IMEANDIKWA NA :
ATUGANILE
MWAKALILE ********************************************************************************* Simulizi
: Nini Maana Ya Mapenzi Sehemu Ya Kwanza
(1) Alikuwa binti mpole ila muongeaji sana,
aliyelelewa katika mazingira ya dini, nyumba yao ilijihusisha zaidi na maswala
ya dini kiasi kwamba hakutaka kujihusisha na maswala ya mapenzi kwa umri mdogo
kwani akiangalia dada zake wote walikuwa kwenye ndoa zako, kwahiyo ndoto yake
yeye ilikuwa ni kumaliza shule, kuanza kazi kisha kupata mchumba na kuolewa. Ni
mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto wanne, wakike watatu na wakiume mmoja
tu. Alikuwa na dada yake mmoja ambaye alipatana nae sana na
kipindi hicho dadake huyo ndoa yake ilikuwa bado changa kwani ndio kwanza
alitoka kuolewa, alikuwa akipenda kupiga nae stori na mara zote dadake alikuwa
akimshauri kuwa makini sana na vijana, “Erica mdogo wangu,
nakupenda sana. Naomba uwe makini sana na vijana, ni wadanganyifu. Unatuona dada
zako, tumejiheshimu hadi tumeolewa, ni fahari kwetu na heshima kwa familia.
Alitangulia dada yetu Maria, nimefata mimi. Najua na wewe utaenda katika
mtiririko unaofaa. Usikubali kushawishiwa kijinga na
wanaume” “Dada Bite najua unanijua vizuri mdogo wako, hayo
mambo sina. Ndio kwanza nipo kidato cha pili” “Ndio upo kidato
cha pili, yani hiko kidato ndio asilimia kubwa huharibikia hapo kuwa makini
sana” “Usijali kuhusu mimi dada” Walikuwa
wakiongea vizuri sana kirafiki kama marafiki wa kawaida vile lakini ilikuwa ni
mtu na dada yake. Beatrice alimrudisha mdogo wake nyumbani kwao
baada ya kutoka kumsalimia kwani mama yao alikuwa anampenda sana binti yake huyo
na alikuwa anamuona bado ni mdogo kutembea mwenyewe. Erica
alikuwa na rafiki aliyeitwa Johari, na alimpenda sana na kupiga nae stori za
kila aina ila tofauti ya Erica na Johari ni kuwa Johari alikuwa mapepe sana, ila
Erica alikuwa mpole sana yani yeye ni uongeaji tu. Wakiwa
darasani siku hiyo aliletwa kijana mgeni kwenye darasa lao, kwa hakika Yule
kijana alikuwa ndio amehamia hapo shuleni, ila alipoingia tu macho yote
yalianguka kwake. Mwalimu akamtambulisha Yule kijana kwa wanafunzi
wote, “Huyu ni mwenzenu anaitwa Erick mpokeeni
vizuri” Darasa lote wakaguna na kumuangalia Erica kiasi cha
kumtia aibu Erica na kuangalia chini, hadi mwalimu akawauliza walichoguna, mmoja
akajibu “Tumeguna sababu kuna pacha wake humu anaitwa
Erica” Wakaangua kicheko wote, mwalimu
akawatuliza, “Kufanana majina ni kawaida tu, kwani hamjawahi
kusikia hayo majina? Acheni habari zenu za ajabu, haya mpokeeni mwenzenu
huyo” Kisha mwalimu akamkabidhi Yule kijana kwa wavulana wenzie
halafu yeye akaondoka zake. Johari akamuangalia Erica na
kumwambia, “Umesikia jina la Yule
kijana?” “Nimesikia ndio” “Sasa mbona
hujafurahia?” “Nifurahie nini sasa?” “Mmmh
kijana mzuri vile, macho yake ya kuvutia kama anaita, halafu kafanana jina na
wewe, huoni kama ni bahati hiyo” “Johari, tafadhali achana na
habari hizo kwangu” “Mmmh wewe nae na ulokole wako, yani hiyo
chance ya kufanana jina ningeipata mimi basi leo leo ningemfata Yule kijana. Ila
Yule kijana mzuri jamani loh kama ameshushwa, lazima nitembee nae, nitampitia
tu” “Johari jamani hivi hatuwezi kuangelea habari zingine zaidi
ya hizo?” “Haya mama Mchungaji, leo umekusanya sadaka kiasi
gani?” Erica alikaa kimya kwani tayari alikuwa ameshachukia
kutokana na watu kuguna pindi tu Yule kijana wakati anatambulishwa na vile
ambavyo Johari amemwambia. Muda wa kurudi
nyumbani ulifika na Erica alirudi nyumbani kwao na kufanya shughuli zake kama
kawaida, alipokaa na kutulia alishangaa picha ya Yule kijana ikimjia kichwani na
jinsi Johari alivyokuwa akimsifia kuwa Yule kijana ni mzuri
sana. “Mungu wangu, sitaki kumfikiria Yule kijana, kwanini
nimfikirie jamani? Sijawahi kumfikiria kijana yoyote maishani mwangu, kwanini
nimfikirie Yule, hapana sitaki” Alitulia ila bado picha ya Yule
kijana ilikaa kwenye mawazo yake na alikuwa akijisemea moyoni kuwa Yule kijana
ni mzuri kweli hata alipoletwa darasana kidogo moyo wake ulipatwa na mshtiko
kuwa kijana mzuri vile katoka wapi ila bado alijipa moyo wa kupambana na zile
hisia kwani hakutaka kabisa maswala ya mapenzi huku akifikiria ushauri aliopewa
na dada yake. Usiku akiwa amelala, alimuona Erick kwenye ndoto
zake, tena aliona kamavile ana mahusiano na Erick, alishtuka
sana. “Jamani mimi ni mtoto wa kike nitaanzaje kumwambia
mwanaume nampenda? Kwanza sio utamaduni wetu, hata hivyo sitaki kumpenda, nataka
nisome nimalize shule name nije kuolewa na kupata heshima kama dada zangu. Erick
ondoka kwenye akili yangu” Kwavile ilikuwa pamekucha tayari,
ikabidi aamke na kujiandaa kwa ajili ya kwenda
shule. Erica alifika shuleni na asilimia
kubwa ya wadada walionekana wakimuongelea Erick tu kuwa ni kijana mzuri
aliyefika shuleni kwao, “Jamani Yule kaka ni mzuri, hadi
natamani anitongoze. Yani akithubutu kunitongoza wala sitalaza
damu” “Unangoja hadi akutongoze subiri uone, mi nitamtongoza
mwenyewe” “Kujidhalilisha huko” “Hata kama
mwenzangu, unaweza ukasubiri mwisho wa siku ukakuta mwenzio kashawahi. Hapa
shule kuna wasichana wazuri eti, unafikiri Yule Erick atafikiria kukufata wewe?
Aache kufikiria wakina Miriam, wakina Manka akufikirie wewe
thubutuuu” Erica alisikiliza kwa makini sana na kuona ni jinsi
gani Erick alikuwa akigombewa shuleni kwao, na kuondoa kabisa tumaini la kuweza
kuwa hata karibu na huyo Erick ila upande mwingine wa roho yake alifurahia maana
kuwa mbali na kijana ambaye ameanza kumpenda kutamuwezesha yeye kutimiza ndoto
zake za kumaliza shule kwanza. Stori nyingi shuleni hapo
zilikuwa ni kuhusu huyu kijana mpya aliyefika yani kila binti alihitaji kumpata
huyu kijana. Zilipita wiki mbili, ilikuwa
siku ya Jumamosi siku hiyo hawakwenda shule, Erica alikuwa nyumbani. Akachukua
kioo na kujiangalia, kisha akasema “Mimi ni msichana wa kawaida
sana, sina uzuri wa kupendwa na kijana kama Yule. Hawezi kunipenda mimi,
natakiwa kumsahau na kumtoa kwenye akili yangu” Akajiwa na
mgeni alikuwa ni rafiki yake Johari, akamkaribisha vizuri sana kisha akaanza
kupiga nae stori ila stori za Johari mara zote ni kuhusu wanaume, na umbea ila
siku hiyo stori yake kubwa ilikuwa ni kuhusu Erick, ingawa stori za vile Erica
alikuwa hapendezewi nazo ila kwavile zilimuhusu Erick alikuwa
akizisikiliza, “Basi bhana, si nimefatilia nyumbani kwao Yule
Erick, loh wana hela hao balaa” “Kumbe” “Ndio
hivyo, halafu nasikia shuleni kuna wadada kama wane wamebambwa na mwalimu
walimuandikia Erick barua za mapenzi” “Kheee, wewe umepona
kweli?” “Hahaha mimi nimtongoze kwa barua nina wazimu au? Mi
nitamtongoza live kabisa, tuangaliane ana kwa ana. Hapo ndio nitajua kama ana
aibu au la” “Kwahiyo utamtongoza lini?” “Nipe
mwezi, nataka nimzoee zoee kwanza” “Je
akikukataa” “Najua atanikataa, ila kwangu hata ile kumtongoza
tu napo ni raha” Erica alikuwa anamshangaa sana huyu rafiki
yake ambaye yeye alikuwa akijionea kila kitu kuwa kawaida
kabisa. Jumatatu yake, siku ya shule kama
kawaida ila leo kidogo Erica alichelewa shule. Sasa muda anaingia darasani kwa
kunyata akajikuta amekumbana kikumbo na Erick maana nae alikuwa anatoka kidogo,
Erica alinyanyua macho yake na kumwangalia Erick kisha
akamwambia, “Samahani” “Hamna shida
usijari” Erica alienda kukaa ila mwili wake ulipatwa na
msisimko mkubwa sana vile alivyokumbana kikumbo na
Erick. Alikaa huku akihema, rafiki yake Johari alimfata na
kumuuliza, “Mbona unahema sana, vipi
wewe?” “Nilichelewa shule leo” “Ndio uheme
hivyo sababu ya kuchelewa? Nimekuona vizuri, uligongana kikumbo na Yule mkaka
mzuri” “Ni bahati mbaya tu” “Sawa, ila umeona
macho yake? Jamani macho ya Yule kaka yanaita, kama anakwambia njoo njoo uwiii
jamani natamani hiyo nafasi ya kugongana nae ningeipata mimi maana
ningemkumbatia pale pale” “Ushaanza hivyo Johari, kwanza mimi
sina uzuri huo wa kuwa na Yule mkaka” “Kwani wewe una ubaya
gani sasa? Kwanza hapa shuleni hujirembi hufanyi nini ila bado unapendeza,
usijidharau Erica wewe ni mzuri, ila tu Yule Erick niachie
mimi” Wakacheka tu na kuendelea na kazi zingine za
darasani. Muda wa mapumziko siku hiyo Erica
hakutoka sababu kuna kazi alikuwa anaimalizia kufanya, kwahiyo alikaa anaandika
wakati wanafunzi wengine wako nje. Mara alisikia kuna sauti imefika na
kumsalimia, “Mambo” Erica alinyanyua macho
yake na kumuangalia aliyekuwa anamsalimia, alikuwa ni Erick kitu ambacho
kilimfanya Erica kukosa ujasiri kidogo huku sauti yake ikitetemeka tetemeka na
kuitikia, “Safi” Halafu akarudisha macho yak
echini huku akiendelea kuandika, “Mbona hujatoka
kupumzika?” “Kuna kazi ya kuandika
naifanya” Erica alikuwa anamjibu huku macho yake yapo kwenye
daftari tu hakutaka kutoa nafasi ya kumtazama Erick kwani aliogopa kijana Yule
kubaki kwenye akili yake. Ila Erick aliendelea
kuongea, “Samahani ile asubuhi, unajua ni kosa langu ndiomana
tumegongana. Nilikuwa siangalii mbele” “Hapana ni kosa
langu” “Sio lako ni langu, naomba unisamehe
Erica” Erica akainua macho yake sasa na kumtazama Erick vizuri
kwani hakutambua kama huyu mkaka angeweza kumuita kwa jina lake, kwa mawazo yake
yeye alijua huyu kijana halijui jina lake. Ila wakati ameinua macho yake,
alifika Johari na kaunza kumsalimia Erick, “Mambo vipi
Erick” “Safi” “Mbona hujatoka kwenda kunywa
chai?” “Nilimuona Erica amejiinamia hapa, ndiomana nikaja
kumuuliza kwanza yeye kuwa kwanini hajaenda mapumziko” “Ana
kazi huyu, nikusindikize basi utembee tembee kidogo mazingira ya
shule” “Sawa, ila ngoja nimuulize kitu
Erica” Erica alivyosikia aulizwe kitu akashtuka kidogo na
mapigo ya moyo kumuenda kwa kasi maana tayari alikuwa anampenda huyu kijana ila
alikuwa akipambana na hisia zake ili aweze kuishi bila mahusiano mpaka
atakapomaliza shule, Erica akainua macho yake kisha Erick
akamuuliza, “Utakula nini mama
nikuletee?” Kiukweli Erica aliona aibu sana na kukataa kuwa
asimletee chochote ila Erick alisisitiza kuwa atamletea chochote kisha akatoka
na Johari. Erica alijikuta kama akiganda kwa muda hivi kwani
akili yake iliruka kabisa kwa wakati huo kila alipoifikiria kauli ya Erick kuwa
utakula nini mama nikuletee yani alijikuta ufahamu ukikatika
kabisa. Muda wa kutoka ulipofika, Erica alifatwa tena na Erick
huku akimkabidhi mfuko, “Nimekununulia juisi na keki ila
kwavile muda wa darasani ulikuwa umefika sikuweza kukuletea tafadahari
pokea” Erick alimshika mkono Erica na kumfanya apokee ule mfuko
huku akitoa asante ambayo hata haikusikika vizuri maana sauti yake ilikumbwa na
tetemeko la gafla. Erica alifika nyumbani kwao akianza kuwa na
mawazo maradufu kuhusu Erick, “Hapana Erick usinipende mimi
tafadhali, sio mimi usinipende” Alijikuta akiongea peke yake
maana alianza kushikwa na hofu ukizingatia yeye tayari ameshampenda Erick halafu
Erick ameanza kumuonyeshea hisia ambazo ni hakika atakuwa naye
anampenda, “Sipo tayari kuwa na mahusiano yoyote, natakiwa
nisome nimalize shule, nianze kazi nipate mume niolewe kama dada zangu. Hapana
sitaki kuwa na mahusiano shuleni” Aliwaza hayo ila muda wote
aliokaa mwenyewe sura ya Erick ilimjia machoni pake na kumfanya akose raha
kabisa, alimfikiria Erick muda mwingi sana na hata usiku alipolala alimuona
Erick kwenye ndoto zake. Siku hiyo alienda
shuleni ilikuwa ni siku ya michezo, wanafunzi walikaa mbalimbali kwa lengo la
kucheza, mara Erick akamfata Erica na kumpa kipande cha karatasi halafu
akaondoka zake, Erica alifungua ule ujumbe ulindikwa “I LOVE YOU” alishtuka sana
na kutetemeka, rafiki yake Johari alifika na kutaka kujua kuwa kile kikaratasi
kimeandikwa nini. Siku hiyo alienda shuleni
ilikuwa ni siku ya michezo, wanafunzi walikaa mbalimbali kwa lengo la kucheza,
mara Erick akamfata Erica na kumpa kipande cha karatasi halafu akaondoka zake,
Erica alifungua ule ujumbe ulindikwa “I LOVE YOU” alishtuka sana na kutetemeka,
rafiki yake Johari alifika na kutaka kujua kuwa kile kikaratasi kimeandikwa
nini. Erica akaona kwamba Johari atakichukua na kukisoma, hivyo
akakitumbukiza mdomoni na kukitafuna, Johari alimwangalia sana rafiki yake na
kumwambia, “Loh Erica jamani yani umekitafuna kweli? Niambie
basi rafiki alikuwa amekuandikia nini?” “Eti alikuwa anaomba
daftari langu la Kiswahili” “Mmmh kama ndio hivyo mbona
umekitafuna?” “Sasa kwani wewe unahisi
nini?” “Mbona unapaniki rafiki yangu? Mimi nimeuliza tu kuwa
hicho kikaratasi kilikuwa kinahusu nini?” “Kwahiyo unahisi
alikuwa ananitongoza au?” Johari alianza kucheka sana kisha
akamwambia rafiki yake, “Hebu nitolee vituko mie, huyo Erick
anavyotongozwa na wasichana wote hapa shuleni aanze kukutongoza wewe kwa lipi?
Mtu mwenyewe binti mlokole, hata vijana wanakuogopa” Erica
alinyamaza kimya tu ila maneno ya Johari yalimuingia vilivyo, alikuwa
akimuangalia Erick kwa mbali alivyokuwa amezungukwa na wadada akicheka
nao. Erica siku hiyo alikuwa na mawazo sana
kiasi kwamba alikuwa kama mgonjwa na kuamua kwenda kuchukua ruhusa kwa mwalimu
na kurudi nyumbani, alienda nyumbani kwao kama mgonjwa siku hiyo akijiuliza
maswali kadhaa kuwa ni kweli kile ambacho Erick alikiandika kwenye kikaratasi
alikuwa anamaanisha? Na kama alikuwa anamaanisha mbona alikuwa akiongea na
kucheka na wanawake wengine, na pia maneno aliyoyasema rafiki yake yalimuondoa
katika hali ya kupendwa kabisa na Erick. Akiwa njiani kurudi
kwao alikutana na rafiki wa dada yake akiwa kabeba mtoto mgongoni, akamsalimia.
Huyu rafiki wa dada yake alianza kumuuliza maswali “Vipi Erica
mbona mapema sana leo?” “Najisikia vibaya Da
Rehema” “Pole, ila mdogo wangu soma. Usiwaendekeze wanaume,
unaona hapa, wengine tunahangaika na watoto migongoni, wengine nyumbani
wanalialia. Hatujaolewa hadi leo tunatanga na njia tu, mdogo wangu soma, achana
na mapenzi kabisa yani wewe jail masomo yako tu” “Asante
dada” Erica aliachana na huyu dada ila maneno ya dada huyu
yalimuingia kwenye akili yake, na kumfanya ile hali ya kujihisi homa iishe
katika mwili wake na kuanza kujihisi yuko salama kabisa, alifika nyumbani na
mamake alimuuliza kuwa nini tatizo ilibidi ajifanye kuwa tumbo linauuma sababu
kwa wakati huo hakuwa na hali ya homa kabisa. Kesho
yake shuleni alikwenda akiwa na hali mpya, fikra za mapenzi alizifuta kabisa
katika akili yake. Alipofika alikutana na rafiki yake
Johari, “Vipi wewe jamani mbona jana ulipotea
tu?” “Nilikuwa najihisi vibaya, tumbo lilikuwa
laniuma” “Kwahiyo ukaomba
ruhusa?” “Ndio” “Ila wewe kuruhusiwa ni lazima
maana walimu wanajuaga kuwa wewe si muongo” Basi Erica alikuwa
akiulizia masomo yaliyompita jana, kwani wazo la mapenzi lilipotea kabisa kwenye
akili yake kwa wakati huo. Muda wa mapumziko akiwa anaandika
kazi ya jana, alikuja Erick na kukaa karibu yake kisha
akamuuliza, “Jana uliondoka mapema sikukuona
tena?” “Kwani ulikuwa unanitafuta?” “Hapana,
ila nilikuangalia tu sikukuona. Vipi nikakuletee nini
nje?” “Sitaki chochote” “Mbona unaongea kwa
hasira?” “Hivi nimeongea kwa hasira eeh! Samahani ila sitaki
chochote” Ilibidi Erick aondoke zake ila Erica alifanya vile
sababu hakutaka tena kujihusisha na maswala ya mapenzi aliona angeharibu maisha
yake. Alipokuwa amekaa pale muda kidogo Johari alirudi, na kama
kawaida alianza kuongea aliyoyaona nje, “Mwenzangu nimemuona
Manka anamuongelea Erick, mmmh Yule mtoto kwa weupe ule na uzuri ule atamuopoa
tu Erick” “Kwahiyo Manka anamtaka
Erick?” “Aaah nasikia Erick ndio anamtaka Manka halafu Manka
nae anampenda Erick, mmh nangoja nione tu picha la malavidavi
litakavyoenda” Kiukweli maneno haya yalimchoma Erica vilivyo
ingawa hakutaka habari za Erick tena ila swala la kuambiwa kuwa Erick anamtaka
Manka na inaonyesha Manka anampenda Erick zilimchanganya vilivyo ukizingatia
akijiangalia yeye na Manka alimuona Manka kuwa na mvuto zaidi kwani yeye
hakujiweka kabisa kwenye kundi la wasichana
wanaovutia. Muda wa kutoka shule, aliweza
kumshuhudia Erick akiwa ameongozana na Manka yani hapo moyo wake ukalia kabisa,
alihisi kupasuka moyo na kuanza kuwa na wivu ila alijipa moyo asiendelea
kumuonea wivu Erick, “Mwanamke yeyote atakaye kuwa nae ni sawa,
sitaki kumpenda” Alirudi nyumbani kwao ila alionekana kuwa na
mawazo sana, alimkuta mama yake na hakuweza kumwambia chochote ukizingatia bado
binti mdogo atamwambiaje mama yake kuhusu mapenzi, alijiuliza tu
moyoni, “Mapenzi ni nini? Kwanini najisikia hivi kwa Erick?
Kwanini nimeumia moyo kumuona Erick yupo na Manka? Aaah sitaki mapenzi jamani,
siku zote nafundishwa ubaya wa mapenzi ila kwanini nijisikie hivi kwa Erick?
Natamani Erick aniambie ananipenda, ila hapana hawezi kuniambia hilo neno. Mmmh
na kile kikaratasi alichoniandikiaga je? Hapana labda alimuandikia mwingine ndio
akajisahau na kunipa mimi” Alikuwa akijiuliza maswali na
kujijibu mwenyewe kisha kuamua kufanya kazi zake za shule na mambo yake ya
masomo. Usiku wa siku hiyo mamake alimuita na
kumwambia, “Mwanangu Erica, umemuona
Aisha?” “Sijamuona, kafanyaje kwani?” “Shule
imemshinda kabeba mimba, tafadhari Erica usinitie aibu ya aina hiyo maana sijui
sura yangu nitaiweka wapi” “Mama jamani mimi naweza kufanya
hivyo!” “Mwanangu, kidato cha pili ndio kidato cha watoto kuota
mapembe maana huwa hamsikilizi nyumbani wala walimu shuleni, na wengi shule
inawashinda hapo. Mwanangu usinitie aibu, soma kama dada zako, maliza upate kazi
ndio uolewe. Yani watoto wako uzae ndani ya ndoa, maswala ya kurukaruka na
vijana hapana, tena ikitokea kuna kijana anakusumbua huko sijui nakupenda sijui
nini na nini njoo uniambie mwanangu. Wewe niambie halafu mimi nitajua nifanye
nini na huyo kijana, sitaki maswala ya mtu kukuchezea binti yangu.
Umenielewa!” “Sawa mama nimekuelewa” Kisha
akamuaga mama yake na kwenda kulala. Akiwa
amelala, Erica alijiona yuko mahali ufukweni halafu Erick yupo pembeni yake na
akimuonyesha mapenzi ya hali ya juu na kumfanya apagawe zaidi. Akashtuka kutoka
usingizini akihema hema, “Shindwa shetani, sitaki maswala ya
mapenzi, sitaki kupenda jamani” Alikaa chini ila wazo la ile
ndoto likafanya kazi kwenye akili yake na kuanza kujihisi akitamani kuwa karibu
na Erick ila alipingana vikali na wazo hilo. Kulipokucha kama
kawaida alijiandaa na kwenda shuleni, ile anafika tu shuleni akashangaa kumuona
Erick akiwa ameongozana na Manka, hakupendezwa na ile kitu kabisa, kisha Erick
akaenda upande mwingine halafu Manka akasogea alipo Erica na
kumsalimia, “Erica
mambo” “Poa” “Mbona leo sio
mchangamfu?” “Kawaida tu, nipo kawaida” “Ngoja
nikuulize kitu” “Niulize” “Hivi mimi na Erick
tunapendezana eeh!” Hili swali Erica hakulipenda kabisa, ila
kwavile alitaka kumuonyesha Manka kuwa yupo kawaida aliamua
kulijibu, “Mnapendezana, ndio shemeji
nini?” Manka akacheka na kujibu, “Hapana, ila
nina mpenzi wangu kafanana na Erick huyo ndio nilikuwa nataka kujua kama
tunapendezana” “Mmmh Manka jamani, si useme ukweli tu kama ndio
shemeji” Manka akacheka na kumuacha Erica halafu yeye akaelekea
darasani kwao, ila Erica aliweza kuelewa pale kuwa Erick na Manka wameshakuwa na
mahusiano tayari ukizingatia toka jana amjibu vibaya Erick wala hakuonekana
kumfata akimuuliza chochote kile. “Alikuwa ananipima tu jana,
sijui kajua kuwa nampenda kwahiyo anataka kucheza na hisia zangu? Simtaki na
sitaki kupenda” Aliingia zake darasani na kumuona Erick akiwa
anazungumza jambo na Johari, alipita kama hawaoni vile maana alienda moja kwa
moja kukaa sehemu yake. Johari alimfata Erica
na kuanza kuongea nae, “Umeniona pale nilikuwa nimekaa na
Erick?” “Nimekuona ndio” “Basi mwenzangu,
Erick alikuwa ananitongoza” “Mmmh
anakutongoza?” “Ndio, Erick alikuwa ananitaka yani anasemaje
hapa shuleni wasichana wote hakuna anayenifikia mimi kwa
uzuri” “Mmmh sasa wewe umemjibu
vipi?” “Nimemkataa” “Mmmh Johari wewe
umemkataa? Unakumbuka ulisema utamtongoza mwenyewe Erick sasa umepata bahati
hiyo amekutaka mwenyewe kweli umkatae” “Nimemkataa ndio,
unafikiri Erick mwenyewe ni mzuri kivile, wala wa kawaida
tu” “Ila jana ulisema alimtongoza
Manka” “Kumbe Erick alimwambia Manka kuwa aje aniambie mimi
kuwa ananipenda ila Manka nae anamtaka Erick hajaja kuniambia ndiomana Erick
kaamua aniambie mwenyewe leo” Ikabidi Erica amueleze rafiki
yake vile ambavyo aliambiwa na Manka na kuhisi kuwa Manka na Erick
washakubaliana, “Hana lolote huyo Manka, anajivunia ule weupe
wake tu. Erick ananitaka mimi ila nimemkataa” Ilibidi Erica
akubaliane na ukweli wa Johari kuwa Erick anamtaka yeye, na moja kwa moja
alihisi kuwa Erick ni kijana muhuni na anataka kuchzea wasichana tu ndiomana
anawatongoza tongoza hovyo. Muda kidogo wasichana wote wakaitwa
na mwalimu wa malezi pale shuleni alikuwa ni mmama wa makamo, aliwaita na kuanza
kuongea nao kuhusu maadili, “Hivi kweli kabisa msichana
unamuandikia barua mvulana ya kumtaka kimapenzi, hamjui kuwa mnajiharibia maisha
yenu! Mapenzi yapo tu na mtayakuta mkimaliza shule, hawa vijana wasiwababaishe
kabisa, mtu anayekupenda hawezi kukuharibia masomo, atasubiri umalize shule
kwanza. Ni aibu kubwa sana kwa jamii ya kiafrika haswaa ya kitanzania kwa mtoto
wa kike kumtongoza mvulana. Muache hiyo tabia mnatutia aibu. Leo siwataji
wahusika wa tabia hii ila safari ijayo msipojirekebisha nitawataja, hiyo tabia
ikome kabisa mnatutia aibu” Yule mama malezi wao aliwaelekeza
vilivyo na kufanya wenye kuelewa waelewe ila wasioelewa kwao ilikuwa ni anapiga
makelele tu. Muda wa kuondoka leo Erica aliongozana na
Johari, “Unajua madam alikuwa anawasema wakina nani
pale” “Wakina nani?” “Mwenangu Manka kabambwa na barua
kamuandikia Erick kuwa anampenda yani Manka bhana hadi ameshindwa kuniambia mimi
ukweli kuwa Erick ananipenda mimi kumbe alishamwandikia barua ya
kumtaka” “Ila mimi hizo hbari za Erick sizitaki” “Mmmh na mfano
akija kukutongoza na wewe?” “Naenda kumsemea kwa mama yani asithubutu
kabisa kabisa. Anafanya wanawake kama mpira eeh kila anayetaka anabutua,
kwakweli anikome ingawa najua hawezi kunitongoza mimi” “Mmmh huwezi jua
ya Mungu mengi, ila unatakiwa kuwa na msimamo shoga yangu. Wanaume wana tamaa,
yani kama Erick anatamaa sana, mtu mgeni lakini anatamani wanawake hapa shuleni
balaa. Yani kuwa makini” Waliachana kisha Erica kurudi nyumbani kwao na
kujiuliza kuwa ni kwanini rafiki yake alikuwa anamsisitiza kuwa awe makini maana
yeye aliona kawaida tu na wala hakufikiria kama Erick anaweza kumtongoza ila
rafiki yake alivyomtahadhalisha ni balaa. Siku hiyo ilikuwa ni
siku ya Ijumaa na iligubikwa na michezo mbalimbali pale shuleni kwao, Erica
alikuwa darasani mwenyewe na rafiki yake Johari walikuwa wakipiga stori za hapa
na pale. Muda kidogo aliingia mule darasani Erick akiwa ameongozana na rafiki
yake Musa walikaa mbele kidogo na walipokaa Erica na johari. Wakati
maongezi yao yanashamili mara Erick aligeuka na
kuita, “Erica” Erica alimuangalia Erick ila hakumuitikia, kisha
Erick akamuita tena Erica na muda huu Erica alivyomuangalia
akamwambia, “Erica nakupenda” Moyo wa Erick ulienda kwa kasi
sana, na kumfanya asijibu chochote ila Erick alisema tana, “Erica
nakupenda” Erica alimuangalia Erick ila hakumuitikia,
kisha Erick akamuita tena Erica na muda huu Erica alivyomuangalia
akamwambia, “Erica nakupenda” Moyo wa Erica ulienda kwa kasi
sana, na kumfanya asijibu chochote ila Erick alisema tena, “Erica
nakupenda” Erica alijihisi vibaya moyoni maana lile swala la kutongozwa
mbele ya rafiki yake Johari na mbele ya Musa hakupendezwa nalo, alinuka na
kutoka nje kwa aibu, cha ajabu wala rafiki yake Johari hakumfata alipotoka,
alikaa peke yake mpaka muda wa kwenda nyumbani. Leo aliondoka akiwa
ameongozana na wanafunzi wengine huku ameweka begi lake mgongoni, mara akavutwa
begi na kuwa kama mtu aliyevutwa kwa nyuma, alipogeuka alimuona Erick halafu
alikuwa akimuangalia kwa jicho la hamasa sana, huku akiongea kwa sauti kama ya
kunong’oneza na yenye mtetemeko ndani yake, “Erica
nakupenda” “Sitaki uniambie maneno hayo Erick, nitaenda kusema kwa
mama” Kauli hii ilimchekesha Erick na kufanya aanze kucheka, kisha
akamuuliza, “Sasa Erica kukupenda wewe kunahusiana vipi na kwenda
kumwambia mama yako? Mimi nakupenda wewe Erica, naomba nielewe” Erica
akaona hii sasa itakuwa ngoma nzito aliamua kukimbia na kumwacha Erick akiwa
ameduwaa pale maana Erica alienda kujichanganya na wanafunzi wengine katika
mlolongo wa kwenda nyumbani. Alifika kwao huku sauti ya Erick ikimjia
kichwani kuwa Erica nakupenda, aliwaza sana na kutafakari ila uoga nao ulikuwa
unamshika vilivyo. Siku hiyo hadi wakati wa kula chakula cha usiku bado
sauti ya Erick ilifanya kazi vilivyo masikioni mwake, hadi akaamua kuwahi kwenda
kulala lakini usingizi haukumpata mapema kwani alikuwa akisumbuliwa na sauti ile
ile ya Erick. Kesho yake akiwa ametulia nyumbani kwao alienda
rafiki yake Johari na kumkuta pale na kusalimiana nae kisha kuanza stori za hapa
na pale, “Eeeh jana uliishiana vipi na Erick?” “Shiiii, punguza
sauti mama yupo ndani atasikia” “Mmmh umemkubalia nini? Sema ukweli
Erica” “Jamani si upunguze sauti nimekwambia, tubadilishe stori
kwanza” “Ila wewe si ulisema akikutongoza utakuja kumwambia mama yako,
saivi unasema nipunguze sauti umemkubali nini?” Mara mama yake Erica
alitoka ndani na kuuliza, “Kitu gani hicho?” Johari alijibu
haraka haraka, “Kuna kijana mama anaitwa Erick kaja shuleni na
amemtongoza Erica halafu huyo kijana anatongoza kila msichana
shuleni” “Amemtongoza?” “Ndio kamtongoza” “Yani nyie
watoto mmeanza habari za kutongozana kweli? Hayo ndio mambo mnayojifunza huko
shuleni, na udogo huo mshaanza kutongozana. Erica niambie hayo maneno ni
kweli?” Erica alikaa kimya na kuinamia chini, mama yake alimuuliza tena
ila Erica alinyamaza tu. Mama yake akamsogelea na kumnasa kibao, “Wewe
Erica si naongea na wewe, unaniletea upunguani eeh! Yani binti mdogo hivyo
unatongozwa shuleni unaacha kusema kwa mama yako? Na Jumatatu tutaenda wote
shuleni nikamuone huyo shababi wa kutongoza tongoza hovyo” Huyu mama
alionekana amechukia vilivyo kisha akaondoka zake, Erica alimuangalia kwa
gadhabu sana Johari na kumwambia kuwa aondoke zake. “Ondoka
kwetu” Johari hakubisha kitu chochote na kuinuka kisha akaondoka
zake. Siku ya Jumapili, mama Erica alienda na Erica kanisani na
baada ya ibada alimpeleka kwa mchungaji, “Naomba umuombee mwanangu, ni
binti mdogo ila anatakwa kutekwa na ulimwengu wa uzinzi” Mchungaji
alimuangalia Erica na kumuuliza, “Umesimama wapi binti yangu? Unataka
kuharibu usichana wako?” Erica hakujibu chochote, mchungaji akamuomba
mama Erica awapishe ili wapate kuongea kidogo na Erica, basi mama Erica alifanya
hivyo. Na baada ya maombi mchungaji alianza kuongea na Erica, “Ni kweli
umeanza uzinzi Erica?” “Hapana baba” “Unajua kama uzinzi ni
dhambi?” “Najua na sijafanya uzinzi mimi” “Sasa imekuwaje mamako
aseme umeanza uzinzi?” “Kuna kijana mmoja shuleni amenitongoza,
sijamkubali ila rafiki yangu kaja kusema nyumbani kuwa
nimetongozwa” “Kidato cha pili mnaanza kutongozana
jamani!” “Sikuwa na lengo la kumkubali, tafadhali mchungaji ongea na
mama anielewe. Mimi sio mtoto mbaya” “Sawa nitaongea naye, ila kumbuka
kuwa hata kwenye biblia Mithali 4:13 inasema “Mkamate sana elimu, usimuache
aende zake” Kuwa makini na masomo yako
mwanangu” “Nimekuelewa” Basi mchungaji aliahidi kupata siku na
kuzungumza na mama yake Erica kwahiyo muda huo akamruhusu
kuondoka. Erica alirudi na mama yake nyumbani ila alimuona mama yake
kama hakuwa na furaha kabisa kwa siku hiyo na hakujua ni kitu gani mama yake
anakipanga moyoni mwake. Jumatatu kama kawaida Erica alijiandaa
na kwenda shuleni, ila nay eye hakuwa na furaha kabisa siku hiyo kutokana na
vile alivyosemewa na Johari na jinsi alivyosemewa na mama yake kwa mchungaji
wao. Akiwa amekaa darasani mara alikuja kuitwa na mwalimu, na kuongozana
nae kuelekea ofisini. Alipoingia tu moyo wake ulishtuka sana kwani alimkuta mama
yake na mwalimu wa nidhamu. Kwakweli raha ilizidi kumuisha kabisa kwani hakujua
kuwa mama yake ameenda kufanya nini, “Haya sogea huku
Erica” Erica alisogea kwa mwalimu na kuanza kumsikiliza, “Ni
kijana gani aliyekutongoza?” Erica alikaa kimya kwani aliogopa kusema
kwa kuhofia ni aibu kwa Erick, ila mama yake alimuangalia kwa gadhabu sana, na
kumsogelea mwenyewe halafu akamnasa tena kofi, “Hebu mtaje huyo
mwendawazimu mwenzako” Mwalimu nae akashika bakora kuwa asipotaja
atamuadhibu, mwalimu akataka kumchapa bakora. Erica aliamua
kusema, “Lakini hakuna mtu aliyenitongoza” Mama yake akawaka kwa
hasira, “Kwahiyo mimi ni chizi? Nimekuja kuleta habari za uongo, hebu
muiteni rafiki yake Johari aje kuthibitisha ujinga wa huyu” Mwalimu
alimuangalia Erica na kumuamuru apige magoti, kisha mwalimu mwingine alienda
kumuita Johari. Alipofika aliulizwa kuhusu mwanaume aliyemtongoza
Erica, “Ni Erick mwalimu, ila msinitaje” “Hebu toa ujinga wako
hapa, na umuite huyo Erick upesi” Basi Johari akatoka na kwendakumuita Erick ambaye alishangaa kufika ofisini na kukuta kuna mmama amekaa huku
walimu wawili wakiwa wamesimama na viboko vyao halafu Erica kapigishwa
magoti. Alipofika nae aliamriwa kupigwa magoti na kuulizwa kama ni kweli
amemtongoza Erica, “Ni kweli mwalimu ila sijamwambia kwa lengo baya ni
kweli nampenda” “Nyamaza upesi, unajua kupenda wewe? Ndio nyie
mnaoanzaga kuharibu maisha ya wenzenu bado mapema kabisa, unakubali kirahisi
rahisi tu.” Wale walimu walimuomba mama Erica aondoke maana walisema
watamshughulikia huyo Erick, kisha wakamwambia Erica ainuke na kwenda
darasani. Kiukweli Erica alishikwa na moyo wa huruma sana, kwani walimu
wale walianza kumuadhibu Erick kwa viboko pale pale, basi Erica
akasema “Mwalimu lakini Erick hajanitongoza” “Nyamaza upesi na
wewe, unataka adhabu tukupe wewe eeh! Haya Erick tongoza tongoza nenda darasani,
adhabu yako apate huyu kipenda roho” Erick aligoma na kuwaambia
walimu, “Mimi ndio naye stahili kuadhibiwa kwani ni kweli nilimwambia
Erica kuwa nampenda, ingawa sikuwa na nia mbaya. Na ninampenda
kweli” “Nyamaza wewe kijana, Erica toka upesi nenda darasani. Na siku
nyingine mtu akikutongoza shuleni uje useme kwa walimu na sio kwenda kusema
nyumbani. Mnawapanikisha sana wazazi” Erica alitoka mule ofisini ila
alijawa na roho ya huruma sana, alirudi darasani ila roho ilikuwa inamuuma
mno. Erica alikuwa kimya kabisa darasani huku watu wakitamani
kumuuliza kuwa imekuwaje kule ofisini walipoitwa, ila walishindwa sababu Erica
alionekana kuchukizwa sana. Baada ya masaa mawili, Erick alirudi
darasani na kuchukua begi lake kisha akaondoka zake. Yani Erica alitamani
kumuuliza kuwa imekuwaje kuwaje, ila hakuweza kufanya hivyo ila Erick alipotoka
tu Johari nae alimfata nyuma kumuuliza, “Pole Erick, imekuwaje
tena?” “Sikujua kuwa Erica ni msichana mjinga kiasi hiki. Kumbe ulijua
kuwa atanisemea kwa mama yake kwanini hukuniambia?” “Ila mimi
nilikwambia Erick usimtongoze Erica yani kaniingizia matatizo na mimi,
nimeshangaa tu ofisini naitwa nithibitishe eti amesema wakati unamtongoza mimi
nilikuwepo. Yani Erica ni muuwaji kwakweli, pole sana Erick. Kwahiyo
imeishiaje?” “Aaah walimu nao wale sijui vipi yani hawaelewi kuna
kupenda” “Kwahiyo umekubali kabisa kuwa kweli
ulimtongoza?” “Kwanini nikatae sasa wakati ni kweli nimemtongoza!
Sikuona sababu ya kukataa ukizingatia ni kweli nampenda Erica, wanaweza sema ni
akili za kitoto ila kutoka moyoni kabisa nampenda Erica” “Jamani ukaamua
ujitoe muhanga hivyo! Ungekataa kuwa hukumtongoza” “Siwezi kukataa kitu
ambacho nimefanya kweli ila nimeshangaa walimu waliponiambia kuwa Erica
amemwambia mama yake kuwa mimi natongoza wasichana hovyo shuleni, jamani toka
nimekuja kwenye shule hii sijawahi kumtongoza msichana yeyote Yule, hata shule
nilizotoka sijawahi kumtongoza msichana ila Erica nimejikuta yupo moyoni mwangu
ila ameniponza” “Duh pole sana, kwahiyo walimu wamechukua uamuzi
gani?” “Wamesema nikamuite mzazi wangu, wewe rudi darasani yani acha
tu” Erick aliondoka na kumuacha Johari akirudi darasani, ila Joharia
alienda moja kwa moja alipokaa rafiki yake na kujaribu kuzungumza
nae, “Jamani Erica usinichukie. Mimi ni rafiki yako ujue, nimefanya yote
haya kukuokoa tu” “Sasa umeniokoa nini na umemuingiza kijana wa watu
kwenye matatizo” “Matatizo gani? Sikia nikwambie, pale nimemfata Erick
na kumuuliza kinafki tu. Akasema kuwa alikutongoza mbele yangu ili roho iniume
kuwa anakutaka wewe wakati kashanitongoza na mimi. Halafu anasema amekubali
ofisini ili wewe umuonee huruma na siku zijazo umkubali ili amalize machungu
yake kwako. Yani wanaume ni wapumbavu sana.” Erica maneno ya Johari
yalimuingia kwa kiasi Fulani kwani aliweza kuona kuwa pengine ni kweli Erick
alikuwa akimjaribu tu na swala la Erick kukubali ofisini inawezekana ni sababu
anahitaji tu amuonee huruma ili mwisho wa siku baada ya zile adhabu
amkubali. Erica alirudi nyumbani kwao ila hakutaka kumuuliza
mama yake kuwa aliongea maneno gani shuleni kwao kwani alijua kama angemuuliza
basi angeanzisha mada upya, ila mamake akamuita mwenyewe, “Yule kijana
mwanangu, walimu wamesema lazima atafukuzwa shule” “Atafukuzwa
shule?” “Ndio, nimemsemea na swala lake la kutongoza kila binti hapo
shuleni kwenu. Yani kijana mzuri vile halafu anakuwa na matendo ya ajabu,
anajivunia uzuri wake. Yani vijana wa vile huwa hawafai, kazi yao ni kuchezea
chezea wasichana” Erica hakutaka kuchangia mada yoyote kabisa alibaki tu
kumsikiliza mama yake kisha kwenda chumbani kwake, ila alikuwa anajiuliza sana
kama kosa alilolifanya Erick lina haki ya yeye kufukuzwa shule. Siku
hiyo hakupata usingizi kabisa maana alijikuta akiwaza kuhusu Erick tu na kile
kilichotokea siku hiyo hadi panakucha alijiandaa tena na kwenda
shuleni. Aliangalia darasani huku na huku hakumuona Erick, akajikuta
akianza kujihisi vibaya katika moyo wake. Akainuka na kutaka kutoka nje ya
darasa kidogo akamuona Erick akiwa ameongozana na mama wa makamo alihisi ni mama
yake Erick, alitamani sana kujua kuwa ni kitu gani kinaenda kuzungumzwa
ofisini. Alitoka vizuri darasani na kuwa kama anaelekea uwani, ila
hakwenda uwani kwani alienda nyuma ya ofisi ya walimu ili kusikiliza kilichokuwa
kinajadiliwa. Alianza kusikia walimu wakiongea na Yule mama ila sauti ya
Erick haikusikika, “Mwanao kaonyesha nidhamu mbovu hapa shuleni
hivyobasi tunamsimamisha masomo” “Jamani walimu, mpeni nafasi nyingine
sidhani kama mwanangu atarudia hiko kitu baada ya adhabu yote
mliyompa” Erica alikuwa makini sana kule nyuma akisikiliza, mara alihisi
kama kuna mtu kamshika kiuno, akageuka haraka na kumuangalia alikuwa ni
Erick. Erica alikuwa makini sana kule nyuma
akisikiliza, mara alihisi kama kuna mtu kamshika kiuno, akageuka haraka na
kumuangalia alikuwa ni Erick. Ila Erick alikuwa akitabasamu tofauti na
Erica alionyesha sura ya kuchukizwa sana kwani hakutegemea kushikwa kiuno na
Erick, basi kabla hajasema chochote Erick alimsogelea na kumbusu, kitendo kile
kilimzubaisha kidogo Erica kisha Erick akamwambia, “Najua sitakuona
kwasasa maana hii shule ndio basi tena! Ila nimekubusu kama ishara ya upendo
wangu kwako” Erica alikuwa kimya tu, basi Erick akasogea na kumbusu tena
ila kwa bahati mbaya wakabambwa na mwalimu wa nidhamu, “Kheeee yani kesi
bado haijaisha mnafanya mambo ya ajabu huku, haya piga magoti” Wakapiga
magoti huku Erica akitetemeka sana na kuanza kumuomba msamaha
mwalimu, “Mwalimu naomba msamaha” “Msamaha gani niutoe kwa mambo
ya kijinga kama hayo? Mimi ni mwalimu wa nidhamu mnataka watu wafikirie nini
kwenye shule yetu ikiwa wanafunzi mnafanya vitendo vya ajabu
hivyo!” Erick nae akaongea, “Lakini mwalimu hakuna kibaya
ulichotukuta tunafanya, mimi nimembusu tu Erica” “Hebu nyamaza na wewe,
haya inukeni hapo twendeni ofisini mkapate adhabu yenu” Basi wakainuka
pale kisha mwalimu akaongozana nao hadi ofisini, “Nimewakuta hawa
wajinga nyuma ya ofisi hapo wanabusuana” “Kheee nyie watoto mna nini
lakini? Ni mapenzi gani hayo? Kwakweli sina mjadala hapa, Erick shule basi, na
wewe Erica kesho uje na mzazi wako. Mama Erick hakuna cha kusikiliza kutoka
kwako, hatutaki vijana wa kuharibu mlolongo wa shule hapa, naomba uondoke na
mtoto wako, barua hii hapa nilishawaandalia” Mama Erick aliona mwanae
kamtia aibu sana, kwahiyo akaondoka nae na Erica alitakiwa kwenda kwao muda ule
ule kuita mzazi wake. Erica aliondoka akiwa na mawazo sana
maana hata hakuelewa kuwa mama yake atamueleza kitu gani sababu ni picha mbaya
tayari, alifika kwao na kunyata kuingia ndani ila mama yake alimuona na
kumuuliza, “Wewe vipi una matatizo gani wewe? Na mbona mapema
hivi?” Erica alianza kujiuma uma kwani hakuelewa ni jinsi gani amueleze
mama yake kuwa anahitajika shuleni na amekutwa na Erick. “Wewe Erica
wewe mbona husemi chochote, kuna tatizo gani mbona mapema?” “Walimu
wamesema nije nikuite” “Mungu wangu, umefanya ujinga gani tena Erica
mwanangu jamani eeh! Niambie ujinga gani umefanya?” “Sijafanya chochote
mama” “Haiwezekani hujafanya chochote niitwe shuleni kwenu, sema
umefanya nini?” “Sijafanya chochote mama” “Usiniletee uchizi
wako kabisa, tunaenda huko shuleni kwenu sasa hivi, unajua kama una mtihani wa
taifa wewe? Unafanya ujinga kweli? Ngoja nijiandae twende” Yule mama
alitumia muda mfupi sana kujiandaa kisha kuanza kukokotana na Erica kwenda
shuleni, kwakweli kile kitendo kilikuwa ni cha aibu sana machoni pa
Erica. Walipofika shuleni, wakati mama Erica anaingia getini akielekea
ofisini, Erica alirudi nyuma na kujificha kisha akatumia njia za panya kuondoka.
Kwahiyo mama Erica alijikuta akiingia mwenyewe ofisini. Erica alirudi
tena nyumbani na kujifungia chumbani kwake akilia, kwakweli alilia sana nah ii
aliiona kuwa ni siku mbaya sana kwake kwani kaonekana ni msichana mbaya mwenye
tabia mbaya, roho ilimuuma sana. Mama Erica alirudi nyumbani
akiwa na hasira sana kwanza kwa kile alichoambiwa mwanae kakifanya na pia kuhusu
swala la mwanae kumkimbia shuleni. Aliingia ndani na kumkuta Erica sebleni
akijiliza, kwakweli mama Erica alimshika Erica na kuanza kumpiga
sana, “Umenitia aibu sana wewe mtoto, nitaiweka wapi sura yangu hii.
Yani siku zote najivunia wanangu wametulia ni wasomi halafu wewe unataka
kuharibu sifa ya familia kweli? Sijapenda ulichokifanya Erica, na umesimamishwa
masomo mjinga wewe, sijui utafanyaje na kuna mtihani wa kidato cha
pili” Erica alilia sana hadi alikosa raha kabisa kwa kulia, akaenda
kujifungia chumbani kwake akilia, yani siku hiyo hakutoka tena nje ukizingatia
alionekana ni msichana mstaarabu halafu gafla kaonekana ni msichana asiye na
maadili kabisa, alijikuta akiyachukia mapenzi na kukosa raha
kabisa. Mama Erica, alipiga simu kwa Bite ili washauriane kuhusu Erica,
naye Bite aliamua kwenda ili akajue imekuwaje. Baada ya mazungumzo na
mama yao aliamua kwenda kuzungumza na mdogo wake, “Pole mdogo wangu
Erica” “Nisameheni dada ila sijafanya chochote kibaya” “Naelewa
ila niambie ukweli jinsi ilivyokuwa ili nijue jinsi ya kukusaidia” Erica
aliamua kumueleza kitendo cha yeye kwenda nyuma ya ofisi ili kusikiliza
alichokuwa anaambiwa mzazi wa Erick na jinsi Erick alivyokuja nyuma yake na
kumbusu kisha mwalimu kuwakuta, “Dada sijafanya chochote kibaya, hata
mimi nilikuwa nikimshangaa tu kunibusu ila nimeshangaa walimu kuchukua maamuzi
mazito sana kwangu” “Sawa mdogo wangu nimekuelewa basi usiwe na mawazo
sana” “Mawazo lazima dada, nipo kidato cha pili natakiwa kufanya
mtihani” “Si bado namba za mitihani hamjaandikisha?” “Ndio ila
nitafanyaje?” “Usijali nitakufanyia mpango haraka iwezekanavyo na
tutaenda kuishi wote kule kwangu hadi umalize kidato cha nne na kumaliza masomo
yoko yote vizuri ila niahidi tu kuwa hutoniangusha. Yani maswala ya mapenzi
hayatakuwepo kwenye akili yako” “Dada nataka kusoma, sitaki habari za
mapenzi kabisa nataka kusoma” “Basi usijali, ngoja niongee na mama.
Tutaondoka leoleo maana mama inaonyesha amechukizwa sana asije akafanya kitu
kibaya bure, ngoja twende ili mama nae apunguze mawazo” “Sawa dada
nimekuelewa” Basi Bite aliamua kwenda kuongea na mama yao ili kuangalia
namna ya kumsaidia mdogo wake huyu. Erica alichukuliwa na dada
yake kisha akatafutiwa shule nyingine na kuanza masomo yake huko, kwakweli
alijikuta akifikiria zaidi masomo na kuyachukia mapenzi kwani yalishamwekea doa
na sifa mbaya, hakupenda ile kitu ijirudie katika maisha yake ya kwenye shule
hiyo mpya kwahiyo alijitahidi kusoma kwa bidii na kujiweka mbali na watoto wa
kiume kwani kila aliporudi nyumbani dadake alikuwa akimuhusia kuhusu mapenzi
kuyaanza mapema yanavyoumiza moyo, “Kwahiyo dada ni kipindi gani kizuri
kuanza mapenzi?” “Usifikirie hayo kwasasa mdogo wangu, kipindi kizuri
ukikua utakijua tu ila kwasasa usifikirie chochote kuhusu mapenzi yani wewe
fikiria elimu yako tu. Mapenzi yapo na utayakuta huko mbele, kwasasa fikiria
masomo” “Sawa dada” “Na kama kuna jambo lolote unakumbana nalo
huko shuleni usisite kuniambia, nieleze mimi ni dada yako na nimepitia mengi
nayajua” Erica alimuelewa sana dada yake huyu na aliona anafanya yote
haya sababu anamuhurumia kwahiyo ikabidi asome kwa bidii, hata akaachana na
marafiki wote aliokuwa nao awali zaidi ya kufatilia masomo
yake. Erica alimaliza kidato cha nne na matokeo yalitoka
alikuwa amefaulu vizuri tu na kuchaguliwa kuendelea na masomo yake kwenye shule
ya bweni ya wasichana, alifurahi maana aliona huko kutamsaidia zaidi
kutokujihusisha na maswala ya mapenzi. Dada yake alimfanyia mipango yote
ya kuweza kuanza shule na alianza shule aliyopangiwa, ila muda ambao marafiki
aliokutana nao kule wakiwa wanaongelea mada za mapenzi kwenye kichwa chake
inamjia picha ya mtu mmoja tu ambaye ni Erick hadi mara nyingine anawaza kuwa
Erick atakuwa wapi, kuwa nay eye je anaendelea na shule? Kwenye moyo wake aliona
ni kweli anampenda Erick na aliamini ipo siku atakutana tena na Erick halafu
Erick atamtongoza tena na kuanza mahusiano, “Sijui kwanini huyu Erick
hatoki kwenye akili yangu, ni siku nyingi lakini Erick bado kaganda kwenye akili
yangu. Kuna siku nitamuona tena kweli? Kama Erick alikuwa ananipenda kweli nina
hakika nay eye atakuwa anasubiri tukutane tena tukiwa wakubwa” Ndio
mawazo yake yalivyokuwa yakimueleza maana moyo wake ulimpenda Erick
vilivyo. Shule ilifungwa na wanafunzi walikuwa wakirudi likizo,
alipanda kwenye basi na wanafunzi wengine, ila siti aliyokaa yeye alipakana na
kijana mmoja ambaye pia alikuwa ni mwanafunzi anarudi kwao likizo, Yule kijana
alianza kwa kumuongelesha Erica, “Naitwa John, sijui mwenzangu unaitwa
nani” “Naitwa Erica” “Oooh jina zuri sana, unajua safari ni
ndefu mno bora tuzoeane tu. Unaishi sehemu gani?” Erica alianza
kuzungumza na yule John na kujikuta wakiongelea habari nyingi za hapa na pale
ila mwisho wa siku John akamuomba Erica namba za simu, “Sina
simu” “Mmmh huna simu mdada wa kidato cha tano?” “Ndio sina
simu, shuleni wanakataza. Nyumbani ndio kabisa, dadangu aliniambia nikimaliza
kidato cha sita ataninunulia” “Sasa itakuwaje? Mi napenda tuendelee
kuwasiliana” “Sijui itakavyokuwa, tutawasiliana tu siku nyingine
tukionana ila simu mimi sina” John akafungua begi lake la mgongoni na
kutoa simu, “Nina simu mbili, naomba uchukue hii moja tuwe
tunawasiliana, natamani niwe na mawasiliano na wewe ya karibu sana Erica.
Tafadhali naomba usikatae” “Mmmh sasa wewe unaniamini nini mimi hadi
kunipa simu?” “Moyo wangu umekuamini Erica, tafadhali chukua simu hii
tuwe tunawasiliana nakuomba, laini ipo nitakuwa nakupigia hata kama ukikosa
vocha uwe unaniambia nikurushie” John alimbembeleza sana Erica naye
Erica aliona John ana moyo wa kipekee sana yani kumpa simu mtu asiye mfahamu
vizuri ni kitu cha ajabu sana. Baada ya kubembelezwa sana Erica alikubali simu
ile kwani kiukweli hata yeye alitamani sana kumiliki simu ila tu kwao walikuwa
wanamzingua kumnunulia kwahiyo bahati ya kupewa simu na Yule kijana ilikuwa ni
nzuri sana kwake ukizingatia Yule ni mwanafunzi mwenzie kwahiyo aliona katoa kwa
upendo tu. Erica alifikia nyumbani kwao maana mama yake alisema
likizo awe anarudi nyumbani, kwahiyo ile simu aliyopewa na John aliificha
chumbani kwake. Ila likizo yake alikuwa akishinda sana chumbani kiasi
kwamba mama yake akajua ni sababu ya kushinda sana shuleni kumbe alikuwa makini
akiwasiliana kwa njia ya ujumbe na John, ila kila mama yake alipomuita aliificha
ile simu. Alikuwa akiwasiliana na John kiasi kwamba aliona kuwa anaanza kumpenda
John hata akasahau kama kuna mtu wa kuitwa Erick kwenye kichwa
chake, “Unajua Erica wewe ni msichana mrembo sana, natamani siku moja
uje kuwa mke wangu” “Jamani John mmmh!” “Tupange kuonana kabla
ya kurudi shule” “Sasa tutaonana wapi?” “Kuna sehemu nzuri sana
mitaa ya Kigamboni, nitakwambia na tutaonana mapema sana halafu utarudi kwenu
jioni” “Sijui kama nitaweza, sijui kama nitapewa
ruhusa” “Kwanini wasikuruhusu binti mkubwa tu!” “Kwetu ni watu
wa dini sana, mama yangu ni mlokole yani hataki nitoke kabisa hata sijui
nitamuagaje” “Huwezi kumwambia unaenda kusalimia ndugu
zako?” “Yani mimi kutoka nyumbani labda dada yangu akijaga kunichukua
kuwa twende nae mahali, na kusalimia ndugu wote anakujaga kunichukua yeye. Yule
dada yangu aliyekuja kunipokea stendi” “Sasa tutaonana vipi
Erica?” “Sijui” “Hutaki kujifunza mapenzi wewe?” “Mmmh
naogopa ujue” “Usiogope nitakufundisha” Erica aliitwa na mama
yake ikabidi aache simu na kwenda kumsikiliza, “Mwanangu Erica mbona
toka umerudi unajifungia tu chumbani au bado una mambo yale yale yaliyopita
mwanangu? Yaliyopitwa si ndwele jamani Erica” “Hapana mama sijifungii
sababu hiyo nakuwa tu nimechoka” “Kuwa mkweli mwanangu, yani nimeomba
likizo urudi hapa nyumbani. Maana toka kipindi kile chote umekaa kwa dada yako,
nikaona mwanangu umeenda mbali sana, nikaomba urudi hapa ili nikae kae na wewe
japo kidogo ila tangu umerudi ni kujifungia ndani tu hadi sielewi kuwa una
tatizo gani?” “Hapana mama sina tatizo lolote” “Basi uwe unakuja
tunaongea ongea kidogo, hujanimiss mama yako jamani! Hutaki kuongea kidogo na
mama yako huoni ni furaha hiyo” “Nimekuelewa mama ila hata rafiki zangu
wa mtaani nimewakumbuka, natamani nikawasalimie” “Ukawasalimie nini
watoto mapunguani wale, Yule rafiki yako Johari unajua kama ana
mtoto!” “Ana mtoto?” “Ndio ana mtoto shule ilimshinda, yani
kaendekeza mapenzi mwishowe ana mtoto. Nilikutana nae siku hiyo anaenda kliniki
kachakaa hatari, ndiomana mwanangu nakwambia usome, hao rafiki zako hata sio
watu” “Ila mama ningeenda kuwasalimia tu” “Unataka ukamsalimie
nani Johari? Nitakupeleka kwao maana mimi pia nahitaji kwenda mitaa ya kule kwao
kesho” Erica ilibidi tu akubaliane na mama yake maana sharia za mama
yake zilikuwa zinambana kiasi kwamba alikosa hata raha ya kufanya mambo yake
mengine. Kesho yake kama alivyopanga na mama yake walienda
kwakina Johari, mama yake alikuwa anaongea na mama Johari halafu Johari alibaki
kuongea na Erica, “Kheee Johari kumbe una mtoto kweli?” “Ndio
rafiki yangu nina mtoto” “Shule tena!!” “Unadhani kuna cha shule
hapa, nalea tu. Ila unajua aliyenizalisha?” “Nani?” “Geuka nyuma
umuone anakuja” Erica akageuka, alipomuona alishangaa sana maana
hakuamini kabisa. “Kheee Johari kumbe una mtoto
kweli?” “Ndio rafiki yangu nina mtoto” “Shule
tena!!” “Unadhani kuna cha shule hapa, nalea tu. Ila unajua
aliyenizalisha?” “Nani?” “Geuka nyuma umuone
anakuja” Erica akageuka, alipomuona alishangaa sana maana hakuamini
kabisa. Alimuangalia tena na kumuangalia Johari kisha akamuuliza kwa
mshangao, “Johari umezaa na mwalimu wa nidhamu!” “Ndio hivyo
rafiki yangu” “Sasa nidhamu iko wapi hapo ikiwa mwalimu anazaa na
mwanafunzi? Huyu mwalimu alisababishwa hadi nifukuzwe shule sababu ya busu la
Erick tu ila leo umezaa nae! Inamaana ulikuwa na mahusiano na
mwalimu?” “Erica yani acha tu haya mambo haya sijui nikuelezeje ila acha
tu” Mama yake Erica alimfata Erica na kushangaa pia uwepo wa Yule
mwalimu, ila Erica hakumficha mama yake ni pale pale alimpasulia kuwa mtoto wa
Johari ni wa Yule mwalimu, “Kheee baba kumbe tulijua unatuchungia wanetu
kumbe wewe ndio fisi loh!” Kisha mama Erica akaondoka na Erica na kurudi
nae nyumbani, walipofika tu akaanza kumpa tena sharia zake, “Hapa
nyumbani hutoenda popote zaidi ya kwenda shuleni shule zikifunguliwa, na
nitauliza walimu wako kama umefika shuleni. Ole wako uniletee upuuzi kama wa
mwenzio Yule sijui hiko kitoto chako utakiweka wapi, sitaki ujinga
mimi” Kwa maneno haya ya mama yake aliona itakuwa ni vigumu kabisa hata
kuonana tena na John ingawa alikuwa akiwasiliana nae kwenye
simu. Aliwasiliana na John kwa hakika hakuweza kukutana nae
hadi likizo inaisha ila wakaahidiana aende na simu shuleni ili wawe
wanawasiliana kinyemela kwani aliamini kuwa wapo wanafunzi wenye simu,
alikubaliana nae kufanya hivyo. Siku ya kurudi tena shuleni ilifika na
alifatwa alfajiri na dada yake ili akapandishwe kwenye basi la kwenda shuleni,
katika harakati za kuwahi akajikuta akisahau simu yake chumbani na aligundua
wakati ameshapanda basi la kwenda mkoa. Kwakweli alipatwa na gadhabu
sana na kuwaza ikiwa mama yake ataiona hiyo simu itakuwaje maana hakuwa na
uhakika wa haswa kuwa wapi ameiacha, “Sijui nimeisahau vipi jamani, si
John ataona kuwa namfanyia makusudi? Sijui imekuwaje nimesahau ile
simu” Alifika hadi shuleni akiwa na mawazo ya kusahau simu yake tu huku
akisubiri likizo nyingine akienda nyumbani kwao, ila ilikuwa tofauti kwani
likizo iliyofuata dada yake naye alikuwa kwenye mkoa huo na kumwambia kuwa
atakuwa nae kwenye likizo nzima kwahiyo hakuweza kurudi nyumbani mpaka tarehe ya
kufungua akarudi tena shuleni, alipatwa na mawazo sana ila mwisho wa siku
akaamua kuachana na wazo hilo na kuona kama ni bahati basi anaweza akaja
kukutana tena na Yule John kwa sehemu nyingine. Alimaliza kidato cha
sita na dada yake alihudhuria kwenye mahafali yake na kumwambia kuna zawadi
amemuandalia ambapo wakati wakirudi nyumbani atampatia. Na kweli kipindi
anarudi dada yake akamkabidhi simu na laini na kumwambia kuwa kafurahishwa nae
sana kuweza kumaliza shule na kumzawadia hiyo simu, “Najua ulikuwa
unatamani sana kumiliki simu, hiyo hapo utatumia na nilishamwambia mama
amekubali pia” “Asante sana dada” Basi safari ilifanyika hadi
wakafika nyumbani na kumkabidhi kwa mama yake, kisha dada yake kuelekea nyumbani
kwake. Sababu walifika usiku alikuwa amechoka sana, hivyo alifikia
kuoga, kula na kulala. Kulipokucha akakumbuka kuhusu simu yake
aliyoiacha nyumbani kwao hapo, akajiuliza kuwa aliiacha sehemu gani na je bado
itakuwa nzima au mbovu akaanza kutafuta mule chumbani, alitafuta sana ila
hakuipata, muda kidogo mama yake akamuita, alitoka na
kumsalimia “Unaonekana upo busy sana, unatafuta nini?” “Hamna
kitu mama” “Mmmh mpaka leo Erica bado unamficha mama yako jamani, najua
unachotafuta ni simu” Erica akashtuka kidogo maana hakudhania kuwa mama
yake anajua kuhusu ile simu, alibaki anamtazama tu na mama yake aliendelea
kuongea, “Umekuwa msichana mkubwa sasa na karibia utaenda chuo kikuu,
mwanangu nilikuwa nafanya yote kukulinda ila bado nikashangaa umepata ujasiri wa
kuhongwa simu! Mwanangu mwanaume aliyekuhonga simu hakukutakia mema na maisha
yako, na Mungu ni mkubwa sana ukaisahau, unajua uliisahau wapi?” Erica
aliangalia tu chini, na mama yake aliendelea kuongea “Uliisahau hapo
kwenye meza ya kula chakula. Nilijua tu ni wewe umeiacha maana humu ndani
tunakaa san asana wawili, sasa unajua kilichotokea kwenye ile
simu?” “Sijui” “Basi ile simu ilianza kuita na hukuweka mlio
zaidi ya mtetemeko tu, nilisikia kitu kikiungurumisha mezani, nikakuta anapiga
mtu aitwaye John maana uliandika jina hilo. Nikataka nipokee nijue mbivu na
mbichi kama ujuavyo mama yako sipendi kinishinde chochote, ila kwa bahati mbaya
muda huo nilikuwa nimeweka ndoo maji ili nideki na ile simu iliniponyoka na
kuingia kwenye maji” Erica alishangaa sana, huku akitamani kujua nini
kiliendelea kwahiyo alimuuliza mama yake, “Kwahiyo ndio ikafa
hapo?” “Hapana, niliitoa na kuifungua nilitaka niweke ile laini kwenye
simu nyingine ila wakati natoa ile laini kwenye ile simu ilivunjika, yani laini
ilivunjika kabisa, na simu nimeiacha ndani nadhani imekuwa kopo sasa. Haya
mwanangu uliitoa wapi na John ni nani?” Erica aliona sasa ni njia pekee
ya kujitetea maana mama yake hajajua ukweli wowote wa ile simu, “Ile
simu haikuwa yangu mama, ila kuna rafiki yangu wakati tunarudi aliisahau kwenye
begi langu na bahati mbaya alisafiri kabla yangu kwahiyo alisema nimpelekee
shuleni, na mimi nikaisahau hata sikujua nimeiacha sehemu gani” “Kheee
kumbe ni ya rafiki yako? Na huyo John?” “Hata simjui mama, huniaminigi
tu mama ila mimi sina mambo hayo, unamuona Yule mwalimu aliyesingizia kuwa
kaniona mimi na Erick, kiko wapi sasa ndio kamzalisha Johari, mama kuna watu
hawapendi tu maendeleo yangu, hayo mambo sina” “Jitunze mwanangu,
jitunze nije kula mahali yako nzuri. Uwe mtoto mwema na mzuri, umalize shule
uolewe, mama zenu tulijitunza ndiomana hadi leo tupo kwenye ndoa
zetu” “Sina mambo hayo mama hata usinifikirie vibaya, mimi mwenyewe
nataka nisome na nipate kazi halafu ndio niolewe. Sitaki kuchezea maisha yangu
mama” “Sasa huyo mwenzio ulimalizana nae vipi?” “Nilimueleza
dada Bite, na alimlipa Yule mwenzangu, ndiomana akaninunulia na mimi
simu” “Kwasasa tumia tu simu ila wasiliana na wasichana wenzio sio
wakina John, sijui Erick hapana utaharibu maisha yako” “Jamani mama,
sina mambo hayo” Erica aliona sasa amefaulu ule mtihani wa kutokuaminiwa
na mama yake ingawa alijua wazi hawezi kuwasiliana tena na John, pia hakujua
kama ingetokea siku aneonana tena na Erick, watu hawa alishawatoa kwenye akili
yake ingawa mara moja moja alipatwa na mawazo kuwahusu ila bado hakujua ni yupi
amchague kati yao maana wote walimvutia. Erica kwasasa alikuwa
nyumbani tu na alijiona kuboreka sana ukizingatia hakuwa na wa kuwasiliana nae
na hakuwa na cha kufanya zaidi ya kufanya kazi za nyumbani na kuangalia
televisheni tu. Siku hiyo akiwa anaangalia televisheni usiku akaona
kipindi kinaitwa cha rafiki nakutafuta, akavutiwa nacho. Ilikuwa kwenye saa tano
usiku na aliona watu wakiandika namba zao za simu kuwa wanatafuta marafiki wa
kuwasiliana nao, akaona ni vyema nae aangalie hapo, ndipo alipoinyaka namba moja
na kuandika kwenye simu yake kisha kujaribisha kuipiga, akashangaa ile namba
ikiita akaogopa na kukata. Muda kidogo ile namba ilianza kupigwa, ikaita hadi
kukatika, ikaanza kuita tena akaamua kuzima televisheni na kwenda chumbani kwake
kupokea, ilikuwa ni sauti yam kaka, “Hallow, mambo
umenibipu” “Samahani, niliona namba yako kwenye tv ndio
nikaijaribisha” “Aaah unapenda kuchat” “Ndio” “Unaitwa
nani?” Erica akajiuma uma akajikuta akiropoka tu jina, “Naitwa
Irene, na wewe je?” “Mimi kama jina langu lilivyotokea kwenye screen
naitwa Babuu” “Aah sawa” “Basi tuwe tunachat” Yule
kijana akamuaga pale Erica na kukata simu, kwakweli Erica alihema kiasi na kuona
kumbe wale watu wanaotafuta marafiki wanakuwaga wa kweli yeye alijua ni watu
uongo, ila alishangaa kuona akiongea ni mtu kweli. Aliamua kulala sasa maana
hakuwa na kingine cha kufanya. Alipoamka asubuhi tu alikutana
na ujumbe kwenye simu yake kutoka kwa Babuu, “Hellow Irene, mambo
vipi?” Akatabasamu, ila kwavile hakuwa na vocha alisema kuwa mpaka
anunue vocha ndio ataweka ili awasiliane nae, kwahiyo akaamka vizuri na kwenda
kufanya kazi zingine za pale nyumbani kwao. Kwenye mida ya saa nne
asubuhi alisikia simu yake inaita na kwenda kuiangalia, aliona akiwa Babuu
anapiga, akapokea kwa uoga, “Mambo Irene?” “Safi
tu” “Mbona nakutumia sms zangu hujibu jamani, tatizo nini
mama?” Erica alianza kujiuma uma na kuamua kuongea, “Simu
haikuwa na salio ila nikiweka salio nitakujibu” “Usijali, ngoja
nikuungie kifurushi” Simu ilikatika, na muda mfupi Erica aliona
ameungiwa kifurushi kwenye simu yake, na kubaki tu, “Wow huyu mkaka hata
hanijui masikini ya Mungu jamani ila ameniungia kifurushi loh ngoja niwasiliane
nae” Akaanza kutumiana ujumbe na Babuu kwa njia ya ujumbe alijikuta
akitumia simu mara kwa mara kuandika ujumbe kwa kuwasiliana na huyo babuu
alishangaa sababu ni mtu ambaye alikuwa kila muda lazima awezeshe kuchat
nae. Toka Erica afahamiane na Babuu ilikuwa ni muda wote kuwa
na simu yake, alikuwa na hiyari akale chakula chumbani ili atumie simu yake
kuwasiliana na Babuu kwa njia ya ujumbe, “Nakupenda Irene” “Mmmh
utanipendaje na hujawahi kuniona!” “Irene, moyo ni kitu cha ajabu sana.
Ni kweli sijawahi kukuona ila huwezi amini, kila siku nakuona kwenye ndoto
zangu. Nakupenda Irene, naimani wewe ndiye mwanamke unayefaa kuwa mke
wangu” “Mmmh Babuu jamani” “Kweli kabisa, ila sijui kama wewe
utanipenda mimi. Mwenzio nakupenda” “Kwani wewe upoje?” “Mimi ni
mfupi kiasi na mweusi kiasi” “Mmmh” “Mbona
unaguna?” “Kiukweli wanaume wafupi na weusi huwa
siwapendi” “Kwanini?” “Basi tu siwapendi” “Jamani Irene
usinifanyie hivyo, basi tupange siku moja tuonane kwa hakika nitaridhika hata
nikikuona” “Hakuna shida tutaonana ila mi naona bora tuendelee
kuwasiliana tu hivi hivi, yani wanaume wafupi halafu weusi siwapendagi hata
kidogo” “Sawa ila siku zote Irene utakaa katika moyo wangu, nakupenda
sana” Erica alijikuta akiwaza sana kuhusu muonekano wa Babuu, alivutiwa
na mawasiliano ya Babuu yalivyo ila hakuvutiwa na jinsi Babuu alivyomwambia kuwa
yupo hivyo. “Aaah hapana siwezi kumpenda hata kama yeye ananipenda
vilivyo ila mimi kumpenda siwezi. Yani mi napenda mwanaume awe mrefu halafu awe
na maji ya kunde, nikimpata kama huyo nitafurahi sana” Akawaza pale,
akakumbuka mwanaume aliyekuwa vile alivyokuwa anapenda yeye alikuwa ni
Erick, “Mmmh kweli Erick alikuwa ninavyopenda mimi ila je Erick
alinipenda kweli? Erick alitongoza wadada wengi shuleni, inawezekana Johari
aliongea ukweli kuwa Erick alitaka kunichezea tu. Ila hivi mimi nitapata mpenzi
kweli? Natamani na mimi niwe na mpenzi, nipate mwanaume nimpende na badae aje
kuwa mume wangu nitafurahi sana, sijui kama nitampata? Muda wote nipo nyumbani
ndani, hata njiani sionekani, kuna dalili yoyote ya kupata mwanaume kweli? Labda
nikienda chuo” Aliwaza sana ila hakupata majibu. Babuu
aliendelea kusisitiza kuhusu swala la kuonana na Erica ambaye yeye alimjua kwa
jina la Irene sababu ndio jina alilojitambulisha nalo kwake, ilibidi Erica
amwambie jinsi ilivyokuwa ngumu kwa yeye kutoka nyumbani kwao, “Jamani
Irene si umesema ndio umemaliza kidato cha sita
wewe?” “Ndio” “Sasa watakukataza vipi na ushakuwa mkubwa? Huwezi
kusema unataka kwenda kumtembelea rafiki yako?” “Hata sijui nyumbani
nitasemaje maana kama ni rafiki wa hapa mtaani mama atasema twende
wote” “Wewe hupendi kutembea ufukweni?” “Napenda” “Basi
mimi nataka tukutane ufukweni, yani tuonane tu nitaridhika. Najua kunipenda
huwezi Irene ila tuonane tu basi ili tufahamiane kwa sura” “Sawa ila
kwetu nitaagaje?” “Ngoja nikufundishe, leo mwambie mamako kuwa kuna
rafiki yako anaumwa na kesho mmepanga kukutana na wenzio ili mkamuone hospitali,
na hakika atakuruhusu tu. Mwambie rafiki yako ambaye hamjui yeye mliyesoma nae
bweni huko, mtaje yeyote” “Basi nitajaribu” “Haya utaniambia ili
kesho nijiandae kukutana na wewe malaika wangu” “Mmmh!” “Usigune
bhana, wewe ni malaika wangu” “Ila si nimekwambia
sitaki” “Nisamehe bure ni moyo wangu ndio king’ang’anizi, ila naomba
tuonane tu Irene” Basi Erica akajaribu tu kuongea na mama yake kamavile
alivyoelekezwa ila mama yake alimkubalia hata yeye mwenyewe akashangaa kuwa mama
yake mbona kawa mwepesi vile kukubali. “Nitakupa na nauli mwanangu, ni
vyema kuwa na ushirikiano hivyo na wenzio” “Asante mama” Erica
alifurahi sana, yani siku hiyo alilala huku akitabasamu. Kesho
yake alijiandaa vizuri kabisa, na kwenda kumuaga mama yake ambaye kweli alimpa
nauli kama alivyomuahidi maana alijua ni kweli anaenda hospitali kumuona mwenzao
anayeumwa ila ukweli ni kuwa Erica alikuwa anaenda kuonana na
Babuu. Erica alifika hadi eneo ambalo alipanga kukutana na Babuu,
akampigia simu alipo ila alishangaa Babuu akimwambia Erica. “Nishakuona
tayari, nakuja hapo sasa hivi” Erica akashangaa kwani Babuu alikuwa
hamjui Erica kwa sura halafu kamwambia nimeshakuona, akashangaa amemuona vipi,
akiwa anashangaa mara kuna mtu alimshika began a
kumuita, “Irene” Aligeuka na kumuangali, ila Erica alipigwa na
bumbuwazi kiasi kwamba hakuweza kuongea chochote kwa wakati
huo. Erica akashangaa kwani Babuu alikuwa hamjui Erica
kwa sura halafu kamwambia nimeshakuona, akashangaa amemuona vipi, akiwa
anashangaa mara kuna mtu alimshika began a
kumuita, “Irene” Aligeuka na kumuangali, ila Erica alipigwa na
bumbuwazi kiasi kwamba hakuweza kuongea chochote kwa wakati huo. Babuu
alimuuliza Erica, “Mbona unashangaa?” Erica alikuwa kimya kwenye
mshangao, na baada ya muda alimuuliza, “Si ulisema wewe
mfupi?” “Ndio mimi ni mfupi, kwani nina urefu gani?” “Si ulisema
wewe ni mweusi?” “Ndio mimi ni mweusi kwani nina weupe
gani?” Erica alikuwa kwenye mshangao bado kwani Babuu aliyekuwa
akimfikiria sio huyu aliyemuona kwenye macho yake, Babuu huyu alikuwa ni kijana
anayevutia sana na alivutia macho yake kiasi cha kumfanya Erica hata aone aibu
kumtazama. Ila Babuu alimshika mkono Erica na kwenda kukaa nae mahali
pale pale ufukweni ili waongee mawili matatu, na waliongea kweli ila Erica
alitumia muda mwingi sana kumuangalia Babuu kiasi kwamba hata Babuu aliposema
kuwa ni muda wa kuondoka ilikuwa ngumu sana kwa Erica kukubaliana na hilo ila
kila alipokumbuka kwao ilibidi tu atake kuondoka na yeye. Ila aliamua kumwambia
Babuu ukweli wa jina lake, “Babuu mimi sio Irene, ila naitwa Erica.
Nilikudanganya tu” “Usijali Irene, ooh sorry Erica, ila nimezoea kukuita
Irene, usijali jina sio tatizo kwangu” “Sawa hamna shida hata ukiniita
hilo Irene sio tatizo” Walienda hadi kwenye stendi ya daladala ambapo
Babuu alihakikisha Erica kapanda basi ya kwenda kwao halafu akampa na nauli,
kisha yeye kuondoka zake. Yani Erica mule kwenye daladala alijikuta
akiwaza kuhusu Babuu tu, alimuwaza sana Babuu hadi anafika nyumbani
kwao. Alipoingia ndani, mama yake alimuuliza, “Mbona
umechelewa?” “Foleni mama” “Kwani ni hospitali
gani?” “Ni Muhimbili” “Anaendeleaje” “Hajambo anaweza
akaruhusiwa kesho” “Eeeh Mungu ni mwema kwakweli, nimekuwa nikimuombea
jamani bora aruhusiwe tu” Erica aliongea ongea pale kidogo na mama yake
kisha kwenda chumbani ila mawazo mengi yalikuwa kwa huyu mtu anayeitwa
Babuu. Alioga na kula huku akiwaza sana, alitamani Babuu amtongoze tena
na kusema iwapo itatokea hiyo nafasi basi atamkubali haraka
iwezekanavyo, “Hivi mkaka mzuri vile kweli anakosa wanawake hadi atafute
kwenye tv? Mbona mkaka mzuri Yule” Ujumbe kutoka kwa Babuu
ukaingia, “Wewe ni msichana mrembo sana, macho yangu yalitamani muda
wote yakutazame wewe, kwa hakika nakupenda. Tafadhali Erica usinikatae
utanitesa” Erica aliusoma ujumbe huu mara mbili mbili, kisha
akamjibu, “Ni kweli kabisa unanipenda Babuu?” “Nakupenda sana
tena sana Erica” “Na mimi nakupenda pia” Inaonyesha Babuu
hakuamini kabisa kwani alipiga na simu ili kuhakikisha kuwa anayewasiliana nae
kwenye ujumbe ni Erica na leo kamjibu kuwa anampenda pia, walianza kuongea
kwenye simu ila Erica alikuwa na aibu sana na kumuomba Babuu kuwa waendelee
kuongea kwa njia ya ujumbe. Ikabidi Babuu akate na waendelee kwa njia ya
ujumbe, “Unajua furaha niliyo nayo hadi siamini kama kweli umenikubalia
Erica, nakupenda sana naahidi kukupenda siku zote za maisha
yangu” “Nakupenda pia Babuu” “Sijawahi kumpenda msichana yeyote
katika maisha yangu, wewe ni msichana wa kwanza kabisa. Nakupenda sana, naimani
nitadumu na wewe mpaka mwisho wangu” Erica alikuwa akitabasamu tu na
alijikuta akiwasiliana na Babuu hadi usiku wa manane wa siku
hiyo. Kesho yake aliamka saa mbili na nusu asubuhi hadi mama
yake akamshangaa maana sio kawaida yake kuchelewa hivyo kuamka, huwa akichelewa
sana basi ni saa moja asubuhi kwahiyo kuamka saa mbili na nusu siku hiyo ilikuwa
ajabu kidogo. “Leo mwanangu umechelewa kuamka?” “Leo usingizi
ulikuwa mtamu mama nahisi ndiomana nimechelewa kuamka” Alifanya shughuli
zake ila alionekana kuwa na furaha sana hata mama yake akashangaa kuwa mtoto
wake kuwa na furaha vile ni kitu cha ajabu. Siku hiyo alifika dada yake
Bite kumsalimia mama yao, kwahiyo nay eye alipata muda wa kuongea nae kidogo
kama kawaida yake, “Dada, hivi mapenzi ni nini?” “Mapenzi ni
kitu flani hivi ambacho unajisikia moyoni kuwa unampenda mtu Fulani halafu mtu
huyo nae anakupenda wewe. Yani mapenzi ni kupendana, ila raha ya mapenzi ni
kupendwa. Kupendwa raha mdogo wangu asikwambie mtu” “Na utajuaje kama
mtu anakupenda?” “Anakujali, anakusikiliza na ana hisia na
wewe” “Mmmh ni hivyo tu?” “Maelezo marefu bhana, kuna mtu
anakupenda nini mdogo wangu?” “Hamna dada nimeuliza tu, na hivi unajuaje
kama unampenda mtu Fulani?” “Unajisikia moyoni kuwa unampenda halafu
unakuwa na wivu na mtu huyo yani inakujaga tu automatically” Erica
alimsikiliza dada yake ila kama alikuwa anamuelewa na kama alikuwa hamuelewi
kwani kwa muda huo mawazo yake ni Babuu tu. Na aliendelea kuwasiliana na
Babuu siku zote ila kuonana nae ilikuwa ngumu sababu ya kukosa ruhusa ya
kutembea tembea kutoka kwao. Erica alibahatika kuchaguliwa chuo
kwahiyo alikuwa na harakati za kuanza chuo ambapo ilimlazimu kukaa hosteli, kitu
ambacho kwa upande mwingine alikipenda sana kwani aliona kuwa atakuwa huru sasa
na kuonana na Babuu na akajiona atapanga vingi sana akiwa anaonana na
Babuu. Alimuona Babuu kama ni kijana pekee katika maisha yake, akampenda
kupita maelezo ya kawaida hata siku zilivyoenda na Babuu kumuomba mapenzi hakuwa
na sababu ya kumkatalia kwani ameshakuwa ni mpenzi wake wa muda mrefu, na
walionyesha kupendana sana. “Pole Erica ila nimefurahi sana mimi kuwa
mwanaume wa kwanza kwako, naahidi kukupenda siku zote za maisha
yangu” “Asante Babuu, natumaini wewe ndiye mume
wangu” Walijikuta muda mwingi sana wakiongea kuhusu maswala ya mapenzi
yao tu, mpaka watu wengine aliokuwa analala nao Erica kwenye chumba walikuwa
wakishikwa na wivu ila pale chuo alipata rafiki aliyeitwa Dora na walipatana
sana. Miezi mitatu tangu aanze chuo alienda kumtembelea dada yake Bite,
ila leo dada yake alimpa usia mpya kabisa, “Mdogo wangu, usikubali
kulala na mwanaume mpaka uolewe” Alimuitikia dada yake lakini huo usia
alishauvunja kwa kulala na Babuu kwani aliamini ndiye mwanaume ampendaye
ukweli. Alimtambulisha Babuu kwa rafiki yake Dora, baada ya
Babuu kuondoka rafiki yake alimuuliza, “Yule Babuu anjishughulisha na
nini?” “Yupo tu, aliishia kidato cha nne na alishindwa kuendelea na
masomo kwahiyo kuna shughuli shughuli anajishughulisha nazo” “Unajua
rafiki yangu unaenda kuwa na shahada, yani mwanaume wa kidato cha nne hakufai
tena” “Una maana gani?” “Aaah usinifikirie vibaya, ila Babuu
hatokufaa tena” “Mimi nampenda Babuu na ninaamini kuwa yeye ndiye
mwanaume bora kwangu” “Mmmh haya, ila mimi nimesema tu usinifikirie
vibaya” Erica hakupenda huo ushauri maana aliona kwa Babuu amefika na
hakutaka mwanaume mwingine zaidi ya Babuu. Jioni ya siku hiyo kama
kawaida Babuu alienda tena kumtembelea Erica kwenye hosteli yao, “Babuu
huchoki kunitembelea, mchana si ulikuwa huku huku?” “Ndio Erica hivi
nawezaje kuchoka kumuona kila muda msichana nimpendae? Sichoki sababu nakupenda
na muda mwingi nahitaji kuwa na wewe Erica” “Naelewa na mimi najisemea
tu kiukweli nafurahi sana unavyokuja mara kwa mara kuniona, unafanya niamini
kweli Babuu unanipenda” Walijikuta wanaongea sana hadi usiku
kabisa, “Mmh Erica leo nimechelewa?” “Umechelewa sana mpenzi, na
usafiri saivi haukatishi huku sijui utafanyaje mpenzi?” “Usijali
nitafika tu nyumbani, mbona siku nyingine nafika” “Lakini huchelewagi
kama leo” “Au niende pale kwenye nyumba ya wageni
nikalale” “Usiniudhi Babuu, sasa kwenye nyumba ya wageni pale ukalale na
nani? Bora uende kwenu, mi siafikiani na swala la wewe kwenda kulala nyumba ya
wageni vishawishi ni vingi” Erica alionyesha kuchukizwa kiasi, ikabidi
Babuu amuahidi kuwa atarudi kwao kwa njia yoyote ile. Basi akambusu kisha
wakaagana na kuanza kuondoka. Erica alirudi hosteli ila usiku huo
ilikuwa ajabu sana maana Babuu hakumtafuta kabisa hata kuwasiliana nae
hakuwasiliana nae na kufanya Erica ashangae maana haikuwa kawaida yao, ikabidi
amtumie ujumbe ila ujumbe wake haukujibiwa, na alipiga simu ila simu yake
haikupokelewa kwa mara ya kwanza Erica alipata maumivu ya mapenzi moyoni mwake
maana hakuelewa ni kwanini Babuu hakutaka kupokea simu yake, alimtafuta vilivyo
ila Babuu hakupokea simu yake kabisa. Siku hiyo hata usingizi hakuupata
kabisa yani hakuweza kulala sababu ya mawazo, alijikuta akifikiria sana kuwa
Babuu kapatwa na majanga gani au kapitia nyumba ya wageni kama alivyosema yani
alijikuta akiwa na mawazo lukuki. Kesho yake alivyofika chuoni
tu, kutokana na mawazo yake alijikuta akigongana na mkaka mmoja kitendo
kilichofanya aangushe vitabu vya Yule kaka, ikabidi ainame na kuanza kumuokotea
huku akimuomba msamaha, “Samahani sana” “Bila samahani, najua ni
bahati mbaya tu. Ila ni vizuri tukafahamiana” “Sawa, naitwa Erica nipo
mwaka wa kwanza” “Sawa, naitwa George nipo mwaka wa tatu. Ni vizuri
kufahamiana, na kama hivyo upo mwaka wa kwanza unapata urahisi wa kusaidiwa na
mimi. Halafu mimi ni waziri wa michezo” “Aaaah sawa, nashukuru
kukufahamu” Basi George akamuomba Erica namba ya simu ili wawe
wanawasiliana, kisha Erica aliendelea na harakati zake za kuwahi
kipindi. Baada ya kipindi tu alitafutwa na George na kumuita mgahawani
waweze kula pamoja na kuongea ongea, Erica alienda kumsikiliza ingawa alikuwa na
mawazo sana kipindi hiko kuhusu Babuu. Alifika mgahawani na kumkuta
George yupo mahali pale, na kumuagizia chakula “Umejuaje napenda chakula
hicho?” “Nimejua tu, unajua kuna vitu tunavyo sisi watoto wa kiume. Yani
Mungu katuumba na upeo wa ajabu sana, huwezi jua ila nimejua kwa kukuangalia tu
kuwa unapenda chakula gani” “Mmmh basi wewe ni noma” Chakula
kililetwa na walianza kula huku wakiongea habari za pale chuoni, :”Chuo
unakionaje?” “Ni kizuri, unajua ndoto zangu ilikuwa ni kusoma chuo hiki
kwahiyo kitendo cha ndoto zangu kutimia kwasasa kimenifurahisha
sana” “Na hujapotea, hiki ni chuo bora kati ya vyuo vyote. Na daima
hutoa watu bora, ndoto zako za badae ni nini baada ya
hapa?” “Nikimaliza, nitatafuta kazi” “Kwahiyo unawaza
kuajiriwa?” “Ndio, sasa nitawaza nini zaidi?” “Ila nyie watoto
wa kike hamna tatizo, sisi watoto wa kiume ndio watafutaji wa haswaaa. Mi
nikimaliza chuo naenda kuendeleza biashara zangu, kwahiyo kazi itakuwa ni akiba
tu, yani labda mshahara wangu wa kwenye kazi ni kumpa mke wangu pesa hizo atumie
labda saluni au matumizi yake mengine kwani najua biashara zangu zinalipa
sana” “Kumbe una biashara?” “Ndio, mimi nasoma huku naendeleza
biashara zangu kwahiyo nikimaliza chuo ndio nitazisimamia vizuri
zaidi” “Hongera sana, ni vijana wachache sana wanaofanya
hivyo” “Vijana wanaofanya hivi ni wale wanaofikiria maisha yao ya badae,
najua badae nahitaji mke wangu na watoto wasipate tabu kabisa. Nataka kuishi nao
maisha ya kifahari” “Mmmh mkeo atakuwa na raha sana” “Kawaida
tu, lazima mke apate raha na afurahie maisha. Ila ukiwa na shida yoyote Erica
usisite kuniambia” Walicheka na kuongea mengi sana kisha kuagana na
kuahidi kuendelea kuwasiliana mara kwa mara. Erica alirudi
hosteli na siku hiyo alijiandaa na kurudi kwao kumsalimia mama yake maana
alimkumbuka tayari na ukizingatia ilikuwa ni mwisho wa wiki, alifika na
kumsalimia mama yake kisha kuongea nae mawili matatu. “Umemuona rafiki
yako Johari?” “Sijamuona” “Kachakaa jamani, yani kachakaa
vilivyo. Unajua nyinyi mabinti mnajiingizaga kwenye mambo mengine bila ya
kufikiria kwa makini, haya sasa huyo mwalimu ni anampa nini zaidi ya kumuongezea
mikosi tu” “Jamani mama kwanini unasema hivyo?” “Unajua Yule
mwalimu alifukuzwa kazi sababu hakuonyesha maadili mazuri shuleni pale, hana
kazi nyingine wala biashara yani yupo yupo tu. Rafiki yako Johari kajidumbukiza
haswaa na atajutia maisha yake yote. Unajua unapoamua kuwa na mwanaume angalia
mwanaume mwenye faida na wewe, kwanza kabisa awe msomi, ajue kutafuta pesa,
asitegemee kazi tu maana kuna leo na kesho akifukuzwa kazi, ujasiliamali
utawawezesha ila wanaume ambao wapo wapo tu sio wanaume wa kupoteza nao muda
kwakweli. Mwanangu kuwa makini, chagua mwanaume sahihi katika maisha yako,
ukipata mwanaume wa kukuoa uangalie vigezo hivyo nilivyosema” Erica
aliongea ongea na mama yake pale ila badae alipokaa na kujifikiria aliona kuwa
sifa anazozisema mama yake basi zote zipo kwa George, “Mmmh ndio kusema
George anafaa kuwa mume wangu jamani!” Aliwaza sana, na upande mwingine
akamfikiria Babuu, “Mmmh kuna Babuu, tulipendana sana ila mbona
hanitafuti tena hewani? Ila Babuu hana sifa anazozisema mama, sio msomi kama
mimi nitakavyokuwa na shughuli zake hazieleweki kabisa, ila George yupo sawa,
halafu nahisi ananipenda na atanitongoza tu” Alijikuta akimlinganisha
George na Babuu ila hakuelewa atafanyaje fanyaje maana bado alikuwa akimpenda
Babuu ila aliona kuwa George ndio mwanaume anayemfaa kwani ana sifa zote
zilizotajwa na mama yake. Erica alienda tena chuoni ila
aliendelea kuwasiliana na George, sema tu toka siku ile hakuweza kumpata Babuu
hewani kabisa na kumfanya kuhisi kuwa Babuu ana msichana mwingine ila kwavile
alimpata George kuwasiliana nae aliona faraja kiasi. Na siku hiyo George
aliomba kuonana nae kwenye vimbweta vya pale chuoni, na alikutana nae na
kuzungumza, “Hivi Erica una mpenzi?” Erica akacheka na
kujibu, “Hapana, sina mpenzi” “Oooh Mungu ni mwema kunikutanisha
na wewe” Wakati anaongea na George pale, aliangalia pembeni gafla
akamuona Babuu akiwa na nguo zile zile ambazo alivaa siku ile usiku na
alionekana akimtafuta yeye mwenyewe. Wakati anaongea
na George pale, aliangalia pembeni gafla akamuona Babuu akiwa na nguo zile zile
ambazo alivaa siku ile usiku na alionekana akimtafuta yeye
mwenyewe. Erica aliona Babuu atamuharibia hapo, ikabidi aombe udhuru
kidogo kwa George kisha akaondoka zake na kwenda sehemu nyingine kwani hakutaka
kabisa kuonana na Babuu. Kwa bahati nzuri Babuu alikutana na Dora na
kumsalimia kisha kumuuliza kuhusu alipo Erica, “Mmmh hata sijui,
sijaonana nae leo. Kwanini usimpigie simu yake?” “Simu yangu
imezimika” “Na mbona upo hivyo una tatizo gani?” “Nilipata
matatizo, niliwekwa selo na nimetoka leo. Moja kwa moja nimekuja hapa ili
nionane tu na Erica halafu niende kwetu” “Pole kwa matatizo, ila na wewe
ulishindwa kwenda kwanza kwenu ndio uje huku kumtafuta Erica?” Babuu
alijiangalia na kweli akajiona kuwa ni mchafu mchafu, kwa aibu akaamua kumuaga
Dora na kuondoka zake. Dora alimuangalia Babuu na kumsikitikia, “Kijana
mzuri ila tatizo hajasoma. Mmmh! Pole yake” Kisha akaondoka zake na
kuelekea hosteli ya kwa kina Erica. Alimkuta Erica amejiinamia
tu nje ya hosteli yao, “Vipi Erica?” “Safi tu” “Umemuona
Babuu?” “Sitaki hata kumuona huyo mtu” “Bora usitake kumuona,
yani kaja mchafu huyo balaa, eti anasema aliwekwa
selo” “Selo?” “Ndio, alikuwa rumande nadhani alikamatwa na
polisi. Ndio mwanaume wa kuwa naye huyo loh hapana jamani, sio saizi yako
kabisa, hakufai” Mara simu ya Erica ilianza kuita alipoiangalia alikuwa
ni George anapiga, akapokea “Erica mbona hukurudi tena au nilikuwa
nakuboa na maswali yangu?” “Hapana George, tumbo liliniuma gafla
nikarudi hosteli” “Aaah pole sana, naomba nielekeze hosteli uliyopo
nije” Basi ikabidi Erica amuelekeze George alipo kisha akakata simu, ila
alitaka kumdanganya Dora ambapo Dora alimshtukia kabla
hajamdanganya, “Mmmh usinidanganye Erica, nimeona sura yako unataka
kunidanganya, bora uniambie ukweli tu. Ni nani huyo ulikuwa unazungumza
nae?” “Humjui” “Nimekusikia unamuelekeza hapa hosteli, nasubiri
nimuone nimjue” “Mmmh na wewe Dora loh!” “Nini sasa kwani
vibaya? Mimi na wewe tumeanza kufichana Erica?” “Hapana, basi
utamuona” Wakaendelea na maongezi mengine, na baada ya muda mfupi George
alifika pale walipo Erica na Dora, ikabidi Erica amtambulishe kwa Dora kuwa ni
rafiki yake, “Na huyu ni kaka yangu anaitwa George” “Mmmh Erica!
Kaka yako!” “Mmmh wewe nae Dora jamani, karibu George” George
alikuwa akicheka tu kwa kuwasikiliza wale mabinti wawili, kisha baada ya muda
kidogo Dora aliaga na kuondoka zake kwani alijua anatakiwa kuwapa nafasi ya
kuongea hawa wawili. Alipoondoka tu, George alimuomba Erica kuwa
ampeleke hospitali, “Hapana George nimeshapona” “Najali afya
yako Erica jamani” “Usijali nimeshapona” “Sawa, kuna jambo
napenda kukuomba” “Jambo gani hilo?” “Napenda kuanzia sasa mimi
na wewe tusiwe marafiki tu bali tuwe wapenzi na badae uje kuwa mke
wangu” Erica alikaa kimya kidogo kwani neno hili alikuwa akilitamani
muda sana, ila hakuweza kujibu kwa muda huo huo sababu ya aibu. George
akamwambia tena, “Naomba nikuachie muda utafakali swala hilo kwani najua
ni gafla tu nimekwambia, Erica tutawasiliana badae” Basi George
alimuacha Erica na kuondoka zake, ila angejua ukweli kuwa Erica alishamkubali
toka kitambo tu na alikuwa akingoja kauli tu kuwa anampenda ila pale pale
alishindwa kumjibu. Usiku wa siku hiyo alikuwa akiona simu yake
ikipigwa na Babuu ila hakupokea kabisa, yani Babuu alipiga na kupiga ila Erica
hakupokea badala yake muda huo alikuwa akiwasiliana na George kwa njia ya ujumbe
kuwa amekubali kuwa mpenzi wake, kwahiyo kwenye moyo wake alianza kumuweka
George na vile alihisi kuwa Babuu ni msaliti hakumtaka tena kuonana na Babuu
wala kuwa na Babuu. Basi wakaahidiana na George kuonana kesho yake ili kuongea
vizuri zaidi. Na kweli kesho yake wakaonana na kuongea mengi zaidi,
George alitaka kupima uaminifu wa Erica na kumuomba simu yake
kidogo, “Naomba simu yako kidogo, nikae nayo tukiwa
tunazungumza” “Mmmh kwanini?” “Niangalie tu picha zilizopo, na
wewe shika ya kwangu” George akampa Erica simu yake naye Erica akampa
George simu yake ila kimoyomoyo alishukuru sababu alikuwa amefuta picha zote
alizowahi kupiga na Babuu pale tu alipoumia moyo na kuhisi kuwa Babuu anamsaliti
kwahiyo hakukuwa na chochote cha Babuu. Wakati George ameshika ile simu
ya Erica akiangalia angalia picha zilizomo mara uliingia ujumbe kwenye simu ile,
na ilionekana umetoka kwa Babuu, George akaufungua ule ujumbe na
kuusoma; “Erica mpenzi wangu, nakupigia simu ila hupokei sijui tatizo ni
nini. Lakini mwenzio nilipatwa na matatizo, siku ile nilipokuwa natoka kuonana
na wewe, nilikamatwa na polisi kwa uzurulaji. Basi niliwekwa rumande hadi
walipokuja kunitoa, ila niligoma kwenda nyumbani hadi nikaja chuoni kwenu ila
sikukukuta. Nielewe Erica, usinifikirie vibaya bado nakupenda
sana” George alisoma mara mbili mbili ule ujumbe, kisha aliufuta kabisa
na kumuangalia Erica kisha akamuuliza tena, “Ni kweli Erica hujawahi
kuwa na mpenzi kabla yangu?” Erica alikaa kimya kidogo ila akona ni
vyema amwambie ukweli maana ipo siku Babuu atatokea halafu atashindwa
kujieleza, “Ngoja nikwambie ukweli, nilikuwa na mpenzi wa kuitwa Babuu
ila alinisaliti na kwenda kuwa na wengine nikaamua kuachana nae” “Je
huyo Babuu hukufanya nae chochote?” Erica alijifikiria sana kuhusu hilo,
ila ikabidi ajibu kuwa hajawahi kufanya chochote na Babuu. George aliposikia
vile alifurahi sana, na kuinuka kisha akamkumbatia Erica na
kumwambia, “Nakuomba unipende mimi tu, achana na mawazo ya Babuu huyo
kabisa. Na ninakuomba kitu kimoja, futa namba zake kwenye simu
yako” Erica alichukua simu yake na kufanya hivyo na kuzidi kumfurahisha
zaidi George kiasi ya kwamba George alimuahidi kumpenda mpaka mwisho wa maisha
yake. Ingawa Erica alifuta namba zote za Babuu kwenye simu yake ila ni
wazi kuwa George hakuridhika kwani kesho yake alikuja na laini mpya na kumpa
Erica kuwa atumie laini hiyo na aivunje ile ya zamani, kwahiyo alichokifanya
Erica ni kukopi majina tu kisha kutaarifu ndugu zake wa karibu kuwa kabadilisha
namba ya simu. Hakuona kama ni tatizo kufanya vile sababu alishamuingiza George
moyoni mwake na aliamini kuwa ndiye mume wake wa badae. Erica
alionekana kuwa na furaha sana, hata alipoenda chuo rafiki yake aliweza kugundua
furaha yake, “Niambie ukweli Erica” “Mmmh sijui
nikwambie” “Niambie bhana” “Yule George kuanzia sasa ni shemeji
yako” “Mmmh nilihisi tu, ila anakufaa sana
Yule” “Kwanini?” “Ni mrefu, mtanashati, msomi kwakweli ndio
mwanaume anayekufaa ila sio wakina Babuu” “Hahaha achana na habari za
huyo Babuu sitaki hata kumuona kwasasa” “Kwanini?” “Msaliti
Yule, aliondoka akaenda kulala guest” “Ila una uhakika gani kama
amekusaliti?” “Nahisi tu ni msaliti bhana, tuongelee habari za George
maana nampenda haswaaa” “Hata kwa Babuu ulisema hivyo
hivyo” “Mmmh Dora jamani, ngoja nikuulize kitu hivi mapenzi ni
nini?” “Mapenzi ni kupendana” “Yani kupendana
kiaje?” “Mapenzi ni kumpenda na yeye akupende” “Kama mimi na
George” Dora alicheka tu na kugundua kuwa ni penzi jipya ndiomana
linauliziwa sana, muda kidogo George alimpigia simu na kuhitaji kwenda nae
kwenye chakula cha mchana. Ilipita kama miezi miwili, Babuu
alikosa mawasiliano na Erica kabisa na alipojaribu kwenda chuoni kwao hakuweza
kuonana nae, ikabidi aende tena ili ajaribu kuonana hata na Yule Dora ambaye ni
rafiki wa Erica. Na alikuwa akienda mara kwa mara ila mara zote hakumpata yeyote
kati ya Erica wala Dora, mpaka siku hiyo ilikuwa kama bahati maana alimuona Dora
na kumuita, “Dora” Dora aligeuka nyuma kuangalia ni nani
anamuita na akamuona ni Babuu, akaitika na kusogea ili kumsikiliza kuwa ana
ujumbe gani. “Naomba kuzungumza na wewe Dora” “Hakuna shida,
twende tukakae pale kwenye kimbweta” Basi wakaenda kukaa kisha Babuu
akaanza kutoa maelezo yake. “Nina matatizo Dora, naomba unisaidie niweze
kuonana na Erica” “Si umpigie simu” “Mwanzoni alikuwa hapokei
simu yangu ila kwasasa simpati kabisa hewani, yani huwezi amini kila siku nakuja
hapa chuoni ili kuangalia kama nitamuona ila leo Mungu mkubwa nimekuona wewe.
Tafadhari naomba nisaidie kuonana na Erica” “Nikuulize swali
Babuu?” “Niulize” “Hivi huwezi kuwa na msichana mwingine zaidi
ya Erica?” “Jamani dora! Natumai unajua kuhusu kupenda, nampenda kweli
Erica ninampenda sana” “Na kama yeye hakupendi tena je?” “Kama
yeye hanipendi tena sijui ila ninachojua nina mpenda sana” “Hivi huwezi
hata kujiongeza, mwanamke ulikuwa unampigia simu hapokei simu zako na siku hizi
ukimpigia humpati hewani yani unashindwa kujiongeza tu kuwa
umeachwa?” “Jamani Dora usiniumize moyo wangu, unajua nampenda sana
Erica yani nampenda sana” Dora alimuangalia jinsi Babuu alivyokuwa
akiongea kwa huruma, na mbele yake kidogo akawaona Erica pamoja na George wakiwa
wameongozana huku wameshikana mikono, Dora alimuangalia Babuu na
kumwambia, “Angalia kule ujionee” Babuu aligeuka na kuangalia,
kwakweli hakuamini macho yake na kuyafikicha fikicha yani hakuamini kabisa kama
Erica aliyemopenda kupita maelezo ya kawaida yupo kwa mtu
mwingine, “Hapana Dora, yani Erica kaniacha kweli?” “Ndio
umeachwa, wakati anakupigia simu wewe na hupokei ulikuwa unamaanisha nini? Kama
kuwekwa rumande alikutuma wewe kwenda kuchokoza polisi?” “Dah!
Unaniumiza Dora ila nashukuru sana ingawa roho inaniuma. Mimi nilikamwatwa na
polisi baada ya kutoka kuonana na Erica yani siku hiyo nilichelewa sana kurudi,
ila kama Erica kaamua kunifanyia hivi sawa bhana Mungu atannilipia” Dora
alicheka sana na kumwambia, “Akulipie kwa lipi? Usinichekeshe mie, haya
ni mapenzi tu, ukitendwa sehemu moja tafuta sehemu nyingine ujiliwaze. Pole
sana” Babuu hakuweza kuendelea kukaa mahali pale na kuamua kuondoka
kwani aliona akizidi kuumia tu kwahiyo hakutaka kuendelea kujiumiza moyo kwa
kitu ambacho ameona kwa ushahidi kabisa kuwa Erica ameamua kuachana nae na kuwa
na mwingine kabisa kabisa. Dora wala hakutaka kujisumbua
kumwambia rafiki yake kuwa Babuu alifika akitia huruma badala yake kila
alipokutana nae alimwambia kuwa George anampendeza sana, na siku zote alikuwa
akimsifia George tu katika maongezi yake. Baada ya siku nyingi kupita,
Dora aliamua kumchunguza rafiki yake kuhusu George na kujua kuwa kuna mipango
gani inaendelea baina ya rafiki yake nba George maana ilionyesha kuwa Erica siku
hizi kuna mambo anamficha, kwahiyo aliamua kutumia mbinu ya kuongea nae kwa
kumsifia George ili ajue kinachoendelea baina yao. “Yani George
anakupendeza rafiki yangu balaa” “Mmh Dora, ya kweli
hayo?” “Ndio ni kweli kabisa, anakupendeza sana. Sipati picha siku ya
harusi yenu” “Amesema akimaliza tu chuo ataenda nyumbani kwetu
kujitambulisha na atanivesha pete ya uchumba” “Wow jamani, hongera sana
rafiki yangu. Umepata bahati haswaa, kumpata mwanaume mwenye upendo kama George
ni vigumu sana kwasasa, unatakiwa shoga yangu na wewe kuwa mjuzi usiwe
mshamba” “Mmh ushamba gani tena?” “Kwani hujatembea nae
tu?” “Sijatembea nae, nimemwambia asubirie ndoa” “Hahaha
usinichekeshe ujue, hiyo ndoa ya lini? Hivi wanaume unawajua au unawasikia? Yani
utaona akipendwa mwenzio halafu wewe ukiachwa yani itakuuma moyo? Hivi unajua
kwanini wanaume wanaamua kuoa?” “Kwanini?” “Mwanaume sio kwamba
anafata kupikiwa, kama kupika anajua, sio kufuliwa yani kufua anajua. Ila
anataka hilo tunda la katikati, sasa wewe endelea kumbania utashangaa unakosa
mwana na maji ya moto. Mpe mtoto wa watu afaidi na akupende zaidi” “Mmmh
unanishawishi” “Sikushawishi ila nakwambia ukweli, mpe tunda mtoto wa
mwenzio achanganyikiwe vizuri na hakika baada ya hapo yani atakupenda
maradufu” Maneno ya Dora yalimuingia kichwani Erica vilivyo ukizingatia
ni mara nyingi tu George amemuomba kufanya nae mapenzi ila alimkatalia kwa
kumwambia kuwa wasubirie ndoa ila maneno ya rafiki yake yalimfanya aseme kuwa
George akimwambia tena basi amkubalie. Ilikuwa siku ya kuzaliwa
ya George na aliamua kwenda kwenye matembezi na mpenzi wake
Erica, “Utanipa zawadi gani kwenye siku yangu hii muhimu?” Erica
alicheka tu, “Tafadhali Erica usiishie kucheka ujue nakupenda, na
ninatamani kuwa na wewe” Erica alijikuta amemkubalia George kuwa yupo
tayari kutembea naye kwa siku hiyo, kwakweli George alifurahi sana na kutafuta
chumba maeneo yale haraka iwezekanavyo. Wakiwa ndani baada ya tendo,
George alionekana kuchukizwa sana kisha kuchukua nguo zake na kuvaa halafu
alimuangalia kwa chuki sana Erica, mpaka Erica aliogopa na
kumuuliza, “Vipi George imekuwaje?” “Vaa nguo
twende” “Imekuwaje tena George?” Safari hii George aliongea kwa
ukali, “Nimesema vaa nguo twende” Kisha George alitoka nje,
ikabidi Erica nae achukue nguo zake na kuvaa upesi upesi huku akijiuliza kuwa ni
kitu gani amefanya. Kisha George alitoka nje, ikabidi
Erica nae achukue nguo zake na kuvaa upesi upesi huku akijiuliza kuwa ni kitu
gani amefanya. Lakini alikosa jibu kabisa maana yeye aliona kuwa ni
kawaida sasa swala la George kuchukia kiasi kile lilimshangaza sana, akatoka nje
ila hakumkuta George kwa maana kwamba alishaondoka muda tu, akachukua simu na
kumpigia ila George hakupokea simu ile. Akajiangalia mfukoni, hakubeba hela
yoyote maana George alimfanyia safari ya kumshtukiza, akawaza sana kuwa
atafanyaje. Akampigia simu rafiki yake Dora, “Best nimekwama huku, una
hela kidogo unitumie nirudi, nikifika nitakupa hela yako” “Umekwama wapi
na kipi kilichokukwamisha?” “Nitakwambia nikifika ila kwasasa nahitaji
msaada wa pesa kidogo niweze kufanya nauli” “Sina sh kumi shoga yangu,
pole weee. Mpigie George” “Hadi nimekupigia wewe jua nimekosa msaada
kote huko, naomba nisaidie rafiki yangu” “Sina hela” “Niazimie
hata kwa mtu nikirudi nitampa” Simu ikakatika maana salio liliisha na
kumfanya Erica achanganyikiwe zaidi ukizingatia kosa alilolifanya kwa George
mpaka muda huo hakulijua na pia hakujua kuwa anarudi vipi hosteli, yani hapo
kichwa kilikosa uelekeo kabisa. Alienda kukaa mahali akilia maana
hakujua hata aanzie wapi na aishie wapi, kuna mmama wa makamo alimuona na
kumsogelea karibu na kumuuliza, “Mwanangu vipi una tatizo gani? Mbona
umejiinamia hapo? Unajua ni usiku huu?” Erica aliinuka na kumuangalia
Yule mama kwa uchungu sana, kisha akamwambia, “Nimeibiwa mkoba wangu
ndio ulikuwa na nauli hata sijui narudi vipi nyumbani” “Pole sana, inuka
mwanangu twende nyumbani kwangu maana huku nilikuwa nafanya mazoezi tu. Twende
nyumbani nikakupe nauli naamini itakusaidia na utafika kwenu” Erica
aliinuka na Yule mama kisha kuanza kuondoka nae taratibu kuelekea anapoelekea
Yule mama, kumbe alikuwa haishi mbali na maeneo yale maana walifika kwenye
nyumba moja na kumkaribisha Erica, “Karibu, hapa ni nyumbani kwangu.
Karibu ndani nikutolee nauli binti yangu” “Usijali mama, nitasubiria
hapa hapa” Erica hakutaka kukaribia ndani maana mambo ya mjini
hayaelewekagi, unaweza kujikuta umekaribia kumbe unaenda kuchinjwa ila Yule mama
nae hakutaka kumlazimisha sana Erica, alienda ndani na kumtolea
nauli. Alirudi na noti ya elfu kumi na kumkabidhi, kisha
kujitambulisha “Naitwa Mrs.Peter unaweza tu kuniita mama. Sijui wewe
binti yangu unaitwa nani?” “naitwa Erica” “Karibu sana nyumbani
kwangu, hapa ni kwangu hata usiwe na mashaka yoyote yale yani wewe ujisikie upo
nyumbani. Sinaga mtoto wa kike, nina watoto wawili tu wa kiume na wote wapo
masomoni nje ya nchi, karibu sana mwanangu” “Asante
sana” “Unaweza ukawa unakuja kunitembeleaga, na vizuri ukinipa na namba
zako za simu” Basi Erica alimpa Yule mama namba zake za simu na
kumshukuru sana kwa ukarimu wake kisha akamuaga na kuondoka
zake. Erica alifika hosteli muda ukiwa umeenda sana, hakuamua
kufanya chochote zaidi ya kuoga na kwenda kulala ila alikuwa na mawazo mengi
sana kwani George hakumtafuta hewani kabisa na kumfanya akose
raha. Kulipokucha alioga na kuanza tena kumtafuta George hewani ila
hakupokea simu zake na kuamua kumtumia ujumbe, “George mpenzi wangu
nimekukosea nini kwani? Kwanini unanifanyia hivi jamani?” Ila ujumbe
wake haukujibiwa, alijaribu kutuma tena na tena ila hakujibiwa kabisa na
kumfanya akose raha zaidi, hata chai siku hiyo hakuweza kunywa kwani alikuwa na
mawazo mengi sana muda huo kiasi kwamba alitaka hata kwenda nyumbani kwao kwani
anamtindo wa kwenda kila mwisho wa wiki ila alishindwa sababu ya mawazo na
kutokuwa na raha. Wakati anawaza sana chini ya mti alikuja rafiki yake
Dora na kumsalimia, “Hapana Dora wewe sio rafiki kabisa, yani wewe wa
kushindwa kunisaidia mimi? Hata ulishindwa kuniombea hela kwa
mtu?” “Jamani rafiki yangu nisamehe bure, yani jana nilivurugwa usione
vile. Yani kuna mwanamke kanipigia simu kuwa ana mahusiano na mpenzi wangu yani
akili yangu yote ikaruka. Nisamehe rafiki yangu, na wewe yamekusibu
yepi?” Erica baada ya kuambiwa maneno hayo na rafiki yake na jinsi
alivyoweza kuona kweli mapenzi yanachanganya, akamuamini na kuamua kumuelezea
kilichotokea ila baada ya maelezo Dora alicheka sana na kumfanya Erica amuulize
kilichomchekesha, “Sasa unacheka nini?” “Samahani rafiki yangu,
usinifikirie vibaya kwa kucheka ila sijui kama nikifikiriacho ni cha
kweli” “Kipi hicho?” “Hivi Erica unafikiri George miaka yote
mitatu hii aliyokaa chuoni hakuona mwanamke kweli akaja kukuona
wewe” “Kwanini unasema hivyo Dora?” “Siamini kama kweli George
anakupenda maana kama angekuwa nakupenda hata kama umemfanyia kitu gani
asingethubutu kuondoka na kukuacha mwenyewe” “Ni kweli usemayo, sasa
ndio kimekuchekesha hicho?” “Hapana, ukiongea na George nitakwambia
kilichonichekesha” “Kivipi?” “Twende nikupeleke anapokaa George
uweze kuongea nae” “Kumbe unapajua?” “Sio kupajua anapokaa tu
ila George namjua vizuri yani in and out ndiomana sikushtuka sana
uliponitambulisha na ndiomana toka siku ya kwanza nilikwambia unanidanganya
kusema kuwa ni kaka yako” “Mbona unanitisha Dora, George unamjua vipi
wewe?” “Erica usijipe presha ya bure, twende anapokaa George uongee nae,
swala la mimi kumjua utamuuliza mwenyewe vizuri” Erica aliwaza sana ila
alikubali kwamba Dora ampeleke akaongee na George maana aliamini ana mengi ya
kuongea nae. Erica aliongozana na Dora hadi mahali
alipoonyeshwa kuwa George anakaa hapo, basi Dora alimwambia Erica aende nae
akafanya hivyo. Alivyofika akagonga mlango, na George ndiye
aliyemfungulia, Erica akashangaa nae George akashangaa, “Nani amekuleta
hapa?” “Kumbe kweli unaishi hapa?” “Sasa unashangaa nini? Ulijua
naishi kwenye kiota cha ndege?” “Hapana sio hivyo ila nimeshangaa sababu
hujawahi kunionyesha unapoishi kumbe sio mbali na chuo” “Sasa ulitaka
nikuonyeshe ili iweje?” “Khee yamekuwa hayo? George mbona umebadilika
gafla, tatizo ni nini?” George hakumjibu kitu na kuingia ndani, ilibidi
Erica nae amfate ambapo alimkuta amekaa tu kwenye kochi kwani chumba kile
kilikuwa na kochi moja na kitanda, kwahiyo Erica alisimama tu na kuendelea
kumuuliza George kuwa kwanini anamfanyia vile, “Hivi wewe si umeahidi
kuwa mume wangu jamani? Sasa mbona unanifanyia hivi?” “Usitake
kunichekesha Erica, hivi una sifa za kuwa mke wewe? Mke gani anaongea na mtu
huku amesimama?” Erica akajiangalia pale aliposimama, hata hivyo
hapakuwa na sehemu nyingine ya kukaa zaidi ya kitandani na chini kwahiyo ilibidi
akae chini na kumuuliza tena, “Kwahiyo hatma yangu ni
nini?” “Unadhani ukikaa chini ndio utaonekana mke mwema? Kwani kitanda
hukukiona kuwa unaweza kukaa pale?” “George jamani, si uniambie tu kuwa
nimekufanyia nini kuliko kunifanyia hivi?” “Sikia nikwambie Erica, wewe
hufai kuwa mke wangu yani hufai kabisa. Nilipenda mke wangu, mimi ndiye niwe
mwanaume wake wa kwanza, ila sio mwanamke ambaye ameshapitiwa na wanaume
wengine. Erica nilikuuliza kuhusu mahusiano yako ya nyuma ili uniambie ukweli
lakini ulisema kuwa mimi ni mwanaume wako wa kwanza, kumbe ushapitiwa. Kweli mtu
ni mpaka umuone ndani ila nje haitoshi kuonyesha mtu anayefaa. Yani kwa nje
unaonekana ni binti mpole, mlokole kumbe ni mchafu tu” Erica alikaa
kimya kwa muda na kumfanya George aendelee kuongea, “Umeona unashindwa
kujieleza? Ningekukuta ni msichana bikira basi hata leo ningeenda kwenu
kujitambulisha ila ilimradi ushapitiwa siwezi hata kuendelea na mahusiano na
wewe” Erica aliumia sana, alijikuta akiinuka na kuondoka bila ya
kuaga. Muda huu alienda kupanda gari kwani hata hakutaka tena kuonana na
mtu yeyote maeneo yale, moja kwa moja alienda ufukweni. Alifika
ufukweni na kukaa mahali peke yake, kisha alilia sana yani alilia kama mtu
aliyefiwa vile hadi macho yalimvimba, hakuwa na raha kabisa hapo ndio alipoona
kuwa mapenzi yanaumiza kiasi kile maana hakufikiria kuwa mapenzi yangemuumiza
kile kiasi. Alilia sana, yani hata Dora alipompigia simu hakupokea,
akakumbuka siku ya kwanza kukutana kimwili na Babuu ilionyesha Babuu kafurahi
sana tofauti na alivyokutana na George, “Ndiomana dada aliniambia
nijitunze mimi, ni mjinga sana mimi sijui nilikubali vipi kutembea na Babuu na
sijui nimekubali vipi kutembea na George kumbe ni mwanaume mpumbavu
kabisa” Alilia sana, kuna mtu alisogea na kumshika bega, Erica
akanyanyua kichwa kumtazama alikuwa ni mkaka aliyemuuliza kwa
upole, “Vipi dada una matatizo gani?” Erica alikaa kimya tu huku
akiendelea kulia, “Pole dada ila una tatizo gani?” Alikuwa
akilia sana na kadri huyu kaka alivyomuuliza maswali ndivyo alivyozidi kulia
kwani alihisi kama yale maswali yakimuumiza kichwa zaidi. Yule kijana
hakukata tamaa kwani alikaa pale pale akisubiria Erica anyamaze kulia huku
akijitahidi kumbembeleza. Erica alisikiliza wosia wa Yule kaka na kuamua
kunyamaza kwani muda nao ulikuwa umeenda sana, “Naitwa Bahati, sijui
wewe mwenzangu unaitwa nani?” “Naitwa Erica” “Jina zuri, je nini
kimekupata Erica hadi unalia?” “Ni historia ndefu sana” “Huwezi
kuniambia hata kwa kifupi?” Machozi mengine yalimtoka Erica na kumfanya
Bahati kumbembeleza tena huku akijaribu kumpa maneno ya
kumshauri, “Matatizo tumeumbiwa, sio siku zote mtu utaishi kwa raha tu.
Kuna kipindi utajikuta ukipatwa na matatizo ila si vizuri kuyaacha matatizo
yachukue nafasi katika maisha yetu. Erica pole sana ila muda umeenda na si
vizuri kuendelea kukaa mahali hapa, nakuomba tuondoke” Erica aliamua
kukubali na kumwambia kuwa anahitaji kwenda nyumbani kwao, kwavile Bahati
alijitolea kumsaidia alimuomba ampeleke nyumbani kwao. “Usijali nitafika
tu” “Hapana ni usiku sana kwasasa, naomba nikupeleke. Mimi ni mtoto wa
kiume tofauti na wewe mtoto wa kike” Basi Erica akakubali kisha
akaongozana na Bahati hadi nyumbani kwao kwani Erica aliamua kurudi kwao tu na
sio kwenda tena hosteli. Alivyofika tu kwao, Bahati aliamua kuaga na
kumuomba namba ya simu ambapo Erica alifanya hivyo kisha akagonga mlango wao na
mama yake kumfungulia. Alipoingia ndani, mama yake
alifoka, “Erica mwanangu mbona usiku huu? Unajua ni saa tano sasa
hivi!” “Nisamehe mama ila nilipakumbuka nyumbani halafu leo kipindi
kilichelewa kuisha, na muda narudi kulikuwa na foleni sana
njiani” “Kipindi kimechelewa kuisha Jumamosi? Si unakujaga asubuhi
wewe?” “Mama leo tulikuwa na kipindi cha dharula na tulitangaziwa jana
jioni halafu kikawekwa leo jioni ndiomana imekuwa hivi” “Na hayo macho
vipi mbona yamevimba?” “Nadhani ni sababu ya kusoma sana” “Kheee
pole mwanangu, nenda kaoge ule halafu ukapumzike” Erica alienda kuoga
ila alikula kidogo sana kwani kiukweli hakuwa na raha kabisa, kisha akaenda
chumbani kwake kwa lengo la kulala. Siku hiyo hakutaka kurudi hosteli
kwani hakupenda wajue kuwa alikuwa na mawazo kiasi kile, kwahiyo alipoingia
chumbani kwake alikaa kitandani huku bado akiendelea na mawazo yake. Akakumbuka
siku ya kwanza kuwasiliana na Babuu, akakumbuka jinsi alivyokutana na George
alijikuta akijisemea, “Hakuna mwanaume mwenye upendo duniani, Erick
nilijua ananipenda ila alitaka wasichana wote shuleni. John nae alinitaka
kimapenzi tu, hivi alishindwa hata kuja kunitafita kwenye shule yangu? Babuu nae
niliamini ananipenda kumbe alikuja kuniharibia maisha yangu, nimeharibu usichana
wangu mimi nani atanioa ikiwa hata George amenikataa?” Machozi mfululizo
yalimtoka, kidogo akapokea ujumbe kwenye simu yake, “Mambo Erica, mimi
nimefika nyumbani salama kabisa. Je unaendeleaje?” Erica alisoma ule
ujumbe na kutamani hata ungekuwa umetoka kwa George ila sio kwa mtu ambaye
amekutana nae ufukweni tu, ila ujumbe mwingine ukaingia. “Naweza
kukupigia simu Erica japo tuongee kidogo tu?” Huu ndio
akaujibu, “Hapana tutaongea kesho” “Basi hakuna tatizo, usiku
mwema Erica. Kumbuka kuwa Mungu anakupenda sana ndiomana upo hadi
leo” Kidogo hili neno la kusema Mungu anampenda sana lilimuingia kwenye
moyo wake na akajihisi fiuraha kidogo kwani aliona japo kuna vitendo vingi
alivyoviona kwake vya ajabu ila Mungu anampenda sana. Akaamua kulala sasa na
kupumzisha mawazo yake. Kesho yake baada ya kutoka kanisani
alifika dada yake Bite na kumkuta pale nyumbani, na baada ya kusalimiana nae tu
dada yake alimuuliza, “Hivi kwanini ulibadilisha namba
Erica?” “Nilipoteza laini dada” “Ulipoteza laini?
Ulipotezaje?” “Kuna mtu aliomba kuweka laini yake kwenye simu yangu,
basi yangu tuliitoa na kuja kuitafuta tena sikuiona” “Sawa kwanini
usiende kurenew laini ile upate mpya kama ile” “Mmmh wazo hilo hata
sikuwa nalo halafu niliona ni mbali sana ndiomana nikanunua laini mpya
tu” “Erica mdogo wangu laini niliyokupa ilikuwa na maana sana, siku zote
sikupati hewani hadi leo nimeamua kuja nyumbani na nimebahatika kukukuta. Laini
hiyo mpya kila nikikupigia inatumika, yani mdogo wangu umekuwa kama kibanda cha
simu?” “Nisamehe dada” “Nataka uirudishe ile laini ya
awali” “Sawa dada nitairudisha” Ila Bite alimuona mdogo wake
kama hana furaha ila kila alipojaribu kumuuliza, Erica alikuwa anabadilisha mada
ili asiendelee kuulizwa kuwa kwanini anaonekana ana mawazo sana. “Mdogo
wangu unanificha hadi mimi dada yako? Unajua mimi ndio msiri wako, unatakiwa
kuniambia mimi vitu vinavyokutatiza, nakuona kabisa huna furaha lakini
unanificha” “Hapana dada sikufichi chochote” “Nyumbani kwangu
unapafahamu, ukiona mambo yanakutatiza uje nyumbani nikushauri” “Sawa
dada” Basi dada yake akaongea ongea nae kisha akajiandaa kwaajili ya
kuondoka kwahiyo ikabidi aondoke nae maana nay eye alitaka kuelekea
hosteli. Alifika hosteli na baada ya muda kidogo tu Dora nae
alifika, ikabidi atoke nae nje kuzungumza nae, “Jamani Erica una tabia
mbaya, yani jana umeondoka bila hata ya kuniaga?” “Nilichanganyikiwa
rafiki yangu” “Ulichanganyikiwa na nini?” “Acha tu rafiki
yangu” “Mmmh niache nini si uniambie tu ukweli kuwa George hakukukuta na
bikra” “Umejuaje?” “Najua vizuri, George huwa anapenda mabinti
bikra na ndiomana alikupenda wewe ila hivyo kakuta huna bikra hawezi kukutaka
tena” “Kumbe unajua, mbona hukuniambi?” “Na mimi mwenyewe
sikujua kama wewe ushatumika” Kisha akaanza kucheka, “Sasa
unacheka nini?” “Usichukie rafiki yangu, kwa muonekano wako unaonekana
ni msichana aliyetulia sana. Hata mimi sikujua kama umetumika tayari, George
huwa anapenda mabinti bikra ndiomana akakupenda wewe” “Ila wewe sio
rafiki mwema, hata kama hukujua chochote kuhusu mimi ulitakiwa kunitahadhalisha
na sio kunishawishi ili mwenzio niumbuke ufurahi” “Hapana sijafurahi
Erica” “Nimegundua, wewe si rafiki mwema. Kwaheri” Erica
aliinuka na kurudi ndani kwani maneno ya rafiki yake hayakumfurahisha hata
kidogo imekuwa kama alimpangia mpango ili aumbuke. Akakumbuka jinsi
alivyokuwa akimshawishi kuwa alale na George na kumfanya azidi kumchukia maana
alimfanyia kitu kibaya. Erica alitulia ila ujumbe pekee
alioupata kwenye simu yake kwa siku hizo ulikuwa unatoka kwa Bahati na
ilionyesha huyu mkaka amempenda pia Erica, “Anitolee balaa na yeye hata
sitaki tena mapenzi, wanaume ni waongo sana” Ila Bahati alizidi kumtumia
ujumbe mbalimbali na jumbe zingine zilikuwa za kumpa moyo na kumfanya asikate
tamaa, kwa sehemu nyingine alimuona Bahati kama rafiki mwema kwani muda wote
alikuwa akimtumia ujumbe wa maana tu na sio wa kumtongoza. Erica
alijikuta akimaliza mawazo yake kwa kusoma ujumbe ambao anatumiwa na Bahati,
kwahiyo siku zote alijiliwaza kwa ujumbe tu aliotumiwa na Bahati na katika siku
zote hizo hakuna siku ambayo alitumiwa ujumbe na George. Ilitokea siku
moja alitumiwa ujumbe na dadake Bite, “Umefikiria nini kuhusu swala la
kurudisha laini yako ya mwanzo?” Ila kabla hajajibu ujumbe huo
alishangaa kupokea ujumbe kutoka kwa George, “Erica, njoo uchukue picha
zako” Kwahiyo alijikuta akipaniki na kujibu kwanza ujumbe
huo, “Hizo picha kaa nazo, mwanaume wa ajabu sana wewe. Ulikuwa na lengo
la kutembea na mimi tu eti hunitaki tena sababu mimi sio bikra. Kama ungetaka
mabikra si ungeenda kuoa kijijini kwenu. Baki nazo hizo picha
sizitaki” Akatuma, baada ya hapo akaona ujumbe umefika, alipoangalia
vizuri alikuta ujumbe ule umefika kwa dada yake Bite na si kwa George kama
alivyodhamilia. Ilitokea siku moja alitumiwa ujumbe na
dadake Bite, “Umefikiria nini kuhusu swala la kurudisha laini yako ya
mwanzo?” Ila kabla hajajibu ujumbe huo alishangaa kupokea ujumbe kutoka
kwa George, “Erica, njoo uchukue picha zako” Kwahiyo alijikuta
akipaniki na kujibu kwanza ujumbe huo, “Hizo picha kaa nazo, mwanaume wa
ajabu sana wewe. Ulikuwa na lengo la kutembea na mimi tu eti hunitaki tena
sababu mimi sio bikra. Kama ungetaka mabikra si ungeenda kuoa kijijini kwenu.
Baki nazo hizo picha sizitaki” Akatuma, baada ya hapo akaona ujumbe
umefika, alipoangalia vizuri alikuta ujumbe ule umefika kwa dada yake Bite na si
kwa George kama alivyodhamilia. Akatetemeka sana na kuogopa hadi akaamua
kuzima simu, na kujilaza kwa uoga huku akiwaza sana kuwa dada yake
atamfikiriaje. Badae akawasha simu yake kwa uoga sana kwani
alikuwa anawaza kuwa atamweleza nini dada yake, alipowasha tu alipigiwa simu na
dada yake, akaipokea kwa uoga, “Nipo hapa kwenye baa ya karibu na
hosteli kwenu njoo” Erica akainuka pale kitandani kwa uoga uoga kwani
ingawa ni mchana ila alilala sababu hakudhamiria kumtumia ujumbe kama huo dada
yake. Alienda alipo dada yake na kumuangalia kwa aibu sana, kisha dada
yake akamwambia twende, akainuka nae na kwenda kupanda gari la dada yake kisha
safari ya kwenda kwa dada yake ikaanza. Walifika nyumbani kwa
dada yake na kuingia ndani, Erica alikuwa amesimama kama mlingoti, dada yake
akamuamuru akae, “Hivi Erica wewe ni wa kunificha mimi? Umeanza lini
mambo ya ajabu haya? Kuwa muwazi mimi ni dada yako na najua jinsi ya
kukusaidia” “Nisamehe dada” “Kukusamehe ndio nini? Kumbuka
umetoa mwili wako, nini maana ya msamaha kwenye mwili
wako?” “Sikudhamilia dada” “Hukudhamilia? Au nikosomee tena
ujumbe wako? Yani unamwambia mwanaume kama angekuwa anataka bikra angeenda kuuoa
kwao, wewe ushatembea na wangapi hadi huyo kakukuta umetumika?” “Dada
itakuwa hukuielewa tu meseji yangu” “Sikuielewa? Kwahiyo mimi nimepaniki
bila kuelewa? Unajua mimi ni mtu mzima Erica, kumbuka dada zako wote tumeolewa
tena kwa ndoa za heshima sasa wewe kwanini unataka kutuaibisha kiasi hiki
jamani!” “Dada umenifikiria vibaya” “Kama nimekufikiria vibaya,
niambie ni kweli wewe sio bikra?” “Mimi bado ni bikra
dada” “Kuwa mkweli Erica” “Ni kweli dada, mimi ni
bikra.” “Sasa ule ujumbe ulikuwa unamaanisha nini? Ngoja nikusomee tena
labda huelewi ulichotuma “Hizo picha kaa nazo, mwanaume wa ajabu sana wewe.
Ulikuwa na lengo la kutembea na mimi tu eti hunitaki tena sababu mimi sio bikra.
Kama ungetaka mabikra si ungeenda kuoa kijijini kwenu. Baki nazo hizo picha
sizitaki” Ujumbe wako huo ulikuwa unamaanisha nini?” “Dada, huyo mkaka
alikuwa ananitongoza na aliniuliza kama mimi ni bikra nikamjibu kuwa mimi si
bikra ili nipime imani yake, sasa kugundua hivyo akadai hanitaki tena ndio
akasema nikachukue picha zangu. Kuna picha zangu alijipendekeza kuzichukua kwa
mpiga picha, ndio nikamjibu vile dada ila sina mahusiano na huyo kijana wala
sijawahi kutembea na kijana yeyote” “Erica, Erica mdogo wangu, hivi
unajua kuwa uzinzi ni dhambi? Unakumbuka ulivyocheza na kufurahi kwenye harusi
yangu? Je wewe hutaki tucheze na kufurahi kwenye harusi yako? Erica mdogo wangu
nilikwambia jitunze, ukijitunza ndio utapata mwanaume wa maana wa kukuoa ila
ukiwa unaruka ruka ni ngumu kuolewa. Hakuna mwanaume anayependa msichana
aliyetumika” “Sijatumika dada” “Sitaki kutafuta ushahidi ila
sitaki aibu kwenye ukoo wetu, kuanzia sasa utaishi hapa kwangu na chuo nitakuwa
nakupeleka nikiwa naenda kazini, ila kurudi utarudi mwenyewe na ufikie hapa.
Hatutaki aibu Erica” “Kwahiyo leo sirudi hosteli?” “Leo utalala
hapa, kesho utaenda chuo” “Jamani dada, vitabu vyangu vyote vipo kule.
Nitajisomea nini sasa?” “Ulikuwa unajisomea wewe au unawasiliana na
wanaume kwenye simu? Utakaa hapa kwa mwezi mmoja nichunguze tabia yako halafu
ndio utarudi tena kukaa hosteli, hivyo vitabu vyako utaenda kuvichukua
kesho” Erica hakutaka kubisha sana kwani kwa upande mwingine alimuogopa
sana dada yake huyu ingawa ni dada waliyefatana ila alimzidi mbali sana kimiaka
na kimaisha, kwahiyo ilibidi awe mpole tu. Kesho yake alienda
chuo kama kawaida ila kwa kipindi hiko hakutaka kuwa karibu na rafiki yeyote
maana aliona wanazidi kumpoteza kimalengo, akiwaza jinsi Dora alivyomdumbukiza
kwa kijana George ndio anakosa hamu ya marafiki kabisa. Siku hii
alikutana na George njiani, kwakweli hakusalimiana nae kabisa kwani alimuona
kama ni mwanaume asiyefaa, aliposogea mbele kidogo akageuka nyuma kumuangalia
George alikuwa akielekea wapi, akashangaa kumuona George amesimama na Dora huku
wakiongea na kucheka, ilimuuma sana na kuzidi kumlaumu Dora katika maisha yake,
wakati anawashangaa alitokea kijana mmoja nyuma yake na
kumuuliza, “Mbona unawashangaa hivyo wale?’ “Aaah nawashangaa
tu” “Wazoee, yani wale wana mipango ya ajabu ajabu hapa
chuoni” “Kivipi?” “Nitafute kwa muda wako
nikueleze” Yule kijana akaondoka, Erica akaanza kumfata nyuma kwani kwa
hakika alitamani kujua kuwa wana mipango ya ajabu ajabu ipi, alipomfikia
alimuomba tena amueleze, “Saivi nipo busy, kama vipi niachie namba yako
nitakucheki” Erica akampa namba na kumwambia, “Naitwa Erica,
sijui wewe unaitwa nani?” “Naitwa Adam” Basi Yule Adam akaondoka
na kumuacha Erica akiwa na hamu ya kujua kuwa ni kitu gani kinaendelea kati ya
George na Dora. Akamaliza mambo yake yote chuoni akisubiri dadake aende
kumchukua ila dada yake hakufanya hivyo, ikabidi ampigie simu kumuuliza kuwa
imekuwaje, “Wewe njoo tu mwenyewe, shemeji yako anarudi leo naenda
kumpokea” Ni muda mrefu tangu shemeji yake huyo asafiri, kwahiyo ile
kama siku ya kurudi huyo shemeji yake lazima dadake aandae mazingira ya
kumpokea. Bahati alimtumia ujumbe Erica mara baada tu ya kukata simu ya
dada yake akimuomba waonane, Erica akaona vyema amtajie mitaa ya kuonana karibu
na kwa dadake ili iwe rahisi kwa yeye kurudi nyumbani. Alimtajia mitaa hiyo nae
Bahti aliafiki. Erica alifika mahali alikopanga kuonana na
Bahati, na kweli Bahati nae alifika mitaa ile na kukaa chini kuanza kuzungumza
nae. “Sijui Erica nimekukosea kitu gani, hujibu meseji zangu. Kiukweli
unaniumiza sana” “Pole” “Mmmh haya asante, ila Erica mie mwenzio
kama jina langu lilivyo yani najiona ni mwenye bahati sana kukutana na
wewe” “Kheee na wewe unataka kunianzia hoja za kunitongoza eeh! Mwenzio
nina maumivu moyoni hata sitaki wanaume” “Kuwa na maumivu moyoni
suluhisho lake sio kutokutaka wanaume, ukumbuke kila binadamu kaumbwa na vitu
vyake na tabia yake. Tunaweza kufanana sura ila tusifanane tabia, si kila
mwanaume ni muongo. Tupo wengine wa kweli” “Yani ndio ulichotaka
kukutana na mimi hiko Bahati? Nilijua huwezi kuniambia ujinga maana siku zote
hunitumiagi meseji za ujinga, imekuwaje leo?” “Erica, toka ile siku ya
kwanza nakuona hubanduki kwenye akili yangu, kiukweli nakupenda Erica. Unaweza
kuona mimi ni mjinga ila mimi si mjinga nakupenda kweli, na leo sikuwa na lengo
la kukwambia haya ila nimeshindwa kujizuia, ni kwelki nakupenda” “Haya,
ngoja nikuulize maswali nione kama una vigezo vyangu” “Niulize
tu” “Umesoma hadi wapi?” “Nimeishia la saba” Erica
alicheka sana yani sana na kumuuliza kwa mshangao, “La
saba!!!” “Ndio la saba” “Halafu bila hata aibu unakuja
kunitongoza mimi mdada wa chuo?” “Mapenzi Erica hayaangalii elimu,
kabila, dini wala umri” “Usinichekeshe mie, sina ndoto ya kuolewa na
mwanaume wa la saba. Samahani Bahati, huna bahati kwangu, siwezi
kukukubali” “Jamani Erica?” “Ndio hivyo sikutaki, kwanza dini
gani wewe?” “Mimi ni Mwislamu” “Kheee Mwislamu kumbe!! Mimi ni
Mkristo, uliona wapi Mwislamu na Mkristo wakaendana?” “Mapenzi Erica,
hayaangalii dini” “Kwanza unafanya kazi gani?” “Mimi ni
mvuvi” “Usinichefue, kwaheri yani bora hata ungekuwa na kazi ya maana
labda ningekufikiria kidogo, yani mvuvi ndio uwe na mimi loh!” Erica
akaondoka zake na kumuacha Bahati akiwa peke yake, ila Bahati alimfatilia Erica
bila ya Erica kujua, ila alimfatilia hadi kwa dada yake, alipohakikisha anaingia
ndani ndipo akaondoka. Bite alimkaribisha mdogo wake na
kumuonyesha shemeji yake tena, “Umemuona shemeji yako, baada ya miaka
mingi” “Kheee huyu ndio Erica, amekuwa mdada siku hizi” “Ndio
yupo chuo” “Hongera sana Erica” Alitabasamu pale na kuongea
ongea kidogo na shemeji yake. Kisha akaenda kwenye chumba chake ambacho huwa analala. Siku hiyo alitumiwa ujumbe
mwingi mwingi na Bahati ila hakujibu hata ujumbe mmoja kwani alimuona Bahati sio
hadhi yake, “Natakiwa nipate mume kama wa dada, msomi na ana hela. Sio
wakina Bahati, kuniekea gundu tu. Mwanaume kaishia la saba, halafu mvuvi loh
nitamtambulishaje kwa rafiki zangu? Anitolee balaa mie” Siku iliyofuata
ilikuwa ni mwisho wa wiki kwahiyo Erica hakwenda chuoni na alibaki nyumbani,
muda huo shemeji yake alikuwa ametoka kwenda kutembelea ndugu, jamaa na
marafiki. Erica alimuuliza dada yake, “Dada ulimpataje
shemeji?” “Ni mwanaume niliyempata kwa bahati sana halafu ananipenda
balaa maana alinikuta bikra. Unajua mwanaume akikukuta bikra anakupenda sana,
yani James ananipenda mdogo wangu jamani ananipenda balaa” “Kwahiyo
hawezi kukusaliti?” “Umefikiria nini kuuliza hivyo?” “Nasikia
asilimia kubwa ya wanaume ni wasaliti, yani wanakuwa na nyumba
ndogo” “Mambo hayo si kwa James wangu, kumbuka kuwa kanikuta bikra na
nimekamilika kila idara, ataanzaje kunisaliti yani kwa mwingine anafata nini
labda” “Hongera dada” “Sio hongera tu, na wewe ujitunze. Hakuna
kitu wanaume wanapenda kama kuoa mwanamke bikra” “Sawa dada
nitajitunza” Aliinuka Erica na kwenda chumbani, kiukweli alikuwa akiumia
sana moyoni na kujiona kuwa atakosa bahati kabisa, “Hivi kwanini kwangu
imetokea hivi? Kuna atakayenioa wakati mimi sio bikra kweli? Hivi wadada wote
walioolewa wameolewa wakiwa bikra mmh jamani! Sijui nifanyeje?” Aliumia
sana kwenye moyo wake, mara ukaingia ujumbe kutoka kwa Bahati, “Erica
nakupenda sana, usijali kuhusu elimu yangu, kuhusu dini yangu, kuhusu kazi yangu
au kabila langu angalia upendo wa kweli. Nakupenda sana Erica, haijalishi
umepita na wanaume wangapi wakakuumiza moyo ila mimi nakuahidi nitakusahaulisha
yote” Erica akamuuliza kwa ujumbe, “Je upo tayari kuoa mwanamke
asiye bikra?” “Kwani bikra ni kitu gani katika mapenzi? Watu wanaoa
wanawake walioathirika sembuse kuoa mwanamke asiye na bikra! Erica haijalishi ni
wanaume wangapi wamepita kwako ila mimi najiona kama ni mwanaume wa kwanza
kwako, hao makapi wote siwapi nafasi uwakumbuke” Kidogo haya maneno
yakaanza kumuingia akilini, na kutaka kumkaribisha Bahati katika moyo wake, ila
akawaza hoja ya elimu na kuona kuwa atachekwa na watu, ikabidi asijibu chochote
hadi atakapojihoji kwenye akili yake. Ilikuwa ni siku ya
Jumapili, Bite alienda kanisani ila Erica hakwenda na mume wa Bite nae alidai
kuwa bado anauchovu na safari kwahiyo hawezi kwenda kanisani, kwahiyo nyumbani
walibaki wawili. Erica hakwenda sababu alikuwa yupo na simu tu akipeana
ujumbe na Bahati kwani kwa kiasi Fulani ulikuwa unamfariji, akiwa chumbani
shemeji yake akamuita. “Erica, toka nimerudi hatujapata muda wa
kuzungumza” Erica alitabasamu tu, na James aliendelea
kuongea, “Unatumiaga kilevi?” “Hapana situmii
kilevi” “Aaah upo kama dada yako?” “Siye kwetu wote hatutumii
kilevi” “Hahaha walokole eeeh! Sawa, ila siku hizi umekuwa
mtamu” “Kivipi?” “Umekuwa umependeza yani ulikuwa mzuri wakati
upo mdogo ila saivi umezidi kuwa mzuri” “Asante shemeji” “Mume
mwenzangu ni nani?” “Kivipi?” “Namaanisha mpenzi
wako” “Hapana sina mpenzi” James akainuka na kwenda chumbani,
baada ya muda kidogo alimuita Erica chumbani kwao, “Mmmh nije kufanya
nini huko shemeji?” “Kuna kitu naomba uje kunisaidia” Erica
hakuwa na wazo baya juu ya shemeji yake, akaenda na kumkuta James akiwa
amejifunga taulo tu, kabla Erica hajashangaa vizuri James alikuwa tayari
ameshamvuta karibu yake. Itaendelea kesho
usiku……!!!! Jamani nyie mnaochukua story zangu na kuziweka huko kwenye
page zenu au magroup yenu bila kunishirikisha na chochote, sipendi hiyo tabia.
Mananivunja moyo kwakweli. Kwa wale wanaohitaji story ya maisha yangu
wanifate inbox sababu ile ni ya private kwa
walioguswa. Erica hakuwa na wazo baya juu ya shemeji
yake, akaenda na kumkuta James akiwa amejifunga taulo tu, kabla Erica
hajashangaa vizuri James alikuwa tayari ameshamvuta karibu yake. James
alikuwa na lengo moja tu muda huo ni kumbaka Erica maana alijua hatotoa
ushirikiano kwake, na katika purukushani hadi alichana blauzi ya
Erica. Hapo Erica akajiongeza kuwa hata akifanya fujo haitamsaidia kitu
sababu mtu ameshadhamilia kumbaka, kwahiyo ilibidi awe mpole na kuongea nae
taratibu. “Shemeji unajua hiki kitendo hakinogi kama ukitaka kunifanya
kwa nguvu?” “Mimi sitafanya kwa nguvu, taratibu tu” “Sina tatizo
juu ya hilo shemeji hata nashangaa umejukua jukumu la haraka sana kutaka
kunibaka wakati ingewezekana ungeongea kawaida tu na mimi. Tunatakiwa wote
tufurahie na kama tunataka kufurahi basi tusifanye hapa nyumbani maana
hatutakuwa huru, dada atarudi muda wowote” “Kwahiyo unataka tukafanye
wapi?” “Twende mahali shemeji hata guest, huko tutafurahi
pamoja” James akatabasamu kwani maneno ya Erica yalikuwa matamu sana kwa
upande wake ukizingatia alikuwa akiongea kwa sauti ya kuvutia
sana, “Tunaweza kwenda saizi?” “Ndio, kwanini
nikatae?” “Na dadako akirudi bila kutukuta utamwambiaje?” “Swala
la dada ni dogo sana, wewe utasema ulienda safari zako, na mimi nitasema
nilienda chuo wenzangu waliniita. Mbona sio shida hiyo” Shemeji yake
alifurahi sana na kumsogelea Erica halafu akambusu, Erica
akamwambia, “Basi jiandae na mimi nikajiandae tuondoke” “Mtoto
mtamu wewe dah! Yani nitamuacha hata dada yako kwaajili yako, unaonekana
unavutia sana halafu mambo unayaweza. Nakupenda Erica” “Nakupenda
pia” Basi Erica akatoka chumbani kwa shemeji yake, alienda chumbani
kwake na kuchukua blauzi, akavaa haraka haraka na kutoka kimya
kimya. Alivyofika nje alishangaa kumuona Bahati, “Khee
wewe umefata nini hapa?” “Nimekufata wewe Erica” “Basi, naomba
tuondoke” Akamvuta mkono na kuondoka nae, mbele kidogo walisimamisha
bodaboda na kwenda nayo stendi. Kufika stendi Erica aligundua kuwa hakutoka na
pochi yake yenye hela ila aliogopa kwenda kuifata tena nyumbani, “Bahati
unajua sijatembea na pochi yenye hela!” “Hela ya nini Erica, huyo
bodaboda nitamlipa mimi” Kisha Bahati akamlipa Yule wa bodaboda na
kupanda daladala kisha kuondoka pale, ila hakujua Erica anataka kwenda wapi kwa
muda huo ilibidi amuulize na Erica akamjibu kuwa anataka kwenda ufukweni, kisha
wakaelekea huko. Walifika ufukweni ila Erica alionekana kuwa na mawazo
sana, ikabidi Bahati amuulize, “Mbona una mawazo sana
Erica?” “Wewe acha tu, ngoja nikuulize. Pale nje kwetu ulikuwa unafanya
nini? Na kama ulinifata mimi, ulijuaje kama naishi pale?” “Siku ile
nilikufatilia hadi unapokaa, na leo nilikuja kwa lengo moja nilihitaji kukuona.
Nilijua umeenda kanisani, kwahiyo nilikuja na kukaa pale nje kwenu ili ukirudi
kanisani nikuone” “Kheee huoni kama ni tatizo, mfano dada yangu
angekukuta je?” “Ningemwambia ukweli kuwa nahitaji kukuona wewe sababu
ni kweli nakupenda” “Mmmh ila nyie wanaume ni waongo sana” “Sio
wanaume wote ni waongo, uongo ni hulka ya mtu Erica” “Unaweza ukaoa, na
mkeo akakupa kila kitu unachohitaji ila bado unatamani wanawake wa
nje” “Hiyo ni tabia ya mtu Erica” “Mmmh na nyie waislamu kuoa
wake wengi siwawezi” “Sikia nikwambie Erica, kuna mwanaume anaweza kuoa
mke mmoja, wake wawili, watatu au wanne ila akawaheshimu wote na kuwatimizia
mahitaji yao yote sawa kwa sawa halafu wanajuana wote. Na kuna mwingine anakuwa
na mke mmoja ila nyumba ndogo kila mahali, Kwa hapo inakuwa bora hata aliyewaoa
kuliko huyu anaoewachezea wanawake wengi halafu anajifanya kaoa mmoja. Na si
kila mwanaume wa Kiislamu ni lazima aoe wake wengi” “Kwahiyo wewe utaoa
wangapi?” “Mimi nataka kuoa mke mmoja tu, ninayempenda, nitamtunza na
kumuheshimu siku zote. Na si mwingine zaidi yako Erica, na sitakuwa na nyumba
ndogo yoyote ile” “Mmmh kama kweli vile” “Ni kweli Erica,
sikudanganyi wala sitanii” Erica alimuangalia Bahati na kutabasamu tu
kwani kiukweli alikuwa anaongea nae tu ila mawazo yake yalikuwa mbali
sana. James alivyotoka chumbani alikuwa ameshavaa na kukaa
sebleni akimsubiria Erica ila alishangaa kuona Erica hatoki chumbani kwake,
ikabidi aende akamuangalie Erica. Alishangaa sana kutokumkuta, akajaribu kumuita
ila hakumuitikia, wakati akimuita ita Erica mule chumbani kwake, mkewe nae akawa
amerudi na kumshangaa James akiwa ametoka chumbani kwa Erica, “Kheee
vipi tena, ulifata nini kwa dogo huyo?” “Nimemuita nikaona kimya, ndio
nikaenda kumuangalia maana siku hizi ya dunia mengi” “Sasa yuko
wapi?” “Sijui, hata mimi mwenyewe sielewi maana hajaniaga. Sasa nilikuwa
namuita ili nimuage ndio sijamkuta” “Na wewe ulitaka kwenda
wapi” “Si kutembea tembea jamani mke wangu” “Ndio ulishindwa
kunisubiria nikitoka kanisani twende wote, jamani James!!” “Basi yaishe
mke wangu” Kisha Bite akaanza kuulizia vizuri kuhusu mdogo wake kaenda
wapi na kwanini kaondoka bila kuaga, alipokosa jibu la maana aliamua kumpigia
simu mdogo wake, “Wewe Erica uko wapi? Na kwanini umeondoka bila ya
kuniaga?” “Nisamehe dada, ila kuna kazi ya muhimu sana niliitiwa
chuo” “Kwahiyo upo chuo kwasasa?” “Ndio dada” “Ukitoka
urudi huku nyumbani” Kisha Bite akakata ile simu ila Erica alikuwa
anawaza sana kurudi kwa dada yake na kuwaza endapo dada yake akaondoka tena kwa
bahati mbaya si shemeji yake atambaka na hawezi kumdanganya tena maana
atajulikana ni muongo ukizingatia alishamdanganya, ila tatizo hakuchukua vitabu
vyake kwahiyo ilibidi akubaliane na swala kwamba anatakiwa arudi kwa dada yake
ila alipanga kesho yake abebe vitabu vyake na kurudi hosteli tu kwani aliona
pale kwa dada yake si salama tena kwake. Muda ulifika
alimwambia bahati kuwa anataka kurudi nyumbani, ila kwakweli Bahati hakumuelewa
Erica kuwa ana tatizo gani sema sababu alitokea kumpenda hakutaka kumuuliza
uliza sana kwa kuhofia kuwa atamkera, kwahiyo alivyosema anataka kurudi nyumbani
aliongozana nae hadi nyumbani kwa dadake. “Mmmh si ushanifikisha ondoka
basi” “Naondoka ila nasubiri uingie ndani” Mara shemeji yake
akatokea, kumbe alikuwa mitaa ya nje ya nyumba kwahiyo akamkuta Erica amesimama
na huyo Bahati, aliwaangalia kwa ukali kama mkaka anayemlinda mdogo
wake, “Vipi wewe kijana una shida gani?” Aliuliza kwa ukali mno,
ikabidi Erica ajibu kwa niaba ya Bahati, “Ni rafiki yangu,
alinisindikiza tu” Mara dada yake nae akatoka ndani na kuwakuta pale
nje, ilibidi aulize kuwa kuna nini, James alijibu, “Hata mimi nashangaa
maana nimekuta wamesimama tu hapa nje” “Erica mdogo wangu jamani,
umeanza kuongozana na wanaume?” Bahati akaanza
kujitetea, “Msilaumu tu mimi nilimsindikiza” James akamuangalia
kwa ukali na kumwambia, “Kelele wewe, utamsindikiza kama nani? Ndio nyie
mnaoharibu watoto wa watu, ondoka hapa upesi” Bahati alisimama tu
ikabidi Erica ampe ishara kuwa aondoke tu, kisha Bahati akaondoka na wao kuingia
ndani. Bite alienda moja kwa moja na Erica chumbani kwa Erica ili kuzungumza
nae, muda huo kumbe James alimfata Bahati, ndani walijua James yupo ndani nao
ila alimfata Bahati. Bite kama kawaida alianza kumsema mdogo
wake, “Erica mdogo wangu lini utajifunza wewe jamani? Yani unaanza
kuongozana na wanaume jamani, mbona unataka kututia aibu?” “Ila dada,
mimi ni msichana mkubwa tayari” “Kuwa chuo haimaanishi kuwa wewe ni
msichana mkubwa Erica, angalia maisha yako ya badae. Kijana kama Yule atakupa
maisha gani eeh! Jitathmini, ana hadhi ya kuwa na wewe Yule? Nimekwambia wanaume
wanapenda sana wasichana bikra ila usiuze bikra yako kwa mwanaume asiyekuwa na
maana, mwanaume asiyekuwa na maisha. Yule si mwanaume wa kuwa na wewe, unasoma
nae?” “Hapana” “Amesoma hadi wapi?” “Kaishia la
saba” “Haya sasa, mwanaume wa la saba kweli ukampe maisha yako? Kwanini
kujidhalilisha kiasi hiko wakati wewe ni binti msomi jamani, angalia dada yako,
nimeolewa na mwanaume mwenye maisha na ananipenda kupindukia sababu alinikuta
bikra” “Mmmh!” “Unaguna nini sasa? Usitutie aibu, sitaki kumuona
tena Yule kijana umenisikia eeh! Sitaki tena kumuona, na ukirudi nitamueleza
mama hadi ule ujumbe uliotuma kwangu” “Basi yaishe dada” Kisha
Bite akatoka na kumuacha Erica mule chumbani. James alimuita
Bahati na kumsimamisha, kisha akamnasa kofi, “Ila kaka
unanionea” “Nakuonea nini mshenzi mkubwa wewe, unataka kuharibu maisha
ya Erica nikuangalie tu” “Nampenda kweli na sina haja ya kuahribu maisha
yake” Akamnasa tena kibao, “Na ole wako nisikie umetembea nae,
nitakuchinja na utanijua vizuri mimi ni nani. Kuanzia sasa, Yule muone kama
kituo cha polisi, nitakufunga mimi. Potea mbele yangu” James alikuwa na
hasira sana maana kila akikumbuka jinsi Erica alivyomlaghai halafu anakutana na
kijana wa ajabu ajabu alikuwa na Erica roho ilimuuma sana kamavile Erica ni mke
wake. Alirudi nyumbani na kumkuta mkewe sebleni, “Kheee ulienda
wapi na wewe?” “Yani Yule mjinga nilienda kumpa onyo sababu sikuridhika
kabisa” “Asante mume wangu kwa kumjali mdogo wangu” “Kwanza yuko
wapi? Anatakiwa nae tumpe onyo asituletee tena watu wa kijinga jinga hapa
nyumbani” “Yupo chumbani kwake, ila nishaongea nae” “Haitoshi,
mimi ndio baba mwenye nyumba. Aibu ikija hapa tutadhalilika wote” “Kweli
mume wangu, yupo chumbani kwake kule” James akaenda kwenye chumba cha
Erica na kufungua mlango ila ulikuwa mgumu na kuonyesha kuwa umefungwa kwa
ndani, James akasema kwa hasira, “Wewe Erica fungua
mlango” Erica nae akajibu kwa kwa kujiamini, “Sifungui mlango,
dada ameshanisema inatosha” “Una kiburi eeh!” Erica akawa kimya
na kumfanya James achukie zaidi, akarudi sebleni alipo mkewe na
kumwambia, “Dogo lako lina kiburi sana, unajua limegoma nisiongee
nalo!” Bite akachukia pia na kuinuka, akafungua mlango wa Erica ukawa
haufunguki na kumwambia, “Wewe Erica nifungulie mlango kichaa
wewe” Erica akafungua mlango, dada yake akamzaba
kibao, “Unajifungia milango nyumba yako hii? Nyumba ni yangu na mume
wangu halafu bila aibu unajifungia milango na kugoma kutufungulia. Na kwanini
umegoma shemeji yako asikuseme?” “Dada ulishanisema nimesikia jamani,
nianze kusemwa tena kwanini?” “Hivi unajua kama Yule ndio baba mwenye
nyumba?” “Najua dada” “Sasa unabishaje kusemwa na shemeji
yako?” “Dada, ngoja nikuulize swali. Hivi ni tamaduni za wapi eti
shemeji aje chumbani kwangu kunisema? Hata kama hii ni nyumba yenu, ila hiki
chumba nalala mimi na sidhani kama ni jambo linalofaa eti shemeji aingie
chumbani kwangu? Hiki ni chumba cha msichana, naweka vitu vya kike, yani shemeji
akutane na chupi zangu kweli? Au akutane na pedi zangu? Labda kama nimezidiwa
sijiwezi kabisa na hakuna msaada anaweza kuja kunisaidia ila sio nikiwa mzima
hivi, ni tamaduni za wapi hizo? Kama mnahitaji kunishambulia kwa kunisema si
mniite sebleni hapo, mnisemeee weee hadi yaniingie ila sio kwa shemeji kunifata
chumbani kwangu” Kwa kiasi Fulani haya maneno yalimuingia Bite ila
ilibidi ajitete kidogo, “Sasa kwani wewe unahisi nini kama angeingia na
kukusema humu? Yule si kama kaka yako tu?” “Ni kweli kama kaka yangu ila
kumbuka si kaka yangu ni shemeji yangu” “Usimfikirie vibaya mume wangu,
hawezi kufanya ujinga kwako hata mara moja, kwanza anakuona kama mwanae hata
sijui umeanzaje kumfikiria vibaya hivyo shemeji yako Erica! Huyu ni mume wangu,
hajawahi kuwa na mwanamke mwingine yeyote nje zaidi yangu, iwe kumtamani mdogo
wangu kweli?” “Sijasema hivyo dada labda kama umefikiria vibaya na wewe
pia ila nimekwambia sio tamaduni zetu” Bite kwa kiasi maneno ya mdogo
wake yalimuingia na kwa kiasi yalimchukiza na kuamua kutoka zake mule chumbani
kwa Erica. Siku hiyo Erica hata kula hakwenda sababu muda wa
kula dada yake alimuita hakutoka, sasa aliwaza akitoka muda ambao shemeji yake
amebaki mwenyewe sebleni itakuwaje, kwahiyo aliamua kukaa chumbani tu huku
akijisemea, “Sitaki kuharibu ndoa ya dada yangu, siwezi kumwambia ukweli
wowote ila mimi nitajiepusha na hapa. Huyu shemeji si mzuri tena kwangu. Hivi
ndio dada anasema mwanaume akikukuta bikra hakusaliti kweli mmh!! Mimi tu mdogo
wa mke wake alinitamani, je wa huko nje inakuwaje? Hakuna cha kuolewa na bikra
wala nini, asinibabaishe na yeye, kwanza nishaharibu siwezi kurudisha siku
nyuma” Aliwaza na kupanga vizuri vitabu vyake kwaajili ya kujiandaa
kesho kwenda chuo. Asubuhi alikuwa ashajiandaa na kutaka kutoka na dada
yake, ila Bite alidai kuwa siku hiyo alichelewa sana kazini, basi James akasema
sababu na yeye anatoka basi atampitisha chuoni, mmh Erica akaona hiyo sio sawa
kwake ilibidi amuombe dada yake amshushe hata stendi maana alikuwa na haraka
sana asingeweza kumsubiria shemeji yake, dada yake alivyopanda tu kwenye gari
yake, Erica nae alikuwa amepanda na kumuomba amuache tu kituoni, ilibidi dadake
afanye hivyo. Erica alienda moja kwa moja hosteli, ila hakuwa na kipindi
chochote siku hiyo kwahiyo alikuwa na lengo tu la kurudi chuo na si kukaa pale
nyumbani na shemeji yake. Akawa amekaa tu akiwasiliana na Bahati kwa
njia ya ujumbe, Bahati alimuomba Erica aende kumuona maana anajisikia vibaya,
ukizingatia hakuwa na kitu chochote cha kufanya kwa siku hiyo akaona ni vyema tu
kwenda kumuona Bahati na kupafahamu anapoishi. Alifika
anapoishi Bahati na kumkuta, walikuwa wawili tu ndani, Bahati akamuuliza
Erica, “Unajua ninachoumwa?” “Unaumwa nini?” “Naumwa
mapenzi Erica” “Unaumwa mapenzi? Kivipi?” “Erica, wewe ndiye
tiba yangu, wewe ndiye wa kunifanya nipone” “Sikuelewi” Bahati
alimuangalia Erica kwa macho ya huruma sana huku akiongea kwa sauti ya
huruma, “Kheee kwahiyo umeniita ili ufanye mapenzi na
mimi?” “Usinifikirie hivyo Erica, nakupenda” “Hapana, sipo
tayari Bahati. Sipo tayari kabisa” Erica akainuka ili aondoke, Bahati
akashika kisu na kumwambia Erica, “Ukiondoka najiua, ni heri nife kuliko
kukukosa wewe” Huruma ikamshika Erica ila hakutaka kulala na mwanaume
kwakweli huo ulikuwa mtihani mgumu sana kwake, ila hakuwa na jinsi kwani hata
taswira ya kawaida ya Bahati ilibadilika kabisa, ikabidi Erica
akubali. Baada ya lile tendo, Bahati alimuangalia Erica na
kumwambia, “Pole Erica” “Pole ya nini?” “Najua
nimekuumiza Erica, ila nashukuru kwa kunipokea” Erica alimuangalia tu
huyu Bahati ambaye aliendelea kuongea, “Asante Erica, asante kwa
kunitunzia” “Sikuelewi” Hunielewi Erica? Nakushukuru sana, yani
siamini kuwa mimi ni mwanaume wa kwanza kwako, asante sana Erica kwa kunitunzia
bikra yako” Erica alimshangaa sana huyu
Bahati. Itaendelea kesho kutwa Usiku…..!!!! Kwa wale wa
story ya maisha yangu mnifate inbox. Ile story siitoi public, ni story ya
private, kuna sababu za mimi kutokuiweka public na ukibahatika kuisoma utaelewa
ni kwanini sijaiweka public. Erica alimuangalia tu
huyu Bahati ambaye aliendelea kuongea, “Asante Erica, asante kwa
kunitunzia” “Sikuelewi” Hunielewi Erica? Nakushukuru sana, yani
siamini kuwa mimi ni mwanaume wa kwanza kwako, asante sana Erica kwa kunitunzia
bikra yako” Erica alimshangaa sana huyu Bahati. Ila Bahati
aliendelea tu kumsifia Erica kuwa ni msichana wa pekee sana, Erica aliamua
kumuaga Bahati kuwa anarudi hosteli. Bahati aliinuka na kutaka kumsindikiza
Erica, “Kheee si ulisema unaumwa wewe?” “Ndio nilikuwa naumwa
ila nilikuwa naumwa mapenzi” Erica alimuangalia Bahati kisha kuanza
kuondoka na Bahati alikuwa akimsindikiza, na alimpeleka hadi
hosteli. Muda wote Bahati alikuwa akimsifia Erica kwa uzuri aliokuwa
nao, “Erica mpenzi wangu, wewe ni msichana mrembo sana najua kuna vijana
wengi watakufata na kukudanganya kuwa wanakupenda huku wakikusifia kuwa wewe ni
mzuri, wakikwambia kuwa wewe ni mzuri na mrembo waambie unajua utaweza kwa kiasi
Fulani kuwakata makali yao. Wakikutaka kimapenzi waambie kuwa una mpenzi, Erica
sikudanganyi wala sikutanii nakupenda sana” Erica alikuwa anamsikiliza
tu anavyoongea hadi alivyofika hosteli na kuagana nae. Kufika
hosteli alipoenda kuoga alijilaumu sana kwa kujiingiza kwenye mapenzi na
Bahati, “Uuuh Mungu wangu, kwahiyo sasa nimetembea na wanaume watatu. Si
ndio nimekuwa Malaya jamani? Na kati yao hakuna wa kuwa mume wangu, ila mimi
nina kilanga, kilichonifanya nitembee na Bahati ni nini? Nadhani ni mawazo
niliyonayo sababu ya George, ila Yule mwanaume ni mpuuzi sana, wa kuniacha mimi
kweli? Mbona Yule Bahati amejisifia kuwa yeye ndio wa kwanza kwangu? Au wanaume
wapo tofauti? Ila Mungu anisaidie nisije kutembea na mwanaume mwingine tena,
kama nimeamua kuwa na Bahati basi niwe naye yeye tu” Aliwaza sana, na
kumaliza kuoga kisha kwenda ndani kuvaa nguo, alipomaliza alifika mtu na
kumwambia “Erica kuna kijana anakuita nje” Erica hakuelewa
kuhusu huyo mtu anayemuita, kwahiyo alitoka kwenda kumuangalia na ilikuwa tayari
saa mbili usiku. Alishangaa kumuona kuwa ni Adam, Yule kijana
aliyemwambia kuwa anaelewa kuhusu George na Dora. “Adam, umejuaje kama
nakaa hosteli hii?” “Nimejua tu, nilikuwa nikiulizia
unapokaa” “Haya karibu” “Asante, ila ni vyema tukitafuta mahali
tuongee” “Usiku huu? Ungeongea tu hapa hapa au tuongee
kesho’ “Hapana tusingoje kesho” Erica akashangaa sana kuwa
wasingoje kesho, ni ujumbe gani anataka kumwambia ila bado hakujua ni wapi
angekaa nae na kuzungumza nae. Adam akamuomba wakakae kwenye vimbweta vya
bustanini ili azungumze nae, Erica alikubali. Walifika kwenye
vimbweta vya eneo hilo na kujikuta wakiwa wawili tu maana lile eneo taa zake
ziliharibika kwahiyo palikuwa na giza na kufanya hata watu kujisomea eneo hilo
iwe ni vigumu sababu ya giza, basi Adam alikaa pale na Erica kwaajili ya
maongezi yao. “Eeeh nakusikiliza Adam” “Unajua Erica wewe ni
msichana mrembo sana?” “Najua, sema lingine” “Mmmh ngoja
tuachane na hiyo mada kwanza. Nilitaka kukueleza kuhusu George na
Dora” “Eeeh” “Yani George ni mwanaume muongo sana,
kashawadanganya wasichana wengi sana, na kuharibu maisha ya wasichana wengi
sana. Tena alishwahi kuwa na mahusiano na Yule Dora ila badae wakawa marafiki.
Dora aliwahi kuwa mpenzi wangu, kwahiyo George alimpora Dora kwangu iliniuma
sana” “Kumbe! Dora si rafiki mwema na sitaki tena urafiki
naye” “Ila mimi nina Wazo” “Wazo gani?” “Najua wewe
ulikuwa na mahusiano na George na umeumizwa na George na Dora, mimi nimewahi
kuwa na mahusiano na Dora na rafiki yangu alikuwa George, wameniumiza pia watu
hawa. Naomba tuwafanyie revenge” “Kivipi?” “Mimi na wewe tuwe
pamoja” “Pole, ila umechelewa Adam” “Kivipi?” “Mimi nina
mahusiano na mtu mwingine kwasasa” “Mmmh Erica jamani, najua unasema
hayo sababu hunijui kwa undani vizuri. Ila ungenijua usingesema
hayo” Adam akawa anamsogelea Erica ili ambusu mdomoni, ila Erica
alimrudisha nyuma na kumwambia, “Adam, nina mpenzi tayari hata hapa
unaponiona nimetoka kufanya nae mapenzi” “Unasemaje?” “Ndio
hivyo, siwezi kuwa na mpenzi mwingine tena” Adam akaona kuendelea
kumuomba Erica kuwa wapenzi ni kujisumbua tu kwa hivyo aliamua kuagana nae,
kisha Erica akarudi hosteli. Na alipofika tu uliingia ujumbe kutoka kwa
Bahati, “Nakupenda sana Erica, wewe ni mwanamke muhimu sana katika
maisha yangu” Alisoma ujumbe huu na kutabasamu alijiuliza kuwa inakuwaje
wakati kwa kawaida wanaume wanapokutana kimwili na mwanamke ndio wakati wa
mwanaume huyo kutokumtaka tena huyo mwanamke ila ilikuwa tofauti sana kwa
Bahati. Kwnye mida ya saa tano usiku akapokea simu kutoka kwa dada yake
Bite, “Wewe mbona hujarudi nyumbani?” “Dada, nimeamua kurudi
hosteli” “Hivi una akili wewe, yani unafanya jambo bila hata ya
kunishirikisha kweli?” “Dada nisamehe ila sikuwa na la kufanya zaidi ya
kurudi hosteli” “Ili iwe rahisi kufanya madudu yako?” “Hapana
dada usinifikirie hivyo” “Kesho shemeji yako atakuja kukuchukua na
utarudi nyumbani sawa” “Lakini dada” “Sitaki cha lakini,
nimemaliza” Bite akakata simu na kumuacha Erica akiwa na mawazo sana
kwani alifikiria cha kufanya sababu hakutaka tena kurudi nyumbani kwa dada yake
na hakutaka kumwambia dada yake ukweli kwa kuhofia atavunja mahusiano ya dada
yake na shemeji yake. Yani usiku wa siku hiyo alikuwa akiwaza tu kesho
anamkwepaje shemeji yake. Kulipokucha mapema kabisa, aliamshwa
na simu ya Bahati na alikuwa akimsalimia na kumtakia masomo mema. “Mmmh
huyu mwanaume nae ana kibarua loh!” Akainuka na kujiandaa kwaajili ya
kwenda chuo maana siku hiyo alikuwa na kipindi cha asubuhi. Wakati
anaingia kwenye bwalo la kusomea, akapishana na George ambaye alionekana
kumuangalia sana Erica ila Erica alipita kamavile hamuoni, akaingia zake
darasani. Wakati anatoka, Dora alimfata nyuma na
kumsalimia, “Erica mambo” “Safi ila sitaki mazoea na wewe
Dora” “Erica jamani, kumbuka tunasoma wote” “Tunasoma wote?
Kwani na wewe ni mwaka wa kwanza kama mimi? Wewe si mwaka wa pili, umecarry hili
somo ndiomana tunaonana” “Hata kama Erica, ila sio vizuri
unavyonifanyia” “Ila ni vizuri kwako kwa mwanaume uliyetembea nae wewe
kumlengesha atembee na mimi! Hivi mkoje watu jamani? Yani hata huoni kinyaa kwa
mwanaume uliyekuwa na mahusiano nae kuja kuwa na mahusiano na rafiki yako?
Usiniambie ndio usomi au uzungu, huo ni uchafu? Na kwa taarifa yako, hutoniona
tena nikimfatilia huyo George wala nikiumia kwaajili yake, kwangu mimi ni kama
mtu ambaye hajawahi kuwepo katika maisha yangu” Erica akaondoka zake,
ila mbele kidogo kuna mdada alimsimamisha Erica na kumwambia kuwa amesikia
alichokuwa anaongea na Dora. “Pole sana, unajua sisi wasichana mara
nyingine ni sisi wenyewe ndio tunaharibiana ndiomana wanasema adui wa mwanamke
ni mwanamke” “Kweli kabisa, yani Yule Dora kanifanya nisiwe na hamu na
marafiki kabisa” “Ila si wote wenye tabia zisizofaa” “Sijawahi
kuwa na rafiki mwenye tabia njema, yani napataga vimeo tu” “Hapana
usiseme hivyo, By the way naitwa Tumaini sijui mwenzangu unaitwa
nani.” “Naitwa Erica” “Ningependa tuwe marafiki, hata kwa
kawaida tu yani tuwe tunaongea na kubadilishana mawazo” “Hakuna
shida” “Unajua Yule Dora uongo ndio uliomfanya hadi akafeli na kurudia
lile somo” “Kumbe unamjua” “Ndio namjua” Basi Erica
aliongozana na huyu mdada hadi hosteli na kugundua kuwa anaishi nae hosteli moja
kasoro vyumba tu. Akaagana nae na kuelekea kwenye vyumba
vyao. Erica alitulia na kupigiwa simu na namba ngeni
akapokea, “Erica, mimi ni shemeji yako James. Nakuuliza nije saa ngapi
kukuchukua?” “Hapana shemeji, mimi hosteli pananitosha” “Ila
dada yako kasema nije nikuchukue” “Hapana shemeji” “Nakuja
Erica” James akakata simu, kwakweli Erica alijiona yupo kwenye mtihani
mzito sana kwake kwani hakutegemea kabisa kama shemeji yake huyo anaweza kuwa
king’ang’anizi kiasi hiko, akawaza sana, akataka kuondoka hapo
hosteli. Ila wakati anatoka tu akakutana na Tumaini, “Khaa kumbe
ulitaka kuondoka Erica, mi nilikuwa nakufata. Unataka kwenda wapi
kwani?” “Kutembea tembea tu” “Basi twende pamoja, mimi nilikuwa
nakufata ili nikuonyeshe chumba ninachoishi” “Si ushanionyesha ni
pale” “Hapana, pale nakaa kihosteli ila kipo chumba mtaani nimepanga.
Twende Erica” Kwasababu Erica alitaka kuondoka hapo hosteli na hakuwa na
mahali pa kuelekea kwa muda huo akaamua kukubali tu kwenda na
Tumaini. Walifika nyumbani kwa Tumaini na kumkaribisha ndani, alishangaa
sana kuona Tumaini ana kila kitu kwenye chumba chake, “Kheee hongera,
umewezaje kumiliki vyote hivi?” “Boom, yani boom ninalopata ndio
nanunulia vitu ninavyotaka. Unajua kwetu wananipa hela ya kila kitu na hawajui
kama Napata mkopo, kwahiyo ule mkopo ndio nafanyia mambo yangu” “Kwahiyo
ada” “Mimi Napata mkopo asilimia mia, na kwetu huwa wananipa ada yote,
sasa nitafanya nini hapo zaidi ya kujipendezesha” “Mmmh hongera
sana” Mara simu ya Tumaini ikaita na akaongea nayo kwa muda, alipokata
akamuangalia Erica na kumwambia, “Ni mdogo wangu nilikuwa nawasiliana
nae, kasema anakuja kunitembelea.” “Aaah sawa basi, ila kwenu wewe una
deka sana?” “Hahaha hapana bhana, halafu kwa baba tupo wawili tu mimi na
huyo mdogo wangu anayekuja ila mama tofauti.” “Wazazi wako wanaishi
pamoja?” “Hapana, baba na mama yangu hawajaoana, ila baba ana hela sana
kwahiyo huwa anatuhudumia kwa kila kitu. Sijui kuishiwa mimi, Yule mdogo wangu
anayekuja ndio balaa maana baba anamuhudumia na mama yake nae anamuhudumia yani
baba na mama yake wanashindana kumuhudumia, hajaanza kazi ila ana hela
uchafu.” Erica alijikuta akitamani sana maisha ya Tumaini na kutamani
hata yeye ndio angekuwa Tumaini. Muda kidogo mdogo wa Tumaini alifika na kugonga
mlango, Tumaini akamfungulia na kuingia ndani. Erica alibaki anamshangaa
tu kwani alikuwa ni Erick, Yule aliyesoma nae. Itaendelea kesho
usiku…..!!!! Wale wa story ya maisha yangu mnifate inbox ila sio mnifate
kwa kunilaumu tu, mimi pia ni binadamu kama kuna mahali nakosea niambie kwa
ustaarabu. Utaratibu wa story hiyo ni private na sio public, naomba mnielewe,
nashukuru kwa wale mnaonielewa mbarikiwe
sana. Erica alijikuta akitamani sana maisha
ya Tumaini na kutamani hata yeye ndio angekuwa Tumaini. Muda kidogo mdogo wa
Tumaini alifika na kugonga mlango, Tumaini akamfungulia na kuingia
ndani. Erica alibaki anamshangaa tu kwani alikuwa ni Erick, Yule
aliyesoma nae. Tumaini ndiye aliyemshtua Erica na kumtoa kwenye
mshangao, “Erica mbona unashangaa hivyo? Huyu ni mdogo wangu anaitwa
Erick. Karibu Erick, huyu ni rafiki yangu na ni mdogo wangu pia anaitwa
Erica.” Erick alimuangalia sana Erica, ila Erica nae alimuangalia sana
Erick kisha Erick akampa mkono Erica na kumwambia, “Nashukuru
kukufahamu” Hii hali kidogo ilimchanganya Erica maana Erick ni mtu
anayemjua fika ila leo anaishia kumpa mkono tu na kumwambia kuwa anashukuru
kumfahamu, alishindwa hata kujibu na kujikuta akikaa kimya na kutikisa kichwa
tu. Kisha Tumaini akaanza kuongea na mdogo wake, “Naona
uenifanyia surprise leo” “Aaah nilikuwa napita mitaa ya huku ndio
nikaamua kuja kukutembelea dada” “Nimefurahi sana” “Dada
kaninunulie kinywaji basi” “Aaah kwa mara ya kwanza leo umetaka
kinywaji, basi sawa ngoja nikakununulie kinywaji chako
unachopendaga” Tumaini akatoka na kuwaacha Erica na Erick ndani, kisha
Erica alimuita Erica, “Erica” “Abeee” “Mbona umetulia
sana?” “Nifanyeje sasa na umejifanya hunijui” “Mmmh sio hivyo
nakukumbuka vizuri Erica ila nakumbuka pia ulivyofanya nidhalilike shuleni,
sikutaka dada ajue kuwa wewe ni msichana uliyefanya mdogo wake nipate aibu
shuleni ndiomana nikajifanya sikufahamu. Ila ni vyema tukipeana mawasiliano
halafu tutaongea vizuri zaidi” Erica alimpa Erick namba zake, muda
kidogo Tumaini alirudi na vinywaji mkononi. Kisha akawafungulia na
kuwakaribisha, “Hapana mimi situmii kilevi” “Kwanini
Erica?” “Situmii tu” “Mmmh unakosa uhondo basi” Ikabidi
achukue ile bia kisha amuwekee juisi Erica maana yeye hajalelewa katika
mazingira ya kunywa kilevi. Waliongea ongea pale kisha Erick
alimtumia ujumbe Erica kuwa aage na amsubirie mahali ili waongee, kwahiyo Erica
akamuaga Tumaini, “Dada, mi naona niende” “Jamani kwani una
kipindi jioni hii? Mbona mapema?” “Hapana, ila kuna mahali natakiwa
kwenda” “Subiri basi, mdogo wangu akiondoka nikusindikize” Erick
akadakia kwa dadake, “Unajua mimi naondoka muda gani?” Ikabidi
wacheke tu kisha Tumaini akamruhusu Erica kuondoka huku akimsindikiza
kidogo. Wakiwa njiani, Erica alitumiwa ujumbe na
Erick, “Jitahidi umkwepe huyo dada maana huwa akiamua kumng’ang’ania mtu
anamng’ang’ania huyo balaa. Hashindwi kukupeleka na ukarudi nae” Kisha
Tumaini nae akamuuliza tena, “Kwani Erica unawahi wapi
jamani?” Mara Erica akapigiwa simu na shemeji yake, “Nakuja
kukuchukua Erica” “Sawa shemeji” “Ushajiandaa?” “Ndio
nishajiandaa” James alishangaa pia muda huu yani Erica kaongea nae bila
kubisha chochote kile kumbe Erica alikuwa anaongea vile ili kumuaminisha Tumaini
kuwa kuna mahali anawahi, “Natakiwa kuwahi hosteli maana shemeji anakuja
kunichukua” “Unaenda nae wapi” “Naenda nae nyumbani, alisema
dada jana aje anichukue” “Aaah sawa, basi usije ukachelewa
kujiandaa” Basi Tumaini akaita bodaboda na kumlipa kisha akamwambia
amfikishe Erica hosteli, kwahiyo Erica alipanda ile
bodaboda. Baada ya Tumaini kurudi tu Erick nae
akamuaga, “Jamani Erick kumbe unaondoka muda huu huu si ungeniambia tu
mi nimpeleke Erica?” “Mmmh dada nawe yani unaanza kuthamini wageni
kupita mimi jamani?” “Basi yaishe” Basi Erick alitoka pale na
kuondoka, kisha akawasiliana na Erica, sababu alikuwa na gari ilikuwa rahisi
kumfata Erica hosteli kwao. Alipofika maeneo ya karibu na pale hosteli
alimshtua Erica naye alitoka kisha Erick akamuomba apande kwenye gari yake na
kuanza kuondoka, “Mmmh tunaenda wapi Erick?” “Nahitaji kuongea
na wewe Erica, hujui tu ni furaha gani ipo moyoni mwangu baada ya kukuona na
wewe” Basi Erick alipeleka gari hadi hotelini na kukodi chumba, kisha
akaingia na Erica huku akimwambia kuwa lengo lake anahitaji tu kuongea
nae. Walifika chumbani na kukaa kwaajili ya maongezi, “Erica
nilikutafuta sana ila sikujua ni wapi pa kukupata, nashukuru nimekupata sasa.
Vipi bado unanipenda?” “Mmmh!” Erica aliguna maana alifikiria
kuhusu Bahati, na vipi amkubali Erick itakuwaje kwa Bahati wakati anaonyesha
akimpenda sana, “Mbona unaguna Erica,
hunipendi?” “Hapana” “Nini sasa
Erica?” “Sijui” “Hujui nini?” “Sielewi” Erick
alimsogelea karibu Erica na kumbusu, kwakweli Erica hakuweza kukataa chochote
kwa Erick sababu ni mwanaume aliyekuwa katika moyo wake kwa kitambo sana, na ile
hali ilimpa urahisi Erick wa kufanya chochote kwa Erica. Erica
alijikuta akifanya mapenzi na Erica na walipomaliza katika siku zote ile siku
alijawa na aibu kupita maelezo ya kawaida, alishikwa na aibu sana baada ya
kumaliza lile tendo na Erick kiasi kwamba hakuweza hata kumuangalia tena usoni,
hadi Erick aliamua kumuuliza “Erica vipi mbona umejawa na aibu kiasi
hiko?” “Hapana” “Usijali Erica, nakupenda ujue. Usijali kwa yote
yaliyopita kati yetu, najua una maisha yako na mimi nina maisha yangu kwasasa
ila upendo ni kitu cha ajabu sana, bado utaendelea kuishi moyoni mwangu kama
mimi ninavyoishi moyoni mwako. Usinionee aibu Erica” Bado Erica aliona
aibu sana, basi Erick aliinuka na kwenda kuagiza chakula. Erica alioga
na kuvaa kisha kuchukua simu yake, akakuta kuna simu ambazo hazikupokelewa za
shemeji yake pamoja na Bahati, kisha akakuta ujumbe kutoka kwa
Bahati, “Kumbuka nakupenda sana Erica, tafadhali
usinisaliti” Alisoma ule ujumbe huku moyo wake ukimsuta sana kwani
tayari alishamsaliti Bahati kwa kulala na Erick, alijiuliza cha kufanya lakini
hakuwa na jibu, “Erick nampenda tena nampenda sana, naye ananipenda ila
sijui maisha yake kwasasa na sijui anafikiria nini kuhusu mimi. Bahati
ananipenda sana, hata sijui nifanyeje” Aliwaza sana na kukosa jibu,
Erick alikuja na chakula ambapo alimbembeleza Erica wale kile
chakula. Walipomaliza alimbembeleza kuwa alale pale na ampeleke hosteli
kesho yake, “Hapana Erick, inabidi nirudi leo” Wakati anabishana
na Erick pale kuna ujumbe kwenye simu yake ukaingia kutoka kwa shemeji
yake, “Erica uko wapi? Nimekuja kukuuliza kwenye hosteli yenu hapa
wamesema hawajui ulipoenda? Uko wapi na nilikwambia nakuja kukuchukua? Nakungoja
hapa nje ya hosteli yenu nipo kwenye gari yangu” Erica alisoma ule
ujumbe na kumuangalia Erick ambaye alimuuliza kuwa tatizo ni nini ila akajikuta
ameropoka tu kuwa amekubali kulala nae hapo hotelini hadi asubuhi, jambo hilo
lilikuwa ni furaha sana kwa Erick huku akimpa Erica ahadi za kila
aina. Erica aliamua kuzima simu ili shemeji yake asimpate tena hewani
ila hakujua kama kile kitendo chake cha kuzima simu kilimuumiza sana
Bahati. Bahati alipoona kuwa hampati hewani Erica akaamua
kwenda hosteli kwa Erica, alipofika moja kwa moja alienda kumuulizia akaambiwa
kuwa Erica hayupo na kumfanya azidi kupatwa na mashaka kuwa huenda Erica kapatwa
na matatizo, wakati anatoka ndipo alipokutana na shemeji wa Erica ambaye alikuwa
anataka kuondoka sababu alishamsubiri sana Erica bila ya matokeo
yoyote. Bahati alishtukia tu akikamatwa na kuingizwa kwenye gari kisha
akapuliziwa kitu machoni na kumfanya apoteze fahamu. Kuja kushtuka
alikuwa baharini anapigwa tena inaonyesha alipigwa sana, “Kaka
nisamehe” “Nikusamehe nini mbwa wewe, yani mimi naenda kumchukua Erica
halafu wewe ulimfungia!” “Si kweli kaka” Ila James hakutaka
kumsikiliza zaidi ya kumuongezea kipigo na kumuacha pale pembezoni mwa
bahari. James aliondoka hadi hosteli kwakina Erica tena, alimuulizia
Erica ila bado hakuwepo alichukia sana na kurudi nyumbani kwake. Bite alimuuliza
mume wake, “Vipi Erica yuko wapi?” “Mdogo wako ni mjinga sana
kati ya wajinga, unajua alikuwa na Yule jamaa hadi simu
kanizimia” “Jamaa gani?” “Si Yule wa siku ile, ila nimempiga
sana yani mimi vijana wa kuharibu mabinti siwapendi kabisa” “Jamani huyu
Erica mbona anataka kututia aibu jamani! Itabidi kesho niende kwa dada yetu Yule
mkubwa nikamueleze habari za huyu Erica maana atatutia aibu
kwakweli” Bite alichukia sana kwa mwenendo huo wa mdogo wake maana
aliona sasa amekuwa mtu wa ajabu. Palipokucha, Erica alijiandaa
vizuri kabisa kisha Erick alimrudisha hosteli. Alikuwa amechoka sana kwahiyo
alifikia kulala kwanza mpaka jioni ndio akajiandaa kwaajili ya kwenda chuo maana
alikuwa na kipindi muda huo. Alirudi jioni kabisa na kuwasha simu yake,
alikutana na jumbe mbali mbali zilizoongozana ila ujumbe uliomshtua zaidi ni
ujumbe wa Bahati, “Jana nilikuja hosteli kwenu maana sikukupata hewani,
ila nilikamatwa na Yule ndugu yako wa kiume wa siku ile na amenipiga sana akidai
kuwa nimekufungia” Erica aliamua kumpigia simu Bahati, hata ongea yake
ilionyesha wazi kuwa ni mtu mwenye maumivu sana, ila aliongea nae na akamueleza
ilivyokuwa ila yeye hakuweza kumueleza kuwa ni kwanini alizima simu yake maana
hakujua ni jinsi gani amwambia ukizingatia kapigwa kwaajili yake. Wakati
anawasiliana na Bahati, Erick nae akamtumia ujumbe kuwa amemkumbuka
sana, “Erica kipenzi cha moyo wangu nishakukumbuka
tayari” Akatabasamu na kusahau kabisa kama kuna mtu alikuwa anawasiliana
nae aliyekuwa na maumivu ya kupigwa. “Nakukumbuka pia
Erick” “Naomba nikuulize swali Erica” “Niulize tu” “Je
una mpenzi?” Erica alifikiria na kuona kama atamwambia ukweli Erick basi
atamkosa kwahiyo hakuwa na budi zaidi ya kumdanganya kuwa hana
mpenzi, “Hapana sina, vipi wewe?” “Upande wangu ni historia
ndefu, ila tuachane na hayo. Unajua nakupenda Erica” Lile swala la kwa
upande wangu ni historia ndefu lilimpa changamoto kubwa sana Erica kwani alihisi
huenda kuna mwanamke ana mahusiano na Erick, alijikuta akimuonea wivu
kupindukia, ila hakuweza kumwambia Erick amueleze huo mlolongo wa stori
ndefu. Basi Erick akamuomba Erica kuwa aonane nae
keshokutwa. “Nitakuja hosteli kwenu kukufata” “Sawa
Erick” Akakubaliana nae kuwa atafika kuonana nae, moyoni mwake kwa muda
huo alikuwepo Erick tu tena hakukumbuka wengine wote zaidi ya kumuwaza
Erick. Swala hilo lilimfanya apotezee kabisa simu za Bahati kwani aliona
akimpotezea ndipo Bahati ataacha kumfatilia ukizingatia kashamwambia Erick kuwa
hana mahusiano mengine yoyote yale. Ilifika siku aliyopanga
kuonana tena na Erick, na kweli Erick kama alivyopanga alienda hosteli anapokaa
Erica na kumsubiria kwa nje, Erica alipofika nje alikutana na Bahati akiwa na
alama alama za kupigwa kumbe Bahati alipoona tena kimya aliamua kuja kumuona
Erica, kwahiyo wakati Erica akimshangaa Bahati kuwa kafata nini tena, muda ule
ule Bahati alisogea alipo Erica na kumkumbatia kisha akambusu, wakati huo Erick
alikuwa mbele yake akiwaangalia kwa mshangao. Ilifika
siku aliyopanga kuonana tena na Erick, na kweli Erick kama alivyopanga alienda
hosteli anapokaa Erica na kumsubiria kwa nje, Erica alipofika nje alikutana na
Bahati akiwa na alama alama za kupigwa kumbe Bahati alipoona tena kimya aliamua
kuja kumuona Erica, kwahiyo wakati Erica akimshangaa Bahati kuwa kafata nini
tena, muda ule ule Bahati alisogea alipo Erica na kumkumbatia kisha akambusu,
wakati huo Erick alikuwa mbele yake akiwaangalia kwa mshangao. Erica
akona sasa picha yake itavurugika, akajitoa kwenye mikono ya Bahati, kisha
Bahati akamuuliza, “Vipi tena Erica?” Erica akawa anaondoka
akielekea alipo Erick, ila Erick aliingia kwenye gari yake akapanda na kuondoka
zake. Ila Bahati nae alikuwa akimfata kwa nyuma, na ilionyesha jinsi gani Erica
amechukia kwa Erick kuondoka kwahiyo mbaya wake kwa muda huo alikuwa Bahati,
akageuka nyuma kwa gadhabu ili amseme Bahati, ila kabla hajamsema Bahati
akamwambia, “Yani Erica hukutaka kukumbatiwa na mimi sababu ya kijana
mwenye gari? Sina gari ndio ila nina mapenzi ya dhati kwako Erica, nakupenda
sana” “Sitaki kuusikia huo wimbo tena” “Erica jamani, kosa langu
ni nini kwako? Kosa langu ni kukupenda? Angalia nilivyoumia kwa kipigo sababu ya
kukupenda wewe” “Usinibabaishe, umeyataka mwenyewe. Bahati sitaki tena
unifatilie” “Siwezi Erica, siwezi kamwe nakupenda sana” “Lakini
mimi sikupendi” “Hunipendi sababu ya Yule kijana mwenye gari Erica? Muda
ukifika, Mungu akipenda na mimi nitamiliki gari yangu” “Sitaki kusikia
hizo ngonjera, kwaheri” Erica alirudi zake ndani mule hosteli kwani
aliona kashaharibu na hakujua ni kwa jinsi gani anaweza kufanya aweze kuelewa na
Erick. Alipokuwa ndani alipigiwa sana simu na Bahati ila
hakupokea hata moja, akapata wazo kuwa inabidi aende kwa Tumaini ili ajaribu
kumdadisi kuhusu Erick, ila akawaza kuwa lazima Bahati atakuwa chini akaimsubiri
maana huwa hakati tamaa kwahiyo ikabidi atumie njia ya kumkwepa ili aende
kiurahisi. Alijiandaa na kutoka, ni kweli wakati anatoka alimuona Bahati
amejikalia chini ya mti akimsubiria, “Yani huyu mkaka wa ajabu hakati
tamaa loh!” Akamsogelea, kisha Bahati akainuka ili
amsikilize, “Bahati mpenzi wangu yani bado unanisubiri hapa
nje?” “Nitafanyaje sasa na wewe umechukia Erica?” “Mimi
sikuchukia ila nilikuwa napima tu upendo wako, nimegundua una upendo wa hali ya
juu Bahati. Ila ukapumzike kwasasa mpenzi wangu, pole sana umeumia kwaajili
yangu. Yani moyo umeniuma kweli” Bahati alitabasamu kusikia maneno haya
kutoka kwa Erica maana hakutegemea kabisa kama Erica angemwambia maneno yale ya
kumbembeleza, alimuahidi kuwasiliana nae muda wote na kupokea simu zake huku
akimbembeleza kuwa aondoke, hadi Bahati akakubali kuondoka. “Mimi nina
kipindi, kwahiyo ukiona sijapokea simu zako ujue nipo kwenye kipindi kwasasa.
Tutakuwa tunawasiliana mpenzi wangu, hata usijali” Basi wakaagana pale
kisha Bahati akaondoka halafu Erica akaenda kwa
Tumaini. Ilikuwa Bahati kwani ni muda ule ule Tumaini alikuwa
ndio amerudi toka kwenye matembezi yake, “Karibu Erica, jamani si
ungesema nikupitie” “Nilikukumbuka tu dada yangu” “Karibu, za
tangu siku ile” Wakaanza kuongea huku wakifurahi sana ilikuwa kama watu
ambao wamefahamiana kwa muda mrefu sana kumbe sio siku nyingi tangu wawe
marafiki, ilionyesha wanapatana sana. Erica alianza kumuuliza kwa
kumtega, “Vipi Yule mdogo wako Erick ana mchumba?” “Mmmh Erica
usiniambie kuwa umempenda mdogo wangu Yule?” “Aaah jamani dada nimeuliza
tu” “Erica nakupenda sana mdogo wangu ten asana, siwezi kukushauri uwe
na Erick kwakweli” “Kwanini?” “Nimejua tu ushampenda, Erick huwa
anapendwa na wadada wengi sana sababu ana sura ya mama yake na mwili wa baba. Ni
mzuri kwakweli wa kuvutia na wengi wanampenda” “Kwasababu watu wengi
wanampenda ndio hafai kuwa na mimi?” “Aaah hiyo sio sababu ila Erick
nahisi kuna kipindi aliathirika kisaikolojia” “Kwanini?” “Ni
anabadilisha wasichana Yule kama nguo, yani kila siku nafanya kazi ya kumpa
ushauri maana magonjwa mengi ila anajidai wanamfata wenyewe. Erick amekuwa na
msichana mmoja anaitwa Sia, ni mvumilivu sana yani Yule Sia hata amfumanie hapo
Erick hakubali kumuacha, yani atanipigia simu na kujiliza sana ila hamuachi
Erick, yani Yule dada anampenda Erick balaa ila mdogo wangu Yule ni pasua
kichwa” “Aaah mfano mimi ananifaa kijana wa aina gani?” “Wewe
anakufaa kijana mpole, mtulivu na mwenye upendo wa dhati. Erica nakupenda sana
na hakika ningependa urafiki wetu ukuwe na ningefurahi uwe wifi yangu ila sio
kwa Erick, hapana kabisa Erick hafai, ni mdogo wangu ila hafai” Tumaini
alimwambia Erica ila hakujua alivyoumiza moyo wa Erica kila alipomwambia kuwa
Erick hamfai ukizingatia nanampenda sana. Basi akaongea ongea nae pale na
kumuaga, kama kawaida Tumaini alimkodia bodaboda Erica imfikishe
hosteli. Erica alikuwa na mawazo sana siku hiyo, akikumbuka
kuwa Erick alimuona na Bahati wakikumbatiana ila Erick aliondoka kwa hasira na
mpaka muda huo hakumtafuta, Erica akiwaza kuwa amtafute yeye na kujaribu
kumuelewesha ila kila alipokumbuka aliyoambiwa na Tumaini hakutaka tena
kuwasiliana na Erick, “Sijui kwanini nimetembea nae, itabidi kesho
nikapime ukimwi. Kumbe Erick kawa muhuni vile, najuta mimi
Erica” Aliwaza sana na kumfanya aumie sana moyoni mwake, ila jumbe
alizozipata toka kwa Bahati zilimpa faraja sana. Kesho yake hakuweza
kufanikisha lile swala lake la kwenda kupima maana masomo yalikuwa mengi sana,
kwahiyo akajikuta akiwa yupo makinisana na masomo yake, na alishtukia kuwa mwezi
huo ni mwezi wa mitihani kwahiyo alijishughulisha sana na masomo hata hakutaka
kuwasiliana sana, hata dadake alipompigia simu na kumwambia kuhusu kuongea nae
alimwambia kuwa kipindi hiko ana mitihani kwahiyo aongee nae kwa kipindi
kingine. Kwahiyo karibia mwezi mzima alikuwa busy sana na masomo yake
hadi pale walipomaliza mitihani na kufunga chuo kwaajili ya kuingia mwaka
mwingine, mtu pekee aliyekuwa akiwasiliana nae mara moja moja kwa kipindi hiko
alikuwa ni Bahati tu. Erica alirudi kwao likizo ila alijiona
kuwa yupo tofauti sana na siku zote, kwanza alikuwa akichoka sana na muda mwingi
alijisikia usingizi na kujiuliza kuwa atakuwa na tatizo gani, akawaza kuwa kesho
yake aende hospitali ili akaangalie hali yake vizuri. Kesho yake
ilivyofika, kabla hajajiandaa kuondoka, walifika nyumbani dada zake wawili, dada
yake Bite akiwa ameongozana na dada yake Mage, aliwasalimia na
kuwakaribisha. “Mama yupo?” “Ametoka ameenda kwenye
kikoba” “Haya, kilichotuleta sio mama ila tuna shida na
wewe” “Shida gani?” “Erica, inabidi tukakupime
ujauzito” “Mkanipime ujauzito kwanini?” “Erica usije ukatutia
aibu, hebu nenda kajiandae huko twende hospitali, tulikuwa tunangoja tu ufunge
chuo mjinga wewe” Erica aliwashangaa sana dada zake hawa ila hakuweza
kuwabishia maana walikuwa wakimfatilia vilivyo, basi akajiandaa ili aende nao
huko hospitali, ila Mage akawakatisha “Bite, kwanini tujisumbue kwenda
mpaka hospitali wakati kuna vile vipimo vya mimba!” “Vinapatikana wapi
sasa” “Maduka yote ya madawa, nenda kanunue basi” Mage
akamuelekeza Bite kisha Bite akaondoka na kwenda kununua, kwahiyo Erica alibaki
na dada yao mkubwa Mage ambaye alimuita Erica karibu, “Mdogo wangu
kwanini umekuwa na tabia za ajabu?” “Hapana dada sina tabia za
ajabu” “Yani kweli wanaume wanakufata hadi nyumbani unasema huna tabia
za ajabu kweli?” “Sasa dada mnavyonifanyia hivi mnaona ni sahihi? Mimi
ni msichana mkubwa sasa” “Hatukatai ni mkubwa ila bado hujaolewa, upo
kwenye uangalizi wetu. Unafikiri leo na kesho ukileta matatizo hapa aibu kwa
nani? Sisi ndio tutaaibika Erica. Katika watoto wote wa mama sikufikiria kama
wewe unaweza kuwa na tabia za ajabu kiasi nilichoambiwa” “Hapana dada,
sina tabia za ajabu mimi” “Sasa mdogo wangu huwa unahangaika na nini, si
utulie tu ukimaliza chuo utaolewa” “Dada, aliyewaambia mimi nahangaika
nani? Mbona mimi ni mpole tu” Mage alitumia muda mwingi sana kumshauri
mdogo wake huyu na kumwambia kuwa kwanini wameamua kuja kumpima ujauzito maana
wamekuwa na mashaka nae halafu habari zake wamezisikia. “Mmezisikia wapi
dada?” “Jua kwamba habari zako tunazijua” Erica alijiuliza sana
kuwa wanajua habari zake zipi na wanazijua jua vipi ila hakupata
jibu. Bite alirudi na kipima mimba, kisha wakamtaka Erica kukinga mkojo
wake ambapo alifanya hivyo na wakapima pale nay eye akiwa
anaangalia, “Mungu wangu Erica una mimba? Aibu gani hii umetupa jamani
Erica?” “Nilijua tu dada, ndiomana nikakuzania tuje tumpime ujauzito,
aliyeniambia anamjua sana huyu mdogo wetu, kipindi hiki alikuwa na mitihani ila
alikuwa analala sana badala ya kujisomea, kumbe ana mimba loh!” Erica
alikuwa kimya tu akiwaza maana ni swala la aibu kweli ila hakujua afanye nini,
dada zake nao waliongea kwa ukali sana na gadhabu kubwa. “Bite mdogo
wangu twende kwanza tukajadiliane cha kufanya, tukikaa hapa na huyu mtoto
tutampasua bure” Wakaondoka na kumuacha Erica pale, muda kidogo mama yao
alirudi ila Erica hakumwambia ukweli mama yake kuwa dada zake walifika maana
aliona ni swala la aibu sana na hakujua hata ataanzia wapi kumwambia mama yao,
kwani hata yeye swala lile lilimchanganya vilivyo. Aliingia
chumbani kwake na kuwaza sana, aliwaza kuwa kama hiyo mimba itakuwa ya
nani, “Mungu wangu, mdada wa chuo kweli na sijui mimba ya nani? Si akili
mbovu hii! Je ya Erick au ya Bahati? Mungu wangu” Aliwaza sana na
kukumbuka kuwa alilala na Bahati halafu kesho yake akalala na
Erick, “Mmmh nimefanya umalaya na sasa nina mimba, hata sijui ni ya
nani. Sijui nitafanyaje?” Aliwaza sana, kisha akachukua simu yake na
kumtumia ujumbe Erick, “Nina mimba yako” Kisha akamtumia ujumbe
huo huo Bahati halafu akatulia kusikilizia kuwa yupi kati yao
atakayejibu. Muda kidogo simu yake ilianza kuita na mpigaji alikuwa ni
Bahati, hakutaka kupokea kwani hakutaka kusikika akiongelea habari za mimba kwa
mama yake, kisha Bahati aliamua kumtumia ujumbe. “Erica kweli uyasemayo?
Kama ni kweli basi nimefurahi sana, maana ndoto yangu ni wewe kuwa mke wangu na
kuwa mama wa watoto wangu, nakupenda sana Erica” Alingoja ujumbe kutoka
kwa Erick ila hakutumiwa ujumbe wa aina yoyote ule na kumfanya aumie sana moyoni
mwake kuwa kwanini Erick amemfanyia vile ilihali amemwambia kuwa ana
mimba. Muda kidogo simu yake ilianza kuita na namba ilikuwa mpya
akaipokea, “Habari, naitwa Sia. Nimeona ujumbe wako kwenye simu ya
mpenzi wangu, tafadhari achana na Erick, habari za mimba utajijua mwenyewe ila
naomba uachane na Erick. Tuache kwa amani tunapendana
sana” “Kheeee” “Usishangae, habari ndio hiyo. Erick ni mpenzi
wangu. Kama ulikuwa hujui basi ujue, Erick ana mpenzi ambaye ndio mimi. Sitaki
tena uwe karibu na Erick achana nae” Erica alikata ile simu kisha
alijikuta akilia sana, tena alilia mno kama siku ambayo alisingiziwa shuleni
kuwa amekutwa na Erick wakibusiana yani alilia sana, hakuamini kuwa angeambiwa
yale maneno na msichana wa Erick. “Kumbe Erick ana mwanamke kweli?
Alikuwa ananidanganya tu jamani! Mapenzi ni mabaya sana” Alilia mno
kwani moyoni mwake alimpenda Erick vilivyo na hata wangesema kuhusu ile mimba
kama ingekuwa ya Erick wala asingejali kitu ila kwanza hana uhakika na mimba ya
nani halafu alichoambiwa na msichana wa Erick kilimuumiza sana, alijikuta siku
hiyo akishindwa kulala kabisa na kuwa macho siku nzima. Kesho
yake walifika dada zake Erica na kumwambia mama yao kuwa wanataka kutoka na
Erica, walimwambia kuwa ajiandae kisha alipomaliza wakaondoka nae. Erica
hakuelewa ila dada zake walikuwa wakienda nae hospitali, walipofika Bite alibaki
nje kisha mage akaenda nae kwa daktari, “Huyu hapa ndiyo tuliongea
habari zake umtoe mimba” Erica akahamaki, “Kutoa
mimba!” “Ndio, tena ufunge bakuli lako hilo hakuna kupiga makelele,
ulibeba mwenyewe mimba kwenye starehe zako, hakuna atakayekubali umletee aibu
nyumbani” Basi daktari akawaelekeza chumba cha kumpeleka Yule mgonjwa,
yani Erica hakuweza kubisha chochote kwa dada zake maana akifikiria kuwa mama
yake ataambiwa ukweli ndio pale aliona uchizi kabisa. Aliingia kwenye
chumba na daktari aliingia na kumuandaa kwaajili ya kumfanyia zoezi la kumtoa
mimba, muda kidogo Yule daktari akapigiwa simu na kupokea. Erica alisikia tu
daktari alichokuwa akijibu, “Usiondoke bhana, nisubirie nje ya chumba
cha mwishoni, kuna kazi nafanya naimaliza sasa hivi usijali…….. Nitakwambia
nikitoka, ni muda mfupi tu hata nusu saa haifiki……. Mimi na wewe tena, sisi ni
kama ndugu rafiki yangu, nitakwambia bhana” Kisha daktari akakata ile
simu na kuanza kumshughulikia Erica, kwakweli maumivu aliyoyapata Erica
alijikuta akiapa kutokufanya mapenzi tena katika maisha yake, yalikuwa ni
maumivu ya muda mfupi ila yalikuwa ya hali ya juu. Daktari alivyomaliza
alimpa pole, kisha akamwambia, “Pumzika kidogo, nitamuandikia dadako
dawa za wewe kwenda kutumia pole sana” Daktari alitoka, kwakweli Erica
hakuwa na furaha kabisa kwani kile kitendo hakukitegemea na kilikuwa ni kitendo
cha ajabu kwake, akajifikiria kuwa Erick na Bahati watamfikiriaje maana
ataonekana kuwa muuwaji, akajiambia kuwa atamwambia Bahati kwamba alimdanganya
kuhusu mimba, ukweli ni hakuwa na mimba wala nini kwahiyo swala la Bahati kwake
halikuwa tatizo kabisa, akafikiria pia kuhusu Erick kwanza hata kuhusu mimba
Erick alikuwa hajui sababu ujumbe ulijibiwa na mwanamke wake kwa maana hiyo
mwanamke wake ndio alisoma ule ujumbe na lazima atakuwa ameufuta, kwahiyo hakuna
tena wa kumuhofia kati yao. Hakutaka kuendelea kupumzika zaidi mahali
hapo kwani palimfanya awaze vitu vingi sana, kwa muda huo alitaka tu kwenda
nyumbani, na kama kupumzika basi akapumzike nyumbani kwao. kwahiyo aliinuka na
kujiandaa kutoka ili awafate dada zake waondoke. Erica alitoka kwenye
kile chumba, kupiga jicho mbele yake aligongana macho na Erick akiwa amesimama
na Yule daktari, kumbe ni Erick ndiye alikuwa akiwasiliana na daktari muda ule
ndani. Erica alitoka kwenye kile chumba, kupiga jicho
mbele yake aligongana macho na Erick akiwa amesimama na Yule daktari, kumbe ni
Erick ndiye alikuwa akiwasiliana na daktari muda ule ndani. Erica
alitamani hata kurudi ndani ila hata kama akirudi Erick alishamuona, kwahiyo
akajifanya anaondoka kamavile hajamuona Erick ila aliitwa, “Erica,
Erica” Alisimama na Erick akamsogelea na kumuuliza, “Kumbe ni
wewe Erica uliyekuwa unafanya yale yasiyofaa kwenye kile chumba?” Erica
alimuangalia, na pale pale akamgeuzia kibao maana hakutaka apewe lawama kwa muda
huo, alimwambia, “Sasa kinachokushangaza ni nini?” “Umeanza lini
mchezo huo?” “Leo” “Kwanini Erica? Hujihurumiii, hujui kama watu
huwa wanakufa kwa kufanya hivyo?” “Usitake kunitibua Erick, nilikutumia
ujumbe kuwa nina mimba yako ukampa simu mwanamke wako anitukane. Halafu leo
ulitegemea nifanyeje? Huyo mtoto ningezaa nilee peke yangu? Tena achana na mimi
kabisa” Erica akaondoka na kumuacha Erick akimshangaa sana maana
alivyokuwa anaongea kana kwamba kitu alichokifanya ni sahihi wakati hakiruhusiwi
kabisa ila yeye aliongea bila hata ya mashaka. Erick alirudi kwa Yule
daktari na kuagana nae, ila muda anatoka ndio aliwaona Erica pamoja na ndugu
zake wakiondoka pia ikabidi awafate nyuma ili apajue anapoishi
Erica. Ilikuwa tofauti maana Bite alienda nao mpaka nyumbani
kwake, alitaka mdogo wake augulie hapo kwanza, kwahiyo Erick alijua pale ndio
nyumbani kwakina Erica, kisha akaondoka zake. Erica alionekana
kutokupakubali kabisa kwa dada yake, “Hapana dada, mngenirudisha
nyumbani tu” “Hapana, nyumbani nitakupeleka kesho kutwa, uugulie hapa
kwangu” “Hapana dada, nawaomba nirudi nyumbani” “Erica usiwe
mbishi, unajua haupo sawa na mama hajui ni sisi tu tunaojua, keshokutwa
nitakupeleka nyumbani ubaya uko wapi?” Erica alikubali kukaa kwa dada
yake kwa muda ila kwa shingo upande kwani hakupenda kabisa kukaa hapo kutokana
na vile alivyotaka kufanyiwa na shemeji yake, yani aliamua kukaa kwa machale
sana. Kesho yake Erica aliwasiliana na Bahati na kumuomba
amtumie hela kwenye simu yake, “Nitakutumia shilingi ngapi Erica? Simu
yangu haina hela ya kutosha” “Nitumie yoyote tu” “Kwani uko wapi
kwasasa” “Nipo huku kwa dada na nina shida na hela” Basi
akatumiwa shilingi elfu tano na Bahati, kisha akatoka nje na kumuaga dada yake
kuwa anaenda dukani kununua vocha, “Niagize mdogo wangu nitaenda
kukununulia” “Hapana dada, dukani hapo tu acha niende
mwenyewe” Basi Erica aliondoka, na moja kwa moja alienda kutoa ile elfu
tano na kufanya nauli ya kurudi kwao. Mama yake alishangaa sana
alipomuona, “Vipi mbona hujarudi na dada yako wakati yeye kasema utarudi
naye?” “Mama, sitaki kukaa kwa dada. Nimemtoroka tu” “Kwanini
umefanya hivyo?” “Mama, nimekumiss sana mama yangu hata sitaki kukaa
mbali na wewe ndiomana nimemtoroka maana ningemuaga aisngekubali
niondoke” Muda kidogo mama yake alipigiwa simu na Bite akimwambia kuwa
Erica haonekani, “Yani ndio kafika huku muda huu huu” Kisha mama
akampa simu Erica aongee na dada yake, “Hivi wewe Erica una matatizo
gani? Mfano ungeniaga ungepungukiwa na nini? Kwanini unapenda kufanya mambo ya
kijinga lakini” “Nisamehe dada” “Kiukweli unakera yani unakera
sana” Dada yake akakata simu, kisha Erica akaelekea chumbani, alikaa na
kulia kwanza maana tayari alifanya kitendo ambacho hakutarajia kukifanya katika
maisha yake, tayari alikuwa ametoa mimba, roho ilimuuma sana. “Labda
mtoto wangu ndio alikuwa huyo huyo, Mungu wangu jamani. Hivi familia zingine
zikoje hizi? Eti nitawatia aibu, hivi ni aibu yangu au aibu zao? Yani mdada
mkubwa wa chuo bado nachungwa kiasi hiki kweli?” Alilia sana, hakuwa na
raha hata kidogo, aliamua kulala tu. Erica hakuwa na hamu hata
na simu yake kwani hakutaka kuwasiliana na yeyote Yule, akaiweka mbali naye
kabisa akajikuta akipiga mahesabu tu ya wanaume aliotembea
nao, “Nilimpata Babuu, tulipendana sana tena sana ila Babuu kaishia
kidato cha nne na kazi zake ni za kubangaiza, nikaachana nae na kuangukia kwa
George, kweli kabisa kwa sifa za George ni msichana gani ambaye mahusiano yake
hayaeleweki atamkataa George? Aliahidi kunioa na alionyesha kunipenda sana kumbe
nae hamna kitu, sasa huyu niliyekutana nae ufukweni ndio balaa, anajitia hadi
kulia kwasababu yangu ila hali yake ya maisha ni ngumu sana. Nikaamua kumkubali
Erick ambaye ni mwanaume wa maisha yangu ila kumbe ana wanawake kibao. Hivi
mapenzi ni nini? Mbona yananitenda hivi jamani? Sitaki kuwasiliana na yeyote
kati yao, bora hata Babuu ila sidhani kama atanipenda tena” Alikuwa na
mawazo sana na kuamua kulala tena hadi kunakucha. Siku hiyo siku nzima
alijishughulisha na kazi za nyumbani hata simu hakutaka kushika tena ingawa
alijua atakapoichukua atakutana na simu za kutosha toka kwa Bahati ila hakujali
kwa muda huo . Kwenye mida ya saa mbili usiku ndipo alichukua
simu yake kuona waliompigia, ila alikuta waliompigia sana ni wawili tu yani
Bahati na Erick, kwa mara ya kwanza alikuta Erick amempigia simu zaidi ya mara
tatu ingawa sio kawaida yake, anayepigaga simu hovyo ni
Bahati. Akakutana na ujumbe wa Bahati kwanza, “Erica
ulichonifanyia sikutegemea kabisa, nimekuja kukuona kwa dada yako kumbe alikuja
na Yule bwanako mwenye gari! Erica umefanya nipigane sana na Yule jamaa, na
kasema kuwa umetoa mimba, Erica umetoa mimba yangu kweli? Nalia tu mimi, jamani
mwanangu wa kwanza umemuua Erica” Ni pale alipogundua kuwa Bahati
kakutana uso kwa uso na Erick nyumbani kwa dadake ila alijiuliza kuwa Erick
alipafahamu vipi pale hakuwa na jibu, akashuka chini na kukutana na ujumbe wa
Erick, “Erica unajua wazi ni kwajinsi gani nakupenda, wewe msichana
umekuwa fimbo kwangu ya kuumiza moyo wangu kila kukicha. Uliniumiza kipindi kile
nikajua sababu ya utoto, umefanya niwe na tabia za ajabu sana kwa kukukosa, na
muda nakupata kumbe ndio umekuwa hufai kabisa, Erica wa kunidanganya mimi huna
mwanaume kumbe unaye? Wa kwenda kutoa mimba yangu Erica kweli? Na mimba yenyewe
umemdanganya na jamaa kuwa ni yake. Kwakweli Erica umeniumiza sana, sikutegemea
kama kuna mwanamke wa kuniumiza kiasi ambacho umeniumiza Erica. Niliwahi
kukwambia kuwa sitoacha kukupenda, na kweli sitoacha kukupenda Erica.
Kwaheri” Ule ujumbe ulipasua moyo wa Erica, na ulionekana kutumwa jana
yake, yani kwa muda huo hata hakuelewa kuwa ni kitu gani afanye, alichukua simu
yake na kuanza kumpigia Erick ila ile simu haikupokelewa, akaamua kuandika
ujumbe, “Tafadhali pokea simu yangu Erick” Ujumbe haukujibiwa
pia, na kumfanya Erica kupatwa na mawazo yasiyokuwa na mwisho. Siku hiyo
hakuweza kulala kabisa na aliona kuwa usiku ni mrefu sana, alijitoa muhanga kuwa
kesho akamtafute Tumaini ili amuelekeze alipo Erick akaongee nae, “Kumbe
Erick ananipenda kweli? Mungu wangu jamani, nitafanyaje mimi Erica
jamani” Muda huo Bahati nae alikuwa akimpigia simu ila zile simu za
Bahati alihisi zikimpigia kelele tu kwani kwa muda huo alitaka kuona simu ya
Erick tu. Saa kumi na mbili asubuhi akaanza tena kumpigia simu Erick ila
haikupokelewa simu yake, akaamua kumtumia tena ujumbe, “Erick nakuomba
pokea simu yangu usikie ninachotaka kusema” Baada kama ya lisaa limoja
ujumbe ule ulijibiwa, “Useme nini kwangu? Ni kipi cha kuniambia Erica
ambacho sikijui? Leo saa nne asubuhi naondoka na baba kwenda Afrika kusini,
haikuwa safari ya kwenda mimi ila nimemuomba baba kwenda nae, nahitaji kutuliza
akili yangu kwanza. Kama unataka kuongea na mimi njoo uwanja wa ndege kabla ya
hiyo saa nne uniage, kwaheri” Erica alihisi kuchanganyikiwa kabisa,
akaenda bafuni kuoga kisha akajiandaa kwaajili ya kuondoka ili akamuwahi
Erick. Wakati anatoka, mama yake akamuuliza, “Unaenda wapi
asubuhi asubuhi hii Erica?” Akawa anajiuma uma maana hakufikiria kama
kuna maneno ya kumdanganya mama yake kwa muda huo, “Mbona unajiuma uma,
hebu kaa pale tuzungumze kwanza” Yani Erica alitamani hata kumtukana
mama yake maana hiyo ilikuwa saa mbili asubuhi nay eye alikuwa anataka awahi,
ila atafanyaje sasa lazima amsikilize mama yake, “Erica mwanangu ni siku
nyingi sijakaa kuzungumza na wewe? Unaendeleaje kwanza?” “Naendelea
vizuri, ila mama si tuzungumze wakati nikirudi” “Erica utanipangiaje
muda wa kuzungumza na wewe lakini? Ujue mimi ni mama yako!” Ilibidi
Erica awe mpole na kumsikiliza mama yake ila kiukweli alikuwa akikereka tu na
mabayo mama yake alimwambia kuhusu maisha maana alitaka kuondoka na mama yake
alimkawiza hadi saa tatu na robo ndio akampa ruhusa ya kuondoka. Erica
alikata tamaa ya kuonana na Erick ila bado alienda uwanja wa
ndege. Alifika uwanja wa ndege kwenye saa nne na nusu, yani
hakuwa na furaha kabisa, wakati anasonga pale uwanjani akiwa na mawazo
akagongana na mtu, alimuangalia na kumuomba msamaha, “Uwe makini binti,
mtoto mdogo hivyo unawaza nini?” Erica alimuangalia vizuri sasa huyu mtu
alikuwa ni mkaka wa kishombeshombe, Erica alikuwa kama akimshangaa hivi, Yule
mkaka aliamua kujitambulisha, “Naitwa Rahim, sijui mwenzangu unaitwa
nani?” “Naitwa Erica” “Mbona unaonekana kuwa na mawazo
sana?” Erica alikuwa kimya tu akimtazama, Yule mkaka alimwambia
Erica, “Anyway, chukua kadi yangu hii tutawasiliana” Erica
akachukua ile kadi na kuiweka kwenye pochi yake, kisha akaendelea na safari yake
halafu Yule mkaka nae akaondoka zake. Aliposogea mbele alishikwa bega,
alipogeuka tu alikutana na Tumaini, “Kheee Erica unafanya nini tena
huku?” Erica alijiuma uma, alitamani kumwambia ukweli ila alihofia
ikabidi amrudishie swali yeye, “Na wewe unafanya nini huku
dada?” “Mimi nimekuja kumsindikiza mdogo wangu Erick na baba wanaenda
South” “Kumbe mdogo wako kasafiri?” “Ndio, yani mdogo wangu hadi
namuhurumia” “Kwanini?” “Ngoja tukae mahali
nikusimulie” Wakaondoka mahali hapo na kutafuta sehemu yenye mgahawa na
kukaa kisha kuagiza vinywaji na kuendelea na maongezi, ila kabla hawajaongea
kitu chochote simu ya Tumaini iliita na Tumaini aliipokea, “Tutaongea
badae, saivi kuna sehemu nipo mara moja” Alivyokata akamuangalia Erica
na kumwambia, “Yani huyu msichana king’ang’anizi
huyo?” “Msichana gani?” “Si Yule Sia nilikwambiaga kuwa ni
mchumba wa Erick” “Kafanyaje tena?” “Huyu msichana hajielewi
hata sijui kwanini anamng’ang’ania hivyo mdogo wangu wakati mdogo wangu mwenyewe
yupo kama kachanganyikiwa. Bora aende zake huko labda ajipatie hata
mzungu” Erica akatabasamu kidogo ila kiukweli alikuwa anaumia moyo,
akamwambia tena Tumaini, “Eeeh nieleze sasa” “Sikia nikwambia,
mdogo wangu Yule Erick kuna kipindi alikuwa akiishi na mamake mdogo na kuna
shule moja alipelekwa mgeni tu halafu akafanya madudu na kufukuzwa, nilimuuliza
mdogo wangu kwanini alifukuzwa shule akasema ni sababu ya msichana Fulani
hajawahi kunitajia jina la huyo msichana ila alisema kuwa alimtongoza huyo
msichana halafu huyo msichana akamsemea kwa walimu, kitendo kilichofanya Erick
achukiwe na kufukuzwa shule ingawa mamake mdogo aliomba sana Erick asamehewe.
Nilimuuliza kuwa ni kweli alimpenda huyo msichana huwa ananijibu hadi leo
anampenda sana. Unajua sisi wanawake mara nyingine tunasababisha wanaume kuwa na
tabia za ajabu ajabu, yani mdogo wangu Erick kawa mlevi, unajua anakunywa Yule
balaa, kawa mtu wa wanawake lakini chanzo chote ni huyo dada” “Kheee
jamani masikini yake, je unatamani kumjua huyo mdada?” “Sitaki hata
kumjua maana nitamuumiza nikimjua, kaumiza sana maisha ya mdogo wangu, hili
nililosikia sasa ndio balaa” “Lipi hilo?” “Nasikia Erick
alikutana tena na huyo mdada na mdada akadai kuwa ana mimba yake, ila Erick
kamshuhudia kwa macho yake Yule mdada akitoka kwa dokta kutoa mimba yake, yani
katoa mimba ya mdogo wangu kumbe Yule mdada ana mwanaume mwingine. Juzi mdogo
wangu kapigana na huyo mwanaume balaa, jamani mdogo wangu hajawahi kupigania
mapenzi ndio mara yake ya kwanza. Huyo dada ni shetani
kwakweli” “Inasikitisha lakini” “Kwakweli inasikitisha sana,
yani mimi sipendi mwanamke anayetoa mimba simpendi kabisa. Unajua kutoa mimba ni
uuwaji! Hivi sisi tungetolewa na wazazi wetu, tungekuwepo leo? Ila mwanamke
muuwaji hana hata huruma anatoa mimba kwakweli, nawachukia watoa mimba. Huyo
msichana nikimjua nitamraruwa kwakweli” Erica hakuwa hata na usemi kwani
muhusika alikuwa ni yeye tena ilionyesha Tumaini akiongea kwa uchungu sana jinsi
gani alivyo na hasira na huyo msichana ambaye ndio yeye, “Nimemwambia
mdogo wangu, huyo msichana hakupendi labda anapenda pesa ulizonazo tu lakini
upendo hana. Hivi Yule msichana anajiona kutoa mimba ndio kashinda, anadhani
anabaki kuwa binti loh! Hapana hajui tu, anakuwa mama wa marehemu na sio binti
tena” Erica alinyamaza kwani yale maneno yalimgusa vilivyo, na kuuliza
tena “Kwahiyo mdogo wako atarudi lini?” “Si oleo wala kesho,
kwanza hakutakiwa kusafiri ila kwa hali aliyokuwa nayo, baba ameona bora aende
nae. Halafu sasa mpaka tupo nae airport bado anajipa imani kuwa huyo msichana
atakuja kuongea nae, cha kushangaza hadi wameingia ndani hakuna huyo msichana
kuja wala nini. Mdogo wangu anatia huruma kwakweli, ila Erica huku airport
ulifata nini?” “Aaah dada alinipa mzigo kuna mfanyakazi wa hapa nilikuwa
nimempelekea, na nimefika muda sana sema nimechelewa tu kuondoka, ningejua mpo
hapa hata ningewatafuta. Namuonea huruma mdogo wako, mpe pole
sana” “Yani kuna wakati natamani kumjua huyo mama marehemu na
atanitambua kwakweli, atanieleza sababu za kumuumiza moyo kaka yangu na sababu
za kumuua aunt yangu” Erica aliamua kuagana na Tumaini huku akidai kuwa
anatakiwa kurudi kwao mapema ila ukweli ni kwamba maneno ya Tumaini yalimuingia
vilivyo na moyo kumuuma sana. Ila Tumaini alimwambia kuwa anahitaji
waende wote nyumbani kwao ili akapafahamu anapoishi Erica, hakubisha juu ya hilo
na kuamua kuondoka nae. Walifika nyumbani kwao, kupiga jicho
getini alimuona kuna kijana amekaa chini, aliposogea akagundua kuwa ni Bahati,
kwakweli Erica alitamani kurudi na Tumaini walipotoka ila kabla hajafanya
chochote Bahati aliinua kichwa chake na alipomuona kuwa ni Erica aliinuka na
kwenda kumkumbatia huku akilia, ikabidi Erica amuulize, “Sasa unalilia
nini?” “Nalilia kiumbe changu Erica, namlilia mwanangu” Erica
aligeuka na kumtazama Tumaini kama naye anayasikia yale maneno anayoyasema
Bahati. Walifika nyumbani kwao, kupiga jicho getini
alimuona kuna kijana amekaa chini, aliposogea akagundua kuwa ni Bahati, kwakweli
Erica alitamani kurudi na Tumaini walipotoka ila kabla hajafanya chochote Bahati
aliinua kichwa chake na alipomuona kuwa ni Erica aliinuka na kwenda kumkumbatia
huku akilia, ikabidi Erica amuulize, “Sasa unalilia
nini?” “Nalilia kiumbe changu Erica, namlilia mwanangu” Erica
aligeuka na kumtazama Tumaini kama naye anayasikia yale maneno anayoyasema
Bahati. Akamuona Tumaini akimuangalia pia, kwahiyo alijua moja kwa moja
Tumaini amesikia kile kilichokuwa kikiongelewa na Bahati, kwahiyo alijishauri
pale pale na halmashauri ya kichwa chake na kumsukuma Bahati
pembeni, “Erica unanifanyia hivi Erica?” “Una matatizo gani
wewe? Nishakwambia usinizoee” Kisha akamuangalia Tumaini na kumshika
mkono, “Dada twende ndani” Aliingia getini na Tumaini na
kumuacha Bahati pale nje, Tumaini alikuwa na maswali mengi sana juu ya Erica
kwanini kamfanyia kaka wa watu vile, kwahiyo akamuuliza, “Erica, kwanini
lakini umemfanyia vile” “Nitakuhadithia ndani, ni chizi
Yule” Basi waliingia sebleni, kisha Erica akaenda chumbani kwa madai
kuwa anaenda kuweka mkoba ila kiukweli alienda kumpigia simu Bahati maana kwa
vyovyote vile Bahati asingeondoka pale kwao na angezidi kumsababishia matatizo,
alipiga simu na Bahati alipokea, “Samahani mpenzi wangu kwa
nilichokufanyia nisamehe bure” “Ila kwanini umenifanyia hivi
Erica?” “Nitakusimulia vizuri ila kwasasa naomba uondoke, unajua yule ni
dada yangu na sikutaka ajue mahusiano yetu. Wakati ukifika watajua tu ila sio
kwasasa, nakuomba mpenzi wangu niokoe mwenzio maana na mama nae akikukuta hapo
ni balaa” “Sawa, basi badae nitakupigia tuongee. Nakupenda
Erica” “Usijali, nakupenda pia” Ilibidi ampe maneno ya
kumlainisha ili iwe rahisi kumuondoa pale kwao maana angemuharibia sifa yake kwa
Tumaini. Kisha akarudi kwa Tumaini, ambapo Tumaini alitaka
haswaa kujua kuhusu Yule mkaka pale nje, “Iko hivi, Yule mkaka alikuwa
na mke wake anayeitwa Erica. Sasa inasemekana mkewe alikimbia na watoto kwahiyo
Yule mkaka kama kaathirika kisaikolojia, yani yeye kila mdada anayeitwa Erica
anadhani kuwa ni Yule mkewe basi ndio shida yake mara ukutane nae aanze kulia
sijui leta mwanangu sijui nini na nini, ananikera balaa” “Duh! Pole,
sasa kama ndio hivyo atakuharibia sana ukija kupata mchumba” “Kweli
ataniharibia” “Erica, sijawahi kukuuliza. Hivi una mchumba mdogo
wangu?” “Hapana dada” “Kwanini?” “Nayaogopa mapenzi,
wanaume hawaaminiki” “Ila wapo wenye mapenzi ya kweli, sema ni vigumu
kuwatambua. Ila unaweza kwa mara ya kwanza usimpende mwanaume ila ukimkubali
unaanza kumpenda taratibu, wenye mapenzi ya kweli wapo Erica” “Basi
nasubiria hao wenye mapenzi ya kweli, mmoja wapo anipende mimi” Tumaini
akatabasamu tu na kuanza kumuuliza Erica kuwa pale anaishi na
nani, “Hapa naishi na mama tu, hizo nyumba mbili hapo nje wanaishi
wapangaji wetu. Mimi na mama tuna funguo kwahiyo asiponikuta atafungua na
nisipomkuta nitafungua na kuingia ndani” “Aaah sawa” Simu ya
Tumaini ikaanza kuita, akaichukua na kuingalia kisha akasema, “Aaah ni
Sia tena, huyu nae loh” Akapokea na kuanza kuongea nae, Erica alitulia
kimya akisubiri amalize kuongea halafu amuulize kuwa kuna nini tena kwa huyo
Sia. Tumaini alipomaliza tu kuongea Erica alimuuliza, “Kwani huyo Sia
anataka nini?” “Yani huyu Sia ananichekesha tu hadi nakereka na mashtaka
yake, mwanaume mwenyewe kashaondoka sijui anafikiri huo msamaha nitamuombea
wapi” “Kafanyaje kwani?” “Nasikia Yule mama marehemu wa Erick
alituma sms kuwa ana mimba ya Erick halafu Sia akaifuta ile sms sijui na kuongea
nae huyo mama marehemu, nasikia huyo mdada alishtaki kwa Erick basi ndio Erick
kamchukia Sia na hata hii kuondoka hajamuaga” “Kheeee!!” “Ndio
hivyo, wasichana wengine jamani. Ila mimi ningekuwa Erick ningempenda sana Sia,
ana mapenzi ya dhati Yule dada ila sio huyo mama marehemu wake yani na nikimjua
huyo mama marehemu jamani atanikoma” “Inaonyesha Erick alimpenda sana
huyo mdada” “Ndio alimpenda sana ila msichana mwenyewe hapendeki, kwanza
sio msichana ni mama marehemu. Yani simfahamu huyo mdada ila namchukia balaa,
maisha yangu yote nitamchukia ni kivuruge Yule kaivuruga akili ya mdogo
wangu” Erica alipumua kwanza sababu laiti kama Tumaini angejua kuwa
anayemsimulia ndio muhusika mwenyewe sijui angefanyaje ila
hakuelewa. Mama yake alirudi na alimtambulisha Tumaini kwa mama yake
kisha Tumaini akaaga na kuondoka zake. Erica alienda chumbani
kwake ila alihisi akili yake yote ikivurugika kwani alijikuta akifikiria sana
kuhusu Erick, akakumbuka toka siku ya kwanza ambayo Erick alifika shuleni kwao,
akakumbuka jinsi Erick alivyomtongoza na jinsi walivyofukuzwa shule, akakumbuka
jinsi alivyokutana nae tena na vile ilivyokuwa, aliumia sana
moyoni, “Kumbe ilikuwa ni kweli Erick ananipenda, nimempoteza Erick
wangu mimi. Hivi na Tumaini akija kujua kuwa mwanamke mwenyewe ndio mimi? Mungu
wangu, ila sijatoa mimba kwa kupenda, ni nani atakayeniamini kuwa sikutoa mimba
kwa kupenda? Erick ndio anafaa kuwa na mimi na si mwingine yoyote, roho inaniuma
mimi, nitampata wapi tena Erick jamani?” Aliwaza sana na kumwambia
ukweli Tumaini hakuweza kuwa labda aombe namba za Erick atakazokuwa anatumia
kule alipo , hakuweza chochote alibaki akilia tu na moyo wake na kuzidi kutokuwa
na raha wala furaha, kwa wakati huo hakuna aliyekuwa anaumiza akili yake zaidi
ya Erick tu. Aliamua kulala tu maana akili yake ilikuwa imevurugwa
haswaaa. Kesho yake akiwa anapangapanga vitu kwenye mkoba wake, akaona
kadi alipo iangalia ilikuwa ya Rahim, “Aaah Yule mkaka wa jana uwanja wa
ndege, mmmh sijui nimpigie? Hapana kwakweli nitaingia kwenye majaribu mengine
bure, mkaka mwenyewe mzuri vile na hivi nina mawazo ya Erick nisije kujikuta
majaribuni bora niache tu” Akaichukua ile kadi na kwenda kuitupa nje
kwani hakutaka kujiingiza kwenye majaribu mengine maana aliona aliyo nayo yana
mtosha. Baada ya kuitupa alijishangaa akikaa hivi sura ya Yule mkaka
ikimjia akilini, “Shindwa shetani, sitaki mawazo ya kijinga mie, niliyo
nayo yananitosha” Akatoka tena nje na kuitafuta ile kadi kwenye
matakataka kisha akaenda kuichoma moto kabisa ili asishawishike kumtafuta Rahim
kabisa maana aliona kama ipo kwenye matakataka kuna muda atajisahau na kuichukua
tena kwahiyo akaona ni vyema kuichoma moto kabisa, kisha akarudi ndani na
kuendelea na kazi zake zingine. Zilipita kama siku mbili huku
Bahati akimuomba muda wa kuzungumza nae, alimuomba sana ikabidi Erica akubali
kwenda kuongea na Bahti, walienda ufukweni kwaajili ya maongezi kwani Bahati
alitaka kujua kuhusu mimba. Alivyofika alimkuta Bahati ameshafika muda tu
kwahiyo alikaa na kuanza maongezi nae, “Niambie ukweli Erica, ulitoa
mimba yangu” “Bahati, hivi ni nani aliyekupa hizo habari unajua
unanishangaza” “Nilikutana na Yule mwanaume wako mwenye gari, nikaanza
kugombana nae ndio akasema umetoa mimba yake, nikamwambia ni yangu basi ndio
ugomvi wetu ulikuwa hapo” “Una uthibitisho gani kuwa mimi nilikuwa na
mimba na una uthibitisho gani kuwa mimi nilitoa mimba” “Sina uthibitisho
zaidi ya ujumbe ulionitumia kuwa nina mimba” “Nikikwambia kuwa ule
ujumbe nilituma kukupima imani yako utaniamini?” “Kunipima
imani?” “Ndio, nilitaka kujua kama unanipenda kweli. Wanaume wengi
wanaposikia wanawake zao wana mimba huwakimbia ndiomana nilitaka kujua na wewe
utafanyaje” “Kwahiyo si kweli kwamba ulikuwa na
mimba?” “Sijawahi kuwa na mimba Bahati” “Na si kweli kama
umetoa?” “Nitatoaje mimba ambayo sijawahi kuwa nayo, hata nakushangaa
kwakweli. Huyo mkaka atakuwa na yake tu, sijawahi kuwa ni mimba mimi na sijawahi
kutoa mimba mimi” “Erica unaniambia ukweli?” “Ndio, kwanini
nikudanganye sasa?” Bahati alimuangalia Erica ila kwavile alikuwa
anampenda sana ikabidi amkubalie kwa chochote alichokisema wala hakuweza
kumpinga. “Kaninunulie juisi basi, kweli unanikalisha hapa tunaongea tu
bila hata kinywaji?” Bahati akaona ni kweli, kwahiyo akainuka ili
akamnunulie juisi, muda huo Erica nae akainuka na kuanza kutembea tembea
pembezoni mwa maji, alijisemea mwenyewe, “Mwanaume kununua juisi tu
anapata mawazo, je kulea mtoto ataweza huyo! Yani hapa nimebugi, nimebugi kabisa
sijui nifanyeje kumuepuka mtu huyu na kaniganda kama ruba” Wakati
anajisemesha aligongana na mtu mbele yake, kumuangalia ni Yule mkaka aliyekutana
nae uwanja wa ndege Rahim, na huyu mkaka alimkumbuka vizuri sana Erica, kwani
alimuita kwa taratibu, “Erica” “Samahani” “Usijali,
inaonyesha mar azote unakuwa na mawazo sana. Na mbona
haukunitafuta?” Erica alikuwa akijiuma uma tu kwa maelezo, Yule mkaka
akatoa kadi yake nyingine ya namba na kumpa Erica, “Naomba unitafute,
nina kitu muhimu sana cha kukwambia wewe. Au huna vocha?” “Hapana
ninayo” Yule kaka alitoa elfu ishirini mfukoni mwake na kumkabidhi
Erica, “Tafadhali pokea, weka vocha unipigie” Erica alichukua
ile hela na kuiweka mfukoni, kisha akaondoka zake na kurudi alipokaa, akamkuta
Bahati amechukia sana, “Mbona umechukia hivyo?” “Yule ulikuwa
unaongea nae pale ni nani?” “Mmmh jamani Bahati ndio uchukie hivyo
kweli?” “Ndio, ni nani Yule?” “Alikuwa ananiuliza tu mazingira
ya huku hayajui vizuri” “Anakuuliza hajui kama wewe ni mke wa
mtu” “Mmmh ushaanza na wivu wako, hebu tuondoke” Bahati
alionekana wazi kuchukizwa na kile kitendo cha Erica kuzungumza na Yule mkaka,
kwahiyo Erica aling’ang’ania kuondoka na ikawa bora kwao kuondoka tu kwa muda
huo. Erica alifika tena nyumbani kwao na kuchukua kile kikadi chenye
namba ya Rahim, akataka ampigie ila moyo wake ukasita akaamua kwenda tena nje
kukichoma moto akiogopa kuingia mtegoni. Erica alijaribu kumuweka Bahati
moyoni ila ilikuwa ngumu sana kwake kwani upendo wake ulikuwa kwa Erick tu na
kitu hiko kilisumbua sana akili yake, akajikuta akitamani sana kuwasiliana na
Erick. Siku hiyo aliamua kwenda kumtembelea Tumaini ila lengo
lake lilikuwa ni kuweza kuongea nae apate namba ya Erick yani alitaka ajaribu
kutumia maneno ya ujanja apewe namba ya Erick kwani hakutaka Tumaini ajue ukweli
kuwa kivuruge ndio yeye. Alifika kwa Tumaini na kusalimiana nae, ila
kabla hajaanza nae maongezi mengine Tumaini alipata ugeni, na mgeni huyo alikuwa
mdada ambapo Tumaini akamtambulisha Erica, “Erica, huyu ni wifi yangu
mchumba wa Erick anaitwa Sia. Sia, huyu ni mdogo wangu pia anaitwa
Erica” Basi Erica akasalimiana na Yule Sia ila alishangaa sana kwani
yeye alihisi kuwa labda Sian i mdada asiyevutia, alishangaa kumuona Sian i
msichana mrembo sana tena anavutia hata akashangaa inakuwaje na yeye
anasumbulkiwa na penzi la Erick wakati anaweza akamuacha na kupendwa na mkaka
mwingine. Sia alionekana kuwa na maongezi binafsi na Tumaini ila Tumaini
aligoma kwenda pembeni, “Sia, ongea tu hapa hapa
nakusikiliza” “Mmmh wifi jamani!” “Ndio, mi nina mambo yangu
hapa, wewe ongea tu” “Umewasiliana na Erick?” “Hapana, vipi wewe
umewasiliana nae?” “Ndio, nilimpigia simu ila inaonyesha alikuwa amelewa
sana” “Ila kulewa si ndio kawaida yake” “Dada nisaidie, nampenda
Erick ujue, yani nampenda sana. Kiukweli hataki hata kuongea na mimi,
nimembahatisha tu na anasema alijua ni mtu mwingine hakujua ni mimi. Akaanza
kulalamika kuwa namba nimepewa na nani, na kusema hapokei tena simu yangu. Dada
nampenda sana Erick” “Sasa Sia, mimi nitakusaidiaje hapo wifi yangu?
Maana hata mimi mwenyewe namuonea huruma sana mdogo wangu” “Dada, nina
wazo” “Wazo gani?” “Ongea na Erick akuelekeze anapoishi huyo
msichana tumtafute, maana nahisi huyo msichana kuna kitu amemfanyia Erick sio
bure” “Umesema jambo la msingi, sasa tukishampata tutafanya nae
nini?” “Tukishampata najua cha kumfanya wifi, mi nataka Erick arudi
kwenye akili sawa na mwanzo. Yani sijui kwanini alikutana tena na huyo
shetani” “Sasa nawaza, hivi Erick atakubali kweli kututajia jina au
anapoishi huyo mdada? Atakubali kweli Erick?” “Hapo pagumu wifi, ila
tukimfahamu tu mchezo umeisha” Erica akaona sasa yupo hatarini ila
akayatumia maongezi yale kama nafasi ya yeye kupata namba ya Erick, akatumia
uongo wa kuwashawishi ili apewe yeye namba ya Erick, “Dada nina
wazo” “Wazo gani tena Erica” “Nipe namba za Erick, niwasiliane
nae najua hajanizoea kivile ila nitajaribu kuongea nae hadi anitajie huyo
mwanamke, nitamwambia kuwa sitakwambia wewe wala nini ila nitamdanganya mpaka
atanitajia” “Mmmh Erica utaweza kweli? Unajua humjui Erick vizuri eeh
tena akijua ni mtu usiyemjua atakuzimia na simu kabisa” “Sidhani kama
anaweza fanya hivyo” Sia nae akaunga mkono hoja ya Erica, laiti kama
angejua ndio mke mwenzio yani asingekubali kabisa. “Wifi nadhani ungempa
tu huwezi jua akamtajia labda, tujaribu tu maana Erick hashikiki
kwasasa” Basi Tumaini akamtajia namba Erica halafu wakaendelea kupanga
mipango yao ya kufanya akipatikana huyo kivuruge. Erica alirudi
kwao akiwa na mawazo sana kuwa laity wakijua kuwa mtu wanayemtafuta yupo karibu
yao itakuwaje, yani alihisi kudata kabisa. Alivyofika tu alianza kupiga
ile namba ila iliita bila ya kupokelewa na kujiambia kuwa ataendelea kuipiga
kesho yake, ila muda kidogo alipigiwa simu na namba mpya, “Hallow Erica,
mimi ni mrs.Peter sijui unanikumbuka?” “Nakukumbuka ndio,
shikamoo” “Marahaba mwanangu, umenitupa sana, naomba uje unisalimie
jamani” “Nitakuja mama” “Naomba uje kesho, nakuomba
Erica” Basi Erica akaongea na Yule mama na kukubaliana nae kuwa kesho
yake ataenda kumsalimia. Kesho yake ilivyofika alijiandaa na kwenda
kumsalimia Yule mama, alifika hadi kwa Yule mama na kukaribishwa na Yule mama
hadi ndani, tena alionyesha kuwa na furaha sana. “Erica jamani,
nilikukumbuka sana. Mbona ulinitupa hivyo?” “Nisamehe bure mama
yangu” “Haya nimekusamehe, mwanangu wa kwanza karudi toka uingereza,
yani nimetafuta namba yako hatimaye jana nikaipata. Nataka nikutambulishe
umjue” Basi Yule mama aliinuka na kwenda kumuita mwanae, Erica alikuwa
ametulia tu pale sebleni na hakuwa na wazo lolote lile. Yule mama
alifika na mwanae, Erica akainua macho yake kumtazama mtoto wa Yule mama,
alikuwa ni Rahim Yule ambaye amekuwa akichoma kadi ya mawasiliano
nae. Yule mama alifika na mwanae, Erica
akainua macho yake kumtazama mtoto wa Yule mama, alikuwa ni Rahim Yule ambaye
amekuwa akichoma kadi ya mawasiliano nae. Erica alikuwa ameduwaa tu,
hadi Yule mama akamshtua, “Erica mwanangu jamani una mawazo gani? Huyu
ni mwanangu anaitwa Rahim” “Nashukuru kumfahamu” “Rahim, huyu ni
mwanangu pia anaitwa Erica” Basi Erica na Rahim wakapeana mikono ya
kusalimiana kamavile hawajawahi kuonana sehemu yoyote. Baada ya salamu,
Rahim aliondoka na kurudi chumbani kwahiyo pale alibaki Erica na Yule
mama, “Huyu ni mwanangu wa kwanza” “Aaah ila mbona yeye kama
mpemba mpemba hivi?” “Hahaha Erica, safari ya ujana ina mambo mengi
sana. Baba yake na Rahim ni mpemba kweli ila sikuweza kuoana nae sababu kwao
hawakutaka aoe mwanamke ambaye sio sawa na wao, ila nashukuru alimuhudumia mtoto
vizuri kabisa na mpaka kawa mkubwa hivyo” “Na mwanao mwingine ni mpemba
pia?” “Hapana, yeye nilizaa na mwanaume mwingine ila sikuolewa nae kwani
alikuwa ni mume wa mtu halafu mimi nilizaa nae bila kujua. Mwanangu, unatakiwa
kujua sana hawa wanaume kabla hujajiingiza kwenye mapenzi” “Asante kwa
ushauri, ila umepata bahati ya kuolewa tena” “Nimepata bahati kweli
maana aliyenioa sijazaa nae kabisa ila ana upendo na mimi. Sikia mwanangu
nikwambie, linda sana ujana wako. Wewe ni binti wa kike, mzuri, mpole unaonyesha
ni mtulivu. Tulia hivyo hivyo mpaka pale utakapopata anayekufaa katika maisha
yako, msichana unapozaa mtoto wa kwanza kama bado hujaolewa jua kwamba
unajipunguzia nafasi za kuolewa na mwanaume umtakaye. Maana ukiwa hujazaa bado
una nafasi kubwa sana ya kuolewa tofauti na ukizaa, ukija kuzaa mtoto wa pili
nyumbani, thamani yako inashuka zaidi, watatu na kuendelea utajikuta kuolewa
inakuwa ni ndoto kwako au unaolewa na mwanaume usiyemtaka sababu tu amesema
atakuvumilia. Inatakiwa uwe makini sana, wanaume waaminifu wapo na wachezeaji
wapo” Maneno haya yalimuingia akilini Erica, wakaongea ongea na huyu
mama kisha Erica akamuaga huyu mama kuwa anaondoka ila huyu mama akamuita mwanae
Rahim kuwa ampeleke Erica kwao, “Rahim, hakikisha unamfikisha kwao
kabisa” “Sawa mama, hakuna tatizo” Basi Erica akaondoka na Rahim
kwa kutumia gari ya Rahim. Walipokuwa njiani, Rahim alimuuliza
Erica kuwa anapendelea kula nini, “Mmmh napenda sana ice
cream” “Aaah kuna supermarket hapo mbele wanauza nzuri sana, ngoja
tupitie mara moja” Basi Rahim akapeleka gari lake mpaka kwenye
supamaketi moja wapo na kushuka pamoja na Erica, kisha wakaingia kwenye lile
duka kubwa, wakati wanachukua zile koni kuna mtu alimgusa bega Erica, alipogeuka
na kumuangalia alikuwa ni Tumaini, basi akakumbatiana nae kwa
furaha, “Mmmh Erica mdogo wangu ndio upon a shemeji nini?” Erica
akawa anacheka tu, ila Tumaini akamvuta pembeni na kumnong’oneza “Mdogo
wangu unajua kuchagua, mshikilie haswaa unaendana nae” Kisha Tumaini
akawaaga, nao ndio walikuwa wanatoka wakaelekea kwenye gari. Rahim
alihakikisha kweli anamfikisha Erica hadi nyumbani kwao, kisha
akamwambia “Sasa leo itabidi unipe namba zako maana kila siku
hunitafuti” Erica hakuona tatizo kumpa Rahim namba zake kwani alijua
hata asingempa basi lazima Rahim angepewa na mama yake, basi akaagana nae pale
kisha Erica akaingia ndani kwao. Alipoingia tu ndani alikuwa anapigiwa
simu, na alipoangalia ni namba mpya akapokea “Erica, ni Rahim hapa.
Unajua nishakumiss tayari” Erica akawa anacheka tu, kisha Rahim
aliendelea kuongea, “Kama hutojali naomba kesho kutwa tuonane Erica,
niongee na wewe japo kwa ufupi tu moyo wangu utaridhika” Erica alikuwa
anatabasamu tu na hakuelewa kuwa akubali au akatae, ikabidi
akamwambia, “Basi nitakwambia badae kama itawezekana” “Naomba
iwezekane Erica, please nakuomba” Basi akaongea ongea nae na kukata
simu, Erica akajikuta akiwaza sana, ila akakosa majibu kwani aliona ni jinsi
gani Rahim akiingia kwenye moyo wake kiasi kwamba kumtoa ilikuwa ngumu sana ila
akakumbuka pia kuwa anampenda Erick ila akawaza kuwa je Erick atampenda tena
baada ya ile kushuhudia kuwa alitoa mimba. Usiku wa siku hiyo alipigiwa
simu na Tumaini pia, na alipopokea swala lilikuwa lile lile la kumsifia Rahim
kuwa Erica kachagua mwanaume wa maana, “Yani kama Yule kaka ningemuona
miyeyusho ningekwambia pale pale mdogo wangu, ila Yule ni mwanaume tena ni
mwanaume haswaa anayeendana na wewe” “Mmmh dada” “Kweli mdogo
wangu, Yule Rahim ni mwanaume anayekufaa” Erica alikuwa akitabasamu tu
kwani moyoni mwake alimpenda sana Erick ila alivutiwa na huyu
Rahim. Ilipokatika simu ya Tumaini iliingia simu ya Bahati nayo ilimkera
sana ila aliamua kupokea maana akili za Bahati alizijua vizuri kuwa asipopokea
basi kesho atakuja hapo kwao. “Nimekumiss
Erica” “Asante” “Mmmh hata wewe hujanimisi
jamani!” “Sasa unataka nikwambie nini?” “Niambie kuwa umenimiss
pia” “Kheee makubwa, haya nimekumiss pia” “Naomba kesho kutwa
tuonane mpenzi” “Aaah hapana, kesho kutwa nipo busy sana” “Busy
na nini Erica wakati chuo mmefunga?” “Aaah kuna sehemu naenda kesho
kutwa, labda tuonane kesho” “Kesho nitakuwa kazini Erica ndiomana
nimekuomba kesho kutwa” “Basi haitawezekana maana kuna sehemu
naenda” “Jamani Erica, basi nikusindikize” “Hapana, hairuhisiwi
kwenda na mwanaume” “Duh! Haya bhana” Akaongea ongea nae na
kukata simu huku akichukia jinsi gani Bahati amekuwa akimfatilia
vile, “Sijui yukoje, yani kahisi kesho kutwa nina mtoko anajifanya
kutaka kuonana na mimi. Anakera huyu loh!” Erica alikuwa akichukizwa
sana na mwenendo wa Bahati kwani hakupenda kabisa jinsi Bahati alivyokuwa
akimfatilia, basi akaamua kulala. Kulipokucha baada ya kufanya
kazi zake za hapa na pale, alishangaa kutembelewa na rafiki yake na
alimkaribisha vizuri sana. Ni muda mrefu sana tangu rafiki yake huyo kumtembelea
ni tangu wakati wanasoma sekondari, alikuwa ni Johari. “Nilikuwa
najaribisha tu kama nitakukuta” “Nipo rafiki yangu, nipo
likizo” “Hongera sana kwa kuchagua njia sahihi ya kusoma rafiki yangu,
ila hata mimi nataka nirudi shuleni” Walishauriana pale umuhimu wa
masomo, na baada ya maongezi ya hapa na pale ilibidi leo Erica amuulize vizuri
Johari kuhusu Erick kipindi kile. “Hivi Johari, ni kweli Erick alikuwa
muhuni sana kipindi kile?” “Kwanza nisamehe Erica kuhusu huyo Erick,
kiukweli rafiki yako nilisumbuliwa na wivu. Erick hajawahi kunitaka tena hata
Manka hajawahi kutongozwa na Erick, kumbe Manka ndio alikuwa anamfatilia
Erick” “Mmmh kumbe, sasa kwanini ulikuwa unaniambia vile kuwa Erick ni
muhuni?” “Sikia Erica, kipindi kile moyo wangu ulikuwa unaendeshwa na
wivu yani nilikuwa na wivu sana kiasi kwamba niliona wewe hufai kuwa na Erick,
mvulana mzuri vile. Kiukweli Erick alinifata na kuniambia nikwambie kuwa
anakupenda sana sababu mimi ni rafiki yako, ila mimi nilirudi na kumwambia kuwa
Erica hataki hata kusikia habari hizo na amesema siku ukimtongoza basi
atakusemea kwa walimu. Erick alionekana kujisikia vibaya ila alinihakikishia
kuwa lazima atakuja kukwambia ukweli kuwa anakupenda. Ndiomana nikatumia njia ya
kumchafua Erick kwako kwa kukwambia kuwa ni muhuni sana ili
usimkubali” “Aah Johari jamani, kwanini ulinifanyia hivyo? Umefanya niwe
na chuki na Erick kwa kipindi chote jamani Johari!” “Ndiomana naomba
msamaha maana chuki zaidi niliijenga mimi mwenyewe kwa Erick nakumbuka kuwa mimi
ndio nilimueleza ukweli mama yako na mimi ndio niliwaeleza ukweli walimu. Na
baada ya Erick kufukuzwa shule nilimfata na kumwambia kuwa wewe ndio
umesababisha yote, nilisema kwamba umemsemea kwenu na umeenda kumsemea kwa
walimu, nilisema maneno mengine hata hayafai ili kuhakikisha tu kuwa Erick hawi
karibu na wewe” “Ndio urafiki huo Johari? Ni urafiki au uuwaji huo?
Unajua mara nyingine mtu unapata laana bila ya kujua umepata vipi laana kumbe ni
mambo uliyotenda kwa wenzio. Sikia hata kama sikuwa katika rika la kujiunga na
mapenzi ila ningetafuta njia bora ya kutokuwa na Erick kwa kipindi kile kuliko
njia ambayo umeiweka wewe. Johari, nadhani hujui ila jua kwamba nampenda sana
Erick kwahiyo umehusika kuliua penzi la watu waliopendana” “Nisamehe
Erica, hata nikikutana na Erick siku moja nitamwambia ukweli” Kiukweli
Erica hakupenda kabisa vile ambavyo rafiki yake alimfanyia kwa kipindi cha nyuma
kwani anaona kama hayo mambo yamechangia yeye kuwa tangatanga wa mapenzi na
mwisho wa siku kumpata hadi king’ang’anizi kama Bahati. Johari baada ya
kuona Erica hana furaha tena aliamua kuaga na kuondoka
zake. Erica aliingia chumbani kwake na kuwaza sana kuwa amekosa
penzi la mwanaume mwenye mapenzi ya dhati kwake kwa kusikiliza maneno ya watu
kuwa hafai, akachukua tena simu na kujaribu kupiga ile namba aliyoiomba kwa
Tumaini ila alipiga weee bila ya kupokelewa na kumfanya azidi kupatwa na mawazo
na kukosa raha kabisa. Muda kidogo akapigiwa simu na Rahim na
kupokea, “Erica natumaini swal la kukutana na wewe kesho bado lipo
palepale, tafadhari usibadili mawazo” Erica akacheka tu na kukubali
kuonana nae, kisha wakapanga mahali pa kukutania, baada ya kukata simu
akajiambia, “Usikatae wito, kata neno. Ila mmmh huyu kaka akinitongoza
nitaweza kumkataa kweli? Ila bora kuwa na huyu kuliko Bahati maana kumpata tena
Erick ni ndoto kwangu” Wakati anawaza hayo tu iliingia simu ya Bahati na
akaona huyu anamzingua sasa hakupokea kabisa na akaamua kuzima simu kabisa baada
ya Bahati kumpigia kwa muda mrefu. Kisha alitoka na kwenda kuongea na
mama yake, “Hivi mama, mimi nafaa kuolewa na mwanaume wa aina
gani?” “Umeshapata mchumba nini?” “Hahaha hapana mama, si
ulisema mpaka nimalize chuo!” “Sio mpaka umalize chuo mwanangu, ila hata
kama bado kumaliza chuo ila ukapata mchumba wa maana mlete nyumbani
ajitambulishe na ikiwezekana alipe mahali kabisa, halafu harusi tunaweza
tukafanya pia ila kama anaeleweka” “Sasa ni mwanaume wa aina
gani?” “Erica mwanangu, unatakiwa uolewe na mwanaume msomi, mwenye kazi,
awe na pesa, ikiwa ana nyumba na gari itapendeza zaidi. Usije ukaniletea kapuku
hapa, nitaweka wapi sura yangu mtaani mimi? Inatakiwa ulete mwanaume wa
maana” “Aaah sawa mama, ikiwa ana pesa je halafu sio msomi?” “Na
wewe huyo asiye msomi unadhani kuna la maana anaweza fanya na hizo hela? Huoni
kama ni sifa kuwaambia wenzio mume wangu kamaliza chuo kikuu, ana degree au ana
masters au phd huoni kama ni sifa hiyo! Sio kusema mume wangu kaishia form four
sijui la saba. Hebu mwanangu ondoa mawazo ya watu ambao hawajasoma, lete msomi
hapa nyumbani lakini awe na hela” “Sawa mama nimesikia” Erica
aliinuka na kwenda chumbani kwake ila kwa maneno ya mama yake aliona kuwa ni
Rahim tu ndiye anayemfaa kwa wakati huo ila sio Bahati maana hana kigezo hata
kimoja anachokitaka mama yake. Alifikiria sana, hakuwasha simu
yake kabisa kwa kuhofia kupigiwa na Bahati wakati amelala na kupata
usumbufu. Asubuhi palipokucha aliwasha simu yake na akapata wazo la
kumpigia tena Erick kwani licha ya kwamba alimpenda sana Erick ila alitaka
kuongea nae kuhusu swala la yeye kutokutajwa kwa Tumaini kuwa ndiye muhusika
maana atamchukia, kwahiyo alitaka kuongea na Erick kuhusu swala hilo na kujaribu
tena kumwambia kuwa anampenda, aliipiga tena namba ile ya Erick kwa zaidi ya
mara tatu ila haikupokelewa na kumfanya ajihisi vibaya. Akatoka na
kwenda kufanya shughuli zake za hapa na pale huku akisubiria muda ambao Rahim
atamwambia kuwa ajiandae waonane, alipomaliza shughuli zake alichukua tena simu
yake na kupiga namba ya Erick ila haikupokelewa kama kawaida, kwa wakati huu
akaamua kutuma ujumbe kwa Erick, “Erick, mimi ni Erica. Nina shida sana
na wewe, tafadhali pokea simu yangu. Usinichukie Erick” Akamtumia na
kukaa kwa muda ila haikuingia simu yoyote, muda kidogo akapigiwa na Rahim na
kumwambia kuwa ameshafika lile eneo ambalo wamepanga kukutana kwahiyo
anamsubiri. Erica aliinuka na kujiandaa kisha kutoka, akamkuta mama yake
sebleni “Eeeh wapi saa hizi!” “Naenda kwa rafiki yangu
mama” “Mmmh siku hizi sikuelewi kabisa Erica, kama umepata mchumba mlete
tu ajitambulishe kuliko kujificha ficha hivyo!” “Hamna mama, ni rafiki
yang utu. Yule dada wa siku ile” Alimaanisha kuwa ni Tumaini, na
kumfanya mama yake kumruhusu bila ya kinyongo chochote. Erica alitoka na
kuondoka zake, ila kitu pekee ambacho hakukijua Erica ni kuwa siku hiyo Bahati
alikuwa nje ya nyumba yao akimsubiri amuone anapoelekea kwahiyo alipotoka na
kuondoka, Bahati alimfata kwa nyuma bila yay eye kujua
chochote. Erica alifika hadi alipoahidiana na Rahim, ilikuwa ni
hotelini na walikaa mahali Fulani kwenye bustani. Kwakweli Erica alifurahia sana
mandhari yale, “Jamani mbona sijawahio kufika sehemu ya
hivi?” “Ukiwa na mimi utafika kila mahali” Erica akatabasamu,
kisha Rahim aliendelea na porojo zake ambapo cha kwanza kabisa alimuomba Erica
simu yake kuwa aangalie picha, “Mmmh jamani, mbona kuna picha za kawaida
tu humu?” “Naomba hivyo hivyo, nawe chukua yangu uangalie” Erica
hakuona kama ni tatizo kufanya hivyo, akabadilishana simu na
Rahim. Wakati wakiendelea na maongezi, Erica aliomba kwenda msalani na
Rahim alimuelekeza, Erica alienda ila alisahau simu yake kwa Rahim. Huku
nyuma simu ya Erica ilianza kuita, Rahim akaitazama ile simu akaona namba
imeandikwa Erick, akajua kwa vyovyote vile ni mwanaume,
akaipokea “Hallow” “Namuomba mwenye simu” “Una shida nae
ipi?” “Hiyo si simu ya Erica? Namuomba mwenye simu” “Una shida
gani na mke wangu?” “Erica ni mke wako?” “Ndio ni mke wangu,
wewe una shida nae ipi” “Aaah basi, mwambie asante” Ile simu
ikakatika, na kumfanya Rahim ajiulize sana kuwa huyo Erick ni nani na
anamahusiano gani na Erica. Basi Erica aliporudi, alianza kupiga nae
story akamuuliza, “Erica una mchumba” “Kwanini umeniuliza
hivyo?” “Nimekuuliza tu, una mchumba?” “Aaah hapana
sina” Rahim akapumua kidogo, kisha akaendelea kumwambia
Erica “Je upo tayari kuwa mchumba angu na badae kuwa mke wangu?
Tafadhali kubali Erica nakupenda sana” Kabla Erica hajamjibu Rahim,
alifika Bahati kwenye maongezi yao na kusema, “Nimekuja mbele yako Erica
unikane kwa macho yangu kuwa mimi si mchumba
wako” Rahim akapumua kidogo, kisha akaendelea
kumwambia Erica “Je upo tayari kuwa mchumba angu na badae kuwa mke
wangu? Tafadhali kubali Erica nakupenda sana” Kabla Erica hajamjibu
Rahim, alifika Bahati kwenye maongezi yao na kusema, “Nimekuja mbele
yako Erica unikane kwa macho yangu kuwa mimi si mchumba wako” Kwanza ni
kitu ambacho Erica hakukitegemea kwahiyo alipigwa na bumbuwazi hivi kwa muda na
kujikuta akiwa hana cha kujibu kwa muda kidogo, ila akakumbuka kuwa simu yake
ipo kwa Rahim, akamuangalia na kumpa simu yake kisha akamwambia, “Na
mimi nipe simu yangu” Rahim alimshangaa kwa muda kidogo Erica na
kumuuliza kwa mshangao, “Kwani imekuwaje? Huyu kijana ni
nani?” “Simjui” Bahati akaongea kwa mshangao, “Leo hii
hunijui mimi Erica sababu ya huyu kijana wa kitajiri? Unanidharau sababu sina
uwezo wa kukupeleka sehemu za aina hii Erica? Nilihisi yote haya maana huyu
kijana simsahau kabisa toka siku ile beach” Rahim
akashangaa, “Mlikuwa wote beach?” “Ndio, huyu Erica ni mpenzi
wangu” Rahim akamuangalia Erica na kumwambia, “Erica kwanini
unakuwa muongo hivyo? Hupendezi kuwa muongo msichana mzuri kama wewe, kumbuka
umeniambia hapa muda sio mrefu kuwa huna mchumba, kumbe unaye. Basi sema hapa ni
yupi unayempenda kati yetu!” Bahati akadakia, “Ukweli ni kuwa
Erica ananipenda mimi, ila wewe kakudanganya sababu kakuona ni
tajiri” Erica alichukizwa sana na maneno ya Bahati na kujikuta akiongea
kwa jazba, “Tena wewe Bahati unikome, nikome kabisa. Sijawahi kukupenda
maisha yangu yote, nilikuwa na wewe sababu ya kukuonea huruma tu. Katika maisha
yangu nampenda kijana mmoja tu anayeitwa Erick, na kwa ujinga wako huu huu
umefanya nimkose Erick wangu” Kisha akachukua mkoba wake na kuondoka,
halafu akawaacha pale Rahim na Bahati wakiwa wanashangaa tu. Na wao hawakuweza
kuendelea kuongea kwani muhusika alishaondoka na walimuona akipanda bodaboda na
kutokomea, kwahiyo waliangaliana kisha Rahim akamwambia Bahati, “Hakuna
haja ya kugombana mimi na wewe ikiwa muhusika ameondoka, hata angekuwepo bado
yeye ndio angekuwa na muafaka, sio mimi na wewe” “Sawa lete simu
yake” “Hukunikabidhi wewe, nitairudisha mwenyewe” “Usiwe mbishi,
jua mimi ni mpenzi wake” “Ila amekukana mbele yangu kuwa hajawahi
kukupenda. Yani tusibishane bure hapa, si wewe wala si mimi anayependwa na Erica
bali ni Erick. Kwaheri” Rahim aliondoka zake, ikabidi Bahati nae aondoke
zake ila bado alikuwa hajaridhika na moyo wake. Erica alirudi
nyumbani kwao huku akijua wazi kuwa siku hiyo amechanganya mafaili vilivyo, ila
akajisemea, “Natakiwa kuachana kabisa na mambo ya mapenzi maana
yataniumiza kichwa tu. Sitaki tena mapenzi kwasasa, huyu Bahati hapana kwakweli
simtaki tena anikome kabisa” Akaingia chumbani kwake na kuoga, aliporudi
kukaa akakumbuka kuhusu simu yake, “Mungu wangu, simu yangu jamani
nitafanyaje na nimemuachia Rahim!” Akawaza sana kuwa aende muda huo
akawaza, kuwa mama yake akirudi bila kumkuta itakuwaje na muda utakuwa umeenda
akaona ni vyema aende kesho yake kuchukua hiyo simu yake maana hakuwa na
namna. Alitulia hadi mama yake aliporudi na kumkuta nyumbani, ila
alimuona kama binti yake hakuwa na raha kabisa, alimuita na kujaribu kuongea
nae, “Erica vipi mwanangu, mbona unaonesha huna
raha?” “Nilipoenda leo nilisahau simu yangu yani ndio nawaza
sasa” “Sasa kwanini hukwenda kuifata?” “Niliona muda umeenda
sana mama” “Sawa, basi usiwaze sana utaenda hata kesho
kuichukua” Basi akakubaliana na mama yake kuwa ataenda kesho yake
kuchukua hiyo simu, aliona ni vyema kumwambia vile ili kesho akiwa anatoka
asiulizwe chochote na mama yake. Alienda kulala ila kiukweli alikuwa na
mawazo sana, aliwaza mno kuhusu simu yake na akawaza pia alivyomjibu Rahim na
Bahati na pia akiwaza jinsi ya kuachana na mapenzi kabisa maana yalizidi
kuivuruga akili yake. Kesho yake baada ya kazi zake za hapa na
pale alijiandaa kisha akamuaga mama yake na kuondoka, moja kwa moja kuondoka
alienda nyumbani kwakina Rahim yani kwa Mrs.Peter, ambaye alimkaribisha vizuri
sana, Erica alikaribia ndani ila kabla hajasema chochote, Yule Mrs.Peter
alimwambia Erica, “Tena kuna mzigo wako, bora umekuja leo maana
ningesahau bure” Yule mama alienda ndani kumletea Erica huo mzigo, Erica
alijua kwa vyovyote vile ni simu aliyoisahau kwa Rahim ila hakujua ni kwanini
Yule mama kamwambia ni mzigo. Muda kidogo Yule mama alirudi na kiboksi
kidogo kwenye mfuko, na kumkabidhi, “Mzigo wako huo, Rahim alisema
nikupe” “kwani yeye yuko wapi?” “Rahim hayupo mbona, kasafiri
leo ameenda Marekani kuna mambo anaenda kumalizia, alirudi mara moja
tu” “Aaah sawa” “Basi, kaniachia mzigo wako tu huu anasema sijui
siku ile mlivyoondoka mlipitia supermarket ila ukasahau mzigo kwenye gari yake,
ndio kakufungia humo” “Aaah asante sana, nashukuru. Nilijua bado
yupo” “Hapana, kaondoka leo. Yule mwanangu angekuwa na mambo ya wanawake
basi ningehisi anataka kukutongoza ila Yule mwanangu namwamini sana, hana kabisa
mambo ya wanawake” “Ila mimi na yeye ni kama dada na kaka” “Ni
vizuri sana hivyo Erica, mi sipendi nione kuna mtu anachezea maisha yako au kuna
mtu anachezea maisha ya mwanangu. Nashukuru Mungu mwanangu Yule, sio mlevi,
havuti sigara na wala hana maswala ya wanawake, na sijui kama ataweza kutongoza
mwanamke yule” Erica akacheka na kumuuliza tena, “Unapenda aoe
mwanamke wa aina gani?” “Mwanamke mwenye hofu ya Mungu tu basi, yani
huyo atakuwa mke mwema kweli kwa mwanangu” “Na atampataje ikiwa
kutongoza hawezi?” “Nadhani mwanangu ataoa mzungu Yule sababu wale ndio
waelewa hata wasipotongozwa ila sio waafrika hawa, au labda nitamtafutia
mwenyewe mwanamke ila mwanangu Yule kutongoza hawezi kabisa, na sijawahi kumuona
na mwanamke.” Erica akacheka tu kisha akaongea ongea kidogo na Yule mama
kisha akaaga na kuondoka. Alikuwa akirudi nyumbani kwao huku akiwaza
kuwa kwenye boksi lile kuna kitu gani zaidi ya simu, ila akaamini tu kuwa kuna
simu labda Rahim ameweka kwenye boksi lile ili mama yake asijue kama alikutana
tena na Erica. Alifika nyumbani na cha kwanza kabisa ni kuingia
chumbani kwake na kufungua lile boksi kuona kuna kitu gani, aliona simu yake
halafu kuna boksi lingine, alivyolifungua alikuta kuna simu mpya ya kisasa na
kumfanya ashangae sana, kisha kulikuwa na bahasha iliyokuwa na pesa taslimu
shilingi laki mbili, kisha kuna karatasi lililokuwa limeandikwa, “Erica,
najua upatapo ujumbe huu sitakuwepo nitakuwa nimeshaondoka. Nakumbuka neno lako
ulilosema kuwa unampenda sana Erick ila tambua kwamba na mimi nakupenda sana na
nategemea kuwa wewe ndiye utakuwa mke wangu. Achana na watu ambao hawaeleweki
kwako kama Yule kijana, sijapenda kujikuta nikibishana eti na Yule kijana
tukikugombea wewe, sijapenda kwakweli. Ile sio type yako Erica, nakupenda sana.
Nimekupa hiyo simu ya kisasa ili iwe rahisi kuwasiliana, maana humo utapata
mitandao ya kijamii na tutawasiliana kwenye facebook, itakuwa rahisi sana.
Nimekuwekea na laini yenye vocha kabisa, nadhani itakusaidia kwa siku kadhaa.
Erica nakupenda sana, sijamwambia ukweli mama ila nataka nae tumshtukize tu siku
nikimwambia kuwa nataka kumtambulisha mchumba wangu, nakupenda sana Erica.
Nimerudi Marekani ila tutakuwa tunawasiliana, jitunze Erica, nakupenda sana
sana” Kwakweli Erica alichanganywa sana na ujumbe huu na alichanganywa
zaidi na zile zawadi alizopewa na Rahim, “Mmmh huyu ndio mwanaume sasa,
natumai hata mama atampenda. Ila mmmh nampenda Erick sijui
nifanyaje?” Akawaza na kuchukua ile simu mpya aliyopewa na kuiweka
kwenye chaji ilia aanze kuitumia. Aliwasha simu yake ya siku zote na
kukuta ikiwa haina jumbe hata moja wala haina simu yoyote iliyopigwa, hapo
hakuelewa kuwa inawezekana Rahim amefuta au alibadilisha vitu kwenye simu yake,
ila haikumuuma chochote kwani cha msingi alikuwa amepata simu
mpya. Asabuhi alianza kuitumia ile simu mpya, aliipenda sana
kwani siku zote alitamani kupata simu nzuri zaidi ila hakuweza kumwambia mama
yake kuwa anataka simu nyingine, kwahiyo kitendo cha kupata simu hiyo
kiliufurahisha sana moyo wake, akakumbuka kuwa ni Tumaini ambaye alimuona
akitumia simu ya aina ile, aliamua kumpigia simu ilia amuelekeze baadhi ya
vitu. Aliongea na Tumaini, naye Tumaini alimuelekeza jinsi ya kufanya
kwenye ile simu, kitu cha kwanza kabisa aliitafuta facebook na kujiunga nayo,
huku akisubiri kwa hamu pale ambapo Rahim atamtafuta, ila rafiki yake wa kwanza
facebook alikuwa ni Tumaini na kumshauri aweke picha zake mbali mbali kwani ndio
itakuwa rahisi kwa watu kumfahamu. Siku hiyo alijiweka vizuri kabisa na
kuchukua ile simu kisha kujipiga picha kadhaa na kuziweka kwenye
facebook, “Mmmh hapo atajua tu ni mimi” Simu yake ya kawaida
ikaanza kuita, akaona anayepiga ni Bahati, na kumfanya achukie sana ila
akapokea, “Erica jamani, Erica mpenzi wangu nakupenda
sana” “Bahati, tafadhari achana na mimi” “Kwahiyo Erica ulienda
kwa Yule jamaa kuchukua simu au alikuletea
kwenu?” “Hayakuhusu” “Erica, wewe ni mwanamke wa muhimu sana
kwangu. Kumbuka mimi ni mwanaume wako wa kwanza Erica” “Hivi wewe una
kichaa nini? Hukuwa mwanaume wangu wa kwanza wewe, ulikuwa watatu” Erica
akakata ile simu huku akisema kuwa Yule asimzoee zoee, kwani alikuwa yupo makini
na kutafuta marafiki kwenye mtandao wa facebook yani siku hiyo hata akasahau
kufanya majukumu yake mengine sababu ya simu. Mamake akamuita maana
ilikuwa ni jioni na siku hiyo mama hakumuona kabisa Erica akitoka nje zaidi ya
mara moja moja tu, “Erica, hivi umekula wewe leo?” Erica
akagundua kuwa siku hiyo hata kula hakula kwani alikuwa na simu tu akihangaika
nayo kila kurasa akiangalia vitu mbali mbali. “Vipi mwanangu
unaumwa?” “Hapana mama” “Sasa mbona upo hivyo?” Hakuwa
na jibu la kumpa mama yake kwahiyo kwa kujigelesha ilibidi aende jikoni na
kuanza kufanya kazi za hapa na pale. Kisha akarudi chumbani kwake kwa
lengo la kulala ila hakulala mapema siku hiyo kwani alijikuta na simu tu ingawa
mtu pekee aliyekuwa akiwasiliana nae kwa muda huo alikuwa ni Tumaini, ila muda
mwingi alikuwa akiwaza kuhusu Rahim na kujaribu kumsahau Erick, “Hata
hivyo natakiwa kumsahau kabisa Erick, kwanza hawezi kunisamehe maana amenihisi
kuwa na tabia mbaya. Ila pia nikimkataa mwanaume kama Rahim nitaonekana ni
msichana mjinga sana kati ya wasichana wote, hivi ni nani asiyependa mwanaume
anayejua kuhonga? Kila mwanamke anatamani ampate mwanaume anayejua kuhonga kama
Rahim, hebu ona sifahamiani nae vizuri ila kapata uthubutu wa kuninunulia simu
na kunipa pesa. Erick nampenda ndio, na hela anazo ila hajawahi kunihonga
tofauti na huyu Rahim ambaye hata hanijui vizuri, nadhani huyu ndiye mwenye
upendo. Ila sijui nitamsahau vipi Erick!” Aliwaza waza kiasi, yani kwa
wakati huo Bahati hakuwepo hata kidogo kwenye akili yake, alishamfuta kabisa.
Kisha akalala. Kulipokucha aliamka na kuendelea na shughuli za
hapa na pale, kisha alipomaliza alienda tena chumbani na kuzama kwenye simu
yake. Ila leo mama yake alimuita tena na kumkalisha kitako, “Erica
mwanangu kakuona upo busy sana, ngoja nirudie hoja yangu niliyokugusia gusia
siku zilizopita. Kwenye nyumba yangu sitaki uniletee mwanaume aliyechoka, yani
mwanaume asiye na uwezo sitaki umlete yani ukithubutu nitamtoa na panga
kwakweli” “Jamani mama” “Jamani nini? Unajua kwanini nimekwambia
hivi?” “Sijui mama” “Nimekwama kwenye hela zangu za vikoba huko,
sasa kila siku namtegemea Bite tu maana ndio kaolewa na mwanaume anayeeleweka
ila dada yenu Mage uuuh sijui alikumbwa na zimwi gani, kaolewa na mwanaume hana
mbele wala nyuma. Leo nimewapigia simu kuwa nimekwama hela ya kikoba wanasema
hawana hela, yani wameniudhi sana, hivi kila siku nimtegemee Bite tu wakati nina
watoto wengine? Huyo kaka yenu naye ameenda kuoa masikini huko yani wanamtegemea
yeye tu, Erica tafadhari sana usije ukaolewa na waliochoka. Umenielewa
eeh!” “Nimekuelewa mama” “Haya sasa, kaendelee na shughuli zako
ila jua kabisa mauza uza siyataki kwenye nyumba yangu. Hapa nina mawazo kweli na
hela ya kikoba” Erica aliingia ndani na kutoka na elfu hamsini kisha
akamkabidhi mama yake, kitendo hiko kilimfurahisha sana mama
yake, “Jamani huyu mkwe aliyekupa hizi pesa ndio namtaka kwakweli, ila
tutaongea vizuri ngoja niende kwenye kikoba kwanza” Mama yake aliondoka
kisha Erica akaenda chumbani na kuendelea kuperuzi mtandao wa
facebook. Leo alipigiwa simu na namba mpya, aliipokea kwa shauku sana
maana ilikuwa ni namba ya marekani na akahisi tu atakuwa ni Rahim, na kweli
alikuwa ni yeye, Erica aliongea nae huku akicheka cheka tu. “Naona
umefurahi sana Erica!” “Ndio nimefurahi” “Furahi mama na jua
kwamba Rahim anakupenda sana” Erica alizidi kutabasamu, kisha Rahim
akamuuliza Erica kama ameshajiunga na mtandao ambapo alimkubalia na kuamua
kuhamia kwenye mtandao sasa na kuendelea kuwasiliana nae. Erica
alitabasamu muda wote alipokuwa akiwasiliana na Rahim, kwa wakati huo alianza
taratibu kusahau kuhusu uwepo wa Erick, ingawa akimtaja anahisi kumkumbuka ila
alijitahidi kwa kadri awezavyo amsahau kabisa. Simu yake ya kawaida iliita mara
kwa mara na mpigaji alikuwa ni Bahati, Erica aliamua kuizima ili kuepuka
usumbufu. Aliwasiliana sana na Rahim siku hiyo kwa njia ya ujumbe bila
ya kujua kuwa kule aliko Rahim kumekucha na kwao ni usiku, aliwasiliana nae sana
hadi kuja kushtukia ni saa kumi na moja kasoro, “Mmmh nimekesha
jamani” Ikabidi amuage Rahim na kulala. Asubuhi
aliamshwa na mama yake, kwenye mida ya saa nne, “Erica, umelala mpaka
muda huu kweli? Hebu njoo kuna kijana anakuulizia na wala
simuelewi” Erica aliinuka na kujiuliza kuwa ni nani huyo aliyekuwa
anamuulizia, aliamka na kuvaa, kisha akatoka kumuona aliyekuja kumuulizia,
alishangaa kuona ni Bahati ndio yupo sebleni
akimsubiria. Asubuhi aliamshwa na mama yake, kwenye
mida ya saa nne, “Erica, umelala mpaka muda huu kweli? Hebu njoo kuna
kijana anakuulizia na wala simuelewi” Erica aliinuka na kujiuliza kuwa
ni nani huyo aliyekuwa anamuulizia, aliamka na kuvaa, kisha akatoka kumuona
aliyekuja kumuulizia, alishangaa kuona ni Bahati ndio yupo sebleni akimsubiria.
Yani Erica alishindwa hata cha kusema na alishindwa jinsi ya kushangaa maana
alikuwa anaona maajabu tu ya huyu Bahati, alisimama akimuangalia, mama yake
Erica nae alikuwa ametulia pembeni akisubiri utambulisho ila alishangaa kuona
kimya kikitawala, Bahati aliamua kutoa ule ukimya, “Erica, mambo
vipi?” Erica alisogea na kumshika mkono Bahati kisha kutoka nae nje,
mama yake alikuwa pale pale sebleni akishangaa tu. Erica alifika nje na
Bahati na kumwambia “Umekuja kufata nini wewe?” “Nimekufata wewe
Erica” “Si nishakwambia sikutaki” “Erica
nakupenda” Akapiga na magoti huku akitaka kulia, Erica akaona hilo balaa
lisije kuonekana na mama yake akamuinua pale chini na kumtaka
aondoke, “Erica sitaondoka hapa hadi uniambie kuwa
unanipenda” “Haya nakupenda, basi nenda” “Erica, niahidi kwamba
utapokea simu zangu” “Ndio nitapokea, haya kwaheri” Bahati
alisogea ili ambusu Erica ila Erica alisogea kwa nyuma kidogo akiashiria kuwa
hataki busu la Bahati, ila aliamua kumuaga kwa uzuri ili asimtie aibu kwa mama
yake. Aliporudi ndani tu, mama yake alimuuliza, “Erica, ni nani
Yule?” Erica alifikiria kidogo na kumjibu mama yake, “Yule ni
kijana anayenileteaga samaki hosteli sasa nilimuelekeza kwetu ndio leo amekuja
kupafahamu” “Jamani, sasa mbona hujanitambulisha na unajua fika mama
yako napenda samaki? Mwambie awe ananiletea” “Sawa mama
nitamwambia” Erica aliitikia ila kiukweli hakupanga kumwambia kabisa
Bahati kwani alijua wazi kwa jinsi Bahati anavyopenda sifa basi yupo tayari
kupeleka samaki kila siku ilimradi apendwe. Alirudi ndani
kujiweka sawa kwa siku hiyo maana hata kuoga hakuoga, kwahiyo alienda kuoga na
alipomaliza alivaa kabisa na kutoka tena sebleni, mamake
akamwambia, “Mwanangu, Yule kijana ametuletea samaki” Erica
alishangaa sana kuwa Bahati amejuaje kama mama yake anataka samaki, na amewezaje
kuwapata kwa muda mfupi vile, alijiuliza sana ila alitabasamu tu kwa mama
yake. Aliporudi ndani alimpigia simu Bahati na kumuuliza kuhusu samaki
alizozileta, “Nilirudi nje kwenu na nikasikia uliyokuwa ukiongea na mama
yako, najua usingeniambia Erica ndiomana nilijiongeza na kuleta wale
samaki” “Yani wewe akili zako loh!” “Usinifikirie vibaya Erica,
familia yako ni sawa na familia yangu ndiomana nikafanya hivyo” “Haya
kwaheri” Erica alikata ile simu na kujiuliza kuwa huyu Bahati ataacha
usumbufu wake lini, maana alishangaa kuwa ni mtu wa aina gani anakataliwa lakini
bado anang’ang’ania. Na ikawa vile mara kwa mara alipeleka samaki
kwakina Erica kiasi kwamba mamake Erica alimzoea vilivyo hadi pale Erica
alipofungua chuo na kurudi hosteli bado Bahati alikuwa akipeleka samaki nyumbani
kwakina Erica. Safari hii Erica hakuwa na marafiki wa kuongea
nao zaidi ya kuongea na Tumaini na kumalizana na simu yake baada ya masomo, leo
Tumaini alimuuliza “Erica, ulichukua namba ya Erick vipi uliishia nae
wapi maana Sia anaulizia” “Erick hajawahi kupokea simu yangu hata mara
moja” “Ila nae ana facebook mtafute, andika tu Prince Erick utaona picha
yake. Mule anaweza akakujibu” “Sawa, nitajaribu” Hakutumia muda
mwingi sana kuongea sababu muda wake uliishia kwenye masomo na kwenye
simu. Siku ya leo alitafutwa na dada yake Bite, ambapo alionana nae na
kuongea nae, “Mdogo wangu dadako natafuta msichana wa kunisaidia kazi za
ndani, niulizie ulizie huko” “Dada msichana wa kazi wa nini na wakati
pale mko wawili tu wewe na shemeji?” “Dada yako nina ujauzito, yani
unanisumbua huo balaa” “Kumbe! Ila mimi nilikuwa sishauri kuweka mdada
wa kazi” “Kwanini?” “Bora hata uweke mkaka wa
kukusaidia” “Mkaka? Shemeji yako hawezi kukubali huo ujinga, niulizie
bhana mdada anisaidiage” “Wadada siwaamini dada, unaweza shangaa
akakusaidia vyote. Unashangaa akamchukua na mumeo” “Unaongea nini wewe
Erica, mume wangu unamchukulia kirahisi eeh! Sio wa hivyo shemeji yako
anajiheshimu sana, na pia ananipenda sana mimi yani mimi ndio kila kitu katika
maisha yake” “Dada naomba nikuulize tu, hivi ni kitu gani kilikufanya
ugundue kuwa shemeji anakupenda sana?” “Mume wangu si mtu wa wanawake,
na alinikuta bikra akaniambia Bite sitakuja kutembea na mwanamke mwingine yeyote
zaidi yako, mume wangu hata akisafiri na kukaa miaka hata miwili najua
anavumilia mpaka arudi kwangu. Muombe sana Mungu akupe mume wa dizaini hii,
mwenye upendo wa kweli” “Wewe dada una uhakika gani kuwa hanaga wanawake
wengine zaidi yako?” “Erica, naona unaanza mada zisizoeleweka. Wewe
elewa tu kuwa ananipenda mimi tu na hana mwanamke mwingine zaidi
yangu” Ilibidi Erica asiongee zaidi maana yeye kwa siku chache alizokaa
na shemeji yake aliona kuwa ana tabia zisizofaa kwahiyo swala la dada yake
kumsifia kiasi kile lilimchanganya sana, aliongea ongea nae pale na kumuahidi
kumsadia ila kiukweli hakupanga kumsaidia wala nini ila alimpa moyo tu kwani
alielewa tabia ya shemeji yake kuwa lazima atapita na huyo dada wa
kazi. Erica alifikiria sana kuhusu wanaume, alifikiria zaidi
kuhusu dada yake aliyekuwa anajiona anapendwa asilimia mia moja wakati mwanaume
mwenyewe anamtongoza hadi mdogo wake, aliwaza sana, “Naweza nikaona
Rahim ananipenda sana ila nyuma ya pazia kumbe ana wanawake wengi, ila mama yake
alisema kuwa hana maswala ya wanawake. Kwa upande wa Erick, ni kweli ananipenda
nampenda ila Yule kashakuwa na wanawake wa kila aina ataacha kweli? Mwenye asili
haachi asili, kwa upande wa Bahati, naona huyu mtu ni msumbufu tu na sidhani
kama ataacha usumbufu kwangu, labda nikiolewa ndio atakoma” Aliwaza sana
kuhusu wanaume na kukosa jibu la moja kwa moja, akiwa pale hosteli aliambiwa
kuwa kuna mgeni wake anamuita nje. Erica alitoka, na kumkuta George,
akamshangaa “Kheee George si umemaliza chuo wewe?” “Ni kweli
nimemaliza chuo ila kuna kitu bado sijakikamilisha na kinaumiza sana moyo
wangu” “Kitu gani hiko?” “Niliahidi kukuoa Erica, na sijafanya
hivyo kwakweli moyo unaniuma sana” “Hata usiumie, mimi sina mpango tena
wa kuolewa” “Kwanini Erica?” Kabla hajamjibu alitokea Bahati,
kiukweli kipindi hiki Erica alikuwa hata hapendi kumuona Bahati kabisa kwahiyo
kile kitendo cha kumuona tu pale alijua ni wazi lazima atapaniki kwa kumuona
amesimama na mwanaume, Erica alimuacha George pale kasimama kisha akaondoka zake
na kumuacha George akiwa amesimama pale, muda ule Bahati nae alikuwa na hasira
sana kwahiyo alihisi moja kwa moja ni Yule anayemsumbua Erica kwa kipindi hiko
ndiomana Erica hataki kumuona tena. Bahati alienda moja kwa moja alipo
George na kumkunja, hata George alimshangaa sana Bahati, ambapo Bahati akampiga
ngumi George iliyomuangusha hadi chini na kisha kuanza kumshambulia ila George
hakumgusa popote Bahati, watu wakaanza kujaa lile eneo la tukio na mwisho wa
siku walinzi wa pale hosteli walisogea na kuwakamata kisha wakawapeleka kituo
cha polisi. Ikawa gumzo pale hosteli kuwa vijana wawili wamepigana
sababu ya Erica, ila Erica mwenyewe alikuwa ndani na wala hakufatilia
kilichotokea nyuma. Alienda msichana mmoja na kumwambia
Erica, “Kheee Erica, ama kweli wewe ni kiboko yani inatokea mpaka
wanaume wanapigana kwasababu yako!” “Wanaume gani?” “Ina maana
kelele za hapo nje hujazisikia?” “Kelele gani? Sijasikia
chochote” “Wale wanaume zako uliowaacha nje, wamepigana sababu yako.
Wewe ni noma Erica? Mmmh nipe siri ya mafanikio, na mimi nataka wanaume wapigane
sababu yangu” Erica akacheka tu, na kuamua kutoka nje ili akaone kuwa
imekuwaje, alipokuwa nje aliona kuna askari mmoja kafika kumbe alikuwa
anamuulizia yeye mwenyewe, kwahiyo akachukuliwa na kupelekwa
kituoni. “Erica, vijana hawa wameletwa na imesemekana kuwa wamegombana
kwasababu yako. Je una mahusiano nao wote?” “Hapana, kwanza siwajui.
Mimi nina mtu wangu” Polisi wakaandika maelezo ya Erica na kumpa ruhusa
aondoke. Aliondoka ila hakutaka tena kurudi hosteli, siku hiyo alimpigia simu
dada yake Mage ili aende kwa dada yake huyo akalale huko sababu hakutaka kurudi
hosteli na hakutaka kwenda nyumbani kwao kwani alihisi kuwa mama yake
angemuuliza maswali mengi sana ukizingatia sio mwisho wa wiki na kwenda kwa dada
yake Bite alipopazoea hakutaka kwani bado alikuwa na hofu na Yule shemeji
yake. Erica alifika kwa dada yake Mage kwenye mida ya saa kumi
na mbili jioni, na dada yake alimkaribisha vizuri sana, “Kwa mara ya
kwanza leo umeamua kuja kwangu kulala? Unanitenga sana mdogo
wangu” “Nisamehe dada” “Haya, usijali karibu. Ila mimi ni dada
yako, mimi ndio dada yako mkubwa, hutakiwi kunikwepa” Basi Erica
alikaribia pale kwa dada yake na kuongea ongea nae, kisha watoto wa dada yake
walifika kumsalimia maana alikuwa na watoto watatu, na aliona jinsi watoto
walivyokuwa wakubwa. Walipoondoka akamuuliza dada yake, “Ila kwanini
wanao huwa huwaleti nyumbani waje kukaa na bibi yao?” “Mdogo wangu,
hujui tu. Mama ni mama yetu, napenda sana kumletea wajukuu zake akae kae nao ila
mama alinisema toka siku naolewa hakumpenda mume aliyenioa kabisa ila alikubali
tu sababu nilikuwa mjamzito” “Kheee kumbe uliolewa na
mimba?” “Ndio, niliolewa na mimba mdogo wangu” “Sasa mbona mimi
mlienda kunitoa mimba?” “Erica, sitaki upitie tuliko pitia wengine.
Napenda umalize shule, ndio uolewe na kuzaa. Hapo unakuwa kwenye maisha yenye
furaha sana , tofauti na kuishi kwa stahili hii” “Mmmh dada jamani,
kwahiyo nyie mnataka niolewe mwanaume wa aina gani?” “Swala sio kuolewa
na mwanaume gani, swala ni kutokupata mimba kabla ya ndoa. Subiri uolewe kwanza,
kuna njia nyingi tu za kujizuia kupata mimba” “Ila wewe binafsi
ungependa niolewe na mwanaume wa aina gani?” “Mimi sikuchagulii mwanaume wa kuolewa nae, ila kwa ushauri wangu ukitaka kufurahia maisha basi olewa na
mwanaume anayekupenda kwa dhati. Kwa hakika hutojutia maisha yote” “Na
nitamjuaje mwanaume anayenipenda kwa dhati?” “Siku uje tena nikupe
darasa kabisa la mapenzi, ila kwa leo tuendelee na mada zingine.” Erica
alitamani sana dada yake amwambie jinsi ya kumjua mwanaume anayempenda kwa dhati
ila aliamua asikilize shauri lake kuwa atamueleza siku nyingine, kwahiyo
akazungumza nae mazungumzo mengine kabisa kwa wakati huo, na mwisho wa siku
walienda kula na kulala. Erica alielewa kwanini mama yake anataka wanaume wenye
hela sababu mazingira aliyokuwa akiishi dada yake hayakuvutia kabisa, na alilala
sababu ni kwa dadake ila ingekuwa vinginevyo asingelala pale, ila alimuheshimu
sana mume wa dada yake kwani mwanaume huyu siku zote alimuona Erica kama mtoto
wake, na akiongea nae ni kama baba anaongea na mtoto na si vinginevyo, Erica
alijisemea moyoni, “Mtu anaweza asiwe na pesa nyingi ila akawa na
mapenzi ya dhati, na mtu anaweza akawa na pesa na akakosa mapenzi ya dhati.
Nadhani mapenzi ni jinsi mtu anavyofanya yeye mwenyewe tu, ni tabia ya mtu bila
kujali kipato chake” Basi kesho yake akajiandaa vizuri na kuwaaga kisha
kurudi hosteli ambapo alienda kubadilisha nguo na kwenda
chuo. Alivyofika chuo, alipishana na Dora ambaye alimfata
nyuma, “Erica” Erica akasimama na kumsikiliza kuwa
anasemaje, “Erica, ulichofanya sio sawa” “Kitu gani
hicho?” “Yani unasababisha George apigwe na kijana asiyeeleweka halafu
polisi unajifanya kumkana George?” “Sikia Dora, habari za George kwangu
zilishafutika hata nashangaa kwa wewe kuzifufua tena, George sina mahusiano nae
kwahiyo polisi ningekubali kuwa nina mahusiano na George? Siwezi, na sijamwambia
anifatilie kayataka mwenyewe” “Erica najua humjui George vizuri, ila
nikwambie tu George hawezi kuridhika kwa ulichomfanyia na
atakukomesha.” “Usinitishe Dora, kwahiyo atanifanya
nini?” “Sikutishi ila nakwambia ukweli halisi, George huwa hapendi
ujinga kabisa, na kwa mambo haya ya kijinga uliyomfanyia utajutia” “Hebu
achana na mimi Dora” “Sawa ila George atakufanya kitu kibaya wewe,
hutakuja kusahau katika maisha yako” “Nimekwambia achana na mimi Dora,
siogopi chochote.” Kisha Erica akaondoka zake na kuelekea kwenye
kipindi, alipomaliza kipindi kuna mkaka alimfata nyuma na kumshika
mkono. “Samahani dada, naitwa Derick sijui wewe unaitwa
nani?” Erica alimuangalia vizuri huyo aliyejitambulisha kwake maana jina
kidogo tu liendane na Erick, akamuangalia sana na kumwambia “Naitwa
Erica” “Nafurahi kukufahamu, naweza kupata mawasiliano
yako?” Katika swala ambalo lilikuwa halimpi shida Erica ni swala la
kutoa mawasiliano yake, yani kwa yeyote aliyehitaji mawasiliano yake alimpa ila
swala la kutongozwa ndio alikuwa anaangalia sana mwanaume mwenye mvuto ndio
amkubali. Kwahiyo alimpa namba Derick bila ya tatizo lolote lile, naye
Derick alimshukuru sana Erica kisha akaagana nae. Erica alirudi
hosteli na jioni ya siku hiyo alikuwa na kipindi kwahiyo alienda tena chuo, muda
anaenda alipigiwa simu na namba mpya na mwenye ile namba alijitambulisha kuwa ni
Derick. “Naweza kuonana nawe muda huu Erica?” “Hapana nina
kipindi” “Basi ukitoka kwenye kipindi” “Hapana, nitaenda kulala
hosteli” “Basi naomba nije nikusindikize hosteli tu” “Hapana,
usijisumbue” Kisha Erica akakata ile simu, na kuingia kwenye kipindi.
Alipotoka alishangaa akiitwa na aliyekuwa akimuita alikuwa ni Dora, akasimama na
kumsikiliza kuwa amemuitia nini. “Erica, nakuomba tumalize tofauti
zetu” “Dora, mi nilishamalizana na wewe ila kuwa tena marafiki mimi na
wewe hilo haliwezekani na halitawezekana kamwe” Dora bado alikuwa
akimbembeleza Erica huku akimpa maneno mbali mbali, kiasi kwamba kuja kushtukia,
chuo kilikuwa kimya kabisa na kuona kamavile kabakia yeye na Dora tu. Ikabidi
Erica amuage Dora kuwa anaondoka, “Huogopi peke
yako?” “Siogopi” Kiukweli alikuwa anaogopa ila hakutaka
kumwambia Dora kwamba anaogopa, Dora akawa anacheka tu maana yeye alikuwa
anaishi ndani ya hosteli za chuo ila Erica alikuwa akiishi hosteli za nje ya
chuo. Erica aliondoka pale huku akitembea haraka haraka, alisikia kuna
mtu anamuita nyuma yake ila hakutaka kusimama kabisa kwani alikuwa na uoga sana,
ila kufika mbele alikuta kuna vijana watatu wamemzingira na kumfanya aogope
zaidi, na kabla hajafanya chochote alitokea George mbele yake, yani akiwa ni
kijana wa nne. Erica aliondoka pale huku akitembea haraka
haraka, alisikia kuna mtu anamuita nyuma yake ila hakutaka kusimama kabisa kwani
alikuwa na uoga sana, ila kufika mbele alikuta kuna vijana watatu wamemzingira
na kumfanya aogope zaidi, na kabla hajafanya chochote alitokea George mbele
yake, yani akiwa ni kijana wa nne. Uoga ulimzidi zaidi Erica, ila George
alimsogelea na kumnasa kofi kisha akamkunja na kumwambia, “Leo nadhani
utataja jina la marehemu baba yako, maana leo tunaenda kukubaka wote
wane” Erica machozi yakamtoka, akashtukia akipigwa teke tu na kuanguka
chini yani pale pale wale vijana walianza kumvua nguo kwa nguvu sana, huku
George akitelemka chini na kuwa wa kwanza kumuingilia, Erica alitamani kupiga
makelele ila mkaka mmoja alitumika kumziba mdomo Erica huku mwingine akimshika
mikono na mwingine akimkamata miguu na kufanya iwe ngumu hata kufurukuta, Erica
alikuwa akiugua moyoni na kumuomba Mungu muujiza utokee. Ila gafla alitokea mtu
mbele ya wale vijana akiwa na mbwa na kuanza kuwabwekea huku akimfata George
ambaye alikuwa chini na Erica na kumng’ata kwenye makalio, kitendo hiko
kilifanya wale vijana wengine wamuachie Erica na wakimbie na George nae
alimuachia Erica na kukimbia ambapo yule mbwa alikuwa akiwambiza. Kisha
aliinama Yule kijana aliyeenda na mbwa na kumuinua Erica pale chini huku akimpa
pole kwa kilichotokea, kwakweli Erica alishangaa sana moyo wa huyu msamalia ila
kwa wakati huo hakumgundua sababu ya mawenge ya kutaka kubakwa, Yule kijana
alimsaidia Erica kujisitiri nguo zake kisha kumsaidia kutembea hadi walifika
mahali penye mwanga karibu na hosteli, Erica alimtazama Yule kijana kumshukuru,
akashangaa sana kuona Yule kijana alikuwa Derick, alimshukuru sana kwakweli na
kumuomba akapumzike kwanza kuwa atazungumza nae kesho, ila Derick aliongozana na
Erica hadi alipofika kwenye mlango wa chumba cha Erica ndipo akaondoka
zake. Erica alienda kubadilisha nguo na kuoga, kisha kurudi
kitandani yani siku hiyo hata hamu ya kula hakuwa nayo alikuwa akijitafakari
tu, “Kwahiyo asingetokea Yule Derick ningebakwa na vijana wane leo, duh
ningekuwa mtu kweli? Hivi kwanini wanaume wana tabia za hivi jamani, huyu George
aliuumiza sana moyo wangu, na ni yeye aliyefanya hadi nimeangukia kwa Bahati
sababu ya mawazo, leo hii ananifata tena mimi, anagombana na Bahati halafu
anataka kunifanyia mimi mambo ya ajabu. Kwani mimi kibaya nilichofanya kwake ni
nini? Hivi amesahau kuwa aliniacha mahali hata nauli ya kurudia sina jamani?
Kwanini lakini wanaume wanakuwa hivi?” Aliwaza sana Erica na
kujihurumia, yani siku hiyo hata hamu ya kuwasiliana kwenye facebook hakuwa nayo
maana moyo wake bado ulikuwa unatetemeka kwa kile kitendo
kilichotokea. Aliamua kulala tu muda huo maana alikuwa na uoga balaa,
asubuhi na mapema aliamka na kilichomuamsha ni simu ya Derick aliikariri namba
yake sababu alimpigia jana yake, akaipokea “Erica samahani ila naomba
nikufate twende hospitali ukapime ili uangalie kama wale vichaa hawajakuwekea
madhara, na kama kuna madhara basi upate dawa mapema” Erica aliona ni
ushauri mzuri aliopewa na Derick kwahiyo alikubali na kujiandaa kisha Derick
akampitia na kwenda hospitali kupima. Walipima na kukutwa hana
maambukizi yoyote ila alipewa dawa tu za kumzuia endapo kuna vilivyokuwemo na
kutajiwa siku nyingine ya kuenda tena hospitali. Waliondoka pale
hospitali kisha Derick kumwambia Erica kuwa waende mgahawani wakapate jambo kitu
cha kula maana walikuwa hawajala kitu chochote. Walikaa
mgahawani na kuanza mazungumzo ambapo Erica aliendelea kumshukuru sana Derick na
kumuuliza kuwa alijuaje kuwa yupo mashakani, “Sikia Erica, kwanza
utambue kuwa nakupenda na yote haya nimefanya sababu ya upendo wangu
kwako” Erica hakujibu chochote ila aliendelea
kumsikiliza, “Erica, mimi sikukutana na wewe muda ule ulipomaliza
kipindi ila nilikuona muda tu na yule rafiki yako, nikakupenda na muda ule
kipindi kimeisha nilikufata na kukuomba namba, nashukuru ulinipa. Sasa kuna muda
nilimuona Yule rafiki yako uliyekuwa unaongea nae ule mchana, nilimkuta mahali
akiongea na mkaka mmoja hivi, nikamsikia akisema nitamgelesha ili achelewe na
awe peke yake wakati wa kuondoka na iwe rahisi kwenu. Sikuelewa ila nilihisi
kama unaongelewa wewe, nilijiuliza ni kitu gani wanapanga kwako, sikupata jibu
ndipo nilipoamua kukupigia simu jioni, nikiwa na lengo la kuzungumza na wewe ila
ulisema kuwa una kipindi, nikakuomba kuwa nikusindikize ukitoka kwenye kipindi
ila ulikaa, nilijisikia vibaya kwakweli na nikasema niache tu kama ilivyo. Ila
kadri nilivyokaa ndivyo moyo ulivyoniuma, nikaamua kupigia simu tena ili
nikutahadharishe hata kwenye simu ila sikukupata hewani, nilijua ni sababu ya
kwenye kipindi ndiomana umezima ila sikuwa na raha kabisa, nilirudi ninapokaa
bado sikuwa na raha, nilipoona ni mida ya kutoka kwenye kipindi nikaamua kuja
tena chuoni kukusubiri, nikaona umetoka na Yule rafiki yako akiongea na wewe
nilisema sitaondoka hadi nijue mwisho wake, sikutaka kukufata pale sababu
nilihisi huwenda ukanishushua, najua ilichukua mud asana hadi wewe kuondoka,
ulipokuwa unaondoka nilikuita ila hata nyuma hukugeuka ndio nikashangaa mbele
umezingirwa na vijana, nikajua wale ndio walipanga kukufanyia vibaya wewe,
nilijua peke yangu nisingeweza ila kwavile mimi huwa naelewana sana na mbwa
sababu nishawafuga sana, nilisogea sehemu yenye mbwa na kumpa ishara kisha
nikaja nae na kukuokoa wewe” “Dah! Kwakweli Derick una upendo wa ajabu
na una utu sana, nashukuru kwakweli nashukuru sana, maana bila wewe sijui
ningekuwa wapi muda huu” “Asante pia Erica, ila nakupenda sana Erica,
tafadhali usinikatae” “Ila nina mchumba tayari” Derick akashtuka
kidogo na kumuuliza, “Yuko wapi huyo mchumba?” “Yupo
Marekani” “Erica, ngoja nikwambie kitu. Unaweza sema naongea tu ila ndio
ukweli ulivyo, mwanaume wa mbali utawasiliana nae ndio na atakwambia anakupenda
ila hakuna mwanaume anayeweza mahusiano ya mbali hivyo. Lazima huko Marekani ana
wanawake ila kwasababu wewe anakuhitaji pia lazima akwambie
anakupenda” “Mmmh!” “Ndio ilivyo, ila hata hivyo huyo sio mume
kwahiyo bado hawezi kunikosesha nafasi ya kuwa na wewe. Huwezi jua Erica, labda
mimi ndio Mungu amekupangia niwe mume wako, huwezi jua ni kwanini Mungu
amenituma nikufatilie hadi nikuokoe” “Mmmh!” “Usigune Erica,
nakupenda. Mapenzi mazuri ni mtu umuone, akuonyeshe mapenzi ya dhati sio ya
kuwasiliana, nakwambia huyo jamaa atakuliza bure, wanaume wa kweli tupo.
Usihangaike kunijibu sasa ila nakupa muda ufikiria na uone jinsi gani Mungu
anataka tuwe pamoja” “Sawa, ngoja nifikirie basi” “Ila usipange
kunikataa Erica, nakupenda sana” Kisha Erica akamuomba Derick arudi
hosteli tu naye Derick alimsindikiza hadi hosteli na kumwambia, “Erica
ukiwa na kipindi cah jioni mpaka usiku uwe unaniambia tafadhali ili niwe nakuja
kukusindikiza” “Sawa” Kisha akaagana nae na kuelekea kwenye
chumba chake. Erica aliwaza sana, kwanza aliwaza kuhusu Dora
kuwa msichana aliyemuamini kuwa ni rafiki yake siku zote ndio amekuwa adui yake
namba moja hata baada ya kuacha urafiki naye, alishangaa kwakweli kuwa hata
angepatwa na matatizo Yule rafiki yake angepata faida gani, alishangaa sana. Ila
pia alifikiria kuhusu Derick kuwa atamkubali vipi wakati siku hizi mawasiliano
yake na Rahim ni motomoto, ndio Rahim ni mpenzi wa kuwasiliana nae tu ila Derick
amemsaidia sana na anadai kumpenda sana, je anamkataaje na je atakubali vipi
kuwa na mahusiano na wanaume wawili yani alijiona yupo njiapanda
kabisa. Alikuwa na kipindi, akaenda kwenye kipindi ila alipotoka alienda
kwa Tuamini maana ni siku nyingi kidogo hakuonana nae, alimkuta na wakaongea
mengi sana ila kubwa zaidi lililomshtua ni pale Tumaini alipomwambia habari za
Erick, “Yani nimefurahi kuhusu mdogo wangu Erick” “Kafanyaje
tena?” “Erick kaachana na Sia, ila sijamlaumu sabau Erick hajawahi
kumpenda Sia” Hii habari ilikuwa nzuri sana kwa upande wa Erica na
kutaka kujua zaidi “Kheee au kampata huyo msichana wake
anayempenda?” “Yule tahira, mama wa marehemu loh! Erick hawezi kumrudia
Yule mama wa marehemu hata kwa dawa. Ila huwezi amini, Erick amesema amepata
mwanamke kule Afrika kusini na wanapendana sana, amesema akirudi atarudi
kumtambulisha kwetu. Amenitumia na picha zao, inaonyesha wanapendana sana yani
Erick hataki hata kuongelea habari za mama marehemu, nimefurahi sana kwa mdogo
wangu kupata faraja ya moyo” Kisha Tumaini akafungua simu yake na kuanza
kumuaonyesha Erica picha za Erick na huyo mwanamke, Erica alitabasamu tu ila
kiukweli hizi habari zilichoma moyo wake, alijihisi wivu uliopitiliza, alihisi
kama tumbo lake likiungurumisha, kiukweli alikosa raha kabisa. Muda ule ule
aliamua kumuaga Tumaini na kuondoka. Alirudi hosteli, akaenda chooni na
kulia sana, kwani ingawa alikuwa anawasiliana na Rahim ila ukweli kwenye moyo
wake ulibaki pale pale kuwa alimpenda sana Erick, “Yani Erick
nimekupigia simu hutaki kupokea, nimekutumia ujumbe hutaki kunijibu jamani Erick
kumbe ushaamua kuanzisha maisha na mwanamke mwingine? Erick, nitakuwa na
mahusiano mengi kila leo ila ukweli uko pale pale, nakupenda sana Erick,
nakupenda sana” Alikuwa akiongea mwenyewe chooni huku akilia sana kwani
hakutegemea kabisa kupata habari kama zile kuwa Erick kashaamua kuwa na mwanamke
mwingine na kapanga kumtambulisha akirudi kwao, “Kumbe ndiomana Erick
hutaki kwenu wanijue, yani hata dadako hukutaka ajue kama mimi ni mwanamke
unipendaye. Hukunipenda Erick kweli hukunipenda kabisa, umeona huko wasichana
wazuri umenisahau kabisa mimi” Alikuwa akilia huku akiwaza sana,
akajikuta kwa muda huo akimchukia hata Rahim, “Hata Rahim nae ni kama
Erick tu, sababu angekuwa muwazi kwa mama yake ila kanificha nisijulikane.
Mwanaume pekee aliyenitambulisha kwa ndugu zake ni Bahati, ila simpendi jamani.
Nakupenda Erick, kwanini umenifanyia hivi?” Kila alipokumbuka zile picha
alilia sana na kuzidi kukosa raha kabisa, alirudi chumbani na kujifunika shuka
kama mtu aliyelala ila kiukweli bado alikuwa akilia, na hapo aliweza kujua ni
jinsi gani alimpenda sana Erick na alimuhitaji katika maisha yake. Hakuwa na
raha kabisa kiasi kwamba alikuwa na kipindi kingine jioni ila hakwenda maana
alijikuta na mawazo kupita maelezo ya kawaida, alimuwaza Erick na alitoa machozi
sababu ya Erick. Erica alilia sana pale kitandani na kulala, hakutaka
wale wa kwenye chumba chake wajue ndiomana alijifunika na shuka hadi usoni, na
kwavile hakuwa na mahusiano nao ya karibu sana zaidi ya kulala nae kwenye chumba
kimoja kwahiyo ilikuwa ngumu sana kwa wao kumuuliza kuwa vipi amelala vile kwa
kujifunika na hajatoka kula. Usingizi ulimpitia pale
pale. Asubuhi kulipokucha alikuwa anapigiwa sana simu na kuamua
kuipokea, mpigaji alikuwa ni Derick, “Mbona unaongea hivyo Erica,
unaumwa?” “Hapana” “Naomba kuonana na wewe, twende basi tukanywe
chai pamoja” “Basi ngoja nijiandae” Erica aliinuka pale
kitandani na kwenda kuoga, kisha kutoka nje ili ampigie simu Derick, ila
alishtuliwa na Yule msichana wa siku ile aliyekuwa anamwambia Erica kuwa ampe
ujuzi ili na yeye apiganiwe na wanaume, “Erica
mambo” “Safi” “Mbona macho yamekuvimba hivyo?” Mbele
kidogo akatokea Derick kumfata Erica kwahiyo alimuita ili waondoke, ikabidi
Erica amuage Yule binti, “Badae Fetty” Aliondoka na kumuacha
Fetty akimuangalia tu. Derick alienda kwenye mgahawa na Erica, wakaagiza
chakula, akamuangalia Erica usoni naye alimuuliza kwa mshangao, “Mbona
macho yamekuvimba hivyo” “Aaah sijui, kwani yamevimba
sana?” “Sio sana, ila inaonyesha umelia sana. Nini kilikuwa kinakuliza
Erica, kuwa muwazi kwangu. Mimi ni muelewa sana” Erica aliinama na
machozi kidogo yalimtoka, na kumfanya Derick amsogelee na kumuuliza kwa upole
kuwa kipi kinamliza, “Sikiliza Erica, kukaa na kitu moyoni sio suluhisho
kwani kitaendelea kuumiza milele. Wote wanaojiua sio kwamba wamependa ila
hutokea sababu waliweka vitu moyoni na kushindwa wa kumshirikisha mtu mwishowe
wakaona bora wajiue wakati kama wangeeleza matatizo yao wala isingepelekea
kujiua. Usiupo moyo wako mateso ya kubeba mizigo ambayo haibebeki, unaposema
unaupa moyo wako mwangaza na uhuru yani utajikuta moyo umeachia kabisa. Usipende
kitu kikutese moyoni, niambie Erica una tatizo gani?” “Sikia Derick,
kuna mwanaume mmoja nampenda sana tena sana, yupo nje ya nchi ila nimesikia ana
mwanamke mwingine” “Pole Erica? Najua mapenzi yanavyoumiza, ila mimi si
nilikwambia, hakuna mwanaume mwenye mapenzi ya dhati anapokuwa mbali. Mimi
nikija kuoa, kama natakiwa kusafiri kikazi basi nitasafiri na mke wangu, siwezi
kumuacha mke wangu na upweke. Usijali Erica, ndio mapenzi yalivyo. Utamsahau
kabisa huyo mtu” “Hujui tu jinsi gani nampenda, nampenda sana
Erick” “Anaitwa nani?” “Anaitwa Erick” “Wow, ona sasa
Mungu alivyo mwema huyo alikuwa anaitwa Erick, na mimi naitwa Derick yani jina
langu na lake limetofautiana kwa herufi moja tu yani D. Ila Mungu ana makusudi
yake kukuletea mimi, acha huyo aende sababu hakutakiwa kuwa na wewe ila mimi
ndio mwenye sifa za kuwa na wewe Erica, yani mfute Erick kabisa katika maisha
yako na sasa muwaze Derick tu. Nahitaji ufurahi, huwa unapenda kwenda
wapi?” “Napenda kwenda ufukweni” “Basi tupange siku, twende
tukapunge upepo. Erica, mtoe Erick kabisa katika akili yako, je kuna mwingine
anayeisumbua akili yako zaidi ya Erick?” “Hapana” “Basi usijali,
Derick nipo na nimeletwa kwako ili huyo mtu asikusumbue tena mawazo yako. Mimi
ni mwanaume wa tofauti sana,najua kupenda, kujali na kumdekeza mwanamke yani
kwangu utapata ambavyo huyo Erick hajawahi kukupatia. Elewa nakupenda sana
Erica” Maneno ya Derick yalikuwa yakimuingia kwenye akili yake vilivyo
ingawa kiukweli hakudhania kama anaweza tokea mtu wa kumsahaulisha yeye kumpenda
Erick, ukizingatia ni muda mrefu ameanza kumpenda toka wako shuleni na hajaweza
kuacha kumpenda. “Sasa naomba jioni, twende kwenye mgahawa moja tukale,
ni mzuri sana yani utaupenda” Erica alikubali kisha kuagana na Derick na
kurudi hosteli, siku hii hakuwa na kipindi chuo kwahiyo alirudi tu hosteli na
kukusanya nguo zake chafu na kwenda kufua. Wakati anafua alienda Yule
Fetty na kuanza kumuongelesha Erica huku akimwambia, “Hongera sana,
sijui una kismati gani wewe mdada, majuzi tu wamepigana wakaka kwaajili yako
halafu leo nakuona unaondoka na Yule Derick” “Kwani unamjua
Yule” “Namfahamu ndio” “Unamfahamu vipi?” “Namfahamu tu,
ila anaonekana yupo romantic sana mmh hongera” Erica alicheka tu maana
hizi hongera alizokuwa anapewa wakati alikuwa akimuwaza Erick tu muda wote
huo. Alimaliza kufua na kuendelea kupiga stori tu na huyu Fetty, kwa
siku hizo mbili hakuwa na habari kabisa ya kuingia kwenye mtandao wa kijamii
wala hakutaka kujua kama Rahim alimtafuta au la, kwahiyo alikuwa tu akiongea na
Yule Fetty pale na kufurahi ili kusogeza siku tu. “Kumbe wewe Fetty ni
mcheshi sana” “Ndio, si wewe unajiweka peke yako pake yako ndiomana watu
wanaogopa hata kukukaribia” “Hapana bhana, marafiki walinitenda ndiomana
sitaki hata kuwa na marafiki wa karibu” “Ila unatakiwa kuwa na rafiki,
kuna mambo yanakupata unaona umuhimu wa kuwa na marafiki sema cha msingi ni
kuchagua marafiki wema kwako” Wakati wanaongea ongea, Derick alifika
eneo lile kwa lengo la kumfata Erica na kwenda nae alipomuahidi. “Mmmh
Derick, mbona mapema sana” “Ndio vizuri mapema” “Basi ngoja
nikajiandae” Erica aliinuka pale na kumuacha Derick akiwa na Fetty, na
baada ya muda alikuwa tayari na kumuaga Fetty kisha akaondoka na
Derick. Walikuwa wakitembea huku wakipiga stori za hapa na pale
sababu Derick alisema sio mbali sana na maeneo yale, kwahiyo waliamua kutembea.
Wakati wanaendelea kutembea, Erica alimuona mdada mmoja akija mbele yake,
akamkumbuka vizuri huyo dada ni dada yake Bahati, Yule dada alivyofika alipo
Erica alimnasa kofi, wakati Erica akigusa pale aliponaswa kofi, alishangaa kuona
akinaswa kofi upande mwingine. Wakati wanaendelea
kutembea, Erica alimuona mdada mmoja akija mbele yake, akamkumbuka vizuri huyo
dada ni dada yake Bahati, Yule dada alivyofika alipo Erica alimnasa kofi, wakati
Erica akigusa pale aliponaswa kofi, alishangaa kuona akinaswa kofi upande
mwingine. Ilibidi Derick aende mbele kwa Erica ili kumzuia Yule dada
asiendelee kumpiga kofi, “Sogea wewe kijana” Yule mdada aliongea
kwa ukali sana, “Kwani tatizo nini dada? Umefika tu na kumpiga, tatizo
ni nini?” “Wewe acha kumtetea huyo Malaya, anajua kila
kitu” Kisha Yule dada alimuangalia kwa jazba sana Erica na
kusema, “Binti mshenzi sana wewe, yani wa kumsababishia mdogo wangu
matatizo halafu anaenda jela ila wewe hujali unakula raha tu na wanaume wengine,
sogea na wewe nitakuchakaza sasa hivi” Akamsukuma Derick pembeni na
kuanza kumshambulia vizuri Erica ilibidi Derick atumie uanaume wake
kumgombelezea Erica, “Wewe kijana hujui tu, ila mwenzako akinyolewa zako
tia maji, huyo binti ni shetani wa mashetani” Kisha Yule dada
akamuangalia Erica na kumwambia, “Bado sijamalizana na wewe mwanaizaya,
siku yako inakuja mwanaharamu wewe” Yule dada akaondoka huku anasonya
sana, kiukweli hata hamu ya kuendelea kula na Derick ilimuisha Erica kwanza
alikuwa amechafuka maana Yule dada alimuangusha chini, kwahiyo akaomba kurudi
hosteli tu, ikabidi wakodi bajaji iwarudishe hosteli maana ni aibu hata
kutembea. Walifika hosteli, na kwa aibu alishindwa hata kumuaga
Derick kwani moja kwa moja alienda chumbani kwao, ila Fetty alimuona na kumfata
Derick, “Vipi tatizo nini?” “Sijui, yani kuna mwanamke
tumekutana nae njiani kaanza tu kumshambulia Erica hata sijui
kwanini” Fetty akacheka kidogo na kupiga makofi kama ya umbea kisha
akasema, “Mapenzi bhana ni kitu cha ajabu sana, yani leo unaweza
sababisha wanaume wakapigana sababu yako ila kesho unapigana na mwanamke mwenzio
sababu ya mwanaume. Mmh Derick, huyo mwanamke aliyemshambulia Erica humjui
kweli? Ni mwanamke wako” “Kwanza sikuelewi Fetty, unazungumzia
nini?” “Majuzi hapa palitokea gumzo kubwa sana, kulikuwa na vijana
wawili wanapigana na chanzo kilikuwa ni Erica halafu leo eti Erica kapigana na
mwanamke mwingine, mmmh chanzo ni wewe” “Unajua bado sikuelewi Fetty,
unamaanisha kuna wanaume wamepigana sababu ya
Erica?” “Ndio” “Mbona Erica mchumba wake yupo nje. Hao
waliopigana ni wakina nani?” “Kalagabao, umeambiwa upo peke yako? Jua
kuna wenzako msururu, yani mapenzi ya siku hizi ni ngoma droo, wewe una wanawake
msururu na yeye ana wanaume msururu” Derick hakutaka hata kuendelea
kusikiliza haya maneno, aliamua kumuaga Fetty na kuondoka zake huku akitafakari
kwa kina yale aliyoyasikia. Erica alienda kubadilisha nguo
kisha akakaa na kujitafakari ila alipaona hosteli pagumu kwa muda ule,
akajiuliza kuwa aende wapi, akaona bora arudi nyumbani kwao hata mama yake
akimuuliza maswali amdanganye tu. Kwahiyo akajitahidi na kuondoka pale
hosteli akarudi nyumbani kwao, na kama kawaida mama yake alimuuliza kulikoni
amerudi mapema yani sio mwisho wa wiki, “Mmmh mama hivi hujisikiagi
upweke kukaa nyumba yote hii mwenyewe?” “Najisikia upweke ndio ila
napenda usome” Akaamua amuanzishie mada nyingine ili mama yake
asiendelee kumuuliza kuwa kwanini amerudi nyumbani siku ya chuo. “Mama,
najiuliza sana kwa dada Mage kuna wajukuu zako ila kwanini hakuna siku uliyosema
waje kukaa hapa nyumbani kama una upweke?” “Wewe Erica, mada hizo
umeanzia wapi?” “Si nakuuliza tu mama, unajua Yule ni dada yetu tena ni
mtoto wako wa kwanza. Kukaa mwenyewe humu ndani kama mkiwa si vizuri, ila
angekuwepo hata mjukuu wako mmoja angekuchangamsha.” “Tayari
nimekuelewa” “Kama umenielewa mama, chukua hatua basi umwambie dada
alete watoto wake” “Erica, tafadhali usinipande kichwani unajua ujinga
alioufanyaga dada yako hapa? Wakati baba yenu yupo, Mage alituletea Yule
mwanaume wake, tulimkataa kabusa maana hakua anafaa, Yule dadako mjinga kuona
vile akaamua kubeba mimba na kujipeleka kukaa kwa mwanaume, ilibidi tumkubali
hivyo hivyo ila baba yenu alimkataa kabisa hata mahali yake hakupokea. Sasa
unadhani naanzaje kupokea watoto wake hapa nyumbani? Watoto nitakaopokea hapa ni
watoto wa Bite tu na wewe ukiolewa ila siwezi kupokea watoto wa
Mage” “Sasa mama, makosa tayari yalishafanyika. Hata ukiwachukia watoto
wa dada Mage bado haitasaidia kitu, kwasasa ungesema tu ni kitu gani wafanye ili
uwasamehe. Mama dada Mage ni mwanao na hilo halipingiki, kumbuka watoto wake
wana haki kwako kama bibi yao, ukiwatenga ni kuwatesa tu. Mama kwasasa ni kusema
kitu gani wafanye uweze kuwasamehe” “Sina kinyongo nao, ila nadhani
labda waje upya kujitambulisha. Nitawapokea maana baba ndio hakuwataka kabisa
ila hayupo tena, sema hata alipokuwa anakufa alisema kama wakifata taratibu
niwapokee ila mpaka leo hawajajiongeza. Ni matahira wale” “Jamani
mama” “Hata usiniambie habari zao” Erica alifanikiwa kubadilisha
mada kwa mama yake na kwenda chumbani kwake, ila pia alifanikiwa cha kumsaidia
dada yake maana alimuona kwa hakika anatia huruma maana naye alionekana kutamani
watoto wake wawe wanaenda kwa bibi yao hata likizo ila haikuwezekana sababu ya
mambo ambayo alikuwa hajamalizana na mama yao. Erica alikaa
akijitafakari jinsi yeye alivyo, akaanza kuhesabu idadi ya wanaume aliokuwa nao
na kuangalia wapi alipokosea, “Nilikuwa na Babuu ila huyu alinisaliti,
alienda kwa wanawake zake akasingizia kuwa aliwekwa rumande kwa uzurulaji,
nikampata George na kuamini kuwa nimempata mume wa maisha yangu ila akaniacha
sababu sikuwa bikra, akaja Bahati yani huyu mwanaume sijawahi kumpenda ila
nilimkubali sababu nilikuwa na mawazo sana ila ndio amekuwa msumari wa miba
kwenye maisha yangu. Alikuja mwanaume niliyempenda kupita kiasi, sikuweza
kumkataa sababu nilimpenda sana ila Bahati ndio kaniharibia kwa huyu Erick,
kaenda kupigana nae na dada zangu nao wamechangia kwa kunitoa mimba ila
ningekuwa nayo hadi leo kwa hakika kusingekuwa na mahusiano mazuri ya mimi na
mama yangu sababu anasisitiza nisome siku zote. Haya sasa, Bahati imemkataa,
George nae nimemkataa ila wamejifanya wamepigana kwasababu yangu mwisho wa siku
wananipangia kunibaka mara dada yake Bahati anipige na kusema nitaona, kwani
kosa langu nini jamani? Mbona wananifanyia hivi jamani mpaka najihisi
vibaya” Aliwaza sana yani kwa muda huo hakutaka kumtafuta yeyote Yule na
hakutaka mawasiliano na yeyote, alipanga kwenye akili yake kuwa kesho yake aende
kwa dada yake Mage bila ya kumwambia mama yake maana atamuaga kuwa anaenda chuo,
kwa muda huo alichukua simu yake na kuizima kwani hakutaka kupatikana hewani
kabisa. Muda wa kulala ulipofika akalala, na kulipokucha aliamka na
kujiandaa kwaajili ya kwenda kwa dada yake kama alivyopanga, “Utakaa
huko huko chuoni au utarudi nyumbani?” “Nitarudi mama” Aliondoka
zake na safari yake kama alivyopanga alienda moja kwa moja kwa dada yake, kwa
muda huo alimkuta dada yake pekee maana watoto wa dada yake walienda shule na
shemeji yake alienda kwenye shughuli zake, alizungumza na dada yake vile
alivyoongea na mama yao. “U na uhakika mama atatukubali tukifata sharia
tu?” “Mama kasema, mkifata sharia atakubali yani nyie ni kujiongeza tu
ila usimwambie kabisa kama mimi ndio nimekwambia” “Asante mdogo wangu,
sikuwahi kufikiria kama ungekuwa na busara kiasi hiki, anachojua Bite ni
kuniletea mashtaka tu ila hajawahi kufikiria kuwa naweza kupatana tena na mama
kiasi cha kuwakubali wanangu maana huwa nakuja kumsalimia tu, ila umenipa
muangaza mdogo wangu kwani hata wanangu nina uhakika watapenda kuwa karibu na
bibi yao” “Usijali dada, tuko pamoja. Nakupenda dada yangu na pia
napenda kushirikiana nawe. Ila leo naomba unijibu na mimi nawezaje kumjua
mwanaume anayenipenda?” “Ngoja nikwambie kwa ufupi tu ila ipo siku
nitakufundisha kwa undani zaidi” “Niambie dada hata hiyo kwa ufupi
nitaridhika” “Yani mdogo wangu ipo hivi, mtu anaweza akawa na pesa
kupindukia ila asiwe na mapenzi ya dhati na mwingine akawa na pesa na mapenzi ya
dhati akawa nayo, ila kuna mwingine ni masikini kabisa ila akawa na mapenzi ya
dhati hadi ukaogopa, sasa kuna namna ya kumjua mtu mwenye mapenzi ya
dhati” “Namna ipi hiyo dada?” “Mtu anayekupenda kwanza kabisa
anakujali, anachukulia tatizo lako kama lake, anapenda kukuona ukiwa na furaha,
na ukiwa na huzuni atatafuta namna ya kukufanya usijisikie vibaya. Hawezi
kukuchukia sababu ya mapungufu yako, na atakusaidia kurekebisha tabia yako kama
haiko sawa, mtu wa hivi ana mapenzi ya dhati kwako, hapendi kuona
ukiumia” “Mmmh dada sikuelewi” “Hunielewi sababu kichwa chako
kinafikiria vitu vingi sana, nina uhakika hapo unajiuliza kuwa uliyenaye ana
mapenzi ya dhati kwako?” “Umejuaje dada?” “Nimejua tu, haya
niambie uliyenaye ana sifa gani?” “Mmmh kusema ukweli dada hata
sijielewi, ila kuna kijana simpendi kabisa ila ananifatilia huyo hadi kero yani,
hata anikute nimesimama na mwanaume mwingine ananifatilia, ila
simpendi” “Ila hilo ni tatizo, ingekuwa unataka kuolewa ningekwambia
utajifunza kumpenda ndani ya nyumba, ila nadhani ni vyema ukimleta nimfahamu
huyo kijana, nitakwambia kama anakufaa” Erica alimuahidi dada yake kuwa
atampeleka huyo kijana, kisha muda huo akajiandaa kwenda tena chuoni ila alitaka
akaangalie tu mambo yameendaje maana hata kwa siku hiyo hakuwa na kipindi
kabisa. Wakati anaingia chuo, aliitwa na kugeuka alimuona
Derick, ambaye alimsimamisha na kumuuliza, “Na mbona jana hukupatikana
hewani?” “Simu yangu ilizima chaji” “Ila nilikuja hosteli
hukuwepo” “Nilienda nyumbani” “Erica, mbona umekuwa na majibu ya
mkato hivyo kwani nimekufanya nini?” “Hujanifanya
chochote” “Erica, ningekuwa na hasira nawe kwa hakika nisingekutafuta
tena, kwanza ulinidanganya kuwa ni mwanaume mmoja tu uliyekuwa naye kumbe kuna
wengine walipigana hosteli. Ila Erica mimi sitaki kupigana na yeyote Yule, yani
sitaki niwe na ugomvi na yeyote Yule. Kila kitu kifute katika maisha yako na
tuanze kurasa mpya ya mapenzi, nakupenda Erica, na napenda tuwe pamoja mpaka
mwisho. Sitakuchukia kwa lolote lile maana kwangu ni kama changamoto tu, na
kwavile nakupenda basi nataka niwe nawe milele” Erica alikuwa kimya tu
akisikiliza maneno ya huyu Derick ambaye alikuwa akimchombeza
vilivyo, “Erica haijalishi ni wanaume wangapi wamepita kwako na
haijalishi wamefanya nini kwako ila bado swala litabaki palepale kuwa nakupenda
sana” “Nimekuelewa Derick, naomba tuongee badae kwasasa kuna mambo
nayaweka sawa” Wakaagana na Derick huku akimuahidi kumfata badae
hosteli, wakati akiwa pale chuoni akakutana na Tumaini tena na kusalimiana
nae, “Jamani Erica uliondoka gafla juzi hadi sikukuelewa kabisa, ila
unaendeleaje mdogo wangu” Kabla hajamjibu, simu ya Tumaini ikaanza kuita
na Tumaini akamwambia Erica asubiri kidogo aongee na ile simu kwahiyo Erica
alikaa pembeni akisubiri Tumaini amalize kuongea na ile simu. Tumaini
alipomaliza kuongea na ile simu alionekana kuwa na furaha sana kiasi kwamba
Erica ilibidi amuulize kuwa kitu gani kimemfurahisha, “Yani Erick
kanipigia simu, na kanipa huyo msichana wake niongee nae jamani ana sauti nzuri
huyo dada balaa, anaitwa Jack. Oooh natamani nimuone huyo wifi yangu, nimefurahi
sana” “Kwahiyo ndio yupo nae muda huu?” “Ndio, anasema Yule dada
kamwambia mpigie wifi yangu simu ndio kanipigia, jamani nimefurahi sana yani
mdada yupo vizuri Yule duh sauti yake tamu hiyo, kwakweli mdogo wangu kabahatika
jamani” Tumaini hakujua kuwa kadri alivyokuwa akisifia kuhusu Yule
msichana wa Erick ndivyo alivyozidi kuumiza moyo wa Erica maana muda huo huo
Erica aliamua kumuaga kuwa anawahi kipindi ila haukuwa ukweli, kwani alipoondoka
pale alijifanya kama anaenda kwenye kipindi ila mbele yake alikatisha na kuanza
safari ya kutoka chuo kwani moyo wake ulikuwa na maumivu sana kwa muda
huo. Wakati anatoka pale chuo alishikwa bega, na aliyemshika
alikuwa ni Derick alijikuta akimkumbatia kwa kilio, na kumfanya Derick atambue
kuwa lazima atakuwa ana matatizo na kumfanya ampe ushauri, “Twende
mahali Erica” Derick alikodi bajaji na kuondoka eneo lile na
Erica. Moja kwa moja alienda na Erica ufukeni na kuanza kuongea nae
maneno ya kumpa faraja, “Najua una matatizo Erica, name nimejitolea
kubeba matatizo yako kama yangu. Niambie sasa kinachokusibu ni nini au bado ni
kuhusu Erick?” Erica alitikisa kichwa huku akiendelea kulia, Derick
alijitahidi kumpa maneno ya faraja sana mpaka giza liliwakutia
palepale, “Erica, naomba usirudi hosteli kulala ila twende mahali
tukacheze, tufurahi usahau kila kitu” “Wapi huko?” “Twende
club” “Hapana, sijawahi kwenda club maisha yangu yote. Kwanza kucheza
sijui” “Sio wote wanaoenda disko wanajua kucheza ila hata ile midundo na
mziki ukiusikiliza unakuliwaza, twende club Erica tafadhali, hautacheza, tutakaa
tu mahali tukitazama watu” “Basi, ngoja nirudi hosteli nikabadilishe
nguo ila hata mavazi ya club sina” “Hata usiumize kichwa, vaa tu suruali
na tisheti basi” Kisha akaondoka nae hadi hosteli kujiandaa, ambapo
Erica alioga na kuvaa alivyoshauriwa kisha kutoka na kuondoka na Derick, ambapo
alienda nae kwanza sehemu ya kula ili kupoteza poteza muda. “Mpaka saa
hizi?” “Ndio, club pananoga muda ukienda enda.Twende
sasa” Walienda disko, kwakwelki ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Erica
kujishuhudia watu wakiwa disko na kucheza maana siku zote alisikia tu kwenye
stori ila siku hiyo alijionea mwenyewe, walifika mahali na kukaa kisha Derick
akaagiza vinywaji, Erica akadakia “Mimi nataka soda” “Erica my
dear, humu hakuna soda” “Basi mimi sinywi, situmii pombe
kabisa” “Kwanini hutumii pombe?” “Sababu ni
chungu” “Aaah sasa kuna kinywaji kimoja hivi kinaitwa Reds kipo humu
yani hata sio kichungu na wala hakina mandhari ya pombe, ngoja nikuagizie
ukijaribu” Basi Derick akamuagizia Erica kile kinywaji na kweli Erica
alikunywa na kkukipenda, akajikuta anakunywa tu huku akifurahia mziki
unavyopigwa na watu wanavyocheza, ilikuwa kikiisha tu Derick anaita kingine
kwahiyo Erica alikunywa sana na akaanza kujihisi kizunguzungu huku mara nyingine
akilia peke yake, mara amkumbatie Derick na kumwambia anampenda yani pombe
ilianza kufanya kazi kwenye akili yake. Derick aliamua kutafuta chumba
maeneo yale ya karibu ili akapumzike na Erica. Kulipokucha,
Erica alijikuta yupo kifuani mwa Derick akiwa hana nguo kwamaana kwamba alifanya
mapenzi na Derick, kiukweli alichukia sana na kumshtua Derick, “Ndio
umefanya nini na mimi sasa?” “Usinilaumu Erica, tulikuwa tumekunywa
wote, ni pombe ndio zimepelekea tukafanya hivi” “Ulijua fika ndiomana
ukanishawishi mimi ninywe zile pombe” “Ila usijali Erica, huu ni mwanzo
mzuri wa mahusiano yetu” “Kwenda zako huko” Erica aliinuka na
kuanza kuvaa nguo zake, “Tukaoge basi mpenzi” “Achana na mimi,
nitaenda kuoga hosteli” Ila akajifikiria akaona ni vyema akaoge kuliko
kutembea na mijasho ya mtu mwingine, alienda na nguo zake chooni na kuoga kisha
akavalia huko huko. Alipotoka alimkuta Derick ameshavaa, “Mbona wewe
hujaenda kuoga?” “Nataka niwe nanusa jasho lako mwilini mwangu muda
wote” Erica akamsonya Derick kisha kutoka kwenye kile chumba, Derick
alitoka na kufatana na Erica kwa nyuma hadi kwenye kituo cha daladala ndipo
alipogundua yale maeneo ni karibu na kwa dada yake Mage, uoga ulimshika wa
kukutana na dada yake, ila jambo la bila kutarajia dada yake alitokea mbele
yao, “Kheee Erica, unakuja kwangu kwa kunishtukiza hivi, umeniletea na
mgeni jamani! Kwanini hukuniambia?” Kisha akamuangalia Derick na
kumwambia, “Khee Derick umekuwa jamani, karibuni nyumbani. Kweli damu
nzito kuliko maji yani Erica na Derick mmekumbukana? Karibuni sana
nyumbani” Erica alipigwa na mshangao kwa muda kidogo maana alijiona
haelewi kabisa, kuwa Derick ni ndugu yake kwakweli
hakuelewa. Kisha akamuangalia Derick na
kumwambia, “Khee Derick umekuwa jamani, karibuni nyumbani. Kweli damu
nzito kuliko maji yani Erica na Derick mmekumbukana? Karibuni sana
nyumbani” Erica alipigwa na mshangao kwa muda kidogo maana alijiona
haelewi kabisa, kuwa Derick ni ndugu yake kwakweli hakuelewa. Mshangao
aliokuwa nao Erica ni sawa na mshangao aliokuwa nao Derick, huyu mdada
alimfahamu ila Erica hakumfahamu hata akashangaa kuwa undugu wake na Erica
umetokea wapi, kisha Mage ndio akawaondoa kwenye mshangao na kuwaambia kuwa
wakaribie nyumbani kwake. Waliongozana na Mage hadi nyumbani kwake, muda
wote si Erica wala si Derick aliyekuwa akiongea chochote zaidi ya
Mage. Alifika nao nyumbani kwake na kumwambia Derrick, “Derick,
hapa ndio nyumbani kwangu. Jisikie upo huru, najua siku zote ulijiuliza kuwa
Yule dada anaishi wapi, ila naishi hapa. Karibu sana” Akashukuru na
kisha Mage kuwauliza, “Mmekutana wapi jamani na mmekumbukana vipi?
Nakumbuka mara ya mwisho nyie kuonana mlikuwa wadogo sana, toka hapo Derick
hukuweza tena kufika kwetu. Sasa sijui mmefahamiana vipi? Najua utajiuliza kuwa
kwanini mimi sijafika kwenu kwa siku nyingi ila mamako alihama bila hata ya
kuniambia, ila upendo wangu upo pale pale. Kwakweli Mungu mkubwa jamani,
mmefahamiana vipi?” Muda wote Erica alikuwa kimya kabisa, ila muda huu
aliamua kumuuliza dada yake kwa mshangao, “Dada, mimi na huyu Derick
tunasoma chuo kimoja ndio tulikofahamiana, ila huo undugu na huyu uko vipi maana
hata sielewi” “Kwahiyo hamkuwa mnakuja kwangu eeh!” “Ni kweli
hatukuwa tunakuja kwako” “Mlikuwa mnaenda wapi?” “Tuachane na
hizo habari kwanza dada, ila tueleweshe undugu wetu uko vipi” Erica
alitaka kujua undugu wake na Derick ukoje maana hakuelewa kabisa, “Iko
hivi, baba yetu alizaa mtooto mwingine nje yani huyu Derick kazaliwa umepishana
nae mwaka mmoja tu. Mwanzoni wakati wewe una miaka mine huyu Derick aliletwa
nyumbani ila mama alimkataa sababu hakutaka mtoto wa nje ya ndoa, ila baba
alikuwa akimuhudumia tu vizuri na ni mimi aliyekuwa ananituma nipeleke hela za
matumizi kwakina Derick, yani hadi kipindi baba anakufa alisema nimuangalie sana
Derick na ndio sababu ya mimi kwenda mara kwa mara kumuona Derick ila
sikumwambia mama kwani sikupenda ajue kuwa naendaga, nimeacha kwenda mwaka juzi
maana mama yake Derick alihama pale alipokuwa anakaa na sikuwa na mawasiliano
nae” “Kwahiyo dada unamaanisha kuwa mimi na Derick ni watoto wa baba
mmoja?” “Ndio, na ndiomana nikasema damu nzito. Yani wewe na Derick ni
baba mmoja ila mama mbalimbali, yani Derick ni ndugu yetu kwa mama mwingine,
tumechangia baba” Alishangaa kuwaona wote wakiinamia chini yani Derick
na Erica, ikabidi awaulize, “Vipi kwani, hamkupenda muwe ndugu? Nisamehe
mimi Derick nilisema ningekuja kukuchukua ufahamu ndugu zako wengine, ila sio
kosa langu, ni sababu mama yako alihama” “Ila kwanini baba hakutaka
tufahamiane?” “Erica, sio kosa la baba ni kosa la mama. Baba hakuwa na
sauti yoyote kwa mama, kwahiyo kila alichoambiwa na mama
alikubali” “Kwanini?” “Erica, hujui mambo mengi katika ujana wa
mama na baba nasikia nyumbani kwakina mama walikuwa na uwezo sana hata zile
nyumba ni mama amejengewa na wazazi wake, kwahiyo baba hakuwa na kauli yoyote,
pale mama aliposema sitaki kukiona hiki kitoto nyumbani kwangu, ilibidi atii
amri tu. Ila sio kosa lao wote, nakumbuka babu yani baba yake mama alikuwa mkali
sana na alimwambia mama asikubali mtoto wa nje kwenye nyumba aliyojenga yeye.
Nakumbuka baba aliniomba nifanye siri hata swala la kumtembelea Derick na
kupeleka hela ya matumizi, ndiomana hata baada ya kifo cha baba bado haikuwa
rahisi kwa mama Derick kuja kudai mirathi ya mwanae” Kwa kiasi Fulani
Erica alisikitika na Derick nae alisikitika, ila dada yao Mage aliendelea
kuzungumza, “Ndiomana mama habari zake huwa anasisitiza watoto wake
kuolewa na wanaume wanaojiweza maana anasema kuwa mwanaume kudharauliwa na ukoo
inauma sana, inasemekana ukoo wa mama walimdharau sana baba” Derick
alitokwa na machozi maana zile habari kuwa baba yake alidharaulika zilimuumiza
na kilichomuumiza zaidi ni kitendo chake cha kutembea na dada yake bila ya kujua
alijihisi maumivu sana moyoni, dada yao hakuelewa ila wadogo zake waliinama
chini kwa muda na kushindwa kuongea chochote. Derick aliinua kichwa na
kuamua kumuaga dada yao kuwa anawahi chuoni, Erica nae alimuaga dada yake. Mage
hakuwaelewa kwakweli ila yeye aliendelea kuwakaribisha tu nyumbani kwake, na
kuchukua mawasiliano ya Derick pamoja na mawasiliano ya mama Derick ila Derick
aliinuka kuondoka mpaka pale Mage alipomsimamisha kuwa awasindikize wote,
walipofika stendi walipanda gari moja ila hakuna mmoja aliyemuongelesha
mwenzie. Mage aliwaacha wamepanda gari ila hakuwaelewa kwakweli kiasi
kwamba alijiuliza maswali mengi bila majibu. Erica alifika
njiani na kushuka kwenye lile gari kwani alipanda gari la kwenda kwao, ila
Derick hakumuuliza chochote kile Erica. Alienda hadi kwao na kukuta mama
yake ametoka, alitulia akimsubiri kwa hamu kwani alijikuta ana maswali mengi
sana kwa mama yake bila hata majibu, alijiuliza kuwa hata kama babu yao alikataa
yeye alitakiwa awe na uamuzi wa mwisho, kwanini amfanyie hivyo mtoto wa baba yao
asiye na hatia? Alikosa jibu kwakweli, pia alimlaumu baba yao kuwa walikuwa na
haki ya kufahamiana hata kwa siri na sio kufahamishwa kwa mtoto mmoja
tu. Alimsubiria mama yake afike kwa hamu sana, na baada ya muda kidogo
mama yake alifika na kumshangaa sana kuwa vipi yupo nyumbani muda wa kuwa
chuo, “Mama, sina hata hamu ya kuwa chuo ndiomana
nimerudi” “Kivipi?” “Nimekutana na mtoto mmoja anaitwa Derick,
kumbe ni mtoto wa baba jamani? Kwanini hukuniambia?” “Kwahiyo kukutana
na mtoto wa baba yako sijui ndio kukukoseshe hamu ya kuwa
chuoni?” “Hapana mama” “Ila nini?” “Mama, dunia ina
mambo mengi sana kama watoto tunapaswa kufahamiana maana kuna leo na kesho,
naweza patwa na matatizo au yeye akapatwa na matatizo tukashindwa kusaidiana
kumbe ni ndugu, ilitakiwa tufahamiane. Na ni nyie ndio wazazi wa kutufahamisha
watoto wenu” “Erica, usiwe unaongea kama unatapika kama kitu hujui bora
kuuliza kuliko kunipa lawama za kijinga” “Nisamehe mama, ila ningependa
kujua” “Najua sasa umekuwa na unaweza kuelewa, baba yenu nilimpenda tena
nilimpenda sana na yeye alinipenda sana. Aling’ang’ania kutaka kunioa ila kwetu
walimkataa sababu ukoo wao hawakuwa na hela za kutosha ila mimi nilimpenda na
kung’ang’ania kuwa wakubali niolewe. Ikawa wamekuja kwetu na kukubaliwa kunioa,
wakatajiwa mahali, ila ilikuwa ni kubwa sana kwa upande wa baba yenu ila kuna
kitendo nilifanya nyumbani. Babu yangu mimi alikuwa na ng’ombe wengi sana,
nilitumia kumlaghai Yule mchunga ng’ombe hadi nikafanikiwa kuuza ng’ombe watano,
kisha pesa nilimpelekea baba yenu na kufanikisha swala la mahali hadi swala la
kuoana. Baba hakutaka niishi kwenye mazingira magumu alinizawadia nyumba na
kiwanja. Nyumba hii alinijengea mwenyewe alisema niishi kwenye nyumba ya kisasa,
kwahiyo nyumba aliyonizawadia tulipangisha pia na tukaweza kujenga nyingine
mbili hapo na kupangisha. Nilimpenda baba yenu, nilimuamini na nilifanya
chochote alichotaka ila alinichefua siku moja nilipoletewa mtoto hapa nyumbani
kwangu kuwa kazaa na mwanamke mwingine. Nilijiuliza hivi huyu mwanaume kakosa
nini kwangu? Kama watoto nilimzalia, wakike kwa wakiume, kwakweli kama
nisingekuwa nimezaa na baba yenu ningemkimbia. Kwakweli hakuna cha kusema sijui
masikini ana mapenzi ya dhati, baba yenu alikuwa masikini na nilimpenda na
kufanya chochote alichosema ila bado alinisaliti ndiomana huwa nawaambia watoto
wangu sitaki mwanaume masikini hapa kwangu.” Kwa kiasi Fulani maneno ya
mama yake yalimuingia akilini, ila mama yake aliendelea kuongea “Hivi
mwanaume nimsaidie, nimzalie watoto, nilee watoto halafu aniletee mtoto kazaa
wapi sijui nilee. Samahanini sana huo upuuzi siwezi kufanya, nilisikia ushauri
wa baba yangu kuwa nyumba yake asikae mtoto wa kufikia, nilimwambia baba yenu
kama kidume basi ajenge nyumba ya kuweka hao watoto wake aliowaokota kwenye
umalaya. Toka kipindi hiko nilimchukia baba yenu yani nilikuwa nae tu sababu ni
mume wangu, nikikumbuka vijana wengi walinitaka enzi za ujana wangu, vijana
waliokuwa na pesa zao ila sikuwakubali sababu ya kuamini kuwa yeye atakuwa
muaminifu kwangu. Wanaume uhuni wameumbiwa” “Kwahiyo mama, hukumpenda
baba hadi amekufa?” “Niavche Erica. Si kweli. Upendo ulipungua ila
haukutoka kwani siku zote atabaki kuwa mwanaume niliyempenda sana, na hakuna
pigo nililopata maishani kama kifo cha baba yenu. Ukizingatia hapa mwishoni ndio
alianza kujitahidi kweli kusaka pesa ila ndio hivyo akafa. Nikikumbuka kifo cha
baba yenu naumia sana” “Ila mama kwanini baada ya kifo cha baba
usimuenzi kwa kututambulisha kwa huyo mtoto wake?” “Erica, mama wa huyo
mtoto hajawahi kuwa karibu na mimi wala baada ya kifo cha mume wangu bado
hakuweza kujileta kwangu ili tumalize tofauti zetu. Siwezi kujipendekeza mimi
sio mwenye shida, aje mwenyewe kumleta mwanae ajuane na watoto
wangu” Erica hakuwa na maswali zaidi kwa mama yake kwani aliona hata
akiendelea kumuuliza ni kazi bure kwani mengi
ameshajibiwa. Erica alienda chumbani kwake, alioga na
kubadilisha nguo. Alikuwa akitafakari sana vitu ambavyo hakuwa na majibu navyo,
alitafakari sana kuhusu mapenzi. “Nimetembea na kaka yangu sababu ya
mawazo ya mapenzi, najuata kufanya vitu bila kufikiria na kusema ukweli siwezi
kabisa. Hivi Yule Bahati ananipenda kweli? Mama kasema wanaume wote ni wasaliti
haijalishi ni tajiri au ni masikini, ukiangalia Rahim ameshindwa hata
kunitambulisha kwa mama yake, mmh ananipenda kweli? Ila yote ni Erick wangu
jamani, kaamua kweli kuwa na mwanamke mwingine? Hapana jamani, Erick nakupenda,
nimetembea na kaka yangu mimi hata sijui nitamuangaliaje?” Aliwaza sana
ila aliona kichwa kikimzunguka tu, leo alipigiwa simu na namba mpya,
alipoiangalia ilikuwa ni namba ya nchi nyingine, akapokea, “Erica, mimi
ni Rahim. Mbona kimya hivyo mpenzi? Nini nimekukosea?” “Hujanikosea
chochote kile Rahim, ni masomo tu yalinibana” “Ila ukiwa na tatizo
lolote niambie Erica, nipo kwaajili yako” “Sawa Rahim,
nimekuelewa” “Naomba tuwasiliane basi
Facebook” “Sawa” Erica alikata simu ya Rahim ila kiukweli kwa
muda huo kama angepigiwa simu na Erick basi angejisikia vizuri sana, lakini
haikuwa hivyo aliamua kuwa mpole tu na kwenda kujilaza kwani alikuwa na mawazo
kupitiliza. Alilala sana siku hiyo yani kuja kushtuka ni usiku wa saa
tatu na kichwa chake kilikuwa kizito sana, akatambua kuwa hata kula hakula,
akamsikia tu mama yake akimuita kwa kulalamika, “Wewe mtoto ndio kuchoka
gani na masomo huko jamani, yani unalala kama mzigo hadi unapitiliza.
Nishakuamsha sana hadi nimetamani nikaite daktari, hebu amka ule” Erica
alijinyoosha nyoosha na kwenda kula ila alikula kidogo sana kwani alihisi mwili
kuchoka vilivyo, alimaliza na kwenda tena kuoga kisha kurudi
kitandani, “Itakuwa Yule mwanaume jana alinipindua pindua vilivyo, mmh
Mungu wangu ni kaka yangu eti! Aibu hii sijui nitaiweka wapi” Akashangaa
kuona Derick akimpigia simu, ila kwa uoga na aibu akaipokea “Erica,
naomba tusameheane ila sio kosa langu na wala sio kosa lako, sijui ni namna gani
ya kukutazama tena ila sitaki kuamini kuwa wewe ni dada yangu” “Derick,
sisi ni ndugu kweli. Ni wakati kwa wazazi wetu kuwa pamoja na kutukutanisha ila
kwa kilichotokea kwetu naomba ibaki kuwa siri yetu” “Hata mimi nilitaka
kukwambia hivyo hivyo, sikulala na wewe kwa kutaka Erica ila ni pombe ndio
zilipelekea kufanya vile naomba unisamehe ila ibaki kuwa siri yetu
milele” “Sitamwambia yeyote siri hii, kwanza ni aibu sana yani nililala
na ndugu yangu? Hapana sitaki kuamini kabisa, naomba tusionane Derick hadi mambo
haya yakae sawa” “Nimekuelewa Erica” “Siku tukija kuonana iwe
kama dada na kaka yani kama hakuna kitu kilichotokea kati yetu tusahau
kabisa” “Ni ngumu kusahau ila nitajitahidi” Simu ilikatika ila
Erica alizidi kuwa na mawazo yani kuna vitu alikuwa akijiuliza bila ya kupata
majibu, “Baba kuwa na mtoto mwingine si vibaya wala si dhambi, mimi
kumfahamu mtoto wa baba si vibaya kwani ni ndugu yangu ila kwanini mimi na
Derick tufahamiane kwa njia hii? Kwanini Derick anipende dada yake? Hivi
hapakuwa na njia nyingine ya kunifahamisha mimi kwa Derick zaidi ya njia ya
kufanya naye ngono? Sielewi jamani yani sielewi kabisa, hivi Derick alianzaje
kuwa na hisia na dada yake jamani? Aaah Erica mimi yani kuna muda hata sijui
nifanyeje” Alijiona tu hana raha, na akakumbuka kuwa Rahim alimwambia
awasiliane nae facebook ila hata hakuwa na hamu ya kufanya hivyo maana bado
akili yake ilizingirwa na mambo mengi sana. Akaamua kulala tena
tu. Kesho yake akajiandaa na kwenda chuoni ila kiukweli
hakupanga kabisa kuonana na Derick, kiasi kwamba alikuwa akimaliza kipindi tu
anarudi kwao yani hata harandirandi maeneo ya chuo kwani bado aibu na dhamira ya
moyo wake vilimsuta. Akiwa nyumbani, akaingia facebook ili aweze
kuwasiliana na Rahim atulize mawazo yake, akakuta kuna jumbe alitumiwa na
Tumaini, kufungua jumbe zile zilikuwa ni picha zikimuonyesha Erick na huyo
mwanamke wake mpya, kisha Tumaini akamuandikia ujumbe, “Huyo ndio wifi
yangu, mwanamke mpya wa Erick yani kwangu ni raha tu kila siku” Erica
hakujibu ule ujumbe kwani ulikuwa ukimkera tu, alijiuliza kuwa pengine huyu
Tumaini anamfanyia makusudi, “Mmmh lakini haiwezekani maana hanijui
jamani kama ni mimi niliyekuwa na mahusiano na Erick, anawezaje kunifanyia vitu
vya kuniumiza moyo? Itakuwa anajisikia tu” Ila aliona cha muhimu ni
kuacha kabisa kuwasiliana na Tumaini kwenye mtandao wa kijamii ili asiendelee
kuumiza kichwa chake kwa picha za Erick na mwanamke wake. Alikaa vile
vile mwenye mashaka moyoni kwa mwezi mzima yani anaenda chuo na kurudi kwao,
hakutaka kulala hosteli kabisa kwani alihisi kama akilala hosteli huenda
akaonana na Derick. Siku hiyo akiwa nyumbani, chumbani kwake, mama yake
alienda kumuita “Erica, Yule muuza samaki amekuja tena
kuulizia” Erica moyo ulilia paaa kwani alijua kwa vyovyote vile ni
Bahati, na kweli alitoka na kumkuta Bahati, kwa kipindi chote hiko alijiona
amepumua kwa Bahati na wala hakujua kama Bahati angejitokeza tena katika maisha
yake. Akamvutia nje Bahati ilia aongee nae, ambapo walivyotoka tu nje
Bahati alianza kwa kulalamika, “Kwakweli Erica ulichonifanyia sio haki
kabisa, mimi nilifungwa kwaajili yako ila wewe hata siku moja ya kuja kuniona
hakuna? Hata kutaka kujua kuwa kipi kilinikuta hakuna? Erica kweli unanifanyia
hivi binadamu mwenzio?” “Bahati, kwanza pole ila na wewe hujui kuwa
ugomvi wako pale hosteli umenisababishia matatizi gani mimi. Unaniona sikai tena
hosteli sababu ya ukorofi wako ulioufanya yani hadi napaona hosteli kama kituo
cha polisi. Hapana kwakweli” “Ila Erica bado nakupenda” “Kheee,
wewe mwanaume hivi umerogwa au?” “Nimekuletea na samaki,
hizi” Bahati akachukua mfuko aliofika nao ulikuwa na samaki akamkabidhi
Erica, ila Erica alipopokea tu ule mfuko gafla akajihisi kichefuchefu cha hali
ya juu na kwenda kutapika sana. Bahati alishangaa na kuuweka ule mfuko
wenye samaki pembeni, “Bahati, ondoka na samaki zako
sizitaki” “Kwani una matatizo gani Erica? Mbona samaki huwa unazipenda
tu” “Nimekwambia ondoka na samaki zako” Ila Bahati hakukubali
bali alienda tena ndani kwakina Erica na kuacha ule mfuko wake wa samaki mezani
kisha akatoka nje alipo Erica huku akimpa ushauri kuwa waende
hospitali, “Hospitali nikafanye nini? Kwani kutapika ndio kuumwa? Labda
ni minyoo” “Sawa, ila hata kama ni minyoo Erica unatakiwa
kupima” “Aaah na wewe hebu achana na mimi, tutaongea siku nyingine kwa
muda huu naenda kupumzika ndani” Erica alionekana kuchukizwa kabisa, na
kwenda ndani kwao ikabidi Bahati aondoke tu. Mama yake Erica
alishangaa kukuta mfuko wa samaki mezani, “Yani Erica umeshindwa hata
kuwashughulikia hawa samaki jamani! Yani umeletewa na kuwaacha hapa
mezani?” Erica alienda kuwachukua kwa kinyaa sana ili akawashughulikie,
ila kabla ya kufanya chochote alitapika sana mpaka mama yake akaenda
kumdaka, “Una tatizo gani Erica” “Najisikia vibaya tu
mama” “Basi twende hospitali” “Ngoja nikajiandae” Erica
aliingia ndani kama anajiandaa kwaajili ya kwenda hospitali ila alifika
kitandani na kujilaza, na usingizi ukampitia pale pale. Mama yake alisafisha
wale samaki na kuwapika ila Erica alikuwa bado kalala, ikabidi hadi mama yake
amuamshe ila alidai ni uchovu tu wala hajihisi vibaya kiasi cha kwenda
hospitali. Ila kesho yake aliamua kwenda mwenyewe hospitali kupima
minyoo, ila daktari alimshauri wapime na ujauzito. Majibu yalipotoka
yalionesha kuwa Erica ana mimba, yani swala hilo likaichanganya kabisa akili
yake. Ila kesho yake aliamua kwenda mwenyewe hospitali
kupima minyoo, ila daktari alimshauri wapime na ujauzito. Majibu
yalipotoka yalionesha kuwa Erica ana mimba, yani swala hilo likaichanganya
kabisa akili yake. Daktari alimuangalia sana kwa makini Erica alivyokuwa
amechanganyikiwa, akamuuliza, “Vipi hukutarajia
au?” “Sikutarajia dokta na hata sijui nifanye nini mimi!” “Kama
huna mpango na hiyo mimba nakushauri utoe” Yani huu ushauri ulipenya
vilivyo kwenye akili ya Erica na aliona kuwa unamfaa sana, akamuangalia dokta
kwa makini na kumuuliza, “Kwahiyo inawezekana kutoa?” “Ndio,
inawezekana, ila kuna gharama zake” “Shilingi ngapi” “Sababu
mimba yako ina zaidi ya wiki nne ni laki moja na
nusu” “Duh!” “Ndio, hivyo. Kutoa mimba ni gharama, nenda jipange
ila usichelewe sana maana kadri inavyozidi kukua ndivyo gharama
inavyoongezeka” Erica alimuaga Yule dokta ila kiukweli alikuwa
kachanganyikiwa na hakujua hata aanzie wapi na aishie wapi, akijangalia hakuwa
na hela hiyo kwa kipindi hiko na hakujua ni wapi ataipata. Akasogea mahali na
kuamua kumpigia simu Derick na kumuomba kuwa waonane siku hiyo ana mazungumzo
nae. Walikutana na Derick ila hata Derick aliweza kuona mashaka
aliyokuwa nayo Erica, alimuuliza kwa makini kuwa tatizo ni
nini, “Nimetoka hospitali kupima nimekutwa na mimba” “Una
mimba?” “Ndio nina mimba” “Ya nani?” “Ya kwako
Derick” “Yani siku moja tu erica ndio upate mimba kweli? Haya sasa
tunafanyaje” “Nataka kutoa” “Kutoa? Unajua kama kutoa mimba si
vizuri!” “Haya ngoja nikuulize, mimi na wewe ni ndugu, je huyo mtoto
atatuitaje unajua mambo mengine yalifanywa bila ya kufikiria! Naomba sapoti yako
Derick, nisaidie nitoe hii mimba” “Sasa mimi nitakusapoti
vipi?” “Unipatie hela nikatoe, dokta kaniambia ni shilingi laki moja na
nusu” “Kheee laki na nusu? Hela yote hiyo, si bora uzae tu. Kwanza sina
hiyo hela” “Sasa kama laki na nusu ya kutolea huna, hiyo hela ya kulea
mtoto utakuwa nayo? Umeniharibia maisha yangu Derick halafu unagoma hapo,
unataka ndugu zetu wajue kama tulikuwa na mahusiano” “Ila Erica, hebu
kuwa mkweli basi hiyo mimba ya nani? Yani mimi siku moja tu nikupe mimba
kweli?” Erica aliona huyu Derick anamfanyia masihara wakati yeye
alishachanganyikiwa na swala lile la mimba, alimuangalia kwa gadhabu sana na
kumwambia, “Hivi aliyekwambia mimba inaingia ukifanya mapenzi wiki nzima
nani? Mimba inaingia siku moja tu na wakati mmoja” “Kama ndio hivyo basi
zaa halafu nitaangalia mtoto kama atafanana na mimi” “Katika watu
waliowahi kunichefua katika maisha yangu, wewe ni namba moja.
Kwaheri” Erica aliondoka zake, alisimamisha bodaboda na kwenda kwao huku
ana mawazo tele akiwaza kuwa atafanya nini na ile mimba maana hakutaka mama yake
ajue na hawezi kwenda kumuomba hela dada yake Bite maana atauliza tu kuwa hela
ya nini, alihisi kuchanganyikiwa kabisa. Usiku ulifika ila
hakuwa na usingizi, mawazo yalijaa kwenye akili yake maana aliwaza kuhusu ile
mimba, yani kwa akili iliyojaa kichwani mwake ni kutoa tu ile mimba na si
vinginevyo. Alichukua simu yake na kuingia facebook, akamuona Rahim yuko
hewani akaamua kumtumia ujumbe, “Nina shida na laki moja na
nusu” Akaituma kisha akaizima kabisa simu huku akiwaza maswali
kadhaa, “Lazima ataniuliza ya nini, sijui nitamjibu vipi mimi? Akisema
sina, oooh nitakuwa nimeumbuka mimi Erica” Akachukua simu yake ya
kawaida na kuandika ujumbe mfupi, kisha akamtumia Tumaini, “Naomba
nikopeshe laki moja na nusu” Akatuma huku akiwaza pia kuwa lazima
Tumaini atamuuliza kuwa ana shida nayo ipi, na kweli ujumbe toka kwa Tumaini
uliingia ukimuuliza, “Una shida gani na hiyo hela
Erica?” Hakuweza kujibu kwani hata hakujipanga kuwa aseme ana shida ipi
na hiyo hela, badala yake akatuma ujumbe kwa dada yake Bite, “Dada,
naomba laki moja na nusu nina shida nayo” Muda kidogo baada ya kutuma,
dada yake alianza kumpigia na kumfanya ashindwe kupokea kwani bado hakujipanga
na maelezo. Ikabidi sasa aanze kujifikiria kuwa akiulizwa hiyo laki moja na nusu
ya nini atafute uongo wa kusema, alijiuliza sana na kukosa jibu. Aliamua
kutokuangalia simu yake kuwa ni ujumbe gani amejibiwa au ni nani anampigia, ila
kuna muda simu yake iliita sana na kila ilipokatika ilianza kuita tena ikabidi
aichukue kuipokea maana alipoangalia alikuwa na Bahati na akaona asipopokea Yule
Bahati hatoacha kumpigia na kama akizima simu basi dada yake atamuuliza kuwa
kwanini alizima simu, “Erica mpenzi wangu una matatizo
gani?” “Usiniulize bhana nina matatizo gani, mimi nina shida na
hela” “Shilingi ngapi unataka mpenzi wangu?” “Nahitaji laki moja
na nusu” “Duh hela yote hiyo ya nini mama?” “Kama huna sema huna
sio kuniuliza hela yote ya nini” “Erica, wewe ni mpenzi wangu na nina
wajibu wa kuhoji kuwa una tatizo gani. Hata hivyo hiyo hela sina, ila nina elfu
ishirini, naomba nikutumie huenda ikakusaidia kidogo” “Haya
tuma” Kisha Erica alikata simu, na baada ya muda kidogo alikuwa
ametumiwa elfu ishirini na Bahati, “Yani angekuwa na hela huyu
ningefaidi sana, ila sema mtu mwenyewe masikini” Alipigiwa tena simu na
Bahati na kupokea, “Hata kama hujataka kuniambia kuwa una tatizo gani,
ila nipo tayari kukusaidia. Kesho nitajitahidi kupambana na nitakachopata
nitakutumia mpenzi wangu” “Haya asante, usiku mwema” Kisha Erica
akakata simu na kulala, ila kiukweli usingizi bado haukuja kabisa maana alikuwa
akiwaza kuhusu ile mimba na atafanya kitu gani aweze kupata pesa za kuitoa,
hakuwa na marafiki wengi na wachache alionao hawakuwa na uwezo wa kumkopesha
laki na nusu, mwenye uwezo ni Tumaini ila hakuweza kumwambia tatizo lake kwani
Tumaini anapinga vikali swala la kutoa mimba. Akawaza kuwa amuulize
Johari, akaona hapana maana hapo siri zake za kutoa mimba zitajulikana,
akakumbuka kuna siku aliwahi kusikia watu wakisema kuwa kunywa majivu kunatoa
mimba. Akainuka na kwenda jikoni, akakoroga majivu kwenye kikombe na kunywa
kisha akarudi chumbani ili kusikilizia matokeo ya majivu
yale. Hadi kesho yake hakuona dalili yoyote ile na kuhisi
huenda ni dawa ya uongo au hakusikiliza vizuri kuhusu njia za kutolea mimba kwa
kutumia majivu. Akawasha tena simu yake na kuingia facebook ili kuona
kama Rahim kamjibu ila akaona hajajibiwa, akakosa raha kabisa, muda kidogo
aliona ujumbe facebook kutoka kwa Rahim, “Yani leo ndio nimeingia kwenye
mtandao na kukuta una shida na hiyo pesa, naomba kesho nikutumie kwa western
union, nitumie tu details zako Erica” Yani Erica alisoma ule ujumbe mara
mbili, hakuamini macho yake hata akawaza kuwa aandike kwanza asante au atume
taarifa zake kwanza, alihisi kuchanganyikiwa maana kati ya wote aliowaomba ni
Rahim tu ambaye hakumuuliza kuwa pesa ile anaihitaji ya nini, alichukua simu
yake na kumtumia taarifa zake kisah chini yake kumshukuru ila Rahim
alimjibu, “Usijali, hayo ni mambo madogo sana kwangu” Erica
alitabasamu na kuweza kuendelea na shughuli zake zingine maana alikuwa na
uhakika wa kuipata ile pesa. Jioni yake alitafutwa na Bahati pia kwenye
simu, akaamua kupokea simu yake, “Erica mpenzi wangu, nimepambana kadri
niwezavyo, nimemkopa rafiki yangu na nimepata elfu hamsini tu naomba nikutumie
tafadhali” Erica akaona kama akikataa basi atamfanya Bahati ajisikie
vibaya, kwahiyo alimkubalia na baada ya muda mfupi Bahati alimtumia ile elfu
hamsini kwahiyo ikawa jumla elfu sabini ukiongeza na ile elfu ishirini ya jana
yake, kiukweli alijua ni wazi kabisa kama Bahati angekuwa na hela za kutosha
basi angemsaidia ni kwavile tu hakuwa na hela za kutosha. Akamshukuru pia huku
akingoja hela atakayotumiwa na Rahim kesho yake. Usiku wake Rahim
alimtumia taarifa za kwenda kuchukua hela zake, na kusema kuwa kesho asubuhi
angeenda kuchukua. Na kweli alienda kuchukua na kushangaa sana, maana
alijua Rahim kakosea kusema nimetuma laki tano, akakuta kweli anapewa laki tano,
alistaajabu sana na kuona ni kweli anapendwa sana na Rahim, moja kwa moja
alienda kule hospitali alipoahidiana na Yule dokta na kupewa muda wa kufanyiwa
tukio la kutoa mimba. Muda ulipofika alielekea alipoambiwa ila moyoni
mwake alijiapia, “Hii itakuwa ni mimba ya mwisho kutoa katika maisha
yangu yote, nikija kupata mimba tena nitazaa bila kujali chochote. Nimejifunza
sasa na sitarudia tena” Daktari alifika na kumfanyia ile shughuli,
maumivu aliyoyapata siku hii yalikuwa makali sana ila dokta alimaliza kumtoa
mimba na kumuandikia dawa kisha kumuacha apumzike
kidogo. Alirudi nyumbani sasa na kwenda kulala ila alishukuru
sana kwa kufanikisha swala lake la kutoa mimba, ila akajisemea kuwa hataki tena
kujihusisha na maswala ya ngono, “Ilimradi mwanaume anipendaye yupo nje
ya nchi basi akirudi labda ndio nitakuwa nae pamoja, ila kwasasa sitaki kuwa
karibu na mwanaume yoyote Yule. Bahati naweza kummudu, ni msumbufu sana ila
naweza kummudu najua nikimwambia sitaki hawezi kunilazimisha ila sitakaa na
mwanaume yoyote Yule kwenye maeneo hatarishi” Lile lilikuwa somo kubwa
sana kwake maana kutembea na kaka yake lilikuwa swala la ajabu na aibu sana
katika maisha yake. Alijifikiria kuhusu elfu sabini aliyopewa na Bahati
akaona kama atamrudishia basi Bahati atajisikia vibaya sana, akaona ni vyema
amnunulie Bahati zawadi kwa ile hela au aongezee kidogo ampatie ila swala la
kumrudishia litamfanya Bahati ajisikie vibaya, akajifikiria sana kuwa ampatie
zawadi gani Bahati, akakumbuka kuwa ndani kwa Bahati kuna jiko la mkaa tu
kwahiyo akawaza kuwa amnunulie jiko la gesi. Akalala muda huo akiwa na
amani moyoni mwake, alikuja kushtuka wakati usiku umeshaingia mama yake ndio
alienda kumuamsha, “Una matatizo gani siku hizi mwanangu, unajua
sikuelewi? Toka umerudi yani hueleweki kabisa, una tatizo gani, niambie unajua
mimi ni mama yako” Muda ule ulke simu ya mama yake ikaita, na akaipokea
ilionyesha kuwa alikuwa akiongea na Bite kwani alikuwa akimueleza matatizo
aliyokuwa nayo Erica kwa kipindi hiko, Erica akainuka na kwenda kuoga kwani
alijua baada ya hapo angeitwa tu na mama yake kuulizwa kuwa ana tatizo gani
tena. Na kweli baada ya kumaliza tu kuoga, mama yake alimuita na
alipoenda alianza kumuuliza, “Ulimuomba dada yako laki moja na nusu ya
nini?” “Mmmh jamani dada Bite nae, yani kakwambia” “Ndio lazima
aniambie mimi ndio mama yenu, na amekuuliza ya nini hujamjibu. Haya niambie sasa
hiyo hela ulitaka ya nini?” “Mama, kuna rafiki yangu anaolewa sasa
nilikuwa nataka hela ya mchango maana nilimuahidi nitamchangia yani sikuwa na
furaha sababu sherehe yake imepita jana” “Hivi wewe kama kuna jambo kama
hilo kwanini usiseme mapema?” “Mama, yani sikuelewa nimekuja kushtukia
tu siku zimeisha na nimeogopa kumwambia dada sababu najua
angenishushua” “Ndio lazima akushushue, mtu unasoma halafu unataka
kuanza kujishughulisha na kuchanga michango mikubwa hiyo ya harusi. Ujinga huo,
michango waniambie mimi” Erica alishukuru mama yake akubaliana na uongo
aliomdanganya kwani muda wote alikuwa anatafuta uongo wa kusema kuhusu kukaa na
mawazo vile na kuomba hela. Kesho yake alienda kwenye maduka ya
gesi na kununua mtungi mdogo wa gesi uliokuwa na kila kitu kwa elfu tisini,
kisha akakumbuka kuwa ndani kwa Bahati kuna joto sana, aliamua kumnunulia na
feni ya chini ya elfu sabini maana hela alikuwa nazo kwa kipindi hiko. Akakodi
bajaji hadi alipokuwa akiishi Bahati maana alifanya kwa kumshtukiza
tu. Alimkuta Bahati anafua, yani Bahati hakuamini kile alichokiona kuwa
Erica kamnunulia zawadi, Erica alishusha zile zawadi na kumwambia Bahati kuwa
anawahi chuo ila hakujua kama kile kitu kimetengeneza kitu gani kwenye moyo wa
Bahati, kwani Bahati alijiona kuwa ni mwanaume anayependwa na Erica kuliko watu
wote duniani kwani hakufikiria kama inawezekana kwa mwanamke asiyekupenda
kukufanyia vile, ukizingatia hata hela aliyompa Erica haikufikia vitu ambavyo
Erica alimnunulia. Erica hakutaka kukaa sana kwa Bahati kwani aliogopa
maswala ya kujikuta akiingia tena kwenye uzinifu kwa kushawishiwa, alishajisemea
kuwa hatokuwa kwenye mazingira hatarishi tena kwahiyo alijizuia hata kuingia
ndani kwa Bahati. Alipokuwa chuoni, jioni yake alifatwa na Bahati,
hakupinga kwenda kuongea nae, “Kwakweli Erica nimeamini unanipenda, na
nakuahidi kukupenda hadi pumzi yangu ya mwisho” Erica alimuangalia tu
Bahati, huku Bahati akiendelea kuongea, “Sasa lini utahitaji
nikufurahishe kwa mapenzi mpenzi wangu?” “Naomba nikwambie jambo hili
Bahati, sitaki tena ngono hadi pale nitakapoingia kwenye ndoa” “Hilo sio
tatizo Erica, si ukubali tu nikuoe hata sasa” “Hapana siwezi kuolewa
hadi nimalize chuo, kama unanipenda basi kubaliana na mawazo yangu, sitaki
kufanya chochote tena hadi ndoa” Bahati hakuwa na usemi zaidi ya
kukubali kile ambacho Erica alisema kwani alimpenda sana Erica, “Pia
naomba usiwe unakuja mara kwa mara hapa hosteli nakuomba” “Sawa, hakuna
shida” Kisha Erica akaagana nae, hakutaka kuendelea kumkataa wakati mtu
bado anajilazimisha kwake akaona njia pekee ni kumuomba asiwe anaenda mara kwa
mara pale hosteli, na alishukuru kuona vile amekubali. Kitu ambacho
hakukifahamu Erica ni kuwa watu wengi pale chuoni walikuwa na habari zake mbali
mbali nzuri na mbaya, alizozijua na asizozijua, sababu hakutaka kuwa karibu na
marafiki maana siku zote walitumika kuumiza moyo wake, ilikuwa ni ngumu sana
kujua habari yoyote inayoendelea juu yake pale chuoni, alichojali yeye ni
kufanya masomo yake tu. Mawasiliano ya Erica na Rahim yalipamba
moto kiasi kwamba walijikuta hadi wakipanga mipango ya ndoa kwenye simu na idadi
ya watoto watakaowazaa, Erica alianza taratibu kuuweka moyo wake kwa Rahim kwani
aliona ndiye mwanaume ampendaye. Siku hiyo akiwa anawasiliana nae kwa
njia ya ujumbe facebook kama kawaida yao, alishangaa kuona kuna mtu kamtumia
ombi la urafiki, kumuangalia mtu Yule akaona ni Erick, moyo ulimlipuka paa,
akamfungua mtu huyo na kuangalia picha zake vizuri, akaona ni Erick Yule Yule
anayempenda siku zote, alihisi akili yake kuhama kwakweli maana kila akimfikiria
mtu huyu huwa anashindwa kuelewa kama anaweza kukubali kuolewa na mwanaume
mwingine ikiwa Erick hajaoa, ingawa taarifa za kuambiwa kuwa Erick ana mwanamke
zilimuumiza sana na kujiapia kuwa atamsahau ila kitendo cha kuona kamuomba
urafiki facebook kilihamisha akili yake kabisa na kujikuta akikubali ombi la
urafiki wa Erick huku akitamani kumtumia ujumbe ila kabla hajamtumia alishtukia
tu kuna ujumbe ukitoka kwa Erick kwenda kwake, “Hongera Erica,
ulinitafuta ilihali ukijua kuwa umeshaolewa? Iliniuma sana kuongea na mume
wako” Erica alishangaa sana na kumuandikia ujumbe, “Hizo habari
za mimi kuolewa umezitoa wapi Erick? Mimi sijawahi kuolewa na wala simu yangu
haijawahi kushikwa na mwanaume” “Acha uongo Erica, mwanaume wako
alipokea hadi usiku akisema umelala nae, niliumia sana Erica yani wewe msichana
unaumiza akili yangu” Sasa muda huo wakati anasoma huo ujumbe kuna
ujumbe uliingia kutoka kwa Tumaini ukimwambia, “Erica toka siku ile
hujanijibu hadi leo kuwa hela ile ulikuwa unataka ya nini, halafu ni mwezi sasa
hatujaonana kwanini mdogo wangu? Una matatizo gani? Usinifiche, kuna habari
nyingi sana nimesikia kuhusu wewe, ndiomana nakuuliza kwa makini ikiwezekana
tuonane na tuongee kuhusu hizi habari kama zina ukweli maana zinaniumiza
sana” Aliisoma na kujiuliza sana kuwa ni habari gani hizo ila hakupata
jibu, ila akaona ni vyema amjibu Erick kwanza, halafu ndio aendelee kuulizana na
Tumaini “Unajua ninavyokupenda Erick, siwezi kufanya huo
upuuzi” Akatuma, na kushtuka kwani aligundua kuwa ule ujumbe ametuma kwa
Tumaini na sio Erick. Aliisoma na kujiuliza
sana kuwa ni habari gani hizo ila hakupata jibu, ila akaona ni vyema amjibu
Erick kwanza, halafu ndio aendelee kuulizana na Tumaini “Unajua
ninavyokupenda Erick, siwezi kufanya huo upuuzi” Akatuma, na kushtuka
kwani aligundua kuwa ule ujumbe ametuma kwa Tumaini na sio Erick. Erica
alitetemeka sana na hakujua hata aseme nini, ujumbe ukatoka kwa
Tumaini, “Erica, unamuongelea Erick mdogo wangu eeh! Nimeona taarifa
hapa kuwa mmekuwa marafiki leo, eeh niambie umeanza lini kumpenda mdogo wangu
Erica?” Erica alijifikiria sana kuwa amjibu kitu gani Tumaini, alijihisi
hadi kuchanganyikiwa kabisa, alikuwa kimya na ujumbe mwingine ukaingia kutoka
kwa Tumaini, “Nijibu Erica umeanza lini kumpenda mdogo wangu? Ndio
sababu ya kuniomba namba eeh! Kumbe ulikuwa unatukejeli pale na Sia wakati
unampenda mdogo wangu?” Ikabidi Erica amjibu, “Hapana dada, sio
Erick mdogo wako” “Mwehu wewe, usinitanie, kama sio mdogo wangu nitumie
jina analotumia humu facebook nimuulize, unadhani tabia yako sijaambiwa?
Unaonekana binti mpole ila una mambo ya ajabu sana, usinidanganye lolote,
niambie umeanza lini kumpenda mdogo wangu?” “Nisamehe dada, ila sio
Erick mdogo wako” Erica aliamua kumjibu hivyo maana aliona jumbe
zinazotumwa na Tumaini ni za kuchukizwa sana ingawa hakujua kuwa ni vitu gani
ambavyo Tumaini amesikia kuhusu yeye. “Kesho tuonane Erica, nina shida
na wewe” “Sawa, hakuna shida” Kwa muda huo Erica hakuwa na hamu
tena ya kuendelea kutuma meseji kwa mtu yeyote kwani hadi pozi zilimuisha
haswaa, alihisi kuchanganyikiwa huku akijiuliza kuwa Tumaini anamuhitaji kuonana
nae ili aongee nae kuhusu tabia yake ipi, aliamua kulala tu huku akisubiri kesho
yake akaonane na Tumaini. Kesho yake kama kawaida alienda chuo
kwenye kipindi, na alipotoka tu kwenye kipindi alitafutwa na Tumaini na kutajiwa
mahali ambako Tumaini yupo kisha akaenda kumsikiliza. Alimkuta na kumsalimia ila
Tumaini hakuitikia salamu ya Erica, akamuuliza “Haya sasa nionyeshe huyo
Erick uliyekuwa unamwambia kuwa unampenda facebook” Erica hakutaka
kumdanganya Tumaini ila pia hakutaka kumwambia ukweli kama ni yeye ndiye
aliyekuwa anasemwa na Erick, kwahiyo akamwambia “Ni kweli niliyekuwa
nawasiliana nae ni Erick mdogo wako ila sikutaka kukwambia ukweli maana
ulishachukia tayari” Tumaini akamzaba kibao Erica na
kumuuliza, “Ni lini umeanza kumpenda mdogo wangu?” Erica alikuwa
akijishika shika shavu pale alipozabuliwa kofi, “Ni tangia nilipomuona
kwako” “Nilijua tu mwanaizaya wewe, mtoto shetani kabisa wewe. Kwan je
unaonekana mstaarabu kumbe mbwa mwitu, kwahiyo siku ile ulitulaghai na Sia ili
uchukue namba ya mdogo wangu na uanza kumchombeza? Ndiomana kila nikikwambia
kuhusu mchumba wa Erick unapata kimuhemuhe na kuaga” “Nisamehe
dada” “Nikusamehe nini shetani mkubwa wewe, ninachotaka ni uachane na
mdogo wangu atulie na mchumba aliyempata kwanza ni mzuri sana. Sitaki mdogo
wangu aanze kuhangaika na watanzania tena, haswaa mtu kama wewe mwenye skendo
kila kona ya chuo hiki” “Ila dada kwani mimi nina skendo
gani?” “Tena utulie, unafikiri mambo yako ni siri? Kila mtu hapa chuo
anayajua mambo yako, ulisababisha vijana wawili wapigane hosteli sababu yako,
hapo ulipo ushabakwa na wanaume wane unafikiri ni siri? Kila mtu anajua, tena
ulivyomzoefu wa hayo mambo yani ulibakwa na kuonekana kujionea sawa tu. Na zaidi
ya yote nimepata habari kuwa ulikuwa na mahusiano na Derick, hakuna asiyejua
hapa chuoni kama Derick ni mwanaume Malaya chuo kizima yani kazi yake ni
kubadilisha wanawake tu, ila kwako akakuzoa maana ushazoea kuzolewa na wanaume.
Hivi wa kumtaka mdogo wangu wewe? Hapo ulipo unanuka zinaa, mwanaharamu
wewe” Erica alikuwa kimya kabisa maana hakuamini kama maneno haya
yanaongelewa na Tumaini, aliyemuona kama dada yake hapo chuoni, aliona kuwa
amepata ndugu na si rafiki na ndiomana akawa nae karibu, ila leo amemwambia
maneno makali sana ambayo alibaki kuyashangaa tu. Kitendo cha Erica kuwa kimya
kilimfanya Tumaini aendelee kuongea, “Nakuomba Erica uachane na mdogo
wangu tafadhali, au kwavile kwetu nilikwambia tuna uwezo? Achana na Erick
nakuomba, achana nae kabisa. Niahidi sasa hivi kuwa utaachana na
Erick” “Nakuahidi dada, sitaendelea nae tena” “Yani wewe
loh” Akatema na mate chini na kuendelea kuongea, “Unatia hata
kichefuchefu yani, msichana mzuri hivyo, unaonekana mpole tena binti mlokole
kumbe hakuna kitu ni jamvi la wageni yani wewe kila anayekutaka anakupata, na
isitoshe ushabakwa na watu zaidi ya wanne halafu bila haya unamwambia mdogo
wangu unampenda, na nitamtafuta Erick nimwambie skendo zako ili hata asikukubali
mwanaizaya wewe” Tumaini akaondoka na Erica akaondoka pia bila ya
kumjibu chochote maana alikuwa akishangazwa tu, kichwa chake kilijaa mawazo ya
kila aina na kufanya akose raha kabisa huku akijiuliza kuwa ni wapi alipokosea
maana hakuelewa kabisa, swala lake la kutafuta penzi la kweli limemfanya
aonekane Malaya na hafai kabisa kwa jamii, Erick ni mwanaume anayempenda sana
ila dalili ya kumpata tena hakuwa nayo kwa zile skendo alizosikia kuhusu
yeye. Alirudi hosteli akiwa na mawazo sana, akaona kuwa atawaza
sana bila ya kuwa na majibu yanayoeleweka, akajiangalia ni kweli hakuwa na
rafiki pale chuoni sasa ni nani anayeweza kumwambia ukweli kuwa zile kashfa za
ajabu ajabu kwake zimeenezwa na nani na zimeanza vipi, akamkumbuka Fetty kuwa
anaongeaga ongeaga nae, akatoka kwenda kumuulizia kwenye chumba chake ili
akaongee nae maana alimuona kuwa na maneno mengi sana na kwa vyovyote vile
lazima atakuwa ni binti mbea. Alienda kumuulizia na kweli alimkuta na
kwenda nae nje kwenye kivuli kisha akaa nae ili kuzungumza
nae, “Samahani Fetty, eti ni habari gani zinazoenea kuhusu
mimi?” “Tatizo lako Erica huna marafiki na ndiomana huwezi kujua kitu
chochote kinachoendelea kuhusu wewe, ila kiukweli habari zako ni mbaya sana yani
ningekuwa wewe hata chuo ningehama” “Niambie Fetty ni habari zipi
hizo?” “kwanza kabisa, lile swala lako la wanaume kupigana sababu yako
limeenea hosteli hapa kote na sio hosteli tu hadi chuoni habari hizo wanazo yani
hakuna mtu anayejua, halafu swala lako la kubakwa na wakaka wane limeenea
kote” Erica alimkatisha kwanza Fetty na kumuuliza kwa
makini, “Nimebakwa! Jamani hizo habari kazieneza nani? Mbona mimi
sikubakwa jamani!” “Erica, wewe unasema hujabakwa ila wakaka waliokubaka
wameeneza habari hosteli kote hya kwamba walikubaka siku hiyo saa nne, eti
ulijichelewesha kuondoka na kuna jamaa yako ulikuwa unamsubiri ila hakutokea, na
wale walikuwa wamekuvizia maana ulishawadanganya wote na umekula hela zao,
kwahiyo wakakubaka” “Jamani jamani loh! Hiki chuo kina mambo ya ajabu
jamani, sijawahi kubakwa mimi, sijawahi kubakwa kabisa katika maisha yangu. Na
kuhusu Derick je maana nimesikia sikia habari” “Shoga, Derick ni Malaya
koko ila sikutaka tu kukwambia siku ile maana sijui kama ungenielewa ila Derick
ni Malaya koko. Sasa kitendo cha wewe kuwa na mahusiano na Derick kimejulikana
chuo kizima yani watu wamekuzania kuwa na wewe ni malaya maana kumkubali Derick
anayejulikana chuo kizima kuwa ni malaya ni swala la ajabu” “Jamani!
Kumbe Derick ni malaya? Sikujua Fetty” “Utajulia wapi na hauna mashoga,
katika maisha unatakiwa kuwa na marafiki ili kutambua vitu kama hivi, watu
wanakuwa na marafiki ili kujua mambo mbalimbali. Kidole kimoja hakivunji chawa
shoga yangu, unatakiwa kuwa na marafiki ili kuweza kuisafisha sifa yako. Sasa
swala la kubakwa ungekuwa na marafiki hata wangekutetea kwa watu kuwa hukubakwa
ila marafiki huna na habari imeenea chuo kizima kuwa ulibakwa” Erica
alipumua kidogo huku akijiuliza kuwa ni nani aliyeeneza habari zake kuwa
alibakwa wakati hakubakwa, kiukweli hakupendezewa kabisa na zile habari ila
alimshukuru Fetty kwa kumwambia ukweli, “Tena nasikia kuna habari yako
hiyo kubwa kuliko zote ila bado mwenye nayo hajapata ushahidi
vizuri” “Habari gani hiyo?” “Sijui, ila wanasema tu kuna habari
yako mbaya inakuja kuenea chuoni. Erica kuwa makini sana, kuwa makini na watu
unaoanza nao mahusiano ya kimapenzi, nahisi habari zako nyingi zinaenezwa na
Derick, kuwa nae makini sana, ni mvulana malaya Yule na anapenda kumchafulia
sifa msichana ndiomana wengi wanamkwepa kuwa nae kwenye
mahusiano.” “Nashukuru sana Fetty, inatosha kwa uliyoniambia
asante” Erica aliondoka na kuingia ndani hosteli, akapabeba mkoba wake
na kuondoka zake, yani muda huo aliondoka na kwenda nyumbani kwao kabisa kwani
zile habari hazikumfurahisha kabisa. Alipokuwa kwao alifikiria
sana, na kuanza kuhisi huenda maneno aliyoyasema Fetty yana ukweli kuwa huenda
Derick ndio amesambaza habari mbaya kuhusu yeye, “Itakuwa ni Derick tu
maana ndio aliyeshuhudia wale vijana waliotaka kunibaka, jamani kwanini
ananifanyia hivi wakati ni ndugu yangu! Na habari kubwa anayotaka kueneza kuhusu
mimi ni ipi?” Akawaza sana na kusema, “Mungu wangu, asije
akaeneza kuwa nimetoa mimba, jamani nitaweka wapi sura yangu mimi Erica? Najuta
kumfahamu huyu mtu, ni kwanini nimempata ndugu wa aina hii?” Aliwaza
sana, na kusema kuwa kesho yake ataenda kumtafuta Derick ili aongee nae na aache
kumfanyia vitu vya ajabu kiasi hiko kama kumsambazia vitu vya uongo, kiukweli
Erica hakuwa na raha kabisa na alijiona akikosa amani moyoni mwake kila siku
maana ni kama liliibuka jipya kila siku, usiku ulifika na mama yake alimuuliza
kuwa imekuwaje amerudi tena kutoka chuoni, alisema uongo wake wa kumkumbuka ila
kiukweli chuo kile kilianza kumchosha kwa kipindi hiko. Kesho yake
alienda chuoni na alimtafuta Derick hewani ili aonane nae, na kweli Derick
alikubali kuonana nae na kwenda kuongea nae, “Derick kwanini lakini
umeamua kunifanyia hivi? Kweli kabisa wewe ni wa kueleza habari mbaya kunihusu
mimi?” “Habari gani Erica?” “Wewe umewaambia watu kuwa mimi
nilibakwa na wanaume wane sijui, jamani Derick, unajua fika kuwa sikubakwa,
kweli ni wa kunisambazia habari za hivyo?” “Erica, kwani habari hizo ni
za uongo” “Ndio ni uongo, kwani wewe hukuona kama
sikubakwa?” “Kama hukubakwa mbona ulikubali twende kupima mimba na
magonjwa ya zinaa? Erica, unaweza kumdanganya mtoto ila sio mimi, na kila leo
unajiliza liza, hata hivyo habari hizo zilizagaa kipindi kile kile hata
sijagundua kuwa wewe ni ndugu yangu” “Sasa umepata faida gani kwa mfano
kunisema hivyo? Unataka watu wanichukie eeh! Unajua wewe ni
muuwaji?” “Hivi uuwaji wangu mimi unaweza kufikia uuwaji wako wa kutoa
mimba? Nyie kwenu ni wauaji ndiomana mamako hakunitaka” “Hivi wewe
Derick unaongea au unaropoka? Jamani siku ile da Mage si amesema maneno ambayo
mimi na wewe hatukuyajua kabisa, kwanza kumbuka ulilala na mimi bila ridhaa
yangu, halafu unataka nionekane malaya, hivi ukoje Derick, wewe ni mtoto wa baba
kweli? Labda baba alisingiziwa tu” Derick akacheka kwa kejeli na
kusema, “Mamako hajanipa haki zangu sababu naye akikazania kuwa mimi ni
mtoto wa kusingiziwa, sikia nikwambie Erica, siku niliyogundua kuwa wewe ni
ndugu yangu nimekuchukia balaa. Katika watoto wa baba nampenda dada Mage tu
sababu amekuwa name bega kwa bega maisha yote, hivi wewe ulishindwa kuzaa hadi
kwenda kutoa ile mimba kama sio mchezo wako? Hata kama nilifanya mapenzi nawe
kwa bahati mbaya ila si ungezaa tu na tungeendelea kufanya iwe siri maana kama
mapenzi tumefanya kweli” “Basi yaishe, tushakuwa ndugu sasa naomba
yaishe. Niheshimu kama dada yako” “Nitaanza kukuheshimu pale tu
nitakaposema kuwa ulitoa mimba na watu wote wajue rangi yako halisi, maana
unaonekana binti mpole kumbe hakuna lolote” Erica alihisi
kuchanganyikiwa kabisa maana huyu ndugu yake hakumuelewa hata kidogo aliona
akimchanganya tu akili hata akajiuliza kuwa baba yao alianzaje kuzaa nje mtoto
wa aina ile asiyekuwa na akili ya utu hata kidogo. “Hivi Derick, undugu
wa wewe na mimi uko wapi? Hivi unajua kuwa mimi ni dada yako?” “Tena
nitasambaza kuwa huna aibu umelala na kaka yako hadi ukapata mimba na mimba hiyo
ukaenda kutoa, yani Erica utapata sifa chafu sana kutoka kwangu. Unafikiri
maisha niliyoishi mimi niliyafurahia? Mama yangu alipata shida sana sababu ya
mama yako na tena alisema baba alikataa nisilelewe pale sababu mkewe alikuwa na
mtoto mdogo, umefanya nikose upendo wa baba, halafu unajishauwa nini? Nataka
upate uchungu nilioupata mimi wa kuishi bila upendo wa baba” “Derick
unadhani utapata faida gani kufanya hivyo? Au maisha uliyoishi wewe kutaka
wengine wayaishi kutakufaidisha nini? Sasa mimi nahusika vipi na kuteseka kwako?
Wakulaumiwa sio mimi ni baba” “Sikia Erica, mimi nimeteseka sana sababu
sijawahi kupata upendo wa baba, kila mwanaume aliyetaka kumuoa mama yangu
haikuwezekana sababu mama ana mtoto ambaye ni mimi, baba amemfanya mama yangu
asifurahie kama kuna kitu kinaitwa ndoa maishani mwake, nimeteseka sana mimi, na
wewe ukaenda kutoa mimba kama ambavyo baba alitaka mimba yangu
itolewe” “Sasa ulitaka nizae mtoto wa laana, tena bora hata mimba yako
ingetolewa tusingeletewa machizi kama wewe duniani” “Mimi chizi eeeh!
Subiri, uchizi wangu utauona vizuri, hiki chuo kitakuwa kichungu sana
kwako” Erica alimshangaa sana huyu Derick yani hakumuelewa kabisa, Yule
Derick akaondoka zake kisha Erica nae akaondoka zake na kurudi hosteli huku
akiwa na mawazo mengi sana maana akili yake alihisi ikiruka
kabisa. Alifika hosteli na kukaa kwenye kitanda chake huku
akiwa na mawazo mengi sana akachukua simu yake na kuiwasha ambapo alikutana na
ujumbe toka kwa Rahim, “Mbona kimya mpenzi? Kwani una tatizo gani?
Nieleze” Ilibidi aanze kumjibu kuwa hana tatizo ila kiukweli alihisi
moyo wake kuuma sana, na alijihisi kuwa na matatizo mengi sana ila hakuweza
kuyaweka wazi. Akapokea na ujumbe mwingine toka kwa
Tumaini, “Kesho nitakuja hosteli hapo, nina shida nyingine na
wewe” Aliisoma bila ya kujibu maana akili yake ilikuwa imevurugwa
kabisa, muda huo Bahati nae alikuwa akimpigia, akaamua kupokea, “Erica,
hupokei simu zangu siku hizi, kwani una tatizo gani mpenzi?” “Sina
tatizo” “Erica, nakuhisi tu kuwa hauko sawa mpenzi wangu” “Nipo
sawa” Erica alivyoona maswali mengi sana akaamua kukata ile simu ya
Bahati na hata alipompigia tena hakupokea kabisa. Muda kidogo akaona
ujumbe toka kwa Erick, “Ndio mumeo alikukataza nini kuchat na mimi maana
toka siku ile kimya?” “Sio hivyo Erick” “Naomba nikuulize
kitu” “Niulize tu” “Je dada yangu amejua chochote kuhusu mimi na
wewe? Je amejuwa kama tulishawahi kuwa na mahusiano” “Hapana, ila tu
nilimwambia kuwa nakupenda” “Sitaki ajue Erica maana atakuchukia sana,
na sitaki dada yangu akuchukie. Ameniambia kuwa kuna kitu ataniambia kuhusu
wewe, ndiomana nilitaka kujua kama umemwambia chochote” Erica akawaza
kwanza kuwa ni kitu gani Tumaini anataka kumwambia Erick, alihisi tumbo
kumsokota na kuamua kwenda kwanza chooni. Alitoka chooni na kumtumia
tena ujumbe Erick, “Ni vitu gani hivyo anavyotaka
kukwambia?” “Sijui ila kaniambia vinakuhusu wewe” Erica
alishindwa hata kuendelea kuwasiliana na kuamua tu kulala huku akisubiri kesho
kitajiri kitu gani. Kulipokucha alijiandaa kwaajili ya kwenda
chuo kwanza alishasahau kama Tumaini alisema kuwa ataenda kuonana nae, yeye
kwenye mida ya saa nne akaenda zake chuo, wakati akipita maeneo ambayo wanachuo
walikaa vikundi vikundi aliweza kuhisi ni jinsi gani wanamsema maana walionekana
kumuangalia sana hadi akajishtukia yani kamavile ni mtu aliyetenda mambo ya
ajabu kweli katika jamii, aliingia kwenye kipindi, ingawa hakuwa na marafiki ila
aliona ni jinsi gani watu walivyomkwepa, alihisi kutakuwa na habari mbaya zaidi
zimesambazwa kuhusu yeye, alijisikia vibaya sana. Kipindi kilipoisha
alirudi hosteli, na moja kwa moja alienda kitandani kwake na kujilaza, ila
hakulala usingizi, alijifunika shuka tu na huku akilia, alijisikia vibaya sana
watu kuonekana dhahiri wanamnyanyapaa utafikiri ni kitu gani kipo
kwake. Wakati amejilaza, alifika Fetty chumbani kwake na
kumuita, “Erica, kuna mgeni wako nje” Erica alijifuta machozi
yake vizuri ndani ya shuka kisha kushuka kitandani kuongozana na
Fetty, “Ni mgeni gani huyo?” “Utamuona tu, pole Erica naona
ulikuwa unalia. Najaribu kuyahisi maumivu yako pole sana, kwakweli habari
zinazoenea kuhusu wewe si nzuri kabisa” “Habari gani
nyingine?” “Inasemekana Erica una ukimwi” Kwakweli Erica alihisi
moyo wake ukijaa machozi ila hakutaka kujionyesha kwa Fetty kama zile habari
zimemuumiza kiasi gani, alifika kwa aliyekuwa mgeni wake akamtazama alikuwa ni
Bahati. Kwakuwa Erica alikuwa na maumivu sana moyoni mwake, alimsogelea
Bahati na kumkumbatia kwa nguvu huku machozi yakimtoka. Mara gafla alisikia mtu
akipiga makofi, kumuangalia mtu Yule alikuwa ni Tumaini
akamwambia, “Nimekupiga na picha Erica, namtumia Erick sasa
hivi” Erica alikuwa ameduwaa tu huku macho yake yakiwa yamejaa
machozi. Kwakweli Erica alihisi moyo wake ukijaa
machozi ila hakutaka kujionyesha kwa Fetty kama zile habari zimemuumiza kiasi
gani, alifika kwa aliyekuwa mgeni wake akamtazama alikuwa ni
Bahati. Kwakuwa Erica alikuwa na maumivu sana moyoni mwake, alimsogelea
Bahati na kumkumbatia kwa nguvu huku machozi yakimtoka. Mara gafla alisikia mtu
akipiga makofi, kumuangalia mtu Yule alikuwa ni Tumaini
akamwambia, “Nimekupiga na picha Erica, namtumia Erick sasa
hivi” Erica alikuwa ameduwaa tu huku macho yake yakiwa yamejaa
machozi. Ila Tumaini aliendelea kuongea, “Usijilize Erica,
ujinga wako wote leo unafika sehemu husika” Bahati hakupendezewa na
kitendo cha kumuona Erica akiwa amejawa machozi kiasi kile, alimshika mkono na
kwenda nae barabarani kisha akakodi bajaji na kwenda nae ufukweni kwani alijua
jinsi gani Erica aliyapenda maeneo ya ufukweni, na hata hivyo alijua tu Erica
hayupo sawa kwa wakati huo. Walifika na kukaa kwenye michanga, ni kweli
Erica hakuwa sawa kabisa, Bahati alimuuliza, “Nini tatizo
Erica?” “Najiona kama sina faida tena hapa duniani, sina thamani ya
kuishi” “Kivipi ukose thamani Erica?” “Sipendwi tena, watu wote
hawanipendi kwa maneno ya uongo. Natamani hata kufa” “Erica jamani
usiseme hivyo, siku zote jua kuna Bahati wako anakupenda sana hata iweje. Kwanza
ni maneno gani waliyokutangazia?” “Wamezusha eti mimi nilibakwa yani
habari imeenea chuo kizima na wamesema kuwa mimi nina ukimwi, kwakweli sina raha
mimi bora hata nife” “Erica usinichekeshe yani utamani kufa sababu ya
habari hizo, wamesema umebakwa, hayo ni maneno tu hata kama kweli ulibakwa ndio
nini sasa? Wanasema una ukimwi, kwani unao kweli? Hata kama unao kwani
utawaambukiza wao? Utaniambukiza mimi, yani maneno kama hayo ningekuwa
ningeambiwa mimi ningewashushua kwakweli, Erica ngoja nikwambie kitu, wewe hata
uwe malaya dunia nzima wakufahamu sababu ya umalaya ila mimi sikuachi. Wewe hata
uwe na ukimwi na vipimo vyote vionyeshe kuwa una ukimwi, mimi sikuachi.
Nakupenda Erica, na ninakupenda kweli yani kupita yeyote Yule aliyewahi
kukwambia kuwa anakupenda” Erica alimuangalia Bahati na kumshangaa
kwakweli maana alikuwa anaongea maneno kama mfu, yani alishangaa kuwa Bahati ni
mwanaume wa aina gani ambaye hakati tamaa kwake, yani yeye anamuimbia wimbo wa
nakupenda kila siku. Bahati alimshauri Erica asirudi hosteli bali aende
kwao akapunguze mawazo, “Ila nataka kuchukua na nguo zangu
hosteli” “Inamaana kwamba hutaki tena kukaa hosteli?” “Sitaki
ndio, bora nikae nyumbani, hata kile chuo chenyewe sikitaki natamani hata
kuhama” “Hivi inawezekana kuhama chuo?” “Nitaenda kuulizia,
kwakweli Bahati nahitaji akili yangu ipumzike. Najua nimebakiza mwaka mmoja ila
sitaki kumalizia pale chuoni, bora nihame” “kama inawezekana, sina
pingamizi mimi. Ilimradi wewe ukiridhika basi na mimi
nimeridhika” Akakubaliana nae arudi kwanza hosteli akachukue nguo zake,
na alirudi hosteli kwenye mida ya saa moja jioni, Bahati alibaki kwenye bajaji
akimsubiria, siku hiyo Bahati alikuwa na hela kwahiyo haikuwa shida kwa yeye
kukodi bajaji. Erica aliingia hosteli na moja kwa moja alienda
kwenye chumba alichokuwa analala, na kubeba nguo zake huku zingine akiziweka
kwenye mkoba, ilibidi wenzie wa kwenye chumba hicho wamuulize, “Vipi
Erica mbona unabeba nguo zote, unahama?” “Mmmh hapana, nitarudi tu.
Nataka nikabadilishe baadhi ya nguo” Akawaaga pale na kutoka, alikutana
na Fetty nje ambaye alimuuliza pia, “Vipi Erica
unahama?” “Nataka nikapumzike kidogo nyumbani” “Ila Erica hata
mimi kama ningekuwa wewe kweli tena ningeenda kupumzika, jamani yani wanaume
wengine sio wa kutembea nao kabisa, lete begi nikusaidie” Erica alimpa
begi lake ambapo Fetty alimsaidia kubeba huku wakielekea nje, na Fetty
akiendelea kuongea, “Yani Derick shetani kabisa Yule, unajua amesema eti
umetoa mimba” “Nimetoa mimba!” “Ndio, kasema umetoa mimba jamani
Derick anakuchafulia sifa zako balaa, ila shoga yangu siku nialike tukutane na
Derick yani siku hiyo nitamchamba sitamuacha chochote yani mwanaume mzima hovyo.
Naomba namba yako Erica” Ikabidi Erica ampatie huyu Fetty namba yake,
kisha akafika kwenye bajaji na kuagana nae ambapo Erica alipandisha mabegi yake
na kuondoka na Bahati. Alifika kwao kwenye mida ya saa tatu usiku, na
kumfanya mamake ashangae sana alipoenda na mabegi, kwa wakati huo alikuwa
ameshaagana na Bahati. “Kheee vipi wewe na mabegi?” “Nimechoka
kukaa hosteli mama” “Sasa utaweza kutoka huku nyumbani kila siku kwenda
chuo?” “Nitaweza mama” “Kwani tatizo ni nini Erica mbona
unaonekana huna raha mwanangu?” Erica alishindwa kujizuia kwa mama yake
na kuangusha machozi, ilibidi mama yake ambembeleze na kumuuliza kwa makini,
Erica aliamua kumueleza mama yake baadhi ya maneno yanayomliza huku yale ya
ukweli akiyaficha, “Mama, hivi Yule Derick kwanini alikuwa mtoto wa
baba?” “Kafanyaje kwani?” “Analalamika kuwa mimi ndiye
nilimfanya akose upendo wa baba sababu hata nyumbani mligoma kumuhudumia sababu
nilikuwepo mimi” “Kwani nani amekukutanisha na huyo
mwanaharamu?” “Dada Mage ndio kanifahamisha kuwa Yule ni mtoto wa
baba” “Aaah Mage nae, hanaga akili Yule ndiomana akaolewa na choka
mbaya. Sasa huyo Derick ndio anakuumiza kichwa hadi unalia
mwanangu?” “Silii sababu ya Derick ila ninalia sababu ya maneno ya uongo
aliyoeneza juu yangu eti nipate uchungu kama alioupata yeye kwa kukosa upendo wa
baba” “Maneno gani hayo?” “Derick katangaza chuo kizima, na
habari zimeenea kote sababu mimi sio muongeaji, eti ametangaza kuwa mimi
nilibakwa na nina ukimwi” “Kheee mtoto ana wazimu huyo eeh! Ukimwi aache
kuupata mama yake kwa umalaya wake, uje uupate wewe” “Yani mama chuo
kizima wananinyanyapaa” “Unajua wanaume nao mara nyingine sijui akili
zao zipo kwenye makalio yani hata hawajifikiriagi, unamsaliti mkeo unaenda kuzaa
na mwanamke mwingine basi msaliti na mwanamke mwenye akili timamu, unaenda
kumsaliti na chizi na unazaa nae, yani baba yenu sijui alikuwa na akili gani,
Yule mwanamke hana akili hata kidogo ndiomana nilimtimua hapa na vitoto vyake,
mwanamke ni tahira Yule. Nyumba yangu mwenyewe halafu anakuja na mitoto yake
hana hata aibu, Yule mwanamke ni malaya wa kutupwa., halafu anajifanya kama yeye
ni mke kwenye familia hii yani atoe amri anavyojisikia, nikasema sitaki kuona
uchafu wake wala watoto wake. Sikufanya kosa kuwatimua kwakweli, ona shetani
alilolikuza sasa, hivi ndio linatumika kuharibu furaha ya mtoto wangu! Nyamaza
Erica wangu, mama yako najua mwanangu hujawahi kubakwa na huna ukimwi, maneno ya
hao watu yasikuumize” “Mama hujui tu, chuo chote wananinyooshea vidole,
halafu kanizushia kuwa nilitoa mimba” “Hivi anataka nini huyo mtoto
jamani! Kwanini kukuzushia habari za kijinga namna hii. Baba Mage, unaona ujinga
uliofanya kwenda kuzaa na matahira, mwanetu anadhalilika sasa bila sababu, Erica
naomba kesho nikakutane na huyo Derick, mbwa mkubwa huyo” Erica akaona
mama yake akienda kukutana na Derick itakuwa soo kubwa zaidi, akamuomba jambo
moja mama yake, “Mama, usiende ila mimi nataka kuhama
chuo” “Umebakiza mwaka mmoja tu mwanangu” “Ndio huo mmoja nataka
nikamalizie kwenye chuo kingine” “Yani yote haya kayataka babako, yani
wanaume hawaelewagi tu kama mwanamke unayezaa nae inabidi umtambue uelewa wake
mapema sana, sio kila mwanamke ni wa kuzaa nae, ndio mwisho wa siku kuzaa na
matahira kama hao. Yani hilo litoto litakuwa na akili za mama yake na labda
limeambiwa lifanye visasi, unafikiri babako angezaa na mwanamke makini ningegoma
kulea mtoto? Hata kama kwetu hawakutaka ila nisingegoma kulea, ila siwezi kulea
toto la mwanamke tahira kama mama yake Derick. Siku ukimuona huyo mama utagundua
maneno yangu, huyo mama hajisomi yani yupo yupo tu. Ila mwanangu, kuhama
kunataka pesa hiyo pesa nitatoa wapi kwa kipindi hiki?” Erica akafikiria
akaona ni kweli kuhama kunahitaji pesa, ila aliamua kwenda chumbani tu
kujifikiria vizuri zaidi. Alienda kuoga na kurudi kulala maana
siku hiyo kichwa chake kilikuwa kibovu sana na alifikiria mambo mengi sana,
aliwaza kuwa afanye kitu gani kwa muda huo, akapata wazo la kuongea na dada yake
ampe namba za mama yake Derick ili akazungumze na mama yake Derick kwani hata
kuhama chuo bado isingekuwa suluhisho kwake ikiwa bado kuna sifa mbaya kuhusu
yeye zitazungumzwa, akawaza pia pesa ya kuhama chuo ataipata wapi maana aliwaza
vitu vingi sana ambavyo vitamuingia gharama ikiwa pia ni kujaribu kuhonga ili
apate nafasi ya kuhamia chuo kingine, aliwaza sana. Alichukua simu yake
na kumpigia dada yake, “Samahani dada Mage, nilikuwa naomba namba ya
mama yake Derick” “Si ungemuomba Derick!” “Jamani dada, ukiona
hivyo nina shida nayo, nataka kumshtukiza tu Derick” “Sawa, nakutumia
basi” Kisha Mage akakata simu na kumtumia Erica namba ile, Erica
alifurahi sana kuipata huku akiwaza kama akimpigia huyo mama atakubali kukutana
nae? Hakutaka kufikiria sana, akaamua kumpigia tu, kisha mama Derick akapokea na
kumsalimia, kisha aliulizwa kuwa ni nani, “Mimi ni rafiki wa Derick
mama, nina shida na wewe sijui naweza kuja nyumbani kesho kuonana
nawe?” “Unaonekana ni binti mpole sana, karibu nyumbani” “Basi
nielekeze mama, ila sitaki Derick ajue kama nakuja” “Hakuna shida
mwanangu” Kisha Yule mama alimuelekeza Erica anapoishi na Erica
alimuahidi kwenda kesho, baada ya hapo akakata simu na kufurahi sana kwani shida
yake kwa muda huo ni kuonana na huyo mama yake Derick na kuongea nae maana
hakuelewa kabisa kwanini Derick anafanya vile. Alipokuwa anataka tu
kulala aliamua kuingia kwenye mtandao kidogo ili kuangalia kama kuna chochote
kipya kinaendelea, muda huo huo akapokea ujumbe toka kwa Rahim, “Mpenzi
kimya sana, tatizo nini au una shida gani?” Erica akafikiria ila akaona
ni vyema amwambie Rahim kuhusu swala lake la kuhama chuo, “Yani Rahim
nina mawazo sana, chuo ninachosoma kinanipa kero. Wanafunzi hawanipendi sababu
tu sina urafiki nao, wananitangazia mambo mabaya hadi sina
furaha” “Jamani mpenzi wangu pole, ila kama sehemu haikupi furaha si
uhame tu!” “Natamani kuhama kweli ila tatizo pesa maana najua itakuwa
gharama sana” “Erica mpenzi wangu, unajua mimi nipo kwaajili yako na
nimekwambia kuwa ukiwa na shida yoyote usisite kuniambia, kweli kitu kama hicho
ni cha kukupa mawazo mpenzi wangu? Sikia, wiki hii nitakutumia pesa, natumai
itakutosha katika shughuli za kuhama. Kwani ada anakulipiaga nani au ni
mkopo?” “Sina mkopo, ada analipaga mjomba na hela za matumizi nazo
ananipaga” “Sawa, na umebakiza miaka mingapi kumaliza? Je ada ni
shilingi ngapi?” “Ni mwaka mmoja tu, ada ni milioni moja. Najua ada
mjomba atanilipia ila swala la kuhama chuo hawezi kunishughulikia” “Je
wewe mwenyewe utaweza kujishughulikia uhamisho?” “Nitaweza Rahim,
nimechoshwa na masimango” “Basi usijali mpenzi, aiki hii nitakutumia
hela itakayokusaidia mambo ya uhamisho na matumizi kidogo” “Nashukuru
sana” Kwakweli Erica alishangazwa sana na Rahim maana kwake kutoa pesa
hakukuwa tatizo hata kidogo, alijisemea mwenyewe tu “Jamani huyu
mwanaume ananipenda hadi naogopa, nikimwambia mama kuhusu huyu mwanaume ni
atamkubali asilimia mia moja ila nitawezaje kumuacha Bahati maana ni
king’ang’anizi hakuna mfano, nitapata tu njia ya kumuepuka Bahati ila kwasasa
nijitunze kwaajili ya Rahim natumai yeye ndio atakuwa mume
wangu” Aliagana na Rahim pale kwa njia ya ujumbe na kulala zake, huku
akiwa na tabasamu zito usoni. Kesho yake alijiandaa kama
alivyopanga kuonana na mama yake Derick, aliwasaliana nae kisha kuondoka kwao
mpaka sehemu aliyoelekezwa akawasiliana nae tena na kufika hadi nyumbani kwakina
Derick na kukutana na huyo mamake Derick na kumsalimia kisha Yule mama
akamkaribisha vizuri sana na kwenda kukaa nae ndani. “Karibu sana binti
yangu, natumaini wewe ni mchumba wa mwanangu” Erica akacheka tu kisha
akamwambia, “Hapana mama, ila mimi nasoma na Derick naitwa Erica ni
mtoto wa mzee Joseph ambaye pia ni baba wa Derick” “Kheee kumbe mtoto wa
Jose!! Nani amekupa namba yangu na imekuwaje umetaka kuonana na
mimi?” “Sina nia mbaya mama, maana nakuchukulia wewe kama mama yangu.
Mwanzoni sikujua kama Derick ni ndugu yangu na kujikuta tukiwa kwenye mahusiano
ila badae nikajua kama Derick ni ndugu yangu, nikamwomba tusahau yaliyopita kati
yetu na tuchukuliane kama ndugu. Ila anachonifanyia Derick chuoni ndio
kilichofanya nije hapa” “Kwanza mwanangu, nafurahi sana umekuwa mkweli
maana Derick aliwahi kunieleza kuwa kuna msichana alikuwa na mahusiano nae na
amegundua kuwa ni mtoto wa babake. Nimefurahi umekuwa mkweli kwa hilo, pole kwa
hayo maana tatizo ni kwetu wazazi kutowaweka wazi watoto wetu. Haya niambie sasa
tatizo lingine ambalo Derick anakufanyia chuoni” Erica alimshukuru huyu
mama kwa kuwa muelewa kwanza, kisha akamueleza jinsi Derick alivyomsambazia yeye
kuwa alibakwa na kumsambazia kuwa ana ukimwi na kumsambazia kuwa ametoa mimba na
jinsi wanavyomnyooshea kidole na kumuita malaya, “Na amesema atafanya
mpaka nione chuo kichungu ili nipate uchungu alioupata yeye kwa kukosa mapenzi
ya baba, kwakweli mama mimi sijui kosa langu, ananiumiza sana, yeye ni ndugu
yangu wa kuwa karibu na mimi ila yeye ndio anafanya kuniumiza mimi yani sina
raha kabisa, chuo nakiona kichungu kweli, watu wananinyanyapaa sina raha wala
amani” “Kwanza pole sana mwanangu, sikia nikwambie mimi siwezi kumtuma
Derick afanye huo upuuzi kwanza kabisa huwa sipendi mabinti kama nyie mpitie
maisha ambayo nilipitia mimi. Ngoja nikwambie kwa kifupi kuhusu mimi na utaweza
kuelewa ni maisha gani niliyopitia, ilifikia hatua ya kuitwa malaya na majina
yote mabaya na iliniuma sana ila mwanangu sipendi kuona mwingine anaopitia
maisha haya” Erica alitulia kwa makini akimsikiliza mama yake
Derick, “Derick sio mwanangu wa kwanza, ila mtoto wangu wa kwanza yupo
na nilizaa nikiwa shuleni. Mwanangu thamani ya mwanamke inapungua sana akizaa
yani mwanamke ukiwa na mtoto kisha Yule baba mtoto hakutaki tena ujue itachukua
muda mrefu sana kumpata mtu sahihi wa kukupenda wewe na mwanao, kiukweli
mwanaume aliyenipa mimba wakati nasoma alinikimbia na kufanya nikose uelekeo ila
nikasaidiana na nyumbani kumkuza Yule mtoto, nikapata mwanaume wa kuishi nae ila
alionekana wazi hampendi mwanangu huku akinilazimisha nimzalie na yeye, nilizaa
nae ila akanikimbia hapo nikawa na watoto wawili wasio na baba, sifa mbaya juu
yangu zikaanza nikajisikia vibaya sana. Ndipo nikakutana na Jose, na aliniambia
kuwa ana mke ila aliahidi kunioa mimi pia, nikawa tayari ili angalau nipate baba
wa kulea watoto wangu, alinipangia chumba ikawa ni faraja kwangu ndipo nikazaa
nae Derick, nikamwambia sababu ameahidi kunioa anipeleke nyumbani kwake mkewe
anijue, akagoma, basi nikamvizia siku anaenda kwake nikamfata nyuma na kwenda
hakuweza kunifukuza, nikaenda kuwachukua na wanangu kuishi nao pale ila mama
yako alinitukana sana majina yote mabaya aliniita na siku hiyo alinifukuza mimi
na wanangu na kusema nata Yule mtoto hamtambui, nilichukia sana nikakaa na ile
chuki kwenye moyo wangu, wakati wangu wanakuwa siku zote niliwaambia
nilivyomchukia mama yenu na ninyi haswa Derick nilikuwa naongea nae sana habari
hizi sababu alikuwa baba yake nahisi ndiomana Derick anakuchukia ila saivi ni
mtu mzima naelewa, nimejifunza kuwa halikuwa kosa la mama yenu maana naye
alikuwa akitetea penzi lake, ila mimi ndio niliyeharibu maisha yangu toka mwanzo
kwa kuchanganya mapenzi na shule. Nilikuwa naumia sana kuitwa malaya kwakuwa na
watoto watatu wenye baba tofauti halafu baba wote hawataki watoto wao ila Jose
alikuwa tofauti sana kwani alikuwa anamtuma mwanae mkubwa Mage aniletee hela za
matumizi hadi kifo chake bado Mage aliendelea kuniangalia hadi nilipohama pale
nilipokuwa nakaa. Erica nisamehe mimi maana ndio nimeweka chuki hiyo kwa
mwanangu, ila nitaongea na Derick na hatokuumiza tena” “Pole mama kwa
yote hayo yaliyokupata, najua hukupenda yakupate hayo ila ni bahati mbaya tu,
yani mimi natamani kuhama hata chuo” “Hata usihame chuo mwanangu,
nitaongea nae Derick atanielewa tu. Sitaki maisha niliyopitia mwingine ayapitie.
Ila kuwa makini sana mwanangu, nitafurahi siku ukinialika nije kusherekea harusi
yako” Kiukweli Erica alimpenda sana huyu mama kwa jinsi alivyokuwa
akiongea, na ilionyesha jinsi gani alikuwa akiyajutia makosa
aliyoyafanya. “Nafurahi sana kuongea na wewe, sikutegemea kama ungekuwa
mzuri kwangu kiasi hiki” “Usijali mwanangu, hata hivyo nimeongea tu na
wewe bila hata kinywaji chochote! Dah sio vizuri kwakweli, unakunywa nini
mwanangu?” “Aaah usijali mama” “Niambie bwana, unakunywa nini?
Hutoondoka hapa bila kunywa kinywaji kwenye nyumba yangu” “Basi maji tu
yananitosha” “Sawa, ngoja nikakuletee” Mama Derick aliinuka na
kutoka nje, Erica akasikia mlio wa meseji kwenye simu yake, akachukua na
kufungua akakuta Rahim kamtumia meseji ya kawaida kabisa, “Hellow
kipenzi changu, tayari nimekutumia pesa kwaajili ya kuhama chuo. Ukiingia
facebook utaona nimekutumia taarifa za kuchukua pesa hiyo, nimekutumia milioni
tatu, isipotosha utaniambia. Nakupenda sana, saizi nalala. Byee” Erica
alisoma mara mbili mbili huu ujumbe na alijiona kama anaota vile, alichukua simu
yake nyingine na kufungua mtandao kweli alikuta ujumbe wa Rahim wenye taarifa
zote za msingi za kuipata pesa hiyo, yani alihisi kimuhemuhe kabisa tayari ile
hela ilishamchanganya. Mama Derick alirudi na maji ya dukani, Erica
aliyapokea kisha kumuaga huku akimshukuru sana, “Sasa mbona mapema hivyo
mwanangu?” “Nahitajika chuo mama, ila tutaendelea
kuwasiliana” “Sawa mwanangu ila usihame chuo, nitaongea na Derick halafu
mwambie mama yako nilishamsamehe kwa yote na yeye anisamehe kwa
yote.” Erica aliaga na kuondoka, kwakweli alikuwa na harakati sana,
kwani muda huo akili ilikuwa ikiwaza zile pesa alizotumiwa na Rahim
tu. Akiwa njiani kuelekea benki, kuna gari ilisimama karibu
yake na kwenye hiyo gari alishuka Mrs.Peter yani mama yake na Rahim, kisha
akasalimiana na Erica pale na kumkumbatia, “Umenitupa
mwanangu” “Sijakutupa mama” “Ngoja nikutambulishe
basi” Kisha Yule mama alimuita binti aliyekuwa nae kwenye gari kisha
Yule binti akashuka, kisha Mrs.Peter akamwambia Yule binti, “Salma, huyu
anaitwa Erica ni kama binti yangu. Mimi sinaga mtoto wa kike kwahiyo kumpata
huyu imekuwa bahati sana kwangu, ni mwanangu pia huyu kwahiyo ni wifi
yako” Neno la wifi yako lilimshangaza kidogo Erica ila alitulia kusikia
zaidi, kisha mrs.Peter akageuka kwa Erica na kuendelea na
utambulisho, “Erica, huyu anaitwa Salma ni mkwe wangu yani ni mchumba wa
Rahim” Erica alionyesha mshangao wa wazi wazi, “Mchumba wa
Rahim? Kwani Rahim ana mchumba?” “Najua lazima ushangae, ila Rahim
kampigia simu baba yake kuwa amtafutie mchumba si unajua Rahim kutongoza hawezi,
ndio baba yake kamtafutia huyu na tumemtumia Rahim picha kasema amempenda. Hivyo
ndio nampeleka na nyumbani kwangu akapafahamu” Erica alihisi kama
masikio yameziba asikii vizuri maana hakuelewa
kabisa. “Erica, huyu anaitwa Salma ni mkwe wangu yani
ni mchumba wa Rahim” Erica alionyesha mshangao wa wazi
wazi, “Mchumba wa Rahim? Kwani Rahim ana mchumba?” “Najua lazima
ushangae, ila Rahim kampigia simu baba yake kuwa amtafutie mchumba si unajua
Rahim kutongoza hawezi, ndio baba yake kamtafutia huyu na tumemtumia Rahim picha
kasema amempenda. Hivyo ndio nampeleka na nyumbani kwangu
akapafahamu” Erica alihisi kama masikio yameziba asikii vizuri maana
hakuelewa kabisa. Mpaka Yule mama alimshtua tena Erica maana alionekana
kushangaa sana, “Unashangaa eeeh! Ipo hiyo ya kutafutiana wachumba,
ulikuwa hujui? Inafanywa sana na wazazi kama mtoto hawezi kutafuta, unajua Rahim
amekuwa eeh! Anatakiwa kuwa na mwanamke” “Sawa mama, nashukuru
kumfahamu” Kisha Erica akampa mkono Yule dada ila ni mkono wa kinafki
kwani kiukweli alikuwa anaumia sana moyoni mwake, na hapo hapo akaaga na
kuondoka, akaiweka akili yake sawa kuwa asilie muda huo ila akaenda kwanza benki
alipokuwa anaenda kuchukua hizo pesa alizotumiwa na
Rahim. Erica alipochukua zile pesa akarudi nyumbani kwao moja
kwa moja, ila aliwaza sana kuwa ni kwanini mwanaume kama Rahim anafikia hadi
kiwango cha kumtumia pesa halafu huku kuna mwanamke mwingine amesema atafutiwe,
akawaza sana akaona kichwa kinamuuma tu kwa kuwaza, akapigiwa muda huo simu na
Bahati, “Erica upo sawa?” “Nipo sawa ndio” “Nahisi kama
unatakiwa uwe sehemu upigwe na upepo kidogo, hisia zangu zinasema haupo sawa.
Kwani uko wapi sahizi” “Nipo nyumbani” “Twende beach
basi” “Muda huu jamani!! Si saa kumi na moja hii” “Ndio kwani
kuna ubaya gani, si hata tukikaa nusu saa itatosha mpenzi wangu!” “Mpaka
nijiandae, kuondoka hapa saa kumi na moja” “Ndio ukiwa tayari niambie,
nije nikufate na pikipiki. Kuna rafiki yangu kaniachia pikipiki yake leo
nitembee tembee nayo” Erica alikubali tu kwani kweli alihitaji apate
mahali atakapotuliza akili yake kidogo kwani aliona ikivurugika haswaaa maana
kila alipomfikiria Rahim alikosa raha, akainuka na kujiandaa kisha akampigia
simu Bahati na ilionyesha hakuwa mbali na kwao maana muda huo huo alifika na
kumchukua kisha wakaenda ufukweni. “Ulikuwa unanisubiria nini mitaa ya
nyumbani, maana muda huo huo umefika” “Yani muda nakupigia simu nipo
mitaa ya kwenu, nikasema kama utakuwa chuo basi ningekufata, unajua ni jinsi
gani nakupenda Erica! Najua hujui sababu ungejua basi ungeona hata dunia yote
hii ipo chini yako kwa upendo wangu kwako. Nakupenda Erica yani hadi nahisi neno
lenyewe la nakupenda halitoshi kueleza hisia zangu kwako. Niambie nifanye nini
ili unipende pia” Erica akacheka kisha akamwambia, “Kwani leo
umetambua kuwa sikupendi?” “Erica sikia nikwambie, hata ukinieleza mara
ngapi kuwa hunipendi ila moyo wangu utasema kuwa wewe ni wangu na umeumbwa
kwaajili yangu, Erica siku moja nitakuwa na pesa kama hao wenye majumba na
magari, nakupenda sana na wala sitokuacha nikiwa hivyo kwani sikuzote wewe
utabaki kuwa thamani yangu” Erica alisikiliza maneno ya Bahati ambaye
alikuwa tofauti kabisa na wanaume wengine, ila aliamua kumpinga
kidogo, “Ila wanaume wote ndio zenu, nakupenda, nakupenda kumbe hakuna
lolote. Siku moja unakuja kunisaliti, nyie wanaume sio watu kabisa, nyie ni
waongo maradufu, hamuaminiki” “Erica, sikatai kuna wanaume waongo
duniani ila wakweli nao wapo. Katika wanaume wakweli mfano wapo ni mimi, Erica
hakuna chochote ninachoweza kukudanganya wewe, nitaona wasichana mbalimbali ila
wewe ni zaidi ya wote, najua umona wanaume wengi, au umeona wengi kwa rafiki
zako ama kwa ndugu zako wakiwa ni waongo ila sio mimi Erica, najua maneno yangu
utayaamini tu ipo siku, maana mimi hata nikizeeka bado nitakupenda wewde hadi
naingia kaburini” Kwakweli Erica alimuona Bahati kuwa mwanaume wa ajabu
sana kati ya wanaume wote aliokuwa nao tatizo ni moja tu, hakuwa na upendo hata
kidogo kwa huyu Bahati. Akajifikiria jambo na kuamua kumuuliza kitu
Bahati, “Ngoja nikuulize” “Niulize tu” “Unajua mimi
sipendi kazi yako ya uvuvi wa samaki, sasa ni kitu gani unaweza kufanya
kuboresha biashara yako ili angalau uwe na thamani” “Erica, kwasasa sina
pesa ila uvuvi unalipa vizuri tu. Nikipata pesa nitaboresha kazi yangu, kwanza
nitatafuta eneo, nitanunua friji kubwa ya kuhifadhi samaki na nitakuwa nauza kwa
watu wengi sana, nitapata faida kubwa sababu navua mwenyewe. Na nikiendelea
vizuri naanza kufuga samaki wengine sababu kuwahudumia najua” “Ungetaka
kama kiasi gani?” “Kwa kuanzia nikipata kama milioni mbili nitakuwa
mbali sana. Kwanini umeniuliza hivyo Erica?” “Aaaah hamna
kitu” Wakaaongea ongea mambo mengine na muda ulikuwa umeenda hivyo Erica
akasema arudi kwao maana anaelewa kuwa mama yake atakuwa amerudi
tayari. Na kweli alifika kwao na kumkuta mama yake anakula,
akamuita, “Eeeeh umegfikia wapi swala lako la kutaka kuhama
chuo?” “Bado mama, ila nadhani nisihame tu” “Hata mimi nilitaka
nikushauri hivyo mwanangu, angalia mjomba wako anavyojitoa kwaajili yako halafu
asikie umehama chuo atasemaje? Usihame chuo mwanangu, huyo Derick nitamtafuta
mama yake na nitamwambia ni vibaya anavyofundisha watoto” Erica aliamua
kumwambia mama yake jinsi alivyomtafuta mama yake Derick na jinsi alivyosema
kuwa atamkanya mtoto wake, “Mama kumbe Yule mama wala hana hata roho
mbaya, usimchukie mama ni baba alimlagkai kuwa atamuoa mke wa pili. Usimchukie
mama Derick, kasema msameheane” “Wewe nae ni mtoto hata huelewi ila
nishamsamehe, hivi unadhani kutembea na mume wa mtu ni sifa? Eti aliahidiwa
kuolewa mke wa pili, aondoe mashetani yake hapa, aseme lingine ila aongee tu na
huyo shetani wake” “Amesema ataongea nae, ila usimchukie
mama” “Kwahiyo unataka nimchukie baba yenu au? Wanawake hawajielewi
hawa, nisingemtoa kitimutimu angejizalisha watoto kama kumbikumbi hapa. Hebu
kula ukalale huko usiniletee habari za vichaa” Yule mama akainuka zake
kisha Erica alikula pale na kwenda kuoga kisha akaenda kulala, kwakweli hata
hakutamani kuingia kwenye mtandao na wala hakuzitamani hela za Rahim maana yeye
alishaanza kumkaribisha kwenye moyo wake halafu anakuja kugundua mambo ya ajabu,
hakutaka kabisa kumfikiria. Kulipokucha alijiandaa asubuhi, akaweka
vitabu vyake vizuri kwa lengo la kwenda chuo, ila alitaka kufanya kitu cha
kushtukiza kwa Bahati. Aliondoka kwao na kwenda moja kwa moja hadi kwa
Bahati, na kweli lilikuwa jambo la kushtukiza kwani Bahati hakufikiria kama
Erica angeenda kwake kwa muda huo, “Karibu mpenzi wangu, naona leo
umeamua kunishtukiza” “Nawahi chuo ila nimeona ni vyema nipitie hapa,
nina zawadi yako” “Zawadi!!” “Ndio zawadi yako” Erica
akatoa bahasha kubwa kidogo na kumkabidhi Bahati, “Nini hiki
Erica?” “Utafungua nikiondoka, ngoja niwahi chuo” Bahati alitaka
kumsindikiza ila Erica alikuwa ameenda na bodaboda kwahiyo akatoka na kumuaga
Bahati kisha akapanda bodaboda na kuondoka. Bahati alipata kimuhemuhe
cha kufungua ile bahasha, akaifungua akashangaa ni hela kwakweli Bahati
alishangaa sana, akaanza kuzihesabu akakuta ni milioni mbili na laki
tano. “Kheee kwahiyo Erica ameamua kunipa hela ili nifanye vizuri hii
biashara! Jamani huyu mwanamke ni ananipenda tena ananipenda sana ila hataki tu
kujionyesha. Erica bila ya chochote kile naahidi kukupenda maisha yangu yote,
najua unafanya haya ili nifanane na aina ya wanaume ambao unatamani kuwa nao.
Sitakuangusha Erica, nitafanya kazi kwa bidii hadi ujisikie fahari
kunitambulisha kwa rafiki zako kuwa mimi ndiye mume wako. Nakuahidi Erica,
nitakupenda hadi pumzi yangu ya mwisho.” Bahati alijikuta akisema peke
yake tu kama mjinga maana si kitu alichokitegemea kabisa. Erica
alienda chuo maana alikuwa na kipindi ila alipomaliza kipindi tu alipanda gari
na kurudi nyumbani kwao kwani kiukweli hakutaka kukaa maeneo ya chuo kabisa,
alijisikia amani kutoa zile pesa na kumpa Bahati, “Sababu kasema anataka
kuboresha biashara yake, acha aboreshe. Mimi nitabaki nah ii laki tano ila nayo
hata siitamani sijui hata nifanyie kitu gani, yani mwanaume kanichefua Yule
amefanya niione dunia chungu kuliko uchungu wenyewe” Akamsikia mama yake
anajiongelesha ongelesha sebleni akaenda kumsikiliza, “Yani mwanangu
safari hii kikoba kitanitokea puani” “Kwanini mama?” “Unajua
nategemeaga biashara yangu ya vitambaa ila vimebuma yani wengi nimewakopesha
hawajalipa, halafu dadako Bite toka amepata mimba yani hakuna msaada tena
kwangu, kila ukipigia simu habari yake ni mimba mimba yani kama wimbo wa taifa.
Huyo Mage ndio sio wa kumtegemea kabisa, mtoto wa kiume sasa, ninae kama sina ni
hana msaada wowote toka anaishi kwa mjomba wake. Yani nahisi kukwama, sijui
mwezi huu nitapata hela wapi ya kupeleka kwenye kikoba, maana ni kesho hapo na
ukichelewa kupeleka faini” “Kwani ni sh ngapi mama?” “Si elfu
hamsini, yani hapa sielewi kabisa” Erica aliondoka pale sebleni na
kuelekea chumbani, mama yake alijua mwanae kamdharau, ila baada ya muda Erica
alirudi na kumkabidji mama yake hela, “Laki mbili hiyo mama, najua
itakusaidia” “Kheee wewe mtoto wewe jamani Mungu akuweke, Erica hujaanza
kazi ila nakula matunda yako mapema hivi. Ukianza kazi si nitanenepa mimi
jamani, Erica mwanangu, nakupenda sana jamani” Mama Erica alifurahishwa
sana na ile hela kwani hakuitegemea pia, na wala hakumuuliza kuwa kaitoa wapi.
Erica alirudi zake chumbani kwake na kujilaza. Alipokuja kushtuka
ilikuwa tayari saa mbili usiku, akakutana na ujumbe wa kawaida kutoka kwa
Rahim, “Mpenzi hata salamu jamani! Facebook huingii kabisa, nini tatizo
Erica kipenzi changu? Unajua nakupenda sana, ingia basi facebook tuchat
kidogo” Erica alisonya kisha akachukua simu yake na kuingia facebook
kuona kuwa huyu Rahim ana kipi kipya, akakutana na ujumbe wa
Rahim “Nimefurahi umeingia facebook mpenzi, najua umechukizwa na vitu
visivyokuwa na uhalisia. Mama aliniambia kuwa kakutana na wewe sijui
kakutambulisha msichana walionitafutia” Erica alipumua kidogo, kisha
akamtumia ujumbe pia, “Ndio, Rahim kumbe unanidanganya tu hunipendi wala
nini!” “Hivi Erica kama ningekuwa sikupendi ningekuwa nahangaika na wewe
kiasi hiki ili iweje? Wasichana wangapi wananitaka mimi huku nilipo ila kwanini
nahangaika na wewe?” “Sijui mwenyewe una maana gani?” “Najua
huelewi mambo ya familia yangu, yule mwanamke wameshauriana wenyewe kumtafuta
sababu mama yangu huwa anafikiria kuwa mimi siwezi kutongoza na wanaona umri
unaenda, wanataka nioe ila mimi ninayekutaka ni wewe. Sitarudi nchini mpaka
umalize chuo, sijataka kuwakatalia kwani sitaki kuanza kuumizana nao vichwa
kwasasa, sijamwambia mama kama ni wewe nikupendae sababu mama yangu namjua
ataanza kukusumbua. Yule ni mama yangu namjua vizuri sana Erica, wewe unamjua
kwa juu juu ila mimi namjua vizuri sana Erica. Tambua kwamba wewe ndiye mwanamke
nikupendaye na ninafanya vyote hivi sababu ya upendo wangu kwako, jitunze Erica
nakupenda sana” Kwakweli Erica hakuelewa hata ajibu nini kwa Rahim,
alisoma ule ujumbe mara mbili mbili huku akijaribu kutafakari ila alishindwa
amjibu kitu gani huyu Rahim, akamuuliza tena, “Kwahiyo Yule msichana
humpendi?” “Erica nielewe ninaposema nakupenda wewe, hakuna msichana
mwingine yeyote ninayempenda zaidi yako, ila nakuomba usiwe karibu kabisa na
mama yangu, atakupa presha za bure, yani jitenge na mama yangu. Ukimuona A, basi
wewe pita B. Nielewe mimi Erica, mimi ndiye ninayekupenda na si
mwinginewe” Erica alianza kulainika kwa maneno yale ya Rahimu maana
alijisikia vizuri sasa kuwa Rahim anampenda ila hela ndio alishazigawa tayari,
ila kabla hajamuandikia Rahim ujumbe mwingine wowote
alimuandikia, “Nitakutumia pesa nyingine kwaajili ya matumizi yako ya
hapa na pale Erica, tambua nakupenda sana. Mapenzi mengi huvunjika kwa
kusikiliza maneno ya watu ila nakuomba usisikilize maneno ya watu bali angalia
vitendo vyangu mimi” Alijikuta akiwasiliana nae kwa muda mrefu sana hadi
pale alipoamua kumuaga na kulala. Alipoamka alikuwa
akijifikiria sana, huku akijiuliza kama Rahim anampenda kweli au la, alikosa
jibu kabisa huku kichwani mwake akishindwa kumtoa Erick ila akishindwa pia
kumtafuta hewani maana alihisi kuwa Tumaini alimwambia mambo mengi sana maana
toka siku ile hakuona tena meseji kwenye simu yake kutoka kwa Erick wala kwenye
facebook yake. Alijiandaa na kwenda chuo kama kawaida, alipotoka tu
kwenye kipindi aliitwa na Derick, aliamua kwenda kumsikiliza, “Erica,
naomba unisamehe na tuanze maisha mapya. Nimetambua makosa
yangu” “Nishakusamehe tayari, ila kama umetambua makosa yako ni
vizuri” “Sasa nitakulinda dada yangu, nitakutunza sitapenda kuona
wakikusema vibaya. Nisamehe sana” “Usijali nishakusamehe” “Ila
dada yangu, naomba ujitulize. Usituamini sana sisi wanaume, tuna maneno matamu
kushinda asali ila ni waongo wa kupindukia, dada yangu napenda tuishi kindugu na
endapo utakuwa na swala lolote la kunishirikisha mimi niambie tu nitakuwa nawe
bega kwa bega, au hatakama unahitaji kuniuliza kama mwanaume yupi anakufaa
nifate nitakuambia. Ila dada yangu usirudie tena kutoa mimba ni hatari kwa afya
yako, hebu jihurumie dada yangu isije siku ukashindwa hata kuzaa kumbe sababu ya
kutoa mimba” “Nimekuelewa” Kiukweli hizi mada za kutoa mimba
Erica hakuzipenda kabisa, aliamua tu kumuaga Derick pale na kumuahidi kuwa
watakuwa wakiwasiliana vizuri tu. Erica aliondoka akielekea nyumbani
kwao ila hakuwa na sababu tena za kuhama chuo kile akajisemea kuwa hatohama ila
atamdanganya Rahim kuwa amehama ili Rahim asione kuwa pesa yake imeenda
bure. Alifika nyumbani kwao na kuongea ongea kidogo na mama yake ila
kwakuwa usiku ulikuwa umefika akaona vyema aende kulala, ila kabla ya yote
aliingia kwanza facebook ili kuangalia kama kuna jipya, alipofungua tu akakutana
na ujumbe wa Rahim, “Nimetoka sasa hivi kukutumia milioni mbili, najua
itakutosha kwasasa.” Erica alitabasamu na kuona kweli kuwa Rahim
anampenda ingawa hataki mama yake ajue, akamshukuru sana na kuongea nae mambo
mengi sana, “Erica, kaa mbali na mama yangu. Namjua mama yangu alivyo,
sipendi kuumia moyo, mama huniambia kitu hata nisipomuuliza, halafu namuamini
sana, naomba ukae mbali na mama yangu” “Ila hata nikiwa nae karibu kwani
nitafanya nini?” “Mama akijua una mahusiano na mimi atakufatilia kila
nyendo zako, unaweza kusimama na mwanafunzi mwenzio tu ila mama akajua ni
mchumba wako, akiniambia nitaumia sana na nitakuchukia Erica, naomba ujitenge na
mama yangu name niendelee kukuamini. Najua unanipenda, naomba ukae mbali na mama
yangu” “Sawa, nimekuelewa Rahim nitafanya hivyo” “Hata swala la
kukutana na wewe, sikumuuliza ila aliniambia tu ilivyokuwa na jinsi sura yako
ilivyoonyesha mshangao hadi akaniuliza kuwa kuna nini baina yetu ila nikamwambia
sina mazoea na wewe, tafadhali kaa mbali na mama yangu. Sitaki uumie moyo,
sitaki uniumize moyo” “Nimekuelewa Rahim” Alizungumza nae sana
kisha akamuaga kuwa analala, na akalala. Kulipokucha alijiandaa
kama kawaida kwenda chuo ila siku hiyo hakuwa na vipindi chuoni aliamua kwenda
kwanza benki kuchukua pesa ambayo Rahim alimtumia, alifika na kuzitoa kisha
kutaka kurudi tena kwao ila kabla hajapanda basi alipigiwa simu na Bahati
akimuomba afike mahali ambako yeye yupo, naye Erica alienda kwani alijua
asipoenda basi Bahati angefika nyumbani kwao, “Nimekuita hapa
kukuonyesha mahali nilipopatafuta kwaajili ya biashara yangu” “Aaah
kumbe! Ndio umepata kwa haraka hivyo!” “Ndio, kuna mama mmoja
nampelekeaga samaki ndio kanipatia eneo hilo, nimemwambia kuwa nataka kufanya
biashara na mchumba wangu. Amefurahi sana, twende yupo pia,
akakufahamu” Basi Erica akaongozana na Bahati hadi kwenye eneo hilo na
kuingia ndani, mama mwenye eneo alifika na Bahati kuanza kumtambulisha Erica kwa
Yule mama, “Mama, huyu anaitwa Erica ni mchumba wangu yani mke wangu
mtarajiwa” Muda huo mapigo ya moyo ya Erica yalikuwa yakienda kwa kasi
sana kwani mama Yule alikuwa ni Mrs.Peter yani mama yake na
Rahim. Basi Erica akaongozana na Bahati hadi kwenye
eneo hilo na kuingia ndani, mama mwenye eneo alifika na Bahati kuanza
kumtambulisha Erica kwa Yule mama, “Mama, huyu anaitwa Erica ni mchumba
wangu yani mke wangu mtarajiwa” Muda huo mapigo ya moyo ya Erica
yalikuwa yakienda kwa kasi sana kwani mama Yule alikuwa ni Mrs.Peter yani mama
yake na Rahim. Huyu mama aliuona uoga aliokuwa nao Erica,
akamuuliza “Mbona hivyo Erica?” Ndio Bahati akashangaa kuwa
wanafahamiana, “Kumbe mnafahamiana?” Mrs.Peter
akajibu, “Ndio, yani huyu Erica ni kama binti yangu vile. Nimefurahi
sana kuona mko pamoja, Erica bingti yangu mshike sana huyu kijana. Anakutajaga
sana ila sikujua kama anayekutaja ni wewe, huwa anasema anakupenda sana, hadi
anatamani dunia yote ijue ni jinsi gani anakupenda. Mshike sana
huyu” Erica aliitikia tu ila kinafki kwani haikutoka moyoni, hakutaka
hata kuendelea kuangalia mandhari ile kwani aliaga kuwa anawahi chuo na
akaondoka na kurudi kwao huku akiwa na mawazo mengi sana. Alifika kwao
na kuwaza sana, aliwaza kuwa aanze yeye kumtafuta Rahim na kumwambia au aache
kwanza kinuke ndipo atafute njia za kujitetea, alikuwa anawaza kuwa hata
kujitetea atajiteteaje, aliwaza sana bila ya jibu. Mama yake aliporudi
alimfata kuongea nae, “Mama nina rafiki yangu mmoja hivi kapatwa na
matatizo, sasa anaomba ushauri” “Matatizo gani?” “Ana mchumba
wake yupo nje ya nchi na huyo mchumba wake anamjali haswaa yani kama hela
anamtumia na kila kitu, ila sasa kuna mwanaume hapa nchini ni anamfatilia hadi
kero, kuna siku alikuwa kwenye matembezi yake Yule mwanaume nae alienda mara
gafla akakutana na mamake Yule mchumba wake wan je ya nchi, sasa anawaza kuwa
afanye nini maana Yule mchumba wake ataambiwa na mama yake” “Huyo rafiki
yako nae ni chizi, yani ni chizi kabisa namba moja. Mtu unapata mwanaume
anayekujali na pesa anakutumia halafu unaanza kuzunguka na hawa vinuka mkojo
wakusaidie nini kwanza kama sio utahira huo? Unajua wanasema unaposhikwa
shikamana, sasa huyo rafiki yako atakula jeuri yake. Ila na wewe mwanangu wakati
wenzio wanapata wanaume nje ya nchi kwanini wewe hupati? Kwani una kasoro gani
mwanangu jamani!” “Mama utamjua tu mchumba wangu hata
usijali” “Usije ukanitambulisha Yule muuza samaki, kwakweli Erica
nitakunyofoa macho hayo. Sitaki ujinga kabisa, tafauta na wewe wanaume wan je ya
nchi ndio wanakuwaga na hela” “Mama jamani, kwahiyo kwako hela ni bora
kuliko mapenzi ya kweli!” “Hebu nitolee balaa za mapenzi ya kweli,
tumepitia haya mambo ndiomana nakupa ushauri wa kumng’ang’ania mwenye hela. Mimi
nilimpenda baba yenu ingawa alikuwa fukara ila sababu ya upendo wa kweli
nikaowana nae, ona sasa alichokuja kunifanyia, kujitia yeye mashuhuri wa kuoa
wake wawiliwawili wakati bila mimi asingepata heshima hii iliyomfanya ajidai
duniani. Mwanangu unaweza ukawa na fukara na akakusaliti na unaweza ukawa na
mwenye pesa na akakusaliti sasa bora kusalitiwa na mwenye pesa haiumi sana ila
kusalitiwa na fukara inauma mwanangu asikwambie mtu” “Sawa mama
nimekuelewa, kwahiyo ushauri wako kwahuyo rafiki yangu” “Huyo sina
ushauri kwake, atachagua mwenyewe kusuka au kunyoa. Wenzie wanatafuta wanaume
kama hao wenye pesa halafu yeye anachezea bahati. Yani ingekuwa enzi zangu
nipendwe na mwanaume mwenye pesa yani njiani hata salamu ya mwanaume mwingine
nisingeiitikia” “Mmmh mama hata salamu ya baba
usingeitikia?” “Achana na mambo hayo bhana” “Sasa mama kwahiyo
hakuna ushauri kwa huyo rafiki yangu?” “Sina ushauri maana hayo matatizo
ni ya kujitakia. Ngoja nifanye shughuli zangu mie, ushauri kuwapa watu wasiokuwa
na akili sitaki” Mamake aliondoka, Erica nae alienda chumbani kwake,
akawaza sana kuwa hata mama yake kamtoa akili, “Kwani kosa langu mimi ni
nini? Najifikiria sana ila sijui kosa langu kabisa, kosa langu ni kujiingiza
kwenye mahusiano ya kimapenzi au kosa langu ni nini? Na kwanini kila neema
inapokuja kwangu linatokea jambo la kuharibu neema hiyo, kosa langu ni nini
haswaa? Erick nimemkosa na huyu Rahim nimkose pia jamani! Yani mwanaume pekee
anayekuwa na mimi bega kwa bega ni Bahati, sielewi kwakweli” Aliamua
kulala tu ingawa hakuwa na usingizi kwa muda huo ila aliamua
kujilaza. Ilipofika usiku aliingia kwenye mtandao huku akiwaza
kama Rahim ameshapata habari ila siku hiyo aliwasiliana vizuri sana na Rahim,
ikionyesha kwamba habari hajapata, akawa anamuomba Mungu mamake Rahim asahau na
asimwambie ukweli Rahim, kitu pekee ambacho alisisitizwa na Rahim kwa siku hiyo
ni kuwa asome basi na sio swala lile kabisa, hakuulizwa. Aliendelea na
mawasiliano na Rahim na hakuna siku ambayo Rahim alimuuliza chochote kuhusu
Bahati na kuhisi kuwa huenda mama yake Rahim hajamwambia chochote. Dada
yake alikuwa kajifungua kwahiyo alikuwa akihudumiwa pale nyumbani kwao, muda
mwingi alijikuta akimdadisi dada yake kuhusu shemeji yake maana
hakumuamini, “Dada. Kwahiyo Yule msichana wako wa kazi ndio umemuacha na
shemeji” “Ndio, maana mume wangu atashindwa kwenda kazini anatakiwa
kuhudumiwa kila kitu, kufuliwa nguo, kupigiwa pasi, kupikiwa lazima Yule mdada
abakie” “Ila pia na huku kuna kazi, kumuangalia mtoto, kumuhudumia,
kufua nguo za mtoto. Kwanini usingekuja nae huku
akusaidiage?” “Unayosema ni kweli ila kule mume wangu nae anatakiwa
kuhudumiwa, kuna msichana nimeagiza atakuja kunisaidia hapa
nyumbani” “Kwahiyo utakaa hapa hadi uzazi uishe?” “Kwani mdogo
wangu vipi? Hutaki kuniona hapa nyumbani au? Nakuzibia nini hapa? Mbona shughuli
zote anafanya mama, kwani ni wewe unatumwa kufanya kazi za hapa” “Hapana
dada, ila nasikiaga wanaume kipindi wake zao wakitoka kujifungua hupenda sana
kutembea na wasichana wa kazi” “Ushindwe na ulegee, sio kwa mume wangu
mimi. Kashindwa kunisaliti kote huko ulaya alikokuwa, aje kunisaliti na msichana
wa kazi? Hiko kitu hakunaga, mume wangu ana kinyaa sana hawezi tembea na
msichana wa kazi” “Dada, ila wanaume si wa kuwakatalia sana maana hata
msichana wa kazi naye ni mwanamke kama wewe” “Weee mtoto wewe, ujue mimi
ni mkubwa wako na mapenzi nimeyajua kabla yako, au kwavile ulibeba mimba ya Yule
taahira ndio unazani mapenzi yapo hivyo? Kwanza wewe mdogo wangu sijui ukoje,
huna kinyaa, hivi kweli wewe wa kwenda kutembea na Yule mwanaume? Loh! Uchafu
mtupu, mwanaume huendani nae hata kidogo, yani wewe mdogo wangu wewe, ndiomana
unahisi kusalitiwa tu. Wanaume masikini na wachafu wachafu ndio wanaosaliti ila
sio wanaume wasomi na waliondelea” “Mmmh dada, haya
yaishe” Erica hakutaka kumwambia vitu vingi dadake kuhusu shemeji yake,
ila alikuwa na hisia mbaya sana kuhusu shemeji yake maana hakumuamini kabisa.
Ila alimshangaa sana dada yake kuwa na imani vile na mume
wake. Erica alikuwa akienda chuo akitokea nyumbani kwao,
walipokuwa wanakaribia kumaliza mwaka wa pili walitakiwa kutafuta sehemu
watakayo fanya mafunzo kwa vitendo, na kwa bahati alipata kwenye ofisi ya
shemeji yake James. Alifurahi ila akafikiria sana namna itakavyokuwa hapo
ofisini kwa shemeji yake, ni kweli kapata sehemu ya mafunzo ila mtihani uliopo
ni kuwa kwenye mafunzo hayo ni kwa shemeji yake ambaye amekuwa akimtaka, ila
kwavile alishajisemea kuwa hatotembea na mume wa dada yake akaamua kushikiria
msimamo wake huo huo. Kwahiyo walipofunga chuo, walihamia kwenye mafunzo
kwa vitendo, na alikuwa akienda mara kwa mara kama alivyohimizwa na dada
yake. Siku hiyo shemeji yake alimuita ofisini, “Mbona unanikwepa
sana Erica? Au ule uongo wako ndio unafanya unikwepe sana siku
hizi!” “Hapana shemeji” “Si ulininyima ukaenda kuwapa wale
mabwege, ila nakutamani mtoto wewe” Erica alikuwa kimya tu ila shemeji
yake aliendelea kumuongelesha, “Basi naomba siku tutoke Erica wangu
jamani” Erica bado alikuwa kimya kabisa kwani hakujua hata amjibu nini
huyu shemeji yake ukizingatia ndio yupo kwenye ofisi yake akiendelea na mafunzo,
aliwaza kuwa ni kitu gani kinaweza kumfanya huyu shemeji yake asimsumbue
kabisa. Akaona akifika nyumbani atapata wazo kuwa afanye kitu gani ila
kwa muda huo hakuweza kumjibu shemeji yake. Muda wa kuondoka ulipofika, shemeji
yake alimkazania kuwa ampe lifti ya kumpeleka nyumbani na akamuangalie na mtoto,
kwa bahati kuna mtu alitokea na kumuita shemeji yake kwahiyo yeye akaondoka na
kwenda nyumbani. Aliwaza sana maana ndio kwanza alikuwa na siku
ya tatu kwenye ile ofisi ila shemeji yake kashamuanzishia tamaa, akawaza sana
kuwa atafanya kitu gani, akapata wazo moja kuwa amuombe Bahati awe anaenda
ofisini kumchukua ili shemeji yake akose hata ile nafasi ya kusema kwamba nikupe
lifti kumbe ana mambo yake mengine. Akampigia simu Bahati na kumwambia
hilo swala, kwakweli hilo swala lilikuwa ni swala la furaha sana kwa Bahati na
alijiona kuwa ana bahati kama jina lake maana hiyo nafasi aliihitaji sana na
kipindi hiko akaipata, “Erica, nitakuwa nafunga biashara zangu mapema
ili nije kukuchukua mpenzi wangu. Nashukuru kwa kuniamini” Erica
alikubaliana nae muda wa kwenda kufatwa pale ofisini na kumuelekeza ofisi ilipo,
maana yeye toka siku ile amuone mrs.Peter hakutaka tena kwenda kwenye ofisi ya
Bahati ili kumuepuka na vile ambavyo Rahim hakumuuliza kulimfanya kuona kuwa
Rahim hajaambiwa chochote kuhusu yeye. Na siku zote alikuwa akiwasiliana
kawaida tu na Rahim na hakuthubutu kumwambia kuwa kwa kipindi hiko yupo kwenye
mafunzo ya vitendo kwani alihisi labda atazua maswali mengi sana kwa
Rahim. Kesho yake alienda ofisini kwa shemeji yake kama kawaida, ila
muda wa kutoka alifika Bahati na kumfanya yeye aondoke nae, shemeji yake
akamuita, “Erica, jana umenikimbia tusiongozane na leo tena unakimbia.
Kwanini unafanya hivyo?” “Aaaah shemeji kuna mtu huwa anakuja
kunichukua” “Mtu gani huyo?” “Ni mchumba wangu” Kisha
Erica akamuaga shemeji yake na kuelekea nje, kitendo ambacho kilimfanya James
kutoka pia ili kuona ni nani huyo anayeenda kumchukua Erica, alichukia sana
baada ya kumuona ni Bahati maana hakumpenda kijana huyo toka siku ya kwanza
aliyomuona na Erica. Ila swala la shemeji yake kuchukia halikumfanya
Erica ajali chochote kwani yeye cha msingi yupo salama tu, akaenda nyumbani
kwao. Baada ya kufika tu nyumbani muda kidogo James nae alifika
kwenda kumuona mtoto wake, na akaanza kulalamika kwa mke wake kiasi kwamba Bite
aliamua kumnuita mdogo wake, “Wewe Erica, kwanini usingekuwa unasubiri
lifti ya shemeji yako?” “Dada kuna rafiki yangu huwa anakuja
kunichukua” “Rafiki? Rafiki yako yupi?” James alidakia pale
pale, “Si kile kimwanaume chake” “Kheee yani Erica mdogo wangu
umeanza tena na kile kimwanaume? Hivi hujisikii aibu?” “Dada, mimi ni
msichana mkubwa sasa na wala hakuna sababu ya kunigombeza. Nina machaguo yangu
na mimi maana nimekuwa sasa. Haijalishi yukoje ila ndio chaguo
langu” “Aaah umekuwa eeeh! Na usiniombe hela tena” “Lini
nimekuomba tena hela dada?” “Kheee wewe Erica wewe, ndio anakupa kiburi
Yule mwehu eeeeh! Subiri sasa, atakusimulia.” Erica aliondoka zake kwani
swala la kulazimishwa kuwa yeye aongozane na shemeji yake hakulifurahia kabisa,
ukizingatia shemeji yake huyo aliyajua mambo yake. Siku hiyo
dada yake alimuaga kabisa kuwa kesho yake atakaporudi hatomkuta sababu anarudi
kwa mume wake, “Kesho mdogo wangu narudi kwangu, mwanangu amechangamka
sasa. Na mimi nisharudi katika hali yangu” “Na kweli umerudi katika hali
yako, maana kukaa uzazi miezi mitatiu sio mchezo, na mwezi mmoja wa matamazio
kweli mumeo atakuwa amekumiss sana maana ni muda umepita” “Kweli
uyasemayo, lazima kanimiss sana hadi namuoneaga huruma ila ndio nilikuwa nafata
sharia” “Sasa, utakuwa na wafanyakazi wawili au mmoja
utamuondoa?” “Kwasasa nadhani inabidi niwe nao wote wawili maana mmoja
atakuwa na mtoto halafu mwingine shughuli za nyumbani si unajua nitaanza na
kwenda kazini!” “Sawa dada, nakutakia maisha mema” Aliongea
vizuri na dada yake ila alikuwa na hofu kubwa sana juu ya msichana wa kazi
ambaye dada yake kamuacha kule kwake. Kesho yake akaelekea kazini kama
kawaida, alifanya kazi zake ila akaitwa na shemeji yake, “Hivi Erica
unajua unavyonifanyia sio vizuri kabisa” “Kwanini
shemeji?” “Yani wewe Erica wa kunikataa mimi kweli sababu ya kile
kimwanaume jamani! Sikia Erica, mimi ukinikubali nitakufanyia vitu vingi sana
vizuri” “Mbona dada yangu hujamfanyia?” “Achana na habari za
dada yako, sikia kitu kizuri naomba leo umwambie jamaa yako asije kukufuata kuna
sehemu nataka niende na wewe. Ni sehemu special kwako” “Kheee shemeji,
badala leo uwahi kurudi nyumbani unataka tena uwende mahali na uchelewe
kwako!” “Kwanini niwahi sasa?” “Dada leo amerudi nyumbani kwako,
wahi ukacheze na mtoto” Ila ile habari ilionekana kumshtua kabisa
James, “Ameendaje nyumbani bila kunitaarifu jamani?” “Kheee pale
si nyumbani kwenu? Akutaarifu nini sasa? Labda alitaka
kukushtukiza” “Aaaargh yani Bite akili zake ni ziro
kabisa” James aliondoka na kumwambia Erica akaendelee na kazi, kisha
yeye aliaga na kuondoka kabisa pale ofisini, Erica alihisi kuwa lazima kuna
tatizo maana sio swala rahisi, akaamua kumpigia simu dada yake ili amuulize tu
kwa kimtego na ajue tatizo ni nini, ila dada yake alipokea simu na kuongea kwa
jazba sana, “Erica, huyo James yupo ofisini
hapo?” “Ametoka” “Kwakweli sielewi mdogo wangu, unaweza kuamini,
nimemkuta huyu msichana ni mjamzito yani nashindwa kuelewa James aliishi vipi na
mdada mwenye mimba hapa” “Usipaniki dada, kwani umemuuliza kuwa mimba ni
ya nani?” “Ananichanganya kwakweli nachanganyikiwa, ananijibu kwa nyodo
kuwa yeye ni mke mwenzangu. Nimechanganyikiwa hapa mdogo wangu” “Subiri
kidogo dada” Erica aliamua kumpigia simu dada yao Mage ili kumuharakisha
kuwa aende nyumbani kwa Bite maana yeye kidogo ana busara, pengine wanaweza
wakaelewana. Kisha nay eye alianza kumalizia kazi zake ili akimaliza aende kwa
dada yake pia ajue kilichojiri. Erica alimaliza shughuli
alizopangiwa kisha akaaga ili kuondoka, ila alipotoka ofisini tu alimkuta Bahati
akimsubiriria nje, na alipomuona alimsogelea na kumkumbatia ila kilichomshangaza
ni kumuona Mrs.Peter akiwapiga picha, akaanza kumuuliza Bahati kabla
hawajamsogelea huyu mama, “Vipi umekuja na mama huyu?” “Aliuliza
kila siku nawahi wapi, nikamwambia huwa nawahi kumpitia mke wangu nimrudishe
nyumbani kwanza. Ndio akasema leo tuje wote” “Sasa mbona alikuwa
anatupiga picha?” “Kuhusu picha sielewi, labda ngoja
tumuulize” Walisogea karibu na kumsalimia, Yule Mrs.Peter alianza
kujieleza mwenyewe kabla hata hajaulizwa, “Nimekupiga picha Erica ili
kupata picha ya ukumbusho na uthibitisho. Unajua Rahim nilimwambia kuwa
nimemuona mumeo akanikatalia katakata kuwa huna mume, sasa leo nataka nimtumie
na picha kabisa aone” Erica alihema kwanza na kumuuliza, “Khaaa
mama, sasa picha za mimi na mume wangu umtumie Rahim za nini?” “Unajua
ulivyoongea hivyo nimekurekodi na nishamtumia? Picha nazo nishamtumia kwani kuna
ubaya gani?” Erica alimuangalia huyu mama na kutamani hata kumnasa
vibao. Walisogea karibu na kumsalimia, Yule Mrs.Peter
alianza kujieleza mwenyewe kabla hata hajaulizwa, “Nimekupiga picha
Erica ili kupata picha ya ukumbusho na uthibitisho. Unajua Rahim nilimwambia
kuwa nimemuona mumeo akanikatalia katakata kuwa huna mume, sasa leo nataka
nimtumie na picha kabisa aone” Erica alihema kwanza na
kumuuliza, “Khaaa mama, sasa picha za mimi na mume wangu umtumie Rahim
za nini?” “Unajua ulivyoongea hivyo nimekurekodi na nishamtumia? Picha
nazo nishamtumia kwani kuna ubaya gani?” Erica alimuangalia huyu mama na
kutamani hata kumnasa vibao. Huyu mrs.Peter aliona jinsi Erica
alivyoonekana kuchukizwa na swala lile, akamuuliza tena, “Kwani
nimefanya vibaya mwanangu?” Erica alikuwa kimya tu, Yule mama
akamuangalia Bahati na kumuuliza “Eti baba nimefanya
vibaya?” “Hapana mama, naona ni vizuri tu maana mimi na Erica
tunapendana sana” “Asante, ndio nilichokuwa nakitaka,
kwaheri” Yule mama aliondoka na kuwaacha pale wamesimama, ila kiukweli
Erica hakuwa na raha hata safari ya kwenda kwa dada yake aliahirisha na kutaka
tu kwenda moja kwa moja nyumbani kwao. Erica alifika kwao ila
mama yake hakumkuta kwa muda huo akahisi labda mama yake amechelewa kwenye
vikoba vyake siku hiyo, ila sababu alikuwa na mawazo aliamua kwenda kulala tu,
ila hata usingizi wenyewe haukumpata kwani alikuwa na mawazo lukuki, akawaza
kuwa pesa ambazo huwa anapewa na Rahim zitakuwa zimefikia mwisho maana akiambiwa
tu na mama yake na kutumiwa ushahidi wa picha na sauti yeye atakuwa ameisha
kabisa, aliwaza sana na muda nao ulienda ila mama yao alikuwa bado hajarudi hadi
akataka kumpigia simu ili ajue tatizo ni nini. Ila wakati anawaza kumpigia simu
alisikia sauti yake ikiita, ikabidi aende kumsikiliza, “Kila siku huwa
nasema wanaume ni mbwa jamani tena mbwa kabisa” “Kwani vipi
mama?” “Si Yule shemeji yako James, kumbe kampa mimba Yule msichana wa
kazi, yani sokomoko la huko leo lilikuwa balaa, hujashangaa hujanikuta hapa
nyumbani!” “Nimeshangaa na nikajiuliza kuwa imekuwaje, nikadhani labda
upo kwenye kikoba” “Kikoba wapi? Mambo yalikuwa sio mambo huko, Mage
alinipigia simu ndio nikaenda, jamani mwanaume Yule anaonekana mstaarabu kwa nje
kumbe mbwa tu” “Ila mama kwani wanaume wote wapo hivyo?” “Hakuna
mwanaume aliyetulia mwanangu, yani kuhusu usumbufu wa wanaume ni kilio cha kila
mwanamke” “Mmmh mama ila si huwa unawasema makapuku tu, kumbe wenye hela
nao hawafai” “Hakuna cha mwenye hela wala kapuku, yani kiukweli mwanangu
mimi hata sielewi kama kuna wanaume wanaishi bila usaliti jamani” “Wapo
mama” “Hawapo, labda ashushwe toka mbinguni. Usimkatalie mwanaume hata
mara moja, uwezi jua mambo anayoyafanya nyuma ya pazia” “Mmh sawa mama,
ila mmeishia vipi kwa dada sasa?” “Yani Bite alitamani kurudi nyumbani
ila nimemshauri kurudi nyumbani sio suluhisho, kwani ni lazima akae hapo na
mumewe na wajue ni wapi alikosea mpaka mume wake akamsaliti.” “Kwahiyo
huyo mwenye mimba kaenda wapi?” “Tumemfukuza, unajua unapokuwa mke wa
mtu inabidi ujivike moyo wa ukatili maana ukiwa mpole sana mumeo atawapa mimba
hadi kuku na kukuletea nyumbani. Tumemfukuza pale, atajua mwenyewe pa
kwenda” “Na shemeji?” “Hajarudi hadi tunaondoka ila kwa
nilichomfundisha Bite Yule mumewe ataelewa tu. Nawajua wanaume kupita hata
wanavyojijua wenyewe” Erica alimuangalia mama yake anayesema anawajua
wanaume sana ila alishindwa kumshauri mwanae kuwa akae karibu na mumewe asiibiwe
na msichana wa kazi maana ingewezekana kabisa Bite angejifungulia kwa mume wake
na mama yake angekuwa anaenda kumtazama ila kwavile alitulia kwao ilitoa upenyo
mkubwa sana kwa mumewe kuwa na msichana wa kazi ukizingatia mume wake mwenyewe
ni penda penda. Erica aliagana na mama yake na kwenda kulala
maana ilikuwa ni saa tano usiku, hakuwa na usingizi sababu ya mawazo ila aliamua
kwenda tu kujilaza, ila kabla hajajibembeleza vizuri na usingizi akapokea ujumbe
wa kawaida ukitoka kwa Rahim, “Naomba uingie facebook muda
huu” Ilibidi Erica achukue simu yake na kuingia kwenye mtandao kwani
alijua lazima atakutana na lawama sababu Yule mama inaonyesha tayari alishasema,
alipoingia tu akakutana na jumbe kadhaa kutoka kwa Rahim, kwanza aliona picha za
yeye na Bahati pia akatumiwa zile sauti ya kwanza akasikia yeye akisema “Khaaa
mama, sasa picha za mimi na mume wangu umtumie Rahim za nini?” na sauti ya pili
ilikuwa ya Bahati na ilisikika, “mimi na Erica tunapendana sana” Erica
alizisikiliza na kumshangaa sana mrs.Peter “Jamani Yule mama ana mambo
ya Kiswahili loh! Sasa kumtumia mwanae picha na sauti ili iweje jamani? Kwani
anahisi natoka na mwanae au? Sasa anamchunga hivyo mwanae na kumtafutia wachumba
wa nini sasa? Loh mama mswahili sijapata kuona” Kisha akaendelea
kuangalia ujumbe utakaofatia toka kwa Rahim, “Erica naomba unieleze
kuhusu hizo picha na hiyo sauti” “Rahim hata sijui nikwambie
nini” “Unajua Erica umeniumiza sana, hivi unajua hilo? Umeumiza sana
moyo wangu, kwanini kunifanyia hivi? Yani unanifanya mimi kama
poyoyo” “Hapana Rahim usinifikirie vibaya, nadhani tu mama amenielewa
vibaya” “Hivi nyie wanawake mkoje? Mnataka mpewe nini ndio mridhike
nyie? Kwenu mwanaume akikupa pesa ni shida, akikupa mapenzi ni shida, hivi
mnataka nini haswaa? Kuna kitu hupati kwangu Erica? Nimekwambia ukiwa na shida
yoyote niambie nitakusaidia, nimejitoa kwaajili yako Erica halafu wewe unaenda
kunifanyia upuuzi huu kweli?” “Rahim hata sijui nikueleze nini ila mama
kanielewa vibaya tu” “Erica nilishakutahadhalisha kuhusu mama yangu,
hata hivyo mama yangu sio chizi kusema akurupuke tu kufanya mambo. Sikutegemea
Erica kama ungeweza kudanganywa na kijana mwingine ilihali nakupa kila kitu cha
kukuonyesha kwamba nakupenda. Unajua kinachoniuma zaidi ni nini? Ni huyo kijana,
nakumbuka nilibishana nae kuwa kati yake na mimi anapendwa nani? Sasa kama mimi
na huyo tu hujui umchague nani, je huyo Erick akisema arudi utanifikiria mimi
kweli?” Erica alisoma huu ujumbe mara mbili mbili na kushindwa ajibu
vipi ila aliishia tu kutuma meseji, “Nisamehe Rahim” “Erica,
kuna siku nitakufanyia kitu ambacho hutokuja kukisahau katika maisha
yako” “Jamani Rahim, ndio unafikia huko kweli? Naomba unisamehe maana
hata nikikuelezea hautaniamini ila naomba unisamehe” “Erica umeniudhi
haijapata kutokea yani leo umefanya siku yangu iwe mbaya kuliko siku zote,
umeniudhi sana Erica hata sijui nifanyeje” “Naomba unisamehe
Rahim” “Erica, sijui niseme nini ila kwavile nakupenda. Kwasasa lala tu,
sina cha kukwambia” Erica alibaki kuandika jumbe za kuomba msamaha tu
bila ya kujibiwa tena huku akiwaza kuwa ni kitu gani kibaya atakachopangiwa na
Rahim, hakuelewa ila pia hakujua kama Rahim anaweza kumsamehe na aendelee
kuwasiliana nae kama zamani kwani kwa kipindi hiko ni kweli hela ya Rahim ndio
iliyokuwa inamtia kiburi. Akaamua kulala tu maana hata akiendelea
kufikiria sana haina maana na muda huo ulikuwa umeenda ilikuwa ni saa nane
usiku, halafu kesho yake anahitajika aende kule kwenye mafunzo asubuhi halafu
anachelewa hivyo kulala. Ikabidi tu atafute usingizi ingawa kwa nadra, akalala,
huku akifikiria kuanza kumuweka moyoni mwake Bahati maana hakujua ni kitu gani
Rahim kapanga kwaajili yake, akawaza ile hela aliyopewa na Rahim ile milioni
mbili kuwa alifanya vyema kupunguza milioni moja na kumpa Bahati aongezee mtaji
ambao ni hela nyingine aliyoipata kwa Rahim ila kwa muda huo alihisi huenda
Bahati ndiye mwanaume wa kutengeneza nae maisha. Kulipokucha
siku hiyo aliamshwa na mama yake maana yeye alilala hoi hata habari hakuwa nayo,
aliamka na kujiandaa kisha kwenda ofisini, alimkuta shemeji yake yupo ofisini
tayari kanakwamba alilala palepale na alikuwa na nguo zile zile za jana, ikabidi
aende ofisini kwa shemeji yake kuongea nae vizuri maana zile ofisi zilikuwa za
vioo ambavyo vilikuwa vinaonyesha kama bosi yupo au hayupo. Erica
aliingia kuzungumza nae, “Shemeji vipi? Inaonyesha hukurudi nyumbani
kwako!” “Na kweli sikurudi hata sijui ni jinsi gani nitamuangalia mke
wangu” “Ila mbona jana uliondoka hapa kama unaenda
kwako?” “Unajua nimechanganyikiwa eeh Erica, ni kweli nilikuwa naenda
nyumbani kwangu ila nilipofika tu nilimsikia mke wangu akigombana na kile
kisichana halafu kwa mbali nikamuona dada yenu Mage anakuja, mmmh namuogopa Yule
dada, nikaona hapa balaa ndio nikaondoka sijarudi kabisa nyumbani
tena” “Sasa utaweza kufanya kazi hivyo?” “Hata sijui, kichwa
chote kimenivurugika. Jana nilienda kunywa pombe, na nilizinywa sana ili mawazo
yakae sawa” “Basi, ilitakiwa leo unywe supu kwanza” “Basi
nisindikize Erica, nakuomba na wala sitakwambia tena mambo ya
mapenzi” Kiukweli James alionekana mtu wa kujutia kwa kile
alichokitenda, na Erica alikubali kumsindikiza shemeji yake akapate supu kwahiyo
ilibidi amuachie maagizo msaidizi wake na kuondoka na Erica. Walifika
kwenye baa kisha akaagiza supu, ikabidi naye Erica aagize supu huku akijaribu
kuongea na huyu shemeji yake maana lazima kuna kitu kinachomfanya shemeji yake
kuwa katika ile hali, “Hivi shemeji, kwani humpendi
dada?” “Hapana, nampenda” “Sasa kwanini
unamsaliti?” “Erica, ngoja leo nikwambie sababu ya mimi kumsaliti dada
yako. Mimi ni mwanaume, nahitaji mapenzi yale yenyewe yenyewe kiasi kwamba
nikiyapata wala nisitamani mwanamke mwingine. Jamani Erica, dada yako hajui
mapenzi kabisa yani hajui kitu hata najuta kuoa mwanamke mshamba kama yeye. Kwa
nje anaonekana mjanja ila kumbe mshamba” “Mmmh jamani! Nyie wanaume
hamna shukrani, umepata mwanamke bikra unasema ni mshamba, ila ukipata
aliyetangatanga ndio mjanja halafu wakati huo huo mnapenda kuoa mabikra sababu
ndio heshima. Ushamba wa dada yangu hauwezi kufanya wewe umsaliti, kumbuka wewe
ndio wa kumfundisha mapenzi dada, hivi usipomfundisha wewe atafundishwa na
nani?” “Erica, hujui tu. Nilipoenda ulaya nilijua nikirudi atakuwa
amejifunza mambo mengi ila ndio kwanza yupo kama gogo hata hajishughulishi na
alivyopata mimba ndio kabisaaa kila ukimshika anadai anaumwa, hivi kuna wanawake
wangapi wanaishi vizuri na waume zao na mimba zao? Dadako anadeka sana, yani
yeye ndio anapelekea mimi kumsaliti” “Ila unavyofanya sio vizuri, wewe
ndio wa kumbadilisha dada, mwambie hupendi ambavyo anakosa ubunifu nina uhakika
dada atajifunza vitu vipya vya kufanya na wewe. Usihangaike nje shemeji yangu,
magonjwa mengi sana.” “Una maneno ya busara sana, hadi natamani wewe
ndio ungekuwa mke wangu, yani Bite nilimuoa basi tu” “Umeanza maneno
yako shemeji” “Sio nimeanza Erica, kiukweli natamani wewe ndio ungekuwa
mke wangu. Upo tofauti sana Erica, wewe ni msichana kati ya wasichana ambao
sijawahi kukutana nao maishani. Erica ungekuwa aina nyingine ya msichana
ungeshatangaza kwenu kuwa nilikutaka kimapenzi ila mpaka leo imebaki kuwa siri
yako kwa kulinda penzi la dada yako. Erica kiukweli, mume atakaye kuoa atakuwa
amepata mke haswaaa, tofauti na dada yako kitu kidogo lazima aseme nyumbani
kwenu hadi najuta kumuoa” “Mmmh jamani! Ulilazimishwa
kwani?” “Hapana sikulazimishwa ila kuna mwanamke nilikuwa nae kabla ya
Bite, alikuwa ni binti wa ukweli ila sikuweza kuoana nae sababu ya itikadi. Na
nilivyokutana na Bite, binti mpole basi nikatangaza ndoa maana Yule msichana
niliyempenda nae alikuwa ameolewa” “Mmmh mapenzi bhana, kizunguzungu tu.
Kwahiyo wewe ulimpendea nini dada?” “Kiukweli Bite nampenda akicheka
anavyobonyea mashavuni yani hapo roho yangu burudani, ila sikujua kama atakuwa
mshamba vile kwenye mapenzi” “Yani ulimpendea dimpozi tu? Ila kwasasa si
unampenda dada kushinda Yule wa zamani?” “Ndio, nampenda sana Bite
halafu nampenda kweli ila kwasasa naomba unisaidie jambo moja tu, naomba wewe
uende kwanza nyumbani kwangu. Ongea kwanza na dadako ndio mimi nitakuja maana
najua una maneno ya busara na unaweza kumfanya dadako anisamehe na tuendelee
vyema kumkuza mtoto wetu” Erica alikubali na shemeji yake alimuomba muda
ule ule aende kwahiyo James alimuombea tu udhuru ofisini, “Ila shemeji
usinywe tena pombe basi” “Sinywi, ukiongea nae tu vizuri akikaa kwenye
mstari niambie nije” Sawa” Erica aliondoka pale na kwenda kwa
dadake, huku akiwaza kuhusu vitu vingi sana, aliona kuwa mapenzi ni kitu cha
ajabu sana kumbe mtu anakwambia anakupenda halafu alimpendaga mwingine ila
hayupo nae tena kwahiyo inabidi aishie kukwambia wewe tu anakupenda, ila
hakufikiria kama ushamba wa dada yake ndio unamfanya shemeji yake awe msaliti
ila ile ni tabia ya shemeji yake ndiomana ameweza kumtongoza hata
yeye. Alifika na kumkuta dadake kajiinamia tu, na alionyesha
kuwa na mawazo mengi sana. Alimkaribisha ila alikuwa na unyonge wa hali ya
juu, “Pole dada, naelewa matatizo unayopitia” “Yani acha tu
mdogo wangu” Erica alijaribu kuongea na dada yake kwa maneno ya busara
ili hata akirudi mume wake asije akamfanyia hasira, “Dada najua
unavyompenda shemeji na yeye anakupenda, wala usiruhusu shetani ayaingilie
mapenzi yenu. Msamehe Yule ni mumeo, akirudi mkaribishe na akipumzika muulize
kwa upendo tu kuwa ilikuwaje akafikia hatua ile, unajua na yeye ni binadamu,
kila binadamu ana mapungufu yake hakuna aliyekamilika ila usiruhusu shetani
kuyavuruga mapenzi yenu. Yani mchukulie huyo msichana kama shetani
tu” Erica alijaribu kumuelewesha dada yake hadi alionyesha kuwa yupo
kwenye mstari kisha akamtumia ujumbe shemeji yake kuwa arudi tu
nyumbani. Halafu yeye akamuaga dada yake kuwa anaondoka kwani alitaka
shemeji yake akifika apate muda wa kutosha wa kuzungumza na dada yake maana
alijua kwa vyovyote vile kama mtoto angesumbua basi angekaa na Yule msichana wa
kazi ambaye kazoea kumlea mtoto Yule tokea wapo kwao. Muda huo aliondoka
na kwenda kwa dada yake Mage, na alifika na kumkuta kisha akamsalimia na kuanza
kuongea nae, “Sasa dada kwanini mlifikia hatua ya kumfukuza Yule dada
aliyepewa mimba na shemeji?” “Kwanini aachwe? Kwanza msichana ana kiburi
sana Yule, anajisema eti mi mke mwenzio, na sisi tukasema hutujui eeh! Dawa ya
kiburi ni jeuri Erica, yani tulivyomtimua pale hajaamini macho yake. Sipendagi
ujinga kabisa mimi” “Ila dada, wewe hujawahi kuletewa mtoto wa
nje?” “Sikia Erica nikwambie kitu, kwasasa sijui kama mume wangu kazaa
huko nje ila siwezi sema kuwa namuamini na hawezi kuzaa nje, siwezi sema hivyo.
Ila ikitokea nikiletewa mtoto wan je nitamlea tu tena kama mwanangu wa kumzaa
ila mama yake huyo mtoto akiwa mstaarabu nitaongea nae kistaarabu hata kuwa na
urafiki nae ila akijifanya jeuri yani hatokanyaga hata hapa kwangu kuja
kumsalimia mwanae.” “Mmmh dada, haya kuhusu swala la kuja nyumbani na
shemeji mmejipangaje?” “Tumejipanga ujue, yani mwezi huu hauishi
tutakuwa nyumbani tayari. Ila mdogo wangu najisikia kukwambia tu, kuwa makini
sana na hawa wanaume maana mwingine anaweza kuonyesha anakupenda kweli kumbe
nyuma ya pazia wala hakupendi ila anavutiwa nawe tu sababu ya kitu
Fulani” “Hivi inawezekana mtu akavutiwa nawe kwa kitu Fulani na
akaonyesha kuwa anakupenda?” “Inawezekana ndio, utasikia mwingine
nakupendea macho yako, jiulize kwamba hivi niking’olewa macho itakuwaje? Yani
hutonipenda tena? Nakupendea miguu yako, hivi miguu ikikatika hutonipenda? Kuna
vitu tunatakiwa kujiuliza, mwenye mapenzi ya kweli huwa hana sababu ya kukupenda
yani yeye huwa anakupenda tu hata uweje” Kwa maneno haya ya dada yake
yalionyesha kuwa mwanaume pekee anayempenda yeye ni Bahati tu sababu ndio
anaonekana anampenda bila kujali sababu yoyote, akaongea ongea pale na dada yake
ila akapigiwa simu na Bahati akimuomba akamuonyeshe kitu nyumbani kwao. “Natumaini sio kwa Yule mmama
tena, sitaki kuonana na Yule bosi wako” “Usijali Erica, ni nyumbani
kwetu” Basi Erica akakubali na kumuaga pale dada yake na
kuondoka. Alifika hadi mitaa ya kwakina Bahati kisha Bahati
akaenda kumchukua na kwenda nae nyumbani kwao, akampeleka mahali ambapo kulikuwa
na mabwawa ya samaki, “Erica nimekuja kukuonyesha kuwa, ile milioni moja
uliyoniongezea nilikuja kutengeneza mabwawa ya samaki, na sasa samaki
wanaendelea vizuri. Mpenzi wangu Erica tutakuwa matajiri sana
sisi” Bahati akamkumbatia Erica, na ilionyesha alikuwa na furaha sana
kwani alikuwa akitabasamu tu, muda kidogo simu ya Bahati ikaita akaipokea na
kuongea nayo, alipomaliza alimuangalia Erica na kumwambia, “Kuna rafiki
yangu kaja, sasa yupo stendi na hapa nyumbani hapajui inabidi nikamfate stendi.
Sasa twende wote au utabaki unaangalia samaki!” “Mimi nitabaki
tu” “Sawa, ila sitakawia kurudi, jisikie upo nyumbani kabisa maana hapa
ni kwenu pia” “Sawa” Erica aliendelea kuangalia wale samaki
jinsi wanavyoogelea mule kwenye bwawa. Gafla alifika dada wa Bahati,
Yule ambaye alikutanaga na Erica na kumpiga kibao, alikuwa ameongozana na wadada
wengine wawili wa Bahati na mama yao. Yule dada alimsogelea Erica karibu
na kumwambia, “Yani msichana mpumbavu wewe, umeona mdogo wetu kaanza
kupata vipesa umeanza kujipendekeza tena” Kisha akamuangalia mama yao na
kumwambia, “Mama, ndio huyu msichana aliyesababisha mwanao alale jela
mwezi mzima tena hata hakujishughulisha kuja kumuona” “Khaaa kumbe ndio
huyu firauni” Yule mama alimsogelea Erica na kumnasa kibao, wakati Erica
akijishika shavu Yule mama akamsukuma Erica kwenye bwawa la
samaki. Kisha akamuangalia mama yao na
kumwambia, “Mama, ndio huyu msichana aliyesababisha mwanao alale jela
mwezi mzima tena hata hakujishughulisha kuja kumuona” “Khaaa kumbe ndio
huyu firauni” Yule mama alimsogelea Erica na kumnasa kibao, wakati Erica
akijishika shavu Yule mama akamsukuma Erica kwenye bwawa la
samaki. Halafu wakawa wanacheka pale juu, Erica akajitahidi kwa
kuhangaika sana na kutoka kwenye lile bwawa la samaki kwa upande mwingine, ila
wakamfata na kumvutia pembeni kisha kila mmoja alianza kumshambulia kwa makofi
yake, mmoja kati ya wale dada wa Bahati akashauri kwamba aachiwe
ameshakoma, “Akome wapi? Malaya anakomaga? Huyu msichana ni malaya,
kasababisha mdogo wetu kaka ndani mwezi mzima, halafu kwa umalaya wake nikamkuta
na malaya mwingine wanakumbatiana kumbatiana njiani. Huyu msichana hafai ni
kichefuchefu” Mama Bahati, akamsimamisha Erica pale chini kisha
akamuangalia na kumwambia, “Yani wewe binti naomba uelewe swala moja,
kama ulifikiri ya kwamba kuna siku utakuja kuolewa na mwanangu yani isahau
kabisa hiyo siku labda niwe nimekufa” Dada yake akadakia, “Sio
wewe tu mama, labda ukoo mzima wa Bahati tuwe tumekufa. Yani huyu mwanamke
hajielewi hata robo, umemuona Bahati kaanza kushika hela vizuri, kaanza kuwa
tajiri ukaona hapa ndio umalizie shida zako na familia yako. Umenoa
kwakweli” Erica alikuwa kimya kabisa, kajikunyata kama kikuku
kilichonyeshewa na mvua, nguo zote zimelowa, na makofi ya kutosha hadi amebaki
na alama usoni, hakujua hata afanye nini kwa muda huo. Yule mama Bahati
akamwambia, “Sasa muda huu fanya upesi uondoke hapa kwangu, sitaki
kukuona maana tutakufanya mboga bure. Ondoka” Erica alianza kukimbia tu
na alipotoka nje ya uwanja wa nyumba ile aliiona bodaboda ikipita akaisimamisha
na kupanda huku akimuomba ampeleke hadi kwao na hela atampa akifika kwao maana
hata mkoba wake ulikuwa chapachapa. Yule wa bodaboda alimuhurumia na
aliona kuwa baridi lingempiga sana ikabidi ampe koti lake avae kisha wakaanza
kuondoka. Njiani akapishana na Bahati anarudi kwao, ila Bahati pia
alimshangaa Erica akiwa kwenye bodaboda na kujaribu kuisimamisha ile bodaboda
lakini Erica alimwambia Yule wa bodaboda asisimame kwahiyo Yule dereva
aliendeleza mwendo tu. Bahati hakuelewa, akarudi kwao na kumkuta dadake
nje akamuuliza kuwa imekuwaje hadi Erica kaondoka, “Kwani wewe umemuona
wapi?” “Nimemuona kwenye bodaboda halafu kama amevaa koti la Yule
mwendesha bodaboda!” Dadake akacheka na kumwambia, “Ila wewe
sijui una akili gani? Sijui unataka tukwambie kwa lugha gani, Yule msichana ni
malaya, tena ni malaya koko. Nadhani anajuana na huyo mwendesha bodaboda maana
mi nilikuwa hapa nikashangaa anaongea na simu gafla namuona katoka mara kapewa
koti na Yule dereva kavaa na kupanda bodaboda akaondoka. Kwanza msichana hana
adabu Yule loh! Hata kunisalimia kaona shida” “Mmmh dada jamani, Erica
anaweza kufanya hivyo kweli?” “Hebu na wewe kuwaga na akili, unamuona
kabisa mwanamke anaondoka na mwanaume mwenzio halafu unabaki kutetea ujinga hapa
eti hawezi kufanya hivyo, hebu kuwa na akili basi” Bahati hakuridhika
kabisa na majibu ya dada yake, akasogea pale kwenye bwawa lake la samaki,
akashangaa kuona maji kwa pembeni, alijiuliza kuwa imekuwaje lakini alikosa
jibu, na akapata wazo kuwa mgtu pekee atakayekuwa na jibu ni Erica
tu. Erica alifika kwao na kumuuliza Yule bodaboda ni shilingi
ngapi, “Hapana dada, mimi nimekusaidia tu” “Hii ni biashara kaka
yangu sio swala la kunisaidia. Naomba nisubiri hapo mara moja, ikuletee hili
koti lako” Erica aliingia ndani kwao, na kwa bahati hakumkuta mama yake
kwahiyo alienda kubadilisha nguo kisha akatoka na hela na kumkabidhi Yule
bodaboda pamoja na lile koti, “Kheee zote hizi, hapana” “Aaah
usijali, umenisaidia sana. Nenda nazo tu, maana hata hili koti lako ingebidi
nilifue, ila nakuomba utapitisha kwa wale wafua nguo, nakuomba” Yule
bodaboda akawa anakataa ila Erica alimuomba achukue kisha akachukua na kuondoka
zake, halafu Erica alirudi ndani kwao amabapo cha kwanza alienda kuoga maana
alihisi mwili wake wote unanuka samaki. Alimaliza na kukaa chumbani
kwake akitafakari, “Hivi kosa langu haswaa ni nini jamani? Mbona kila
ninachoshika hakishikiki? Sina raha ya mapenzi kabisa mimi, hakuna ninachofanya
kikafanyika, kila kitu kwangu ni majanga.” Aliwaza sana kuwa yeye ndiye
aliyempa pesa Bahati ila leo hii anaonekana yeye ndio anafuata pesa kwa Bahati,
roho ilimuuma sana na kujiona kwa hakika hana bahati na mapenzi
kabisa. Akachukua simu zake kwenye mkoba, na kwa bahati hazikuingia maji
ila zilikuwa zimezimika, akaziwasha na alikuwa na mawazo sana huku akijisemea
kuwa ni vyema angerudi kwao tu kuliko kupitia alikoitwa na Bahati. Alipokaa
kidogo simu yake ikaanza kuita, mpigaji alikuwa ni Bahati kwakweli hakupokea
kabisa kwani hakujisikia hata kuongea nae kila akifikiria maneno ya ndugu wa
Bahati na vile walivyomfanyia hakuwa na hamu kabisa. Mama yake hata aliporudi
alimkuta amelala, ila hakulala kwa raha kwani kiukweli alikuwa na mawazo
sana. Kulipokucha alihisi viungo vyote mwilini vinauma, akagundua ni
sababu ya ile misukosuko aliyoipata jana yake, basi akampigia simu shemeji yake
na kumtaarifu kuwa anajisikia vibaya na hatoweza kufika ofisini, shemeji yake
alimkubalia ukizingatia huwa anampenda kwahiyo hawezi kukataa kuwa asipumzike
kwenda ofisini halafu yupo mafunzoni tu sio kazi kamili. Kwenye
mida ya saa nne asubuhi alikuwa akikereka sana na zile simu za Bahati ambazo
alikuwa akipiga kila baada ya dakika chache, akajiandaa kisha akaenda mjini, kwa
mara ya kwanza alienda kwenye ofisi za laini na kurudisha ile laini yake ya
zamani kabisa, alipokuta hakuna mtu mpya anayeitumia alifurahi sana, akairudisha
ile laini na kurudi nyumbani kwao kisha kuiweka kwenye simu. Halafu ile laini
yake ya siku zote aliikata kata huku akijisemea kuwa atakuwa Erica mpya, hataki
tena ujinga wala masikhara, kwani alihisi kuwa hii laini aliyotafutiwa na George
ndio iliongeza mkosi kabisa katika maisha yake. “Ngoja nikumbuke kwanza,
laini hii nilitafutiwa na George halafu alinifanyia vituko sana kiasi kwamba
nilijiona sina thamani, kwa mawazo nilikutana na mama yake Rahim na kwa mawazo
nilikutana na Bahati halafu watu hawa wote wamekuwa ni changamoto kubwa sana
katika maisha yangu, ngoja niangalie ukurasa mpya wa maisha yangu
kwasasa” Ile laini ambayo aliwekewa na Rahim, hakuitumia kupiga zaidi ya
kwenye mtandao tu, kwahiyo alikuwa akitumia bando tu la ile simu
basi. Baada ya kubadilisha hii laini aliamua kumpigia simu shemeji yake
maana akaona ni vyema kumtaarifu sababu anaweza akamtafuta, “Kumbe
Erica, mbona umebadilisha namba?” “Ndio nilikuwa nakutaarifu tu kuwa
nimebadilisha namba” “Sawa, ila nikitoka ofisini nakuja
kukuona” “Hapana usijali shemeji, naendelea vizuri” “Lazima nije
nikuone Erica, usinikatalie” Erica hakuwa na jinsi ila alitaka tu muda
atakaokuja shemeji yake basi na mama yake awepo ndani. Kiukweli mwili
wake ulikuwa umechoka choka sana, aliamua kwenda kupumzika, wakati amelala na
kujisahau kumbe giza lilishaanza kuingia, akasikia tu mtu akigonga mlango wa
ndani kwao kwa nguvu, Erica aliinuka na kwenda kumfungulia, akamkuta ni shemeji
yake akiwa anathema halafu alionyesha kuwa na hasira sana, “Vipi
shemeji, kuna nini?” “Naomba maji kwanza” Erica akaenda kuchukua
maji na kumpa, akayanywa kwa haraka sana kwani ilionyesha alikuwa na hasira
vilivyo, kisha akamuangalia Erica na kumuuliza, “Erica, Yule mbwa umempa
nini wewe mpaka anakung’ang’ania hivyo?” “Mbwa gani
shemeji?” “Si kile kibwana chako, aaargh nitakimaliza
mimi” “Sikuelewi shemeji, imekuwaje?” “Kwanza mama yuko
wapi?” “Mama, katoka kidogo ila sasa hivi anarudi” “Nimemkuta
nje kwenu hapo Yule bwanako muuza samaki, ndio nimetoka kugombana
nae” “Kwanini umegombana nae sasa shemeji?” “Sitaki
akufatilie” Erica alimuangalia shemeji yake na kushindwa hata
kumtafakari maana anamuonea wivu wa nini sasa, muda kidogo mama yao alirudi na
kumkuta James pale na kumkaribisha, wakasalimiana kisha James akasema dhamira
yake ya kuja kumuona Erica, “Endelea na moyo huo huo baba angu, ni
wachache sana wanaojali ndugu wa upande wa pili. Kwakweli mwanangu kapata
mume” James mwenyewe alishangaa ambavyo mama huyu hakumkumbusha kabisa
kuhusu makosa aliyoyafanya ya kumpa mimba msichana wa kazi, baada ya muda kidogo
akaaga maana asingeweza kuendelea na zile mada zake zisizoelewekaga mbele ya
mama mkwe wake. Kisha akamuuliza Erica kama ataweza kwenda ofisini kesho yake
naye alisema kuwa ataenda. Kisha akaaga tena na kuondoka
zake. Muda huu Erica alikaa na mama yake na kujaribu kuongea
nae vitu vichache vichache kama kumdadisi, “Hivi mama, mfano mwanamke
kaolewa ila familia ya mume hawampendi huyo mwanamke inakuwaje
hapo?” “Mmmh mwanangu huo ni mtihani mkubwa sana, japo wengi wanasema
akikupenda mume inatosha ila kiukweli usopopendwa na familia kuna karaha yake,
raha ya ndoa upendwe na mume na ndugu nao wakupende hapo utajiona kama upo pepo
dogo, ila mume anakupenda halafu ukizunguka huku masimango, ukienda huku
masimango yani utaiona ndoa chungu kwakweli. Utasema mume akikupenda inatosha je
hutashirikiana na wale ndugu zake kwenye jambo lolote? Yani kiukweli ili furaha
itimie basin a wao wakupende hata kama sio wote ila wawepo ambao
watakupenda” “Sasa mtu huwa anafanya nini kupendwa na ndugu wa
mume?” “Hiyo huwa inatokea tu, mwingine ana damu ya kupendwa basi
wanajikuta wanampenda ila mwingine ni mume ndio anatakiwa afanye ndugu zake
wakupende. Kwani mume ana nafasi kubwa ya kufanya ndugu zake wakupende au
wakuchukie, yani hatakiwi kusema mabaya yako kwa ndugu zake, yani hata kama una
mabaya basi atafute hata mazuri ya kujitungia ili ndugu zake
wakupende” “Mmmmh mama, ila ndoa ni ngumu sana?” “Vipi mwanangu
unataka kuolewa nini? Ndoa si ngumu ila kabla hujaolewa mchunguze huyo muowaji,
maana unaweza kuangukia pua uione dunia chungu.” “Hapana sio nataka
kuolewa ila nauliza tu nijue, hivi ndugu wa mume wakikuchukia kuna namna unaweza
fanya wakupende kweli?” “Mwanangu umechukiwa na ndugu wa mume au?
Sikuelewi, na kwanini uchukiwe?” “Nimeuliza tu mama” “Basi
nitakujibu siku nyingine” Erica alienda chumbani kwake akawa
anajiongelesha mwenyewe, “Erick, dada yake hataki hata kunitazama mara
mbili yani hanipendi kabisa. Kuolewa na huyu ni mtihani maana yeye na dada yake
ni wanapatana balaa halafu dada yake hanipendi. Rahim nae mama yake nahisi
hataki ukaribu wangu na mwanae maana anafatilia kila njia yangu, na siku
akisikia nina mahusiano na mwanae atakuwa mbogo kwakweli. Bahati sasa, mwanaume
niliyemuamini kuwa hateteleshwi na chochote, nikaanza kumkabidhi moyo wangu
maana na yeye ananipenda sana, ila ndugu zake wote hawataki hata kunisikia,
mbona sina bahati na mapenzi jamani! Nina mkosi gani mimi
Erica?” Hakujielewa, akafungua simu yake ile nyingine na kuingia kwenye
mtandao, akakutana na jumbe toka kwa Rahim, “Mbona namba yako nimeipiga
haipatikani?” “Nimebadilisha laini” “Kwanini?” Erica
alifikiria cha kumwambia Rahim, badae akapata wazo, “Sitaki tena
kuwasiliana na watu wa ajabu ajabu ndiomana nimebadilisha laini” “Kweli
Erica? Kwahiyo Yule Bahati hutowasiliana nae tena?” “Ndio, siwasiliani
nae, nimeanza maisha mapya” “Kama umeamua hivyo Erica nimefurahi sana
ten asana” “Ndio nimeamua hivyo” “Niambie zawadi gani
unataka?” Erica akatabasamu kwa kuweza kurudisha moyo wa Rahim tena
kwake, yani kwa siku hiyo akawasiliana nae vitu vingi sana kwani ilikuwa ni
furaha mno sana kurudisha moyo wa Rahim, hadi anamuaga kulala amejawa na furaha
kwenye uso wake, yani kwa muda huo hakujali swala la kusema kuwa mama yake Rahim
hampendi wala nini. Kulipokucha alienda ofisini kama kawaida
ila alikuwa akijitahidi kutoka kwa muda ambao Bahati hamkuti nje, yani alikuwa
anajitahidi kumkwepa Bahati kwa vyovyote vile kwani aliona kuwa Bahati si
mwanaume wake maana hata tena namna ya kufanya ndugu wa Bahati
wasimchukie. Siku hiyo wakati anatoka ofisini na anakaribia na kwao,
simu yake ikaita kwa namba ngeni kabisa, akajiuliza kuwa ni nani ila
akapokea, “Erica” “Ndio, mimi ni Erica” “Siamini masikio
yangu, naongea na Erica kweli?” “Ndio, kwani wewe nani?” “Mimi
ni Babuu” “Babuu? Kumbe upo?” “Nipo ndio Erica, siamini kama leo
nimekupata hewani. Uko wapi saizi?” “Naelekea nyumbani” “Naomba
nipajue nyumbani kwenu, walau nije nikusalimie” Basi Erica akamuelekeza
Babuu nyumbani kwao, na muda mchache tu baada ya Erica kufika kwao Babuu nae
alikuwa amefika, na Babuu alipomuona Erica alimkumbatia kwa furaha
sana, “Siamini kama nimekuona Erica, nimekusaka wewe mwanamke dah!
Umejua kuutesa moyo wangu Erica” “Ila mimi nina mwanaume
mwingine” “Shiiiii sijakuuliza habari za kuwa na mwanaume Erica, ila
nimefurahi kukuona naomba uwe unaniruhusu kuja kukuona maana moyo wangu utakuwa
na amani. Erica, wewe ni msichana wangu wa kwanza, na mimi ni mvulana wako wa
kwanza. Siwezi kukutoa kwenye akili yangu Erica, yani kwenye mawazo yangu
unatembea wewe tu” “Ni kweli usemayo Babuu ila mimi sio kama Erica Yule
wa mwanzo, nimebadilika sana siku hizi” “Haijalishi Erica, kubadilika
kwako hakuwezi kufuta kumbukumbu zako kwangu. Erica haijalishi ni kitu gani
kilitokea kati yetu ila bado upo moyoni mwanagu, haijalishi upo kwenye mahusiano
na nani ila moyoni mwangu bado unaishi” Erica alimuangalia Babuu ambaye
alionekana kuwa na maneno matamu kama aliyokuwa nayo mwanzo, kisha Babuu
alimuuliza Erica kuwa anafanya nini kwa kipindi hiko. “Niko field, na
kesho ndio siku ya mwisho maana karibia tutafungua chuo na ndio utakuwa mwaka
wangu wa mwisho” “Field upo sehemu gani?” Erica akamuelekeza,
Babuu akamuomba kuwa kesho akitoka waonane ili angalau amsindikize hadi hapo
kwao, Erica alimuitikia kisha akamuaga na kuingia ndani kwao. Alipokuwa
ndani alimuwaza sana Babuu, akakumbuka siku ya kwanza kuonana na Babuu jinsi
akili yake ilivyoruka, alikuwa binti mbichi kipindi hiko hata nyumbani kwao
haruhusiwi kutoka ila kwasasa kawa gumegume, kashatoa mimba mbili yani thamani
yake imebaki machoni pa watu tu ila kiukweli imepungua, hata akashangaa kwa
Babuu kuendelea kumwambia maneno ya upendo kuwa bado anampenda sana. Kiukweli
siku hiyo, hadi alilala alikuwa bado akimuwaza Babuu ingawa hakujua kama
angeweza kumfikiria namna hiyo. Siku iliyofuata alijiandaa na
kwenda ofisini ila ilikuwa ndio siku yake ya mwisho kwa mafunzo, alikuwa
akifurahia mwenyewe kwani tangu amekuwa pale kazini hajawahi kukorofishana na
mtu yeyote. Alipofika ofisini, shemeji yake alimuita kwa furaha
sana, “Leo ni siku ya mwisho kuwa hapa ofisini Erica, ila ningependa
tule chakula cha jioni pamoja” “Hakuna tatizo shemeji, wapi
hapo?” “Kuna hoteli Fulani hivi, wanapika chakula kizuri
sana” “Nitajie shemeji” James akamtajia na kumwambia kuwa
akitoka ofisini ajiandae, basi Erica akakaa kwenye meza yake na kukumbuka kuwa
Babuu alimuomba aende ampitie ofisini siku hiyo, ikabidid amtumie ujumbe kuwa
ataenda kwenye chakula cha jioni na shemeji yake kisha akamtajia hoteli
watakayokuwepo, Babuu alipiga simu ya Erica na kuanza kuongea nae huku
akimuuliza vizuri kuhusu hapo mahali atakapokuwepo, “Erica, mimi
nitakuja hata hapo hotelini hata nikikaa mbali tu nikakuona
nitaridhika” “Ila usijali, huyu ni shemeji yangu atanirudisha mwenyewe
nyumbani” “Ndio Erica ila nitakuja tu” “Khaa wewe nae mbishi,
kwaheri” Erica akakata simu na kuendelea kuweka mambo yake
sawa. Jioni ilipofika shemeji yake alimshtua mpaka kwenye hiyo hotel,
walishuka kwenye gari na kuingia hotelini kisha wakakaa bustanini, huku kwa
mbali ukisikika mziki laini na kisha kuletewa vinywaji na chakula ila kile
kinywaji Erica alipokunywa tu alianza kujihisi kizunguzungu hatari kama mtu
aliyekunywa pombe balaa, James akainuka na kwenda kuongea na
muhudumu, “Naomba kile chakula utubebee utupelekee chumbani kule
nilipokodi maana mpenzi wangu hawezi kula hapo amelewa” Wakati James
anarudi ili amchukue Erica, alishangaa kuona Erica akikokotwa na kijana mwingine
wakitoka nje ya ile hoteli. Jioni ilipofika shemeji
yake alimshtua mpaka kwenye hiyo hotel, walishuka kwenye gari na kuingia
hotelini kisha wakakaa bustanini, huku kwa mbali ukisikika mziki laini na kisha
kuletewa vinywaji na chakula ila kile kinywaji Erica alipokunywa tu alianza
kujihisi kizunguzungu hatari kama mtu aliyekunywa pombe balaa, James akainuka na
kwenda kuongea na muhudumu, “Naomba kile chakula utubebee utupelekee
chumbani kule nilipokodi maana mpenzi wangu hawezi kula hapo
amelewa” Wakati James anarudi ili amchukue Erica, alishangaa kuona Erica
akikokotwa na kijana mwingine wakitoka nje ya ile hoteli. James alipigwa
na bumbuwazi kuwa Yule kijana ni nani na kwanini kamchukua Erica, akaanza
kumfata kwa nyuma ila alipofika nje alimuona Yule kijana akimpakiza Erica kwenye
bajaji kisha kuondoka na ile bajaji, bado James alikuwa na bumbuwazi, akaenda
akapanda gari yake ili kufata ile bajaji, ila alipofika barabara kuu tu ile
bajaji ilimpoteza kabisa yani hakuelewa ilipoenda, kile kitendo kilimfanya
ajilaumu kwanza, muda wake, pesa yake kila kitu chake alichofanya kwa siku hiyo
ilikuwa ni bure kabisa. Kuna muhudumu wa ile hoteli alipewa madawa ya
kulevya na James ili aweke kwenye kinywaji cha Erica, naye alitimiza wajibu
wake, James alijilaumu sana kuwa ni bora angemkokota na kwenda nae chumbani
kuliko kubembwa na mtu asiyejulikana. Kwa muda huo hata hakuelewa kuwa aende
wapi kumtafuta Erica, akajaribu kupiga simu ya Erica ila iliita sana bila ya
kupokelewa hadi kukatika, alipiga tena na tena ila simu yake haikupokelewa na
mara ya mwisho wakati anajaribu namba ya Erica haikupatikana na kuhisi kuwa simu
ya Erica imezima, yani hapo ndio akili yake ilichanganyikiwa kabisa. Akapata
wazo kuwa aende nyumbani kwao akamuulizie kwanza kwani hata kurudi pale hotelini
hakutamani ukizingatia mambo yake hayajawa alivyotaka, halafu akawaza kuwa kama
Erica akiwahi nyumbani basi atamsemea sifa mbaya yeye, kwahiyo akaona bora yeye
awahi nyumbani kwakina Erica. James alifika nyumbani kwakina
Erica na kugonga, kisha mama mkwe wake akamfungulia mlango na kumkaribisha,
James akamsalimia na kumuuliza, “Erica kashafika
nyumbani?” “Bado hajafika, hata namshangaa leo kachelewa chelewa halafu
hajaniambia kama atachelewa” “Samahani mama ila utaona kama namfatilia
binti yako, ila Yule ni kama mdogo wangu ndiomana namfatilia kwa lengo zuri
tu” “Hakuna tatizo mwanangu, tena unavyomfatilia ndio vizuri, sasa
atakuwa wapi?” “Unajua leo ni siku yake ya mwisho kufanya mafunzo pale
ofisini, sasa nikaongea nae vizuri kuwa anisubiri nimalize kazi zangu nimrudishe
nyumbani. Nikiwa sina habari najua ananisubiri, nikashangaa tu kuna mtu kaja
kunitonya kuwa njoo umuone shemeji yako, nikatoka nikamuona Erica kashikiliwa na
mwanaume halafu akionekana kuwa amelewa kisha akapanda bajaji na Yule mwanaume
na kuondoka. Yani….” “Subiri, subiri kwanza. Erica anakunywa pombe?
Jamani Mungu wangu, yani binti yangu mimi anakunywa pombe? Eeeh Mungu,
nimekukosea wapi mimi? Binti yangu kawa mlevi?” Mama Erica machozi
yalikuwa yakimlenga lenga kwani kwa binti zake wote hakuna hata mmoja aliyepata
sifa ya kunywa pombe, kwahiyo kuambiwa swala la Erica alilewa lilimshtua sana,
akamuuliza tena, “Kwahiyo akaenda wapi na huyo mwanaume?” “Sijui
mama, nimejaribu kuwafatilia lakini wamenipotea, nikampigia simu Erica kwakweli
kaniambia vitu vya kunitia simanzi sana” “Vitu gani
baba?” “Erica kaniambia, acahana na mimi, usinifatilie huna undugu na
mimi. Nikamwambia naenda kuwaambia ndugu zako mambo haya, akasema tena
usithubutu kusema maana ukisema nitakusingizia kuwa ulitaka kunibaka. Kwakweli
mama hiyo kauli imeniuma sana” “Jamani huyu Erica kapatwa na shetani
gani mwanangu jamani? Yani akusingizie wewe kubaka? Erica jamani, mbona hana
fadhila mwanangu! Yani kumsaidia kote huko aseme maneno ya ujinga kama hayo?
Ngoja aje hapa nyumbani, nashukuru kwa taarifa mwanangu ingawa zimenichanganya
haswaa” “Pole mama, ila Erica nampenda kama mdogo wangu. Sikutaka
aharibikiwe maana yupo kwenye ofisi yangu na ni mimi mtasema sikumuangalia
vizuri, ila Erica alinishushua mbele ya dada yake kuwa nisimfatilie maisha yake,
mwanaume yoyote anayetaka kuwa nae ni yeye. Maana mwanzoni kulikuwa na
kimwanaume kimoja kinakuja kumchukua akitoka kazini, namuhurumia Erica
mama!” “Na wewe kwanini hukuja kuniambia siku zote hizo mpaka maji
yamemwagika?” “Mama, siku zote Erica ananiambia nisiseme chochote, yani
siamini kuwa ndio mtoto Yule mdogo wa kipindi kile ndio kawa hivi” “Hizi
habari zimenichanganya kabisa yani sielewi, narudia maneno kama kichaaa,
sielewi” James akaaga na kuondoka, mamake Erica alikuwa na mawazo sana
huku machozi ya hasira yakimjaa kuwa binti yake kaanza lini ulevi na zaidi ya
yote tabia ya kuanza kuzunguka na wanaume, “Erica leo utanieleza
kwakweli, sijalea mtoto mlevi mimi, sijalea mtoto malaya mimi, sijalea mtoto
muongo mimi. Hiyo tabia umeitoa wapi Erica, yani mtu anayekusaidia eti unataka
umtungie stori kuwa alitaka kukubaka! Erica huna hata uso wa
aibu!” Alikuwa na huzuni sana na hasira kwani katika mabinti zake wote
hakuwahi kumtegemea Erica kuwa binti wa tabia zisizofaa. Mama Erica
alikaa macho hadi usiku sana ila bado Erica hakurudi hadi aliamua kwenda kulala
kuwa akirudi atagonga mlango kwani mpaka usiku sana Erica
hakurudi. Kulipokucha huyu mama alizidi kupatwa na hasira kwani
bado Erica hakurudi nyumbani, akili yake ikakosa uelekeo kabisa maana kila
alipopiga simu ya Erica haikupatikana, akaamua kwenda kwa mwanae Bite maana
alishachanganyikiwa. “Mumeo hajakueleza kuhusu mambo ya
Erica?” “Kaniambia juu juu na nimeshangaa kwakweli, vipi
karudi?” “Bado hajarudi nyumbani jamani mtoto huyu ananitaka nini
mimi?” Ikabidi Bite amueleze mama yake kuhusu kijana anayekuwaga na
erica na jinsi hata walivyomkataza na mumewe alivyowajibu, “Alisema yeye
ni msichana mkubwa na tumuache na maisha yake, kwakweli mama niliumia sana maana
Erica ni mdogo wangu natakiwa kuwa nae makini ila akasema tuachane nae
kabisa” “Hapa nimechanganyikiwa, huyu mtoto sijui atakuwa
wapi” Mama akaamua kupiga simu kwa Mage ambaye alipopata ile taarifa
ilibidi aende kwa Bite pia ili wajadiliane, walijaribu kupiga simu ya Erica
haikupatikana na hapo ikawa ni hofu kubwa sana kwao kuwa ni kitu gani
kilichompata ndugu yao. “Sasa huyo mwanaume hamjui anapoishi
jamani?” “Hatujui mama, ila Yule kijana ndio anatokaga sana na Erica
yani tumefanya mambo ambayo hata haiwezekani kukwambia mama, huyu Erica huyu
loh!” Mage akaamua kumpigia simu Derick ili kujaribu kumuuliza alipo
Erica labda alijua ila Derick alijibu kuwa hajui popote alipo
Erica, “Kwani imekuwaje hadi Erica apotee?” “Inavyosemekana
alikuwa amelewa sana na akaondoka na huyo mwanaume hadi muda huu hakuna anayejua
Erica yuko wapi jamani, na ubaya zaidi hata simu zake hapokei” “Ila dada
mngepunguza presha tu, Erica ni binti mkubwa na hawezi kupotea kirahisi hivyo,
atapatikana tu hata msiwe na mashaka” “Derick tumechanganyikiwa, Erica
ni mtu mzima kweli ila yupo chini ya wazazi angetakiwa kusema sehemu alipo, au
hata angeongea kwenye simu ingekuwa afadhali kidogo kuliko hivi, hewani
hatumpati na hatujui alipo” “Ila cha kuwashauri tu ni kuwa muwe wapole
jamani, nina uhakika Erica atarudi akiwa salama salimini” Ila Derick nae
alishangazwa nah ii taarifa kuwa Erica alikuwa amelewa maana kwa ajuavyo Erica
hanywi pombe, akawaza kuwa labda amenza kunywa pombe. Ila kitendo cha familia ya
Erica kumuulizia Erica kwa Derick hawakujua tu kuwa ni swala ambalo lingezua
utata mkubwa sana pindi Erica atakaporudi maana Derick sio mtu wa
kunyamaza. Walikaa pale na kujadiliana ila hawakupata shuluhisho, James
nae alirudi mapema kujifanya anasaidia swala la kupotea kwa Erica, ila akashauri
warudi nyumbani tu ili kuangalia kama Erica amerudi, basi waliondoka James, Mage
na mama yao. James alifanya vile ili kuwaondoa tu pale nyumbani
kwake. Kufika nyumbani wakamkuta Bahati getini kumbe nae
alikuwa akimsubiria Erica baada ya kumkosa hewani kabisa kwa siku kadhaa
mfululizo maana Erica alibadilisha laini ya simu, kwahiyo alihisi akifika
nyumbani kwao itakuwa rahisi kumuona. James alipomuona Bahati akamwambia mama
mkwe wake, “Eeeh mama, kijana mwenyewe ndio Yule pale anayesumbua akili
ya Erica” “Khaaa si muuza samaki huyu!” Mama Erica alimfata
Bahati kwa hasira sana, na kumkunja kisha James akasogea na kumpiga vibao kadhaa
kisha akasema kuwa wasimsikilize chochote kwani huyo ndio mtuhumiwa namba moja,
walimpandisha kwenye gari ya James na kwenda nae kituo cha polisi. Kwakweli
Bahati alikuwa akishangaa tu, maana hata hakuelewa kuwa imekuwaje kuwaje yeye
kushikwa kama mwizi kiasi kile maana hata hakujua kama Erica
alipotea. Walivyofika kituoni, James alishuka na Bahati na kuwaambia
wale wamsubirie kwenye gari, James alienda na Bahati kwa mapolisi, na aliimuita
polisi mmoja pembeni na kumpa kitu kidogo ili amshikishe adabu Bahati, na Yule
polisi pale pale alianza kumshurutisha Bahati. Kisha James akarudi
kwenye gari na kuwaambia wale kuwa Erica atapatikana tu, akaenda kuwarudisha
nyumbani, kisha akaondoka. Mage nae alikaa kidogo tu na kumuaga mama
yao, kwani kuna mahali alitakiwa aende, “Mama naomba uniruhusu
tu” “Sawa, ila hapa sina hata hamu ya kula” “Ila mama jaribu
hata kunywa juisi tu, twende ninavyoondoka uchukue juisi dukani. Badae
nitarudi” Mama Erica alikubali na kwenda na Mage dukani ila kiukweli
alikuwa na mawazo sana. Erica alishtuka kichwa chake kikiwa
kizito sana kiasi kwamba hakuna alichoelewa kimetendeka juu yake, akaangaza
macho huku na huku akagundua yupo kwenye chumba asichokijua kwani hayakuwa
mazingira ya nyumbani kwao, akiwa anashangaa shangaa akamuona Babuu akiingia
kwenye kile chumba, “Ooooh Erica, umezinduka asante Mungu” Erica
alikuwa akishangaa tu na kumuuliza Babuu, “Kwani imekuwaje? Hapa wapi?
Nafanya nini hapa?” “Erica, hapa ni nyumbani kwangu” “Nyumbani
kwako! Nimekuja kufanya nini hapa?” “Usiwe na jazba erica, nisikilize
kwanza nikwambie” “Haya niambie” Aliongea huku akionekana
kuchukizwa sana kupelekwa pale, “Erica, jana nilifika kwenye ile hoteli
mliyopanga kwenda na shemeji yako kabla hata ya muda wenu na hadi mnaingia pale
nawaona. Sasa shemeji yako alienda kuagiza vinywaji sijui na chakula, nilimuona
akiongea na kijana mmoja na kumpa pesa, ilibidi nifatilie ili nijue ni kutu
gani. Yule kijana nilimuona akibeba vinywaji ambapo kimoja wapo ilikuwa ni juisi
kwenye glasi ila nilimuona akitia kitu kwenye ile juisi, nikafatilia kuona ni
nini kinaendelea. Pale mlipokaa vikaletwa vinywaji na chakula, ukaanza kunywa
ile juisi ila taratibu ulionekana kuregea hadi kulaza kichwa chako kwenye meza,
nikamuona Yule shemeji yako ameinuka. Sikutaka kujua ameenda kufanya nini ila
nilichohisi ni kuwa ana lengo baya na wewe, ikabidi nianze kukukokota pale ili
nikutoa eneo lile. Tulifika nje nikakodi bajaji tukaanza kuondoka ila shemeji
yako akawa anatufata nyuma ikabidi nimwambie Yule dereva bajaji atupitishe njia
za panya na tukampoteza mwelekeo Yule shemeji yako. Nilitaka nikupeleke kwenu
ila nikakumbuka kuwa mama yako ni mlokole na hatopendezewa kukuona kwenye hali
kama ya ulevi, yani Erica ulikuwa kama mtu aliyekuwa pombe saana, ikabidi
nikulete hata nyumbani kwangu. Erica hakuna chochote nilichofanya kwako, siwezi
kufanya jambo lolote bila ridhaa yako, furaha yangu mimi ni kuona ukizinduka
tu” Erica alijaribu kufikiria na kukumbuka vizuri, akakumbuka pale
alipokunywa kinywaji na kuzidiwa na kizunguzungu basi ila mengine hakuyakumbuka
ila alitambua kwamba shemeji yake alikuwa na lengo baya kwake, “Yani
Yule shemeji yangu jamani, kweli alitaka kunibaka loh! Asante kwa kuniokoa
Babuu, nashukuru sana. Saa ngapi saa hizi?” “Ni saa sita mchana hii yani
hadi nilikuwa na mashaka nikasema usipozinduka nikupeleke hospitali ila nilikuwa
nahofia kuwa nitaenda kujielezea nini” “Mungu wangu, mama atakuwa na
wasiwasi balaa, naomba niende nyumbani” “Hakuna shida, nitakusindikiza
ila ngoja unywe kahawa kwanza” Babuu alimmiminia Erica kahawa na kumpa
anywe ili angalau aweke kichwa vizuri, “Na simu yako iliita sana jana
ila nilipoangalia jina niliona Shemeji james, na alikuwa akipiga sana kwahiyo
nikaamua kuizima. Samahani kwa hilo kama litakukwaza” “Hata usijali
Babuu, cha msingi umeniokoa toka kwenye mikono ya lile shetani. Yani mtu
anatembea na dada yangu, bado haridhiki anataka kunibaka na mimi loh! Sijui
wanaume mmeumbwaje!” “Sio wote bhana Erica, hiyo ni tabia ya mtu hata
kuna wanawake wengine wenye tabia hizo” “Hapana, wanaume nyie sio watu
kabisa mna tamaa sana” “Erica, kumbuka na mimi ni mwanaume pia ila
umelala hapa bila kujitambua na sijakufanya chochote. Tumetofautiana wanaume, na
hiyo ni tabia ya mtu tu. Huyo shemeji yake itakuwa ndio tabia yake
hiyo” “Sawa ila kwa muda huu nahitaji kumuona mama yangu tu maana najua
atakuwa na mawazo sana” Baada ya hapo Babuu alimsaidia kujiweka sawa
Erica kwani bado kichwa chake hakikuwa vizuri. Kisha wakatoka nje na kukodi
bajaji ya kuwapeleka nyumbani kwakina Erica. Walifika nyumbani
kwakina Erica, Babuu alitaka aingie nae ndani ila Erica
alimzuia, “Hapana Babuu, nenda tu. Sitapenda mama aone nimefika nikiwa
nimeongozana na mwanaume, nashukuru sana kwa msaada wako” “Haya Erica,
ila kumbuka upatapo jambo lolote juwa yupo Babuu bega kwa bega na wewe
kukusaidia. Siwezi kuacha kukupenda Erica” Babuu alisogea na kumkumbatia
Erica, kisha akambusu na kumuaga halafu Erica akaingia ndani kwao. Kumbe
mama Erica alikuwa ametoka dukani kwahiyo kile kitendo cha Babuu kumkumbatia
Erica na kumbusu alikishuhudia vilivyo, alipatwa na hasira sana yani alijikuta
hata alichonunua amekitupa, huku akijaribu kuwakimbilia ila Babuu nae
alishapanda kwenye ile bajaji na iliondoka. Mama Erica alifika na
kuingia ndani kwa gadhabu sana na kuita, “Erica, wewe Erica, hebu njoo
hapa” Erica alitoka chumbani na kwenda sebleni maana alitaka kujiandaa
akaoge, mamake alimshika na kuanza kumpiga, “Umefanya usiku wote
nishindwe kulala, kumbe umeenda kufanya umalaya wako” Huyo mama alimpiga
sana Erica bila hata kusikiliza kuwa Erica ana jambo gani la kueleza maana
hakumuuliza na wala hakumpa nafasi ajieleze ila yeye alimpiga tu, hadi Erica
alizimia. Baada ya kuzimia alihamaki, “Mungu wangu, mwanangu!
Erica mwanangu jamani, mwanangu Erica!” Erica alikuwa kimya kabisa na
kufanya mamake achanganyikiwe. Huyu mama alimpiga sana
Erica bila hata kusikiliza kuwa Erica ana jambo gani la kueleza maana
hakumuuliza na wala hakumpa nafasi ajieleze ila yeye alimpiga tu, hadi Erica
alizimia. Baada ya kuzimia alihamaki, “Mungu wangu, mwanangu!
Erica mwanangu jamani, mwanangu Erica!” Erica alikuwa kimya kabisa na
kufanya mamake achanganyikiwe. Alishindwa hata aanzie wapi na aishie
wapi, akachukua simu yake na kumpigia Mage kumpa taarifa kuwa Erica amerudi na
kuzimia kwahiyo awahi na usafiri wampeleke hospitali, kwa bahati Mage hakuwa
amefika mbali sana kwahiyo alirudi nyumbani akiwa kwenye bajaji, alishuka kisha
kusaidiana na mama yao kumbeba Erica na kumpakia kwenye bajaji kwaajili ya
kumpeleka hospitali. Wakiwa kwenye bajaji Mage alimuuliza mama
yake, “Kwani imekuwaje mama?” “Usiniulize habari hizo Mage,
ngoja kwanza tukamuhudumie hospitali” Walifika hospiatali na kupokelewa
ambapo moja kwa moja Erica alikimbizwa kwa daktari. Kwakweli mama yao alikuwa
amechanganyikiwa sana, hata hakujua ni nini afanye kwa wakati huo. Mage akapata
wazo la kumpigia simu shemeji yake kwani alijua hapo hospitali lazima kutakuwa
na maswala ya pesa, kwahiyo mtu wa kuwasaidia kwa haraka ni shemeji yake
James, “Shemeji tupo hapa hospitali tumemleta Erica amezidiwa yani hata
hatuelewi” “Imekuwaje kwani?” “Sijui shemeji” “Basi
nakuja” Mage alikata simu huku akiendelea kumpa moyo mama yake kuwa
Erica atakuwa sawa kabisa. Baada ya muda kidogo Erica alitolewa kwa
daktari na kupelekwa wodini, kisha wakataka kwenda kumuona ila daktari aliwazuia
kwa muda na kuwaita pembeni, “Msijali amezinduka na atakuwa sawa
kabisa” “Ooooh asante Mungu jamani mwanangu dah!” “Usijali mama,
ila tulia kuna mambo nataka nikuulize” “Niulize tu” “Kwani
mwanao mara ya mwisho alikuwa wapi? Ameangukia wapi?” “Ameangukia
nyumbani, ila mara ya mwisho sijui alikuwa wapi” “Inaonekana mwanao
alitumia madawa ya kulevya” Mage na mama yake walishtuka sana na
kumuuliza daktari kwa mshangao, “Madawa ya kulevya?” “Ndio, sasa
sielewi alitumia kwa ridhaa yake au imekuwaje ila inaonekana ametumia madawa ya
kulevya tena mengi, halafu alipigwa maana ana alama” Wakati akiendelea
kuwaelezea alifika James eneo lile na kuingilia kusikiliza yale mazungumzo,
kitendo kile cha kusikia kuwa Erica alitumia madawa ya kulevya kilifanya amvute
dokta pembeni ili aongee nae cha kuwaambia wale ndugu wa Erica na sio habari za
madawa tena. Kwenye mida ya saa mbili usiku, Erica aliruhusiwa
kurudi nyumbani kwahiyo walirudi nae, kwakweli Erica alikuwa kimya tu huku
akimuangalia shemeji yake akiwaendesha kuwarudisha nyumbani, alikuwa na chuki
nae kwakweli na laiti angejua shemeji yake alichosema kwao basi hasira
zingemzidi maradufu. Walifika nyumbani na kumuacha akapumzike, kwani
alionyesha kutokutaka kuongea jambo lolote ukizingatia mwili wake ulikuwa na
maumivu maumivu ya kupigwa na mama yake. Alienda kuoga na kukaa
kitandani huku akijiuliza sana, “Hivi kosa langu nini lakini? Kwanini
mimi? Sielewi, yani nataka kubakwa nafanyiwa kitu cha kikatili kama kuwekewa
madawa kwenye kinywaji change, ila narudi nyumbani mama anashindwa nata
kuniuliza anafikia tu kunipiga jamani hii ni haki kweli? Kwanini nafanyiwa hivi
lakini? Kichwa chote bado kinaniuma” Aliamua kujilaza tu kwani hata
akiendelea kujiuliza ni kuendelea kujiumiza kichwa tu. Kulipokucha mama
yake alienda kumuamsha na kumuomba akanywe chai, “Nakuomba uje kunywa
chai mwanangu” “Sawa mama” Erica aliinuka na kwenda kuoga kwanza
kisha akaenda kunywa chai, na alipomaliza sasa alienda kukaa na mama yake ili
ajue ni kwanini mama yake alichukua jukumu la kumpiga tu, “Mama, mbona
jana ulinipiga tu bila kuuliza ilikuwaje!” “Mwanangu, kwanza nisamehe
bure ila mimi ni mzazi na nina umia sana pindi nikisikia kuwa mwanangu kaanza
tabia mbaya. Ngoja nikuulize tu kidogo, umeanza lini kunywa pombe
mwanangu?” “Hapana mama, mimi sio mlevi” “Unajua mwanzoni
daktari alisema kuwa inaonyesha ulitumia madawa ya kulevya ila badae alikuja
kusema kumbe sio madawa ni pombe kali. Mwanangu umeanza lini kunywa pombe?
Kumbuka nimekulea katika maadili ya dini, na siku zote nakufundisha kuwa pombe
ni mbaya. Umeanza lini kunywa pombe? Niambie ukweli mimi ni mama
yako” “Hapana mama, situmii pombe mimi” “Niambie ukweli Erica,
mimi ni mama yako. Ukinificha mimi utamwambia nani tena? Halafu Yule mwanaume
muuza samaki uliniambia anakuleteaga samaki kumbe ni mwanaume
wako!” “Kheee mama, nani kakwambia kuwa ni mwanaume
wangu?” “Erica na hilo unanificha kweli?” “Sikufichi mama ila
nashangaa aliyekupa hizo taarifa” Ilibidi mama Erica, amuelezee Erica
jinsi walivyomkuta Bahati pale mlangoni na jinsi James alivyosema hadi kumpeleka
polisi, “Kheee mama, kwahiyo kijana wa watu mmempeleka
polisi!” “Ndio, kama mtu kaenda kunifichia binti yangu kwanini
nisimpeleke polisi!” “Jamani mama, hausiki na kupotea kwangu huyo. Ni
nani aliyetoa wazo hilo la kumpeleka Bahati polisi? Ni James
eeeh!” “Kheee wewe mtoto huna adabu yani James unamuita James badala,
umuite shemeji yako!” Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake, akachukua
simu yake ilikuwa bado imezimwa, akaiwasha na baada ya muda akampigia simu
shemeji yake, “Erica mrembo, unaendeleaje?” “Mbwa wewe,
usiniulize chochote. Kwanini umemuweka Bahati polisi? Eeh! Sasa naenda huko
polisi, halafu nasema ujangili uliotaka kunifanyia” “Sasa polisi unaenda
kufanya nini?” “Naenda ili wamuachie Bahati” “Acha kunichekesha
Erica, unafikiri huyo Bahati anaweza kuachiwa kwa njia ya jazba kama usemayo
wewe? Hiyo sio njia ya kuachiwa huyo Bahati, hivi unajuaga mimi ni mtoto eeeh!
Nina akili kukuzidi na huwa nafanya vitu kwa akili, unatakiwa kuwa mpole niombe
kwa adabu kuwa nimtoe Bahati na sio kwa kunikaripia” Erica alinyamaza
kwa muda na alikuwa na hasira sana na huyu shemeji yake, ila kwavile alitaka
Bahati atoke ikabidi awe mpole tu, kwani kiukweli nay eye ni muoga wa polisi
balaa, “Basi shemeji nakuomba umtoe Bahati” “Sawa, nitamtoa ila
kwa sharti moja yani ukilivunja namrudisha tena rumande” “Naomba lisiwe
sharti gumu” “Hata sio gumu, naomba usiseme chochote kuhusu
mimi” Erica alimuitikia shemeji yake kwa shingo upande na shemeji yake
aliahidi kumtoa Bahati, kiukweli roho ilimuuma sana Erica kwani shemeji yake
ndio muhusika halafu anawekwa ndani mtu hata asiyehusika. Alikata simu huku
akiwa na kinyongo sana kwenye moyo wake, alikaa kule kule chumbani akiwa na
mawazo ila mama yake akamuita tena na kumwambia, “Erica, hutakiwi kukaa
na mawazo kwakweli, ujue mamako nipi. Niambie nini kinakusibu?” “Hakuna
kitu mama” ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment