Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

THAMANI YA MOYO - 3

 





    Simulizi : Thamani Ya Moyo

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Thamani Ya Moyo...Maumivu Ni Haki Yangu



     ilishia pale Daudi Msomwa amesikia sauti ya Zuhura kwa mara nyingine. Baada ya kupokea simu kwenye jioni moja. lakini mambo yanabadilika ghafla, je ni mambo yapi hayo? Sasa tuwemo kwenye sehemu ya tisa ilituweze kuyafahamu.



    Jambo ambalo sikulitegemea kabisa. Mara kadhaa nimezoea kusikia na hata kuwaona wazembe sana watu wanaoibiwa haswa linapokuja suala la wizi wa simu, pasipo kujua maumivu ya jambo hilo. Lakini jioni hiyo ya aina yake nami niliyapokea maumivu ya kuibiwa.

    Nikiwa kwenye pilikapilika za usafiri pasipo mategemeo yangu, vibaka waliniotea kuja kutahamaki sikuwa na simu tena. Walichonibakiza ni nauli tu, kidogo ilinitoa fedheha ya kudhalilika ndani ya gari.



    Kitendo ambacho kiliniumiza sana. Niliniumia katika namna mbili nilijiuwa wazi uwezekano wa kupata mawasiliano na Zuhura hakuwepo tena. Kwa maana Laini ambayo Zuhura alikuwa akiitambua hiakuwepo tena na uwezo wa kulinew sikuwa nao. Kwa sababu sikuwa mimi nimesajili ile laine. Maana simu nilipewa na mama ikiwa pamoja na laini, na wakati huo nilikuwa chuoni. Hakukuwa na uwezekanao wa kuipata hata kidogo.

    Hakika niliumia mno sikuwa na cha kufanya zaidi ya kumshukuru Mungu, ilikuwa kama nimetoa sadaka.

    *********

    Sauti yake, ilibaki nami kwenye wiki nzima. Moyo wangu ukiweza kunipatia majibu ya maswali kadhaa wa kadhaa ambayo nilikuwa nikijiuliza hapo awali.

    Safari hii majibu yakiwa mepesi kuliko hata maswali yenyewe. Ni kama vile kuna kitu kilikuwa kina kosekana moyoni mwangu, licha ya kujihusisha kwenye mapenzi na wasichana tofauti lakini bado kunakitu nilikuwa nikiona kinakosekana kabisa. Jina la Zuhura likionekana kuridhisha moyo wangu zaidi kuliko wasichana wote katika jicho langu kawaida tu na mizani ya kichwa changu ilipima na kuliweka jina lake katika kilele cha juu na thamani zaidi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mvuto na msukumo wa moyo wangu, bado ulikuwa ukimuhitaji Zuhura, nikiona ni mbadala sahihi sana kwenye moyo wangu safari hii ikiwa tofauti sana. Nilipima huenda angekuwa mtu sahihi sana katika maisha yangu. Lakini sasa sikuwa na uwezo walau wa kuisikia sauti yake. Hakika nilibaki njia panda kwa mara nyingine tena pasipo mategemeo.

    Ndugu yasikie tu mapenzi usiombe ukapenda kwa maana mapenzi yanaweza yakayabadilisha maisha yako pasina kutumia nguvu.

    *************

    Mwezi moja ulipita baada ya sekeseke hilo sikuchelewa sana, kununua simu mpya. Lakini upya wake ulinitesa kwa maana hata laini ilinihitajika kununua nyingine, kwa sababu sikuwa na uwezo wa kuipata ile ya zamani.

    ***********

    Katika siku moja baada ya kuwaza na kuwazua jina la Niko likanirudia. Nilikumbuka vituko vingi ambavyo nilifanyia, nikiweka uhasama kubwa naye, nikiamini moja kwa moja atakuwa akimchukua Zuhura.

    Kumbukumbu yake ilinipitia nikiamini kwa sasa angekuwa anafahamu upatikanaji wa Zuhura na hata angeweza kunisaidia kunifikishia maagizo yangu kwa Zuhura iliniweze kupata mawasiliano naye kwa mara nyingine.

    _____________

    Baada ya kuweka azimio langu la kumtafuta Niko, wakati nambari yake ya simu sikuwa nayo. Ila niliamua kucheza mchezo wa bahati nasibu kweli baada ya kuitafuta katika namba yake kwenye mtandao wa facebook, nilifanikiwa kuipata mawasiliano naye.

    Sikuchelewa, nikiwasilisha ujumbe wangu. Alipokea japo kama vile nilikuwa nikimlazimisha kwa namna vile alivyokuwa akiyapokea maneno yangu. Sikujali sana, japo kuna wakati ilinitia shaka kama ujumbe wangu ungeliweza kufika kwa muhusika huo ukabaki mtihani usikuwa na majibu.



    Miezi ilienda mwaka ukatika pasipo matumaini ya kupata chochote kutoka kwa Zuhura. Lakini sikuchoka kumsumbua Niko, naye hakuchoka kunizungusha alinipa maneno mengi ya matumaini lakini hakuna kilichoonekana kunijengea faraja.

    Siku zilizofatia ni kama vile nilikumbwa na ugonjwa wakutupenda kukaa karibu na wasichana kwa maana hali yangu ilibadilika sana hata mazoea na watoto wa kike chuoni yalikata ghafla pasipo hata marafiki zangu wa karibu kufahamu nini kilichokuwa kinanisibu kwa upande wangu.

    Nilijikuta najiweka mbali kabisa na watu wa jinsia hiyo.



    Ugonjwa wangu ulibaki kuwa wangu. Chuki kali dhidi ya viumbe hivyo iliiniingia na kila nilipokuwa nikiwaona msisimko wa baridi kali ulikuwa ukinipitia nikishindwa kuizua hiyo hali.

    Ilitumia muda mrefu sana hali hiyo kubaki nami pasipo kubaini dawa yake. Hata maongezi yangu tu mdomoni yalitosha kubaini hali iliyokuwa ikinikumba.

    Na kumbuka kuna siku niliwahi kuvurumisha makonde msichana moja darasani tulipopishana kauli ya kawaida tu. Lakini jambo lile mimi nilishikiria kidete na hata kunisababishia matatizo chuoni. Hali iliyozidi kuongeza tofauti kwa upande wangu. Laiti isingekuwa busara za mwanafunzi yule kwa hakika ilibaki kidogo ningeweza kutimuliwa chuoni pale. Na hata kunijengea picha mbaya kwa mzazi wangu.

    ***********

    Mwaka wa pili chuoni ukaingia, nikifaulu vizuri masomo yangu pasipo shaka. Wakati huo nirudi uwanjani baada ya ushawishi mkubwa kutoka kwa marafiki zangu. Nilifanya mazoezi kwa nguvu, siku hadi siku zilivyokuwa zinaenda kiwango changu kilianza kuimalika na kurudi katika siku kadhaa za nyuma.

    Niliendelea kufanya mazoezi kwanguvu sana, miezi miwili tu nilijumuhishwa katika kikosi cha timu ya chuo kilichokuwa kinashiriki mashindano ya vyuo mbalimbali nchini.

    Mechi kadhaa za mwanzo niliingia kama mchezaji wa akiba. Nilizitendea haki vilivyo katika kila mechi ambayo niliyopata nafasi.

    Jambo ambalo liniweka katika hali nzuri ya kujiamini kwenye mechi za kuishindani, kitendo ambacho kiliianza kupotea kwangu kutokana kukosa kucheza mechi nyingi za kiushindani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mashindano hayo kumalizika huku nikiwa nimefungia timu yangu magoli matatu nikiwa kama mchezaji wa akiba. Kitendo ambacho kilinipatia namba ya kudumu ya kuanza kwenye kikosi cha chuo nikiwa nambari kumi tegemeo.

    Mambo ya starehe niliweka pembeni kabisa. Jina langu uwanjani lilianza kuwa kubwa, nilifunga kila nilipokuwa nikitaka. Hiyo iliniwekea katika nafasi nzuri hata kuja kuchukuliwa kama mchezaji wa kukodiwa katika ligi mbali mbali zilizokuwa zikifanyika nje ya chuo. Sikuwa nikifanya makosa, niliendelea kuwa mwiba mkali kwa mabeki wa timu pinzani ambao asilimia nyingi walibaki kunichezea faulo nyingi na mimi niliendea kuwaadhibu vile nilivyokuwa nikijisikia.



    Nilipachikwa majina tofauti ya wachezaji wa nje na nchi yetu ambao walikuwa wakitamba ndani ya ulaya. Yote ilitokana na juhudi na uwezo wangu binafsi. Watu ambao walinizoe mwanzo pale chuoni kwa vile nilivyoingia sikujihusisha na mchezo huo walibaki kunishangaa na la zaidi niliwafanya wawe watu wa kuniuliza maswali tofauti tofauti na kunipa sifa nyingi, zilizonishinda hata uwezo wangu kutokana na mambo kadhaa wa kadhaa niliyopitia kwenye maisha yangu.

    Wakati huo nilijikuta nikibadilika kabisa sasa sikuwa mtu wa kujirusha. Muda mwingi niliutumia kufanya vitu vya maana chuoni na uwanjani.



    Watu walionizoe kwa tabia yangu ile ya awali pia sikuacha kuwastajabisha. Sasa nilikuwa ni mimi yule Daudi Msomwa, wa hapo awali. Walimu walinipenda wanafunzi pia licha ya uwezo wangu ila sikuwa nikijiona bora sana mbele ya wezangu.

    Tabia yangu nzuri haikuishia chuoni, likizo ya iliyofata niliporudi nyumbani wazazi walishangazwa mno na mwenendo wangu. Hawakusita kunipongeza kwajinsi nilivyokuwa nimebadilika. Kiukweli nilikuwa nimebadilika haswa!

    ____________

    Nikiwa katika likizo nzima hakuna kilichoonekana kuwa kimeenda tofauti sana kwa upande wangu. Nilimshukuru Mungu kwa namna moja ama nyingine katika kuniwezesha kuwa katika hali njema.

    Ni kweli kama siku zilivyokuwa njema. Katika jioni moja nilipokea taarifa.



    Taarifa ya kwenda kufanya majaribio, ilikuwa ni habari njema sana kwa upande wangu. Kwa maana kwa wakati wote licha ya kucheza kwa kiwango cha juu sana, suala la kwenda kufanya majaribio sikuwahi kuliwaza kabisa kwenye kichwa changu.

    Isitoshe mjomba ndio aliileta habari hiyo. Ilinishangaza kidogo kwa sababu ilipita kipindi kirefu sijazungumza naye. Kutokana na kuwasiliana naye kwa nadra sana na mara nyingi salamu zake huwa na zipata kutoka kwa mama au baba. Kwa sababu hatukuwa na ukaribu sana wakuwasiliana kila wakati na mjomba wangu.



    Ilikuwa taarifa yenye kuvutia sana masikioni mwangu. Nilitamani kila mtu wangu wa karibu asikie furaha niliyokuwa nayo baada ya ngoma za masikio yangu kuipokea taarifa hiyo katika namna ya aina yake yenye kutia ladha masikioni.

    Timu ya Simba si timu ndogo nchini. Ni timu ambayo ina historia nzuri na yenye kuvutia kwa wale wapenzi wa soka nchini na zaidi la ziada wachezaji wengi nchini wamekuwa wakipenda na hata kuwa na ndoto ya kucheza kwenye timu hiyo. Kitendo cha mama kuniambia kuwa mjomba amewapa taarifa ya kuwa nilikuwa nikitakiwa kwenda kufanya majaribio ndani ya timu hiyo kiliniweka katika shauku kubwa sana.



    Wachezaji kadhaa maarufu wa timu hiyo walinipitia kichwani mwangu, nikivuta taswira ya kuwa ningepata nafasi ya kuwaona kwenye mboni zangu moja kwa moja tofauti na mara zote ambazo nilikuwa nikiwashuhudia tu kwa kuwaona kwenye runinga pale wanapocheza na timu pinzani.

    Na la zaidi zaidi lilikuwa likinitia kimuhemuhe si kuwaona tu ningeenda kupata fursa ya kufanya mazoezi na kuzungumza nao kabisa.

    Bahati iliyoje ilikuwa imeniangukia kwangu. Ni kama vile safari ya kwenda kucheza timu hiyo ilikuwa ikikaribia, namna nilivyokuwa kwenye morali ya mchezo ilinipa hamasa ya kutamani kwenda kucheza hata kwa muda ule.

    ********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilizungumza na wazazi namna nilivyolipokea jambo lile, walionekana kupendezwa na kile hivyo walibaliki jambo lile, ikisubiriwa siku muafaka ya kwenda kufanya majaribio ambapo mjomba hakusema tarehe rasmi ya kwenda kufanya. Lakini tu alisisitiza nijiandae vya kutosha siku yoyote ningehitajika mkoani Dar es salaam.

    Jambo likazua jambo, usiku wa siku hiyo ulikuwa mrefu, nilitakari kwa kina ni jinsi gani ambavyo ningeweza kufanya majaribio hayo, na namna gani ningeweza walau kufanya mambo mazuri yenye kuvutia, kiasi cha kwamba viongozi wa timu hiyo kunipatia nafasi ya kunisajili ilikuchezea timu hiyo kwa dhumuni la kuwa mchezaji wa kulipwa si kwa wakutumikia timu za mitaani na timu ya chuo.



    Suala la kusoma na kucheza mpira halikunipa shida kwa sababu ufahamu wa kusoma elimu ya chuo nilikuwa nao hilo halikunitia shaka hata kidogo. Shaka ilikuwa ni jinsi gani nitaweza kufanya mambo mazuri nami nipate kusikika kwenye redio hata kuonekana kwenye runinga.

    Japo niliupata usingizi lakini sikulipata jibu ni jinsi gani nitakavyoweza kufuzu mtihani huo kwa maana mara zote nilikuwa nikijiamini kuwa ni moja kati ya wachezaji wa zuri. Na jambo moja sikutaka kumwangusha mjomba ambaye hapo awali alishawahi kuichezea timu hiyo na kuweka historia kubwa sana. Na hata nafasi yenyewe niliipata kupitia mgongo wake.

    _________________

    Asubuhi niliamka na hamu ya kufanya mazoezi saa kumi na mbili kasoro nilikuwa uwanjani nikizunguka kujimalisha vyema katika mazoezi ya kuongeza pumzi kabla ya kufanya ya kuongeza stamina.

    Zoezi likawa hilo hilo kwa takribani wiki moja na nusu kabla ya kupokea simu kutoka kwa mjomba akinihitaji kuelekea kwenye majaribio huku akisisitiza kutomuangusha.

    Swala lilikuwa limeiva haswa hakukuwa na utani hata kidogo.



    Mapema asubuhi ya siku iliyofata baada ya kuipokea simu ya mjomba nilikuwa ndani ya basi nikitokea nyumbani Morogoro kuelekea mkoani Dar es salaam. Mkoa haukuwa mgeni kwangu kwa sababu elimu yangu ya chuo nilikuwa nikichukua katika chuo kimoja pembezoni mwa mkoa huo. Masaa matatu baada ya purukushani za safari hatimaye harufu ya jiji Dar es salaam ikanipokea. Sikushangaa shangaa kero za wanaume walikuwa kazini kwenye eneo hilo, haraka nilijitoa ndani ya basi kuelekea nyumbani kwa mjomba maeneo ya Mabibo nusu saa nilikuwa na tazamana na nyumba ya mjomba.



    Ugeni ulikaribisha na chai nzito, baada ya kupokelewa na tabasamu nzito la mke wa mjomba, wakati huo mjomba hakuwa nyumbani nadhani alitoka kuelekea kwenye michakato yake ya kujipatia kipato.

    Nilifurahi chai ile zaidi la zaidi soga za hapa na pale za mke wa mjomba zilinivutia mno. Ni kama vile nilikuwa nimeondoa ukimya ulikuwa umetawala ndani mule kwa maana watoto zake wawili Azam na Sada walikuwa wapo katika mashule ya bweni, hivyo kukosekana kwa wanae ilikuwa ikifanya nyumba kupooza sana, kitendo cha kufika pale ni kama vile nilishangamsha nyumba.



    Tuliongea mengi na shangazi na hata kuhusu suala langu la kwenda kufanya majaribio pia tulizungumza na hapo nilipata kufahamu kwa kina juu ya suala lile. Kumbe sababu haswa ilitokana na mashindano yaliyopita ya vyuo ambapo kuna kiongozi moja wa timu ya Simba alinishuhudia uwezo wangu na huyo kiongozi alikuwa na ukuaribu sana na mjomba. Katika maongezi yao alihusisha jina langu ndipo mjomba alipopata kufahamisha kuwa mambo yale nilikuwa nikiyafanya mimi.

    Nilijisikia furaha sana kwa jambo lile, likioniongezea kujiamini sana. Miguu yangu ilionekana pia kufurahia jambo kupitiza maelezo.

    *********

    Saa kumi jioni mjomba alirejea nyumbani na kukaribishwa na ugeni wangu alifurahia mno. Baada ya kuweka mambo sawa tuliingia kwenye mazungumzo marefu alinieleza kwa kina kile ninachotakiwa kwenda kukifanya ilikuweza kunipatia nafasi ya kuwemo ndani ya timu yao. Sikuwa na hiyana nilimueleza mjomba ni namna gani nilivyokuwa nilivyozipokea habari zile. Nikimuahidi kwenda kufanya kitu kizuri pengine zaidi ya uwezo wangu wa kawaida.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilinipaswa kusubiri kwa siku tatu nikiwa pale nyumbani kwa mjomba wakati huo mjomba alinifahamisha kiwanja cha kufanyia mazoezi. Nilicheza kwa taadhari ya kuepuka kuumia. Hilo nilifanikiwa baada ya kupita siku hizo, siku ya mwisho mjomba aliyasimamia mazoezi yangu.

    Kwa namna nilivyokuwa nikipokea mipira, uimara wangu mjomba alinisifu mno, akiamini suala la majaribio lisingenishinda kabisa. Alinipa asilimia nyingi za kufanya vizuri.



    Mapema asubuhi ya siku ya nne, tulijitoa pale kuelekea kwenye makao makuu ya timu ya Simba, baada ya muda mchache tulikuwa tunazama na jengo hilo. Kulipendeza sana, bendera ya rangi nyekunde na nyeupe ilipepea vyema.

    Wakati nashangaa shangaa yale mageni kwangu. Ghafla katika namna ya kushangaza.

    Mmh ghafla katika namna ya kushangaza. Namna gani tena hiyo Daudi kutwa huachi vituko? Msikilizaji huu si mwisho wa haya, nikuombe tu tuangane wote kwenye sehemu ya kumi na moja ya simulizi hii ilitubaina namna hiyo ya kushangaza.



    Sauti nzuri ya kike ilitupokea eneo hilo na kutufahamisha mahali pa kwenda baada ya kumpatia maelekezo ya kile ambacho tulikuwa tumekuja kufanya ndani ya ofisi za timu hiyo.

    Sauti ile ilinishangaza kwenye ngoma za masikio yangu haikuwa ngeni hata kidogo. Ilinitafakarisha kidogo “Ni kama kunasehemu niliwahi kusikia?” Nilijiuliza , jibu sikulipata swali lingine likanipitia. “Wapi nilipowahi kusikia?” Ukawa mtihani lakini sikulijali sana.

    Tulielekea kule tulipopewa maelekezo, baada ya hatua chache tulikuwa tunatazamana na kiongozi moja ambaye alionekana ana nafasi kubwa ndani ya timu.

    Alifahamiana na mjomba haswa baada ya maongezi ya mjomba, yule kiongozi alinikaribishwa nami nikakaribia. Ugeni ukanitoka kabisa, nilianza kuyazoea majengo.

    Saa kumi kasoro nilikuwa uwanjani nikaanza kufanya kile kilichokuwa kimenileta. Ilikuwa tofauti kidogo na mawazo yangu. Kwa maana mawazo yangu moja kwa moja ilikuwa ni wazi ningefanya majaribio ndani ya kikosi cha timu ya wakubwa. Haikuwa hivyo kumbe walikuwa wanatimu ya vijana, hiyo haikunitia sana shaka ili niongezea kujiamini. Ni kiamini majaribio yangu yanaweza kuwa mepesi kuliko hata nilivyokuwa nikiweka shaka mwanzoni.

    Niliingia uwanjani nikiwa nimekabidhiwa jezi yenye namba arobaini na tano mgongoni. Baada ya kufanya mazoezi ya viungo na wachezaji wengine. Kocha wa timu ya vijana ya Simba alitugawa katika vikosi viwili. Kila mtu akipewa jukumu lake.

    Hakuwa na shaka ya kuniuliza nambari gani nilikuwa nikicheza uwanjani kwa maana taarifa zangu alikuwa nazo. Hivyo niliambiwa nicheze nambari kumi. Nambari ambayo haswa nilikuwa nikipendelea kucheza licha ya kuweza kumudu nafasi nyingi uwanjani. Ni kama vile alijichanganya, mazoezi mpaka yanaisha niliwafanya vile nilivyokuwa nikiwajisikia mabeki wa timu hiyo, nikiingia kambani mara tano.

    Niliyafunga magoli vile nilivyokuwa nataka ndani ya wiki nzima ya majaribio nilifunga si chini ya goli kumi na mbili. Hilo lilinifurahisha sana na kuniongezea kujiamini, kutokana na kile nilichokuwa nikikionesha, nikiamini njia ilikuwa nyeupe kuelekea kujiunga ndani ya timu hiyo.

    Baada ya mazoezi ya wiki kama moja, nilipata fursa pia ya kucheza mechi kadhaa za kirafiki na timu hiyo ya vijana. Kwenye mechi hizo nazo nilizidi kuweka uhai na tumaini la kujiunga na timu hiyo pasipo kujua kama mambo yangeenda kuwa mabaya katika jioni moja ya siku ya mwisho wa majaribio yangu.

    Ni kama vile siku hiyo nilikuwa nikifahamu kuna jambo baya lilikuwa linaenda kunitokea kwa maana nilicheza kwa taadhari sana lakini hakutosha kuniepusha kuvunjika mguu.

    Nilichezewa rafu mbaya sana na mchezaji wa timu pinzani rafu ambayo ilinifanya kushindwa kuendelea na mchezo, nikiwaishwa hospitali haraka kwa matibabu.

    Saa tatu usiku nilikuwa ndani ya hospitali ya Amana nikifungwa bandeji gumu kwenye mguu wangu.

    Maumivu niliyokuwa nikayasikia hayakuwa ya madogo. Kila upande wa mwili wangu uliniuma kupita maelezo. Licha ya kuendelea kupata maumivu makali lakini wazi akili yangu haikuwa sawa, nilihisi ndio mwisho wa kucheza mpira na habari zangu kuishia pale.

    Nilimuliza maswali mengi daktari juu ya kuweza tena kurejea uwanjani. Majibu yake nayo hayakuwa yakinipa faraja zaidi ya kuniongezea machungu. Aliongea yakuwa inategemea na uponaji wa mguu wangu. Kama hatuleta usumbufu basi ningeweza kurejea uwanjani bila tatizo lolote. Mjomba na mke wake wao ndio walibaki faraja yangu.

    Baada ya huduma zile za hospitali kukaa sawa saa tano usiku tulirejea nyumbani. Usiku wa kuamkia siku inayofata ulikuwa mrefu sana kwangu. Maumivu ya mguu yaliendelea kunitesa kwenye usingizi wangu, na hata kunifanya kutokumbuka muda gani ambao niliweza kulala kabisa.

    ___________CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Mapema asubuhi, nilipokea simu kutoka kwa mama akinipa pole kwa kile nilichokuwa nimekipata, mama alinisihi sana ni vumilie kipindi kama kile kwa maana kila kitu kinachangamoto zake. Akinisitiza kufuta suala la kuacha kucheza mpira kama lilikuwa kichwani mwangu.

    Maneno yake niliyaelewa sana na uzuri sikuwa nikifikiria kitu kama hicho. Jambo hilo lilinipa faraja sana nikiamini kuwa mambo yakikaa sawa kama daktari alivyosema ningeendelea na mchezo huo kwa maana wazazi walikuwa radhi mimi kuendelea kucheza.

    **********

    Baada ya wiki mjomba aliniletea taarifa ya kuwa nilikuwa nimefuzu majaribio, na nilichotakiwa tu baada ya kupona, ningewasili ndani ya timu hiyo kutoa taarifa ya uwepo wangu na hata kufanya taratibu za kusajiliwa.

    Taarifa hiyo nilipokea katika namna iliyokonga moyo wangu, nikiwa siamini kile alichokuwa akikisema mjomba. Mjomba hakuishia hapo aliniambia mchana wa siku hiyo timu ya Simba ingemtuma mwakilishi wake kuja nyumbani kuniona na hata kuniletea pesa kidogo kwajili ya kujiuguza. Hakika ilikuwa taarifa njema sana, nikikaa mkao wa kumsubiri mwakilishi wa Simba kuja nyumbani ili maneno ya mjomba yapate kutimia kama vile alivyokuwa akinena.

    *********

    Kweli baada ya mjomba kwenda kazini masaa kadhaa tuliokea ugeni nyumbani. Ugeni ambao si mara ya kwanza kuona kwenye mboni zangu. Sauti yake ilinikumbusha mbali sana, haikuwa mara ya kwanza pia kuisikia, wakati huo nilipoisikia iliniacha na tafakari nzito mwanzoni kabla ya kuamua kuipotezea.

    Sasa nilisikia vizuri ikipenya kwenye ngoma za masikio yangu. Tofauti tu sauti nilihisi ya mtu fulani ambaye hapo awali niliwahi kuona naye. Lakini ajabu sura yake sikuwahi kuiona hapo nyuma.

    Alivalia suruali ya jinsi iliyochora umbo lake nzuri la Kibantu na kuongeza nakshi ya urembo wa msichana huyo wa makamo. Macho yake yalivalia miwani iliyoongeza haiba ya uzuri wake kwa yule aliyekuwa akimtazama.

    Alijitambulisha kwajina la Maria, jina nalo likawa geni kabisa masikioni mwangu na kunipa uhakika huenda tu ni ufanano wa sauti na mtu ambaye wazi sasa nilielewa nilikuwa nikifanisha ile sauti na mwanadamu gani. Hakuwa mwingine sauti yake ilifanana sana na Zuhura msichana ambaye nilimpenda sana.

    Utambulisho wake ulipita vyema kwetu, akijibaraguza vilivyo. Kazi yangu ikibakia kumeza mate tu uzuri wa msichana huyo. Hakika Mungu naye alijua kumuumba katika namna ya kipekee sana. Upekee uliondelea kuleta hali ya burudani katika mazungumzo yetu.

    Tulizungumza kwa muda kidogo kile ambacho kilikuwa kimemleta eneo lile, akinipa pole zisizokuwa na idadi kutokana na hali yangu. Nami nilizipokea kwa mikono miwili.

    Alinipatia kiasi kadhaa cha pesa kisha akaniomba jambo. Nilimtazama, naye akanitazama. Tukabaki tukitazama kwa muda kidogo, ni kama vile nilikuwa siamini kile nilichokuwa nakisikia. Na hakika sikukitegemea mpenzi msomaji.



    Aliniomba nimpatie nambari ya mawasiliano yangu. Nilisita kidogo nikimtazama. Akaniangalia katika mfumo wa kumanisha jambo. Nilijikuta na kwepesha macho yangu, aibu ilinipita. Nilijikaza kiume kisha nikazitaja namba zangu kwa umaridadi sana. Kicheko kikampita, tabasamu lake, likaonekana vyema kwenye mboni za macho yangu na kuongeza nakshi ya uzuri wa msichana huyo.

    Hakuchelewa kuzihifadhi kwenye simu yake. Tulizungumza maneno machache hatimaye alituacha mimi na mke wa mjomba tukiujadili ujio wake, huku tukipambana kuhesabu kiasi cha pesa alichotukabidhi.

    *********

    Wiki mbili zikakatika, wakati sahihi wa kurejea chuo ukawadia kwenda kuendelea na masomo, hali yangu ya mguu ilikuwa nzuri lakini ilinipaswa kutembelea magongo, kwa maana bado sikuweza kutembea mwenyewe wakati bandeji gumu liliendelea kushikiria mguu wangu.

    Nilirejea chuoni, niliomba kusoma masomo ya nje ya chuo. Sikutumia nguvu sana, nilifanikiwa kupata usajili wa kusoma masomo hayo. Niliamua kufanya hivyo baada ya kushauriwa na mjomba. Wazazi hawakuwa na tatizo lolote kwa maana walishajua lengo na dhumuni la mimi kusoma masomo hayo ya nje ya chuo. Ingenipa nafasi nzuri ya kufanya majukumu mengine nje ya elimu.

    Katika wiki hizo, nilizipokea simu nyingi kutoka kwa Maria, simu ambazo zilileta ukaribu sana na msichana huyo. Urafiki ulikuwa mkubwa sana akiwa mzoefu hata nyumbani kwa mjomba, uzoefu uliotokana na safari zake za kuja kunitembelea kila baada ya siku kadhaa. Nilifurahia ujio wake, ukinifariji kabisa baada ya kuweka ukaribu na msichana huyo.

    ************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wiki ya nne, nilirudi hospitali, habari za hospitali zilikuwa njema sana. Daktari aliniambia uwezekano wa kurudi uwanjani ni mkubwa sana, kuliko vile alivyokuwa akidhani. Mwili wangu ulikuwa tofauti sana, akinipongeza na kusema mazoezi ndio yamesadia mwili wangu kuwa tofauti na watu wengine.

    Baada ya kutolewa bandeji gumu. Wiki iliyofata nilianza mazoezi mepesi mepesi hatimaye niliweza kutembea vizuri kabisa. Maria aliyasimamia mazoezi hayo, nilijishangaa kabisa kuweka ukaribu uliozidi na msichana huyo. Pia Maria hakusita kunisisitizia ushauri wa Daktari wa ya kuwa nilihitajika kufanya mazoezi mepesi ya kukimbia kwa wiki mbili kabla ya kujihusisha na mazoezi ya mpira hivyo wiki zilizofata tulikuwa pamoja katika mazoezi hayo.

    __________

    Mambo yaliendelea kuwa mazuri kwangu, nilipopona kabisa kama nilivyotakiwa kwenda kuripoti ndani ya timu ya Simba. Mapema katika asubuhi ya siku moja, tuliongozana na mjomba kwenda katika ofisi za timu hiyo. Baada ya kufika mapema, tulipokelewa na Maria, kisha kupelekwa katika ofisi ya msajili mkuu wa wachezaji wa timu hiyo.

    Usajili wangu ukafanyika, miaka mitatu nikaipokea, ilikuwa ni usajili wa aina yake sana, katika maisha yangu ya mpira. Kwa maana kitendo cha kusajili katika timu hiyo wakiwa wamenipeleka katika timu ya vijana. Ulikuwa mkataba wenye kuridhisha sana kwa maana jambo la kupandishwa mapema kwenda timu ya wakubwa kulikuwa na ongezeko la pesa kama mkataba wangu ulivyokuwa ukinena.

    Jioni ya siku hiyo, sherehe ndogo ya kujipongeza ilifanyika ikiuzuliwa na wazazi wangu wote na mke wa mjomba na mjomba mwenyewe. Nilifurahi mno kwa jambo lile, lakini bado kuna kitu kilikuwa ninakikosa ndani ya faraja yangu.

    Nilitamani kuisikia sauti nzuri ya Zuhura ambaye kila kukicha alikuwa akiisifu sana uwezo wangu wa kucheza mpira, nikiyatoa magoli kadhaa niliyokuwa nikiyafunga vile nilivyokuwa nakijisikia kwajili yake.

    Lakini sasa alikuwa mbali na hata kukosa kufahamu ni lini haswa ningepata kumsikia Zuhura japo nipate kumwambia ni jinsi gani moyo wangu ulivyokuwa ukiguswa na hisia za mapenzi juu yake.

    Hisia zenye kueleza na namna gani nilivyokuwa nikipata wakati mgumu katika nyakati ambazo nilikuwa nilikosa penzi lake. Ijapokuwa nilishaumizwa na mapenzi katika vipindi tofauti tofauti. Niliamini ya kuwa Zuhura ni msichana ambaye kamwe nisingeyapokea maumivu ya mapenzi pindi tu nitakapoipata nafasi kutoka kwake. Kwa maana nilimuweka katika sehemu nyingine kabisa ya wanawake.

    *********

    Usiku wa siku hiyo ulikuwa wa tofauti sana kwangu, kumbukumbu nyingi kuhusu maisha ya nyuma kidogo yalinijia nilimkumbuka sana Zuhura na ile siku ya mwisho nilivyopata kuisikia sauti yake. Maneno yake yalikuwa faraja sana kwangu. Hakika penzi dhidi yake halikuwa limezikwa kwenye moyo wangu. Moyoni ilionekana wazi nyakati zote niliendelea kuishi nalo. Na hata nilipojaribu kupima kwenye mizani ya kichwa changu mwanamke pekee aliyeonekana kuwa katika nafasi nzuri kwenye moyo wangu bado aliendelea kubaki kuwa yeye.

    ___________

    Asubuhi ya siku iliyofata, nilichelewa kuamka kuliko kawaida na hata sikufanikiwa kwenda kufanya mazoezi binafsi katika asubuhi ya siku hiyo. Maria ndio alinitoa kwenye rindi la usingizi, sauti nzuri ya kike yenye kufanaa na Zuhura ilipokelewa nyema kwenye ngoma za masikio yangu.

    Niliyasikiliza maneno yake, viungo vyangu vya uzazi vikionekana kuitii vyema sauti ile ya kike, nilijitahidi kuvikanya lakini vilionekana kunishinda na muhemko wa hali ya juu nilikuwa nikipata, wakati nikiendelea kumsikiliza Maria, aliongea kichokozi mno.

    Nilimuelewa nini anamaanisha lakini, bado nilikuwa mbali sana kwa yale aliyokuwa akizungumza japo tulikuwa na urafiki wa hali ya juu kabisa. Katika mazumgumzo yake aliniomba kuonana katika jioni ya siku hiyo. Nilifikiri kidogo kwa muda kisha nikamjibu kuwa nimelikubali ombi lake. Aliokana kufurahia sana. Tuliyamaliza mazungumzo kwa namna hiyo.

    **********

    Niliingia bafuni, kuoga baada ya kujitoa kitandani, chai nzito ya maziwa ikanipokea pindi tu nilipotoka bafuni, wakati huo nikipokelewa na mazungumzo ya mama na baba, tulizungumza sana, wakinisihi na namna gani ambavyo natakiwa kuwa katika kipindi kama hicho, niuongeze juhudi kwenye mchezo bila ya kusahau kusoma hayo yakabaki maneno muhimu kwangu. Maana maneno yao yalikuwa faraja sana kwangu katika kipindi adimu kabisa kama hicho.

    Saa sita mchana walijitoa nyumbani kwa mjomba, wakiniomba kuwasindikiza stendi. Niliwasindikiza mimi pamoja na shangazi mpaka Ubungo, soga za hapa na pale tulizipiga kabla ya kuwapandisha basi nao wakirejea nyumbani Morogoro nasi tulijitoa eneo hilo kurudi nyumbani taratibu.

    ************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali ya hewa kwa siku hiyo ilikuwa tofauti sana, ghafla hali ilibadilika machoni mwa kila mtu. Kitendo cha kurejea nyumbani mvua kubwa ilikuwa ikionesha umwamba wake kwenye uso wa dunia.

    Raha iliyoje upande wangu, nilipenda sana kulala wakati mvua inanyesha hali hiyo bado hakuwa imenitoka licha ya umri wangu kuongezeka.

    Hivyo wakati mvua ikiendelea kunyesha nilikuwa juu ya kitanda nimejikunja kama samaki. Mvua ilinyesha kweli, wakati huo usingizi hakuchelewa kuja kunichukua. Ulinichukua kwa aina yake.

    Wakati mvua inanyesha alikuwa juu ya kitanda. Usingizi ukamchukua kwa aina yake? je ni aina gani ndugu msikilizaji? Kumbuka Maria naye anajaribu kujisogeza kwa Daudi Msomwa vipi atafakiwa au la? Naam hayo na mengine mengi utayapata ndani ya simulizi hii. Usikose kungana nasi kwenye sehemu inayofata.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog