Search This Blog

Friday, 3 June 2022

SURPRISE YA AIBU - 3

 







    Simulizi : Surprise Ya Aibu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Kwa vile ulikuwa usiku hata mandhari ya mji wa Mwanza kutoka Uwanja wa ndege sikuiona japokuwa ilionesha jiji la Mwanza lilikuwa limejengeka sana. Baada ya muda alisimamisha gari mbele ya hoteli moja iliyokuwa na gharofa tatu lakini ilikuwa ipo katika hali nzuri na kunifanya nipapende hata kabla ya kukaa.

    Niliingia na kukodi chumba kisha nilimlipa hela yake na asante nilimuongezea elfu ishirini. Alinishukuru na kuniachia namba yake ya simu ili niwapo na shida nimjulishe. Niliagana naye na kuingia ndani ya chumba changu kilichokuwa kwenye hali nzuri kilichokuwa ghorofa ya kwanza na kujilaza kwanza kabla ya kuoga na kutafuta chakula.

    Baada ya kula niliagiza pombe kali na kunywa nusu chupa, nilijikuta nililewa na kupitiwa usingizi bila kujua mpaka siku ya pili. Kwa vile nilikuwa mgeni siku hiyo nilishinda ndani nikiangalia picha kwenye tivii.

    Jioni nilitoka na kukaa sehemu ya bar iliyokuwa palepale kwenye ile hoteli ambayo ilikuwa na watu wengi majira ya kuanzia jioni. Nilikaa nje mpaka saa nne usiku niliporudi ndani kulala.

    Katika hoteli ile ilikuwa na wapanaji wengi mmoja wapo dada mmoja wa kizungu ambaye alitokea kunizoea haraka. Muda mwingi nilikuwa naye kitu kilichofanya tuwe mtu na shogaye.

    Japokuwa alikuwa mzungu alikuwa amechangamka sana kama mswahili, akikueleza kazaliwa Tanzania tena uswahilini ungekubali kutokana na kuyajua mambo kiswahili na lugha ya kiswahili aliizungumza vizuri sana.

    Kwa kweli kupata rafiki yule ambaye alinipunguzia upeke, kila jioni alinipeleka kumbi za starehe kama Delux, Kapili Kabana na kumbi nyingi za jiji la Mwanza ambazo nazo zilikuwa zimekucha.

    Kama ujuavyo Mungu alivyonipendelea kila kona wanaume walinitolea macho, kila mmoja alitangaza dau nene ili kunikamata. Wengi walipitia kwa shoga yangu Carloliner. Japokuwa nami niyatamani maisha ya kujimwaga na kumpata mtu wa kunikata kiu yangu ya mapenzi.

    Lakini sikuwa tayari kujiingiza kwenye shimo jingine la kifo baada kuponea tundu la sindano. Nilitamani maisha ya utulivu kwa muda mrefu ili kujipanga kimaisha ikiwezekana niichukue familia yangu niishi mwanza baada ya kuufurahia mji huu ambao ulikuwa na pilikapilika kama Dar.

    Ili kujiweka mbali na wanaume, waliomtuma Callo niliwadanganya kuwa mimi ni mke wa mtu nipo pale kwa ajili ya kumsubiri mume wangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wapo walioomba kufanya mapenzi na mimi hata kwa dakika moja ili wanihonge milioni. Nilijua nikikubali dakika hiyohiyo moja inaweza kunipeleka kaburini.

    Pia ilionesha wanaume wengi walinitamani ili kutaka kujua ndani ya mwili wangu kuna nini kimefichwa kwenye umbile lenye utata.

    Baada ya mwezi Callo aliondoka na kuniaga kuwa anasafiri kidogo na kuniacha peke yangu lakini baadhi ya wafanyakazi wa hoteli ile tayari nilikuwa nimeisha jenga nao urafiki kwa kuwatembelea maeneo waliokuwa wakikaa.

    Wengine walikuwa wakikaa Igogo, Igoma Nyakato, Mabatini, Mkuyuni na Pasiansi. Kwa kweli nilijikuta nikifurahia maisha ya Mwanza na kusahau ya Dar japokuwa moyo uliniuma kukaa mbali na familia yangu.

    Nilijikuta nikipata wazo la haraka kwa nini nisiwasiliane na shoga yangu aniletee wanangu Mwanza ili niweze kuyaanza maisha mapya.

    Lakini siku zote bandubandu humaliza gogo ndani ya miezi tisa niliyokaa Mwanza pesa ilianza kunikatikia kutokana na matumizi bila mahesabu.

    Hapo ndipo nilipojikuta wenye wakati mgumu wa kushindwa nianzie wapi maisha kutokana kutokuwa na mradi wowote. Lakini bahati nzuri wakati huo rafiki yangu Callo alikuwa amerudi akiwa na pesa nyingi sana.

    Alinieleza nisiwe na wasi atanisaidia, kwa kweli Callo alinisaidia vitu vingi ikiwepo kunipa pesa za matumizi na kunilipia pesa ya hotel kwa miezi miwili zaidi.

    Nilimshukuru sana lakini siku zote Callo sikujua kazi zake japokuwa mawazo yangu huenda ni mfanyakazi wa mashirika ya kujitolea kusaidia umaskini Afrika.

    ********

    Nakumbuka siku moja ambayo kulikuwa na sherehe ambayo tulikunywa sana, japokuwa nakumbuka sikunywa kinywaji kikali sana kutokana na kutokuwa na mzoefu na maeneo yale.

    Siku ya pili nilipoamka nilijikuta nipo sehemu ambayo ilikuwa siijui, lakini ilionesha ni nyumba ya wageni. Nilipoangalia pembeni yangu nilishangaa kumuona mwanaume amelala usingizi mzito akikoroma.

    Nikiwa bado nimo kwenye shuka ya hotel ile iliyokuwa na jina la Aspen. Moyo ulinilipuka baada ya kuona kondomu zaidi ya tatu zilizokuwa zimetumika. Nilijikuta nikinyanyuka kitandani huku nikiitupa shuka pembeni.

    Sikuamini kujikuta nikiwa mtupu bila nguo yoyote, moyo uliniuma na kujiuliza pale nimefikaje. Nilichukua nguo zangu haraka na kuzivaa ili niondoke.

    Kabla ya kumaliza kuvaa sauti ya yule mwanaume ilinishtua:

    "Mrembo mbona haraka subiri haki yako."

    "Pumbavu unikome," nilimtukana huku nikimalizia kuvaa nguo zangu.

    "Sikiliza mrembo umbile na kauli yako ni vitu tofauti, japokuwa pesa niliishampa Zungu lakini mahaba yako motomoto lazima nikuongezee ya asante."

    Kauli ile ilinifanya nisite kuvaa nguo na kushtuka huku nikiweka mkono mdomoni kwa mshangao. Kauli ile ilionyesha jinsi gani Callo alivyo nifanyia biashara bila mwenyewe kujua. Wakati huo yule bwana alikuwa ameisha amka na kutoa pesa mfukoni na kunihesabia wekundu watano.

    Kutokana na hasira nilimpiga nazo usoni pesa zake na kutoka kwa hasira huku nikimalizia kuvaa vizuri nje ya chumba kwenye korido. Japokuwa sikuwa na pesa muda ule ambao ulikuwa ni saa moja asubuhi, sikuwa na haja ya gari nilitembea kwa miguu huku nikiapa Callo atanitambua kwa kitendo alichonifanyia.

    Nilijiuliza kwa nini hakunishirikisha akajua nitasemaje na mimi. Nilipofika hotelini nilikwenda moja kwa moja chumba cha Callo sikumkuta.

    Wafanyakazi wa hotelini walinieleza kuwa tangu tulipotoka pamoja jana yake hajarudi. Nilikwenda kuoga huku nikimsubiri kwa hamu kubwa.

    Baada ya kupata supu ya nguvu nilijilaza kitandani kutokana na uchovu usingizi haukuchelewa kunichukua.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mkono wa mtu kunitikisa begani ulinifanya nifumbue macho. Hakuwa mwingine zaidi ya Callo.

    "Vipi Shosti mbona umelala umerudi saa ngapi?" aliniuliza huku akitabasamu bila kujua ameniudhi sana.

    Nijikuta nikijaa kifua na kushindwa nimjibu nini, nilimpandisha na kumshusha nisipate jibu.

    "Sikiliza Suzy kwa vile wewe ni rafiki yangu kipato cha jana sichukui hata senti tano, hela zako hizi hapa."

    Callo alisema huku akihesabu elfu 50 na kunikabidhi. kabla ya kuzipokea nilimuuliza.

    "Za nini?"

    "Suzy kutokana na kazi ya jana, kwenye pati kuna mtu alijipendekeza nami sikuwa na jinsi kwa vile najua hata shemeji akirudi haipungui utamu hiyo."

    Mmh! Maneno ya Callo yalinikata makali nilimuangalia nisimmalize, kwa sauti ya chini nilimuuliza:

    "Callo kwa nini usiniambie mapema ili nami nikajindaa?"

    "Suzy japokuwa sasa hivi mambo yako si mazuri lakini umekuwa mtu mwenye msimamo. Kwa vile hata mimi kazi inayoniweka mjini ni hii, ndiyo maana nimeamua kukushirikisha ili mambo yako yakiwa mazuri utajua jinsi ya kujipanga huenda mumeo ameingia mitini.

    Huyo mwanaume gani asiyejua mkewe mwaka sasa unakatika haonekani wala kukutumia pesa za matumizi yeye anajua unakula mawe?"

    "Sawa, lakini ulitakiwa kunijulisha mapema."

    "Lazima ungekataa," alizungumza huku akinikabidhi elfu 50 ambazo sikuwa na jinsi ya kuzipokea na kujilaumi kuzikataa zile elfu 50 zingine nilizopewa hotelini asubuhi.

    "Suzy kwa sura na umbile lako ndani ya mwaka utajenga nyumba na kupata usafiri wa kutembelea. Mimi napata pesa kwa uzoefu tu, lakini ningekuwa kama wewe mbona ningenunua hata ndege," Callo alinimwagia sifa.

    Bila kutegemea nilijikuta nikirudi kulekule nilipotoka kazi ya uchangudoa. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuifanya ili kujikomboa maana mambo yalivyokuwa yakielekea yalinitisha nisijue hatma yangu.

    Niliingia kilingeni rasmi na changudoa mzoefu Callo ambaye alinipa mbinu za kimataifa ambazo yeye ilizitumia kufanya mapenzi na wanaume wengi bila kuchoka. Ikiwa pamoja na kutumia madawa ya kuongeza nguvu ili kukabiliana na wanaume wengi.

    Kwa kweli kazi yangu haikuwa ngumu kutokana na kupata wateja kwenye hoteli zote kubwa za jiji la Mwanza. Kutokana na upendeleo niliopewa na Mungu na maelekezo ya kuifanya kazi ile kimataifa, niliweza kutengeneza pesa kama sina akili nzuri.

    Kazi ile ya ukahaba ilikuwa inatofauti kubwa na ile tuliyokuwa tukiifanya Dar. Hatukuwa tukienda kujiuza barabarani na kujinadi uchi kama mnadani. Kule ilikuwa ni kujipamba na kuingia hotel kubwa na kutafuta meza ya pembeni huku ukiagiza kinywaji cha bei kubwa kwani hata mwanaume itakaye jigonga kwako lazima atakujua wewe ni mtu wa matawi ya juu.

    Hata akikutaka dau lake lazima litakuwa la juu tu. Sio unaingia hotelini unaagiza soda moja na kuinywa zaidi ya masaa zaidi ya matatu au matano.

    Hata mwanaume ukiwa pembeni akikufuatilia atakujua wewe mtu wa hadhi ya chini. Siku zote ukitaka kukamata samaki mkubwa lazima uweke chambo mkubwa ama sio utaendelea kukamata vidagaa vya maji mafupi.

    Na dau lake sanasana atakupa elfu kumi akizidi sana kumi na tano au ukopwe kabisa. Ukitaka faida ya biashara yako lazima uingie gharama ya matangazo. Wahindi wanasema weka mingi upate mingi, siku nyingine naweza kutumia hata elfu 30 na ukatoka kapa.

    Lakini mambo yakiwa mazuri mpaka asubuhi unaweza kutoka na laki mbili mpaka tatu kama siku kijiwe kimekubali, lakini pesa ya chini ilikuwa elfu hamsini.

    Tulikuwa tukipata pesa nyingi, kazi tulikuwa tukiifanya mara tatu kwa wiki jumatano jumamosi na jumapili siku nyingine tulikuwa tukipumzika.

    Nilijikuta nikiyafurahia maisha ya Mwanza ambayo nilitengeneza pesa ambazo baada ya mwezi nilikuwa nimeisha fungua akanti mpya na kuweza kuweka milioni moja na laki tano ambazo zilikuwa hazina kazi kwa muda ule. Niliweza kusafiri miji mbalimbali kama Machimboni ambako kwa kweli tulitengeneza pesa sana. Kule watu walitoa pesa bila kuifikiria, kwa kweli Machimboni nilikuwa nikitembea na wanaume zaidi ya saba kwa siku.

    Mwanzo nilipata shida kwa kutembea na wanaume watatu au wanne, kila nilipomaliza nilikuwa nipo hoi na kushindwa kujitambua. Kuna siku nilitembea na wanaume watano japo nilipata fedha ya maana, lakini siku hiyo nilipoteza fahamu na nilipopata fahamu ilibidi nikimbizwe hospitali. Kitu kilichonifanya nipumzike kazi kwa miezi miwili.

    Baada ya kupona ndipo shoga yangu Callo aliponifundisha kutumia dawa za kuongeza nguvu ambazo tulizinunua kwa bei kubwa. Nilizitumia kwa muda na kuona faida yake kwa kuweza kufanya mapenzi na wanaume shababi zaidi ya kumi bila kuchoka.

    Biashara ilikuwa nzuri iliyotuongezea kipato na kuweza kufikisha milioni saba kwa miezi sita. Callo alipingana na wazo langu la kutafuta chumba kupanga kwani alinieleza kazi ile haitaki bughuza.

    Nilikubaliana naye kutokana na kipato tulichokipata kiliweza kutupatia pesa ya kulipia chumba na matumizi ya kawaida pamoja na pesa ya kuweka benki.

    Niliweza kwenda naye baadhi ya mikoa na nje ya nchi za kama Kenya Uganda Rwanda, Burundi mpaka Zaire ambako tulitengeneza pesa za kumwaga. Callo alikuwa mzoefu wa kazi ile alinifundisha njia nyingine ya kujiongezea kipato ambayo kwa njia nyingine ilikuwa ya hatari.

    Alinifundisha kuwaibia watu pesa kwa mtindo wa kuwawekea dawa za kulevya kisha kuwaibia wakiwa wamelala fofofo hawajitambui kwa kuleweshwa na dawa. Hapo unamsachi na kuchukua pesa zake na kutimka usiku uleule.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa mlevi tulikuwa tukimwekea kwenye kinywaji kwa asiye mlevi tulikuwa tukimpakia dawa kwenye matiti na katikati ya mapenzi, unamuomba akunyonge matiti ili kukupandisha mzuka. Akijidanganya tu kunyonya anakwenda na maji na kufanya vitu vyetu.

    Ile haikuwa ngeni kwangu ndiyo njia niliyotumia kulipizia kisasi ila shoga yangu alikuwa mtaalamu sana kuliko mimi. Huwezi kuamini safari zetu tulikuwa tukirudi na pesa zaidi ya Milioni tano kwa wiki.

    Japokuwa tulipata pesa lakini tulikuwa tukiishi maisha ya kujificha tunapokuwa tupo nje ya nchi. Lakini tulipokuwa tukirudi tulijiachia kisawasawa.

    Callo kila nililokuwa nikilitaka kulifanya kwa wakati ule alinikataza. Kama kununua nyumba au gari la kutembelea. Alinieleza pesa niliyokuwa nayo zaidi ya milioni kumi na tano zilikuwa kidogo sana alipenda nipate wazo lile nitakapokuwa na zaidi ya milion 50 mpaka 100.

    Kwa biashara ile nilikuwa nikiamini ndani ya mwaka mzima ningekuwa nimefikisha, kwani wakuja walikuwa ni wengi ambao tuliwaingiza mjini. Pia tulijichanganya kwenye magulio ya ng'ombe ambako tuliwaokota wakuja kama hatuna akili nzuri.

    Callo alikuwa jasusi la kimapenzi ilifikia hatua ya kunifundisha hata kuua japokuwa kitu kile hakikuwa kigeni kwangu lakini nilifanya mchezo ule katika kulipa kisasi si katika uchangudoa.

    Kitendo kile tulikifanya kwenye Machimbo ya almasi na dhahabu Jamhuri ya Kongo. Kule tulitoka na pesa zaidi ya milioni 50.

    Taratibu nilianza kuvutika na kufika hatua ya mimi kuwaza kuua pale mtu atakapoingia kwenye anga zangu. Mimi na Callo tulikuwa kama mapacha hasa Callo alinitumia kutengeneza pesa nyingi kutokana na mimi kukubalika sana kwa wanaume.

    Tulijikuta tukiingia katika kazi ya ujambazi kuwaibia watu waliokuja kununua dhahabu kwa kuwapulizia dawa za kulevya na kuchukua fedha zote kisha tulitoroka usiku huo na kurudi Mwanza.

    Lakini kila kizuri kina ubaya wake, siku moja tukiwa tupo Geita kwenye machimbo tukiwa tumepanga guest moja na mtu mmoja aliyekuwa na pesa za manunuzi ya dhahabu. Callo kwa uzoefu wake alimgundua.

    Yule bwana pamoja na kumtega aliruka vihunzi lakini Callo aliniambia nimuache kwani alijua angemfanya nini.

    Siku ile Callo alinikataza kuchukuliwa na mwanaume yoyote hata kama angenihonga milioni.

    " Moureen leo hatufanyi biashara ya mwili."

    "Kwa nini?"

    "Kuna kazi moja ina hela kuliko hata kulala na wanaume saba."

    "Hakuna tatizo."

    Nikiwa nimelala chumbani kwangu

    Callo alinishtua usiku wa manane na kuniomba tuondoke pale. Niliniamka na kutoka, kutokana na kunijulisha nilale kama nipo kwenye lindo yaani nilale na nguo zangu.

    Nilipoamka nimkuta Callo ana begi lilionyesha amelichukua kwa yule mwanaume.Tuliondoka Geita usiku uleule na kuingia Mwanza Alfajiri. Tulipofika tuliteremkia mjini na kukodi gari jingine hadi hotelini kwetu. Tulipofika tulikwenda moja kwa moja hadi chumbani kwake na kulifungua lile begi lililokuwa na pesa nyingi.

    Kwa vile tulikuwa tumechoka sana kila mmoja alipumzika chumbani kwake ili baadaye tuweze kuzihesabu na kugawana. Nilikwenda chumbani kwangu na kujimwagia maji ili nijilaze kutokana kulala usingizi wa machugamachuga. Baada ya kuoga na kupanda kitandani na kulipitiwa na usingizi mzito.

    *****

    Sauti kali ya mlango kugongwa ilinishtua katika usingizi mzito nilijikuta nikifoka kwa ukali

    "Ni ustaarabu gani huo?"



    Kwa vile tulikuwa tumechoka sana kila mmoja alipumzika chumbani kwake ili baadaye tuweze kuzihesabu na kugawana. Nilikwenda chumbani kwangu na kujimwagia maji ili nijilaze kutokana kulala usingizi wa machugamachuga. Baada ya kuoga na kupanda kitandani na kulipitiwa na usingizi mzito.

    *****

    Sauti kali ya mlango kugongwa ilinishtua katika usingizi mzito nilijikuta nikifoka kwa ukali

    "Ni ustaarabu gani huo?"

    SONGA NAYOO

    Sauti kali ya juu toka nje uliniamuru nifungue mlango:

    "Fungua!"

    Nikiwa nimejifunga taulo tu nilikwenda hadi mlangoni na kufungua, nilishangaa kuona askari wenye bunduki wakiwa na mhudumu wa hoteli wakiwa mlangoni kwangu, nilishangaa na kuwauliza:

    "Jamani kuna nini?" niliuliza kwa woga kidogo.

    "Mwenzio amekwenda wapi?" askari aliyekuwa mbele aliniuliza.

    "Mwenzangu nani?"

    "Muuaji mwenzio."

    Kauli ile ilinishtua na kujikuta nikibakia kinywa wazi na kukumbuka safari yetu ya usiku Callo alifanya mambo yake.

    "Tunakuuliza muuaji mwenzako amekwenda wapi?"

    "Kwa kweli sijui lolote wala mimi sio muuaji na sijui lolote kuhusiana na huyo mnayemtafuta."

    Nilijitahidi kujitetea lakini hawakunielewa na kuamliwa nichukuliwe na kupelekwa polisi tayari kufunguliwa mashtaka la mauaji baada ya kuonekana Callo amekimbia na mimi kuwa naye siku ya tukio.

    *************

    Nilichukuliwa na kupelekwa polisi ambako nilifunguliwa mashtaka ya mauaji, pamoja na kujitetea hakuna aliyenielewa. Nilikaa ndani miaka miwili bila kuhukumiwa, Wakati naingia gerezani kumbe nilikuwa na ujauzito wa mwezi mmoja wa mwanangu wa mwisho. Nilijikuta mtoto wa kike kujiingiza kwenye kesi mbaya ya wizi na uuaji. Kibaya sijukua wanangu wanaishi maisha gani japokuwa niliacha fedha nyingi ya matunzo.

    Nilimshukuru Mungu nilijifungua salama na mwanangu kukua katika hali nzuri kipindi chote nilichokuwa gerezani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku zote nilijiuliza Callo alitakuwa amekwenda wapi na kwa nini alikimbia na kuniacha bila kunijulisha hatari ile. Mungu mkubwa baada ya kusota gerezani kwa miaka miwili. Nilitoka kwa msamaha wa Rais baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha wa kunitia hatiani.

    Nilitoka kwenye gereza la Butimba na kurudi hadi mjini na kwenda moja kwa moja benki angalau nichukue pesa kidogo za matumizi ili nijipange upya. Namshukuru Mungu nilikuta fedha zangu zaidi ya milioni 35. Niliona ndicho kipindi changu cha kurudi Dar kuungana na familia yangu.

    Nilirudi Dar na kumshukuru shoga yangu kunitunzia wanangu kipindi chote nikiwa mbali naye. Nilifurahi kuwakuta wanangu wapo katika hali nzuri, nilimshukuru sana Mungu.

    Fedha niliyokuwa nayo nilinunua nyumba kisha nilijifikiria kuanzisha biashara ya salon ili kujiingizia kipato. Kwa vile sikujua hali yangu ya mbele niliwapeleka watoto wangu shule ya kulipia ya kulala hukohuko kwa miaka mitatu ili nijipanga kwa kuamini mpaka ada ya miaka mitatu.

    Niliamini mpaka ada inakwisha nitakuwa nimepata fedha nyingine.

    *****

    Baada ya kupumzika nilijikuta nikipata hamu ya kurudi kwenye kazi yangu japo sikuwa na shida ya kimaisha. Kwa vile jasiri haachi asili kukaa hivihivi nilishindwa nikajikuta nakuwa na hamu ya kuingia kwenye kazi yangu ya asili. Kwa kweli nilirudi kijiweni na kuendelea na kazi yangu kwa vile sikufanya kwa shida nilifanya biashara kwa kuchagua wateja.

    Niliwapenda wateja wa ndani ya gari kuliko kwenda kulala naye, kwa kweli ile ilinisaidia kufanya mapenzi mepesi pia kupata malipo mazuri na kulala nyumbani.

    Kwa kweli kazi niliifanya kwa kupenda huku ikiniongezea fedha ya matumizi ambayo ilinifanya nisitumie fedha zangu. Kwa vile nilikuwa peke yangu kwa kweli fedha niliyopata kila nilipotoka ilinitosha na nyingine kuweka ndani. Maisha yalikwenda vizuri huku nikifurahia mpangilio wangu wa biashara.

    Siku moja nikiwa kijiweni lilikuja gari la kifahari na kusimama mbele yetu, kwa vile nilikuwa kibiashara ya kuchagua na si kukimbilia kama wenzangu. Kutokana na kujiamini na kutofanya kazi kwa njaa nilisimama nyuma yao, lakini mwenye gari alinitaka mimi. Nilipita mbele yao na kuonana na mzee aliyekuwemo kwenye gari ambaye alikuwa amevaa kofia ya pana.

    “Ingia mrembo.”

    Niliingia bila kusema kitu na kukaa siti ya mbele, baada ya kukaa mzee yule alinisamilia.

    “Habari mrembo?”

    “Nzuri.”

    Japokuwa alikuwa mtu wa mzima umri wa baba yangu kwenye biashara yetu hakukuwa na shikamoo, akitaka kuamkiwa aende kwa watoto wake.

    “Nikupatie shilingi ngapi?”

    “Elfu hamsini.”

    “Mpaka asubuhi?”

    “Hapana huwa silali kwa mtu pia ukitaka mapenzi na mimi tunamalizana kwenye gari siku hizi wanaume haaminiki.”

    “Kwa nini?”

    “Wengi wamekuwa na tabia mbaya anakupeleka guest na kukulewesha kisha anakufanyia mchezo mbaya.”

    “Aah! Binti mimi mtu wa heshima siwezi kufanya hivyo.”

    “Wengi walisema hivyo, lakini mwisho wake nilijuta.”

    “Sasa mapenzi ndani ya gari yana raha gani?”

    “Hujawahi kufanyiwa?”

    “Bado, napenda sana kitandani.”

    “Basi leo jaribu kesho utanitafuta.”

    “Poa ngoja nijaribu leo, lakini mbona gharama kubwa.”

    “Hata huduma yake ni kubwa.”

    Mzee mzima alipaki gari pembeni na kuteremsha suruali nusu mlingoti na kuanza kumpatia huduma ambayo ilimpagawawisha na kuniomba twende hotelini ili nimpe raha zaidi.

    “Binti unajua, sijawahi kufanyiwa mchezo kama huu toka nizaliwe.”

    “Mzee punguza mapepe leo hamu zako zote zitaishia humuhumu ndani ya gari.”

    Niliendelea kumpa huduma mzee iliyompagawisha na kuniomba kesho tena nionane naye.

    “Mrembo kazi unaijua badala ya elfu hamsini ninakupa laki mbili.”

    “Asante mzee wangu, kwenye gari hivi kitandani si ungehonga nyumba.”

    “Binti fedha ninayo na uzee wangu fedha niliyonayo nakula raha tu.”

    “Na mama nyumbani?”

    “Mama kachoka kawa kawa mti uliokauka unatia mapengo panga langu, lakini wewe binti laiini hata kwa wembe unakatika.”

    “Kwa hiyo nikija mchana utanipa shilingi ngapi?”

    “Japokuwa nilikuwa nataka kuondoka kesho lakini kwa ajili yako nitakupa milioni.”

    “Weweee acha utani!” macho ya tamaa yalinitoka pima.

    Tamaa iliniingia na kuitamani ile fedha lakini niliamini huduma niliyompa kwa usiku ule na malipo ya laki mbili si haba. Niliamini sikuwa na haja ya kurudi kijiweni baada ya kutoka kwa babu ningekodi gari na kurudi nyumbani.

    “Kweli binti, raha nilizopata sikuwa kupata katika ujana wangu na wenzako wengi wanajali fedha kuliko huduma.”

    “Kwa hiyo upo hoteli gani?”

    “Selena.”

    “Kesho nije saa ngapi?”

    “Kuanzia saa nne asubuhi nitakusubiri wewe tu.”

    “Poa, wacha niwahi home.”

    “Kwa jinsi ulivyonifurahisha nitakuongezea laki ya nauli ya kukupeleka nyumba na nyingine ya kukuleta hotelini.”

    “Asante mzee wangu.”

    Kabla ya kuondoka mzee yule alinipa business card, ili kesho nikifika nimpigie simu kama yumo ndani. Niliichukua na kukodi teksi hadi kwangu huku nikifurahi siku ile kuwa yenye bahati. Nilipofika nilioga na kula kisha nilichukua pombe kali kwenye friji na kunywa kisha nilijilaza kuitafuta siku ya pili.

    ****

    Asubuhi aliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kuonana na mteja wangu huku nikijiandaa kumpa penzi takatifu mteja wangu ili niendelee kula zaidi vitu vya yule mzee aliyekuwa akipata mapenzi ya kulipua. Siku hiyo nilijipamba kwa nguo nzuri yenye mvuto ambayo nilipoivaa kila mwanaume alinimezea mate.

    Baada kuhakikisha nipo sawa nilichukua business card na kuitazama, jicho langu lilishtuka kukuta jina kama la baba yangu mzazi.

    “Mmh! Ina maana majina yana fanana? Hapana labda siyo yeye ngoja nikamuone. Baba yangu hawezi kufanya vitu kama hivi.”

    Nilijikuta nikiwaza hivyo, lakini akilini nyingine iliniambia nisiende moja kwa moja, nikifika nikae sehemu ili kumuona atakaye tokea isiwe baba yangu mzazi ukawa kizaazaa.

    Baada ya kuamini nipo sawa nilitoka na kukodi gari mpaka Selena Hoteli kuonana na mwanaume wangu ambaye nilimchanganya kwa mapenzi. Moyoni nikipanga kumfanyia mambo makubwa mwanaume ambaye alionekana mgeni katika medani ya mapenzi. Pamoja na kupanga yale bado moyo wangu ulikuwa na wasiwasi na jina la yule mwanaume kufanana na la baba yangu mzazi, japokuwa tayari nilikuwa nimeishafanya naye mapenzi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipofika hotelini niliteremka na kuingia hadi mapokezi kisha nilipiga simu. Niliamini kwa jinsi nilivyokuwa nimevaa wigi na miwani isingekuwa rahisi kunitambua.

    Baada kuketi kwenye kochi nilipiga simu ambayoiliita kidogo na kupokelewa mara moja kuonesha alikuwa ameshikilia simu mkononi.

    “Haloo.”

    “Haloo bebi,” nilijibu kwa pozi.

    “Vipi umefika?”

    “Ndiyo.”

    “Basi njoo ndani chumba namba 220.”

    “Hapana bebi nifuate sijawahi kuingia naogopa.”

    “Basi ingia mpaka mapokezi.”

    “Noo, bebi naogopa njoo nipo nje ya hoteli.”

    “Haya nakuja umevaaje?”

    “Jamani bebi jana tu umenipotea?” nilijishauwa mtoto wa kike.

    “Si unajua ilikuwa usiku sikukutazama usoni.”

    “Mi mbona nakukumbuka, nikukuona tu nakufuata.”

    “Hakuna tabu nakuja.”

    Baada ya kukata simu nilitulia huku nikiitengeneza vizuri miwani yangu kuhakikisha nampoteza atakayetoka kunifuata. Kilichonifurahisha zaidi kilikuwa kutonifahamu usiku ule, ile ilikuwa nafasi ya kumtambua kama ni baba au la, japokuwa niliamini baba yangu hawezi kuwa na tabia chafu kama zile.

    Niliwa nimeinama nikisoka ujumbe kwenye simu, nilishtuliwa na sauti.

    “Samahani binti.”

    “Bila samahani,” nilijibu huku nikinyanyua uso wangu.

    Moyo ulishtuka kidogo usimame, aliyekuwa amesimama mbele yangu ni baba yangu mzazi mzee Hans Mouses. Nilijitahidi kuficha hofu yangu na kumtazama kupitia msaada wa miwani.

    “Mgeni wangu?” baba aliniuliza bila kujua niliyekaa pale ni mwanaye wa kumzaa.

    “Hapana,” nilikataa huku nikitikisa kichwa kwa msisitizo.

    “Ok, samahani.”

    “Bila samahani.”

    Mzee Hans Mouses aliyekuwa amevaa penzi ya maua na flana kwa juu na chini alivaa sandoz aliondoka kuelekea nje. Hapo ndipo nilipoamini kumbe jana yake nilitembea na baba yangu mzazi.

    Lakini nilitaka kupata ukweli, baada ya kunipa mgongo akielekea nje niliipiga simu yake.

    Baada ya kuita nilimuona akipokea huku akitokomea.

    “Haloo mpenzi upo wapi?” aliniuliza.

    “Wee upo wapi?”

    “Mi ndo’ natoka nje ya hoteli.”

    “Nikwambie kitu mpenzi?”

    “Niambie tu.”

    “Lakini naomba usikasilike.”

    “Siwezi niambie tu.”

    “Nimeondoka nyumbani kwa haraka ya kukuwahi nimeondoka na ufunguo wa geti, hivyo nimepigiwa nirudishe funguo ili baba atoe gari,” nilitengeneza uongo.

    “Ooh! Kwani unakaa na nani?”

    “Na wazazi.”

    “Kwa hiyo?”

    “Naomba nifikisha ufunguo nyumbani na kurudi mara moja.”

    “Basi haina tatizo, leo nipo kwa ajili yako.”

    “Poa ila samahani kwa kuonekana mswahili.”

    “Usihofu bebi wahi basi.”

    “Ok.”

    Nilikata simu na kutulia huku macho yangu nikiyaelekeza mlango wa kutokea nje. Baada ya muda nilimuona baba akirudi kuonesha anaamini kabisa mpenzi wake amerudi nyumbani.

    Baada ya kunipita na kuelekea chumbani nilinyanyuka na kuelekea nje. Nilipofika nje nilikodi gari hadi nyumbani, nilipofika nilijilaza kitandani kichwa kikiwa kinaniuma baada ya kugundua nimefanya mapenzi na baba yangu mzazi kwa sababu ya kufanya mapenzi gizani. Nilijiuliza kama asingenipa busness card ingekuwaje pale ambapo ningekwenda moja kwa moja chumbani na kumkuta baba amejaa tele.

    Nilijikuta nikipata wazo lingine na kujinga kwa kujilaumu kuondoka, nilitakiwa kwenda chumbani kwake ili aone faida ya kunifukuzwa kwake.

    Lakini wazo kama lile sikukubaliana nalo, niliamini nilitakiwa kumuheshimu mzazi wangu kwa vile kosa lilikuwa langu na tulio la jana yake litabaki kama bahati mbaya.

    Sikutaka kujilaumu kwa kitendo kilichotokea kwa vile niliamini ilikuwa ajali kazini.

    Nilijikuta nikijawa na mawazo kuhusu baba yangu kujiingiza kwenye tabia ya kutembea na changudoa hasa nikizingatia alikuwa akiwalaani watoto wa watu waliokuwa wakijiuza.

    Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa naye jana yake ilionesha tabia ile ni mtindo wake kila alipokuja Dar na hakupata mwanamke anayejua mapenzi kama mwanaye aliyefanya naye mapenzi bila kujua.

    Moyo ulinituma lazima nimpigie simu baba na kumueleza kitendo chake cha kunifukuza na ushahidi wa kutembea na mwanaye kwenye gari lake. Nilijua atashtuka lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kuusema ukweli.

    Kutokana na kichwa kuchanganyikiwa nilikwenda kwenye friji na kuchukua pombe kali na kunywa kwa fujo kisha nilijilaza kwenye kochi kwa vile niliamini siku ile ilikuwa ni nuksi kwangu.

    ***

    Nilishtuka saa moja usiku njaa ikiniuma kama kidonda, nilikwenda kwenye bar ya jirani na kuchukua mchemsho kisha nilirudi ndani na kuushambulia wote kutokana na njaa ya toka asubuhi.

    Baada kushiba nilikwenda kuoga kisha nilijilaza kwenye kochi na kuwasha tivii kuangalia vipindi huku nilichukua simu yangu niliyokuwa nimeiacha juu ya kochi.

    Nilikuta missed calls zaidi ya ishirini na sms zaidi ya tano zote zikuwa za baba.

    Nilifungua upande wa ujumbe mfupi na kukutana na ujumbe wa lawama wa kwanza ulisema:

    Bebi mbona kimya, kwa nini hupokei simu?

    Wa pili ulisema: Vipi, kuna tatizo?

    Wa tatu: Nijulishe basi mpenzi ili nijue umepatwa na nini?

    Nilipotaka kuufungua wa nne simu iliingia nilipoangalia kwenye kioo alikuwa baba Mzee Hans Mouses. Nilijiuliza nikiipokea nitamjibu nini.

    Lakini niliamini lazima nimpe makavu live kisha sionani naye tena. Niliamini ukweli nitakaompa ataondoka akijua kabisa kitendo alichonifanyia cha kunifukuza kama mbwa ni cha kinyama na matokeo yake tukafanya mapenzi bila kujuana.

    Wakati nikiwaza yale simu ilikatika, niliichukua na kuitazama huku nikiwa na mambo mawili nimpigie au niache. Kabla sijapata jibu simu iliita tena. Nilibofya kwenye kitufe cha kupokelea na kuweka simu sikioni.

    “Haloo.”

    “Haloo, bebi umefanya nini? Yaani hapa nimeshindwa kuondoka kwa ajili yako umepatwa na nini mpenzi?” baba aliuliza kwa shauku ya kujua.

    “Kuna tatizo,” nilimjibu.

    “Tatizo gani?”

    “Kuhusu wewe.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mimi?” alionesha kushtuka.

    “Ndiyo.”

    “Tatizo gani?”

    “Samahani wewe ni kweli unaitwa Mzee Hans Mouses?”

    “Bebi swali gani hilo ikiwa business card nilikupa, kuna tatizo?”

    “Naomba ujibu swali langu kama lilivyokuja.”

    “Ndiyo.”

    “Unakaa Arusha?”

    “Ndiyo bebi, mbona unaniuliza hivyo?”

    “Utajua tu, Moureen unamjua?”

    “Moureen gani?”

    “Moureen Hans Mouses.”

    “Si..si..simjui,” alipata kigugumizi kidogo.

    “Mbona kama unasita?” nilimuuliza.

    “Hapana nilijitahidi kumkumbuka lakini kumbukumbu haiji.”

    “Mouses Hans Mouses naye humfahamu?”

    “Huyo namfahamu.”

    “Unamfahamu kivipi?”

    “Mwanangu wa kwanza.”

    “Yupo Marekani?”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog