma, alikuwa akiamini sana katika msemo wa ‘ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni’.
Wavulana wa Magomeni Mapipa walikuwa wamepanga foleni lakini hakukuwa na mtu ambaye alifanikiwa kumpata Rose ambaye sifa za uzuri wake zilikuwa zikienea kwa kasi sana kila siku masikioni mwa watu. Vijana wengine ambao walikuwa wakikaa Magomeni Mikumi na sehemu nyingine walikuwa wakifika Mapipa kwa ajili ya kumuona Rose tu ambaye alikuwa akitikisa sana katika miaka hiyo.
Rose hakuonekana kuwa mtu wa hasira, kila alipokuwa akitongozwa, tabasamu pana lilikuwa likionekana usoni mwake, tabasamu ambalo lilimpa faraja kila mwanaume ambaye alikuwa akijaribu bahati yake ila tatizo lilikuwa moja tu, jibu lake alilokuwa akilitoa lilikuwa tofauti na tabasamu lile jambo ambalo lilionekana kuwashangaza wavulana wengi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rose alikuwa binti pekee wa mzee Shedrack, mzee ambaye alikuwa mwanajeshi ambaye kambi iliyokuwa Lugalo. Mzee Shedrack alijua fika kwamba binti yake, Rose alikuwa msichana mzuri ambaye alikuwa na mvuto mkubwa kwa kila mwanamume ambaye alikuwa akimwangalia, alichokifanya yeye ni kumpa tahadhari juu ya kila uamuzi ambao alikuwa akiufanaya kuhusiana na wanaume ambao walikuwa wakimfuata kila siku.
Rose alionekana kuwa muelewa, kila wakati maneno ya baba yake yalikuwa yakijirudia kichwani mwake. Maneno yale yakamfanya kutokutamani wanaume, maneno yale yakamfanya kuwachukia wanaume na kuwaona kwamba wote walikuwa wadanganyifu. Maneno yale ya baba yake ndio yalikuwa chachu kubwa katika maisha yake, yalikuwa maneno ambayo yalimpa nguvu kubwa ya kumkataa kila mwaume ambaye alikuwa akisimama mbele yake kumtongoza.
Pamoja na hayo yote, ukali wa baba yake ulikuwa ukimuogopesha kupita kawaida. Mikanda ambayo ilikuwa ikitumika kumchapa katika kipindi cha nyuma ndio ambayo ilimfanya kumuona baba yake kutokuwa na masihala hata kidogo. Mikanda ile ndio ambayo ilimfanya kusimama mbali na wanaume ambao alikuwa akiongea nao kwa ajili ya kumuogopa baba yake ambaye alikuwa mkali kupita kawaida.
Wanaume wengi ambao walikuwa wakimfuatilia Rose walikuwa wakipigwa na mzee Shedrack ambaye alionekana kuwa katili mtaani pale. Japokuwa vijana walikuwa wakipigwa sana na mzee huyo lakini hakukuwa na mvulana ambaye alionekana kukata tamaa kumfuata Rose, msichana huyo bado alikuwa chaguo la kila mvulana ambaye alikuwa akimwangalia.
Siku ziliendelea kukatika na mwisho wa siku wasanii wakubwa wa muziki na maigizo kuanza kumnyemelea Rose. Mtu wa kwanza kabisa ambaye alikuwa maarufu kuanza kumnyemelea Rose alikuwa msanii wa muziki ambaye katika kipindi hicho alikuwa juu sana, Yusufu au The Ruler kama ambavyo alikuwa akijulikana na wengi. Yusufu alikwenda kwa kujiamini sana, jina lake lilikuwa likimpa kiburi kwa kujiona kwamba angempata Rose lakini mwisho wa siku akajikuta akimaliza soli za viatu kwa kutembea kutoka Kijitonyama mpaka Magomeni pasipo kufanikiwa kumpata msichana huyo.
Watu hawakuishi hapo, mtu wa pili kumfuata Rose alikuwa mwandishi wa hadithi ambaye alikuwa akivuma sana nchini Tanzania kwa wakati huo, Andrew Carlos. Nae alijaribu sana kumfuata Rose, alitumia kila njia ya kumpata Rose, alilitumia sana jina lake katika vitabu vyke vya hadithi pamoja na kuwaambia watu dhahiri kwamba alikuwa akimpenda Rose lakini mwisho wa siku akajikuta akipoteza muda wake kwa ajili ya kumfuatilia msichana huyo.
Rose hakuonekana kuwa mwepesi hata mara moja, alijua fika kwamba kulikuwa na wanaume wengine walikuwa wakimpenda kwa moyo mmoja lakini bado hofu ilikuwa kubwa kwa baba yake. Alikuwa akimuogopa sana baba yake ambaye mara kwa mara alionekana kuwa kama muuaji mbele ya macho yake.
Ukiachana na Rose, mzee Shedrack alikuwa na mtoto mwingine wa kiume, huyu aliitwa John. John alionekana kuwa kama mlinzi katika maisha ya Rose, mara kwa mara yeye ndiye ambaye alikuwa akimpelekea kesi baba yake kuhusiana na Rose. Kila alipokuwa akimuona kasimama na mwanaume, John alikuwa akimfikishia taarifa baba yake ambaye alionekana kuwa kwenye hasira kali.
“Kuna siku nitakuua wewe malaya wa kike” Mzee Shedrack alimwambia Rose huku akionekana kuwa na hasira.
“Wao wananitaka baba….mimi nawakataa” Rose alijitetea huku akilia.
“Hata kama. Yaani kila siku wakutake wewe tu, yaani kila siku wakusimamishe wewe tu. Nitakuua. Rose nitakuua. Wewe ngoja ulete mimba humu ndani. Nitakuua. Narudia tena, NITAKUUA” Mzee Shedrack alimwambia Rose huku akionekana kuwa na hasira mpaka mishipa ya shingo ikasimama.
Kila siku maisha ya Rose yalikuwa ya woga, maneno makali ambayo alikuwa akiongea baba yake kila siku yalionekana kumuogopesha. Katika kipindi hicho hawakuwa wakiishi na mama yao kwani alikuwa amefariki miaka mitatu iliyopita huku tetesi zikisema kwamba mzee Shedrack ndiye abaye alikuwa amemuua kutokana na wivu wa mapenzi, kifo ambacho kilikuwa na utata mkubwa.
Hayo ndio yalikuwa maisha ya Rose, kila siku wanaume walikuwa wakijileta kwake, hakutaka kuwapa nafasi hata mara moja, baba yake alionekana kuwa makini sana katika maisha yake. Rose akawa mtu wa kuwakatalia wanaume kila siku. Japokuwa alikuwa amevunja ungo, kuwa na matamanio kama wanawake wengine lakini hakuweza kuwa na mwanaume yeyote kwa ajili ya kukidhi tamaa ya mwili wake, sababu kubwa ni kwamba alikuwa akimhofia baba yake.
Kila siku Rose alikuwa mtu wa kushinda ndani, mzee Shedrack akaendelea kumuweka John kuwa mlinzi wa dada yake. Kila siku ambazo Rose alikuwa akitoka ndani ya nyumba, John alikuwa akimfikishia baba yake taarifa, alipokuwa akirudi, ilikuwa ni kama vita ndani ya nyumba mpaka pale alipoeleza sababu iliyomfanya kutoka ndani ya nyumba.
Maisha yaliendelea kuwa hivyo kila siku, Rose hakuonekana kuwa na amani kabisa nyumbani kwao. Japokuwa katika kipindi hicho alitakiwa kuanza kidato cha tano lakini baba yake hakuonekana kuwa tayari kumpeleka shule binti yake, kila siku alikuwa akimtaka kubaki ndani ya nyumba hiyo hiyo. Kitendo hicho ndicho ambacho kilianzisha mawazo mengine kichwani mwa Rose kwamba baba yake alikuwa akimtaka kimapenzi na ndio maana hakumpa hata nafasi ya kutoka ndani ya nyumba hiyo.
Mawazo hayo yaliendelea kuwepo ndani ya kichwa chake lakini kila siku alikuwa akiyapuuzia tu kwa kuyaona ni mawazo machafu ambayo yalikuwa yakipandikizwa na shetani kichwani mwake. Mara kwa mara alipokuwa chumbani kwake, Rose alikuwa na tabia ya kusimama mbele ya kioo na kisha kuanza kujiangalia, alikuwa akiliona umbo lake kuvutia kupita kawaida, matiti yake yaliyosimama pamoja na sura yake nzuri vilikuwa vitu ambavyo vilimvutia kupita kawaida.
“Mtoto wa shangazi yako atakuja hapa. Nataka ukae nae kwa amani na huo umalaya malaya wako uuache, usinitie aibu” Mzee Shedrack alimwambia Rose.
“Nani?”
“Irene. Anakuja kwa ajili ya likizo ya chuoni kwao. Nakuomba umuonyeshee upendo wote. Umenisikia?”
“Nimesikia baba” Rose alimjibu baba yake.
Baada ya siku mbili, msichana Irene akafika nyumbani hapo. Kama alivyokuwa Rose, Irene nae alikuwa mrembo sana. Umbo lake nae lilikuwa la mvuto sana, makalio yake yalikuwa makubwa jambo ambalo lilimfanya kujivunia kila alipokuwa akijiangalia katika kioo. Kwa muonekano tu, Irene alionekana kuwa msichana mtulivu sana, uso wake ulikuwa ni uwa upole kupita kawaida.
Kwa kumwangalia tu, usingeweza kujua kwamba ile sura ambayo ilionekana kwa Irene ilikuwa ni kama kinyago tu kwani maisha yake ya nyuma ya pazia yalikuwa mabaya, maisha ambayo kusingekuwa na mzazi yeyote ambaye angetamani msichana Irene kukaa pamoja na binti yake.
Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Irene alionekana kuwa msichana mpole ambaye alikuwa akiwaponda wanaume kila siku mbele ya mjomba wake jambo ambalo lilimfanya mzee Shedrack kumsifia kila siku na kumtaka Rose kuiga maisha yale na si kila siku kusimama na wanaume njiani.
“Umemuona mwenzako. Hawapendi kabisa wanaume na si kama wewe. Kila siku ni kusimama na wanaume tu njiani. Narudia tena. Siku ukipata mimba, bora utafute pa kwenda” Mzee Shedrack alimwambia Rose huku akimsisitizia kwamba ilikuwa ni lazima awachukie wanaume.
Irene ndiye ambaye alikuwa karibu nae sana katika kipindi hicho, Irene ndiye ambaye alionekana kuwa rafiki yake mkubwa ambaye alikuwa akiishi nae karibu yake kila siku. Mara kwa mara walikuwa wakielekea sokoni pamoja na kurudi nyumbani. Kwa wanaume, wakaonekana kuchanganyikiwa kwa Irene, makalio yake makubwa yakaonekana kuwadatisha kupita kawaida.
“Mmmh! Una umbo zuri Irene” Rose alimwambia Irene ambaye alikuwa amesimama akiwa mtupu mbele ya kioo.
“Asante shosti. Ila mbona na wewe una umbo zuri sana” Irene alimwambia Rose.
“Hapana. Umbo langu wala sio zuri. Hebu niangalie” Rose alimwambia Irene huku akisimama.
“Una umbo zuri sana. Hebu jaribu kuvua nguo zako uone” Irene alimwambia Rose ambaye akaanza kuvua nguo na kubaki mtupu.
“Hebu jiangalie Rose. Unavutia” Irene alimwambia Rose huku akiwa amemsogelea. Kitu cha kwanza ambacho alikuwa ameanza kukifanya ni kukipeleka kinywa chake katika matiti ya Rose.
Rose akaonekana kushtuka, hakuamini kama Irene angeweza kumfanyia kitu kama kile, alichotaka kukifanya ni kutaka kumtoa, lakini kila alipotaka kufanya hivyo, alijisikia kuwa katika hali ambayo hakuwahi kuwa nayo kabla.
Irene hakuishia hapo. Bado aliendelea vile vile kuuchezea mwili wa Rose mpaka pale ambapo alianza kumuona Rose akianza kuchanganyikiwa na yeye mwenyewe kukifuata kitanda na kulala. Irene hakutaka kuishia hapo, alichokifanya ni kuelekea katika mkoba wake na kisha kutoa kitu ambacho kilikuwa kwenye karatasi.
“Nini hicho?” Rose aliuliza huku sauti yake ikiwa imebadilika.
“Uume wa bandia” Irene alimjibu huku akimsogela pale kitandani.
“Unataka kufanya nao nini?”
“Kwa ajili yako Rose. Unapokuwa na huu, hata hamu ya mwanaume unakuwa hauna” Irene alimwambia Rose ambaye alionekana kumshangaa.
“Hapana. Haiwezekani. Sitaki Irene. Haiwezekani” Rose alimwambia Irene.
“Kwa nini?”
“Sijawahi kufanya mapenzi”
“Hilo si tatizo. Tena wewe ndiye mtu mzuri. Usimfanye mwanaume kuimwaga damu yako kitandani. Wengi wanakuwa makatili, hawaoni hata huruma” Irene alimwambia Rose kwa sauti ya chini.
“Hapana. Haiwezekani” Rose alimwambia Irene huku akisimama na kisha kuanza kuvaa nguo zake.
**************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rose hakuonekana tena kuwa na imani juu ya Irene ambaye kwake tayari alionekana kuwa msagaji. Kila wakati alikuwa mkimya huku akimwangalia Irene kwa macho ya mshangao, Irene hakutaka kujisikia aibu, kila siku alikuwa akimsisitizia Rose kwamba ili kuepukana na wanaume mbalimbali ambao walikuwa wakimsumbua basi ilikuwa ni lazima akubaliane na kile ambacho alikuwa amemwambia akifanye.
Kwa Rose jambo lile likaonekana kuwa gumu sana kufanyika, isingekuwa rahisi hata mara moja kufanya mapenzi na uume wa bandia, alikuwa akijiheshimu sana, kufanya jambo lile lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo lingeweza kumsumbua sana katika maisha yake.
Irene hakukoma, kila siku ishu yake ilikuwa ile ile moja tu kwamba ni lazima Rose akubaliane nae kwani ile ndio ilikuwa njia pekee ya kuwaepuka wanaume ambao walikuwa wakimfuata kwa kasi sana. Bado msimamo wa Rose ulikuwa pale pale na alipoona kwamba Irene alikuwa akimlazimisha, alitamani kumwambia baba yake lakini alihofia kufanya hivyo.
Kila siku usiku Irene alikuwa na kazi ya kumpapasa Rose mgongoni katika kipindi ambacho walikuwa wakilala usiku. Japokuwa Rose hakuwa akipenda lakini mipapaso ile ilikuwa ikimfanya kuwa katika hali ya tofauti sana. Mwili wake ulikuwa ukimsisimka kila alipokuwa akipapaswa na viganja vya Irene ambavyo vilikuwa vimebobea utaalamu wote wa kumfanya mtu yeyote kuingiwa na hisia za kufanya mapenzi.
Katika kipindi hicho Irene akaona ilikuwa ni bora kwanza kubadilisha lengo lake kwa ajili ya kumtia upofu Rose. Alichokifanya katika kipindi hicho, alitaka awe anamlainisha hivyo hivyo na kumsaga huku akiwa hatumii kifaa kile. Jambo lake likaonekana kukubalika mwilini mwa Rose, kila siku usiku kazi yao ilikuwa moja tu, kushikana hapa na pale na kisha kuanza kubadilishana mate.
Rose hakuonekana kuwa na jinsi katika kipindi hicho, aliuona mwili wake ukiwa katika uhitaji mkubwa sana wa kuwa na mwanaume au mtu yeyote ambaye angeweza kuzimaliza tamaa za mwili wake ambazo zilikuwa zikimshika kupita kawaida. Kwa kitendo cha Irene ambacho alikuwa akikifanya kilionekana kuanza kumbadilisha, miguso mbalimbali ya kimahaba ambayo alikuwa akishikwa ikaonekana kumpagawisha.
Irene hakutaka kumuacha Rose hivi hivi, yeye ndiye alikuwa kungwi wa mambo yale. Kila siku alihakikisha anamsaga Rose ambaye alikuwa akilalamika kimahaba kupita kawaida. Tayari ndani ya wiki moja Rose akaanza kubadilika, japokuwa hakuwa akifanya mapenzi na mwanaume yeyote yule lakini tamaa za mwili wake zikaonekana kuanza kumuisha.
Ile hali ya kuwatamani wanaume ikaanza kutoweka kabisa, badala ya kuwatamani wanaume akawa akianza kumtamani Irene. Kila alipokuwa akimuona, Rose alikuwa akiweweseka, kwake alimchukulia kama mume wake ambaye alikuwa amkimridhisha sana kitandani.
“Ila ikitokea siku baba akajua” Rose alimwambia Irene.
“Atajuaje sasa? Kwani utamwambia?”
“Nimwambie! Sijitaki!”
“Sasa atajuaje?”
“Si unajua dunia haina siri hii. Anaweza kujua”
“Hakuna kitu kama hicho. Dunia ina siri kama watu mtaamua kutunza siri mke wangu” Irene alimwambia Rose.
“Wewe jiamini tu. Inaweza kutokea siku baba akajua halafu ikawa balaa”
“Hawezi kujua. Hebu njoo juu yangu my baby” Irene alimwambia Rose ambaye akamfuata kwa juu na kisha kumkalia.
Hiyo ndio ilikuwa michezo yao ya kila siku. Japokuwa katika kipindi cha nyuma Rose alionekana kutokuuzoea lakini uwepo wa Irene ndani ya nyumba ile ukaonekana kumfanya kuanza kuuzoea mchezo ule ambao ulikuwa mchezo mbaya sana hasa kwa wasichana ambao walikuwa wakiufanya.
Kila siku walikuwa wakijiridhisha chumbani mwao, hawakuwa wakitoka nje ovyo, mara kwa mara walikuwa wakibadilishana mate. Kwa Rose, akaanza kujisikia wivu kila alipokuwa akimuona Irene akisimama na msichana mwingine au mvulana. Alikuwa akimhitaji sana Irene kiasi ambacho hakutaka kuachana nae kabisa.
Wivu wa mapenzi ukaanza kumsumbua. Kama ambavyo msichana alivyokuwa akijisikia wivu kila alipokuwa akimuona mwanaume wake akiwa amesimama na msichana mwingine ndivyo ilivyokuwa ikitokea kwa Rose. Alimpenda sana Irene, kwake alimuona kuwa kama mume bora ambaye alikuwa akimridhisha kupita kawaida.
“Ushaanza kuniudhi mpenzi” Rose alimwambia Irene.
“Kwa nini tena?”
“Ulikuwa ukiongea na nani simuni muda wote huo?”
“Nilikuwa naongea na Asha, msichana ninayesoma nae”
“Unataka kunikasirisha sasa. Unaanza kuuumiza moyo wangu. Unataka waanze kuniibia nini?” Rose alimuuliza Irene huku dhahiri akionekana kushikwa na wivu mkali moyoni.
“Hapana. Huwezi kuibiwa. Wewe ndiye kila kitu kwangu. Ila hata wewe pia unanikasirisha bwana” Irene alimwambia Rose.
“Toka lini nimekukasirisha?”
“Si umekataa kuutumia”
“Upi?”
“Ule”
“Ule nini?”
“Si ule wa siku ile”
“Ule wa bandia?”
“Ndio”
“Hapana. Siutaki wa bandia wala wenyewe. Mimi nakutaka wewe, sina haja na wa namna ile” Rose alimwambia Irene.
Japokuwa Rose ndio kwanza alikuwa ameanza kuingia katika mchezo wa usagaji lakini akaonekana kuuvamia kwa kasi kupita kawaida. Mwilini mwake, hakuwa na haja na wanaume, Irene ndiye ambaye alionekana kumridhisha kimwili. Kila siku kazi yao ilikuwa ni ile ile, kuchezeana usiku kucha na asubuhi kujifanya kama hakukuwa na kitu ambacho kilikuwa kikiendelea.
Mpaka katika siku ambayo Irene alikuwa akitakiwa kurudi chuoni Rose akabaki kwenye majonzi makubwa, moyo wake ulikuwa umeumia kupita kawaida. Alikuwa amemzoea sana Irene, kwake alimchukulia kama mume wake ambaye alikuwa akimtimizia haja zote za mwili wake. Alichokifanya Irene ni kumuachia ule uume wa bandia.
“Ufanyie kazi huu. Nikirudi tena nikute kupo fresh” Irene alimwambia ambaye alibaki akiuangalia uume ule.
“Ila sijawahi kukiingiza kitu chochote kile” Rose alimwambia Irene.
“Hilo sio tatizo kabisa. Wewe anza taratibu taratibu na mwisho wa siku utazoea” Irene alimwambia Rose katika kipindi ambacho walikuwa wakiongea simuni.
Irene alijua fika kwamba Rose alikuwa akiogopa lakini kitu ambacho alikifanya yeye ni kumuondoa wasiwasi kila siku. Maneno matamu ya Irene ambayo yalikuwa yakisikika mara kwa mara masikioni mwake yakamfanya kutamani kuujaribu uume ule ambao ulikuwa ni wa plastiki laini.
Usiku wa siku hiyo Rose akajaribu kuutumia uume ule. Maumivu yalikuwa makubwa chini ya kitovu kiasi ambacho akaamua kuuacha. Kila siku alikuwa akitamani aendelee zaidi na zaidi lakini bado alikuwa akiumia kupita kawaida kitu kilichompelekea kuachana nao.
“Sasa kwa nini uachane nao?” Irene alisikika akimuuliza simuni.
“Unauma”
“Acha masihala. Hiyo si siku ya kwanza mke wangu. Jitahidi, baadae maumivu yatakwisha, hakuna kinachouma milele” Irene alimwambia Rose.
“Nimeshindwa. Labda uje kunisaidia”
“Usijali. Nitakuja huko mwezi ujao” Irene alimwambia Rose.
Maisha ya usagaji yakawa yamekwishamuingia Rose na hakujua ni kwa namna gani alitakiwa kujinasua kwa wakati huo. Matamanio kwa mwanaume wala hayakuwepo kabisa, kila siku alikuwa akiwatamani wanawake wenzake tu. Kila alipokuwa akimuona mwanamke ambaye alikuwa na makalio makubwa, mwili wake ulikuwa ukimsisimka kupita kawaida, alikuwa akitamani kusagana tu.
Matiti yake ambayo yalikuwa madogo ya wastani katika kipindi hicho tayari yalikuwa yamekwishaanza kuwa makubwa kutokana na kushikwa sana na Irene. Kwa wakati huo akaanza kuvaa sidiria kitu ambacho hakuwahi kukivaa toka anazaliwa. Umbo lake likaongezeka, uzuri wake ukaongezeka zaidi. Katika kipindi hicho, Rose hakutamani mwanaume yeyote yule, mtu ambaye alikuwa akimtamani ni mwanamke tu, hasa Irene ambaye alikuwa akimridhisha sana kitandani.
****
“Ila kiukweli ninataka kumuoa Rose” Kijana Peter alimwambia baba yake, mzee Edward.
“Umempenda kweli?” Mzee Edward alimuuliza Peter.
“Ndio baba”
“Basi hakuna tatizo. Nenda kasome kwanza na kisha ukirudi utamuoa tu” Mzee Edward alimwambia kijana wake.
“Atakubali kweli?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa nini asikubali? Nitaongea na baba yake”
Hayo yalikuwa maongezi ya watu wawili. Kila siku Peter alikuwa akimwambia baba yake kuhusiana na Rose ambaye katika kipindi hicho alikuwa kidato cha nne katika shule ya Jangwani jijini Dar es Salaam. Rose ndiye alikuwa msichana ambaye alikuwa akimpenda kupita kawaida moyoni mwake.
Siku ya kwanza kuonana na Rose ilikuwa katika kipindi ambacho wanajeshi walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya kufanya sherehe ya kuwapongeza wanajeshi ambao walikuwa wamepandishwa vyeo hasa mara baada ya kutoka katika mafunzo ya kikomandoo nchini Cuba. Katika sherehe hiyo ndipo ambapo Peter aliweza kukutana na msichana Rose.
Moyo wa Peter ukafa na kuoza kwa Rose, uzuri wake machoni mwake ulionekana kuwa mithili ya malaika, alijaribu kuongea nae siku ile lakini Rose hakuonekana kuwa radhi kuongea na Peter kwa sababu katika maisha yake hakutaka kuwa karibu sana na wanaume. Peter akaumia ila alichokifanya ni kupeleleza Rose alikuwa mtoto wa nani. Alipokuja kufahamu kwamba alikuwa mtoto wa Bwana Shedrack, hapo akaona kwamba kungekuwa na wepesi wa yeye kumpata Rose kutokana na ukaribu wa baba yake na Bwana Shedrack.
Bwana Edward hakuwa na jinsi, alipoambiwa na mtoto wake, Peter kwamba alikuwa akimtaka Rose na kuwa wapenzi na baadae kufunga nae ndoa akamfikishia ujumbe ule mzee mwenzake, Bwana Shedrack ambaye aliona kwamba kwa kitendo cha Rose kuwa na Peter basi urafiki wao ungedumu zaidi.
“Hilo nalo neno. Nitaongea nae” Bwana Shedrack alimwambia Bwana Edward ambaye akakenua kuonyesha furaha aliyokuwa nayo.
“Utaongea nae lini sasa?”
“Bado. Si unajua kwamba kwa sasa hivi anasoma”
“Basi haina tatizo. Wewe ongea nae, katika kipindi ambacho Peter atarudi kutoka masomoni Afrika Kusini, basi aweze kumuoa. Itapendeza sana” Mzee Edward alimwambia Bwana Shedrack.
“Hakuna tatizo. Atarudi baada ya miaka mingapi?”
“Miwili tu”
“Basi hakuna tatizo kabisa. Unajua sisi ni marafiki, vitu kama hivi vitatufanya tuwe karibu sana na kuwa kama ndugu wa hiari” Bwana Shedrack alimwambia Bwana Edward.
“Hata mimi nimeliona hilo”
Bwana Shedrack hakutaka kufanya vitu kwa haraka sana, kwanza akamuacha Rose amalize shule na kisha kumfikishia kile ambacho aliambiwa na Bwana Edward. Katika kitu ambacho alikiona kama kingefaa sana kumfanya Rose kutokuwa na mwanaume ni kumfungia sana ndani. Hivyo ndivyo ilivyokuwa, mara baada ya kumaliza shule, Bwana Shedrack hakutaka Rose atoke nje.
Hata matokeo yalipotoka na Rose kufaulu na kutakiwa kujiunga na shule ya Benjamin William Mkapa ya jijini Dar es Salaam, hakutaka kumpeleka shuleni. Alichokiamua ni kwamba Rose aendelee kubaki ndani ya nyumba tu kwa kuogopa kwamba kama angekwenda tena shule, hasa Benjamin na kukutana na wanaume mbalimbali, wangeweza kumshawishi, afanye nao mapenzi na hatimae kuanguka kabisa mapenzini kwa kijana mmoja hivyo kuwa mtihani mkubwa kwa Peter hapo baadae.
Hiyo ikawa mwanzo wa sababu kwa Bwana Shedrack kuwa mkali kwa binti yake. Hakutaka kumuona akisimama na mwanaume, na kila alipomuona alikuwa akimkaripia sana na hata kumpiga. Kwake, alitaka Rose aendelee kuwa vile vile, msichana ambaye hakuwa amekutana na mwanaume katika maisha yake na kulala kitanda kimoja. Japokuwa alikuwa makini kwa kila kitu, Bwana Shedrack alifanya kosa sehemu moja tu, kumleta Irene ndani ya nyumba ile, msichana ambaye alikuja kuharibu kila kitu.
Katika kipindi chote ambacho Peter alikuwa chuoni nchini Afrika Kusini kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Rose, msichana ambaye alitokea kumpenda kuliko msichana yeyote maishani mwake. Kila alipokuwa akimkumbuka Rose, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi huku akianza kujisikia amani moyoni.
Katika kipindi hicho, Peter alikuwa katika mapenzi ya dhati, hakuona sababu yoyote ile ya kuchukua msichana yeyote chuoni hapo na wakati kulikuwa na msichana ambaye aliandaliwa kwa ajili yake nchini Tanzania, Rose. Wasichana wengi wazuri wa Kizulu pamoja na Xhosa walikuwa wakitamani sana kuwa na Peter ambaye alikuwa Mtanzania lakini Peter hakuonekana kuwa rahisi kutekwa na wasichana hao.
Kwake, ndani ya moyo wake kulikuwa na msichana mmoja tu, Rose ambaye alikuwa ameingia moyoni, akavuta kiti na kisha kutulia Hakuwa na habari na wasichana wengine, japokuwa mara nyingi walikuwa wakimletea mitego mingi lakini hiyo wala haikuwa sababu iliyomfanya Peter kuwafuata na kumtoa Rose moyoni mwake.
Rose alikuwa kila kitu ndani ya moyo wake, Rose alikuwa kama malkia mpya ambaye aliingia ndani ya moyo wake na kuanzisha utawala wa kimapenzi. Katika kila kitu ambacho alikuwa akikifanya, bado alimuamini sana baba yake, Bwana Edward ambaye alimuachia kazi ya kuweza kuongea na baba yake Rose, Bwana Shedrack kuhusiana na Rose kwamba alikuwa akikamilisha kila kitu taratibu.
“Usijali. Kila kitu kinakwenda safi kabisa. Unasubiriwa wewe tu” Bwana Edward alimwambia kijana wake, Peter.
“Kwa hiyo kila kitu safi?”
“Yeah! Si unajua wazee tunajuana bwana. Tunajua namna ya kuongea kiutu uzima. Wewe maliza chuo na kisha njoo” Bwana Edward alimwambia kijana wake.
“Sawa sawa. Umekwishanifanya niione miaka miwili kuwa mingi. Kama kila kitu kipo freshi, nitakuja na kisha kufunga nae ndoa” Peter alisema huku akionekana kuwa mwenye furaha.
“Usijali. Unasubiriwa wewe tu” Bwana Edward alimwambia kijana wake.
Hapo ndipo presha ilipozidi kuongezeka zaidi moyoni mwa Peter, mawazo juu ya Rose yakaongezeka zaidi na zaidi. Hakuamini kama kazi ambayo alimuachia baba yake ilikuwa imekwishafanyika kwa urahisi sana tofauti na jinsi alivyokuwa akifikiria kabla. Muda mwingi chuoni alionekana kuwa na furaha, kitendo cha kufanyiwa kazi yake kilimpa furaha kupita kawaida.
Mwaka wa kwanza ukakatika chuoni, hakutaka kurudi nchini Tanzania kwa sababu alikuwa na mambo mengi ya kufanya. Akabaki nchini Afrika Kusini mpaka mwaka wa pili kuingia. Katika kipindi hicho bado mawazo yake juu ya Rose hayakuweza kumtoka hata kidogo, alikuwa akiendelea kumfikiria msichana huyo.
Miezi ikaendelea kukatika mpaka kufikia kipindi ambacho alitakiwa kufanya mitihani yake ya mwisho. Alijitahidi sana kusoma, moyo wake ulikuwa umegawanyika katika vyumba viwili kwa wakati huo. Nusu ulikuwa ukifikiria kuhusiana na masomo na nusu ulikuwa ukimfikiria Rose. Mitihani ilipokwisha, akaanza kujiandaa na safari yakurudi nchini Tanzania.
Ndani ya ndege, aliiona ndege hiyo ikichelewa kufika nchini Tanzania. Alitamani yeye ndiye angekuwa rubani aweze kuiendesha ndege hiyo kwa kasi zaidi na kuingia nchini Tanzania. Hakukuwa na kitu ambacho alikuwa amekipanga wa kwa wakati huo zaidi ya kufika nchini Tanzania na kisha kufunga ndoa na Rose ambaye mpaka katika kipindi hicho aliamini kwamba uzuri wa msichana huyo ulikuwa umeongezeka maradufu.
Mpaka ndege inakanyaga ardhi ya Tanzania, mapigo ya moyo ya Peter yalikuwa yakimdunda kupita kawaida, hamu ya kumtia machoni Rose ilikuwa imemkaba kupita kawaida. Kwa mwendo wa haraka haraka akaanza kushuka katika ndege ile na kisha kuanza kuelekea katika jengo la uwanja wa ndege ule wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kisha kuchukua mzigo wake.
“Nimewakumbuka sana” Peter aliwaambia wazazi wake, Bwana Edward pamoja na mama yake, Bi Stella na kisha kuwakumbatia.
“Karibu tena nchini Tanzania” Bwana Edward alimwambia Peter.
“Nimekwishakaribia. Nilidhani mngekuja na Rose kuja kunipokea” Peter aliwaambia katika kipindi ambacho alikuwa akiingia ndani ya gari.
“Usijali. Hatukutaka kumtaarifu kwani tulitaka kumfanyia sapraizi” Bwana Edward alimwambia Peter na kisha kuwasha gari na kuondoka mahali hapo.
Kila kitu kikaonekana kukamilikia kwa wakati huo. Walipofika nyumbani, Bwana Edward hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kuanza kuwasiliana na Bwana Shedrack na kumwambia kwamba kijana wake tayari alikuwa amekwishaingia nchini Tanzania na hivyo alitaka kuonana nae.
“Hilo si tatizo. Tunaweza kuonana” Bwana Shedrack alimwambia Bwana Edward simuni.
“Sawa. Nije hapo hapo nyumbani kwako au?”
“Vyovyote vile lakini kama tukionana sehemu yoyote tulivu ya vinywaji itakuwa bora zaidi” Bwana Shedrack alimwambia Bwana Edward.
Hapo wakapanga sehemu ya kukutania na kisha kuongea kile ambacho walitakiwa kukiongea kuhusiana na watoto wao. Wakakutana, kila mmoja akaonekana kuwa na furaha, wakakubaliana kwamba ilikuwa ni lazima vijana wao wafunge ndoa na hatimae kuishi pamoja kama mume na mke na hivyo kuufanya urafiki wao kuwa karibu zaidi ya ndugu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walichokiona ambacho kilikuwa bora zaidi ni kumtaka Peter kuja nyumbani ili aweze kuonana na Rose kama hatua mojawapo ya kumzoea na kisha mambo mengione kufuata. Hilo halikuonekana kuwa tatizo kwa Peter, siku iliyofuata, wakati wa mchana akaanza kwenda nyumbani kwa Bwana Shedrack kama ambavyo aliambiwa.
Alipofika nyumbani hapo, akapiga honi, mlinzi akafungua geti na kisha kuanza kumhoji Peter maswali. Peter akajitambulisha, geti likafunguliwa na kisha kuliingiza gari lake na kuliegesha. Peter akateremka, katika kipindi hicho, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi kupita kawaida, akaanza kuufuata mlango wa kuingilia sebuleni na kisha kuanza kuugonga.
Mlango ukafunguliwa na John, kwa sababu kwa kiasi fulani alikuwa akifahamiana na John, wakaanza kuongea kwa furaha na kisha kuingia ndani. Macho ya Peter hayakutulia, japokuwa John alikuwepo mahali hapo huku akiongea nae maneno mengi lakini macho yake yalikuwa na kiu ya kumuona Rose tu.
“Rose yupo?” Peter alimuuliza John.
“Yupo. Nimuite umsalimie?” John alimuuliza Peter.
“Itakuwa vizuri sana” Peter alijibu.
John hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuelekea chumbani kwa Rose kwa ajili ya kumuita msichana huyo. Peter alibaki akiwa na presha kubwa, hakuamini kwamba mara baada ya kusubiri kwa miaka miwili siku hiyo ndio ilikuwa siku ya kumtia machoni Rose kwa mara nyingine tena. Alibaki kochini kwa dakika kadhaa, John akarudi mahali hapo huku akiongozana na Rose.
Mapigo ya moyo ya Peter yakaongezeka kasi zaidi, mzunguko wake wa damu ukawa mkubwa kupita kawaida. Peter akajihisi kama kipindi chochote kile alikuwa akizimia kwa presha kubwa mara baada ya kumtia machoni Rose. Ule uzuri ambao alikuwa nao katika kipindi cha nyuma ukaonekana kuongezeka maradufu kwa wakati huo, hakuamini kama Rose alikuwa akionekana kuwa mrembo namna ile.
Miguu yake ikawa mizito kusimama, macho yake hayakuweza kutoka usoni mwa Rose, lipsi za mdomo wake zikaanza kuchezacheza huku kwa mbali akiuhisi mwili wake kuanza kutokwa na kijasho chembamba cha wasiwasi.
“Habari yako” Rose alimsalimia Peter ambaye bado alikuwa akimwangalia huku akionekana kuwa na mshangao.
“Nzuri. Karibu Rose” Peter alimwambia Rose.
Rose, msichana ambaye alikuwa akimfikiria kwa takribani miaka miwili leo hii alikuwa mbele yake, msichana ambaye alikuwa akimpa nafasi kubwa moyoni mwake leo hii alikuwa amekaa mbele yake huku akimwangalia. Muda wote Peter alionekana kuwa na furaha, hakuamini kama yule Rose ambaye alikuwa akimfikiria kwa kipindi kirefu leo alikuwa mbele yake. Wakati mwingine alijiona kuwa na uhitaji wa kumfuata Rose na kisha kumkumbatia kwa dakika kadhaa japo aanze kulihisi joto la mwili wake.
“Rose” Peter alijikuta akiita bila kupenda.
“Abeeee”
“Nimekukumbuka sana” Peter alimwambia Rose ambaye alibaki kimya kwa muda. John akaonekana kuhisi kitu, muonekano ambao alikuwa nao Peter ulionekana kuwa muonekano mwingine kabisa, alichokifanya ni kuinuka na kisha kuelekea chumbani.
“Umekuwa mzuri maradufu” Peter alimwambia Rose ambaye alibaki kimya.
Peter akaona kwamba kama angeongea maneno matupu ilikuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kitu huku ukisubiria yasagike. Alichokifanya ni kuinuka pale kochini na kisha kuanza kumsogelea Rose katika kochi lile na kisha kukaa karibu yake. Alipoupeleka mkono na kumgusa tu, Peter akajihisi akisisimka kupita kawaida.
“Rose…!” Peter aliita kwa sauti ya chini.
“Abee” Rose aliitikia.
“Nakupenda” Peter alimwambia Rose.
“Nafahamu”
“Ninahitaji kukuoa na kuwa mke wangu wa ndoa hapo baadae” Peter alimwambia Rose huku akiwa ameushika mkono wake.
“Kunioa?”
“Ndio”
“Sidhani”
“Kwa nini tena?”
“Nahisi sistahili kuolewa”
“Kwa nini?”
“Basi tu”
“Hapana Rose. Nimekuwa nikikusubiria kwa miaka miwili mpaka sasa, nimekuwa nikiwakataa wasichana wengine kwa ajili yako, hebu fikiria muda wangu nilioupoteza kwa ajili yako Rose” Peter alimwambia Rose.
“Najua”
“Sasa kwa nini hutaki nikuoe?”
“Unakumbuka nilikwambia nini kipindi cha nyuma?”
“Hapana”
“Nilikwambia kwamba sikutaki”
“Rose…pleaseeee”
“Huo ndio ukweli. Mbaya zaidi sina hata ndoto za kuolewa na mwanaume yeyote yule” Rose alimwambia Peter na kisha kusimama kutoka kochini pale na kisha kuanza kuondoka.
“Rose…Rose…Rose…” Peter aliita lakini Rose hakusimama wala kugeuka, akapotea machoni mwake.
Peter aliumia, aliumia zaidi ya maumivu ambayo aliumia katika maisha yake ya nyuma. Hakuamini kwamba kwa miaka miwili ambayo alikuwa ameipoteza kwa ajili ya kumsubiria msichana huyo leo hii alikuwa akimwambia kwamba hakuwa akimpenda na wala hakuwa na ndoto za kuolewa na mwanaume yeyote yule.
Peter alijihisi kuchanganyikiwa kupita kawaida, bila kutegemea akayahisi macho yake yakianza kulengwa na machozi na baada ya dakika kadhaa machozi yakaanza kutiririka mashavuni mwake. Maneno ya Rose yalikuwa yamemchoma moyo wake kupita kawaida, alikuwa ameumia katika maumivu ambayo hakuwa akiyafikiria kabla.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapo ndipo akaanza kushikwa na mashaka kwamba inawezekana Bwana Shedrack hakuwa ameongea na binti yake zaidi ya kumtaka Peter mwenyewe kufika mahali hapo na kisha kuanza kuongea na Rose kuhusiana na maisha yao. Peter akaoneana kuchanganyikiwa, alichokifanya ni kusimama na kisha kutoka nje. Katika kipindi hicho, safari yake ilikuwa ni kuelekea katika kambi ya kijeshi ya Lugalo kwa ajili ya kuonana na Bwana Shedrack na kumuuliza kile ambacho kilikuwa kimetokea kwani kama angekuwa ameongea nae kabla basi msichana huyo asingeweza kumkataa kiasi kile.
Peter akaanza kuondoka mahali hapo. Akaingia ndani ya gari lake na kisha kuliondoa. Moyo wake bado ulikuwa na maumivu makali kupita kawaida. Hakuamini kwamba kweli msichana Rose alikuwa amemkataa namna ile huku akimwambia dhahiri kwamba hakufikiria kuolewa na mwanaume yeyote yule.
Peter hakujua, hakujua kwamba nyuma ya kila kitu kulikuwa na mtu mmoja tu ambaye alifanya kila kitu kutowezekana kwa wakati huo. Peter hakujua kwamba kwa kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kulikuwa na mtu aliyeitwa Irene, mtu ambaye alikuwa amepigilia msumali wa mwisho katika moyo wa Rose wa kumkataa kila mwanaume ambaye angemfuata maishani mwake.
Kauli ya Rose kwamba hakuwa tayari kuolewa na mwauame yeyote wala haikueleweka moyoni mwa Peter, hakuelewa kama kauli ile ilimaanisha kwamba hakuwa tayari kuolewa na mwanaume yeyote yule bali alikuwa tayari kuolewa na mwanamke, hasa Irene ambaye alikuwa amemuingiza katika ulimwengu mpya wa mapenzi.
Maneno ya Irene kila siku yalikuwa moyoni mwake, moyo wake ukatokea kumuamini Irene kupita mtu yeyote katika dunia hii, hakuona sababu ya kumuamini mtu mwingine zaidi ya Irene ambaye kwake alimuona kuwa zaidi hata ya baba yake. Kila siku alikuwa akiwasiliana nae simuni na kuongea maneno ya kimapenzi huku wakiitana mke na mume.
Walikubaliana katika kila kitu lakini suala la Rose kutumia uume wa bandia bado lile likaonekana kuwa zoezi gumu sana ambalo wala hakuweza kulikubali kutokana na maumivu ambayo alikuwa akiyasikia kila alipojaribu kuutumia uume ule.
Siku ziliendelea kukatika mpaka siku ambayo Irene alikuja nyumbani hapo kufikia. Ile kumuona tu, Rose akashindwa kuvumilia, akamfuata na kumkumbatia kwa furaha tukio ambalo lilionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa amemkumbuka mtu huyo. Bwana Shedrack ambaye alikuwa amekuja na Irene ndani ya nyumba hiyo akaonekana kutabasamu kwa kuona kwamba Rose alikuwa akiufurahia uwepo wa Irene mahali hapo bila kujua kitu ambacho kilikuwa kikiendelea nyuma ya pazia.
Siku ile ikaonekana kuwa furaha kwa Rose, hakuamini kama kweli Irene, msichana ambaye alikuwa akipenda kumuita mume wake alikuwa amefika ndani ya nyumba ile. Kitu cha kwanza mara baada ya kupeleka mizigo chumbani ni kuanza kubadilishana mate kitendo ambacho kiliwachukua muda wa dakika moja nzima.
“Nimekukumbuka mume wangu” Rose alimwambia Irene ambaye alionekana kuwa mwenye furaha kubwa zaidi.
“Nimekukumbuka pia” Irene alimwambia Rose na kisha kuanza kupeana mabusu mfululizo.
Siku hiyo walibaki chumbani huku wakiongea mambo mengi. Kwa sababu Irene alikuwa na muda wa wiki moja tu kukaa ndani ya nyumba hiyo kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka, akajitahidi sana mpaka anaondoka Rose awe amekwishaanza kuutumia uume ule wa bandia ambao alikuwa amemuachia.
Usiku ndio muda ambao zoezi lile likaanza kufanyika. Yalikuwa ni maumivu makubwa lakini alitakiwa kuvumilia kwa sababu alikuwa akiingia katika hatua nyingine. Rose alikuwa akipiga kelele za kimahaba huku kifua chake kikiwa juu na huku Irene akijitahidi kumtumikisha Rose uume ule wa bandia.
Damu zikaanza kutoka katika sehemu zake za siri, bikira ambayo alikuwa nayo ikawa imetolewa na uume wa bandia ambao alikuwa amekabidhiwa na Irene huku msichana huyo akiwa kungwi wake. Yalikuwa ni maumivu makubwa lakini kila uume ule ulivyokuwa ukizidi kufanya kazi na ndivyo ambavyo alishikwa na raha zaidi na zaidi, yaani yakawa maumivu yaliyo matamu.
Kitendo kile kilichukua dakika zaidi ya thelathini, mishipa ya damu ambayo ilikuwa imeungana ukeni ikawa imekwishakatika na sehemu ile kubaki wazi na kutengeneza njia. Hapo ndipo maisha ya Rose yakazidi kubadilika, japokuwa alikuwa msagaji lakini moyoni mwake akagundua kwamba kutumia uume wa bandia kulikuwa na raha zaidi ya kusagwa na Irene ambaye kwake aliendelea kuwa kungwi wake.
Rose akaanza kufikiria kitu kimoja, tayari alikuwa amekwishaonja raha ya uume wa bandia ambao alikuwa ameutumia na sasa alijiona kuwa na kila sababu ambazo zilimfanya kutumia uume ambao haukuwa wa bandia kwa ajili ya kuona utofauti wake.
Moyoni alikuwa amekubaliana na nafsi yake kwamba ilikuwa ni lazima ajaribu kwa namna yoyote ile kuonja raha ya uume ambao haukuwa wa bandia kama ule ambao alikuwa ameutumia Irene mwilini mwake, kwa kifupi, alikuwa akitamani kufanya mapenzi na mwanaume.
Kitu ambacho alikuwa akikitaka kilikuwa kimoja tu, alitaka kuona ni raha gani ilikuwepo kwa mtu ambaye alikuwa akifanya mapenzi na uume ambao haukuwa wa bandia. Kusagana hakukuisha hata mara moja, mwili wake ulikuwa ukihitaji kusagwa kama msichana ambaye alikuwa akihitaji kufanya mapenzi na mwanaume na Irene alikuwa kwa ajili yake tu.
”Kumbe nao una raha yake” Rose alimwambia Irene.
“Nini?”
“Si ule uume wa bandia”
“Achana nao. Sidhani kama una raha kama hivi ninavyokufanyia mpenzi” Irene alimwambia Rose.
“Mmmh! Ule umezidi mume wangu. Ningependa kila siku tuwe tunautumia” Rose alimwambia irene.
“Mmmh!”
“Mbona unaguna tena”
“Naona nikiondoka bora niondoke nao”
“Kwa nini sasa?”
“Unaweza kukufanya usinitamani” Irene alimwambia Rose.
“Hapana bwana. Usifanye hivyo”
“Manake naona umekwishaanza kuidharau kazi zangu”
“Wala sijadharau”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa unavyosema ule una raha zaidi si inamaanisha kwamba umeanza kuidharau kazi yangu!” Irene alimwambia Rose.
“Hapana. Kazi yako bado bora na itaendelea kuwa bora mwilini mwangu” Rose alimwambia Irene.
Usagaji bado ulikuwa ukiendelea kama kawaida. Mawazo ya Rose katika kipindi hiki yakaanza kuhama kabisa, tayari alikwishaona kwamba kulikuwa na kitu tofauti sana mara unapoamua kutumia uume wa bandia na ile staili ya usagaji ambayo alikuwa akiifanya Irene mwilini mwake, moyo wake ukabadilika, bado alikuwa akitamani sana kufanya mapenzi na mwanaume ili kuona kulikuwa na kitu gani.
“Mjomba aliniambia kwamba kuna mwanaume anataka kukuoa” Irene alimwambia Rose.
“Aliniambia pia. Ni mwanaume ambaye alikuwa akinifuatilia toka zamani lakini nikawa simpendi” Rose alimwambia Irene.
“Kwa nini sasa haumpendi?”
“Basi tu. Sijisikii kuwa na mwanaume katika kipindi hiki” Rose alimwambia irene.
“Safi sana. Wanaume ni watu wabaya sana. Wale hawana huruma kabisa, kwanza ukiwapenda sana, wanauumiza moyo wako” Irene alimwambia Rose.
“Kweli?”
“Ndio hivyo” Irene alijibu.
“Basi nitaendelea kuwachukia”
“Hilo ndilo la maana”
Tayari Irene alikuwa amekwishausoma mchezo, alikwishaona kwamba kama asingeweza kutumia njia nyingine za kumfanya Rose kuwachukia wanaume basi angeweza kumpoteza msichana huyo kwani alikwishaona kwamba aliona raha sana kila autumiapo uume wa bandia ambao alikuwa amemkabidhi. Akajiona kutumia nguvu za ziada akilini mwake, nguvu ambazo zingemfanya Rose kuendelea kumuamini yeye na kuachana na wanaume.
“Nitajaribu kufanya mapenzi na mwanaume nione” Rose alijisemea moyoni.
Wiki moja ikakatika na hatimae Irene kurudi chuoni. Japokuwa alikuwa akitamani sana kuondoka na uume wake wa bandia lakini Rose akaung’ang’ania sana na hatimae kumuachia. Irene hakutamani kabisa kuuacha lakini hakuwa na jinsi, kwa sababu hakutaka kumuona Rose akiwa amekasirika, akaamua kumuachia.
Kazi ikabaki kwa Rose. Kila alipokuwa akiutumia uume ule aliuona kuwa wa tofauti sana kuliko mikono ambayo alikuwa akiitumia Irene katika kuutomasa mwili wake. Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hamasa kubwa ya kutamani kuwa na mwanaume ikazidi kumwingia mwilini mwake.
Katika kipindi ambacho Peter alifika nyumbani, mwili wake ulikuwa katika matamanio makubwa sana ila tatizo lilikuwa moja tu, Peter alikuja na gia za kutaka kuwa mke wake. Rose hakuwa tayari, alichokuwa akikihitaji katika kipindi hicho ni kuwa na mwanaume ambaye angefanya nae mapenzi na kumuonjesha radha tu na si kuwa mume wake wa ndoa kwa sababu bado alikuwa pamoja na Irene.
Hakumkubali Peter kwani aliona kama alikuwa akimzingua. Alichokifanya Rose katika kipindi hicho ni kuchukua simu yake na kisha kuanza kuziangalia meseji ambazo alikuwa ametumiwa na wanaume mbalimbali anaowafahamu na asiowafahamu. Akaanza kuzipitia moja moja mpaka alipotua katika jina la Joshua. Akaifungua meseji hiyo na kisha kuanza kuisoma. Kama ilivyokuwa kwa wengine, Joshua alikuwa amejielezea vya kutosha kwamba alikuwa akimpenda sana Rose na alikuwa akimuhitaji, alichokifanya ni kumtumia meseji moja tu.
“Nataka kukuona mchana wa leo, tafuta sehemu isiyokuwa mbali na nyumbani, sehemu ambayo tutakuwa wawili tu” Meseji ile ilisema na kisha kuituma. Wala haikuchukua muda mrefu, meseji ile ikajibiwa.
“Unataka nionane nawe wapi? Bar au wapi?” Meseji hiyo kutoka kwa Joshua ilisomeka.
“Huko sitaki. Kuna watu wengi”
“Basi njoo gheto kwangu, hakuna mtu zaidi yangu”
“Sawa. Nitakuja saa nane. Naomba uwepo na usimwambie mtu yeyote yule”
“Usijali. Nitakuwa nakusubiria” Meseji ya Joshua ilisomeka.
Rose akaonekana kuridhika, tayari alijiona kwamba katika siku hiyo ingekuwa siku maalumu ya kuonja radha waliyokuwa nayo wanaume katika kufanya mapenzi. Uume ule wa bandia ukaonekana kama kumchanganya na kwa sasa alikuwa akitaka kitu chenyewe na wala si cha bandia tena. Kwake, katika kipindi hicho aliuona muda ukichelewa sana, kila wakati alikuwa akiangalia simu yake ya mkononi, mshale wa sekunde ulikuwa ukichelewa kwenda.
Saa nane kasoro tano mchana Rose akatoka chumbani kwake. Hakutaka kupitia sebuleni kwa kuona kwamba John angemuona, akapitia geti la nyuma na kisha kuondoka. Siku hiyo Rose hakuonekana kuwa na amani, muda wote macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule.
Alipofika katika sehemu ambayo kulikuwa na nyumba ambayo alikuwa amepanga Joshua, akaanza kuangalia huku na kule, macho yake yakagongana na macho ya Joshua. Joshua hakutaka hata kuongea nae, alichokifanya ni kuanza kuelekea ndani ambapo Rose akaanza kumfuata mpaka kuingia chumbani.
“Karibu mgeni” Joshua alimwambia Rose huku akionekana kuwa na hamu japo kuyaona mapaja ya msichana huyo.
“Asante” Rose alisema huku akikaa katika kistuli.
“Hicho kibovu. Utaanguka” Joshua alimwambia Rose huku akitaka akae tu kitandani na wala stuli haikuwa mbovu.
Rose akainuka na kisha kukaa kitandani. Alichokifanya ni kuitoa kanga ambayo alikuwa ameivaa na kisha kukibakisha kisketi kifupi ambacho kiliyafanya mapaja yake meupe kuwa nje. Joshua hakutulia, mara alikuwa akifanya hili, mara lile, yaani kila wakati mishemishe hazikuisha chumbani hapo. Wakabaki wakipiga stori tu. Kitu ambacho alikuwa amekifuata Rose mahali hapo kilikuwa ni kimoja tu, kufanya mapenzi na Joshua ila alikuwa na wasiwasi ni sehemu gani ambapo alitakiwa kuanzia.
Huku akiwaza ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, kichwa chake kikaonekana kukumbuka kitu kwamba siku hiyo ilikuwa ni siku ya hatari kwake, siku ambayo kama angefanya mapenzi na mwanaume basi kulikuwa na uwezekano wa kupata ujauzito. Akajikuta akiinuka na kutaka kuondoka.
“Vipi tena?” Joshua alimuuliza Rose.
“Nataka kuondoka nyumbani” Rose alijibu.
“Yaani umekuja na kukaa kwa dakika kumi tu unataka kuondoka. Usifanye hivyo Rose” Joshua alimwambia Rose
Joshua akashindwa kuvumilia, kwa jinsi alivyokuwa akiyaangalia mapaja ya Rose pamoja na kifua chake ambacho kilikuwa kimesimamishwa na sidiria ambayo alikuwa ameivaa akashindwa kuvumilia. Kama angethubutu kumuacha Rose aondoke ndani ya chumba hicho pasipo kufanya mapenzi lingeonekana kuwa kosa la jinai kwake.
Akamshika Rose mkono na kisha kumkarisha kitandani. Alichokifanya bila kuchelewa ni kuanza kubadilishana mate pamoja na kuanza kuupapasa mwili wa Rose. Hapo ndipo utaofauti ukaanza kugundulika kwa Rose. Mikono ya Joshua ilikuwa ni tofauti na Irene, mwanaume, kwake akaonekana kuwa na kitu cha ziada, bila kinyongo chochote kile, akajikuta akimruhusu Joshua aendelee huku kichwa kikiwa kimesahau kama alikuwa katika siku za kupata ujauzito.
“Nakupenda Rose. Nakupenda sana Rose. Nakwenda kufanya mapenzi nawe siku ya kwanza na kuanza mahusiano ya kimapenzi rasmi” Joshua alimwambia Rose ambaye alimkubalia kwa kutingisha kichwa chake juu na chini.
Hapo ndipo ambapo Rose akafanya mapenzi na mwanaume kwa mara ya kwanza, kila wakati alikuwa akiuona utofauti mkubwa zaidi, raha ambayo alikuwa akiipata ilikuwa ni tofauti na ile ambayo alikuwa akiipata kwa Irene. Walichukua muda wa dakika hamsini, kila mmoja akawa hoi.
“Hivi ulitumia mpira?” Rose alimuuliza Joshua.
“Hapana”
“Haukutumia?”
“Sikutumia?”
“Kwa nini?”
“Dah! Nilikuwa kwenye mzuka, nikasahau mpira” Joshua alijibu.
Rose akaonekana kushtuka sana, hakuamini kama alikuwa amefanya mapenzi na Joshua bila kutumia mpira. Moyo wake ukaanza kusononeka, hakuamini kama kweli kitendo kile kilikuwa kimechukua nafasi katika maisha yake. Mtu wa kwanza kumfikiria alikuwa baba yake, angemwambia nini endapo angegundua kwamba alikuwa mjauzito, amani ikatoweka moyoni mwake.
“Acha niondoke” Rose alimwambia Joshua huku akionekana kuwa na haraka.
“Kuna nini tena?”
“Acha niondoke. Tutaongea kwenye simu” Rose alimwambia Joshua na kisha kuondoka ndani ya chumba hicho.
Mbegu za Joshua zikawa zimeingia katika mayai ya uzazi ya Rose na kuanza hatua zote za kutengeneza kijusi na kisha mtoto kuumbwa ndani ya tumbo lake. Hilo likaonekana kuwa kosa kubwa kwa Rose, kumruhusu Joshua kufanya nae mapenzi ndani ya siku ile ikaonekana kuwa kosa kubwa sana. Hakujua, hakujua kabisa kama kuruhusu kufanya kitendo kile ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mapya, maisha ambayo asingeyapenda ila yalikuwa maisha ambayo alibidi kuyaishi kwa kuwa hakuwa na jinsi wala uamuzi wowote wa kuyakwepa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
****
Uzuri wa Rose ulikuwa umewateka vijana wengi waliokuwa wakiishi Magomeni Mapipa, kila mvulana ambaye alibahatika kumuona Rose alitamani kuwa msichana wake kwani alikuwa akionekana kuwa na mvuto mkubwa kupita kawaida. Wanaume hawakutaka kutulia, kila siku walikuwa wakimfuatilia msichana huyo ambaye alionekana kumhofia kila mwanaume ambaye alikuwa akimfuata.
Watu wakajua kwamba baba yake, Bwana Shedrack ndiye ambaye alimfanya mrembo huyo kuwa namna hiyo. Wavulana hawakukoma, kila siku walikuwa wakiweka mitego yao lakini hakukuwa na mtego hata mmoja ambao ulimnasa Rose. Hapo ndipo watu walipoanza kuzitafuta namba za simu za Rose. Walichokifanya, ni kumtumia msichana Lucy ambaye akajiwekea ukaribu kidogo na Rose na kisha kuchukua namba zake.
Kila mwanaume alikuwa akizitaka namba hizo huku wengine wakidiriki hata kuzinnunua. Kwa maneno walishindwa hivyo walitaka kumteka kwa kutumia maandishi. Kwa siku, Rose akawa anapokea meseji kutoka kwa wanaume zaidi ya thelathini huku kila mmoja akizielezea hisia zake za kimapenzi kwa msichana huyo ambaye hakuonekana kuwaelewa kabisa.
Kati ya wanaume wote, pia kulikuwa na Joshua, mvulana ambaye kila siku alikuwa akimpenda sana Rose ila hakuwa akipata muda wa kumwambia kwani kila siku Rose alipokuwa akitoka, alikuwa pamoja na wavulana wengine ambao kama walikuwa kwenye mashindano ya kumtaka Rose.
Siku mbili za nyuma kabisa ambazo Joshua alionana na Rose na kisha kuongea nae ndizo siku ambazo wakaonekana kufahamiana lakini baada ya hapo, hawakuonana tena. Hata siku ambayo Joshua alikuwa akimtumia Rose meseji, Rose alikuwa akimfahamu sana Joshua ambaye alikuwa akijitambulisha lakini katika kipindi hicho hakuwa tayari kuwa na mvulana.
Kila siku Joshua alionekana kuwa mtu wa kuumia tu, kila meseji zake alizokuwa akimtumia Rose hazikuwa zikijibiwa jambo ambalo lilikuwa likimfanya kutokuwa na furaha kabisa. Katika chumba ambacho alikuwa amepanga, usiku kilionekana kuwa kikubwa, kitanda chake alikiona kama kumwagiwa maji kwani kila alipokuwa akijaribu kulala, usingizi haukuja kabisa.
Mawazo juu ya Rose yalikuwa makubwa, kuna wakati mwingine aliatamani kumfuata Rose mpaka nyumbani kwao na kumuulizia lakini ilipofika asubuhi, alikuwa akihofia kufanya hivyo. Vijana ambao mara kwa mara walikuwa wakipewa mkong’oto mbele ya macho yake kutoka kwa Bwana Shedrack walionekana kumuogopesha sana Joshua kiasi ambacho akaamua kutulia huku akiyauguza maumivu yake chumbani kwake.
Mapenzi yakawa mazito moyoni mwake, mapenzi yakaonekana kumchoma kupita kawaida. Hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya kwa wakati huo, hakujua ni hatua gani ambayo alitakiwa kuichukua mpaka kuonana na Rose kwa mara nyingine tena na kuendelea kumsisitizia juu ya uamuzi wa kumpenda ambao ulikuwa moyoni mwake.
Mapenzi yalimuuma, mapenzi yalimchoma, kumpenda mtu ambaye wala hakuwa na taarifa na yeye ilionekana kumuumiza sana Joshua kiasi ambacho kila siku alikuwa akiulaumu moyo wake kwa nini ulikuwa ukimpenda sana Rose kupita kawaida. Hakujua ni kwa namna gani angeweza kumpata, ingekuwa anamuona nje ya nyumba yao akiwa peke yake ingekuwa afadhali, ila tatizo lilikuwa moja tu, kila alipokuwa akitoka, wasindikizaji walikuwa wengi.
Joshua akakata tamaa, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya kwa wakati huo. Kama kupenda alikuwa amependa sana na wakati huo moyo wake ukaonekana kama kukata tamaa. Maneno juu ya uzuri wa Rose bado yalikuwa yakiendelea kusikika kama kawaida lakini hakutaka kumwambia mtu yeyote kwamba na yeye pia alikuwa mmoja wa wafuatiliaji wazuri wa Rose.
Katika siku hii ya leo, Joshua hakutaka kufanya jambo lolote lile, kwa kuwa alikuwa amechoka, hata kufuatilia biashara zake akapuuzia na kisha kukaa tu nyumbani. Siku hiyo ndio alichukua muda mrefu sana kumfikiria Rose ambaye kwake alionekana kuwa kama malaika mzuri aliyeshushwa kutoka Mbinguni. Huku akiwa katika hali hiyo, mara meseji ikaingia. Hakutaka kupoteza muda, hapo hapo akaichukua simu yake na kuufungua ujumbe huo.
Kwanza akashtuka pale kitandani alipokuwa amelala, akainuka na kisha kukaa kitako. Akayafikicha macho yake na kisha kuuangalia vizuri ujumbe ule, ulikuwa ni ujumbe ambao ulitoka kwa Rose. Bila kuchelewa, bila kuuliza kwamba ilikuwaje, akaujibu.
Siku hiyo ndio ambayo Joshua akafanya mapenzi na msichana Rose na kisha kuziruhusu mbegu zake kuingia katika mfuko wa uzazi wa Rose na hatimae kuanza kutengeneza kijusi.
Peter akaliegesha gari lake nje ya geti la kuingilia katika kambi ya kijeshi ya Lugalo. Kwa kuwa alikuwa ni mtoto wa mwanajeshi, akatoa kitambulisho chake na kisha kumuonyeshea mwanajeshi ambaye alimtaka kufanya hivyo na kisha kuruhusiwa. Akaliendesha gari lake mpaka katika sehemu ya maegesho na kisha kuteremka.
Kichwa chake kilikuwa kwenye mawazo mengi, hakuamini kwamba Bwana Shedrack hakuwa amemwambia Rose kile ambacho alikuwa ameambiwa na baba yake, Bwana Edward. Kitu ambacho alikijua ni kwamba kila kitu kingekuwa chepesi kwake, yaani kamakumsukuma mlevi katika mteremko wa mlima kumbe hali ilikuwa tofauti kabisa.
“Nipo hapa sehemu ya kuegeshea magari” Peter alimwambia Bwana Shedrack.
“Sawa. Nakuja” Bwana Shedrack alimwambia Peter simuni.
Peter akabaki akiwa amesimama ndani ya eneo lile huku akiwa ameegemea gari lake. Baada ya dakika tano, Bwana Shedrack akatokea mahali hapo na kisha kumsalimia.
“Naona mambo hayaendi vizuri mzee” Peter alimwambia Bwana Shedrack baada ya kuongea maongezi machache.
“Kivipi?”
“Kuhusu Rose”
“Amefanya nini tena?”
“Nimetoka kwako hapa na nimeongea nae” Peter alimwambia bwana Shedrack.
“Kasemaje?” Bwana Shedrack aliuliza huku akionekana kuwa na furaha.
“Kanikataa”
“Kakukataaa! Kivipi?”
“Sijui. Yaani inaonekana kwamba haujamwambia kitu chochote kile” Peter alisema kinyonge.
“Hapana. Nilimwambia. Tena nilimwambia kila kitu” Bwana Shedrack alimwambia peter.
“Basi ndio hivyo. Kanikataa” Peter alimwambia Bwana Shedrack.
Bwana Shedrack akaonekana kuchanganyikiwa, hakuamini kile ambacho Peter alikuwa amekisema ndicho ambacho kilikuwa kimetokea. Moyoni mwake alikuwa na uhakika kwamba kwa jinsi alivyokuwa ameongea na binti yake, Rose mpaka kwa wakati huo kila kitu kingekuwa safi yaani ingebakia kitendo cha Peter kuja na kuongea maneno machache ya kumalizia.
Bwana Shedrack hakutaka kuendelea kuongea na Peter, alichokifanya ni kuondoka mahali hapo, akaingia ndani ya gari na kuelekea nyumbani kwake. Ndani ya gari, hasira zake zilikuwa juu ya Rose tu. Ni kweli alijua kwamba hakutakiwa kumlazimisha binti yake katika kupanga maamuzi ya maisha yake lakini katika suala kama hilo, suala la kuufanya ukaribu wake na Bwana Edward kuzidi kushamili, aliona ana kila sababu ya kumlazimisha Rose kukubaliana nae hata kama alikuwa akifanya makosa.
“Hawa watoto wengine bwana, wanataka kuniaibisha mtu mzima” Bwana Shedrack alijisemea huku akionekana kuwa na hasira.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Njia nzima Bwana Shedrack alionekana kuwa na mawazo mengi, kichwa chake kilikuwa kikimuuma sana kwa ajili ya kumfikiria binti yake ambaye alikuwa amemkataa Peter. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kukifanya kwa wakati huo, hakujua ni hatua gani madhubuti ambazo alitakiwa kuzichukua mara atakapofika nyumbani.
Alipofika nyumbani, akaliegesha gari na kisha kuingia ndani. Siku hiyo Bwana Shedrack alionekana kubadilika sana, alionekana kuwa mwingi wa hasira kupita kawaida. Alipofika ndani, macho yake yakatua kwa John ambaye alikuwa akiangalia televisheni sebuleni.
“Shikamoo baba” Joh alimsalimia.
“Dada yako yupo wapi?” Bwana Shedrack aliuliza huku akionekana kuwa na hasira.
“Yupo chumbani kwake” John alijibu huku akionekana kuwa na wasiwasi.
Bwana Shedrack hakutaka kuongea kitu kingine chochote kile, alichokifanya ni kuanza kuelekea ukumbini na alipoufikia mlango wa chumba cha Rose akaanza kuugonga. Alisimama na kuugonga kwa muda mrefu lakini haukufunguliwa wala kusikia sauti ya mtu yeyote ndani jambo ambalo lilimfanya kuingia ndani, alipoingia, hakukuwa na mtu yeyote yule.
Bwana Shedrack hakuishia hapo, akaanza kwenda katika kila sehemu, akaelekea jikoni, akaelekea mpaka stoo, bafuni na chooni huko kota Rose hakuonekana. Hapo ndipo ambapo akaonekana kuwa na wasiwasi, akaelekea nje ya nyumba hiyo upande wa nyuma, alipoangalia geti, lilikuwa halijafungwa vizuri kitu ambacho alijua fika kwamba Rose alikuwa ametoka nje kupitia geti la nyuma, na kama alikuwa ametumia geti hilo ina maanisha kwamba hakutaka kuonekana na John. Alichokifanya akaanza kulifuata geti lile, alipotaka kulifunga tu, Rose akalifungua kutokea nje na kukutana uso kwa uso.
****
Mawazo ya Irene yalikuwa yakimfikiria Rose ambaye alikuwa amemuacha nyumbani, tayari aliona dhahiri kwamba uhusiano wake wa kimapenzi pamoja na Rose ulikuwa ukienda kuharibika muda si mrefu. Maneno ya Rose kwamba alikuwa akijisikia raha zaidi kila alipotumia uume wa bandia ndio ilikuwa kauli ambayo ilimtia sana wasiwasi.
Alijua fika kwamba kama asingefanya kazi ya zaidi basi alikuwa akienda kumpoteza Rose ambaye kwake alionekana kuwa msichana muhimu kwa sababu tu alimkuta bikira na hivyo hakutaka kumuachia. Uume wake wa bandia ambao alikuwa amemuachia alijua fika kwamba ule ndiio ambao ungeleta kizaazaa hapo baadae.
Kuna wakati mwingine alitamani sana kurudi nyumbani na kuuchukua uume ule lakini kila alipotaka kufanya hivyo,. Akapuuzia kwa kuona kwamba hakukuwa na umuhimu wowote ule. Hakujua, hakujua kwamba kile kitu ambacho alikuwa akikifikiria ndicho ambacho kilikuwa kikiendelea kufanya kazi akilini mwa Rose. Katika kipindi hicho, alikuwa na kiu ya kufanya mapenzi na mwanaume yeyote yule.
Siku ziliendelea kukatika mpaka siku ambayo alipokea simu na kupewa taarifa kwamba Rose alikuwa njiani kufunga ndoa na kijana Peter. Kwanza akashtuka, taarifa zile zilionekana kumshtua kupita kawaida. Ilikuwaje Rose aamue moja kwa moja kwamba anafunga ndoa pasipo kumtaarifu, Irene akaonekana kuchanganyikiwa sana.
Moyoni akashikwa na kimuemue cha kutaka kufahamu sababu ambayo ilimfanya Rose kukubali kufunga ndoa kirahisi bila kumfahamisha, akagundua kwamba kulikuwa na uwezekano wa Bwana Shedrack kumlazimisha kufunga ndoa ile. Irene haukutaka kuvumilia kubaki chuoni, alijiona kuwa na uhitaji wa kuonana na msichana huyo ambaye kila siku alikuwa akimuita mke wake na kuzungumza nae.
Ila kabla hajaamua kuelekea nyumbani huko, akachukua simu yake na kisha kuanza kumpigia Rose. Kwanza alitaka kufahamu kila kitu, sababu ambayo Rose aliamua kutaka kufunga ndoa na Peter na wakati alijua fika kwamba yeye alikuwepo kwa ajili yake. Simu ikaanza kuita, iliita kwa muda fulani na kisha kukatika. Irene hakutaka kuacha, akapiga tena, simu ikaanza kuita tena na hatimae kupokelewa.
“Ndio umefanya nini sasa?” Irene aliuliza bila hata kujua ni mtu gani alikuwa akiongea.
“Nakuuliza wewe. Ndio umefanya nini tena mpenzi. Yaani mahaba yote ambayo nilikupa kitandani, yaani kuyacheza matiti yako yote mpaka mtoto wa kike kulegea kitandani, eti leo hii unakubali kuolewa na mwanaume, au haujui kwamba mimi ndiye mwanaume wako? Au haujui kwamba mimi ndiye mtu ambaye nimekutoa bikira kwa kutumia uume wa bandia? Hivi kwa nini unaamua kunisaliti Rose? Hivi kwa nini umeamua kufanya jambo kama hili kwangu. Au mjomba kakulazimisha? Na kama alikulazimisha kwa nini usiongeondoka nyumbani ukaja japo huku hosteli ukaja tukakaa pamoja? Umenikasirisha mke wangu, mahaba yangu yameonekana kuwa si kitu” Irene aliongea kwa sauti ya hasira bila kusikia sauti ya upande wa pili.
“Umenikasirisha…umenikasirisha sana…umenisikia..halllow” Irene alisema kwa hasira na kuita baada ya kutokuisikia sauti ya Rose.
“Hallow. Endelea nakusikiliza” Sauti ya mwanaume ilisikika simuni, alikuwa Bwana Shedrack.
Irene akaonekana kushtuka, hakuamini kwamba maneno yote ambayo alikuwa akiyaongea kumbe yalikuwa yakisikika masikioni mwa Bwana Shedrack ambaye alikuwa ameipokea simu ile. Kwa haraka sana bila kupoteza muda, akakata simu na kuizima kabisa.
Mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu, hofu ikamuingia moyoni kwa kuona kwamba Bwana Shedrack alikuwa amefahamu kila kitu ambacho kilikuwa kimeendelea. Hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, kila kitu kilikuwa wazi kwa Bwana Shedrack kitu ambacho kilimfanya kujilaumu sana kwa kuongea mfululizo bila kusikiliza sauti ya upande wa pili.
“Mmmh! Nitafanya nini sasa! Mjomba anaweza hata kuniua” Irene alijisemea huku akionekana kuwa na hofu kubwa.
Kwa wakati huo, kila kitu kikaonekana kuwa wazi, Bwana Shedrack akaonekana kufahamu kila kitu ambacho kilikuwa kikitokea chumbani katika kipindi ambacho Irene alikuwa akielekea katika nyumba ile. Irene hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, kitendo cha mjomba wake kufahamu kila kitu kikaonekana kumtia hofu kupita kawaida.
****
Rose alibaki akiwa amepigwa na mshtuko mkubwa, hakuamini kama baba yake ndiye ambaye alisimama mbele ya geti lile. Alikuwa akimwangalia huku akitetemeka kupita kawaida. Hofu kubwa ikaingia moyoni mwake, uso wa baba yake ukaonekana kuwa kwenye hasira kubwa kupita kawaida.
Rose akaihisi miguu yake ikitetemeka sana, alitamanai kurudi kule alipotoka lakini akajikuta akikosa nguvu kabisa za kurudi.
Bwana Shedrack alikuwa akitetemeka kwa hasira, kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka kwa wakati huo, macho yake yakaanza kupata wekundu fulani, hakuamini kama kweli Rose alikuwa ametoka nje ya nyumba ile bila ruhusa yake. Kichwani mwake kwa wakati huo, akili yake ikaanza kumwambia kwamba ile ndio ilikuwa tabia yake kwamba kila siku anaondoka nyumbani hapo na kwenda nje ya nyumba ile.
Hata kabla Rose hajajua ni nini cha kufanya, akashtukia akishikwa mkono na kuvutwa ndani. Bwana Shedrack alionekana kuwa mwingi wa hasira, kitendo cha Rose kutoka nje ya nyumba ile kilionekana kumkasirisha kupita kawaida. Huku akimvuta kuelekea ndani, alikuwa akiuvua mkanda wake, alipomfikisha sebuleni, akamtusukumia kwenye kochi.
Kabla ya kuchapwa mikanda, Rose alikuwa akilia kupita kawaida, kwake, tayari aliona kuwa kipindi hicho kilikuwa kipindi cha hatari kwake. Hasira ambazo alikuwa nazo baba yake zilionekana kuwa hasira kubwa ambazo zisingeweza kupoa hata mara moja.
Kabla ya kuanza kumchapa, Bwana Shedrack akalisogelea kochi moja na kukaa, alikuwa akihema kwa nguvu kana kwamba alikuwa ametoka kukimbia mbio ndefu. Hakutaka kumchapa Rose katika hali ya hasira ambayo alikuwa nayo katika kipindi hicho kwa kuona kwamba angeweza kumuua, alisubiria kwanza hasira zake zipungue.
“Naomba unisamehe baba” Rose alimuomba msamaha baba yake huku akianza kutembea kwa magoti na kulia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Umetoka wapi?” Lilikuwa swali la kwanza kutoka kinywani mwa Bwana Shedrack.
“Nimetoka kutembea” Rose alijibu huku akitetemeka.
“Wapi?”
“Nje” Rose alijibu.
“Sawa. Nipe simu yako” Bwana Shedrack alimwambia Rose.
Rose akashtuka kupita kawaida, hakutarajia kuambiwa maneno kama yale. Meseji zote ambazo alikuwa akitumiwa na wanaume wengine zilikuwa katika simu yake na wala hakuwa amezifuta. Akazidi kutetemeka, hakujua kama alitakiwa kumpa simu baba yake au la.
“Nipe simu yako” Bwana Shedrack alimwambia Rose kwa mara ya pili.
Rose hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kuchukua simu yake na kisha kumpa baba yake huku akitetemeka kupita kawaida. Bwana Shedrack akaichukua simu ile na kisha kuanza kuangalia angalia. Alifungua kila sehemu, akasoma meseji zote ila meseji za mwisho ambazo zilitumwa siku hiyo kwenda kwa Joshua zikamfanya kufahamu kila kitu.
“Umetoka kufanya mapenzi” Bwana Shedrack alimwambia Rose kwa hasira.
“Sijafanya baba”
“Umetoka kufanya mapenzi mpuuzi wewe. Nilikwishakwambia, nitakuua” Bwana Shedrack alimwambia Rose.
Siku hiyo hakutaka kumwadhibu, alijua fika kwamba kama angemuadhibu basi asingeweza kufanikisha kumshawishi juu ya suala la kuolewa na Peter ambaye alikuwa tayari kwa moyo mmoja kumuoa Rose.
“Naomba utulie Rose. Wewe ni binti yangu ambaye ninakupenda sana, tulia binti yangu. Kila kitu katika dunia hii kinapita. Wanaume wapo na wataendelea kuwepo” Bwana Shedrack alimwambia Rose.
Kwanza Rose hakuamini, hakuamini kama baba yake ndiye ambaye aliongea maneno yale mara baada ya kuonekana kuwa na hasira katika kipindi kichache kilichopita. Bwana Shedrack akasimama na kisha kumuinua Rose na kumkumbatia kitendo ambacho kilimshangaza mpaka John aliyekuwa pembeni.
“Badilika binti yangu. Mapenzi yapo tu” Bwana Shedrack alimwambia Rose.
“Nimebadilika baba. Nisamehe baba” Rose alimwambia baba yake.
Kuanzia siku hiyo Bwana Shedrack akajifanya kuwa na upendo wa dhati kwa Rose, hakutaka kumfokea kwa kitu chochote kile, kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo ni kuitengeneza akili ya Rose na hatimae mwisho wa siku aje kukubali kuoana na Peter.
Kitu alichokifanya Bwana Shedrack ni kuchukua simu ya Rose na kisha kukaa nayo.Kila simu ambayo ilikuwa ikipigwa, alikuwa akiangalia kioo, alipoona kwamba ilikuwa namba ngeni, alikuwa akiachana nayo.
Maisha yaliendelea zaidi na zaidi mpaka kufikia siku ambayo Bwana Shedrack akaamua kumwambia Rose ukweli juu ya Peter ambaye alikuwa akimpenda sana na alikuwa tayari kumuoa na kuishi kama mume na mke.
“Sitaki kuolewa baba” Rose alimwambia baba yake.
“Kwa nini tena binti yangu mzuri?” Bwana Shedrack aliuliza.
“Nitakutia aibu”
“Kivipi? Una mimba?”
“Hapana”
“Sasa kivipi?”
“Simpendi Peter” Rose alijibu.
“Hapana. Unajua mapenzi si lazima mtu umpende siku hiyo hiyo, wakati mwingine unaweza kupita muda mrefu, halafu baadae ukaja kumpenda kwa dhati” Bwana Shedrack alimwambia Rose.
Kila siku Bwana Shedrack alikuwa mtu wa kubembeleza mpaka pale ambapo Rose akakubaliana nae. Kwanza kitu cha kwanza akawasiliana na Peter na kisha kumueleza kila kitu. Peter hakuonekana kuamini.
“Amekubali?”
“Ndio. Mimi ndiye mzazi, yeye ni mbegu yangu, kwa nini akatae”
“Nashukuru sana mzee. Kwa hiyo lini tuanze mipango ya harusi?”
“Siku yoyote ila kwanza njoo uonane nae” Bwana Shedrack alimwambia Peter.
Siku iliyofuata Peter akafika mahali hapo na kisha kuanza kuongea na Rose. Japokuwa Rose hakuwa akimpenda Peter, hakuwa na jinsi, akauruhusu moyo wake kumuingiza Peter ila wasiwasi wake ulikuwa sehemu moja tu, juu ya ujauzito aliokuwa nao.
“Huyu huyu nitambambikia” Rose alijisemea.
Kwa kuwa aliamini kwamba Peter alikuwa akimpenda, akataka kufanya nae mapenzi, Peter hakuwa na kizuizi, hakujua Rose alikuwa ametega nini. Peter akafanya mapenzi na Rose, mbegu zake zikaingia ila hazikuweza kufanya chochote kile.
“Mbona unahuzunika tena?”
“Leo ni siku yangu ya kupata mimba” Rose alimwambia Peter huku akijifanya kulia.
“Mungu wangu!”
“Ndio hivyo”
“Ila hakuna tatizo. Nitakuoa, tutamlea mtoto wetu pamoja” Peter alimwambia Rose.
Lengo la Rose likaonekana kukubalika, tayari aliona kwamba alikuwa amempatia sana Peter kwa kumuweka tayari kulea mtoto ambaye hakuwa damu yake. Kwa Peter ikaonekana kuwa kawaida, muda wote alikuwa tayari kulea mtoto hasa kwa Rose ambaye alikuwa akimpenda sana.
Mara baada ya kumaliza kila kitu wakatoka chumbani na kisha kuanza kumpeleka Rose nyumbani kwao kwa kutumia usafiri wake. Hawakuchukua muda mrefu, wakafika nyumbani hapo, Rose akateremka na kisha kuanza kuelekea ndani huku akiwa na furaha ya kukamilisha kile alichotaka kukikamilisha. Alipoufikia mlango wa sebuleni, akaufungua, macho yake yakatua usoni mwa baba yake ambaye alionekana kuwa na hasira.
“Kuna nini tena baba?” Rose aliuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Irene……!” Bwana Shedrack alisema huku akiobnekana kuvimba kwa hasira na kuiweka simu ya Rose mezani kitendo ambacho kilimshtua sana Rose.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bwana Shedrack akajiona kumaliza kila kitu, kitendo cha yeye kuchukua simu ya Rose na kisha kuanza kukaa nae aliona kwamba hiyo ingempa unafuu kutokana na tabia ambayo alijua kwamba Rose alikuwa ameianza, tabia ya kutoka nje ya nyumba na kisha kuonana na wanaume. Simu akawa nayo yeye, kila meseji ambayo ilikuwa ikitumwa, alikuwa akizipuuzia kwa sababu zilikuwa zikitoka katika namba ngeni kabisa.
Katika kipindi hicho ndicho ambacho alikuja kugundua kwamba binti yake alikuwa mwaminifu sana na hakuwa na habari na mwanaume yeyote yule. Malalamiko ya wanaume ambao walikuwa wamekataliwa yakamfanya kufurahia sana kwa kuona kwamba binti yake hakuwa mtu wa kupenda wanaume kama ambavyo alifikiria kabla.
“Huyu ndiye binti anayetakiwa kuishi nami kama mwanangu. Ila huyu mtu…huyu…Mhh! Sijui” Bwana Shedrack alikuwa akijiseme katika kila kipindi ambacho alikuwa akiangalia meseji ambazo zilikuwa zikitumwa katika simu ya Rose.
Kuna mtu mmoja tu ambaye alikuwa akimhofia sana juu ya binti yake, mtu huyu kila wakati alikuwa akituma meseji za mapenzi, meseji ambazo alikuwa akizituma yeye hazikuwa za kulalamika au za kumtaka Rose kimapenzi bali meseji ambazo alikuwa akizituma yeye ni zile ambazo zilionyesha kwamba walikuwa kwenye mahusiano kwa kipindi fulani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bwana Shedrack akashikwa wasiwasi sana na mtu huyu kwa kuona kwamba angeweza kuleta mambo fulani hapo baadae. Kila alipokuwa akiliangalia jina la mtu huyo, Joshua, moyoni mwake alikuwa akikosa amani na kukereka sana.Tayari alikuwa amekwishaanza kuhisi kitu lakini kutokana na ukaribu ambao alikuwa ameuweka kwa binti yake pamoja na kumbana kupita kawaida, aliona kila dalili kwamba mwanaume huyo asingeweza kupata nafasi.
Bwana Shedrack hakutaka kubaki hivi hivi tu bila kufanya chochote kile, alichokifanya ni kuhakikisha kwamba Peter anapata nafasi kubwa zaidi ya kuwa na binti yake. Mara kwa mara Peter alikuwa akifika ndani ya nyumba hiyo, alikuwa akiongea sana na Rose na mwisho wa siku kuwa wapenzi ambao walitegemea kuoana na kuwa mume na mke.
Hiyo ndio ikaonekana kuwa furaha kwa Bwana Shedrack, kile ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo kikaonekana kukamilika bila matatizo yoyote yale. Kitendo cha Peter kuanza mahusiano na binti yake kikaonekana kumpa amani. Japokuwa kila kitu kilikuwa kimekamilika lakini hakutaka kumrudishia simu ile kwa kuona kwamba Joshua, mwanaume ambaye alikuwa akituma sana meseji za kimapenzi angeweza kuharibu kila kitu.
Kila siku alikuwa na simu ya Rose chumbani kwake, hakutaka kuiacha mbali, alikuwa akikaa nayo karibu huku muda mwingi akizisoma meseji ambazo walikuwa wakizituma wanaume mbalimbali ambazo kwake zikaonekana kuwa kama kichekesho vile.
“Binti yangu hamuwezi kumpata kirahisi” Bwana Shedrack alikuwa akijisemea huku akiwa amekenua meno yake.
“Yule ni mtoto wa mwanajeshi, ana kila ulinzi mahali hapa. Ila huyu Joshua nae ananichanganya sana. Hivi hizi meseji zake mbona zipo tofauti na wengine? Yaani yeye anaziandika kimapenzi zaidi, au kashamchukua binti yangu? Hapana. Hebu ngoja nichunguze” Bwana Shedrack alikuwa akijisemea kila alipokuwa akiziangalia meseji ambazo Joshua alikuwa akiendelea kuzituma ndani ya namba ile.
Siku zikakatika kama kawaida mpaka siku ambayo aliisikia simu ya Rose ikianza kuita. Alichokifanya, kama kawaida yake akaichukua simu ile na kisha kuangalia jina la mpigaji, haikuwa namba ngeni, ilikuwa ni simu kutoka kwa Irene huku namba ikiwa imehifadhiwa kama ‘My Hubby Irene’.
Kwanza Bwana Shedrack akashtuka kidogo, namna ya jina lile lilivyokuwa limehifadhiwa ndani ya simu ile likaonekana kumtia wasiwasi kupita kawaida. Hakutaka kujipa sana presha kwani alikwishasikia kwamba wanawake huwa wanayahidhi majina ya wanawake wenzao kwa namna ambayo mwanaume hawezi kutumia kulihifadhi jina la mwanaume mwenzako. Akakibonyeza kitufe cha kijani na kisha kuipeleka simu sikioni.
“Ndio umefanya nini sasa?” Sauti ya Irene ilisikika simuni na kuendelea huku Bwana Shedrack akibaki kimya.
“Nakuuliza wewe. Ndio umefanya nini tena mpenzi. Yaani mahaba yote ambayo nilikupa kitandani, yaani kuyacheza matiti yako yote mpaka mtoto wa kike kulegea kitandani, eti leo hii unakubali kuolewa na mwanaume, au haujui kwamba mimi ndiye mwanaume wako? Au haujui kwamba mimi ndiye mtu ambaye nimekutoa bikira kwa kutumia uume wa bandia? Hivi kwa nini unaamua kunisaliti Rose? Hivi kwa nini umeamua kufanya jambo kama hili kwangu. Au mjomba kakulazimisha? Na kama alikulazimisha kwa nini usiongeondoka nyumbani ukaja japo huku hosteli ukaja tukakaa pamoja? Umenikasirisha mke wangu, mahaba yangu yameonekana kuwa si kitu” Irene aliongea kwa sauti ya hasira huku Bwana Shedrack akiwa kimya akimsikiliza tu bila kuongea chochote kile.
“Umenikasirisha…umenikasirisha sana…umenisikia..halllow” Sauti ya irene iliita kwa hasira na kuita baada ya kutokuisikia sauti ya Rose.
“Hallow. Endelea nakusikiliza” Bwana Shedrack aliitikia na ghafla simu kukatwa.
Bwana Shedrack akabaki akitetemeka kwa hasira, tayari akaonekana kubadilika kupita kawaida, akakunja ngumi na kisha kuupiga ukuta kwa hasira. Maneno ambayo alikuwa ameyasikia kutoka kwa Irene yakaonekana kumkasirisha kupita kawaida. Akaanza kuliangalia tena jina la Irene, akapata jibu ya namna ambavyo jina lile lilikuwa limehifadhiwa ndani ya simu ile.
Mwili ulikuwa ukitetemeka kwa hasira, kijasho chembamba kikaanza kumtoka huku akiwa amekunja ndita kwa hasira. Hakutaka kubaki chumbani, alichokifanya ni kutoka na kuelekea sebuleni. Furaha yote ambayo alikuwa nayo ikawa imemtoka, hakuamini kama msichana Irene ambaye alikuwa amemleta ndani ya nyumba yake alikuwa msagaji na ambaye alikuwa akimsaga binti yake, Rose.
“Haiwezekani. Irene msagaji!” Bwana Shedrack alikuwa akijisemea kwa hasira.
Kila kitu ambacho alikuwa akijiuliza mahali hapo alikosa jibu kabisa, hakuamini kama kweli Irene alikuwa msagaji. Huku akiwajifikiria jambo hilo, akapata jibu juu ya hali ya mapokezi makubwa ambayo Rose alimpokea Irene katika kipindi ambacho alikuwa amefika nyumbani hapo kwa mara ya pili mara baada ya kutoka chuo, hakuishia hapo tu bali akapata jibu juu ya sababu iliyowafanya wawili hao kuchukua muda mrefu kujifungia chumbani.
“Nitaua mtu” Bwana Shedrack alijisema.
Wala hazikupita dakika nyingi, akasikia muungurumo wa gari kutoka nje, akasimama na kisha kuchungulia, lilikuwa gari la Peter na kisha Irene kuteremka. Bwana Shedrack akajikuta akishikwa na hasira zaidi, hata Rose alipoingia ndani ya nyumba hiyo, bado hasira zake zilionekana kuwa waziwazi.
“Kuna nini tena baba?” Rose aliuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Irene……!” Bwana Shedrack alisema huku akionekana kuvimba kwa hasira na kuiweka simu ya Rose mezani kitendo ambacho kilimshtua sana Rose.
Alipoiweka simu ile mezani, kwa haraka sana akamwangalia Rose machoni ili kuona angeonyesha hali gani. Alipomuona Rose ameshtuka, akajua kwamba kile ambacho alikuwa kikihisi kilikuwa chenyewe, hakuwa amebahatisha. Rose akabaki kimya, kwa mbali akaonekana kutetemeka kupita kawaida, alitamani kuichukua simu ile na kisha kuondoka nayo lakini akajikuta akikosa nguvu, akajiweka kochini.
“Niambie kuhusu mahusiano yako na Irene” Bwana Shedrack alimuuliza Rose.
“Ni ndugu yangu” Rose alijibu.
“Usitake kunikasirisha. Niambie mahusiano yako na Irene” Bwana Shedrack aliuliza kwa hasira huku akionekana kuanza kubadilika.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rose hakujibu kitu, hakuwa tayari kumwambia baba yake kwamba Irene alikuwa msichana ambaye alikuwa akimsaga kila siku chumbani, hakuwa radhi kumwambia kwamba Irene alionekana kuwa kama mume wake wa ndoa kutokana na kufanya mambo mengi ambayo wanandoa hufanya chumbani.
“Umeanza lini usagaji?” Bwana Shedrack alimuuliza Irene.
“Nisamehe baba”
“Hilo si jibu ninalolitaka. Nimekuuliza umeanza lini usagaji? Sijauliza kuhusu msamaha hapa” Bwana Shedrack alimuuliza Rose huku akionekana kukasirika kupita kawaida.
“Irene alikuwa akinilazimisha”
“Alikuwa akikulazimisha! Kukulazimisha kivipi na wakati inaonyesha kabisa kwamba nyie ni wapenzi, tena wapenzi waliokubuhu” Bwana Shedrack alimuuliza Rose.
“Nisamehe baba” Rose alisema huku akianza kuomba msamaha.
“Yaani mwanajeshi mimi shupavu eti leo nimezaa mtoto msagaji, yaani hii skendo hata wanajeshi wenzangu wakisikia, watanishangaa sana” Bwana Shedrack alimwambia Rose.
Rose akaanza kulia, moyo wake ukaanza kuumia hasa mara baada ya kuona kwamba hata baba yake alikuwa amekwishajua kwamba alikuwa msagaji. Akaendelea kuomba msamaha zaidi na zaidi lakini Bwan Shedrack hakutaka kuelewa kabisa, katika kipindi hicho, alikuwa akijitahidi kuzungumza maneno mengi ambayo aliamini kwamba yangemchoma Rose moyoni.
“Yaani unataka kuniambia kwamba vidole vya msichana mwenzako vinakuridhisha, yaani unataka kuniambia kwamba unachukua muda wako kuunyonya mdomo wa msichana mwenzako! Hivi hauoni kwamba huo ni uchafu, hivi hauoni kufanya mapenzi na mwanamke mwenzako ni uchafu, uchafu uliokithiri, uchafu ambao hata Mungu haupendi kabisa. Hivi mna tofauti gani na mashoga, hivi mnatofauti gani na wale watu wa jinsia moja ambao wanakwenda kanisani na kutaka kufunga ndoa ya jinsi moja? Nisikilize Rose, sikuwa nikikufungia ndani ili uwe msagaji, nilikuwa nakufungia ndani kwa sababu nilitaka uwe binti mzuri zaidi ya ulivyokuwa. Hiyo ndio ilikuwa maana yangu kubwa. Badala ya kuwa binti mzuri zaidi, umekuwa zaidi ya binti mbaya, sasa kazi yote ambayo nilikuwa nikiifanya ikaonekana kuwa ni bure kabisa. Yaani ni bora, ni bora ungefanya mapenzi na wanaume wote wanaokutaka hapa Magomeni kuliko kufanya mapenzi na msichana mwenzako. Acha nikwambie Rose, sitaki kuyafuatilia maisha yako, sitaki kumwambia mtu yeyote juu ya uchafu wako, nakuachia wewe na mume wako mtarajiwa. Akijia kufahamu, mtajijua kivyenu. Kwa huyu mshenzi mwenzako, nitamuua, nakwamba kwamba NITAMUUA. Haijalishi atakimbia nchini Tanzania au la…NITAMUUA” Bwana Shedrack alimwambia Rose, akachukua simu ile aliyoiweka mezani na kisha kuondoka mahali hapo.
Rose akabaki akilia tu, hakuamini kama baba yake, Bwana Joshua alikuwa amefahamu kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea. Hakunyamaza, aliendelea kulia zaidi na zaidi. Kuanzia siku hiyo, akawa tu wa kulia kila siku, moyo wake ukapoteza furaha, kila alipokuwa akimwangalia baba yake, alikuwa akijisikia aibu, moyo ulikuwa ukimsuta kupita kawaida.
Siku zikaendelea kukatika kama kawaida. Rose hakutakiwa kutoka nje ya nyumba hiyo, hata katika kipindi ambacho Peter alikuwa akifika mahali hapo kwa ajili ya kumchukua Rose, alikuwa akizuiliwa. Lengo kubwa ambalo alikuwa amelipanga Bwana Shedrack ni kumuua Irene ambaye kwake alionekana kuwa msichana mmoja mbaya ambaye hakutakiwa kuishi katika dunia hii.
Alihofia kwamba kama angeruhusu Rose kutoka nje ya nyumba hiyo, basi angeweza kutumia simu kumtaarifu Irene juu ya uamuzi ambao alikuwa ameupanga baba yake juu yake. Hata Peter alipokuwa akifika mahali hapo, alikuwa akiongea na Rose huku Bwana Shedrack akiwa pembeni yake.
Baada ya kipindi fulani, hali ya Rose ikaanza kubadilika, akaanza kujisikia uchovu, muda mwingi akawa akitamani kulala na kilipofika kipindi fulani kuanza kutapika. Dalili zote za mwanamke mjauzito zikaanza kuonekana mwilini mwake. Hali hiyo haikujificha, John akamwambia baba yake, Bwana Shedrack ambaye akaamua kumuita Rose.
“Una mimba?” Bwan Shedrack alimuuliza Rose.
“Ndio”
“Ya nani?”
“Ya Peter.
“Safi sana. Bora muoane tu”
Mimba ile ikaonekana kuwa sababu, mipango ya harusi ikaendelea kuchangwa kwa kasi, watu wakazidi kupewa taarifa juu ya harusi hiyo kiasi ambacho kilionekana kuwafurahisha wazazi wa pande zote mbili.
Bado dukuduku la kutaka kumuua Irene lilikuwa likiendelea moyoni mwake, kila alipokuwa akimwangalia Rose mawazo yake yalikuwa yakimfikiria Irene ambaye alionekana kumharibu mtoto wake. Siku ambayo aliipanga kuwa siku maalumu ya kumuua Irene ikawadia, alichokuwa amekiamua ni kumfuata Irene usiku na kisha kumuua katika kifo ambacho kingetangazwa kufanyika katika mazingira ya kutatanisha.
Rose akaonekana kuhisi kitu, siku hiyo baba yake akaonekana kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa, toka alipokuwa amerudi kutoka kazini, hakuonekana kama alikuwa wa kawaida kama siku nyingine, kila alipokuwa akimwangalia, aligundua kwamba kulikuwa na kitu.
Ilipofika saa mbili kasoro usiku, Bwana Shedrack akaondoka mahali hapo huku bunduki yake ikiwa kiunoni. Macho ya Rose yalipotua katika bunduki ile iliyokuwa kiunoni, hakutaka kujiuliza, tayari alijua kwamba baba yake, Bwana Shedrack alikuwa akiondoka kuelekea katika hosteli aliyokuwa akiishi Irene kwa lengo la kumuua.
“Leo ndio siku yake” Bwana Shedrack alijisemea huku akiingia ndani ya gari huku akionekana kuwa na hasira na kisha kuondoka mahali hapo huku akimuacha Rose akiwa hajui afanye nini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rose akaonekana kama kuchanganyikiwa, tayari hali ya hatari ikaonekana mbele yake, alijua fika kwamba baba yake alikuwa akielekea katika hostel ya Irene kwa ajili ya kumuua msichana huyo. Kwake, hakutaka kuona jambo hilo likitokea, hakutaka kumuona Irene akiuawa na baba yake, kitu ambacho alikifikiria kwa wakati huo ni kumpigia simu Irene na kumtaarifu juu ya ujio wa baba yake.
Simu angetoa wapi kwa wakati huo? Kutoka nje na kwenda kutafuta simu kwa watu wengine likaonekana kuwa jambo gumu kufanyika kwa wakati huo, angefanya nini? Kila alichokuwa akikifikiria, alikosa jibu kabisa. Rose akabaki kimya huku kichwa chake kikionekana kuwa na mawazo lukuki, alichokifikiria ambacho kilikuja kwa haraka sana kichwani kwake ni kuelekea chumbani kwa baba yake kwa ajili ya kuchukua simu yake na kisha kumpigia Irene na kumpa taarifa.
Kwa mwendo wa haraka haraka akaanza kukifuata chumba kile, alipokifikia, akakishika kitasa na kisha kujaribu kuufungua mlango, mlango ulikuwa umefungwa kwa ufunguo. Mpaka kufikia hatua hiyo Rose hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, akarudi sebuleni na kukaa kochini.
Muda bado ulikuwa ukiendelea kusogea mbele na alitakiwa kufanya jambo lile kwa haraka sana kwani kama angechelewa basi Irene angeweza kuuawa na baba yake. Rose alibaki kwa muda wa dakika kadhaa, mara akasimama kama mtu ambaye alikuwa amepata wazo jipya juu ya kitu ambacho alitakiwa kukifanya kwa wakati huo.
Kwa haraka haraka akaelekea chumbani kwake na kisha kuanza kuangalia darini. Kumbukumbu ilikuwa imejia kwamba ndani ya chumba cha baba yake, juu kulikuwa na mlango wa kuingilia darini, hivyo alitakiwa kuingia ndani ya chumba kile kwa kupitia mlango wa dari. Angeanzia wapi? Japokuwa nyumba ilikuwa yao na alikuwa ameizoea sana lakini katika kipindi hicho akaona bora kuanza kutafuta mlango mwingine wa dari.
Alipotoka chumbani kwake, kwa haraka sana akaelekea katika chumba cha John ili kuangalia kama kulikuwa na mlango wa dari, huko haukuwepo. Rose akaonekana kuchanganyikiwa kupita kawaida, muda mwingi alikuwa akiangalia saa yake ya mkononi, aliuona muda ukienda sana.
Alizunguka katika vyumba vingi vya ndani ya nyumba hiyo, hakukuwa na mlango mwingine wa dari. Huku akionekana kkata tamaa, akaonekana kukumbuka kitu, akagundua kwamba kulikuwa na chumba ambacho kilikuwa na mlango wa dari, chumba hicho kilikuwa stoo.
Bila kupoteza hata dakika moja akatoka mbio mpaka katika chumba kile, kila alipotaka kuufungua mlango ule, mlango ulikuwa umefungwa jambo ambalo lilimfanya kuanza kuzitafuta funguo katika droo za makabati yaliyokuwa pale jikoni, hakuziona funguo hizo. Akakishika tena kitasa cha mlango ule na kuanza kukitekenya, aliona kulikuwa na kila sababu ya kuuvunja mlango ule.
“Vipi tena Rose?” John ambaye alitokea mahali hapo aliuliza huku akionekana kumshangaa.
“Funguo za mlango huu zipo wapi?” Rose aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Wewe za nini?”
“Unaniuliza za nini tena! Niambie funguo za mlango huu zipo wapi” Rose alimwambia John huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Zipo pale”
“Wapi?”
“Kwenye ile droo ndogo” John alimwambia Rose ambaye akaanza kuelekea katika droo ile.
Alipoifikia akaifungua na kisha kuanza kupekua pekua vizuri. Aliangalia kwa sekunde kadhaa, akauona funguo mbili, alichokifanya akzichukua na kisha kuufuata mlango ule na kuufungua. Mlango ukafunguka, alichokifanya ni kuanza kuelekea chumbani kwake na kisha kuchukua tochi na kurudi mahali pale.
“Kuna nini Rose?” John aliuliza huku akionekana kushangaa.
“Njoo unishikie hili gunia la mkaa nipande juu” Rose alimwambia John huku akimshika mkono na kumvuta.
“Unataka kwenda wapi?” john aliuliza.
“Darini”
“Darini! Kufanya nini tena?”
“Wewe njoo unishikie” Rose alimwambia John ambaye akamshikia gunia lile.
Tayari kijasho chembamba kikaanza kumtoka, kila kitu ambacho alikuwa akikifanya mahali hapo alikuwa akikifanya kwa haraka sana. Alipoukaribia mlango ule, akautoa mlango na kisha kuutoa na yeye kushika vizuri na kuingia darini.
Darini bado kulikuwa na joto kupita kawaida, Rose hakuonekana kujali kabisa, akaingia darini mule na kuanza kutembea mwendo wa kuchuchumaa chuchumaa mpaka katika usawa wa chumba cha baba yake na kuutoa mfuniko wa dari na kisha kurukia ndani.
Rose hakutaka kuchelewa, kwa haraka sana akaanza kulifuata kabati la baba yake na kisha kulifungua, akaiona simu yake na kisha kuichukua. Huku mikono ikitetemeka na huku akiwa na uharaka akaanza kulitafuta jina la ‘Hubby Irene’ alipoliona,a akabonyeza kitufe cha kijani na kisha kuipeleka simu sikioni.
Simu ikaanza kuita, Rose aliona kama Irene hapokei simu ile. Kwa uharaka ambao alikuwa nao mahali hapo, alitamani kumvuta Irene mahali alipokuwa na kisha kumgawia simu yake na kuongea nae. Alisubiria kwa zaidi na zaidi, simu ikapokelewa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hallow” Sauti ya Irene ilisikika ikiita.
“Irene ondoka. Irene kimbia hapo hostel” Rose alisema huku akitetemeka kwa woga.
“Kuna nini tena? Mbona unanitisha?” Irene aliuliza.
“Baba anakuja kukuua. Kimbia, toka hapo ulipokuwa” Rose alimwambia Irene ambaye akakata simu.
Hapo, Rose akajisikia kuwa na amani, alichokifanya ni kuanza kuutafuta ufunguo mwingine wa mlango ule, alipouona, akaufungua mlango na kisha kutoka ndani ya chumba kile. Moja kwa moja akaelekea chumbani kwake huku akiwa na simu yake mkononi, alipofika akachukua nguo zake na kutoka nje.
“Umepitia wapi?” lilikuwa swali kutoka kwa John.
“Usijali” Rose alisema na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea nje.
John akashindwa kuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo, alikuwa akimshangaa dada yake kwa uamuzi ule ambao aliuchukua. Mkononi alikuwa na begi na alikuwa akiondoka kuelekea sehemu ambayo yeye kama John hakuwa akiifahamu.
Rose akatoka ndani ya nyumba hiyo, begi lilikuwa mkononi mwake kwa wakati huo, alichokifanya ni kuondoka na kuelekea alipokuwa akiishi Joshua. Kitendo cha Joshua kumuona Rose akiwa amesimama mlangoni kwake huku akiwa na begi kukaonekana kumtisha, akapigwa na mshangao, hakujua sababu ambayo ilimpelekea Rose kufika mahali hapo akiwa hivyo. Alichokifanya, hakutaka kumuuliza chochote, akamkaribisha na wote kukaa kitandani.
“Kuna nini tena?” Joshua aliuliza huku akionekana kushangaa.
“Nimeondoka nyumbani mpenzi” Rose alijibu huku akianza kulia.
“Kwa nini?”
“Nimeondoka nyumbani mpenzi” Rose alimwambia Joshua.
“Najua. Kwa nini tena?”
“Sitaki kuishi pale”
“Kwa nini hutaki kuishi pale?”
“Baba ataniua”
“Mbona unanichanganya Rose. Kuna kitu gani kimetokea?”
“Naomba unielewe mpenzi. Nataka kulala hapa na kesho nitaondoka” Rose alimwambia Joshua.
“Bado unanichanganya. Unataka kuelekea wapi hasa?”
“Popote pale”
“Kama wapi?”
“Popote pale” Rose alijibu.
Katika kipindi hicho hata Joshua alionekana kuchanganyikiwa, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimemtokea Rose mpaka kuamua kile ambacho alikuwa amekiamua mahali hapo. Rose alionekana kuchanganyikiwa, alionekana kuwa kama mtu aliyakata tamaa na ambaye alichoshwa na maisha ambayo yalikuwa yametokea nyumbani kwao.
“Naomba maji ya kunywa” Rose alimwambia Joshua.
“Hapa sina maji. Ngoja nikakununulie” Joshua alimwambia Rose na kisha kuondoka chumbani hapo, akafunga mlango kwa nje na kuondoka kwenda dukani kununua maji ya kunywa. Joshua alichukua muda wa dakika kumi, akarudi huku akiwa na maji ya lita moja na kisha kumgawia Rose ambaye akayachukua na kuanza kunywa.
Muda wote huo Joshua alikuwa akimwangalia Rose usoni, hakuonekana kuwa katika hali ya kawaida kwa wakati huo, hakuonekana kama alikuwa na furaha yoyote ile, alionekana kukata tamaa, alionekana kutokuhitaji kurudi nyumbani kwao.
Kutokana na Rose kuwa kwenye hali hiyo ambayo wala haikuonekana kuwa hali salama, Joshua akamuacha alale chumbani hapo japokuwa aliamini kwamba msichana huyo hakuwa na amani kabisa. Katika kipindi hicho hakukuonekana na mtu yeyote ambaye alionekana kuwa na uhitaji wa kufanya mapenzi japokuwa hawakuwa wameonana kwa muda mrefu sana. Wote walijikuta wakiwa wamelala chali huku wakiangalia juu.
“Kuna nini kimetokea mpenzi?” Joshua alimuuliza Rose.
“Hakuna kitu”
“Baba yako amejua kwamba una mimba?”
“Ndio” Rose alitoa jibu lilimshtua Joshua.
“Amesemaje? Hiyo ndio sababu?”
“Hapana. Alikuwa ameniandalia mtu wa kunioa”
“Hiyo ndio sababu iliyokufanya ukimbie nyumbani?”
“Hapana ila nayo imechangia” Rose alijibu.
“Pole sana mpenzi” Joshua alimwambia Rose na kisha kumkumbatia.
Walijitahidi kuuvuta usingizi lakini wala haukuonekana kupatikana kwani kila mmoja alikuwa na mawazo kwa wakati huo. Ilipofika saa sita usiku, mara wakasikia vishindo vya mtu nje ya chumba kile. Kila mmoja akaonekana kushtuka, alichokifanya Joshua ni kushuka kutoka kitandani kwa ajili ya kwenda kufungua pazia ili achungulie. Hata kabla hajalifikia pazia, sauti ya Bwana Shedrack ikasikia nje ya mlango.
“Fungua mlango. Nasema fungua mlango kabla sijauvunja” Sauti ya Bwana Shedrack ilisikika kwa nje, sauti ambayo ilikuwa na hasira kupita kawaida.
Je nini kitaendelea?
Je Bwana Shedrack atafanya nini baada ya kumkuta binti yake ndani ya chumba hicho?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Je huo ndio mwisho wa kila kitu?
Je kahaba kutoka China ni nani?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment