Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

NIFUNDISHE KUNYAMAZA - 3

 





    Simulizi : Nifundishe Kunyamaza

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Mara baada ya yule askari katiri kuyaongea hayo alinisogelea tena akanipiga Kofi la usoni na hapo hapo akanisukuma nikaenda kuanguka juu ya yale matofali ya block .Niliponyanyuka kwa kujivuta vuta niliyasikia maumivu makali sana kwenye mkono wangu wa kulia ,,kuja kuuchunguza vizuri ule mkono nilibaini umepatwa na jeraha kubwa sana ambalo liliifanya damu yangu ianze kuchuruzika kwa kasi ya ajabu.Niliipangusa ile damu taratibu huku nikijiongelesha kimya kimya mithili ya mwendawazimu .Niliyaongea maneno tofauti tofauti ambayo hata sikuyaona yakinisaidia kwa chochote kile kunitowa ndani ya lile dimbwi la mateso,,siku zote sikutegemea kama ningekuja kupatwa la mateso kama hayo lakini ilinibidi tu ni ya kubali maana sikuwa na ujanja wowote wa kujitoa kwenye hayo mateso yasiyokuwa na pumzi hata kidogo ya furaha.Basi sikumrudishia chochote kile yule askari bali nilimuangalia tu nikabakiza kukitikisa tikisa kichwa changu kwa uchungu.Nilisimama wima nikaupiga konde moyo wangu nikauambia,,

    "Tulia moyo wangu, wamekuonea lakini hawatakaa wayasahau mateso yatakayo wapata kwa kosa la kuinyonga haki yako.Jipe matumaini moyo wangu maana ndiwe pekee uliyebakia kuwa faraja yangu maana dunia imenisaliti na wala sikuwa na hatia yoyote ile. Ila hukumu yangu najua haitawaacha watu salama". Nilipomaliza kujiongelesha hayo maneno niliyafuta machozi yaliyokuwa yakinitoka na taratibu nikajaribu kuyapepesa macho yangu kuyaelekeza ule upande ambao wale wenzangu walikuwa wakipata chakula. Niliwaangalia kidogo tu kisha nikajiangalia tena na kubaini ni kweli zile tofali nilikuwa nimeachiwa nizihamishe Mimi peke yangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***********

    Kwa kweli inauma sana ,niliitafakari ile kauli ambayo nilimwambia yule askari nikairudia Mara mia mia nikaja na jibu la kwamba kauli hiyo haikuwa na hatia yoyote bali ilikuwa na lengo moja tu la kuitetea huruma.Mwanadamu huyu huyu aliyeumbwa kwa udongo kama Mimi ni kweli ameshindwa kunionea huruma? Nilijaribu kulitafuta kosa langu lililomfanya yule askari anipe hiyo adhabu na kuwakataza wafungwa wengine wasiifanye lakini nikashindwa kulipata.Sijui kosa langu la kumwambia nimepatwa na tatizo la kung'atwa na nge ndo lililo sababisha nipewe ile adhabu isiyokuwa na chembe ya ubinadamu? Nilijihoji lakini nikaishia kunyamaza tu.Nilianza kuyasomba yale matofali moja baada ya jingine,,nilipobakiza tofali mia niligeuka na kuwaona wale wenzangu tayari wameshamaliza kula chakula chote na baada ya muda kidogo vyombo vyote vilivyokuwa vimewekewa chakula vilitolewa pale nikashuhudia kwa macho yangu kwamba tayari nimeshashinda njaa.Basi nikazidi kujitia nguvu hivyo hivyo japokuwa zilikuwa zikizidi kunikimbia hatimaye nikabakiza tofali hamsini niimalize ile adhabu ya kikatiri .

    "Bwana mdogo hii ndo Jela na usipoangalia siku mbili au tatu tutakuzika.Sasa endelea kufanya usenge wako...Mimi ni afande Swey ,ni afande niliyejaliwa moyo wa huruma sana lakini huruma hiyo hufunikwa mithili ya wingu jeupe lifunikwalo na wingu zito la mvua endapo utaniletea mambo ya kipumbavu.Sasa hiyo adhabu niliyokupatia ni nusu thelusi tu ,siku nyingine ukijifanya wewe nunda utajuta".

    Afande Swey alipomaliza kuongea hivyo aliachia msonyo wa ajabu sana kisha akaenda na kusimama pembeni. Kwa mbali nilianza kuyasikilizia maumivu mazito ndani ya tumbo na baada ya muda kidogo nikaanza kusikia maumivu makali sana karibia mwili wangu wote .Nilijitutumua hatimaye nikawa nimefanikiwa kuyamaliza matofali yote.Mungu wangu nilipoyamaliza tu ghafla nilianza kuweweseka na hapo hapo nikadondoka na kupoteza fahamu.

    ************

    Upande mwingine alionekana Manka akiwa ndani ya gari akielekea ngomeni kwa master Kill ,,ndani ya moyo wake alijisikia faraja sana kumuona Imma kijana aliyekuwa akimuwinda kama mnyama amesha hukumu ya kifungo cha maisha. Alikuwa akiishia kutabasamu tu ,basi baada ya kuifikia ile ngome,aliisimamisha gari yake akashuka na kuanza kuzipiga hatua kuingia ndani ya ile ngome.

    " Waoo mrembo wangu yaani umependeza sana...mithili ya malaika aliyeshuka kutoka juu mbinguni".Aliongea Master Kill kwa basha basha nyingi sana Mara baada ya kumuona Manka akija mbele yake.Manka alikuwa akitembea kwa maringo sana utadhani dunia yote ilikuwa chini ya mikono yake."Waoo! Kamanda wangu Master Kill mwenyewe hata wewe umependeza sana jamani ".Baada ya Manka kuongea hivyo alimsogelea Master Kill wakakumbatiana,,wakapigana mabusu kisha wakashikana mikono yao na kuanza kuelekea upande wa eneo la kupumzikia...

    " Hey! Kipanga waambie hao vijana watuletee vinywaji hapa,umenisikia?" Aliuliza Master Kill."Ndio mkuu nimekusikia".Alijibu Kipanga na hapo hapo akaita vijana wawili akawaagiza waifanye hiyo kazi Mara moja na mambo mengine yaendelee.Huku hayo yakiendelea,Manka alikuwa amekaa juu ya mapaja ya Master Kill akiendelea kukichezea chezea kidevu chake.

    "Unajua nini baby..yaani siku ile hakimu alinifurahisha sana ,furaha ambayo niliipata siku hiyo nahisi sijawahi kuiona tangia nizaliwe.Afadhari huyu kinyago amefungwa maana angetusumbua sana.Nilijaribu kumtafutia sababu yoyote ya kumharibia lakini sikuipata kwa muda huo hatimaye Leo moyo wangu umefarijika kumuona Imma amefungwa tena kile kifungo cha mbwa cha kufia gerezani,, yaani safi sana na akomee". Aliongea Manka kwa furaha sana ." Hahaha! Mimi ndiye Master Kill bwana,nani mwenye nguvu na uwezo kama wangu? Siku zote ukiwa na pesa,pesa ndiyo inayoongea.Yule hakimu nilimtoa kiasi kikubwa sana cha pesa na ndio maana ile kesi ilipelekwa haraka haraka...pesa ni mfalme wa nchi kavu.Sasa huyu mwendawazimu atafia gerezani tena naafe kabisaaa, hahahaha". Baada ya Master Kill kuongea hivyo alizipokea glasi mbili zenye vinywaji akampa Manka ile glasi moja na yeye akabaki nayo nyingine wakaendelea kula maisha,, nadhani ndani ya mioyo yao walijiona wamebarikiwa sana kiasi kwamba hawatakuja kufa.

    "Sasa baby tutaishi kwa amani wakutusumbua hayupo tena.Maana yule jamaa nilikuwa simpendi afadhari kinyesi jinsi nilivyokuwa nikimchukia". Aliongea Manka huku akiubinua mdomo wake kwa dharau.

    *********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa pale chini ..kwa mbali nilihisi baridi kali sana...ghafla nikakurupuka.Kumbe nilikuwa nimemwagiwa maji.Niligundua kwamba nimemwagiwa maji baada ya kubaini nguo zangu zilikuwa zimelowana zote.Sijui Yale maji yalikuwa ya chooni, maana nilisikia harufu kari ikinisumbua sana .

    " We mwendawazimu nyanyuka hapo haraka.. Unajifanya kuzimia! Yaani bora ungekufa kabisa, unajua nini ungekufa Mimi ningepandishwa ngazi aisee.Simama,,una shangaa shangaa nini.Nimekwambia huku hakuna starehe ni afadhari na maisha matakatifu ya kuzimu".Afande Swey aliongea kwa sauti ya kikatiri sana kisha akanisogelea hadi pale nilipokuwa nimekaa akaninyanyua kwa fujo kisha akanipiga Kofi la mgongoni,,

    "Pumbavu tangulia hapoo ...yaani Leo mpaka uharishe utumbo ndipo nijue umechoka...Songaa...Sasa unawaona hao wenzako hiyo kazi wanayoifanya ,,,nataka uende pale ukang'oe visiki hamsini,,,utajua mwenyewe utapatia wapi vitendea kazi ". Aliongea afande Swey na kuondoka mbele yangu.



    Nilibaki nimezubaa pale mithili ya kichaa aliyenyimwa chakula katikati ya umati mkubwa wa watu.Niliitafakari sana ile adhabu nikajikuta nikiishia na wazo la kwamba, kwa vyovyote vile nisingeweza kuifanya ile adhabu...kila nikiyakumbuka yale maumivu ambayo yalikuwa yametokana na Mimi kuzisomba zile tofali zaidi ya elfu moja peke yangu pamoja na Yale ya kung'atwa na Nge ama hakika nguvu zangu ziliniishia."Mh! Hivi huu ni ungwana ? Yaani tunatesana mithili ya wanyama na ili hali sote tumeumbwa kwa udongo, kweli nimeamini mnyonge hunyongwa kwa vyovyote vile maana hana cha kujitetea ".Nilijiongelesha hayo kimya kimya,nikatafakari kidogo kisha nikaamua kumfuata yule askari aliyenipa ile adhabu.Niliona bora nifanye hivyo tu maana niligundua kwamba endapo ningeendelea kubaki kimya basi ningeumia.Nilizipiga hatua taratibu nikawa nimemfikia,Sasa kabla hata sijamuongelesha chochote alininyooshea mkono wake wa kulia kuashiria kwamba hakuwa tayari kuisikia neno lolote kutoka kwangu.

    " We boya ishia hapo hapo..usinisogelee maana ukinisogelea tu basi umeumia maana Mimi kama unavyonifahamu huwa sipendagi ujinga.Sasa sogea uone".Aliongea afande Swey kwa sauti ambayo haikuwa na dalili yoyote ya kunionea huruma.Nilijikaza kisabuni nikajisemea lolote na liwe acha nimfikishie tu huu ujumbe wangu hata Kama atashindwa kunielewa.Nikabakiza hatua moja nimfikie..sasa nikamuona amechomoa bastora yake na kuinyosha kuelekea usawa ule nilipokuwa nimesimamia .Mimi kwa muda huo nilikuwa nimeyakubali yote ,,ama aniue au aniache hai maana hata kama angeniua basi angenipunguzia chungu nzima ya mateso iliyokuwa ikiniandama.

    "Ndugu yangu,, kumbuka sote tuko duniani.Sote tumeumbwa kwa udongo...tutakufa na tutakwenda kuhukumiwa, sasa kwa nini tutesane kiasi hiki? Kumbuka Mimi ni binadamu kama ulivyo wewe..Nina nyama kama uliyonayo wewe,,,Huwa napumua kama unavyopumua wewe Sasa kwa nini unipatie adhabu kubwa kiasi hiki? Kwani kosa langu ni nini afande ..Au kwa vile wewe unalipwa mshahara kwa kutesa watu kuliko Mimi ambaye si ambulii chochote!!. Unalipwa mshahara kwa sababu ya kuonea watu lakini yote kwa yote tutakutana wote kaburini".Niliongea lakini nikajikuta nikimiminiwa risasi mbili mguuni kwangu hapo hapo sikuwa na nguvu zozote za kuniwezesha kusimama hivyo nilidondoka chini nikaanza kujiburuza buruza mithili ya nyoka huku maumivu yakiendelea kunisonga ,,maumivu yalianza kunitesha na uvumilivu ukanishinda nikajikuta nikiyaacha tu machozi yanitoke maana nilijua tayari ameniumiza.Nikiwa pale chini,yule afande alinisogelea akaninyanyua na kunisukumizia upande wa mbele nikadondoka vibaya nikausikia mguu wangu mwingine umelia kabisa kuashiria kama si kuvunjika basi uliteguka.

    ********

    Siku hiyo kule ngomeni kwa Master Kill hali haikuwa shwari kabisa. Master Kill aliwaandaa vizuri vijana wake wapatao ishirini akawapa maagizo magumu kisha akawapa na silaha za kwenda kupambana na lolote lile litakalo tokea mbele yao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Vijana Leo ni siku maalumu ya kwenda kuishambulia ngome ya yule jamaa anayejiita Mr Stanley,nataka mkifika pale mkaangamize kila kiumbe mtakacho kiona mbele yenu.Hakikisheni kabla hamjalifanya hilo kila mmoja wenu ajitathimini maana mkienda kichwa kichwa tu mnaweza msirudi kabisa maana ile ngoma ni hatari sana.Kwa hiyo mnatakiwa muwe makini sana". Baada ya Master Kill kuyaongea hayo aliwapigisha kwata vijana wake hao kisha akawaamuru wapotee mbele yake.Siku hiyo Master Kill aliwaandaa vijana wake kwa ajili ya kazi moja tu ya kwenda kuishambulia ngome ya Mr Stanley baba mzazi wa Manka .Master Kill hakukurupuka kuivamia hiyo ngome bali ilitokana na maelewano ambayo walielewana yeye pamoja na Manka...walipanga siri nzito sana iliyokuwa imejificha nyuma ya pazia.Manka tangu amuone baba yake mzazi amemiliki Mali nyingi sana pamoja na magari ya kila aina ,alikuwa akimfuatilia sana huyo baba yake...kiasi kwamba uchu wa tamaa ulimlemea hadi akaamua kuyachukua hayo maamuzi magumu ya kushirikiana na Master Kill kuivamia ngome yake na wakati mwingine Kuapa kumwangamiza kabisa Mr Stanley mwenyewe endapo watabahatika kumuona akizagaa zagaa mbele yao.Basi wale vijana walipanda ndani ya gari mbili nyeusi wakaianza safari ya kuelekea ngomeni huko.

    Safari yao ilichukua muda wa lisaa limoja ikawa imekamilika.Waliifikia ngome hiyo mnamo majira ya saa mbili na nusu za usiku wakapaki gari zao pembeni kabisa kisha wakaanza kuizunguka ile ngome kimya kimya.Sasa usoni mwao ilikuwa ni vigumu sana kuwafahamu maana walikuwa wamevalia mask usoni na wote walikuwa wamevaa makoti meusi marefu.Walizitoa baadhi ya silaha zao huku wakiwa wamechukua tahadhari kubwa sana.Kipanga ambaye ndiye aliachiwa jukumu hilo la kuwaongoza wenzake na boss wake Master Kill ,alitoa amri moja ya kwamba,, kila mmoja aanze kutega mabomu yasiyopungua ishirini kabla hawajaanza rasmi kufanya mashambulizi ya moja kwa moja.Sasa kazi ya kuyatega hayo mabomu ikaanza ,,waliifanya kwa umakini sana hadi wakaimaliza na kusubiri muda ufike waishambulie hiyo ngome.Kipanga akaitoa darubini yake akaanza kuchunguza,,akagundua ngome hiyo ilikuwa na maaskari kadhaa tu.Alipoendelea alibaini katikati ya lango kuu la kuingilia kulikuwa na maaskari wawili tu ambao hawakuwa na silaha yoyote ile zaidi ya virungu tu.Kipanga alipojiridhisha na hilo alinyanyuka yeye mwenyewe akaanza kutembea kwa kuchuchumaa hadi akalifikia hilo lango .Sasa kwa vile wale askari walikuwa hawajui hili wala lile aliwaibukia akawakaba shingoni wote na hapo hapo akawageuza na kuwadunga visu vya tumboni kitu ambacho kiliifanya damu yao iruke juu mithili ya maji.

    **********

    Katika uwanja wa denge wa Mwalimu Nyerere alionekana Queen akishuka ndani ya ndege moja iliyokuwa na nembo ya USA akiwa ameambatana na baba yake mdogo Albert yaani mdogo wake na Imma wakaanza kuzipiga hatua kuisogelea gari moja iliyokuwa upande wao wa kulia .Queen alikuwa ametoka USA huko huko alipokuwa masomoni...Muda huo alikuwa akielekea nyumbani kwa baba yake Imma maana kilikuwa ni kipindi cha likizo.Baba yake mdogo nae alikuwa ametoka USA Mara baada ya kumaliza mafunzo yake ya ukomando wa majini na nchi kavu uliokuwa umechukua takribani jumla ya miaka saba.Sasa ameamua kurudi nyumbani kuja kumsalimia kaka yake kipenzi Imma.

    "Baba mdogo yaani nimepamisi sana nyumbani,, unajua miaka karibu minne sasa sipo ,,sijui ni furaha gani tu ambayo nitakuwa nayo Mara baada ya kuwaona wazazi wangu pamoja na mdogo wangu Prince. Yaani nimewakumbuka sana". Aliongea Queen huku akimwangalia baba yake mdogo kwa macho yaliyojaa tabasamu la furaha.Albert huku kifua chake kikiwa kimetuna alimwangalia Queen kwa jicho la furaha kisha akaachia tabasamu kidogo na kuongea.." Hata Mimi Mwanangu nimepakumbuka sana hapa nyumbani, unajua kazi zetu za kijeshi huwa zinatuweka bize sana yaani huwezi amini Mimi hapa tangia niwasiliane na kaka yangu Imma mwaka jana sijawahi kuwasiliana nae ,,nimemkumbuka sana kaka yangu huyo.Tulizaliwa wawili tu na marehemu mama yetu yaani kaka Imma pamoja na Mimi hivyo tunapendana sana.Huwa sipendi kusikia kaka yangu amepatwa na tatizo lolote lile yaani huwa nachukia sana...Na ukitaka kuuona ukichaa wangu basi mtukane kaka yangu huyo utajuta kuzaliwa.Kaka Imma namheshimu kama mzazi wangu maana kipindi mama anatuacha duniani alimuachia jukumu la kunisimamia Mimi .Daah! Yaani sijui itakuaje tu nikikutana nae huko nyumbani kwake. Hata shemeji yangu Nancy nae nimemkumbuka sana".

    Daah!! Sijui itakuaje tu....Komando Albert anarudi nyumbani Tanzania akitokea USA Baada ya kumaliza mafunzo yake ya kijeshi huku akiwa na furaha kubwa ya kuonana na kaka yake Imma pamoja na shemeji yake Nancy....Sasa nini kitatokea? Imma yuko gerezani,,, Nancy hayupo duniani. ..Nini kitatokea??



    "Harafu unajua nini Mwanangu Queen,, nimemkumbuka sana shemeji Nancy..yaani tangu nihudhurie kwenye harusi yake miaka kumi iliyopita hadi Leo bado sijabahatika kukutana nae sasa Nina hamu ya kumuona.Hivi Prince yeye ulimuacha pale nyumbani akiwa na umri wa miaka mingapi?"..." Aaah! Nilikaacha kakiwa kadago mno,yaani kalikuwa na umri wa miaka miwili tu.Sasa nadhani katakuwa kameshakua sasa hivi maana miaka imesogea baba mdogo ".Baada ya Albert kumaliza mazungumzo hayo na Queen walikuwa tayari wameshaifikia gari ambayo ilikuwa upande wa kulia kwao...walipanda na safari ya kuelekea Magomeni njia panda ikaanza .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Oyaa kutoka hapa kwenda hadi maeneo ya Magomeni njia panda utatufanyia shilingi ngapi?" Aliuliza Albert huku akiwa amemuangalia yule dereza kwa jicho kavu.."Ni buku mbili tu broo" Aliongea kwa ufupi huku akiendelea kukanyaga mafuta."Punguza bwana hujui hali ya kiuchumi ni tete aisee? Fanya angarau buku moja hivi hapo itakuwa fresh" aliongea Albert. "Broo kwa kweli hilo haliwezekani..sasa hiyo ndo bei halisia,tofauti na hapo tutasumbuana bure tu brother" dereva taksii aliongea. "Punguza wewe kwani kuna shida gani hapo? Kwanza barabara zote naona zina lami sasa iweje tuzinguane kiasi hicho? Punguza bwana". Albert nae aliendelea kuushikilia msimamo wake ." Brother kama vipi shuka tu chini,masuala ya kuendelea kuzungushana kiasi hicho aisee Mimi hayo yote sijayazoea..kama unaona hiyo elfu mbili imekuwa kubwa basi shuka chini utembee kwa mguu na huyo demu wako".Dereva Aliongea kwa hasira sana na wakati mwingine kuikunja hadi sura yake."Oya! Mimi sijakuongelesha kiukatiri kiasi hicho...tafadhari chunga sana hayo maneno yako,,Mimi huwa ni mpole sana lakini ukinikasirisha huwa nakuwaga mkali zaidi ya manyigu sasa narudia tena,chunga hayo maneno yako ".Aliongea Albert kwa hasira kidogo." Brother acha usenge,,kama huna hiyo elfu mbili shuka chini,tusipotezeane muda aisee Nina mambo mengi ya kufanya ".Aliongea Dereva na kwa Mara hii akaisimamisha gari yake kabisa.. Sasa Mara baada ya kuyaongea hayo,, hasira ya Albert ikawaka.Laiti kama angejua kwamba anazungumza na nani asingediriki hata kuyaongea hayo aliyoyaongea,,Komando Albert ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wakiogopewa sana,,hadi president mwenyewe alikuwa akimfahamu vizuri huyu jamaa.Yeye alikuwa akipiga hakuna wa kumkamata wala kumwongelesha." Nadhani wewe hunifahamu vizuri.. Naomba toka nje ....nahesabu hadi Mara tatu uuachie huyo usukani..moja....?" ...."Sitoki kwani wewe nani hadi nikuogope,,sasa kama unajiamini wewe ni dume la mbegu nisogelee uuone moto unavyowaka, mjini shule,huwa hatuogopani,,sasa wewe dhubutu uone ".Aliongea Dereva kwa kujiamini sana." Kijana nasema toka nje..nimehesabu mbili,,toka njee !! ".Aliongea Albert lakini yule Dereva hakumuelewa kabisa. Sasa kimbembe kikaanzia hapo,,Albert alisimama akazipiga hatua kumsogelea hadi pale kwenye usukani.Alipomfikia akamlamba Kofi la usoni...jamaa akahisi amepigiwa kitu kama chuma." Broo unanipigia nini...unanipigia nini?? Msenge wewe ngoja sasa....".Dereva huyo akajaribu kurusha ngumi kuelekea usawa wa kifua cha Albert lakini hakikufika popote,, alishtukia tu mikono yake imekamatwa yote mithili ya chuma kilichonaswa na sumaku.Albert alimnyanyua juu juu kwa kutumia mkono wake wa kushoto akamrusha huyo jamaa kupitia dirisha la hiyo gari hadi nje usawa wa mita kama tano hivi.....Jamaa huyo alipokuja kudondoka tayari alikuwa kashapoteza fahamu.

    *****************

    Kule ngomeni kwa Mr Stanley hali ilizidi kuwa tete sana...Baada ya Kipanga kumaliza kuwachoma visu wale walinzi wawili wa getini aliwaamurisha vijana wake kwamba walipue mabomu kama matano hivi ili wawakurupushe walinzi wote wa hiyo ngome,na wakishatawanyika basi wabakize kazi moja tu ya kuwateketeza kabla hawajaanza kuchukua Mali za mle ndani ya hiyo ngome.

    ***********

    Basi Mara baada ya Albert kumtupilia mbali yule dereva tax alichukua jukumu la kukaa usukani yeye mwenyewe na kuanza kuiendesha hiyo gari huku akiwa hana hofu kabisa. Queen moyo wake ulianza kudunda akawa anajiuliza itakuaje endapo watabainika ni wao waliomfanyia vile yule dereva tax,,alijiuliza pia je itakuaje wakifika huko ,ni nani ataiijia hiyo gari ..Ama hakika maswali hayo yalimchanganya sana huyo binti.

    "Maskini baba mdogo, Mimi naogopa...sasa umempiga yule dereva harafu ukamuacha pale si hiyo itakuwa hatari? Baba mdogo tutakamatwaa!! Tafadhari baba tumrudie huyo mtu maana sipati picha kabisa, kwamba nini kitatokea, kumbuka akija kuzinduka pale anaweza akayahatarisha maisha yetu....baba mdogo Mimi naogopa kwa kweli". Aliongea Queen kwa sauti ya uoga huku akijaribu kuyaangaza macho yake huku na huko." Usiogope,,Ule msemo wa samaki mtungoni utaeleweka tu...Mimi ni mtu special huwa sikamatagwi ovyo ovyo,hata maaskari wenyewe wanalijua hilo .Mimi sikutumwa na serikali nikatalii Marekani Bali nilitumwa huko nikayapate mafunzo special ya ukomando ili nilete ujuzi Kwa wanajeshi wa huku.Sasa wote wananifahamu vizuri mno maana hawatadiriki hata kunitamkia neno lolote lile ,,wewe vuta pumzi yako vizuri kisha twende hadi huko nyumbani... Kuhusu gari,watajua wenyewe kwamba wataifataje huku".Aliongea Albert. "Sawa baba mdogo nimekuelewa maana nilikuwa na hofu sana".

    Basi safari ikaendelea hatimaye mataili ya hiyo gari yakatua moja kwa moja hadi kunako nyumba ya Imma.Waliposhuka ndani ya hiyo gari na kujiandaa kuzipiga hatua kulisogelea geti lililokuwa mbele yao, watu kadhaa wakiwemo majirani walikuwa wakiwashangaa sana.

    " Mh! Hawa watu wa wapi hawa? Yaani sijui wanaenda wapi tu..au kwenye hiyo nyumba? Harafu yule binti mbona kama namfananisha,si ndiye binti wa Imma aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela?"..."Ndiyo ndo yeye harafu amekua sana..nilisikia baba yake alikuwa amempeleka huko nchini Marekani...sasa sijui "..." Mh! Kazi ipo ,sasa hii nyumba si ilipigwa mnada na serikali ya kijiji Mara baada ya Imma kubainika amemuua Mkewe pamoja na kijana wake wa kiume?"..."Ndio ! Tena nasikia ipo katika hatua za Mwisho kabla ya kununuliwa rasmi,nashangaa hawa wanaendapo,au hawajui kwamba nyumba ishauzwa?"..."Hahaha! Labda hawajui lakini wataelewa tu".

    Hayo yalikuwa ni maongezi baina ya wamama watatu waliokuwa wakiwaangalia sana kina Albert pamoja na Queen. Basi Albert akalisogelea lile geti,alishangaa kidogo Mara baada ya kuliona kufuli kubwa limefungwa pale,akalichunguza vizuri akabaini halikuwa kufuli la kawaida.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mh! Ina maana nyumba hii imeuzwa au? Mbona hili kufuli si la kawaida,, mh! Mambo gani tena haya ? Lakini kaka yangu hawezi kufanya upuuzi kama huu ..Sasa hebu ngoja nimtafute kwenye simu.....". Kabla hajaanza kumtafuta Imma kwenye simu Mara akasikia sauti ikimwambia....

    " Chini ya ulinzi...nasema chini ya ulinzi".Albert alipogeuka nyuma yake akawakuta watu kama kumi hivi waliokuwa wamevaa nguo za kaki...alipowachunguza vizuri akabaini walikuwa ni maaskari polisi .Wote walikuwa wameshikilia bunduki mikononi mwao....."Ee mwenyezi Mungu Nifundishe Kunyamaza maana hawa watu nitawaangamiza tu".Alijiongelesha Albert kimya kimya huku akiwa amewakodolea macho.

    "Kwani nyie kina nani hadi mniambie Mimi chini ya ulinzi... Okey sipo tayari kuitii hiyo amri yenu maana nyie ni Sawa na viroboto tu kwangu!!" Alizungumza Komando Albert kwa kujiamini sana."We mpumbavu nini ,tunapokuambia upo chini ya ulinzi hatutaki utuletee uchwara wako hapa,tutakutoa utumbo sasa hivi".Aliongea Afande Swey huku akimsogelea Albert.. Sasa alipomkaribia tu alishtukia amelambwa mtama wa juu ju hapo hapo akapiga mweleka mmoja mbaya sana kwenda chini...."Pumbavu simamaa!!" Aliongea Albert kwa hasira.Sasa wale wenzake wakaziweka sawa bunduki zao kuelekea sehemu alipokuwa amesimamia Albert. "Tumeshakwambia upo chini ya ulinzi,, sasa leta ubishi wako tukibomoe hicho kichwa chako.Si unajifanya gaidi siyo...utaelewa tu" Aliongea askari mwingine. Pasipo kutarajia Mara Albert akachomoa kitambulisho chake cha ukomando na kuwaonyesha huku akiwa amekunja ndita.Ile wanakiona tu Mara wakashusha silaha zao chini na kuinyanyua mikono yao juu!!

    "Samahani afande...tulikuwa hatujui....Samahani sana". Aliongea askari mmoja na wote wakawa wamepiga magoti chini. Albert aliwaangalia,,kisha akatikisa kichwa chake na kuwaambia." Tokeni hapaa !!".Walisimama haraka haraka,,wakamshukuru kisha wakaondoka hatua kama tano na baada ya hapo wakatimua mbio.

    "Baba nakufaaa...baba nakufaaaa". Ilisikika sauti ya Queen ikilia.Albert alipogeuka tu akamkuta Queen amekabwa shingoni na jamaa moja lililokuwa na kisu mkononi .Jamaa hilo lilikuwa limevaa koti jeusi na usoni lilivaa mask.



    "We boya ! Ama ning'oe kichwa cha huyu binti au uinyoshe mikono yako juu...kabla sijaitekeleza sheria nataka uchague moja kati ya hayo mawili". Ilisikika hiyo sauti kutoka kinywani mwa lile jamaa lililokuwa limemkaba Queen shingoni. Albert alibaki amesimama tu huku akiwa hana wasiwasi kabisa...

    " Mimi huwa sibishani na wapumbavu...nataka umwachie huyo binti haraka iwezekanavyo".Aliongea Komando Albert huku akiyachezesha chezesha macho yake.Sasa lile jamaa halikuelewa likajifanya nunda.Albert akarudia tena .."We boya ! Nasema umuachie huyo binti hivi hunielewi si ndio?" Sasa Albert alipouliza tu hivyo akayanyanyua macho yake juu ghafla akaruka juu juu kuelekea upande wa nyuma kule alipokuwa amesimamie yule jamaa,alipokuja kutua tayari alikuwa kashamkaba shingoni. Albert alimpokonya kisu chake alichokuwa amekishikilia akamburuza yule jamaa hadi kwenye mti uliokuwa karibu. Kwa kutumia mkono wake wa kulia alimnyanyua juu akamweka kwenye usawa wa shina la huo mti..."Niambie wewe ni nani na umekuja hapa kufanyaje?" Aliuliza Albert kwa sauti ya kikatiri."Mi...miii!! Naitwa Master Kill nimekuja kuiteketeza hii nyumba... Brother... Brother una...unaaa...unaniumizaaa".Aliongea Master Kill huku akiwa amening'inia juu juu."Master Kill ndo nini ,acha kunitania sema jina lako...lasivyo Leo nitakung'oa shingo "...." Brother utaniuwaa...naitwa Master Kill..naitwa Master Kill"...."Pumbavu naona tunataniana,,utaelewa tu si unajifanya zuzu".Albert alimuachia jamaa akadondoka vibaya mithili ya gunia la mchanga...akamkamata tena kisha kumbamiza kwenye huo mti kabla hajamnyanyua na kumkata mtama uliomfanya apige mweleka huku akiwa ametanguliza tumbo lake .

    *******

    "Brother utaniuwa tu kwa kweli hilo ndo jina langu utaniuwa tuu!!" Aliongea Master Kill huku akigaa gaa pale chini kwa maumivu makali .Albert aliunyanyua mguu wake wa kulia uliokuwa umevikwa kiatu kisichopungua kilo tano akauweka juu ya mgongo wa Master Kill,,huku yote hayo yakiendelea Queen alikuwa amesimama pembeni akitetemeka kwa hofu,,kumwangalia yule jamaa anavyochezea kichapo."Kama hutaki kuniambia jina lako Leo utaondoka hapa ukiwa huna kichwa ".Aliongea Albert kisha akasimama kabisa juu ya mgongo wa huyo jamaa anayejiita Master Kill..Master Kill uvumilivu ulimshinda akaanza kulia kwa sauti kama mtoto mdogo huku akiwa ameutoa ulimi wake nje nje..." Nitasema...nitasemaaa....Mimi naitwa Athumani Maziku ni gaidi linaongoza kikosi cha magaidi wasiopungua ishirini hapa hapa Magomeni pia ndimi niliyesababisha hadi Imma akafungwa gerezani ".

    " Ati nini! Ina maana baba yangu amefungwa? I can't believe !! Baba yangu amefungwa kwa kosa lipi! Na mama yangu yuko wapi?".Alidakia Queen na kuyauliza hayo maswali huku akimsogelea master Kill ajulikanae kwa jina la Athumani Maziku."Ndio, Imma amefungwa tena kifungo cha maisha,, harafu mkewe sijui wanamwita Nancy! Huyo ni kitambo sasa hayupo duniani pamoja na mwanae wa kiume..sasa huo ndo ukweli wangu".Alipoongea hivyo tu ,ghafla Queen akaangua kilio cha juu huku akiruka ruka mithili ya mtu aliyechanganyikiwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mamaaa....mama! Hivi mama yangu amekufa ,ayayaaa!! Mama yangu amekufaa!! Kwa nini lakini, kwa niniii!!'.Aliyaongea hayo huku akiendelea kulia .Albert aliunyosha mkono wake wa kushoto akamshika Queen na kuanza kumtuliza.Baada ya Queen kuonekana kama ametulia japo maumivu bado alikuwa nayo .Komando Albert alimgeukia tena Master Kill na kumuuliza;

    " Ina maana wewe ndiye uliyeyasababisha yote haya ? Lengo lako hasa lilikuwa ni nini au Imma alikuwa amekukosea nini mpaka ukaamua kumfanyia vitendo vya kikatiri kama hivyo?".Master Kill aliulizwa hilo swali lakini akashindwa namna ya kulijibu akaamua Kunyamaza tu.

    *********

    Huku nyuma,,Mara baada ya wale vijana wa Master Kill kumaliza kuiteketeza ile ngome ya Mr Stanley na kuchukua kila walichokiona cha thamani...walirudi ngomeni wakiwa wamejawa na furaha kubwa sana.Walipofika hapo walipaki zile gari zao kisha wakashuka na kuanza kuzipiga hatua kuelekea ndani.Sasa cha ajabu walipojaribu kumuita boss wao ili wamkabidhi zile Mali pamoja na kumfikishia mafanikio waliyoyapata huko hakuweza kuitika.Walizunguka ndani na nje kujaribu kumtafuta lakini hawakuweza kumpata ,,walianza kuchanganyikiwa ..

    "Oyaa!! Boss ameelekea wapi wadau?". Aliliuliza hilo swali Kipanga lakini hakuna aliyejitokeza kulifafanua zaidi ya kuishia kusema " hatujui".Walishauriana mawili matatu kisha wakaonekana kukubaliana....baada ya muda kidogo, Kipanga alizunguka hadi nyuma ya ngome hiyo akaitoa simu yake ya mkononi kisha akabofya kitufe kimoja Mara cha kushoto akaiweka sikioni.

    "Haloo!! Haloo!!"... Mara simu ikakatwa.Hiyo ilizidi kumtatanisha sana Kipanga akahisi huenda boss wake huyo atakuwa amepatwa na matatizo makubwa... Alijaribu tena kubiga,kwa Mara hii simu ilikuwa ikiita tu bila hata kupokelewa...." Shitii! Boss amefanyaje?...aisee hapana,,hapa lazima kuna kitu...lazima kuna kituu ".Alijiongelesha Kipanga huku mapigo ya moyo wake yakizidi kuongezeka .Alichuchumaa baadae akasimama tena na kuanza kuzunguka zunguka pale huku akijiongelesha peke yake akazipiga hatua,akauendea mti mmoja akasimama kwa kuuegemea...hazikupita hata dakika mbili akatoka hapo na kuanza kujongea mbele. Alisimama tena akalivua koti lake refu ,,kisha akawaendea wenzake...

    " Vijana! Boss nimejaribu kumpigia simu lakini hapokei...sasa hii ni hatari,huenda ametekwa.Maana hii si kawaida yake kabisa. Hapa tusipoteze muda...tuondokeni tukamtafute boss..akili yangu imecheza machale.Aisee acheni kushangaa shangaa tuondokeniii!!".Aliongea Kipanga kwa sauti iliyoashiria kuchanganyikiwa..."Lakini boss....."Lakini nini tuondokeniii".

    ***********

    Upande wa master Kill hali yake ilizidi kuwa tete...Komando Albert alikuwa amemkaba shingoni kwa nguvu huku akimnyanyua juu na kumshusha chini utadhani alikuwa ameshikilia bua.

    "Yaani wewe umletee matatizo makubwa kiasi hiki kaka yangu? Chuki yako binafsi Ndiyo iliyokudanganya umfanyie hivi kaka yangu? Aisee hutapumzika kwa amani...hivi unajua ni kiasi gani ninavyompenda kaka yangu? Sasa utaelewa tu.Umeshirikiana na wapumbavu wenzio kumuua Nancy shemeji yangu pamoja na mtoto asiyekuwa na hatia pasipo sababu yoyote... Basi nyie wote mtafia gerezani.Wewe ,,yule hakimu mpumbavu pamoja na wenzako wote lazima mfie gerezani... Mmekosa kazi za kufanya.. Munaanza kuleta upumbavu ndani ya nchi huru ...Nawaambia mtajuta".

    Aliongea Komando Albert kisha akamnyanyua juu Master Kill akamlamba ngumi ya mdomoni na kumpelekea kutapika damu pamoja na meno matano.Master Kill akaanza kujuta huku akimlaumu shetani kimya kimya ni kwa nini alimdanganya kwenda pale..Alilia mpaka akachoka,yakabaki machozi tu kuendelea kumtiririka.

    " Kwanza hilo gereza alipofungwa Imma lipo upande upi ? Ongea haraka usitake kunipotezea muda".Aliongea Albert. "Lipo upande wa Magharibi kamandaa...shiiii". Aliongea Master Kill huku damu zikiendelea kumtoka mdomoni ." Tangulia twendee".Aliongea Albert na kumfanya Master Kill asimame juu na kujaribu kutembea kitu ambacho hakukiweza.Master Kill alihisi miguu yake imeteguka maana kila akijaribu kutembea miguu ilikuwa haimpi ushirikiano kabisa.

    "Kamanda nimeshindwa kutembea".. Aliongea Master Kill huku akianza kukaa".

    " Pumbavu! Simamaaa!! Usiniambie Mimi sijui umeshindwa kusimama....Leo utatembelea mikono...Hebu Queen mwanangu niletee hiyo fimbo".

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog