Search This Blog

Friday, 3 June 2022

SURPRISE YA AIBU - 2

 





    Simulizi : Surprise Ya Aibu

    Sehemu Ya Pili (2)



    Nilipata fahamu ziku ya pili jioni wakati huo nilikuwa nimeishapatiwa matibabu ya hali ya juu ikiwa pamoja kupigwa bomba. Kabla ya kutoka polisi walifika kuchukua maelezo. Kwa vile sikuwajua vizuri ila nilikuwa nawafahamu nilitoa maelezo nao waliahidi kuwasaka mpaka kuwatia nguvuni.

    baada ya wiki mbili walifanikiwa kuwakamata baada ya kutega mtego seheme yenye tunayofanya biashara ya miili. Kitu cha ajabu baada ya kukamatwa wale wazungu waliandika maelezo na kuwekwa ndani kisha nikaelezwa nirudi siku ya pili.

    nilikwenda nyumbani na siku ya pili nilirudi polisi nikiwa na ushahidi wa shoga zangu waliokuwepo siku nilipochukuliwa. Kila kitu kilikuwepo ikiwemo taarifa ya daktari vilionesha kweli niliingiliwa na mbwa, kilichotakiwa kuwafikisha mahakamani na kufunguliwa mashtaka

    usitaajabu ya musa utayaona ya filauni, siku ile nilipofika kibao kikanigeukia mimi eti kumbe wale wazungu walikuwa na rb yangu alikuwa nayo aliyofungua muda mrefu ya kuwaibia dola laki moja na walikuwa wakinitafuta. Basi wanangu mimi ndiye niliye ingizwa hatiani na kufikishwa mahakamani mara moja na kufungwa mwaka mmoja baada ya kujitetea nina watoto wadogo. Hebu wanangu ona jinsi uonevu ulivyo fanywa juu yangu kwa vile nilikuwa mnyonge sina kitu.

    nilikubali matokea lakini moyoni nilijiapiza nitakapotoka kila aliyehusika hastahili kuishi duniani. Basi sikuwa na jinsi nilitumikia mwaka gerezani.

    nilipotoka nilianza msako wa kuwasaka wabaya wangu, wanangu nilimuua mmoja mmoja kila kukicha. Kwa wale wazungu niliua mpaka mlinzi na mbwa wao. Nilipomaliza kumuua mkuu wa polisi aliyeshiriki kubadilisha kesi yangu ndipo nilipotorokea mwanza.

    "uliwauaje wote hao bila kushikwa?" edna alijikaza na kumuuliza mama yake.

    "mnajua wale wazungu walikuwa ma x-part waliokuwa wakisimamia miradi mingi nchini na walikuwa wakilindwa na serikali. Kesi kama ile haikuwa kwangu tu kumbe mchezo ule tulifanyiwa wanawake wengi waliokuwa wakifanya biashara kama yangu.

    ilionesha mkuu wa polisi niliyemuua alikuwa akihongwa na kuwageuzia makosa wote waliokwenda kushtaki na kuwafanya wasichana wengi wakitendewa unyama kukaa kimya.

    baada ya kutoka gerezani nikiwa na hasira na wote walionitenda kuanzia mkuu wa polisi hakimu na hao wazungu ambao waliendelea na tabia za kutudhalilisha wanawake."

    "mama wakati unafungwa kina kaka walikuwa wapi?" edna aliuliza tena kwani kaka zake walikuwa wamepigwa na bumbuwazi na kuona kama aliyokuwa akiyasema mama yao ni hadithi ya ndotoni.

    "kuna shoga yangu mmoja aliwachukua na kukaa nao, bahati nzuri nilikuwa na fedha ya kutosha katika akaunti yangu hiyo niliamini hata ningefungwa miaka miwili ingeweza kuwasaidia. Basi baada ya kurudi nilitembelea sehemu zangu kuendeleza kazi yangu ya ukahaba kuendeleza kujipatia riziki baada ya akiba yangu kukuta imebakia kidogo kwa vile sikuwa na kazi nyingine niliamini kazi ile ndiyo mkombozi wangu.

    kwanza niliwauliza mahoga zangu kuhusu mchezo wa wale wazungu kuwafanyisha mapenzi na mbwa. Niliambiwa mzungu mmoja alifukuzwa nchini baada ya kesi kumkalia vibaya baada ya msichana mmoja kumpata mtu wa kumsimamia kwenye kesi yake na kulipwa fedha nyingi lakini na yeye kazi ya ukahaba ilikuwa kwenye damu hakuacha japo alipunguza na kuchagua wanaume wenye fedha kwani alikuwa akija kazini na gari lake.

    nilielezwa wakati narudi walikuwa wakiwachukua wanawake na kukubalia kufanya nao mapenzi wote watatu. Japokuwa wanasema ulitaka ule ushibe lakini ulikuwa ukitoka na fedha nzuri. Baada ya kuelezwa vile niliendelea kuwawinda kwa siri bila mashoga zangu kujua dhamilia yangu ni nini kwa washenzi wale nilitembea na dawa ya kulevya ya kupaka kwenye matiti ambayo huitumia kama unataka kumwibia mtu pia kisu nilichokificha kwenye mkoba wangu.

    nilifanya kazi kwa taadhari kubwa ili nisirudie kosa la awali, sikuwa tayari kwenda na mtu mwenye gari bali kufanya mapenzi ya papo kwa papo na kumalizana. Niliendelea na kazi yangu huku nikifanya mawindo ya watu wangu. Sikutaka kuanza na mkuu wa polisi na hakimu kwanza kwa vile nilijua wale ni watu wa kumalizia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    siku moja nikiwa lindoni mwangu lilikuja gari na kushangaa kuona mashoga zangu hawalikimbilii, nilijiuliza kuna nini. Nilipouliza niliambiwa:

    "shoga leo hatutaki wale wazungu wana mchezo mbaya, leo hawapati mtu tumewaambia kama kwenda na mmoja sawa lakini wote watatu hatutaki."

    kauli ile ilinifanya nichekelee moyoni, nilijisogeza mbele hadi kwenye lile gari waliponiona walinieleza kama nitakubali watu watatu sawa ilionesha wamenisahau.

    nilikubali kuwa nipo tayari, niliongozana hadi kwao, moyoni nilikuwa na dhamila mbaya kila nikikumbuka moyo unanitetemeke na kumuomba mungu anisamehe.

    tulipofika niliwaeleza nitafanya mapenzi na wote lakini kwanza na mmoja mmoja kisha baadaye nitafanya na wote kwa pamoja. Tena niliwaeleza kwanza nitafanya mapenzi kwa kila mmoja kuwa chumbani kwake. Bila kujua nimedhamilia nini walikubali. Basi nilianza kwa kuingia kwenye chumba cha mmoja na kuondoa nguo zote nikijifanya nimepandwa maruhani ya mapenzi.

    wakati wa kuandaana nilipaka dawa yangu kwenye matiti bila kujua kisha nilimwambia anyonye ili kunipandisha mdadi, bila kujua alifanya nilivyotaka. Haikuchukua muda alinyonya kisha nilimuona akilegea na kujilaza pembeni.

    nilichukua mto na kumziba pumzi usoni, sikuutoa mpaka alipotulia nikijua nimemaliza kazi kisha nilimlaza vizuri.

    nilijipaka dawa yangu tena kwenye nyonyo na kutoka bila kitu mwilini na kwenda chumba cha mzungu mwingine aliyekuwa akinisubiri kwa hamu sana.

    kama kawaida baada ya kupanda kitandani nilimuomba anyonye matiti na yeye alinyonya baada ya muda alilegea na kummaliza kama mwenzake.

    kumbe wakati nammalizia yule mzungu wa pili mzungu wa tatu sijui alishtukia vipi nilimuona akija huku akimwita mwenzake kwa sauti ya juu.



    Nilijipaka dawa yangu tena kwenye nyonyo na kutoka bila kitu mwilini na kwenda chumba cha mzungu mwingine aliyekuwa akinisubiri kwa hamu sana.

    Kama kawaida baadaya kupanda kitandani nilimuomba anyonye matiti na yeye alinyonya baada ya muda alilegea na kummaliza kama mwenzake.

    Kumbe wakati nammalizia yule mzungu wa pili mzungu wa tatu sijui alishtukia vipi nilimuona akija huku akimwita mwenzake kwa sauti ya juu.

    "Mr Rich kuwa makini Mr Rich kuwa makini."

    Kwa haraka niliteremka kitandani na kujificha nyuma ya mlango, aliingia na bastola mkononi akili yake ikiwa kwa mwenzake ambaye nilikuwa nimeisha msafirisha kuzimu. Nilijua nimekufa kwa vile sikuwa na ujanja wowote wakujiokoa kwa mzungu yule aliyekuwa na siraha mkono pili hatamwili wake kama angenikamata basi ningefia mkononi kwake.

    Nikiwa natetemeka mpaka haja ndogo ilinitoka baada ya kuona akimpima mwenzake mapigo ya moyo. Niliona ile ndiyo nafasi yangu ya kutoka mbio, nilikurupuka nyuma ya mlango na yeye alimuacha mwenzake nakunifuata. Kwa vile nilijua mlango umefungwa nilijitahidi kuufunga ule mlango ili nimfungie ndani. Wakati huo yule mzungu alikuwa akija mbio, nilifanikiwa kuufunga ule mlango na kumfanya ajigonge mlango nina kuanguka chini.

    Alianguka kwa kishindo, nilifunga mlango kwa komeo kwa nje kisha nilichungulia ndani na kumuona amelala chini damu zikimtoka kichwani. Nilikwenda mpaka jikoni na kufanikiwa kupata kisu kikubwa ambacho nilirudi nacho na kuufungua mlango wakati huo roho yadamu ilinijaa.

    Nilimfuata chini alipolala huku nikiwa na hasira niliteremsha mapigo mfululizo ya kifuani mpaka alipotulia. Nilinyanyuka na kujifuta damu kisha nilivaa nguo zangu. Nilianzakupekua kila kona na kufanikiwa kupata dola laki nne, nilizifunga vizuri kisha nilichukua bastola hadi kwenye banda la mbwa na kuwauambwa wote na kwenda kwenye moja la gari lao na kutoka nalo.

    Mlinzi alipoangalia ndani ya gari na kuniona mimi alishtuka nakunihoji:

    "Vipi mbona unatoka na gari?"

    "Siyo juu yakofungua geti," nilimjibu kwa sauti ya ukali.

    "Kazi yangu niulinzi nina haki ya kuuliza," mlinzi naye alikuwa mbishi.

    "Sikilizawe kidampa hebu fungua geti kabla sijakupoteza!" nilimtisha afungue mlango.

    "Siwezi mpaka nipate ruhusa ya mabosi wangu."

    Nilionakama ananichelesha nilichukua bastola iliyokuwa pembeni yangu nakumshuti. Niliteremka haraka na kwenda kufungua geti kisha nilirudikwenye gari na kuliondoa kwa kasi.

    Nilitembea huku moyo wangu ukiwa na hasira ya kunywa damu ya mtu.Nilikwenda na gari hadi mjini ambako nililiacha njiani na kuchukua teksi iliyonipeleka nyumbani.Kwa wasiwasi wa kukamatwa sikutoka ndani kwa siku tatu hukunikisikiliza taarifa kwenye vyombo vya habari ambavyovililipoti vifo vya wazungu watatu na mlinzi wao waliouawakinyama na mtu asiyejulikana.

    Nilitulia kwa muda wa mwezi mzimanikiwa mtu wa kujificha ikiwemo kuhama nilipokuwa nakaa na kuhamianje ya mji. Baada ya hali kutulia nilianza msako wa mkuu wa polisi nahakimu. Nilifuatilia nyendo zao na kujua kila mmoja anakunywawapi.

    Pia niliona kuwapata siyo kazi kutokana na tabia zao za unywaji na kupenda wanawake. Niliona nianze na hakimu kwa kujua polisi msako wake ni mkubwa kuliko wa hakimu. Hakimu alikuwa akikaamaeneo ya Mikocheni na alikuwa akipenda kunywa kwenye baa moja maarufu iliyopo Kinondoni.

    Niliamua kumfuatilia nyendo zake ambazo nilizielewa, siku moja nilimkuta kwenye baa hiyo akiwa amekaa pekeyake akinywa bia yake huku akichati na simu. Kwa vile nilikuwa nimevaa kiutata niliamini kila mwanaume alitamani kuwa na mimi.Nilisogelea meza yake na kumsalimia:

    "Habari za saizi?"

    Kablaya kuitikia alinyanyua uso na kunitazama kisha alishusha pumzi ndefuna kusema:

    "Ooh! Sorry, karibu mrembo."

    "Hapana nakusalimia," nililegeza sauti.

    "Ooh! Nzuri mrembokaribu."

    "Asante, vipi una mtu hapa?"

    "Nipo peke yangu karibu mtoto mzuri."

    Nilikaa na kujifanya natoa simu kwenye mkoba na kujifanya nasoma kitu kumbe ilikuwa kumlia pozi.

    "Mmh!Binti unatumia kinywaji gani? Aliniuliza baada ya uhudumu kuja kusimama mbele ya meza yetu.

    "Heinken."

    "Na ninimrembo?"

    "Kwanza hiyo inatosha kuanzia mi si mnywaji sana."

    Baada ya vinywaji kuletwa nilitulia na kunywa kistaarabu,kitu kilichomfanya hakimu kutaka kunijua zaidi.

    "We nimgeni?"

    "Si sana."

    "Mwenyeji wa wapi?"

    "Arusha."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ooh!Nimefurahi kuwa na wewe nina imani leo tutakuwa pamoja."

    "Mmh!Na mkeo?" nilijifanya kulia wivu.

    "Mke wangu nikirudi kwangu,sasa hivi mimi nipo na wewe mtoto mzuri."

    "Mmh! Kama hivyobasi wewe tu," nilijifanya kulegea.

    Baada ya chakula tulikubaliana kwenda nyumba ya wageni si kwa kulala kwa mapenzi yamuda mfupi kwa kisingizio nipo kwa baba yangu mdogo siruhusiwi kulalanje. Tulitoka pamoja kwenye gari lake na kuingia, nilipata wazo la haraka la kumuulia ndani ya gari ili kufuta ushahidi.

    Baada yakutoka eneo la baa niliacha gari liende mbele kidogo na kumuombaalisimamishe pembeni.

    "Kuna nini sweet?"

    "Nina hamumpenzi naomba uninyonye matiti kidogo uzipunguze."

    "Vumilia nitazishusha sasa hivi."

    "Hapana ninyonye," nilisema huku nikizitoa matiti yangu ambazo yalimbabaisha na kukubali kupaki garipembeni na kuanza kuyanyonya matiti yangu. Japokuwa alinipandisha mzuka lakini lengo langu lilikuwa roho yake.

    Aliendeleakulinyonya kwa ufundi mkubwa sana mpaka nikajikuta namaliza hajazangu bila kupenda, lakini lengo langu kwa siku ile halikuwa hilozaidi ya roho yake. Baada ya kunyonya kwa muda nilimuona akianzakulegea na kuliachia ziwa kisha alijilaza pembeni.

    Nilimtikisa nakugundua amelegea nilichukua mto ndogo ndani ya gari na kumziba naousoni kwa kumkandamiza kwa nguvu. Kwa vile hakuwa na nguvu hakuwezakunizuia nilimbana mpaka alipopoteza uhai nilimlaza pembeni nakuteremka zangu kwenye gari, nilifunga mlango na kuondokazangu.

    Nilitembea haraka mpaka mbele na kukodi bodaboda mpakaMagomeni ambako nilikodi teksi mpaka nyumbani. Nilitulia ndanisikilizia kwenye vyombo vya habari vitaripoti vipi kifo kile. Taarifaya asubuhi kwenye radio zote zilielezea Hakimu Kiondo alivyokutwaamekufa kwenye gari lake.

    Vyanzo vya habari vilisema alionekanaameongozana na mwanamke mmoja mrembo na kwenda kwenye gari lake nabaadaye gari lake kuonekana hatua chache na baa aliyokuwaakinywa.

    Polisi walisema wanamsaka mwanamke aliyetoka naye japoilikuwa vigumu kunigundua kwa vile hakuna hata mmoja aliyekuwaakinifahamu pia alikuwa mgeni maeneo yale. Baada kufanikisha kifo chaHakimu nilitulia kwa miezi mingine miwili kujipanga kwa ajili yakummaliza mkuu ya kituo ambaye wakati huo alikuwa OCD katika wilayamoja mkoani Morogoro.

    Mwanamke baada ya kujipanga nilifunga safarimpaka Morogoro na kupanga kwenye hoteli moja yenye hadhi mkoniMorogoro. Nilianza kumfuatilia OCD Mzizire kwa siku tatu nakugundua bado wana tabia zilezile za kunywa kwenye baa kubwa piakupenda watoto wazuri.

    Baada ya kujua baa anayokunywa nilikwendasiku moja kwenye ile baa na kutafuta siti ya karibu na alipokuwaamekaa na wapambe wake wakinywa. Nilimwita mhudumu.

    "Habaridada."

    "Nzuri, karibu."

    "Asante, samahani dadayangu."

    "Bila samahani."

    "Eti mzee Mzizire anakunywakinywaji gani?"

    "Serengeti."

    "Na wenzake?"

    "Kunaanayetumia ndovu, konyagi na Tusker."

    "Kila mmoja mpe tatutatumwambie mzee Mzizire ofa yangu kwake."

    "Sawa."

    "Shilingingapi?"

    "Usiwe na wasi nitakwambia baada ya kuhudumia, weweje, huagizi?"

    "Mi niletee Heinken moja."

    "Baridi,moto?"

    "Moto hali ya hapa ni baridi."

    "Dada barudi ipowapi wewe mgeni?"

    "Si sana."

    Yule msichana aliondoka nakunifanya niendelee kumtazama kwa uchu mzee Mzizire, kilanilipokumbuka alivyonifanyia moyo uliniuma na sikutaka kumsamehe hatakidogo, kwa tabia zake za kuwakandamiza wanawake na kuwatetea wazungu waliowafanya vibaya wanawake kwa kuwafanyisha mapenzi na mbwa namwisho wa siku wanafungwa wao bila kosa.

    Baada ya muda nilimuonayule mhudumu akiweka tlei la vinywaji kwenye meza. Nilimuonaakiuliza, mhudumu alinionesha mimi ambaye alimpokea kwa tabasamukali. Niliwaona wote wakinishuku kwa kushika vifuani vyao naminilijibu kwa kushika changu kuonesha nikubali.

    Alipotoka palealiniletea heinken yangu na kunifungulia na kutaka kuniwekea kwenyeglasi, nilimkataza na kujiwekea mwenyewe na kupiga funda moja nakutulia. Nilifanya kuangalia chini ili niwape nafasi ya kuusanifuuzuri wangu ambao ulinifanya nijiamini muda wote.

    Siku zote huwanaamini wakubwa ndiyo wanapenda kujipendelea kizuri lazima wakitakewao. Baada ya muda yule dada alikuja na bei nne na kutaka kuziwekajuu ya meza yangu.

    "Vipi dada?" nilimuuliza.

    "Mzeeamesema nikuhudumia nikupe chochote unachokitaka."

    "Mwambieasante, leo sijisikii kunywa sana, sina uhakika hata kama bia hiimoja nitamaliza."

    "Dada si ungechukua hata kama hunywi ungenipa mimi mdogo wako."

    "Usiwe na wasiwasi we rudisha nitakupa elfu kumi ya matumizi unasemaje?"

    "Duh! Dada yanguutaokoa maana leo hali ni mbaya."

    Nilifungua mkoba wangu nakuchukua noti ya elfu kumi na kumpa.

    "Hii ya nini?"

    "Yako."

    "Nabili?"

    "Hujaniambia kiasi gani pia hujawaongezea bianyingine."

    "Kwa hiyo niwaambiaje kuhusu bia hizi?"

    "Mwambiekama nilivyokwambia kuwa sijisikii kunywa bia leo, labda keshonitaungana nao."

    "Haya dada, asante sana."

    Yule mhudumu aliondoka na kuniacha nikiibembeleza bia yangu ambayo niliiweka kuzugia tu kwa siku ile sikuwa mnywaji kabisa zaidi yakumtamani Mr Mzizire kama Simba mwenye njaa aliyemuona Swali akinywamaji pembeni yake.

    Baada ya muda yule mhudumu alinifuata nakuniletea kimemo toka kwa Mr Mzizire.

    Sorry mrembo tunaweza kuwapamoja leo?

    Baada ya kukisoma nilitabasamu kumfanya aliyeleta ujumbe ambaye nilijua alikuwa akinifuatilia kujua nitaupokeaje.Tabasamu langu lilikuwa la kwanza kumpa matumaini.

    Baada ya kusomanilimuomba kalamu mhudumu na kunipa na kugeuza kalatasi kwa nyuma nakuandika.

    Kwa leo au kwa siku zote?

    Nilimpa mhudumu aliyempelekea baada ya kusoma naye aliandika kikalatasikingine.

    Nimekupenda sana nina imani itakuwa sikuzote.

    Nilipoletewa nilisoma na kumjibu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sawa, lakini sipendi kuchezewa na wanaume! Nilijifanya kutoa onyo.

    Mhudumu alichukua ujumbe ule na kumpelekea baada ya kuusoma alijibu:

    Nimekuelewa,naomba tuzungumze faragha.

    Baada ya kuletewa niliusoma nakumjibu:

    Hakuna tatizo.

    Baada ya kupelekewa jibu langu, niliona akijadiliana na mpambe wake baada ya muda nilimuona yule mpambe akijanilipokuwa nimekaa na kuniinamia.

    "Samahani naombaunifuate."

    "Sawa ngoja nilipe kwanza."

    "Hapana mzeeatalipa."

    "Hapana, vinywaji hivi nimeagiza mimi."

    Baadaya kulipa nilitoka na yule mpambe aliyenipeleka mpaka kwenye hoteli moja iliyokuwa nje kidogo ya mji. Moyo wangu ulijawa furaha baada yakuona mtego wangu umenasa kirahisi tofauti na nilivyofikiria. Jamaa baada ya kunifikisha chumbani aliniacha na kuondoka.

    Baadaya kuondoka nilibakia chumbani peke yangu nikiwa katika wakati mgumuwa kutimiza nilicho dhamilia. Wasiwasi wangu ulikuwa kujulikana mimindiye muuaji hivyo kunifanya nishikwe mara moja na kukamatwa kablasijafika mbali.

    Nilijikuta nikiingiwa wasiwasi kuhusiana nampango wangu kwa vile kama ningemuua basi ningekatatwa mara moja.Wazo la kumuua siku ile sikutaka kulitekeleza kwa vile mazingirayalikuwa tata kwa kujua wapambe wake hawakuwa mbali niliaminibaada ya kuonekana natoka lazima watamfuatilia na wakimkuta amekufamsako wake ungekuwa mkubwa na mimi nisingefika mbali lazima wangenikamata.

    Siku zote niliamini mpango mzuri ni katiyangu na adui yangu asiwepo wa tatu mwenye kujua mpango ule ambayeanaweza kuwa shahidi wa kuweza kunitia hatiani. Nilikubali siku ilenifanye mapenzi tu bila kuingiza kitu chochote huku nikiapakujituma ili kumfanya aombe tukutane siku nyingine.

    Nikiwa katikaya mawazo mkuu wa polisi wa wilaya OCD mzee Mzizire aliingia na kujamoja kwa moja nilipokuwa nimejilaza kwenye kochi.

    "Niambiempenzi wangu?"

    "Mmh! Nakusikiliza wewe."

    "Mimi ninalozaidi ya kuhitaji mapenzi yako."

    "Lakini kweli unanipenda au unanitamani?" nilijifanya kujibalaguza huku nimelegeza macho nasauti.

    "Siyo siri mrembo, sijawahi kumpenda mtu kwa haraka hivikama nilivyokupenda wewe."

    "Muongo! Unanidanganya unatakakunichelea tu leo kisha uniache," nilijifanya kudeka.

    "Kwelikabisa nakupenda kwa dhati wala si kukuchezea."

    "Kweli?"

    "Kwelikabisa, unataka nikufanyie kitu gani uamini nakupenda?"

    "Unipende tu wala sitaki kitu kingine."

    "Wewe ni mgenihapa?"

    "Ndiyo."

    "Unatokea wapi?"

    "Arusha."

    "Ooh! Vizuri na hapa Morogoro umefikia wapi?"

    "Nipokatika mapumziko tu."

    "Unafanyakazi?"

    "Ndiyo."

    "Ipi?"

    "Kwenye kampuni yautalii."

    "Upo likizo?"

    "Ndiyo, leo ni siku ya tano, ila kesho nitakuwa Dar ambako nitakaa siku mbili na kwenda Zanzibar kidogo kisha nitaenda Mwanza na kurudi Arusha, kidogo nitakuwanimeosha macho."

    "Duh! Inaonekama utalii imekukaa sana."

    "Upondani ya damu yangu."

    "Kwa nini usimalize likizo yako hapa ilituwe pamoja, nitakupangia kwenye hoteli hii kwa muda wote utaokuwahapa."

    "Asante, kwa vile nimeishapanga ratiba zangu,nitakutafutia nafasi yako hata ya kusema uongo kazini kuwa nauguliwahivyo nitakuja unifiche unifaidi."

    "Basi ondoka keshokutwa."

    "Hapana naomba kesho uniache niondoke, naweza kuachakwenda Mwanza nikarudi kwako niache niende Dar na Zanzibar."

    "Mmh!Sawa."

    Baada ya kukubaliana tuliondoana nguo zetu kwa kupeana msaada kisha tulikwenda kuoga na kurudi kitandani ambako nilimpa rahakamili zilizomfanganya mzee wa watu. Kwa vile nilikuwa mzoefu wakukutana na wanaume pia nilijua kuitaka hela ya mwanaume ambayealikuwa akiitoa bila kusita hata tuliyokubaliana lazima uiongeze kwapenzi ninalompa.

    "Mpenzi kwa nini kesho usihahirishe safariyako, kwa penzi unalonipa sijawahi kupewa sema unataka nikupe niniili usiondoke."

    Nilitaka kumwambia naitaka roho yake, lakini ilibakia siri yangu ambayo niliijua mimi na Mungu wangu. Niliendelea kumpa vitu vipya mtoto wa kike huku nikikataa kila alichotaka kunipakujifanya sina tamaa kumbe naitaka roho yake.

    "Mpenzi sihitajichochote bali penzi lako."

    "Penzi umepata, nakuahidi kukujengea nyumba na kukununulia gari hata kesho."

    "Nimekuelewampenzi wangu ila nina ombi moja kwako."

    "Ombi gani mpenziwangu?"

    "Kwa vile kesho nitakuwa Dar, naomba uje hata jionituwe pamoja, nimefurahia penzi lako naomba niwe nyumba yako ndogo,"nilizidi kumtia ujinga.

    "Umeipata hata ukitaka nimfukuze mkewangu nipo radhi."

    "Hapana mkeo usimfukuze bali mimi niporadhi kuwa nyumba ndogo lakini naomba uniheshimu tu."

    "Nakuhahidikukuheshimu zaidi ya heshima hata ukitaka nikupikie nakukufulia."

    "Hapana sivyo hivyo nataka utambue mimi kuanzialeo ni mpenzi wako."

    "Jamani Bebi au nipige kelele kuoneshanimekubali."

    "Basi nimekuelewa lakini hajajibu ombilangu."

    "Lipi bebi?"

    "La mimi na wewe kuwa keshoDar."

    "Kumbe hilo, usiwe na wasi nakuahidi mpaka saa kumi nambili jioni nitakuwa Dar, unataka tuwe hoteli gani?"

    "SeaCliff."

    "Hakuna tatizo mpenzi wangu."

    "Nimefurahikusikia hivyo, naomba fedha ya hoteli nilipe mimi."

    "Naombampenzi wangu nilipe mimi."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikutaka kulazimisha nilimkubalia nakunieleza asubuhi kabla ya mimi kuondoka atakodi yeye chumba ilinikifika nifikie kwenye hicho chumba.

    Siku ile tulilala mpaka sikuya pili alfajiri aliponiaga anakwenda nyumbani kuvaa sare ya kazi iliaingie kazini na saa tisa alasiri ataondoka Moro kuja Dar.

    Kablaya kuondoka alibuku chumba Sea Cliff hoteli na kuniuliza aandike jinala nani.

    Ili kupoteza ushahidi nilimwambia aandike jina lake,baada ya kupata chumba namba 215 kwa jina Kaka Mkubwa aliondoka nakuniacha nimejilaza kitandani ili kujiandaa kurudi Dar hukunikifurahia mpango wangu umekwenda vizuri. Nilitamani kupiga vigelegele vya furaha. Moyo mwingine uliingia huruma kumuua mzee kama yule aliyekuwa na familia nilijikuta kwenye wakati mgumu wa maamuziyangu.

    Niliondoka Morogoro na basi majira ya saa moja kasoro asubuhi na kufika Dar saa tatu na kukodi teksi hadi kwangu.Nilipofika nilijipumzisha kwa kuoga na kujilaza, majira ya saa kumina mbili niliamka na kuoga ili kujiandaa kwenda Sea Cliff hoteli kumsubiri mtu wangu ili nimalize kazi ilibaki ili kufanya mambomengine.

    Baada ya kujiandaa na kuchukua vifaa vyangu vya kazinilikodi teksi hadi Sea Cliff , nilifika majira ya saa moja nanusu tofauti na muda tuliokubaliana wa saa kumi na mbilikasoro. Kwa vile mzee Mzizire alikuwa ameisha chukua chumban ili kwenda moja kwa moja mapokezi na kuomba funguo, nilimkuta dadammoja mrembo.

    "Habari dada?"

    "Nzuri, karibu."

    "Asante,naomba ufunguo wa chumba namba 215."

    Yule msichana alipekuakitabu na kuniuliza.

    "Samahani dada mbona chumba hiki kimechukuliwa na mtu anayeitwa Kaka Mkubwa?"

    "Ndiye mpenzi wangu, chumba hiki tumechukua kwa kubuku kwa simu alfajiri yaleo."

    "Ooh! Mpenzi ndo unafika," sauti nyuma ilinishtua ilikuwa ya mzee Mzizire.

    Niligeuka mzimamzima na kwenda kujitupa kifuani kwake, kwa usanii niliokuwa natumia hata ungekuwa na moyomgumu kiasi gani angekubali nampenda sana.

    Kwangu hakikuwa kitukigeni kwa vile ile ndiyo kazi yangu iliyokuwa ikinipatia kipato,hivyo nilikuwa najua jinsi na kumpumbaza mwanaume na kuamini nampenda kumbe nina yangu.

    "Waaawooo mpenzi," nilijifanyakuchanganyikiwa.

    "Waaawoo."

    "Yaani ndo nafika na kukutanana maswali kama polisi," nilijifanya kudeka.

    "Jamani dada yangu sasa ningetoa chumba bila kuwa na uhakika?" msichana wa mapokezi alijitetea.

    "Basi mpenzi, vipi umefika zamani?"

    "Kama ningefika zamani si ningeumbuka."

    "Basi yameisha, tunaomba ufunguo," mzee Mzizire alisema.

    Tulipewa ufunguo na kuelekea kwenye vyumba tukiwa tumekumbatiana mtoto wa kike nilideka kuoneshanimemmisi sana. Tulikwenda mpaka chumbani na kujilaza kitandani kablaya kwenda kuoga. Wakati mwenzangu akiwaza mapenzi mimi nilikuwa naitamani roho yake ambayo niliamini sehemu ile ilikuwa nzuri sanaisiyo na ushahidi.

    Tulipotoka kuoga sikuhitaji auchezee mwili wangu tena kwa vile pale nilikuwa na kazi moja naye. Baada ya kutokakuoga nilipaka dawa yangu kwenye matiti na kumuomba anyonye.

    "Mpenzi..mpenzi naomba uninyonye matiti nisikie raha."



    Tulipewa ufunguo na kuelekea kwenye vyumba tukiwa tumekumbatiana mtoto wa kike nilideka kuonesha nimemmisi sana. Tulikwenda mpaka chumbani na kujilaza kitandani kabla ya kwenda kuoga. Wakati mwenzangu akiwaza mapenzi mimi nilikuwa naitamani roho yake ambayo niliamini sehemu ile ilikuwa nzuri sana isiyo na ushahidi.

    Tulipotoka kuoga sikuhitaji auchezee mwili wangu tena kwa vile pale nilikuwa na kazi moja naye. Baada ya kutoka kuoga nilipaka dawa yangu kwenye matiti na kumuomba anyonye.

    "Mpenzi..mpenzi naomba uninyonye matiti nisikie raha."





    Mzee wa watu zikiwa zimempanda alivamia nyonyo zangu na kunyonya kama mtoto aliyelikosa ziwa la mama yake toka asubuhi. Kutokana na kuipaka dawa nyingi hakuchukua muda mzee mzima alilegea. Kama kawaida nilichukua mto na kumziba pumzi sikumuacha mpaka alipotulia.

    Baada ya kupata uhakika nimemaliza kazi nilinyanyuka na kuvaa nguo zangu na kutoka. Niliuacha ufunguo kwa ndani kwa kuamini hakuna mtu wa kuingia kwa siku ile mpaka siku ya pili. Nilitoka na kutembea kwa haraka kuelekea barabara ya Salenda Bridge.

    Kwa vile ilikuwa giza hakuna aliyeniona, ilipita teksi niliyoipiga mkono baada ya kusimama nilikwenda nayo mpaka Kinondoni kwa Manyanya na kuchukua nyingine mpaka nyumbani.

    Kama kawaida yangu baada ya tukio nilikaa ndani kusikilizia nini kitaendelea, mpaka kunakucha hakukuwa na taarifa yoyote kutoka katika vyombo vya habari kuhusiana na niliyoyafanya. Niliamini mwili wa mzee Mzizire utagundulika siku ya pili kwa mfanya usafi atakapoingia ndani.

    Asubuhi ilikuwa tulivu hakukuwa na taarifa yoyote muda mwingi niliutumia kuangalia na kusikiliza taarifa za habari ya kwenye redio na tivii. Majira ya saa sita vyombo vya habari vya redio na tivii vilitoa taarifa iliyoitwa ya kushtusha pale waliposema mwili wa mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro Bwana Mzizire umekutwa umekufa kwenye hoteli ya Sea Cliff katika chumba namba 215 ukiwa umekufa.

    Taarifa iliendelea kusema kwa mujibu wa maelezo ya mhudumu wa hoteli ile aliyekuwa zamu alisema majira ya saa moja na nusu waliingia marehemu na mwanamke mmoja aliyeonekana ni mpenzi wake. Lakini majira ya saa nne asubuhi siku ya pili wakati wa kufanya usafi ndipo ilipogundulika hali ile iliyowashtua na kutoa taarifa polisi.

    Baada ya maelezo msichana wa mapokezi aliyeionekana kuchanganyikiwa alifuata mkuu wa upelelezi wa mkoa kusema kuwa watafanya uchunguzi wa kifo kile ikiwa pamoja na kumtafuta mwanamke yule aliyefanya mauaji yale.

    Moyoni nilifurahia kusikia wabaya wangu wote nimewamaliza.

    Niliamini muda ule ulikuwa muafaka kuondoka jijini Dar na kwenda kuishi mkoa wowote. Sikutaka kurudi Arusha niliamua kwenda mbele kwa mbele. Wazo la haraka lilikuwa kwenda kujificha mkoani Mwanza jiji ambalo lilikuwa limechangamka hata mtu kukutilia mashaka ni vigumu tofauti na mikoa mingine ukiingia mgeni unajulikana haraka.

    Sikutaka kukurupuka kwa siku zile nilitulia kwa wiki huku nikifanya mambo yangu ikiwa pamoja na kuwakabidhi wanangu kwa shoga yangu ambaye nilimuachia kiasi kikubwa cha fedha cha kuwatunza. Baada ya kila kitu kwenda vizuri niliondoka bila kumjulisha nakwenda wapi ila nilimweleza nitamjulisha baada ya kufika ninapokwenda.

    Niliondoka na ndege ya jioni na kufika Mwanza saa mbili usiku, kwa vile nilikuwa mgeni nilimuomba dereva anipeleke kwenye hoteli nzuri iliyo nje kidogo ya mji. Kama jiji Dar basi iwe maeneo ya Temeke siyo Mbagala au Kibamba.

    "Dada wewe mgeni?" dereva aliniuliza.

    "Kaka nimekueleza nitafutie hoteli maswali ya nini?" sikupenda maswali yake.

    "Lazima nikuulize ili nijue hoteli gani inakufaa."

    "Yoyote nzuri lakini isiwe nje kidogo ya mji."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwani Mwanza hujawahi kufika?"

    "Zamani sana, baba yangu aliondoka nina miaka kumi," nilimdanganya.

    "Mmh! Zamani sana, ulikuwa unakaa wapi?"

    Mmh! Lile kidogo lilikuwa gumu kidogo na kunifanya ninyamaze kidogo kukumbuka maeneo ya jiji la Mwanza. Baadhi ya maeneo niliyakumbuka nilipokuwa Dar niliwahi kuzisikia kama Igoma, Ilemela kwenye kituo cha Redio free Afrika na Star tv, Mabatini na Isamilo. Nilitafuta jina moja na kulitamka.

    "Tulikuwa tunakaa Isamilo."

    "Mmh! Inaonekana mlikuwa nayo!"

    "Baba yangu alikuwa mkuu wa polisi."

    "Ndiyo maana, vipi umekuja kibiashara?"

    "Kaka yangu mbona maswali kama natafuta pasipoti?"

    "Basi dada, nitakupeleka kwenye hoteli nzuri pia nitakuipa namba yangu ukiwa na shida nijulishe."

    "Hakuna tatizo," nilimjibu kwa mkato kwa vile nilikuwa tayari nimechoka na maswali yake kama mpelelezi.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog