Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

WAKILI WA MOYO - 4


Simulizi : Wakili Wa Moyo

Sehemu Ya Nne (4)


“Zitachukua muda gani kurudi?” mama Cecy aliuliza. “Hatuwezi kujua ubongo umecheza kiasi gani, lakini msiwe na wasiwasi hii ni hali ya kawaida kwenye ajali za namna hii,” dokta aliwapa moyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Tunaweza kwenda kuwaona?” aliuliza mama Cecy. “Kwa leo bado kuna baadhi ya mambo tunashughulika nayo kuanzia kesho mna nafasi ya kuja kuwaona.” “Sawa.” Mama Colin na mama Cecy walitoka ofisini kwa mganga mkuu na kukutana na Mage na mama yake wakiwasubiri, walipotoka waliwauliza. “Vipi wanasemaje?” Mage alikuwa wa kwanza kuuliza. “Bado wapo chini ya uangalizi maalumu,” alijibu mama Colin. “Hatuwezi kuwaona?” mama Mage aliuliza. “Kwa leo haiwezekani.” “Mmh! Basi watakuwa wana hali mbaya sana,” Mage alisema. “Anayejua ni dokta, sisi hatujui kwa vile hatujawaona,” alijibu mama Colin ambaye alionesha kuchoshwa na maswali ya Mage. “Jamani hatuna cha kufanya maombi yetu yote yawe kwa watoto wetu ili Mungu awaepushe na matatizo yaliyo mbele yao,” alisema mama Mage. “Ni kweli dada yangu,” alisema mama Cecy ambaye muda wote alikuwa kimya kutokana na mshtuko alioupaka kwa ajali ya watoto wao. Walikubaliana kurudi nyumbani mpaka kesho ambayo wangerudi kuwaona, mama Mage aliwashauri wote waongozane nyumbani kwa mama Colin kufanya maombi ya pamoja ili Mungu awaepushe na matatizo yale. Waliongozana wote hadi nyumbani kwa mama Colin ambako walifanya maombi ya pamoja yaliyoongozwa na mama Mage. Walipiga magoti na kushikana mikono kisha mama Mage alishusha maombi. “Baba Mungu tumepiga magoti mbele yako tunajua hakuna chochote chini na juu ya jua kiwezacho kufanyika bali kwa idhini yako. Baba Mungu lisilowezekana kwa mwanadamu kwake linawezekana, lililo zito kwa mwadamu wako ni jepesi. Eeh, Baba tunaomba uwaepushe watoto wetu na matatizo mazito kama ulivyoweza kumuepusha mwanao mpendwa pale msalabani. Kama ulivyoweza kumponya Ayubu na maradhi ya ajabu ambayo alipona kupitia kwa uweza wako. Baba Mungu unaweza kumponya aliye mahututi unaweza kumfufua aliyekufa kwako wewe hakuna kinachoshindikana baba waponye wenetu ambao hatujui hali zao ni wewe pekee mwenye kuugeuza usiku ukawa mchana basi yaondoe maradhi miilini mwao wape afya njema. Baba vunja pepo wa maumivu vunja pepo wa mauti vunja pepo wa maradhi kwa jina la mwanao Yesu Kristo aliyehai Amen.” “Ameni,” waliitikia pamoja. Baada ya maombi walinyanyuka na kukaa kwenye makochi, kwa vile hawakuwa na la kuzungumza mpaka siku ya pili watakapokwenda kuwaona wagonjwa wao. Mama Mage na mwanaye waliaga na kuondoka kurudi nyumbani na kuwaacha mama Colin na Cecy wakiwa wamekaa kila mmoja akiwaza lake. *** Siku ya pili alfajiri walikutana wote hospitali ya Muhimbili , kwa vile daktari alikuwa hajafika ilibidi wamsubiri mpaka saa moja asubuhi alipofika, alipowaona aliwaeleza wasubiri ili afike wodini kwanza. Dokta Bukos baada ya kuwazungukia wagonjwa wote na kuchukuwa taarifa kutoka kwa daktari wa zamu aliwafuata kwenda kuwaona wagonjwa wao. Waliingia mmojammoja kutokana na taratibu za kuingia chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Colin alikuwa akipumulia mashine akiwa amelala bila kutikisika. Lakini dokta Bukos aliwaeleza kuwa kidogo ameanza kupata fahamu kwa misuli ya mwili kuanza kufanya kazi taratibu japo hakuonesha mabadiliko yoyote zaidi ya kulala vilevile walivyomkuta. Katika chumba kingine Cecy naye alikuwa vilevile amejilaza akitumia mashine kupumua, yeye alionekana ufahamu bado kabisa japokuwa mapigo ya moyo dokta alisema yapo mbali sana. Lakini aliwaomba wazidishe kumuomba Mungu na si kulia. WIKI MOJA BAADAYE Baada ya wiki moja hali ya Colin ilimalika kidogo kwa kuweza kutambua watu japo bado alikuwa hawezi kuzungumza kwa haraka kwa kutafuta maneno. Cecy hali yake ilikuwa bado mbaya pamoja na mwili kuanza kurudisha hisia bado alikuwa akiendelea kutumia mashine za kumsaidia kupumua. Walijikuta katika wakati mgumu baada ya hali ya Cecy kuonekana kuchelewa kuimalika. Mganga mkuu aliomba kama wana uwezo basi Cecy apelekwe India kwa ajili ya matubabu zaidi baada ya kuamini uwezo wa madaktari wa Tanzania uliishia pale kuweza kuuamsha mwili lakini hali ilikuwa bado tofauti na Colin ambaye aliweza kula hata kufanyishwa mazoezi japokuwa alikuwa akizungumza kwa shida. Madaktari waliwahakikisha ndani ya wiki nyingine hali itaimalika zaidi na kuweza kuanza mazoezi ya peke yake. Fedha iliyokuwa ikitakiwa kwa ajili ya matibabu na nauri ya Cecy na msaidizi wake ilikuwa kubwa ambayo mama Cecy hakuwa nayo. Kwa hali ya mgonjwa ilivyokuwa ikionekana mama Colin aliamini kabisa Cecy hawezi kupona hivyo kutoa kiasi hicho cha fedha ni sawa na kuzitupa. Mama Cecy alikuwa radhi kuuza nyumba ili tu mwanaye akatibiwe, lakini mama Colin alimshauri asisumbuke kwa vile wagonjwa wa aina ile huwa hawaponi heri asiipoteze nyumba kwani Cecy akifa atakuwa na sehemu ya kukaa. Mama Cecy alikuwa radhi kulala nje lakini ajue hatima ya hali ya mwanaye, ili kujitoa kwenye lawama alichangia milioni tano katika milioni ishrini na tano zilizotakiwa. Mama Cecy alitafuta dalali wa kuiuza nyumba kwa bei ya kutupa ili tu mwanaye akatibiwe India kama kufa basi afe akijua alikuwa akipigania maisha yake. Wiki ile ndiyo ilikuwa wiki ya malipo ya Cecy kutoka katika kampuni ya jarida la Ebony ambayo iliijngiza kwenye akaunti ya Cecy pia walifunga safari mpaka Tanzania kuonana na Cecy kwa ajili ya kumpiga picha zingine kwa ajili ya matoleo mengine. Jarida lililotoka na picha ya Cecy ilivunja rekodi ya mauzo ya kampuni ile toka ianzishwe. Uongozi wa kampuni ile ulipanga kumpa mkataba mnono wa muda mrefu zaidi pia kumfunga asitumike kwenye majarida mengine. Walipofika walitaka kuonana na meneja wake ambaye ni mchumba wake Colin mmiliki wa kampuni ya Urembo. Taarifa walizopata ziliwashtuka kusikia Cecy na mchumba wake walipata ajali mbaya sana. Walikwenda mpaka hospitali na kuwaona wagonjwa. Colin alionekana hajambo lakini Cecy bado hali yake ilikuwa tata, walionana na mganga mkuu na kutaka kujua nini hatma ya mgonjwa kwa siku alizokaa hospitali. Aliwaeleza hatua walizochukua tokea mwanzo kwa wagonjwa wote na kufanikiwa kwa mmoja na sehemu walipokwama na kuhitaji msaada wa matibabu zaidi nje ya nchi. Waliulizia kama kuna uwezekana wa mgonjwa kupona, walijibu upo wa hamsini kwa hamsini. Waliuliza gharama ya matibabu yote walielezwa milioni ishirini na tano kwa awali kama itazidi watajulishwa kwa vile mgonjwa hakuwa wa kutoka mapema. Walikubali kugharamia matibabu ya Cecy mpaka hatua ya mwisho. Baada ya makubaliano zilifanywa taratibu zote za kumsafirisha mgonjwa na mtu wake wa karibu. Siku ya tatu Cecy alisafirishwa pamoja na mama yake kwenda India kwa matibabu ambayo wengi waliamini madaktari wa Tanzania waliona aibu kusema ukweli kuwa Cecy ameisha kufa anachosubiri kupoa tu. Baada ya safari ya angani Cecy alitua katika jiji la Mumbay na kupelekwa katika hospitali ya Apolo. Alipokelewa mara moja alianza kupatiwa matibabu kwa kuchukuliwa vipimo vyote ili kuangalia tatizo lipo wapi. Baada kurudi majibu ya vipimo ilionesha Cecy atapona lakini itachukua muda kurudi katika hali ya kawaida kutokana na kupoteza kumbukumbu na ubongo wake kucheza kidogo, lakini alikuwa na bahari nzuri ubongo haukuvia damu. TANZANIA Hali ya Colin iliendelea vizuri kwa kuimalika kwa kasi kubwa tofauti na walivyotegemea. Baada ya wiki aliweza kuzungumza vizuri na kuanza kumkumbuka mpenzi wake Cecy. Wakiwa wamekaa kitandani Colin alimuuliza mama yake. “Mama mbona simuoni Cecy wala mama yake leo siku ya tatu?” “Cecy alisafiri walifiwa na bibi yao kabla hujapata ajali.” “Mama ina maana nilipata ajali peke yangu?” Swali lile lilimchanganya sana mama yake aliyeamini mwanaye baada ya ajali alipoteza kumbukumbu na hakutaka kumshtua kutokana na hali na mchumba wake ambaye aliamini aliondoka mfu kwa asilimia tisini na tano. “Kwani unakumbuka nini?” “Unajua mama nakumbuka wakati napata ajali nilikuwa na Cecy tukitoka mazoezini na sababu ya ajali ni Mage.” “Mage?” mama yake alishtuka. “Ndiyo mama.” “Mage kasababisha kivipi?” Colin alimweleza tukio zima la ajali ilivyotokea mpaka kupata ajali, baada ya kumsikiliza aliguna na kusema: “Kwani Mage aliandika ujumbe gani?” “Kwa kweli sikuuona bali usomaji wa Cecy ulionesha ujumbe siyo mzuri.” “Sasa wewe nini kilikupelekea kupata ajali.” “Mama baada ya kumwangalia Cecy usoni moyo ulishtuka na kujua hakuna tena usalama kwa vile aliisha mshutumu Mage mapema baada ya hukumu ya mchumba wake kabla ya simu na kutishia kusitisha mkataba. Mage alinipigia simu na kuzungumza maneno ambayo ni uchokonozi kwa vile anajua kabisa nipo na nani.” “Inaonekana alikuacha bado anakupenda ulikuwa una hiyari kukubali au kukataa au hata kumfanya spea taili.” “Mama Cecy ni kila kitu kwangu ndiye mwanamke wa pekee moyoni mwangu sina nafasi nyingine.” “Lakini ulitakiwa kujua ameandika ujumbe gani kabla ya kupagawa na kusababisha ajali mbaya.” “Kwani gari limeharibika sana?” “Limeungua lote na moto.” “Mungu wangu na..na Cecy?” “Naye alipata majeraha kama yako.” “Yupo hapa hospitali?” “Hapana yeye inaonekana alipata matatizo makubwa na kukimbizwa India.” “Maskini mpenzi wangu,” Colin alishika kichwa kwa mshtuko. “Lakini taarifa zinasema anaendelea vizuri,” mama yake alimpa moyo. “Hospitali natoka lini?” “Wiki hii lakini utatakiwa kuja kila siku asubuhi kufanya mazoezi ya viungo ili kuurudisha mwili katika hali ya kawaida.” “Nikijisikia vizuri kidogo nakwenda India kumwona mpenzi wangu.” “Hakuna tatizo tutakwenda wote,” mama Colin alimkubalia mwanaye kumpa moyo lakini aliamini kabisa Cecy hakuna kitu siku zake zilikuwa zikihesabika walichosubiri taarifa za msiba wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mama Mage na mwanaye walikuwa wakizungumza kuhusiana na hali ya Colin na mchumba wake. “Mama unafikiri mchumba wa Colin anaweza kupona?” “Mmh! Kwa kweli ni Mungu tu mwenye uwezo wa kumponya, taarifa nilizopata kutoka kwenye hospitali aliyokuwa anatibiwa kupona ni asilimia ndogo na hata akipona bado hata kuwa sawa.” “Kwa hiyo mama nina imani hii ni nafasi yangu ya kurudi kwa Colin?” “Ni nafasi yako kama ukiifanyia kazi bila hivyo itakupita huku unaiona.” “Sasa mama niifanyie kazi ipi au niende wa Karumanzila?” “Si kwenda kwa Karumanzila bali kujipendekeza muda huu wa matatizo kuonesha unamjali sana Colin kwa kwenda asubuhi unarudi usiku ikiwezekana ulale hukohuko.” “Mama tena naondoka muda huu.” “Mwanangu kijua ndicho hiki lazima uuanike sasa, huenda Mungu alikuwa na kusudio lake la kuirudisha ndoa yetu iliyoyeyuka kwa kifungo cha Hans na kufa kwa Cecy.” “Umeona eeh, mama utakuwa nabii kwa kuiona hilo, japo siwezi kufurahi kwa matatizo ya Cecy lakini kila kitu hupangwa na Mungu.” “Halafu nimeambiwa Colin atatakiwa kila siku asubuhi apelekwe hospitali kwa mazoezi, nataka kazi hiyo uifanye wewe tena utachukua gari la kifahari la kumpelekea hospitali.” “Mama hilo si la kusema mbona kikohozi kimepata mkohoaji nitahakikisha mahaba ninayo mpa anamsahau marehemu wake(Cecy).” Baada ya mazungumzo Mage alimuaga mama yake kwenda kumwona Colin nyumbani kwao ili aurudishe ukaribu wao kutokana na matatizo ya mchumba wake Cecy. Mage maombi yake alitaka Cecy afie India, Tanzania urudi mwili tu usio na uhai, aliendesha gari hadi nyumbani. Mama Colin alimpokea Mage aliyejionesha mwenye huzuni kutokana ugonjwa Colin. “Karibu mkwe.” “Asante mama, mume wangu anaendeleaje?” “Mmh! Kiasi hajambo vipi nyumbani hamjambo.” “Hatujambo kiasi.” “Kuna anayeumwa?” “Hapana ila huwezi kuamini toka Colin apate matatizo nimekuwa sili wala silali vizuri utafikiri naumwa mimi.” “Pole, la muhimu kumuomba atapona tu.” “Mama maombi yangu yote kila dakika ni kwa Colin.” “Mama yako hajambo?” “Hajambo, mume wangu yupo wapi?” Mage alijifanya ana shauku ya kumuona Colin. “Yupo chumbani kwake amepumzika.” Kwa vile chumba cha Colin alikuwa akikijua alikwenda moja kwa moja na kuingia ndani bila hodi. Alimkuta amesinzia aliinama na kumpiga busu la shavu lililomfanya Colin afumbue macho. Alishtuka kukutana na Mage aliyekuwa amemchanulia tabasamu pana amesimama pembeni ya kitanda. “Colin mpenzi wangu pole sana,” Mage alisema huku akikaa kitandani, lakini Colin hakumjibu alikuwa kama anamshangaa. “Vipi inaendeleaje mpenzi?” alimuuliza tena. “Mage unatafuta nini hapa?” Colin alimuuliza akiwa amemkunjia uso. “Colin mpenzi wangu maswali gani hayo wakati unajua wewe ni mgonjwa?” “Hata kama mgonjwa sikukuita uje unione labda ungekuja kuona jeneza langu na si mwili wangu.” “Kwa nini unasema hivyo mpenzi wangu?” majibu la Colin yalimshtua Mage. “Kwanza naomba jina la mpenzi lifutike mdomoni na moyoni mpenzi wako, mpenzi wangu ni mmoja tu Cecy.” “Kumbuka kabla ya Cecy nilikuwepo miye.” “Kuna mtu aliye mpenzi wa moyo wako si mwingine bali Hans si Colin.” “Colin, Hans amefungwa si mpenzi wangu mwenye nafasi hiyo ulibakia wewe peke yako.” “Mimi ulinipenda lakini Hans ulimpenda zaidi kwa hiyo ndiye chaguo sahihi la moyo wako si mimi. Nami wewe nilikupenda lakini Cecy nilimpenda zaidi naye ndiye aliyenipenda kuliko kiumbe chochote kilichopo chini ya jua. Malaika sijawaona nina amini hata wao ningewaona wasingeuzidi uzuri wa Cecy.” “Wewe Colin acha kukufuru Cecy ana uzuri gani kumshinda malaika?” “Malaika uliisha muona?” “Sijamuona lakini nasikia mzuri sana.” “Basi uzuri wao haufiki kwa Cecy, kwa vile ulichokitaka kimefanikiwa naomba uachane na mimi.” “Colin nimefanya nini?” Mage aliuliza huku akilia. “Unajua umeniumiza mara ya kwanza hukutosheka umeniumiza kwa mara ya pili bado hujaridhika naona kimebakia roho yangu tu.” “Colin usiseme hivyo unaniumiza?” “Ulitaka tufe sote lakini nakuhakikishia Cecy atapona na atarudi tufunge ndoa hata kama Cecy atakufa nitafunga ndoa na maiti ya Cecy si mwanamke mwingine.” “Colin usiseme hivyo, Cecy akifariki siyo mwisho wa dunia maisha yataendelea, nina imani hakutakuwa na mwanamke mwingine atakayechukua nafasi ya Cecy bali mimi.” “Ninacho kisema hakitafutika moyoni mwangu Cecy ndiye mwanamke wangu wa maisha nawe msubiri Hans mfunge ndoa au nenda mkafungie ndoa gerezani.” “Kwa nini Colin unanichukia hivyo?” “Sitakusamehe mpaka nakufa naomba utoke nje,” Colin alisema kwa sauti ya juu. “Colin ukikataa najiua.” “Kajiue kwani ukifa mimi napungukiwa nini labda muuaji mwezio Hans.” Maneno yale yaliuchoma moyo wa Mage ambaye alikuwa na matumaini ya kuchukua nafasi ya Cecy ambaye aliamini kupona kwake ni asilimia ndogo sana na hata kipona hataweza kuwa sawa. Kutokana na maelezo ya kidaktari aliyemfuata baada ya Cecy kupelekwa India. Alimweleza kuwa kama atapona angeweza kuwa na tatizo la kusahau au kupoteza kumbukumbu ambacho huwa sawa na kichaa cha kipindi kama maji kupwa maji kujaa kuna wakati inakaa sawa kuna wakati inahama. Baada ya kuumizwa na maneno ya Colin yaliyomkatisha tamaa alitoka nje akilia kilio cha kwikwi kitu kilichomshtua mama Colin aliyekuwa amekaa sebuleni akisoma Biblia. “We, Mage unalia nini, Colin kazidiwa?” “Ha..ha..pana mama, Colin kanifukuza eti hataki kunioa.” “He! Kwa sababu gani?” “Hata sijui, yaani anasema yupo radhi kufunga ndoa na maiti ya Cecy kuliko kunioa mimi. Eti mama, siombi ila kwa bahati mbaya Cecy amekufa mwanamke wa kuolewa na Colin kuna mwingine zaidi yangu?” “Hakuna.” “Sasa kwa nini ananidhalilisha kwa maneno makali?” “Labda umemkuta leo hayupo vizuri.” “Mama naomba kama Cecy atakufa basi nafasi yake nipewe mimi kwa vile tunajuana vizuri, inawezekana kufungwa kwa Hans na hii ajali ilikuwa mpango wa Mungu kuirudisha harusi yetu iliyofungwa mbinguni.” “Mmh! Makubwa,” mama Colin aliguna maneno ya Mage. “Mama naomba ukazungumze na Colin, si ulisema anatakiwa kupelekwa hospitali kila asubuhi, kazi hiyo nitaifanya mimi hata kumpikia chakula kumfulia kipindi chote nitafanya nini. Nipo tayari kuhamia hapa kuhakikisha Colin hapati tatizo lolote.” “Basi tulia nitazungumza na Colin.” Mama Colin alikwenda chumbani kwa Colin ili ajue kimetokea nini mpaka apishane kauli na mpenzi wake wa zamani. Alimkuta Colin amejilaza macho kaangalia juu, mlango ulipofunguliwa aligeuza shingo kuangalia nani anayeingia alimkuta ni mama yake. “Vipi baba?” mama yake alimuuliza. “Safi tu,” alijibu akiwa bado ameangalia juu. “Upo sawa baba?” “Sipo sawa,” alijibu akiwa bado macho yake yakiangalia darini. “Kwa nini tena mwanangu?” “Nani kampa ruhusa huyu shetani kuingia ndani?” aliuliza huku akigeuka kumtazama mama yake. “Colin! Shetani nani?” “Mage, sitaki kumuona machoni mwangu,” alisema kwa sauti ya juu kidogo. “Kwa nini baba?” “Aliyonifanyia madogo, leo ni Mungu tu nipo hai lakini kifo changu angechangia yeye hata mateso ya mpenzi wangu chanzo ni yeye. Kaniumiza mara ya kwanza hajafurahi karudia mara ya pili kaniumiza na mpenzi wangu bado tu ananifuata anataka nini kama siyo uhai wangu?” “Lakini kwa nini unamhukumu bila kujua ujumbe alioandika umeandikwaje?” “Mama, ulikuwa mbaya, Cecy hawezi kulia kwa ujumbe wa kawaida.” “Colin bado hutakiwi kumhukumu kwa kitu usichojua, inawezekana ulikuwa wa kawaida lakini kwa vile mpenzi wako aliisha jenga chuki kwa Mage huenda hakufurahia ujumbe ule.” “Lakini mama hata kama, ni haki mtu kutuma ujumbe au kupiga simu akijua kabisa mimi ni mchumba wa mtu na tupo katika hatua gani?” “Hapo anaweza kuwa amefanya makosa lakini hakuna adui wa maisha, adui wa leo rafiki wa kesho, msamehe mwenzio nimemwacha analia kwa maneno yako makali.” “Mama nitamsamehe Mage labda Cecy apone asipopona sitamsamehe mpaka nakufa.” “Sikiliza mwanangu, ni wazi Mage anakupenda sana hujui tu, kama Mungu anapitisha uamuzi wake, Cecy anafariki Mage ndiye mwenye nafasi ya kuwa mkeo.” “Mama kwa nini unakimbilia kufa mpenzi wangu, nataka nikuambie kitu. Cecy akifanya nitafunga naye ndoa kabla ya kuzikwa.” “We’ Colin umerogwa yaani ufungwe ndoa na maiti ili iwe nini?” “Kutimiza ahadi niliyomuahidi Cecy ambayo ndiyo ndoto yake kubwa kwangu ya kuwa mke na mume. Mama Cecy nampenda lakini yeye ni mwalimu wangu wa mapenzi ndiye wakili wa moyo wangu kanipigania wakati wote kuonesha ana mapenzi ya kweli kwangu Cecy hanipendei kitu bali mimi kama mimi.” “Mmh! Na ukiisha muoa?” “Nitaendelea kuwa muaminifu katika ndoa yangu mpaka mauti yatakaponichukua.” “Kwa hiyo huoi tena?” “Mama ndoa ipo moja tu dunia ikiisha fungwa duniani mpaka mbinguni haitafunguliwa.” “Sasa kama amekufa si ndiyo mwisho wa ndoa yenu.” “Kwangu itakuwa mwanzo kwa vile sijaitumikia ndoa yetu.” “Colin mwanangu upo sawa?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Tena akili zangu zipo timamu.” “Hebu pumzika naona kama haupo sawa.” “Mama wala usisumbuke kufikiria unavyotaka kufikiria sina jibu zaidi hilo nililokupa.” “Kwa mfano Cecy atarudi hayupo sawa na ugonjwa wake hauponi au amepooza utafanya nini?” “Kama nitaweza kufunga ndoa na mwili wake usio na pumzi sitabadilika nitafunga ndoa na Cecy katika hali yoyote.” ”Mmh! Sawa.” Mama Colin alitoka bila kuongeza neno huku akijiuliza Mage kamfanya nini Colin mpaka kufikia uamuzi mzito kama ule. Lakini aliamini zile ni hasira za kumwona Mage lakini baadaye zitashuka na kuelewana. Aliamini kabisa ugonjwa wa Cecy si wa kupona na kama akipona hata kuwa sawa hivyo mwanamke aliyeona anamfaa mwanaye ni Mage kwa vile tayari waliisha kuwa wapenzi kabla ya hapo. Mage baada ya kutokeza mama Colin alikaa mkao wa kutaka kujua amezungumza nini na mwanaye. “Vipi mama, Colin kasemaje?” “Hii kazi niachie mimi, najua bado ana hasira zikipoa atanielewa tu.” “Yaani mama siamini maneno anataka kuoa maiti ya Cecy kwani wanawake wamekwisha? Hata kama hanitaki mimi lakini bado wapo wazuri na wenye tabia nzuri kuliko Cecy.” “Hilo lisikutie presha, nammudu kwa vile ni mwanangu na wala hataoa mwanamke mwingine zaidi yako. Ninyi mnafahamiana na vile mlikuwa mnapendana hivyo mtaendelea uliposimamia.” “Umeona eeh mama, yaani Colin namshangaa kweli.” “Sasa sikiliza kesho anatakiwa kupelekwa hospitali kwa mazoezi njoo asubuhi umpeleke.” “Mamaa! Kwa hali hii atakubali?” Mage aliishangaa kauli ya mama Colin. “Mage we njoo mimi nitajua nitafanya nini, nakuhakikishia lazima ataolewa na mwanangu.” “Mmh! Mama nitafurahi, bado naona kama nipo ndotoni.” “Wala si ndotoni, amini Colin wewe ndiye mkewe.” “Nashukuru sana mama, basi nikuache niwahi nyumbani.” “Hakuna tatizo msalimie mama yako.” “Salamu zimefika.” Mage aliagana na mama Colin na kurudi nyumbani kwao huku dua lake likiwa kwa Cecy asirudi hai ili aichukue nafasi ambayo aliamini ilikuwa yake hapo awali. Hakutaka kuyajutia maamuzi yake ya kuachana na Colin na kurudiana na Hans kwani kwake ulikuwa uamuzi sahihi ilitokea bahati mbaya ya kufungwa maisha. Moyoni mwake alikuwa tayari kumsubiri Hans hata miaka kumi ili waoane lakini kifungo cha maisha kilimvunja nguvu na kuamini mtu sahihi kwake alikuwa Colin. Aliapa kumpigania Colin kwa nguvu zote kumrudisha mikononi mwake hata kwa kutoa uhai wa mtu. Alipofika nyumbani kwao alimweleza mama yake kilichotokea na kumshtua sana. “Mmh! Yamekuwa hayo unafikiri utafanyaje naona kila kitu kimevurugika.” “Lakini mama Colin kasema kesho niende nikampeleke Colin hospitali.” “Utampeleka vipi ikiwa hataki hata kukuona?” “Mama yake kasema yeye anajua kila kitu kinachotakiwa kufanyika na ameniahidi lazima nitaolewa na mwanaye.” “Mmh! Sawa kwa vile kasema mama yake lakini maneno ya Colin yamenitisha kusema, eti yupo tayari kufunga ndoa na maiti ya Cecy kuliko kuoa mwanamke mwingine.” “Mama au akili ya Colin imepata tatizo baada ya kujigonga kwenye ajali?” “Inawezekana maana ajali haikuwa ya kawaida.” “Mmh! Inawezekana maana alivyonigeuka si kawaida yake, mama naamini Colin ananipenda.” “Au yule mtoto alimwendea Colin kwa Karumanzila?” “Inawezekana kabisa si bure ana urembo gani wa kumfanya Colin atake kufunga ndoa na maiti yake.” “Hata mimi naona, lazima nasi tuhangaike ili kuhakikisha nafasi hiyo unaipata wewe.” “Yaani huwezi kuamini sara zangu zote namuomba Ziraili amtokee Cecy na kummaliza kabisa tufikirie mambo mengine.” “Duh! Kweli wewe kiboko, wenzio dua zao wanaomba amani wewe shari.” “Siku zote adui yako muombee matatizo.” “Mmh! Haya.” MUMBAY INDIA Katika hospitali ya Apolo katika mji wa Mumbay nchini India madaktari waliendelea kuumiza kichwa kutokana na ugonjwa wa Cecy ambao uliwachanganya akili baada ya kuweza kufumbua macho lakini mwili bado haukuwa na mawasiliano kwa asilimia zote. Waliufanyia vipimo vyote na kukaa jopo la madaktari mabingwa kuchunguza Cecy ana tatizo gani lililopelekea kuwa katika hali ile. Hali iliyojitokeza ilikuwa tofauti na maelezo ya ajali yake, walijikuta wakifikia uamuzi wa kumrudisha Tanzania kwani waliamini hakutaka na mabadiliko yoyote kwa muda mfupi. Matumaini ya kupata nafuu yalikuwa asilimia ndogo sana kuliko kupoteza maisha. Uhai wake waliamini hautachukua muda mrefu kwa vile mawasiliano hayakuwepo zaidi ya mapigo ya moyo yalienda kawaida pia hata mapafu yalifanya kazi vizuri. Kilichowashangaza kuweza kupita kwa chakula laini na kufanyiwa kazi na kutoka kinyesi chepesi ambacho alisaidia bila habari. Mama yake alikuwa na kazi ya kumgeuza na kumsafisha anapojisaidia pia kumbadili ubavu ili kutoweka vidonda kwa kulalia upande mmoja kwa muda mrefu. Mama Cecy naye alikata tamaa ya mwanaye kupona kutokana na kutotokea mabadiliko yoyote makubwa zaidi ya kuweza kutazama na kula kitu kilichokuwa kikitia matumaini kidogo. Baada ya jopo la madaktari kukubaliana kumrudisha Tanzania, kwa kuamini kwa kuwa Tanzania ataweza kupata vitu viwili, moja kulikava taratibu akiwa nyumbani hivyo kupunguza gharama. Pili hata akifa wasipate gharama za kuusafirisha mwili wa marehemu. Walimwita mama Cecy kumpa taarifa zile walizokubaliana kuhusu mwanaye kurudishwa Tanzania. Baada ya kuingia kwenye ofisi ya madaktari bingwa alikaa kitini huku akiwa na mkalimani daktari aliyeongozana naye. “Mama Cecy, tumekuita hapa ili kukujulisha hatua tuliyofikia, inaonesha ugonjwa wa mwanao utachukua muda mrefu kupona. Hivyo tumeamua kumrudisha Tanzania ili uweze kumhudumia nyumbani pia kupata msaada wa matibabu ya kusaidia kuusisimua mwili.” “Mmh! Sasa itakuwaje ikiwa hospitali inayotegemewa mmeshindwa, mwanangu si ndiyo anakwenda kufa?” “Hapana si kufa bali huduma za muhimu tumejitahidi kadri ya uwezo wetu, hatuwezi kuendelea kumweka hospitali na kuongeza gharama wakati huduma zingine anaweza kuzipata akiwa hukohuko Tanzania. Sisi kazi yetu kubwa tumemaliza kilichobakia na kazi ya Mungu.” “Mmh! Sawa.” Mama Cecy alikubali kwa sauti ya kukata tamaa kwani siku zote watu waliokwenda India hurudi wamepona na ikishindikana basi mtu huyo huwa wa kumzika. Aliamini ile ilikuwa kauli ya kumpa moyo lakini siku za kuishi mwanaye zilikuwa zinahesabika. Iliandaliwa mipango yote ikiwa pamoja na tiketi ya kurudi Tanzania na kupangiwa siku ya kurudi. Habari zile zilikuwa pigo mujarabu moyoni kwa mama Cecy mwanaye mmoja kama mboni ya jicho lake alimuona akitoweka katika sura ya dunia. Lakini yote alimuachi Mungu kwa vile muweza wa kila kitu. Taarifa za kurudishwa Tanzania Cecy baada ya ugonjwa wake kuonekana utachukua muda mrefu kupata nafuu. Zilimfikia mama Colin na kuamini ile ndiyo nafasi ya pekee kwa Mage kuichukua nafasi ile baada ya kupata uhakika hali ile inaweza kuchukua muda mrefu kupata nafuu au maisha yake yote yawe ya kitandani alijua ilikuwa kuwapa moyo lakini Cecy alikuwa maiti mtalajiwa. Kwa taarifa ile aliamini mwanaye pamoja na msimamo lazima atabadilika na kukubali kumuoa Mage huku akijitolea kumsaidia Cecy kwa kumwekea mtu wa kumhudumia na kumlipa kwa maisha yake yote ili tu kumfurahisha mwanaye. Alitamani siku moja aitwe bibi na hakuwa na mtoto mwingine zaidi ya Colin ambaye ndiye aliyemtegemea kumleta mjukuu. Ugonjwa wa Cecy ulionesha hakukuwa na dalili zozote kuweza kubeba ujauzito na yeye kupata mjukuu. Moyoni alijikuta akipata mawazo mabaya ya kumuua Cecy kama mwanaye atasimamia msimamo wake wa kutotaka kuoa mwanamke mwingine. Lakini kuna kitu kilimtisha baada ya kukumbuka kauli ya mwanaye kufunga ndoa hata na maiti ya Cecy. Hiyo ilimpa wakati mgumu. Lakini alipanga kumtumia Mage kuyabadili mawazo yake na kukubali kumuoa. Siku ya pili Mage alifika kama alivyoelekezwa na mama Colin lakini hakutakiwa kuonana na Colin mpaka mpango wake autekeleze. Baada ya Mage kufika alifikia chumba cha msichana wa kazi na mama Colin alikwenda chumbani kwa Colin kumwamsha ili ajiandae kwenda hospitali. “Jiandae basi ukafanye mazoezi.” “Sawa mama.” Colin aliingia bafuni kuoga baada ya kuoga alibadili nguo na kutoka chumbani kwake na kwenda kukaa sebuleni kumsubiri mama yake ili waende kwenye mazoezi ya viungo (Physiotherapy). Mama Colin alitoka chumbani kwake akiwa tayari kwa safari begi lake begani. Colin alipomuona mama yake alinyanyuka ili waondoke. Lakini ghafla alishtuka kumwona mama yake akiweka mkono kichwani katika paji la uso huku amekunja uso. “Nini mama?” Colin alishtuka. “Kichwa,” mama alisema kwa sauti ya kujilazimisha. “Mungu wangu! Kimefanya nini tena mama yangu?” Colin alishtuka na kujitahidi kumfuata mama yake ili amshike. “Hapana baba , niache nitakaa mwenyewe,” mama Colin alisema huku akisogea kwenye kochi na kukaa. “Nipe maji,” alisema akiwa ameinama mkono kichwani. Colin alipotaka kwenda kumchukulia maji alimkataza na kutaka amwambie msichana wa kazi. Baada ya kuitwa alileta maji kwenye glasi na kumpa mama Colin aliyeyanywa yote na kupumua pumzi nyingi kisha alisema. “Duh! Afadhali kidogo.” “Sasa itakuwaje maana kwa hali hiyo huwezi kuendesha gari?” “Na kweli siwezi kuendesha gari, nimekumbuka Mage alisema atakuja kukuona asubuhi.” “Mage gani?” “Si aliyekuwa mchumba wako.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Mama niseme mara ngapi kuwa sitaki kumuona yule shetani wa kike,” Colin alisema kwa hasira kidogo. “Mwanangu wewe ndiye uliyekuwa ukinieleza siku zote nisikae na jambo baya moyoni muda mrefu naweza kupata matatizo. Kwa nini unamchukia hivyo Mage? Hata kama alifanya kosa lililosababisha ajali bado alitakiwa kusamehewa. Humtaki kuwa mpenzi wako lakini bado ni mwanadamu anayetakiwa kusamehewa na kumwona rafiki, hujui adui wa leo ni rafiki wa kesho.” “Ni kweli mama, najitahidi kumsamehe lakini moyo wangu umekuwa mzito.” “Huyo ni pepo mchafu tunatakiwa kumkemea.” “Sawa mama nitajitahidi.” “Kwa vile siwezi kuendesha gari leo basi naomba Mage atatupeleka hospitali.” “Sawa mama,” Colin hakutaka kukataa kwani angemuudhi mama yake. “Ngoja nimpigie simu.” Mama Colin alijifanya kipiga simu na kujizungumzisha peke yake: “Eeh! Umekaribia... tena umefanya vizuri... wahi basi utupeleke hospitali...haya tunakusubiri... Umekaribia... sawa... hakuna tatizo tupo tayari,” mama Colin alijifanya kukata simu. “Kwani kafika wapi?” Colin aliuliza. “Yupo nje ya geti.” “Sawa.” Mama Colin alijifanya kuelekea upande wa vyumbani na kwenda chumba cha msichana wa kazi na kwenda kuzungumza Mage. “Mambo yamekwenda vizuri japokuwa imenibidi nilazimishe kwa cheo cha umama, sasa pitia mlango wa nyuma kisha ingilia mlango wa mbele kujifanya ndiyo unaingia.” “Sawa mama.” Mage alitokea mlango wa nyuma na kwenda kulichua gari alilokuwa amelipaki nje na kuingia nalo. Aliteremka kwenye gari na kuingia ndani. “Karibu mama.” “Asante, za hapa?” “Nzuri.” Mage alisogea kwa Colin na kumsalimia: “Umeamkaje?” “Namshukuru Mungu.” “Nina imani hali yako itatengemaa muda si mrefu ili urudi katika majukumu yako, sara zangu zote hukutanguliza mbele nina imani Mungu ataipokea.” “Amina.” “Mage tunaweza kwenda.” Mage alimshika mkono Colin na kunyanyua, alitoka naye hadi nje na kuingia kwenye gari la Mage ambalo aliomba walitumie kwa siku ile. Colin muda wote alikuwa kimya hakutaka kutia neno kwa kuhofia kumuudhi mama yake ambaye muda huo aliamini kabisa hali yake siyo nzuri hakutaka kuharibu kote kwani bado hali ya mpenzi wake Cecy ilibakia kitandawili. Walikwenda mpaka kwenye kitengo cha mazoezi ya viungo (Physiotherapy), walipofika mama Colin alikaa pembeni na Mage alimsaidia Colin kufanya mazoezi kwa kumshikilia sehemu zingine ambazo alihitaji msaada. Kila dakika Mage alikuwa akitokwa na machozi kitu kilichomshtua Colin. “Mage unalia nini?” “Sijui moyoni mwako una hasira kiasi gani juu yangu.” “Sina hasira yoyote.” “Hapana Colin una kitu kizito juu yangu kutokana na yaliyotokea, ile ni mipango ya Mungu tu, naomba Colin unisamehe najutia kilichotokea ni mapenzi ndiyo yaliyonisukuma kufanya vile. Hata kama hutaki kuwa na mimi naomba unione rafiki na si adui.” “Mage ningekuwa sijakusamehe tusingekuwa karibu hivi na kuweza kukusikiliza.” “Nashukuru Colin kwa kunisamehe, naamini wewe ni mume mwema hakika Cecy kapata lulu kwenye chaza.” “Nashukuru.” “Vipi hali ya Cecy?” “Kwa kweli mpaka sasa sijajua, mama amekuwa akinificha japo walinieleza inaendelea vizuri.” “Mungu atamsaidi siku moja atasimama na kufanikisha mlichokipanga,” Mage alimpa moyo kinafiki. “Amina.” “Colin.” “Naam.” “Baada ya Cecy moyoni mwako yupo nani?” “Bado sijamuona labda mwenetu atakaye zaliwa.” “Basi naomba baada ya mwenenu nafasi inayofuata nipe mimi, naomba usiniweke mbali na mawazo yako.” “Hakuna tatizo.” “Naomba niwasiliane na wewe wakati Cecy yupo mbali.” “Mage, suala la mawasiliano naomba tuliweke pembeni kwanza.” “Kwa nini Colin, kukujulia hali tu.” “Ukitaka kuwasiliana na mimi tumia simu ya mama lakini kwa sasa sitatumia simu kwa vile ndiyo iliyoleta yote haya.” “Colin basi hujanisamehe.” “Kukusamehe si kunilazimisha kufanya vitu nisivyo vitaka, nimekueleza sitaki kutumia simu unanilazimisha kwa kisingizio cha kutokusame. Kumbuka ubishi huo ndiyo uliosababisha yote haya.” “Nimekuelewa Colin, nisamehe sana, nitajitahidi kukuelewa ili tusije kosana tena.” “Itakuwa vizuri.” “Colin nashukuru kunisamehe moyo wangu sasa mwepesi nilikuwa kama nimebeba mawe.” “Kawaida katika maisha kuna kukosana na kupatana.” “Nashukuru sana.” Mama Colin aliyekuwa mbali kidogo mazungumzo yale yalimtia moyo na kuamini mpango wake umeweza kufanikiwa kwa kuamini Mage ndiye chaguo lake la awali kabla Cecy kuingilia penzi lile. Taarifa ya kurudishwa Cecy kutoka India hakutaka kumweleza haraka mwanaye mpaka akapotua nchini kwani kwa taarifa siku inayofuata ndiyo aliyokuwa akiwasilia nchini. Alipanga kuonesha ushirikiano mkubwa lakini alibakia na siri yake juu ya Cecy na ugonjwa wake ambao kama ulishindikana India basi Tanzania ilikuwa ni kusubiri kifo. Kumweka Mage karibu na Colin kungemsaidia kumweka karibu kimapenzi hata akifa Cecy basi Mage achukue nafasi ile. Baada ya mazoezi walirudi nyumbani huku kila mmoja akiwa na furaha moyoni mwake japokuwa furaha ya Colin ilikuwa usoni na mdomoni lakini moyoni bado halikosa raha kushindwa kupata mawasiliano ya kujua hali ya mpenzi wake Cecy. Lakini aliamini baada ya muda hali yake itatengemaa na yeye mwenyewe kwenda India kumuona Cecy. Siku ile Mage alishinda pale na kufanya kila kitu kwa ajili ya Colin, kuanzia usafi wa chumba chakula cha mchana vyote alifanya yeye na muda mwingi alikuwa karibu yake ili kuhakikisha anairudisha nafasi iliyoipoteza kupitia matatizo ya Cecy. Kitu kile kilimfurahisha sana mama Colin na kuuona mpango wake taratibu utafanikiwa. Siku ile taarifa ilifika kwa Cecy anawasili toka India, mama Colin hakutaka kumwambia mwanaye ila saa sita usiku alikwenda kuwapokea pekle yake. Baada ya ndege tukutua abiria waliteremka na kutoka nje. Alisimama macho yakiwa ndani huku akijiuliza Cecy atarudi katika hali gani, akiwa mapokezi alikiona kitanda kikisukumwa nyuma yake alikuwepo daktari aliyeondoka naye na nyuma ya daktari alikuwepo mama Cecy ambaye alionekana amepururuka mwili kutokana na matatizo ya mwanaye. Mama Colin alijitokeza kuwapokea kwa kumkumbatia mama Cecy. “Jamani dada karibuni, poleni na safari.” “Mungu ni mwema.” “Karibuni,” alikwenda kitandani kumwangalia Cecy ambaye muda huo alikuwa amepitiwa usingizi. “Vipi anaendeleaje?” “Tutazungumza nyumbani, vipi Colin naye anaendeleaje?” “Kweli Mungu ni mwema anaendelea vizuri.” Kwa vile alikuwa amekuja na gari aina ya Toyota Noah aliyeelezwa ndiyo inayotakiwa kumpokelea mgonjwa, walimweka kwenye gari na kuelekea nyumbani kwa mama Cecy ambako siku ile kulifanyika usafi na kuiweka nyumba katika hali nzuri. Hivyo walikuta nyumba ipo vizuri pamoja na msichana wa kazi aliyeachwa kwa ajili ya kuangali nyumba kwa muda wote ambao hakuwepo. Baada ya kufikishwa nyumbani aliingizwa chumbani na kulazwa kitandani, muda wote mama Colin alimfuatilia Cecy na kuonesha hakuwa na dalili zozote za kupona. Pamoja na huruma kumjia lakini bado aliamini kama Cecy atakufa basi Mage ndiye mbadala wake. Baada ya kumlaza kitandani daktari aliyekwenda na Cecy India alikaa na wazazi wawili na kuwaeleza: “Jamani nina imani maelezo tulipewa India unayakumbuka, lakini kwa kuongezea ninataka kuwaeleza, mgonjwa hali yake bado japo kuna mabadiliko makubwa sana tofauti na alivyokwenda. Ugonjwa wa Cecy umekuwa tofauti na ugonjwa mwingine ambao madaktari bingwa wamekutana nayo huu kidogo umewala akili.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Inaonekana mwili wa Cecy anajenga mawasiliano taratibu sana inaweza chukua muda mrefu sana kunyanyuka kitandani. Hivyo anatakiwa uangalizi wa karibu sana, kama kuna uwezekano aajiliwe mtu kwa kazi hii ili kumpumzisha mama yangu hapa kwani namhurumia amefanya kazi kubwa usiku na mchana kwa ajili ya kumwangalia mwanaye japo nilimsaidia bado muda wote alikuwa halali. “Mgonjwa ataendelea kupata huduma ya kuchuliwa kila siku mwili mzima ili kusisimua misuli ya mwili. Nina imani kwa uwezo wa Mungu anaweza kupata nafuu upesi kwa vile mwisho wa akili ya mwanadamu ndipo uwezo wa Mungu huchukua nafasi yake,” dakta Mariamu Shaka aliwapa moyo kwa maneno ya hekima. “Nina imani mpaka leo yupo hivi lazima turudishe shukrani zangu kwa Mungu wetu,”mama Colin alisema. “Kingine mama, huoni maajabu pamoja na mwili kukosa mawasiliano lakini vitu vyote vya ndani vinafanya kazi hata kuweza kula japo chakula laini kitu ambacho kimewashangaza hata madaktari bingwa.” “Ni kweli tuna kila sababu ya kumshukuru alichotupa si haba, kama leo katupa kidogo na kurudisha shukurani kwake basi hatasita kutupa kikubwa nina imani mwanangu siku moja atasimama,” alisema mama Cecy kwa hisia kali. “Amina, Mungu wetu ni msikivu,” alijibu dokta Mariamu. Kwa vile muda ulikuwa umekwenda mama Colin aliaga kurudi nyumbani na kumwacha mama Cecy mgonjwa na daktari ambaye alilala pale ili kesho yake baada ya kumpatia mgonjwa huduma arudi nyumbani kwake. Kutokana na hali aliyomuona nayo Cecy hakutaka kumweleza mwanaye kwa kujua atamshtua hata kukosa raha na kumuongezea matatizo kwa vile alimpenda sana mchumba wake. Lakini alijiuliza mwanaye akijua lazima atamweleza vibaya, alipanga kumwambia baadaye kuwa Cecy amerudi. Aliamua kukaa kimya huku wiki ilikatika bila kumweleza kitu chochote mwanaye juu ya Cecy kurudi toka India. Siku zote alitoka peke yake kwenda kumwona Cecy na kuonesha kugushwa na hali ile huku akimlipa daktari aliyekwenda naye India pesa nyingi ili kumpatia huduma ya kumchua na kumwangalia kila siku baada ya kazi. Wema wake ulikuwa wa mamba wa kutoka machozi lakini alikuwa na siri moyoni mwake kujionesha anamjali mgonjwa. Lakini aliamini kupona kwa Cecy ni ndoto, kila alipoulizwa na mama Cecy kuhusu hali ya Colin alisema hajambo kiasi. “Hawezi kutembea?” “Mmh! Kwa sasa amekatazwa kutembea.” “Kwa nini basi usimlete aje amwone mchumba wake?” “Atakuja hali yake ikitulia.” “Kwa hiyo hali yake inaonekana bado.” “Ni kweli.” “Mmh! Mpe pole isingekuwa hali ya Cecy ningekuja kumwona mkwe wangu.” “Mungu atawapa afya na kuweza kunyanyuka.” “Mungu atasikia dua zetu, kila jambo la heri Mungu ulishika mkono nina imani Cecy na Colin watasimama na siku moja kusherehekea harusi yao.” “Amen,” mama Colin aliitikia huku moyoni akijisemea “Labda harusi aliyosema mwanaye ya kufunga ndoa na maiti ya Cecy, lakini harusi ya sherehe ukumbuni itakuwa muujiza.” Mama Cecy aliamini hali ya Colin ni mbaya ila mama yake anampa moyo, alipanga siku akipata nafasi afike kumwona kwani haikuwa vizuri mzazi mwenzie kuja kumuona mwanaye na yeye kutokwenda kumuona Colin. Kwa vile hali ya mwanaye alijua alipanga siku moja baada ya kumpatia chakula akilala atoke mara moja kwenda kumwona Colin na kuwahi kurudi. Siku ya tatu ambayo mama Colin alipiga simu kuwa hatakwenda kwa vile kuna sehemu ambapo angerudi usiku. Siku hiyo mama Cecy aliitumia kumwandaa Cecy ambaye alishangaa kuona mabadiliko madogo baadhi ya sehemu kupata joto kama miguuni ambako kulikuwa na ubalidi kwa muda mrefu. Baada ya kumpatia chakula chepesi na dawa alimwacha apumzike na yeye kukodi gari mpaka kwa mama Colin kumjulia hali mgonjwa. Wakati huo Mage alikuwa akiendelea kuwa karibu na Colin ili kujivuta karibu kwa kuamini baada ya kifo cha Cecy basi nafasi ile ni yake. “Colin nina imani sasa hivi afya yako ni nzuri unaweza hata kuendesha gari.” “Namshukuru Mungu, pia nashukuru kwa msaada wako kwangu kwa muda wote wa kuniangalia.” ”Usijali nipo kwa ajili yako, nitapigania afya yako hata kwa gharama yoyote.” “Usiwe na wasi nina imani sasa hivi sijambo na wiki ijayo nitakwenda India kumwangalia Cecy.” “Lakini hali yako si bado kwa nini usisubiri upone kabisa.” “Mage, mimi sijambo sasa hivi naweza kufanya lolote, lakini afya ya mpenzi wangu siijui. Mpaka leo bado yupo hospitali huenda yupo kwenye hali mbaya lazima niende nikajue hali yake.” “Mmh! Sawa,” Mage aliogopa kutia neno kwa kuhofia kukorofishana na Colin ambaye alionekana bado ana mapenzi mazito na Cecy. Alijua msimamo wake ni kwa vile hajamwona lakini akimwona hali yake aliamini lazima angebadili mawazo na nafasi ile kumpa yeye. Wakiwa katika ya mazungumzo walishtuliwa na hodi, waliponyanyua macho Colin hakuamini kumwona mama Cecy aliyejua yupo India na mpenzi wake, lakini afya yake ilioneka imedhoofu sana. “Ha! Mama ni wewe?” Colin alisema huku akinyanyuka na kwenda kumpokea mama mkwe. “Ni mimi mwanangu, unaendeleaje na wewe?” “Namshukuru Mungu, hali yangu sijambo. Sasa hivi nilikuwa nasema wiki ijayo nakuja India kumwona mchumba wangu. Ha..ha..lafu mbona uko huku Cecy umemwacha na nani hospitali?” “Kwani mama yako hajakwambia?” “Kuhusu nini?” “Kurudi kwetu, nimemuulizia ameniambia hali yako bado si nzuri, hivyo nikaona nije nikujulie hali baba yangu na kumwacha mchumba wako na msichana wa kazi.” “Mama unataka kuniambia Cecy yupo Tanzania?” Colin alishtuka huku macho yamemtoka pima. “Colin unauliza ukweli au unatania?” “Mama mimi na wewe hutujawahi kutaniana, hata muulize Mage muda si mrefu nilikuwa namwambia lazima nije India kumjulia mchumba wangu hali yake baada ya mimi kuamini nimepona.” “Siamini unachokisema najua unaumwa hivyo hukuwa na uwezo wa kuja kumpokea mchumba wako, lakini sikubali kauli yako kuwa huna taarifa yoyote kuwa mimi na Cecy tupo nchini kwa wiki sasa.” “Wiki!?” Colin alishtuka. “Colin hebu acha kujitoa akili, ina maana mama yako hajakwambia?” “Hajaniambia, ina maana mama anajua?” “Mbona ndiye aliyetupokea na kila siku lazima afike kumuona mgonjwa kasoro leo.” “Mmh! Una maanisha mama yangu, mama Colin?” “Ndiye huyohuyo, ina maana hajakwambia?” “Haki ya Mungu sijui kitu, sikuwa ugonjwa wa kushindwa kuja kumpokea mpenzi wangu, kwa nini mama kanificha hivi, Cecy mpenzi wangu atanielewa vipi?” Colin alisema kwa uchungu. “Sijui, labda muda wake wa kukueleza bado, lakini namshukuru sana amejitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha afya ya mpenzi wako inatengemaa.” “Vipi hali ya mpenzi wangu?” “Bado, lakini ana afadhali kwa mbali sana.” Colin alinyanyuka na kumwomba mama Cecy aende akamwone mpenzi wake. “Mama naomba nikamwone mpenzi wangu.” “Colin pumzika kwanza hujapona vizuri, nilikuja kukuona tu.” “Hapana...kama Cecy ana wiki hapa mama kanitendea unyama mkubwa sana,” Colin alisema huku akionekana kuchanganywa na taarifa zile ambazo hakutegemea kusikia kwa kuamini Cecy bado yupo India. Colin hakusema kitu alikwenda ndani na kuchukua ufunguo wa gari na kutoka. “Mama naomba twende,” Colin alipagawa na kusahau muda mfupi alikuwa na Mage alitoka bila hata kumuaga na kumfanya Mage aumie moyoni kuona ana kazi kubwa ya kuubadili moyo wa Colin. Lakini aliamini kifo cha Cecy ndiyo tiketi yake ya kuwa na Colin, aliendeleza dua za kuomba kifo cha Cecy. Colin japo alikuwa hajaruhusiwa kuendesha gari alikwenda kuchukua gari na kumwomba mama Cecy waondoke. Waliongozana hadi kwenye gari na kuondoka kuelekea kwa Cecy. Wakiwa ndani ya gari Colin alimdodosa mama Cecy. “Mama kwanza vipi hali ya mchumba wangu?” “Hajambo, lakini bado.” “Bado nini kinamsubua?” “Siwezi kukueleza kwa vile unakwenda mwenyewe kila kitu utakiona.” “Mmh! Sawa.” Colin aliendesha gari huku akiwa na mawazo mengi juu ya mama yake kukaa kimya huku kila siku anakwenda kumwona mgonjwa bila kumwambia aljiuliza alikuwa na maana gani na mchumba wake angemwelewa vipi kama amerudi bila kwenda kumwona. Walipofika walikwenda hadi ndani, Colin alionekana mwenye kimuhemuhe cha kumwona mpenzi wake. Kwa vile alikuwa akikijua chumba cha Cecy aliingia moja kwa moja. Lakini chumbani kwake hakuwemo alitoka na kukutana na mama Cecy. “Mama mpenzi wangu yupo wapi?” Colin aliuliza macho yamemtoka pima na presha juu.“Colin taratibu umefika utamuona, subiri,” mama Colin alisema huku akielekea chumba alicholazwa Cecy. Alipakaribia alipogusa mlango alishtuka kusikia Cecy akimwita sauti ambayo ilipotea toka alipopata ajali iliyokuwa ikimwita. “Ma..a..ma...ma..a..ma.” Alisogea haraka kitandani na kuitikia. “Abee mwanangu.” “Nigeuze nimechoka kulala hivi?” Mama Cecy aliona ule ni muujiza mkubwa kwake kwa vile siku zote mgonjwa alikuwa wa kulala bila kujitikisa wala kusema neno zaidi ya kutumbua macho tu bila kuyapepesa. Alimgeuza na kumlaza vizuri. “Niwekee mto chini.” Mama yake haraka alichukua mtu na kumwekea mwanaye. “Mama ulikuwa wapi?” “Nilikuwepo nje.” “Mbona dada alisema ulitoka?” “Nilifika dukani.” “Mume wangu Colin yupo wapi?” “Yupo sebuleni.” “Ana fanya nini?” “Ndiyo amefika sasa hivi.” “Alikuwa wapi?” “Kwao.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Cecy kusikia Colin yupo sebuleni alitaka kunyanyuka na kuishia kukaa kitako na kurudi tena chini. Kitendo cha kujinyanyua peke yake yalikuwa maajabu mengine kwa mama Cecy ambaye alipiga ishara ya msalaba na kumsukuru Mungu kwa kile alichokionesha muda ule mbele yake. “Asante Mungu... Asante baba... Asante kwa kila akifanyacho mbele ya macho yangu.” “Mama,” Cecy alimwita mama yake. “Abee.” “Naomba niende kwa Colin.” “Subiri.” Mama Colin alitoka hadi sebuleni ambapo Colin alikuwa akizungumza na dada wa kazi juu ya hali ya Cecy. Alimdodosa na kuelezwa yote toka akipofika na hali aliyokuwa nayo na maajabu ya siku ile alipokuwa akimtengeneza kitandani na kushtuka kumsikilia akiiita jina la Colini na baadaye aliita mama yake. Dada wa kazi alimweleza ametoka, ndipo alipoanza kumuuliza maswali ambayo alimjibu kwa vile mambo mengi alikuwa akiyaelewa. Baada ya mazungumzo na dakika ishirini Cecy aliomba kugeuzwa tofauti na siku za nyuma alikuwa wa kulala tu na kugeuzwa kwa kipindi. “Kwa hiyo toka apate ajali ndiyo kazungumza leo?” “Ndiyo najua hata mama ataona muujiza.” “Mmh!” Colin aliguna na kujiuliza nini hatima ya mpenzi wake ikiwa sehemu inayotegemewa na watu wote imeshindwa. Ile kwake ilikuwa picha mbaya sana kwake na kukiona kifo cha Cecy kipo mbele. Aliamini yote aliyasababisha yeye alijikuta akitokwa na machozi ya uchungu. “Colin baba,” Colin alishtuliwa na mama Cecy. “Naam mama,” Colin aliitikia huku akinyanyua kichwa. “Ha! Unalia nini tena?” mama Cecy alishtushwa na machozi ya Colin. “Inauma.” “Cecy anakuita.” Colin bila kujibu alinyanyuka na kuelekea chumbani ambako alimkuta Cecy amelala kitandani mwili ukiwa umepururuka kwa ugonjwa. “Cecy,” aliita kwa sauti huku akisogea kitandani na kumkumbatia mpenzi wake. “Colin mume wangu,” Cecy alisema huku akijitahidi kumkumbatia mpenzi wake. Ilikuwa ajabu nyingine Cecy kuweza kumkumbatia Colin kwa mwili uliobakia mifupa mitupu. “Ni mimi Cecy mke wa maisha yangu.” “Colin nifurahi kukuona mpenzi wangu japokuwa nina muda mrefu nilikuwa siwezi kuzungumza wala kujigeuza. Lakini kuja kwako kumekuwa dawa ya kupona kwangu. Hata nikifa sasa hivi moyo wangu utakuwa na furaha kwa vile nimekuona chakula cha nafsi yangu,” Cecy alisema kwa sauti ya chini. “Ni kweli naamini Mungu alituumba kwa ajili yetu, siamini niliyoyasikia na niliyo kutana nayo leo,” Colin bado alikuwa kama yupo ndotoni. “Ni Mungu tu mpenzi wangu.” Siku ile Colin alishinda pale mpaka jioni pembeni ya Cecy, pamoja na yeye hali yake kuwa katika uangalizi lakini hali aliyomkuta nayo mpenzi wake aliamini amepona kabisa. Jioni daktari aliyempeleka India alipopitia kuangalia hali mgonjwa wake alishikwa na mshangao baada ya kukuta hali ya Cecy ina mabadiko makubwa. “Mungu mkubwa siamini ninachokiona leo,” mama Cecy alisema huku akifuta machozi kwa kiganja cha mkono. “Ni kweli Mungu katenda muujiza wake,”Colin alisema huku naye akifuta machozi. “Jamani msinililie tena, kama nilikuwa nusu mfu kwa muda mrefu na leo nipo hivi, basi aminini nimepona,” Cecy alisema kwa kujiamini. Siku ile kazi ya masaji aliifanya Colin huku akimpa moyo mpenzi wake kuwa atapona. “Kweli nitaweza kutembea? Maana kwa hali ya kulala kitandani kama nyoka nimechoka.” “Utapona tena na kusimama, nakuahidi baada ya kupona nakufanyia bonge la surprise.” “Colin nawe kwa kunipa moyo, je nisipopona?” “Ugonjwa utakuwa wetu sote.” “Hutafuti mwanamke mwingine?” “Cecy baada ya kukufungia moyoini mwangu ufunguo niliutupia baharini, mimi ni kipofu mbele yako. Wewe ndiye uliyekuwa mwanamke wa mwisho kuonwa na macho yangu. Siamini kama nitapenda tena katika maisha yangu kama tutatengana. “Nakupenda Cecy zaidi ya kupenda. Amini usiamini muda si mrefu utasimama na kutimiza ndoto yetu ya kuwa mke na mume.” “Colin sikuwahi kumwamini mtu katika maisha yangu lakini wewe kwangu sina la kuongeza nakuamini mpenzi wangu. Mungu ana maajabu yake amani kila litendekalo lina makusudio yake.” “Cecy Mungu waajabu wewe ni yule wa jana leo na kesho, Mungu alikupa azina ya busara na hekima ni mtaji mkubwa katika maisha yetu.” “Asante kwa kulitambua hilo.” Pamoja na Cecy kuwa mgonjwa aliweza kuzungumza mengi mpenzi wake mpaka ulipofika muda wa kumwacha apumzike. Colin hakutoka alilala pembeni ya mpenzi wake. Daktari Mariam alishangazwa na hali aliyomkuta nayo Cecy ulikuwa muujiza mkubwa maishani mwake. “Kweli Mungu mkubwa hutenda pasipo mtu kutegemea, siamini... siamini kuna kila sababu ya kumshukuru Mungu wetu,” dokta Mariam Shaka alichanganyiwa na hali aliyomkuta nayo Cecy. Dokta Mariam alisema baada ya kumwona Cecy akijigeuza kitandani na kumwita mpenzi wake. “Colin.” “Naam mpenzi.” “Nataka kwenda msalani.” Colin alimnyanyua na kumkalisha kisha aliomba chombo cha kujisaidia na kupewa, kazi yote ya kumhudumia mpenzi wake alifanya mwenyewe. Baada ya kumwogesha alimrudisha kitandani. Baada ya huduma zote dokta Mariam alimchunguza ilionesha kila kiungo kimepata ufahamu. Kila alipomminywa kwa nguvu alipiga kelele, ile ilikuwa dalili nzuri kuonesha mwili mzima umeisharudisha mawasiliano. Baada ya kufanyiwa uchunguzi alikalishwa kitako na kuelezwa aliyekuwepo mbele yake ni dokta Mariam Shaka dokta aliyekwenda naye India kwa siku zote alizokuwa naye huko katika kukuchua mwili. “Asante dada yangu Mungu atakulipa,” Cecy alisema huku machozi yakimtoka. “Usijali, Mungu mkubwa naamini muda si mrefu utasimama tena, hatua ya leo ni kubwa kweli kila lililo zito kwa mwanadamu kwa Mungu ni jepesi.” “Hakika,” alisema mama Cecy. Colin alikuwa karibu muda wote kuonesha jinsi gani anavyomjali mpenzi wake ambaye aliamini ni mwanamke wa maisha yake. Siku hiyo kila kitu Colin aliomba amfanyie mpenzi wake. Ilikuwa faraja kubwa kwa Cecy ambaye pamoja na kuwa bado mgonjwa lakini ukaribu wa kipenzi chake uliongeza faraja moyoni mwake. *** Upande wa pili baada ya Colin kuondoka na mama Cecy, Mage hakuondoka alibakia kumsubiri Colin kwa kuamini kutokana na maelezo ya mama yake Cecy alikuwa nusu mfu mtu wa kulala tu. Hivyo asingekaa muda mrefu angerudi mapema na kumkuta, alitumia muda mwingi kuangalia mikanda ya video. Mama Colin alirudi saa mbili kasoro usiku na kumkuta Mage peke yake amejaa tele sebuleni. Mage alipomwona mama mkwe zilipendwa alinyanyuka na kumpokea. “Wawooo, karibu mama.” “Asante mwangu, za kushinda?” “Mmh! Nzuri.” “Mbona kwanza umeguna kabla ya kujibu.” “Hamna mama.” “Mwenzio yupo wapi?” “Ametoka.” “Ametoka! Kaenda wapi?” “Kumwona mgonjwa.” “Mgonjwa! Mgongwa gani?” “Cecy.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Cecy! Nani kamwambia kama Cecy yupo?” mama Colin alishtuka kusikia habari zile. ITAENDELEA  

0 comments:

Post a Comment

Blog