Simulizi : Wakili Wa Moyo
Sehemu Ya Tatu (3)
“Sawa mama msalimie Colin, naendelea kumuombea naye apate mke mwenye mapenzi naye ya kweli.” “Amen.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Mama Colin alimwita mama Mage amuage, baada ya kuja alimweleza: “Dada nikukimbie.” “Jamani, mbona haraka mmeelewana na mwanao?” “Tumeelewana na nimemuelewa vizuri sana.” “Basi nikutoe.” Waliongozana kutoka nje walipofika nje mama Mage alitaka kujua kama mwanaye amebadili uamuzi. “Vipi amesemaje?” “Amesimamia msimamo wake, nami naheshimu alichokisema kwa vile amekuwa mkweli. Japo inauma lakini ndiyo ukweli wenyewe.” “Bado hatujakata tamaa nitazungumza naye.” “Muache tu, kwa aliyo zungumza hata kwa mtutu wa bunduki habadili uamuzi wake.” “Mmh! Sawa, lakini Mage ni mtoto bado nina nafasi kama mzazi,” mama Mage alisema kwa sauti ya kukata tamaa. Waliagana na mama Colini aliingia kwenye gari lake kurudi kwake akipata uhakika wa ndoa ya mwanaye kuvunjika. *** Siku ya pili Mage alimuamsha mama yake aliyekuwa bado amelala, baada ya kuamka alimuaga. “Mama nasafiri kidogo.” “Unakwenda wapi?” “South.” “Una maanisha Afrika ya kusini?” “Ndiyo mama.” “Na nani?” “Na mchumba wangu.” “Nani, Colin?’ “Hapana mama, ya Colin yameishafutika moyoni mwangu itabaki kama historia.” “Unakwenda na Hans?” “Mama kuna mwingine? huyo ndiye aliyeshikilia maisha yangu.” “Mmh! Sawa.” “Bai mama,” Mage alimsogelea mama yake na kumbusu shavuni. “Mage mwanangu ndiyo umeamua kunivua nguo mbele za watu?” mama yake bado hakuamini. “Mama nakuahidi nikitoka South barua ya posa inakuja na ndoa itakuwa ya haraka sana. Najua utasahau yote.” “Mage mwanangu unamuamini vipi Hans mwanaume alikuacha katika wakati mbaya?” “Lile lilikuwa shinikizo la wazazi wake si uamuzi wake najua kabisa Hans ananipenda sana hata mimi kama ningeolewa na Colin lilikuwa shinikizo letu.” “Mage mwanangu nani alikulazimisha, si ulikubali kwa hiyari yako?” “Nilikubali ili kufunika kombe mwanaharamu apite.” “Mmh! Sawa, safari njema,” mama alisema kwa sauti ya unyonge ambayo haikumshitua Mage. Mage alitoka hadi nje na kuchukua gari la nyumbani ambalo alikwenda kuliacha uwanja wa ndege. Aliungana na mpenzi wake kwenda Afrika ya kusini kupumzika kwa wiki moja kabla ya kurudi kwa ajili ya maandalizi ya harusi kabambe. Wakati Mage na zilipendwa wake wakienda kutuliza mawazo Colin naye aliamini kuendelea kuwepo Tanzania kwa muda ule akili yake haitakuwa sawa. Alipanga siku inayofuata aende Afrika ya Kusini kwa wiki moja ili arudi na mawazo mapya. Kwa vile ndege ilikuwa ikiondoka saa sita mchana Colin alipanga kuondoka saa nne asubuhi ili awahi saa moja kabla ndege haijaondoka baada ya taratibu zote alijiandaa kwa siku ya pili. Siku ya pili Colin akiwa amejilaza kitandani alikumbuka kitu na kunyanyuka kwenda kwenye kabati na kutoa picha alizompiga Cecy siku ya birth day yake. Alizichukua na kuziweka juu ya kitanda, katika zile picha aliikuta picha moja ya Mage. Alipitia picha mojamoja, aliona kitu cha ajabu mbele ya macho yake Cecy alikuwa msichana mrembo kuliko Mage na kujiuliza kipi kinachomfanya amng’ng’anie Mage wakati kuna almasi juu ya mchanga. Alitulia akiitazama picha ya Cecy na Mage, mara simu yake iliita, alipoangalia ilikuwa ya rafiki yake Lukonge. “Niambie Musoti,” alimwita kwa jina alilokuwa akipenda kumtania kutokana na kufanana na umbile la mchezaji wa timu ya Simba, Donald Musoti raia wa Kenya. “Mzee vipi?” “Poa za siku?” “Nzuri naona namba ya South, lini tena huko?” “Na wiki sasa.” “Naona mzee umenikumbuka?” “Kawaida tu, Colin kuna kitu kinanitatiza sina uhakika nacho?” “Kitu gani?” “Ngoja nitume picha kwenye WhatsApp kisha utanipa jibu.” “Poa tuma.” Baada ya sekunde chache picha iliingia kwenye simu kupitia WhatsApp, aliifungua na kukutana na picha tofauti za Mage akiwa na mwanaume wakiwa katika mkao wa mahaba mazito. Alituliza macho na kushindwa kuelewa picha ile imepigwa lini na Mage yupo wapi. Baada ya muda Lukonge alipiga simu na kuuliza: “Umeelewa?” “Ndiyo, hii picha umetoa wapi?” “Nimezipiga muda si mrefu, huyu si shemeji Mage?” “Kwani wewe upo wapi kwa sasa?” “Nipo Hilton hotel hapa Daban.” “Musoti ni historia ndefu niache kwa muda nitakupigia.” “Poa.” Baada ya Lukonge kukata simu, Colin aliziangalia upya zile picha jinsi Mage alivyojiachia na mwanaume Afrika ya kusini. Akiwa katikati ya lindi la mawazo na kumuangalia Mage ambaye aliamini kabisa hakuwa na mapenzi naye na ukweli ilizidi kudhihirika. Mlango uligongwa, aliweka simu pembeni na kunyanyua uso wake kuangali mlangoni bila kusema kitu. Alijua ni mama yake amerudi baada ya asubuhi kuondoka kwenda kwa mama Mage kutaka kutafuta muafaka. Aliamini picha zile ndizo zitapunguza presha ya mama yake aliyeng’ang’ania kuokoa ndoa yake na Mage ambayo iliisha kufa. Alikumbuka ameacha simu alirudi kitandani na kuichukua ili amuoneshe mama yake zile picha za Mage akiwa na mwanaume nchini Afrika ya kusini. Baada ya kuichukua simu alirudi hadi mlangoni na kufungua, alishtuka kumuona mwanamke mgeni kwake akitabasamu aliyekuwa na miwani ndogo nyeupe. Aliwekewa kidole mdomoni na kumsukuma kumrudisha ndani, naye hakuwa mbishi alirudi hadi kitandani na kukalishwa. Msichana yule mrembo alifunga mlango na komeo na kugeuka huku akitoa miwani ndogo na kutabasamu. Colin alikuwa kama anaota baada ya kumuona aliyekuwa amesimama mbele yake ni Cecy hakika alikuwa amependeza sana. “Ha! Cecy?” “Ndiyo mimi,” Cecy alijibu kwa madaha. “Siamini…Siamini Cecy wewe ni mwanamke mzuri sana tena sana.” “Simshindi Mage.” “Cecy naomba uachane na kile kichefuchefu.” “Colin leo unamuona Mage kichefuchefu kwa vile amekukataa?” “Ilikuwa shinikizo la mama tu lakini ukweli sikuwa na mapenzi naye kama ninavyokupenda,” Colin alijitetea. “Colin napita nilitaka kujua kama upo,” Cecy baada ya kusema vile aligeuka na kutoka nje. “Cecy hebu nisikilize.” “Ungekuwa na shida na mimi ungenifuata nyumbani kwetu.” Colin aliamini kabisa Cecy alikuwa amechukizwa na kitendo cha kumterekeza na ahadi za uongo. Alitoka mbio kumuwahi Cecy nje, alimkuta amekaribia getini alimfuata na kumshika mkono asiondoke. “Cecy najua nimekukosea naomba unisamehe.” “Colin najua hunipendi bali mimi najipendekeza kwako, endelea na Mage wako.” “Hapana Cecy nakuapia haki ya Mungu wewe ndiye moyo wangu,” Colin alipiga magoti mbele ya Cecy ambaye siku ile alionekana mrembo mara dufu. “Colin wewe ndiyo wa unifanya hivi au kwa vile mimi ni maskini mbumbumbu sijui lolote, asante,” Cecy alisema kwa sauti ya kilio. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Ha..ha..Si..si…” Colin alinyamaza baada ya kusikia honi lakini alishindwa kunyanyuka kwa vile alikuwa bado kamshika mkono Cecy akimuomba msamaha. Geti lilifunguliwa na gari la mama Colin liliingia na kushangaa kumuona mwanaye amepiga magoti mbele ya binti mrembo. Cecy alipomuona mama Colin akiteremka kwenye gari alimsukuma Colin na kutimua mbio kwenda nje. “Cecy…Cecy rudi na..na..” Cecy hakugeuka alitoka hadi nje ya geti, bahati nzuri aliona bajaj inapita aliisimamisha na kupanda kisha alimweleza dereva ampeleke nyumbani kwao. Colin alipotoka nje alikuta ameisha ondoka. Alirudi ndani mbio na kumwambia mlinzi afungue geti, alipanda kwenye gari alilokujanalo mama yake na kumfukuzia Cecy kwa kuamini hasira za Cecy hazikuhitaji kupewa muda zaidi ya kutulizwa haraka la sivyo atakosa bara na pwani. Mama Colin toka afike alikuwa akijionea vihoja asijue kumetokea nini na yule binti mrembo ni Cecy gani. Alimsogelea mlinzi na kumuuliza. “Eti yule msichana ni nani?” “Hata sijui, alikuja na kukuuliza kama upo nikamwambia haupo, akaniuliza Colin nikamwambia yumo ndani. Basi aliingia ndani hata hajakaa niliona akitoka mara nikamuona Colin akimkimbilia na kumshika yule msichana akawa mkali. Nilishangaa kumuona akipiga magoti kumuomba msamaha.” “Nimesikia anamwita Cecy, ni Cecy yupi?” “Mmh! Ndiyo leo namuona.” “Mmh! Sasa atakuwa amekwenda wapi?” “Hata najua! Labda atakuwa amemfuata huyo msichana.” Colin aliendesha gari kwa kasi kuitafuta bajaj ambayo ilikuwa imeishapotea kuonesha Cecy alimwambia dereva aikimbize. Aliakanyaga mafuta kuitafuta bajaj kuifuata njia ya kuelekea nyumbani kwao Cecy. Alipokaribia nyumbani kwao alimuona akiteremka kwenye bajaj na kuingia ndani. Colin alisimamisha gari mbele ya nyumba ya kina Cecy na kuteremka, hakufunga mlango alikimbilia ndani, Cecy alishangaa kumuona Colin pale alimuuliza kwa sauti ya juu. “Colin umefuata nini hapa kwa masikini?” “Cecy mpenzi naomba unisikilize.” “Nikusikilize nini, ni wazi nalazimisha mapenzi nenda kwa Mage mwanamke mwenye uwezo na elimu, niache mimi maskini nisiye na elimu.” “Ukifanya hivyo utakuwa ukinifunga mikono na kunipiga sitaweza kujitetea, naomba unipe nafasi.” “Umetudhalilisha vya kutosha kwa kutudanganya kuishi maisha ya peponi leo yapo wapi, najua una chaguo lako naomba uondoke utuache na umaskini wetu.” “Cecy najua nimewakosea lakini nami ni mwanadamu ninayehitaji kusamehewa kwa vile si mkamilifu.” Mama Cecy aliyekuwa nyumba ya pili akichota maji aliporudi alishangaa kumkuta Colin kampigia magoti Cecy. “Kuna nini?” aliuliza kwa mshangao. “Mama huyu si alikuja hapa kusema nini na alifanya nini?” Cecy aliuliza kwa sauti hasira. “Mama najua sikuwa mkweli lakini mpango wangu upo palepale.” “Baada ya kukataliwa na Mage eeh?” Cecy alimuuliza huku amemshikia kiuno. “Hapana majukumu yalinibana, mama naahidi nikitoka hapa kila nilichoahidi nakitimiza nisipofanya hivyo chukue uamuzi wowote.” “Tuchukue uamuzi gani ikiwa hatukudai ni hitari yako si lazima,” mama Cecy alisema. “Mama nilikuwa katika kipindi kibaya ambacho naamini ningelezimisha ningeweza kuwatia kwenye matatizo.” “Colin, maisha yetu ndiyo haya hatuhitaji msaada wako, hatujaja kwenu kuomba msaada, hata masikini ana nafasi kwa muumba,” Cecy alisema huku machozi ya uchungu yakimtoka. “Cecy usifike huko, najua unanipenda,nakuhakikishia kulipa upendo mara mbili.” “Sihitaji,” Cecy alijibu kwa nyodo japo moyo wake wote ulikuwa kwa Colin alitaka kutikisa kibiriti kuona kama kimejaa. “Cecy najua nimekukosea lakini amini huu ni wakati wako wa kuponya maumivu ya moyo wako.” “Cecy msamehe mwenzako,” mama Cecy aliingilia kati. “Basi amka,” Cecy alinyanyua Colin ambaye alikuwa bado amepiga magoti kama muumini aliyekuwa akiungama kanisani. Colin alinyanyuka na kukumbatiana na Cecy ambaye alijilaza kifuani kwa mpenzi wake, mama yake alikuwa pembeni alitabasamu huku akiomba dua Colin amuoe Cecy ili kutimiza ndoto ya mwanaye. “Cecy nataka kukuhakikishia mbele ya Mungu, mama yako na mchana wa jua kuwa wewe ndiye mke wangu wa maisha.” “Muongo Colin unanidanganya,” Cecy alisema kwa sauti ya kudeka. “Unataka nifanye nini ili uamini ninayosema.” “Nioe niwe mkeo.” “Nakuhakikishia kukuoa uwe mke wangu na mimi niwe mumeo.” “Asante.” “Naomba sasa hivi twende nyumbani nikamueleze mama mbele yangu.” “Akikataa?” “Hawezi, hii ni nafasi yangu ambayo hakuna wa kuiingilia, naomba uniamini.” “Mmh! Sawa wacha nikaoge ili tuondoke.” Colin alipewa kiti ili amsubiri Cecy aliyekwenda ndani kubadili nguo, alitoka amejifunga upande wa khanga na kutoka kuelekea bafuni kuoga. Colin alimsindikiza kwa macho baada ya kupata nafasi ya kuliona umbile la Cecy katika vazi la kanga rangi adimu ya isiyochanganywa madawa ya ngozi. Aliamini chaguo la kwanza la mama yake lilikuwa sahihi, alijua ni wakati wa mama yake kuamini chaguo la pili halikuwa sahihi bali tamaa ya macho ndiyo iliyompoteza. Cecy baada ya kumaliza kuoga alirudi ndani na kubadili nguo kwa kujipamba kwa vazi la kitenge lililompendeza alionekana mwanamke wa Kiafrika hasa. Alisimama mbele ya Colin na kutabasamu. “Colin tunaweza kwenda.” “Duh!” Colin alisema akiwa haamini. “Ndiye mimi Cecy, mwafrika asilimia ninayejivunia rangi yangu nyeusi.” “Basi mama inatosha, “Colin alisema huku akinyanyuka na kumshika mkono. “Mama tunaomba tukukimbie,” Colin alimuaga mama Cecy. “Haya baba Mungu awatangulie mfike salama.” “Amina.” Walishikana mikono na kutoka nje kuelekea kwenye gari, mama Cecy aliwasindikiza kwa macho na kunyanyua mikono juu na kurudi kuomba dua yake ya Colin kumuoa mwanaye ili roho itulie. Hakuteremsha jicho mpaka gari lilipopotea machoni mwake. Ndani ya gari Cecy moyo wake ulikuwa na furaha nusu kwa vile aliamini lazima Colin atumie nguvu nyingi bila hivyo hakuna mapenzi kwa vile mama yake aliishajenga uadui mapema. Alionekana mtu mwenye mawazo mengi kitu kilichomfanya Colin amshtue. ”Vipi mpenzi?” “Colin bado moyo wangu una wasiwasi.” “Wa nini?” “Jinsi mama yako atakavyonipokea.” “Ondoa wasi kila kitu niachie mimi.” Colin alisimamisha gari mbele ya geti na kupiga honi, mlango ulifunguliwa na kuliingiza gari ndani. Alizunguka upande wa pili na kumfungulia Cecy na kumshika mkono kuteremka kwenye gari kwa heshima kisha alielekea naye ndani. Walitembea taratibu kama mtu na mkewe angetokea mtu na kuwaona angejua ni wapenzi wa muda mrefu wanaopendana sana. Walipofika mlango wa kuingia sebuleni Colin alisema kwa sauti ya unyenyekevu: “Karibu malkia wangu.” “Asante mfalme wangu,” Cecy naye alijibu kwa unyenyekevu. Sauti zile zilimfanya mama Colin aliyekuwa ameinama akisoma biblia kunyanyua macho na kumuona mwanaye na msichana mrembo ambaye aliamini ndiye aliyeondoka muda mfupi uliopita. “Shikamoo mamkwe!” Cecy alimsalimia mama Colin kwa unyenyekevu huku akipiga magoti ya heshima. “Marahaba mama, karibu.” “Asante,” Cecy alijibu huku akinyanyuka na kumfuata Colin aliyekuwa amesimama pembeni yake na kumshika mkono. Colin alimuongoza Cecy mpaka kwenye sofa na kumkaribisha tena: “Karibu.” “Asante,” Cecy alijibu huku akikaa. “Unatumia kinywaji gani?” “Chochote utakachonichagulia mfalme wangu.” “Colin si ungemwita dada wa kazi awahudumie,” mama Colin aliingilia kati. “Hapana huyu ni mgeni wangu, kila kitu chake nitafanya mimi.” “Mmh! Haya.” Muda wote mama Colin alikuwa bado hajaipata picha ya yule msichana mrembo, alituliza macho kwa wizi ndipo alipomgundua kuwa ni Cecy msichana muuza ndizi. Alikunja uso kwa hasira na kuamini kabisa lile si chaguo sahihi kwa mwanaye bali ni papara ya kuachwa na Mage. Alinyanyuka na kuelekea chumbani kwake, alipotoka eneo la sebule alimwita Colin. “Colin.” “Naam mama.” “Njoo mara moja.” “Nakuja,” Colin alisema huku akimwekea juisi kwenye glasi na kunywa kidogo kisha alimkaribisha. “Karibu malkia wangu.” “Asante mfalme wangu.” “Samahani namsikiliza mama mara moja.” “Nenda mpenzi kamsikilize mama.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Colin alimfuata mama yake kwenye korido alipokuwa amesimama, alimsogelea karibu na kumuuliza: “Unasemaje maana umenitoka kama kuna kitu?” “Yule nani?” aliuliza huku akinyoosha kidole sebuleni. “Mke wangu mtarajiwa chaguo sahihi la moyo wangu.” “Colin… Colin una tatizo gani wanawake wote wameisha mpaka umfuate huyu maskini mbumbumbu asiyejua kitu. Mwanangu tuna fedha tunaweza kumuona msichana yeyote mzuri mwenye elimu yake kwa fedha yoyote na popote duniani.”“Mama naomba kwa hili usizungumze chochote uniache kabisa, umetafuta mwanamke ambaye leo katuvua nguo kwa vile ulimfuata msomi mwenye uwezo.” “Lakini suala la Mage bado tulikuwa tunalishughulikia bado lilikuwa halijafika mwisho. Hivi leo Mage aje na mama yake wakikute kinyago hiki kuna ndoa kweli?” “Penzi langu na Mage liliishia Bagamoyo, lilikufa tukalizika halitafufuka tena.” “Lakini bado wazazi hatajabariki uamuzi wenu.” “Mama si uamuzi wetu bali wa Mage, kasema ukweli ana mtu anayempenda tatizo lipo wapi?” “Basi Cecy si chaguo langu.” “Mama, mimi ni mwanao umenizaa na kunilea na kunifundisha kila kitu, lakini suala la nimpende nani ni matakwa ya moyo wangu. Nilikukubalia kwa Mage kwa vile ni mzazi wangu zoezi lako limefeli sasa huu ni muda wangu.” “Lakini siyo kwa Cecy.” “Mama Cecy ni zaidi ya mwanamke ndiye mwenye nafasi moyoni mwangu zaidi ya hapo sitakuwa na mwanamke mwingine.” “Colin, Cecy umemjulia wapi kama siyo mimi?” “Basi hili ndilo chaguo lako lililokuwa sahihi hujui tu.” “Nilikuwa namtania tu lakini si kwa ajili ya kuwa mkeo.” “Basi imekuwa hivyo bila kutegemea.” “ Basi mimi simtaki.” “Kwa hiyo unatafuta aibu nyingine?” Colin alisema huku akifungua simu upande wa picha na kumuonesha mama yake. “Umeona unayempenda?” Aliangalia picha za Mage na kuuliza: “Hizi picha za nani?” “Mage na mpenzi wake,” Colin alimjibu huku akimtazama usoni. “Picha hii imepigwa lini?” “Leo.” “Wapi?” “Wapo Afrika ya kusini wanakula raha katika hoteli ya Hilton jijini Durban, sasa naomba uniache na Cecy wangu.” “Colin bado hujanieleza kitu, tafuta msichana mwingine lakini kwa Cecy sipo radhi kuingiza uchafu katika familia yangu.” “Mama nakupenda na kukuheshimu sana naomba kuhusu Cecy usiniingilie kabisa zaidi ya hapo nitaondoka na kukuacha na fedha zako.” “Colin mwanangu mbona umefika mbali,” mama alishtuka. “Kwa sababu umeingilia haki ya moyo wangu, wewe ni mzazi gani usiye na huruma nimeumizwa badala ya kunihurumia bado unataka kuniongezea maumivu,” Colin alisema kwa uchungu. “Lakini kumbuka wewe ni msomi unawezaje kuoa mwanamke mbumbumbu?” “Mama mapenzi si cheo, elimu wala fedha, Cecy ni zaidi ya vyote hivyo kwangu.” “Sawa, lakini utakuja kunikumbuka na uamuzi wako hata nikifa.” “Ni kweli mama nitakukumbuka kwa kunitafutia mchumba aliye bora kuliko Mage. Cecy ni lulu iliyokuwa imejificha kwenye matope.” “Nimekuelewa mwanangu, naomba unisamehe kwa kukukwaza.” “Nilikusamehe kabla hujatenda.” “Basi naomba ya huku yaache hukuhuku.” “Sawa mama.” Baada ya makubaliano Colin alirudi kwa Cecy na mama yake kwenda chumbani, alipofika alimpigia simu mama Mage kutaka kupata ukweli wa kauli ya mwanaye. Baada ya simu kuita ilipokelewa upande wa pili: “Haloo, dada vipi?” “Mmh! Yaani bado nachanganyikiwa ulisema Mage kaenda wapi?” “Nilikuambia amekwenda kwa shoga yake.” “Wapi?” “Aliniaga anakwenda Kibaha,” mama Mage alidanganya. “Mmh! Mbona Colin anasema katumiwa picha za Mage akiwa na mwanaume Afrika ya kusini wakila raha kwenye ufukwe wa Hilton Hotel?” “Mmh! Labda maana ametoka toka jana, dada wee hebu tuachane na Mage tufanye mambo zingine.” “Sawa dada nimekuelewa.” Baada ya kukata simu alitulia kwa muda akiwaza, alijikuta akimchukia Cecy na kuuapia moyo wake hatakuwa tayari kuona mwanaye akioa mwanamke asiye na hadhi. Alipanga kuhakikisha anauvunja uhusiano ule kwa hali na mali ili Colin aoe mwanamke mwingine mwenye elimu na kutoka familia yenye uwezo. Alitoka chumbani na kujifanya kujichekeza kwa Cecy huku akimtania. “Jamaniii mmependezaje wapenzi!” “Asante mkwe,” alijibu Cecy kwa furaha huku Colin aliuona unafiki wa mama yake uliojificha moyoni ambao mpenzi wake hakuujua. Kwa vile mama Colin hakupenda Cecy kuwa pale aliondoka na kwenda chumbani kwake na siri yake nzito moyoni. JIJINI DURBAN AFRIKA KUSINI Katika ufukwe wa hoteli ya Hiltoni wapenzi wa wawili walikuwa wakila raha, Mage alikuwa amelala kifuani kwa Hans huku akichezea kidevu chenye ndevu chache. “Hans nikuambie kitu?” “Niambie mpenzi.” “Ningebugi vibaya kuolewa na mrugaruga kama yule(Colin).” “Si haraka zako, nilikueleza piga ua lazima mke wangu utakuwa wewe pamoja na wazazi kunilazimisha kumuoa yule mwanamke.” “Nilichanganyikiwa baada ya kuona umepata mtoto.” “Ilikuwa lazima iwe vile ili wasijue nimepanga nini mbeleni.” “Asante Hans kwa kuponya majeraha ya moyo wangu.” “Nami nashukuru kukubali kurudi mikononi mwangu.” “Kwa hiyo ndoa lini?” “Tukirudi tu nyumbani mipango inaanza mara moja.” “Nitafurahije mpenzi wangu.” “Usijali nipo kwa ajili yako.” “Basi naomba turudi nyumbani ili tukalisema hili mbele ya wazazi wetu wote.” “Hakuna tatizo nakusikiliza wewe.” “Nataka kesho jioni tuwe mbele ya wazazi wako ukiwaeleza kwa mdomo wako kuwa mimi ndiye mkeo baada ya hapo twende kwetu nikamweleze mama kuwa wewe ndiye mume wangu.” “Hakuna tatizo mpenzi wangu.” Walikubaliana kuondoa Afrika ya kusini siku ya pili mchana warudi Tanzania ili kwenda mbele ya wazazi wao kuthibitisha mapenzi yao ya dhati. *** Colin na Cecy baada ya kutoka nyumbani walikwenda Bagamoyo katika hoteli ya Malaika ambako alipanga kukaa kwa siku moja. Majira ya jioni wakiwa wamejilaza mchangani huku wakipepewa na upepo mwanana wa bahari Colin aliyaangalia mawimbi ya bahari na mitumbwi ya wavuvi aliokuwa wakivua samaki. Baada ya kugandisha macho baharini alijikuta akitokwa na machozi baada ya kukumbuka sehemu kama ile ndiyo iliyotumika kuvunja uchumba wake na Mage japokuwa ilikuwa hoteli tofauti lakini ni Bagamoyo ileile. Machozi yalimdondoka bila kujua na kuangukia kwenye paji la uso la Cecy aliyekuwa amejilaza mapajani kwa mpenzi wake na kumfanya anyanyue macho kumwangalia. Alishtuka kumuona akibubujikwa machozi kitu kilichomfanya amuulize. “Vipi mpenzi wangu mbona unalia?” “Nimekumbuka kitu ambacho kimesababisha nitokwe machozi.” “Kitu gani mpenzi wangu?” Cecy alimuuliza huku akimfuta machozi kwa upande wa mtandio aliojifunga. “Ni juzi tu maeneo hayahaya yaliujerudi moyo wangu lakini, leo hii maeneo yaleyale yameujenga upya na kujiona kama nimezaliwa upya.” “Kwa nini unasema hivyo?” “Juzi tulikuja huku na Mage kuvunja uchumba wetu ambao ulinishtua sana na kuumiza moyo wangu japokuwa haikuwa hoteli hii, lakini ni hukuhuku Bagamoyo. Lakini leo nimezaliwa upya kwa kulipata penzi la kweli ambalo naamini nilitaka kulipoteza haya ni machozi ya uchungu na furaha.” “Nifurahi kusikia hivyo, lakini moyo wangu bado haujaamini kama tayari wewe ni wangu.” “Kwa nini Cecy?” “Naogopa Mage anaweza kurudi na wewe kunitosa, nitaumia mara mbili kwa vile nimeonja utamu wa mapenzi naweza kufa kwa presha kama utafanya hivyo,” Cecy alisema kwa sauti ya kulalamika. “Cecy unataka kuamini vipi wakati penzi langu lilikuwa wazi mbele ya mama yangu.” “Mama yako alikuitia nini pembeni?” “Tulikuwa na yetu wala haikuhusiana na sisi,” Colin alitengeneza uongo ili kuendeleza furaha ya siku ile. “Mmh! Nilikuwa na wasi labda chokoraa nilimeingia kwenye nyumba ya malkia,” Cecy alitania utani wenye ukweli.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Hapana wewe ndiye malkia wangu.” “Nashukuru kusikia hivyo,” Cecy alimkumbatia mpenzi wake kwa furaha bila kujua palichimbika mpaka yeye kuwa pamoja muda ule. *** Mage na Hans waliwasili katika aridhi ya Tanzania katika jiji la Dar na ndege ya shirika la Afrika ya Kusini. Nje ya uwanja wa ndege walisubiriwa na gari la kifahari Land Cruiser V8 nyeusi. Baada ya ndege kutua waliteremka na kwenda moja kwa moja ndani ya gari lililokuwa likiwasubiri na kuingia. Gari liliondoka kuelekea Mikocheni anapoishi Hans, njiani Mage alikuwa na furaha ya ajabu kurudi mikononi kwa mpenzi wake mwanaume wa maisha yake. Baada gari kuingizwa ndani na kusimama Hans alizunguka upande wa pili na kumfungulia Mage mlango na kumkaribisha.” “Karibu utamu wangu.” “Asante raha zangu.” Walishikana mikono na kuingia ndani, mapokezi ya familia ya Hans yalikuwa tofauti na siku za nyuma waliufurahia ugeni wa Mage huku wadogo zake wakimwita wifi na shemeji na wazazi wakimwita mkwe. Ilikuwa ni faraja kubwa moyoni kwa Mage aliona sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano kukubalika katika familia ile. Moyoni alijilaumu kukubali kuolewa na Colin kumbe ahadi ya kuvumilia ili ndoto yao ya muda mrefu waliyoahidiana kutenganishwa na kifo ilikuwa njiani. Familia haikuwa na tatizo tena kuingilia uamuzi wa mtoto wao kwa vile chaguo lao Mungu alilichukua hawakuwa na jinsi. Baada ya mapokezi mazuri katika familia ya mpenzi wake Mage na Hans walielekea Kigamboni nyumbani kwao Mage ili kujitambulisha rasmi kwa mzazi wake. Walipofika Kigamboni Mage alimkaribisha Hans nyumbani kwao. “Karibu mume wangu.” “Asante mke wangu.” Walishikana mikono na kuingia ndani kwa mwendo wa mahaba, sebuleni walimkuta mama Mage. Mage alimuachia mkono Hans na kumkimbilia mama yake na kumkumbatia. “Waaawoo mama.” “Mage mwanangu karibu mama.” “Asante mama.” Mage alichukua nafasi ile kumtambulisha Hans. “Mama leo nimemleta mume wangu chaguo la moyo wangu.” “Nimemuona, karibu baba,” mama Mage alisema kwa sauti ya unyonge. “Asante mama, shikamoo.” “Marahaba.” “Mama mbona mnyonge unaumwa?” Mage alimuuliza mama yake. “Walaa, mwili umechoka tu.” Mama Mage alinyanyuka na kuelekea chumbani kuwapisha alipoondoka eneo la sebule alimwita mwanaye. “Mage mama njoo mara moja.” “Nakuja mama,” kabla ya kuondoka alimuaga mpenzi wake. “Mpenzi nakuja.” “Hakuna tatizo msikilize mama.” Mage alimbusu shavuni Hans na kuchepua mwendo kwenda kumsikiliza mama yake. “Abee mama.” “Njoo chumbani.” Waliongozana hadi chumbani, walipofika mama yake alisimama na kumwambia Mage akae kwenye kochi, baada ya kukaa alimgeukia na kumwita. “Mage.” “Abee mama.” “Hivi ndiyo umeamua kunivua nguo?” “Kukuvua nguo! Kivipi mama.” “Kwa hiyo hutaki kuolewa na Colin?” “Mamaaa! Mbona hilo tuliisha limaliza, si nimekueleza ukweli wangu na Colin anajua kila kitu. Sasa swali kama hilo linatoka wapi?” “Mage kwa nini unalamba matapishi yako?” “Mama Hans si matapishi ni chakula kilichowekwa kwenye Hot port nimekipakuwa bado kina moto. Unajua jinsi gani nilivyoteseka baada ya Hans kulazimishwa kuona mwanamke mwingine. Ni wewe uliniambia niwe na subira sasa leo karudi mikononi mwangu unaniuliza hivyo?” “Kama ungekuwa huna mchumba nisingekuuliza lakini wewe tayari umeishakuwa mchumba wa mtu tena upo kwenye hatua za mwisho za ndoa.” “Mama wewe ndiye unayekuza mambo Colin tumeisha malizana na sasa hivi tunatoka nyumbani kwao Hans ambako sikuamini kama wangenipokea kama malkia. Yaani mama nimefurahi kukubalika katika familia ya mpenzi wangu.” “Mwanangu siku zote mkataa pema pabaya panamwita.” “Mamaa maombi gani hayo?” “Nakuambia utamkumbuka Colin, ipo siku Hans atakukimbia na kurudi kwa Colin utambembeleza ukitembea kwa magoti, kibaya ukute ameoa mwanangu utakuja jutia uamuzi wako,” mama alitoa taadhali. “Mama kuwa na Hans sitajuta katika maisha yangu ni chaguo sahihi la moyo wangu.” “Mmh! Sawa.” “Kuonesha Hans hataki kunichezea wiki ijayo barua inakuja na baada ya majibu maandalizi yanaanza mara moja. Kinachotakiwa vikao vya harusi visogezwe mbele ili michango ya harusi yangu na Colin iwe yangu na Hans. Hapo nina imani hakuna kitakacho haribika.” “Sawa, siwezi kukuingilia kwa vile umeamua mwenyewe, ila kila aliyae ushika kichwa chake.” “Mama hiyo misemo, ninacho shukuru nimepata tiba ya moyo wangu, kuna lingine?” “Hakuna.” “Basi mama yangu naomba unipe baraka zako kinyongo chake kinaweza kuvuruga ndoto zangu.” “Siwezi kuna na kinyongo kwa vile nipo kwa ajili ya kuyaona maisha yako yanakuwa mazuri na salama.” “Asante mama,” Mage alimshukuru mama yake kwa kumkumbatia. Mage baada ya kuachana na mama yake alikwenda sebuleni alipokuwa amemuacha mpenzi wake. Alirudi sebuleni na kumvamia Hans kwa mahaba motomoto bila kujali yupo sehemu gani. Mama yake hakutoka ndani alijikuta moyo ukimuuma na kuanza kulia peke yake huku akilaumu mapenzi ya mumewe kumuharibu mtoto. **** Siku ya pili Colin na Cecy alirudi nyumbani, alimpitisha nyumbani kwa kisha yeye alirudi nyumbani kwa vile kulikuwa na mambo ya kufuatilia kuhusiana na shughuli zake alizoanza ikiwemo kupata kibari cha kuanzisha kampuni ya mitindo na mavazi ambayo alipanga kumtumia Cecy kwa ajili ya maonesha ya mitindo ya nguo. Walipofika kabla ya kuondoka Colin alimwambia Cecy: “Mpenzi pumzika ila jioni nitakufuata tutakuwa na mazungumzo marefu ila utarudi kulala nyumbani najua bi mkubwa amekumisi.” “Hakuna tatizo msalimie mkwe.” “Kuanzia wiki ijayo nategemea kutimiza ile ahadi.” “Ahadi gani?” “Ya ujenzi wa nyumba yenu, leo nitamtuma mtu awatafutie nyumba ili kesho muhame ili kupisha ujenzi.” “Kama ni kweli tutashukuru.” Colin alimwita mama Cecy na kumpa laki mbili. “Mama utakunywa soda.” “Asante baba.” “Hakuna tatizo.” Colin aliaga na kuondoka kuwahi nyumbani ili awahi mjini kwenye mipango yake na kumuacha Cecy akikumbatiana na mama yake kwa furaha. Kwa vile alikuwa na haraka alifika nyumbani hakukaa alibadili nguo na kuvaa suti ili kwenda kwenye miadi yake. Wakati anatoka alikutana na mama yake sebuleni. “He! Baba umerudi saa ngapi?” ”Sasa hivi mama, Leo namiadi ya jamaa wale wa kampuni ya matangazo.” “Na mwenzio yupo wapi?” “Nimemuacha kwao.” “Sawa baba baadaye.” “Sawa mama baadaye.’ Colini aliagana na mama yake na kutoka nje ambako alichukua gari kuwahi Posta mpya katika Jengo la Benjamini Mkapa ghorofa ya kimi na nne. Baada Colin kuondoka mama yake aliamini ile ndiyo nafasi ya kwenda nyumbani kwao Cecy ili kuhakikisha ndoa na mwanaye haifungwi. Alioga harakaharaka na kutoka kwenda nyumbani kwao Cecy, aliendesha gari kwa kasi kidogo ili kuwahi kabla mwanaye hajarudi. Aliamini kutumia fedha zake ataweza kuisambaratisha ile ndoa. Alisimamisha gari mbele ya nyumba ya kina Cecy na kuteremka. Alimkuta mama Cecy amekaa kwenye kibalaza cha nyumba, alipomuona alimkaribisha kwa furaha na bashasha. “Ooh! Karibu dada.” “Asante, za hapa?” “Nzuri, karibu japo maisha yetu ya kuungaunga.” “Aah! Kawaida tu wala msijali.” Alipotaka kumkaribisha ndani alikataa alisimama mbele ya nyumba, aliyatazama mazingira wanayoishi Cecy na mama yake moyo wake ulichefuka kwa kuona jinsi gani mwanaye alivyopotea maboya kutaka kumuona mwanamke fukara kama yule ambaye halingani na sifa na hadhi ya familia yao.Lakini alijenga tabasamu la uongo ili kuonekana amefurahi kuonana naye. “Dada karibu ndani.” “Napita tu siku nyingine nitaingia, vipi mkwe wangu yupo?” “Mmh! Amerudi muda si mrefu alikuwa na mwenzake muda si mrefu na kufikia kulala.” “Naomba uniamshie.” “Hakuna tatizo dada.” Mama Cecy alikwenda kumuamsha mwanaye. “Cecy mwanangu amka kuna ugeni mzito.” “Nani tena mama?” “Mama Colin.” ”Uongo!” “Kweli, amekataa kuingia ndani ana shida na wewe mara moja.” Cecy aliamka na kujifunga kanga na nyingine alijitanda mabegani na kutoka nje, alipofika nje na kumuona mama Colin aliteremka ngazi haraka na kwenda kumkumbatia kwa furaha. “Waaawooo! Jamani mama mzaa chema.” “Ndiye mimi.” “Mama mbona umeishia nje si uingie ndani.” “Hapana nina haraka kidogo naomba tuzungumze kwenye gari.” “Hakuna tatizo.” Cecy na mama Colin waliingia kwenye gari na kumwacha mama Cecy amekaa kwenye kibaraza huku akiamini ile ni dalili njema za ndoa ya mwanaye baada ya adui kugeuka rafiki. Baada ya kuingia kwenye gari walifunga vioo vyote na kuwasha AC, Cecy alikuwa mtulivu ili kumsikiliza mama mkwe kipi kimemleta. Baada ya kimya kifupi Cecy alikuwa wa kwanza kuzungumza. “Ndiyo mama, una habari gani?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Cecy nataka kukuliza kitu kimoja, umempenda mwanangu kwa ajili ya mapenzi au kufuata fedha?” “Kimapenzi,” alimjibu kwa upole huku akimtazama usoni. “Muongo, wewe mwanangu unampenda kwa ajili ya fedha hivyo nataka uniambie unahitaji kiasi gani ili umuache mwanangu?” “Mmh! Haya yameenza lini mama na kipi nilichokiomba toka katika familia yenu kuonesha nahitaji fedha?” “Sikiliza Cecy narudia tena, mwanangu huna mapenzi naye sitaki yatokee ya Mage hivyo naomba uachane naye. Sema unataka kiasi gani?” “Kuachana na Colin wala sihitaji pesa yako mimi ni maskini niache na umaskini wangu. Unaweza kununua kila kitu lakini huwezi kununua moyo wa mtu.” “Sikiliza Cecy nitayabadili maisha yenu kwa kuwajengea jumba la kisasa na kuwanunulia wewe na mama yako magari ya kutembelea pia kukufungulia duka kubwa la nguo na vipodozi katikati ya jiji ili tu uachane na Colin.” “Nimeridhika na umaskini wangu wala usipoteze fedha na nguvu nyingi kuliua penzi letu.” “Cecy nielewe si kuliua penzi lenu bali kumuokoa mwanangu na mateso, kingine sitaki nawe kuingia kwenye mkumbo huo kwa vile Colin bado anampenda Mage wakirudiana watakuumiza.” “Sawa nimekuelewa unaweza kwenda,” Cecy alisema kwa mkato. “Ila ukitoka hapa naomba hili libakie siri yetu.” “Sawa, ila nami nakutuma kitu kimoja, ukitoka hapa kamkanye mwanao asije hapa la sivyo!” “Utamfanya nini?” “Siyo nimfanye nini asije hapa na wewe ukiondoka hapa usikanyage tena, nenda kwa matajili wenzio,” Cecy alisema kwa hasira. “Cecy usifanye hasira hujui vitu gani vizuri nilivyovipanga kwako.” Mama Colin alifungua mkoba na kutoka mabunda matano ya milioni mojamoja na kumpa Cecy huku akisema: “Ukiachana na Colin utapata zaidi ya hizi.” INAENDELEA HAPA... ILIPOISHIA: Cecy alizipokea na kumfanya mama Colin kutabasamu kwa kuamini fedha ni sabuni ya roho. Alizitazama zile fedha kwa uchungu huku machozi yakimtoka na kuona jinsi gani umaskini wao ulivyotumiwa kama kisu butu cha kuupasua moyo wake bila ganzi. Alitulia akilia huku machozi yakidondokea kwenye zile fedha. SASA ENDELEA... Kwa hasira alizinyanyua na kumpiga nazo usoni mama Colin na kutoka ndani ya gari, kitu kilichomuacha mdomo wazi mama Colin. Mama yake alishangaa kumuona mwanaye akitoka ndani ya gari akilia. “Cecy kuna nini?” “Mama niache kwanza, huyu mama ni mchawi.” “Mchawi! Kafanya nini?” mama yake alishtuka. Wakati huo mama Colin kwa aibu aliwasha gari lake na kuondoka bila kuaga. Aliushangaa ujasiri wa Cecy msichana maskini lakini mwenye kujiamini kupita kiasi kwa kukataa fedha zile na ofa ya kuyabadili maisha yao. Hakuamini binti muuza ndizi kukataa fedha zile wakati maisha yao ya kubahatisha. Lakini alijiapiza kwa nguvu kwa hiyari kwa fedha kwa damu lazima Cecy ataachana na Colin. Mama Cecy alimfuata mwanaye aliyeingia chumbani huku akilia na kushindwa kuelewa mazungumzo ya ndani ya gari yalikuwa ya nini. Alikumta akiendelea kulia kitu kilichomfanya ajiulize kipi kikubwa walichokizungumza ndani ya gari. Alimkuta amelala kifudifudi akilia kwa sauti ya kwikwi, wasiwasi wake labda Colin amepata tatizo. “Cecy mwanangu kuna tatizo gani tena?” “Mama inaumiza sana.” “Kuna nini mpenzi wako kapata tatizo?” “Mama mtu anaweza kuununua moyo wangu hata kuuchukua bure nikiwa nimekufa, lakini nikiwa hai siuuzi kwa gharama yoyote kwa vile furaha ya mtu hainunuliwi dukani.” “Una maana gani?” mama yake alikuwa bado njia panda. Cecy alimweleza mama yote aliyozungumza na mama Colin, mama yake macho yalimtoka pima kusikia taarifa ile baada ya kuamini kila kitu kilikuwa vizuri kilichobakia ni ndoa ya mwanaye na Colin. “Mmh! Mbona makubwa madogo yana nafuu,” mama Cecy alisema akiwa amechoka na maneno yale. “Mama mimi na Colin basi,” Cecy alisema kwa hasira. “Huo ni uamuzi wa hasira lazima umsikilize mwenzako si amesema atakupitia jioni basi msubiri umsikilize naye anasemaje kama lao moja na mama yake una haki ya uamuzi wako.” “Mama kosa langu nini? Yaani anatumia fedha zake kuinunua furaha yangu?” Cecy alisema kwa uchungu. “Mwanangu kama Colin si chaguo la Mungu basi hamtaoana lakini kama ni chaguo la Mungu hakuna kitakachozuia.” “Yule mwanamke ni mnafikia akiwa na mwanaye ananichekea kicheko cha mamba lakini kumbe ananitamani kunimeza.” “Wee yaache tusubiri jioni.” “Sawa, lakini nina amini hakuna ndoa yangu na Colin labda mapenzi ya sisi wenyewe lakini mama yake hanipendi na yupo radhi kutumia njia yoyote kukwamisha mapenzi yetu.” ”Ngoja tumsubiri Colin anasemaje.” “Namsubiri kwa ajili yako lakini ningekuwa peke yangu asingekanyaga hapa.” **** Majira ya jioni Colin alimpitia Cecy kama alivyomweleza, aliposimamisha gari alishangaa kutomuona mpenzi wake kama kawaida, kwani aliisha mzoesha vibaya kumpokea kwa kumrukia kwa mahaba motomoto. Baada ya kusimamisha gari aliteremka na kwenda ndani huku akiita jina la Cecy mkononi alikuwa amebeba zawadi za mpenzi wake. “Beeeebi.” Hakuwa na jibu zaidi ya kusikia sauti ya kilio toka ndani kitu kilichomshtua na kufanya akimbilie ndani kwa kuamini mpenzi wake yupo kwenye matatizo. Alimkuta Cecy amelala kifudifudi akilia kilio cha sauti. “Cecy mpenzi una nini?” “Colin unaweza kununua kila kitu chini ya jua lakini si furaha ya mtu,” Cecy alisema bila kugeuka. “Kuna nini mpenzi wangu?” Colin alishangaa. “Umenikuta maskini hata siku moja sikuja kwenu kuomba pesa ya kula, nimeishi kwa kuuza ndizi nitaendelea kuuza ndizi lakini hamuwezi kuutumia umaskini wetu kama siraha ya kununua haki ya moyo wangu.” “Cecy hebu geuka mpenzi wangu, kipi nimekukosea mpaka useme maneno makali hivyo?” “Najua hunipenda lakini usitumie gharama kubwa kuniacha, tamko lako ni tosha kuliko gharama na nguvu mnayotaka kuitumia. Ni kweli nakupenda jambo ambalo lipo wazi mbele ya muumba. Lakini ni vigumu kulazimisha mapenzi ni sawa na kumvuta punda mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji.” “Cecy mpenzi wangu mbona toka jana tumekuwa na siku nzuri ambayo nilitegemea kuimalizia leo. Kipi nilichokufanyia ikiwa nimekuaga nimekwenda kwenye mipango ya maisha yetu ya mbeleni. Nimekuja na furaha ili kukujulisha nimekupatia chuo cha mambo ya urembo ambacho utasoma miezi sita na ukitoka hapo utakuta nimeisha kukufungulia kampuni yako ya urembo. “Kwa nini wanawake mnapenda kuumiza moyo wangu, Cecy kabla hatujaanza mapenzi ulionesha kunijali lakini kuanza kwa ukaribu wetu hata mwezi bado unataka kuupasua moyo wangu bila ganzi. Cecy niliamini wewe ndiye tiba ya moyo wangu, lakini unataka kuongeza msumali wa moto kwenye kidonda. Naomba basi mnihurumie nami binadamu ninayehitaji upendo. Mapenzi yangu yamekuwa kama mtu anayemwaga maji baharini yasiyoonekana. “Kwa nini hukuniambia mapema Cecy umeacha nijirushe juu ya ghorofa ya mapenzi nikiamini utanidaka, lakini najiona naangukia pabaya nawe umekataa kunidaka nitakufa kifo kibaya. Cecy utajiri wetu hauingiliani na mapenzi yetu, fedha inaweza kununua kila kitu lakini si penzi la kweli bali upendo wa dhati toka chini ya uvungu wa moyo wa mtu mwenye mapenzi ya kweli asiyeangalia kitu bali mtu mwenyewe alivyo. “Ni kosa gani nililokufanyia mpaka kufikia kusema maneno mazito yaliyoushtua moyo wangu, kama moyo ungekuwa ukitoka nje naamini ungekuwa unavuja damu kutokana na mshtuko na maumivu ya kuona unatolewa sehemu salama na kutupwa kwenye miba.” Maneno ya Colin ambaye alionekana hajui kilichokuwa kikiendelea kilimfanya Cecy aongeze sauti ya kilio na kujinyanyua alipokuwa amejilaza na kwenda kujitupa kifuani kwa Colin kitu kilichomshangaza mpenzi wake. “Cecy mpenzi wangu hebu kuwa mkweli tatizo nini mpaka kusema maneno makali? Nipo radhi kujitoa muhanga ili kuliokoa penzi letu.” “Colin najua unanipenda lakini mama yako hanipendi,” Cecy alisema kwa sauti ya kilio. “Bebi, maneno gani hayo ikiwa jana uliona alivyokufurahi, yasahau yote yaliyopita.” “Colin, mama yako mnafiki, ana tabia ya unafiki wa mamba anakuchekea machoni lakini moyo anakuchukia.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Kwa nini unasema hivyo?” Colin alishtuka kusikia vile. “Mama yako hataki tuwe pamoja yupo radhi kutumia gharama yoyote kuhakikisha anatutenganisha.” “Lakini mbona yaliisha.” Cecy aliamua kumweleza ukweli, ujio wa mama yake na ahadi na fedha aliyotoa kwa ajili kulivunja penzi lao. Colin alibakia macho yamemtoka pima asiamini maneno ya Cecy. “Cecy unayosema ni kweli?” “Nimzulie uongo mama yako ambaye kama tungeoana angekuwa mama mkwe wangu.” “Kama kafikia hatua hiyo naomba kwanza unisamehe sana, najua nitafanya nini. Ila nakuahidi kwa kuonesha msimamo umezisha upendo moyoni mwangu, pia hela aliyotaka kukupa nitakupa mara kumi yake na kutimiza ahadi yangu kwa kulijenga penzi letu.” “Colin, narudi huwezi kuununua moyo wangu.” “Kwa nini unasema hivyo?” “Sihitaji pesa zako kwa ajili yakuonesha kuwa unanipenda bali mapenzi ya dhati toka kwako. Pendo langu halina gharama japo ni ghali kwa vile nilikubali kukupenda kama ulivyo wala si kwa ajili ya gari, majumba au fedha zenu.” “Asante kufahamu hivyo, basi naomba ukaoge ili twende nilipokueleza jana.” “Sawa mpenzi wangu.” “Pia, kesho mtahama ili kupisha ujenzi wa nyumba yenu kwa muda, nimewatafutie nyumba nzima ambayo nimelipia kwa mwaka mzima.” “Kwani hiyo nyumba unachukua muda gani kujengwa?” “Nitaka ijengwe vizuri hata miezi miwili au mitatu.” “Basi si ungechukua miezi mitatu?” “Msiwe na wasi, niliwaambia wakakataa wakataka mwaka mzima.” “Ipo wapi?” “Kimara Baruti.” “Asante mpenzi wangu,” Cecy alimkumbatia Colin kwa furaha na kuyasahau maumivu yote. Cecy alikwenda kuoga akimuacha Colin ambaye alihisi kichwa kinataka kupasuka kwa mawazo kutokana na alichokifanya mama yake aliyeamini ndiyo muongozo wake na kuitengeneza furaha lakini kwake ilikuwa kinyume. Alipanga akitoka pale kwenda na Cecy nyumbani kwao ili mama yake akayasema yale mbele yake. Baada ya Cecy kumaliza kuoga na kubadili nguo ambazo zilizidi kumpandisha chati na kumfanya aonekane binti mrembo kuliko wanawake wote duniani mbele Colin. Walishikana mikono na kuelekea ndani ya gari na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwao Colin. “Colin unanipeleka wapi?” Cecy alishtuka. “Usihofu naomba unifuate na mimi.” “Mmh! Sawa.” Gari lilipiga hodi na geti lilifunguliwa na Colin kuliingiza ndani, kama kawaida alizunguka na kumfungulia mlango kisha alimshika mkono na kuingia naye ndani. Sebuleni alikuwa mama Colin akizungumza na msichana wa kazi alipomuona Colin alinyanyua macho na kumuona ameongoza na hasimu wake. Alijikuta akiponyokwa na glasi ya juisi aliyokuwa ameshikilia. Cecy alisogea hadi karibu na mama Colin na kumsalimia. “Shikamoo ma mkwe,” kama kawaida alipiga goti la heshima mpaka chini. Mama Colin alinyanyuka alipokuwa amekaa na kumfuata Cecy na kumnyanyua alipokuwa bado amepiga magoti na kumkumbatia kwa muda huku machozi yakimtoka. Colin alishangazwa na mama yake kufanya vile aliamini alifanya vile kujitakasa mbele ya macho ya mwanaye lakini moyoni alikuwa na nia mbaya kuliko bomu la kutegwa. Alijiuliza mama yake atamwambia nini kwa kitendo cha kigaidi alichokifanya cha kusambalatisha penzi lake. “Cecy,” alimwita huku akimshika mabegani na kumtazama usoni kwa macho yaliyojaa machozi. “Abee ma’ mkwe,” Cecy aliitikia huku naye machozi yakimtoka. “Najua siku ya leo huenda hutanielewa, unaweza kuwa msichana wa kwanza kunionesha kitu si cha kawaida. Lakini nilichokifanya leo ni mtihani wangu wa mwisho kwako, nakili kwa moyo wangu katika wasichana niliowapenda ulikuwa wewe namba moja. “Lakini sikumaanisha kuwa utakuwa mke wa mwanangu kwa vile nilikuwa na Malengo makubwa kwa mwanangu baada ya kutumia kiasi kikubwa kumsomesha. Niliamini mwanamke atakayemfaa ni mwenye elimu kama yake pia anayetoka katika familia yenye uwezo ambaye atakuwa na mapenzi ya kweli na hatafuata mali aliyonayo mwanaume. “ Niliamini chaguo langu lilikuwa sahihi la kumchagua Mage kwa vile ni msomi tena anatoka katika familia yenye uwezo pia mama yake ni shoga yangu. Lakini kumbe siyo, nakiri toka moyoni mwangu mapenzi niliyokuwa nikimpenda Cecy yaligeuka na kumuona ni adui namba moja anayetaka kuvuruga ndoto zangu. “Mwanzo nilidhani utani lakini siku ya birthday ya Colin nilivyokuona ulivyopendeza mpaka kukusahau na picha nilizomkuta nazo Colin niliona ndoa hakuna. Moyo wangu ulikosa amani mpaka mipango ya harusi kwenda vizuri huku nikiwa sisikii taarifa yako. “Kwa kweli niliumia sana kwa kitendo cha Mage kuuvunja uchumba tukiwa katika hatua za mwisho. Siku zote nilikosa usingizi nimekuwa nikipungua siku hadi siku. Kitendo cha kuibuka wewe kwa kweli kilinichanganya sana, sikuamini kama una mapenzi ya kweli na mwanangu zaidi ya kufuata mali zetu. “ Mtihani niliokupa leo umenipa sababu sahihi ya mwanangu kukuchagua wewe kuwa mkewe. Cecy kitendo cha leo kilifukua mapenzi yote ya nyuma na kukiri mapenzi si elimu wala mali bali upendo wa dhati toka moyoni mwa mtu. Umenionesha jinsi gani unavyo mpenda mwanangu mapenzi ya dhati si kwa ulichonacho. “ Napenda kuwaomba radhi wote kwa kuwakwaza kwa namna moja ana nyingine. Colin mwanangu nataka kukutamkia hili mbele ya mpenzi wako na Mungu shahidi yangu kama nitakwenda kinyume naomba anifanye kitu chochote kibaya. Kuanzia leo namtambua rasmi Cecy kama mkwe wangu na mipango ya harusi itaanza mara moja. “Cecy mkwe wangu kuna zawadi nitakupa kwa kuonesha msimamo na mapenzi ya dhati kwa mwanangu naamini wewe ndiye mke aliyechaguliwa na Mungu.” Mama Colin alisema huku machozi yakimtoka, kila mmoja alitokwa na machozi, yalikuwa maneno yenye kuumiza moyo yaliyotaka moyo wa chuma kukufanya usidondoshe chozi. Colin hakuwa na la kumuuliza mama yake baada ya kila kitu kuwekwa wazi. Mama yao aliwakusanya na kuwakumbatia wote kisha aliwaachia na kutaka kupiga magoti kuwaomba msamaha lakini walimuwahi mama yao kabla hajapiga. “Hapana mama huna kosa, bali sisi ndiyo tulikwenda tofauti na mawazo yako, tunaomba utusamehe sana. Ombi letu utupe idhini toka moyoni mwako ili tufunge ndoa yenye baraka,” Colin alimwambia mama yake. “Mungu ananisikia nimeibariki ndoa yenu duniani na mbinguni.” “Ma’ mkwe, naomba usinipe zawadi yenye gharama kubwa bali kunipa mume wa ndoto yangu, inawezekana uliponiita mkwe na kunieleza nitaolewa na mwanao anayesoma Ulaya ulidhani utani. Na siku nilipomuona nilichanganyikiwa zaidi, moyoni niliamini nimeokota dhahabu katikati ya soko. “Lakini niliumia siku nilipojua kumbe kuna chagua sahihi la Colin, kuanguka kwangu si ungonjwa bali presha ilipanda na kushindwa kujizua. Niliamua kujitoa na kukaa pembeni huku nikiwa nimejikatia tamaa. Niliumia zaidi siku Mage alipomshusha Colin kwenye gari na kumdhalilisha kwa kweli japo nilikuwa sipendwi niliingilia ugomvi kwa vile chenye thamani kwenye moyo wangu nikikiona kikidhalilishwa. “Mpaka leo mama unasema maneno matamu kama haya si kwa urahisi bali nimetoka jasho la damu. Nashukuru mama mkwe, nakuahidi kuwa mke bora na kufurahia chaguo lako la awali.” Ilikuwa furaha siku hiyo iliagizwa shampeni na kufurahi kutambulika rasmi kwa Cecy katika nyumba ya kina Colin. **** Mipango ya harusi ya Hans na Mage ilikwenda vizuri, mama Mage hakuwa na haja ya kukusanya tena michango ya sherehe zaidi ya kugawa kadi za send of ya harusi ya mwanaye. Katika watu waliopelekewa kadi ya send of ya Mage ni familia ya mama Colin, tena Mage alisisitiza Colin ahudhulie send of yake. Taarifa zilifika Colin alikubali kuhudhulia kwa kujua hataumia kwani Cecy alikuwepo. Siku ya sherehe ya send of Colin na Cecy waliingia wakiwa watu wa mwisho, ilikuwa siku ambayo Cecy aliitafuta kwa udi na uvumba kuwaonesha walimwengu kuwa kila mguu hutulia kwenye kiatu saizi yake wala si kuvaa kikubwa kikakupwaya au kidogo kikakubana lakini kwake kilikuwa kimetulia. Wakiwa wamependeza Colin katika vazi la shati refu la kitambaa cha maua laini na suruali nyeusi na viatu vyeusi vilivyo chongoka kidogo mbele. Cecy alivaa gauni refu jekundu la mikanda mabegani la kitambaa chepesi na viatu virefu vilivyoongeza mzuri wake. Waliingia taratibu huku Cecy akiuweka mkono wa Colin kwapani kwake na kuushika kwa mbele. Waliingia taratibu na kufanya watu wote wageuze shingo kuwatazama wapenzi wawili walionekana kama ndiyo wamepata shahada ya mapenzi muda si mrefu. Mage alishtuka kumwona Colin akiwa amependeza sana akiwa na msichana mrembo ambaye alimsahau kama ndiye aliyempa kipigo siku alipomdhalilisha Colin. Moyo ulimlipuka na kujikuta akiingia wivu, Colin alikuwa na tofauti kubwa na Hans kimuonekana alikuwa ana mvuto kwa mwanamke yoyote. Lakini mapenzi yake Hans yakuwa makubwa kuliko kitu chochote chini ya jua. Colin pamoja na umbile na sura nzuri lakini kwake moyoni kwake alikuwa na nafasi ndogo. Naye mke matarajiwa alipendeza katika gauni la kitenge alililoshonwa kwa ustadi mkubwa na kumwongezea urembo wake. Aliamini kabisa msichana aliyechukua nafasi yake alikuwa kama maji ya bahari na yeye, kuvunja uchumba na Colin ilikuwa sawa na kuchota maji kwa kikombe ndani yake na kufanya pengo lake lisionekane kabisa. Sherehe ilienda vizuri kila mtu aliyekuwepo aliisifia jinsi ilivyofana kwa burudani iliyoandaliwa ilifanya wageni wasichoke kuwepo ukumbuni pale.Katika watu walikuwa na furaha siku ile alikuwa mama Colin baada ya kumwona mwanaye alivyopendeza akiwa na Cecy msichana aliyekuwa kama dhahabu iliyokuwa imechafuliwa na tope lakini mwanaye aliisafisha na thamani yake kuonekana mbele ya macho ya watu. Katika kitu kilichomvutia siku ile ni jinsi Cecy alivyojiamini sana, kwake lilikuwa kama jibu ambalo alitamani siku moja Mage alipate baada ya kumuacha mwanaye. Kitendo cha kuonesha mapenzi mazito kwa mwanaye kilimpa faraja kubwa moyoni mwake na kujiapiza kumpa zawadi kubwa japokuwa alionesha Cecy haitaji zawadi ambayo aliitafsiri kama hongo. Alipanga siku ya harusi ya mwanaye ampe Cecy zawadi ya nyumba ambayo ataanza kuijenga wakati wowote na zawadi ya gari la kifahari ili kurudisha shukurani kwake kumwokoa mwanaye aliyeachwa ghafla kama chuma cha moto kilichozimwa kwa kumwagiwa maji ya baridi lazima kipinde. Aliamini kitendo Mage kumuacha ghafla lazima angekuwa kwenye hali mbaya lakini yeye alikuwa wokozi wake na kulipigania penzi la mwanaye mpaka mwisho kuibuka mshindi. Kila alipoyafikiria yale na kuangali mwanaye na Cecy walivyopendeza alimshukuru Mungu kutenda muujiza. Sherehe iliendelea ilifika wakati wa Mage kwenda kumnyanyua mumewe matarajiwa alipokaa. Alinyanyuka alipokuwa na kuanza kumtafuta Hans aliyekuwa amekaa nyuma, alizunguka taratibu kwenye meza akimtafuta. Kwa vile toka Colin aingie na msichana mrembo alikuwa na hamu ya kutaka kuthibitisha uzuri aliouona kwa mbali ni kweli au cosmetic na vazi ndivyo vililompandisha chati. Alitembea taratibu kwa kumtafuta kila meza iliyokuwa na mwanaume, alikwenda hadi kwenye meza aliyokuwa amekaa Colin na Cecy. Akitembea kwa mwendo wa taratibu alisogelea karibu macho yake yakiwa kwenye uso wa Cecy. Pamoja na kupata jibu lililokuwa akiusumbua moyo wake tangu Colin alipoingia akiwa ameongozana na msichana mrembo ambaye aliamini yule msichana ndiye mrembo kuliko wote waliokuwepo pale ukumbini. Alishtuka kuiona sura ya Cecy, moyo ulimshtuka baada ya kumkumbuka ndiye aliyemshushia kipigo siku alipomteremsha Colin kwenye gari lake. Moyo ulimuuma kuona pamoja na kumpenda Colin kumbe alikuwa na msichana wa pembeni. Japokuwa sura ilikuwa yenyewe alitaka kujua jina lake kwa vile jina aliloitwa na Colin siku ile alikuwa akilikumbuka ili kupata uhakika asilimia mia. “Mambo Colin?” Mage alisimama kidogo meza ya Colin na kumsemesha. “Poa, hongera.” “Asante, huyu ndiye wifi?” “Si wifi ni mke mwenzio,” Cecy alijibu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Mmh! Anaitwa nani?” “Cecy.” “Si..si ndiye aliye ni…ni..” “Shoga ndiye mimi, wee kamtafute mumeo mengine achana nayo,” Cecy alimpa makavu huku akibinua midomo ya dharau na kumpiga busu Colin. Mage hakuwa na jibu aliondoka bila kuongeza neno akitamani kuomba Cecy aondolewe kwenye sherehe yake na kujilaumu kumwalika Colin kwani aliharibu furaha yake yote ya siku ile. Baada ya kuzunguka meza kadhaa alifika alipokuwa Hans, alimshika mkono na kufanya ukumbi ulipuke kwa furaha. Aliongozana hadi meza iliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya kukaa pamoja. Sherehe iliendelea huku zoezi la chakula likianza kwa kutangulia Mage na mumewe mtarajiwa. Baada ya maharusi watarajiwa kuchukua chakula, wengine walifuata na kurudi kwenye nafasi zao. Wakiwa katika ya chakula aliingia mwanaume mmoja mtanashati lakini mwenye mwili mkakamavu hadi kwa MC na kuzungumza naye kitu na kuonesha meza aliyokaa bibi na bwana harusi watarajiwa. Yule bwana alikwenda kwenye meza ya chakula alipokuwa amekaa bwana harusi na kumwomba wazungumze nje ya ukumbi. Hans alikitaka wazungumze pale ilibidi yule bwana amnong’oneze kitu. Ghafla Hans alikuwa mpole na kumwambia Mage. “Samahani mpenzi nakuja.” “Kuna nini?” Mage alishtuka. “Nakuja sasa hivi.” “Fanya haraka bwana.” “Poa.” Hans alijibu kwa mkato na kuongozana na yule mtu hadi nje ya ukumbi, alipofika nje alielekezwa gari la kuingia lilikuwa limesimama pembeni ya ukumbi. Alipofungua mlango na kukaa alikutana na pingu huku akiambiwa. “Tuna imani kosa lako unalijua?” Hans hakujibu alikaa kimya, baada ya kutojibu askari alimuuliza swali lingine. “Unamjua huyu?” Alioneshwa kijana mmoja aliyekuwa amemekaa pembeni yake ameinamisha kichwa. Alipomwangalia vizuri alimkumbuka na alishtuka na kujisema moyoni. “Nimekwisha.” Hans alichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi. Alipofika aliingizwa chumba maalumu kwa ajili ya mahojiano. Kila aliloulizwa kuhusiana na kuhusika na njama za kuuawa mkewe na mwanaye alibakia bubu, baada ya kubana sana alikubali kuhusika kwa namna moja japo yeye hakuua. Nyuma sherehe iliendelea huku Mage akiamini mchumba wake atarudi wakati wowote, baada ya muda bila kuonekana ilibidi aulize kuhusu mchumba wake. Mara moja walianza kufuatilia, kwa kumuuliza rafiki kipenzi cha Hans, Ndubikile ambaye alikuwa amekaa bila kujua nini kinaendelea. Hata yeye alishtuka sana na kuamua kupiga simu yake ambayo ilipokelewa na mtu mwingine. “Haloo una shida gani?” “Samahani nina imani napiga namba ya Hans?” “Ndiyo.” “Mwenye simu yupo wapi?” “Yupo kituo cha polisi cha kati.” “Ha! Amefanya nini?” “Ukifika kituoni utajua kila kitu.” “Sawa.” Baada ya kukata simu aliwageukia waliokuwa wakitaka kujua kutoweka ghafla kwa Hans. “Jamani waliomchukua hapa ni askari ambao wamempeleka kituoni cha kati.“ “He! Kwa kosa gani?” waliuliza wote kwa mshangao. “Wamesema tufike kituoni tutajua kila kitu.” Ilibidi watu watumie busara na kuficha kilichokuwa kikiendelea na kumdanganya Mage ili shughuli isivurugike kwa kumwambia Hans amekimbilia hospitali mdogo wake kapata ajali. Wakati sherehe ikiendelea familia ya Hans ilipewa taarifa zile nayo iliondoka kufuatilia kituoni. Walipofika walielezwa kuwa Hans anashikiliwa na polisi kwa kosa la kupanga mauaji ya mkewe na mwanaye. Wote walishtuka na kutaka isibitisho wa habari zile, walielezwa jinsi walivyofuatilia mauaji yale taratibu mpaka kuwakamata wauaji ambao walijitetea kutumwa na Hans ili aweze kumuona mpenzi wake wa zamani. Waliomba kukutana na Hans, walikutana naye na kutaka kujua habari zile zina ukweli wowote. “Wazazi wangu hakuna ukweli wowote, haiingii akilini nimuue mke wangu na mwanangu kwa ajili ya mwanamke.” “Basi mwanangu haki itapatikana, nina imani mpaka kunakucha utakuwa umetoka nje,” baba Hans alimpa moyo mwanaye ambaye moyoni alijua kila kitu kinachoendelea. Kuondoka ghafla kwa familia ya Hans ilizidi kumshtua Mage na kujikuta akikata kususa sherehe. Ilibidi achukuliwe na kupelekwa pembeni na kuelezwa ukweli kuwa mpenzi wake kachukuliwa na polisi. Aliomba kupelekwa kituo cha polisi ili akamwone mpenzi wake kwa kuamini kupitia kwa rafiki wa baba yake mkuu wa polisi atatoka. Alifikishwa kituo cha polisi na kupelekwa chumba alichokuwemo mpenzi wake na kuonana naye. Mage akiwa amechanganyikiwa macho yakiwa yamemvimba kwa ajili ya kumlilia mpenzi wake ambaye hakujua yupo pale kwa kosa gani. “Vipi mpenzi kuna nini?” “Mmh! Mambo magumu.” “Kivipi?” “Ile ishu imebumburuka.” “Ishu gani?” “Off air” “Mungu wangu! Sasa itakuwaje?” “Sijui, lakini naamini imekaa vibaya kwa vile kuna ushahidi mkubwa wa kunimaliza naamini siwezi kutoka.” “Kwa nini?” “Kila kitu kipo wazi lazima nitaozea gerezani.” “Sasa harusi yetu itakuwaje?” “Mmh! Itategemea muujiza wa ngamia kupita katika tundu la sindano.” “Yupo ba’ mkubwa naamini utatoka tu,” Mage alimtia moyo mpenzi wake. “Nami ndicho ninachokiomba.” “Hebu subiri.” Mage alichukua simu na kumpigia baba yake mkubwa mkuu wa polisi mzee Clarence. Baada ya kuita ilipokelewa upande wa pili. “Haloo.” “Haloo baba,” Mage alisema kwa sauti ya kulia. “Vipi mama, mbona unalia?” “Baba mchumba wangu amechukuliwa kwenye send of yangu na kuwekwa ndani.” “Kwa kosa gani?” “Hakuna kosa lolote zaidi ya uonevu.” “Naomba kuzungumza na mkuu wa kituo.” “Sawa baba.” “Mpenzi nimeisha zungumza na baba utatoka sasa hivi ngoja nipeleke simu kwa mkuu wa kituo,” Mage alimueleza mpenzi wake huku akielekea kwa mkuu wa kituo. “Hakuna tatizo.” “Samahani kaka kuna simu kutoka kwa mkuu anataka kuzungumza na mkuu wa kituo,” alimwambia askari mmoja aliyekuwa kaunta. “Mkuu gani?” “Mkuu wa polisi wote.” “Nenda chumba cha pili mkono wa kushoto.” Mage alikwenda hadi mlangoni na kuingia bila hodi kitu kilicho mkasirisha mkuu wa kituo na kutaka kumfukuza. “We binti toka nje unaingiaje kama msalani.” “Kuna simu yako toka kwa mkuu wako unatakiwa kuzungumza naye.” “Mkuu gani?” “IGP.” “He! Nipe,” mkuu wa kituo Aloyce Jacob alishtuka na kuichukua simu haraka aliweka sikioni na kusema kwa sauti ya juu. “Samahani afande.” “Bila samahani pole na majukumu.” “Asante mkuu.” “Kuna kijana mmemkamata usiku huu akiwa kwenye send of ya mchumba wake?” “Ndiyo mkuu.” “Kwa kosa gani?” “Lile la mauaji tulilokuwa tukipeleleza.” “Sasa yeye anahusika vipi?” “Ndiye mtuhumiwa mkuu.” “Una uhakika?” “Kila kitu kipo wazi, kesho faili lake tunaifikisha mahakamani.” “Nipe huyo binti.” Simu alipewa Mage aliyekuwa akifuatilia mazungumzo ambayo yalimtisha na kuona tatizo la mpenzi wake lilivyo zito lakini aliamini kupitia wadhifa wa baba yake mkubwa lazima ataachiwa tu. “Haloo baba.” “Sasa mama suala la mpenzi wako lipo kisheria sana, hivyo nakuomba rudi nyumbani ili vyombo vya dola vifanye kazi yao.” “Sasa baba harusi yangu itakuwaje?” “Naomba urudi nyumbani kesho nitakuja.” “Sawa baba.” Mage alirudi kwa Hans kumweleza alipofikia, Hans aliamini hali ilivyo kulikuwa hakuna dhamana mpaka upelelezi ukamilike. Aliamini ukikamilika lazima utamtia hatiani na kufungwa. Ilibidi Mage arudi nyumbani kwao akiwa amechanganyikiwa kutokana na tukio lile aliamini ndoa hakuna na atakuwa amepoteza mwana na maji ya moto. Kwa vile sherehe ilimalizwa alirudi nyumbani. Mama yake naye aliona sherehe ya mwanaye imeingia nuksi alitaka kujua kipi kilichompeleka mchumba wake polisi. “Si lile tatizo lililoniweka ndani.” “La kifo cha mke wa Hans?” “Ndiyo.” “Sasa yeye anahusika vipi?” “Eti kahusika kumuua mkewe.” “He! Ili iweje?” mama Mage alishtuka kusikia habari zile. “Mimi sijui, eti mama mtu akishtakiwa kwa kosa la kupanga mauaji hukumu yake ipo vipi?” “Kama hajatenda hawezi kufungwa lakini kama kweli amehusika hukumu yake ni miaka 30 au maisha.” “Mungu wangu nimekwisha!” Mage alisema kwa sauti ya kukata tamaa. “Mbona unasema hivyo?” “Mashtaka ya Hans ni ya kupanga njama za kifo cha mkewe.” “Sasa wasiwasi wako nini ikiwa haimuhusu, nitampigia simu baba yako mkubwa yataisha.” “Mama nilizungumza na baba na kutaka kuzungumza na mkuu wa kituo baada ya mazungumzo aliniambia mashtaka yapo kisheria hivyo tuache vyombo vya dola vifanye kazi yake.” “Mmh! Kama baba yako kasema hivyo itabidi tuwe watulivu.” “Mama nina wasiwasi huenda harusi yangu haipo.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Kwa nini?” “Nina wasiwasi mpenzi wangu atafungwa.” “Kwa nini unasema hivyo?” “Hata sijui, mama hivi nikimfuata Colin atakubali kweli kunirudia?” “Mage umefikiria nini tena mama! Kwa nini umefikia huko, mchumba wako yupo ndani na hana kosa asilotenda atatoka tu.” “Sasa tutafanyaje?” Mara simu ya Mage iliita ilikuwa ikitoka kwa mama Hans, alichukua na kuiweka sikioni. “Haloo mama.” “Nina imani sasa imefurahi.” “Nifurahi nini mama?” “Haya sasa mwanangu anafungwa kwa ajili yako, haya fanya sherehe kwa vile dhamira yako imetimia, imekuwa kama jini wa kutumwa humuachi mtu mpaka uone amefukiwa. ” “Mama utanionea bure.” “Tunashukuru ila Mungu yupo,” baada ya kusema vile alikata simu na kumuacha Mage kasimama kama sanamu kitu kilichomshtua mama yake. “Nini tena?” “Mama huu mkosi gani?” Mage alisema huku akilia. “Kwani kuna nini tena mwanangu mbona unatakaa kuniuguza presha?” mama yake alitaharuki. “Siamini maumivu ninayosikia juu ya mpenzi wangu kuwekwa ndani na kubambikiwa kesi nzito halafu familia yake inasema eti nimefurahi! Mimi Mage nifurahi kufungwa kwa mpenzi wangu?” Mage alimuuliza mama yake huku akibubujikwa na machozi ya uchungu. “Nani amekuambia hivyo?” “Mama Hans.” “Unaona mwanangu ile siyo familia badala ya kukuonea huruma ndiyo kwanza wanakulaumu, ufanye vile ili iweje ungeweza kuvuruga ndio yako kama mtu humpendi.” “Mama nakuapia Hans akinioa sitaki kuwaona ndugu wa mume.” “Mage mwanangu hayo siyo maneno, bado tunataka kuonesha upendo kwa wenzetu kipindi hiki kigumu.” “Mama wakati Hans yupo ndani nataka kuzungumza na Colin naamini ananipenda sana.” “Ukiisha zungumza naye?” “Ili nikamate huku na huku kama Hans atafungwa basi niwe na Colin.” “Na Hans akitoka gerezani na kukuta umeolewa?” “Nitajua, nina imani Colin nammudu, nitamweleza ukweli kuwa kwake nilikuwa najiegesha na nimpendaye karudi. Mbona anajua kuwa kwa Hans nimekufa nimeoza.” “Mage kumbuka ukianzisha uhusiano na Colin mpaka kufikia kufunga ndoa lazima watu watasema umehusika kumfunga mpenzi wako hapo ndipo utaongeza uhasama na familia ya kina Hans.” “Nitafanya kwa siri.” “Colin akitaka kukuoa?” “Nitamvuta kwa muda ili kumsubiri Hans, kama anafungwa maisha sina jinsi kama miaka saba nitajishikiza kwa Colin.” “Ulivyomuacha atakukubali kweli, ha..ha..lafu leo kaingia na msichana mrembo ni nani yake?” “Mpenzi wa rafiki yake,” Mage aliongopa. “Mmh! Ili kutengeneza mazingira mazuri unatakiwa kujipendekeza kwa mama Colin.” “Nitafanya hivyo, najua yule mama ananipenda sana nikimfuata na kumweleza nimerudi kwa mwanaye nina imani atapiga vigelegele.” “Mmh! Haya.” Mage aliachana na mama yake na kwenda chumbani huku mawazo yake yote yakiwa kwa Colin kutokana na kuujua ukweli wa kesi ya Hans kwa kuamini kutoka kutakuwa muujiza. Alipanga kuanza kujipendekeza kwa familia ya kina Colin wakati akisubiri hukumu ya mpenzi wake. **** Colin alimpeleka Cecy chuo cha urembo ambako alisoma kwa miezi mitatu, muda wote walikuwa kama kumbikumbi kila mmoja alionesha mahaba mazito. Taarifa ya kukamatwa mchumba wa Mage iliwafikia na kushagaa taarifa ya kukamatwa kwake kuwa alihusika na kifo cha mkewe na mwanaye ili tu amuoe Mage. “Colin yaani naomba kama mama yako atasababisha tutengane usifanye kama mpenzi wa Mage alivyofanya. Heshimu uhai wa mtu, kama ipoipo tu, Mungu ana maajabu yake ameweza kutukutanisha pamoja bila sisi wenyewe kujua. Kwa hivyo ni makosa kulazimisha kitu.” “Cecy kila dakika nakuwa mwanafunzi wako, wewe ni zaidi ya mwanamke pamoja na umri mdogo lakini Mungu amekupa busara na hekima.” “Kama ni kweli mpenzi wa Mage anahusika kutenda unyama ule kwa ajili ya Mage atakuwa ametenda dhambi kubwa sana.” “Mi’ siamini mtu anaweza kumuua mke na mwanaye kwa ajili ya mpenzi wake.” “Kwa hiyo ungemuoa Mage, mimi ningekuwa na nafasi gani moyoni mwako?” Cecy alimuuliza swali la kizushi. “Cecy tuachane na hayo, unakumbuka wiki ijayo ndiyo onesho lako la kwanza la mavazi, mazoezi yako yamenipa matumaini ya kuishtua dunia.” “Mmh! Nitafunikaje maana nguo zote nilizojipima hadi mwenyewe najione wivu, si vibaya kujisifia mi’ mzuri bwana.” ”Siyo mzuri bali mrembo,” Colin alimrekebisha. “Bwana eeh, urembo unatengenezwa lakini uzuri ni wa asili.” “Sawa mama umeshinda.” Wiki moja baadaye liliandaliwa onesho la kwanza la mavazi la kampuni ya Colin litakalo ongozwa na Cecy. Matangazo yalirushwa mwezi mzima katika vyombo vyote vya habari na kufanya watu wengi wavutike na kuapa kutolikosa. Miongoni mwa watu walipanga kwenda kwenye onesho hilo la kwanza la kimataifa alikuwa ni Mage na shoga yake Brenda. Washiriki walikuwa wengi kutoka ndani na nje ya nchi na kufanya onesho lile lizidi kuvutia watu wengi. Siku ya onesho ilipowadia Mage na shoga yake Brenda walikuwa miongoni ma watu waliohudhulia onesho hilo lililojaza watu wengi. Muda ulipofika maonesho yalianza kwa kuanza kupita wageni ambao walionesha mavazi ya kigeni na kuwafanya watu walipuke mayowe. Baada ya kumaliza wageni lilianza vazi la Kitanzania kuanzia vazi la vitenge, khanga na vikoi.Walianza kutangulia mabinti ambao nao walikuwa katika kampuni hiyo. Baada ya kupita wote ikafika kipindi akatokea Cecy katika vazi la kitenge chenye kilemba kirefu na kufanya ukumbi ulipuke mayowe. Alipita na mavai zaidi ya kumi ya ubunifu na kuacha historia kwenye onesho lile. “Mage huyu si yule msichana aliyeingia na Colin siku ya Send of yako?” Brenda aliuliza baada ya kumfananisha Cecy. “Ndiye yeye.” “Mage tuache utani msichana huyu mzuri tena ana uzuri wa asili,” Brenda alimsifia Cecy. “Hana lolote uzuri upo wapi?” Mage aliponda. ”Wivu huo, kwenye ukweli uongo hujitenga, yule msichana mzuri.” “Brenda tutakorofishana tumekuja kuangalia mavazi au kuja kumsifia mtu, kwanza mavazi aliyovaa ya kishamba nani sasa hivi anavaa mavazi ya khanga na kitenge. Angejua wala hakupendeza lolote,’ Mage alimbeza Cecy. “Mageee! Siamini kama una nafasi katika moyo wa Colin, kitu kama hiki hata mimi nikimuona yupo na mpenzi wangu lazima nipate presha,” Brenda alizidi kumuumiza roho shoga yake. “Brenda naona umetumwa kuja kuniumiza roho, kosa langu kuja na wewe pamoja?” Mage alikuja juu. “Lakini Mage kwani nikimsifia yule mwanamke kuna ubaya gani ikiwa wewe ni mchumba wa mtu na Colin si mtu wako?” “Unajuaje kama nitarudiana na Colin.” “Mrudiane kivipi ikiwa wewe utaolewa na Hans na Colin anaweza kumuoa huyo msichana.” Wakiwa katikati ya onesho Colin ambaye alifahamika kama mkurugenzi wa kampuni ile ya urembo na mavazi alifuatwa na watu wenye majarida ya urembo kumtaka Cecy kwa ajili ya kuyapamba majarida yao kwa sura yake kwa mkataba mnono. Pia makampuni mengine ya Afrika ya kusini na Ufaransa ambao walikuwa wageni waalikwa walivutiwa Cecy na kuomba kufanya naye kazi kwa mkataba mnono. Nyota ya Cecy ilizidi kung’aa, Colin aliwakubalia lakini walitakiwa waonane kesho kwa ajili ya mazungumzo zaidi, walikubaliana. Siku ile pia ilikuwa maalumu kwa Colin. Wakati burudani ikiendelea Mc alisimamisha kwa ili mkurugenzi aseme neno. Colin alichukua kipaza sauti na kuwasalimia wote kisha alisema: “Ndugu zangu kwanza nashukuru kwa muitikio katika onesho la leo ambalo limekuwa na mafanikio makubwa tofauti na nilivyofikiria. Mpaka sasa tumepata naombi ya kumtaka Malkia Cecy kupamba majarida na pia kwenda kufanya maonesho Afrika ya kusini Marekani na Ufaransa,” kauli ile ilifanya ukumbi ulipuke kwa mayowe. “Lakini hilo silo lililonifanya nimnyang’anye kipaza sauti Mc, nia yangu nilikuwa nimeweka ahadi moyoni mwangu siku ya leo nifanye kitu gani. Naomba nimwite malkia wa usiku wa leo Cecilia hapa mbele.” Cecy alitoka chumba maalumu akiwa na gauni refu jekundu lililokuwa likiburuza kwa nyuma, lililokuwa limempendeza sana kama bi harusi. “Ndugu zangu, wazazi wangu na wageni waalikwa katika onesho hili la kwanza la kimataifa. Leo ndiyo namtambulisha kwenu wakili wa moyo wangu binti mrembo Cecy kuwa ndiye mke wangu mtalajiwa,” ukumbi ulilipuka tena kwa mayowe. Colin aliendelea kwa kujipapasa na kutoa mkebe mdogo na kusema: “Cecy mpenzi fumba macho,” Cecy alifanya vile. Colin alitoka pete ya tanzanite iliyochanganywa na almasi na kukishika kidole cha Cecy na kumvisha na kufanya ukumbi wote kulipuka kwa mayowe kila mtu akisema kuwa kila mmoja kampata mwenzake. Lile lilikuwa pigo mujarabu kwa Mage aliyekuwa na ndoto za kurudi kwa Colin kama Hans atafungwa. Mapigo ya moyo yalianza kumwenda mbio na jasho kumtoka kwa wingi, kizungumzungu kikali kilimshika na kiza kinene kilitanda mbele yake na kumfanya adondoke alipokuwa amekaa. Alichukuliwa haraka kwenda kupewa huduma ya kwanza kwa vile pale ukumbuni kulikuwa na kila kitu. Shughuli ilendelea kwa Mc kulitangaza vazi jipya la wachumba siku ya kuvishana pete lililompendeza vilivyo Cecy. Baada ya onesho yale Colin alijiandaa kuingia mkataba mnono wa Cecy na hayo makampuni. *** Cecy aliingia mkataba wa mamilioni ya fedha ya miaka miwili kwa makampuni mawili ya majarida makubwa Marekani moja la Vibe na Ebony kwa ajili ya kupamba ukurasa wa mbele pia aliingia mkataba mnono wa kampuni ya maonesho ya mavazi ya Ufaransa ambayo yabadili maisha ya Cecy toka umaskini wa kutupa mpaka msichana bilionea. Baada ya kuingia mkataba mnono uliomtaka aanze kazi hiyo mwezi mmoja baadaye kwa ajili ya mazoezi ya mwezi mmoja na kujifunza lugha vizuri kabla ya kuianza kazi hiyo mara moja. Cecy aliomba kuzungumza kwanza na familia yake pamoja na mpenzi wake Colin ili ajue ataanza lini kazi yake, walikubalia na kumpa siku mbili za kutoa jibu ili wakiondoka wajipange vipi. Ilikuwa tofauti na mapokeo ya Cecy baada ya kulala maskini na kuamka tajiri mkubwa. Ndoto yake ilikuwa kuolewa na Colin na si kufanya kazi ya mabilioni, alijiuliza kukaa miaka mwili nje ya nchi lazima Colin atatafuta mwanamke mwingine na yeye kupoteza kitu muhimu maisha zaidi ya fedha atakazolipwa katika kazi yake. Kwake alichokitafuta kilikuwa kuwa karibu na Colin na kufanikiwa kuwa naye karibu na kubakia kitu kimoja ndoa ambayo aliiota siku zote. Baada ya kuachana wa wenye makampuni toka nchini za nje. Cecy alionekana mtu mwenye mawazo tofauti na kitu alichokipata cha kugeuka bilionea kwa kufanya onesho lake moja na kuonekana. Baada ya kufika nyumbani ilibidi amuulize: “Vipi mpenzi wangu mbona kama hauna furaha wakati leo umeuaga umaskini?” “Mi kwangu naona kama ndiyo unataka kuniongezea umaskini,” Cecy alijibu kinyonge. “Kivipi?” “Hivi nikiwa huko tutakuwa pamoja?” “Hapana ila tutaonana mara chache kwa vile utakuwa bize na kazi yako ya kuizunguka dunia kufanya maonesho.” “Uoni kama nitakuwa nimepata fedha zisizo na faida kwangu.” “Kivipi?” “Colin wewe ni kila kitu kwangu, niliapa kuwa mbali na wewe ni pale mmoja wetu akichukuliwa na umauti na si vinginevyo.” “Hilo tu, nitakuwa naonana na wewe kila mara wala usihofu.” “Colin nina wasiwasi nikiwa mbali kuna vipanga watu watakunyakuwa na mimi kuichukia dunia, kukupata nimetoka jasho la damu. Furaha yangu ni kuwa karibu yako na si kuingiza mamilio ya fedha.” “Najua mpenzi unanipenda lakini hili dili ni zaidi ya mapenzi kwa vile litayabadilisha maisha yako sasa hivi una uwezo wa kujenga gharofa Masaki au Kunduchi.” “Colin mimi huko siendi na hizo hela zao sizitaki.” “Usifanye hivyo, ukilipoteza hutakuja kujuta maisha yako yote.” “Moyo wangu naujua hauna shida ya mabilioni ya watu bali upendo toka kwako, pia naona umekwenda kinyume na makubaliano yetu.” “Kivipi mpenzi?” “Ulisema unataka kunifungulia kampuni ili niwe nafanya maonesho na si kwenda kufanya kazi nje ya nchi.” “Mpenzi, yaani dili ulilopata fedha utakayoipata kwa miaka yote hiyo unaweza kukaa bila kufanya kazi na kuishi maisha ya juu.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Sina maana hiyo, uliniahidi baada ya kumaliza masomo unanioa sasa ahadi yetu ipo wapi? Au ndiyo unanitoa kijanja urudiane na Mage baada ya mpenzi wake kufungwa?” Cecy alilia wivu. “Ahadi yetu ipo palepale, we fanya kazi mwaka mmoja kisha tunafunga ndoa ndipo nitajua nitafanya nini.” “Cecy mpenzi hujui tu kiasi gani cha fedha utakacholipwa, ni wasichana wachache dunia wenye bahati hii. Tukitaka tufanye harusi itachukua muda wakati mwezi ujao unatakiwa Afrika ya Kusini kwa mazoezi ya wiki mbili kabla ya kwenda Ufaransa. Kutokana na makubaliano picha za jarida la Ebony watatumia za kwenye onesho na zile walizokupiga siku ile. Malipo yako ya kwanza yataingia mwezi ujao ya dola elfu mia mbili arobaini(408,000,000) kwa mwaka. Baada ya mwaka malipo yataongezeka na kuwa dola elfu mia tatu (510,000,000). Pia utapata bonas ya asilimia tano kutokana na mauzo huoni kwa miaka miwili utakuwa mbali mpenzi wangu kwa kutengeneza dola elfu mia tano arobaini (918,000,000). Bado kampuni ya maonesho itakulipa dola elfu mia tatu (510,000,000) kwa mwaka na bonasi kila onesho la nchi kubwa barani Ulaya na Amerika. Unataka nini tena mpenzi wangu, kipindi hiki hebu ndoa iweke pembeni tupige pesa.” “Colin nakuona kama unampigia mbuzi gitaa, nakueleza kwa mara ya mwisho pesa inaweza kununua kitu chochote chini ya jua lakini si furaha ya moyo wa mtu dawa ya mtu ni mtu si kitu.” “Mmh! Sasa wewe ulikuiwa unatakaje?” “Kwanza tuoane kisha tutajua kama kwenda au kufanyia kazi hapa lakini si kukaa mbali na wewe.” Ulikuwa mtihani mzito kwa Colin kutokana na msimamno wa mpenzi na kuliona kama dili lile litapeperuka kwani walikuwa wapo wapo nchini wakisubiri kauli yao ataanza lini kufanya kazi. Lakini kwa Cecy alikuwa haelewi kitu bado ya kutetea ndoa yake pia kuwa karibu na mpenzi wake kwa kuogopa vibaka vya wapenzi wa watu.Jioni ya siku ile Colin alikutana na mama Cecy na kumuelezea hatua waliyofikia na uamuzi wa Cecy. “Mama nilikuwa naomba umweleze mwenzangu akubali kwanza kwenda kufanya kazi ndoa itafuata baadaye.” “Mmh! Nitajaribu kumweleza, nina imani atanielewa.” “Yaani nitashukuru sana, sijawahi kuona mwanamke mwenye msimamo kama Cecy.” Kwa vile Cecy alikuwa amekwenda kuoga aliporudi alikaa pembeni ya mama yake na kumuacha Colin aliyekuwa amekaa kochi la peke yake. Baada ya ukimya mfupi mama Cecy aliuvunja ukimya ule. “Cecy mama.” “Abee mama.” “Nina imani leo Mungu atuangazia maisha yetu?” “Ni kweli mama, lakini maisha hayatakuwa na furaha bila kutimiza ndoto yangu.” “Najua una hamu ya kutimiza ndoto yako, lakini kilichotokea ni muhimu kwa wakati huu ndoa yako ipo palepale.” “Hilo nalijua, siku zote fimbo ya mbali haiuwi nyoka, kama nitaanza kazi naweza kukaa hata miezi mitatu bila kumuona Colin na wakati penzi langu limenitoa jasho la damu. Naweza kupata fedha lakini nikapata jeraha lisilopona mpaka nakufa na pengine likawa ndio sababu ya kifo changu.” “Kwa nini unasema hivyo?” “Mama kama unavyojua mchumba wa Mage yupo ndani na kesi yake ni nzito, kwa habari za juujuu kweli anahusika katika vifo vya mkewe na mwanaye ili arudiane na Mage. Kwa hiyo uwezekano wa kutoka ni mdogo huoni muda huo nikiwa mbali na Colin penzi linaweza kuzaliwa upya na nafasi yangu kupotea. “Kama nilijitoa kwa ajili ya Colin ifike wakati nimkose hizo fedha zitakuwa na faida gani kwangu. Nipo tayari kupoteza hata fedha zilizojaa bahari lakini si kumpoteza Colin, moyo wangu ndiyo unaojua thamani yake si yeyote. Mama hujui kiasi gani niliumia niliposikia Colin akioa lakini machozi yangu hayakwenda bure, Mungu alisikia kilio changu na kunirudishia mpenzi wangu mikononi mwangu na kuamini haki ya mtu huwa haipotei bali hucheleweshwa.” “Sasa kama unafahamu hivyo kwa nini una wasiwasi na Mage?” “Mama, Golden chance never came twise.” “Hapo umeniacha feri una maanisha nini?” “Kwangu hii ni nafasi ya dhahabu kamwe haijirudii mara mbili.” “Cecy nakuahidi wewe ndiye mwanamke wa maisha yangu, nilivyofahamu thamani yako ndani ya moyo wangu upengo wangu uliongezeka mara dufu. Cecy wewe ndiye wakili wa moyo wangu uliyenitetea wakati wa matatizo hakuahidi sitamfungulia mwanamke mwingine moyo wangu nilipokufungia moyoni mwangu ufunguo niliutupa baharini,” Colin alimuhakikishia mapenzi yake ya dhati kwake. “Colin ufunguo kuutupa baharini ni usemi tu lakini mnasahau ufunguo unaweza kumezwa na samaki na kuurudisha watu wakauokota na kuufunguo moyo wako na mimi ukanitoa moyoni mwako. Colin unanipenda?” Cecy alimuuliza Colin huku amemkazia macho. “Zaidi ya sana na kama kuna kauli nyingine zaidi ya hiyo ungeijua ningeisema mbele yako.” “Naomba unioe.” “Nitakuoa kwa vile wewe ndiye mwanamke wa maisha yangu.” “Si kwa wakati mnaotaka ninyi bali kabla ya kuanza kazi yangu nataka nikisimama sehemu nijulikane kama mrs Colin na si miss Cecy.” “Muda tuliopewa ni mdogo sana wa maandalizi ya harusi, hivyo ungekwenda kufanya kwanza kazi kisha ukirudi tutafunga ndoa utakuta maandalizi tayari ukifika tunafunga ndoa na kuondoka.” “Kwani kazi si naanza mwezi unaokuja huu muda hatuwezi kufunga ndoa?” “Cecy wewe sasa si Cecy muuza ndizi bali wa kimataifa kwani wiki ijayo sura yako inaruka dunia nzima kwenye Jariba la Ebony harusi yako haitakiwi ya kulipua bali iendane na wewe mwenyewe.” “Mimi Cecy hata niwe vipi bado nitabakia Cecy muuza ndizi, kwa hiyo kama mna nia nifanye kazi tufunge ndoa ya kawaida ila sherehe nikirudi zaidi ya hapo kazi yenyewe siitaki na msiambie kitu kinachohusu hiyo kazi. Fedha inatafutwa kwa njia yoyote lakini upendo kwa kweli ni adimu kama maji jangwani. “Naweza kumsifu Mage kwa kuvunja uchumba wetu si kwanza nimepata nafasi bali amezieleza hisia zake za kweli toka moyoni kwake kuwa kuna mtu aliyekuwa akipenda kwa dhati. Kosa walilofanya kuua viumbe wasio na hatia lakini walikuwa wapo sahihi kabisa. Kama mliona Mage yupo radhi kulaaniwa na dunia kwa ajili ya mapenzi basi na mimi nipo tayari kufa maskini kwa ajili ya mapenzi,” Cecy alisema kwa sauti kavu isiyo na mzaha hata kidogo. “Mmh! Mwanangu Colin mpaka hapo mimi sina neno siku zote mwenye kujua maumivu ya moyo ni mhusika, wengine ni washauri na mwisho wa siku ana uamuzi wa kukubali au kukataa anabakia nao mwenyewe na mwenzio amekataa,” mama Cecy hakuwa na kuongeza baada ya kauli ya mwanaye. “Mama nimesikia yote nitayafanyia kazi, najua kabisa Cecy ananipenda na ameteseka juu yangu. Nimemuhakikishia yeye ndiye chaguo la moyo wangu na mwanamke wa maisha yangu kwa vile moyo wake imeingia wasiwasi basi nitafanya anavyotaka mpenzi wangu ili aamini mbegu yake ya upendo imemea kwangu na kuzaa matunda.” “Hilo ndilo neno nililokuwa nikilisubiri usiku na mchana, najua hukupenda maamuzi yangu lakini utaamini siku moja kwa nini nimeharakisha harusi.” Baada ya makubaliano ya kufunga ndoa kabla ya kwenda kuanza kazi, Colin alikwenda kwa mama yake kumweleza taarifa ya Cecy kupata mkataba mnono na kutakiwa kwenda kufanya kazi nje na alivyong’ang’ania kuolewa kuliko kufanya kazi. Alipofika nyumbani alimkuta mama yake amekaa sebuleni, alimsalimia na kukaa pembeni yake. “Vipi baba, una jambo?” mama yake alimuuliza kwa vile alifahamu vizuri mwanaye. “Ndiyo mama.” “Ehe,” mama yake aliweka vitu vyake chini na kugeuka amsikilize vizuri mwanaye kwa vile kila kukicha alikuwa na jakamoyo. Hasa baada ya ndoa ya mwanaye na Mage kuvunjika katika hatua za mwisho. Colin alimweleza mkataba alioingia Cecy na makampuni yote ambayo yalimuacha mama yake kinywa wazi kufikia hatua ya kusema. “Yaani Cecy muuza ndizi alipwe mamilio ya fedha kwa kazi ya kupamba jarida na kuonesha mavazi huoni atakutana na watu wengi wenye fedha na wewe kumkuacha. Kwa nini umemtafutia kazi kama hiyo wakati shida yako ilikuwa awe mkeo kwa vile hatuna shida katika maisha yetu.” “Mama, yote hayo tisa kuna kitu Cecy kanichanganya sana yaani mpaka kichwa kinaniuma,” Colin alisema kwa sauti ya unyonge. “Kitu gani? Nilijua lazima uhusiano wenu utaingia dosari pesa atakazolipwa ni nyingi sana hasa akizingatiwa alikuwa hohehahe,” mama Colin alichangia bila kujua anataka kuambiwa nini. “Sivyo unavyofikiria, mama Cecy anataka ndoa kabla ya kwenda kuanza kazi.” “He! Si umesema mwezi ujao anatakiwa kuondoka?” “Ndiyo, lakini yeye amesema bila ndoa na kazi hataki.” “Mbona sikuelewi hataki kazi kwa ajili ya ndoa?” “Ndiyo mama, anataka akiondoka hapa awe tayari mke wangu.” “Kwa nini anafanya haraka hivyo, kwa nini asiende kwanza kisha arudi kufunga ndoa wakati huo maandalizi yatakuwa yamekamiliksa anaolewa na kuondoka.” “Amekataa, amesema nikimlazimisha kwenda na kazi yenyewe hataki.” “Kweli elimu ni muhimu. Yaani anataka kuyakataa mamilioni kwa ajili ya ndoa tu?” mama Colin alishangaa. “Mama Cecy ni tofauti na wanawake wengi, mimi kwake ni kila kitu hasikii wala haoni anasema anaweza kuondoka huku nyuma Hans akafungwa hivyo naweza kurudiana na Mage na yeye kupoteza alichokitafuta muda mrefu. Yupo radhi kuendelea kuuza ndizi lakini si kunikosa mimi.” “Mmh! Kazi ipo, sasa utafanyaje?” “Nilikuwa naomba ushauri wako japo nilimkubalia kufunga naye ndoa kabla ya kuanza kazi.” “Ninafikiri wazo lako zuri, japokuwa sikupenda harusi ya aina hiyo, lakini kwa vile naujua msimamo wa yule msichana sina budi kukubaliana nawe. Sijawahi kuona mwanamke msimamo mkali kama yule binti. Anajiamini katika kitu anachokitafuta hasa akiwa na haki nacho.” Walikubaliana kufanya maandalizi ya harusi kwa kuandaa vikao vya wiki tatu, wiki ya nne inakuwa harusi. *** Baada ya upelelezi wa kesi ya Hans kupanga njama za kifo cha mkewe na mwanaye kukamilika ilisomwa hukumu katika mahakama kuu. Siku hiyo walijaa watu pomoni kutaka kusikiliza nini kitakacho amuliwa juu ya tuhuma za Hans kumuua mkewe. Baada ya jaji kukaa kwenye kiti chake na watu wote kukaa chini alitulia kupanga kalatasi zake vizuri kisha alikohoa kidogo kuwafanya watu wote wakae tayari kumsikiliza wakiwemo Mage, mama yake shoga yake Brenda, familia nzima ya Hans pia alikuwepo mama Colin, Colin na mchumba wake Cecy. Watu wote walitulia kumsikiliza jaji huku mioyo ikiwadunda wakiomba utokee muujiza utakao badili damu kuwa maji meupe. Kwa sauti yenye kusikika alisema:CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Nina imani wote uliopo hapa mnajua tupo hapa kwa sababu gani, leo ndiyo siku tunayo hitimisha kesi inayomkabiri Hans Simgao ambaye anakabiriwa na kesi ya mauaji iliyochukua takribani mwezi mzima na leo ndiyo siku ya hukumu yake. Kama kawaida kesi hii ilianza kusikiliza mahakama ya mwanzo ambayo haikuwa na uwezo wa kuhukumu na kuamuliwa kuletwa huku mahakama mkuu yenye uwezo wa kutoa hukumu kwa kesi yoyote nzito. Baada ya hukumu kama mtuhumiwa hata ridhika na hukumu hii bado ana nafasi ya kwenda mbele zaidi kwenye mahakama ya rufaa. Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote za mashtaka na utetezi na mahakama kuridhika utetezi wa pande zote. Kutokana na maelezo upande mashtaka unaosema kuwa mtuhumiwa aliwatuma watu kumuua mkewe ili arudiane na mpenzi wake wa zamani ambaye wakati huo alikuwa kwenye maandalizi ya kuolewa na mwanaume mwingine. Baada ya mashahidi wote waliopanda kizimbani akiwemo mchumba wa marehemu kutoa ushahidi wao ambao ulifanyiwa kazi na hatimaye kujiridhisha na ushahidi upande wa mashtaka ambao unatia hatiani moja kwa moja mtuhumiwa kwa hiyo mahakana inamuhukumu Hans Simgao kifungo cha maisha gerezani na kazi ngumu. Narudia tena kusema kuwa kama hamjalidhika na hukumu hii mna nafasi ya kukata rufaa mahakama ya rufaa,” hakimu alimaliza hukumu yake. Hakimu baada ya kutoa hukumu ile iliamsha vilio mahakamani huku mama mzazi na Mage kuanguka chini na kupoteza fahamu. Ilibidi huduma ya kwanza ifanye kazi yake ya ziada kutoa huduma ya kwanza kutokana na watu wengi walipoteza fahamu baada ya hukumu nzito iliyompoteza Hans uraiani. Baba yake hakukubaliana na huku ile na kuapa kukata rufaa kuhakikisha mwanaye anachiwa huku kwa vile makosa yalionekana ya kutengeneza lakini aliamini mwanaye hawezi kumuua mkewe kwa ajili ya mwanamke. Wakili aliyewekwa kutetea kesi ile aliomba nakala ya hukumu ili waweze kukata rufaa. *** Mage alizinduka na kujikuta amelala kwenye kitanda cha hospitali akiongezwa maji, pembeni alikuwa mama yake na shoga yake Brenda. Alipowaona aliangua kilio upya huku akisema: “Mama mkosi gani nimekosa Bara na Pwani, hivi nitaweka wapi uso wangu mbele ya jamii wakijua mimi ndiye niliyesababisha kifo cha mke wa Hans huku wengine wakiniona mimi ndiye sababu ya Hans kufungwa maisha.” “Mage aliyoyafanya Hans hukumtuma kafanya kwa matakwa yake siamini kama angekushirikisha ungemkubalie afanye unyama kama ule. Ni heri angempa talaka kuliko alichokifanya,” alisema Brenda. “Brenda naamini nuksi ndiyo nyota yangu haiwezekani Hans afungwe maisha Colin naye awe na mpenzi. Nina imani sina faida ya kuendelea kuishi.” “Mage unataka kufanya nini?” Brenda alishtuka. “Mwanangu hayo ni mawazo gani, Hans kufungwa si mwisho wa maisha bado una nafasi ya kuitafuta furaha,” mama yake alimtia moyo. “Sasa mama hiyo furaha nitaipata wapi ikiwa hata aliyemweka kama spare tyre ana mwanamke mwingine ambaye ni mzuri kuliko mimi.” “Brenda yote umeyataka mwenyewe ungenisikiliza sasa hivi ungekuwa kwa mumeo.” “Mama sikubali nitalipiganie penzi la Colin kwa gharama yoyote.” “Sasa Mage unataka kuchanganyikiwa, juzi tu Colin kamtangaza mchumba wake mbele za watu tena mtu maarufu utaanzia wapi?” Brenda alimuuliza. “Kama mnataka niendelee kuishi naomba hili ninalotaka kuamua mniachie mimi mwenyewe zaidi ya hapo mtaokota mzoga wangu,” Mage alitoa vitisho. “Lakini Mage wanaume wameisha? Mbona kuna wavulana wazuri kuliko huyo Colin na Hans?” Brenda alimuuliza. “Ni kweli wapo wanaume wazuri lakini si kila mbegu humea kwenye udongo wowote. Mapenzi yangu kwa Hans na Colin ni kama mtende kwenye jangwa si rahisi mti mwingine kumea sehemu ile basi ndivyo mapenzi ya Hans na Colin walikuwa kama mapacha ndani ya moyo wangu.” “Basi ndivyo hivyo mtaka pupa hadiliki kula tamu.” “Jamani nimewaeleza naomba mniache ni uwamuzi wangu mtu atakayeingilia uamuzi wangu ajue ndiye atakayehusika na kifo changu.” “Mmh! Fanya mchezo utakwenda kufunga ndoa na Hans gerezani,” mama Mage alitoa taadhari kwa mwanaye aliyetaka kuingilia mapenzi ya watu. *** Kufungwa kwa Hans kuliongeza umakini kwa Cecy kuhakikisha kila kona aliyokuwepo Colin na yeye yupo huku moyo wake ukimpa tahadhari ya yeye kuwa mbali na Colin lazima kuna kitu kitatendeka. Wazo lake lilikuwa kuachana na kazi ya kufanya maonesho ya mavazi ili kumlinda mumewe na Mage msichana aliyebakia kama genda heka ambalo linaweza kuvamia mume wa mtu bila aibu. Baada ya kutoka gym wakati wa kurudi nyumbani Cecy alionekana mtu mwenye mawazo mengi kitu kilichomfanya apoteze mchangamfu wake wa kawaida. “Bebi.” “Abee, Cecy alitikia huku akichukua chupa ya juisi. “Vipi mazoezi ya leo yamekuchosha?” alimuuliza huku akimtazama. “Hapana kawaida tu,” Cecy alimjibu bila kumtazama. “Mbona huna uchangamfu wako wa kawaida.” “Kuna kitu kinaniumiza kichwa nafikiria kubadili uamuzi.” “He! Uamuzi tena mpenzi wangu?” Colin alishtuka kidogo agongane uso kwa uso na gari lililokuwa likija kwa mbele yao lakini alijitahidi kulirudisha sehemu yake. “Ndiyo mpenzi kuna jinamizi linataka kuivamia furaha ya moyo wangu.” “Jinamizi gani tena mpenzi wangu?” Colin aliipaki gari pembeni ya barabara ili amsikilize vizuri mpenzi wake. “Colin naomba unisikilize vizuri.” “Sawa mpenzi.” “Nimeamua kuvunja mkataba wa kwenda kufanya maonyesho nje ya nchi.” “He! Kwa nini jamani? Si nimekubali kufunga nawe ndoa ndipo uondoke,” Colin alishtuka. “Hukumu ya Hans imeondoa kabisa amani ya moyo wangu.” “Kivipi mpenzi?” “Najua nikiondoka utarudiana na Mage.” “Siwezi...siwezi mpenzi, yule ni matapishi sitayarudisha mdomoni mwangu.” “Hapana Colin, yule mwanamke nikiondoka lazima atatumia hila za kike kukurudisha mikononi mwako na mimi kutoka kapa. Kwa hiyo mimi siendi popote wapigie simu waeleze nimevunja mkataba yote.” “Mpenzi utafungwa, una hela za kuwalipa ili kuvunja mkataba?” “Kwani kazi nimeanza?” “Hakuna kitu kama hicho, ukitaka fanya hata mwaka mmoja ndipo uvunje.” “Basi kama hivyo tutaondoka wote kwenda huko nitakapokuwa.” “Sawa hakuna tatizo lakini usiache kazi.” “Hapo tutaelewana kidogo na sitaki kumuona Mage kwenu wala kukupigia simu.” “Yote yanatekelezeka mpenzi wangu.” Kauli ya Colin ilirudisha furaha ya Cecy na kujikuta akitabasamu na kumnywesha juisi mpenzi wake aliyekuwa amezima gari kwa mshtuko. Aliwasha gari na safari ya kurudi nyumbani iliendelea. Wakiwa njiani simuya Colin iliita Cecy aliichukua na kuangalia na kukuta haina jina alimpa Colin. “Mpenzi pokea simu.” “Kapiga nani?” “Haina jina.” “Achana naye.” “Hapana pokea hujui nani anakupigia.” Colin aliichukua siku na kupokea: “Haloo.” “Ooh! Mpenzi wa maisha yangu, za toka jana mahakamani nina imani unajua kabisa sasa ndiyo nafasi yetu ya kufunga ndoa na kuwa mke na mume.” “We! Nani?” Colin pamoja na kujua aliyepiga simu ni Mage alijifanya hamjui aliyepiga ili Cecy asijue kitu. “Colin mpenzi kipi kilichokufanya usahau sauti ya malkia wa moyo wako au sababu ya hicho kinyago?” “Jitambulishe au siyo nakata simu,” Colin alijifanya kuja juu. Cecy alishtuka majibu ya mpenzi wake lakini alitulia amalize kuzungumza ndipo amuulize. “Ni mimi Mage mwanamke pekee uliyeshushiwa na Mungu, amini kufungwa kwa Hans Mungu ametenda ili ile ndoa yetu ya ahadi itimie.” “Umekosea namba,” Colin alisema huku akikata simu. “Nani?” Cecy alimuuliza. “Kuna mtu anaonekana amekosea namba.” “Basi unakuta mtu anapiga simu na kuanza kutoa maagizo mengi bila kujua anazungumza na nani,” Cecy alimuunga mkono mpenzi wake. “Umeona eeh, mpenzi nawe yamekukuta?” “Mara chache.” “Mara nyingi watu huwa wanachanganya namba badala ya sita wanaandika tisa basi akipiga inakwenda kwa mwingine,” Colin alizidi kuficha kilichopita. Wakiwa katika ya mazungumzo ujumbe uliingia kwenye simu ya Colin, aliichukua simu haraka kwa kuamini unatoka kwa Mage. Kabla hajafungua upande wa ujumbe Cecy alidaka na kusema: “Nipo kwa ajili yako nitasoma na kukueleza kimeandikwa nini.” Colin alipoangalia namba ya ujumbe ule ilikuwa iliyopigwa muda mfupi na Mage, alijikuta njia panda kumuachia simu Cecy asome ujumbe ule ambao aliamini si mzuri kusomwa naye. Lakini hakuwa na jinsi huku akiomba usiwe ujumbe mbaya ambao utamchanganya mpenzi wake na kulizua jipya pengine kukataa hata kazi yenyewe.. Cecy alichukua simu na kufungua upande wa ujumbe na kuanza kusoma, ghafla macho yalimtoka pima na mapigo ya moyo yalianza kumwenda mbio huku jasho likitanda kwenye maji la uso. Ujumbe ulikuwa umeandikwa: Colin wewe ndiye mpenzi wangu wa maisha, kumbuka ahadi yetu tuliyoahidiana kuwa mume na mke ipo palepale. Huu ndiyo wakati wangu hicho kinyago chako hakina nafasi mimi na wewe tunajulikana kwa wazazi wetu na mbele ya Mungu. Colin nakupenda zaidi ya kupenda, kufungwa kwa Hans Mungu ametenda ili ahadi yetu itimie. Mimi ndiye mkeo uliyechangulia na Mungu. I love you my husband to be Colin forever and ever mmmmwaaa. Colin aliyekuwa akifuatilia uso wa Cecy alishtuka kuona macho ya Cecy yakikodolewa pima kisha kuanza kutoka machozi, alijua kimenuka, kwa mchecheto bila kujielewa kama yupo barabarani gari lilihama njia na kwenda kujingonga kwenye nguzo ya umeme na kufanya utokee mlipuko mkubwa baada ya waya za umeme kugusana.Mlipuko ule ulifanya watu wakimbie kuokoamaisha yao , ghafla gari lilianza kuwaka motokabla hawajatoka. Watu walishtuka nakukimbia kuangalia kuna nini . Waliwakuta watuwawili wamejilaza mwanamke kwenye dashibodi na mwanaume kwenye usukani hukudamu zikiwatoka vichwani .Haraka waliwatoa kwenye gari na kuwalazapembeni huku wengine wakijitahidi kuzima gariambalo moto wake ulikuwa mkubwa . Kwaharaka walisimamisha gari na kuwapakizamajeruhi waliokuwa hawana ufahamu nakuwawahisha hospitali.Kutokana na hali zao ambazo hazikujulikanakama wapo hai au wamekufa waliwawahishaHospitali ya Taifa ya Muhimbili. Gari alilokuwaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/akiendesha Colin liliendelea kuteketea nahatimaye lilishika moto lote kutokana namiundo mbinu midogo ya kuzimia moto na kuteketeza kila kilichokuwepo pamoja na simu zote za Colin na Cecy.Msichana mmoja shoga wa Brenda rafiki wa Mage ambaye alikuwa akimfahamu Colin kutokana na kuwepo siku Colin alipomvisha pete Mage. Alikuwepo kwenye ajali ile kutokana na kutemka kwenye daladala na kukuta watu wakitolewa kwenye gari lililokuwa likiwaka moto. Kwa vile hakuijua namba ya simu ya mama Colin aliamua kumpigia simu Brenda amweleze Mage ili ampigie mama Colin kumjulisha ajali ile. Baada ya kupigiwa simu Brenda alipokea upande wa pili: “Haloo Loveness, niambie shoga!” “Aisee kuna tatizo,” alisema kwa sauti iliyojaa wasiwasi. “Mbona unanitisha kuna nini?” Brenda alishtuka. “Colin kapata ajali mbaya sana.” “Colin! Yupi?” “Aliyekuwa mchumba wa Mage.” “Wewe! Ajali ya nini tena Mungu wangu?” “Gari alililokuwa akiendesha nimepata ajali mbaya barabara ya Sam Nujoma jirani na Mlimani City kwa kugonga nguzo ya umeme.” “Mungu wangu, vipi hali yake?” “Mmh! Kwa kweli kuna taarifa nyingi japo si rasmi.” “Mungu wangu nisaidie mja wako, taarifa gani tena Love?” “Wapo wanaosema wamekufa papohapo.” “Jamaniii! Kwani alikuwa na nani?” “Na msichana mmoja ambaye anaonekana alikuwa na nguo za mazoezi.” “He! Yaani nimechoka, siamini kama Colin amekufa kirahisi namna hiyo.” “Sasa shoga nina imani Mage ana namba ya mama yake, mpigie ili awajulishe nina imani hawana taarifa.” “Poa, lakini siamini mpaka niuone mwili wa Colin kwenye jeneza.” Brenda akiwa amechanganyikiwa alimpigia simu Mage aliyekuwa amekaa kwao huku akichezea simu yake. Baada ya kumtumia ujumbe Colin alipiga simu ambayo iliita bila kupokelewa na mwisho ilizimwa kabisa. Baada ya kuzimwa alijikuta akijiapiza: “Lazima nimpate Colin kwa hiyari kwa nguvu, nitahakikisha nampoteza kinyago wake ili niipate nafasi yangu bila hiyo sina maisha heri ninywe sumu.” Akiwa katikati ya mawazo simu yake iliita, wazo lake alijua Colin alikuwa akitafuta sehemu nzuri ili ampigie. Alipoangalia alikuta inatoka kwa shoga yake Brenda, aliipokea. “Niambie shoga.” “Mage kuna taarifa siyo nzuri.” “Taarifa gani?” “Zinamhusu zilipendwa wako.” “Nani, Hans?” “Hapana, Colin.” “He! Colin kakupigia simu?” “Siyo kunipigia simu bali kapata ajali mbaya.” “Acha utani, acha kunirusha roho unione kama nampenda, sio siri Colin ndiye aliyebeba uhai wangu.” “Mage hebu tuliza akili unisilize.” “Haya niambie mpenzi.” “Colin amepata ajali mbaya barabara ya Sam Nujoma jirani na Mlimani City na haijulikani kama mzima au amekufa.” “Brenda sipendi utani wa kujinga, nimetoka kuzungumza na Colin hata robo saa haijapita.” “Sasa wewe fanya utani naomba umpigie simu mama yake sasa hivi, mweleze Colin amepata ajali na amekimbizwa Muhimbili. Naomba usiongeze lingine usije muua mama wa watu kwa mshtuko. Najua anampenda sana mwanaye ndiye kama mboni ya macho yake.” “Japo siamini nitampigia tu.” “Fanya haraka, unaambiwa hata gari alilokuwa akiendesha limeteketea lote.” “Mungu wangu ! Brenda unasema kweli?” Mage aliuliza kwa sauti ya kilio. “Kweli, siwezi kukutania kwa jambo zito kama hili.” “Mungu wangu hii nuksi gani? Kama Colin akifa nitakuwa na faida gani ya kuendelea kuishi,” Mage alizungumza peke yake huku macho yamejaa machozi na mikono kumtetemeka wakati wa kutafuta namba ya mama Colin. Kila alivyokuwa akilitafuta machozi yalizidi kuyafunika macho yake hata alipoyafuta kwa mkono yalijaa tena. Alitoka chumbani na simu mkononi hadi sebuleni na kumkuta mama yake. “Mage nini?” mama yake alishtuka na hali ya mwanaye. “Colin, mama,” alisema huku akilia na kumpa simu mama yake. “Colin! Kafanya nini?” “Ajali.” “He! Lini?” “Sasa hivi.” “Taarifa umezitoa wapi?” “Kanipigia Brenda sasa hivi?” “Dah! Vipi hali yake.” “Na..na..sikia a..a..meku..” “Wewe mtoto ushia hapohapo,” mama Mage alimkata kauli mwanaye hakutaka kulisikia neno la mwisho kwa vile aliamini litamuumiza moyo wake. “Mama mpigie simu mama yake hana habari.” “Mmh!” Mama Mage alichukua simu yake kutafuta namba ya mama Colin huku naye mikono ikimtetemeka. Baada ya kuipata alipiga simu ambayo ilipokelewa upande upande wa pili. “Haloo dada vipi?” “Kwema, una habari gani?” “Za nini?” “Kuhusu Colin.” “Mmh! Sina habari zozote.” “Kuna taarifa kapata ajali.” “Ajali!?” mama Colin alishtuka. “Eeh, ndiyo, kuna mtu kampigia simu Mage na kutaka tukujulishe kwa vile hakuwa na namba yako ya simu.” “Mungu wangu wee, yupo katika hali gani?” “Hebu subiri,” alisema na kuziba sehemu ya kuzungumzia na kumgeukia Mage. “Eti Mage mwili wa Colin umepelekwa hospitali gani?” “Mama sijasema amekufa ila watu wanafikiria hivyo,” Mage alimgeuka mama yake. “Sasa kapelekwa wapi?” “Mama mwambie amekimbizwa muhimbili, ila usimwambie yupo kwenye hali gani mengine atayajua hukohuko mwenyewe. ” Baada ya kuzungumza na mwanaye aliachia sehemu ya kuzungumzia na kuzungumza na mama Colin. “Anasema baada ya ajali wasamalia wema wamewapeleka Muhimbili.” “Wanasema hali yake ipo vipi?” “Hawajajua kwa vile amebebwa na kuingizwa kwenye gari na kuwahishwa hospitali.” “Na..na.. Cecy?” “Sijajua hebu subiri...Eti Cecy alikuwepo? Alimuuliza mwanaye. “Ndiyo.” ‘Ndiyo walikuwa pamoja.” “Na..nashukuru dada.” “Nami nakuja huko.” “Sawa tutakutana.” Baada ya kukata mama Mage alinyanyuka kuelekea chumbani kuchukua funguo ya gari, baada ya kuchukua alitoka nje na Mage alitoka kumfuata mama yake waliingia kwenye gari na kutoka kuelekea Muhimbili. Muda wote Mage alikuwa akilia kitu kilichomfanya mama yake kuingilia kati. “Unasema hajafa unalia nini mbona unamchulia mwenzio.” “Mama inauma Colin ndiye lilikuwa tumaini langu mwisho.” “Muombee basi apone.” “Yaani Mungu asikie dua langu, Colin apone lakini mchumba wake afe.” “Wee mtoto roho gani hiyo?” “Mama wakipona wote sina changu.” “Hebu achana na mawazo hayo,” mama Mage alisema huku kanyaga mafuta kuwahi hospitali. Mama Colin baada ya kuzipata taarifa zile alimpitia mama Cecy aliyekuwa hana taarifa zozote kwa kujua mwanaye alikwenda mazoezi asubuhi na mpenzi wake. Naye alishtuka lakini mama Colin alimpa moyo wafike hospitali ili wajue kipi kinaendelea japokuwa hakujua watoto wao wapo kwenye hali gani. Walijikuta wakifika pamoja na Mage na mama yake, waliongozana wote mapokezi kuulizia taarifa za wagonjwa wao. Waliambiwa wote wamekimbizwa chumba cha wagonjwa mahututi kwa vile hali zao si nzuri. Walikwenda kuonana na mganga mkuu, aliwakaribisha ofisini kwake. “Ndiyo wazazi wangu kwanza poleni sana.” “Mmh! Hatujapoa kwani hatujui hali za watoto wetu,” alijibu mama Colin. Dokta Bukos kwanza alitulia kama anasoma taarifa kwenye kalatasi kutafuta neno la kuwaeleza ili wasipagawe kutokana na hali za wagonjwa wao. Baada ya kutulia kwa muda alinyanyua uso wake na kusema kwa sauti ya upole. “Wazazi wangu hali za wagonjwa si mbaya wala nzuri sana lakini bado tunapigania maisha yao.” “Lakini baba mtu mpaka kuletwa chumba cha wagonjwa mahututi lazima hali yake ni mbaya sana?” aliuliza mama Colin. “Ni kweli, chumba hicho ni kwa ajili ya uangalizi wa karibu kwa mgojwa.” “Kwani hali zao zikoje?” aliuliza mama Cecy.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Bado kwa vile wameletwa hawajitambui hivyo kwanza tunashughulika na suala la kurudisha ufahamu kisha tutajua tufanye kitu gani.” “Mbona nilisikia wamekufa?” Mage aliropoka. “Si kweli, kama wangekuwa wamekufa wodini tumewapeleka kufanya nini?” daktari alijibu kwa ukali kidogo. “Wee Mage acha kuropoka,” mama yake alimkanya. “Jamani naomba kuzungumza na wahusika wa wagonjwa wengine msubiri nje,” daktari alisema. Mage na mama yake walitoka nje na kubakia mama Colin na Cecy, baada ya kubakia wawili dokta alitaka kujua uhusiano ya waliobakia na wagonjwa. Wote walijitambulisha. “Basi wazazi wangu ajali waliyopata ilikuwa mbaya sana, majeraha si makubwa sana lakini inaonesha wamejigonga kwenye kitu kigumu wakati gari likipata ajali hivyo kusababisha mtikisiko wa ubongo uliopelekea kupoteza fahamu. Lakini tunahangaika ili kurudisha fahamu zao.”ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment