Simulizi : Niliua Kumlinda Mama Yangu
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walichokifanya polisi ni kuuchukua mwili wa marehemu na kuwachukua watu hao kwa ajili ya kwenda kutoa maelezo zaidi kituoni.
Ndani ya nusu saa tu tangu kifo cha mchungaji Yekonia kujulikana, tayari watu walishasambaziana taarifa hiyo katika mitandao ya kijamii kitu kilichoibua maswali mengi kama taarifa zile zilikuwa ni za kweli au la.
Kila mmoja, kwa jinsi alivyolielezea tukio ni kama mtu aliyekuwa sehemu husika kwani wengine walikwenda mbele zaidi na kusema kwamba mchungaji huyo aliamua kujiua kwa sababu alitaka kwenda Mbinguni haraka hata kabla Mungu hajaamua kumchukua.
Hakukuwa na aliyeamini juu ya taarifa zile, washirika wake, wakalia sana, mchungaji Yekonia alikuwa mtu muhimu sana katika jamii kwani mbali na huduma yake ila alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba wenye matatizo binafsi hasa ya kifedha wanasaidiwa haraka iwezekanavyo.
Tanzania ikawa kama imetetemeka, vifo vya watu muhimu watatu tena ndani ya miezi miwili vikawashtua wengi, tena kitu kilichowapa maswali zaidi ni namba zile zilizowekwa ndani ya ofisi ile iliyofanyikiwa mauaji. Hapo ndipo watu walipogundua kwamba muuaji wa mauaji hayo ni yuleyule ambaye alimuua bwana Kambani na Nkone.
“Huyu muuaji ni nani hasa?” aliuliza jamaa mmoja.
“Wakati wewe unajiuliza huyu muuaji ni nani, mimi najiuliza kwa nini anaweka namba hizi, tena kwa kuitaja miaka ya enzi hizo,” alisema jamaa mwingine.
“Hapa cha msingi ni polisi kufanya kazi ya ziada, haiwezekani mtu aue anavyotaka halafu asikamatwe,” alisema mwanamke mwingine.
Katika msiba wake, idadi kubwa ya watu ilikuwa mahali hapo, vilio vilisikika kila kona, viongozi mbalimbali wa serikali na dini walifika kwa ajili ya kuhudhuria mazishi hayo yaliyoigusa Tanzania. Kila mmoja alikuwa na maswali juu ya muuaji huyo, wengi wakawa na hofu, matajiri wengi wakawa si watu wa kukaa nchini, walikuwa wakisafiri kuelekea nje, kote huko, walikuwa wakimkimbia muuaji huyo ambaye alizidi kuitetemesha Tanzania.
“MUUAJI NI NANI?, NINI MAANA YA NAMBA HIZI? NANI ANAYEFUATA?” Vilikuwa vichwa vya habari vya magazeti mbalimbali ambavyo vilifanya magazeti hayo kununuliwa sana. Watu walitaka kufahamu ukweli, ni nani alikuwa muuaji na kwa nini alifanya mauaji hayo.
Maswali mengi yalikusanyika vichwani mwa watu lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa na majibu yoyote yale. Mpaka siku ambayo mchungaji Yekonia alikuwa akizikwa katika makaburi ya Kinondoni, bado minong’ono ilikuwa mingi, kila mtu alikuwa akiuliza kuhusu muuaji huyo.
*****
“Karibu sana mzee....” alisema polisi huku akionekana kuwa na heshima ya hali ya juu.
“Asante sana. Nimekuja mnifunge jela...” alisema mzee mmoja aliyeingia, tena huku akiwa anatetemeka.
“Unasemaje?” polisi aliuliza huku akionekana kushtuka, yaani alikuwa kama mtu asiyeamini maneno yale aliyoyasikia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimekuja mnifunge jela, nitauawa, naomba mnifunge, ninauza madawa ya kulevya...” alisema mzee huyo.
“Hebu punguza munkari, mbona hatukuelewi?”
“Naomba mnifunge jela...atakuja kuniua na mimi pia, naomba mnifunge jela.”
Polisi walipigwa na mshangao, hawakuamini kile walichokuwa wakikisikia kutoka kwa mtu aliyesimama mbele yao ambaye alikuwa bilionea mkubwa. Walimfahamu, kwa jina aliitwa James Marimba, alikuwa miongoni mwa mabilionea wakubwa nchini Tanzania.
Kipindi cha nyuma alikuwa hakimu ila baada ya kupata fedha, akaachana na kazi hiyo na kuwa mfanyabiashara ambapo alijiingizia kiasi kikubwa cha fedha. Leo, mwanaume huyo alikuwa ameingia katika kituo cha polisi na kutaka kufungwa jela kwani kulikuwa na mtu aliyekuwa akimuwinda.
“Mzee Marimba...hatukuelewi...”
“Mtanielewa baadaye, naomba mnifunge kwanza...”
Polisi waliokuwa kituoni hapo walishindwa kumuelewa mzee huyo, kwao, alionekana kama kuchanganyikiwa, yaani mtu atoke huko alipotoka halafu kung’ang’aniwa kufungwa gerezani, hakika kilikuwa kitu cha kushangaza mno.
Mbali na hiyo, mtu huyohuyo alisema kwamba yeye alikuwa muuzaji wa madawa ya kulevya, vyote hivyo viliwashangaza polisi ambao walibaki na mshangao tu, hawakuonekana kumuelewa mzee huyo, walibaki wakimwangalia tu.
****
Kadiri bwana Mapimba alivyokuwa akizungumza maneno ya kutaka kufungwa jela ndivyo polisi wengine walivyofika katika kaunta hiyo na kuanza kumsikiliza kile alichokuwa akikizungumza.
Hakukuwa na mtu aliyeamini, wengi walimuona kama mtu aliyechanganyikiwa, ilikuwaje atake kufungwa jela na wakati hakuwa amefanya kosa lolote lile? Kitu kingine alisema kwamba yeye alikuwa akifanya biashara ya kuuza madawa ya kulevya, ilikuwaje hiyo? Polisi walijiuliza sana lakini hakukuwa na mtu aliyekuwa na majibu.
Walichokifanya ni kumuita mkuu wa kituo ambapo wakamchukua na kwenda naye katika chumba kilichokuwa ndani ya kituo hicho kilichokuwa maalumu kwa ajili ya kufanyia mahojiano tu.
Walipofika humo, wakamuweka kitini na kuanza kuzungumza. Mzee Marimba aliwaambia ukweli kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa akiwawinda, ndiye huyohuyo ambaye alifanya mauaji kwa matajiri wengine ambao walikuwa maswahiba wake.
Polisi walikuwa kimya wakimsikiliza, walikuwa na maswali mengi lakini hawakutaka kuuliza kwanza, walitaka kumsikiliza mpaka mwisho angehitimisha kwa kusema kitu gani. Alichukua dakika kumi nzima, ndipo akamaliza.
“Kwa nini amewaua wote hao, na kwa nini anataka kukuua na wewe?” aliuliza mkuu wa kituo.
“Kambani alifanya mchezo mbaya sana,” alijibu mzee Marimba.
“Mchezo gani.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kuhusu utajiri...”
“Ilikuwaje kwani?”
Hapo ndipo mzee Marimba akaanza kuhadithia tena kila kitu kilichokuwa kimetokea, tangu bwana Kambani amtapeli mwanamke mmoja aliejulikana kwa jina la Anita mali zake kisha kumtesa na kumfukuza.
Haikuishia hapo, alihadithia kila kitu, ukatili wotempaka waliposuka miango ya kumuua yeye na mtoto wake lakini ilishindikana kwa sababu nyuma kulikuwa na watu waliokuwa wakimsaidia.
“Watu gani?”
“Hata sifahamu! Ila mipango yote iligonga mwamba na vijana wote waliuawa...” alijibu mzee Marimba.
“Kwa hiyo chanzo cha utajiri wa bilionea Kambani ni huyo mwanamke?”
“Ndiyo! Tena mimi ndiye niliyesimamia kesi na mwisho wa siku kumfanya bwana Kambani kuwa mmiliki halali....uwiiiii,” alisema mzee Marimba na kuanza kulia kama mtoto.
“Na vipi kuhusu madawa?”
“Kweli ninauza madawa ya kulevya, sisi wote wanne tulikuwa tukihusika na uuzaji wa madawa ya kulevya...” alijibu mzee Marimba.
“Safi sana. Na vipi kuhusu zile namba?”
“Namba zipi?”
“Zile anazoziandika muuaji baada ya kuua...”
“Zile ni idadi ya watu aliotaka kuwaua, tupo wanne, na alikuwa akitupa taarifa kila anapoua, hauwezi ukazifahamu kama wewe si mhusika, ila sisi tulizifahamu zote. Mwisho, nimebaki mimi tu na ndiyo maana nimeona nije kujisalimisha,” alisema mzee Marimba.
Walimuuliza maswali mengi na mwisho wa siku, kupitia maelezo yake alionekana kuwa na kesi ya kujibu hivyo kuwekwa chini na ulinzi na kusukumizwa sero. Kwake, hiyo ilionekana kuwa nafuu, alikuwa akiogopa sana, wenzake waliokufa walikuwa na ulinzi mkubwa lakini kutokana na ujuzi wa muuaji, wote wakajikuta wakiuawa kikatili.
Hakutaka hilo litokee, alikuwa tayari kukaa jela lakini si kukaa uraiani tena kwa wasiwasi mno. Ndani ya sero, alibaki akilia, alijaribu kumuomba Mungu msamaha kwa ubaya wote alioufanya kwa kukusudia au kutokukusudia, alijiona kuwa na dhambi kubwa ambazo zote hizo zilihitaji msamaha kutoka kwa Mungu.
Taarifa za kujisalimisha polisi kwa mzee Marimba zilimshangaza kila mtu, maelezo ambayo yalitolewa na polisi yalimshtua kila mmoja. Kilichotokea ni kuanza kufuatilia kwa kina kuona kama kweli mzee huyo alikuwa akijihusisha na biashara za madawa ya kulevya, kwenye kufuatilia kwao, wakabaini kwamba kweli mzee huyo alikuwa muuzaji mzuri, hata vijana wake waliokuwa wakisimamia biashara hizo wakachukuliwa na kupelekwa sero kama yeye na kusubiri hukumu.
Kwake, hilo halikuwa tatizo, aliona ni bora kuwa nyuma ya nondo lakini si kuona akiishi kwenye jumba lake la kifahari tena akiwa mwenye hofu ya kuuawa kila wakati. Baada ya wiki mbili, kesi hiyo ikaanza kusikilizwa mahakamani, ikahahirishwa na kusukumizwa siku nyingine.
Vyombo vya habari, vikapata vya kuandika, kila siku ilikuwa ni lazima kuandika kuhusu taarifa kuhu mzee Marimba, na kilichowashtua watu zaidi ni kwamba hata wale mabilionea wengine walikuwa wakijishughulisha na biashara hiyo, tena walikuwa marafiki wakubwa.
“Kwa hiyo mpaka bwana Kambani?” aliuliza jamaa mmoja.
“Ndiyo! Si umemsikia mwenyewe...tena kasema mpaka yule mchungaji Yekonia...”
“Acha utani kaka?”
“Kwani hukumsikia kwenye televisheni?”
“Sikumsikia, nilikwenda kulala...”
“Alizungumza sana.”
“Na ile miujiza yake?”
“Kumbe ilikuwa danganya toto, hakuna cha uponyaji wala nini!”
“Jamani! Mbona tunamkosea sana Mungu?”
Kesi ile iliendelea kuunguruma mahakamani na baada ya miaka miwili, mzee Marimba akaonekana kuwa na kesi ya kujibu hivyo kuhukumiwa miaka kumi na tano gerezani, hilo kwake halikuwa tatizo, alikuwa tayari kuitumikia kwa mikono miwili lakini si kurudi uraiani ambapo aliamini kwamba alikuwa akisakwa kwa udi na uvumba.
****
“Nimekuja kufungua kesi ya madai...” alisikika bi Anita.
“Madai dhidi ya nani?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Marehemu Kambani...”
“Yanasemaje hayo?”
“Kwamba mali zote alizokuwa nazo zilikuwa zangu...”
“Una uhakika?”
“Ndiyo!”
Bi Anita alifika mahakamani na kupeleka vithibitisho vyake kwamba mali zote alizokuwa akimiliki bwana Kambani zilikuwa zake hiyo ilikuwa taarifa yenye kushtua sana, mahakimu hawakuamini kile walichoambiwa, walibaki wakimwangalia mwanamke huyo, kwao, alionekana kuwa miongoni mwa watu waliokuwa na tamaa ya kuuchukua utajiri mkubwa aliokuwa ameuacha mwanaume huyo.
Hawakutaka kumpuuzia, walichokifanya ni kuwasiliana na familia ya marehemu Kambani na kuhitaji kwenda na vithibitisho vyote kwamba mali zile walizokuwa wameachiwa na bwana Kambani zilikuwa zao.
Walipofika huko huku wakiwa na mwanasheria wa familia, wakaonyesha nakala zao, zikachukuliwa zote na za Anita na kwenda kuzihifadhi tayari kwa kesi kuanza kuuanguruma.
Hapo, mambo yakaanza upya, kesi ikaanza kusikilizwa mahakamani huku waandishi wa habari wakiifuatilia kwa umakini kabisa. Madai ya Anita yaliwashangaza watu wengi, wengi wakashtuka kwani hawakutegemea kama kuna siku kungekuwa na mwanamke angeibuka na kudai kwamba mali zote alizokuwa nazo bwana Kambani ambazo kwa wakati huo zilikuwa chini ya familia yake zilikuwa zake.
“Una uhakika nitashinda kesi hii?” aliuliza Anita, alikuwa akimuuliza mumewe.
“Utashinda tu, wala usihofu.”
“Nashukuru kwa kunitia moyo!”
“Tupo pamoja.”
Kesi iliendelea kuunguruma, walichokifanya mahakimu ni kupitia mafaili
ya kipindi cha nyuma kabisa, jinsi mafaili yalivyoonyesha, kulionekana kuwa na
mianya mingi ya rushwa hivyo kuanza kuisimamia tena kesi ile.
Mawakili kutoka pande zote mbili wakawasilisha hati za umiliki wa nyumba
na biashara mbalimbali, hati hizo zikafikishwa kwa hakimu ambaye alitaka
kuangalia pamoja na baraza lake la wazee.
Siku hiyo, kesi ikaahirishwa tena na kutakiwa kusomwa tena baada ya wiki
mbili. Kila siku ilikuwa ni kuahirisha kesi hiyo ila baada ya miezi miwili,
hukumu ikatolewa kwamba zile hati ambazo familia ya bwana Kambani iliziwakilisha
mahakamani, zilionekana kuwa na kasoro nyingi na hazikuwa halali kabisa, ila
hizi ambazo alizipeleka Anita, zilikuwa ni za halali na zilionyesha kwamba yeye
ndiye alikuwa mmiliki halali wa mali hizo.
“Mmiliki halali wa mali hizo ni bi Anita Philip..” alisema hakimu, bi
Anita akashindwa kuvumilia, hapohapo akaanza kurukaruka kwa
furaha.
Maisha yakaanza upya, mali hizo aliachiwa Anita aziendeleze kama kawaida
huku mume wake, bwana Philip akiendelea kuwa nchini Madagaska. Hakutaka kurudi
tena nchini Tanzania, kila kitu, hasa maisha yake yangeendelea kuwa hukohuko
nchini Madagaska.
*****
“Kweli duniani wawiliwawili...”
“Kwa nini?”
“Mmh! Nilikutana na msichana kama wewe!”
“Kwa nini?”
“Mmh! Nilikutana na msichana kama wewe!”
“Wapi?”
“Kwa bosi wangu! Yaani kama wewe...”
“Yupo wapi?”
“Sikumfuatilia sana mara baada ya bosi mwenye kuuawa, nilichanganyikiwa ati mpaka nikawa namuita kwa jina lako...” Joshua alimwambia Cynthia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa bosi wangu! Yaani kama wewe...”
“Yupo wapi?”
“Sikumfuatilia sana mara baada ya bosi mwenye kuuawa, nilichanganyikiwa ati mpaka nikawa namuita kwa jina lako...” Joshua alimwambia Cynthia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda wote waliokuwa Joshua alionekana kuwa na furaha, kila
alipomwangalia msichana wake, Cynthia, kumbukumbu za msichana aliyekutana naye
kwa bwana Kambani zilimjia kichwani mwake.
Alikuwa Cynthia huyohuyo lakini hakuweza kuligundua hilo kwa kuwa mpenzi
wake huyo aliamua kumficha. Kilichotokea baada ya kukaa kwenye uhusiano kwa muda
wa mwaka mzima, hapo ndipo wawili hao walipopanga kuoana kama walivyopanga
kipindi cha nyuma.
Hilo halikuwa tatizo, kila mmoja alikuwa tayari na baada ya
kutambulishana kwa wazazi, wawili hao wakafunga ndoa kwenye kanisa la St.
Patrick lililokuwa Masaki jijini Dar es Salaam.
Siri ya kuwa mpelelezi kutoka nchini Madagaska iliendelea kubaki moyoni
mwake, hakutaka kumwambia mumewe. Kwa upande wa pili, mpelelezi Cosmas
aliendelea kupeleleza lakini kila alipokuwa akifikia, hakuweza kuendelea,
hakupata ushahidi wowote ule, kila sehemu aliyokuta mwili wa marehemu, hasa wale
mabilionea, hakukuwa hata na alama za vidole.
Alichanganyikiwa, baada ya miaka miwili ndipo akapokea barua pepe
iliyomwambia kwamba alitakiwa kuachana na kila kitu kwani kuuawa kwa watu hao
kulikuwa na mpango kabambe nyuma, hasa kuua mizizi ya biashara ya madawa ya
kulevya.
Hakujua barua pepe hiyo ilitoka wapi ila alipoifuatilia sana, aliona
ikiwa imetoka katika shirika kubwa la kijasusi nchini Marekani, CIA hivyo
akaamua kufunga mafaili yake na kusafiri tena kwenda nchini Marekani kula bata
kama kawaida yake.
Huku nyuma, kila kitu kilichotokea kilisahaulika, mapenzi motomoto kati
ya Philip na Anita yalirudi tena, binti yao aliwafanya kuwa na furaha siku zote,
kazi kubwa aliyokuwa amepewa, aliifanya kwa kiasi kikubwa na hakutaka
kujishughulisha na bwana Marimba ambaye alikuwa nyumba ya
nondo.
Yote hayo, mauaji aliyofanya, alifanya kwa kuwa alimlinda mama yake ili
hapo baadaye asije kuuawa na watu hao walioonekana kuwa na roho mbaya.
Cynthia na mumewe waliishi nchini Tanzania kwa miaka miwili kabla ya
kuamua kuhama na kuhamia nchini Madagaska ambapo wanaishi huko mpaka leo
hii.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHOOO
0 comments:
Post a Comment