Simulizi : My Rose
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilicheza naye sana Generose pale chumbani,kila ujanja niliutumia ili asije nisahau maishani mwake. Generose alibalikiwa kwa kila kitu, siyo nje tu! tena akivaa mavazi yake nadhifu bali hata akiyavua alikuwa bado anavutia tena sana. Hatimaye baada ya kuchezeana sana pale kitandani ukafika ule muda ambao kila mtu alikuwa anauhitaji. Generose akiwa hajielewi hata kidogo kwa mambo niliyomfanyia, muda wote alikuwa akijisogeza kiuno chake kwenye kiuno changu.Sikufanya makosa kama mnavyoomba niyafanye nyie wasomaji.
Kwa mara ya kwanza Generose aliutoa usichana wake kwa kunikabidhi mimi ambapo baadaye alinisisitiza sana kuhusu kulilinda penzi letu. Sikusita kumshukuru Generose kwa kitu alichokifanya na zaidi nilimsifu kutokana na ujasiri wake wa kuniachia mwili wake.
Kila mmoja alifumfurahia mwenzake kwa matendo tuliyofanyiana. Nilimtoa nje huku dada zangu wakiwa wapo ndani kwa wakati ule,hivyo Generose alijisikia huru sana. Nilimpigia simu dereva wa tax ambaye mara nyingi huwa namtumia katika safari zangu ndefu. Alikuja na kisha nikapanda kwenye tax hiyo pamoja Generose na safari ya kumrudisha kwao ikaanza.Nilimfikisha na kisha tuliagana kwa kila mmoja kwenda makwao.
Kama kawaida ya dada zangu, hawakuisha utani na kwa kuwa niliwazoea wala sikuwa na neno la kuongeza kwa wakati huo na nashukuru MUNGU waliamini kuwa nampenda sana Generose.
.
Tuliendelea kuwasiliana kwa pamoja na kila Generose alipokuwa anakuja nyumbani, tuliyajenga zaidi mapenzi yetu kwa kufanya mapenzi.Nilizidi kumpenda Generose zaidi na zaidi na haikuwa kificho tena hata kwa wakina Babuu japo mara ya kwanza walinicheka kiaina ila baada ya kuwaelewesha jinsi ya Generose alivyojitoa juu yangu, ingekuwa dhambi sana ningemchezea na kumuacha.
“Sikiliza dogo, Rose ananipenda sana, na yupo radhi kufanya chochote juu ya penzi letu, hivyo itakuwa si vizuri hata kidogo kumsaliti au kumfanyia tendo lolote la kumuumiza”.Nilikuwa namuambia Babuu maneno hayo siku moja wakati tunaongelea masuala ya mahusiano yetu.Wakati huo na yeye tayari alishafanikiwa kuwa na Ritah na walikuwa wanapendana sana.
“Ha hahaaa,ina maana ulikuwa hulioni hilo eeh, wewe si ulisema kuwa huwezi kumpenda demu yoyote dunian? Nini kimekukuta sasa”.Babuu alikuwa anaongea huku ananikumbusha maneno yangu niliyoyasema mida ya nyuma.
“Haijalishi, kwani nikisema kuwa leo siendi shule halafu nikaenda.Itakuwa dhambi au kosa?”
“Siyo kosa,ila ulijidai sana nunda wewe. Majigambo kibao kama muimba mziki”.
“Ndiyo hivyo sasa, nishapenda mwenzako. Ukitaka kufa,ukipenda jinyonge”. Niliongea hayo huku nikimpa Babuu mgongo kama nataka kuondoka.
“Haha haa, lazima uyajue machungu ya mapenzi wewe,si ulijidai kidumee!!!. Sasa subiri wakati wako ufike, nitakucheka kichizi”.Aliongea Babuu maneno ambayo kwa wakati ule kwangu yalikuwa changamsha bongo tu! Wala sikuyatilia maanani au kuyaogopa.
“Hayo maneno tu! hata kwenye hela siku hizi yanaandikwa”.Nikamjibu huku nafungua mlango kwa ajili ya kuondoka.
“Haya bwana, na wakina Paul nitawaambia”.Babuu akawa anazidi kuongea wakati huo mimi nilikuwa nishatoka zangu nje.
“Na usisahau kuwakumbusha kuwa demu wako mi ndo nilitoboa wa kwanza”. Nilijibu kiutani na kupotea kabisa kwa akina Babuu.
Hatimaye mwezi wa pili na nusu ukawa unakatika huku mapenzi kati yetu yakizidi kutawala fikra zetu na kila mmoja hakuwa na hamu ya kusikia kuwa mwenzake ana tatizo au mwenzake hampigii simu.
Ilikuwa raha kwangu na raha kwake. Kila usiku saa sita ilikuwa ni lazima niongee na Generose hadi usiku wa manane.
Wengi wanasema mapenzi na shule hayaendani, lakini hawaelezei ni vipi hayaendani. Kwangu mimi naona kuwa,mapenzi na shule hayataendana pale yule umpendaye atakapokuwa hana muda na wewe au anapokuwa anajali kuhusu yeye pekee na kusahau kuna mtu ambaye anafaa kumpa matumaini na kumfanya afanye vizuri hata darasani. Na kuna wengine wao hufikilia zaidi kuhusu miili yao kuridhishwa zaidi ya kumridhisha pia mtu aliyenaye.
Kifupi, mapenzi na shule hayaendani pale unapokutana na mtu ambaye hajali hisia zako bali kujali hisia zake binafsi. Kwangu mimi na Generose tulithibitisha kuwa mapenzi na shule yanaendana sana, na yanafanya mtu afanye vizuri zaidi darasani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila nilipokuwa nasoma usiku,nilimpigia simu Generose ili na yeye aamke kusoma na alikuwa anafanya hivyo, na kama alikuwa kachoka hataki kusoma basi nilimpa nafasi ya kuniuliza maswali ambayo hayawezi, na mimi nilimjibu vizuri sana.Alijikuta anafauru sana yaani kuliko hata hapo mwanzoni wakati hajawa na mimi, huku na mimi nikizidi kuwa na furaha na kuzidi kufanya makubwa pale shuleni. Wakati huo tulishatimiza miezi sita katika uhusiano wetu.
