IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI
*********************************************************************************
Simulizi : Niliua Kumlinda Mama Yangu
Sehemu Ya Kwanza (1)
DAR ES
SALAAM
“Anita...” ilisikika
sauti ikiita kwa nyuma.
“Anitaaa...Anitaaa...”
iliendelea kusikika sauti ya mwanaume mmoja nyuma.
Watu waliokuwa
wakipiga hatua kuelekea katika boti ya Royal Palm iliyokuwa ikifanya safari zake
kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, wengi wao wakageuka nyuma na kumwangalia
mwanaume huyo aliyekuwa akiita huku akikimbia kuelekea kule alipokuwa mwanamke
yule aliyemuita.
Mwanaume yule
aliendelea kupiga hatua kumfuata msichana aliyekuwa amemuita ambaye alimbeba
mtoto mikononi huku pembeni yake kukiwa na mwanaume
mwingine.
Mara baada ya kusikia
ameitwa, hapohapo Anita, mwanamke aliyeonekana kuwa na uzuri wa asili, nywele
ndefu akageuka nyuma kumwangalia mtu aliyemuita. Sauti ile alipoisikiliza vizuri
masikioni mwake, haikuwa ngeni, aliwahi kuisikia kipindi cha nyuma, kichwa chake
kikaanza kujifikiria ni mahali gani aliwahi kuisikia sauti
hiyo.
“Oooh! Edson...”
alisema Anita mara baada ya mwanaume huyo kumfikia.
Mwanaume aliyesimama
mbele yake ambaye ndiye alikuwa huyo Edson, alionekana kupigwa na maisha, mwili
wake ulikonda, kichwani hakuwa na nywele, alizinyoa zote na kuwa na upara
uliokolezwa sana mafuta ya mgando.
Anita alipomwangalia
Edson, hakuamini kama huyo ndiye alikuwa Edson, alionekana kuwa tofauti na jinsi
alivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo alikuwa miongoni mwa wanafunzi ambao wazazi
wao walikuwa na fedha nyingi katika shule ya international iitwayo St. Augustine
iliyokuwa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
“Edson...are you
alive?” (Edson! Upo hai?) aliuliza Anita huku akimwangalia Edson
usoni.
“Yeah! Long time no
see...where have you been?” (Ndiyo! Kipindi kirefu hatujaonana! Ulikuwa wapi?)
aliuliza Edson huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana, alionekana kuwa
mwanaume masikini ambaye kwa kumwangalia tu, ilikuwa ni vigumu kuamini kama
aliwahi kuingiza hata laki moja siku za karibuni.
“What had happened to
you?” (Nini kilikutokea?)CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“My mom and dad died
after completing my O level education, then after, my relatives took everything
I had,” (Mama na baba yangu walifariki baada ya kumaliza elimu yangu, baada ya
hapo, ndugu zangu wakachukua kila kitu nilichokuwa nacho) alisema Edson kwa
sauti ya chini.
“Where is your
sister?” (Dada yako yupo wapi?)
“Who? Sophia?” (Nani?
Sophia?)
“Yes!”
(Ndiyo!)
Edson hakujibu swali
hilo, alibaki kimya na baada ya sekunde kadhaa machozi yakaanza kumtoka. Anita
alionekana kuelewa kilichokuwa kikiendelea kwamba dada wa Edson alikuwa
amefariki dunia, hivyo akamsogelea na kumkumbatia kwa mkono mmoja huku mwingine
ukiwa umembeba mtoto wake.
“Pole sana Edson,
amini kwamba kwa kila kinachotokea, kimepangwa na Mungu,” alisema Anita kwa
sauti ya chini.
Mwanaume yule
aliyekuwa amesimama pembeni ya Anita, alibaki akiwaangalia watu hao walivyokuwa
wamekumbatiana huku Anita akijitahidi kumbembeleza Edson, hakukasirika wala
hakuumia, kwake, kila kitu kiliendelea alikichukulia
kawaida.
“Edson, huyu ni mume
wangu, anaitwa Phillip Mnyome,” alisema Anita huku akijitahidi kuachia tabasamu
pana.
“Nashukuru kumfahamu
shemeji.”
“Mpenzi! Huyu anaitwa
Edson, nilisoma naye kitambo sana kidato cha kwanza, anaitwa Edson Mawela,”
alitambulisha Anita.
“Nashukuru
kumfahamu,” alisema Phillip huku akichia tabasamu pana.
Edson alifurahi
kumuona Anita mahali hapo, muda wote uso wake ulikuwa kwenye tabasamu pana,
hakuamini kama mwanamke yule aliyesoma naye kitambo hatimaye mwisho wa siku
walikuwa wameonana.
Anita na Edson
walisoma pamoja, miaka ya nyuma walipokuwa kidato cha kwanza ambapo walisoma
mpaka kidato cha nne na kila mmoja kuondoka zake
shuleni.
Katika kipindi
walichokuwa shuleni, Anita alijulikana kama Cleopatra na hii ilikuwa ni kwa
sababu ya uzri wa sura aliokuwa nao. Kila mvulana aliyemwangalia Anita,
alimpenda, sura yake ya upole, umbo lake maridadi, mwendo wake wa kinyonga
viliwapagawisha wavulana wengi kiasi kwamba wakapanga msururu kumfuatilia
msichana huyo.
Kila mmoja shuleni
hapo alitoka katika familia yenye fedha hivyo kitendo cha kumfuatilia msichana
huyo, wengi walijitambia utajiri wa wazazi wao kitu kilichomchanganya sana
Anita.
Alipofika kidato cha
nne ndipo alipojikuta akiangukia katika mikono ya mvulana Edson, wakatokea
kupendana, kila mmoja alimuona mwenzake kuwa kila kitu kwake.
Mara kwa mara
walikuwa pamoja, walitembea pamoja na hata kusoma pamoja. Mapenzi baina yao
wawili yakawateka, wakashindwa kuyafanya kuwa siri hivyo kuacha kila mtu
kufahamu kilichokuwa kikiendelea.
Kutokana na mapenzi
ya dhati waliyoonyeshana, wanafunzi wengi wakawaita Romeo na Juliet. Edson akawa
aambiwi kwa Anita na hata kwa msichana huyo hakuwa akiambiwa lolote kwa
Edson.
“Nitakupenda maisha
yangu yote,” alisema Anita.
“Kweli?”
“Niamini!
Maisha yangu yote utakuwa wangu peke yangu,” alisema
Anita.
Hayo ndiyo maneno
waliyokuwa wakiambiana, kila siku walikumbushiana kwamba walitakiwa kuishi
pamoja, kupendana na mpaka kuoana na kuishi kama mume na mke na hatimaye
kutengeneza familia moja.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku zikasogea, wiki
zikakatika na miaka kwenda mbele mpaka pale Edson, mtoto wa tajiri mkubwa
kutengana na msichana Anita. Kuanzia siku hiyo, huo ukawa mwisho, hawakuweza
kuonana tena.
Anita akawa na mawazo
mno, hakukuwa na mtu aliyetokea kumpenda kama Edson, maishani mwake, hakukuwa na
mtu aliyeuteka moyo wake kama mvulana huyo.
Hata alipoingia
kidato cha tano katika shule ya kimataifa ya St. Marrys bado moyo wake ulikuwa
kwa mvulana huyo ambaye mpaka katika kipindi hicho hakujua alikuwa wapi na kitu
gani kiliendelea katika maisha yake.
Alikaa na mawazo
mengi, alikosa raha, furaha ikapotea, kila siku alikuwa mtu wa mawazo mno.
Shuleni, hakuwa na mpenzi mwingine, kila mwanaume aliyemfuata, alimwambia kweli
kwamba alikuwa na mpenzi hivyo hakutaka kuwa na mtu
mwingine.
Wanaume wengi
waliumia lakini hawakuwa na jinsi, walitakiwa kukubaliana na ukweli kwamba
msichana huyo hakutaka kuwa na mwanaume mwingine zaidi ya yule aliyekuwa naye
aliyeitwa Edson.
Baada ya kumaliza
shule na kwenda nchini Marekani kusoma, huko ndipo alipokutana na kijana mmoja
mtanashati, mvulana mwenye uzuri wa sura ambaye aliutetemesha sana moyo wake,
huyu aliitwa Phillip Mnyome.
Walianza kama
marafiki wa karibu, kuambiana maneno mengi ya mapenzi na mwisho wa siku kujikuta
wakiogelea katika dimbwi la mahaba. Uhusiano wao ukaanza rasmi, wakawa pamoja
kila kona, wakaendelea kupendana mpaka pale walipomaliza chuo na kurudi nchini
Tanzania, kilichofuatia ni kufunga ndoa tu.
Hakukuwa na mtu
aliyewazuia, wakatambulishana kwa wazazi wao na hatimaye kufunga ndoa katika
Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
Katika kipindi chote
hicho, Anita hakukumbuka kama kulikuwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Edson,
alishamsahau, mtu pekee ambaye alimkumbuka vilivyo na ambaye alimpa moyo wake
kwa asilimia mia moja alikuwa mumewe tu, Phillip.
Baada ya kukaa mwaka
mzima kwenye ndoa hapo ndipo walipofanikiwa kupata mtoto waliyempa jina la
Cynthia. Alikuwa mtoto mzuri, mwenye afya ambaye alichukua sura za wote
wawili.
Kila walipomwangalia
mtoto wao, mioyo yao ilikuwa na faraja mno, hawakuamini kama kukaa ndani ya ndoa
kwa kipindi cha mwaka mmoja Mungu aliamua kuwapa mtoto wa
kike.
Mwaka wa kwanza
ukapita na wa pili kuingia. Huku akiwa amemsahau kabisa Edson, kwa bahati
akakutana naye katika kituo cha kupanda boti kuelekea Zanzibar kwa ajili ya
mapumziko ya wiki nzima.
Edson huyu
waliyekutana naye hakuwa yule wa nyuma. Alizaliwa kwenye familia ya kitajiri,
alikulia huko ila baada ya wazazi wake kufariki, mali zote zilikwenda kwa ndugu
zake waliokuwa na tamaa na yeye kumuacha.
Maisha yakampiga,
nyumbani akafukuzwa na kukimbilia mitaani, huko, alisulubika, alilia usiku na
mchana, hakuwa na amani, wakati mwingine hata kula, chakula chake kilikuwa cha
shida mno.
Alipambana lakini
akashindwa, akaanza kutafuta kazi za kufanya, kila alipokwenda, kwa jinsi
alivyoonekana hakukuwa na mtu aliyeamini kama mtu huyo alikuwa raia mwema,
alionekana mchafumchafu, alifanana na mhuni, mvuta bangi na mbwia madawa ya
kulevya.
Baada ya kuteseka
sana ndipo akafanikiwa kupata kazi katika kampuni ya Mediteranian ambayo ilikuwa
na boti zenye jina la Royal Palm ambazo zilikuwa zikifanya safari zake kutoka
Dar es Salaam kwenda Zanzibar.
Huko, alikwenda kama
mbeba mizigo. Japokuwa kipindi cha nyuma aliiona kazi hiyo kuwa mbaya lakini kwa
kipindi hicho, hiyo ilionekana kuwa bora kuliko kukaa mitaani akiombaomba hela
kwa kila rafiki yake aliyemuona.
Kidogo akapata
ahueni, akapanga chumba maeneo ya Manzese na kuanza maisha huko. Hakuwa na
mshahara mkubwa, alipata kidogo na hichohicho ndicho alichokitumia kuyatengeneza
maisha yake.
Siku zikakatika,
maisha yakaanza kuwa mazuri japo si sana. Kila siku alihakikisha anafika kazini
na kuanza kazi yake ya kubeba mizigo. Kwa kumwangalia, ingekuwa vigumu kuamini
kama mtu huyo aliwahi kuishi maisha ya kitajiri kabla ya wazazi wake kufariki
dunia.
Mara nyingi alikuwa
akisafiri na boti mbalimbali kuelekea Unguja na Pemba, huko, kama kawaida
alikuwa na kazi ya kushusha mizigo na kupandisha, ndiyo kazi ambayo aliizoea na
ndiyo hasa iliyomuweka mjini.
Kutokana na maisha
mabovu aliyokuwa nayo, hakukuwa na mwanamke aliyetamani kuwa naye. Wanawake
wengi walifikiria fedha, waliwafuata wanaume wenye fedha hivyo kwa mtu kama
yeye, hakukuwa na msichana aliyemfuata, tena wengi walipomuona,
walimdharau.
Moyoni aliumia,
alitamani kuwa na heshima, alitamani kupendwa kama watu wengine lakini hiyo
haikuwezekana, hakuwa na uwezo wa kuwa na fedha, hakuamini kama ingetokea siku
angeweza kupata fedha.
Baada ya kupita
miaka hiyo miwili ndipo akakutana na msichana wa ndoto yake, msichana
aliyempenda kuliko mtu yeyote yule, huyo alikuwa Anita, msichana yule wa kipindi
cha nyuma ambaye alimwambia kwamba alikuwa akimpenda sana.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Leo hii, msichana
huyuhuyu ambaye waliwekeana ahadi kwamba wangeoana alikuwa na mwanaume mwingine,
mwanaume mwenye sura ya kipole ambaye hakuonekana kama alikuwa mtu katili, uso
wake tu ulionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa kwenye mapenzi ya dhati kwa mke
wake.
“Mnakwenda wapi?”
aliuliza Edson huku akimwangalia Anita machoni, bado alihisi mapenzi mazito kwa
msichana huyo.
“Tunakwenda
Zanzibar....”
“Pemba au
Unguja?”
“Unguja.”
“Waoo! Sawa!
Nitahakikisha nawasaidia, hasa kubeba mizigo, tena bila gharama yoyote ile,”
alisema Edson huku akiachia tabasamu.
“Sawa! Tutashukuru
sana,” alisema Anita.
Moyo wake ulikuwa
kwenye maumivu makali, hakuamini kama yule aliyekuwa akimwangalia alikuwa Edson,
yuleyule mvulana aliyempenda sana tangu walipokuwa
shuleni.
Hali hiyo hakutaka
mumewe aione, hakutaka kugundulika ila mara nyingi alimwangalia kwa macho ya
mahaba yalioonyesha kuwa na uhitaji wa kuwa na mwanaume
huyo.
Baada ya dakika
kadhaa, abiria walipotimia ndani ya boti, ikawashwa na safari ya kuelekea Unguja
na Pemba kuanza huku Edson akiwa bize katika sehemu ya kutunza
mizigo.
****
“Yule ndiye Edson
mwenyewe?” aliuliza Phillip.
“Ndiye yeye!
Amekwisha sana, ni vigumu kuamini kama huyu ndiye yule Edson niliyesoma naye,”
alisema Anita huku akionekana kuhuzunishwa na hali aliyokuwa nayo
Edson.
“Ndiyo maana
nimeshangaa, jinsi ulivyoniambia na jinsi alivyo, ni vitu viwili tofauti
kabisa,” alisema Phillip.
“Ndugu wamechukua
kila kitu alichoachiwa na wazazi wake, anatia huruma sana,” alisema
Anita.
Muda huo, boti
ilikuwa safarini, ilianza safari ya kuelekea Zanzibar huku bahari ikiwa imetulia
kabisa. Ndani ya boti ile kila mmoja alikuwa bize kuzungumza na mwenzake,
walitegemea kutumia saa moja baharini mpaka kufika
Zanzibar.
Kadiri muda
ulivyozidi kwenda na ndivyo idadi ya watu waliokuwa wakipiga stori walivyozidi
kunyamaza na hivyo kulala. Japokuwa Edson alilala lakini Anita hakuthubutu hata
kuyafumba macho yake.
Kichwa chake
kilikuwa na mawazo tele juu ya mwanaume wa kwanza kuwa naye katika uhusiano wa
kimapenzi, Edson. Aliuhisi moyo wake kuwa kwenye mapenzi na mwanaume huyo kwani
hata kipindi cha nyuma walipokuwa wameachana, hawakuachana kwa maneno wala
ugomvi, waliachana kwa sababu tu masomo yaliwatenga.
Alitaka kupata
nafasi ya kukaa naye na kuzungumza naye, alitaka kufahamu mengi yaliyotokea, si
maisha yale aliayopitia ambayo yalijaa shida, bali alitaka kufahamu kama bado
alikuwa akimpenda au la.
Alibaki kwenye kiti
huku akijifikiria ni kwa namna gani angekwenda kule alipokuwa Edson na
kuzungumza naye, mume wake alikuwa pembeni yake ila alikuwa amelala lakini
hakuona kama ingekuwa rahisi kwake kumfuata na kupiga naye
stori.
Muda ulizidi kwenda
mbele, akajua kwamba endapo boti ingefika Zanzibar basi asingeweza kuzungumza na
Edson, hivyo ilikuwa ni lazima aonane na mwanaume huyo hata kabla boti haijafika
Zanzibar na kuachana.
“Ni lazima
nikazungumze na Edson, siwezi kusubiri hapa,” alisema
Anita.
Hakutaka kuendelea
kusubiri, ilikuwa ni lazima akazungumze na mwanaume huyo, hakuwa tayari kujiona
akisubiri zaidi, alichokifanya ni kusimama na kuanza kuelekea upande ambao
ulikuwa na mizigo, sehemu ambayo ndipo Edson
alipokuwepo.
Wakati anapiga hatua
kuelekea huko, ghafla akashtukia tumbo likianza kuchafuka, akaanza kuyumba huku
na kule na hapohapo kuanza kutapika. Hakuchukua mifuko kama abiria wengine,
hivyo matapishi yake yote yakaenda chini.
Mawimbi yaliendelea
kupiga huku na kule, meli ile ikaanza kuyumbishwa, kila mtu akaonekana kuogopa,
bahari ilichafuka na hali ya hatari kuonekana ndani ya meli
hiyo.
Haikuwa kawaida, ni
kweli wakati mwingine bahari huchafuka lakini kwa siku hiyo ilikuwa zaidi. Boti
ilipigwa na mawimbi mazito kiasi kwamba hata wale abiria waliokuwa wamelala,
wakaamka.
Phillip aliposhtuka
kutoka usingizini, mtu wa kwanza kabisa kumwangalia alikuwa mkewe, hakuwepo pale
alipotakiwa kuwepo, akajaribu kuangalia huku na kule lakini hakumuona, si yye tu
bali hata mtoto, naye hakuwepo.
Alichanganyikiwa,
hakutaka kubaki mahali pale, tayari abiria walianza kupiga kelele za kutaka
kuokolewa kwani kwa jinsi hali ilivyoonekana hakukuwa na dalili kwamba wangebaki
salama kabisa.
Phillip akatoka nje
ya sehemu aliyokuwa amekaa na kuanza kuangalia huku na kule, alipoona kwamba
mkewe hamuoni, akaanza kuita huku akionekana
kuchanganyikiwa.
“Anita...Anita...”
aliita huku akiangalia huku na kule lakini hakuweza kumuona
mkewe.
Watu wakaanza
kukimbia huku na kule kwa kuamini kwamba wangeweza kuyaokoa maisha yao lakini
hilo halikuwafanya kutoka nje ya meli, walibaki mule mule.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mawimbi mazito
yaliendelea kuipiga boti ile, katika hali ya kushangaza, maji yakaanza kuingia
ndani ya boti ile hali ilizidi kumtia hofu kila abiria.
“Tusaidieni
tunakufaaaa...” alisema abiria mmoja.
Hali ikawa mbaya,
mawingu mazito yakaanza kujikusanya angani na wala hazikupita dakika nyingi,
mvua ikaanza kunyesha. Ndani ya meli hakukukalika, kila mmoja alikuwa
akihangaika kuyaokoa maisha yake.
Anita pale alipokuwa
alikuwa kwenye hali mbaya, alijitahidi kusimama ili kurudi alipotoka lakini
hakuweza, boti ilikuwa ikiyumbayumba sana kutokana na kupigwa na
mawimbi.
Maji yaliendelea
kuingia ndani ya boti, nahodha na wafanyakazi wengine walijitahidi kutafuta
mawasiliano ya simu lakini hayakupatikana kutokana na hali ya hewa kuwa
mbaya.
Baada ya dakika
kumi, boti ikaanza kuzama kutokana na maji mengi kuingia ndani. Hakukuwa na
maboya ya kutosha hivyo abiria wengi kuhofia kufariki dunia ndani ya boti
ile.
“Tunakufaaa...”
walisema abiria katika kipindi ambacho boti iliendelea
kuzama.
Hakukuwa na mtu
aliyemsaidia mwenzake, walikuwa katikati ya bahari, katika kila upande,
hakukuonekana kuwa na dalili za nchi kavu, hakukuwa na aliyejua pande za dunia
yaani Kusini ilikuwa wapi na Kaskazini ilikuwa wapi.
Boti ilizama, abiria
wenye ujuzi wa kuogelea wakaanza kuogele kwa staili ya kulegeza miili yao na
kubaki juu wakielea, kwa wale ambao hawakuwa na uwezo wowote ule, wakaanza
kuzama na kufa huko baharini.
Wakati boti ikizama,
Edson alikuwa katika chumba cha mizigo. Kwa jinsi boti ile ilivyokuwa
ikiyumbishwa, hali iliyokuwepo baharini alijua kwamba kulikuwa na hatari ya boti
kuzama humo baharini, alichokifanya ni kuelekea nje.
Huko, hapohapo
akaanza kumtafuta Anita, alijua kwamba msichana huyo hawezi kuogelea hivyo
hakutaka kuona akifa, alimpenda kwa moyo mmoja, aliendelea kumtafuta
zaidi.
Mpaka boti inaanza
kuzama, hakuwa amemuona Anita. Alijitahidi kuita huku na kule, tena kwa sauti
kubwa lakini hakusikia msichana huyo akiitikia, moyo wake ulimuuma
mno.
Kwa kuwa alikuwa na
ujuzi wa kuogelea, akaanza kuogelea na kumtafuta Anita. Kila alipopita, watu
walikuwa wakilia na kuomba msaada. Hakutaka kumsaidia mtu yeyote yule, kwa
wakati huo, mawazo yake yalikuwa kwa Anita tu. Alikuwa akimtafuta kwa kupiga
mbizi huku na kule.
Ndani ya dakika tano
nzima tangu boti izame, hakuweza kumuona Anita.
****
Maji yaliingia ndani
ya boti na hivyo kuanza kuzama. Anita alipiga kelele za kuomba msaada huku
mkononi akiwa na mtoto wake lakini hakukuwa na mtu aliyemsaidia, kila mmoja
alikuwa bize kuyaokoa maisha yake lakini si kumsaidia mtu
mwingine.
Mbele yake alikiona
kifo, hakuwa na uhakika kama angepona, kwake, alijua kwamba ilikuwa ni lazima
kufa, hivyo akaanza kusali sala yake ya mwisho na kuyakabidhi maisha yake na ya
mtoto wake mikononi mwa Mungu.
Boti ilipozama,
hakukuwa na msaada wowote ule, alikuwa radhi kunywa maji lakini si kuona maji
yakimuua mtoto wake, hivyo alijitahidi kumshika kwa mkono mmoja na kumpeleka juu
huku miguu yake ikifanya kazi ya kukata maji ili
asizame.
Wakati akiwa kwenye
harakati za kujiokoa yeye na kumuokoa mtoto wake, akaanza kusikia akiitwa jina
lake. Kitu cha kwanza akaisikiliza sauti ile kwa makini, alichohisi ni kwamba
alikuwa akiitwa na mumewe, Phillip lakini alipoisikia vizuri sauti ile, haikuwa
ya mumewe bali ilikuwa ni ya aliyekuwa mpenzi wake,
Edson.
“Anita…..Anita…Anita….” iliendelea kusikika sauti ya
Edson.
“Edson…Edson
nisaidie naku…” alisema Anita lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake akaanza
kunywa maji.
Japokuwa kulikuwa na
kelele mahali hapo lakini Edson aliweza kuisikia sauti hiyo, alijua ilipotokea
hivyo kuanza kupiga mbizi kuelekea kule sauti ilipotokea.
Alipofika huko,
akaanza kuangalia huku na kule, tayari watu wengine walikuwa wamekufa, miili yao
ilielea hivyo watu wengine kuishikilia miili hiyo ili
wasizame.
Edson alipomuona
Anita, hapohapo akaanza kumsogela, alipomfikia, kitu cha kwanza akamchukua
Cynthia.
“Vipi Anita?”
aliuliza Edson.
“Ninakufa Edson,
ninakufaaaa.”
“Huwezi kufa! Hautoweza kufa. Kama utakufa, basi acha na mimi nife,” alisema Edson huku macho yake tu yakionekana kumaanisha alichokisema.
“Huwezi kufa! Hautoweza kufa. Kama utakufa, basi acha na mimi nife,” alisema Edson huku macho yake tu yakionekana kumaanisha alichokisema.
Alichokifanya, mkono
mmoja ukamshikilia mtoto Cynthia aliyekuwa akilia huku akipiga mbizi na
kumwambia Anita amfuate kule alipokuwa akielekea. Safari yao fupi iliishia
sehemu iliyokuwa na pipa moja kubwa lililokuwa likielea na kumwambia Anita
alishikilie pipa hilo kwani ndiyo ulikuwa msaada pekee waliokuwa
nao.
Watu wengine
waliendelea kufa, kelele zilianza kupungua kwani pamoja na kuwa kwenye hali
mbaya, mvua ile iliyokuwa ikiendelea kunyesha ikasababisha baridi kali
lililowamaliza watu wengi baharini hapo.
Alichokifanya Edson
ni kumshikilia vizuri Cythia, akamwambia Anita ajitahidi akae juu ya pipa lile
kwani ndiyo ingekuwa nafasi pekee ya kuyaokoa maisha
yake.
Alichokifanya Anita
ni kuanza kupanda pipa lile. Haikuwa kazi nyepesi hata kidogo, alijitahidi sana
kupanda, alitumia muda wa dakika kumi nzima ndipo akafanikiwa na hivyo kuwa juu
ya pipa lile kisha Edson kumpa Cynthia.
“Na wewe
panda!”
“Hapana Anita!
Sitoweza kupanda.”
“Nashukuru kwa
msaada wako Edson, nashukuru kwa kuokoa maisha yangu,” alisema Anita huku
akimwangalia Edson usoni.
“Usijali! Nimefanya
hivi kwa kuwa ninakupenda sana Anita. Siku zote nimekuwa nikikufikiria, sikujua
ni kwa namna gani ningeweza kukuona tena,” alisema Edson huku akimwangalia
Anita.
Huo haukuwa mwisho,
waliendelea kukaa baharini mpaka ilipofika jioni ya saa kumi na mbili ndipo kwa
mbali walipoona Boti ya Mv Space ikiwa inakaribia kule
walipokuwa.
Walikuwa kwenye hali
mbaya, baridi liliwapiga na njaa ziliwauma mno. Kuna kipindi walifikiria kwamba
hata Cynthia alikufa kwani alikuwa kimya kabisa hali iliyomfanya mara kwa mara
Anita kumtingisha, alipoona akianza kulia, alimuacha.
“Edson…Edson…boti,”
alisema Anita kwa sauti ya chini, alikuwa akimwamsha Edson aliyeonekana kuwa
kwenye mawazo mengi.
“Unasemaje?”
aliuliza Edson huku akitetemeka, nusu ya mwili wake ilikuwa
majini.
“Boti…”
Aliposikia neno boti
akapata nguvu na kuona kwamba hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yao ya kuokolewa.
Akatupia macho kule alipoambiwa kwamba kulikuwa na boti, kweli aliiona ikiwa
inasogea kule walipokuwa.
Alichokifanya ni
kupunga mkono wake mmoja huku akipiga kelele za kuomba msaada. Hiyo ilionekana
kusaidia kwani watu waliokuwa kwenye boti ile waliamua kuzungukazunguka katika
eneo lile boti ilipozama ili kuona kama kuna majeruhi basi wawasaidie kwani hali
ilionekana kuwa mbaya.
“Tupo haiiiii….tupo
haiiiiii….” alipiga kelele Edson.
Hiyo ilisaidia kwa
kiasi kikubwa, watu wale waliokuwa kwenye boti ile walipoisikia sauti ya Edson,
wakaanza kuangalia kule sauti hiyo ilipotoka, kwa bahati nzuri wakamuonaAnita
akiwa juu ya pipa, kwa pembeni alikuwepo mwanaume
mwingine.
“Wale kule…” alisema
mwanaume mmoja na hivyo kusogea kule kisha kuwatupia boya lililofungwa kamba,
walipolishika, wakaanza kuwavuta. Huo ndiyo ukawa msaada
kwao.
****CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taarifa zilitolewa
katika vyombo vya habari hasa redio na televisheni kwamba boti moja ya Royal
Palm ambayo ilikuwa ikifanya safari zake kwenda Unguja na Pemba ilipata ajali na
abiria wengi kufariki.
Kila mtu aliyesikia
taarifa hiyo, alisikitika, wengine hasa waliokuwa na ndugu zao wakalia na
kuomboleza kwa kujua kwamba wasingeweza kuwaona tena ndugu wao
hao.
Miili ya watu
waliokufa katika ajali hiyo ikaokolewa na kupelekwa hospitalini ambapo huko watu
walitakiwa kwenda ili kuona kama kulikuwa na ndugu zao hivyo kuichukua miili
hiyo na taratibu nyingine kufuata.
Mtu ambaye alikuwa
mmoja wa watu waliofika hospitali na kuiangalia miili hiyo alikuwa Anita na
baadhi ya ndugu zake. Alifika hapo kwa ajili ya kuutafuta mwili wa mume wake
aliyempenda, Phillip.
Walipelekwa katika chumba kilichokuwa na miili hiyo, walifunuliwa miili yote na kuonyeshewa, hakukuwa na mwili wa Phillip kitu kilichoonyesha kwamba mume wake huyo alikufa na mwili wake kuliwa na samaki.
Walipelekwa katika chumba kilichokuwa na miili hiyo, walifunuliwa miili yote na kuonyeshewa, hakukuwa na mwili wa Phillip kitu kilichoonyesha kwamba mume wake huyo alikufa na mwili wake kuliwa na samaki.
“Miili ndiyo hii
tu?” aliuliza Anita huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Ndiyo hii tu!
Hakuna mingine.”
“Kweli?”
“Ndiyo! Lakini subiri kwanza,” alisema daktari mmoja.
“Ndiyo! Lakini subiri kwanza,” alisema daktari mmoja.
Akaondoka na
kuwaacha watu hao wakiwa katika mabenchi hospitalini hapo wakilia tu. Anita
alimuomba Mungu ili amfanikishe kumuona mume wake na hata kama hatomuona basi
angeridhika zaidi kama angeuona mwili wake tu.
Ndugu zake
wakajaribu kumbembeleza lakini hakunyamaza, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu
makali mno, hakutaka kusikia la mtu yeyote yule, kile alichotaka kukisikia ni
kuhusu mume wake tu.
Daktari yule
aliporudi, wakasimama na kumsogelea, walitaka kusikia kile kilichotokea kule
alipokwenda kama aliweza kumuuona mwili wa Phillip au
la.
“Vipi?”
“Huko nilipokwenda
wamesema kwamba miili ya wahanga wa ajali ya boti ni hii tu,” alisema daktari
yule.
Kilio zaidi kikaanza
kusikika kutoka kwa Anita, hakuamini kama kweli huo ndiyo ulikuwa mwisho wa
kumuona mume wake mpendwa. Alibaki akiwa na maumivu mazito moyoni mwake, huzuni
aliyokuwa nayo haikuweza kusimulika.
Alilia na kulia
lakini ukweli ulibaki palepale kwamba mwili wa mume wake haukuwepo na kulikuwa
na uwezekano kwamba ulilikuwa na samaki huko baharini.
Kilichofuata baada
ya hapo ni kuweka mazishi, watu wengi walikwenda katika msiba huo mzito. Kilio
cha Anita kilimhuzunisha kila mtu aliyekuwepo mahali pale, alilia kwa kulalamika
kwamba Mungu aliamua kumuonea kwani hata mwili wake ungekuwa umepatikana, kwake
ingekuwa faraja kubwa mno.
Baada ya saa kadhaa,
jeneza likaletwa, padri akasimama na kuomba sala maalumkisha safari ya kuelekea
makaburini kuanza.
Ndani ya jeneza lile
hakukuwa na mwili wake, kulikuwa na nguo zake tu na baadhi ya vitu alivyokuwa
navyo. Phillip alifariki kwa maana hiyo mali zote alizokuwa nazo, ule utajiri
mkubwa aliokuwa akiumiliki ulikuwa chini ya mke wake ambaye alimuacha akiwa na
mtoto wake mdogo, Cynthia.
“Pole sana Anita!
Mungu atakupigania tu,” alisema mama yake, bi Lydia.
“Nashukuru mama,
asante kwa kunitia moyo katika kipindi hiki kigumu,” alisema
Anita.
*****
Kitu kilichokuwa
kikimuumiza Anita ni kumuona mpenzi wake wa kipindi cha nyuma, Edson akiwa
kwenye hali ya umasikini mkubwa. Moyo wake uliumia mno, hakuamini kama kulikuwa
na mwanaume aliyekuwa akipata tabu kama alizokuwa akipata
Edson.
Moyo wake ulimpenda
mno, mbali na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa mwanaume huyo, pia alihitaji
kuishi naye, yaani lile penzi la dhati alilokuwa nalo lirudi na kuwa kama
zamani.
Anita hakutaka
kutulia, ni mwezi mmoja tu ndiyo ulikuwa umepita tangu mazishi ya mumewe
yalipofanyika lakini hakutaka kutulia, kila siku akawa mtu wa kumpigia simu
Edson na kuzungumza naye, alishindwa kuzizuia hisia za kimapenzi alizokuwa nazo
juu yake hivyo kumwambia ukweli.
Edson hakutaka
kupinga, alijua hilo lingetokea na yeye mwenyewe alimpenda mno mwanamke huyo,
hivyo kuanza kwenda kwake na kufanya mambo mengine kama
wapenzi.
Kwenye kitanda
kilekile alichokuwa akikitumia na mumewe ndicho hichohicho alicholala na Edson,
hakutaka kujali sana kuhusu Phillip kwani kama kufa alikwishakufa hivyo
asingeweza kurudi tena duniani.
Uhusiano huo
uliendelea kwenda mbele, waliendelea kupendana kama zamani. Ndugu wa Phillip
waliposikia kwamba Anita aliamua kuwa na mwanaume mwingine, mioyo yao iliumia
sana, hawakuamini kwamba Anita hakusubiri hata miezi sita iishe, aliamua kuwa na
mwanaume mwingine kwa haraka sana.
“Jamani! Nasikia
Anita amepata mwanaume mwingine!” alisema ndugu mmoja huku akionekana kushangaa
mno.
“Hata mimi mwenyewe
Joshua aliniambia hivyohivyo, bado sijapata uhakika, hebu nikamuulize Joyce,
anaweza akawa anajua,” alisema msichana mwingine.
“Lakini mbona
amefanya haraka sana?”
“Hata mimi sijui kwa
nini, unajua ni miezi miwili tu imepita.”
“Ndiyo hivyo! Ninachojiuliza, ni kwa muda gani alikutana na mwanaume huyo, kuzungumzia mapenzi mpaka kuwa wapenzi, ni muda mchache sana, yaani sijui nini kilitokea,” alisema msichana huyo.
“Ndiyo hivyo! Ninachojiuliza, ni kwa muda gani alikutana na mwanaume huyo, kuzungumzia mapenzi mpaka kuwa wapenzi, ni muda mchache sana, yaani sijui nini kilitokea,” alisema msichana huyo.
Kila mmoja
alishangaa, kila walichojiuliza, hawakupata jibu lolote lile. Mioyoni mwao
waliumia lakini hawakuwa na jinsi, Anita aliamua kuwa na mwanaume mwingine hivyo
hakutaka kuingiliwa.
Baba yake Edson
aliposikia hivyo, hakutaka kukubali hata kidogo, alichokuwa akikiangalia ni
mjukuu wake, Cynthia tu, alichokifanya ni kuwasiliana na Anita, majibu aliyopewa
ni kwamba asiingiliwe, alichokiamua kilikuwa ni matakwa yake, hivyo hakutaka
kuingiliwa.
“Unasemaje?”
“Ndivyo
alivyoniambia! Tusimuingilie,” alisema baba Edson.
“Anita hawezi
kubadilika namna hiyo! Kweli?”
“Ndiyo!”
“Hapana!”
“Hapana!”
“Kwani kwenye simu
hujasikia mke wangu? Amenijibu tena kwa nyodo.”
“Yaani Anita
huyuhuyu?”
“Ndiyo!”
“Ndiyo!”
Alichokifanya baba
Edson ni kuwasiliana na wazazi wa Anita ambao wakamuita binti yao na kumwambia
kwamba hakutakiwa kuwa na uhusiano na mwanaume yeyote yule mpaka kipindi cha
miezi sita kipite.
MAjibu waliyopewa na
binti yao, hayakuwa mazuri, bado msichana huyo hakutaka kuingiliwa katika maisha
yake. Wazazi wake walihuzunishwa na majibu ya binti yao, walijaribu kumuomba
kwamba auondoe moyo wake kwa Edson lakini msichana huyo hakukubali, kwa wakati
huo, hakukuwa na mwanaume aliyeuteka moyo wake zaidi ya
Edson.
“Tunataka uachane
naye, mlee mwanao kwanza,” alisema baba yake.
“Jamani mbona
tunaingiliana? Baba, ulivyoanza uhusiano na mama kuna mtu aliwaingilia?” alihoji
Anita.
“Anita…maneno gani
hayo?”
“Nimeuliza tu! Kama
hakuna aliyewaingilia, kwa nini nyie mnaniingilia mimi?” aliuliza
Anita.
Anita alibadilika,
alionekana kuwa jeuri, hakutaka kusikia kitu chochote kile kutoka kwa mtu
yeyote, alichokiangalia kwa wakati huo ni kuwa na Edson tu. Alimpenda zaidi ya
mtu yeyote, katika maisha yake, hakukuwa na mtu ambaye angeweza kumtenganisha na
Edson.
Miezi ikakatika,
mwaka mwingine ukaingia, Cynthia akatimiza miaka mitatu hivyo kuanza kusoma
shule ya chekechea katika Shule ya Kimataifa ya St. Augustine, shule
iliyokusanya watoto wengi wa watu wenye hela.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Japokuwa maisha
yalikuwa ya kifahari, alipata alichokitaka lakini Edson hakuonekana kuwa na
furaha, kila siku alionekana kuwa na mawazo mengi, alionekana kama mgonjwa hali
iliyomuweka Anita kwenye wakati mgumu.
Hakupenda kumuona
mwanaume wake akiwa hivyo, kitendo cha kuonekana mnyonge hata yeye mwenyewe
kilimshangaza mno. Aliumia moyoni, alijua kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa
kikiendelea ila Edson alifanya kuwa siri kubwa.
Kuvumilia kwake
kukaisha, hakutaka kuendelea kujiuliza maswali mengi juu ya kilichomsibu Edson,
alichokifanya Anita ni kumuita na kumuuliza kile kilichokuwa kikiendelea ambacho
kilimfanya kuwa kwenye hali ile.
“Tatizo nini
mpenzi?” aliuliza Anita.
“Hivi unanipenda
kweli?” aliuliza Edson.
“Ndiyo! Ninakupenda
mpenzi.”
“Kweli?”
“Hakika! Hakuna mwingine zaidi yako!”
“Kweli?”
“Hakika! Hakuna mwingine zaidi yako!”
“Haiwezekani!
Sidhani kama ni kweli!”
“Kweli mpenzi!
Ninakupenda. Unataka nikufanyie nini mpaka ujue kwamba ninakupenda?” aliuliza
Anita.
Edson hakuzungumza
kitu, akabaki kimya huku akiwa amejiinamia. Bado alijifanya kuwa na mawazo
mengi, Anita alibaki akimwangalia huku akihisi moyo wake kuumia mno.
Alichokifanya ni kumsogelea na kumuinua, alipomwangalia Edson, machozi yalikuwa
yakimtoka mwanaume huyo.
“Unalia nini tena
mpenzi?” aliuliza Anita.
“Kwa sababu
haunipendi!”
“Ninakupenda mpenzi!
Ninakupenda na ndiyo maana upo hapa!”
“Hapana Anita!
Sidhani kama ni kweli!”
“Edson! Niambie
mpenzi nikufanyie nini!”
“Mimi ni nani
kwako?”
“Mpenzi wangu!”
“Mpenzi wangu!”
“Na umesema kwamba
muda si mrefu tutaoana, si ndiyo?”
“Ndiyo mpenzi!”
“Ndiyo mpenzi!”
“Sasa mbona kila
kitu unajimilikishia wewe tu?”
“Sijakuelewa.”
“Namaanisha mali. Yaani kila kitu unataka uonekane wewe tu.”
“Yaani bado sijakuelewa.”
“Sijakuelewa.”
“Namaanisha mali. Yaani kila kitu unataka uonekane wewe tu.”
“Yaani bado sijakuelewa.”
“Namaanisha mbona na
mimi hutaki kunipa haki yangu!”
“Ipi?”
“Ya kumiliki!”
“Ipi?”
“Ya kumiliki!”
“Hizi
mali?”
“Ndiyo!”
“Sasa hilo ndiyo linakufanya uhuzunike hivyo?”
“Ndiyo!”
“Sasa hilo ndiyo linakufanya uhuzunike hivyo?”
“Sasa unafikiri
nitakuwa na furaha? Naendesha magari ya kifahari, ila sina haki nayo, naishi
kwenye nyumba nzuri, ila sina haki nayo, nasimamia mpaka biashara ambazo sina
haki nazo. Sasa haki zangu zipo wapi?” alihoji Edson.
“Sasa ndiyo
ukasirike na kuonekana kama mgonjwa?”
“Ndiyo
hivyo!’
“Basi usijali
mpenzi, nitakuandikisha na wewe uwe na haki nazo,” alisema Anita maneno
yaliyomfanya Edson kuwa na furaha mno.
Hilo ndilo
alilolitaka, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali kila alipojiona akiendesha
magari ambayo si yake au kuishi ndani ya nyumba ambayo haikuwa na haki yake.
Kila siku katika maisha yake alitamani naye awe na asilimia fulani katika
kumiliki mali zile alizokuwa nazo Anita.
Kutokana na mapenzi
mazito aliyokuwa nayo Anita kwa Edson, akajikuta akimuita mwanasheria wake na
hatimaye kumuandikisha Edson kuwa mmiliki halali kama
alivyokuwa.
Kwa Edson, hiyo
ilikuwa furaha kubwa, hakuamini kama kila kitu kingekwenda kwa wepesi kama
kilivyokuwa. Akajikuta akimkumbatia Anita na kummwagia mabusu mfululizo, hapo,
akamwambia kwamba moyoni mwake alikuwa na amani, furaha aliyokuwa nayo
haikuelezeka.
Anita alimpenda sana
Edson lakini mwanaume huyo, moyoni mwake alikuwa akifikiria kitu kingine kabisa,
hakujiona kama alikuwa na mapenzi makubwa kwa msichana huyo kama kipindi cha
nyuma, kitu ambacho kilimfanya kujifanya kuwa na mapenzi mazito kwa msichana
huyo ni mali alizokuwa nazo tu.
Alizitamani mali
zile, alitaka sana ziwe zake, hivyo kitendo cha kuandikishwa kama mmiliki halali
wa zile mali, moyoni mwake ilikuwa ni shangwe kubwa.
Akapanga mipango
yake, kitu pekee alichotaka kufanya ni dhuluma tu, alitaka kumdhulumu mwanamke
huyo mali zile, ziwe zake na kufanya mambo yake, azitumie
atakavyo.
“Ameingia kingi!
Ataisoma namba sasa,” alisema Edson huku meno yote yakiwa
nje.
****
Siku zikaendelea
kukatika, baada ya miaka miwili kupita huku Cynthia akiwa na miaka mitano, hapo
ndipo Edson alipoanza kubadilika. Akaanza dharau kwa Anita, kila alipoambiwa
hili na lile, alibadilika na hakutaka kusikia hata mara
moja.
Akawa mtu wa kunywa
pombe, kurudi usiku wa manane na hata wakati mwingine kuwaingiza wanawake ndani
ya nyumba hiyo kitu kilichomuuma sana Anita.
Hakuwa na msemo
wowote ule. Kwa kipindi kirefu alimwambia kwamba ilikuwa ni lazima waoane lakini
kwa kipindi hicho, Edson hakutaka kusikia chochote kile, hakutaka kusikia mambo
ya ndoa kwani kile alichokitaka alikifanikisha kwa kiasi
kikubwa.
Alitaka kila kitu
kiwe chake, hivyo akaanza kuhamisha fedha zilizokuwa kwenye akaunti za Anita na
kuziingiza katika akaunti yake. Kiasi cha shilingi bilioni sitini kikaamishwa na
kuingizwa katika akaunti yake.
Anita hakufahamu
kilichokuwa kikiendelea, kila kitu alichangia na Edson, hakujua kama mule ndani
ya akaunti yake ni milioni kumi tu ndizo zilizokuwa
zimebaki.
Maisha yalibadilika,
hayakuwa yale yenye mapenzi kama yalivyokuwa kipindi cha nyuma, Edson yule
alibadilika, Anita hakuamini kama mwanaume yuleyule aliyemkuta akiwa amechoka
katika kampuni moja ya boti za Royal Palm ndiye ambaye leo hii alikuwa
akimfanyia mambo yale.
Moyoni aliumia,
wakati mwingine alijuta sababu ya kumwandika kama mmoja wa wamiliki wa mali
zile.
Hapo ndipo tabia
halisi ya Edson ilipoanza kuonekana, ulevi ukamteka, mara kwa mara akawa mtu wa
kurudi usiku wa manane. Kila Edson anapokuwa nje, Anita hakulala, alibaki macho
huku akimsubiria mwanaume huyo.
Mateso aliyoyapata
yalikuwa siri, hakutaka kumwambia mtu yeyote kwa kuogopa kuchekwa na
kudharauliwa. Alikuwa mtu wa kujifungia chumbani, wakati mwingine alibaki akilia
tu, kila kilichokuwa kikiendelea, hakika kilimuumiza
mno.
“Edson…mbona
umebadilika hivi?” aliuliza Anita.
“Nani?
Mimi?”
“Ndiyo! Haukuwa hivi
zamani, nini kimekubadilisha?” aliuliza Anita, machozi yalianza
kumlenga.
“Hebu niondolee
uchuro wako huko,” alisema Edson huku chupa ya Saint Anna ikiwa mkononi
mwake.
Kubadilika kwa Edson
kuliendelea kumshangaza sana Anita, hakutaka kukubali, alijua kulikuwa na kitu
kilichomfanya kuwa hivyo, akili yake ikamwambia kwamba ilikuwa ni lazima
afuatilie suala la fedha katika akaunti zake kwa kuhisi kwamba Edson angeweza
kumtapeli.
Hapo ndipo alipoanza
kufuatilia, alipokwenda kwenye akaunti ya kwanza, hakukuta kiasi cha fedha
kikubwa, ni milioni tano tu ndizo zilizokuwa zimebaki.
Alishtuka mno,
hakuamini macho yake, hakutaka kuishia hapo, alipoangalia akaunti ya pili, pia
kulikuwa na shilingi milioni tano tu. Alijikuta miguu yake ikiisha nguvu,
ikalegea na hapohapo kuanza kulia kama mtoto.
“Kuna nini dada?”
aliuliza mfanyakazi wa benki, si yeye aliyeshangazwa na kilio cha Anita, hata
wafanyakazi wengine na wateja waliokuwa humo ndani walishangazwa
naye.
Watu wakaanza
kumbembeleza Anita, walimtaka anyamaze lakini pia walitaka kufahamu tatizo
lilikuwa nini. Anita hakunyamaza, kilichokuwa kimetokea, wakati mwingine alihisi
kama yupo ndotoni na baada ya muda mchache angeamka kutoka
usingizini.
Anita hakutaka
kubaki hapo benki, alichokifanya ni kuondoka huku akiwa amechanganyikiwa,
alipofika nje, akalifuata gari lake la thamani na kuingia, safari iliyoanza ni
kwenda nyumbani kwake.
Aliendesha gari huku
akiwa amechanganyikiwa, kila aliposogea mbele, alisikia maumivu mazito moyoni
mwake. Hakuamini kama Edson yuleyule ndiye aliyefanya vile, hakuamini kama
shukrani ya punda aliamua kumpiga mateke.
Kwa kuwa hakukuwa na
foleni, hakuchukua muda mrefu akawa amekwishafika nyumbani, geti likafunguliwa
na kuingia ndani.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hili gari la nani?”
aliuliza Anita mara baada ya kuingia ndani ya eneo la nyumba
yake.
“Kuna wageni
wamekuja.”
“Wakina nani?”
“Wakina nani?”
“Sijui! Ila shemeji
amesema ni wateja wamekuja kununua nyumba.”
“Nyumba
ipi?”
“Hiihii!”
Anita alihisi
kuchanganyikiwa zaidi, hakuamini kile alichokisikia kwamba kuna wageni wamekuja
kwa lengo la kununua nyumba. Akaingia ndani mpaka sebuleni, macho yake
yakagongana na wanaume wawili waliovalia suti ambao walikaa kwa kujiachia
sebuleni pale.
Mbali na wanaume
hao, pia Edson alikuwa sebuleni hapo akiwa amejiachia tu, uso wake ulikuwa
kwenye tabasamu pana.
“Milioni mia moja na
hamsini,” alisema Edson, alijifanya kama kutokumuona
Anita.
“Basi hakuna tatizo!
Hati iko wapi?”
“Hilo halina
tatizo!”
“Sawa! Kesho
nitakuandikia cheki,” alisema mwanaume mmoja, alikuwa kijana
tu.
Anita hakuamini
alichokisikia, mapigo ya moyo wake yalidunda kwa nguvu, hakuamini kile
alichokiona, hakuamini kama hao waliofika nyumbani hapo walikuwa wateja
waliotaka kununua nyumba pasipo yeye kushirikishwa.
Moyo wake ulikuwa na
hasira mno, alitoka benki ambapo huko alikuta kiasi kikubwa cha fedha kikiwa
kimechukuliwa, wakati akirudi nyumbani huku akionekana kuwa na hasira, akakutana
na kitu kingine kabisa, wageni walifika mahali hapo kwa ajili ya kununua nyumba
yake.
“Edson! Unataka
kuiuza nyumba yangu?” aliuliza Anita huku akionekana
kutokuamini.
“Kuuza nyumba yako
au yetu?”
“Yetu! Tangu lini?
Umechangia hata tofali humu?” aliuliza Anita, hakuamini kama siku hiyo alimfokea
Edson.
“Kwani hati ya
nyumba inaonyesha ni nani mmiliki halali wa nyumba
hii?”
“Mimi?”
“Umenisahau hata mimi? Sikiliza Anita, mimi kama mmoja wa wamiliki wa nyumba hii, nimeamua kuiuza kwa kuwa nimechoka kuishi humu, ni bora nyumba iuzwe, tugawane pesa halafu kila mtu afanye yake,” alisema Edson.
“Mimi?”
“Umenisahau hata mimi? Sikiliza Anita, mimi kama mmoja wa wamiliki wa nyumba hii, nimeamua kuiuza kwa kuwa nimechoka kuishi humu, ni bora nyumba iuzwe, tugawane pesa halafu kila mtu afanye yake,” alisema Edson.
Anita alibaki
akibubujikwa na machozi tu, hakuamini kama kile kilichokuwa kikitokea. Aliachiwa
mali na mumewe, aliachiwa fedha nyingi lakini mwisho wa siku, kila kitu kilikuwa
kikiporwa na mwanaume aliyeonekana kuwa katili.
Hakuacha kulia,
aliumia mno lakini machozi yake yote, hasira zake zote hazikuweza kubadilisha
kitu chochote kile, ukweli ulibaki palepale kwamba nyumba ilitakiwa kuuzwa na
kisha agawane hela na Edson, mtu ambaye hakuwahi hata kutokwa jasho
kuzitafuta.
Baada ya wiki moja,
uuzaji wa nyumba ile ukakamilika, haikuwa mali yake tena, ilikuwa mali ya mtu
mwingine, mmiliki mpya aliyejulikana kwa jina la Andrew
Nkone.
Hilo lilikuwa pigo
kubwa kwa Anita, bado hakuamini kilichokuwa kimetokea kwamba alipoteza nyumba na
kiasi kikubwa cha fedha. Hakukuwa na sehemu ya kukimbilia, kila alipokwenda,
hakupata msaada wowote ule mpaka pale alipoashauriwa kwamba ilikuwa ni lazima
kesi hiyo ifikishwe mahakamani ili aweze kushinda haki
yake.
“Itawezekana
kweli?”
“Kwa nini
isiwezekane?”
“Naona inaweza kuwa
na ugumu.”
“Hakuna kitu kama hicho! Wewe nenda tu.”
“Hakuna kitu kama hicho! Wewe nenda tu.”
Alichokifanya ni
kuonana na mwanasheria wake na kumwambia kile kilichokuwa kikiendelea hivyo kesi
kufunguliwa na kuanza kusikilizwa mahakamani.
“Hii ni kesi ya
madai, nina uhakika utafanikiwa tu, utashinda na kila kitu kurudi kwako,”
alisema mwanasheria wake aitwaye Sifaeli Mambo.
“Nitashukuru sana,
naomba unisaidie.”
“Hilo wala usijali.”
“Hilo wala usijali.”
Kilichotokea ni
Edson kuitwa mahakamani na kusomewa kesi ya madai iliyokuwa imepelekwa katika
mahakama hiyo huku mshtaki akiwa Anita. Edson hakuonekana kuwa na wasiwasi
wowote ule, kila kitu kilichokuwa kimetokea, alikuwa na uhakika kwamba
angeshinda kesi ile na hivyo kujimilikisha haki za umilikaji wa mali na fedha
zile moja kwa moja.
Wakati kesi
ikiunguruma mahakamani, hakukuwa na ndugu yeyote wa Anita au marehemu mume wake
aliyekwenda mahakamani, walitokea kumchukia Anita kutokana na kile alichokuwa
amekifanya hivyo nao walimwachia afuatilie kila kitu peke
yake.
Mtu ambaye alikuwa
tumaini lake kwa wakati huo alikuwa mtoto wake tu ambaye katika kipindi hicho
alikuwa na miaka sita. Kila siku Cynthia alionekana kuwa na huzuni mno, kila
alipomuona mama yake akilia, moyo wake ulimuuma sana, hakujua mama yake alilia
nini, alijitahidi kuuliza lakini Anita hakutaka kumwambia ukweli,
alimficha.
Tofauti na kesi
nyingine, kesi hiyo ilisikilizwa kwa muda wa miezi miwili tu tena huku
ikisimamiwa na hakimu aliyejulikana kwa jina la James Marimba. Hukumu ya kesi
ile ilivyotoka ilionyesha kwamba Anita alipoteza haki zake za kumiliki mali
zote, si hizo tu na hata fedha ambazo alitakiwa kuzimiliki, hakuwa na haki
nazo.
Kilisikika kilio
kikubwa mahakamani hapo, hakuamini kama hakimu ndiye aliyetoa hukumu hiyo nzito.
Alipoteza kila kitu, alimpenda Edson, alimthamini na kumpa kila kitu
alichokihitaji kikiwepo uhalali wa kumiliki mali lakini mwisho wa siku ni
maumivu makali ndiyo yaliyofuata.
Akaachwa yeye kama yeye, hakuwa na fedha, hakuwa na mahali pa kuishi,
akajaribu kwenda kwa ndugu zake, wote aliowafuata, hakukuwa na aliyetaka kuishi
naye, wengi walimfukuza.
Huku akiwa na mtoto wake, hakuwa na jinsi, akaondoka na kwenda mitaani.
Huko, akaanza kuishi maisha ya mitaani, hakukuwa na aliyeamini kwamba mwanamke
yule aliyekuwa na utajiri mkubwa hatimaye ndani ya miaka mitatu tu, alikuwa
masikini wa kutupwa, aliyelala mitaani huku akiwa na binti yake
mdogo.
Aliogopa kwenda nyumbani kwao, alikumbuka namna wazazi wake walipomuita
na kumwambia kuhusu Edson, walimkataza kuwa na mwanaume huyo hivyo abaki peke
yake na kumlea mtoto wake lakini majibu yaliyotoka kinywani mwake, yalionyesha
dharau ya hali ya juu.
Leo hii, hakutaka hata kwenda huko nyumbani, moyo wake ulimuhukumu,
hakuwa na furaha, alijiona kutengwa na dunia nzima, kulia ikawa sehemu ya maisha
yake ya kila siku.
Kwa sababu hawakuwa na fedha, waliingia kwenye umasikini mkubwa, Cynthia
akafukuzwa shule ya kimataifa aliyokuwa akisoma ambayo kwa mwaka ada yake
ilikuwa ni zaidi ya milioni mbili.
Wakati akiendelea kuteseka mitaani ndipo alipofuatwa na watu wawili na
kupewa taarifa kwamba alikuwa akihitajika na wazazi wake, walimsamehe kwa kila
kitu kilichotokea na hivyo walihitaji kuishi naye.
Kidogo kwake ikaonekana kuwa nafuu, akaelekea nyumbani kwa wazazi wake
ambapo baada ya kuwaona tu, akaanza kuwaomba msamaha kwa yote yaliyotokea.
“Usijali binti yetu, tumekusamehe,” alisema baba yake.
Nyumbani kwao hakukuwa na maisha mazuri, kipindi cha nyuma alikuwa
akiwasaidia sana wazazi wake lakini baada ya mali kuzikabidhi kwa Edson, kila
kitu kikabadilika, misaada haikwenda tena kwa wazi wake, fedha zile zilizokuwa
kwenye akaunti zikawekewa mipaka, na kwa sababu alimpenda sana Edson, hakutaka
kujali sana kwani mapenzi yalimlevya.
Leo hii, aliona ubaya wa Edson, alijuta kwa kutokuwasikiliza wazazi
wake.Mapenzi yalisababisha kila kitu kilichotokea, mapenzi yakasababisha
kupoteza kila kitu alichokuwa nacho.
Kulia hakukusiha, hata kula hakula, moyo wake ulimuuma sana. Mara kwa
mara aliwasiliana na wakili wake na kumuuliza namna kesi ile waliyoshindwa.
Kwa jinsi ilivyoonekana tu, ilionyesha kuwa kulikuwa na mazingira ya
rushwa yaliyohusika na ndiyo maana ilikuwa nyepesi mno kwa Edson na ngumu mno
kwake.
Alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya. Wakati
mwingine alikaa na kumlaumu Mungu sababu ya kumchukua mume wake mapema mno hata
kabla binti yake hajawa mkubwa.
“Mungu! Kwa nini mimi? Kwa nini Edson amenidhulumu mali zangu?’ aliuliza
Anita huku akilia.
Pamoja na machozi yote, pamoja na huzuni zote, majonzi lakini ukweli
ulibaki palepale kwamba alidhulumiwa mali zake na mwanaume aliyekuwa akimpenda
ambaye aliamini kwamba angesaidiana naye kuzikuza mali zile.
*****
Kila kitu kilikamilika, kwenye suala la fedha, Edson alionekana kuwa
makini mno, alitaka kumtumia rafiki yake ambaye alikuwa na fedha nyingi, Nkone
kwa ajili ya kuhakikisha kwamba nyumba ile inakuwa yake.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kazi kubwa ya Nkone ilikuwa ni kujifanya mnunuaji wa nyumba ile, kwamba
mara Anita atakapoulizia mnunuaji basi Nkone ajitokeze na kusema kwamba yeye
ndiye mnunuzi lakini ukweli ulibaki palepale kwamba mwanaume huyo hakuinunua
nyumba ile bali ilikuwa mikononi mwa Edson.
Walifanikiwa kufanya mchezo huo mchafu, Anita akadhulumiwa nyumba yake na hivyo kwenda kuishi na wazazi wake. Edson na Nkone walibaki wakipongezana kwa kazi kubwa waliyokuwa wameifanya.
Walifanikiwa kufanya mchezo huo mchafu, Anita akadhulumiwa nyumba yake na hivyo kwenda kuishi na wazazi wake. Edson na Nkone walibaki wakipongezana kwa kazi kubwa waliyokuwa wameifanya.
Baada ya kuona kwamba Anita alitaka kuipeleka kesi mahakamani,
walichokifanya ni kuzungumza na hakimu James Marimba na kumwambia jinsi hali
ilivyokuwa na kwamba kama angefanikisha kushinda kwa kesi ile basi kitita cha
shilingi milioni mia mbili kilikuwa mezani.
Kilikuwa ni kiasi kikubwa cha fedha ambacho kusingekuwa na mtu yeyote
ambaye angekikataa, alichokifanya ni kukubaliana nao na ndiyo maana kesi
ikapelekwapelekwa tu na mwisho wa siku Edson kushinda katika mazingira ya
kutatanisha sana.
Baada ya kufanya michezo hiyo michafu ndipo walipoamua kukutana na
kusherehekea, kwao ulionekana kuwa ushindi mkubwa. Wakaitana kwenye Hoteli ya
New Paradise ambapo huko, wakala na kunnywa na baada ya hapo Edson kuingizwa
katika idadi ya mabilionea wakubwa nchini Tanzania.
“Karibu katika ulimwengu wa mabilionea,” alisema Nkone.
“Asante sana, cha msingi ni kuziongeza fedha hizi ziwe nyingi zaidi,
nitataka kufungua biashara nyingi,” alisema Edson.
“Hilo ni la maana sana. Nitakuwa pamoja nawe, nitakuonyeshea michongo
mingi ya biashara,” alisema Nkone.
Hicho ndicho kilichofuata, Edson akajiingiza katika biashara za kuuza
magari ambazo kwa namna moja au nyingine zikamfanya kuwa tajiri mkubwa. Kila
siku aliogelea katika bwawa la fedha, hakumkumbuka kabisa Anita, wakati mwingine
aliona kwamba msichana huyo na mume wake waliandaliwa kwa ajili yake, yaani
wapate utajiri ambao baadaye ungekuja na kuwa wake.
Jina lake likaanza kuwa kubwa, wanawake wakaanza kumpapatikia, kila
alipopita, watu walimzungumzia yeye kwa kuwa tu alikuwa na utajiri mkubwa ambao
hakukuwa na mtu aliyejua kwamba utajiri wote huo alikuwa amemdhulumu
Anita.
Wanawake wa mjini waliojua namna ya kuzitafuna pesa za wanaume
hawakumuacha Edson, kila siku walijilengesha kwake, walijiweka katika mikao
iliyojaa mitego ambayo ilimfanya mwanaume huyo kuingia kwenye kumi na nane zao,
kilichofuata ni kuponda raha naye.
Katika wanawake wote aliokuwa akiponda nao raha, alikuwepo mmoja ambaye
alimshikilia hasa, huyu aliitwa Jamila. Alikuwa msichana mrembo wa sura, mweupe,
mwembamba lakini huko nyuma ndiyo ilikuwa balaa.
Kila alipotembea, kulitingishika, kwenda kulia na kushoto. Siku ya
kwanza Edson alipomuona Jamila, alishtuka, hakuamini kama angeweza kumuona
msichana kama huyo jijini Dar es Salaam kwani aliamini wanawake wengi wa namna
hiyo walipatikana Mombasa.
Akashindwa kuvumilia, siku ya kwanza alipopewa penzi, likamchanganya,
hakutaka kusikia chochote kile, yeye na Jamila wakawa kama mama na mwana, kila
walipokwenda, walikuwa pamoja, waliyafaidi mapenzi huku Edson akipewa kila
alichokitaka kutoka mwilini mwa Jamila.
“Baby! Nataka wiki ijayo tusafiri!” alisema Jamila.
“Kwenda wapi?”
“Popote penye baridi kidogo, Tanzania joto sana.”
“Popote penye baridi kidogo, Tanzania joto sana.”
“Basi twende Uingereza au Hispania, unaonaje?”
“Hakuna tatizo! Tutakwenda huko.”
Maisha yalihitaji nini tena? Hakuwa na shida kama kipindi cha nyuma, kwa
wakati huo Edson alikuwa akinukia pesa, hakukumbuka kama miezi michache
iliyopita alikuwa katika maisha ya ufukara yaliyomfanya kurandaranda mitaani
kutafuta chakula tu.
Baada ya miezi miwili, akapata taarifa kwamba yule hakimu ambaye
alisimamia kesi yake, bwana James Marimba aliachana na kazi hiyo na hivyo
kujiingiza kwenye biashara.
Hapo ndipo walipoanza kujenga urafiki mkubwa. Yeye na bwana Nkone
wakamchukua Marimba na kumuingiza katika system yao na hivyo kuanza kushirikiana
katika biashara zao.
Wao watatu wakatengeneza mtandao mkubwa, wakapanua biashara zao na hivyo
kuingiza kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti zao. Maisha yalibadilika,
wakajikuta wakianza kujulikana nchini Tanzania, wakatengeneza majina yao kwa
kuwatumia vijana.
Walijua kwamba vijana walikuwa na nguvu kubwa hivyo wakawashikilia
vilivyo. Wakaanza kuwapatia fedha, kuwasaidia katika kununua pikipiki za
kufanyia biashara, hiyo yote ni kwa sababu walitaka kujitangaza na kujulikana
nchini Tanzania.
Walitaka kuonekana kama watu wema, wawasaidie vijana wengi lakini upande
wa pili walikuwa na mpango kabambe wa kufanya biashara za magendo, kuuza madawa
ya kulevya na kuua tembo katika mbuga mbalimbali za wanyama.
Walifanikiwa katika mipango yao, vijana waliwatangaza, wakaonekana kuwa
watu bora, matajiri wasiokuwa na sifa ambao kila siku walitamani watu wengine
kupata hata robo ya kile walichokuwa nacho.
Ili kuwafanya watu kutokuingilia mambo yao ya biashara za magendo ambayo
walitaka kufanya, kwanza wakajiweka karibu na jamii, yaani kwa Nkone, kitu
alichokifanya ni kuisaidia jamii kwa kuwaletea chakula kutoka
mikoani.
Alipokwenda Mbeya, alinunua mpunga kwa bei waliyoitaka wakulima,
hakujali kama ilikuwa kubwa au la, alipohakikisha manunuzi yamefanyika,
alisafiri mpaka Dar es Salaam huku akiwa na tani zaidi ya mia moja na kuelekea
masokoni, huko, mchele aligawa bure kabisa kwa kila mtu
aliyetaka.
Ilikuwa ni kazi ya kujitoa ambayo ilimfanya kupoteza kiasi kikubwa cha
fedha, yeye, hakuangalia hicho, alichokitaka ni kuhakikisha kwamba kila kitu
kinakuwa kama kilivyotakiwa kuwa.
Watu wakawapenda, hakuishia kwenye mpunga tu, bali ngano, unga na vitu
vingine vyote alivipeleka jijini Dar es Salaam na kuwasaidia watu mbalimbali
waliofika jijini humo na hata wale waliotoka mikoani.
Jina la bwana Nkone likawa kubwa, akajulikana sana kiasi kwamba kila
alipopita, watu walikuwa tayari kulisimamisha gari lake, kulisafisha kisha
kumwambia aendelee na safari na huku wakati mwingine wakidiriki mpaka kupiga
deki barabara.
“Huyu jamaa atakuwa malaika tu,” alisema kijana mmoja.
“Kwa nini?”
“Haiwezekani kuwe na binadamu mwenye roho nzuri kama hii. Jamaa anatoa chakula kutoka mikoani na kuja kugawa bure, hivi kuna mtu anaweza kuwa na moyo huo?” alihoji kijana huyo.
“Haiwezekani kuwe na binadamu mwenye roho nzuri kama hii. Jamaa anatoa chakula kutoka mikoani na kuja kugawa bure, hivi kuna mtu anaweza kuwa na moyo huo?” alihoji kijana huyo.
Ukiachana na huyo, mtu mwingine, bilionea ambaye aliibuka alikuwa bwana
Marimba. Huyu naye alikuwa na moyo wa kuwasaidia Watanzania, alitaka watu wote
waliokuwa na magonjwa ya moyo wapate tiba bure kabisa na kusiwepo na wagonjwa wa
kusafiri kwenda India kutafuta tiba.
Akajenga hospitali kubwa jijini Dar ambayo iliwashughulikia zaidi
wagonjwa wa magonjwa ya moyo. Kwake, hiyo ilikuwa sifa kubwa, watu wengi
walimsifia kwamba alikuwa na moyo mzuri kama bwana Nkone.
Hakuishia hapo, alichokifanya ni kupanga mikakati kabambe ya kuhakikisha
kwamba dawa zinapatikana bure kabisa kwenye hospitali zote, gharama zilikuwa
chini yake.
Alipoteza kiasi kikubwa cha fedha lakini hakuangalia, alichokitaka ni
kujenga uaminifu katika jamii kwani kile alichotaka kukifanya na mabilionea
wenzake kilikuwa kikubwa mno ambacho kingewaingizia fedha kupita
kawaida.
“Gharama za dawa kiasi gani?” aliuliza mgonjwa mmoja katika hospitali
moja jiji Dar es Salaam, alionekana kuwa hoi.
“Zote ni elfu themanini!”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mmh! Jamani dokta, nitaweza kulipia kweli na maisha yangu
magumu?”
“Usijali! Umekwishalipiwa.”
“Nimelipiwa! Na nani?”
“Na bwana Nkone. Analipia gharama za dawa zote,” alisema daktari.
“Usijali! Umekwishalipiwa.”
“Nimelipiwa! Na nani?”
“Na bwana Nkone. Analipia gharama za dawa zote,” alisema daktari.
Kama ilivyokuwa kwa Nkone hata kwake alijijengea heshima kubwa,
Watanzania wakachanganyikiwa, mapenzi waliyokuwa nayo juu yake yalikuwa makubwa
mno, hawakuamini kama kungetokea mtu ambaye angekuwa tayari kuingia gharama kwa
ajili ya Watanzania.
Wagonjwa wa magonjwa ya moyo wakafika katika hospitali yake, huko,
walipatiwa matibabu bure tena kutoka kwa madaktari waliobobea katika magonjwa
hayo.
Ilikuwa sifa kwa Watanzania kwani pia wagonjwa wengi kutoka Rwanda,
Kenya na Uganda walifika Tanzania kwa ajili ya kupatiwa matibabu katika
hospitali hiyo.
Edson ambaye baada ya kupata ubilionea aliamua kuitwa jina lake la pili
la Kambani kama ubini wake, akaamua kuwasaidia Watanzania katika kujenga viwanda
vya makaratasi, viatu na nguo na kuwaajiri Watanzania wengi tena wa rika
zote.
Alipoona amefanikisha katika hilo, akaanza kujenga vituo vya watoto
yatima, watoto wote waliokuwa wakizurura mitaani wakachukuliwa na kupelekwa
katika vituo hivyo ambapo huko walisomeshwa, walilishwa na kuvarishwa kama watu
wengine.
Kambani hakuishia hapo, alichokifanya ambacho kikaonekana kuwa kama
kujitangaza zaidi ni kusaidia kujenga misikiti na makanisa. Kupitia msaada huo,
akajikuta akipata jina kubwa zaidi nchini Tanzania.
Japokuwa kulikuwa na watu wengi waliosema maneno mbalimbali lakini
hakuacha, misikini na makanisa ambayo ilisimamisha ujenzi kwa kuwa watu walikosa
fedha, aliimalizia na maisha kuendelea.
Akajijengea jina kubwa, utajiri wake ukaongezeka, kila alipopita, watu
walimpongeza, walimsifia kitu kilichomfanya yeye na mabilionea wengine kuitwa
sana ikulu.
Huko, walipongezwa kwa kazi kubwa waliyoifanya pasipo Watanzania kujua
kwamba mbali na misaada hiyo, watu hao walikuwa na mawazo ya kujiingiza katika
biashara haramu za kuuza madawa ya kulevya na kuua wanyama mbugani ili kuongeza
utajiri wao. Hilo, Watanzania hawakulifahamu.
*****
Miaka mitano ikapita, utajiri wao ulikuwa mkubwa zaidi, ile mipango
waliyokuwa wameiweka, ikafanikiwa na katika kipindi hicho walikuwa wakiingiza
kiasi kikubwa cha fedha kupitia madawa ya kulevya na kuua wanyama wengi
mbugani.
Hakukuwa na mtu aliyefahamu kama yale madawa ya kulevya ambayo
yaliingizwa sana nchini yalikuwa chini yao. Kwa viongozi ambao walijua,
walinyamazishwa kwa kupewa kiasi fulani cha fedha, hivyo
wakanyamaza.
Mara kwa mara waliwatuma vijana wao kwenda Pakistan ambapo huko
walichukua madawa kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa na kuyaleta nchini Tanzania
ambapo yaliuzwa hapo na mengine kupelekwa sehemu mbalimbali barani
Afrika.
Wao ndiyo walikuwa wasambazaji wakubwa wa madawa ya kulevya barani
Afrika. Kila mzigo uliokuwa ukiingia Afrika ilikuwa ni lazima upite mikononi
mwao na kuwatuma vijana kusambaza katika nchi mbalimbali.
Wakawa na genge la watu zaidi ya ishirini, tena vijana wa kike na wa
kiume ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kusambaza madawa hayo sehemu
mbalimbali.
Ilikuwa ngumu mno kuwagundua, misaada waliyoitoa kwa jamii iliwafanya
watu kutokuamini hata pale tetesi za chini ziliposikika kwamba watu hao
walijihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Kwa kuwaangalia, walionekana kuwa wapole sana ambao waliwapenda watu
wote pasipo kujua kwamba upande wa nyuma watu hao walikuwa wauaji wakubwa ambao
kamwe hawakutaka kupata hasara.
Kila mtu aliyefika mbele yao na kusema kwamba mizigo ilikamatwa, aliuawa
kwani katika biashara yao hiyo hawakutaka kupata hasara ya aina yoyote
ile.
“Nisikilize Ali, unazingua...” alisema Kambani huku akionekana kuwa na
hasira, mkononi mwake alikuwa na bastola.
“Nisamehe bosi, ilikuwa bahati mbaya.”
“Huo ni uzembe na lazima uulipe, yaani tupoteze bilioni moja kwa ajili
yako, haiwezekani Ali ni lazima ufe,” alisema Kambani huku akiichukua bastola
yake kutoka kiunoni.
“Bosi subiri kwanza.”
“Nisubiri nini? Hivi unafikiri tunafanya kazi ya kanisa? Hivi unafikiri hizi fedha tuliziokoka tu sehemu?” aliuliza Kambani.
“Nisubiri nini? Hivi unafikiri tunafanya kazi ya kanisa? Hivi unafikiri hizi fedha tuliziokoka tu sehemu?” aliuliza Kambani.
“Bosi...bosi....”
“Paaa...paaaa...”
Ilisikika milio ya bastola ndani ya jumba hilo la kifahari, hapohapo,
kijana yule aliyeitwa kwa jina la Ali akaanguka chini na damu kuanza kumtoka.
Tofauti na mabilionea wengine waliokusanyika mahali hapo, Kambani alionekana
kuwa na hasira mno, alijua kwamba alitoka kwenye maisha ya shida, yaliyojaa
umasikini ambayo hakutaka kurudi tena, hivyo alitaka kuhakikisha anafanya lolote
lile lakini mwisho wa siku utajiri wake kuendelea
kuwepo.Miaka mitano ilipita tangu aachane na Anita, hakutaka kumkumbuka kabisa, ule utajiri aliomdhulumu, alitaka kuuendeleza na kuwa bilionea mkubwa barani Afrika, hivyo ilikuwa ni lazima kuwamaliza vijana ambao walileta masihara.
“Nkone, hawa vijana wapumbavu sana, ukiwachekea, mwisho wa siku utajikuta unaendesha mkokoteni Tandale,” alisema Kambani huku akimwangalia Nkone.
“Kweli kabisa, ila ungempa nafasi nyingine.”
“Hakuna cha nafasi! Unafikiri amekamatwa kweli? Alitaka kutuchezea dili tu. Marimba, tunatakiwa tuwe makini sana. Umeachana na uhakimu ili utengeneze pesa, sasa wapumbavu kama hawa wakitokea, si utarudi tena kuwa hakimu na kula rushwa za shilingi elfu kumikumi? Tusitake masihara kabisa na pesa,” alisema Kambani.
Biashara zao za madawa ya kulevya zilizidi kusambaa, walizidi kupata wateja wengi barani Afrika, wakagawana majukumu kwamba ilikuwa ni lazima wahakikishe wanapata matawi zaidi, hivyo walichokifanya ni kuwafuata wasanii wa muziki na watu wengine maarufu na kuwatumia katika usambazaji wa madawa yao.
Ukiachana na hayo, pia walihakikisha wanacheza michezo michafu katika viwanja vya ndege, wakawakamata polisi wote ili kila mtu wao anapopita asiweze kupekuliwa, na hilo likafanyika kwa haraka sana.
Hakukuwa na uwanja wa ndege barani Afrika uliokuwa hatari kwao, kila uwanja walihakikisha wanaukamata vilivyo. Waliingiza fedha, walitanua kwa kununua magari ya kifahari ila pamoja na yote hayo, walihakikisha kwamba jukumu lao la kuisaidia jamii lilikuwa palepale na ndiyo kitu pekee ambacho kiliifanya hata serikali kutokuwafuatilia sana.
“Ni lazima tuishi kwa akili Kambani! Vipi kuhusu wale Waarabu?” aliuliza Nkone.
“Waarabu gani?”
“Wale wa Tunisia!”
“Wako poa, leo asubuhi walinitaarifu kwamba mizigo imeingia bila matatizo na fedha watatuma jioni,” alisema Kambani.
“Safi sana!”
“Ila kuna kitu,” aliingilia Marimba.
“Kitu gani?”
“Unamkumbuka yule malaya uliyekuwa ukiishi naye?”
“Nimeishi na wengi! Yupi?”
“Yule mwenye mali.”
“Unamaanisha Anita?”
“Ndiyo!”
“Amefanya nini?”
“Unafikiri huu ndiyo utakuwa mwisho?”
“Kivipi?”
“Nina uhakika kuna siku atalianzisha tu! Yaani ile kesi inaweza kufufuliwa upya na akaja kushinda,” alisema Marimba.
“Ila wewe si ndiye uliimaliza mahakamani?”
“Ndiyo! Ila nimekumbuka kwamba nilifanya kosa!”
“Kosa lipi?”
“Nilipomaliza kesi ile nilisema kwamba mahakama ilikuona hauna hatia,” alisema Kambani.
“Si ndiyo sikuwa na hatia!”
“Ndiyo! Ila kuna kitu ambacho ni lazima ukifahamu.”
“Kipi?”
“Kuna utofauti kati ya mahakama kutokukuona kuwa na hatia na mahakama kukuachia huru,” alisema Kambani.
“Utofauti wake ni upi?”
“Mahakama inapokuona hauna hatia, inamaanisha kwamba jalada linafungwa na hivyo kesi kuisha ila mahakama inapokuachia huru, inamaanisha kwamba inawezekana kuna vipengele fulani havipo ila vipengele hivyo vikipatikana, kesi inaweza kuanza tena,” alisema Kambani.
“Sasa nani ataianzisha?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kama huyo Anita akienda mahakamani, ni lazima jalada lifunguliwe tena, kesi ianze kuunguruma.”
“Daah! Kwa hiyo?”
“Tumuue huyu Anita kupoteza ushahidi! Vinginevyo, baadaye itakula kwako,” alishauri Marimba.
“Hakuna tatizo! Nipo tayari kuua ili kuzilinda mali zangu! Nipo tayari kumuua Anita.”
“Basi fanya hivyo! Anapoishi si unapajua?”
“Ndiyo!”
“Basi tuma vijana wakammalize.”
“Haina tatizo! Nitafanya hivyo leo hiihii,” alisema Edson Kambani na kuchukua simu yake, akawaambia vijana wake kwamba wafanye lolote liwezekanalo ili Anita aweze kuuawa haraka iwezekanavyo!
Alichokifanya ni kuwaambia mahali alipokuwa akiishi. Vijana hao wakasema kwamba ni lazima wafanye kazi hiyo. Hivyo wakajiandaa.
****
Binti yake alikuwa na miaka mitano tu, maisha yalimpiga mno mpaka yule Anita aliyeishi kitajiri kupigika, mwili kuchoka sababu ya mawazo mengi huku mara kwa mara akiumwa magonjwa mbalimbali, hiyo ilitokana na mawazo lukuki aliyokuwa nayo.
Bado moyo wake haukuamini kama yeye ndiye aliyekuwa akipitia maisha yale, kwake, hiyo ilionekana kuwa kama ndoto ambapo baada ya muda fulani angeshtuka na kujikuta kitandani, akiwa na mume wake mpendwa huku pembeni yake akiwepo binti yake aliyekuwa akimpenda mno.
Moyo wake ulimchukia mno Edson, hakuamini kama duniani kulikuwa na mtu aliyekuwa na roho mbaya kama alivyokuwa Edson, kila siku maisha yake yalikuwa ni kusali tu, yaani Edson apate matatizo, augue ugonjwa usiopona au kama itawezekana afe kabisa.
Hilo likawa kama dua la kuku, kamwe halikumpata mwewe, wakati akiomba Edson apate matatizo au afe ndiyo kwanza mwanaume huyo alizidi kufanikiwa na kuwa bilionea mkubwa.
Siku zikakatika, miezi ikaenda mbio na miaka nayo kusogea, muda haukumsubiri mtu. Baada ya miaka mitano, ndiyo kwanza mtoto wake, Cynthia alikuwa na miaka kumi.
Shule aliyokuwa akisoma ilikuwa ni shule za watu masikini ambazo zilijulikana kama Kayumba. Huko, alionekana kuwa na mawazo mno, ndiyo kwanza alikuwa darasa la tatu lakini kwa jinsi mama yake alivyokuwa na huzuni kila siku, kukamuathiri, akawa na mawazo lukuki kiasi ambacho kila siku alionekana kutokuwa na furaha kabisa.
“Cynthia, tatizo nini mwanangu?” aliuliza mwalimu Asha, aliamua kumuita Cynthia kwa lengo la kumuuliza kwani kila siku mtoto huyo hakuwa na furaha kabisa.
“Hakuna kitu mwalimu.”
“Kweli?”
“Ndiyo! Hakuna kitu.”
Japokuwa alijitetea sana lakini bado walimu walijua kwamba kulikuwa na tatizo ambalo mtoto huyo hakutaka kuliweka wazi. Walitaka kujua kwani hali ile ilimfanya mpaka kufanya vibaya darasani.
Walichoamua kama walimu ni kumuagiza kumuita mama yake, kesho akafika naye shuleni hapo. Anita alikonda sana, alivyoonekana kwa walimu wale, walihisi kwamba mwanamke huyo alikuwa mgonjwa, tena wa wa kifua kikuu kilichokomaa ambao waliishi katika hatua za mwisho za kuvuta pumzi ya dunia hii.
Walimu walishtuka mno, hawakuamini kama kweli yule alikuwa mama yake Cynthia, mtoto mrembo aliyemvutia kila mtu aliyemwangalia. Alipofika mbele ya walimu hao, Anita akaanza kukohoa mfululizo, hiyo ilionyesha kwamba alikuwa akiumwa, hivyo wakamchukua na kumpeleka ofisini.
“Wewe ni nani?” aliuliza mwalimu Asha, ndiye alikuwa mwalimu wa darasa wa Cynthia.
“Mama yake Cynthia.”
“Unaitwa nani?”
“Anita.”
“Kuna kitu kinaendelea nyumbani kwako?”
“Kitu gani?”
Alichokifanya mwalimu ni kumwambia Cynthia aende nje ya ofisi ile kisha wao kama walimu kuanza kuzungumza na Anita. Mwanamke huyo hakutaka kuwaficha, alichokifanya ni kuwahadithia kila kitu kilichotokea maishani mwake tangu alipokuwa na mumewe, alipofariki katika ajali ya boti ya Royal Palm, alipokuja kuwa na Edson mpaka kumuacha na kumdhulumu mali zake.
“Huyuhuyu Edson Kambani au?”
“Ndiye huyohuyo! Alichukua kila kitu kutoka kwangu,” alijibu Anita.
“Hapana! Haiwezekani!”
“Kweli tena!”
“Labda useme kingine lakini si hicho,” alisema mwalimu mmoja.
Hakukuwa na aliyemwamini, walimfahamu Kambani, alikuwa mmoja wa watu waliosaidia sana jamii, alikuwa tayari hata yeye kulala njaa lakini mwisho wa siku watu waliokuwa na shida wapate chakula.
Kitendo cha Anita kusema kwamba mali alizokuwa nazo Kambani zilikuwa zake, hakukuwa na mtu aliyemwamini hata kidogo , tena ndiyo kwanza walimu haohao walimsuta.
Anita aliumia moyoni mwake, hakuamini kama hakuaminika hata kidogo, kilichobaki ni kuumia moyoni mwake, hakuamini kama watu hao walifikia hatua ya kumwamini sana Kambani kiasi kwamba hata aliposema kwamba mwanaume huyo alimdhulumu mali yake, hakukuwa na aliyemwamini hata kidogo.
Akaondoka shuleni hapo huku akilia, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno, walimu wale badala ya kumfariji kutokana na matatizo aliyokuwa akipitia ndiyo kwanza walimsabababishia maumivu makubwa moyoni mwake.
Wakati amefika barabarani, kituoni kwa ajili ya kuchukua daladala kurudi nyumbani, ghafla, gari moja lisilokuwa na namba likasimama mbele yake. Hata kabla hajajiuliza lilikuwa gari la nani, mara vijana wanne waliokuwa na bunduki mikononi wakateremka na kumfuata.
Watu waliokuwa karibu naye wakapigwa na taharuki, hawakujua watu wale walikuwa wakina nani. Wakati raia walipojaribu kutaka kumsaidia Anita, risasi kadhaa zikapigwa hewani, wote waliokuwa mahali hapo wakakimbia.
Anita akachukuliwa na kupakizwa ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea asipopafahamu. Mapigo yake ya moyo yakaanza kumdunda, hakujua watu hao walikuwa wakina nani na walihitaji nini. Alipojaribu kuuliza, akapigwa vibao viwili mfululizo kama ishara ya kuonyeshwa kwamba watu hao hawakuhitaji maswali yoyote yale. Akabaki kimya.
*****
Kilichokuwa kimepangwa ni kumuua Anita tu, Edson Kambani alijipanga, hakutaka kusikia kitu chochote kile, alichoambiwa kwamba mwanamke huyo alikuwa hatari na hivyo alitakiwa kumuua haraka iwezekanavyo.
Akawatuma vijana wake kwa ajili ya kukamilisha kazi ambayo kwake ilionekana kuwa kubwa, alitulia nyumbani huku mara kwa mara macho yake yakiwa kwenye simu yake kwani alitegemea muda wowote ule angepokea simu kutoka kwa vijana wake wakimpata taarifa ya ushindi mkubwa.
Aliisikilizia simu ile mpaka pale aliposikia ikiita, kwa harakaharaka akaichukua na kuipeleka sikioni ambapo sauti ya mwanaume kutoka upande wa pili ikaanza kusikika.
“Tumekamilisha mkuu! Nini kinafuata?” aliuliza mwanaume huyo.
“Mpo naye?”
“Ndiyo mkuu! Tunasikia neno lako tu, kama kumuua au la.”
“Nyie muueni tu, hakuna zaidi ya hilo,” alisema Kambani huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
Vijana wale waliokuwa na Anita waliendelea na safari yao, mwenzao alipokuwa akizungumza kwa simu na kupewa maagizo kwamba Anita alitakiwa kuuawa, nao walisikia ila wakawa wanahitaji kusikia zaidi kama kweli kile walichokisikia ndicho walichoagizwa au la.
Anita alibaki akitetemeka, kila alipowaangalia vijana wale, walionekana kama walikuwa maadui zake ila hakujua ni nani aliwatuma kwa ajili ya kummaliza. Kichwa chake kilikuwa na maswali mengi, hata simu ilipopigwa na mwanaume mmoja kuzungumza na huyo mtu aliyejifanya kuwa bosi, alijitahidi kuisikiliza sauti hiyo ili kuona kama aliitambua lakini aliambulia patupu.
“Bosi kasemaje?” aliuliza mwanaume mmoja.
“Tumuue tu.”
“Hakuna noma.”
Anita alivyosikia hivyo, akachanganyikiwa, akaanza kulia kwa uchungu mkubwa. Aliogopa kuzungumza lolote lile kwani bado alikumbuka vema lile kofi alilopigwa dakika chache zilizopita.
Vijana wale hawakuzungumza kitu chochote kile zaidi ya kuanza kuzikoki bastola zao tayari kwa kufanya mauaji mbele ya safari kwani piga ua ilikuwa ni lazima Anita auawe kikatili.
Wakati huo gari lilikuwa likielekea katika Msitu wa Pande. Njiani, walikuwa wakizungumza tena kwa kupongezana kwa kazi kubwa waliyoifanya na baada ya muda wangeikamilisha na hivyo kugaiwa kiasi cha fedha kilichobaki.
“Jamani nimewafanya nini?” aliuliza Anita, aliona kama kupigwa, acha apigwe lakini ilikuwa ni lazima ajue alichokifanya mpaka kutekwa.
“Nilikwambiaje?” aliuliza mwanaume yule aliyempiga mara ya kwanza.
“Jamani! Mnanionea, sijamfanya mtu kitu chochote, nimetoka kumpeleka binti yangu shule, jamani, nimef...” alisema Anita lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake akakatishwa na sauti nzito ya kiume.
“Nyamazaaa...hayo maswali utamuuliza Kambani mkikutana ahera, sisi tunakamilisha kile alichotuagiza,” alisema mwanaume huyo.
Hapo ndipo Anita alipopata jibu ya kile kilichokuwa kikiendelea, moyo wake uliumia mno kwani kitendo cha kuambiwa kwamba mtu aliyekuwa nyuma ya tukio hilo alikuwa Kambani kilimshtua sana.
Alijua kwamba mwanaume huyo ndiye aliyemdhulumu mali zote na kisha kumfukuza, sasa ilikuwaje mpaka leo hii bado alikuwa akimtafuta na kutaka kumuua? Miaka saba ilipita, leo hii aliwatuma watu ili wakamuue, akajikuta akimchukia zaidi.
“Jamani! Hivi nimemfanya nini Edson...jamani, nimemfanya nini mimi? Kanidhulumu mali zangu, bado hajaridhika mpaka kutaka kuniua?” aliuliza Anita huku akilia kama mtoto.
Hakukuwa na mtu aliyeongea kitu chochote kile, walichokifanya ni kuendelea na safari yao. Mara baada ya kupita Mbezi Mwisho, wakaendelea mbele zaidi kuufuata msitu wa Pande, walipokwenda kwa umbali fulani, wakawa wamekwishakaribia.
“Simamisha gari kwanza,” alisema mwanaume mmoja mwenye sauti ya uongozi. Gari likasimamishwa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tumuueni hapahapa au tuingia ndani ya msitu?” aliuliza mwanaume huyo.
“Tungeingia ndani ya msitu, hapa noma,” alisema mwanaume mmoja.
“Basi poa, liingize gari ndani.”
Wakati dereva akiwa amekwishapiga gia tayari kwa kuingia msituni, ghafla mlio mkubwa ukasikika nyuma, gari lile walilokuwemo likagongwa kwa nyuma na gari lililoonekana kuwa kwenye mwendo wa kasi.
“Puuuuuu...” mlio huo wa kugongwa ulisikika.
Kwa kuwa dereva hakuwa amefunga mkanda, akajikuta akikigonga kichwa chake katika kioo cha mbele, wale wanaume wengine nao wakarushwa mpaka mbele ya gari lile na kujibamiza kwenye kioo kile ila kwa kuwa Anita aliwekwa chini, hata lile gari lilipogongwa, hakwenda mbele, alijigonga kwenye kiti cha mbele tu kitu ambacho hakikumletea hata maumivu yoyote yale.
Huku kila mmoja akiwa anaugulia maumivu, mara wanaume watatu waliokuwa na bunduki mikononi mwao wakatokea mahali hapo, wakaufungua mlango mkubwa wa gari lile na kisha kuanza kuwamiminia risasi wanaume waliokuwa ndani ya gari lile.
Anita ambaye alikuwa amechanganyikiwa, hakujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea, alijikuta akiikutanisha mikono yake na kuanza kumuomba Mungu ili amuokoe na kile kilichokuwa kikiendelea garini mule.
Alitetemeka mpaka kujisaidia haja ndogo pale alipokuwa. Wanaume wale wakaanza kuangalia huku na kule ndani ya gari lile, walikuwa wakimtafuta Anita aliyekuwa humo, walipomuona, wakamshika mkono na kuanza kumtoa kinguvu.
“Let’s get out of here,” (Tuondoke hapa) alisema mwanaume mmoja kwa Kiingereza.
“Who are you? What have I done to you?” (Nyie ni wakina nani? Nimewafanya nini?) aliuliza Anita.
“Don’t ask any question, you have to do what we want you to, otherwise, we’ll kill you,” (Usiulize swali lolote, unatakiwa kufanya tunachotaka ukifanye, vinginevyo tutakuua) alisema mwanaume huyo. Anita akabaki kimya.
Walichokifanya ni kumchukua na kisha kuondoka naye mahali hapo. Ndani ya gari, bado Anita alikuwa akitetemeka, watu wale waliokuwa ndani ya gari lile walionekana kama si Watanzania kwani muda mwingi wa mazungumzo yao walikuwa wakizungumza Kiingereza tu.
Mbali na hilo, hata ngozi zao hazikuonyesha kama walikuwa Watanzania, walionekana kama watu kutoka katika nchi za Uarabuni waliokuwa na wazazi wenye mchanganyiko wa rangi.
Anita hakujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea, alijiuliza maswali mengi kuhusu watu hao lakini hakupata jibu lolote lile. Aliokolewa kwenye hatari ya kuuawa na watu hao lakini bado hakuwa na uhakika kama watu hao walikuwa watu wema kwake au watu wabaya.
“Who are you?” (Nyie ni wakika nani?)
“Calm down, we are good people to you,” (Tulia, sisi ni watu wema kwako) alisema mwanaume mmoja.
Anita hakuweza kunyamaza, muda wote alikuwa na hofu moyoni mwake, japokuwa aliambiwa na watu hao kwamba asiwe na wasiwasi wowote lakini hilo halikutosha kumfanya kujiachia ndani ya gari hilo.
Gari lilikwenda mpaka lilipofika Magomeni Mapipa alipokuwa akiishi na wazazi wake, gari likasimama nje ya nyumba hiyo na kumtaka kuteremka. Kwa kuwa gari lilikuwa na vioo vyeusi, hakugundua hapo kulikuwa wapi ila aliposhuka na kugundua kwamba palikuwa nyumbani kwao, akashtuka.
“Imeakuwaje tena? Nyie ni wakina nani?” aliuliza Anita huku akionekana dhahiri kuchanganyikiwa.
“Usijali! Nenda nyumbani! Kuwa makini, watu wabaya bado wanakutafuta. Tutakufuata wiki ijayo, tunakutafutia nyumba na utakwenda kuishi huko,” alisema mwanaume mmoja.
“Nyie ni wakina nani lakini?” aliuliza Anita kwa mshangao.
“Tulikwambia sisi ni raia wema. Anita! Roho yako inahitajika sana, ila usijali, tutakulinda wewe na mtoto wako,” alisema mwanaume yule.
“Sawa! Nani anataka kutuua?”
“Edson Kambani.”
Watu wale hawakutaka kuzungumza zaidi, walichokifanya ni kuondoka mahali hapo huku wakisisitiza kwamba ilikuwa ni lazima wamlinde mwanamke huyo na mtoto wake.
Bado Anita alibaki kuwa na maswali mengi, watu wale walimshangaza sana, hakuwafahamu, hakujua ni wakina nani na walihitaji nini na kwa sababu gani waliamua kumlinda.
Hakutaka kulipuuzia suala hilo, alichokifanya ni kuwaambia wazazi wake ambao hata nao pia wakaonekana kushtuka sana.
“Haiwezekani! Ni wakina nani hao?” aliuliza baba yake.
“Hata mimi siwajui, ila ni watu wazuri nahisi.”
“Mhh! Nina wasiwasi! Isije ikawa wanakutengenezea mazingira mazuri ya kukuua!” alisema mama yake.
“Sidhani mama! Ngoja niendelee kupeleleza nijue ni wakina nani,” alisema Anita huku akiingia chumbani mwake, kichwa chake kilichanganyikiwa mno.
*****
Kambani alichanganyikiwa, hakuamini kile alichokuwa akikiangalia kwenye televisheni kwamba watu aliokuwa amewatuma, walikutwa wameuawa Mbezi ya Kimara huku miili yao ikiwa imepigwa risasi.
Aliiangalia televisheni ile na kuwasikiliza mashuhuda wa tukio hilo ambalo walilieleza tukio kwa ujumla kwamba gari hilo lilisimamishwa pembeni mwa msitu na baada ya muda kulikuwa na gari jingine ambalo liliigonga gari hilo kwa nyuma.
Baada ya tukio hilo, wanaume watatu wakateremka na kulifuata lile gari kisha kuwapiga risasi watu hao na kuondoka na mwanamke ambaye hakuweza kujulikana.
Kambani hakujua hao watu walikuwa wakina nani, alijua dhahiri kwamba mwanamke huyo alikuwa Anita, kitu kilichomsumbua kichwani mwake ni juu ya watu hao, kwa nini waliamua kuwaua vijana wake? Kila alichojiuliza, alikosa jibu kabisa.
Alichokifanya ni kuwapigia simu mabilionea wenzake kwa ajili ya kuzungumza nao, alitaka kuwaambia kila kitu kilichotokea ili kujua kama alitaka kuchukua hatua ya pili kumuua Anita, alitakiwa kufanya nini.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment