Simulizi : Nilivyokutana Na Mzimu Wa Kifo Oman
Sehemu Ya Pili (2)
Sasa Hussein anafanya mapenzi na nani? Nilijihoji huku nikijawa na wivu mwingi kifuani kwangu, donge zito lilinikaba kooni kila nilivyozisikia kelele za kilio cha mahaba kutoka mule ndani. “Yanii huyu mwanaharamu anipe mimba halafu kama haitoshi ananisaliti!” kwa nguvu zangu zote niliusukuma mlango na kuingia ndani.
Sikuamini macho yangu, Hussein Jabal na Zakia mke wa Abdallah Mustapha walikuwa uchi wa mnyama kitandani, niliduwaa mbele yao, macho yamenitoka, mikono yangu ilifunika mdomo wangu uliokuwa wazi kwa mshangao!
Wao pia, walipatwa na taharuki, wakakurupuka kitandani na kunyakua nguo zilizokuwa kando na kujistiri, tukatizamana bila yeyote kati yetu kusema kitu, ilikuwa ni picha mbaya kwenye macho yangu.
“Unaona sasa, haya yote nilikueleza, lakini ubishi wako matokeo yake ndiyo haya” Hussein aliongea kibwege akiwa na wasiwasi usoni, Zakia hakutia neno zaidi ya kuanza kuvaa nguo zake upesiupesi.
“We Mbwa umetoka chumbani kwako kuja kunifumania humu chumbani?” Zakia alisema, safari hii macho yake hayakuwa na wasiwasi tena, yakawa ni macho yenye chuki na hasira dhidi yangu.
Nakuuliza wewe Malaya mweusi..” alisema huku akinichapa kibao ambacho hakikunifanya niyumbe wala kupepesa macho.
Nilikosa cha kumjibu yule mke wa bosi wangu, nikabaki nimeganda kama sanamu huku moyo wangu ukiteketea kwa dhuruma ile, yanii nidhulumiwe penzi langu na mitusi nitukanwe na makofi nipigwa! Niliwaza kimoyomoyo nafsi yangu ikizidi kukaangika kwa maumivu.
“Why this black bitch come in here?” (Kwanini huyu Kahaba mweusi kaja humu ndani?) Zakia alimuuliza Hussein kwa ghadhabu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kahaba ni wewe siyo mimi” nilisema huku nikimwangalia Zakia kwa jicho la chuki.
Alinigeukia kwa hasira na kunipiga kibao kingine, nilipepesuka, na kupata maumivu makali, lakini safari hii na mimi sikukubali, kwa wepesi wa ajabu nilimrukia nikampiga kibao cha uso kilicho mpeleka chini, sura yake ikawa imejaa mshangao wa kutotegemea jambo lile, akanitizama kwa ghadhabu na kunifuta kwa hasira huku akiunguruma kama paka vidole amechanua tayari kwa kuniparua kwa makucha. Ndani ya sekunde zilezile mlango wa chumba kile ulisukumwa, bila kutegemea mumewe aliingia.
Tukabaki tumeduwaa, ndani ya nukta chache sana, akili ya Zakia alifanya kazi mithili ya kompyuta, hapohapo alimkimbilia mahali aliposimama mumewe Abdallah Mustapha na kumkumbatia kifani, akaongea kwa mideko:
“These two people want to kill me just because I found them sexing” (Hawa wawili wanataka kuniua kisa nimewakuta wakifanya mapenzi) lilikuwa ni shambulio la moja kwa moja kwa upande wangu, na ikawa zamu yangu kutaharuki.
“What!.” Abdallah alihamaki. Akatutizama mimi na Hussein kwa zamu, macho yake yakiwa na hasira. Ghafla alinirukia na kunipiga kibao cha uso kilicho nipeleka chini, akamsogelea Hussein na kumipiga teke la tumboni.
“Mnafanya ufuska ndani ya mji wangu, kama haitoshi mnataka kuondoa uhai wa mke wangu, si ndivyo..” alisema kwa ukali ndita zilizojichora kama mkeka wa kizaramo zilionekana.
“Watu weusi mnataka kuua mtu mweupe..! tena kwenye ardhi ya nchi yake..! hii ni kali kuliko zote nilizowahi kuziona! mmefanya makosa makubwa sana, hili ni taifa la warabu hili, siyo Afrika..” alisita kidogo, akatutizama kwa zamu kisha akasema:
“Jiwekeni tayari kunyongwa hadhalani washenzi ninyi”Sauti yake ilikuwa ya kunong’ona lakini yenye kutisha, walitoka mule ndani kisha wakatufungia mlango kwa nje na kutia kufuli.
“Get ready for wriggle! I repeat again you are going to die die die” (narudia tena, kaeni tayari kwa kufa, na mtakufa, kufa, kufa) Alirudia kusema kwa msisitizo.
“Ulijuaje kuwa hawa washenzi wako huku wakifanya huu ujinga?” nilisikia Abdallah akimuliza mkewe.
“Niliona dalili za mahusiano tangu zamani, ndipo nilipoanza uchunguzi wa siri”
“Lazima tuwasiliane na polisi na kuwaeleza juu ya haya ili watu hawa wapewe adhabu ya kifo.”
“Lini?”
“Sasa hivi”
Nilisikia mazungumzo hayo yaliyozungumzwa kwa sauti kubwa, kila neno nililisikia vizuri kabisa. Muda mfupi badae nilimsikia tena Abdallah akiwasiliana na polisi na kuwaeleza polisi kisanga chote kilichotokea pale nyumbani kwakwe.
“Hadi sasa wamo ndani wote wawili, tumewafungia kwa nje iliwasije kutoroka”
“Mmoja anatokea Tanzania mwingine Somalia” Abdallah aliendelea kutoa maelezo kwa polisi, kisha nikasikia polisi wakimuahidi kufika ndani ya dakika ishirini.
Niliketi chini, donge zito likinikaba kooni, machozi yalinitoka, nilijiona ni kimbe niliyedhulumiwa haki yangu kwa kiwango kikubwa, kwa wakati huo sikuwaza madhala yanayoweza kutoke kutokana na lile tukio, lililokuwa akilini mwangu ni mapenzi.
“Mmoja anatokea Tanzania mwingine Somalia” Abdallah aliendelea kutoa maelezo kwa polisi, kisha nikasikia polisi wakimuahidi kufika ndani ya dakika ishirini.
Niliketi chini donge zito likinikaba kooni, machozi yalinitoka, nilijiona ni kimbe niliyedhulumiwa haki yangu kwa kiwango kikubwa, kwa wakati huo sikuwaza madhala yanayoweza kutoke kutokana na lile tukio, lililokuwa akilini mwangu ni mapenzi.
“Alinilazimisha” hatimaye Hussein alisema kwa sauti ya upole akiniangali kwa macho ya upole.
“Nini!”
“..Alinilazimisha kufanya mapenzi” alisema tena huku akinitizama kwa huruma.
“Unafikiri naweza kuwa hayawani wa kiwango hicho? tangu lini mwanaume akalazimishwa kufanya mapenzi na mwanamke! tafuta uongo mwingine wa kuniongopea siyo huo”
“Haki ya Mungu nakuapia, Zakia amekuwa akinitaka kimapenzi kwa siku nyingi sana na nimekuwa nikitishiwa kwa mambo mengi, najua ni ngumu kunielewa, muhimu kwa sasa tufanye mpango wa kujinasua kwenye hili songombingo kwani nijuavyo sheria za nchi hii, kesho asubuhi tutanyongwa hadhalani kwa makosa ya uzinifu na kutaka kuua”
Kauli ile ndiyo iliyozindua ufahamu wangu na kuelewa hatari iliyokuwa inaninyemelea. Wivu uliokuwa umegubika nafsi yangu uliyeyuka kama bonge la balafu kwenye jua, hofu ikachukua nafasi.
“Hussein umeniponza, ona maisha yangu ulivyoyaingiza matatani”
“Hayo tutayaongea badaye, muhimu kwa sasa ni kuhakikisha tunatoweka eneo hili”
Huko nje tuliendelea kuwasikia Zakia na mumewe wakiendelea kutujadili kwa namna kifo chetu kitakavyokuwa funzo kwa watu wengine hususani wafrika waliko nchini Oman.
Dakika chache nilisikia ngurumo za magari ambayo haikuhitaji kuuliza ni magari ya nani, upesi nilifahamu yalikuwa ni magari ya polisi.
“Wako wapi?” nilisikia sauti ikisema huko nje.
“Tumewafungia chumba hiki” Abdallah alijibu, mlango wa chumba ulifunguliwa askari kama saba wenye bundu ki wakaingia mule ndani.
Hatukuulizwa chochote na wale askari zaidi ya kuchezea kipigo, tulipigwa na kupigwa tukapigika haswaa. Kila sehemu ya mwili wangu kulikuwa na maumivu, sikuweza kusimama kwani nilikuwa na maumivu makali maeneo mbalimbali.
“Wasilianeni na ndugu zao waliopo huku kwa ajili ya kuja kuchukua maiti zao kwa kusafirishwa nchini mwao kesho baada ya kutumikia adhabu yao ya kifo” Askari mmoja aliyeonekana kama kiongozi wao alisema.
Tuliondolewa mule ndani tukiwa tumefungwa pingu mikononi, tukapandishwa kwenye gari la polisi, kisha safari ya kuelekea mahali ambapo sikupaelewa ikaanza, muda wote nilikuwa nikilia kwa uchungu, maisha yangu yalikuwa yamebadilika ghafla mno.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nisamehe Agripina” Hussein alisema, akionekana kukata tamaa.
“Najua hadi kesho, muda kama huu, miili yetu itakuwa mochwari ndani ya friji lenye baridi kali, ikingojea kuzikwa kwenye makaburi mawili tofauti, nataka moyo wako ufahamu kuwa sikukusudia safari ya mahusiano yetu iwe hivi, ndoto zangu za kukupeleka Mogadishu zimegonga mwamba, naumizwa na hilo Agripina, lakini naumizwa zaidi na mtoto aliye tumboni mwako” alisema huku akinionyesha kipimo changu cha mimba alichokuwa amekimata mkononi, machozi yakijikusanya machoni mwake.
Sikujibu chochote, zaidi ya kutiririkwa na machozi, polisi walikuwa wametuweka kati huku mitutu ya bunduki ikitutizama kwa uchu. Tulipelekwa hadi kwenye eneo moja lenye uwazi mkubwa, kukiwa na majengo yaliyokuwa kama mabweni, ukingoni mwa eneo hilo kukizungushiwa ukuta mrefu wenye mitambo yenye shoti za umeme.
“Teremka” tuliamriwa.
Taswira ya kunyongwa ikawa inanitesa akilini, kwakweli niliogopa sana, tukiwa kwenye lile eneo ambalo badae nilifahamu kuwa ilikuwa gereza, tuliingizwa kwenye ofisi ndogo tuliyo andikisha majina yetu na kuandikiwa makosa mawili yanayotukabili, kwa maana ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa, sanjari na kutishia kuua.
Baada ya hapo, Hussein alichukuliwa na kupelekwa eneo ambalo sikujua ni wapi. Nilitolewa mule kwenye kile kiofisi kidogo na kuingizwa kwenye chumba pweke ambacho hakikuwa na kitu chochote, kulikuwa na mwanga hafifu wa njano uliotokea kwenye balbu ndogo iliyokuwa ikining’inia kwenye dari.
Niliegemeza mgongo wangu kwenye ukuta, taswira ya kijiji cha Makose mkoa wa Tanga huko nchini Tanzania ikanijia, kwa mara nyingine nililia mno kuona ndoto zangu za kuikomboa familia yangu katika maisha duni zimegonga mwamba huku nikisubiri kunyongwa hadi kufa masaa machache yajayo.
Nilikaa ndani ya kile chumba hadi asubuhi, mwanga wa jua la asubuhi ukapenya kupitia matobo ya kwenye bati na kuingia hadi ndani ya chumba kile, niliumia nilipo baini kuwa jua hilo ndio jua la mwisho kuliona duniani, masaa mawili badae, mlango ulifunguliwa wakaingia askari wawili na kuniamulu nitoke nje tayari kwa kupelekwa mahali niliko takiwa kusomewa mashitaka yangu na kutumikia adhabu yangu ya kifo.
Nilitolewa nje na kupelekwa tena kwenye ile ofisi ndogo ambayo niliingizwa jana usiku nikiwa na Hussein Jabal, kusomewa mashtaka kabla ya kutumika adhabu ya kifo. Ajabu nyingine nilipo ingizwa ndani ya kiofisi kile nilijikuta nipo pekee yangu Hussein Jabal hakuwepo.
“Yuko wapi Hussein?” niliuliza.
“Unamuuliza nani maswali ya kijinga, kaa kimya” Afande ambaye alionekana kuwa kiongozi wao alinifokea.
“Nifanyie ikhisani ya jambo moja” nilisema kwa upole huku machozi yakinilenga.
“Jambo lipi?”
“Naombeni msaada wa kuwasiliana na ubalozi wa nchi yangu sanjari na mwenyeji wangu aitwaye Maliamu ambaye yupo hapa Muscut maeneo ya Deira ili wajue madhila yanayonisibu”
“Tunasikitika hilo pia hatuwezi kufanya , taarifa zitakazo wafikia nduguzo ni kuja kuchukua maiti yako.” Alisema tena yule askari mkuu.
Nilijikuta nikilia kama mtoto, hofu ya kunyongwa kwa kamba ilisambaa ndani ya kifua changu vibaya sana, muda mchache badae walinifunika kitambaa cheusi usoni, mikono yangu ikiwa kwenye pingu. Nikachukuliwa na kupelekwa mahali ambapo nilisikia wakipataja kuwa panaitwa slaughuter place.
Nilifikishwa slaughuter place na kufunguliwa kitambaa, mbele yangu nikajiona nipo eneo lenye uwazi kama uwanja wa mpira, kulikuwa na jukwaa kubwa ambalo lilitengenezwa kama goli la mpira wa miguu, kamba nyingi zenye vitanzi zilikuwa zikining’inia kwenye goli lile nikabaini eneo hilo ndipo eneo lililohusika kwa kunyongea watu.
Katika kutazama huko nikaendelea kuona kitu kingine kilicho upasua moyo wangu vibaya mno, nilimwona Hussein akiwa kando ya jukwaa lile la kunyongea akiwa anafanya ibada.
“Husseiiiin!!” niliita kwa nguvu huku nikiamini kivyovyote vile Hussein amepewa nafasi ya kusali sala ya mwisho kabla ya kuning’ininzwa kwenye kitanzi. Wale askari wa kijeshi walinikabili kwa kunifunga kitambaa mdomoni ili nisiweze kupiga kelele.
“Wewe hujui kama kuleta ghasia kwa mtu anaye fanya ibada ni jambo baya..eeh”
Nilishindwa kujibu kwakuwa tayari nilikuwa nimefungwa kitambaa mdomoni, nikaishia kulia, wakati huo nilimwona Hussein akiwa amemaliza kufanya ile ibada na sasa askari walimfunga pingu mikononi mwake. Aligeuka akanitizama huku akitoa tabasamu lenye kila dalili ya kukata tamaa
“Agripina naenda kunyongwa, usijali kuhusu hilo, kubwa ni kunisamehe kwa kushindwa kukupeleka Mogadishu, nisamehe hata kwa kukusababishia kifo ilihali ukiwa na mtoto tumboni mwako, Nisamehe kwa kukusaliti na kutembe na mwanamke mwingine, nisamehe kwa kila kitu Aglipina, naamini tutaonana badae, Inshallah” Hussein alipaza sauti kunieleza hayo, sikuweza kujibu chochote zaidi ya kububujikwa na machozi mdomo wangu ukiendela kuzibwa kwa kitambaa kigumu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walimvalisha kitambaa cheusi usoni wakamwongoza kumpandisha kwenye jukwaa la kunyongea, askari wawili walimvisha kitanzi cha kamba ngumu shingoni na kuhakikisha wamekikaza vizuri kisha wakashuka chini wakimwacha peke yake kwenye jukwaa.
Niliendelea kulia nikimwomba Mungu kimoyomoyo afanye mujiza wake kubadilisha kile kilichokuwa kikiendelea wasaa ule, lakini haikuwa hivyo, askari aliyehusika na kubonyeza swichi ya kupandisha kamba juu alikuwa akingojea amri kutoka kwa kamanda mkuu.
“Nyongaa!”amri ya kunyonga ilitoka kwa kamanda mkuu, mnyongaji alibonyeza swichi, kamba ikaanza kujiviringisha taratibu kwenda juu, ilivyokuwa ikijivingirisha ndivyo ikawa inamnyanyua Hussein taratibu, na hapo ikawa inamkaba shingoni kwa nguvu.
Walimvalisha kitambaa cheusi usoni wakamwongoza kumpandisha kwenye jukwaa la kunyongea, askari wawili walimvisha kitanzi cha kamba ngumu shingoni na kuhakikisha wamekikaza vizuri kisha wakashuka chini wakimwacha peke yake kwenye jukwaa.
Niliendelea kulia nikimwomba Mungu kimoyomoyo afanye mujiza wake kubadilisha kile kilichokuwa kikiendelea wasaa ule, lakini haikuwa hivyo, askari aliyehusika na kubonyeza swichi ya kupandisha kamba juu alikuwa akingojea amri kutoka kwa kamanda mkuu.
“Nyongaa!”amri ya kunyonga ilitoka kwa kamanda mkuu, mnyongaji alibonyeza swichi, kamba ikaanza kujiviringisha taratibu kwenda juu, ilivyokuwa ikijivingirisha ndivyo ikawa inamnyanyua Hussein taratibu, na hapo ikawa inamkaba shingoni kwa nguvu.
Sekunde kumi badae Hussein alikuwa akining’inia juu na kutapatapa huku na kule, miguu yake ilikuwa kirukaruka huku kiwiliwili chake kikitetemeka kana kwamba anapigwa na shoti ya umeme, kwa macho yangu niliweza kuona Hussein akijikojolea na wakati mkojo huo unapita sekunde tano zilizofuata Hussein alitulia tuli. Tayari alikuwa maiti.
Bila kutegemea nilijkuta na mimi nikijikojolea kwa mara ya pili, nilikuwa na woga isiyo kifani, niliona mwili wa Hussein ukiendelea kubembea kwenye kamba, kilichokuwa kimebakia ni kushushwa kupelekwa mochwari kisha kuzikwa.
“Anayefuata kunyongwa ni wewe” nilistushwa na sauti ya kamanda mkuu, nilijikuta tumbo likinichafuka nikahisi kutapika, wakati huohuo pasina kutarajia nikajikuta haja kubwa ikinitoka na kujiharishia vibaya sana.
Nilifunguliwa kile kitambaa mdomoni na kusogezwa eneo lilitandika zuria dogo kando kukiwa na maji kwenye ndoo ambayo nilitakiwa kunawa kabla ya kusali sala zangu za mwisho kisha kunyongwa kama ilivyokuwa kwa mpenzi wangu Hussein Jabal.
“Niacheni nirudi nyumbani, sitaki kufa mimi..sitaki aagh!.” nilisema kwa mahamaniko makubwa huku nikilia kama mtoto, hata hivyo hakuna aliyenijali wote walinitaka nijinawishe kwa maji kisha waninyonge.
Niliendele a kuwasihi waniachie nirudi nyumbani kwetu Tanzania, lakini nao waliendela kunisihi nisali sala zangu za mwisho kwani muda wa mimi kufa utakapo wadia hawatakuwa na cha kusubiri zaidi ya kunitundika kweye kamba na kuninyonga.
Nilibaki nikilia na kulia na hatimaye muda wa kunyongwa ulifika. Walinikamata askari wawili waliokuwa na nguvu na kunisukumiza kwenye jukwaa tayari kwa kunivisha kitanzi na kunyongwa.
“Mungu uko wapi wewe Mungu..aggh!..fanya kitu kwa ajili yangu baba, fanya sasa hivi Mungu wangu, nisaidie ” Nilijikuta nikitamka maneno hayo kwa nguvu huku nikilia kama mtoto, sikuwa tayari kufa, bado niliona nina haki ya kuishi na kuwa mtu huru kwenye dunia.
Hata hivyo fikra hizo zilibakia kuwa kichwani mwangu tu, nilivishwa kitambaa cheusi kisha kitanzi, kamba ikakazwa shingoni mwangu na askari anayebonyeza swichi inayoruhusu kamba kunivuta kwa juu aliiendea swichi na kuibonyeza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kamba ilianza kuivuta shingo yangu na kunining’iniza kwa juu, niliona pumzi zinagoma kutoka huku maumivu makali ya kubanwa na kamba yakiniumiza, nikawa natapatapa huku na kule, nikatamani ninyanyue mikono yangu ili nizuie kamba isiendelee kunikaba, ila mikono yangu ilikuwa imefungwa kwa pingu.
Giza la ajabu likazikumba mboni zangu na wakati huohuo nikajiona nikiwa naelea angani hata hivyo nikiwa kwenye hali hiyo nikajiona naanguka kwa kasi kueleka kwenye shimo ambalo lilikuwa na giza, kwenye shimo hilo sikuona mwisho wake. Hapo nikaendelea kubaini kuwa zile ni dalili za kifo.
“Kumbe ndiyo hivi mtu akiwa anakufa inavyokuwaga” niliwaza.
Nukta zilezile sikujua tena kilicho endelea ingawa kabla sijajua kilicho endelea tayari nafsi yangu ikakubali kuwa mimi ni maiti!.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment