Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

NIFUNDISHE KUNYAMAZA - 2

 





    Simulizi : Nifundishe Kunyamaza

    Sehemu Ya Pili (2)



    Baada ya Master Kill kumaliza kuyatoa hayo maagizo yasiyokuwa na chembe ya huruma ndani yake aliwaamuru vijana hao watoweke mbele yake wamuache Kipanga peke yake .Master Kill alijiona amebarikiwa sana kwa vitendo vya kikatiri alivyokuwa akinifanyia,silitambui hata kosa nililomkosea huyu binadamu aliyeumbwa kwa udongo kama Mimi.Ameniondolea mke wangu kipenzi pamoja na mwanangu Prince akaona hiyo haitoshi akaamua kuanza kuiwinda roho yangu ambayo ilionekana dhahili kuwa haina hatia.Master Kill anaona ni jambo la maana sana kuniondolea roho yangu pasipo kutafakari kuwa hata yeye atakufa,,,Ila vyote kwa yote binadamu ndivyo tulivyo,,tunachukiana bila ya hatia yoyote na tunawindana mithili ya wanyama wakali wa mwituni.

    **********

    Basi baada ya Manka kuitoa simu yake na kulilipoti hilo tukio kituoni,hazikupita hata dakika ishirini askari polisi wakaja pale.Maskini wa Mungu sijui nimuamini nani hapa duniani tu maana kila ninayejaribu kumuamini bado anakuja kuniona mbaya tu mbele ya macho yake .Baada ya wale maaskari kufika eneo hilo nilijikuta wakiniweka katikati na kuanza kunishtumu kuwa Mimi ndiye muuaji niliyemuua mke wangu pamoja na mtoto wangu tena kwa ncha ya upanga,,Eti dalili za kwamba Mimi ndiye muuaji zilijionyesha dhahili.Shati langu lililokuwa limechafuliwa na michirizi ya damu lilijulisha kwamba ndimi niliyemuua mtoto wangu pamoja na mke wangu.Hawakujua kwamba niliumia sana nikamkumbatia mke wangu hivyo hivyo ingali ana jeraha tumboni ishara ya kuchomwa kisu.Walinitupia pingu wakanifunga nazo mikononi wakaanza kuniburuza chini mithili ya gunia huku wakinirushia mabanzi ya nguvu mgongoni,kichwani na kila sehemu ya mwili wangu.Nilijaribu hata kujitetea lakini bado waliyapuuza maneno yangu na kuyaona hayafai,,ule ushahidi wa ile barua ya mwisho ya mke wangu Nancy nao waliupuuza wakautupilia mbali kwa kisingizio eti nimeuandika Mimi mwenyewe ili kupoteza ushahidi.Niliumia sana jama ,sikumuona mtetezi wangu yu atatoka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wapi.Nilijaribu hata kuyainua macho yangu labda nijaribu kuitazama milima napo sikuiona zaidi ya kuiona michirizi ya machozi tu ikinitoka ndani ya macho yangu .Imma maskini Mimi nitaponea wapi? Sasa nikiwa nimezungukwa na wale maaskari moja kwa moja huku wakizidi kunizonga zonga,niliyapepesa macho yangu taratibu nikamwona Manka mtoto pekee wa boss wangu Mr Stanley akitabasamu tena akiwa hana hofu kabisa.Nilitaka kumwuliza kwa nini amenisaliti either kwa kunichonganishia kwa maaskari au kula njama na binadamu katiri Master Kill lakini moyo wangu ukasita.Sikuweza kumwelewa Manka kwa kweli ,mwanzo toka aniokoe zidi ya mikono hatari ya Master Kill hadi ananipeleka hospitalini nilijua huyu ndiye binadamu mwenye huruma ndani ya hii dunia iliyojaa dhuruma na uonevu.Nilimwangalia kwa nje nikajua ndiye mwanamke atakaye nifariji labda,Mara baada ya kuondokewa na kipenzi changu Nancy kumbe maskini Mimi nilikuwa nikilisubiri embe chini ya mnazi.Sikujua kama na Manka mwenyewe pamoja na kutoka katika familia ya kitajiri alikuwa kibaraka wa kikundi kiovu cha Master Kill.Basi nikiwa sijui hata cha kufanya nilimtazama Manka kwa macho ya huzuni sana kisha nikaufungua mdomo wangu taratibu nikamuuliza.

    "Why Manka,Kwa nini Manka,kumbe wewe ni adui yangu?". Hilo swali sikumuona hata mmoja wa kulijibu tofauti na kurushiwa ngumi moja ya usoni na askari aliyekuwa akijiona amebarikiwa sana na Mungu kwa kuyafikia maisha halisia ya ulimwenguni.Taarifa zikasambaa kwa kasi sana eneo hilo na Mimi nikajulikana ndiye niliyemuua Nancy mke wangu pamoja na Prince mwanangu na hapo ndipo nikayakumbuka maneno ya mwisho ya marehemu mama yangu;

    " Mwanangu Mimi nitakufa na nitakuacha peke yako hapa duniani.Muombe sana Mungu akusaidie katika maisha yako maana unao maadui wengi sana wanaokunyemelea kila uchao.Kumbuka taarifa za usingiziaji huwa hazienezwi na miti ila wanadamu unaoishi nao na unao kula nao".

    Sijayasahau hayo maneno ya mama yangu na Leo hii yamejizihirisha rasmi.Baba yake na marehemu mke wangu Mzee Hendrix alitaarifiwa na hakuchelewa sana akawa amefika pale nyumbani akiwa ameambatana na mkewe.

    ***********

    "Umemuua mwanangu Leo hii utamla nyama.Nilikuamini wewe nikaamua kukupa huyu mwanangu kumbe wewe ni mbwa mwitu...Nasema Leo hii utamla mwanangu". Maneno hayo kutoka kinywani mwa mama Nancy yalinivunja moyo nikawa nayafumba fumba tu macho yangu na kujiona mkosaji mkubwa mbele ya wanadamu wengi waliokuwa wakinizunguka.Laiti kama wangeyatambua maumivu yaliyomo ndani ya moyo wangu wasingedhubutu kunifanyia hivyo.

    Nilishtumiwa sana hatimaye nikakosa hadi cha kuongea nikaamua kuwa kimya tu.Nilimuomba tu Mungu angarau anifundishe kunyamaza maana kama nikujitetea nimejitetea sana lakini maneno yangu yote yote yalionekana hayana maana yoyote mbele ya wote waliokuwa wamenizunguka,nilimuomba Mungu wangu aliyeniweka tumboni mwa mama yangu kwa miezi tisa na kuruhusu nizaliwe anitetee.Basi kelele za watu zikiwa zinaendelea Mara Manka akajitokeza tena mbele ya mboni ya macho yangu,akaniangalia kwa jicho la husuda kisha akaniambia;

    " We handsome unaikumbuka siku ile nilipokutana na wewe pale njia panda ya Ubungo? Yes nilikuwa ni Mimi na yule niliyekuwa nae alikuwa ni rafiki yangu, so the game is over,nenda kawasalimie kuzimu maana utaenda kufia jela na hautatoka milele ,umeua ndugu yangu".

    Maneno hayo aliyoyaongea Manka yaliniumiza sana,nikatamani kumjibu lakini mdomo wangu ulikataa kunipa ushirikiano.Nikiwa nashangaa shangaa nilishtukia narusha ndani ya gari ya polisi huku nikiwa nimefungwa pingu.Kwa mbali niliiona gari ya kubebea wagonjwa ikija kwa kasi eneo hilo na bila shaka ilikuja kuuchukua mwili wa mke wangu Nancy pamoja na Prince mwanangu.Manka alipanda ndani ya gari yake akatokomea,,Mimi nikapelekwa mahakamani.

    "Nateseka jama ....Nateseka jama ....Nancy umeenda ,Mimi umeniachia mateso".



    Waliponipandisha ndani ya hiyo gari ya polisi huku wakiwa wamenifunga pingu mikononi na miguuni walianza safari ya kunipeleka mahakamani.Sikuwa na ujanja wowote ule ila nilinyamaza tu nikawa nawaza mambo mengi sana ndani ya kichwa changu.Bado sikuitambua hatia yangu ya kwa nini nimekamatwa kama muuaji na ili hali mikono yangu haikudhubutu hata kidogo kufanya kitendo kama hicho.Maumivu ndani ya moyo wangu yaliendelea kuninyonga huku nikiendelea kujiuliza na kujihoji maswali mengi sana mengine yakiwa hayana hata majibu.

    **********

    Tangu mama yangu aondoke duniani nimekuwa nikiendelea kukumbwa na matatizo mengi ,mengine yakukatisha kabisa tamaa.Siku zote sikuwahi kufikiria kabisa kama na Mimi ningesingiziwa kesi kama hiyo na kupelekwa mahakamani.Mafunzo ya mama yangu tangu enzi za utoto wangu niliyashika sana, si kwamba niliyashika kwa sababu ya kumfurahisha mama yangu,hapana Bali niliyashika ili yawe nguzo na msaada wa maisha yangu yote ya hapa duniani.Kwa sababu nilijua kwamba hii ni dunia na ipo siku mama ataondoka na kuniacha peke yangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mwanangu tambua upo duniani,na katika dunia hii yapo mambo mengi sana ya kuvunja moyo pamoja na kukatisha tamaa.Dunia imejaa dhuruma,dunia imejaa dhiki ,dunia imejaa miiba ya kila aina inayoweza kukuchoma hadi ndani ya moyo wako lakini yote haya yataonekana si kitu endapo tu utavumilia.Wapo watu wengi sana ambao wao hujiona kana kwamba hii dunia ni yao huendekeza vitendo vibaya vya kuwapuuza wenzao na wakati mwingine kuwaumiza kabisa,lakini kama nilivyokuambia, ya kupasa kuvumilia.Ishi vizuri na watu,jenga amani na maadui zako ili hata kama wanakuchukia waje wapate chochote cha kuzungumza siku ukitoweka kwenye usawa wa mboni za macho yako.Usisahau kumwomba Mungu ili akufundishe kunyamaza maana bila kufanya hivyo utayajutia sana maisha yako .Wakikutukana wewe waombee na wala usiwatukane,,wakikudharau wewe wapende na wala usiwachukue maana binadamu ndivyo walivyo.Usije kujaribu kulipiza kisasi kwa yeyote atakaye kukosea maana huwezi jua Mungu ana mpango gani katika maisha yako ya siku za usoni".

    Hata siku moja yapata miaka zaidi ya ishirini sasa tangu mama yangu anisimulie hayo, sijakaa na kuyasahau hadi Leo hii.Hayo hayo ndiyo niliyokuwa nikiyatumia katika maisha yangu ya kila siku. Nilijitahidi sana kuishi vizuri na watu maana niliijua thamani yake hata kupitia maandiko matakatifu.Hayo maneno ya mama yamenikuza,Japo nimekua kwa neema ya Mungu tu lakini yote nilishukuru kwa uhai ambao huyu baba wa yatima alinijalia maana maisha yetu Mimi na mama yangu yalikuwa magumu sana.Sijalisahau chozi la mama lililonidondokea begani kwangu kipindi niliporudishwa nyumbani kwa kukosa ada ya shule ili hali nilikuwa nimebakiza siku chache niufanye mtihani wangu wa kidato cha nne .Maneno aliyoyaongea mama siku hiyo yalinichoma sana si kwamba yalinichoma tu Bali hata kuniliza yaliniliza na kuusononesha sana moyo wangu.

    "Mwanangu Mimi hapa nilipo nimsindikizaji tu wa jua.Sina pesa wala dhahabu mwanangu Imma,labda kama ningekuwa hata na kipande kidogo cha shamba nisingekubali uteseke kiasi hiki mwanangu. Wamekurudisha toka shuleni hadi hapa kwa sababu ya ada sijui utasomaje tu mwanangu. Mungu ameniweka hai hadi muda huu ili nikulinde mwanangu, nguvu za kukulinda sina ila maneno yangu naamini hayo hayo ndiyo yatakayo kulinda.Siipatii picha siku yangu ya kusindikizwa kaburini itakuaje maana nahisi msiba wangu hautahudhuriwa na watu wengi maana Mimi ni maskini wa kutupwa ,watu wananidharau sana kwa sababu ya kuvaa nguo zilizo chakaa na kuishi maisha ya kuunga unga.Mvi zangu hazitasindikizwa kwa amani mwanangu lakini pamoja na hayo bado nitaenda kupumzika tu hata kama wasiponizika wengi.Basi mwanangu, maadamu umerudishwa kwa sababu ya ada nenda kavue sare zako hizo za shule,twende popote tupajuapo tukatafute hizo pesa hata kwa njia ya kuponda kokoto ,kuhusu hela ya chakula basi hilo lisikupe taabu,tutalala hata njaa".

    Hadi Leo bado namlaumu sasa baba yangu ni kwa nini alimkimbia mama Mara baada ya Mimi kuzaliwa.Japo nilimsamehe lakini sitokaa nimsahau popote pale alipo kwa kitendo hicho alichomfanyia mama yangu. Huenda angeshirikiana nae hayo yote yasingenipata

    **************

    Basi njia nzima nilikuwa nikiyawaza hayo tu ,niliyakumbuka sana maneno ya marehemu mama yangu, kila nikiitazama mikono yangu nakuikuta imekazwa pingu yayakumbuka haya maneno "Mwanangu muombe sana Mungu akufundishe kunyamaza maana wanadamu wamejaa dhuruma,wasamehe tu mwanangu". Kila nikiitazama hiyo mikono yangu isiyokuwa na hatia na kuyakumbuka maneno ya mama niliyaacha tu machozi yanitoke maana sikuwa na namna hata ya kuyapangusa.Safari ya kuelekea mahakamani ikawadia.

    Nilishushwa ndani ya gari hiyo mkukumkuku huku nikipigwa na kurushiwa matusi mazito ya kumtukana hadi mama yangu mnyonge asiye na hatia aliyeniacha peke yangu duniani na kuzidi kuumiza moyo wangu.Hadi dakika hiyo nilikuwa nimeshaiona dunia chungu nikabakiza kutamani tu na Mimi niondoke duniani ili hayo mateso yaniepuke maana nimeonewa na haki yangu imenyongwa.Ikafikia kipindi nikawa najilaumu kabisa ni kwa nini nilikata shauri ya kuoa mwanamke duniani. Maana huenda hata hili lisingenitokea.Mke wangu Nancy nilimpenda sana lakini kwa hili lililonitokea kwa kusingiziwa ndimi niliyemuua niliijutia nafsi yangu.

    Siku hiyo kwa vile ilikuwa ni siku ya mangojeo ya hukumu niliwekwa rumande siku nzima huku nikiwa sijala chochote.Usiku nilipata taabu kubwa sana maana mbu walinizungukia sana huku wakizidi kunishambulia kana kwamba hata wao nilikuwa nimewakosea.Kichwa changu kilibaki kimejiinamia tu na Mimi kuniacha niendelee kuumia.

    ***********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye kukakucha na siku ya hukumu yangu ikawa imewadia.Walikuja maaskari watatu wakanikamata na kuanza kuniburuza huku wakinitukana,

    "Msenge wewe uliyezaliwa na mbwa Leo utafia gerezani, umeua kwa sababu ya upumbavu wako....Tanguliaa...Pumbavu ,kenge mkubwa wewe".

    Sikujua siku hiyo itakuaje maana hata marafiki zangu wote waligeuka wakawa maadui zangu.

    " Ee Mungu nisaidiee....Mnyonge nimenyongwa nitakimbilia wapi???"



    Siku ya Mimi kuhukumiwa ikawadia,maaskari wakanitoa mle ndani ya rumande wakanipeleka ndani ya mahakama huku wakizidi kunitesa sana.Nilishindwa kuendelea kuzungumza chochote kile maana hata kama ningediriki kuufungua mdomo wangu ili nizungumze,sidhani kama ningesikika au kama maneno yangu yangeeleweka miongoni mwa watu hao ambao walikuwa wakijiona wameshaimaliza safari yote ya maisha yao.Ndugu yangu sijui hata nielezeje tu ,lakini ngoja niyapanguse kwanza machozi yangu harafu nikueleze.Mimi sikuwa na hatia yoyote nimehukumiwa hiki kifungo cha maisha jela ,hivyo napenda kukuombea ndugu yangu usije na wewe ukakubwa na jambo hili lililonikumba Mimi maana si zuri kabisa, jela panatisha ndugu zangu ni afadhari na maisha ya kuzimu.Katika maisha yangu sikutegemea kabisa kama ningekuja kufungwa lakini hii ndiyo hali halisia ya maisha yalivyo.

    *****

    Basi nilizidi kunyamaza kimya tu kuendelea kuwasikiliza kwa vyovyote vile watakavyoamua dhidi yangu.Nilitulia kimya nikawa nafikiri sana na wakati mwingine kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.Niliyakumbuka sana maneno ya mama yangu aliyoniambia enzi za uhai wake kwamba nijitahidi sana kuishi vyema na walimwengu,hilo nililizingatia,sasa kwa nini wanadamu hawa wamenigeuka na ili hali nilijitahidi kuishi nao vyema? Hilo kwa kweli liliendelea kukiumiza sana kichwa changu .Nilijiinamia chini nikazidi kujiongelesha Mimi mwenyewe kimya kimya na wakati mwingine kubaki nikiyaacha tu machozi toka machoni mwangu yatoke maana sikuwa hata na uwezo wa kuyapangusa.Pande zote kila nikijaribu kuyapepesa macho yangu naliona kundi kubwa la watu wakiwa wamenizunguka,,sikuweza kuwaelewa watu hao walikuwa pale kwa lengo gani,lakini akili zangu za haraka haraka nilijua tu watakuwa wanasubiria Mimi nihukumiwe harafu waachame midomo yao kunicheka.Niliyainamisha tena macho yangu kuelekea usawa wa mikono yangu.Nilipoiona imefungwa pingu sikuwa na ujanja tena,zaidi ya kumuomba Mungu aendelee kunifundisha kunyamaza maana kwa maumivu yaliyokuwa ndani ya moyo wangu ningeongea vyovyote vile nikazidi kumchukiza muumba wangu.Basi nilizirudisha kumbukumbu zote nikaanza kuwakumbuka ndugu zangu wote waliotangulia mbele ya haki huku nikijisemea laiti kama wangekuwepo najua wangejitoa kwa nguvu zao zote kusimama kunitetea maana kwa kipindi hicho sikuwa na mtetezi hata mmoja.

    ***********

    "Baba hivi ni kwa nini ulimkimbia mama? Ulimkimbia mama yangu kwa kosa lipi! Mbona kama ni tabia mama alikuwa na tabia nzuri tu,au kwa vile alikuwa ni mbaya ndomaana uliamua kumkimbia.Baba uliniachia maumivu mazito sana baba yangu.Laiti kama baba usingefanya hivyo ungekuwepo hapa kunitetea lakini haupo baba,macho yangu yananishuhudia kwamba nipo peke yangu ,sina hata pa kukimbilia.Mama na wewe haupo? Mama yangu uko wapi?? Nimeyakumbuka sana maneno yako mama ila uliondoka mapema sana mama yangu...kwa nini hukusubiri ili mwanao nipate faraja?.Mwanao nimeonewa mama...fufuka mama uje ulione chozi langu linavyonyongwa...Mikono yangu haijafanya kosa wala hatia yoyote ile lakini imefungwa pingu.Mama mwanao naenda jela ,sina matumaini tena,nimebakiza kuzihesabu siku tu,,Imma mwanao nimeonewa lakini nitafanyaje wakati ya ulimwengu ndivyo yalivyo? Tutaonana mama yangu .Laiti kama ungekuwepo ungenitetea mama lakini basi tu".

    Hayo maneno niliyaongea kimya kimya huku nikiendelea kuuambia moyo wangu utulie.Niliubembeleza moyo wangu hadi ukanielewa.Baada ya hayo yote niliyainua macho yangu nikamwona Master Kill mtu katiri aliyesababisha kifo cha mke wangu pamoja na mwanangu Prince na Mimi kuniweka katika haya matatizo ,akitabasamu kwa furaha,nadhani ndani ya nafsi yake alijiona ni mtu wa maana sana kwa ushindi alioupata kutokana na kushtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji .Pembeni yake nilimuona Manka akijaribu kumnong'oneza Master Kill huku akitabasamu bila shaka alijiona amebarikiwa sana kuliko wanawake wote ndani ya hii dunia.Maskini Mimi sikujua kama siku hiyo wangetokea maadui wengi wa kuishangilia hukumu ile ,sikuamini kabisa maana hata marafiki zangu,wote walinigeuka siku hiyo.Sikujua kwa nini walinifanyia hivyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndani ya moyo wangu sikuwa na kinyongo cha aina yoyote ile ,nilikuwa tayari hata wanifunge maana Baba wa yatima,Mume wa wajane na Mungu wa wanyonge nilikuwa nikimuelewa sana.Ndiye yeye pekee aliyeshuka na kumtetea Joseph kijana aliyefungwa gerezani bila ya hatia yoyote ile,, Bado sijaisahau safari ndefu ya wana waisrael jinsi Mungu alivyo wapigania na kuwatetea dhidi ya safari yao hiyo iliyokuwa imejaa machungu pamoja na mateso ya kila aina.Sijausahau muujiza wake wa kuitoboa bahari ya Sham ikawa njia ya kutokea dhidi ya maadui zao na kuwashindia wana wa Israel.Niliitambua kazi ya Mungu wangu,,nilimtumaini yeye peke yake maana ndiye atakaye nitengenezea njia hata pale pasipokuwa na njia kunitetea kama alivyowatetea wana wa Israel.

    ***************

    Baada ya hukumu yangu kutolewa na Mimi kuhukumiwa kifungo cha maisha Jela wote walioisikia hiyo hukumu walishangilia sana kwa furaha huku wengine wakiinua mikono yao juu kuashiria kufurahishwa na hukumu hiyo .Niliumia sana,,Maumivu ndani ya moyo wangu yaliongezeka maradufu nilipomuona rafiki yangu kipenzi Filbert akiishangilia ile hukumu na kuipigia makofi.Sikujua kama na yeye angenifanyia hivyo maana tulikuwa tukiheshimiana sana.Ni yeye pekee aliyezijua siri zangu na zake nilizijua.

    Mimi pekee ndiye niliyeyabadirisha maisha ya Filbert .Nilimfanya na yeye aivae tai kwa kuhangaika kumtafutia kazi,kumbe shukurani yake ilikuwa ni hiyo?.Kiukweli siku hiyo niliyaelewa sana maneno ya wahenga yasemayo "Kikulacho kinguoni mwako" na kila anayekuonyesha tabasamu usoni mwake amefurahishwa na kitendo chako.Wapo wengi huyaonyesha matabasamu ya uwongo ili mradi wakuvute karibu ili waweze kukuangamiza.

    Basi maaskari wakanishika na kuanza kuniburuza mithili ya mnyama kunipeleka gerezani kwa ajili ya kuitumikia adhabu yangu. Nilijitahidi kunyamaza kimya lakini moyo wangu uliponibembeleza niyaongee haya ,niliyaongea,kwa aliyenisikia alinielewa maana walikuwa wamenishikilia tayari kwa kunipeleka gerezani.

    "Ndugu zangu adhabu mmenipa,lakini siku zote samaki ndiye aumizwaye ndani ya bahari.Haki hunyongwa na kutupiliwa mbali pale inapostahili iwe haki.Nendeni mkamsalimie mwanangu Queen, mwambieni baba yake nitarejea endapo Mungu akicheka ila nikifia jela msisite kumwonyesha kaburi langu ".



    Niliyaongea hayo maneno kwa ukakamavu sana lakini nikaonekana kama kinyago tu mbele ya wale maaskari waliokuwa wamenikamata.Kuna askari mmoja Mara baada ya Mimi kuyaongea hayo nilimuona ameukunja uso wake na hapo hapo akanikamata shingoni na kunipiga kofi la usoni .Sikumwelewa ni kwa nini amenipiga hivyo lakini moyo wangu uliniambia nimsamehe tu maana kila mtu awapo hapa dunia huwa ana muda wake wa kujidai.Nilijua tu huyo askari huo ndo ulikuwa muda wake wa kujiona amebarikiwa chini ya hii ardhi.Sikumurudishia chochote Bali nilinyamaza tu.Japo uso wangu uliumia sana lakini faraja iliyotolewa ndani ya moyo wangu ilitosha kuufariji uso wangu.

    ***********

    Basi baada ya kunifikisha gerezani walinisukumizia nikaenda kudondokea ndani kama siyo binadamu vile,mpaka nikajiuliza kabisa ni kwa nini wanadamu huwa hatuna huruma ili hali sote tu mavumbi na mavumbini tutarudi.Baada ya kuniweka humo waliufunga mlango wakaenda zao.Nilistaajabu sana kukuta sehemu ya humo gerezani ikitisha,,kulikuwa hakuna taa zozote mle na madirisha yake yalikuwa ni madogo sana kiasi kwamba hali ilikuwa si ya kibinadamu kabisa. Sasa kwa vile muda ulikuwa ni wa mchana nilielewa labda kulikuwa na taratibu zingine kuhusiana na suala la mwanga hususani nyakati za usiku.Basi nilibahatika kuwaona wafungwa kama watano ndani ya chumba hicho cha gereza akili yangu ikanishuhudia huenda wale walikuwa ni wafungwa wa kudumu yaani waliohukumiwa miaka ya maisha jela.Mimi huku nikiwa nimejawa na huzuni kubwa sana ndani ya moyo wangu nilijivuta vuta nikausogelea ukuta nikaa na hapo hapo nikajiinamia.Kwa mbali nilianza kuhisi matone ya machozi yakikirowanisha kifua changu .

    "Vipi brother mbona unaonekana ni mtu wa huzuni sana? Izoee tu hii hali broo maana hata ukihuzunika kiasi gani hakuna atakaye kuhurumia huku.Gerezani brother watu wamekaliwa na mioyo ya kishetani,,kwa hiyo jikaze kiume kumbuka wewe si mwanamke wa kulia lia ovyo ovyo wewe ni mwanaume". Hiyo sauti ilipenyeza vyema ndani ya maskio yangu nikakinyanyua kichwa changu juu kumbaini ni nani aliyekuwa akiniongelesha hayo maneno.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Vipi broo changamka maisha ya humu yanatakiwa uyachangamkie maana ukiwa una bung'aa bung'aa unaweza kuolewa aisee.Kwanza unaitwa nani na humo umeletwa na mshkaji yupi?" Hiyo sauti iliongea tena.Baada ya kuyapepesa macho yangu huku na huko nilimuona jamaa mmoja aliyekuwa amekonda sana akiniongelesha.Yaani alikuwa amekonda utadhani alikuwa mgonjwa wa ukimwi.Nilipomtizama tu mwili wangu ukasisimka nikajikuta nikitetemeka maana kiukweli hali yake ilikuwa ikitisha sana yaani ndugu msomaji hata wewe ungebahatika kumwona bila shaka ungeogopa sana kama siyo kutetemeka.Nilishindwa hata nimjibuje nikawa nimebaki mdomo wazi tu.

    "Broo!! Mbona kimya sana,au wewe ni bubu nini! Nijibu broo, huku ukijifanya kauzu lazima uumie maana maisha ya huku ni afadhari na yale ya kuzimuni.Kwanza maisha ya kitaa unatakiwa uyasahau kabisaa Bali uanze kuyazoea maisha ya gerezani. Una masaa tu harafu unahuzunika kiasi hicho je ukikaa miezi sasa si utakufa kabisa. Sie hapa tulipo tumekaa humu zaidi ya miaka thelasini na bado tunaendelea kukaa,sasa wewe jifanye kauzu tu". Baada ya yule jamaa kumaliza kuyaongea hayo nilimuona amejongea pembeni na hapo hapo akakaa na kutulia .Nilishusha pumzi kidogo nikataka nimfuate yule jamaa kumuulizia masuala ya gerezani yanavyo kwenda lakini moyo wangu ukasita nikatulia tu na kuanza kujifariji kimya kimya .Muda nao ukazidi kwenda hatimaye ule muda wa kupata chakula ukawadia.Tulitolewa ndani ya hilo gereza tukatoka nje kuungana na wafungwa wengine kukipata chakula cha mchana.

    ************

    " Wafungwa wote waliohukumiwa kifungo cha maisha, panga mstari mmoja hapa,,Fanya faster!!".Ilisikika sauti moja kutoka kwa jamaa mmoja aliyekuwa amevaa magwanda ya ugoro.Basi tulipoisikia tu hiyo sauti wafungwa wote wa maisha tulijongea tukapanga mstari mmoja tu,,sasa Baada ya Mimi kuwahesabu wafungwa hao kimya kimya niligundua kwamba tulikuwa jumla ya wafungwa kumi tu ,,lakini wafungwa wengine walikuwa ni wengi sana tofauti na sisi.

    "Sasa ili mfanikiwe kukila chakula hiki cha mchana,,lazima mhakikishe rundo hili linatoweka hapa,msipofanya hivyo aisee mtaishia kuisikilizia tu harufu ya chakula,, basi poteeni". Jamaa yule bila kujali watu walikuwa wamechoka kiasi gani aliamua kutupa kazi ya kuyahamisha matofali zaidi ya elfu moja yaliyokuwa yamerundikwa upande wa kulia kutoka pale tulipokuwa tumesimamia...Basi kwa vile adhabu ile ilikuwa ikitulenga sisi tulilikaribia lile rundo la tofali tukapangiana kila mtu asombe tofali zaidi ya mia moja ,,,Daah! kazi tukaianza,,Mimi nikajivuta vuta nikafanikiwa kuhamisha tofali kama tano hivi..Sasa niliporudi tu,ili niendelee kuisogeza idadi ya zile tofali Mara kwenye kidole gumba changu cha kulia nikahisi nimeng'atwa na mdudu ,kuja kuangalia kumbe ni Nge ndiye aliyekuwa amening'ata.Nilijaribu kujikaza kiume lakini uvumilivu ukanishinda nikaamua kuisitisha ile kazi kuyasikilizia maumivu.Sasa Mara baada ya Mimi kusimama tu,alikuwa askari mmoja akanipiga mjeredi wa mgongoni bila hata kuniuliza na hapo hapo akaniongezea maumivu maradufu,,,Nilimwangalia yule askari nikashindwa hata cha kumwambia.

    " We fala nini ,sasa unauleta ujinga wako hapa,,huku siyo nyumbani kwako aisee Fanya kazi ,acha ujinga,,nataka hizo tofali zitoke zote hapo".Aliongea yule askari kwa sauti ya kikatiri.Mimi niliendelea kumwangalia hatimaye uvumilivu wa kukaa kimya huku nikiumia ulinishinda nikaamua kuuvunja ukimya,

    "Ndugu yangu naomba unisamehe...Hapa nilipo nimeng'atwa na Nge ndo maana unaniona nipo hivi,,nivumilie kidogo tu kaka yangu ". Nilipoongea hivyo nilimuona yule askari amekunja uso wake.

    " Nani kaka yako hapa? Oyaa nyie wengine acheni kuifanya hii kazi nendeni mkale.Huyu anayejifanya mjanja sijui ameng'atwa na sisimizi..nataka hii kazi aifanye peke yake,,hizi tofali azisombe peke yake".



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog