Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

SIRI YA MKE - 3

 





    Simulizi : Siri Ya Mke

    Sehemu Ya Tatu (3)





    ***********



    “NASHUKURU umetimiza ahadi,” Adrian alimweleza Grace kwa lengo la kuuondoa ukimya kati yao.

    “Kwani ulifikiri sintafika?” Grace akamuuliza na kuongeza. “Mimi nina ahadi za kizungu…”

    “Basi vizuri, je, unatumia kinywaji gani niagize?” Adrian akamuuliza.

    “Nitakunywa soda aina ya Mirinda,” Grace akamjibu.

    “Hunywi bia?”

    “Hapana, situmii kilevi chochote...”

    “Poa, ngoja niagize...” Adrian akasema, halafu akaunyanyua mkonga wa ile simu ya ndani, ambapo alipiga simu kule mapokezi na kuomba wahudumiwe vinywaji.

    Muda siyo mrefu, mhudumu aliingia pale chumbani akiwa na soda mbili zilizokuwa kwenye sinia, ikiwa ni kwa ajili ya wote wawili, kwani Adriana hakupenda kunywa bia, akihofia kumuudhi Grace. Soda zikafunguliwa na mhudumu huyo na kuwaacha yeye akitoka nje. Wakaendelea kunywa taraibu huku wakiendelea na maongezi yao. Kila mmoja alikuwa na mawazo yake kichwani, hasa Grace aliyekuwa akiwaza mbali sana akifikiria juu ya usaliti ule wa mapenzi uliotiwa baraka na mumewe!

    “Kwa jina ninaitwa Adrian Asenga...ni mfanyabiashara...sijui wewe mwenzangu?” Adriana aliamua kuuvunja ule ukimya uliokuwa umetawala.

    “Naitwa Grace...” alijibu Grace huku akiendelea na ukaguzi wa chumba kile, ambacho kwa wakati ule kilikuwa na jbaridi mkali uliotokana na kiyoyozi kilichokuwa kinapuliza hewa.

    “Vizuri sana, je, umeaga nyumbani?”

    “Nimeaga...”

    “Mume wako hawezi kujua?”

    “Ah, achana na ua mume wangu, tuongelee yaliyotuleta hapa.”

    “Mambo si hayo?” Adriana limwambia Grace na kuongeza. “Sasa huu ni muda muafaka wa kukueleza dhumuni la kukuita sehemu hii. Ukweli bila kuficha ni kwamba nimekuzimia kimapenzi muda mrefu sana, ingawa najua kuwa wewe ni mke wa mtu....” Adriana alimweleza yote kwa kirefu kuhusu madhumuni yake ya kumwalika pale Rufita Gesti. Hakumficha, alimweleza kuwa alimhitaji kimapenzi, maneno ambayo hayakumshangaza Grace kwa vile alishaifahamu dhamira yake, hivyo hawakuzungushana. Jambo zuri zaidi ni kwamba Grace alishapata ruhusa kutoka kwa mumewe ya kutembea na mwanaume anayempenda. Hivyo ilikuwa ni kazi moja tu, kutekeleza kitendo!

    Dakika tano zilizofuata, wote wawili walikuwa wameshasaula nguo zao. Katika kipindi hicho, mapigo ya moyo wa Grace yaliongezeka kutokana na woga na wasiwasi aliokuwa nao, hasa ikizingatiwa kwamba ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana kimapenzi na mwanaume. Akabaki kumkodolea macho Adrian kwa mshangao!

    “Sasa?” Adrian akamuuliza Grace baada ya kuuona ule mshangao aliokuwa nao!

    “Unajua mimi sijawahi kufanya tendo la ndoa?” Grace akamwabia!

    “Unasemaje?”

    “Ndiyo hivyo, mimi sijawahi kukutana na mwanaume!”

    “Ina maana ulikuwa hujakutana kimwili na mume wako?”

    “Ndiyo...”

    “Kwa sababu gani?”

    “Ah, hayo najua mwenyewe...cha muhimu nifundishe, kwani ndiye mwanaume wangu wa kwanza...”

    “Mungu wangu!” Addriana akasema kwa mshangao!

    “Ndiyo, inabidi unitunzie heshima yangu, sijui unanuelewa?”

    “Nakuelewa vizuri sana.”

    Baada ya kumaliza mazungumzo yao, wote walijitupa kitandani, na kilichoendelea kilikuwa siri yao. Kwa kifupi ni kwamba walipeana penzi moto moto, ambayo yalimpagawisha Grace. Adrian alikuwa mjuzi wa shughuli ile pevu, mpaka walipomaliza, Grace alikuwa ameridhika kiasi cha kumsifia Adrian kwamba ni mwanaume wa shoka!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******

    TANGU siku hiyo, Grace alikuwa amenogewa na mchezo ule. Akawa kama mnyama, Fisi, aliyeonyeshwa mfupa wa binadamu. Baada ya mume wake kumruhusu kufanya mapenzi nje ya ndoa kwa minajili ya kupata mtoto, ikawa sasa Grace ameonjeshwa raha adimu!

    Ikawa sasa Grace anaondoka nyumbani kwake muda wowote anaotaka na kwenda kukutana na Adrian, wakawa wanaponda starehe na kushiriki katika tendo la ndoa. Grace akaona kama alikuwa amepata bahati ya mtende, na kwa vile Adrin alikuwa ameshamkoleza, ilimbidi amgande na wakati mwingine kupitisha usingizinyumbani kwake au hata katika nyumba ya wageni, Kitendo kile kikamfanya Geofrey aanze kuingiwa na wivu kwa kujiona alikuwa mjinga kwa kumruhusu mke wake kutembea nje ya ndoa. Akawa anajiuliza, inakuwaje mke wake alale nje na kumwacha ndani peke yake?

    Isitoshe, hakujua kitakachotokea zaidi ya hapo, iwapo mke wake atajihusisha kimapenzi na zaidi ya mwanaume mmoja, hasa akifikiria hatari ya ugonjwa wa Ukimwi, ambao hadi sasa haujapata tiba! Ukweli ni kwamba alianza kuzichoka tabia za mke wake, kwani badala ya kutafuta motto kama walivyokubaliana, sasa ilionekana kama vile alikuwa anafanya mchezo mchafu zaidi. Akaamua kumketisha chini ili walizungumzie suala lile!

    Siku moja wakiwa wamekaa sebuleni, wakiburudika na vinywaji baridi, huku wakitazama runinga, Geofrey akaamua kumpasulia ukweli mume wake!

    “Grace mke wangu mpenzi...” Geofrey alimwita kwa sauti ya chini.

    “Unasemaje mume wangu,” Grace aliitika huku akimwangalia mume wake kwa jicho la pembeni.

    “Hebu naomba uniambie, ni kitu gani kinachoendelea?”

    “Kinachoendelea kivipi?”

    “Yaani kukupa ruhusa kutembea nje ya ndoa ili kutafuta mtoto imekuwa nongwa?”

    “Mbona sikuelewi?”

    “Nasema hivi, kukupa ruhusa kutembea nje ya ndoa ndiyo imekuwa kosa mpaka unaamua kulala hukohuko?”

    “Oh, mume wangu!”

    “Lakini si kweli?”

    “Ndiyo, ni kweli. Lakini si wewe mwenyewe uliniruhusu?”

    “Nilikuruhusu, lakini sasa imezidi!”

    “Si unajua kutafuta mimba siyo kazi ndogo? Na lazima nipate mtu anayejua kulenga! Kama ni hiyo, basi mimi nitakuwa nikishinda hapa nyumbani, halafu ujitahidi jogoo lako liwike ili tupate mtoto, umeielewa?”

    “Mungu wangu!” Geofrey akasema kwa uchungu mwingi!

    “Huo ndiyo ukweli!” Akaongeza Grace!

    “Hakika umefika mbali!”

    “Ndiyo, inabidi iwe hivyo, maana nakuona unaanza kuwa mkali sasa!”

    “Basi mke wangu, yamekwisha, endelea tu kutafuta mtoto huko nje, lakini ni bora uchague mwanaume mmoja aliye mwaminifu, siyo wa kudandia! Kuna gojwa la ukimwi mke wangu!”

    “Hilo naelewa mume wangu, nitakuwa makini sana na matokeo yake yatakuwa mazuri!”

    “Sawa,: alijibu Geofrey, kisha wakaufunga ule mjadala!

    Geofrey alikubali yaishe, lakini rohoni alikuwa akiumia, hakuwa na la kufanya zaidi ya kuukubali ukweli ule. Ingawa alimketisha chini na kumweleza yote, lakini ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa! Tabia ya Grace iliendelea kuwa mbaya kiasi kwamba alianza hata kunywa pombe, kitu ambacho ahapo zamani alikuwa hatumii, na hiyo ilikuwa ni kazi ya kijana, Adrian aliyekuwa akifanya matanuzi naye kiasi cha kumshawishi kunywa pombe. Kwa vile alikuwa ameshampenda, Grace akaamua kuufuata ushauri wake!

    Wakati mwingine Grace alikuwa akirudi nyumbani amelewa na heshima kwa mume wake kupungua, kikiwa ni kitendo ambacho kilishuhudiwa hata na majirani, kiasi cha kuanzisha minong’ono ya hapa na pale. Kama kawaida, majirani zao wakiwa wamekaa kibarazani, pamoja na shoga yake mkubwa, Mwantumu, walikuwa wakiongelea suala lile, ikiwa ni umbea uliozoeleka maeneo ya uswahilini.

    Ile ilikuwa ni baada ya Grace kupita pale walipokuwa wamekaa na kuwasabahi kisha akaondoka zake huku akiwa ameupara vilivyo!

    “Mh, huyu mwanamke mwenzetu amezidi, Malaya kwelikweli!” Alisema jirani mmoja mwanamke!

    “Na kweli...” akaongeza mwingine aliyekuwa bonge la mtu!

    “Hafai kabisa, atamuua mumewe kwa ukimwi!”

    “Sijui amekosa nini? Mtu ana midhahabu kibao, lakini haridhiki?” Yule wa kwanza alisema huku akiubetua mdomo wake.

    “Siyo bure, amemtengeneza mumewe,” akadakia yule wa pili.

    Wakati wote huo, Mwantumu alikuwa akiwasikiliza wenzake walivyokuwa wanaongea. Naye akaamua kupasua jibu, hasa ukizingatia kuwa ndiye aliyemshawishi Grace atoke nje ya ndoa.

    “Jamani, acheni tu,” Mwantumu aliwaambia.

    “Tuache nini?” Aliuliza mmoja wa wanawake pekupeku!

    “Ni lazima mwanamke mwenzetu afanye hivyo...hana jinsi...” Mwantumu akasema.

    “Kwa nini unasema hivyo?”

    “Hakuna anachotimiziwa ndani ya nyumba na mwanaume wake,” Mwantumu akawaambia.

    “Fafanua shoga, hatukuelewi!”

    “Mumewe hafai!” Akapasua!

    “Hafai kivipi? Au siyo rijali?”

    “Ndiyo manaake,” Mwantumu alisema Mwantumu na kuendelea. “Yaani wanalala kama mtu na dada yake, au na mwanamke mwenzake, jogoo hawiki!”

    “Mtumeee! Hakika hayo makubwa!”

    “Yaani wameishi hivyo kwa muda mrefu?”

    “Ndiyo, tokea walipofunga ndoa...”

    “Hapana, hii ni mpya, walipatana wapi wakati mwanaume ana matatizo?”

    “Walikopatana wanajua wenyewe, lakini hali halisi ndiyo hiyo!”

    Pamoja na maneno mengi ya majirani waliyokuwa wanayasema, uzi uliuliendelea kuwa uleule kwa Grace. Kazi ilikuwa moja tu, kutafuta mtoto, utaratibu ukawa huohuo. Mumewe Geofrey akazidi kusononeka, lakini hakuweza kufanya kitu!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******

    JIJINI Arusha, hali ya maisha ilikuwa nzuri kwa familia ya mzee Kisamo. Lakini tatizo dogo lililokuwa linamkabili mzee huyo, ni kwamba mdogo wake Geofrey, aitwae Deo, alikuwa masomo yake ya sekondari, kidato cha nne na hakufanikiwa kuendelea na elimu ya juu. Hivyo akawa anazurura tu bila kuwa na kazi ya kufanya. Mbali ya kutofanyakazi, Deo alipenda kukaa katika makundi ya vijana wenzake, kiasi kwamba alikuwa akikumbwa na mabalaa ya kukamatwa na polisi mara kwa mara katika kundi la watu wanaoitwa wazururaji.







    Mara nyingi alikuwa akitolewa na mzee Kisamo. Kukamatwa mara kwa mara kwa Deo, kulimkera mno baba yake kwa vile alikuwa akipoteza fedha nyingi kwa ajili ya kumtoa polisi. Akaamua kupanga la kufanya ili kuondokana na adha hiyo. Kwa kushirikiana na mkewe, mzee Kisamo aliamua kupanga jinsi ya kumsaidia Deo, ili asije kuharibikiwa au kujihusisha na mambo mabaya kama vile utumiaji wa dawa za kulevya au ujambazi, mambo ambayo yangeweza kumfanya aozee jela kama siyo kuchomwa moto na raia wenye hasira!



    “Mama Geofrey...” mzee Kisamo alimwita mke wake siku moja walipokuwa wamekaa sebuleni.



    “Nakusikiliza baba Geofrey...” aliitikia mama Geofrey.



    “Unalionaje suala la mtoto wetu, Deo...”



    “Hata mimi bado linanitatiza...”



    “Mimi nimepata wazo zuri...” mzee Kisamo akamwambia.



    “Wazo gani hilo?”

    “Naona tumpeleke Dar es Salaam kwa kaka yake. Labda ataweza kumtafutia kazi kitakachomfanya abadilike na kutulia...”



    “Ni wazo zuri baba Geofrey kwasababu hata mimi naona hapa Arusha hapamfai, asije kufungwa bure!” Mama yake akasema na kuongeza. “Lakini bado kuna kitu kinanitatiza. Je, Deo atawezana na shemeji yake, Grace?”



    “Kwa nini wasielewane? Kule hakuna kazi nyingi za nyumbani. Ingekuwa yule mwanamke amezaa, tungeweza kusema atapewa kazi nyingi kama vile za kufua nepi za mtoto, lakini watu wenyewe hawajazaa!” Mzee Kisamo alimwambia!



    “Basi, itabidi tumjulishe kwa njia ya simu. Nadhani ni bora umjulishe leo hii...”



    “Baada ya majadiliano yale, mzee Kisamo hakupoteza muda. Alichukua simu yake ya mkononi na kumpigia Geofrey. Na baada ya kusalimiana, alimweleza yote juu ya mdogo wake, Deo.



    “Hakuna tatizo baba. Mwandaeni tu aje huku Dar, nitajitahidi kumtafutia kazi...” Geofrey alimwambia baba yake.



    “Basi, tunashukuru sana, tutamwandaa,” mzee Kisamo akasema.

    Walipomaliza maongezi yao, wakaendelea na ratiba nyingine, huku mzee Kisamo akifurahi kuona kuwa Geofrey amekubali kumchukua mdogo wake, Deo, ili akaishi naye Dar...



    ********

    WIKI moja baadaye, Deo aliwasili Dar es Salaam na kupokewa vizuri na kaka yake pamoja na shemeji yake, Grace. Ukweli ni kwamba Grace alifurahi mno kumpata mtu wa kumuondolea upweke, hasa ikizingatiwa kuwa, walikuwa wakiishi wawili tu, hali iliyosababishwa nyumba iwe imepooza.



    Baada ya Deo kupumzika na kuyaanza maisha mapya, kaka yake aliamua kumketisha chini na kumweleza madhumuni ya kumleta kwake Dar. Akamwambie, “Mdogo wangu, nafikiri umeyafurahia maisha ya Dar au siyo?”



    “Kwa kiasi fulani nimeyafurahi kaka, lakini nitayafurahia zaidi mara baada ya kuanza kazi,” alisema Deo.



    “Basi, usijali, mimi ni kaka yako, niko mbioni kukutafutia kazi, hivyo usiwe na wasiwasi,” Geofrey alimjibu.



    “Nitashukuru sana kaka.”

    Baada ya muda, Geofrey alimuuliza Deo, “Tangu umefika, unayaonaje maisha hapa nyumbani?”



    “Kivipi kaka?”



    “Mambo siyo mazuri...”



    “Kwa nini unasema hivyo kaka?”



    “Shemeji yako amebadilika kitabia...”



    “Amebadilika kivipi?”



    “Nasema hivyo kwa sababu siku hizi anaweza kuondoka hapa nyumbani mapema, lakini kurudi kwake ni saa sita usiku!”



    “Huwa anatokea wapi usiku huo?”



    “Sijui. Kisha hunigongea mlango nimfungulie, sijui huwa anatokea wapi!”



    “Hali hiyo imeanza lini?” Deo akaendelea kumuuliza.

    “Ni muda kiasi,” Geofrey akasema na kuongeza. “Hali hiyo imenifanya nisononeke sana kwa kubaki peke yangu hapa nyumbani. Maadam umekuja, tutakuwa wote.”



    “Pole sana kaka, lakini mmefikia suluhisho gani?”



    “Hakuna kilichosuluhishwa zaidi ya kubaki hivyohivyo. Yaani tunaishi kila mmoja na maamuzi yake!”



    “Hapana kaka, tutajaribu kulisuluhisha jambo hili. La sivyo, hakutakuwa na amani ndani ya nyumba na mwishowe kufukuza baraka zote,” Deo alimwambia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni kweli usemayo. Tutajitahidi kuyasuluhisha mdogo wangu,” Geofrey akamwambia huku nafsi yake ikimsuta. Ukweli ni kwamba ni yeye aliyekuwa na makosa kwa sababu alimruhusu mkewe kufanya mapenzi nje ya ndoa kwa lengo la kuficha aibu yake ya kimaumbile.



    Hata hivyo, Deo alikuwa mtu mzima na mwenye akili timamu. Haikuwa mara yake ya kwanza kuusikia mgogoro ule. Aliwahi kumsikia baba yao, mzee Kisamo akiilalamikia ndoa ya Geofrey na Grace kwa vile waliishi muda mrefu bila kupata mtoto.



    Alielewa wazi kwamba mgogoro ule ulisababishwa na hali hiyo ya hali hiyo ya kimaumbile ya Geofrey ndiyo sababu Grace aliamua kutembea nje ya ndoa kwa lengo la kujiridhisha kimatamanio ya mwili. Baada ya Geofrey kumweleza mdogo wake kuhusu mambo anayofanya Grace, huku nyuma, Grace naye alipokuwa akibaki na shemeji yake, Deo, alikuwa na mengi ya kumweleza.



    “Shemeji yangu Deo,” Grace alimwita Deo siku moja walipokuwa wamekaa barazani.



    “Sema shemeji,” alijibu Deo.

    “Yaani naona raha sana baada ya kuja kwako. Maana nyumbani palikuwa pamepooza sana,” alisema Grace.



    “Kwa nini unasema hivyo?”

    “Si unaona mwenyewe palivyopooza?”



    “Ah, shemeji bwana, kwani kaka si yupo? Tatizo nini?”



    “Ndiyo, kaka yako yupo, lakini nimekwambia anashinda kazini.”



    “Na usiku je?”



    “Usiku anakuwepo, lakini...” Grace alishindwa kuendelea.



    “Mh, pole sana shemeji...” Deo akasema na kuishia hapo.



    Siku hiyo Grace hakuondoka nyumbani, kitu ambacho kilimshangaza sana Deo, hasa baada ya kukumbuka kauli ya kaka yake, kwamba alikuwa hatulii nyumbani. Deo akaamua kuvuta subira kwa vile tatizo alishajua liko wapi.



    *******

    USIKU mmoja, Deo na shemeji yake, Grace walikuwa wamekaa sebuleni wakiangalia runinga huku wakiongea mambo mbalimbali yanayohusu maisha kwa ujumla. Wakati huo Geofrey alikuwa bado hajarudi kutoka kazini, hivyo Grace alikuwa na jambo moja ambalo lilikuwa linamkereketa moyoni, alivuta pumzi ndefu na kumuuliza Deo:



    “Shemeji Deo, kuna jambo kukuuliza...”

    “Jambo gani shemeji? Uliza tu...” Deo akamwambia huku akimwangalia.



    “Naomba usinifiche...”



    “Usijali, wewe uliza, usiwe na wasiwasi......” Deo alimtoa wasiwasi.



    “Hebu nieleze juu ya wazazi, baba na mama, kule Arusha wanasemaje?”



    “Juu ya nini?”



    “Juu ya maisha yetu, mimi na kaka yako Geofrey. Ni muda mrefu tumekaa bila ya kuzaa mtoto, au vipi shem?”



    “Ohoo, kumbe ni hilo?” Deo akasema na kuongeza. “Bila kuficha, kwa mtazamo wangu, wana wasiwasi sana shemeji.”



    “Wasiwasi wa nini?”

    “Baba anashangaa mpaka leo hamjapata mtoto. Nafikiri labda ana wasiwasi kuwa wewe ndiye mwenye matatizo, kwa hisia zangu lakini...” Deo akamwambia Grace.



    “Mimi nina matatizo?” Grace akadakia huku akimwangalia shemeji yake kwa jicho la ukali! Uzuri wake wote ukayeyuka!



    “Kwa kweli sijui, lakini baba anadai kuwa kaka Geofrey ndiye mwenye matatizo, sijui ukweli ni upi...”



    “Na wewe unaamini hilo?” Grace akauliza.



    “Kwa kweli mimi niko njia panda, sielewi. Na sipendi kuingia sana katika unyumba wa watu!”



    “Mungu wangu!” Grace akasema na kuanza kulia kilio cha chini chini!



    “Vipi shemeji, mbona unalia?” Deo akauliza, kisha akanyanyuka kutoka kwenye kochi alilokuwa amekalia na kumwendea Grace.



    “Hebu tulia...” akamwambia.



    “Siyo hivyo shemeji, naona uchungu sana kuambiwa mimi nina matatizo, wakati ni mzima kabisa na mwenye uwezo wa kuzaa. Bila kukuficha, tatizo liko kwa kaka yako, Geofrey, siyo mzima kabisa, amini nakuambia...”



    “Unasema siyo mzima?Hebu fafanua!”



    “Kaka yako si mzima. Ni mwanaume, lakini jogoo lake halifanyi kazi...” Grace akamwambia yote kwa kirefu huku akiendelea kulia. Halafu akamalizia. “Tena amefikia hatua ya kunipa ruhusa nitembee na wanaume wa nje, ili mradi nimpatie motto. Sasa ukiangalia hapo kosa langu liko wapi shem?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi shem, acha kulia...” Deo akamwambia Grace huku akimbembeleza.

    Bila kutarajia, Deo alijikuta akimbembeleza Grace huku amemkumbatia. Joto la kila mmoja wao lilitikisa fahamu zao za mapenzi. Kutokana na maelezo aliyoelezwa na Grace, Deo aliamini wazi kwamba, Geofrey hakuwa mzima, mawazo machafu yakamjia kichwani mwake na kufikiria kuwa amwingie kwa njia gani ili aweze kumpata. Hakupenda asikie kuwa alikuwa anagawa penzi kwa mtu wanje ili kutafuta mtoto wakati yeye yupo. Ibilisi mbaya akamwingia!

    Deo aliendelea kumkumbatia shemeji yake huku akijifanya anambembeleza kiasi cha kuufanya mwili wake teketeke utikisike. Mawazo machafu yakaendelea kumwandama Deo na Ibilisi kumkalia haswa kiasi cha kutowaza jambo jingine zaidi ya kujaribu kumwaga sera kwa shemeji yake!

    “Vipi shemeji yangu...” Deo alimuuliza shemeji yake kwa sauti ya chini.

    “Mh...acha tu...” Grace akajibu huku moyoni mwake akiwaza yake. Akawa anajiuliza afanye mbinu gani ili amnase shemeji yake Deo ili aweze kumpata mtoto atakayefanana na Geofrey, kwani wote wawili walikuwa wanafanana!

    Kilio cha Grace kilimweka pabaya Deo kiasi cha kumfanya awaze ni kwa nini aliyaanzisha mazungumzo yale. Ndipo aliposimama na kumshika mkono.

    “Basi shemeji, twende chumbani tukapumzike,” Deo alimwambia huku akiwa amemshika mkono!

    Grace akanyanyuka kutoka pale kwenye sofa, halafu wakaelekea chumbani kwake. Baada ya kuingia mle chumbani, Grace alijibwaga kitandani huku akimwangalia shemeji yake kwa macho malegevu.

    “Shemeji nyamaza, ukiendelea kulia, na mimi nitalia bure...” Deo alimwambia huku akimweka vizuri pale kitandani. Ingawa alifanya kosa kubwa kuingia mle chumbani kwa kaka yake, hakujali sana!

    “Nifunike shuka shemeji,” Grace alimwambia Deo, ambaye bila ajizi alimfunika shuka shemejiye kabla ya kuondoka mle chumbani huku akiwa na mawazo mengi kutokana na vibweka alivyokuwa akifanyiwa na shemeji yake. Akabaki akijiuliza, ataivumilia hali hii mpaka lini?



    *******

    BAADA ya Deo kutoka mle chumbani, Grace alibaki amejilaza kitandani huku akiwaza mengi. Akabaki akijiuliza ni kwa nini apewe lawama kwamba yeye ndiye mwenye matatizo wakati siyo kweli? Akaendelea kuwaza iwapo Geofrey alikuwa na matatizo ya kimaumbile tangu alipozaliwa ama alipata kilema hicho ukubwani.

    Pia, akajiuliza atakuwaje na uhakika na hali hiyo ya Geofrey bila kuthibitisha? Na swali jingine lililokuwa likimtatiza Grace ni juu ya kijana, Adrian. Alishajihusisha naye kimapenzi mara nyingi, lakini alishindwa kunasa mimba! Sasa kosa lilikuwa la nani?

    Hatimaye Grace akapitiwa na usingizi baada ya kulia kwa muda mrefu kutokana na mawazo yaliyokuwa yametawala kichwani mwake. Mume wake, Geofrey aliporejea usiku wa saa tatu, alimkuta Grace ameshalala wakati ilikuwa siyo kawaida yake:

    “Vipi mke wangu, unaumwa?” Geofrey alimuuliza.

    “Hapana, siumwi,” Grace alijibu huku akionekana kuwa na huzuni.

    “Haiwezekani mke wangu, lazima una tatizo, siyo kawaida yako,” aliendelea kusema Geofrey.

    “Ni kwamba nimechoka tu,” Grace akamwambia.

    “Oh, pole sana...”

    “Ahsante.”

    Baada ya Grace kumweleza mumewe kwamba alikuwa amechoka, Geofrey hakumsemesha tena. Aliona kwamba angeendelea kumbughudhi na kumbukumbu juu ya suala lake la kutaka mtoto, ambalo lilikuwa limekaa kichwani mwake angekasirika. Alishamzoea kutokana na vibweka vyake.

    Alipomaliza kuzungumza na mke wake mle chumbani, Geofrey alitoka na kuelekea sebuleni, ambapo alijiunga na mdogo wake, aliyekuwa anaangalia tamthilia kwenye runinga. Wakaende;ea na maongezi mengine, ikiwa ni pamoja na kupata mlo wa usiku, ambao ulikuwa umeshaandaliwa na Grace.

    “Deo mdogo wangu...” Geofrey akamwita mdogo wake kwa sauti ndogo lakini iliyoweza kusikika.

    “Naam kaka...” Deo akaitikia huku naye akimwangalia kaka yake.

    “Naona shemeji yako amelala mapema leo...”

    “Ndiyo, naona anajisikia vibaya. Nilikuwa nimekaa naye hapa, lakini baadaye akaenda chumbani kulala...”

    “Hata mimi nimemuuliza, akasema anajisikia vibaya...nafikiri itakuwa ni uchovu tu...”

    “Aisee?” Deo akaishia kusema hivyo. Hakupenda kuongea zaidi, hasa kwa kuwa alishajua tatizo lililopo kati ya kaka yake na mkewe.

    Geofrey hakuendelea kuzungumza. Aliendelea kula chakula na alipomaliza, ambapo aliagana na mdogo wake, halafu akaenda kulala, kuashiria kumalizika kwa siku ile na kusubiri siku mpya ya kuingia katika mihangaiko ya maisha.



    ********

    SIKU mbili zilipita tangu Grace na shemeji yake, Deo walipozungumzia suala lile la mgogoro wa ndoa yao. Waliendelea kuishi vizuri ingawa palikuwa na kile kiwingu cha kutopata mtoto, ambacho kilikuwa sehemu ya maisha ya Grace na mumewe Geofrey. Kwa upande wa Grace simanzi ilizidi kuongezeka, kiasi kwamba, ilibidi shemeji yake, Deo amliwaze kwa maneno mazuri.

    Na katika siku hizo, ndipo Geofrey alipigiwa simu kutoka nyumbani, Arusha, kwamba baba yake, mzee Kisamo alikuwa mgonjwa. Ujumbe ule wa simu ulieleza kwamba mgonywa alikuwa katika hali mbaya, na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru. Ilibidi Geofrey aombe ruhusa kazini kwake, ili kwenda kumjulia hali baba yake. Alikubaliwa na likizo fupi, na kabla ya kuondoka alimwita mdogo wake, Deo na kumpa maelekezo:

    “Kwa hivyo bawana mdogo, mimi naondoka kwenda nyumbani kumjulia hali baba. Wewe utabaki na shemeji yako hapa nyumbani, nakutegemea wewe kwa vile ni mtoto wa kiume...”

    “Sawa kaka, safari salama na urudi salama. Hakutakuwa na tatizo hapa nyumbani...” Deo alisema huku moyoni akifurahia sana kuondoka kwa kaka yake, kwa vile alikuwa na uhakika kuwa huo ni muda muafaka kwake kuwa karibu na shemeji yake, na hatimaye kutimiza matamanio ya moyo wake. Pia aliona ni wakati mzuri kwake kumpa mamba, kwa lengo la kumzalia mtoto kaka yake.

    Kwa upande wake, Grace naye alikuwa na mawazo kama ya Deo. Aliona kuwa hiyo ilikuwa nafasi nzuri kwake kumnasa shemeji yake na kumtimizia mpango alioupanga na mumewe wa kutafuta mtoto nje ya ndoa yao! Aliwaza kuwa, iwapo mpango huo utafanikiwa, ataachana kabisa na kijana, Adrian, ambaye hadi wakati ule alishindwa kazi ya kumjaza mamba!

    MUDA muafaka wa siku ya safari ulipowadia, Geofrey aliondoka nyumbani, Tabata, akisindikizwa na mkewe, Grace, pamoja na mdogo wake, Deo, mpaka walipofika kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani, Ubungo. Walitumia usafiri wa teksi, iliowafikisha mapema, ambapo Geofrey alikata tiketi ya basi la kampuni ya Sai Baba, linalokwenda Arusha..

    Muda wa basi kuondoka ulipowadia, basi liliondoka Ubungo huku Geofrey aliwapungia mkono Deo na Grace. Baada ya kuhakikisha basi limeondoka, wote wawili wakaondoka kurudi Tabata kwa kutumia usafiri wa teksi, huku kila mmoja akiwa na mawazo yake kichwani. Katika muda huo, Deo alikuwa akijisemea moyoni kwamba, akifika nyumbani, ni kumwaga sera zake kwa shemeji yake. Aliwaza kuwa, kwa vyovyote vile Grace asingeweza kumkatalia kwa vile alikuwa akihitaji kupata mtoto kwa udi na uvumba!

    Deo aliona kuwa, kuondoka kwa Geofrey, ilikuwa ni nafasi nzuri kwake kujirusha na Grace. Ni kama mawazo yao yalikuwa sawa, kwani Grace naye alikuwa akiwaza yaleyale moyoni mwake, kwamba, angemfanyia vibweka shemeji yake Deo, mpaka azimie. Alipania kushirikiana naye katika suala la tendo la ndoa ili kutimiza makubaliano kati yake na mumewe.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Teksi ilipowafikisha Tabata, walishuka na kuingia ndani, ambapo walipokelewa na ukimya wa aina yake. Moja kwa moja, Deo akafikia kweye sofa, ambapo alijibwaga. Kichwa chake kilikuwa hakifanyi kazi kazi kabisa kutokana na mawazo yaliyokuwa yakipishana kwa kupanga la kufanya. Akiwa pale, aliweza kumwona shemeji yake akipitiliza moja kwa moja hadi chumbani, na kabla ya kuingia chumbani, aligeuka na kumwangalia kwa jicho la mahaba, ambalo Deo aliliona! Mwili ukasisimka!

    Alipoingia chumbani, Grace alivua nguo zote na kubakiwa na nguo ya ndani ya rangi nyekundu, kikiwa ni kivazi pekee tu, halafu akauchukuwa upande wa khanga nyepesi yenye rangi nyeupe na maua machache meusi, ulioweza kuonyesha mpaka ndani, akaivaa. Kwa jinsi umbile lake lilivyokuwa, ukweli ni kwamba alitamanisha, hivyo akatoka tena mle chumbani na kuelekea pale sebuleni na kukaa jirani na aliopokuwa amekaa shemeji yake. Harufu ya mafuta mazuri iliingia sawia kwenye tundu za pua za Deo, kiasi kwamba uvumilivu ulimshinda, akageuka na kumtazama Grace kwa macho ya matamanio.

    Grace alikuwa amekaa mkao wa hasara, akameza mate na kujifanya kuuchuna! Hata hivyo aliendelea kumwangalia Grace kwa muda wa dakika tano hivi bila kusema lolote. Moyoni mwake akiwa ameridhika kuwa shemeji yake alikuwa ameumbika ipasavyo, na aliporidhika kuwa amemaliza kumwangalia, Deo akageuza shingo na kuangalia runinga iliyokuwa inaendelea na vipindi. Baada ya Grace kugundua mguso uliompata Deo, akaamua kumshika began a kumsemesha:

    “Shemeji Deo, vipi?” Akamuuliza.





    “Ah, safi tu...” Deo akajibu.

    “Mbona uko kimya?”

    “Sasa nisemeje shemeji?”

    “Si maongezi tu?”

    “Ok, yaanzishe basi?”

    “Hakuna shaka...” Grace akasema na kuendelea. “Naomba unielewe shemeji. Mimi ni mzima kabisa, siyo kwamba sizai kama wanavyofikiria. Kaka yako ndiye mwenye matatizo, ananiweka katika wakati mgumu...”

    “Ndiyo, ulishawahi kuniambia...” Deo akasema huku akimwangalia shemeji yake.

    Grace naye akamsogelea Deo kiasi cha kugusana, kitu kama shoti ya umeme kikamtokea Deo, kiasi cham kumfanya apumue kwa nguvu Kamchezo alichokuwa akimfanyia Grace, kalimzingua si mchezo!

    “Mbona hivyo?” Grace akamuuliza Deo baada ya kuona akisuasua!

    “Oohps!” Deo alipumua kwa nguvu na kuendelea. “Oh, shemeji yangu...” akashindwa kumalizia!

    “Unasemaje?” Grace akamuuliza kwa sauti iliyotokea puani.

    “Hivi shida yako ni kuzaa tu?” Deo akamuuliza.

    “Baaasi!” Akadakia Grace na kuongeza. “Nitazeeka bure mtoto wa watu!”

    “Sasa unataka kuzaa na mimi?”

    “Samahani shemeji kama nitakueleza kilichoko moyoni mwangu...”

    “Wewe nieleze tu...”

    “Mimi naomba kuzaa na wewe shemeji yangu. Lakini jambo la muhimu ni kaka yako asijue, iwe siri kubwa baina yangu na wewe!” Grace akamwambia kwa msisitizo!

    “Hivi unasema kweli shemeji?” Deo akamuuliza huku mapigo ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu!

    “Ni kweli kabisa, nimedhamiria na wala si uongo. Elewa kwamba ninahitaji mtoto...”

    “Kama umeamua poa...” Deo akasema huku akiwa amehamasika kwa kauli ile ya shemeji yake. Akaanza kumpapasa mwilini huku akiwa bado ameuvaa ule upande wa khanga!

    “Oooh!” Grace akalalamika kimahaba huku akimwachia Deo afanye anavyotaka, hasa ukizingatia alikuwa amemruhusu mwenyewe!

    Kama vile walikuwa wamejisahau kama walikuwa sebuleni, walianza kubinuana pale kwenye sofa na kuzama kwenye bahari kubwa ya mapenzi, bahari ndefu ya huba huku Grace akiendelea kulalamika kimahaba! Na baada ya kumaliza tendo lile ambalo hawakulitarajia, kila mmoja alikuwa amechoka. Grace akajiegemeza kwenye ukingo wa sofa huku akirembua macho yake. Kifua chake kilionekana kikipanda na kushuka kutokana na kule kuhema kwa uchovu!

    “Ahsante shemeji...” Grace akamwambia kwa sauti ndogo ya kutetemeka!

    “Ahsante ya nini?”

    “Umeniridhisha si utani...”

    “Nimekuridhisha sivyo?”

    “Si utani..sanaa! Sijui nikupe nini!”

    “Unipe nini zaidi ya ulichonipa?”

    “Na kweli...”

    Wote wakaishia kucheka na kugongeana mikono. Hakikia siku hiyo ilikuwa ya aina yake kwa Deo na Grace. Ni kama vile Paka alikuwa ametoka na sasa ni zamu ya Panya kutawala!

    Baada ya kula chakula cha mchana na kupumzika, kazi ilikuwa ni ileile ya kuendeleza zoezi lile. Kinywani mwake Grace kukatawala maneno ya kumsifu Deo, badala ya kaka yake, Geofrey au Adriana, mpenzi wake wa mwanzo aliyemfungulia njia ya kuujua ulimwengu wa mapenzi!

    Basi, hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa siku zote ambazo Geofrey alikuwa Arusha, akimuuguza mzee Kisamo. Deo alikuwa akimsaidia kaka yake ile kazi iliyokuwa imemshinda kwa muda wote, tangu alipofunga ndoa na Grace. Amani ikarudi tena ndani ya nyumba huku vicheko vikitawala baina ya watu wawili, Grace na Deo!



    *******

    Baada ya wiki mbili na nusu, Geofrey alirudi kutoka safari ya Arusha. Akaendelea na kazi yake bila kujua kilichokuwa kinaendelea kati ya Grace na Deo. Waliendelea kufanya mapenzi kwa siri sana kwani walikuwa wameshanogewa. Hali ile ilimfanya Grace asiwe anatoka sana nje kama ilivyokuwa mwanzo wakati Geofrey alipomruhusu kufanya mapenzi nje kwa minajili ya kusaka mtoto.

    Kitendo kile kilimshangaza sana Geofrey, kwa vile walikuwa wameshapanga kupata mtoto kwa udi na uvumba. Usiku mwingine wakiwa wamepumzika chumbani, ilimbidi Geofrey amuulize mke wake kinachoendelea juu ya mpango wao huo.

    “Mke wangu...” Geoferey alimwita.

    “Bee mume wangu...” aliitikia Grace huku akijigeuza pale kitadani na kumwangalia. Halafu akaendelea, “Nakusikiliza, unasemaje?”

    “Vipi, mbona kimya kimezidi?”

    “Kimya gani tena mume wangu?”

    “Naona hunipi maendeleo?”

    “Maendeleo yapi tena?”

    “Si kama tulivyokuwa tumepanga? Ina maana baada ya kukuruhusu umeshindwa kupata mimba? Mwenzio naumbuka...” Geofrey akamwambia.

    “Sijashindwa mume wangu...”

    “Sasa mbona siku zinakwenda tu!”

    “Wewe poa tu mume wangu, usiwe na wasiwasi...”

    “Ni lazima niwe na wasiwasi, si unajua kwamba mimi nakutegemea wewe kunificha siri yangu?”

    “Hilo naelewa sana mume wangu...”

    “Naomba usiniangushe...”

    “Siwezi kukuangusha kamwe, amini nakuambia,” Grace alisema huku akimvuta mumewe upande wake akijiandaa kumpiga busu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kweli?” Geofrey akauliza.

    “Kweli kabisa,” Grace akajibu huku akimpiga busu zito mumewe, ambaye naye alilipokea, lakini mwili haukusisimka. Hata Grace alilielewa hilo, kwani mawazo yake yalikuwa kwa shemeji yake, Deo, aliyekuwa amemwingia akilini.

    “Basi nashukuru sana,” alisema Geofrey, halafu akagekia upande wa pili wa kitanda, wakazima taa na kulala.

    Grace yeye alilala chali huku akiwaza mbali. Kwa muda huo alitamani kama angepata angalau wasaa wa kujirusha na shemeji yake, ili amuondolee kiu iliyokuwa imemkamata punde tu baada ya kupigana mabusu na mume wake, ambaye hakuwa rijali wa kumkata kiu yake kwa muda ule hali ilivyokuwa mbaya, yeye akiwa kama mwanamke! Hakuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia!

    Usiku ule ukapita.



    ********

    UKIMYA mwa Grace ulimtesa sana kijana Adrian Senga, ambaye alikuwa amshamfanya kama mke wake. Ukweli ni kwamba alikuwa amenogewa sana na penzi alilokuwa anapatiwa na Grace, na hasa ukizingatia yeye ndiye mwanaume wa kwanza kufungua njia, na kuiondoa bikira yake, kitu ambacho ni adimu sana kwa wanawake wa kileo!

    Kwa muda wote waliokuwa wakijihusisha kimapenzi, Adrian alikuwa akimhitaji wakati wowote alikuwa akimpata bila kipingamizi chochote, lakini hivi karibuni alikuwa amebadilika kabisa na kuwa mkimya hata kumpigia simu na hata wakati mwingine kuipokea ilikuwa shughuli pavu. Ilifikia wakati mwingine Adriana alijitahidi kupita karibu na nyumba ya akina Grace, angalau tu amwone, lakini hakufanikiwa kumwona.

    Uvumilivu ule ulimshinda Adrian na kuendelea kuutesa moyo wake, hivyo siku nyingine aliamua kumtafuta tena Grace kwenye simu yake ya mkononi, na kweli akafanikiwa, ambapo upande wa pili simu ile ilipokelewa:

    “Haloo...”

    “Haloo...mpenzi, hali yako...” Adrian akasema upande wa pili.

    “Nani mpenzi wako?” Grace akamuuliza Adrian.

    “Si wewe mpenzi?” Adriana akasema huku akishangaa baada ya kujibiwa vile na Grace! Hakutegemea!

    “Si unajua kuwa mimi ni mke wa mtu?” Grace akaendelea kumuuliza.

    “Ndiyo...natambua hilo, wewe ni mke wa mtu...”

    “Sasa kama unatambua ndiyo unataka kunimiliki kabisa?”

    “Siyo hivyo mpenzi...”

    “Au kukuonjesha ndiyo imekuwa nongwa kiasi cha kutaka kunimiliki kabisa?”

    “Hapana...umefika mbali sana...”

    “Siyo mbali huo ndiyo ukweli...”

    “Najua unatambua kuwa nakupenda...usifanye hivyo. Naomba kama nimekuudhi unisamehe...”

    “Hujaniudhi chochote,” Grace akamwambia na kuongeza. “Mimi ni mke wa mtu, hivyo cha kukushauri ni kwamba utafute mchumba uoe. Kwangu huna nafasi tena...namheshimu mume wangu!”

    “Usifanye....”

    “Achana na mimi!” Grace akasema na kukata simu!

    “Shit!” Adrian akasema!

    Kisha Adriana akabaki ameikamata ile simu mkononi. Hakuamini kile alichojibiwa na Grace, mwanamke ambaye alikuwa amemweka mawazoni mwake, na pia kuwa tayari hata kumuoa kama angeachana na mume wake. Ni kitu gani kilikuwa kimempata hasa ukizingatia zile habari za mume wake kuwa siyo rijali, zilitapakaa kote mtaani pale. Je, mume wake atakuwa amepona tatizo lake? Ukweli ni kwamba hakujua!

    Baada ya kutambua kuwa hatakiwi tena na Grace, Adriana akaukubali ukweli kuwa alikuwa amemwagwa jumla, na pia akagundua baadaye kuwa Grace alikuwa akijihusisha kimapenzi na shemeji yake, Deo, aliyekuwa ametoka Arusha hivi karibuni. Basi, yeye ndiye aliyekuwa kiinio cha tatizo lile, hivyo hakuwa na njia nyingine zaidi ya kumuachia, ingawa roho ilimuuma sana!



    ********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MIEZI miwili ilipopota, Grace alinasa mimba kutokana na ile kazi waliyokuwa wanaifanya kwa bidii na shemeji yake, Deo. Kwa upande wa Geofrey, hakutambua kabisa ule usaliti wa hali ya juu uliofanywa na mdogo wake wa kuzaliwa tumbo moja.



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog