Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

NILIVYOKUTANA NA MZIMU WA KIFO OMAN - 3

 

    -




    Simulizi : Nilivyokutana Na Mzimu Wa Kifo Oman

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Giza la ajabu likazikumba mboni zangu na wakati huohuo nikajiona nikiwa naelea angani hata hivyo nikiwa kwenye hali hiyo nikajiona naanguka kwa kasi kueleka kwenye shimo ambalo lilikuwa na giza, kwenye shimo hilo sikuona mwisho wake. Hapo nikaendelea kubaini kuwa zile ni dalili za kifo.

    “Kumbe ndiyo hivi mtu akiwa anakufa inavyokuwaga” niliwaza.

    Nukta zilezile sikujua tena kilicho endelea ingawa kabla sijajua kilicho endelea tayari nafsi yangu ikakubali kuwa mimi ni maiti!.

    **************

    **************

    NILISTUKA ghafla nikajikuta nipo kwenye eneo lenye baridi kali na ukimya wa ajabu, nilikuwa nimelala chali huku nikiwa kama nilivyozaliwa, nilikuwa natetemeka kutokana na baridi.

    Niligeuka nikatizama upande wa kulia na kushoto nikajiona nipo kwenye kitu kama

    box kubwa lenye kuzalisha baridi, sikuhitaji muda mrefu zaidi kutambua kuwa nilikuwa nimewekwa kwenye jokofu la kuhifadhia maiti ndani ya Mochwari!.

    Ndani ya nukta zilezile nilikumbuka kila kitu, kichwa changu kikabaki na maswali mengi ambayo majibu yake sikujua pakuyapatia, katika mengi niliyojiuliza swali kubwa lilikuwa ni vipi nipo hai ilihali nilinyongwa kwa kamba hadi kufa!.

    Wakati nikiwa naendelea kujiuliza swali hilo mara nilisikia mlango wa Mochwari ukifunguliwa, nikasikia sauti za watu wawili wakizungumza, mmoja mwanaume mwingine wa kike, Almanusura nipige kelele baada ya kusikia sauti ya mtu ninaye mfahamu, lakini nikajionya kutokurupuka kwa namna yoyote ile, nikajenga utulivu mwilini na akilini mwangu huku nikifuatilia mazungumzo yao vizuri sana.

    Wakawa wanazungumza huku wakisogea karibu zaidi na jokofu nililokuwa nimelazwa, nikasikia yule mwanaume akimuhadithia songombingo lilitokea nyumbani kwa Abdallah Mustapha hadi kupelekea mimi na Hussein kunyongwa.

    “Kikawaida huwa hatuna utaratibu wa wanawake kuingia kwenye chumba cha kuhifadhia maiti na kutizama maiti, lakini kwakuwa umeniomba sana, utamwona ndugu yako,”

    “Nitashukuru sana”

    “Uko tayari kuona maiti ya ndugu yako?” mlinzi wa Mochwari alimuuliza Mariamu kwa msisitizo.

    “Ndiyo niko tayari” Baada ya jibu hilo kutoka kwa mariamu, tumbo langu likapata joto, mate mepesi yakajaa mdomoni, hofu ikanitawala. Wakati huohuo droo ya jokofu nilimokuwa nimelazwa ikavutwa.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Uko tayari kuona maiti ya ndugu yako?” mlinzi wa Mochwari alimuuliza Mariamu kwa msisitizo.

    “Ndiyo niko tayari” Baada ya jibu hilo kutoka kwa mariamu, tumbo langu likapata joto, mate mepesi yakajaa mdomoni, hofu ikanitawala. Wakati huohuo droo ya jokofu nilimokuwa nimelazwa ikavutwa.

    Nilijikuta nakosa utulivu ambao nilikuwa nimeutengeneza, bila kutarajia nikajikuta nafumbua macho. Tendo lile la mimi kufumbua macho mbele ya mariamu na yule mlinzi wa mochwari kuliibua kizaazaa.

    “Mamaaaa. Uwiiii, maiti..imefufuka..waiii, mzimu..mzimu!” Mariamu na mlinzi yule wa mochwari walipiga kelele huku wakikurupuka na kuvaa mlango wa kutokea nje, kwa upande wangu nilijitoa ndani ya ile droo ya jokofu nikasimama katika ya chumba kile nikaona nimezingirwa na maiti nyingi zilizokuwa zimelazwa chini huku zimefunikwa kwa mashuka meupe, wakati huohuo nikasikia kelele nyingi zilizopigwa na Mariamu na mlinzi yule zikishadadiwa na watu wengine huko nje.

    Nilibaki nimeduwaa kama teja aliyebwia unga, katika kuduwaa huko nikavutiwa na maiti moja iliyokuwa imelazwa chini huku kukiwa na kibao kidogo kilichowekwa juu ya mwili wa ile maiti kikiwa na maandishi ya kingereza yaliyosomeka ‘taday buria’

    Mpenzi msomaji, hadi leo ninapo simulia mkasa huu nashindwa kuelewa ni msukumo gani ulionikumba na kufanya kile nilichofanya, kwani pamoja na kulindima kwa kelele huko nje zenye kushadadia kufufuka kwa maiti ndani ya mochwari, ndiyo kwanza mimi nilipiga hatua kuusogelea ule mwili, kisha nikaufunua. Sukuamini nilicho kiona.!..

    Kwa mara nyingine nilijikuta nikiduwa baada ya kuona kitu kilicho nifanya nihisi mwili wote ukipata ubaridi, mpenzi wangu Hussein Jabal alikuwa amelala chali akiwa amekufa, uso wake ulionyesha kama mtu aliyepatwa na maumivu makali kabla ya kukata roho.

    Machozi yalinitoka nikahisi donge zito kooni, kwa mara nyingine nilimlaumu mno Mungu, niliona sitendewi haki kwenye dunia, maisha yangu yalikuwa yamevurugika vibaya mno, kamasi jepesi lilichungulia kwenye tundu za pua yangu huku machozi yakiendelea kumiminika.

    “Mzimu, mzimu, mzimu” ghafla nikasutushwa na kelele zilizo endelea kulindima kwa kasi ya ajabu kutokea huko nje, hapo akili yangu ikazinduka, bila kufikiri mara mbili nikachomoka kufuata malango wa kutokea nje na kutoka. Nilipojitokeza tu nje nikashangaa kukuta mlundo wa watu waliokuwa umbali wa hatua kama ishirini wakiwa wamezunguka jengo lile la mochwari wakiwa mkao wa kusubiri kuona mzimu ulioibuka ndani ya mochwari.





    “Mzimu, mzimu, mzimu” ghafla nikasutushwa na kelele zilizo endelea kulindima kwa kasi ya ajabu kutokea huko nje, hapo akili yangu ikazinduka, bila kufikiri mara mbili nikachomoka kufuata malango wa kutokea nje na kutoka. Nilipojitokeza tu nje nikashangaa kukuta mlundo wa watu waliokuwa umbali wa hatua kama ishirini wakiwa wamezunguka jengo lile la mochwari wakiwa mkao wa kusubiri kuona mzimu ulioibuka ndani ya mochwari.

    Baada ya kujitokeza kwenye mboni za macho ya watu wale nikashangaa kuona kukizuka taharuki nyingine ya aina yake, kelele na mayowe ya hofu yalilindima huku kila mmoja akishika njia yake, bila kupoteza muda na mimi nikaanza kutimua mbio bila kujua wapi ninapokimbilia. Ndani ya nukta hizo hizo nikagundua jambo jingine lililonifanye nizidi kuchangaikiwa. Kwenye mwili wangu nilikuwa sina chochote nilicho vaa, nilikuwa uchi wa mnyama.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikazidi kuhamanika, nikageuka na kurudi ndani ya chumba cha mochwari kisha nikakwapua shuka moja miongoni mwa zile zilizokuwa zimefunika miili ya watu wengine, nikajifunika na kutoka tena nje.

    Nikashika uelekeo wa upande wa kusini mwa hosptali ile, nikawa nakimbia huku nimejifunika shuka jeupe, kwakweli kwa mwenekano nilifanana dhahili na mzimu, , nilikimbia nikiwa nimechanganyikiwa vibaya sana, katika kukimbia huku na kule nakajikuta nimetokeza upande wa nyuma wa hosptali ile, eneo lile kulikuwa na bustani ya mauwa iliyopandwa kiusatadi, bahati nzuri lilikuwa ni eneo ambalo halikuwa na mtu yeyote.

    Kando ya mauwa kulikuwa na pipa la kuhifadhia takataka, nikaamini hapo ndiyo maficho sahihi kwa wakati ule, nikafunua mfuniko na kutumbukia ndani ya pipa lile kisha nikajibanza humo.

    Nilikuwa nimejikunyata huku nikitweta, nafsi yangu ilikiri kuwa uhai wangu ulikuwa mashakani, niliamini kama nitaingia kwenye mikono ya serikali ya nchi ya Omani kamwe hawawezi kuniacha nikiwa hai, niliendelea kuamini kuwa endapo nitatiwa nguvuni dola ya nchi hiyo itahakikisha ninanyongwa hadi napoteza uhai wangu, kwa mara nyingine kiu ya kuwa mtu huru ikatanda kwenye fikra zangu, hapo ndipo shauku ya kurudi Tanzania ilipozidi kutekenya hisia zangu.

    Nilikaa ndani ya pipa lile la takataka kwa makisio ilikuwa ni zaidi ya masaa saba ama nane, eneo lile liliendelea kuwa kimya, sikusikia chakalachakala yoyote, nilijinyanyua taratibu na kuchungulia, nilishangaa nilipona giza lilikuwa limeingia, nikajivuta na kuruka nje ya pipa lile, nikaanza kutembea kuelekea gizani, wakati napiga hatua ya kwanza tu nikabaini jambo jingine lisilo la kawaida mwilini mwangu.

    Viungo vya mwili wangu vilikuwa vizito, njaa kali ilikuwa ikiniuma, nikagundua nilikuwa nina muda mrefu sijapata chochote, sikutaka kuwaza sana juu ya njaa niliyo kuwa nayo, akili yangu nikairejesha kwenye kujinasua kuingia kwenye mikono ya serikali ya nchi ya Omani. Nafsi yangu ikakiri kuwa hatua ya kwanza ya kuwa mtu huru ilikuwa ni kutoka nje ya hosptali ile.

    Nikawa natembea kwa kupepesuka lakini kwa umakini wa kutooenekana na mtu yeyote mwilini nikiwa nimejifunika lile shuka nililotoka nalo mochwari, nilitokeza kwenye eneo ambalo lilinipa faraja zaidi, nikaona kwa kutokea eneo lile ni hatua nyingine muhimu ya kunitoa ndani ya hospitali. Ilikuwa ni eneo la kufulia nguo na nguo nyingi zilikuwa zimeanikwa katika kamba.

    Nilinyata na kuanua gauni moja na mtandio, upesi nikavaa gauni lile na kujitanda mtandio kisha nikatoka nikiwa natetemeka, nilipishana na watu wawili watatu hapakuwa na yeyote aliyenijali na hatimaye nikatokeza kwenye lango kuu la hosptali.

    Kulikuwa na wanajeshi wenye bunduki waliokuwa wamezagaa kwenye geti lile, nikaanza kutetemeka, lakini sikuacha kujongea kuufauta mlango wa kutokea, hatimaye nilifika getini na kutoka nje, jasho liliendelea kunitoka huku mwili wote ukinitetetemeka, hatua ya kwanza, ya pili, ya tatu, mara nikasikia sauti kali ya kiume ikiniita nyuma yangu

    “Agripina”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bila kufikiria mara mbili nikageuka, lilikuwa ni kosa kubwa sana. Ulikuwa ni mtego, hapo hapo nikaona sura za wale wanajeshi zikimakanika bunduki wakazielekeza mbele yangu, ndani ya nukta hizohizo nikisikia amri kutoka kwa mwanajeshi mmoja akisema:

    “Kamata huyoo! ndiye yeye, msimwache akatoroka” sikupoteza muda hapo hapohapo nikakurupuka na kutimua mbio.

    “paaaaaaa!” sauti kali ya risasi ilisikika



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog