IMEANDIKWA NA : SAMWEL EMMANUEL
*********************************************************************************
Simulizi : Nifundishe Kunyamaza
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ilikuwa ni mishale ya saa mbili na robo za asubuhi nilipomuaga Nancy mke wangu na mama watoto wangu kwamba naenda kazini kwenye mihangaiko yangu ya kila siku,,niliamua kufanya hivyo kwa sababu niligundua ameingiwa na hofu furani ambayo sikuitambua."Ni sawa mume wangu lakini kwa nini leo usipumzike harafu kesho ndo unaenda? Tafadhari baba watoto wangu naomba kwa Leo upumzike! Kumbuka jana tu tumetoka Marekani kumfuata mwanetu Princes masomoni sasa najua bado umechoka na una uchovu kwa nini usipumzike kwa leo tu?".Aliongea mke wangu Nancy kwa sauti ambayo niliisikia kama imegonga karibu na ngoma ya masikio yangu.Nami bila hiyana kwa sababu ya upendo wangu kwake niliona bora nilimweleze tu ukweli halisi."Hayo unayoyasema mke wangu Nancy ni ya kweli kabisa lakini sina jishi mke wangu.Kumbuka Mimi ni mtumishi wa kawaida tu na si boss pale ofisini labda kama ile ofisi ingekuwa yangu ningeamua vyovyote,lakini kwa sasa siwezi,nikiwa mtoro mtoro pale ofisini watanifukuza kazi mke wangu.Tafadhari nakuomba uniruhusu niende nikayatetee maisha yetu kupitia hii kazi ,wewe usiwaze wala kunung'unika sana cha msingi niombee nifike huko salama na nirudi salama".Sasa nilipoyaongea hayo maneno nilimuona Nancy mke wangu amejiinamia chini,,nilipozipiga hatua na kuishika mikono yake laini na kumwinua niligundua alikuwa akitokwa na machozi,,sasa hayo machozi yalizidi kunichanganya sana nikawa najiuliza kwa nini mke wangu analia baada ya Mimi kumuaga kwamba naelekea kazini? Kwa nini asifurahi kwamba naenda kazini kufanya kazi na si kuzurura? Sikuweza kupata jibu mwafaka la kwa nini analia baada ya mimi kumwabia naenda kazini.Nilipomnyanyua nilimweka kifuani kwangu nikawa nambembeleza na kumfariji mpaka akanikubalia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa mume wangu Mimi nimekuruhusu uende huko kazini lakini chunga sana huko uendako maana moyoni mwangu kuna kitu kinanusumbua sana juu yako lakini Mimi sikielewi na sijui kina maana gani tu". Aliongea mke wangu Nancy huku akiyafuta taratibu matone ya machozi yaliyokuwa yakimtoka.Nilimpa moyo kwamba asihuzunike sana wala kuteteleka juu yangu maana Mimi ni mmoja wa wanaume wanayoijua thamani ya mwanamke dunia,kwa hiyo nilimwambia aniamini.Basi mke wangu Nancy akaniruhusu nikawa nazipiga hatua kuelekea mbele,,nilipoifikisha hatua ya tatu nilimsikia Nancy mke wangu akiniita.Nilipogeuka nilimuona akinikimbilia na aliponifikia alitabasamu kidogo akaniambia;
" Mume wangu nigeukie Mimi,ona tai yako ilivyokaa unataka ukaniaibishe huko uendako?".Baada ya hapo Nancy mke wangu aliitengeneza vizuri tai yake pamoja na kulisafisha vizuri begi langu dogo la mkononi.Baada ya hapo aliusogeza mdomo wake kwenye mdomo wangu akafumba macho na kunipiga busu ambalo lilinisisimua sana."By mume wangu Mungu akutangulie huko uendako".Mke wangu aliongea na kuunyanyua mkono wake kama ishara ya kuniaga kisha akasimama kuniangalia mpaka nilipotoweka kwenye mboni ya macho yake .
**************
Safari yangu ya kuelekea kazini ikapamba moto,,kwa vile niliona muda ukienda mbio sana niliongeza mwendo wa kutembea maana sikuwa na usafiri kwa siku hiyo."Daah! Kwa vile muda umeenda acha nipite njia za mkato ili niwahi kufika".Moyoni nilijisemea hayo nikaafikiana nayo na hapo hapo nikapita njia moja ya vichochorani nikaendelea na safari yangu.Hatua chache baada ya kuiacha hiyo njia nilipishana na wadada wawili waliokuwa wamevaa suruali nyeusi aina ya jinzi,,,walikuwa weupe kiasi na machoni mwao walivaa miwani za jua.Kwa vile Mimi nilikuwa na haraka sana,sikuweza hata kuwajulia hali bali niliwaacha tu nikawa naendelea na safari yangu.Sasa ile wanatembea kidogo tu kabla hawajaniacha hata hatua tano niliwaona wamesimama na kuanza kuniangalia,,sijakaa sawa Mara yule msichana aliyekuwa amevaa ramba nyekundu nikamsikia akiniongelesha.
"Imma mambo? Sasa Imma kwa nini tunapishana kama hatufahamiani vile? Eneway kwa vile una haraka sana wacha tukuache uende huko uendako lakini kiukweli wewe ni handsome japo ombi langu kwako umelipuuza lakini ipo siku tu". Alipoongea hivyo waliondoka na kutokomea na sikujua walikuwa wakielekea wapi,,sasa pamoja na yule binti kuniongelesha hivyo bado moyoni mwangu sikumwelewa kwamba alikuwa akimaanisha nini maana hata kumfahamu nilikuwa simfahamu.Basi hilo wazo lilizunguka kidogo tu akilini mwangu baadaye nikalipuuza na kuondoka zangu.
***********
Baada ya dakika kumi na tano na sekunde ya tatu kwa mjibu wa saa yangu ya mkononi nilianza kuingia maeneo ya kazini.Sasa kuna kitu ambacho kilianza kuusumbua moyo wangu,hicho kitu kilikuwa Mara mbili, kimoja kilikuwa kikiniambia nisiendelee kupiga hatua kuipanda ngazi ya kwanza kabla sijaingia ghorofa ya tatu zilipo ofisi zetu na kingine kiliniambia niendelee.Moyoni mwangu nikawa nadhani labda hayo ni mawazo tu ya kawaida kama yalivyo mawazo mengine.Kile kitu kilichokuwa kikiniambia nisiendelee nilikipinga vibaya mno nikazidi kuikaribia ngazi ya kwanza kabla sijaunyanyua mguu wangu wa kulia kuanza kuipanda.Baada ya kuifikia nilianza kuipanda huku nikiwa sifahamu chochote kile kilichokuwa kikiendelea mbele yangu wala nyuma yangu.Sasa bila Mimi kufahamu chochote kumbe nyuma yangu kulikuwa na watu ambao walikuwa wakinifuatia na Mimi sikujua walikuwa na malengo gani juu yangu.Kabla sijafika popote ghafla nikashtukia nimepigwa risasi begani ,nikiwa najibalaguza ni nini cha kufanya nikashtukia mguu wangu wa kushoto nao umepigwa risasi.Nguvu ziliniishia na hapo hapo nikadondoka hadi chini kabisa ya ile ngazi ya kwanza.
"Ahahahaaaa!!" Bwana Imma nadhani utakuwa unanikumbuka vizuri.Kama umenisahau Mimi naitwa Master Kill,Sasa sina muda wa kupoteza hapa ninachotaka ni wewe kunipa pesa zangu,na hapa kuna chaguo moja tu,utoe pesa ama ufe".Hiyo sauti niliisikia vizuri sana lakini sikuielewa maana akili zangu zilikuwa zimevurugika.Sasa kwa vile macho yangu nilikuwa nimeyafumba kwa maumivu ya risasi,niliyalazimisha kuyafumbua,,duuh! Nilijikuta nipo katikati ya jamaa saba waliokuwa wamevaa makoti meusi pamoja na miwani za jua.Nikiwa sijui hili wala lile ghafla nikasikia paaaaaaa!! Paaaa!!" Kuashiria kwamba ilikuwa ni milio ya risasi.Kwa vile hofu ilikuwa imenipanda fahamu zangu zote zikakatika nikawa naona sijui kama nipo wapi tu.Hivyo sikuelewa chochote.
**************
Mara nikakurupuka nakujikuta nipo wodini tena kitandani kabisa huku nikiwa nimetundikiwa dripu nyingi nyingi mikononi na miguuni.Pembeni yangu alikuwa amekaa Dada mmoja mrembo sana.
"Imma mambo?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huyo mrembo alinisalimia huku akiniangalia kwa macho ambayo hata Mimi sikuyaelewa kwa kweli.Ndani ya akili yangu nikawa napanga mafaili na kuyapangua."Huyu Dada aliyekaa hapa karibu na Mimi ni nani mbona Mimi simfahamu,amelijuaje jina langu ?".Hilo swali nilijiuliza kimya kimya na kulijibu Mimi mwenyewe japo majibu yake sikuwa na uhakika nayo ,sasa kwa akili yangu ya haraka haraka nikawa nafikiri labda huyu binti atakuwa ni yeye aliyeniokoa katika ile hatari iliyokuwa imenikumba.Niliona kuendelea kuwa kimya pasipo kuongea chochote niliona huo utakuwa ujinga ambao haujawahi kutokea,niliamua kuijibu salamu yake japo sikumtambua vizuri.
"Poa tu Dada yangu ila samahani kwa usumbufu,Dada kwa kweli sikufahamu na sifahamu hata hapa nimeletwa na nani". Huo ujasiri wa kuyaongea hayo sijui niliutoa wapi tu maana kwa maneno hayo nilihisi hata Mimi mwenyewe sikuyaelewa vizuri ." Bila samahani kaka Imma kwa kweli acha niuseme tu ukweli uliojificha ndani ya moyo wangu.Kwa jina Mimi naitwa Manka ni binti wa mzee Stanley na Nina kaa hapa hapa mjini".Binti alipoongea hivyo nilishtuka kidogo nikajisemea "Mr Stanley? Huyu si ni boss wangu anayemiliki makampuni tofauti tofauti hapa jijini Dar es salaam! Ina maana huyu ni bintiye au?". Hilo swali nilijiuliza lakini sikulipatia jibu la moja kwa moja kwa kipindi hicho,niliona labda niendelee kumsikiliza huenda akafunguka zaidi na zaidi." Imma najua utakuwa unajiuliza maswali mengi sana kuhusiana na Mimi huku kubwa zaidi likiwa ni lile la nimefika fikaje hapa? Na ni nani amenileta hapa!.Kiukweli ile siku unajiandaa kupanda ngazi kuingia ofisini na ukavamiwa na wale jamaa akiwemo Master Kill Mimi ndiye niliyechukua jukumu la kukuokoa zidi ya mikono ya wale jamaa,nilijitoa mhanga kukuokoa kwa kadri niwezavyo maana ndani ya moyo wangu hakuna ninaye msamini na kumheshimu kama wewe ".Manka aliongea kwa sauti ya chumbani.
*****************
Kumbe yule jamaa anayejiita Master kill pamoja na wenzake walikuwa wakipafahamu hadi nyumbani kwangu .Sasa walipoona wamenishindwa Mimi waliamua kwenda hadi nyumbani kwangu kumfanyia fujo mke wangu Nancy.Wakiwa na idadi yao ile ile waligonga lile geti la nyumba yangu walipoona hakuna anayewajali walilisukuma kwa nguvu wakaingia moja kwa moja hadi ndani ya hilo geti .Ile wanafika tu na kuyaangaza macho yao huku na huko walimuona mlinzi wangu Fred wakamteka na hawakuongea nae maneno mengi walimkaba na hapo hapo wakayapoteza maisha yake kwa kumchoma kisu.Waliuacha mwili wake ukiwa umetapakaa damu wakaanza kuzipiga hatua kuingia ndani ya nyumba yangu."Mh! Mbona kupo kimya sana kuna watu kweli humu ?" Master Kill aliliuliza hilo swali mbele ya wenzake,hata na wao hawakuweza kulipatia jibu ila walishauriana kidogo hatimaye wakaufikia mlango na kuanza kuugonga taratibu ,kumbuka kipindi hicho yalikuwa ni majira ya saa tisa na nusu za mida ya kuelekea jioni na mke wangu Nancy hakuwa anafahamu chochote kile kuhusiana na Mimi.Basi wale jamaa wakaendelea kuugonga ule mlango,dakika mbili baadaye alitoka Nancy na kuwakuta wamesimama karibu na mlango huku wakionekana kuwa wageni kabisa mbele ya Nancy.Maana walikuwa wamevaa makoti meusi na machoni mwao walivaa miwani ya jua hivyo kuwafanya wasijulikane kwa haraka.Nancy baada ya kuwaona alishtuka akawa anajiuliza maswali mengi sana ambayo hayakuwa na majibu.Sasa akiwa anatafakari namna ya kufanya ,Mara Master Kill akaanza kuongea,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Waoo! Mrembo uliyeumbika mithili ya malaika wa mbinguni,Leo nina furaha sana kukutana na wewe .Kwanza wewe ni mzuri sana yaani ungefaa uwe mke wangu kabisa,au wewe unaonaje? Kama vipi achana na Imma uolewe na Mimi ". Aliongea Master Kill kwa kujiamini sana.Sasa Nancy akawa anaingiwa na hofu akijiuliza hawa ni kina nani na wamjuaje mume wangu Imma wakati Mimi siwafahamu,kina nani hawa,mbona wanaonekana kama si watu wa kawaida!!.Aliona kuendelea kujiuliza kimya kimya hakutosaidia kitu;
" Nyie kina nani na mmekuja hapa kufanyaje?" Aliuliza Nancy kwa sauti ya uwoga.Master Kill alicheka kidogo tena kwa dharau na kusema,,"Ah! Kwa Sasa wewe upo chini ya mikono yangu unachotakiwa ni kukaa kimya tu na kunisikiliza Mimi ,kwanza Mimi ni mumeo kwa Sasa".Master Kill alipoongea hivyo aliipandisha jazba ya Nancy mke wangu,,Sasa kwa vile alikuwa ni mwanamke wa hasira sana aliamua kumjibu "Mke wako mama yako,nikome kama ulivyokoma kulinyonya titi la mama yako,nani mke wako hapa? Usinichefue,nitakuitia polisi Sasa hivi na hao vibaraka wako,sikufahamu na wewe hunifahu kwanza tokeni hapa nyumbani kwangu,tokaa". Nancy aliongea kwa hasira sana huku akihema juu juu." Ahahahaa!! Punguza jazba mrembo wangu,kwanza wewe ukikasirika unazidi kupendeza njoo unibusu basi maana natamani kulipokea busu lako".Ile anaongea hivyo,Master Kill,Nancy alimshukia akamzaba Kofi moja la shavuni akawa anaona maruweruwe.Nancy akawa anajitahidi kupambana na hao watu waharibifu kwa kadri awezavyo.Sasa huku ndani Prince akiwa anaangalia TV alishtuka kusikia kelele za ajabu nje,akaamua kutoka kwenda kushuhudia ni kitu gani kimetokea.Alipofika na kumkuta mama yake ameshikiliwa aliogopa sana akawa ana wakimbilia wale jamaa kwenda kujaribu kumwokoa,Sasa msaada wake haukusaidia chochote maana alikuwa ni kijana mdogo hivyo akaishia mikononi mwa jamaa moja lililokuwa na sura ya kibabe."Mwachieni mama yangu mnampeleka wapi huko mwachieniii".Prince alijitahidi kuipaza hiyo sauti lakini wala haikuwa na msaada wowote.Wale jamaa kwa sababu idadi yao ilikuwa kama saba hivi walimtweza nguvu Nancy jamaa wawili wakamkamata kwa nguvu wakawa wanampeleka moja kwa moja hadi chumbani,,Prince jamaa wengine waliendelea kumshikiria pale sebureni huku wakimtishia mtutu wa bastora,basi walimziba mdomoni asiweze kupiga kelele ,,kule chumbani Master Kill akiwa ndo mhusika mkuu aliwaamuru wamvue nguo haraka haraka Nancy ili wamfanyie mambo ya kipumbavu,,Nancy alijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini hazikufika popote,,basi Master Kill bila huruma aliamua kumbaka Nancy mke wangu bila hata ya kumkosea chochote.Alipomaliza yeye aliwaruhusu na wenzake wakawa wanafanya hivyo mpaka wakaridhika na kutoka.Sasa wakati wanatoka hawakutoka hivi hivi,Master Kill kama kiongozi wao aliwaamuru wachukue vitu vya thamani ndani ya nyumba yangu kama,Skleni,yaani flat screen na vifaa vyote pamoja na vifaa vya ukutani kama saa vyote wakavivunja vunja.Walipomaliza kuifanya hiyo kazi walitoka ndani ya geti wakapanda gari yao na kutokomea.
**************
Kwa upande wangu Mimi nikiwa bado nipo hospitalini pamoja na yule binti mtoto wa Mr Stanley maongezi yetu yaliendelea huku nikiwa sijui chochote kile kilichotokea nyumbani kwangu." Kwa hiyo Imma Mimi kama Mimi nilikubali kufa ili mradi niyatetee maisha yako.Nilipokuta umetekwa na hao watu nilichukua bastora zangu mbili nikaziseti na kuanza kumimina risasi kuelekea juu nikawakurupusha wakakimbia na kukuacha wewe ukiwa umepoteza fahamu.Nilikuchukua nikakuweka ndani ya gari yangu nikakuleta hapa hospitalini,kwa hiyo huo ndo ukweli halisia".Manka aliendelea kuongea,,Mimi nilimshukuru sana kwa msaada wake lakini nilimwambia angarau atoke pale kitandani akakae pembeni maana alikuwa amenisogelea sana kiasi kwamba tungekutwa na mtu yoyote yule angetuelewa vibaya sana,,basi tuliongea mambo mengi mwishowe tukamaliza na Mimi kwa vile afya yangu ilitengemaa jioni hiyo hiyo niliagwa nikawa nimeianza safari ya kurejea nyumbani kwangu.Sasa kutokana na ukaribu alioujenga Manka kwangu ambao Mimi niliuona kama urafiki tu wa kawaida alinisindikiza kwangu kwa kutumia gari yake hadi akanifikisha nje kabisa ya geti langu .
***************
Nilifika pale nikawa nabisha nje ya geti hilo lakini sikusikia dalili zozote za mtu kuja kunifungulia.Kwa tahadhari kubwa nililisukuma geti hilo nikaingia hadi ndani ,,duuh! Nilishtuka nilipoyaangaza macho yangu nakuona mwili wa Fred mlinzi wangu ukiwa umetapakaa damu na ilionekana kabisa amepoteza maisha,,wasiwasi ulinipanda zaidi nilipoangalia kulia kwangu nikakuta vifaa vyangu vimeharibiwa.Sasa nilianza kutetemeka,,nilitembea kwa kunyata hadi ndani ya nyumba yangu. Ile najiandaa tu kumwita Nancy mke wangu huku nikielekea chumbani nilipokelewa na michilizi ya damu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipoiona ile michirizi ya damu moyoni niliogopa sana nikawa nawaza kivingine kabisa maana sikutegemea kama ningekuja kukutana na tukio kama hilo nyumbani kwangu.Sikuweza kutambua ni kitu gani kimetokea Bali niliendelea kusimama tu pale mlangoni kama sanamu nisijue hata cha kufanya maana kama nikuogopa niliogopa sana mpaka kijasho chembamba kikawa kinanitoka makwapani ,usoni,na wakati mwingine kifuani.Basi kwa kujipa tu moyo niliona nimuite Nancy mke wangu labda angeniitikia,
"My sweet!,,Nancy mke wangu upo wapi?". Nilijaribu kuitoa hiyo sauti kumwita lakini sikupokelewa na sauti nyingine tofauti ya kupokelewa na ukimya tu.Nilijitahidi sana kumwita kwa kadri ya uwezo wangu lakini bado sikuambulia chochote.Wasiwasi ulizidi kuongezeka ndani ya moyo wangu na kunifanya nianze kutetemeka kwa uwoga.Sasa nilipoona mke wangu haniitikii nilijaribu kumwita Prince mwanangu maana nilijua tu na yeye atakuwemo humo ndani kwa sababu kipindi namuaga mke wangu kwamba nataka kwenda kazini alikuwepo.Nilipoanza kuipaza sauti yangu kumwita nilijikuta nikipigwa na butwaa Mara baada ya kugundua bado ukimya unaendelea kunipokea.Nilijipiga konde nikaona kuendelea kusimama pale mlangoni mithili ya sanamu niliona huo utakuwa ni ujinga.Nililisogeza pazia la mlangoni hapo hapo nikaunyanyua mguu wangu wa kushoto nikaingia hadi ndani ya hicho chumba,,,Lahaula nguvu ziniliniishia nikajikuta nikisimama wima kama zoba nisijue hata cha kuamua.Nancy mke wangu nilimkuta amedondoka chini huku akiwa ameilalia michirizi ya damu ambayo ilionekana kuwa mibichi kabisa.Nilimkimbilia nikaanza kulia kama mtoto mdogo aliyepokonywa ziwa la mama yake .
"Nancy....Nancy....Mke wanguu ,,amka mke wangu ! Kwa nini umelala mke wangu wakati Mimi mume wako nimerudi? Nancy mke wangu amkaaa!!.Usife kwanza mke wangu kwa sababu ukifa hata Mimi thamani na furaha ya kuendelea kuishi hapa duniani itatoweka,,,Please Nancy amkaaaa". Niliyaongea hayo maneno huku nikijaribu kumtikisa mke wangu kwa bidii sana lakini hakuamka maana tayari macho yake alikuwa ameshayafumba.Nililia sana nikajipa nguvu ambazo sikuzitambua zimetoka wapi nikakaa na kumkumbatia mke wangu bila ya kujali kwamba mwili wake ulikuwa umetapakaa damu.Nilimgusa maeneo ya kifuani pamoja na kumchunguza kwa makini nikagundua tayari Nancy kashaniacha peke yangu chini ya hii ardhi.Bila kujizuia nilijikuta nikiangua kilio cha nguvu sana nisiweze kuamini kabisa kama mke wangu wa maisha niliyekuwa nikimpenda kwa moyo wangu wote kashanikimbia na kuniacha.Furaha yangu yote ilitoweka na hamu ya kuendelea kuishi duniani nayo ikapotea nikaanza kuona huo ndo utakuwa mwisho wa maisha yangu maana sikumuona wa kuja kuliziba pengo la Nancy .Nililia sana nikawa najiuliza mengi ambayo sikuyapatia majibu kabisa.
********
Sasa wakati naendelea kutokwa na machozi huku nikiomboleza kifo cha mke wangu Nancy ,wazo moja liliniijia nikamweka kando mke wangu na hapo hapo nikawa namchunguza.Kumbe tumboni kwake alikuwa na jeraha kubwa sana lililonijulisha kwamba mke wangu alikuwa amechomwa na kisu.
"Why...why?? Nani amekuua mke wangu nani amekuua? Maskini mke wangu kumbe lile busu ulilonipa kipindi unaniaga kabla ya Mimi kwenda kazini kumbe lilikuwa la kuniaga? Maskini Mimi nitabaki na nani sasa hapa duniani?".
Niliyatoa hayo maneno kwa uchungu sana huku nikijilaumu ni kwa nini nilimuacha Nancy nikaenda kazini bila ya kukubali kubaki kumlinda.Sikuwa na jinsi lakini haki ya nani maumivu niliyoyapata pale hayakuwa na mfano.Mwanamke huyo nilimpenda sana na sikutarajiwa wala kufikiria kama angekuja kuaga dunia na kuniacha mapema mapema kiasi hiki.Basi huku nikilia kwa kwikwi nilijaribu kuyaangaza macho yangu huku na huko nikayaelekeza chini na hapo nikaona kijikaratasi kimoja kimekunjwa,,nilijivuta vuta nikakichukua na kuanza kukikunjua kabla sijakisoma.
***********
" Imma mume wangu najua nimekuacha katika kipindi ambacho hukukitarajia lakini nakuomba uupige konde moyo wako.Najua utakuwa na msululu mrefu sana wa maswali ya kwa nini mke wangu amekufa mapema kiasi hiki,,Jibu la hilo swali ni gumu sana kulipata lakini nakupa moyo tu mume wangu uvumilie kwa hiki kipindi kigumu nilichokuachia.Nimeyachukua maamuzi magumu sana ya kujitoa uhai wangu Mimi pamoja na Prince mtoto wetu baada ya kugundua heshima yangu kama mwanamke imetoweka.Nadhani majibu utakuwa nayo ,nisingeendelea kuishi kwa amani hapa duniani kwa sababu moyo wangu ulitiwa doa ambalo isingekuwa rahisi kuliondoa.Nilikupenda sana mume wangu na nilitamani kuendelea kuishi na wewe maana sikuwa na samani tena hivyo sina budi tena kukuaga na kukutupia mkono wa kwaheri.Uliniingiza ndani ya ulimwengu wa mapenzi kwa Mara ya kwanza kabisa,lakini utu wangu haupo tena mume wangu.Ninachosema ni kwa heri ya kuonana japo nimekuachia kidonda kikubwa ndani ya moyo wako .Nisamehe tu mume wangu pia na Mungu anisamehe maana nimemkosea,,Nimejiua kwa kisu na mwanangu Prince nimemuua kwa sumu,acha tuondoke tu labda huko tuendako tutakuja kuonana tena ,,Sitamsahau aliyenifanyia huu unyama ambaye si mwingine Bali ni Master Kill maana ndiye aliyenibaka na kunisababisha Mimi niyaamue haya.Baki salama mume wangu.
Ni Mimi Mkeo Nancy Alfred ".CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Usema ukweli Mara baada ya kumaliza kuisoma hiyo barua,nilijikuta nguvu zikipungua kwa kasi sana ndani ya mwili wangu.Huku nikitetemeka niliyanyanyua macho yangu hadi pale kitandani nikamuona mwanangu Prince amenyooka pale kitandani huku akiwa hana dalili yoyote ya kuwa hai.Nilijongea na kumfuata hapo hapo nikaangua tena kilio cha nguvu sana huku nikiyaacha machozi yaendelee kukirowanisha kifua changu.
Sikulitambua kosa langu lililomfanya huyu binadamu anayejiita Master Kill kuendelea kunifanyia vitendo kama hivi vya kikatiri bila hata ya kumwogopa Mungu.Huku nikitetemeka nilimbeba juu juu Prince nikatoka nae sebuleni ,na kwa Mara hii nilitamani hadi Mimi mwenyewe nife .Maana sikuona umhimu wowote wa kuendelea kuishi.
*Nancy....Nancy....Amkaaaaaa!!!"
Niliitia kiushahidi tu lakini hali halisia ndani ya moyo wangu niliitambua maana hata ningefanyaje au ningeliaje bado kamwe nisingeubadirisha huo ukweli.Nancy nishampoteza na mwanangu pia nimempoteza,japo niliumia sana lakini nilijikaza kiume nikaamua kuyapangusa machozi yote yaliyokuwa yakinitoka,wote walionifanyia hivyo kwa kumdharirisha mke wangu niliwasamehe na niliwaombea kwa Mungu awasamehe.Nilijiongelesha maneno mengi sana lakini yote nikajikuta yakikizunguka kichwa changu na kupotea ghafla tena papo kwa hapo pasipo kujua hata yalikoelekea.Ndugu yangu unayeisoma makala yangu hii omba sana usitokewe na mambo kama haya tena kwa kushtukizwa pasipo kuwa na habari kwamba yangekutokea unaweza kutamani na wewe ufe tena kwa wakati huo huo.Hebu vuta picha mkeo amekuaga asubuhi na wewe umemuaga kwamba unaenda kazini kupambana katika ridhiki yako ya kila siku na wewe ukawa na imani kwamba masaa kumi au tisa siyo mengi,mke wangu nitamkuta salama harafu ukarudi jioni nakumkuta ameaga dunia tena kwa hali ya kushtusha kama ile ungetoa maamuzi gani? Bila shaka hata wewe mwenyewe jibu la hili swali unalo tena linazunguka sana ndani ya kichwa chako.Bila kuwa na moyo wa kiume au kuupiga konde moyo wako unaweza kudondoka na kufariki hapo hapo,,,Hayo yaliyonikuta Mimi yaani hapa nilipo hadi mikono yangu ninavyokuandikia hivi huweza amini kabisa kama ningekuambia inatetemeka mithili ya mtu aliyevamiwa na baridi Kali ndani ya maji marefu ya bahari.Matumaini yangu na furaha yangu imebaki ya kuunga unga tu na sijui nitamuona nani tu wa kuja kuliziba pengo la Nancy aliyeondoka na kuniacha peke yangu.Hata mwanangu nae wa kiume Prince niliyekuwa nikimpangia malengo mengi zile siku za wahenga jama tayari na yeye kashanikimbia.Ila amebaki Queen mwanangu wa kike aliyeko masomoni nchini Marekani labda huyo atakuwa ndo kifuta machozi changu ,lakini je angenielewaje iwapo nitamwambia kwamba mama yake kashaondoka duniani tena kwa kifo kama kile ?.Kwa kweli hilo swali liliniijia sana kichwani mwangu lakini sikuweza kulipatia jibu kabisa,nikifikiria kwa kijishi gani mambo yatakayo tokea mh! Sijui yaani...Sijui.Basi Nilimuweka kitandani Nancy mke wangu pamoja na Prince nikawa nimepiga magoti kumwomba Mungu anisaidie na anitie nguvu kwa hili gumu lililonipata.Huku nikiwa nimeinua mikono yangu juu na macho yangu nimeyanyanyua juu nilimuomba sana Mungu anisaidie maana kwa akili yangu kweli hata ningefanyaje nisingeweza hata kidogo .Sasa wakati naendelea kufanya hivyo huku nikiwa sitambui hili wala lile ghafla begani kwangu nikahisi nimeguswa na mtu .
***********
Upande mwingine kule ngomeni kwa mtu katiri na muuaji,Master Kill kilisikika kicheko cha dharau sana ambacho hakikueleweka hata kimefurahishwa na nini au kimechekwa kikiwa na maana gani.
"Hahahahaha....Ahahahaha,,,Kipanga wewe ni kiboko yaani saluti kwako mjomba unafaa kuwa bodigadi wangu.Siku ile tunaivamia nyumba ya huyu jamaa Imma yaani ulinifurahisha zaidi ya sana". Master Kill aliongea kidogo akasitisha na kuvuta sigara yake iliyokuwa haitoki mdomoni daima." Kivipi boss mbona umeongea na kuniacha njia panda?" Aliuliza Kipanga huku akiliweka vizuri koti lake la kijambazi lililokuwa refu sana."Namaanisha kwamba ,siku ile nambaka yule mwanamke mrembo na mtamu kama asali ulimshikilia vizuri sana kijana wangu na unastahili tuzo.Sasa Mimi nasema hivi,kuanzia Leo na kuendelea wewe utakuwa mkuu msaidizi wa hii ngome ya mheshiwima Master Kill".Master Kill alipozungumza hivyo alimshangaza sana Kipanga pamoja na kuwashangaza wale wenzake.
"What?.Unayoyasema ni ya kweli boss wangu??".
************
Kwa upande wangu bado sintofahamu isiyoeleweka iliendelea kuutesa moyo wangu.Sasa baada ya kugundua begani kwangu hususani katika mkono wangu wa kulia nimeshikwa,bila hiyana au wasiwasi niligeuka,ile nayainua tu macho yangu ili nibaini ni nani alikuwa ameingia ndani na kunigusa bega langu .Nikakutana na sura nyororo ya binti aliyeniokoa mbele ya mikono hatari,ya master Kill na vijana wake.Huyu hakuwa mwingine Bali alikuwa ni Manka,binti pekee wa boss wangu Mr Stanley. Sasa Mara baada ya kumuona tu amesimama mbele yangu huku akiwa haamini kilichotokea,Mimi machungu yaliniijia upya nikaanza tena kudondokwa na machozi.Manka alistaajabu sana akawa anatapa tapa huku na huko mwisho akanisogelea na kuninyanyua pale chini nilipokuwa nimejiinamia akaanza kunibembeleza huku na yeye machozi yakianza kumlenga lenga.Alichukua kitambaa chake cheupe akawa anayafuta machozi yangu huku akiendelea kunibembeleza.Alinipa moyo ambao sijawahi kupewa na rafiki yangu yeyote na akanihakikishia atakuwa bega kwa bega katika gumu hilo lililonipata.
" Imma nyamaza usilie ,ya dunia ndivyo yalivyo,Mungu siku zote huwa hamtupi mja wake .Leo umempoteza kipenzi chako kesho ataibuka mwingine wakuyapangusa hayo machozi machoni mwako.Usilie tafadhari Mimi Niko pamoja na wewe nitakufariji".Baada ya Manka kumaliza kuyaongea hayo alitoa simu yake akaanza kupiga,,kulitaarifu hilo tukio.
************CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sasa vijana wangu natoa tamko.Imma atafutwe popote pale alipo.Akamatwe na aletwe hapa akiwa hai maana Mimi mwenyewe kwa mikono yangu nitamuua".
Alitoa amri hiyo ya kikatiri,Master Kill huku akiwa ameshikilia kisu chake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment