Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

ULAANIWE - 2

 





    Simulizi : Ulaaniwe

    Sehemu Ya Pili (2)



    Siku ya pili tukiwa tunapata kifungua kinywa, siku ambayo nilikuwa nimejipanga kuanza rasmi kusaka makala za kusisimua. Mezani nilipokuwa mara alifika muhudumu akiwa na bahasha, akamgusa begani mmoja kati ya wanahabari wenzangu. Kisha akampatia na kumweleza kuwa bahasha ile ililetwa mapokezi kwa ajili ya mmoja kati yetu. Kwa sababu yeye ndiye alikuwa mwenyekiti wa msafara aliipokea kisha akaifungua na kusoma palepale.

    “Duuh! Mwandiko huu ni zaidi ya daktari…”aliguna na kusema. Mimi nilikuwa nimejikita katika kunywa chai.

    “Natamani kufanyiwa kipindi cha redio au ataKama ni kwenye ViDEO, Hiro ndilo rengo langu hasaa naitwa JoSIA MWinYI. ASaNte”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kiongozi wa msafara akaisoma kama ilivyokuwa. Kwa pamoja tukajikuta tunacheka! Na hapo kila mmoja akatamani kuiona barua. Mimi sikuishika niliishia kuangalia tu…

    Mkuu wa msafara akaihifadhi katika pochi yake. Kisha akamuita yule muhudumu na kumuuliza huyo mtu hajaacha namba za simu wanampataje sasa ikiwa wamekubali ama wamekataa ombi?

    Älisema atakuja kati ya kesho ama keshokutwa.

    Mkuu wa msafara akacheka na kupuuzia!! Akaiacha ile barua katika pochi yake.

    Hakuna hata mmoja kati yetu aliyejua lijalo!!

    Laiti kama tungelijua!!

    Ama! Ya Mungu mengi kwakweli!!

    SIKU MBILI BAADAYE!!

    Nikiwa nafanyia uhariri wa sauti kutokana na makala niliyokuwa nimeifanya tayari nilipokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa mkuu wangu wa msafara. Alinihitaji mara moja katika chumba maalumu tulichokuwa tumekilipia kwa ajili ya kuwa tunaandalia vipindi vyetu ambavyo vilikuwa vinaruka hewani moja kwa moja wakati sisi tukiwa nje ya mkoa.

    Nilitumia kama dakika tano kufika eneo ambalo alikuwa amenihitaji.

    Nilimkuta nje akiwa ameghafirika, kwa sababu ilikuwa kawaida yake kuwa na tabasamu muda wote usoni mwake. Na pale ambapo anakuwa na hasira tabasamu hutoweka kabisa usoni.

    Ni kitu gani nimemkera? Nilijiuliza huku nikizidi kujongea na huku nikitengeneza tabasamu hafifu kabisa usoni mwangu!!

    “Hivi ndó huu mkoa upo hivi!!”alianza kuzungumza baada ya kumfikia karibu.

    “Kivipi?”

    “Yaani jitu linakuja kutoka linapoua na kulazimisha kufanyiwa mahojiano eti….” Alitokwa na ile kauli huku akitupa mikono yake huku na kule.

    “Jitu? Jitu gani?”nilimuuliza huku lile jina jitu likinisisimua na kuogofya japokuwa nilijua hamaanishi kama nilivyodhania.

    “Ni mtu tu ukimuona kama ana akili timamu, anyway anataka kufanyiwa mahojiano juu ya mapenzi… sekta yako hiyo Jimmy. Malizana naye fasta….”

    Alizungumza huku akiondoka, nilitaka kuuliza kitu lakini sikujua nauliza nini.

    Niliufungua mlango wa kile chumba, nikapokelewa na harufu ya marashi mwanana kutoka katika kile chumba.

    Harufu ile kila mmoja alikuwa kiisifia huku akiifananisha na ile inayopatikana katika jingo la Mlimani city ama Quality center jijini Dar es salaam.

    Nilipiga hatua hadi nikaingia chumba cha kurekodia, nikamkuta mwanaume nadhifu akiwa ameketikatika kiti. Aliponiona alitabasamu.

    Yale maneno ya mkuu wa msafara juu ya jitu yakafutika mara moja.

    Jitu! Kwanini anamuita mwanaume nadhifu kama huyu jitu!!

    Nilisalimiana na yule bwana kwa kushikana mikono.

    Baada ya hapo nikaketi na kuisikiliza shida yake.

    “Jimmy…. “aliniita mtu yule nikatikisa kichwa kumaanisha kuwa hilo ni jina langu haswa.

    Badala ya kuzungumza akasimama na kuenda mahali ulipo mlango.

    “Vipi ndugu mbona una…” nilitaka kumuuliza.

    Ghafla akageuka, mkononi alikuwa na kisu kikali chenye mpini wa dhahabu!

    “Naitwa Japhet Sudi….”alijitambulisha jina lake katika namna ya ushari shari. Wakati huo nilibaki nikiwa nimekaa natetemeka nisijue ni kitu gani nifanye. Kikubwa nilichofanya japo kuwa hakikuwa na msaada wowote kwa wakati ule niliwasha vi8nasa sauti mle ndani ili hata kama akiniua yule mtu basi ushahidi ubakie duniani. Naama sauti zikawa zinanaswa…

    “Jimmy Elkael Sumo!!”akaniita jina langu na hapo nikaipata sauti yake vyema. Alikuwa ni Jitu, lile jitu nililokutana nalo usiku.

    Jitu la maajabu!!

    “Ni kipi unataka kwangu Sudi… ni nini niambie nikupatie..”

    “Hakuna kikubwa sana ambacho nakihitaji kutoka kwako Jimmy, sihitaji kitu kikubwa kabisa. Ninahitaji unihoji, nahitaji kukupa mkasa wa maisha yangu mkasa unaonifanya unione kama jitu la kutisha. Nahitaji kuzungumza na Tanzania Jimmy.. sihitaji uhai wala mali yako, mimi si muuaji bali mwanaume kama wewe tu….

    Jimmy, hata ufurukute vipi sina uwezo wa kuzamisha hiki kisu katika mwili wako. Ninachohitaji unifanyie mahojiano, ni mimi niliyeandika ile barua ya kuwachekesha, mmenicheka vilevile ambavyo Maria alinicheka. Mmenicheka Jimmy kwa sababu sijui kuandika vizuri.

    Ningejua vipi kuandika wakati sikusoma hadi ngazi za juu kama mlizosoma nyinyi pamoja na huyo Maria. Eeh! Ningeweza vipi kuandika mwandiko ambao mnautaka nyinyi Jimmy.

    Jimmy!! Siwalaumu nyinyi hata kidogo, ni kwa sababu hamkuajua lolote kuhusu mimi hivyo ilikuwa haki yenu kunicheka vile, na hata huyu bwana aliyekuleta wewe humu ndani simlaumu hata chembe. Amenisemesha maneno mengi ya kiingereza, nimeshindwa kumjibu kiusahihi. Si kwa sababu ya kiburi ama kwa sababu ya hiki kisu laah! Ni kwa sababu sijui alichokuwa akiniambia.” Jitu lile likatoa tabasamu, sasa hakuwa akitisha tena. Na nikaamini kweli lile sio jitu bali alikuwa ni Japhet Sudi kama alivyokuwa amejitambulisha.

    Tabasamu lile likaambatana na unyonge mkubwa.

    Sasa akaketi katika kiti ambacho mbele yake palikuwa na kinasa sauti ambacho nilikuwa nimekiwasha tayari kwa ile tahadhari ya kuuwawa.

    “Jimmy! Naelewa kuwa upo katika mshangao bado unashangaa mimi ni kiumbe wa aina gani….

    Mimi ni mwanaume tu Jimmy. Mwanaume kama wewe sema mimi ni mwanaume mpumbavu wa akili na matendo!!

    Sikiliza Jimmy, maisha hayana tafsiri ya moja kwa moja kama unavyoweza kudhania. Hakuna hata mtu mmoja ulimwenguni mwenye tafsiri ya neno maisha.

    Hata mimi sikujua kuwa maisha ni fumbo wakati nakutana na Maria katika kile kijiji ambacho nilikutana nawe usiku.

    Wewe umefika katika kijiji kile walau watu wanayo nafuu ya maisha lakini muulize vyema mjomba wako atakueleza ni ugumu kiasi gani tumepitia.

    Lakini mapenzi huja hata vitani Jimmy.

    Na maisha yako ya leo unayoishi na wenzako mnalalamika njaa usidhani miaka miwili ijayo wote mtakuwa mkiendelea kulalamikia jambo lilelile. Maisha yanabadilika!!!

    Jimmy elkael Sumo!! Nimekwambia mimi ni mwanaume wa kawaida kama ulivyo wewe, lakini nikisema mimi ni mpumbavu nielewe.

    Enzi za kwenda shuleni tukiwa peku tukisomea chini ya mwembe wakati huo mwalimu Mathias akiwa bado kijana, Maria naye alikuwa anakuja shule pekupeku. Shati lake la shule kuukuu lilisababisha hata wakati anabalehe matiti yake madogo yaweze kuonekana wazi tu.

    Lakini hakuna aliyejali, nitamcheka vipi matiti yake yako nje wakati bukta yangu ilikuwa imepasuka matakoni na kuniacha uchi mara kwa mara. Viraka vilikuwa vingi hadi bukta yenyewe ikasema basi.

    Enzi hizo mwalimu Mathias mjomba wako alikuwa ndiye mtanashati anavaa kandambili za bluu na kuja nazo shuleni.

    Ama! Mwalimu Mathias ni mzalendo sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Urafiki kati yangu na Maria ulikuja kwa sababu sote tulikuwa masikini. Wale watoto kadhaa waliokuwa wakivaa viatu hawakuwa rafiki zetu.

    Wao kwa wao na sisi kwa sisi!!

    Jimmy! Sikuwahi kujua kuna kitu kinaitwa mapenzi, ila nilianza kujua kuwa kuna hisia.

    Tukiwa darasa la sita , siku hiyo nilikutana na Maria kisimani akiwa anateka maji.

    Ndoo ilikuwa kubwa sana na alikuwa hana mtu wa kumtwisha. Nilipofika pale kisimani nilimsaidia kujitwisha.

    Na hapo nakumbuka tulitazamana machoni kwa sekunde kadhaa na kila mmoja kujikuta akitabasamu.

    Ile haikuwa mara ya kwanza kuliona tabasamu la Maria lakini la pale kisimani lilikuwa la tofauti. Alitabasamu nami nikatabasamu.

    Baadaye sana nkatambua kuwa nafsi zetu zilizungumza!!

    Aliondoka na kuniacha pale kisimani nikiwa najiuliza ni kitu gani nilikiona machoni kwake.

    Sikujua bado ni kitu gani lakini nikatamani kukiona mara kwa mara.

    Kitu kile kilikuwa kinanivutia.

    Kutokea pale urafiki ukaimarika sana, licha ya kutembea matako yakiwa nje na yeye matiti yake yakiwa karibu na nje bado tulijiona matajiri.

    Nyumbani mama akipika magimbi nilijitahidi kubeba pande moja na kwenda nalo shuleni na kugawana na Maria, na yeye ikiwa bahati nyumbani kwao wakachemsha mahindi, alinibebea pia.

    Ikafikia hatua mmojawetu asipokuja shule basi mwenza anakosa raha na amani.

    Mwalimu Mathias alikuwa wa kwanza kabisa kuelewa kuwa kuna kitu kati yetu!!!

    Jimmy, hisia hazidumu milele. Yule Maria ambaye nilikuwa namsaidia akipewa adhabu ya kulima mashamba ama vichuguu, yuleyule niliyekuambia kuwa mioyo yetu ilizungumza hapo kabla. Ni huyu huyu ambaye usiku tuliokutana nawe nilikueleza kuwa ni shetani mkubwa. Shetani muua moyo kisha anauacha mwili wako uzirura.

    Wanawake watu wabaya sana Jimmy. Kama mwanamke wako ni mtu sahihi nisamehe kwa kauli zangu mbovu juu ya wanawake, lakini ni Maria kaka, ni Maria anayenifanya leo hii naonekana mjinga kila kona, ni Maria anayenifanya unaniogopa. Jimmy…. Ni Maria Jimmy.”…. Japhet alishindwa kuendelea kuzungumza, akainama katika meza iliyokuwa mbele yake kwa sekunde kadhaa. Kisha ghafla akainuka na kuzungumza huku akilia kwa kwikwi na machozi yakimbubujika.

    “Eti Maria akasema hawezi kukaa walau chumba kimoja na mimi, hawezi na hajawahi kamwe kuwa na mwanaume kama mimi.”

    “Hayo maneno alikwambia ukiwa peke yako ama?” kwa mara ya kwanza nikajivika ujasiri na kumuuliza swali.

    “Aaargh! Jimmy si bora ningekuwa mwenyewe basi, si bora ningeweza kuvumilia. Ameniropokea mbele ya watu wengi kabisa. Amenivua nguo hadharani. Sawa sikuwa na uwezo wa kumnunulia nguo za gharama kubwa, ni kweli hata kumpa pesa ya kupanda taksi kila siku sikuwa nawez akuimudu. Lakini wakati nafsi zetu zinazungumza hivi vitu havikuwepo, Maria alikuwa msichana tu tena mchafu, sidhani hata kama alikuwa anaoga kila siku mwanaharamu mkubwa yule. Maria si alikuwa mjinga mjinga tu yule. Wasichana wenzake walikuwa wanamtania sana eti ni kikojozi, sikuyajali hayo japokuwa ukweli alikuwa akinuka mkojo. Eti akafikia hatua ya kusema nanuka harufu ya mbuzi beberui la kijijini, na akamalizia kauli kuwa ana mashaka kuwa nimetokea Kitunda huko nilikuwa mchunga ngómbe na huenda nimemfananisha tu kwa sababu yeye ni mtu maarufu!!” alilalamika Japhet kama mtoto mdogo huku akijifuta machozi kwa kutumia kiganja cha mkono wake.

    Hakika alikuwa katika huzuni kuu!

    Sikuwa na hofu tena, nilisahau kuhusu kile kisu chake kikali alichonitishia

    “Nilikwambia usiku ule kuwa asipolaaniwa Maria, ntamlaani mimi mwenyewe kwa mkono wangu nitakilaani kizazi chake na mtu wa mwisho kabisa atakuwa ni yeye.” Alimalizia kusema kisha akasimama ili aweze kuondoka.

    Awali nilitamani utokee muuajiza apotee mle ndani lakini sasa nilimsihi asiondoke kwa sababu nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza





    “Sikiliza Jimmy wewe niache tu niende, usiku nina kazi ya kufanya. Nalaani watu, kuna watu nawasaka nianze kuwalaani. Na lazima niwe kijijini leo, laana tamu huanzia kijijin i. alipe nauli kuja kuzika ndugu mmoja baada ya mwingine, huku akitokwa machozi na kamasi tele. (akasita akacheka kidogo kisha akaendelea).. inafurahisha eeh binti mrembo kama yule kulia huku anagalagala chini, naam! Inafurahisha ni kama mimi tu nilivyowafurahisha kule Dar es salaam nilipoenda kwa mara ya kwanza nikiamini naenda kwa mwanamke nimpendaye na yeye akinipenda kwa dhati.

    Unaiona hii suruali niliyovaa Jimmy, hii ni suruali ndogo sana, enzi zile suruali ilikuwa mithiri ya gunia, nikaenda nayo mjini kumtembelea Maria.

    Jimmy, naamini wewe umesoma ten asana tu! Hivi ni kitu gani elimu huwa inaweka katika akili ya mtoto wa kike, kwa mwanaume anapata akili ya kutafuta maisha kama wewe hivi Maria yeye elimu ilimsaidia nini labda. Eeh!” aliniuliza nikawa sina cha kujibu kwa sababu hata huyo Maria sikuwa namfahamu japo kwa sura acha mbali juu ya historia yake.

    Alipoona sina jibu akatabasamu kisha akaendelea.

    “Tazama Jimmy… wale wanaume wasiotaka kuoa wanawake wanaowazidi kiwango cha elimu wako sawa kabisa. Elimu ni kitu kibaya sana kwa wasichana. Nd’o maana wazee wetu hawakutaka kuwaelimisha hawa viumbe.

    Nilijifunza na kupata jibu kutoka kwa Maria.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Halafu hizi dalili niliziona mapema tu sema tu nd’o utumwa wa mapenzi.

    Awali tulikubaliana kuwa akimaliza kidato cha sita tutaoana, lakini mambo yakabadilika alipomaliza kidato cha sita hapo akasema kuwa mpaka amalize miaka mitatu ya shahada ya kwanza.

    Ningefanya nini Jimmy wakati nilikuwa nampenda huyo shetani. Nikaona miaka mitatu si mingi, Jimmy nimegombana na mama yangu alikuwa akilalamika kila siku kuwa natakiwa kuwa na mtoto. Hakutaka kuiaga dunia bila walau kuwa na mjukuu wake.

    Lakini nilikataa kata kata nikamueleza kuwa sipo tayari kuoa bado nayatafuta maisha, wasichana wengi sana walijigonga mbele yangu ili niweze kuwaona mama naye akanionyesha wasichana na adabu zao hapo kijijini lakini ungeniambia nini mimi mbele ya Maria wangu.

    Nikapuuzia na ili kuwakata maini nikaikuza picha moja ya Maria nikaibandika chumbani kwangu! Sasa kila aliyenitembelea alikutana na picha kubwa ya Maria.

    Sikujua mwenzangu alikuwa anafanya nini jijini Dar es salaam.

    Miezio kadhaa tu baada ya kufika jijini akasema kuwa hawezi kuwasiliana tena kwa njia ya barua ninachotakiwa kufanya ni kutafuta simu.

    Naam! Nikatafuta simu na kuipata, lakini ili kuupata mtandao nililazimika kunyonga baskeli yangu vijiji vitatu mbele zaidi na hapo ndipo ningeweza kuzungumza naye tena kwa shinda.

    Kuna siku nilinyonga baiskeli yangu ikapata pancha taili zote mbili, nikaisukuma hadi nikafikia kijiji ambacho kilikuwa na mtandao. Nikampigia simu Maria, akapokea na kuongea upesiupesi ‘nipo kwenye diskasheni n’takucheki kesho’ kisha akakata simu.

    Maria! Hivi ni kwa sababu niliishia darasa la saba kila kitu ukaniona sijui na sitakiwi kujua, hivi ni kwa sababu sikuwa najua nini maana ya neno diskasheni. Yaani hata kunipa dakika moja ya kuzungumza nawe ukashindwa zaidi ya kuaga!

    Hakika niliumia Jimmy! Nilifanikiwa kuziba pancha na kisha nikarejea nyumba, hakika ulikuwa ni usiku wa kiza kinene.

    Nilichukia sana kwa mara ya kwanza katika maisha yetu ya mahusiano!

    Na hapo nikakumbuka jinsi marafiki zangu walivyokuwa wakinisema tukiwa mashambani ama vijiweni. Waliniambia nijitahidi nimjue Maria la sivyo watamjua wengine na baada ya hapo ataniona mimi mpuuzi.

    Huenda sina sabnabu ya kumlaani Maria, nilikuwa mpuuzi nilipomruhusu kila siku aje na kuondoka nyumbani pasi na kuugusa mwili wake eti akaniahidi na kisauti chake cha kutolea puani ‘nakutunzia bikra yako mume wangu’.

    Maneno yale ya marafiki yakaanza kunipa mashaka nikahisi kuna kitu kinaenda kutokea.

    Nililala na hasira kali lakini cha kushangaza sasa sikuamka na tone la hasira. Hapa nikagundua kuwa nilikuwa nampenda Maria kupita maelezo.

    Siku hiyo tena nilikifikia kijiji kwa ajili ya kuzungumza naye, ajabu sasa hakuniuliza juu ya siku iliyopita ilhali alijua wazi kuwa alinikera.

    Tulizungumza kwa muda mfupi akaniaga, nikakumbuka kumwambia kuwa nampenda!

    Akajibu kwa sauti ya chini ‘me too’.

    Jimmy! Sitaisahau sauti ya huyo shetani! Sitaisahau kamwe!!

    Hivi kwanini hakunieleza nijue moja tu kuwa si wangu tena. Akaniacha nikasubiri hadi kushuhudia kwa macho yangu!!

    Kwanini alimuacha hadi mama yangu akapoteza uhai bila kumuona mjukuu wake.

    Jimmy! Halipo neno lolote la kuniambia ili nimsamehe binti yule!! Naondoka lakini utazisikia taarifa zangu!!

    Hapo sasa sikuweza kumzuia tena Japhet akachomoka kwa kasi na kupotea mbele ya macho yangu!!

    Nilitegemea kuwa atarejea siku inayofuata lakini haikuwa hivyo, nikategemea kuwa nitasikia mauaji yoyote yale katika juma hilo. Lakini hali ilikuwa tulivu sana, nikataraji labda kupata taarifa za mtu kujinyonga huku akiacha ujumbe lakini haikuwa vile.

    Nilisubiri kwa siku, juma, mwezi na hatimaye miezi ikakatika nikamsahau bwana Japhet Sudi huku nikihesabia kuwa ni jitu lililorukwa akili na kuja kusimulia kisa cha kusisimua kisichokuwa na ukweli ndani yake.

    Nikalisahau jitu! Na maisha yakaendelea.

    *****

    MIAKA MITATU NA NUSU BAADAYE!!

    NILIKUWA na miezi minne tu tangu nipate ajira mpya katika kituo kipya cha redio baada ya kudumu miaka lukuki katika kile kituo cha awali nilichokuwa.

    Kipindi nilichokuwa nimepangiwa kilikuwa kinaenda kwa jina la YALINITOKEA YANANITOKEA, kipindi ambacho kilikuwa mahususi kwa ajili ya kusikiliza simulizi mbalimbali kutoka kwa wasikilizaji mbalimbali, simulizi za kweli za maisha yao ambazo zilikuwa zinakonga nyoyo.

    Jinsi ya kushiriki, wakati mwingine tulikuwa tunampokea mgeni na kumuhoji moja kwa moja na wakati mwingine akiwa mbali alikuwa akitutumia barua ya kawaida ama barua pepe.

    Usiku huu nilikuwa nyumbani kwangu nikiwa napitia barua pepe kadha wa kadha ili nione kuna nini ndani yake, ni wadau wachache sana walikuwa wakituma barua zao kwa njia hiyo ya mawasiliano, wengi walitumia barua za kawaida ama kufikisha studio moja kwa moja barua zao.

    Katika kufungua jumbe zilizotumwa nilikutana na moja ikiwa na kichwa cha habarti ‘JS’ haikuwa na maandishi zaidi. Nilitaka kuipuuzia lakini nikagundua kuwa kulikuwa na kiambatanishi cha sauti kilichokuwa kimetumwa.

    Nikakiona ukubwa wake ulikuwa ukubwa wa kutishia usalama wa salio nililokuwa nalo katika kifaa cha kuwezesha mtandao wa intaneti.

    Nikaingiwa na ubahiri lakini nilipotazama saa ilikuwa saa sita usiku, nikakumbuka kuwa muda huo ni bure kupakua na kupakia katika intaneti.

    Nikabofya kuruhusu upakuzi wa kilichotumwa.

    Nilipomaliza kupakua likaja tatizo jingine, kompyuta yangu ilikuwa na tatizo katika spika hivyo nisingeweza kusikiliza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikapapasa huku na kule na kukutana na éarphone’nikazitumia zile kupachika.

    Nikawasha ili nisikilize!

    Sauti ikaanza kwa kukohoa kisha kucheka kwa sekunde kadhaa, na hapo ikaendelea kuzungumza.

    “Za miaka bwana Jimmy Elkael Sumo!!” ilianza ile sauti na kuingia moja kwa moja katika ufahamu wangu, ilikuwa sauti ya bwana Japhet Sudi p.a.k Jitu!

    “…. Sasa ninakaribia kuwa na furaha bwana Jimmy, furaha niliyoitafuta miaka kadhaa… kabla hujaendelea kusikiliza umepata nafasi ya kuangalia picha zangu nilizotuma. Kama bado tazama kisha uje hapa tena upoteze muda wako kunisikiliza rafiki yangu!!”

    Niliendelea kusikiliza na kukuta ujumbe mwingine juu, nikaufungua na kukutana na picha za mwanaume akiwa amekonda sana, nyingine akiwa kitandani na nyingine akiwa amesimama wima.

    Hakika! Alikuwa ni Japhet Sudi… lakini mbona sasa alikuwa amedhoofu kiasi kile, ni furaha gani hiyo ambayo anayo ilhali yu katika wakati ule mgumu!!

    Nikarejea tena ili niweze kusikiliza ni ujumbe gani kutoka katika ile sauti nilitakiwa kuupata.

    “Sina maneno mengi ya kukueleza Jimmy…. Ila ni kukupatia ujumbe mmoja tu. Mbona ukoo wako umejiingiza katika matatizo yasiyowahusu kabisa rafiki yangu eeh! Kwa nini Jimmy unataka nionekane mbaya sasa… wewe ni rafiki yangu kabisa lakini kwa mambo ambayo ndugu zako wamenifanyia naweka urafiki kando. Kama utaweza kuwahi kabla hayajawa mabaya itakuwa sala kwenu lakini vinginevyo…. Vinginevyo Jimmy. Hasira yangu na iwe juu yenu!! Siku tatu.. nakupa siku tatu… rekebishya palipoharibika.” Haikuendelea kuzungumza ile sauti badala yake ukaingia wimbo wa Parapanda italia parapanda!! Ulipoisha huo ukaja wimbo mwingine tena wa misibani uitwao tuonane paradise! Yaani ikawa nyimbo baada ya nyimbo…

    Ama kwa hakika nilipagawa!!

    Sijaonana na Jimmy miaka lukuki, sasa ananiambia kuwa kuna jambo ukoo wangu umemfanyia.

    Mbaya zaidi akanipatia siku tatu tu za kubadili ambacho anataka kukifanya!!

    Ni kitu gani sasa?? Swali hili likanifanya nishindwe kulala.

    Nikajaribu kumpigia mjomba Mathias simu lakini iliita tu bila kupokelewa! Bila shaka alikuwa amelala….

    Mkojo ukanibana ghafla na tumbo nalo likaanza kuuma... vipele vya baridi vikaniota kwa fujo!!

    **SIMULIZI hii bado ni fumbo lakini kifuatacho ni kulifumbua hilo fumbo!!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog