Simulizi : Siri Ya Mke
Sehemu Ya Pili (2)
***********
Walipomaliza kuoga, Geofrey na Grace walijitupa kitandani. Ni kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita, kilichokuwa kimetandikwa shuka zuri la rani ya zambarau, iliyolandana na mito ya kulalia. Hakika ilikuwa ni ishara nzuri ya mapenzi hasa kwa watu waliofunga ndoa na kuwa kitu kimoja. Hata hivyo, hofu kuu iliendelea kumwandama Geofrey, na kumfanya aanze kutetemeka kama mtu aliyekuwa na homa kali sana. Ikamlazimu kumeza dawa ya kutuliza maumivu, aina ya Panadol alizokuwa amezihifadhi ndani ya mkoba wake, kwani alishajiandaa kwa mchezo ule wa kuvunga!
“Oh, vipi mume wangu?” Grace alimuuliza mumewe huku akimpapasa!
“Ni kama nilivyokwambia, hali imebadilika ghafla,” geofrey akamwambia.
“Oh, bahati gani mbaya hii iliyonikuta, hasa leo hii wakati wa harusi yetu? Pia, ukizingaia nina hamu na wewe!” Grace aliendelea kulalamika huku mapigo ya moyo wake yakipiga kwa kasi!
“Vumila tu mpenzi…” Geofrey akamwambia mkewe kwa huzuni kubwa huku akifunika sehemu yake nyeti. Ni sehemu iliyokuwa imepooza na kuwa baridi kiasi cha kutoonyesha uhai!
Hata hivyo mkewe, Grace hakumsumbua sana mume wake kwa vile alishamtaarifu mapema kwamba hali yake ilikuwa mbaya. Akasubiri mpaka atakapokuwa amepata ahueni. Akaamua kujilalia kando ya Geofrey, akiwa amemkumbatia! Hakika ulikuwa ni usiku wa aina yake kwa watu wale wawili waliokuwa wamependana, kwani Grace alikuwa akiota ndoto za mang’amung’amu kutokana na ile furaha ya kufunga ndoa kutumbukia nyongo. Alichotegemea kukipata kwa usiku ule hakukipata kabisa zaidi ya kuusindikiza usingizi kando ya mumewe aliyekuwa taaban!
Hakika alijiona kama mtu mwenye mkosi!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
KULIPAMBAZUKA afajiri ya siku ya pili, na hakuna mtu yeyote aliyekuwa amepata usingizi katika usiku ule wa fungate, na mambo yalikuwa ni bila kwa bila. Wote wawili, Geofrey na Grace walikuwa wamejifunika viwiliwili vyao kwa blanketi, kila mmoja akiwa na mawazo yake kichwani, hasa kwa Geofrey, ambaya alikuwa hawezi kumridhisha mkewe. Upande wa ubavuni mwake, alikuwepo Grace, aliyemkumbatia kwa kuhitaji kitu muhimu sana, na kukamilisha kitendo cha ndoa!
Hamu ilikuwa imemshika siyo mchezo!
“Vipi mume wangu,” Grace alimwita mume wake aliyekuwa mbali!
“Mke wangu…ah…” Geofrey alisema bila kumalizi.
“Ninahitaji mpenzi, naomba unikumbatie, nasikia baridi…” Grace alisema kwa sauti ambayo ilikuwa imejaa mahaba mazito!
“Usihofu,” Geofrey akamwambia Grace huku akimkumbatia pale kitandani.
“Mume wangu unajua kuwa nakupenda sana?” Grace akamwambia huku macho ya udadisi yakiwa yameua usoni mwa Geofrey.
“Naamimi unanipenda mke wangu, ndiyo maana nikaamua tuoane, lakini nahisi mimi ndiye niliyezimia kwako zaidi,” Geofrey alimwambia huku wakiwa wamekumbatiana na mabusu motomoto yakashamiri, si mashavuni, mdomoni na kwenye paji la uso! Yalikuwa ni mabusu ya upendeleo!
Geofrey alisikia mapigo ya moyo wake yakipiga kwa kasi na jasho jembamba kumchuruzika taratibu kiasi cha kushindwa afanyeje ili aweze kumridhisha mkewe. Kila alipomshika kwenye kona za huba, alimsikia akizizima, alikini akaamua kutulia kidogo baada ya kuona mambo yote aliyokuwa akimfanyia yalikuwa bure, kwa vile hakuwa na nguvu za kiume!
“Ooooh! Geff mume wangu…” Grace alisema.
“Nakusikiliza mke wangu…” Geofrey akaitika.
“Unajua kuwa mimi sijawahi kuguswa kabisa?”
“Unasemaje mke wangu?” Geofrey akauliza kana kwamba hakumwelewa!
“Nasema kuwa mimi ni bikra,” Grace akasema kwa sauti mya huzuni na kuendelea. “Sijawahi kufanya mapenzi tokea nizaliwe. Naomba unifundishe katika muda huu mchache tulio ndani ya fungate yetu, kwani kumeahapambazuka.”
“Oh! Mungu wangu!” Geofrey akajisemea kwa sauti ndogo. Halafu akaanza kulia, akiwazia ile hali yake ya kutokuwa na nguvu za kiume, na pia alitamani kumkabili mume wake! Alishindwa kuelewa ugonjwa wa kupooza ulitoka wapi!
Na je, angemwambia nini mke wake?
“Unalia nini tena mume wangu?”Grace alimuuliza mume wake huku akiwa amelala chali, kama mgonjwa aliye mahututi!”
Mwili wake mweupe ulizidi kupendeza na kung’ara kila alipomtazama. Kwa ufupi alikamilika katika kila idara, ambapo Geofrey alitamani kumrukia lakini hakuwa na nguvu!
“Mke wangu, bado nimeshikwa na kichomi…ooooh!” Geofrey aliendelea kumwambia mkewe huku akijishika kifuani, na machozi yakaanza kumtoka taratibu. Aliamini kwamba maneno ya kusema, ‘naumwa,’ mkewe angemuonea huruma!
“Basi mume wangu, usije ukapata matatizo mengine zaidi…” Grace akamwambia huku akimwonea huruma.
“Nashukuru mke wangu kwa kutambua hilo…” Geofrey akasema. “Hivyo ni vyema tuamke na kwenda kujiswafi.”
“Ni sawa, lakini ni lazima uende hospitali ukapatiwe huduma…”
“Wewe usijali, hili tatizo litaisha. Ni lazima leo niende kwa daktari,” Geofrey aliendelea kumpa moyo mke wake.
Lakini wasiwasi ulikuwa umetanda kuhusu hali ile. Grace alikuwa ameinamisha kichwa magotini mwake kama mtu aliyekuwa akisujudu. Geofrey hakujua alichokuwa anawaza akilini mwake, akahisi yote yalikuwa juu ya matatizo aliyokuwa nayo na kushindwa kumridhisha!
Baada ya muda takriban dakika tano hivi, kitu kama majimaji yenye uvuguvugu yalidondokea gotini tone moja moja. Geofrey akajua ni machozi, akaamua kuuinua uso wake kutizama ni kitu gami hasa. Kila alipojaribu kumuinua Grace, alikaza shingo yale!
Makubwa!
“Mke wangu…” akaita Geofrey.
“Bee…” Grace akaitikia huku akimwangalia kwa uso wa huzuni.
“Mbona unalia?”
“Hata silii…”
“Hulii wakati naona machozi yanakutoka? Vumilia, hili ni jambo dogo sana!”
“Mume wangu, nateseka! Utafanya nini ili unisaidie? Kwani najisikia vibaya…”
“Oooohps!” Geofrey akavuta pumzi ndefu na kuishia kunyamaza tu, kwani maneno yale ya Grace yalimuumiza moyo wake.
Akamuonea huruma Grace alivyokuwa akijigaragaza pale kitandani. Mwili wake ulikuwa umelegea, macho mekundu na ya kurembua, hakuweza kuvumilia zaidi ya kulia! Ukweli ni kwamba Geofrey alishindwa kumtimizia mke wake haki yake ya ndoa, kikiwa ni kitendo kilichomshangaza sana mke wake huyo mpya! Lakini hakuwa na la kufanya kwa sababu ilikuwa ni mapema mno!
Geofrey alimbembeleza sana Grace, halafu wakaelekea bafuni kuoga. Baada ya kumaliza kuoga, walivalia vizuri na kubeba baadhi ya mizigo midogo waliyokuwa nayo na kutoka mle chumbani, na kuteremka chini kwa kutumia ngazi, ambapo walikuta gari likiwa linawasubiri tayari kwa kuwarudisha nyumbani baada ya kumaliza fungate. Lilikuwa ni gari aina ya Mercedes Benz, la rangi nyeusi, ambalo lililokodishwa maalum kwa kazi ile ya kuwahudumia maharusi wale.
Geofrey na Grace walipakiza mizigo yao yote, huku wakisaidiwa na dereva, na baada ya kumaliza kupakia, nao wakaingia ndani ya gari na dereva akaliondoa kuelekea katika makazi yao mapya waliyokuwa wameandaliwa tayari kwa kuishi kama mke na mume. Kwa ujumla, wote wawili walikuwa wamenyamaza kimya ndani ya gari, kila mmoja akiwa na mawazo yake, kwa kile kilichotokea ndani ya chumba kule hotelini. Ni kwamba hawakuridhishana kimwili, kama ilivyokuwa inategemewa punde watu, mume na mke wanapokuwa kitu kimoja.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Geofrey na Grace walikuwa wamepewa nyumba moja nzuri, ndogo kwa ajili ya familia yao. Ni nyumba ambayo walikuwa wamepewa na mzee Kisamo, ikiwa ni zawadi aliyoiahidi ndani ya ukumbi jana yake. Ilikuwa ni nyumba ya vyumba vitatu, sebule, pamoja na mahitaji mengine kama vile, choo na stoo. Nyumba hiyo ilikuwa imejengwa eneo lile la Kijenge, mbali kidogo na makazi ya mzee Kisamo. Hakika ilikuwa ni zawadi nzuri sana, iliyowafurahisha wote wawili, ingawa kwa upande mwingine nafsi ilimsuta Geofrey, kwa kufikiria kwamba angeishije huku akiwa katika hali kama ile ya kutokuwa nam uwezo wa kumridhisha mkewe?
Ukweli unajulikana kwamba hakuwa mwanaume rijali wa kuweza kumtekelezea suala la unyumba, mke wake yule mrembo! Ni hatari sana! Sasa afanyeje na huku alishafunga ndoa? Alibaki katika matata mazito!
Baada ya kufikishwa nyumbani, Geofrey na Grace waliingia ndani, ambapo ndani yake palikuwa na samani za gharama, vyote vikiwa ni zawadi walizoandaliwa na mzee Kisamo. Hivyo ndivyo wanandoa hao walivyoanza maisha yao mapya, ambayo waliapa mbele ya Kasisi, kwamba wataishi kwa shida na raha, mpaka mauti yatakapowatenganisha!
*******
BAADA ya wiki chache tokea wafunge ndoa, mwanadada, Grace alianza kuonja adha ya maisha ya ndoa kutoka kwa mume wake, Geofrey. Aliweza kushuhudia jinsi mume wake alivyokuwa na matatizo ya kushindwa kumtimizia haki yake ya msingi ya ndoa, kitu ambacho kilimnyima raha, hasa ukizingatia alikuwa hajawahi kukutana kimwili na mwanaume yeyote. Aliyemtegemea kumtoa bikra yake ni mumewe Geofrey, ambaye ndiye alikuwa na matatizo yale ya kutokuwa na urijali!
Kwa upande wa Geofrey, aliendelea na shughuli zake ingawa hali ile ilimuathiri kiasaikolojia. Lakini hakukata tamaa zaidi ya kumpa maneno mazuri ya kimapenzi mke wake, ambaye kwa kiasi fulani yalimliwaza. Hata hivyo, usiku mmoja, wakiwa chumbani wakijiandaa kwa kulala, Grace aliamua kuliongelea suala lile la mume wake ili kujua kulikoni.
“Mume wangu…” Grace aliita.
“Mke wangu,” Geofrey aliitika huku akimwangalia.
“Unajua ninashindwa kukuelewa?”
“Kunielewa nini mke wangu?”
“Kuhusu hali hii tuliyonayo mume wangu,” Grace alisema na kuendelea. “Unajua nina hamu sana na wewe, yaani tukutane na kunipa ‘unyumba,’ sasa nashindwa kuelewa. Naona mwenzangu unazidi kuwa kimya!”
“Oohps!” Geofrey alivuta pumzi ndefu halafu akaendelea kumwangalia mkewe kwa huzuni kubwa na kuendelea kusema. “Wewe acha tu mke wangu, ni masahibu makubwa yaliyonikumba mwenzako…”
“Masahibu gani hayo?”
“Ni historia ndefu sana, lakini sina budi kukuelezea ukiwa mke wangu…” Geofrey alimwambia mkewe, Grace.
“Ni vizuri unieleze ili uweze kunitoa tongotongo machoni mwangu,” Grace alimwambia huku akimwangalia kwa huzuni kubwa!
“Sawa mke wangu, tambua kwamba wewe ndiye tegemeo la maisha yangu…”
“Hilo naelewa, ndiyo maana tumeoana. Natambua kwamba wewe ndiye wangu, na pia nimeachana na wazazi wangu, baba na mama, wewe ndiye baba yangu.”
“Ukweli ni kwamba ni kwamba nina matatizo makubwa sana…” Geofrey alimwambia mke wake, Grace, kwa kuamua kumwambia ukweli kuhusu yale matatizo ya kimaumbile yaliyokuwa yanamkabili!
“Niambie hayo matatizo yaliyokukabili ili na mimi niweze kuyajua…” Grace akamwambia huku akijiweka tayari kumsikiliza.
“Mimi nimezaliwa na kujikuta katika hali kama hii. Inasemekana kwamba mama yangu aliponizaa tu, nilidondokewa na kitovu katika sehemu zangu za siri, kitu ambacho kina madhara kwa mtoto wa kiume. Hata hivyo, mama yangu hakuweza kuthibitisha bayana zaidi ya kuwa siri yake mpaka nilipokuja kuwa mtu mzima na kujikuta katika hali hii!” Geofrey alimwambia mkewe, Grace huku akimwangalia kwa uso wa huzuni.
“Oh, Mungu wangu!” Grace akasema baada ya kusikia alichokuwa anazungumzia mumewe.
“Baada ya kubalehe, nilipata shida sana nasoma shule ya sekondari, kwani wenzangu walikuwa wakinicheka baada ya kuniona sijihusishi na masuala ya wanawake kama walivyokuwa vijana wengine wa umri wangu. Tatizo hilo liliendelea hadi nilipomalioza shule na kuanza shughuli zangu na hatimaye kukutana na wewe mke wangu…” Geofrey akanyamaza kidogo huku akimwangalia Grace mkewe, aliyekuwa akimsikiliza kwa makini.
“Ili kuondoa aibu yangu,” Geofrey akaendelea kusema. “Nionekane mwanaume rijali, niliamua kufanya urafiki na wewe, na hatimaye uchumba na kuamua kukuoa. Hiyo ndiyo hali halisi mke wangu, na hata siku ile ya fungate nilipokuambia kwamba ninaumwa, haikuwa kweli, bali ni ili kuficha kilema changu, sikuwa na jinsi…oh, Mungu wangu!”
“Oh, pole sana mume wangu…” Grace alimwambia huku akimwonea huruma na pia akijawa na simanzi kubwa moyoni.
“Nimepoa, lakini sijapoa, kwa vile ni kilema changu cha kudumu, ambacho nitaishi nacho milele!” Geofrey aliendelea kumwambia mkewe.
“Sina jinsi. Kwa vile tumeshafunga ndoa kanisani na kuapa kuwa tutaishi wote kwa raha na shida mpaka mauti yatakapotutengenisha, wewe ni mume wangu na tutaendelea kuishi hivyohivyo…” Grace alisema huku akiendelea kububujikwa na machozi.
“Nashukuru mke wangu kwa kulielewa hilo,” Geofrey akamwambia Grace. Kisha wakakumbatiana kwa upendo na kuanza kulia kwa sauti za chini hadi walipojitupa kitandani…
*******
UPANDE wa pili, mzee Kisamo, baba yake Geofrey alikuwa akiwaza sana juu ya mwanawe, kwa vile alifahamu ukweli kwamba hakuwa na nguvu za kiume. Vilevile alizinyaka habari kwamba tangu Geofrey amwoe Grace, mtoto wa mzee Ramson Laiser, hakuwahi kumtimizia haki yake ya ndoa, jambo ambalo lilimkuna sana na kuona kuwa Grace alikuwa akipata shida!
Hivyo basi, mzee Kisamo akaona kwamba, jambo lile ni vyama amshirikishe mke wake, Bi. Bernadeta, kuzungumzia suala lile, ingawa pale mwanzo mke wake alikuwa ni mmoja wa aliyepinga suala lile la Geofrey kuoa kutokana na matatizo yake ya kimaumbile aliyokuwa nayo. Lakini cha muhimu ilikuwa ni kupata suluhu!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mama Geofrey,” mzee Kisamo alimwita mkewe.
“Bee,” Bi. Benedeta akaitikia.
“Kuna jambo nataka kuongea na wewe…”
“Jambo gani?”
“Ni kuhusu mwanetu Geofrey…”
“Amefanya nini tena?”
“Unajua tulifanya kosa kubwa sana kwa kumkubalia kuoa?”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Ni kutokana na ile hali aliyokuwa nayo!”
“Si niliwahi kukwambia?” Bi. Benadeta akasema na kuendelea. “Lakini wewe ukasema tumwache tu kwa kuwa nia uamuzi wake. Sasa huoni kwamba mtoto wa watu anapata shida sana? Hapati haki yake ya ndoa kama walivyo wanawake wengine!”
“Ni kweli uliniambia, lakini kwa sasa hakuna haja ya kulaumiana. Tupange jinsi ya kuwasaidia,” mzee Kisamo akasema.
“Hatuwezi kwa sasa. Watoto wameshafunga ndoa kanisani, tene ni pingu ya maisha. Hawawezi kuachana mpaka pale kifo kitakapowatenganisha!”
“Mungu wangu, sasa tufanyeje?”
“Ukweli ni kwamba hakuna jinsi…”
“Basi, tuwaache tu kwa vile walikuwa wameshapendana!”
“Hilo ndilo jambo la msingi.”
Mjadala wao uliishia hapo. Mzee Kisamo na Bi. Benadeta hawakuendelea kujadili tena suala la Geofrey na mke wake, Grace. Wakabaki wakiumia rohoni na hawakutegemea kamwe kama wangeweza kupata mjukuu kwa mtoto wao wa kwanza. Vilevile hawakutegemea kwamba upande wa pili wa wazazi wa Grace walikuwa na mawazo gani.
Mawazo yaliendelea kumtesa mzee Kisamo, punde anapokuwa peke yake. Ni mawazo ambayo yalitaka kumfanya Ibilisi mbaya amtawale na kutaka kufanya jambo baya, na kama asingekuwa mtu aliyetawaliwa na imani kali ya kidini, basi angefikia pabaya! Ni kwamba alitaka kupanga kuwa amshauri Grace, mkwe wake, awe anafanya naye mapenzi kwa siri, ili aweze kupatan uja uzito na kuzaa mtoto kwa lengo la kumfichia siri Geofrey, mwanawe. Hata hivyo aliuona kuwa uamuzi ule haukuwa wa busara na ni dhambi kubwa!
*******
KWA bahati nzuri, Geofrey alikuwa amefanya usaili katika kampuni moja inayotoa huduma za usafirishaji na upokeaji wa mizigo, iliyojulikana kwa jina la Mangi Forwarding & Clearing Agency, iliyokuwa na tawi lake jijini Arusha, huku makao yake makuu yakiwa jijini Dar es salaam. Alikubaliwa na kupata ajira na kuitwa kufanya kazi mara moja, ambapo alipangiwa kufanya jijini Dar, badala ya Arusha.
Yeye Geofrey na mke wake, Grace, walizipokea habari hizo kwa furaha kubwa, huku Geofrey akiwa ndiye mwenye furaha zaidi ya kulihama jiji la Arusha akiwa na mke wake, Grace, ikiwa ni moja ya kukwepa aibu ile ya kutozaa. Alijua kuwa atakapokuwa Dar, hakuna atakayeijua siri yake, hivyo baada ya maandalizi, wote wakasafiri na kwenda katika kituo kipya cha kazi, ambao waliamua kuyaanza maisha mapya yaliyojaa furaha.
Kazi ile aliyokuwa anaifanya Geofrey, ilikuwa na mshahara mzuri pamoja na marupurupu mengi, yaliyoweza kutatua shida zao na kupangilia mambo yao. Katika kipindi hicho chote, Geofrey alikuwa akimjali sana mke wake, kiasi kwamba alikuwa akimtimizia mahitaji yote muhimu, isipokuwa tendo la ndoa pekee.
Grace naye akawa ni mtu mvumilivu, hakupenda kuivujisha ile siri, ukizingatia alikuwa anaishi maisha ya raha mustarehe na hakuna kitu chochote alichokikosa. Kwa vile walikuwa peke yao kwa kutokuwa na mtoto, walikuwa wakijipangia sehemu za kwenda kustarehe siku za mwisho wa wiki, ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Walipendelea kwenda kustarehe sehemu kama, Club Billicana, Sea Cliff au California Drimmer, kwa lengo la kujirusha na kuyafurahia maisha yao ya ujana. Ni nguo gani ambayo Grace hakuwahi kuvaa? Ni kiatu gani ambacho hakuwaho kuvaa mguuni mwake? Grace alikuwa akivaa nguo na viatu vya gharama, ambavyo ukipiga hesabu, vilifikia maelfu ya shilingi za kitanzania. Pia, alikuwa na kawaida ya kuvaa vito vya thamani, kama herein, pete, mikufu na bangili, vyote vya dhahabu.
Hakika Geofrey alikuwa amedhamiria kumpendezesha mke wake, kwani alijua siku zote kuwa, mwanamke nip ambo la nyumba. Je, usipompendezesha mke wako utampendezesha nani? Achana na hayo, kutokana na nafasi ya kazi ya mumewe, katika nyumba waliyokuwa wamepanga, eneo la Ilala, kulikuwa kumeenea samani zote za ndani.
Baada ya kufanya kazi kwa kipindi kirefu, huku pia akiwa na wivu wa kimaendeleao, Geofrey alifanikiwa kujenga nyumba yao, eneo la Tabata. Wakahamia huko kwa lengo la kupunguza gharama za kupanga, na kuendelea na maisha yao huku Grace akiendelea kukosa haki yake ya ndoa, ya kupeana unyumba.
Tangu walipooana hawakuwahi kukutana kimwili, kitu ambacho kwa mtu wa kawaida asingeweza kuvumilia, lakini ndivyo ilivyokuwa kwa mwanamke kuvumilia namna ile. Na katika kipidi chote hicho, kamwe Grace hakukubali tamaa za kimwili zimwandame na hatimaye ajikute amejiingiza katika usaliti wa ndoa kwa kutoka nje.
Tena Grace akiwa msichana mbichi kabisa na mwenye umbile la kusisimua, ilikuwa yataka moyo! Ni wanaume wengi wakware waliokuwa wakimmezea mate na hata kudiriki kutupa ndoana zao, lakini ziligonga mwamba, hawakuambulia kitu!
Hata hivyo, ili kumliwaza kidogo, Geofrey aliamua kumfungulia Grace duka linalouza bidhaa, ambalo lilikuwa katika ile nyumba yao, upande wa mbele ambapo palikuwa na nafasi ya kutosha. Na ile yote ni ili kumuweka bize, asikae bila kazi ya kufanya, na pia kusaidiana katika mapato zaidi. Ni duka ambali lilikuwa linauza bidhaa za aina mbalimbali, kuanzia za vyakula, vinywaji baridi na vitu vinginevyo. Grace akawa akijishughulisha na biashara ya duka, kitu ambacho kilimliwaza kidogo…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
SIKU zilizidi kwenda, na baada ya kuishi Tabata kwa muda wa miezi sita, Grace alijikuta akijenga urafiki na mwanadada mmoja, aliyejulikana kwa jina la Mwantumu. Yeye alikuwa anaishi katika nyumba ya jirani tu, na mara nyingi alikuwa akimtembelea Grace pale nyumbani, katika kununua bidhaa dukani, ambapo wakawa wanaongea mambo mengi sana kama walivyo wanawake wengi wanapokutana na kujenga urafiki mkubwa.
Walikuwa marafiki wakubwa, kiasi hata cha kuhadithiana mambo yao ya siri juu ya maisha yao. Ni katika kipindi hicho, ndipo Grace alipojaribu kuomba ushauri kwa Mwantumu, juu ya hali ile iliyokuwa inamkabili mume wake, Geofrey. Hakika ilikuwa ni siri kubwa ya ndani, ambayo alikuwa ameihifadhi muda mrefu sana, lakini akaamua kuimwaga kwa shoga yake baada ya uvumilivu kumshinda.
Mchana wa siku moja, walipokuwa wamekaa katika kibaraza cha nyumba yao, Grace aliamua kulitoa lile dukuduku lake lililokuwa moyoni mwake kwa muda mrefu. Ukweli ni kwamba, japokuwa alimwamini sana Mwantumu kama shoga yake, kwa upande mwingine hakuwa na ushauri mzuri, kwani alikuwa ni mtu wa kubomoa badala ya kujenga, hasa alipogundua kwamba suala lile lilikuwa ni la kimaendeleo. Grace hakugundua hilo zaidi ya kumwamini na kuanza kumwagia mambo yake ya siri!
“Ndiyo shoga, naona jinsi mnavyoishi maisha ya peponi. Mtoto wa kike unavyotunzwa vilivyo. Hakika mumeo anakupenda si mchezo!”
“Ni kweli mume wangu ananipenda, ten asana. Lakini kuna kitu ninachikikosa kutoka kwake. Bila kukuficha, mume wangu mpendwa siyo mzima kabisa! Naamua kusema ukweli, kwani hakuna sababu ya kukuficha wewe shogangu ati. Kwani wahenga walisema mficha maradhi, mauti humuumbua!”
“Uko wazi kabisa shogangu…mwanamke lazima azae…” Grace akamwambia huku uchungu ukiongezeka.
“Mbona leo sikuelewi shoga?” Mwantumu akamuuliza. Ukweli ni kwamba ingawa walikuwa wameunda ushoga na Grace kwa muda sasa, hakuna hata siku moja aliyowahi kumwambia maneno kama yale. Akahisi kuna sababu
“Utanielewa tu shoga. Natumaini unaona jinsi maisha yangu na mume wangu yalivyo ya raha mustarehe…”
“Shogangu Mwantumu,” Grace alimwita.
“Bee shogangu…”Mwantumu akaitikia.
“Kuna kitu nataka kukwambia…”
“Kitu gani shogangu?”
“Mwenzio nina shida…”
“Shida gani tena shoga?” Mwantumu akamuliza na kuendelea. “Wewe ni mtu wa kulia shida kweli? Acha kukufuru!”
“Binadamu lazima awe na shida…” Grace akaendelea kusema.
“Haya, shida gani?”
“Ni shida ambayo ni tofauti na wewe unavyofikiria shoga…”
“Haya mwaya, hebu nieleze.”
“Kuna shida au tatizo moja, ambalo nimekaa nalo kwa muda mrefu sasa bila kumweleza mtu yeyote, zaidi ya wewe ninayekueleza muda huu tukiwa wawili tu,” Grace akaendelea kumwambia. Halafu Grace akaendelea kumwangalia Mwantumu kama ujumbe wake unamwingia.
“Hivyo shoga, nitakachokueleza naona unaweza kunisaidia hata kwa mawazo,” Grace alisema huku akiwa na uchungu mwingi na machozi yakimtoka. Akaanza kuyafuta kwa upande wa khanga.
“Usijali, nieleze tu, kama nina uwezo wa kukusaidia, nitakusaidia. Halafu mbona unalia? Unaanza kunitisha mwenzio?”
“Hivi shogangu, si unajua kwamba nimeolewa?” Grace akamwambia Mwantumu huku akimwangalia kwa macho ya udadisi!
“Ndiyo, najua kwamba umeolewa…”
“Baada ya kuolewa kinachofuata ni nini?”
“Kinachofuata ni maisha ya ndoa, yaliyojaa upendo na furaha, kupeana unyumba na kuzaa watoto. Hiyo ndiyo hali halisi shogangu,” Mwantumu akamwambia Grace.
***********
“Utanielewa tu shoga. Natumaini unaona jinsi maisha yangu na mume wangu yalivyo ya raha mustarehe…”
“Ndiyo shoga, naona jinsi mnavyoishi maisha ya peponi. Mtoto wa kike unavyotunzwa vilivyo. Hakika mumeo anakupenda si mchezo!”
“Ni kweli mume wangu ananipenda, ten asana. Lakini kuna kitu ninachikikosa kutoka kwake. Bila kukuficha, mume wangu mpendwa siyo mzima kabisa! Naamua kusema ukweli, kwani hakuna sababu ya kukuficha wewe shogangu ati. Kwani wahenga walisema mficha maradhi, mauti humuumbua!”
“Mh, unasema mumeo siyo mzima kivipi?”
“Hawezi lolote! Unalala kama ndani kama mtu na dada yake! Sijui itakuwaje wakati mimi nataka mtoto!”
“Ina maana mtambo haufanyi kazi?” Mwantumu akamuuliza.
“Ndiyo manaake, hausimami kabisa!”
“Oh, hali hiyo imeanza lini?”
“Ni muda mrefu, tangu tuanze uchumba wetu na hatimaye kufunga ndoa. Hatujawahi kukutana kimwili, na nilijua hali hiyo wakati tukiwa katika fungate!”
“Unasema ulimkuta katika hali hiyo?” Mwantumu akaendelea kumuuliza.
“Ndiyo, nilimkuta hivyo!”
“Na umesema hamjakutana kimwili?”
“Ndiyo hivyo shoga, kweli ni makubwa yamenikuta, si mchezo!”
“Mh! Kweli ni makubwa!
“Hivyo shogangu nakuomba ushauri. Tambua kuwa wewe ndiye mtu wa kwanza kukueleza siri hii, sijamwambia mtu yeyote…oh!”
“Ni kweli unahitaji ushauri…”
“Ni kweli…ninateseka sana.”
“Ama kweli unayaweza. Kama ingekuwa ni mimi Mwantumu binti Korongo, mbona ningetoka nje ya ndoa, nipate mwanaume wa kuniridhisha?”
“Nitoke nje ya ndoa?”
“Ndiyo manaake!”
“Si dhambi shoga?”
“Dhambi? Usiwe mjinga!” Mwantumu akamwambia na kuongeza. “Tafuta mwanaume wa nguvu akuzalie mtoto! Utazeeka na uzuri wako bure nakwambia!”
“Ni kweli shoga, ushauri wako nimeusikia. Lakini siku hizi magonjwa ni mengi sana, hasa ugonjwa huu hatari wa Ukimwi, ambao hauna tiba, ukizingatia nia ya kukutana na mwanaume, ni kwa nia ya kuzaa. Sasa unafikiri kuna kutumia kondomu?” Grace akamwambia Mwantumu huku akimwangalia kwa makini.
“Kuwa mwelewa shogangu, siyo wanaume wote wenye magonjwa,” Mwantumu akamwambia na kuendelea. “Wewe ni mtu msomi, na ufanye mambo yako kisomi, siyo mpaka hilo nikuelekeze shoga.”
“Basi, nitajaribu kufanya hivyo, pengine nitafanikiwa na hatimaye kuitwa mama Fulani kama walivyo wanawake wengine…” Grace akasema akiwa ameukubali ushauri wa shogake, Mwantumu.
Ulikuwa ni usaliti wa hali ya juu!
Usaliti wa ndoa!
“Ndiyo, fanya hivyo. Ukikwama nitakusaidia zaidi shoga, siwezi kukuangusha,” Mwantumu akamwambia.
“Nashukuru sana shoga…” akamaliza kusema Grace.
Baada ya Grace kuupata ushauri ule, aliamua jambo moja tu, ni lazima aufanyie kazi. Alijiona kuwa bado yungali msichana mbichi, mruri na mrembo. Wanaume wengi waliokuwa na uchu walikuwa wakimtongoza kila kona aliyokuwa anakatiza. Ni kitu ambacho kilikuwa kimepangwa na kupangika, kwani wiki ileile, ambayo Grace alizungumza na shoga yake, Mwantumu kuhusu hali ile iliyokuwa inamkabili, jambo jingine lilimtokea, Geofrey, mume wake.
Mzee Joel Kisamo, akiwa jijini Arusha, aliamua kumpigia simu mwanae, Geofrey, katika kumuulizia maendeleo yake kwa ujumla, kwa vile walikuwa mbali. Vilevile ile hali ya kutokuwa rijali, ilizidi kumsumbua sana!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
GEOFREY alikuwa amekaa ndani ya ofisi yake, katika kampuni ya Mangi Fowarding & Clearing Agency. Ilikuwa ni saa nne za asubuhi wakati simu yake ya mkononi ilipoita, na alipoangalia namba za mpigaji, zilionyesha ni za mzee Kisamo, baba yake mzazi. Akaamua kuipokea:
“Haloo…baba…”
“Haloo…Geofrey mwanangu…”
“Ndiyo mimi baba naongea…
“Hamjambo na mwenzio?”
“Hatujambo baba, shikamoo…”
“Marahaba mwanangu. Na sisi hapa nyumbani hatujambo.”
“Naashukuru sana baba…”
“Nimeamua kukupigia simu mwanangu, ili niweze kujua maendeleo yenu na mkeo kwa ujumla.”
“Maendeleo yetu ni mazuri tu baba…”
“Nashukuru sana kama ni mazuri, lakini mkeo ameshajaaliwa kupata ujauzito?”
“Mh,” Geofrey akaguna, halafu akaendelea. “Bado baba…”
“Ni kwa sababu gani mpaka leo hii?”
“Ni kazi ya Mungu baba…”
“:Hapana, siyo kazi ya Mungu!” Mzee Kisamo akamwambia na kuongeza. “Hebu niambiae mwanangu, una matatizo gani?”
Swali hilo lilikuwa gumu sana kwa Geofrey, ukizingatia kuwa ni kweli hakuwa na nguvu za kiume. Sasa ulikuwa ni wakati muafaka wa kumweleza baba yake!
“Mbona kimya mwanagu?” Mzee Kisamo akauliza upande wa pili wa simu.
“Ah, nashindwa hata la kusema…” Geofrey akamwambia baba yake.
“Ni kweli, najua kuwa unashindwa la kusema. Na mimi nimeuliza hivyo kwa sababu nina mashaka na nguvu zako za kiume…” mzee Kisamo akamwambia ili ampashe ukweli!
“Mungu wangu!” Geofrey akatamka huku mapigo ya moyo wake yakipiga kwa kasi!
“Ndiyo hivyo mwanangu, tafakari hilo,” mzee Kisamo akamaliza kusema, kisha akakata simu.
Geofrey akabaki ameikamatia simu yake, huku akiwa amepigwa na bumbuwazi. Alikosa raha kabisa, hasa akifikiria jinsi baba yake alivyotamka maneno yale yenye ukweli ndani yake. Alikuwa na kasoro kwa jogoo lake kutoweza kupanda mtungi!
Daima siku zote ukweli huwa unauma, lakini angefanyeje? Ilimbidi apange na kuyapangua mawazo kichwani mwake, kiasi cha kufikia uamuzi wa kumketisha chini mke wake, Grace, ili kupanga namna ya kulitatua tatizo lile. Siku hiyo alifanyakazi bila raha kabisa hadi ilipofika muda wa kufunga ofisi jioni, akarejea nyumbani kwake, Tabata.
Kabla Geofrey hajamweka kitako mkewe Grace, ili kuzungumzia suala lile, yeye Grace alimuawahi hata kabla hajaanza kumwelezea. Wakiwa wamekaa sebuleni baada ya kumaliza kula chakula, Grace aliona kuwa ulikuwa wakati muafaka wa kumweleza tatizo lile mumewe Geofrey. Kwa upande wa Geofrey, alionekana kama mtu aliyekuwa na mawazo mengi kutokana na ule ujumbe wa simu kutoka kwa baba yake, mzee Kisamo, hakujua aanzie wapi!
“Mume wangu,” Grace alimwita kiasi kwamba Geofrey alishtuka kutoka katika lindi la mawazo!
“Naam mke wangu…” Geofrey akaitikia na kumwangalia mke wake.
“Napenda kukutaarifu kuwa siku ya leo nina mazungumzo muhimu na wewe…” Grace akamwambia mumewe, kasha akachukuwa kitendea mbali na kupunguza sauti ya runinga. Akajiweka sawa ytayari kuongea na umewe!
“Maongezi gani tena?” Geofrey akamuuliza.
“Ni maongezi muhimu juu ya maisha yetu kwa ujumla.”
“Sawa mke wangu, nakusikiliza…”
“Wewe si mume wangu?”
“Ndiyo, ni mumeo, hilo nalielewa…”
“Si unajua tumeishi muda mrefu sasa?”
“Ndiyo, ni muda mrefu…” Grace akasema huku akiendelea kumkazia macho mumewe. Akamaliza, “Lakini pamoja na kuishi kwa kipindi chote hicho, hakuna kinachoendelea…”
“Hakuna kinachoendelea kivipi?” Geofrey akamuuliza!
“Ndiyo, hakuna kinachoendelea. Hivi wewe huoni jinsi tunavyoishi?”
“Mh,” Geofrey akaguna. Halafu akanyamaza kimya bila kusema chochote. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka ingawa pale juu ya dari palikuwa na pangaboi lililokuwa likileta upepo mzuri. Hakika mke wake alikuwa amemtonesha donda lake!
“Ninachotaka kusema mume wangu,” Grace akaendelea kusema. “Wewe ndiyo hivyo tena, huwezi kuzaa motto kama ilivyo kawaida kwa mwanamke. Mimi nataka kuzaa, kwani muda unazidi kwenda, na uzee unaingia, nitakufa bila kuwa na mtoto? Na pia najua nikirudi Arusha nitawaambia nini kwa kutokuwa na mtoto? Yaani nirudi kama nilivyoondoka?”
“Ooopsi!” Geofrey akavuta pumzi ndefu, halafu akamwangalia mke wake kwa uchungu na huzuni kubwa. Akiwa ni mtu mwenye akili timamu, aligundua kuwa mke wake alikuwa amechoka na si vinginevyo!
“Mke wangu mpendwa nimekuelewa unachosema, naomba tuelewane…” Geofrey akamwambia.
“Tuelewane nini?”
“Naomba unitunzie siri yangu…”
“Niitunze mara ngapi?”
“Nisikilize kwanza mke wangu. Ni kwamba nataka tupange jambo moja!”
“Jambo gani tena?”
“Nataka nikuruhusu kitu…”
“Kitu gani hicho? Naomba unieleze.”
“Nimekaa nikawaza na kuwazua. Nimepanga kwamba kutokana na tatizo nililonalo, nakuruhusu utafute mwanaume yeyote, ambaye utafanya naye mapenzi ili upate ujauzito, tupate angalau mtoto wa kufutia machozi na kuiondoa hii aibu inayotukabili! Ukweli ni kwamba hata mimi nakosa raha kabisa!”
“Mungu wangu!” Grace alisema kwa mshangao na kuongeza. “Unajua sijakuelewa mume wangu?”
“Ndiyo hivyo. Nielewe nilichokueleza, tafuta mwanaume, kisha uzae naye!” Geofrey akamweleza mkewe kwa msisitizo!
“Ina maana umeniruhusu kufanya mapenzi nje?”
“Ndiyo manaake!”
“Kweli?”
“Sina jinsi. Imenibidi kufanya hivyo, ili mradi unitunzie siri yangu. Vilevile ufanye kwa heshima kubwa!” Geofrey akaendelea kumwambia mke wake huku akiwa na uchungu mwingi sana na pia akimwangalia jinsi alivyokuwa amenona na umbile la tipwatipwa!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
“Maadam umekubali mume wangu, itabidi kufanya hivyo, ingawa roho inaniuma sana. Yaani kufunguliwa ‘njia’ na mwanaume mwingine, badala ya wewe mume wangu niliyekutunzia?” Grace akasema kwa uchungu mkubwa!
“Hakuna haja ya kujadili. Mimi nimeshakuruhusu, bora heshima mke wangu…” Geofrey akamwambia huku akimpigapiga begani.
“Sawa mume wangu…hakuna jinsi. Kazi ni moja katika kulitekeleza zoezi hilo mara moja,” Grace akamwambia mumewe.
“Ndiyo hivyo, naona muda mwingi sasa, ni muda muafaka wa kwenda kulala…” Geofrey akasema huku akinyanyuka na kuelekea chumbani. Akamwacha Grace akiweka vitu sawa pale sebuleni, ikiwa ni pamoja na kuzima runinga na pia taa ya sebuleni.
Grace alipomaliza kuzima taa, akaingia chumbani, ambapo alimkuta Geofrey ameshajilaza kitandani. Usingizi ulikuwa hamjampata, lakini alionekana ni mtu mwenye mawazo mengi sana. Hata hivyo hakumsemesha, zaido ya yeye kujilaza kando yake katika kitanda kile kikubwa cha futi sita kwa sita. Mawazo mengi yakaanza kumwandama pia, kuhusu ule uamuzi aliokuwa ameamua mumewe, juu ya kutembea nje ya ndoa!
Ukweli ni kwamba kwa upande wake alikuwa ni mwanamke mwaminifu, lakini baada ya kupewa ruhusa ile, hakuwa na la kufanya zaidi ya kuutekeleza. je, atautekeleza na mwanaume gani? Siyo rahisi kumtongoza mwanaume njiani, sasa afanyeje? Akaendelea kujiuliza Grace!
Hata hivyo, Grace alikumbuka kitu kimoja. Ni kijana Adrian Senga, ambaye alikuwa akimtongoza mara kwa mara, na yeye akawa anamtolea nje! Ndiyo, alikuwa ni kijana mvumilivu kwa jinsi alivyokuwa hakati tamaa katika kumfuatilia, basi akaona huyo ndiye atakayejaribu naye kama alivyoruhusiwa!
Adrian Senga alikuwa kijana mtanashati na mwenye kujipenda, ambaye walikuwa wamepishana kiumri kidogo na Geofrey. Alikuwa bado hajaoa, kiasi cha kumfanya awe anamzengea Grace kwa muda mrefu baada ya kuvutiwa naye. Huyu Adrian alikuwa anaishi mtaa wa tatu kutoka nyumbani kwa Geofrey, akiwa amepanga chumba, na kikazi alikuwa mtu wa ‘misheni tauni’ katikati ya jiji la Dar es salaam.
Ni kila mara kijana Adrian alikuwa akijaribu kumsemesha Grace, lakini alipata kipingamizi kikiubwa kutokana na mwanamke kutotaka kumsikiliza ule upuuzi aliokuwa anataka kumwambia, akimtahadharisha kwamba alikuwa mke wa mtu. Hata hivyo Adriana hakukata tamaa, akijua kuwa iko siku atafanikiwa kumpata ndege mlengwa. Na mwombaji huwa achoki na akichoka amefanikiwa!
*******
JUMAMOSI moja, siku ya pili tangu Grace na mumewe Geofrey wapange ule mkakati wao, Grace alikuwa akitokea katika saluni, iliyokuwa katika mtaa wa tatu, ambapo alikuwa amekwenda kutengeneza nywele zake. Wakati akiwa anarejea nyumbani, alikutana na Adrian katika uchochoro mmoja uliotenganisha nyumba na nyumba. Kwanza kabisa baada ya kuonana tu, moyo wake ulipasuka kuashiria jambo Fulani, hasa Grace aliyekuwa akitongozwa na Adrian kwa muda mrefu, lakini akawa anamkataa.
“Hujambo anti?” Adriana alimsalimia.
“Sijambo, hali yako…” Grace aliitikia bila kinyongo chochote huku akitabasamu. Kwa vyovyote vile, aliona kuwa bahati yake ilikuwa imemshukia kwa kukutana na kijana Adrian, aliyekuwa anamkataa siku zote.
“Mimi sijambo,” Adriana aliitikia huku akiwa amesimama mbele ya Grace. Halafu akaongeza kusema. “Naona leo imekuwa kama bahati tumekutana!”
“Kwa nini unasema hivyo?” Grace akamuuliza bila kufanya ukorofi kama alivyokuwa amezoea.
“Kwa sababu ni mara nyingi unanichunia kuongea na mimi,” Adrian akamjibu.
“Kuongea nini?”
“Kuna suala nataka kukuambia…”
“Naona wewe ni king’ang’anizi…” Grace akamwambia na kuendelea. “Hebu nieleze basi, si unajua mimi ni mke wa mtu? Sasa kusimama vichochoroni siyo vizuri.”
“Na kweli hapa hapafai kuongea…”
“Sasa?”
“Tutafute sehemu yoyote yenye usalama, kwani naheshimu wewe ni mke wa mtu. Naomba twende pale Mariana Pub, ili tuweze kuongea nap engine kupata kinywaji kidogo…” Adriana akamwambia.
“Hapana, siwezi kwenda pale, kwa sababu ni sehemu ya wazi sana, ambapo kila mtu anaweza kutuona, akiwemo mume wangu.”
“Kwa hiyo?”
“Panga tukutane kesho Jumapili, sehemu iliyojifiocha…”
“Hakuna tatizo, naomba namba za simu yako ya mkononi, halafu nitakujulisha.”
Grace na Adriana walipeana namba za simu, baada ya kukubaliana kukutana kwenye nyumba ya wageni ya Rufita Gesti, iliyoko eneo la Ubungo, ili waweze kumaliza mazungumzo yao. Baada ya hapo, wakaagana na kila mmoja akaelekea na uelekeo wake, ambapo kwa upande wa Adriana alijikuta akiwa na mshangao mkubwa baada ya kukubaliwa kirahisi namna ile na mwanadada mrembo, Grace, aliyekuwa akimzungusha kwa muda mrefu na kumkwepa.
Na hata kwa Grace naye hakujua bahati ile ilivyotokea. Kichwani mwake alikuwa akipanga jinsi ya kumpata mwanaume wa kutembea naye na kuhakikisha anapata motto kama walivyokuwa wamepanga na mume wake, Geofrey. Ilikuwa ni vigumu sana kwa Grace kusimamisha wanaume ovyo barabarani kwa lengo la kuwataka kimapenzi. Lakini kwa Adrian, alijikuta akishindwa kujizuia siku hiyo, hasa baada ya kufikia makubaliano na mume wake. Kuanzia muda ule, Adrian akawa ndiyo chaguo lake, mwanaume ambaye nduye atakayefungua njia katika mwili wa Grace, mwanamke ambaye alikuwa bado hajaguswa na mwanaume yeyote tokea azaliwe kuwa mwanamke!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
MAJIRA ya saa saba za mchana siku ile ya Jumapili, Adriana Asenga, alikuwa ndiye mtu wa kwanza kufika Rufita Gesti, iliyoko Ubungo. Na ile walikuwa wamepanga kila mtu afike kwa wakati wake na kwa siri ili Grace asionekane na watu ukizingatia tukio lile lilikuwa ni la kuiba nje ndoa. Huwenda kidudu mtu akamwona na kwenda kumwaga umbea kwa watu na hata kwa mume wake! Watu hawana dogo, kila watakaloliona hawana subira zaidi ya kupayuka!
Adrian alipofika tu, hakupoteza muda, bali aliingia ndani ya gesti ile hadi sehemu ya mapokezi ambapo alimkuta mhudumu wa kiume anayeshughulika na kazi za pale. Baada ya kumwelezea shida yake, akapanga chumba namba 12 ambacho kilikuwa mwisho kabisa. Alipokabidhiwa ufunguo, akaelekea na kuingia ndani ya chumba kile kilichokuwa nadhifu. Chumba alichopanga kilikuwa na huduma zote, zikiwemo choo na bafu ndani yake. Bila kusahau friji ndogo, simu na runinga ndogo iliyokuwa kwenye pembe ya chumba. Hakukuwa na usumbufu kwa wateja kutoka nje kwenda kujisaidia, na hii yote ilionyesha jisi Adrian alivyokuwa mwizi mzoefu wa wake za watu.
Baada ya kuingia mle chumbani, ndipo Adrian alipompigia simu Grace, ambapo alimweleza juu ya namba ya chumba alichopanga na atamkuta anamsubiri. Grace naye alifika pale baada ya robo saa, ambapo alipoingia alimkuta mhudumu ambaye alimweleza kuwa ni mgeni wa Adriana aliyekuwa ameshatangulia. Akaelekezwa ndani ya chumba alichokuwemo Adrian, ambacho alikiendea na kugonga mlango mara mbili. Mlango ulikuwa haujafungwa kwa ndani, hivyo akashika kitasa na kuufungua taratibu, halafu akaingia ndani ya chumba huku mapigo ya moyo wake yakipiga kwa kasi, kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuingia ndani ya chumba cha gesti!
“Oh, karibu sana…” Adrian akamkaribisha, wakati huo akiwa amekaa kwenye kiti akiangalia runinga iliyokuwa inaendelea kuoyesha sinema.
“Ahsante sana,” Crace alijibu huku akiingia mle ndani, halafu akaendea kukaa kwenye kiti kingine kilichokuwepo mle chumbani. Akaanza kuchunguza mandhari ya mle ndani na kuridhika kuwa kilikuwa kisafi kuanzia kwenye kitanda kile kikubwa cha futi sita kwa sita kilichotandikwa shuka safi nyeupe, na pia kukiwa na mito miwili.
“Nashukuru umetimiza ahadi,” Adrian alimweleza Grace kwa lengo la kuuondoa ukimya kati yao.
“Kwani ulifikiri sintafika?” Grace akamuuliza na kuongeza. “Mimi nina ahadi za kizungu…”
“Basi vizuri, je, unatumia kinywaji gani niagize?” Adrian akamuuliza.
“Nitakunywa soda aina ya Mirinda,” Grace akamjibu.
“Hunywi bia?”
“Hapana, situmii kilevi chochote...”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment