Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

THAMANI YA MOYO - 1

 





    IMEANDIKWA NA : YONA FUNDI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Thamani Ya Moyo

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Thamani Ya Moyo...Maumivu Ni Haki Yangu





    Hali ya hewa ya ubaridi, uliyokuwa ikipinga vyema kilipo kitanda changu, kutokana na mvua iliyonyesha siku nzima ndani ya viunga vya jiji la Dar es salaam. Ilifanya kubadili mwili wangu kwa muda.

    Hakika baridi lilikuwa limenikamata vilivyo, nililitafuta shuka zito kwajili ya kulifukuza baridi. Hatimaye nilifanikiwa walau kupata ahueni, lakini kufanikiwa huko hakuniacha hivi hivi! Kuliniacha na namna nyingine kabisa. Baada ya usingizi kunipitia ulinipeleka mbali takribani miaka kumi iliyopita.

    Ilikuwa hivi!

    **************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majina yangu halisi ni Daudi Msomwa. Safari yangu ya maisha kwa kiasi kikubwa ilibadilisha na mazingira ni ngali mwanafunzi wa kidato cha tatu tu! Mwaka 2001, mazingira yaliamua kufanya vile yatakavyo katika maisha yangu. Nikajikuta na jenga chuki kali na sehemu iliyonipa hifadhi ya kuianza safari yangu ya kiitafuta elimu. Nikiwa kidato cha tatu tu nililazimika kuihama shule ya sekondari Askofu Adrian mkoba. Baada ya kutumia ushawishi mkubwa sana kwa wazazi wangu.

    Taratibu za kuihama shule nilizifanya haraka sana. Si kuwa na raha tena ya kuishi eneo hilo. Kila nilipokuwa nikinyanyua uso wangu na kuangaza huku na huku bado roho yangu haikuwa ikikubaliana nami kuendelea kuishi mahali hapo!

    Nilisahau kwamba ilinipokea kwa furaha sana miaka mitatu nyuma iliyopita, nilisahau ya kuwa nilishajizolea marafiki wengi wa namna tofauti tofauti, wale wa faida na hasara. Ilo si kuliwaza tena mazingira yalinichukia na kunitumbukia nyongo kabisa. Hatimaye nilihama na kuelekea shule nyingine mbali kabisa na mahala hapo. Hiyo yote ilichangiwa na sababu kadha wa kadhaa kwenye maisha yangu.

    _____________

    Katika Jumanne moja tulivu kabisa ya mwezi wa tisa mwaka 2001, safari ya kwenda katika mazingira mpya ndiyo ilipoanzia safari ambayo mpaka hii leo inaendelea kubaki kumbukumbu kwenye maisha yangu!

    Asubuhi iliyonga’rishwa vyema na nuru iliyoangaza kwenye dunia. IIinipa tena wasaa wa kuendeleza safari yangu ya elimu, punde tu nilipokelewa ndani ya shule ya sekondari ya Nguzuko . Baada ya kuoneshwa mazingira mpya ndani ya shule hiyo, kidogo nilijikuta nikitanabai. Tabasamu mwanana nilitoa mbele ya mama yangu pindi alipokuwa akinikabidhisha kwa uongozi wa shule hiyo.

    ______________

    Baada ya kupokelewa na uongozi wa shule na kumaliza taratibu zote za usajili. Nilifikishwa darasani na kupokelewa na wanafunzi, wengi wao wakiwa wanashangaa ujio wangu katika nyakati kama zile. Kwa kawaida tu huwa ni ngumu sana, wanafunzi kuhamia shule mwishoni mwa muhula. Hivyo ujio wangu ulikuwa wakushangaza.

    ____________

    Hata hivyo nilipata wasaa wakukaribisha vizuri sana! Baada ya muda mwalimu wa somo la Kiswahili aliingia darasani. Hivyo nami nikajumuika nao, kusoma kile walichokuwa wanafundishwa.

    Niliendelea kumsikiliza mwalimu kwa makini sana. Sikutaka kinipite kitu, mpaka anamaliza kipindi nadhani nilikuwa nimeelewa kuliko wanafunzi wote, na uzuri nililipenda sana somo la Kiswahili.

    Muda wa vipindi ulimalizika kwa namna ya kupendeza tu machoni mwangu. Wakati wote nilikuwa kimya sana, ushamba wa mazingira mapya uliendelea kunitesa. Kama mtu ambaye alikuwa amewahi kuniona huku nyuma angekuwa shahidi. Utulivu wa hali ya juu ulinitawala sana kuliko ilivyokuwa desturi yangu. Si kuwa yule ambaye aliyekuwa muongeaji huku nikiyamaliza yote yale yalikuwa yakija kwenye kinywa changu.

    ___________CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya siku kadhaa hatimaye niliweza kuyazoea mazingira, katika mwisho ya wiki moja kuna moja ya wanafunzi wa darasani kwetu alikuja kuniulizia habari za mpira. Mchezo ambao nilikuwa nikiucheza vizuri sana. Katika nafasi mbali mbali uwanjani. Ila kwa namna alivyokuja kuniuliza kama vile alikuwa akinidharau kwa maana sikuwa sawa kabisa katika jioni hiyo.

    Sikutaka kumwonesha hali ile. Pasipo na papara.Nilimjibu, huku nikwepesha macho.

    “Sijawahi kuupenda wala kucheza mchezo huo.” Nilimaliza hivyo.

    “Poa kijana”, alinijibu akionekana kugadhibika. Wakati huo hakutaka kuendelea kukaa karibu yangu. Alitimua zake.

    Si kutaji usumbufu sana kutokana na maswali yake ambayo niliona kama vile alikuwa akiongea pumba mbele yangu hivyo kuondoka kwake pia niliona baraka.

    Akili yangu ilikuwa mbali sana tofauti yeye alivyokuwa akiniona. Japo nilikuwa na miaka kumi na saba tu. Lakini tayari nilikuwa na jeraha la moyo. Moyo wangu ulikuwa umeshajeruhiwa. Mapenzi yalishauathiri moyo wangu na kuuacha na makovu katika kila pembe.

    Ungeniuliza kwa wakati huo kama nitakuja kupenda tena, basi jibu lingekuwa rahisi kuliko hata lilivyo kwa sasa. Janety alishafanya vile alivyokuwa akitaka kwenye moyo wangu.

    Msichana ambaye nilimpenda kuliko nilivyojipenda mwenyewe. Kwanini nisimpende? Ushawishi wake ulikuwa kivutio sana kwangu. Si kuwa na pesa la kusema pesa lingeongoza penzi letu. La sikuwa na pesa ya kuitwa pesa. Nilitegemea pesa za wazazi nazo zisingefaa kudumisha penzi langu.

    Loo! Kwa upande wa utanashati si kuwa mtanashati wa kutisha mbele ya watanashati. Mwili wangu mdogo, wenye kimo kisichopendeza kwenye macho ya wachaguzi wengi. Lakini hiyo hakuninyima kuipata nafasi ndani ya moyo wa Janety. Aliupa hifadhi moyo wangu na mimi nikapenda mazima. Nikayasahau kuwa ni hayo mapenzi ambayo kila kukicha watu wamekuwa wakiimba kuumizwa nayo. Labda ingenipa kumbukumbu nzuri ya kujianda kimazingira kuwa ipo siku nami ningekuwa muhanga wa mapenzi.

    Ndugu msikilizaji yasikie tu mapenzi ama ya furahie tu. Madhari usiombe ukawa muhanga wa mapenzi unaweza ukawa shahidi mzuri wa hiki nikisemacho.

    Miezi sita tu ulitosha kulifurahia penzi, sijui kilikuwa kimemsibu nini Janety? Si kuwa tena na thamani kwake, namna alivyokuwa akiniona ni kama vile ameona na mtu ambaye kamwe asingependa kumuoana kwenye macho yake. Si kuwa na jinsi tena sikupenda kumuona akijisikia vibaya kwa sababu yangu mimi.

    Taratibu mazingira niliyokuwa nikiyapenda nami yakinifurahia. Yakaanza kunichukia, yalinichukia vilivyo, kila nilipokuwa nikimuona Janety, ni kama vile kunadonge zito la chuki lilikuwa likinitawala.

    Kwa nini nijenge chuki kisa mapenzi? Suala hilo likaendelea kunitesa siku hadi siku. “Janety, Janety, ahhh!!! Ni vipi nijenge chuki nawe, chuki kisa mapenzi?” Kiapo nikakiweka kuanzia siku hiyo. Sitakuja kupenda tena na tena!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kuepusha kumwona Janety na mazingira nikayahama, lakini sasa alikuwa amejirudi upya kwenye moyo wangu. Nguvu ya penzi lake bado ilikuwa ikiishi nami, siku nzima niliyoona chungu.

    _____________

    Jioni ya siku hiyo, kulikuwa kuna mechi kali sana. Mechi ambayo ilituhusisha kidato chetu cha tatu na kidato cha pili. Nami niliamua kujumuika kwenda kuangalia mechi ile. Kipindi cha kwanza kilianza vizuri sana kwa upande wa timu yetu ilijipatia mapema goli. Goli ambalo halikudumu sana kabla ya wapinzani kufunga magoli mawili na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza.

    Namna walivyokuwa wakicheza mpira miguu yangu ilikuwa ikiniwasha sana, japo sikuwa na mpango wa kucheza ukizingatia nilishakanaa kuwa si chezi mpira. Hilo kidogo lilinitia shaka.

    Niliendelea kuvumilia nikibaki mtazamaji. Kidato cha pili waliendelea kutawala mchezo haswa haswa eneo la kiungo.

    Kwa namna walivyokuwa wakicheza, niliendelea kusoma mchezo kwa dakika kama ishirini hivi. Uvumilivu ulinishinda nikamuendea mwanafunzi ambaye alikuwa akijihusicha na kuisimamia timu yetu. Nikamueleza kile nilichokuwa nikiona huku nikimuomba niweze kuingia kulikoa jahazi.

    “Kaka naweza kupata nafasi?”,...Nilisita kidogo kisha nikaendelea kumsemesha….Aliniangalia kabla ya kuibuka na jibu.

    “ A...hhh.…sawa angalia viatu vya kukufaa ubadilike haraka.”

    Nilifanya kama vile alivyonigiza. Dakika chache nikawemo uwanjani. Kuingia kwangu uwanjani kuleta tumaini eneo la kiungo la timu yetu. Nilicheza kiufundi zaidi tofauti hata walivyokuwa wakitegemea. Hakika kila nilivyokuwa nikipata mpira niliwasumbua vilivyo wapinzani. Nikiwaacha midomo wazi washabiki wa timu pinzani.

    Kadri muda ulivyokuwa ukienda timu yetu ilipata uhai. Ilinichukua dakika tisa tu. Kuandika timu yetu goli la kusawazisha kupitia shuti kali la nje ya kumi na nane. Hiyo ndiyo ilikuwa kawaida yangu. Mara chache sana nikiingia uwanjani huwa na kosa kutoka na goli.

    Dakika zilizofata niliendelea kuwanyanyasa wapinzani vile nilivyokuwa nikitaka mpaka mpira unamalizika kidato cha tatu goli mbili na kidato pili goli mbili. Hivyo goli langu liwanyamazisha wapinzani.

    Nilizipokea pongezi za kila aina kila mtu akiyaongea yake. Nilikuwa kimya sana wakati tunatoka nje ya uwanja baada ya mechi kumalizika taratibu. Wakati huo sikuwa hili wala lile ghafla katika namna ya kushangaza.



    Sauti mbembelezi ya kike ilipenya kwenye ngoma za masikio yangu. Sauti ambayo ilikuwa ikipaza kusheherekea matokeo akilitaja na jina langu.

    Niligeuka kumtazama, hakuwa mgeni kwenye mboni za macho yangu. Pengine ingeongeza mshangao wangu la! Ni vile alivyokuwa akiningalia. Aliniangalia kuashiria kuna jambo tofauti zaidi na lile liliomfanya aniangalie kiasi hicho.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Si kujali kuhusu vile, haraka shingo yangu niligeuza kulekea kule miguu ilipokuwa ikiongoza. Si kutaka kuweka dhana ya dhania ndani yake. Kwa maana si vyema kulidhania jambo, wakati mwingine unaweza ukawa haupo sahihi. Na jambo la kutokuwa sahihi wakati mwingine linaweza kukugharimu pasipo kujijua.

    ____________

    Baada ya mechi ile iliyonifanya nijulikane haraka Nguzuko.Ndugu msikilizaji, maisha nikaanza kuyazoea, habari za Janety na ya Askofu Adriani mkoba, yakaanza kunipitia mbali. Sasa nikawa mtu wa Nguzuko rasmi. Msichana ambaye sauti yake ilisikika ikipaza akalisifia jina langu. Sasa tulifahamiana vyema kwa maana tulikuwemo ndani ya darasa moja tukiyatimiza majukumu yalituleta shuleni. Zaidi la zaidi iliyonifanya niwe na msichana huyu karibu. Ni uwezo wake wa darasani.



    Ni msichana ambaye binafsi alikuwa vizuri sana darasani. Alituongoza vile alivyokuwa akitaka tangu nihamie shuleni mpaka nilipoimaliza shule. Hakuna aliyekuwa akifurukuta.

    Ukaribu wetu uliongezeka zaidi kutokana na ushirikiano wetu katika vikundi mbalimbali vya masomo.

    Hisia za kupenda msichana huyo hazikufichika, ghafla nilijikuta nikimpenda japo nilishaapa kutopenda tena. Baada ya kile nilichokiona ni mateso ya moyo wangu. Lakini hisia za ghafla dhidi ya msichana huyo zikaendelea kunisurubu siku hadi siku.



    Kuna nyakati nilitamani kumweka wazi kwa kile nilichokuwa nikijisikia ila ugumu ukawa umenikumba. Mdomo wangu ulikuwa mzito kulitamka neno nakupenda mbele yake.

    Ni kama vile nilikuwa mtoto nikijifunza kuongea mbele ya mama yangu. Maneno yote nilikuwa nikiyamaliza lakini neno ‘nakupenda’ lilinishinda. Ni vivyo hivyo mtoto anapomaliza mama nyingi za kutosha lakini anashindwa kutamka neno la kuomba kujisaidia pindi anapobanwa na haja kubwa au kidogo.

    Ni kwa vile neno na kupenda kwangu nilihitaji kulitamka kwa thamani zaidi. Huku nikienda sambamba na thamani na ukweli wa moyo wangu juu ya kulitamka neno hilo mbele ya msichana ambaye ndio alikuwa mmliki hali ya majina haya. Zuhura Rahman. Japo nilishawahi kuyasikia majina mengi ya kufanana na jina hilo, lakini yeye alikuwa ana kitu cha ziada kwenye jicho la kawaida ni ngumu kuliona. Ni mimi pekee ndio nilikuwa nimefanikiwa kuliona pasipo mwenyewe kujua. Hakuwa wakutisha labda kwa uzuri wa umbo la, alikuwa wa wastani. Wastani wa kawaida usiochukiza mbele ya mwanaume mwenye jicho la tatu katika kuwatambua wanawake.



    Ni hapa ambapo iliwahi kunipitia kumkumbuku mwalimu wangu moja wa philosophy. Alipokuwa akiwashambua wanawake katika namna ambayo iliniacha hoi. Aliniambia kuna tofauti kubwa sana ya mwanamke na mke. Angalau wote wanajisia moja. Kwa vile alikuwa akimaanisha kuwa si kila mwanamke hana uwezo wa kuitwa mke. Katika hili alitoa mapendekezo kadhaa. Kabla ya mwanaume kuwa na mke. Kwa maana mke ni kilele cha juu cha mwanamke. Ni kilele kinachompa hadhi kila mwanamke mwenye sifa ya kuwekwa ndani na kuwa mke.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Basi Zuhura Rahman alikuwa ni aina hiyo ya mwanamke, nitampataje likawa swali lingine? Msichana ambaye sikuwahi kuzipata taarifa zake ya kuwa alishawahi kuwa kwenye mahusiano au la. Atanionaje nikiziweka hisia zangu wazi kwake? Atayapokeaje maneno yangu? Mtihani ukaza mtihani ndani ya kichwa changu. Siku hadi siku ukaendelea kuzaa majibu yasiyokuwa na tija kwenye kichwa changu. Mbaya zaidi alionekana kuyafurahia sana maongezi yangu ya kila kukicha, kiasi cha kwamba zilianza kusikika minongo’no ya kuwa nilikuwa nikitoka na msichana huyo. Nilikanusha vikali ingawa moyoni nilikuwa nikifahamu ni jinsi gani nilivyokuwa nikiumia.

    Naye kama alikuwa akifanya sifa aliendelea kunipagawisha kila nilipokuwa nikimuona kwenye mboni za macho yangu. Zuhura aliendelea kuninyanyasa moyo wangu. Moyo wangu ulitamani kusema vile ulivyokuwa ukijisikia. La ulibaki katika dhoruba kali.



    Ndugu msikilizaji asikuambie mtu kama kuna vitu katika dunia hii ambavyo vinaweza kukuacha na historia nzuri au mbaya katika maisha yako basi ni mapenzi. Mapenzi yanaweza kukutengenezea historia katika maisha, historia yenye kuweza kuwa na mvuto ama majuto ndani yake. Zuhura aliuteka moyo wangu pasipo kutegemea nami nilikuwa nimezama kwa mara nyingine, lakini sasa ndani ya kina kirefu cha bahari.



    Ni hapo nilipokili kuwa haya ni mapenzi. Mapenzi gani sasa likawa swali kichwani mwangu? Swali la kizembe pengine kati ya maswali yote niliyowahi kujiuliza ama kuulizwa.

    “Eehe Mungu ni epushe na jambo hili”, neno lilinitoka, machozi haya kuchelewa kuja. Nilililia kama mtoto. Nililia kwa sababu ya mapenzi. Nilisahau ya kuwa niliwahi kuwa sugu namba moja linapokuja suala la kupokea adhabu ya viboko darasani. Lakini sasa sikuguswa sehemu yoyote pengine ingenisababishia maumivu. Ikawa ndio sababu haswa ya kilio.



    Hakika mapenzi yalishanipoteza. Nilisahau kama ni hayo niliyokuwa nikiyafurahia katika miezi kadhaa ya nyuma. Janety alinifanya vile anavyotaka. Nikayachukika mapenzi nayo yakanichukia. Lakini sasa yalikuwa yamejirudi katika namna nyingine. Ni huyu Zuhura sasa amekuwa kikwazo ananirudisha katika dhana ya kupenda.

    Basi kwa namna hiyo aliendelea kunipagawisha nikiiamini ipo siku, nitapata kuwa naye. Wakati wote huo, si kuwahi kumgusia habari zote kuhusu mahusiano. Nilipenda kuheshimu sana hisia za mtu mwingine kama nilivyokuwa nikiziheshimu za kwangu. Ndio maana ilikuwa ni rahisi kuhama shule, madhari kuiweka sura yangu mbali na Janety ambaye penzi langu lilimtia kinyaa. Nami sikutaka kumtapisha. Nikayahama mazingira kwa urahisi kabisa pasina mabavu.

    ____________

    Kidato cha tatu tukawa tumekimaliza . Mwaka 2002 ukaingia katika namna nyingine, huku uzoefu ukiongezeka kwenye mazingira yale, urafiki wa kutosha kati yangu na Zuhura uliongezeka sana. Urafiki ambao ulizidi kuwaduwaza wale watafuta fununu ndani ya shule. Lakini jibu langu lilikuwa lile lile, sikuwa na mahusiano na msichana yule. Ndio moyo wangu ulikuwa umezama kwake ila ni yeye je? Hilo likaendelea kubaki kuwa kweli. Kweli usiyokuwa na usahihi kwenye kichwa changu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usahihi unatokea wapi? Mapenzi ni hisia. Hisia ziambatanazo na mguso. Mguso uhusisha pande mbili. Baina ya wale waliamua kuanzisha safari ya mapenzi. Na mguso huu utegemeana na lazima pande zote ziguswe ndipo zilete hisia. Hisia ambazo hupelekea kuzaliwa penzi.

    Mimi pekee ndio nilijifahamu kuwa nimeguswa. Lazima ni usemee moyo wangu. Yawezekana kuwa wake hakuguswa. Hivyo moja kwa moja kujidhirisha kuwemo ndani ya penzi hilo. Ni kosa kubwa sana. Kosa ambalo lingiweza kunigharimu na kuwapa nafasi, wapenda fununu kufurahi zaidi pindi zitakapo kuja habari mbaya ya kuwa Zuhura hakuwa akinifikiria mimi ama kuwa ipo siku atakuwa na mwanaume wa aina yangu. Kitu ambacho sikutaka kitokee hata kwa siku moja maana ingeniharibia kwenye harakati zangu.

    Niliendelea kuzichanga karata zangu, kwa namna ya taratibu sana. Nikijaribu kutaka kufahamu mtazamo wake. Huo ndio ukawa mtihani wangu wa kwanza katika kuhakikisha anakuwa wangu.



    Si kuwa na papara, nilitaji kumkimbiza mwizi pasipo kupiga kelele za kuitia mwizi. Hii ndio niliona ingekuwa njia nzuri ya kumkamata Zuhura.

    Unajua mwanaume unapojaribu kuingia katika mapenzi lazima uwe na kanuni kana kambwa unafanya mahesabu. Hivyo mbinu zangu zilikuwa za taratibu sana katika kuhakikisha na muweka sawa.

    Ajabu mwezi ulikatikana si kuweza kuambulia chochote. Nikaendelea kuumia. Kiuweli aliniweka katika namna nyingine. Bora ningekataliwa loo! Ningeugulia maumivu ya kukataliwa hatimaye kuitafuta dawa ya kupoza machungu ya kukataliwa naye.

    Kuna nyakati, alionesha kuwa kama yupo upande wangu. Hilo likawa linanipa tumaini. Lakini vikwazo vikawa vinajileta. Zuhura akiwa wa leo basi usitegemee kesho atakuwa huyo huyo! Kila siku akawa mtihani wa kuanza kutafuta majibu upya. Majibu ambayo haya kuonekana yanatija sana kwa upande wake. Basi nikaendelea kubaki kwenye mtihani.



    Wakati wote nilijitahidi kufanya kile ambacho nilikiona walau kingeniongezea alama kwa upande wake. Lakini ilibaki kuwa mtihani kwa upande wangu na mbaya zaidi katika siku moja ndio ilinichosha zaidi, katika moja ya mazungumzo yetu huku nikiamini kile alichokuwa akisema ndio sababu haswa ya kipindi chote kuingia katika mizunguko ambayo mwisho wa siku haikuwa na tija kwangu.

    Jina la Niko likahusika katika mazungumzo yetu. Niko hakuwa moja ya wanafunzi wa shule ya Ngazuko, Niko nilimfahamu vizuri kwa sababu niliwahi kusoma naye katika mwaka moja nyuma ndani ya shule ya Sekondari Askofu Adrian mkoba, hivyo jina lile halikuwa geni sana kwangu.

    Zuhura alimchambua Niko vizuri, vile alivyokuwa anajisikia. Hiyo hakunitia shaka mwanzoni, lakini siku hadi siku zilivyokuwa zinaenda. Nilianza kuhisi moja kwa moja huenda si kuwa nafasi mbele ya Zuhura, kwa sababu ya Niko yeye alionekana kunizidi nami nikionekana si chochote wala lolote.

    Ilizidi kuniweka katika hali tofauti mno. Ikianza kukatisha na wazo la kuwa na Zuhura, nikiamini vyema sasa sikuwa na nafasi kabisa na jambo la kumweleza ya kuwa nilikuwa nikivutiwa naye, na moyo wangu upo radhi juu yake. Ingekuwa sawa ya kujisumbua tu. Kwasababu akili yake tayari ilitawaliwa na mwanaume mwingine. Na ubaya kwa namna nilivyokuwa nimefanya uchunguzi wangu wa kina Zuhura hakuwa msichana ambaye unaweza ukayumbishwa katika maumuzi yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimfikiria Niko katika namna nyingine. Si kuwa bora sana kwake. Kuanzia darasani, hata utanasharti. Alionekana mpole kushinda mimi ambaye hakuna aliyekosa kulijua jina langu. Utundu wote ni kiwa naumaliza. Mdomoni ndio usiseme nilizungumza bila hata kuangalia vituo. Sasa katika kupambana na mtu mstarabu ambaye hata mimi nilikili ya kuwa sikuwa nikimzidi inapotokea mwanamke wa aina ya Zuhura.



    Ndugu naomba uelewe mwanamke wa aina ya Zuhura mara nyingi upenda kufanya machaguo katika kuingia kwenye mahusiano. Na mara nyingi utumia akili nyingi katika kufanya machaguo na kuingia katika mahusiano kwa taadhari kubwa sana. Na hicho ndio kilifanya mpaka mimi kufika kushindwa kupata ripoti yoyote iliyoonesha Zuhura alishawahi kuwa katika mauhusiano hapo nyuma.

    Ama kwa hakika nilikuwa ndani ya mtikisiko. Mtikisiko wa nafasi. Nilimpenda sana Zuhura lakini yeye hakuonekana kuvutiwa nami. Ushawishi wote nilioutumia lakini alibaki kuwa yule yule. Kuna nyakati nilijikanya mwenyewe kwa kuwa na ukaribu na msichana huyo. Kwasababu mazoea niliyoanza kuyajenga taratibu pasipo mategemeo. Ndio ilikuwa chanzo cha kuzaa penzi ndani ya moyo wangu. Penzi lilikosa sehemu ya kujihifadhi.



    Suala moja nilifikiria kujiweka mbali na Zuhura baada ya kuona uwezekano mdogo wa kumpata. Nilijitahidi kujiweka mbali naye haikuwa kazi nyepesi. Moyo wangu bado ulikuwa ukipata maumivu makali pindi nimuonapo na suala la kumwona halikuwa likizuhilika. Tulisoma darasa moja na ubaya zaidi bado aliendelea kuwa na mazoe nami.

    Ila nilijitahidi kumweka mbali kwa kuanza kujenga chuki ndani ya moyo wangu. Lakini bado nilishindwa. Kitu kimoja niliona kinafaa labda kujifariji kwa kulikosa penzi. Nikuanzisha mapenzi na Lina.



    Lina msichana ambaye kila kukicha nilizipokea ujumbe zake nyingi hakionesha kuhitaji huduma ya penzi langu. Hapo nyuma si kuwa tayari kuwa naye kutokana moyo wangu hakuwa haki yake. Hivyo kulikosa penzi la Zuhura likalipa nafasi penzi lake kwangu.

    Sikumpenda Lina kutoka katika moyo wangu. Ila nilitaji faraja zaidi kwenye kipindi kilichobakia pale shule ili niwe mbali na Zuhura huenda ningelisahau penzi lake. Hiyo ndio ilikuwa lengo langu haswa. Huku nikisahau, moyo wangu ulikuwa ukihitaji mapenzi ya dhati na si maigizo ya mapenzi.



    Nilijitahidi kuvaa uhusika wa kuwa na Lina, nikiweka taadhari Zuhura asifahamu husiano wetu. Ni kiviweka vikwanzo vingi kwa Lina ili penzi lake lisiwe huru sana, kufanya kila mtu aelewe pale shule.

    Lina alinipenda, alinisikiliza sana kile nilichokuwa nikisema. Ubaya tu moyo wangu ulikuwa hakuipata thamani yake halisi. Hivyo licha ya upendo wote alikuwa akiwoonesha Lina kwangu si kuumtilia manani kabisa.

    Siku zilienda ni kiwa shule nikijitahidi kiyaficha mapenzi ya Lina kwa Zuhura. Ili isitokee hata chembe Zuhura akafahamu husiano uliopo kati yangu na Lina.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waswahili hawakukosea kusema ‘penzi kikozi na kulificha huwezi’. Pasipo mategemeo katika jioni moja nilipokea ujumbe kutoka kwa Zuhura akinihitaji kuzungumza nami. Si kuelewa dhumuni la wito ule ila nilitoa uhakika kuwa ningeenda kuitia wito wake.

    Baada ya kufanya shunghuli zangu. Jioni mwanaume nilielekea kule nilipoitwa. Lakini nilichokuwa nakisika kwenye masikio yangu. Hakika kilininyongonyesha na kuhisi sasa nilishaipoteza thamani yangu kabisa.





    Naam! tuendelee kwenye sehemu ya nne tufahamu zaidi.

    Ni kweli yale maneno yalikuwa yakimtoka Zuhura kwenye kinywa chake. Hakuwa mwingine, kiasi cha kwamba ningeleta kipingamizi na kile nilichokuwa nakisikia.

    Kwa taratibu yaliendelea kupenya kwenye ngoma za masikio yangu, na kuniweka katika hali nyingine.

    Utetezi wa kile alichiokuwa anakiongea si kuwa nao. Huku nikiamini ni ngumu kuuficha ukweli. Aliongea kwa uhakika sana. Si kwa kuhisi kabisa. Penzi langu na Lina lilikuwa tayari kwa Zuhura. Akinipongeza kuwemo kwenye uhisiano na msichana hukuchelewa kunipa taadhari kubwa dhidi ya kuwa na msichana huyo. Akidai ya kuwa Lina hapo nyuma alishawahi kuwa na wanaume kadhaa. Na hao alishia kuachana nao bila kuwepo sababu maalumu.



    Zuhura aliongea sana, ni kama vile kuna jambo lilikuwa akilifikiria juu yangu.

    Maneno yake, yalizidi kuniweka sehemu tofauti sana nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu, kuupindisha ukweli lakini kweli ilibaki kuwa kweli. Si kuwa na cha kujitetea, hoja nilizikosa kabisa. Mpaka kikao hicho cha dharua kinaisha hakuna nilichoweza kuweka sawa.

    Sasa mambo yalikuwa hadharani. Mwanzo wa kuikikosa thamani ya moyo wangu niliyona kabisa kwenye jicho langu!

    ______________

    Wiki nzima kwangu ilikuwa mbaya sana, uso wangu kwa Zuhura nilishindwa kuweka. Ucheshi na uongeaji wangu ulipungua kabisa, suala hilo lilifanya hata baadhi ya marafiki zangu kuuona utofauti wangu, lakini si kuweka wazi kile kilichokuwa kinanifanya niwe vile mbele ya maswali yao lukuki.

    Katika wiki hiyo, nilijiweka mbali kabisa na Lina, si kutamani kumwona Lina, nilimwona kama adui yangu, ijapokuwa hapo mwanzo ilikuwa faraja yangu.

    Nilijuta maamuzi yangu ya kuwa na Lina, athari ya penzi lake, ilianza kuonekana kwangu. Hakika mapenzi yalianifanya nijione tofauti kabisa. Maumivu ya moyo hayakuwa na zuilika, mpenzi msomaji.

    Siku zilifaata uhusiano wangu na Lina ulivunjika ghafla, mimi ndio nikiwa muhusika wa kulitengenesha penzi hilo.

    Ijapokuwa penzi langu Lina lilimkolea sana, hata kitendo cha kutopata mawasiliano nami kwa kipindi cha wiki nzima kilinyima raha. Na haswa nilipomweka wazi ya kuwa mimi na yeye basi. Lina alilia sana! Alilia kwa sababu alionekana kunipenda kweli wakati mimi moyo wangu hakuwa kwake kabisa. Lakini hakuweza kuzuia kile nilichokuwa nimekipanga.

    ____________

    Baada ya kuachana na Lina, nilitumia muda mwingi sana, mpaka kuurudisha urafiki wangu na Zuhura ambaye kwake yeye bado hakuwa akiniweka katika mizani ya moyo wake. Ijapokuwa nilihisi huenda Zuhura alikuwa akitoka na Niko lakini, bado akili yangu ilikuwa ngumu kuamini moja kwa moja kama Niko anaweza kuwa na Zuhura.

    Kwa sababu nilimdodosa sana lakini niliambua kufahamu tu walikuwa ni marafiki kama nilivyokuwa mimi. Hivyo hiyo kidogo ikanipa nafasi ya kuamini ningeweza kuipata nafasi kutoka kwake, nami moyo wangu uweze kufarijika.

    Kwa vile nilimpenda sana Zuhura, hivyo suala la uvumilivu nikalipa nafasi sana, nikiomba Mungu Zuhura awe wangu hata ikiwa kwa miaka ya baadae, kwa sababu nilimpenda mno, nilimpenda katika namna ya kupenda.

    Yeye pekee ndio alimrudisha moyo wangu katika dhana ya mapenzi. Hivyo nilijitahidi kuonesha hisia zangu kwa ubunifu wa hali ya juu. Pasipo kujali yeye ana waza nini juu yangu, kwa maana nilihitaji kulitengeneza penzi.

    Niliamini kuna nyakati ni ngumu kupendwa ila unaweza fanya mwanamke akakupenda kwa sababu ya kulitengeneza penzi katika namna halisi ya penzi.

    Matendo yangu niliyofanya yaliashiria ni namna gani nilivyokuwa nikiguswa juu yake. Ijapakuwa yeye hakuwa akionesha mguso juu yangu.

    ______________CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwezi wa sita ulikuja kwa aina yake. Madarasa yote yaliingia katika mashindano, ya mpira wa miguu yaliyohusisha madarasa tofauti tofauti, pale shuleni.

    Kutokaa na uwezo wangu, hali ilikuwa tete kwa wapinzani, kila moja aliongea lake, jambo ambalo liliniongezea sana alama kwa Zuhura kwa namna vile watu walivyokuwa wakinizungumzia. Nami si kumuungusha mara kadhaa kabla darasa letu halijaingia kwenye mechi nilikuwa nikizungumza na Zuhura. Nikiyatoa magoli, nitakayo funga kwenye mechi husika kama zawadi yake.



    Kitendo hicho kilikuwa kinamfurahisha sana kwa maana aliupenda sana mchezo wa mpira. Na mimi nikipata nafasi yakuingia uwanjani nilikuwa sifanyi masihara, nilihakisha na toka na magoli ya kutosha katika kila mechi husika. Hapo nilikuwa nakijisikia raha sana, kutokana lilikuwa jambo muhimu la kumweka Zuhura katika hali iliyokuwa ikifanya hata kunifikiria.

    ***********

    Mpaka ligi tunamaliza darasa letu lilibuka mabingwa huku mimi nikibuka mfungaji bora.

    Jina langu lilizidi kuwa kubwa walinizungumzia kila kona ya Nguzuko visichana navyo vilinipapatikia mno. Lakini hakuna ambaye alipata nafasi kwangu, moyo wangu alikuwa nao Zuhura, si kuona wakumkabidhi, hivyo nilijiweka mbali sana nao.

    _____________

    Jioni moja baada ya mashindano kuisha, niliupokea ujumbe kutoka kwa Zuhura, ni kiwa sehemu ya kuchukua chakula, kitendo cha kupokea ujumbe wake, ambao sikujuwa ndani yake ulikuwa umeandikwa nini, kilinifanya hata chakula nile kwa haraka haraka.

    Nikiwazia sehemu ambayo nitapata utulivu wa kusoma ujumbe wake.

    Kweli baada ya kutoka sehemu ya kulia chakula. Kwa vile siku hiyo tulikuwa hatuendi darasani jioni kwajili ya kujisomea hivyo nilivyomaliza tu, niliwahi bwenini kwenye kitanda changu.

    Nilianda mazingira mazuri ya kusoma ujumbe wake pasipo mtu kunifatiria, baada ya kuhakikisha niliweka sawa mazingira . Dakika chache mikono yangu ilikuwa ikipambana kufungua ujumbe ule. Macho nayo hayakuchelewa kuyasoma maandishi yalichanganyika na herufi ndogo na kubwa. Nilisoma taratibu sana, nikirudia rudia kwa umakini wa hali ya juu.



    Maandishi yale yalibaki kuwa vile vile. Hakuna kilichokuwa cha ajabu zaidi ya kuonesha ni jinsi gani alivyokuwa akiguswa na uwezo wangu wa kucheza mchezo wa mpira, akinisifia sana.

    Maandishi yake yalinipa faraja sana, hakika niliona sasa Zuhura alishaanza kunielewa taratibu.

    Usiku wote nilishi kwa kucheka cheka, utadhani nilikuwa nikienda kuwa chizi katika muda mchache, hata wanafunzi wenzangu walibaini hali ile. Kikweli nilifurahi sana!



    Asubuhi ilifika kwa aina yake, maana nilivyo ulaza mwili wangu juu ya kitanda, ndoto nzuri ya mapenzi ilipita nami, nikumuota Zuhura, katika ndoto hiyo.

    Niliamka kwa tabasamu moyoni mwangu.Tabasamu ambalo sikujuwa lilikuwa likimaanisha nini?

    Daudi Msomwa bado ana unguluma. Sasa ndani ya tabasamu ambalo hakujua linamaanisha nini kwenye asubuhi ya aina yake? je nini jambo gani hilo? Ni kusihi tu ndugu msikilizaji kuendelea kufatiria simulizi hii…Hakika ni Thamani ya moyo.. maumivu ni haki yake

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog