Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

USIKU WA MANANE - 3

 







    Simulizi : Usiku Wa Manane

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Hancy alimwomba Fina waondoke na kurejea nyumbani. Fina hakukataa ombi la Hancy ambaye alionekana kuwa na hasira ambazo Fina alikuwa anazielewa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hancy hakwenda kwa pita. Alihamia Tabata Makuburi nyumbani kwao. Alimwomba Peter akakae Tabata katika nyumba yao ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikipangishwa. Ni baada ya Hancy kuomba ndipo wapangaji waliokuwa wamepangisha hapo kumaliza mkataba wao na kuondoka.



    Hancy alimpeleka kwanza Fina nyumbani kwao kisha akaelekea nyumbani kwake Tabata Makuburi.



    ****

    Hancy aliamka na kukumbuka kwamba alikuwa na gazeti lenye habari kuhusu jambazi aliyeuliwa. Na siku hiyo alikuwa aende hospitali ili kuona kwamba yule alikuwa ni moja wa watu ambao alikuwa akiwatafuta.



    Alitaka kupitia tena kwa fina ili akamwonyeshe gazeti lile na juu ya habari ile. Alimaliza kunywa chai yake ambayo ilikuwa imeshatayarishwa na mlinzi wa nyumba hiyo ambaye walikuwa wakikaa pamoja. Hakukuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa akiishi katika hiyo nyumba tofauti na wao, Hancy na Rajabu Mkwesi.



    Rajabu baada ya kumwona Hancy akitia gari moto alifungua geti haraka.



    "Poa Rajabu, baadaye."



    "Mchana au?” aliuliza Rajabu.



    "Hapana, kuna mambo nafatilia kutwa nzima nadhani we kama ni chakula, tengeneza cha kwako tu."



    "Sawa mkuu,” alijibu Rajabu huku akifunga geti baada ya Hancy kuondoa gari.



    Hancy alimfuata tena Fina. Alichukua gazeti ambalo alisahau kumwonyesha Fina jana yake. Ni mwendo wa dakika kumi na tano zilimtosha kufika Mbezi. Alimkuta Fina nje akiwa ananyweshea maji.



    “Naona unaremba mazingira,” Hancy alimtania Fina.



    “Ndiyo, Jumapili ni zamu yangu,” Fina alisema huku akimfuata Hancy, alimkumbatia na kumbusu. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Fina kufanya vile tangu Hancy arudi.



    “Wee, huogopi watu madirishani kule wanatuona?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hancy, siwezi kujizuia eti kisa watu. Wewe ni wangu tayari na sitajizuia kufanya lolote kwako. Isitoshe watu wanajua,”

    alisema Fina huku akiendelea kumkumbatia Hancy.



    “Sawa Fina, nashukuru,” Hancy alimshukuru Fina huku akimpa lile gazeti alilolinunua jana yake.



    “Najua kuhusu hili Hancy, inaelekea umedhamiria sana.”



    “Ila nataka nimwone mtu mwenyewe kama ni kweli

    niliyewachora wanafanana, pia ntaka nkaangalie ilea lama yao kama atakuwa nayio mkononi.”



    Fina alibaki akimwangalia Hancy ambaye alikuwa akirudi nyuma kuashiria alikuwa akiondoka.



    “Sasa unaenda wapi Hancy?” alihoji Fina.



    “Naenda Muhimbili mara moja, nitawahi kurudi ili tutoke.”



    “Sawa, lakini hata kusalimia ndani?”



    “Nisaidie,” Hancy alimwomba Fina huku Fina akirusha maji kuelekea alikokuwa Hancy kummwagia.



    “Acha yutani wako mpenzi,” alilalamika Hancy huku akiyakwepa maji.



    “Umeniudhi ndo maana,” alisema Fina.



    “Nmekuudhi nini tena.”



    “Umekuja kunionyesha tu gazeti halafu unaondoka…” alisema Fina huku akionekana mpole akitamani Hancy abaki.



    “Ntarudi baadaye nkitoka huko,” Hancy alisema huku akiingia kwenye gari.



    “Okey, baadaye. Take care Hancy.”



    “Poa Fina,” alisema Hancy huku akitabasamu baada ya kumwona Fina ameridhika na alichokisema.



    *****

    Nusu saa ilimtosha Hancy kufika Hospitali ya Muhimbili. Njiani foleni haikuwa kubwa na hivyo aliwahi kufika kama matarajio yake yalivyokuwa. Watu walikuwa ni wengi sana.



    Alipita moja kwa moja na kwenda kuegesha gari lake nje ya hospitali kabla hajaingia. Wagonjwa wengine waliingizwa na wengine wakiwa ndio walikuwa wakiletwa. Watu wengine waliingia kuona ndugu zao na wengine walikuwa wakitoka baada ya kuonana na ndugu zao. Hancy aliiingia na kutafuta upande ambao chumba cha uhifadhia maiti kilikuwapo.



    Hakuwahi kuingia katika hospitali hiyo na hivyo ilimbidi aulizie kwa mmoja wa watu ambaye alikuwa akitokea upande ambao Hancy aliona kuna watu wengi.



    “Samahani kaka,” alisema Hancy.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Bila samahani…. Vipi mbona kama una wasiwasi… jamaaa ni ndugu yako nini?” alihoji yule mtu baada ya kumwona Hancy kama mwenye hamu ya kumwona mtu ambaye alikuwa chumba cha maiti ambaye ndugu zake bado walikuwa hawajafika kuchukua maiti yake.



    “Mtu gani huyo?”



    “Si hilo jambazi ambalo limeuliwa na wenzake…. Nakuambia kama ni ndugu yako una hasara sana. Eti wanagombea hela walizoiba wenyewe… na walikuwa wamelewa. Hao ndo Kobra bana,” alimaliza kusema yule mtu huku akiondoka na kumwacha Hancy pale pale. Hancy alishangaa kusikia jina Kobra. Hapo hapo aliukumbuka ule mchoro aliouona kipindi akiwa mdogo pamoja na kwenye picha za Soo. Alitamani kutabasamu lakini alimwona yule jamaa akiondoka na kumuuliza.



    “Lakini… chumba gani ndo yupo?”



    “Kwani hujui chumba cha maiti… nyoosha hukohuko kwenye watu wengi utaonana naye.”



    Aliona watu wakiwa wamesimama nje ya chumba hiko.

    Alielekea moja kwa moja hadi katika chumba cha maiti. Aliomba ruhusa ya kuuona mwili wa jambazi yule. Askari walimshuku huenda akawa mwenzao. Walimruhusu huku mmoja wa wale askari akiwasiliana na polisi.



    “Tuko hapa nje, kuna nini?” mmoja wa polisi aliuliza baada ya yule askari wa mlangoni kuwasiliana naye.



    “Kuna mtu tunamhisi ni moja wa majambazi wanaotafutwa. Kaingia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti kuona mwili wa marehemu sasa hivi. Tunaomba mfike hapa.”



    “Sawa tunakuja.”



    Kama vile Hancy alisikia juu ya waliyoongea. Hakuogopa. Aliendelea na upekuzi wake. Akligundua kuwa kwenye mkono wa ile maiti kulikuwa na ilea lama ya tattoo ya picha ya Kobra.



    “Afadhali… sasa nimeshawajua. Na hii sura ndo ileile kwenye picha yangu. Mmoja kashaondoka.



    Askari wa mlangoni walikuwa wakimsubiri ilia toke. Polisi nao walikuwa wameshafika na kusimama pale waliposimama wale askari wa mlangoni. Hawakumwona akitoka.



    “Mbona hatoki. Afande Graham. Ingia utoke naye,” askari mmoja alimwamuru afande Graham aingie ili amtoe. Afande Graham aliingia lakini hakukuta mtu.



    “Hakuna mtu kule ndani,” Afande Marwa aliwaangalia wale askari wa mlangoni.



    “Ina maana mnatudanganya? Nyinyi mliona mtu akiingia?”



    “Ndiyo afande, amevalia tisheti nyeusi na suruali ya bluu.”



    Afande Marwa aliingia mwenyewe, alikagua kila mahali lakini hakuona mtu. Alielekea katika dirisha la kile chumba ili achungulie. Alishika kitasa. Kitasa cha dirisha kilikuwa kimevunja. Alitoka nacho hadi nje na kuwaonyesha wale askari.



    “Katoroka,” alisema Afande Marwa. Alitoa simu yake ya upepo ‘radio call’ na kupiga makao makuu kuwa taarifu juu ya kuonekana kwa mmoja wa wale majambazi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hancy hakuwa tayari kufanya kazi na polisi kwa wakati huo. Alijua polisi watatumia sharia zao kuwafikisha mahakamani na kuwafunga. Yeye hakutaka hivyo. Alitaka wote wafe.

    Hilo ndilo lililomfanyua atoroke bila ya kujulikana. Hakujali kama atatafutwa kwani alikuwa na imani ya kwamba hakuna aliyemjua kwani ni kipindi kirefu sana alikuwa nje ya nchi.



    Alilifuata gari lake na kurudi Mbezi nyumbani kwa kina Fina.

    Alisimama getini kwa kina Fina huku akimwangalia Fina ambaye alionekana mchangamfu kupita siku zote. Alikuwa akicheza na watoto ambao alikuwa akiishi nao nyumbani kwao.



    Alimwona mrembo zaidi. Alipenda kumwangalia sana. Alimtamani na pia alimpenda sana. Alimchora kuanzia juu hadi chini na umbile lake lote. Alifurahi sana kuwa na Fina, hasa baada ya kujua Fina alimpenda sana. Alitabasamu wakati wote huo aliokuwa akimwangalia akicheza na watoto. Pale aliposhindwa kuzizuia hisia zake aliamua kumwita.



    “Fina,” aliita Hancy.



    “Wooouw… Hancy karibu. Karibu tucheze na watoto. Ingiza gari ndani basi,” Fina alisema huku akimfuata Hancy getini. Alifungua geti ili Hancy aingize gari ndani. Hancy naye alifanya kama alivyoambiwa na Fina.



    Alilipaki gari lake na kuteremka. Alimshika Fina na kumkumbatia kwa nguvu bila ya kujali lolote kuhusu kuonwa kama ilivyokuwa asubuhi wakati alipofika hapo.



    "Nakupenda sana Fina.”





    “Nakupenda pia Hancy.”



    *****

    Miaka yake ishirini na minne ya kuwepo kwake duniani, imemfanya kujiona kama ni mwanamke aliyekamilika kwa kile ambacho aliamini kwamba anaweza. Akiwa na urefu wa wastani na mwembamba kiasi mwenye umbo ambalo lilijionyesha hata pasipo kuongezea nakshi za kulazimisha kuwavutia.



    Fina Finias, alikuwa ni msichana mrembo. Urembu uliowahadaa wanaume wengi wakware bila mafanikio ya kumpata. Aliyejua utu wake lakini pia ambaye alijua zaidi kujiachia mjini. Hakuna ambaye angeweza kumdhani kwa maisha aliyokuwa akiyaishi.



    Uzuri wa Fina ulimfanya awe mwepesi kushawishi mtu wa aina yeyote. Hakujali kingine zaidi ya pesa kwa wakati huo. Ujanja wake ulimfanya ajulikane na watu wengi. Wengine walimwona tapeli lakini ikawa ni vigumu kuhoji kwani hakueleweka. Angeweza kusababisha lolote na akasimama kizimbani na kujitetea bila woga na kushinda kesi.



    Alipenda sana kampani. Adeline shynes ni moja wa marafiki zake wakubwa ambao kila mahali alikuwa akiongozana naye. Wakati mwengine alienda na kushinda kwao ili mradi tu awe ni mwenye furaha wakati wote. Alimpenda Adelina kutokana na ustaarabu wake na tabia yake ya upole na huruma.



    Pamoja na vituko vyake pamoja na ujanja wake aliokuwa nao. Fina alipenda sana kusikiliza ushauri wa Adelina na kuufanyia kazi.

    Adeline pia alikuwa si msemaji sana. Wakati wote alikuwa kimya akimsikiliza Fina kile ambacho angependa wafanye kwa siku hiyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yeye alikuwa akimshauri tu kwa lile ambalo aliona halifai kwa siku hiyo. Hivyo Fina alimpenda sana rafiki yake huyo ambaye hata hivyo hawakudumu sana kwani Adelina alipata safari baada ya wazazi wake kuhamia nchini Uingereza ambako baba yake alipata kazi na hivyo kutakiwa kuishi nchini huko.



    Fina starehe kwake ilikuwa ni sehemu ya maisha yake. Hakukosa kuingia klabu kubwakubwa na hata katika matamasha na sherehe kubwa zilizokuwa zikifanyika katika sehemu mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam. Alijichanganya na kila mtu na hakujali lolote kwani lengo lake kubwa ilikuwa kupata burudani ambayo alijisikia kuipata kwa siku ile.



    Fina alikuwa akifanya kazi katika ubalozi wa Marekani kama ofisa Uhamiaji. Aliijua kazi yake vyema. Wafanyabiashara mbalimbali walimjua kwani wengi wao walisafiri kwa msaada wake. Pamoja na kazi yake. Asingekosa kustarehe apendavyo. Hata nyumbani kwao alihama ili ttu aweze kutawala maisha yake na kuwa karibu na kile alichokitaka.



    Moja ya watu waliomfahamu sana Fina alikuwa ni Deogratius Mbila au Deo kama alivyopenda kuitwa na watu wake na wengi waliomfahamu. Walifahamiana wakati wakiwa katika moja ya klabu za usiku iitwayo Maisha baada ya kitambo kirefu ambapo walikutana mara kwa mara katika ubalozi wa Marekani. Ndipo Deo alipomkumbuka Fina. Siku na mara ya kwanza kumwona ilikuwa ni Ubalozi wa Marekani. Ni yeye ndiye aliyemsaidia Deo mpaka akafanikiwa kupata hati yake ya kusafiria. Safari yake ya kwanza kwenda Marekani. Aliishusha miwani yake na kumtazama vizuri. Alikumbuka siku hiyo.



    “Dada samahani,” Deo alisalimia.



    “Bila samahani, karibu, nikusaidie nini kaka?”



    “Nashukuru sana,” Deo alitoa miwani yake nyeusi na kuweka juu ya meza tayari kuzungumza na Fina. Macho yake yalionekana makubwa kidogo yenye rangi ya damu ya mzee. Alikuwa mwenye kifua kipana na umbo lililojengeka kwa mazoezi mazito ya kunyanyua vyuma. Kichwani mwenye upara uliomeremeta kwa kuongezea na mafuta aliyokuwa amepaka. Weusi wake pia uliongeza mng’ao.



    “Nimefuatilia pasipoti yangu ya kusafiria. Niliambiwa nije leo.”

    Alisema Deo huku akimwangalia Fina maeneo ya kifuani na usoni.



    “Unaitwa nani?” aliuliza Fina.



    “Deo Mbila, I mean Deogratius Mbila,” Fina alimwangalia kidogo akacheka. Hata hivyo hakuonyesha kujali aliyoyasikia.



    “Unatabasamu zuri dada,” Deo alimwambia Fina.”



    “Nashukuru kaka. Samahani, sioni pasipoti yako hapa, nadhani itakuwa inashughulikiwa bado. Ntakusaidia kuifatilia kwa ofisa mwingine.”



    “Ntakushukuru sana dada yangu,” alisema Deo huku akikichukua kitabu ambacho kilikuwa pale mezani ili akisome.



    Fina bila kujali kumwacha Deo pale mapokezi aliondoka na kuingia chumba cha ofisa ambaye alikuwa akitoa pasipoti za kusafiria.

    Alirudi akiwa kaishika na kumkabidhi Deo. Aliutizama sana mkono wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Vipi dada angu,” Deo alimwangalia na kumsemesha huku akitabasamu.



    “Nimeipenda Tatoo yako,” alisema Fina huku akimkabidhi Deo pasipoti yake.



    “Ooh…Nashukuru. Mi natoka,” alisema Deo huku akitoka baada ya kuichukua pasipoti yake na kuiweka mfukoni.



    “Okey, karibu tena siku nyingine,” aliaga Fina.



    Deo alitoka na kuwasha gari lake na kuondoka.



    njiani Deo aliwaza kuwa mizigo yake ambayo alikuwa aipeleke nchini Marekani itafika salama kwani kuhusu kupitiosha kiwanja cha ndege isingekuwa tabu kwake kwani alijua ni namna gani angewahonga wafanyakazi wa pale kama kawaida yake.



    Safari hii hakutaka kumshirikisha mtu yeyote katika dili hilo kwani halikuwa kubwa sana la kugawana na watu wengi.



    Alihitaji muda ili aanze safari yake ya Marekani bila kadhia yoyote. Alianza mara moja mawasiliano na wafanyakazi hao ili siku ya safari aweze kupita buila ya vikwazo vyovyote.



    *****

    Mwaka mmoja ulipita baada ya fina kuonana na Deo. Safari hii walikutana pamoja katika klabu ya Sansiro. Fina alikuwa amesimama na mwarabu mmoja aitwaye Nizar ambaye alikuwa ameshika glasi ya wine wakizungumza mambo mbalimbali. Deo alikuwa wa kwanza kumwona fina na kumkumbuka. Aliamua kumfuata alipo. Alimwangalia Nizar aliyesimama naye. Alimshika Fina bega bila wasiwasi ili ageuke. Nizar hakumfahamu Deo.



    Alionekana kuogopa baada ya kuwaona watu wa deo wakiwa pembeni wakimsubiri mkuu wao, Deo. Hakuweza kuongea lolote zaidi ya kuangalia kile Deo alichotaka kukifanya kwa Fina. Fina aligeuka kumwangalia Deo.



    “Ohh, its u Deo. Sijakosea nadhani. Habari za Marekani?” Fina alimgeukia Deo na kumwambia kwa kumtania.



    “Aaah, hahahaaa,” Deo alicheka kisha akaendelea kusema, “Nzuri tu, nimeenda nimerudi mrembo, ni siku nyingi nimerudi kwani sikukaa sana huko,” Deo alimjibu huku akitoa miwani yake ilimfanya Fina kumtambua vizuri. Alishaiona ile Tatoo ya Deon a hapo akawa amejidhihirishia kabisa kuwa ni yeye.



    Deo alimsalimia yule Mwarabu na kisha aliwaaga Fina na Nizar na kwenda kujumuika na wenzake.



    “Nani yule?” Nizar alimuuliza Fina. Fina alimgeukia akatoa miwani yake kisha akamjibu kwa dharau, alimwangalia kwa kitambo kidogo kisha akamwambia…



    “Ni rafiki yangu….. kama ulivyo wewe?” kusikia vile Nizar aligeuka na kuondoka. Hamu ya kuendelea kuwepo pale Sansiro ikamwondoka na kuamua kulifuata gari lake na kuondoka kabisa kuelekea nyumbani kwake.



    Fina hakuhitaji kuwepo pale tena, alihisi Nizar amemchafua roho kwa wivu wake kwa kitu ambacho hakijui.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unafikiri nakutaka mpaka uniulize yule nani,” alijisemea Fina huku akitoka kulifuata gari lake. Aliingia na kuwasha. Hakufika mbali simu yake iliita na kuipokea.



    “Hallow, nani wewe?” aliipokea kwa ukali kidogo.



    “Mbona unakuwa mkali sana?” Fina kusikia vile alikata simu na kuiweka kwenyi siti ya abiria. Hakutaka usumbufu. Hakujua aliyempigia ni nani na wala hakujali hilo.

    Aliendesha kwa kasi hadi kufika nyumbani. Akiwa getini alishtuka baada ya kukumbuka namba ile ambayo aliona namba za kuanzia za nchi husika ‘Country code’ aliitambua kwamba ilikuwa ni ya Uholanzi. Namba hiyo ilisoma +31, lakini pasipo kuiona alijikuta akiongea kwa jazba na kukata simu hali iliyosababisha kumlazimu aliyekata kukaa kimya.



    Alitamani aingie ndani haraka ili akapige hiyo namba kwani alijua lazima atakuwa ni Hancy.



    *****



    Mlinzi wa lango lake alikuwa ameshatambua ujio wake, alikuwa tayari ameshasikia mngurumo wa gari likielekea katika geti hilo. Fina alikuwa ameachiwa nyumba baada ya familia yao kwenda Nairobi kuishi huko. Yeye alishindwa kuhamia huko kwa sababu ya kazi yake ambayo ilimlazimu kubaki. Ni nyumba jirani na kwa mzee Peter, mlezio wa Hancy maeneo ya Mbezi Beach, ambapo kila mara Fina alikuwa akipita kuulizia hali ya Hancy huko alipo. Na jibu la Justin ambaye ndiye aliyekuwa amemzoea sana lilikuwa ni ‘bado kidogo atarudi’. Jibu hilo Fina alilizoea huku akiwa na hamu sana ya kuonana na Hancy. Mawazo juu ya Hancy yalimjia kila mara japo alijitahidi kujizuia kuwaza kwa imani ya kwamba atarudi siku moja.



    Baada ya mlinzi kufungua geti saa nane na nusu usiku, Fina aliingiza gari na kulipaki vizuri. Hakuwa amelewa kama sikun zote arudipo. Na siku hiyo hata mlinzi aliona Fina amewahi sana kurudi kwani huwa anarudi hata saa kumi au saa kumi na moja. Alishuka na kuingia moja kwa moja hadi chumbani kwake na kujirusha kitandani.



    Kabla hajapata usingizi, Fina aliwaza mengi yaliyomtokea siku hiyo. Alikumbuka jinsi Deo alivyokuja pale na jinsi alivyomjibu Nizar. Hakujali hilo, alitamani siku moja amwambie ukweli Nizar ambaye amekuwa akijisogeza karibu yake akiwa anamaanisha wanauhusiano, kitu ambacho kwa Fina alikuwa akipuuza na kumwacha kama alivyo. “Mpuuzi Yule ana wivu sana, tangu lini nikatembea na mwarabu mimi?” alisema kwa kupuuza huku akiigeukia simu iliyokuwa pembeni yake na kuishika.



    Moja ya jambo ambalo lilimkurupua wakati akisinzia na kuwaza ni ile namba ambayo muda mfupi tu alikuwa ameikumbuka, alishtuka tena na kuichukua simu yake upesi. “Nani huyu aliyenipigia?” aliwaz.Aliitafuta ile namba. Aliamua apige.



    “Itakuwa Hancy huyu…. Najua tu,” alisema huku akitabasamu mkono mmoja akiwa kauweka juu ya kifua chake akitamani namba ile iwe ni ya Hancy aliyeko Uholanzi. Alihisi machozi kumtoka na mapigo ya moyo kwenda mbio. Simu ilikuwa ikielekea kuunganika nay a mpokeaji. Alisubiri akisikiliza mpokeaji apokee ambaye hakumjua hata hivyo bali kumdhania tu.



    “Hallow,” Fina aliita upande wa simu ili kuzungumza naye. Kimya kilitawala kabla ya mzungumzaji wa upande wa pili hajaitikia hali iliyompa Fina wasiwasi ya kwamba hataitikia.



    “Haloo, Fina. Mambo vipi?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Poa sijui nani mwenzangu, nilikuwa kwenye gari tukawa hatusikilizani ndiyo mana n’kaona hadi nifike nyumbani?” Fina alijitetea baada ya kuhisi sauti aliyokuwa ameisikia ilikuwa ni ya Hancy. Alikuwa akisikiliza kwa makini ili asikie jibu ambalo alilitarajia kuwa ndo hilohilo.



    “Usijali. Ni mimi Hancy.”



    “Whaat! Hancy? Is this you?” Fina hakuamini macho yake kama yule aliyekuwa amempigia ni Hancy. Alijiona mpya. Aliamka pale alipokuwa amelala na kukaa kitako. Usingizi wote ulimwisha na kukaa vizuri kitandani kwa ajili ya kujiliwaza kwa Hancy baada ya misukosuko aliyokutana nayo klabu. Hakuamini kabisa kama angekuwa ni Hancy aliyempigia.



    “Ulikuwa unatokea wapi usiku hivyo Fina?”



    “Hancy, am sorry, nilikuwa klabu, hata hivyo kuna watu wamenikera sana n’kaamua nirudi nyumbani. Ni wewe kweli Hancy?” aliuliza kwa kutokuamini kama kweli alikuwa akiongea na Hancy.



    “Ni mimi Fina… lakini unaniogopesha sana kwa kile ambacho nimekisikia ukikisema sasa hivi, japokuwa sina amri wala sihitajiki kukuuliza hivyo lakini kwa sababu nakujali itanibidi…. Unajua ni muda mwingi sana niko huku na sielewi ni kipi kinaendeleo huko?” alisema Hancy huku akimuuliza Fina ambaye wakati huo alikuwa anasikiliza kwa makini kile ambacho Hancy alikuwa akikisema.



    “Unaogopa nini Hancy?... ” aliuliza fina kwa shauku kubwa ya kujua lililomtokea Hancy au analotaka kuliweka bayana kwake.

    “Fina, unajua tulikuwa karibu sana tangu tukiwa watotot wadogo sana na kabla sijaja huku, hata nilivyokuwa narudi likizo wewe ndo ulikuwa ukinikaribisha, tunakuwa wote mara nyingi na mara nyingine unanizungusha sehemu tofauti nilizozisahau.



    Unakumbuka kweli Fina?” aliuliza Hancy.



    “Ndiyo Hancy, nakumbuka,” alijibu Fina.

    “Hata nyumbani kwetu nako nilipasahau ila wewe ndiye



    uliyenipeleka,” unajua hilo.



    “Mmmh, kweli Hancy,” Fina alijibu huku akifurahia kusikia sauti ya Hancy na kile alichokuwa anasema.



    “Isitoshe kinachoniuma zaidi na kuogopa ni kwa sababu tulikuwa hivi lakini sijawahi kukuambia kitu muhimu Fina. Hujawahi kusikia lolote ambalo hukulitegemea kutoka kwangu wala mimi kusikia lolote kutoka kwako.”



    “Kitu muhimu?... kitu gani Hancy?.... ni kitu gani unadhani sijawahi kukuambia na wewe hukuwahi kuniambia toka utotoni?” fina aliongea taratibu huku moyo wake ukidunda akitamani kujua.



    “Fina,” aliita Hancy.



    “Nakusikiliza Hancy,” aliitikia Fina.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nakupenda sana, imani yangu itatulia kama utasema unanipenda pia. Tafadhali sema hivyo tukamilishe ndoto yetu. Kwani ni kitu ambacho sikuwahi kukuambia pamoja na ukaribu wetu. Na nitajuta kama nitakuwa nimechelewa na umeshapata mtu mwingine.”



    “Hancy,” Fina aliita.



    “Nakusikiliza Fina.”



    “Nakupenda sana Hancy… Haitakaa itokee nimpende mtu mwingine zaidi yao. Ni kweli hukuwahi kusema hivyo. Lakini hata mimi sijawahi kuwa na mtu mwingine. Nilitamani sana nikuambie jambo hilo lakini nilikuwa naamini ipo siku utaniambia na ndiyo siiku kama ya leo ambayo nlikuwa naisubiri Hancy. Nimefurahi sana leo kuniambia hivyo. Bado nakukumbuka sana na nakupenda kuliko kitu chochote. Sitegemei kuwa na mtu mwingine zaidi yako kwa kipindi ambacho upo huko. Zaidi ni kwamba najua kujilinda na hakuna ambaye ameshawahi kunigusa. Naenda sana kwenye starehe lakini nikukumbukapo mara nyingi huwa natoka kwani wanaume wakware wengi lakini siwapi nafasi hii ya kipekee ambayo ni kwa ajili yako.”



    “Nashukuru sana kwa kuniambiahilo Fina. Naamini utakuwa wangu milele. Naamini sina mwingine zaidi yako. Nakuhitaji kwa kila hali, nilipo huku nakukumbuka sana. Nafurahi sana kusikia sauti yako mpenzi.”



    “Hata mimi naamini utakuwa wangu milele Hancy. Fina alisema huku akilia. Hali hiyo ilipelekea kimya cha muda mfupi kabla ya Hancy kuendelea na mazungumzo yao.”



    “Najua si muda mrefu nitakuwa nimerudi huko na sidhani kama nitarudi huku tena kwani nitakuwa nimemaliza masomo yangu kabisa. Nitarudi ili nijipange na maisha yangu ya baadaye tukiwa pamoja mpenzi.”



    “Sawa mpenzi, nakusubiri kwa kila hali,. Natamani sana urudi mpenzi.”



    “Tutaonana tu Fina, nakupenda sana Fiana.”

    Nakupenda sana Hancy.”



    Hancy na fina wakawa wamefungua ukurasa mpya wa uhusiano. Uhusiano ambao ulifichika kwa miaka nenda rudi. Kauli ya Hancy ya kumpenda Fina ilimfanya fina akumbuke mengi sana walivyokuwa na Hancy tangu wakiwa wadogo ikiwa ni pamoja na na kucheza pamoja. Sasa ukawa sio urafiki tu bali ni wapenzi. Furaha ambayo Fina alishindwa kuizuia na kujikuta akipiga kelele ziilizomfanya mlinzi akimbilie mlangoni na kuuliza kuna nini kilichotokea.



    “Dada Fina, kuna tatizo?”



    “Usijali Seba, niimejikuta tu nimefurahi,” Fina alisema huku akirudi kitandani na kujirusha tayari kwa kuutafuta usingiza ambao ulikuwa umeshapotea.





    *****

    Hancy na Fina walikuwa pamoja kuanzia wakiwa wadogo. Fina alionyesha kila dalili za kumpenda Hancy kabla hata hajajua nini maana ya kupenda. Ni muda mfupi tu baada ya wazazi wake Hancy na ndugu zake kuuliwa na kuzikwa Hancy alipohamia kwa Peter ndipo Fina alipomwona Hancy kwa mara ya kwanza. Alikuwa na miaka mitatu wakati Hancy alikuwa na miaka minne.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Fina alipenda kucheza na Hancy kila wakati. Hata pale alipokuja kuchukuliwa na dada yake alilia sana akitaka kuendele kucheza na Hancy. Hiyo ilimjengea pia Hancy mazingira ya kuzoea kucheza na Fina.



    Walijenga uhusiano mzuri ambao uliwafanya hata wazazi wao wafahamu urafiki wao na hivyo kuwaacha wawe karibu.

    Waliachana baada ya Hancy kuondoka na Peter na kwenda kusomea Uholanzi. Hiyo il;ikuwa ni pigo kubwa sana kwa Fina ambaye alikuwa akikosa raha kila wakati Hancy akiwa safari.



    Pale Hancy aliporudi ilikuwa ni sherehe kwa Fina kwani siku hiyo angeonekana kuwa ni mwenye furaha sana tofauti na siku zote. Hata pale alipoona Hancy amekaa muda mrefu sana bila kurudi, alikuwa akimuulizia sana kwa Justin. Hakujua lolote kuhusu Hancy na familia yake kwa wakati huo wakiwa wadogo. Alijua Hancy ni mdogo wake Justin ambaye alipenda sana kumtania mengi kuhusu Hancy kila alipokuja kumuulizia nyumbani kwao.



    “Shikamoo kaka,” alisalimia Fina huku akiwa ameshikilia mdoli wake pamoja na chupa ya Juisi.



    "Marahabaa mtoto mzuri, karibu…. Umekuja kwa mchumba ako,” alijibu Justin huku akimfuata Fina.



    “Hancy kaenda wapi?” Fina alimuuliza Justin.



    “Mchumba wako hayupo, kaenda na harudi tena,” alisema Justini huku akimbeba Fina juu juu. Kauli hiyo ilimnyong’onyesha sana Fina ambaye alitarajia kumkuta Hanc.



    Justin alimcheka kwa furaha baada ya kumwona Fina ambaye ni mtoto mdogo lakini kwa kauli alioitoa ananuna.



    “Yani Fina ananuna kwa sababu Hancy hayupo,” alisema Justin huku akimcheka Fina.



    “Anarudi lini kaka Justin??” alihoji Fina. Justin alimweka chini. Hakuona haja ya kumdanganya kwani alimwona Fina japo ni mtoto mdogo lakini anakosa raha kwa sababu Hancy hakuwepo ili wacheze naye. Hivyo, aliamua kumwambia ukweli ili afurahi.



    “Kasafiri ila atarudi. Kaenda na baba sehemu atarudi, sawa mdogo wangu?”



    “Haya kaka Justin,” Fina aliridhika na jibu la Justin. Alikuja tena na tena kwenye nyumba ya kina Justin ili kubahatisha kama Hancy atakuwa amesharudi.



    Wakati huo fina alikuwa na umri wa miaka mitano wakati hancy akiwa na miaka sita.



    Baada ya miezi miwili Hancy alirudi tena Tanzania. Mtu wa kwanza kufika na kumwona nyumbani alikuwa ni Fina. Peter aliiona furaha ya Fina kila alipomwona na Hancy. Alijua kwamba Fina anapenda sana kuwa karibu na Hancy.



    Hata alipomnunulia Hancy zawadi alijua lazima Hancy ampelekee Fina. Hata wazazi wa Fina walijua upendo kwa watoto hao. Fina asingeweza kupewa kitu kwao bila kumtaja Hancy na kumpelekea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mamaaa, nampelekea Hancy,” Fina aliropoka tu pale mama yake alipompa Choculate. Alitoka nayo hadi nyumbani kwa kina Hancy.



    Hakujali ni saa ngapi. Hali iliyowafanya wazazi wake wasimpe chochote wakati wa usiku kwani angetafuta tu njia ili aende akampe Hancy. Hivyo hivyo kwa Hancy ambaye aliiga upendo na ukarimu wa Fina. Wazazi wa pande zote mbili wakajua watoto wanapendana sana.





    *****

    Alibaki akiyakumbuka mengi kichwani kwake. Mengi ambayo alifanya na Hancy kuanzia utotoni hadi wakati huo. Na sasa Hancy amerudi na mipango yake yote ameshamwambia. Lengo lake ni kulipa kisasi. Yeye ndiye anayewajua watu wale vizuri wanaojiita Kobra.



    Uhusiano wake na Hancy ungependeza zaidi kama wazazi wake Hancy wangekuwepo. Sasa hawapo nay eye ndiye rafiki wa watu hao.



    Aliwaza sana Fina juu ya hilo. Hakujua kwamba Hancy alikuwa akitaabika sana siku zote kutaka kujua watu wale waliofanya mauaji nyumbani kwao wakati akiwa mdogo.



    Alimuwaza Deo, ghafla sura ya Chacha ikamjia. Hao ndio waliokuwa watu wake wa karibu zaidi. Walikuwa ni wakorofi sana. aliwatumia kama kivuli chake pale alipoona mambo hayaendi vizuri.



    Sasa analazimika kuwageuka. Pengine ni kwa sababu pia alikuwa hapendi mienendo yao. Alikumbana na masaibu mengi p[ale aliokuwa nao. Wakati mwingine alipelekwa hadi kituo cha polisi ili kuhojiwa na kuwatetea juu ya mambo yao. Wakati mwingine alidiriki kujificha ili asionekane. Yote hayo ilikuwa ni kuwasaidia ili wasikamatwe na polisi.



    Deo alimpenda sana Fina kwa kuwa alikuwa ni mjanja na aliyekuwa akijiamini sana. hivyo aliona hiyo ndiyo nafasi nzuri kwa kumtumia Fina japokuwa Fina pia aliwakwepa wakati mwingine akiwatoroka na kuwadanganya. Wao waliamini.



    Alikumbuka matukio yote yaliyofanywa na Deo. Kuanzia lile la kumjeruhi Nizar siku mbili tu baada ya kukutana na Fina. Nizar hakumjua Deo japo Fina alimsihi kukaa mbali na Deo.



    Wakati Deo akiingia klabu saa tatu usiku. Nizar alikuwa kasimama nje akiongea na Fina. Deo aliyekuwa na watu wake alifika na kumsalimia Fina. Nizar hakupenda vile. Kwani kwake ilikuwa ni wakati wake kumshawishi Fina ili wawe pamoja. Alijua Deo anamwingilia katika harakati zake za kumpata Fina.



    Deo alimshika Fina na kumvuta pembeni kwa makusudi. Nizar alipandwa na hasira na kumhoji Deo.



    “Vipi kaka, huwezi kuwa mstaarabu?



    “Fuata yako,” Deo alimjia juu Nizar. Hapo hapo Nizar alitaka kumvamia Deo ili ampige. Watu wa Deo wakawa wameshafika na kumkamata hali iliyompa nafasi Deo kumtandika ngumi za uso na kumjeruhi. Fina alivyoona vile haraka alimfata Deon a kumtolea maneno yaliyosababisha watu kujaa pale nje ya klabu. Deo aliwahimiza watu wake waondoke na kuapa kwamba atamtafuta Nizar.



    “Hatujamaliza bado, nitakutafuta.” Deo alisema huku akiondoka kuelekea klabu. Fina alibaki tu akimwangalia pasipokusema neno lolote hukun akijaribu kumnyanyua Nizar aliyekuwa akitokwa na damu sehemu za usoni.



    “Nilikuambia lakini Nizar, huyu mtu ni hatari. Ona sasa.”



    “Asinitishie mimi, mimi ntamsubiri aje.”



    “Ntakupeleka kwako. Twende kwenye gari langu.”



    Fina alimchukua Nizar hadi nyumbani kwake. Alimwacha akiendelea kuhudumiwa na mfanya kazi wake wa ndani na kuondoka. Hakurudi tena klabu bali alielekea nyumbani kwake Sinza Shekilango.



    Baada ya siku mbili Fina alisikia taarifa ya mtu kupigwa na kuumizwa vibaya kisha akatupwa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi. Mtu huyo alikuwa ni Nizar. Wasamaria wema walimwona na kumpeleka Hospitali ya Muhimbili. Watu hao wanasema kwamba alikuwa katika hali mbaya na watu waliofanya hivyo hawakujulikana.



    Fina alimpigia simu Deo na kumuuliza kuhusiana na tukio lile. Deo alikataa kuhusika na kumhakikishia Fina kwamba alimaliza hasira zake siku ya kwanza kugombana na Nizar na hakuona haja ya kumtafuta kama alivyosema awali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upelelezi uliendelea bila kuhusishwa kwa tukio la Nizar na Deo kupigana nje ya Klabu. Katika uchunguzi huo Fina alikuwa ni moja kati ya watu waliohojiwa na polisi kwani walionekana mara nyingi na Nizar katika sehemu za starehe.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog