Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

NILIVYOKUTANA NA MZIMU WA KIFO OMAN - 5

 





    Simulizi : Nilivyokutana Na Mzimu Wa Kifo Oman

    Sehemu Ya Tano (5)



    Niliendelea kupigwa na bumbuwazi baada ya Casper kuanza kunishikashika chuchu zangu huku akiwa ananivutia kwakwe, macho yake yakionesha ananitaka kimapenzi. Nilibaki nimeduwaa nisijue kama nilitakiwa kukataa ama kukubali, Casper akaendelea kunibinyabinya chuchu huku pumzi zikimtoka kwa kasi, mara akanivua gauni langu, nikabaki uchi, niliendelea kuganda kama sanamu.

    Mara akavua surauli yake halakahalaka kama anakimbizwa, nikaona kitu cha ajabu kwenye sehemu zake za siri.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sehemu zake za siri zilikuwa kubwa na zilikuwa wima mithili ya ukuni mkavu, zilikuwa zimekakamaa huku zikinitizama kwa uchu. Yule jamaa akawa anahema kwa tabu ilionesha mzuka wa ngono ulikuwa ushampanda.

    Hatimaye akawa ananiingilia kimwili, sikuhisi chochote zaidi ya maumivu makali sehemu zangu za siri, kwa lugha nyepesi naweza nikasema alikuwa akinibaka, alinibaka na kunibaka mpaka hamu yake ilipokwisha, hadi anatoka juu ya mwili wangu nilikuwa nahisi mwili mzima ukiniwaka moto.

    Sikuwa na lakufanya kwakuwa kitu nilichokuwa nakitaka kwa wakati huo ni kurudi nyumabni kwetu Tanzania, nilikubaliana na udhalilishaji wote sanjari na maumivu yote yatakayo nisibu ilimradi nifikishwe nyumbani.

    “Bila shaka utanifikisha nyumbani salama” nilisema kwa sauti ya upole mbele ya yule mwanaume mwenye kuitwa Casper.Alinitizama kwa chati kisha akasema

    “Nina kisasi na wanawake wote kwenye hii dunia, sijawahi kumpenda mwanamke yoyote tangu nilivvyopata akili, tangu nilipogundua viumbe hao walinifanyia mambo ambayo sikupaswa kufanyiwa niliwachukia mno.

    “Niliapa kuwaliza machozi kisha kuwamaliza popote watakapo ingia kwenye anga zangu, nimekwisha ua wengi hadi sasa, bado nina kiu ya kuua zaidi, hata wewe tayari nisha kuua” alisema yule jamaa kwa sauti ambayo haikuwa na mzaha hata kidogo.

    “Casper kwanini unaongea maneno hayo mbona unanitisha”

    “Sikiliza wewe mwanamke, hapo ulipo tayari nishakuambukiza ukimwi na kwa taarifa yako siwezi kukusafirisha hadi huko unakotaka kufika. Umebakiza muda mfupi wa kuendelea kuishi kwenye hii dunia, kitu cha msingi ni kusali sala zako za mwisho”

    Bila kutegema nilijikuta nikianza kulia kama mtoto aliyetelekezwa na mama yake, mambo aliyonieleza yalikuwa ya kutisha mno.

    “Umeniambukiza ukimwi!”

    “Ndiyo nimekupa ukimwi”

    “Kwanini lakini! kwanini eeh!”

    “Kimya kenge wewe, kimya unamlilia nani hapa”

    “Kwani nimekukosea nini hadi uniambukize Ukimwi”

    "Nasema kimya we mtu mweusi huelewi..alaa!”

    “Kwanini uniambukize Ukimwi” niliendelea kulalama huku machozi yakinitoka.

    Ghafla hali ya hewa mule ndani ilichafuka, yule jamaa alitoka akiwa na hasira dhidi yangu, nilimwona mtu yule kama alipandwa na majini kichwani mwake, sikutegemea kabisa kwa ukalimu alionionyesha awali kama angeweza kunibadilikia muda mfupi kiasi kile.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilibaki nikilia kwa uchungu, kwakweli sikujua nini hatma ya maisha yangu, kwa dakika zile chache nilijikuta nikikata tamaa vibaya mno, sikuona thamani ya uhai kwenye huu ulimwengu, kiotendo cha kuambukizwa ukimwi kiliniuma mno.

    Nikiwa sijawa vizuri kiakili mara Casper akarudi akiwa kama mbogo aliyejeruhiwa na risasi.

    “Toka toka humu ndani toka” alisema huku akinisukuma, alikuwa kifua wazi, mkononi alikuwa ameshikilia kamba pamoja na kisu chenye makali.

    Nilitoka nje, nilikutana na watu wengineambao kwa mwonekano walikuwa ni wafanyakazi wa meli ile, walionekana ni watu wenye kumwogopa sana Casper.

    “Mfunge kamba huyu kahaba” amri ilitolewa na Casper, upesi vijana wale walinidaka na kunifunga kamba miguu na mikono, haikuishia hapo walinifunga mwilini mwangu pamoja na chuma kizito.

    Nilitambua nini kinacho kwenda kutokea, nilitambua kinachokwenda kutokea ni kutupwa baharini nikiwa nimefungwa mikono na miguu sanjari na chuma kizito mwilini wangu.

    Nilijiona ni kiumbe mwenye bahati mbaya kwenye maisha, nilizaliwa kwenye familia masikini na nimekuwa ndani ya umasikini huo kwa muda mrefu, katika kipindi ambacho niliona nakwenda kubadilisha histria ya maisha yangu mara mambo yanabadilika na kukutana na majanga mazito na yenye kuogopesha.

    Machozi yalinibubujika, picha ya familia yangu ilijitengeneza kichwani mwangu, nilimia nilipobaini kuwa nakwenda kufa pasina wao kuona hata mwili wangu, wakati wote familia yangu itakuwa na amani kwa kuamini mtoto wao niko nchini Oman nikifanya kazi za ndani na mwisho wa siku nitarejea nyumbani na kubadilisha hali ya maisha ya nyumbani.

    Niliumizwa na nililia sana juu ya hilo, uchungu uliokuwa kifuani kwangu ulikuwa haumithiliki, niliamini mambo yote hayo chanzo chake ni umasikini na sasa nilikuwa nikionja chungu ya umasikini. Mpenzi msomaji pengine haya ninayo simulia leo unaweza kuona ni kama riwaya za kubuni, amini nakwambia mambo yote haya yemenitokea na hakuna hata moja la kubuni.

    Nikiwa nimejinamia nikiwaza na kuwazua mara nikastushwa na sauti ya Casper ikisema:

    “Mtupeni baharini huyo Kahaba” amri ilitoka.

    Hapohapo wakanibeba juu tayari kunitosa baharini, wakawa wanasogea ukingoni mwa meli tayari kwa kunitosa baharini. Nilinyanyua shingo yangu kwa juu kidogo nikaona bahari ikiwa na mawimbi mazito yaliyokuwa yakijipiga katika kuta za meli ile kubwa na kutawanyika kila mahali.

    Nikaona ubuluu wa maji mazito nikaendelea kubaini kuwa sehemu ile ilikuwa na kina kirefu, sikuwahi kujua kuogolea ingawa hata kama ningekuwa najua kuogelea bado nisingeweza kufanya lolote kwani mikono na miguu yangu ilikuwa imefungwa kwa kamba huku shingoni nikiwa nimefungwa kwa kamba nyingine iliyo unganishwa na chuma kizito.

    “Moja..mbili..tatu twendee!” wale jamaa walihesabu na hapohapo wakanirusha baharini, nilijibamiza kwenye maji ‘pwaaa’ maji yakaruka na kusambaa kila mahali, nikaanza kuzama kuelekea chini huku nikinywa vikombe kadhaa.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Moja..mbili..tatu twendee!” wale jamaa walihesabu na hapohapo wakanirusha baharini, nilijibamiza kwenye maji ‘pwaaa’ maji yakaruka na kusambaa kila mahali, nikaanza kuzama kuelekea chini huku nikinywa vikombe kadhaa.

    nilikuwa siwezi kufurukuta kwakuwa chuma kizito kilikuwa kimefungwa shingoni mwangu, mikono na miguu ikiwa imefungwa kwa kamba, nilipojaribu kuvuta hewa kwa ndani nikajikuta navuta maji mengi puani na mdomoni tendo hilo likanifanya nianze kutapatapa kwa namna halisi ya mafa maji.

    Nilibwia vikombe vya maji huku nikiwa sipati pumzi, hatimaye nikawa nazama kwa kasi kuelekea chini kabisa ya bahari, sikuwa na lakufanya zaidi ya kusubiri mauti, nafsi yangu ilikuwa tayari kabisa kufa.

    Nilibwia vikombe vya maji nikiwa sipati pumzi, nikaanza kuliona giza la ajabu mbele yangu, hatimaye sikujua tena kilicho endelea na kabla sijajua kilicho endelea nafsi yangu ilikiri kwamba mimi tayari ni maiti.

    ******

    “Jina lako nani?”

    “Nani?”

    “Wewe hapo”

    “Jina langu....jina langu... jina langu, dah nimelisahau”

    “Pole sana binti”

    “Pole ya nini?”

    “Umeokolewa na wanajeshi wa majini waliokuwa katika nyambizi wakielekea nchini Syria kulinda amani” Yalikuwa ni mazungumzo ya daktari mmoja akiongea na mimi niliyekuwa kitandani.

    Kauli ya mwisho ya daktari huyo ndiyo iliyofungua milango ya kumbukumbu zangu, mtiririko wa kumbukumbu zilianza kujaa kwenye kichwa changu mithili ya simu iliyokuwa imezimwa data kwa muda mrefu na sasa imefunguliwa.

    “Mungu wangu!”nilimaka.

    “Nini?”

    “Nimekumbuka kila kitu”

    “Kweli?”

    “Kabisa”

    “Haya sema, jina alako unaitwa nani?”

    “Naitwa Agripina”

    “Kwanini ulitupwa baharini?”

    “Ni stori ndefu, ila nataka kujua hapa niko wapi?”

    “Upo hosptali ya Ahlal bayty mjini Muscut”

    “Unataka kuniambia nimerudi nchini Oman”

    “Hujarudi ila umeletwa na wanajeshi wa kulinda amani nchini Syria, ndio walio okoa maisha yako”

    Nilishindwa kuelewa kama nilitakiwa kufurahia ama kulia, nchi ya Omani kwangu ilikuwa sehemu rafiki, sikutamani kabisa kuendelea kuishi juu ya mgongo wa ardhi ya nchi hiyo.

    Pamoja na kufikiria yote hayo mwisho wa siku nilimshukuru Mungu kwa kuendelea kuonyesha miujiza ya ajabu kabisa kwenye maisha yangu na kunifanya niendelee kuwa hai.

    Nililala pale kitandani kwa masaa mengi hadi badaye aliporudi tena yule daktari niliyekuwa nikizungumza naye.

    “Ulisema jina lako unaitwa Agripina?”

    “Ndiyo” nilijibu kisha nikamwona akiandika kwenye kitabu chake kidogo na kuondoka.

    Akaondoka, kama dakika kumi akarudi tena akiwa ameongozana na watu wengine wawili mwanaume na mwanamke. Wakaja na kukizunguka kitanda changu.

    “Agripina” aliniita.

    “Abee”

    “Unamfahamu huyu dada?” alisema akimsonta binti aliyeingia naye mule ndani.

    Nilipo mtizama vizuri yule binti nikamkumbuka ni yule mdada aliyenikuta ndani ya chumba nilichokimbilia kujificha nikiwa nakimbizwa na wanajeshi, ndani ya chumba kukiwa na mtu amelala muda mfupi mtu yule akaanza kukoroma huku akitokwa na damu mdomoni na puani kisha akafa.

    “Nisha mkumbuka”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi upo chini ya ulinzi kwa makosa ya mauwaji lakini pia kwa makosa mengine ya kutishia kuua na kufanya zinaa ndani ya nchi hii” alidakiza yule jamaa mwingine aliyeongozana na daktari.

    Alitoa pingu na kunifunga, kusema ukweli safari hii sikuwa na hofu hata kidogo, matukio na mikasa kwenye maisha yangu nilisha ona ni kawaida, nilichokuwa nangoja kwa wakati huo ni siku yangu ya kufa.





    Alitoa pingu na kunifunga, kusema ukweli safari hii sikuwa na hofu hata kidogo, matukio na mikasa kwenye maisha yangu nilisha ona ni kawaida, nilichokuwa nangoja kwa wakati huo ni siku yangu ya kufa.

    “Nafikiri hutakiwi kuendelea kulalia kitanda cha hosptali hii, utatakiwa kupelekwa selo, mahakamani kisha kutumikia adhabu utakayokuwa imetoka juu yako,” alisema tena yule askari aliyekuwa amevaa kiraia.

    Nilichukuliwa na kupelekwa selo, haikuwa selo ile ambayo niliwahi kupelekwa kipindi cha nyuma, hii ilikuwa ni tofauti, hii ilikuwa ni selo ambayo haikuwa na tofauti na selo za nchini kwetu. Nilichokikuta ndani ya selo hizo niliogopa.

    Kulikuwa na utitiri wa wasichana wa kitanzania ambao walikuwa ni mahabusu na wafungwa wenye mashtaka mbalimbali wengine walisha hukumiwa kifo huku wengine wakiongoja hukumu. Wengi wao walikuwa ni wasichana waliokwenda kufanya kazi za ndani.

    Pamoja na hali hiyo ya kuhuzunisha, Kwa mara ya kwanza nilijihisi siko peke yangu katika ulimwengu, kitendo cha kukutana na watanzani wenzangu ambao wengi wao walikuwa ni wenyeji wa Zanzibar, kilinipa matumaini mno, tulikaa pamoja na kuzungumza mambo mengi ya nyumbani Tanzania.

    Kila mtu alikuwa na kiu ya kurudi nyumbani lakini hilo lilibaki kuwa ndoto ya alinacha nyuma ya milango ya nondo.

    Siku chache badaye nilipelekwa mahakamani, sikuwa na imani na mahakama za nchi hiyo, namna kesi zilivyo endeshwa kwakweli zilimnyima mtuhumiwa haki ya kijitetea kwa kiwanngo kikubwa, jambo jingine ubalozi wa nchi yangu ulitupa kisogo kwa asilimi kubwa. Hatukuthaminiwa kama ambavyo raia wa kigeni wanavyo thamaniwa na balozi zao nchini kwetu.

    Nilihukuwa kifo, kwa kuzingatia kwamba nilisha wahi kunyongwa kwa kamba na badaye kurudiwa na fahamu nikiwa mochwari safari hii nilihukumiwa kuchomwa sindano ya sumu hadi kufa, haki niliyopewa ni mwili wangu kusafirishwa nchini kwangu hadi kijijini kwetu kwa ajili ya mazishi.

    Nilishukuru japo kwa hilo kwani niliona angalau sasa ndugu zangu watapata fursa ya kuona maiti yangu na kuzikwa kwenye ardhi ya nchi yangu, nafsi yangu haikuogopa kufa, ila kilichoniumiza ni kufa nikiwa na mtoto tumboni, hilo liliniliza machozi.

    “Usilie Agripina ndivyo maisha yalivyo, hujafa hujaumbika” mtu mmoja mwenyeji wa Zanzibar alinipa moyo.

    “Silii kwa sababu ya hukumu, namlilia mwanangu aliye tumboni”

    “Una mtoto tumboni?”

    “Ndio”

    “Nafikiri huwezi kutumikia adhabu ya kifo hadi pale utakapokuwa umejifungua mtoto”

    “Labda ngoja tusubiri” nilisema kinyonge huku matone ya machozi yakijikusanya kwenye macho yangu.

    Siku na miezi ikayoyoma, niliendelea kuishi ndani ya gereza kama mfungwa ninayesubiri siku ya kutumikia adhabu yangu ya kifo. Wakati nikingoja siku ya hukumu pia tumbo langu lilizidi kuwa kubwa.

    Siku moja nikafuatwa na askari magereza walikuwa kama sita, mikononi mwao walibeba bunduki, walinizunguka huku wakionekana kuwa makini na mimi, mmoja miongoni mwao akanisogelea na kunieleza ilibakiza wiki moja tu kabla ya kutumikia adhabu ya kifo.

    Nilihisi mate mepesi yakijaa mdomoni, pamoja na kwamba nilikuwa sina hofu dhidi ya kifo lakini kwa mara ya kwanza nikahisi mwili ukinisisimka, hofu ikanisambaa kifuani mwangu, taswira ya tukio la mtu kunyongwa likajitengenza kwenye akili yangu, kwa kweli niliogopa mno.

    Walipoondoka wale askari, wafungwa wenzangu walinifuata na kuniuliza nilikuwa naambiwa nini, niliwaeleza yote nilioambiwa na wale askari wa kiarabu, simanzi na hofu ilienea katika nyuso za wafungwa hasa Watanzania wenzangu ambao pia walihukumiwa kifo.

    “Ndiyo maana wameanza kuwa makini na wewe, kuanzia leo unaweza usiwe na sisi tena ndani ya selo, unajua siku za mfungwa kunyongwa zikikaribia huwa anawekwa mbali na watu kwa imani kwamba anaweza kufanya lolote dhidi ya mtu yeyote ili mradi asife peke yake” alisema mfungwa mmoja miongoni mwa waliokuja kunipa pole.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Saa kumi na mbili jioni niliojiwa tena na wale askari wenye bunduki, kama alivyonieleza yule mfungwa mwezangu nilihamishwa na kupelekwa katika selo ya peke yangu, niliingizwa kwenye chumba kimoja kizuri ambacho kilikuwa na kila kitu cha thamani, chumba hicho kilikuwa ndani ya jela hiyo.

    Sikujua mantiki ya kuingizwa kwenye chumba nadhifu ingawa wakati mwingine nilihisi hizo ni itifaki za kumkirimu mtu ambaye hukumu yake ya kifo ipo jirani, hata hivyo wakati mwingine nilipingana na fikra hizo kwa kuwa mwanzoni nilipohukumiwa kifo sikufanyiwa ikhisani ya mambo haya.

    Niliishi ndani ya chumba kile nadhifu, kila siku nikiletewa vyakula vizuri ambavyo nafikiri vingine sijawahi kuvila hadi leo ninaposimulia mkasa huu. Wiki ile moja ilienda harakaharaka hatimaye siku ya hukumu ikafika.

    Walikuja askari wenye bunduki na kunitoa nje ya chumba kile, nilifungwa minyororo miguuni, mnyororo huo ukaunganishwa na shingo yangu ukapita hadi mikononi, kisha nikavikwa soksi nyeusi usoni.

    Nilishikwa bega kwa nguvu na askari mmoja miongoni mwa waliokuwa wamenizunguka huku mkono mmoja wa askari yule ukiwa umekamata silaha yake vizuri.

    Akawa ananiongoza na kunipeleka mahali nisikokujua, mapigo yangu ya moyo yakawa yananidunda “duk duk duk” nikaanza kutokwa jasho mwilini, hofu ya kifo ikawa kubwa, hatimaye nikaanza kulia, machozi na kamasi vilinitoka ndani ya ile soksi nyeusi iliyofunika uso wangu. Hata hivyo hakuna aliyejali hilo..

    Nilifikishwa ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa na baridi kali kisha nikaondolewa ile soksi usoni, nikashangaa nilipojikuta nipo ndani ya mochwari, moyo wangu ukalipuka “paaa” niliogopa.

    Ndugu msomaji hapa ngoja niseme kitu, hakuna hukumu mbaya ambayo inavuruga saikorojia ya mtu kama hukumu ya kifo, kama wadau wa sheria watapata bahati ya kusoma maandishi haya ni vema wakafanyia marekebisho sheria hii kwani sheria hii inamtafuna binadamu kisaikolojia kabla ya kuitumikia.

    Baadhi ya nchi za ulaya na Marekani, sheria ya hukumu ya kifo haipo kidogo na baadhi ya nchi za Afrika, lakini kwa bara la Asia bado sheria hii inaendelea kutesa saikolojia ya binadamu kwa kiwango kibaya sana.

    Basi, baada ya kujiona nipo ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti nilianza kuhisi kizunguzungu, maiti nyingi zilikuwa zimetapakaa chini huku zikiwa zimefunikwa kwa mashuka meupe, kulikuwa na harufu kama ya jiki (ile dawa ya kuondoa madoa), nikatambua hiyo ni dawa ambazo maiti zile zimechomwa ili pengine zisiharibike.

    Nafsi yangu ikazidi kuzongwa na jinamzi la hofu baada ya kubaini kuwa kumbe na mimi dakika chache nitakuwa maiti kama zile zilizolazwa pale chini kisha nitachomwa sindano yenye dawa ambayo ina harufu ya jiki kisha nitalazwa chini na kufunikwa shuka jeupe nikingoja kuzikwa.

    “Mlazeni juu ya kitanda” alisema daktari huku akivuta sumu kwa kutumia sindano kwenye kichupa kidogo.

    Nilishikwa na askari wawili nikalazwa juu ya kitanda, nikawa nimelala chali, mtoto wangu aliyekuwa tumboni nikamsikia akichezacheza. Machozi yalinitoka.

    “Tutaonana mbinguni kwa baba mwanangu, samahani kwa kutumikia adhabu yangu, pengine ni sahihi tu kufa na mama yako maana kama usipokufa sasa utakufa baadae kwa ukimwi ambao naamini tayari nimekwisha kuambukiza”

    Nilizungumza maneno hayo kwa kunong’ona huku nikisubiri kudungwa sindano yenye sumu hadi kufa, nilimwona daktari yule akiinyanyua sindano iliyokuwa imejazwa dawa ya tetrodotoxin ambayo ni sumu maalumu kwa kuulia watu waliohukumiwa kifo, akaibonyeza kidogo ile sindano matone madogo ya sumu yakaruka angani, kisha akanisogelea pale kitandani nilipolazwa tayari mkononi akiwa amekamata sindano tayari kwa kunidunga.

    “Nina mimba jamani, msiniue” nilisema huku nikilia, macho yangu yakimtizama mtu yule kwa huruma.

    “Nina mtoto tumboni baba yangu niache tafadhali, usinichome sindano ya sumu” niliendela kulalama, hakuna kilicho badilika, mtu yule hakuwa na taimu na mimi, ilivyo onekana alikwisha zoea huruma zile, kwahiyo jambo lile mbele yake ilikuwa ni kitu cha kawaida, hakunijali kabisa hata usoni hakuniangalia.

    Alitizama saa yake ya mkononi nikaona ameganda kwenye saa hiyo, ni kama alikuwa akingoja muda fulani uwadie ndipo afanye kazi yake, naam hisia zngu zilikuwa sahihi kwani baada ya sekunde kadhaa akanigeukia tena na kunikabili.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mfungeni mikanda” alitoa amri, askari wenye bunduki wakaanza kufanya kazi hiyo, pamoja na kwamba nilifumgwa minyororo mikono na miguu lakini nilifungwa tena mikanda.

    Nikawa siwezi kufurukuta, jamaa alinisogelea tena akiwa na sindano mkononi, akanijia usawa wa shingo yangu kisha akaniinamia na kunidunga sindano ile ya sumu kwenye shingo yangu.

    Nilifumba macho wakati tendo hilo linafanyika ingawa niliusikia uchungu wa sindano ile hasa wakati daktari anaibinya sumu ya tetrodotoxin kuingia ndani ya mishipa ya mwili wangu.





    Sekunde tatu zilitosha kunifanya nianze kuona maluweluwe, nikajiona napatwa na maumivu makali mwili wote, yalikuwa ni maumivu kama vile nababuliwa na moto, nikataka kupiga kelele mdomo nao ukawa mzito, mara povu zito likaanza kunitoka modomoni.

    Giza la ajabu likazikumba mboni zangu, muda mfupi badae sikujua tena kilicho endelea duniani.

    *********

    “Agripina, we Agripina, Agripina amka, amka upesi!” nilisikia sauti ikiniamsha, sauti hiyo haikuwa ngeni masikioni mwangu, nilifumbua macho kivivu, ingawa niliona kwa mbali lakini sura ya mtu ninaye mfahamu ilijidhihilisha mbele yangu.

    “Mama!”

    “Bee mwanangu”

    “Nmekufa na mungu ameniingiza peponi!”

    “Hahaha! hapana mwanangu, upo kijiji cha Makose wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, hujafa”

    “Nipo Makose!i inamaana niko Tanzania?” niliuliza huku macho yangu yakitizama huku na kule ndani ya chumba ambacho pia hakikuwa kigeni machoni mwangu

    Kabla mama yangu hajanipa jibu mara akaingia mtu ambaye sikumtegemea kumwona, alikuwa ni Mariamu Rashidi huyu ni yule wakala wa wasichana wa kazi wanaokwenda kufanya kazi za ndani nchini ya Oman, alikuja na kuketo karibu yangu.

    “Mambo Agripina, naona mzimu wa kifo uliokukumba Oman umekurejesha Duniani” alisema kwa masikhara huku akiachia tabasamu pana na kuketi karibu yangu.

    Nikiwa sijakaa sawa nikendelea kushangazwa na utitiri wa ndugu walioingia ndani ya chumba kile nilichokuwa nimelala. Kila ndugu aliyekuja kuniona alionekana kufurahi kwa kuona nikiwa hai.

    “Naombeni tusikilizane jamani” alisema Mariamu, ndugu wote waliokuwa mule ndani wakanyamaza.

    “Kila mtu angependa kujua nini kilifanyika hadi Agripina kwa sasa yupo hai ilihali taarifa zilienea kuwa tayari binti huyu kisha chomwa sindano ya sumu na kafa” aliposema sentesi hiyo watu wote walijenga utulivu zaidi ili kujua nini kilitokea.

    “Kwanza kabisa shukrani na pongezi zote anastahili mwenyezi Mungu kwakuwa ni yeye ndiye anayejua nini hatma ya maisha ya mja wake, Agripina alikuwa katika hukumu ya kifo na alikwisha ingizwa katika chumba cha kuhifadhia maiti tayari kwa kuchomwa sindano yenye sumu.

    “Kitu ambacho wanajeshi na serikali ya nchi ya Oman haifahamu hadi sasa ni kwamba mtu anayehusika na kutoa adhabu ya kuwachoma watu sindano ya sumu nilimuhonga Dolla 600 ili mradi afanye lolote lile kumwepusha binti huyu na kifo.

    “Siku ya hukumu ya Agripina ilipowadia mipango yote ilikuwa sawa, alichofanya mtu yule ni kumdunga Agripina sindano yenye dawa ya Ketamine benzodiazepine ambayo ilimfanya apatwe na maumivu makali sanjari na kumtoa povu mdomoni lakini ambacho askari waliokuwa hawajui ni kwamba chupa yenye sumu aina ya tetrodotoxin chupa hiyo ilikuwa na dawa ya benzodiazepine ambayo ilikuwa ni dawa ya usingizi.

    “Baada ya Agripina kupoteza fahamu kilichofuata ilikuwa ni kuusafirisha mwili wake kama ambavyo mahakama ya nchi ile ilivyokuwa imeahidi, kwahiyo tulimsafirisha Agripina akiwa kama maiti hadi hapa Tanzania, hivyo ndivyo ilivyokuwa” alimaliza kusimulia Mariamu.

    Kila mtu mule ndani maelezo yale yalimsisimua, kwakweli hata mimi nafsi yangu ilikiri kuwa Mungu hashindwi na jambo. Nilipewa pole nyingi na ndugu na jamaa, ilikuwa ni furaha kubwa mno kwa mama yangu, wakati wote alikuwa akibubujikwa na machozi. Kwa upande wangu, jambo lile nililiona ni kama ndoto nzuri inayopita kichwani mwangu.

    Muda mfupi baadaye ilikuwa ni zamu yangu kusimulia mambo yote yaliyo nisibu tangu siku ya kwanza naikanyaga ardhi ya nchi ya Oman, hadi nafika nukta ya mwisho kila kila mtu alilia machozi

    Ndugu zangu waliumizwa zaidi kusikia naisha na maambukizi ya virusi vya Ukimwi hata hivyo hapakuwa na mwenyekuweza kubadili ukweli wa jambo hilo.

    Maisha yaliendela kama kawaida nikiwa kijijini kwetu Makose, miezi michache badaye nilijifungua mtoto wa kiume ambaye kwa bahati mbaya pia alizaliwa akiwa anamambukizi ya virusi vya Ukimwi.

    Wito wangu kwa wasichana wenzangu wa kitanzani hasa wenye ndoto za kwenda kufanya kazi za ndani nchi za nje ni vema mkawa makini huko mwendako, bila kuwa makini unaweza kujikuta unatumbukia katika shimo la mauti bila kutegemea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kabla ya kusema kwaheri. Napenda nimshukuru mwandishi wa mkasa huu, kaka yangu Ally katalambula ambaye alibadilisha maelezo yangu kuwa maandishi yaliyonakshiwa na kachumbali za kifasihi.

    MWISHO!.

0 comments:

Post a Comment

Blog