Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

NIFUNDISHE KUNYAMAZA - 5

 





    Simulizi : Nifundishe Kunyamaza

    Sehemu Ya Tano (5)



    Albert aliyaangaza macho yake huku na huko na baada ya kujiridhidha kwamba wale magaidi wametoweka kabisa katika ile ngome Albert aliyainua macho yake akamtazama Queen baadae Imma kisha akaachia tabasamu la kikomandoo akajisemea "Hawa washenzi wamaniacha sasa watajuta kuzaliwa". Baada ya Komando Albert kujisemea hayo maneno alisimama kwa nguvu na kamba zote alizokuwa amefungwa miguuni na mikononi zote zilikatika mithili ya uzi wa katani upitishwapo kwenye miali ya moto.Aliposimama,alikibeba kile kiti kwa kutumia mkono mmoja akakirusha juu na kilipokuja kutua chini alikipokea kwa kutumia kichwa na baada ya hapo akakikunja kunja na kukitupa juu ya bati moja lililokuwa karibu maana kiti hicho kilikuwa cha chuma .Alisimama wima akavitengeneza vizuri viatu vyake vyenye uzito wa kilo tano akaanza kuzipiga hatua za pole pole akawasogelea kina Imma walioonekana kupigwa na bumbuwazi akasimama mbele yao na kuwaambia " Tuondokeni hapa maana Nina kazi kubwa sana ya kuifanya hapo mbeleni hivyo tuondokeni".Komando Albert alipomaliza kuyaongea hayo alianza kuyaangaza macho yake huku na huko kuona kama kuna usafiri wa aina yoyote ambao angeutumia,,kwa bahati nzuri wakati anaendelea kufanya hivyo alikuja kuiona gari moja nyeusi ndogo aina ya Toyota T246 akaisogelea na kujaribu kuikagua kagua.Alipochungulia ndani ya hiyo gari alikuja kugundua kwamba funguo zilikuwemo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    "Kaka Imma pamoja na Queen nawaomba mje hapa tupande ndani ya gari hii harafu tuondoke hapa Mara moja,,mambo mengine mtaniachia Mimi nitajua cha kufanya". Aliongea Komando Albert ,Imma alionekana kusita kuikaribia ile gari lakini alipoitwa tena kwa Mara nyingine hakuwa na kipingamizi,,alisogea huku akitetemeka na baada ya kuifikia hiyo gari aliingia hadi ndani.Queen nae hakubaki nyuma,alifika hapo akapanda na Komando Albert akawa wa mwisho kupanda ndani ya gari hiyo.Sasa alipohakikisha hao ndugu zake wameshapanda ndani ya gari hiyo,,,aliisoma vizuri ramani ya ile ngome akaiweka kichwani kisha nae akapanda humo na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza .Safari yao haikuwa ndefu sana maana walitumia kama muda wa dakika kumi na tano tu wakawa wamefika.Walipofika walishuka na kuanza kuingia moja kwa moja hadi ndani ya geti hilo ,,naam waliingia ndio maana zile funguo za ule mlango wa geti kumbe alikuwa nazo Imma mwenyewe.Basi walifanikiwa kuingia hadi ndani ya nyumba yao hiyo wakakuta bado mambo si mabaya.Kwa vile kila kitu kilikuwa sawa hakuna hata kimoja kilichokuwa kimeharibika...vyote vilikuwa sawa.Walipumzika kidogo na baada ya dakika kumi Komando Albert aliwaaga akaanza safari ya kuelekea benki kwa ajili ya kutoa pesa pamoja na kununua mahitaji mengine ya mhimu.
    *****************
    "Ayayaya!! Wajameni tumekwisha,,yule jamaa tumemuacha peke yake kule ngomeni!! Aisee tumekwisha". Aliongea Kipanga baada ya kugundua kwamba wamemuacha Komando Albert peke yake pale ngomeni bila ya kumuacha mlinzi yoyote.Waliifahamu vizuri shughuli ya Komando ilivyo na ndio maana Kipanga aliongea hivyo." Kipanga sasa tutafanyaje? Wewe ndiye uliyetuvuruga kumbuka kabisa ndugu yangu.Yule mtu ni hatari kwa nilivyomuona siku ile anawashushia kichapo wale maaskari mpaka wakatoka nduki...sasa tunafanyaje? Pendekeza cha kufanya Kipanga maana wewe ndie boss wetu kwa sasa".Aliongea kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Martin."Ah! Unaponiambia nini cha kufanya aisee nitakushangaa sana maana kipindi tunaondoka tuliondoka wote na hatukuacha mtu huko ngomeni sasa tusilaumiane maana hatuna namna.Labda tufanye hivi,,tutume vijana wawili wakaangalie huko ngomeni kama watamkuta huyo jamaa".Aliongea Kipanga. "Ulichokiongea ni sahihi kabisa, lakini una uhakika wakienda hao vijana unafikiri watamkuta? Kumbuka tuliwaacha watu watatu huko na wengine walikuwa hawajafungwa chochote...sasa sidhani kama watawakuta,,hapa labda tuanze tu kujiandaa kisaikolojia namna ya kupambana ya huyo jamaa maana najua hata yeye alichukizwa sana na kile kitendo tulichomfanyia na ninavyojua lazima jamaa atalipiza kisasi tu". Aliongea Martin huku akimwangalia Kipanga kwa wasiwasi sana." Ah..ah!! Huu ushenzi sasa,,hivi kwa nini tuliondoka kienyeji kiasi hicho daah!! Sijui tufanyaje tu maana nahisi petroli itaturipukia sasa".Aliongea Kipanga huku akionekana kuchanganyikiwa kabisa. "Oya tuacheni sasa basi kumbukeni hapa tupo barabarani tunaelekea hospitalini kuufata mwili wa boss wetu Master Kill,,,kama vipi kanyaga gia hapo twenzetu hayo mengine tupilia mbali". Aliongea kijana mwingine aitwaye Mshama." Oya we jamaa acha uboya basi wewe unaona kabisa hapa tunatafuta namna ya kumkabiri yule jamaa harafu wewe unatuletea ukuku hapa...au tukupige chini uchape lapa?".Aliongea Kipanga. "Sasa Mimi ninavyoona hapa mnatwanga maji kwenye kinu labda tuombe tu tuikute ngome yetu ipo salama ila tukisema sijui tumkute huyo jamaa hilo haliwezekani kabisa.. Sasa cha msingi hapa twendeni tu ,baadae tutajua cha kufanya". Aliongea Martin na baada ya kuonekana kukubaliana kwa hilo ,Kipanga aliiendesha hiyo gari hadi wakafika huko hospitalini wakamkuta Manka akiwasubilia kwa hamu.Baada ya kuzungumza mawili matatu na wale madaktari...mwili wa Master Kill ulipelekwa hadi chumba cha kuhifadhia maiti na mipango mingine ya masuala ya mazishi wakaanza kupanga wakiwa hapo hapo hospitalini.
    Baada ya kumaliza kupanga mipango yao hiyo .Manka aliungana na wenzake hao wakaanza safari yao ya kurudi ngomeni. Walipofika huko kweli hawakumkuta Komando Albert pamoja na ndugu yake Imma,,walikuta tu vipande vya kamba vilivyokatwa katwa na hawakujua hata cha kufanya wakabaki kushangaa sana.Walizunguka huku na huko kuwatafuta labda watabahatisha kuwaona lakini jibu likabakia lile lile tu kwamba wameshasepa tayari.Baadae Kipanga akaonekana akijikuna kuna kichwani huku akitembea kwa wasiwasi kuelekea sehemu moja iliyokuwa na mti aina ya mbuyu.Alifika hapo akasimama kama mwendawazimu akaushika huo mti kisha akaanza kujiongelesha peke yake huku akianza kujikuna kuna mgongoni na kiunoni."Daah! Jamaa limeshakimbia,sijui tutalipatia wapi tu! Boss wetu kashatoweka duniani,, yaani ni hasara juu ya hasara...labda..labdaaa ah!!".Kipanga alishindwa aongeaje aliona kama anapoteza muda tu pale.Aliondoka hapo akaanza kuizunguka ngome yote huku akijiongelesha peke yake asifikie hata mwafaka wa nini cha kufanya. Baada ya kurudi kwa wenzake alimwita Manka Pembeni akaanza kuzungumza nae maneno mawili matatu,
    "Manka hali imeshakuwa tete sana...ningependa tumzike boss haraka iwezekanavyo ili tujiandae kwa lolote maana tumeshachokoza nyuki". Aliongea Kipanga huku akitoa kitambaa chake na kujifuta kijasho kilichokuwa kikimtoka usoni." Kipanga sijakuelewa! Unasema tumechokoza nyuki,,tumechokoza nyuki wa aina gani hao?" Aliongea Manka huku akimkazia macho Kipanga. "Manka kuna lijamaa limoja sijui likomando tuliliteka tukajisahau tukaliacha peke yake kipindi tunakuja huko hospitalini sasa hatuna cha kufanya na hatujui tutafanyaje,,ila lazima tujipange.Harafu inasemekana hilo jamaa ni li ndugu yake na Imma"...." What!! What!! Ndugu yake na Imma? ".
    ***********************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Upande mwingine alionekana Komando Albert akimalizia kuzipiga hatua baada ya kuifikia nyumba ya kaka yake Imma ,,,Mkononi alikuwa ameshikilia briefcase moja kubwa ambayo sikujua ilikuwa imewekewa nini ,,huo ulikuwa ni ule muda wa kutoka benkini alipokuwa ameenda.Basi akaingia ndani ya kumkuta Queen amekaa sebuleni... Alikuwa amejishika shavuni na ilionekana alikuwa na wazo furani." Mwanangu Queen mbona una mawazo mengi hivyo? Punguza mawazo,kumbuka wewe bado binti mdogo sana sasa unapowaza hivyo utazeeka mapema sana na utakonda".Aliongea Albert huku akimsogelea Queen na kumshika begani ."Kawaida tu baba maana haya mambo acha tu".Aliongea Queen. "Acha kuwaza utakonda...nimeshasema hayo mambo niachieni Mimi yaani nibebesheni mgongoni nitajua cha kufanya.. Si Mimi ni Komando bhana". Aliongea Albert." Ehee!! Vipi baba yako ameenda wapi?" Aliuliza tena Komando Albert. "Baba yupo chumbani amepumzika". Alijibu Queen. Baada ya hapo waliongea mambo mengine mpaka usiku ukaingia Walipata chakula cha usiku wakaenda kupumzika .
    Siku iliyofuata Komando Albert aliamka asubuhi na mapema akavaa vesti nyeusi ya Kikomando akatoka nje na kwenda hadi uwanja wa wazi kupiga mazoezi ya kufa mtu.
    Alipofika ndani ya huo uwanja ,alitafuta mafiga ya mawe yapatayo manne yaliyokuwa tambalale.Akayapanga mawili mbele na mawili nyuma.Alipomaliza alilala akaiweka mikono yake kwenye yale mafiga mawili na miguu yake akaiweka juu ya mafiga yale mawili mengine.Alikunja ngumi akaanza kupiga pushapu.Alipiga pushapu zaidi ya hamsini bila kupumzika baada ya kulimaliza zoezi hilo alisimama .Alichukua tofali la kuchomwa akalirusha juu na kulipiga ngumi moja hewani hewani likasambaratika lote.Baadae alienda hadi kwenye rundo moja la kokoto akaanza kupiga pushapu pale kwa kutumia vidole huku misuli yake ikiwa imetuna hatari...Alipomaliza alizipiga hatua za haraka haraka hadi kwenye ukuta mmoja wa nyumba iliyobomoka,,akausogelea na kuupiga ngumi moja tu hapo hapo huo ukuta ukaanguka.


    Komando Albert alipomaliza kuuangusha ule ukuta kwa kutumia ngumi ,,aliangua kicheko cha dharau kisha akazipiga hatua za haraka haraka hadi kwenye mti mmoja uliokuwa na upana wa sentimita mia moja na hamsini ,aliusogelea na baada ya kuufikia alianza kuurushia ngumi za haraka haraka mpaka ule mti ukakaribia kuvunjika maana ilikuwa ni zaidi ya hatari .Alipolimaliza hilo zoezi alirudi tena kwenye lile rundo la kokoto akajitupa kwa nguvu huku Mara hii akiwa kifua wazi akaanza kujiviringisha mithili ya taili huku akicheka utadhani mwendawazimu .
    "Baba chai tayari nimeshaivishaa!!".Hiyo ilikuwa ni sauti ya Queen Mara baada ya kumaliza kuandaa chai na kisha kutoka nje kumjulisha baba mdogo wake huyo ." Ah! Queen mwanangu nadhani wewe utakuja kuwa mwanajeshi sasa kama nilivyo Mimi baba yako.Yaani kufumba na kufumbua umeshamaliza kuandaa chai !! Au umetuandalia chai maji nini ?".Aliuliza Albert huku akinyanyuka baada ya kumalizia kuzipiga pushapu zaidi ya sitini."Ah! Acha hivyo babaa,tangu lini Mimi nikaandaa chai au chakula kibichi..appreciate kazi yangu baba bila shaka utaipenda,we njoo tu uone".Aliongea Queen. "Sawa! Yote kwa yote tutaona kama ukizungumzacho ni cha kweli ama laa ".Aliongea Albert, baada ya maongezi hayo kumalizika ,Albert aliinyanyua mikono yake juu kuashiria ameikamilisha kazi kisha akaishusha chini na kuanza kuzipiga hatua kuingia ndani kupata chai .Kweli chai ilikuwa ni nzuri pamoja na vitafunwa vyake hivyo walikunywa na mambo yote yakaenda sawa sawia .Maongezi ya hapa na pale nayo yaliendelea; " Mdogo wangu unajua hadi dakika hii siamini kabisa kama umenitoa kuzimuni maana maisha ya kule gerezani ni kama jehanamu kabisa,, kiukweli yalinitesa na kuniumiza sana".Aliongea Imma wakati anamalizia kuibugia chapati moja iliyokuwa imebakia."Ah!! Usijali kaka unajua wewe ni kama mzazi wangu kwa sasa kwa hiyo siwezi kukubali kuona unateswa na kuonewa ovyo ovyo wakati na Mimi nipo,,niliapa tangia zamani nitakuheshimu na nitakulinda na haya ndo matokeo yake .Bora nife Mimi kwa kukuokoa kuliko ufe wewe maana sitaishi kwa amani duniani ". Aliongea Komando Albert huku akijilazimisha kutabasamu." Yaani afadhari kabisa maana kule sipakuomba kule ni jehanamu,,nadhani wote walionifanyia kile kitendo watakuja kukilipa na mabaya yote lazima yatawarudia tu".Aliongea Imma,,basi waliendelea na maongezi mengine tofauti wakafurahi na kufarijiana mpaka wakachoka na kuamua kupumzika maana kwa muda huo tayari yalikuwa ni majira ya saa sita za mchana.
    *********************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    "We mpumbavu hivi utaendelea kukaa kimya mpaka lini ! Hujui kwamba Mimi nina mamlaka ya kukufunga au kukuachia! Sasa nakuuliza kwa Mara ya mwisho...ni nani aliyemruhusu Komando Albert aje au aingie ndani ya maeneo ya gereza? Hii ni Mara ya mwisho ukishindwa basi utafia gerezani". Hiyo ilikuwa ni sauti ya hakimu kipindi anamhoji afande Swey aliyekuwa amepandishwa kizimbani kwa kutokuzingatia sheria na kanuni za Magereza kama Mkuu wa kitengo hicho.Muda wote huo afande Swey alikuwa amekaa kimya tu,si kwamba alipenda akae kimya Bali ilimbidi afanye hivyo maana hakuwa na kitu cha kujitetea.Alizitafuta sababu za kujitetea lakini zote zilimkimbia na kukiacha kinywa chake kikiwa hakina hili wala lile." Ah! Nina...ninaaaa.....Ah!!".Alijaribu kuongea lakini akashindwa na kumlazimu kunyamaza tu kimya kukubali lolote litakalo mpata basi na liwe .Hakimu hasira zilimpanda akachoka kumbembeleza ikamlazimu asimame tu kutoa maamuzi.
    "Ndugu Swey Abdala tumejaribu sana kukusihi utueleze ukweli kuhusiana na lile tukio lakini umeshindwa kutupa ushirikiano.Sasa mahakama inakuhukumu....kutokana na vifungu na ibara za katiba ya jamhuli ya muungano ya mwaka elfu sabini na saba,,inasema endapo mtuhumiwa atashindwa kutoa maelezo yaliyo sahihi kuhusiana na kile anachoshitakiwa basi mahakama itamweka katika kundi lile lile la waharifu hata Kama alikuwa na haki .Kwa vile ndugu Swey ameshindwa kuiambia mahakama kuhusiana na kitendo cha wafungwa kutoroka na kukimbia gerezani inaonyesha ukweli halisia alikuwa akiufahamu lakini akashindwa kuieleza mahakama,,, bila vipingamizi na vizuizi vyovyote vile inaonekana Ndugu Swey,,alikula rushwa.Sasa huo mzigo wa wafungwa wote waliokimbia ataubeba yeye mwenyewe.Leo tarehe 25/8/2017 namhukumu kifungo cha maisha gerezani ndugu Swey Abdala na adhabu hiyo akaanza kuitumikia Leo ".
    " Ayayayaaa!! Hakimu nina swaliiii"...."Funga domo lako swali la nini wakati umeshahukumiwa...tangulia gerezani pumbavuu ".
    *******************
    Upande mwingine lilionekana kundi kubwa la magaidi wakiwa wamekusanyika katikati ya msitu wakijiandaa kuupumzisha mwili wa aliyekuwa kiongozi wao wa muda mrefu.Magaidi hao hawakuwa wengine Bali walikuwa ni hao hao kina Kipanga na wenzake wakati wakijiandaa kumzika jemedari wao Master Kill aliyefariki dunia.Sijui Komando Albert alifika fikaje tu pale.Sasa wakati wanaendelea na taratibu zao za mazishi muda huo Albert alikuwa amepanda juu ya mti mmoja wenye matawi na majani mengi akiendelea kuwasikiliza.Nguo alizokuwa amezivaa zilifanana sana na hayo majani hivyo kuwa kazi ngumu kutambua uwepo wake eneo hilo .
    " Jamani hizi ndizo heshima zetu kwa boss.Master Kill ama hakika wewe ulikuwa master japo umetutoka lakini hatutokusahau.Leo tunaenda kukuhifadhi ndani ya nyumba yako ya milele na hatutakuja kuonana tena labda tubahatike kuonana huko ahera.Tunakutakia maisha mema huko uendako lakini....? ".Kabla Kipanga hajalimalizia hilo neno Mara walishtukia kikidondoshwa kisu kutoka juu pasipo kufahamu aliyekidondosha.Wote waliingiwa na hofu kubwa sana iliyowafanya wayatoe macho yao kwa mshangao.Kile kisu kilichozama na kusimama ardhini wima kiliwashtua sana.
    " Oya nani katupa kisu hapa..nani katupa kisuuu?" Aliuliza Kipanga huku akiyainua macho yake juu...,"Hatujui boss...hatujuii".Walijibu kwa pamoja. Manka nae hakuwa na cha kufanya alibaki tu kuyakodoa kodoa macho yake .Sasa wakati wanaendelea kufanya uchunguzi ni nani aliyekitupa kile kisu Mara kijana mmoja aliyekuwa amesimama upande wa nyuma alisikika akitoa sauti ya uchungu;
    "Jamaniii..jamaniii...nakufaaa...nakufaaa!!.Kipanga alipogeuka na kumwangalia huyo kijana aliukuta mshale mmoja ukiwa umemdunga mgongoni na kutokea tumboni." Haaaaa!! Haaaaa!! Jamani hatariii".Mshama alipoongea tu hivyo Ghafla Komando Albert aliruka kutoka juu ya ule mti hadi chini na kutua katikati yao huku sura yake ikiwa imejaa vitu vyeusi mithili ya mkaa.
    "Wote chini ya ulinziiiiii".Albert alipolitamka tu hilo neno,Magaidi wote akiwemo Kipanga walitimua mbio kila mtu njia yake wakauacha mwili wa boss wao Master Kill ukizagaa pale.Yule kijana aliyedungwa na ule mshale alidondoka chini akapoteza maisha hapo hapo.
    " Mamaaaaa...mamaaaaa!!! Nisaidieeeee mamaaaaaa!!.Manka alibaki nyuma akikimbia huku akigeuka geuka nyuma wakati huo akiyatoa hayo maneno. Alikimbia kama hatua kumi tu hivi,,,akajikwaa na kudondoka chini.


    Manka alihangaika sana kunyanyuka pale chini alipokuwa ameangukia,,alijaribu kujikokota kokota akafanikiwa kusogea kama hatua mbili mbele, baadae akabonyea tena chini na kumbidi atulie tu maana nguvu nazo zilianza kumwishia na presha ikaanza kumpanda.Manka alipogeuka nyuma na kumkuta Komando Albert akimfuatia kwa mwendo wa kunyata nyata huku akiwa amevaa gwanda la kijeshi suruali yake na mkoti kama vesti wa kikomando uliokuwa umetuna alianza kutapatapa pale chini huku akijitahidi sana kunyanyuka ili aweze kukimbia kitendo ambacho hakikufanikiwa.Ghafla akaangua kilio cha juu;
    "Mamaaa...mamaaa!! Siyo mimiii...siyo mimiii!!". Manka aliyaongea hayo maneno na kujikuta mwili wake ukianza kulowa jasho wote mithili ya mtu aliyemwagiwa maji.Suruali yake aina ya jenzi aliyokuwa ameivaa alianza kuiona kama haimtoshi vile.Huku nyuma Albert aliendelea kumkaribia bila hata kumwongelesha chochote, yeye alikuwa amenyamaza tu.Alipomfikia pale alisimama pembeni yake akaanza kumtazama,,alimtazama kwa umakini sana kisha akaufungua mdomo wake na kumwambia;
    " We mwanamke upo chini ya ulinzi,na kama unayapenda maisha yako naomba usimame juu na uinyoshe mikono yako...tii sheria bila shurutii,ila ukijifanya we ni mbegu la jike basi sitaona tabu kuyanyofoa mananihii yako hayo.Sina mjadala ninachotaka ni utekelezaji".Aliongea Albert kwa sauti ambayo hata wewe ungeisikia basi usingeuzuia mkojo usikutoke,Komando Albert alichomoa kisu kimoja kilichokuwa kiking'aa sana akakinyoosha na kumwonyesha binti huyo aliyekuwa akitetemeka kupita kawaida."Unaiona hii kitu,,sasa leta ubishi uone,,yaani hapa nilipo sicheki na nyani nacheka na silaha..ukijifanya mjuaji natoboa hayo makitu yako harafu nawapa mbwa,haya simamaa!!".Aliongea Albert na kuzidi kumwogopesha Manka,,Manka alitamani ardhi ipasuke immeze lakini kitu hicho kikawa ndoto tu mbele ya ufahamu wake.Huku akitetemeka alisimama na kwa Mara hii miguu yake ilianza kucheza cheza kama amekunywa pombe tena ile ya kienyeji kabisa. Aliinyanyua mikono yake juu akayainamisha macho yake chini kwa woga kisha akatulia na kusubiri kitakachozungumzwa na Komando.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    "Haya pita hukuu ...sogeaa..sogeaa,,hapo hapo.Sasa nataka uniambie wewe ni nani na hapa ulikuja kufanyaje,nakupa dakika mbili tu". Aliongea Albert." Mimi na..naa..naitwa Mank ...naa..naitwa Manka,nii..ni..niii..ni mtoto wa Mr Stanley ".Aliongea Manka kwa kigugumizi huku akiendelea kutetemeka kwa hofu." Hujamalizaa!! Au unataka ubonyee chini sasa hivi?" Aliuliza Albert na kuzidi kuyahamisha kabisa mafaili yote ya Manka."Nisamehe kaka nisamehee".Aliongea Manka."Nikusamehe kwa lipi toa maelezo yaliyonyooka,acha upumbavuu!!".Albert alipoongea hivyo alimsogelea akamtwanga mtama mmoja wa hewani hewani ,Manka akajikuta akidondoka chini kama gunia la mchanga.Albert huku amenuna alimsogelea tena na kusimama mbele yake ."Bado umekaa tu hapo chini,,simama hii ni dawa ya kitoto tu yaani utaelewa tu,,kabla sijayavuta hayo manywele yako sitaki niongee harafu unaniangalia tu simama".Komando Albert aliongea lakini Manka akaendelea kukaa tu huku akianza kulia ."Nadhani tunataniana,unadhani Mimi ni mume wako sivyo? Subirii".Albert alimnyanyua kwa nguvu akampiga Kofi la usoni lililomfanya akokoe na kutapika damu.Uweupe wake ulianza kubadirika na michirizi kama ya damu ikawa imejionyesha dhahili usoni mwake ."Haya ongea wewe huwa unafanya kazi gani hapa au huwa unajiuza kwa hawa wapumbavu? Si bado binti mdogo kabisa wewe ? Zungumza acha kupenga kamasi ovyo ovyo".Aliongea Komando Albert. "Kiukweli Mimi sikupenda kujiingiza katika hili kundi la kigaidi ila niliingizwa kwa kulazimishwa na Mjomba wangu huyu aliyefariki kwa kunitishia kwamba angeniua endapo ningekataa,,huyu Mjomba aitwaye Master Kill!"..." Master Kill?".Aliuliza Albert kwa mshangao."Ndio alikuwa akipenda sana kujiita jina hilo ,sasa alinilazimisha Nikiwa binti wa miaka kumi na sita tu akawa ananitumia kama chambo cha kufanikishia mipango yake ya kigaidi na alinikataza katakata nisimwambie baba wala mama kuhusiana na tabia yake hiyo kwa kutishia kuniua.Sasa kwa woga wa kuyalinda maisha yangu nikaona bora ninyamaze tu kuliko kuongea na kuangamia.Hata Mimi nilijuta sana kuwa katika kundi hili lakini sikuwa na ujanja wa kujinyofoa hivyo ndo maana unaniona nipo hapa.Huyu Mjomba pamoja na kumzoea alinitesa sana maana ilionekana kama Mimi si mtoto wa Dada yake ,,ilifikia kipindi akawa ananivua hadi nguo na kunifanya kama mke wake pamoja na kunifundisha kuvuta bangi lakini hiyo bangi ilinishinda nikaachana nayo hadi sasa Nikiwa na huu umri wa miaka ishirini na miwili ".
    Manka alipomaliza kuyaongea hayo roho ya huruma ikamwingia Komando Albert akatambua kuwa kumbe huyo binti hakupenda kujiingiza katika hilo kundi bali alilazimishwa." Kaka nisamehe nakuahidi sitayarudia tena haya makosa ".Aliongea tena Manka ." OK Mimi nimekusamehe,haya tuondoke ndani ya huu msitu maana unatisha".Komando Albert alipoongea hivyo alimshika Manka kwa kutumia mkono wake wa kulia akaanza kukimbia nae kuelekea upande wa mbele. Sasa walipoziacha hatua kama kumi kutoka nyuma Mara uso kwa uso na vijana watatu wa master Kill,ambao ni Alfred, Jay na Mshama .
    *********************
    "Hahahaha!! Nadhani kila siku ule msemo wa mbio za sakafuni huwa zinaishia ukingoni,,sasa nadhani huu msemo umetimia.Upo chini ya ulinziii". Aliongea Mshama huku akiwa ameinyoosha tayari tayari bastora yake ." Nani yuko chini ya ulinzi hapa?". Aliuliza Komando Albert kwa kujiamini.Sasa akiwa hajui hili wala lile ghafla nyuma yake akamiminiwa risasi kama tano mgongoni na mtu ambaye hakumwona miongoni mwa wale vijana. Komando Albert alidondoka chini na hapo hapo akaonekana Martin akizipiga hatua kutokea upande wa nyuma huku akicheka kwa dharau .
    "Manka umetusaliti si ndio?". Aliuliza Martin huku akimshika Manka begani baada ya kumkaribia.Manka alinyamaza kidogo akawa anamwangalia Komando Albert pale chini jinsi anavyojigeuza geuza kwa uchungu,huku akimhurumia.
    " Mimi sijawasaliti nyie,tuko pamoja kabisa".Aliongea Manka na kumsogelea Martin kisha akamshika mabegani.Sasa wakati amemshika hivyo alimtabasamia kisha akamwibia na kumpiga goti la tumboni lililomfanya Martin adondoke chini na kuiachia bastora yake aliyokuwa ameishikilia.Haraka haraka aliichukua ile bastora akaiweka mikononi mwake na kuwanyoshea hao vijana.
    "Shusheni silaha zenu chinii ..sitanii". Aliongea Manka huku akiwa amewabadirikia kabisa." Aaaa!! Manka umetusaliti au unatutania?".Aliongea Jay huku akiwa haamini kabisa kama huyo binti kashawasaliti.
    "Siongei na mbwa na ongea na mwenye mbwa..Mimi kwa sasa si mwenzenu tena,hivyo....?" Wakati Manka hajaendelea alishtukia amepigwa na kitu kama kiwiko mgongoni mwake kilichomfanya aende chini na kuanza kugaa gaa.Kumbe wakati anaendelea kuwashurutisha kina Jay wanyanyue mikono juu ,Martin alisimama huku akiwa amejawa na hasira akampiga mgongoni. Sasa wakati Manka anataabika pale chini,Martin alimsogelea akamnyanyua juu na kumshinga shingoni.Alimsukuma hadi kwenye mti akambana hapo kisha kuanza kumpiga ngumi na makofi maeneo tofauti tofauti ya mwili wake ."Jamanii ..niachiee".Manka alijitahidi kujinasua mikononi mwa Martin lakini akashindwa."Hahahah!! Unajifanya wewe msaliti ee ? Sasa ngoja nikuonyeshe kazi ".Baada ya Martin kuongea hivyo,alimbeba Manka juu juu akambwaga chini na kumfanya apoteze fahamu huku damu nazo zikianza kumtoka puani na mdomoni.Martin aliichukua ile bastora akaikoki na kuinyosha kuelekea usawa aliokuwa Manka.Sasa kabla hajafanya chochote, Komando Albert alinyanyuka pale chini mzima mzima akaruka na kwenda kumpiga teke moja la kifuani lililomfanya ahisi ardhi yote imetapakaa damu.Martin alidondoka chini akawa anagaa gaa huku akihisi huenda kifua chake kimepasuka.
    Wale kina Jay walipoiona hiyo hali walishtuka sana wakaanza kukimbia ovyo ovyo,maana walidhani huenda Albert akawa si binadamu wa kawaida,kutokana na kuamini kwamba alikuwa ameshafariki.
    Albert alimsogelea Martin akaunyanyua mguu wake wa kulia uliovikwa kiatu kisichopungua kilo tano kisha akamkanyaga kwa nguvu kifuani .
    ******************
    Muda huo huo alionekana Kipanga akikimbia ovyo ovyo peke yake kuelekea ngomeni kwao akipitia ile ya msituni.Alipiga kona moja Kali lakini ya pili yake akajikuta akipiga mweleka mmoja hatari uliomfanya adondokee korongoni na kwenda kukibamiza kichwa chake kwenye rundo moja la kinyesi na kuwa kizaa zaa!!.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    "Mh nipo duniani ama jehanamu? Mbona nimebaki peke yangu mithili ya mtoto yatima! wenzangu wapo wapi mbona siwaoni?". Hayo maswali alijiuliza Kipanga huku akitafuta majani na kuanza kukipangusa kile kinyesi ambacho tayari kilikuwa kimeshashikamana kichwani mwake .Taratibu alinyanyuka akalivua koti lake na kulitupilia mbali akabaki na vesti tu kifuani akatoka haraka haraka mle korongoni na kuanza kutimua mbio kuelekea ngomeni.
    Upande mwingine walionekana vijana wengine kadhaa wa Master Kill wakibishana na kurushiana lawama za hapa na pale baada ya kukimbia kwa muda mrefu siku ile walipokutana na balaa kule ngomeni.
    " Ah! Washkaji hivi hii ngome inatupa faida gani aisee? Mi ninavyoona ni bora tuachane nayo tu harafu tupambane na hali zetu au vipi wadau?"..."Kweli kabisa broo kwanza kwa sasa hivi hatuna chetu pale zaidi ya kujitafutia balaa tu,,kwanza mtu mhimu tuliyekuwa tukimtegemea ndo hivyo tena kashatangulia mbele ya haki kule msituni,kwa hiyo tubadirikeni tu wadau tukajaribu kuwa raia wema katika hii nchi"..."Okey ulivyoongea bwana kaka ni sahihi kabisa na alivyoongea huyo bwana mdogo ni sahihi lakini swali la kujiuliza ni hili jamii itatuchukuliaje tukifika huko ? Maana huu ugaidi tuliokuwa tukiufanya ulikuwa ukijulikana sana,sasa labda tushauriane hapo tufanyaje?"..."Ah! Mimi najilaumu sana sijui ni nani aliniroga tu nijiunge na hilo kundi la kipumbavu, nadhani haya yote yasingenipata,lakini siyo mbaya siku zote kufanya kosa si kosa ila kurudia kosa hilo ndo kosa lisilovumilika,,tumefanya uhalifu wa kutosha,tumeibia sana watu na tumeua sana sasa yatosha huu ndo muda mwafaka wa kutubu na kujipanga upya kwa safari nyingine ya matumaini katika hii dunia "....." Mi nadhani tutakuwa wajinga wa kutupwa endapo tutashindwa kumtafuta Imma na kumwomba msamaha kwa upumbavu wote tuliomfanyia ili atusamehe maana hakuna kitu kiletacho furaha na maelewano katika hii dunia bila kusameheana"..."Umeongea point broo kule ngomeni hatuendi,ugaidi tumeuacha kilichobaki ni kuanza kupambana na maisha yetu kupitia jasho letu wenyewe na si kuibia watu.Huko tuendako tukajitahidi sana kuishi vizuri na watu,,zaidi tusiwe watu wa visasi...tuilinde amani ya nchi yetu tuliyojaliwa na mwenyezi Mungu ".
    Baada ya vijana hao kuyamaliza mazungumzo yao walighairi kurudi tena kule ngomeni kwa master Kill wakakata shauri ya kurudi kwenye jamii kuiomba msamaha ili iwasamehe na zaidi washirikiane kwa pamoja katika kuijenga nchi yao.
    *****************
    Baada ya Komando Albert kuhakikisha amemwangamiza gaidi yule ajulikanae kwa jina la Martin, alimbeba juu juu akalitafuta pango moja akautupa humo mwili wake,, aliurudia na ule mwili wa Master Kill uliokuwa ndani ya jeneza akaubeba na kuupeleka hadi mle pangoni,,baada ya kuziba hilo pango kwa kutumia jiwe kubwa alirudi akambeba Manka na kuanza kuelekea mbele. Hatua tano mbeleni akakumbuka kitu,,,alimshusha Manka aliyekuwa amezirai akatoa mabomu kama mawili hivi akayarusha kwenye ile ngome ,akambeba tena Manka na kuanza kudondoka ndani ya hiyo ngome huku akiuacha moshi mzito ukizuka hewani kuashiria kwamba ile ngome imesharipuka yote.Aliondoka muda huo huo akampeleka Manka hospitalini kupatiwa matibabu.
    *****************
    Upande wa Kipanga, wakati anaendelea kukimbia kuelekea ngomeni kwao alihisi amechoka,,sasa ile ana si mama tu ili kupumzika kidogo ghafla akawaona kina Mshama wakikimbia kuelekea upande wa kushoto...
    "Mshama.. Mshamaaa...Jay...Jay". Aliita Kipanga huku akiwa amepigwa na butwaa.Kina Mshama wakasimama na kuanza kuzipiga hatua kumsogelea ,walipomfikia walikuwa wakihema sana kuashiria kwamba walikuwa wamekimbia kwa muda mrefu." Kipanga kwa kweli kuanzia ..kuanzia muda huu usituhesabu sisi kama wanakikundi wako,, kwa tuliyoyashuhudia tuache tu tuendelee na safari yetu".Aliongea Jay huku akiwa amechanganyikiwa kabisa. "What!! Acheni upuuzi wa kiboya,,nyie ni vijana wangu na mtabaki ndani ya ngome yangu milele, Mimi ndiye nitakayeichukua nafasi ya Marehemu Master Kill mpende msipende!!". Aliongea Kipanga kwa sauti ya kumaanisha." We msenge tu nenda huko ngomeni peke yako sisi usituambie".Aliongea Mshama na kumkasirisha sana Kipanga,,, Kipanga bila kuuliza Mara mbili mbili aliichomoa bastora yake akawamiminia risasi wote watatu akawaangamiza kabisa kisha akaitupa ile bastora na kuendelea kupiga mbio kuelekea huko ngomeni.
    Kipanga hakutaka kuyaamini kabisa macho yake kwa alichokuwa akikiona mbele yake .Ngome yote ilikuwa ikiteketea kwa moto na hakuna kilichokuwa kimesalia pale vyote vilikuwa vikiteketea kwa moto,,Kipanga alijaribu kuyaangaza macho yake huku na huko kuona labda atampata mwenzake hata mmoja lakini haikuwa hivyo..Bali alikuwa amebaki peke yake .Alienda hadi pale alipouacha mwili wa boss wake Master Kill napo hakuuona.Huzuni ilimtanda na kumfanya aikose kabisa furaha ya hapa duniani. Kipanga alichuchumaa na kujikuta akitiririkwa na machozi machoni mwake ambayo hakuyafuta hata kuyafuta.Alinyanyuka akatoa kisu alichokuwa amekihifadhi mfukoni akaongea neno moja tu la "Bora nife ". Kisha akayafumba macho yake na kujichoma kisu tumboni akaanguka chini na kugaa gaa kidogo tu baadae akatulia tuli,na hapo hapo akayafumba macho yake na kuipa mkono wa kwa heri dunia. Huo ukawa ndo mwisho wa maisha ya Kipanga hapa duniani.
    ******************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zilipita siku tatu mfululizo hatimae hali ya Manka ikatengemaa na akapona kabisa ." Albert asante kwa kuyaokoa maisha yangu, nilikuwa hatarini lakini wewe umejitahidi kwa kadri uwezavyo kuniokoa..asante sana".Hayo maneno yalitoka kinywani mwa Manka wakati wakiwa wamepanda ndani ya gari moja wakijiandaa kuelekea nyumbani kwa Imma.
    Siku iliyofuata Manka akiwa nyumbani kwa Imma alisimama mbele ya watu wanne akiomba msamaha huku machozi yakimtoka kwa uchungu machoni mwake.Watu hao walikuwa ni Imma,,Queen, Albert pamoja na baba yake Mr Stanley, wote walikuwa wameketi sebuleni.
    "Imma nipo hapa nimeyapiga magoti mbele ya mboni za macho yako kukuomba msamaha. Imma siku zote nimekuwa adui mkubwa mbele ya maisha yako,nilikuwa nikikuumiza sana Imma,nilikuwa nikikutesa na kukudharirisha sana lakini Leo nimerudi na kutambua kumbe nilikuwa nikifanya upumbavu mbaya tena usiofaa katika maisha ya binadamu yeyote aishiye hapa ulimwenguni.Kwa upumbavu wangu nilisababisha kifo cha mkeo Nancy pamoja na mwanao wa kiume Prince lakini nakuomba Leo hii unisamehe Imma.Japo nilikutesa na kukuumiza kwa ujinga wangu usiokuwa na faida naomba uyasahau yote hayo,,unisamehe na tuendelee kuyaganga yajayo.Nakuahidi sitakutendea ubaya wa aina yoyote ile na nitakusaidia kwa kadri niwezavyo kukusaidia kabla sijaondoka na kuipa mkono dunia.Babaaa!! Nisamehe mwanao,nipokee tena babaaa!! Najua dunia imenifunzwa lakini nakuomba unipokee mwanao,,nilikuwa nimepotea njia babaa,lakini Leo hii nayakili makosa yangu. Naomba unisamehe". Sasa kwa Mara ya kwanza akaonekana Komando Albert akibubujikwa na machozi ya huzuni Mara baada ya Manka kuyaongea hayo maneno. Imma pia alibubunjikwa na machozi vile vile hata Mr Stanley nae alitokwa na machozi,, Queen ndo usiseme kabisa. Imma aliyafuta taratibu machozi yake akasimama na kwenda kumnyanyua Manka pale chini aliyekuwa akilia kwa kwikwi .
    "Manka usijali Mimi sina usemi kabisa". Aliongea kidogo Imma baadae akainama na kuipangusa michirizi ya machozi iliyokuwa ikipiga mbio kuelekea kifuani mwake." Manka,,Mimi nilishakusamehe zamani sana..labda kilichobaki nikumuombea tu mke wangu Nancy pamoja na mwanangu Prince roho zao zipumzishwe kwa amani popote walipo maana sisi sote tu mavumbi na mavumbini lazima turudi...usijali Nancy.Japo ni mengi niliyoyapitia yaliyo magumu lakini siku zote sikuchoka kumwomba Mungu a "NIFUNDISHE KUNYAMAZA" na hiyo ndiyo ilikuwa kauli mbiu ambayo nilikuwa nikiitumia.Tuko pamoja Manka".Aliongea Imma kisha akamkumbatia Manka na hapo hapo akaunyosha mkono wake wa kulia na kumsogeza Queen kisha akamkumbatia.Komando Albert alipoona hivyo taratibu alijongea akaungana nao katika suala zima la kukumbatiana,,,Mr Stanley nae hakubaki nyuma, alisimama na kumkumbatia mwanae huyo baadae akamkumbatia na Imma na kutoa ahadi ya kumrudisha kazini Imma ikiwemo pamoja na kumpandisha cheo na mshahara wake.
    **************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Baada ya mwaka mmoja kupita Imma alivaa tai pamoja na suti akafanikiwa kurudishwa tena kazini na maisha yake yakawa mazuri zaidi ya mwanzo ,,na akafanikiwa kumrudisha tena Queen nchini Marekani kuendelea na masomo yake ya chuo kikuu kuitafuta shahada yake ya udaktari.Mateso yote aliyokuwa akiyapitia aliyasahau yote ikatawala furaha tu.
    Komando Albert alifanikiwa kufunga pingu za maisha na Manka na ndoa yao ikadumu huku akiwa ameajiliwa kama jenerali Mkuu wa kikosi cha makomandoo wa nchi kavu.
    "Ndugu zangu tujifunzeni kunyamaza hiyo ndo siri ya kuwashinda maadui wote wanaotuzunguka". Hayo yalikuwa ni maneno ya Imma wakati anamalizia kuzipiga hatua kuingia kanisani kumshukuru Mungu kwa wema na fadhiri zote alizomtendea.
    ________MWISHO______
    ==>MBARIKIWE WOTE NA KILA LA KHERI.

0 comments:

Post a Comment

Blog