MWANZO WA MATATIZO…
Kama kawaida yetu. Wapenzi wakupigiana simu nyakati za usiku na kuongea hadi usiku wa manane. Tabia hiyo ikawa imekomaa baina yetu. Nakumbuka siku hiyo niliongea na Generose hadi mida ya saa tisa za usiku, na baada ya hapo nikawa nataka kukata simu ili tulale, lakini kabla sijaikata nikawa namuomba jambo Generose anifanyie.
“Rose, unaweza kunikiss me thru the phone?”Nilimuomba Generose anibusu kupitia simu.Nakumbuka kipindi kile ule wimbo wa Kiss Me Thru The Phone wa Soulja Boy ndiyo ulikuwa umetoka na karibu kila mtu kwenye akili yake alikuwa nao.
“Ha ha haaaa, wewe. Hayo maneno umeyaanza lini? Ha ha haa”.Generose alijikuta akijisahau na kucheka kwa nguvu sana wakati ilikuwa ni usiku.
“Sasa nini cha ajabu jamani?We si unibusu tu!”.Nikawa nambeleza Generose.
“Haha haaa, haya ngoja. Kaa vizuri, weka shavu iloo. Haya anza kulipo…….”.Generose hakumaliza kauli yake, simu ikawa imekatika. Kwa kuwa nilikuwa na usongo wa kupewa busu kwenye simu, basi nikapiga fasta fasta. Iliita kidogo tu! Halafu ikapokelewa, na wala sikuwa na wasiwasi. Nikaanza kuongea tena kwa sauti ya mahaba.
“Baby, mbona umekata simu?”. Nikaanza kuongea hivyo.
“Hamna, tuendelee sasa”.Ilijibu upande wa pili.
“Haya nikiss me thru the phone ili nilale salama”.Nikarudi kwenye mada bila wasiwasi tena kwa ujasiri wenye mahaba mengi ya sauti.Kimya kikatawala kwa muda na kisha sauti upande wa pili ikaitika tena,lakini safari hii ilikuwa tofauti sana.
“Wewe na mbwa mwenzako mnaongea hadi usiku wa manane si ndiyo eeh! Hivi unajua ni kiasi gani sisi tunaha…….”. Sikutaka yale maneno yaendelee kuingia masikioni mwangu, hivyo niliikata simu na kuizima huku nikiwa natetemeka na kujiuliza maswali mengi sana kuhusu ile sauti. Ilikuwa inafanana sana na ya Generose ndio maana nilishindwa kuitambua ni ya nani na kuzidi kuropoka maneno yangu kwa mahaba zaidi.
Baada ya dakika tano kupita akili yangu ikiwa imetulia. Ndipo niliamua kuifungua simu yangu huku nikijisemea liwalo na liwe. Baada ya kuifungua,hakuna kilichoendelea,iwe kupigiwa au kutumiwa meseji jambo ambalo lilinipeleka mbali na kuhisi kuwa Generose alikuwa katika wakati mgumu. Baada ya kuwaza sana bila kupata majibu, usingizi ukanibeba huku wazo la mwisho likiwa kumtegea kesho asubuhi nipate kujua nini kilitokea.
Kwa kuwa wote tulikuwa wanafunzi hivyo sikupata shida sana kumtegea. Niliamka mapema na kujiandaa, kisha nikaanza kwenda njia ambayo Generose alikuwa anapenda kuipita. Baada ya kumtegea sana sehemu fulani, nilimuona akija na aliponiona alianza kutabasamu huku akija pale nilipo.
“Mambo”Alianza kwa salamu baada ya kunifikia
“Poa niambie mtoto”.Nilimjibu huku nikizirudisha nywele zake kama nazilaza kwa nyuma.
“Mimi poa, vipi jana”.Aliruka hadi napotaka.
“Mh! Ndo nipo hapa ili uniambie nini kilitokea”.
“Ha ha haa, usijal.i, we wakikupigia waambie mimi ni mwanafunzi mwenzako”.
“Poa. Ila niambie nini kilitokea kwanza”.
“Uliongea na mama jana”.
“Unasemaje?”.Niliuliza kwa hamaki huku yeye Generose akiwa anacheka kana kwamba ni kitu cha kawaida.
“Uliongea na mama jana, huelewi au?”. Alisisitiza Generose.
“Unajua nilimuambiaje?”.
“Ha ha haaa, ulipokata simu alianza kukuigiza ulichokisema”
“Sasa mbona unacheka kama mazuri?”
“Basi tu! kanipora na simu ila atanirudishia tu!”.
“Mi naogopa mwenzako”.
“Usijali baba yangu, si nilikuambia nipo tayari kufanya lolote kwenye mahusiano yetu?”.
“Mh! Haya bwana, mi nakuachia wewe mama”.
“Basi poa, ngoja twende shule, halafu nitawahi kurudi ili tuonane si wajua simu yangu mama kaichukua, hivyo leo maongezi yote huku huku”.
“Haya bwana, baadaye basi”.
“Poa, I Love You Frank”. Huku akinipungia mkono kuniaga.
“Love you too,Rose”.Niliongea hayo huku narudi nyuma kimgongo mgongo uso ukiwa unamuangalia yeye.
Kifupi sikumuelewa Generose kwa sababu alichukulia lile jambo kwa ukawaida sana wakati huo kwangu lilikuwa ni jambo la hatari sana ambalo kama wazazi wake wakilifatilia basi ningekuwa matatani.
Nilienda zangu shule na siku hiyo wala sikukaa sana.Mida ya saa sita nikawa najirudisha nyumbani huku nikiwa na wazo moja tu! La kuwa na Generose. Sikuwa na wasi wasi ni vipi nitampata kwa sababu pale nyumbani alishazoeleka sana.
Baada ya kufika nyumbani, moja kwa moja nilienda chumbani kwangu na nilipofungua sikuamini macho yangu nilipokutana na mwili wa Generose ukiwa umejilaza kwenye kitanda changu. Alikuwa kalalia tumbo na miguu yake kuining’iniza kwenye kile kitanda changu,wakati huo sketi yake ya shule ilikuwa imepanda kiasi na kusababisha maungio ya magoti yake kuonekana vizuri kwa nyuma na kuhamsha hisia tofauti kwenye mwili wangu.
Sikuwa na shaka wala papara tena, kwa sababu ndege alikuwa tayari tunduni hivyo ilikuwa ni mimi tu! kuchagua nimkamate kwa njia gani.
Nilinyata taratibu huku nikiwa makini nisimshtue na kisha nilitoa shati langu la shule na kubaki na singlend ambapo baada ya kufanya hivyo,nilijikuta ile tamaa ya mwili ikiniondoka na kujiona kama mjinga kwa ninachotaka kukifanya. Badala yake nilimvua viatu Generose kwa utaratibu ili asishtuke na baada ya hapo nilimpandisha miguu yake kitandani.Na baada ya kufanikiwa na mimi nilala kwa pembeni yake na kisha nikaanza kuutathimini uso wa Generose bila kuupatia majibu, zaidi ya kupata jibu moja tu! la kuwa ninampenda sana Generose.
Alikuwa amelala usingizi wa kweli ambao sidhani kama ulikuwa una zuri ndani yake,kwani kitendo cha yeye kulala pale nyumbani kilikuwa si kitendo cha kijinga hata kidogo. Generose alikuwa hata akitoka saa mbili shule, hawezi kukaa nyumbani hata kwa nusu saa, lakini siku ile Generose alilala kabisa. Nilichogundua kutoka kwa Generose ni kuna kitu anakificha ndani ya tabasamu lake alilokuwa ananitolea asubuhi. Generose alificha siri kubwa ndani ya tabasamu lake,kitu kilichokuwa kinanipa wasiwasi sana katika kichwa changu.
Kwa kuwa sikuzoea kulala mida ya mchana, basi niliendelea kuwa pale kitandani nikiendelea kuzihesabu pumzi za Generose alizokuwa anazitoa wakati kalala. Baada ya kama nusu saa tangu na mimi nijilaze pale kitandani,ndipo Generose naye aliamka na aliponiona alitabasamu kama kawaida yake na kunifanya na mimi nitabasamu zaidi. Generose alikuwa anapendeza sana akitabasamu,kitu ambacho kilikuwa kinanivutia na kunifanya nimpende maradufu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Umefika saa ngapi?”.Alianza kwa swali baada ya kufungua macho kabisa.
“Kama nusu saa hivi imepita”.Nilimjibu huku namfuta alama za machozi ya usingizini.
“Sasa mbona hukuniamsha?”.Aliongea tena huku akitabasamu.
“Nilikuacha tu!upumzike. Inaonekana una mambo mengi sana kichwani ila unanificha”. Niliongea hayo na kumfanya atabasamu tena huku akishindwa kuongea. Nikaendelea,
“Sikiliza Rose, wewe ndiyo kila kitu kwangu, naomba unifanye niwe kila kitu kwako. Niambie nini kilichokukuta jana usiku”. Generose aliniangalia na ghafla lile tabasamu lake akalipoteza na kisha kwa nguvu alinyanyuka na kunikumbatia huku akilia na kuongea maneno kwa uchungu sana.
“Frank, sipo tayari kukuacha wewe kwa sababu ya maneno ya wazazi wangu. Nitapigana hadi kufa kwangu ili mradi nitimize ahadi ya kuwa na wewe katika maisha yangu yote nitakayoishi duniani. Sipo tayari kukupoteza Frank,nakupenda sana ten asana. Nkuahidi Frank wangu,sitokuacha wala kumsikiliza mtu kwa wakati huu zaidi ya moyo wangu”.Aliongea hayo Generose huku akizidi kunikumbatia kwa nguvu zaidi. Maneno yale yaliamsha maswali mengi sana kichwani,kitu kilichonifanya nichimbue zaidi ili nipate undani wa maneno yale.
“Una nini Rose?”.Nilimuuliza.
“Ni mama, Frank”.Alijibu kifupi huku anavuta mafua yaliyotokana na kulia.
“Mama kafanyaje sasa Rose, mbona waniweka kwenye mabano?”.
“Mama kasema hataki mimi niwe na wewe, na kamwambia Baba kuhusu hilo, na Baba kasema nije nikuambie kuwa endapo utaendelea kuwa na mimi, basi kuna makubwa yatakukuta na atakufanya kitu kibaya. Frank, siwezi kukuacha wala sijali maneno yao, nitapigania pendo langu kwako hadi pale nitakapokata pumzi yangu ya mwisho”.Generose aliongea maneno ambayo nilishindwa kuvumilia na kujikuta nikimkumbatia pia huku nikitoa machozi.
“Rose, wewe ndiye mama yangu, kumbuka haya maneno niliwahi kukuambia. Bila wewe mimi siyo kitu.Chochote kitakachokutokea na mimi kitanitokea. Ukiruka nami Nitaruka, kumbuka hili”.Nilimpa faraja kwa maneno yale na vile vile sikuchoka kumuongezea ujasiri wa kuzidi kuvuta subira huku nikijitahidi kumzuga kwa kuficha hisia za uwoga wangu kwa sababu maneno aliyoyaongea baba yake, yalikuwa yana vitisho sana ndani yake.
“Sikiliaza Rose, hata hao wazazi wako, walianza hivi hivi kwa kificho na hadi sasa wapo ndani ya ndoa.Wewe unadhani walianza mapenzi kwa kujionesha onesha kwa wazazi wao?.Cha msingi tuvumiliane hadi hapo tutapokuwa tayari kwa ajili ya kuwa wazi kwa wazazi wetu”.Nilimfariji Generose ambaye kiasi fulani alianza kuelewa nini namaanisha.
“Ila Frank,baba kawa mkali balaa. Jana siyo mara ya kwanza, walianza kunifatilia tokea muda kidogo. Kuna siku nilikuwa napika, ukawa unapiga. Nilipo pokea tukaanza kutaniana,kumbe mama alikuwa nyuma yangu,akawa anasikiliza yote. Ile ulivokata tu! Akanipola simu halafu akaanza kuangalia meseji zako na kisha akazifuta zote pamoja na namba zako”.Alizidi kuongea Generose maneno ambayo yalizidi kunipa wasiwasi kiasi fulani lakini sikuonesha wasi wasi huo kwa wakati ule.
Kifupi ni kwamba.Baba yake Generose alikuwa ni Mwanajeshi mstaafu huku Mama yake akiwa Usalama wa Taifa,yaani mpelelezi huku akiwa amefanya kazi ya Upolisi kwa miaka karibu kumi. Kwa jinsi hiyo nadhani hata wewe msomaji lazima uanze kuogopa japo haijakutokea wewe.
“Sasa mbona ukuwahi kuniambia hata mara moja?”.Nikamuuliza.
“Nilikuwa sitaki kukuweka roho juu, si unajua kiasi gani nakupenda Frank”.
“Rose bwana, kwa hiyo sasa hivi hujaniweka roho juu?”. Nikamuuliza tena huku nikiwa nimepoa.
“Siyo hivyo Frank, it’s all about love. Ni mapenzi yanayonituma nifanye hivi Frank, nakupenda sana”.
“Basi isiwe tabu. Mimi nitapigana daima kulinusuru penzi letu, na ninaomba na wewe upigane kuhusu ilo”.
“Frank, nipo tayari kupoteza uhai kwa ajili yako na nipo tayari kufanya chochote ili ufurahi”
“Rose usiseme hivyo bwana, sasa ukifa mimi nitabaki na nani?.Itabidi na mimi nife tu!”.
“Ha haaa, usijali mme wangu. Ila zingatia niliyosema, sitanii. Nitapigana mpaka kufa”.
“Ukiruka na mimi Nitaruka, ni hilo tu! naweza kukwambia kwa sasa”.
“Hivi huo msemo umeutoa wapi?Mbona unaupenda sana?”
“Msemo gani tena?”.
“Si huo UKIRUKA nami NITARUKA”.
“Ha ha haa, huo kwenye ile ‘movie’ ya Titanic, pale wakati yule jamaa (Leonard Decaprio) anamtongoza yule wewe (Rose), ndio alimuambia hayo maneno. Halafu na pale wakati jamaa yupo baharini kamuweka yule wewe kwenye kile kidude cha meli baada ya kuzama, jamaa aliongea maneno mengi hivi halafu akamaliza kwa kusema ‘You jump, I jump, remember’.Alikuwa anamkumbusha hayo maneno kuwa aliyasema kipindi cha nyuma, halafu jamaa alipomaliza hakusema tena,ndio akawa amekufa”.
“Ahaaa, sawa nimekumbuka hiyo. Ha ha haaa,shauri yako ukinifata mimi nikiruka”.
“Nakufata ndiyo, subiri uone”.Tulikuwa tunaongea huku tunacheza cheza ili kuondoa fikra za uoga vichwani mwetu,jambo lililofanya Generose kurudi katika hali yake kiasi.
Tuliongea mengi sana siku ile,kiasi kwamba kila mtu alipata faraja kutoka kwa mwenzake.Ila Generose kama nilivyosema hapo mwanzo,alikuwa anaficha machungu yake kupitia tabasamu lake,na kwa kuwa nilishaliona hilo basi nikawa makini kwa kila alichokuwa anaongea. Japo aliongea huku anatabasamu,lakini alikuwa anamaanisha kwa asemayo.
Tulikaa mle chumbani kwangu tukichezeana hapa na pale katika miili yetu na mwisho wa siku tulijikuta nguo zetu za shule zikiwa pembeni na kilichoendelea hapo siyo vizuri kukihadithia.
Kila mmoja alijikuta yupo pembeni akitweta na kutoa kijasho chembamba baada ya ule mchezo kumalizika. Tuliangaliana na kushindwa kuongea kitendo kilichofanya tutoe vicheko kwa pamoja kwa kujiona kama wajinga.
“Sasa unacheka nini”.Alianza Generose baada ya kumaliza cheko yake na kubakiza tabasamu.
“Sijui, labda nikuulize wewe”.Nikamjibu huku na mimi nikiwa na tabasamu.
“Mi sijui, wewe si ndo umeanza kucheka”
“Ha ha haa, sasa mimi ndo nilianza au wote kwa pamoja”.
“Wewe ndio ulianza, mimi ndio nikafata”.
“Haya bwana, ngoja nimalize ubishi maana nakujua kwa ubishi mwanamke”.
“Ndiyo bora utulie tu! Nisije nikakuchapa hapa”.
“Haya mama.Ila siku hizi unaweza”.
“Naweza nini?”. Huku anaona aibu fulani lakini ya kijasiri. Yaani ile aibu ambayo bado unamuangalia mtu usoni.
“Kucheza kitandani”.
“Kuchezaje? Hivi?”. Huku anarusha rusha mikono hewani.
“Siyo hivyo, wala siyo huko kwenye mikono”.
“Sasa wapi?”
“Hapo”.Nikawa naonesha kwa kidole sehemu yake ya kiunoni.
“Wapi? Mbona mimi sipaoni”.
“Hapa bwana”.Nikaongea kama na kihasira kidogo huku nimeshika kiuno chake. Kumbuka wakati huo wote tulikuwa hatujavaa nguo zaidi ya yeye kujifunika shuka na mimi nikiwa nipo na kikaptula changu cha maua madogo madogo.
“Ahaaa, kama hivi”.Akaanza kukatika wakati huo bado mkono wangu upo kiunoni mwake jambo lililofanya lihamshe hizia za ajabu tena mwilini mwangu na kujikuta nikimtoa lile shuka na kukikamata kiuno chake kwa mikono miwili kisha nikamvutia kwangu na kuanza kucheza na mwili wake tena hasa maeneo yale yanayompa hisia za kufanya mapenzi. Muda kidogo, tayari kila mmoja alikuwa anayasikia mapigo ya moyo ya mwenzake kwa kutumia vifua vyetu vilivyokutana kwenye shughuli ile ya kijinga lakini yenye raha na furaha ndani yake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
____________
Ni kama wiki ilipita tangu Generose anapokonywe simu na mama yake,hivyo tulikuwa hatuna mawasliano pale anapofika nyumbani jambo lililokuwa linaninyima sana raha japo Generose alinipa moyo kwa kuniambia itarudishwa tu!.
Siku hiyo nikiwa nimetulia nyumbani,ghafla simu yangu ilianza kuita, nilipoangalia alikuwa na Generose. Nilitabasamu na kasha nikaipokea na kuanza kuongea naye huku nikiwa makini na sauti isije kuwa tena ya mama yake.
“Haloo”.Nilianza hivyo baada ya kupokea simu.
“Haloo,mambo”
“Poa mzima wewe”.
“Mimi mzima, nipigie basi”.
“Poa,kata simu”.Alikata simu na kitendo bila kuchelewa nikampigia.
“Eheee, umerudishiwa simu?”.Nikaanza tena baada ya simu kupokelewa.
“Ndiyo,ila walifuta namba zako zote na meseji zako”.
“Sasa wewe umeipataje namba yangu”.
“Ha ha haaa, watafuta pote ila kichwani mwangu hawawezi”.
“Duh! Halafu eti nilisahau kuwa umekariri namba yangu, asante Rose”.
“Usijali.Halafu wewe hujakariri yangu eeh”.
“Thubutuuu. 0752 353039, utaniambia nini”.
“Ha ha haaa, ndo maana nakupenda”.
“Sasa hivi wako wapi sasa, hauogopi wakikukuta?”.
“Hamna, wametoka mara moja,wameenda sokoni”.
“Poa, baadaye basi mtoto mzuri, naona salio linaanza kuisha”.
“Poa, wasalimie mawifi zangu”.
“Zimefika”.Simu ikakatwa na mimi nikaanza kufanya mambo yangu mengine ambayo nilikuwa nayafanya.
Maongezi yalirudi tena kati yangu na Generose lakini safari hii tulikuwa makini sana ili tusikamatwe tena. Mara nyingi tulikuwa tunaogea kwa lisaa limoja na kisha kulala.Hayo ndio yakawa maisha yetu mapya kati yangu na Generose.
___________
Siku moja,ambayo nahisi ndiyo siku mbaya katika maisha yangu ya mapenzi kati yangu na Generose. Siku hiyo kwanza simu ya Generose haikupatiakana tangu asubuhi na ilipopatikana hakuongea Generose bali Baba yake.
“Sikiliza kijana.We si unasoma Jamhuri na upo kidato cha sita,mchepuo wa HGL?”.Mzee aliongea hayo huku yakiwa ni kweli kila kitu.
“Ndiyo, kwani wewe nani?”
“Mimi ni Baba yake Rose. Nakuomba uachane na binti yangu. Yaani achana naye kabisa, sitaki kukusikia wala kuona ukiwa na binti yangu. Muache na yeye asome japo kama wewe hapo ulipofikia,sawa kijana?”.
“Lakini mzee,siyo kwamba nacheza na Rose. Nampenda sana Rose, na yeye ananipenda pia. Naomba uniwekee kikwazo kingine lakini siyo kuachana naye. Nipo tayari kumsubiri afike unapotaka,lakini na mimi nikiwa mmoja wa watu muhimu kwake”.
“Sikiliza kijana, nimemuheshimu sana Baba yako.Bila Baba yako ningekusweka lupango kwa kosa la kutembea na ‘Under 18’. Namjua Baba yako vizuri sana,na ninafanya naye biashara. Nomba ukae mbali na mwanangu”. Hakusubiri niweke neno lolote baada ya yeye kumaliza.Alikata simu,na hata nilipopiga tena, haikupatiakana.
Kiukweli siku hiyo nilikaa kama nimechanganyikiwa akili,kila nilichogusa,kilikuwa kama kinataka kuniponyoka na kuharibika. Japo niliongea na mzee yule kiujasiri sana,lakini kiukweli nilikuwa naogopa sana endapo atamuambia Baba.Mbaya zaidi alinionya na kujua hadi naposoma.
Siku ile ikapita bila mawasiliano na Generose. Ikaja siku ya pili, nayo ikatitia.Ya tatu,ya nne hadi wiki ikaisha bila mawasiliano na Generose,na kibaya hata shule alikuwa haji na mimi kwenda kwao, naogopa.Ikabidi niende kwa Babuu kupata ushauri wa nini cha kufanya japo nilijua ataanza kejeri zake.Nilimkuta kwao,tukasalimiana na kisha nikamueleza mkasa mzima uliyonitokea na kumwambia hali yangu halisi itakayonikuta endapo Generose nitaachana naye.
“Ha ha haaa, James Bond leo kawa fala la mapenzi. Wewe si ndo ulijisifiaga hapa kuwa huwezi kuzinguliwa na mapenzi, haya nini kimekukuta? MUNGU kweli mkubwa, kajibu maombi yangu.Ha ha haaaa”.Alikuwa Babuu akikejeri baada ya kumsimulia mkasa mzima.
“Sasa mwanangu umeamua kunicheka kwanza ndo unijibu au ndo niambulie maumivu tu!”.Niliongea hayo huku nikionesha sura ya kuchoka na ya huruma.
“Siyo kama nakucheka, tatizo ulitukana Mamba kabla ujavuka mto.Hukujua nini kitakachotokea mbeleni.Ngoja nikupe siri moja”.Babuu akakaa kimya kidogo kabla hajaendelea kuongea hiyo siri yake.Kisha akaendelea.
“Generose anajua kila kitu kuhusu maisha yako kabla ujakutana naye. Tulimuambia tabia zako zote za kutembea na visichana vya hapa mtaani. Na kwa kuwa alikuwa anakupenda,akaapa kukubadilisha na kwa hilo kafanikiwa kichizi. Yaani mwanangu ume change ile mbaya”.
“Kwa hiyo Rose anajua kuwa mimi nilikuwa kicheche?”.
“Ndiyo hivyo, na tulimuambia siku ilee, ambayo jana yake wewe ndiyo ulimtokea.Tulikuwa mimi na Seth”.Alizidi kuongea Babuu.
“Okey, hilo siyo kitu. Embu nishauri cha kufanya kwa hili jambo linalonikabiri sasa hivi. Mi nitakufa Dogo, haki ya MUNGU nitakufa”.Niliongea hayo huku nikiwa sina hata tone la utani katika sura yangu.
“We sikiliza mwanangu, subiri kwanza. Just subiri,atapiga tu! simu. Mpe muda wa yeye kuongea na wazazi wake, wanaweza kumuelewa”.Babuu alitoa ushauri ambao kwangu sikudhani kama ndiyo suruhisho.
“Dogo mimi siwezi, unajua wiki sasa sijaongea naye”.
“Kwa hiyo unataka ufanyaje?”.Babuu akauliza.
“Nataka niende kwao nikajue kuna nini kinachoendelea”.Nikamjibu Babuu.
“Aaah! hee hee!. Hivi wewe ushawahi kuliona dingi lake?”.
“Sijawahi na wala siogopi,nachojua mimi napigania penzi langu”.
“Yaani wewe unacheza. Dingi lake ni bonge la mtu. Lilikuja pale skuli na kibaluni chake, limejaa kwenye gari peke yake. Bonge la mwili kama Shoziniga, halafu limepiga para hilo la hatari.Mi nahisi lile Dingi ni Jambazi maana Generose tukimuulizaga, hasemi kazi ya dingi yake”.
“Hamna, siyo Jambazi.Dingi ni mwanajeshi mstaafu na sasa hivi anapiga biashara,na ndo maana anafahamiana na mzee”.
“Sasa kama mwanajeshi mstaafu, nenda kwake uone. Utaruka kichura chura,utapiga pushapu,utakimbizana na mambwa yake yale hadi ukome. Cha msingi wewe tuliza akili na subiri uone nini kitakachofuata”.Babuu aliongea hayo huku kiundani nikianza kukubaliana naye. Nivute subira nikingoja kujua nini kitakachoendelea.
Nilikaa na Babuu hadi usiku huku akiwa ananipa ushauri na maneno ya kunifanya nijikaze ili nisikurupuke na kufanya utumbo mwingine.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wiki na nusu ikapita bila mawasiliano na Generose huku machungu na wasiwasi vikizidi kutawala maisha yangu.Sikuwa na raha tena kwa wakati ule,jambo lililofanya hata mama na dada zangu kushindwa kuelewa nini kinachonisumbua.
Nakumbuka ilikuwa ni Jumapili ya Asubuhi, ndipo nilipokea simu ambayo mpigaji iliandika ni Generose lakini aliyekuwa akiongea ni mama yake huku akiwa na msisitizo mkubwa kwa akiongeacho.
“Halow”. Niliongea baada ya kupokea simu huku nikiwa makini zaidi nisije nikakurupuka na kuanza kuongea maneno ya kuraumu kabla sijamjua ni nani.
“Halow,we ndiyo Frank?”.Ilisikika sauti upande wa pili ikiuliza.
“Ndiyo, kuna jipya?”Nilimjibu na kumuuliza.
“Mimi ni mama yake”.
“Ahaaa, samahani mama, shikamoo”.
“Marahaba”.Aliitikia na kukaa kimya kidogo huku akivuta mafua kana kwamba alikuwa analia.
“Mama, kuna jipya?”.Nikamuuliza tena.
“Mwenzako huku,mwanangu”.Akanijibu huku akiendelea kuvuta mafua yake.
“Nani? Rose!!!?”.Nikauliza kwa sauti ya juu huku nikiamka nilipokuwa na kusimama wima huku nikijiuliza maswali kibao ya kuna nini kinaendelea kwa akina Generose, na zaidi nilitegemea mama yake atakuwa mkali, lakini alikuwa mpole na kuonesha kuwa anahitaji kitu kutoka kwangu.
“Ndiyo mwanagu, sijui kafanya nini. Siku ya tatu leo hatoki nje wala kula. Jana alitoka nje mara moja na kwenda dukani alivyorudi akaingia ndani na kujifungia, ndiyo hadi sasa hivi hajafungua mlango zaidi ya kusema anataka wewe uje,tena alikuwa anaongea kwa sauti ya chini sana”.Hadi mama Generose anamaliza kuongea hayo yote,mimi tayari mwili wangu ulishakufa ganzi na zaidi nilihisi kama nataka kudondoka au kutaka kama kuchanganyikiwa.
“Nakuja mama”.Ndicho nilichomjibu Mama Generose. Nilitoka chumbani kwa kasi huku navaa tisheti,na moja kwa moja nikaenda wanapokodisha baiskeli na kuanza kuelekea inapoishi familia ya akina Generose. Sikumuambia mtu yeyote naenda wapi kwa sababu nilikuwa kama nimechanganyikiwa. Hata baiskeli nilivyokuwa naiendesha,ilionekana dhahiri kuna jambo limetokea.
Baada ya dakika zisizopungua kumi,nilishafika kwa akina Generose na moja kwa moja bila hata kusita na nikiwa tayari kwa lolote. Niliuendea mlango wao na kuanza kuugonga ili niingie. Ulifunguliwa na mama ambaye kwa haraka nilijua kuwa yule ni mama yake Generose kwa jinsi walivyofanana. Macho yake yalikuwa mekundu naona ni sababu ya kulia,kitu ambacho kilinipa mashaka na kutaka kujua ni nini kinachoendelea.
“Mama kuna nini? Mama, Rose yupo wapi?”.Nilijikuta nauliza maswali mfurulizo huku nikishindwa kwenda mbele wala kurudi nyuma bali kubaki pale mlangoni nikitazamana na mama yake Generose.
“Mwanangu embu tulia kwanza uingie ndani”.Mama Generose aliniambia hayo huku akinipisha mlangoni ili niingie ndani. Nikavua viatu vyangu na kuingia ndani ambapo nilikutana na sura ambayo moja kwa moja nayo nikaijua ni ya Baba yake Generose nikitengeneza picha ya Babuu alivyoniambiaga muonekano wa Baba Generose.
“Shikamoo Baba” Huku nampa mkono.
“Embu nitokee hapa, nitakuumiza kijana”.Alijibu Baba Generose kwa hasira huku akionesha dhahiri anaweza kufanya alichokisema .
“Baba Rose, embu msikilize huyu kijana, tumsaidie Rose”.Aliongea mama yake Generose kwa utaratibu akijaribu kumsihi mme wake.
“Na mwanangu akifa wewe. Nakuambia utanitambua mimi ni nani”.Baba Rose aliongea huku ananioneshea kidole kwa ukali.
“Baba Rose, embu acha maneno ya kukata tamaa hayo.Muache kijana aende kuongea na Rose labda atamuelewa”.Mama Generose alizidi kumbembeleza mme wake,wakati huo mimi nilishaelewa kuwa Baba Generose alikuwa hajapenda ujio wangu pale nyumbani kwake.
“Ninyi mtajuana wenyewe,mimi siwezi kukaa nyumba na huyu mpumbavu akiwepo”.Baba Generose aliongea hayo huku akinyanyuka kwenye kochi alilokaa na kufungua mlango,kisha akatokomea nje.
“Mwanangu, japo Rose ni mdogo na wewe pia ni mdogo,lakini mimi sikuwa na tatizo juu ya mahusiano yenu.Kifupi nilifurahi sana baada ya Generose kubadilika kimasomo na hata hapa nyumbani alikuwa anafanya mambo yake kwa uhuru na furaha. Nilipochunguza ni nini kinasababisha hayo yote,niligundua ni kwa sababu yako.Na nilikuwa nataka niwaite ninyi nyote na kuwahasa sana kuhusu mahusiano mliyoanzisha,na zaidi nilitaka kukuhasa wewe kumlinda mwenzako dhidi ya magonjwa na mimba zisizotarajiwa.Lakini tatizo ni la huyu Baba yake, yaani hataki kabisa kusikia ni nini ambacho najaribu kumuambia. Matokeo yake,mtoto hajala leo siku ya tatu na tangu alivyojifungia jana, hadi leo hajafungua mlango”.Mama Rose alikuwa akiongea hayo huku akiwa na uchungu pamoja na wasiwasi kitu ambacho kilinifanya na mimi niondoe ule wasiwasi wangu na kujivisha moyo wa ujasiri pamoja na kujikaza nisijioneshe kuwa Generose ana kitu kibaya kitamkuta japo nilijua ni lazima kuna kitu Generose anategemea kukifanya hasa kutokana na maongezi aliyokuwa anayaongea kipindi cha nyuma kuhusu mahusiano yetu.
“Mama usijali,Rose atakuwa salama tu! Cha msingi wewe nipeleke sehemu alipo ili niongee naye”.Nilimpa moyo Mama Generose na kitendo bila kupoteza muda alianza kuelekea chumba ambacho alisema ndipo Generose alipo.
“Rose….., Rose……., Rose mama yangu”.Nilikuwa nagonga mlango wa chumba chake huku namuita,wakati huo mama yake alikuwa kaniacha pale peke yangu.
“Frankyyyyyyy”.Ilisikika sauti kwa mbali sana kama ya kunilaki lakini ikionesha ina maumivu mengi sana. Hatimaye Generose alifungua mlango na sidhani kama alitegemea nitakuwepo pale kwa muda ule. Alitoa tabasamu moja kubwa sana ambalo tayari nilishagundua maana ya tabasamu lile, tabasamu lenye kuficha vitu vingi sana ndani yake.Alinirukia na kunibusu kwa midomo yake mikavu iliyoonesha kukosa maji kwa kipindi kirefu sana.
Hakuwa Generose yule niliyemzoea,wala hakuwa Generose yule niliyemsikia wakina Babuu wanamsifia kwa mara ya kwanza siku ile kwenye mabishano yao, na wala hakuwa Generose yule niliyemuona kwa mara ya kwanza siku ile anatoka shule na wenzake.
Generose huyu wa sasa alikuwa ameisha mwili na vidonda kwenye midomo yake vilikuwa vimemtoka kama kapata ajari ya moto au kadondokea uso na kujikwaruza. Licha ya hivyo, Generose alikuwa rangi yake ilianza kubadilika na kuwa nyeusi kutokana na kutohudhuria bafuni kwa muda mrefu.
Japo alitabasamu,lakini mimi nilishindwa kuvumilia na kujikuta nikidondosha chozi na kumkumbatia kwa nguvu na kisha nikaanza kulia kwa uchungu huku nikimuuliza kwa nini kaamua kufanya yale yote?.Kilio kile kutoka mdomoni mwangu kilihamsha kilio kingine kutoka kwa Generose jambo lililosababisha Mama Generose kuja pale tulipo ili kuja kushuhudia ni nini kinajiri kati ya wapenzi sisi. Bila kutegemea Mama Generose naye alikuja na kutukumbatia kwa pamoja, na kujiunga kwenye msiba wetu usio na jina.Baada ya hapo tukatengeneza sauti za ajabu pale ndani,sauti ambazo zingemfanya hata mpita njia asimame au kuja kuulizia pale kuna nini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya dakika kama mbili za majonzi yale niliamua kuuvaa ujasiri tena na kuanza kuwabembeleza wanawake wale kana kwamba mimi sikuwepo pale. Walinisikia na kunyamaza,kisha Generose alimuomba mama yake atoke kidogo kwani alikuwa na maongezi na mimi.
Baada ya mama Generose kuondoka, Generose alinishika mkono na kuanza kuniingiza ndani kwake huku akipepesuka kitu ambacho kilinifanya nimshike na kumyanyua kwa mikono yangu miwili na kumuweka kama vile Bibi harusi kitu kilichomfanya Generose aniangalie usoni na kutoa tabasamu lake kadiri alivyoweza ilimradi aoneshe kuwa amefurahia kitendo kile.
Wakati nimembeba vile alinivuta kichwa changu ambapo midomo yake aliielekeza kwenye sikio langu jambo lililomaanisha kuna kitu anataka kukifanya sikioni mwangu.Na kama mawazo yangu yalivyonipeleka,Generose alininong’oneza sikioni mwangu kwa kusema.
“Natamani siku kama hii ingetokea wakati huo tukiwa tunatoka kanisani kwa furaha na siyo kama siku ya leo.Natamani sana, lakini haitowezekana Frank, haitowezekana mme wangu”.
Nilimwangalia Generose kwa huruma wakati anaongea yale na wala sikutaka kumjibu neno kwa muda ule japo alikuwa anaendelea kuongea.
“Baby, kwani siku yetu ya harusi wewe ungevaaje?”.Alikuwa ananiuliza huku mimi nikiwa namshushia kitandani. Sikujibu swali lile zaidi ya kuendelea na kazi yangu ya kumshusha pale kitandani huku namshangaa usoni kwa asemayo. Wakati naendelea kumshusha,ndipo aliponiganda kwa kuifunga mikono yake shingoni kwangu akikataa kushuka hadi nimjibu swali lake.
“Hapa sishuki ng’oo, hadi unijibu swali langu nililokuuliza”.Aliongea Generose.
“Tatizo Rose una maongezi ya ajabu bwana. Wewe unaongea hivyo kama leo ndiyo mwisho wako bwana”.Niliongea hayo huku nikiwa na maumivu mengi moyoni,kitu kilichofanya niwe kama nafoka.
“Ha ha haaa, kumbe na wewe muoga wa kufa eeh. Kila mtu atakufa muda wake ukifika, na ninahisi mimi muda wangu umefika”.Alizidi kuongea maneno ya kukatisha tama,wakati huo alikuwa ananiachia na kuanza kushuka kitandani.
“Ujue ungeniona wakati nakuja kufungua mlango, mbona ungecheka hadi ukae!!! Ha ha haaaa, yaani nilikuwa natambaa kama mtoto mdogo. Ha haaa”.Generose hakuisha maneno mdomoni na tene huku akitabasamu kana kwamba yale aliyokuwa anaendelea kuyasimulia ni mazuri.
“Rose umekula nini?”.Nikamuuliza swali.
“Ha ha haaa, nimekula upendo wangu kwako. Ni mtamu sana,lakini kuna watu wanataka kuukatisha na sitokubari”.Alijibu Generose huku akinifanya nizidi kuumia nafsini mwangu.
“Nakuomba Rose, niambie mama yangu. Umekula nini tangu juzi?”. Nikamuuliza tena, safari hii kwa kubembeleza.
“Sijala kitu zaidi ya jana nilipotoka nje na kwenda dukani,halafu nikapitia pale bombani kwetu na kunywa maji. Ndiyo basi hadi sasa hivi”.Alijibu Generose huku sauti yake ikizidi kuwa kavu kutokana na kuongea sana wakati hana maji mdomoni na anasikia njaa.
“Dukani ulienda kufanya nini?”.Nikamtupia swali linguine.
“Nilienda kununua dawa”.
“Dawa gani?”.
“Dawa za kutibu kelele za hapa nyumbani kuhusu mimi”.
“Hiyo inatibu nini mwilini mwako?”
“Haitibu kitu zaidi ya kuwatibu midomo yao”.
“Ujue sikuelewi Rose una maana gani”.
“Sasa huelewi nini mme wangu?. Furaha yao na ukitaka kuona wanakaa kimya, ni mimi kuondoka dunia hii”.
“Ina maana umeshameza hivyo vidonge?”
“Siyo vidonge, ni dawa”.
“Dawa gani sasa uliyoimeza?”.Akaa kimya kidogo na kisha akajibu.
“Dawa ya panya, ha ha haaaa”.Alijibu kama utani, lakini haikuwa utani tena kwa mimi niliyejua maana ya cheko zake.
“Embu ngoja”.Nikatoka nje haraka na kwenda dukani kasha nikanunua maziwa na kuingia nayo ndani kwake ambapo nilimkuta Mama yakeakimuomba Generose ale lakini alikataa.
“Mwanangu, embu nisaidie huyu mwenzako ili ale chakula”.Mama Generose aliniambia baada ya mimi kuingia mle ndani tena.
“Usijari mama, atakula tu! We kiache hapo”.Nilimjibu mama Generose na kisha aliondoka mle na kutuacha mimi na Generose tena.
“Na utakila mwenyewe, wewe si unajidai unajua sana. Na ukile hicho chakula”.Aliongea Generose huku akikioneshea chakula kile kidole.
“Hivi Rose, mimi nimekuja hapa kuteseka nafsi yangu kwa ajili ya kukuona wewe unavyohangaika hivi? Embu fikilia nimetoka wapi ili nije kukuona nakuhakikisha kuwa upo salama? Embu niangalie mwenzako navyoteseka, tafadhari Rose nionee huruma. Kama unataka kunipa furaha na nijisikie amani, naomba ule chakula”.Niliongea hayo kwa sauti ya kusikitika na ya huruma ambapo kiasi fulani nilifanikiwa kumshawishi Generose na kukubari nachoomba.
“Basi njoo unilishe,wewe si ndo unataka nile.Haya njoo hapa kitandani ukae na kianza kunilisha”.Kitendo bila kusita nikawa tayari nipo kitandani huku kichwa chake kikiwa mapajani kwangu, na taratibu nikaanza kumlisha mtoli ambao mama Generose aliuandaa.
“Frank, naomna nikuambie jambo”.Alianza tena kuongea Generose baada ya kula nusu sahani ya mtori ule.
“Kunywa na haya maziwa halafu utakuwa huru kusema chochote juu yangu na kuniambia chochote utakacho”.Nilimuambia Generose huku namimina maziwa yale kwenye glasi iliyokuwepo mle ndani.
“Haitosaidia Frank, ila nitakunywa kwa sababu yako”.Aliongea hayo huku anatanua mdomo kwa ajili ya kuruhusu maziwa yale yaingie kinywani mwake.
“Haya niambie sasa unachotaka kuniambia,ila kisilenge sana mambo ya kifo”.Nilimuambia baada ya kuridhika na unywaji wake wake wa yale maziwa.Alitabasamu kidogo baada ya kumpa ruhusa ile na kuanza kuongea aliyodhamilia kuyaongea.
“Frank, nayajua maisha yako yote ya mapenzi uliyoishi kabla hujawa na mimi. Yasint na Seth waliniambia kila kitu kuhusu tabia yako,na kwa kuwa nulikupenda,basi niliapa kukubadilisha. Sikutaka uendelee na tabia zile hata kidogo,na kwa kiasi fulani naweza kusema nimefanikiwa.
Frank,kabla sijaondoka duniani.Ha ha haa, samahani kama nitakuwa nimekukera kwa hayo maneno ya mwisho, nimepitiwa. Ila nataka nikuambie kuwa, waheshimu sana wanawake,usiwafanye kama chombo cha starehe katika maisha yako,usiwafanye wawe wanalia kwa ajili yako na kamwe usiruhusu kuona chozi la mwanamke likidondoka kwa kuonewa au labda ana shida ambayo unaweza kumsaidia.
Frank, natangulia. Ila nitakuwa nakuangalia kwa kila kitu utakachofanya na kuwafanyia wanawake na nitakulaani kwa chochote kibaya utakachowafanyia, kumbuka mimi ni mama yako japo sijakuzaa”. Generose alikuwa anaongea haya huku akiwa na msisitizo wa maana katika kutamka alichodhamilia kukitamka.
“Rose, naamini bado nitakuwa na wewe katika maisha yangu yote. Utakapoenda na mimi nitakufata. UKIRUKA namI NITARUKA kumbuka huu msemo”.Nilimuambia Generose huku chozi likitaka kunitoka lakini nililizuia kwa kuangalia pembeni kama nakohoa halafu nikalifuta chozi lile kwa mkono.
“Frank tafadhari,usije ukafanya jambo lolote litakalokwaza maisha yako. Na ninaomba, uwe wazi kupenda tena. Acha moyo wako upende tena,usivunjike moyo na kuapa kuwa hutokuja penda tena. Frank nakuomba tena na tena, usije kufanya kitu kibaya katika maisha yako baada ya mimi kutoweka. Ni lazima nife Frank, kitu nilichokunywa hakina dawa na nimekunywa kwa muda mrefu sasa. Hayo maziwa siyo kitu, ushachelewa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikuumizi moyo kwa haya niyasemayo bali ni ukweli usijificha. Nakufa ila nakufa kwa kupigania mtu ninayempenda, na ninidhani sasa watatulia na kelele kupotea midomoni mwao. Nakupenda sana Frank.” Alizidi kuniongezea machungu Generose na safari hii nilishindwa kulizuia chozi langu bali kuliacha litililike toka kwenye jicho langu na kupita kwenye shavu langu kisha kudondokea kwenye paji la uso wa Generose ambapo kichwa chake bado kilikuwepo kwenye mapaja yangu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment