Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

THAMANI YA MOYO - 5

 





    Simulizi : Thamani Ya Moyo

    Sehemu Ya Tano (5)



    Thamani Ya Moyo...Maumivu Ni Haki Yangu





    baada ya Daudi Msomwa kuifungia timu yake goli la ushindi dhidi ya mtibwa. Asubuhi magazeti ya na amka na jina lake, bila kujua kuwa kuna kitu kilikuwa kinajitengeneza. Je ni kitu gani hicho? Ungana nami kwenye sehemu hii ya kumi na saba.

    Mpenzi msikilizaji, mambo yalibadilika sana, katika namna ya haraka mno, jina langu kuanzia kwenye timu hadi kwenye ligi liliongezeka thamani maradufu, ikileta chuki wa baadhi ya wachezaji ambao tulikuwa tukicheza katika nafasi moja na hata kwa mabeki wa timu pinzani namna nilivyokuwa nikiwaweka katika wakati mgumu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa maana baada ya mechi hiyo. Mechi iliyofata mwalimu pia alinijumuisha katika kikosi kitachoanza kwenye mechi iliyofatia, japo siku anza ila safari hii, nilipewa dakika nyingi za kucheza uwanjani pindi nilipoichukua nafasi ya mchezaji mwingine. Dakika hizo nazo sikuzifanyia ajizi magoli mawili nikaweka kwenye mguu wangu, katika ushindi wa goli tatu tulipata katika siku hiyo.

    Naam! habari ikawa nyingine kama ilivyokuwa kwa mara ya kwanza , kila kituo cha habari kilizungumza jina langu, harufu ya umaarufu ikaanza kuninukia haraka kuliko hata mategemeo yangu , kwa maana kitendo cha kucheza mechi tatu nikitokea bechi nikifunga magoli katika kila mechi ilinipa nafasi moja kwa moja ya kupata namba katika kikosi cha kwanza katika mechi zote ambazo zilikuwa zimebakia katika msimu wa ligi ambapo, timu yetu ilifanikiwa kuchukua ubigwa wa mashindano japo mimi sikufanikiwa kuchukua tunzo ya mfungaji bora, ila jina langu lilipendekezwa katika tunzo za wachezaji katika ligi kuu, mimi nikiweka katika kipengele cha mchezaji bora kijana, wakati huo huo ndani ya timu nililipewa tunzo ya mfungaji bora kijana zaidi, ikiambatana na mchezaji bora wa miezi miwili mfululizo.

    Hakika habari ilikuwa nyingine kabisa katika maisha yangu. Kwa maana thamani ya timu ilikuwa kubwa mno. Hivyo jina langu lilivuma haswa!

    __________

    Mwaka ulikuwa wa bahati sana, kila tunzo nilipendekezwa kugombea, nilifanikiwa kuzipata. Sasa jina langu lilikuwa katika wakati mgumu sana, usumbufu kutoka kwa watu tofauti tofauti, ambao walikuwa wameipata namba yangu ya mawasiliano, ilifanya hata baadhi ya simu muhimu kushindwa kuzipokea kutokana na tabia ya watu ambao kila kukicha, hawakuchoka kunipigia simu wakihitaji huduma yangu.

    Katika namna tofauti wapo wale ambao walikuwa wakinihitaji kimapenzi, na wale viongozi wa timu fulani kubwa zikihitaji huduma ya miguu yangu. Hiyo ilinitia shaka sana hata kufanya kushindwa kupokea nambari ngeni ambazo hazikuchoka kunisumbua bila kujua huenda nilikuwa nikikosesha raha mtu fulani upande wa pili, aliyeonekana kunihitaji zaidi katika kipindi hicho.

    _____________

    Wakati huo, penzi langu na Maria lilikuwa likiendelea katika namna iliyokuwa ikiendelea kuniridhisha sana, uwepo wa Maria kwangu, nilifurahia mno hasa hasa sauti yake iliyokuwa ikifanana na Zuhura iliniweka katika namna ambayo ilizidi kunikonga nyoyo zangu na kusahau machungu mengi niliyopitia kwa kukosa penzi la Zuhura. Hivyo hata ukosefu wa Zuhura kwenye moyo wangu haukuwa pengo kubwa sana kwa nyakati hiyo kwa maana Maria alioneka kuliziba.

    Mpendwa msikilizaji Maria alinipenda kweli, wivu ukalichukua penzi letu, Maria alikuwa anawivu mkali kupita maelezo wakati mwingine ulikuwa ukiniweka katika hali ya tofauti sana, haswa kutokana na simu ambazo nyingi nilizokuwa nikizipokea kutoka kwa Janety ambaye naye kila kukuicha alijitahidi kulipigania penzi ambalo halikuwa hai tena kati yangu na yake. Lakini Maria hakulilielewa hilo.

    Ndugu asikuambie mtu mapenzi yana nguvu katika namna ya aina yake, Maria hakuwa akinielewa hata kidogo inapotokea simu ya Linda ijapokuwa ukweli juu ya Janety niliweka wazi kwake, lakini hiyo haikufanya kukubaliana na hali ile aliyekuwa ikimpeleka puta. Pasipo mategemeo yangu Maria aliamua kufanya jambo ambalo liliniweka katika hali nyingine sana, baada ya kile kinachoitwa uvumilivu kumshinda.

    Maana kitendo cha kuchukua namba ya Janety kwenye simu yangu hakuchelewa kufanya kile kichwa chake kilivyokuwa kikimtuma. Shambulizi la aina yake Maria alilifanya dhidi ya Linda, shambulizi lililoteka magazeti ya udaku wiki nzima katika kile cha kujitafutia wasomaji zaidi ilikuongeza vipato vyao.

    Naam! Shambulizi hilo liliniweka katika hali mbaya zaidi kuanzia kwa wazazi hadi kwa mjomba walizungumza mno, kwa maana magazeti ya udaku hayakuchelewa kunimulika mapapalazi kila kukicha walinitafuta pale nipokuwa nikiingilia na kutokea.

    Wakati huo Maria aliingia katika mgogoro na vyombo vya dola kwa maana kitendo cha kwenda kumshambulia Janety, kilisababisha kuingia katika kesi kati yake na vyombo vya dola. Kwa maana baba yake Janety alikuwa anamkono mrefu kwenye vyombo hivyo, hilo lilikafanya Maria atokemee mahali pasipo julikana, japo nilijitahidi kumtafuta Maria sikumpata, hiyo akainiangaukia mimi, lakini hakunisumbua sana mambo ya kaweka katika mstari.

    Ni wakati huo ambao Janety alimua kuyaacha maisha yangu naye kuangalia maisha yake katika namna nyingine, kwa maana ilikuwa ni aibu kubwa sana kwake, kitendo alichofanyiwa na Maria kiliidhalilisha hata katika familia yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ____________

    Mwezi mzima nilingia katika misukosuko, wakati huo Maria hakouonekana kabisa hata kuisikia sauti yake nilikosa, mazoea ya kuwa na mawasiliano naye yalinitafuna kidogo kidogo, na kunisababishia msongo wa mawazo katika nyakati fulani.

    Nijitahidi sana kupambana na hali iliyokuwa ikinikabili, katika kipindi ambacho nilikuwa nikibaliwa na mitihani ya chuo. Nikipindi hicho ambacho pia timu ilikuwa ikijiindaa kwenye michezo yake ya kimataifa, ijapokuwa nilifanikiwa kupata matokeo ya wastani ambayo yaliniweka katika hali nzuri kidogo, lakini haikuwa kabisa mategemeo yangu. Wakati huo kiwango changu kilichelewa kukaa sawa kuendena na kasi ya timu, hivyo ilinibidi nifanye mazoezi ya kasi sana nikiwa binafsi kabla ya kufanya mazoezi ya pamoja na timu kutokana na mambo kadhaa wa kadhaa yalikuwa yamejitokeza kwa upande wangu.

    Wiki mbili, mbeleni tulikabiliwa na mechi ya ligi ya mabingwa, mechi ambayo ilituhisisha na timu ya Enyimba kutoka Naigeria, ni moja kati ya timu kubwa barani afrika kwa nyakati hizo. Mechi ilijawa na shauku kubwa sana kwa upande wangu, kwa maana nilifahamu wazi katika mechi hiyo ya kwanza ya kimataifa, kwa mara ya kwanza katika historia ya timu ya Simba. Nilikuwa nikiandika jambo lingine la kuvutia mno.

    Maandalizi ya mechi tuliyafanya kwa ustadi wa juu, ikichangiwa zaidi sisi ndio tulikuwa wenyeji wa mechi hiyo. Hivyo viongozi walichakarika mno kuweka mazingira ya uwanja vizuri, wakaisidiwa na shirikisho la uongozaji wa mpira nchini kuhakikisha kila kitu kinaenda kuwa katika mstari ulikuwa umenyooka. Siku hazikuongopa, ya kwanza ilikatika, ya pili, hatimaye siku ya mechi ilitimia, wakati huo tulibakiza dakika chache kuingia uwanjani, wachezaji tukiwa katika homa ya mpambano. Amini usiami mpenzi msikilizaji.

    Kweli siku hazikuongopa, ya kwanza ya pili hatimaye siku ya mechi.



    Uwanja ulikuwa umefulika katika kila kona, washabiki wa timu yetu, walionekana kuwa na morali ya juu sana, jambo ambalo lilituzidishia kujiamini kwa kila mchezaji wa timu yetu. Wakati huo nami nilikuwemo katika wachezaji wa kikosi cha kwanza walikuwa wamevalia jezi kuwa kabili wapinzani wetu.

    Baada ya salamu za timu zote mbili, mpira ulianza katika kipindi cha kwanza, wapinzani walionekana kuja na mbinu ya kuzuia. Kwa upande wetu tulifanya mashambulizi mengi sana lakini hayakufanikiwa kuzaa goli, dhumuni ambalo tulikuwa tukilihitaji kwa udi na uvumba.



    Mabeki wa timu ya Enyimba walionekana kujipanga vyema sana, kwa maana hata yale mambo yangu ya kuwasumbua mabeki kwa chenga za maudhui, wao hawakuchelewa sana kuja kuchukua mipira miguuni mwangu. Japo nilionekana kuwa msumbufu sana kwao.

    Wakati huo mipira yote ilionekana kucheza kwangu, kwa maana kidogo nilikuwa na utilivu ukilinganisha na mshambuliaji mwenzangu, hii waliijua wapinzani hivyo hawakuwa wakiniacha nicheze na mchezaji moja kwa maana nisingechelewa kuwaadhibu. Miguu yangu ilioneakana kuwa na nguvu zaidi. Tabia yangu ya kufanya mazoezi binafsi kabla ya wenzangu iliniweka fiti sana.

    ____________

    Baada ya kwenda mapumziko, hali ilikuwa tofauti sana tulivyorejea kipindi cha pili, Enyimba walitushambulia haraka haraka, hawakuchelewa kupata goli.

    Hakika walikuwa timu yenye mipango na uzoefu wa ligi ya mabingwa ukilinganisha na timu yetu licha ya kuwa timu kongwe nchini. Kwa maana dakika kumi na tano za kwanza za kipindi cha pili walizitumia kutufunga alafu kilichofata hapo walirudi nyuma kuzuia. Sisi tukihaha kusaka goli la kusawazisha tena, baadala ya kutafuta ushindi katika mechi hiyo.

    Mpaka dakika ya sabini mambo yalikuwa magumu kwetu, lakini kosa moja walilolifanya sikuchelewa kuwaadhibu na mpira mdogo wa adhabu uliomshinda mlinda mlango wao, akiniacha nikiaandika historia nyingine kwenye maisha yangu ya soka.

    Uwanja mzima ulilipuka kwa shangwe, wakiliimba jina langu, kiukweli japo tulikuwa tunatamani tupate ushindi dhidi yao, mpango wao wakutafuta suluhu ulifanikiwa kwa namna hiyo. Mechi ikaasha kila timu ukitoka na goli moja moja.



    Waandishi wa habari hawakuchelewa kuja kutumulika hasahasa mie, nami sikuvikimbia kwa maana nilishakuwa mzoefu wa kuzungumza na vyombo hivyo. Ni nyakati hizo ambazo nahodha wa timu ya Enyimba alipokuja kuomba tubadilishane jezi, hiyo ikiwa habari nyingine, habari ya kuvutia zaidi kwa upande wangu na taifa kwa ujumla. Ilikuwa heshima sana kwa mchezaji wa kiwango cha kimataifa kuja kuiomba jezi yangu ilionekana wazi alikuwa amevutiwa na uchezaji wangu.

    __________

    Mabadilishano ya jezi na mchezaji yule, yakaitengezeza historia nyingine ndani ya timu yetu, kila moja alisifu uwezo wangu niliouonesha ndani ya mechi hiyo, kocha naye hakusita kuonesha furaha yake kutokana na kile ambacho mchezaji mdogo kabisa kama mie kwa namna gani nilivyokuwa nikijituma kuijengea timu heshima.

    Nilizipokea ofa nyingi sana, za kwenda kupumzika baada ya mchezo ule wadhamini wa timu yetu, hawakuchelewa kuninunulia nyumba, habari ikawa nyingine kabisa, nilipahama kwa mjomba nikahamia nyumbani kwangu. Baada ya kuweka mambo yote sawa na wazazi hawakuwa na shida katika jambo hilo walinipatia baraka.

    Sasa jina la Daudi Msomwa lilikuwa kubwa, licha ya kutolewa mapema katika mashindano ya ligi ya mabigwa lakini kiwango nilichokuwa nimekionesha kilinipa heshima sana kikinifungulia njia ya kwenda kufanya majaribio katika timu kadhaa za bara la ulaya.

    __________

    Nilifanya majaribio katika timu kadhaa za kule nje, karibia zote zilionekana kuvutiwa na huduma yangu. Kilichokuwa kinashindikana kukamilisha dili la usajili. Dirisha la usajili kwa wakati huo lilikuwa bado halijafunguliwa hivyo wakanihitaji ni subiri mpaka dirisha la usajili litakapo funguliwa. Iliwaweze kunifanyia vipimo vya afya na taratibu zingine za kimasirahi kufanyika, mjomba akiwa msimamizi mkuu ya mambo yangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/***********

    Ni nyakati hizo ambazo nami nilikuwa nikimaliza ngazi nyingine ya elimu yangu, hiyo ikanifanya niwe huru kwa maana, sikuhitaji tena kurudi kuendelea na chuo katika ngazi nyingine. Kwa maana nilihitaji kujikita zaidi kwenye maswala ya soka na yalionesha dhahiri kuwa yapo katika mstari ulinyooka.

    Mkataba wangu na timu ya Simba uliboresha vilivyo, mshahara wa maana nikawa na upokea, na kwa vile sikuwa mtu wa starehe, wazazi waliyafaidi matunda yangu kwa kiasi kikubwa sana. Wakati huo sikuwa na mwanamke, Maria hakujulikana wapi alikuwa ametokomea na hata nilipozitafuta habari zake sikuzipata kabisa.



    Hivyo maisha ya mapenzi hayakuwa yakichukua nafasi kwenye mwili wangu. Ijapokuwa kuna nyakati kama mwanadamu nilikuwa nikishikwa na hisia kali sana. Lakini mapenzi yote nilikuwa nimeyaamishia kwenye miguu yangu.

    Hapo ikaleta tofauti sana kati yangu na wachezaji wengi wenye majina makubwa kwenye ligi kuu. Kwa maana wengi sana walikuwa wakinishangaa, kwa namna nilivyokuwa nikipokea mshahara mzuri lakini sikuwa mtu wa starehe kama ilivyokuwa wao. Si kwamba nilikuwa sipendi starehe la hasha mara kadhaa nimekuwa mtu wa kupenda kuheshimu hisia za moyo wangu unataka nini? Kwa wakati gani? Na kwanini unahitaji hicho kitu? Nikijiridhisha na kile ninachokiona kwenye macho yangu na fikra za ubongo wangu hapo ndipo walau naweza kumtakia msichana neno nakupenda. Na mara kadhaa huwa nikipenda napenda kweli. Sipendi sana maigizo kwenye mapenzi, kwa sababu najua athari za kuleta maigizo kwenye mahusiano yoyote yale.



    Mpendwa msikilizaji nikusihi tu, ni vyema ukazitendea haki hisia zako, hata kama itachukua muda mrefu mpaka pale utakapoguswa kisha kuwemo kwenye dhana iitwayo mapenzi. La sivyo unaweza ukajikuta unapata wakati mgumu sana kuingia katika jambo ambalo ni kama ulikuwa umelazimishwa kwa namna moja ama nyingine.

    Naomba nikupe siri moja tu, penzi la kwanza daima huwa na mguso wa hali ya juu kushinda yote, kwa maana hapo karibia wengi wetu huwa tunapenda katika maana halisi. Na hii hupelekea hata mtu kuishia katika namna ya kuyachukia mapenzi ama kuyafurahia. Yote kwa yote ni kutokana na matokeo chanya ama hasi ya penzi hilo.

    Kwa upande wangu licha ya kupitia kwa wasichana wengi bado moyo wangu kwa nyakati hizo ulikuwa haujapata kile ambacho inakihitaji. Ilinihitaji kusubiri zaidi. Kama ilivyokuwa na hamu shauku yako ya kutaka kujua mengi kuhusu maisha yangu. Basi nami ilinihitaji kusubiri zaidi ili kupata thamani ya moyo wangu kwenye dhana ya mapenzi.

    Baada ya dirisha la usajili kufunguliwa barani ulaya. Nilipanda ndege na kwenda kufanya majaribio kwa mara nyingine, wakati huo nikipitia kwenye timu tofauti kabisa na zile za mwanzo.

    Nilifanya majaribio wa wiki moja kwenye timu ya Sevira ya nchi Hispania katika wiki hiyo. Majibu hayakuja mapema, hivyo kwa vile bado nilikuwa na mikakati hiyo nilipata fursa ya kwenda nchini Swideni kufanya majaribio na timu ya White Star.

    Naam! majaribio ya nchini Swideni yalikuja na namna nyingine katika maisha yangu. Labda niweka wazi kabla sijaendelea, mpenzi msikilizaji ni ngumu kujua ni namna ipi? Hata nikupa nafasi ya kuzungumza baadala yangu.



    Wiki mbili zilikuwa za faraha sana ndani ya nchi ya swideni safari hii nikiwa nimeongozana na mjomba na kiongozi moja wa timu yangu ya Simba. White Star walionekana kukubaliana na kiwango changu kwa asilimia kubwa sana. Hivyo hawakutaka kuchelewesha usajili wangu kama uongozi wangu walivyokuwa wakichelewesha kutokana na kusubiri ofa ya Sevira ambao nao walionesha kunihitaji kwa udi na uvumba. Lakini pesa waliokuwa wakitaka kuitoa White Star ilikuwa ina masilahi sana na hata mkataba ambao, walikuwa wakiingia nami ulikuwa upo na vipengele vizuri. Hivyo haraka nilitakiwa kufanya vipimo vya afya. Ilikukamilisha mchakato wa usajili.

    Zoezi lilikuwa rahisi tu, baada ya kufanyiwa vipimo vya afya, jezi namba kumi na saba walinikabidhi, habari zilikuwa za kuvutia mno, kuanzia nchini Swideni hadi nchini Tanzania.

    Usajili wangu ukakamilika namba kumi na saba, jina Daudi Msomwa mgongoni lilikawa limetambulisha rasmi ndani ya timu hiyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wiki tatu, nilitumia kuyazoea mazingira mpya, wakati huo nilipangishiwa nyumba eneo ambalo halikuwa mbali na uwanja wetu wa kufanyia mazoezi. Tofauti na kwetu wenzetu walikuwa wameendelea sana, nyumba ilikuwa ya kuvutia mno. Huduma muhimu za kibinadamu zilikuwa zikipatikana kwa urahisi.

    Hali ya hewa nayo ilikuwa nzuri zaidi na ilinipenda sana, kitendo cha kukaa wiki tatu tu, hata kiwango changu kilimalika na kuwa imara zaidi sasa nilijiona mchezaji wa hadhi ya juu sana.

    Wiki ya nne, ligi ya Swideni ilianza nikiwa sura ngeni kabisa kwenye timu ya White Star, na bahati nzuri wageni katika timu hiyo tulikuwa wachezaji kama wa tano hivi kutoka nchi tofauti tofauti za bara la Afrika.Tulizoeana haraka haraka na kujenga urafiki kwa upande wetu, jambo ambalo lilikuwa nikinifanya nijione niko nyumbani kabisa.

    Sikuchelewa kuingia kwenye kikosi cha kwanza wakati huu majukumu yangu yakabadilika, sasa mimi ndio nilipewa nafasi ya kuanza katika mfumo wa kocha nikiwa mshambuliaji wa mwisho kabisa. Mfumo hakunipa shida kilichofata hapo, mpaka msimu unamalizika nilifunga magoli arobaini. Wakati timu yetu ikiamaliza nafasi ya pili.

    Mimi nilibuka mfungaji bora na hata kupata tunzo ya mchezaji bora ndani ya timu yetu. Habari ilikuwa nyingine kwa mabeki wa timu pinzani, niliwanyanyasa vile nilivyokuwa nataka.

    __________________

    Baada ya ligi kumalizika nilipata fursa ya kurejea nyumbani, nyumbani kukanipokea nchini Tanzania kwa aina yake kabisa, habari zangu zilisikika kila pande, ikinitengenezea ukaribu na mwanadamu mwingine.

    Kwa maana siku tatu baada ya kurejea nyumbani, sikuchelewa kuipokea simu kutoka kwa msichana, msichana ambaye hakika bado alikuwa akiishi kwenye moyo wangu. Sauti mbembelezi ya kike ilipenya kwenye masikio yangu na kadri ilivyokuwa ikipenya kuna jambo lilikuwa linajirudi kwenye ubongo wangu.

    Hakuwa mwingine mpendwa msikilizaji, ile sauti iliyokuwa ikipenya kwenye ngoma za masikio yangu ikipita kwenye simu yangu, alikuwa Zuhura alibadilika katika maongezi yake, kuliko kawaida safari hii alionekana kukomaa kiakili.

    Tulizungumza kwa muda mrefu sana, mazungumzo yaliyojaa na kumbukumbu za zamani, hata hamu ya kuulizana nikipi kinaendelea kati yetu hakikuwepo. Hakika kila moja alionekana kuwa na hamu na mwenzake, hakuna aliyeonekana kuchoka kumsikia mwenzake. Simu hiyo hakumaliza hamu yangu mpendwa msomaji.

    Maana ilikatishwa na jambo fulani kwa upande wa Zuhura huku akihidi kunitafuta baadae ilikuendeleza yale maongezi yetu. Siku amini kabisa kile nilichokuwa nakisikia kwenye masikio yangu. Lakini ukweli ulibaki kuwa kweli ile sauti ilikuwa ni ya Zuhura kabisa. Msichana ambaye nilipenda haswa!

    Kwa wakati huo moyo wangu ulihisi kupitiwa na baridi kali, baridi lilikuwa likiamsha hisia ambazo zilianza kujizika ndani yake. Hisia za mapenzi dhidi ya Zuhura. Naweza sema, penzi la kweli ni ngumu sana kupotea kwenye nyoyo za watu, kwa maana kwa upande wangu bado nilijihisi ni na deni kubwa ndani ya maisha yangu. Moyo wangu ulihitaji kitu, kitu cha kuupa faraja ya hali ya juu.

    Hakika nilijihisi kusuhuzika mno. Msuhuzo ulikonga nyoyo katika kila pande ya moyo wangu. Siku nzima niliona tamu kwa upande wangu. Wakati huo, mambo yalikuwa mazuri sana kwa upande wangu, pesa nilikuwa nayo ya kutosha jambo la mapenzi ndio kitu ambacho nilikuwa nimekikosa kwa muda mrefu. Lakini namna nilivyokuwa nikizungumza na Zuhura sasa niliona wazi huenda nafasi nikaipata kwake na ile kadhia ya mapenzi kuweza kupotea kwenye maisha yangu kwa kuwa na msichana ambaye moyo wangu ulikuwa ukiridhika naye.

    Usiku wa siku hiyo, sikio lilikuwa na shughuli ya kuisikia sauti ya Zuhura, hakika kama nilikuwa bwege katika miaka yote, safari hii ilikuwa tofauti sikuchelewa kuweka wazi namna gani moyo wangu ulivyokuwa ukiapata maradhi ya kulikosa penzi lake.

    Nilitumia muda mwingi kuelezea jinsi gani nilivyokuwa nikipata shida kwa miaka yote. Zuhura akibaki msikilizaji wa maombi yangu. Nilalama kama vile nilikuwa nikidai haki yangu Mahakamani la hasha, wazi nilikuwa nikiweka jinsi gani ya kuwa nimeshindwa kuishi bila ya penzi lake. Nikiliweka kusudio langu wazi la kuitaji kufunga ndoa na Zuhura.

    Jibu halikuwa jibu, Zuhura akuzungumza chochote kuhusu namna gani ameyapokea maombi yake, alinihitaji kusubiri kwa siku mbili mbeleni. Ni siku hizo ambazo likizo yangu ya kukaa nchini ilikuwa ikimalizika. Nilimsihi sana ya kuwa aweze kunipatia kabla sijaacha ardhi ya Tanzania kwenda katika majukumu ya kikazi.

    Zuhura alinielewa, usiku wa kumkia safari alikuja na jibu; jibu la kushangaza mno kwako, lakini ilikuwa la kuvutia kwenye moyo wangu. Zuhura kwa mara ya kwanza alinitamikia ananipenda, na si tu kwa kunifurahisha la hasha yuko wazi kwa lolote. Yote kwa sababu ya upendo ambao pia naye ulikuwa ukamtafuna kwenye maisha yake, alizungumza sana namna gani alivyokuwa ameishi muda mrefu bila ya kuweka wazi ukweli ambao ulikuwa ukimtafuna!

    __________________

    Ghafla nilishutuka usingizini nikiwa natokwa na machozi nikijitoa kitandani. Nililia kwa namna kumbukumbu ya maisha niliyoishi na Zuhura iliendelea kuninyanyasa, miaka kumi sasa, imeendelea kubakiza kumbukumbu mbaya kwenye maisha yangu. Nilitumia nguvu sana kumpata Zuhura lakini Mungu alimchukua kwa urahisi zaidi ugonjwa wa ghafla wa shinikizo la damu. Umefanya kuipoteza thamani ya moyo wangu kwa hali ya urahisi zaidi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliishi na Zuhura kwa miaka kumi tu, miaka saba katika ndoa, kilichofata hapo, kimebakiza historia mbaya kwenye maisha yangu. Tangu hapo moyo wangu hakulipata chaguo lingine la kuishi naye kwenye maisha yangu. Faraja yangu pekee ni Maua, mtoto pekee nilijaliwa kuzaa na Zuhura kabla ya kifo chake. Hakika moyo wangu bado upo kwenye rindi la kulikosa Thamani yake halisi. Licha ya umarufu nilikuwa nimejizolea na uwezo wa kifedha nilikuwa nao. Kwa maana tangu hapo habari za mahusiano kwangu, imekuwa hadithi ya kufarahisha mwishowe kuhuzunisha.

    Mmhh aiseh pole sana ndugu Daudi Msomwa. Hakika ni Thamani ya moyo maumivu ni haki yangu. Ni seme jambo moja tu, huu ndio mwisho wa simulizi hii ya kuvutia na ya kuudhunisha. Kumbuka tu imeandikwa na mwandishi Yona fundi na kusimuliwa nami msimulizi Tony Terrio usikose kuungana nami kwenye simulizi zingine.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog