Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

MSICHANA NDOTONI MWANGU - 2

 





    Simulizi : Msichana Ndotoni Mwangu

    Sehemu Ya Pili (2)





    KILA nilipokumbuka tukio la Monalisa la kupata ajali mbaya na kupooza mwili, tena akiwa amesafirishwa na wazazi wake kupelekwa nchini Uingereza kwa



    matibabu niliumia sana.



    Niliumia kwa sababu nilikuwa najua kila kitu kuhusu ajali yake. Mimi ndiye chanzo, jambo ambalo lilinitesa sana moyoni wangu. Mbaya zaidi ni Zamaradi



    ambaye kila wakati alinitokea usiku kwenye ndoto na kunieleza ukweli kwamba kamwe hawezi kumsamehe!



    Zamaradi alinitisha sana kunieleza kwamba hata kama alikuwa amesafirishwa kwenda nje ya nchi, ni kazi bure maana hawatafanikiwa kumtibu na kupona.



    Alinihakikishia kuwa lazima atamtoa uhai.



    Nikiwa bado sijapona maumivu hayo ambayo yalinisumbua sana, Linna naye akafanya tukio ambalo halikumfurahisha Zamaradi, akanieleza wazi wazi kuwa



    atamkomesha.

    Ilikuwa lazima nichanganyikiwe sana. Usiku huo ukawa mgumu sana kwangu, sikufanikiwa kupata usingizi hata kidogo. Niliona maluweluwe huku matukio ya



    ajabu yakizunguka kichwani mwangu juu ya Linna.



    Namfahamu vizuri sana Zamaradi, huwa haahidi uongo hata mara moja na katika siku zote za maisha yangu na yeye ya kimapenzi, hajawahi kuniahidi ahadi ya



    uongo. Hilo liliniumiza sana, nilijua lazima kuna jambo baya lilikuwa njiani kumkuta Linna.



    Nilichanganyikiwa sana, nikatamani Zamaradi anitokee tena ili niendelee kumuomba msamaha, lakini hilo halikutokea. Niliamka asubuhi nikiwa sijaonana tena



    na Zamaradi, taa za hatari zikawa zinawaka ubongoni mwangu.



    ***

    Ilikuwa Jumapili, nilipoamka sikutaka kwenda kanisani, kumbukumbu za Zamaradi zikaendelea kunitesa. Nilijihisi kama muuaji wa watu wasio na hatia. Nafsi

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    yangu ilinisuta na hakika sikutaka Linna afe kwa kosa ambalo alilifanya bila kujua.

    “Lazima nifanye kitu fulani hapa, Linna anaweza kupata matatizo,” nikawaza kichwani mwangu.



    Hata hivyo kwa hakika sikujua ni jambo gani hasa ambalo nilipaswa kulifanya kwa ajili ya kumuokoa Linna. Kichwa changu kikawa kama kimejaa mambo



    mengi ambayo yalikuwa nje ya uwezo wangu.



    “Sijajua...lakini lazima nikutane naye,” nikaendelea kuwaza kichwani mwangu.

    Nilichokifanya ni kutoa simu yangu ya mkononi na kubonyeza namba zake. Simu iliita kwa muda mfupi sana, Linna akawa amepokea, akizungumza kwa furaha



    sana.

    “Hello Phillip!”

    “Vipi Linna?”



    “Poa.”

    “Kwa nini jana ulifanya vile?”

    “Nilifanyaje?”

    “Umesahau mara hii?”

    “Ni kuhusu kukubusu?”

    “Ndiyo!”



    “Mh! Yaani mpaka leo bado unakumbuka kitu hicho hicho jamani? Basi samahani kama nitakuwa nimekuudhi, lakini halikuwa lengo langu kukuchukiza.”

    “Unachukulia rahisi sana tatizo hili.”

    “Kwa nini?”

    “Unavyoongea tu!”



    “Kwani ni jambo kubwa kiasi hicho?”

    “Sikiliza Linna, hili ni jambo kubwa, nahitaji kuongea na wewe leo jioni. Utakuwa na nafasi tukutane?”

    “Hata sasa hivi nipo tayari.”



    “Hapana, iwe jioni tafadhali, maana sina muda kwa sasa.”

    “Saa ngapi?”

    “Tukutane saa 10.00.”

    “Unapenda wapi?”

    “Udasa Bar.”

    “Poa.”



    “Usipuuze ni lazima tuongee.”

    “Hamna shida Phillip, mtanashati wa chuo, nitakuja.”

    “We’ endelea kuchukulia utani, lakini ni kwa faida yako Linna!”

    “Faida yangu?”



    “Ndiyo!”

    “Kivipi?”

    “Utajua jioni.”

    “Haya tutaonana.”



    Tukakata simu zetu nikiwa na mawazo mengi sana, lakini ukweli ni kwamba sikupenda jinsi Linna alivyochukulia utani katika mambo muhimu kwa maisha yake



    kama yale. Hata hivyo isingekuwa rahisi kumlaumu kwa sababu hakujua alichokuwa akikifanya.



    ***

    Nilifika katika Baa ya Udasa iliyokuwa ndani ya chuo chetu mapema sana. Cha ajabu wakati naingia tu, niliona gari lake limeegeshwa nje. Nikajua wazi kuwa



    alikuwa amenitangulia kufika.



    Nikampigia simu, akanielekeza mahali alipokuwa amekaa. Nikajongea taratibu na kumfuata. Alikuwa amekaa kimya akiendelea kunywa maji ya matunda.

    “Karibu Phillip,” akanikaribisha.

    “Ahsante, umefika muda mrefu?”

    “Tangu nusu saa iliyopita nilikuwa hapa. Ilikuwa lazima niwahi kabla yako.”



    “Vizuri.”

    Nilitulia kwa muda nikimwangalia na kujiridhisha kweli alikuwa mwanamke mrembo sana. Kwa hakika hakustahili kabisa kufa. Moyo wangu ukaenda mbio,



    nikashindwa kujua mahali pa kuanzia.



    Kwa jinsi ilivyoonekana, Linna alikuwa na shauku sana ya kutaka kujua nilikuwa nataka kumwambia nini. Alikuwa kimya kuliko kawaida, akionesha utayari wa



    kusikia chochote kutoka kwangu.

    Kinywa changu kilikuwa kizito kuongea, nilimwangalia kwa nukta kadhaa bila kutamka chochote. Naye alionekana kuanza kuingiwa na wasiwasi kidogo.



    “Linna, kwa nini jana ulifanya vile?” Nilimwuliza nikimwangalia usoni.

    “Samahani kwa kukuudhi, najua hukupenda lakini lazima niwe mkweli kwamba, nilifanya vile kwa hisia zangu za ndani kabisa kutoka moyoni.”

    “Hisia zipi?”



    “Phillip tambua kwamba wewe ni mwanaume mtanashati sana, hakuna mwanamke ambaye atakubali kupata nafasi ya kukaa na wewe sehemu ya peke yenu,



    akaacha kutamani angalau kupata busu lako. Ndivyo ilivyokuwa kwangu, nilitamani unibusu. Kama nilikukosea naomba unisamehe.”

    “Kwa hiyo unataka kusema kwamba unanipenda?”

    “Ndiyo!”



    “Acha kabisa Linna, mimi sitakiwi kuwa katika uhusiano wa aina hiyo kabisa.”

    “Hutakiwi kivipi, kwani wewe hunipendi?” akaniuliza.

    Lilikuwa swali gumu sana, nilichukua muda kidogo kumjibu. Ni kweli ndani ya nafsi yangu nilijihisi kumpenda sana Linna, lakini isingewezekana kutokana na



    masharti magumu ya Zamaradi.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Elewa tu hivyo.”

    “Mh!”

    “Usigune, ndiyo ukweli wenyewe ulivyo...halafu, vipi tangu hiyo jana hakuna tukio lolote lililotokea?” Nikamwuliza, lakini nikiogopa sana.

    “Tukio, unamaanisha nini?”



    “Basi, kama hakuna.”

    “Sijakuelewa Phillip, unamaanisha nini?”

    “Usijali,” nikamwambia na kubadilisha kabisa maongezi.



    Nisingeweza kuongea zaidi ya pale, maana kama baadaye angepatwa na tukio lolote, ingekuwa rahisi kulihusisha na maelezo yangu. Tukaanza kuzungumza



    mambo tofauti kabisa na yale.

    Saa tatu na dakika zake, usiku nikarudi zangu bwenini, lakini bado moyoni mwangu nilikuwa na wasiwasi mwingi. Zamaradi aliendelea kunitesa mawazoni.



    ***

    Ndani ya gari alikuwa msichana mrembo sana, akiendesha gari kwa mwendo wa kasi. Alikuwa akitumia Barabara ya Sam Nujoma akitokea Ubungo. Muziki laini



    uliendelea kumsindikiza katika safari yake huku kiyoyozi kikimpuliza!



    Alipita eneo la Mlimani City kwa kasi sana, mbele kidogo ya kituo hicho akiwa anakaribia kufika katika mzunguko zinapokutana Barabara za Ardhi na Sam



    Nujoma, akashangaa kumuona mwanamke akiwa amesimama barabarani, mikononi mwake amebeba mtoto.



    Akashtuka sana na kupunguza mwendo, akiwa anajaribu kumkwepa akashangaa yule mwanamke anabadilika, wakaonekana wanawake wengi wanaofanana na



    yule aliyemuona awali, wote walikuwa wanalia, machozi yao yakitoka damu.



    Akakata kushoto ili aingie kwenye sheli ya Bonjour, lakini cha kushangaza akiwa anajaribu kukanyaga breki, gari ndiyo likaongeza kasi, kama amekanyaga



    mafuta! Akaenda kuvaa pampu moja ya mafuta aina ya petroli.



    “Puuuuuu....” mlio ukasikika na hapo hapo, moto mkali ukaanza kulipuka.

    Gari likaanza kushika moto, msichana huyo akiwa ndani yake. Alipiga kelele bila msaada wowote, magari mengine yaliyokuwa karibu yakatolewa, yeye



    akiendelea kuteketekea ndani ya gari.



    Akajitahidi kufungua mlango na kutoka ili kuinusuru roho yake, akiwa ndiyo anamalizia mguu wa mwisho, akahisi kama kuna mtu anamvuta. Akarudishwa



    ndani kwa kasi! Akaendelea kuungua!

    Sasa hakupiga tena kelele, alikuwa kimya! Msichana huyo mrembo alikuwa ni Linna



    Sauti ya msichana iliendelea kusikika kutoka katikati ya moto kuomba msaada lakini hakuwepo mtu mwenye uwezo wa kumsaidia, kila aliyekuwa karibu



    alijaribu kuokoa maisha yake. Lilikuwa ni tukio la kusikitisha, wote walimhurumia lakini hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kushuhudia akifa.



    “Nakufa! Nisaidieni. Nateketea, niokoeni!” alizidi kupiga kelele msichana huyo akiomba msaada.

    “Tufanyeje?” mmoja wa wafanyakazi wa kituo alimuuliza mwenzake.

    “Tuwapigie simu Zimamoto.”



    “Hawa ambao wakifika eneo la tukio wanakuwa hawana maji?”

    “Sasa tufanyeje?”

    “Mimi nashauri tuwapigie Knight Support au Ultimate Security, hao kidogo ni wepesi na huwa wanaegesha magari yao karibu kabisa na maeneo ya viwanda



    huku Mwenge.”

    “Uamuzi wa busara.”



    Wakati wanafikia uamuzi huo bado kituo kilikuwa kikiendelea kuteketea, Linna akiwa tayari amekwishanyamaza kuashiria kabisa kuwa roho yake ilishatoka.



    Kitendo cha mguu wake kubanwa na moja ya vyuma vya bodi ya gari ndicho kilichosababisha akumbwe na mkasa huo, laiti mguu wake ungeachwa huru



    angefanikiwa kutoka ndani ya gari lake kabla moto haujawa mkubwa na kuokoa maisha.



    “Ultimate Security hapa.”

    “Ndiyo, kuna kituo cha mafuta kinateketea.”

    “Wapi?”

    “Hapa Mwenge karibu kabisa na Mlimani City.”

    “Hicho cha kwenye kona ya Chuo Kikuu?”

    “Ndiyo.”



    “Wewe ni nani?”

    “Mfanyakazi wa kituo.”

    “Nani atalipia gharama ya kuzima?”

    “Nyinyi njooni tu mzime, bosi wetu atalipa.”

    “Una uhakika?”

    “Ndiyo.”

    “Basi tunawasiliana na wenzetu walioko Mwenge, Coca Cola.”



    ***

    Bahati nzuri dereva wa gari la Zimamoto lililomilikiwa na Kampuni ya Ultimate Security alikuwa njiani kuelekea maeneo ya Ubungo, simu yake ilipoita



    aliipokea na kupewa maelekezo ya kwenda haraka eneo la tukio ili kujaribu kuokoa mali na maisha ya watu. Akabadilisha gia na kuwasha king’ora kilichokuwa



    kimezimwa na kuongeza kasi.



    “Nilishauona huo moto, moshi wake ni mkubwa mno, niko umbali wa kama mita mia mbili tu kufika eneo la tukio.”

    “Uzimeni haraka, watatulipa baada ya kazi.”

    “Sawa.”



    Dakika moja na nusu baadaye kwa sababu hapakuwa na msongamano wa magari barabarani, gari la Zimamoto lilifika na watu waliokuwa wamesimama mbali



    kuanza kushuhudia maji yakiruka na moto kuzimwa ndani ya dakika kumi. Gari la Linna lilikuwa limeteketea kabisa, yeye mwenye akiwa amelala nje ya gari hilo



    mguu mmoja ukiwa umebanwa.



    Alilala kifudifudi juu ya ardhi, hakuna sehemu ya mwili wake mgongoni kuanzia kichwani hadi miguuni iliyobaki bila kuungua, walichokifanya askari wa



    Zimamoto ni kumbeba haraka na kumpakia ndani ya gari lao kisha kuondoka kwa kasi kuelekea hospitali wakiwa hawajui ni ipi iliyokuwa karibu na kama mtu

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    waliyekuwa wakijaribu kuokoa maisha yake alikuwa hai au la.



    “Wapi?” Dereva aliuliza.

    “Tutawahi Muhimbili kweli?”

    “Siyo rahisi.”

    “Sasa tutaelekea wapi?”



    “Tujaribu hospitali ya jeshi Lugalo.”

    “Ni mzima huyu kweli?”

    “Hakuna mwenye uhakika, wewe twende tu madaktari watajua baada ya kumpima.”

    Gari lilizidi kuendeshwa kwa kasi huku king’ora kikilia na kufanya magari mengine yaliyokuwa barabarani yapishe, dakika tano baadaye gari hilo liliegeshwa



    Idara ya Mapokezi Hospitali ya Lugalo na wauguzi wakafika na machela yao.



    “Mungu wangu.” Mmoja wa wauguzi alisahau maadili ya kazi yake na kujikuta akitamka neno hilo baada ya kuushuhudia mwili wa Linna.

    Haraka wauguzi wakavaa mipira mikononi mwao na kuushusha mwili huo ambao kila sehemu waliyogusa ilibanduka ngozi, hakika Linna alikuwa ameungua



    vya kutosha, hakuna sijui ni maneno gani yangetamkwa kuelezea vizuri hali hiyo zaidi ya mtu kushuhudia mwenyewe. Akashushwa na kulazwa juu ya machela



    kisha kukimbizwa chumba cha daktari.



    “She is still breathing, but this is a severe case of third degree burn!” (Bado anapumua, lakini ni mgonjwa aliyeungua vibaya kabisa, kiwango cha daraja la tatu..)



    Aliongea daktari wa kike akiwa amezungukwa na vijana walioonekana kuwa wanafunzi wa udaktari.



    “What is the prognosis in cases like this one?” (Nafasi ya kupona ikoje kwa wagonjwa kama huyu?) Mmoja wa wanafunzi madaktari aliuliza.

    “To be honest the prognosis is very poor, may be until a miracle happens!” (Kusema ukweli nafasi ya kupona ni ndogo, labda utokee muujiza.) Daktari aliongea



    na kuwaamuru wauguzi wamkimbize haraka sana mgonjwa chumba cha wagonjwa mahututi.



    Linna akabebwa na kupandishwa juu ya machela akiwa bado hajitambui.

    Kilichofanyika chumba cha wagonjwa mahututi ni kasi ya kumuongezea maji mfululizo ili kuziba pengo la maji yaliyopotea kwa kuungua, mashine ya hewa ya



    oksijeni ilifungwa puani na mdomoni kwake.



    Yote haya yalifanyika kujaribu kuokoa maisha ya msichana huyu ambaye mpaka wakati huo alikuwa hajatambulika, kwani sura yake ilikuwa imeharibika vibaya



    na hata gari lake pia liliteketea kiasi cha namba zake kutoonekana. Madaktari hawakujali hilo, cha muhimu kwao ilikuwa ni kumponyesha mgonjwa, mengine



    yangefuata baadaye.



    “Will she survive?” (Atanusurika?) Dk. Mafuru, bingwa wa upasuaji kwenye Hospitali ya Lugalo aliwauliza wenzake kwenye kikao cha kumjadili mgonjwa



    huyo.



    “Not possible, even if she does, she will never be the same again, the deformities caused by the scars will be too bad.” (Siyo rahisi, hata akinusurika, hatakuwa



    yule yule tena, vilema vitakavyosababishwa na makovu vitakuwa vibaya mno.)

    “Kama wazazi wake ni matajiri, wanaweza kumpeleka kwenye hospitali kubwa nje ya nchi ambako atafanyiwa upasuaji wa marekebisho, si chini ya operesheni



    hamsini au sitini hivi ndiyo zinaweza zikamsaidia, tofauti na hapo atakuwa na maisha magumu sana.



    Sijui kama anaweza kuona tena.” Dk. Matilda aliyempokea Linna kwa mara ya kwanza aliongea.

    “Nawashauri kwanza tushughulikie kuokoa maisha yake mengine yatafuata, ila kwa kweli ameungua, sijawahi kuona mtu aliyeungua kiwango hiki tangu nianze



    kazi hii miaka thelathini iliyopita.”



    “Tunaendelea na matibabu gani sasa?”

    “Drip za Normal saline kwa kasi na prophylactic anti-biotics, kuzuia maambukizi.”

    “Kama ipi hiyo anti-biotic?”

    “Urgumentin.”

    “Haya jamani tuwasiliane baadaye.”

    Kikao kikamalizika na madaktari wakasambaa kwenda kuendelea na kazi nyingine za kuhudumia wagonjwa.



    ***

    “Mh!”

    “Mbona unaguna?”

    “Sijamsikia Linna akirudi.”

    “Hata mimi au tulipitiwa na usingizi?”

    “Hebu ngoja nikaangalie chumbani kwake, haiwezekani awe hajarudi mpaka saa hizi na hata kutupigia simu kutoa taarifa kwamba yuko na rafiki zake mahali



    fulani.” Mama yake Linna alisema na kukurupuka kitandani kisha kutembea moja kwa moja na kushusha ngazi hadi chini kilikokuwa chumba cha Linna, mlango



    ulikuwa wazi akaufungua na kuingia ndani.



    “Mh!” Akaguna tena baada ya kukuta binti yake hayupo, saa ya mezani ilisomeka saa 6:20. Haikuwa kawaida ya Linna kukaa nje mpaka muda huo bila kutoa



    taarifa kwa mama yake ambaye pia alikuwa rafiki yake mkubwa, mama akapandisha ngazi moyo wake ukiwa umejawa na hofu, hisia zilimtuma kuanza kuamini



    kulikuwa na tatizo lililompata mwanaye baada ya kuusikia kabisa mwili wake hauko sawa.



    “Hayupo.” Alimwambia mume wake.

    “Mh! Hebu piga simu yake.” Mzee alisema pia akianza kuingiwa na wasiwasi moyoni mwake.

    Simu ya Linna ilipopigwa ilionekana imezimwa, wakajaribu kupigwa kwa rafiki zake ambao mara nyingi alikuwa nao usiku jibu likawa wote walikuwa



    nyumbani kwao wamelala na hawakujua mahali Linna alikokuwa. Wasiwasi ukazidi kuongezeka.

    “Sasa atakuwa wapi?”

    “Hata sijui.”









    angu utotoni kijana Phillip alikuwa akimuota msichana mrembo na baadaye yeye na msichana huyo walifunga ndoa ndotoni na kuzaa mtoto mmoja. Kwenye



    ulimwengu halisi, hivi sasa Phillip ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako wasichana wanahangaika kumpata bila mafanikio.



    Msichana wa ndotoni (Zamaradi) alishamuonya kwamba kila mwanamke atakayekuwa na uhusiano naye atamdhuru. Jambo hili ni siri yake, kamwe asidiriki



    kuwaeleza wasichana waliomtaka kimapenzi kuwa yeye ni mume wa jini mkali na mwenye wivu.



    Wasichana wakidhani Phillip alikuwa mvulana mwoga, wakamfanyia njama na kumfanya ashiriki mambo ya mapenzi bila ridhaa yake. Kilichowapata wasichana



    hao ni ajali za gari; wa kwanza alikuwa ni Monalisa ambaye akiendesha gari kwa kasi, alishitukia mwanamke mwenye mtoto akisimama mbele yake.



    Wakati akijaribu kumkwepa gari lake lilipinduka, akaumia ubongo na uti wa mgongo hivi sasa amepooza na wazazi wake wanahangaika kutafuta matibabu



    sehemu mbalimbali duniani.

    Linna msichana wa pili naye akamshawishi Phillip na kumbusu kwa nguvu, muda mfupi tu baadaye akiendesha gari lake kuelekea nyumbani, mwanamke



    akaonekana katikati ya barabara, wakati akimkwepa gari liliacha njia na kuingia kwenye kituo cha mafuta na kugonga pampu ya mafuta ya petroli, moto mkubwa



    ukalipuka na kumuunguza vibaya.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zimamoto walifanikiwa kuuzima moto na kumtoa Linna akiwa katika hali mbaya, wakampeleka hospitali ambako madaktari wamempokea wakiwa na uhakika



    kabisa asingepona. Wazazi wake walipogundua usiku kwamba Linna hayuko ndani ya nyumba, walipiga simu yake bila mafanikio, wasiwasi mwingi ukawaingia



    zaidi hasa baada ya kuwapigia hata rafiki zake ambao pia walithibitisha kutomuona. Hivi sasa wamechanganyikiwa, hawajui cha kufanya.





    Wazazi walikuwa wamechanganyikiwa kabisa, Linna ndiye mtoto pekee aliyebaki, tegemeo lao na mrithi wa utajiri wao baada ya kaka yake kufariki miaka



    michache iliyopita. Hawakuwa tayari kumpoteza, kulifikiria jambo hilo tu peke yake kulimfanya mama yake Linna aanze kulia na mume wake kumpigapiga



    mgongoni akimfariji na kumwambia asiwe na wasiwasi Linna angerejea.



    “Kweli?”

    “Usiwe na shaka.”

    “Moyo wangu unaniambia mwanangu yupo katika matatizo.”

    “Hizo ni hisia tu mke wangu.”

    Waliendelea kumsubiri bila mafanikio, kila walipoisikia muungurumo wa gari nje ya nyumba yao, walisimama na kuchungulia wakiamini Linna alikuwa



    amerejea, haikuwa hivyo, magari mengi yaliyopita yalikuwa ni ya majirani. Walishangaa siku hiyo jinsi masikio yao yalivyokuwa na uwezo mkubwa wa kusikia



    kuliko siku nyingine.



    Mpaka saa kumi na mbili asubuhi Linna alikuwa hajarejea, walishapiga simu yake bila kufanikiwa kumpata na walikuwa hawajasinzia kabisa. Baba akainuka



    kitandani na kuchukua rimoti ya televisheni iliyokuwa juu ya meza ndogo kando mwa kitanda, akaibonyeza akiwa ameilenga runinga na kuiwasha.



    “Hii ni taarifa ya habari kutoka Shirika la Utangazaji la Taifa, msomaji wako ni mimi Leodgar Masome, …

    Dar es Salaam; Ajali mbaya ya moto imetokea jijini Dar es Salaam baada ya gari dogo kuacha njia na kugonga kituo cha mafuta cha Bonjour, dereva wa gari hilo



    ambaye amejeruhiwa vibaya kwa moto na hali yake ni mbaya amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili… tuungane na mwandishi wetu Brighton Masalu aliyefika



    eneo la tukio…



    Mama yake Linna aliyekuwa amejilaza kitandani, aliposikia maneno hayo alikurupuka na kuisogelea runinga, yeye na mume wake wakaanza kuangalia namna



    moto ulivyokuwa ukiwaka huku gari la zimamoto likiendelea kuzima na baadaye majeruhi alivyotolewa ndani ya gari ambalo lilikuwa limebadilika kabisa na



    kuwa na rangi nyeusi.



    “Anaweza kuwa Linna huyu?” Mama yake aliuliza.

    “Hapana!”

    “Hata kama ni yeye, naomba hii isiwe ukweli, iwe ndoto!”

    “Hawezi kuwa yeye, gari lile si lake.”

    “Ile inaonekana kama Peugeot, siyo BMW!”

    “Kabisa.”



    “Afadhali, angekuwa yeye sijui ingekuwaje.”

    “Lakini atakuwa wapi, hata kama yuko kwa mpenzi wake ni bora arudi nyumbani, anatutesa sisi wazazi wake.”

    “Ni kweli kabisa.” Mama alijibu akihema kwa nguvu, mapigo yake ya moyo yalikuwa yamebadilika kabisa.



    Waliendelea kusubiri huku wakiwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki ili kuona kama Linna alikuwa amefika kwao lakini kote hawakufanikiwa. Hii iliendelea



    kuwajaza wasiwasi, hatimaye ilipofika saa sita mchana wakafikia uamuzi wa kuondoka nyumbani kwenda kituo cha kati cha polisi ambako waliulizia kama kuna



    ajali yoyote ilikuwa imetokea, wakaelezwa ni ya moto peke yake iliyohusisha gari kwenye kituo cha mafuta.

    “Huyo majeruhi yuko hospitali gani?”



    “Muhimbili wodi ya wagonjwa mahututi.”

    “Ni vyema twende tukamuone, huwezi kujua anaweza kuwa ni mtoto wetu.”

    “Ushindwe katika jina la Yesu!” Mama yake Linna aliongea akimuangalia mume wake.

    “Nisamehe mpenzi wangu, ni mawazo tu.”



    Wakaingia ndani ya gari na kwenda moja kwa moja hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako gari liliegeshwa na wakashuka kisha kutembea kwa haraka hadi



    chumba cha wagonjwa mahututi, ingawa muda wa kuona wagonjwa ulikuwa umeisha, baba yake Linna alitumia kufahamika kwake kumshawishi muuguzi



    angalau awaruhusu waingie kumuona majeruhi wa moto.



    “Baba nawapa dakika mbili tu!”

    “Zinatosha sana mwanangu.”

    “Asante binti.” Mama alisema na wote wakaingia haraka na kupelekwa mpaka kwenye kitanda alicholazwa Linna, wakaanza kumwangalia kuanzia kichwani hadi



    miguuni, nywele zote zilikuwa zimeungua na ngozi ya mwili ilikuwa imebabuka na kuufanya uwe nyama iliyo wazi.



    “Ni yeye?” Baba yake aliuliza.

    “Hapana, huyu siye, afadhali!” Mama aliongea akitabasamu, kitendo cha kukuta mtu aliyeteketea ndani ya gari si Linna kilimfurahisha na kumfanya atamani



    Linna arejee nyumbani.

    “Lakini urefu ni sawa.”

    “Hata kama ni sawa, huyu si Linna.”



    Walipotoka hapo walirejea nyumbani, mioyoni wakidhani wangeweza kumkuta Linna amekwisharejea lakini haikuwa hivyo, mpaka saa moja jioni. Wakazidi



    kuchanganyikiwa, usiku wa siku hiyo pia hawakulala mpaka asubuhi ambapo walifikia uamuzi wa kwenda kituo cha polisi wakitaka kujua kama kweli gari



    lililoungua halikuwa la Linna.



    Walipofika kituoni walijitambulisha, bahati nzuri baba yake Linna alifahamika na watu wengi, hivyo haikuwa kazi ngumu kumuona mkuu wa kituo na



    kumweleza tatizo lake. Yeye ndiye aliyewachukua na kuwapeleka nyuma ya kituo ambako gari lilikuwa limeegeshwa, kwa jinsi lilivyokuwa limeteketea haikuwa



    rahisi hata kidogo kulitambua.

    “Ni lenyewe?” Mkuu wa kituo aliwauliza.



    “Siyo.” Mama yake Linna aliitikia.

    “Lakini mimi nina wasiwasi kidogo, muundo ndiyo wenyewe, nashauri nikimbie nyumbani mara moja nikachukue faili la gari la Linna ili tupate namba za



    chesisi yake, hiyo ndiyo itatupa uhakika kama kweli gari hii siyo ya mtoto wetu.”

    “Baba Linna, ya nini yote hayo? Au unataka mwanangu ndiyo awe ameteketea kwenye gari hii?”



    “Siyo hivyo mke wangu, moyo wangu umeingiwa wasiwasi, twende!” Aliongea mzee huyo na kwa pamoja wakamuaga mkuu wa kituo na kuingia ndani ya gari



    lao, safari kuelekea nyumbani iliwachukua dakika kumi na tano wakawa wameshafika, kuegesha na kupandisha juu kwenye chumba cha Linna ambako



    walifungua kabati na kulipata faili, haraka wakashuka hadi kwenye gari na kuondoka tena kuelekea kituoni.



    Mkuu wa kituo aliomba msaada wa maaskari ambao walifungua sehemu ya mbele ya gari na kukuta injini ikiwa imeungua lakini si kiasi cha maandishi ya



    kuchimbwa kwenye injini kushindwa kusomeka, haikuchukua muda mrefu namba za chesisi zikapatikana, wote wakasogeza vichwa vyao karibu na kuanza



    kusoma namba moja baada ya nyingine.



    “Uuuuwi! Maskini mwanangu Linna! Uuuuuwi!” Ilikuwa ni sauti ya mama yake akilia baada ya kugundua namba ya chesisi iliyoonekana ni ya gari la Linna,



    ilimaanisha mtoto wao ndiye alikuwa ameteketea ndani ya moto, yalikuwa ni maumivu makali yasiyopimika, kama mkuki wa moto kuuchoma moyo wa mtu



    akiwa hai.



    Mama akaanguka chini na kuanza kugalagala akilia, kazi ya mume wake ikawa ni kumbembeleza mpaka alipotulia ndipo kwa msaada wa polisi akasaidiwa



    kutembea mpaka kwenye gari, wakaondoka pamoja mpaka hospitali na kupelekwa tena kwenye kitanda cha mgonjwa.



    “Linna! Linna! Linna!” Mama aliita lakini Linna hakuitika, bado hakuwa na fahamu, alipumua kwa kutumia mashine ya oksijeni iliyokuwa kando ya kitanda

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    huku dripu nyingi zikiingia mwilini mwake kupitia mirija.

    “Mama hawezi kukusikia, tangu amekuja hapa hana fahamu, ni ajali mbaya sana ya moto kuliko zote ambazo nimewahi kushuhudia.”



    “Mwanangu atapona daktari?” Baba yake Linna aliuliza, naye akijifuta machozi, haikuwa rahisi kujizuia kwa jinsi hali ilivyokuwa.

    “Ni kazi ya Mungu, tunajitahidi sana kufanya kazi yetu ambayo ni kutibu, lakini mponyaji ni Mungu.” Daktari huyo aliongea.

    “Bila shaka wewe ni Dk. Mafuru?”

    “Ni kweli.”



    “Nakufahamu sana.”

    “Hata mimi nawafahamu sana wazee wangu, sikujua tu kwamba huyu ni Linna, si rahisi kumtambua.”

    “Tusaidie daktari, angalau mtoto wetu apone.”

    “Mungu atasaidia, ila hata kama akipona, ukweli ni kwamba hawezi kuwa Linna yule yule tena, roho inaniuma sana, lakini sina jinsi. Sijui ni kwa nini Mungu



    huwa anaruhusu matukio kama haya?”



    “Sisi tunamshukuru Mungu, najua ni kwa nini ameruhusu jambo hili litokee.” Baba yake Linna aliongea kwa huzuni.

    Mama yake Linna alipiga magoti kando ya kitanda na kuendelea kulia huku akimuomba Mungu amsaidie mwanaye apone, muda huo baba yake Linna alikuwa



    akiwasiliana na uongozi wa Chuo Kikuu kuwapa taarifa za kupatikana kwa mtoto wao akiwa katika hali mbaya. Taarifa hizo zikabandikwa kwenye ubao wa



    matangazo na kuwataka wanafunzi wenye nafasi wafike haraka Hospitali ya Muhimbili kumuona mgonjwa, tayari ilikuwa saa tisa na nusu alasiri.



    ***

    Baada ya chakula cha mchana, Phillip alikuwa katikati ya mawazo mengi chumbani kwake, akiyapitia mambo yaliyokuwa yakitokea maishani mwake, kuanzia



    kwa Monalisa aliyekuwa amepooza na sasa alikuwa hajui ni wapi alipokuwa Linna baada ya kumlazimisha busu mara ya mwisho walipoonana. Hisia zilimtuma



    kufikiri lazima kuna jambo lililokuwa limetokea, Zamaradi alikuwa amemtenda jambo, pengine kumuua na maiti yake kupotea.



    “Acha niende chuoni labda nitakuta amerejea, namuomba Mungu asaidie ili asije akawa ameingia kwenye matatizo.” Aliwaza Phillip na kunyanyuka kitandani



    kisha kuchukua begi lenye kompyuta yake na kuanza kutembea taratibu kuelekea darasani.

    Alishangazwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekusanyika mbele ya jengo la utawala, wakiwa katika vikundi vidogo vidogo wakijadili jambo huku



    wengine wakiwa kwenye ubao wa matangazo, wote wakisoma jambo.



    Akawahi hapo na kupenya katikati ya watu mpaka akaufikia ubao na kuanza kusoma, muda wote alipokuwa akisoma machozi yalikuwa yakimbubujika kwani



    alielewa kilichotendeka, hasira dhidi ya Zamaradi zikampanda akiamini kabisa alikuwa akiwadhuru watu wasio na hatia.



    “No! Something has to be done! I can’t let her continue tormenting innocent being.” (Hapana! Jambo fulani linahijika kufanyika, siwezi kumwacha aendelee



    kutesa viumbe wasio na hatia.) Alijisemea moyoni mwake Phillip na kwenda kando ambako alianza kulia kama jinsi wanafunzi wengine wengi walivyokuwa



    wakibubujikwa na machozi.



    Haukupita muda mrefu sana mabasi matatu yakafika na wanafunzi wakapanda, wote walikuwa wakielekea Hospitali ya Muhimbili kumuona mwanafunzi



    mwenzao, Phillip akawa miongoni mwao ili akamuone Linna. Moyoni alikuwa na maumivu makali mno, sababu alielewa kila kitu kilichokuwa kikiendelea na



    alihisi kuwajibika.





    Aliketi kiti cha nyuma kabisa dirishani, akiendelea kububujikwa na machozi, kando yake akiwepo Tyra, msichana mrembo ambaye pia alikuwa katika ligi ya



    kumpata. Mkono wa Tyra ulikuwa begani kwa Phillip akijaribu kumbembeleza asilie, kwake nafasi hiyo ilikuwa muhimu na alitaka kuitumia vyema



    kumuonyesha Phillip kwamba ni kiasi gani alimjali.



    “Tyra.”

    “Bee!”

    “Toa mkono begani, usinipapase, utapata matatizo!”



    “Matatizo gani? Kama ni mapaparazi wa chuo mimi siwaogopi, siwezi kukuacha uendelee kulia, najua matukio ya Monalisa na Linna yamekuumiza sana.



    Usisikitike, Mungu hakuwapangia wao, pengine hii ilikuwa ni riziki yangu…”

    “Tyra!” Phillip aliita akimuangalia kwa jicho la huruma, alielewa ambacho kingefuata kama msichana huyo angeendelea na mpango wake, yeye pia angekutwa na



    matatizo kama yaliyowapata wenzake.



    “Bee!”

    “Nisikilize mimi, ninajua ninachokisema, tafadhali usinilazimishe nizungumze mambo mengine ambayo mimi sipendi kuyaongea.”

    “Mambo gani Phillip?”

    “Basi tu, wewe toa tu mkono.” Phillip aliongea akiutoa mkono wa Tyra begani kwake, wanafunzi wengine waliokuwa jirani waliangaliana, Tyra msichana mzuri



    na mwenye maringo kuliko mwingine yeyote katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alijisikia vibaya mno.



    “Haya bwana, sitakufuatilia tena, hii ni mara ya mwisho.”

    “Nashukuru.”

    Tayari basi walilopanda likawa linakata kona kutoka Barabara ya Umoja wa Mataifa na kuingia Barabara ya Malik kuelekea Muhimbili, hawakuongea tena kitu



    chochote mpaka wanashuka Idara ya Mapokezi. Walishangazwa na umati wa wanafunzi waliowakuta, kumbe wengi walitangulia hospitalini kutoka mabwenini,



    zaidi ya wanafunzi elfu nne walikuwa wamejaa mbele ya jengo la mapokezi, walikuwa wamezuiliwa kwenda chumba cha wagonjwa mahututi kumuona Linna,



    baadhi walikuwa wakilia.



    Aliposhuka ndani ya basi, Phillip hakutaka kuongea na mtu tena, alichagua eneo la pembeni karibu kabisa na Idara ya Maabara na kuketi kwenye msingi wa



    nyumba , akainamisha kichwa chake chini na kuendelea kulia, huku mkononi akiwa ameshikilia kijiti na kuandika juu ya ardhi; I love you, don’t die! maneno ya



    Kiingereza yaliyomaanisha; Nakupenda, usife.



    Akayasoma maneno hayo mara nyingi na kuzama ndani yake, kwa mara ya kwanza akaamini moyoni mwake alikuwa akimpenda sana Linna, bila Zamaradi



    kuwepo maishani mwake na akapewa nafasi ya kuchagua mwanamke wa kuoa, asingemchagua mwingine yeyote isipokuwa yeye, sasa alikuwa ameungua na



    moto, Zamaradi alikuwa amemteketeza, kwa hali aliyokuwa nayo lazima angekufa, moyo ukamuuma.



    “Haya tukusanyikeni! Wanafunzi wote tukusanyikeni, daktari anataka kuongea na sisi” Ilikuwa ni sauti ya Jason Mbwambo, rais wa serikali ya wanafunzi katika



    Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.



    Sauti hiyo ndiyo iliyomgutua Phillip na kumuondoa katika dimbwi la mawazo alilokuwa amezama ndani yake, akanyanyuka taratibu na kujikongoja mpaka



    mahali ambako wanafunzi wote walikuwa wakijikusanya, minong’ono ikaanza kusambaa kwamba Linna alikuwa amefariki dunia, taarifa hizo zilimuumiza sana,



    akabaki kimya katikati ya wanafunzi wenzake akimsubiri daktari aje atangaze. Dakika ishirini baadaye daktari alifika na kusimama mbele ya wanafunzi.



    “Habari zenu!”

    “Nzuri shikamoo daktari.”

    “Marahaba, naitwa Dk. Mafuru, mimi ndiye ninashughulika na tatizo la mwanafunzi mwenzenu, rafiki yenu Linna, nimejitokeza hapa kuwapeni habari kwamba,



    hali yake si nzuri, ameungua sehemu kubwa sana ya mwili wake. Tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuokoa maisha yake, hatuwezi kusema atapona kwa sasa, ila



    tuendeleeni kumuombea! Hizo ndiyo habari nilizotaka kuwapatia. Kama kuna swali mnaweza kuniuliza.” Alimaliza daktari na kuanza kuwaangalia wanafunzi,



    mkono mmoja ulikuwa hewani.



    “Naitwa Phillip, sina swali ila nilikuwa naomba nikamuone mgonjwa.”

    “Suala la kumuona nyinyi nyote ni gumu, mgonjwa anahitaji utulivu, hivi sasa hana uwezo wa kuzungumza, hivyo kuwaruhusu kwa wingi wenu muingie

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    itakuwa ni sawa na kumsumbua mgonjwa, lakini tunaweza kuruhusu viongozi wenu wawawakilishe.”

    “Sawa daktari!” Wanafunzi wengi waliitikia.



    Phillip hakuwa miongoni mwa viongozi wa serikali ya wanafunzi, lakini alishinikiza mpaka kujikuta yuko kati ya wanafunzi saba walioruhusiwa kuongozana na



    daktari hadi ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi, hakuamini alichokiona Linna alipoondolewa kifaa kilichomfunika juu yake kukiwa na mashuka na kubaki



    wazi, Phillip alilia, hakuwa Linna bali kiumbe kingine tu kilichochunwa ngozi na moto.



    “No! Huyu siyo Linna, nionyesheni mwingine.” Aliongea akijiunga na wanafunzi wenzake wote kulia, ilikuwa picha mbaya mno kuishuhudia.

    Haikuwezekana kabisa kubaki ndani ya chumba hicho, wote baada ya kupiga magoti pembeni mwa kitanda na kusali walinyanyuka, wakawapa pole wazazi kisha



    kutoka hadi nje ambako walishindwa hata kuwasilimulia wenzao walichokishuhudia. Dakika ishirini baadaye walipanda kwenye mabasi na safari kurejea chuo



    kikuu ikaanza, huko Phillip hakuwa na la kufanya zaidi ya kushuka na kwenda moja kwa moja bwenini kwake, akajifungia na kuanza kulia.



    Baadaye fahamu zilimpotea, ulikuwa ni usingizi mzito uliomchukua, akamshuhudia Zamaradi pamoja na mwanaye akimwijia, uso wake ukiwa na tabasamu,



    mkononi akiwa ameshikilia boksi na kuliweka juu ya meza. Phillip alikurupuka kitandani na kuanza kumfokea akilalamika ni kwanini alikuwa akitesa watu bila



    huruma kiasi hicho, Zamaradi hakuwa na la kusema zaidi ya sentensi “Samahani, nakupenda mno, niko tayari kufanya lolote kukulinda mume wangu.”



    Aliposema maneno hayo Zamaradi alipotea, Phillip akafumbua macho yake na kushuhudia juu ya meza kukiwa na boksi kama alivyoona ndotoni. Taratibu



    akajinyanyua kitandani kulisogelea boksi hilo, alipofungua ndani yake alikuta kuna mkufu, saa ya dhahabu na bulungutu la dola za Kimarekani.



    Pia kulikuwa na karatasi ndogo ambayo juu yake iliandikwa maneno “I am sorry!” kwa kutumia damu ambayo Phillip hakuelewa ilikuwa ni ya binadamu au



    mnyama gani. Taratibu akaanza kuhesabu noti za dola mia alizozikuta, zikatimia elfu kumi! Moyo wake ukaanza kushuka, hasira aliyokuwa nayo ikaanza



    kupungua hasa baada ya kuivaa saa mkononi pamoja na mkufu shingoni, tabasamu likarejea.



    ***

    Hali ya Monalisa ilikuwa mbaya kupita kiasi, juhudi zote za madaktari zilionekana kugonga mwamba lakini wazazi wake hawakuwa tayari kukata tamaa. Ni



    kweli alikuwa amepooza na asingenyanyuka kitandani siku zote za maisha yake kwa maelezo ambayo madaktari waliyatoa lakini bado wazazi hao walitaka



    kujaribu njia nyingine, fahamu zilishamrejea binti huyo na alikuwa akilia akiwaomba wazazi wake wasihangaike sana.



    “Baba!”

    “Naam!”

    “Msihangaike, mliyoyafanya yanatosha, bila shaka huu ndiyo ulitakiwa kuwa mwisho wangu. Jambo moja tu naomba mnifanyie, nitafurahi sana.”

    “Jambo gani mwanangu?”

    “Nahitaji kuongea na mwanafunzi mmoja chuo kikuu anaitwa Phillip.”





    “I think this is beyond our control, we cant save the life of this victim, she has severe bruises and burns which penetrated into her body. She must be referred,”

    (Nafikiri hii ni nje ya uwezo wetu, hatuwezi kuokoa maisha ya mwathirika huyu, ana malengelenge na majeraha ya moto yaliyopenya hadi ndani ya mwili wake.



    Lazima tumtafutie rufaa) aliongea Daktari Mafuru wakati akijadiliana na Bodi ya Madaktari wa Muhimbili juu ya hali ya mgonjwa yule.



    Hospitali ya Muhimbili ndiyo iliyokuwa kubwa zaidi nchini Tanzania, hivyo kumtafutia rufaa kulimaanisha kumpeleka nje ya nchi kwenye hospitali bora zaidi.



    Wakati madaktari wakijadiliana, baba na mama yake Linna nao walikuwa wakifikiria suala hilo hilo.

    “Tangu tumlete mwanangu hapa hospitali sioni mabadiliko yoyote, mume wangu tusipochukua uamuzi wa haraka tutampoteza mtoto huku tunashuhudia.”



    “Ni kweli mke wangu, lazima tufanye jambo haraka. Hata kama tutalazimika kuuza kila tulichonacho ilimradi mtoto wetu akatibiwe mimi niko tayari,” aliongea



    baba yake Linna huku akijifuta machozi. Japokuwa alikuwa ni mwanaume na baba wa familia, hali ya mwanaye ilimfanya ashindwe kuyazuia machozi. Ikawa



    kila mmoja anajifuta machozi kutokana na hali aliyokuwa nayo Linna.



    Muda mfupi baadaye waliitwa kwenye chumba cha Daktari Mafuru na kuelezwa kile madaktari walichoona kinafaa.

    “Tumependekeza mkajaribu kwenye Hospitali ya Johannesburg Trauma Centre, pale huduma zao ni za hali ya juu hasa kwa wagonjwa waliopatwa na majanga



    kama hili lililomkumba binti yenu. Mungu atawasaidia na naamini atapona ingawa hataweza kuwa kama alivyokuwa kabla ya kupatwa na matatizo.



    Bila kupoteza muda, madaktari wa Muhimbili wakiongozwa na Dokta Mafuru walianza kufanya mawasiliano na wenzao wa Johannesburg Trauma Centre. Baba



    yake Linna alishughulikia taratibu za uhamiaji, akafuatilia vibali ubalozini na hatimaye kila kitu kikawa tayari.



    Kwa kutumia ndege maalum iliyokodiwa, Linna akasafirishwa hadi jijini Johannesburg sambamba na wazazi wake. Ndege iliyowabeba ilipotua nchini humo,



    tayari gari la wagonjwa (ambulance) kutoka kwenye hospitali ile lilikuwa likiwasubiri uwanja wa ndege. Linna akashushwa kwenye ndege na kuingizwa moja



    kwa moja kwenye ambulance, safari ya hospitalini ikaanza.



    Alipofikishwa Johannesburg Trauma Center, alipitishwa mpaka chumba cha wagonjwa mahututi ambapo alianza kutibiwa haraka. Kitu cha kwanza ilikuwa ni



    kumuunganisha na mashine ya kusukuma hewa ya Oksijeni iliyomsaidia kupumua.



    “She has been dehydrated! Her body is running a severe shortage of water and mineral salt. We need to hydrate her first before we proceed.”

    (Amepungukiwa na maji mwilini. Mwili wake una upungufu mkubwa wa maji na madini ya chumvi. Tunapaswa kumuongezea kwanza kabla ya kuendelea)



    Daktari Amstrong Reymann, mkuu wa kitengo cha majanga ya moto hospitalini pale alikuwa akitoa maelekezo kwa madaktari wenzake. Muda mfupi baadaye



    Linna akatundikiwa dripu ya maji na chumvi, huku akipakwa dawa za kuua wadudu (Antibiotics) mwili mzima.



    Kwa kipindi hicho chote, Linna alikuwa amelala usingizi wa kifo, akiwa haelewi chochote kilichokuwa kinaendelea kwenye ulimwengu wa kawaida.

    Baada ya dripu karibu sita kutiririka kwa kasi mishipani mwa Linna, mapigo yake ya moyo yalianza kuongezeka taratibu. Madaktari wakawa wanapishana



    kwenye kitanda chake kuhakikisha mgonjwa huyo anapona.



    Huduma bora za kiwango cha juu ilikuwa ni miongoni mwa sifa zilizoitangaza hospitali ile dunia nzima. Kila aliyewahi kutibiwa pale, hakuacha kusifia huduma



    bora kabisa za afya. Hali ile iliwapa matumaini wazazi wa Linna, wakapata moyo kuwa mtoto wao anaweza kupona ingawa hawakujua kama atarudia hali yake



    kama ya zamani.



    Baada ya mapigo ya moyo, kiwango cha maji na chumvi mwilini kuanza kuridhisha, Dokta Amstrong Reymann alishauriana na madaktari wenzake namna ya



    kuifanyia marekebisho ngozi ya Linna iliyokuwa imeharibika vibaya mwili mzima.

    “We need to implant her body with the modern skin grafting method, at least we can minimize the damage.”

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    (Tunatakiwa kupandikiza ngozi mpya juu ya mwili wake kwa kutumia mbinu ya kisasa ya upandikizwaji wa ngozi, angalau tutapunguza madhara mwilini



    mwake)

    Kilichofuatia ilikuwa ni utekelezaji lakini kilichowakwamisha ikawa ni mahali pa kuipata ngozi ambayo ingetumika kwa zoezi lile.



    Mwili wote wa Linna ulikuwa hautamaniki na hakukuwa na sehemu ambayo ngozi yake haikuungua. Baada ya madaktari kukwama, waliwaita wazazi wake na



    kuwaeleza hali halisi. Suluhisho pekee lililoonekana kufaa ilikuwa ni wazazi wake kukubali kupimwa ngozi zao na kama zingeendana na mtoto wao,



    wangekatwa ili kumsaidia Linna.



    Waliingizwa maabara ambapo vipimo kadhaa vya ngozi vilichukuliwa. Majibu yalipotoka, wote walionekana kuendana na mtoto wao, hivyo zoezi ambalo



    lilifuatia lilikuwa ni kukata sehemu ya ngozi miilini mwao na kumpandikiza Linna. Wakaambiwa wakasubiri maelekezo nje.

    “Mmh! Unajua mke wangu mi naogopa sana. Niliwahi kusikia kuwa wakitaka kukutoa ngozi wanakata makalio.”



    “Baba Linna nawe, huachi woga wako wa kitoto. Hata kama ingekuwa usoni, si unamtolea mwanao? Au unataka afe?”

    “Basi mke wangu, nilitaka kukuchangamsha kidogo kwani ulikuwa umepooza sana,” aliongea Baba Linna wakati wakisubiri maelekezo ya daktari.



    Alichokizungumza baba yake Linna kilikuwa kweli kwani daktari Amstrong alipowaita ofisini kwake aliwaeleza kuwa kama watakubali, ngozi ya kwenye



    makalio yao ndiyo itakayokatwa kwa ajili ya kuipandikiza kwenye mwili wa Linna. Waliangaliana machoni kwa muda kisha wakatabasamu, kwa pamoja



    wakatingisha vichwa vyao kuonesha kuwa wako tayari.



    Kilichofuatia ikawa ni kuingizwa chumba cha upasuaji, mmoja baada ya mwingine. Wakakatwa ngozi kisha Linna akaanza kufanyiwa ‘skin grafting’. Baada ya



    baba yake kumaliza kufanyiwa zoezi lile, mama yake naye aliingizwa maabara. Matibabu kwa Linna yaliendelea na angalau akaanza kuonesha matumaini ya



    kupona ingawa bado alikuwa hajarejewa na fahamu zake.



    Licha ya wote kujitolea ngozi kwa ajili ya mtoto wao, bado haikutosha kuufunika mwili wote wa Linna. Ikabidi taratibu zifanyike za kuwaita ndugu zao wengine



    waliokuwa Tanzania kwa ajili ya kwenda kujitolea kuokoa maisha ya Linna.



    Ndugu saba wa ukoo wa akina Linna wakasafirishwa mpaka Afrika Kusini. Walipoenda kupimwa damu na ngozi zao, watano kati yao walionekana kuendana na



    Linna. Wakaingizwa maabara na kufanyiwa kama wenzao. Angalau ngozi ikatosha kufunika maeneo yote muhimu.

    Madaktari walihakikisha kuwa ngozi waliyoibandika mwilini mwa Linna inajishikiza vizuri na kuungana na mwili wake. Wakawa wanampa dawa nyingi za kuua



    wadudu na kulainisha ngozi.



    Hilo lilifanikiwa kwani mwezi mmoja tangu zoezi lile lifanyike, hatimaye Linna alirejewa na fahamu zake na kufumbua macho kwa mara ya kwanza. Tofauti na



    alivyokuwa awali kabla hajapatwa na ajali ile mbaya, upasuaji wa kupandikiza ngozi ulimfanya abadilike kwa kila kitu. Hakuwa Linna yule wa zamani, binti



    mrembo mwenye tabasamu pana muda wote. Alikuwa mtu mwingine tofauti kabisa, hali iliyomliza mno mama yake.



    Uso ulikuwa na alama nyingi za mishono, kichwa hakikuwa na nywele hata moja. Mwili mzima ulikuwa na viraka kama nguo iliyopelekwa kwa fundi mara



    nyingi. Hata hivyo wote walimshukuru Mungu kwa miujiza aliyoifanya kwani hakuna ambaye alikuwa na matumaini ya Linna kufumbua macho yake tena.





    Siku ya kwanza tangu Linna arejewe na fahamu ilipita, wazazi wake wakawa bado hawajamwambia nini hasa kilichomsibu. Kumbukumbu zake zilikuwa



    zikirejea taratibu sana, kiasi kwamba hakukumbuka nini kilichomtokea mpaka akawa pale.



    “Lakini kwani hapa ni wapi? Mbona hamtaki kuniambia ukweli?”

    Baba na mama yake walitazamana kwa muda kama wanaoulizana wamwambie au la. Wakapeana ishara ambayo waliielewa wenyewe kisha mama yake akaanza



    kumweleza.

    “Hapa ni hospitali mwanangu, pole kwa yote yaliyokupata. Tunamshukuru Mungu kwa kukulinda mpaka leo.”



    “Kwani nini kilinipata mpaka nikaletwa hapa?” Alizidi kuhoji Linna lakini hakuna aliyemjibu.

    “Nataka kwenda ‘toilet’!”

    “Utaweza kusimama kweli, ngoja tumwambie nesi aje atusaidie kukuinua.”

    “Mbona naweza kuinuka mwenyewe,” Linna aliongea huku akijivuta pale kitandani na kusimama.



    Kwa kuwa alishatolewa dripu na ile mashine ya kusukuma Oksijeni aliyokuwa amefungiwa, haikumuwia vigumu kusimama. Mama yake akamsaidia kushuka



    kitandani na wakamshikilia huku na huku, wakampeleka chooni.



    Wakati wanaelekea chooni, walipofika sehemu iliyokuwa na vioo vikubwa ukutani, Linna alisimama kwa muda. Akawa ni kama anajishangaa kupitia vile vioo



    kwani tangu alipopatwa na masaibu yale, hakuwahi kujiangalia jinsi alivyo.



    “Yule ni nani?” Alinyoosha kidole kujionesha mwenyewe kwenye kioo. Baba na mama yake walitazamana tena, machozi yakawa yanawalengalenga. Mama yake



    alimkumbatia na kumwambia kuwa yule aliyekuwa anamuulizia ni yeye mwenyewe.



    “Mbona nimebadilika hivi? Noo! Siyo mimi, labda ni mtu mwingine,” aliongea Linna huku akianza kulia. Alikuwa amebadilika mno. Ilibidi wazazi wake



    wafanye kazi ya ziada mpaka akatulia na kukubaliana na matokeo.



    Walimfikisha msalani, akamaliza haja zake kisha wakamrudisha wodini. Alipofika tena eneo lile lenye vioo vikubwa, alizidi kujishangaa huku safari hii



    akishindwa kujizuia kulia.

    “Mi nafikiri tukamuite daktari kwa ajili ya kumjenga upya kisaikolojia ili akubaliane na hali halisi, vinginevyo atapata shida sana kuyakubali mabadiliko



    makubwa aliyonayo.”



    “Ni sawa, lakini kabla ya kumuita daktari hata sisi wenyewe tunaweza kumsaidia. Nafikiri huu ni muda muafaka wa kumueleza nini kilichompata mpaka akawa



    hivi.”

    “Unafikiri itasaidia?”

    “Yaah! Itasaidia sana.”



    Baada ya kuteta pembeni kwa muda mfupi, baba na mama Linna walirejea kwenye kitanda alichokuwa amelala mtoto wao aliyekuwa anaendelea kulia kwa



    uchungu, wakaanza kumbembeleza na kumweleza kila kitu kilichomtokea. Ni hapo ndipo kumbukumbu zake zilipomrudia vizuri. Alikumbuka siku aliyopata



    ajali mbaya kisha gari lake kulipuka baada ya kugonga pampu ya mafuta.



    “Mamaa nakufa! Niokoeee!” Alipiga kelele Linna kumbukumbu za jinsi ajali ilivyotokea zilipomrudia.

    “Tulia Linna, mshukuru Mungu kwamba mpaka muda huu uko hai,” aliongea mama yake huku akimshika mwanaye na kumtuliza pale kitandani.



    “Mamaa, nilimuona mwanamke akivuka barabara akiwa amembeba mtoto, nilipojaribu kumkwepa ndiyo gari likanishinda,” aliongea Linna huku akitetemeka



    mwili mzima. Zilikuwa ni kumbukumbu mbaya ambazo ama kwa hakika zilimfanya atie huruma.

    Maneno yale aliyoyasema kuwa alimuona mwanamke akivuka barabara akiwa amembeba mtoto, yaliwafanya wazazi wa Linna kuanza kuhusinisha ajali ya mtoto



    wao na ya mwanafunzi mwenzake, Monalisa.



    “Mbona Monalisa na yeye alipopata ajali alisema aliona mwanamke akivuka barabara akiwa amembeba mtoto?”

    “Lazima kuna jambo hapa! Siyo bure.”

    “Inawezekana kuna siri nzito iliyojificha nyuma ya pazia. Mimi si mwepesi wa kuamini nguvu za kishirikina, lakini katika hili nahisi zinahusika.”



    “Tumwachie Mungu, cha msingi mtoto wetu ameanza kupona.”

    Daktari Amstrong aliingia wodini na kukuta mama na baba Linna wanambembeleza mtoto wao. Alitambua matatizo ya kisaikolojia yanayoambatana na tatizo



    kama lile lililokuwa limemsibu Linna. Aliwaomba wazazi wake wamfuate ofisini kwa ajili ya maelekezo zaidi juu ya tiba ya Linna.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Japokuwa mgonjwa amerejewa na fahamu, bado tuna kazi kubwa ya kuurekebisha mwili wake. Hii ni hatua ya awali tu kwani kuna zaidi ya oparesheni nyingine



    50 ambazo inabidi tumfanyie ili angalau kurejesha mwonekano wake wa awali.”

    “Oparesheni hamsini? Zote hizo za nini?”

    “Bado tunahitaji kurekebisha viungo kama macho, pua, midomo, masikio na vingine vingi, ajali ya moto ilimharibu kabisa.



    ***

    Hali ya Monalisa ilizidi kuwa mbaya licha ya kusafirishwa hadi nchini Uingereza. Kauli ya mwisho aliyoitoa ilikuwa ni kuwaomba wazazi wake wamkutanishe



    na Phillip kabla hajafa.

    Wazazi wake walimhakikishia kuwa watatimiza ombi lake. Kilichofuatia baada ya hapo ikawa ni baba yake Monalisa kusafiri hadi jijini Dar es Salaam kwa lengo



    la kumfuata Phillip.



    Alipowasili, alienda mpaka kwenye uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuomba kuonana na Phillip.

    “Mimi ni baba yake Monalisa! Amenituma nije kuonana na wewe na kukufikishia ujumbe kuwa anahitaji kuonana na wewe.”

    “Sasa atanionaje wakati yuko hospitali, tena Uingereza?”

    “Usiwe na wasiwasi, familia yangu itakugharamia usafiri na malazi, cha msingi ni utayari wako.”



    “Mimi niko tayari mzee wangu, hata sasa hivi!””Ok, safi kijana! Sasa jiandae, ngoja mimi nifuatilie taratibu zote za vibali vya usafiri. Naomba ukapige ‘passport’



    na unipe kitambulisho chako, kesho mambo yote yatakuwa tayari,” aliongea baba Monalisa kisha akaagana na Phillip.



    Baada ya kuachana naye, alitamani Zamaradi amtokee na kumuombea tena msamaha Monalisa kwani kwa hali ilivyokuwa, uwezekano wa kupona ulikuwa



    mdogo. Phillip alibaki na msongo mkubwa wa mawazo juu ya hali ya Monalisa. Aliumia kuona mtu asiye na hatia akiangamia kwa sababu ya wivu wa Zamaradi.



    Alimuomba Mungu wake ampe ujasiri kwenye safari ile ngumu ya kwenda kuonana na Monalisa. Alijikuta machozi yakimlengalenga.

    Ndege ya Shirika la British Airways ilikuwa ikiiacha ardhi ya Tanzania na kupaa kuelekea jijini London, Uingereza. Phillip na baba yake Monalisa walikuwa ni



    miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya ndege ile. Hakuna aliyemsemesha mwenzake japo walikaa siti zilizokaribiana.



    Masaa machache baadaye, ndege ile ilikuwa ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow jijini London. Abiria wote waliteremka, Phillip akiwa



    miongoni mwao sambamba na baba yake Monalisa.

    Hawakuwa na muda wa kupoteza. Waliunganisha moja kwa moja mpaka hospitali. Walipofika, baba yake Monalisa alimuomba Phillip amsubiri sehemu ya



    mapokezi kwa ajili ya kwenda kumuandaa mgonjwa.



    Katika hali ambayo hakuitegemea, Phillip alishtuka kumuona baba yake Monalisa akitoka wodini huku amejiziba uso wake kwa kitambaa. Alipomchunguza



    vizuri aligundua kuwa alikuwa akilia.

    “Mungu wangu! Nini tena?” aliongea Phillip na kuinuka kwa kasi kumfuata baba Monalisa.

    “Mzee kwani vipi?”



    “Hatunaye tena! Monalisa ametangulia mbele za haki?”

    “Niniii?” Phillip akiwa katika hali ya kutoamini kile alichokisikia, alishangaa mwanamke wa makamo akitoka wodi ile ile huku akilia na kuja kumkumbatia



    baba yake Monalisa. Alimtambua kuwa ni mama yake Monalisa.



    “Pigo kubwa kiasi gani? Yaani safari yote kutoka Dar es Salaam kumbe nakuja kuiona maiti yako? Kwa nini usingesubiri japo nikuone mara ya mwisho



    Monalisa! Eeeh Mungu, mpumzishe kwa amani!” aliongea Phillip huku akilia kilio cha kwikwi. Hakuna aliyekuwa na uwezo wa kumtuliza mwenzake, ikawa ni



    maombolezo wakati mwili wa Monalisa ukitolewa wodini na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.







    Lilikuwa ni tukio la kusikitisha mno, Phillip alilia kuzidi hata wazazi wa Monalisa. Moyoni mwake aligundua wazi kuwa hata yeye alimpenda msichana huyo



    kupita kiasi. Lakini sasa alikuwa amekufa kabla hawajaongea chochote, safari yake kuja Uingereza haikuwa na matunda. Alimlilia Monalisa kwa nguvu zake



    zote, hasa alipokumbuka namna walivyoishi vizuri chuoni.



    Hasira zake zote zilielekezwa kwa Zamaradi, alimchukia, tena sana. Hakutaka tena kuwa naye kwa sababu alikuwa muuaji, aliyemuua Monalisa bila hatia na



    kumjeruhi Linna kwa moto ambaye pia Phillip aliamini, kwa hali aliyokuwa nayo, asingeweza kupona. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kufikiria namna ambayo



    angeweza kujinasua kwa mwanamke huyo hatari.



    “Nataka kuishi maisha ya ukweli, nataka kuishi maisha halisi, sitaki tena maisha ya chini ya maji, lakini nitajitenganisha nayo vipi? Zamaradi ataniua,” Phillip



    alijiuliza bila kupata jibu.



    Taratibu za kuusafirisha mwili wa Monalisa kutoka Uingereza zilishughulikiwa na Watanzania waishio nchini humo kwa kushirikiana na ubalozi wao, wakati



    huo Phillip akiwa amechukuliwa chumba kwenye Hoteli ya Conrad ambako pia wazazi wa Monalisa waliishi.



    Hakuwa na jingine la kufanya akiwa chumbani isipokuwa kulia, hakulala wala kula chochote mpaka siku iliyofuata ambapo walipanda ndege na kusafiri watatu



    na mwili wa Monalisa hadi uwanja wa ndege, Dar es Salaam.



    Maelfu ya watu walikuwepo uwanjani, wengi wakiwa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, marafiki na majirani wa familia ya kina Monalisa



    maeneo ya Upanga. Vilio vilisikika kwa mbali, wanafunzi wakimlilia Monalisa. Alipotoka nje ya uwanja, Phillip alikumbatiwa na Tyra ambaye alimchukua hadi



    kwenye maegesho ya magari, akafungua mlango na kumpakia.



    Baadaye msafara mrefu wa magari uliondoka uwanjani kuelekea Upanga, Phillip na Tyra wakiwa peke yao ndani ya gari, muda wote Tyra akimfariji na



    kumwambia asijali kwa yaliyotokea. Kwake kifo cha Monalisa kilimuumiza lakini pia ilikuwa nafasi ya yeye kumpata Phillip kwa urahisi hasa baada ya Linna



    kuungua vibaya kwa moto, alihisi Phillip alikuwa amemaanishwa kwa ajili yake.



    “Usilie Phillip.”

    “Sawa lakini inaniuma.”

    “Najua, ulikuwa unampenda sana Monalisa na pia Linna.”

    “Siyo hivyo, ananiuma kwa sababu amekufa akiwa bado kijana sana. Isitoshe ninajua kilichosababisha kifo chake.”



    “Si ni ajali au kuna kitu kingine?”

    “Siwezi kukuambia, niache tu nilie.”

    “Usiumie sana, mimi nipo, nitakufariji.”

    “Sawa. Una habari gani za Linna?”



    “Hali yake bado ni mbaya, amefanyiwa tena oparesheni nyingine jana. Ameharibika sana sura, havutii tena, sidhani kama kuna mtu atakuja kumpenda Linna



    kabisa.”

    “Hayo anayajua Mungu, hujafa hujaumbika. Pia yeye halikuwa kosa lake, najua kilichosababisha akaungua kwa moto.”

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni nini? Maana nasikia maneno yanasambaa kwamba kuna mkono wa mtu, eti walimuona mwanamke mwenye mtoto katikati ya barabara kabla ya ajali



    kutokea.”

    Phillip hakujibu kitu tena, hakuwa tayari kujadiliana juu ya Zamaradi.



    Gari likazidi kusonga mbele mpaka wakafika nyumbani kwa kina Monalisa maeneo ya Upanga, ambako pia kulikuwa na mamia ya watu wakisubiri. Ulikuwa ni



    msiba mkubwa tena wa kifahari uliojaza watu wote maarufu na matajiri sababu baba yake Monalisa alikuwa miongoni mwao.



    “Naweza kubaki humu humu ndani ya gari?” Phillip alimuuliza Tyra.

    “Hakuna tatizo, tunaweza kubaki tu humu humu ndani mpaka baadaye.”

    “Hauna safari yoyote?”

    “Sina.”



    Phillip alilaza kiti naye kujilaza akiwa amefumba macho. Mawazoni aliendelea kumfikiria Monalisa, akahamia kwa Linna na baadaye kuendelea na Zamaradi.



    Roho ilimuuma sana hasa alipogundua kwamba hata Tyra pia kama angediriki kumshawishi au kumlazimisha kufanya tendo la mapenzi, pia angepatwa na ajali



    mbaya na hata kufa. Hapo Phillip akafumbua macho na kumuangalia Tyra.



    “Mbona unaniangalia kwa jicho hilo?”

    “Nakusikitikia.”

    “Kwa nini?”

    “Tyra!”

    “Bee!”



    “Naomba tu uniache, usije ukajaribu kunilazimisha kuwa mpenzi wako, utapata matatizo.”

    “Matatizo gani?”

    “Huoni yaliyowakuta wenzako?”

    “Toka hapa… Unataka kunitia woga? Hakuna chochote, hizi ni ajali za kawaida, usitake kujichukulia umaarufu kwamba wewe ndiye umezisababisha.”



    “Sijazisababisha mimi lakini yupo aliyezisababisha.”

    “Nani?”

    “Siwezi kukutajia ila fuata maneno yangu.”

    “Sitaki.”

    “Shauri yako.”



    Hivyo ndivyo ilivyokuwa, wote wawili walilala ndani ya gari, saa kumi na moja alfajiri, Phillip akiwa katikati ya usingizi alishitukia mwili wake unapapaswa,



    mwanzoni alidhani ni ndoto kwani hakutambua mahali alipokuwa lakini akili yake ilipokaa sawa, tayari Tyra alishamfungua zipu ya suruali yake na kuzitoa



    sehemu zake za siri nje.



    “Tyra! Utakufa,” alisema Phillip kwa sauti huku akinyanyuka.

    “Nakupenda Phillip, wewe ni haki yangu ndiyo maana akina Monalisa na Linna wamenipisha. Tafadhali nipe haki yangu,” aliongea Tyra kwa sauti ya upole uso



    wake ukiwa umejawa na aibu.



    “Haiwezekani, nakupenda mno ndiyo maana nakataa.”

    Tyra hakukubali, akaanza kulia huku Phillip akimuangalia kwa jicho la huruma, kwani alielewa ambacho kingefuata kama angeruhusu jambo hilo litendeke.



    Walishinda msibani Phillip akihuzunika kwa kifo cha Monalisa, huku Tyra akihuzunikia kitendo cha Phillip kumnyima penzi.



    “Unaweza kunipeleka bwenini nikabadili nguo?” Phillip alimwambia Tyra ilipotimia saa kumi jioni.

    “Hakuna shida.”

    “Twende basi.”



    Wakaondoka mpaka chuo kikuu ambako Phillip alishuka na wote wawili wakapandisha hadi ghorofa ya tatu kilipokuwa chumba chake, katika hali ambayo



    hakuitarajia, Phillip alibadilisha mawazo na kuamua Tyra aondoke ili yeye apumzike sababu alisikia usingizi, tena alikuwa mkali wakati akiongea maneno hayo.

    “Nikufuate baadaye?”

    “Nitakuja mwenyewe.”



    Tyra hakuwa na la kufanya isipokuwa kushusha ngazi hadi kwenye gari lake ambako alipanda, kuwasha na kuondoka kwa kasi kuelekea Upanga, akiwa amepanga



    kupitia njia ya Ubungo, Manzese, Magomeni, Faya na baadaye kuingia Upanga msibani kuungana na wanafunzi wenzake.



    ***

    Zamaradi aliyashuhudia yote yaliyotokea ndani ya gari na hasira kali kumpanda, ilikuwa ni zamu ya Tyra kufa, tena alidhamiria kumuua pale pale ambapo ajali



    ingetokea. Baada ya hapo wabaya wake wote wangekuwa wamekwisha. Phillip akiwa usingizini alimtokea na kumpa taarifa ya jambo alilokuwa anakwenda



    kulifanya, akamsihi asifanye hivyo badala yake amsamehe Tyra.



    “Tena ukizidi kunizuia hata wewe nitakuua.”

    “Usifanye hivyo, hawana hatia, ni hisia za kimapenzi zinawasumbua, cha muhimu ni kwamba mimi nina msimamo.”

    “Haiwezekani. Lazima Tyra afe.”

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tyra aliendesha gari lake kwa kasi akiwa hajui Zamaradi alikuwa akimsubiri kwa hamu kubwa kwenye taa za kuongozea magari za Faya. Kabla hajakata kona



    kuelekea Upanga, alipanga kuzipasua tairi zake zote za mbele na kisha kulipindua gari mara tano na hatimaye ligongane na gari jingine, huo ndio uwe mwisho



    wa Tyra.

    Alishuhudia gari likishuka maeneo ya Magomeni kuelekea Jangwani, akajiandaa kwa ajili ya kazi.







    Jini Zamaradi, mke wa Phillip katika ulimwengu usioonekana amedhamiria kuwaua wasichana watatu (Tyra, Monalisa na Linna) ambao ni wanafunzi katika



    Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako pia Phillip anasoma. Hakuna anayejua siri ya Phillip kuwa ni mume wa mtu kwenye ulimwengu usiooonekana,



    wasichana hao wanamuona ni mvulana mzuri na wanapanga kila mbinu ili waweze kumpata kimapenzi, hapo ndipo wakakutana na hasira ya Zamaradi.



    Kwanza alikuwa ni Monalisa, akamsababishia ajali mbaya ya gari iliyosababisha msichana huyo kupooza baada ya kuumia ubongo. Hivi sasa ameaga dunia na



    kurejeshwa nchini kutoka Uingereza kwa mazishi.



    Wa pili alikuwa Linna ambaye pia Zamaradi alimsababishia ajali mbaya ya gari iliyomfanya msichana huyo kuungua vibaya ndani ya gari lake alipogonga pampu



    ya mafuta ya petroli kwenye kituo cha Bonjour kilichoko njia panda ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam karibu na eneo liitwalo Mlimani City.



    Hivi sasa msichana huyu aliyeungua vibaya mwili wake yupo nchini Afrika Kusini akifanyiwa upasuaji kurekebisha mwili wake, sura imebadilika kabisa kwa



    sababu ya moto na Zamaradi anafurahia jambo hilo lakini Phillip anaumizwa sana kwani anajua kinachoendelea.



    Hawa wakiwa na hali hizo, Tyra pamoja na maonyo yote aliyopewa na Phillip anamfungua kijana huyo zipu ya suruali yake kwa lengo la kufanya naye mapenzi



    ndani ya gari lake, jambo hili lilimuudhi Zamaradi ambaye yupo kwenye taa za kuendeshea magari za Faya akimsubiri Tyra afike, apasue tairi za mbele za gari



    lake kisha kulipindua, huo ndiyo uwe mwisho wa msichana huyo mrembo.



    Tyra yupo maeneo ya Jangwani kwenye Barabara ya Morogoro, amebakiza mita chache tu afike Faya ambako jini Zamaradi anamsubiri kwa hamu kubwa akiwa



    amedhamiria kuing’oa roho yake bila huruma.





    “He is so handsome, I can’t resist him.” (Ni mzuri mno siwezi kujizuia nisimpende.) Tyra aliwaza akiwa ndani ya gari lake dogo aina ya Volkswagen New Model,



    muziki laini ukiporomoshwa na Celine Dion kupitia kwenye spika zilizoko kwenye mlango.



    Hakika msichana huyu alikuwa na kila kitu maishani mwake, kuanzia sura, umbile na utajiri wa wazazi wake. Simu yake haikutulia, wanaume wakimpigia simu



    kumtaka mapenzi na wote aliwakatalia, hakuwa na mpenzi kabisa ndani na nje ya Tanzania baada ya kuachana na mpenzi wake wa kwanza miaka mitano kabla,



    sasa alimtaka Phillip kwa gharama yoyote.



    Kwa kuwatazama watu hawa wawili na historia za maisha yao, utajiri wa familia zao, Basi msichana kama Tyra hakutakiwa kabisa kuwa na uhusiano wa



    kimapenzi na Phillip hata kama alikuwa na sura nzuri kiasi gani, lakini sasa alikuwa amenasa, akili yake haikufanya kazi sawasawa, taswira ya Phillip ilionekana



    kichwani mwake kila alikokwenda, hakuwa na nafuu yoyote hata alipolala usingizi, Phillip alionekana katika ndoto.



    Alishangazwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika kwenye viwanja vya Jangwani huku wengine wengi wakizidi kumiminika kuelekea kwenye viwanja



    hivyo, bila kutarajia akajikuta akishusha kioo cha gari lake na kuanza kusikiliza spika zikitangaza kwa sauti ya juu kutoka kwenye viwanja hivyo, mguu wake wa



    kulia ukahama kulia na kuja katikati, gari likapunguza mwendo.



    Najua mnayo masumbuko mengi maishani mwenu, wengine mna kila kitu lakini bado mnateseka, Yesu anawaita ili aje awatue mizigo yenu. Imetosha



    kusumbuka, iwe kwa magonjwa au maumivu ya moyo sababu kuna watu wamekutenda vibaya, Mungu wetu analijua hilo na sasa anataka kukuweka huru…



    Njoo kwake leo, hutajuta…



    Tyra aliyasikia maneno hayo kupitia masikio yake yote mawili, bila kupanga akakata kona kuelekea kwenye viwanja hivyo, hata siku moja hakuwahi kufika hapo



    kusikiliza neno. Hakuwa mtu wa kanisa sana, ni kweli alimwamini Mungu na alikuwa Mkristo lakini si mhudhuriaji wa ibada, siku zote alikuwa mtu wa starehe



    na kuhudhuria kumbi za starehe huku akiwacheka wanafunzi wenzake walioonekana wacha Mungu, akiwaita wanafiki.



    Aliegesha gari lake kando, akashuka na kujichanganya katikati ya maelfu ya watu waliokuwa wamekusanyika kwenye viwanja hivyo kumsikiliza Mhubiri wa



    Neno la Mungu, Mchungaji Moses Lubala kutoka Kanisa la Word Alive la jijini Dar es Salaam aliyekuwa akiendesha mkutano katika viwanja hivyo.



    Tyra alisimama na kuendelea kusikiliza mafundisho ya Mchungaji huyo, akiwataka watu wote kugeuka na kuacha njia zao mbaya, kwamba Yesu alikuwa



    amekaribia kurudi kuja kutoa hukumu ya kutupwa katika ziwa la moto, maneno hayo yakaingia moyoni mwa Tyra moja kwa moja, akiwa amefumba macho



    akaanza kuyapitia upya maisha yake, akajiona mwenye dhambi aliyestahili msamaha wa Mungu. Machozi yakambubujika, kwa mara ya kwanza maishani mwake



    akajikuta akitamani kumfahamu Mungu zaidi ya alivyokuwa akisikia kutoka kwa wazazi wake.



    “Wangapi wako tayari kukabidhi maisha yao kwa Yesu jioni ya leo ili aweze kuwabadilisha na kuwafanya wapya, ili hatimaye waweze kuurithi ufalme wa Mungu



    na pia kulindwa na mwovu Shetani ambaye kazi yake ni kuharibu… Kama wapo naomba wapite mbele.”



    Mtu wa kwanza kufika mbele ya jukwaa alikuwa ni Tyra, machozi yakimbubujika na mwili wake kutetemeka. Alikuwa amejisikia mwilini mwake hali ambayo



    hata siku moja haikuwahi kumtokea, akapiga magoti na kusujudu mbele ya jukwaa huku watu wengine wakizidi kumiminika.



    Mchungaji akawaongoza watu hao sala ya toba ili Mungu apate kuwasamehe dhambi zao, alipomaliza aliwaruhusu kuondoka lakini Tyra hakufanya hivyo,



    akaomba kuongea na Mchungaji baada ya mkutano kumalizika. Hicho ndicho kilichotokea, akamweleza mtumishi huyo wa Mungu kila kitu kuhusu maisha yake



    na hasa alivyoteswa na mapenzi ya Phillip, Mchungaji hakuwa na cha kufanya zaidi ya kumwombea ili roho hiyo imtoke.



    “Mchungaji naomba twende nyumbani ukawaone wazazi wangu!”

    “Unaishi wapi binti?”

    “Upanga.”

    “Nisubiri basi tumalize shughuli zote tutaongozana.”

    “Asante mtumishi.”



    Saa moja na nusu ndipo Tyra alimuongoza Mchungaji hadi kwenye gari lake, wote wawili wakapanda na kuondoka. Walipoingia tu barabarani, Zamaradi ambaye

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    bado alikuwa hajaondoka eneo hilo alijiweka tayari kwa mashambulizi, hasira yake ilikuwa palepale na alitamani kumuondoa Tyra duniani ndipo kazi yake



    ikamilike. Gari lilipofika, alinyosha mkono wake ambao ulitoa kitu kama moto uliokwenda moja kwa moka kwenye gari kwa lengo la kupasua tairi, cha



    kushangaza tofauti na siku nyingine zote moto huo uligeuka na kuanza kumrudia yeye, ukampiga pamoja na mwanaye wote wakaanguka chini.



    “Mh!” Tyra aliguna.

    “Vipi binti?”

    “Gari imetingishika.”

    “Twende, nimekwishaelewa kilichokuwa kinaendelea, roho wa kifo alikuwa hapa akikusubiri wewe lakini Mungu amekunusuru.”

    “Kweli?”

    “Ndiyo.”



    “Kwani imekuwaje?”

    “Nimemwona mwanamke mmoja ana mtoto, akanyosha mkono wake ambao ulitoa nguvu za giza lakini nikaziamuru zimrudie yeye.”

    “Mh! Mwanamke na mtoto tena, inawezekana akawa ni yuleyule aliyewatokea rafiki zangu wawili, Monalisa na Linna, magari yao yakapinduka. Hivi sasa



    ninavyoongea na wewe Mchungaji Monalisa ni marehemu, Linna ni majeruhi wa moto aliyeungulia ndani ya gari lake…”



    Waliongea mengi Mchungaji akimsimulia Tyra juu ya mapepo na namna yanavyofanya kazi na kwamba kinga pekee ilikuwa ndani ya Mungu, ambako watu wote



    wamchao hawakuwa na hofu ya mapepo hata kidogo. Tyra akamuahidi Mchungaji kumcha Mungu kwa uwezo wake wote tangu siku hiyo.



    Kilichofanyika nyumbani kilikuwa ni utambulisho wa Mchungaji kwa wazazi wa Tyra ambao kwanza walishangaa sana kusikia mtoto wao aliyewahangaisha



    kwa muda mrefu amempokea Yesu, wakamtaka awe anakwenda kuabudu kanisani kwa Mchungaji Moses Lubala ili azidi kukomaa kiroho.



    Hivyo ndivyo ilivyotokea, kwani baada tu ya mazishi ya Monalisa, Tyra alianza kuhudhuria mafundisho na ibada kwenye kanisa hilo. Chuoni wanafunzi



    walimshangaa sana kwani tabia yake ilibadilika kabisa, hakuwa na makundi tena na hata hakudiriki usiku kutoka kwenda disko kama ilivyokuwa siku za nyuma.



    Kitu pekee kilichomsumbua akili ni Phillip, pamoja na kuokoka lakini bado alijisikia kumpenda kijana huyo, hiyo ndiyo vita aliyokuwa amebakiza na ilikuwa



    ngumu sana kupata ushindi. Hata hivyo, aliuahidi moyo wake kupambana mpaka hatua ya mwisho asirejee dhambini, baadhi ya wanafunzi Chuo Kikuu



    walimcheka na kudai alikuwa akiigiza ulokole, kwamba muda si mrefu angeanguka na kurejea tena kwenye dhambi zake.



    “Umebadilika sana siku hizi, nini siri ya mafanikio yako? Kifo cha Monalisa kimekuumiza sana labda?” Ilikuwa ni sauti ya Phillip alipomfuata kuzungumza



    naye.

    “Hapana. Ni Mungu, ameamua kubadili maisha yangu, nakukaribisha sana kanisani kwetu pale Sinza Mori.”

    “Ningependa kufika hapo kanisani ili nione kitu gani kimefanyika, wewe? Wewe Tyra? Ndiyo umekuwa hivi, siyo rahisi kuamini.”

    “Karibu.”



    Mazungumzo hayo ndiyo yaliwaunganisha zaidi, tangu siku hiyo wakawa karibu kuliko ilivyotokea baada ya tukio lililotokea ndani ya gari nyumbani kwao na



    Monalisa wakati wa msiba. Phillip akahudhuria kanisani ambako mafundisho yalimgusa, akakabidhi maisha yake kwa Yesu pia na kusimulia mkasa mzima



    uliomtokea wa kuoa jini ambaye alizaa naye mtoto na alikuwa na wivu mkubwa uliosababisha kuwashambulia wanawake wote waliompenda, Tyra hakuamini



    alichokisikia ndani ya ofisi ya Mchungaji, akalia machozi mbele ya Mchungaji.



    “Ndiyo maana nilikuwa nakwambia uniache.Wenzako niliwakataza hawakunielewa, roho inaniuma sana kwa yaliyowapata,” akamwambia Tyra akimpapasa



    mgongoni.

    “Usiwe na wasiwasi Phillip, Zamaradi hutamuona tena akikusumbua, wala mwanao ambaye pia ni jini, tulikutana nao njiani wakimsubiri Tyra, nguvu ya Mungu



    ikawashughulikia.”

    Phillip alilia kwa uchungu, akajisikia huru moyoni mwake. Taratibu akamnyanyua Tyra na kumkumbatia kisha kunong’ona sikioni mwake “I LOVE YOU



    TYRA, CAN YOU MARRY ME?” (Nakupenda Tyra, unaweza kukubali nikuoe?)



    “Oh, my God! I can’t believe this, are you sure?” (Oh, Mungu wangu! Siwezi kuamini hivi, una uhakika?) Tyra aliuliza maswali mfululizo akilia kwa furaha.

    “Absolutely! Our Pastor is my witness.” (Kabisa. Mchungaji ni shahidi wangu.)

    “Yes, I can marry you Phillip, I love you too.” (Ndiyo, niko tayari unioe, nakupenda pia.)



    Wiki moja baadaye walivalishana pete ya uchumba kanisani mbele ya waumini, ndugu na jamaa na kubatizwa, Tyra akabadilisha jina na kuitwa Genevieve, huku



    Phillip akiendelea na jina lile lile. Ndoa ilipangwa kufungwa baada ya kumaliza masomo yao, muda wote wakiwa chuoni wangeendelea kuwa wachumba. Mioyo



    yao ilijaa furaha.







    Phillip na Tyra ambaye sasa alikuwa akiitwa Genevieve waliendelea na masomo huku kila mtu chuoni pale akiwashangaa. Wengi walikuwa wakimshangaa



    Genevieve kwani ndani ya muda mfupi tangu alipotangaza kumpokea Mungu, maisha yake yalibadilika sana. Hakuwa tena Genevieve wa kwenda kwenye kumbi

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    za starehe na kuvaa mavazi ya kidunia.



    Kila jambo alilifanya kwa upole huku jina la muumba wake likitawala mdomoni mwake. Hali kadhalika, Phillip naye alibadilika sana na sasa akawa mtakatifu



    kwa kila alichokuwa anakifanya. Japokuwa haikuwa rahisi kwake kuwasahau Zamaradi na mwanaye, alimshukuru Mungu kwa kumfungua kwenye kifungo



    kilichomtesa siku nyingi maishani mwake. Mawazo, akili na moyo wake alivielekeza kwa Genevieve na aliamini hakuna kitakachowatenganisha zaidi ya kifo.



    Siku zilizidi kusonga huku mapenzi yao yakiwa gumzo kila walikopita. Wapo waliowabeza na kuwaona kama watu waliokuwa wakiigiza ingawa pia wapo



    waliokuwa wanawaombea mema kwenye maisha yao.

    “Hivi mapenzi ya kilokole yanakuwaje?”

    “Yanakuwa kama mapenzi mengine, kwa nini unauliza hivyo?”



    “Nauliza kwa sababu nawashangaa sana Phillip na Genevieve, eti wanaigiza mapenzi ya kilokole, ina maana hawajawahi kuduu?”

    “Wewe nawe, maswali gani hayo unauliza, kwani hujui amri kumi za Mungu zinavyosema?”

    “Sawa najua kuwa Mungu amekataza watu kuvunja amri ya sita, lakini ukiwaangalia Phillip na Genevieve watakuwa hawajahi kukutana kimwili kweli?”



    “Bwana eeeh, hayo maswali kawaulize wenyewe, mi ninachojua ni kuwa haitakiwi wachumba kufanya tendo la ndoa mpaka watakapohalalishwa madhabahuni,”



    wanafunzi waliokuwa wakifanya ‘discussion ‘chini ya mti mkubwa kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliacha kujadili masomo na sasa wakawa



    wanawajadili Genevieve na Phillip.



    Kila mmoja alikuwa akiongea lake lakini ukweli walikuwa nao wenyewe. Kwa kutambua kuwa wanafuatiliwa sana na wenzao, Phillip na Genevieve hawakutaka



    kuingia kwenye skendo yoyote, wakawa wanajitahidi kuishi kwa kufuata maagizo yote ya Mungu. Hawakuacha kusali kila asubuhi, mchana na jioni bila kujali



    kama ilikuwa Jumapili au la.

    Siku zilizidi kuyoyoma na hatimaye wakamaliza chuo na kutimiza ahadi waliyokuwa wamewekeana, wakafunga ndoa na kuwa mume na mke halali.

    ***

    MWAKA MMOJA BAADAYE

    “Haya ndiyo maisha niliyokuwa nayaota siku zote za uhai wangu,” aliongea Phillip wakiwa wamepumzika kwenye bustani nzuri za maua na mkewe, Genevieve.

    “Unamaanisha nini mume wangu?”



    “Siku zote nilikuwa nikiota kumpata mke mwema ambaye nitaishi naye maisha ya raha mustarehe, unajua mi nimekulia kwenye shida na dhiki sana,” aliongea



    Phillip huku akijaribu kuvuta kumbukumbu za maisha yake ya utotoni.



    “Jamani mume wangu, Mungu ndiyo anapaswa kushukuriwa kwa yote, najua umepitia mambo mengi magumu tofauti na mimi mkeo, lakini hatimaye ndoa



    imetuunganisha na sasa tumekuwa mwili mmoja,” aliongea Genevieve na kumbusu mumewe shavuni. Alishatambua kuwa kumbukumbu za maisha ya zamani ya



    mumewe zilikuwa zikimuumiza, jambo ambalo hakuwa akipenda litokee. Akawa mfariji mkubwa kwake.



    “Nakupenda sana mume wangu, mimi pia nilikuwa naota kumpata mwanaume kama wewe, una kila kitu nilichokuwa nakihitaji,” aliongea Genevieve huku



    akijilaza kifuani kwa mumewe. Hawakuitana tena majina yao waliyokuwa wanayatumia tangu wakiwa chuoni.

    Licha ya maisha ya kifahari waliyokuwa wakiishi, nyumba nzuri ya kifahari waliyoijenga baada ya kuunganisha mishahara yao na magari ya kisasa ya kutembelea,



    bado walikosa kitu cha muhimu, watoto.



    Mwaka mzima waliokaa ndani ya ndoa haukuwa na mafanikio yoyote, wakaanza kuandamwa tena na walimwengu ambao walikuwa wanawatania kuwa



    wanamaliza magodoro na kujaza choo.

    “Unajua mume wangu mi’ najisikia vibaya sana majirani na ndugu wanavyotudharau na kutunanga eti kwa sababu hatuna mtoto,” aliongea Genevieve huku



    akilengwa lengwa na machozi.



    “Usiwajali mke wangu, kuzaa ni majaliwa ya Mungu, mara ngapi tumefunga na kusali tukimuomba Mungu atupe mtoto? Naamini ameshasikia maombi yetu,



    hatupaswi kutilia mashaka ahadi za Mungu wetu,” aliongea Phillip kwa hisia.

    “Sawa mume wangu, lakini wakati tunasubiri majibu ya Mungu, kwa nini na sisi tusijaribu kwenda hospitalini?”



    “Wazo zuri mke wangu, lakini kama ikibainika mmoja wetu ana matatizo huoni ndiyo itakuwa sababu ya mapenzi yetu kupungua?”

    “Hapana mume wangu, nakuahidi kuwa hata kama ni wewe ndiyo mwenye tatizo, kamwe upendo wangu kwako hautapungua, nitazidi kukupenda daima.”



    “Hata mimi mke wangu nakuahidi kuwa kama mimi nikiwa mzima na tatizo likionekana lipo kwako, sitakutenga bali nitazidi kukupenda kwa siku zote za



    maisha yangu,” aliongea Phillip, wakakumbatiana kwa furaha. Walikubaliana kuwa siku inayofuata waende pamoja mpaka hospitalini kwenda kuonana na daktari



    anayeshughulikia masuala ya uzazi.

    Kesho yake waliongozana mpaka hospitalini, wakaonana na daktari ambaye aliwafanyia vipimo kwa kina.



    Majibu yalipotoka, Genevieve hakuwa na tatizo bali Phillip ilibainika kuwa mbegu zake za kiume hazina uwezo wa kurutubisha yai la mwanamke na



    kusababisha ujauzito.

    “Uliwahi kupata mtoto enzi za ujana wako kabla hujaoana na huyu mkeo wa sasa?” aliuliza daktari, swali ambalo lilimfanya Phillip azame kwenye dimbwi la



    mawazo.

    “Mume wangu daktari si anakuuliza?”



    Phillip alishindwa kujibu kwani ni kweli aliwahi kuwa na mtoto lakini siyo katika ulimwengu huu unaoonekana. Alishindwa kujua daktari atamuelewaje



    atakapompa ukweli huo wa maisha yake.



    “Sijawahi daktari, huyu ndiyo mke wangu wa kwanza na sina mtoto yeyote nje ya ndoa,” alijibu Phillip huku mkewe akimuangalia kwa huruma. Alipomueleza



    vile, daktari aliandika kitu kwenye cheti na kuwaomba wakasubiri nje kwa muda wakati anatafuta ufumbuzi wa tatizo lao.



    Aliwaita madaktari wenzake wawili na kujadiliana nao nini cha kufanya ili kumsaidia Phillip apate mtoto.

    “Her wife is physically fit, her uterus can conceive and the fallopian tubes are in good condition,” ( Mke wake yuko fiti, mji wake wa uzazi una uwezo wa



    kutunga mimba na hata mirija yake ya uzazi ipo kwenye hali nzuri)

    “How about him?” ( Vipi kuhusu yeye)



    “His sperms are not viable. They lack motility ability and they can’t swim to the uterus,” (Mbegu zake za kiume hazina rutuba. Zinakosa uwezo wa kujongea na



    haziwezi kuogelea kwenda kwenye mji wa mimba)

    Madaktari waliendelea kujadiliana juu ya tatizo la Phillip. Mwisho walifikia hitimisho la kumpa dawa ambazo zingeenda kuongeza nguvu na rutuba kwenye



    mbegu zake. Daktari aliyewapima akawaita Phillip na Genevieve ofisini na kuanza kuwapa ushauri nasaha kabla ya kumpa Phillip dawa za kutumia.



    “Mama jitahidi kumpikia mumeo vyakula vyenye wanga na mafuta ya asili kwa wingi. Pia inashauriwa mjizuie kukutana kimwili mara kwa mara ili kuzipa muda



    mbegu zake zikomae, mkizingatia haya naamini mwezi huu hautaisha bila majibu kuonekana,” aliongea daktari na kuwapa maelekezo mengine ya ziada.



    Alipomaliza waliaga na kuondoka, njiani wakawa wanamshukuru Mungu wao kwa kuwasaidia. Waliamini kwake hakuna linaloshindikana. Hakuna kitu



    walichokuwa wanakisubiri kwa hamu kama mtoto kwenye ndoa yao.



    Hata baada ya mwezi mmoja kupita, bado hawakuona dalili yoyote, Genevieve hakuwa amenasa ujauzito. Hali ile ikaanza kusababisha huzuni miongoni mwao.



    Ni kweli walikuwa wakipendana kwa dhati lakini walihitaji kitu kuurutubisha upendo wao.

    Genevieve alikuwa na kazi ya ziada ya kumfariji mumewe kwani majibu yale yalionekana kumsononesha zaidi, hasa baada ya kuambiwa tatizo lilikuwa kwake.



    “Au bado Zamaradi analipa kisasi kwenye maisha yangu? Lakini mbona tangu niokoke na kuoana na Genevieve hajawahi kunitokea tena? Na kama kweli sina



    uwezo wa kumzalisha mwanamke, mbona yeye alibeba ujauzito wangu na kunizalia mtoto?” Maswali mengi yaliyokosa majibu yalikuwa yakipishana kichwani

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mwa Phillip na kumfanya awe kama mwendawazimu.



    Licha ya hali ile, Genevieve aliendelea kumpenda huku akijitahidi kuwa karibu naye kwa kila jambo.

    “Mke wangu!”

    “Abee mume wangu?”

    “Kwa nini tusiende kujaribu kwa waganga wa kienyeji? Nasikia wengi wamefanikiwa.”

    “Haaa! Yaani mume wangu unaweza kukosa imani kiasi hicho hadi kuamua kutumia njia hiyo badala ya kumwamini Mungu?”



    “Kwani waganga wanaotibu si wanatumia miti iliyoumbwa na Mungu kututibu? Kibaya ni kupiga ramli mke wangu, sioni kama kuna tatizo kwenda kujaribu,



    hatuwezi kundelea kuishi maisha kama haya.”



    “Hapana mume wangu, niko radhi nisizae kabisa maishani mwangu, lakini kamwe siwezi kuabudu miungu wengine zaidi ya Mungu aliye juu.”

    Phillip na Genevieve walikuwa kwenye mjadala mzito juu ya hali ile yakutopata mtoto iliyowatokea. Phillip alionekana kuanza kukata tamaa kiasi cha kujaribu



    mbinu mbadala lakini mkewe hakuwa tayari.









    Phillip anakombolewa kutoka kwenye mateso ya jini Zamaradi baada ya kuokoka na kukabidhi maisha yake kwa Mungu, aliyemfanya aokoke ni Tyra ambaye



    muda mfupi baadaye alimchumbia na hatimaye kufunga ndoa mara tu walipomaliza masomo yao ya chuo kikuu.



    Zamaradi hayuko tena katika maisha yake, wala hamtokei katika ndoto kama ilivyokuwa huko nyuma. Hivi sasa wanaishi vizuri kama mke na mume, wakiwa



    wamefanikiwa kimaisha kwa msaada mkubwa kutoka kwa wazazi wa Tyra ambao ni matajiri wa kutupwa. Wote wawili hawana taarifa tena juu ya Linna na



    kilichomtokea baada ya kufanyiwa upasuaji kurekebisha mwili wake.



    Kinachowatesa pamoja na mafanikio makubwa waliyo nayo ni mtoto, Phillip na Tyra wameshindwa kabisa kupata mtoto baada ya kuishi kwenye ndoa kwa



    miaka zaidi ya miwili. Jambo hili ndilo linawakosesha furaha pamoja na kwamba wana kila kitu.



    Baada ya kutafakari sana hatimaye walifikia uamuzi wa kutafuta msaada wa daktari, huko ndiko baada ya uchunguzi ilibainika kuwa, chanzo cha tatizo alikuwa



    ni Phillip ambaye mbegu zake hazikuwa na uwezo wa kumfanya mwanamke ashike mimba!



    Jambo hili linamuumiza sana Phillip na kumfanya akose kabisa raha ya maisha kwani anachohitaji ni mtoto, walipotafakari kwa muda, hatimaye Phillip alifikia



    uamuzi wa kutafuta tiba za jadi jambo ambalo Tyra hakukubaliana nalo.





    “Sasa tutafanya kitu gani mke wangu, mimi ndiyo mwenye tatizo na ninahitaji tiba ili niwe na uwezo wa kukupa ujauzito.”

    “Si kwa kwenda kwa waganga Phillip, tuendelee kumwamini Mungu, sisi tumeokoka hatuwezi kufanya jambo hilo. Tatizo ni kwamba umepoteza imani kabisa,



    hata maombi yako hayamfikii Mungu.”



    “Siyo rahisi kuendelea kuwa na imani, swala hili limeniumiza sana, nataka mtoto, nataka mtoto Tyra.”

    “Kuwa na imani, Mungu atajibu kwa wakati wake, Sara alisubiri miaka mingi kabla Isaka hajazaliwa, wewe umeshindwa nini?”



    Phillip akamuelewa mkewe, imani yake ikarejea tena. Tangu siku hiyo akawa ni mtu wa kuhudhuria maombi, aliposikia mhubiri mpya ameingia jijini Dar es



    Salaam alihudhuria na kueleza shida yake, maombi yakafanyika lakini bado hakuwa na uwezo wa kumfanya Tyra mjamzito, imani yake ikazidi kuporomoka tena.



    Kwa siri kubwa akaanza kuwa anamdanganya mke wake kwa safari za kikazi, kumbe alikwenda kwa waganga na waganguzi ambako alipewa dawa za mitishamba



    na kuzitumia kwa siri lakini nazo pia hazikumsaidia mpaka mwaka mmoja mwingine baadaye ukaisha wakiwa hawana mtoto, jamii nzima kuwateta kwa sababu



    tu hawakuwa na mtoto, jambo hili lilimuumiza sana Phillip na kumfanya wakati mwingine ajifungie chumbani na kulia.



    Hata kazi ilimshinda, ikabidi achukue likizo bila malipo.

    “Hakuna sababu ya kulia, kitu cha muhimu tutafute jibu la tatizo letu na usiwe na wasiwasi Phillip, nakupenda mno, tuwe na mtoto, tusiwe na mtoto, mimi



    nitaendelea kukupenda tu.”



    “Najua Tyra, lakini roho inaniuma sana, naamini anayenifanya hivi ni huyo huyo Zamaradi, kwa kweli simpendi.”

    “Usijali, yote yatapita.”



    Alikuwa ni Tyra, mwezi mmoja baadaye akipitia mtandaoni kujaribu kufuata suluhisho la tatizo lao aliposoma juu ya Dk. Zim Kohrer, Mjerumani bingwa wa



    masuala ya urutubishaji wa mayai ya uzazi na masuala ya viumbe vidogo ambaye kwa Kiingereza walimwita Consultant Embryologist.



    Daktari huyu maarufu nchini Ujerumani alikuwa amewasaidia watu wengi ambao hawakuwa na tegemeo la kupata mtoto, hatimaye kufanikiwa, nguli wengi



    kutoka Hollywood huko Marekani walimiminika katika Jiji la Berlin kupata huduma yake iliyowafanya baadhi kuzaa mpaka watoto pacha.



    “Nina habari njema!” Tyra alimwambia Phillip aliporejea kutoka kazini na kumkuta ameketi sebuleni akiwa mwenye mawazo mengi, Phillip akanyanyua kichwa



    na kumwangalia.

    “Habari gani?”

    “NImepata daktari wa kutusaidia tatizo letu.”

    “Wapi?”



    “Ujerumani.”

    “Ujerumani? Umempataje?”

    “Mtandaoni.”

    “Kweli?”

    “Ndiyo, ningependa tumjaribu naye.”



    “Siyo gharama kubwa?”

    “Ni kubwa lakini tutamwambia baba atusaidie…” Tyra hakumalizia sentensi yake simu ya mkononi ikaita, mara moja akabonyeza kitufe cha kupokea na kuiweka



    sikioni, akaanza kuongea.

    “Halo! Halo! Nini? Mama mbona unalia?...Nakuja.” Aliuliza maswali kwa mshituko.

    “Kimetokea nini tena?” Phillip aliuliza.

    “Baba ameanguka bafuni…. Twende haraka”



    Ilikuwa imetimu saa kumi na nusu jioni wakati wanaingia ndani ya gari, Phillip akiwa kwenye usukani na kuendesha moja kwa moja kuelekea nyumbani kwa



    wazazi wake Upanga wakitokea Mikocheni. Walipofika walipewa taarifa kuwa mzee alikimbizwa Hospitali ya Muhimbili, hawakutaka kupoteza muda wao



    hapo, gari ikageuzwa na kunyoosha hadi Muhimbili Idara ya Wagonjwa Mahututi ambako walikuta mama yake Tyra akilia, huku wauguzi na majirani wakiwa



    wamemzunguka.



    “Mama nini?”

    “Baba yako katutoka.”

    Tyra alianguka chini na kuanza kugalagala huku akilia kwa uchungu, Phillip akawepo kumnyanyua hadi kwenye gari ambako alianza kumbembeleza na kumpa



    maneno ya kumtia moyo. Ukweli haukubadilika, taarifa ilipotolewa baadaye na daktari ilithibitisha kuwa mzee huyo alikuwa amefariki kwa shambulio la moyo,



    Tyra alilia kupindukia kwa siku zote mpaka walipomzika huko Machame mkoani Kilimanjaro mamia ya watu wakiwa wamehudhuria kumzika mtu tajiri.



    Mpaka mwezi mmoja baadaye, Tyra na Phillip walikuwa bado wako kijijini Machame wakiomboleza msiba, tatizo lao la kukosa mtoto lilishapotea kabisa



    ubongoni, kilichokuwa kikifikiriwa wakati huo ni msiba mzito ulioipata familia.

    Kikao cha ndugu kilipokaa, mwanzoni mwa mwezi wa pili Tyra alisimikwa kuwa mrithi wa utajiri wote wa baba yake uliokadiriwa kuwa mamilioni ya dola



    yakiwa katika viwanda na biashara mbalimbali, kufumba na kufumbua jina la Tyra likabadilika, akaanza kuitwa Mkurugenzi.



    Kutajirika kwa Tyra, kulikuwa pia kutajirika kwa Phillip, watu hawa wawili walikuwa mtu na mke wake, hivyo kila alichokuwa nacho Tyra kilimstahili Phillip



    na alichokuwa nacho Phillip pia kilimstahili Tyra. Wote wakaacha kazi ili wasimamie mali za familia, pamoja na utajiri wote huo suala la mtoto liliwasumbua,



    walihitaji mtoto, hiyo ilikuwa furaha yao.



    “Kwanini tusisafiri kwenda Ujerumani kumuona Dk. Kohrer? Tuna fedha ya kutosha sasa kulifanya jambo hili.” Ilikuwa ni sauti ya Tyra siku moja wakiwa



    wamelala ndani ya chumba chao kikubwa chenye kila kitu.



    “Sina tatizo. Nahitaji sana mtoto mke wangu, inaniumiza sana mimi kuwa chanzo cha tatizo hili”

    “Usijali, hatuhitaji mtoto tu, tunahitaji watoto pacha kwa mara ya kwanza ili tufidie muda uliopotea, niko tayari kulipa chochote kwa daktari huyo ili awezeshe



    mimi kupata watoto wawili kwa wakati mmoja.”



    “Nitafurahi mno.”

    Kama utani, mwezi mmoja baadaye walikuwa ndani ya ndege ya shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa, shirika la gharama kubwa pengine kuliko mengine yote



    duniani, wakiwa wameketi kwenye daraja la watu maarufu. Hii ilikuwa safari ya kwenda kwenye Jiji la Berlin kuonana na daktari aliyewasaidia watu wengi

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kupata watoto.



    Ilikuwa ni safari ya saa kumi na mbili, kwanza waliruka mpaka Amsterdam, Uholanzi, ambako waliunganisha na ndege nyingine ya shirika hilo hilo hadi Berlin,



    wakapokelewa na wafanyakazi wa Hospitali ya Freiburg ambao waliwapeleka kwanza hotelini ili wapumzike na siku iliyofuata waweze kumwona Dk. Kohrer.



    Mioyoni mwao walijawa na furaha kubwa kama vile tayari walishapata watoto waliowatarajia, hakuna walichokihitaji zaidi ya watoto wawili kwa wakati mmoja



    tena wote wawe ni wa kike.





    PHILLIP alikuwa akikoroma huku mkewe akiwa amemkumbatia, walionekana kuufaidi usingizi lakini ghafla Genevieve aligutuka na kujikuta akitoka jasho



    jingi ingawa chumba chao cha kulala kilikuwa na kiyoyozi.

    “Vipi?” Phillip aliuliza baada ya kuzinduka usingizini na kumkuta mke wake ameketi kando ya kitanda akitetemeka.

    “Sidhani kama ni ndoto.”



    “Kwani vipi?”

    “Nimeota ndoto ya kutisha.”

    “Ndoto gani?”

    “Eti Mzee Mpangala amefariki kwa shambulio la moyo, halafu mimi na wewe tumesafiri kwenda Ujerumani kumuona daktari uliyekuwa unamzungumzia.”

    “Ni ndoto tu, Mzee Mpangala hajafa ingawa ni kweli Dk. Zim Kohrer tumempata.”

    “Inawezekana ni kwa sababu ya mazungumzo yetu ya jana.”



    “Kweli kabisa.”

    “Acha nimpigie baba angalau niongee naye.”

    “Ni usiku sana atakuwa amepumzika.”

    “Phillip! Ni ndoto tu hii, yaani nimeona kila kitu mpaka tukiwa Machame kwenye mazishi.”

    “Ni ndoto tu mke wangu.”



    “Acha niongee na baba.”

    “Haya mpigie.”

    Huku Genevieve akitetemeka, moyo wake ukiwa bado hauamini kama kilichotokea ni ndoto alimpigia baba yake na kuzungumza naye, ingawa hakumweleza



    chochote juu ya ndoto aliyoota. Baada ya maongezi hayo ndipo alirejea kitandani na kujilaza kando ya mume wake, hawakupata usingizi tena muda wote



    walizungumzia habari ya watoto na safari ya Ujerumani.



    Wiki moja baadaye walisafiri mpaka Berlin na kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Schonefeld ambako walipokelewa na wafanyakazi wa hospitali



    ya Freiburg ambao waliwapeleka moja kwa moja hospitalini kuonana na Dk. Zim Kohrer, mzee mfupi na mwenye mvi nyingi na aliyevaa miwani muda wote,



    uso wake ukiwa umejawa na tabasamu.

    “Mnahitaji kupumzika ili tuanze matibabu kesho?” Aliwauliza baada ya salamu ofisini kwake.



    “Hakuna sababu, hatujachoka kiasi hicho, karibu safari yote tulikuwa tumelala vitandani.”

    “Aha! Mmesafiri kwenye daraja la watu wazito bila shaka.”

    “Ni kweli.”

    “Basi tuanze.”



    Dk. Kohrer akafungua kompyuta yake na kuanza kuandika maelezo yao yote tangu walipooana, madaktari waliowaona na namna walivyofanya tendo la ndoa,



    mwisho akamuuliza Genevieve maswali mengi kuhusiana na mzunguko wake wa hedhi. Alipomaliza maswali hayo aliwaeleza juu ya vipimo ambavyo



    vingefanyika katika kulitafuta tatizo.

    “ Kwanza tutaupiga picha mfuko wa uzazi, mirija ya viwanda vya mayai ya Genevieve.



    Pia tutapata manii yako kwa ajili ya kuzichunguza ili tuone kama mbegu zako zina tatizo lolote, lazima tujue idadi yake na kama zina uwezo wa kurutubisha yai



    au la, yote haya ni muhimu tuyafahamu kabla ya kuchukua hatua yoyote.”

    “Hakuna tatizo lolote daktari, tumeacha shughuli zote kuja kukuona na tunaamini utakuwa na jibu la tatizo letu.”



    “Hakuna kisichowezekana, wengi wamepata furaha yao hapa hapa kwenye chumba hiki.” Dk. Kohrer aliongea akitabasamu.

    Kilichofuata siku hiyo ni kuchukuliwa vipimo, zoezi lilipokamilika waliondoka kwenda Hoteli ya Berlin Hilton ambako walifikia. Ilikuwa ni ya nyota tano,



    chumba kimoja kililipiwa dola elfu moja mia tano kwa usiku mmoja. Hapo ndipo Genevieve na Phillip waliamua kuishi mpaka wapate suluhisho la tatizo lao,



    gharama zote zikilipwa na Mzee Mpangala.



    Siku tatu baadaye wakiwa hotelini walipigiwa simu na Dk. Kohrer akiwataka wafike ofisini kwake mara moja kujadiliana juu ya majibu yaliyopatikana, mioyo



    yao ikiwa imejawa hofu na furaha waliondoka hadi ofisini kwake na kumkuta akiwasubiri kwa hamu kubwa. Tofauti na nyuso zao kuwa na wasiwasi, Dk.



    Kohrer alikuwa na uso wenye furaha na matumaini.

    “Tumekuja daktari.”



    “Imebidi niwaite maana majibu yote yamekamilika.”

    “Sawasawa.”

    “Itabidi niwe mkweli maana lengo ni kusaidia.”

    “Hakuna tatizo.”

    “Uchunguzi unaonyesha kwamba Genevieve huna tatizo lolote kabisa, tatizo liko kwa mumeo, Phillip…” Dk. Kohrer alimalizia kwa kuita.

    “Naam.”



    “Mbegu zako hazitoshi, ni chache na zaidi ya kuwa chache pia hazina mbio, zinashindwa kulifikia yai la mwanamke ili mimba itungwe. Nilipozichunguza zaidi



    nikagundua hata kama zikilifikia yai hazina uwezo wa kutungisha mimba, nimekuja kwenu na jibu lifuatalo, kama kweli mnahitaji mtoto hamna jinsi zaidi ya



    kutafuta mbegu za kiume za mtu mwingine ili tufanye kitu kiitwacho IVF.”

    “IVF ni nini daktari?”



    “Kirefu chake ni In Vitro Fertilization, kitakachofanyika hapo ni kuchukua mbegu za Genevieve na kuziunganisha na mbegu za mwanaume mwingine ili mimba



    itungwe kisha nitaipandikiza ndani ya tumbo la mkeo na itakua vizuri mpaka mpate mtoto au watoto mapacha kama mnataka.”

    “Inawezekana daktari?” Phillip aliuliza.



    “Kwanini isiwezekane, hizo ndizo kazi zangu, huwa nazifanya kila wiki.”

    “Mtu wa kutoa mbegu za kiume tutampata wapi?”

    “Tutatanganza mtandaoni, atajitokeza mtu na kulipwa si chini ya dola elfu kumi ili atoe mbegu zake. Kama mko tayari mnaweza mkaniambia niendelee na



    utaratibu wa kumtafuta mtoa mbegu, gharama zangu mimi zitakuwa dola elfu ishirini na mbili kwa mtoto mmoja na mara mbili yake kwa watoto pacha.”



    “Tuko tayari daktari, tunachohitaji sisi ni watoto.” Phillip aliongea uso wake ukiwa umeinamishwa chini ni kweli alikuwa hajisikii vizuri kuwa na watoto ambao



    si damu yake lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali.



    “Basi kesho fanyeni malipo ili mambo yafanyike haraka.”

    “Tutalipa daktari, wewe tafuta tu mtu wa kutoa mbegu.”

    “Hii hapa ndiyo namba ya akaunti yangu, mnaweza kuniingizia fedha hizo moja kwa moja pale NedBank.”

    “Hakuna shida.”



    ***

    Novotroitsk, Urusi.

    Kilikuwa ni kipindi cha majira ya baridi nchini Urusi, watu wengi walijifungia ndani ya nyumba zao ambao waliwasha mitambo ya kuongeza joto. Watu kidogo



    sana kwenye mitaa ya mji wa Novotroitsk, maarufu kwa viwanda vya vyuma duniani, walikuwa nje sababu ya baridi. Barafu zilikuwa zimeganda juu ya ardhi,



    kiasi cha kuyafanya hata magari yashindwe kutembea kwa mwendo wa kasi.



    Katika hali hii mtu mmoja aitwaye Victor Fedorov, alikuwa nje akipigwa na baridi, hakuwa na mahali pa kuishi, alikuwa maskini kama walivyo maskini wengine



    wengi barani Afrika ingawa aliishi katika taifa lenye utajiri mkubwa. Moyoni alijawa uchungu, akitamani siku moja kuwa na mafanikio ndiyo maana alikimbia



    jijini Moscow alikozaliwa kuja kutafuta maisha kwenye mji huu mdogo wenye idadi ya watu wasiozidi laki moja kwenye mpaka wa Urusi na Kazakhstan.



    “Siku moja nitafanikiwa tu, sina sababu ya kuendelea kuishi Moscow wakati sina hata familia, mke na watoto wangu walishanikimbia sababu ya umaskini..”



    Aliwaza Victor.

    Kila alipotaka kupata joto aliingia kwenye vyumba ambavyo vilitoa huduma kwenye mtandao wa Intaneti kwa malipo, akalipa fedha kidogo na kupata joto huku

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akitafuta taarifa mbalimbali mtandaoni. Mchana wa siku hiyo baridi ilipomzidi alielekea kwenye chumba kimoja cha huduma hiyo na kuingia ndani ambako



    alilipia na kuonyeshwa kompyuta, akakaa na kufungua kisha kuanza kupita kwenye mitandao mbalimbali.



    “Sperm donor needed urgently! Ten thousand dollars will be paid.” (Mtu wa kutoa mbegu za kiume anahitajika haraka, dola elfu kumi zitalipwa.) Aliyasoma



    maneno hayo kwenye mtandao na moyo wake kushituka, alihitaji fedha kuliko kitu kingine chochote wakati huo na aliamini dola elfu kumi zingetosha kabisa



    kuanzisha biashara ya kununua vyuma na kuuza, kwa muda mrefu sana alikuwa ametamani kufanya hivyo lakini kikwacho kilikuwa ni mtaji.



    Haraka akajaza fomu iliyokuwepo akielezea utambulisho wake na mahali alipokuwa nchini Urusi ikiwa ni pamoja na kuweka anwani ya barua pepe na namba



    yake ya simu, baada ya kumaliza akaendelea na kupitia mitandao mingine. Masaa mawili kabla hajatoka ndani ya chumba hicho, simu yake iliita, namba



    iliyoonekana kwenye kioo haikuwa ya Urusi.

    “Halo!”

    “Halo! Victor?”



    “Ndiyo.”

    “Naitwa Dk. Kohrer, napiga simu kutoka Ujerumani nimeiona fomu yako sasa hivi mtandaoni kwamba uko tayari kutoa mbegu kwa gharama ya dola elfu kumi.”

    “Ndiyo.”

    “Unaweza kunielezea jinsi ulivyo?”

    “Ni Mrusi, mweupe, mrefu na nina nywele nyeusi.”



    “Unaweza kupiga picha na kunitumia sasa hivi?”

    “Niko kwenye chumba cha Intaneti, hivyo ndani ya dakika kumi nitakuwa nimeishatuma.”

    “Nasubiri, nikishaipokea mara moja nitakupigia.”



    Dakika kumi na tano baadaye walikuwa kwenye simu tena, Dk. Kohrer akiongea na Victor kumthibitishia kuwa alikuwa amekubalika na angesafirishwa hadi



    Ujerumani kwa ajili ya kutoa mbegu ingawa kwa sharti moja tu kwamba hakutakiwa kukutana na watu ambao walihitaji mbegu yake, kazi yake ingekuwa ni



    kutoa mbegu, kulipwa na kuondoka.



    “Hilo si tatizo kwangu, cha muhimu ni malipo.”

    “Hakuna shida, nitakutumia sasa hivi namba ya tiketi na fedha ya matumizi njiani ili kesho usafiri kuja hapa Berlin.”

    “Hakuna shida.”









    BAADA ya Phillip na Genevieve kukubaliana na Dk. Kohrer juu ya gharama zinazohitajika kwa ajii ya kufanya IVF, njia ya kupandikiza mbegu za mwanaume



    mwingine ndani ya mji wa uzazi wa Genevieve kwa lengo la kupata mtoto, wawili hao walikamilisha malipo kupitia Benki ya NedBank kama walivyokubaliana



    na kilichofuatia ikawa ni kumtafuta mwanaume ambaye atakubali kutoa mbegu zake kwa malipo ya dola elfu kumi.



    Baada ya kutangaza mtandaoni, Victor Fedorov, mwanaume fukara anayeishi kwenye Mji wa Novotroisk, Urusi alijaza taarifa zake mtandaoni kuonesha kuwa



    yupo tayari kuchangia mbegu zake za kiume kwa malipo ya dola elfu kumi. Baada ya kujaza taarifa zake, Dk. Kohrer alimpigia simu na wakakubaliana kufanya



    kazi hiyo haraka kwa sharti moja la kutokutana na watu waliokuwa wakihitaji mbegu zake.



    Baada ya makubaliano,Victor alitumiwa tiketi ya ndege mpaka Ujerumani na siku iliyofuatia akawa tayari amewasili kwenye Hospitali ya Freiburg aliyokuwa



    akifanyia kazi Dk Kohrer.



    “Karibu bwana Victor, naitwa Zim Kohrer, mtaalamu wa embryology, kama tulivyozungumza kupitia mtandao, kuna biashara hapa ya kuuza mbegu zako za



    kiume kwa ajili ya kuwasaidia wanandoa wenye matatizo ya kupata mtoto.



    Hundi yako ya dola elfu kumi hii hapa, cha msingi twende maabara ukafanyiwe vipimo kuona kama huna matatizo yoyote kisha mambo mengine yatafuatia,” Dk.



    Kohler alikuwa akizungumza na mwanaume mrefu, mweupe mwenye nywele nyeusi, Victor kutoka Urusi.



    Hakuwa na kipingamizi chochote, kwake fedha ndiyo kitu alichokuwa anakihitaji kuliko vitu vyote. Baada ya kuingizwa maabara na kufanyiwa vipimo vya kina



    kuchunguza kama hakuwa na tatizo lolote, majibu yalipotoka alionekana kuwa na afya njema.



    Kilichofuatia ikawa ni kuingizwa tena kwa mara nyingine maabara ambapo alitolewa mbegu zake za kiume kwa kutumia utaalamu wa hali ya juu. Alipomaliza



    alikabidhiwa hundi yake kisha akaaga na kuondoka. Kwake ile ilikuwa ni zaidi ya bahati ya mtende kuota jangwani. Ufukara uliomtesa kwa kipindi kirefu hadi



    kusababisha mkewe na wanaye wamtoroke, sasa ulikuwa umefikia mwisho.



    Kwa kutumia dola elfu kumi alizozipata, alipanga kuanzisha biashara ya kununua vyuma na kwenda kuviuza, kazi ambayo aliitamani kwa siku nyingi lakini



    akawa anakwama kutokana na kukosa mtaji.

    Hakutaka kupoteza muda, jioni ya siku ile ile kwa kutumia tiketi aliyokuwa amekatiwa na Dk. Kohrer, alisafiri hadi Novotroisk, mji aliokuwa akiishi na



    kuanzisha biashara ya kununua vyuma kama alivyopanga.



    *******

    Phillip na Genevieve walikuwa chumbani kwao ndani ya hoteli wakiendelea kufarijiana, mara simu ya mezani ikaita. Kwa haraka, Phillip aliinua mkonga na



    kuongea na upande wa pili. Alikuwa ni Dk. Kohrer akiwataarifu kuwa kazi ya kupata mwanaume wa kutoa mbegu za uzazi tayari imekamilika na aliwataka



    wafike haraka hospitalini kwa ajili ya Genevieve kuchukuliwa mbegu zake tayari kwa kuunganishwa na mbegu ya mwanaume aliyepatikana, ambaye wote



    hawakutakiwa kukutana naye.



    “Mke wangu, kila kitu kipo tayari, daktari amesema tujiandae kwenda hospitali sasa hivi,” aliongea Phillip kwa furaha huku akimkumbatia mkewe. Kwa pamoja



    walimshukuru Mungu kwani hawakudhani kuwa kazi ya kumpata mtoa mbegu ingekuwa rahisi kiasi kile.

    Baada ya kujiandaa, Phillip na mkewe walishuka ngazi hadi kwenye maegesho ambako dereva wa hoteli alikuwa akiwasubiri, wakaondoka wakimhimiza



    aendeshe kasi hadi Hospitalini, gari likaegeshwa na wakashuka na kwenda moja kwa moja hadi ofisini kwa Dk. Kohrer aliyekuwa akiwasubiri.



    Bila kupoteza muda aliwaeleza mafanikio ya mpango wao huku akiwaonesha picha ya mwanaume aliyetoa mbegu zake na kila mmoja akaridhika na mwonekano



    wake.

    “Hamtakiwi kukutana naye kabisa, wala yeye hapaswi kukutana nanyi ili mradi amekwishatoa mbegu, kazi yake imekwisha!” Aliongea kwa msisitizo Dk. Kohrer.



    Kilichofuata kikawa ni Genevieve kuchukuliwa hadi chumba cha upasuaji mdogo ambapo zoezi la kuzinyonya mbegu kwenye viwanda vyake vya mayai



    lilifanyika, bahati nzuri alikuwa katika kipindi ambacho mayai yake yalikuwa tayari kwa kurutubishwa.



    Ilikuwa ni operesheni ndogo lakini ilichukua muda wa masaa matatu, ndipo mayai yakapatikana na Dk. Kohrer kuyachukua kwenye chombo maalum kiitwacho



    Incubator hadi maabara ambako alishirikiana na wataalamu wengine kuliunganisha moja ya mayai hayo na mbegu ya Bwana Victor Fedorov iliyogandishwa,



    ambaye tayari alikuwa ndani ya ndege akirejea Urusi.



    Zoezi la kurutubisha na kupandikiza kiumbe hicho ndani ya mfuko wa uzazi wa Genevieve na uchunguzi kama hakikuwa na matatizo yoyote lilipokamilika



    masaa arobaini na nane baadaye, alipewa muda wa mwezi mmoja kupumzika wodini ili kuhakikisha kiumbe hicho kinapata muda wa kuzamisha mizizi yake



    kwenye mfuko.



    Mambo yote yalipokamilika ikiwa ni pamoja na kulipa gharama zote zilizokuwa zinahitajika, Phillip na Genevieve waliruhusiwa kurejea Tanzania kwa



    makubaliano ya kuendelea kuwasiliana na Dk. Kohrer katika hatua zote za ukuaji wa ujauzito ule.

    Saa kadhaa baadaye wakawa ndani ya ndege ya shirika la usafiri wa anga la Ujerumani, Lufthansa. Mioyo yao ikiwa imejawa na furaha, hakika safari yao ilikuwa



    ya mafanikio makubwa.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walipowasili Dar es Salaam, waliendelea na maisha yao kama kawaida na baada ya wiki kadhaa kupita, Genevieve akaanza kuonesha dalili zilizoamsha



    matumaini mapya kwao. Alianza kusikia kichefuchefu na kuanza kuchagua aina ya vyakula.



    “Kaniletee ndimu mume wangu, halafu samaki wabichi siwatamani hata kuwaona, wananifanya nijisike kichefuchefu,” aliongea Genevieve kwa kudeka akiwa



    amejilaza kwenye kifua cha mumewe. Dalili zile zilimfurahisha zaidi Phillip kwani aliamini sasa na yeye atapata heshima kama wanaume wengine wenye



    familia.



    Mwezi wa nne wa ujauzito huo ulipoingia, afya ya Genevieve ikiwa nzuri, walikwenda hospitali kupima ili wapate uhakika wa jinsi mtoto alivyokuwa



    akiendelea kukua. Wakati wa kuwapa majibu, sura ya daktari ilikuwa imejawa na tabasamu.

    “Mimba inaendelea vizuri sana, tena nina habari nzuri za kuwapa... Genevieve una mimba ya watoto pacha!”



    “Asante Mungu, furaha yangu itakuwa mara mbili!”

    Hakuna aliyekuwa anaelewa namna walivyofanikisha suala lile la Genevieve kupata ujauzito, wakaendelea kuifanya siri kama walivyokuwa wamekubaliana.



    Kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda mbele, ujauzito wa Genevieve ulizidi kuongezeka, tumbo lake likawa kubwa, hali iliyowafanya wote wawili



    kujisikia fahari kubwa mioyoni mwao.



    Ujauzito wake ulipofikisha miezi sita, Genevieve alilazimika kupumzika nyumbani na kuacha shughuli zote alizokuwa akizifanya, kama walivyokuwa



    wameshauriwa na Dk. Kohrer, lengo la kufanya hivyo likiwa ni kuzuia ujauzito ule kuharibika katika hatua za mwisho. Phillip akawa na kazi ya kumtunza



    mkewe kwa uangalifu, huku wakizidi kumuomba Mungu wao kila uchao.



    Hatimaye miezi tisa ilitimia, Genevieve akashikwa na uchungu wa kujifungua. Kwa kuwa Phillip alikuwa amemuandalia mkewe kila kitu, alipoanza kuonesha



    dalili za uchungu tu, alimkimbiza haraka hospitali.



    Alipofika mapokezi akiwa anaendesha gari mwenyewe, Phillip aliwasiliana na manesi wakunga ambao kwa haraka walisogeza kitanda cha magurudumu karibu



    na gari lake, Genevieve akateremshwa na kuwekwa juu yake, akawa anakimbizwa kuelekea kwenye wodi za wazazi huku akijinyonganyonga kutokana na



    maumivu makali aliyokuwa akiyahisi.



    Aliwekwa kitandani, Phillip akawa kando yake akishuhudia hatua kwa hatua namna mke wake alivyokuwa akifanya kazi ya kuwaleta watoto hao duniani!



    Jukumu lake lilikuwa ni kumfariji na kumtia moyo.







    Hospitali ya Aga Khan ilikuwa umbali wa kama mita mia mbili na hamsini tu kutoka walipoishi Phillip na Genevieve, ilikuwa hospitali kubwa ya gharama pale



    ambapo mtu alihitaji huduma kutoka kwa madaktari wake. Kwenye chumba ambacho mlangoni kilikuwa na kibao kilichoandikwa “Labour Room” ndimo



    alimokuwa amelala Genevieve akihangaika na maumivu, Phillip akiwa kando yake, akimpapasa tumbo na kiuno kama njia ya kumpunguzia maumivu.



    “So painful!” (Inauma sana.) aliongea machozi yakimtoka.

    “I know, just be strong because soon you are going to be happy. Our dream is going to be realized and you are the dream bearer” (Najua, kuwa imara tu, sababu



    muda si mrefu utafurahi, ndoto yetu itatimia na wewe ndiye uliyeibeba ndoto.) Phillip alimwambia mke wake.



    Wauguzi walikuwepo muda wote kutoa kila aina ya msaada uliohitajika lakini kwa saa zote kumi na mbili lakini bado Genevieve hakuweza kujifungua, daktari



    akafikia uamuzi wa kumchoma sindano ya kuongeza uchungu, Oxytocin, ambayo ilipochomwa tu, muda wa kama masaa matatu baadaye, mtoto wa kwanza wa



    kike alitoka na akafuatiwa na mwingine wa pili ambaye pia alikuwa wa kike.



    Genevieve akainua kichwa chake na kuwaangalia watoto wake, machozi ya furaha yakamtoka, Phillip akasogea karibu na kumkumbatia. Hakika ndoto ilikuwa



    imetimia, haikujalisha kabisa mbegu za watoto hao zilitoka wapi, walikuwa ni watoto wao, Mungu alikuwa amewapa ili wawalee na kuwatunza.

    “Mwaaa!” Phillip alimbusu mke wake usoni.



    “Thank you, finally we are going to be the happiest couple on earth.” (Asante, hatimaye tutakuwa wanandoa wenye furaha kuliko mwingine yeyote duniani.)

    “Yeah!” (Ndiyo.)

    Watoto waliondolewa na kupelekwa kwenye chumba maalum ambako walivalishwa nguo na kufanyiwa huduma zote, Genevieve akatundikiwa dripu ya maji ya



    Glucose ili kumuongezea nguvu mwilini maana alikuwa amedhoofika sababu ya kusukuma watoto kwa muda mrefu. Masaa mawili baadaye, Phillip akiwa bado



    na mke wake wazazi wa Genevieve waliingia, wakiongozwa na mzee Mpangala, wote nyuso zao zilikuwa zimejawa na furaha.



    “Hongera mwanangu.”

    “Asante baba, nimekuletea wake wazuri wawili, kama ndoto yangu ya kwamba umekufa niliyoota ingekuwa kweli, basi ungewakosa.” Genevieve aliongea



    akiikumbuka ndoto mbaya aliyoota kabla hawajasafiri kwenda Ujerumani kuonana na Dk. Kohrer.



    “Ilikuwa ni ndoto tu mwanangu, hongera sana, ukoo unazidi kuongezeka.”

    “Kweli baba.”

    Ilikuwa ni siku ya furaha mno kwa kila mmoja wao, kitu kilichomsumbua Phillip moyoni ni historia ya watoto hao, bado alielewa kabisa uwazi kwamba hakuwa



    baba yao halisi. Kwa mbali hili lilimuumiza, kwani hakujua nini kingetokea iwapo yeye na Genevieve siku moja wangeshindwa kuelewana na hatimaye



    kutengana, hiyo ilimaamnisha angeweza kuambiwa watoto wale hawakuwa wake. Akajipa moyo kwamba Genevieve asingeweza kumfanyia kitendo hicho.



    Muda mfupi baadaye watoto walitolewa chumbani walikopelekwa na kuletwa kitandani kwa Genevieve, wakalazwa kando yake, kwa furaha akawafunua na



    kuanza kuwabusu.

    Mzee Mpangala na watu wote waliokuwa chumbani walionyesha mshituko kwa rangi za watoto hao hazikuwa za Waafrika halisi lakini hakuna aliyediriki



    kufungua mdomo wake kuulizia jambo hilo.

    “Wanafanana sana na marehemu bibi yetu mzaa mama, yeye alikuwa na asili ya Kibeligji,” Phillip aliongea baada ya kuzisoma kwa makini nyuso za watu

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    waliokuwemo chumbani na kuugundua wasiwasi wao, hakutaka mtu yeyote aelewe siri ya kupatikana kwa watoto hao.



    “Duh! Tulitaka kushangaa, imekuwaje nyinyi Waafrika mzae watoto wa aina hiyo.” Mzee Mpangala aliongea.

    Hawakukaa sana baada ya hapo, ndugu na marafiki wakaondoka na kuwaacha Phillip na Genevieve peke yao wakiendelea kuweka msimamo wa kuificha siri ya



    watoto hao. Siku mbili baadaye waliruhusiwa kuondoka hospitali na kurejea nyumbani Upanga ambako furaha iliendelea mtindo mmoja, ndugu na jamaa



    wakiendelea kumiminika kuwaona watoto pacha wa Genevieve na Phillip.

    “Naomba nipewe nafasi ya kuwapa watoto wangu majina.” Genevieve aliongea mbele ya ndugu na jamaa.

    “Endelea.” Watu wote wakaitikia.



    “Hawa watoto wataitwa Dorice na Dorica!”

    “Yupi Dorice, yupi Dorica?” Phillip akauliza.

    “Wa kwanza kutoka ni Dorica na wa pili ni Dorice!”



    Makofi yakapigwa watu wakishangilia, majina yalikuwa yamewafanana kabisa watoto kwa jinsi sura zao zilivyokuwa nzuri. Miezi mitatu baadaye watoto



    wakiendelea kukua vizuri, Phillip alirejea kazini kwake kwenye kampuni ya simu za mikononi iliyoitwa T-Mobile ambako alifanya kazi kama mwanasheria na



    Genevieve akaendelea kufanya kazi kwenye kampuni ya baba yake ambako alitumia elimu yake ya uchumi akiwa Mkurugenzi Msaidizi, lengo la Mzee Mpangala



    lilikuwa ni kumrithisha kila kitu ili aendeleze mambo aliyoyafanya, muda wa kustaafu ukifika.



    Miezi tisa baadaye watoto walitimiza mwaka mmoja, sherehe kubwa ya kuzaliwa kwao ikafanyika, mpaka wakati huo hakuna mtu hata mmoja aliyejua siri ya



    namna walivyopatikana. Dk. Kohrer alialikwa siku hiyo kusherehehea mafanikio lakini aliombwa kutoongea chochote juu ya namna mimba ilivyotungwa, hiyo



    ilitakiwa kubaki siri mpaka mwisho wa dunia.



    ***

    Victor Fedorov alipoingia nchini Urusi, taarifa ya kwanza aliyoipokea ni juu ya kifo cha mke na watoto wake kwenye milima ya barafu walikokwenda kushiriki



    mchezo wa kuteleza kwenye barafu. Ingawa siku zote alimchukia mke wake, Fedorov aliwapenda mno watoto wake Misha na Kunin, alilia na kuomboleza,



    kilichomsikitisha zaidi ni kwamba hakuweza kuziona maiti zao.



    Kilichofanyika baada ya hapo maishani mwake, hakikuwa kufanya biashara ya vyuma kama alivyokuwa amepanga baada ya kupokea dola elfu kumi kutoka kwa



    Dk. Kohrer, akaamua kuingia kwenye ulevi. Kazi yake kubwa ikawa kunywa na kulewa, lengo likiwa ni kupoteza mawazo ya kupoteza mke na watoto, maisha



    yakaharibika, akawa mtu wa kulala baa na mtaani.

    “Sina sababu ya kufanya kazi au biashara tena, acha ninywe tu.” Aliwaza na kila siku hilo ndilo jambo alilofanya; kunywa.



    Miezi mitatu baadaye, fedha zote ilikuwa imekwisha, akaanza kuteseka tena. Mwisho akiwa amebakiza dola tano mfukoni aliamua kuitumia kununua tiketi ya



    bahati nasibu kubwa iliyokuwa ikifanyika nchini Urusi, zawadi yake ikiwa dola milioni moja kwa ambaye angeshinda. Alifanya hivyo kama jaribio la bahati yake,



    ingawa hakuwa na uhakika wa kushinda.







    Be the next Millionaire, ulikuwa ni mchezo mkubwa sana nchini Urusi, maelfu ya watu walishiriki wakijaribu bahati yao. Kila mwaka alipatikana mshindi



    mmoja tu katika nchi hiyo kubwa yenye idadi ya watu wasiopungua milioni 141, ushindani ulikuwa mgumu, hata Victor aliponunua tiketi yake alijua



    angeshindwa, hata hivyo alitaka kujaribu kwa sababu hakuwa na jambo jingine la kufanya.



    “Huwezi jua pengine naweza kushinda, hakyanani nikipata fedha tena safari hii sitafanya mchezo, namuahidi Mungu kwamba nitabadilika kabisa, sitakunywa



    pombe tena na nitatoa sehemu ya kumi kwake kama Zaka…Ee Mungu nisaidie”

    Aliitunza tiketi yake kwenye karatasi la nailoni ili isiweze kuharibika kwa unyevunyevu uliosababishwa na umande, kila siku jioni akiwa mtaani kwenye veranda



    alilolala ilikuwa ni lazima aifungue na kuanza kuzisoma namba zake.



    “18243004!” alitamani siku ya kutangazwa mshindi namba hiyo ndiyo isomwe, akiteseka kwa ubaridi aliendelea kusubiri mtaani kwa hamu kubwa, akipata



    msaada wa fedha ya chakula kwa kuombaomba kwa wapita njia, moyoni akijilaumu kwa kuchezea fedha aliyopata baada ya kuuza mbegu.

    “Siku itafika tu! Matangazo yatoke kwamba mimi ndiye mshindi wa Bahati Nasibu…ni Machi 16, siyo mbali, itafika tu!” aliwaza Victor akiwa mtaani.



    ***

    Dorice na Dorica walikuwa wazuri mno, kila mtu aliwapenda, tena walikuwa ni wapole waliobebwa na kila mtu. Watu hawakusita kusema wangesumbua sana



    vijana wa kiume kama wangefikisha umri wa miaka kumi na sita, sura zao zilikuwa ni mchanganyiko wa baba na mama yao ambao kwa hakika walikuwa na



    mvuto wa kutosha.



    Wakaendelea kukua vizuri, siri ya walivyopatikana ikaendelea kufichwa, watu wote mpaka familia waliamini mbegu za Phillip ndizo zilizotumika jambo ambalo



    halikuwa kweli. Jambo hilo halikutakiwa kabisa kuvuja, hata wao wenyewe waliliongelea mara chache na hawakupenda kabisa lijitokeze, Genevieve



    alimheshimu Phillip kama baba wa watoto wake.



    “Hivi itakuwaje kama itakatokea siku moja siri ikavuja na aliyetoa mbegu zake akajitokeza na kudai Dorice na Dorica ni watoto wake?” Phillip alimuuliza mke



    wake siku moja akicheza na watoto wake sebuleni.

    “Haiwezekani, atajuaje?”

    “Huwezi kuelewa, lakini ikitokea hivyo, nakuhakikishia mke wangu kwamba nitakufa au nitaua mtu, hawa ni watoto wangu kabisa, ndivyo ninavyojisikia



    ingawa sikutoa mbegu, nawapenda kuliko kitu kingine chochote maishani mwangu, najua ndiyo watarithi kila kitu nitakachokipata!”



    “Ina maana unawapenda kuliko hata mimi mama yao?”

    “Siyo hivyo mke wangu, nyote nawapenda kwa upendo mmoja, teh! teh! teh!” Phillip alimaliza kwa kucheka.

    Miaka miwili na nusu baadaye Genevieve akiendelea kuendesha kampuni za baba yake kama Mkurugenzi Mkuu na Phillip akipandishwa cheo kuwa Mwanasheria



    Mkuu wa T-Mobile, Dorice na Dorica waliandikishwa chekechea katika shule ya Awali iitwayo Upanga Maranatha Kindergaten school.



    Ilikuwa ni siku ya furaha mno kwa watoto na hata wazazi wao, huko walijifunza kuandika, kuimba, kusoma na hata kuhesabu na uwezo wao ulikuwa mkubwa



    sana kuliko watoto wengine kituoni hapo, jambo hili liliwapa Phillip na Genevieve tumaini kubwa.

    “Wanaendelea vizuri sana, tumaini letu ni kwamba hata wakianza darasa la kwanza watakuwa na akili hivi hivi!” Ilikuwa ni sauti ya mwalimu akiwaeleza Phillip



    na mke wake siku ya mkutano wa wazazi na walimu shuleni.



    “Tutafurahi mno, ahsanteni sana kwa jinsi mnavyowafundisha watoto wetu”

    “Pia ninyi, kwa ushirikiano mnaotupa na malezi bora kwa watoto, hiyo inafanya kazi ya kuwafundisha iwe rahisi, ni wasikivu sana na wana adabu”

    Miaka miwili baadaye na nusu baadaye, Dorica na Dorice wakiwa na umri wa miaka mitano taratibu za kuwatafutia shule ya kuanza darasa la kwanza zilianza



    kufanyika, walikuwa wamekuwa kiasi cha kutosha, kiasi kwamba haikuonekana sababu yoyote ya kusubiri mpaka watimize umri wa miaka saba ambao watoto



    wengi walianza nao darasa la kwanza.



    “Mom I am so happy, tomorrow am going to be a big girl!” (Mama nina furaha mno, kuanzia kesho nitakuwa msichana mkubwa) ilikuwa ni sauti ya Dorica



    akimwambia mama yake huku uso wake ukiwa umejawa na tabasamu lililomfanya azidi kuvutia na kufanana kabisa na mama yake.

    “Me too mom!” (Mimi pia mama) Ilikuwa ni sauti ya Dorice.

    “Why?” (Kwanini?)

    “We are going to start Primary School!” (Tutaanza darasa la kwanza) wote wawili wakaitikia wakimkumbatia mama yao.



    Siku hiyo walilala usingizi wa mang’amung’amu, wakiifikiria siku iliyofuata, ya kwanza kuanza darasa la kwanza. Ilibaki kidogo tu walale wamevalia sare za



    shule kwa furaha waliyokuwa nayo. Phillip na mke wake walicheka sana, wao pia walilazimika kuingia kitandani saa nane usiku sababu wasingeweza kuwaacha

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    watoto wakiwa macho peke yao.



    Kulipokucha Phillip na mke wake walishirikiana kuwaandaa, baadaye Phillip aliondoka akimwacha Genevieve ili muda ukifika awapeleke kwenye kituo ambako



    basi la Shule ya Holy Ghost lingepita na kuwachukua, baada ya hapo ndiyo yeye angerejea nyumbani kuendelea na shughuli nyingine.



    ***

    Mamilioni ya watu nchini Urusi walikuwa nyuma ya runinga zao, ilikuwa ni siku ya Machi 16, kila mtu mkononi akiwa ameshika kipande cha karatasi, kilikuwa



    ni tiketi ya Bahati Nasibu ya Be the next Millionaire, kila mmoja aliamini yeye ndiye angekuwa mshindi na maisha yake yangebadilika kuanzia siku hiyo.



    Victor Fedorov, alikuwa nje ya baa iitwayo Zona, ambako watu wengi maarufu walikwenda kuburudika siku za mwisho wa wiki. Alikuwa hapo akiomba kwa



    watu waliokuwa wakiomba kuingia na kutoka ndani ya baa hiyo maarufu, yeye pia alikuwa na kipande chake cha tiketi mkononi, akichungulia ndani kwenye



    runinga kubwa iliyokuwa ukutani, ambayo ililengwa na macho ya watu wote wakitaka kushuhudia nani angeibuka Milionea.



    “Na mshindi ni mwenye tiketi namba…!” Mtangazaji, msichana mwembamba mrefu mwenye sura ya kuvutia aliyejaa sawasawa kwenye kikoo cha runinga



    alisema, watu wote wakawa kimya, mapigo ya moyo yakisikika namna yalivyogonga kifua, huku macho yao yakiwa yameelekea kwenye kipande cha karatasi na



    masikio yakiwa yameongezewa uwezo wa kusikia. Victor alikuwa kimya, yeye pia akiisoma tiketi yake.

    “Narudia tena mshindi ni mwenye namba 1824300…!”



    “Mungu wangu! Mungu wangu! Mungu wangu!” Victor alisema kwa sauti ya chini chini, mwili wote ukitetemeka na machozi yakimtoka, alikuwa amebakiza



    hatua moja tu maishani mwake awe milionea!

    Kilichofuata baada ya hapo, sekunde chache tu baadaye ni kelele nyingi nje ya ukumbi, mtu akipiga kelele na kushangilia, watu wote wakatoka mbio kwenda



    kuona nini kilichotokea lakini hawakumwona, alishapotelea gizani. Wakarudi ndani kuendelea na vinywaji, kila mmoja wao akisonya na kujisikia ni mwenye



    bahati mbaya.









    …4!” ndivyo alivyomalizia mtangazaji.

    Victor hakuamini alichokisikia, hisia zake zilimtuma kuwa huenda masikio yake yalikuwa yamemdanganya au alikuwa akiota ndoto. Mshindi wa bahati nasibu



    wa dola milioni moja awe yeye? Lilikuwa ni jambo lisilowezekana kwa maskini ambaye hakuwa hata na mahali pa kulaza ubavu wake kuibuka na kitita hicho.



    Kwa hofu kubwa aliyokuwa nayo ya kuuawa na pengine kunyang’anywa tiketi yake, Victor alikimbia umbali wa kama mita mia tano hivi na kuingia chini ya



    daraja ambako alizama huku akihema kwa nguvu katikati ya mapipa mawili ya takataka.



    “Siamini! Ahsante Mungu,” alijisemea moyoni mwake huku akiendelea kububujikwa na machozi ya furaha.

    Hakutoka hapo, wadudu waliendelea kumuuma lakini alijikaza mpaka kulipokucha. Saa kumi na mbili kasorobo ndipo alipoondoka katikati ya mapipa na kuanza



    kutembea kuelekea mjini ambako alianza kuzitafuta ofisi za Be a Billionaire mpaka akazipata na kuketi mbele ya mlango wake.



    Tayari mwanga wa siku ulishajitokeza na kulikuwa na baridi kali iliyomfanya atetemeke kiasi cha meno kugongana kama vile alikuwa na homa kali. Hakujali,



    mawazo yake yote yalikuwa kwenye dola milioni moja, tayari alikuwa tajiri. Kwa fedha hizo asingelala nje tena, angenunua nyumba nzuri yenye mitambo ya



    kuongeza joto.



    “Pombe basi tena! Sitafanya makosa ya mwanzo. Mungu amenipa nafasi nyingine,” aliwaza Victor.

    Saa mbili kamili mfanyakazi wa kwanza wa ofisi hiyo alifika na kumkuta Victor ameketi mbele ya mlango, haraka akamuamuru aondoke akidhani ni watu



    wasiokuwa na makazi, Victor aligoma kuondoka na kumwambia alikuwa na shida kwenye ofisi hiyo.



    “Hakuna msaada hapa.”

    “Sijaja kutafuta msaada, kwa fedha niliyonayo naweza kukuajiri wewe uwe unafua nguo zangu za ndani tu! Wala si suruali na mashati”

    “Kaka usinitukane, nahisi wewe ni punguani.”

    “Baada ya muda si mrefu utaanza kuniamkia.”

    “Akuamkie nani?” aliuliza mwanaume huyo huku akifungua mlango kisha kuingia ndani, Victor alimfuata kwa nyuma.



    “Kaka nimekwambia subiri nje.”

    “Soma hii…” Victor aliongea akimwonyesha tiketi.

    “Mungu wangu! Ni wewe? Shikamoo kaka, karibu kiti, utatumia kinywaji gani?”

    “Sihitaji chochote, hivi sasa ndiyo unaanza kuniamkia?”

    “Samahani sana, sikufahamu.”



    “Naomba fedha yangu niondoke.”

    “Kaka subiri, meneja anakuja muda si mrefu, atawaita waandishi wa habari na kukutangaza, hongera sana.”

    Victor hakujibu, alibaki kimya akionekana mwenye chuki sababu ya dharau alizofanyiwa. Nusu saa baadaye mwanaume mfupi mnene mwenye kitambi chenye



    uzito usiopungua kilo hamsini aliingia, mfanyakazi aliyetangulia akasimama kwa heshima na kumwamkia kisha kumtambulisha kwa Victor, yeye pia alionesha



    hali ya kutoamini.



    “Ni wewe?”

    “Ndiyo”

    “Unaishi wapi?”

    “Sina makazi, naishi mtaani.”



    Mchana wa siku hiyo, Victor alinunuliwa suti nzuri ya vipande vitatu, akanyolewa nywele zake vizuri, akavaa pamoja na viatu vyeusi vya ngozi vipya tayari kwa



    mkutano na waandishi wa habari akitangazwa kama mshindi wa dola milioni moja. Uso wake ulikuwa umejawa na tabasamu, hakuwahi katika maisha yake



    kupigwa picha nyingi kiasi hicho. Gazeti la jioni lilipotoka lilikuwa na kichwa cha habari kisemacho A homeless become a millionaire (Asiye na makazi aibuka



    milionea). Ilikuwa ni furaha isiyo na kifani.



    Urusi na dunia nzima ilisoma habari za Victor Fedorov, siku hiyo hakulala nje, alipangishiwa chumba kwenye hoteli ya nyota tano ya Hilton akifanyiwa kila kitu



    kama mfalme. Siku iliyofuata asubuhi taratibu za kufungua akaunti na kuhamisha fedha zake zilifanyika, dola milioni moja zikaingizwa kwenye akaunti yake.



    Kitu cha kwanza alichokifanya ilikuwa ni kuchukua moja ya kumi ya fedha hizo zote na kuzipeleka kanisani kama alivyomuahidi Mungu, kisha kuwakusanya



    watu wote wasio na makazi walioishi katika Mji wa Novotroitsk na kuwafanyia sherehe kisha kuwapatia mitaji wa biashara. Baada ya hayo hakutaka kuchezea



    fedha kama alivyofanya awali, alikimbia haraka kwenye soko la hisa ambako alionana na madalali na kuambiwa kampuni ya vyuma iitwayo Novic Metals,



    ilikuwa ikiuza hisa zake kwenye mnada.



    “Kwa dola laki tisa naweza kununua asilimia ngapi ya hisa?”

    “Asilimia themanini.”

    “Niko tayari.”

    “Unazo fedha?”

    “Ninazo.”



    “Wapi?”

    “Kwenye akaunti yangu.”

    “Benki gani?”

    “Russian Commercial Bank.”

    “Unaweza kuniruhusu nimpigie meneja wa Benki?”

    “Hakuna shida.”



    Hilo lilifanyika, dalali mkuu wa soko la hisa la Urusi akapata uhakika na biashara ikafanyika. Bila kutarajia wala kupanga, kampuni hiyo kubwa ya uchimbaji wa



    chuma ikawa mali ya Victor Fedorov. Wanahisa wote wakatangaziwa na kukutana naye kwenye mkutano wa wanahisa siku tatu baadaye. Hakuna aliyekuwa



    tayari kuamini kwamba mtu ambaye hakuwa na makazi, waliyempita mtaani akipigwa na baridi ndiye sasa alikuwa mmiliki wa kampuni hiyo.



    Victor akaanza kuchapa kazi akiwa na uchungu mkubwa wa maisha, alitaka kufanikiwa na alitamani kuwa tajiri. Hivyo alifanya kazi usiku na mchana, akiwa na



    chumba cha kuishi ndani ya kiwanda chake. Hii iliwafanya wafanyakazi wote wafanye kazi kwa kujituma, huku akitoa motisha kwa wale waliofanya kazi kwa



    bidii kuliko wengine.



    Miezi michache baadaye aligundua kuwa kilichoifanya kampuni hiyo isipate faida kilikuwa ni uvivu na kutojituma kwa wafanyakazi. Aliporekebisha tatizo, faida



    kubwa ilipatikana ndani ya miezi sita tu, kampuni ikaanza kukua na ndoto ya Victor kuwa tajiri ikaanza kuonesha njia. Akanunua nyumba kubwa na gari la



    kifahari kisha kumuoa binti mrembo aitwaye Maria Nosh kwenye harusi iliyokusanya matajiri na wanasiasa wengi kwenye mji huo. Tayari alishakuwa miongoni



    mwao.



    Wakati kampuni ikiendelea kukua, Victor ambaye aliwauzia Phillip na Genevieve mbegu zake za kiume, hakuweza kupata mtoto katika mwaka wa kwanza wa



    ndoa yake. Moyo wake uliumia kwani alihitaji mtoto kuliko kitu kingine chochote, alitaka mrithi wa utajiri wake baada ya watoto wake kufa mwaka mmoja

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kabla.



    Haraka yake ya kupata mtoto ilimfanya aachane na Maria Nosh mwaka mmoja na nusu tu baada ya ndoa yao, akamuoa mrembo mwingine aitwaye Milka Vashnic



    ambaye pia mpaka mwaka mmoja baadaye alikuwa hajapata mtoto, Victor akamuacha bila kujiuliza mara mbili.



    “Nahitaji mtoto, haraka iwezekanavyo,” alijisemea moyoni mwake, ghafla akazikumbuka mbegu zake alizouza kwa Dk. Kohrer. Akachukua simu na kuipiga



    namba yake akitaka kufahamu nini kilitokea baada ya yeye kuondoka Ujerumani.



    “Aaa! Yalikuwa mafanikio makubwa, walizaliwa watoto wawili.”

    “Wako wapi?”

    “Siwezi kusema, ni kinyume na taratibu za kazi yangu.”

    “Daktari, nawahitaji hao watoto, ni wa kwangu.”

    “Victor umechanganyikiwa?”



    “Sijachanganyikiwa, nahitaji watoto wangu kwa gharama yoyote.”

    “Utajuaje mahali walipo?”

    “Nitajua. Fedha haishindwi, mimi si maskini mlala nje tena.”

    “Siyo rahisi.”



    “Naapa kwa Mungu kuwa lazima watoto wangu nitawapata. Kama ni dola elfu kumi niliyopewa niko tayari kuirejesha hata kama ni mara kumi au mia moja



    zaidi lakini nipewe wanangu.”

    Tayari simu ilishakatwa upande wa Dk. Kohrer.







    ILIKUWA ni ofisi kubwa iliyopambwa kwa vioo kila upande na kulikuwa na meza kubwa pamoja na kabati iliyotengenezwa kwa fomaika, kando kulikuwa na



    mashine ya kuongeza joto chumbani kwa sababu baridi ilikuwa chini ya nyuzi sifuri kwa wakati huo kwenye mji wa Novotroitsk, nyuma ya meza hiyo aliketi



    mwanaume aliyevalia suti nyeusi ya vipande vitatu, tai nyekundu na shati jeupe, uso wake haukuonekana wenye furaha hata kidogo.



    Alikuwa Victor Fedorov, ambaye miezi michache tu kabla alikuwa akiishi nje sababu ya kukosa makazi huku akipigwa na baridi. Sasa alikuwa mkurugenzi wa



    kampuni ya Novic Metals yenye wafanyakazi zaidi ya elfu mbili na mia tano, yeye akiwa mwajiri wao.



    Kichwani mwake alikuwa na wazo moja tu; watoto. Aliwataka watoto waliotokana na mbegu zake wapatikane na kusafirishwa kuja Urusi mara moja, uwezo wa



    kufanya hivyo alikuwa nao sababu ya utajiri mkubwa alioumiliki akiendesha kampuni ya kuchimba na kufua vyuma iliyoshika namba mbili kwa ukubwa nchini



    Urusi.



    “Nahitaji watoto wangu!” alisema Victor kwa Kirusi huku akipiga meza kwa nguvu.

    Moyoni mwake aliamini kuna jambo lingemwezesha kuwapata watoto hao zaidi ya kutafuta mpelelezi au kampuni ya upelelezi ambayo angeilipa ili ifanye kazi



    hiyo dunia nzima mpaka watoto watakapopatikana. Alizungusha akili yake huku na kule akitafakari na kufikiria kampuni yoyote ambayo ingeweza kumsaidia



    kulifanya jambo hilo hata kama malipo yangekuwa makubwa kiasi gani.



    “Niitie Ditrov,” alimwambia katibu muhtasi wake kupitia katika simu.

    “Sawa bosi!”

    Dakika tano baadaye mlango wa ofisi yake ulifunguliwa, akaingia mwanaume mfupi mwenye misuli aliyevalia suti ya rangi nyeusi pia, kwa kumtazama tu mtu



    yeyote angeamini lazima sehemu kubwa ya maisha yake ilitumika kubeba vyuma. Huyu ndiye alikuwa Ditrov mlinzi wa Victor Fedorov, ambaye historia yake



    ilihusisha mapambano katika vita vya Chechnya, kufanya kazi katika Shirika la Kijasusi la Urusi na kazi nyingi za hatari.



    “Ndiyo bosi.”

    “Nataka unisaidie.”

    “Niko tayari.”

    Victor alikwenda mbele na kumsimulia sehemu ya mkasa uliokuwa ukimkabili na kumwomba amsaidie kama alifahamu mtu yeyote nchini Urusi ambaye



    angeweza kufanya kazi ya kupeleleza mahali watoto wake walikokuwa, akamhakikishia kwamba angekuwa tayari kulipa kiasi chochote cha fedha ili mradi



    amweleze ni wapi watoto walipokuwa na ikiwezekana watekwe na kusafirishwa moja kwa moja hadi Urusi.



    “Inawezekana!”

    “Nani anaweza?”

    “Mimi.”

    “Kweli?”

    “Kabisa.”



    Baada ya mazungumzo ya muda wa karibu saa nzima, walikubaliana malipo ya dola laki moja na elfu hamsini ili kuhakikisha kwamba watoto hao wanapatikana,



    Victor alikubali na akaahidi kulipa kiasi cha dola elfu hamsini kama malipo ya utangulizi na baada ya hapo angeendelea kulipa dola elfu hamsini-hamsini mpaka



    fedha zote zikamilike lakini watoto wapatikane.



    Siku tatu baadaye kila kitu kilikamilika, malipo yakafanyika na Ditrov akapanda ndege na kuruka moja kwa moja hadi Ujerumani kwenye Jiji la Berlin kwenye



    kadi yake ya benki kukiwa na dola elfu hamsini, kwa fedha hiyo alikuwa na uhakika wa kupata kila taarifa muhimu juu ya watoto waliozaliwa kutoka kwenye



    kliniki ya Dk. Kohrer hata kama daktari huyo alikuwa hataki.



    Alitua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Schonefeld saa kumi na mbili jioni kwa majira ya Ujerumani, hakuwa na mtu wa kumpokea, akachukua teksi



    na kumwamuru dereva ampeleke kwenye hoteli ya nyota tano na dereva huyo akampeleka katikati ya jiji ambako alipanga chumba ghorofa ya tano kwenye hoteli



    iitwayo Metropolitan, iliyoaminika kuwa ni ya gharama kubwa kuliko nyingine yoyote nchini humo.



    Baada ya chakula cha usiku na vinywaji kidogo kwenye baa ya hoteli hiyo, alipandisha hadi chumbani kwake ambako alitumia muda wa kama nusu saa kwenye



    mtandao akichunguza kliniki ya Dk. Kohrer, akagundua msichana wa mapokezi ambaye picha yake ilikuwa miongoni mwa picha za wafanyakazi wa kliniki hiyo



    aliitwa Nasha, kwa muonekana alionekana kama Msomali.



    “Huyu ndiye atanisaidia kujua ukweli ninaoutafuta,” alisema moyoni mwake na hakutaka kuendelea kuwaza tena, akavuta shuka yake na kujifunika gubigubi,



    dakika arobaini na tano baadaye alikuwa akikoroma na hakuamka mpaka kulipokucha asubuhi siku iliyofuata.



    Saa nne kamili alikuwa mapokezi ambako aliomba aelezwe utaratibu wa kukodisha gari ambalo angeendesha mwenyewe, akawashangaza wahudumu alipoulizia



    kama angeweza kupata Q7, gari la kifahari kupita kiasi, wakamwangalia kwa mshangao wakiwa hawaamini walichokisikia.



    “Q7?”

    “Ndiyo.”

    “Kwa nini Q7?”

    “Najua ni kwa nini.”

    “Twende,” mmoja wa wahudumu alimwita na kumchukua moja kwa moja hadi kwenye chumba ambacho mlangoni kiliandikwa maandishi: Metropolitan Car



    Hire.



    “Anataka gari la kukodi.”

    “Aina gani?”

    “Q7.”

    “Q7?” msichana aliyekuwa nyuma ya kaunta aliuliza.

    “Ndiyo.”

    “Hatuna Q7.”



    “Mna gari gani nzuri inayonifaa mimi na ya kifahari?”

    “Ferrari!”

    “Safi kabisa, inakodishwa kiasi gani kwa saa?”

    “Dola mia tano.”

    “Naitaka kwa saa ishirini na nne kazi yangu itakuwa imemalizika.”

    “Hakuna shida, unaweza kulipia.”



    Hawakuamini alipojaza fomu na baadaye kutoa kadi yake ambapo fedha zote za kulipia gari hiyo kwa saa ishirini na nne zilikatwa, akakabidhi hati yake ya



    kusafiria na kuonyesha leseni ya kimataifa ya udereva na hapo ndipo akapewa ufunguo wa gari na kuondoka moja kwa moja kuelekea ilikokuwa kliniki ya Dk.



    Kohrer, akiongozwa na kifaa maalum cha kuonyesha njia kilichokuwa ndani ya gari lake ambacho mtu aliandika jina la mahali alikokwenda kisha kilimwelekeza



    mitaa mpaka kumfikisha.



    Akaegesha gari mbele ya jengo kubwa la hospitali ya Freiburg na kushuka, kisha kutembea akiingia ndani ya jengo hilo mpaka mapokezi, haikumsumbua hata



    kidogo kumtambua Nasha, moyoni mwake akakiri msichana huyo alikuwa mrembo kupindukia.

    “How are you Nasha?”

    “I am fine and you?” (Mimi mzima wewe?)

    “I am fine too, do you remember me?” (Mimi mzima pia, unanikumbuka?)

    “Nop!” (Hapana)



    “I came here with my wife last year, you attended us very well, I am here to say thank you.” (Nilikuja hapa na mke wangu mwaka jana, ulituhudumia vizuri sana,



    nimekuja kukuambia ahsante.)

    “You are welcome!” (Karibu!)

    “Is doctor Kohrer in?” (Dk. Kohrer yupo?)

    “Yes, very busy though!” (Ndiyo, lakini ana kazi nyingi sana.)

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok! Say hi to him! Can you come with me to my car? There is something I would like to hand you.” (Sawa, utamsalimia! Unaweza kunifuata kwenye gari?



    Kuna kitu ninataka kukupa.)



    “No problem!” (Hakuna shida) Nasha aliitikia na kuanza kumfuata Ditrov kwenda nje ambapo alifika na kufungua mlango wa gari, sauti ya Nasha kwa nyuma



    ikasikika akisema: “Oh! My God! You are riding a Ferrari? You must be very rich, you didn’t tell me your name sir?” (Oh! Mungu wangu! Unaendesha Ferrari?



    Lazima utakuwa tajiri sana, hukuniambia jina lako) Nasha aliongea akipokea bahasha kutoka kwa Ditrov, ndani yake kukiwa na dola elfu moja.



    “I am staying at the Metropolitan Hotel, please pass by for a cup of tea in the evening if you have time!” (Nimefikia Metropolitan Hotel, tafadhali ukipata nafasi



    jioni unaweza ukapita angalau tupate kikombe cha kahawa.)

    “No problem I will at 7:00!” (Hakuna tatizo nitapita saa moja.)

    “JOB DONE!” (Kazi imekamilika) Ditrov alijisemea moyoni mwake, akimkumbatia Nasha, wakaagana na akaondoka akimwacha amesimama mwenye



    mshangao.







    DITROV aliondoka akiendesha kwa mikogo Ferrari yake ya kukodi huku Nasha akimwangalia kwa mshangao, kwa tamaa zake msichana huyo alihisi hiyo



    ilikuwa ni bahati ya mtende iliyomwijia bila kutarajia. Hakuhisi kabisa kilichokuwa kikiendelea, kwake saa moja ya jioni ikaonekana ni kama mwaka kesho,



    alitaka muda huo ufike upesi ili achukue teksi na kwenda moja kwa moja hotelini kwa Ditrov, hakika alimtaka kwa udi na uvumba.



    “Warum hast du glucklich warden so plotzlisch”(Kwa nini umepata furaha hivyo ghafla?) msichana mwingine wa mapokezi alimuuliza Nasha.

    “Eine reiche person hat mich fur kafee eingeladen am Abend” (Mtu tajiri amenikaribisha kahawa jioni)

    “Vorsichtig sein.”(Uwe mwangalifu)

    “Ich beginne, ihn zu lieben” (Nahisi nimeanza kumpenda).



    Saa zilitembea taratibu mno siku hiyo, hatimaye saa 12:30, muda wa kutoka kazini ukawadia, Nasha akasaini kitabu na kubeba mkoba wake kwapani na



    kutembea hadi nje, kichwani mwake akimfikiria Ditrov tu, alihisi ndiye mwanaume wa ndoto yake ambaye kwa kipindi kirefu alikuwa akimsubiri na alitamani



    awe hajaoa ili baadaye amtamkie kwamba alitaka kuwa mume wake.



    Nje alipanda ndani ya teksi na kumwelekeza dereva ampeleke Metropolitan Hoteli ambayo ilikuwepo umbali wa nusu kilometa kutoka ilipokuwa kliniki ya Dk.



    Kohrer, dakika kumi baadaye waliegesha mbele ya jengo la hoteli hiyo, Nasha akalipa kisha kushuka na kunyoosha moja kwa moja hadi mapokezi.



    “Ich hier, um zu treffen Herr Ditrov” (Niko hapa kumuona bwana Ditrov)

    “Fur einem Moment zu warten”( Subiri muda kidogo) aliongea msichana huyo wa mapokezi na kupiga namba ya simu, akasikika akiongea na mtu upande wa



    pili, alipoweka simu chini alimwita kijana aliyekuwa kando yake ambaye alivalia suti nyeusi ya vipande vitatu na kumwomba ampeleke Nasha chumbani kwa



    Ditrov.



    kwa msaada wa lifti walipandisha hadi ghorofani ambako kengele iligongwa mlangoni, Ditrov akiwa kwenye taulo tu akafungua, moyo ukamwenda mbio Nasha



    alipomtazama jinsi mwili wake ulivyojazia sababu ya mazoezi, hakuonekana kama mzee, kifupi alimvutia kimapenzi. Mlango ulipofungwa nyuma yao, Ditrov



    alimshika mkono na kuanza kumvuta kumpeleka kitandani, akamsukuma na kumlaza chali.



    “You know what?”(Unajua nini?)

    “No!”(Hapana)

    “I love you and I want us to have sex”(Nakupenda na nitaka tufanye ngono)

    “Just like that?”(Hivyo tu?)

    “Yeah!” (Ndiyo)

    “No! Lets talk first!”(Hapana! Tuongee kwanza)



    Ditrov ambaye tayari alishavua taulo na kulitupa pembeni alisitisha zoezi na kuketi kando ya Nasha kisha kuanza kumwambia maneno ya mapenzi akieleza jinsi



    alivyompenda baada ya kumwona tu pale kliniki na hakuwa tayari kumpoteza msichana mrembo kama yeye.

    “I am ready to do anything but have you!”(Niko tayari kufanya lolote niwe na wewe!)

    “Are still married?”(Bado umeoa?)



    “No! I divorce my wife last year, right now I am looking for a woman with lucky, I think you’re the one”(Hapana! Nilimtaliki mke wangu mwaka jana, sasa hivi



    natafuta mwanamke mwenye bahati, nafikiri ni wewe) aliongea Ditrov akitabasamu.

    “Sure?”(Hakika?)

    “Yeah!”(Ndiyo)



    Maneno hayo yalimlainisha kabisa Nasha, akahisi kuishiwa nguvu mwilini mwake, ghafla akajiona mwenye bahati kuliko wanawake wengine wote chini ya jua



    ambayo hakutaka ipotee. Akamruhusu Ditrov azungushe mkono wake begani na kuanza kumpapasa taratibu nyuma ya shingo. Kitu kama umeme wenye nguvu



    kali, ukapita mwilini mwake na kumpiga shoti, akazidi kulegea, mhemo wake ukabadilika na taratibu akalazwa kitandani na kuanza kuvulishwa nguo alizokuwa



    nazo mpaka akabaki mtupu.



    Kilichofuata baada ya tukio hilo, hakielezeki, hakuwahi tangu azaliwe kukutana na mwanaume kama Ditrov, alihisi ni kwa sababu ya mazoezi aliyoyafanya. Ni



    kweli alikuwa na mchumba aliyetarajia kuolewa naye lakini kama Ditrov angetaka kumuoa na kuondoka naye kwenda Urusi, alihisi alikuwa tayari kwa hilo bila



    kuogopa lawama.

    “Ditrov!”

    “Yes” (Ndiyo)



    “Can I tell you something?”(Naweza kukueleza kitu?)

    “Go ahead”(Endelea)

    “You are good!” (Wewe ni mtaalam)

    “In?”(Katika?)

    “Love making!”(Kufanya mapenzi)



    “Thank you, that is just a beginning, lets take a fifteen minutes break and then I will show you who I am!”(Ahsante, huo ni mwanzo, tupumzike kwa dakika kumi



    na tano halafu nitakuonyesha mimi ni nani?)

    “Oh! My God! That’s just a beginning? You gonna kill me”(Oh! Mungu wangu! Huo ni mwanzo tu? Utaniua.)

    “No! You will enjoy it!”(Hapana! Utafaidi)

    Nusu saa iliyofuata ndani ya chumba hicho ilikuwa ni vilio na kelele zilizowasumbua mpaka watu wa vyumba vingine, Nasha alikuwa katika hali ambayo



    hakuwahi kukutana nayo, Ditrov akiwajibika ipasavyo, ghafla akasitisha huduma na kumwangalia Nasha machoni ambaye tayari alikuwa taaban akielekea



    mwisho wa safari yake.



    “Usiache!” Nasha alipiga kelele.

    “Listen, I want you to do me one favour!”(Sikiliza, nataka unifanyie upendeleo mmoja)

    “What is that favour baby? I can do anything for you, I love you so much Ditrov, you name it, I do it!”(Kitu gani hicho mpenzi? Naweza kufanya chochote kwa



    ajili yako, nakupenda mno Ditrov, ukikitaja tu nakifanya)



    “ I need one file from Dr. Kohrer’s Clinic!”(Nahitaji faili moja kutoka kwenye kliniki ya Dk. Kohrer)

    “Whose file is that?”(Faili la nani?)

    “A guy named Victor Federov, who donated sperms to a certain couple few years ago!”(La mtu aitwaye Victor Federov ambaye alitoa mbegu zake za kiume kwa



    wanandoa fulani miaka michache iliyopita)

    “When do you need it?”(Unalihitaji lini?)

    “Tomorrow!”(Kesho)



    “I will do that in the morning!”(Nitafanya hivyo asubuhi)

    “Thank you!” (Ahsante)

    Ditrov hakumwachia Nasha, usiku mzima alimfanyia mambo ambayo msichana huyo hakuwahi kukutana nayo, kifupi hawakulala na wala Nasha hakukumbuka



    kwenda nyumbani kwake. Saa mbili asubuhi ndiyo aliamka na kuanza kujiandaa, sababu hakutaka kwenda kazini na nguo zile zile, Ditrov alishuka hadi ghorofa



    ya chini ambako alimnunulia nguo nyingine mpya na kumletea, akavaa na kumbeba kwa gari hadi kliniki ambako alimwacha na kurejea hotelini.



    Saa nne kamili, simu chumbani kwa Ditrov iliita, akaikimbilia haraka na kuipokea. Ilikuwa ni sauti ya Nasha akipiga simu kutoka kliniki na kumtaarifu kwamba



    alishalipata faili hilo, Ditrov akamwomba alitoe kopi ili akienda hotelini ampelekee nakala.

    “It is an electronic file!”(Ni faili la kielekroniki) alijibu Nasha akimaanisha faili hilo lilikuwa kwenye kompyuta.



    “That is even better, send to my email now”(Hiyo ni nzuri zaidi, nitumie kwa barua pepe sasa hivi)

    “Five minutes!”(Dakika tano)

    Hivyo ndivyo ilivyotokea, dakika tano baadaye Ditrov alipofungua sanduku lake la barua pepe alikuta faili limetumwa, akafungua na kuanza kulisoma,



    hakuamini alichokishuhudia, kazi ilikuwa imekuwa rahisi kuliko alivyofikiria. Akafunga kompyuta yake na kulisogelea begi lake, haraka akalifungua na kuanza



    kukusanya kitu kimoja baada ya kingine akikiweka ndani ya begi.



    ***

    Saa tano kamili Nasha alitoroka kazini kwake na kwenda moja kwa moja hotelini Metropolitan, lengo likiwa ni kwenda kumwona Ditrov, akili yake



    ilishachanganyikiwa kabisa, kazi zilikuwa hazifanyiki. Taswira ya mwanaume huyo ilikuwepo kila mahali, alitaka amwone tena kabla hajaendelea na kazi.

    Mapokezi hakuongea na mtu, akapitiliza moja kwa moja kwenye lifti na kwenda hadi chumbani ambako alikuta mlango umefungwa, akagonga kwa muda bila

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kufunguliwa. Alipohakikisha Ditrov hakuwemo chumbani ndipo akaamua kwenda mapokezi kuulizia.



    “Ameondoka!”

    “Ameondoka?”

    “Ndiyo”

    “Siyo kweli”

    “Amesaini hapa”





    Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu katika ndoa bila kupata mtoto, Phillip na Genevieve wanaamua kusafiri hadi Ujerumani ambako kwa msaada wa Dk.



    Kohrer, inagundulika kuwa mbegu za Phillip hazina uwezo wa kurutibisha yai la mwanamke, hivyo Dk. Kohrer anaamua kununua mbegu kutoka kwa



    mwanaume masikini wa Kirusi, Victor Fedorov.



    Watoto pacha (Dorice na Dorica) wanazaliwa miezi tisa baada ya mbegu za Victor kuunganishwa na yai la Genevieve katika utaalamu uitwayo IVF (In Vitro



    Fertilization). Furaha inarejea kwa Phillip na mkewe Genevieve ingawa kilichotokea kinabaki kuwa siri ili kumlindia Phillip heshima yake. Wanawatunza watoto



    wao vizuri mpaka wanafikia umri wa kuanza darasa la kwanza, siku ya kwanza tu kupelekwa shule, basi ambalo ndani yake Dorice na Dorica walipanda wakiwa



    na watoto wengine kumi na nane lilipuka kwa bomu na watoto wote kuaminika kufa lakini mabaki yaliyopatikana ni ya watoto kumi na sita tu. Hesabu hizo



    zikazua kitendawili.



    Miaka michache baadaye, masikini Victor Fedorov maisha yalimbadilikia na kujikuta akiwa tajiri lakini asiye na mtoto, wanawake wote aliowaoa na kuwaacha



    walishidwa kumzalia hata mtoto mmoja. Hii ilimfanya akumbuke mbegu zake na kuamua kutumia fedha nyingi kutafuta mahali mbegu zake zilikotumika.



    Akampa kazi hiyo mlinzi wake, Ditrov, ili apeleleze na akafanikiwa kulipata faili kutoka kwenye kliniki ya Dk. Kohrer nchini Ujerumani baada ya kumdanganya



    msichana wa mapokezi aitwaye Nasha, ambaye amerejea hotelini kwa Ditrov na kukuta amekwishaondoka.





    KITU cha kwanza alichokifanya Ditrov bila kupoteza muda baada ya kulipata faili ni kumpigia simu Victor Fedorov kumtaarifu juu ya ushindi alioupata ndani



    ya muda mfupi, Victor alifurahi mno akiwa haamini alichokuwa akiambiwa. Mara moja akamtaka Ditrov apande ndege na kuruka hadi Moscow ambako



    angeunganisha ndege nyingine na kusafiri hadi Novotroisk, safari ambayo ingemchukua saa kumi na mbili.



    “Hakikisha unafika hapa ndani ya muda huo, kweli umepata faili?”

    “Ndiyo bosi, utakuja kuona.”

    “Tafadhali njoo, umenifurahisha mno, lazima nikupe motisha.”

    “Hakuna shida, nakuja.”



    Saa mbili baadaye Ditrov alikuwa ndani ya ndege ya Shirika la Ndege la Urusi akikatisha mawingu, fikra zake zilitawaliwa na kazi iliyokuwa mbele yake, ni



    kweli alikuwa amefanikiwa kujua mahali watoto wa Victor Federov walikokuwa lakini hakufahamu njia ambayo angeitumia kuwachukua na kuwasafirisha



    mpaka Urusi bila matatizo yoyote.



    Kompyuta yake ndogo ikiwa imefunguliwa, akiendelea kulisoma taratibu faili alilotumiwa ili apate kulielewa vizuri; Dar es Salaam, Tanzania, Upanga, Ally



    Khan Street, House Number 122, Phillip and Genevieve Mpangala. Alisoma maelezo hayo mara kwa mara akijiridhisha kisha kuitafuta ramani ya Jiji la Dar es



    Salaam iliyopigwa kwa setelaiti, akauona mtaa wa Ally Khan na kuanza kuitafuta nyumba namba 122 mpaka akaipata.



    “Lazima watakuwa matajiri pia, nyumba kubwa sana hii,” aliwaza Ditrov ndege ikizidi kusonga mbele.

    Saa tano baadaye, ndege ilianza kushuka na hatimaye kutua kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo ambako alishuka na kufanya taratibu za kuunganisha na



    ndege nyingine ya shirika hilo hilo iliyompeleka mpaka Novotroisk,

    Nje ya uwanja alipokelewa na Victor ambaye uso wake ulijawa na furaha. Wakaingia ndani ya gari aina ya Benz nyeusi na kuondoka hadi ofisini kwa Victor



    ambako kitu cha kwanza ambacho Victor alichotaka kukiona ni faili, Ditrov akafungua kompyuta yake na kuanza kumwonyesha kila kitu alichokipata.



    “Una uhakika ni wenyewe?”

    “Asilimia mia bosi.”

    “Hebu twende kwenye mtandao wa Google, tuangalie kama wana maelezo yoyote yanayowahusu.”

    “Hakuna shida,” alijibu Ditrov na kuutafuta mtandao huo mpaka akaupata na kuandika majina ya Phillip, Genevieve, Upanga Tanzania na kubonyeza kitufe



    kilichoandikwa Enter.



    Taarifa za Phillip na Genevieve tangu wakisoma chuo kikuu na baadaye kufunga ndoa zikaonekana, upande wa picha ilionekana ile waliyopiga kama familia na



    watoto wao wawili pacha, chini yake ikiwa imeandikwa “A wonderful and happy family of Mr Phillip and Mrs Genevieve”. Moyo wa Victor uliruka mapigo



    kadhaa baada ya kuiona picha hiyo.



    “Ndiyo, hawa ni watoto wangu.”

    “Wanafanana nawe kupita kiasi!”

    “Kabisa, ndiyo wenyewe kwa gharama yoyote ile nawataka hapa Urusi, unanisikia Ditrov?”

    “Nakusikia bosi. Unawataka lini?”



    “Nawataka jana!” alisema tajiri Victor akionesha ni kiasi gani aliwataka watoto wake, kiasi cha kufikiri wangekuwa hapo kuanzia jana yake.

    “Hakuna shida.”

    “Utafanyaje?”

    “Kwa hivi sasa sina jibu, nipe muda mpaka kesho niwasiliane na watu wangu.”



    “Hakuna shida, lakini naomba uelewe kwamba furaha yangu haiwezi kutimia kama watoto hawa sitawapata.”

    “Nitakuja na jibu zuri bosi wangu,” Ditrov akajibu kisha kuaga na kuondoka zake.



    Kufanya kazi ndani ya shirika la kijasusi la Urusi kwa miaka mingi kabla ya kuacha na kuajiriwa na Victor, kulimpa Ditrov nafasi ya kufahamiana na watu wengi



    waliojihusisha na ujasusi, miongoni mwao akiwemo Dimitri Coscov kiongozi wa kundi la uasi la Chechnya. Huyu ingawa alikuwa adui mkubwa wa Urusi, kwa



    upande wa Ditrov alikuwa rafiki yake mkubwa. Kitu cha kwanza alichokifanya baada ya kuondoka ofisini kwa Victor ni kumpigia simu.



    “Nina tatizo, nahitaji utaalamu wako kulitatua.”

    “Tatizo gani?”

    “Sitaki kuongea kwenye simu, napanda ndege sasa hivi kuja Grozny.”

    “Karibu.”



    Kesho yake majira ya jioni tayari alisharejea Novotroisk na kumpigia simu Victor ili kujua mahali alipokuwa, alikuwa bado yuko ofisini kwake kitini



    akiwafikiria watoto wake. Taarifa kwamba Ditrov alisharejea zilimfurahisha akamtaka afike ofisini mara moja ili aeleze mpango aliokuwa nao.

    “Tayari ninalo jibu.”

    “Naomba unieleze.”



    “Gharama yake ni kubwa lakini.”

    “Gharama siyo muhimu, cha muhimu ni watoto wangu.”

    “Tumegundua kwamba watoto hao wanaitwa Dorice na Dorica, wanategemewa kuanza darasa la kwanza wiki mbili zijazo. Ambacho tumepanga mimi na



    wenzangu tutakaofanya kazi hii ni kwenda huko Tanzania na kuthibitisha yote tuliyoyagundua, hatutaki kuamini mtandao moja kwa moja, tukishathibitisha



    kwamba ni kweli, watoto hao watatekwa siku watakayokuwa wanakwenda kuanza darasa la kwanza na wataletwa mpaka hapa Urusi.”



    “Mtafanyaje ili isijulikane?”

    “Watu ninaofanya nao kazi sitaki kukuficha ni waasi wa Chechnya ambao tumekubaliana kusafiri nao hadi Tanzania, ili kuudanganya ulimwengu, basi ambalo



    watoto hao watapanda litalipuliwa kwa bomu la kutengenezwa na waasi humo humo nchini Tanzania!”



    “Kwa hiyo na watoto wangu watafia kwenye basi hilo?”

    “Hapana wao watatolewa sekunde chache kabla basi halijalipuliwa kwa bomu, kitakuwa ni kitendo cha haraka, watu hawatakumbuka sababu ya hofu



    itakayowapata bomu likilipuka.”

    “Watasafirishwaje hadi hapa?”



    “Tulifanya utafiti na kugundua kuna ndege huwa zinasafirisha madini kutoka kwenye mgodi uitwao Deep Search Mining Company ambao uko katika mji mdogo



    uitwao Geita mkoani Mwanza. Ndege huwa zinaruka moja kwa moja kutoka mgodini hadi Canada, na tayari tumekwishafanya mazungumzo na mmoja wa



    marubani kwa malipo ya dola laki mbili ili baada ya kuwateka watoto hao wachukuliwe kwa ndege ya kukodi hadi mgodini na kupakiwa kwenye ndege



    itakayokuwa inaruka kwenda Canada. Huko tutakodisha ndege nyingine itakayoruka mpaka hapa, unauonaje mpango wetu?”



    “Uko sawa, lakini swali moja najiuliza, kuna namna yoyote ile ya kuwafanya watoto hao wasiwe na kumbukumbu kabisa ya mahali walipotoka?”

    “Tumelifikiria hilo bosi na uamuzi tulioufikia ni kwamba, baada tu ya kutekwa, watachomwa sindano ya dawa ya usingizi iitwayo Memory Eraser ambayo kazi



    yake ni kufuta kumbukumbu kwenye ubongo wa mwanadamu ili asikumbuke alikotoka fahamu zikimrejea.”

    “Dawa hiyo ipo?”



    “Ipo. Waasi wa Chechnya wanaitumia sana kupata wapiganaji, hiyo ndiyo tutatumia.”

    “Oh! Ahsanteni sana, kwa utaratibu huo nimewapata watoto wangu.”

    “Lakini gharama ya kazi yote hiyo ni dola milioni moja.”

    “Nitawaongezea laki mbili juu yake kama mtafanikiwa kuwafikisha watoto hapa.”





    SIKU tatu baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati ya Ditrov na Victor, tayari kundi la vijana tisa lilikuwa likishuka ndani ya ndege ya shirika la ndege la



    Urusi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, walionekana kama watu waungwana au wawekezaji waliokuja nchini Tanzania kuleta neema, jambo ambalo



    halikuwa kweli.



    Walikuwa ni waasi wa kundi la Chechnya waliokodiwa na Ditrov kwa kazi moja tu; kuwateka Dorice na Dorica na kuwasafirisha hadi kwenye mji wa



    Novotroitsk na kuwakabidhi kwa Victor, kazi yao ingekuwa imekwisha na kukabidhiwa kitita kisha kurejea Grozny.



    Mzungu mmoja ndiye aliyewapokea kwenye uwanja wa ndege, shati lake la khaki likiwa na nembo iliyoandikwa Deep Search Mining Limited. Alikuwa ni



    Meneja Mkuu wa mgodi huo uliokuweko katika mji wa Geita. Baada ya mazungumzo ya muda mrefu kwenye simu na kuingiziwa na Victor kiasi cha dola laki



    mbili kwenye akauti yake nchini Afrika Kusini, mzungu huyu alikuwa amekubali kuwasaidia Ditrov na vijana wake kukamilisha kazi iliyowaleta.



    “My name is Mike Eaglewood. You are all welcome to Tanzania.” (Naitwa Mike Eaglewood. Wote mnakaribishwa Tanzania.)

    “Thank you, a nice country.” (Asante, nchi nzuri.)

    Wakatembea mpaka kwenye maegesho ya magari na kupanda ndani ya gari aina ya Combi, Mike akaketi kwenye usukani na kuendesha taratibu mpaka maeneo ya



    Masaki nyumbani kwake. Ilikuwa ni nyumba kubwa na aliishi peke yake, hiyo ilimfaa Ditrov na vijana wake sababu walihitaji usiri wa hali ya juu hasa katika



    kazi ya kutengeneza bomu ambalo lingelipua basi lililobeba watoto wa shule.



    Kilichofanyika nusu saa baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo, hakikuwa kingine isipokuwa kikao cha kupanga mikakati ya utekelezaji, Mike akiwahakikishia

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kila kitu kingekwenda kama kilivyopangwa. Makubaliano yakafanyika kwamba yakodishwe magari mawili aina ya Benz ambayo yangetumiwa na kikosi hicho



    siku ya utekaji lakini pia kupeleleza mienendo ya familia ya Phillip.



    Pia uamuzi ukafikiwa kwamba baada ya watoto kutekwa, wangesafirishwa kwa njia ya barabara ndani ya kontena lililofungwa viyoyozi wakiwa tayari



    wamechomwa sindano ya kupoteza kumbukumbu hadi Geita ambako ndege ingekuwa imeandaliwa kwa ajili ya kuwabeba na kuruka nao moja kwa moja hadi



    Canada.Victor akaamua kuongeza dola nyingine laki tano kwenye milioni moja aliyokwishatoa ili kufanya zoezi hilo lifanyike kwa urahisi.

    “Zoezi la utekaji litafanyika siku gani?” Mike aliuliza.



    “Siku watoto watakapokuwa wanapelekwa shuleni.” Ditrov akajibu.

    “Mnaijua hiyo siku?”

    “Ndiyo.”

    “Mnaijuaje wakati nyie ndiyo mmewasili Tanzania?”

    “Phillip na Genevieve wana blog yao, kila kitu wanachokifanya huwa wanaweka huko. Tumesoma mtandaoni.”



    “Itakuwa siku gani?”

    “Tarehe kumi na nne, kama siku kumi na mbili kuanzia sasa.”

    “Tarehe tisa kuna kontena mbili zinaondoka hapa kwenda mgodini, tunaweza tukapakua mizigo kwenye moja ya kontena hizo na kupakia kwenye lori, halafu



    kontena hilo tukalifunga viyoyozi kisha tarehe kumi na nne kama mambo yatakwenda vizuri, tukaondoka na watoto hadi mgodini ambako tarehe kumi na tisa



    kuna ndege inaondoka kwenda Canada.”



    Wote wakakubaliana juu ya mpango huo na Ditrov akajitolea kusafiri na watoto ndani ya kontena akiwalisha mpaka wafike Geita, kilichofuata baada ya hapo ni



    kazi ya kulitengeneza bomu, vijana wawili kati ya tisa kwenye kundi hilo walikuwa ni wataalam wa kutengeneza mabomu ya petroli yanayoweza kutegwa na



    kulipuka baada ya muda uliopangwa.



    Kazi ya kutengeneza bomu kwa vifaa vilivyonunuliwa kwenye maduka na vituo vya mafuta jijini Dar es Salaam, ilikamilika siku ya tarehe kumi na tatu huku



    upelelezi juu ya shule ambayo watoto walitakiwa kupelekwa na gari asubuhi ya tarehe kumi na nne pia ukiwa mezani.



    Kwa kutumia ushawishi wa fedha, Ditrov na kundi lake wakijifanya wafadhili walimzoea dereva wa gari hilo mpaka akawapa ratiba kamili ya kazi yake kwa siku



    na mahali alipoliegesha gari hilo baada ya kazi na kurejea nyumbani.



    Ilikuwa ni kwenye ofisi ya CCM karibu kabisa na nyumbani kwake Magomeni Mapipa ambako pia walihakikisha wanaonekana kwa walinzi ili iwe rahisi kwao



    kurejea usiku na kutega bomu ndani ya gari bila kutiliwa mashaka wakijifanya walikuwa wakilirekebisha kabla dereva hajafika.



    Kwa ushawishi huohuo wa fedha walimfanya mlinzi wa ofisi ya CCM asiwatilie mashaka, watano wakiwa wamemzubaisha kwa maongezi walipofika alfajiri



    kumwuulizia dereva, wanne walikuwa kwenye gari, wawili kati yao wakitega bomu chini ya gari hilo huku kifaa kiitwacho Ignitor ambacho waya wake



    uliounganishwa kwenye betri ya gari na kuanza kuzunguka kikihesabu saa tayari kwa bomu hili kulipuka mara tu Dorice na Dorica wakipakiwa ndani ya gari



    hilo.



    Baada ya kazi hiyo waliingia ndani ya magari yao mawili aina ya Benz, wakimsubiri dereva ambaye kwa ratiba aliyowaeleza, gari lake lingeifika Upanga saa



    mbili asubuhi kwenye kituo ambacho Dorice na Dorica wangetakiwa kupanda.Walianza kulifuata taratibu kwa nyuma na kushuhudia likipakia watoto kituo



    kimoja baada ya kingine mpaka idadi ya watoto kumi na sita wakapanda, tayari likafika kwenye kituo cha Upanga ambako walimuona Genevieve amesimama na



    watoto wake, taratibu akatembea na kuwapakia gari liliposimama kisha kuanza kuwapungua mkono, jumla ya watoto kumi na nane wakawemo ndani ya gari



    hilo.



    Benz moja likapita na kwenda mbele ambako lilisimama ghafla kulizuia gari la shule na Ditrov akiwa na mmoja kati ya vijana wake wa kazi alishuka akiwa na



    bastola mkononi na kwenda moja kwa moja kwenye dirisha la dereva na kumwekea shingoni huku kijana mwingine akifungua mlango na kuwatoa Dorice na



    Dorica kisha kuwakimbiza kwenye gari lao, kilikuwa ni kitendo cha haraka mno kilichochukua sekunde kadhaa kiasi kwamba watu wengi waliokuwa jirani



    hawakushuhudia.



    Hazikupita hata dakika tatu, bomu likalipuka huku magari mawili aina ya Benz yakiondoka kwa kasi, ndani ya moja ya magari hayo Dorice na Dorica walikuwa



    wakipiga kelele huku wakichomwa sindano. Dakika chache baadaye walikuwa wakikoroma na safari iliendelea hadi Masaki, huko waliingizwa ndani ya kontena



    lenye viyoyozi, likafungwa na safari ikaanza.



    Ulikuwa ni msafara wa makontena mawili mbele yakiwa yamebandikwa maandishi makubwa yaliyosomeka “POISON IN TRANSIT” kuonyesha kwamba ndani



    yake kulibebwa sumu, hii iliwafanya maaskari njiani washindwe kuyasimamisha. Dorice na Dorica walikuwa ndani wakisafirishwa huku watu wote wakiwemo



    wazazi wao wakidhani walikufa kwenye mlipuko wa bomu.







    LILIKUWA ni tukio la kusikitisha, watu wengi walioona habari hiyo ya kulipuka kwa basi la wanafunzi na kuua watoto kumi na nane walilia machozi.



    Tanzania ilikuwa imepatwa na msiba mkubwa ambao haukuwahi kutokea kabla, mpaka vyombo vikubwa vya habari duniani kama CNN, Sky News na BBC



    vilitangaza tukio hilo likidaiwa ni la kigaidi na kuhusishwa na Osama bin Laden, hakuna mtu hata mmoja aliyejua kilichotokea, kwamba mwenye watoto wake



    alikuwa ameamua kuwafuata.



    Polisi walikuwa kazini usiku na mchana katika jiji la Dar es Salaam, mipaka yote ikiwa imefungwa, mamia ya vizuizi yakiwa yamewekwa barabarani, ukaguzi



    katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere ukiwa umeongezeka, upekuzi kwenye nyumba za wageni ukifanyika usiku na mchana kuwasaka watu



    waliohusika na tukio hilo ambalo kwa maelezo ya mashuhuda, walikuwa ni wazungu.



    Juhudi zote hizi zikiendelea bila mafanikio, gari lililobeba kontena ambalo ndani yake walikuwemo Dorice na Dorica lilizidi kukata mbuga, likipita mikoa ya



    Morogoro, Dodoma, Singida hatimaye likafika Isaka mkoani Shinyanga na kukata kona kuelekea Kahama ambako lingenyoosha moja kwa moja hadi mgodini



    Geita.



    Hakuna askari aliyediriki kunyosha mkono wake hewani kulisimamisha baada ya kuona maandishi ya POISON IN TRANSIT, wote waliamini ni sumu iliyokuwa



    ikisafirishwa kwenda pengine nchi za Rwanda, Burundi, Congo au migodini.

    “Sumu hiyo.”



    “Inawezekana inapelekwa migodini kwa ajili ya kulipulia miamba.”

    “Ndiyo, hawa wazungu wanaleta tu sumu ambayo mwisho wa siku inaingia kwenye maji yetu ya kunywa na kutusababishia kansa.”

    “Kwani unadhani wao wanajali sana afya zetu, cha muhimu kwao ni dhahabu, basi!”



    “Inabidi serikali yetu ndiyo itulinde sisi wananchi.”

    Hayo yalikuwa ni maongezi ya maaskari wa usalama barabarani na maafisa wa Mamlaka ya Mapato waliolishuhudia kontena likipita mbele yao,bila kuelewa



    kuwa kitambaa chenye maandishi kuonyesha ndani kulikuwa na sumu kilikuwa ni geresha, kwani kama wangelisimamisha na kuomba lifunguliwe wangemkuta



    Ditrov akipulizwa na kiyoyozi huku watoto wawili wakiwa wamelala bila fahamu kando yake.



    Siku tatu baada ya kuondoka Dar es Salaam, gari hilo liliingia ndani ya ngome ya mgodi wa Deep Search Mining Limited usiku wa manane, wafanyakazi wengi



    wakiwa wamelala na Bwana Mike Eaglewood,



    Mkurugenzi wa mgodi huo ambaye alielewa kila kitu kilichoendelea baada ya kupewa kitita cha fedha aliwaongoza mpaka kwenye uwanja wa ndege wa mgodi



    huo ambako ndege iliyokwishapakiwa shehena ya mchanga wa dhahabu kwa ajili ya kupelekwa Canada ilikuwa ikisubiri.



    “Quickly!” (Haraka!) Bwana Eaglewood aliongea kwa sauti ya kuonyesha kwamba hapakuwa na muda wa kupoteza, kila kitu kilikuwa ni muhimu kifanyike kwa



    kasi ili ndege iruke kutoka kwenye uwanja huo akidai ilikuwa iimechelewa.

    “Yes sir!” (Sawa mkuu.) alijibu Ditrov akimalizia kuwachoma Dorice na Dorica sindano ya kuharibu kumbukumbu.



    Watoto hao wakashushwa wakiwa hawajui kinachoendelea na kupakiwa ndani ya ndege, kisha Ditrov na vijana wake pia wakaingia, cha kwanza alichokifanya ni



    kuwasiliana na Victor Fedorov na kumtaarifu juu ya mafanikio waliyoyapata na kumtaka aandae ndege ya kukodi kutoka Ottawa Canada kwenda Moscow



    ambako pia walitakiwa wakute ndege nyingine ya kukodi ambayo ingewapaleka moja kwa moja hadi kwenye mji wa Novostroitsk ambako Victor angewapokea.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hayo ndiyo yakawa makubaliano na Victor akawahakikishia kwamba kila kitu kingekwenda kama walivyopanga, akiwaeleza kuwa alichohitaji si kingine



    isipokuwa watoto wake. Hivyo alikuwa tayari kutumia kiasi chochote cha fedha nje ya makubaliano ya awali ili mradi Dorice na Dorica waingie mikononi



    mwake, hicho ndicho kitu pekee alichoamini kingempa furaha.



    Dakika kumi na tano baadaye injini za ndege ziliwashwa, mapanga yakaanza kuzunguka na ndege ikaanza kusogea mbele kisha kupaa na kuiacha ardhi ya



    Tanzania, Ditrov akatabasamu akiwaangalia wenzake.



    “Give me five, mission accomplished.” (Nipe tano, mpango umekamilika.) akaongea Ditrov akiinua mkono wake wa kuume juu na kuanza kugonganisha na



    wenzake.



    Ilikuwa ni safari ndefu yenye kuchosha lakini wao waliiona kuwa fupi sababu muda wote walikuwa wakinywa pombe, kuimba na kushangilia, fedha ambayo



    walikuwa wanakwenda kulipwa na Victor Fedorov ilikuwa kubwa mno, maisha yao yasingekuwa kama yalivyokuwa, wote waliamini tangu siku hiyo



    wangemiliki biashara kubwa na kujiepusha na mambo ya ugaidi.



    Saa kumi na tatu baadaye walitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ottawa ambako muda mfupi tu baada tu ya ndege kutua na injini kuzimwa,



    mwanaume mrefu mwembamba aliingia kwenye ndege akiwa amevaa suti nyeusi na kuwaangalia watu wote walioketi vitini, kisha akamgusa Ditrov begani,



    ilivyoonekana alikuwa na maelezo ya kutosha kabisa ya mtu aliyekuwa akimtafuta.



    “Carry the children and follow me!” (Bebeni watoto na mnifuate.) aliongea mwanamume huyo.



    “Ok!” (Sawa.) Ditrov akaitikia na kunyanyuka alipokuwa ameketi na kuzunguka kiti cha kwanza, akambeba Dorice na kumuomba mmoja wa vijana wake



    ambebe Dorica, wakashuka hadi chini kulikokuwa na gari maalumu na kupanda,likaondoka na kutoka nje ya uwanja kupitia mlango wa nyuma na kuendeshwa



    hadi kwenye uwanja mwingine mdogo wa ndege ambako walipanda katika ndege ambayo nusu saa baadaye iliruka wakiwa pamoja na mwanaume



    aliyewaongoza.

    “Where to?” (Tunaelekea wapi?) Ditrov aliuliza.

    “Moscow.”



    “Thank you.” (Asante.)

    Watoto walikuwa bado wako usingizini, mpaka wakati huo walikuwa hawajaweka chakula chochote mdomoni, hata maji ya kunywa. Safari yao ilitegemewa



    kuwachukua muda wa masaa matano ndiyo watue kwenye uwanja wa ndege wa Sheremetyevo, jijini Moscow.



    Kwa maelezo ya mtu aliyekuwa anawaongoza, ndege nyingine ya shirika hilo hilo la kukodisha ingewapeleka moja kwa moja hadi Novotroitsk na hapo ndio



    ungekuwa mwisho wa safari yao. Ditrov na watu wake walikuwa na furaha mno, walikuwa wakisubiri kitu kimoja tu mbele yao; kufika na kukabidhiwa kitita,



    kisha kusambaa.

    ***

    Ilikuwa yapata majira ya saa tatu na nusu za usiku, mvua ilikuwa ikinyesha sana kwenye mji wa Novotroitsk, sababu ya baridi kali watu wachache sana walikuwa



    nje, wengi walijifungia ndani ya nyumba zao kuota moto.



    Hali ilikuwa tofauti kwa Victor Fedorov, pamoja na utajiri wake wote, alikuwa uwanja wa ndege akiwa amebana kwenye moja ya kona, simu yake ikiwa



    kiganjani, subira yote hiyo ilikuwa ni kwa watoto wake, alitarajia wakati wowote kupokea simu kutoka kwa Ditrov ikimweleza kuwa tayari walishatua.



    “Driiiii! Driiiii! Driiiii!” ulikuwa ni mlio wa simu yake, haraka akaipokea na kuiweka sikioni na kuanza kusikiliza.

    “Ditrov?”

    “Ndiyo.”

    “Mmefika?”

    “Ndiyo.”

    “Subirini hapo hapo nakuja,” aliongea Victor na kuanza kutembea kwenda mahali alipoliacha gari lake na kuingia, kisha kuliwasha na kuondoka kuelekea



    kwenye lango la kuingilia uwanjani, askari akafika akitaka kujua ni nani alitaka kuingia uwanjani muda huo wa usiku.



    “Ah! Mzee,” askari huyo alisema baada ya Victor kuvua kofia yake kichwani, aliheshimika mno kwenye mji huo na alikuwa na uwezo wa kufanya chochote



    serikalini hata kumuachisha au kumhamisha mtu kituo cha kazi kama tu angegombana naye, hii iliwafanya wafanyakazi wengi wa serikali wamwogope.

    “Naomba nikampokee mgeni wangu.”

    “Hakuna shida, pita tu”



    Victor akaendesha gari lake mpaka ndani kabisa mwa uwanja mahali ilipoegeshwa ndege ya shirika la ndege la Cross Atlantic ambayo aliikodisha kuwasafirisha



    watu wake mpaka kwenye uwanja huo, mlango wa ndege ukafunguliwa, Ditrov na kundi lake akashuka wakiwa wamewabeba Dorice na Dorica ambao walikuwa



    bado wako usingizini, miili yao ikiwa imesinyaa sababu ya kukosa chakula na maji.



    Wakapanda garini, kabla gari haijaondoka, Victor alishuka kwenye usukani na kuzunguka upande wa pili, akapanda na kuanza kuwabusu watoto mfululizo huku



    akilia kwa furaha na kukiri kwa mdomo wake kuwa hakuwahi kutarajia siku moja angewaona watoto waliotokana na mbegu zake ambazo aliziuza sababu ya



    umaskini.

    “Huu ni ukombozi,” alisema maneno hayo akiliendesha gari lake kwa kasi kuelekea nyumbani, furaha aliyokuwa nayo ilikuwa ni kubwa mno, alitaka afike



    nyumbani haraka ili awachunguze vizuri watoto wake.



    Je, nini kitaendelea watoto wakizinduka? Nini kinaendelea nchini Tanzania kwa sasa ambako inaaminika watoto hao wamelipukia ndani ya gari lililolipuliwa



    kwa bomu? Kitendawili cha mafuvu kumi na sita wakati watoto waliokuwemo ni kumi na nane kitateguliwaje?









    MVUA kubwa ilizidi kunyesha kwenye Mji wa Novotroitsk ikiambatana na baridi kali iliyofanya watu wengi wajifungie majumbani mwao. Gari aina ya Volga



    GAZ-24 (New Era) la kisasa lenye vioo vyeusi lilikuwa likikatiza kwenye ukungu mzito kutokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Novotroitsk kuelekea mahali



    yalipokuwa makazi ya Bilionea Federov. Ndani ya gari kulikuwa na wanaume wawili, Federov mwenyewe na mlinzi wake, Ditrov ambaye ndiye aliyekuwa



    kiongozi wa msafara ulioenda kuwateka Dorice na Dorica na kuwafikisha Urusi.



    Kwenye siti ya nyuma walikuwa wamelala watoto wawili, Dorice na Dorica ambao hawakuwa wakijitambua kutokana na kuchomwa sindano ya dawa ya



    Memory Eraser iliyokuwa na kazi ya kufuta kumbukumbu kichwani. Miili yao ilikuwa imesinyaa kwani hawakula chochote tangu walipotekwa jijini Dar es



    Salaam wakati wakipelekwa shule hadi wakati ule.



    Vijana wa kazi’ wa Kundi la Chechniya waliofanikisha kazi ile sambamba na Ditrov lilikuwa likiwafuata taratibu. Walikuwa wakielekea nyumbani kwa Federov



    kukabidhiwa mamilioni yao waliyoahidiwa baada ya kuikamilisha kazi ile.



    Walipofika nyumbani kwa Federov, tafrija fupi ya kuwapongeza wote waliofanikisha zoezi lile ikafanyika na makabidhiano ya fedha walizoahidiwa



    yakakamilishwa. Kila kitu kilikuwa kikifanyika chini ya ulinzi mkali kuzuia siri ile isivuje na kutua mikononi mwa watu wasiohusika.



    Siku ile ile daktari maalum akatafutwa na kupewa kazi ya kuhakikisha Dorice na Dorica wanarejea kwenye hali zao za kawaida lakini wakiwa hawakumbuki kitu



    chochote kuhusu maisha yao yaliyopita. Fedha ilitumika kisawasawa kwani waliongezwa dozi nyingine ya Memory Eraser, wakaachwa walale mpaka siku



    iliyofuatia.



    Furaha aliyokuwa nayo Federov haikujificha. Hakuamini kuwa hatimaye kazi ile ya kuwarejesha mikononi mwake watoto wake imefanikiwa. Alikuwa na furaha



    kubwa ambayo ilimfanya amuongezee Ditrov mshahara mara tatu zaidi ya ule wa awali aliokuwa anaupata.



    Siku iliyofuatia, Dorice na Dorica walirejewa na fahamu, kazi ya kuwalisha chakula bora ikaanza ili kufidia muda mrefu waliokaa bila kula chochote. Licha ya



    kuwa walikuwa wamerejewa na fahamu zao, hawakuonekana kukumbuka kitu chochote maishani mwao. Hata kula ilibidi waanze kufundishwa upya. Kila kitu



    kwenye vichwa vyao kilikuwa kimefutika kama kompyuta ‘iliyofomatiwa’.



    “Hawa ni wanangu waliokuwa wanaishi barani Afrika, nimeamua kwenda kuwachukua baada ya kuona nimezidiwa na upweke,” alisema Federov wakati



    akiwatambulisha Dorice na Dorica mbele ya walimu watatu ambao aliwapa kazi ya kuhakikisha wanawafundisha kila kitu upya kwani hakuna walichokuwa



    wanakikumbuka.

    Wakabadilishwa majina na kupewa ya Kirusi, Dorice akiitwa ‘??????’ au Mahreenah (Marina) na Dorica akiitwa ‘?????’ au Mahreeyah (Mariya).

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakafundishwa lugha ya Kirusi na taratibu wakaanza kuzoea majina yao na mazingira mapya.

    Walimu wale waliwafundisha kwa bidii kwani walikuwa wakilipwa mshahara mnono na ndani ya wiki moja wakawa na uwezo wa kutamka maneno machache ya



    Kirusi.



    Wakaamini kuwa walizaliwa kwenye mazingira yale na Federov ndiyo baba yao kama walivyofundishwa na walimu wao. Walibadilika kwa kila kitu na



    hawakukumbuka chochote kuhusu Tanzania.



    Siku zilizidi kusonga na watoto wale wakawa wanazidi kuzoea mazingira mapya. Waliendelea kufundishwa mambo mbalimbali ikiwemo tabia njema na maadili



    ya Kirusi, na taratibu wakaanza kufanana na watoto waliozaliwa eneo lile. Suala lile lilimpa faraja kubwa Federov, ule upweke uliomtesa kwa miaka mingi sasa



    ukabakia kuwa historia.



    “Baba, kwani mama yetu yupo wapi?” Dorice ambaye sasa alikuwa akiitwa ?????? (Marina) alimuuliza Federov jioni moja wakati wakitoka kwenye matembezi



    ya jioni.



    “Mama yenu alifariki wakati mkiwa bado wadogo kwa ajali ya gari, lakini msiwe na wasiwasi kwani baba yenu nipo,” aliongea Federov na kuwafanya watoto



    wale waamini kile walichoambiwa.



    Kwa jinsi alivyokuwa anawapenda, alihakikisha wanapata mahitaji yote muhimu yakiwemo chakula, mavazi mazito yasiyoruhusu baridi kupenya na kila kitu



    kilichokuwa muhimu kwao. Hakutaka wapate shida kabisa. Alipofikiria kuwaandikisha shule, walimu wao walishauri kuwa wanapaswa kuendelea kufundishwa



    nyumbani kwa angalau mwaka mzima mpaka watakapozoea kabisa mazingira.



    ***

    Phillip alikuwa na kazi ya ziada baada ya tukio lile la ajali iliyohusisha gari la shule ambalo kila mtu alikuwa anaamini kuwa Dorice na Dorica nao walikuwa



    ndani yake mpaka wakati linalipuliwa na bomu. Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa mkewe, Genevieve ambaye alishindwa kukubaliana na ukweli kuwa hatawaona



    tena watoto wake, akapatwa na mshtuko mkubwa siku ile ya tukio na kupelekwa hospitalini kulazwa. Licha ya madaktari kujitahidi kwa kila namna kumsaidia,



    bado hakuweza kuzinduka.



    “Amka mke wangu, kila kitu kinapangwa na Mungu. Tazama amewachukua watoto wetu na kuwatanguliza mbele za haki, na wewe unataka kuondoka? Nitabaki



    na nani kwenye hii dunia mimi?” Phillip alikuwa akilia pembeni ya kitanda alicholazwa Genevieve hospitalini na machozi yake yakawa yanamdondokea usoni.



    Phillip akawa na kazi ya kuomboleza, kwanza kwa ‘kufiwa’ na wanaye, pili kwa hali aliyokuwa nayo mke wake kipenzi. Jitihada za kumrejesha Genevieve



    kwenye hali yake ya kawaida zilishindikana, akawa ni mtu wa kitandani saa zote.



    Madaktari waliielezea hali ile iliyompata kuwa ni huzuni kali ambayo huumaliza nguvu na kuudhoofisha ubongo na kusababisha ushindwe kufanya kazi yake



    ipasavyo, hali ambayo husababisha mgonjwa kupoteza fahamu kwa kipindi kirefu.



    “Inaonekana aliwapenda sana watoto wake, ubongo wake umeshambuliwa kwa kiwango kikubwa na uwezekano wa kurejea kwenye hali yake ya kawaida ni



    mdogo. Hata akizinduka atakuwa na tatizo la kuzimia mara kwa mara kwani ubongo wake utakuwa unazalisha chaji za umeme kila atakapokuwa anawakumbuka



    wanaye, hali ambayo ni hatari sana,” alisema daktari aliyekuwa akimhudumia wakati akimuelewesha Phillip hali ya mkewe.



    Hilo lilikuwa ni pigo lingine kwenye maisha ya Phillip. Furaha yote aliyokuwa nayo wakati familia yake ikiwa imekamilika, ilipotea kama mshumaa uzimikavyo



    gizani, akawa ni mtu wa kuomboleza na kulia muda wote.



    Hakuweza hata kuendelea na kazi yake kama awali, muda mwingi akawa anautumia hospitali kumuuguza mkewe ambaye kila siku hali yake ilikuwa inazidi



    kuwa mbaya.



    “Eeeh Mungu, nimekukosea nini mimi mja wako mpaka kustahili mateso makali namna hii?” alisema Phillip akiwa pembeni ya kitanda cha mkewe wodini huku



    machozi yakimbubujika kama chemchemi ya maji.







    PHILLIP alikuwa kwenye kipindi kigumu kuliko kingine chochote maishani mwake, kufiwa na watoto wawili pekee aliokuwa nao katika ajali pamoja na



    kuuguliwa na mkewe mpendwa ambaye alikuwa amepoteza fahamu baada ya kushuhudia mlipuko wa bomu ulioua watoto wake, hayakuwa matukio madogo,



    hakika yalivuruga kabisa akili yake na kutamani siku zirudi nyuma ile ya mlipuko wa bomu iondolewe katika historia ya maisha yake.



    Kwa hali ilivyokuwa, akiwa amechanganyikiwa kabisa, baada ya kuzunguka huku na kule mikononi mwa matabibu wa kitaalam na kienyeji, akiongozana na baba



    mkwe wake, hatimaye aliamua kuandika barua ya kuacha kazi ili ajikite moja kwa moja kwenye tiba ya mkewe.



    Maisha yalikuwa yamebadilika, kila siku alipobaki peke yake alilia. Genevieve alimuumiza sana moyo kwa alivyokuwa akiteseka, kichwani mwake hakuwa na



    kumbukumbu hata kidogo za yeye alikuwa nani, watoto wake walikuwa wapi, alionekana kama zezeta tu jambo lililomuumiza sana Phillip na kumfanya awe



    tayari kutumia kila alichokuwa nacho akitafuta tiba za mke wake mpendwa.



    Pamoja na yote hayo, hakusahau jambo moja kubwa kuwaombea marehemu watoto wake na hata kutembelea kaburi lao kila siku ya Jumapili, huo ndio ulikuwa



    utaratibu wake wa maisha. Alimsikitikia sana mke wake kwa sababu hakuelewa chochote kilichokuwa kikiendelea na kila siku ya Jumatano ya kila wiki



    alilazimika kumpeleka hospitali.



    “Hivi iko siku mke wangu atapona na kurejewa na kumbukumbu zake za nyuma?” alimuuliza Dk. John Lupimo, bingwa wa magonjwa ya akili katika hospitali



    ya Muhimbili.

    “Ndio.”



    “Tatizo lake ni nini?”

    “Linaitwa kitaalam Amnesia.”

    “Amnesia? Ndio nini? Na inasababishwa na nini?”



    “Ni tatizo la ubongo pale hasa unaposhindwa kuyavuta mafaili ya kumbukumbu kutoka kwenye stoo zake au kushindwa kutunza kumbukumbu, husababishwa



    na magonjwa ya akili au wakati mwingine ajali kwenye kichwa.



    Hii ndio iliyotokea kwa Genevieve baada ya kushuhudia gari lililowabeba watoto wake likilipuka, akaanguka chini na kupiga kichwa ardhini.”

    “Sasa itakuwaje?”



    “Tunampa dawa iitwayo Amytal, hii inasaidia kurekebisha kumbukumbu, ipo siku Genevieve atarejea kwenye hali ya kawaida, hutaamini!” Daktari aliongea na



    kumfanya Phillip atabasamu, kauli hiyo ikawa imempa matumaini makubwa kwamba siku moja mke wake atarejewa na fahamu zake ili wote wawili wachangie



    maumivu ya kufiwa na watoto wao ambayo Genevieve hakuwa na habari nayo sababu ya tatizo lake la akili.



    Kadiri siku zilivyozidi kusonga wakiwa wodini, ndugu na jamaa wakifika kuwasalimu, hali ya Genevieve iliendelea kuwa mbaya siku hadi siku, akazidi kukonda



    sababu ya kutokula chakula, matumaini yake ya chakula yakawa ni kwenye mpira kupitia puani au dripu.



    Yote hayo hayakuweza kusaidia, hatimaye mwezi mmoja baada ya bomu kulipuka, Genevieve akaaga dunia na kuzikwa kando ya kaburi la watoto wake, katika



    mazishi yaliyohudhuriwa na maelfu ya watu wengi waliomlilia, Phillip alilia kama mtoto mdogo na kuzimia mara kadhaa.



    “Life has no meaning any more, I better die!” (Maisha hayana maana tena, bora nife!) Phillip aliongea akibubujikwa na machozi mbele za watu waliokusanyika



    kumfariji, wengi wakiwa ni wafanyakazi wenzake pamoja na familia ya Phillip.



    Baada ya mazishi Phillip hakuongea tena, muda wote akawa kimya kuliko ilivyokuwa kawaida yake, alitambulika kama mtu mcheshi mwenye mazungumzo kwa



    ajili ya kila mtu lakini sasa akachagua kubaki kimya sababu ya simanzi



    alilokuwa nalo. Kitu kingine kilichojitokeza ni wakati wa usiku, alipiga kelele na kudai mke na watoto wake walikuwa wakimtokea na kumwambia awafuate,



    jambo ambalo hakuna hata mmoja aliyelithibitisha ingawa yeye alidai kila siku dirisha la chumba chake liligongwa na akaitwa jina.



    Habari hii iliwashtua watu wengi na kuwafanya waamue kuwa wanakesha usiku ili waone kama kweli kilichodaiwa na Phillip kilikuwa ni cha kweli, wiki nzima



    baadaye hakuna aliyewaona Genevieve na watoto wake wakipita, hiyo kathibitisha kabisa kwamba Phillip alikuwa akinyemelewa na tatizo la akili, hii ilifanya



    siku chache baadaye abembelezwe na kukubali kupelekwa kwa daktari ambako awali alikuwa hataki kwenda akidai yeye alikuwa mzima wa afya.



    “Kila siku mke na watoto wangu wanakuja kunigongea wakitaka niongozane nao, mimi sitaki kwenda huko ambako wao wanaishi, kuna mateso sana, hivi njia



    ya kwenda Kigoma inapitia Kigamboni? Ng’ombe na mbuzi yupi ni paka?” aliongea sentensi nyingi zisizo na maana.



    Tayari daktari akawa ameshaligundua tatizo lake, hapohapo hakupoteza wakati, akatoa maamuzi kwamba mgonjwa alazwe kwenye wodi ya wagonjwa wa akili



    kwa matibabu ili pia awe anakutana na mtoa nasaha ambaye angebadilisha maisha yake baada ya kufiwa na mke pamoja na watoto wake.



    Akaanza kupewa dawa ambazo hazikumsaidia chochote, aliendelea kuwa kimya huku mara kwa mara akilia na kuwaita mke na watoto wake. Kibaya zaidi



    alianza tabia ya kutupa nguo na kutembea utupu bila kujali heshima yake, hii ilifanya madaktari wamwandikie dawa zilizomfanya alale kwa muda mrefu ili



    kusaidia akili ikae sawa.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dawa hizo ziliposimamishwa wiki mbili baadaye, angalau aliweza kujisikia vizuri, madaktari wakaridhika kabisa na kuamua kumruhusu arejee nyumbani



    kuendelea na dawa taratibu.



    Huzuni yake ilikuwa pale pale, kila alipoyaona makaburi ya mke na watoto wake alipokwenda kuyatembelea alilia mno. Hakika alitamani kufa, akazidi kukonda



    sababu ya mawazo na hakujijali tena, wengi walimchukulia kama mtu aliyechanganyikiwa na akili sababu ya matatizo yaliyomkuta, alitembea sehemu nyingi



    akiongea peke yake.



    “Hallow!” ilikuwa ni sauti ya mwanamke nje ya duka kubwa la Imalaseko ambako Phillip alikuwa akipita, akageuka na kuangalia upande sauti ilikotokea.

    “Ndio dada.”

    “Wewe ni Phillip?”



    “Ndio, wewe ni nani? Sauti yako sio ngeni.”

    “Nini kilitokea mpaka ukawa hivi?”

    “Maisha tu dada yangu. Dunia inazunguka kwenye mhimili wake, watu tunaingia na kutoka.”



    “Nimesikitika sana.”

    “Kila mtu anayeniona anasikitika. Wewe ni nani lakini?”

    “Unataka kunifahamu?”

    “Ndio.”

    “Njoo ndani ya gari yangu tuongee, nitakukumbusha kila kitu.”

    “Kweli?”

    “Ndio.”



    “Naogopa kuingia kwenye gari lako!”

    “Hakuna sababu ya kuogopa, wewe njoo tu nataka kukuonyesha jambo.”



    “Mh!” Phillip aliguna, taswira ya Zamaradi ikamwijia kichwani, akaanza kuhisi pengine mtu huyo aliyekutana naye alikuwa jini ambaye angeweza



    kumdhuruHata hivyo, baada ya kusisitiziwa sana alijikuta anakubali na kuingia ndani ya Land Cruiser mpya ya rangi ya fedha, akaketi kitini kando ya dereva



    ambaye alikuwa ni mwanamke aliyekutana naye.

    “Unataka kufahamu mimi ni nani?”

    “Ndio.”



    “Subiri!” mwanamke huyo aliongea akijifunua wigi usoni mwake, akaiondoa pia sura ya bandia na yake halisi kuonekana. Macho yakamtoka Phillip kwa



    mshangao akiwa amejifunika kwa mikono yake yote miwili mdomoni, bila kusema chochote alianza kulia.

    “Usilie ndio dunia.”



    Je, mwanamke huyo ni nani? Nini kinaendelea kwa watoto Dorice na Dorica ambao tayari wapo nchini Urusi wakiwa wamepoteza kumbukumbu zote za



    Tanzania na

    wazazi wao baada ya kuchomwa sindano ya dawa iitwayo Memory Eraser ambayo hutumika kufuta kumbukumbu kwenye ubongo wa mwanadamu ili aanze



    upya kujifunza? Majina yao hivi sasa si Dorice na Dorica tena bali ni Mariya na Merina.







    BASI la shule lililobeba watoto kumi na nane linalipuliwa kwa bomu, watoto wote wanakufa palepale lakini baadaye yanapatikana mabaki ya watoto kumi na



    sita tu! Hiki kinakuwa ni kitendawili kwani kila mtu alikuwa na uhakika watoto waliopanda ni kumi na nane.



    Ukweli wa tukio hili ni kwamba, watoto wawili (Dorice na Dorica) waliondolewa kwenye gari na watekaji kabla ya bomu kulipuliwa. Watekaji hao walitumwa



    na Victor Federov, Mrusi bilionea asiye na mtoto ambaye wakati wa umasikini wake aliwahi kuwauzia Phillip na Genevieve mbegu zake za kiume.



    Phillip na mke wake Genevieve hawaelewi juu ya jambo hili, wanalia kwa kupoteza watoto wao wawili katika ajali hiyo mbaya iliyomfanya Genevieve aanguke



    chini na kupoteza fahamu, mshipa wa damu ukapasuka kwenye ubongo kwa sababu ya kupanda kwa shinikizo.



    Maisha ya Phillip baada ya hapo yanabadilika, akawa na kazi moja tu ya kumuuguza mke wake mpaka alipofariki na kufanya jumla ya watu waliofariki kwenye



    familia yake kufikia watatu. Amechanganyikiwa na kuwa kama mwendawazimu, akitambea na kuongea peke yake njiani.



    Kwa msaada wa ushauri wa kisaikolojia aliopewa hatimaye alirejea katika hali ya kawaida, ndipo akakutana na mwanamke nje ya duka kubwa la Imalaseko



    katikati ya jiji, wakapanda kwenye gari kwa ajili ya maongezi, mwanamke huyo alipovua wigi na kujifunua uso wake, Phillip alishtuka na kuanza kulia.





    “NINI kilikupata dada yangu?”

    “Hunikumbuki?”

    “Kabisa.”

    “Mbona umelia?”

    “Nakuonea huruma.”



    “Nikikusimulia historia ya maisha yangu utanikumbuka, umewahi kuwa na rafiki msichana aliyeungua vibaya ndani ya gari?”

    “Wewe ni Lina?!” Phillip aliuliza tena mshangao macho yakiwa yamemtoka, hakuwa tayari kuamini kama kweli msichana aliyekuwa mbele yake ndiye Lina



    aliyewahi kuwa msichana mrembo ambaye sasa uso wake ulikuwa umejaa makovu.



    “Ni mimi, habari za siku nyingi Phillip?”

    Phillip hakujibu, akaendelea kububujikwa na machozi, kichwani mwake taswira ya Lina wa zamani ilikuwa ikionekana, hakika alikuwa ameharibika, uso wake



    ukiwa umejaa makovu makubwa, ilivyoonekana upasuaji wote wa kumrekebisha sura haukuwa na mafanikio makubwa kwani sura yake ya awali haikurejea.



    Hasira nyingi sana akazielekeza kwa Zamaradi.



    “Nisamehe!” Phillip alisema neno hilo pekee kwikwi ya kulia ilipomwachia.

    “Kwa kipi Phillip?”

    “Nahusika sana na ajali yako.”

    “Unamaanisha nini? Ulijua itatokea? Ilikuwa ya kupangwa?”

    “Hapana, ni historia ndefu naomba tu unisamehe.”



    “Hakuna shida, naweza kukusamehe lakini ni vizuri ukanieleza pia ni kwa nini unaniomba msamaha?”

    Phillip akajifuta machozi kisha kuanza kumsimulia Lina kila kitu kuhusu maisha yake, namna alivyoishi katika dunia mbili tofauti, inayoonekana na



    isiyoonekana akiwa mume wa Zamaradi, jini mwenye hasira ambaye alimshambulia kila mwanamke aliyemtaka kimapenzi. Lina alikuwa kimya akisikiliza.



    “Ndiyo maana nilikuwa sikubali uhusiano wa kimapenzi na msichana yeyote, lakini mabinti walinilazimisha na Zamaradi akawadhuru, ajali yako ilisababishwa



    na Zamaradi, yeye ndiye aliyemuua Monalisa pia katika ajali! Nisamehe sana kwa yaliyotokea, haikuwa nia yangu.”



    “Mh! Hii ni habari mpya, sikuwahi kufahamu jambo hili.”

    “Huo ndiyo ukweli.”

    “Huyo Zamaradi yuko wapi sasa?”



    “Nilipokutana na marehemu mke wangu na kuamua kuwa na uhusiano naye kimapenzi, Zamaradi alijaribu kutushambulia lakini kwa sababu tulikuwa



    tumekabidhi maisha yetu kwa Mungu na tulilindwa saa ishirini na nne alishindwa kutudhuru, tangu siku hizo sikuwasiliana tena na ulimwengu usioonekana,



    nikamuoa mke wangu na kuzaa watoto wawili mapacha ambao sasa wote wameniacha!”



    “Pole sana, nimesikia kila kitu kilichotokea, tuyasahau ya zamani tuangalie ulimwengu unaofuata mbele yetu.”

    “Umeolewa?”

    “Hapana, bila shaka hakuna mwanaume ambaye anavutiwa na mimi kwa jinsi nilivyo.”

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usiseme hivyo, mshukuru Mungu.”

    “Ahsante kwa kunitia moyo lakini mimi pia nataka nikuambie hata kama umepoteza mke na watoto wako, simama imara, endelea na maisha, usivunjike moyo,



    unakumbuka sura yangu mimi?”

    “Ndiyo”



    “Ilikuwa ya kuvutia, nikaipoteza katika ajali ya moto lakini bado nilisonga mbele, baada ya upasuaji wa kurekebishwa kufanyika, angalau kuwa hivi nilivyo



    niliendelea na masomo kwa msaada wa Umoja wa Mataifa mpaka nikapata shahada mbili za Uchumi na kuajiriwa nchini Marekani, nimehamishiwa hapa mwezi



    uliopita kuwa Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP!”



    “Kweli?”

    “Ndiyo”

    “Umenitia moyo.”

    “Hivyo ndivyo maisha yalivyo Phillip, Wazungu wanasema life is a series of events, yaani maisha ni mfululizo wa matukio, linaondoka hili linaingia lile, hivyo



    unatakiwa kusimama imara.”



    “Ahsante sana.”

    “Unaelekea wapi hivi sasa Phillip?”

    “Nazungukazunguka tu!”

    “Karibu nyumbani basi.”

    “Hakuna shida twende nikapafahamu.”



    Lina akashuka na kuzunguka upande wa pili ambako alikaa kwenye usukani, akawasha gari na kuondoka moja kwa moja kupitia Barabara za Ohio, Ali Hassan



    Mwinyi na baadaye Haile Selasie kuelekea Masaki ambako Lina alipiga honi kwenye jumba lenye lango kubwa na likafunguliwa.

    “Mh!” Mlinzi akaguna.



    “Vipi?”

    “Gari ni lenyewe, sauti ni ile ile akini bosi siye.”

    “Mungu wangu…” Lina aliongea akijigusa kichwani na usoni, alikuwa amesahau kuvaa wigi na sura yake ya bandia ndiyo maana mlinzi wake akashtuka, kwa



    muda wote walioishi pamoja hakuwahi kumwonesha jinsi alivyokuwa.



    “Wewe fungua lango, mambo mengine hayakuhusu.”

    “Bosi haruhusu wageni kuingia bila miadi.”

    “Nakuambia fungua, unataka kazi au?”

    “Eebwana ee, usinizingue, rudi kinyumenyume egesha pale nje umsubiri mpaka aje.”



    “Sawa, ngoja nikamlete.” alijibu Lina na kuanza kurudi kinyumenyume bila ubishi, akaligeuza gari kwa kasi na kuondoka hadi barabarani ambako alizunguka



    upande wa pili na kuvaa wigi pamoja na sura yake ya bandia, akarejea tena kwenye usukani na kuendesha kwenda nyumbani kwake ambako baada ya honi lango



    lilifunguliwa.



    “Karibu bosi!”

    “Ahsante sana.”

    “Walikuwa wamekuacha barabarani?”

    “Ndiyo, kazi nzuri sana, nilitaka kukujaribu ili nione kama watu wanaweza kuingia hapa kwangu kwa urahisi tu. Safi sana, chukua hii elfu kumi utakunywa



    soda”



    “Teh! Teh! Teh! Ahsante bosi nitaendelea kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa.”

    Gari likaingizwa ndani ya kuegeshwa sehemu yake, Lina akashuka na kumfungulia Phillip mlango kisha kumwita mlinzi na kumtambulisha kwamba huyo



    alikuwa rafiki pekee aliyeruhusiwa kumtembelea wakati wowote usiku na mchana bila kizuizi, Phillip na mlinzi wakashikana mikono.



    “Naitwa Phillip.”

    “Mimi ni Marwa, kutoka Taa-rime!”

    “Nafurahi kukufahamu.”

    “Na mimi hibyo, hibyo!”



    Phillip na Lina wakaanza kupandisha ngazi kuingia ndani ambako tofauti na watu wenye uhusiano wa kawaida, Lina akaanza kumtembeza Phillip kwenye



    nyumba yake kuanzia jikoni kisha kupandisha ngazi hadi kwenye chumba chake cha kulala ambako aliketi kitandani na kumwomba Phillip afanye hivyo hivyo.

    “Kaa tu usiogope, hakuna tatizo, jisikie uko nyumbani.”



    “Ahsante.”

    Kwa mara ya kwanza tangu apoteze familia yake, Phillip alijisikia faraja ya kweli moyoni mwake, akaketi kitandani kando ya Lina na wakaanza kuongea mambo



    mbalimbali kuhusu maisha tangu walipoachana, Lina hakuficha ukweli wake kwamba tangu aungue kwa moto hakuwahi kukutana na mwanaume hata



    akamwambia neno “Nakupenda” ingawa alikuwa na mafanikio makubwa mno maishani mwake.



    “Pole!”

    “Ahsante Phillip.”

    “Nakupenda.”

    “Kha!”

    “Mbona unashangaa?”

    “Una uhakika?”



    “Ndiyo.”

    “Hausemi tu kwa sababu una mfadhaiko baada ya kupoteza mke na watoto?”

    “Hapana, nakupenda Lina, nilivutiwa na wewe wakati ule ukiwa na sura ile, sidhani kama nahitaji kubadilika leo ukiwa na sura hii, upendo wangu ni wa kweli,



    naomba uniamini.”



    “Ghafla mno…”

    “Mapenzi ya kweli hayana maandalizi, isitoshe mimi ndiyo chanzo cha yote yaliyokukuta, naomba uamini nakupenda. Wewe ndiyo utakuwa faraja ya mtima



    wangu, utanipunguzia maumivu niliyonayo ndani, nikiwa na wewe nitakuwa mtu tena”



    Lina akainamisha kichwa chake chini, machozi yakaanza kudondoka na kulowanisha sakafu. Phillip akamsogelea na kumnyanyua, kisha kumkumbatia, akamvua



    wigi na sura ya bandia, halafu akamlaza chali kitandani na kuanza kumpiga mabusu mfululizo. Hisia za Lina zikawa kama mtu aliyekuwa akipigwa na shoti ya

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    umeme.

    “Usinishangae Phillip, ni miaka mingi sijakutana na jambo hili.”

    “Basi leo ndiyo leo.”



     ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog