Simulizi : Ukweli Wenye Kuuma ( Painful Truth )
Sehemu Ya Tano (5)
Ilikuwa ni taarifa njema kwa Watanzania hasa mara baada ya kupewa habari kwamba mwanaume ambaye alikuwa amemuua Spika wa Bunge, Annastazia Kapama alikuwa amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Watu wakashindwa kujizuia, wakaanza kuandamana huku wakimtaka Andy ahukumiwe kifo katika kipindi ambacho atakanyaga katika mahakama kuu ya Tanzania. Vyombo vya habari ndivyo ambavyo vilikuwa vikitangaza habari hiyo zaidi na zaidi na kufanya vyanzo vyao vya habari kusikilizwa na kununulika kupita kiasi.
Maandamano ya kumtaka Hakimu kumuhukumu Andy kifo yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Mara ya kwanza yalikuwa yameanzia Dar es Salaam lakini kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo maandamano hayo yalivyozidi kuongezeka.
Watu wa Morogoro nao wakaanza kuandamana, Dodoma wakafuata huku nao Tanga wakishika nafasi. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo yalizidi kuenea mpaka kufika mkoani Kigoma. Katika maandamano yote hayo, mabango ambayo yalikuwa yakimtaka Andy ahukumiwe kifo ndio ambayo yalikuwa yakionekana muda wote.
Watanzania hawakutaka Andy aendelee kuishi, walimtaka auliwe kwa kunyongwa au hata kwa kuchomwa sindano iliyokuwa na sumu kali. Kifo cha Spika wa Bunge, Annastazia ambacho kilitokea wiki iliyopita kilikuwa kimewagusa sana, mioyo yao ilikataa katakata kumsamehe Andy ambaye alionekana kuwa kijana mdogo.
Ndani ya masaa mawili tu, dunia nzima ikapata taarifa juu ya kuamatwa kwa Andy. Dunia ikagawanyika, kuna wengine ambao walifurahi lakini kuna wengine ambao hawakupenda akamatwe kwani bado alikuwa akihitajika kutengeneza zile dawa zake ambazo zilikuwa zikitibu magonjwa ya moyo na mengine ndani ya mwili wa binadamu.
Mbali na Dawson, hakukuwa na mtu yeyote duniani ambaye alikuwa akifahamu kama Andy huyo ndiye ambaye alikuwa ametengeneza virusi vya Katapillar ambavyo vilikuwa vikisambaza ugonjwa hatari wa PENINA. Kwa kuwa Andy alikuwa na uraia wa Tanzania, serikali ya Marekani haikutaka kuingilia kwa chochote kile japokuwa mtu huyo alikuwa muhimu sana katika maisha yao.
Jina lake na picha zake ndivyo vilikuwa vitu ambavyo vilitawala sana katika vyombo mbalimbali vya habari. Kila mtu ambaye aliiangalia picha ya Andy alionekana kushtuka kwa sababu alionekana bado kijana mdogo sana ambaye alithubutu kunyanyua kisu na kumchoma Annastazia.
Kutokana na maandamano kuongezeka kila siku, siku ya kusomwa kwa hukumu ya Andy ikatangazwa. Kesi hiyo ikapelekwa moja kwa moja mpaka mahakama kuu tayari kwa kusomwa. Muda wote Andy alionekana kuwa na huzuni kitu kiliwapelekea watu kuona kwamba alikuwa akijuta kwa kile alichokuwa amekifanya.
“Ninawahuzunikia wanaume wa nchi hii. Hivi hawajui kwamba wanawake hawa ni wanyama na shetani wakubwa sana? Nilikuwa tayari kuwatetea lakini badala ya kuhuzunika kwamba nimekamatwa, wao ndio kwanza wanashangilia” Andy alisema huku akionekana kuwa na majonzi.
“Ni lazima niue mamilioni ili kuokoa mabilioni” Andy alijisemea.
Bado hali ya hewa nchini Tanzania ikaonekana kuchafuka, kila siku idadi ya watu ambao walikuwa wakiandamana ilikuwa ikiongezeka barabarani. Mapolisi walikuwa wakizidiwa nguvu na wananchi hao ambao walionekana kuwa na hasira kupita kawaida.
Wao, kiu yao ilikuwa ni kutaka kumuona Andy akihukumiwa kifo tu, ingawa siku ya hukumu ilikuwa imepangwa lakini watu waliiona siku hiyo ikichelewa kufika. Hawakutaka kumuona Andy akiendelea kuendelea kuvuta pumzi ya dunia hii.
Maandamano yaliendelea na hatimae fujo kuanza kutokea. Vibanda vilikuwa vikichomwa moto huku hata wakati mwingine mapolisi ambao walikuwa wakiwazuia katika maandamano yao wakianza kupigwa. Watu hawakutaka kusikia kitu chochote zaidi ya hukumu ya kifo tu.
Makaratasi yakachapishwa na picha za Andy kuweka huku maneno ambayo yalikuwa yakimtaka kuhukumiwa kifo yakiwa yanasomeka vizuri. Vijana wadogo ambao hawakuwa wakifuatilia kitu chochote kile nao wakapandikizwa sumu ya kutaka Andy ahukumiwe kifo.
****
Mchungaji Wayne na mkewe, Happy walionekana kuhuzunishwa na taarifa ile ambayo walikuwa wameipata kutoka katika vyombo vya habari. Hawakuamini kama kweli mtoto wao alikuwa amefanya mauaji kwa mwanamke ambaye alikuwa na uhusiano nae wa kimapenzi.
Walionekana kufahamu sababu ambayo iliwapelekea Andy kumuua mwanamke yule lakini kamwe hawakutaka kumwambia mtu yeyote sababu ile. Walichokifanya kwa wakati huo ni kuwaandaa mawakili wao ambao walionekana kuwa na uwezo wa kuwasaidia wateja wao kushinda kesi kubwa kama ile.
Wakili akapangwa na kisha kuanza safari ya kuelekea nchini Tanzania. Alichokifanya wakili yule ni kukutana na Andy na kisha kuanza kuongea nae. Aalitamani sana kumsaidia kwa nguvu zote mpaka pale ambapo angeshinda kesi ile na kurudi nchini Marekani.
“Ni kweli uliua?” Wakili Kelly aliuliza.
“Ndio” Andy alijibu.
“Kwa nini uliua?”
“Unajua wanawake hawa wajinga sana. Nimeua kwa sababu tu alinisaliti” Andy alijibu.
“Niko hapa kwa ajili ya kukusaidia Andy. Nina uhakika utatoka tu. Nitasimamia kesi yako mpaka mwisho” Andrew alimwambia Andy.
“Itakuwa vizuri sana kama ukinisaidia kwani nitafanikiwa kuifanya kazi yangu” Andy aliwaambia.
“Kazi gani?” Kelly aliuliza.
“Kazi nzito ya kuwamaliza wanawake wote wa nchi hii” Andy alitoa jibu lililoonekana kumshtua Kelly.
“Kwa nini unataka kuwaua?”
“Unajua ni bora kuua mamilioni ili kuokoa mabilioni. Nyie acheni tu. Ni bora kumpenda shetani, ukae nae chini na kuzungumza kuliko kumpenda mwananamke wa Kitanzania” Andy alimwambia.
Wakili hakutaka kuendelea kuuliza maswali japokuwa alionekana kushtushwa na maneno mazito ambayo aliyaongea Andy. Hakuonekana kujali, alichokuwa akitakiwa kukijali kwa wakati huo ni kuifanya kazi yao hiyo ambayo ilikuwa imemleta nchini Tanzania.
Siku ziliendelea kukatika na hatimae siku ya kwanza ya kusikiliza kesi yake ikawadia. Wananchi walikuwa wamejazana mahakamani huku kila mmoja akitaka Andy ahukumiwe kifo wa kunyongwa au kuchomwa sindano ya sumu.
Bwana Wayne na mkewe walikuwa ndani ya mahakama hiyo pamoja na binti yao, Esther. Muda wote walionekana kuwa katika hali ya mawazo kupita kawaida huku macho yao yakiwa mekundu hali iliyoonyesha kwamba katika kipindi kichache kilichopita walikuwa wakilia.
Baada ya muda fulani Andy akaanza kuingizwa ndani ya mahakama hiyo. Kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia alionekana kumchukia, mioyo yao wala haikuwa na upendo wowote juu ya Andy kutokana na mauaji yale aliyokuwa ameyafanya ya kumuua mtu ambaye walikuwa wakimpenda kupita kiasi.
Wala hazikupita dakika nyingi, hakimu, Bi Beatrice akaanza kuingia mahakamani hapo huku watu wote wakiamriwa kusimama. Kila mtu alimwangalia hakimu Beatrice, uso wake ulionekana kuwa wa kipole sana jambo ambalo liliwafanya wananchi kuona kwamba ni lazima hakimu huyo angemuonea huruma Andy.
Siku hiyo ya kwanza Andy hakutakiwa kuongea kitu chochote kile, alitakiwa kusikiliza kesi yake tu. Kesi ikasomwa na kisha kuahirishwa mpaka baada ya wiki mbili. Hakimu akaondoka mahakamani hapo na Andy kurudishwa rumande kusikilizia siku hiyo ya kesi ambayo alitakiwa kurudishwa tena mahakamani.
Nje ya mahakama watu walikuwa wakipiga kelele za kumtaka Andy ahukumiwe kifo. Kila wakati Andy alipowasikia wanaume wakipiga kelele za kumtaka ahukumiwe kifo alibaki akihuzunika tu. Hakuamini kama wanaume ambao alikuwa na lengo la kuwatetea walikuwa wakimpinga namna hiyo kwa kutaka ahukumiwe kifo. Andy akashindwa kujizuia, machozi yakaanza kumtoka.
Andy akaingizwa ndani ya karandinga hilo na kisha kuanza kurudishwa rumande huku akisubiria siku nyingine ya kesi hiyo.
****
Kesi hiyo ya mauaji ambayo ilikuwa ikimkabili Andy ndio ambayo ilikuwa ikisikika sana katika vyombo vya habari duniani huku kila mtu akitaka kufahamu nia aina ya hukumu gani ambayo angepewa Andy, dokta mwenye jina kubwa kutoka nchini Marekani japokuwa alikuwa na uraia wa Tanzania.
Mitaani bado watu walikuwa wakiendelea kuandamana huku kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo idadi ya watu ilikuwa ikiendelea kujaa. Wanafunzi ambao walikuwa wakihitajika kwenda shuleni kusoma, hawakwenda, wanachuo ambao walikuwa wakihitajka kwenda vyuoni nao hawakwenda, waliungana na watu waliokuwa na hasira kali na Andy na kisha kuandamana nao katika zile siku ambazo zilikuwa zimepangwa maalumu kwa maandamano ya amani.
Ingawa wakili Kelly alikuwa na uhakika wa kumfanya mteja wake, Andy kushinda kesi lakini maandamano yale yakaonekana kumtia wasiwasi. Wananchi walikuwa wamehamasika kupita kawaida, kiu yao kubwa kwa wakati huo ilikuwa ni kutaka kumuona Andy akihukumiwa kifo au kufungwa kifungo cha maisha jela.
Siku ziliendelea kukatika na hatimae siku ya kesi kusikilizwa kwa mara ya pili kuwadia. Kama kawaida yao idadi kubwa ya wananchi ilikuwa imefurika mahakamani hapo huku kila mtu akitaka kumuona huyo Andy ambaye alikuwa amefanya mauaji yale ya kinyama.
Karandinga likaanza kuingia katika eneo la mahakama hiyo, waandishi wa habari wakajiweka tayari kwa ajili ya kupiga picha. Flashi zikaanza kuonekana mahali hapo, waandishi wakaonekana kuwa bize wakimpiga picha Andy kwa ajili ya kuziweka kwenye kurasa za mbele katika magazeti yao.
Andy alikuwa kimya huku uso wake akiwa ameuinamisha chini. Kichwani alionekana kuwa na mawazo mazito, kitendo cha kuingia mahakamani na kutaka kuhukumiwa kifo au kifungo cha maisha jela kilionekana kumuumiza. Siku hiyo napo, kesi ikaahirishwa kama kawaida hasa mara baada ya hakimu kumsomea mashitaka ambayo yalikuwa yakimkabiri. Kila kitu kilipomalizika, Andy akarudishwa katika karandika lile na kurudishwa mahabusu.
Magazeti mbalimbali bado yalikuwa yakiendelea kuuza sana kutokana na habari zilizojaa mvuto ambazo walikuwa wakiziandika huku zikiwa na vichwa vya habari ambavyo vilikuwa vikimfanya mtu kutotaka kuacha kununua magazeti hayo.
Katika kipindi hicho cha kesi hiyo ndicho kilikuwa kipindi cha biashara sana. Fulana mbalimbali ambazo zilikuwa na picha za Andy zikaanza kutengenezwa jambo ambalo kwa wale ambao walikuwa wakitaka kuzinunua wazinunue. Chuki kubwa ya watanzania juu ya Andy ilizidi kuota mizizi mioyoni mwao, walimchukia Andy kuliko mtu yeyote.
“Ni afadhari wafungwa wote jela waachiwe huru kuliko huyu mtu kushinda kesi hii” Mwananchi mmoja ambaye alionekana kuwa na hasira aliwaambia wenzake.
Bwana Wayne na mkewe, Bi Happy hawakuonekana kuwa na furaha kabisa. Kila siku walikuwa watu waliokosa amani mioyoni mwao, walizidi kumuomba Mungu aweze kumuepushia adhabu yoyote kijana wao.
Kila siku usiku walikuwa wakishikana mikono chumbani na kisha kuanza kumuombea kijana wao, Andy. Kila mmoja moyoni mwake alikuwa na uhakika kwamba Andy angeshinda kesi ile kutokana na kumuamini Mungu wao wa miujiza.
“Atashinda kesi. Naamini atashinda na maisha yake kumkabithi Yesu” Bwana Wayne alimwambia mkewe.
“Hata mimi naamini ila hii isiwe mara yetu ya mwisho kumuomba Mungu” Bi Happy alisema.
“Sawa sawa. Kila siku tutakuwa tukimuomba Mungu” Bwana Wayne alisema.
Maombi yao hayakukoma hata siku moja, kila siku alikuwa waliendelea kushikana mikono na kumuomba Mungu wao. Mbele yao waliona dhahiri Mungu kwenda kufanya miujiza na hatimae kijana wao kushinda kesi ile ngumu ambayo ilikuwa iimkabiri.
Siku zikaendelea kukatika, wiki zikaanza kusogea mpaka siku ya kesi ile kufikia. Watu kama kawaida yao walikuwa wamekusanyika mahakamani pale kwani waliona kwamba siku hiyo ndio ilikuwa siku ya kutangaza hukumu ile. Kutokana na wananchi kuweka shinikizo la kutaka kuiona kesi ile, kituo cha televisheni ya Taifa kikaruhusiwa kurusha moja kwa moja kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea mahakamani.
Andy akasimama kizimbani huku macho yake yakiwaangalia wazazi wake pamoja na mdogo wake, Esther. Moyoni alikuwa anaumia sana hasa kila alipokuwa akiwaangalia wanaume ambao walikuwa wamekusanyika mahali hapo.
Wakili Kelly akaanza kazi yake ya kumtetea Andy ambaye alikuwa amesimama kizimbani kimya. Wakili Kelly alionekana kuwa mjanja katika kila kitu abacho alikuwa akiongea mahali hapo huku kila mtu akiona dhahri kwamba Andy alikuwa akielekea kushinda kesi ile. Wakili Kelly aliendelea kuongea mambo mengi huku utetezi wake ukionekana kuwa na nguvu, zamu yake ilipokwisha, hakimu akaingilia.
“Tumesikiliza mambo mengi kutoka kwa wakili wa kujitegemea, Kelly. Hata kabla mahakama haijaamua kesi yako, kuna lolote ungependa kuiambia mahakama?” Hakimu wa kesi hiyo, Bi Beatrice alimuuliza Andy.
Andy akayatoa macho yake usoni mwa hakimu na kisha kuanza kuwaangalia watu ambao walikuwa wameingia ndani ya mahakama ile. Idadi kubwa ya watu ambao walikuwa ndani ya mahakama ile walikuwa wamekunja sura zao kuonyesha ni jinsi gani walikuwa na hasira juu yake.
“Mheshimiwa hakimu. Najua kwamba kila mtu ana hasira kali na mimi hasa kwa kile ambacho nimekifanya. Naomba watanzania waelewe kwamba nilifanya mauaji yale huku lengo langu likiwa ni kulipa kisasi” Andy alisema na kuendelea.
“Mara nyingi najifananisha na mkulima ambaye anatamani sana shamba lake liwe na mazao mazuri, kwangu mimi, Annastazia alionekana kama gugu, tena gugu kubwa ambalo lingeweza kuyaharibu mazao yote. Nilichokifanya kama mkulima, nikalikata gugu hilo” Andy alisema na kuendelea.
“Annastazia hakuwa mwanamke mzuri, alikuwa msaliti tena mkubwa hata zaidi ya Yuda. Nilimpenda sana mwanamke yule lakini kutokana na kuwasikiliza sana wazazi wake, akaamua kunisaliti. Niliumia sana, nilijiahidi kumuua kwa njia yoyote ile. Mara ya kwanza nilijaribu kulilipua gari lake, akanusurika na ndio maana nikaamua kumuua kwa mkono wangu mwenyewe” Andy aliiambia mahakama maneno ambayo yalionekana kumshtua kila mtu kwa kuona kuwa kumbe lile tukio la kulipuliwa kwa gari lilikuwa limefanywa na mtu huyo.
“Nimemuua Annastazia na wanawake wote kufuata baada yake kwani nimegundua kwamba wote hao wana roho kama yake. Ni bora niue mamilioni ili niokoe mabilioni mheshimiwa hakimu. Nitakapotoka hapa, nitaanza kazi yangu rasmi. Wanawake wote wa Tanzania watakuwa halali yangu” Andy aliiambia mahakama .
Kila mtu mahakamani akaonekana kushtuka. Maneno ambayo aliyaongea Andy yalionekana kumstaajabisha kila mtu aliyekuwa akiyasikia. Wakabaki wakimwangalia mara mbili mbili huku wakionekana kutokuamini kile ambacho alikuwa amekiongea.
Maswali mfululizo yakaanza kumiminika vichwani mwao, ilikuwaje Andy aongee maneno yale? Je alikuwa na uhakika wa kushinda kesi ile au la? Na kama alikuwa na uhakika, angeweza kutimiza kile ambacho alikuwa akikiongeakwa wakati ule? Kila maswali ambalo watu walijiuliza vichwani mwao wakakosa majibu.
“Nina kazi na wanawake wa Tanzania. Na ni lazima kazi hiyo niimalize. Nafikiri watoto ndio watakaobaki hai, ila hao wengine ni lazima niwamalize” Andy aliiambia mahakama.
“Kazi gani?” Hakimu alidakia.
“Kazi kubwa sana. Ni na uhakika kama kazi hiyo ningekuwa nimeifanya ni uhakika hata wewe usingekuwepo mahali hapa, inawezakana kwamba ungekuwa umekwishaoza kaburini” Andy alimwambia hakimu.
Hakimu akayatoa mawani yake kutoka machoni mwake na kisha kuanza kuyafuta. Maneno ambayo alikuwa ameyaongea Andy yalionekana kumchanganya, kitu ambacho alikiamua mahali hapo ni Andy kwenda kupimwa akili siku inayofuata kabla ya kesi kuendelea wiki ijayo na hukumu kusomwa.
Mahakama ikafungwa na hakimu kutoka. Minong’ono ilikuwa imetawala midomoni mwa watu ambao walikuja mahali hapo kushuhudia kesi ile. Andy akatolewa mahakamani huku akiwa katika ulinzi mzito na kisha kupandishwa kwenye karandinga kwa ajili ya kurudishwa remande ili kesho aende kupimwa akili kabla ya kesi kuendelea kwa siku ya mwisho ya hukumu.
****
“Watu wanaangamia. Dawa zinaelekea kuisha. Ninamtaka Andy mahali hapa haraka iwezekanavyo. Hata kama atakuwa akishikiliwa na mapolisi, sitojali kitu chochote. Ni ndani ya siku tatu tu, ninamtaka mahali hapa” Bwana Dawson aliwaambia vijana wake ambao aliwaajiri maalumu kwa ajili ya kumleta Andy mahali hapo.
“Sawa mkuu. Kuna kingine?”
“Ndio” Bwana Dawson alisema na kisha kuingia ndani, alipotoka alikuwa na sura ya bandia mkononi mwake na kuwapatia vijana wake pamoja na mfuko wa kaki ambao ulikuwa na dokumenti fulani ambazo aliziona kuhitajika mbele ya safari.
“Ninamtaka ndani ya siku tatu. Nitawapeni dola laki tano kuwasaidia. Kama mtaona kumpata itakuwa ngumu, tumieni risasi ili mladi tu apatikane niendelee na kazi nae” bwana Dowson alisema.
“Sawa mkuu”
Powell alikuwa mmoja wa vijana ambao walikuwa wametumwa na Bwana Dawson kwa ajili ya kumleta Andy nchini Marekani na kuendelea na mchakato wake wa kutengeneza fedha. Ilikuwa ni lazima Andy apelekwe nchini Marekani kwa ajili ya kufanya kile ambacho alitakiwa kukifanya kwa wakati huo.
Mikakati kabambe ikaandaliwa, vijana nane wakatafutwa, vijana ambao hawakuwa na hata na chembe yoyote ya woga, vijana ambao walikuwa na uzoefu mkubwa wa kutumia bunduki wakati wowote na sehemu yoyote bila kuogopa kitu chochote kile.
Vijana nane tayari walikuwa wamekamilika na kitu ambacho kilifanyika ni kuanza kusafiri kuelekea Tanzania. Kwa kuwa walitumia usafiri wa ndege ya kukodi ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Bwana Dawson wala hawakutumia muda mrefu angani wakawa wamekwishafika Tanzania.
Walichokifanya mahali hapo ni kuchukua vyumba katika hoteli ya The Cape na kisha kupumzika. Usiku hawakulala, kitu ambacho walikuwa wakikifanya ni kukusanyika katika chumba kimoja na kuanza kupanga mipango juu ya namna ya kumchukua Andy na kuanza kurudi nae nchini Marekani.
Nchi ya Tanzania wala haikuwaogopesha hata kidogo kwani kwao waliuona ulinzi wa nchi hiyo kuwa ndogo sana na hivyo kuwapa nafasi kubwa sana ya kumchukua Andy salama salimini. Kikao chao cha siri kilichukua dakika thelathini, kila mmoja akaelekea chumbani mwake huku wakimuacha Powell ndani ya chumba kile.
Hawakutaka kuchelewa, siku iliyofuata wakakodi gari moja kwa moja kuanza kuelekea katika sehemu ambayo waliiona kufaa kwa kufanya tukio moja muhimu ambalo walitakiwa kulifanya kwa wakati huo huku wakiwa na bunduki zao zilizokuwa zimejaa risasi.
“Na vipi kuhusu Michael?” Shawn aliuliza
“Amekwishafika jana usiku kwa kutumia boti ile ile ya bosi iendayo kasi. Kinachosubiriwa ni sisi tu” Powell alijibu.
“Na umekwishamwambia wapi pa kuonana?”
“Ndio. Kuna ufukwe unaitwa Coco ambapo hapo ndipo tutakapokutania na kuanza safari yetu. Natumaini hii itakuwa kazi nyepesi sana” Powell alisema huku wakiwa wanaingia eneo la Mnazi Mmoja ikiwa imetimia saa moja na nusu asubuhi.
****
Watanzani walikuwa wakizidi kumiminika ndani ya mahakama kuu ya Tanzania kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi hiyo ya mauaji ambayo inamkabili Andy ambayo ilikuwa imevuma kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili.
Kila mtu alikuwa akitamani hakimu amhukumu kifo Andy kwa kile ambacho alikuwa amekifanya kwa kumuua Spika wa Bunge la Tanzania, Bi Annastazia Kapama. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo watu walizidi kuongezeka mahakamani hapo kiasi ambacho watu wengine wakazuiliwa na kutakiwa kusimama nje ya mahakama hiyo.
Kama kawaida, waandishi wa habari walikuwa wakiendelea na kazi yao ya kupiga picha na kuandika mambo mbalimbali ambayo yalikuwa yakiendelea mahali hapo. Ingawa karandinga ilitakiwa kuingia hapo saa mbili kamili asubuhi hiyo lakini watu waliiona karandinga hiyo ikichelewa kufika mahali hapo.
“Ni lazima auhukumiwe kifo mjinga yule. Hawezi kutuwekea vidonda mioyoni mwetu” Mwanaume mmoja alisema huku akionekana dhahiri kuwa na hasira.
Muda ulizidi kwenda mbele, saa moja na nusu ikafika, hakimu akawa amekwishafika nje ya mahakama ile lakini bado karandinga halikuwa limeingia mahali hapo. Watu wakaendelea kusubiri zaidi na zaidi, saa mbili kamili ikaingia lakini hali bado ilikuwa vile vile, karandinga halikuwa limeingia mahali hapo jambo ambalo likaonekana kumtia wasiwasi kila mtu.
****
Pikipiki mbili zilikuwa mbele, nyuma ya pikipiki zile kulikuwa na gari aina ya defender ambalo lilikuwa limewapakiza maaskari saba ambao walikuwa na bunduki. Nyuma ya defender ile kulikuwa na karandinga ambalo lilikuwa limewabeba watu ambao walitakiwa kufika mahakamani siku hiyo huku Andy akiwa mmoja wapo.
Ving’ora vilikuwa vikiendelea kusikika hali ambayo iliwataka watu kuyapaki pembeni magari yao kwa ajili ya kuyapisha magari yale ambayo yalikuwa yakielekea Mahakama kuu. Nyuma ya karandinga lile kulikuwa na defender moja ambalo nalo lilikuwa limewabeba maaskari saba waliokuwa na bunduki mikononi mwao.
Walipofika maeneo ya Mnazi Mmoja, kila mmoja akapigwa na mshangao mara baada ya kuona magari mawili ambayo yalikuwa yamepata ajali. Kila polisi alikuwa akishangaa, mazingira ya magari yale kupata ajali yalikuwa yakishangaza na hata kuchekesha, mazingira ambayo kwa mtu ambaye alikuwa na leseni basi hakutahili kupata ajali kama ile.
Magari yote yalikuwa yamesimama huku foleni ikiwa katika eneo hilo. Ving’ora vilisikika zaidi na zaidi lakini hakukuwa na dereva yeyote ambaye alikuwa na uwezo wa kusogeza gari lake kutokana na msongaano wa magari ambao ulikuwa mahali pale.
“Tunazidi kuchelewa kufika mahakamani. Tufanye nini?” Polisi mmoja aliwauliza wenzake.
“Hakuna jinsi. Tushukeni na tujaribu kuyasogeza magari haya upande mwingine na kisha tuende upande mwingine, natumaini tutaweza kupita” Polisi mmoja alijibu.
Hata kabla hawajafanya kitu chochote kile, polisi mmoja akaanguka chini, damu zilikuwa zikimtoka kifuani huku akitupa miguu na mikono yake kila upande. Kila polisi ambaye alikuwa akimwangalia polisi yule alikuwa akipigwa na mshangao, hali ambayo ilikuwa imetokea haikuonekana kueleweka mbele ya macho yao.
Wala hazikupita hata sekunde kumi, mapolisi wawili wakaanguka chini, damu zilikuwa zikiwatoka vifuani. Hapo ndipo walipopata picha kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo. Walichokifanya mapolisi wale ni kupiga risasi hewani, watu wakaanza kukimbia ovyo.
Mapolisi ambao walikuwa katika defender ya nyuma wakaanza kuja kule mbele huku wakiwa wameziweka sawa bunduki zao. Tayari waliona kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kinaendelea, wakaanza kulipa ulinzi zaidi karandinga lile.
Kila walipokuwa wakiangalia wala hawakuweza kumuona mtu yeyote ambaye alikuwa na bunduki au hata kuisikia milio ya bunduki za maadui zao. Mapolisi bado walikuwa wakianguka chini mmoja baada ya mwingine, risasi zilikuwa zikiendelea kuingia miilini mwao.
Mapolisi wakaona kwamba wangeendelea kumalizika kama tu wasingefanya kitu cha ziada, walichoamua kukifanya mahali hapo ni kuanza kujipigia risasi ovyo pasipo kuwaona maadui zao. Kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa, vichwani mwao walijua wazi kwamba watu ambao walikuwa wakiwashambulia walikuwa wakitumia bunduki zilizokuwa na vyombo vya kuzuia milio ya risasi.
“Wako wapi?” Polisi mmoja alimuuliza mwenzake huku wakiwa wamebakia wanne tu.
“Sijui. Yaani mimi naona wenzetu wanaanguka tu” Polisi mwingine alijibu huku akiweweseka tu.
“Kwa hiyo tufanye nini?”
“Nafik......” Polisi yule alijibu lakini hata kabla hajamalizia jibu lake, akaanguka chini, damu zilikuwa zikitoka kichwani mwake.
Ni ndani ya dakika tano tu, mapolisi wote walikuwa chini wamekufa. Vijana watatu wa kizungu ambao walikuwa na risasi mikononi wakatoka kule walipokuwa wamejificha na kuanza kuelekea kule ambako kulikuwa na karandinga. Kila askari magereza ambaye alikuwa ndani ya karandinga lile alikuwa akipigwa risasi tu.
Washitakiwa zaidi ya kumi walikuwa ndani ya karandinga lile huku kila mmoja akionekana kuogopa. Wazungu wale wakaanza kumtafuta Andy ndani ya gari lile huku wakionekana kuwa na haraka sana.
“Andy.....” Mmoja wao aliita hali iliyomfanya Andy kuuinua uso wake.
“Tuondoke” Mzungu mwingine alisema, akachukua bunduki yake na kuipiga kufuri ambayo ilikuwa imeshikilia wavu na kuachia, wakamchukua Andy na kuondoka nae.
Wazungu wengine watano nao wakajitokeza kutoka kule walipokuwa wamejificha na kisha wote kwa pamoja kuanza kuondoka mahali hapo. Mpaka tukio lile linakamilika, zilichukua dakika sita tu, walikuwa wamekamilisha kila kitu.
Wala gari haikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi, walikuwa wakienda taratibu sana kwa kuhofia kugundulika. Kutoka Mnazi mmoja mpaka katika ufukwe wa Coco walichukua dakika ishirini tu, wakawa wamekwishafika na kuanza kuchukua mtumbwi mmoja uliokuwa pembeni na kisha kuanza kuifuata boti yao ambayo ilikuwa imepaki karibu mita elfu moja kutoka nchi kavu.
“Kazi imekamilika. Kila kitu kimekamilika kwa amani” Powell alisema huku akionekana kuwa na furaha.
“Nyie ni wakina nani?” Andy aliwauliza huku akionekana kushangaa.
“Hauwezi kutufahamu ila tumetumwa na bosi kuja kukuchukua” Powell alijibu.
“Bosi gani?”
“Dawson” Powell alijibu.
Hapo Andy akapata picha ya kila kitu ambacho kilikuwa kimeendelea, tayari alikwishajua kwamba bado Dawson alikuwa akitaka kukamilisha kazi zake ili aendelee kuingiza fedha. Moyo wa Andy ulikuwa ukitamani kufika haraka nchini Marekani na kukutana na Dawson na kisha kumshukuru kwa kile ambacho alikuwa amemfanyia.
“Safi sana, nadhani sasa lengo langu litakamilika” Andy aliwaambia huku akionekana kuanza kutabasamu.
“Lengo gani?”
“Kuwaua wanawake wote wa nchi hii” Andy alijibu.
“Unataka kuwaua? Kwa nini? Na utaweza vipi kuwaua wanawake wote hao?” Powell aliuliza.
“Ni kazi rahisi sana. Nataka ndani ya mwaka mmoja asilimia tisini na tano ya wanawake wawe wamekufa” Andy alijibu.
“Bado unanichanganya. Utawaua vipi?”
“Nyie mtasikia tu”
“Kwa risasi? Au kwa mabomu? Mbona sipati picha kabisa. Utawaua vipi?” Powell aliendelea kuuliza.
Usijali. Usiwe na haraka ya kutaka kufahamu. Unachotakiwa kujua ni kwamba nitawaua wanawake wote ndani ya nchi hii” Andy alijibu.
“Mmmh! Sawa bwana. Ila itakupasa kuwa makini wakati huu” Powell alimwambia.
Hapo hapo Andy akagaiwa sura ya bandia na kuivaa huku akipewa dokumenti zote kama pasipoti ambayo ilikuwa na sura ile ya bandia. Ilikuwa ni vigumu sana kumfahamu Andy, alionekana kubadilika sana huku sura ile ya bandia ikionekana kuwa ndio sura yake halisi.
“Kwa sasa utaitwa Donavan Sinclaire” Powell alimwambia Andy huku akimwangalia vizuri.
Mara baada ya kuifikia boti ile ambayo ilikuwa ikiwasubiri, wakateremka na kuanza kuingia ndani ya boti ile. Kazi ile kwao ilionekana kuwa nyepesi kuliko kazi zote ambazo walikuwa wamepitia kabla, kila mmoja alikuwa akionyesha sura iliyojaa tabasamu yaliyokuwa na mafanikio.
“Sasa kisasi kimebaki kwangu. Ni lazima niwaue wanawake wote wa Tanzania” Andy alijisemea huku akionekana kumaanisha kile ambacho alikuwa akikizungumza.
****
Watu walikuwa bado wapo mahakamani huku wakisubiri karandinga ambalo lilikuwa limembeba Andy pamoja na watuhumiwa wengine kufika mahakamani hapo. Muda ulikuwa ukizidi kwenda lakini karandinga lile halikufika mahali hapo.
Kila mmoja akaonekana kukata tamaa, na hapo ndipo taarifa za kile kilichokuwa kimetokea Mnazi Mmoja kuanza kusambaa. Watu walikuwa wakipigiwa simu na kuelezwa kila kitu hasa juu ya mapigano kati ya polisi na wazungu ambao walikuwa na bunduki zilizokuwa na vyombo vya kuzuia milio ya risasi.
Hizo zilikuwa taarifa mpya, kila mtu akaonekana kushangaa na kushtuka, taarifa za kushambuliwa kwa mapolisi ziilionekana kuwashtua. Zaidi ya hiyo, taarifa kwamba Andy alikuwa ametorshwa ndio ambazo ziliwashtua zaidi.
Taarifa zile zikaanza kusambaa. Mipaka ya nchi ikatakiwa kufngwa haraka iwezekanavyo huku navyo viwanja vya ndege vikiagizwa kufngwa. Kila mtu alikuwa na uhakika kwamba Andy bado alikuwa nchini Tanzania ambako angetarajiwa kuondoka siku yoyote pamoja na hao wazungu ambao walikuonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia bunduki.
Msako wa ghafla ukaanza. Wapelelezi wakasambazwa kila kona. Siku ya kwanza ikapita, siku ya pili, ya tatu na hatimae wiki lakini Andy wala hakuweza kupatikana na wala tetesi kwamba alikuwa ameonekana sehemu fulani
Wazazi wake, Bwana Wayne na Bi Happy hawakuonekana kuwa na furaha, kitendo cha mtoto wao kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kilionekana kuwakosesha amani mioyoni mwao. Bado walikuwa wakiendelea kumuomba Mungu amuepushie kifo pale popote alipokuwa kwa kuwa tu bado walikuwa na imani kwamba siku moja angekuja kumtumikia Mungu.
Maombi kwao ndio kilikuwa kitu chochote kile, kila siku walikuwa wakishikana mikono na kuanza kuomba Mungu, imani juu ya mtoto wao kuja kumtumikia Mungu katika siku za usoni ilikuwa imejengeka kwa kiansi kikubwa mioyoni mwao.
Baada ya kukaa kwa wiki mbili huku wakitembelea Machame, wakaamua kuondoka kurudi nchini Marekani kuendelea na kazi yao ya kumtumikia Mungu huku maombi yakiendelea kufanyika.
Safari ya kutumia boti bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Muda mwingi Andy alikuwa akionekana kuwa kimya huku akionekana dhahiri kuwa na hasira. Safari hiyo walitaka kufika nchini Kenya kwa kutumia boti ile ambapo hapo wangeweza kupanda ndege na kurudi nchini Marekani salama.
Kwa kuwa walikuwa na fedha za kutosha, kuhonga kwao ikawa moja ya mambo ambayo walikuwa wakiyafanya njiani. Mioyoni mwao walikuwa na furaha kwa kuona kwamba walikuwa wamefanikisha kila kitu ambacho waliambiwa kuja kukifanya nchini Tanzania.
Walitumia masaa kumi wakawa wamekwishafika nchini Kenya katika mji wa Mombasa. Hapo, wakateremka na kuanza kuelekea mitaani ambapo huko wakachukua basi na kuanza kuelekea katika jiji la Nairobi ambapo wangetaka tiketi ya ndege na kurudi nchini Marekani.
Vyombo vingi vya habari vya Kenya vilikuwa vikitangaza kuhusiana na ile ambacho kilikuwa kimetokea nchini Tanzania, mauaji ya mapolisi ambao waikuwa katika karandinga wakiwapeleka watu ambao walikuwa wakienda kusomewa kesi akiwepo dokta mkubwa aliyekuwa akifanya kazi nchini Marekani, Andy Wayne.
Powell na wenzake walikuwa wakicheka tu huku wakijiona kuwa wajanja ambao siku zote walitakiwa kupewa heshima kwa kile ambacho walikuwa wamekifanya, kumuokoa Andy pasipo usumbufu mkubwa kutokea.
Baada ya masaa mawili, basi likafika jijini Nairobi ambapo wakaelekea kukata tiketi katika shirika la ndege la Amecan Airlines na usiku wa saa sita kuanza safari ya kuelekea nchini Marekani. Kwa kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia Andy hakuwa akimgundua kutokana na sura ya bandia ambayo alikuwa ameivaa na kubadilishwa jina kwa kuitwa Donavan Sinclaire.
“Hakika tumefanikiwa kwa kila kitu” Powell alimwambia Andy ambaye alikuwa karibu nae.
“Namshukuru Mungu sana ila ni lazima nifanye kile ambacho nilikiahidi moyoni mwangu” Andy alimwambia Powell.
“Kile cha kuwaua wanawake wa Kitanzania?”
“Ndio hicho hicho” Andy alijibu.
Walichukua masaa ishirini na mbili hewani na ndipo ndege ilipoanza kutua katika uwanja wa ndege wa John F. Kennedy ndani ya jiji la New York. Wote wakateremka na kuanza kuelekea nje ya uwanja huo ambapo magari manne ya kifahari yalikuwa yakiwasubiria.
Baada ya kuingia ndani ya magari hao, moja kwa moja wakaanza safari ya kuelekea Binsbury, mtaa ambao alikuwa akiishi Bwana Dawson. Moyo wa Andy bado ulikuwa na shauku kubwa ya kutaka kufika haraka iwezekanavyo ili aanze kazi yake mara moja. Kadri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hasira juu ya wanawake wa kitanzania ilivyozidi kumpanda.
Bwana Dawson akaonekana kuwa na furaha, ujio wa Andy nchini Marekani ukaonekana kumfuraisha kupita kiasi. Kwa mwendo wa furaha akaanza kumfuata na kisha kumkumbatia. Bwana Dawson akaona kwamba huo ulikuwa ni wakati mwingine wa kutengeneza fedha kama zamani na ndio maana wala hakuona hatari kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kumrudisha Andy nchini Marekani.
“Inatakiwa urudi tena kazini” Bwana Dawson alimwambia Andy.
“Nitarudi hata ukisema sasa hivi. Ila kuna kitu nataka unisaidie” Andy alimwambia Bwana Dawson.
“Kitu gani?”
“Nataka kuua wanawake wote nchini Tanzania”
“Mungu wangu! Kwa nini?” Bwana Dawson aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Hawajui mapenzi wale. Kila siku wanaume wanaumizwa na kusalitiwa huku wengine wakijiua kwa ajili yao. Hawana thamani kabisa kuishi ndani ya dunia hii. Yaani wao ni kama mwanamke yule malaya, Annastazia” Andy alimwambia.
“Kwa hiyo unataka kuwaua kwa kutumia nini? Bomu au? Kama ni bomu sema tuagize kutoka nchini Urusi” Bwana Dawson aliuliza.
“Bomu nitaweza kuwaua hata wanaume ambao wala hawahusiki hata kidogo. Ninachotaka ni kuwaua wanawake tu”
“Sasa utawaua vipi?”
“Ni kazi rahisi sana. Nitatumia bakteria wapya nitakaowatengeneza, hawa wataitwa LETOFOAN yaani nikimaanisha Lets Tost For Annastazia (Acha tusherehekee kwa ajili ya Annastazia)” Andy alimwambia Bwana Dawson ambaye alionekana kushangaa.
“Mmmh! Sasa hao bakteria watawekwa wapi?” Bwana Dawson aliuliza.
“Ni kazi rahisi sana isiyokuwa na ugumu wowote ule. Nitawaweka kwenye pedi zao. Kwa kila mwanamke ambaye atakuwa akiingia mwezini itampasa kununua pedi ambazo zitakuwa na bakteria hawa. Atakapoziweka sehemu zake za siri ndani ya siku yake, bakteria hawa wataanza kushambulia sehemu zake za siri taratibu. Itaanza michubuko ambayo itakaa kwa muda hata wa mwezi mmoja na kisha baada ya hapo sehemu za siri zitaanza kutoka damu na kuharibu mishipa yote ya damu. Hali hiyo itakaa kwa mwezi mmoja pia, sehemu hizo zitaanza kuoza na hivyo kufa kifo kilichojaa maumivu” Andy alimwambia Bwana Dawson.
“Mmh! Kweli unafikiria mbali. Sasa itakuwa vipi na hizo pedi?”
“Nitatumia kiasi kikubwa cha fedha kuzisafirisha mpaka nchini Tanzania. Zile zitakazokuwa za kwanza na za pili zitakuwa ni za kisasa zinazokidhi mahitaji yote. Zitatangazwa sana na kumpelekea kila mwanamke kutamani kuzitumia, na kweli zitakuwa zina ubora mkubwa sana. Baada ya kuanza kupata wateja wengi, hapo ndipo nitakapozipeleka toleo la tatu, hizi ndizo zitakazokuwa na bakteria wa LETOFOAN. Katika hili jua kwamba kuna wanawake wengi sana watakufa. Hapo ndipo nitakapokuwa na furaha” Andy alimwambia Bwana Dawson.
“Ila nafikiri kuna kitu inatakiwa tufanye” Bwana Dawson alimwambia Andy.
“Kitu gani?”
“Kule si kuna pedi nyingine zinauzwa kwa sasa?”
“Ndio. Nilipitia haraka haraka nikaona kwamba ni ALWAYS.”
“Sasa itatubidi tuanze kufanya fitina, pedi hizo zifungiwe na sisi kuzileta zetu. Unaonaje hapo?”
“Hapo umesema. Itatupasa tufanye kitu hicho hicho”
“Sawa sawa. Sasa pedi zetu zitaitwaje?”
“Zitaitwa KIMEAN”
“Mungu wangu! Jina gani sasa hilo?”
“Hili ni kifupi cha Kill Me Andy ila sisi tutawadanganya kwamba jina hilo limetokana na mti mmoja unaopatikana katika msitu wa Amazon ambao una uwezo mkubwa wa kukausha damu hasa zile zinazotoka katika uke wa mwanamke siku anapokuwa mwezini” Andy alisema.
“Hapo nimekupata. Nadhani tengeneza kama tani moja za dawa za huu ugonjwa wetu na baada ya hapo uanze kutengeneza hao bakteria huku mimi nikianza kazi ya kupeleka pedi za Kimean zianze kuuzwa nchini Tanzania” Bwana Dawson alisema.
“Nitashukuru kwa msaada wako. Kazi naianza kesho asubuhi, na nina uhakika kwamba wiki ijayo, bakteria wa Letofoan watakuwa tayari kwa ajili ya kazi miezi sita baadae” Andy alisema.
“Sawa” Bwana Dawson aliitikia.
****
Nchi ya Tanzania ikaanza kuishutumu nchi ya Marekani kwa kile ambacho walikuwa wamekifanya cha kuwatuma watu wake waje nchini na kumuokoa Andy huku wakiua mapolisi ambao walikuwa pamoja na Andy safarini kuelekea mahakamani.
Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akifikiria kwamba watu wale ambao walifika nchini walikuwa wametumwa kufanya kazi na Bwana Dawson, mtu pekee ambaye alikuwa akisambaza dawa za ugonjwa wa PENINA.
Maneno ya chini chini ambayo yalikuwa yakiendelea nchini Tanzania hasa kwa viongozi mbalimbali ndio ambayo yalifanya uhusiano baina ya nchi hizo mbili kuanza kuyumba. Tayari kutokuelewana kukaonekana kuanza kuingia miongoni mwao huku Serikali ya Marekani ikijitetea kwa kusema kwamba hawakuwa wakihusika kwa kile ambacho kilikuwa kimetokea.
Andy bado alikuwa amejificha ndani ya nyumba ya Bwana Dawson huku akihofia kutoka nje ya nyumba hiyo kutoana na kuhofia kukamatwa na kurudishwa nchini Tanzania. Kila kifaa ambacho alikuwa akikihitaji kikanunuliwa kutokana na kutotaka kuvichukua vile vifaa ambavyo vilikuwa nyumbani kwake.
Andy akaamua kufngua akaunti nyingine ya benki ambayo hiyo ingetumika katika kuhifadhia fedha ambazo angekuwa akiwekewa na Bwana Dawson. Kazi ya kutengeneza dawa ya kuulia virusi vya Katapillar ambavyo vilikuwa vikisambaza ugonjwa wa PENINA bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida.
Ilimchukua kipindi cha mwezi mzima, dawa zikawa zimekamilika na kuingizwa tena sokoni na watu kuanza kuzitumia. Kila siku fedha nyingi zilikuwa zikiingia katika akaunti ya Bwana Dawson huku nae akiendelea kumlipa Andy kwa kile ambacho alikuwa akiendelea kukifanya.
Bwana Dawson alikuwa akisifiwa katika kila kona duniani, jina lake likawa kubwa kutokana na kile ambacho alikuwa akikifanya katika dunia hii. Kupitia yeye, dawa zilikuwa zikiuzwa sana, madaktari ambao walikuwa wamesomea kazi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano walikuwa wameangaika sana kutafuta dawa lakini mpaka katika kipindi hicho hawakuwa wamefanikiwa kabisa.
Serikali ya Marekani ikaamuru Bwana Dawson aanze kulindwa, tayari wakaona dhahiri kwamba maisha yange yangekuwa hatarini endapo wangemuacha awe peke yake. Watu wengi walikuwa wakihitaji dawa na kuingiza kiasi kikubwa cha fedha, kitendo cha kumuachana Bwana Dawson kingewafanya watu wengine kumteka na hatakumuua kutoka na watu wengine kuingiza sana fedha kupitia ugonjwa wa PENINA kwakutoa dawa feki.
Maisha ya ndani yalikuwa yakimuumiza sana Andy jambo ambalo akamtaka Bwana Dawson amletee mke wake, Sofia na kuanza kuishi pamoja nae. Kazi hiyo ikafanyika kwa haraka sana, ni ndani ya saa moja, Sofia alikuwa ndani ya nyumba hiyo na kisha kuingizwa katika chumba ambacho Andy alikuwa akikitumia kwa kulalia.
“Karibu Sofia” Andy alimkaribisha mke wake, Sofia huku akiivua sura ya bandia amayo alikuwa ameivaa. Huku akionekana kuwa na furaha na kuchanganyikiwa, Sofia akamfuata Andy na kisha kumkumbatia kwa furaha.
Moyo wa Sofia haukuamini kama ingetokea siku ambayo angekuja kuonana tena na mume wake ambaye alikuwa akitafutwa sana katika kipindi hicho. Hapo ndipo Andy alipopata muda wa kuongea na Sofia, Andy hakutaka kumficha Sofia kitu chochote kile, akamuelezea kila kitu ambacho kilihusu ugonjwa wa PENINA.
“Unasemaje?” Sofia aliuliza huku akionekana kutokuamini.
“Nilichokwambia ndicho ukweli wenyewe. Mimi ndiye niliyetengeneza ugonjwa huu” Andy alimwambia Sofia.
Sofia hakuweza kuvumilia, maneno ambayo aliongea Andy katika kipindi hicho ndio ambayo yakavuta kumbukumbu ya watu mbalimbali ambao walikuwa wakiteseka kwa ugonjwa ule vitandani duniani kote. Machozi yakaanza kutoka machoni mwa Sofia, moyo wake ulimuuma kupita kawaida.
“Kwa nini uliamua kufanya hivi?” Sofia aliuliza huku akilia.
“Kwa sababu ya fedha zaidi” Andy alijibu.
“Unaiteketeza dunia mume wangu. Umeifanya dunia nzima kulia kwa ajili yako” Sofia alimwambia mume wake, Andy huku akizidi kulia.
Alichokifanya Andy kwa wakati ni kumkumbatia na kuanza kumfariji. Japokuwa Andy alikuwa na mkakati wa kumwambia Sofia juu ya kile ambacho alikuwa akijiandaa kukifanya kwa wanawake wote waishio nchini Tanzania, akaamua kunyamaza kwani alijua kwa namna moja au nyingine mke wake, Sofia ni lazima angemzuia.
Siku ziliendelea kukatika huku Andy akiendelea kuishi na mke wake ndani ya nyumba ile ya Bwana Dawson. Maisha yao waliyokuwa wakiendelea kuishi ndani ya nyumba ile yalikuwa siri kubwa. Watu wengi walikuwa wakijiuliza maswali mengi juu ya mahali alipokuwa Sofia katika kipindi hicho huku ikiwa ni siku chache kupotea mara baada ya mume wake, Andy kuanza kutafutwa.
Hakukuwa na mtu ambaye alijua mahali ambapo Sofia alikuwepo katika kipindi hicho japokuwa kila mtu alikuwa na uhakika kwamba katika kipindi hicho Sofia alikuwa akiendelea maisha pamoja na mume wake, Andy.
Baada ya miezi sita kupita, pedi mpya za wanawake zilizojulikana kama KIMEAN zikaanza kuingizwa nchini Tanzania huku zikiwa ni toleo la kwanza ambalo lilionekana kuwa na ubora. Japokuwa nchini Tanzania kulikuwa na pedi za Always, fitina zikaanza kufanyika huku Bwana Dawson akitumia kiasi kikubwa cha fedha mpaka pale ambapo alifanikiwa kuua soko la pedi za Always nchini Tanzania.
Wanawake wa kitanzania wakavutiwa na ubora wa pedi za KIMEAN ambazo zilikuwa zimeanza kuuzwa nchini Tanzania. Ubora wake katika ukaushaji damu ndio ambao uliwafanya wanawake wengi kuzipenda pedi hizo. Kwa kila mwanamke ambaye alikuwa akizitumia pedi zile, alikuwa akieneza sifa kwa wanawake wengine ambao walizinunua na kujione ubora ambao ulikuwa ukipatikana.
Zaidi ya wanawake milioni ishirini kati ya milioni ishirini na tano walikuwa wakitumia pedi za KIMEAN ambazo ubora wake ulizidi kuwa juu kila siku. Kutokana na gharama zake kuwa ndogo sana, si wanawake wa vijijini wala wa mijini, wote walikuwa wakinunua pedi hizo ambazo zilikuwa ni za gharama za chini sana madukani.
Matangazo ambayo yalikuwa yakiendelea kuonyeshwa kwenye televisheni pamoja na kutangazwa kwenye maredio na kuandikwa kwenye magazeti ndio ambayo yalikuwa yakizidi kuwahamasha wanawake wanunue zaidi na zaidi pedi zile ambazo zilikuwa zikizidi kuvuma zaidi na zaidi nchini Tanzania.
“Yaani zinakausha damu mapema hadi raha” Mwanamke mmoja alimwambia mwenzake.
“Kweli?”
“Ndio”
“Ngoja na mimi nianze kuzitumia” mwanamke yule alimwambia mwenzake.
Wanawake walizidi kupeana taarifa zaidi na zaidi, kwa wanawake ambao hawakuwa na aibu, wengine wakaanza kuweka mpaka post katika mitandao ya kijamii na kuanza kuzisifia pedi hizo ambazo zilikuwa zikizidi kuonekana kuwa bota zaidi na zaidi.
Baada ya miezi kumi kupita, toleo la kwanza likamalizika na hivyo kuletwa toleo la pili nchini Tanzania. Bado wanawake wakazidi kuzipapatikia zaidi na zaidi, mauzo ya pedi zile zilikuwa zikizidi kushika kasi nchini Tanzania bila kujua ni hatari gani ambayo ilikuwa inawafuata mbele yao.
Toleo lile la pili liliuzwa zaidi ya mwaka mzima na hapo ndipo maandalizi ya tolea la tatu yalipoanza kufanyika. Pedi zikasafirishwa huku zote zikiwa zimewekewa bakteria aina ya LETOFOAN ambao walikuwa na uwezo wa kuishi sehemu ang’avu kwa muda wa mwaka mzima. Bakteria hao ambao walikuwa wamewekwa kwenye pedi zote walikuwa na kazi moja tu katika mwili wa mwanadamu, kuharibu mishipa yote ya damu sehemu za ukeni na kisha kuiozesha sehemu hiyo.
Wanawake wa Kitanzania wakazipokea pedi hizo kwa furaha bila kufahamu kwamba kitu kile walichokuwa wakikipokea kwa furaha ndicho ambacho kingekuja kuwamaliza sana nchini Tanzania, yaani ni watoto tu ambao hawajavunja ungo ndio ambao wangebaki hai.
Toleo la tatu la pedi za KIMEAN likawa limeingia nchini Tanzania. Wanawake walikuwa wakizidi kuzipapatikia kupita kawaida. Pedi zile zilinunuliwa kwa wingi sana nchini Tanzania bila kufahamu kwamba pedi zile katika toleo hili zilikuwa na bakteria wakali wa Letofoan. Wanawake ambao walikuwa wakiingia katika siku zao katika kipindi hicho wakaanza kuzitumia.
Kwa jinsi ambavyo pedi zile zilivyokuwa zikiendelea kutangazwa na ndivyo wanawake wengi walizidi kuzinunua zaidi na zaidi mpaka kuzifanya kuvunja rekodi ya mauzo katika soko kuu la Tanzania na hivyo kuiingizia serikali kiasi kikubwa cha fedha.
Miezi iliendelea kukatika, baada ya miezi mitano, huku wanawake wengi wakiwa wamekwishazitumia pedi zile, madhara yakaanza kuonekana katika sehemu zao za siri. Kitu cha kwanza ambacho kilikuwa kama dalili za ugonjwa ambao ulisababishwa na pedi zile, sehemu za siri zikaanza kuwasha kupita kawaida.
Wanawake wengi walikuwa wakiwashwa jambo lililowafanya wengine kufanya ngono hovyo kwa sababu ya kutuliza muwasho ambao ulikuwa ukipatikana ndani kabisa ya sehemu zile za siri. Japokuwa waliokuwa wakifanya ngono na wanaume mbalimbali walikuwa wakijisaidia kwa kiasi fulani kupunguza miwasho lakini haikusaidia kwa asilimia mia moja.
Miwasho ile iliendelea zaidi na zaidi. Hilo likaonekana kuwa kama janga la taifa. Wanawake wakashindwa kuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea katika miili yao. Miwasho ile ndio ambayo ilisababisha ndani ya sehemu zao za siri kuanza kuchubuka. Hali hiyo ndio ambayo iliwapelekea wanawake wengi kuanza kuelekea hospitalini ili kuona tatizo lilikuwa nini ambalo lilisababisha hali ile.
Mahospitalini, wanawake walikuwa wakijazana sana kupita kawaida. Zaidi ya wanawake ellfu kumi na tano walikuwa wakimimini katika hospitali mbalimbali za Halmashauri katika kipindi hicho. Serikali ikaonekana kushtuka, halikuwa jambo la kawaida kwa wanawake kumiminika hospitalini kiasi hicho.
Mahojiano yalipofanyika na ndipo habari ikawa imetolewa kwamba kulikuwa na ugonjwa mpya ambao ulikuwa umeingia. Serikali haikutaka kukaa kimya, tayari hali ilionekana kuwa mbaya sana jambo ambalo liliwafanya kuanza kufanya upelelezi ili wajue chanzo cha tatizo hilo lilikuwa nini.
“Nafikiri hizi pedi zitakuwa na matatizo” Waziri mkuu aliwaambia waandishi wa habari.
Mahojiano yakaanza kufanyika, kwa kila mwanamke ambaye alikuwa na tatizo hilo alipohojiwa, alisema kwamba alikuwa akitumia pedi za Kimean jambo ambalo serikali ikatangaza pedi hizo kutokuuzwa tena.
Tayari walikuwa wamekwishachelewa, zaidi ya wanawake milioni ishirini walikuwa wamekwishatumia pedi hizo ndani ya miezi sita. Matatizo zaidi na zaidi yakaendelea kutokea. Wanawake wale ambao walikuwa wakizitumia pedi zile, sehemu zao za siri zikaanza kutokwa na damu.
Janga hilo likaonekana kuwa janga kubwa la taifa, wanawake ambao walikuwa waandishi wa habari, wake wa mawaziri, mke wa rais, wanawake ambao walikuwa madaktari, mapolisi, walimu na wafanyabiashara wote wakaanza kutokwa na damu katika sehemu zao za siri jambo ambalo likaonekana kuwa hatari sana katika maisha yao.
Kwa wale ambao walikuwa na fedha za kutosha wakaanza kwenda nje ya nchi kutibiwa lakini hali haikuonekana kubadilika, bakteria ambao walikuwa wameanza kuziharibu sehemu zao za siri walionekana kutokuwa na dawa. Baada ya wiki moja kupita, sehemu zile za siri zilishambuliwa sana na hatimae mishipa ile ya damu kuanza kuoza.
Balaa likawa limeongezeka zaidi, wanawake wakaanza kufa mfululizo. Hilo likaonekana kuwa pigo kubwa zaidi, mke wa raisi wa Tanzania akafa huku damu zikiwa zimetapakaa sehemu zake za siri, wake mbalimbali wa viongozi nao wakafa kifo kile kile. Ndani ya wiki moja tu, zaidi ya wanawake milioni kumi na tano walikuwa wamekufa kwa ugonjwa ule ambao haukuonekana kuwa na tiba.
Shirika la afya lililo chini ya Umoja wa Mataifa la WHO (World Health Organization) likaingilia kati. Waandishi wengi wa habari duniani kote wakaanza kumiminika nchini Tanzania kwa ajili ya kutangaza kile ambacho kilikuwa kikitokea nchini Tanzania. Pedi zote za Kimean zikapigwa marufuku na kuchomwa moto huku Serikali ikianza kumtafuta mtu ambaye alikuwa akiziingiza pedi zile nchini Tazania.
Shirika la afya la WHO likaanza kutoa tiba mbalimbali nchini Tanzania lakini tiba hizo hazikuonekana kusaidi kabisa, japokuwa wanawake wengi walikuwa wakitumia lakini bado walikuwa wakifa kama kuku. Makanisani, watu wakaanza kuomba, misikitini nao wakazidi kuswali kwa kumtaka Mungu awaepushie na adhabu ambayo alikuwa ameamua kuwapa.
Hali haikuonekana kubadilika, bado wanawake waliendelea kufa mfululizo nchini tanzania. Mahema ya misiba ilikuwa imetawala katika sehemu nyingi nchini Tanzania, vilio vilizidi kutawala. Mwanamke ambaye leo alikuwa akilia kwa sababu ya rafiki yake kufa, kesho alikufa yeye. Hayo ndio yakawa maisha ya wanawake wa kitanzania, waliendelea kufa zaidi na zaidi.
Ugonjwa huo hatari haukuwa na tiba yoyote ile, tiba pekee ambayo ilikuwa ikipatikana ilikuwa ni kuacha kutumia pedi zile za Kimean hasa toleo la tatu. Mwezi ukakatika na wanawake zaidi ya milioni ishirini na tano wakawa wamekwikufa nchini Tanzania.
“Huyu atakuwa Andy” Kamanda mkuu wa jeshi la polisi Bwan Idrisa alisema.
Hapo ndipo kazi ya kupata mikanda ya vidoe ya tukio lile la kupelekwa mahakamani kuanza. Kamera za siri ambazo zilikuwa zikichomekwa katika kila mahakama ndizo ambazo zilikuwa zikihitajika kwa wakati huo. Mkanda wa siku ambayo Andy alikuwa akiongea mahakamani ukapatikana na hatimae kuanza kuuangalia.
“Unamsikia anavyosema kwamba angeua wanawake wote nchini Tanzania kama angefanikiwa kutoka” Mpelelezi wa kimataifa ambaye alikuwa amekamilisha upelelezi wake alisema.
“Kumbe hili lote liko chini yake!” Kamanda Idrisa alisema.
“Ndio. Ila cha msingi inabidi tumtafute huyu hakimu, Beatrice” Mpelelezi wa kimataifa, Bravo alimwambia.
“Nae amekufa kwa ugonjwa huu” Kamanda Idrisa alisema.
Taarifa zikatolewa katika vyombo vya habari kwamba Andy ndiye ambaye alikuwa amehusika katika kila kilichokuwa kikiendelea kwa wakati huo. Kwa sababu taifa la Marekani ndilo ambalo lilikuwa likituhumiwa sana katika kumtorosha Andy, wao ndio ambao waliahidi kumtafuta Andy na kumkamata na kisha kumpeleka katika vyombo vya sheria kwa kosa la kufanya mauaji ya kimbari nchini Tanzania.
Wapelelezi watatu ambao walikuwa chini ya shirika la kipelelezi la F.B.I (Federal Bureau of Investigation), Paul Steven, Kenneth Peter na Swan Huth wakaingia kazini, kazi ambayo walikuwa wamepewa ilikuwa ni kutaka kufahamu Andy alikuwa sehemu gani kwa wakati huo. Wapelelezi hawa hawakuingia mitaani kumtafuta Andy, kitu walichokifanya ni kukaa katika chumba kimoja kikubwa ambacho kilikuwa na kompyuta nyingi na kisha kuanza kazi ya kumtafuta Andy na kujua mahali alipokuwa.
****
Maisha kwake yakaonekana kuwa na furaha kwa mara nyingine tena. Kitendo cha wanawake kuuawa nchini Tanzania kilionekana kumfurahisha kuliko kitu chochote kile. Kila alipokuwa akiangalia Cnn na kuona jinsi wanawake hao walivyokuwa wakifa ndio furaha yake ilivyozidi kuongezeka zaidi na zaidi.
Andy hakujisikia uchungu moyoni wala majuto, kitendo cha kuona kwamba Bakteria wa Letofoan walicyozidi kuwaua wanawake wa Kitanzania na ndivyo ambavyo alizidi kufurahia zaidi na zaidi. Kila siku alikuwa akinywa na kula kwa furaha, maisha kwake yakaonekana kuwa na furaha kupita kawaida. Kwa sababu alikuwa na sura ya bandia, katika kipindi hicho akaamua kununua nyumba ya kifahari ambayo ilikuwa jiji Washington na kuhamia pamoja na mke wake, Sofia.
Hakutaka kujulikana na mtu yeyote yule kwamba alikuwa amehamia jijini Washington zaidi ya Dawson ambaye alikuwa rafiki wake mkubwa. Sura ya bandia ya Sofia ikatengenezwa na wala hakukuwa na mtu ambaye alijua kwamba watu ambao walikuwa wakiishi kwenye moja ya jumba kubwa la kifahari alikuwa Andy pamoja na mke wake, Sofia.
Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele nandivyo ambavyo walizidi kuingiza fedha kwa kitendo kile ambacho kilikuwa kikiendelea cha utengenezaji wa dawa zilizokuwa zikitibu ugonjwa hatari wa PENINA. Andy akaendelea kununua magari ya kifahari hali ambayo ilimpelekea baada ya muda fulani kujenga hospitali yake mwenyewe.
Kila mtu katika kipindi hicho alikuwa akimtambua Andy kwa jina la uongo la Simpson. Kutokana na utaalamu mkubwa aliokuwa nao pamoja a kuwaajiri madaktari waliokuwa na uwezo mkubwa, hospitali yake iliyoitwa WASHINGTON SIMPSON MEDICAL HOSPITAL watu wengi wakaanza kumiminika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupata tiba ya magonjwa mbalimbali.
Jina la hospitali hiyo likakua zaidi na zaidi huku wagonjwa wengi wakizidi kumiminika. Magonjwa mengi ya kansa pamoja na magonjwa mbalimbali ya ngozi yalikuwa yakitibiwa katika hospitali hiyo ambayo ilionekana kuwa na madaktari wengi waliokuwa na uwezo wa juu kuliko madaktari wa hospitali nyingine nchini Marekani.
Wamarekani wakamuamini Andy ambaye alikuwa amejitambulisha kwao kama dokta Simpson, kiasi kikubwa cha fedha kilikuwa kikiendelea kuingia ndani ya hospitali hiyo ambayo wagonjwa mbalimbali nchini Marekani wakaonekana kuwa sehemu yao ya kimbilio.
Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hospitali ile ilivyozidi kupata jina zaidi na zaidi na wagonjwa kuzidi kumiminika zaidi. Kwa yale magonjwa ambayo yalikuwa yakishindikana hasa ya kansa, madaktari walikuwa wakishauri wagonjwa hao kuelekea katika hospitali hiyo ambayo ilikuwa na sifa kubwa ya kutibu magonjwa mbalimbali.
Ndani ya mwaka mmoja tu, tayari hospitali hiyo ikaonekana kuwa maarufu duniani kutokana na kutangazwa sana katika vyombo vya habari kwamba ilikuwa ni moja kati ya hospitali bora duniani. Mara kwa mara Andy kama dokta Simpson alikuwa akiitwa sana katika vyombo vya habari kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano mbalimbali.
Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alifahamu kwamba dokta Simpson ambaye alikuwa akiaminika na kila mtu duniani ndiye alikuwa mtu ambaye alikuwa akitafutwa sana duniani kwa kitendo chake cha kuua mamilioni ya wanawake ambao walikuwa wakiishi nchini Tanzania.
*****
Wapelelezi wale wakaanza ufanya kazi yao, kitu cha kwanza ambacho walikuwa wamekihitaji ni program maalamu iliyoitwa Motherless PC Studio ambayo kazi kubwa ya programu hiyo ilikuwa ni kugundua mtu fulani mahali alipokuwa. Program hii ndio ambayo ilikuwa ikifanya kazi kubwa sana kuwatafuta watu ambao walikuwa wakiisumbua nchi y Marekani.
Program hii ilikuwa ni ya siri sana ambayo ilitengenezwa na mtaalamu wa kompyuta aliyekuwa na uraia wa nchini Israel, Bwana Yehofati Patzan. Program hii ndio ambayo ilikuwa ikitumiwa sana na wapelelezi wengi nchini Marekani hasa wale ambao walikuwa wakitoka katika kitengo kikubwa cha upelelezi cha nchini Marekani, F.B.I.
Mpaka kufikia kipindi hicho program hiyo ilikuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, program hiyo ndio ambayo ilikuwa ikitumika kumtafuta jasusi mkubwa ambaye aliisumbua sana Marekani kwa Miaka ishirini na tano, Carlos the Jackal. Utumiaji wa program hiyo haukuishia hapo, bado ulionyesha mafanikio makubwa sana hasa mara baada ya kuendelea kuwakamatisha watu mbalimbali akiwepo Osama Bin Laden ambaye alijulikana mahali alipokuwa amejificha.
Program hiyo ndio ambayo ilikuwa ikiaminika sana na wapelelezi wa shirika la kipelelezi la F.B.I. Kwa sasa, wapelelezi ambao walikuwa wataalamu wa kuitumia program hiyo ndio ambayo walikuwa wameitwa kwa ajili ya kuitumia kwa ajili ya kumtafuta Andy na kujua mahali alipokuwa amejificha kwa wakati huo.
Siku zikaendelea kukatika lakini hakukuwa na mafanikio yoyote yale. Kila siku kazi yao ilikuwa moja tu lakini hawakuwa wamejua sehemu ambayo Andy alikuwa amejificha jambo ambalo lilionekana kuwashangaza wote. Program ile ilikuwa imewekwa vizuri kabisa kwa ajili ya kumtambua katika kipindi ambacho angekuwa akitumia simu au hata kompyuta ambayo ilikuwa imeunganishwa na internet.
Miezi sita ikakatika na hatimae mwaka kutimia lakini hakukuwa na mafanikio yoyote ambayo yalikuwa yameonekana. Bado serikali ya Marekani ilizidi kuwasumbua wapelelezi wale ambao walikuwa wamepewa kazi ya kumtafuta Andy na kujua mahali ambapo alipokuwa. Wapelelezi wale walifanya kazi usiku na mchana lakini hakukuwa na mafanikio yoyote yale.
“Ila huyu Andy si ameoa?” Swan aliwauliza wapelelezi wenzake.
“Ndio. Mke wake anaitwa Sofia, ana asili ya Venezuela japokuwa yeye ni Mmarekani” Paul alijibu.
“Ngoja tujaribu kumtafuta mke wake, najua kama tutafanikiwa kila kitu kitakuwa sawa” Swan aliwaambia.
Hapo ndipo ambapo kazi ikaanza upya, walichokuwa wakikitaka katika kipidi hicho ni kujua mahali ambapo Sofia alikuwepo. Walijua fika kwamba walishindwa kumpata Andy kwa sababu tu alikuwa akituvaa grops mkononi mwake katika kila kipindi ambacho alikuwa akitumia simu na ndio maana ilikuwa jambo kubwa na zito kumkamata.
Waliendelea kumtafuta Sofia zaidi na zaidi. Kitu cha kwanza ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kutafuta alama zake za vidole tu. Wakaelekea katika sehemu iliyohusika katika utunzaji wa alama za vidole vya wananchi wote wa Marekani na kisha kuchukua vitu vyote ambavyo vilikuwa vikihusiana na Sofia.
Mara baada ya kurudi katika chumba kile, alama za vidole vyake wakaziweka katika sehemu maalumu na kisha kuviscan na kazi kuanza mahali hapo. Kwa kutumia uzoefu mkubwa wa program ile, wakafnikiwa kwa kiasi kikubwa sana kugundua mahali ambapo alama za vidole vile vilipokuwa vimeshika simu. Kompyuta ikaanza kulia, kwa haraka haraka Swan akaifuata na kisha kuanza kuifungua program ile.
Ramani yote ya Marekani ikaonekana katika kompyuta ile. Swan akaanza kutafuta alama zile za vidole zilipokuwa kwa kipindi hicho. Ramani ikazidi kuvutwa zaidi na kisha mshale kuanza kuelekea katika jiji la Washington ndani ya mji wa Macberth uliokuwa Kusini Mashariki mwa jiji lile. Bado program ile ilizidi kufanya kazi yake zaidi na zaidi. Nyumba ikaanza kutafutwa na hatimae mshale ule kusimama katika nyumba moja ya kifahari.
Kila kitu juu ya ile nyumba kikaanza kujiandika. Ikaanza kutokea namba ya nyumba pamoja na kila kitu ambacho kilikuwa kikitumika ndani ya nyumba ile na kwamba mmiliki wa nyumba ile alikuwa dokta Simpson pamoja na mke wake Elizabeth. Mpaka kufikia muda huo wakaonekana kuanza kuhisi kitu.
Walichokifanya kwa wakati huo ni kufungua katika mtandao wa Google na kisha kuandika jina la Simpson Gabriel kama ambavyo Andy alivyokuwa akijiita kwa wakati huo na kisha kuanza kuangalia taarifa zake. Taarifa zote zikajileta mahali pale kwa kueleza kwamba Simpson alikuwa dokta mkubwa ambaye alikuwa akitibu magonjwa ya kansa pamoja na kufungua hospitali yake kubwa iliyokuwa nchini Marekani.
Mara baada ya kupata taarifa hizo, napo wakaanza kuangalia kuhusiana na Andy. Taarifa zote zile zilionekana kufanana, kama jinsi dokta Simpson alivyokuwa mtaalamu wa magonjwa ya kansa basi nae Andy alikuwa mtaalamu wa magonjwa hayo hayo ya kansa jambo ambalo likawafanya wote kuwa na uhakika kwamba mtu huyo ambaye alikuwa akijulikana kwa jina la dokta Simpson alikuwa Andy ambaye walikuwa wakimtafuta.
Hawakutaka kuishia hapo, walichokifanya ni kuanza kuangalia rangi yamacho ya dokta Simpson na dokta Andy, macho yalikuwa na rangi ile ile. Hawakuishia hapo, walitaka kujua vitu vingine zaidi na zaidi, wakaanza kuangalia urefu. Urefu ulikuwa ukionekana kufanana japokuwa dokta Simpson alikuwa amezidi kwa pointi kadhaa.
“Ndiye yeye” Swan aliwaambia wenzake ambao wote wakaonekana kufikia mwisho wa kazi ambayo ilikuwa imewafanya kukusanyika ndani ya chumba kile.
Mawasiliano yakaanza kufanyika kwa wakati huo, tayari mtu ambaye alikuwa akitafutwa sana alionekana kuwa sehemu fulani huku akijifanya kuwa mtu fulani. Mara baada ya mapolisi kupewa taarifa ile wala hawakutaka kuchelewa, kitu walichokifanya kwa wakati huo ni kujiandaa na safari ya kwenda katika nyumba aliyokaa akiishi Andy ambaye alikuwa amejitambulisha kwao kama dokta Simpson.
Bunduki zilikuwa mikononi mwao, zaidi ya mapolisi ishirini walikuwa wakisafiri kuelekea katika nyumba hiyo. Mioyoni mwao walikuwa na uhakika kwamba mtu yule ambaye alikuwa amejitambulisha kama dokta Simpson ndiye ambaye alikuwa Andy kama jinsi ambavyo waliambiwa na wapelelezi wae ambao walikuwa wamefanya kazi kwa zaidi ya mwaka mzima.
Mapolisi wale hawakutaka wote kuelekea katika nyumba hiyo bali walijigawa na wengine kwenda hospitalini. Walikuwa na uhakika kwamba kama Andy hakuwa nyumbani kwake basi ilikuwa ni lazima kwa mtu huyo kuwa hospitalini ambapo hapo wangemkamata na kisha kumfikisha katika vyombo vya sheria.
Hawakuchukua muda mrefu wakawa wamekwishafika katika nyumba hiyo ambapo polisi mmoja akasimama na kisha kuoyesha kitambulisho huku akitaka geti hilo lifunguliwe. Geti likafunguliwa na moja kwa moja kuingia ndani ambapo wakahitaji kuonana na dokta Simpson.
Kwa haraka haraka mfanyakazi wa ndani akatoka mahali hapo na kisha kuingia sebuleni na kuuchukua mkonga wa simu ya mezani na kuanza kupiga katika simu ya Adny ambayo ilikuwa chumbani. Simu iliita zaidi na zaidi lakini wala haikupokelewa. Mfanyakazi alionekana kushangaa kupita kawaida, alijua fika kwamba bosi wake alikuwa ndani ya chumba kile kwani ni dakika chache zilizopita aikuwa ameongea nae huku akimpa maagizo fulani ya nyumbani hapo ambayo yalitakiwa kufanyika.
“Nadhani hayupo” Mfanyakazi yule aliwaambia.
“Sawa. Atakapokuja mwambie kwamba tunamuhitaji” Polisi yule alisema.
Hawakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka na kupeleka taarifa kwa Andy hakuwepo nyumbani kwake. Kwa wakati huo wakaanza kuwasikilizia wale mapolisi ambao walikuwa wamekwenda hospitalini kumwangalia, majibu ambayo yalitoka kwa mapolisi wale ni kwamba Andyau dokta Simpson hakuwepo hospitalini kule.
Jibu lile lilionekana kumchanganya kila mmoja, hawakuelewa mahali ambapo Andy alikuwepo kwa wakati huo. Wakaanza kuwasiliana na wapelelezi wale na kisha kuwaambia kwamba Andy hakuwepo ndani ya nyumba ile. Kitu alichokifanya Swan ni kwenda kwenye kompyuta yake na kisha kuanza kumtafuta mke wa Andy, Sofia.
Kwa wakati huu mambo yakaonekana kuwa tofauti, katika kila kona ambayo alikuwa akimtafuta kwa kutumia alama za vidole pamoja na ile programu ya kompyuta hawakufanikiwa kumpata. Jambo lile lilionekana kmchanganya kupita kawaida, kwa nini Sofia hakuonekana ndani ya nyumba ile na wakati muda mfupi uliopita alikuwa ameonekana, tayari akahisi kwamba kulikuwa na kitu kimetokea.
Hapo dipo alipoamua kuwapigia simu mapolisi na kuwaambia kwamba kwa kipindi hicho iliwabidi waelekee katika nyumba hiyo na kisha kuanza kufanya msako nyumba nzima. Kitu alichoshauri Swan ndicho ambacho kikafanyika kwa wakati huo. Mapolisi wakajiandaa na kisha kuanza safari ya kuelekea katika nyumba hiyo huku wakiwa na vibali vyote vya kufanya upekuzi ndani ya nyumba hiyo.
Mara baada ya kufika katika nyumba hiyo wakawaonyeshea wafanyakazi vibali vile na kisha kuanza kufanya upekuzi ndani ya nyumbaile. Upekuzi ulifanyika kwa takribani nusu saa lakini hakukuwa na mafanikio yoyote yaliyopatikana. Si Andy wala Sofia ambaye alionekana ndani ya nyumba hiyo jambo ambalo lilionekana kuwachanganya mapolisi wale.
“Hakuna mtu” Polisi mmoja, Mark alimwambia Swan.
Andy akaonekana kupotea ndani ya nyumba ile. Hakukuwa na dalili zozote za kuonekana kwa Andy wala mke wake, Sofia. Kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa, katika kipindi cha nyuma waliona kila dalili za kufanikiwa katika kazi ile ya kumtafuta Andy na kumkamata lakini kwa wakati huo kila kitu kikaonekana kupotea,
Walichokifanya ni kuondoka ndani ya nyumba hiyo huu wakipanga kurudi tena ndani ya nyumba hiyo katika siku ambayo haikutarajiwa. Wafanyakazi wa ndani walikuwa waishangaa, hawakujua sababu ambayo iliwafanya mapolisi wale kumtafuta bosi wao.
****
Andy alikuwa amekaa ndani ya chumba chake huku mke wake, Sofia akiwa jikoni akiandaa chakula. Muda wote macho ya Andy yalikuwa katika kioo cha kompyuta. Kwa wakati huo Andy alikuwa akiangalia oda za dawa za ugonjwa wa kansa ambazo watu mbalimbali duniani walikuwa wamezituma katika hospitali yake.
Huku akiwa bize na kuangalia mambo hayo, mara macho yake yakatua katika kioo cha televiheni ndogo ambayo ilikuwa ndani ya chumba chake hasa mara baada ya kusikia sauti ikiongea kutoka getini, alipoangalia kwenye televisheni ile ambayo ilionganishwa na kamera ambayo ilikuwa getini, macho yake yakatua kwa mapolisi kadhaa ambao walikuwa getini pale.
Andy akaonekana kushtuka, alichokifanya ni kuinuka na kisha kwa haraka sana kuelekea jikoni ambako akamchukua mke wake na kuelekea nae chumbani na kumuonyeshea kile kilichokuwa kikionekana kwenye televisheni ndogo pale chumbani. Hakukuwa na muda wa kupoteza, walichokifanya ni kufungua chini ambako kulikuwa na mlango uliokuwa vigumu sana kuonekana kutokana na rangi yake kufanana na sakafu na kisha kuufungua na kuingia ndani na kuufunga.
Ndani ya shimo lile lilionekana sehemu ya kawaida sana, kulikuwa na makochi, televisheni, jiko vitanda huku kukiwa na viyoyozi vya kutosha. Ukiachilia na hivyo, vile vile kulikuwa na njia ya ambayo ilikuwa na zaidi ya umbali wa kilometa moja ambayo ilikuwa ikitokea ufukweni.
Andy pamoja na mke wake wakatulia ndani ya shimo lile huku wakiangalia kila kilichokuwa kikiendelea kwa kupitia kamera ambazo walikuwa wamezifunga katika kona nyingi ndani ya chumba kile. Waliwaangalia mapolisi wale ambao walikuwa wameingia ndani ya nyumba ile na kuwaulizia.
Mapolisi wakaondoka mahali hapo lakini Andy na mke wake, Sofia hawakutaka kutoka ndani ya shimo lile. Baada ya masaa manne mapolisi wale wakarudi tena na kisha kuanza kukagua nyumba nzima. Ndani ya nusu saa mpaka upekuzi unakwisha hawakuweza kufanikiwa kuwaona na kuamua kuondoka ndani ya nyumba hiyo.
Wiki ya kwanza ikapita, wiki ya pili ikapita na hatimae mwezi mzima kumalizika lakini si Andy wala mke wake, Sofia ambaye alikuwa ameonekana sehemu yoyote ile. Bado wapelelezi walikuwa wakiendelea kupeleleza zaidi na zaidi lakini Andy wala hakuweza kuonekana sehemu yoyote ile. Watu ambao walikuwa wakiumwa magonjwa ya kansa wakaonekana kuzidiwa, umuhimu wa Andy ukaanza kuhitajika kwa kuokoa maisha ya wagonjwa ambao walizidi kuteketea.
****
Miezi sita ikakatika, hali ilionekana kuwa mbaya sana kwa wagonjwa wa kansa jambo ambalo likaonekana kuiweka nchi ya Marekani katika hali mbaya. Wengi walikuwa wakifa na wakati walikuwa na uhakika wa kupona kama wangetibiwa na dokta Andy ambaye alikuwa akijulikana kama dokta Simpson.
Ingawa Serikali nchini Marekani ilikuwa ikiendelea kumtafuta Andy kwa ajili ya kumfikisha katika vyombo vya sheria lakini kwa wakati huo mambo yakaonekana kubadilika, Andy akaanza kutafutwa kwa ajili ya kurudishwa hospitalini na kuendelea na kazi yake kama kawaida ya kuwaokoa wamarekani wengi ambao walikuwa wameathiriwa na ugonjwa wa kansa.
Andy hakuonekana kabisa japokuwa alitafutwa katika kila sehemu. Matangazo yakaanza kutolewa kwamba popote alipokuwa alikuwa akihitajika kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu ambao walikuwa wakizidi kufa kwa kansa. Ingawa kila siku tangazo lile lilikuwa likitolewa lakini Andy hakujitokeza kutoka alipokuwa japokuwa alikuwa akiliona tangazo lile.
“Kuna nini?” Kamanda mkuu aliuliza mara baada ya kupokea simu kutoka katika shirika la habari la CNN.
“Kuna mkanda umeletwa hapa” Mwandishi wa habari wa shirika hilo alijibu.
“Mkanda gani?”
“Njoo uuone. Unamhusu Andy”
Kamanda Simons hakutaka kuendelea kukaa ofisini mwake, akainuka na moja kwa moja kutoka nje kwa ajili ya kwenda kuuangalia mkanda huo. Maswali mengi yakaanza kumiminika kichwani mwake juu ya huo mkanda, ulikuwa ukizungumzia nini?
Mara baada ya kusaifiri kwa ndege mpaka kufika Atalanta, moja kwa moja akaanza kuelekea katika kituo kikubwa cha shirika hilo la habari na kisha kuelekea kule alipokuwa akihitajika. Alipoufikia mlango akaugonga na kukaribishwa ndani katika chumba ambacho waandishi wengi wa habari walikuwa wamejazana kana kwamba kulikuwa na kitu kinaendelea.
“Vipi?” Simons aliuliza.
“Kuna mkanda umeletwa ofisini”
“Unahusu nini?”
“Andy amejirekodi. Ameuita UKWELI WENYE KUUMA”
“Mungu wangu! Ukweli gani huo aliouzungumzia? Amesemaje?”
“Anachokitaka yeye ni kwamba mkanda huu tuurushe hewani ili dunia ijue kila kinachoendelea” Mkurugenzi wa shirika lile, Peters alijibu.
“Amezungumzia nini?”
“Mambo ya ajabu, mambo yanayotisha sana”
“Mmmh! Hebu uweke tuuone kabla ya kuurusha hewani” Simons aisema na kisha mkanda kuwekwa.
Mkanda ule wa saa moja ulikuwa ukimuonyesha Andy, tena akiwa katika sura yake halisi. Alikuwa akiongea huku akilia tu. Aliongea kuhusu historia yake toka kipindi ambacho alikuwa amezaliwa mpaka katika kipindi hicho. Hakuficha kitu chochote kile, aliuelezea uhusiano wake na Annastazia, akaelezea kuhusu virusi vya katapillar ambavyo vilikuwa vikieneza ugonjwa wa PENINA.
Andy hakuficha, alieleza kila kitu jambo ambalo lilimfanya kila mtu kushika kinywa kwa mshtuko. Bwana Simons ndiye ambaye alionekana kushtua zaidi, hakuamini kama Andy ndiye ambaye alikuwa nyuma ya kila kitu kilichotokea. Maneno yake ambayo alikuwa ameongea katika mkanda ule yalionekana kumshtua kila aliyekuwa akiuangalia na kuusikiliza.
“Urushe haraka sana” Simons alimwambia Peters huku akionekana kuchanganyikiwa.
Kichwa chake kilikuwa kinauma kwa wakati huo, Andy akaonekana kuwa tatizo kubwa kwa wakati huo. Mkanda ule ukaanza kurushwa, watu walipoona kwamba ni habari zilizofika punde tena zilizomhusu Andy, watu wakatulia katika televisheni zao. Picha ya Andy ilipoonekana tu, kila mmoja alionekana kumuhitaji.
Maneno ambayo yalikuwa yakiongelewa na Andy yalionekana kumuumiza kila mtu, hapo ndipo walipojua kwamba Andy ndiye alikuwa nyuma ya kila kitu. Magonjwa mawili ambayo yalikuwa yakiusumbua dunia kwa wakati huo, dawa ilikuwa ikipatikana kwa mtu mmoja tu, Andy.
“Mtu mbaya ndiye mtu mzuri. Sasa afanywe nini huyu?” Jamaa mmoja aliuliza.
“Tuangalie kwanza umuhimu. Ni lazima tufikirie sana kwamba ni kitu gani kikifanyika kitakuwa suluhisho, kuuawa au kuachwa hai” Jamaa alimjibu mwenzake.
Hiyo ndio hali ambayo ilionekana kusumbua vichwa vya watu duniani kwa wakati huo. Magonjwa hayo mawili yalizidi kuwamaliza watu kupita kawaida. Hakukuwa na jinsi, kwa kuwa Tanzania ilionekana kuwa nchi ndogo ambayo ilikuwa ikitaka Andy akamatwe na kuhukumiwa kifo, ombi lao likafichwa chini ya kapeti, watu walichokuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kumuona Andy akirudi na kuendelea na utengenezaji wa dawa za magonjwa yale.
Matangazo yalizidi kutolewa zaidi na zaidi kumtaka Andy ajitokeze lakini bado alikuwa kimya hali ambayo ilimchanganya kila mtu.
*****
Maisha ya chini ya andaki bado yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Muda mwingi Andy alikuwa akionekana kuwa na mawazo kupita kawaida. Kitu ambacho alikuwa ameamua na mke wake, Sofia kwa wakati huo ni kujirekodi na kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake. Wakafungua mlango wa kutokea ndani ya chumba chao na kisha kutoka na kuanza kutafuta kamera ndani ya nyumba ile na kujirekodi.
“Huu ndio ukweli wangu ambao utakwenda kuwaumiza watu wengi duniani” Andy alisema mara baada ya kamera kuanza kumchukua.
Andy akaanza kuelezea, kila kitu ambacho alikuwa akikielezea katika kipindi hicho alikuwa akilia tu, maneno ambayo alikuwa akiyaongea yalikuwa yakimuumiza hata yeye mwenyewe. Si yeye tu aliyekuwa akilia, bali hata mke wake, Sofia alikuwa akiumia kupita kawaida. Ni kweli alikuwa ameangamiza watu wengi duniani lakini katika kipindi hicho hakutakiwa kuuawa.
Kama angeuawa lisingekuwa suluhisho kabisa kwani watu wengi wangezidi kufa ila kama angeachwa hai basi watu wengi wangetibiwa juu ya magonjwa yale ambayo yalikuwa yakiwasumbua. Mkanda ulichukua dakika thelathini na ndipo ambapo wakampa mfanyakazi wa nyumba yao na kumuambia aupeleke katika jengo la shirika la habari la Cnn na kuwaambia kwamba waurushe hewani ili dunia nzima ijue ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea.
*****
Watu walikuwa wakihuzunika kupita kawaida huku wengine wakilia kupita kawaida. Kitendo cha kuuona mkanda ule ambao alikuwa ameurekodi Andy kwamba yeye ndiye alikuwa nyuma ya kila kitu kilichokuwa kikitokea kuhusiana na ugonjwa mbaya wa PENINA kilionekana kuwauma kupita kawaida.
Ugonjwa ule ulikuwa umemaliza watu wengi duniani, kwa kipindi hicho dawa za ugonjwa ule zilikuwa adimu sana kupatikana na hata kama zilikuwa zikipatikana basi zilikuwa na gharama kubwa kiasi ambacho watu maskini hawakuweza kuzinunua.
Maanamano yakaanza kufanyika mitaani katika nchi ya New York huku yakimtaka Andy ajitoe kule alipojificha ili aje kuiokoa dunia kutokana na janga kubwa la magonjwa ambalo lilikuwa limeikumba dunia hii. Maandamano yale yalipoonekana yakiendelea kufanyika kila siku nchini Marekani, nao nchi nyingine zikaanza kuandamana, na mwisho wa siku nusu na robo ya nchi duniani zilikuwa zikiandamana.
Si Andy wala mke wake ambaye walitoka kutoka kule walipokuwa, bado waliendelea kujificha huku wakiangalia hali inaendelea vipi. Ugonjwa wa PENINA na magonjwa ya kansa ndio yalikuwa magonjwa ambayo yaliwamaliza sana, watu walizidi kuteketea kila siku jambo ambalo uhitaji wa Andy ulikuwa ukizidi kuongezeka.
Mwezi wa kwanza ukapita na ndipo kipindi ambacho Andy akaanza kujitokeza. Ilionekana kuwa furaha ya dunia, matumaini ambayo yalikuwa yamepotea mioyoni mwa watu yakaanza kurudi tena. Waandishi wa habari wakaanza kukusanyika nyumbani kwake, Washington kwa ajili ya kufanya nae mahojiano. Siku hiyo Andy aliongea mambo mengi sana huku akimtaja Dawson kuwa mtu ambaye alimfanyia ushawishi mkubwa wa kutengeneza virusi vile vya Katapillar.
Mapolisi hawakutaka kukaa kimya, walichokifanya ni kufanya maandalizi ya kumkamata Bwana Dawson kwa sababu alionekana kuwa chanzo cha kila kitu. Andy hakukamatwa japokuwa alionekana kuwa na makosa makubwa. Makosa yote ya kuangamiza mamilioni ya watu duniani yakaonekana kusahaulika.
“Bora alivyoua mamilioni ili aokoe mabilioni” Mwananchi mmoja aliwaambia wenzake maneno ambayo alitaka yaandikwe kwenye bango lake huku akijiandaa na maandamano.
Siku mbili baadae, Andy akaitwa Ikulu na kula chakula cha jioni na mheshimiwa rais wa nchi hiyo na baada ya siku mbili kazi ya kutengeneza dawa ikaanza rasmi. Hiyo ikaonekana kuwa neema kwa watu wote duniani, mara baada ya kila kitu kukamilika, dawa zikaanza kusambazwa dunia nzima, haikujalisha kama ulikuwa masikini au tajiri, dawa zile zilikuwa zikipatikana bure kabisa.
Andy hakuishia hapo, akaanza kutengeneza dawa nyingi za magonjwa ya kansa ambazo zilikuwa na nguvu kupita kawaida. Kila dawa ambayo alikuwa akiitengeneza ilikuwa ikipatikana bure na serikali ya Marekani ndio ambayo ilikuwa ikimlipa. Faraja ikaonekana kurejea duniani, watu ambao walikuwa wametumia dawa zile walikuwa wamepona kabisa.
Lengo kubwa la Andy katika kipindi hicho lilikuwa ni kuupoteza kabisa ugonjwa wa PENINA. Alitengeneza dawa usiku na mchana. Kwa sababu yeye ndiye ambaye alikuwa ameutengeneza ugonjwa ule, alitakiwa kuua kwa mikono yake mwenyewe.
Kutoka asilimia thelathini ya watu ambao waliuwa wameambukizwa ugonjwa ule duniani mpaka kufikia asilimia tano ilionekana kuwa kazi kubwa kupita kiasi. Andy hakupata muda mwingi wa kupumzika, bado alikuwa akiendelea kutengeneza dawa zaidi na zaidi.
Maisha yake yaliendelea hivyo hivyo, alizidi kutengeneza dawa zaidi na zaidi. Bwana Wayne na mke wake, Bi Happy walionekana kuwa na furaha kumuona tena mtoto wao machoni mwao. Kwa sababu alikuwa amekiri kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea, wote tena kwa moyo mmoja wakamsamehe na kuendelea na maisha yake kama kawaida mpaka pale ambapo alikuwa kupata mtoto wa kwanza wa kike ambaye alimpa jina la Loveness.
Maisha yaliendelea kama kawaida, kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake kaamua kukisahau. Nchi ya Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa ukawa umemkingia kifua Andy. Hata nchi ya Tanzania ilipokuwa ikilalamika kuhusiana na Angy, hakukuwa na mtu yeyote ambaye aliwaelewa.
Dawa zikatengenezwa za kutosha, Andy akaamua kufungua chuo cha uuguzi nchini Marekani na kuwafundisha wanafunzi namna ya kutengeneza dawa mbalimbali za kuua baadhi ya magonjwa. Ndani ya mwaka mmoja, wanafunzi wote ambao walikuwa wakitoka katika chuo chake alikuwa akiwaajiri katika hospitali yake jambo ambalo lilimfanya kumuingizia fedha kupita kawaida.
**SEMA LOLOTE KUHUSIANA NA SIMULIZI HII...maoni yako
MWISHO
0 comments:
Post a Comment