Simulizi : My Rose
Sehemu Ya Pili (2)
Nilifika nyumbani vizuri na kama kawaida nikakutana na mama pale nje, nikamsalimia na tukaanza viutani vya hapa na pale lakini mwisho wa siku niliingia chumbani kwangu na kama kawaida kulikuwa kusafi na kunanukia manukato mazuri na ya kuvutia. Alikuwa ni Ritah, mtoto wa mwanajeshi kama kawaida yake.
Mara nyingi Ritah huletewa manukato hayo na baba yake kwa sababu baba yake ni mtu wa stoo ya jeshi, hivyo wakileta hayo madude na yeye hujichukulia kwa ajili ya nyumbani kwake.
Baada ya kubadili nguo zangu za shule, nilitoka na nikamkuta mama kakaa pale pale, na kisha bila kuzunguka alinidaka na swali.
“Umeona chumba kilivyo leo?”.Mama akaanza.
“Mmh! Mama na wewe na kiuzee chako hicho lakini unakuwa mbea, utasutwa”.Nilimjibu mama huku naingia sebuleni kwa ajili ya kwenda kula,wakati huo Baba alikuwa yupo safarini tena.
“Yaani mimi nimekuwa mbea Frank. Hivi wewe ungekuwa na mimama mingine unadhani wangekubari yule binti aingie humu?Kwanza ni kitoto,sijui miaka 16 kile. Lakini mimi kwa kuwa nakipenda na ndiyo naona kitakufaa, we unaniona mi mbea,sawa bwana”.Aliongea mama huku akionesha kiasi Fulani kaumia kwa maneno yangu. Nililiona hilo, hivyo nikatoka nje na kwenda pale alipokaa.
“Mama na wewe hutaniwi?Hivi bado hujanizoea tu mwanao? We ndo mama yangu,nikimtania mama mwingine unadhani nini kitatokea?”.Nilikuwa naongea hayo huku nampiga piga vingumi vya kichokozi na baadaye nikaa pembeni yake na kumkumbatia kama kumfariji na njia ya kuomba msamaha kwa nilichofanya.
“Embu niondokee hapa, linataka lijibaraguze baraguze ili na mimi nilikumbatie, sikukumbatii ng’oo. Lione likichwa lake, kama kiazi kitamu”.
“Ha haaa, hapo ndipo napokupendea mama yangu.Utani wako tu! Sasa kiazi kitamu kipo kama kichwa?”.Nilifurahi baada ya kumrudisha mama katika hali yake na nilikuwa naongea yale huku naelekea sebuleni.
“Ila mwanagu uangalie, kile kibinti kinakupenda. Usije ukajidai una roho mbaya halafu ukakiacha”.Aliongezea mama wakati huo mimi nilikuwa naelekea kwenye mlango wa sebule letu.
“Sawa mama, usijari kuhusu hilo”.Nilimjibu mama hivyo huku moyoni nikificha siri kubwa juu ya tabia yangu ya mtaani ya kuwachezea wasichana kama wale na kuwaacha na wakati huo akili yangu ikaamia katika msako wa Generose,binti mwenye mbwembwe na mapozi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kula ugali na nyama pale nyumbani wala sikupumzika,na kwa kuwa ilikuwa Ijumaa hivyo sikuwa na wasiwasi wa sare zangu za shule kwani ni hadi Jumatatu ndiyo nilitakiwa kwenda shule tena kwa ajili ya kupewa rikizo fupi baada ya mitihani. Mguu njiani kwa ajili ya kwenda kwa Babuu ambapo hapakuwa mbali sana na pale kwetu, ni kama dakika kumi nilishafika kwao na moja kwa moja nikaingia chumbani kwake. Siku hiyo nilimkuta yupo na Seth pamoja na Paul,na nilipofika kama kawaida yake alinikaribisha kwa mbwembwe nyingi hadi wenzake wakawa wanamshangaa.
“Oyoooo, Baba Ritah A.K.A wa mazali,au Baba Generose. Niambie”. Yalikuwa maneno ya Babuu.
“Mmmh! We Babuu, mbona unampa jamaa majina mengi hivyo? Baba Ritah mara Baba Generose,kuna nini hapo between”.Ilibidi Seth aulize kabla mimi sijajibu.
“Hata mimi nashangaa, muulizeni ndugu yenu anaweza kuwa anachanganyikiwa”.Na mimi nikaongezea.
“Embu Wa Kitaa toboka”.Paul naye akakomelea maneno ya mwisho.
“Mazee mmenivamia, kama nimeua, basi yaishe bwana. Ehee, Man’Sai leta ma news kwanza ya yule mchuchu.
Eee bwana Seth, leo jamaa kakutana na Generose wacha apagawe.Halafu mtoto akamzingua eti akasema yeye siyo Generose na wala hawamjui, hapo ni baada ya jamaa kuwasimamisha wote pale wakati wanatoka shule na kuwauliza swali kama wanamjua Generose”.Alikuwa anaongea Babuu huku akijaribu kufuta yale maswali aliyo ulizwa na kwa kiasi fulani alifanikiwa hilo.
“Acha wee, ina maana kaka uliwasimamisha wale wote!!?”.Aliuliza Seth kwa hamaki.
“Ishi! mbona kitu kidogo sana kile,kwani wewe Seth huwezi?”. Nilimjibu Seth na kumtupia swali.
“Dah! Mwanangu mimi ningezimia au kutoa haja fulani hivi,iwe kubwa au ndogo.”Alisema Seth na kutufanya wote tucheke mle ndani
“Ina maana Seth wewe domo zege,hahaaa? “. Nikamuuliza tena huku nacheka.
“Hilo zege hatari,usilione hivyo”.Alidakia Babuu
“Sasa kama zege, siku ile alimfataje Generose?”.Niliuliza tena,wakati huo Paul akiwa kaka kimya kama anasubiria wakati wa kuongea.
“Mimi mwenyewe nilishangaa,yaani sijui mashetani yake ya kipare yalimpandaga”.Babuu akazidi kuongeza radha ya maongezi.
“Aaah, mtajuana wenyewe.Oya mimi nimekuja kukupa ule mkakati wangu wa kumpata Generose”.Nilikatisha zile story na kwenda kwenye mada iliyonipeleka pale.
“Sasa hilo ndo kila mtu alikuwa analisubiria hapa, haya tuambie sasa”.Alikuwa Babuu ndio anasema hayo.
“Sasa sikiliza mdogo wangu, huu mkakati nimeutenga kwenye sehemu mbili. Sehemu ya kwanza nimeiita salamu na sehemu ya pili itaitwa uongo”.Nikanyamaza kidogo kuwapa nafasi ya kuongea.
“Sasa hapo sijakuelewa nia yako Yeroo”. Babuu akaongea tena.
“Ngoja nikueleweshe sasa. Tuanze na sehemu ya kwanza ya salamu.
Yaani inatakiwa kila siku ukikutana naye basi mwambie kuwa na msalimia.Hata kama sijakuambia,wewe unatakiwa kumwambia kuwa namsalimia”.Nikawa nimemaliza kuelezea sehemu ya kwanza ya mkakati wangu.
“Kha! Huo uboya kweli kweli, sasa salamu itasaidia nini?”.Babuu akakakandamiza swali lingine.
“Wewe Babuu na wewe unakuwa hata hufikilii haraka haraka. Kitendo cha wewe kupeleka salamu kwa demu kitamfanya demu aone mchizi ana mjali kichizi”. Hapo Paul ndiye aliyeongea.
“Tatizo lenu mnamchukulia Rose ni wa hivyo, muulizeni Seth”. Babuu aliongea huku akionekana kama kutokubaliana na ule mkakati na kisha kumgusia Seth kidogo.
“Sasa mimi nimefanyaje jamani,wewe huwezi kuongea bila kuniweka mimi kama mfano?”. Seth akaja juu huku anamraumu Babuu.
“Seth mzowee huyu,achana naye. Wewe Babuu fanya nilichokuambia na Paul si unaona kaelewa nini lengo langu? Kaa ukijua demu hata awe mgumu vipi, ila ukimuonesha kuwa una mjali tu! Basi huyo ni wako”. Nikawa naendelea kutoa somo kwa Babuu.
“Okey, ngoja nitafanya halafu tutaona”.Aliongea Babuu.
“Nakupa wiki moja ya kufanya hivyo. Mwanzoni lazima atakuwa mgumu tu! Ila ndani ya wiki asiposema na wewe msalimie,basi sipigi saundi tena”.Bado nilikuwa naendelea kutoa maujanja yangu kwa vijana wale ambao muda huo walikuwa kimya wakinisikiliza,nikaendelea..
“Huo mkakati wa pili utaendelea baada ya wewe kuja kuniambia kuwa kajibu salamu zangu na kukwambia kuwa na wewe unisalimie. Niamini dogo kwa haya mambo,mimi ndiyo James Bond”.Nilimaliza hivyo huku nikijifananisha na James Bond yule muigizaji wa filamu nchini Uingereza ambaye kwenye kila filamu lazima awatongoze wanawake na huwa hakataliwi.
“Ayaaa, Mr.Bond. Sisi yetu masikio bwana”.Akaongea Paul huku akitabasamu kwa kusikia nimejiita James Bond. Ilibidi Babuu akubaliane na hilo na aliahidi kuanzia Jumatatu mkakati utaanza kufanyiwa kazi.
Baada ya maongezi yale tukaanza kupiga story ya mambo mengine nazaidi niliwapa habari kuhusu Ritah na wote walishangaa sana kwa yule Binti kuwa na mimi, lakini mimi niliwajibu kuwa hiyo ndiyo kazi ya Mr.Bond.Wote wakacheka kisha nikawafundisha kidogo na baadaye kurudi zangu nyumbani.
Maisha yakaendelea na sasa kwa akina Babuu nikawa mgeni wao kila siku, na habari kubwa ikawa ni jinsi gani Generose ana pokea salamu zangu. Kiukweli kwa siku zile tatu za mwanzoni Generose alikuwa mgumu sana na alikuwa hataki kusikia habari zangu hata kidogo.
Babuu alikuwa anaanza kukata tamaa lakini nilimuambia ajikaze hivyo hivyo hadi aone mabadiliko. Sikuamini hadi wiki inakatika Generose alikuwa mgumu na alimpiga mkwara hadi Babuu kwa ile tabia aifanyayo. Hapo ndipo niliongeza hamasa ya kutaka kuendelea kumtafuta na sasa nikabuni njia nyingine ya kuandika vimeseji vya kwenye karatasi na kisha kumpa Babuu, na yeye Babuu alimpa rafiki wa kike wa karibu wa Generose, ujumbe ukamfikia pale alipo. Mara nyingi nilikuwa naandika kwa kumpa salamu na saa nyingine niliandika kumuomba msamaha kama nakosea kuandika vile viujumbe na uzuri alikuwa hajui kama Babuu ndiye aliyekuwa anavipeleka pale shuleni.
Baada ya wiki mbili kupita na nikiwa nimejitolea kwa moyo mmoja kumpata ndipo, nilipositisha vile vikaratasi na kumuambia Babuu asihangaike tena kwa sababu Generose hakuwa akijibu salamu zangu wala kuonesha kuwa anajali.
Mwanzoni Babuu alikuwa ananicheka nilipomsimamisha kile kitu bila kujua lengo la kumuambia vile na mimi nilimuacha acheke hadi azimie lakini siku zote nilijiamini kwa nifanyacho.Huku Babuu akidhani kuwa nimeshindwa, mwenzake nilikuwa nakamilisha mpango wangu japo ulinichukua muda mrefu sana kuufanikisha.
Babuu hakufanya vile kwa wiki mbili jambo lililofanya nitimize mwezi katika harakati zangu za kumpata Generose. Na kiukweli nilimkubaLi Generose, alikuwa ana msimamo sana kwani hata yule ambaye Babuu alikuwa anampa vile vikaratasi aliwahi kumlalamikia Babuu kuwa Generose anamtishia kuachana naye urafiki. Zilipopita wiki zile mbili za kukaa kimya ndipo nikamfata Babuu na kuongea naye kidogo kuhusu suala lile.
“Nambie dogo”. Nilianza na salamu hiyo.
“Poa, niambie mwenyewe”.
“Mi gado,anasemaje mtoto Rose?”.
“Wewe si umemshindwa bwana”.
“Nilijua tu,utasema hivyo.Lakini mi sikubaligi kushindwa kihivyo”.
“Sasa mbona ulikaa kimya?”.
“Hiyo ni moja ya sumu hatari sana kwa vitoto vinavyojidai vigumu”.
“Aaah wewe, yaani hata huongei halafu unasema ni sumu!!!!?”
“Kwa kuwa hujui kama ni sumu,basi na mimi sikuambii kama ni sumu hadi pale utakapoenda kuhakikisha mwenyewe”.
“Kuhakikisha kivipi sasa?”
“Nenda kaanze kumuambia tena kuwa Frank anakusalimia”.
“Hahahaaa, we ulishadevera pale,humpati tena hata kama nitaenda kumpa na ndege”.
“Dogo sikiliza. Nifanyie hili zoezi kwa siku mbili tu! Fanya leo na Ijumaa, asiposema neno mi nitanyoosha mikono juu kuonesha kuwa nimeshindwa”.
“Ok, poa Sai. Mi nitaenda hizo siku ili mpango wetu ukamilike”.
“Fanya hivyo,halafu utajua nini namaanisha”.
Nikamaliza maongezi hayo na Babuu na tukaanza kama kawaida kupiga stori nyingine za masomo na saa nyingine mapenzi, huku nikimgusia kidogo nachofanyaga na Ritah. Na saa nyingine nilimpa orodha ya mabinti niliokuwa natoka nao.
Babuu alikuwa wa kucheka tu, nakunihasa niangalie nisije kupata UKIMWI.Kitu nilichokijua toka kwa Babuu ni kuwa alikuwa anajua kuongea na wanawake lakini alikuwa muoga wa kuwaambia hisia zake na ndio maana hata Ritah alimkosa.
Ilikuwa ni alhamisi moja tulivu nikiwa nyumbani nimejilaza ndipo nilisikia hodi inagongwa mlangoni mwangu, na nilipofungua mlango nikakutana na Babuu akiwa kachanua tabasamu kubwa usoni pake na mimi kuona hivyo nikashikwa na shauku ya kutaka kujua undani wa tabasamu lile
“Vipi dogo?, mbona tabasamu pana kama umeokota simu”.Nilianza hivyo huku nikimpisha mlangoni aingie ndani.
“Eee bwana nimekukubari,wewe ni Mzee wa Mabinti”.Akajibu Babuu
“Hahahaaa, najua hiyo itakuwa ni taarifa nzuri sana. Haya toboka”
“Mtoto leo nikamwambia kuwa unamsalimia bwana, dah,aisee, kwa mara ya kwanza nikaona anatabasamu kusikia taarifa ile”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwisha habari yake huyo,unacheza na mimi nini”.Nikaongea hayo huku nainuka na kuanza kufanya tambo pale chumbani.
“Sasa sikiliza kwanza,najua umeshafanikiwa”.Babuu akakatisha zile tambo.
“Haya endelea dogo”.
“Basi nilivyo mwambia vile akaanza kutabasamu halafu kama anaona kinoma fulani hivi, mimi nikawa na mcheki tu! Wakati huo tupo nje mapumziko. Ghafla kakaniambia niambia na wewe msalimie halafu kakageuka fasta kakaanza kukimbia”.
“Hahahaaa,dogo umenikubali eeh. Sasa umeamini kuwa mi sijui kushindwa eeh. Sasa hapo sifanyi kazi ya salamu tena. We kesho ukienda mwambie uliongea kwa simu na mimi na nikakwambia kuwa nipo safarini, nimeenda kutoa mzigo wa kompyuta za Baba bandarini”.
“Ishi! Kwani dingi yako anafanya kazi ya kusambaza kompyuta?”.
“Huo ni mkakati wa pili ambao nimeuita uongo. Vitoto vya sekondari kama vile hupenda sana mambo kama hayo. Believe me dogo,lazima atauingia tu!”.
“Mh! Kwa kuwa umefanikiwa hili la kwanza,sasa nimeanza kukuamini mambo yako, nitafanya hivyo”.
“Sijamaliza bado.Mwambie kuwa narudi Jumapili halafu muulizie nikirudi nimletee zawadi gani?”.
“Hapo ndo nimekuelewa nia yako.Embu nipe siri ya kumsalimia ndani ya wiki mbili halafu ukaamua kuuchuna, na pale uliporudi kumsalimia tena mtoto akawa laini”.
“Aaah dogo, hujui kuwa na wale wana akili sana tu! Kitendo cha mimi kumsalimia kwa zile siku kilimjenga kifikra kuwa namjali na nipo siriazi na nikifanyacho. Baada ya yeye kukaa kimya si ndo na mimi nikaamua kuuchuna?. Basi hiyo ilimjengea fikra za kuwa nimechukia au nimekata tamaa au nimemuhisi vibaya hivyo lazima huruma itamuingia na kujigundua kuwa kafanya makosa. Hivyo nilipokuambia msalimie tena, angesipo kubali kurudia tena lile kosa la kuuchuna”. Yalikuwa maelezo yangu juu ya kuuchuna kwangu.
“Aisee nimekubali,naichukua hiyo”.
“Poa dogo”
“Fresh, ngoja mimi nirudi home kwanza nikafanye mengine”.
Babuu alitoka nje baada ya maongezi yale na kuanza kurudi nyumbani huku akiniacha nikiwa na furaha tele baada ya taarifa aliyoniletea.
Siku hiyo nilikuwa na furaha sana kwani na utozi wangu pale mtaani eti na mimi nikamuambia mama apumzike ili nipike mimi.
“Heee, makubwa, tangu lini mwanangu?Na hayo mashanga uliyovaa shingoni unapikaje, heheee”.Alikuwa ni mama akinishangaa na kuziita Culture nilizovaa ni shanga.
“Mama bwana, leo nataka nikupe mapishi yangu ili na wewe ufurahi kidogo, au unataka nife kabla ujaonja mapishi yangu?”.Nilimuambia mama kiutani.
“Haya. Mwiko na unga hivyo hapoo”. Alinikabidhi mama vifaa vya kupikia na hapo nikaanza kumwagia unga kwenye maji jambo lililofanya mama aje juu tena.
“Wee mtoto wee, huo ugali unampikia mbwa au? Liugali litakuwa gumu hilo, utalikata kwa shoka nakwambia”.Alikuwa anaongea huku anaweka utani wake.
“Mama tulia, mi leo ndo Chief Cooker,kwa hiyo tulia kama maji ya mtungini”. Nilimjibu mama huku kichwani nikijua kabisa naenda kubugi kwa sababu sijawahi kupika ugali hata mara moja.
Baada ya dakika tano kupita
“Mama ujue huu ugali mimi nimeukutia njiani,kwa hiyo embu upike mwenyewe nisije kuutoa mbichi bure”
“Umesha haribu ndiyo unajidai kukimbia hapa, na utaula. Lione likichwa lake kwanza”.Aliongea mama huku anapokea mwiko na mimi kumuacha mle jikoni akiendelea kupika ugali niliyo uanza.
“Katirumi”. Na mimi nikamjibu mama kwa kilugha chetu kwa kumaanisha kwa heri.
Sikuwa nimekosea sana kupika sema niliona uvivu kuendelea, hayo niliyaona wakati nakula ugali ule ambao mama alitumia nguvu kidogo kwenye kuumalizia.
Ijumaa ya wiki hiyo sikuenda shuleni kabisa kwa sababu mama alikuwa anaenda hospitali hivyo alinipa na mimi nafasi ya kumuita Ritah na kufurahi naye pale nyumbani.Ritah alikuwa ni msichana mdogo sana na alikuwa anasoma kidato cha pili pale pale Dodoma. Lakini Ritah licha ya kuwa mdogo alikuwa anavutia sana ,kuanzia umbo lake,sura na tabia yake. Alikuja nyumbani siku hiyo na tukafanya mengi ambayo ni kinyume na dini zetu hasa ile amri ya sita. Baada ya kumalizana na Ritah, nilimtoa na kumsindikiza kidogo nje na wakati narudi ndani ndipo nilisikia sauti ikiniita kwa nguvu nyuma yangu, nilipogeuka alikuwa ni Babuu akiniomba nimsubiri.
“Yereee, Man’Sai joo. Naona umetoka kuneemeka kwenye kiuno cha mtoto mzuri”.Alianza Babuu kama kawaida yake.
“Hahaaa, dogo kula kavu kwanza na unipe ma news ya mtoto G”.
“Mtoto ndiyo sababu ya mimi kuja hapa”. Aliongea Babuu huku tukiingia getini na kuelekea chumbani kwangu ambapo Ritah alishaparekebisha.
“Ehee, dogo niambie”.
“Mchuchu si ndo nikamwambia ishu kama ulivyonituma, basi ile kumwambia kuwa unamsalimia, mtoto akatoa bonge la smile huku anakula tuvidole twake. Basi wakati yupo katika hali hiyo nikamchomekea kuwa upo safarini Dar na unarudi Jumapili. Mtoto akazidi kutabasamu huku anaangalia pembeni, basi hapo nikamalizia kwa kumuuliza kuwa anapenda umletee zawadi gani. Unajua nini kilitokea? Nenda kwanza kaniletee fanta,usipoleta sisemi”. Alimaliza Babuu huku akinipiga kamkwara na mimi kwa kuwa nilikuwa na usongo,nikatoka nje kuelekea sebuleni kumchukulia soda aitakayo.
“Ehee, hapo sawa. Haya imenye kwanza”. Aliongoa Babuu huku akinipa soda ile nimfungulie.
“We dogo leo unajidai mfalme eeh, poa bwana”. Nilichukua ile soda na kumfungulia huku nalalamika.
“Sasa nisipokutumikisha leo, unadhani nitafanya hivyo lini. We fanya nachokwambia ili upate habari”.
“Haya endelea basi, maana ukianza kuchonga humalizi”.
“Basi bwana”. Akaanza Babuu kuongea tena baada ya kunywa ile soda funda moja la hatari.
“Mh! Dogo, umemwaga au umekunywa? Pigo moja,soda nusu”. Nilimtania kabla ajaendelea.
“Nitaacha Yeroo, wewe unataka stori au jinsi ya kunywa soda”. Alikuja juu Babuu kwa mkwara.
“Leo kanajidai haka kajinga”. Na mimi nikaongea kwa kunong’ona sauti ile ya chini chini.
“Unasemaje Yeroo?”
“Nasema endelea wewe ndiyo bingwa”.
“Ahaa, nilidhani umesema mimi mjinga”. Nikatabasamu baada ya kujua hakusikia nilichosema. Akaendelea.
“Ona sasa nimesahau,hivi nimeishia wapi?”.
“Si hapo uliposema sijiui ukamwambia nipo safarini Dar na nitarudi Jumapi……”.Hata sikumaliza akadakia
“Ehee, basi si ndiyo nikamuulizia akuletee zawadi gani? Basi kwa vijiaibu vyake huku anang’ata ng’ata vikucha halafu anazunguka zunguka kichwa chake na saa nyingine mwili mzima na kuifanya sketi yake kuwa kama feni. Eti akajibu umletee yoyote. Nikacheka kidogo kisha nikakumbuka ule msemo wako wa “kwisha habari yake” ndio ukazidi kunipa raha”. Bado Babuu alikuwa anaendelea kusimulia huku mimi muda wote,meno nje. Akaendelea
“Mi nikamwambia yeye achague tu! Hata gari utamletea. Mtoto ndiyo akazidi kutengeneza dimpozi kwenye mashavu yake kwa kutabasamu. Akakaa kimya kidogo huku kama anafikilia,halafu baadae akanijibu kuwa baadae nikamcheki kabla hatujarudi skani, na mimi nikakubali”. Babuu akawa anaendelea kutoa simulizi yake huku akizunguka tu! Akanyanyua chupa ya soda ile na kuiweka kwenye midomo yake kisha akaacha imiminike mdomoni, ila sasa hivi alikunywa kidogo.
“Ehee, endelea basi dogo, mbona unaniacha roho juu mtoto wa mwenzako”. Nilimwambia Babuu baada ya kuona kama anajishaua kuendelea.
“Leo zamu yako nakwambia, hadi ufe na presha”
“Embu acha ufala huo, kama hutaki kuongea si unasema tu! Umekuwa Ritah wewe kujishaua”.Nilimuijia juu kidogo Babuu kwa sababu niliona ananizingua tu!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa hiyo mwanangu unanipatia moto? Hahahaaa, kweli una usongo. Ngoja niendelee usije kunifia hapa halafu Mama Masai akaja kunidaba mimi”. Aliongea hayo Babuu na kisha akaendelea kunipa habari.
“Basi nilivyo maliza pale kuongea, yeye akaenda kantini kunywa chai kwa sababu ilikuwa breki, mi nikaenda zangu uwani kutoa urojo”. Bado Babuu alikuwa anaongea vitu nisivyo vitaka na sasa nikaanza kuingiwa na hasira zaidi ila sikutaka kumuonesha,nikawa navuta subira aendelee mwenyewe.
“Kengele ya kuingia klasi ikagonga, tukazama kwenye pindi la dini si wajua leo Ijumaa . Baada ya kumaliza pindi nini, saa saba hiyo, ikagongwa kengele ya kurudi masnika. Ile natoka tu! Namuona mtoto kasimama kwenye kamti Fulani hivi kapo pale skuli. Nikamfata halafu nikamwambia vipi sasa, ushafikilia? Kama kawaida yake, mtoto haishi tabasamu. Akacheki pembeni kama kuna watu wanaenda na muvu, halafu akanipa kikaratasi fasta fasta na kuniambia eti umpelekee maepo”. Akamaliza Babuu simulizi ambayo mi nilishaanza kuichoka ila ikanipa muhemko mwingine tena wa kutaka kujua zaidi.
“Yuhuuuu,epo tunda la wapenzi lile, lazima afe huyo. Sasa ndiyo mtamjua Man’Sai ni nani. Ehee, kakupa kikaratasi gani?”. Nikamtupia Babuu swali
“Ngoja, halafu hata sijakifungua, embu kicheki”. Alikitoa Babuu kile kikaratasi mfukoni nakunipa na yeye akaendelea kunywa ile soda.
“Mambo,pole na majukumu. Dar wazima? 0752353039 namba yangu hiyo, ukirudi nitafute. Zawadi yangu nishamwambia Yasint”. Nilikuwa namsomea Babuu ujumbe ule huku natabasamu kwa furaha. Yasint ni jina analotumia Babuu shuleni kwao.
“Kushinei, kwisha habari yake. Anacheza na Handsome wa kitaa hichi nini. Hata bila shilingi,watakuja tu warembo na wapambe”.Nikawa najigamba pale na Babuu huku nainuka kwenye kitanda na kurudi tena kukaa.
“Mimi nishamaliza kazi yangu na nitawapa wakina Seth habari jinsi ilivyokuwa. Sasa ndiyo tutaona kama utapenda au vipi”. Aliongea Babuu huku akikumbushia lengo la mkakati ule.
“Poa dogo, ila hapa kupenda labda mama yangu tu! Hawa viroboto wenu mi nachakapua tu!”
“Haya bwana, sie yetu macho. Kwa hiyo una mpigia lini?”.
“Nitampigia keshokutwa, Jumapili jioni ili nizuge nilikuwa Dar kweli”.
“Poa Man’Sai, nimekuaminia sana kwa staili yako”
“Poa Wa Kitaa, mi ndo mashine ya hawa ‘species’, taratibu kama nyau, lakini na bonge la mbio kama duma”
“We jamaa kwa kujipa maflagi mi nakuaminia. Poa bwana baadaye, ngoja nikale kwanza na asante kwa soda bwana,hapa najua sinywi tena hadi sikukuu”.
“Haha haaa, poa dogo.Ukiwa unakuja hapa unakunywa tu,siyo hadi ukalazwe”.
“Haya bwana, baadaye si utakuja uwanjani eeh”.
“Nitakuja ila sitocheza,si unajua nini kimefanyika leo getoni”
“Ahaa, poa bwana ila najua utakuja kunicheki Michael Owen navyofanya mambo yangu”. Alimaliza Babuu maongezi wakati huo tayari alishakuwa katoka getini na kuanza safari ya kwenda kwao.
Mambo yakawa yanaenda kama yalivyopangwa, Generose akawa kanipa namba yake na nilikuwa ninasubilia siku ya Jumapili ifike ili nimrukie hewani na kumjulia hali mtoto mzuri yule mwenye kila sababu ya kufanya hata ndege angani kugongana kwa sababu ya kumshangaa yeye.
Siku hazigandi na wala hazina kujiremba remba kama pozi za wadada poa au mwendo wa twiga. Hatimaye Jumapili ikawadia na ili niipeleke ifike hadi jioni,ikabidi nitoe rundo la nguo,zikiwemo zangu na za Baba kwa ajili ya kuzifua. Nilizifua nguo zile huku Ritah akinisaidia kuzianika hadi mida ya saa kumi jioni ambapo nilielekea bafuni kuoga na kumuacha Ritah akirudi kwao kwa ajili ya kufanya mambo mengine.
Kama unakumbuka mwaka 2004 kulikuwa hamna vifurushi kama X.trim au Cheka ila kwa voda ilikuwa ikifika saa sita usiku ni bure hadi asubuhi. Basi na mimi nikamuomba mama hela akanipa elfu tatu (kipindi ilikuwa hela kweli) na mimi kwa ubairi wangu nikaenda kuweka salio la mia tano halafu ile elfu mbili mia tano nikapanga kesho yake kwenda kumnunulia Generose zawadi zake. Baada ya kujaza salio lile sikutaka kupoteza muda, nikafungua kitabu cha majina ya simu na kutafuta jina la Rose kisha nikapiga.
“Haloo”.Ilisikika sauti ya kike upande wa pili baada ya simu kuita kidogo tu.
“Haloo, mambo vipi?”. Nikajibu
“Poa mzima? Kwani wee nani?”.
“Mi rafiki yake Yasint”
“Ahaa, usharudi toka Dar?”
“Ndiyo,nilifika saa tisa. Sasa fanya hivi,hiyo ndiyo namba yangu, sasa hivi na vikazi kidogo. Nitakupigia ile usiku tuongee kwa starehe”.Niliongea hayo baada ya kusikia mlio wa sauti ukinijulisha kuwa salio linakata.
“Poa basi, baadaye”.Akajibu Generose na kukata simu.
Furaha ikanijaa baada ya maongezi yale mafupi, nikatamani kwenda kwa Babuu kujitapa kwake lakini ilikuwa tayari ni usiku kiasi na Baba alikuwepo siku hiyo hivyo ikala kwangu.
Mida ya saa nne nikiwa najisomea mama akaniita kwa ajili ya chakula cha usiku, na baadaye alinipa taarifa kuwa dada yangu Vene na Angel, watakuja kutoka Morogoro walipokuwa wanasoma kidato cha nne. Hivyo kesho nilitakiwa kufanya usafi. Baada ya maneno yale ya mama nikaelekea chumbani kwangu huku nikiwaza ni jinsi gani nitachomoka kwenda kumnunulia zawadi Generose. Baadae nikapanga mpango wa kutoroka asubuhi niende kufanya hivyo japo najua watakuwa hawajafungua.
Katika kuvuta muda kwa kusoma soma,hatimaye saa sita ikawadia na bila kuchelewa nikachukua Kisimensi changu mayai na kumpigia Generose. Simu iliita mara mbili tu! Ikawa imepokelewa……
“Haloo”.Alianza Generose kwa sauti kavu iliyoonekana hakuwa amelala hata kidogo.
“Hey mambo”. Nikamjibu
“Fresh mzima wewe?”.
“Mi mzima, yaani hadi sasa hivi hujalalaga tu!”.
“Nilikuwa najisomea kidogo si unajua cha tatu msuri wake”.
“Haya bwana. Asante kwa kuitikia wito wangu”.
“Wito gani tena?”.
“Si huu wa kupokea simu na sasa naongea na wewe”.
“Ahaa, hilo halina shida. Hivi kwani wewe unaitwa nani?”.
“Mh! Ina maana hunijui?”.
“Ndiyo sikujui”.
“Kwa hiyo unaweza kuwa unaongea na jini bila kujijua”
“Aaa,siyo hivyo bwana”. Hapo sauti yake ilikuja na kicheko kidogo cha chini chini.
“Mh! Una cheko nzuri wewe,embu cheka tena”.
“Embu acha bwana, mbona hivyo?”.Huku akiambatanisha tena na kile kicheko.
“Dah!Aisee una ni kill me softly na hiyo cheko”.
“Kumbe mtundu wewe eeh”
“Aaah, siyo hivyo bwana, yaani mara hii ushajua kama mimi mtundu?”.
“Sasa jee, huto tumaneno twako huoni kama ni utundu?”.
“Mh! Mi sijui hilo,nachojua mimi naongea huku natamka yaliyo moyoni”.
“Haya bwana, nitajie jina lako basi”.
“Kwani wewe umenisevu nani kwenye simu yako”.
“Haha haa, mi naogopa kukwambia”.
“Dah! Umecheka tena Rose, yaani hapa kamoyo kamepiga putuu”.
“Haha haa, embu acha mambo yako bwana, niambie unaitwa nani”.Kiukweli Generose alikuwa ananikosha sana na cheko yake, ilikuwa kama imekauka fulani hivi halafu ilikuwa ni ya kistaarabu sana.
“Haya bwana, we niumize tu na hiyo cheko yako”
“Basi sicheki tena, haya niambie jina lako”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa usipocheka mimi nitalalaje?”.
“Hee, kwani cheko yangu ndiyo kitanda?”
“Siyo kitanda tu! Ndiyo godoro,mashuka,mito na usingizi”.
“Haha haa, we una vituko sana”. Baada ya haya maneno yakiambatana na cheko yake, nilikaa kimya kwa sekunde kadhaa bila kuongea, kitu kilichomfanya Generose kuniuliza.
“Vipi? Mbona kimya ghafla?”
“Daah! Yaani siyo siri, cheko yako mi inanipa ganzi huku”.
“We bwana usiwe hivyo”. Hapo aliongea kidogo kwa kudeka au sijui kwa kubembeleza, utajua mwenyewe unayesoma utavyo tafsiri.
“Mamaaaa, we Rose wee. Unataka unifanyaje mtoto wa mwenzio?”
“Kwani nimefanyaje?”
“Hiyo sauti uliyoongea hapo, unadhani ni sauti ya kunifanya niwe mzima kweli?”
“Haha haa, yaani wewe”.
“Ona, umecheka tena”.
“Hee, haya makubwa sasa, wewe kila kitu nachofanya mimi, kumbe nakutesa”.
“Siyo kunitesa tu! Unaniua huku unanipuliza, yaani sisikii maumivu bali raha”.
“Mh! Hivi wewe msanii?”
“Hapana, kwa nini?”
“Yaani, una vimaneno vya ajabu, sasa nakuuaje huku unasikia raha?”
“Haha haa, hayo maneno tu! Si unajua nakaa karibu na maua waridi, lazima nitanukia”.
“Haya bwana. Kwa hiyo hutaki kunitajia jina lako?”.
“Nitakutajia, ila niambie kwanza umenisevuje”.
“Naogopa bwana.Kwani hutonuna”.
“Sina tabia hiyo, we mwagika tu!”
“Haya ngoja nikwambie. Upo tayari?”
“Nipo tayari,lete mambo”.
“Nimekusevuuu, Mr.Who”.Akataja jina aliloninakili kwenye simu yake huku akiangua kicheko chake kile.
“Ishi! Sasa kwa nini umenisevu hivyo?”
“Si kwa sababu sikujui”.
“Ina maana Babuu akukutajia jina langu?”
“Babuu ndiyo nani?”.
“Aaah, sori. Huku home tunamuita Babuu,ila la shule ni Yasint”.
“Ahaa, alinitajia ila nimelisahau”.
“Ok, poa basi. Futa hilo halafu andika kati ya haya. Frank au Masai au Man’Sai na ukiona hayo marefu basi andika Sai”.
“Mi nimelipenda la Masai. Kwani wewe Mmasai?”
“Hamna, hilo jina tu! Mimi wa Magharibi”.
“Magharibi ndiyo wapi?”
“Rukwa huko, mitaa ya Sumbawanga”.
“Ohoo, usije ukaniroga bure”
“Acha mambo yako bwana, hizo stori tuu!”
“Nakutania bwana”.
“Haya na wewe wa wapi”.
“Mimi wa Iringa”
“Haaa, kumbe wote wa Magharibi?”
“Magharibi kivipi yaani, ujue sikuelewi”.
“Magharibi namaanisha, ile Mikoa ipo Magharibi mwa nchi yetu”.
“Ahaa, nimekuelewa. Mimi Muhehe bwana”.
“Kamwene”. Nikamsalimia Kihehe.
“Mnogage”. Akajibu naye.
“Ahaa, kumbe unajua”.
“Endelea sasa, mbona unaishia hapo?”
“Haina haja, mimi nilikuwa nataka kuakikisha tu!”
“Hiloo, halijui haha haa”.
Kiukweli niliongea sana na Generose siku ile.Ilikuwa ni mara ya kwanza lakini nilikuja kugundua kuwa damu zetu zimepatana sana,alikuwa mtu wa utani na hapa kwangu alikuwa amefika kwa hilo.Maongezi yalinoga hadi saa nane na nusu iligonga bado tukawa tunapiga story tu! Sikumgusia mahusiano yake hata kidogo kwani nilikuwa namvuta vuta kwanza ili aniweke kichwani halafu mambo mengine yangefata kama taratibu za mazishi.
Baada ya kuongea naye sana kuhusu masomo na viutani vingine, sasa kila mmoja akawa anataka kulala.Kwa hiyo tukafanya maongezi ya mwisho.
“Zawadi zako vipi, kesho utazipitia?” Nikamuuliza swali hilo.
“We mpe Yasint aniletee”.
“Kwa nini usije wewe?”
“Mimi tutapanga siku ya kuonana,siyo kesho”
“Ok,poa. Basi itabidi umuambie Babuu aje ile mida ya mapumziko akuchukulie”.
“Haya Masai”.
“Poa wa ukweli, ila nipe kitu cha mwisho”.
“Kitu gani?”
“Cheko yako”.
“Hahaha haa, wee nawe huachi vijimambo?”
“Asanteee, nimeisikia hiyo”
“Haya bwana, usiku mwema”.
“Nawe pia, uamke huna mguu”.
“Haha haa, mi sitaki bwana”
“Acha kabisa, naona sasa hivi umechanganya vyote. Sauti tamu na kicheko ndani yake”.
“Embu toka huko, tulale”
“Haya poa, usiku mwema”.
Nilimaliza kuongea na Generose usiku huo na kunifanya nijisikie raha sana kwani alikuwa ni msichana tofauti sana na wengine niliopita nao. Yeye alikuwa na utani mwingi na anajua jinsi ya kuitumia simu kwa ajili ya maongezi. Wengine hawajui hilo,wao wakipigiwa, unaongea nao dakika mbili halafu utasikia nasikia usingizi, lakini Generose alithibitisha kuwa anajali mtu.
Asubuhi na mapema nilidamka na kuvaa nguo za mazoezi kwa ajili ya kuzugia ili hata nikirudi nyumbani nimechelewa wajue kuwa nilikuwa mazoezini, kumbe mwenzao kiguu na njia hadi mjini kwenye duka moja wanaliita Kwa Mjomba lipo barabara ya kwenda hospitali ya Agakhan karibu na sheri ya GAPCO.
Kwa bahati nzuri nilikuta wameshafungua, hivyo nikanunua maepo matatu kwa shilingi elfu moja mia tano halafu nikamnunulia na kadi moja kubwa kiasi iliyoandikwa kwa kiingereza,
“My heart is still beating your name from the first day I saw you. You made my head to think more about your face than my life”. Yaani “Moyo wangu bado unadunda jina lako tangu siku ile nilipokuona kwa mara ya kwanza. Umefanya kichwa changu kiwaze sura yako kuliko maisha yangu”.
Mimi mwenyewe niliyashangaa yale maneno.Nilijua ni uongo tu! Ila nitafanya nini ili kumvuta mtoto karibu.Hatimaye nikaiweka kwenye bahasha na safari ya kurudi nyumbani ikashika namba.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimkuta mama anahangaika peke yake kusafisha chumba watakachofikia wale dada zangu wa Morogoro, hivyo kabla hajaniona nilinyata na kuingia chumbani na kuficha zile zawadi kisha nikaenda kumsaidia mama kusafisha kile chumba ambapo mida ya saa tano tayari kilikuwa safi na tayari kwa kuishi mtu.
Baada ya kumaliza ile kazi nilikaa kama nusu saa na kwenda kuchukua chakula.Kwa kuwa nilikuwa sinywagi chai asubuhi hivyo mama alikuwa anawaisha chakula cha mchana ili mwanaye nisikae na njaa. Wakati naingiza chakula ndani ndipo nikasikia sauti ya Babuu ikiniita.
“Oya vipi?Fanya fasta mwanangu nipe kimzigo cha Rose kanituma,halafu tushaingia class”.Aliongea Babuu baada ya kumfata pale alipo na kusalimiana.
Nikaenda chumbani na kuchukua zile zawadi na kumletea Babuu na hapo hapo Babuu akaanza safari ya kurudi Shuleni kwao kwa kasi kiasi fulani huku akiwa na baiskeli.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment