Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

THAMANI YA MOYO - 2

 





    Simulizi : Thamani Ya Moyo

    Sehemu Ya Pili (2)



    Thamani Ya Moyo...Maumivu Ni Haki Yangu



     iliishia, baada Daudi Msomwa kusindikizwa na barua ya kuvutiwa kutoka kwa Zuhura, lakini mambo yanakuwa tofauti licha ya kuanza na tabasamu lenye kuvutia kwa upande wake. Je ni jambo gani hilo? Naam tuendelee kwenye sehemu hii ya tano.

    Siku ilianza kwa kupendeza sana machoni mwangu, ikiwa jumapili tulivu kabisa, baada ya kufanya sala kama jumapili zingine.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mapema tu si kuchelewa kumtafuta Zuhura, kwajili ya kuisikia sauti yake kuendana na matakwa ya moyo wangu ulivyokuwa ukiniendesha. Ajabu ilikuwa tofauti sana Zuhura hakuwa yule wa siku mbili za nyuma. Alionekana kuna jambo zito linamkabili. Maana hata maongezi yake, haya kuwa yakionesha kufurahia ujio wangu pale. Tulitumia kama dakika tano kuzungumza kabla kila mtu kutafuta mahali pa kwenda.

    Jambo ambalo lilizidi kunipotezea uchangamfu nilio amka nao.

    Si kuwa na jinsi niliamua kuitafuta sehemu ya kwenda kujichimbia ili kuuridhisha moyo wangu.

    Siku iliishia katika namna hiyo, na ubaya zaidi kama ilivyokuwa katika siku hiyo hata kwa siku mbili mbeleni zilikuwa hivyo. Mawasiliano hafifu na Zuhura, yalikuwa ndani yetu, sikulijua tatizo, au ni wapi nilipokuwa nimekosea? Fikra zangu hazikunipa majibu sahihi katika wakati adimu kama huo.

    Walau tumaini nilikuja kulipata katika siku ya nne. Ni kama vile Zuhura alikuwa akiniigizia. Uchangamfu ulirejea tofauti hata na siku nne zilizokuwa zimepita. Katika kubaini ni jambo gani haswa lilikuwa likimsumbua. Baada ya dodosa dodosa yangu nilifahamu jambo lilikuwa likifanya mawasiliano yetu kuwa hafifu.

    Kumbe ilitokana na kuingia katika siku zake. Nilitamani kucheka, kicheko kikubwa. Kumbe suala la yeye kuingia kwenye siku zake wengine tulianza kuonekana maadui kwake, na hata kutokosesha raha kabisa. Hakika mapenzi yaliendelea kunitesa! Ati! Tatizo la mwingine lilikuwa tatizo langu!

    Baada ya jambo hilo kupita mambo yalikaa sawa, hakuna kilichonekana kuharibu furaha yake, nami nikaendelea kujisogeza taratibu. Lakini nafasi bado ilikuwa ngumu. Na kumbuka kuna kipindi nilipokuwa nikigusia habari za mapenzi Zuhura alijitahidi kwa kiasi kikubwa kubadili mada katika namna ambayo hata mimi ilikuwa ikinifanya kukosa muendelezo wa kile nilichokuwa na kizungumza, hivyo kugeukia katika habari za kawaida. Lengo lilikuwa kuepusha kumuuzi na hata kuleta ukinzani wa maneno yangu.

    Hivyo nikaendelea kubaki na maumivu pasipo kuipata dawa yake, dawa ilionekana kuwa mbali na mahali nilipo.

    Angalabu misemo ya waswahili kama ile ya uvumilivu hula mbivu, pole pole ndio mwendo, ilikuwa kama ganzi ya kupoza maumivu yangu ya mapenzi. Kwa maana juhudi zangu zilionekana kugonga mwamba. Nikitaji kuvumilia zaidi ili kufikia siku ambayo Zuhura angelikuwa wangu.

    _______________

    Miezi ya kumaliza kidato cha nne iliendelea kubaki michache huku tukiziongeza juhudi katika masomo. Zuhura hakusita kunielekeza pale nilipoonekana mbovu nami sikusita kumuelekeza pale alipokuwa kuna mshinda. Hiyo iliendelea kuongeza ukaribu wangu na Zuhura. Kitendo ambacho kilizidi kutafsiriwa vibaya na baadhi ya wanafunzi hata walimu, lakini mimi niliendea kubaki na ukweli wangu.

    Na kumbuka jambo hilo liliwahi kuibua mgogoro mkali kati ya Zuhura na Lina. Lina akidai kuwa Zuhura ndio chanzo haswa, cha mimi kuachana naye. Lakini nilijitahidi kuliweka sawa, baada ya muda kila mtu aliendelea na maisha yake. Mimi nikiisaka thamani ya moyo wangu, pasipo kuchoka.

    Siku hazikuongopa hatimaye kidato cha nne tukakimaliza, hakuna kilichobadilika Zuhura alibaki kuwa yule yule.Katika mwanzo mwingine. Mwanzo wa mboni zangu kutomwona Zuhura. Nililijua hilo hata nilipoanza kujianda kimazingira lakini hakunisaidia kitu.

    Siku ya mahafali yetu, si kuwa na furaha kabisa kama wanafunzi wengine. Furaha ingetokea wapi? Wakati nilijua wazi huo ndio mwanzo ramsi wa kumpoteza Zuhura huku nikiishi na ndoto za kuwa na mwanamke huyo. Mwanamke ambaye nilimpenda katika maana halisi.

    Nambari yangu ya simu niliyompatia hakunifanya kazuia kuwa katika hali mbaya zaidi, kwa maana haikuwa siku wala wiki hata mwezi hakuna nilichokisika kutoka kwake, hata ile sauti yake mbembelezi sikuitia masikioni mwangu kabisa!

    Tabasamu lake likawa linanyanyasa kila kukicha katika ndoto zangu, zilizokosa tumaini la kuonesha kuwa punde ningeweza kupata mawasiliano na Zuhura.

    Habari za Niko zikajirudi upya kwenye kichwa changu na kuanza kuninyasa kwa aina yake. Nilizitafuta nambari za Niko kwa juhudi sana, hatimaye katika wiki kadhaa nilizipata.

    Maongezi yangu na Niko hayakuweza kunifanya kunga’mua chochote ambacho labda kingenifariji. La hasha Niko alionekana kuwa msiri zaidi na kila nilipojitahidi kutaka kufahamu ukweli juu ya Zuhura, hakuonekana kunipa ushirikiano kabisa. Si kuwa na ubavu wa kubadilisha kile kilichokuwa kinamtoka kwenye kinywa chake nami nilichokuwa nikasikia kwenye masikio yangu. Zaidi ya kunisabibisha maumivu makali. Maumivu walikuwa yakisabisha na wivu. Wivu wa namna ya ajabu zaidi. Penzi lilikuwa likiniendesha puta.

    Labda ni seme kitu kimoja tu, ‘mapenzi ni zaidi ya silaha kwenye vita’.

    Mapenzi wanaweza yakaamua maisha ya mtu na hata, hapa ufikia watu kujitoa uhai kwa sababu ya kile ambacho nyoyo zao hukosa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa namna hiyo wivu mkali uliendelea kuninyasa baada ya kulikosa penzi la Zuhura, nikianza kujenga uadui na Niko. Nikidhani yeye ndio alikuwa akiniletea kipingamizi kulikosa penzi la Zuhura.

    Taratibu hata ule urafiki nilikuwa nao na Niko nyuma ukaanza kuondoka, chuki kali dhidi yake ilianza kujengeka ndani ya moyo wangu. Si kumtamani rafiki wa aina yake. Simu zake si kuwa nikizipokea kabisa, nilijitahidi kujiweka mbali naye. Nikiendelea kuugulia maumivu ya kumkosa Zuhura. Kwa maana nilimkosa kwa vyote, si kupata kuisikia sauti yake, kabisa walau ingenipoza machungu ya kutoiona sura yake.

    _____________

    Nyumbani kukanizoea, sasa ni kawa mwana kijiji rasmi, harufu ya uwanafunzi ikinipotea kabisa. Nilijitahidi sana kumsahau Zuhura, ilitumia muda mwingi mno. Hatimaye hali ya kukaa bila kuisikia sauti yake ikaanza kunijengea mazoe, moyo wangu ukiweka utayari wa kuzoe hali ya kulikosa penzi la msichana huyo, nikijiweka mbali sana na masuala ya mapenzi.

    Nilicheza mpira kwa ustadi wa juu sana. Hiyo ikichangia sasa kuniweka mbali na masuala ya mahusiano. Kwa maana si kuona msichana thabiti mwenye kuweza kuvaa viatu vya Zuhura, ijapokuwa sikuwahi kumtamkia yakuwa ninampenda na hata yeye kunitamkia ananipenda lakini ndani ya moyo wangu, aliendelea kuwa mtu muhimu sana. Hivyo kulikosa penzi lake, lika halalisha moyoni mwangu kuifunga nafasi ya mapenzi ndani yake.

    Si kuona umuhimu kabisa wa kuwa na mpenzi. Niliyaogopa mapenzi. Si kuhitaji tena kuwa muhumini wa mambo hayo. Mpenzi wangu akabaki kuwa mpira.

    Miguu yangu ilinisaidia sana katika kutekeleza kile ambacho kichwa changu kilikuwa kimedhamiria. Ili kuutakasa moyo wangu. Maana moyo hauna kazi pekee tu ya kusukuma damu la hasha. Dhana ya penzi na mapendo ndipo chimbuko lake halisi haswa!

    ____________

    Mwaka uliisha, mwaka mpya uliingia na mashahibu mingine kabisa. Ni kama vile nilikuwa ndotoni la hasha si kuwa kwenye ndotoni, nilikuwa ndani ya uhalisia kabisa. Lakini sasa nilikuwa nikipambana na kile nilichokuwa na kiona, kwa namna iliyokuwa ikitaka kunidhalilisha.



    Nilimpenda Naomi katika utoto wangu, nikimuweka katika sehemu nyingine kabisa. Umbo lake, la wastani. Ngozi yake ya maji ya kunde, akiwa na urefu wastani. Ilikuwa kivutio kikubwa kwenye mboni zangu. Akili yangu ya kitoto kabisa nikisumbuliwa na balehe yangu ya kwanza, ilinipa ushawishi sana wa kuwa na Naomi. Sijui nini ambacho kilimvutia kwangu? Alionesha kuwa akinipenda sana. Hata nami kujisifu kwa wenzangu kuwa na msichana wa aina yake.



    Na kumbuka kabisa mboni za macho yangu zilionana na Naomi kwenye ligi ya kitongoji chetu, ni kiwa nahodha wa timu yetu katika mechi ya fanali, ambayo tulifanikiwa kuchukua kombe kwa ushindi wa magoli matatu ambayo mimi nilifunga goli moja. Nikichangia upatikanaji wa magoli mawili. Kiwango nilichokionesha katika mechi hiyo kilivutiwa na kila mtu, na kukonga nyoyo zao barabara!

    Hapo ndipo nilipopata kuona na msichana huyo ikiwa sura ngeni kabisa katika kitongoji chetu, alionekana mgeni bila shaka. Hata kwenye maongezi yetu niliweza kuling’amua hilo. Huo ndio ukawa mwanzo wa mazoea dhidi yake na kisha kuzaa penzi.



    Sababu mbali mbali zikanifanya kulikosa penzi lake. Umbali, shule na mambo mengine mengi yalinifanya kuwa mbali na msichana huyo, wakati huo kichwa changu kikipoteza kumbukumbu sahihi kama nilishawahi kuwa na msichana wa aina yake.

    _________

    Nilijikaza kiume baada ya kumbukumbu yake kunipitia nikiondoa mshangao wangu. Kinywa changu hakikupata tabu kilitaja jina lake. Niliita kwa sekunde kadhaa. Naam! Masikio yake hayakuchelewa kuipokea sauti yangu, hakuchelewa kugeuka kutazama mahali ilipokuwa ikitokea.

    Ghafla macho yetu ya kagongana, alionekana kama amepigwa na butwaa asijue cha kufanya. Mdomo wake ulibaki wazi kwa nutka kadhaa, kabla ya miguu yake kuwahi kunisalimu.

    Harufu nzuri ya marashi ilipokea pua yangu punde nikaanza kuisikia sauti yake. Kiukweli alikuwa amebadilika kila kitu, sauti tu ilinipokea kwa mabadiliko makubwa. Achana na kile nilichokuwa nakiona kwenye macho yangu. Miaka mitatu kama na nusu tangu mboni zangu zilipomuona, msichana huyo zilikili wazi sasa alikuwa amebadilika haswa! Na hata kuongeza mvuto zaidi kwa yule aliyekuwa anamtazama.



    Mdomo wangu ulishindwa kuchagua maneno yapi sahihi ya kuzungumza kwa nyakati huo, zaidi la zaidi ulitoa maneno ya kusifia kile ambacho macho yangu yalikuwa yakipambana nacho.

    Kuepusha macho ya watu, kitendo cha kuzungumza naye kwa dakika kama tano. Nilipata wasaa wa kunakiri nambari yake ya simu kwa mawasiliano zaidi.

    _____________

    Nilijitoa eneo hilo, nikiwahi kwenda uwanjani kwajili ya maandalizi ya mechi. Mechi ambayo ilikuwa ya muhimu sana katika kukaribisha mwaka mpya. Ijapokuwa si kuchelewa mazoezini lakini, hata ufanisi wangu katika mazoezi haukuwa kama kawaida. Nilicheza kwa kiwango cha chini sana na hata nilipokuwa nikiulizwa na kocha kulikoni? Nilijitetea tu ni kwajili ya kugopa kupata majeraha. Ilikuweza kucheza kwa ufasaha katika mechi hiyo.



    Kocha hakuwa na kipingamizi kwa maana kisingizio changu kiliendana na ukweli. Lakini sababu ya kufanya vibaya kwenye mazoezi nilikuwa naijua mwenyewe. Maana kitendo cha kumwona Naomi ikiwa takribani miaka kadhaa sikupata kumwona, namna ambavyo macho yangu yalivyopokea jambo lile nilijikuta tu mawazo dhidi yake yanajia na kushindwa kuwa makini na kile nilichokuwa na kifanya.

    Mawazo ambayo nilishindwa kuyatafsiri mwanzoni, lakini niliporejea kutoka uwanjani, mambo yalikuwa tofauti sana. Jambo la kwanza tu baada ya kupata chakula cha jioni, nilingia ndani mapema kuliko kawaida yangu. Kitu cha kwanza tu ilikuwa nikiungaika na simu, kunakiri ile nambari aliyonipatia kwajili ya mawasiliano.

    Kweli baada ya kunakili nambari zile, na kubonyeza kitufe cha kupigia simu. Hazikupita sekunde nyingi simu ilipokelewa, sauti nyororo ya Naomi ilipenya kwenye ngoma za masikio yangu. Kwa uhakika zaidi alikuwa ni yeye.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alinipa dakika kadhaa za kuzungumza kabla ya kukata simu kwa miadi ya kunipigia baada ya lisaa limoja. Sikubisha nilitikia.

    Muitikio ambao sasa ulianza kutafunwa na ile ahadi. Lisaa limoja niliona lingi sana. Dakika hazikuoneka kwenda kabisa shauku ya kutaka kumsikia Naomi ilinizidi. Hakika nilishikwa na kihoro cha kuisubiri sauti yake. Ni kama vile nilikuwa nikisubiri ahadi za ukombozi.

    Nusu saa, lisaa likatimia. Alikuwa akienda na muda, hakupita hata dakika moja. Simu yangu ilipata uhai. Hakuwa mwingine nambari ya Naomi. Niliweka koo langu sawa kabla ya kuipokea simu yake kwa utulivu wa hali ya juu. Maongezi hayakuwa madogo, masaa matatu yaliisha, ikiwa ameimaliza vocha yake, na hata ya kwangu haikutosha kukamilisha maongezi.



    Tulizungumza mambo mengi mno ya zamani yalitawala maongezi ya sasa yakichukua sehemu chache. Vicheko vikisindikiza maongezi yetu. Mpaka simu inakitika kila moja alionekana ana hamu ya kuzungumza na mwenzake.

    Ilikuwa ngumu kuupata usingizi, niliubembeleza sana mpaka nilipoupata.

    Asubuhi ilikuwa tofauti sana, mara nyingi huwa na wahi kuamka hata kwenda kufanya mazoezi binafsi. Lakini kwa siku hiyo ilikuwa tofauti sana. Hakuna kilichofanyika. Saa ya ukutani ilinipokea punde tu macho yangu yalipoanza kuipokea nuru. “Saa nne na nusu!’’ Kwa hamaki nilikurupuka kitandani, ni kiwa si amini. Hata nilipoliendea dirisha mwanga mkali wa jua ulipenya kwenye macho yangu. Ikihakishia kile nilichokuwa na kiona hakikuwa na tofauti hata kidogo.

    Haraka nilienda bafuni. Niliweka mwili sawa.



    Nilipojitoa bafuni nilianza kukaribishwa na harufu nzuri ya kile ambacho mama alikuwa amekianda kwajili ya kufungua kinywa. Sikutumia dakika nyingi, kuvaa. Ndani ya dakika chache nilikuwa nikisalimiana na mama jikoni.

    Niliweka sawa mazingira ya kupata kifungua kinywa, baada ya kupata kifungua kinywa. Si kuchelewa haraka nilijitoa nyumbani na kuelekea dukani, kwajili ya kujipatia vocha kwa miadi ya kuwasiliana na Naomi

    Sasa Naomi alionekana kuchukua nafasi kwenye kichwa changu. Bila kujua nini ambacho mbele kinakwenda kutokea, na kama ningelijua hakika. Ni singejiweka karibu na msichana huyo.



    Lakini ‘ninge’ waswahili wanena kuwa huja baada ya mwisho wa safari.

    Hivyo kitendo cha kujitoa ndani. Haraka niliokuwa njiani kuelekea dukani. Nukta kadhaa duka likanipokea, si kutumia muda mrefu nilikuwa ndani ya chumba changu, nikiweka mazingira mazuri ya kuwasiliana naye.

    Niliweka tarakimu zilizokuwa ndani ya kadi ya kuongeza salio. Kisha si kuchelewa kumpigia. Pasipo mategemeo simu yake iliita sana, nilijaribu mara kadhaa.

    Kabla ya upande wa pili kupokea, lakini sasa mdomo wangu ulionekana huu mzito, masikio yangu yakishindana na kile kilichokuwa kinasikika.



    Ilikuwa sauti ya tofauti kabisa kwenye ngoma za masikio yangu, katika namna ambayo sikuitegemea. Nilishindwa pakuanzia na hata pakumalizia.

    Haraka, niliona vyema kuikata simu. Hofu ilinipita, ghafla moyo wangu ulienda mbio kupita maelezo, mikono ikiwa inanitetemeka.

    Dakika moja nikawa na pambana kufikiria kile nilichokuwa nakisikia. Sauti nzito ya mwanaume aliyeonekana wa makamo ilinitisha zaidi. Nikitia shaka huenda akawa baba yake Naomi aliyepokea simu.

    Mawazo mabaya juu ya kile yalinipitia nusu saa mzima, kabla ya kichwa changu kukaa sawa. Nikiweka kujiamini kwa chochote ambacho kingeenda kutokea kwa upande wangu.



    Nilishinda ndani muda wote, nikisubiri simu yangu kuita ili walau kuisikia sauti yake. Taratibu aliaanza kuningia kwenye fikra zangu, kumbukumbu za zamani zikiwa chanzo cha kuniweka katika hali ya kunifikirisha sana.

    Nilisubiri simu kutoka kwake, ajabu mpaka muda najiandaa kwenda uwanjani sikuipokea simu yake, hiyo ilinijengea hofu zaidi. Niliamua kuliweka pembeni swala lake, kwa miadi ya kutamfuta tena nitakapo rudi kutokea uwanjani.

    Nilipoweka mambo sawa nyumbani nilimuaga mama kuelekea uwanjani muda ukiwa umeenda sana tofauti, maana zikibakia dakika chache kabla mchezo kuanza. Ilikuwa tofauti sana kwa upande wangu katika siku hiyo, kwanza nilichelewa uwanjani, pili si kuwa na morali ya kutosha katika kuanza kwenye kikosi. Jambo hilo hata kocha aliliona mapema sana. Hivyo hata kwenye kikosi kilichoanza kuingia uwanjani mimi sikuwemo. Kitu ambacho kiliwashangaza wachezaji wenzangu na washabiki wa timu yetu kwa ujumla.



    Kwa upande wangu niliona amani kabisa kwa maana nilikuwa nikiona nisingecheza vizuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo, hivyo kuanzia nje nilioana kunafaa zaidi, sababu kingeniongezea hamu ya mchezo na kufanya vizuri zaidi kadri muda ulivyokuwa ukienda.

    _______________

    Mechi ilianza kwa kasi sana. Timu zote zikifanya mashambulizi kwa zamu, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu ambayo ilifanikiwa kupata goli la kuongoza.

    Wakati wote mimi macho yangu hayakuwa yakitulia sehemu moja. Yalihangika kupambana na shauku ya kumwona Naomi pale uwanjani, nilijitahidi kwa kiasi kikubwa nikijipa tumaini huenda ningefanikiwa kumuona. Kwa maana nilijuwa wazi asingekosa kufika kutokana na mechi yenyewe ilikuwa ikituhusisha timu yetu ya kitongoji na timu ya kitongoji kilichokuwa karibu nasi, hivyo mechi ilikuwa inaupinzani mkali hata kufanya kushuhudiwa na watu wengi, vile vile kuwemo baadhi ya viongozi mbalimbali wa serekali. Jambo ambalo lililofanya kuongeza utamu wa mechi yenyewe. Hivyo kwa jinsi watu walivyokuwa na shauku na mechi yenyewe nilijuwa wazi habari zile hatakuwa amezipata na kushawishika kuja kuangalia kile kilichokuwa kinaendelea.

    *********

    Niliangaza huku na huku wakati kocha akitupatia maelekezo kabla ya kuanza kwa kipindi cha pili, kwa mbali macho yangu yaliweza kumoana msichana ambaye baada ya kumtazama kwa muda mrefu niliweza kubaini alikuwa ni Naomi, hapo hata hamu ya kuingia uwanjani iliongezeka. Nikijiweka ahadi ya kulitafuta goli, punde tu kocha ataponipatia nafasi ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilisikiliza maelekezo ya kocha, nikiwa mbali kimawazo, ghafla kocha aliniambia nijiandae kuchukua nafasi, haraka nilibadilisha nguo.

    Kitendo cha kuanza kwa kipindi cha pili, nikingia kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine. Mchezaji aliyevaa beji ya unahodha, haraka alinikimbilia na kunipa kitambaa cha unahodha kwa heshima kwa maana mimi ndio nilikuwa nahodha mkuu katika timu yetu. Kitendo hicho kiliniongezea kujiamini mno, hazikuchelewa kuibua shangwe uwanja mzima.

    Wapinzani wakianza kupata tumbo joto kutokana na kufahamu vizuri uwezo wangu, jambo ambalo walianza kuongeza ulinzi.



    Taaratibu nilianza kutawala mchezo, siku hiyo ilikuwa tofauti sana kwangu, uwezo wangu uliongezeka zaidi, niliwachambua viungo wa timu pinzani, hawakuchelewa kunikwatu kwatu. Nami si kuchelewa kuwaadhibu kwa mpira wa adhabu moja wapo ambao niliupiga vizuri na mguu wangu wa kushoto ulingia moja kwa moja golini, na kupatia timu yetu goli la kwanza, kitendo ambacho hakichukua muda mwingi nilifanikiwa kufunga goli lingine.

    ___________

    Hakika siku hiyo nilicheza kwa kiwango cha juu kuliko hata nilivyokuwa na tegemea, mpaka mchezo unamalizika timu yetu ilibuka na magoli mawili ambayo yote niliyafunga kupitia mguu wangu wa kushoto.

    Nilifarahia mno matokeo, wakati filimbi ya mwisho mwamuzi inapigwa kumaanisha kumalizika kwa mchezo, si kuchelewa kuzipokea pongezi kutoka kwa watu mbalimbali.

    Wakati wote akili yangu ilikuwa kwa Naomi tu! Niliangaza huku na huku, hakika kama yeye alikuwa pamoja na mimi naye. Haraka alivyoniona aliniwahi kuja kunipongeza, akinikumbatia pasipo hata kutegemea, jambo ambalo liliangaliwa na watu wengi sana likiacha sintofahamu kwa wale walikuwa wakishuhudia kitendo kile.



    Lakini sikukijali sana. Nilipopata wasaa dakika kidogo za kuzungumza naye machache, nikamsisitiza anitafute usiku wa siku hiyo, kwa maana eneo lile sikuliona kama lingefaa zaidi kwajili ya mazungumzo yetu. Hakuwa na tatizo alinielewa, nyakati hizo ambazo kila mtu akijitafutia njia ya kurudi kwao.

    Kwa vile wachezaji tulitakiwa kurudisha vifaa vya michezo kabla ya kurudi manyumbani. Hivyo niliwahi katika mkusanyiko wa timu, tukayapokea maelekezo kutoka kwa mwalimu, wakati huo mimi nikishungulika na zoezi la kukusanya vifaa. Baada ya zoezi hilo tulitawanyika na kurejea nyumbani.

    Nyumba ikanipokea, pongezi kutoka kwa mama nazo nikazipokea, mama yangu alinipenda sana na namna nilivyokuwa nikitumia miguu yangu vizuri katika mchezo wa mpira, ulikuwa ikifurahisha zaidi, akidai uwezo wangu wa kucheza mpira, ulitokana na kaka yake, ambaye hapo nyuma alishavichezea vilabu vikubwa nchini kabla ya kuamua kuachana na mchezo mpira. Hivyo namna hata nilivyokuwa nikiucheza mchezo huo aliniwazia mbali sana, lakini hakusita kunisihi kukazania mazoezi kila siku, kwa maana chochote kingeweza kutokea kwenye maisha yangu.



    Jambo ambalo kiukweli lilikuwa likiniongezea faraja sana kwa maana mama alikuwa akipenda kile nilichokuwa nakifanya, si hivyo tu hata baba alikuwa akinisisitiza kupigania kile nilichokuwa na kiweza. Hakuchelewa kunitadhalisha kuwa mbali sana na wasichana kwa maana mara nyingi huchangia kuharibu viwango vya wachezaji.

    *********

    Usiku wa siku hiyo ulikuwa wa aina yake, baada ya kupata chakula cha usiku kama nilivyoweka miadi ya kutafutana na Naomi, ilipofika saa tatu na nusu nilipokea simu kutoka kwake.

    Maongezi hayakuwa mafupi, niligusia habari za kumpigia simu mchana wa siku hiyo, na kile nilichokisikia. Hakuchelewa kunitoa hofu juu ya kile, pasipo kuniambia ni nani haswa ambaye alipokea simu ile. Nami si kuwa na tatizo kwa maana sauti yake, ilitosha kunipa burudani ya kutosha.

    Maongezi yetu yote hakuna hata moja ambaye alikuwa akigusia habari za mapenzi. Nilijitahidi sana nilipoona mambo yanaanza kuniharibikia nilijikaza kiume na kumweleza hisia zangu juu yake.



    Nilizungumza kwa kumaanisha mno, maneno yaliyojaa ushawishi wa namna yake. Hakika Naomi hakuonesha kuyakataa maneno yangu, aliyakubali. Penzi letu likazaliwa upya, usiku ulikuwa mrefu mno, ahadi kibao niliziweka, nami nikizipokea za kwake zilizojaa utamu kwenye ngoma za masikio yangu, pasipo hata kuelewa kama nilikuwa nikiingia katika bahari, na karibia nilikuwa naelekea kuzama na msaada ukionekana upo mbali na maeneo hayo!



    Penzi jipya likaanza kwa aina yake. Katika namna ambayo moyo wangu, ulifalijika mno kupita maelezo. Penzi jipya lilinibadilisha kweli, ni kama kila kitu kilikuwa kipya kwenye maisha yangu.

    Mazoezi kwenda ikawa kwa nadra sana, sababu kemkemu niliziweka kwendana na kile nilichokuwa nakifanya. Nilitunga uwongo wa kila aina ili mama anipatie pesa kadhaa ambazo nilizitumia kuliendelesha penzi.

    Naomi alizependa pesa nami nilijitahidi kumpatia pale alipokuwa akihitaji. Wakati huo sikuwahi kwenda nyumba yoyote ya kulala wageni, lakini baada ya muda kidogo nilikuwa mwenyeji wa maeneo hayo sehemu mbali mbali nilizikariri kulingana na ubora na utofauti wa nyumba moja na nyingine. Hapo akanifungulia dunia ya mapenzi kutoka kuwa lena hadi kuwa mzoefu.

    Mchezo ukajenga mazoea kichwani mwangu pasipo kujua, madhara gani baadae ningeenda pata. Nanma ya penzi letu lilivyokuwa likienda hakika nilijioa nimefika sana kuwa na msichana wa aina yake. Niliwasahau wote wa nyuma.

    Tabia zangu zikaanza kubadilika taratibu nyumbani, muda mwingi sikuwa tena mtu wa kushinda nyumbani. Mama alijua hilo na kila alipokuwa akiongea maneno yake hayakuwa na mashiko kwangu. Kwa maana yaliingilia huku na kutokea huku.

    Baba taarifa akazipata, lakini maneno yake hayakufaa kabisa. Na kila walipokuwa wakinigusia habari za kuwa katika tabia mbovu nilizikana haswa!

    Kuna kipindi mpaka maelewano mazuri na wazazi hayakuwepo kabisa. Na si pale nyumbani kwenye timu yetu tabia yakutoudhuria kwenye mazoezi na hata kucheza chini ya kiwango kwenye baadhi ya mechi ambazo nilipata nafasi ya kucheza zilinifanya hata kuvuliwa unahodha wa timu lakini hilo mimi sikulijali Naomi alindelea kuniathiri.

    Mwezi wa pili baada ya mwaka mpya, matokeo ya kidato cha nne yalitoka. Katika namna ya ajabu ya kanirudisha habari za Zuhura kutoka na kufahamu daraja la juu alilopata. Lakini sikujali sana kwa sababu kwa upande wangu katika namna isiyotegemewa kabisa sikuweza kufanikiwa kupata daraja la kwenda kuingia kidato cha tano bali nilifanikiwa kupata daraja la kwenda kuanza ngazi ya cheti kwenye elimu ya vyuo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Matokeo yaliwasikitisha sana wazazi. Lakini kwa upande wangu sikujali kitendo cha kwenda shule kusoma elimu ya sekondari sikukitaka kwa maana kingenipa wakati mgumu wa kuona na Naomi.

    Hivyo kupata alama zile kwenda chuo nilizifurahia zaidi kwa sababu kingenipa nafasi ya kuona na Naomi pale nilipokuwa nataka kutokana na kuwa na ufahamu sana na maisha ya wanafunzi wa vyuo. Hilo halikunitia shaka.

    ____________

    Misukosuko ya mapenzi hakuchelewa kunipata kitendo cha kwenda kuanza chuo katika baada ya miezi miwili kupita. Mambo yalianza kuwa tofauti sana. Hali mbaya ya usaliti ilianza kunyemelea penzi letu na kuniweka katika wakati mgumu sana. Nilifahamu wazi usaliti alikuwa akinifanyia Naomi lakini kauli sikuwa nayo na hata pale nilipojaribu kunyanyua mdomo kusema. Hakuna nilichoweza kuambulia zaidi ya maumivu.

    Shubiri ya mapenzi sasa ikawa nyumbani kwake kwenye mwili wangu, vilio visiokuwa na sababu ya wazi kwangu havikuwa vigeni kwenye maisha yangu. Niliishi katika namna ya majuto. Lakini bado sikuweza kukaa mbali na penzi la Naomi.

    Mwili wangu ulianza kupungua siku hadi siku mapenzi yaliendelea kunitesa katika namna yake na weza sema, katika safasi zote nilizowahi kuwemo kwenye mapenzi Naomi ni mwanamke ambaye alinitesa zaidi kwa sababu utamu wa penzi lake uliendelea kuniathiri siku hadi siku kwenye ubongo wangu. Kumbukumbu ya penzi lake halikutaka kuniacha kwenye maisha yangu kabisa!

    Katika namna nyingine ambayo bado nayo inaendelea kuwa kumbukumbu kwangu, kuna nyakati niliwahi kuzifumania ujumbe za kadhaa za mapenzi kwenye simu yake, na kila nilipokuwa nikimuuliza hakuonekana kujali hali ile, wakati wote nilikua nikijiiba sana kukutana na Naomi, nikizitumia pesa za wazazi kizembe ili kuhakikisha na kuwa karibu naye. Upendo wote nilikuwa nikimuonesha lakini hiyo hakaona haitoshi. Ilifika siku kwa macho yangu nilishuhudia akiwa na mwanaume. Jambo ambalo lilinipa tabu sana mpaka kuamua kuchana na penzi lake. Japo nilipitia vipindi vigumu sana lakini nilifanikiwa.

    Maumivu ya mapenzi yakaniweka katika namna nyingine, sikuwapenda wasichana utanasharti wangu nikiwa chuoni, niliwatumia kama chombo cha starehe pale nilipokuwa nikiwahitaji. Tabia ilibadilika sana, uwezo wangu wa kucheza mpira ulibadilika sana kwa kipindi kifupi, ilifika kipindi sikutamani tena mpira.

    ***********

    Mwaka wa kwanza chuo ulikuja na maajabu naweza sema pasipo mategemeo yangu jioni moja, nikiwa nanimejichanganya na baadhi ya wanafunzi wenzangu. Simu yangu iliita kwa vile nilikuwa kwenye makelele sikuweza kuisikia vizuri kama simu ilikuwa inaiita.

    Nikiwa nishangashangaa wakati sina hili wale lile. Nikaitoa simu yangu mfukoni, nikakutana na simu kama tano zilizopigwa kutoka kwenye namba ngeni. Nilitaka kama kupuuza lakini, niliamua kupiga namba ile baada ya kushauriana na kichwa changu.

    Iliita sana bila kupokewa, nilijaribu kwa mara nyingine lakini hali ilikuwa ile ile. Sikutaka kusumbuka namba ile. Hivyo niliendelea kufanya mambo mengine.

    Saa mbili usiku wa siku hiyo ile namba ikanipigia.

    Ghafla baada ya kupokea sauti ambayo takribani mwaka ulikuwa umekatika sasa, ilipenya vizuri kwenye ngoma za masikio yangu. Mdomo ulikuwa mzito ukishindana na kile nilichokuwa nakisikia.

    Hakuitaji utambulisho kama yeye alivyofanya. Niling’amua vyema sauti yake alikuwa ni Zuhura kwa uhakika.

    Dakika mbili zilitosha kumaliza maongezi yetu, yakiniweka kwenye tafakari nzito.

    Ni kweli nilikuwa nimekumbuka sana kutokana na simu yake, lakini ilikuwa muda sana umepita. Ni vipi bado moyo wangu ulikuwa ukimuhitaji kama alivyoniuliza? Jibu nilikosa, nilihitaji kujifikirisha ndani ya moyo wangu. Nikiyapima meneno yake machache lakini yalionekana yana tija ndani yake.

    Usiku ulikuwa mrefu sana, kumbukumbu mbalimbali zilinipitia kuhusu maisha ya Nguzuko. Nililila kwa manyanyaso sana, kiasi cha kwamba hata nilichelewa kuamka juu ya kitanda cha hosteli nilichokuwa nimelalia.

    Niliamka nikijishangaa katika siku ambayo ilianza kwa utofauti mkubwa. Mpaka namaliza siku. Hakika haikuwa njema kwa upande wangu. Jambo baya lilitokea jioni ya siku hiyo.

    Mmh jambo baya lilitokea usiku huo? Aiseh Daudi Msomwa unatuweka tumbo joto. Je ni jambo gani hilo? Naam na imani utatuambia tu… Msikilizaji hakika kuna mengi ndani yake nikusihi tu. Usikose kufatiria simulizi hii kwenye sehemu inayofata ilituweze kubaini yaliyomo yamo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog