Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

MY ROSE - 3

 







    Simulizi : My Rose

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikumuona tena Babuu kwa siku ile, nadhani alikuwa ana mambo mengi ya kufanya ndiyo maana hakuja hata mida ya jioni.

    Dada zangu walifika pale nyumbani na sasa familia ikawa imeongezeka na kuwa na furaha kiasi chake tofauti na mwanzoni. Utani nao ukaongezeka baina ya watoto na wazazi hadi Baba naye alikuwa kwenye kundi lile kitu ambacho sikukitegemea katika kalia yangu pale nyumbani, na tena alikuwa ana utani mkali sana.



    Muda ukasogea na hatimaye ukafika ule muda wa saa sita,muda ambao tulikuwa tunautumia mimi na Generose kuongea. Kama kawaida nilimpigia na kuanza kupiga naye stori za hapa na pale na hatimaye nikamuulizia kuhusu zawadi;

    “Vipi ulipata zawadi zangu?”. Nilimuuliza hivyo na kumfanya atoe kale kakicheko kidogo na kisha akajibu.

    “Niliipata, ndiyo”.

    “Vipi umezipenda?”

    “Eee, nimezipenda”

    “Na kadi yangu, umeipenda?”

    “Sana tu”

    “Haya, na mimi lini utaniletea?

    “Siku yoyote tu!”.

    “Haya bwana.Kwa hiyo sikutani na wewe?”

    “Usijali, ipo siku utakutana na mimi tu!”

    “Poa bwana,we ukiamua tutaonana”.Baada ya maongezi hayo tukaongea mengine mengi sana hadi tukakosa cha kuongea na kubaki kuiga lile tangazo la “Kata basi” halafu yule mwingine anajibu “Kata wewe”, ndiyo ikawa hivyo siku ile.



    Ndiyo yakawa maisha yetu mimi na Generose. Alikuwa halali bila kuongea na mimi. Kila muda wetu ukifika ni lazima anibipu ili tuongee. Maongezi yetu yalikuwa hayana maana,ila yalikuwa yanaenda hadi saa tisa za usiku na saa nyingine kama siku za mapumziko,tuliongea hadi saa kumi na moja. Huyo ndiye Generose Bandari,ambaye nilitafutiwa na wakina Babuu.



    Siku moja nikiwa nyumbani na dada zangu tunapiga soga mbali mbali,ndipo nilipokea simu ambayo ilipigwa na Generose akinitaka niende Saint John nikakutane naye kwa mara ya kwanza na kuonana vizuri. Nilifurahi sana na sikuwa na mpango tena wa soga, nikatoka zangu nje na kuelekea bafuni kuoga, kisha baada ya kutoka nikavaa mavazi yangu nadhifu na safari ya kwenda Chuo Cha St.John ikaanza. Hapakuwa mbali, kwani baada ya dakika kama kumi tayari nilikuwa mbele ya Generose ambaye muda wote alikuwa kapambwa na tabasamu usoni mwake kana kwamba hajui shida.

    “Ndiyo wewe au?” Nilianza kumchokoza kwa maneno hayo na kama kawaida alitoa kicheko chake na kunifanya nigundue kitu kimoja ambacho ni ubovu wangu sana. Ni dimpozi.

    Generose alikuwa ana dimpozi tena mashavu yote ambazo zilinifanya nikae kimya kama nimepigwa mshale wa sumu.

    “Ndiyo mimi,kwani vipi”. Alinitoa kwenye lile ganzi kwa maneno yake, na kisha nikaanza kuongea naye tena.

    “Umependeza sana,halafu kumbe una dimpozi, dah!”.Niliendelea kumwaga porojo zangu kwa Generose.

    “Hivi wewe unataka kuchanganyikiwa eeh, yaani kuwa na dimpozi ndo iwe tatizo?”.Aliongea Generose huku anaendelea kutabasamu na kuzifanya dimpozi zake ziendelee kuutesa mtima wangu na kuugaragaza kabisa moyo wangu ule wa kipindi kile.

    Nikatamani nimuombe nizishike au nizibusu,lakini nilijifikilia kuwa atanionaje? Hata siyo mpenzi wangu wala urafiki wetu haujafikia huko. Ikabidi nigugumie maumivu huku nikijiambia moyoni kuwa ole wake siku ajilengeshe, ndio atanijua kwa nini najiita Mr.Bond.

    “Haya bwana ngoja mimi niumie tu! Maana nikikuambia mateso yangu kwa sasa hivi,sidhani kama hutoacha kunipiga kofi”. Niliongea hayo huku nikijibaraguza kwa kuangalia pembeni kama kuna watu wanaenda na kipindi katika maongezi yetu.

    “Haha haa, halafu wewe. Yaani kumbe siyo kwenye simu tu!. Mambo yako ufanyayo kumbe hata live upo hivyo hivyo”.

    “Yaani ujue jinsi unavyoongea hapa, mwenzako naweza kuwehuka.Hiyo cheko yako na hizo dimpozi basi mimi holoo”.

    “Nitakuchapa sasa, naona unataka kunifanya katoto kadogo kwa kunidanganyishia na pipi”.

    “Haha haa, haya mama, usije kunirapua bure. Twende basi pale Camp David tukakae kidogo”.Nilikubali yaishe huku namuoneshea eneo moja pale Saint John lenye migahawa na huduma nyingine za kijamii na za kiuwanafunzi, eneo lile linaitwa Camp David.

    Huku nikiwa na shilingi elfu tano mfukoni, tukaanza kwenda pale Camp David na kwa makusudi nikaacha atangulie ili niuthaminishe mwili wake vizuri.

    Jamani siwafichi wote mnaosoma simulizi hii.MUNGU hata sijui nimpe cheo gani vya hapa duniani ndiyo mnielewe. Vyeo kama Profesa,Dokta au Mheshimiwa sijui Jiniazi, havifai kumpa MUNGU. MUNGU ni zaidi ya hivyo vyeo. Kiukweli,nimewahi kuona kazi za MUNGU nyingi sana alizoumba hapa duniani, ila kwa Generose, nahisi hakufanya kosa hata kidogo. Maana mtoto kwa huku nyuma alikuwa kafungasha kamzigo fulani hivi kakichokozi chokozi, yaani kale kanachoweza kukupa mshawasha wa kutaka kujua ndani kuna nini. Siyo makubwa sana kama kiti cha baiskeli kilichobeba kiroba chenye nyama na wala siyo kama vijipu au mapunye,bali alikuwa wastani lakini mwenye umbile lililoingia kwa ndani pale kiunoni halafu pakaja kutanuka tena kwa juu pale kifuani kwa kubeba matiti madogo yaliyofanya tisheti yake iende kwa mbele sentimita kama nne hivi,halafu nusu sentimita nyingine ikaachia zile chuchu zilizokuwa hazijazuiliwa na sidiria kuchomoza na kusababisha mapigo yangu ya moyo yatake kusimama na kuachia mapigo mengine kunako nanii yaanze kupanda na kushuka.

    Achana na huko kifuani, panda hadi kwenye shingo yake isiyo na mikato mikato wala michirizi kama kwapa la msukuma chapati.Ilikuwa imebeba cheni ya silva yenye herufi ya G, na usoni pake ndipo hasa paliponifanya leo hii niandike simulizi hii, alikuwa kapambwa na tabasamu kila wakati, tabasamu ambalo akilitoa, basi linaacha vishimo vidogo kwenye mashavu yake mateke na ambayo sidhani kama yaliwahi kuguswa na midomo ya watu wengine zaidi ya baba yake au mama yake tena utotoni kuonesha upendo.

    Tukiacha huko, nataka ujue ni jinsi gani MUNGU ni zaidi ya Maprofesa.Ni ile miguu yake, kuanzia mapajani hadi unyayoni, nyie acheni tu! Wacha watu waimbe “Acheni MUNGU aitwe MUNGU” maana dah! Embu ngoja mimi niachie hapa,maana nikiendelea kusema na jinsi alivyokuwa anatembea kwa maringo na kistaarabu,mtaniona mimi muongo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nawajua wanawake bwana. Kuna wengine kila muda wapo kama wanataka kukimbia, ukiwaambia twende huku, hapo ndio utakoma. Vumbi linatimka kama mafarasi yamesikia mlio wa risasi. Lakini Generose alikuwa anaweza bwana,tena siyo kuweza tu! Generose angekuwepo leo hii, tungesema majanga.



    Nikiwa bado nyuma ya Generose namtafakari kwa makini huku tunaelekea Camp David, ndipo aliponigeukia huku ana tabasamu na kuniambia nisogee mbele,yaani nitembee nikiwa pembeni yake. Na mimi bila hiyana nikafanya hivyo na kusababisha baadhi ya watu kule tulipokuwa tunambea macho yao yaamie kwetu. Generose hakuwa mrefu sana wala mfupi, nilimuacha kidogo sana, kitu kilichofanya tupendeze sana wakati tunatembea pamoja.



    “Mmmh! Watu wanatuangalia kichizi, dah!”.Nikaanzisha maongezi hayo baada ya kuona tunatembea bila hata kuongea,huku maongezi yale yakiwa yana lengo la kutaka kujua atachukuliaje hali ile.

    “Kwani wewe una muogopa nani? Wale wote si binadamu kama wewe, hebu twende”. Kama maongezi yangu yalivyotaka, na Generose alikuwa kaingia mwenyewe. Alinishika mkono na tukaanza kuelekea ulipo mgahawa mmoja ambao waliuza na vinywaji vya aina mbalimbali hasa vinywaji laini.



    Tulikaa meza ya pembezoni na kuagiza vinywaji vyetu huku kama kawaida yangu nikamuomba mhudumu aliniletee Fanta, na Generose yeye aliagiza juisi ya ukwaju iliyochanganywa na ubuyu na kisha tukaanza kuburudika.

    Kitu nilichogundua kutoka kwa Generose, alikuwa ni mstaarabu na mwenye heshima hasa wakati wa kula au kunywa. Hakupenda sana kuongea wakati anafanya matendo haya mawili, na hata akiongea husubiri kwanza ameze anachokula,ndiyo anaongea. Na akiongea haongei maongezi ambayo yatamkwaza mtu mwingine,kwa mfano kumchekesha mtu wakati anakula. Najua mnanuna jinsi navyomsifia, ngoja niishie hapa.



    Wakati tunaendelea kupata vinywaji vyetu pale kwenye ule mgahawa, ndipo nikapata wasaha mwingine wa kutaka kumjua Generose.

    “Rose, nikuulize swali?”

    “Uliza tu, usiogope”. Huku anatabasamu.

    “Hivi una mpenzi?”

    “Pruuuu, koh koh”.Swali lile, likamfanya juisi yake impalie na kusababisha kikohozi kumtoka, huku kikiambatana na machozi kwa mbali. Sikutaka kuipoteza fursa hiyo, nikasogea pembeni yake na kutoa leso,kisha nikaanza kumfuta, jambo ambalo alishindwa kulizuia kwa sababu hakutegemea kama nitafanya vile kwa muda ule mfupi tangu lile tukio litokee.







    “Mbona hivyo sasa jamani”. Nilimuuliza Generose baada ya kumaliza kumfuta ile juisi.

    “Sikutegemea swali kama hilo kwa wakati huu”.Alijibu Generose huku akionesha hali ya mfadhaiko na aibu kwa mbali.

    “Sasa jamani,si swali tu kama maswali mengine?”. Nikazidi kudadisi ili aniambie.

    “Yaani, nashindwa kuelewa kwa nini umeniuliza swali kama hilo kwa wakati huu”.

    “Kwani nimekosea Rose?”.

    “Hamna, sema naona kama umewahi sana kuniuliza”. Nilielewa kwa nini Generose hakutegemea swali lile kwa wakati ule, kwa sababu alijua endapo atalijibu swali lile kitakachofuata hadi hapo ni kutamkiwa maneno matamu na kachaa mimi.

    “Kwa hiyo hutonijibu?”. Niliendelea kumvuta vuta kwa maswali ya mitego.

    “Nitakujibu. Ila sitopenda tuongelee sana hayo kwa sasa”.

    “Ok. Mimi swali langu hilo ni tu, na wala sitakusumbua tena”

    “Sina mpenzi, na wala sijawahi kuwa naye hapo kabla”.Alinijibu Generose na kusababisha aamshe maswali kibao kichwani mwangu hadi nikasahau kuwa nilimuahidi kutoongelea hilo suala tena.

    “Unataka kuniambia wewe niiii………, Oh sorry Rose, nilisema sitakuuliza tena”.

    “Hamna, wewe uliza tu!”. Aliongea Generose kwa sauti ya chini chini iliyojaa aibu,uoga na kama simanzi ndani yake. Huo ndiyo ubovu unaowakumba wasichana wengi hapa duniani, ukisha onesha mwanzoni hutaki kuliongelea hilo suala halafu baadaye unaliruhusu. Wakwale wa mambo hayo kama mimi, hatukuachi.

    “Yaani wewe hujawahi kufanya mapenzi?”. Nikafunguka kamanda. Na hakujibu kwa mdomo bali kuitikia kwa kupeleka kichwa chini na juu kuonesha kusema ndiyo.

    Kichwani nikaona na bonge la bahati, yaani ndani ya mwaka napata wasichana wawili ambao hawajawahi kuguswa. Nikatabamu na kujisemea moyoni kuwa nikimkosa huyu, itabidi niende kuoga maji ya baharini.

    “Hongera mama yangu, na endelea kujitunza hivyo hivyo”. Nilimjibu hivyo huku nikionesha kuwa sina kama haja naye.

    “Asante, kwani wewe unaye?” Na mimi nikatupiwa swali ambalo nilijua lazima lijitokeze na nilisha lipanga tangu nyumbani jinsi ya kulijibu.

    “Sasa kwa muonekano wangu, kweli nitakosa mpenzi?”. Nilimuambia ukweli lakini ni ukweli ambao ulikuwa una jambo dogo ndani yake, wataalamu wachache wanaweza kutumia mbinu kama hiyo. Kiukweli alipoa kidogo lakini alitaka kuificha hali ile kwa kuendelea na maongezi.

    “Hongera sana, inaonekana una mpenda eeh”.Alinyanyua kichwa na kunipa hongera hiyo.

    “Aaaah,we acha tu! Nipo tayari kufa kwa ajili yake kama litaitajika suala hilo”.Nikazidi kukomelea maneno yangu ambayo yalizidi kumtoa mchezoni Generose.

    “Mh! Haya bwana, wenye bahati zenu”. Aliongea huku akilazimisha tabasamu.

    “Siyo wenye bahati zenu,sema wenye bahati zetu”.

    “Haha haa, sasa mpenzi unaye wewe halafu mwenye bahati niwe mimi?”.

    “We umejuaje kama huyo mpenzi mwenyewe siyo wewe?”Swali hilo likamfanya Generose ashituke kiasi na kutoa macho usoni mwangu kana kwamba kaona mdudu ananitambalia.

    “Heee, una maana gani?”Swali juu ya swali, badala ya kujibu langu kwanza, yeye akaniuliza tena.

    “Wewe ndiye mpenzi wangu, sina mwingine. Kama wewe siyo wangu basi nikatae hapa hapa”. Kama nilivyojipanga toka nilipotoka, ndivyo ilivyoenda. Kimya kikamkumba Generose na hapo ile juisi ikaanza kuwa kama chungu vile.Nilipoona hivyo nikaamua kamanda kuanza kufunguka yaliyo moyoni mwangu.

    “Sikiliza Rose, sijaanza leo kukupenda. Ni kitambo sana nilikuwa nakuhitaji.Nadhani ulikuwa hunijui hata kidogo,lakini mimi nakufahamu muda mrefu sana, yaani tangu kidato cha pili, sema ile siku nilikutana na wewe ukiwa na rafiki zako niliona umebadilika sana, na pale ndipo nilianza kukupenda zaidi na zaidi”.Nikaweka kituo kidogo kwa kunywa soda yangu, halafu nikasogeza mikono yangu na kushika mikono ya Generose na kuendelea kutapika maneno aliyonijalia maulana kwa wakati ule.

    “Sipo hapa kwa ajili ya kukutaka kimapenzi,bali nipo hapa kuhitaji uwe wangu mpenzi. Sipo tayari kuishi bila sauti yako na sura yako. Amini usiamini Rose, wewe ndiye ua waridi langu, You’re my Rose baby”.Nikazidi kutema maneno matamu huku nia yangu ikiwa ni moja tu! kuwathibitishia wakina Babuu kuwa mimi ni hatari kwa watoto wa kike na vile vile, sitopenda mtoto wa mtu. Hivyo maneno yote yale yalikuwa ni uongo tu!. Sikuishia hapo kuongea, nikazidi kuuvuta moyo wa Generose.

    “Embu kumbuka nimeanza lini kupigania uwe karibu yangu Rose,najua unajua ni lini.

    Embu angalia macho yangu vizuri Rose,unaona nini?

    Nadhani unaona sura yako. Lakini vipi kwenye moyo wangu, unaweza kuona chochote? Najua huwezi. Lakini jinsi ya kuyaona hayo ya moyoni,ni lazima usikilize maelezo haya nayokupa,na hiyo ndiyo picha utakayo iona kwenye moyo wangu”. Nikatulia tena huku nimemkazia macho Generose ambaye muda wote niliyokuwa naongea alikuwa kimya huku kanishikilia kwa nguvu mikono niliyomshika, naona ni sababu alihisi kutetemeka. Kiukweli hakutoa tabasamu hata kidogo,jambo lililonipa shaka na kudhani kuwa atanikataa.

    “Rose, najua una mengi sana ya kuniambia, lakini nakupa muda wa kwenda kufikilia jibu sahihi ambalo nadhani kwako halitakukwaza. Lakini kama kwako halitakukwaza, naomba na kwangu lisinikwaze pia. Maana ukifanya hivyo moyo wangu utashikwa na ganzi la mapenzi na kamwe sitohisi kupenda”.Nikazidi kumdanganya mtoto wa watu ambaye sasa alikuwa analegeza mikono yake na kisha kuongea.

    “Frank. Mi sijui. Aaah, naomba niende nyumbani”.Generose alifungua mdomo wake lakini alishindwa kuongea kutokana na maneno yangu niliyoyaongea.

    Nilisikiliza ombi lake la kurudi nyumbani, hivyo nilimwambia amalizie juisi yake ndiyo tuondoke.Hakufanya hivyo kitu ambacho kilinifanya kamanda mwenyewe niichukue ile juisi na kuigida bila huruma.

    “Kumbe tamu eeh”.Nilimwambia Generose baada ya kuinywa ile juisi kitu kilichomfanya atabasamu na kuangalia pembeni wakati huo mimi nilimuita mhudumu na kulipia vinywaji vyetu vile.. Baada ya kulipa tulitoka zetu pale kwenye mgahawa na kuanza kumsindikiza Generose kwao ambapo palichukua kama dakika arobaini na tano kufika.

    Nilipenda kutembea naye kwa miguu ili nipate nafasi ya kuongea naye. Mara nyingi nilikuwa naongea maneno ya kuvutia na kumchekesha hili hata akinitosa anikumbuke maneno yangu.



    Muda wote tuliyokuwa tunatembea Generose hakuongea hadi tulipofika karibu na kwao ambapo alioneshea kwa mbali na kuniambia kuwa wazazi wake ni wakali hivyo wangemkemea endapo ningeenda naye. Tuliagana huku nikimuacha bila kumuambia neno lolote na kutokana na hali aliyonionesha, nikajua tayari nishachezea mtoso.



    Nilitembea haraka haraka huku nikiwa na mawazo juu ya Generose na kila nikifikilia maneno niliyokuwa nayaongea, nikawa natabasamu peke yangu huku nikijiuliza nilipoyatoa yale maneno. Wakati naelekea nyumbani ndipo nikapata na wazo la kwenda kwanza kwa akina Babuu.

    Moja kwa moja nikaelekea mawazo yangu yaliponituma na uzuri nilimkuta yupo, tena peke yake.



    “Hilo bwana, Yeroo lenyewe. Nambie kwanza”.Alianza Babuu kwa utani na kisha kunisalimia kwa kunipa tano.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Poa kijana, vipi mbona kimya sana?”Niliitikia na kumtupia swali.

    “Mi nipo tu! Vipi Generose?”.

    “Dah! Leo nimekutana naye bwana”.

    “Haaa, umekutana naye? Ilikuwaje?”.

    “Nimefanya bonge la misteki,yaani ndo leo mara ya kwanza kukutana naye, si nikampiga saundi”.

    “Ishi! Sasa hiyo misteki gani? Mbona poa tu!”.

    “Tatizo ni demu, yaani kaonekana kama kutofurahia kile kitendo”.

    “Kwani kakujibuje?”.

    “Hajanijibu kitu,halafu alipoa sana kitu ambacho alinifanya nijishtukie na kuanza kuropoka ropoka tu! nikidhani nitamrudisha kwenye hali yake”.

    “We tulia tu! atarudi mwenyewe”.

    “Ngoja nitulie bwana,si wajua sijui kubembeleza, kama hataki nabaki na Ritah. Naye akizingua, nasaka mwingine”.

    “Haha haaa, maneno ya mshindwaji hayo”.

    “Sijawahi kushindwa dogo, we subiri atose awamu ya kwanza halafu ndo utaona awamu ya pili navyotema sumu za kobogo, mtoto hadi atalia”.

    “Haya bwana,mimi yangu macho”.

    “Tatizo dogo unadharau, hilo ndilo linanifanya nizidishe hasira za kumsaka.Na nikimpata ujue natembeza mdudu tu!”.

    “Haha haaaa, we jamaa ni mjinga sana, shauri yako mwenyewe”.

    “Halafu bwana, mtoto kaniambia kuwa yeye ni sildi”

    “Sildi ndiyo nini sasa.Halafu wewe una vimaneno vyako binafsi vya kihuni,hata havijulikani. Mara mdudu, sasa hivi unasema sildi. Sasa sildi ndiyo nini?”

    “Yaani ajafunguliwa bado, hajawahi kuguswa na mwanaume”.

    “Ayaaa, ina maana unaenda kufungua tena kama Ritah? Jamaa una zari wewe”

    “Hicho ndo kitu kinachonifanya nisitake kumpoteza Rose”.

    “Haya bwana, ngoja sisi tuangalie mwisho wake tu!”

    “Mi ndo Mr.Bond, wewe tulia na angalia, uone kama nitapenda. Si mmemleta wenyewe,basi hiyo ni kesi yenu”.

    “Haya bwana, ngoja mimi nikaoge basi”.

    “Fresh, ngoja na mimi nirudi nyumbani kwanza”.

    “Poa kijana,nitawapa taarifa na wakina Seth”.Alimaliza Babuu wakati huo mimi nilikuwa natoka chumbani kwake na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.

    Nilipofika nyumbani nilikaa na dada zangu na kupiga stori za hapa na pale hadi mida ya saa tatu usiku nilipoingia chumbani kwangu. Nilimfikilia sana Generose kwa jinsi atakavyo nichukulia kwa kitendo nilichomuonesha. Hatimaye nikapitiwa na usingizi mkali sana.



    Nilikuja kushitushwa na simu iliyokuwa inapigwa mida ya saa saba za usiku na nilipoangalia alikuwa Generose. Nilipoipokea akakaa kimya kidogo na kisha akaanza kuongea.





    “Haloo”. Alianza Generose kwa sauti ya upole kama ametoka kulia au anaumwa.

    “Hey,mambo. Mbona hivyo?”.Na mimi nikamjibu huku namshangaa hali yake.

    “Hamna kitu.Yaani basi tu!”. Aliendelea Generose kwa sauti yake ile ile.

    “Mimi sipendi bwana uwe hivyo”. Nikamwambia hivyo na kumfanya asijibu chochote zaidi ya kusikia anavuta mafua tu!

    “Hey Rose, una nini mama?”. Nilishikwa na uwoga baada ya hali ile, ikanibidi nimuulize huku nikiwa na hamasa ya kutaka kujua kinachomsumbua.

    “Frank, sijawahi hata mara moja kukaa namfikilia mwanaume aliyenitaka.Lakini wewe leo hii umenifanya hata chakula nikione kichungu mdomoni mwangu”. Akakaa kimya kidogo huku nikisikia kama anapenga makamasi, wakati huo mimi roho yangu nilikuwa nafurahia kinachokuja kutokea baada ya haya maongezi. Akaendelea.

    “Frank, wewe ndiye unaweza kunifanya mimi nikalala usiku huu na kesho nikaamka na furaha mwilini mwangu. Nakupenda sana Frank, nakupenda kuliko hata nilivyokuwa nakuonesha pale mchana. Siwezi bila wewe Frank naomba uamini usikiacho, nipo tayari kufanya chochote kwa ajili yako. Lakini tatizo lipo kwako, ni kweli unanipenda au unataka kunichezea tu!? Frank, naomba kama unataka kunichezea basi uniache kama nilivyo kwani kama utafanya hivyo, sitakuwa na sababu ya kuishi hapa duniani.

    Sasa ni heri uniambie kabla sijaingia katika uhusiano na wewe”.Generose aliongea hayo huku akionekana mwenye kumaanisha asemacho jambo lililonifanya nijifikilie mara mbili kabla sijamjibu.

    Kiukweli kwangu nilikuwa nataka kuwathibitishia wakina Babuu kuwa mimi ni mkali wa mambo yale kwa watoto wa kike, hivyo maneno ya Generose yalinigusa kwa mara ya kwanza tangu nianze kuongea na wanawake.

    “Generose, mi ni F na wewe ni G, yaani tunafatana kama majina yetu yanavyojieleza. Sipo tayari kukupoteza na sitakuwa tayari kuichoma nafsi yako motoni kwa matendo yangu. Niamini Generose, umeumbwa kwa ajili yangu na endapo utakufa na mimi nitakufa, UKIRUKA nami NITARUKA, kumbuka nayokwambia”.Nilijikuta nateremka maneno ambayo hata MUNGU aliyeyasikia aliniadhibu ili nimaanishe nayoyasema. Baada ya maneno hayo, Generose alifungua kinywa chake na kuongea.

    “Frank, nakukabidhi moyo wangu kama mwanaume wa kwanza katika maisha yangu, usije ukanifanya nije kuyachukia mapenzi na wanaume wote duniani. Nakupenda sana Frank, narudia tena, nakupenda sana Frank, wewe ndiye kila kitu kwangu. Tangu nilipoanza kuongea na wewe, sikuwahi kununa kwa sababu ulinipa furaha ambayo hata mama alikuwa hajawahi kuiona tangu nizaliwe. Frank, nithamini mimi kama mama yako unavyomthamini. Usije kuitesa nafsi yangu, tafaadhari”. Generose alizidi kusisitizia kuhusu upendo huku mimi taratibu nikaanza kujutia uamuzi wangu wa kumtaka.Ila nikajipa moyo na kujisemea moyoni kuwa hata wale niliowapitia,walikuwa hawana hamu ya kuachwa na mimi,sembuse huyu ambaye hata siwajui wazazi wake. Hapo ni kurapua na kuacha,ndicho kilichokuwa kichwani mwangu kwa wakati ule. Lakini kama ningelijua nini kitakachoenda kutokea mbeleni mwa maisha yangu, kamwe ningesipokuwa karibu na Generose.

    “Sikiliza Rose, mimi siyo kama wanaume wengine wasiyojua thamani ya upendo kwa wasichana na heshima kwa mwanamke. Ni kweli kabisa, wewe ni sawa na mama yangu kwa sababu huu mwanamke kama yeye,nahitaji kukuheshimu kama yeye. Kamwe sitaruhusu kucheza na hisia zako, na kama nitafanya hivyo basi sasa hivi nakuambia, kuwa nitalaaniwa”. Nilijikuta nazidi kuropoka maneno ya ajabu na wala hayakuwa na faida kwa Play Boy kama mimi kwani ingesipo tokea kutomsaliti Generose.



    Niliongea mengi sana usiku ule mimi na Generose na mwisho wa yote ilikuwa ni furaha ya Generose kurudi kama zamani na zaidi alikuwa ana furaha sana nikimuambia kuwa nampenda sana.Huo ndiyo ukawa mwanzo wa furaha yetu mimi na Generose, furaha ambayo sikuwaza kama itakuja kukatishwa na mtu yeyote hapa duniani.



    Kesho yake nilihamka mapema na mwenye tabasamu lililochanua kama ua saa sita lililokutana na unyevu nyevu na jua kiasi. Nilikuwa sihishiwi maneno mdomoni kama kanga aliyeona nyoka. Ilifika kipindi hata dada zangu walinishangaa.



    “We vipi leo, mbona una furaha kama kumepikwa wali?”. Aliniuliza dada yangu mmoja aitwaye Angel.

    “Hivi huyo hamumjui? Ana kibinti chake kizuri hicho, kinakujaga hapa hadi kumpigia deki”.Alidakia mama huku wakiniacha mimi niendelee kutabasamu zaidi na zaidi.

    “Haaa, mbona uniambii My Twin Bro?”.Dada yangu mwingine ambaye nilimzidi miaka miwili naye aliongea.Alikuwa anaitwa Veneranda. Huyu aliniita mimi pacha wake kutokana na tulivyolelewa. Tulianza shule ya msingi pamoja, tena darasa moja. Hadi kidato cha nne tulisoma pamoja, nilikuja kumuacha kidato baada ya yeye kukosa sifa za kuendelea kidato cha tano,hivyo yeye alienda Morogoro kurudia masomo yake. Ilikuwa tukitoka shule au popote pale, ni lazima awe pembeni yangu hadi watu wakatuita mapacha.

    “Atawaambia huyo? Sijakiona muda sana, sijui kanawaogopa nyie”.Aliongea mama.

    “Kwani mama anaitwa nani huyo wiifiiii”.Dada yangu Angel akazidi kupekua. Ukweli nilimkataza Ritah asiwe anakuja nyumbani kwa kisingizio kuwa dada zangu wangeleta longo longo, lakini hiyo ilikuwa ni njia mojawapo ya kutaka kumuweka mbali ili asije kuniaribia mkakati wangu kwa Generose.

    “Anaitwa Ritah, kile kitoto cha Mama Neema. Kinampenda hicho”.Mama akafunguka kwa kuweka mambo hadharani.

    “Haaa, kaka utafungwa.Hivi baba yake si mwanajeshi yule. Kaka ile kesi”.Dada Angel akawa ananishangaa kwa kuwa na Ritah wakati ni mtoto mdogo kwangu, na zaidi alinionya kwa ninachokifanya.

    “Hahaha haa, sister acheni zenu.Mimi yule sipo naye tena. Na kitu kipya kabisa ambacho nitakitambulisha kwenu hivi karibuni”.Ilinibidi nitoe lile zogo kwa kumtosa Ritah, kitu ambacho mama hakukipenda hata kidogo.

    “Ina maana Frank umekaacha kale katoto?Jinsi kanavyokupenda vile….. We mwana weee”.Mama alishindwa kumalizia maneno yake huku dada zangu wakimshangaa kuhuzunika vile.

    “Sasa mama unataka mwanao akafungwe?Huyu ana miaka 21 yule sijui kama 18 kafika, huoni kama kesi hiyo”.Dada Angel aliongea wakati huo mimi nikawa najiuliza umri wa Generose, lakini nilijipa moyo kwa sababu Generose alikuwa ana umbo kubwa kuliko Ritah.

    “Zama nabwa,ijusi pivi, leka totoka nambo dogoka nasa.Niya alivyo apo utadhani laka furaba (Maza bwana,sijui vipi,kale katoto mbona kadogo sana.Yaani alivyopoa utadhani kala barafu”.Dada Angel alikuwa bado anaendelea kumshangaa mama huku akiongea lugha ya kinyume ili mama asielewe.

    Lugha ile tulikuwa tunaitumia sana pale nyumbani ili kumficha mama baadhi ya mambo yetu. Mara nyingi yeye alidhani tunaongea kiingereza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hahaha haa, aniiju waku mi ni ndamaka, nime atipi ngiwe zichiki paha taaki. Wam aju, Rashua na dada keya Aphiso, tewo atipi lepa. Na naku nengike kanatwai Sejonaphi, leka totoka ka Gacham nyemwe kadu lepa. Mbara lepa diha zizawa kewa wakaka shamia Arusha. Yuhu Tari nime taka wenyemwe ziu, haha haaa” {Anijui kuwa mimi kamanda,nimepitia wengi kichizi hapa kitaa. Wamjua Ashura na dada yake Sophia, wote pitia pale. Na kuna kengine kanaitwa Josephina, kale katoto ka Mchaga mwenye duka pale. Ramba pale,hadi wazazi wake wakamuamishia Arusha. Huyu Ritah nime kata mwenyewe uzi}”. Tukazidi kumuacha mama kinywa wazi kwa lugha yetu hadi akaamua kutoka nje ili akaendelee na kazi nyingine.

    “We nawe unaona sifa kufanya hivyo”.Dada yangu Vene akaongea baada ya kimya kifupi cha kumsubiri mama atokomee kabisa.

    “Hee, we Vene, embu muache Bro awafanyie. Mi mwenyewe ningekuwa dume. Hawa wangenikoma. Ila kwa Ritah kaka ulibugi, kale ni katoto. Wewe size yako ni wakina Ashura”.Dada Angel akazidi kusifia na vile vile kukandia.

    “Sister kale kalitaka kenyewe, sasa mimi nitafanyaje?”. Nikajitetea

    “Haya bwana, tuyaache hayo. Huyo mwingine anaitwa nani na lini tutamuona?”

    “Hahaa, huyo anaitwa Generose ndiyo jana tu! kanikubalia, mambo yakiwa safi, nitamleta tu! si unajua ndo tunaanza?, hivyo hawezi kukubali kuja home sasa hivi”.

    “Bro angalia watoto wa watu,usije ukatuletea matatizo hapa”.Dada yangu Vene naye hakuwa nyuma kutoa wasaha wake.

    “Sister usijali,Generose ndiye wa mwisho, sidhani kama nitakuwa Player tena”.Niliwajibu dada zangu hivyo huku moyoni nikijua kuwa Generose naye atapitiwa kama Ritah na kuachwa. Tuliongea mambo mengine huku nikimuomba dada Angel aende kuongea na Ritah kuhusu kuachana na mimi kwa kutumia kigezo cha mimi mkubwa na Ritah mdogo. Alikubali na nahisi alifanikiwa kwa sababu Ritah hakunitafuta tena kitu kilichofanya akili yangu iamie kutaka kufanya juu chini Generose aingie chumbani kwangu…





    BAADA ya utani wa hapa na pale kutoka kwa dada zangu, nilitoka nje na safari ya kwenda kwa akina Babuu ikaanza. Nilikuwa natembea taratibu huku natumiana meseji na Generose ambazo nilizipata kutoka Vodacom baada ya lile shindano la Tuzo Pointi. Tulikuwa tunatumiana meseji nzuri sana,ambazo zilikuwa zinanifanya niwe najisikia raha sana kuendelea kuchat na Generose.

    Hatimaye niliingia kwa akina Babuu na nilimkuta yupo na wale jamaa zake wote niliyowakuta naye siku ile mara ya kwanza. Nilipoingia kama kawaida yao,walinilaki kwa furaha huku kila mmoja alikuwa ana shahuku ya kutaka kujua nini kinachoendelea kati yangu na Generose.

    “Ehee, we jamaa afadhari umekuja, eti mchuchu kazingua?”Alianza Paul kuuliza wakati huo mimi nilikuwa nipo bize kuchat na mtu waliyosema kanizingua na zaidi nilikuwa natabasamu huku nimeitolea macho simu yangu, kitu kilichomfanya Paul aone kama nimemshusha. {Kumbuka Paul ndiye yule dogo tuliyokuwa hatupatani sana na mara nyingi tulikuwa tunapishana kauli zetu}

    “Sasa mwanangu si nakuuliza au ndo full mashau”.Aliongezea Paul lakini kwa kuwa nilikuwa na furaha, sikufatilia sana maneno yake zaidi ya kumpa simu yangu na kumuambia asome zile meseji.

    “Mimi napenda tuwe na watoto wawili, mmoja wa kike na mwingine wa kiume. Wa kiume nitamuita Aman jina la baba na wa kike tumuite jina la mama yako”. Paul ndiye alikuwa anaisoma meseji mojawapo niliyotumiwa na Generose,meseji ambayo iliwafanya watu wote mle ndani kushangilia. Mara ikaingia nyingine, Paul nayo akaisoma.

    “Na huyo mtoto wa kiume napenda atoke amefanana na wewe ili hata ukifa niwe nakukumbuka nikimuangalia yeye”. Baada ya kumaliza kusoma ujumbe huo, wote wakaanza kucheka kutokana na Generose kuombea mimi nife.

    “Huyo ana utani mwingi sana nyie, mkimfatilia mtaona kama anazingua”.Nilimtetea Generose huku nikichukua simu yangu kutoka kwa Paul na kumjibu Generose halafu nikamwambia baadaye kidogo, na vikazi nyumbani. Alikubali na hapo ndiyo nikaanza kuongea na wakina Babuu.

    “Haya sasa vijana, mtoto ndio huyo katua kwa Mr.Bond, hapo tena sina huruma wala amani, ni kichapo tu!”.Yalikuwa maneno yangu kuonesha kuwa sitokuwa na utani endapo atakubari kunivulia nguo.

    “Mh! Bro hadi hapo mimi sina swali, yaani na utata wote ule,sasa hivi mtoto kalegea kama uzi wa mlenda!! We ni noma kaka”.Seth hakusita kutoa pongezi zake baada ya kujua nammiliki Generose.

    “Sasa hapo ndiyo kazi inaanza rasmi, ya kwanza umefanikiwa kumpata kama ulivyosema. Sasa ya pili, Je!? Utampenda ndani ya miezi mitatu? Hicho ndo tunasubiri” Paul alikuwa anaongea hayo kama ananikumbusha majukumu yangu.

    “Haha hahaaa, hiyo sahau kabisa katika akili yako, huyo atamegwa na kuachwa kama wale wengine”.Niliongea hayo huku nikionesha wazi kuwa sina muda naye.

    “Ila mwanangu kwa nini usimfanye awe wako tu! daima? Mtoto mzuri kama yule kwa nini usimuweke awe pamanenti tu!”. Aliongea Seth huku akinitaka nimfanye Generose awe wangu wa daima.

    “Tatizo hilo lipo nje ya makubaliano yetu, nyinyi mliniletea yule muone kama nitamuweza, hilo nimefanikiwa na lingine mmesema kama nitampenda, hilo ndiyo msubiri kuliona”.Nilimjibu Seth.

    “Sisi hatujui hayo,si tunataka kuthibitisha tu hapa. Hayo mambo ya kumtaka awe pamanenti,mtajuana wenyewe”.Aliongea Babuu ambaye alikuwa kimya sana tangu niingie.

    “Poa dogo,kama vipi mfate Ritah, nishaachana naye”.Nilimgeukia Babuu sasa.

    “Kwa hiyo mimi ndiyo wa kula makombo yako?”.Babuu aliniuliza.

    “Kwani mademu wote waliowahi kugongwa ni makombo?”Na mimi nikageuza swali.

    “Tatizo wewe umekula, halafu unataka na mimi nikale tena”.

    “Kwani tatizo ni nini? Wewe una undugu na mimi?”

    “Hata kama sina undugu na wewe, ila siwezi kuchomeka wewe ulipo chomeka” .Babuu akazidi kuwa mgumu.

    “Kwani wewe Babuu unampenda Ritah au haumpendi”.Paul akatupa swali kwa Babuu.

    “Kiukweli nampenda, lakini nikiwa naye huyu jamaa atajigamba na kunikashifu sana”.Babuu akajibu.

    “Ahaa, kumbe uoga wako wewe kukashifiwa na mimi? Hilo ondoa shaka kijana, mimi ni mtu wa masihara mengi, lakini linapokuja suala kama hilo, basi tabia kama hizo siwezi kuzifanya. Hayo mambo ya kujigamba mimi sinaga. Umeshawahi kusikia mimi najisifu kuwa namla demu fulani?” Nikawa naongea maneno ya kumuelewesha Babuu ili anisikilize na aende kwa Ritah,na ili mimi niwe huru kutembea na Generose mahala popote pale mtaani bila kikwazo.

    Mara nyingi huwa natumia njia ya kuwaunganishia rafiki zangu kwa wasichana niliyotembea nao ili mimi nipate nafasi nzuri ya kufurahi na msichana wangu mpya. Na richa ya kutembea na wanawake wengi pale mtaani kwetu, sikuwahi kuwa na wasichana zaidi ya mmoja kwenye mahusiano yangu. Yaani nikipata msichana mpya, naachana na yule wa zamani kwa njia yoyote ili niwe na yule mpya.

    “Nani hakuamini wewe Masai? Jinsi navyokujua kwa kujisifia, haha haa, hilo hunivuti”.Aliongea Babuu kudhihirisha kuwa ana msimamo.Sikuacha kumpa moyo na kumvuta.

    “Hivi wewe unamjua Safina yule demu wa Gasper?”.Nikamuuliza Babuu.

    “Kwa nini nisimjue yule”.Akajibu Babuu.

    “Sasa yule nilipiga mimi kabla sijawa na Salome demu wa Salum. Na hao wote, mimi ndiyo niliwaunganisha ndo wakawa wapenzi. Mnayajua hayo?”.Nikampa kithibitisho Babuu kumuonesha kuwa sikuwa na tabia za kujitangazia.

    “Haaa, ina maana na Salome ulikula jamaa”.Akadakia Paul huku akionesha kutoamini.

    “Mimi nacheka na watoto wazuri kama wale? Nafumua tu!”.Nikamuacha Paul bila swali.

    Hizo ndizo zilikuwa tabia zangu pale mtaani.

    Baada ya kuongea sana mambo kama yale, Babuu alikubali nimuitie Ritah ili wazungumze kuhusu kuwa wapenzi.Wakati huo nilishamwambia Dada yangu Angel aende kumwambia Ritah tuachane kwa sababu ya umri wetu kupishana sana.

    Tuliongea sana siku ile kiasi kwamba nikamsahau hata Generose ambaye baadaye alinishitua na meseji kwa kuniuliza kama bado naendelea na kazi. Nilimjibu bado kidogo, na baada ya hiyo kidogo kupita nilianza kuchat naye tena huku narudi nyumbani,na siku hiyo tulitumiana meseji hadi usiku.

    ************************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    BAADA YA MWEZI MMOJA.



    Generose alikuwa kama kichaa juu yangu kitu ambacho taratibu kikaanza kunibadilisha moyo wangu na kuhisi kama naanza kumpenda. Sikuwahi kumtaka hata mara moja kwenda kufanya naye mapenzi kitu kilichofanya Generose azidi kunipenda kwani ni wanaume wachache sana wangeweza kuvumilia hali hiyo.



    Tofauti na nilivyotegemea, Generose akawa haishi kuwa karibu yangu huku tabasamu na cheko yake vikawa silaha tosha ya kunifanya niwe zezeta kichwani mwangu.

    Kiukweli nilianza kubadilika na kuanza kumpenda Generose, ikawa haipiti hata sekunde bila kuwasiliana naye. Simu yake kama haipatiakani, basi moyo wangu uliteseka sana na kujikuta nikitamka maneno ya uchungu sana baada ya simu yake kuwa hewani. Mabadiliko haya sikutaka kuwaonesha wakina Babuu kwani ningefanya hivyo wangeniona mimi mjinga na kunishusha thamani, hivyo nilikaa kimya huku nikijigamba kuwa siwezi kumpenda Generose.



    Ilikuwa ni kidogo kidogo kuanza kumpenda Generose. Lakini mara ikawa kileleni yaani kama grafu,basi iligusa nukta ya mwisho au kama ni maji ya moto, basi yalichemka kwa joto la 100 F{Wale wa hesabu mnajua}. Siyo kumpigia simu tu! ndo ikawa kazi yetu, bali ilikuwa akitoka shuleni kwao ni lazima apite pale nyumbani na kupata chochote ndiyo aende kwao.

    Dada zangu walimpenda sana Generose na walikuwa wana msaidia sana kimasomo, kitu kilichomfanya Generose amshinde hata Babuu darasani na wakati hapo mwenzoni Babuu alikuwa anamuacha mbali Generose kimasomo.



    Nilikuwa nakaa na Generose kwa muda mrefu sana, na bado alikuwa akirudi nyumbani, ukifia ule muda wa saa sita usiku tunapigiana simu na kuongea kwa masaa mengi sana. Siku moja nilimpigia simu kama kawaida yetu ifikapo saa sita za usiku. Akapokea simu na baada ya salamu na viutani vya hapa na pale aliniuliza swali.

    “Hivi Baby, huna mpenzi mwingine kweli?”

    “Hacha bwana, ina maana umeanza kutoa imani kwangu?”.

    “Hamna, siyo hivyo. Mimi nahisi unanisaliti”.

    “Kwa nini unasema hayo, honey”.

    “We unafanya mapenzi na nani, hadi usinitake hata mara moja tufanye”.

    “Hahaa, Rose bwana. Mimi nimekupenda wewe, hayo mambo ya kufanya mapenzi ni makubaliano kati yangu na yako”.

    “Mh! Haya. Mimi nilikuwa na mashaka na hilo tu!”

    “Usijali mama yangu, upo peke yako. Ila tupange ilo jambo ili tuondoane mashaka au unasemaje?”.

    “Haha haa,embu toka hapa, unataka unichane”

    “Hahahaa, hivi wewe hauachagi masihara tu? Embu nijibu bwana”. Alikaa kimya kidogo kama anafikilia jambo na kisha akaongea.

    “Siku nikija kwenu basi, maana mwenzako sitaki kufa na bikra. MUNGU akiniuliza kwa nini nimeenda nayo mbinguni na wakati nilikuwa na mtu ninayempenda duniani, nitamjibu nini?”.

    “Ha hahaaa, haya bwana, mimi nakusubili hata ukija mwakani utanikuta”.

    “Okey Baby, tulale basi maana leo nimechoka mwenzako”.

    “Poa katoto kangu, lala salama eeh”.Simu ikakatwa baada kunitakia usiku mwema pia na hapo kila mmoja nadhani akawa anasubiri siku iwadie ya kuyajenga.





    Tuliendeleza mawasiliano kati yetu kwa muda mrefu huku kila mmoja akieleza hisia zake juu ya mwenzake, na wakati huo kiukweli nilikuwa nimekubali kila kitu kuwa nampenda Generose lakini kama nilivyosema hapo mwnzo, sikuwaambia wakina Babuu.Nilimpenda sana Generose, kiasi kwamba hata majina niliyokuwa nayaandika shuleni kwenye madaftari yangu na hata kwenye kutunga sentensi ni lazima nimuweke na Generose.

    Siku zikaenda na kukatika na hatimaye ikafika ile siku ambayo kila mtu alikuwa anaisubiria kwa hamu katika maisha yake ya mapenzi. Mimi nikiwa na hamu ya kumuona Generose mwili wake kiundani zaidi na yeye akiwa na hamu ya kuwa msichana.



    Nakumbuka siku hiyo tulishapanga tangu jana yake usiku kuwa kesho yake ni lazima atakuja nyumbani mapema na kufanya kale kamchezo. Ilikuwa ni kazi rahisi sana kwake kuingia chumbani kwani dada zangu walikuwa mstari wa mbele kufanya hivyo.

    Kwa kifupi mnaweza kuwashangaa sana dada zangu, lakini ni dada ambao wapo kisela sana,na ninahisi ni dada bora mimi kuwa nao kuliko mtu yeyote duniani. Ni kweli walikuwa ni wasela sana lakini huwezi kuwasikia wao wakifanya mambo ya kihuni kama nilivyokuwa nayafanya mimi. Kifupi walikuwa wanajiheshimu sana,kiasi cha baba yangu kuwapeleka Morogoro na kuwapangishia chumba ambacho walikuwa wanakaa wao peke yao.Na kuthibitisha kuwa wao wanajiheshimu na walikuwa siriazi, ni baada ya matokeo yao ya kidato cha nne waliyokuwa wanarudia {risit} kutoka. Walifauru vizuri sana kwa kupata alama zote muhimu za kuwapeleka kidato cha tano.



    Baada ya Generose kuja pale nyumbani,wakati huo mama hakuwepo. Walimuelekeza chumbani kwangu.Na kwa tabasamu la aibu, Generose alikuja hadi chumbani ambapo nilikuwa nimepasafisha vizuri na kupapulizia manukato ya ukweli huku nikiwa nimesambaza maua ya waridi chumba kizima, yaani kuanzia pale mlangoni hadi kitandani.

    Nilikuwa nimesambaza maua hayo kwa mtindo wa kapeti na kitendo hicho kilimfanya Generose awe anatabasamu na kuanza kuyakanyaga yale maua taratibu akinyata huku akinifuata nilipokuwa nimelala usingizi ambao kwangu ulikuwa ni wa kinafki tu.

    Alipofika pale kitandani alinirukia mgongoni huku akinivuta vuta kwa nguvu na kwa utani mwingi lakini mimi nikajidai na usingizi mkali sana. Sikushituka hata kidogo kwa matendo aliyokuwa anayafanya ya kunitekenya na saa nyingine kuning’ata sikioni. Nilikaa kimya kwa muda wa dakika kama tatu kitu ambacho kilianza kumkera Generose na kuanza kama kuniraumu kwa nifanyacho.



    Hatimaye nikaamka na kumuangalia usoni mwake kwa furaha ya ajabu na kwa hamasa. Kwa mara ya kwanza nilimvuta Generose kifuani kwangu na kulala naye vizuri huku vinywa vyetu vikiwa vinasemezana kwa lugha za kupeana mate na kunyonyana ndimi kwa dakika kama mbili hivi.Nilimuachia Generose na kumtoa kifuani pangu na kisha nikaelekea kwenye mfuko wangu wa shule na kutoa mdoli mmoja mkubwa, saa ya silva ikiwa na cheni yake pamoja na pete.



    Mapenzi jamani siyo kitu cha kitoto kama tunavyodhani. Mimi nikiwa na umri wa miaka 21 lakini nilikufa na kuoza kwa Generose huku lile neno la kina Babuu likitimia kuwa naweza kumpenda mwanamke nisiyemjua. Baada ya kuchukua vitu vile huku Generose akiwa ananiangalia tu! asijue nafanya nini. Nilichukua vitu vile na kuenda navyo pale alipolala Generose na kisha nikamuomba ainuke na akae kitandani,wakati huo mimi nilikuwa nimesimama na zawadi zangu zile.

    Alinyanyuka na kufanya nilichomuambia na hapo hapo nikawasha radio niliyokuwa nimeweka kanda ya Celin Dion na wimbo wa My heart will go on wenye maneno ya kwenye filamu ya Titanic ndiyo ulikuwa unaanza kuburudisha taratibu. Na mimi hapo hapo niliushika mkono wake wa kuume na kuanza kuongea maneno ambayo kamwe siwezi kuyasahau maishani mwangu, na ndiyo chanzo cha mimi kuwa vile nitakavyokuwa huko mbeleni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Rose, wewe unanishangaza sana. Nimesimama kwa msichana mrembo, mwanamke ambaye sikumjua.

    Sipo tayari kukupoteza Rose, sipo tayari kukuacha uondoke. Ukiruka nami Nitaruka,kumbuka hili. Maisha bila wewe ni sawa na bunduki isiyo na risasi vitani,bila wewe ni heri nife kuliko kuendelea kuona uwepo wako kwangu haupo. Siwezi bila wewe,nasema tena siwezi bila wewe Rose ”nilimaliza kuongea maneno hayo ambayo yalikuwa yanataka kunitoa hadi machozi.

    Niliushika mkono wake vizuri na kuchukua kidole chake na kumvisha pete ile kama uchumba, na baadaye nikampa na ile saa pamoja na yule mdoli ambaye nilimpa jina Hailey.

    “Frank, sina cha kukupa katika maisha yangu zaidi ya kukupenda hadi pale mitakapoingia kaburini.Nakupenda sana Frank”.Generose aliongea hayo na kuinuka kitandani kisha akazungusha mikono yake shingoni mwangu na kunipa ulimi wake. Kwa kuwa nilishawazoea sana wanawake,wala sikuhangaika kwa Generose ambaye kwake ilikuwa ni mara ya kwanza kuwa na mwanaume chumba kimoja kwa lengo la kufanya mapenzi.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog