Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

SIRI YA MKE - 1

 





    IMEANDIKWA NA : PATRICK J. MASSAWE



    *********************************************************************************



    Simulizi : Siri Ya Mke

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    GIZA lilikuwa limeshatanda kote angani usiku ule, na ni sehemu chache tu ndizo zilizoonekana kuwa na mwanga wa taa, hasa katika majumba ya watu na hata katika taa za barabarani. Hali ya utulivu ilishaingia na baadhi ya watu kujifungia ndani, ni baadhi yao tu ndiyo walioonekana wakipita huku na kule mitaani, na wengine wakijirudisha majumbani mwao kwa usafiri wa daladala, baada ya mihangaiko ya mchana kutwa ya kutafuta riziki.

    Wakati hayo yakijiri, kunako majira ya saa mbili na robo za usiku ule, mzee Joel Kisamo, akiwa na mtoto wake wa kiume, Geofrey, walikuwa wamekaa faragha katika kibaraza cha nyumba yao, iliyoko katika mtaa mwembamba, eneo la Kijenge Kati, jijini Arusha. Pale walipokaa, walikuwa pia wakiburudika na vinywaji laini huku wakiongea mambo mengi yanayohusu maisha kwa ujumla, na jinsi ya kukabiliana nayo katika karne hii ya ishirini na moja.

    Ingawa kibaridi cha mwezi Oktoba, kilikuwa kinapuliza kutoka kilele cha mlima Meru, hakikuwazuia kuendelea na mazungumzo yao, ambayo mzee Kisamo alikuwa akiyasubiri kwa hamu, kwani alikuwa ameitikia wito wa mwanae, Geofrey, baada ya kumtaarifu kuwa alimhitaji kwa mazungumzo muhimu, na akiwa kama mtoto wake wa kwanza, mzee Kisamo hakumkatalia. Mazungumzo yao yalifikia pale Geofrey alipoamua kumweleza ukweli baba yake, kuhusu nia yake ya kutaka kuoa, baada ya kuwa mtu mzima sasa, mwenye kuweza kujiamulia mambo yake mwenyewe.

    Vilevile ilikuwa ni baada ya yeye Geofrey kuona vijana wenzake wa umri wake wakioa na kumiliki miji yao na kuziendesha familia zao, kiasi cha kujijengea heshima mbele ya jamii inayowazunguka. Kamwe Geofrey hakupenda adharauliwe na watu kwa kumtolea maneno mabaya kuhusiana na maumbile yake aliyokuwa nayo muda mrefu sasa, ikiwa ni hali ambayo hakupenda kuiweka bayana, ili watu waweze kuijua, zaidi ya kuwa siri yake. Baada ya kumaliza mazungumzo mengine na baba yake, ambayo siyo rasmi, Geofrey alivuta pumzi ndefu na kuzishusha. Kisha akamwangalia baba yake, kana kwamba ndiyo kwanza alikuwa anamwona.

    “Baba…” Geofrey akamwita kwa sauti ndogo yenye adabu.

    “Mwanangu…” mzee Kisamo akaitikia huku naye akimwangalia kwa makini mwanae.

    “Nashukuru sana baba, kwa kunikubalia wito wangu wa kuonana na mimi, kwa ajili ya mazungumzo muhimu.”

    “Hakuna tatizo mwanagu, nakusiliza…”

    “Unajua baba, mimi nimeshakuwa mtu mzima sasa,” Geofrey akaendelea kumwambia baba yake..

    “Hilo naelewa,” mzee Kisamo akasema huku akiwa na shauku ya kutaka kujua mwanae anataka kuongelea kitu gani.

    “Napenda kukufahamisha kwamba nimepata mwenzangu.”

    “Umepata mwenzako?”

    “Ndiyo,” Geofryey akasema na kuongeza. “Nikiwa na maana ya mchumba.”

    “Umepata mchumba mwanangu?” mzee Kisamo akamuuliza.

    “Ndiyo baba…”

    “Vizuri sana..” mzee Kisamo akasema huku akisita kidogo, kisha akaendelea. “Nimekuelewa mwanangu, umeniambia kuwa umepata mchumba, je, umejiandaa vya kutosha?”

    “Ndiyo, nimejiandaa baba…”

    “Sawa, kama umejiandaa, unaweza kunidokezea mchumba mwenyewe ni nani?”

    “Mchumba wangu ni Grace, mtoto wa mzee Ramson Laiza, natumaini unamfahamu baba.”

    “Ndiyo, namfahamu sana si amezaliwa na kukulia hapahapa kwenye kitongoji chetu cha Kijenge?”

    “Basi, ndiyo huyo baba, mimi nimempenda, na yeye vilevile kamenipenda.”

    “Lakini mwenyewe anaelewa hilo?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo baba, anaelewa hilo. Tumeshakubaliana, isipokuwa nilikuwa natafuta muda muafaka wa kukueleza wewe, ili taratibu nyingine zifuate, ikiwa ni pamoja na kupeleka posa.”

    “Sawa mwanangu. Nashukuru sana kwa kunifahamisha jambo hili, ambalo ni la muhimu sana. Hivyo mambo mengine itabidi utuachie sisi wazee wako,” mzee Kisamo akamwambia baada ya kuimwelewa vizuri.

    “Nashukuru sana baba,” Geofrey akasema huku akiwa na matumaini baada ya ujumbe wake kufika.

    “Haya mwanagu, suala lako limefika, je, kuna jingine?” mzee Kisamo akamuuliza.

    “Hakuna jingine baba…”

    “Kama hakuna jingine, basi mimi nakwenda kupumzika.”

    “Sawa baba, usiku mwema…”

    Halafu hatua iliyofuata ni kila mmoja aliondoka kuelekea chumbani tayari kwa maandalizi ya kulala, ambapo Geofrey alielekea katika chumba chake kilichokuwa upande wa nyuma wa nyumba ile kubwa, ambayo ilikuwa imejitenga na upande ule waliokuwa wanaishi wazazi wake. Ina maana alikuwa anajitegemea kila kitu upande ule bila kuleta usumbufu, ukizingatia alikuwa bado anaishi katika mji wa baba yake.

    Mzee Kisamo alielekea ndani, katika nyumba kubwa, aliyokuwa anaishi na mke wake, Bi. Bernadeta. Baada ya kuingia chumbani, mzee Kisamo akakaa kwenye kiti na kuanza kutafakari juu ya kuelezwa na mwanawe nia ya kuoa. Hakika alikuwa amechanganyikiwa badala ya kufurahi kupata mkwe! Ni kwa nini lakini?

    Wakiwa chumbani, mzee Kisamo na mkewe, Bi.Bernadeta, waliingia kwenye mjadala mkali usiku ule, punde tu baada ya mtoto wao, Geofrey kumweleza baba ayake kwamba alikuwa anataka kuoa. Mzee Kisamo hakupenda kulificha jambo lile, na kuliacha limemkaa rohoni bila kumwambia mkewe.

    “Mama Geofrey…” mzee Kisamo alimwita.

    “Bee…” Bi. Bernadeta aliitikia huku akimwangalia mume wake.

    “Hivi unajua alichoniitia mwanetu Geofrey usiku wa leo?”

    “Siwezi kuelewa kwa vile hujaniambia. Kwani alikuwa na shida gani?”

    “Basi, alichoniitia Geofrey, ni kwamba anataka kuoa!”

    “Geofrey anataka kuoa?”

    “Ndiyo hivyo. Ni maelezo yake aliyonieleza baada ya kuomba kukutana na mimi…” mzee Kisamo alisema na kuendelea. “Amenitamkia wazi kwamba amepata mchumba, ambaye wamependana, na wameamua kuoana!”

    “Mungu mkubwa, basi litakuwa jambo la furaha, je, amekutajia huyo mchumba ni nani?” Bi. Bernadeta alimuuliza huku akitabasamu kutokana na habari zile, hasa ukizingatia Geofrey alihisiwa kuwa hakuwa mwanaume rijali!

    “Amenitajia kuwa mchumba wake ni Grace, mtoto wa mzee Ramson Laiser…”

    “Aisee, vizuri sana, mtoto yule ana heshima sana, hivyo atamfaa.”

    “Kwa hivyo umeamuaje mke wangu?”

    “Niamuae nini, si tupange mipango ya posa itumwe kwa wazazi wake?”

    “Lakini…” mzee Kisamo alisema, halafu akasita kuendelea.

    “Lakini nini?” Bi. Bernadeta akauliza.

    “Unajua kuna jambo moja linanitatiza, ambalo nilishawahi kukwambia?”

    “Jambo gani tena?”

    “Ni juu ya Geofrey kutomwona akiwa na uhusiano na watoto wa kike. Pia, habari zimeenea kuwa siyo mwanaume rijali! Sasa unauchukuliaje huo uamuzi wake wa kutaka kuoa?”

    “Wala jambo hilo lisikutie shaka…maadam ameamua mwenyewe, tumkubalie na kukamilisha matakwa yake. Huenda mambo yake yamekuwa mazuri hasa ukizingatia siku hizi kuna dawa nyingi za miti shamba…” Bi. Bernadeta alisema kwa msisitizo, akiwa na matumaini.

    “Basi, hakuna tatizo, nitajipanga na kutuma washenga, pindi tutakapokaa tena na Geofrey na kufahamu amejiandaa vipi kwa ajili ya harusi yake,” mzee Kisamo alisema kwa sauti ndogo, lakini roho yake ikiwa nzito.

    Hata hivyo, baada ya mazungumzo yao yale, hatimaye waliufunga mjadala ule baada ya kukubaliana Geofrey aoe, na taratibu za kutuma washenga zifanyike. Ni utaratibu uliotakiwa udumishwe kiutamaduni wa kimila unaotumiwa na makabila ya Kanda ya kaskazini.

    Mzee Kisamo na mkewe, hawakuendelea na maongezi zaidi ya kujitupa kitandani na kulala, kuashiria kupita kwa siku ile ya aina yake. Hata hivyo, usingizi haukumpata mapema mzee Kisamo, zaidi ya kuendelea kuwaza. Kumbukumbu ziliendelea kumwandama mzee Kisamo usiku huo punde baada ya kujitupa kitandani…





    ******

    MZEE Kisamo alivuta kumbukumbu zake, kuwa siku za nyuma, wakati mmoja, aliwahi kumwuliza mke wake, juu nya mtoto wao wa kwanza, kwa hali ile aliyokuwa nayo, ambayo ilitofautiana na vijana wa rika lake. Wakati huo bado Geofrey alikuwa kijana mdogo, ndiyo kwanza alikuwa anasoma Shule ya Sekondari ya Enaboishu, jijini Arusha.

    “Mama Geofrey…” mzee Kisamo alimwita mkewe.

    “Nakusikiliza baba Geoff…” Bi. Benadeta alisema huku akimwangalia.

    “Kuna jambo moja nataka kukuuliza…” mzee Kisamo alisema na kuendelea. “Nimevumilia kwa muda mrefu sasa, lakini inabidi leo kulisema bayana.”

    “Sema tu jambo hilo, nakusikiliza…”

    “Hivi huyu mwanetu Geofrey, si karibu ana miaka ishirini sasa?”

    “Ndiyo, anakimbilia miaka ishirini…kwani vipi?”

    “Nauliza hivyo kwa sababu sijawahi kumwona akizungumza na vijana wenzake!” Mzee Kisamo alisema huku akimkazia macho mkewe na kuendelea. “Yeye amekuwa ni mtu mkimya kimya tu…”

    “Unasema hazungumzi na vijana wenzake?” Bi. Benadeta alimuuliza. Ni kwamba alikuwa hajamwelewa kabisa!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo, vijana wenzake!” Mzee Kisamo alisisitiza!

    “Si kweli, mbona ni mara nyingi tu marafiki zake huwa wanamtembelea hapa nyumbani?”

    “Vijana gani hao?”

    “Si wale wa mtaa wa pili, kama vile, Juma, Patrick, Innocent…”

    “Ah, wale huwa nawaona. Lakini mimi sina maana hiyo mke wangu!” Mzee Kisamo akamkatiza.

    “Kumbe una maana gani?”

    “Nina maana watoto wa kike! Na Geofrey sijamwona hata siku moja kasimama na binti yeyote hapa mtaani, hivyo nina wasiwasi kama kujana wetu ni mzima! Hayuko kamili!”

    “Kumbe ulikuwa na maana wasichana?”

    “Ndiyo manaake…”

    “Ukweli hata mimi sijui…”

    “Basi elewa hilo. Sisi kama wazazi wake, inatupasa kulijua suala hilo, pamoja na kumchunguza, ukizingatia ni mtoto wetu wa kwanza, na ambaye anapaswa kutuletea wajukuu wetu!” Mzee Kisamo aliendelea kusema kwa wasiwasi!

    “Na kweli, ni wajibu wetu kumchunguza. Basi, itabidi tufanye hivyo kuanzia sasa, kwani tunahitaji wajukuu…” Bi. Bernadeta alimaliza kusema, ingawa kwa namna moja ama nyingine, tatizo la mtoto wake alikuwa analifahamu kutoka udogoni wake, lakini kamwe hakutegemea kama ingefikia katika hali kama ile, alijua tatizo lile lingetengamaa kadri siku zinavyosonga!

    Basi, kumbukumbu ile ndiyo ilimjia mawazoni mzee Kisamo usiku ule ambapo Geofrey alimweleza nia yake ya kutaka kuoa. Lakini baada ya kuoa yule mke, angampa nini, wakati wenzake wanaoa kwa lengo la kupata watoto watakaomsaidia katika maishan ya baadaye?

    Si hayo tu, mke ndani ya nyumba hafuati kula, kuvaa wala kulala, kwani vyote alikuwa anavipata kwa wazaza wake. Daima siku zote mke ndani ya nyumba anafuata unyumba, na si vinginevyo! Sasa Geofrey, mwanawe, ndiyo huyo anataka kuoa, je, angeweza kumridhisha huyo mke anayemsema?

    Hakujua!

    Ukweli ni kwamba Geofrey alimtongoza Grace kwa kumjaribu tu, na pia kuwaridhisha rafiki zake ambao walikuwa wakimsema sema ovyo kutokana na tabia zake za kuwakwepa wanawake! Na yote ile ili aonekane ni mwanaume rijali kabisa. Lakini kitu ambacho hakukitegemea, ni ile kukubaliwa haraka sana na Grace, na urafiki wao ukaanza kwa kasi kubwa mithili ya moto katika nyasi kavu nyikani! Ni urafiki ambao siyo wa kukutana kimwili, ambapo kwa Grace aliona kama kitu cha kawaida, kwani hakulikimbilia sana suala lile la kukutana kimwili.

    Ndipo Geofrey na Grace walipokaa na kupanga kuoana, wawe kitu kimoja, mume na mke. Baada ya makubaliano yale, ndipo Geofrey alipomweleza baba yake azma yake ya kuoa siku ile usiku! Baadala ya habari hizo kupokewa kwa furaha, ikawa kama vile kituko cha mwaka!

    *******

    UPANDE wa pili, Geofrey Kisamo, aliyekuwa ameingia chumbani kwake, alikuwa amejilaza kitandani akiwa na mawazo mengi, ikiwa ni baada ya kumweleza baba yake kwamba alikuwa anataka kuoa. Ingawa ni kweli alikuwa amechukua uamuzi ule, lakini nafsi yake ilikuwa inamsuta ukizingatia tangu azaliwe na kuwa mtu mzima, hakuwahi kufanya tendo la ndoa, au na kuwa na hamu ya kufanya ngono.

    Akiyavuta mawazo yake, ni kwamba yeye alijikuta akiwa katika hali ile, punde tu alipopata akili. Lakini hali hiyo aliendelea nayo hadi alipofikisha umri wa balehe na kuingia katika utu uzima. Pale ndipo lilipokuwa tatizo, kwa vile alikuwa ni kijana mtanashati na kivutio kwa wasichana waliokuwa wakimfuatilia kwa wingi walipokuwa katika shule ya sekondari.

    Basi hali aliyokuwa nayo ni ndiyo hiyo, pamoja na kufuatwa kote, lakini hakuwa na msisimko wowote mwilini mwake. Ukweli ni kwamba ilikuwa inasemekana yeye alikuwa na matatizo ya kimwili, hakuwa na nguvu za kiume, kikiwa ni kilema alichokuwa amezaliwa nacho. Sasa lile wazo la kutaka kuoa hakujua alikuwa amelitoa wapi masikini! Katika kukua kwake, hakuwahi kuonekana hata siku moja akizungumza au kujishughulisha na wanawake!

    Geofrey alitambua kuwa, siyo mzee Kisamo tu, baba yake, aliyekuwa akimshangaa, bali hata baadhi ya marafiki zake, aliokuwa anasoma nao shule. Walikuwa wakimshangaa baada ya kumwona akiwa mbali na wanawake zaidi ya kujisomea tu. Ina maana hata ule utani wa kitoto ambao wanafunzi huwa wanataniana mashuleni, au hata mchezo wa kujificha usiku hakuwahi kushiriki, kitu ambacho huwa kinaashiria kuwa kijana wa kiume ni rijali!

    Kihistoria, Geofrey Joel Kisamo, alikuwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu wa mzee Joel Kisamo, pamoja na mke wake, Bi. Bernadeta Machuwa. Mtoto wa pili alikuwa ni Patricia, ambaye ni wa kike wa pekee na wa tatu ni Deo, ambaye ni kitinda mimba, na wakati ule alikuwa anasoma shule ya sekondari. Geofrey na Patricia walikuwa wameshamaliza shule muda mrefu, na walikuwa wakiendelea na shughuli zao. Hakika mzee Kisamo alijitahidi kuwasomesha watoto wake, kwani aliithamini elimu ambayo ni msingi wa maendeleao.

    Geofrey, akiwa na umri wa miaka ishirini na tisa kwa wakati ule, awali, alifanikiwa kusoma mpaka kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Enaboishu, na baada ya kumaliza, ndipo alipojiunga na chuo kimoja cha binafzi na kusomea kozi inayohusu shughuli za Usafirishaji na upokeaji wa mizigo, ‘Clearing and Fowarding,’ kwa muda wa miaka mitatu. Baada ya kumaliza masomo yake, alifanikiwa kupata Diploma yake katika shughuli zile, ambapo aliweza kuajiriwa na kampuni moja binafsi, iliyokuwa inafanya kazi zake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

    Kwa upande wa Arusha, ofisi ya kampuni ile, ilikuwa ndani ya moja ya majengo ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) kilichoko katikati ya jiji la Arusha.. Basi akiwa katika mizunguko yake ya kikazi ndani ya majengo yale, ndipo alipokutana na mwanadada mrembo, Grace Ramson Laiser, ambapo kila mmoja alikuwa katika mihangaiko kwenye ofisi nyingine zilizokuwepo pale.

    Grace alikuwa ni mwanadada mwenye umri wa miaka ishirini na minne, ambapo alikuwa na sifa zote za kuitwa mrembo, akiwa msomi mwenye elimu ya kidato cha nne, na pia alikuwa amezaliwa na kukulia kwenye familia inayofuatilia maadili ya kidini, hususan ya kikristo. Kwa vile Geofrey alikuwa ni kujana mwenye wajihi wa kupendeza, alimvutia Grace, mwanadada wa kiarusha, kiasi kwamba Geofrey alipotupa ndoana yake haikuacha kunasa!



    ***********



    Geofrey, akiwa na umri wa miaka ishirini na tisa kwa wakati ule, awali, alifanikiwa kusoma mpaka kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Enaboishu, na baada ya kumaliza, ndipo alipojiunga na chuo kimoja cha binafzi na kusomea kozi inayohusu shughuli za Usafirishaji na upokeaji wa mizigo, ‘Clearing and Fowarding,’ kwa muda wa miaka mitatu. Baada ya kumaliza masomo yake, alifanikiwa kupata Diploma yake katika shughuli zile, ambapo aliweza kuajiriwa na kampuni moja binafsi, iliyokuwa inafanya kazi zake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.

    Kwa upande wa Arusha, ofisi ya kampuni ile, ilikuwa ndani ya moja ya majengo ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) kilichoko katikati ya jiji la Arusha.. Basi akiwa katika mizunguko yake ya kikazi ndani ya majengo yale, ndipo alipokutana na mwanadada mrembo, Grace Ramson Laiser, ambapo kila mmoja alikuwa katika mihangaiko kwenye ofisi nyingine zilizokuwepo pale.

    Grace alikuwa ni mwanadada mwenye umri wa miaka ishirini na minne, ambapo alikuwa na sifa zote za kuitwa mrembo, akiwa msomi mwenye elimu ya kidato cha nne, na pia alikuwa amezaliwa na kukulia kwenye familia inayofuatilia maadili ya kidini, hususan ya kikristo. Kwa vile Geofrey alikuwa ni kujana mwenye wajihi wa kupendeza, alimvutia Grace, mwanadada wa kiarusha, kiasi kwamba Geofrey alipotupa ndoana yake haikuacha kunasa!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ukweli ni kwamba Geofrey alimtongoza Grace kwa kumjaribu tu, na pia kuwaridhisha rafiki zake ambao walikuwa wakimsema sema ovyo kutokana na tabia zake za kuwakwepa wanawake! Na yote ile ili aonekane ni mwanaume rijali kabisa. Lakini kitu ambacho hakukitegemea, ni ile kukubaliwa haraka sana na Grace, na urafiki wao ukaanza kwa kasi kubwa mithili ya moto katika nyasi kavu nyikani! Ni urafiki ambao siyo wa kukutana kimwili, ambapo kwa Grace aliona kama kitu cha kawaida, kwani hakulikimbilia sana suala lile la kukutana kimwili.

    Ndipo Geofrey na Grace walipokaa na kupanga kuoana, wawe kitu kimoja, mume na mke. Baada ya makubaliano yale, ndipo Geofrey alipomweleza baba yake azma yake ya kuoa siku ile usiku! Baadala ya habari hizo kupokewa kwa furaha, ikawa kama vile kituko cha mwaka!



    *******

    ULIKUWA ni mchana mmoja wa jumapili, majira ya saa nane na nusu hivi, wakati mwanadada mrembo, na mwenye heshima ya hali ya juu, Grace Ramson, alikuwa amekaa faragha na mama yake mzazi, Bi. Letisia. Walikuwa wamekaa ndani, katika sebule ile nadhifu, wao wawili tu, ikiwa ni baada ya Grace kumwomba wakutane, kwa vile alikuwa na mazungumzo muhimu. Ni mazungumzo yaliyohitajika kuongelewa wao wawili tu, kwa utulivu wa hali ya juu.

    Hivyo basi, akiwa ni mtu mwelewa, mama yake alimkubalia na ndipo walipokutana pale sebuleni tayari kwa maongezi hayo. Baada ya kuongea mambo mengine ya kifamilia kwa ujumla, ndipo Grace alipobadilisha mazungumzo, na kumgusia mama yake juu ya kupata mchumba, ambaye wamekubaliana kuoana na kuwa kitu kimoja. Hakumficha juu ya mchumba wake huyo, bali alimtobolea kuwa ni Geofrey Kisamo, mtoto wa mzee Joel Kisamo, ambaye anaishi eneo lile lile la Kijenge ya Kati. Baadaye Grace akamalizia kwa kusema:

    “Basi, ndiyo hivyo mama, ninapenda kuwataarifu rasmi kuwa mchumba wangu, mume mtarajiwa ni Geofrey Joel Kisamo, mtoto wa mzee Kisamo…”

    “Nimeshakuelewa mwanangu, si unasema mchumba wako ni Geofrey, yule kijana mpole na mtaratibu sana?”

    “Ndiye huyo mama.”

    “Aisee,” Bi. Letisia akasema huku mawazo yake yakijigonga kichwani mwake. Ukweli ni kwamba, alishangaa baada ya Grace kumwambia mchumba wake ni Geofrey, kijana waliyekuwa wanamzungumzia sana pale mtaani, kwamba hakuwa na mishughuliko yoyote na wanawake, na pengine hakuwa mzima! Hata hivyo hakuwa na uwezo wa kumkatalia kwa vile hakuwa na sababu zozote au ushahidi wa kuthibitisha jambo lile!

    “…Basi, ni vizuri,” Bi. Letisia akamwambia na kuendelea. “Umenijulisha ikiwa mimi ni mtu wako wa karibu. Hivyo nitakaa na baba yako, kisha nimweleze yote uliyonieleza, tuone na yeye atasemaje.”

    “Sawa mama, nitasubiri…”

    Baada ya Grace kumjulisha mama yake, wakasitisha mazungumzo yao, kila mmoja akaendelea na shughuli zake za jumapili ile.

    Hakika kwa Grace ilikuwa ni furaha ilioje baada ya kumfahamisha mama yake suala lile, kwani kwa upande wa Geofrey, naye alishamwambia alishawajulisha wazazi wake, ambao pia walikubaliana na uamuzi wa Geofrey amwoe Grace.



    *******

    USIKU wa siku ile ya Jumapili, iliwakuta mzee Ramson Laiser na mkewe, Bi. Letisia, wakiwa wamekaa faragha, katika sehemu ya mapumziko iliyokuwa kando ya bustani, mbele ya nyumba yao.Walikuwa pia wakinywa vinywaji laini huku wakijadili mpango ule wa mtoto wao, Grace kutaka kuolewa na Geofrey, mtoto wa mzee Joel Kisamo.

    “Baba Grace…” Bi. Letisia aliita.

    “Mama Grace…unasemaje?” mzee Ramson alimuuliza huku akimwangalia.

    “Kuna jambo moja nataka kukwambia…”

    “Jambo gani hilo mke wangu?”

    “Ni kuhusu mtoto wetu Grace…” Bi. Letisia kasema na kuendelea. “Leo amenieleza jambo muhimu, ambalo nimeona ni vizuri nikueleze na wewe, ukizingatia linatuhusu sote tukiwa kama mzazi wake.”

    “Ni jambo gani hilo mke wangu?”

    “Ameniambia kuwa eti amepata mchumba, hivyo yuko tayari kuolewa.”

    “Amepata mchumba?” mzee Ramson akauliza huku akiyatoa macho yake!

    “Ndiyo manaake…”

    “Kwa kweli ni habari njema. Je, amekudokezea huyo mchumba wake ni nani?”

    “Ndiyo, ameniambia. Ni Geofrey, mtoto wa Joel Kisamo.”

    “Aisee, si yule mtoto wake wa kwanza?”

    “Ndiye yeye.”

    “Safi, kijana yule hana matatizo. Ni kijana mpole, mstaarabu ma mwenye heshima, kwa kweli sina matatizo kwa upande wangu juu uchumba wao, labda wewe…”

    “Hata mimi sina matatizo, isipokuwa…”

    “Isipokuwa nini tena? Unaanza kutaka kutoa sababu sasa!”

    “Siyo hivyo, si unajua yule ana matatizo?”

    “Matatizo gani?”

    “Watu wanasema siyo mzima…hana nguvu za kiuanaume!”

    “Una uhakika gani? Hayo ni maneno ya watu tu. Mwache mtoto wetu aolewe na kijana yule, ambaye wanapendana!” Mzee Ramson akasema kwa msisitizo!

    “Sawa baba Grace, tutafanya hivyo,” Bi. Letisia akasema akionyesha na yeye kukubali.

    “Ndiyo, tusubiri posa, na kuwaruhusu waoane! Ni bahati ilioje kwa mtoto wa kike kuolewa siku hizi, eti unasema siyo mzima. Kama asingekuwa mzima mwanetu Grace angempendaje?”

    “Na kweli, asingempenda kamwe!”

    Baada ya maongezi yao, walikubaliana waipokee ile posa ya Geofrey punde watakapotuma mshenga.

    Ulikuwa ndiyo uamuzi wa mwisho!

    *******CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    WIKI mbili zilipita baada ya pilikapilika zile za kupeana taarifa za uchumba kwa pande zote mbili. Kwanza kabisa, kabla ya kupeleka posa, wazazi wa msichana mwolewaji walitaarifiwa, kisha wakakaa kikao na kupanga mkakati wao juu ya upokeaji wa posa na sheria zake, ambazo pia zinaambatana na kimila. Baada ya kukubaliana, ndipo wakapanga siku maalum ya waoaji kwenda, ambayo ilikuwa ni mwisho wa wiki, siku ya Jumamosi.

    Basi, katika wiki ile ya tatu, mzee Joel Kisamo aliamua kutuma mshenga kupeleka posa nyumbani kwa mzee Ramson Laiser, kumchumbia binti yale, Grace. Mshenga huyo alikuwa ni, mzee Albert Kileo, mmoja wa watu maarufu kaika eneo la Kijenge Kati, jijini Arusha. Na mara nyingi watu wengi walimtumia kutokana na busara alizokuwa nazo, hivyo akiwa ni mzoefu, mzee Kileo alijua fika kwamba posa ile isingekataliwa kamwe, kwa jinsi alivyokuwa anajua kuremba maneno yaliojaa ushawishi ndani yake!





    Jumamosi hiyo, mzee Kileo akiwa ameongozana na mashahidi wawili wenye umri wa kati, walifunga safari kwenda nyumbani kwa mzee Lamson, ambako walikuwa wakisubiriwa kwa hamu kupeleka posa ya kumwoa Grace. Maandalizi ya kuwapokea yalikuwa yameshaandaliwa juu ya ujio wao. Hakika nyumbani kwa mzee Ramson kulikuwa kumejaa pilikapilika nyingi za kuwapokea wageni hao.

    Baada ya kufika, wageni walipokelewa vizuri na kukaribishwa ndani ya sebule nadhifu, ambapo walikuta baadhi ya ndugu na jamaa wa upande wa mzee Ramson waliofika kushuhudia utoaji ule wa posa. Kwa ujumla watu wote walikuwa ni wanaume, ambao walikaa ndani, lakini kwa upande wa wanawake walikaa sehemu ya nje, wakiendelea na utayarishaji wa maakuli kwa ajili ya wageni waliofika.

    Muda suyo mrefu, baada ya mambo yote kuwa tayari, vyakula viliandaliwa mezani, ambapo waliendelea kula huku wakiongea hili na lile, maongezi ambayo yalikuwa ya kusukuma muda tu, hayakuhusiana na lile jambo muhimu lililowafikisha pale. Walipomaliza kula, wakaendelea kunywa vinywaji, hasa pombe kwa wale waliokuwa wanatumia, na soda kwa wale wasiotumia. Wakati huo mzee Kileo alikuwa akipanga namna ya kuanza mazungumzo yaliyowapeleka nyumbani kwa mzee Ramson. Hata hivyo, mzee Ramson aliamua kuvunja ukimya kwa kusema:

    “Jamani…wageni wetu, karibuni sana…”

    “Tumekaribia, na tunashukuru sana,” mzee Kileo alisema huku akiyazungusha macho yake pande zote.

    “Na huu ni muda muafaka wa kutaka kupata maelezo juu ya ujio wenu, ingawa unafahamika,” mzee Kileo akaendelea kusema.

    “Ni kweli kabisa,” mzee Ramson akasema na kuendelea. “Madhumuni ya safari yetu ya kufika mpaka nyumbani kwako, ni juu ya watoto wetu, Geofrey na Grace, ambao wamependana na kutaka kuoana. Hivyo,mimi ni mshenga niliyetumwa na mzee Kisamo, nilete posa!”

    “Ni sawa kabisa. Ingawa watoto wetu wamependana na kutaka kuoana, mimi sina pingamizi lolote. Isipokuwa ni lazima zifanyike taratibu zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na utoaji wa mahari baada ya kutanguliza posa!” Mzee Ramson alisema.

    “Kuhusu mahari…hakuna tatizo, ili mradi posa yetu ikubaliwe…” mzee Kileo alisema huku akiangalia pande zote.

    Wazee wale walikaa wakijadiliana mengi mpaka walipoafikiana na posa ya Geofrey ikakubaliwa. Mzee Ramson hakuwa na kipingamizi hasa ukizingatia hakuona umuhimu wowote wa kukataa binti yake asiolewe na Geofrey. Vilevile walipanga juu ya utoaji wa mahari, ambayo ingetolewa kwa muda wowote. Baada ya kumaliza, ndipo mzee Kileo na ujumbe wake walipoondoka kurudisha jibu sehemu husika.

    Mzee Kisamo aliporudishiwa jibu, alifurahi sana na kumtaarifu mwanae, Geofrey baada ya kukubaliwa kwa posa yake. Hakika ilikuwa ni furaha ilioje, ambapo kwa Geofrey, alijiandaa kwa utoaji wa mahari mara moja ili mipango ya harusi ifanyike haraka. Hakupenda aibu ile imtawale na kusemwasemwa na watu kwamba alikuwa si mwanaume rijali!

    Na upande wa Grace, naye alikuwa na furaha baada ya baba yake kukubali kupokea posa ile, kwa vyovyote alikuwa na uhakika wa kumpata Geofrey, kijana mtanashati aliyeuteka moyo wake, ambapo kwa asilimia mia moja alihesabu kwamba alishakuwa mumewe. Hivyo basi, kwa muda wote wakawa wanapigiana simu za kupongezana kwa kukubaliwa kwao, kiasi cha watu kusahau ile tofauti iliyokuwa inazungumzwa baina yao, yaani hakuwa mzima! Makubwa!

    Mahari ilipokwisha tolewa, vikao vya harusi vilianza mara moja, ambapo marafiki, jamaa za Geofrey walimsaidia sana. Wote waliamua hivyo, katika kukamilisha ile ndoto yao, kuwa Geofrey alikuwa ni mwanaume kamili aliyekuwa anaoa sasa. Vikao vile vilifanyika kwa muda wa miezi mitatu, na kufanikisha kupata michango mingi iliyoweza kutosheleza katika ukamilishaji wa sherehe ile harusi, ni sherehe ambayo walikuwa wameamua kwamba ni lazima ingekuwa ya kukata na shoka na kuacha simulizi jijini Arusha!

    Pia, kwa upande wa mzee Ramson, baba yake Grace, alihamasisha michango ya nguvu, ili aweze kumuabga binti yake katika sherehe ya Send off. Alifanikiwa kupata michango mingi, na kujiandaa kwa sherehe ile, ambapo pia alitaka iwe ya aina yake. Ukweli ni kwamba wote walikuwa wamejiandaa vya kutosha!

    ********

    HATIMAYE siku ya siku ilifika, ambapo Alhamisi hiyo, kulikuwa na sherehe kubwa ya Send off, ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Sayari, ulioko eneo la Kimandolu, jijini Arusha. Na ile ilikuwa ni sherehe ya kuagwa kwa Grace, na upande wake ndiyo uliowakaribisha upande wa bwana harusi. Bwana harusi na bibi harusi walipendeza sana, ambapo kila mmoja alifika kwa wakati wake, hasa ukizingatia kila mmoja alikuwa akitokea nyumbani kwao. Vigelegele na hoihoi vilitawala kwa muda wote na uiofanikisha sherehe ile na kila mmoja akaridhika.

    Baada ya sherehe ile kumalizika, ndipo ilipofika siku ya Jumamosi, ambapo ndiyo siku ya harusi yenyewe, na muandaaji alikuwa ni bwana harusi.

    Eneo zima la mtaa wa Kijenge, nyumbani kwa mzee, Kisamo kulikuwa na pilikapilika nyingi sana, pakiwa na wageni wa aina mbali mbali waliotoka maeneo mbalimbali katika kusherehekea sherehe ile ya harusi ya kijana wao mpendwa, Geofrey. Pia, nyumbani kwa mzee Ramson, pia palikuwa na pilikapilika hizo, wakisubiri muda muafaka wa kusherehekea. Grace alikuwa akiandaliwa kwa kupelekwa saluni kwa gari maalum, kurembeshwa, hatimaye arudi nyumbani kwao tayari kwa kwenda kanisani kufunga ndoa.

    Maharusi, Geofrey na Grace, walipokuwa tayari, walichukuliwa kwa gari maalum na kuelekea katika Kanisani Katoliki la Kijenge. Nyuma walifuatiwa na msururu mkubwa wa magari hadi walipofika. Misa iliendelea kama kawaida hadi ulipofika muda wa kufungishwa ndoa, ambapo walifunga mbele ya kasisi na kuapishwa kiapo cha ndoa kuwa wataishi maisha yao yote, mpaka mauti yatakapowatenganisha!

    Baada ya kufungishwa ndoa, waliondoka pale kanisani na msururu ule wa magari, ambapo walizunguka katika maeneo maarufu ya jiji la Arusha huku honi za magari zikipigwa. Safari yao ikakomea eneo la bustani ya mzunguko, eneo maarufu la kupigia picha za kumbukumbu. Ni eneo lililoko mkabala na hoteli ya Impala. Walipomaliza kupiga picha za kumbukumbu, ndipo walipoelekea katika ukumbi wa Mezaluna, ulioko Kijenge, palipotegemewa kufanyika kwa sherehe ile. Kwa muda wote maharusi wale walikuwa na nyuso za furaha kiasi cha kufanya wavutie.

    Maharusi wakaingia ukumbini na kupokewa kwa vifijo na vigelegele hadi walipokaa. Sherehe ikaanza huku MC akisherehesha kwa mbwembwe na kuwa kivutio kikubwa. Wazazi wa pande zote mbili walikuwepo, halikadhalika ndugu, jamaa na marafiki pia walikuwepo katika kukamilisha tendo lile muhimu. Lakini kadri muda ulivyokuwa, ndivyo wasiwasi ulivyokuwa unamtawala Geofrey, na kumfanya furaha yake izidi kuyeyuka taratibu, kwani mwisho wa sherehe ulikuwa unakaribia kwisha ili wakapumzike!





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maharusi pamoja na wapambe wao, walikuwa wamepangiwa kwenda kupumzika katika hoteli ya Mango Villa, katika kukamilisha fungate. Hivyo basi, kwa upande wa Geofrey ndiyo kwanza alikuwa anawaza kwamba kitakachoendelea baada ya kupumzika hotelini, ni kwa mke wake, Grace kutaka kupewa penzi motomoto kutoka kwake, ukizingatia walikuwa hawajawahi kukutana kimwili. Ni tendo la ngono tu ndilo litakalowaingiza katika ulimwengu mwingine na si vinginevyo!

    Sasa Geofrey aliona mambo yamezidi kuwa mazito juu ya hali ile aliyokuwa nayo, ambayo aliijua mwenyewe. Ukweli ni kwamba asingeweza kumtimizia mke wake lile tendo linalounganisha mume na mke, afanyeje? Aliendelea kuwaza sana, hata hivyo wazo moja lilimjia kichwani mwake, kwamba ajifanye kuwa anaumwa kwa muda ule wa katikati ya sherehe, aseme amepatwa na homa ya ghafla. Na kweli ujanja ule ulimsaidia sana baada ya kuendelea kugugumia taratibu kiasi cha kuwashtua watu, hasa mpambe wake aliyekuwa karibu naye muda wote! Akamuangalia kwa hofu kidogo na kumuuliza:

    “Vipi Geofrey?”

    “Mh, hali mbaya…” Geofrey akasema kwa sauti ndogo.

    “Hali mbaya?” Mpambe akaendelea kumuuliza.

    “Ndiyo…”

    “Imekuwaje?”

    “Najisikia hali siyo nzuri…”

    “Unaumwa?”

    “Ni kitu kama hicho!”

    “Sasa…niwajulishe watu?”

    “Hapana…” Geofrey akasema na kuendelea. “Ngoja tumalize sherehe tu, nitakwenda kupumzika…”

    “Utapumzika bila kupata matibabu?”

    “Nitameza dawa za kutuliza maumivu.”

    “Unazo dawa hizo?”

    “Ndiyo, ninazo ndani ya mkoba.”

    “Basi hakuna shaka, lakini ukizidiwa useme…” mpambe akamwambia huku akiendelea kumwangalia kwa wasiwasi.

    Hata hivyo baada ya Geofrey kumaliza kuongea na mpambe wake, aligeuka na kumwangalia mke wake, Grace, ambaye naye alikuwa akimwangalia alipokuwa akiongea na mpambe wake. Kwa sauti ndogo Grace akamuuliza:

    “Vipi Geoff?”

    “Ah, ni hali imebadilika ghafla!”

    “Unajisikiaje?”

    “Sijisikii vizuri.”

    “Unaumwa?”

    “Naweza kusema hivyo, lakini siyo sana…”

    “Basi vumilia, kwani karibu sherehe itamalizika, mengi tutaongea hotelini. Mimi ninahisi labda umetawaliwa na hofu tu,” Grace akamwambia huku akimwangalia jinsi mumewe alivyokuwa akivunga kuumwa!

    “Vyote vinawezekana…oh!” Geofrey aliendelea kuvunga!

    “Pole mume wangu…” Grace akaendelea kumfariji.

    “Ahsante sdana,,,nashukuru sana kwa kunijali…”

    Wakati wakiwa katika maongezi yao, sherehe ilikuwa inakaribia kufika ukingoni, kitu ambacho kwa upande wa Geofrey aliona kama ni adhabu kubwa kwa upande wake.‘Msema chochote’, aliendelea kuchombeza maneno kwa kuwasifia maharusi na kuwatakia maisha mema katika ndoa yao, na pia eti kuwaombea wazae watoto mapacha! Ni hatari sana, aliwaza Geofrey!

    Ni hadi sherehe ile ilipoisha kunako majira ya saa saba za usiku. Watu wakaanza kutoka, na maharusi wakachukuliwa kwenda kupumzika katika hoteli ya Mango Villa, kufurahia fungate yao. Msafara wa magari ukaelekea katika hoteli ile iliyoko eneo la Sanawari, na baada ya kufika maharusi wakashuka na kuelekea ndani ya hoteli, na kufikia sehemu ya mapokezi, ambapo walikuwa wamepangiwa chumba namba 0134 katika ghorofa ya tatu. Wapambe wao, walikuwa wamepangiwa chumba namba 0135 jirani yao tu, ikiwa ni sababu za kiusalama.

    Hatimaye baada ya kufanya taratibu zote za pale hotelini, maharusi na wapambe, wakaingia ndani ya vyumba vyao, ambapo vilikuwa vyumba vikubwa, vilivyokuwa na kila kitu ndani, vitanda viwili, sofa, runinga, friji ndogo, simu na huduma za choo zikiwa humohumo chumbani. Wapambe wao wakaingia ndani ya chumba chao tayari kwa kupumzika, na kuwaacha Geofrey na Crace nao wakiingia chumbani mwao.

    Geoffrey na Grace walipoingia, wakakaa kwa muda katika sofa huku wakiongea hili na lile hasa kwa kuulizana hali ya ugonjwa wa ghafla wa Geofrey, hata hivyo wakafikia uamuzi wa kwenda kuoga. Wote walisaula nguo zao na kuingia bafuni kuoga, kila mmoja kwa wakati wake. Kwa muda wote ule Grace alikuwa na hamu kubwa ya kustarehe na mume wake, hasa ukizingatia walikuwa hawajawahi kukutana kimwili, na siku yenyewe ndiyo ile ya fungate!

    Walipomaliza kuoga, Geofrey na Grace walijitupa kitandani. Ni kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita, kilichokuwa kimetandikwa shuka zuri la rani ya zambarau, iliyolandana na mito ya kulalia. Hakika ilikuwa ni ishara nzuri ya mapenzi hasa kwa watu waliofunga ndoa na kuwa kitu kimoja. Hata hivyo, hofu kuu iliendelea kumwandama Geofrey, na kumfanya aanze kutetemeka kama mtu aliyekuwa na homa kali sana. Ikamlazimu kumeza dawa ya kutuliza maumivu, aina ya Panadol alizokuwa amezihifadhi ndani ya mkoba wake, kwani alishajiandaa kwa mchezo ule wa kuvunga!

    “Oh, vipi mume wangu?” Grace alimuuliza mumewe huku akimpapasa!

    “Ni kama nilivyokwambia, hali imebadilika ghafla,” geofrey akamwambia.

    “Oh, bahati gani mbaya hii iliyonikuta, hasa leo hii wakati wa harusi yetu? Pia, ukizingaia nina hamu na wewe!” Grace aliendelea kulalamika huku mapigo ya moyo wake yakipiga kwa kasi!

    “Vumila tu mpenzi…” Geofrey akamwambia mkewe kwa huzuni kubwa huku akifunika sehemu yake nyeti. Ni sehemu iliyokuwa imepooza na kuwa baridi kiasi cha kutoonyesha uhai!

    Hata hivyo mkewe, Grace hakumsumbua sana mume wake kwa vile alishamtaarifu mapema kwamba hali yake ilikuwa mbaya. Akasubiri mpaka atakapokuwa amepata ahueni. Akaamua kujilalia kando ya Geofrey, akiwa amemkumbatia! Hakika ulikuwa ni usiku wa aina yake kwa watu wale wawili waliokuwa wamependana, kwani Grace alikuwa akiota ndoto za mang’amung’amu kutokana na ile furaha ya kufunga ndoa kutumbukia nyongo. Alichotegemea kukipata kwa usiku ule hakukipata kabisa zaidi ya kuusindikiza usingizi kando ya mumewe aliyekuwa taaban!

    Hakika alijiona kama mtu mwenye mkosi!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog