Simulizi : Siri Ya Mke
Sehemu Ya Nne (4)
BAADA ya kutambua kuwa hatakiwi tena na Grace, Adriana akaukubali ukweli kuwa alikuwa amemwagwa jumla, na pia akagundua baadaye kuwa Grace alikuwa akijihusisha kimapenzi na shemeji yake, Deo, aliyekuwa ametoka Arusha hivi karibuni. Basi, yeye ndiye aliyekuwa kiinio cha tatizo lile, hivyo hakuwa na njia nyingine zaidi ya kumuachia, ingawa roho ilimuuma sana!
********
MIEZI miwili ilipopota, Grace alinasa mimba kutokana na ile kazi waliyokuwa wanaifanya kwa bidii na shemeji yake, Deo. Kwa upande wa Geofrey, hakutambua kabisa ule usaliti wa hali ya juu uliofanywa na mdogo wake wa kuzaliwa tumbo moja.
“Haya mume wangu,” Grace alimwambia mume wake katika usiku mwingine.
“Unasemaje mke wangu?” Geofrey akamuuliza.
“Mambo tayari!”
“Umenasa?”
“Ndiyo, mtoto yuko tumboni!”
“Mh, ni kweli?”
“Kweli kabisa!”
“Ina maana karibu nitaitwa baba fulani?” Geofrey alisema kama mtu asiyeyaamini masikio yake. “Hii ni neema!”
“Sana, tena nataka tuchague mapema jina la mtoto wetu!”
“Umenena mke wangu.”
“Ungependa jina gani?”
“Kama ni wa kiume, tumpe jina la baba yake mdogo, Deo, ambalo litamfaa...”
“Baba yake mdogo?” Grace akauliza.
“Ndiyo, kwani wewe hujawahi kuona ama kusikia mtoto akipewa jina la baba yake mdogo?” Geofrey akauliza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mh, makubwa! Kwani hakuna majina mengine mpaka umwite Deo?”
“Mimi ndiyo nalipenda jina hilo.”
“Yaani tumwite Deo? Mh!”
“Mimi ndiye msemaji wa mwisho!” Geofrey alisisitiza. “Jina hilo ndiyo nalipenda kwa mtoto wetu!”
“Ooohps!” Grace akavuta pumzi ndefu na kuzishusha. Hakika hakuwa na ujanja!
Mjadala ule uliishia pale wote wawili walipoamua kusubiri mpaka mtoto wao atakapozaliwa. Wakaendelea na maisha yao kama kawaida huku mabadiliko makubwa yakiwa yametawala ndani ya nyumba ile. Hapakuwa tena na maneno ya chinichini kati ya Geofrey na Grace.
Lakini kazi ilikuwa ni kwa Deo, ambaye alihusika na upatikanaji na ile mimba, kwani alianza kuishi kimachale ili asije akashtukiwa na kaka yake. Alijiwa na hofu hiyo kutokana na jinsi Grace alivyokuwa amemganda kama Kupe. Kwa bahati nzuri, Deo alifanikiwa kupata kazi kwenye kampuni moja ya bibafsi, ambayo ni kazi aliyokuwa ametafutiwa na kaka yake. Ili kukwepa dhahama ile, Deo aliamua kuhama pale nyumbani kwa kaka yake na kupanga chumba eneo la Tabata Bima, mbali kidogo na alipokuwa anaishi kaka yake. Hiyo yote iliwasaidia kumkwepa Grace, ambaye alikuwa anaonyesha kila dalili za kumhitaji kila mara.
Ile kupata mimba kwa Grace kuliwachanganya watu wengi hasa majirani zake, ambao walikuwa wameshagundua siri ile baada ya Grace kuitoa kwa shogake, Mwantumu. Kama kawaida ya wanawake, siku moja wakiwa wamekaa kibarazani, walipomwona Grace akipita, wakaanzisha mjadala juu yake!
“Jamani, mwenzetu kapata mimba!” Jirani mmoja alisema.
“Ni kweli, wamejitahidi sana,” aliongeza jirani mwingine.
“Lakini si mlisema mwanaume hayawezi? Mbona imekuwa hivyo?” Alihoji wa kwanza.
“Unajuaje? Labda kasaidiwa,” alijibu mwingine.
“Inawezekana, maana naona hawaachani na shemeji yake kila wanapokwenda. Jamaa anajitafunia kiulaini kama anakunywa maji vile!”
“Na hata kama ni ya mdogo wake, si itakuwa ni damu yao ya halali? Hakuna kosa, kaka yake si ameshindwa, lazima asaidiwe,” mwingine alidakia.
“Eheheheheeeee!” Wakaangua kicheko kikali!
“Jamani tuyaache hayo, tuendelee na mambo yetu!”
“Na kweli, maana ya kwetu yametushinda!”
“Heheheheeee!” wakaishia na kicheko kingine kikali, kilichowafanya hata kuku waliokuwa jirani wakichakura wapige kelele za mshtuko! Ndiyo mambo ya uswahilini hayo!
Majirani wale waliongea mengi sana na mwishowe wakaamua kuusitisha mjadala ule usiokuwa rasmi. Lakini ukweli ulibaki palepale kwamba Grace alikuwa mjamzito!
********
KUPATA mimba kwa Grace hakukuwashangaza majirani aliokuwa anaishi nao katika eneo lile la Tabata tu, bali hata baba yake mzazi, mzee Kisamo, ambaye alikuwa na mashaka kutokana na ile hali aliyokuwa nayo Geofrey. Ukweli ni kwamba alikuwa hana nguvu za kiume kwa muda wote wa maisha yake, sasa kupata kwake mimba kilimshangaza sana na kutoamini kama ni kweli ilikuwa yake. Kwa muda mrefu alikuwa akisubiri kwa hamu mtoto huyo azaliwe ili ukweli ujulikane.
Akiwa amekaa na mkewe siku moja, mzee Kisamo aliamua kumuuliza kuhusu mimba ile ya mkwe wao.
“Mama Geofrey,” mzee Kisamo alimwita.
“Bee, baba Geofrey...”
“Natumaini umezipata habari za mkweo, Grace amepata mamba....”
“Ndiyo, najua hilo. Hatimaye amepata kilichokuwa kinasubiriwa kwa muda mrefu...”
“Hivi mimba hiyo ni ya mwanetu Geofrey kweli?” Mzee Kisamo akauliza.
“Hata mimi nina mashaka kidogo...”
“Mashaka gani? Hebu nieleze...”
“Inawezekana kasaidiwa...”
“Na wanaume wenzake sivyo?”
“Ndiyo manaake... lakini hatuna la kufanya. Labda siri anaijua mkewe...”
“Cha muhimu ni kusubiri mtoto atakapozaliwa, siri itajulikana...”
“Hilo ndiyo neno...”
Mazungumzo kati yam zee Kisamo na mkewe yaliishia hapo huku yakiwa yamebaki majuma machache kabla ya Grace kujifungua. Swali kubwa lililotawala vichwani mwa wazee hao juu ya mimba ile ya Grace. Wakabaki kujiuliza, ni nani aliyehusika?
*******
MIEZI tisa ilimalizika, halafu ikafika siku ya Grace kujifungua. Usiku mmoja, hali ilibadilika ghafla. Ilikuwa yapata saa sita za usiku hivi, giza nene lilikuwa limetanda angani huku kukiwa na dalili za kunyesha kwa mvua. Geofrey na Grace walikuwa wamelala. Ni wakati huo uchungu ulipomuanza Grace na kuonyesha dalili zote za kujifunguia. Bila kupoteza muda, Geofrey aliamka na kuanza kumpatia huduma ya kwanza.
“Grace...” Geofrey alimwita.
“Bee...” Grace akaitikia huku akiyauma meno yake kwa uchungu!
“Vipi?”
“Uchungu!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Pole sana mke wangu!”
“Tafuta usafiri unipeleke hospitali...oh!”
“Sawa mke wangu...”
Geofrey alichukuwa simu yake ya mkononi na kumpigia rafiki yake mmoja, ambaye ni dereva teksi, na kumueleza juu ya ile hali iliyomkuta mke wake, hivyo aende kumchukuwa mara moja. Baada ya dakika tano hivi, teksi ile ilifika na Grace akapakizwa na safari ya kuelekea kwenye Hospitali ya Amana, Ilala, akiongozana na mumewe, Geofrey. Kwa vile usiku ule magari yalikuwa machache barabarani, walifika salama na Grace akapokelewa na kuingizwa ndani tayari kwa kupatiwa huduma za haraka.
Baada Geofrey kuhakikisha mke wake amepata kitanda cha kulala, alilazimika kuondoka kurejea hospitali huku akiwa na hamu kubwa ya kujua matokeo.
Ni bahati ilioje, kwani Grace alijifungua alfajiri mtoto mzuri wa kiume. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na kilo nne, na moyoni Grace alifurahi sana baada ya kuonyeshwa mtoto wake na wauguzi na kubaini kwamba japokuwa ilikuwa mapema mno kuifananisha sura yake, ilifanana na ya Deo, shemeji yake, ambaye ndiye aliyehusika na kumpa ujauzito ule wenye utata!
Akiwa bado na furaha, Grace alichukuwa simu yake, halafu akampigia Geofrey, ambapo alimjulisha kuwa alikuwa amejifungua salama mtoto wa kiume. Akiwa bado amejilaza kitandani, Geofrey alizipokea taarifa zile kwa furaha, na kumuaambia kuwa muda siyo mrefu, watakwenda kumuangalia, wakiongozana na Deo, shemeji yake, na kuanzia muda huo, Geofrey hakuendelea kulala tena, bali aliamka na kufanya maandalizai ya kwenda kule hospitali...
********
ASUBUHI ya siku hiyo, Geofrey alimpigia simu mdogo wake, Deo, kumjulisha habari za kujifungua kwa mkewe, kisha wakakubaliana kwenda hospitali pamoja. Deo alimpitia Geofrey halafu wakakodi teksi na kuanza safari ya kwenda katika Hospitali ya Amana, Ilala. Baada ya kufika, walimkuta Grace ameshajifungua mtoto, na alishahamishiwa katika wodi ya wazazi, kwa vile hali yake ilikuwa ni nzuri na alijifungua bila matatizo yoyote.
Geofrey na Deo waliruhusiwa kwenda kumuona, ambapo baaada ya Grace kuwaona, alitabasamu kwa furaha. Wakati huo motto aliyezaliwa alikuwa amefunikwa mwili mzima na kubakia sura tu, na ukaguzi ulipomalizika baada ya daktari kuupitisha, Grace aliruhusiwa kurejea nyumbani. Hakika ilikuwa ni siku ya furaha kwa Geofrey, Grace na Deo. Hata hivyo furaha ya Deo ilikuwa ya mashaka, kwani hakuelewa kuwa siri ile itadumu hadi lini, alikuwa na hofu kubwa ya klutokea kwa mfarakano kati yake na Kaka yake iwapo siri ile itabainika.
Hatimaye baada ya kuruhusiwa, Geofrey alikodi tena teksi, ambayo iliwarudisha nyumbani, Tabata, na kichanga kile kikaingizwa ndani na kufikia chumbani. Kuanzia muda ule Grace akaanza kupatiwa huduma zote stahili akiwa kama mzazi aliyejifungua, kwani alipatiwa chakula kizuri, kuanzia supu ya nyama, uji wa ulezi na vinginevyo. Kamwe Geofrey hakutaka mke wake apate shida hata kidogo Kwa upande wake Geofrey furaha aliyokuwa nayo ni ya kupata mtoto, japokuwa hakuwa wa damu yake.
Moyoni alijisemea kuwa potelea mbali, ili mradi siri ile ni kati yake na mkewe, na aliamini kuwa hakuna mtu mwingine anayeweza kuifahamu.
Masikini, Geofrey hakuwaza kabisa kama mtoto yule ni wa mdogo wake Deo, ambaye mke wake, Grace alijitahidi kumrubuni na kuweza kuzaa naye!
Na tatizo lilikuja pale Geofrey alipotaka mke wake amwambie jina la mtu aliyempa mamba. Kila mara alilkuwa akimbembeleza amtajie huyo mwanaume ili amfahamu.
“Mke wangu mpenzi...” Geofrey alimwambia Grace.
“Bee mume wangu...” Grace akaitikia huku akimwangalia.
“Nashukuru sana kwa kuufuata ushauri wangu wa kutafuta mtoto, hatimaye umefanikiwa. Ukweli nashukuru kwa hilo.”
“Hatukuwa na jinsi, nami nashukuru...” Grace alimjibu.
“Lakini, ingekuwa ni vizuri unitajie japo jinma la huyo mtu aliyekupa ujauzito wa motto huyu...”
“Mh,” Grace aliguna, kasha akasendelea. “Wewe ulitaka mtoto, au mwanaume aliyenipa mamba?”
“Usiwe mkali mke wangu...” Geofrey akamwambia kwa upole.
“Alienipa mimba ni Boka, yule dereva wa daladala,” alidanganya Grace baada ya kuona mumewe anapeleleza kijanja!
“Unasema Boka?”
“Ndiyo.”
“Yule mweusi kama mkaa?”
“Ndiye huyohuyo...”
“Ok, hakuna taabu...” Geofrey akasema huku akionyesha kutoridhika na lile jibu. Kidogo akaanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu yule mtoto aliyezaliwa!
“Vipi, hujaridhika?” Grace akamuuliza mumewe baada ya kumuona hakuridhika! Na kweli ilikuwa hivyo!
“Niyo, naona mtoto ni mweupe, wakati Boka ni mweusi,” Geofrey akamwambia.
“Ina maana humtaki huyu mtoto?” Grace akaendelea kuhoji. “Kama humtaki nitampeleka kwa baba yake, Boka...”
“Oh, basi mke wangu, yasiwe makubwa,” Geofrey aliufyata. Hakupenda kuzozana na mke wake, lakini roho ilikuwa inamuuma sana!
Kila Geofrey alivyomwangalia mtoto kwa makini, alibaini kwamba anashabihiana na mdogo wake, Deo. Tofauti yake na Deo ni kwamba yeye ni maji ya kunde, wakati mdogo wake ni mweupe. Hata mkewe Grace ni rangi ya maji ya kunde, hivyo akaendelea kujiuliza kama kweli mtoto yule ni wa Deo?
Mjadala ule ulifungwa na kila mmoja akaendelea na utaratibu mwingine. Lakini siri ilibaki palepale kuwa mtoto hakuwa wa Geofrey!
********
UPANDE wa pili Deo hakuwa na raha kabisa tokea azaliwe yule mtoto. Wasiwasi mwingi ni juu ya kaka yake Geofrey kama angekuja kuugundua ule uasi walioufanya mtu na shemeji yake. Pamoja na wasiwasi ule, hakuwa na jinsi zaidi ya kuwa anatembelea pale nyumbani ili kuwajulia hali kaka yake, shemeji yake na moto. Jumamosi moja, siku ya mapumziko Deo hakwenda kazini, hivyo aliamua kwenda Tabata Mawezi kuwatembelea, lakini hakutegemea katika safari ile angemkuta kaka yake Geofrey.
Alipofika na kuingia ndani, alimkuta kaka yake amejaa tele sebuleni akiangalia sinema katika runinga. Baada ya kumsabahi, naye akajichukulia nafasi na kukaa kwenye sofa la pembeni huku akimuangalia kaka yake kwa chati. Alionekana ni mtu asiyekuwa na furaha hata kidogo, ingawa alijaribu kujificha, na hilo alitambua Deo, kwani tangu mkwe wake, Grace amemzaa yule mtoto na kukataa kumwambia baba yake ni nani, raha ilitoweka, na hakumwamini mtu!
Deo alikaa pale huku wakiongea hili na lile, huku pia wakiburudika na vinywaji baridi. Hata hivyo kuwepo kwa Geofrey siku hiyo, kulimnyima raha Deo, kwani alikuwa anataka kuongea mazungumzo nyeti na Grace, yanayohusu yule mtoto. Baada ya kuona kulikuwa na ugumu kwake kuzungumza na shemeji yake, aliamua kuchukuwa kalamu na karatasi na kuandika ujumbe kwenye kipande cha karatasi, ambao baadaye alimpatia kwa siri Grace walipokutana nje, Grace aliupokea ujumbe ule na kuuficha kwenye khanga ili ausome baadaye.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Deo alipohakikisha amempatia ule ujumbe, aliamua kuaga na kuondoka pale nyumbani kwa kaka yake, na kurejea kwake, Tabata Bima. Huku nyuma, kumbe wakati Grace akiipachika ile karatasi kwenye khanga, ilidondoka bila yeye kujua, na Geofrey akafanikiwa kuiokota karatasi ile pale ilipodondokea karibu na mlango wa jiko. Akaichukuwa na kwenda nayo pale sebuleni, ambapo aliifungua na kukuta ni ujumbe uliokuwa umeandikwa na Deo, mdogo wake!
Geofrey akaanza kuusoma ule ujumbe:
Mpenzi shemeji yangu,
Mimi mzima. Vipi mtoto wetu, hajambo? Naona sasa unafuraha sana, maana ulilia kuzaa na mimi mpaka imewezekana. Lakini fanya juu chini uhakikishe huyo mtoto amebadilishwa hilo jina la Deo. Hawezwi kuitwa jina la baba yake mdogo, ni kitu ambacho hakiwezekani. Tuwasiliane zaidi mama watoto wangu.
Ni mimi Deo.
Baada ya kumaliza kuusoma ule ujumbe. Geofrey alivuta pumzi ndefu na kuzishusha. Alijiona kama mtu aliyekuwa ndotoni, hakuamini kama ule ujumbe ulikuwa umeandikwa na mdogo wake, Deo. Akabaki akijiuliza, “Ina maanaGrace alikuwa anafanya mapenzi na shemeji yake Deo? Ama kweli kikulacho ki-nguoni mwako! Yaani mdogo wangu ananizunguka kaka yake?
Geofrey alikiona kitendo kile ni cha aibu kwake, hivyo akawza kuwa afanye nini, lakini hakupata majibu mazuri zaidi ya mawazo kumjaa kiasi cha kuwaza hata kujiua! Na alichofanya kwa muda ule, ni kwamba aliuficha ule ujumbe bila kumweleza lolote mke wake.
Geofrey akaingia chumbani na kuvalia fulana, halafu akatoka bila kuaga, akaelekea katika mtaa wa pili huku akitembea na mawazo mengi kichwani kiasi kwamba alikuwa akitembea huku akizungumza pake yake kama mwenda wazimu. Safari yake ile ilikomea kwenye duka moja la jirani na nyumbani kwake, ambapo alinunua sumu ya panya kwa lengo la kwenda kuinywa na hatimaye kujiondoa uhai wake na kuondokana na udhia ule. Hakuwa na hamu ya kuendelea kuishi tena duniani! Aliona aibu, sura yake aiweke wapi? Alitamani ardhi ipasuke na kumfunika!
Baada ya kununua ile sumu ya panya, Geofrey akarudi nyumbani kwake, na wakati akiingia ndani, alikutana na mke wake, ambapo sura yake ilionyesha wazi wasiwasi aliokuwa nao. Ni wasiwasi wa kutoiona ile karatasi iliyokuwa imeandikwa ujumbe ule, aliyokuwa ameificha kwenye khanga aliyovaa, kwani alijaribu kuitafuta kila mahali, lakini hakuipata. Akawa na uhakika kuwa karatasi ile ilikuwa imeshafika mikononi mwa mume wake!
“Vipi mume wangu?” Grace alimuuliza mume wake.
“Vipi nini?” Geofrey akamjibu huku akiwa na hasira ambazo zilionekana wazi.
“Ah, nauliza tu, kwani kama vile huna raha” Grace akamwambia.
“Mimi nataka kupumzika, kwani nina usingizi, niache...” Geofrey alidanganya.
“Haya mume wangu, kapumzuke,” Grace akamwambia huku akimtazama mumewe aliyekuwa akielekea chumbani.
Baada ya kuingia chumbani. Geofrey akaufunga mlango, na kisha akakaa kwenye kiti kilichokuwa kando ya kitanda. Juu ya meza, pembeni ya kiti alichokalia, kulikuwa na saraka la kuhifadhia vitu. Akachomoa karatasi moja na kalamu na kuanza kuandika ujumbe kabla ya uamuzi wa kujitoa roho!
Mimi Geofrey Kisamo,
Nimeamua kujiondoa uhai wangu mwenyewe, baada ya kugundua siri kubwa, kwamba mdogo wangu Deo, niliyempenda na kumtegemea kwa mambo yote, amezaa na mke wangu Grace. Na ninaagiza kwamba, Deo amlee motto wake katika maisha yote.
Nawatakia maisha mema.
Buriani.
Baada ya kumaliza kuuandika ujumbe ule, Geofrey aliichukuwa ile sumu ya panya na kuimiminia ndani ya glasi ya maji na kuikoroga vizuri. Halafu akainywa yote kwa mkupuo, na wakati huo akiinywa, alikuwa akiomba dua kwa Mwenyeza Mungu amsamehe kwa kosa lile baya ya kujiua kabla ya siku zake. Na kabla ya kujilaza kitandani, Geofrey akaufungua mlango wa chumbani aliokuwa ameufunga wakati akiandika ule ujumbe ule wa kifo!
Baada ya kurejea kitandani, Geofrey alijilaza chali akiisikilizia ile sumu aliyoinywa ilivyokuwa inafanya kazi yake. Haukupita muda mrefu, alianza kusikia kizunguzungu na nguvu kumwishia mwilini. Povu zito jeupe likaanza kumtoka mdomoni huku tumbo lake likikata. Muda wote huo roho yake ilikuwa inajitahidi kuachana na mwili kwa kulazimishwa, na baada ya sekunde chache, Geofrey alikata roho huku lile povu jeupe lilikwa bado limetanda kinywani na macho kumtoka pima. Hakika alitisha sana!
Wakati huo, Grace alikuwa bado amekaa sebuleni akimnyonyesha mtoto wake. Alikuwa amebanwa na mawazo mengi, akifikiria hatima yake baada ya Geofrey kuusoma ule ujumbe uliokuwa umeandikwa na Deo. Kwa vyovyote alijua kwamba mumewe alikuwa amechukua sana. Alipomaliza kumnyonyesha mtoto yule, aliamua kumpeleka chumbani akalale kwa vile alikuwa anasinzia baada ya kushiba.
Grace aliufungua mlango wa chumbani na kuingia na mtoto, huku macho yake yakayaelekeza kitandani. Hata hivyo alishtuka baada ya kuona kitu ambacho hakukitarajia maishani mwake, kwani mumewe, alikuwa amejilaza pale juu ya kitanda huku povu jeupe likimtoka kinywani! Hakuonyesha dalili zozote za uhai, alikuwa ametulia kimya!
Grace akajikaza na kumlaza yule mtoto kwenye kitanda chake kilichokuwa upande wa pili. Halafu akamsogelea Geofrey karibu na kumtingisha!
“Geofrey...” Grace akamwita!
Kimya!
“Baba Deo...”
Kimya!
“Mamaa! Mume wanguuuu!” Grace akalia kwa sauti ya juu kiasi, ambayo haikuweza kusikika kule nje!
Akaiinamia maiti ile na kuendelea kuitingisha, lakini ilikuwa kimya kabisa! Kilio cha kwikwi kikaongezeka baada ya kuthibitisha kuwa mume wake amekufa. Hata hivyo akaona kuwa kulia sana kusingesaidia kitu, ni kupanga juu ya kuepukana na janga lile alilosababisha yeye. Basi alichofanya, alichomoka mle chumbani, kisha akaufunga mlango wa chumbani na wa nje. Akaondoka kwa mwendo wa haraka kuelekea kwenye kituo cha daladala, ambacho hakikuwa mbali sana.
Baada ya kufika kwenye kituo kile, akapanda basi la daladala, aina ya Toyota Coaster, linaloelekea Tabata Bima, alipokuwa anaishi Deo, shemeji yake. Hakika hakutofautiana na mwendawazimu wa muda kwa wakati ule!
********
DEO alikuwa amekaa kwenye kiti cha plastiki, nje ya nyumba ile anayoishi, akizungumza na mmoja wa mpangaji mwenzake. Walikuwa wamekaa chini ya mti mmoja wa mwarobaini uliokuwa na kivuli, ulioko kando ya nyumba. Baada ya Deo kumwona Grace akielekea pale, mara moja alishtuka na kuhisi mambo mawili, aidha siri ya kuzaa na shemeji yake imefichuka, au kuna jambo baya lilikuwa limemtokea kaka yake, Geofrey.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Deo akanyanyuka na kumkaribisha Grace, aliyeonekana kuwa na taharuki. Wakaingia ndani, ambapo Grace alifikia kujibwaga kwenye sofa huku akihema kwa nguvu. Deo akabaki amesimama huku akimwangalia, na pia kuonyesha wasiwasi mkubwa kiasi cha kumuuliza:
“Vipi shemeji, mbona hivi, nini kimetokea?”
“Mambo mabaya shemeji…” Grace akamwambia huku akifuta machozi yaliyokuwa yakimbubujika kwa wingi!
“Mabaya kivipi, shemeji ameshtuka?”
“Hebu soma huu ujumbe…” Grace akamwambia huku akimkabidhi kile kikaratasi kilichokuwa kimeandikwa ule ujumbe. Deo akakipokea huku akitetemeka ukizingatia hakujua kilichokuwa kimeandikwa!
Huku mikono ikiendelea kutetemeka, Deo alianza kuusoma ule ujumbe ulioandikwa na kaka yake, Geofrey. Baada ya kumaliza kuusoma, akashika kichwa chake na kuonyesha kuchanganyikiwa. Akamuangalia Grace aliyekuwa anaendelea kulia kwa sauti ya chini!
“Unataka kusema kuwa kaka amekufa?” Deo akamuuliza Grace.
“Ndiyo, amejiua kwa kunywa sumu ya Panya, na huo ndiyo ujumbe aliouandika kabla ya kifo chake!”
“Una uhakika na unachokisema?”
“Nina uhakika shemeji…”
“Siamini kama kaka amekufa…oh!” Deo akajisemea pake yake kwa sauti ndogo.
“Ni kweli…oh, sijui tufanyeje? Mungu wangu!”
“Ujumbe huu uliukuta sehemu gani?”
“Niliikuta juu ya meza…”
“Umefanya la maana sana kuichukua hii karatasi,” Deo akamwamia na kuendelea. “Inabidi tusimwonyeshe mtu yeyote, ili ionekane kama ni kifo cha ghafla, au ameamua kujiua bila kuacha ujumbe wowote!”
“Mungu wangu! Tutafanya nini sisi…oh!” Grace aliendelea kulalamima.
“Jikaze shemeji…cha muhimu tuondoke tuelekee nyumbani tukampeleke hospitali kwa uchunguzi zaidi…”
“Sawa shemeji…” Grace akasema.
Halafu wote wawili wakatoka pale nyumbani kwa Deo, Tabata Bima, kisha wakakodi teksi, na kuelekea nyumbani kwa Geofrey. Baada ya kufika, walishuka na kumlipa dereva, halafu wakaingia ndani moja kwa moja na kupitiliza hadi chumbani. Kwa macho yake mwenyewe, Deo akaushuhudia mwili wa kaka yake ukiwa umeshakata roho, umejilaza juu ya kitanda.
“Ni kweli…kaka amekufa…” Deo akasema huku machozi yakimlengalenga!
“Amakufaa…oooh!” Grace akasema huku akilia.
“Usilie kwa sasa hivi shemeji, ngja niwajulishe polisi…” Deo akamwambia huku akiitoa simu yake ya mkononi!
Kabla majirani hawajajua kilichokuwa kinaendelea, Deo aliwapigia simu polisi na kuwataarifu juu ya kifo kile. Askari polisi walifika pale nyumbani wakiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser, ambapo ndani yake walikuwepo askari sita. Baada ya askari wale kufika, wakafanya uchunguzi ndani ya chumba kile na pengine wakimhoji maswali kadhaa Grace kuhusu kifo kile, naye akajibu kadri alivyoweza.
Mwisho wa uchunguzi wao, askari wale waliamua kuichukuwa ile glasi iliyokuwa na mabaki ya sumu ile ya Panya, halafu wakaiweka ndani ya mfuko wa nailoni, kwa ajili ya uchunuzi wa kimaabara zaidi. Pia, waliuchukuwa ule mwili wa Geofrey na kuupeleka kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuhifadhiwa na hatimaye kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuzikwa. Vilevile, Deo na Grace walichukuliwa ili wakaandikishe maelezo yao kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni.
Kwa kweli kilikuwa ni kifo cha ghafla mno, ambacho Deo na Grace hawakukitegemea, na pia hawakutegemea kama Geofrey angekuja kuigundua siri ile ya mtoto aliyezaliwa! Kifo kile kiliwashtua wakazi wengi wa Tabata, ambao walikuwa wamemzoea sana kutokana na upole wake. Wengi hawakusita kusema maneno mengi tu wanayoyajua, ambapo wengine walisema kulikuwa na mkono wa mtu kutokana na mazingira ya kifo chenyewe!
Taratibu zote zilipokamilika, mwili wa Geofrey ulisafirishwa kwenda Arusha kwa ajili ya mazishi na gharama za kuusafirisha mwili huo, zilitolewa na Kampuni ya Mangi Fowarding & Clearing Agency, ambako alikuwa anafanyia kazi kabla ya mauti kumfikia. Wazazi wa Geofrey pamoja na ndugu zake wengine walilia sana kutokana na kifo hicho cha ghafla na kumwacha mwanamke, mjane pamoja na mtoto. Walishangaa zaidi baada ya kuelezwa kwamba kifo hicho kilitokana na kunywa sumu ya Panya. Hawakuelewa ni kwa nini na sababu gani zilizomfanya Geofrey aamue kunywa sumu ile, wakabaki wakimwachia Mungu!
Mazishi ya Geofrey yalifanyika katika makaburi ya Njiro, yaliyoko nje kidogo ya jiji la Arusha. Ni mazishi yaliyohuidhuriwa na watu wengi sana, hasa wakazi wa eneo la Kijenge, ambako ndipo alipozaliwa na kukulia katika nusu ya ujana wake. Baada ya mazishi hayo kumalizika, ndipo siri ile ilipobaki kwa watu wale wawili, Deo na Grace, waliohusika kwa namna moja ama nyingine na kifo cha Geofrey.
Baada ya kumaliza kuandikisha maelezo yao kwenye kituo cha polisi, Deo na Grace waliruhusiwa kurejea nyumbani. Moyoni nafsi iliwasuta ukizingatia walikuwa wahusika wakuu wa kifo kile. Na uchunguzi uliofanywa baadaye na Daktari baada ya mwili wa Geofrey kufanyiwa upasuaji, ulithibitisha kuwa kifo chake kilikuwa kimesababishwa na sumu ya Panya. Lakini polisi hawakuweza kumhisi mtu yeyote kutokana na kifo kile, pengine walihisi labda amejiua mwenyewe!
Taratibu zote zilipokamilika, mwili wa Geofrey ulisafirishwa kwenda Arusha kwa ajili ya mazishi na gharama za kuusafirisha mwili huo, zilitolewa na Kampuni ya Mangi Fowarding & Clearing Agency, ambako alikuwa anafanyia kazi kabla ya mauti kumfikia. Wazazi wa Geofrey pamoja na ndugu zake wengine walilia sana kutokana na kifo hicho cha ghafla na kumwacha mwanamke, mjane pamoja na mtoto. Walishangaa zaidi baada ya kuelezwa kwamba kifo hicho kilitokana na kunywa sumu ya Panya. Hawakuelewa ni kwa nini na sababu gani zilizomfanya Geofrey aamue kunywa sumu ile, wakabaki wakimwachia Mungu!
Mazishi ya Geofrey yalifanyika katika makaburi ya Njiro, yaliyoko nje kidogo ya jiji la Arusha. Ni mazishi yaliyohuidhuriwa na watu wengi sana, hasa wakazi wa eneo la Kijenge, ambako ndipo alipozaliwa na kukulia katika nusu ya ujana wake. Baada ya mazishi hayo kumalizika, ndipo siri ile ilipobaki kwa watu wale wawili, Deo na Grace, waliohusika kwa namna moja ama nyingine na kifo cha Geofrey.
*******
MATANGA yalipomalizika, mzee Kisamo aliamua kuitisha kikao cha faragha kati yake na Deo, ili kuizungumzia kifo kile cha mashaka dhidi ya kaka yake, Geofrey. Haikumuingia akilini mzee Kisamo, kwamba geofrey angeweza kujiua kwa kunywa sumu bila kuwa na sababu za msingi. Alimfahamu vyema mwanae, hivyo wazo hilo halikumjia kabisa akilini. Alihisi wazi kwamba ipo namna si bure!
Ilipofika saa moja za usiku, siku hiyo, mzee Kisamo na Deo walikutana faragha. Sehemu waliyokuwa wamekaa, ni ile sehemu waliyokaa siku ile ya usiku mmoja wa baridi, ambapo mzee Kisamo alikaa ma marehemu Geofrey, wakijadiliana kuhusu masuala ya kupata mchumba, na kumfahamisha anataka kuoa. Na mchumba mwenyewe alikuwa ni Grace!
Mzee Kisamo alionekana kuwa mtu mwenye mawazo mengi sana, kitu ambacho hata Deo alikiona. Na pia, Deo hakujua alichokuwa ameitiwa na baba yake usiku ule uliokuwa na kijibaridi cha upepo kilichokuwa kinapenya ndani ya maungo yao ingawa walijisitiri kwa makoti.
“Deo mwanangu…” mzee Kisamo akasema.
“Naam, baba…” Deo akaitikia huku akimwangalia baba yake.
“Nimekuita ili tuzungumze kidogo kuhusu kifo cha kaka yako…”
“Sawa baba…” Deo akaitikia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nataka kusikia kutoka kwako, kwa sababu wewe ndiye uliyekuwa unaishi na kaka yako huko Dar es Salaam, na ulikuwa naye karibu. Nataka kujua ni kwa nini Geofraey aliamua kujiua kwa kunywa sumu? Unajua kifo chake kinanichanganya sana…” mzee Kisamo aliendelea kusema.
“Kwa nini unasema hivyo baba?” Deo akauliza. “Hainiingii akilini kwamba geofrey alikunywa sumu kwa kupenda tu. Lazima iko sababu, ndiyo hicho ninachotaka kukifahamu…” mzee Kisamo aliendelea kumwambia.
“Baba…ukweli ni kwamba, Geofrey ameshakufa, nami siwezi kujua sababu zilizomfanya anywe sumu…” Deo akamwambia huku akiwa na wasiwasi.
“Laikini si ulikuwa unaishi vizuri na kaka yako?”
“Ndiyo, nilikuwa naishi n aye vizuri…”
“Je, shemeji yako, Grace?”
“Sikuwa na matatizo naye…”
“Vizuri, je, wao walikuwa wanaishi vizuri bila matatizo?”
“Walikuwa wanaishi vizuri, lakini…” Deo akashindwa kuendelea.
“Lakini nini?” Mzee Kisamo akauliza.
“Bla kuficha baba, niliwahi kusikia kwamba walikuwa na matatizo katika ndoa yao.”
“Matatizo gani?”
“Ni ya unyumba…”
“Ni kweli, kaka yako hakuwa mzima, hilo najua. Je, wewe ulikuwa unajua hilo?”D aliguna na kunyamaza.
“Sema, mbona unasita?”
“Nilikuwa najua baba…”
“Sasa niambie, huyo mtoto alizaliwaje wakati yeye hakuwa rijali?”
“Hilo siwezi kulielezea baba, hayo yalikuwa mambo yao ya ndani,” Deo alisema na kuongeza. “Hayo ni mambo waliyokuwa wamekubaliana na kuelewana.”
“Basi, ninachoona mimi, hicho ndicho kilichosababisha kaka yako kunywa sumu!” Mzee Kisamo akasema kwa msisitizo huku akimkazia macho Deo!
Baada ya maongezi yao, Deo na baba yake waliagana, ambapo Deo alielekea ndani ya chumba chake huku maneno ua mzee Kisamo yakirejea mara kwa mara kichwani kwake. Ukweli ni kwamba maneno yale yalimuumiza sana katika nafsi yake!
Deo aliendelea kujuta hasa baada ya kumuona mama yake, Bi. Benadeta akiwa amekaa chemba na Grace, ambapo hakujua walichokuwa wanazungumza. Ni kama walikuwa wamepanga, wakati mzee Kisamo alipokuwa akizungumza na Deo kuhusu kifo kile cha Geofrey, Bi. Benadeta naye alikuwa akizungumza na Grace, juu ya suala lile.
Walikuwa wamekaa sebuleni wao wawili tu, Bi. Benadeta na Grace mkwewe. Ukweli ni kwamba, Bi. Benadeta alikuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua undani wa kifo cha Geofrey, na hicho ndicho kilichomfanya amwite chemba ili kumhoji ilikuwaje mtoto wake yule akajiua?
“Grace mwanangu…” Bi. Benadeta akamwita.
“Bee, mama…” Grace akaitikia.
“Nimekuomba tukutane hapa kwa maongezi machache tu…”
“Ni sawa mama…”
“Lakini samahani sana kwa nitakachokuuliza…”
“Uliza tu mama…”
“Najua kuwa una majonzi ya kuondokewa na mwenzako, lakini ndiyo hivyo, maji yameshamwagika, kamwe hayazoleki. Ninachotaka ni wewe kuniambia ukweli niujue…”
“Ukweli gani mama?” Grace akauliza huku akionekana mwenye wasiwasi!
“Hivi ni kweli kwamba mumeo hakuwa mzima kimaumbile?”
“Ni kweli mama…hakuwa mzima…”
“Kama hakuwa mzima, huyu mtoto uliyezaa ni wa nani?”
“Aliniruhusu nizae nje ya noa ili nimwondolee aibu hii…”
“Sawa, sas huyo mtoto ni wa nani?”
“Siwezi kumtaja mama, kwa sababu ninazozijua mimi mwenyewe…”
“Au tuseme hana baba?”
“Anaye baba.”
“Yuko wapi, na anaitwa nani?”
“Nitamtaja tu mama, usihofu…”
“Je, unaweza kujua sababu za kumfanya anywe sumu?”
“Sielewi ni sababu gani, na wala hatukuwa na ugomvi naye baada ya kuridhika kuwa nimezaa. Isitoshe hakuacha ujumbe wowote, kitu ambacho kinazidi kutuchanganya!” Grace akaendelea kusema.
“Oh, basi nashukuru mwanangu, hicho ndicho nilichokuwa nimekuitia tuongee…” Bi. Benedeta akamwambia.
“Nashukuru mama…” Grace akamwambia.
Baada ya maongezi yao, wakaagana na kila mmoja akaendelea na utaratibu wake, lakini kwa upande wa Bi. Benadeta, alikuwa anawaza mbali sana. Kifo cha ghafla cha mwanawe, kilimweka njia panda!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
WIKI mbili zilipoita, Deo aliondoka jijini Arusha, kurejea Dar es Salaam, Hata hivyo, aliondoka peke yake na kumwacha mjane, shemeji yake, Grace, ambaye wazazi wake waliamua abaki Arusha kwanza mpaka siku arobaini zitakapokwisha. Japokuwa msiba ulikuwa umemalizika, Deo alikuwa bado ana wasiwasi mkubwa, hasa alipokuwa akifikiria kwamba marehemu kaka yake ndiye aliyempokea na kumtafutia kazi. Sasa hakuwepo tena! Amebaki peke yake!
Mara baada ya kufika Dar es Salaam, Deo alirejesha chumba alichokuwa amepanmga kule Tabata Bima na kuhamia nyumbani kwa kaka yake. Hata hivyo, ilimbidi awe na kichwa kigumu, kwani majirani wengi walikuwa wakimnyooshea kidole baada ya kufahamu kuwa ndiye aliyezaa na shemeji yake. Wengi walivumisha kwamba alimuua kaka yake kwa sumu ili aweze kurithi mali zake.
Siku ziliendelea kusonga mbele huku majirani wakisema mengi kuhusu uhusiano wa Deo na Grace. Hata hivyo hakujali maneno yao, na kuamua kutia pamba masikioni. Akaendelea kuchapa kazi kwa bidii zote huku akiwa katika ulimwengu wa pekee kwa kujitenge na watu waliokuwa wakimsema vibaya, kwa vile hawakumsaidia chochote!
Hatimaye siku ya arobaini tangu Geofrey afariki ilifika. Ilimbidi Deo arejee tena Arusha kwa ajili ya kuhudhuria arobaini ya kaka yake, ambapo alisafiri kwa kutumia usafiri wa Basi na kupokelewa vizuri, na baada ya kupumzika ndipo walipoanza maandalizi ya shughuli ile iliyotegemewa kuhudhuriwa na watu wengi, wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki waliokuwepo katika sehemu mbalimbali, mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment