Simulizi : Usiku Wa Manane
Sehemu Ya Nne (4)
***** ***** ***** ***** *****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya siku mbili Fina alisikia taarifa ya mtu kupigwa na kuumizwa vibaya kisha akatupwa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi. Mtu huyo alikuwa ni Nizar. Wasamaria wema walimwona na kumpeleka Hospitali ya Muhimbili. Watu hao wanasema kwamba alikuwa katika hali mbaya na watu waliofanya hivyo hawakujulikana.
Fina alimpigia simu Deo na kumuuliza kuhusiana na tukio lile. Deo alikataa kuhusika na kumhakikishia Fina kwamba alimaliza hasira zake siku ya kwanza kugombana na Nizar na hakuona haja ya kumtafuta kama alivyosema awali.
Upelelezi uliendelea bila kuhusishwa kwa tukio la Nizar na Deo kupigana nje ya Klabu. Katika uchunguzi huo Fina alikuwa ni moja kati ya watu waliohojiwa na polisi kwani walionekana mara nyingi na Nizar katika sehemu za starehe.
*****
Nizar baada ya kupata nafuu baada ya kuwa hajitambui kwa kipindi cha wiki moja kutokana na kipigo alichokipata, hakuwakumbuka wala kuwatambua watu waliomvamia na kumteka, kumpiga na kisha kumpeleka katika ufukwe wa bahari ya hindi na walilopenda wao, hakuamini macho yake kwa kuwa hakuuliwa. Alimchukia sana Fina kwa kumwona kuwa yeye ndiye aliyekuwa chanzo cha matatizo yake hayo.
Fina ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuhojiwa na polisi juu ya suala hilo la kutekwa na kupigwa kwa Nizar. Alifikishwa katika kituo cha polisi cha Mbezi.
Akiwa katika meza maalumu huku chupa ya maji ikiwa mbele yake, aliingia mmoja wa maofisa wa polisi ambaye alikuwa amevalia nguo za kiraia na baada ya kujitambulisha kwa Fina, alianza kumuuliza maswali ambayo fina alikuwa akiyajibu bila wasiwasi.
“Habari yako dada Fina,” alisalimia yule ofisa wa polisi baada ya kukalia kiti chake na kumgeukia Fina.
“Nzuri tu ofisa,” alijibu Fina.
“Unajua kwa ni kwa nini upo hapa?” alihoji ofisa yule.
“Ndiyo, nimeitwa hapa ili kuhojiwa. Ndiyo taarifa nilizopewa baada ya polisi kuja kwangu.
“Sawa sawa,” aliitika yule ofisa kabla ya kuuliza swali lingine kwa Fina ambaye alikuwa hana wasiwasi huku akisubiria maswali ya yule ofisa.
“Tueleze dada Fina. Wewe na Nizar mkoje?... namaanisha mna uhusiano gani?” Ofisa Upelelezi alimhoji Fina ambaye alikuwa ameishika ile chupa ya maji na kuifungua. Alipiga funda moja kabla ya kuanza kuzungumza. Swali hilo halikumfanya Fina awaze alilijibu kiurahisi zaidi.
“Ni rafiki angu. Mara nyingi tulikuwa pamoja.”
“Rafiki yako kivipi?” ofisa yule alimtupia swali lingine ambalo lilifuatana na lile la awali.
“Ni rafiki wa kawaida ofisa. Tufauti na hapo hakuna uhusiano mwingine kati yetu. Sio mpenzi wangu kama itakuwa tunafikiriwa hivyo. Ni watu ambao mara nyingi huwa tunakutana klabu.
“Siku ya tukio wewe ulikuwa wapi?”
“Nilikuwa klabu pamoja nay eye na watu wengine ofisa,” alijibu fina.
“Wakati akishambuliwa wewe ulikuwa wapi?” ofisa alimtupia swali lingine.
“Awali ya yote kulikuwa na vurugu katika klabu ambapo baadaye ziliisha na kukawa na amani ila mimi pamoja na Nizar tuliondoka kwani mlengwa kwenye ile vurugu alikuwa ni yeye. Sikujua kwamba alirudi baada ya hapo kwani nilimfikisha kwake na mimi nikarudi kwangu nikawa sijaenda klabu klwa wiki hiyo hadi nilipopata taarifa za kutekw kwake na kushambuliwa.”
“Mna kawaida ya kutoka pamoja kila siku baada ya starehe.”
“Siyo kila siku maana mi huwa naenda klabu mwisho wa wiki. Ila huwa tunakutana huko”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo namaanisha hizo siku unazokwenda klabu, huwa mnatoka naye?”
“Hapana, ni mara moja moja sana. Ni kwa sababu Nizar amekuwa akinifatilia kwa muda mrefu akinitaka kimapenzi lakini mimi namchukulia kama rafiki yangu. Hivyo mara nyingine huwa anapenda tuongozane wakati nikitoka. Ila huwa tunakutana hukohuko klabu kama watu wengine.”
“Unadhani kwa sababu ya kukufuatilia inawezekana ndo ukaamua kumtafutia watu ili wampige asiwe anafanya hivyo tena?”
“Hapana ofisa,” Fina alitabasabu na kujibu kwa mkato kisha akaendelea. “Siwezi kufanya hivyo kwani hakuwahi kunilazimisha na ni mtu mstaarabu tu na ananiheshimu sana. Hivyo sijaona tatizo na kweli siwezi kufanya hivyo.”
“Sawa, na vipi kuhusu watu aliogombana nao wiki moja kabla ya kushambuliwa, unaweza ukawa unawafahamu?”
“Ndiyo, ulikuwa ni ugomvi wa kawaida. Walijibizana vibaya wakasukumana lakini haukuvuruga jambo na pia mambo yaliendelea tu vizuri kwani niliwahimiza waondoke na kila mmoja alirudi nyumbani. na mtu aliyegombana naye hayupo nchini. Amekwenda marekani hivyo asingeweza kumpiga na nilimuuliza juu ya Nizar akaniambia yeye hayupo nchini toka juzi yaani asubuhi baada ya siku ya ugomvi baina yao.”
"Sawa tutaendelea na uchunguzi vizuri. Tukikuhitaji tutakuita.”
“Nashukuru ofisa.”
Fina alitoka akiwa anajiamini na kwenda moja kwa moja hadi kwenye gari lake. Alipiga moto na kuondoka kituo cha polisi. Njiani alimpigia Deo akitaka waonane haraka.
“Hallo! Deo.”
“Ndiyo, Fina, kuna nini mbona juu juu bibie?” alihoji Deo ambaye alikuwa hana wasiwasi wowote.
“Njoo hapa Ubungo haraka. Nataka tuongee jambo muhimu na hakikisha hauonekani.”
“Sawa nafika hapo,kuna nini lakini?” Deo hakutaka kwenda kwani hakutaka kuonana na askari au mtu asiyemfahamu. Aliamua kumhoji Fina.
“We njoo, nilikuwa polisi na wamenihoji mengi juu ya Nizar.”
“Nizar?” alishtuka Deon a kuendele… “Ok nakuja.”
“Sawa nakusubiri,” alisema Fina.
“Fina, nihakikishie kama uko mwenyewe.”
“Ndiyo Deo, njoo hadi hapa Ubungo mataa barabara ya Mandela utaona gari Vx nyeusi.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Deo alifanya kama alivyoambiwa na Fina. Dakika chache baadaye alikuwa ameshafika mahali ambako Fina alikuwa ameegesha gari lake. Aliingia ndani ya gari la Fina na hapo hapo Fina alianza kumwelezea yaliyotokea.
“Sasa sikia, hapa natokea polisi kama n’livyokuambia. Niambie ukweli kuhusu Nizar. Ni kweli ulimteka?”
“Ndiyo, japo mimi sikuwepo. Yule mtu nataka nimfundishe adabu,” alijibu Deo bila kujali lililotokea kwa Nizar wala polisi ambako Fina alikuwa ametoka.
“Acha hayo mambo Deo, unajiweka katika hatari sasa,” alisema Fina.
“Fina, hii dunia inahitaji mtu akuheshimu umheshimu, kama mtu hakuheshimu haina maana kwako kujiona mnyonge. Unatumia uwezo wako. Sasa ningemwacha yule mshenzi angejisifu sana. nadhani amekoma,” Deo alijigamba huku akiitoa miwani yake na kuishikilia mkononi.
Fina alimwangalia Deo bila kummalliza. Alimwona mtu katili lakini hakumwonyesha wazi kumchukia.
*****
Tukio lingine ambalo Fina alikuwa akilikumbuka kuhusu Deo pamoja na kikundi chake cha Kobra lilikuwa ni tukio moja la utekaji nyara. Utekaji nyara wa mke wa Balozi wa Marekani nchini. Iligundulika kwamba ni Deo ndiye aliyehusika na utekanyi nyara huo. Alifanya hivyo akisisitiza alipwe Dola milioni tano. Tukio hilo lilitikisa nchi nzima na hata nchi za jirani pamoja na Marekani.
Hata hivyo hakujulikana aliyehusika kwani watekaji waliwahi kumwachia na kutokomea pasipojulikana baada ya kusikia FBI walikuwa wamefika Tanzania kusaidia uchunguzi na kuwasaka watu hao. Ni Fina pekee ambaye baadaye alikuja kuujua ukweli juu ya njama hizo ambazo Deo alikuwa amezipanga baada ya kuona namba za simu za mke wa balozi huyo kwenye simu ya Deo.
Katika tukio hilo, Deo aliwatuma watu wake kumfuatilia mke huyo wa balozi na kumteka.
Deo alituma sauti aliyojirekodi na kumrekodi mke wa balozi. Hakuonyesha ukweli wowote katika sauti hiyo ili kuwaficha wasijue ukweli. Watekaji hawakujionyesha sura zao wala mke wa balozi hakujua alipo baada ya kutekwa kwani alikuwa amefungwa na kitambaa cheusi.
Alifungwa kamba na watu wa Deo na kumpeleka na kumtupa ufukweni wakijua ni sehemu rahisi kuonwa. Kisha wakatokomea.
Asubuhi taarifa zilizagaa kila mahali. Ni baada ya wasamaria wema ambao ni wavuvi kumkuta akiwa amelala chini karibu na bahari huku mawimbi ya maji yakiwa yanamgonga.
'Mke wa Balozi wa Makerani akutwa akiwa hajiwezi huku amefungwa kamba mikono na miguu. pia machoni akiwa amefungwa kitambaa cheusi. Mwanamke huyo Elizaberth alikuwa hoi baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni wateka nyara kumteka wiki zaidi ya tatu na kisha kumtupa katika ufukwe wa bahari. Ushunguzi bado unendelea na watuhumiwa wanatafutwa.'
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Fina alisikia taarifa ya habari. Ni mwezi mmoja alikuwa hajaonana na Deo. Na kila alipokuwa akimpigia simu, Deo hakuongea sana. wakati mwingine alizima pia simu. Fina alijua atakuwa kwenye mambo yake. Hakumwona hata rafiki yake mmoja, si Chacha wala John ambao ndio waliokuwa karibu zaidi na Deo..
Ukaribu wa Fina na Deo ukaanza kutoweka taratibu hasa baada ya Fina kugundua na kuona hila za Deo. Alijua atajiweka katika hatari kama angeendelea kuwasiliana na Deo. Ni zile namba za simu za mke wa balozi wa marekani bi Vicky George, ndizo zilizomfanya aamini kuwa Deo alikuwa ndiye mtekaji wa mke huyo wa balozi.
Alijiuliza mengi juu ya Deo kuzipata namba za Vicky. Baadaye alikumbuka kwamba Deo alishawahi kufika ofisini kwao siku ambayo yeye hakuwepo. Alipata taarifa za Deo kupitia kwa mfanyakazi mwenzake ambaye alimjua Deo kupitia kwa Fina.
*******
Deo alikuwa amewahi kuamka. Alifanya hima na kuelekea moja kwa moja hadi ubalozini. Alishawataarifu watu wake juu ya jambo ambalo wlikuwa wamepanga kulitekeleza siku chache zijazo. Alitumia hila zake kuhakikisha anafika tena kwa mara nyingine katika ubalozi huo. Hakutaka Fina afahamu.
Alikumbuka Fina aliwahi kumwambia juu ya siku ambazo huwa haendi ofisini, na kwa hakutaka afahamu, aliitumia siku hiyo.
Ni Jumamosi asubuhi Deo anaingia katika moja ya mageti makubwa ya ubalozi huo. Anapaki gari lake karibu kabisa na geti hilo na kuteremka. Anatembea kuelekea zilipo ofisi za ubalozi huo.
“Habari yako.” Deo alisalimia kwa lugha ya Kiswahili alipopishana na dada mmoja wa kizungu aliyetokea ofisi za ubalozi wa Marekani.
“Muzuri, Hellow Jambo.” yule dada wa kizungu aliitikia huku Deo akimwangalia kwa makini. Alitabasamu baada ya kusikia maneno ya yule mzungu baada ya kumjibu.
Siku hiyo lengo lake kubwa lilikuwa ni kupata mawasiliano ya mke wa balozi. Alizihitaji kwa namna yoyote namba za simu za mke wa balozi. Aliingia moja kwa moja hadi sehemu ya mapokezi na kuona kwamba kulikuwa na mtu katika chumba kile.
“Habari yako dada,” alisalimia Deo.
“Nzuri tu, karibu. Sijui nikusaidie nini?” dada aliyekuwapo pale mapokei alimwitikia Deo huku akiendelea na kazi yake ya kupanga vitabu vilivyokuwepo katika meza iliyoko pale mapokezi.
“Nashukuru sana….Aaah, samahani…. naomba kuonana na balozi,” Deo alisema bila kujali kwamba alimuulizia mtu mkubwa sana ambaye mara nyingi hakuwa akiuliziwa kwa namna alivyomuulizia yeye.
“Balozi!” alihoji yule dada kwa mshangao.
“Ndiyo. Balozi George…. Mbona unashtuka?” alihoji Deo.
“Sikutegemea kama ungemuulizia bosi. Wengi huwa wanakutana hukohuko. Kufika ofisini na kumuulizia huwa sionagi kitu kama hicho. Na ana wasaidizi wake ambao unaweza ukapitia kwao.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndo maana unashangaa…. Mimi unanijua?” alihoji Deo. Swali lile lilimpa woga yule dada na kutikisa kichwa chake akikataa kwamba hamfahamu Deo.
“Hapana.”
“Basi…. Nina miadi na balozi…. Naelewa ndo maana nimekuja hadi hapa. Kuna mambo tutazungumza na aliniambia nitamkuta. Labda kapata dharura lakini hajanitaarifu.”
“Bosi kweli ametoka, na alisema atarudi badaye kidogo. Ila sijajua atakuwa amekwenda wapi.”
“Naweza kumsubiri hapa?... maana sidhani kama itawezekana kuondoka bila kuonana naye na huenda ndo akawa anarudi,” Deo hakuonyesha wasiwasi wowote alijua atapata namna yoyote ilia pate namba ya mke wa balozi huyo.
“Sijajua atawahi au atachelewa.”
“Basi nitamsubiri kwa dakika chache alafu kama vipi nkiona anachelewa nitaondoka nije kesho,” Deo alifurahi kwa kuwa balozi hakuwepo. Alishajua muda huo asingeweza kumkuta hasa baada ya kusikia kwamba rais alikuwa akutane na mabalozi wa nchi za nje Ikulu. Aliona hiyo itamsaidia kupata lile alilolikusudia.
“Sawa. Karibu.” Deo alikaribishwa na kupewa majarida kadhaa ya kusoma. Alivalia suti maridadi ambayo ilimfanya aonekane maridadi kweli na hivyo kuweza kumshawishi mtu yeyote kumvisha vyeo vyovyote alivyotaka kumvisha. Iwe ni mkurugenzi, meneja wa kampuni fulani kubwa, waziri au hata mbunge ambaye hakujulikana sana kwa watu. Vyeo vyote hivyo alistahili kutokana tu na mwonekano wake siku hiyo.
Alitabasamu baada ya kuona yule dada akionyesha kumthamini kama mgeni mashuhuri. Baada ya kumaliza kumkaribisha na kumhudumia Deo, yule sekretari alitoka na kumwacha Deo peke yake.
“Nakuacha mara moja,” alisema yule dada huku akiondoka. Deo alichukua kitabu cha simu na kukikagua. Aliangali jina la nyumba ya Balozi yule na kuipata katika kitabu hicho. Aliangalia namba zilizokuwepo pale. Ghafla tabasamu likamjia la ushindi. Alizipata namba husika. Aliziandika katika simu yake na kurudisha kile kitabu. Akaacha kuvipitia vile vitabu vingine na kumsubiri sekretari arudi.
“Nilikuacha mwenyewe,” alisema yule dada baada ya kurudi.
“Usijali… nipo sawa,” Deo alimjibu huku akisimama.
“Mbona hima... humsubiri tena.”
“Hapana. Kuna simu nimepokea natakiwa niwahi sehemu japo siyo mbali. Sidhani kama nitatumia muda mwingi.”
“Sawa. Kwa heri.”
“Jina lako nani?” aliuliza Deo.
“Suzy,” alijibu yule dada huku akitabasamu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nashukuru Suzy. Mi naitwa Alfonce Makala,” alisema Deo jina hilo. Alimwongopea Suzy. Suzy hakuwahi kumwona Deo awali. Katika ofisi hiyo Deo alimjua Fina peke yake kwani ni yeye aliyekuwa akimshughulikia hati yake ya kusafiria.
“Baadaye,” alisema Suzy.
“Poa,” Deo alisema huku akifungu mlango na kutoka. Alielekea moja kwa moja hadi kwenye gari lake na kuondoka.
*****
Saa kumi na mbili kamili jioni. Deo alikutana na watu wake wa Kobra. Safari hii hawakutana katika ukumbi wa Maisha kama walivyofanya mara kwa mara. Walikuwa nyumbani kwa Deo.
Katika Jumba kubwa la Deo ambalo lilikuwa nje kidogo ya mji mji wa Dar es Salaam maeneo ya Mkuranga. Haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kujua kinachoendelea ndani. Lilikuwa ni jumba kubwa.
Deo alikuwa na banda kubwa nje ya nyumba yake kwa ajili ya kufugia nyoka aina ya Chatu. Kila siku aliwawekea unga na baadhi ya panya ambao alikuwa akiwanunua kutoka kwa wapitanjia ambao walipewa kazi hiyo bila kujua panya hao wanaenda wapi.
Wengi hawakumjua muhusika bali Deo aliwatumia vijana ambao wlikuwa wakifanya kazi hiyo ya kukusanya panya hao.
Kimya kilitawala katika jumba hilo. Deo peke yake ndiye aliyekuwa akisubiria aanze kuzungumza.
“Tumefanya mambo makubwa sana na yote tumefanikiwa,” alisema Deo huku wote wakit6ikisa vichwa vyao kuonyesha kukubaliana na kile alichokisema Deo.
Deo alitoa picha ya mke wa balozi. Aliwaonyesha wenzake na kuwauliza kama wako tayari kwa kazi.
“Tupo tayari mkuu.”
“Nadhani kila mtu anaelewa pesa ni nini na kwa nini anazihitaji.”
“Ndiyo mkuu,” wote waliitikia kwa pamoja.
“Sisi ndio Kobra,” alisema kwa sauti ya kujigamba huku akimrushia panya chatu mmoja katika banda. Yule chatu alimvamia yule panya na kumla. Deo alicheka na kuwageukia tena wenzake.
“Mmeiona hiyo picha?”
“Ndiyo mkuu,” wote waliitikia.
“Nani anamfahamu huyo mama wa Kizungu, mke wa balozi wa Marekani.... mlishawahi kumwona hata gazetini au kwenye tv?...kama hamumjui basi anaitwa Vicky.....namtaka mara moja kama nilivyowaagiza.”
Baadhi ya watu wake walikuwa hawamjui Vicky. Deo aliwaelekeza sehemu ambayo anaishi na muda anaopita akitokea katika shughuli zake za kila siku.
“Sasa, mimi natangulia Mafia. Baada ya kumteka mtakuja naye huko,” alitoa amri hiyo huku akitembea kuelekea liliko banda la Kobra wake.
“Sawa bosi,” walikubali tena kauli ya bosi wao. Ghafla Deo alisimama na kuwaambia.
“Hakikisheni hakuna atakayewaona na kugundua lolote. Kuweni makini. sawa?”
“Sawa bosi.”
“Kobraa.” Deo alisema kwa nguvu.
“Kobraa,” waliitikia wote na kufunga kikao.
*****
Baada ya siku tano, Deo alikutanishwa na mke wa balozi wa Marekani, Vicky. Alikuwa tayari ameshafika Mafia na kusubiri watu wake waje. Hakuna alijua juu ya tukio hilo hadi pale waliposikia taarifa katika vyombo vya habari. Hata wakazi wa Mafia hawakugundua chochote juu ya utekaji huo. Watekaji walimteka wakati akirudi nyumbani saa mbili usiku na kufanikiwa kumvusha bahari hadi katika Kisiwa cha Mafia ambapo Deo alitangulia wiki moja akisubiri.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Habari zilienea kote juu ya utekaji huo. Polisi walianza kufuatilia bila mafanikio baada ya kwenda Mafia. Baadhi ya maofisa wa FBI kutoka Marekani walifika ili kusaidia uchunguzi. Ambapo ilikuwa imechukua wiki nyingine moja bila ya kupewa jibu juu ya pesa alizokuwa ameagiza. Alisikia katika taarifa na kuona askari wakiwa karibu na eneo walilokuwa wamefikia.
Alianza kuchanganyikiwa kwani alijua hataweza tena kufanya alichokusudia na hivyo aliamua kuachana na mpango huo kwani aliamini hakuna aliyejua watekaji kwani walichosikia ni sauti tu za kurekodiwa bila ya video. Aliamua kuachana naye baada ya kuambulia shilingi laki saba alizokuwa nazo katika pochi yake.
Aliwaamuru watu wake wamfunge kamba na kumpeleka ufukweni usiku na kumwacha huko.
“Sasa sikieni… Ili kuwapoteza hawa washamba, fanyeni mpango mhakikishe mnaenda kumwacha katika ufukwe wa Coco. Hiyo itakuwa tumewapoteza na hakuna ambaye atajua kama walivyohisi tupo huku Mafia.”
“Sawa bosi,” waliitikia watu wake huku yeye akitangulia tena na kuvuka maji kurudi Bara. Hakutaka kujulikana.
*****
Fina alitikisa kichwa chake. Ni baada ya kukumbuka siku alipokutana na Deo klabu na kumwona akiwa na namba ya simu ya nyumbani kwa balozi siku hiyohiyo alipotoka ubalozini. Sekretari pia alitoa ripoti ya watu waliofika kwa Fina. Katika daftari la kuweka saini ya wageni mbalimbali waliofika Fina aliona jina la Deogratious Mbila. Mbele yake aliona sababu iliyomleta pale ubalozini kuwa ni kuonana na balozi. Alijua mpango wote ulikuwa ni wa Deo wa kuteka. Alimwogopa sana Deo baada ya kuhisi yote hayo. Pia alijihakikishia baada ya kuambiwa na mfanyakazi mwenzake Suzy.
Matukio ya Deo yalimwingia hasa fina. Alimfikiria sana Hancy ambaye alikuwa akihangaika kujua aliyefanya mauaji ya wazazi na ndugu zake. Akili haikumkaa sawa na hivyo kuamua moja juu ya Deo. Kumsaidia Hancy ili amjue Deo.
Mauaji yaliyofanya na Deo na kumfichia siri ilikuwa ni mtihani mkubwa. Deo mwenyewe alijua kwamba Fina alifahamu kila kitu. Hivyo alijitahidi kuwa naye karibu ili asiweze kusema lolote.Kuna wakati alimfokea na kumtishia asiseme kitu. Hilo halikumtisha Fina kwani alielewa nini cha kufanya baadaye. Alimwahidi Deo kutokusema lolote kwani asingeweza kumsaliti. Lakini mwisho wa maongezi yao aliishia kubenua mdomo akipuuzia alilosema Deo.
Alikumbuka pia siku ambayo walikuwa mitaa ya Kariakoo pamoja na Deo na Deo kufanya uhalifu ambao ulimchanganya sana Fina ambaye kwa mara ya kwanza alisjhirikishwa bila ya kupenda katika uhalifu huo ambao pia hakujulikana na hivyo kupotelea mbali pasipokuwa na ushahidi baada ya tukio lililotokea siku hiyo.
Deo aliingia ndani katika duka moja la Muindi maeneo ya Kariakoo katika mtaa wa Msimbazi. Muindi yule alikuwa peke yake. Alimkaribisha Deo baada ya kumwona kaiingia ndani. Deo alikuwa pamoja na Fina. Fina alikuwa akizunguka kuangalia nguo zilizokuwepo pale dukani. Hakuangaika kumfuata Deo upande aliokuwepo ambapo alimfuata muuzaji huyo. Hakuwa na taarifa ya kinachoendelea kati ya Deo na Muindi yule. Ghafla alisikia kimya. Kimya kilichoashiria jambo fulani. Yule Muindi hakuendelea kuongea tena kumkaribisha Deo na kumwelezea bei za bidhaa. Deo naye alitoka na kumfuata Fina.
Fina aligeuka na kumkuta yule Muindi amelala chini. Alikuwa amekufa. Deo alikuwa amerudi na mfuko wa hela na kumpa Fina. Alimwamuru atoke nao na kuelekea kwenye gari.
“Nenda nao kwenye gari sasa hivi. Asikuone mtu wala usijishtukie,” Fina alifanya kama alivyoambia. Alifanya ili kukwepa kukamatwa. Baada ya muda wa dakika mbili Deo alimfuata. Alienda kumficha yule Muindi ili asionekane. Alimvunja sjingo yake na hivyo hakukuwepo na ushahidi wa damu. Alitoka nje na kuelekea liliko gari ambalo Fina alikuwa ameingia. Deo aliingia kwenye gari na kupiga moto na kutokomea.
“Kwa nini umefanya vile Deo?”
“Tufike kwanza, hapa sio pa kuongelea hayo.”
Deo alipita barabara ya Morogoro na kuingia maeneo ya Magomeni Mikumi. Walitafuta sehemu na kungia na zile hela. Walipata chumba. Walilipia na kuingia. Fina alikuwa muda wote amekasirika. Hakutamani kuendelea kuwa na Deo kwa wakati huo.
Deo alitoa zile hela. Zilikuwa ni zaidi ya milioni 50 baada ya kuzihesabu harakaharaka.
“Aaah! Dili zuri sana,” Deo alifurahia zile pesa huku akimrushiarushia Fina baadhi ya hela hizo.
“Sikujua unakokwenda kama ningejua nisingeenda. Kumbe ulikuwaq unaenda kufanya huu ushenzi.”
“Finaaa… Unaita kazi yangu ushenzi?... huu ni ushenzi?” alikoroma Deo baada ya Fina kusema vile.
“Sikiliza Deo, mi sipendi mambo unayoyafanya. Najuta hata kujuana na hili kundi lenu la Kobra. Hamuoni kama mnajiweka matatizoni na pia mnaniweka mimi hukohuko. Sitakubaliana na hilo.”
“Sikiliza wewe… usijidai mtoto wa mjini wakati sio. Na ukileta mchezo utajuta,” Deo alisema huku akitoka nje na ili kuangalia mambo yanavyoendea kabla ya kurudi na kuchukua pesa zake na kuondoka na Fina.
Fina hakuwa na la kusema. Aliamua kutafuta mbinu ili aondoke na aachane na hilo kundi. Alipata mwanya baada ya Deo kutoka nje. Alifungua dirisha na kupita na kutokea katika ukuta wa nyumba ambao ulikuwa umetenganisha nyumba hiyo na hoteli waliyofikia. Kisha akaondoka bila kuonekana. Hakuchukua hata shilingi katika zile pesa za Deo kwan hakudhamiria kufanya jambo ambalo angelijutia.
“Nadhani sasa tunaweza….” Kabla Deo hajamalizia kuongea, alishangaa kuona chumba lkikiwa chenyewe. Aliona dirisha likiwa wazi. Alicheka kicheko cha taratibu huku akifunga lile dirisha. Alijaribu kumpigia simu lakini simu yake ilikuwa imezimwa.
Fina alifanikiwa kuchukua usafiri wa kumpeleka nyumbani kwake. Bada ya wazazi wake na ndugu zake kurudi kutoka Nairobi, alihamia maeneo ya Shekilango. Alinunua nyumba ambayo ilikuwa inamtosha yeye peke yake. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alifika na kuingia ndani. Siku zote akiwa na Deo hakutaka kumwonyesha nyumba ambayo alikuwa akiishi. Alijua ipo siku atamrudi na hivyo alikuwa akimdanganya mara kwa mara kwamba liishi Mbezi Beach.
Wazo la kwanza alilolipata ni kwamba afanye hima na kuwasiliana na Hancy kabla Deo hajaanza kumfatilia. Alifikiria kuacha kwenda klabu kwa kuhofia kukutana na Deo huko.
Simu ya Hancy haikupokewa. Aliwaza Fina baada ya kupiga mara kadhaa. Hancy hakuipokea kwani alikuwa amelala baada ya mizunguko yake kumchosha. Fina pia aligundua amebadili line na hivyo inawezekana Hancy hakuelewa kama ni yeye.
Alisubiri tena ili baadaye apige tena.
*****
Fina alichukua simu yake baada ya kumaliza kuvaa. Ilikuwa ni jioni ambapo baada ya kufika nyumbani kwake alijitosa bafuni na kuondoa uchovu wa siku hiyo ambao kwa kiasi kikubwa ulisababishwa na Deo. Hakuwa na hamu ya kuonana na Deo. Aliapa kupambana na uhalifu wao. Alijua kwa kumtumia Hancy wataweza kufanikisha hilo kwani alijua Hancy alikuwa na hasira nao sana.
Alipiga namba za Hancy. Safari hii simu yake ilipokewa na Hancy.
“Halow, Hancy,” Fina alianza kumwita Hancy aliyekuwa upande wa pili wa simu.
“Fina, ni wewe?... uko wapi? Nakutafuta muda mrefu sikupati kwenye simu.”
“Nilikuwa mjini. Simu ilikuwa kwenye pochi. Samahani….Hancy nataka tuonane. Serious,” Fina hakutaka Hancy aelewe kwanza lengo lake la kuzima simu. Alijua lazima atashangaa ni kwa nini amebadilisha namba ya simu lakini alijua ni namna gani atafanya ili aweze kumweka sawa.
“Na mbona umebadili line?.... nimekutafuta sana nikuambie uje nyumbani,” alisema Hancy aliyeonekana akiongea kwa uchovu baada ya kuamka jioni ile.
“Nitakuja kukuambia Hancy. Hapa nimeshajitayarisha kama vile nilikuwa najua ntakuja kwako jioni. Nakuja kulala kwako leo.”
“Sawa njoo basi,” alisema Hancy.
“Nakuja Hancy.”
“Poa.”
Fina alichukua gari lake hadi nyumbani kwa Hancy. Mlinzi alikuwa akimtambua na hivyo hakuulizwa swali lolote tofauti na watu wengine waliokuja kumwona Hancy. Imani ya kuonana na watu wema ilikuwa kama imempotea Deo hasa baada ya kuamua kuwa msiri na kile ambacho alikusudia kukitekeleza siku zijazo. Muda mwingi aliutumia kufanya matayarisho juu ya kazi yake hiyo aliyoidhamiria.
Fina aliingiza gari na kulipaki katika eneo ambalo huwa amezoea kulipaki. Ni eneo ambalo alilipenda kwa kuwa ni karibu na linapoegeshwa gari la Hancy ambalo hulipenda zaidi, Toyota Land Cruser. Alishuka kwenye gari huku akitabasamu baada ya kumwona Hancy kwa mbali. Alitembea na kumfuata hadi alipokuwepo. Alimkuta Hancy akinoa panga. Alisimama na kumwangalia Hancy. Alisimama na kumwangalia kwa kitambo kidogo….Aliona mapambano yanaanza. Alitabasamu.
“Hancy,” aliita Fina huku akimfuat. Hancy aligeuka na kumfata Fina na kumkumbatia kwa nguvu.
“Vipi mpenzi, mbona na mapanga sasa hivi?.... au unataka kumchinjia mgeni kuku?” aliuliza Fina kwa mzaha huku akijibandua kwa Hancy baada ya kukumbatiana.
“Niko kazini mpenzi,” alisema Hancy baada ya kumwachia Fina.
“Nakuona…. Acha kwanza. Nataka tuongee kuhusu Deo,” Fina alisema huku akiwa amebadilika sura na kuonyesha kuchukizwa na jambo fulani.
“Deo?.... Deo ndiyo nani?” alihoji Hancy ambaye hakuelewa Fina alikuwa akizungumzia jambo gani.
“Njoo hapa ukae nitakuelezea yote kuhusu Deo,” Fina alimvuta Hancy mkono mpaka kwenye viti ambavyo vilikuwa katika bustani pale nyumbani. Hancy alikaa na kisha Fina kumkalia juu ya mapaja yake. Panga alikuwa ameliweka juu ya kiti kingine. Lilikuwa na makali tayari kwa shughuli aliyotaka kuitekeleza. Fina aliliangalia lakini hakuuliza kitu.
“Fina, ni nani huyo Deo?” alianza kuuliza Hancy huku akizishika nywele za Fina na kuzichezeachezea jambo lililomfanya Fina ahisi raha na kuanza kuzungumza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hancy,” alianza kusema Fina. Deo ndiye hasa mtu unayemtafuta. Ndiye kiongozi mkuu wa kundi la Kobra na aliyeongoza katika mauaji ya familia yako. Ni mtu hatari sana.”
“Deo… alisema Hancy kana kwamba alikuwa akilikumbuka hilo jina.”
“Ndiyo Hancy.”
“Fina. Kwa nini haukuniambia siku zote?” aliuliza Hancy ambaye alikuwa amebadilika sura na kuwa kama simba mwenye njaa.
“Hancy, sikujua kama uliyewatafuta ni wao. Ulivyonionyesha ile picha ndo n’kajua kwamba uliyewatafuta ni wao. Deo alikuwa ni rafiki angu kabla. Nilipogundua hila zake na mambo aliyoyafanya. Niliamua kuachana naye.
“Alikuwa mpenzi wako?” alihoji Hancy kwa ukali.
“Hapana Hancy,” Fina alijibu kwa sauti ya upole iliyoonyesha woga.
“Ulikuwa naye kivipi?”
“Hancy, tulikuwa tunakutana mara kwa mara. Sikujua ni mtu gani ila nilifanya uchunguzi nikagundua mengi mabaya kuhusu yeye na ndiyo maana nataka nikusaidie kumtia nguvuni.”
“Fina, kumtia nguvuni siyo suluhisho. Nataka kuwaangamiza wote mmoja baada ya mwingine. Na hilo panga walilolitumia kuwaua ndugu zangu ndiyo litaamua maisha yao. Sitaacha hata mmoja. Nadhani unawafahamu wote Fina.
“Kweli Hancy, na wote najua wanapoishi,” Fina alijibu huku akiliangalia lile panga lililoko juu ya kiti pembeni yao.
“Hapo utakuwa umenisaidia sana. Nahitaji kuwaona kwa sura wote kabla ya kuanza kwa hili zoezi zito. Baadaye nitaenda huko huko ukumbi wa Maisha. Utaenda kukaa nao ili nikikuona nao niwajue. Sitapenda watu wajue pia tumefika wote kwani wanaweza wakawa ni watu wake wengine wakamweleza.”
“Lakinin Hancy, nimemtoroka Deo leo tu. Kuna mambo kayafanya hadi ikabidi nibadilishe namba ya simu…. Nilikuwa Kariakoo tukaonana. Akaniomba nimsindikize duka moja hivi la Muindi. Kufika pale akamuua yule Muindi na kuiba pesa zake zote. Zaidi ya milioni hamsini hivi. Tukaelekea hoteli moja hivi… hapo ndo nkamtoroka na kuapa kwamba ntafanya juu chini nihakikishe haendelezi hii tabia yake. Ana ua watu wasio na hatia. Juzi tu hapa kamteka mke wa balozi wa Marekani. Anapigaga sana watu klabu na kuwateka. Yeye ndo aliyewaua wazazi wako na pia nilisikia alikuja ofisini kwetu na kumhadaa mfanyakazi mwenzangu na kupata hiyo namba ya mke wa balozi kwa madai ya kwamba alikuwa akimsubiri balozi kwani alikuwa na miadi ya kukutana naye siku hiyo… Sitaki kuonana naye. Na ninahisi atanifanyia kitu kibaya kwa vile nimemtoroka. Nitahakikisha haonani na mimi kwa njia yoyote ile…. Hancy, kuna mzungu mmoja nitakupa mawasiliano naye. Anaitwa Van Brussel. Amekuwa akikutana nao kama mimi na mi nimemjua hukohuko.“
“Van Brussel?” aliuliza kwa mshangao Hancy.
“Ndiyo Hancy… utaenda kukutana naye.”
“Ni nani huyo?” alihoji Hancy ambaye alionekana kuwa na shauku ya kujua kama ni yule aliyemfahamu japokuwa akilini mwake alijua itakuwa ni yeye kwani alikumbuka alishawahi kumwambia ya kwamba alikuwa Tanzania kipindi Fulani na mama yake wakiwa wadogo.
“Sikumzoea sana, ila inawezekana ni mtu mwema sana. Anasaidia sana watu alafu anajua kuchora kaka wewe. Ni wa huko Uholanzi kwenu.”
“Sawa,” Hancy alishtuka kusikia Van Brussel. Alinyamaza. Hakutaka kumuuliza zaidi Fina juu ya huyo Van Brussel.
Alitabasamu kwa mbali baada ya kusikia neno ‘anajua kuchora kama wewe’. Hakutaka kuendelea. Alijua atakuwa ni yule aliyemjua ila hakutaka kumuulizia sana. Alichukua namba za Van Brussel na kuzisave kwenye simu yake.
“Hancy…. Najua utafanikiwa kwa hilo bila ya mimi,” aliuliza Fina baada ya kuona kimya kidogo kilichosababishwa na fikra za Hancy aliyeonekana akifikiria jambo.
“Usijali mpenzi,” ngoja niwafuate hukohuko.
“Hapana Hancy… sikuruhusu kwa leo. Nenda kesho. Hii safari nimekuja kwa ajili yako na nlikuambia leo nalala kwako.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Okey Baby,” Hancy alisema huku akitabasamu. Alimbeba juu juu Fina na kuingia naye ndani. Zoezi zima la kulienzi penzi lao likashika hatamu baada ya wote kuwa na hamu ya mwenzake kwa muda mrefu. Fina hakujionyesha kuogopa kufanya lolote ambalo alijua litrampoza hasira na kumrudisha Hancy katika dunia ya huba na iliyojaa asali ya upendo.
Alijitutumua kila awezavyo hali iliyomfanya Hancy akiri uzuri wa Fina kipenzi chake cha moyo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment