Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

THAMANI YA MOYO - 4

 





    Simulizi : Thamani Ya Moyo

    Sehemu Ya Nne (4)



    Thamani Ya Moyo...Maumivu Ni Haki Yangu





     ilishia baada ya Daudi Msomwa kuweka miadi ya kuonana na Maria asubuhi ya siku hiyo. Mchana mvua ya aina ikasindikiza usingizi wa Daudi. Je nini kitaendelea hapo? Sasa tuendelee kwenye sehemu hii ya kumi na tatu.

    Saa kumi na nusu ya jioni, muito wa simu yangu ndio ulinitoa katika rindi la usingizi mzito, uliokuwa ukileta burudani kwenye mwili wangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati huo hazikusikia kelele za mvua, jua la jioni liliangaza vyema kwenye mboni za macho yangu punde nilipochungulia dirishani. Ni kama vile hakukuwa na mvua kubwa iliyonyesha ndani ya siku hiyo.

    Niliangalia simu yangu, nambari ya mpigaji ikasomeka vyema kwenye kioo. Kama nilivyokuwa nikiwaza kwenye kichwa changu, alikuwa ni Maria. Nilisita kidogo kuipokea baada yakukumbuka miadi yake ya kwenda kuonana. Sikuwa na mpango wa kutoka kabisa licha ya kuwa nilikubali ya kuwa ningeweza kuoana naye katika jioni ya siku hiyo. Lakini mwili wangu ulikuwa mzito sana, nilijihisi uvivu wa kutosha. Na hata hivyo jambo lingine sikuwa nikioana umuhimu wa kwenda kuona na Maria, kwa maana shida yake kama mwanaume nilishaiilewa, na hakika sikuwa tayari kuwa na Maria.

    Ijapokuwa alikuwa ni msichana mwenye kuvutia kwenye jicho la mwanaume rijali. Sijui nini kilikuwa kimenikumba? Ni mimi huyo ambaye niliwabadilisha wanawake katika kipindi fulani cha nyuma kwenye maisha ya chuo. Lakini kwa wakati huo ikawa tofauti sana.

    __________

    Nilipokea simu, tulizungumza kwa dakika kama kumi, kabla ya kumkubalia ombi lake kwa mara nyingine, nikiwekea sharti la kutokaa sana. Ni kama vile nilikuwa nimejiloga mwenyewe kwa maana sikuwa nikifahamu kile ambacho kilikuwa ndani ya moyo wa msichana huyo.

    Na kama ningelijua nisingejtoa nyumbani na kujipeleka kule. Kwa maana hata kama ningeshitaki ya kile alichonifanyia Maria hakuna Jaji wala Mahakama ingenielewa kwa urahisi kiasi kile.

    Mpenzi msikilizaji baada ya kujitoa kitandani, nilienda kuoga. Nilioga kwa kipindi kifupi baada ya kujianda nilimuanga Shangazi. Nilipendeza haswa kwa siku hiyo. Kuliko kawaida, hiyo ilimshitua hata Shangazi lakini nilimtoa hofu kwa maneno machache yaliyojaa ulaghai, hakubisha akanielewa.

    Taratibu kwa maringo nilijitoa kuelekea alipo Maria. Nusu saa nilikuwa na tazamana naye.

    Hali ya hewa ya eneo hilo, lilivutia mno, hata ile hali ya uchovu nilikuwa nayo, ilinitoka. Macho yangu yaliangaza huku na huku. Kila nilichokuwa na kiona kilifanana haswa kuwa eneo hilo.

    Niligiza soda Maria naye akagiza Soda wakati huo tukiendelea na mazungumzo. Alizungumza kwa upole mno, akijitahidi kuziweka hisia zake kwangu.

    Alimanisha kile alichokuwa anakizungumza, lakini yale maneno hayakuwa katika sehemu sahihi kwa maana majibu yangu hayakuwa yakitafsiri wazi wazi kile ambacho moyo wangu ulikuwa ukijihisi.

    Niliongea kwa mafumbo sana, mafumbo ya kumanisha Maria hakuwa Msichana ambaye moyo wangu ulikuwa ukivutiwa naye.

    Mpenzi msikilizaji licha ya Maria kuvalia nguo nyepesi iliyoacha sehemu ya kubwa ya mwili wake, ikiongeza utalii kwa wale ambao walikuwa wakijionea senima ile ya bure, lakini ilikuwa tofauti sana kwangu. Sikuwa na mguso, wala hisia za mapenzi dhidi yake, na mbaya zaidi hata zile za tamaa ya kujingiza katika mchezo mchafu wa ngono zembe ziliniondoka kabisa.

    Hakika hakuna sehemu yoyote ya viungo vyangu vya uzazi vilionekana kustusha na muoenekano wake, kila sehemu ilikuwa doro ikitazama vituko vyake.

    ________________

    Tuliendelea kuzungumza nusu saa ikatika, ni hapo nilipompatia nafasi Maria ya kufanya kile alichokuwa amekidhamiria. Nilijitoa kulekea chooni, Maria aliniangalia kwa jicho ambalo sikuwa nikielewa anamaanisha nini. Lakini hali ilikuwa tofauti sana niliporejea, nilipiga mafunda kadhaa ya kinywaji nilichoacha kwenye Bilauri ndogo juu ya meza iliyofunika vyema miili yetu.

    Robo saa nilikuwa hoi, kichwa kilikuwa kizito. Ulevi gani ulikuwa umenipata? Jibu sikuwa nalo. Mwili ulionekana kunishinda, nilijitahidi kupambana na kile lakini sikuweza, kilichofata kilibaki kuwa historia, yenye kuvutia kwa Maria, mimi ikiniweka katika namna nyingine.

    Sura nzuri, ilificha unyama wa Maria, na weza sema ni unyama kitendo cha kufanya mapenzi na mimi bila ridhaa yangu, kwa upande wangu nilioana nikitendo cha kinyama mno! Na hakika kilinifedhesha, na kunipotezea uaminifu katika nyumba ya mjomba, ikiniweka katika hali mbaya sana kwa usiku nzima wa siku hiyo. Walinitafuta sana simu yangu haikuwa ikipatikana, hilo liliwatia shaka zaidi, ikiwaongeza gadhabu sana.

    Sikuwa na cha kujibu hata niliporejea asubuhi yake, nilijiona mdogo zaidi licha ya ukubwa wa umbo ambalo liliokuwa likiendelea kujengeka kwa mazoezi kila kukicha. Lawama nilizipokea, zikiniweka katika hali mbaya zaidi kuishi kwenye nyumba ya mjomba.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijitahidi kupambana na lile, wiki nzima lilinisumbua kwenye kichwa changu na hata kiwango changu uwanjani hakikuridhisha. Nilicheza chini ya kiwango, kutokana na msongo wa mawazo, jambo lile likiendelea kunitafuna siku hadi siku.

    Ukweli sikutaka kuweka wazi, kwa maana niliona ni ngumu sana kueleweka kwa yule ambaye angelikuwa ananisikiliza maneno yangu.

    ____________

    Nilimtafuta Maria, kipindi chote hicho, lakini alionekana kunikwepa kwepa. Nilijitahidi sana, katika jioni moja nilipata kuoana naye, kwa kweli nilikuwa na hasira sana. Lakini msichana kama alikuwa anadawa vile. Hasira zangu zilitulia sauti mbembelezi ya Maria, ikapoza Hasira zangu. Msamaha wake nikaupokea, tukiweka makubaliano ya kutokuwa wapenzi, Maria akanielewa!

    Katika kunihakishia kuwa hali yangu ya nyumbani inakuwa vyema. Maria alimtafuta Shangazi kisha wakalizungumza suala lile. Hapo kidogo ikaleta amani kwangu. Ilikuwa dawa tosha, kwangu. Taratibu nilianza kulisahau jambo lile, na kurudi sawa.

    Mwezi moja baadae, timu ya yetu ya vijana, iliingia katika maandalizi ya kucheza kombe la vijana. Kombe ambalo lilikuwa likihusisha timu za vijana ambazo zinamilikiwa na timu zote zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara. Hivyo tukalazimika kuweka kambi. Ikiwa mara yangu ya kwanza kuweka kambi, katika maisha yangu ya mpira. Kambi ilivutia mno, karibia kila kitu kilikuwa kipya kwangu. Nilijitahidi kuzoea hali ile, kweli sikuchelewa nilizoea haraka.

    Baada ya ratiba ya mashindano kutoka, kila mchezaji alielewa, na uzuri kabisa mashindano yalikuwa yakichezwa kwenye uwanja wa karume, uwanja ambao mara kadhaa tulikuwa tukipata nafasi ya kuutumia kama uwanja wa mazoezi kwa timu yetu. Hiyo haikunipa wasi wasi maana uwanja huo nilijua vilivyo.

    Tarehe ya mashindano ikawadia, mechi ya ufunguzi kama bahati ikatokutanisha sisi na timu ya Majimaji ya vijana. Mechi ilikuwa kali sana, japo nilicheza kwa karibia dakika themanini za mchezo lakini, hakuna timu iliyofanikiwa kuibuka na goli, walionekana kutukamia mno, na mimi nilicheza kwa taadhari sana. Ijapokuwa jereha la kuvunjika mguu lilikuwa limepona lakini, bado nilikuwa nikicheza kwa kuogopa ogopa. Hivyo sikucheza katika kiwango cha kuridhisha sana, licha ya mwalimu kuonekana kuvutiwa na uwezo wangu.

    Baada ya mechi hiyo kuisha tukapewa mapumziko ya siku mbili, ni kama mapumziko hayo yalikuja na jambo la aina yake pasina mimi mwenyewe kufahamu. Hakika waswahili hawakosea kusema ‘Hakuna ajue kesho yake’



    Ni kweli hakuna ajuea kesho yake, ni kiwa katika matembezi, ghafla katika namna ya ajabu, nilihisi kuguswa kwenye bega langu, niligeuza shingo yangu kupambana na mguso ule. Ni ugeni gani huu kwenye macho yangu? Nilijiuliza kwenye kichwa changu, sikuwa na jibu pengine jepesi kwenye lile nilikuwa nikiliona.

    Naam! Mbele yangu ni msichana, msichana ambaye aliendelea kuyamaliza maneno pasipo kumfahamu ninani, lakini yeye alionekana kunifahamu kinagaubaga.

    Hakika nilikuwa nimesahau, nimesahau yule niliyekuwa nikimuona kwenye mboni za macho yangu. Hakuwa mwingine bali ni Janety, lakini safari hii alikuwa amebadilika sana umbo lake liiongezeka likionekana vizuri kwenye macho yangu, na kuniacha na sintofahamu ya kumtambua hapo mwanzoni pasingekuwa na utambulisho wake kwangu.



    Ama kwa hakika, ‘Milima hakikutani bali binadamu wanakutana’, alikuwa ni yeye Janety. Kwa vile tulikuwa barabarani, tulijivuta kidogo katika kimgahawa kimoja kumaliza hamu aliyokuwa nayo dhidi yangu, japo kwangu ilikuwa ajabu mno. Mpaka tunaingia katika mgahawa moja ulikuwa karibu na eneo la Ilala, mdomo wangu hakuwa na uchaguzi sahihi wa nini cha kuongea, Janety akioenekana muongeji mkubwa sana, tofauti na hata katika miaka ya nyuma aliponiacha pasipo sababu ya wazi.



    Ni miaka mingi sana ilikuwa imepita bila ya kusikia sauti yake, kiasi cha kwamba kwenye kumbukumbu za kichwa changu nilishalitoa jina lake. Kwa maana sikuihitaji kubaki na kumbukumbu ambazo zingendelea kuniumiza katika maisha yangu kadri siku zilivyokuwa zinaenda.

    Lakini sasa nilikuwa nikitazamana naye, niliagiza maji, akanichombeza kuagiza kinywaji chochote la hata ikiwa bia. Sikuwa na neno maji tu yalinitosha. Mimi nikiwa msikilizaji, akayatawala maongezi, aliongea mno. Aliongea bila vituo wala mkato. Loo! jambo lingine la kushangaza kwa upande wangu nilikuwa nikipambana nalo. Hakuwahi kuwa muongeji sana na hata nilipokuwa nikimtongoza aibu ilikuwa imetawala kwenye uso wake, lakini sasa nilikuwa nikipambana na uso wake vizuri kwenye macho yangu, aliniangalia vizuri bila kukwepesha macho, wakati huo akiendelea kunikumbushia mambo kadhaa wa kadhaa ya nyuma.

    Shaka huzalisha hofu. Hofu ya nini sasa? Naam! ya kupambana na kile nilichokuwa na kisikia na kukiona, nilijikaza kiume nikiendelea kuwa msikilizaji kama wasikilizaji wengine.

    ____________CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nusu saa ilitosha kumaliza kuzungumza kile alichoona yeye kinafaa, alioniomba nambari yangu ya mawasiliano, sikusita kumpatia. Wakati huo akinielekeza mahala anapokaa yeye na wazazi wake, nilipafahamu vizuri eneo hilo hapakuwa mbali sana na mtaa wa Karume. Eneo ambalo halikuwa geni machoni mwango ni kama vile tulikuwa tukipishana kwenye mitaa ya ile kwa maana, mara kadhaa nilikuwa nikipita nikielekea uwanjani, na hata nikiwa kwenye pilikapilika zangu.

    __________

    Tuliagana baada ya mabadilishano ya nambari za simu, Janety alionekana kubadilika mno, kuanzia maongezi na hata upande wa mwili wake, alikuwa na mwili wenye kuvutia sana, lakini kwa upande wangu sikusitushwa na mwili wake. Niliuona wa kawaida sana, na hata hisia zozote za mapenzi dhidi yake hazikuwepo kabisa.



    Nilisahau ya kuwa nilishawahi kulitoa chozi kwa sababu ya kulikosa penzi lake, nilisahau ya kuwa niliwahi kuyachukia mazingira nayo yakanichukia kisa ikiwa ni yeye. Wakati huo hakuwa na hata mwili wa kutisha na kuvutia kama ilivyo sasa. Lakini hakuna kilichonitisha mimi nilichokumbuka tu mapenzi ni hisia, hisia chanya ambazo kamwe haziwezi kugusana na hisia hasi.

    Kwa namna hiyo bado kulikuwa na daraja kubwa sana la kuyarudisha mahusiano na msichana huyo. ‘Hata ikiwa kwa dawa’, nilijisema kimoyo moyo, nikikazia kile ambacho kichwa changu kilichokuwa kinafikiri baada ya kuona naye.

    Sikuliweka manani, nilikatiza mitaa kadhaa, nikiendelea na mzunguko wangu, ikiwa lengo la mapumziko tuliyopewa na timu, zikiwa siku mbili tu, siku ya kwanza ikianza kwa namna hiyo.



    Mapema jioni ya siku hiyo, tulipata mtoko. Safari hii nikiwa na watoto wa mjomba pamoja na mjomba na shangazi. Azam na Sada walikuwa wachangamfu mno, kiukweli nilivutiwa sana na uwepo wao kwa upande wangu. Azam alifanana sana na mjomba, wakati Sada kama vile alimfata mama yake, japo hakuicha sana sura ya mjomba. Ni mtoto wa kike lakini mjomba alikuwa na damu kali kupita maelezo kiasi cha kwamba alilandana na mtoto wake huyo wa kike.



    Sehemu tulivu, mziki kwa mbali, yalisindikiza maongezi ya familia, vijwaji visivyo na kilevi, vilikuwa pamoja katika mkusanyiko wetu katika hoteli moja yenye hadhi ya kuitwa hoteli. Vicheko vya furaha vilitawala, utani kidogo wa shangazi na mjomba pia ulinifanya nijihisi tofauti sana, namna walivyokuwa wakataniana, nilitamani siku moja nami nipate mwenza wa kufanana na shangazi.

    Kwa maana ndoa yake ilionekana kupendeza sana, kiukweli kawivu cha mafanikio kidogo kilinitawala.

    Nilikumbuka wanawake wote ambao niliwahi kuwa nao katika mahusiano. Tabasamu na kicheko cha kupendeza cha Zuhura kilinipitia kwenye kichwa changu, na kuningiza katika tafakari nzito, ni kufanisha lile tukio linaloendelea pale ni kama mimi na Zuhura tungekuwepo eneo lile, tukizungukwa na watoto wetu. Lakini ajabu Zuhura sikuwahi kuwa na mahusiano naye, madhari mimi ndio nilikuwa nimezama kwenye penzi lake.

    Loo! Mpenzi msikilizaji haikuwa hivyo, ni muda nilikuwa sijasikia sauti yake na hata kufahamu ukweli ya kuwa angelikubali kuishi nami japo ingelinipa taswira ya kile nikiwazacho.



    Ghafla maumivu ya kumkosa Zuhura yakanipitia. Niliumia mno, niliumia kwa maana ni kama vile nilikuwa katika mtihani ambao hakika kila nilipokuwa nikijiangalia sikuwa na uwezo wa kufaulu mbele ya mtihani ule, na hata ingelikuwa nimeingia na daftari nzima la somo hilo bado nilionekana ningefeli tu.

    Mpenzi msikilizaji, ni vyema ukakutana na mitihani mingi kwenye maisha lakini ugopa sana kukutana na mtihani wa mapenzi. Hakika majibu nitakayojaza mimi, na wewe nikupa nafasi ya kufanya mtihani huo huo hakuna hata moja lingeweza kufafana na ya kwangu.

    Tulitumia masaa kama matatu kuwa eneo hilo, usiku wa saa mbili tulijitoa eneo hilo, na kurejea nyumbani. Hali ya nyumba ilikuwa kama tulivyo iacha hakuna kilichobadilika.

    Baada ya kupata chakula cha usiku, niliingia chumbani, kulala nikiwa na mtoto wa mjomba Azam. Alikuwa na miaka kama nane hivi, alijua kujieleza haswa. Maswali mengi ya kitoto niliyajibu usiku wa siku hiyo katika ustadi wa juu. Lakini swali moja ambalo sikulitegema kama ningeulizwa na binamu yangu huyo katika namna ambayo sikuitegemea, ‘eti ya kuwa nina mchumba?’ Swali lilikuwa zito kwake na ilinihataji kulijibu kwa usahihi pasipo kuleta shaka kwa Azam mtoto wa miaka nane, lakini mwenye akili ya kielevu.



    Nilimvuta pumzi ndefu, kisha nikaliweka sawa koo langu na kumkabili kwa jibu jepesi, jibu ambalo liliharibu hali ya hewa katika usiku huo na kuleta dhoruba kali.



    Ni mimi niliyekuwa nikiyatoa maelezo yale, nilijitahidi kuficha hali ya huzuni iliyoanza kunitafuna nikipambana na jibu nilimpatia Azam ya kuwa kipindi chote kile na umri wangu sikuwahi kuwa na mchumba. Hakika kweli ilianza kunitafuna ndani ya moyo wangu na kuni sababisha maumivu makali sana pasipo mategemeo. Niliumizwa na kile nilichokuwa na kijibu, kikinijengea kumbukumbu mbaya zaidi kichwani mwangu.

    Wachumba hawakuwa wachumba kabisa katika maisha yangu, wote walionekana kutoridhisha moyo wangu. Na hata kunipatia kile kilichokuwa kinaokosa moyo. Hakika moyo wangu ulihitaji thamani ya juu zaidi.

    Aliningalia kiudadisi mno Azam, akiendelea kuniuliza maswali mfululizo, ya kuwa ni vipi mpaka dakika hii sikuwa na mchumba wakati huko shuleni kwao watoto kama yeye tayari wana wachumba zao?

    Sasa nilikuwa katika mtihani mwingine, mtihani ulihitaji usaidizi wa fikra pevu za kutatua jambo.

    Ni ngumu sana kuficha ukweli katika maana halisi na ya kawaida mbele ya jicho la mtoto mwenye kichwa chenye uweledi wa hali ya juu. Mpendwa msikilizaji, sikuwa na jibu la kumridhisha mtoto, ilinibidi tu nitumie nguvu ya kiutu uzima ya kulimaliza jambo bila ya kuhitaji maswali kutoka kwake.

    ________CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usiku wa siku hiyo uliisha katika namna iliyoniumiza mno, moyo wangu ulionekana kuhitaji kitu, kitu ambacho hakionekana kuwa karibu na eneo nililikuwepo walau ingeletea faraja kwa upande wangu.

    Mpendwa msikilizajhi, yasikie mapenzi tu yasike katika masikio yako yote mawili, kwa maana uchungu na raha ya mapenzi ni ngumu kuiona katika jicho lako la kawaida, na kama ingelikuwa na uwezo wa kuyaona maumivu na raha ya penzi. Hakika katika hii dunia hakuna hata moja ambaye angelitamani kuwemo ama kukosa kuwemo kwenye mapenzi katika akili yake ya kawaida tu.

    Baada ya usiku ulikuwa na kila aina ya karaha kwa upande wangu, hatimaye Mungu aliweza kuniamsha mapema sana katika asubuhi ya siku iliyofata, ikiwa siku ya mwisho kwenye mapunziko yangu, lakini ilikuwa tofauti sikukitamani kitanda. Saa kumi na moja na nusu nilikuwa nje nikipambana kuufukuza upepo, lengo kujenga pumzi na kujimalisha zaidi kwajili ya mechi ambazo zilikuwa zinanikabili mbeleni.

    Mazoezi ya siku hiyo yalikuwa mazuri sana kwa upande wangu, mwili ulionekana kufunguka kuliko kawaida, huku miguu yangu ikionesha ukomavu wa hali ya juu na kuniongezea hali ya kujiamini mno.

    Lisaa limoja lilitosha kujiweka sawa, haraka nilijerea nyumbani, bafu likanipokea, maji ya baridi ya kuweka mwili wangu vizuri kwa miadi ya kuanza siku mpya. Wakati huo baada ya kumaliza kuvaa vizuri, mapema tu simu yangu ilitoa muito. Ilikuwa ni simu ya asubuhi sana, mpigaji akionekana ana shauku ya kusikia sauti yangu. Hofu ilijengeka kidogo, nambari ikiwa ngeni kabisa machoni mwangu. Nilisita kuipokea baada ya kuita kwa muda mrefu hatimaye nilipokea ilikuondoa hofu iliyoendelea kujenga nafasi ndani ya mwili wangu.

    Sauti haikuwa ngeni. Nilisikiliza, bila kuleta umakini na kile mzungumzaji alichokuwa anakiongea.

    Hakuwa mwingine alikuwa Maria, bado aliendelea kuishi na ndoto za kuwa na mimi, akionekana kuendelea kuhitaji huduma yangu. Akiyakiuka makabaliano yetu tuliyaweka hapo awali.

    Alizungumza kwa masikitiko zaidi, masikitiko ya kulikosa penzi langu. Akidai huenda kuna jambo atakuwa amelikosea na anaomba nimsamehe. Hakika sikuwa na neno la kukubali msamaha dhidi yake. Mdomo wangu ulishindwa lipi la kumjibu mwanamke yule na hata nilipoihitaji kujibu jambo lolote, ni nyakati hizo nilipokuwa nikitolewa macho na Azam. Loo! Mtoto alikuwa ameshamka hivyo akaninyima nafasi ya kuzungumza faragha na Maria. Udadisi wa Azam ukanifanya kuogopa kuzungumza chochote na Maria, nilichofanya nikumpa miadi ya kunitafuta mchana wa siku hiyo.

    Naam! Nilikata simu kuipokea salamu ya binamu yangu, wakati huo nilijiweka sawa, nikitafakari mambo kadhaa kichwani mwangu. Ni nyakati nilizoona zinafaa kujikumbusha habari za masomo. Nilitumia muda mwingi kusoma mpaka saa tano ya asubuhi, nilikuwa nikiendelea kupitia maandishi kadhaa wa kadhaa kwenye macho yangu.

    Nilitolewa kwenye kisomo na sauti ya mjomba akihitaji kuzungumza nami, nilijitoa ndani, la kumbe siku hiyo mjomba alikuwa ana safari kidogo ya nje ya mkoa. Hivyo alizungumza nami kidogo kisha alituaga.

    Hapo nilipata nafasi ya kupata kifungua kinywa, karibu nikiyapokea maneno ya kuchombeza kutoka kwa binamu zangu. Hakika niliyafurahia mno, yalinitoa upweke katika namna moja ama nyingine. Kidogo maneno yao yalipata kutakasa moyo wangu nami kujiona mtu mbele ya watu.

    Mchana wa siku hiyo kama nilivyoweka ahadi Maria alinitafuta kuzungumza nami, mazungumzo yalikatishwa na miadi ya kuona jioni ya siku hiyo, kwa maana nilihitaji kuona naye ilikuzungumza kwa kina kile alichokuwa anakihitaji kutoka kwangu. Kwa sababu maongezi ya hapo nyumbani nikiwa na simu sikuona ya kifaa zaidi kwa yale niliyoyahitaji kuyafikisha. Lakini safari hii nikiweka taadhari kubwa yasije kutokea kama yale yaliyopita.

    Suala la kumuaga shangazi halikuwa gumu. Ugumu ulikuja pale nilipohitaji kutoka nyumbani. Azam alionekana kuning’ania kutoka wote alipofahamu ya kuwa nilihitaji kutoka kidogo, hapo ilinibidi nitumie akili ya ziada na kumuacha solemba.

    Saa kumi na nusu nilikuwa nikitazama na sura ya mrembo Maria, alikuwa ana kila sifa ya kuitwa mrembo, ajabu hakuwa akinishutua licha ya urembo wake. Alivutia machoni, pua zangu ziliendelea kupambana na harufu nzuri ya marashi aliyokuwa amejipulizia Maria.

    Hali ya hewa ilikuwa ya kuvutia sana eneo hilo, vinguo vifupi vya wahudumu wa eneo hilo na wale wageni viliendelea kuleta mvuto zaidi ya wale wanaume walikuwa wamevikalia viti katika eneo hilo, ikiongeza nakshi kubwa katika mtazamo wa akili za binadamu ambazo zilikuwa zikijipa hadhi kubwa kuwemo ndani ya eneo hilo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hayo na mengine ya kushangaza naya kuvutia yalilitosha kabisa kusindikiza maongezi yetu tukiwa eneo hilo. Mimi nikipata nafasi ya kuwa mzungumzaji wa kwanza kwenye maongezi yetu. Niliongea ukweli wa kile kilichokuwa ndani ya moyo wangu, hakuna nilichokuwa nimeficha namna nilivyokuwa nikijisikia. Sikuweka taadhari ni jinsi gani yule aliyekuwa akinisikia atayapokeje maneno yangu. Hilo sikulijali nilizijali hisia zangu kwa kiasi kikubwa.

    Nilitumia uchaguzi sahihi wa maneno kwenye mdomo wangu. Maneno ambayo nilikuwa nikihakikisha kila nitakalo litoa litakuwa bakora kwa yule aliyekuwa ana nisikiliza, nikihitaji kumwadhibu kutokana na kile nilichokiona ubaya kwenye mtazamo wa akili yangu.

    Maria aliendelea kunisikiliza, alinisikiliza kwa makini sana, akionekana kutuguswa kabisa na kile nilichokuwa nikiongea kwa upande wangu. Sikutaka kuonesha na shindwa na kile nilichokiamua, lakini jambo nilifanya kumpatia nafasi ya kuzungumza. Hakika ilikuwa fimbo, fimbo ya kuumiza kwenye mwili wangu.





    Maria alizungumza kana kwamba maneno yangu yote niliyokuwa nikiyasema haya kumfaa kabisa. Hakika aliendelea kuniachapa fimbo, fimbo iliyoendelea kuniumiza pasipo kujitegemea, maumivu ambayo hayakuoneka wazi wazi kwenye mwili wangu.

    Maria alizungumza kwa ushawishi mno, ijapokuwa nilikuwa na msimamo wa hali ya juu lakini namna alivyokuwa akizungumza taratibu alianza kuniathiri kiasakolojia, kiasi cha kwamba nikijikuta na kubaliana na kile alichokuwa anakitaka. Nusu saa tu ilitosha kunibadilisha mawazo yangu, na kuingia rasmi kwenye penzi lake katika namna ya kushangaza mno.

    _____________

    Miadi tukaiweka ya kuonana siku nyingine, wakati huo muda ulikuwa umeenda sana, sikuhitaji kuitokea kama jambo la mara ya kwanza, Maria hakuwa na neno ila aliniomba anisindikize nami nikakubaliana na ombi lake.

    Wakati huo alijaribu kunisogelea karibu sana nami nilikaribisha. Hakika taratibu mgusano wa mwili wangu na Maria ni kama vile ilikuwa ikipalilia penzi lile jipya. Penzi lilianza kuchipua, jambo ambalo lilikuwa la tofuati sana. Siku hiyo kwa mara ya kwanza Maria alionekana kunivutia, sijui sababu ilikuwa nini? Ni kama vile nilikuwa nimelogwa.

    Mpaka ananifikisha nyumbani, Maria alipata nafasi kubwa sana kucheza na mwili wangu nami kucheza na mwili wake, na kuibadili jioni yangu. Nilimuwaza yeye kwenye kichwa changu hadi siku inaisha. Mpenzi msikilizaji Maria haswa aliniingiza katika tafakari nzito. Nilimuweka katika sehemu nyingine bila hata kuelewa uzuri na ubaya wa kuwemo katika penzi na Maria.

    ______________



    Asubuhi ya kuamkia siku iliyofata mapema sana, ilinibidi nianze kujianda ili kuwahi kambini, ni nyakati hizo nilipokea simu kutoka kwa Janety, alizungumza kwa bashasha sana nami nilionekana kuchangamkia simu yake, sikuhitaji kumweka katika namna ambayo ingenisababishia usumbufu hapo mbeleni. Dakika kumi zilitosha kumaliza maongezi yetu, ijapokuwa hakukuwa na jambo la maana sana kwenye mazungumzo yetu.

    Baada ya kumaliza kuzungumza naye, ni muda huo, nilipokuwa nikamalizia kuweka vitu vyangu sawa, na kwenda kupata kifunguo kinywa, wakati huo watoto wa mjomba na shangazi walikuwa wameshamka, wakishindana na habari za mimi kuondoka, lakini hakuona ambacho kingeweza kunizuia nilihitajika kwajili ya kuitumikia timu wale watoto hawakuwa wakilijua hilo.



    Saa mbili na nusu, tayari nilikuwa kambini mapema kabisa kuliko wachezaji wote, hakuna kilichokuwa kimebadilika baada ya wachezaji wote kufika, walimu walitueleza maswala ya timu, saa kumi na jioni, tulikuwa uwanjani kufanya mazoezi mapesi mepesi. Baada ya siku tatu, mechi tulikabiliwa na mechi ya pili.

    Mechi ilikuwa tofauti sana, tofauti hata na ya kwanza wapinzani wetu Ruvu shooting wakitukamia mno, lakini ilituchukua mpaka dakika ya themanini, sikuchelewa kuwa wadhibu, niliwadhibu kwa shuti kali, ilitupatia goli la kwanza. Hakika lilikuwa goli bora sana kwa upande wangu, likiwa goli la ushindi. Likinifungulia idadi ya magoli kadhaa wa kadhaa niliyoyafunga kwenye ligi hiyo mpaka tunafika fainali na timu ya Majimaji. Thamani yangu ikiongezeka, na kuwa tishio ndani ya timu, na hata habari zangu zilianza kuwa vutia timu kubwa nyingine za ligi kuu.

    Hiyo haikutosha mechi ya fainali niliwadhibu kwa magoli yangu matatu, timu yetu ikishinda goli tatu dhidi ya moja dhidi ya wapinzani wetu wa Majimaji. Ligi tulimaliza kwa namna hiyo nikibuka mfungaji bora na mchezaji bora wa mashindano.



    Hali iliyoleta faraja sana kwa upande wangu, zikiendeleza uvumi wa kujiunga na timu mbali mbali za ligi kuu ambazo zilikuwa zikionesha kunihitaji. Suala la mimi kuendelea kucheza Simba ya vijana, lilibaki kwa viongozi wa timu na mjomba ambaye yeye ndio alikuwa akinisimamia.

    Wiki mbili baada ya kumaliza mashindano ni wiki hizo ambazo nilikuwa nikihitajika chuo kwajili ya mitihani, nilijianda vya kutosha mitihani hakunisumbua sana, na hata majibu yalikuwa katika wastani wa kile nilichokuwa nimekisoma kikinihakishia kuwa hakuna kilichoonekana kunichanganya, licha ya kutokaa chuo.

    Wakati huo nilizipokea simu nyingi kutoka kwa Janety, lakini nilishia kumkwepa kwepa, sikuhitaji kujichanganya naye, kwa maana Maria alionekana kunikolea haswa, katika siku moja moja ambazo nilipata nafasi ya kuonana naye. Maria alionekana kuniridhisha kwa kiasi kikubwa, alijua kucheza nami, nami nilijua kucheza naye, kuna kipindi mpaka nilikuwa nikijutia kwanini sikuwa na msichana huyo hapo mwanzoni.



    Hakika ‘majuto ni mjukuu’, Maria alinivuta mno kwenye penzi lake, alijua kuziteka hisia zangu, na mimi niliamua kuwa naye, japo ilikuwa kwa taadhari sana, nikihofia kushuka kwa kiwango changu. Hivyo licha ya kuwa na Maria nilikuwa na nidhamu ya juu sana na kiwango changu.

    Mwezi wa moja baadae baada ya dirisha la usajili mdogo kufunguliwa timu ya Simba aliamua kunipandisha katika timu ya wakubwa, wakati huo katika timu ya vijana tulifanikiwa kupanda mimi na goli kipa wa timu yetu ya vijana. Furaha iliyoje kwangu, hakika nilifurahia mno jambo la kwenda kucheza ligi kuu, liliongezea thamani ya hali ya juu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanzo ulikuwa mgumu sana sikufanikiwa kucheza mechi kama nne hivi niliambulia kukaa bechi tu, nikishuhudia wachezaji wengine wakicheza, sikukata tamaa niliamini miguu yangu, niliamini kabisa kitendo cha kupata nafasi siku moja kingenipatia hata namba ya kudumu ndani ya kikosi hicho kwa maana bado sikuona wakunizuia kabisa licha ya kutokuwa na uzoefu wa kucheza ligi kuu. Wakati huo hali ya timu ilikuwa katika kiwango kilichokuwa kinavutia mno, na hata kwenye ligi tulikuwa nafasi ya pili nyuma ya timu ya Mtibwa.



    Mechi ya tano, ilikuja na mbinu nyingine ya kocha, mechi likuwa ni ya muhimu sana kwa maana kitendo cha kushinda ili kuwa ikituwezesha kuongoza ligi. Katika mechi hiyo kwa namna nisiyoitegemea niliwekwa katika wachezaji watakaotumika katika mchezo siku hiyo. Mpaka dakika ya sabini timu hatukuwa tukiongoza mbele ya timu ya Prison.

    Mwalimu alinijanyua kutoka bechi, hakinihitaji nipashe iliniweze kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine, jambo ambalo sikulitegemea kabisa, nilijenga kujiamini nikipasha misuli moto dakika tano nilikuwemo uwanjani wakati huo, dakika zilibaki chache sana uwanjani.

    Kitendo cha kupokea mpira kwa mara ya kwanza, sikuchelewa kufanya yale niliyokuwa nikiyafanya kwenye timu mbali mbali, haikunitumia nguvu sana, niliwalamba chenga mabeki wa timu pinzani, na kubaki na kipa kilichofata kwa ufundi wa hali ya juu, niliweka mpira katika eneo sahihi, na kuipatia timu goli la kuongoza, goli ambalo lilidumu mpaka mpira unamalizika. Na kutufanya tuongeze ligi.



    Asubuhi ya siku hiyo, magazeti yote yaliamka na jina langu, pasipo kujua kuwa jambo lile lilikuwa likinitengenezea kitu cha aina yake namna.



    Asubuhi ya siku hiyo unasema Magazeti yaliamka na jina lako? Wakati hawakujua kama kuna kitu kinajitengeneza. Mmh kitu gani tena hicho ndugu Daudi? Mpendwa msikilizaji bado Daudi Msomwa anaendelea kuunguluma. Ni kusihi tu ni muhimu kukifahamu hicho kitu? Basi usikose kuungana nasi kwenye sehemu inayofata.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog