Search This Blog

Friday, 3 June 2022

SURPRISE YA AIBU - 5

 





    Simulizi : Surprise Ya Aibu

    Sehemu Ya Tano (5)





    Nilijifanya kubadili uamuzi kwa kutaka kujengewa nyumba na kununuliwa gari vitu vilivyotimia ndani ya miezi miwili.

    Mzee wa watu fedha kwake haikuwa tatizo ndani ya muda huo nilipata vitu vyote nilivyotaka. Baada ya kuponea kwenye tundu la sindano niliachana na mchezo wangu ule mchafu na kutafuta njia nyingine wa kupunguza shombo nililokuwa napakwa na mzee Kupe.

    Wakati nikitafuta njia muafaka niliamua kutulia kwa muda ili kumfanya mume wangu aamini ule ni uongo. Ili kurudisha imani kwangu hata kutembea nilikuwa sitaki zaidi ya kukaa ndani na nilitoka kwa taarifa kitu kilichoongeza mapenzi kwa mume wangu na kuamini yote aliyo ambiwa ni uongo.

    ***

    Nakumbuka siku moja kabla ya kuelekea mjini nilipeleka viatu vyangu kwa shoe shine Mlemavu wa miguu aliyekuwa nje ya uzio wa nyumba yetu. Na yule mlemavu ni mimi niliye mkingia kifua baada ya mume wangu kusema kuwa eti ni uchafu kuwepo kwenye ukuta wa uzio wa nyumba yetu.

    Lakini nilimueleza mume wangu na kunielewa na kumuacha afanye kazi pale nje ya uzio wa nyumba yetu. Kwa upande mwingine alinisaidia kunisafishia viatu vyangu ambavyo awali nilikuwa nikienda mjini nilisafishia huko huko.

    Japo kutokana na ukarimu wangu alipenda anisafishie viatu bure lakini nilimkatalia kwa kujua ile ndiyo kazi yake na sisi ndio tunaotakiwa kumsaidia kimaisha. Japokuwa alikuwa akinisafishia viatu kwa shilingi mia tatu mimi nilikuwa nampa kila kiatu elfu moja.

    Kwa kweli kwa muda mfupi nilizoeana naye na yeye alipenda kuniita mchumba nami nilimkubalia ili naye asijione kuwa mlemavu wa miguu hana haki ya kupata upendo kwa watu hasa wanawake wazuri kama mimi.

    Kutokana na ukaribu na mazoea siku nyingine huacha viatu kila nilitoka mjini na yeye alikuwa akinisafishia kumtuma mfanyakazi anifuatie. Siku hiyo nakumbuka vizuri kabla ya kutoka kwenda mjini nilitoka nje kupeleka viatu vyangu visafishwe na kupigwa dawa.

    Nilipokaribia kijiweni kwake hakuniona kutokana na kunipa mgongo, alikuwa akisafisha viatu vya mmoja wa mteja wake. Kwenye benchi kulikuwa na vijana watano wa kijiweni. Mazungumzo yake yalinifanya nisimame nyuma yake bila kuzungumza ili nisimkatishe kwa kujitokeza.

    Nilimsikia akiwaambia wateja wake juu ya uwezo wake wa kufanya mapenzi na wanawake.

    "Hivi mnajua kwa nini naitwa Side Butamu?"

    "Hatujui" mmoja alijibu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Maana yake ni jinsi mtoto wa kiume nilivyo mtamu kitu kilichosababisha wake za watu niwaone nuksi."

    "Nuksi kivipi."

    "Hivi ndugu yangu Side mimi na viguu hivi kama vijiko leo hii lizuke vagi nitaanzaje kukimbia?"

    "Acha uongo umeisha onja mke wa mtu?"

    "Kaka kila aliyeonja alitangaza kuachana na mume wake na kutangaza kunioa."

    Kauli ile iliwafanya wote waliokuwa pale waangue kicheko pamoja na mimi nilicheka kwa kushika mdomo ili sauti isitoke nna kukatisha utamu.

    "Side utani huo."

    "Kama utani nipe mkeo nimuonje kisha jibu utapata kama hakuomba taraka. Wengine wapenzi tunafanyia kazi sio starehe, sio ukigusa kidogo kama bata hupandi tena.

    “Nikipanda juu nakuwa mdogo kama kidumu cha lita tano hapo mwanamke atamaliza maneno yote. Wengi hujiuliza nimeungwa kwa viungo gani asali si asali, sukari si sukari. Kibaya zaidi nikiwakoleza huvinyonya viguu vyangu kama nimevipaka sukari."

    Kauli ile nilinifanya nicheke kwa kushika mdomo, huku nikiangalia viguu vyake vidogo.

    "Side mbona huna mke?" mmoja alimuuliza.

    "Toka nifike hapa sitaki wanawake nitakaye muonja lazima atawahadithia wenzake na kuwafanya wanikimbilie kama mzinga wa nyuki. Mi mtamu bwana utafikiri nimetolewa kwenye pipa la asali."

    Maneno ya Side yalinifanya nicheke kwa sauti na kumfanya agundue nipo nyuma yake. Alipogeuka aliona aibu na kuniomba msamaha kutokana na kuheshimiana sana.

    "Ooh! Mchumba samahani sikukuona, si unajua nipo na wahuni."

    "Aah! Side ya kawaida, nifanyie chapuchapu nawahi mjini."

    Nilimuachia viatu na kurudi ndani huku nikichekea moyoni kila nilipokumbuka maneno ya Side Butamu kama apendavyo kujiita. Nilijikuta nikijiuliza swali juu ya yale yote aliyokuwa akiyazungumza kama ni kweli au ni porojo.

    Nilijikuta nikipata wazo la kutaka kufanya naye mpenzi uhakikiwa wa maneno ya Side Butamu yana ukweli gani. Baada ya kunisafishia viatu vyangu nilielekea mjini huku mawazo makubwa yakitawala kichwani kuhusiana na maneno ya Side Butamu.

    Kweli ugonjwa wa ngono ulikuwa ukinisumbua kila nilipokumbuka maneno ya Side Butamu nilihisi kuwa na hamu ya kufanya naye mapenzi na kutaka kuthibitisha kwa vitendo. Nilijikuta nikimtamani Side Butamu kufanya naye mapenzi japo mlemavu.

    Akili yangu ilinituma kama kweli asemayo nitayakuta basi nilipanga kuyabadili yaisha yake kwa kumuhamisha mji na kumpangia nje ya mji na kumpatia huduma zote muhimu.

    Pia nilipanga kumnunulia gari ya Automatic gear ambalo atalitumia kuijia mjini. Lakini nilijiuliza nitaweza kumuingiza ndani bila mtu yeyote kujua, baada ya kupanga na kuwazua nilipata jibu la kufanya.

    Siku ya pili mume alinijulisha kuwa mchana anaweza kuchelewa kutokana na kubanwa na mkutano muhimu ofisini. Ilikuwa kawaida yake panapotokea mabadiliko yoyote lazima anijulishe.

    Niliamini siku ile ndiyo ya kudhihilisha kauli ya Side Butamu kama ina ukweli. Majira ya saa nne nilitoka hadi nje ya geti na kumkuta Side akisafisha viatu juu ya benchi kulikuwepo mtu mmoja tu.

    Side aliponiona alidaka juu juu:

    "Ooh! mchumba wangu huyo!"

    "Ni mimi mpenzi wangu Side Butamu."

    Kauli yangu ilimfanya aone aibu lakini sikutaka kumkosesha raha nilimweleza kilicho nieleka pale.

    "Sasa Side nilikuwa naomba ukimaliza kazi hii usipokee kazi ya mtu yeyote njoo ndani kuna kazi kusafisha mikoba yangu."

    "Mingapi?"

    "Ipo mingi sidhani kama leo utaimaliza naona itakuwa kazi yako ya kutwa nzima," nilitengeneza uongo wa kuingiza ndani bila yeye kujua.

    "Poa mchumba nakuja."

    Baada ya kukubaliana na Side nilirudi hadi chumbani na kutandika kitanda vizuri kuliko siku zote. Kisha nilikwenda bafuni kuoga ikiwa kuufanyia usafi uwanja utakaotumiwa katika mechi.

    Mtoto wa kike nilisimama mbele ya kioo nikiwa mtupu na kuuangalia mwili wangu na kugeuka huku na kule huku nikurusharusha makalio yangu yaliyokuwa laini kama mchicha pori.

    Nilijipamba nikapambika na kujipulizia utuli ambao hata mtu angepumua ungemeza uvundo wote. Nilijifunga kanga moja nyepesi bila nguo ndani na kukaa mkao wa kumsubiri huyo Side butamu aliyejisifia mtamu zaidi ya vitamu. Baada ya muda mfanyakazi wangu wa ndani alinifuata chumbani kwangu.

    “Dada Mou.”

    “Judy vipi?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Dada Side amekuja.”

    “Mwambie apite ndani.”

    Nilisubiri kwa muda bila kumuona kitu kilichonifanya nitoke kumfuata. Nilimkuta bado yupo sebuleni akiwa kwenye zulia.

    “Vipi Side?”

    “Mchumba niletee hapahapa.”

    “Mchumba utaniuzi umesikia nakula watu?”

    “Basi hakuna tatizo tangulia nakuja.”

    Nilitangulia chumbani, baada ya muda Side aligonga mlango, nilitoka hadi mlangoni na kufungua, kweli alikuwa Side Butamu kama alivyojiita. Mtoto wa kike nilipomuona nilikuwa na shauku kama mwenye kiu aliyeona dimbwi la maji.

    Pamoja na kujisifu bado nilikuwa na wasiwasi wa kunikata kiu yangu iliyokuwa ikinitesa kila kukicha.

    “Side mpenzi pita ndani.”

    “Noma mchumba babu ataniua akinikuta,” Side aliingia wasiwasi.

    “Akukute ili iweje?”

    “Si unajua mazingira,” Side alijitetea.

    “Side hebu ingia ndani umalize kazi uliyoitiwa mara moja uwahi kazi zako, kumbuka nje wateja wanakusubiri,” nilimuhimiza aingie ndani ili anipe alichokinadi mbele za watu kuwa mtamu kama katumbukizwa kwenye pipa la asali.

    Side aliingia chumbani kwa woga baada ya kuingia niliufunga mlango kwa komeo. Side kuona vile alishtuka na kuhoji.

    “He! Mchumba mbona unanitisha?”

    “Acha woga kipi cha ajabu?”

    “Nyumbani kwa mtu hapa usinitoe sadaka nikakatwa masikio.”

    “Walaa, hofu yako kwani na mimi sijipendi?”

    “Mmh! Haya hebu nipe hiyo kazi niifanye maana sehemu hii si salama kabisa hasa mtoto kama wewe umbile na vazi alilovaa ni mtihani mzito kwangu.”

    “Ukizidiwa nitakupa wala usihofu, mtoto wa kike nyama isiyo na mfupa kwa mwanaume.”

    “Mmh! Mtihani huo, lakini nipe kazi maana nisije fanya kazi isiyo nihusu ukamsahau mzee wako bure.”

    Mmh, Side bila kujua alikuwa akiingia kwenye mtego mwenyewe, sikutaka kuipoteza nafasi ile. Khanga moja niliyokuwa nimejifunga niliidondosha makusudi, jicho la Side lilipotua mwilini mwangu alishtuka na kuangalia chini.

    Niiokota kanga kwa pozi kujifunga kisha nilimsogelea pale chini alipokuwa amekaa na kukaa pembeni yake.

    “Side,” nilimwita kwa sauti ya uchokozi.

    “Mmh,” maskini Side aliingiwa na aibu kama mwari.

    “Side unajua kazi niliyokuitia?”

    “Ya kusafisha mikoba.”

    “Hapana, kumbe hukusikia vizuri,” nilifanya kama hakusikia vizuri.

    “Mbona nilisikia kusafisha mikoba,” Side alijitetea.

    “Kuna kazi nyingine kabisa ukiifanya vizuri nakuhakikishia umasikini utakutoka utasahau kusafisha viatu vya wanaume wenzako.”

    “Kazi gani hiyo?” aliuliza macho yamemtoka pima.

    “Nataka unipe ulichokinadi kwa wanaume wenzako huko nje.”

    “Kipi hicho mchumba?”

    “Nataka unipe ule utamu iliouahidi kuwa ukimpata mke wa mtu anachanganyikiwa.”

    “Hakuna mchumba nilikuwa nawatania tu”

    “Muongo Side usiniogope.”

    “Kweli mchumba zile porojo tu,” kauli ya Side kidogo initoe machozi.

    “Side hebu nionee huruma mpaka kukuleta huku kuna kitu nakitaka kwako.”

    “Lakini humu ndani noma, mchumba unataka babu aniue.”

    “Side babu mwanaume jina hana lolote nakaa naye kwa vile ana pesa lakini nikimpata mtu wa kuzimaliza haja zangu haki ya nani nakununulia nyumba na gari,” mtoto wa kike hamu zilinipanda na kujikuta nikitoa siri ya ndani huku nikitangaza bingo.

    “Siwezi kukataa ofa nono kama hiyo, lakini mazingira yenyewe hayaruhusu. Unafikiri mumeo akinifuma ndani kuna kupona kweli?”

    “Side mume wangu huwa harudi bila kunijulisha na pia huwa harudi mchana.”

    “Tufanye kesho mchumba popote tofauti na hapa,” Side alikuwa na maneno mengi kiasi cha kuanza kunirusha stimu.

    “Side nionee huruma mtoto wa mwenzako, siwezi kuvumilia hali ni mbaya nione jinsi ninavyo teseka mpaka kisima kimejaa maji ya kumwaga bondeni. Hata mwili wangu umebadilika rangi na kuwa mwekundu kama nyoka mwenye sumu kali hebu nionee huruma mwana wa mwenzio,” nilijitetea kwa Side baada ya hali kuwa mbaya.

    Nilizungumza sauti ambayo hata mlokole asingeweza kuruka, huku nikiitambaza mikono yangu laini kuelekea kwenye shamba la muhogo. Side taratibu alianza kulainikia, kama umeme nilimbeba kama kifurushi na kumuhamishia kitandani. Sikumchelewesha muda mfupi wote tulikuwa salesale maua.

    Mtoto wa kike zilikuwa zimenipanda kila kona niliyoguswa nilihisi msisimko wa ajabu. Mmh! Side alinitisha na mtindo wake wa kuniandaa aliouita mboga saba. Kila kona ya mwili aliyonigusa aliigusa kwa ufasaha na kunifanya nisikie raha ya ugwadu usiojulikana ni tamu au chachu.

    Baada ya mtoto wa kike kulainika kama mchicha pori, ngoma iliwekwa uwanjani. Side alianza kwa mkwala mzito kama katika ngumi alishambulia bila kupumzika kitu kilichonifanya nijihami muda wote huku nikienda wavuni zaidi ya mara mbili mfululizo.

    Mmh! Mtoto wa kike nilianza kuamini kauli za Side Butamu kwamba yeye kaumwa kwa viungo vyote vitamu duniani. Japokuwa niliinjoi mapenzi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu. Lakini niliona fedheha kushindwa na kinyangarakata kama Side ambacho hata mkononi hakijai. Mpaka tunakwenda mapumziko Side alikuwa anaongoza tena kwa pointi nyingi.

    Niliamini nilimdharau na tamaa zangu za mwili ndizo zilizofanya nifanye mapenzi na mtu asiye na hadhi kama Side Butamu kama alivyojinadi. Kwanza alikuwa maskini pili alikuwa mlemavu wa miguu iliyolemaa na kutembea kwa kujivuta kwa makalio.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimuangalia Side Butamu aliyekuwa amejilaza pembeni yangu kama kifurushi cha mzigo akiangalia juu kwenye dali bila wasi kuonesha hakubahatisha.

    “Side ni kweli au umenibahatisha?”

    “Mara nyingi ukisema kilicho ndani ya uwezo wangu, siwezi kukuhonga pesa ila nina uwezo wa kukupa penzi la kweli. Na leo ni woga kama tupo sehemu tulivu mbona leo ungeomba talaka kwa mumeo,” Side alijitapa.

    “Utani huo Side?”

    “We mwenyewe si umeuona muziki usio zima kwa umeme wa mgao?”

    Mmh! Side jamani alinitisha kwa majingambo yake, lakini sikuwa wa kukubali kushindwa kirahisi. Baada ya mapumziko mafupi tulirudi kwenye ungwe ya pili. Kama kawaida Side alianza kwa kasi ile ile ya mwanzo na kuzidi kuniweka katika wakati mgumu.

    Nami sikutaka kurudi nyuma tukakutana wote katikati ya uwanja ikawa piganikupige, Side alikuja juu nami nilimfuata huko huko. Nilijikuta nikimwaga chozi mtoto wa kike kwa penzi tamu la Side Butamu. Mtoto wa kike wazimu wa mapenzi ulinipanda na kujituma vilivyo kulinda hadhi yangu.

    Sikuamini mtu kama yule mlemavu asiye na hadhi yoyote kunipeleka puta kama gari kwenye njia mbovu. Katika ya mpambayo nilishangaa kumuona Side akitulia na kuanza kutokwa povu zito mdomoni. Macho yalimbadilika na kutazama juu kama ugonjwa wa kifafa.

    Mungu wangu! Nilijua nimeishaua kumzidishia dozi kaka wa watu, yeye mapenzi starehe mwenzie sehemu ya maisha yangu kama kuvuta pumzi.

    Nilishtuka na kuruka pembeni na kuanza kumwita.

    “Side...Side.. Side Buta..”

    Side hakuitikia zaidi ya kukoroma huku povu likimtoka, tumbo lilikuwa limerudi ndani kidogo likutane na mgongo. Wakati nimepagawa nafikiria jinsi ya kumsaidia Side, mlango uligongwa kwa nje. Sauti ya mume wangu ilizidi kunichanya na kujiona nimekwisha mtoto wa kike.

    Nilijiuliza imeanza lini mume wangu kurudi bila kunijulisha, niliona nimeumbuka mchana kweupe. Talaka niliiona mbele ya sura yangu, wazo la haraka lilinituma nikamfiche Side bafuni. nilimbeba kama furushi na kwenda kumbwaga bafuni kisha nguo zake nilizificha chini ya uvungu. Muda wote huo mume wangu alikuwa akigonga mlango huku akiniita kwa jina langu.

    Nilijifuta jasho lililokuwa likimwagika kama maji, kisha nilifungua mlango na kukutana na mume wangu aliyekuwa amefura kwa hasira.

    “Imeanza lini kujifungia mlango kwa ndani?” mzee Kupe alifoka.

    “Nawe imeanza lini kurudi bila kunijulisha?” badala ya kumjibu nami nilimbana kwa swali.

    “Nimekupigia simu hupokei, nimetuma mtu hufungui ulitaka nisifanye kazi zangu, nimeamua kuja mwenyewe. Mbona kama ulikuwa una...!!” Moyo ulipasuka pa! nikajua nimeumbuka mtoto wa kike, lakini niliwahi kumkata kauli.

    “Nafanya nini? si nilikuwa nimelala.”

    “Mbona mwili unatoka jasho?” akiniuliza huku akinichunguza.

    “Niliota ndoto mbaya sana.”

    “Ndo utoke jasho namna hiyo kama ulikuwa unacheza mieleka?”

    “Mume wangu hata sijui ni nini, kama jinamizi lilinikaba na kuteseka kwa muda huku jasho likinitoka. Yaani kugonga kwako mlango ndio kumenitoa kwenye ndoto hiyo sijui ungechelewa ingekuwaje labda ungekuta mkeo nimekufa,” nilitengeneza uongo huku nikijifuta jasho ambalo bado liliendelea kutoka japo chumba kilikuwa na kiyoyozi.

    Mume wangu alinipita na kuelekea msalani, nilitaka kumzuia lakini nilijiuliza atanielewaje ikiwa sijawahi kufanya kitendo kama kile hata siku moja. Nilijikuta nikisimama kama sanamu na kumsindikiza kwa macho. Nilijiuliza mlango wa bafuni niliufunga au la, niliamini kwa mchecheto niliokuwa nao sikukumbuka kuufunga.

    Nilimuomba Mungu asimuone kwani ilikuwa aibi kubwa kukutwa na mwanaume nikifanya mapenzi wenye kitanda chake kibaya zaidi mlemavu. Nikiwa naomba dua kimoyomoyo, haikuzuia chochote. Dua langu halikufika popote nilisikia sauti kali ya mume wangu ikiniita.

    “Mooreen hiki nini?”

    Mara alitoka na Side akimburuza kwa kukishika kiguu chake kimoja.

    “Moureen mke wangu ni uchafu gani unafanya? Unadiliki kufanya mapenzi na mlemavu, ni aibu gani hii?” Mzee Kupe alianza kulia.

    “Nisamehe mume wangu ni shetani tu kanipitia,” nilijitetea huku nikipiga magoti mbele yake.

    “Sawa kakupitia, lakini si kwa mlemavu kama huyu mke wangu aibu gani hii. Umelazimisha tumpe nafasi afanye kazi kumbe mwanaume wako?” Mzee Kupe alisema kwa hasira.

    Mume wangu angejua wala asingesema kauli ile, Side alikuwa zaidi ya wale wanaovaa masuti na miili mikubwa ya mazoezi. Kwangu Side ndiye niliyemuoina mwanaume wangu wa shoka.

    “Kweli ni mlemavu, lakini yote umeyataka wewe,” mtoto wa kike baada ya kuona maji yapo shingoni nilimtolea uvivu kwa kumwaga mchele mbele ya kuku.

    “Yapi hayo?” nilimuona akishtuka macho yamemtoka pima.

    “Unikidhi haja zangu muhimu umekuwa ukinipaka shombo tu kila siku.”

    “Kwa mtindo huo utaniua kwa ukimwi.”

    “Kwa hiyo unaamua nini?” Nilimuuliza nikiwa nimemshikia kiuno nilijua kama mbwai, mbwai tu.

    “Kila mtu achukue chake, nitaendelea kuchukua Changudoa kama zamani nijue moja kuliko kufuga changudoa mama huruma.”

    “Vyovyote vile, hata mimi nimechoka kupakwa shombo, mwili huu unatakiwa kutumiwa na wanaume wenye nguvu sio wewe kibabu. Kwanza shukuru nimekuvumilia muda wote lakini nimekuwa nikiteseka kila kukicha,” nilijua chakula hakiliki tena kwa vile Mzee Kupe alikuwa amemwaga ugali nami nikamalizia kwa kumwaga mboga.

    “Kabla ya yote uondoe uchafu wako mbele ya macho yangu.”

    Muda huo Side alikuwa amerudiwa na hali yake ya kawaida, kutokana na woga uliomtawala haja ilimtoka pale chini. Nilimtolea nguo zake chini ya uvungu na kumpa, kutokana na kuchanganyikiwa Side alijikuta akivaa kaptula yake kichwani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijikuta nikitaka kucheka, lakini nilimuonea huruma nilimsaidia kuvaa nguo zake na kumruhusu aondoke. Niliamini Side hakuamini jinsi alivyoachwa bila kuguswa. Baada ya kuondoka vita ikabakia kwangu, mume wangu aliamua tuachane.

    “Mi nafikiri tumeshindwana, siwezi kutunza uchafu ndani mwangu.”

    “Nami siwezi kukaa na mwanaume mchelemchele.”

    “Ndiyo nini, unanitukana?”

    “Sikutukani, ukweli ndiyo huo.”

    “Sawa hata ukinitukana, lakini kama nilivyosema kila mtu achukue ustaarabu wake kwa vile wewe ni kunguru hufugiki.”

    “Poa, mi’ kunguru nawe nyoka mtembelea tumbo unayetaka kukimbia wakati miguu huna, unataka wanawake vijana wakati mwenyewe nguvu za kupepea, utaliwa mali zako kila siku.”

    “Maliza matusi yote, leo ndiyo mwisho wa kufanya uchafu kwenye nyumba hii.”

    “Hii nayo nyumba wakiitwa wenye nyumba utapita wewe?” niliendelea kumpa makavu.

    Sikumlazimisha tulikwenda kwa mwana sheria na kugawana mali. Alinipa nyumba mbili za nguvu magari mawili na pesa za kuanzia maisha.

    Mtoto wa kike baada ya talaka, chaguo langu la kwanza lilikuwa Side Butamu mwanaume aliyenigusa nikagusika. Japokuwa nilitaka kumtoa roho baada ya kichaa cha mapenzi kunipanda. Nilimtafuta Side ambaye alikuwa amehama kufanyia kazi nje ya jumba la mtalaka wangu kuhofia usalama wa maisha yake.

    Baada ya kumpata niliushangaza ulimwengu kwa kuolewa na Side Butamu, hakika alinipa utamu usio niisha hamu. Kila nilipokuwa Side alikuwa pembeni yangu, japo wanaume wenye pesa zao waliniijia na dau kubwa kutaka kunitoa mikononi mwa Side.

    Kutokana na mapenzi mazito aliyonipa Side Butamu nilijikuta nikimuamini kupita kiasi. Niliyabadili maisha ya Side na kumfanya aishi kama mfalme kushona na kuweka viraka viatu vya wanaume wenzake akasahau. Kumbe mwanaume yule japokuwa mlemavu alikuwa na roho mbaya kuliko ya nyoka. Kumuamini kote na kumhurumia alitumia nafasi ile kunitapeli na kuchukua sehemu kubwa ya mali yangu, kitu kilichonifanya nichanganyikiwe na kuuza zilizobaki kisha kurudi kwangu.

    Baada ya kurudi nyumbani wanangu mliendelea kusoma kama kawaida kwa vile sehemu kubwa ya fedha yangu niliiwekeza kwenye elimu yenu. Baada ya kutendwa na Side Butamu ambaye wakati huo alikuwa amechukuliwa na shoga yangu, niliondoka huku nikijipanga kumfanyia kitendo kibaya.

    Kwa kweli Mungu atanisamehe Side Butamu nilimuua kifo kibaya sana. Niliwatuma watu wakamkamata na kumleta. Nilimtia kwenye gunia na kumpiga mpaka akapoteza fahamu kisha nilimmwagia petrol dumu la lita tano lote na kumtia kiberiti.

    Sikuondoka mpaka mwili ulipobakia majivu, alikufa kifo kibaya sana kwa kweli. Yale yalikuwa malipo ya usaliti baada ya kuyabadili maisha yake, lakini kumbe nilikuwa nafuga nyoka aliyekuwa na kunimeza. Baada ya kifo cha Side nilitimkia Mwanza ili kutuliza akili yangu kwa muda.

    Kama kawaida nilifikia hoteli niliyokaa siku za nyuma, fedha zilipoanza kuniishia nilirudi kwenye kazi yangu ya ukahaba kwa vile nilijiamini mtaji ulikuwa mwili wangu. Nilikuwa nikitoka usiku na kwenda kwenye hoteli za kifahari na kununua kinywaji kisha baada ya muda nilielekea msalani ili kuwakonga wanaume wakwale. Kutokana na umbile nililojaaliwa midume mikwale alinitolea macho na kurusha ndoano.

    Niliporudi ofa zilimiminika, niliangalia mwenye kisu kikali ndiye niliyetoka naye. Kwa vile nilirudi upya baada ya kulelewa na mzee Kupe, maisha ya ndoa yana raha zake niliamini kweli mimi kunguru sifugiki kwa kuyakataa maisha ya raha kama yale. Nilivyokuwa nimenawili na kupendeza kwenye macho ya wanaume nilijikuta nikiwaokota kama senene.

    Nakumbuka vizuri ilikuwa siku ya jumapili nikiwa hoteli ya Kapil Cabana, kama kawaida yangu niliagiza pombe ya bei mbaya na kunywa kidogo kisha nilikwenda msalani. Baada ya muda alikuja Mzungu kwenye meza yangu ambaye alijipendekeza kunilipia kisha aliomba usiku wa siku ile tuwe pamoja.

    "Upo peke yako au una mtu?" aliniuliza.

    "Nipo peke yangu."

    "Tunaweza kwenda?"

    "Bila wasi."

    Baada ya kinywaji niliongozana naye kwenye gari lake, tuliondoka hadi hotelini alipopanga. Ilionekana ni wale wataalamu kutoka nje ya nchi waliokuja kwenye miradi ambao hawajapata nyumba wanaishi hotelini. Alikuwa amepanga High Clasic Hotel. Kama kawaida usiku nilimpa mshikemshike na kumpa penzi zito lililomrusha akili.

    Tulijikuta tunafanya mapenzi kwa nguvu hadi kufikia hatua ya kuchoka wote kama majogoo yaliyochoka kupigana na kila mmoja usingizi ulimpitia. Niliwahi kushtuka na kumkuta bado akikoroma, saa ya ukutani ilinionyesha ni saa kumi na moja kasoro.

    Nilijikuta napata wazo la zamani la wizi japokuwa sikulipenda kwa kuhofia akiamka anaweza kunikamata na kunipiga kisha kuninyang'anya dola mia mbili alizonipa. Lakini roho nyingine iliniambia liwalo na liwe biashara ina kanuni mbili faida na hasara.

    Nilijinyanyua kitandani taratibu na huku nikimuacha Mzungu aliyenitajia jina lake Mr Hourison akiwa anakoroma. Huku nikitetemeka nilinyata taratibu hadi kwenye kabati na kuanza kupekua. Nilikutana na mkoba mdogo, nilipokifungua sikuamini macho yangu. Zilikuwa dola tupu kwa uoga haja ndogo nilishindwa kuizuia.

    Sikuwa na haja ya kuzihesabu nilizibeba zote, huku nikiwa natetemeka nilimuomba Mungu Mzungu asiamke. Nilivaa nguo zangu harakaharaka na kuupakatia ule mkoba kwa ustadi mkubwa.

    Nilipofika getini kidogo mlinzi anizuie hapo nilijua nimekwisha, nilimpa dola kumi na kuniachia nitoke. Nilipotoka getini tu, nilipata teksi mpaka hotelini. Niliingia chumbani kwangu nikiwa siamini, baada ya kufunga mlango nilizimwaga zile dola juu ya kitanda. Kwa furahanilizichota na kujimwagia. Nilikwenda kuoga kisha nilianza kuzihesabu, mmh! Sikuamini zilikuwa dola elfu ishilini na tano. Niliona umasikini umenitoka na wanangu mtaendelea kusoma shule muda wote wa uhai wangu hata kama nitatangulia mbele ya haki.

    Sikutoka mbali ya hoteli kwa muda wa wiki nzima, wakati huo taarifa za kuibiwa Mzungu na changudoa zilizagaa jiji la Mwanza na msako mkali uliendelea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Baada la tukio lile nilitoroka na kurudi tena Dar kwa vile Sibe Butamu hakujulikana amepotelea wapi. Nilitulia nyumbani kwa muda wa mwaka mzima. Lakini bado nilikuwa siwezi kuvumilia japokuwa nilipata bwana lakini tabia yake ya kunipiga kila akilewa ilinifanya niachane naye. Niliamua kupumzika tena nyumbani. Lakini siku moja mojamoja nakwenda viwanja ili nipate mwanaume kwa dau dogo. Nilikuwa kama mvuta sigara bila kupata hata pafu moja nilikuwa silali.

    Miaka ilikatika na wanangu mlisoma na kupata mafanikio makubwa kwa kwenda nje kusoma masomo zaidi na kufanikiwa kupata kazi nzuri.

    Wanangu wote kwa pamoja mlinijengea jumba kama kasri ya mfalme. Pamoja na maisha mazuri mliyokuwa nayo mlitaka kumjua baba yenu. Lakini kupitia maelezo yangu ya kina kila mmoja amejifahamu sidhani kama kuna mtu ataniuliza juu ya baba yake.

    Najua mwanzo niliwadanganya kuwa baba yenu alinikimbia na kuniachia watoto, lakini siri yangu ilikuwa moyoni. Kwa vile leo kila kitu kipo wazi ni wewe Martin pekee baba yako anajulikana ni Shauri Kati mchora Katuni.

    Pamoja na wanangu kunifanya niishi maisha kama nipo peponi, lakini damu ya ukahaba bado ilikuwa mwilini na kutoka siku mojamoja kwa siri. Sio siri ule usemi siku ya kwenda uchi ndiyo siku ya kukutana na mkwewe ilijidhihirisha.

    Kama kawaida nilitoka mara nyingi na kurudi usiku, nikichelewa sana nilirudi kabla ya alfajiri. Nilikuwa na wanaume zangu watano ambao yeyote aliyeniwahi aliondoka na mimi. Na ratiba yangu waliijua ilikuwa siku ya jumatano, jumamosi na jumapili.

    Siku hiyo kama kawaida nilikutana na mmoja wa wateja wangu kumbuka nilikuwa sifanyii ziki bali hobi. Tukiwa tunapata nyama choma na mtu wangu ili twende kwenye shughuli si ndio wakatokea wanawake zaidi ya watatu wakisema nimezoea kuwachukulia bwana yao na kuanza kunipa kipigo mpaka nikapoteza fahamu na kujikuta nipo hospitali.

    Kwa kuwa maumivu hayakuwa makubwa niliruhusiwa asubuhi na kuamua kurudi nyumbani. Kumbe ndiyo siku ya kuumbuka mbele ya wanangu.

    ****

    Baada ya maelezo marefu yaliyo watoa machozi watoto wake Moureen aliwapigia magoti wanaye wamsamehe kwa aibu waliyoiona. Wote walisimama na kumnyanyua mama yao na kumketisha kwenye kiti.

    "Mama huna kosa mbele yetu najua tabu zote ulizozipata ni kwa ajili yetu, sisi kama wanao tumekusamehe ila tunaomba msamaha. Tunaomba utusamehe kwa kuja bila kukutaarifu ni sawa kuingia chumbani kwako bila hodi. Lazima hali hii ingejitokeza.

    “Mama tusamehe sana kwa yote uliyosema imeonyesha jinsi gani ulivyokuwa na mapenzi mazito kwetu na kupitia mitihani mizito lakini ulisimama kidete kututafutia maisha mazuri wanao. Mama sisi wanao hatuna la ziada ila tunaomba tena utusamehe si wewe utuombe msamaha mkubwa hakosi," Martin mwanaye mkubwa alisema kwa niaba ya wadogo zake.

    Maneno yale yalimfanya mama yao abubujikwe na machozi huku akisema:

    "Wanangu najua leo ndiyo siku Mungu alifanya hivi kwa makusudio makubwa kama ingeendelea kuwa siri nami ningeendelea kufanya uchafu na kumkosea Muumba wetu. Najua wanangu mlitaka kunifanyia mama yenu Surprise lakini limegeuka aibu kwangu na kuumbuka mama yenu. Leo hii naahidi kuachana na mambo yote machafu na Mungu anitie nguvu, nasema ukahaba basi."

    Moureen alikumbatiana na wanaye kwa furaha na kusahau yote yaliyopita huku akiamini kuanzia pale amekuwa kiumbe mpya. Tokea siku ile Moureen aliachana na ukahaba na kumtafuta mzee mwenzie na kufunga ndoa ya uzeeni. Moureen mpaka anakufa hata sahau Surprise ya aibu iliyomkuta na mambo yake yote kuwa hadharani.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    T A M A T I



0 comments:

Post a Comment

Blog