Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

MREMBO ALIYEPOTEA - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ANDREW CARLOS





    *********************************************************************************

    Simulizi : Mrembo Aliyepotea

    Sehemu Ya Kwanza (1)



     Umati wa waumini wa dini ya kikristo ulikuwa unaendelea kumiminika katika kanisa kubwa la Mtakatifu John. Shangwe kubwa ziliendelea kusambaa ndani ya kanisa hilo ikiwa ni msisitizo kwamba waumini wake wameguswa sana na mahubiri yaliokuwa yakiendelea ndani ya kanisa ambayo yalikuwa yakitolewa na mchungji Joseph. Mmoja wa waumini katika kanisa hilo alikuwa ni Majaliwa na mkewe Juliana. Japokuwa alikuwa ni fundi mabomba na kila siku alitakiwa awe anafanya kazi hata kama ni jumapili, lakini kwake Majaliwa haikuwa hivyo kutokana na kuheshimu sana siku ya jumapili kwani aliitenga kama siku muhimu kwake na yakutubu dhambi zake zote. Upole na ucheshi aliokuwa nao Majaliwa ulizidi kumuongezea marafiki kila kukicha ikiwa ni kanisani mpaka mtaani alipokuwa akiishi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tatizo kubwa lililokuwa likimuandama Majaliwa ni juu ya mtoto. Pamoja na umri wake kufika miaka thelathini na tano lakini bado alikuwa hajabahatika kupata hata mtoto. Alihangaika yeye na mke wake kwenda karibu kila hospitali kujaribu kuangalia pengine mmoja wapo anamatatizo lakini karibu kila hospitali waliyoenda jibu lilikuwa ni hilo hilo kuwa wanauwezo wa kupata mtoto ila kinachotakiwa ni subira na kuomba sana kwa mwenyezi Mungu. Ndani ya miezi takribani mitatu tayari mke wa majaliwa alikuwa ameshanasa mimba. Furaha ya ajabu ilimtawala Majaliwa na mkewe Juliana nakuamini kile kilio alichokuwa akikililia kila siku sasa kimepata ufumbuzi. Hakutaka hata kumwacha mke wake abaki nyumbani peke yake mpaka atakapojifungua. Kutokana na kuwa na kipata kidogo alichokuwa akikiingiza kupitia kazi yake ya ufundi mabomba hakikutaosha hata kutafuta msichana wa kazi japokuwa pia ilikuwa ni tatizo kubwa kwake kwanza sehemu aliyokuwa amepanga ni ya chumba kimoja. Majaliwa aliendelea kuwa bega kwa bega mkewe mpaka alipofikisha miezi tisa ambayo mke wa Majaliwa alizidiwa na uchungu wa mara kwa mara.

    “..Mume wangu..?? sijiskii vizuri nakuomba nisidie kunyanyuka hapa!!”

    Aliongea mke wa Majaliwa huku uchungu ukizidi kumzidia hali iliyomfanya majaliwa atafute usafiri na kumkimbiza hospitali haraka. Woga uliochanganyana na kutetemeka mara kwa mara huku akijihisi kama mkojo unamtiririka kupitia suruali aliyokuwa amevaa Majaliwa. Muda wote alishikilia mikono yake kwa nguvu nje ya hospitali huku kila muda akionesha ishara kama ngumi juu kwa kusali na kuomba mkewe ajifungue salama hapo hospitali. Jasho jembamba liliendelea kumteremka Majaliwa kupitia kwenye kola ya shati lake huku dhahiri likionesha vifungo kupishana sababu ya haraka aliokuwa nayo ya kumuwaisha mkewe hospitali. Kila mlango wa wodini ulipofunguliwa Majaliwa alikuwa akitetemeka nakuona kama analetewa majibu juu ya maendeleo ya mkewe huko ndani. Hatimaye ndani ya muda mchache akatoka daktari aliyevaliwa mavazi makubwa meupe huku mikononi mwake akilishikilia karatasi na kalamu,

    “..Wewe ndio Majaliwa..?”

    “ndio mimi dokta.. dokta..?”

    Majaliwa aliitikia kwa kutetemeka huku akiendelea kumtolea macho yule dokta.

    “..twende ofisini kwangu..”

    Majaliwa aliongoza na yule daktari mpaka ofisini kwake kisha akamkalisha kwenye kiti na maongezi yakaendelea.

    “..kwanza kabisa nikupe hongera mzee mwenzangu..”

    Majaliwa hakutaka kabisa kuamini yale maneno kutoka akwa yule daktari, kwanza alihisi ni ndoto aliyokuwa akiiota kila siku halafu akizinduka inayeyuka. Majaliwa alijaribu kufumba macho nakufumbua ili kuamini kwamba anachokiona na kukisikia ni kweli kabisa na hayo maneno yanayotoka kwa daktari aliyekuwa amemuita mpaka ofisini kwake au la!

    “kwahiyo dokta, embu niambie Mke wangu kajifungua mtoto wa kike au wakiume maana natamani kumuona wee acha tu..”

    “..Anhaa, umefanikiwa kupata mtoto wa kike bwana Majaliwa..”

    “oohh!! Ashukuliwe Mungu, Apewe sifa Baba yetu aliye Mbinguni, Nasema ahsante sana Mungu umejibu maombi Baba, ulisema hakuna lishindwalo chini ya dunia Baba..”

    Majaliwa alijisahau kabisa kama tayari yupo katika himaya ya hospitali na akadhania yupo kanisani tena alijihisi yupo kwenye kipindi cha maombi, alianza kushukuru taratibu lakini hali ilivyozidi ukichanganya na furaha aliokuwa nayo Majaliwa alijikuta akiitoa sauti kubwa mule ofisini mwa daktari hali iliyomfanya Daktari amuondoe ampeleke mpaka alipo Mke wake ajionee mtoto wake. Majaliwa alipofika na hapo wodini hali ilimzidia akaanza kutangaza neno la Mungu huku kelele akiziachia karibu wodi nzima kwa kulitaja neno la Mungu na kushukuru kupata mtoto wa kike. Majaliwa alikuwa kama kituko pia kama kivutio katika ile wodi ya wakinamama.



    ***************



    Ndani ya miaka Kumi na nne hali ya Majaliwa ilikuwa imeshabadilika. Hakuwa Majaliwa tena kwani alitambulika kama Baba Alice kutokana na Yule motto aliyempata. Ule ulokole aliokuwa nao kipindi cha nyuma kabla ya kumpata Alice sasa ulikuwa haupo tena. Majaliwa alibadilika sana na haikujilkana haswa kipi kilichofanya akabadilika. Mama Alice na Alice walikuwa na kazi ya ziada juu ya kumfanya Baba Alice abadilike lakini hali ikawa pale pale. Ulevi wa pombe za kienyeji ulikuwa umeshamuathiri halmashauri ya kichwa cha Majaliwa. Kurudi kwake usiku wa manane nakuanza kutukana ovyo mitaani na hata kuamsha majirani waliolala kwa kuwaporomoshea matusi mengine ya nguoni kilikuwa ni kitendo kilichomsononesha sana Mama Alice na Alice kwa ujumla. Ile kazi ya ufundi Mabomba ambayo ilimsaidia Alice japo kumaliza darasa la saba sasa Baba alice akawa ameachana nayo huku akiamini kazi ya kuuza na kukaanga samaki aliokuwa akiifanya Mama Alice itawasaidia huku akijifariji kwa kuomba kwa ndugu jamaa na marafiki na akizipata ni kukimbilia kilabuni kunywa pombe za kienyeji.

    Siku moja usiku wa sana Baba Alice alikuwa ametoka kunywa pombe zake na alipofika kwake alichukuwa kipande cha kuni ambayo Mama Alice uvitunza ndani kwa ajili ya kukaangia samaki zake. Bila ya kuwa na sababu zozote za msingi Baba Alice aliingia mpaka chumbani kwake huku mkononi mwake akiwa na ukuni mkubwa nakuanza kumpiga nao Mama Alice kwa nguvu zote. Mama Alice alijitahidi japo kujikomboa lakini haikuwezekana huku Baba Alice akimnyamazisha kwa kumnyoshea ishara ya kumnyamzisha kwa vidole mdomoni. Maumivu makali aliokuwa anaendelea kuyapata Mama Alice yalimfanya atafute upenyo na kukimbia huku akielekea nje kusikojulikana.

    Ndani ya wiki hali ilizidi kuwa mbaya kwa Alice kutokana na kutoelewa Mama yake alipoelekea toka mara ya mwisho apate kipigo kutoka kwa Baba yake. Alice aliendelea kukaanga na kuuza samaki huku akiamini Mama yake atarudi tu. Hali ya Baba yake nayo iliendelea hivyo hivyo ya kilevi japokuwa siku nyngine alikuwa akirudi kwake akiwa amepooza na wala hajanywa. Alice alijitahidi sana kumpenda Baba yake kwa kuwa aliamini dhahiri yeye ni mtoto pekee kutoka kwa Baba na Mama yake hivyo inabidi awapende kwa hali yeyote. Siku moja usiku kwenye muda wa saa tatu usiku Baba Alice aliwahi kurudi kwenye mizunguko yake na hali yake ilikuwa si kilevi kama ilivyozoeleka. Alimkuta alice kishamtayarishia chakula cha jioni hivyo alipofika akatengewa akala na kisha akaelekea kulala. Ilimchukuwa masaa matatu tu Baba Alice alikurupuka usiku sana akaenda kuwasha mshumaa kisha akasogea hadi maeneo alipokuwepo Alice amelala. Alimwangalia mtoto wake Alice kwa masikitiko kisha akavua zipu ya suruali yake na baada ya hapo akavua nguo zake zote na kubaki mtupu. Usingizi mkali uliokuwa umempitia Alice ukichanganya na pilika pilika alizokuwa nazo siku nzima za kuandaa samaki na kuwakaanga pia kutengeneza chakula zilimfanya alale fofofo. Baba Alice alivyomaliza kuvua nguo zake zote alimfuata Alice na kisha kuanza kumvua gauni lake nakubakiwa uchi kama alivyozaliwa. Baada ya hapo Baba Alice akaanza kufanya tendo la kujamiiana na mtoto wake tena huku akitumia nguvu zake zote..

    “….Mamaaa nakufaaa..???”

    Alice alishtuka kutoka usingizini huku jasho likimtoka akimtazama Baba yake ambaye bado alikuwa juu ya kifua chake huku akiendelea kujamiiana. Machozi yalianza kumtiririka Alice. Maumivu makali aliokuwa anaendelea kuyapata kupitia sehemu zake za siri yalizidi kumuumiza akili yake. Baba alice alimtishia kwamba endapo atapiga kelele atamchoma na moto kupitia ule mshumaa. Alice alikuwa bikra ambayo alitamani sana siku moja mume atakayekuja kumuoa ndio aitoe lakini tayari Baba yake akawa ameshaitoa na kumsababishia maumivu makali..

    “..Nakupenda mwananagu Alice..!!”

    Aliongea Baba Alice huku akimwambia Alice kwa kumbusu kifuani mwake..



     Alice alijitahidi kuchukuwa mikono yake nakumsogeza Baba yake kutoka juu ya kifua chake lakini haikuwezekana. Kwanza Baba Alice alizidi kuwa mkali kama mbogo huku akiendelea kufanya mapenzi na Alice hali iliyomfanya kuendelea kupata maumivu. Machozi ya uchungu yaliokuwa yakiendelea kumwagika Alice pale kitandani yaliochanganyikana na hasira kali ni kati ya vitu ambavyo Baba Alice alivigundua lakini kutokana na hamu aliokuwa nayo ilimbidi kufanya hivyo. Baba Alice alipomaliza kufanya mapenzi na Alice alirudishia suruali yake vizuri kisha akazima ule mshumaa nakuelekea kwenye kitanda chake tayari kwa kulala. Usiku wote ulikuwa ni mkubwa kwa Alice kwa sababu ya mambo makubwa mawili. Kwanza kabisa kitendo cha kuingiliwa na Baba yake mzazi na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri. Na pili ni kumtoa bikra yake aliyokuwa ameitunza kwa muda mrefu.



    ******



    Ndani ya mwezi Maisha ya Alice yalikuwa yameanza kubadilika kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja nakupungua mwili. Kutokumuona Mama yake takribani miezi tangu Baba yake ampige na kuni na kasha kutoroka mara ya mwisho ni kati ya mawazo yaliokuwa yakimtawala sana Alice. Tayari ilikuwa kama tabia kwa Baba Alice kufanya mapenzi na Alice. Baba alice alimchukulia Alice kama mke wake badala ya mtoto. Japokuwa wakati mwingine alikuwa akitumia nguvu mpaka kufanya mapenzi na Alice. Kadri siku zilivyokuwa zikienda na hali ya Alice ilianza kubadilika na kudhohofika. Ule mtaji aliokuwa nao wa samaki ulipukutika wote kutokana na Baba yake kuchukuwa zile pesa kinguvu na kila Baba Alice akiondoka asubuhi kurudi kwake ni usiku na lazima ahakikishe ametukana nyumba yote ndipo aingie ndani na hata akifika ndani asipokutana na chakula basi Alice atapigwa na vile vile kufanya naye mapenzi. Na huo ndio ulikuwa mchezo wa Baba Alice kila kukicha. Sasa akili ya Alice ikawa ni kutafuta ni jinsi gani ataweza kujinasua katika tatizo la njaa yeye na Baba yake.

    Kuna kipindi Alice alikuwa akikata tamaa kabisa kimaisha kwanza kutokana na elimu yake ndogo aliyoishia ya darasa la saba, ambayo aliona ni vigumu kwa yeye kupata kazi. Kuvaa kwake ilikuwa ni mabaki ya kanga ambayo Mama yake alikuwa akiyatumia pindi alipokuwa akipika samaki. Moyo wa Alice ulikuwa tayari ni mkakamavu kwa mateso na manyanyaso ambayo alikuwa akikutana nayo kila kukicha kutoka kwa Baba yake.

    Maisha ya kiukatili yaliokuwa tayari yameukomaza ubongo wa alice yalimuamuru moja kwa moja kuwa mtoto wa mtaani. Alice sasa alikuwa ni mtu aliyedhamiria kuondoka pale tena kutoroka bila ya Baba yake kujua wala majirani. Usiku ndio ulikuwa muda muafaka wa yeye kuondoka. Siku nzima Alice alivumilia kushinda na njaa huku akitamani sana usiku ufike aweze kuondoka pale kwao nakutokomea kusikojulikana. Ndani ya saa mbili za usiku Alice alikuwa tayari kishaiacha nyumba yao aliokuwa akiishi yeye na Baba yake na wapangaji. Hasira kali zilizochanganyika na mateso aliyokuwa akiyapata kutoka kwa Baba yake yalimfanya hata kutokuandika ujumbe wowote juu ya kumjulisha Baba yake kama ameondoka au la! Alice aliumia sana moyo kitendo cha kumuacha Baba yake peke yake kwani alijua kuwa Baba yake kamwe hawezi kuishi peke yake bila msaada wowote.

    “..nani sasa atampikia..?, nani atamfulia..?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni kati ya vitu alivyokuwa akijiuliza Alice mara mbilimbili kichwani mwake bila ya jibu lolote.

    Alice hakupajua vizuri mjini zaidi ya kuishia feri tena alikuwa akija kununua samaki na dagaa kwa ajili ya kukaanga na kuuza. Alizurura mjini usiku kutwa huku akipishana na magari yaliokuwa yakimuwashia taa kali. Njaa sasa ikawa imeanza kumzidia alice. Hakujua ni wapi atapata chakula, mfukoni hakuwa na hata senti ya kununua chochote na hata kama angekuwa na hela kwa maeneo ya katikati ya mji aliokuwepo hakukuwa na duka hata moja lililokuwa wazi kwa muda ule. Tumbo lake lilikuwa linakoroma na kumkumbusha kuwa toka asubuhi hajaingiza chochote. Alice alibaki kutoa machozi huku akiliangalia lile furushi la nguo alizobeba nakuona kama linazidi kumlete uzito hivyo kuamua kulitupa na kuendelea na safari yake kwa masikitiko makubwa. Akiwa njiani huku katika dimbwi la mawazo Alice alijikuta akipuliziwa moshi mzito wa sigara. Alihema juu juu kisha akatoa macho kuangaza huku na kule lakini bado hakuambulia kujua moshi huo unatokea upande gani. Ile hali ya usingizi na njaa ambayo tayari ilikuwa ikimnyemelewa ikaanza kuisha taratibu kutokana na woga ambayo tayari ulishatawala katika halmashauri ya kichwa chake. Na sasa Alice akanyanyua mguu na kuanza kuondoka katika lile eneo.

    “..unafanya nini hapo wewe..?”

    Kinadada takribani watatu waliovalia vinguo vifupi huku eneo lote la juu wakiachia nusu ya matiti yao wazi wakawa tayari wameshamzunguka Alice. Mapigo ya moyo ya Alice sasa yakawa yamebadilisha uelekeo na kuanza kwenda kwa kasi huku akijihisi kuishiwa nguvu katika viungo vyake vya mwili. Mdomo wake ulibaki kumtetemeka huku akijihisi jasho kumtoka katika kila pembe za mwili wake.

    “..nipo na na naa..”

    Akiwa katika hali ya kujing’atang’ata ghafla alishangaa vicheko vikirindima kumzunguka kutoka katika lile eneo.

    “..bwana tuondokeni katatupotezea muda hapa.., embu tukachangamkie pesa sisi..?”

    Aliropoka mmoja wa wale madada hali iliyomfanya Alice asielewe wana maana gani waliposema wakatafute pesa.

    “..inamaana pesa kumbe inatafutwa hadi usiku..?”

    Alice alijiuliza kimoyo moyo huku akitamani kuwauliza wale wadada lakini hali ya uwoga aliokuwa nao ilimfanya kukaa kimya huku akiendelea kuwatolea macho. Katika maisha yake yote Alice hakuwa anajua kuwa pesa inatafutwa hadi usiku tena na kina dada zaidi ya kuamini wanaotafuta pesa usiku ni walinzi peke yao. Mmoja kati ya wale wadada alionesha kumuonea sana huruma Alice. Kila wenzake wakitaka kuondoka yeye alionesha kuweka mgomo na kubaki na Alice katika lile eneo.

    “..nyie nendeni nitawakuta, si mtakuwepo hapo mtaa wa ohio..? tangulieni nakuja..”

    Alice alishangaa yule dada kuwaambia wenzake vile kisha wakaondoka na kuwaacha wawili tu usiku ule.

    “..embu niambie binti unaitwa nani..?”

    “..mimi..?”

    Alice bado alikuwa muoga na mtu wa kutokujiamini. Woga uliokuwa umeendelea kumwandama ulisababisha hata kupoteza ujasiri japokuwa walikuwa wamebaki wawili tu.

    “..ndio naongea na wewe binti, kwani si tupo wawili tu jamani..?”

    “anhaa, mimi naitwa Alice..”

    “..Alice mbona usiku wote upo peke yako..?, na kwa jinsi ulivyovaa unaonesha una matatizo kwani nyumbani wapi jamani..?”

     “..hapana dada wala sina hata tatizo..”

    Alice alimjibu yule dada huku akijiuma uma kwa kushika vidole vyake huku akivikunja kunja.





    ********



    Angel Mahipsi kama jina lilivyozoeleka kwa baadhi ya marafiki zake haswa anaofanya nao kazi. Weupe aliokuwanao na hata maumbile mazuri ya mwili wake ni kati ya vitu ambavyo vilikuwa kivutio kikubwa sana kwa wanaume haswa wale wenye tamaa za kimapenzi. Angel alijipenda sana na mara nyingi alipenda vitu vizuri, kuvaa vizuri, kula vizuri na hata kuishi maisha mazuri japokuwa alitoka kwao Kigoma na kuja Dar kutafuta maisha nakuwaacha wazazi wake huko kigoma wakiwa katika hali mbaya ya kimaisha ya kutegemea milo miwili kwa siku. Tangu alipoingia Jiji la Dar akitokea kwao Kigoma Angel hakuwa na ndugu wakuweza kusaidiana naye katika maisha. Alipitia maisha ya mtaani mpaka alipokuja kufanikiwa kufanya kazi za ndani kwa mzee wa kitajiri Mzee Khalfani. Hata hivyo Angel hakudumu sana kufanya kazi kwa mzee Khalfani kutokana na kudharaulika na kufanyishwa kazi nyingi na familia ya Mzee Khalfani hivyo miezi mitatu ilimtosha kabisa kuingiza kipato alichokihitaji nakuamua kuachana na kazi za kufanya kazi za ndani kwa mzee Khalfani nakujitafutia maisha yake. Kwa mara ya kwanza Angel alifanikiwa kujinunulia godoro, kitanda na vyombo vya ndani viwili vitatu. Chumba alichokipata hakikuwa hata na umeme kutokana na hela aliyolipa haikukidhi kupatiwa chumba chenye umeme. Maisha yalikuwa yakibadilika kadri siku zilivyokuwa zinaenda. Kile kiasi cha hela ambacho alikivuna kwa mzee Khalfani alipokuwa akifanya kazi za ndani kilizidi kupungua mpaka nakubakiwa kiasi cha shilingi elfu thelathini tu. Wazo la kuanza kuuza matunda kwa kuweka kwenye beseni na kutembeza mtaani lilikuwa sahihi sana kwa Angel. Alihangaika kila kukicha kutanga na jua huku akitembeza matunda mbalimbali zikiwemo ndizi, machungwa, maembe, matango na mananasi maeneo ya mjini. Kuna waliokuwa wakiidharau biashara yake kutokana na uzuri aliokuwa nao na biashara aliokuwa akiifanya. Wengi wa wateja wake walikuwa wakimshauri aachane nayo lakini ilikuwa ni kama kumtukana Angel tena matusi ya nguoni kwa kuwa siri kubwa aliijua moyoni mwake juu ya biashara hiyo iliokuwa ikimuingizia kipato kiduchu kwa siku. Kutoka kwake asubuhi na kurudi jioni huku akiwa amechoka kulimfanya ajikaze na kuamini ipo siku matatizo yake yataisha. Ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuja kuwa Mwanamke mashuhuri Tanzania na Duniani kwa ujumla na mwenye kuwakomboa kina Mama wenye matatizo mbali mbali kwa kuwashauri na hata kuwawezesha kwa vipato. Lakini sasa ndoto hiyo ilikuwa nzito kwa angel kufikia malengo yake, iliyeyuka mithili ya barafu linapokutana na maji ya moto. Kadri siku zilivyokuwa zinakwenda ndipo na Angel alikuwa akikata tamaa kila kukicha nakuamua sasa kuachana rasmi na biashara ya kuuza matunda mtaani iliokuwa imeshamchosha haswa kwa kipato kidogo cha shilingi elfu tatu kwa siku alichokuwa akikiingiza. Biashara ya kuuza mwili ndio ilikuwa jibu sahihi kwa Angel kubadilisha kutoka kuuza matunda. Hakujua kunywa pombe wala kuvuta sigara lakini sasa Angel akawa ni msichana mmoja wapo anayejua kupuliza sigara na hata kunywa bia zaidi ya sita na wala asilewe. Kulala na wanaume zaidi ya watano kwa siku kwake ilikuwa ni jambo la kawaida na wala halikumuumiza kutokana ana mazoea ambayo tayari yalikuwa yamejijenga katika halmashauri ya kichwa chake. Angel hakuwa na mahusiano mazuri na majirani wake alipopangisha kwani hakutaka urafiki kabisa na majirani anaoishi nao na pia alikuwa msiri sana katika mambo yake haswa katika biashara hii ya kujiuza mwili ambayo hakukuwa na jirani yeyote aliokuwa akijua zaidi ya kila mmoja kumuhisi kwa kitendo cha yeye kutoka usiku na kurejea alfajiri. Mawindo yake yalikuwa ni Ohio, Kinondoni na Magomeni kwa Macheni japo hakupendelea sana kwenda kwenye makasino kwa sababu aliamini kuwa katika makasino wazungu wako wengi nayeye elimu yake ya darasa la saba ilimfanya asijue kabisa lugha ya kiingeeza ambayo huzungumzwa na wazungu wengi wa kwenye makasino. Marafiki aliokuwa akipenda kuongozana nao katika Biashara hiyo ya kujiuza mwili walikuwa ni wawili tu, Miriam na Josephina na sasa walimuacha Angel akiwa na Alice pale barabarani huku wao wakienda kujitafutia wanaume kwa upande mwingine.

    “..Sasa unawaona marafiki zangu wameniacha..?, ila nipo pamoja na wewe mdogo wangu Alice..”

    “sawa, Dada..”

    Angel aliongea na Alice kwa sauti ya chini chini huku akionesha dhahiri kutaka kumsaidia Alice kwa kumchukuwa na kuishi naye. Ile dhahama anayokutana nayo kila kukicha akirudi nyumbani akiwa amechoka na hata ile hali ya kujipikia nyumbani na kufua nguo ilikuwa imemchosha sana Angel. Na sasa aliona amepata mfumbuzi baada ya kukutana na Alice mjini. Hakuwa akimjua vizuri lakini tayari Angel alijiwekea moyoni kwamba Angel atakuwa msaidizi katika kumsaidia kazi ndogondogo za nyumbani kwake.

    “..Alice..?”

    “..Abee..”

    “..kwani nyumbani kwenu wapi..? na Baba yako na Mama wako wapi…?”

    Alice aliposikia anaulizwa tu wazazi wake alishindwa kujizuia nakuachia mchozi huku makamasi yakiwa karibu katika pua zake. Alikohoa na mishipa ya pembeni taratibu ilianza kujikusanya na kumvimba kwa haisra kali. Siri kubwa ilikuwa bado imebaki moyoni kwa Alice na alihaidi kutokumwambia mtu yeyote juu ya wazazi wake.

    “..mhh.., Mama na Baba wanaishi Bukoba..”

    “..kwani wewe ni Muhaya..?”

    “..ndio Dada..”

    Alice alijitahidi kudangaya tena kwa kujiuma uma huku mkono wake mmoja akiutumia kufuta machozi ambayo tayari yalikuwa yameuzunguka uso wake na mengine yakilowesha kifua chake. Angel aliamua kughairi kufanya kazi yake ya kujiuza mwili kwa siku hiyo. Wateja watatu aliokuwa amewapata walimtosha kujipatia kiasi kidogo cha pesa kwa siku hiyo.

    Alimchukuwa Alice kisha wakakodi bajaji iliowasaidia kuwapelekea mpaka nyumbani alipokuwa akiishi angel. Ukarimu aliounesha Angel kwa Alice ilikuwa ni faraja kubwa nakuona sasa amepata mkombozi. Alijitahidi kulificha tabasamu lake ambalo lilizungukwa kwa machozi karibu uso mzima. Safari ya kutokea Ohio alipokuwa akijiuza Angel ilianza na sasa alikuwa na Alice ambaye alidhamiria kumchukuwa kwa lengo la kumpekela mpaka kwake kisha kumsaidia kazi ndogo ndogo zinazokuwa zikimkabili. Iliwachukuwa mwendo wa nusu saa kwa kutumia bajaji mpaka kulifikia eneo la tabata bima ambapo Angel alikuwa amepanga. Angel alimlipa dereva bajaji hela yake kisha akamshika mkono Alice nakuongozana naye mpaka ndani. Alifungua mlango na kutafuta kiberiti ambapo aliwasha mshumaa na kuingia mpaka ndani.

    “..Jisikie uko nyumbani mdogo wangu Alice..”

    “..ahsante sana Dada..”

    “..hapa ndipo ninapoishi na tena naishi peke yangu mdogo wangu..”

    Alice alitoa macho karibu kila pande ya chumba. Mwanga wa mshumaa haukutosha kujua ukubwa wa chumba kile zaidi ya kushuhudia kitanda kikubwa cha tano kwa sita na kochi mbili za kawaida na beseni lililojaa vyombo vya kupikia.

    “..kwakuwa ni usiku sana sasa hivi nakuomba asubuhi ikifika ndio ukaoge mdogo wangu ila tulale tu kwa sasa hivi..”

    “..sawa Dada nimekuelewa..”

    Kwa mara ya kwanza Alice alijihisi mtu tofauti kwa kulala katika makazi mengine. Pia ile hali ya kupigiwa makelele na Baba yake na kisha kupigwa na hata kubakwa sasa ilikuwa ndio kikomo kwake. Alijihisi kama barafu ya baridi inapenya ndani ya kifua chake. Aliona ni kama bahati imetoka mbinguni ya yeye kukutanishwa na Angel. Moyoni aliahidi kumthamini sana Angel na kufanya kazi kwa bidii kila atakavyohitaji. Aliingia hivyo hivyo na kanga zake kitandani zilizokuwa zinanuka moshi wa na harufu ya samaki aliokuwa akiwakaanga kipindi cha nyuma, mawazo mengi yalizunguka kichwani mwake na kumkoseha usingizi usiku kutwa, mipangilio ilimzidia kichwani mwake.

    “..Alice mdogo wangu..”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “..Abee Dada..?”

    “…Yaani bado huko macho mpaka sasa..?, embu tulale nini unafikiria hivyo..?”

    Angel alimuuliza Alice kwa sauti ya chini chini nay a kumbembeleza baada ya kwenda kuuzima ule mshumaaa na kumshuhudia Alice akiwa katika hali ya mawazo.

    “..nitalala tu Dada wala usihofu..”

    Alice alimjibu Angel na kisha akajigeuza upande wa pili na kufumba macho tayari kwa kulala. Asubuhi na mapema Alice alikuwa mtu wa kwanza kuamka. Alibaki kitandani akimtolea macho Angel ambaye bado alikuwa katika usingizi mkali. Mkojo ulimbana sana Alice lakini alijikaza na kuubana huku akishindwa jinsi ya kumuamsha Angel japokuwa kulikuwa kumeshakucha. Muda wa dakika arobaini bado ulikuwa kama masaa matatu kwa Alice ambaye sasa mkojo alihisi unamvuja kupitia nguo yake ya ndani. Kule kujibana sasa kukawa kumemshinda. Alijikaza akasogea mpaka kwenye kochi pembeni yake.

    “…Dada..?? Dada..?”

    Alice aliita kwa sauti ya uoga uoga huku akiwa hajiamini bila majibu yeyote kwani ndio kwanza Angel alijigeuza na kuendelea kuuchapa usingizi. Uzalendo ukamshinda baada ya kuona Angel hashtuki wala kuamka. Alichokifanya alifungua mlango taratibu huku akinyata nakutoka nje.

    “..Samahani..!! , eti uani wapi..?”

    Sasa Alice alikuwa amekutana uso kwa uso na jirani mmojawapo. Yule jirani alimsikiliza na kumwangalia Alice kwa jicho la dharau kisha akamfyoza na kuendelea na shughuli zake. Alice alijiskia mwenye bahati mbaya na watu lakini alijikaza moyo na kuendelea kuangaza kila pande hadi alipofanikiwa kuuona mlango wa choo. Kitendo cha yeye kuongoza mpaka chooni na kisha kuvua nguo haraka haraka. Ule mkojo uliokuwa unamsumbua sasa ukawa haupo tena kwake kwani ulishaijaza nguo yake ya ndani na sasa ilikuwa imelowa tepetepe. Alice aliogopa sana kutoka chooni akiwa amelowa katika nguo yake ya ndani, woga ulimtanda na hakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kukaa chooni huku akitafakari ni jinsi gani ataweza kurudi chumbani akiwa amelowa nguo yake ya ndani tepe tepe?..

    “..Alice.?, Alice mdogo wangu upo chooni..?”

    Sauti ya Angel tayari ilikuwa nje ya choo ikimtafuta Alice na sasa alikuwa nje ya kile choo akigonga ili Alice atoke..

    Woga ulikuwa bado umemtanda Alice. Mwili wote ulikuwa ukiendelea kumtetemeka, mdomo wake ulikuwa ukiumana huku mapigo yake ya moyo yakianza safari ya kwenda kasi mithili ya gari liliopo katika mteremko mkali. Aliiangalia ile nguo yake ya ndani kwa hasira huku akijuta kitendo cha yeye kuchelewa kuwahi chooni.

    “..Abee Dada..!! , nipo huku chooni..”

    “..Aanhaa..!! , nilishtuka mdogo wangu nilidhani umeondoka..”

    “hapana Dada..!”

    “haya endelea tu.., mimi nipo chumbani nakusubiri..”

    “..sawa Dada”

    Alice aliitika kwa sauti ya chini naya kunyenyekea. Aliendelea kuishikilia ile nguo yake ya ndani vyema na kuikamua kisha akahakikisha kojo lote limekauka vilivyo. Dakika tano zilimtosha kabisa Alice kuikausha kwa kuikamua ile nguo yake ya ndani na kisha kuivaa. Aliivaa hivyo hivyo japokuwa ilikuwa bado ina unyevu nyevu na kisha kurudi chumbani alipomuacha Angel.

    “Dada nimeshamaliza..?”

    Alice alimwambia Angel kwa kuogopa ogopa kutokana nay eye kutokumfahamu vizuri. Alijitahidi kukaa katika kochi japokuwa bado alikuwa hajakakuka vizuri katika nguo yake ya ndani. Baada ya muda Alice alielekea na Angel sokoni ambapo walinunua vitu vidogodogo vya kupika na vingine wakavihifadhi kama akiba ya baadaye. Alice alifurahia maisha yale, ushamba bado ulikuwa umemtawala. Japokuwa alipewa nguo mbili tatu na Angel lakini yeye bado aling’ang’ana kuvaa kanga zake alizokuja nazo. Hali ya kutokwa damu ya hedhi hakuwa anajua zaidi ya kutetemeka nakuhofia huenda anafanyiwa vitendo vibaya usiku anapokuwa amelala. Alinyemelea muda ambao Angel anaenda kwenye mawindo yake basi yeye akatumia muda huo huo kuvikata vipande vidogo vidogo vya kanga yake ili viwe vinamsaidia kukinga damu iliyokuwa ikimtoka kila kipindi cha hedhi kinapomfika. Takribani miezi miwili Alice hakuwa akijua kama kuna kitu kinaitwa pedi. Kutokana na biashara ya Angel ya kujiuza mwili kila siku hivyo Angel alikuwa akitumia vidonge vya uzazi na hata wakati mwingine alikuwa akichomwa sindano za kuzuia bleed. Maisha ya Angel na Alice yalikuwa ni mazuri sana, Alice alihakikisha anafanya kazi vizuri ili kumfurahisha Angel. Kwa upande wa Angel Alijitahidi kumchukulia kama ndugu yake wa damu. Alimfanya Alice apendeze na alihakikisha anampa mahitaji karibu yote aliyokuwa akiyataka. Weupe kidogo aliokuwa nao Alice akiongozana na Angel lazima utasema mdogo wake wa damu. Kama kawaida ya Angel kutokuwa karibu na majirani zake ndio tabia ikajijenga mpaka kwa alice. Alice alijifunza mengi kutoka kwa Angel. Hakutaka hata kuwa karibu na majirani zaidi ya kuwaangalia tu na kuwapita tena bila hata salamu. Biashara ya kujiuza mwili aliokuwa akiendelea nayo Angel sasa ilizidi kumtajirisha. Alipata pesa nyingi zaidi kupitia biashara hiyo. Kamwe aliapa kutokubali Alice ajihusishe na biashara hiyo hivyo alikuwa mkali sana na kumuonya mara kwa mara ajitahidi kuepukana na vijana walaghai pindi yeye anapotoka usiku na kwenda mawindoni. Karibu kila mwisho wa wiki Angel alikuwa akiupumzisha mwili wake kuufanya kazi na wanaume hivyo alijijengea mazingira ya kutoka na Alice sehemu mbali mbali kama vile kwenye kumbi za starehe na hata maonesho makubwa makubwa ili mradi Alice ajisikie vizuri na ajione mtu tofauti kidogo. Lile eneo alikokuwa akiishi Angel na Alice ambalo hata halikuwa na umeme wakaamua kulihama na kutafuta nyumba kubwa yenye vyumba viwili na sebule. Alice alijitahidi sana kusahau maisha ya nyuma japokuwa picha ya Mama yake lilikuwa ilkimjia sana ndotoni na akiamka huwa anatoa sana machozi. Hasira iliyoambatana na dukuduku kubwa aliyokuwa ameiweka rohoni kwa muda mrefu juu ya Baba yake bado ilikuwa ikimsumbua mara kwa mara pindi anapofikiria kitendo cha yeye kubakwa na Baba yake mzazi. Bado ilikuwa ni siri kubwa moyoni mwake na hata Angel hakuwa akijua chochote zaidi ya kuamini kuwa Baba na Mama Alice wako hai na wanaishi Bukoba.





    *******



    Mabadiliko yalianza taratibu kwa Angel. Uchovu wa mara kwa mara ulikuwa umeanza kupenya katika mwili wake hali iliyomsababishia homa za hapa na pale. Alice ndiye alikuwa mtu wa karibu kwa Angel. Alihakikisha anamjali kwa kumhudumia kwa hali na mali. Kadri siku zilivyokuwa zikisonga na hali ya Angel nayo ikawa inabadilka kila kukicha na kuzorota. Mwili wake ulianza kubabuka na vipele vyeusi vodogo vidogo vilianza kuchukuwa nafasi yake. Wiki mbili zilimpita hivi hivi Angel akiwa kitandani bila hata ya rafiki yake mmojawapo kati ya wanaofanya nao biashara ya kujiuza mwili kutokea. Ni Alice peke yake aliokuwa akijua Angel anavyojisikia. Sasa ilifika kipindi Angel alikuwa akichagua vyakula vya kula. Akipewa wali anatapika na kukohoa sana. Vyakula alivyohitaji ni wali ule wa kusaga kama uji uji na mtori.

    “..Dada Angel jitahidi basi hata umalizie hiki kijiko cha mwisho..”

    “..Hapana mdogo wangu Alice inatosha.., peleka tu jikoni nitakula tena baadaye..!!”

    Alice alijitahidi sana kumbembeleaza Angel lakini haikuwezekana zaidi ya kutapikiwa kile chakula na hata kukimwaga. Mwezi mzima Angel alikuwa bado yupo hoi kitandani. Hakutaka kupelekwa hata hospitali japokuwa na miguu yake ilikuwa imemvimba sana na mwili kukosa nguvu. Ule weupe wake uliokuwa ukifananishwa na Alice pamoja na mahipsi ambayo yalikuwa yakigombaniwa sana na wanaume pindi anapokuwa mawindoni katika kujiuza mwili sasa ukawa umebadilika. Hakuwa Angel mahipsi tena bali aliukuwa ni Angel mchina kwa kuwa yale mahipsi aliokuwa nayo yote yalishuka mpaka magotini. Rangi ya ngozi il nyeupe aliokuwa nayo sasa ilikuwa ni mchanganyiko wa nyeusi na kijani. Sura ya chanjo chanjo mithili ya wamakonde ndio ilikuwa imemvaa Angel. Mwili wote ulimwisha na ulikuwa huwezi kumwangalia mara mbili mbili kwa jisi mdomo ulivyokuwa ukimtoka maudenda tena yale mazito. Siri kubwa alikuwa nayo Angel juu ya ugonjwa aliokuwa nao na ndio maana hata hakutaka kupelekwa hospitali, sasa akawa ni mtu aliyekata tamaa ya kuishi. Siri kubwa aliyojijengea rohoni mpaka moyoni mwake sasa ikawa imedumu kwa wiki tatu tu baada ya kuona hali tete. Alice akawa ameshaambiwa kila kitu na kuujua ukweli.

    “..kumbe ukimwi hatari hivi..?”

    Alice alijisemea kimoyo moyo huku akiendelea kumnywesha Angel uji. Alikuwa akishuhudia kwenye Televisheni na magazeti juu ya waathirika wa ugonjwa wa ukimwi na sasa alishuhudia moja kwa moja. Mpaka miezi inafika mitatu bado Alice hakuweza kupata usingizi wenyewe zaidi ya kuwa karibu na Angel masaa yote na kama akipitiwa na usingizi basi ni nusu saa au lisaa tu anashtuka nakuendelea kumuuguza. Kuugua kwa angel kwa muda mrefu kulichochea mawazo mengi sana kwa Alice nayeye kusababisha kupungua lakini kupungua huko kwa Alice kulitokana na kuwa na mawazo mengi sana juu ya Angel. Aliona sasa ndoto zake zinaenda kukatika kwa mara ya pili baada ya ile ya kwanza alipokuwa akiishi na Baba yake na kisha akaambuliwa kubakwa. Dawa za miti shamba kutoka Kigoma alizokuwa akitumia Angel tangu alipotoka Kigoma ambazo zilikuwa zikimpa sana nguvu pindi anapoumwa sana haswa haswa viungo au anapokuwa hoi sasa hazikuweza kusaidia chochote zaidi ya kumfanya ajisaidie haja zote kitandani. Kazi kubwa ya Alice ilikuwa ni kuhakikisha Dada yake Angel anakuwa msafi muda wote kwa kumfulia nguo zake pindi anapojisaidia na pia kumvalisha nguo nyingine. Mwili wake wote Angel ulipukutika na sasa alikuwa akingojea siku yake ifike. Akiba ya pesa ambayo Angel alikuwa amejiwekea ndani sasa ikawa imeisha yote kutokana na kununua mahitaji madogo madogo. Matatizo yakahamia kwa Alice ni jinsi gani atatafuta pesa ya kuweza kumtibia Angel. Alice alijitahidi kukopa hapa na pale baadhi ya maduka ambayo Angel aliuwa akipendelea kununua vitu. Madeni yalizidi nakuamua kubadilisha hadi njia napo kila kona kukawa ni madeni tu. Kuna kipindi alidiriki kushinda na njaa mpaka kesho yake yeye na Angel. Hakukuwa na dalili yoyote kuashiria Angel atapona wala kupata unafuu zaidi ya kuendelea kuumwa na kukohoa sana tena kile kifua kikali na kikavu. Mwezi wa nne sasa ulikuwa ukielekea kukatika ambapo hali ya Angel ilionesha kufikia ukingoni kutokana na kubanwa sana na pumzi. Usiku huo Alice hakupata kabisa usingizi kutokana na Angel kushindwa kuongea kabisa. Kile kikohozi kikavu ambacho Alice alikuwa akikisikia kila inapofika alfajiri sasa kikawa kimekatika. Mwanzoni Alice alijua ni usingizi utakuwa umempitia lakini jibu lilikuwa pale pale kwamba Angel alikuwa ameshatangulia mbele ya haki kifupi ameshafariki..

    “..Angel…??, Dada angel…??.”

    Alice aliita kwa sauti ya juu huku akimtingisha kwa kutumia nguvu kidogo, lakini Angel hakushtuka wala kutoa macho. Alice alikisogeza kichwa chake mpaka kifuani mwa Angel lakini bado hakuambulia chochote kusikia zaidi ya kuhisi masikio yake yamezibwa. Nguvu zilimelegea Alice akajikuta akidondoka na kupoteza fahamu papo hapo..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Tatizo la kutokuweza kupata mtoto liliendelea sana kumsumbua John Mapunda. Pesa nyingi alizokuwa akizipata kupitia kazi yake ya kusimamia shughuli za urembo hazikuweza kumpa furaha ya nyumba kabisa. Toka alipofunga ndoa na mkewe Janet miaka mitatu iliyopita alizidi kukosa furaha ndani ya nyumba kutokana tatizo la mkewe kutokushika ujauzito. Mwanzoni alijihisi pengine tatizo litakuwa upande wake lakini haikuwa hivyo. Kila hospitali aliyokuwa akiongozana pamoja na mkwewe kujua nani ana tatizo jibu lilikuja pale pale kuwa mkewe John, Janet ni mgumba na kamwe hawezi kupata mtoto. Furaha ya nyumba ikaanza kubadilika siku baada ya siku ndani ya miaka mitatu. John akawa ni mtu wa kulewa na kutembea na wasichana ovyo. Maisha yake yote sasa akawa ameyahamishia kwenye wanawake. Mwanzoni alifanya kama siri kutembea na wanawake tofauti lakini mwishowe alijionesha dhahiri kutembea na kila mwanamke amtakaye mbele ya mkewe. Hali ile ya John kubadilika kulimuumiza sana mkewe janet. Janet alijihisi ni mtu mkosaji duniani, alijutia ndoa waliyofungishwa kanisani miaka mitatu iliyopita. Uzuri aliokuwa nao Janet na unyenyekevu ilikuwa jibu tosha kwa aliyemuona. Kuimba kwaya kanisani ndio kazi aliyokuwa ameichagua katika maisha yake ya kumtolea Mungu kupitia kipaji alichokuwa nacho. Janet hakuwa na kazi ya maana zaidi ya kujiendesha kwa biashara za mikononi ambapo alikuwa akikopesha kinamama wenzake nguo za watoto na kulipwa baada ya wiki mbili hadi tatu. Kuimba kwake kwaya kulimfanya ajiepushe na mengi japo siri kubwa alimganda moyoni kuwa hana uwezo wa kushika ujauzito. Janet alifanya kila njia kuhakikisha anamuweka mumewe John katika hali ya kutokujisikia tofauti kwa kutopata watoto na akiamini kuwa ipo siku Mungu atawashushia Baraka na watapata mtoto wa maisha, Alihangaika sana kwenda kwenye semina mbali mbali za maombezi na kuombewa sana lakini bado hakuwa na dalili yeyote ya kuondoka ugumba wake. Siku, wiki, Miezi, miaka ilizidi kukatika bila mafanikio yeyote kwa Janet. Kipindi hiki sasa John ndio akaamua kuzidisha ule umalaya aliokuwa akiifanya mwanzo. Kwake kutembea na wanawake hata watatu kwa siku na kuwahonga lilikuwa ni jambo dogo sana. Ushauri aliokuwa akipata kutoka kwa baadhi ya marafiki zake juu ya tabia yake hiyo alikuwa akiupuuzia na hata mwingine kuuweka kichwani japokuwa alikuwa mzito sana katika kuufanyia kazi. Taratibu John akaanza kubadilika. Sasa akawa anatembea na mwanamke mmoja tu. Nusu ya mshahara wake akawa anagawana na mwanamke huyo. Hakuwa mwingine bali alikuwa ni Angel. John alijivunia sana kumpata Angel katika maisha yake na akiamini kuwa atamfanya nyumba ndogo na kumuahidi kuwa endapo atamzailia mtoto basi nusu ya mali zake zitakuwa mikononi mwa Angel . John alifanya siri kubwa kutembea na Angel na hata makutano yao mara nyingi yalikuwa ni hotel maarufu pale kariakoo ya Royal Image mtaa wa Livingsotne na hakutaka kabisa kwenda kwa Angel kwani aliamini angefuatiliwa na mkewe hivyo kungemletea matatizo Angel na mkewe Janet. Angel ambaye alizoea kutembea na wanaume wengi sasa akawa ameachana nao baada ya kumpata John na kumpa kila alichokitaka, na hata pesa za kuhama alipokuwa akikaa zamani ni John pekee ndio alizozitoa. Angel hakupenda kabisa kumshirikisha wala kumjulisha mdogo wake Alice juu ya kutembea na john na ahadi walizoahidiana. Hata kipindi walichokuwa wakitoka wote katika matembezi ya pamoja Alice alikuwa akimuona tu John akiwa karibu na Angel lakini hakujua ndani yao kuna kitu gani. Ilimchukuwa wiki chache tu Angel kunasa mimba ya John na hata John mwenyewe alipopewa taarifa juu ya kushika hiyo mimba hakuamini mpaka alipokutana naye hotelini wanapokutana na kumkimbiza hospitali nakugundua kuwa kweli Angel ni mjamzito wa wiki chache. Furaha ya ajabu ilimtanda John, siri kubwa alikuwa nayo na hakutaka hata rafiki wala mkewe Janet wajue mpaka Angel atakapojifungua. Kadri siku zilivyokuwa zinasonga ghafla mawasiliano ya John na Angel yakakatika ghafla. Na ni Angel pekee ndio aliyoyavunja mahusiano hayo kwa haraka baada ya hali kumzidia juu ya ugonjwa wa ukimwi uliokuwa ukimsumbua. Hakutaka kuiona hata imu ya John ikiita kwani aliamini angekosa cha kujieleza kutokana na kuwa hoi kitandani. Kutokana na kuendelea kukaa kimya kukamuharibu kabisa John kisaikolojia, ule utendaji wa kazi ukaanza kupungua kazini kwao. Siku zote alijiona kama msaliti asiye na bahati hapa duniani. John hakujua aanzie wapi kumtafuta kipenzi chake Angel. Alitembea usiku kumbi zote walizokuwa wakitembea wote bila kupata jibu haswa alipokuwa akiishi. Wazo likamjia kumtafuta rafiki yake wazamani sana na Angel ambaye alijulikana kwa jina la Miriamu. Alifanikiwa kuonana na Miriam kwenye mawindo yake usiku wa manane..

    “..Miriam bora nimekuona mambo rafiki..??”

    “..safi tu..!!, niambie sasa.., leo shosti wako hayupo twende wote tukalale basi..??”

    “..hapana Miriam..!!, yani nipo hapa kujua tu anapoishi huyo Angel..??, na kuhusu kulala na wewe haitawezekana ila nitakupa hela yako ya siku unayoingiza hapa..!!”

    “..daahh..!!, sijui nianzie wapi kukueleza John, yaan nina muda mrefu sijui hata Angel yupo wapi na anafanya kazi gani kwa sasa kwani tangu kipindi kile unakuja kumchukuwa sijamuona tena na wala kwake nimepasahau kidogo..”

    John alizidi kunyong’onyea baada ya kuambiwa maneno hayo na Miriam.., akilli ilizidi kumchanganya hadi akaiona dunia chungu.

    “..Lakini Miriam alipokuwa akiishi zamani si unapakumbuka..???”

    “..ndio napakumbuka lakini si sana..?”

    “..basi mie nipeleke tu mpaka hapo halafu nitajua cha kufanya..”

    John aliingia kwenye gari na Miriam kisha safari ikaanza mpaka nyumba ya zamani alipokuwa akikaa Angel napo alipofika tu hakufanikiwa kupata jibu sahihi sehemu alipoamia kutokana na Angel pamoja na mdogo wake Alice kuwa viburi na wenye dharau kwa majirani wenzake. Sasa Shati la John likawa kama limetoka kufuliwa linasubiri kuanikwa. Mwili wote ulikuwa umetapakaa majasho japokuwa alikuwa akiendesha gari tena ndani yake mlikuwa na kipupwe.

    ..hatua tatu mbele na moja nyuma ndizo zilikuwa zimemtawala John huku akiutoa mikono wake mmoja nakuurusha juu mithili ya mchungaji akiwa madhabahuni akihubuiri. Akiwa bado nje ya ile nyumba aliyekuwa akiishi Angel zamani mara Miriam naye akashuka ndani ya gari na kumfuata John alipo..

    “..mbona sikuelewi..??, umeambiwaje..?”

    “hapana Miriam.., ni kwamba hawajui alipohamia Angel, na mie lazima nimpate le oleo sirudi kwangu..”

    Miriam hakuwa na roho ya huruma toka aanze kujijihusisha na biashara hii ya ukahaba, kwake kumdai mwanaume hadharani au kumkunja shati na kutaka kumpiga kwa kudai pesa kwake ni jambo la kawaida sana. Na sasa Miriam alikuwa ameshamvumilia John vya kutosha, lile giza lililokuwa linazidi kufunika ndilo lillikuwa linampa hasira zaidi Miriam na sasa alitamani pesa zote zote na alitaka achukue pesa kwa John aliohadiwa na vile vile arudi tena mawindoni kutafuta zingine.

    “..haya mie msaada wangu umeishia hapa John.., nipe changu nitambae…??”

    Bado sura ya John ilikuwa katika majonzi na kuchanganyikiwa kwa kile ambacho hakiamini juu ya mpenzi wake Angel anapoishi. Hakutaka kusikia maneno tena ya Miriam kwakuwa dhahiri alishaonesha kuchukizwa na kuchelewesha hivyo John alichukuwa mkono wake wa kulia nakuingiza ndani ya suruali yake kisha akachomoa shilingi elfu thelathini nakumpatia Miriam. Miriam alizipokea kisha akajigeuza kwa jicho la dharau na kuondoka zake. Ilimchukuwa nusu saa nzima John kuzubaa pale na majirani wale waliokuwa wakiishi na Angel zamani kwa kuwabembeleza kisha akaingia ndani ya gari nakuondoka zake. Ramani ambayo alibembeleza baadhi ya majirani wakampa sasa ilikuwa imehamia kichwani mwa John. Hofu yake ilikuwa juu ya mimba ambayo alimwachia Angel na aliamini sasa inazidi kukuwa. Alijipa moyo hata kama Angel atakuwa amepata bwana mwingine lakini yupo tayari kumlipia mtoto gharama zote ili mradi damu yake aliyoitafuta kwa miaka mingi isipotee bure. Dakika ishirini ndani ya gari zilimtosha John kutoka lile eneo la Tabata bima alipokuwa akiishi Angel zamani mpaka eneo jipya. Nyumba kubwa yenye uzio wa matofali huku ikilembwa kwa geti lenye kila aina ya urembo ndilo lilizuzua macho ya John. Kabla hajashuka kwenye gari john aliangalia kwanza saa yake lakini tayari ilikuwa inamuonesha imetimia saa tano za usiku, haraka haraka akashuka nakuongoza mpaka eneo la geti nakuanza kugonga. Hakukuwa na mlinzi yeyote, John alitumia dakika tano nzima kugonga bila ya majibu yeyote, ile hali ya hofu na uwoga vikaanza kumtawala nakujihisi huenda amedanganywa na wale majirani ama yeye mwenyewe amekosea ramani. Lakini kwa upande mwingine akawa anajipa moyo kuwa huenda Angel wake na mdogo wake wamelala kwakuwa usiku umeshaingia na tena mida inayoyoma. Ile hali ya kugonga taratibu alioanza nayo John sasa ikawa imebadilika, alichukuwa kipande cha jiwe na kugonga kwa nguvu lakini bado haikusaidia chochote, na sasa akawa ameshikilia geti la upande wa kuingilia huku akisukuma kwa ndani napo bado geti halikufunguka. Akili ikamjia kwenda pembeni yake ambapo kulikuwa na bar ambayo bado ilikuwa haijafugwa watu wanakunywa, moja kwa moja akamfuata muhudumu mkuu pale.

    “..samahani Anti..??”

    “..bila samahani Kaka..”

    “..eti nilikuwa naulizia hawa wanaoishi nyumba hiyo hapo wapo..?”

    John aliuliza kwa sauti ya uwoga na kutokujiamnini na anachouliza huku akionesha kutetemeka mwili wote.

    “..unaulizia hao wadada weupe..??”

    John aliitikia kwa kichwa moja kwa moja na kwa haraka haraka.

    “..mida ya asubuhi nilimuona yule mdogo akipita kashikilia mfuko mkubwa kama ametoka sokoni asubuhi ila huyo mkubwa hajaonekana muda kidogo anakaribu mwezi, kwani umeshawagongea hapo getini kwao..??”

    “..ndio.., nimepiga hodi sana lakini hakuna majibu yeyote ya mtu kuitika ama kufungua..”

    “..basi watakuwa wamelala kajaribu kuwagongea tena..”

    Akili ya john sasa ikawa tofauti naya mwanzo lile wazo la kuambiwa akawagongee tena lilimkaa na sasa akili yake ikajazwa kuwa aende akaruke tu ukuta aingie ndani labda akigonga kwenye madirisha yao watasikia nakumfungulia. Ilimchukua dakika mbili yu tayari John akawa amesharuka ndani ya ukuta wa ndani anapioshi Angel. Woga wote ulimfutika ghafla huku akituna macho yake kuangaza hapa na pale mule ndani ya geti. Giza tororo lililokuwa limeanza kugubikwa ndani ya nyumba hii bado halikumsababishia John kuwa muoga, hakukuwa na taa ya aina yeyote iliowashwa, akili za John bado zillimtuma kuwa Angel na Alice watakuwa wamelala ndani, alichungulia chumba kimoja baada ya kingine kupitia madirishani napo haikusaidia chochote kujua kinachoendelea ndani. Wazo la kuvunja na kuufungua mlango ndilo lililomtawala halmashauri ya kichwa chake na sasa akawa ameshikilia kitasa ambacho hakikuwa kimefungwa kwa funguo yeyote. John alifanikiwa kuingia ndani na kuwasha taa za sebuleni na nje. Hatua kumi zilimtosha sana kufungua chumba kimoja bila kuambulia chochote na sasa akawa amebakiza chumba cha mwisho mbele ya macho yake. Akashusha pumzi yake kwanza aliokuwa akihema juu juu na kisha akatoa tabasamu kwa furaha huku akiamini atakuwa amemfanyia ‘surprise’ mpenzi wake Angel. Kitendo cha kufungua tu mlango na kuwasha taa mule chumbani hakuaamini alichokiona. Wote wawili, Alice na Angel walikuwa wapo chini na hawaongei na Angel alionesha kubadilika rangi ya mwili nakuwa mweusi sana huku matapishi na mikojo vikitapakaa pembeni na kuweka mfereji.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hofu kubwa iliendelea kujengeka mwilini mwa John, na sasa akawa anatetemeka huku akijihisi mkojo wa moto unatoka kupitia suruali yake alioukuwa amevaa. Midomo yake ilionesha kabisa kukosa ushirikiano kwani lipsi zote za juu na chini zilikuwa zikimtetemeka huku zikiyasukuma meno yake kugongana yenyewe mithili ya vyombo vikipitiwa na panya kabatini tena wale panya sugu wa usiku wanaokimbizana ovyo.

    “..Oooohh my God..!! Oohh my God..!! nini tena hiki...? Mkosi gani tena huu..??”

    John hakujua aanzie wapi na wala amalizie wapi kwani alitoa mkono wake nakuingiza mfukoni kwa dhumuni la kutoa simu apige polisi lakini alivyoitoa tu simu napo akachanganyikiwa nakusahau asijue ni mtu gani alikuwa akitaka kumpigia akairudisha tena mfukoni. Alirudi tena mpaka mlangoni hatua mbili tena akarudi pale pale walipokuwa wamelala Angel na Alice. Machozi ya kiutuuzima yakawa yameshatawala sura yake huku mashavu yakionesha dhahiri kupokea rundo la machozi na kuyatelezesha kupitia kidevuni mwake mpaka kwenye shati lake la ofisini. Akili aliokuwa nayo John ni kuinama mpaka chini na kwa kutumia kichwa chake moja kwa moja nakukiinamisha kifuani kwa Angel lakini mawasiliano kati ya kichwa cha John na kifua cha Angel hayakuwa sahihi kwani hakuweza kuusikia muungurumo wowote kuonesha kuwa mapigo ya moyo ya Angel yapo sawa.

    “…Angel my love..??, Angel..? Angel..? Angeeeeeeeeeel??? amka jamani, amka unione mumeo nimekuja..?? nimekuja kukufanyia ‘suprise’ mke wangu..! pliiz Angel japo fungua macho basi nikuone.. rudisha furaha yangu kipenzi..”

    John bado hakutaka kuamini kama Angel kapoteza maisha, alimtingisha sana bila kuambulia chochote na sasa alichokifanya aliinuka nakuvua shati lake nakubakiwa kifua wazi kilichojaa nywele za kiume sambamba nakulowana na jasho kisha akainamisha kichwa chake kwa angel kwa mara ya pili tena kusikilizia mapigo ya moyo napo hali ikawa kama ile ile ya mwanzo. Akili ikamganda mithili ya barafu linapokutana na ubaridi asijue nini cha kufanya ikabidi aamie pembeni yake alipokuwa amelala Alice nakuanzaa kumuasha kwa kumtikisa ama alivyofanya kwa Angel..

    “.. Alice..?, Alice…??? amkeni jamani nini tatizo..??”

    John alijihisi kuchanganyikiwa zaidi kwa kutikujibiwa na mtu yeyote wala kuonesha mshtuko wa aina yeyote, alichokifanya hapo alilichukuwa lile shati lake aliokuwa amelivua hapo mwanzo nakuanza kuwa pepea kwa nguvu zote mithili ya feni. Ndani ya dakika takribani tano John akashangaa Alice akijikunja kunja mithili ya mtu anayesumbuliwa na ndoto usingizini, akazidisha zaidi kupuliza kwa kutumia lile shati lake huku akihamishia na kwa Angel haraka haraka. Taratibu Alice akaonesha matumaini, akayafungua macho yake nakumtazama John kwa tabasamu huku akioneshawa kutokwa na ufahamu juu ya kilichomfanya azimie. Mshangao ambao alikuwa akiendelea nao sasa ukawa umefika pembeni yake ambapo ulikuwepo mwili wa Angel akiwa bado hajazinduka.

    ”..Dada ni kweli umekufa Dada…?? nani sasa nitaishi naye Dada yangu..?? Maisha yangu yatakuwaje na umeniacha bila mtetezi wa maisha yangu Dada..? kwanini kila mikosi ni mimi tu dada yangu..??, Dada Angel amka basi japo uniage mara ya mwisho amka Dada yangu John wako amekuja kukuona Dada..? nitaishi na nani tena mie Alice..??”

    Muda wote John alikuwa kashikwa na butwaa na asielewe cha kufanya zaidi ya kuendelea kumshangaa Alice alivyokuwa amezinduka toka usingizini nakumlilia Dada yake Angel. Akili ya kiutu uzima ikaanza kumtawala John katika halmashauri ya kichwa chake nakutambua kuwa zile damu alizokutana nazo pindi akiingia zilikuwa zikitoka kwa Angel na si kwa Alice. Macho yake yakaanza kuufata ule mchiriziko wa zile damu ulipotokea mpaka kwenye gauni alilokuwa amelivaa Angel.

    “..Angel umemuua mtoto wangu…? Kwanini umekufa na mtoto wangu Angel..? kwanini jamani..?, nini kimekusibu si ungeniambia hata kwa simu..?, ona sasa nani tena atakayenizalia na mke wangu matatizo yake unayajua Angel.., mke wangu hawezi kuzaa na wewe ndio ulikuwa mtetezi wangu kwa hiki kiumbe..??.. nitakuwa mgeni wa nani tena John mimi..?”

    Nyumba nzima ikageuka vilio lakini havikuwa vilio vya makelele sana bali vilikuwa vilio vya chini chini ambavyo vilikuwa vikitolewa na Alice na John huku kila mmoja akioneka kumlalamikia Angel ambaye tayari alikuwa amefariki. Vilio hivyo vilifungua ukurasa upya ndani ya sura za John na Alice kwani sura zao zikawa zimefunikwa kwa machozi na kwikwi za hapa na pale. Kuna kipindi John alijitahidi kujikaza kiume lakini uzalendo ukawa unamshinda nakujikuta akitoka sauti kubwa. Sasa Alice akawa amedondoka chini kwa mara ya pili hali iliyomfanya Johna kuzidi kuchanganyikiwa akijua tayari na Alice amekufa. Alichukuwa mkono wake nakuulaza kwenye kifua cha Alice lakini mapigo yake ya moyo yakawa kama ya yamegoma kudunda. Ule mkojo uliokuwa ukimchuruzika John kidogo kupitia suruali yake kwa uoga sasa ukawa umeongeza kasi nakuwa mwingi sana hali iliyofanya suruali yake yote kulowana na lilie kojo. Alijikaza kiume na kisha akamnyanyua Angel kwa kumbeba mithili ya wacheza mieleka kisha akaongoza mpaka kwenye gari lake nje nakumuhifadhi halafu akarudi tena ndani nakumchukuwa Alice naye akampakazia kwenye gari lake nakuelekea hospitali ya Amana.

    “..Mungu nisidie nifike salama.., Eeeh Baba niongoze ningoze Baba…” OOohhh..!!”

    Barabara haikuwa na foleni kabisa sababu ilikuwa ni usiku sana, gari zilikuwa chache sana alizokuwa akipishana nazo John, njia nzima alikuwa akimuomba Mungu afike salama. Japo mikono yake ilikuwa ikimtetemeka lakini alijitahidi kujikaza kiume mpaka akafanikiwa kuingia katika hospitali ya Amana kisha akaomba msaada pale mule ndani.

    “..Umesema umekuja na maiti au mgonjwa..”

    “..Mimi nahisi watakuwa wote wagonjwa maana nahisi kama wamezi mia kwani huyu mmoja alizinduka baada ya kumpepea sana akazimia tena ila huyu mwingine sikumuona akizunduka..”

    John alikuwa akiongea na Daktari wa zamu ambaye kwa muda huu alikuwa karibu na ile miili ya Alice na Angel kwenye wodi ya wagojwa mahututi akiikagua vizuri.

    “..Umesema walipatwa na nini..?”

    “..Hapana Dokta wala sijui mie nilikuwa ofisini sasa nimerudi nakuta wote wamezimia..”

    “..Hawa ni kama nani kwako..??”

    “..Huyu hapa mmoja ni mke wangu anaitwa Angel na huyu ni mdogo wake anaitwa Alice wote wanaishi pamoja..”

    Dakatri alichukuwa vipimo vyake kwa kuwapima mapigo ya moyo kisha akaingiza mkono wake mifukoni na kutoa tochi za kupimia wagonjwa waliokufa halafu akafungua macho ya Alice na kummulika..”

    “..Huyu hapa mzima hana tatizo.., itakuwa kaishiwa na pumzi tu hivyo atapelekwa mule wodini akawekwe oksijeni..”

    “..Na huyu mke wangu Dokta..”

    John alikuwa na haraka zaidi ya kujua jibu gani atapewa na yule daktari kuhusiana na Angel. Yule dokta aliendelea na zoezi lake la kuchukuwa ile tochi kisha akamfungua Angel macho yake na kummulika huku akiandika kwenye karatasi yake. Muda wote John alibaki akiyatolea macho yale maandishi aliokuwa akiyaandika yule Daktari bila kuelewa yana maana gani..

    “..Alikuwa ni mjamzito..??”

    “..Ndio Dokta.., alikuwa mjamzito tena mimba ni changa sana ndio kwanza ilikuwa ikikuwa..”

    Yule Daktari sasa akaichukuwa ile tochi yake nakuingiza mpaka sehemu za siri za Angel huku akichungulia kwa kutumia ile tochi yake akainuka huku akiwa na ile damu katika glovu zake nakuendelea kuandika maelezo katika ile karatasi yake ya mwanzoni.

    “..Bwana mkubwa..?? embu njoo kwa hapa pembeni mara moja..”

    Yule daktari alimvuta John kwa pembeni huku akionesha kuwa anajambo anataka kunena.

    “..Samahani lakini ndio ukubwa pia.., na pia uvumilivu wako kama mwanaume. Kujikaza ni jambo la busara katika maisha haya haswa kwa sisi wanaume tunapopatwa na matatizo..”

    John tayari akili yake ikawa imeshagundua ni kitu gani anachotaka kuambiwa, bahari ya machozi ikawa imeanza kujikusanya tena katika uso wake huku kamasi likianza kuteleza kupitia mdomo wake. Mishipa ya hasira pembezoni mwa uso wake ikawa imechukuwa nafasi na kuamsha kwikwi huku akijilaziimisha kuvuta pumzi kwa haraka na kuchochea mapigo yake ya moyo ambapo sasa yalikuwa kama yamechochewa na kuni. Alijihisi mwili wote upo katika karai lililojaa mafuta ambapo chini yake kuna mafiga matatu yaliozungukwa na kuni zenye kuwaka ule moto mkali.

    “..Dokta niambie tu mke wangu kafa.., Angel kafaaa..?”

    “..Ndio maana nikakwambia jikaze wewe mwanaume mwenzangu.., hali kama hii lazima itamtokea kila mmoja aliye ndani ya ndoa.., na haya yote ni matakwa ya mwenyezi Mungu.. Mungu kampenda zaidi..”

    “..Hapana dokta na kiumbe changu..”

    “..Ni kwamba mimba inaonesha ilikuwa ndogo sana hivyo imesharibika na hii harufu kali unayoendelea kuisikia ambayo hii damu iliobadilika rangi na kuwa ya kijani na manjano imetokana na hii mimba iliyoharibika, Na huenda mimba ikawa imechangia kifo cha huyu japo sijapima vipimo vingine vilivyompelekea kifo chake. Cha muhimu ni kumshukuru Mungu kwa kazi yake aliyoitenda..”

    “..Noo, Noo, Nooo Dokta siwezi kuvumilia..!!, Dokta nashindwa kujizuia..!!, ni nani ataliziba pengo hili.., nani atanizalia Doktaaaa….”

    Daktari akabaki na mshangao, Mshango wa kile anachoendelea kukishuhudia kwa John, Alijitahidi sana kumbembeleza lakini ndio kwanza alikuwa akizizidisha hasira za John ambazo sasa zilikuwa zinamshinda nguvu na kusababisha mdomo wake kuanza kuropoka ovyo na kwa sauti ya ukali. John na yule daktari Wakiwa bado wodi ya wagonjwa mahututi mara Nesi akatokea huku akionesha anahema sana na amekuja kwa taarifa.

    “..Dokta..??, Dokta…??, Dokta..?? Yyyuuu uule mgonjwa uliyetuambiaa tut u tuumpeleke kule wooddini.., tumemuwekea ile oksijeni ili apate hewa lakini oksijeni yote imejaa damu na sasa yupo anafurukuta kama anataka ku..”

    “..Unasemaje..??, Alice anakufaa..?”

    John alishikwa na butwaa nakuropoka.., hakuamini maneno ya yiule Nesi, wakaondoka wote na Yule Dokta mpaka kwenye wodi alipokuwa amelazwa Alice napo walipofika walishuhudia kitanda chote kikifurika bahari ya damu huku Alice akijikunja kunja mithili ya mtu anayetaka kukata roho..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******************************



    ITAENDELEA





0 comments:

Post a Comment

Blog