Simulizi : Niache Na Moyo Wangu
Sehemu Ya Tano (5)
Ilipoishia ijumaa…
Alihisi ni kitu cha kawaida lakini hakuwa na jinsi kutokana na kukabwa na kinakakamega hali iliyomfanya Sara kuishiwa nguvu kabisa. Alikuwa ameshajitolea kufa. Hakuweza kutoa neno hata moja zaidi ya kuhema juu juu.
Songa nayo sasa…
“Unaitwa munani wewe?” Aliuliza Thiwa.
Sara hakuweza hata kutoa neno moja. Alikuwa amebanwa vilivyo na Thiwa maeneo ya shingoni mwake. Hoi!!
Lengo kuu la Thiwa ni kumuweka Sara na yeye awe miongoni mwa kina Kakamega. Sara aweze kuishi kuendana na maisha waishio watu wa Kakamega. Maisha ya nusu uchi kwa kutumiwa majani makavu ya msituni tena maeneo ya mbele tu. Maisha ya kushindia nyama za msituni. Maisha ya kusindikiza watu wakamatwao nje kwa ajili ya kupelekwa katika jiwe kuu la kutolea kafara. Jiwe waliloliamini kina Kakamega kuwa endapo watakuwa wakitoa kafara mungu aliokuwa ndani ya jiwe hilo atafurahia. Ataufanya msitu ujazane mahitaji wanayoyahitaji kuanzia wanyama wa porini. Majani kujaa maji na kuweza kuishi maisha mazuri kila siku.
Alama nne katika mwili wa Sara zilimtosha kabisa kuwa mwanachama hai wa Kakamega. Alama za duara ambapo Thiwa alifanikiwa kumtoa Sara vipande vidogo vya ngozi kuanzia maeneo ya mkononi kipande kimoja. Eneo la pajani kipande kimoja, eneo la mgongoni kipande na mwisho kabisa Thiwa alimalizia kutoa kipande cha ngozi ya mwili eneo la shingoni. Mwili wa sara ni kama ulikuwa umeingiwa na ganzi kwa muda. Hakuweza kusikia tena hata ile ngozi aliokuwa akitolewa na Thiwa. Alikuwa amelegea vya kutosha kiasi cha kutokusikia chochote.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mpelekeni kwa bibi Mwenda?” Aliamrisha Thiwa.
Kina Kakamega wakambeba Sara juu juu mpaka katika nyumba ya pembeni. Nyumba ambayo anaishi bibi mzee sana. Bibi mkongwe kwa eneo lote la Kakamega. Bibi ambaye hushughulika na matatizo ya wanawake wa Kakamega katika kuwafunza. Bibi ambaye umri tayari ulikuwa umeshamtupa! Hakuweza hata kutoka kitandani. Miguu yake ilishazeeka na maisha.
“Nani huyu mmeleta” Aliongea bibi Mwenda.
“Thiwa katutuma tumpeleke hapa”
Bibi mwenda alikuwa na hisia za ajabu sana. Hisia za kuweza kumtambua mtu pasipo kumuona bali kwa kumpapasa. Macho yake madogo sana mithili ya watu wale wa ‘Vietnam’ au wajapani ndio yalikuwa na nguvu sana kuona. Alimuona Sara. Sahawia!!
“Msogezeni karibu yangu?” Aliamuru bibi Mwenda.
Wakamsogeza Sara karibu ya bibi mwenda. Sara bado hakuweza kushtuka. Alikuwa kama nusu mfu. Hakujitambua!!
Bibi mwenda akaitoa mikono yake nakuanza kumpapasa sara mwilini mwake. Alimpapasa mpaka zile alama alizokuwa amepigwa na Thiwa. Alama za utambulisho wa kinakakamega. Alama zilizotoa vipande vya ngozi yake.
Bibi mwenda akazipapasa zote. Akaitoa mikono yake katika mwili wa Sara. Mikono yake akaihamisha dira nakuelekea katika majani majani ya miti yaliokuwa pembeni yake. Akavuta jani refu lilokuwa na hirizi moja kubwa. Akachomoa ile hirizi. Ikangatuka!!
Akaiosogeza mpaka katika nguo ya Sara. Akaanza kuifunga kwa nguvu. Hirizi ikashikamana na nguo ya Sara pasipo Sara mwenyewe kujitambua. Bibi mwenda akatoa mikono yake nakuitafuta hirizi ya pili. Safari hii ilikuwa ni hirizi ndogo sana ambapo aliitoa na kumuwekea Sara mdomoni mwake kisha akaufunga mdogo wa Sara kwa kumbana kwa kutumia mikono yake. Akampiga ngumi ya mgongo. Sara akashtuka. Kitendo cha Sara kushtuka kutoka usingizini ile hirizi ikamzidi ujanja. Ikapenyeza!!
Ikaomba njia katika koromeo laini la Sara. Koromeo lisilo na hatia yoyote katika jamii. Hirizi ikaingia na kutulia tumboni mwa Sara. Sara akashtuka!
“Mnanifanya nini? hapa wapi” Sara aling’aka.
Hakujitambua wala kuelewa kinachoendelea kutokana na upofu wake.Alionesha tabasamu kana kwamba tayari ni mwana Kakamega mpya. Alinywea kwa muda kisha akatoa neno.
“Nashukuru sana bibi mwenda! nakuhaidi kuwa pamoja na wewe na wote hapa msituni!!” Aliongea Sara akifikicha eneo la usoni mwake ambao lilikuwa bado katika mshono. Halikuwa na uwezo wa kuona. Hisia na nguvu ya ile hirizi ndio ilimchochea Sara kuongea maneno yale.
Kilichofuatia ni makelele tofauti kutoka kwa kina Kakamega katika kumpokea mwenzao mpya.
**********
Jua la upole lilianza kupenyeza katika jiji la Dar es salaam. Jua la asubuhi ambalo lilileta joto la ajabu. Kila mmoja alionekana kuwa na kitambaa cha kufuta majasho. Wenye magari nao kiyoyozi kilikuwa ni kama hakifanyi kazi ipasavyo. Waliweza kufungua viyoyozi vyao sambamba na vioo vya magari yao kuvishusha. Wale wasukuma mikokoteni kwao ilikuwa ni bora riziki ipatikane lakini jasho lijitokee tu. Waliweza kutoa mashati yao na kubakiwa tumbo wazi pasipo kujali ukubwa wa matumbo yao.
Mchungaji John pamoja na yule mzee walikuwa wameshafika katika Gereza kuu la Segerea. Walikuwa nje ya lango na fuko lao kubwa lililokuwa limejaa vitafunwa sambamba na chupa kubwa iliokuwa na chai ndani yake.
“Watapita huku kweli” Aliongea yule mzee kwa kukata tamaa.
“Lazima hili si ndio lango lao kuu la kuingilia? tumuombe Mungu aweze kutukutanisha naye kwa mara nyingine ili tumpatie hivi vitu mtoto wetu” Alijibu mchungaji John.
Haikuchukuwa muda sana.Ndani ya lisaa msafara wa gari ndogo aina ya ‘Defender’ ilikuwa mstari wa mbele kuingia eneo la gereza kuu la Segerea kisha kwa nyuma basi kubwa la kubebea watuhumiwa liliingia. Mapolisi waliokuwa kwenye ile ‘Defender’ wote walishuka mikononi mwao wakiwa na silaha za moto. Wakatanda kote kote na kilichofuatia ni lango kuu kufunguliwa. Mtuhumiwa mmoja baada ya mwingine alishushwa nakuelekea ndani ya lango la kuingilia gereza kuu. Macho ya mchungaji John yakisaidia na macho ya yule Mzee yalikuwa na kazi moja ya kuhakikisha wanamuona Stan na kuomba kama kutakuwa na uwezekano apelekewe ile chai. Walilitazama gari karibia lote lakini hawakuweza kumuona Stan wala huyo baba Devotha.
“Yupo wapi sasa? watakuwa wamempeleka wapi sasa?” Aliropoka mchungaji John baada ya kumshuhudia mpaka mtu wa mwisho kushushwa.
“Au tutakuwa tumeangalia vibaya nini? haiwezekani kwa kweli hayupo?” Aliendelea kuongea yule mzee.
Bumbuwazi!! kila mmoja hakuwa akielewa haswa kilichomfanya Stan asiwepo katika ule msururu. Stan ambaye walimshuhudia akipakizwa katika basi lile lile la polisi. hakuwepo kabisa. Wale mapolisi walifunga mlango wa lile basi la polisi baada ya wote kuhakikisha wameshuka na kupelekwa lango kuu la gereza la Segerea. Basi likawashwa nakuondoka zake na baada ya hapo wale mapolisi nao wakapaki gari yao vizuri nakuingia ndani ya Gereza kwa ulinzi zaidi.
“Embu twende tukaulize na kumpelekea hii chai. Lazima atakuwa amepelekwa ila hatukuwa makini katika kuangalia tu!” aliongea yule Mzee.
Walikubaliana. Wakajisogeza na chupa yao mpaka eneo la lango la kuingilia. Hatua moja baada ya nyingine waliweza kufika mpaka mapokezi kuu. Kaunta kuu ya polisi.
“Jambo afande” Aliongea yule mzee kwa kutetemeka.
“Salama tu tuwasaidie nini?”
“Enhh!!, Mhh!! kuna kijana wetu anaitwa Stanley yeye alikuwa kituo kikubwa cha polisi kule Kimara na basi limeshampakiza…
Kabla hajamalizia kuongea yule Mzee, polisi mmoja alidakia.
“Sema shida yako moja kwa moja unataka nini hapa au hujui hili ni eneo gani na muda gani huu? Sema nini kilichowaleta hapa?”
Woga ulizidi kumtanda yule mzee. Vidole vyake vikakosa kabisa ushirikiano. Vikatetema!! Akajiumauma!! Akajimezameza!! Akajitusu lakini akashindwa!!
Mchungaji John ikambidi kuingilia kati kumsaidia kujieleza vizuri.
“Afande hapa tuna chai na vitafunwa tumemmletea kijana wetu anaitwa Stan.”
“Hivyo ndivyo mnapaswa kuongea sio kuzunguka zunguka pasipokueleweka!! haya huyo kijana mmeambiwa huku hawapewi chai?”
“Hapana hatumaanishi hivyo”
“Bali?”
“Alikuwa amewekwa kule kituo kikuu cha Kimara, na tulikuwa tumempelekea chai ila sasa muda ukawa hautoshi wakampakiza kwenye basi na sasa hivi tumeliona basi likiingia. Tunaomba japo mumpatie hata kama ni nyinyi pasipokumuona sisi lakini anywe hii chai na vitafunwa”
“Mzee” polisi aliita kwa ukali.
“Naam mkuu!!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapa hakuna utaratibu wa kuleta vyakula. Utaratibu huo hufanyika vituoni hukoo na sio hapa gerezani. Hapa kuna watu wa kuwatengenezea vyote hivyo. Na kuhusu basi kutoka kimara bado halijafika. Hapa kuna mabasi mengi sana ya kila kanda hili lililotoka ni la kanda ya ilala bado la kinondoni. Na hapa bora mpotee na hivi vitu vyenu. Poteeni tafadhali” Aliongea yule polisi kwa ukali.
Mchungaji John pamoja na yule Mzee hawakuwa na jinsi yoyote tena. Walikuwa ni kama waliolowa na mvua mwilini mwao. Jasho liliwaelemea sana. Hawakuwa na jinsi zaidi ya kuondoka wakiwa wamenywea. Wakaongozana mpaka katika gari lao nakuingia. Wakiwa katika hali ya kukata tamaa ndani ya lile gari mara basi la polisi jingine likaingia ndani ya lile eneo. Basi la kijani lililokuwa limewabeba watuhumiwa wengine. Yule mzee alikuwa na mchecheto kwa kunyooshea lile basi kidole. Mchungaji John naye akaliona. Basi likaingia na kupaki kama lililvyofanya lile jingine. Mapolisi wakashuka katika ‘Defender’ yao na kutanda. Basi Likapaki nakuanza kushusha mmoja mmoja. Baada ya zoezi la kushusha mmoja baada ya mwingine. Safari hii tena Stan hakuweza kuonekana hata akishuka. Mchungaji na yule mzee akili zoa zikajijenga tofauti kama walivyoelezwa na yule polisi pale kaunta kuu. Wakahisi huenda tena lile basi ni lakutoka kanda nyingine.
“Na hapa patupu? Stan atakuwepo wapi sasa?” aliuliza yule mzee.
“Itakuwa sio hili basi”
“Hapana ndio lenyewe bwana wewe humuoni yule baba Devotha akiingizwa mule ndani?”
Wakiwa katika kuulizana mara polisi wakamshusha mwisho kabisa Stan. Stan aliokuwa amefungwa mikono yake kwa nyuma kwa kutumia pingu. Alishushwa kwa ulinzi mkali na mapolisi watatu wakiwa wamemzunguka japo alikuwa ni kijana mdogo sana. Taharuki!!
Defender ile ya polisi ilisogea mpaka eneo alilokuwepo Stan na wale mapolisi. Wale mapolisi wakampakiza Stan kwa haraka. Stan akazidisha ubishi. Hakuwaweza!! Wakamlazimisha na kufanikiwa kumuingiza katika ‘Defender’ yao ya polisi. Defender ikazungushwa kwa haraka na kutimua mavumbi. Mchecheto!!
Mchungaji John pamoja na yule mzee hawakuwa wakijielewa kwa lile tukio. Mikono yao bado ilikuwa imeingiwa na barafu. Ilikuwa ya baridi yenye kutetema. Hata kuliwasha gari alishindwa mchungaji John. yule mzee naye hakuwa akijua kuliendesha gari. Maombi ya chinichini yakaanza kurindima ndani ya gari lao ili tu waweze kujinusuru mikono yao nakuweza kuliendesha ili tu wafuatilie ile ‘defender’ iliyokuwa ikimpeleka Stan tena chini ya ulinzi mkali.
****************
*********
Umati wa wananchi ulizidi kumiminika barabarani. Barabara na njia za magari yapitao shotikati zilionekana nazo kujaa watu. Magari yaliokuwa yamekatiza njia hiyo hayakuweza kusogea hata kidogo kutokana na umati ule wa watu. Mabango mbalimbali ya kuhamasisha maandamano yalikuwa mikononi mwa watu. Makelele na miluzi vilizidi kutikisa masikio ya wapitao bila kujihusisha na maandanmano hayo.Walianza taratibu lakini kadri muda ulivyosogea ndivyo walizidisha makelele yao. Walishachoshwa manyanyaso ya mtaa kupendelewa wahindi. Wahindi walionekana kuuteka mtaa kwa kuwaondoa kwa nguvu ya pesa na kuporomosha majumba yao na kuweka makazi yao wenyewe.Wahindi walikuwa wakipitia njia za panya katika kuwahonga madiwani wenyeviti wa mitaa mpaka halmashauri kisha kuporomosha maghorofa yao na wakati mwingine kujenga katika viwanja vya mipira na hata barabara ili mradi waweke makazi yao.
“Tunataka waondoke!!! Hatutaki wabaguzi!!, Waondokee Wabaguzi!!”
Si kina baba wala kinamama wote walikuwa mstari mmoja. Kuna wakinamama walionesha wazi kuchoshwa hata kumwaga radhi hadharani ili mradi tu wachochee ule mkusanyiko. Wananchi waliwachukia sana madiwani,watu wa halmashauri mpaka mapolisi. Waliwachukia kwa jinsi wanavyowalelea Wahindi nakuwaonea masikini wa Ilala. Tayari walikuwa wameshateketeza nyumba ya diwani wa kata yao nyumba yake pamoja na familia yake iliokuwa ndani kwa kuichoma moto kila kona. Na sasa ilikuwa zamu ya kila kituo cha polisi cha mtaa na lengo lao kuu likiwa ni kuteketeza vituo vyote vya polisi vya mtaani.
Wakiwa katika maandamano katikati ya foleni ya magari baadhi ya raia waliiona defender ya polisi ikiwa imepaki katika foleni ile ile ya magari yapitao shotikati. Wananchi wenye hasira wakaifuata ile defender kwa ukaribu na kuirushia mawe makubwa eneo la mbele. Vioo Vikapasuka!! Mapolisi takribani wanne wote wakatoka katika ile gari uku watatu kati ya wanne wakiwa na bunduki kubwa.
“Tutawasambaratisha sasa hivi pumbavu!! tokeni hapa nyie ndio mnasababisha hii foleni siyo?” Aliongea polisi mmoja baada ya kuchoshwa na makelele ya maandamano. Walikuwa wakijua ni maandamano ya kawaida na hayana madhara.
Mara jiwe kubwa la haja likatumwa upande wa pili. Likampata yule polisi kichwani. Polisi hakuwa na chochote cha kuzuia kichwa chake. Akadondoka hapo hapo. Raia mmoja mwenye ujasiri akawahi kuivua ile bunduki kwa yule polisi lakini akawahiwa pale pale na askari mwingine, akamnyunyizia risasi mfululizo. Wakasambaratika baadhi huku mawe yakiendelea kuvugumishwa hapa na pale. gari yote ya polisi ikabonyea kwa kukandamizwa mawe makubwa. Mapolisi wale waliotoka wengi walikuwa waoga katika kuachia risasi. walijikuta wakidondoka kwa kupigwa mawe ya nguvu vichwani mwao. Umati ukaongezeka zaidi mara mbili yake. Defender mbili zikawasili nakuachia mabomu ya machozi baadhi ya raia wakasambaratika lakini tayari walikuwa wameshawauwa wale mapolisi wote wa ile defender ya kwanza ya polisi kwa kutumia mawe makubwa na nondo nene.
Stan alibaki peke yake ndani ya ile defender ya kwanza ya polisi baada ya mapolisi wote kuuliwa. Alikuwa na pingu mikononi mwake. Aliweza kutoka kwenye ile defender kwa kujikokota. Macho yake yakasalimiana na mabomu ya machozi kutoka kwa mapolisi wengine waliokuwa wakituliza ghasia. Stan hakuweza kuona mbele wala nyuma. Akawa akitangatanga!! akiweweseka!! akiyumbayumba!! akigotagota!! akathubutu lakini akashindwa hata kujua uelekeo wake. Kuna baadhi ya mawe madogo dogo yalimpata kwa bahati mbaya lakini aliweza kuyavumilia uku akikimbia. Akiwa hajielewi mara akasikia sauti ya jina lake akiitwa. Akabaki na butwaa!! akasikamama asielewe wala kumuona huyo anayemuita kutokana na macho yake kuingiwa na mabomu ya machozi.
***********
Mchungaji John akiwa pamoja na yule mzee waliendelea kujinasua kwa muda mrefu mikono yao iliokuwa kama imeingiwa na ubaridi. Mikono ambayo ilikuwa ikitetemeka sana kwa hofu. Baada ya kufanya maombi ya kimya kimya kwa muda kidogo wakastaajabu mikono yao kuingiwa na jasho. Majimaji yakalowesha mikono yao. Mikono ikawa na furaha kupata joto joto mithili ya maji yale ya mtoni yaliopigwa na jua kwa muda mrefu.
“Hapa ni kuondoka tu na sijui kama tutaweza kujua walipoelekea” Aliongea mchungaji akimwambia yule Mzee.
Hawakuwa tena na cha kusubiria. Mchungaji alitekenya funguo zake za gari kisha safari ikaanza. Hawakutoka na mwendo wa kawaida. Tangu mchungaji awe na gari yake ile hata siku moja hakuwahi kuikimbiza lakini alifanya hivyo na lengo kuu ni kujua Stan anapelekwa wapi. Walirudi na babaraba ile ile waliotoka nayo na kila baada ya hatua kadha walisimamisha gari lao nakuulizia kama kuna defender ya polisi imepita. Kila walipokuwa wakisimama walipewa jibu sahihi kuwa imeonekana ikipita kwa spidi. Waliendelea kujijaza moyo wa ziada katika miili yao. Yule mzee pembeni alikuwa na kazi ya kuomba tena kwa sauti tu ili Mungu aweze kufungua njia waweze kukutana na defender iliyokuwa imembeba Stan.
Baaada ya mwendo mrefu kidogo walifanikiwa kuiona defender. Defender ya polisi lakini haikuwa katika mwendo waliokuwa wakidhania. Waliisogelea nyuma nyuma kadri ilivyokuwa ikitembea. Ile defender ikahisi kama inafukuziwa nyuma. Ikapiga breki. Balaa!!
Hofu ikaanza tena kutanda upya katika mikono ya Mchungaji John. Mikono ikataka kujawa na ubarafu kama wa awali. Mkojo wa moto ukatiririka katika suruali aliokuwa ameivaa mchungaji John. Akajihisi homa ya ghafla kwani kutetemeka kulimzidia mara mbili yake tofauti na mwanzo.
“Endesha twende, twende tuwazunguke kwa mbele!” Aliongea yule Mzee.
“Endesha?, Niendeshe nini wewe huoni wameshatungundua na wamesimamisha gari yao. Haya sasa tutafanyaje na wewe kujieleza huwezi?” Aliongea mchungaji John kwa kupaniki.
Wote hasira kali ziliwashika lakini waliapa ni lazima watakuwa upande wa Stan popote pale alipo Stan. Waliapa mbele ya Mungu kumsaidia kwa lolote. Mchungaji John alichokifanya kwa kuwa alikuwa akitetemeka alilizima lile gari lake sambamba nakujifuta michirizi ya kojo lililokuwa limeshaomba njia ya kutoka katika mguu mmoja wa suruali yake. Yule mzee pembeni yake alishaligundua kuwa mchungaji kashajikojolea. Cheko la kimya kimya lilimtawala. Akapiga Ganzi!, Akasizi!, Akakausha!, tuliii!!
Ile defender ya polisi baada ya kusimama alishuka polisi mmoja akiwa na silaha mkononi na kulifuata gari la mchungaji John. Alilisogelea mpaka karibu kisha akalichungulia kwa upande wa mbele wa dereva nakushuhudia mchungaji John na yule mzee wakiwa tuli wakikodoa mimacho.
“Vipi nyie mnatatizo gani? kwanini mnatufuata nyuma nyuma? mnataka msaada?” Aliongea yule polisi.
“Ndio tunataka msaada!!” Aliropoka yule Mzee.
Kitendo cha kusema hivyo yule polisi akaiweka bunduki yake vizuri begani. akawasogelea tena kwa ukaribu.
“Mnataka msaada gani tuwasaidie”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni kuhusu kijana wetu Stan, tunaomba jamani tumpatie japo hii chai” Aliendelea kuropok yule Mzee na muda wote mchungaji John alikuwa ni kama haijelewi kwa kinachoendelea kutokana na kuwa na kigugumizi cha muda.
“Huyo Stan yupo wapi? na ni nani?” Alihoji polisi.
“Stan ni mtoto wetu na mpo naye ndani ya hilo defender mmepakiza kwa nyuma hapo kwenye hilo turubai lenu siti ya nyuma. Chukuwa jamani mumpe japo chai” Aliongea yule mzee kwa kuchanganyikiwa uku akiitoa ile chupa ya chai na kuanza kuinywa chai kuashiria kuwa haina tatizo lolote.
“Ngoja ngoja, Umesema Stan yupo wapi? na alikuwa wapi mpaka awepo katika gari yetu? unajuwa tupo na kina nani mule nyuma ya lile turubai? Aliendelea kuhoji polisi safari hii alikuwa mkali kidogo.
“Mkuu wewe chukuwa tu mpelekee ni kijana mdogo mdogo anaitwa Stan ukitaja jina hilo ataitika tu mpe mwambie mchungaji John amemletea.” Yule mzee alizidi kuongea.
Hakuwa akijitambua kabisa. Jasho lilimtiririka mwili mzima. Jasho la kuchanganyikiwa kwa alichokuwa akikifanya. Kwanza alikuwa kaingiwa woga wa kuhojiwa na polisi pili alikuwa na woga wa kuhojiwa juu ya Stan.
“Hivi eti mzee mwenzangu kuna Stan wa kike kweli hapa duniani?” Alihoji yule polisi na safari hii alimgeukia mchungaji John akimuuliza.
“Hapana, hakuna!” Alijibu mchungaji John.
“Sasa basi nataka muelewe kuwa kwenye lile gari hakuna Stan. Tumewakamata machangudoa wanauojiuza usiku na walikuwa wamelazwa katika kituo cha hapa Tazara na sasa tunawapeleka kituo kikuu buguruni sokoni. Embu wewe mmoja shuka ukawaone na uniambie sasa huyo Stan wakumpelekea chai yupo wapi au Stan ndio mke wako aliokamatwa akijiuza?” aliongea polisi kwa kejeli.
Ilimbidi yule Mzee amuache Mchungaji John ndani ya gari kwakuwa suruali yake ilikuwa imelowa kwa mkojo. Alishuka kwenda kuhakikisha kama mule ndani ya defender hakukuwa na Stan, aliona kama anadangwa na kitu alichoamini ni defender ile ile ya bluu ndio ilikuwa na Stan na hata namba zake ni zile zile.
“Haya Stan wako yupo wapi? au jamani humu kuna mama Stan au mtu anaitwa Stan atokee mumewe huyu?” Aliendelea kuongea yule polisi kwa kejeli.
“Basi mkuu nimeamini hakuna mwanaume yoyote, Samahani kwa usumbufu mkuu” Alimaliza kuongea yule Mzee akijiondokea zake kwa kunywea.
Aliachiwa aondoke zake aelekee kwenye gari lake. Alipofika kwenye gari ya mchungaji John.
“Enhee vip wamekwambiaje umemuona Stan?” Alihoji Mchungaji John.
“Hapana washa gari twende tu, ile sio defender tuliokuwa tukiitaka. Mule hakuna Stan ni kweli wako wasichana na wengine watu wazima wakiwa nusu uchi wamekamatwa wakijiuza kweli aisee. Dahh dunia imekwisha Mchungaji” Alioongea yule Mzee.
Waliliwasha gari lao na safari ya kutokea maeneo ya Tazara kueleke njia ya upande mwingine ikaanza. Wakaanza kuifuatilia njia ya buguruni wakielekea Ilala. Safari hii hawakuwa na ujanja tena ndani ya jiji. Hawakuwa na ujanja wa kuuliza kwa mtu kutokana na njia kuwa moja.
“Tuelekee uku itatubidi tukisie tu kwani hakuna ujanja wa kumpata tena Stan zaidi ya kuotea, au, au ngoja! hawawezi kuwa wamempeleka mahakamani kisutu kweli wale?” Alihoji yule Mzee.
Alikuwa ni kama ameshachanganyikiwa bado.
“Sijaujua lakini jana tu wamemkata leo mahakani hakunaga kitu kama hicho tumtafute sehemu nyingine tu tunaweza kubahatisha.
Wakiwa katika maongezi ya hapa na pale ndani ya lile gari mara walishangaa kupita defender mbili za polisi zikiwa katika kasi ya ajabu. Si yule mzee wala Mchungaji John wote walishikwa na butwaa ghafla. Hawakuelewa zinatokea wapi na zinaelekea wapi zaidi ya kuwapita zikiwa mwendo kasi sana.
“Watakuwa wenyewe. Ndio hao hao watakuwa na Stan” Aliongea yule Mzee kwa mchecheto.
Mchungaji John naye alijikuta furaha ya ajabu kumtawala. Akaliongeza gari lake spidi nakukimbiza kwa kasi ya ajabu akifuatilia zile defender mbili za mapolisi.
Woga wake safari hii aliuweka pembeni. Hakutaka kabisa kuwapoteza hata chembe. Hakuwahi kuliendesha gari lake kasi lakini kwa safari hii hakuwa na jinsi. Magari mengi yaliokuwa yamewekwa foleni yalipisha zile defender kana kwamba kuna moto unawaka uko wanapokwenda ama kuna mgonjwa mahututi anakimbizwa kupatiwa huduma. Mchungaji John na yeye alifanikiwa kujiunga nao. Kila kona zilipokatikaza zile defender nyuma yake kulikuwa na gari moja tu ya mchungaji John nayo ilikuwa kasi moja. Baada ya mwendo mrefu kwa kuruka viunzi vya hapa na pale zile gari ziliingia njia inayotumika gari kupitia shotikati kama foleni ikiwa kubwa. Zikasimama. Baada ya hapo polisi mmoja baada ya mwingine alishuka huku usoni mwao wakiwa na kofia zile za waendeshao bodaboda. Wale mapolisi walisogea hatua kama kumi mbele yao ambapo walikumbana na rundo la watu wakiwafuata kwa upande wao. Mapolisi wakaanza kuwarushia mabomu ya machozi wale watu. Kuona vile mchungaji john akalirudisha gari lake nyuma haraka akaliweka mwendo wa kutoka spidi na kisha wakafunga vioo vyao nakukaa kimya wakisikilizia.
Baada ya kukaa kwa muda wakisikilizia milio ya mabomu na mawe yakirushwa mchungaji John akaitoa miwani yake nakumpatia yule Mzee. Yule mzee akaivaa kwa kujifunika na kitambaa kwa upande wa pembeni ya ile miwani kwa lengo la kuzuia mabomu yale ya machozi kisha akashuka nakuanza kujipenyeza kujua kama anaweza japo kumshuhudia Stan kati ya hizo defender mbili za mapolisi zilizoingia. Alienda kwa kujibanza ukuta wa nyumba ya jirani kiupande upande nakufanikiwa kuchungulia karibu defender zote mbili nazo zilikuwa patupu. Hakukuwa na mtuhumiwa hata mmoja zaidi ya wale mapolisi waliokuwa wamevalia sare wakichukuwa mabomu ya machozi kisha kutoka. Yule mzee akatembea kwa mbele kidogo nakujificha kwenye kagenge ambapo muuzaji alikuwa amejificha chini kabisa.
“Eti hapa kuna nini? vipi na hizi vurugu” Aliuliza yule mzee.
“Kuna maandamano ya wananchi kwa kero za diwani kuruhusu hawa wahindi kujenga ghorofa ile pale ambayo haijaisha. Leo wananchi wamemuua diwani na wameamua kuufunga mtaa huu.” Alijibu muuza genge.
“Na magari haya ya polisi vipi ndio yamekuja kutuliza ghasia?” Aliendelea kuhoji yule mzee.
“Ujue wengi hupenda kutumia hii njia hapa ya shotikati kama kule barabara kuu kukiwa na foleni kubwa sana upande wa kutokea kule ilala. Sasa leo wamekutana na wenye hasira zao waliochoshwa na wahindi na mapolisi wapokea rushwa kwa wahindi ona mziki wake ule cheki mbele pale kuna defender ya polisi nayo ilipita shotikati hii hii na limeharibiwa vibaya sana na polisi wane wote wameuliwa na raia wenye hasira kali kwa mawe na nondo nene tu. Yaani ni balaa!!”
Yule mzee alipoambiwa tu habari ya defender moja kukatisha maeneo hayo na ndio lipo mbele ya macho yake pale pale hakutaka kuendelea kumsikiliza yule muuza genge. Aliinuka na kusogea maeneo yale. Raia wengi walikuwa wakitapakaa kutokana na mabomu ya machozi kuwaingia na hata wengine kukimbilia maji kujiosha macho yao yaliokuwa yakiwasha. kila mmoja alionekana kupoteza uelekeo kutokana na kutokuweza kuona mbele kutokana na yale mabomu ya machozi kuwaingia machoni vilivyo. Gari chache ziliharibiwa kwa mawe na wananchi wenye hasira kali bila kujua wengi wao walikuwa ni wapitaji wa shotikati.
“Staaaan?? Staaaan” Staaaaan???” Aliita yule mzee.
Macho yake yalishaweza kuiona shati ya stani ikipepea uku akiwa na pingu mikononi kwa upande wa nyuma. Hakuwa akijitambua anapoelekea kutokana na mabomu ya machozi kumuingia machoni vilivyo. Alikuwa akijigonga kwenye ukuta anahama anajigonga tena ukuta mwingine. Hakuwa na uwezo wa kujua anapolekea kutokana na mabomu ya machozi.
Kitendo cha yule mzee kumuita tu Stan. Stan alihisi kama kuitwa jina lake. Alibaki akizubaa kuangalia uku na kule pasipo kuweza kuona kutokana na yale macho yake kumezwa na mabomu ya machozi. Polisi mmoja aliokuwa akirusha yale mabomu tayari macho yake yalikuwa yameshamuona Stan akiwa amefungwa pingu nyuma. Aliikoki bunduki yake nakutupa yale mabomu yake pembeni. alishagundua kuwa Stan atakuwa mmoja kati ya watuhumiwa waliokuwa katika ile defender yao iliokuwa imeharibiwa kutokana na Stan kuwa na pingu mikononi.
******
Yule polisi alizidisha mwendo kuelekea sehemu alipokuwa amezubaa Stan.Hakutaka kabisa kulazia damu hata kidogo. Sura ile ya polisi ilishajijenga kichwani mwake na alishaona kuwa endapo atazubaa tu basi zoezi lake la kumtafuta Stan lingeishia hapo hapo.
“Staaaan kimbiaaaaa, kimbiaaaaa anakufuata huyooo!” Aliropoka yule Mzee.
Ile sauti kubwa ya yule mzee ikazama masikioni mwa Stan. Stan akageuza mwili wake nakuanza kutoka mbio uku mikononi zile pingu zikiwa bado zimemng’ang’ania vilivyo.
Yule mzee aliokota mawe makubwa kiasi akisaidia na wananchi wenye hasira kali waliokuwa tayari wameshamuona yule askari akija upande wao. Wakaanza kumshambulia yule askari kwa mawe yale makubwa. Askari akajitahidi kuyakwepa lakini ikashindikana kwani mengi yalikuwa yamempata maeneo ya kichwani. Hakuweza kumfikia Stan japokuwa Stan alikuwa amekimbia mwendo kidogo nakujikalia zake kwa kuchoka. Idadi kubwa ya mawe ilishaharibu kichwa cha yule askari. Alidondoka chini na kilichofuatia ni raia wenye hasira kali kumsogelea nakumvamia kwa kumkanyaga kanyaga mwili wote sambamba na kumpora ile bunduki begani mwake. Kiujanja ujanja kitendo cha wale raia wenye hasira kali kumshambulia yule askari, yule Mzee alijipenyeza mpaka alipo Stan, akamshika mkono.
“Stan mwanangu pole sana, watakuua wale sio watu wazuri, twende mwanangu?” Aliongea yule mzee.
“Niache tu, hapa nilipofikia nitaweza kujiokoa mwenyewe nakujua wapi naendelea. Asante mzee kwa ukarimu wako” Alijibu Stan.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Stan hakuwa ni mtu wa kujielewa hata mara moja. Alikuwa ni kama amepoteza ufahamu wa kujitambua. Hakuwa akiamini hata mara moja kwa kilichomtokea kuanzia kusingiziwa kesi ya kuua na mpaka kupelekwa rumande na siku ya pili kumtokea vurugu wakati akipelekwa kusikojulikana.
“Hapana Stan mwanangu! Nipo na mchungaji John na tupo hapa kwa ajili ya kuwa na wewe na tutahakikisha upo mikononi mwetu Stan. Mikono Salama!!” Alionge a yule mzee kwa kubembeleza.
“Hamsikii!!!! Nimesema niacheni mimi, niacheni na moyo wangu. Yatosha kwa msaada wenu mlioonesha kwangu. Asanteni!!” Alijibu Stan. Safari hii alikuwa amekunja ndita. Alikuwa mkali kidogo.
“Stan unamkumbuka mchungaji aliyekupa ile biblia vizuri? yupo kwenye gari lake anakusubiri. Angalia wema wake aliokufanyia. Tumekaa leo ni siku ya pili hata kula wala kunywa hiyo chai hatuwezi. Tumekuwa tukikuombea wewe mwenyewe usiku kucha na mchana. Mungu ameweza kuonyesha njia lakini bado Stan unatukataa? Stan kumbuka kuwa kwa Mungu hakuna lisiloshindikana, chukuwa ile biblia yako tafuta Warumi 15: 4-6 sasa hivi. Tafuta Stan?” Aliongea yule Mzee.
Machozi yalimbubujika hali iliyomfanya Stan kumuonea huruma sana. Maneno yale yakagusa roho yake. Akatabasamu na huruma pana.
“Mchungaji yupo wapi umesema?” aliuliza Stan.
“Yupo nimemuacha kapaki gari lake upande ule wa kule chini kutokana na vurugu zinazoendelea twende tupite kwenye hizi kona kona usije kukamatwa tena mwanangu!!” Alijibu mzee.
Stan aliweza kunyanyuliwa na yule mzee pale chini. Wakaanza kujikongoja uku wakikatiza njia za panya ili watokee eneo aliokuwa amemuacha mchungaji John. Baada ya muda mchache waliweza kukutana na gari ya mchungaji John ikiwa bado imepaki. Mchungaji John hakuwepo eneo hilo lakini milango ilikuwa wazi. Haikuwa imelokiwa. Yule mzee akafungua nakumpakiza Stan kisha akafunga nakuchukuwa simu yake kumpigia mchungaj John.
“Halo mchungaji?”
“Ndio mko upande gani nyie” Alijibu mchungaji John kwa upande wa pili wa simu.
“Nimeshamchukuwa Stan nimefanikiwa kumpata na nipo hapa ulipoacha gari lako”
“wapi?”
“Pale tulipoachana mara ya kwanza na nipo na Stan katika gari lako njoo haraka twende zetu”
“Gari languuu??? Gari mbona ninayo mimi hapa naendesha nyie mpo gari ipi sasa?? Mimi nipo upande wa mbele kabisa nimesogea mara moja ngoja nigeuze nakuja maeneo hayo hayo tena....
Kabla mchungaji John hajamaliza kujieleza pale pale yule Mzee akakata simu yake. Kitendo cha kumaliza tu kukata ile simu. Tahamaki!! watu watatu wakiwa pamoja na yule kamanda mkuu wa kikosi, Rafaeli alikuwa mbele yao kidogo akiongea uku akizungukwa na mapolisi waliokuja kuchukuwa miili ya wenzao pamoja na kutuliza ghasia. Alikuwa kama akiwaambia kitu kwa kuwafokea na kwa msisistizo!
**********
“Haiwezekani!! Haiwezekani lazima atengwe na asiwe kitu kimoja na wenzake. Kama hajaua basi ukweli wote atakuwa akiujua. Tumshikilie na apewe uangalizi mkali sambamba na mahojiano ya watu wachache!” Aliongea Rafaeli.
Alikuwa bado yupo katika kituo kikubwa cha polisi,Kimara. Alikuwa akibishana juu ya Stan. Alitaka kwa amri yake Stan atengwe na awe chini ya uangalizi mkuu na mahojiano ya peke yake juu ya tukio la kuuwawa kwa mfanyabiashara maarufu, Laurent Kimaro.
“Kwani mmepeleka wapi? Segerea?” Alihoji Rafaeli.
“Ndio mkuu”
“Sitaki kusikia hivyo. Akachukuliwe sasa hivi haraka iwezekanavyo apelekwe kanda ya mahojiano na wapelelezi pale Ilala boma sasa hivi. Wote nyie watatu chukueni defender hiyo akachukuliwe mara moja na mhakikishe amepelekwa pale Kanda ya Ilala. Mie natokea hapa moja kwa moja naenda Ilala tukutane uko?” Aliongea Rafaeli kwa ukali. Rafaeli aliwaandikia kibali maalum kikapigwa muhuri wa kituo kikuu cha kimara kisha akawapa waende nacho kwa ajili ya kumtoa Stan kumhamisha eneo.
Wale wapolisi wakawa wameshahafikiana na kamanda wao mkuu wa kikosi,Rafaeli. Waliafikiana juu ya kijana mdogo kiumri lakini kesi iliokuwa ikimkabili alionekana kama ni mtu mzima. Walikuwa wakitaka kuujua ukweli mapema juu ya aliyefanya mauaji ya Laurent Kimaro. Waliona endapo watatumia njia za nguvu au kufanya baya lolote kwa Stan isingekuwa rahisi kuupata ukweli nakumjua aliyehusika. Kwa mwendo wa haraka sana wale maaskari walitoka katika kile kituo kikuu cha polisi Kimara na kuelekea Segerea moja kwa moja lengo lao kuu ni kulikimbiza lile basi lililokuwa limebeba watuhumiwa mbali mbali na Stan akiwemo. Kila kona waliopita lile basi lilikuwa limeshatangulia kwenda Segerea. Ndani ya muda mchache wakafanikiwa nao kuingia katika gereza kuu la Segerea. Kitendo cha kuingia wakakuta na basi nalo likiwa katika kuwashusha watuhumiwa na kuelekea rumande. Pale pale polisi mmoja akamfuata dereva wa basi pamoja na wale maofisa wengine wa polisi. Akawaoneshea kikaratasi kidogo kutoka kwa mkuu wao. Wakamuachia Stan. Walimshusha Stan katika basi lile nakumhamisha katika defender yao chini ya uangalizi mkali. Defender ikaondoka kwa spidi zote lakini kitendo cha kufika maeneo ya Ilala bungoni walistaajabu kukutana na foleni kubwa ya magari. Haraka waliokuwa nayo ikawabidi kupita njia ya upenyo. Njia ya shotikati. Wakapita shotikati ambayo wangeweza kutokea Amana hospitali halafu ndio waingie Ilala boma walipokuwa wakielekea. Umati mkubwa wa wananchi wenye hasira kali waliokuwa katika maandamano walikutana nao. Wananchi wale waliacha magari mengine binafsi yaliokuwa yamepita shotikati nakudili na lile defender la polisi. Walirushia mawe na kuanza kuwapiga mmoja baada ya mwingine kila aliyetoka katika ile defender kwa kutumia mawe na nondo nene. Baaada ya wote kutoka katika ile defender ndipo na Stan akapata nguvu ya kutoroka mule ndani ya gari kwasababu alikuwa amebaki peke yake tu. Hakupigwa mawe na raia kutokana na kuonekana na pingu mikononi.
Taarifa juu ya kutokea vurugu nakusababisha ile defender kuwa nyang’anyang’a na mapolisi kupoteza ufahamu kwa kupigwa na mawe na nondo ndio iliyomchanganya sana kamanda wa kikosi,Rafaeli. Alishajua atakuwa moja kwa moja ameshampoteza Stan na kesi itakuwa ni kama imeshakwisha. Alichokifanya alichukuwa gari yake binafsi nakutoka mwendo kasi mpaka maeneo ya Ilala vurugu zilipokuwa zimetokea. Alipofika, alikuta tayari mapolisi walikuwa wameshasambaratisha ule umati kwa kuwatupia mabomu ya machozi. Akashuka ndani ya gari lake nakuelekea eneo la mbele kidogo walipokuwa mapolisi wengine wakijadiliana. Akawaweka kati nakuongelea swala la Stan alipotorokea. Wakiwa katika maongezai mara yule kamanda akageuza kichwa kuangalia katika gari lake. Taharuki!!
Stan pamoja na yule mzee walikuwa wameingia katika gari ya Rafael. Maskini hawakuwa wakijua kama ni gari binafsi la kamanda mkuu wa kikosi,Rafael.
********
Watuhumiwa wa kesi mbali mbali walijikusanya pamoja ndani ya gereza kuu la Segerea. Hawakuwa wamehukumiwa kesi bali walikuwa katika kusubiri siku zao za kusomewa mashitaka. Waliwekwa kwa pamoja katika chumba kubwa. Baba Devotha alipoingia tu mule ndani alionekana ni kama Shujaa wao. Wale watuhumiwa wengine aliokuwa ametoka nao katika kituo kikuu cha Kimara walishaona cheche zake kidogo alizotaka kumfanyia Stan. Walipoingizwa tu ndani ya kile chumba ambacho kilikuwa na giza na uwazi mdogo sana uliokuwa ukipitisha mwanga kutoka katika kidirisha kidogo kilichokuwa juu kabisa kama kile kituo cha kimara. Baadhi ya watuhumiwa walimfuata kwa ukaribu.
“Sasa mzee vipi Kakakumega sijui!!, Hatuendi tena? Ndio muda huu tusichelewe mwenzako nakabiliwa na kesi kubwa sana nitafungwa tu na sina uwezo!!” Aliongea kijana wa makamo aliokuwa amejazia mwili wake.
“Hata mimi nina kesi kubwa sana na kwetu masikini na walioshikilia usukani ndio wenye nazo nashindwa hata nifanye nini, kama uko kakakumega mnakosema hakuna kiingilio tupeleke tu” Aliropoka mtu mwingine upande wa pili.
Wote wakamzunguka baba Devotha. Alikuwa tuli akicheka na moyo wake. Aliwacheka pasipo wao kujijua kwani alikuwa ni kama akihesabu kafara atakazoenda nazo Kakamega.
“Wangapi mnataka niende na nyinyi Kakamega?” Aliongea baba Devotha.
Wote walinyoosha mikono. Walikuwa ni zaidi ya kumi na nane waliokuwa wakimtaka baba Devotha awatoroshe kuelekea huko Kakamega.
Mikono yao haikuwa na pingu kutokana na kufunguliwa walipoingizwa ndani tu. Mbwembwe!! Baba Devotha akafanya kama alivyokuwa akifanya awali alipokuwa katika kituo kikubwa cha polisi cha Kimara. Safari hii alibadilisha kidogo sana.
“Nani ameingia na wembe humu ndani?” Aliuliza baba Devotha.
Watuhumiwa watatu kati yao kila mmoja alikuwa ameingia na wembe. Walimsogezea baba Devotha haraka haraka. Akaichomoa ile hirizi yake katika pindo la suruali yake na kisha akaichana ile hirizi. Kilichotokea baaada ya hapo ni mwanga mkali sana ukawamulika wote kutoka katika kile kihirizi. Baba Devotha akachukuwa kile kiwembe tena.
“Kila mmoja anipe mkono wake wa upande wa kulia hapa” Aliongea baba Devotha uku akitokwa na macho kwa kuangalia pande zote.
Hakuna hata mmoja aliyetamani kubaki mule rumande. Wote walimsogezea baba Devotha mikono yao. Akawachanja kila mmoja upande wa kulia wa mkono nyuma ya kiganja. Damu hazikumtoka hata mmoja kutokana na kile kiwembe kukigusisha na ile hirizi. Akachukua zile chembe chembe za unga kutoka katika ile hirizi kwa kutumia kile kiwembe kisha akawadumbukiza wale watuhumiwa kila mmoja eneo la mkono aliokuwa amewakata. Aliwafanyia karibia wote. Ukimya wa hali ya juu ukatanda juu ya kumsikiliza baba Devotha kitakachofuata.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mnaziona hizi kona za hili jumba?” Aliongea baba Devotha.
“Ndiiooo” Waliitika wote kwa pamoja.
“Kila mmoja ataelekea kona kwa mmoja mmoja na ukifika katika kona tu utanyoosha mkono niliouchanja nakuuwekea dawa moja kwa moja utakuwa umetokea Kakamega. Karibuni sana Kakamega kwa wale wote waliochanjwa na mimi” Alimaliza kuongea baba Devotha.
Vurugu za kila mmoja kung’ang’ania kwenda katika kona zilianza. Walizidiana nguvu na hata wengine kutishiana kupigana na kutukanana. Kila mmoja aliona kama anaachwa. Mikono yao ilikuwa na nguvu za ajabu sana kila walipofika kona ya ukuta wakinyoosha tu ile mikono wote walijikuta kuyeyeyuka papo hapo. Idadi ya watuhumiwa takribani ishirini ikawa imeshayeyuka na baba Devotha akiwemo kwa kupitia kona ya ule ule ukuta.
*************
Dalili za mawingu kujiweka karibu zilimaanisha kuwa mvua haikuwa mbali kushuka katika maeneo ya Kijiji cha Kakamega. Wale kinamama ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kutafuta maji asubuhi na mapema kupitia katika majani mapana yale yatambaayo chinichini walikuwa wakifanya hivyo. Ni Sara pekee alioonekana kulemewa na kazi hii kuotokana na kutokuona kwakwe. Upofu wa kutokuuona afanyacho mbele yake ulimfanya kutumia hisia kali katika kufanya kazi yake aliyopewa ya kukusanya maji kutoka katika majani mapana. Ule mchezo wa kina Kakamega kumtolea macho mara kwa mara kutokana na upofu wake uliachwa. Ni Thiwa ndio aliingilia kati nakuwaaambia kuwa Sara ni binadamu wa kawaida wasimshangae wala kumchukulia tofauti. Thiwa alimchukulia Sara kama binti yake. Sara akapendeka kwa baba asiyemuona kwa sura kutokana na ule upofu. Zile dawa za kikakamega zikawa zimeuathiri ubongo wake. Sara akajiona ana baba na hata yale yote yaliotokea nyuma akawa hayafahamu yote kutokana na kupotezwa akili na kujazwa akili za Kikakamega. Akili za kuyaishi maisha ya kikakamega.
“Mama nahisi kama kuna kitu kinakuja kwa mshindo?” Aliongea Sara akimwambia mama wa jirani yake mwanakakamega mwenzake.
“Ndio mwanangu hiyo ni dalili njema sana kwetu wala usiogope ni Neema hizo zinakuja, umesikia upande ule wa shimo la kafara sauti ya vicheko?”
“Ndio mama naisikia mpaka sasa”
“mungu wetu huyo ameshahisi kafara kubwa inakuja na mara nyingi ukisikia vicheko kutoka upande wa kule aishipo mungu wetu ujue kuna kafara zinaletwa”
“Sasa mama huyo nani anayeleta hizo kafara sasa hivi?”
“Sijajua ila hapa Kakamega mwanangu wapo wengi waishio makwao huko mijini lakini nguvu zote wanazipata hapa na kila wanavyoleta kafara mungu wetu akishiba tu basi huwapatia Baraka kubwa sana ya kuwaongezea nguvu mara mbili na pia kijiji chetu kinafurika wanyama tunapata kuishi kwa kula nyama hizo.”
“Mama upofu huu unanipa shida sana maishani mwangu, nateseka sana naumia sana unaweza kunisaidia kumwambia mungu wetu?” Aliongea Sara.
“Sara! Sara! hilo linawezekana wewe tayari unaongozwa kwa hisia na unachotakiwa kukifanya leo jioni tutakwenda mimi na wewe tu katika jiwe la kafara kuongea na mungu halafu akupe njia ya wewe kuweza kufunguliwa upofu”
“Lakini mama!!..
“Lakini nini?”
“Mama mimi nilitolewa kabisa macho yote nikashonwa, sina jicho hata moja. Yote yalishaharibika yakatolewa nakutupwa”
“Kwa mungu wetu hashindwi kitu tutakwenda akueleze cha kufanya sawa Sara?”
“Sawa mama..”
Sara akiwa bado katika maongezi na yule mama. Kile kishindo walichokuwa wakikisikia kikaongezeka mara mbili yake. Ikawa ni mshindo haswa!!
Upepo mkali ukawapuliza wakina Sara. wakawahi kujishika eneo la siri kulipokuwa kumejisitiri kwa majani makavu. Upepo ukapuliza kwa muda kisha ukaacha.
Vijana takribani kumi na nane walikuwa wametanda mbele. Walikuwa katika mavazi ya nguo za kawaida. Walikuwa wameongozwa na baba Devotha.
“Karibuni Kakamega! kwenye kila sifa ya kila kitu, maisha mepesi na rahisi.” Aliongea baba Devotha akiwaambia wale vijana aliokuja nao.
“Ndio hapa Kakamega kwani?” Aliropoka mmoja kati ya wale vijana.
“Naam!! hapa ndio Kakamega, hamuwezi kushikwa tena maishani mwenu!” Aliongea baba Devotha akiwaondoa woga.
Yule mama na Sara pamoja na wasichana wote waliokuwa wakitafuta maji katika majani mapana baada ya kuziona zile sura wote walijikusanya pamoja na kurudi kwenye makazi yao. Walishajua nini kinafuatia baada ya baba Devotha kuwafikisha wale vijana. Mioyo yao wale wasichana walifurahia kupata maji kwa wingi na mahitaji kutoka kwa mungu wao. Walichekelea kimoyo kafara kubwa iliokuwa imeletwa na baba Devotha.
“Cecy?” aliita baba Devotha akimuita yule mama aliokuwa akiondoka na Sara.
“Abee?”
“Huyo binti ni wa kwetu? Sura hii niliiacha kule mjini?”
“Ndio aliletwa juzi hapa, aliletwa na Devotha”
“Nani alimleta? si mlemavu huyo? na imekuwaje mko naye mpaka sasa?”
“Ni story ndefu nendeni kwanza kwa mungu halafu mkirudi nitakwambia yote na kama sio mimi atakwambia Thiwa usiwe na shaka!”
Maneno yale yalimuweka baba Devotha njia panda. Hakujielewa!! Aliijua wazi sheria ya kuleta mtu mlemavu katika msitu wa kakamega. Aliijua kabisa adhabu yake ni kuuwawa.
“Inamaana Devotha wangu watakuwa wamemuua? hapana wangeniambia na mbona binti bado yupo?”” Alijiuliza Baba Devotha na kujijibu mwenyewe.
Taarifa juu ya baba Devotha kushuka na kafara zilitawala kijiji chote cha kinakakamega. Vijana karibu wote waliokuwa wakitafuta wanyama kwa ajili ya kujipatia nyama pasipo mafanikio walikuwa wameshakusanyika wakiwazingira wale vijana waliokuwa wameletwa na baba Devotha. Walikuwa wameshikilia mikuki yao kama wafanyavyo.
“Mzee vipi salama kweli kijiji hiki?” Aliropoka mmoja wa watu waliokuja na baba Devotha.
“Hakuna usalama hapa!!” Alifoka baba Devotha
Akili ya baba Devotha haikuwa imekaa sawa kabisa. Ilikuwa moja kwa moja kwa mtoto wake Devotha. Alimpenda sana kutokana na kuwa naye huyo huyo mmoja katika maisha yake. Aliachana na wale watu aliowaleta nakuongoza moja kwa moja mpaka katika nyumba nyumba waishizo Kakamega kwa lengo la kuiona sura ya mtoto wake Devotha. Wale vijana aliowaacha pale walitaka kumfuata nyuma nyuma lakini tayari walikuwa mbele ya mishale yenye sumu kali ya Kakamega.
“Haiwezekani, Tumekuja naye atuache hapa, wewe mzee unakwenda wapi sasa? mimi nitakufuata tu kumbuka ahadi yetu kule ulivyotuambia kabla hatujaja huku?” aliongea yule kijana kwa hasira kali.
Ukubwa wa mwili wake uliojijenga ulimfanya kujiamini sana lakini mbele ya mishale ya kina Kakamega ulimfanya kuwa mpole. Mmoja wa kina Kakamega alishatelezwa na mshale wake nakumpata yule kijana aliyetaka kumfuata baba Devotha kifuani mwake. Kifua kilichokuwa kimetuna kwa kubeba chuma. Akadongoka mpaka chini nakutapatapa hali iliowafanya wale wenzake wote waliokuja na baba Devotha kuingiwa na woga. Wakawa wapole, Kimya kikatawala!!
Kama kawaida ya Kakamega. Walichuma kambakamba za miti katika msitu ule nakuwafunga mmoja baada ya mwingine na baada ya hapo Safari ya kuelekea katika jiwe la kutolea kafara ikaanza. Hakukuwa na mbishi hata mmoja aliojitokeza kutokana na mwenzao kuuliwa na mshale wenye sumu pale. Wote walihisi huenda wanapelekwa himaya kuu ya kakamega alipoelekea baba Devotha lakini haikuwa hivyo. Walijikuta kwenye kabonde kadogo juu kukiwa na jiwe kubwa sana. Kakamega wakawakokota mmoja baada ya mwingine mpaka kwenye kamlima lilipokuwa lile jiwe la kutolea kafara. mungu wao akaisikia ile kafara kwa mara nyingine ikiwa karibu yake. Alishaijua imeletwa na nani kutokana nakutoa ishara ya kucheka tangu mwanzo kuwa kuna kafara inakuja.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wale vijana wote wakadumbukizwa katika jiwe la kutolea kafara. Walikuwa ni wabishi sana lakini kuna baadhi walijikuta wakipigwa mishale na kakamega na wengine wakidumbukia wenyewe pasipo kujitambua. Msitu ukawameza! wakaisha. mungu wao akatoa cheko kubwa tena kumaaanisha ameridhika waende tu porini wanyama wapo wengi sana wakatafute mlo.
***********
Bado kamanda wa kikosi alikuwa akiyatoa macho yake katika gari lake. Hakuweza kujua kiurahisi ni kina nani wapo katika gari lake.
“Mkuu vipi mbona tena unahamaki pembeni?” aliongea mmoja wa kamanda.
“Washenzi wamejileta wenyewe” aliongea kamanda wa kikosi Rafael.
Akili yake ilikuwa imeshanasa tukio la mbele yake. Aliiona sura ya Stan akiwa amelowa jasho akiwa siti ya mbele ya gari lake binafsi. Akaachana na wale maaskari na kuongoza moja kwa moja mpaka eneo walipo wakina Stan. Kabla hajawafikia tu rundo la vijana wale waliosumbua mtaa kwa maandamano wakiwa mikononi na mawe pamoja na nondo walitokea kona kwa fujo zote.
Polisi mmoja alishawaona akamuwahi kamanda wake wa kikosi,Rafael. Akamshika mkono kwa kumkinga asiweze kuendelea kwa kumuwekea ulinzi. Rafael hakuweza kuwaona zaidi ya akili yake yote kuielekeza kwa Stan. Aliona kama polisi mwenzake anamzuia kumfuata Stan.
“Niache, Niacheni vipi tena, Pumbavu!!” Aliongea Rafael kwa hasira akijigeuza kichwa.
Tayari yule askari aliokuwa amemkinga Rafael alikuwa amedondokewa na nondo kubwa iliorushwa na wale vijana waliokuwa wakiandamana. Waliokuwa na hasira kali na mapolisi kwa kitendo chao cha kuwalea wahindi wa mtaa wa Ilala na pili kuwachanganya wenzao kwa kuwatupia mabomu ya machozi. Waliona mapolisi wana makosa makubwa sana ya kutowasikiliza matakwa yao.
Mapolisi karibia watatu waliokuwa wakiongea muda si mrefu na kamanda wa kikosi Rafaeli, walikuwa chini ya ulinzi na vijana wa mtaa. Walikuwa wamewashikiliwa kama vile majeruhi wa ajali. Walionesha kuchoka hawajiwezi kwa lolote.
Muda wote Stan na yule mzee walikuwa wakifuatilia lile tukio. Waliona ni kama sinema kutokana na kukata tamaa baada ya kumuona Rafaeli akiwafuata kisha kwa ghafla wakatokea vijana waliokuwa na hasira kali na kuwakamata.
“Amini Stan Mungu yu pamoja nasi! hakika bwana ametenda miujiza mbele yetu mwanangu Stan” Aliongea yule mzee akitazamana na Stan wakiwa bado ndani ya ile gari ya Rafael.
“Tushuke tu mzee hapa hapatufai tena!!. Tuondoke hata kwa mguu tutafika Mbezi, njia za mkato zipo nyingi sana?” Aliongea Stan.
Alikuwa ni kama aliyekata tamaa. Aliona muda wowote mambo yanaweza kuwaendea kombo. Wakiwa katika kutoka ndani ya ile gari ya Rafael mara mchungaji John na yeye akawa ameshatokea upande wao. Mzee akaonesha tabasamu nakuingia katika gari ya mchungaji John hali iliowafanya wale vijana watata wa mtaa wasiwafanye kitu chochote kutokana na kuwa katika nguo za kiraia pia kina Stan walionekana kabisa ni wananchi wa kawaida. hawakuwa polisi.
Kamanda Rafael alibaki akiwaangalia kwa hasira zote. hakuwa na jinsi ya kutoka katika ule umati wa vijana wa mtaani wenye hasira kali wakiwa na nondo nene wengine fimbo wengine mawe makubwa. Alijiona ni kama jambazi sugu likiwa chini ya ulinzi.
“Nitawapata tu nimeshawaona walioondoka nao” Aliongea Rafael kimoyo moyo na kwa uchungu baada ya mchungaji John kuondoka na Stan akiwa pamoja na yule mzee.
“Wote hawa ni wa kuwaburuza tu mtaa wote waone uozo uliofanywa na hawa wenzao wakuporomosha mijumba nakutuondoa pia kuziba uwanja wa michezo kule kona ya Chabasi. Hakuna kumuonea hata mmoja huruma hapa. Hawa ndio wauzaji wa nchi. Na hii ni komesha yao kwa wenzao” Aliongea kijana mmoja kiongozi wao wale waandamaji wenye hasira kali.
Waliwashika wale askari wote sare zao za kipolisi wakiongozwa na kamanda wao mkuu Rafael nakuanza kuwaburuta chini chini kwa kuwatembeza mitaani. Walichubuka sana kutokana na ile barabara kutokuwa na lami. Kokoto walizokuwa wakisalimiana nazo zilitosha kuwatakatisha ngozi zao. Walipokuwa wabishi walijikuta wakipigiliwa na nondo nene pamoja na fimbo zile za mkonge!
********
“Leta mafuta ya taa, Side lete tairi pale lile kubwa!” Aliongea mmoja ya waandamaji aliyeonekana kuwa mtata.
“Ndio hawa wakuchoma moto maana ni sawa na wezi tu hawa!!, hawatufai na hawana utetezi wowote juu ya mali zetu” Aliropoka Side,mmoja wa waandamaji uku akienda kuchukua tairi kubwa la gari kwa madhumuni ya kuwachoma moto.
“Jamani, hivi tumekosa nini haswa? kwanini mnataka kuiaibisha serikali yetu na sisi wenyewe?” Aliongea kamanda Rafael.
“Kaa kimya boya wewe!!, Pumbavu!!” Side alimtuliza.
Umati ulizidi kuongezeka na kuwa mkubwa zaidi na zaidi wakizingira. Kila mmoja alitamani kuona kile kikosi cha polisi kikitekea kwa moto uku kikiwa ndani ya sare zake za polisi na kofia zake.
“Leta fasta fasta side tuwachome hivi hivi wakiwa bado hai ndio vizuri”
Side alikuwa ameshafika na tairi kubwa la trekta. Ule umati ulilipukwa kwa shangwe baada ya tairi kuingia maeneo yale. Muuza duka wa jirani akajitolea mafuta ya taa lita tatu. Yakawasili pale. Haraka haraka wakalifunika lile tairi kati kati ya wale mapolisi. Si kamanda Rafael wala wenzake wote wakawa wamefunikwa na lile tairi. Wakawa katikati ya lile tairi. Wale waandamaji wakaanza kupiga kelele za shangwe na miluzi uku mmoja wao akichukua kiberiti tayari kwa kuanza kuwachoma moto. Rafael nguvu za ajabu zikamjaa, nguvu za kikamanda. Akajifanya mjanja kukurupuka baada ya moto kuwashwa. Akainuka na moto ukiwa mgongoni mwake umeanza kumchoma. Hakuuweza umati uliokuwa umemzidia. Ule umati ulimsukuma mara mbili yake kumrudisha. Akadondokea tena lile tairi chini. Akafurukuta!!
“Hawatuwezi!!, Wapumbavu!!, Hawatuwezi!! Wamekwishaaa!! Wamekwishaaa!! Wamekwishaaaa!!” Waliimba waandamaji.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakiwa bado katika shangwe zao juu ya kuwaadhibu wale mapolisi kwa kuwateketeza kwa kutumia tairi la trekta mara defender kama sita za polisi zikiongozana na gari kama la zimamoto zikawasili pale. Umati ule ukatishia kutanda barabara kuwazuia. Ile gari iliodhaniwa ni zimamoto haikuwa hivyo. Ilikuwa ni gari spesho kwa bomba la kutolea maji ya kuwasha. Wale mapolisi wakayamwaga yale maji kwa kutanda. Wakaanzia pale chini kwa askari wenzao kwa kuwatuliza na yale maji japo yalikuwa yanawasha lakini walihitaji kuuzima ule moto ulioshika tairi la trekta. Wakauzima na kilichofuatia wale askari walishuka garini wote nakutanda eneo lote kwa kumwaga yale maji ya kuwasha na wengineo wakiwaokoa wenzao katika tairi la trekta. Si Side wala wale wenzake waliokuwa wakiongoza maandamano walisalimiana na ule muwasho wa maji makali. Maji yakateka eneo lote. Hawakuweza kukimbia zaidi ya kusimama nakujikuna muwasho wa yale maji makali. Upupu si Upupu na wala PiliPili si PiliPili. Yalikuwa yakiwasha hata zaidi ya mdudu washawasha. Yalikuwa ni mithili ya mgonjwa aliotoka na vipele vya joto au mwenye kuugua ugonjwa wa tetekuwanga mwili mzima tena nyakati za usiku au kwenye joto. Kiurahisi!! Simpleeeee!!
wale mapolisi walifanikiwa kuwazoa vijana wengi sana nakuwapakiza katika karandinga lao la polisi chini ya ulinzi mkali. Kamanda Rafael na wenzake wao walipakizwa gari jingine kwakuwa walikuwa katika hali mbaya zaidi. Hawakuwa wakiongea na baadhi yao walionekana kama kupoteza maisha kutokana na moto ule wa tairi kugusana na ngozi zao nakubabuka vibaya. Walikuwa hawatamaniki kwa weusi waliokuwa nao kuanzia sura mpaka miili yao. Hawakuweza kutoa neno hata moja zaidi ya kuwaachia wale mapolisi wafanye watakavyoweza.
***********
“Mwanangu yupo wapi? nawauliza nyie kina mama nimeambiwa mwanangu alikuja uku yupo wapi?” Aliuliza kwa ukali baba Devotha.
Alikuwa ameingia moja kwa moja upande wa kinamama wa Kakamega. Nyumba ya kiongozi wa kike wa Kakamega,Cesy.
“Habari juu ya mtoto wako nenda kwa Mkuu anajua yote!” Aliongea mmoja kati ya kina Kakamega wakike.
Hasira kali zilimzidia baba Devotha. Alishaapa na moyo wake kama uKakamega uishie leo lakini ni lazima amuone mwanaye na waachane na tabia za Kakamega.
Njia nzima kutoka kwenye nyumba za kinamama wa Kakamega mpaka kwenye nyumba za wanaume wakakamega baba Devotha alikuwa ni mtu wa kuongea mwenyewe na kujijibu. Punde akawa ameshafika.
“Thiwa!! Thiwa!! Thiwa!!” Aliita baba Devotha kwa hasira.
“Nani aniita hivyo? mimi ni Mkuu nani ananitaja jina langu hivyo tena likiwa kwa ukali?” Alihoji Thiwa akiwa kitandani kwake ametulia.
Baba Devotha alichofanya alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwa Thiwa.
“Thiwa mkuu!” Aliita baba Devotha.
“Naam!!” Aliitika Thiwa.
“Nipo hapa kujua mwanangu yupo wapi na yule binti kipofu alikuwa naye imekuwaje kuwepo katika himaya hii?” Alihoji baba Devotha.
“Kumbe wajua na washangazwa juu ya binti kipofu kuwepo Kakamega?”
“Ndio najua walemavu hawaruhusiwi ndani humu Kakamega”
“Sasa bora wajua na je kwanini hukumwambia mwanao kuwa hawapaswi?”
Baba Devotha akabaki akitafakari,mwenyewe kwa muda. Akashindwa kujibu swali.
“Lakini mimi nilikuwa nimete…
Kabla hajamalizia kuongea baba Devotha alishangaa Thiwa kumuwahi kwa neno.
“Lakini nini? unajua adhabu zake kama mtu akileta mlemavu hata kama akiwa ameshakufa? unajua adhabu kutoka kwa mungu wetu inakuwaje? zamani mungu wetu alikuwa akipokea hao walemavu lakini siku hizi kila kitu kimebadilika toka mimi niwe kiongozi wa huu msitu. mungu wetu hawataki tena walemavu ndani ya msitu huu wakipelekwa kwake.”
“Inamaana Thiwa mwanangu Devotha ndio mmeshampeleka kwa mungu mbadala wa yule binti kipofu?” Aling’aka baba Devotha akishika mikono kichwani kwa hasira na mchozi kumdondoka taratibu.
“Ndio! Devotha ameshamezwa na msitu! mungu wetu alishampokea na yule binti kipofu ndio atakuwa anaishi badala yake hivyo basi kama unamtaka mwanako bado yupo hai na hapa nilikuwa nafikiria hao kinakakamega wenzako waniletee macho ya mnyama niweze kumuwekea nakumjaza nguvu za Kakamega sambamba na akili tofauti utakuwa naye kama zamani. Amini mwanao yupo na ni yule kipofu.” Alimaliza kuongea Thiwa akishuka katika kitanda chake nakuchukuwa fimbo yake kubwa kwa kuinuka vizuri.
“Thiwa? Thiwa?” Aliita baba Devotha.
“Sihitaji tena maswali kutoka kwako na ninachohitaji kitendo. Safi kwa kafara uliyoleta leo nimeambiwa na wanaKakamega umempelekea mungu wetu watu wengi sana, safi subiri kujazwa nguvu na mungu wetu. Hongera sana” Aliongea Thiwa uku akijikokota na kutaka kutoka nje.
Bado hasira kali zilikuwa zimemganda baba Devotha. Kwikwi si Kwiki ilikuwa imembana. Alijihisi hasira kupitiliza katika ubongo wake.
“Liwalo na liwe lazima nimuue!!” Alijisemea kimoyo moyo baba Devotha.
Hakuwa ameridhika kabisa na maneno ya Thiwa. Kitendo cha kupelekwa mtoto wake Devotha katika shimo la kafara kilimuuama sana. Kila akifikiria kwa jinsi alivyokuwa akiishi na mwanaye Devotha maisha ya shida na mpaka Devotha amekuwa. Akifikiria ahadi alizomuahidi Devotha juu ya maisha yake. Akajuta na moyo wake kitendo cha kuishi na Stan. Akafikiria sana kitendo cha kulirudia lile gari miaka 15 iliyopita pale alipomuokota Stan akiwa mdogo sana. Gari ambalo baadaye lilihifadhiwa kituo cha polisi. Akaikumbuka sana siku ile alivyoirudia ile gari usiku na kukuta vitu kama ujiuji umetapakaa siti ya mbele. Akavuta picha kitendo cha kuushika ule uji uji ndio siku aliokutana na mauza uza yaliomfanya kujikuta yupo katika himaya ya Kakamega chini ya watu wa kakamega na ndio siku aliyomjua baba na mama wa Stan.
“Mwanangu Devotha si mmetupa kwa mungu wetu? si mmemtoa kafara siyo?” aliongea baba Devotha kwa hasira.
“Tushamsahau na nimekwambia sasa mwanako ni yule binti kipofu na kuanzia leo nitamtoboa nakumuwekea macho ya mnyama pori sambamba na nguvu zetu ili apate kuona. Na yule tutamwita Devotha nikishamuwekea.” alijibu Thiwa.
“Hapana, hapana kwa kweli!! kama ni hivyo ni bora tukakosa wote, Leo leo naenda kumchukuwa Stan nakuja kumuonesha wazazi wake wote. Na leo ataujua ukweli si kila siku mlikuwa mnanizuia asiweze kujua chochote kutokana nakujazwa nguvu nyingi za Mungu wao. Leo ndio namleta Kakamega.” Aliongea baba Devotha.
Hakuwa mtu mwenye kujitambua hata mara moja. Thiwa alinyamaza kimya akimwangalia kwani alitambua wazi ni hasira za kuondokewa na mwanawe ndizo zinamfanya kuropoka maneno ovyo. Alimwacha baba Devotha akiondoka zake kwa hasira.
Baada ya kufika kwa nje ya nyumba ya Thiwa, ndani ya msitu wa Kakamega. Baba Devotha alichukuwa majani chini kisha akaitoa ile hirizi yake katika pindo la suruali yake nakupikicha kwa nguvu zote na punde akaimeza ile hirizi na kilichofuatia alijikuta akiyeyuka pale pale msituni Kakamega na kwenda kumtafuta Stan alipo popote Dar es salaam.
*************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kitendo cha kujinusuru kutoka tu pale kwenye maandamano ambapo kamanda mkuu wa kikosi Rafael alikuwa akiongea na wenzake. Mchungaji John aliendesha gari lake kwa fujo zote akikatiza mitaaa. Njia nzima aliamini ni lazima mapolisi watawafuatilia kwa nyuma kutokana na kitendo cha Kamanda wa kikosi Rafael kuwaona wakiingia na kutoa maneno yale. Kitendo cha vijana wa mtaa wale waliokuwa wakiandamana kumshikilia Rafael na mapolisi wenzake kiliwapa ahueni Yule mzee na Stan wakatoroka kwa kuingia katika gari la mchungaji John.
“Mchungaji? Yaani bado siwezi kuamini kama tupo salama?” Aliongea yule mzee.
“Ndio yaani kwa hapa ashukuliwe Mwenyezi Mungu na sio mimi!! Yeye ndio ametenda miujiza na imetendeka ashukuliwe Bwana wa majeshi.” Aliongea Mchungaji John uku akiwa bado akiliendesha lile gari kwa mwendo kasi.
Muda wote Stan hakuweza hata kutoa neno moja kutokana na kushikwa na bumbuwazi kwa kilichotokea. Aliona ni kama tamthiliya tena zile za kifilipino zikiendelea mbele ya macho yake. Alijiona kama ni Steringi mkuu wa tamthiliya ya kifilipino. Alikuwa amewekwa siti ya nyuma kabisa. Mchungaji John na yule mzee wao walikuwa siti za mbele.
“Saasa hapa tunampeleka wapi huyu kijana wetu ?” Aliongea yule mzee.
“Kwanza inatakiwa tukatulize akili zetu juu ya kufanya maamuzi sahihi na nilipenda kwanza twende kwa haki kwani hata mwenyezi Mungu hapendi. Tukamtafute wakili wetu wa kujitegemea na tumkuelezee kila kitu naamini hakuna lishindikalo na kama gharama zote za kumlipa wakili mimi nitatoa” Aliongea mchungaji John kwa msisitizo.
Walienda mwendo mrefu na lengo lao kuu lilikuwa ni kurudi mpaka Mlandizi. Mchungaji John alifikiri sana juu ya kufuatiliwa na mapolisi endapo akiweka kambi kibaha kwake kutokana na kuonekana kituo kikuu pale Kiamara na pia kule Segerea. Aliona endapo polisi watafanya msako wa haraka atapatikana kiurahisi.
Sasa walikuwa katika foleni ubungo wakitokea Ilala. Stan muda wote alikuwa kashapitiwa na usingizi. Uchovu wa siku mbili mfululizo uliutesa sana mwili wake. Hakupata hata nafasi ya kupumzika vizuri. Aliuachia usingizi wa haja. Ndoto ikamvuta!! Akavutika!! Akaingiamo!!, Akaotamo!!
Walivuka foleni ya Ubungo na walikuwa wakielekea maeneo ya mbezi. Wakiwa katika mwendo wa kawaida tu mara mchungaji akahisi kitu ndani ya gari lake. Akafunga vioo vyote vya gari na kuendelea na mwendo wake wa kawaida. Bado moyo wake ulishajifungua, Moyo uliokuwa umetekaswa kwa imani ya bwana Yesu ulitikisika. Akasimamisha gari pembeni.
“Nini tena mchungaji? vipi?” Aliulizia yule mzee kwa mshangao.
Mchungaji John alijishika kifuani mwake akihema juu juu.
“Siko salama!! hapa hatuko salama nahisi kuna kitu kibaya mbeleni!! kunakitu kibaya kinatokea muda si mrefu…
Kabla hajamalizia kuongea mchungaji John alisikia mshindo wa haja juu ya gari lake na punde alishangaa kuiona sura ya baba Devotha ikiwa siti ya nyuma ya gari lake. Akiwa amemshikilia Stan kwa kumkaba shingoni. Stan aliyekuwa bado katika usingizi mzito. Baba Devotha akaitapika ile hirizi yake aliyokuwa ameimeza akiwa kule Kakamega. Ikatoka na utelezi akaishika kwa meno kisha akamsogezea Stan mdomoni mwake kwa lengo la kumlisha ile hirizi kwa kutumia mdomo. Stan akashtuka kutoka usingizini ile hirizi ipo mdomoni mwake.
“Stan?? Stan chukuwa ile biblia yako, ipo wapi?” Aliongea mchungaji John.
Mchungaji hakuwa na nguvu zaidi ya mwili wake wote kujikuta ukikosa nguvu kabisa ya kukemea wala viungo kufanya kazi yoyote.
Stan hakuwa na ujanja mbele ya mikono ya baba Devotha. Alichokifanya baba Devotha alichukuwa mkono wake mmoja na kudumbukiza ile hirizi kwa nguvu zote mdomoni mwa Stan. Yule mzee aliyekuwa pembeni ya Mchungaji John akataka kuingilia kati lakini alijikuta akipigwa kibao cha nguvu kutoka kwa baba Devotha. Akaungulia maumivu pembeni. Baba Devotha akiwa amamkaba Stan alimburuta mpaka kwenye kona ya lile gari alipotokea na kuyeyuka naye.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
************
MWISHO
0 comments:
Post a Comment