Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

NILIVYOKUTANA NA MZIMU WA KIFO OMAN - 4

 



    -

    Simulizi : Nilivyokutana Na Mzimu Wa Kifo Oman

    Sehemu Ya Nne (4)



    Kulikuwa na wanajeshi wenye bunduki waliokuwa wamezagaa kwenye geti lile, nikaanza kutetemeka, lakini sikuacha kujongea kuufauta mlango wa kutokea, hatimaye nilifika getini na kutoka nje, jasho liliendelea kunitoka huku mwili wote ukinitetetemeka, hatua ya kwanza, ya pili, ya tatu, mara nikasikia sauti kali ya kiume ikiniita nyuma yangu

    “Agripina”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bila kufikiria mara mbili nikageuka, lilikuwa ni kosa kubwa sana. Ulikuwa ni mtego, hapo hapo nikaona sura za wale wanajeshi zikimakanika bunduki wakazielekeza mbele yangu, ndani ya nukta hizohizo nikisikia amri kutoka kwa mwanajeshi mmoja akisema:

    “Kamata huyoo! ndiye yeye, msimwache akatoroka” sikupoteza muda hapo hapohapo nikakurupuka na kutimua mbio.

    “paaaaaaa!” sauti kali ya risasi ilisikika, kukazuka kizaazaa kingine , watu wachache waliokuwa eneo lile la lango la hosptali kila mtu akashika njia yake huku sauti za taharuki zikiwatoka.

    Nilifahamu wazi risasi ilikuwa imepigwa angani ili kunitisha nisikimbie, nilikuwa tayari kufa nikiwa nakimbia nikijaribu kujiokoa kuliko kusimama kisha nikatiwa nguvuni kikondoo.

    “Simama wee mwanamke Simamaa!” sauti za amri zilizidi kunishurutisha. Sikujali nilizidi kukimbia kwa nguvu zangu zote, nilibahatika kuona kichochoro mbele yangu, mita kama kumi, nikaona pale ndiyo mahali sahihi pakuwapoteza wale wanajeshi waliokuwa wakinifuata nyuma yangu kwa kasi.

    Nilikifia kile kichochoro na kutokomea ndani yake, nikakutana na mazingira ambayo yalizidi kunipa nguvu ya kukimbia, nilikuwa ndani ya makazi ya watu hohehahe maarufu kama uswahilini, nikapita kwenye vichochoro viwili vitatu hatimaye nikajikuta nimetokea katika eneo ambalo halikuwa na njia.

    Nikatazama kulia kwangu nikajiona nipo katika nyumba eneo la uwani, nikaona kuna vyumba kadhaaa katika lile eneo la uwani vikiwa wazi, nikakurupuka na kuingia kwenye moja ya chumba ambacho kwa kukiangalia kilikuwa kikikaliwa na kijana wa kileo.

    Nilisukuma mlango kwa nguvu na kuzama ndani kisha nikaufunga, naam dhana yangu ilikuwa sahihi, chumba kile kilikuwa kikikaliwa na mvulana, alikuwa ni mvulana wa kiarabu mrefu na mwenye nywele nyingi kichwani alikuwa amelala fofo!

    Pamoja na kwamba nilisukuma mlango kwa nguvu na kuingia ndani kwa fujo lakini mtu yule aliyekuwa amelala fofo hakustuaka!. Nilijikunyata nikiwa nahema kama nimetoka kwenye mbio za marathoni.

    Ukimya wa ghafla ukashika hatamu. Nikawa najiuliza maswali mwenyewe mule ndani kama nitoke ndani ya chumba kile nitimkie mahali pengine ama niendelee kubaki mule ndani hadi hapo mwenyeji wa chumba kile aliyekuwa akikoroma kitandani atakapo amka na kunikuta mule ndani.

    Katika kuwazawaza huko nikapata wazo ambalo niliamini ni zuri. kabla sijalifanyia kazi wazo hilo mara nikasikia kitu kingine cha ajabu, yule mtu aliyekuwa amelala kitandani akawa anatoa mkoromo usio wa kawaida, nikasimama na kumtizama sikuamini kile nilicho ona.

    Mtu yule alikuwa akitokwa damu puani, masikioni na mdomoni damu ile ilichanganyika na povu lilikuwa likimtoka mdomoni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ngo ngo ngo” ndani ya sekunde hizohizo nikisikia mlango wa chumba kile ukigongwa kwa nguvu!.

    Nilibaki nimeganda kama sanamu, nilihisi akili yangu ikisimama kufanya kazi kwa muda, wakati nikiwa nimeduwaa mbele ya mtu yule aliyeonekana yupo kwenye hekaheka za kuipigania roho yake nikastushwa tena na sauti kali ya mlango ukigongwa.





    sijalifanyia kazi wazo hilo mara nikasikia kitu kingine cha ajabu, yule mtu aliyekuwa amelala kitandani akawa anatoa mkoromo usio wa kawaida, nikasimama na kumtizama sikuamini kile nilicho ona.

    Mtu yule alikuwa akitokwa damu puani, masikioni na mdomoni damu ile ilichanganyika na povu lilikuwa likimtoka mdomoni.

    “Ngo ngo ngo” ndani ya sekunde hizohizo nikisikia mlango wa chumba kile ukigongwa kwa nguvu!.

    Nilibaki nimeganda kama sanamu, nilihisi akili yangu ikisimama kufanya kazi kwa muda, wakati nikiwa nimeduwaa mbele ya mtu yule aliyeonekana yupo kwenye hekaheka za kuipigania roho yake nikastushwa tena na sauti kali ya mlango ukigongwa.

    Hapo ni kama akili yangu ilikurupuliwa ilipokuwa imelala, nikatambua hatari iliyokuwa inaninyemelea.

    “Ngo,ngo,ngo!..open the door” Sauti ya mwanamke ilisikika ikisema kwa wahaka huku akiendelea kuugonga mlango kwa nguvu, jasho lilinichuruzika maungoni mwangu, nikaona hatimaye ninaingia kwenye mikono ya serikali ya nchi ya Oman, sikutaka kabisa kujiongopea kwamba siwezi kuhusishwa na kifo cha yule jamaa aliyekuwa akiweweseka kitandani huku damu ikimtoka puani na mdomoni.

    Nikaamini kabisa hilo ni jumba bovu jingine linalokwenda kuniangukia, nikajionya kama nisipofanya kitu lazima nitaingia kwenye mikono ya serikali na sikuhitaji mwalimu wa kunieleza kuwa kama nikingia kwenye mikono ya dola nini kitatokea.

    “Ngo,ngo,ngo” Mgongaji aligonga tena safari hii kwa nguvu zaidi, nikatizama kulia na kushoto nikaona mahali pekee pakujificha ni kuingia chini ya uvungu wa kitanda. Lakini kabla sijazama uvunguni mara mlango ulisukumwa kwa nguvu na ukafunguka.

    Aliingia msichana mmoja wa kiarabu akanikodolea macho yenye mshangao kisha akayahamisha macho yake kwa kwa mvulana aliyekuwa hoi pale kitandani, nikamwona akipigwa na bumbuwazi baada ya kuona hali ya yule mtu pale kitandani.

    Nilikuwa nimesimama nikiendelea kumwangalia yule dada namna alivyo taharuki kwa kile alichokuwa akikishuhudia mbele yake, nikawa makini na yule msichana kufuatilia kila tendo alilokuwa akifanya, akayatupa macho yake tena kwangu, akanitizama kwa chati kisha akasema kitu, lakini sikumwelewa kwakuwa alizungumza kwa lugha ya kiarabu.

    Ingawa sikumwelewa lakini nilibaini alichokuwa anataka kwangu nini, alitaka kufahamu mimi ni nani,kwanini nipo mule ndani na nimemfanya nini mtu yule anayetokwa na damu nyingi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitendo cha mimi kubaki kuwa bubu huku yeye akiniuliza maswali lukuki kilimkera vibaya sana yule msichana, nikaona anatoa simu yake ya mkononi kisha akapiga namba fulani na kuanza kuzungumza na mtu upande wa pili. Sikutaka kujiongopea kwamba haiti polisi.

    Machale yakanicheza, hapohapo nikamrukia na kumkwapua ile simu na kuitupa, baada ya kufanya kitendo kile kilichofuata kilikuwa hakielezeki, tulikamatana na yule msichana na kuvingirishana huku na kule, pamoja na kwamba nilikuwa na njaa lakini niweza kumthibiti msichana yule.

    Nilimvuta nywele nikamkandamiza kwa chini huku nikiwa nimemkanyaga kifuani.“Kimyaa, nasema kimyaa, nyau wewe nani aliyekwambia uite polisi? Umeniona mimi ndiyo nimemua huyu fala wako aliyelala hapa kitandani..eh?” nilisema kiwazimu nikiwa nimevurugwa vibaya sana.

    Nilichofanya ni kumfunga kwa kamba mikono na miguu yake kisha nikampiga sachi na nikamkuta na kiasi cha fedha ambazo sikumbuki zilikuwa ni shilingi ngapi, nilizikomba pesa zote nikiamini zitanisaidia mbele ya safari, baada ya tukio hilo niliyatupa macho yangu kwa yule kijana mvulana mwingine aliyekuwa hoi kitandani, nilichanganyikiwa baada ya kumwona mtu yule akiwa amekoda macho huku akiwa ahemi. Nikatambua tayari mtu yule alikuwa amekwisha fariki dunia.

    “Hapanifai tena hapa” Niliwaza, sikupoteza muda niliondoka mule ndani upesi nikimwacha yule binti akijizoazoa pale sakafuni, niliingia mtaania na kuendelea kukimbia, kwakweli naweza nikasema niligeuka kuwa mkimbizi katika nchi mwa watu.

    Nakumbuka baada ya kutoka mule ndani nilichofanya ni kwenda katika hoteli iliyokuwa mafichoni kidogo, ilikuwa karibu na pwani ya bahari, haikuwa hotel ya kitalii ila nakumbuka jina la hotel hiyo iliitwa Kuluthumu hotel, ingawa ilikuwa ni usiku nilipata stafutahi ya chai ya maziwa na mkate wa siagi ambao kwa hakika ulijaza tumbo langu.

    Na katika kipindi chote ambacho nilikuwa nikipata stafutahi ile nilikuwa nimekwishapata wazo moja ambalo niliamini kama nikiliweka katika uhalisia ni wazi litaleta matunda na kuweza kutoroka kabisa katika nchi ile na kurudi nyumbani Tanzania.

    Baada ya kushiba nilinyanyuka na kuanza kuyafanyia kazi mawazo yangu, nilitoka na kutembea kwa mguu kuufuata fukwe ile ambayo ilinipeleka hadi ukingoni mwa bandari ya Muscut, nilisimama katika uzio wa bandari ile nikawa natizma huku na kule kama nitamwona mtu yeyote.

    Wakati huo kwa makisio ilikuwa yapata kati ya saa nne ama saa tano usiku, nikaelendelea kusimama kwa muda hadi badae nilipostuliwa na sauti kali iliyotokea nyuma yangu:

    “We ni nani na unafanya nini?” sauti ya amri ilisikika, nilipogeuka nikamwona mtu mmoja mzee wa makamo kasimama huku akiwa amekamata bunduki aina ya gobole. Kimwonekano alikuwa ni kama mlinzi wa eneo lile la bandari.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “My name is Agripina, I want to go back home, East Africa. I need your help to get there and I can give you anything you want,” (naitwa Agripina, nataka nirudi nyumbani, Afrika Mashariki. Nataka unisaidie kufika huko na nitakupa chochote unachokitaka) nilimwambia mlinzi.

    Yule mlinzi alinitizama kwa chati tochi yake ikiendelea kunimulika, kisha akavuta pumzi ndefu halafu akasema:

    “I’ve never seen you in my life but you seem like you need some help. I can do that for you but let me tell you something,” (sijawahi kukuona maishani mwangu lakini unaonekana kuhitaji msaada. Nitakusaidi lakini acha nikwambie kitu kimoja) alisema kwa sauti ya kukoroma kama ambavyo kamanda wa kijeshi anavyoweza kutoa maelekezo kwa kikuruti.

    “We have a cargo ship, Zaghol 153 which travels to Mombasa this night. Captain can take you there in one condition,” (tuna meli ya mizigo, Zaghol 153 inayosafiri kwenda Mombasa usiku huu. Nahodha anaweza kukupeleka kwa sharti moja)

    “Which one?” (lipi hilo?) niliuliza kwa kiherehere....





    “Nifuate” badala ya kunijibu yule mtu alisema huku akianza kutembea kuingia ndani ya bandari.

    Nilibaki nikimkodolea macho nikiwa njia panda nisijue kama nilistahili nimfuate ama niachane naye, nasema hivyo kwa sababu niliona kama jambo lile nililoliomba kwa mtu yule lilikubalika kirahisi mno, machale yakawa yananicheza, nikawa njia panda, nilifikiria kwa muda mwisho wa siku nikajiambia potelea mbali litakalo kuwa na liwe. Nikamfuata.

    Alinipeleka hadi kwenye ofisi moja ndogo ambayo ilionekana ni kama ofisi ya walinzi waliyoitumia kwa kufanyia mambo yao ndani ya bandari ile.

    “Ningoje hapa” alisema yule mzee na kunipa kiti, aliniacha pale na kwenda mahali ambako sikujua ni wapi, dakika chache badae alirejea na kunitaka nimfuate.

    Nilimfuata lakini swali kuu kichwani mwangu lilikuwa ni vipi mtu yule ajitoe kunisaidia mimi kiasi kile, kwa malipo gani? Kwa ushawishi upi? Na kwa huruma gani aliyonayo juu yangu mtu ambaye nimekutana naye si zaidi ya dakika ishirini.

    Pamoja na kuyawaza hayo, bado sikutaka kabisa kurudi nyuma, nilitaka nishindwe nikiwa kwenye harakati za kujaribu kujiokoa kuliko kuogopa kufanya nikingoja kukamatwa kikondoo, niliamini adui namba moja wa mustakabali wa uhai wangu kwa wakati ule ni hofu, hivyo nilipiga moyo konde na kusonga mbele.

    Safari yetu ilishia kwenye kontena moja ambapo baada ya kuingia ndani ya kontena lile nilishangaaa nilipoona mandhali ya ndani yakiwa ni mithili ya sebule nzuri ya kisasa yenye kila kitu ndani yake.

    “Anaitwa Casper ndiye atakaye kusadia kukupeleka kwenu,” alitoa utambulisho yule mwenyeji wangu.

    “Sawa” nilitikia.

    “Mimi naondoka, mambo mengine atakueleza mwenyewe” yule mlinzi alisema tena huku akituangalia kwa zamu, nilitikisa kichwa kumkubalia, alinyanyuka na kusogea kwa yule jamaa kisha yule jamaa akatoa burungutu la pesa na kumpa yule mlinzi, “isije ikawa ndiyo nimeuzwa” nilijisema kimoyomoyo. Tukabaki na yule jamaa aliyetambulishwa kwangu kama Casper nahodha wa meli ya mizigo Zaghol 153.

    Tulibaki kimya kwa dakika zaidi ya moja, hakuna aliyeanza kumsemesha mwenzake, jamaa alikuwa bize na sigara zake, akionekana kutokunijali hata kidogo, kwa haraka nikagundua jamaa yule alikuwa na chembechembe za dharau, hata hivyo sikujali nilibaki kimya nikisubiri niambiwe ni nini malipo ya kusafirishwa kutoka Muscut hadi Mombasa.

    “Una mzigo wowote au ndivyo hivyo ulivyo utakavyo safari?” hatimaye jamaa aliniuliza.

    “Ndivyo hivi nilivyo, sina mzigo”

    “Ok, twende kwenye meli”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulisimama na kutoka mule kwenye lile kontena na kupita katikati ya makontena mengi tukipishana na watu lukuki waliokuwa wakiendelea na majukumu yao mule bandarini.

    Safari yetu ikaaishia mbele ya meli kubwa ya rangi ya kijivu, ubavuni mwa meli hiyo kukiwa na maandishi makubwa yaliyosomeka Zaghol 153. Tulijitoma ndani ya meli ile, nikapelekwa kwenye moja ya vyumba vilivyokuwa mule ndani nikatulia mule nikingoja kupewa maelekezo mengine.

    Saa tisa kamili usiku Meli ile kubwa ilipiga honi dakika chache badae ikaanza kuondoka. Bado nilikuwa siamini kama hatimaye naweza kuiacha nchi ya Oman, nilisali na kumshukuru Mungu kimoyomoyo.

    Nilikuwa nimekaa ndani ya chumba kile juu ya kitanda huku nikijiona ni mwenye furaha isiyo ya kawaida kwa kuona narejea nyumbani kwetu Tanzania, nakumbuka nilikaa ndani ya chumba kile kwa masaa mengi mno hadi usingizi ukanipitia, nililala masaa mengine mengi mno hadi nilipo amshwa na njaa.

    Nilipotupa macho kwenye saa ya ukutani iliyokuwa mule ndani nilishangaa nilipo ona ilikuwa ni saa sita mchana wa siku mpya. Njaa ilikuwa inaniuma, ajabu ni kwamba bado Casper hakuwa ameniambia ni jambo gani nitakalo stahili kumlipa kama malipo ya msaada ule.

    Nikiwa bado natafakari mara mlango wa chumba kile uligongwa kiustarabu, niliruka na kwenda kuufungua, alikuwa ni Casper. Alikuwa amesimama sigara ikiwa mdomoni mwake, mkononi akiwa ameshika sahani lililokuwa na chakula aina ya baga pamoja na glasi yenye juisi nzito ya nanasi.

    “Pole, nimekuletea chakula” alisema huku akitoa moshi wa sigara katika tundu za pua yake.Nilipokea chakula kile huku nikitoa tabasamu lililosema ahsante kwa wema wako.

    “Kula, ukishiba tutatakiwa kuzungumza” alisema tena Casper, nilikula upesiupesi baada ya kushiba nikaketi kitako kumsikiliza yule jamaa.

    “Kwanini unakimbia Oman kwa kujificha..umeua?” Casper aliuliza, swali lilikuwa kama mjeledi wa moto kifuani mwangu mate mepesi yalinijaa mdomoni nikapatwa na kigugumizi. Na hata kabla sijajibu akasema tena:

    Hata hivyo siyo kazi yangu kujua kwanini unakimbia nchi ile ya kiarabu, kazi yangu ni kukupeleka unakotaka kwa malipo ya ngono,” kwa mara nyingine nilibaki tena nimeduwaa baada ya kauli ile, nikajiona ni mjinga kwa kutohisi jambo lile kama linaweza kunitokea.

    Niliendelea kupigwa na bumbuwazi baada ya Casper kuanza kunishikashika chuchu zangu huku akiwa ananivutia kwakwe, macho yake yakionesha ananitaka kimapenzi. Nilibaki nimeduwaa nisijue kama nilitakiwa kukataa ama kukubali, Casper akaendelea kunibinyabinya chuchu huku pumzi zikimtoka kwa kasi, mara akanivua gauni langu, nikabaki uchi, niliendelea kuganda kama sanamu.

    Mara akavua surauli yake halakahalaka kama anakimbizwa, nikaona kitu cha ajabu kwenye sehemu zake za siri.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog