Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

SIRI YA MKE - 5

 





    Simulizi : Siri Ya Mke

    Sehemu Ya Tano (5)



    HATIMAYE siku ya arobaini tangu Geofrey afariki ilifika. Ilimbidi Deo arejee tena Arusha kwa ajili ya kuhudhuria arobaini ya kaka yake, ambapo alisafiri kwa kutumia usafiri wa Basi na kupokelewa vizuri, na baada ya kupumzika ndipo walipoanza maandalizi ya shughuli ile iliyotegemewa kuhudhuriwa na watu wengi, wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki waliokuwepo katika sehemu mbalimbali, mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

    Siku hiyo ilianza kwa misa ya mkesha na kufuatilia kwa shughuli ya chakula na vinywaji vya kikabila. Baada ya shughuli hiyo kumalizika, familia ya mzee Kisamo ilikutana kwa ajili ya kupanga mikakati baada ya kumalizika kwa zile siku arobaini. Kikao kile cha wazee kilifanyika kwa kufuata mila na desturi za kabila la mzee Kisamo, ambazo nyingine zilikuwa zimepitwa na wakati wa kizazi cha sasa. Walipanga kuwa, Grace, mke wa marehemu Geofrey, arithiwe na Deo, mdogo wake na marehemu, kama angekubali.. Uamuzi huo ulilenga kuufanya ukoo wa mzee Kisamo usipotee.

    Lengo lingine la uamuzi huo lilikuwa kuhakikisha mali zote za marehemu Geofrey hazipotei, waliona kama Grace angeolewa na mwanaume mwingine, mali zile zingeweza kuangukia kwa watu wengine. Baada ya kikao kile cha wazee hao kumalizika, jopo lao lililoongozwa na mzee aliyekuwa mshenga wa Geofrey, lilikutana na kumketisha chini Deo. Wakamweleza kwa kirefu kuhusu taratibu za kimila zinavyosema, ambapo Deo aliwasikiliza kwa makini sana huku akizungusha macho yake kwa wazee wale waliokuwa wamemzunguka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tunajua kuwa wewe Deo ni mtu mzima…” alisema mzee Kileo, aliyekuwa kiongozi wa jopo lile.

    “Ndiyo, mimi ni mtu mzima…” Deo akasema huku akiwa na hamu ya kusikia kilichokuwa kinaendelea juu ya kikao kile.

    “Inabidi tukueleze taratibu muhimu kuhusu mila zetu, kwani kama unavyojua, kaka yako amefariki na ameacha mke na mali nyingine kadhaa, ambazo lazima ziwe na mrithi…sijui unanipata?” Mzee Kileo akaendelea kusema.

    “Nakupata mzee, endeleea…” Deo akamjibu.

    “Pamoja na kaka yako kuacha mjane, kuna kitu muhimu sana. Ni lazima mjane huyo aishi kama mwanafamilia na kuuendeleza ukoo wa Kisamo. Pili ni juuya nyumba. Marehemu kaka yako ameacha nyumba lule Dar es Salaam. Sasa nyumba hiyo inaweza kupotea iwapo mkewe ataolewa na mwanaume mwingine ikizingatiwa kuwa ni mali ya mtoto!” Mzee Kileo alimaliza kusema na kubaki akimwangalia Deo kama ujumbe ule ulikuwa umemwingia vizuri, au hata kama angechangia chochote baada ya kuisikia kauli ile!

    Deo hakuweza kusema lolote kwa muda ule, kwani alihisi balaa lilikuwa likimjia na kuona hatari ya kurithishwa shemeji yake Grace.Kamwe hakupenda kitu kama hicho kitokee, inagawa ni kweli alizaa na yule mtoto.

    “Naona unanisikiliza kwa makini,” mzee Kileo akamwambia Deo na kuendelea. “Jambo la tatu kijana, ni kwamba tunavyoona sisi wazee wako, inabidi umrithi mke wa kaka yako kwa lengo0 la kuuendeleza ukoo. Umenielewa?”

    “Nimekuelewa mzee…lakini…” Deo akamwambia kwa kusita.

    “Lakini nini?” Mzee Kileo akamuuliza.

    “Haiwezekani! Siwezi kumrithi mke wa kaka yangu hata kidogo…”

    “Punguza jazba kijana…” mzee Kilea akamwambia kwa sauti ya taratibu.

    “Nasema haitawezekana!” Deo alisisitiza!

    “Lazima tuelewane kwa sababu jambo hili lina manufaa makubwa…”

    “Hapana…afadhali apewe uhuru wa kuolewa na mwanaume mwingine lakini siyo mimi!”

    “Kwa nini hutaki kijana?”

    “Nimeamua tu…”

    “Nia yetu ni kurejesha mali za marehemu kaka yako mikononi mwako. Sielewi kwa nini unapinga suala hili…”

    “Wazee wangu, hizo taratibu za kurithi wanawake zimepitwa na wakati, hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa kuna ugonjwa hatari wa Ukimwi. Mtu anaweza kurithi mke, kumbe mumewe alikufa kwa ugonjwa huo, sasa si kuna hatari ya kuiambukizana?”

    “Laini kaka yako hakufa kwa ugonjwa huo…eti!”

    “Hapana, hamuwezi kunishawishi kwa jambo kama hilo wazee wangu!” Deo aliendelea kuwa na msimamo!

    “Unautia ukoo wetu nuksi kijana, hivi unaelewa hilo?” Mzee mwingine aliyekuwa kimya muda mrefu, alidakia.

    “Pamoja na kuutia nuksi ukoo, mila hizo zimepitwa na wakati. Kamwe hamuwezi kunilazimisha nimrithi mke wa kaka yangu,” Dea akamwambia.

    “Ooohps…kijana mgumu huyu! Nadhani imeshindikana!” Mzee Kileo alisema huku akiwaangalia wazee wenzake, mmoja baada ya mwingine. Kila mmoja alionekana akiwa amepigwa butwaa!

    Je, wangemlazimisha? Haiwezekani



    *******

    UPANDE wa pili, lilikuwepo kundi jingine lenye mchanganyiko wa vijana, ambao walikuwa wakinywa vinywaji, kila mmoja alikuwa akisikiliza kile kilichokuwa kinaongelewa na wazee wale waliokuwa wamemweka kati kijana Deo, aliyekuwa anashinikizwa amrithi shemeji yake. Pia, vijana wale waliweza kumsikia jinsi Deo alivyokuwa anakataa katakata ushauri ule wa kumrithi mke wa marehemu kaka yake!

    Pia, wakati huo, Grace alikuwa amekaa kwenye mkeka pamoja na akina mama wengine, akiwemo mama mkwe wake, Bi. Benedeta. Alikuwa akifuatilia kwa makini majadiliano yale kati tya Deon a wale wazee. Alimsikiliza kwa makini Deo alivyokuwa akiwakatalia kumrithi kaka yake. Moyoni hakuamini iwapo maneno yale yalitoka kinywani mwa Deo. Hakitarajia kamwe, hasa alipowaza kuwa mtoto aliyenaye, amezaa na Deo!

    Awali, akilini mwake, Grace alijua kuwa Deo angeupokea uamuzi ule kwa mikono miwili ili waishi kwa furaha wakiwa mke na mume. Sasa mbona amekataa? Bila kutegemea, Grace alijikuta akichanganyikiwa na kuona wingu zito likitanda mbele ya macho yake! Akajikuta akilia kwa uchungu!

    Grace akanyanyuka na kuekekea sehemu ile aliyokuwa amekaa Deo. Watu wote wakabaki wakimwangalia hadi alipomfikia Deo, na kusimama karibu yake!

    “Usiseme hivyo shemeji…” Grace akamwambia Deo.

    “Kwa nini nisiseme?” Deo akamuuliza huku akimwangalia.

    “Ni afadhali ya wewe Deo!”

    “Afadhali ya nini?”

    “Ndiyo, ni afadhali ya wewe kuliko kaka yako marehemu kaka yako!”

    “Kwani imekuwaje?”

    “Jogoo lake lilikuwa halipandi mtungi!”

    “Yametokea wapi tena hayo shemeji?” Deo akamuuliza!

    “Lazima niseme ukweli, maana naona unaanza kuniruka!”

    “Mh!” Baadhi ya watu waliguna na kubaki wamepatwa na mshangao. Wakabaki wakiangaliana baada ya kusikia yale matamshi ya Grace.

    Mzee Kisamo aliyekuwa anasikiliza kwa makini mazungumzo yale, akadakia kwa kuuliza, “Unasemaje, jogoo halipandi mtungi?”

    “Ndiyo baba,” Grace akasema kwa kujiamini huku akimwangalia Deo.

    “Mh, makubwa,” mzee Kisamo akasema.

    “Hii mpya,” akadakia mzee mwingine!

    “Ina maana Geofrey alikuwa hazai?” Mzee Kileo akamuuliza Grace ili apate ufafanuzi zaidi.

    “Ndiyo, alikuwa hazai!” Alisisitiza Grace.

    Bi. Benadeta, ambaye alikuwa amenyamaza muda mrefu, aliyasikiliza maneno yale ya mkwe wake kwa makini. Mapigo yake ya moyo yakapiga kwa kasi, halafu akamuuliza.

    “Unasema nani hazai?”

    “Marehemu Geofrey, mume wangu…”

    “Kwani alikuwaje?”

    “Alikuwa siyo mwanaume kamili…” Grace alijibu bila wasiwasi wowote!

    “Kama alikuwa hazai, huyo mtoto ni wa nani sasa?” Bi. Benadeta akamuuliza Grace huku akimkazia macho!

    “Ni historia ndefu sana…” Grace akasema huku akiendelea kumwangalia Deo aliyekuwa ameinama akisubiri bomu lile lipasuke! Hakuwa na raha kabisa, akijilaumu kwa kushirikiana kumapenzi na shemeji yake, Grace, na hatimaye kutokea kile kinachojadiliwa muda ule!

    “Hebu ieleze hiyo historia ndefu…” mzee Kisamo akamwambia Grace.

    “Bila kuficha wazee wangu, nimeishi nam marehemu kwa muda mrefu baada ya kufunga ndoa. Amini msiamini, tokea tuoane, hakuna siku hata moja aliyonitimizia haki yangu ya msingi ya ndoa, yaani kunipa unyumba. Nikisema hivyo, nina maana kwamba hakuwa na nguvu za kiume kabisa!”

    “Unasema kweli?” Bi. Benadeta aliuliza.

    “Ni kweli kabisa. Na ndiye aliyenishauri nitembee nje ya ndoa ili niweze kumzalia mtoto!”

    “Upuuzi mtupu!” Bi. Benadeta akasema akionyesha mwenye hasira!

    “Ndiyo hivyo mama…”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa tueleze, huyo mtoto ni wa nani kama siyo wa Geofrey?”

    “Ni lazima niseme ukweli bila kuficha chochote wala kusingizia. Huyu mtoto nimezaa na shemeji Deo. Sikuona sababu yoyote ya kuzaa na mtu mwingine!”

    “Uuuuwiii!” Bi.Benadeta alipiga kelele, na bila kutarajia, alisimama na kuanza kusaula nguo zake na kuzitupa ovyo. Kwa jisi alivyokuwa, hakutofautiana na mtu aliyechanganyikiwa kiakili!

    “Kumbe Deo ndiye uliyemuua kaka yako! Wewe ndiye chanzo cha yeye kunywa sumu, Mungu wangu!” Alizidi kulalamika Bi.Benadeta!



    “Mh, balaa gani hili tena?” Mzee Kisamo alisema huku akimwangalia Deo na kuendelea. “Umefanya nini mwanagu?”

    “Siyo kosa langu baba…” Deo alijitetea!

    “Ni kosa la nani?”

    “Ni kosa la shemeji yangu Grace, ambaye alinishawishi!”

    “Unasema umeshawishiwa?” Mzee Kisamo akauliza.

    “Ndiyo, alinishawishi, kwa vile kaka hakuwa na uwezo wa kuzaa!”

    “Hii ni hatari sasa!” Mzee mwingine akadakia!

    Ghafla Deo akaanza kuhisi kizunguzungu. Akapiga yowe kubwa na kisha kuanguka chini na kupoteza fahamu. Kuanguka kule kwa Deo, kuliwashtua wale wazee waliokuwa wakizungumza naye. Wakamzunguka na kuanza kumpatia huduma ya kwanza kwa kumpepea hadi alipozinduka. Baada ya kuzinduka, Deo hakuweza kuwa na kumbukumbu na kile kilichotokea wakati ule, na alipojaribu kunyanyuka na kutembea, alikuwa akiyumbayumba. Watu wote wakawawanamwangalia kwa hofu na mashaka!

    “Hakika hii ni aibu kwangu! Siwezi kuishi hapa duniani!” Deo akasema baada ya fahamu kuanza kumrudia kichwani mwake.

    “Pole sana…” kijana mmoja akamwambia.

    “Pole aisaidii kwa wakati huu!”

    “Kwa nini?”

    “Ni lazima nikajinyonge!” Deo akasema huku akiangalia pande zote.

    Baada ya kusema vile, Deo akachomoka mbio kutoka sehemu ile alipokuwa amesimama na kuanza kukimbilia sehemu isiyojulikana. Mara baada ya Deo kukimbia, kundi la vijana na wazee waliokuwa eneo lile, likapatwa na hali ya mshangao kabla ya kuamua la kufanya!

    Grace naye aliposhuhudia Deo akikimbia, naye alichomoka mbio kumfuata huku akisema, “Na mimi naondoka, huwezi kuniacha. Nakwenda kujitia kitanzi ili nikufuate!”

    “Hawa wamechanganyikiwa!” Mzee Kisamo akasema huku akikiodolea macho kule walipokimbilia Deo na Grace!

    “Mungu wangu, wototo wetu jamani!” Bi. Benadeta alilalamika huku ameshika kichwa chake!

    “Wafuatiliwe!” Mzee Kisamo akasema.

    Wote waliokuwa kwenye kikao kile, walinyanyuka na kuanza kuwafuatilia nyuma ili kuyaokoa maisha yao!



    *******

    AKIWA anakimbia kwa mwendo wa kasi, Deo alipogeuka nyuma, aliweza kumwona Grace akimfuata. Hivyo basi akazidisha mbio huku akikatiza vichochoro kadhaa vya eneo lile la Kijenge hadi alipofika katika barabara kuu. Baada ya kufika pale, akasimamisha teksi iliyokuwa inapita, akaufungua mlango wa mbele na kuingia. Muda ule alikuwa akihema kwa nguvu na mapigo ya moyo wake yaliongezeka mara dufu!

    “Nipeleke Tengeru…” Deo akamwambia dereva.

    “Sawa braza…” dereva akamjibu huku akiiondoa teksi. Lakini alikuwa na wasiwasi na yule abiria wake!

    “Endesha kwa kasi, nyoosha mguu!” Deo akamwambia yule dereva, ambaye bila kupende alifuata matakwa yake.

    Wakati huo, Deo alipotazama kwenye kioo cha gari kilichokuwa mbele yake juu ya kipaa cha gari, aliweza kumwona Grace akisimamisha teksi nyingine.

    “Kwani vipi braza?” dereva yule akamuuliza Deo.

    “Kuna mtu namkimbia!”

    “Mtu gani? Au polisi?”

    “Hapana, siyo polis. Namkimbia yule mwanamke!”

    “Mwanamke gani?”

    “Yule anayepanda teksi nyuma yetu!”

    “Wanawake wa sasa hivi bwana, wanang’ang’ania wanaume kama Luba. Ni kwa sababu hakuna waoaji,” dereva yule alisema baada ya kumwelewa Deo. Akabadili gea na kuongeza mafuta!

    Baada ya Grace kusimamisha teksi, alimwamuru dereva aifuiatilia ile teksi aliyokuwa amepanda Deo. Ikawa mfukuzano hadi walipofika katika barabara kuu iendayo Moshi. Magari yote yakaifuata barabara inayoelekea Moshi huku wakivipita vitongoji kadhaa. Kwa ujumla watu wote walikuwa wamenyamaza kimya ndani ya magari yale.

    Kwa bahati mbaya, ile teksi aliyokuwa amepanda Deo, ilipasuka gurudumu la mbele upande wa kulia, na kuifanya iserereke. Kwa vile ilikuwa katika mwendo wa kasi, iligota upande wa pili wa barabara. Hakuna aliyeumia!

    “Mungu wangu, balaa gani hili?” Dereva akasema huku akijiandaa kuufungua mlango ili kushuka chini!

    “Na kweli ni balaa!” Deo akaema huku akiufungua mlango. Kisha akashuka chini huku akiangalia kule walipotokea!

    “Itabidi nifunge gurudumu la akiba…” derive akamwambia Deo huku akizunguka nyuma ya gari.

    “Utawahi kweli?”

    “Sasa unafikiri nitafanyeje? Hii ni ajali!”

    “Atanikuta ninayemkimbia!” Deo akasema huku akijiandaa kukimbia!

    “Vipi braza, mbona unataka kuondoka bila kunilipa fedha?” Dereva akamuuliza Deo.

    “Ah,” Deo akaguna. Na bila kutarajia, alichomoka mbio na kuelekea ndani yam situ mkubwa uliokuwa upande wa kushoto mwa barabara. Lengo lake lilikuwa ni kumkimbia Grace ili asimkute mahali pale, kwani alishapania kujitia kitanzi!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Shenzi sana!” Derva yule akatoa tusi kubwa la nguoni. Hakuwa na la kufanya, na pia hakuweza kumkimbiza Deo!

    Hazikupita hata dakika tano, ile teksi iliyokuwa imembeba Grace, ilifika katika eneo lile, ambapo waliikuta ile teksi imegota kando ya barabara. Grace akafungua mlango na kuchomoka mbio kumfuatilia Deo, kitu ambacho kilizidi kuwachanganya madereva wale wa teksi.

    “Imekuwaje braza?” Dereva wa teksi iliyopata ajali akauliza!

    “Hata mimi sijui kinachoendelea braza!” Dereva wa pili akajibu huku akiangalia kule alipokibilia Grace. Ukweli ni kwamba alikuwa amechanganyikiwa. Alijihisi kama mtu aliyekuwa ndotoni akitazama sinema ya kusisimua!

    “Sijui hawa watu ni wenda wazimu?”

    “Inawezekana, kwani yule mwanamke alinikodi ili nikufukuze wewe, kwa sababu alikuwa na shida na yule abiria uliyembeba…”

    “Hata mimi yule abiria wangu aliniambia anamkimbia yule mwanamke!” dereva wa kwanza akasema.

    “Ama kweli wametufanya majuha!

    Madereva wale walibaki wamechanganyikiwa, kwani abiria waliokuwa wamewabeba hawakuwalipa fedha. Yule wa kwanza alikuwa amepata hasara mara mbili. Hasara ya kwanza ni ya kuharibikiwa gari lake, nay a pili ni kutolipwa ujira wake. Walichofanya ni kusaidiana kulitengeneza gari lililopta ajali.

    Hawakuwa na muda wa kuwafuatilia abiria wao!

    *******

    UPANDE mwingine, lile kundi la vijana na wazee lililokuwa linawafiatilia Deo na Grace, baada ya kufika barabarani, wakakuta wote wameshakodi teksi. Hawakuwa na fedha, hivyo wakabaki wamepagawa! Hata hivyo, mzee Kisamo aliamua kukodi gari aina ya Land Rover 110 iliyokuwa ikipita barabarani, wakapanda vijana kumi, akiwemo na yeye. Wakaanza kuwafuatila hasa kwa mzee Kisamo akihofia usalama wa mtoto wake, hasa kila mmoja kusema kwamba atajitia kitanzi!

    Dereva wa gari lile aliliendesha kwa mwendo wa kasi kuzifuatilia zile teksi mbili, hata hivyo hawakuweza kuziona, hali iliyomfanya mzee Kisamo apatwe na wasiwasi mwingi. Moyoni mwake aliwaza kwamba, alikuwa mbioni kumpoteza mtoto wake wa pili, baada ya wa kwanza, Geofrey kufa kwa kula sumu ya panya!

    Hatimaye walifika katika sehemu ile ambayo, teksi ile iliyokuwa imembeba Deo ilipata ajali. Wakayakuta magari yote mawili huku madereva wakiwa wanasaidiana kubadilisha gurudumu baada ya kupiga jeki. Baada ya gari kusimamishwa, mtu wa kwanza kushuka alikuwa ni mzee Kisamo, halafu akawafuata wale madereva huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi kwa kutowaona Deo na Grace! Hakujua wameelekea wapi!

    “Hamjambo jamani!” Mzee Kisamo aliwasalimia wale madereva waliokuwa wakimalizia kufunga gurudumu.

    “Ah, mbaya mzee wangu!” Dereva mmoja akasema.

    “Mbaya sana!” Dereva mwingine wa gari ya pili akadakia.

    “Imekuwaje jamani?” Mzee Kisamo akaendelea kuuliza.

    “Gurudumu limepasuka…”

    “Poleni sana!”

    “Ahsante mzee…”

    “Wale abiria mliokuwa nao wako wapi jamani? Maana ndiyo hao tunaowafuatilia!”

    “Wale machizi?” Dereva mmoja akasema.

    “Una haki ya kuwaita machizi,” mzee Kisamo akamwambia.

    “Washenzi sana, baada ya gari yangu kupasuka gurudumu, jamaa akachomoka kwenye gari na kukimbilia msituni,” akasema dereva wa teksi iliyokuwa imembeba Deo.

    “Na mimi baada ya kufika hapa,” akasema yule dereva wa gari ya pili. “Yule mwanamke naye akatoka mbio kumfuatilia mwanaume kuelekea msituni. Sijui wana matatizo gani watu wale!

    “Mbaya zaidi hawjatulipa nauli!” Akamalizia dereva mwingine.

    “Mungu wanmgu!” Mzee Kisamo akasema huku mikono yake ameiweka kichwani! Ukweli ni kwamba alikuwa amekata tamaa!

    “Mzee, ni wanao?” Dereva akamuuliza mzee Kisamo baada ya kumwona amechanganyikiwa!

    “Ndiyo, ni wanangu…”

    “Wana matatizo gani?”

    “Ah, acha tu!” Mzee Kisamo akasema huku akiangalia upande ule wa msitu walipokimbilia Deo na Grace.

    “Mzee, tuwafuatilie!” Kijana mmoja akatoa wazo.

    “Sawa, tufanye hivyo vijana…” mzee Kisamo akaunga mkono.

    Ndipo vijana wale na mzee Kisamo walipoamua kuuvaa ule msitu mzito waliokimbilia watu wale. Walikuwa wakitembea kwa kupita kwenye nyasi zilizokuwa zimelala, wakiamini wamepitia huko. Hakika ulikuwa ni msitu mzito unaotisha kutokana na miti iliyokuwa imefungamana!

    Hata hivyo hawakukata tamaa!





    ********

    WAKATI huo, ndani ya msitu ule, Deo na Grace walikuwa bado wanafukuzana, Deo akiwa mbele na Grace akimfuata nyuma. Ni hadi walipochoka na kuendelea kufukuzana kama kuku huku wakikwepa miti na vichaka!

    “Deo simamaaa!” Grace alimwambia!

    “Sisimami, una shida gani!”

    “Simama tu, oh!”

    “Nimeshakwambia sisimani! Nakwenda kujinyonga!”

    “Usifanye hivyo!”

    “Nitafanya hivyo!”

    “Ooohpsi!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye mbio zao zile zilikomea kwenye gema moja kubwa, lililokuwa limezungukwa na majani mengi, ambapo hawakuweza kutambua mara moja kuwepo kwa gema hilo. Akatangulia kuangukia mzimamzima Deo, halafu akafuatia Grace. Wakabiringita kwa kasi hadi walipofika chini ya gema lile, kiasi cha kujikuta wameanguka sambamba wakifikia sehemu isiyokuwa na nyasi nyingi zaidi ya udongo laini na nyasi chache.

    Deo alikuwa upande wa kulia na Grace upande wa kushoto, na kwa vile walikuwa wamechoka sana, walibaki wakihema kwa nguvu, na hakuna aliyemsemesha mwanzake zaidi ya kujisikilizia walivyofika katikati ya msitu ule baada ya kukimbia katika kikao kilichohitishwa na wazee, nyumbani kwao, Kijenge. Baada ya kupumzika vya kutosha, Deo alivuta pumzi ndefu na kusema:

    “Gracee…oh!”

    “Oh, nakusikiliza Deo…oh!” Grace aliitikia kichovu.

    “Sasa umefanya nini?”

    “Kivipi Deo?”

    “Kwa nini umenifuata mpaka huku?”

    “Si ulisema unakwenda kujinyonga?”

    “Ndiyo, sioni umuhimi wowote wa kuishi…”

    “Oh, na wewe unataka kujinyonga?”

    “Ndiyo!”

    “Na mtoto je?”

    “Mtoto atabaki yatima!”

    “Oh, Mungu wangu!”

    “Ndiyo ukweli wenyewe!”

    “Hakika hii ni dhambi kubwa sana!”

    “Lakini tumefanta dhambi kubwa sana shemeji Deo…”

    “Huu siyo wakati wa kulaumiana…”

    “Isipokuwa…”

    “Tupange la kufanya…hakuna sababu za kujiua Grace.”

    “Ooohps! Tufanyeje sasa?”

    “Cha muhimu tuishi kama mume na mke, kwani hakuna jinsi…”

    “Itawezekana kweli?”

    “Itawekana mbelekwa mbele…” Deo akasema na kuongeza. “Twende zetu nyumbani tukapange na wazee!”

    “Sawa,” Grace akasema huku nuru ya matumaini ikionekana katika sura yake.

    Wote wawili wakanyanyuka na kutoka ndani ya gema lile waliloangukia ndani yake. Halafu wakapanda huku wakivutana mikono hadi walipofanikiwa kutoka hadi juu, ambapo walianza kuondoka huku angali bado wameshikana mikono. Walikatiza ndani ya msitu ule kuelekea katika barabara kuu, sehemu waliyokuwa wametokea mwanzo. Muda wote walikuwa wakishindana na nyasi ndefu zilizokuwa zimejaa katika eneo lile, hadi walipoweza kusikia sauti za watu waliokuwa wakizungumza ndani yam situ huo. Ndipo walipowaona watu waliokuwa wanawafuatilia!

    “Unaona kulee?” Deo akamwambia Grace.

    “Ndiyo, ni watu!” Grace akadakia!

    “Wanatufuatilia sisi!”

    “Bilam shaka!”

    Ndiyo, walikuwa ni watu wale waliokuwa wanawafuatilia, mzee Kisamo na kundi lile la vijana.

    “Deoooo!” Mzee Kisamo akasema mara tu baada ya kuwafikia.

    “Baba!” Deo akaitikia!

    “Imekuwaje mwanangu?”

    “Acha tu baba…”

    “Unataka kujitundika kitanzi?”

    “Ilikuwa iwe hivyo baba!”

    “Oh, usifanye hivyo, basi twendeni nyumbani tujajadilioane upya kuhusu suala hili!” Mzee Kisamo akamwambia Deo.

    “Sawa baba…” Deo akakubali baada ya baba yake kumwambia vile.

    Hivyo basi, wote wakaongozana kuelekea katika arabara kuu walipokuwa wameliacha lile gari aina ya Land Rover. Baada ya kufika wakalikuta gari limeegeshwa kando ya barabara, nao wakapanda na kuanza safarim ya kurudi jijini Arusha. Pale ndipo Deo na Grace walipokumbuka kuwa walikuwa wamewatelekeza wale madereva teksi wakati walipokuwa wanafukuzana. Lakini hawakujua kilichokuwa kinaendelea na waliondoka baada ya kutengeneza gurudumu la gari yao.

    Hatimaye, mzee Kisamo, na watu wake, walifika tena nyumbani huku wakiwa wamechoka baada ya kukimbizana kule msituni, ambapo Deo alitala kwenda kujitia kitanzi kwa vile alikuwa anapinga maamuzi ya wazee!



    *******

    MZEE Ramson Laiser na mkewe, Bi. Letisia, wazazi wa Grace, walikuwa wamekaa sebuleni nyumbani kwao, wakijadiliana juu ya mtoto wao, alivyokuwa akidhalilishwa na familia yam zee Joel Kisamo, punde tu baada ya kufiwa na mume wake, Geofrey. Kitu kilichowashangaza ni kwamba walikuwa wakijipangia mambo mengi bila kuwashirikisha wao kama wazazi wenzao!

    Habari zilizowasikitisha na kuwatisha zaidi, ni juu ya kusikia kwamba walipanga kumrithisha mtoto wao Grace, kwa Deo, mdogo wake na marehemu, Geofrey, ili awe mke wake! Ni utaratibu ambao haukuwezekana kabisa kwa kizazi cha sasa, na ukiwa ni udhalilishaji mkubwa wa kijinsia. Hivyo mzee Ramson akiwa amechukia, alivuta pumzi ndefu na kuzishusha, kasha akamwambia mkewe:

    “Mama Grace…”

    “Bee…” Bi. Letisia akaitikia.

    “Hivi unalifikiriaje hili suala la Bw. Kisamo kumwozesha binti yetu kwa mtoto wake, Deo?”

    “Kwa kweli mimi sikubaliani nalo!” Bi. Letisia akasema huku amekunja sura!

    “Kwa hivyo unasemaje?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naona njia iliyobaki ni kwenda kumchukuwa haraka iwezekanavyo, na kumrudisha hapa nyumbani!”

    “Hilo ni jambo la maana…”

    Baada ya mzee Ramson na mke wake kukubaliana, wakaondoka nyumbani kwao, na kuelekea Kijenge Kati, nyumbani kwa mzee Kisamo, ambapo hapakuwa mbali sana kiasi cha kuwafanya watembee kwa miguu tu. Baada ya kufika, walikuta katika eneo la mji wa mzee Kisamo, walikuta umati wa watu umejazana, kushuhudia, mzee Kisamo na vijana wao, Deon a Grace walipokuwa wanarudi kutoka msituni walipokuwa wamekimbilia kwa ajili ya kwenda kujinyonga!

    Lile gari aina ya Land Rover lilikuwa limeegeshwa nje ya nyumba na waliokuwa ndani wakaanza kuteremka. Ndipo Grace alipomwona mama yake akiwa amesimama na baba yake, mzee Ramson Laiser. Akachomoka mbio na kumkimbilia huku akilia, na baada ya kumfikia akamrukia!

    “Oh! Mama!” Grace akasema!

    “Oh! Mwanangu!” Mama yake akasemas huku akimkumbatia na kumpigapiga mgongoni!

    “Kidogo ningejitia kitanzi mama!”

    “Kwa nini mwanangu?”

    “Ah, ni makubwa mama…”

    “Basi, tulia mwanangu, ndiyo maana tumekuja na baba yako…”

    Wakati wote ule, mzee Kisamo bado alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa huku akitweta. Baada ya kuwaona wageni wale, mzee Ramson na mkewe, Bi. Letisia, akawakaribisha ndani. Hawakupinga, wageni hao wakaingia hadi ndani na kufikia sebuleni huku wakiwa na hamu ya kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea kutokana na misukosuko ile iliyotokea katika kitongoji kile!

    “Ndiyo mzee mwenzangu, hebu niambie kinachoendelea…” mzee Ramson akamwambia punde baada ya hali ya utulivu kurejea.

    “Ni matatizo yametokea…”

    “Matatizo gani?”

    “Watoto walikuwa wamekimbia!”

    “Walikimia kwa sababu gani?”

    “Ni kwamba tulikuwa tumepanga kuwaozesha Grace na Deo, ili waweze kuuendeleza ukoo wetu baada ya mumewe, Geofrey kufariki…” mzee Kisamo alimweleza yote mzee Ramson, jinsi walivyokuwa wamepangilia mwanzo mpaka mwisho, kiasi kwamba haikumuingia akilini mzee Ramson, ambapo hakukubaliana na uamuzi ule waliokuwa wamepanga.

    “Mzee mwezangu, mbona mnajipangia mambo kiholela?” Mzee Ramson aliuliza huku akitetemeka kwa hasira!

    “Kwa nini unasema hivyo?” Mzee Kisamo akasema na kuona kuwa hakukuwa na kosa lolote lililotokea!

    “Mtamrithishaje binti yangu kwa mwanenu Deo?”

    “Ndiyo, tuliona tufanye hivyo ili ukoo usije ukapotea…”

    “Mbona hukunishirikisha?”

    “Sikuona umuhimu wowote kwa shughuli ambayo hata mimi kama mzazi ningeweza kufanya…au vipi?”

    “Haiwezekani! Hayo ni mabo ya kizamani, hivyo nakuambia kuanzia sasa hivi, sitaki kusikia hayo!” Mzee Ramson akabwata, halafu akaendelea. “Mimi ninaondoka na mwanangu, msinifanye mjinga!”

    “Umefika mbali mzee mwenzangu!”

    “Nimeamua hivyo, kama alikuwa ameshaolewa na marehemu Geofrey, basi ameshatangulia mbele ya hakli, si vyema kumlazimisha aolewe na mdogo mtu!”

    “Lakini tambua kwamba ni Grace mwenyewe amethibitisha kwamba amezaa yule mtoto na Deo!” Mzee Kisamo akasema kwa kusisitiza!

    “Kama amezaa naye hakuna tatizo. Mimi nitamlea huyo mjukuu, lakini lazima niondoke na mwanangu!” Mzee Ramson alimaliza kusema!

    Baada ya kumaliza kusema vile, mzee Ramson akamgeukia Grace na kumuangalia takriban dakika mbili hivi, halafu akamuuliza:

    “Grace…”

    “Bee…” Grace akaitikia huku akimuangalia baba yake.

    “Hebu niambie ukweli!”

    “Ukweli upi baba?”

    “Ni kweli kwamba umezaa na Deo?”

    “Ni kweli baba…”

    “Kwa ninim uliamua kufanya hivyo?”

    “Ni shetani alitupitia baba…” Grace akasema na kuendelea. “Vilevile ilichangiwa na mume wangu, ambaye alikuwa hana nguvu za kiume, kiasi cha kushindwa kunitimizia haki yangu ya ndoa! Sasda unafikiri mimi kama binadamu, na mwanamke kam ili, ninefanyeje? Nilizidiwa!”

    “Oh! Mungu wangu!” Mzee Ramson akasema huku ameshika kichwa chake! Makubwa!

    “Ndiyo hali halisi baba…”

    “Kwa hivyo mwanangu unaamuaje?”

    “Sina la kuamua…ukweli ni kwamba nimechanganyikiwa!” Grace akamwambia baba yake kisi cha kumwacha njia panda!

    “Umechanganyikiwa nini? Yaani umekubali kurithiwa?” Mzee Ramson akaendelea kumuuliza!

    “Wanadai mila ndiyo inasema hivyo…”

    “Hakuna kitu kama hicho, mila gani hiyo iliyopitwa na wakati? Hapa tunaondoka wote, mguu kwa mguu mpaka nyumbani!” Mzee ramson akasema kwa hasira huku akijiandaa kunyanyuka pale kweye sofa alipokuwa amekaa!

    “Sawa baba, nakusikiliza…” Grace naye akasema huku akinyanyuka tayari kumfuata baba yake.

    “Mengine tutapanga siku ya kuweka kikao cha kutatua matatizo haya!”

    Baada ya kumaliza majadiliano yale, mzee Ramson hakupenda kupoteza muda, kwani alimwamuru mkewe, Bi. Letisia amchukuwe Grace pamoja na mtoto wake, waende nyumbani. Walitoka na kuwaacha, mzee Kisamo na watu wengine wamechanganyikiwa!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda siyo mrefu, watu waliokuwa wamejazana kule nje kushuhudia tukio lile la aina yake, wakatawanyika na kuendelea na shughuli nyingine. Hata hivyo, ilikuwa ni furaha kwa upande wa Deo baada ya kuokoka katika janga lile la kurithishwa mke, ambaye ni shemeji yake Grace.

    Hivyo kuanzia muda ule Deo akaanza kupanga mpango wa kuondoka haraka sana ndani ya jijini Arusha na kurudi Dar es Salaam, kuendelea na mipango mingine, lakini si kwa baba yake, mzee Kisamo ambaye alikuwa amepanga kuwa ni lazima Deo amwoe Grace hata kama baba yake hataki, ukizingatia alikuwa ni mtu wa kung’ang’ania kitu, akiamua ameamua, hakuna mtu wa kuweza kumshawishi aache!

    Ndiyo tabia yake!



    ********

    INGAWA mzee Kisamo alikuwa analazimisha watoto wale, Deo na Grace, mke wa marehemu kaka yake waoane, lakini hakujua kitu ambacho kingeweza kuja kumtokea kiasi cha kumfanya asitishe ule mpango mara moja. Na baada ya watu wote kutawanyika, mzee Kisamo aliyekuwa ametoka nje kuwasindikiza wageni, alirudi na kuingia ndani ambapo alijibwaga kwenye sofa sebuleni na kuanza kuwaza na kuwazua.

    Mzee Kisamo hakupenda kupata usumbufu kabisa, hasa ukizingatia alikuwa amechoka vilevile katika pilikapilika zile za kuwafukuzia Deo na Grace, waliokuwa wamekimbilia msituni kujitia kitanzi. Mara baada ya kujilaza tu, kitu kama usingizi kikampitia na kuanza kuota njozi ya ajabu. Upande wake wa kushoto, kwenye kona ya ukuta wa sebule, kulitokea mwanga Fulani, ambao ulikuwa umefifia. Mzee Kisamo alipotupa macho yake na kuangalia, ndipo alipokumbana na kitu cha ajabu!

    Aliweza kuona mtu mmoja aliyekuwa amesimama akiwa amejifunika shuka nyeupe mwili mzima na kubakiza sura tu! Ulikuwa ni mzimu wa mwanawe, Geofrey, ambao kwa muda ule ulikuwa ukimkazia macho! Uliingiaje mle ndani? Hakujua!

    “Babaaa!” Mzimu ule wa Geofrey uliita kwa sauti kubwa, ambayo aliisikia mzee Kisamo peke yake!

    “Oh, nani wewe?” Mzee Kisamo akasema kwa hofu kubwa!

    “Ni mimi baba!”

    “Wewe Geofrey?”

    “Ndiyo!”

    “Si ulikufa wewe?”

    “Ndiyo baba…lakini sasa ni mzimu!”

    “Oh! Unasema ni mzimu?”

    “Ndiyo, nimekuja kutoka kuzimu!”

    “Mungu wangu…una shida gani? Oh!”

    “Nimekutokea kwa sababu maalum!” Mzimu ule ukamwambia huku ukiendelea kumkazia macho!

    “Sababu gani?” Mzee Kisamo akauliza.

    “Ninakujulisha kwamba uachane kabisa na mpango wako wa kumrithisha Deo mke wangu! Hilo ni onyo! La sivyo mtanifuata kuzimu!”

    “Oh, nimesikia, sitafanya hivyo!” Mzee Kisamo akasema huku wasiwasi ukiongezeka!

    “Haya, mimi naondoka!” Mzimu ule uklasema. Halafu ukatokomea na hali ikabaki kama ilivyokuwa mwanzo, na mzee Kisamo akabaki anashangaa!

    Baada ya kupata fahamu baada ya mzimu ule kuondoka, mzee Kisamo alikurupuka kutoka pale kwenye sofa, na kukimbilia chumbani, ambapo mke wake, Bi. Bernadeta alikuwepo. Akamshangaa baada ya kumwona akiingia kwa kasi mithili ya mtu aliyekuwa anakimbizwa!

    “Vipi mume wangu, mbona mbio?” Bi. Bernadeta akamuuliza!

    “Oh, makubwa! Mzee Kisamo akasema huku akitetemeka!

    “Imekuwaje?”

    “Hatari!”

    “Hatari ya nini?”

    “Mzimu wa Geofrey!”

    “Unasema kweli?”

    “Ni kweli mke wangu!”

    “Hebu nieleze vizuri…”

    “Nilikuwa nimejilaza pale kwenye sofa sebuleni, halafu kikajitokeza kitu cha ajabu, ambacho kilinijulisha kama mzimu…” mzee Kisamo akamueleza yote, halafu akamalizia. “Amenipa onyo kuwa tusithubutu kumrithisha deo mke wake, la sivyo tutamfuata kuzimu!”

    “Mungu wangu, sasa tufanyeje?”

    “Hakuna cha kufanya zaidi ya kuachana na mpango huo, tutakuja angamia bure!”

    “Na kweli, kama yametokea hayo, tuachane na mpango huo kabisa!”

    Wote wakakubaliana kuusitisha ule uamuzi, baada ya kutokewa na mzimu wa Geofrey. Ukweli ni kwamba uliwatia hofu kubwa kiasi kwamba walishindwa wafanye nini ili usiweze kuwatokea tena?



    *******

    DEO alikuwa amelala chumbani usiku ule. Mawazo mengi yalikuwa yakimwandama hadi usingizi ulipomchukua. Lakini katikati ya usiku ndipo aliposhtuka katikati ya usingizi, alipokuwa anaota ndoto ya kutisha. Wakati huo chumbani palikuwa na giza la kutisha ukizingatia taa ilikuwa imezimwa baada ya kulala, lakini ghafla mwanga ulienea ndani na kumfanya Deo azidi kuwa na wasiwasi!

    “Nini hicho?” Deo alijiuliza huku akinyanyuka kutoka pale kitandani na kukaa. Mwanga ukazidi kuongezeka, na alipotupa macho katika kona ya chumbani, ndipo alipomuona marehemu, kaka yake, Geofrey akiwa katika umbile la mzimu, amejifunika shuka nyeupe! Macho yake aliyakodoa kuelekea kwake! Hakika alitisha si mchezo!

    “Deo mdogo wangu!” mzimu ule ukasema kwa sauti kubwa yenye mwangwi!

    “Naam kaka!” Deo akaitikia huku akiwa na wasiwasi mwingi!

    “Naona umefurahi sana!” Mzimu uliendelea kumwambia!

    “Nimefurahi nini?”

    “Kwa kumrithi mke wangu!”

    “Mimi sijamrithi!”

    “Ndiyo, mmepanga hivyo!”

    “Siyo mimi…ni baba!”

    “Kwa hiyo ulipenda nife ili umchukue mke wangu Grace?”

    “Siyo hivyo kaka…” Deo aliendelea kusema na kuongeza. “Ni Ibilisi tu aliyenipitia, naomba unisamehe!”

    “Kama ni Ibilisi kweli alikuwa amekupitia baada ya kukushawishi, basi nakuomba usimuoae!”

    “Sawa kaka…nitafanya hivyo! Sitokubali kumrithi!”

    “Cha muhimu sasa, rudi Dar es Salaam haraka sana, ukaendelee na shughuli nyingine!

    Mzimu ule ulipomaliza kusema vile, ukatoweka pale chumbani na kumwacha Deo akishangaa! Akawa anafikicha macho yake na kujiuliza nini kilichokuwa kinaendelea? Mwili mzima ukawa unamtetemeka Deo, huku akiamua moja tu, kuwa ni lazima aondoke jijini Arusha haraka sana!

    Akiwa bado amekaa pale kitandani, mara mlango wa chumba chake ukagongwa, kitendo ambacho kilimfanya ashtuke sana!

    “Nani!” deo akauliza kwa sauti!

    “Ni mimi baba yako,” mzee Kisamo akamwambia kwa nje.

    “Oh!” deo akaguna, halafu akanyanyuka na kwenda kuufungua ule mlango.

    “Upo mwanangu?” Mzee Kisamo akamuuliza huku akimwangalia kana kwamba alikuwa anamkagua!

    “Nipo baba, kwani vipi?” Deo akamuuliza huku akimshangaa baba yake!

    “Ah, makubwa mwanangu!”

    “Imekuwaje baba?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mzimu wa kaka yako, Geofrey umenitokea jioni ya leo! Ni miujiza!”

    Unasema kweli baba?”

    “Ni kweli kabisa! Mzee Kisamo alisisitiza na kuendelea. “Hu8wezi kuamini, lakini ndivyo ilivyokuwa!”

    “Hata mimi sikupingi baba, kwani mzimu huo umenitokea muda siyo mrefu!”

    “Baada ya kukutokea ukaasemaje?”

    “Umenionya nisimrithi Grace!”

    “Basi, hata mimi baada ya kunitokea, umenionya hivyohivyo!”

    “Ni makubwa baba!”

    “Na kweli, inabidi tusitishe mpango wa kumrithi Grace, ni muhimu ujiandae urudi Dar ukaendelee na shughuli zako,” mzee Kisamo akamwambia Deo.

    “Nitafanya hivyo baba, kwani Mzimu umekasirika!”

    Baada ya majadiliano yale kati yam zee Kisamo na mwanawe, Deo, wakaufunga mjadala, ambapo mzee Kisamo alikwenda kulala. Deon aye akajilaza kitandani, lakini hakupata lepe la usingizi kutokana na tukio lile la kutisha kwa kutokewa na mzimu wa kaka yake, Geofrey, mtu aliyekuwa amekwisha kufa!



    *******

    ULIKUWA ni usiku wa patashika. Mzimu wa Geofrey ulicharuka na kuanza kutembea sehemu zote husika, katika kutoa ujumbe wake dhidi ya wote waliokuwa wakishikilia msimamo wao wa mila zilizopitwa na wakati, hasa kwa kurithiwa kwa mke wake, Grace. Hivyo baada ya kutoka nyumbani kwa mzee Kisamo, ulikwenda kwa akina Grace, katika mji wa mzee Ramson Laiser. Baada ya kufika, mzimu ule ukaingia ndani ya chumba alichokuwa analala Grace, na wakati huo alikuwa amelala usingizi wa mang’amung’amu kutokana na kuwaza sana matukio yale.

    Kama kawaida, mzimu ule ulisimama mbele ya kitanda chake, kama hatua tano hivi, na kubaki ukimkodolea macho makali. Mwanga mkali ukatokea mle chumbani na kufanya pawe peupe, kiasi cha kumfanya Grace ashtuke kutoka usigizini! Akauona mzimu wa Geofrey umemsimamia mbele yake!

    “Mamaa!” Grace alishituka sana baada ya kuuona mzima.

    “Grace mke wangu!” Mzimu ulimuita!

    “Bee!” Grace akaitikia huku akiwa amejawa hofu.

    “Ni mimi mzimu wa Geofrey, mumeo!”

    “Oh, Mungu wangu!”

    “Nimeamua kukujia katika hali hii ili nikupatie ujumbe muhimu!”

    “Oh! Oh!” Grace akliendelea kuweweseka!

    “Nitakuuliza swali moja!”

    “Ndiyo!”

    “Ina maana umefurahi sana baada ya mimi kufa?”

    “Hapana…sikufurahi…”

    “Kwa nini uliamua kuzaa na Deo, mdogo wangu?”

    “Ni Ibilisi tu kanipitia…”

    “Ndiyo mkaamua kurithiana?”

    “Hapana…”

    “Hapana nini?” Mzimu ukaendelea kumuuliza kwa ukali na kuongeza. “Sasa nakuonya, hakuna kuolewa na mdogo wangu deo. Ukipenda tafuta mwanaume mwingine, ukikaidi amri hii, nitawamaliza wote mnifuate kuzimu! Sijui unanipata?”

    “Nakupata…”

    “Haya…kwa heri!”

    Baada ya kutoa ujumbe ule, mzimu wa Geofrey ukatoweka pale chumbani, na hali ikabaki kama ilivyokuwa mwanzo, giza likatawala. Grace akapiga ukulele wa nguvu, ambao uliwaamsha mzee Ramson na Bi. Letisia, mama yake. Wote wakaamka na kwenda kugonga mlango wa chumba chake, ili kujua kilichomsibu binti yao. Ama kweli ulikuwa ni usiku wa aina yake!

    Haraka, Grace alinyanyuka haraka na kwenda kuufungua mlango, ambapo baada ya kuufungua, akakutana na mama yake pale mlangoni!”

    “Oh, mamaaa!” Grace akasma kwa woga huku akimkumbatia mama yake!

    “Vipi Grace?” Bi. Letisia akamuuliza.

    “Mama…oh!” Grace akasema bila kumalizia na kubaki analia.

    “Kitu gani mwanangu?” Mzee Ramson naye akamuuliza.

    “Ah, hali mbaya!”

    “Mbaya vipi? Mbona hueleweki?”

    “Amenitokea!”

    “Nani kakutokea?”

    “Geofrey!”

    “Unasema kweli au unaota?”

    “Ni kweli baba!”

    “Geofrey si amekufa?”

    “Basi amenitokea!”

    “Grace,” Bi. Letisia alisema. “Nafikiri wewe unaota kutokana na matukio haya!”

    “Sioti mama, ni kweli!”

    “Sasa baada ya kukutokea amesemaje?”

    “Amenipa onyo!”

    “Onyo gani?”

    “Amesema nisirithiwe na Deo!”

    “Na sisi hatutaki hilo balaa!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naogopa baba…”

    “Basi, usiogope…ni njozi tu, endelea kulala…”

    “Hapana…mimi silali peke yangu, kwani nimemwona kwa macho yangu!” Grace aliendelea kulalamika!

    Baada ya kusema vile, ikabidi Grace alale na mdogo wake, Matilda, halafu mzee Ramson na Bi. Letisia wakarudi chumbani mwao na kuanza kujadiliana kuhusu hali ile iliyomkuta Grace, hakika ilikuwa inatisha!

    “Baba Grace umeyaona?” Bi. Letisia akamuuliza.

    “Kweli nimeyaona…” mzee Ramson akasema.

    “Mtoto ameuona mzimu wa mumewe!”

    “Na kweli ameuona!”

    “Sasa tufanyeje?”

    “Ni muhimu kusitisha kabisa mpango huo ili tusije tukaangamia!”

    “Ni kweli kabisa!”

    Wote wakasitisha mpango wa kuwaozesha kwa nguvu!



    ****MWISHO*****



    NB: UNAKARIBISHWA KUTOA MAONI KUHUSU RIWAYA HII.

0 comments:

Post a Comment

Blog