Search This Blog

Thursday, 24 November 2022

NGUVU YA MAPENZI - 2

 


    Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

    Sehemu Ya Pili (2)





    Usiku ulipofika, Erica alienda chumbani kwa Erick ili kumpa pia taarifa ambayo alikuwa akimpa baba yake, ila ile taarifa ilimchukiza sana Erick na kusema,

    “Yani simpendi Elly jamani simpendi kabisa, na mama yake simpendi”

    “Kwanini sasa? Kwnai Elly kosa lake nini?”

    “Elly ananikera, kwanini anakubali kutumwa ujinga na mama yake? Yani hapo ni mama Elly ndio kamtuma Elly kufanya hivyo, namuhurumia dada yangu jamani maana kuanza kupatwa na mawazo ya huyu mama kwasasa dah!”

    “Kwani mama yake Elly ana ubaya gani? Maana hata baba nimeona alivyochukia na kumsema mama yake Elly”

    “Huyo mama ni mtu mbaya sana, kumbuka vile visheti ambavyo baba alikula na kuanza kuumwa, je alikuwa na maana gani kufanya vile? Kwakweli yule mama hatufai kuanzia Elly na mama yake wote hawatufai katika familia yetu”

    “Ila kwanini?”

    “Erica na wewe kama huelewi basi endelea kutokuelewa hata hivyo ukielewa ni balaa maana sijui utayapeleka wapi”

    Halafu Erick aliinuka na kwenda chumbani kwake, na muda ule Erica pia aliamua kulala tu.

    Kulipokucha kama kawaida, Erica aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda shule.

    Leo, baba Angel nae alienda mapema kwenye ofisi yake kwani alipanga kuwa akitoka tu basi moja kwa moja aende kwa mama mkwe wake ili kuongea nae kidogo kuhusu Angel kwani alihitaji awe nae makini zaidi kwani hakuelewa kuwa Sia ana lengo gani kwa binti yao

    Ila wakati Erica anatoka kwenda shuleni alimuona mwanamke ambaye alitambulishwa na Elly kuwa ni mamake, kwahiyo alimuona mamake Elly, na alimuona kama anaelekea kwao, pale hakuelewa kuwa yule mama anaenda kufanya kitu gani pale kwao.



    Basi muda huu, mama Angel aliamua kurudi kulala tu kwani watu wote waliokuwa wanatoka walikuwa
    tayari wameshatoka ile asubuhi, basi wakati anajilaza tu akafuatwa na Vaileth na kugongewa mlango,“Ndio Vaileth kuna nini?”“Kuna mgeni wako sebleni mama”Kwakweli mama Angel alishangaa kidogo kuwa kwa muda huo ni nani yupo sebleni kumsubiri, basi alitoka ili kumuangalia akamkuta Sia ndio amekaa sebleni, ila kiukweli mama Angel aliona kuongea na Sia mahali hapo ni kujipa ugonjwa wa moyo tu basi moja kwa moja alienda kufungua mlango na kumwambia Sia,“Naomba uondoke”“Niondoke kitu gani? Siwezi kuondoka mimi kama hujanisikiliza”“Sihitaji kukusikiliza, kama unahitaji kuongea na Erick mfate ofisini kwake”“Hapana, sijaja kwaajili ya Erick hata mimi najua kama yupo ofisini muda huu ila nimekuja kuongea nawe mke mwenzangu”Mama Angel alipatwa na hasira muda huo ila akajituliza tu hakujibu kitu, sema muda huo huo akarudi ndani na kuchukua simu yake na kumpigia mumewe,“Yule shetani Sia kaja na leo, yani hapa tu kashaanza kunichefua”“Usijali mke wangu nakuja”Basi baada ya muda kidogo tu baba Angel alikuwa amewasili, na alivyoingia tu pale sebleni alionana na Sia, moja kwa moja baba Angel alimshika Sia mkono na kumtoa nje na alitoka nae hadi nje ya geti na kumwambia mlinzi,“Sitaki tena uruhusu hii takataka kwenye nyumba yangu tafadhali”Kisha baba akamsukumia Sia nje na kurudi ndani, moja kwa moja alienda kwa mke wake na kumkumbatia huku akimwambia,“Usijali mke wangu, hii kitu haitotokea tena”“Ila kwanini ananifanyia hivi jamani! Sia ananikosesha raha kabisa na amani”“Achana nae mke wangu, utakosaje amani sababu ya mjinga mmoja!!”Basi baba Angel alienda na mama Angel chumbani, kwakweli siku hiyo aliamua kutokutoka tena yani alishinda tu pale pale na mke wake, ingawa alijua kuwa kuna kazi zake zinakwama ila kwake ilikuwa sawa tu kuliko kumuona mke wake akihudhunika.Muda huu Sia alienda moja kwa moja kwenye lile duka ambalo linasimamiwa na Steve na kumwambia Steve,“Nimetumwa na mwenye mali, kuwa unipatie laki mbili”“Aarrgh usinichanganye wewe mwanamke kabisa, nadhani unafikiri mimi ndio bwege lako”“Kheee mbona umekuwa na hasira kiasi hiko? Nini kimekukera? Unapata shida kupata mwanamke? Ila mimi bado nipo?”“Yani wewe mwanamke sikukujua tu na dawa zako ndio zilinichanganya kipindi kile hadi nikakuoa, ila laity kama ningejua una akili mbovu kiasi hiki basi nisingethubutu”Mara simu ya Steve ilianza kuita, alitoka ofisini na kwenda kuongea nayo basi Sia alifungua droo na kuchukua kiasi cha pesa alichokitaka na kumuachia ujumbe mezani tu halafu akaondoka zake, yani Steve aliporudi alikuta tu ujumbe,“Nimechukua laki tatu”Yani Steve alijishika kichwa, kwakweli hakuelewa kabisa, kwanza hakuelewa kwanini ameenda kuongea na simu bila kufunga droo ya pesa, na pili hakuelewa ni kwanini aliamua kumuacha Sia ofisini, yani hakuelewa kabisa mahali hapo basi alikaa na kutafakari kisha aliamua kumtumia bosi wake ujumbe kwa kile ambacho kimetokea kwa siku hiyo, kiukweli alikuwa akisikitika sana kwa kilichofanywa na Sia kwa muda huo.Alipotuma ule ujumbe kwasasa alitulia kwani aliamini kuwa ujumbe umefika na bosi wake ataufanyia kazi.Muda huu Erica na Erick walitoka shuleni, yani siku ya leo walirudi pamoja ila wazazi wao walikuwa sebleni wakiangalia tv tu na moja kwa moja Erica baada ya salamu tu akawaambia kuwa asubuhi alimuona mama Elly kama anaelekea nyumbani kwao, basi baba yake alimkatisha pale kwani alijua kuwa atayasema nay a jana yake bure. Alimuuliza tu,“Hivi kesho ndio mnafunga shule eeeh!”“Ndio baba, kesho ndio kufunga shule”“Haya, mwanangu”Kisha Erica sasa alienda chumbani kwake, ila muda huu baba Angel alipata wazo na kuona ni vyema kupiga simu kwa Tumaini, basi akainuka na kwenda chumbani, ila alipochukua simu yake ndio alibambana na ujumbe wa Steve, kwakweli alishangaa sana na kujiuliza kuwa Sia ana maana gani kufanya vile dukani kwake, mama Angel nae alipoingia alimuonyesha ile meseji ya Sia,“Sasa kwanini kafanya hivyo!!”“Najua basi mke wangu? Kwakweli sijui huyu mwanamke anahitaji kitu gani kutoka kwangu! Ngoja nimpigie Tumaini nimueleze na jambo hili”Baba Angel alimpigia Tumaini kwa muda huo na alimueleza yale aliyoyafanya Sia,“Jamani mimi nimetoka kumtimua nyumbani kwangu hapa, nadhani sasa sio wakati wa kumchekea zaidi huyo mwanamke, sasa laki tatu kachukua kwa kazi gani jamani! Mimi naenda kumpokonya”“Aaah muache tu dada, ila naenda kuongeza ulinzi kwenye duka langu”“Hivi Sia wa sasa unamuelewa lakini! Kwakweli sijawahi kufikiria kama ipo siku Sia atakuwa wa aina hii, pole sana mdogo wangu ila fundisha vijana wenzio sasa wasifanye kama wewe maana wewe nawe ulikuwa muongo sana kwa wanawake na uliwaaminisha mno ndiomana huyu Sia kawa kichaa, fundisha wenzio ila pole”Baba Angel aliona kuwa dada yake hana ushauri, kwahiyo aliamua tu kukata simu ile na kufikiria mambo mengine kwa wakati huo.Wakati wa kulala, baba Angel alikuwa na mawazo sana ila hakutaka mkewe agundue jambo hilo, alichokuwa akiwaza ni namna ya kufanya na huyu Sia, yani alitamani kupata kitu cha kumfanya Sia, ila muda ule alipigiwa simu na mama yake na kuipokea halafu akaanza kuongea nayo,“Hujambo mwanangu”“Sijambo kabisa mama”“Sia kanipigia simu, kasema mtoto anaumwa”Baba Angel hakuwahi kumkatia mama yake simu ila siku hii alimkatia na kuizima kabisa, mkewe alimuuliza kuwa tatizo ni kitu gani ila alimgeresha tu pale kwahiyo hakumueleza ukweli wowote ule.Basi waliamua tu kulala na kulipokucha kwa siku hiyo ilimbidi baba Angel ajiandae kwaajili ya kwenda ofisini kwake ambako hajaenda kwa siku mbili na alikuwa na kazi za kufanya.Alifika ofisini kwake na kuanza tu kazi zake, ila muda huu mama yake alimpigia tena simu na kupokea,“Erick, ndio nini jana kunikatia simu?”“Mama, kwa kifupi sitaki uniambie habari za huyo Sia, yani sitaki kabisa tuwe tunaongea mambo mengine tu”“Kweli mwanangu huyu Sia kakutoka loh! Ila kasema mtoto amelazwa”“Mama jamani, nakuomba mama yangu nakuomba sana, habari za Sia sizitaki kabisa mimi”Baba Angel alikata tena ile simu aliona na mama yake akimchanganya tu, basi akaendelea na kazi zake kama kawaida.Mchana wa siku hiyo, ofisini kwake alifikiwa na madam Oliva, basi alimkaribisha na kuanza kuongea nae,“Nilikuwa napita maeneo haya ya karibu, nikaona ni vyema kama nikija kukusalimia baba Erick”“Oooh nashukuru sana mwalimu”“Unaonekana kuchoka sana na kazi, hivi umekula kweli!”“Sina hata hamu ya kula, halafu muda sina kwanza nimechoka hapa najilazimisha tu”“Jamani, ungekula hata matunda”“Naona hata uvivu kuyaagiza”Basi madam Oliva aliinuka na kutoka na baada ya muda kidogo alirudi na matunda na kumuwekea baba Angel mezani ili aweze kula,“Asante sana, unaonekana ni mkarimu sana wewe”Madam Oliva alitabasamu na kusema,“Unajua maisha huwa yanatufundisha mambo mengi sana, nilikuwa napita hapa ila moyo ukaniuma hadi nimekuja kukuona, na nilipokuona nimehisi kuwa umechoka sana na hujala kitu ndiomana nikakuuliza”“Nashukuru sana madam”“Unakaribishwa muda wote baba Erick, shule zimefungwa leo kwahiyo nitakuwa huru muda mwingi sana. Siku ukiwa upo tu huna wa kuongea nae jua nipo”“Aaaah madam nitakosaje wa kuongea nae!! Yupo mke wangu kipenzi ambaye huniliwaza wakati wote”Kiukweli madam Oliva alihisi wivu kwa muda huu ila alijikaza tu na kusema,“Hongera sana kwa kupata mke anayejua nini maana ya mume, ila huwa natamani sana ningeolewa maana mume wangu angepata kila kitu kutoka kwangu”“Usikate tamaa, muda bado upo wa kutosha tu, usijali utaolewa madam”“Umri umeenda jamani, yani saivi sina mvuto tena!”Baba Angel alisimamisha kidogo kazi zake na kumuangalia madam Oliva kisha akamwambia,“Nani anakuongopea kuwa huna mvuto tena!! Wewe ni mzuri sana madam, usisikilize maneno ya watu walioshindwa”Kisha baba Angel aliendelea na kazi yake, ila kile kitu cha baba Angel kumuangalia kilimfanya madam Oliva ajihisi vyema sana katika moyo wake, kisha aliongea ongea nae na kumuaga pale huku akimuuliza,“Jumatatu si utakuwa hapa ofisini?”“Ndio nitakuwepo, hata kesho pia nitakuwepo ila mara nyingi Jumamosi huwa sikai sana”“Oooh basi, tutawasiliana”Kisha madam Oliva aliondoka na kumuacha baba Angel aendelee na kazi zake.Kwakweli ingawa alipanga kwenda kwa mkwe wake ila aliona kuwa kazi zake zilihitaji muda kumaliziwa kwahiyo alikaa mpaka jioni kabisa ndio aliondoka nakurudi nyumbani kwake.Leo usiku wakati wa kulala, kama kawaida Junior alikuwa chumbani kwa Vaileth na walianza kuongea mambo mbalimbali kwanza, ambapo leo Vaileth alimwambia Junior,“Unajua mama na baba humu ndani wanapendana sana, hadi raha kuwaangalia. Natamani na sisi maisha yetu yawe hivyo!!”“Usijali Vai, mimi na wewe tunapendana sana yani tunaweza tukawa zaidi yao”“Yani nikawa nawaonea raha sana”“Jamani mke wangu, ona raha na kwenye haya mapenzi yetu”Basi Junior alianza kumpapasa pale Vaileth na mwisho wa siku kulala nae kawaida.Ila leo asubuhi kulivyokucha tu, Vaileth ndio aliwahi kuamka ila simu ya Junior ilikuwa ikiita basi Vaileth aliisogelea na kukuta namba mpya akaipokea ile simu na kuiweka sikioni,“Mpenzi, jamani mwenzio toka tumetoka kutoa ile mimba basi natokwa na dam utu hadi leo. Nakupigia simu hupokei, nashukuru leo umepokea, meseji zangu hujibu, ni kwanini unanifanyia hivi Junior?”Kiukweli Vaileth alihisi kama moyo wake umekumbwa na mripuko vile, kisha alimshtua Junior na kumuwekea ile simu sikioni huku akimsikilizia amalize kuongea nayo,“Nani wewe? Sikufahamu bhana”Kisha Junior alikata ile simu na kumgeukia Vaileth na kumuangalia kwa muda, wakati huo Vaileth alikuwa kajiinamia huku akilia. Kiukweli Vaileth alihisi kama moyo wake umekumbwa na mripuko vile, kisha alimshtua Junior na kumuwekea ile simu sikioni huku akimsikilizia amalize kuongea nayo,“Nani wewe? Sikufahamu bhana”Kisha Junior alikata ile simu na kumgeukia Vaileth na kumuangalia kwa muda, wakati huo Vaileth alikuwa kajiinamia huku akilia.Basi Junior aliamua kumuuliza,“Kwani umeongea na huyu mtu mke wangu?”“Toka hapa, nani mke wako? Wewe Junior ni mchafu sana sikujua tu”“Jamani Vai kwani tatizo liko wapi?”“Hivi Junior wewe ndio wa kukaa na kuniongopea mimi? Unaniambia unanipenda kumbe unawanawake zako wengi tu, mpaka wengine umewapa mimba na kwenda kuzitoa? Haya sasa damu zinawatoka huko hadi leo”“Sikia Vaileth, huyo mtu atakuwa amekosea namba”“Aaaah kakosea na jina lako eeeh kusema kuwa Junior kumbe ni Junior mwingine. Hivi Junior unaniona mimi mtoto mdogo eeeh!”Mara Vaileth alisikia akiitwa na mama Angel kwahiyo aliacha kuongea na Junior pale na kwenda kumsikiliza mama Angel,“Jamani Vaileth siku hizi unachelewa sana kuamka sijui ni kwanini?”“Samahani mama”“Haya, asubuhi hii kuna mahali nataka kukuagiza maana kuna kitu nakihitaji mapema hii basi nenda kajiandae nikuagize”Vaileth alienda kujiandaa na bila ya kuongea na Junior wala nini na alipomaliza tu alimwambia Junior,“Na utoke chumbani kwangu, sitaki hata kukuona”Halafu Vaileth alienda kuchukua maagizo kwa mama Angel na kuondoka zake.Vaileth alipofika alipoagizwa, wakati anasubiria alimuona kuna mwanamke ameshuka kwenye gari na kukutana na mwanamke mwingine pale walikumbatiana na kusalimiana kisha walikaa karibu na Vaileth ila hawakumtilia maanani, basi walianza kuongea pale,“Ila mwenzangu mbona siku hizi upo hivyo yani kuna muda unakuwa na mawazo sana”“Mwenzangu, yani sijui nikwambiaje, unajua sijawahi kumpenda mume wa mtu ila safari hii nampenda mume wa mtu balaa”“Kwahiyo upo nae?”“Mmmh sipo nae wala nini, yani huyo mume wa mtu mwenyewe anajifanya anampenda mke wake balaa ila na mimi nampenda sana”“Sasa shoga yangu kama swala ni kumpenda mume wa mtu na hujui jinsi ya kumpata si ungeniambia mapema! Ila ana pesa?”“Kheee yani ana pesa uchafu ila sio kwamba nahitaji pesa zake ila mimi ninachohitaji nilale nae hata mara moja tu”“Aaaah mbona kazi rahisi hiyo shoga yangu, kumdaka mwanaume ni rahisi sana. Kwanza anaitwa nani?”“Anaitwa Erick”Hapo Vaileth alishtuka kwani hakujua ni Erick gani anazungumziwa ila alipatwa na hisia kama anayezungumziwa ni baba Angel, ila alishaletewa alichokifata ikabidi tu aondoke zake huku akitamani kufahamu zaidi kuhusu Erick anayetajwa mahali pale ni nani.Vaileth alirudi nyumbani na kumpatia tu mama Angel alichomuagiza ila aliogopa kumwambia kuhusu wale wanawake ukizingatia hakujua ni Erick gani aliyekuwa akizungumziwa na wale wanawake.Leo baba Angel alipokuwa ofisini na akikaribia kufunga ofisi yake kwani siku hii alitaka kuondoka mapema ili kwanza aende dukani akaelewane na Steve na kuangalia kama kuna uwezekano wa kwenda kwa mkwe wake, ila wakati anafunga ofisi tu alishangaa kumuona madam Oliva akiwa ameenda kumtembelea na kuanza kuongea nae,“Ila ndio nilikuwa nafunga ujue”“Kwani huwa unafunga ofisi yote!”“Hapana, huwa nafunga ofisi yang utu na wengine wanaendelea na kazi kama kawaida hadi muda wa kufunga”“Oooh sawa, sio tatizo basi nimekuja muda mzuri”“Aaah sio muda mzuri huu sababu naondoka muda huu huu”“Unaelekea wapi kwani”“Kuna duka langu mahali ndio nataka niende huko”“Basi, twende wote”“Kheee kwani ndio ratiba yako ya leo”“Hapana, ila nilikuwa nimeboreka na nilikuwa nahitaji mtu niongee ongee nae kidogo kwahiyo ndio nikaja huku ofisini kwako, kwahiyo ni vyema kama tukienda wote huko dukani kwako”Basi baba Angel hakutaka kumkatalia kwani hawezi kujua kuwa pengine Oliva nae akapenda bidhaa za duka hilo na kununua.Basi walitoka nje na kuingia kwenye gari ya baba Angel kwani madam Oliva alisema kuwa kwa siku hiyo hakwenda na gari na safari ilianza huku madam Oliva akiongea vitu mbalimbali na baba Angel,“Unajua napenda sana vile unavyopendana na mke wako, mlianzia wapi nay eye hadi kufahamiana vizuri na kupendana hivyo”“Unajua upendo mwingine ni mpaka mzoeane ila mimi jamani siku ya kwanza kabisa kumuona mke wangu nilimpenda ten asana, nakumbuka ilikuwa kidato cha pili”“Kheee kidato cha pili? Mliweza vipi sasa kutengeneza mapenzi na kutengeneza shule?”“Yani kulikuwa na vikwazo vingi sana, ila Mungu ni mwema kwani mwisho wa siku nikampata mke wangu na kumuoa. Kwakweli huyu ni mwanamke wa ndoto zangu, na kama ningeoa mwanamke mwingine mbali na yeye basi huyo mwanamke mwingine ningemuacha na kumuoa yeye nampenda sana mke wangu”“Kheee hadi raha jamani, natamani mimi. Natamani sana hata ningepata mpenzi tu wa kuniambia kuwa mimi ni mwanamke wa ndoto zake, napenda sana kupendwa jamani kwakweli mwanamke mwenzangu huyo ana bahati sana, hivi anatambua kweli?”“Anatambua ndio, na uzuri ni kuwa hata yeye ananipenda sana”“Ila katika maisha yako hujawahi kufikiria kuwa na mwanamke mwingine?”“Mwingine wa nini sasa wakati mke wangu ananitosheleza, sijawahi kufikiria na wala siwezi kufikiria hilo maana mke wangu ndio maisha yangu”“Duh! Watu wanasema hapa duniani wanawake ni wengi kuliko wanaume, ndiomana wanaume wanakuwa na mahusiano na wanawake wengi wengi ili wasiwepo wanawake watakaokosa wanaume. Je wewe unasemaje kuhusu hiyo dhana ya wanawake wapo wengi kuliko wanaume?”“Hiyo dhana mimi naona ni dhana ya kujitetea tu ili mtu aendelee kufanya uhuni, hakuna cha wanawake wengi kuliko wanaume wala nini sababu kama ni hivyo kwanini ukifatilia asilimia kubwa ya wanawake utasikia nina mtu wangu halafu asilimia kubwa ya wanaume utasikia nimeachwa au sina mtu! Tatizo la wanawake wengi wanachagua sana, yani kuna wanaume wengine hawapati kabisa wanawake sababu tu ya muonekano wao, au sababu hawana pesa ya kutosha au sababu ni walemavu yani wanawake mnachagua sana. Mimi naamini Mungu katuumba wote kwa idadi kamili, kwahiyo yule ni mke wangu na kama nikiamua kuwa na mwanamke mwingine sio kwa kigezo mpo wengi hapana ila ni tamaa tu. Ila mimi naamini na nitaendelea kuamini hivi, tupo kwenye idadi sawa kabisa”“Mmmmh kwahiyo wewe hufikiriii kabisa kuchepuka?”“Nakwambia nichepuke ili iweje wakati mke wangu yupo!”“Mfano mkeo kapatwa na ulemavu je!”“Ningempenda na ulemavu wake kwani mimi upendo wangu kwa mke wangu upo moyoni na sio muonekano wake, yani yeye akiwa mwembamba au bonge bado nitampenda ten asana tu, akiwa mweusi au mweupe bado nitampenda, akiwa mfupi au mrefu bado nitampenda sana tu. Upendo wangu kwake upo moyoni, vingine hivi ni ziada tu”“Hivi wanaume kama wewe Erick wapo kweli kwenye dunia hii?”Baba Angel alicheka na kusema,“Kwani mimi naongea toka mbinguni!”Walikuwa wamefika dukani, ila kiukweli madam Oliva alizidi kumpenda baba Angel yani alizidi kuvutiwa nae kila alipokuwa akiongea nae, alimtamani sana.Baba Angel na Oliva waliingia dukani, basi Oliva alikuwa akiangalia angalia bidhaa za pale huku baba Angel akienda kuongea na Steve kuhusu tukio la Sia.“Kwahiyo ilikuwaje Steve maana ule ujumbe sijauelewa hata kidogo”Basi Steve alianza kumueleza vile ilivyokuwa mpaka Sia alipochukua hiyo pesa na kuondoka nayo,“Yule mwanamke ana wazimu”“Ni kweli ana wazimu hata sijui cha kufanya nae”“Ila akija tena mwambie kuwa Erick anasema nahisi umesahau akili zake za zamani. Maana nahisi yule mwanamke kanisahau ila mimi ni chizi zaidi yake, nikiamua kumfanyia uchizi atalia kwakweli, mwambie asitake kunirudisha nilikotoka kabisa, hili ni duka langu na hizo ni pesa zangu na huo ujinga wake iwe ni mara ya kwanza na ya mwisho maana sitarajii tena kuusikia. Sitamfatilia kwasasa wala nini andika tu kwenye kitabu kuwa hizo pesa tumeingia hasara ila kitu kama hiki asifikirie kukifanya tena maana nitamfanyia kitu kibaya, mimi huwa nacheka ila nina roho mbaya sana. Ukimuona Sia mkanye juu ya hilo”Kisha baba Angel akapitia pitia vitu vya duka lake hili na vitabu vitabu vya pale na aliporidhika sasa alimfata Oliva ili waondoke ambapo bado Oliva alikuwa akiangalia bidhaa za duka hilo na kwa wakai huo alishanunua nguo kama mbili, basi alimwambia baba Angel,“Kwakweli duka lako lina bidhaa nzuri sana nimelipenda bure, hadi nimechukua nguo”“Oooh vizuri sana, umeona zitamfaa mwanao eeh!”Madam Oliva alitabasamu kisha aliongoza hadi kwenye gari la baba Angel na kupanda, basi baba Angel alipanda pia na kumwambia,“Kwasasa nahitaji kwenda kwa mama mkwe wangu ila kama muda umeenda hivi!! Itabidi tu nirudi nyumbani, je nikuache wapi au unataka kwenda nyumbani kwangu?”“Ni kweli nahitaji kufika nyumbani kwako, nahitaji kuona mke wako ila hatonipiga kweli?”“Aaah akupige kwa lipi jamani! Kwani umemkosea nini?”“Kuna wanawake huwa wakiona mumewe kaongozana na mwanamke mwingine basi huwa wanahisia mbaya”“Oooh hawajiamini hao ila mke wangu anajiamini, hawezi kuwa na hisia mbaya na wewe ila kama una shughuli zingine basi useme nikuache wapi?”“Hamna sina shughuli yoyote, nifikishe tu kwako”Basi baba Angel alienda na madam Oliva hadi nyumbani kwake.Muda huu mama Angel alikuwa amekaa sebleni na kwavile shule zilikuwa zimefungwa basi Erica alienda kwa mama yake na kumtaka mama yake aanze kumsuka suka nywele zake yani azitonee maana Erica alikuwa akinyoa ila kipindi hiko alitamani kusuka,“Mama, na mimi nataka kuwa na nywele ndefu kama za dada Angel si zitakuwa eti eeeh!”“Zitakuwa ndio, ila mimi nitakuwa hata sikusuki vizuri, nitakupeleka saluni huko mwanangu wakakusuke vizuri upendeze”“Nitafurahi sana mama”Basi mama Angel alikuwa akijaribu pale kuzisuka suka nywele za Erica, na muda huo huo baba Angel pamoja na madam Oliva waliwasili pale nyumbani na kumkuta mkewe wakiwa sebleni akijaribu kumsuka suka Erica, basi waliwasalimia pale na baba Angel alikaa kwaajili ya utambulisho,“Samahani mke wangu, huyu anaitwa madam Oliva, ndio mwalimu wa nidhamu shuleni kwakina Erick. Halafu madam, huyu ndio mke wangu, kwahiyo mama Erick ndio huyu sasa”“Ooooh nimefurahi kumuona”Basi madm Oliva aliinuka na kupeana mikono pale na mama Angel, kisha alikaa na kuanza kuongea mawili matatu, basi akamwambia Erica aende kumwambia Vaielth alete juisi waweze kunywa na mgeni wao yule.Baada ya muda Erica alirudi na madam Oliva akawa anamwambia mama Angel,“Jamani unahangaika na vinywele vifupi hivyo vya mtoto!”“Yani acha tu, anataka urembo, nifanyeje sasa”“Mimi nina saluni yangu kwaajili ya watoto na wakibwa, yani hizo nywele wanamshika vizuri tu, atasukwa rasta na kupendeza sana huyo”Erica aliposikia alifurahi sana na kumgeukia mama yake,“Mama, nahitaji kusuka rasta”Basi mama Angel alicheka sana na kumwambia yule madam,“Hakuna tatizo, basi ataletwa na baba yake”Baba Angel nae akadakia,“Lini tena jamani, mimi nipo na kazi nyingi sana”Basi madam Oliva akadakia,“Hata msijali, Jumatatu nitakuja kumchukua hapa na kumpeleka huko saluni halafu nitamrudisha au nikiona mbali huku nitamrudisha ofisini kwako baba Erick ili urudi nae nyumbani maana saluni kwangu sio mbali na ofisini kwako”“Kama ndio hivyo sawa, na wewe Erica unataka urembo wa nini si uwe tu kama kaka yako!”“Jamani baba, nataka kuwa tofauti. Mimi ni mtoto wa kike na Erick ni mtoto wa kiume”Basi Vaileth alileta juice na kuwamiminia pale, ila alipomuona madam Oliva alishtuka kiasi sema hakutaka kuonyesha mshtuko wake, basi alimimina tu ile juisi na kuwakaribisha halafu akaenda kuendelea na shughuli zake, ila baba Angel alisema kuwa anahitaji kupumzika kwa muda huo na madam nae aliaga ila kwavile hakuwa na usafiri basi baba Angel alimuita Erick ili aongozane na Erica waweze kumsindikiza yule madam kwa muda ule nao walifanya vile na kuanza kumsindikiza ila mama yao aliwaambia kuwa wasifike mbali.Pale nyumbani baba Angel aliamua muda huo kwenda kuoga tu na kwenda kulala kwani alijihisi uchovu sana, basi Vaileth alienda sebleni kutoa vile vikombe vya juisi na kumuuliza mama Angel ambaye bado alikuwa pale sebleni,“Kwani yule madam unamjua vizuri mama?”“Hapana, ndio leo siku ya kwanza kumuona”“Oooh nilidhani unamfahamu”“Kwani kuna nini?”“Hakuna kitu mama, nimeuliza tu”Bado Vaileth aliogopa kusema, kwahiyo alitoa tu vile vyombo na kurudi jikoni kusafisha vyombo huku mama Angel nae akienda chumbani.Basi Erick na Erica walimsindikiza madam Oliva hadi kwenye stendi ya daladala huku wakiongea nae mambo mbalimbali tu, na madam aliendelea kumsisitiza Erica kuwa ataenda kumchukua Jumatatu kama alivyosema. Basi hadi yule madam alipanda daladala ndipo na wao wakaanza kurudi nyumbani huku wakiongea,“Jamani leo bahati hii! Sijui baba kafikiria nini kusema tumsindikize huyu madam!”“Yanileo tunaweza kuangalia vizuri mandhari ya sehemu mbalimbali ilivyo, hivi wewe huchokagi kukaa ndani Erick! Mimi nachoka jamani, natamani mama angekuwa ananiruhusu nizunguke kila sehemu ninayoitaka”Basi njiani karibia na stendi waliona watu wengi wamesimama wakiangalia kitu, ikabidi na wao waende kuangalia walikuta kuna watu wakitangaza vitu vynye madhara na dawa za kutumia,“Mayai hayo ya kisasa mnakula ila hamjui ni sumu katika miili yenu, leo tutawaonyesha jinsi sumu kwenye yai la kisasa inavyofanya kazi, soda hizo ni sumu kali sana, hayo mafuta ya kupikia mnayotumia ni sumu, hizo soseji mnazokula ni sumu, hizo permpers mnazowazalisha watoto ni sumu na zina madhara makubwa sana, hizo pedi mnazotumia dada zetu zina madhara makubwa sana, leo tutawaonyehs jinsi sumu inavyoingia mwilini na namna ya kuitoa sumu hiyo”Kwakweli Erick na Erica walikuwa wakishangaa sana, maana yule aliyetangaza alisema karibia kila kitu ni sumu na kuwafanya wabaki pale kushangaa tu mara Erica akavutwa bega, alipogeuka nyuma alimuona mtu anayemfahamu ambapo alimuona Bahati basi akamshtua Erick ambapo walisogea kidogo na Bahati akawasalimia kisha akawaambia,“Nyie mmesimama kuwaangalia hao, wengi wao ni matapeli, msijisumbue wala nini”“Matapeli kivipi? Mbona wanasema vitu vya ukweli?”“Ndio wanasema vitu vingine vya ukweli ila kwa njia zisizo na ukweli, msiwasikilize mtaharibu fikra zenu. Kwanza nyie mkiwasikiliza mtajiona mmekula sumu tupu na kununua dawa zao ambazo hamna kitu zitafanya kwenye miili yenu zaidi zaidi mtaharisha tu basi”“Wewe umewajulia wapi?”“Mama yangu ni mnene, aliwasikia hawa wakitangaza sumu na dawa mbalimbali, basi walitangaza na dawa za kupunguza mwili na mama alinunua, ila nini kilitokea aliharisha tu siku nzima na hakuna kupungua mwili wala nini”Erica na Erick walibaki wakimuangalia kisha akasema,“Kwani mnaenda wapi muda huu?”“Tunarudi nyumbani”“Basin i vyema nikapafahamu hata nyumbani kwenu”Erica alianzisha safari ila Erick hakupenda kabisa kwani alimuhisi Bahati kumnyemelea mdogo wake na hakupenda kabisa kile kitu.Basi walifika hadi kwakina Erica ila Bahati hakuingia ndani ila aliwaahidi tu kuwa ipo siku ataenda kuwasalimia.Mama Angel alichukia sana kwa ambavyo watoto wamechelewa kurudi, na moja kwa moja kwenda chumbani na kumuamsha mume wake,“Hivi leo kitu gani kimekutuma uwaambie wakina Erick wamsindikize yule mgeni!”“Kwani bado hawajarudi! Nimechoka sana mama Angel, niache nipumzike”“Unapumzikaje na watoto hawajarudi”“Hapo kidogo palimshtua baba Angel na kumfanya akae kwanza, na kusema,“Jamani, wamepitia wapi hawa watoto?”“Mimi sijui ila hawajarudi na kumbuka niliwaambia wawahi”“Ila mke wangu naamini watarudi tu”“Watarudi muda gani?”“Kwahiyo unataka niende kuwatafuta kweli jamani mama Angel?”Mama Angel alikaa kimya kidogo na kurudi sebleni, baada ya muda kidogo Erick na Erica walirudi kwakweli mama Angel alikuwa na hasira nao kiasi kwamba hakuwauliza kuwa wamechelewea wapi wala nini zaidi zaidi aliwavuta na kuanza kuwatandika na fagio kiasi cha baba yao kufika na kuwaamulia pale kupigwa kwahiyo Erica na Erica walikimbilia tu vyumbani kwao.Basi baba Angel alimchukua mke wake na kwenda nae chumbani kuongea nae,“Mke wangu, watoto hawafundishwi hivyo”“Sitaki mtu wa kunielekeza namna ya kufundisha watoto wangu”“Mmmmh haya mke wangu, ngoja mimi niendelee kupumzika ila usiende kuwapiga tena watoto”Basi baba Angel aliendelea kulala tu.Kesho yake jioni, familia nzima ilikuwa nyumbani baada ya kufanya ibada kwa siku hiyo kwahiyo muda huu walikuwa wametulia tu nyumbani ila kwa upande wa Junior hakuwa na raha kabisa kwani tangu alipogombana na Vaileth basi Vaileth hakutaka kabisa kulala nae wala hakumuhitaji tena aende chumbani kwake kwani muda wote alifunga mlango wake kwahiyo Junior alikuwa hafunguliwi mlango.Basi muda huu wakati wamekaa wote, baba Angel aliwaambia pale,“Wanafunzi wamefunga shule, ila napenda wote humu ndani mchague sehemu ambayo tutaenda kutembelea kwa kipindi hiki, basi Vaileth akasema“Jamani mimi naomba twende ufukweni maana sijawahi kutembelea huko”Basi wote wakacheka sana kwani walikuwa wakiona ufukweni ni kitu cha kawaida kabisa na wao walitaka kitu kingine, basi Erick akasema,“Bora twende mbugani tukaangalie wanyama”Mara simu ya baba Angel ikaita na kumfanya aipokee kwani mpigaji alikuwa ni mama yake,“Kesho nitakuja ofisini kwako maana nina maongezi na wewe”“Sawa, hakuna tatizo”Baada ya kuongea nayo aliwaangalia wanae sasa na kuwaambia,“Jamani, hatujafika muafaka sasa ni mbugani au ufukweni?”Wote walisema mbugani kasoro Vaileth tu aliyedai ufukweni basi baba Angel akasema,“Jamani, mbugani tutaenda siku nyingine ila kwa siku hiyo twendeni ufukweni ili Vaileth nae afurahi”Kisha mama Angel akasema,“Hivi katika hizo safari zenu mnanifikiria na mimi jamani! Naona mnapanga tu mara mbugani sijui ufukweni, na mimi naendaje na huyu Ester? Au baba Angel utawapeleka tu kisha mimi na wewe na Ester tutashinda nyumbani hadi muda wao wa kurudi”“Aaah mama Angel kwanini nijisumbue hivyo! Erick na Junior wanaweza kuendesha gari, basi nitawapatia gari moja na pesa na kuwaelekeza ufukwe wa kwenda halafu wataenda huko na kurudi hapa nyumbani halafu mimi na wewe tutashinda hapa nyumbani”“Oooh hapo sawa mume wangu, halafu Vaileth utafanya kazi ya kuangalia wadogo zako hawa”Vaileth aliitikia tu, laiti kama angejua Junior huwa anamuita Vaileth mke wangu hata asingejisumbua kumwambia Vaileth kuwa aangalie wadogo zake maana kuna mume wake pale, kuna shemeji yake na wifi yake ila hakujua ukweli tu.Basi kwa siku ya leo familia hii ilifurahi sana na kupanga siku ya hiyo safari, kiukweli walikuwa na furaha hasa watoto kwani waliona rah asana kama wataenda kwenye hiyo safari bila ya wazazi wao kwani huwa wanaona kuwa wanawafatilia sana.Siku hii waliongea ongea kwa pamoja, na muda wa kulala ulipofika, kila mmoja alienda zake kwenye chumba chake kulala.Asubuhi kwenye mida ya saa tatu hivi, madam Oliva alifika pale nyumbani kwa ahadi yake ya kumchukua Erica ili ampeleke saluni na uzuri ni kuwa alimkuta Erica ameshajiandaa kwahiyo akaaga pale na kuondoka nae.Siku hiyo alikuwa na usafiri kwahiyo walitembea kwenye gari la huyo madam huku akiongea na Erica mambo mbalimbali,“Erica, kitu gani cha kutafuna tafuna huwa unapenda?”“Napenda sana chokleti”“Nadhani baba huwa anakuletea kila siku!”“Alikuwa ananiletea ndio ila toka mama kamleta mdogo wangu imekuwa basi tena, baba haniletei tena yani haniletei kabisa”“Oooh basi mimi nitakuwa nakuletea”Muda huo akapita nae dukani na kumnunuliza chokleti ambapo Erica alifurahi sana kununuliwa ile chokleti na madam Oliva. Basi walirudi kwenye gari huku madam Oliva akiendelea kumuuliza maswali mbalimbali Erica kisha akamwambia,“Mimi na wewe Erica tutakuwa marafiki, tutakuwa tunaambiana vitu vingi sana ila itakuwa siri yetu”“Sawa madam”Basi madam akampa mkono Erica kama ishara ya urafiki wao na kumfanya Erica afurahi sana.Leo Angel aliachiwa simu na bibi yake halafu bibi yake alitoka, kutokana na Samir kumwambia kuwa ana hamu sana ya kumuona ilibidi amtumie ujumbe kuwa siku hii bibi yake katoka,“Oooh Angel unaniambia ukweli? Yani katoka na kukuachia simu!”“Ndio, nadhani kajisahau”“Basi jiandae, nakuja hapo kukuchukua ili twende mahali Angel, nahitaji tuwe mahali wawili tu”“Mmmh wapi hapo Samir lakini? Bibi je akirudi?”“Atakuwa kaenda kwenye kikundi chao maana hata bibi yangu nyumbani nimeulizia na kuambiwa hivyo na huko huwa wanachelewa sana kurudi, nakuomba Angel jiandae”Basi Angel alijiandaa haraka haraka , na kweli baada ya muda tu Samir alikuwa amefika mahali pale na kutoka nje na Angel.Ila wakati wanatoka getini, walishangaa sana kumkuta bibi Angel nae akiwa anarudi kwa kasi kidogo ila huyu bibi alivyomuona Samir na Angel alichukia sana na moja kwa moja alienda kumnasa Samir kibao. Ila wakati wanatoka getini, walishangaa sana kumkuta bibi Angel nae akiwa anarudi kwa kasi kidogo ila huyu bibi alivyomuona Samir na Angel alichukia sana na moja kwa moja alienda kumnasa Samir kibao.Kwakweli kile kibao kilimuingia Samir, kiasi kwamba aliamua kukimbia tu kwani angeendelea kusimama mahali hapo basi angepigwa tena na huyu bibi na alimtambua vizuri mambo yake, hivyobasi alikimbia, basi bibi alimshika Angel mkono na kuingia nae ndani, kwakwlei kwa wakati huo Angel alijiandaa kupigwa tu kwani alijua wazi kuwa atapigwa sana na bibi yake huyu, ila walipoingia ndani bibi alimkalisha Angel chini na kumuuliza,“Una uhakika kuwa huyo Samir anakupenda?”Erica alinyamaza kimya tu huku akiangalia chini kwa aibu, kisha bibi yake akamwambia tena,“Mjukuu wangu, huyo Samir hakupendi wala nini hebu jiulize anayekupenda kweli anaweza kukimbia sababu ya kupigwa kibao kimoja? Mtu akikupenda huwa tayari kwa lolote lile, kuna kijana mmoja aliitwa Bahati basi alikuwa akimpenda dada mmoja hivi na kumfatilia sana, yani yule kijana alikuwa tayari hata kumwagiwa maji ya moto sababu ya mwanamke, yule kijana aliwahi kukaa rumande sababu ya mwanamke, hakuwa na kosa ila alikaa rumande sababu ya upendo wake tu kwa mwanamke”“Kheee bibi, sasa kwanini aliwekwa rumande?”“Ndugu wa mwanamke hawakumtaka, kwahiyo alivyokuwa hataki kuondoka hadi aonane na mwanamke ndipo walipomuweka rumande ila badae walimuhurumia sana na kumuachia huru. Kijana huyo alikuwa akihudumia familia ya mwanamke kama familia yake akiwaletea kuku na samaki, kijana huyo alikuwa tayari kulea mtoto wa mwanaume mwingine ambaye huyo dada alimzaa kabla, yani huyo kijana alikuwa na upendo wa dhati tena upendo mkubwa sana”“Bibi, vijana kama hao wapo?”“Wapo ndio, msubirie wa kwako ila sio huyu Samir anakuongopea tu, kibao kimoja kakimbia vile, hata hajali kuwa nitakupiga wewe au nini! Nakwambia ingekuwa huyo Bahati angetaka apigwe yeye badala yako, usimfikirire Samir mjukuu wangu hakupendi wala nini. Haya nipe na simu nikaiweke”Basi Angel aliitoa ile simu na kumpa bibi yake ili aiweke, kisha bibi aliinuka yani Angel kwakweli hakuamini kama kapona kipigo toka kwa bibi yake maana alihisi muda huo angepigwa vibaya sana ila hakupigwa wala nini zaidi ya kuambiwa kuwa Samir hafai kabisa kwake.Basi madam Oliva alifika na Erica saluni na kumuweka pale huku akiwaelekeza wasusi namna ya kumsuka nao walianza jambo lile, huku muda huo madam akiwaaga kuwa anaenda kwanza kuangalia chuo chake, kisha alimuuliza Erica,“Nikirudi nikuletee nini? Maana leo itabidi ule huku”“Chochote tu”“Sawa, nitakuletea chips kuku basi”“Sawa, asante”Erica alitabasamu halafu madam Oliva alitoka. Alipotoka tu wale wasusi waliokuwa wakimsuka Erica walianza maongezi, kwanza kabisa walimuuliza Erica,“Huyu madam ni ndugu yako?”“Hapana, ila ni mwalimu wa kaka yangu”“Ooooh sawa”Kisha mwenzie akasema,“Jamani, huyu madam leo alivyo na furaha utafikiri kitu gani. Halafu naona huyu mtoto kampenda sana”“Inaonekana, maana sio kawaida yake. Asubuhi kapita kuwa anamleta mtoto tumsuke, alivyokuwa anatuambia kuhusu huyo mtoto basi nikajua mtoto mdogo sana kumbe binti tu. Sijui muusuke taratibu, msimsumbue, msimvute nywele, mpeni anachotaka”Wakaanza kucheka huku mmoja akisema,“Kwani jamani yule madam ana mume yule?”“Mume hana, eti anasema yeye yupo kutafuta pesa tu hana shida na mume wala shida ya kuolewa”“Ila ana mpenzi au?”“Yani kwa kifupi yule madam hana mpango kabisa na wanaume, yani yeye anasema anawaza pesa tu ndio ya muhimu kwake.”“Na kama pesa ni anaitafuta kweli, maana yule kaajiriwa halafu ana biashara zake. Ana chuo chake cha kompyuta, ana hii saluni na ana shule yake ya kujifunza ushonaji”“Kweli yupo vizuri ila kuna umuhimu wa kuwa na mwanaume katika maisha, mtu anaishi vipi jamani bila mwanaume! Tamaa zake za kimwili anazimaliza vipi?”“Hapo sasa, au mwenzetu hana tamaa za kimwili jamani! Kuna mambo mengine ndiomana mtu unakuwa na hasira muda wote, kwanza toka nimfahamu huyu madam ndio leo namuona anacheka”Mwingine akadakia,“Usikute kashaonja tamu ya asali”Mmoja akawanyamazisha wenzie,“Badilisheni mazungumzo jamani, kumbukeni mnayemsema katuajiri na anafanya turinge mjini”“Kheee bwana eeeh anasemwa raisi sembuse yeye!!”Basi wakacheka na kuendelea na maongezi mengine.Baba Angel akiwa ofisini kwake kwa muda huo, akaja mama yake kama ambavyo aliongea nae kwenye simu jana yake basi alimkaribisha na kumsalimia pale kisha kuanza maongezi nae ambapo mama yake alianza kuongea,“Mwanangu sikia, naomba niache niongee kwanza halafu zamu yako ikifika ndio utasema yani usinikatishe wakati naongea”“Sawa mama”“Ni hivi, Sia alinipigia simu kuwa mtoto anaumwa, kwakweli na mimi ni mama halafu na mimi nimepitia mazingira ya kulea mtoto bila ya baba kwahiyo najua uchungu wake na ninajua ni hali gani inakuwa. Nimekulea wewe, nimehangaika na wewe kipindi hiko baba yako hana hata habari hata wewe mwenyewe unakumbuka wazi kuwa baba yako umefahamiana nae ukiwa mkubwa kabisa unajitambua tena ukiwa unatangatanga huko baada ya kufukuzwa shule. Kiukweli nilipatwa na uchungu kusikia mtoto mdogo anaumwa na mama yake hana pesa, ilibidi niende. Nilipofika pale nilimkuta mtoto kalala, yani nilienda kwa kuelekezwa na Sia mwenyewe, na nilivyofika alimuamsha mtoto aje anisalimie maana kuna zahanati alimpeleka na alipatiwa dawa ila aliacha deni tu pale zahanati, ilibidi nitoe pesa aende kulipa hilo deni maana afya ya mtoto ni ya muhimu zaidi ya vyote. Kingine ni kuhusu yule mtoto mdogo Elly, kwakweli kwa jinsi nilivyokuwa namuangalia ananikumbusha zamani kabisa kipindi cha udogo wako, wewe ulikuwa ni mtoto mpole na mchangamfu basi ndio alivyo yule Elly, mwanangu mimi naomba jambo moja tu hata kama Sia humpendi basi mpende yule mtoto, nakuomba ukubali kupima DNA na Elly”“Umemaliza mama?”“Ndio, nimemaliza nakusikiliza wewe sasa”“Kwanza kabisa siwezi kwenda kupima DNA na Elly, nikifanya hivyo inamaana sijiamini. Pili ngoja nikuulize mama, inamaana Ellyn i mwanangu halafu Erick sio mwanangu?”“Mmmh mimi sijasema Erick sio mwanao, kwanza itakuwaje Erick asiwe mwanao jamani! Erick si kazaliwa na mkeo, sasa itakuwaje sio mwanao? Ninachohitaji mimi ni Elly kupata haki sawa na wenzie wote, una watoto pale kuna Angel, Erick, Erica, Ester na sasa Elly awepo kwenye familia”“Kwa misingi ipi mama?”“Ellyn i mtoto wako ambaye umezaa na Sia”“Mama, mimi ndio mwanaume ambaye Sia anadai amezaa nae, ila mimi nakataa mbele ya vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana kuwa sijazaa na Sia mimi.”“Ila mwanangu unakumbuka tabia zako vizuri wewe, ni wadada wangapi waliokuwa wakilalamika kwangu kuwa wana mimba zako sembuse Sia ambae muda wote alikuwa na wewe! Je kama akitokea mdada mwingine na mtoto utakataa kuwa sio mwanao wakati ulikuwa muhuni sana wewe!”“Ni kweli mama, yani siwezi kukataa kuwa sikuwa muhuni, kama uhuni nimeufanya sana tu, ila niliufanya sababu ya stress nilikuwa siwezi kumpata mwanamke nimpendaye ndiomana nilikuwa nafanya ule uhuni, kuna wanawake wakija kusema Erick tulizaa na wewe naweza nikakubali ila sio Sia, unajua nini Sian i mwanamke ambaye alikuwa akiniganda sana. Na toka nimetoka Afrika kusini na kuanza kuishi na Erica kw aupendo ile ikawa mwisho wa mimi na Sia yani sikuwa na ukaribu nae tena, alikuwa akifanya kila mbinu lakini ilishindikana kuwa na mimi, halafu leo useme Sia kazaa na mimi tena mtoto ambaye ni umri sawa na watoto niliozaa na Erica, hapana kwakweli Sian i muongo tena muongo namba moja. Kuna mwanamke mmoja angesema hivyo ningesema labda maana kipindi kile Erica alinikatalia kabisa hadi ndoa na mimi ni mwanaume ila yule mwanamke alikuwa akijua kila kitu kuhusu mimi na Erica hadi siku namuacha nikamwambia mimi na wewe basi maana nimerudi kwa Erica wangu, yule mwanamke alikubali kwa roho moja na hajawahi kunitafuta tena hadi leo kwani anajua kuwa nina familia yangu ila kwanini Sia anakuwa hivi jamani! Kwani wanaume wameisha duniani au kitu gani?”Mama yake akapumua kidogo na kusema,“Haya, mfano huyo mwanamke aseme pia ana mtoto wako utasemaje?”“Haiwezekani sababu yule mwanamke nilikuwa nae na aliweka kijiti cha miaka mitatu, na wakati niko nae ilikuwa ni mwaka wa pili, mama katika maisha yangu kitu mimba nilikuwa nakihofia sana na kukuheshimu kwani nilitambua wazi kuwa Erica akiona nina watoto wengi basi hatonikubali, kwahiyo nilikuwa makini sana”“Sawa mwanangu ila mimi hoja yangu bado ni moja tu, ukapime DNA na Elly”“Mama, tafadhari hilo swala kwangu halikubaliki. Yani hiyo kitu haipo, labda ukapime wewe na ukikuta mnafanana basi jua kuwa ni mwanao na sio mwanangu sababu mimi sijazaa na Sia”“Sasa hayo matusi mwanangu, yani unanitusi mama yako. Inamaana mimi nimezaa na Sia? Yani wewe mtoto loh! Mitoto mingine tunabebaga change tu tumboni”Kisha mama yake akanyanyuka na kuondoka zake, inaonyesha alikuwa amekasirika ila baba Angel wala hakujali zaidi zaidi aliendelea na kazi zake tu.Madam Oliva alimpelekea Erica kama alivyoahidi na Erica alikula pale, kisha walipomaliza kumsuka alimwambia kuwa anampeleka ofisini kwa baba yake ili aondoke na baba yake maana yeye alidai kuwa kuna kazi anataka kuifanya.Basi aliondoka na Erica pale huku akimsifia kuwa kapendeza sana hadi kabadilika, basi Erica alikuwa akifurahi sana kuambiwa vile, yule madam nae alikuwa akifurahi kuona Erica anafurahi ndipo Erica alipomwambia,“Madam, wale wafanyakazi wako mule wanafki”“Wamefanyaje tena?”Erica alianza kumueleza moja baada ya jingine ambalo wafanyakazi wale walikuwa wakisema na kuelekeza kabisa yupi kasema lipi na yupi kaongea lingine, kiukweli yule madam alichukia sana,“Yani badala ya kufanya kazi wanafanya kazi ya kunisema!”“Tena mwenzao alipowakatisha wakasema anasemwa raisi sembuse wewe!”Yani madam Oliva alizidi kuchukia kwakweli na kuona kuwa wafanyakazi wake wabaya, basi alienda na Erica hadi ofisini kwa baba yake ambaye kwa muda huo alikuwa amekaa tu maana hata yeye kichwa chake kilikuwa kimevurugwa ila alipomuona binti yake alimsifia sana kuwa kapendeza kisha akamshukuru madam Oliva na kumuuliza pale,“Eeeeh ndio pesa ngapi hapo?”“Aaaah hii leo nimempa ofa”“Kumbe ofa!! Jamani madam kwanini lakini!”“Hamna jamani, hii ni ahadi yangu kwake, na sio kwa leo tu kwani siku zote akiitaji kusuka basi nitampeleka saluni kwangu na atasuka bure kabisa”Basi baba Angel alicheka tu, kwavile hata yeye alichoka aliamua kuondoka kwahiyo aliagana na madam Oliva halafu yeye kuelekea kwake huku madam akirudi kwenye saluni yake.Basi Erica kama kawaida alianza kumsimulia na baba yake maneno ambayo wale wadada wa saluni walivyokuwa wakiongea na jinsi na yeye alivyomueleza madam Oliva,“Aaah mwanangu, unajua utakuwa umewafanya hao wadada wafukuzwe kazi!!”“Ila baba, mimi sijasema kwa ubaya, nimesema tu ili madam Oliva ajue kuwa wafanyakazi wake ni watu wa aina gani!”“Mmmh ila Erica mambo yako jamani!”Baba Angel alicheka na kutikisa kichw atu huku wakielekea nyumbani.Walipofika nyumbani, kila mtu alikuwa akimsifia Erica kuwa kapendeza sana na kumfanya hata yeye afurahie sana zile sifa alizokuwa anapewa.Basi waliongea ongea kidogo pale halafu Erica alienda chumbani kwake halafu mama yake alimfata na kumuuliza,“Eeeh Erica, nipe habari za huko”Erica kama kawaida alimuelezea kila kitu yani hakuacha hata kimoja, kisha akamwambia,“Wale wasusi wanasema madam yupo kutafuta hela ila kapewa hela na baba kaikataa”“Hela ya nini?”“Si ya kunisuka mimi, eti kasema ni ofa”“Kheee kumbe!!”“Ndio mama, kwahiyo nimesukwa bure”“Haya sawa mwanangu, mimi nashukuru kwa ujumbe”Mama Angel alijua kuwa mwanae lazima atamwambia kila kitu, sababu ya kumuuliza ni kujiridhisha kuwa madam Oliva sio mtu mbaya katika maisha yao, na kwa yale maongezi ya mwanae hakuona ubaya wa madam huyo sababu ameambiwa kuwa huyo madam yupo kwaajili ya kutafuta pesa tu.Basi usiku wa siku hii, baba Angel aliongea na watoto wake maana Erica alienda kuomba kuwa hiyo safari ya ufukweni iwe kesho, na kwavile alijihisi uchovu sana akaona hakuna tatizo kwahiyo aliwaambia tu kuwa kesho yake wataenda huko ufukweni kutembea, ila ilikuwa nu furaha kubwa. Basi siku hiyo walilala huku wakiwaza uhuru ambao kesho yake watakuwa nao.Basi kulipokucha, baada ya kazi za hapa na pale ndio walienda kujiandaa sasa na walipokuwa tayari ndio walienda kuchukua ruhusa mapema naye aliwaruhusu na kuwapa pesa kwaajili ya matumizi ya huko watakapokuwa kutembea ila baba yao aliwaambia,“Ila kule ni kuzuri sana mwisho wa wiki, sema leo siku ya kawaida mtakuta kumepooza sana”“Aaaah baba, sisi hatuna tatizo ni bora tukashuhudie maji tu”Basi akawaruhusu na wao wakaondoka kisha pale nyumbani alibaki na mkewe tu huku wakiongea na kupanga mambo mbalimbali.Muda huu mama Angel ndio alikuwa na simu ya mume wake, basi ujumbe mara ukaingia kwenye simu ya mume wake,“Baba Elly, mbona unafanya hivyo?”Moja kwa moja mama Angel alitambua kuwa aliyetuma ujumbe ule alikuwa ni Sia, basi alimuangalia mumewe na kumuuliza,“Eeeeh mume wangu huyu Sia ana ajenda gani za kukuita baba Elly?”Akampa simu mumewe ambapo naye aliangalia ule ujumbe na kumwambia mke wake,“Aaaah si mjinga huyu, hutambui hilo mke wangu. Naomba usifatilie mambo ya huyu”“Ila amekazana sana mume wangu?”“Achana nae, yani yeye ilimradi kapata namba zetu basi anaona cha kufanya ni kutusumbua tu, usimjali kwa lolote huyu mtu mke wangu”“Na akija tena hapa nyumbani!”“Hawezi, nishamwambia mlinzi kuwa sitaki kuiona ile takataka hapa nyumbani kwangu, hebu tufanye vitu vya muhimu mke wangu. Eeeh watoto wote wameondoka, leo tutakula nini?”“Mmmh hata sijui halafu naona uvivu kupika leo hatari”“Hakuna tatizo mke wangu, basi leo nitakupikia naamini utapenda chakula changu”Mama Angel alicheka na kumkumbusha kitu mume wake,“Ndio unipikie kama ugali aliopika dada yako nyumbani kwetu, na maharage yenye macho”Baba Angel alicheka sana, yani alicheka muda huo na kusema,“Yani Tumaini kashasahau ujue kama alikuwa hajui kupika, saivi anajiona ndio mwenyewe wakati aliumbuka ukweni. Ila kwenu sio watu wazuri, yani kumfanyia vile dada yangu dah! Haya sasa nikupikie nini mke wangu?”“Chohote utakachokipenda wewe basi nami nitakipenda tena leo nimepikiwa na mume wangu basi nitakulaje!”Wakacheka pale na kuendelea na mambo mengine.Wakina Erick walifika ufukweni walikokuwa wakienda, basi baada ya kufika pale Junior akawaambia,“Jamani, mimi nitatembea na Vaileth huku nikimuonyesha mandhari ya ufukwe halafu nyie kaka na dada ongozaneni huko kwingine sio tuanze kufatana fatana”Erick na Erica wakaguna ila wakakubaliana nae tu na moja kwa moja Junior aliongozana na Vaileth ila kwakweli Vaileth hakutaka kuongozana na Junior sema tu hakutaka Erick na Erica watambue chochote kile.Vaileth na Junior waliongozana huku Junior akijifanya kumuonyesha Vaileth baadhi ya vitu vya ufukweni, kisha alimuomba wakae mahali kwenye mchanga ili amuonyeshe vizuri, na walipokaa tu alianza maongezi nae,“Kwanza kabisa Vaileth, ni kwanini umenichukia?”“Hivi unadhani kuna mtu anaeweza kufurahia ujinga Junior, sikia umenidanganya mimi kuwa unanipenda kumbe una wanawake zako kibao. Najua unanifanyia yote haya sababu unaniona mimi mjinga kwakuwa ni mtu mzima halafu nimekupenda wewe kijana mdogo”“Ngoja nikukatishe kuhusu umri wako, kwanza kabisa tambua kuwa umri ni namba tu, mapenzi hayaangalii umri wala nini. Halafu unaweza kuona mimi ni mdogo ila nikawa natambua mambo mengi sana katika mapenzi kutokana na niliyopita. Siwezi kukataa hili, ni kweli mimi nilikuwa muhuni sana na nilikuwa na wanawake wengi, ila nilipokupata wewe nikasema kwanini nihangaike na wanawake wengine wakati wewe nakupenda! Sasa yule msichana niliachana nae kitambo sana na alisema kuwa ana mimba yangu na anahitaji kuitoa, basi nilimpatia pesa za kuitoa na hapo nikamwambia kuwa mimi na yeye ndio basi. Sasa hata namshangaa kunitafuta tena sijui damu zinamtoka, kwanza kabisa mimba alikuwa nayo yeye na sio mie, halafu ni yeye ndio aliyeenda kutoa, sasa anamlalamikia nani kuwa damu zinamtoka? Achana na yule msichana, kwanza nilimwambia kuwa mimi nina mke aniheshimu ila hataki ndiomana kafanya huo ujinga, jamani Vai nakupenda sana”“Mmmh kwa mtindo huu ndio tutakuwa kama mama na baba kweli kule nyumbani! Wale wanapendana kwa dhati na wala baba hana uhuni kabisa”“Sikia nikwambie, mama yangu nilimsikia akiongea na baba na walikuwa wakiongea kuhusu bamdogo huyo, nasikia alikuwa ni malaya tena malaya koko, hata mbwa mwenyewe akasome”“Jamani Junior, punguza ukali wa maneno”“Aaah basi, ila usione watu wametulia kwenye ndoa zao ukadhani wameibuka tu, penzi la kweli linatengenezwa na maelewano mema na masikizano, sasa unanifungia mlango kabisa hutaki hata kusikia upande wangu naongea kuhusu nini au nitajitetea vipi ila unabaki kuumia moyo na kunilaumu. Jamani Vaileth mimi nakupenda sana”“Mmmh lakini swala la kusema baba alikuwa muhuni nakukatalia”“Haya, endelea kukataa tu ila wanaomfahamu wenyewe wanasema, kuwa alikuwa ni kiwembe balaa kinakata kulia na kushoto, unaambiwa akiwa anatembea na wewe mdada na ukamtambulisha rafiki zako basi jua wote hao atawapitia”“Duh!!”“Mbona mimi mstaarabu sana, ila maisha huwa yanabadilisha mtu. Muangalie sasa, katulia na ndoa yake, hanywi pombe na unaambiwa alikuwa analewa yule hadi anazima”“Junior! Nani kakwambia maneno hayo?”“Yani licha ya kumsikia mama ila kuna mama mmoja hivi, sijui alikuwaga mwanamke wa zamani wa bamdogo basi huwa nikikutana nae ananiambia mambo mengi sana ya bamdogo kipindi hiko”“Kwahiyo na yeye alimvumilia tu! Yani mwanaume analewa hadi anazima, anatembea na rafiki zako wote, bado alimvumilia tu”“Si alimpenda, tena sio marafiki tu hata ndugu zako ikiwezekana anatembea nao. Unajua ukiona mwanaume wa hivyo tambua kabisa hakupendi kwani mwanaume anayekupenda atawaheshimu ndugu zako, atawaheshimu rafiki zako na atakuheshimu na wewe pia. Yule mmama nilimwambia kuwa basi hakukupenda, ila yule mama anavyoongea kwa uchungu hata nina mashaka nae”“Ni mama gani huyo?”“Siku moja nitakuonyesha, nikimuona tu nje ya geti basi nitakuita ili tuongee nae, kiukweli utabaki unamuangalia tu. Ila sijui alinihadithia mimi tu au huwa anawahadithia wengi sijui. Kiukweli siwezi kumueleza bamdogo yale maneno najua atachukia sana”“Ila kwakweli imenishangaza sana, kwahiyo wewe unanipenda kweli?”“Vaileth jamani, mimi ninakupenda sana tu, kiasi kwamba hata siwezi kumtamani mwanamke mwingine zaidi yako. Naomba unisamehe na tuanze kurasa mpya ya mapenzi yetu”Vaileth alitabasamu tu na kumfanya Junior atambue kuwa pale ameshasamehewa kwahiyo ilikuwa ni furaha sana kwake kwani alitamani mno kusamehewa na Vaileth.Erick na Erica nao walikuwa wakitembea tembea pembezoni mwa maji huku wakichezea maji na kukimbizana, basi Erica akasema,“Jamani, mimi huwa nikimuona Sarah yupo karibu na wewe basi roho huwa inaniuma sana”“Kwanini?”“Hata sijui kwakweli”“Sikia basi tufanye kitu kimoja”“Kitu gani?”“Mimi na wewe tupeane ahadi ya jambo moja ambalo wewe hutolifanya katika maisha yako na mimi sitolifanya katika maisha yangu”“Jambo gani”“Iwe hivi, yani mimi nisiwe na rafiki yoyote wa kike zaidi yako yani wewe uwe ndio rafiki yangu na kila kitu kwangu, na wewe usiwe na rafiki yoyote wa kiume zaidi yangu yani mimi niwe kila kitu kwako”“Unamaanisha hata kuongea nao tusiongee nao!”“Unaweza kusalimiana nao tu ila ukiona wanaleta maongezi mengi unaachana nao na mimi iwe hivyohivyo, unajua na mimi naumia sana moyo nikimuona yule Bahati na unavyoongea nae vizuri kwakweli naumia sana. Sisi ni mapacha, yatupasa tupendane”“Kweli kabisa, kwahiyo tule kiapo?”“Ndio”“Sasa kiapo hiko tunakulaje?”Twende pale kwenye ukingo wa bahari nikuelekeze cha kufanya”Basi Erick na Erica wakaongozana hadi kwenye ukingo wa bahari na kwenda kuelekezana namna ya kula kiapo.Muda huu Tumaini alikuwa ametoka kwenye shughuli zake ila njiani alimuona Sian a kumfanya asimamishe gari ili aongee nae maana mama Erick alishampigia simu kwa kumwambia kuwa inatakiwa wamshawishi baba Angel kwenda kupima DNA na mtoto wa Sia.Basi alishuka kwenye gari na kusimama nae nje huku akiongea nae,“Eeeh Sia, nimesikia ishu za kwenda kupima DNA sijui Erick na mtoto wako, jamani Sia rafiki yangu mbona una makubwa wewe, unajua wazi mtoto sio wa Erick, kitu gani kinakusumbua lakini”“Tumaini, najua huelewi uchungu ambao upo katika moyo wangu ndiomana unasema hivyo”“Huo uchungu ni uchungu gani wa miaka hiyo hadi leo! Inamaana wewe huwezi kupata mwanaume zaidi ya Erick, kwani Sia una kasoro gani wewe hadi ukose mwanaume? Unachong’ang’ania kwa Erick ipo siku utakipata”“Ndio, nataka sana anioe”“Hilo swala la Erick kukuoa hebu lifute katika mawazo yako, halipo na kamwe halitakuwepo. Unajua na mimi nimeolewa kwahiyo naujua uchungu wa mume, usitake Erica aone ndoa yake chungu eti sababu yako Sia. Hebu acha wenzio wafurahie ndoa yako, sijui umeibuka wapi wewe”“Sijaibuka ila nampenda sana Erick”“Oooh tena kabla sijasahau, Erick alinipigia simu kasema…..”Kabla Tumaini hajamalizia mara kuna mkaka alitokea mbele yao na kumzaba kibao Sia halafu akamkunja pale na kumwambia,“Wewe mwanamke nataka mtoto wangu, nishapata habari zako unachokifanya kwa mwanangu namtaka”Tumaini alibaki ameduwaa kwani hakuelewa ni kitu gani kinaongelewa pale.Ila wakati wanatoka getini, walishangaa sana kumkuta bibi Angel nae akiwa anarudi kwa kasi kidogo ila huyu bibi alivyomuona Samir na Angel alichukia sana na moja kwa moja alienda kumnasa Samir kibao.Kwakweli kile kibao kilimuingia Samir, kiasi kwamba aliamua kukimbia tu kwani angeendelea kusimama mahali hapo basi angepigwa tena na huyu bibi na alimtambua vizuri mambo yake, hivyobasi alikimbia, basi bibi alimshika Angel mkono na kuingia nae ndani, kwakwlei kwa wakati huo Angel alijiandaa kupigwa tu kwani alijua wazi kuwa atapigwa sana na bibi yake huyu, ila walipoingia ndani bibi alimkalisha Angel chini na kumuuliza,“Una uhakika kuwa huyo Samir anakupenda?”Erica alinyamaza kimya tu huku akiangalia chini kwa aibu, kisha bibi yake akamwambia tena,“Mjukuu wangu, huyo Samir hakupendi wala nini hebu jiulize anayekupenda kweli anaweza kukimbia sababu ya kupigwa kibao kimoja? Mtu akikupenda huwa tayari kwa lolote lile, kuna kijana mmoja aliitwa Bahati basi alikuwa akimpenda dada mmoja hivi na kumfatilia sana, yani yule kijana alikuwa tayari hata kumwagiwa maji ya moto sababu ya mwanamke, yule kijana aliwahi kukaa rumande sababu ya mwanamke, hakuwa na kosa ila alikaa rumande sababu ya upendo wake tu kwa mwanamke”“Kheee bibi, sasa kwanini aliwekwa rumande?”“Ndugu wa mwanamke hawakumtaka, kwahiyo alivyokuwa hataki kuondoka hadi aonane na mwanamke ndipo walipomuweka rumande ila badae walimuhurumia sana na kumuachia huru. Kijana huyo alikuwa akihudumia familia ya mwanamke kama familia yake akiwaletea kuku na samaki, kijana huyo alikuwa tayari kulea mtoto wa mwanaume mwingine ambaye huyo dada alimzaa kabla, yani huyo kijana alikuwa na upendo wa dhati tena upendo mkubwa sana”“Bibi, vijana kama hao wapo?”“Wapo ndio, msubirie wa kwako ila sio huyu Samir anakuongopea tu, kibao kimoja kakimbia vile, hata hajali kuwa nitakupiga wewe au nini! Nakwambia ingekuwa huyo Bahati angetaka apigwe yeye badala yako, usimfikirire Samir mjukuu wangu hakupendi wala nini. Haya nipe na simu nikaiweke”Basi Angel aliitoa ile simu na kumpa bibi yake ili aiweke, kisha bibi aliinuka yani Angel kwakweli hakuamini kama kapona kipigo toka kwa bibi yake maana alihisi muda huo angepigwa vibaya sana ila hakupigwa wala nini zaidi ya kuambiwa kuwa Samir hafai kabisa kwake.Basi madam Oliva alifika na Erica saluni na kumuweka pale huku akiwaelekeza wasusi namna ya kumsuka nao walianza jambo lile, huku muda huo madam akiwaaga kuwa anaenda kwanza kuangalia chuo chake, kisha alimuuliza Erica,“Nikirudi nikuletee nini? Maana leo itabidi ule huku”“Chochote tu”“Sawa, nitakuletea chips kuku basi”“Sawa, asante”Erica alitabasamu halafu madam Oliva alitoka. Alipotoka tu wale wasusi waliokuwa wakimsuka Erica walianza maongezi, kwanza kabisa walimuuliza Erica,“Huyu madam ni ndugu yako?”“Hapana, ila ni mwalimu wa kaka yangu”“Ooooh sawa”Kisha mwenzie akasema,“Jamani, huyu madam leo alivyo na furaha utafikiri kitu gani. Halafu naona huyu mtoto kampenda sana”“Inaonekana, maana sio kawaida yake. Asubuhi kapita kuwa anamleta mtoto tumsuke, alivyokuwa anatuambia kuhusu huyo mtoto basi nikajua mtoto mdogo sana kumbe binti tu. Sijui muusuke taratibu, msimsumbue, msimvute nywele, mpeni anachotaka”Wakaanza kucheka huku mmoja akisema,“Kwani jamani yule madam ana mume yule?”“Mume hana, eti anasema yeye yupo kutafuta pesa tu hana shida na mume wala shida ya kuolewa”“Ila ana mpenzi au?”“Yani kwa kifupi yule madam hana mpango kabisa na wanaume, yani yeye anasema anawaza pesa tu ndio ya muhimu kwake.”“Na kama pesa ni anaitafuta kweli, maana yule kaajiriwa halafu ana biashara zake. Ana chuo chake cha kompyuta, ana hii saluni na ana shule yake ya kujifunza ushonaji”“Kweli yupo vizuri ila kuna umuhimu wa kuwa na mwanaume katika maisha, mtu anaishi vipi jamani bila mwanaume! Tamaa zake za kimwili anazimaliza vipi?”“Hapo sasa, au mwenzetu hana tamaa za kimwili jamani! Kuna mambo mengine ndiomana mtu unakuwa na hasira muda wote, kwanza toka nimfahamu huyu madam ndio leo namuona anacheka”Mwingine akadakia,“Usikute kashaonja tamu ya asali”Mmoja akawanyamazisha wenzie,“Badilisheni mazungumzo jamani, kumbukeni mnayemsema katuajiri na anafanya turinge mjini”“Kheee bwana eeeh anasemwa raisi sembuse yeye!!”Basi wakacheka na kuendelea na maongezi mengine.Baba Angel akiwa ofisini kwake kwa muda huo, akaja mama yake kama ambavyo aliongea nae kwenye simu jana yake basi alimkaribisha na kumsalimia pale kisha kuanza maongezi nae ambapo mama yake alianza kuongea,“Mwanangu sikia, naomba niache niongee kwanza halafu zamu yako ikifika ndio utasema yani usinikatishe wakati naongea”“Sawa mama”“Ni hivi, Sia alinipigia simu kuwa mtoto anaumwa, kwakweli na mimi ni mama halafu na mimi nimepitia mazingira ya kulea mtoto bila ya baba kwahiyo najua uchungu wake na ninajua ni hali gani inakuwa. Nimekulea wewe, nimehangaika na wewe kipindi hiko baba yako hana hata habari hata wewe mwenyewe unakumbuka wazi kuwa baba yako umefahamiana nae ukiwa mkubwa kabisa unajitambua tena ukiwa unatangatanga huko baada ya kufukuzwa shule. Kiukweli nilipatwa na uchungu kusikia mtoto mdogo anaumwa na mama yake hana pesa, ilibidi niende. Nilipofika pale nilimkuta mtoto kalala, yani nilienda kwa kuelekezwa na Sia mwenyewe, na nilivyofika alimuamsha mtoto aje anisalimie maana kuna zahanati alimpeleka na alipatiwa dawa ila aliacha deni tu pale zahanati, ilibidi nitoe pesa aende kulipa hilo deni maana afya ya mtoto ni ya muhimu zaidi ya vyote. Kingine ni kuhusu yule mtoto mdogo Elly, kwakweli kwa jinsi nilivyokuwa namuangalia ananikumbusha zamani kabisa kipindi cha udogo wako, wewe ulikuwa ni mtoto mpole na mchangamfu basi ndio alivyo yule Elly, mwanangu mimi naomba jambo moja tu hata kama Sia humpendi basi mpende yule mtoto, nakuomba ukubali kupima DNA na Elly”“Umemaliza mama?”“Ndio, nimemaliza nakusikiliza wewe sasa”“Kwanza kabisa siwezi kwenda kupima DNA na Elly, nikifanya hivyo inamaana sijiamini. Pili ngoja nikuulize mama, inamaana Ellyn i mwanangu halafu Erick sio mwanangu?”“Mmmh mimi sijasema Erick sio mwanao, kwanza itakuwaje Erick asiwe mwanao jamani! Erick si kazaliwa na mkeo, sasa itakuwaje sio mwanao? Ninachohitaji mimi ni Elly kupata haki sawa na wenzie wote, una watoto pale kuna Angel, Erick, Erica, Ester na sasa Elly awepo kwenye familia”“Kwa misingi ipi mama?”“Ellyn i mtoto wako ambaye umezaa na Sia”“Mama, mimi ndio mwanaume ambaye Sia anadai amezaa nae, ila mimi nakataa mbele ya vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana kuwa sijazaa na Sia mimi.”“Ila mwanangu unakumbuka tabia zako vizuri wewe, ni wadada wangapi waliokuwa wakilalamika kwangu kuwa wana mimba zako sembuse Sia ambae muda wote alikuwa na wewe! Je kama akitokea mdada mwingine na mtoto utakataa kuwa sio mwanao wakati ulikuwa muhuni sana wewe!”“Ni kweli mama, yani siwezi kukataa kuwa sikuwa muhuni, kama uhuni nimeufanya sana tu, ila niliufanya sababu ya stress nilikuwa siwezi kumpata mwanamke nimpendaye ndiomana nilikuwa nafanya ule uhuni, kuna wanawake wakija kusema Erick tulizaa na wewe naweza nikakubali ila sio Sia, unajua nini Sian i mwanamke ambaye alikuwa akiniganda sana. Na toka nimetoka Afrika kusini na kuanza kuishi na Erica kw aupendo ile ikawa mwisho wa mimi na Sia yani sikuwa na ukaribu nae tena, alikuwa akifanya kila mbinu lakini ilishindikana kuwa na mimi, halafu leo useme Sia kazaa na mimi tena mtoto ambaye ni umri sawa na watoto niliozaa na Erica, hapana kwakweli Sian i muongo tena muongo namba moja. Kuna mwanamke mmoja angesema hivyo ningesema labda maana kipindi kile Erica alinikatalia kabisa hadi ndoa na mimi ni mwanaume ila yule mwanamke alikuwa akijua kila kitu kuhusu mimi na Erica hadi siku namuacha nikamwambia mimi na wewe basi maana nimerudi kwa Erica wangu, yule mwanamke alikubali kwa roho moja na hajawahi kunitafuta tena hadi leo kwani anajua kuwa nina familia yangu ila kwanini Sia anakuwa hivi jamani! Kwani wanaume wameisha duniani au kitu gani?”Mama yake akapumua kidogo na kusema,“Haya, mfano huyo mwanamke aseme pia ana mtoto wako utasemaje?”“Haiwezekani sababu yule mwanamke nilikuwa nae na aliweka kijiti cha miaka mitatu, na wakati niko nae ilikuwa ni mwaka wa pili, mama katika maisha yangu kitu mimba nilikuwa nakihofia sana na kukuheshimu kwani nilitambua wazi kuwa Erica akiona nina watoto wengi basi hatonikubali, kwahiyo nilikuwa makini sana”“Sawa mwanangu ila mimi hoja yangu bado ni moja tu, ukapime DNA na Elly”“Mama, tafadhari hilo swala kwangu halikubaliki. Yani hiyo kitu haipo, labda ukapime wewe na ukikuta mnafanana basi jua kuwa ni mwanao na sio mwanangu sababu mimi sijazaa na Sia”“Sasa hayo matusi mwanangu, yani unanitusi mama yako. Inamaana mimi nimezaa na Sia? Yani wewe mtoto loh! Mitoto mingine tunabebaga change tu tumboni”Kisha mama yake akanyanyuka na kuondoka zake, inaonyesha alikuwa amekasirika ila baba Angel wala hakujali zaidi zaidi aliendelea na kazi zake tu.Madam Oliva alimpelekea Erica kama alivyoahidi na Erica alikula pale, kisha walipomaliza kumsuka alimwambia kuwa anampeleka ofisini kwa baba yake ili aondoke na baba yake maana yeye alidai kuwa kuna kazi anataka kuifanya.Basi aliondoka na Erica pale huku akimsifia kuwa kapendeza sana hadi kabadilika, basi Erica alikuwa akifurahi sana kuambiwa vile, yule madam nae alikuwa akifurahi kuona Erica anafurahi ndipo Erica alipomwambia,“Madam, wale wafanyakazi wako mule wanafki”“Wamefanyaje tena?”Erica alianza kumueleza moja baada ya jingine ambalo wafanyakazi wale walikuwa wakisema na kuelekeza kabisa yupi kasema lipi na yupi kaongea lingine, kiukweli yule madam alichukia sana,“Yani badala ya kufanya kazi wanafanya kazi ya kunisema!”“Tena mwenzao alipowakatisha wakasema anasemwa raisi sembuse wewe!”Yani madam Oliva alizidi kuchukia kwakweli na kuona kuwa wafanyakazi wake wabaya, basi alienda na Erica hadi ofisini kwa baba yake ambaye kwa muda huo alikuwa amekaa tu maana hata yeye kichwa chake kilikuwa kimevurugwa ila alipomuona binti yake alimsifia sana kuwa kapendeza kisha akamshukuru madam Oliva na kumuuliza pale,“Eeeeh ndio pesa ngapi hapo?”“Aaaah hii leo nimempa ofa”“Kumbe ofa!! Jamani madam kwanini lakini!”“Hamna jamani, hii ni ahadi yangu kwake, na sio kwa leo tu kwani siku zote akiitaji kusuka basi nitampeleka saluni kwangu na atasuka bure kabisa”Basi baba Angel alicheka tu, kwavile hata yeye alichoka aliamua kuondoka kwahiyo aliagana na madam Oliva halafu yeye kuelekea kwake huku madam akirudi kwenye saluni yake.Basi Erica kama kawaida alianza kumsimulia na baba yake maneno ambayo wale wadada wa saluni walivyokuwa wakiongea na jinsi na yeye alivyomueleza madam Oliva,“Aaah mwanangu, unajua utakuwa umewafanya hao wadada wafukuzwe kazi!!”“Ila baba, mimi sijasema kwa ubaya, nimesema tu ili madam Oliva ajue kuwa wafanyakazi wake ni watu wa aina gani!”“Mmmh ila Erica mambo yako jamani!”Baba Angel alicheka na kutikisa kichw atu huku wakielekea nyumbani.Walipofika nyumbani, kila mtu alikuwa akimsifia Erica kuwa kapendeza sana na kumfanya hata yeye afurahie sana zile sifa alizokuwa anapewa.Basi waliongea ongea kidogo pale halafu Erica alienda chumbani kwake halafu mama yake alimfata na kumuuliza,“Eeeh Erica, nipe habari za huko”Erica kama kawaida alimuelezea kila kitu yani hakuacha hata kimoja, kisha akamwambia,“Wale wasusi wanasema madam yupo kutafuta hela ila kapewa hela na baba kaikataa”“Hela ya nini?”“Si ya kunisuka mimi, eti kasema ni ofa”“Kheee kumbe!!”“Ndio mama, kwahiyo nimesukwa bure”“Haya sawa mwanangu, mimi nashukuru kwa ujumbe”Mama Angel alijua kuwa mwanae lazima atamwambia kila kitu, sababu ya kumuuliza ni kujiridhisha kuwa madam Oliva sio mtu mbaya katika maisha yao, na kwa yale maongezi ya mwanae hakuona ubaya wa madam huyo sababu ameambiwa kuwa huyo madam yupo kwaajili ya kutafuta pesa tu.Basi usiku wa siku hii, baba Angel aliongea na watoto wake maana Erica alienda kuomba kuwa hiyo safari ya ufukweni iwe kesho, na kwavile alijihisi uchovu sana akaona hakuna tatizo kwahiyo aliwaambia tu kuwa kesho yake wataenda huko ufukweni kutembea, ila ilikuwa nu furaha kubwa. Basi siku hiyo walilala huku wakiwaza uhuru ambao kesho yake watakuwa nao.Basi kulipokucha, baada ya kazi za hapa na pale ndio walienda kujiandaa sasa na walipokuwa tayari ndio walienda kuchukua ruhusa mapema naye aliwaruhusu na kuwapa pesa kwaajili ya matumizi ya huko watakapokuwa kutembea ila baba yao aliwaambia,“Ila kule ni kuzuri sana mwisho wa wiki, sema leo siku ya kawaida mtakuta kumepooza sana”“Aaaah baba, sisi hatuna tatizo ni bora tukashuhudie maji tu”Basi akawaruhusu na wao wakaondoka kisha pale nyumbani alibaki na mkewe tu huku wakiongea na kupanga mambo mbalimbali.Muda huu mama Angel ndio alikuwa na simu ya mume wake, basi ujumbe mara ukaingia kwenye simu ya mume wake,“Baba Elly, mbona unafanya hivyo?”Moja kwa moja mama Angel alitambua kuwa aliyetuma ujumbe ule alikuwa ni Sia, basi alimuangalia mumewe na kumuuliza,“Eeeeh mume wangu huyu Sia ana ajenda gani za kukuita baba Elly?”Akampa simu mumewe ambapo naye aliangalia ule ujumbe na kumwambia mke wake,“Aaaah si mjinga huyu, hutambui hilo mke wangu. Naomba usifatilie mambo ya huyu”“Ila amekazana sana mume wangu?”“Achana nae, yani yeye ilimradi kapata namba zetu basi anaona cha kufanya ni kutusumbua tu, usimjali kwa lolote huyu mtu mke wangu”“Na akija tena hapa nyumbani!”“Hawezi, nishamwambia mlinzi kuwa sitaki kuiona ile takataka hapa nyumbani kwangu, hebu tufanye vitu vya muhimu mke wangu. Eeeh watoto wote wameondoka, leo tutakula nini?”“Mmmh hata sijui halafu naona uvivu kupika leo hatari”“Hakuna tatizo mke wangu, basi leo nitakupikia naamini utapenda chakula changu”Mama Angel alicheka na kumkumbusha kitu mume wake,“Ndio unipikie kama ugali aliopika dada yako nyumbani kwetu, na maharage yenye macho”Baba Angel alicheka sana, yani alicheka muda huo na kusema,“Yani Tumaini kashasahau ujue kama alikuwa hajui kupika, saivi anajiona ndio mwenyewe wakati aliumbuka ukweni. Ila kwenu sio watu wazuri, yani kumfanyia vile dada yangu dah! Haya sasa nikupikie nini mke wangu?”“Chohote utakachokipenda wewe basi nami nitakipenda tena leo nimepikiwa na mume wangu basi nitakulaje!”Wakacheka pale na kuendelea na mambo mengine.Wakina Erick walifika ufukweni walikokuwa wakienda, basi baada ya kufika pale Junior akawaambia,“Jamani, mimi nitatembea na Vaileth huku nikimuonyesha mandhari ya ufukwe halafu nyie kaka na dada ongozaneni huko kwingine sio tuanze kufatana fatana”Erick na Erica wakaguna ila wakakubaliana nae tu na moja kwa moja Junior aliongozana na Vaileth ila kwakweli Vaileth hakutaka kuongozana na Junior sema tu hakutaka Erick na Erica watambue chochote kile.Vaileth na Junior waliongozana huku Junior akijifanya kumuonyesha Vaileth baadhi ya vitu vya ufukweni, kisha alimuomba wakae mahali kwenye mchanga ili amuonyeshe vizuri, na walipokaa tu alianza maongezi nae,“Kwanza kabisa Vaileth, ni kwanini umenichukia?”“Hivi unadhani kuna mtu anaeweza kufurahia ujinga Junior, sikia umenidanganya mimi kuwa unanipenda kumbe una wanawake zako kibao. Najua unanifanyia yote haya sababu unaniona mimi mjinga kwakuwa ni mtu mzima halafu nimekupenda wewe kijana mdogo”“Ngoja nikukatishe kuhusu umri wako, kwanza kabisa tambua kuwa umri ni namba tu, mapenzi hayaangalii umri wala nini. Halafu unaweza kuona mimi ni mdogo ila nikawa natambua mambo mengi sana katika mapenzi kutokana na niliyopita. Siwezi kukataa hili, ni kweli mimi nilikuwa muhuni sana na nilikuwa na wanawake wengi, ila nilipokupata wewe nikasema kwanini nihangaike na wanawake wengine wakati wewe nakupenda! Sasa yule msichana niliachana nae kitambo sana na alisema kuwa ana mimba yangu na anahitaji kuitoa, basi nilimpatia pesa za kuitoa na hapo nikamwambia kuwa mimi na yeye ndio basi. Sasa hata namshangaa kunitafuta tena sijui damu zinamtoka, kwanza kabisa mimba alikuwa nayo yeye na sio mie, halafu ni yeye ndio aliyeenda kutoa, sasa anamlalamikia nani kuwa damu zinamtoka? Achana na yule msichana, kwanza nilimwambia kuwa mimi nina mke aniheshimu ila hataki ndiomana kafanya huo ujinga, jamani Vai nakupenda sana”“Mmmh kwa mtindo huu ndio tutakuwa kama mama na baba kweli kule nyumbani! Wale wanapendana kwa dhati na wala baba hana uhuni kabisa”“Sikia nikwambie, mama yangu nilimsikia akiongea na baba na walikuwa wakiongea kuhusu bamdogo huyo, nasikia alikuwa ni malaya tena malaya koko, hata mbwa mwenyewe akasome”“Jamani Junior, punguza ukali wa maneno”“Aaah basi, ila usione watu wametulia kwenye ndoa zao ukadhani wameibuka tu, penzi la kweli linatengenezwa na maelewano mema na masikizano, sasa unanifungia mlango kabisa hutaki hata kusikia upande wangu naongea kuhusu nini au nitajitetea vipi ila unabaki kuumia moyo na kunilaumu. Jamani Vaileth mimi nakupenda sana”“Mmmh lakini swala la kusema baba alikuwa muhuni nakukatalia”“Haya, endelea kukataa tu ila wanaomfahamu wenyewe wanasema, kuwa alikuwa ni kiwembe balaa kinakata kulia na kushoto, unaambiwa akiwa anatembea na wewe mdada na ukamtambulisha rafiki zako basi jua wote hao atawapitia”“Duh!!”“Mbona mimi mstaarabu sana, ila maisha huwa yanabadilisha mtu. Muangalie sasa, katulia na ndoa yake, hanywi pombe na unaambiwa alikuwa analewa yule hadi anazima”“Junior! Nani kakwambia maneno hayo?”“Yani licha ya kumsikia mama ila kuna mama mmoja hivi, sijui alikuwaga mwanamke wa zamani wa bamdogo basi huwa nikikutana nae ananiambia mambo mengi sana ya bamdogo kipindi hiko”“Kwahiyo na yeye alimvumilia tu! Yani mwanaume analewa hadi anazima, anatembea na rafiki zako wote, bado alimvumilia tu”“Si alimpenda, tena sio marafiki tu hata ndugu zako ikiwezekana anatembea nao. Unajua ukiona mwanaume wa hivyo tambua kabisa hakupendi kwani mwanaume anayekupenda atawaheshimu ndugu zako, atawaheshimu rafiki zako na atakuheshimu na wewe pia. Yule mmama nilimwambia kuwa basi hakukupenda, ila yule mama anavyoongea kwa uchungu hata nina mashaka nae”“Ni mama gani huyo?”“Siku moja nitakuonyesha, nikimuona tu nje ya geti basi nitakuita ili tuongee nae, kiukweli utabaki unamuangalia tu. Ila sijui alinihadithia mimi tu au huwa anawahadithia wengi sijui. Kiukweli siwezi kumueleza bamdogo yale maneno najua atachukia sana”“Ila kwakweli imenishangaza sana, kwahiyo wewe unanipenda kweli?”“Vaileth jamani, mimi ninakupenda sana tu, kiasi kwamba hata siwezi kumtamani mwanamke mwingine zaidi yako. Naomba unisamehe na tuanze kurasa mpya ya mapenzi yetu”Vaileth alitabasamu tu na kumfanya Junior atambue kuwa pale ameshasamehewa kwahiyo ilikuwa ni furaha sana kwake kwani alitamani mno kusamehewa na Vaileth.Erick na Erica nao walikuwa wakitembea tembea pembezoni mwa maji huku wakichezea maji na kukimbizana, basi Erica akasema,“Jamani, mimi huwa nikimuona Sarah yupo karibu na wewe basi roho huwa inaniuma sana”“Kwanini?”“Hata sijui kwakweli”“Sikia basi tufanye kitu kimoja”“Kitu gani?”“Mimi na wewe tupeane ahadi ya jambo moja ambalo wewe hutolifanya katika maisha yako na mimi sitolifanya katika maisha yangu”“Jambo gani”“Iwe hivi, yani mimi nisiwe na rafiki yoyote wa kike zaidi yako yani wewe uwe ndio rafiki yangu na kila kitu kwangu, na wewe usiwe na rafiki yoyote wa kiume zaidi yangu yani mimi niwe kila kitu kwako”“Unamaanisha hata kuongea nao tusiongee nao!”“Unaweza kusalimiana nao tu ila ukiona wanaleta maongezi mengi unaachana nao na mimi iwe hivyohivyo, unajua na mimi naumia sana moyo nikimuona yule Bahati na unavyoongea nae vizuri kwakweli naumia sana. Sisi ni mapacha, yatupasa tupendane”“Kweli kabisa, kwahiyo tule kiapo?”“Ndio”“Sasa kiapo hiko tunakulaje?”Twende pale kwenye ukingo wa bahari nikuelekeze cha kufanya”Basi Erick na Erica wakaongozana hadi kwenye ukingo wa bahari na kwenda kuelekezana namna ya kula kiapo.Muda huu Tumaini alikuwa ametoka kwenye shughuli zake ila njiani alimuona Sian a kumfanya asimamishe gari ili aongee nae maana mama Erick alishampigia simu kwa kumwambia kuwa inatakiwa wamshawishi baba Angel kwenda kupima DNA na mtoto wa Sia.Basi alishuka kwenye gari na kusimama nae nje huku akiongea nae,“Eeeh Sia, nimesikia ishu za kwenda kupima DNA sijui Erick na mtoto wako, jamani Sia rafiki yangu mbona una makubwa wewe, unajua wazi mtoto sio wa Erick, kitu gani kinakusumbua lakini”“Tumaini, najua huelewi uchungu ambao upo katika moyo wangu ndiomana unasema hivyo”“Huo uchungu ni uchungu gani wa miaka hiyo hadi leo! Inamaana wewe huwezi kupata mwanaume zaidi ya Erick, kwani Sia una kasoro gani wewe hadi ukose mwanaume? Unachong’ang’ania kwa Erick ipo siku utakipata”“Ndio, nataka sana anioe”“Hilo swala la Erick kukuoa hebu lifute katika mawazo yako, halipo na kamwe halitakuwepo. Unajua na mimi nimeolewa kwahiyo naujua uchungu wa mume, usitake Erica aone ndoa yake chungu eti sababu yako Sia. Hebu acha wenzio wafurahie ndoa yako, sijui umeibuka wapi wewe”“Sijaibuka ila nampenda sana Erick”“Oooh tena kabla sijasahau, Erick alinipigia simu kasema…..”Kabla Tumaini hajamalizia mara kuna mkaka alitokea mbele yao na kumzaba kibao Sia halafu akamkunja pale na kumwambia,“Wewe mwanamke nataka mtoto wangu, nishapata habari zako unachokifanya kwa mwanangu namtaka”Tumaini alibaki ameduwaa kwani hakuelewa ni kitu gani kinaongelewa pale. Kabla Tumaini hajamalizia mara kuna mkaka alitokea mbele yao na kumzaba kibao Sia halafu akamkunja pale na kumwambia,“Wewe mwanamke nataka mtoto wangu, nishapata habari zako unachokifanya kwa mwanangu namtaka”Tumaini alibaki ameduwaa kwani hakuelewa ni kitu gani kinaongelewa pale.Yule mwanaume aliendelea kumkunja Sia na kumfanya Sia aanze kumlalamikia,“Hebu niachilie jamani, yani huwezi kuongea kistaarabu!!”“Kistaarabu gani na mwanangu napata habari kuwa umemfanya ombaomba huko”“Jamani nimemfanya ombaomba wapi una uhakika? Mbona unaongea maneno ambayo huna ushahidi nayo?”Muda huu Tumaini alisema,“Mtajuana wenyewe”Kisha akaingia kwenye gari lake na kuondoka zake.Kwahiyo Sia alibaki na yule mwanaume akibishana nae,“Kwanza hebu niachilie halafu ndio tuongee”Yule mwanaume alimuachilia Sia ili kumsikiliza anasemaje ila muda ule ule Sia alimkimbia yule mwanaume na mbele kupanda pikipiki yani yule mwanaume hakuweza kumpata tena Sia, kitendo hiko Tumaini alikiona wakati akigeuza gari yake na kumfanya ajiulize sana kuwa kuna nini kati ya Sia na yule mwanaume? Ila kwa mawazo yake akahisi kuwa huenda Sia amezaa na yule mwanaume, tena akahisi kuwa huenda Elly ndio mtoto ambaye yule mwanaume anamdai maana mtoto huyo inaonekana Sia kamfanya kitega uchumi, ukizingatia mama Angel alimuelezea kuhusu lile swala la Sia kumtuma mtoto nyumbani kwake kuwa anaumwa, basi moja kwa moja alihisi kuwa yule mwanaume alikuwa akidai mtoto Elly tu kwa Sia.Muda huu Erica na Erick walivyokubaliana na kumaliza kula kiapo, ila waliona kuwa muda umeendaenda kwahiyo waliona ni vyema wakaungane na wakina Junior ili kuangalia kama watarudi nyumbani muda huo.Basi waliwafata wakina Junior pale ambao walionekana wamepatana huku wakifurahi sana, basi waliwashtua na kukaa nao karibu ambapo Junior aliwauliza,“Kheee kwahiyo ndio mshamaliza kutembea tembea!”Erica akamjibu,“Kheee jamani, unataka tutembee tembee hadi muda gani? Sisi tushamaliza kilichotuleta huku”“Kitu gani hicho?”“Leo tumeamua kula kiapo”Junior akashangaa,“Kiapo, kiapo gani”Basi Erick alikuwa akimtonya Erica asielezee ila Erica hakuona kama kuna tatizo au ubaya wowote na kuanza kuelezea,“Mimi na Erick tumeamua jambo moja, yani yeye hatokuwa na rafiki mwingine wa kike zaidi yangu, siri zake na kila kitu chake atakuwa ananiambia mimi. Na mimi sitokuwa na rafiki yoyote wa kiume zaidi yake, siri zangu na kila kitu change basi namshirikisha Erick”Junior na Vaileth waliangaliana kwa mshangao, kisha Junior akasema,“Hivi hamjui kama ni ndugu nyie!”“Kwani ndugu hawapaswi kula kiapo?”“Sijasema hivyo ila nimesema kutokana na aina ya kiapo chenu, nyie ni mapacha hilo sikatai wala sipingi ila sio kwamba ndio mtakuwa kila kitu mnafanya pamoja. Hapo badae Erica utaolewa na Erick ataoa, sasa mtawezaje kuoa na kuolewa bila kuwa na urafiki na wenzi wenu sababu tu mmesema mtakuwa marafiki wenyewe! Hivi mmefikiria hili kwanza kabla ya kula hiko kiapo chenu!”Erick akajibu,“Katika maisha yangu sitegemei kuja kuoa”“Kheee usinishangaze Erick, kwahiyo wewe ni Padri?”“Na mimi sitegemei kuolewa”“Kheee nyie watoto mnanivuruga mjue, kwahiyo Erica ni Sister halafu Erick ni Padri, nyie wawapi jamani! Mbona mnanishangaza sana”“Sasa tunachokushangaza ni kitu gani? Kula kiapo au kitu gani?”“Ila sio kosa lenu ni utoto tu unawasumbua, najua mkikua na kufikia kwenye rika kama langu basi mtaona umuhimu wa marafiki mbalimbali. Siwashangai sana maana ni utoto tu huo unawasumbua, haya twendeni tukale pale kwenye hoteli halafu ndio turudi nyumbani yani tunafika tukiwa tumeshiba kabisa sio kuanza kutafuta chakula nyumbani tena”Kisha waliinuka wote na kuelekea kwenye hoteli ya karibu na pale ufukweni ili kupata chakula.Muda huu baba Angel akiwa yupo kuzunguka zunguka kwenye nyumba yake ili kuangalia maeneo ya bustani yake vizuri, akapigiwa simu na dada yake na kuanza kuongea nae,“Jamani Erick, leo njiani si nikakutana na Sia halafu akaanza zile mada zake za mtoto ila Mungu si Athumani jamani akatokea mbaba yule sijui wa wapi, akamzaba vibao Sian a kumkunja huku akimdai mtoto wake, yani mwanamke mbaya yule jamani! Kutaka kutudanganya tunaona hivi ndio nini!”“Kwahiyo na wewe ulikuwa unaamini kuwa mtoto ni wangu?”“Hapana, mimi nilikuwa siamini na ndio nilikuwa naongea nae anakazana tukapime DNA ndio mara katokea huyo mbaba, jamani Sia yule asipoangalia anafia kwenye mikono ya watu halafu sijui alimponyokaje yule baba maana tu nilimuona akipepea na bodaboda, jamani Sia kawa mbaya sana”“Ila ni vizuri umetambua hilo dada yangu maana nilikuwa naumia sana kuona mnamuamini yule mjinga”Tumaini aliongea na ndugu yake kwa furaha sana, na ile simu ilipokatika basi baba Angel alienda kumpelekea mama Angel ujumbe ule na kumfanya mkewe ajihisi vizuri sana kwani siku zote alihisi kuumizwa kichwa sana na Sia, kwahiyo kupata habari kama hiyo kwake ilikuwa nafuu sana.“Mke wangu, kesho nitaenda kazini ila nitawahi kutoka na kwenda kumuona Angel kwa mama”“Oooh utakuwa umefanya jambo jema sana mume wangu, nashukuru kwa hilo”Basi waliongea pale huku wakipanga ratiba vizuri tu.Muda huu ndio wakina Junior walikuwa wanarudi nyumbani, na kweli walishashiba kwahiyo walifika tu na kuwashuku wazazi wao kwa kuwaruhusi siku hiyo kwenda kutembea na moja kwa moja walienda kulala kwani kila mmoja alikuwa amechoka sana ila kama kawaida leo Junior aliweza kwenda chumbani kwa Vaileth tena maana walikuwa wamepatana, basi akamwambia,“Nakuomba kitu kimoja mke wangu, tuaminiane yani mimi na wewe tuwe letu moja”“Ila kuna jambo mimi nataka”“Jambo gani?”“Erica na Erick ni mapacha ila wamekula kiapo cha kuwa marafiki wao wawili tu daima na milele, tumewaponda ila kiukweli nimependa maamuzi yao. Basi nilikuwa naomba mimi na wewe tule kiapo pia cha kuwa pamoja milele na kutokusalitiana yani usinisaliti na nisikusaliti”“Hakuna tatizo mke wangu, tutakula tu hiko kiapo”“Ndio tule muda huu, ni kiapo cha damu”“Mmmh jamani Vai, mambo gani hayo yakutoana damu tena! Unajua mimi ni muoga sana, tutakula kiapo kama cha wakina Erick”“Sasa mpaka twende ufukweni ni lini tena! Wakati kiapo cha damu ni rahisi tu hapa”“Mke wangu napenda sana tule hiko kiapo ila mimi ni muoga sana kutobolewa na kitu yani nikiona damu inatoka basi Napata hofu maradufu, nakuomba mke wangu niamini halafu mimi na wewe tutakula tu kiapo. Amini nakupenda sana Vaileth, leo tumechoka sana mama njoo tulale, maswala ya viapo tutakula tu hakuna tatizo”Basi Junior akafanya kumpapasa pale Vaileth ili asahau ile ajenda yake na kweli mwisho wa siku waliamua kulala tu.Kwenye mida ya saa nne asubuhi, Angel akiwa na bibi yake basi bibi yake kulikuwa na watu anahitaji kuwasalimia ila simu yake haikuwa na salio hivyo ilimbidi amuagize Angel kununua vocha, kwakweli Angel alifurahi kwa kiasi Fulani aliyapenda maisha ya kwa bibi yake ingawa kuna muda huwa anakosa raha sana ila aliyapenda maisha yale sababu hata alikuwa anapata uhuru wa mwenda dukani, kwaniyo kwake ilikuwa ni furaha.Aliondoka muda huu na kuelekea dukani alikotumwa na bibi yake, moja kwa moja alienda kununua vocha ila alipotoka tu kununua vocha alishikwa bega akashtuka kugeuka akamuona yule Ally ambaye ni dereva bodaboda, kwakweli alimshangaa sana na kusogea pembeni huku akisalimiana nae,“Kheee Ally, umefikaje huku?”“Hata mimi sijui nimefikaje huku ila nadhani ni kusudi la Mungu ili mimi na wewe tupate kuonana”“Kheee!”“Kweli Angel, nilikuwa naumia sana kwa kutokukuona maana furaha yangu ni kukuona tu kwahiyo swala la kutokukuona lilikuwa linaniumiza sana”“Oooh pole, mimi nawahi nyumbani nampelekea bibi vocha”Basi Angel akawa anaondoka huku Ally akimfata nyuma na kumuongelesha,“Kwahiyo unaishi huku siku hizi!”“Ndio, naishi na bibi yangu”“Natumai bibi yako hatachukia nikimfahamu”“Mmmh sio leo, hapana jamani usiniletee matatizo bure”“Kwanini?”“Kwanza bibi yangu hapendi kabisa niwe na marafiki wanaume, kwahiyo nisamehe tafadhali”Angel alifika kwa bibi yake na kuingia na moja kwa moja kumpelekea bibi yake vocha ambaye alimuuliza kidogo,“Mbona umechelewa Angel, ulisimama na wanaume eeeh!”“Hapana bibi”“Maana mkishaona mna rangi rangi na vinywele vya kuongopea wenzenu basi ndio mnajifanya mnamiliki dunia sababu ya kujiona nyie ndio wazuri dunia nzima. Angel mjukuu wangu, sifa ni ile tutakayokupa sisi tu na si mtu wa njiani, atakwambia mzuri kumbe anakusabifu, sisi tukikusifia inatosha mjukuu wangu. Haya niwekee hiyo vocha na uniungie kifurushi”Basi Angel alifanya hivyo ila alipomaliza alituma ujumbe kwa Samir,“Nimekumiss sana Samir, ila bibi bado hajanipa simu yangu. Akinipa nitakushtua ili tuwasiliane, usinijibu hapa maana hii simu ya bibi”Akamtumia na kuifuta ile meseji kisha kumpa simu bibi yake ambapo alianza kuitumia kwa kuwapigia aliotaka kuwapigia.Baba Angel leo akiwa ofisini tu, muda kidogo akafatwa na madam Oliva ambaye alikuwa akilalamika kwanza,“Jamani baba Erick, kumbe jana ulipanga kutokuja ofisini! Basi mwenzio nikaja nikakukosa, niliumia moyo ujue!”“Oooh pole sana, ulikuwa na ujumbe gani madam?”“Nina ujumbe basi!! Nilikuwa nataka kukusalimia tu, yani mimi huwa napenda sana kuongea na wewe maana wewe ni mwanaume ambaye una maneno yenye busara sana, halafu huwa unanipa moyo sana yani nikiongea na wewe basi najihisi vizuri kwenye moyo wangu”“Nafurahi kusikia hivyo, karibu sana”“Asante, leo una ratiba gani? Maana nilitaka twende kwangu ukapafahamu”“Madam tutaenda siku nyingine, maana leo nahitaji kwenda kumuona mwanangu kwa bibi yake”“Sawa hakuna tatizo, mwanao huyo ni wa kike au wa kiume?”“Ni wa kike, anaitwa Angel”“Oooh nimefurahi kufahamu hilo swala, basi ni hivi ngoja nitoke kidogo halafu nitarudi muda sio mrefu naomba usiondoke kabla sijarudi”Basi madam Oliva aliondoka, kiukweli baba Angel hata hakujua ni kitu gani huyu madam anahitaji kufanya, kwahiyo yeye aliendelea na kazi zake tu kama kawaida.Muda kidogo madam Oliva alirudi akiwa na kimfuko na kumkabidhi baba Angel, kisha akamwambia,“Humo kuna zawadi ya Angel, naomba usifungue yani mpelekee Angel mwenyewe kisha umwambie kuwa umepewa na madam Oliva”“Asante sana kwa kumkumbuka mwanangu”“Yani mimi kwa jinsi ninavyokuona hadi naona watoto wako wote kama watoto wangu jamani. Ila hakuna tatizo, sema tu kumbuka hilo kuwa mfikishie zawadi yangu hiyo Angel”“Nitaifikisha madam, hakuna tatizo lolote”“Haya, mwambie Angel kuna siku ataniona naamini atanipenda sana”Madam alikuwa akiongea haya huku akitabasamu kwani alijihisi raha sana kwenye moyo wake na alitamani watoto wote wa baba Angel wampende yeye ili kama atazungumza nao chochote kile wapate kumsikiliza na kumuelewa.Basi baba Angel nae aliinuka pale kwani aliona kuwa muda wake umefika wa kwenda kumtembelea mama mkwe wake kama alivyopanga, kwahiyo waliachana na madam Oliva nje ya ofisi halafu moja kwa moja baba Angel alipanda kwenye gari na kuondoka zake.Fetty leo ndio aliweza kumshawishi mumewe ili waende kwa mama Erica yani bibi Angel maana alishamshauri muda kufanya hivyo ili wakapate ushauri wa ziada.Basi walijiandaa na kutoka ambapo moja kwa moja walienda mpaka kwa bibi Angel na kufika mpaka mlango wa mbele ya nyumba hiyo na kubisha hodi huku mume wa Fetty akisema,“Ila pamebadilika sana siku hizi”“Lazima pabadilike ni muda mrefu umepita”Basi walifunguliwa mlango na Angel na kukaribishwa ndani, walimkuta bibi Angel amekaa na mgeni ambaye alikuwa ni baba Angel ila kiukweli mume wa Fetty alipomuona huyu mtu yani baba Angel alijihisi vibaya sana moyoni, basi waliingia na kuwasalimia na kuongea mawili matatu baada ya muda mume wa Fetty alitoka nje na aliporudi ndani alisema kuwa kuna mahali kaitwa kwahiyo ilibidi tu awaage, kwahiyo hata mkewe hakuwa na namna zaidi zaidi ya kuongozana nae tu.Bibi Angel aliwaambia pale,“Jamani, Fetty ungebaki jamani, si ni yeye ndio anawahi!”“Aaaah mama usijali, tutakuja siku nyingine yani lazima tuje, usijali mama”Basi wakaagana nao pale na moja kwa moja walitoka na kwenda kupanda gari yao na kuondoka ila njiani mume wa Fetty alinza kusema,“Na bahati yako hujakubali kubaki maana ungekubali ndio ungenieleza ajenda yako vizuri”“Ajenda kivipi?”“Unafikiri yule Erick namuamini basi! Sina imani nae”“Huna imani nae wapi? Si useme tu ukweli kuwa bado unampenda Erica, hivi lini Bahati akili yako itakuwa kawaida jamani! Unajua siku ya harusi ya Erick na Erica ulitoa risala ambayo binafsi nilifurahishwa nayo na kuona ni kweli mume wangu kawa muelewa sasa, yani ulitoa risala nzuri sana kama mwalimu wa mapenzi ila leo hii wewe ndio wa kuwaonea wivu Erick na Erica kweli!”“Aaaah hapana, sio hivyo ingawa ni kweli Erica nilimpenda”“Basi ule upendo ambao ulikuwa nao kwa Erica uonyeshe kwangu, unashindwa nini? Au ngoja nikuulize ni kitu gani kinakufanya umpende Erica hadi leo yani hadi mume wa Erica pale umuonee wivu maana naelewa wazi kuwa huna safari wala hujaitwa popote ila umeona tuondoke tu”“Ni kweli mke wangu hata sio utani, yani nilipomuona Erick tu nimeshangaa kuwa sipendi tena kuwa eneo hilo kabisa, nisamehe kwa hilo tafadhari”“Haya niambie, ni kitu gani kinakufanya uone wivu au ni kitu gani kinakufanya umpende sana Erica mpaka ushindwe kumsahau”“Nadhani sijawahi kukwambia haya, ni hivi. Mimi kwa Erica nilikuwa ni mwanaume wake wa kwanza kabisa, hiyo inaonyesha jinsi gani Erica alijitunza kwaajili yangu, hiko kitu kinafanya nimpende sana Erica na nishindwe kumsahau”“Wewe ulijuaje kuwa ulikuwa mwanaume wa kwanza kwa Erica?”“Yani siku namuingilia, Erica alikuwa akilalamika maumivu tu, na Erica hakujua mambo yoyote ya mapenzi, kwakweli najivunia kuwa mwanaume wa kwanza kwa Erica”“Mmmh! Kwahiyo roho ikakuuma sana kunipata mimi gumegume”“Hapana mke wangu sina maana hiyo”“Haya kingine”“Kingine ni kuwa, mimi kwa hali niliyokuwa nayo mwanzoni ilikuwa ni ngumu sana kukubaliwa na mwanamke mrembo kama Erica, ila Erica alikubaliana na hali yangu na kuwa na mimi na huo ni upendo wa dhati alionionyesha, sikuwa na kitanda mimi ila Erica alikubali kulala na mimi kwenye godoro chini, vitu vingi sana sikuwa navyo ila Erica alinikubali na umasikini wangu. Kitu kingine, Erica aliniambia wazi, anapenda mwanaume wake awe hivi na vile na vile ila kwakuwa mimi sikuwa na pesa basi kuna mambo mengine nilitamani kuyafanikisha lakini nilishindwa ila asilimia tisini ya mafanikio yangu katika maisha basi imefanikishwa na Erica, alianza kuninunulia vitu vya ndani ya nyumba na kufanya chumba change kivutie, Erica alinipa mtaji wa kufuga samaki, Erica alinipa mtaji wa kufuga kuku, Erica alinipa mtaji wa kufungua lile duka langu kubwa la samaki na kuku, kwakweli siwezi kumsahau Erica katika maisha yangu. Hapo ndio msemo wanaosema kwenye mafanikio ya mwanaume basi mwanamke yupo nyuma, nauona kuwa ni kweli maana mafanikio yangu yamewezeshwa na Erica. Sasa roho iliniuma kipindi nimekuwa na pesa, na mimi naweza kutembea kwa kujitapa nikamuona jamaa Erick kaniibia mwanamke aliyenitengeneza kwa muda mrefu!! Kwakweli roho iliniuma sana. Nisamehe mke wangu ila siwezi kuficha hili, nampenda sana Erica”Fetty akapumua kidogo na kumwambia mumewe,“Unampenda sana, ila kumbuka hata yeye anampenda sana Erick na ndio kaamua kuolewa nae na kweli wanapendezana hata upendo wao tunaweza kuuona machoni. Hata kama Erica alikupenda basi hakuweza kukupenda kama ambavyo amempenda mume wake. Kuhusu kukutengeneza kimaisha, Mungu alijua ni kwanini Erica kafanya vile maana kumbe alikutengeneza kwaajili yangu”“Ushaanza kujipigia debe, yani kuna mambo nakumbuka na moyo unaniuma sana. Ile nyumba yangu niliyoamua kupangisha, basi ile nyumba ndio niliyojenga ili niishi na Erica, kiukweli bila fitna za ndugu zangu basi kwasasa Erica angekuwa mke wangu”Fetty hakutaka kuongeza neno kwa hapo kwani alijua maneno mengine atakayoongea mume wake yatamkarahisha tu.Baba Angel alipomaliza yale maongezi, akaenda kuitoa ile zawadi aliyokabidhiwa na madam Oliva na kumpa Angel ila Angel alifurahi sana maana huyu mtoto alikuwa na kawaida ya kufurahi na alipenda sana kufurahi kwahiyo yeye alifurahi kabla hata ya kujua kuwa ni zawadi gani ambayo imewekwa kwenye mfuko.Basi kwa muda huo baba Angel aliwaaga na kuondoka zake. Angel alienda chumbani kwake ili kuangalia ule mfuko umebeba vitu gani, kwanza alikuta kitabu kimoja kidogo halafu alikuta hereni, cheni na bangili. Basi akakisoma kile kitabu kidogo ambacho kiliandikwa juu“Mtoto wa kike jithamini, wewe ni wa thamani sana”Yale maneno yalimvutia na kujikuta akianza kusoma, kile kitabu kilielezea namna ya mtoto wa kike anavyopaswa kuwa msafi na namna ambavyo wanaume wanaonyesha tamaa kwa watoto wa kike, basi alikuwa akisoma na kwenda nacho kwa bibi yake na kumuonyesha, kwakweli alipomsomea kidogo tu bibi yake nae alipenda sana na kuuliza,“Ndio nani kakupa mjukuu wangu?”“Baba kasema ni madam Oliva”“Natamani kumfahamu kwakweli, amefikiria nini kukuletea kitabu kama hiki!! Jamani Angel maneno yangu hayakukai, umeletewa kitabu sasa na kama bado maneno yake hayakukai basi hapo sijui ni shetani gani atakuwa kwako”Angel alitabasamu tu, na bibi yake akasema tena,“Labda shetani mwenye vichwa saba, ila nitaongea na baba yako kuwa atuletee huyo madam Oliva tumfahamu”“Oooh bibi, tena nina hamu kweli ya kumfahamu ngoja nikakuonyeshe vingine alivyoniletea”Angel alienda kumletea bibi yake ambaye aliviangalia vile vitu na kuvipenda sana huku wakimsifia madam Oliva kuwa ni mtu mzuri sana.Baba Angel anarudi nyumbani kwake na kumuelezea taarifamkewe kuhusu sehemu aliyotoka, yani mama Angel akafurahi sana kwa mumewe kuitimiza hiyo ahadi, kitu pekee ambacho baba Angel hakukisema ni kuhusu kumpelekea Angel zawadi iliyotoka kwa madam Oliva, hakuona umuhimu wa jambo lile ndiomana hakusema wala nini, baada ya hapo aliulizia mambo ya watoto,“Eeeeh watoto hapa nyumbani wameshidaje?”“Uuuh leo maajabu, jamani baba Angel huwa huna kawaida ya kuulizia hali ya watoto kabisa, yani leo ni maajabu yamefanyika,, wamwshinda salama mume wangu hawajambo”“Oooh jana si walienda ufukweni nikajua Erica kakuletea mada za huko”“Halafu namshangaa safari hii hajaja kusema, yani Erica hata angeona mchanga unagongana anagekuja kusema. Hivi huyu mtoto katoa wapi hizi tabia za umbea jamani! Yani hadi huwa nashangaa na kujiuliza sana. Unajua kwetu hawapo watu wa namna hii na kwenu pia, sasa Erica kaitoa wapi tabia hii ya umbea?”“Hilo hilo jambo ilitakiwa mimi ndio niwe nashangaa ila sio wewe mama Angel jamani, yani wewe hata usingeshangaa ila tu ungemuweka mtoto vizuri asizungumze umbea kupitiliza maana itafikia hatua atatoa siri zake mwenyewe”“Kwahiyo katoa wapi umbea hadi unasema wewe ndio wa kuniuliza mimi?”“Kwani Derrick yukoje jamani! Yani Derrick ni mbea sana tena Derrick ni mbea na muongo, tumuombee tu Erica asianze uongo na huo umbea apunguze maana atagombanisha watu. Yani wewe muangalie ndugu yako Derrick vizuri, angalia umbea aliokusambazia wewe tena Derrick ni mtoto wa kiume kumbeka, ila Erica ni mtoto wa kike. Yani kwenye ukoo wenu huko lazima kuna mtu yuko hivi ndio anarishisha hawa watu”Mama Angel alisikitika kidogo kwani alimkumbuka huyu ndugu yake Derrick ambaye hadi sasa hawapatani sababu ya mambo ambayo Derrick amemfanyia, basi akasema,“Ila kweli, sema mwanangu asiwe kama Derrick jamani! Unajua yule Derrick ilivuka mipaka jamani!”“Ni wewe kukaa chini na Erica na kumwambia cha kusema na kutokusema, ila naona ameanza kukua maana jana alivyotoka ufukweni tu angekuja kukueleza kila kitu kilichotokea”“Ila mimi huwa napenda sana ambavyo anasema maana kuna mambo yamejificha ila Erica ananiletea habari na kunifungua macho”“Aaaah kumbe unapenda umbea wake eeeh!”Mama Angel alicheka pale kwani kuna baadhi ya maneno ya mwanae aliyaona kuwa yapo sawa kabisa.Kulipokucha, mapema kabisa baba Angel alienda zake kwenye kazi yake na kuanza kufanya kazi zake basi alikuwa pale kwenye kazi muda wote, na kama kawaida yake yani alisahau hata kula kwa muda huo maana alijiona kuwa kuna kazi lazima aimalize kwanza na kweli alifanya juu chini hadi aliimaliza.Ila alipoimaliza tu, alifika madam Oliva, yani kama alivizia vile kuwa muda huu baba Angel atakuwa kamaliza kazi, basi alimsalimia pale na kumwambia,“Jamani, hivi na leo umekula kweli?”“Aaah kuna kazi iliniweka busy sana siku ya leo, hivyobasi hata kula sijala ila hakuna tatizo sababu muda sio mrefu narudi kwangu kwahiyo nitakula nyumbani”“Aaaah jamani, nimekuletea matunda haya”Basi madam Oliva alitoa yale matunda na kumpa baba Angel, ila kiukweli baba Angel alikuwa akipenda sana matunda basi alimshuru pale na kula yale matunda, huku wakiongea ongea,“Leo baba Erick nahitaji ufike nyumbani kwangu ili upafahamu. Nakuomba sana”“Aaaah madam Oliva sio kwa leo”“Lini sasa jamani baba Erick? Wewe mwenyewe muda wako unajua jinsi ulivyo, mimi nitakufahamisha kwangu lini? Unajua binadamu ni kufahiana eeeh! Yani inatakiwa ufahamu kwangu kama nilivyofahamu kwako. Nakuomba tafadhari ufike kwangu leo”“Ila sitakaa sana”“Hamna tatizo yani swala la wewe kufika tu kwangu linatosha”Baba Angel alikubali na baada ya muda kidogo aliinuka na kufunga ile ofisi yake kisha kuondoka na madam Oliva.Wakiwa njiani na madam Oliva alimuona mtu kama Sia kwenye bodaboda tena ikienda kwa kasi sana ila hakutilia maanani ukizingatia huwa anakerwa sana na mtu huyu, kwahiyo aliendelea tu na maongezi na madam Oliva basin a mwisho wa siku walifika hadi kwa madam Oliva.Aliweza kuiona nyumba ya madam huyu ambayo ilikuwa ni nzuri ila ndani hapakuwa na mtu mwingine yoyote zaidi ya mlinzi ambaye alikuwa getini yani madam Oliva ndani ya nyumba yake hapakuwa hata na msichana wa kazi, basi baba Angel akauliza,“Mbona kimya hivi? Wanao wako wapi?”“Nina mtoto mmoja tu, ila bibi yake huwa anamng’ang’ania sana, kwahiyo yupo kwa bibi yake na hapa naishi mwenyewe tu”“Aaaah nimekuelewa hapo”Basi madam Oliva alimkaribisha baba Angel sebleni na kwenda jikoni kuleta juisi ili waweze kunywa kidogo ila muda huo alivyoenda kuleta juisi baba Angel alipigiwa simu na Steve na kufanya aipokee,“Bosi, ni hivi. Sia alikuja tena dukani leo ila kilichotokea sasa ni kimoja kuna wale walinzi uliwaweka na kusema kuwa Sia asiingie dukani kabisa, basi walimzuia ila Sia alisisitiza kufanya hivyo na wale walinzi wamempiga Sia ameanguka hata sijui imekuwaje maana hatingishiki”:Ile habari kidogo ilimshtua sana baba Angel na muda huo huo akasimama na kutoka nje ya nyumba ile. Basi madam Oliva alimkaribisha baba Angel sebleni na kwenda jikoni kuleta juisi ili waweze kunywa kidogo ila muda huo alivyoenda kuleta juisi baba Angel alipigiwa simu na Steve na kufanya aipokee,“Bosi, ni hivi. Sia alikuja tena dukani leo ila kilichotokea sasa ni kimoja kuna wale walinzi uliwaweka na kusema kuwa Sia asiingie dukani kabisa, basi walimzuia ila Sia alisisitiza kufanya hivyo na wale walinzi wamempiga Sia ameanguka hata sijui imekuwaje maana hatingishiki”:Ile habari kidogo ilimshtua sana baba Angel na muda huo huo akasimama na kutoka nje ya nyumba ile.Kiukweli alitoka nje na kuondoka akielekea dukani kwake ambapo kaambiwa kuwa kuna tatizo, basi madam Oliva muda huo alitoka jikoni na glasi za juisi ila hakumkuta baba Angel, ikabidi akamuulize mlinzi wake ambaye alisema kuwa yule mgeni kaondoka zake, basi madam Oliva alirudi ndani na kupiga simu ya baba Angel na kuanza kuongea nae,“Jamani baba Angel ndio hata kuaga hakuna!”“Aaah samahani madam, kuna tatizo kidogo limetokea ndio naenda kushughulikia”Kisha baba Angel akaikata ile simu kwakweli madam Oliva hakujihisi vizuri kabisa na muda huo alimpigia rafiki yake simu,“Jamani shoga yangu kumbe kumpata mume wa mtu ndio kazi hivi!!”“Kivipi!! Kwanza kabisa hakuna mwanaume rahisi kumpata kama mume wa mtu sababu wengi wao huwa wanakuwa na stress za kutosha walizopewa na wake zao”“Jamani huyu mume wa mtu ananipa mawazo haswaa, leo nimekuja nae hadi nyumbani basi nikaenda kufanya vile ulivyosema, nafika sebleni hayupo kumbe kapata dharula kaondoka, jamani dharula gani muda huu huu!”“Uikate tamaa madam, hiyo moja imeshindikana ila endelea kujaribu”Aliongea na mwenzie pale aliyeonekana kumpa ushauri mbalimbali.Basi baba Angel alifika dukani na kuulizia kuwa Sia yuko wapi, alikuta wamemuhifadhi mahali kwani pale waliogopa watu wangeweza kujaa,“Mmmmh nyie mbona mna akili mbovu hivyo, yani mtu alianguka halafu nyie mmenda kumuhifadhi mahali? Akitufia huko je! Hata kama nilisema mumfukuze ila sio kwa stahili ya kumpa kipigo mpaka kuzimia”“Ila bosi, hatujampiga hivyo unavyodhani!”Baba Angel alichukia, ingawa hakumpenda Sia ila bado hakupenda yeye awe chanzo cha kifo cha Sia, kwahiyo alichukia sana, akaonyeshwa sehemu waliyomuweka Sia na hapo alimbeba na kumpeleka kwenye gari yake kisha na yeye akapanda ili aelekee nae hospitali.Wakati gari inaondoka akamsikia Sia akiongea,“Habari yako Erick”Baba Angel alishtuka sana hadi alisimamisha gari pembeni na kuita,“Sia!!”“Ndio ni mimi ulidhani imekuwaje?”“Umenishtua sana”“Kheee ulidhani nimekufa! Hapana sijafa, bado nipo hai”“Sasa ilikuwaje kwani?”Kwavile baba Angel alimlaza Sia siti za nyuma ya gari, kwahiyo Sia akaruka na kukaa ile siti ya mbele ili aonane nae vizuri zaidi, kisha alianza kuongea nae,“Unajua sikujua kama bado utanijali kiasi hiki baada ya yote yale”“Sikuelewi”“Huwezi ukanielewa, ni hivi. Mimi sikuzimia kama kuzimia ila nilikuwa nimeigiza tu, na nilijua kuwa wale vijana watafanya vile ila nilikuwa namuomba Mungu ukipigiwa simu basi ufanye hima kufika. Unajua wale vijana wamenizaba kibao kimoja tu, kiukweli siwezi kuzimishwa kwa kibao kimoja labda kama kuna namna nyingine”“Kwahiyo Sia ulikuwa unaigiza kuzimia ili iweje?”“Sikia nikwambie Erick, unajua mimi huwa nakufatilia sana. Ipo hivi na huwezi kuibadilisha. Mimi sio adui yako na wala sio adui wa Erica, mna maadui wengine tu ila sio mimi na kama kutumiwa na maadui zenu basi nilitumiwa mwanzoni. Mimi siwezi kumuumiza mtoto wako, bora hata mtoto wa Erica”“Unamaanisha Angel!”“Nimesemea tu, ila mimi siwezi kumuumiza mtoto wako wa aina yoyote. Kuna vitu vingine nafanya vinakukera haswaa, sema kuna wakati mwingine nakuwa na uhitaji wa pesa ndiomana nafanya vile. Nilikwambia kuwa Erick ni mwanangu hujawahi kuniamini, nikasema Elly nimezaa na wewe hujataka kuniamini wala sihitaji uniamini wala nini kwani sina ugomvi na wewe ila mara nyingine ni pesa inanitesa sababui sina pesa. Ila kwasasa ningeomba basi umuhudumie Elly kama unavyomuhudumia Angel yani uwe unamsaidia tu, mbona Angel unajua fika sio mwanao lakini unampenda, unamjali, unamthamini na kumlinda! Naomba iwe hivyo na kwa Elly pia”“Unajua wewe mwanamke una wazimu, kwahiyo Elly mwanangu sio mwanangu?”“Aaaah tusiongee hayo kwa wakati huu hata nikikwambia hutonielewa”“Sikia kwanza, kuhusu swala la Angel natambua wazi kuwa sio wangu ila nilishamkubali yule mtoto toka mdogo na nilimwambia mama yake kuwa Angel nitamlea siku zote kama mwanangu na siku zote ataishi hivyo na ndugu zangu wote hata waseme kitu gani ila wanatakiw akukubaliana na kauli yangu kuwa Angel ni mwanangu. Mwanzoni walisema sema hadi kutaka nikapime damu na Angel sasa nipime damu gani wakati ukweli naujua? Ila mimi nilibaki na msimamo wangu kuwa Angel ni mwanangu na maisha yanataka uwe na msimamo. Ila wewe naona upo kujikanyagakanyaga, mara Erick mwanao tukikuuliza kivipi unajiuma uma, mara Elly mwanangu na sasa umekuja na hoja mpya sijui nimsaidie Elly kama ninavyomsaidia Angel. Dah! Wewe mwanamke wewe aliyekuroga kiukweli amekufa jamani. Kwahiyo hiko kitu cha kuomba msaada kuhusu Elly ndio kilikufanya uzimie?”“Hapana, hiko wala kisingenifanya nizimie kwani ningejua ni wapi pa kukuvizia hadi tukaongea pamoja, ila kilichonifanya nifanye hivi ni hiki. Nilikuona wewe na yule madam mnaondoka na kwa haraka haraka nilihisi tu mnaenda nyumbani kwa yule madam, inawezekana hujui au unajifanya hujui wakati dalili zote zinaonekana, yule madam anakutaka Erick ndiomana yupo karibu sana na wewe. Nimefatilia muda, anakuletea matunda sijui nini, anawapeleka wakina Erica kusuka, anakupa zawadi umpelekee Angel, nimemfatilia sana, utajua wewe ni muda gani nimetumia kumfatilia ila nilishamfatilia sana. Na nilishawahi kumsikia akiongea na mwenzie yani mwenzie alikuwa akimpa mbinu ya kukupata wewe kuwa ukienda nae kwake akuleweshe kisha ungelala nae na yeye ingekuwa ndio njia moja wapo kwanza ya kukupata maana ukilala nae sasa ndio ataanza kufanya mazoea ya kulala nawe mara kwa mara”“Mmmh!”“Ndio hivyo, kwahiyo nilivyokuona nikaona njia pekee ya kufanya ni kujifanya nimeenda kufanya fujo dukani kwako kwani naelewa wazi kuwa umeweka walinzi kwaajili yangu nami nilijifanya nataka kuingia kwa nguvu basi wakanizaba kibao nami nikazimia ila dah kibao kinauma kile, wale walinzi wamekomaa sana.”Baba Angel alicheka kidogo na kutikisa kichwa maana huyu mwanamke kiukweli alikuwa akiumiza sana kichwa chake, kisha Sia aliendelea kuongea,“Basi ndiomana nikafanya vile sababu nilijua wakikutaarifu utakuja na kuachana na yule mwanamke. Erick ngoja nikwambie kitu, kipindi upo na mimi ulikuwa ni mwanaume muhuni sana, ulikuwa na wanawake wengi na wengine nakufumania nao kitandani ila bado nilivumilia, ila sio kwamba niliipenda ile hali sikuipenda hata kidogo sema tu nilivumilia sababu nakupenda. Namfahamu Erica alivyo, nafahamu udhaifu wake, pia nafahamu kuwa Erica anapenda sana kulia. Jamani aje agundue kwasasa upo na yule madam utamfanya mwenzio alie hata siku mbili kama ana msiba vile, ukizingatia kwake unaishi kama mwanaume wa tofauti kwani umebadilisha tabia zote na wala hawezi kukuhisi vibaya, ila gafla sikie mumeo anatoka na yule madam kiukweli ataumia sana na utamuweka kwenye wakati mgumu sana, ndiomana mimi nikafanya vile kukuokoa wewe na kuokoa ndoa yenu. Mimi nilikuomba unioe ila sikukuomba uachane na Erica, ila najua pia kuwa swala hilo ni gumu kutokana na mlivyokubaliana wakati wa ndoa kuwa ndoa yenu ni ya mke mmoja na mume mmoja, ila ombi langu mimi ni ndoa tu. Sema tuachane na hilo kwanza, ila tuongelee hili la leo, kwahiyo hiko ndio kitu kilichotokea, nisamehe bure, nisamehe kwa kukukwaza ila sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivyo”“Sasa madam Oliva alitaka anileweshe na kitu gani?”“Sijui ila alitaka kukulewesha, na ungelewa tu basi kwisha habari yako, kwanza yule madam ana uchu wa muda mrefu sana. Ungelewa wewe mbona ingekuwa balaa humo ndani, na ninavyokufahamu ukilewa mmh! Sema umeacha pombe tu siku hizi”“Hebu acha habari zako hizo, ila hata sijui niseme kitu gani? Haya cha kukusaidie kwasasa nitakurudisha tu kwako”Sia alifurahi sana, na muda huo huo alianza kumuelekeza baba Angel nyumbani kwake ambapo ni kweli baba Angel alimfikisha Sia hadi nyumbani kwake na hapo palikuwa na Elly ambaye aliona lile tukio na kumfanya atabasamu pia, kwani alikuwa akiumia sana kuona hakuna hata mwanaume anayeongozana na mama yake, kwahiyo alivyomuona vile mama yake alifurahi sana huku akijisemea,“Hata kama baba yangu amekufa, ni heri mama akanipatia baba wa kambo kama hivi”Basi Sia alipokuwa anashuka alimwambia baba Angel,“Ila Erick samahani, hapa ndani kwa siku ya leo kidogo biashara zangu hazijaenda vizuri na sina chakula”“Unajua kuna kipindi una wazimu wewe mwanamke”“Jamani, kwanini Erick?”“Haya, unahitaji mtaji wa kiasi gani ili kuboresha biashara yako na uache kuisumbua familia yangu”“Ningepata milioni moja, ingenisaidia sana”“Basi subiri hapo nitakuja muda sio mrefu”Sia alishuka na baba Angel muda huo alienda hadi benki na kutoa pesa kisha akaweka kwenye bahasha na kumpelekea Sia kisha akamwambia,“Sihitaji tena kuona ukiisumbua akili yangu au familia yangu”“Ila naomba usinikataze kufatilia kama kuna wanawake wanaokuvizia kama madam!”“Dah! Unajua wewe jamani! Usiniumize kichwa, yani acha kunifatilia kabisa. Kwaheri”Baba Angel alirudi kwenye gari yake na muda huo moja kwa moja alienda nyumbani kwake.Kwakweli, leo Sia alikuwa na furaha sana hadi Elly alifurahi pia jinsi mama yake alivyokuwa na furaha basi akaongea nae,“Mama, leo nimefurahi sana jinsi ulivyofurahi. Sikutoka nje kumsalimia yule mgeni ila kama namfahamu hivi! Nitambulishe mama”“Ni kweli unamfahamu, yule ni baba yake Erica”Elly akashtuka kidogo kwani hakufahamu kama yule ni baba yake Erica wala nini ila kawahi kuonana nae mara kadhaa, kisha alimuuliza mama yake,“Mama, lakini si ulisema ile familia ya wakina Erica ni ndugu zetu lakini wanakuchukia kumbe hawakuchukii?”“Ni hivi mwanangu, huyu baba hana roho mbaya hata kidogo ila mke wake kuna muda anakuwa kama mwendawazimu. Leo nimefurahi sana kukutana naye”“Nakuona mama”Kisha Sia alitoa ile bahasha na kuweka zile hela kitandani na kuanza kuzihesabu, kwakweli alichekelea sana na kusema,“Oooh furaha yangu ya leo, nitaipumzisha ile familia kwasasa hawatoniona maana nitakuwa makini na shughuli zangu. Oooh kumbe kanipa milioni tatu na laki tano!! Aaaah nimefurahi sana”Elly nae alifurahi sana maana kile kitendo cha kumuona mama yake akiwa na furaha kilimfanya afurahi pia kisha akamuuliza,“Kwani mama umefanyeje leo hadi imekuwa hivyo!!”“Yani mwanangu nilichokifanya leo hata sikutegemea kama kitaniletea matunda haya, ila mwanangu usijali kitu yani katika maisha ukitaka kufanya kitu basi fanya tu huwezi jua muda kitu hiko kitakapofanikiwa kama mimi leo”Sia alikuwa akiongea huku akitabasamu tu, kisha mama yake akasema,“Hii milioni tatu nitaiwekeza kwenye biashara yangu halafu hii laki tano ndio itatuisaidia kwasasa hapa nyumbani. Unajua shule yako nayo imenikomba sana hela, ila usijali kitu mwanangu yani mama anaweza kila kitu katika maisha maana yule baba yake Erica kaahidi kukusomesha mwanangu”“Mama, hiyo ni habari njema sana, nilikuwa naumia ukihangaika kulipa ada, nimefurahi sana”“Usijali mwanangu, nikiwepo mimi basi kila kitu kinaenda kwenye mstari ulionyooka”Basi siku hiyo aliamua kwenda kupika mapema kabisa ili ale na watoto wake maana kwenye nyumba yake kulikuwa na watoto wengine anaishi nao zaidi ya Elly.Baba Angel akiwa njiani kurudi nyumbani kwake, alisikia simu yake ikiita ila kwa muda huo hakuichukua kwani alikuwa makini na kuendesha gari yake, basi alivyofika nyumbani na kuingiza gari ile simu ikaanza kuita tena ikabidi aichukue na kuangalia mpigaji alikuwa ni madam Oliva, basi akaipokea na kuanza kuongea nayo,“Baba Erick, ndio bado hujamaliza tu hilo tatizo?”“Aaah nimemaliza, ila nimerudi nyumbani”“Jamani kwanini lakini”“Usijali madam, nimeshapafahamu kwako sidhani kama ni tatizo sana kwani kama kufahamiana tumeshafahamiana”“Mimi nilihitaji angalau ule chakula na tuongee mawili matatu sababu nina biashara yangu nataka nikushirikishe”“Oooh basi njoo ofisini kesho”Kisha baba Angel hakukata simu, kuna muda alitaka kuamini maneno ya Sia kuhusu huyu madam ila kuna muda anaona maneno ya Sia kuwa ni uzushi tu kwani alimuona madam kama ni mtu asiyekuwa na tatizo ambalo Sia alikuwa akilizungumzia.Basi akaingia ndani kwake na kumkuta mkewe na kuendelea nae na mambo mengine ila kuhusu swala la Sia hakumwambia kabisa kwani anamfahamu vizuri mkewe alivyo.Kesho yake ilivyofika, baba Angel alijiandaa vizuri kabisa na kwenda kazini kwake, ila kuna mahali alikuwa na shamba halafu alikuwa akihitaji kufanya ujenzi ila kutokana na shughuli zake kuona zitakuwa nyingi siku hiyo basi aliondoka pale nyumbani akiwa na Junior pamoja na Erick na moja kwa moja alienda nao kwenye hilo eneo na kuwaelekeza cha kufanya kisha akawaacha hapo halafu yeye akaenda ofisini.Yani ile anaingia tu ofisini kwake, na madam Oliva alikuwa kashawasili,“Eeeh madam”“Eeeeh nilikuwa nakusubiri ufike”“Haya, karibu ofisini”Basi waliingia ofisini na madam Oliva na kuanza kuongea nae mawili matatu,“Eeeh kuna biashara ulisema unataka unishirikishe, ni biashara gani hiyo?”“Mmmh kwanza mke wako anafanya kazi au ni mama wa nyumbani tu!”“Aaaah nilioa msomi bhana, atakuwaje mama wa nyumbani! Yupo nyumbani sababu analea tu, sema kwa mimi huwa napenda mke wangu awe nyumbani tu ila yeye hapendi. Yani mimi kitendo cha kurudi nyumbani na kupokelewa na mke wangu huwa najihisi raha sana, ila akianza shughuli zake sasa hadi huwa namwambia pumzika sasa mama tule maisha.”“Kheee kwahiyo mke wako angekuwa mama wa nyumbani ungefurahi zaidi?”“Ndio, si mimi najishughulisha kwaajili yao! Yani yeye angekuwa anakaa tu nyumbani kulea watoto ningefurahi ila mke wangu hataki kabisa, hata hivyo nilimkatalia kuwa na kazi ya kumfanya awe busy kwa muda mrefu kwahiyo kazi yake anayoifanya ni huru sana.”“Oooh sawa, kuna biashara nataka nikushirikishe. Ushawahi kusikia biashara za mtandao?”“Aaaah na wewe madam una mambo mengi sana, saivi unakuja na biashara za mitandao tena!”“Ni nzuri sana, ukiianza hutojutia, watu wanatengeneza hadi milioni mia kwa wiki!”“Jamani madam, ila kwa mimi biashara zangu hizi zinanitosha, wala usinishirikishe hiyo”“Basi nitamwambia mke wako, ni nzuri sana kwanza unaifanya kwa muda wako wa ziada”“Asante madam, mimi niletee biashara za kuona ila za mitandao zisiwezi kwanza sio mzuri sana kwenye mitandao mimi. Ila kwa leo nina kazi nyingi sana sitaweza kuongea sana na wewe”Basi madam Oliva aliamua kuaga tu kwani aliona kama ni ujanja tu baba Angel kautumia ili aondoke.Mama Angel akiwa nyumbani, kwahiyo aliyebaki alikuwa Erica tu sababu Erick na Junior waliondoka na Vaileth muda huo alikuwa akipika.Basi alikaa sebleni pale na mwanae huyo, mara simu yake ikaita akaichukua na kuipokea, alikuwa ni dada yake Mage,“Mdogo wangu nipigie, kuna jambo muhimu sana nataka tuongee”Kisha ile simu ikakatika, basi mama Angel akaanza kupiga ila simu ikamwambia kuwa salio lako halitoshi kupiga simu na kumfanya achukie sana,“Aaaarggh kumbe sijaweka vocha, kehee sasa nitafanyaje jamani! Nitamtuma nani dukani kuninunulia vocha?”Erica akamwambia mama yake,“Nitume mimi”Basi hakuwa na njia nyingine mama Angel zaidi ya kumtuma Erica vocha ambapo Erica alitoka huku akifurahia,“Jamani, leo kama maajabu vile nimetumwa dukani. Ila mama anatufuga sana dah!”Basi akaenda moja kwa moja hadi dukani na kununua vocha, ambapo yule muuza duka akamuuliza,“Hivi wewe ni mtoto wa yule baba ambaye watoto wake hawatoki nje eeh!”Erica alicheka kusikia kuwa mtaani wanaitwa kwa jina hilo, alitikisa kichwa na kuanza kuondoka. Ila kwa hatua chache tu akashikwa bega, kugeuka akakutana na Elly kwakweli alifurahi sana na kuanza kuongea nae,“Elly jamani, mitaa yetu umekuja kutafuta nini?”“Aaah mama yangu ana mgahawa wa mama lishe maeneo ya huku, sasa leo nilikuwa nae maana tunapaboresha na kuanza tena biashara”“Kumbe, hongereni”“Ila unajua mama yangu kapata hela wapi?”“Eeeh wapi?”“Jana, mama kaletwa nyumbani na baba yako kisha baba yako akaondoka na baada ya muda alirudi na bahasha na kumkabidhi mama. Tulipoenda kuhesabu zile hela zilikuwa milioni tatu na laki tano. Halafu nasikia baba yako kamuahidi mama kuwa atanisomesha mimi kwahiyo ada hatolipa tena mama bali italipwa na baba yako”“Mmmh kumbe!”“Ndio, nasikia baba yako ana roho nzuri sana ila mama yako kuna wakati anapatwa na uwendawazimu!”“Jamani Elly! Mama yangu hawezi kupandwa na uwendawazimu ujue!”“Ndio mama alivyoniambia sasa, kasema mimi na nyie ni ndugu, na baba yako anatupenda sana wote kwa pamoja”“Kheee haya, twende kwetu basi ukamsalimie mama”“Siku baba yako akiwepo nitakuja, ila mama yako namfahamu maana hata siku ile aliniangalia kwa chuki sana. Ila hata hivyo kuna kazi naimalizia na mama”Basi Erica aliagana na Elly pale ila alikuwa akitembea huku akijiuliza maswali mengi sana kuwa baba yake imekuwaje hadi ampe pesa mama Elly, akajiuliza,“Hivi mama atakuwa anajua kweli? Hivi baba anaweza kufanya kitu mama asijue!”Akaendelea kwenda nyumbani na alipofika alimpa mama yake ile vocha ambaye aliikwangua na kuanza kuiingiza kwenye simu yake basi Erica akaanza kuongea,“Basi leo dukani mama nimekutana na….”Mama yake akamkatisha,“Ushaanza umbea wako, nataka kwenda kuongea na simu mimi aaargh maana wewe hata ukikutana na mende unataka uje kunisimulia”Kisha mama Angel aliinuka na kwenda kuongea na simu ile, kiukweli Erica hakupenda kabisa jambo lile yani aliona kama mama yake kamfanyia makusudi, hakujua ni kwanini mama yake hakutaka kumsikiliza, basi akahisi huenda mama yake anafahamu hiko kitu ila ilimuuma kushushuliwa kabla ya kusema umbea, hivyobasi akaamua kwenda kulala.Mama Angel alimpigia simu dada yake na kuanza kuongea nae, ambapo walisalimiana kwanza kisha dada yake akaanza kumwambia dhumuni la yeye kumtafuta hewani,“Ni hivi mdogo wangu, unajua tukiacha mambo yote yaliyotokea baina yako na Derrick ila bado ni ndugu yetu yani hatutakiwa kulipinga hilo maana Derrick ni mtoto wa baba yetu”“Kwani unaongelea kitu gani dada?”“Nasikia Derrick kawa tapeli”“Mmmh jamani, Derrick kawa tapeli!”“Ndio hivyo, Derrick ni tapeli. Sasa tusipoamka kama ndugu tutakaoumia ni sisi, inatakiwa mimi wewe, Bite na Tony tuungane na Derrick ili tumsaidie kisaikolojia”“Sikuelewi dada”“Kitu gani ambacho hunielewi Erica jamani! Kumbuka Derrick ni ndugu yetu yani unavyomuona Tony unatakiwa kumuona hivyo hivyo na Derrick”“Kwakweli dada unanichanganya tu”“Nakuchanganya na nini jamani, nakwambia Derrick kawa tapeli”“Kwanini wakati kasoma na ana kazi nzuri tu”“Aliyekwambia matapeli ni watu wasiosoma tu nani? Huoni kila leo wanagundua njia mpya za utapeli? Wengine wamesoma na wengine hawajasoma ila utapeli ni tabia tu, mwingine utaona kavaa vizuri anapendeza kumbe tapeli ndio ilivyo kwa Derrick ni wengi kawaliza kwa utapeli wake, tusiposhirikiana pamoja ili Derrick aache utapeli itakuwa ni kazi kwetu”“Ila dada Derrick si ana kazi jamani!”“Nasikia kuna matatizo yalitokea kazini kwao, kwahiyo Derrick hana kazi tena ila hiyo sio sababu maana nasikia utapeli kaanza toka yupo kazini kwahiyo kwasasa ni kama anaendeleza tu. Kwakweli Derrick anaweza fanya mpango hata tutapeliwe sisi wenyewe, mdogo wangu kama ndugu tunatakiwa tuwe na lengo moja ili tuweze kumuokoa Derrick, haijalishi ni kitu gani kilitokea kati yenu ila bado Derrick ni ndugu yetu, tumpende, tumjali na tumthamini”“Kheee haya dada nimekuelewa, hakuna tatizo utanipa taarifa basi”“Sawa, wasalimie wanangu huko”Kisha mama Angel aliagana na dada yake ila bado hakuafikiana nae wala nini kuhusu kumsaidia Derrick kwani kiukweli huwa mtu huyu anamkera sana.Usiku wa leo Erick akiwa kajilaza sababu alichoka sana kwa safari ambayo jana yake walienda na baba yao kwahiyo aliwahi sana kulala, basi Erica akaenda moja kwa moja chumbani kwa kaka yake ambaye alimkuta amejilaza ila siku hii alisahau kufunga mlango wa chumba cha Erick alivyoingia, kwahiyo alianza tu kumuamsha, basi Erick aliamka huku akiwa na usingizi na alimuangalia Erica kwa macho ya usingizi halafu aliendelea kulala ambapo Erica alienda kumgusa tena, na kumfanya ageuke sasa akiendelea kumuangalia kwa jicho la usingizi kisha akamwambia,“Niambie malaika wangu nini tatizo”“Wewe mimi sio Angel bhana, mimi ni Erica”Erick aligeuka upande wa pili na kulala tena, basi Erica alichukia na kusema,“Ndio shida yako ukilala unakuwa kama pono, sasa mimi huu umbea nitamwambia nani jamani! Mama hataki na wewe umelala jamani mwenzenu nina maneno nataka niseme”Ila muda huu Erick alikuwa amelala kabisa yani hana hata habari, basi Arica alianza kuongea peke yake yani aliongea tu hata kama kaka yake amelala basi alianza kusema ila muda huu mama Angel nae alikuwa akipita pale karibu na chumba cha Erick na kukuta mlango uko wazi, sema alielewa kuwa mwanae siku hiyo alichoka sana kwahiyo akasogea ili afunge mlango sema akasikia sauti ya Erica ikisema,“Basi leo mama alinituma dukani, wakati natoka tu si nikakutana na Elly, tukasalimiana pale akaanza kuniambia kuwa baba na mama yake wamepatana kiasi kwamba baba kampeleka mama yake nyumbani kwao, halafu baba akaondoka na kurudi tena kwao kisha akamkabidhi mama yake hela kiasi cha milioni tatu na laki tano, kitu kingine baba kaahidi kumsomesha Elly na kila kitu kuhusu Elly kitakuwa juu ya baba. Nilivyotoka dukani nikatamani nikumueleza mama ila nilivyoanza tu kanishushua balaa hadi nimejihisi vibaya mimi, halafu nakuja kukwambia wewe unayenisikilizaga nawe unajifanya umelala. Ila ndio nishakwambia hivyo, ukiona kama ulikuwa unaota shauri yako ila mimi ndio nishakwambia. Usiku mwema”Erica akainuka na kumfunika kaka yake shuka vizuri halafu alitoka ila hakumkuta mtu mlangoni pale kwahiyo hakuelewa kama mama yake alisikia kile alichokisema, basi alifunga mlango wa Erick na kuondoka zake.Mama Angel alienda chumbani kwake na kuwa na mawazo sana, yani alijikuta akikosa raha kabisa huku moyo ukimuuma sana kwani wivu ulijengeka kwake, muda huu mumewe alikuwa ameenda kuoga, alikuwa amejiinamia tu kwa mawazo aliyokuwa nayo.Gafla alisikia mlio wa meseji na hivyobasi akachukua simu ya mumewe na kuanza kuangalia ule ujumbe ulioingia, ilikuwa ni namba tu na ujumbe ulisema,“Erick, kwakweli jana nilifurahi sana. Ngoja nikupe matumizi ya ile hela, laki tano nimetumia nyumbani na milioni tatu kwenye biashara yangu. Kwakweli asante sana, sitakufatilia wala kukusumbua kwasasa maana ahadi zako zimenitosha. Nitakupenda siku zote za maisha yangu”Mama Angel alirudia ujumbe huu mara mbili mbili huku akiumia sana moyo wake hadi machozi yalianza kumlengalenga. Gafla alisikia mlio wa meseji na hivyobasi akachukua simu ya mumewe na kuanza kuangalia ule ujumbe ulioingia, ilikuwa ni namba tu na ujumbe ulisema,“Erick, kwakweli jana nilifurahi sana. Ngoja nikupe matumizi ya ile hela, laki tano nimetumia nyumbani na milioni tatu kwenye biashara yangu. Kwakweli asante sana, sitakufatilia wala kukusumbua kwasasa maana ahadi zako zimenitosha. Nitakupenda siku zote za maisha yangu”Mama Angel alirudia ujumbe huu mara mbili mbili huku akiumia sana moyo wake hadi machozi yalianza kumlengalenga.Baba Angel alitoka bafuni na kumshangaa mkewe akiwa na simu yake huku machozi yakimlengalenga, basi alimfata karibu na kukaa naye kisha alianza kumuuliza,“Tatizo liko wapi mke wangu? Mbona unaonekana haupo sawa?”Kisha mama Angel alimpa baba Angel ile simu yake na kumfanya ausome ule ujumbe, moja kwa moja baba Angel alitambua wazi kuwa ule ujumbe ulitoka kwa Sia, basi alimuangalia mke wake na kumwambia,“Erica mke wangu, kweli ni wakati wa wewe kuchukia huu! Inamaana huniamini mume wako mpaka leo? Kweli nianze kuhangaika na wanawake wa kazi gani, unatakiw akuniuliza kwanza tena kwa ustaarabu tu ila sio kutoa machozi mke wangu jamani”“Nikuulize kitu gani wakati kila kitu kinaonekana hapo”“Sikia mke wangu, ningekuwa ni mwanaume muhangaikaji kwanza kabisa nisingekuwa nakuachia simu yangu, ungekuta simu yangu ina kufuli kila mahali ila simu yangu huwa naicha peupe kabisa sababu najiamini sana, kwanini wewe huniamini? Tumekuwa pamoja kwa miaka sasa mpaka tuna watoto wanne ila bado huniamini jamani! Nifanye nini mke wangu?”“Haya nieleze kwanza huyo mwanamke ulimpatia pesa kwa misingi ipi? Ni nani?”“Huyu ni Sia mke wangu, sikuwa hata na nia mbaya ila nilimuuliza tu anachotaka ni kitu gani ili asiisumbue tena familia yetu, ndio akasema nikimpa milioni moja basi hatotusumbua tena. Nikampa hiyo milioni tati na laki tani sababu sitaki usumbufu wake tena, sio kwamba sina matumizi na hela, ninayo sana ila sikupenda vile anavyoikosesha amani familia yetu”“Kwahiyo umeona kumpa hela ndio suluhisho? Na kumepleka kwake je? Kumuahidi kumsomeshea mwanae na kumtunza je! Hebu niweke wazi Erick, ni kweli ulizaa na Sia?”“Sikia mke wangu, kama ningezaa na Sia wala nisingekuwa na sababu ya kukataa ujue! Kwanza nikatae damu yangu ili iweje! Siwezi kufanya hiko kitu hata kama simpendi mwanamke, ila Erica nakupenda wewe na ninachokwambia ni ukweli ila swala la kunichunguza hivyo mke wangu inaonyesha wazi huniamini”“Aaaagh Erick, nitolee swala la kutokukuamini kabisa eti nakuchunguza inamaana sikuamini naomba ulitoe. Katika mahusiano yetu tunaishi siku zote kwa namna hii, ni kawaida kwangu kushika simu yako nawe ni kawaida kushika simu yangu hata kupokea pia, sasa mimi kusoma ujumbe ndio kukuchunguza! Naomba jamani usianze kufanya niongee hadi asubuhi hapa, nataka tu kujua ajenda yako ya kumsomesha mtoto wa Sia imekuwaje?”“Hakuna kitu kama hiko mke wangu, sijapanga hivyo na Sia”“Erick, nitajua tu ukweli. Unaona nalea ndio unafikiri siwezi kujua, najua unajua kama akili zangu zikoje, sishindwi kukuchunguza mimi tena zaidi ya kukuchunguza kwa simu naweza yote, ila nahitaji tuendelee kuishi kwa amani, kuwa mkweli kwangu kama zamani. Mume wangu najivunia kuwa nimekutengeneza na kukufanya uwe hivyo ulivyokuwa kwasasa, najua kuna wengi wanajiuliza ni kwanini wale wanadumu au ni kwanini wana furaha ila ni sababu ya kukutengeneza na kujenga mazingira safi ya kupendana na kuaminiana. Kipi unachoniambia nikapinga mimi? Kwanini sasa unanificha mambo kama haya kweli!! Jambo limetokea jana ulishindwa kuniambia hadi leo kweli!!”“Oooh mke wangu nisamehe tafadhari, nakuomba tusimkaribishe shetani bure katika ndoa yetu, naomba unisamehe”“Niahidi kuwa unaenda kubadilika, kiukweli sijapenda hii kitu yani sijapenda kabisa. Naomba chochote kinachotokea uwe unaniambia kama zamani”“Sawa mke wangu, naomba tena msamaha”Mama Angel aliitikia ila bado alionekana kuwa na kinyongo moyoni mwake, hivyo mumewe ilibidi aanze kumbembeleza ili arudi katika hali ya kawaida.Basi wakaamua kulala, sema kwavile baba Angel nae alikuwa amechoka sana kwahiyo alivyojilaza tu akapitiwa na usingizi ila kwa mama Angel ilikuwa tofauti kwanza alikuwa na mawazo na pia huwa analala sana mchana na mtoto kwahiyo alijikuta akiwa macho, kwani bado moyo wake ulikuwa ukiumia kwahiyo alichukua simu ya mume wake na kuanza kuwasiliana na Sia yani akijifanya kama yeye ndiye baba Angel,“Umelala Sia? Ile hela inakutosha lakini?”“Oooh Mungu yu mwema, umenikumbuka leo jamani naona maombi yangu yanaanza kujibiwa. Imenitosha ndio, nilikuwa nalala hapa ila niliposikia ujumbe ndio naangalia naona ni wewe nimeshtuka sana. Nashukuru, leo umechat na mimi mkeo hakuoni au?”“Aaah kalala, yupo hoi si unajua analea?”“Oooh naelewa ndio, sasa huu ndio muda muafaka ungekuwa na mimi wakati mkeo analea. Unajua ndiomana wenzetu kuna sharia ya mwanaume kuoa wake wengi, achana na imani hiyo ya mke mmoja, twende tufunge ndoa hata bomani ili tusizini”Mama Angel akapumua kidogo na kuendelea kuwasiliana na Sia,“Aaah jamani, ndoa nyingine mke wangu hawezi kukubali”“Naelewa hilo sababu Erica ana roho mbaya, na akijua kuwa umenipa pesa kama namuona atakavyonuna hata kutamani kujiua”“Hahaha, mke wangu hayupo hivyo bhana. Hawezi kuchukia, mbona ana roho nzuri tu huyu”“Kama ana roho nzuri mwambie nataka kuongeza mke wa pili, nataka kumuoa Sia uone patakavyochimbika hapo bila jembe”“Basi nitamwambia hakuna tatizo, vipi mtoto kalala?“Kalala ndio, leo maajabu umeulizia hadi kuhusu mtoto?”“Ndio, mwanangu huyo”“Mmmh jamani, Erick wewe au mwingine. Wewe kirahisi tu hivyo useme Elly mwanao! Au leo umekunywa kidogo?”“Aaah hapana, nitamlea Elly”“Kheee jamani usinifanye nishindwe kulala kwa furaha, miaka yote hii natafuta wa kunisaidia kulea mtoto, unajua nani alikuwa akinisaidia? Simtaji hadi unioe”“Nakutania jamani usichukulie serious maneno yangu, usiku mwema.”“Nakupenda Erick, na nitakupenda siku zote za maisha yangu yani leo nalala huku natabasamu kwa kuwasiliana tu na wewe maana sikutegemea kitu cha namna hii. Nakupenda sana”Mama Angel alikuwa akisoma hizi jumbe mara mbilimbili ila ni yeye mwenyewe zilikuwa zikimuumiza maana mumewe alilala muda huo hana hata habari, kisha mama Angel alizifuta zile jumbe na kuweka simu pembeni, ila kitu ambacho kilimpa amani ni kule kugundua kuwa mumewe hajasema swala la kuhudumia mtoto wa Sia, wala hajakubali kuwa mtoto wa Sia ni wake, kisha akalala kwa muda huo.Kulipokucha, na leo baba Angel aliwachukua Junior na Erick na kuondoka nao kuelekea kwenye sehemu yake ya ujenzi kwani bado alikuwa na kazi ofisini na alihitaji sehemu ile isimamiwe kwa ukaribu sana kwahiyo aliwaamini watoto wake hao kuwa watafanya vizuri sana.Basi yeye alifika ofisini na kuanza kazi zake, wakati akiendelea ujumbe kwenye simu yake ukaingi na namba mpya ila aliitambua kuwa ni namba ya Sia,“Umeamkaje Erick kipenzi cha moyo wangu, yani jana usiku nimefurahi sana kuwasiliana na wewe. Hizi meseji zako nazipitia tu leo na zinanipa nguvu sana ya kuendelea mbele, nakupenda sana Erick”Kwakwlei baba Angel alishtuka sana kwani hajawasiliana na Sia kw anjia ya ujumbe kwa siku nyingi sana, kwani siku zote huwa anapuuzia jumbe zake kwahiyo siku hiyo alishangaa sana na kuona kweli Sia ana wazimu, basi akaamua kumpigia simu,“Ila Sia una wazimu au kitu gani? Mimi na wewe tulikubaliana nini kwani? Si ulisema hutoisumbua familia yangu tena, imekuwaje sasa? Unaanza uongo, mimi nimeongea nawe saa ngapi jana na kuhusu nini?”Basi Sia alijaribu kumuelewesha jinsi jana alivyokuwa akiwasiliana nae, kwakweli baba Angel alishangaa sana sababu hakufanya hivyo, Sia akamwambia,“Hadi nilikuuliza umelewa leo?”“Hebu nitumie hizo jumbe yani hata sikumbuki”Basi Sia akamtumia zile jumbe ambazo alikuwa akiwasiliana nae jana usiku, baba Angel alizipitia na kujua moja kwa moja ni mke wake tu, ila hakutaka Sia ajue kuwa ni mke wake ndio kaona, kisha akamwambia,“Sia, mimi na wewe tumemalizana naomba uiache familia yangu na uache kunitumia jumbe za kijinga jinga”Kisha baba Angel alikata simu na kukaa sasa akimtafakari mke wake kuna mke wake ana tatizo gani ambalo yeye binafsi halielewi, alijisemea,“Sijui ni kitu gani unaweza kumfanyia mwanamke naye akaona na kuamini kuwa hakuna mwanamke mwingine unayemuhitaji katika maisha yako zaidi ya yeye, ningejua hiko kitu basi ningemfanyia mke wangu yani anachukia bila sababu ananichunguza bila sababu halafu nampenda sana jamani”Mara madam Oliva alifika ofisini kwa baba Angel ambaye alimkaribisha na kuanza kuongea nae,“Oooh naona na leo umekuja madam”“Yani mimi huwa nikikaa ofisini kwangu na kujiona nimeboreka, naona ni vyema nije tu huku ili tuongee mawili matatu”“Haya, karibu”“Asante, hivi baba Erick ni kitu gani unakipenda kwa mwanamke?”“Dah hilo swali ni gumu sana, ila nadhani siku ukikaa sana na mke wangu halafu muangalie alivyo basi utapata jibu ya swali lako maana ninachopenda kwa mwanamke basi vyote anavyo mke wangu ndiomana nampenda sana”“Oooh mke wako ana raha sana, yani kupata mume kama wewe kwakweli ana raha sana tena ana Bahati sana. Haya, ngoja nikuulize swali jingine ukiambiwa kitu ufanye na mama yako halafu mke wako akakwambia kitu kingine utafanya kipi?”“Sijui lengo lako ni nini kuniuliza maswali hayo, ila katika maisha kila kitu kina wakati wake, kipindi nikiwa mdogo nakuwa chini ya mama na mama yangu ndio anakuwa kila kitu kwangu, ila kwasasa nimeoa basi niko chini ya mke wangu, yani mke anatakiwa kuniongoza mimi ndiomana kuna usemi unakwambia katika maisha kosea vyote ila usikosee ndoa, kwani ndoa ndio inatufanya tuwe jinsi tulivyosasa, mwanamke mwenye busara basi atamthamini mama mkwe wake kama mama yake mzazi kwahiyo atamuheshimu na kumthamini mama yangu, kiasi kwamba mama akitaka jambo na yeye akitaka kwa muda huo huo basi atatumia busara yani hata yeye yupo radhi kusubiri maana anamuona mama kama mama yake, labda mimi mwenyewe tu nikengeuke. Na ndivyo ilivyo kwa mke wangu, yani ndugu zangu ni ndugu zake, wazazi wangu ni wazazi wake, anawapenda, anawaheshimu na kuwathamini halafu kingine mimi ninavyompenda, kumjali na kumthamini mke wangu ndivyo ninavyowajengea chachu ndugu zangu kumjali mke wangu pia, ila mimi nikimchukia hao ndugu watampenda kitu gani kama sio unafki!”“Ooooh baba Erick unaongea, hata sikutegemea. Ila samahani kwa maswali yangu, hivi mwanamke akikutongoza unajisikiaje?”“Kipindi cha ujana wangu, nikitongozwa na mwanamke nilikuwa naona ufahari sana na kumkubali muda huo huo ila tangu nimeoa, basi nikitongozwa na mwanamke nampa onyo kuwa mimi ni mume wa mtu asinisumbue, kama hasikii huwa namueleza kila kitu mke wangu ili naye ajue kilichopo”“Kheee hadi hayo mambo huwa unamwambia mkeo!”“Nisipomwambia yeye nitamwambia nani tena”Simu ya baba Angel iliita na alihitajika kule kwenye ujenzi kwahiyo aliona vyema kuagana na madam Oliva, ila kiukweli huyu madam humfanya asimamishe kazi zake maana akiwa na mazungumzo nae basi hujiona akiongea nae ujinga tu.Junior na Erick wakiwa kwenye usimamizi mahali pale, baba yao alifika na kufanya wenyewe kuanza kuzunguka kidogo kiwanja kile ambacho kilikuwa ni kikubwa sana, ila wakati wanazunguka kuna mtu walimuona akipita na mtu huyu walimfahamu, alisogea kuwasalimia, alikuwa ni Samia, basi Junior akamuuliza,“Samia, kwani kwenu ni huku!! Si uliniambia sehemu nyingine!”“Huku sio kwetu, huku ni kwa bibi yangu mzaa baba. Saivi si tupo likizo basi ndio hivi nipo kwa bibi”“Aaah kumbe, kwahiyo kwa bibi yako sio mbali na hapa?”“Eeeh sio mbali wala nini, ni hapo tu mbele kidogo. Bibi alinituma kumuita kaka yangu ndio nilienda kumuita”Basi yule kaka yake nae alisogea na kumfanya Samia kuanza kuwatambulisha wakina Junior,“Kaka, huyu anaitwa Junior na huyu ni Erick ni kaka zake na rafiki yangu Erica. Jamani huyu ni kaka yangu anaitwa Rahim”Basi wakashikana mikono pale kisha Rahim akatangulia kuondoka na kuwaacha pale wakiwa wamesimama na Samia, ila muda kidogo Erick aliitwa na baba yake kwahiyo alibaki Junior na Samia ambapo Samia aliaga ila Junior aliamua kumsindikiza Samia hadi kwa bibi yake, kwahiyo njiani walikuwa wakiongea,“Eeeh Samia, yani huwa napenda unavyoongea, unavyotabasamu napenda sana. Mimi nakupenda kiukweli”“Kheee makubwa”“Makubwa yapi Samia? Mimi nakupenda, natamani tuwe na mahusiano ila mahusiano ya siri”“Unanipenda kweli?”“Ndio nakupenda”“Baba aliniambia kuwa, ikiwa kuna mwanaume kaja kukwambia anakupenda mwambie akupe pesa”“Kheee hela ya nini jamani Samia? Mapenzi sio pesa”“Hiyo ni kutokana na wewe ila kwa mimi nasema nilichoambiwa na baba yangu, kaniambia kuwa mtu akisema ananipenda nimwambie kuwa anipe pesa”“Kwahiyo nikikupa pesa ndio utanikubali?”“Nitakufikiria”“Jamani Samia mbona unanifanyia hivyo mtoto wa mwanamke mwenzio? Haya basi chukua hii elfu tani ya vocha”Junior alitoa elfu tano na kumpa Samia ambaye aliipokea ila akamwambia,“Hii hela ndogo hainitoshi”“Kheee kwahiyo unataka pesa ngapi?”“Nipe kuanzia laki tano, baba yangu hapendi nije kuolewa na masikini. Kwahiyo ukinipa hela nitajua kuwa wewe ni tajiri na unafaa”“Kheee Samia, unajua wewe bado ni mtoto mdogo!”“Nina miaka kumi na nne, ni mdogo kweli ila hakuna cha kunidanganya maana nishafundishwa kila kitu na ninaelewa kila kitu”“Kwahiyo nikikupa laki tano ndio utanikubalia? Ulishawahi kuwa na mpenzi?”“Sijawahi sababu huwa wanashindwa kutafuta hiyo laki tano ya kunipa mimi kwahiyo sijawahi kuwa na mchumba na nadhani itakuwa hivyo hadi nimalize shule”“Ila unaonekana mjanja sana wewe”Walikuwa wamefika kwa bibi yake Samia, hivyobasi Junior aliagana na Samia pale hukua akiahidi kumtafuta tena tu,“Ukinitafuta tena iwe tunaongelea maswala ya kawaida ila kama unataka kunitongoza bila hiyo laki tano hapana kwakweli”Kisha Samia akaingia kwa bibi yake halafu Junior akarudi kule ambako ujenzi unaendelea na kumkuta Erick,“Ulimsindikiza Samia?”“Ndio, nimempeleka hadi kwa bibi yake, ila wewe naona huwa unamfagilia yule Sarah maana akifika nyumbani huwa lazima umsindikize ila huyu Samia wala huwa hujiangaishi nae”“Aaaah tatizo Sarah nimemzoea sana ila Samia sina mazoea nae kivile wala nini”Baba yao alifika na kuwauliza maswali matatu pale kuwa wanauonaje ujenzi na mengine mengine. Walipomaliza jioni kabisa ndio waliondoka kuelekea nyumbani kwao maana walikuwa wameshachoka.Kwkweli Erick ndio alikuwa anaongoza kwa kuchoka sana ukizingatia bado kukurukakara kama hizi hajazizoea tofauti na Junior kidogo mambo yale kayazoea.Basi kwenye gari ni Junior tu na baba Angel ndio walikuwa wakiongea ongea ila Erick alikuwa amelala muda tu kwa uchovu,“Baba si unaona Erick hajazoea haya mambo, mwambie mamdogo aache kumkalisha ndani hadi Erick kama watoto wake wengine wakike”“Aaaah atazoea tu, ndio kama hivi nampa mpa zoezi la kazi”“Sawa, bamdogo”Basi waliendelea tu na safari ila kichwani kwa Junior muda huo ilikuwa ni kupata tu laki tano ambayo aliona ingemsaidia sana.Leo Angel na bibi yake wakiwa wanajiandaa kulala, Angel alimuomba bibi yake simu kwa siku hiyo ili aweze kuwasiliana na rafiki zake,“Angel, sio ndio uanze kuwasiliana tena na wakina Samir jamani!”“Siwezi bibi, kwanza kile kitabu kimenifungua sana siwezi kufanya hivyo bibi nawasiliana tu na marafiki zangu wa kawaida yani wakina Husna, Yusna, Hanifa nimewakumbuka sana”Basi bibi yake akampa simu na kumfanya Angel afurahi sana na kuanza kwenda nayo moja kwa moja chumbani kwake. Ila bibi yake akamkumbusha jambo moja,“Ila si unajua kuwa huu ni muda wa kulala?”“Najua bibi, nawasiliana nao kidogo tu halafu nakuletea simu”“haya, saa nne kamili ulete simu chumbani kwangu siwezi kuacha uitumie hadi asubuhi”“Hakuna tatizo bibi yangu”Basi Angel alienda nayo chumbani kwake huku akijisemea kuwa siku hiyo kweli hatomtafuta Samir wala nini na alikuwa na mpango kweli wa kutafuta rafiki zake wa kike ila muda alipoiwasha tu ile simu alipokaa kidogo tu kuna ujumbe ukaingia kutoka kwa Samir, hata yeye alishangaa kuwa Samir kajua vipi kuwa kashika simu kwa muda huo, ujumbe ulimwambia“Najua mpenzi unaupata ujumbe wangu muda huu, ni kwamba nakupenda sana”Basi akamjibu kwa kumuuliza,“Umejuaje kama nitakuwa na simu muda huu?”“Ni Mungu tu ambaye ameunganisha mioyo yetu Angel, mimi nakupenda sana”“Mmmh!”“Sasa unaguna nini Angel”“Wewe ungekuwa unanipenda siku ile usingekimbia baada ya kumuona bibi yangu na ungebaki kunitetea”“Aaaah kumbe unahitaji hiyo kitu kutoka kwangu, usifikiri siwezi Angel, yani naweza sana hata kuwa nakuja hapo. Kwani bibi yako hanifahamu mimi? Ananifahamu huyo toka udogo wangu, ila nitaanza kuwa nakuja sasa”“Ndio, onekana kwa bibi na usimuogope ndio nitajua ni kweli unanipenda”“Sawa, hakuna tatizo lolote”Kisha waliendelea kuwasiliana kwa vitu mbalimbalia na kwavile hakuwakuwasiliana kwa siku nyingi kwahiyo wakajikuta wana mada nyingi sana za kuongelea mwisho wa siku Angel alijikuta amelala akiwa na ile simu mkononi.Kuja kushtuka ni wakati pamekucha kabisa, basi aliwasha ile simu na kufuta jumbe zote kisha kuizima halafu alinyata na kuipeleka chumbani kwa bibi yake ambaye alimkuta kashaamka na yupo nje maana bibi yake huwa anawahi sana kuamka.Alivyoiweka ile simu akarudi chumbani kwake na kuendelea kulala, baada ya muda kidogo tu bibi yake alienda kumuamsha,“Wewe Angel hebu amka huko, nadhani ndio umetumia simu hadi usiku sana maana hujanirudishia na umelala mpaka muda huu, simu iko wapi?”“Jamani bibi, mbona simu niliirudisha saa nne usiku kama ulivyosema”“Umeiweka wapi sasa?”“Pale mezani kwako bibi”Bibi aliwaza ila hakuwa na kumbukumbu kama aliangalia mezani, basi alienda chumbani kwake na kweli aliikuta mezani kwake kwahiyo akaona kuwa Angel alikuwa akisema ukweli na kuamini maneno yake.Leo, Angel na bibi yake walitembelewa na mgeni ambaye alikuwa ni mama mkubwa wa Angel, basi walimkaribisha pale vizuri kabisa na bibi Angel alianza kumlaumu,“Yani Mage kuja kwangu siku hizi naona hutaki kabisa hadi usikie mama yako nimekufa!”“Hapana mama, sio hivyo tatizo ni nyie wenyewe yani naona kwasasa maisha yako yote yapo kwa Erica”“Kwanini jamani?”“Nyumbani kwa Erica ndio unapoweza kwenda kukaa hata mwezi ila kwangu huji wala kwa Bite nasikia huendagi”“Hizo lawama sasa, mimi nilienda kukaa kwa Erica sababu ya uzazi. Kwanza nakushangaa unajilalamisha wakati mdogo wako toka ajifungue hujawahi kwenda kabisa, ila upo hapa kulalamika kwanini sikutembelei, ukiacha mambo yako na kuja kunitembelea mimi unapungukiwa na nini? Kumbuka mimi ni mama na nitabaki kuwa hivi, huwezi kukaa chini na kusema mama sijui alifanya hivi basi na mimi nafanya vile, kila mtu atakushangaa kutaka kushindana na mama yako”“Basi nisamehe mama”“Sio basi nisamehe, yani unastahili kuniomba msamaha tena haswaaa. Ni kweli kulikuwa na matatizo baina yetu ila yaliisha, yani nakushangaa sana Mage, wewe habari za ndugu wa baba yako ndio unazo, unaenda huko kuwasalimia muda wote na kufanya nao kila kitu ila kuja kunisalimia mimi unaona shida, mdogo wako kajifungua pale hujaenda hadi leo! Hata Bite na mumewe wamekushinda kwani walikuwa wa kwanza kuja, hata Tumaini kakushinda yani mwanangu umekuwa na roho ya ajabu sana. Ila nishakusamehe tayari maana mtoto akinyea kiganja huwezi kukata”“Jamani mama, nashukuru kwa kunisamehe lakini. Ila leo nimekukumbuka sana, na licha ya kukukumbuka kuna jambo nataka tuongee”“Jambo gani?”Basi Mage alianza kumueleza mama yake kuhusu Derrick na kumuomba awaombe ndugu zake yani Erica, Bite na Tony wakubali kukutana nae na kufanya kikao cha namna ya kumsaidia,“Unaona sasa Mage, hayo ndio mambo unayoyaweza wewe. Sijui Derrick imekuwaje sijui imekuwaje, jamani yule si ana mama yake? Si ana ndugu zake huko watamsaidia”“Ila mama kumbuka kuwa Derrick ni mtoto wa baba yani ni ndugu yetu”“Ndio ni ndugu yenu nyie ila sio mimi, simtambui Derrick mimi. Sijawahi kumtambua na sitomtambua kamwe”“Ila mama kigeugeu wewe, mamake Derrick si aliwahi kufika hapa tena alikuwa anakuja na unaongea nae vizuri tu kumbe una kinyongo hadi leo!”“Sina kinyongo ila usitake kunichanganya tafadhari Mage, usinichanganye kabisa. Kama umepanga kukutana na ndugu zako basi kutana nao uzungumze nao kuhusu hilo ila mimi mniache kama nilivyo, ya kwangu yananitosha”Kiukweli Mage huwa kuna wakati anamshangaa sana mama yake, kuwa anamchukia kiasi hiko mtoto ambaye baba yao alizaa nje ya ndoa, yani Mage hakuona kama kuna sababu ya kumchukia wakati ni ndugu yao ila ikabidi tu abadilishe mada.Muda kidogo alisogea msichana wa kazi kwa Angel na kumwambia kuwa kuna mgeni wake nje, ikabidi Angel atoke ili akaonane na huyo mgeni.Angel alitoka na kushangaa kumuona Ally, maana kwa haraka haraka alihisi ni Samir sababu jana yake aliongea nae kuwa ataanza kumtembelea kwahiyo alishangaa sana kumuona Ally basi ikabidi asalimiane nae na kumuuliza,“Jamani, umekuja hadi kwa bibi yangu!”“Ndio, sababu nakupenda kwahiyo lazima nije ulipo”Angel alitabasamu na kumuuliza,“Kwahiyo Ally unamaanisha unataka kuwa mpenzi wangu?”“Ndio, nahitaji tuwe pamoja”“Wewe si dereva wa bajaji!!”“Haijalishi, leo utaona naendesha bajaji ila kesho utaona naendesha hummer”“Khaaa jamani, wanaume mna swaga duh!! Ila Ally hapana jamani, mimi nina mpenzi”“Aaaah Angel usiseme hivyo, hebu ona tunavyoendana, pale Angel hapa Ally yani mimi na wewe tumeumbiwa kuwa pamoja kabisa”Angel akacheka tu, ila muda huo mamake mkubwa yani Mage alitoka ndani akiwa na bibi yake inaonyesha alikuwa ameaga, ila alipofika pale nje ambapo Ally kasimama na Angel aliwaangalia kwa mshangao na kusema,“Jamani Ally umefika hadi huku kweli kufata mwanamke!”Bibi Angel alishangaa pia na kuuliza,“Kwani ni nani huyu?”Mage alimuangalia mama yake na kusema,“Mama, kuna haja ya Angel kujua ukweli wa uhalisia wake bila hivyo atatembea na ndugu zake na kuleta mabalaa aliyoleta mama yake”Kisha akawaangalia Angel na Ally na kusema,“Nyie ni ndugu wajinga nyie, mmesimama hapo kutamaniana tu”Angel na Ally walishangaa sana kusikia kuwa wao ni ndugu. Mage alimuangalia mama yake na kusema,“Mama, kuna haja ya Angel kujua ukweli wa uhalisia wake bila hivyo atatembea na ndugu zake na kuleta mabalaa aliyoleta mama yake”Kisha akawaangalia Angel na Ally na kusema,“Nyie ni ndugu wajinga nyie, mmesimama hapo kutamaniana tu”Angel na Ally walishangaa sana kusikia kuwa wao ni ndugu.Basi waliuliza kwa mshangao,“Sisi ni ndugu!!”Bibi yake Angel aliingilia kati pale ili yule mwanaume aondoke,“Wewe kijana ondoka nyumbani kwangu sitaki ujinga, halafu Angel rudi ndani”Ila bado Angel na Ally walisimama pale pale kwani walitaka kusikia ile kauli juu ya undugu wao iko vipi, ikabidi bibi aongee kwa ukali zaidi na ambapo alivyoona hawamsikii akamshika Angel mkono na kumuingiza ndani kisha alifunga mlango kwa nje ili Angel asitoke kabisa, kisha alivyotoka nje akamtimua Ally na kumvuta Mage kwa pembeni na kuanza kuongea nae,“Wewe Mage wewe, wale ni ndugu kivipi? Badala uwafokee wewe unasema ni ndugu!!”“Ni ndugu ndio mama, ni sababu tu Ally kafanana na mama yake, ila huyo Ally pia ni mtoto wa Rahim”“Kheee huyo Rahim alikuwa anazaa zaa hovyo hovyo eeeh!”“Ndio, Rahim ana watoto wengi sana. Kwahiyo kuna umuhimu mkubwa sana wa Angel kuujua uhalisia wake, la sivyo atatembea na kaka zake”“Ila Erica hataki kabisa hilo lifanyike, hataki Angel atambue ukweli”“Mama, hata sisi tumwambie tu Angel ukweli. Unajua haijalishi baba wa mtoto alikufanya nini ila kuna ulazima wa mtoto kutambua baba yake halisi ni nani, kwahiyo kama Erica hawezi hata sisi tumwambie Angel”“Mmmh mwanangu, unajua mapenzi ya watu tena. Erick na Erica wenyewe walikubaliana juu ya Angel halafu sisi tufungue midomo mipana kama funiko la choo kumwambia Angel kuwa baba yako sio Erick ni Rahim! Jamani itakuwa tuna wazimu eti”“Ila mama kwani siri hapo iko wapi, hivi huyo Angel hakuna hata kimoja alichofanana na Erick, halafu mseme mnatunza siri, hadi lini mambo hayo? Mwambieni Angel ukweli na aamue mwenyewe kusuka au kunyoa ila mwambieni ukweli kuwa Erick sio baba yake mzazi. Kwanza namshangaa sana Erica, yani mtoto baba yake mzazi ni mwingine halafu kaenda kumuandikisha jina la mwanaume mwingine! Yani mapenzi ni uchizi sana, kuna mambo mtu anafanya kama anawazimu vile”“Ngoja nikuombe kitu mwanangu, naomba kuhusu hilo uwe na busara na uwe mstahimilivu, hebu kwanza kumbuka mdogo wako wakati ana mimba ya Angel alikuwa na hali gani? Hakuwa na raha kabisa mpaka nimembamba akajifungua, baada ya hapo ni kulia tu kila akikaa mwenyewe chumbani basi ujue analia na kumkuta amevimba macho tu, ila Mungu ni mwema akatokea Erick na kumfuta machungu yote na kuanza kumlea Angel na kumuhudumia kama mwanae, je Erica angefanyeje zaidi ya kutimiza matakwa ya Erick na kumuandika Angel jina la Erick? Unadhani Erica angefanyeje? Alikuwa kwenye wakati mgumu sana, nilimsema mno nakumbuka ila badae nilielewa ni kwanini alifanya vile. Huyo Rahim si ndio wale wanaume wanaozaa hovyo na kusema mtoto akikua basi atanitafuta, hivi huwa inatokeaje kwa wanaume wa aina hiyo? Si ndio mama anaamua tu kumpa mtoto ubini wake! Sasa kama huyo Rahim ana watoto wengi basi ni lazima mwisho wa siku watoto wake wataoana tu”“Ila mama umeongea mengi sana, sema mada yangu sio hiyo ila mada yangu ni Angel aujue ukweli”“Sasa ukweli huo ataambiwa na mama yake na sio sisi watu wengine, nadhani umenielewa Mage? Tafadhari muache Erica afanye maamuzi yake mwenyewe kwa watoto wake”“Mmmhhh”“Usigune, ndio hivyo. Mwache mdogo wako afurahie ndoa yake na watoto wake, muda ukifika na akiamua kusema ukweli basi atausema tu”Muda huu bibi Angel alighairi hata kumsindikiza Mage kwahiyo Mage aliondoka mwenyewe na bibi Angel alirudi nyumbani.Kisha bibi Angel moja kwa moja alienda ndani na kumkuta Angel kajiinamia tu, basi akamsogelea na kumuuliza,“Angel mjukuu wangu jamani tatizo ni nini kwani?”“Nahitaji kujua ukweli bibi, yule Ally ni ndugu yangu kivipi? Je naye ni mtoto wa baba?”“Mwanangu, huyu mamako mkubwa usimuone hivi ni ana matatizo mengi sana, kwanza ushawahi kumuona akija kwenu mara kwa mara?”“Huwa haji”Mara simu ya bibi Angel ikaanza kuita, kuiangalia aliyekuwa anapiga ni Mage, basi akaipokea na kuanza kuongea nayo,“Kwakweli mama, mimi sina amani natamani Angel aujue ukweli yani sina amani kabisa. Narudi mama kumwambia Angel ukweli”“Kwani uko wapi muda huu?”“Nipo stendi ila narudi, nahitaji Angel aujue ukweli jamani mama mtamficha Angel hadi lini? Inapaswa mtoto ajue ukweli”“Ila Mage una wazimu au ni kitu gani lakini”“Hapana mama ila lazima Angel ajue ukweli”Mage akakata simu, yani kwa muda huo bibi Angel hakuelewa cha kufanya na kuhisi kama kuchanganyikiwa kwani hakuona kama ni sahihi kwa wao kumwambia Angel ukweli wakati wazazi wa mtoto wapo.Basi na Angel nae akaendelea na maswali kwa bibi yake,“Nielezee basi bibi”“Mjukuu wangu, natoka kidogo nikirudi nitakuja kukwambia uchizi wa huyu mamako mkubwa”Kwa muda huo aliona kitu pekee cha kumzubaisha nacho Angel ni simu, basi akampa Angel simu na kweli Angel alifurahi sana na kwenda nayo chumbani kwake. Muda huo bibi Angel aliwahi kutoka nje ili akutane na Mage, na ile anafika tu nje na Mage nae alikuwa amefika, kwavile bibi Angel alikuwa amechukizwa akamnasa Mage kibao na kumwambia,“Hivi wewe mtoto una nini lakini? Kwanza huna mazoea ya kwenda kwa mdogo wako ingawa mdogo wako hakujali chochote kuhusu kwako na kuja mara kwa mara ila wewe huna mazoea”“Kwani kwani kuna nini?”“Unafikiri kuwa na watoto wengi vile kama timu ya mpira kuna mgeni yoyote anapenda? Ulikuwa nao wanne na sasa una watoto sita Mage, kuna mgeni anapenda? Na bora ungekuwa na nyumba kubwa, kwa nyumba gani ile mgeni anarundikana na mitoto yote chumbani”“Mama, sasa naona umeamua tu kunidhalilisha. Kwani kuwa na watoto wengi ni dhambi? Mume wangu tumetulia nae kwa miaka na miaka, kwanini nisimzalie akafurahi! Kwahiyo ndiomana unaenda kwa Erica sababu ana jumba kubwa, ila huo ni ujinga kwani hilo jumba ataikwa nalo! Mnaacha kumwambia Angel ukweli sababu ya mali za huyo Erick, kama mali Angel akazitafute kwa babake huko mwenye watoto kama kumbikumbi ila sio kujidanganyishia kwa Erick, na yule mwanao alivyo na wivu najua pale hata asikie Erick ana mtoto mwingine atatamani hata kujiua na kusahau yote ambayo Erick amemtendea yeye. Jamani hebu muhurumieni na huyo Erick, kashamlea sana huyu Angel, kwanza nilivyomkuta kwako huku nimeshukuru Mungu, kuna siku Erick atambaka huyu Angel kufidia mali zake”Mama yake akamzaba tena kibao na kumwambia,“Hivi wewe Mage una wazimu au kitu gani? Sikia nikwambie, kuolewa ni Bahati ila kuolewa na mwanaume kama Erick ni Bahati zaidi, hebu muache mdogo wako aishi kwa amani. Kwahiyo yale maisha ya kwenda huko kijijini na kufanyiwa mila ulikuwa unayapenda? Hebu muache, Erick kamkubali mwenyewe mtoto, na yeye mwenyewe alisema kuwa mtoto awekwe jina lake na siku zote anamjali na kumpenda, huyo baba yake angafanya nini?”“Ila mama, nashukuru kwa vibao ulivyonipiga wala siwezi kuvirudisha kwani wewe ni mama yangu, ila mimi nitasimama kwenye ukweli tu Angel lazima amtambue baba yake. Hata kama ukinizuia leo jua kuna siku nitakuja na kumwambia Angel ukweli kuhusu baba yake mzazi”Kisha Mage akaondoka, kwakweli mama yake akasikitika sana na akaona kuna umuhimu wa kumwambia mwanae Erica ili ajue kuwa dada yake anataka kufanya nini yani bibi Angel aliingia ndani akiwa na mawazo sana ila kitu kikubwa alichowaza ni swala la kumpa Angel simu kwa muda huo, akawaza huenda Angel akimuuliza mama yake kuhusu lile swala basi mama yake anaweza kupaniki ni bora yeye mwenyewe kumueleza mama yake Angel ilivyokuwa kwahiyo aliona ni vyema akamnyang’anye Angel ile simu.Angel alitulia na simu yake huku akiwasiliana na watu mbalimbali na siku hiyo akabahatika kuwasiliana na Mussa pia,“Nimekukumbuka sana Angel”“Unajua mimi ni shemeji yako kwa Samir”“Aaaah Angel, achana na Samir kwakweli utajutia, ni ndugu yangu yule namjua vizuri tu. Unamuona Samir kuwa kijana mwenzio ila ana mambo makubwa kushinda huo ujana wenyewe, kwakweli Angel huyo Samir hakufai kabisa”“Mmmmh!”“Usigune Angel, lini tukutane tuyajenge?”“Aaaah mimi naishi kwa bibi halafu siruhusiwi kutoka kwahiyo ni ngumu kwa sisi kukutana”“Nielekeze kwa bibi yako basi nije”Wakati huo kuna ujumbe uliingia pia kutoka kwa Samir ukisema,“Angel mpenzi wangu nimekukumbuka kweli yani, sijui nije lini kukuona”Sasa Angel hakusoma vizuri na kujua ni Mussa ndio kaandika vile basi akajibu na kumwambia,“Mussa, acha zako jamani uje wapi wakati huku hupajui?”Muda huo huo Samir alianza kupiga simu maana tayari na yeye alishahisi kuwa Mussa bado anamnyemelea mpenzi wake, ila muda huu bibi Angel nae alienda chumbani kwa Angel na kumtaka ampe ile simu, basi Angel hakuwa na namna aliizima tu na kumpa bibi yake kisha akamuuliza,“Eeeh bibi kwahiyo hujanimalizia mambo ya mamkubwa Mage”“Aaaah ila Angel nimekumbuka kile chakula chako cha siku ile, naomba unipikie tena mjukuu wangu”Kwahiyo bibi aliamua kumzuga Angel kwa namna hiyo kwani alijua lazima kile chakula kitachukua muda wake wa kutosha kisha akamwambia kuwa akimaliza kupika atampa simu ili aendelee kuwasiliana na marafiki zake, kwakweli Angel alifurahi na kwenda kuanza kupika ila wakati huo tu akafika mama Junior yani mama mkubwa mwingine wa Angel, basi walifurahiana pale kisha mama Junior alienda kumsalimia mama yake ambaye alifurahi sana na kusema,“Naona leo nimekumbukwa sana jamani, wanangu mmeniota nini?”“Aaaah mama jamani, nimekukumbuka tu”“Haya, karibu mwanangu tena bora umekuja maana nina dukuduku hatari”“Lipi tena hilo mama?”“Niambie kwanza ya kwako”“Ya kwangu ni kuhusu dada Mage na habari zake za Derrick, kiukweli huwa simuelewi kabisa Mage akianza habari za huyo mtu”“Kwanza nikukatishe, twende nje kuzungumza hayo”Basi mama Junior alitoka nje na kuamua kuaga kabisa kwani muda nao ulikuwa umeenda kwahiyo aliona ni vyema kuongea na mama yake nje na kuondoka moja kwa moja.Walipofika nje ndipo walipoanza kuongea,“Kwanza huyo Mage kaniudhi hatari, bora umekuja nikwambie hili dukuduku na ujue cha kufanya”Kisha bibi Angel alianza kumuelezea mama Junior mambo yote yaliyotokea siku hiyo, muda huo walikuwa wakiongea huku wakitembea kuelekea stendi na walifika mahali wakasimama, bibi aliamua kufanya hivyo ili Angel asisikie yale maongezi yao, basi alivyomueleza kila kitu mama Junior akamwambia,“Mama, kwahiyo tumekuja kuongelea huku barabarani kwanini lakini wakati tungeweza hata kuongea chumbani kwako au hata nje ya geti?”“Nimehofia mwanangu, Angel asije akatusikia”Mama Junior alicheka na kusema,“Jamani mama, unajua Angel hana tabia za kimbea hata kidogo yani yule mtoto anaishi kizungu, umbea ni mtu ampelekee mwenyewe. Hapo angekuwa Erica uwiii hata huku barabarani angekuja kutusikiliza tu, kitoto kimbea kile nahisi hadi anakaribia kupewa medali. Jana niliongea na mama yake anasema Erica akiwa na umbea asiposikilizwa basi anaanza kuongea mwenyewe, yani angekuwa Erica ningekwambia wazi kuwa hakuna la kuficha ila kwa Angel hakuna tatizo lolote maana Angel sio mfatiliaji wa mambo yasiyomuhusu”“Ila haya yanamuhusu mwanangu!”“Hata kama, bado Angel hawezi kuja kutegesha sikio sehemu asiyoitwa kuja kusikiliza mazungumzo yani Angel hayupo hivyo, na kuhusu huyo Mage tulia mama yani tulia kabisa, wote ndani hatumuwezi Mage maana akiamua lake kaamua ila kiboko yake ni mama Angel tu. Nitamueleza mama Angel kila kitu hata usihofu na huyo Mage ajipange maana mama Angel ndio huwa wanawezana wale. Unafikiri mama unaweza kumwambia chochote Mage akakuelewa akishaamua lake? Huwa haelewi kitu, ila unadhani ni kwanini hajasema ukweli wa kuhusu Angel hadi leo? Tulia mama, tena ngoja nianze na hilo halafu hili la Derrick litafatia. Rudi tu nyumbani mama ngoja niondoke mimi”Basi wakaagana pale na bibi Angel akarudi zake nyumbani kwake.Baba Angel akiwa nyumbani leo ilibidi amuelezee mke wake kuhusu ujenzi unaoendelea maana kila siku amekuwa akiondoka na wakina Junior halafu mkewe anajua tu kuna ujenzi ila hajui ni sehemu gani,“Mke wangu, ngoja nikuelezee kuhusu ujenzi unaoendelea”“Kwanza ni ujenzi wa nini?”“Unajua unapoamua kuwa mjasiriamali basi lazima uwe mbunifu yani ujaribu kuona vitu vinavyoingiza hela zaidi, nimefanya sana biashara za maduka ya nguo za watoto, nimefanya sana biashara za magari ila pale ninajenga kiwanda kidogo kwa kuanzia kwani nimeona uhitaji wa watu wa eneo lile. Ila nataka pia kuanza kumfundisha Erick ili asiwe mzembe, nahitaji Erick awe kama mimi”“Oooh ni vizuuri ila ni eneo gani hilo?”Baba Angel alimtajia eneo ambalo anafanya ujenzi huo na kumfanya mama Angel ashtuke sana, basi mumewe akamuuliza,“Mbona umeshtuka hivyo mke wangu?”“Mmmh sijui, unajua nini hiyo sehemu ndio ambako wanaishi yule mr.Peter na mke wake”“Unamaanisha wazazi wa Rahim?”“Ndio”“Aaaah watajijua wenyewe, cha muhimu sie tunafanya mambo yet utu. Yani tusindwe kutafuta sehemu bora za biashara sababu yao! Watajijua wenyewe”Huwa baba Angel hapendi kufanya akili yake iwaze mambo kama hayo yani huwa hapendi kabisa ukizingatia ana mambo mengi ya kuwaza.Wakati wote wameondoka nyumbani kwa siku hii, alibaki tu mama Angel na Vaileth na muda huu Erica alikuwa amelala ila mama Angel alipigiwa simu na mama Junior ambaye alimpa habari ya dada yao mkubwa Mage, basi aliamua kwenda chumbani kuongea nae,“Hivi kwani dada ananitakia nini mimi jamani? Unajua mistake kunikumbusha mambo ya ajabu ambayo mnataka kunifanyia, hivi mtoto wangu wa kwanza si angekuwa wa Erick kama msingeenda kunitoa ile mimba? Sasa tatizo liko wapi nikimpa Angel Erick? Na hata isingekuwa hivyo bado Erick yupo upande wangu sana, kaifuta aibu yangu na fedheha, tatizo liko wapi nikimtunuku mtoto ambaye baba yake haeleweki. Yeye kinamuuma nini ikitokea Angel katembea na kaka yake? Kwanza asinichanganye kabisa, huyo Rahim ana watoto kila kona ya nchi halafu na mwanangu nimdumbukize huko, halafu huyo dada Mage, ni siku nyingi haji kwangu kumbe ana yake ameyatunza, anitolee balaa mie”Basi aliongea nae ila mama Angel alichukia sana ila hakutaka hata kumpigia simu kwa siku hiyo dada yake.Alivyokata ile simu alirudi sebleni, na kutoka nje ila alimkuta Vaileth amejiinamia tu basi alianza kumuuliza pale kuwa tatizo ni nini,“Yani huko nyumbani wamenipigia simu kuwa mvua zimeanza na nyumba ya wazazi wangu inavuja, natamani ningekuwa na pesa niwaweke bati wazazi wangu”“Oooh pole jamani Vaileth, ila usijali nitajadili na mume wangu jioni ya leo”“Oooh asante sana mama, nashukuru kwa hilo ila pia mama kuna ndoto ambazo sio nzuri nazipata”“Ndoto gani hizo Vaileth?”“Samahani mama kama nitakukwaza, ni kuhusu huyu madam Oliva, yani nikilala nahisi kama kuna mambo anataka kumfanyia baba, nahisi kama anataka kumvuta baba”“Mmmh asante kwa ujumbe Vaileth”Kisha muda huo huo mama Angel alirudi ndani kwani aliona akili yake ikianza kuchanganyikana sasa.Baba Angel akiwa kazini siku ya leo akiendelea na kazi zake, mara kama kawaida alifika madam Oliva na kumsalimia pale huku akijiongelesha mambo mbalimbali kisha akatoa bakuli ambalo aliweka matunda, ni kweli yale matunda yalikuwa yanavutia sana kiasi cha kumfanya baba Angel kuyatamani, basi madam Oliva huku akitabasamu akamwambia,“Leo nimeona utakuwa na hamu sana na matunda baba, nimekuletea haya”“Oooh nashukuru sana madam Oliva”“Ni matamu sana, hebu onja kidogo”Mara simu ya baba Angel kuna ujumbe uliingia, basi akaangalia na kuona kuwa ujumbe ule umetoka kwa mke wake basi alianza kuusoma,“Erick nakuomba mume wangu usiwe karibu na madam Oliva, nakuomba sana usile chochote kile anachotaka ule. Kama unataka chochote utakipata nyumbani mume wangu, nakupenda sana”Kwanza kabisa baba Angel alitabasamu kwani ujumbe wa namna hii umekuwa adimu sana kwake toka kwa mke wake toka wawe ndani ya ndoa, kwahiyo akajikuta anafuraha sana kisha akamuangalia madam Oliva na kumwambia,“Oooh madam samahani, nimekumbuka kitu jamani dah! Uroho huu, kumbe nimefunga leo”“Khaaa kumbe huwa unafunga baba Erick! Ila kwenye kufunga wanasema ukitamani kit utu umefungulia kwahiyo ni bora ule tu”“Aaaah hapana bhana, mimi nishakubaliana na mke wangu kuwa tutafungulia jioni nikiwa nyumbani, hata kama nimetamani basi nitatubu tu mbele za Mungu ila kula siwezi kwakweli, nisamehe sana madam”“Mmmh jamani, sawa basi”Madam Oliva hakutaka hata kukaa zaidi kwani aliaga na kubeba bakuli lake la matunda na kuondoka zake.Baba Angel alikaa kwa muda akimtafakari mke wake, yani alijihisi amani kubwa sana katika moyo wake na kujisemea,“Oooh leo nitaenda tena kwenye duka lile kumnunulia mke wangu zawadi”Na muda huo huo aliinuka na kutoka ofisini kwake, na moja kwa moja alipitia kwanza kwenye lile duka kununua zawadi halafu ndio aende kwenye ujenzi, aliwakuta baba Emma na Mama Emma wapo kama kawaida ila hawa wana ndoa nao walionekana kufurahiana sana kuwa pamoja na kufanya shuguli pamoja, basi walimkaribisha vizuri sana na moja kwa moja aliongea nao kuwa anahitaji zawadi nyingine ya mke wake, basi baba Emma akamshauri,“Leo mchukulie mkoba, anaweza kuwa na mikoba mingi sana ila utakaomchukulia wewe ndio atauona maridadi. Na ubora wa mikoba yetu ya hapa ni lazima mke wako apende”Baba Angel akatabasamu na kuuliza,“Sasa nitamchukulia mkoba gani jamani!”Baba Emma alionyesha mkoba ambao hata mama Emma aliupenda na hata baba Angel aliupenda pia basi walimfungia na kuondoka nao kwani alitaka kumpelekea mke wake.Junior na Erica kwenye ule ujenzi, muda mwingi Junior alionekana na mawazo kiasi na kumfanya Erick amuulize,“Kwani tatizo nini Junior?”“Hivi katika maisha yako umewahi kupenda?”“Ndio kusema unampenda hivyo dada Vai?”“Nampenda ndio ila…!”Baba Angel alifika muda ule na kuangalia nao ujenzi na kufatilia ya hapa na pale kisha baada ya hapo kuwataka wote warudi nyumbani.Walipofika nyumbani tu baba Angel alimkabidhi mke wake ile zawadi na kumfanya mke wake afurahi sana,“Asante kwa zawadi mume wangu, naona siku hizi unapatia sana ninavyovipenda”“Ndio, sababu wewe ni mke wangu wa pekee”Mama Angel alikuwa akitabasamu tu kisha mumewe akamwambia,“Unajua ujumbe wako wa leo umenihamasisha sana, jamani mama kuwa hivi hivi kwangu na ikiwezekana ongeza zaidi ili nipagawe mtoto wa mwanamke mwenzio”Mama Angel alicheka na muda huo aliamua kumwambia pia swala la Vaileth ila sababu baba Angel alikuwa na furaha sana akamwambia mke wake,“Kuna hela nilitaka kwenda nazo kesho mahali, ila naenda kumpatia Vai ili atume kijijini kwao, maana kumbuka tuliahidi kumsaidia, naomba mke wangu usikatae”“Mmmh sikatai, ni kiasi gani?”“Milioni mbili”“Jamani yote hiyo mume wangu!”“Aaaah jamani mke wangu kumbuka huyu kabeba dhamana zetu, huyu anatutunzia nyumba yetu kwasasa, anatuandalia chakula na kutufanyia mambo mengi sana”Kisha baba Angel alimsogelea mke wake na kumbusu halafu akamuuliza tena,“Tumpe ngapi mke wangu?”“Hakuna tatizo, mpe tu hiyo uliyosema”Basi baba Angel alimkabidhi ile pesa mke wake ili akampe yeye mwenyewe, kwahiyo mama Angel alitoka na kwenda kuongea na Vaileth na kumkabidhi ile pesa, kwakweli Vaileth alifurahi sana maana aliona kama ndoto vile.Vaileth alimshukuru sana baba Angel na mama Angel kwa moyo wao wa kipekee sana.Usiku wa siku hiyo, wakati Junior yupo na Vaileth, alimuona akiwa na furaha sana na kumuuliza kilichomfyrahisha vile basi Vaileth alimueleza kile kilichotokea kuhusu pesa aliyopewa na bosi zake,“Oooh jambo jema hilo mke wangu jamani, ila kuna kitu nataka nikuombe”“Kitu gani hiko?”“Katika hiyo hela naomba unikopeshe laki tano maana kuna mambo ya maendeleo nataka kufanya ila niliwaza kuwa pesa nitapata wapi, sema Mungu ni mwema sana naomba unifanyie hivyo Vai”“Mmmh jamani Junior!”“Kwani hunipendi Vai!”“Nakupenda sana Junior”“Basi naomba nifanyie hivyo”Vaileth hakuwa na namna zaidi ya kumpa hizo laki tano Junior ambaye alifurahi sana na siku hiyo alimpa Vaileth mapenzi mazito sana maana hela aliyokuwa akiitaka aliipata tayari.Kulipokucha tu siku hiyo Junior na Erick waliondoka mapema sana kwani walitakiwa kuondoka na dereva ila baba Angel alikuwa bado kalala kwani hakupanga kuwahi kwa siku hii.Ile asubuhi mama Angel aliongea na mumewe wakati akijiandaa kwenda kazini,“Ila unajua mume wangu hatujafanya kitu kizuri kumpa pesa mkononi Vaileth”“Sasa tungefanyeje mke wangu?”“Yani tulitakiwa kuongea nae halafu tuwatumie wazazi wake moja kwa moja na kama nyingine ya kumuwekea tumuwekee ila hivi tulivyofanya hatujafanya vizuri maana yeye mpaka aende kutuma kwenye simu huko, wakimuibia je!”“Nimekuelewa mke wangu, ila hakijaharibika kitu muite Vai akupatie ile pesa ili mimi nikaweke kwenye simu yako kisha wewe utamtumia kwa namba za ndugu zake hapa au tufanyeje?”“Sawa mume wangu”Basi mama Angel alienda kumuita Vaileth na kumwambia,“Vai, naomba ile hela ya jana ili tuitume moja kwa moja”Vaielth alipumua na kuangalia tu chini kimya Basi mama Angel alienda kumuita Vaileth na kumwambia,“Vai, naomba ile hela ya jana ili tuitume moja kwa moja”Vaielth alipumua kwanza huku akimkodolea macho tu mama Angel.Mama Angel alimshangaa na kumwambia tena,“Wewe Vai hunisikii au ni kitu gani?”“Nakusikia mama”“Sasa unangoja nini kutekeleza?”Vaileth akaondoka na kwenda chumbani kwake na kuzitoa zile milioni moja na laki tano huku akiwaza kuwa itakuwaje, aliwaza kwa muda sana kule chumbani hadi mama Angel alimuita tena kwa nguvu na kurudi na zile pesa, basi mama Angel akamuuliza,“Vipi wewe upo sawa?”“Nipo sawa mama”“Haya, zilete”Muda huo baba Angel alitoka chumbani pia na aliuliza,“Zipo zote?”Vaileth alijiuma uma tu na kujibu,“Zipo milioni moja na laki tano”Mama Angel alishangaa sana na kumuuliza,“Laki tano nyingone iko wapi?”Vaileth aliinama tu chini bila ya kujibu chochote, basi baba Angel akasema,“Itakuwa kaiweka kwaajili ya matumizi yake”“Matumizi gani ndani ya nyumba hii laki tano jamani! Eeeh Vain i matumizi gani hayo?”Vaileth alikuwa kimya tu, kiukweli hata jinsi ya kuanza kujieleza hakujua kuwa aanzie wapi maana wakimwambia hata alete wazione ni kazi bure maana hana hizo pesa, basi baba Angel ikabidi akate yale maneno na kumuomba mke wake asifoke sana kisha akachukua zile pesa na kuondoka nazo ili kwenda kufanya kama ambavyo aliahidi.Walibaki mama Angel na Vaileth sasa ambapo mama Angel alimwambia Vaileth,“Vaileth, mimi ndio ningekuwa wewe nimepata kazi mahali kama hapa ambapo mabosi wana upendo basi ningepatumia kama njia kwangu ya kupata maendeleo. Unashindwa kusema kuwa jamani ninahitaji kitu Fulani au kitu Fulani unashindwa Vai? Unashindwa hata kusema naomba mnifungulie akaunti ili niweke japo hela zangu humo kuna leo na kesho ujue, unatakiwa kujiandaa katika maisha. Shauri yako, kaa na pesa upigiwe simu zisizoeleweka kukukopa hizo hela, oooh nimekumbuka kitu kwanza simu yako ninayo mimi taarifa za ndugu zako ulizipata wapi?”“Niliwapigia kwa simu hiyo ya mezani mama”Basi mama Angel alienda ndani kwake na kutoa ile simu ya Vaileth na kumkabidhi maana tangu ameichukua kipindi kile hakuirudisha.Leo walivyofika tu kwenye ujenzi baada ya muda kidogo Junior aliondoka, yani hata Erick hakujua kuwa Junior ameenda wapi ila muda huo Junior moja kwa moja alienda kwa bibi yake Samia ili kuonana na Samia.Alifika pale na kugonga geti halafu akaamuulizia Samia ambaye aliitwa na kutoka ndani na kumkaribisha junior,“Karibu sana Junior”“Asante, nakupenda sana Samia”“Oooh kumbe hunielewi au? Nilikwambia kunitongoza mimi ni laki tano”“Nimekuletea Samia”“Wow, iko wapi?”Junior akamtolea Samia hela ambayo alienda nayo kwa lengo la kumpa na Samia akafurahi sana kisha Junior akamwambia,“Sasa Samia, inatakiwa mimi na wewe tupate sehemu ya kuzungumza vizuri ili tuyajenge”“Sehemu gani?”“Ikiwa guest itapendeza zaidi”“Mmmh guest? Hapana, siwezi kupelekwa guest mimi”“Kwahiyo wapi unataka?”“Nataka twende labda hotelini”“Mmmh jamani Samia mbona unapenda vitu vya gharama hivyo?”“Sababu na mimi ni wa gharama, baba yangu huwa ananiambia kuwa mimi ni wa gharama sana. Ngoja nikutajie hoteli ya kwenda, sitaki za ajabu ajabu”“Mmmh hoteli gani hizo?”Samia akamtajia na kumfanya Junior ashtuke kidogo ambapo Samia akamwambia,“Yani nimekutajia hoteli ya chumba cha kulala laki moja umeshtuka hivyo ningekutajia zaidi je ingekuwaje?”“Hamna Samia, sijashtuka kwa ubaya mpenzi wangu. Ila Samia ni kweli hujawahi kuwa na mahusiano wewe? Hujawahi kulala na mwanaume?”“Ndio sijawahi, unanionaje kwani? Mimi siwezi kuwa na mwanaume mtu mzima, na wanaume wadogo wengi hawana hela, huwa nikiwaambia waniletee laki tano wanajiuma uma ila naona wewe umeweza, na kwa hakika utakuwa mpenzi wangu tu”“Basi Samia, naomba Jumamosi hii tukutane”“Aaaah sio Jumamosi, fanya Ijumaa maana Jumamosi nahisi kamavile baba atakuwepo”“Sawa hakuna tatizo, basi Ijumaa tutakutana ila naomba umaanishe Samia”“Usijali, tutakuwa tunawasiliana basi”Na muda ule Samia akampa Junior namba anayotumia kwa siku hizo na kumfanya Junior afurahi sana basi waliongea sana pale na kuagana ambapo Junior akamwambia Samia,“Jamani hata kunikumbatia au kunibusu?”“Mmmh haiwezekani kwa muda huu, itawezekana Ijumaa”Basi Junior hakuwa na namna ila alichotaka ni kumpata Samia tu, yani yeye alihisi kuwa akishalala nae tu basi ataridhika na roho yake.Alirudi kule kwenye ujenzi na kumkuta Erick na baba Angel basi baba Angel alimuuliza,“Kheee Junior ndio ushazoea huku na kuanza kuzurula?”“Hapana bamdogo ila kuna rafiki yangu hakai mbali na hapa nikaona ni vyema nikienda kumsalimia”“Oooh sawa hakuna tatizo”Basi waliendelea na kazi ndogo ndogo za pale na walipomaliza tu waliondoka na kurudi nyumbani.Wakiwa njiani kurudi nyumbani, leo Erick alimuona Elly na binti mwingine ambaye alikuwa kama kipofu ila Erick hakumshtua baba yake kuhusu hilo na kukaa kimya tu hadi wanaingia nyumbani kwao hakusema lolote kama kuna mahali kamuona Elly.Basi usiku wa leo, baba Angel aliwaita Junior na Erick na kuwaambia kuwa kesho yake watapumzika kwenda kwenye ujenzi halafu wataenda tena kesho kutwa,“Kesho Alhamisi mtapumzika ila Ijumaa kuna kazi kubwa kidogo kwahiyo inabidi twende mapema sana, yani Ijumaa hata mimi sitaenda ofisini”Waliitikia pale ila Junior alikuwa na miadi yake Ijumaa kwahiyo aliwaza jinsi gani ataikwepa siku ya Ijumaa ili aweze kwenda kukutana na Samia na hata hivyo alihitaji pesa za kufanya hivyo, basi akiwa anawaza baba Angel akawaambia jambo lingine,“Ila Ijumaa baada ya kazi ile nitawapa pesa ili Jumamosi kila mmoja akajinunulie kitu anachokitaka”Ile ilikuwa ni habari njema sana ila kwa upande wa Junior kidogo haikukaa vizuri kwani alikuwa na mawazo mengi sana juu ya Samia ila aliitikia tu kwani aliwaza kumshawishi Samia ili wakutane Jumamosi.Kwahiyo baada ya kuwaambia hayo kila mmoja alirudi chumbani kwake, na Junior kitu cha kwanza kabisa ni kuwasiliana na Samia ili amsikie atasemaje,“Samia mpenzi wangu, naomba tuonane Jumamosi”“Mmmh si nimekwambia Junior kuwa Jumamosi haitawezekana, ni Ijumaa tu”“Unajua Ijumaa kuna dili la hela nyingi sana nataka kufanya ili Jumamosi nikununulie zawadi nzuri sana Samia”“Oooh sasa utaangalia mwenyewe kati ya hilo dili na mimi kipi ni cha muhimu, kwahiyo utaamua kama kukutana na mimi au kwenda kwenye hilo dili. Sina maneno mengi mimi nimemaliza”“Mmmh jamani Samia mbona unakuwa hivyo!!”“Sio kosa langu ila ni baba yangu ndio kanifundisha jinsi ya kumchunguza mwanaume”“Mmmh ila jaribu basi iwe Jumamosi”“Nishakwambia Jumamosi haiwezekani mbona hunielewi Junior!”“Basi malkia wangu, tutakutana Ijumaa”Yani muda huo akili ya Junior inagonga mwamba tu kila muda, kiukweli hakuelewa kabisa cha kufanya kwake ilikuwa moja haikai wala mbili haikai akajikuta siku hiyo hata anasahau kwenda kulala chumbani kwa Vaileth wakati ni kawaida yake kwenda kulala chumbani kwa Vaileth.Alijikuta akiwa na mawazo hadi usingizi ulimpata na kushtuka wakati pamekucha kabisa, akawaza cha kufanya kwa muda huo,“Nitapata wapi hiyo laki moja ya kukodi chumba? Ila lazima niipate maana kale kajinga kashamaliza laki tano yangu! Na nikimpata huyu binti atasimulia ukoo wake mzima”Basi likamjia wazo kuwa aende kwa mama yake kumuomba hela ila hakuwa na uhakika kama mama yake angempatia pesa kwa siku hiyo, yani akachekecha akili yake sana, akachukua simu yake na kukutana na ujumbe toka kwa Vaileth,“Jana ndio ulichoka sana Junior? Mbona hukuja chumbani kwangu, nilitaka uje ili tuongee kuhusu hili swala”Alijua kuwa alifanya makosa na kujisema,“Ila sisi wanaume loh! Kwa Vai Napata kila kitu yani hakuna ambacho sipati na ninaishi nae kama mke wangu ila nimechukua na laki tano yake kwenda kumpelekea mwanamke mwingine ili tu nikamuonje huyu mwanamke, sijui tamaa nitaacha lini mimi! Nitaacha hadi nikilala na Samia kwakweli, huyu mtoto kaniingia sana akilini”Basi akaamka na kuoga na kujiandaa ili aende kwa mama yake.Ila moja kwa moja Junior alienda kwanza jikoni ili kumpooza Vaileth kwani anajua kuwa amechukia, basi alimkuta jikoni na kumbusu ambapo Vaileth alishtuka kidogo halafu alianza kumwambia kwa sauti ya chini,“Nisamehe mpenzi wangu, yani jana nilichoka sana halafu usiku nikajiwa na ndoto mbaya kuwa mama yangu ni mgonjwa, nikaamua kumpigia simu na kukuta kweli anaumwa ila hakutaka nimueleze mtu yoyote kuhusu kuumwa kwake kwahiyo hata mamdogo usimwambie, namuaga tu kuwa naenda kumsalimia mama si unajua mimi ni mtoto wa pekee kwetu”“Naelewa hakuna tatizo”“Basi kwaheri”Junior akambusu tena Vaileth na kutoka ila kwenye mlango wa kuingia jikoni akapishana na Erica ambaye alikuwa anaenda jikoni pia ila hakufikiria kama Erica amesikia chochote kile maana alikuwa akiongea na Vaileth kwa sauti ndogo sana.Basi alisalimiana nae tu na kuondoka zake na hata Erica jikoni hakumuuliza chochote kile Vaileth zaidi ya kuanza kumsaidia kazi tu.Junior alienda kumuaga mama Angel kuwa anaenda kumsalimia tu mama yake, naye mama Angel hakumkatalia zaidi ya kumpatia Junior nauli tu ya kwenda huko kwa mama yake.Basi Junior aliondoka ila huku akiwaza vitu mbali mbali vya kufanya, aliwaza kupata pesa kwa mama yake na kuona ni kazi ila akasema acha aende kujaribu tu.Junior alivyofika tu alimkuta mama yake nyumbani na kukaribishwa vizuri tu,“Oooh naona mwanangu umenikumbuka leo”“Ndio, nimekukumbuka mama”Basi baada ya maongezi ya hapa na pale, Junior akamjaribu mama yake,“Halafu mama, nilikuwa na shida na kama laki moja hivi!”Mama Junior akashtuka kidogo na kumuuliza,“Weee Junior, laki moja ya nini tena?”“Nina shida nayo mama”“Junior mwanangu, naona huko kwa babako mdogo kunakuchanganya akili jinsi unavyowaona wanamiliki pesa nyingi, mwanangu pesa zinatafutwa kwa kufanya kazi. Sasa wewe laki moja unataka ya nini jamani! Mara mwisho umesema sherehe, haya leo ya nini?”“Mmmh mama na wewe jamani, angekuwa mamdogo hapa angenipa haraka sana”“Mbona hujamuomba sasa umekuja kwangu!”“Jamani, wewe ndio mama yangu yani nitegemee kwa mama mdogo kila kitu kweli! Wewe ndio mama yangu na unajukumu la kunihudumia sababu mimi ni mwanao”“Ila sio kwa huduma hizo za kukupa laki moja, mimi sina hela kwanza hapa nilipo nina kadi za michango ya harusi kibao ndani kwangu hata sielewi itakuwaje, na wewe unazidi kuniumiza kichwa tu. Sina hela Junior”“Sawa mama, sijakulazimisha ila leo nipo hapa nitalala hapa kwahiyo kwa mamdogo nitarudi kesho”“Oooh sawa”Junior akampigia tu simu mama yake mdogo kumtaarifu kuwa siku hiyo hatorudi nyumbani sababu analala kwa mama yake, naye mama Angel alimuelewa sababu ni muda kidogo Junior hakwenda nyumbani kwao.Basi leo baba Angel akiwa yupo kazini akiendelea na shughuli zake za kikazi maana huwa lazima azimalize kwanza halafu ndio aende kwenye ujenzi wake, akatembelewa na madam Oliva ila huyu madam leo alionekana kutabasamu sana kanakwamba sio yule aliyekataliwa matunda, kisha madam Oliva bila hata salamu alimwambia baba Angel,“Nina habari njema kwako”“Eeeh habari gani hiyo?”“Matokeo ya kidato cha nne yametoka, halafu Angel na Junior wamefaulu vizuri tu”“Oooh hizo ni habari njema kweli, kumbe majina ya wanangu unayajua eeh!”“Ndio nayajua, nimewafatilia maana niliwauliza shule walizokuwa wakisoma. Basi nilipoona tu matokeo yametoka ikawa ndio kitu cha kwanza kabisa kuangalia matokeo yao”“Nashukuru sana madam kwa kujitoa kwako”“Kwahiyo ni muda wa kushereke, unajua watoto wakifaulu ni furaha sana kwa wazazi, inatakiwa kusherekea na kuwatafutia watoto zawadi”“Ni kweli, ni jambo jema sana, ila mimi nina shughuli nyingi mno, hata muda wa kuwatafutia zawadi watoto huwa sina”“Mke wako je!”“Oooh yule ni wa muhimu sana kwangu, yani siwezi fanya kitu bila kumfikiria yeye. Nikimuahidi zawadi hata kama nimetoka kwenye shughuli zangu saa tano usiku basi hiyo zawadi nitaitafuta tu. Nampenda sana mke wangu”“Mmmh!”“Unaguna nini madam?”“Unajua wewe ni mwanaume wa tofauti sana, jamani ni ngumu kwa mwanaume kumsifia mke wake mbele ya mwanamke mwingine, ni ngumu sana. Ila wewe muda wote utamsifia mke wako na utasema jinsi gani unavyompenda”“Mbona hivi bado sijamsifia kabisa, hizi sio sifa, nikianza kutoa sifa za mke wangu mimi utabaki umeduwaa tu, kwanza mke wangu ana akili sana, mke wangu ni mcha Mungu, mke wangu sio malaya, mke wangu sio mchafu, mke wangu ni mzuri, mke wangu ana upendo, mke wangu….”“Eeeeh basi jamani, hukawii kusema mkeo ndio bora zaidi hata chumbani kuliko wanawake wote”“Ni kweli, mke wangu ni namba moja kuliko wanawake wote, acha nimpende mke wangu maana kakamilika kila kitu”Madam Oliva akapumua kidogo ila hata hakutaka kukaa sana na kusema,“Shule walizopangiwa zikitoka nitakuja kukwambia, kwaheri”Basi madam Oliva aliinuka na kutoka nje ya ile ofisi ila baba Angel hakujali kitu chochote maana yeye aliona ni kawaida kwake kumsifia mke wake.Kwakweli madam Oliva aliumia sana kwa siku hii kupata siku zozote anazoongea na baba Angel na kwa muda huo aliamua kwenda mahali ili kupumzisha akili yake, ila akiwa huko akakutana na rafiki yake ambaye nae alikuwa sehemu hiyo kwahiyo walifurahiana na kuanza kuongea mawili matatu,“Kumbe na wewe Oliva huwa unakuja huku!!”“Mimi mwenzio bachela, nikushangae wewe mke wa mtu unafanya nini huku?”“Aaaah mke wa mtu bongo!! Mimi nipo huku kutuliza mawazo, wee ndoa hizi ziachege tu yani mambo ya ndoa jamani loh!”“Nini tena wakati tusio na ndoa tunatamani kuingia kwenye ndoa!!”“Ingia tu shoga yangu ila kuna watu tuna mawazo hadi tunatamani kutoka, sema watoto wangu ndio wananiumiza kichwa inabidi tu nivumilie. Eeeh vipi Oliva ni shemeji gani huyo umempata? Nakumbuka wakati tupo Sekondari ulikuwa ukiponda wanaume wewe, nadhani ndio sababu ya kutokuolewa hadi leo. Hata ulipozaa kila mtu alijiuliza imekuwaje kwa Oliva kuzaa jamani, hata baba mtoto wako hutaki kumuonyesha, sasa nani huyo kapata Bahati ya kukubaliwa na wewe kwenye swala la ndoa?”Madam Oliva alicheka na kusema,“Mwenzangu, nihurumie tu mwenzio nampenda mume wa mtu”“Aaai shoga yangu, mume wa mtu tena!! Aaah hata sikushauri jamani, mume wa mtu wa kazi gani jamani! Kuna wanaume wengi tu wapo hawajaoa, sasa wewe ukazane na mume wa mtu wa nini?”“Ana mapenzi ya dhati shoga yangu, katika maisha yangu sijapata kuona mwanaume wa aina yake, kiukweli nahitaji kuolewa nae, natamani akubali niwe hata mke wa pili jamani nimezama shoga. Ila tatizo lake kila ukikutana nae ni kumsifia mkewe tu”“Nimekwambia shoga hebu acha hayo mambo utajiumiza kichwa bure, wewe ni mwanamke msomi na una pesa kwanini uhangaike na mume wa mtu jamani. Mke wake akijua unajua atakudhalilisha, hebu achana na mambo hayo. Kwanza ndoa haina maana yoyote. Mwenzio hapa mume wangu ananiletea watoto kila siku nyumbani, karibia tunakuwa na timu mbili za mpira tuanzishe mechi mule mule ndani”“Mmmh Fetty usiniambie jamani, mbona shemeji anaonekana mpole!”“Wapole hao waogope shoga yangu, hawana maana hata kidogo, waogope kabisa. Najuta mimi ila nitafanyeje sasa, navumilia tu”Basi wakaongea pale na kuanza kukumbushana mambo ya zamani ya shuleni na kucheka sana kisha kuamua kuondoka, na muda huu madam Oliva aliamua kumpa lifti rafiki yake hadi nyumbani kwake.Siku hii baba Angel alichelewa kiasi kurudi nyumbani ila alimpa mke wake ile habari ya kufaulu kwa Junior na Angel, naye mama Angel alifurahi sana hata kutamani kupiga simu muda huo ila sababu aliona muda umeenda akasema kuwa atapiga kesho yake, basi baba Angel alimuulizia Junior na kuelezwa kuwa Junior kaenda kwao,“Aaah jamani Junior nae, kwanini lakini wakati tulipanga vizuri, basi nitaenda na Erick tu”Ila sababu baba Angel alikuwa amechoka sana akaamua tu kulala muda huo.Kulivyokucha, ikabidi baba Angel aondoke na Erick tu maana Junior hakuwepo wala nini.Basi nyumbani walibaki wale wale wa siku zote, baada ya kazi zake mama Angel aliamua kwend kukaa sebleni na kuangalia Tv ila muda huo alishasahau habari za matokeo ya wakina Angel na Junior.Kwa muda huo alikuwa amekaa na Erica tu, mara kuna habari ilipita,“Matokeo ya kidato cha nne mwaka huu, wasichana wang’ara”Erica akamshtua mama yake,“Mama, je matokeo ya kaka Junior na dada Angel yakoje?”“Oooh nilisahau eti, wamefaulu maana baba yenu aliangalia tena ngoja nimpigie bibi yenu ili Angel apate habari juu ya ufaulu wake, halafu nimpigie mama Junior”“Mmmh!”“Mbona umeguna Erica?”Erica akasogea karibu kwa mama yake na kuanza kumwambia,“Basi nikwambie mama, mama Junior anaumwa ndiomana Junior kaenda huko jana na hajarudi”“Kheee dada yangu anaweza akaumwa kweli na mimi nisipate habari!”“Kweli mama, ila nasikia wamesema usiambiwe wewe ni siri”“Hivi kuna ugonjwa wa siri jamani! Hebu kaniletee simu yangu washanichanganya tayari, kweli dada yangu anaumwa kimya kimya jamani loh!”Erica akaenda kumletea mama yake simu ila alipiga aliona simu inakatwa na kumfanya achukie sana, yani akatamani hata kwenda ili akaangalie mwenyewe hali ya dada yake.Muda huu Junior alikuwa na mama yake, na aliona dalili ya kupata pesa kwa mama yake ilikuwa ni ndogo mno, basi akaamua kumuomba simu mama yake,“Mama, samahani naomba simu nimpigie mamdogo maana alisema nikitaka kutoka huku nimtaarifu”Basi mama yake alimpatia simu yake halafu yeye akaenda kuendelea na kazi zake zingine, basi Junior alipekua majina ya ile simu akakuta kuna namba mama yake kaandika ‘Daktari’ Junior akatabasamu kisha akatuma ujumbe kwenye ile namba,“Ndugu yangu nina shida sana, nimekwama hapa na ninahitaji sana pesa. Naomba uniazime laki mbili, kwenye siku mbili hizi nakurudishia ndugu yangu”Basi ujumbe ukarudishwa muda huo huo,“Usijali mama Junior, shida yako ni kama yangu nakutumia muda sio mrefu”Na kweli muda sio mrefu ikaingia laki mbili kwenye simu ya mama Junior, basi muda huo huo Junior akairusha kwenye simu yake na kuandika ujumbe mwingine,“Asante sana ndugu yangu, yani ndani ya siku mbili hizi nakurudishia”Mara simu ile ilianza kuita, kuangalia akaona ni mama yake mdogo anapiga, basi akawa anaikata ili isimsumbue, kisha ukaingia ujumbe toka kwa yule daktari,“Hakuna tatizo Bite, wewe ni kama ndugu yangu”Basi Junior alifuta zile jumbe zote kisha akamrudishia mama yake simu na kumuaga kwani muda huo huo aliondoka zake ukizingatia alishapata hela aliyokuwa akiitaka tena na zaidi.Junior alifika kwenye hoteli ambayo kapanga na Samia, basi alikodi chumba na kununua vinywaji halafu akakaa chumbani sasa akimsubiria Samia huku akiwasiliana nae,“Samia mpenzi, mimi nishafika tayari”“Oooh vizuri sana Junior, nipe kama nusu saa nitakuwa hapo, ila ushakodi chumba?”“Ndio, nipo chumbani sasa”“Hapo sawa, nakuja basi muda sio mrefu si unajua mimi bado mdogo sio vizuri tukionekana nje, ni bora umekodi chumba”“Nakusubiri basi kipenzi changu”“Yani nusu saa tu, usijali Junior”Basi Junior alikuwa akimsubiria Samia ila yalipita masaa mawili bila ya Samia kuonekana wakati kamwambia ndani ya nusu saa, akaanza kupiga simu ya Samia ila ikawa haipokelewi wala nini yani Junior alichukia sana, mara ukaingia ujumbe toka kwa Samia,“Samahani Junior, baba alikuja na kunilazimisha kwenda kuswali. Na sasa nipo nae nyumbani kwahiyo sitaweza kuja leo, nisamehe sana” Basi Junior alikuwa akimsubiria Samia ila yalipita masaa mawili bila ya Samia kuonekana wakati kamwambia ndani ya nusu saa, akaanza kupiga simu ya Samia ila ikawa haipokelewi wala nini yani Junior alichukia sana, mara ukaingia ujumbe toka kwa Samia,“Samahani Junior, baba alikuja na kunilazimisha kwenda kuswali. Na sasa nipo nae nyumbani kwahiyo sitaweza kuja leo, nisamehe sana”Junior alisoma huu ujumbe wa Samia mara mbili mbili na kuhisi akili yake ikiruka kabisa, basi aliamua kumpigia simu ila simu iliita tu bila kupokelewa na mwisho wa siku simu ilikuwa haipatikani, kwakweli Junior alichukia sana na kujisemea,“Kwakweli mimi ni lofa, tena bonge la lofa, nimechukua hela kwa Vaileth mwanamke anayenipa mapenzi yote na kumpelekea yule mjinga Samia, na sasa nimeenda kumuwekea mama yangu deni ili nije kujivinjari na Samia, kwakweli mimi ni lofa sana. Yani Samia anajifanya mtoto wa mjini eeeh! Kweli maisha ni tofauti sana, Vaileth ni mkubwa ila mengi hayajui, ila Samia ni mdogo na mengi anayajua. Dah huyu dogo kaniweza ila lazima nitamkomesha tu”Basi alikuwa akijifikiria pale, roho ilimuuma sana kwani tayari alishatoa hela pale ya chumba, na tayari alishanunua vinywaji yani akili yake haikufanya kazi kabisa, akawaza tena,“Au niende kununua changudoa nije kulala nae humu! Jamani, hela yangu iende bure bure tu”Hapo akaona ni vyema akanunue wanawake wa kujiuza ili hela yake isiende bure.Bado mama Angel alikuwa akijiuliza sana kuwa ni kwanini dada yake amfiche kuhusu ugonjwa, basi muda huo aliamua kumpigia tena simu ila muda huu mama Junior alipokea na kusalimiana nae pale,“Dada nasikia unaumwa ila unafanya siri, kwanini dada jamani!”“Kheeee jamani niumwe halafu nifanye siri!! Haiwezekani kwakweli, nani huyo aliyekupa hizo habari?”“Nasikia ndivyo Junior alivyosema jana”“Jamani Junior niliongea nae muda gani mimi! Kwanza jana nilionana nae huku nyumbani ila kabla ya hapo hakuna chochote ambacho niliongea nae, mimi ni mzima wa afya njema kabisa”“Sawa dada, yani nilishtuka sana kusikia unaumwa ila unafanya siri”“Siwezi kufanya hivyo mdogo wangu”Basi mama Angel aliagana na mama Junior na kumuita Erica sababu alitaka kujua kuwa Erica maneno hayo kayatoa wapi, alitambua kama mwanae ni mbea ila katika swala la uongo hakumuweka maana huwa mara nyingi anasema kitu alichokisikia, basi Erica akaenda,“Eeeh na wewe, hiyo habari kuwa mama Junior anaumwa ila anafanya siri umeitoa wapi? Nimempigia simu ni mzima wa afya njema, jamani mwanangu mbea wewe hadi unachukua habari sio zenyewe. Haya umeitoa wapi?”“Mama, ngoja nikwambie ukweli. Asubuhi nilikuwa naenda jikoni ila nikasikia sauti ya Junior jikoni basi nikasogea taratibu na kusikiliza ndio nikasikia Junior akimwambia dada Vaileth kuwa yeye anaenda kumuona mama yake sababu mama yake ni mgonjwa ila hataki watu wajue”Mama Angel aliamua kumuita Vaileth, sababu hakuelewa kabisa, basi Vaileth alipofika alimuuliza,“Vai, jana asubuhi Erica alikusikia wewe na Junior mkiongea jikoni yani Junior alikuwa akikwambia kuwa anaenda kumuona mama yake sababu alikuwa mgonjwa ila hataki watu wajue, je ni kweli?”Vaileth alinyamaza kimya hadi mama Angel aliamua kumuuliza kwa ukali zaidi ndipo alipojibu,“Ni kweli mama”“Sasa Junior alikuwa ni misingi gani kusema hivyo jamani!”Erica akauliza,“Kwani mama yake haumwi kweli?”“Haumwi wala nini, na unaambiwa Junior katoka kwao muda mrefu sana kasema anakuja huku ila hadi jioni hii hajafika huku jamani, huyu Junior anamaana gani sijui”Basi Vaileth alinyanyuka na kuwa kama anaenda jikoni ila alienda chumbani kwake kwani kwa muda huo alijikuta akijiuliza maswali mengi sana,“Kwani Junior kaenda wapi? Na kwanini anidanganye kuwa mama yake anaumwa?”Akaanza kuvuta matukio kwanza, alivuta tukio la Junior kurudi akiwa na mawazo sana, pia alivuta tukio la Junior kuomba laki tano yake, alivuta tukio la Junior kudai kuwa amechoka sana na kulala chumbani kwake, akavuta pia tukio la kudanganywa kuwa mama Junior ni mgonjwa, akajikuta machozi yakimtoka kwani alihisi kuwa Junior anamsaliti.“Kwanini Junior ananifanyia hivi lakini? Mbona mimi nampenda sana, mbona namjali, kwanini ananifanyia hivi!! Junior hata angechoka vipi ni lazima angekuja chumbani, kwanini Junior kabadilika? Lazima kuna mwanamke mwingine kampata tu”Kwa muda huo huku machozi yakimtoka alikuwa akiwaza kuwa ampigie simu Junior kumuuliza au afanye kitu gani, yani alijikuta kuwa na mawazo sana ila kwa muda huo aliampigia simu kwanza ndugu yake Prisca maana simu ya awali alikuwa nayo,“Oooh leo Nyanda umenikumbuka, nimefurahi sana”“Jamani wewe, huzoei tu kuniita Vaileth jamani!!”“Samahani Vaileth jamani, mazoea yana tabu nishazoea nyanda mimi”“Hivi kwa mfano una mwanaume wako, akakukosea unatakiwa kufanya kitu gani?”“Kheee ushapata mwanaume au yule baba mtoto wako karudi? Unataka ushauri gani kwangu? Ushauri wa kawaida ni kuwa kama mwanaume wako kakukosea mchambe tu tena umchambe haswaaa hadi ahisi kizunguzungu. Ila ushauri wenye busara na wa kudumisha mahusiano, kama mwanaume wako kakukosea, kwanza kabisa huwezi jua ni kwanini kakukosea, unatakiwa kumbembeleza, mnyenyekee muulize kwa ustaarabu, muonyeshe mapenzi na yeye atajishtukia kwa makosa yake. Kwahiyo utachagua wewe!”“Mmmh ingekuwa wewe ungechagua nini?”“Inategemea na aina ya mwanaume, kama anayenipa pesa nitamnyenyekea hata kama kanikosea ila mwanaume ngonjwa ngojwa akinikosea namchamba hadi anasahau jina la mama yake mzazi”“Mmmh jamani!”“Kwanza nimefurahi sana upo hewani kwasasa”“Basi nitakupigia tena tuongee”Vaileth alikata ile simu huku akijiuliza kama ampigie simu Junior au vipi.Kwa muda huu, Junior alikuwa ameshafanikiwa kumpata mwanamke mmoja anayejiuza ambaye alikubaliana nae kumlipa elfu ishirini, basi alienda na yule mwanamke kwenye ile hoteli na mwanamke akasema,“Kheee kumbe una hela jamani, sasa mbona hukusema hadi nimepanga dau dogo hivyo!! Nilikuona mdogo kumbe una mawe, utaongeza dau ili tuwe wote hadi asubuhi”Mara simu ya Junior ilianza kuita, basi aliichukua na kuona mpigaji ni Vaileth, kiukweli aliumia moyo wake na kuamua kupokea ile simu,“Junior mpenzi wangu, upo wapi?”“Karibia narudi nyumbani”“Nakuomba mpenzi, ukihisi kutamani mwanamke mwingine jua kuwa mimi nipo na ninakupenda sana mpenzi wangu, maradhi ni mengi sana siku hizi”“Nimekusikia”“Nakupenda sana, naomba urudi nyumbani Junior. Natamani sana kukuona mpenzi wangu”Basi ile simu ikakatika ila kwa muda huo Junior alihisi moyo wake kuumia sana jinsi akimfikiria Vaileth, basi akamuangalia yule kahaba aliyemuita na kumwambia,“Subiri nikanunue kinga”“Hakuna tatizo”Junior alitoka ila bado kauli ya Vaileth ilifanya kazi kichwani kwake kuwa rudi nyumbani moenzi wangu, alijihisi kuwa na hatia sana. Basi alivyofika nje, alisimamisha bodaboda na kuondoka nayo kuelekea nyumbani kwa muda huo, hata hakumjali tena yule Kahaba aliyemchukua.Wakati baba Angel na Erick walipokuwa wakirudi nyumbani, basi baba Angel alimpa Erick hela kama ambavyo alikuwa ameahidi kufanya hivyo naye Erick alimshukuru sana baba yake kisha baba Angel alimuuliza.“Utaenda kununua nini na hiyo hela?”“Aaah zawadi baba ila nyingine naiweka kwanza”“Oooh haya mwanangu, kwahiyo hiyo zawadi unaenda kununua lini?”“Kesho baba’“Je mama yako yupo kwenye watakaopata zawadi au ni za kwako mwenyewe? Au mama yako utampa zawadi ya pipi? Yani zawadi wewe unanunua kwaajili ya nani?”Erick akacheka kwanza na kumwambia baba yake,“Mama, nitamnunulia zawadi ila sina tatizo sana na mama sababu huwa anapata zawadi kutoka kwako, ila zawadi ninayopanga kununua napanga kumnunulia Erica”“Wow, mwanangu ni vizuri sana kumpenda dada yako, kumbe huwa unamkumbuka eeeh! Oooh ni vizuri sana, nina uhakika Erica atafurahia sana zawadi utakayomnunulia”Erick akatabasamu tu, kisha baba yake akasema,“Unajua mwanzoni nilikuwa najiuliza kuwa unapanga kununua zawadi ya nani? Nimejiuliza sana, nakumbuka mimi jamani wakati nimeanza mahusiano na mama yenu basi katika swala la zawadi ni yeye tu aliyekuwa akinijia kichwani mwangu”“Na kabla ya hapo baba?”“Kabla ya hapo, sikuwa mzuri sana kwenye swala la zawadi ni mpaka mtu aniambie kuwa nataka zawadi, kama dada yangu alikuwa na mtindo wa kuniambia nataka zawadi, basi ndio naenda kumnunulia. Badae nilipoanza na mama yenu alinifundisha umuhimu wa zawadi basi hata mama yangu nikaanza kumpelekea zawadi, dada yangu nae na ndugu zangu wengine. Nafurahi mwanangu umejua umuhimu wa zawadi ukiwa mdogo hivi, kwakweli dada zako wamepata kaka wa kujivunia haswaa”Baba Angel alionekana kumfurahia sana mtoto wake na waliongea mengi sana hadi wanaingia nyumbani.Basi kutokana na uchovu uchovu wa siku hiyo walikula tu na kwenda moja kwa moja vyumbani maana hakuna aliyekaa kuongea na wengine zaidi ya kuoga na kulala tu.Usiku wa leo, Junior alikuwa chumbani kwa Vaileth huku akijaribu kuweka sawa baadhi ya mambo,“Ila kwanini Junior ulinidanganya mpenzi? Yani umesema mama yako anaumwa wakati haumwi jamani Junior!”“Kwanza naomba unisamehe sana, yani hata sijui nisemaje. Unajua mama alinidanganya pia kuwa anaumwa kumbe shida yake ilikuwa kuniona tu, si unajua huwa siendi mara kwa mara! Halafu kitu kingine, hata mamdogo kanisema sana nilivyorudi, jamani kitoto Erica ni kimbea hadi kimeshindikana. Kweli kwa sauti ile jikoni ni ya kusikiwa jamani!”Vaileth alicheka kwa muda na kusema,“Hujamzoea tu Erica, ila kumbuka katufichia siri”“Kwanza tujiandae wakati wowote ule litabumburuka, katoto kambea kale wala sio ka kukaamini sana”“Je ikibumburuka itakuwaje?”“Yani hapo ni kukataa tu hakuna namna”“Mmmh unajua kuwa Erica ni mbea ila sio muongo ndiomana anaaminiwa sana! Hapa ni kuombea tu asije kusema ukweli”“Ila sijapata kuona mtu mbea kama yule mtoto, yani akija kuolewa mumewe atapata shida, hao mawifi zake na mama mkwe wajipange maana kanauwezo wa kusambaratisha ukoo mzima kwa umbea wake, atatoka kwa mama mkwe na hili na kupeleka kwa wifi hili, katoto kambea hadi kameshindikana”“Sasa karithi wapi?”“Aaaah sijui kwakweli, ila Vaileth kwakweli nimekumiss sana mke wangu yani nilikuwa na mambo mengi ila mawazo yote ni juu yako”Moyo wa Vaileth uliridhika sana kwa maneno yale ya Junior na kujikuta akitabasamu tu kisha wakalala kama kawaida yao.Mama Junior akiendelea na kazi zake za hapa na pale, mara alipigiwa simu na rafiki yake daktari, basi alitabasamu na kupokea ile simu,“Bite, habari. Jana ndugu yangu hata hatukuongea vizuri kwani ulikumbwa na nini rafiki yangu”“Mmmmh nini tena!!”“Unajua nilivyopokea ule ujumbe wako tu nikaamua kutuma muda ule ule na hata sikukuuliza ndugu yangu”“Ujumbe gani tena!”“Khee Bite, si wewe jana umenitumia ujumbe wa kuazima laki mbili!”“Mmmh jamani Maimuna, mimi nimekutumia huo ujumbe!! Muda gani?”“Ngoja nikutumie zile jumbe kwanza tulizokuwa tukiwasiliana”Basi Daktari alikata ile simu na kumtumia mama Junior zile jumbe za jana, kwakweli mama Junior alikuwa akishangaa tu maana hakumbuki kabisa kuwasiliana na huyu daktari kuhusu maswala ya hela, kwahiyo alikuwa na mshangao, kisha daktari akampigia tena simu,“Unajua nini Maimuna naomba unipe muda tafadhari, mimi na wewe hatuwezi kujivunjia heshima kwa vitu vidogo kama hivi. Ngoja tu nitapata ukweli”“Duh! Ila inashangaza, au uliibiwa simu?”“Hapana, simu ninayo mwenyewe muda wote, ngoja tu Maimuna nitakujibu”Basi mama Junior alikata ile simu, kiukweli hakuelewa kabisa aliamua kujiandaa na kwenda moja kwa moja kwenye kwenye ofisi za mtandao wa simu ili apate taarifa za akaunti yake ya simu.Alipopewa alistaajabu sana kuona kweli alitumiwa laki mbili na yule daktari tena sio laki mbili tupu ila ilikuwa laki mbili na elfu kumi, halafu akaona yote ilirushwa kweye namba ya Junior, kwakweli alichoka kabisa na kusema,“Kheee tuzaege tu jamani, mambo yenyewe ndio kama haya loh! Huyu Junior angebaki tumboni kwangu si angenipatia uvimbe huyu jamani! Khaaa mtoto gani huyu!!”Basi aliondoka zake kurudi nyumbani kwake ila alikuwa na hasira sana.Baba Angel leo hakwenda ofisini ila alienda kwenye ujenzi wake kuangalia tu mwenyewe, na pale yule fundi wake mkuu alimwambia,“Kwakweli hongera sana”“Hongera ya nini tena?”“Una kijana mwenye akili sana, yani mtoto wako ana mawazo ya kikubwa hatari tofauti na umri wake”“Erick huyo!”“Ndio, Erick yani akiwa hapa anasimamia utadhani ni mtu mkubwa sana yani anauelewa wa kila kitu, nakwambia karibia utaacha kutembelea kweye hizi saiti na kumuachia yeye tu afanye hivyo. Kwakweli una kijana mwerevu sana, hongera kwa hilo”Baba Angel alifurahi sana na kujisifia zaidi,“Yule ni mwanangu pekee wa kiume, na amechukua jina langu maana Erick ni jina langu”“Aaaah kumbe! Yani nimemtamani hata awe ni mwanangu, jamani mtoto ana akili yule na yupo vizuri sana kichwani nina uhakika hata maendeleo yake shuleni ni mazuri. Yule mwingine sasa, na yeye ana akili sana ila asione mwanamke kapita uwiii macho juu juu mpaka namuhurumia kwakweli, ila Erick yupo makini sana”Baba Angel alizidi kufurahi sana na kufanya upendo wake kwa Erick uwe maradufu kwani aliona fahari sana kwa kila aliyekutana nae halafu akamsifia Erick.Basi siku hii hakukaa sana kule kwenye ujenzi na kuamua kuondoka tu sababu hakukuwa na mambo mengi sana wala nini.Moja kwa moja baba Angel alirudi nyumbani kwake, na kumkuta mkewe akiwa chumbani muda huu akimlaza mtoto basi alisalimiana nae pale na kumuuliza,“Erick yuko wapi?”“Nilimuona anaenda bustanini kukaa, naona siku hizi anapenda sana lile eneo”“Sawa, ngoja nikaongee nae”Basi baba Angel aliondoka na kwenda bustanini ila muda huo huo mama Angel alipigiwa simu na mama Junior,“Mdogo wangu unajua alichokifanya Junior?”“Kafanya nini tena?”“Ngoja tukionana nitakueleza vizuri, yani huyu mtoto ni pasua kichwa hatari”“Ila kafanyaje dada?”“Nitakuelezea tu hakuna tatizo”Basi mama Junior alikata simu na kumfanya mama Angel kujiuliza kuwa tatizo ni nini ila hakupata jibu.Mama Junior muda huu alishindwa kumueleza mdogo wake sababu ya mume wake kumkataza, yani alipotaka kuongea basi mumewe alikuwa karibu na kumkataza, kwahiyo alivyokata simu alianza kumsema,“Ila nawe mke wangu umezidi jamani, sasa unataka kumuelezea mdogo wako wakati hata muhusika mwenyewe hujamuuliza”“Nimuulize nini sasa wakati inaonekana wazi kitu gani amefanya jamani, nilikuwa nataka nimueleze mdogo wangu ili anisaidie kulipa hii pesa unafikiri mimi natoa wapi laki mbili na elfu kumi kwasasa?”“Ila mke wangu, unajua kama wale ndio wanaishi na Junior kwasasa, na ukiwaambia juu juu swala hilo hivi huoni kama watamtimua mtoto pale kwao? Mara nyingine uwe unafikiria kwanza, yule Erick usimuone vile, anacheka na kufurahi ila yule ni ana hasira sana tena hasira za karibu hata nashangaa mdogo wenu kamuweza vipi yule na kumtuliza tuli kabisa. Sasa unataka kumcharusha, Erick atataka kuishi na mtoto tapeli? Si ataona kuwa atawafundisha wanae tabia mbaya, yani atamtimua tu na kumrudisha hapa nyumbani. Huoni kama kwasasa tunaishi kwa amani hapa!”“Kumbe humtaki mwanangu hapa eeeh!”“Sina maana hiyo mke wangu ila nakwambia tu kuwa sio vizuri kuanza kumtangazia mtoto wakati hata hujaongea nae bado, sikia mimi nitakupa laki moja ili upunguze deni halafu nyingine mwambie tutammalizia”“Oooh asante sana mume wangu”Mama Junior aliona nafuu sasa, kisha muda huo huo alimpigia simu mtoto wake na kumwambia,“Junior, tayari nimejua ujinga ulioufanya kwenye simu yangu, kwa hakika sijapenda kabisa jambo hili”“Nisamehe mama”“Yani wewe mtoto hufai kabisa hata kwa kulumangia hufai wewe, kesho uje nyumbani kwangu mara moja”“Sawa mama, ila kesho naenda Kanisani”“Kwani huko Kanisani utakaa milele? Nakwambia uje nyumbani, usiniletee ujinga mie”“Sawa mama, nitakuja”Mama Junior alikata simu ila kwa kiasi alikuwa amechukizwa sana na tabia ya Junior.Baba Angel alikaa kwenye bustani na Erick na kuanza kuzungumza nae,“Ila mwanangu mbona kama umejitenga hivi, kwanini umekaa mwenyewe?”“Kuna mambo natafakari baba”“Mambo gani hayo?”“Yani nawaza maisha yangu ya badae yatakuwaje na nitafanya nini”“Sawa mwanangu, hayo usiyawaze ila waza zaidi masomo yako maana kuhusu maisha yako ya badae mimi nayaandaa mwanangu hatausijali, ndiomana nakushirikisha mambo mbalimbali mwanangu. Haya hizo zawadi ulishanunua?”“Ndio, nilishanunua baba”“Umenunua nini?”“Nimemnunulia gauni na viatu”“Oooh mwanangu huyo, najivunia sana kuwa na wewe. Kwahiyo ushamkabidhi?”“Hapana, sijampa mkononi ila nimemuwekea chumbani kwake kitandani, yani akiingia tu atakumbana navyo halafu badae ndio nitamwambia kuwa ni mimi”Baba Angel alifurahi sana kiasi kwamba hata hakumuuliza kama na mama yake kamnunulia au la, yani yeye alifurahi tu kusikia Erick kamnunulia Erica zawadi.Basi waliongea sana pale na mwisho wa siku waliingia ndani maana usiku ulishaingia na wote walielekea mezani kupata chakula cha usiku ambacho kwa siku hiyo kiliandaliwa na Vaileth pamoja na Erica kwahiyo muda mwingi Erica alikuwa jikoni siku hiyo.Walianza kula pale na baba Angel akauliza,“Hizi njegere kapika nani jamani!”Vaileth akajibu,“Mambo ya Erica hayo”Baba Angel alitabasamu na kusema,“Hakika mume atakayekuoa mwanangu atakuwa na furaha sana kama mimi baba yako, yani hiki chakula umepika vizuri sana. Hongera sana”“Asante baba”Erica alikuwa akitabasamu tu, na mama yake akaongea“Naona huyu Erica kafata upishi wangu”“Kweli kabisa mama Angel ila katoto kamekuzidi haka”“Aaaah mimi ndio fundi wake bhana”“Ila kumbuka vya kurithi vinazidi”Wote wakacheka tu pale na kila mmoja alisifia kuwa chakula kilikuwa kizuri na mboga ilikuwa ni nzuri sana.Basi alimaliza kula pale na kila mmoja alienda kwenye chumba chake.Erica ndio aliingia muda huu chumbani ambapo cha kwanza alienda kuoga kwanza, ila alipotoka bafuni alishangaa kuona mzigo kitandani kwake, basi akafungua ule mzigo na kushangaa sana kukutana na gauni zuri sana na viatu vizuri sana halafu alikuta na nguo za ndani mpya kabisa, basi akajaribisha lile gauni, lilimpendeza sana alijiangalia mara mbilimbili kwenye kioo chake kikubwa, akajaribu na viatu navyo vilimpendeza sana kwakweli alishangaa mno aliyemuwekea hizo zawadi, akataka kutoka kwenda kumuuliza mama yake ila alipofungua tu mlango wake alikutana na Erick ambaye alikuwa akitabasamu na kuingia mule chumbani kwake.Erick nae alivyomuangalia Erica ndani ya ile nguo alifurahi maana ilimpendeza sana,“Eeeeh Erica umependeza sana”Erica alitabasamu na kusema,“Ila sijui ni nani kaniletea”“Aaaah Erica jamani, nimekuletea mimi”Erica alifurahi sana na kwenda kumkumbatia kaka yake kwa furaha na kumbusu, kwakweli ile ilikuwa ni furaha sana kwa Erick pia maana aliona raha kwa Erica kuipenda zawadi yake, kisha Erica akamwambia,“Asante sana Erick”“Ni wajibu wangu Erica kufanya hivi, kwanza mimi ni kaka yako na rafiki yako kwahiyo ni wajibu wangu kufanya hivi kwako”“Nashukuru sana Erick, nimeipenda sana hii nguo”Basi Erick alivyoona kuwa Erica kaipenda sana ile zawadi ndipo alipomuaga usiku mwema na kuondoka zake kwenda kulala.Jumapili hii, Erica alivaa zile nguo alizoletewa na Erick na wote pale nyumbani kwao walimsifia kuwa kapendeza sana na alipenda na kufurahi maana yeye licha ya umbea pia ni binti ambaye anapenda sana kupewa sifa, yani akisifiwa huona ufahari mkubwa sana.Junior alipotoka Kanisani tu siku hii, aliwaaga na moja kwa moja kwenda nyumbani kwao ili akaonane na mama yake na alijua kuwa atasemwa sana siku hiyo ila alivyofika tu alimkuta mama yake kajiandaa na alisema,“Yani ungechelewa tu kidogo ningekupigia simu, haya twende”Junior alimfata mama yake tu bila kujua kuwa anaelekea nae wapi, wakapanda daladala mpaka walipokuwa wakielekea, basi Junior akamuuliza mama yake,“Mama, ni wapi huku?”“Wewe mjinga, umeniingiza madeni makubwa sana, nimepata laki moja ndio nimekuja kumlipa hapa mwenyewe, kwahiyo hapa ni nyumbani kwa daktari”“Jamani mama”“Hakuna cha jamani”Basi mama Junior alimshika mkono Junior hadi kwenye ile nyumba na kugonga, walikaribishwa vizuri tu na daktari alikuwepo, walisalimiana pale na mama Junior alimtambulisha Junior kwa yule daktari kisha akamwambia Junior,“Huyu ndio rafiki yangu daktari, anaitwa dokta Maimuna, ndio uliyemuongopea ile hela”Basi mama Junior alianza kumueleza huyu rafiki yake kilichotokea, mara alifika mtoto wa yule daktari na kuwasalimia pale ila Junior na mtoto huyu walibaki kuangaliana kwa mshangao kwani mtoto huyu alikuwa Samia. Basi mama Junior alimshika mkono Junior hadi kwenye ile nyumba na kugonga, walikaribishwa vizuri tu na daktari alikuwepo, walisalimiana pale na mama Junior alimtambulisha Junior kwa yule daktari kisha akamwambia Junior,“Huyu ndio rafiki yangu daktari, anaitwa dokta Maimuna, ndio uliyemuongopea ile hela”Basi mama Junior alianza kumueleza huyu rafiki yake kilichotokea, mara alifika mtoto wa yule daktari na kuwasalimia pale ila Junior na mtoto huyu walibaki kuangaliana kwa mshangao kwani mtoto huyu alikuwa Samia.Ila kiukweli Junior alionekana na sura ya kuchukizwa sana, basi daktari aliwatambulisha pale,“Jamani huyu ni mtoto wangu wa mwisho, anaitwa Samia”Kisha daktari alitambua jicho baya la Junior na kufanya amuulize,“Mbona unamuangalia mwanangu kwa jicho baya hivyo!!”Junior hakusema kitu ila aliinuka na kutoka nje yani kitendo kile hata mama yake alishangaa sana kuwa Junior amekuwaje vile, ila alivyofika nje alisimamisha bodaboda na kuondoka zake.Kwahiyo daktari na mama Junior walibaki wakishangaa huku daktari akimuuliza mwanae,“Samia, kwani unamfahamu Junior?”“Hapana, simfahamu”Samia alikataa halafu akaenda zake chumbani kwahiyo mama Junior na daktari walibaki kushangaa, basi mama Junior alianza kuongea na yule rafiki yake daktari,“Jamani watoto wana mambo sana, ila tuachane na habari hizo ndugu yangu, unajua nini siku ile kumbe ni mwanangu ndio alichukua simu yangu na kukuandikia ule ujumbe”“Kheee jamani, watoto hawa!!”“Kisa tu aliniomba hela nikamnyima, basi akaniomba simu ili apige mahali kumbe jamani ana mambo yake ndio kama vile ndugu yangu, nisamehe sana nakuomba. Halafu naomba nitangulize hii laki moja kwanza, ila nyingine nitakutafutia ndugu yangu kwenye siku mbili hizi”“Eeeh kwanza pole sana Bite, ndio mambo ya Junior hayo!! Pole sana”Basi mama Junior akawa anataka kuchukua pochi yake ndogo ilia toe hela yake ila hakuiona na kushangaa,“Jamani pochi yangu ilikuwa hapa, iko wapi tena?”“Pochi gani hiyo?”“Pochi ndogo ndogo nyekundu”“Mmmh mbona mtoto wako alitoka nayo”“Kheee Junior jamani, kwanini lakini jamani uuuh!”“Kwani vipi?”“Ile pochi ndio niliyoweka hela”Kisha mama Junior akaamua kumpigia simu Junior ili kumuuliza kwanini ameondoka na pochi, na kweli Junior alipokea ile simu yake,“Wewe Junior kwanini umeondoka na pochi yangu!”“Mama, sina mengi ya kuongea ila mwambie huyo Samia amlipe mama yake”“Kivipi sasa?”“Mtoto mjinga sana huyo, ile laki mbili ni yeye ndiye aliyesababisha nikamuomba huyo rafiki yako, tena ni vizuri sana ni mama yake kwahiyo yeye ndio amlipe mama yake”“Wewe Junior wewe una kichaa au?”“Sina kichaa, nina akili zangu timamu, mwambie huyo Samia amlipe mama yake”Kisha Junior alikata ile simu, basi mama Junior alimuangalia rafiki yake na kumwambia,“Unajua hata sielewi yani sielewi kabisa ujue, huyu mtoto sijui kakumbwa na nini?”“kwanini rafiki yangu?”Mama Junior akamueleza vile ambavyo aliongea na Junior kwenye simu, kuna kitu Fulani yule daktari alikigundua na kusema,“Mama Junior, kwakweli watu tunazaa ila muda mwingine tunazaa vitu visivyoeleweka sababu ya kuzaa na watu wasioleweka. Bite acha tu, nitajua cha kufanya kuhusu hiyo hela, si amesema Samia anajua? Basi acha tu najua ni jinsi gani nitambana huyu mtoto”“Jamani ila hata sijui imekuwaje?”“Usijali rafiki yangu, niachie mwenyewe tu halafu tutawasiliana, aaarggh watoto hawa jamani dah!”Kwakweli mama Junior hakuelewa kabisa, kwahiyo aliamua kumuaga tu rafiki yake na kuondoka ake kuelekea nyumbani kwake.Mama Samia alimfata Samia chumbani sasa huku kashika bakora maana alielewa kuwa mwanae kuongea ni mpaka fimbo, yani aone fimbo ndio aongee,“Haya niambie, unamjua Junior?”“Namjua ndio mama”“Oooh mbona muda ule ulikataa, kaone vile. Haya unamjua vipi?”“Nilimuona nyumbani kwakina Erica, ni ndugu yao”“Halafu ikawaje, niambie ukweli mtupu sababu ukinificha basi hii bakora itakuishia”Samia aliamua kumueleza mama yake kila kitu kilivyokuwa mpaka alivyopewa ile laki tano na Junior,“Kumbe yule Junior ndio mjinga hivyo!! Kukutongoza wewe kweli!! Mitoto mingine ni laana. Haya na wewe hiyo laki tano iko wapi?”“Nilimpa baba”“Hivi si nilikukataza maswala ya wewe kuchukua hela kwa wanaume lakini?”“Ndio ulinikataza ila baba kaniambia niwe nafanya hivyo ili wanaume wasinifatilie”“Haya unaona unachukua hadi hela za vichaa, huyu anaonekana ni kichaa yani anaweza kukukuta mahali na kukubaka maana akili yake inaonekana sio nzuri”“Nisamehe mama”“Nikusame nini? Ngoja huyo baba yako arudi na aniambie ujinga anaokufundisha wewe halafu mnapeana hela, sasa laki mbili yangu mtanilipa wewe na baba yako maana uliyemchukulia hela ni mwehu, angekuwa mwingine asingethubutu kufanya hivi, sipendi huu mchezo Samia, ukirudia tena nakupeleka hospitali kukuchoma sindano, mjinga wewe”Kisha mama Samia akamuacha Samia chumbani ila yale maneno ya mama yake wala hayakumuingia kwenye akili kwani alisema,“Mama anadhani mimi ni mjinga, huyo Junior anajifanya mwehu ila mimi ni mwehu zaidi yake, si alinipa mwenyewe ile hela! Tamaa tu, na nimemkomesha mjinga yule”Kisha Samia alikuwa akipanga mipango yake mingine tu.Kwakweli mama Junior hadi alifika nyumbani kwake bado hakuwa na amani kabisa, akampigia simu Junior,“Wewe mjinga hebu rudisha laki moja yangu”“Mama, hii hela isahau tu. Nilikuomba ukaniambia huna hela, kwahiyo hii isahau tu au kamavipi nenda kamdai yule yule Samia”Halafu Junior akakata simu na kumfanya mama yake achukie zaidi ila muda huo mumewe nae alikuwa amerudi basi alimuelezea mlolongo mzima wa siku hiyo na jinsi Junior alivyofanya na vile alivyompigia simu muda huo na alichomjibu,“Oooh kweli mke wangu Junior ulizaa kama mtoto ulizaa tena haswaa ila unajua kwanini Junior ana jeuri kiasi hiko?”“Kwanini?”“Sababu yupo peke yake, kila siku mke wangu nakwambia tuzae umekazana oooh una watoto wengi, ni kweli nina watoto wengi ambao nimezaa enzi hizo ila mimi na wewe hatujazaa wa kwetu ndiomana nikakwambia tuzae, Junior angekuwa na wadogo zake kidogo angekuwa na adabu”“Jamani, ila yule mtoto nimemlea vizuri sana hata nashangaa”“Unaona umemlea vizuri ila Junior umemdekeza sana, yani Junior ndio jicho lako wewe hata kwasasa umekubali akake kwa mdogo wako sababu unaona mambo yamekushinda ila yule Junior ungemuongoza toka mdogo kidogo ingekuwa afadhari, yani Junior hana mashaka na wewe, ndiomana anakujibu atakavyo sababu anajua huna cha kumfanya, kuna malezi mengine sio mazuri kuwapa watoto eti sababu yupo mmoja, unatakiwa kutoa malezi ya kumfanya awe mtoto mwema, kiukweli hata mimi huwa sipendi kumuona Junior hapa nyumbani”“Jamani mume wangu!”“Ndio, nimesema ukweli leo. Muache akae huko huko kwa mdogo wako, kama hiyo laki unaitaka basi nitakupatia ila wala huyo Junior wako asije hapa”Kisha mumewe akaingia ndani na kumfanya mama Junior atafakari vitu vingi sana, na kukumbuka toka wanaanza kuishi na huyo mwanaume, ni wazi hakupenda kuishi na Junior ila kwavile ni mtoto wa mke wake ndiomana alikuwa akiishi nae tu, basi akajisemea,“Ndiomana utakuta mtu ndoa inamsumbua hatari ila anavumilia tu ili kulea watoto na mume wake, kwakweli mtoto anahitaji mapenzi ya baba na mama. Sasa huyu Deo hajawahi kumpenda mwanangu, sasa nisingekuwa karibu na mwanangu vile si ningemfanya ajihisi upweke wa kutokuwa na wazazi jamani! Hata sijui ni kwanini ile ndoa ya kwanza ilinishinda, ila sababu mume wangu alikuwa ni muhuni sana, ila mbona kama Dora alitulia nae, labda sikuumbwa kuwa na yeye ila nimemkosesha Junior vitu vingi sana, kwa baba yake mzazi hapati kitu na kwa huyu Deo pia hapati kitu maana leo kanidhihirishia wazi kuwa mwanangu hampendi, inabidi mimi mwenyewe niamke ili kutengeneza maisha ya badae ya Junior maana sina namna nyingine tena. Ila huyu mwanaume jamani, kaniendekeza sana, nilikuwa nafanya kazi nzuri sana, akalazimisha nichukue mkopo na tukaenda kutengeneza kwao, na sasa nagundua kuwa hana upendo kabisa na mwanangu jamani! Bora James angekuwepo ningempelekea mtoto wake, kweli kabisa mtu hawezi kupenda mtoto asiye wake ila mbona kwa Erick ni tofauti sana! Nadhani ni roho ya mtu tu, nahisi kuchanganyikiwa jamani. Itabidi nipate muda wa kuongea na mtu wa kunishauri”Alijisemea na moja kwa moja kuingia ndani pia.Junior alivyoondoka na ile hela ya mama yake, moja kwa moja alienda dukani na kumnunulia Vaileth zawadi kwani moyo wake ulikuwa ukimsuta sana kwa kitendo alichomfanyia Vaileth.Basi alirudi wakati giza limeshaingia na aliwakuta wote wapo sebleni yani kamavile kuna kikao, kwahiyo akawasalimia pale na kupeleka vitu vyake chumbani kisha alienda kuunganika nao kwenye kile kikao basi baba Angel ndio alikuwa anaongea,“Jamani kesho kutwa tutaenda kwa bibi yenu kule alipo Angel, tutaenda kuwatembelea na kuwasalimia na mengi sana tutaongea kule, hatuwaambii sababu tutaenda kuwashtukiza tu”“Hilo ni swala zuri sana, maana nimemkumbuka sana bibi”“Na wengine je!”“Hata sisi tumemkumbuka”“Ila inaonyesha Erick ndio kamkumbuka sana bibi yake, maana ndio kajibu haraka sana”Wengine wakatabasamu tu, basi baba yao akamaliza kwa kuwaambia,“Usiku mwema jamani”Kisha akamuinua mke wake na kuondoka zao kwenda chumbani na wengine wakainuka pia.Basi Junior alienda chumbani kwake ila alishangaa sana kutokuulizwa kuwa katokea wapi wakati kachelewa kurudi, kwakweli aliona ni ajabu sana basi alienda kuoga na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Vaileth na kumkabidhi zile zawadi alizokuwa amemchukulia, kwakweli Vaileth alifurahi sana na kusema,“Kweli Junior nimeamini kuwa unanipenda sana”“Ndio, nakupenda sana Vai. Wewe ndio kiboko yangu”Basi Vaileth alifurahia sana ile sifa na siku hiyo walilala vizuri sana.Kulipokucha, malango wa chumbani kwa Vaileth uligongwa na kufanya Vaileth ashtuke sana na kumwambia Junior,“Mmh jifiche, huenda akawa ni mama”“Leo, itabidi niingie uvunguni”Basi Junior akaingia uvunguni ili ajifiche, na Vaileth akaenda kufungua mlango ila akakuta ni Erica ndio yupo mlangoni na kumshangaa,“Erica!! Mbona asubuhi asubuhi?”Erica aliingia chumbani kwa Vaileth na kumuuliza,“Junior yuko wapi?”“Mmmh yupo chumbani kwake”“Chumbani kwake hayupo, ni lazima yupo humu”Kisha Erica akaenda kuangalia chooni na kumfanya Junior atoke tu kule uvunguni ili Erica asijue kuwa alijificha wapi na kumuuliza,“Erica, unanitafuta nimefanyaje?”“Baba, anakutafuta huko kaenda chumbani kwako anagonga tu pale basi mimi nikajua tu upo huku”“Mmmh mtoto una mambo wewe”Kisha Junior aliondoka na kuelekea chumbani kwake na moja kwa moja kuelekea kwa baba Angel ili asikie alichokuwa anaitiwa.Vaileth alibaki kumuangalia tu Erica na alimuangalia kwa muda sana ambapo Erica alimuuliza Vaileth,“Una uhakika gani kuwa Junior anakupenda sana?”“Mmmh Erica ndio maswali gani hayo? Mapenzi unayajua wewe?”“Nayajua ndiomana nimekuuliza”“Najua ananipenda, ila Erica tafadhari nakuomba tusiongee mada hizo!”“Mmmh!”Kisha Erica akatoka mule chumbani na kuelekea sehemu nyingine.Junior alienda hadi kwa baba yake mdogo na kuitikia wito,“Bamdogo, nasikia umeniita”“Mmmh nimekuita! Muda gani nimekuita?”“Nimeambiwa kuwa ulikuwa ukigonga chumbani kwangu”“Nigonge chumbani kwako usisikie, kwani ulikuwa wapi?”“Aaaah nilitoka nje kidogo”“Ni kweli niligonga chumbani kwako ila niligonga mara moja tu, upo tayari leo twende kwenye ujenzi ila leo mtawahi kurudi”“Nipo tayari”“Haya, kajiandae”Junior alienda kujiandaa na muda huo huo alipomaliza tu waliondoka zao na kuwaacha waliobaki nyumbani tu.Wakati wapo njiani, kuna mtu alikuwa amejitanda khanga na akasimamisha gari, basi baba Junior akasimamisha na kukuta mtu huyo ni Sia,“Khaaa ni wewe tena!!”“Samahani, naomba tuongee kidogo tu”Baba Angel akaangalia watoto wake kwa muda, ila akashuka kwenye gari na kusimama na Sia nje ya gari pale akimsikiliza,“Haya niambie kilichofanya usimamishe gari?”“Ni hivi, unajua yule Oliva anakutaka tena anakutaka kwa udi na uvumba”“Umeanza tena mambo yako ya kunifatilia”“Nilikwambia kuwa siwezi kuacha kukufatilia sababu nakupenda, nahitaji katika maisha yako tubaki wanawake wawili tu yani mimi na Erica”“Umeanza tena mambo yako, hebu sema ulichonisimamishia hapa”“Ni hivi, kuna siku Oliva alikuletea matunda ofisini, na leo nimegundua kuwa kuna kitu aliweka katika yale matunda yani ungekula tu basi ingekuwa ndio kumfata Oliva tu. Halafu kuna kitu kingine nimesikia ila sina uhakika nacho, nasikia Oliva amepanga kukununulia zawadi Fulani hivi ila sijajua ni zawadi gani, nakuomba usiitumie hiyo zawadi tafadhari”“Mmmh ila wewe jamani!! Kwaheri”Baba Angel alirudi kwenye gari na kuendelea na safari ila Junior na Erick hawakumuuliza chochote kile, basi alienda nao moja kwa moja kwenye eneo la ujenzi na kuwaacha pale kisha yeye akawaaga kuwa anaenda zake ofisini,“Leo sikupanga kwenda ofisini kabisa ila inanibidi kufanya hivi maana kuna vitu naenda kushughulikia, ila nitawahi kurudi kuja kuwachukua ili tufanye maandalizi ya kwenda kwa bibi yenu kesho”Basi baba Angel aliondoka pale na kuelekea ofisini kwake.Baba Angel alipofika tu ofisini kwake, alikutana na ujumbe toka kwa mtu wake wa mapokezi,“Bosi kuna mzigo wako huu”“Asante”Basi baba Angel aliingia na ule mzigo mpaka ofisini kwake, akauweka pembeni na kuanza kufanya kazi zake, ila mara simu yake ikaita na kumfanya kuipokea kwani aliyekuwa akipiga alikuwa ni madam Oliva,“Baba Erick, umepata ujumbe wako?”“Ujumbe gani tena?”“Kuna mzigo nimeacha hapo kwa mtu wa mapokezi”“Oooh nimeupata”“Uangalie basi”Ikabidi baba Angel afungue ule mzigo, na kukuta ni viatu vizuri sana, kwahiyo madam Oliva alikuwa amemnunulia zawadi ya viatu, kwakweli vilikuwa ni vizuri na madam Oliva akampigia tena simu,“Umeona?”“Ndio nimeona, asante”“Jaribisha kwanza, nakuja muda sio mrefu”“Sawa, hakuna tatizo”Basi akakata ile simu na baba Angel akataka kujaribu vile viatu ila kwa muonekano tu vilikuwa ni viatu ambavyo vingemtosha kabisa, ila alipotaka kuweka mguu akajikuta akijiwa na maneno ya Sia kuwa kuna zawadi analetewa na madam Oliva na asiijaribu hiyo zawadi, basi akajisemea,“Ila Sia nae kama kachawi kale kamwanamke jamani! Inawezekana kweli asemayo mmmh! Ila huyu madam nae kasema anakuja muda sio mrefu, ngoja niondoke ili asinikute”Baba Angel alifunga kazi yake na kuondoka zake ambapo moja kwa moja alienda tu kule kwenye ujenzi kwani aliona kama siku yake imeharibika na hata kwenye ujenzi hakukaa sana na kuwataka watoto wake warudi nae tu nyumbani kwa muda huo.Siku ya leo pale nyumbani kwao Erica alitembelewa na rafiki yake Samia na kufurahi sana, basi kwa siku ya leo alienda kukaa nae bustanini huku wakiongea mambo mbalimbali,“Kheee leo Junior na Erick hawapo au wanaangalia mikanda?”“Hawapo, baba kawapeleka huko kwenye ujenzi”“Oooh sawa, sasa bhana kuna jambo nataka nikwambie shoga yangu”“Jambo gani hilo?”“Si kuhusu Junior, ni kwamba Junior alinitongoza”“Mmmh jamani!”“Ndio hivyo, na mimi nikamwambia kuwa bila laki tano siwezi kukubali, sijui Junior kapata wapi zile hela maana akaniletea laki tano kamili, akataka kulala na mimi basi nikamwambia kuwa akatafute hoteli ya chumba laki moja, akatafuta halafu mimi sikwenda, si ndio amechukia hivyo! Wakaja nyumbani na mama yake, kumbe Junior katumia simu ya mama yake kumkopa mama yangu hela, basi imebidi nimwambie mama ukweli”“Mmmh Junior alitaka kulala na wewe!!”“Ndio, alitaka kulala na mimi”“Kwahiyo ungekubali Samia?”“Nisingekubali ndiomana nilimdanganya”“Ila umepata wapi ujasiri wa kumwambia akuletee hela?”“Ndio nilivyofundishwa, baba huwa ananiambia kuwa mimi ni wa gharama sana na mwanaume anayenitaka anatakiwa kunigharamia ndio anipate, sasa Junior ni mjinga hata kama alilipia hoteli si ndio sehemu ya kunigharamia, alitakiwa kuendelea kunifatilia tu sio kuja kuniabisha nyumbani vile”“Kwahiyo Junior anakupenda wewe! Mpaka akakuletea laki tano! Aliipata wapi?”“Sijui, ila Junior kaniletea laki tano kamili. Na Bahati yake hayupo leo, kanikera sana kwanza mimi simpendi yeye yupo mwingine nimpendaye”“Nani huyo?”“Yupo kwenye nyumba hii hii ila simtaji”“Jamani nitajie!”“Aaah natakiwa kuwahi nyumbani leo, kwaheri Erica”Basi Samia aliinuka na kuaga, kwakweli Erica aliwaza vingi ila kwa muda huo kikubwa alichowaza ni Junior kumpa laki tano Samia, na kujisemea,“Kumbe Junior sio muaminifu kabisa, atampendaje Samia wakati anampenda dada Vai!!”Basi akaingia ndani huku akijifikiria kidogo na muda huo huo alitaka kumwambia mama yake,“Ngoja nikwambie kitu mama”“Eeeeh kitu gani hiko”“Basi, Samia kaniambia kuwa….!!”Mara baba Angel na wakina Junior walikuwa wamewasili, kwahiyo Erica ilibidi asiseme tena kwa muda huo.Usiku wa leo, mama Angel na baba Angel walikuwa wakipanga namna ya kesho yake kwa mama yao watakachokifanya,“Kwanza kabisa tutapika chakula hapa cha kwenda nacho”“Sawa mke wangu, hilo ni jambo zuri, halafu mimi niliwaza kuwa labda tununue chakula cha kwenda nacho”“Aaaah tununue cha nini wakati kupika naweza, nipo mimi, yupo Vai na yupo mpendwa wetu Erica yani hakuna kitu kitakachobadilika”“Oooh mtoto wetu Erica yupo vizuri, yani hawa watoto wananifurahisha sana, huko kila ninapoenda na Erick wanamsifia kuwa ni mtoto mwenye akili sana yani hadi najihisi ufahari kuwa baba wa Erick, halafu huku Erica ni binti mwenye tabia nje na yupo vizuri”“Ila umbea wake ndio unamuharibia sifa zake zote”Mara simu ya baba Angel ilianza kuita, na mama Angel alikuwa wa kwanza kuitumbulia macho simu ile na jina liliandikwa ‘Madam Oliva’“Mmmh madam Oliva huyo anakupigia”“Aaaah achana nae”“Mmmh unanipa mashaka sasa, nipe niipokee”Baba Angel hakutaka kurumbana na mkewe kwahiyo alimpa aipokee ambapo muda ule ule madam Oliva alianza kuongea,“Mbona simu zangu hupokei leo nimekukosea nini? Nilikuja ofisini ila uliondoka, hujapenda zawadi yangu?”“Zawadi gani?”“Oooh samahani mama Erick, kwaheri”Kisha madam Oliva alikata simu na mama Angel alimuangalia mume wake na kumuuliza,“Ni zawadi gani hiyo ambayo madam Oliva kakuletea?”“Kaniletea zawadi ya viatu, ila usijali mke wangu hata sivihitaji na nimeviacha kule kule ofisini”“Aaaah ila leo siongei mengi sana, tulale tu muda huu”Baba Angel hakuelewa ni kwanini mkewe leo hajalalamika sana wakati ni kawaida yake yani alishangaa jinsi mkewe alivyokuwa muelewa vile maana huwa inachukua muda mrefu sana kumuelewesha.Kulipokucha walianza kujiandaa wote huku wakiandaa chakula cha kuondoka nacho, muda huu baba Angel alikuwa chumbani akijiandaa pia ila ukaingia ujumbe kwenye simu yake,“Samahani baba Erick, sina nia mbaya mimi mwambie mkeo asinifikirie vibaya, leo nitakuja ofisini kwako ili tuongee vizuri”Baba Angel hakujibu ule ujumbe wala nini zaidi zaidi ya kuufuta na kumalizia kujiandaa tu na alipomaliza, mkewe nae alifika na kujiandaa kwaajili ya safari ambayo walikuwa wameipanga.Basi kila mmoja alipomaliza kujiandaa wakatoka na kuingia kwenye gari ambayo iliwatosha wote kisha safari ilianza ila njiani kuna kijana walimuona na Erica alimuona vizuri na kusema,“Jamani, Elly yule pale. Tumsalimie basi”Mama Angel alimuangalia Erica na kumwambia,“Una kiranga sana wewe, muone vile. Hamna kusimama baba Angel”Basi baba Angel akaendelea kuendesha gari yake bila hata kusimama ila Erica alikuwa akiangalia tu hadi alipomuona Elly ametokomea.Walifika kwa bibi Angel na kupokelewa kwa furaha sana yani bibi Angel aliona raha sana kwa mshtukizo ule aliofanyiwa, basi walikaa wote na kufurahi na muda ule ule walipakua kile chakula ambacho walikibeba ili waje kula kwa pamoja.Wakati wanakula, kuna mgeni alifika na mgeni huyo alikuwa ni dada wa mama Angel yani Mage ambaye walimkaribisha vizuri tu naye ila baada ya salamu tu alikaa na kusema,“Eeeh ni vizuri leo nimewakuta wote, mwambieni Angel ukweli sasa” Wakati wanakula, kuna mgeni alifika na mgeni huyo alikuwa ni dada wa mama Angel yani Mage ambaye walimkaribisha vizuri tu naye ila baada ya salamu tu alikaa na kusema,“Eeeh ni vizuri leo nimewakuta wote, mwambieni Angel ukweli sasa”Kwakweli mama Angel alishtuka sana na kuhisi ubaridi ukipita katika mwili wake sababu hakutaka mwanae apewe siri yake kwa wakati ambao hajaupanga yeye, basi akainuka na kumshika mkono dada yake kisha kutoka nae nje kabisa halafu ndio akaanza kuongea nae,“Dada Mage, nakuheshimu sana ila sipendi unachotaka kunifanyia, kwanini vitu vidogo kama hivi vikatuondolea heshima kwanini? Unajua niliambiwa ila sikuchukulia kwa makini ila leo ndio nimeelewa sasa, kitu gani unachotaka kuifanyia familia yangu?”“Erica, nisikie mdogo wangu si kwa ubaya, unajua Angel amekuwa mkubwa sasa nahofia kisije kutokea kitu kama wewe”“Kitu gani?”“Leo umesahau Erica, si ulitembea na Derrick sababu mlikuwa hamfahamiani!! Nahofia isije kutokea kwa Angel nae akatembea na kaka zake?”“Kwani mwanangu Angel umemuonaje? Haya nilitembea na Derrick kitu gani kilitokea sasa?”“Erica jamani, unakumbuka hadi tulienda kufanya tambiko kwasababu hiyo!!”“Basi ikitokea na kwa Angel tutaenda kufanya tambiko pia, ila usiniharibie familia yangu.”“Sikia nikwambie Erica, kosa kubwa tunalolifanya wanawake ni kumficha mtoto baba yake halisi, halafu huwa tunaona kuwa tumefanya sawa kabisa, ila kuna umuhimu mkubwa sana wa mtoto kumfahamu baba yake halisi, mtoto huyo mmemdanganya akiwa mdogo hadi leo jamani! Mnamkosesha mtoto haki yake”“Kwani akishamjua baba yake halisi ndio inakuwa nini sasa? Dada tafadhari niache, kwanza kabisa unatakiwa umuheshimu mume wangu, ni yeye ndiye amefuta aibu yangu, mlikuwa wa kwanza hapa kunisema kuwa nimezalia nyumbani, mlikuwa wa kwanza kusema nimkubali yoyote wa kunioa, ila akatokea Erick mwenye mapenzi na mimi, sasa nimefanya kosa lipi kumzawadia mtoto? Angel nitamwambia ukweli siku ambayo Erick atasema kuwa tumwambie Angel ukweli ila sio kwa maneno yenu. Halafu dada, katika vitu vyote ukifanya unachotaka kufanya kuhusu Angel kwa hakika tutaonana wabaya, mimi mdogo wako nina roho mbaya sana nikitaka, naomba uniache na familia yangu, nitajua mwenyewe inapoelekea”“Eeeeh yamekuwa hayo, hadi kuonana wabaya kisa kumwambia Angel ukweli!! Yani tatizo lako wewe huyo Erick kakushika masikio sana nadhani huoni kama kuna mwanaume zaidi ya Erick duniani”“Ndio hakuna”“Hahahah sasa ngoja siku moja mumeo akuletee mke mwenzio ndio akili itakukaa sawa, kumbuka mwanaume sio ndugu yako na sio mama yako wala baba yako anaweza kubadilika wakati wowote haijalishi mmeishi kwa amani kwa muda gani. Ila siku akipatikana mwanamke mjanja mbona utabaki kulia tu, usijiamini kupata kiasi”“Kiukweli dada unanichefua”“Kheee kukwambia ukweli ndio nakuchefua!!”“Ndio unanichefua sana yani nahisi kichefuchefu kukuangalia”“Kheee haya kwaheri, fanya unachojisikia”Mage aliondoka zake yani hata hakuingia ndani kuaga wala nini na wala mama Angel hakuona kuwa ni tatizo ila aliona akili yake ikielemewa tu, akikumbuka mambo ya zawadi ya madam Oliva kwa mumewe na vile dada yake alivyosema akipatikana mwanamke mjanja alihisi kizunguzungu tu na yale mambo ambayo dada yake anataka kuyazindua alihisi kuumia kichwa, basi alifikiria kidogo jambo la kifanya kwa muda huo.Mama Angel alirudi ndani ila walimuuliza kuwa imekuwaje, na Angel ndio alikuwa wa kwanza kuuliza basi akamwambia,“Mwanangu, nikirudi nitakueleza vizuri”Wote wakamuangalia na bibi Angel akamuuliza,“Kwani unataka kwenda wapi?”“Mama, wakati nipo nje na dada Mage hapo alipita mdogo wake Johari na kaniambia kuwa Johari yupo kwao. Kwakweli nahitaji kumsalimia maana ni muda mrefu sana, ila sitakawia kurudi”Basi alimuangalia mume wake pale na kumuaga halafu akamwambia,“Tena ni vizuri niende na gari ili niwahi kurudi, sio mbali kutoka hapa”Basi baba Angel akampa funguo ambapo mama Angel alitoka nje na kuingia kwenye gari na kuondoka zake.Safari ya mama Angel ilikuwa ni kwenda ofisini kwa mume wake, kwani alitaka kwenda kuona hiyo zawadi ya viatu ambavyo mumewe aliletewa na madam Oliva, alikuwa akiendesha gari huku akiwaza moyoni,“Nikishachukua hivyo viatu naenda kuvitupa baharini, sitaki ujinga mie au navichoma moto”Yani maneno ya dada yake yalimfanya kuhisi kuwa ndoa yake kwasasa haipo sehemu salama.Alifika ofisini kwa mumewe kama kawaida, mtu wa mapokezi alimruhusu kuingia kwani anatambua kuwa ni mke wa bosi wao kwahiyo walimkabidhi tu funguo, basi aliingia moja kwa moja na kukuta boksi likiwa pembeni ya meza ya mume wake na alipofungua akakuta kuna viatu vile ambavyo vililetwa na madam Oliva, basi aliviangalia kwa makini sana ila muda huo wazo lake la kuvitupa baharini au kuvichoma moto lilipotea na kusema,“Mmmh viatu hivi ni vizuri sana halafu vinaonekana ni vya gharama, nikienda kuvitupa au kuvichoma moto nitakuwa natenda dhambi, ila sitaki mume wangu avae hivi viatu. Kwahiyo cha muhimu nikampe tu mtu mwingine kama zawadi pia”Basi akavichukua vile viatu na kutoka, halafu akafunga mlango wa mume kwenye ile ofisi vizuri kabisa na kurudisha funguo kwa watu wa mapokezi kisha akaondoka zake, alikuwa akiondoka na gari huku akiwaza kuwa vile viatu akampe zawadi nani ila kuvichoma moto roho ilimuuma maana vilikuwa vizuri sana.Wakati yupo njiani alimuona madam Oliva akitembea basi akasimamisha gari ili kumsalimia tu aone anaichukuliaje salamu yake,“Madam habari”Madam Oliva alishtuka kidogo kwani inaonyesha hakufikiria kukutana na mama Angel kwa muda huo, basi akasimama na kuitikia,“Salama, mama Erick”“Unaenda wapi nikupe lifti?”“Aaah hamna, usijali kitu naenda hapo mbele halafu nipo kufanya mazoezi”“Ila mbona hujaja tena kunitembelea?”“Nitakuja tu, kwaheri”Yani madam Oliva alionekana kama ana haraka sana ila mama Angel alihisi kuwa madam Oliva anajishuku tu kwa tabia yake ya kumtaka mume wake.Mage alivyoondoka kwao, moja kwa moja alienda ofisini kwa mdogo wake Tony kwa bahati nzuri siku hiyo alimkuta mdogo wake yupo ofisini basi alisalimiana nae na kuanza kuongea nae,“Mmmh dada leo ofisini kwangu kuna jema kweli! Au yale yale ya kuhusu Derrick”“Mmmh umasikini mbaya sana jamani!”“Kwanini dada, ni mambo ya kuhusu Derrick au kitu gani?”“Hayo, pia yapo ila cha zaidi kilichonileta ni kuhusu Erica”“Kwani Erica kafanyaje?”“Erica, hataki kumwambia Angel ukweli.Wanamnyima mtoto haki yake ya kumtambua baba yake wa ukweli”Kisha akamuelezea vile ambavyo aliongea na mama Angel na ambavyo mama Angel alimjibu, kwakweli Tony alisikitika na kumuuliza dada yake,“Ila dada, kwani Angel kadai hiyo haki ya kumjua baba yake wa ukweli?”“Hapana”“Unajua mtoto hufikia hatua ya kudai kufahamu kuhusu baba yake mzazi ikiwa yule baba anayeishi nae hamjali, hampendi, hamuangalii ndio pale mtoto hujiuliza hivi sina baba mwingine kweli! Sasa kama Angel maisha anayoishi na anayopewa na huyo Erick anaanzaje kudai kumfahamu baba yake halisi? Ikiwa Erick anampenda na anamjali kama mtoto wake kabisa?”“Ndiomana nilianza na kauli ya kusema umaskini mbaya sana”“Sasa umasikini unauhusiano gani na hayo?”‘Nilijua tu utawatetea Erick na Erica kwani ndio waliyokupa maisha hayo uliyonayo”“Sikia dada, unajua mara nyingine unaweza kufanya kitu na kuona unapata faida kumbe ilitakiwa upate faida kubwa zaidi ila tu sababu huna muongozo unaofaa inakuwa ni ngumu sana kwako, ukipata mtu wa kukupa muongozo unatakiwa kumshukuru sana. Mimi nilikuwa nafanya kilimo, sio nilikuwa nib ado nafanya mpaka sasa ila kilimo changu cha kipindi hiki na kipindi kile ni tofauti, Erick kanisaidia kupata ofisi hii na kanisaidia niwe na masoko makubwa kawahiyo kilimo changu kimekuwa bora sana na ninamshukuru kwa hilo, ila wewe ni nani usiyekuwa na shukrani upo hapa tu kulalamika umasikini mbaya kisa umekataliwa kusema yasiyokuhusu!”“Mbona maneno mengi yanakutoka! Hiyo ipo wazi kwasasa mnamuheshimu sana Erica na mumewe Erick, tena mmeacha hata kunisikiliza dada yenu”“Yani dada maneno mengine unayataka tu, wenyewe washakwambia kuwa hawataki umwambie mtoto wao sasa wewe kinakuuma kitu gani? Tena mimi ingekuwa wewe hata wakina Erica nisingewasumbua kabisa”“Ndiomana nasema umasikini mbaya, kwahiyo unataka niwanyenyekee wakina Erica?”“Sio kuwanyenyekea, ila unatakiwa kuwaheshimu pia. Dada kumbuka, mlikuwa mnaishi kwenye nyumba ya urithi na mumeo ila Erica kawapigania hadi sasa mnaishi kwenye nyumba yenu na alifanya kwa upendo tu, alikupa hela ya biashara ila ukaitumia yote, bado Erica hakulalamika bali alikufungulia biashara, hivi unataka mtu akufanyie nini? Na haya mambo uliyoyaanza naanza kuingiwa na wasiwasi”“Wasiwasi wa nini?”“Nahisi biashara uliyofunguliwa umeshaiua na kama bado basi unakaribia kuiua ndiomana umeweza kupata nguvu ya kutaka kuharibu familia ya wenzio na nguvu ya kumfatilia Derrick”“Nilijua tu kuwa nitaonekana naongea porojo sababu tu Erica kawawezesha kwa kupitia mume wake, haya kwaheri”Mage aliamua kuondoka pia kwa Tony ila Tony hakutilia maanani kabisa maneno ya dada yake kwa zaidi zaidi aliendelea tu na kazi zake.Leo Steve alitembelewa dukani na rafiki yake wa muda mrefu sana ila rafiki yake huyu alimkuta Steve yupo muda wote akiangalia simu yake na kumuuliza,“Mmmh hivi na kazi zako unafanya muda gani?”“Kama hamna wateja ndio unanikuta hivi na simu halafu unafikiri huwa nawasiliana na mtu basi!! Huwa naangalia picha tu”“Picha gani?”“Kuna mama mmoja hivi ni mwalimu, jamani huyu mama napenda sana misimamo yake basi huwa naangalia sana picha zake yani nampenda jamani, angenikubali ningemuoa”“Aaaah wewe nawe, hujaoa hadi leo, unatakiwa kutafuta wasichana wadogo, sasa hao wamama si utakuta ni wake za watu!”“Huyo sio mke wa mtu”“Una uhakika gani?”“Kwenye ukurasa wake wa facebook kaandika hivi, ngoja nikusomee ‘single and happy’ umesikia inamaana hana mahusiano yoyote ila huwa anaandika maneno yenye busara sana”“Ushawahi kuwasiliana nae?”“Mmmh yani kila nikiMtumia ujumbe hanijibu, yani nishamtumia hadi basi ila hajawahi kunijibu hata mara ila sichoki”“Basi ngoja nikufundishe njia rahisi itakayomfanya akujibu”“Njia gani hiyo?”Mara Steve akafikiwa na mke wa bosi wake pale dukani yani mama Angel kwahiyo ilibidi aende nae ofisini kuzungumza nae,“Unafikiri Steve nakaa basi!!”“Karibu mama”“Sasa nimekuletea zawadi,ilikuwa ya mume wangu ila havimtoshi ndio nimekuletea wewe”Basi mama Angel akampa Steve vile viatu ambapo Steve alivyoviona alivipenda sana yani na muda huo huo alivijaribisha na vilimtosha vizuri kabisa basi alikuwa akifurahia na kumshukuru sana mama Angel.Muda huo huo mama Angel alimuaga kuwa anaondoka zake, basi aliagana nae pale na kuendelea kumshukuru sana.Alipofika kwa rafiki yake nje akamwambia,“Ona sasa tunaopendwa na mabosi zetu, kaniletea kiatu kizuri sana”“Halafu ni cha gharama sana hiko, nimewahi kuvikuta duka flani hivi nikaulizia bei yake nikaambiwa ni laki tatu na elfu tisini”“Duh!! Hebu nipige picha nijiweke facebook leo”Basi rafiki yake alichukua simu na kumpiga picha Steve ambaye alifurahi sana kupigwa ile picha na muda huo huo aliiweka facebook ila pia alihisi akili yuake kutotulia kabisa na vile viatu alitamani wengi waone kuwa kavaa viatu vya gharama, yani alifunga biashara na kuondoka zake kwa muda huo.Nyumbani kwa bibi Angel walikuwa wakijiuliza sana kuhusu mama Angel hata bibi Angel alijaribu kwenda hadi kwakina Johari ila mama Angel hakumkuta na hakuna aliyesema kuwa alikwenda pale, basi bibi Angel alirudi huku asijue hata cha kumjibu mkwe wake, basi baba Angel akamuuliza,“Eeeh mama, na huko wamesemaje?”“Mmmh!”Mara ndio wakasikia honi ya gari na kujua kuwa mama Angel amerudi kwa muda huo, na kweli muda kidogo tu aliingia ndani ila muda ulikuwa umekwenda sana kiasi kwamba hata hakuelezea alipokuwa zaidi ya kuwaambia kuwa wajiandae ili waondoke halafu alienda kuongea na mama yake ila kama kawaida yake sababu alikuwa na tabia Fulani ya kutokusema ukweli aliweza kumdanganya mama yake na kumfanya mama yake amuamini maana aliona akimwambia vile mama yake basi hatomuelewa kabisa.Walijiandaa pale na kufanya safari ya kuondoka kuelekea nyumbani kwao, ila kwakweli baba Angel hakufurahishwa kabisa yani na alikuwa na hasira sana kwa kile alichokifanya mke wake ila aliona ni vyema akifika nyumbani waanze kuongea na mke wake.Na kweli walivyofika nyumbani tu, walipoingia chumbani baba Angel alitaka kumuuliza mama Angel ila kabla ya hapo mama Angel alianza kumuelezea,“Mume wangu nisamehe sana najua nimekuudhi mno naomba unisamehe, ni hivi mume wangu kwakweli mimi toka jana kuhusu zawadi aliyokupa madam sikuwa na amani nayo kabisa moyoni, nilichokifanya leo nilienda ofisini kwako na kuichukua, nia yangu ni kutoka kuchoma moto vile viatu ila niliona ni vya gharama sana na ni vizuri basi sikuona vibaya kumpelekea mtu mwingine kama zawadi”“Kwahiyo ukampelekea nani?”“Nimempelekea Steve, naomba unisamehe mume wangu”“Ila kwanini unapenda kufanya mambo bila kunishirikisha? Hivi ungeniambia ningekataa kwani? Kwanini mke wangu unakuwa hivyo jamani eeeh! Ungeniambia nisingekataa, na kesho tungeenda wote ofisini kuvichukua ila nadhani ingekuwa ni vyema sana ungenishirikisha kwanza kabla ya kufanya maamuzi yote hayo”“Naomba nisamehe mume wangu”“Unajua una mtoto mdogo ila mke wangu jamani kwanini unafanya haya!! Kwanini huna imani na mimi jamani, nakupenda Erica, kwanini huniamini? Hao wakina Oliva wanini mimi jamani, unajua mtu ukifanya sana uhuni kuna muda unafika unakuwa umechoka na huwezi tena kutenda maovu wala kutamani wanawake tena, jamani mke wangu nakupenda tena sana, kwanini huniamini Erica?”“Nakuamini mume wangu”“Hapana, huniamini hata kidogo laiti kama ungekuwa unaniamini basi usingekuwa unafanya mambo bila kunishirikisha kama leo, kiukweli sijapenda kabisa”“Nisamehe mume wangu”“Unajua umeniabisha mbele ya watoto mke wangu maana wote walikuwa wakiuliza mama yuko wapi? Halafu sina jibu lolote la kuwaambia, umenitia aibu sana leo Erica”Ikabidi mama Angel ambembeleze mume wake kwani alijua ni wazi kafanya makosa ila hakuwa na namna kwa muda huo zaidi ya kufanya vile.Madam Oliva kwa muda huu alikuwa amekutana na rafiki yake Fetty na walikuwa wakiagana sababu alikuwa akirudi nyumbani kwake, ila alishika simu na kushtuka pale pale Fetty alimuuliza basi alimuonyesha kilichomshtua na pale Fetty akamshangaa na kumuuliza,“Sasa umeshtuka nini?”“Viatu alivyovaa na kupiga picha huyu kijana vimenishtua sana”“Kwanini jamani, au sababu ni vizuri sana”“Licha ya uzuri wake, ni hivi yani unajua yule mume wa mtu nilikwambia nampenda basi ndio nilienda kumtafutia zawadi ya viatu kama hivi ndio vimenichanganya akili hapa”“Mmmh na wewe una kilanga, yani mume wa mtu ushaanza kumgharamikia hadi viatu!”“Jamani, nampenda, yani nampenda sana na nahitaji kumpata ila kwa hivi viatu hachomoki”“Kivipi?”“Nitakwambia shoga yangu hata usiwe na wasiwasi, ila huyu kijana inaonekana hali yake ni ya kawaida sana hivi amejigharamikia kweli kununua kiatu kama hiki!!”“Soma kwanza alichoandika juu”Madam Oliva akaanza kusoma,“Zawadi kutoka kwa madam le boss”Basi madam Oliva akaguna,“Mmmmh! Eti zawadi”“Ndio, kwani yeye hawezi kupewa zawadi!! Mbona anaonekana ni kijana mzuri sana halafu mstaarabu”“Aaaah usiku saivi, kwaheri shoga yangu tutaonana tena tu”Basi madam Oliva alirudi nyumbani kwake ili alikuwa na mawazo sana kama baba Angel alivaa vile viatu au la, tena hakufikiria kama viatu alivyokuwa anaviona kwenye mtandao ndio hivyo hivyo alivyompa baba Angel.Kulivyokucha tu, baba Angel leo aliamka na kujiandaa ila alipoondoka kwake hakwenda kwanza ofisini zaidi ya kwenda dukani kwake na kumkuta Steve akiwa tayari ameshafika, cha kwanza bila hata salamu alimuuliza,“Viatu alivyokuletea jana mama Angel viko wapi?”“Vipo nyumbani bosi”“Aaaah naomba kesho uje navyo”Kisha baba Angel akaondoka zake na kuelekea ofisini kwa muda huo, kwakweli Steve alishangaa sana kwani aliletewa vile viatu kwa uzuri kabisa na mama Angel ila alishangaa sana baba Angel kuvihitaji tena akatafakari kwa muda na kumpigia simu mama Angel,“Mama, kuna tatizo kidogo huku”“Tatizo gani hilo?”“Sijui ni kwanini ila baba kaja hapa anahitaji vile viatu ulivyonipa jana”“Mmmh!”“Ndio, kasema kesho nije navyo ofisini ili nimpatie”“Sasa sikia usifike navyo wala nini ila mimi nitakuletea kesho asubuhi viatu vya kufanana na hivyo umpatie, sawa!”“Sawa mama hakuna tatizo”“Na kama kuna lingine atasema niambie mapema, ila usimwambie kama umeongea na mimi. Nikiweza kuvileta leo basi nitakuletea leo leo ila nikishindwa basi nitakuja kesho asubuhi”Kisha mama Angel alikata ile simu huku akitafakari kuwa kwanini mumewe ameamua kufanya vile!alifikiria sana kwani siku hiyo hata mumewe hakumchukua Erick na Junior kuwa aende nao kwenye ujenzi kumbe alikuwa amepanga kwenda dukani kwanza, alijiuliza ila tu hakuhitaji kumuuliza mumewe wala nini, na moja kwa moja alienda kwa dereva wao na kumuelekeza aina ya vile viatu ili akamtafutie dukani ambapo yule dereva aliondoka muda ule ule.Baba Angel alifika ofisini kwake na kuwa kama mtu anayetafakari jambo Fulani na kuchukua simu yake huku akiangalia ujumbe wa simu ambapo kulikuwa na ujumbe wa madam Oliva, na ujumbe huu ndio uliomchanganya na kumfanya ile asubuhi kabisa aende kwenye duka lake, basi alisoma tena ule ujumbe,“Baba Erick kama zawadi yangu huitaki basi nitakuja ofisini kwako kuichukua”Muda kidogo alifika madam Oliva na kusalimiana nae halafu walianza kuongea,“Hujaniambia chochote kuhusu ile zawadi nilikupa, viko wapi vile viatu?”“Vipo nyumbani kwangu”“Ila kwanini baba Angel hutaki zawadi yangu jamani!! Ungeona nilivyojikakamua kuitafuta zawadi ile dah!”“Naelewa madam, na zawadi yako ni nzuri sana ila vile viatu havinitoshi”“Jamani, si nilikwambia ujaribu ukakataa siku ile, unadhani mimi sijui namba unayovaa? Kabla sijakuchukulia kiatu nilichunguza kwanza namba unayovaa, sema tu hujapenda kiatu changu. Kikowapi sasa?”“Njoo kesho uchukue, maana nimeviacha nyumbani”“Sawa, ni zawadi gani nikuletee ambayo utaipenda?”“Mmmh labda saa ya mkononi”“Basi nitakuletea hakuna tatizo, ila naomba yani naomba ukubali zawadi yangu”“Usijali madam, hivi shule bado wakina Angel hawajapangiwa?”“Bado, ila wakipangiwa tu nitakuja kukwambia kwani una mpango wa kuwapeleka shule za Serikali? Kesho nitakuja tuongee shule nzuri za kuwapangia watoto”“Sawa madam, hakuna tatizo”Basi madam aliaga na kuondoka zake, ila siku hiyo baba Angel hakukaa sana ofisini pia kwani muda kidogo tu aliamua kurudi nyumbani kwake.Yule dereva alirudi nyumbani na viatu ambapo mama Angel alipoviangalia akaona vile viatu havifanani na vile anavyovitaka,“Duh! Umenunua bei gani hivi?”“Nimenunua elfu hamsini mama”“Mmmh sio hivi kwanza havifanani na vile nilivyokuelekeza kabisa, vile sidhani kama vinauzwa chini ya laki tatu. Naelewa viatu vya aina ile. Ila ngoja niende mwenyewe basi”Mama Angel akaenda ndani kujiandaa ili aende mwenyewe ila muda huo huo mumewe alirudi nyumbani na kumfanya ashindwe kutoka tena na kubaki tu na mumewe ila hakumuuliza chochote kuhusu kwenda dukani zaidi zaidi alimuuliza ratiba ya kesho,“Mume wangu, leo naona hujaenda kabisa kwenye ujenzi, tatizo ni nini? Na kesho je ratiba yako ikoje?”“Aaaah leo, sijui hata ila akili yangu haikuwa sawa nadhani. Halafu kesho ni lazima niende kwenye ujenzi, tunaenda kumalizia ujue, halafu kuna vitu natakiwa nikaangalie vizuri, kwahiyo kesho nitaondoka na wakina Erick asubuhi na kwenda nao kwenye ujenzi halafu nitaondoka na kwenda kazini mara moja”“Oooh sawa mume wangu, kwahiyo inabidi niwaambie wakina Erick wajue eeeh kama kesho mtatoka”“Ndio, ni vizuri ukawaambia”Basi mama Angel alienda kuongea na wakina Erick ila baba Angel alishangaa sana moyo wake ukimuuma sana yani hakuwa na amani kabisa, viatu vile aliona vikimkosesha amani basi akajisemea kuwa kesho yake akitoka kwenye ujenzi ndio ataenda dukani kuchukua viatu halafu ataenda navyo ofisini,“Yani nikishafanya hili nahisi moyo wangu utaridhika, sijui kwanini nimekosa amani kiasi hiki jamani! Sio kawaida yangu yani sielewi”Aliamua tu kujilaza huku akitafakari mambo mbalimbali.Siku hii kulivyokucha tu baada ya baba Angel kuondoka na wakina Erick, basi mama Angel nae alijiandaa na kuamua kuondoka nyumbani kwake kwenda dukani, kwahiyo mtoto alimuacha chini ya uangalizi wa Vaileth.Alifika duka kubwa la viatu na kuangalia vile viatu avitakavyo, basi akaviona na kuvichukua kisha akaenda kulipia hela, ila wakati anatoka hapo dukani alikutana na rafiki yake wa muda mrefu sana Fetty na kufurahi kumuona na kuanza kuongea kidogo,“Umebeba nini Erica?”“Mmmh wewe nawe, umbea huachi jamani ni viatu hivi”Fetty alichukua ule mfuko na kuviangalia kisha akasema,“Kheee ndio umeamua kuja kumnunulia shemeji, naona viatu vimeingia hivi ila wanavaa wenye hela zao. Kuna shoga yangu kanunua kama hivi kumpelekea mume wa mtu huko”Mama Angel alacheka na kusema,“Umeanza sasa, yani yote yanakutoka wewe, hata kama hayupo utasema yupo”“Kweli nakwambia, sasa kwanini nidanganye? Shoga yangu anaitwa Oliva”Mama Angel akashtuka kidogo na kuamua kumvuta pembeni Fetty ili waongee vizuri, kisha akamuuliza,“Sijakuelewa, yani kanunua kumpelekea mume wa mtu?”“Ndio, yani Oliva anampenda huyo mwanaume kufa na kupona na amesema akivaa tu vile viatu basi kampata”Mama Angel alihisi kama tumbo lake kuunguruma kidogo. Mama Angel akashtuka kidogo na kuamua kumvuta pembeni Fetty ili waongee vizuri, kisha akamuuliza,“Sijakuelewa, yani kanunua kumpelekea mume wa mtu?”“Ndio, yani Oliva anampenda huyo mwanaume kufa na kupona na amesema akivaa tu vile viatu basi kampata”Mama Angel alihisi kama tumbo lake kuunguruma kidogo.Fetty alihisi kitu kwa mama Angel na kumuuliza,“Vipi tena shoga yangu ndio unaibiwa mumeo nini?”“Hata sielewi, hebu muulize vizuri huyo Oliva kuwa ameweka nini kwenye hivyo viatu hadi aweze kumteka kirahisi huyo mume wa mtu!”“Basi hivyo huniamini wewe, nakwambia ukweli huniamini. Oliva nimesoma nae sekondari ni rafiki yangu mkubwa sana, yeye kila leo kuponda tu wanaume yani hakuna mwanaume ambaye huwa anasifiwa na Oliva, sasa siku nimekutana nae na kuanza kumsifia huyo mume wa mtu kwa hakika nilishangaa sana ila ndio hivyo anampenda huyo mume wa mtu kufa na kupona”“Unajua nini Fetty, wewe ni rafiki yangu na sio rafiki yang utu ila upo kama ndugu yangu kwani ni mengi sana umenisaidia, hebu tuingie kwanza kwenye gari halafu nikueleze kidogo”Basi waliingia kwenye gari, na muda ule mama Angel hakuona kama ni vyema kumficha Fetty kwani alijifunza pia kuwa mambo mengine ni vyema kusema ili uweze kupata msaada kuliko kukaa nalo moyoni peke yako likakutesa tu, basi alianza kumuelezea,“Unajua ulivyoniambia Oliva nimeshtuka maana kuna mtu anaitwa madam Oliva, kwakweli nina mashaka nae sana kwa mume wangu. Huyo Oliva ni mwalimu?”“Ndio ni mwalimu, tena ana vituo vyake vya kufundisha kozi mbalimbali na ana saluni yake”“Mmmh ndio huyo huyo wala sio mwingine”“Kwahiyo mwanaume anayemnyemelea ni shemeji?”“Ndio, ngoja nikuelezee kidogo”“Eeeh niambie”Basi mama Angel alimueleza vile ambavyo madam Oliva kaweka ukaribu na mume wake, na ambavyo alivyompelekea zawadi ya viatu na yeye kwenda kuvitoa na ambavyo mumewe alivyobadilika,“Duh! Pole sana, unajua hata siamini kama Oliva kaanza mambo ya ushirikina sababu ya mwanaume tena mume wa mtu!! Dah siamini, tena mume mwenyewe ni mume wa shoga yangu kipenzi, jamani! Ila dunia duara bhana, unayemfahamu wewe kumbe anamfahamu mtu mwingine. Sasa Erica shusha presha shoga yangu, namuendea Oliva hewani muda sio mrefu halafu nitaweka sauti kubwa kama yupo sehemu nzuri basi ataongea tu vizuri”Basi muda huo huo Fetty akachukua simu yake na kumpigia madam Oliva ambaye hakuchukua muda aliipokea ile simu,“Kheee shoga yangu uko wapi?”“Nipo kwangu”“Nataka kuja kwako leo”“Aaaah sio leo jamani, nitakuja kukuchukua siku nyingine”“Mmmh jamani kwanini?”“Yani ni hivi, yule mume wa mtu nilikwambia basi leo nitamuweka mikononi mwanangu na kuja nae nyumbani kwangu yani sitamuachia wiki nzima”“Mmmh Oliva jamani, humuonei huruma mke wake?”Yani wakati huo mama Angel alikuwa akihisi tumbo kumuunguruma tu na akitetemeka kwa hasira, basi madam Oliva aliendelea kuongea,“Nimuoneehuruma ya nini sasa wakati hata yeye mwanaume huyo alimuiba kwa mwanamke mwenzie? Mbona yeye hakumuonea huruma yule mwanamke?”“Mmmh kwahiyo hata yeye alivuruga ndoa ya watu? Ila Oliva huyo mume wa mtu imekuwaje hadi umtake?”“Yani siku moja nilikumta huyo mwanamke wa kwanza wa huyo mwanaume akilalamika sana kuhusu huyo mwanaume na kusema hawezi kumfanya kitu sababu anampenda sana, nikamuuliza kwanini ila alidai hakuna mwanaume kama huyo duniani, kiukweli na mimi nahitaji mwanaume wa tofauti kwahiyo nikaona huyu ndio atanifaa”“Haya sasa utampataje?”“Mwanzoni si nilikwambia kwenye viatu nilivyompelekea kuna siri kubwa sana, sasa leo nampelekea saa na lazima ataivaa tena nitamvisha mwenyewe maana kuna siri nzito sana na baada ya hapo nitaondoka nae, hapa naweka mambo sawa kwanza hapa nyumbani ndio niende”“Kheee sikuwezi, basi utaniambia hiyo siri”“Tukionana nitakwambia hakuna tatizo, ila leo ni siku yangu muhimu sana”Basi Fetty alikata ile simu na kumuangalia mama Angel ambaye alikuwa akitoa machozi tu kwa muda huo, akamwambia“Sasa shoga yangu kwasasa kulia hata hakusaidii, cha msingi unatambua mumeo alipo basi fanya juu chini ukamfate na urudi nae nyumbani na ujaribu kumueleza kila kitu ili uokoe ndoa yako ila kulia hakutakusaidia ndugu yangu”“Yani nimechanganyikiwa ujue”“Najua ndio, inauma na lazima ikuchanganye ila chukua hatua sasa, muda ni huu nenda kamfate mumeo kabla huyo Oliva hajamfikia, unajua tatizo ni rahisi kuingia ila ni gumu kutoka, utatambua ukweli mume wangu karogwa ila kila siku utaomba na kulia, mpaka siku akiachiwa ni umehenya sana, shukuru Mungu umeonyeshwa ni kitu gani kinaendelea juu ya mume wako, basi chukua hatua ili umuokoe mapema”Basi mama Angel aliagana na Fetty ambaye alishuka kwenye gari na muda ule ni moja kwa moja alienda ofisini kwa mume wake.Mama Angel alivyofika ofisini hakumkuta mume wake, yani hapo ndio tumbo joto kwani alihisi pengine huyo madam ndio kashamchukua, basi akampigia simu,“Uko wapi mume wangu?”“Kuna mahali nipo nakunywa supu”Mama Angel aliumia pia, akakumbuka kipindi wakienda kazini na mumewe basi mambo mengi mumewe alimwambia kabla ya kuyatenda yani baba Angel kama akitaka kunywa supu lazima amwambia mkewe na ampitie ofisini kwake waende pamoja, na muda wa kutoka mara nyingi alikuwa akirudi na mumewe nyumbani, kwahiyo aliona kama shughuli za uzazi zimemzuilia yeye kufanya mambo mengi sana, akaamua kumpigia tena simu,“Mimi nipo hapa ofisini kwako mume wangu, niambie ulipo nije”“Kheee mama Angel, umekuja ofisini!! Basi nakuja muda sio mrefu”Na kweli muda sio mrefu baba Angel aliwasili, basi mke wake akamwambia,“Kuna jambo nahitaji kuongea na wewe ila sio hapa inatakiwa tukaongelee nyumbani”“Jambo gani hilo mama Angel, mimi nina kazi nyingi sana leo”“Nakuomba sana mume wangu, nipo radhi kesho tuje wote ofisini nikusaidie kazi zako”“Na mwanangu utamuacha na nani? Kwa mfano leo mtoto umemuacha na nani?”“Erick, hebu kumbuka uliwahi kuniambia kuwa watoto hawabadilishi chochote katika maisha yetu maana sisi ndio tunaopendana zaidi, nitabaki kuwa Erica wako na utabaki kuwa Erick wangu, unakumbuka hilo!! Ulisema watoto ni sehemu tu ya kuchangamsha familia, sasa leo kwanini uchukie sababu ya mimi kumuacha mtoto!!”“Kwanza umenielewa vibaya mke wangu, sijachukia ila nimekuuliza maana mtoto yule bado mdogo sana, nakupenda mke wangu na hilo halitabadilika”“Basi twende nyumbani, nakuomba Erick”Ingawa Erick alikuwa na kazi nyingi ila kwa hamasa za mke wake aliona kweli mkewe anahitaji kwenda nae nyumbani, ikabidi tu akubali na wakatoka nje ya ofisi, kisha baba Angel akamuuliza,“Tutaondoka na gari yangu au yako?”“Tutaondoka na gari yangu halafu gari yako tutamtuma dereva aje kuifata, nakuomba usikatae mume wangu”Baba Angel alikubali na kupanda kwenye gari na mke wake ila wakati wanaondoka tu mama Angel alimuona madam Oliva akifika kwenye ofisi ya baba Angel lakini lile tukio la kufika madam Oliva wala baba Angel hakuliona na kumfanya mama Angel kutokuliongelea wala nini.Nyumbani nako, Ester alikuwa akilia sana na kila walichokuwa wakijaribu kumpa alikuwa akikataa na kuendelea kulia, basi Erica na Vaileth wakashauriana kuwa wapi simu ila muda wanapiga simu tu na wazazi wao walikuwa wamefika hivyobasi mama Angel akamchukua mwanae na kwenda kumbembeleza na kumnyonyesha, mumewe aliingia chumbani na kumlalamikia,“Unaona mke wangu, nilikwambia kuwa mtoto huyu bado mdogo na anakuhitaji sana kwa ukaribu ukaona sijui naongea nini, hivi ungenipigia simu nisingerudi nyumbani jamani hadi unifate!”“Sio hivyo mume wangu, kuna matukio yamefanya mimi niwe hivi leo unajua nakupenda sana na pia naogopa sana kukupoteza mume wangu”“Ooooh leo umeniambia neno tamu sana mke wangu, haya sasa malizia kumnyonyesha mtoto tuweze kuongea sasa”Basi mama Angel aliendelea kumnyonyesha mtoto huku akifikiria kwanza jinsi ya kuanza kuongea nae mpaka mumewe amuelewe, Ester alilala basi mama Angel alimlaza na kumsogelea mumewe kisha akamtaka wasimame na kumwambia,“Naomba tushikane mikono na tuombe”“Kheee mama Angel, tuombe kuhusu nini sasa?”“Nahitaji tuombe na tuvunje hila za shetani ila nitakachoongea na wewe kwa muda huu upate kunielewa”“Jamani, inamaana mimi sielewi mpaka maombi!”“Sina maana hiyo mume wangu, ila hili swala kabla hatujaliongelea inahitajika maombi kwanza”Ilibidi tu baba Angel akubali ila kiukweli yeye binafsi hata hakujiandaa kwaajili ya maombi halafu alikuwa akilna uvivu sana, yani mwili wake ulikuwa na uzito sana kufanya maombi kwahiyo pale aliyekuwa akiomba ni mama Angel mwenyewe.Baada ya maombi yale ndio alianza kuongea na mume wake,“Unajua Mungu anatupenda sana sisi, kwanza kabisa katuvusha vikwazo vingi sana, kama milima na mabonde kwakweli tumevuka, penzi letu limepigwa vita sana ila tuliweza kufanikisha hadi mwisho wa siku tukaoana na leo ni mke na mume, nakupenda na unanipenda mume wangu. Mungu bado hajatuacha na anaendelea kulinda penzi letu ndiomana ikiwa kuna mtu mbaya anataka kujiingiza kwetu basi Mungu atatufunulia mtu huyo”“Mtu gani sasa mbaya kajiingiza kwetu”“Madam Oliva”Baba Angel akashtuka, ndipo mama Angel aliamua kumwambia baba Angel mlolongo mzima yani kwa muda huo hakumficha kitu chochote kile, kwakweli baba Angel nae alibaki akishangaa sana kuwa ile kitu inakuwaje kwa namna ile, mara gafla ujumbe ukaingia kwenye simu yake baba Angel alipouangalia ulikuwa umetoka kwa madam Oliva, basi akampa mkewe ile simu ilia some ule ujumbe,“Uko wapi Erick, nimekuletea ile zawadi ya saa ni nzuri sana maana ina jina lako katikati, uko wapi muda huu?”Kisha mama Angel akamuangalia mume wake na kumwambia,“Ndio ningekuwa nakukosa hivi mume wangu!!”Baba Angel aliinuka na kumkumbatia mkewe kisha akamwambia,“Asante kwa kunijali, unajua sikuelewa kuwa huyu mwanamke ana akili mbovu kiasi hiki! Ukimuona ni mwanamke mwenye akili timuma kumbe ana akili mbovu kabisa, mimi nakupenda wewe mke wangu na hilo halitabadilika”Mara madam Oliva alianza kupiga simu baada ya kuona kuwa ujumbe wake haujibiwi, na mama Angel ndio alipokea simu ile na kuanza kuongea nayo,“Madam, nakuomba kwa amani kabisa muache mume wangu, mimi ndio ninayejua kuwa huyu mwanaume nimetoka nae wapi, naomba niachie mume wangu. Hila zako zote unazozifanya ili umteke mume wangu nimezijua, mara umtegeshee kwenye viatu na sasa kwenye saa, tafadhari niachie mume wangu”Madam Oliva hakuweza kuendelea kusikiliza kwani muda huo huo alikata ile simu, basi mama Angel na baba Angel walianza kuongea vizuri sasa kuhusu maisha yao.Kwakweli madam Oliva hakupendezewa kabisa na kujiuliza kuwa ni mtu gani ambaye anafanya kazi ya kutoa siri zake, kwani hakupenda yale mambo yamfikie mama Angel bila hata kufanikiwa, kwahiyo alichukia sana na muda huu alitafuta mtu wa kuongea nae na moja kwa moja alimpigia simu Fetty,“Uko wapi muda huu?”“Nipo nyumbani kwangu”“Naomba nije nikuchukue tuje wote nyumbani kwangu”“Kheee yule mgeni vipi tena shoga yangu?”“Dah! Sijui hata nikuelezeje ila nitakuelezea tukifika nyumbani, nahitaji mtu wa kuongea nae kwa wakati huu”“Sawa, hakuna tatizo njoo tu unichukue”Basi madam Oliva akaamua kwenda kumfata Fetty nyumbani kwake.Madam Oliva alifika nyumbani kwa Fetty na kumchukua Fetty kwenda nae nyumbani kwake ili kuongea nae kiasi, basi walivyofika akaanza kumwambia,“Unajua sielewi yani sielewi kabisa, sijui nani kamwambia mke wa yule mwanaume jamani! Sielewi mimi”“Kwani imekuwaje?”“Mke wake kaja juu, yani nimempigia simu yule baba kapokea mke wake na kusema nimuache mumewe, dawa ninazotaka kumfanyia ameshazigundua. Sijui nani kamwambia”“Pole, kwani ni dawa gani hizo? Halafu Oliva umeanza lini mambo ya madawa hayo shoga yangu?”“Sikia nikwambia, nilitokea kumpenda sana huyu mume wa mtu na hata sikujua kama nitaweza kumpata, basi nina shoga yangu mmoja hivi anafanya kazi kwenye shirika flani la kifedha huwa naongea nae mambo mengi sana, nikamwambia akasema kuna bibi mmoja ana dawa za asili, sio limbwata la kumfanya mwanaume bwege sijui hapana ila ni dawa za asili hata yeye alizitumia kumpata mume wake, basi nikaona ni vyema anipeleke kwa huyo bibi na mimi ili niweze kupata hizo dawa za kumteka huyu mume wa mtu. Basi nikaenda nae na huko nikajifunza mambo mengi sana”“Eeeeh mambo gani?”“Ni hivi, yule bibi aliniambia kuwa inatakiwa kwanza nijue udhaifu wa huyo mke wa huyo mwanaume ili iwe rahisi kwangu kumteka mumewe maana udhaifu wake ndio nitautumia kama fimbo, ila nikamwambia udhaifu wa huyo mwanamke mimi siujui maana sijamzoea basi akasema ngoja afanye dawa zake za asili na kweli aliniambia udhaifu wa yule mwanamke”“Udhaifu gani?”“Basi aliwasha moto na kutupia dawa kwenye moto huo akaniuliza jina la huyo mwanaume nikamwambia anaitwa Erick basi akaanza kuniambia kuwa mke wa huyo mwanaume anaitwa Erica halafu huyo mwanaume ni anampenda sana mke wake tena sana ila mkewe ana udhaifu mwingi sana sema huyu baba anamvumilia tu mkewe, aliniambia udhaifu mmoja tu ambao ndio nilikuwa nataka kuutumia kwasasa kumteka mumewe kwani alisema nikishamteka basi udhaifu mwingine wa huyo mwanamke ningeujua kwa kupitia mkewe na hapo ndio ningeboresha zaidi na kufanya anipende mimi zaidi maana hizi dawa ni za muda tu”“Sasa alikwambia kuwa huyo mwanamke ana udhaifu gani?”“Nasikia huyu mwanaume ana upendo sana halafu anajua kujali ila mkewe sio mtu wa kujali, kitu kidogo tu nasikia huyu mwanamke hana kawaida ya kumnunulia mumewe zawadi kabisa ila yeye anapenda kuletewa zawadi na mume wake. Yule bibi akaniambia kuwa, yule baba anapenda mtu awepo wa kumpatia zawadi ila hayupo, yule mwanamke hana tabia hiyo sababu anahisi mumewe hana uhitaji, basi ndio akaniuliza zawadi gani nzuri ninayoweza kumpatia huyo mwanaume? Basi nikafkiria na kuwaza vile viatu, alisema nikatafute nimpelekee kwanza, basi nikanunua na kumpelekea yule bibi ambapo alivinuizia kuwa huyu baba akiviona tu kwanza awe anatamani kuvivaa na asipovivaa ahisi kichwa chake kumvuruga sana, akivivaa basi mawazo yote ni juu yangu kiasi nikimwambia twende nyumbani anakubali bila ubishi na anaanza kunipenda sana, na vile mimi nampenda basi inakuwa maradufu. Ila viatu hata sijui imekuwaje, nilimuuliza nimpelekee zawadi gani nyingine akasema nimpelekee saa basi nayo ndio nikaipeleka kwa bibi na akainuizia na kusema nifanye juu chini nimvishe na baada ya hapo angeondoka na mimi na kurudi nami nyumbani, basi hapa ndio ningemfanyia makeke yote sababu kuna dawa nishanawa sehemu za siri ambapo lazima angeomba mechi na hapo asingeganduka kwangu, unajua hapa nimechanganyikiwa sana”“Duh pole, kwahiyo na dawa yenyewe ushaitumia hiyo ya sehemu za siri?”“ndio kwani nilijua leo hapindui nilijua lazima nitarudi nae tu na tungekuwa wote, sijui ni nani ananizunguka jamani”“Pole sana shoga yangu, nakuhurumia sana sijui hata utafanyeje?”“Yani acha tu, hebu nishauri ndugu yangu sielewi kitu hapa”“Sasa, ngoja nirudi nyumbani pia nitulize akili yangu halafu nitakupigia simu ili tuongee vizuri zaidi ndugu yangu na nitakwambia cha kufanya”Sababu muda nao ulikuwa umeenda ikabidi tu madam Oliva amruhusu Fetty kuondoka, kwakweli akili yake ilikuwa imechanganyikana kiasi kwamba hata kumsindikiza hakumsindikiza.Fetty aliondoka huku akifikiria mambo mengi sana na kujiuliza,“Jamani, sasa Erica anashindwa kumnunulia mumewe zawadi jamani!! Ila simshangai sana ni kawaida ya wanawake wengi tukiolewa tunasahau jambo hili ni dogo ila huwa tunasahau ni kama baadhi ya wanaume nao huwa wanasahau jambo hilo. Zawadi ni kitu kidogo sana ila kumbe zawadi inaweza kufanya ukaribishe mchepuko ndani!! Nitamwambia shoga yangu ajirekebishe halafu na mimi pia nimejifunza jambo jamani, kesho nitaenda kumtafutia mume wangu zawadi mmmh makubwa haya ya leo”Basi Fetty alivyofika nyumbani kwake tu alimpigia simu mama Angel na kuongea nae,“Kuna mambo nahitaji kuzungumza na wewe, kwahiyo tukionana nitakwambia rafiki yangu”“Mambo gani hayo?”“Tukikutana tutazungumza, ikiwezekana kesho tuonane ndugu yangu”“Sawa, hakuna tatizo basi njoo nyumbani maana si unajua ninalea!”“Sawa, nitakuja. Utanilekeza basi”Wakaongea pale ila alivyokata ile simu tu muda huo huo alipigiwa simu na madam Oliva na kuanza kuongea nae,“Tatizo nini Oliva?”“Jamani, mwenzio sipo sawa yani sipo sawa kabisa”“Kwanini?”“Nahitaji mwanaume, kiukweli nahitaji mwanaume jamani!”“Kheee pole jamani, zile dawa ulizotumia”“Yani acha tu, dawa zinanitesa hizi, nahitaji mwanaume kwasasa hata sijui nifanyeje? Yani nimejikuta nikimtamani hata mlinzi wangu, Eeeh Mungu anisaidie jamani nisifikie hatua ya kujidhalilisha namna hii”“Pole ndugu yangu, sasa ngoja nikushauri kitu”“Kitu gani?”“Chukua simu yako, ingia kwenye mtandao wa kijamii halafu angalia picha za watu, matukio mbalimbali, tafuta zile kurasa za vichekesho ucheke humo hadi siku ipite, pole sana”“Mmmh huo ushauri wako jamani sijui kama utanisaidia, nipo na hali mbaya sana mwenzio”“Pole, kesho nitakutafuta ili tuongee kidogo”“Asante, ila sipo sawa kabisa yani”Alikata ile simu kiukweli Fetty hakujua ni njia gani ya kumsaidia Oliva ila alimuhurumia sana na kusema,“Ila huyu nae ni kilanga chake, hivi mwanaume hata hamjakubaliana unaenda kutumia dawa jamani!! Si ndio mwanzo wa kutembea na mbwa mmmh!! Halafu ni mwalimu, kwakweli Oliva kajiharibia sifa kwaajili ya ujinga wa kutaka kuiba mume wa mtu”Alimsikitikia sana maana hakujua ni kitu gani rafiki yake angekitenda.Steve alikuwa ametoka zake kuoga na akijiandaa kulala ila alichukua simu yake na kutembelea kwenye mtandao kidogo, ila alivyoingia tu alibambana na picha ya madam Oliva hapo moyo wake ukalia paaa na kuzidi kumpenda huyu madam, aliona kabisa kuwa anashindwa kuzuia hisia zake, basi aliamua kumfata sehemu ya ujumbe na leo alimuangikia ujumbe,“Nakupenda sana”Ila hakufikiria kama madam Oliva angemjibu kwani ilikuwa ni kawaida yake kutokujibu jumbe za huyu mtu ila alishangaa kuona madam kama anaandika vile alijikuta akiwa na hamu sana ya kupata jibu la huyu madam,“Wewe nawe kila leo naona jumbe zako, kwani unataka nini kwangu?”“Nakuhitaji, kwakweli nakupenda sana. Natamani uwe mke wangu na tuishi pamoja”“Unamaanisha hayo unayoyasema?”“Ndio namaanisha, nakupenda sana yani sijielewi juu yako”“Unaweza kuja nyumbani kwangu muda huu?”“Naweza ndio, nielekeze nije”Basi madam Oliva alimuelekeza na muda huo huo Steve alijiandaa haraka haraka na kutoka kwao na moja kwa moja alipanda pikipiki na kwenda hadi alipoelekezwa na madam Oliva, hakujali umbali ila alichojali yeye ni kuonana na madam Oliva.Na kweli alifika na kumtumia ujumbe,“Tayari, nipo nje ya nyumba uliyonielekeza”“Mmmh upo serious kumbe, gonga hapo namwambia mlinzi akufungulie”Ni kweli Steve aligonga na kufunguliwa na mlinzi na moja kwa moja akaingia kwenye ile nyumba na kukaribishwa na madam Oliva ambaye jambo la kwanza alimuuliza,“Hivi wewe umejiamini vipi kufika kwa mtu ambaye humfahamu tena kwa muda kama huu?”“Ni sababu ya upendo nilionao juu yako, nimejikuta nikijitoa muhanga tu na kuja”“Halafu umenishangaza ujue, hata namba yangu ya simu hukuwa nayo?”“Nilisahau kabisa kuhusu simu jamani, yote sababu nakupenda sana”“Ulipanga ukifika na kuniona ufanye kitu gani?”Basi Steve hakutaka kupoteza muda kwani alimsogelea madam na kumkumbatia kisha akambusu na wote kwa pamoja waliingia chumbani na kulala huko hadi asubuhi kabisa kwahiyo wakawa wamefungua ukurasa mpya wa mapenzi, kilishomshangaza madam Oliva ni kuwa alijikuta akimpenda huyu Steve kupitaLeo Fetty alienda nyumbani kwa rafiki yake yani mama Angel kama ambavyo walipanga jana yake kuwa waonane na waweze kuzungumza, na alipofika pale wanaenda kukaa bustanini na kuongea mambo mbalimbali ambapo Fetty alimueleza kila kitu ambacho kaambiwa na Oliva kisha alimuuliza rafiki yake,“Ila na wewe unashindwa nini kumnunulia mumeo zawadi?”“Mmmh sijui ni kwanini jamani, huwa naona mume wangu ni mtu wa kuzunguka sana, kwahiyo huwa nahisi kama akitaka kitu chochote basi lazima atakiona kwenye mizunguko yake na atakinunua”“Ila kama ukimtafutia wewe zawadi inakuwa vyema zaidi, anazunguka kweli ila zawadi kwenye mahusiano ni muhimu sana haijalishi ana pesa kiasi gani”“Ni kweli usemayo, kwanza umenifungua akili na mawazo rafiki yangu, kwakweli nitaanza kumtafutia mume wangu zawadi pia nitaanza kupeleleza ni tabia gani ninazo ambazo mume wangu hazipendi ili nizirekebishe, ni kweli ananivumilia kwa mengi sana”“Ndio hivyo, mumeo anakupenda na usitake kuwa sababu ya mumeo kutoka nje ya ndoa halafu uje usingizie shetani. Mpende mumeo, mjali, mthamini na umuone kama kitu cha thamani kubwa sana katika maisha yako”Kwakweli yale maneno yalimuingia sana mama Angel na aliona kuwa anapaswa kujirekesbisha ili kutetea ndoa yake, basi waliongea mengi ila Fetty sababu alitaka kwenda pia kwa madam Oliva kwahiyo aliamua kumuaga mama Angel.Ilibidi mama Angel amsindikize kidogo Fetty, ila wakati wanatoka nje ya geti gafla akatokea Sia, ni kwavile hawakumtarajia walibaki kumshangaa kwa muda ila gafla Sia akamzaba kibao mama Angel. Kwakweli yale maneno yalimuingia sana mama Angel na aliona kuwa anapaswa kujirekesbisha ili kutetea ndoa yake, basi waliongea mengi ila Fetty sababu alitaka kwenda pia kwa madam Oliva kwahiyo aliamua kumuaga mama Angel.Ilibidi mama Angel amsindikize kidogo Fetty, ila wakati wanatoka nje ya geti gafla akatokea Sia, ni kwavile hawakumtarajia walibaki kumshangaa kwa muda ila gafla Sia akamzaba kibao mama Angel.Kile kitendo kiliwashangaza sana Fetty na mama Angel, basi Sia alinyoosha tena mkono wake kutaka kumzaba kibao kingine mama Angel ila Fetty alimkamata ule mkono na kumshusha chini halafu alienda katikati ya Sia na mama Angel na kumuuliza Sia,“Tatizo ni nini? Unafika kwenye mji wa watu na kuanza kunasa vibao wenye nyumba!”“Hata na mimi ni mwenye nyumba hii”“Khee makubwa haya”Fetty alifikiria kidogo na kumuuliza mama Angel,“Erica, kwahiyo huyu ndio Sia?”“Eeeeh ndio huyo!!”Sia nae akajibu,“Kumbe unanifahamu eeeh! Nilitaka nishangae unaacha vipi kunifahamu wakati mimi nakufahamu kila kitu na familia yako nzima, kwahiyo ndio mnajitia mashoga na huyo Erica, kuna ushoga kati yenu au unafki tu”“Kheee jiheshimu wewe mwanamke, wengine na utu uzima huu huwa hatupendi kugombana kabisa, kwani tatizo lako nini?”“Huyo Erica, kwenda kumvesha mume wangu viatu vya limbwata la yule madam ni nini mpaka muda huu yule madam kamuweka Steve ndani kwake”Mama Angel alicheka na kutikisa kichwa, kisha alimuuliza Sia,“Huyo mumeo ni nani jamani! Mbona una mapya kila siku lakini!”“Inamaana hujui kama mimi na Steve tulifunga ndoa!!”Fetty akasema,“Sasa wewe nishakuelewa vizuri, kumbe wewe ndio uliyesababusha mdogo wake Dora akakuoa, na ndio ukamfanyia visanga, kwanza hukuwa na aibu mtu mzima wewe kuwa na yule mtoto!”“Kwani huyo madam ni mtoto!!”“Hata kama, naomba uende maana hata sioni kama una maneno yanayoeleweka. Erica rudi ndani tu, huyu mimi nitamalizana nae”“Utamalizana na mimi kitu gani mnafki mkubwa wewe, hivi kweli marafiki wa damu wanaweza kushea mwanaume? Yani mwanaume anayeachwa na rafiki yako ndio wewe unaenda kujipeleka ili akuoe wewe, kwa mtindo huo si ndio nyie mnaoweza kuolewa hata na mume wa dada yako wa damu! Hivi Erica unafikiri huyu anashindwa kutembea na mumeo? Subiri uone picha, unaruka jivu unakanyaga moto”Fetty alimuangalia Sia na kumsikitikia kisha akamgeukia mama Angel na kumwambia,“Ndugu yangu rudi ndani, huyu humuwezi, nitawezana nae mwenyewe”Na kweli mama Angel alijiona wazi kuwa hamuwezi Sia kwani mama Angel hakuwa mtu wa kuweza kujibishana sana ndiomana mara nyingi alikimbilia kulia, basi aliamua tu kurudi ndani ila Sia alitaka kuingia pia ambapo Fetty alimshika mkono na kumvuta kisha akamwambia,“Njia ya kuondokea ni hii hapa, haya niambie hilo dukuduku lako ulilonalo. Kwani wewe inakuuma nini mimi kuolewa na mwanaume aliyeachana na Erica? Katika dunia hii ni wapi utampata mwanaume wako peke yako? Akiwa na wewe ujue kuna mtu kaachana nae, ni wapi utampata wako tu! Hebu tumia akili muda mwingine”“Ila sijapenda kwa alichokifanya Erica, mimi ananifahamu akili zangu zilivyo nitamfanyia kituko hicho hatasahau maisha yake yote”“Sasa wewe hujapenda kitu gani, yani kitu gani kimekufanya uchukie hivyo?”“Steve haelewi kitu hatambui kitu, nimeenda dukani sijamkuta, nimempigia simu anasema yupo kwa Oliva”Ndio hapa kidogo Fetty alishtuka yani mwanzoni alikuwa kama haelewi vile, ndio hapa kajua kuwa rafiki yake Oliva kamuopoa Steve ila hakuelewa ni sababu ya viatu ambavyo Sia anasema au ni sababu ya nini? Basi wakati akifikiria yale ni sauti ya mtoto wa kiume ndio ilimshtua, mtoto huyu alikuwa ni Elly ambaye alisogea kumuita mama yake na alivyofika pale alimsalimia Fetty na kuongea na mama yake ambapo Fetty alikuwa kasimama tu akiwaangalia na walipomaliza kuongea alimuuliza Sia,“Huyo ni mtoto wako kweli?”“Kwanini?”“Umepata wapi mtoto mstaarabu na mwenye heshima kiasi hiko!”“Mbona hapa bado, ukimuona wangu wa ukweli nadhani ndio utapagawa na kustaajabu zaidi”Muda huu Sia aliondoka na mwanae na kumfanya Fetty amuangalie tu huku akitikisa kichwa na kusema,“Hivi kuna mwanaume mwenye akili zake timamu kabisa aamue kuwa na huyu Sia kwasasa!! Labda ampe limbwata kama huyo mdogo wake Dora”Kisha aliondoka zake kuelekea kwa madam oliva.Fetty alifika nyumbani kwa madam Oliva, ila mlinzi getini alimwambia kuwa madam Oliva hayupo,“Kheee kaenda wapi kwani?”“Sijui, ila kuna kijana alikuja jana usiku hapa na leo madam kanitambulisha kuwa yule ndio baba wa mwanae yani ndio mumewe, na muda ule walikuwa wanaenda kuchukua mizigo ya yule mwanaume maana anahamia hapa”“Kheee yamekuwa hayo!! Jamani Oliva sio mzima mmmh!”Fetty aliamua kuondoka zake, ila alipokaribia kufika nyumbani kwake alikutana na Dora na kuanza kusalimiana pale,“Umetokea wapi Dora?”“Nimetokea nyumbani huko mama aliniita mara moja”“Vipi tena?”“Unajua mdogo wangu tokay ale majanga ya Sia hadi kuoana nae na kuishi nae pamoja, walivyoachana basi alirudi nyumbani na mama alimuomba jambo moja kuwa akipata mwanamke wa kuishi nae basi aje kuishi nae nyumbani maana tuna nyumba kubwa tu kwasasa. Cha kushangaza nasikia jana usiku kaondoka tena bila hata ya kumuaga mama yani mama kamuona tu akitokomea na pikipiki akanipigia simu basi leo nimeenda, loh muda kidogo Steve kaja na huyo mwanamke na wamefika pale na kusema wamekuja kuchukua nguo za Steve kwani anaenda kuishi na huyo mwanamke, jamani mdogo wangu lini akili yake itamkaa sawa? Atalelewa na wanawake hadi lini? Mwishowe wanamdhalilisha, ila nadhani yule mwanamke kampata mdogo wangu kwa madawa tu ila nitajua mchezo wote nadhani kuna watu wanataka kutibua akili yangu”“Mmmh jamani, mbona haya mapya?”“Ndio hivyo”Simu ya Dora ikaita alikuwa akiitwa tena kwao kwahiyo ilibidi aagane na Fetty, yani hapo Fetty ndio akaelewa wazi kuwa kitu gani kinaendelea kati ya madam Oliva na Steve ila ambacho hakuelewa ni kitu gani kimewakutanisha pamoja watu hawa ni vile viatu na malimbwata ya Oliva au ni kitu gani, hakuelewa kabisa.Kuna mambo Angel alikuwa akijaribu kuyaunganisha kwenye kichwa chake bila ya kupata jibu, kwanza alikumbuka maneno ya mama yake mkubwa pindi alipomuona na Ally, akakumbuka na siku ambayo wazaziwake walikuwa hapo halafu mama yake mkubwa akaenda hapo, kwahiyo aliwaza kitu ambacho mama yake mkubwa alisema na kujiuliza,“Sasa ni ukweli gani ninaopaswa kuufahamu?”Alitamani kujua, basi muda huu alimfata bibi yake na kumuuliza,“Bibi samahani, eti ni ukweli gani ambao mimi napaswa kuufahamu ila nyie hamtaki nifahamu?”“Sikia Angel, unajua vitu vingine sio vya kujiumiza kichwa wewe kama wewe, ukiona jambo ambalo wazazi wako wameamua kukuficha basi tambua kwamba hutakiwi kulijua jambo hilo na pengine ukilijua linaweza kukupa madhara makubwa”“Jamani bibi!”“Ngoja tubadili kidogo mada, hivi kati ya baba yako na mama yako unampenda zaidi nani?”“Mmmh wote nawapenda”“Ndio wote unawapenda ila unayempenda zaidi ni nani?”“Nampenda zaidi baba”“Kwanini?”“Sijui jinsi gani ya kueleza ila nampenda zaidi baba, naamini kuwa baba ananipenda sana, ananijali na kunithamini”“Hivi gafla ukaletewa taarifa kuwa baba yako amekufa utafanyaje?”Kwanza Angel alishtuka sana na kumwambia bibi yake,“Bibi usiseme hivyo jamani, mimi nitakufa ujue. Naomba umpigie simu baba yangu niongee nae, nakuomba bibi”Bibi Angel akakumbuka tabia ambayo alikuwa nayo Angel wakati mdogo alipenda sana kuongea na baba yake kwenye simu kiasi kwamba wasipopiga simu anaweza kugoma hata kula, alifikiria kidogo na kumpigia simu baba Angel ambaye kwa muda mfupi tu alipokea na moja kwa moja bibi alimpa Angel,“Shikamoo baba”“Marahaba mwanangu”“Unaendeleaje baba, ni mzima kabisa wewe?”“Salama mwanangu, mimi ni mzima kabisa. Naona umenikumbuka leo, nitakuja kukuchukua mwisho wa wiki nikupeleke matembezi kidogo binti yangu”“Asante sana baba”Kisha alikata simu halafu Angel alimuangalia bibi yake na kumwambia,“Unaona bibi, yani baba atakuja kunichukua anipeleke matembezi, jamani huyu baba ananipenda mimi tena ananipenda sana nadhani katika watoto wote basi mimi ndio namba moja ndiomana huwa anasema nimefanana na nyanya yake”Basi bibi yake alimuangalia Angel, yani malezi ambayo Erick alimpa huyu mtoto yaliwafanya kupatwa na uoga kidogo kumwambia Angel ukweli kuwa yule sio baba yako maana walikuwa wakijifikiria je Angel ataichukuliaje ile hali ya kugundua kuwa Erick sio baba yake wa ukweli na ikiwa kila mahali anajitapa kuhusu baba yake huyo!! Yani hata bibi ilibidi ake kimya kwa muda kwani kuzungumza ukweli kwa wakati huo ilimuwia vigumu sana.Angel ndio alimshtua bibi yake kutoka kwenye yale mawazo,“Bibi zimebaki siku mbili halafu baba yangu anakuja kunichukua kunipeleka matembezi, hivi bibi kwa hali hii kwanini nisimpende baba yangu! Kwakweli baba ni kila kitu katika maisha yangu”“Na Samir je!”“Jamani bibi, mbona umebadilisha mada. Ila bibi nyie hamjanigundua vizuri, hakuna kitu napenda kama kukatazwa kufanya jambo Fulani na baba sababu yeye sio kwamba ananikataza kila kitu, shughuli kwa mama kila kitu anakukataza, jambo kidogo tu anafoka, siku moja niliunguza mboga uwiii mama alisema sana ila baba hakuongea jambo zaidi ya kwenda kununua mboga nyingine na kuileta nyumbani, tena mboga iliyopikwa, kisha akaniambia usijali mwanangu hiyo ni Bahati mbaya, nampenda sana baba yangu kuliko kitu chochote duniani”“Unajua wewe ni mtu wa kwanza kusema hivyo, katika dunia hii kila mtu anampenda mama yake kuliko kitu chochote. Wewe Angel vipi wewe?”“Mama nampenda tena sana tu ila baba nampenda zaidi”Bibi akapumua tu na kuamua kwenda kuendelea na mambo mengine huku akifikiria mambo mbalimbali ila muda kidogo Angel alienda kumuomba simu ili aweze kuwasiliana na rafiki zake, siku hiyo bibi hakukataa wala nini kwani alimpa tu ile simu akawasiliane nayo.Leo usiku baba Angel alimwambia mama Angel namna alivyowasiliana na Angel na vile alivyomwambia,“Wewe nawe unamuendekeza sana huyo Angel”“Ila mke wangu unajua kuna muda huwa sikuelewi kabisa, nikifanya hiki kwa mtoto huyu unasema nampendelea huyu, jamani mbona mimi nalea watoto kwa usawa? Hebu siku moja muulize Erica, unamuonaje baba nae atakwambia halafu siku nyingine muulize Erick halafu useme kama kuna mtoto yoyote nampendelea”Mara simu ya mama Angel iliita naye aliyepiga alikuwa ni dada yake Mage, basi akaipokea na kuanza kuongea nayo,“Mdogo wangu unajua leo nimekutana na nani?”“Nani huyo?”“Nimekutana na Rahim”“Kheee dada nawe!”“Na nimemuuliza kuhusu Angel kasema anamkumbuka, yani kwa kifupi ni kuwa Rahim anamkumbuka vizuri kabisa mtoto wake, tena anasema akikutanishwa nae atafurahi sana maana ni damu yake”Mama Angel alikata hii simu na kuizima kabisa, basi mumewe alimuuliza,“Tatizo ni nini mke wangu? Nani huyo aliyekuwa anakupigia?”“Ni mtu kakosea namba sasa akawa anongea sana”“Mmmh Erica umeanza uongo tena halafu hapa hapa tuko wote, nimekusikia kabisa hapo ukisema dada nawe inaonyesha wazi ni dada yako halafu saivi kusema ni mtu kakosea namba kweli jamani mkwe wangu ndio aina ya maisha tunayotaka kuichagua hiyo!!”“Nisamehe mume wangu, ni hivi dada Mage kanipigia simu na kuanza kunikumbusha zile zile mada za kutaka Angel aujue ukweli kuhusu baba yake”“Kwani Mage yeye cha zaidi nikipi kwake yani kitu gani kinamuumiza akili sana? Ni Angel kutokumjua baba yake au ni maisha ya Angel?”“Yani yeye anakazana kusema kuwa Angel anaweza kuolewa na kaka yake halafu ikawa balaa kwetu”“Hivi Angel akiolewa na kaka yake balaa ni kwetu au kwa Rahim maana si ndio ukoo wake? Mimi nasema tu ila ukiona umuhimu wa Angel kufahamu ukweli basi mwambie tu”“Unadhani ni rahisi hivyo! Kumbuka wakati Angel akiwa mdogo kipindi tunamruhusu Rahim kuja nyumbani kucheza cheza na Angel ili amzoee ni nini kilitokea? Mtoto alikuwa akilia muda wote ambao Rahim atafika nyumbani halafu na ule ujinga alioufanya ndio kabisa ukafanya tujifiche wasijue tulipo ila najua familia haielewi ni yapi nimepitia ni yapi huyo Rahim kanitendea, najua hawaelewi ila siku moja nitakayomwambia Angel ukweli basi nitamwambia na ujinga wote ambao baba yake kanifanyia”“Mmmh ila naiogopa hiyo siku naiogopa sana, nilimwambia Rahim mapema sana, unatakiw auje mtoto akuzoee hata akiambiwa ni baba yake mtoto anakuwa hana mashaka yoyote na anakuwa na furaha, hivi kwa ile tabia ya Rahim kama utaamua kumueleza Angel atataka kweli kumfahamu baba yake? Atataka Rahim kuwa baba yake? Sijui lakini ila kuna umuhimu wa mtoto kumfahamu baba yake mzazi”“Ila ngoja mwanangu akue vizuri hata nikimueleza anielewe na asichukie kwanini nilimficha kwa kipindi chote hiki”Walibaki tu kuongea ila hawakuweza kuelewana kuwa wakati sahihi wa kumwambia Angel ukweli kuhusu baba yake ni wakati gani.Kulivyokucha tu, Erica aliamka tena siku hiyo aliamka mapema sana kutokana na ndoto aliyoota ambapo alitaka kwenda kumsimulia kaka yake ili waweze kushauriana juu ya ndoto hiyo, basi moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa Erick na kufungua mlango ambapo bado Erick alikuwa amelala ule usingizi wa asubuhi, basi aliaenda kumtikisa,“Erick, Erick”Erick alishtuka na kuanza kufikicha macho, mara Erica alianza kucheka na kumfanya Erick amuulize,“Nini unacheka?”“Nini hiko kimetuna kwenye kaptula yako?”Aliuliza huku akiendelea kucheka basi Erick akavuta shuka na kujifunika vizuri kisha akasema,“Yani wewe Erica dah!! Una mambo ya ajabu ujue, kwahiyo unataka kujua nini kimetuna kwenye kaptula yangu kweli!! Aaah tuachane na hayo, hebu niambie kilichokuleta asubuhi hii maana lazima una jambo”“Ni kweli nina jambo, mwenzio leo nimeeta bhana”“Umeota nini?”“Ndoto yangu ilikuwa hivi, nilimuona dada Angel anaolewa halafu yule mwanaume aliyekuwa anamuoa dada Angel kama namfahamu vile ila sijui simfahamu, mara nikamuona mama na baba halafu akatokea mama mwingine sijui ni mama wa bwana harusi akasema, sikufahamu kama huyu ni baba yake Angel, kwamaana hiyo Angel na huyu kijana ni ndugu yani mtu na dada yake. Nikashtuka sana kutoka kwenye ile ndoto, nimetafakari bila ya kupata jibu ndiomana nikaona nije nikushirikishe, eti au baba ana watoto wengine nje?”“Mmmh hapana bhana, sidhani kama baba ana watoto wengine”“Sasa kwanini niote hivi kuwa dada Angel anaolewa na mtu ambaye inasemekana ni kaka yake! Lazima baba atakuwa na watoto wengine nje”“Na wewe Erica, kwani umeambia hiyo ni kweli? Hiyo ni ndoto tu kama ndoto zingine, kama baba angekuwa na watoto wengine nje basi angekuja kusema kuwa hawa ni watoto wangu, kwanza baba ana upendo sana kwahiyo hawezi kuacha watoto wake sehemu nyingine wahangaike, sidhani kama baba ana watoto wa nje”“Ila sisi tuna Bahati ujue, yani Samia anasema kuwa kwa baba yake ana watoto hao hadi wengine hawafahamiani, yani na wewe Erick usiwe kama babake Samia”“Sasa mimi nitakuwaje kama huyo jamani wakati hata wazo la kuoa halipo kwenye akili yangu, wazo la kuwa kwenye mahusiano halipo kwangu kabisa sasa nitaanzaje kufikiria kuwa kama babake Samia!”“Sawa, hapo utakuwa kijana mzuri. Ila niambie kilichotuna muda ule kwenye kaptula yako ni nini?”“Unajua wewe ni chizi sana, ngoja nikaoge kuna siku nitakuonyesha hiko unachokiulizia”“Mmmh!”“Sasa unaguna nini? Si umeuliza mwenyewe? Kuna siku nitakuonyesha”“Haya bhana”Kisha Erica akainuka na kutoka chumbani kwa kaka yake.Leo baba Angel hakwenda ofisini wala hakwenda kwenye ujezi sababu ujenzi alikuwa amemaliza karibu kila kitu kwahiyo alikuwepo nyumbani tu, muda huu alikuwa ameshika simu ya mke wake mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu hii basi aliufungua na kuusoma,“Sasa umeamua kumfanyia hivi mume wangu ilihali unajua wazi kuwa mimi na Steve tulifunga ndoa ya uhalali kabisa, basi nakwambia hivi mimi nitaendelea kumng’ang’ania mumeo mpaka mwisho wangu”Yani baba Angel alijihisi kucheka na kutikisa kichwa kisha akasema,“Ndiomana huwa nasema huyu mwanamke ni chizi, hivi mtu mwenye mume kweli anaweza kupoteza muda wake kukazana ili ampate mume wa mwanamke mwingine! Halafu bila aibu yupo kulalamika kuhusu Steve, jamani huyu Sia ni wa kumsamehe tu”Akacheka pale na kuweka simu ile pembeni na moja kwa maoja aliinuka na kwenda kwenye chumba chake cha kujisomea na kuanza kusoma magazeti mbalimbali ambayo yaliletwa. Wakati baba Angel akisoma yale magazeti, akapigiwa simu na rafiki yake mmoja,“Uko wapi Erick?”“Aaaah leo nipo nyumbani tu, sijaenda popote”“Kuna jambo la maana sana nahitaji kuongea nawe kuhusu ile ofisi yako mpya”“Mmmh sasa utaweza kuja nyumbani kwangu!!”“Sawa, nielekeze nakuja”Basi baba Angel alimuelekeza yule rafiki yake ambaye aliahidi baada ya muda mfupi kufika mahali pale.Alipofika aliwasiliana na baba Angel ambapo alitoka nje kumkaribisha na moja kwa moja alienda nae kwenye kile chumba cha kujisomea kwani aliona hata maongezi kama watafanyia humo ni vizuri zaidi, muda huo mkewe likuwa yupo na mtoto chumbani kwahiyo hata hakujua kama kuna mgeni amefika pale kwao.Basi baba Angel akaanza kuongea na yule mgeni,“Kwanza Erick, yule mwanao uliyekuwa unaendaga nae kwenye ujenzi yuko wapi?”“Nilikuwa naenda na wawili ujue, kuan Junior na kuna Erick”“Mmmh siwajui kwa majina ila naweza mtambua kwa sura”Basi baba Angel aliwaita Junior na Erick kuwatambulisha kwa yule mgeni,“Jamani, huyu ni rafiki yangu anaitwa Juma, halafu hawa ndio Junior na Erick”Yule mgeni alifurahi kuwafahamu kisha baba Angel akawaruhusu waendelee kwenye shughuli zao ambapo waliondoka, basi yule mgeni akamwambia Erick,“Niliyekuwa nataka kumsema ni yule Erick, kwakweli umepata kichwa kile ni hatari nadhani ndiomana umempa jina lako. Sasa sikia nikufundishe ujanja, yani Erick unampeleka pale kiwandani na umwambie tunahitaji kufanya moja mbili tatu ila itakuwa chini ya uangalizi wako, halafu muache ashughulike na hiyo kazi mwezi mmoja tu utaona matunda yake yani utafurahi na kusema kweli una mtoto mwerevu”“Mmmh ila bado anasoma”“Anasoma ndio, ila weka utaratibu Fulani hivi hata kuanzia Ijumaa hadi Jumapili ni siku za yeye kushughulika na biashara tu, matunda yake utaniambia kuwa nilisema. Ila kuna jambo nataka kukuuliza”“Jambo gani?”“Huyu mtoto mwingine Junior, mbona kafanana na James?”Baba Angel alicheka kidogo na kusema,“Kumbe James ulimfahamu, basi yule ni mtoto wake kabisa”“Jamani!! James alikuwa ni rafiki yangu sana. Kumbe ni mtoto wake yule!! Nitakuja kufanya kitu kwaajili yake kama ukumbusho kwa baba yake!”“Itakuwa vizuri sana ndugu yangu kumbe ulifahamiana sana na James!! Inawezekana hata mke wangu unamfahamu maana mke wangu ni mdogo wa aliyekuwa mke wa James”“Aaaah kumbe!! Basi inawezekana namfahamu”Ikabidi baba Angel aende kumuita mke wake ili waonane na rafiki yake, na kweli mama Angel alifika pale na kutazamana na huyu mgeni kwanza alimshangaa kidogo kufahamiana na mume wake maana alikuwa akimfahamu huyu mtu, basi alisalimiana nae pale,“Kumbe ni wewe ndio mke wa Erick!!”“Ndio ni mimi, karibu sana. Rafiki yangu hajambo?”“Hajambo kabisa, atafurahi sana nikimwambia kuwa nimekutana na wewe”Ndio baba Angel nae akauliza kwa makini,“Kumbe mke wako na mke wangu ni marafiki!!”Ndio mama Angel alipomjibu,“Ndio, kumbe humfahamu mke wa huyu Juma? Mke wake ni Johari”“Kheee kumbe Johari, yule tuliyesoma nae!!”“Ndio huyo huyo”“Kumbe mlisoma na mke wangu!! Halafu sikujua yani hata urafiki wa mke wako na mke wangu nilijua tu ni urafiki kwavile wanaishi sehemu moja kumbe mmesoma wote, ngoja siku moja nimlete mke wangu hapa nadhani atafurahi sana”Basi ikawa ni furaha na waliongea mambo mengi sana, basi maam Angel ilibidi aende kuandaa chakula ili wale pamoja na mgeni wao maana yeye hakujua kama kuna mgeni amefika kwao kwa siku hiyo.Basi kwa pamoja walienda kula chakula huku wakiongea mambo mbalimbali ya maisha na jinsi mambo yalivyo, akamkumbusha pia jinsi alivyomtafutia leseni ya udereva,“Unakumbuka nilikutafutia leseni ya udereva!”“Nakumbuka vizuri, unafikiri naweza kusahau hilo Juma!!”Basi wakacheka pale na kuendelea kula.Kwa upande wa Sia alizidi kuwa na hasira yani yeye alichukia kuona kwanini mama Angel alimpelekea vile viatu Steve, aliona kamavile amemfanyia makusudi wakati mama Angel hakujua ukweli wa jambo lolote lile, basi siku hiyo alijiandaa tena na kwenda dukani ili ajaribu kuongea na Steve vizuri na aweze kumzindua ufahamu wake.Ila alivyofika dukani hakumuona Steve yani duka lilikuwa limefungwa, na kuwaona tu wale walinzi pale nje basi aliwafata na kuwauliza,“Ila wewe mwanamke si uliambiwa usifike hapa!”“Hiyo sio sababu, hivi nyie mnajua kuna mambo mnafanya halafu hamjifikirii mnakumbuka siku mliyonizaba kibao halafu nikaanguka? Mnakumbuka alivyofika mwenye mali alifanyaje?”“Alikupakia kwenye gari lake na kukupeleka hospitali”“Unajua kwanini alifanya hivyo!! Sababu anajua umuhimu wangu katika maisha yake, anaijua thamani yangu ni kitu gani ndiomana hamjawahi kumuona hata akinyoosha mkono wake kunizaba kibao. Haya huyu Steve yuko wapi jamani! Hadi leo hajafungua duka!”“Katupigia simu kuwa hafungui leo, na hapa tuliambiwa tumsikilize Steve kwahiyo ndio hivyo mpaka atakapoamua yeye kufungua hata wale wafanyakazi wengine wa kawaida wale wawili walifika na kuondoka maana Steve hajafungua duka”“Duh!! Yani huyu mwanamke kamshika sana Steve, ila yote haya ni Erica ndio kayataka”Basi akaondoka pale bila hata ya kuwaaga wale walinzi, muda huo alikuwa akienda tu nyumbani kwa Erica ili akaonane na Erica,“Yani leo ndio atanitambua vizuri, nimeachana na Steve ndio ila sio sababu ya kumfanya Steve awe na mwanamke mwingine, sitaki hilo jambo kabisa. Na leo lazima nikamdhalilishe Erica”Basi moja kwa moja alienda kupanda pikipiki ili awahi kufika huko kwa Erica na kufanya fujo anazotaka kuzifanya.Muda huu Juma alikuwa ameaga kwani aliona kama muda umeenda kiasi halafu kuna mahali alitaka kwenda, basi walitoka pale nje na hakuwa ameenda na usafiri basi baba Angel alitaka kupanda nae kwenye gari lake ili amfikishe hata stendi ila alikataa,“Aaaah hapana, unajua mimi huwa sipendi sana kutumia usafiri kuna muda huwa napenda tu kupanda daladala na kutembea, kwahiyo nitaenda tu stendi hakuna tatizo”“Ni vizuri lakini maana ni mazoezi pia hayo”Basi waliamua kutoka na kumsindikiza kidogo muda huo walikuwa wameongozana mama Angel, baba Angel pamoja na mgeni wao Juma.Wakati wametoka tu nje ya geti, walikutana macho kwa macho na Sia ila gafla kitu ambacho hawakukitarajia ni Sia kuanza kutimua mbio tena alikimbia sana kama mtu aliyeogopa kitu Fulani, kwakweli mama Angel alibaki kushangaa sana. Wakati wametoka tu nje ya geti, walikutana macho kwa macho na Sia ila gafla kitu ambacho hawakukitarajia ni Sia kuanza kutimua mbio tena alikimbia sana kama mtu aliyeogopa kitu Fulani, kwakweli mama Angel alibaki kushangaa sana.Yani baba Angel ndio alimtoa mama Angel kwenye mshangao,“Hivi yule sin i Sia jamani!!”“Ndio mwenyewe, sijui alikuja kufata nini na kitu gani kilichomkimbiza!”Basi Juma nae akauliza,“Kwnai yule mwanamke aliyekimbia ni nani? Maana hata sijamuangalia vizuri”“Ni historia ndefu sana, ila anaitwa Sia na hata sijui ni kwanini amekimbia”Kisha baba Angel akamuangalia mkewe na kumtaka arudi ndani tu, ila kama kawaida ya wivu wa mama Angel kwahiyo hakutaka kurudi ndani peke yake ukizingatia kamuona Sia mahali hapo ilibidi baba Angel aagane tu hapo na mgeni wake huyo ambaye aliamua kumuitia pikipiki ili impeleke stendi halafu yeye alirudi ndani na mke wake.Basi baba Angel na mama Angel walipokuwa ndani waliulizana kwanza kuhusu Sia ambapo mama Angel aliuliza,“Ni kwanini kakimbia sasa?”“Sijui na alikuwa anafata nini?”“Nikuulize wewe ambaye huwa unampa hela, unajua unampa kiburi sana huyu mwanamke, halafu sikukwambia tu alikuja na kunikuta getini nikimsindikiza Fetty akaninasa kibao, yani huyu Sia unampa jeuri sana na hela”“Yani alikunasa kibao wewe!”“Ndio”“Mbona hukuniambia kuhusu hilo mke wangu!! Yule mwanamke ni kichaa sana, ila tusimfatilie wala nini tuendelee na mambo yet utu”Baba Angel alikuwa ameongea hivyo ila alikuwa ameumizwa sana na kusikia kuwa Sia alimnasa kibao mke wake, yani kitu ambacho huwa hapendi ni kusikia kuna mtu kamuonea mke wake ndiomana hata dada yake aligombana nae alipomnasa kibao mke wake.Mama Junior leo alitembelewa na rafiki yake daktari na kufurahi sana halafu akamkaribisha vizuri sana nyumbani kwake kisha walianza kuongea,“Unajua siku ile hatukumaliza vizuri maongezi yetu yani kuna mambo hatukuyaweka sawa, najua hukuelewa inakuwaje kwa mwanao kusema hela zipo kwa mwanangu, sasa nimepata ukweli wote”“Eeeh ukweli gani huo?”Daktari alimueleza mama Junior kuhusu swala la Junior kumtongoza Samia na jinsi Samia alivyomwambia na vile Junior kutekeleza,“Kheee jamani, huyu Junior jamani. Hiyo laki tano aliitoa wapi sasa?”“Sijui, mwanangu anasema alimpelekea laki tano keshi kabisa”“Ila mwanao duh!! Au ndio watoto wa siku hizi jamani, mjanja huyo balaa, nimempenda bure, enzi zetu tulikuwa wajinga wajinga, utakuta mwanaume anamdanganya mwanamke kwa kitu kidogo tu na anampata ila huyo Samia duh nimempenda jamani, yani Junior na laki tano yake haijafua dafu!”Wakacheka kidogo kisha daktari akamwambia,“Unajua mwanangu hiyo tabia hata sijui kaitoa wapi jamani maana nishamsema hadi basi na siku zote huwa anasema anafundishwa na baba yake, kwakweli yule mume ananiharibia mtoto jamani!!”“Kheee anamfundishaje hivyo mtoto?“Yani usione watu tunavumilia ndoa, ila huwa tunavumilia mambo mengi sana, kiukweli mimi ile ndoa naivumilia kwa mikiki mikiki mingi sana, kwa kifupi yule mume wangu najua humjui sababu hujawahi kumuona ila alikuwa ni muhuni hatari kiasi kwamba ana watoto yule baba hata wengine hajui wako wapi, basi huwa namwabia hadi watoto wako wataoana, ila huwa anasema hilo haliwezi kutokea, na yeye anaamini kwamba kuna siku watoto wake wote watamtafuta alipo, yani huwa hana muda wa kutafuta mtoto. Ukimuona mtoto wake ujue mama wa huyo mtoto kapambana hadi mtoto amfahamu baba ila asipopambana basi na yeye hana hata habari”“Mmmh huyo mumeo kiboko, yani mimi nilikuwa nahisi wangu tu ndio hatari maana nimemkuta na watoto watatu halafu wengine wawili kumbe walikuwa bado wadogo ndio mama zao wakawaleta nilivyoanza tu kuishi nae kiasi kwamba hata nimeona ni vyema nisizae tena, sasa wewe mwenangu wangapi?”“Sijui ni wangapi, ila kwa wanaofahamika hadi kwao na wanaendaga kwa bibi yao wapo kumi ila sijui hao wengine sasa. Naona uhuni wake anaogopa watoto wake kufanywa kama yeye alivyokuwa akiwafanya watoto wa wenzie ndio anamfundisha ujinga mwanangu, unajua nahofia siku anaweza akala hela ya mwanaume chizi na kupelekea kubakwa maana wanaume wa siku hizi akili zao wanazijua wenyewe”“Kweli hapo umeongea, ila bado nipo kwa mwanangu Junior alipata wapi hiyo laki tano ya kumuhonga Samia? Naona Junior atakuwa anampenda sana binti yako”Daktari akacheka kwanza na kusema,“Junior ana maisha?”“Maisha kivipi?”“Unajua siku hizi hata sisi wazazi tunatakiwa kuamka, tukisikia kuna kijana anataka kuwa na mwanao lazima tuangalie ana maisha ya mbeleni sio kumpa shida tu mtoto wangu”“Jamani Junior wangu yupo vizuri si unaona alipata hiyo laki tano kiurahisi tu”“Unajua mwanao kazitoa wapi hizo laki tano!! Hebu fatilia na ukumbuke kuwa mwanao hana kazi yoyote, ila naona anampenda sana binti yangu sema pole yake maana Samia hana mambo ya mapenzi kabisa”Basi waliongea mengi sana na mwisho wa siku daktari alimuaga tu mama Junior na kuondoka zake, ila mama Junior alikuwa anawaza jambo kuwa ni lazima apange siku aende kwa mdogo wake ili kuuliza kwa makini hiyo laki tano Junior aliitoa wapi.Usiku wa leo, Vaileth alikumbuka jambo na kuamua kumuuliza Junior kuhusu lile swala ambalo alilikumbuka,“Samahani Junior, hivi ile laki tano ambayo uliichukua kwangu ulienda kufanyia kitu gani?”“Aaah ile hela, kuna jambo Fulani hivi nimefanya ni la muhimu sana katika maisha yetu ila sikwambii kwasasa na siku ukiligundua utaamini ni kiasi gani nakupenda”“Basi mwenzio nilishindwa kujieleza kuhusu hiyo hela wakati nimeulizwa, yani nilihisi kupata kizunguzungu kabisa yani, ila nashukuru kama umefanya jambo la maana”“Sasa unafikiri mimi naweza kwenda kufanya ujinga jamani Vai!! Nichukue hela kwako halafu nikafanye ujinga! Hapana sipo hivyo na siwezi kabisa kufanya hivyo. Niamini mke wangu, amini kuwa Junior anakupenda sana”Vaileth alikuwa akihisi raha sana moyoni mwake kila Junior alipomwambia kuwa anampenda sana.Basi waliamua tu kulala kwa muda huo, ila palivyokucha tu Vaileth alisikia akiitwa mlangoni na sauti ilikuwa ya mama Angel basi alikurupuka na kumkurupua Junior,“Mmmh nasikia sauti kama ya mama Angel, kajifiche”Kama kawaida, Junior alienda kujificha chooni, basi Vaileth alienda kufungua mlango na kumsalimia mama Angel ambapo aliuliza,“Hivi maji kwenye choo chako yanatoka?”Mama Angel alipouliza vile alikuwa kama anataka kwenda chooni kuhakikisha ila Vaileth aliwahi haraka haraka na kumwambia,“Yanatoka mama”“Aaaah maana kuna fundi anarekebisha mabomba, jana usiku kuna vyumba vilikuwa havitoi maji chooni”“Kwangu yanatoka mama”Basi mama Angel akaondoka na kumfanya Vaielth apumue kidogo kisha alimfungulia Junior mlango na kuongea nbae,“Unajua presha ilikuwa inapanda balaa, nikawaza hivi angekukuta chooni ingekuwaje jamani!! Sijui yani sipati picha”“Naona chimbo la chooni limeanza kuzoeleka”“Ndiomana mimi nilikwambia kuwa ni bora ujifiche uvunguni, ila haya mapenzi dah!!”“Usijali mke wangu ila naamini kuwa hakuna siku watakayotubamba”“Mmmh ila tuwemakini sana”Kisha Vaileth akatoka nje ili kwenda kuanza kazi mbalimbali muda huu, huku Junior naee akitoka ila wakati anatoka tu akabambana na Erica ambaye alisema,“Nilijua tu, muda huu utatokea humo ndani”Junior alikuwa akimnyamazisha kwa kidole ili asiendelee kusema, huku akitoka na kufung mlango halafu akawa anaondoka ambapo Erica akasema,“Kwani ukitoka humo ndio huruhusiwi kuongea?”Junior akaendelea kutembea huku akielekea chumbani kwake, basi Erica akamwambia,“Junior kama hunijibu nakusemea”Junior akasimama ila muda huu mama Angel nae alikuwa anapita pale na kuuliza,“Kumsemea kitu gani?”Junior akamsalimia mamake mdogo na kusema,“Aaaah mimi na Erica huwa tuna mtindo wa kutaniana, si eti Erica eeeh!”“Ndio”Basi kila mmoja akaelekea kwenye sehemu yake ila mama Angel alikuwa akijiuliza na kuhisi kuwa lazima kuna kitu maana hakuelewa kama ni kawaida tu kufanya vile.Leo baba Angel alivyotoka asubuhi kwenda kazini, hakwenda kazini moja kwa moja ila alienda nyumbani kwa Sia kwani alichukia sana kwa kile kitendo cha mkewe kusema kuwa alizabwa kibao na Sia, na alipofika tu alimkuta Sia yupo kufagia nje ya nyumba yake ila Sia alivyomuona baba Angel kwakweli alifurahi sana alijikuta akiwa na furaha mno na kumsogelea karibu ila baba Angel akanyoosha mkono wake kama kumzuia kuwa asimsogelee karibu sana,“Kheee jamani hata kukukumbatia?”“Sasa unikumbatie ili iweje? Jiheshimu wewe, tambua kuwa mimi ni mume wa mtu”“Ila kumbuka kuwa ulikuwa mpenzi wangu, wapenzi huwa hawaachani hata kama mtu akioa na kuolewa”“Kwa mtindo huo mtu si utakuwa kwenye ndoa na msululu wa watu, mfano mimi kama unavyosema kuwa nisiachane na wapenzi ni wangapi wangekuwepo sasa? Wengine hata majina siwajui”“Achana na hao ambao ulikuwa nao siku mbili na kuachana nao, kuna wanawake hata mwezi hukuweza kufika nao, hata wiki ilikuwa ni ngumu, katika mahusiano yako ya kimapenzi kabla ya ndoa kuwa muwazi tu kuwa mimi ndiye niliyekuwa mwanamke niliyedumu na wewe, nilikupenda, nilikujali na nilikuheshimu bila kujali chochote kile, nilikufumania na bado nilikusamehe na kufanya penzi letu liweze kustawi. Unajua mara nyingine ambavyo unanifukuza mimi uwe unakumbuka na mazuri yangu ambayo nimefanya kwako sio unakumbuka mabaya tu, laiti kama ungejua mimi nilivyo na siri nyingi basi ungekaa karibu yangu ili nikuambie mengi ninayoyafahamu”“Hata sina haja ya kujua unayoyafahamu, ila kilichonileta leo ni kukuuliza wewe kitu gani kimekuleta tena nyumbani kwangu wakati tulikubaliana kuwa hutokuja tena kwangu, na kwanini ulikuja na kumzaba kibao mke wangu? Unajua mimi huwa sipendi kuongea sana, katika wanawake zangu wote basi sijawahi kumpiga mke wangu, kama kupiga basi wewe nishakupiga sana na unaelewa kabisa jinsi nilivyo ila ukaja na kumpiga mke wangu kwanini? Na ushukuru sana nimekuja na kukuuliza kwa ustaarabu hivi”“Kwanza naomba unisamehe sana, haikuwa dhamira yangu kuja kumzaba mkeo kofi ila ni hasira tu. Ngoja nikueleze kwanza, unajua wewe ni mwanaume nikupendaye sana ila sijaweza kukupata sababu ya mkeo licha ya kuwa kwenye mahusiano na wewe kwa muda mrefu sana, nakiri wazi kuwa nilifanya dawa ili nikupate ila dawa zangu zilimpata Steve na mwisho wa siku nikaishi nae hadi kuamua kuzaa nae nakuoana kabisa, unajua kilichomfanya Steve aondoke kwangu sio kuisha kwa dawa maana dawa ziliisha na Steve sababu aliamua kuishi na mimi na kunioa inamaana alinipenda kweli, kilichonifanya niachane na Steve ni ndugu zake ambao walianza chokochoko baada ya mtoto kuzaliwa na kusema kuwa mtoto sio wa Steve, yani pale ndio walianza kuniachanganya akili na kusababisha mimi na Steve kutengana ila nilivumilia tu na kuchukulia ni changamoto maana mengine nilijitakia mwenyewe. Haya unajua mkeo alichokifanya nae?”“Kafanyaje?”“Steve alikuwepo tu hana mwanamke yoyote na Steve namfahamu fika kuwa asingeweza kuwa na mwanamke yoyote yule, sababu nazijua mwenyewe, ila mkeo kaenda kumpa Steve viatu ambavyo madam Oliva alikuletea wewe sijui, kaenda kumpa na vile viatu vimechanganya akili ya Steve kwa maana hiyo Steve yupo kwa madam Oliva, yani Steve sio yule Steve uliyemfahamu mwanzoni maana kawa mwingine kabisa”“Kheee kwahiyo hivyo viatu vya madam Oliva vilikuwa na mambo?”“Ndio, Oliva alikukusudia wewe, ila mkeo nilijua ataenda kuvichoma moto ila nilivyogundua kampelekea Steve wangu nimeumia sana”Baba Angel akacheka kidogo na kusema,“Ila unajua wewe mwanamke unachekesha sana, sasa ulikuwa unanipenda mimi au Steve? Maana hizo nguvu ulizokuwa ukitumia kwangu nina uhakika ungezitumia kwa Steve basi angekubali na mngeishi pamoja tena, ila kweli wewe ni chizi”“Sikia Erick,kumbuka Steve ni baba wa mtoto wangu”“Unaendelea kunichekesha, baba wa mwanao kumbe ni Steve ila kila siku kunisumbua mimi na familia yangu kuhusu mtoto wako, jamani wewe mwanamke ukweli wote unaufahamu ila kila siku kunishikilia kuwa mimi ni baba wa mwanao, leo Steve anakuumiza kichwa, unajua wewe ni mgonjwa wa akili!”“Nadhani hujanielewa Erick, ila ipo siku utanielewa. Mimi nakupenda sana wewe, nilitamani pia awepo mtu wa kunipenda sana mimi yani ambaye hawezi kufanya kitu bila ya kunifikiria mimi”“Kwahiyo mtu huyo ndio ulitaka awe Steve?”“Nilitaka Steve anipende sana na niwe kila kitu katika maisha yake”“Wewe mwanamke ni mgonjwa, ulitaka akupende wakati unajua wazi alikupenda kwa madawa? Halafu kwanini utake kumtesa mtu kwa upendo, unatakiwa kumpenda akupendaye ndio uishi salama. Haya leo nakupa onyo la mwisho, kwakweli nikisikia tena umekuja nyumbani kwangu na kufanya fujo kwa mke wangu nakwambia wazi utanifanya niwe vile nilivyokuwa kwa muda halafu utajutia kitendo chako cha kuamua kufanya ujinga kwa mke wangu”“Ila hujui tu, laity ungejua huyo Steve hayupo kazini hadi leo sababu ya Oliva hata usingesema hayo, ni kweli nakufatilia na familia yako ila nakusaidia kwenye mambo mengi sana ili kukuokoa wewe na familia yako. Nakupenda sana Erick”Baba Angel hakusikiliza zaidi kwani kwa muda huo akili yake iliruka kusikia kuwa Steve hajaenda kabisa kazini, kwahiyo aliingia kwenye gari yake na muda huo alikuwa akielekea kwenye ile biashara yake.Kwa muda huu yani ilikuwa ni tofauti kwa Steve kabisa kwani alisahau shida zake zote, alisahau kila kitu kinachohusiana na yeye sijui kazi, sijui vitu gani alisahau kabisa kwahiyo muda mwingi alikuwa akikaa na madam Oliva ndani ya nyumba, kisha walianza kuongea,“Unajua tutaishi hivi kwa wiki nzima, kisha ndio itawezekana kufanya mambo mengine”“Sina tatizo mimi, nakubaliana nawe kwa kila kitu”“Kwanza, ulikuwa unafanya kazi gani awali”“Oooh umenikumbusha, Mungu wangu sijui itakuwaje. Nilikuwa nauza duka la nguo za watoto na mimi ndio nilikuwa nimeishika biashara ile kwahiyo siku zote hizi sijafungua”Mara simu ya Steve ilianza kuita na alipoiangalia akaona ni bosi wake anampigia simu basi aliogopa kupokea ambapo madam Oliva alimuuliza,“Kwani nani anapiga?”“Ni bosi wangu”Madam Oliva akachukua ile simu na kuangalia akaona jina bosi Erick, basi akamuangalia vizuri Steve na kumuuliza,“Kwani huyu Erick ni nani? Ni yule ninayemfahamu mimi au? Watoto wake wanaitwa kina nani?”“Ana watoto wanne kwasasa, kuna Angel, Erick, Erica na Ester”“Oooh ndio huyu huyu ninayemjua mimi ila imekuwaje jamani! Mbona sielewi”Kisha akakumbuka vile viatu ambavyo alimuona Steve amevaa katika facebook, akamuuliza sasa,“Kwahiyo vile viatu ndio huyo bosi wako Erick alikupatia?”“Hapana, ni mke wake ndio aliniletea alisema mumewe havimtoshi kwahiyo aliona ni vyema kuniletea mimi”“Dah!! Kuna kitu naanza kuelewa sasa, hivi wewe ulianza kunipenda kipindi gani?”“Mimi, ni siku nyingi sana nilikuwa nakupenda”“Basi mimi toka siku nimekuona umepiga picha na vile viatu, nikajua na wewe umeanza kunipenda baada ya vile viatu?”“Hapana, ni siku nyingi sana ila kwasasa ndio sijielewi kabisa maana nakupenda kupitiliza”Madam Oliva alitikisa kichwa tu kwani alielewa kinachoendelea, kisha simu ya Steve ilianza kuita tena na kufanya Steve aogope maana alikuwa ni bosi wake anapiga ila madam Oliva alimwambia acha apokee yeye basi Steve alimpatia ile simu ambapo madam Oliva aliipokea,“Wewe Steve uko wapi kwa siku zote hizi jamani hujafungua biashara yangu!!”“Erick, samahani sana. Steve yupo kwangu, naomba umsamehe bure maana sio kosa lake”“Nani wewe?”“Mimi madam Oliva”“Kheee madam olive!! Sasa Steve anafanya nini kwako?”“Mimi na mwanamke na Steve ni mwanaume unadhani atakuwa anafanya nini kwangu? Nitakuja ofisini kwako na tutaongea vizuri ila naomba umsamehe bure tu Steve”Baba Angel alikata ile simu kwani alionekana kuwa na hasira ila kwa upande wa madam Oliva ilikuwa kawaida kabisa maana hakuwa na mashaka na jambo lolote lile, kisha alimwambia Steve,“Usijali, maana hata ukikosa kazi kwake basi nitakupa kazi kwenye ofisi zangu, najua bado hunifahamu vizuri ila mimi ni mwanamke ambaye najitosheleza”Steve alikaa kimya tu akimuangalia madam Oliva kwani kila muda alijikuta akizidi kumpenda madam Oliva kupita kawaida.Baba Angel alikuwa ofisini kwake huku akisikitika sana, kwanza alikumbuka maneno ya Sia ambayo alimwambia awali akimtahadharisha kuhusu madam Oliva, alikumbuka pia maneno ya mke wake, na kile kilichotokea kuhusu Steve basi aliwaza sana na kusema,“Inamaana muda huu isingekuwa Steve bali ingekuwa ni mimi ndio nipo nyumbani kwa madam Oliva na kuisahau kabisa familia yangu, dah nauchukia uchawi jamani. Sasa ndio mambo gani haya, yani mtu anaweza kukupa dawa hadi unasahau familia yako!! Ka jinsi ninavyompenda mke wangu, kwa jinsi ninavyowapenda watoto wangu halafu leo hii niwakimbie na kwenda kwa mwanamke mwingine sababu ya madawa kweli! Aaaarghh nauchukia uchawi, nani huyo kaweka dawa za mapenzi jamani!!”Akitafakari hayo alimuona Oliva akiingia ofisini kwake, kiukweli kwasasa baba Angel alikuwa akimuogopa madam Oliva yani alimuogopa na kumuhofia sana kiasi kwamba hata hakuweza kumkaribisha ila madam alifika na kukaa kisha akaanza kuongea,“Mbona unaonekana kuniogopa sana baba Erick? Mimi sio mtu mbaya kama ambavyo unafikiria, usiniwazie vibaya, mimi nilikufanyia tu kile ambacho mke wako alishindwa kukufanyia na si vinginevyo”“Kwani nilikuomba usaidizi?”“Hapana, ila sikuwa na nia mbaya. Nataka ujue kwamba sikuwa na nia mbaya, na hili nitalidhihirisha kwako kwa kupitia huyu Steve, sikuhisi kama ningeweza kumpenda ila nashangaa kuona nikimpenda sana kiasi cha kutokutaka awe mbali na mimi. Twende nje ukamsalimie maana yupo kwenye gari yangu”“Hapana madam, nenda tu”Yani baba Angel hakuwa na amani na madam Oliva hata kidogo, hivyo ilibidi tu madam Oliva aondoke zake yani baba Angel hakuwa na amani na madam huyu hata kidogo kabisa.Jioni ya leo Angel alienda kumuomba simu bibi yake ili aweze kuwasiliana na rafiki zake mbalimbali, ila bibi yake anampatia na kumwambia,“Kesho si ndio unaenda matembezi na baba yako, unikumbuke tu kwenye zawadi”Angel alicheka na kuchukua simu kisha alienda chumbani kwake ambapo alipofika tu akaanza kumtafuta Samir maana ni muda hakuwasiliana nae,“Jamani Samir ndio toka siku ile unashindwa tena kufika kwetu kuniona, au hujanimiss”“Nimekumiss sana Angel, ila huyo bibi yako humjui vizuri”“Kwanini sasa?”“Huyo bibi yako hashindwi kummwagia mtu maji ya moto”“Jamani, bibi yangu hana roho mbaya ya kiasi hiko, kweli kabisa ammwagie mtu maji ya moto jamani kwa lipi sasa?”“Sikia nikwambie Angel, huyo bibi yako ni rafiki mkubwa sana wa bibi yangu kwahiyo namfahamu vizuri sana. Muone hivyo hivyo ila huyo bibi yako ana roho mbaya sana”“Mmmh jamani!! Kwahiyo nikikaa kwa bibi basi hutokuja kabisa kuniona?”“Nitakuja tu, ila siku nikijitoa muhanga kufanya hivyo. Halafu vipi kuhusu shule, mimi nilitafutiwa shule ila nimekataa maana nataka kusoma shule utakayosoma wewe”“Mmmh tusome tena pamoja Samir?”“Ndio, tena itakuwa vizuri maana kwasasa mimi na wewe tuna mahusiano, tofauti na pale mwanzoni tulikuwa tunasumbuliwa akili tu ila kwasasa tutaishi vizuri sana shuleni”“Hapo nimekuelewa kabisa, ngoja nikijua ni shule gani wamenitajia nitakwambia Samir”“Tena itakuwa raha sana kama itakuwa ni shule ya bweni halafu mbali ili kipindi cha likizo tuwe tunarudi wote”“Mmmh jamani Samir unawaza mambo ya mbali sana, ila mimi sipendi kusoma bweni, naona sitaweza napenda sana kukaa nyumbani”“Naomba kwaajili yangu kubali utafutiwe bweni mpenzi”Basi Angel alikubali kwani alihisi kumpenda sana Samir na alitamani mno kuwa nae pamoja kama wapenzi, basi wakati ule akatumiwa tena ujumbe na Ally, ujumbe ule ulisema,“Angel, ushaulizia vizuri kuwa undugu wangu mimi na wewe ukoje?”“Ooh bora umenikumbusha, ngoja kesho nitamuuliza baba yangu kama ana mtoto mwingine”“Kwani baba yako anaitwa nani?”“Baba yangu anaitwa Erick”“Hata hivyo hatuna undugu maana mimi niliambiwa kuwa baba yangu anaitwa Rahim, kwahiyo haiwezekani tukawa ndugu nadhani yule sijui mamako mkubwa atakuwa amesema vile ili tusiwe pamoja”“Ila hata hivyo mimi nina mtu wangu”“Angel, naongea na wewe kwa kawaida kabisa. Sikia hunitaki ndio nimekubali, una mtu wako ndio nimekuabali ila kuna siku mimi na wewe tutakuwa pamoja tena mke na mume labda mimi Ally nife ila nikiwa hivi mzima basi tambua hilo”“Mmmmh!”“Usigune, ndio ukweli huo”“Kwahiyo utafanyaje?”“Tena Angel lazima utanizalia watoto mapacha”Angel akaogopa kidogo na kuamua kuzima ile simu na kwa muda huo aliamua kulala tu maana usingizi ulimshika muda huo.Kulivyokucha Angel aliamka na kumkabidhi bibi yake simu kisha yeye alianza kufanya kazi mbalimbali huku akijiandaa kwaajili ya kutoka na baba yake.Leo mchana, ndipo mama Junior alienda nyumbani kwa mama Nagel ili kuongea nae kwahiyo alivyofika alimkuta yupo kwakweli mama Angel alifurahi sana na kuanza kuongea nae mawili matatu kwanza kabisa aliwaulizia wakina Junior,“Junior yuko wapi?”“Junior hayupo, yeye na Erick kuna mahali wameenda”“Wapi tena jamani!!”“Sijui, wameniambia tu wanaenda kwenye matembezi”Kisha mama Angel akamuita Vaileth na kumtaka amletee Juisi mgeni, basi alimsalimia pale na kwenda kumletea juisi, basi mama Junior akamwambia sasa mama Angel,“Yani umemuachia Junior aende matembezi na Erick kweli, ujue Junior anatabia mbaya sana. Sikukwambia haya mdogo wangu ila natakiwa nikwambiae sasa”“Yapi hayo tena?”“Junior kuna binti anampenda bhana, sasa huyo binti kamwambia Junior ampelekee laki tano”“Kheee Junior atatoa wapi hiyo hela sasa?”“Sio atatoa wapi, kwa kifupi Junior kampa huyo binti laki tano taslim”Mara gafla walisikia gafli ikianguka chini na kupasuka, walipogeuka ilikuwa ni Vaileth ambaye alikuwa akileta ile juisi. Kisha mama Angel akamuita Vaileth na kumtaka amletee Juisi mgeni, basi alimsalimia pale na kwenda kumletea juisi, basi mama Junior akamwambia sasa mama Angel,“Yani umemuachia Junior aende matembezi na Erick kweli, ujue Junior anatabia mbaya sana. Sikukwambia haya mdogo wangu ila natakiwa nikwambiae sasa”“Yapi hayo tena?”“Junior kuna binti anampenda bhana, sasa huyo binti kamwambia Junior ampelekee laki tano”“Kheee Junior atatoa wapi hiyo hela sasa?”“Sio atatoa wapi, kwa kifupi Junior kampa huyo binti laki tano taslim”Mara gafla walisikia gafli ikianguka chini na kupasuka, walipogeuka ilikuwa ni Vaileth ambaye alikuwa akileta ile juisi.Basi walimshangaa sana kisha mama Angel akamuuliza,“Wewe Vai una matatizo gani wewe?”“Samahani mama”Kisha Vaileth akaenda kuchukua tambala na kutoa zile chupa na kufuta ile juisi kisha kwenda kuleta juisi nyingine, basi muda huu mama Angel alimwambia,“Hebu kaa chini kwanza nikuulize maswali”Ilibidi Vaileth akae kwenye kochi na kusikiliza maswali ya bosi wake,“Eeeeh kilichokiustua hivyo ni kitu gani hadi kuangasha kikombe!”“Samahani mama, sijui ni vipi mkono umeteleza tu”“Hapana, lazima ulikuwa na mawazo yaliyofanya mkono wako ukateleza”Ilibidi mama Junior amtetee pale,“Hapana jamani,kuna wakati huwa inatokea tu, kwahilo namtetea”“Haya, kaendelee na kazi zako”Vaileth aliinuka na kurudi jikoni ila hakuwa na raha kabisa ukizingatia ni yeye aliyetoa laki tano na kumbe laki tano hiyo imeenda kupelekwa kwa mwanamke mwingine kwakweli roho ilimuuma sana.Junior na Erick wakiwa kwenye gari, Erick alimuuliza Junior,“Kwani tunaelekea wapi?”“Utaona tu, ila kuna jambo nataka unisaidie”“Jambo gani hilo?”“Kuna mwanamke namuhitaji halafu kashakula hela yangu kwakweli, leo nahitaji kuwa nae karibu”“Kivipi?”“Ngoja twende”Walifika mbele ya nyumba moja hivi na kusimamisha gari, kisha Erick alimuuliza Junior,“Kwahiyo hapa ni wapi?”“Hapa ni kwa mtu mmoja hivi unamfahamu, hebu shuka halafu ukimuona muite na akija panda nae kwenye gari”Basi Erick alishuka chini, na alivyoshuka tu baada ya muda kidogo alishangaa kumuona Samia akipita kuelekea kwenye ile nyumba, basi alimuita“Samia, Samia”Samia aligeuka, kwakweli hata Samia hakuamini kama aliyemuita ni Erick, yani alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha huku akimuongelesha ila Erick alikuwa kama anamshangaa vile,“Jamani Erick, kweli unanipenda umefika kwetu bila hata kukuelekeza”“Kheee kwani unaongelea kitu gani Samia, njoo kwenye gari”Basi Erick alifungua mlango na Samia akapanda kisha na yeye akapanda ila alishangaa kuona Samia alivutwa siti ya nyuma kwenye gari, mwanzoni hakujua ni kwanini Junior alikaa siti ya nyuma ila muda huo ndio akaelewa. Samia alikuwa amezibwa mdomo na Junior ambaye alikuwa akimwambia,“Wewe si mjanja, ukaamua kula hela zangu sasa na mimi leo lazima nipate changu. Erick ondoa gari sehemu hii”Erick alikuwa akimshangaa na kumuuliza,“Kwani Junior tatizo ni nini? Unataka kufanya nini na Samia?”“Nataka kumbaka”“Kheee kumbaka? Kakufanya nini kwani?”“Kala hela zangu mjinga huyu”“Sasa na wewe si umdai tu hizo hela zako, kwani ukimbaka ndio utakuwa umelipwa hizo hela?”“Erick hujui tu”“Najua vizuri, ila sipo tayari kushiriki na wewe katika hili, ukitaka kufanya huo ujinga wako basi uje ufanye peke yako ila sio ukiwa na mimi, naomba muachie Samia ashuke”Junior hakutaka kusikia hivyo kabisa zaidi zaidi alianza kumpapasa Samia kifuani na kumvuta blauzi kisha akaanza kumnyonya maziwa, kitendo kile kilimchukiza sana Erick ambaye alifungua mlango na kwenda kufungua mlango wa nyuma na kumshusha Samia kisha akamwambia,“Kimbia nenda kwenu”Halafu akarudi ndani ya gari na kuondoa gari na hakuongea chochote na Junior ila Junior ndio akaanza kulalamika,“Yani wewe kama sio mwanaume vile”“Kwani mwanaume anatakiwa kuwa vipi? Kama kubaka ndio uanaume basi nakubali ni kweli mimi sio mwanaume”“Nakushangaa sana, ndiomana ulikula kiapo na dada yako kuwa yeye ndiye atakuwa rafiki pekee wa kike katika maisha yako yani hujawaza hapo mbeleni utahitaji mpenzi au utahitaji mke, yani wewe wa ajabu sana, mambo yako hayaendani na ulivyo”“Ongea tu ukimaliza tutakuwa tumeshafika nyumbani”Aliendele tu kuendesha gari wakielekea nyumbani kwao ila Junior alimuomba jambo,“Sikia Erick nakuomba kitu kimoja tu, unajua akili yangu haipo sawa, naomba nipeleke hata ufukweni basi nikapate kidogo upepo wa bahari”Erick alikubali na kwa muda huo safari ilikuwa ni kuelekea ufukweni tu.Angel akiwa na baba yake siku hiyo ilikuwa ni furaha sana kwake kwahiyo aliamua kumuuliza pia kuhusu shule ambayo atatafutiwa,“Baba, ni shule gani nitaenda kusoma kidato cha tano na cha sita?”“Kuna shule nishakutafutia binti yangu, ni shule nzuri nina uhakika utaipenda”“Inaitwaje baba?”“Nadhani utaijua siku ya kufanya usahili ingawa usahili wenyewe hatufanyi kwenye shule, kwahiyo usiwe na wasiwasi bingti yangu amini lazima baba akupeleke sehemu nzuri inayokufaa”“Asante baba, ndiomana nakupenda sana”Basi Angel aliongea mambo mengi sana na baba yake hadi muda ulipofika wa baba yake kumrudisha nyumbani ambapo aliingia nae kwenye gari yake na kuelekea kwa bibi yake ila njiani Angel alikumbuka jambo,“Nimekumbuka zawadi ya bibi”“Oooh vizuri sana, unataka kumpatia zawadi gani?”“Mmmh sijui, ila nataka kumnunulia kiatu”“Unajua anavaa namba ngapi?”“Najua baba”Basi moja kwa moja baba Angel alienda na Angel kwenye duka la viatu na kuchagua kiatu cha kumpelekea bibi yake ila wakati wanaondoka hapo, baba Angel alishtuliwa na mtu ambaye alikuwa akimfahamu basi walianza kusalimiana pale,“Johari, za siku nyingi?”“Nzuri tu, yani mume wangu ndio akaniambia kuwa kaonana nanyi dah nikatamani sana nije kuwaona jamani, rafiki yangu Erica hajambo!!”“Hajambo kabisa, karibu sana nyumbani”“Asante, oooh nimekumbuka. Unamkumbuka Manka?”“Manka yupi?”“Mmmh wewe nawe, yani wewe usimfahamu Manka kweli? Leo hii humkumbuki Manka jamani!! Ila wanaume mna mambo sana, nilikutana na Manka ana mtoto mkubwa wa kike, nikamuuliza tu pale mtoto umezaa na nani kacheka nina mashaka ni mwanao”Baba Angel alimuangalia Angel ambaye alikuwa amesimama pembeni yao kisha alimuangalia Johari na kumwambia,“Acha maneno hayo hakuna kitu kama hiko kwangu, karibu nyumbani. Kuna mahali nawahi na binti yangu hapa”Basi muda ule ule baba Angel alipanda na mwanae kwenye gari ili kuelekea kwa bibi wa Angel, ila wakati wanaondoka Angel alimuuliza baba yake,“Kwani baba una watoto wengine tofauti na sisi?”“Aaaah kumbe ulikuwa unamsikiliza yule! Hapana bhana mwanangu, sina mtoto mwingine mimi zaidi yenu”Angel alitabasamu tu huku safari nayo ya kurudi kwa bibi ikiendelea.Mama Junior hakuwa na mambo mengi zaidi ya kumueleza mdogo wake kuhusu hiyo laki tano ila mama Angel aliwaza pia kuwa hiyo hela Junior aliitoa wapi? Alikosa jibu kabisa, basi wakati wanaendelea na maongezi simu ya mama Junior iliita ambapo alipokea maana mpigaji alikuwa ni dada yao Mage,“Ndio dada?”“Uko wapi?”“Leo nilikuja huku kwa Erica”“Oooh sikujua jamani, unajua mimi nipo huku kwako”“Aaaah jamani, basi nisubiri nakuja muda sio mrefu ngoja nichukue pikipiki”Basi mama Junior aliamua kumuaga mama Angel ambapo mama Angel alimuuliza,“Kwanini usimwambie yeye ndio aje huku?”“Unadhani angekuja? Hawezi kuja, ngoja niende na nitajua kilichokuwa kimemleta nyumbani kwangu maana lazima ana maneno”“Nimekumbuka kitu, unajua hapa nyumbani kuna kiumbe wangu huyu wa kuitwa Erica ni mbea hakuna mfano ila naanza kuhisi umbea Erica kautoa wapi, naona kwetu kuna asili Fulani ya umbea maana dada Mage nae dah ni mtihani sana”Mama Junior alicheka tu na kuondoka maana alitaka kumuwahi dada yao ajue ni kitu gani ambacho kimempeleka kwake.Junior na Erick wakiwa ufukweni, kuna mahali wanaona watu wamezunguka kwahiyo nao wakaona ni vyema waende kushuhudia kuna nini, wakakumbana na sauti ya mtu aliyekuwa akichezesha karata tatu,“Jamani ukipata basi umekula na ukikosa basi umeliwa, ni mchezo mrahisi sana unaoweza kukufanya uondoke na pesa nyingi za kutosha”Wakaangalia watu waliokuwa wakicheza, kuna wengine waliliwa hadi viatu walivyovaa, wengine hadi nguo walibaki tu kuondoka na kaptula, waliangaliana kwa makini na kuona kuwa ule mchezo ni mchezo wa kitapeli, ila aliyekuwa akichezesha mchezo ule ndio alikuwa akiwashangaza, basi walisogea pembeni kidogo ambapo Erick alimuuliza Junior,“Hivi yule sio mjomba Derrick!!”“Ndio, mwenyewe yule ila ngoja tukahakikishe”Basi wakati akiendelea kuchezesha ule mchezo, ni Junior ndio alienda kumshtua na kumfanya ashtuke sana, kisha alisogea nao pembeni na kuwauliza,“Nyie watoto mnafanya nini huku?”“Sisi tupo kutembea tu, ndio tunakushangaa wewe mjomba”Derrick aliwacha hapo na kama kuwatonya rafiki zake aliokuwa nao pale na uondoka kabisa eneo lile, kwahiyo Junior na Erick walibaki tu wakimshangaa hata wao waliamua tu kuondoka.Basi wakiwa kwenye gari Junior alianza kusema,“Mimi ndiomana mara nyingine hata sitaki kusoma, unajua huyu mjomba ni amesoma sana tu ila saivi kawa tapeli”“Ila utapeli sio kusoma au kutokusoma ni tabia ya mtu tu.”Basi wakarudi zao moja kwa moja nyumbani kwa wakati huo.Usiku wa leo, Vaileth alikuwa na mawazo sana na uchungu wa pesa yake kugundua kuwa ameenda kupelekewa mwanamke mwingine, basi alikuwa kajiinamia tu,mpaka Junior alipoingia bado Vaileth alikuwa akilia tu na kumfanya Junior ahisi lazima kuna jambo,“Vai nini tatizo?”“Umenifanya mjinga Junior tena umenifanya mjinga wa kwanza, kweli jamani wewe wa kuja kuchukua laki tano kwangu na kwenda kumpelekea mwanamke mwingine jamani Junior hivi hata hukupata haya katika kunifanyia jambo kama hilo!!”“Jamani, nani huyo kakwambia maneno ta uongo Vai!”“Maneno ya uongo eeeh! Wakati mama yako kaja kuelezea hapa mwanzo mwisho halafu unasema ni uongo. Kwakweli umenishinda tabia, hivyobasi kuanzia leo mimi na wewe basi”Junior akafikiria na kujiona ni kweli ametenda makosa kwa Vaileth, ila kwa wakati huo alishindwa kusema lolote na hata kumbembeleza sana Vaileth hakummbembeleza zaidi ya kuinuka na kurudi chumbani kwake, hiko kitendo kilimuumiza sana Vaileth, aliwaza jinsi alivyojitoa kwa mwanaume huyo, jinsi alivyomuhudumia kama mke na mume, kwakweli roho ilimuuma sana na kumfanya akose raha kabisa, kilichotokea kwake ni kujikuta akilala na dukuduku moyoni mwake.Kulivyokucha tu, Erica alienda chumbani kwa Vaileth ila leo alifungua tu mlango na kuingia kisha akamuuliza,“Kheee leo hukufunga mlango dada!! Junior yuko wapi?”“Nadhani yupo chumbani kwake”“Mbona unaonekana umevimba Macho dada?”“Aaaah macho tu yalikuwa yakinisumbua ila usijali nipo sawa”Erica alimuangalia na kutoka na wala hakusema jambo lililompeleka kwahiyo hataVaileth hakutambua ni kitu gani kilimpeleka Erica chumbani kwake kwa muda huo.Ila Erica alivyotoka chumbani kwa Vaileth moja kwa moja alienda bustanini maana alimuona Junior akielekea huko basi alimkuta na kuanza kuongea nae,“Umemfanya nini dada Vai?”“Kwanini?”“Nimemkuta macho yamemvimba, kanidanganya kuwa macho yanamuuma ila anavyoonekana ni kuwa amelia sana”“Mmmh mimi sijui kitu”“Halafu kitu kingine, siku ile Samia amekuja amesema kuwa ulimpatia laki tano”“Mmmh huyo Samia chizi eeeh!”“Ndio kasema, pia kasema wewe hakupendi wala nini ila kuna mwanaume mwingine kwenye nyumba yetu ndio anampenda”“Haya sasa umeona kama Samia ni chizi, anamaanisha kuwa anampenda Erick”Hapo Erica akashtuka kidogo na kuuliza tena,“Unasema?”“Ndio hivyo anampenda Erick, sasa unashtuka nini? Samia ni msichana na Erick ni mvulana, tatizo liko wapi wakipendana? Hutaki wifi wewe? Ndio nyie ambao huwa mnagombana na mawifi zenu bila sababu”“Kwani mimi nimesema jambo lolote”“Hata kama ila nakuelewesha”“Ila umebadili mada tu, umemuhonga Samia laki tano!!”Vaileth akaenda kule bustanini pia maana alikuwa anataka kufagia kidogo na kuweka mazingira safi, kwahiyo alisikia haya maneno ya mwishoni na kumfanya aelewe zaidi kuwa kwanini Junior aling’ang’ania kumsindikiza Samia siku ile, kwahiyo Vaileth akazidi kupata ushahidi.Basi alisogea pale na Junior alimsalimia ila hakumuitikia yani moyoni mwake alikuwa na kinyongo sana.Kisha muda wa kwenda kanisani leo wote walijiandaa na kwenda Kanisani kama kawaida ya nyumba hii, na leo ni nyumba nzima waliondoka na kwenda Kanisani.Huku nyumbani alifika Derrick ambaye alikaribishwa na mlinzi tu na kwenda kukaa kwenye kibaraza kwani familia nzima hii haitakuwepo kwa siku hiyo.Basi alikaa pale kwenye kibaraza hadi akasinzia pale pale, ila wakati amesinzia akajiwa na ndoto na hiyo ndoto aliona watu wengi wamemzingira huku wakisema mwizi huyooo, mwizi huyooo piga pia, Derrick alishtuka sana huku akihema, akaamka na kujisemea,“Ila mimi sio mwizi, mimi siibi na simpori yoyote ila wanatoa kwa hiari yao, nitakuwaje mwizi sasa?”Akaona hapo hata hapamfai kuendelea kusinzia sababu alikuwa na mambo yake mengi tu ya kufanya basi aliinuka na kumuaga mlinzi na kuondoka zake.Wakati anaondoka ndipo akakutana na Tumaini ambaye nae alikuwa akienda mahali hapo, ila alikuwa ameongozana na rafiki yake kwa muda huo basi akamuuliza Derrick,“Kheee Derrick, leo ulikumbuka kuja kwa dada yako!”“Ndio, nilitaka kumsalimia maana nimemkumbuka sana ila sijawakuta”Huyu rafiki yake Tumaini alishtuka kidogo na kumuuliza Derrick,“Kaka, hunikumbuki?”“Nikukumbuke kwani tumesoma wote?”“Hapana sio hivyo, mimi nakukumbuka vizuri ulinitapeli wewe”“Kuwa na adabu mwanamke, hivi unavyoniona nina muonekano wa kitapeli? Kuwa na heshima”Kisha akamuaga Tumaini na kuondoka zake, ambapo yule dada alimwambia Tumaini,“Huyu kaka ni tapeli, yani alinitapeli mimi kila kitu nilichokuwa nacho”“Lazima umemfananisha, unajua anafanya kazi gani huyu? Unajua elimu yake, hawezi kuwa tapeli hata kidogo”“Namkumbuka vizuri dada, alinitapeli huyu”“Haiwezekani nakwambia, wewe nawe ujue tunaenda nyumbani kwa dada yake kwenye ofisi yake anatafuta mtu wa kumsaidia ndio nakupeleka wewe unaanza kumuita kaka yake tapeli, hebu usije sema hivyo mbele yake kabisa”Ila sasa hata na wao waliposogea kwa mlinzi waliambiwa vile vile kuwa wale watu bado wapo Kanisani na siku hiyo walichelewa sana kutoka Kanisani tofauti na siku zingine, waliwasubiri pia na kuchoka ikabidi waondoke zao tu.Siku ya leo, walipotoka Kanisani baba Angel aliamua kuwapeleka wote kwenda kula hotelini, yani siku hiyo alikuwa na furaha sana ya kumaliza ujenzi wake wa kile kiwanda kidogo, kwahiyo alikaa na familia yake na kuagiza nao chakula ambapo walikuwa wakila huku wakifurahi, kasoro Vaileth ambaye muda mwingi alikuwa kimya kwani alikuwa akifikiria laki tano yake, ila walipomuuliza sababu ya kuwa kimya kiasi kile alisingizia kuwa siku hiyo hakuamka vizuri tu.Basi walikuwa wanakula huku wakiongea mambo mbalimbali ndipo Junior alipoingizia swala la kumuona Derrick ufukweni,“Halafu mamdogo, tulimuona mjomba Derrick mahali anacheza ile michezo ya kitapeli”“Michezo gani?”“Ule mchezo wa karata tatu”Baba Angel alishtuka kidogo na kusema,“Hivi ule mchezo bado upo!! Kwahiyo kuna watu wanapeliwa bado kwa ule mchezo, nakumbuka zamani sana utakuta mtu anatapeliwa hadi nguo”“Hata hapo ilikuwa hivyo hivyo, unajua bamdogo mjini kila siku washamba wanaongezeka, yani kuna watu hawajui kama ile ni michezo ya kitapeli”“Hivi mmesema Derrick, mna uhakika nyie mnamfahamu Derrick?”“Tumemuita na kumuita, akasogea na kuuliza tunafanya nini halafu akaondoka”Mama Angel alikaa kimya tu kwani alishawahi kuambiwa tabia ya kaka yake huyo kwa siku hizo kwahiyo akajikuta hana cha kusema, mumewe akamuangalia na kumuuliza,“Kwahiyo unaamini haya maneno ya watoto?”“Tutaongea zaidi tukirudi nyumbani ila sio muda huu”Yani mama Angel alikatisha yale maneno ya kuhusu ndugu yake, mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake basi akafungua na kusoma,“NImekuja kwenu nimekaa sana hadi nimechoka, by Derrick”Mama Angel akashtuka kidogo kwani kwa tabia ya utapeli aliyosimuliwa kuhusu Derrick akajikuta akihofia kuwa isikuwa Derrick kamtapeli hadi mlinzi wao ila akaona ni vyema asiwaze hayo sana sababu atashindwa kukaa vizuri mahali pale na kufurahi na familia yake.Basi waliendelea tu na mazungumzo mengine hadi pale walipomaliza na kufurahi.Sia akiwa katika harakati zake za biashara, anakutana na Dora na kumsimamisha kisha kuanza kuongea nae,“Leo sijakusimamisha kwa ubaya Dora maana hapo ulipo tayari ushakunja sura jamani, pole sana”“Kwani mimi nimesema kuwa umenifananisha kwa shari? Hata hivyo niambie ulichonisimamisha, kwanza upo kwenye biashara saa hizi hukwenda kwenye ibada leo?”“Leo sijaenda, yani mimi kwenda kuna watoto wa Erick, wakiniona kanisani wanaona kama mzuka vile”“Jamani! Mbona una mambo ya ajabu Sia, kwani wale watoto wanakufahamu?”“Tuachane na habari hiyo, Kwa kifupi ni hivi, mdogo wako kapewa dawa na yule mwanamke”“Kivipi?”Sia alianza kumueleza toka yule madam Oliva alivyokuwa akimtaka Erick, na jinsi ambavyo alimpelekea Erick viatu halafu mama Angel akavipeleka kwa Steve,“Kheee kumbe ndio ilivyokuwa!”“Ndio hivyo”“Jamani kwanini mdogo wangu mmemuonea hivi!! Hivi kweli haiwezekani kwa yeye kumpenda mwanamke anayemtaka mpaka mumkorogee madawa, kuna kipindi mtaharibu akili ya mdogo wangu”“Mmmh usiniseme mimi, mseme huyo wifi yako mpya”“Simtambui kama ni wifi yangu”“Hata mimi hujawahi kunitambua ingawa nimezaa na kaka yako, yani wewe Dora una matatizo sana”“Ila samahani, unapafahamu nyumbani kwa huyo mwanamke?”“Napafamu ndio”“Nakuomba basi unipeleke ili nikaongee nao mwenyewe”Sia alikubali kumpeleka na aliweka vitu vyake vizuri kisha yeye na Dora waliondoka eneo lilena kwenda nyumbani kwa madam Oliva.Walifika pale na kugonga geti ambapo mlinzi wa nyumba ile alienda kufungua mlango, ila macho ya Diora na yule mlinzi yalipokutana kila mmoja alionekana kupata mshangao dhidi ya mwenzie. Sia alikubali kumpeleka na aliweka vitu vyake vizuri kisha yeye na Dora waliondoka eneo lilena kwenda nyumbani kwa madam Oliva.Walifika pale na kugonga geti ambapo mlinzi wa nyumba ile alienda kufungua mlango, ila macho ya Dora na yule mlinzi yalipokutana kila mmoja alionekana kupata mshangao dhidi ya mwenzie.Waliangaliana kwa makini sana, ila mwisho wa siku Dora alijihisi vibaya kwani huyu mlinzi wa madam Oliva alikuwa ni mtoto wa James ambaye alizaa na msichana wa kazi, maana alimuuliza,“Unaitwa nani kijana?”“Naitwa James”“Imekuwaje hadi umekuwa mlinzi?”“Unajua mimi naishi na mjomba, sasa kila kitu namtegemea mjomba, nikaona ni vyema nitafute kazi ila Mungu mwema ndio nikapata kazi mahali hapa”Kwakweli Dora aliacha hadi kufikiria kilichompeleka mahali pale na kujikuta akimuangalia kwa makini sana huyu kijana kwani moyo ulikuwa ukimuuma sana, basi Sia alimuuliza,“Inamaana huyu ni James, mtoto wa James!”Dora aliitikia kwa kichwa tu kisha Sia akamwambia,“Mimi nilishawahi kukwambia haya, nadhani leo umenielewa ni kitu gani nilichokuwa nazungumzia, unaishi kwenye nyumba nzuri, una maisha mazuri, unafanya utakacho ila watoto wa huyo mtu wanaishije? Je wanalalamikaje kwa Mungu. Haya kama wamefikia hatua ya kuwa walinzi ni mara ngapi wamelalamika kwa Mungu, na wakati wewe unaouwezo wa kuwasaidia?”Basi Dora akamuangalia yule kijana na kumuandikia namba yake kwenye karatasi kisha akampatia na kumwambia,“Naomba utanitafuta”Halafu Dora akaondoka, ikabidi Sia nae aondoke zake maana aliyempeleka alikuwa ameondoka kwa muda huo.Dora alirudi nyumbani kwake na kujifikiria vitu vingi sana, kuna muda alihisi machozi yakimtoka na kusema,“Ingawa mwishoni James hakunifanyia vitu vizuri ila alikuwa akiniambia nikumbuke watoto wake, alikuwa akimtaja James, Junior na Jasca, kwanini nimekuwa mbinafsi kiasi hiki!! Kwani wokovu ndio unatufundisha hivi? Neno la Mungu ndio linafundisha hivi kudhurumu mali ya mtu! Si wanasema mtu mwenye dhuruma hatouona ufalme wa Mungu, eeeh Mungu naomba unisamehe”Basi akafikiria pale cha kufanya kwani aliona ni wazi anawajibu wa kuwasaidia watoto wale ili na wao waishi kama Jesca na watambuane maana ni mali za baba yao wote watatu.Wakati akifikiria hayo, simu yake ya mkononi ilianza kuita na alipoangalia aliona namba ngeni na kupokea na kuanza kuongea nayo,“Ni Sia anaongea hapa”“Eeeh Sia unasemaje?”“Unajua ni jambo gani lilitupeleka pale? Yani ulipomuona yule kijana umesahau kila kitu, mdogo wako karogwa wewe!”“Unajua naweza kukazana kumfatilia huyo aliyemroga mdogo wangu wakati mimi kuna dhambi nimefanya na ninazifumbia macho, acha kwanza nijisafishe na dhambi yangu hii”“Kheee haya, ila mimi nilikwambia ukanipuuzia. Kuna muda unaona unaishi kwa amani sana ila kuna mtu umedhuruma nafsi yake na kila siku analia kwaajili yako”“Kwaheri maana wewe nawe ukianza humalizi”Dora alikata ile simu huku akiendelea kutafakari mambo mbalimbali.Familia ya mama Angel, kwa muda huu wote walikuwa wakirudi nyumbani huku wakiongea mambo mbalimbali kwenye gari, ila njiani mama Angel alikuwa akiangalia nje na alimuona Derrick kasimama na mdada halafu Derrick akaondoka muda huo magari yalikuwa kwenye foleni kwahiyo mama Angel alikuwa akiona karibia kila kitu kilichoendelea, mara alimuona yule dada akilia hadi kukaa chini, ndipo alipomuomba mumewe asimamishe gari pembeni kwanza ili akaongee na yule mwanamke, na kweli magari yaliporuhusiwa baba Angel alisimamisha pembeni halafu mama Angel alishuka na kumfata yule mwanamke aliyeonekana amechanganyikiwa,“Vipi dada tatizo ni nini?”“Nimetapeliwa dada, yani kuna mbaba nilisimama nae hapa kumbe ni tapeli, kanitapeli kila kitu hadi hela ya nauli”“Yani kakutapeli kivipi?”“Yule kaka nimetoka nae mbali kidogo, kaniambia kuwa yeye huwa anawasaidia watu kuongeza kipato chao, basi aliniambia vitu vingi sana hadi tumefika hapa akaniambia nimpe mkoba wangu na simu yangu nami sijui vipi nikampatia ila alipoondoka ndio nimegundua kuwa nimetapeliwa hapa sijui hata nyumbani narudi vipi”“Duh pole sana”Kisha mama Angel akampa yule mdada elfu tano ili iweze kumsaidia kama nauli ya kurudi, basi alirudi kwenye gari ya mume wake na safari iliendelea.Usiku huu baba Angel aliona vyema kuuliza kuhusu mkewe kwenda kuongea na yule mwanamke, kuwa ni kitu gani kilimfanya aende kuongea na yule mwanamke, basi alimwambia tu kuwa yule mwanamke alikuwa katepeliwa ila hakusema kama tapeli mwenyewe ni Derrick kwani aliamini kuwa aliyemuona Derrick alikuwa ni yeye mwenyewe, basi alimulezea mumewe tu lile tukio la yule mwanamke, basi baba Angel akasema,“Ila tamaa ya kupata hela kwa haraka haraka ndio inayofanya wengi watapeliwe, ukianza kufatilia utaona wengi kweli walitamani hela za haraka. Ila mke wangu kuna tatizo lingine”“Lipi hilo”“Sikukwambia sijui, ila ni hivi Steve hajaenda ofisini kabisa, nilimpigia simu akapokea madam Oliva, kwahiyo Steve yupo kwa madam Oliva”“Kheee jamani huyu mwanamke ni nyoka, kwahiyo ndio alitaka akuweke wewe hivyo jamani!! Si ningekuwa chizi mimi loh!! Ila pale dukani itabidi tumpe mtu mwingine, la sivyo huyo Steve atahonga duka letu kwa huyo madam wake”“Mmmh sijui, ila tutafanya hivyo”Basi waliaongea ongea pale na kuamua tu kulala kwa muda huo.Angel kama kawaida alimuomba bibi yake simu na kuanza kuwasiliana na wale watu wake aliokuwa akiwasiliana nao sana, yani kitu pekee ambacho huwa kinamfanya kuomba simu kwa bibi yake ni kuwasiliana na Samir, na huwa akiipata hiyo simu anaanza kumtumia ujumbe Samir,“Samir”“Oooh niambie malaika wangu, unajua Angel nakupenda sana”“Jamani Samir unafanya nihisi hakuna mwanaume tena katika ulimwengu huu mwenye mapenzi kama wewe, ukimtoa baba yangu”“Ni kweli kwa waliobaki hakuna kweli, tumebaki wachache sana. Ila Angel siku za mbeleni huko tutaishi pamoja na kuwa mke na mume”“Nitafurahi sana Samir”“Vipi na shule bado hujatajiwa”“Sijatajiwa ila baba alisema kuwa naweza leo kwenda kufanya usahili”“Basi ukienda kuwa makini sana Angel ili unitajie hiyo shule maana nataka tusome pamoja ili niwe nakulinda kipenzi changu”“Mmmh Samir una vituko sana”Mara simu ya Angel ilianza kuita, alipoangalia ni Mussa aliyekuwa anapiga, ila kwavile alipenda zaidi kuwasiliana na Samir, kwahiyo hakupokea ile simu ya Mussa na kuendelea kuwasilina na Samir.Kesho yake mapema kabisa, baba Angel alijiandaa na kwenda ofisini kwake, kisha alienda kwenye ujenzi wake ambapo alitaka kufanya sherehe kidogo ya ufunguzi wa jingo lake hilo ila alitaka kumshtukiza tu mke wake kwahiyo hakutaka kumwambia ni kitu gani kitaendelea.Basi alipomaliza hapo, kuna mwalimu aliwasiliana nae kuhusu Angel kwenda kufanya usahili basi alipoondoka hapo alienda kumfata Angel ambaye alifanya ule usahili na kumrudisha nyumbani, ila wakati wa kurudi simu ya Angel ilianza kuita maana siku hiyo alisahau kumrudishia bibi yake, basi baba yake alisimamisha gari pembeni na kuanza kumuuliza Angel,“Nasikia simu inaita?”Angel hakuwa na jibu, basi baba yake akamwambia,“Hebu nipe hiyo simu niione”Angel hakuwa na namna zaidi ya kutoa ile simu ili baba yake aweze kuiona, basi baba Angel alichukua ile simu na kuiangalia kwakweli ilikuwa ni simu ya gharama sana, akamuuliza,“Hii simu umepewa na nani Angel?”“Samahani baba, nilipewa na babu”“Na babu? Babu yupi huyo?”“Nilimfahamu kwa bibi kule nilipokuwa, ndio akaniletea hii simu”Kwakweli baba Angel aliiangalia sana ile simu ila hakuongea jambo lingine lolote na kurudisha ile simu kwa Angel, kisha safari iliendelea ambapo alimfikisha Angel kwa bibi yake halafu yeye akarudi katika ujenzi wake ili kupanga na baadhi ya vijana kuwa mahali hapo atafanikisha vipi kwaajili ya sherehe yake fupi ya ufunguzi wa kiwanda chake, basi alipanga nao pale na kisha kuondoka zake kurudi nyumbani, kiukweli alikuwa amechoka sana siku hiyo kutokana na matembezi aliyokuwa nayo.Kulipokucha leo kabla baba Angek hajaondoka aliona ni vyema kwanza akiongea na mke wake, basi alianza kuongea nae pale kuhusu Angel,“Halafu mama Angel unajua mwanao anamiliki simu ya aina gani?”“Eeeh ya aina gani?”“Mwanao anamiliki simu ya gharama sana, niliwahi kuulizia zile simu wanauza milioni, mbili nimemuuliza tu nani kampatia ile simu kasema baba yake kule kwa bi I yake alipokuwa yani kwa mama yangu, kwakweli nimesikitika na kushindwa hata kuongea lolote”“Kheee na mama yangu nae kamuachia simu jamani wakati niliongea nae!”“Kuongea na mama hakusaidii kitu ila hapa naona cha muhimu ni wewe kuongea na Angel”“Niongee nae nini sasa?”“Yule ni mtoto wa kike na wewe ndio mama, tafuta siku na uongee na mtoto ukweli”“Unamaana nimuelezee kuhusu uhalisia wake”“Aaaah sijasema hivyo maana hayo ni maamuzi yako, ila ninachoongelea hapa ni ile hali ya mama kuongea na mtoto wake wa kike”“Unajua sikuelewi mume wangu, niongee nae kuhusu nini?”“Sikia nikwambie, kaa chini na Angel mueleze ukweli wote kuhusu mahusiano, najua umepitia changamoto nyingi pia kwahiyo unaweza kumueleza mtoto wako hata kwa kuto kusema ni wewe yani ukasema kuna rafiki yako yalimpata haya na haya na haya, mueleze ukweli mtoto ajue kuhusu mahusiano kwanza, hata ukimueleza ukweli kuhusu uhalisia wake na bila kumueleza ukweli kuhusu mahusiano basi atatembea na hao unaosema ndugu zake maana ataona ni kawaida, sasa kaa na echini mwambieukweli jinsi mahusinao yalivyo hata yakimtokea puani bado atakumbuka kuwa lakini mama alisema, kwani tukiendelea kumthibiti kuhusu simu bila kumwambia ukweli napo ni kazi bure, utamzuia na simu hii kuna jamaa atamnunulia simu nyingine. Angel ni bvinti mzuri tena mzuri sana ila akiharibikiwa basi ule uzuri wake hautoonekana kwani kila sehemu atakuwa akielezewa kuhusu sifa mbaya, mama Angel kaa chini na mtoto”“Nitajitahidi mume wangu, kwani sitaki mtoto aharibikiwe”“Maana naona kuna wanaume wameanza kuichanganya akili yake kiasi kwamba nahisi ana mawazo yupi ni yupi katika maisha yake, na ikiwa tukiona kuna mwanaume anamfatilia sana mtoto wetu basi hatuna budi kufatilia uhalisia wa huyo mwanaume ingawa ni ngumu sana kuchunga kila mwanaume anayemfatilia mtoto wetu. Ila mueleze mtoto ukweli ili aweze kujilinda na kujichunga”Mama Angel alimuelewa vyema kabisa mume wake, kwahiyo alikubaliana nae na kile alichokuwa akikisema na kusema kuwa atakitekeleza.Usiku wa leo, Vaileth bado aliamua kuwa mbali kabisa na Junior kwani kila akifikiria kuhusu laki tano ambayo Junior aliichukua kwake na kukumbuka aliyoyasikia kuwa alipeleka hela hiyo kwa mwanamke, alijikuta akiwa hana furaha tena na Junior kiasi cha kufanya amchukie sana, ila kabla hajalala alitumiwa ujumbe na Junior,“Vaileth mpenzi wangu, nifanye nini ili uweze kunielewa, sijui hata nikuelezeje ila mama yangu si mkweli”“Oooh mama yako si mkweli, kwahiyo mama yako kapanga na Samia au? Halafu usiniongezee hasira Junior”“Basi, ila niambie nifanye kitu gani kwasasa uweze kunisamehe”“Nirudishie laki tano yangu, sitaki maneno mengine”“Sawa hakuna tatizo, hiyo hela nitakupatia tu hakuna tatizo”Vaileth hata hakuendelea kuwasiliana nae zaidi ya kutafuta usingizi tu muda huo ila akapigiwa simu na ndugu yake Prisca na kuipokea,“Unajua nini Vai, natamani kuja kwenye hiyo nyumba kukuona ila naogopa na ninaona aibu”“Pole sana, kwa yale mambo lazima uone aibu”“Kwanza hongera sana, nasikia matusi uliyofanya kijijini huko”“Matusi gani tena?”“Si umerekebisha nyumba ya wazazi, nasikia wameweka bati na wamerekebisha kote yani nasikia pamependeza nyumbani kweli, halafu mjomba kawasaidia kuvuta umeme kwa ile hela”“Oooh swala zuri sana, kwahiyo nyumbani kuna umeme kwasasa?”“Ndio, unajua nguzo za umeme zilipita pale pale ila sababu ya pesa ndiomana hawakuvuta, halafu nyumba ya bati zilizooza na umeme wa kazi gani? Ila Vai umefanya kazi kubwa sana, hongera mdogo wangu umefanya jambo la akili. Ila ngoja nikuulize, zile pesa ndio mshahara au kitu gani? Na mimi natamani kupata kazi za ndani jamani, kwa miezi michache tu umeweza kufanya kitu cha namna ile nyumbani!! Oooh na mimi nitafute kazi za ndani sasa”“Sikia kwanza, ile pesa sio mshahara ila ile pesa nimepewa na wazazi hapa, nilipowaambia tu kuhusu nyumbani basi wakanipatia ile pesa, tena mama aliituma mwenyewe kwa mama nyumbani kupitia simu ya mjomba, tuliwasiliana nao na kutuma ile pesa, kwakweli hii familia wananipenda sana na wananilea sana, kwakweli nawapenda”“Haya, ila nasikia kule kijijini kuna mkaka mwalimu anafundisha shule ya jirani, toka kaambiwa kuhusu wewe basi anasema ukirudi tu anakuoa, kwahiyo jiandae na ndoa”“Jamani ndugu yangu, usinichekeshe mie, ngoja nilale halafu tutaongea vizuri siku nyingine unajua ni usiku huu!”“Najua ndio, ila huu ni muda mzuri wa kukupata hewani ila hakuna tatizo usiku mwema”Basi Vaileth alikata ile simu ila hakutaka kutilia maanani kuhusu huyo kijana mwalimu wala nini zaidi ya kufikiria mambo mengine na kulala tu.Leo baba Angel kabla ya kwenda ofisini, alipitia kwanza kwenye ujenzi wake kuangalia maandalizi ya ufunguzi yatakavyokuwa maana alishaongea nao, kwahiyo alienda tu kuangalia na kupanga zaidi,“Ila bosi, kukipambwa kidogo hapa nje basi shughuli itapendeza zaidi”“Kwahiyo kuna umuhimu wa kutafuta mpambaji?”“Ndio, kuna umuhimu wa kufanya hivyo”“Mimi sijuani sana na watu wengi, basi mtanitafutia mtu mnayeona anafaa na kumpa hii kazi”“Oooh kuna baba mmoja hivi anaitwa Babuu ni hatari kwa mapambo, yani akikupambia mahali lazima ubaki mdomo wazi”“Basi nitafutieni huyo Babuu na muelekezeni tunachotaka halafu mtaniambia gharama zake”“Sawa, hakuna tatizo juu ya hilo”“Nataka ile siku ikifika mimi na familia yangu yote tuwe hapa na nitaongea machache kidogo kwani hiki ni kiwanda changu cha kwanza kufungua na ninahitaji kifanye vizuri”“Usijali bosi, kwanza eneo umepata zuri na kubwa, lazima kiwanda kitafanya vizuri sana”Basi alikubaliana na huyu kijana na kutembelea tembelea baadhi ya vifaa alivyoviweka kwani kuna watu aliwaweka watengeneze bidhaa ambazo zitakuwepo siku ya ufunguzi na kufanya watu wafahamu bidhaa zake, basi alipomaliza aliondoka zake na kuelekea kazini kwake.Ila leo alipoingia ofisini tu kuna mgeni alikuja ofisini kwake, mgeni huyo alikuwa ni Sia, basi akamuuliza,“Kheee Sia, umefata nini kwani?”“Sijaja kwa nia mbaya ila nimekuja kukupa habari flani hivi”“Habari gani?”“Shemeji yako Derrick ni tapeli”“Kivipi?”“Ni hivi, Derrick ana michezo ya kitapeli na wengi sana kawatapeli na kuwaliza, mimi mwenyewe alitaka kunitapeli, nikamuangalia na kumuuliza Derrick mbona mimi nakufahamu vizuri sana, yani unataka kunitapeli kweli! Basi akaona aibu na kuondoka, kwakweli Derrick sio mtu mzuri kwasasa”“Duh!! Ila kwanini umekuja kuniambia hayo?”“Nimekuja kukwambia ili nyie mjue cha kufanya na huyu ndugu yenu, unajua utapeli sio sifa nzuri eeeh!! Tapeli hana tofauti na mwizi, ila tofauti yake ni kuwa yeye hapori bali unampa mwenyewe na mwizi anaphora ila tapeli ni kama mwizi tu kwani anakuumiza kimaisha na kisaikolojia, kwahiyo mnatakiwa mjue cha kufanya”“Sasa cha kufanya ni kipi hapo?”“Sikia nikwambia, kwasasa unaona hakuna cha kufanya ila hii ni sifa mbaya ambayo haitaishia kwa Derrick tu bali itasambaa hadi kwenye familia yenu, hebu angalia ulivyo na pesa na jina zuri mjini halafu Derrick anamtapeli mtu na kusikika kuwa yule ni shemeji wa Erick, unajua sio sifa nzuri kabisa hiyo. Hebu kuweni makini na ndugu yenu, yule Derrick ni msomi, na mpaka kawa vile lazima kuna kitu kimemfanya awe vile, msikubaliane na ile hali kabisa, nyie mnasali siku hizi na uzuri ni kuwa mnatambua jinsi gani nguvu za giza zinafanya kazi, mkomboeni ndugu yenu”“Kheee ulivyoongea kwa uchungu, sawa mama nimekuelewa”“Jamani, leo mbona nitalala huku nikitabasamu, Erick umeniita mama!! Asante sana”Baba Angel alicheka tu huku akitikisa kichwa, basi Sia aliinuka na kumuaga baba Angel huku akimwambia,“Naomba ufanyie kazi hilo nililokwambia, msimuache Derrick aendelee kupotea, ha[endi kuwa vile, msaidieni”Sia akaondoka zake, ila kuna muda kama aliona kuwa Sia anazungumza ukweli kuwa wanapaswa kumsaidia Derrick, ila kwavile siku ile alikuwa na mambo mengi ya ufunguzi wa kampuni yake ambao karibia unafanyika basi ndio kitu alichofikiria zaidi.Leo, mama Angel alikuwa amekaa sebleni na Erick wakiangalia Tv, kidogo ilikuwa ni tofauti kidogo kwani mara nyingi Erick sio mpenzi wa kuangalia Tv, basi kulikuwa na kipindi cha mahusiano na kuna mtu alipiga simu kuwa ameachwa na mpenzi wake, alipomaliza kuongea kwenye simu, wale watangazaji wakaanza kudadavua sasa ambapo mmoja akasema,“Jamani kuachw akunauma tena sana”Mwingine akadakia,“Ni kweli kunauma ila inatakiwa ifikie hatua watu waone kuachwa au kuachana ni kawaida tu, sasa mtu mmekutana kimjini mjini asikuache kwasababu gani? Akipata mpya anayefaa anakuacha tu, mtu mwenyewe mmekutana na meno yote mdomoni, asikuache umezaliwa nae tumbo moja huyo? Ni pacha wako hadi asikuache”Wale watangazaji walikuwa wakicheka sana huku wakiongea kwa furaha, basi Erick alimuangalia mama yake na kumuuliza,“Kwani kuna mahusiano ya kimapenzi kwa watu waliozaliwa tumbo moja au mapacha?”“Mmmh mahusiano ya kimapenzi? Haiwezekani maana ni ndugu”“Sasa hawa mbona wanasema kuwa mtu ambaye hujazaliwa na tumbo moja au mtu ambaye sio pacha wako ni lazima akuache, sasa kuna umuhimu gani wa kuwa na mahusiano”“Hujaelewa hapo mwanangu, ni hivi katika mahusiano kuacha na kuachwa ni kawaida kwani mtu anahitaji apate mtu wa kuridhika nae, anaweza kuona tabia ambazo hazifai kwake na akakuacha, ila ndugu kuachana ni ngumu, sio kimahuano ya kimapenzi bali kimahusiano ya kindugu, kuachana ni vigumu sana kwani ni ndugu wanajuana toka watoto na damu zao zimewaunganisha, kwa undugu wa mapacha ndio ngumu kabisa kuutenganisha. Ila kuna usemi usemao ndugu wakigombana chukua jembe ukalime kwahiyo mambo ya ndugu kidogo ni mambo ambayo yana gusa sana”“Kwahiyo mama ndugu hawawezi kuwa wapenzi”“Jamani Erick, uliona wapi ndugu wakawa wapenzi jamani! Kuna baadhi ya kabila tu ndio zinaruhusu mabinamu kuoana ila ndugu kuwa wapenzi ni kinyume kabisa”“Ila mama, ukisoma kwenye Biblia unaona kuwa mtu wa kwanza kuumbwa ni Adam halafu akafatia Eva, hiyo inamaanisha kuwa duniani wote ni ndugu hivi ni kweli ndugu hawaoani? Au Mungu aliumba watu wengine tofauti na hao kwanza?”“Kheee wewe mtoto usinitie kiungulia mie, mambo ya uumbaji nitayajulia wapi jamani, kwanza nenda kaoshe ile gari pale nje maana unaongea sababu huna kazi za kufanya kwasasa”Basi Erick aliinuka na kwenda kuosha gari ambalo mama yake alimwambia ila bado alikuwa na maswali yake ambayo mama yake hakuwa na majibu na hayo maswali.Wakati akiosha gari lile, alienda Erica kule ambapo kaka yake alikuwa akiosha gari, alimnyatia kwa nyuma na kumwagia maji na kufanya Erick ashtuke sana, kisha walianza kukimbizana na kusahau hata kile alichokuwa akifanya.Walikuwa wakikimbizana huku kila mmoja akipata maji anamvizia mwenzie na kummwagia, kitendo hiko kilifanya kummwagia maji baba yao ambae alikuwa ndio amerudi,“Nyie watoto vipi kwani?”“Samahani baba”‘Hebu njooni hapa”Erica na Erick walisogea kwa baba yao ambaye alianza kuongea nao,“Haya, huo mchezo wa kumwagiana maji mmeutoa wapi?”“Baba, nilikuwa naosha gari ila Erica akaja nyuma yangu na kunimwagia maji”“Eeeh Erica kwanini umefanya hivyo?”“Baba, zamani tulipokuwa watoto basi mimi na Erick tulikuwa tukicheza michezo mingi sana ila siku hizi huwa simuelewi Erick maana muda mwingi kama ananikwepa basi ndio nikaamua kuja kuanzisha mchezo wa kummwagia maji”Baba Angel alitikisa kichw akama kusikitika kidogo halafu akacheka na kusema,“Yani nyie watoto mnaakili mbovu sana, hebu cheki mlivyolowa chapachapa jamani. Haya Erick acha tabia ya kumkwepa mdogo wako, uwe unaongea nae na kucheza nae”Basi Erica akasema,“Tena ni vyema baba kama mimi na Erick tukisoma shule moja kama zamani”“Hilo tutaliongelea pia, Erick wewe ndio mlinzi wa dada yako na sio mtu wa kumkwepa. Haya nendeni mkabadilishe nguo”Basi waliingia ndani na baba yao nae aliingia ndani na moja kwa moja kwenda chumbani kwa mke wake na kuongea nae,“Kesho, naomba uwaandae vijana wetu wote maana kuna mahali tunaenda halafu tutaenda kumpitia na Angel, na mama kwenda nae hiyo sehemu”“Ni wapi huko?”“Aaaah utajua tu mke wangu, ni surplise”Basi mama Angel hakuongea zaidi, aliwafata tu watoto na kuwaambia kuwa wajiandae kuna mahali wataenda siku ya kesho.Kulipokucha, kila mtu alijiandaa kama walivyoambiwa kisha safari ikafanyika ya kwenda kumfata Angel ila kwa bahati mbaya hawakumpata Angel maana alikuwa kaondoka na bibi yake, kuna mahali walienda basi mama Angel akamwambia mumewe,“Unaona sasa mambo yako ya kushtukiza, hatujawapata wala nini ni bora watu kuwaandaa kwanza”“Sawa, hakuna tatizo nitawapeleka wao siku nyingine”Kisha waliondoka pale na kuelekea kwenye safari yao.Moja kwa moja walifika kwenye kile kiwanda ambacho baba Angel alikuwa amejenga, na palikuwa pamepambwa sana na kumfanya mama Angel afurahi kwani ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kuwa yeye na mume wake siku moja wamiliki kiwanda chao, na akajua kuwa kiwanda kile ndio ufunguzi wa wao kuwa na viwanda mbalimbali.Basi baba Angel aliwatembeza kwenye kile kiwanda huku akiwaelekeza mambo mbalimbali, basi mama Angel akamwambia,“Ila umekosea sana kutokutushirikisha, unajua ungetushirikisha basi ingekuwa rahisi kwa ndugu zetu wote kuwepo mahali hapa”“Hakuna tatizo, kuna siku nitafanya sherehe mahali hapa, na ndugu wote nitawaalika”Basi mama Angel na familia nzima walifurahi na kukaa pamoja huku wakiongea mambo mbalimbali, muda huu baba Angel aliingia tena kiwandani ili kuelekezana kidogo na aliamua kumchukua Erick kwani kuna kitu aliwahi kuambiwa kuhusu Erick kwahiyo alitaka kusikia kwanza mawazo yake.Muda huu Erica alikuwa akizunguka maeneo ya nje ya kiwanda kile, huku mama yao akiwa amekaa na mtoto mara mama Angel alishangaa Erica kufika na mtu pale kwake huku akimwambia mama yake,“Mama mtu huyu nimekutana nae njiani, kaniuliza jina nikamwambia naitwa Erica, akasema anahitaji kumuona mama yangu ndio nimemleta”Mama Angel alikuwa kimya tu akimuangalia mtu huyu kwani mtu huyu alikuwa ni Rahim, yani baba mzazi wa Angel.Sia alikubali kumpeleka na aliweka vitu vyake vizuri kisha yeye na Dora waliondoka eneo lilena kwenda nyumbani kwa madam Oliva.Walifika pale na kugonga geti ambapo mlinzi wa nyumba ile alienda kufungua mlango, ila macho ya Dora na yule mlinzi yalipokutana kila mmoja alionekana kupata mshangao dhidi ya mwenzie.Waliangaliana kwa makini sana, ila mwisho wa siku Dora alijihisi vibaya kwani huyu mlinzi wa madam Oliva alikuwa ni mtoto wa James ambaye alizaa na msichana wa kazi, maana alimuuliza,“Unaitwa nani kijana?”“Naitwa James”“Imekuwaje hadi umekuwa mlinzi?”“Unajua mimi naishi na mjomba, sasa kila kitu namtegemea mjomba, nikaona ni vyema nitafute kazi ila Mungu mwema ndio nikapata kazi mahali hapa”Kwakweli Dora aliacha hadi kufikiria kilichompeleka mahali pale na kujikuta akimuangalia kwa makini sana huyu kijana kwani moyo ulikuwa ukimuuma sana, basi Sia alimuuliza,“Inamaana huyu ni James, mtoto wa James!”Dora aliitikia kwa kichwa tu kisha Sia akamwambia,“Mimi nilishawahi kukwambia haya, nadhani leo umenielewa ni kitu gani nilichokuwa nazungumzia, unaishi kwenye nyumba nzuri, una maisha mazuri, unafanya utakacho ila watoto wa huyo mtu wanaishije? Je wanalalamikaje kwa Mungu. Haya kama wamefikia hatua ya kuwa walinzi ni mara ngapi wamelalamika kwa Mungu, na wakati wewe unaouwezo wa kuwasaidia?”Basi Dora akamuangalia yule kijana na kumuandikia namba yake kwenye karatasi kisha akampatia na kumwambia,“Naomba utanitafuta”Halafu Dora akaondoka, ikabidi Sia nae aondoke zake maana aliyempeleka alikuwa ameondoka kwa muda huo.Dora alirudi nyumbani kwake na kujifikiria vitu vingi sana, kuna muda alihisi machozi yakimtoka na kusema,“Ingawa mwishoni James hakunifanyia vitu vizuri ila alikuwa akiniambia nikumbuke watoto wake, alikuwa akimtaja James, Junior na Jasca, kwanini nimekuwa mbinafsi kiasi hiki!! Kwani wokovu ndio unatufundisha hivi? Neno la Mungu ndio linafundisha hivi kudhurumu mali ya mtu! Si wanasema mtu mwenye dhuruma hatouona ufalme wa Mungu, eeeh Mungu naomba unisamehe”Basi akafikiria pale cha kufanya kwani aliona ni wazi anawajibu wa kuwasaidia watoto wale ili na wao waishi kama Jesca na watambuane maana ni mali za baba yao wote watatu.Wakati akifikiria hayo, simu yake ya mkononi ilianza kuita na alipoangalia aliona namba ngeni na kupokea na kuanza kuongea nayo,“Ni Sia anaongea hapa”“Eeeh Sia unasemaje?”“Unajua ni jambo gani lilitupeleka pale? Yani ulipomuona yule kijana umesahau kila kitu, mdogo wako karogwa wewe!”“Unajua naweza kukazana kumfatilia huyo aliyemroga mdogo wangu wakati mimi kuna dhambi nimefanya na ninazifumbia macho, acha kwanza nijisafishe na dhambi yangu hii”“Kheee haya, ila mimi nilikwambia ukanipuuzia. Kuna muda unaona unaishi kwa amani sana ila kuna mtu umedhuruma nafsi yake na kila siku analia kwaajili yako”“Kwaheri maana wewe nawe ukianza humalizi”Dora alikata ile simu huku akiendelea kutafakari mambo mbalimbali.Familia ya mama Angel, kwa muda huu wote walikuwa wakirudi nyumbani huku wakiongea mambo mbalimbali kwenye gari, ila njiani mama Angel alikuwa akiangalia nje na alimuona Derrick kasimama na mdada halafu Derrick akaondoka muda huo magari yalikuwa kwenye foleni kwahiyo mama Angel alikuwa akiona karibia kila kitu kilichoendelea, mara alimuona yule dada akilia hadi kukaa chini, ndipo alipomuomba mumewe asimamishe gari pembeni kwanza ili akaongee na yule mwanamke, na kweli magari yaliporuhusiwa baba Angel alisimamisha pembeni halafu mama Angel alishuka na kumfata yule mwanamke aliyeonekana amechanganyikiwa,“Vipi dada tatizo ni nini?”“Nimetapeliwa dada, yani kuna mbaba nilisimama nae hapa kumbe ni tapeli, kanitapeli kila kitu hadi hela ya nauli”“Yani kakutapeli kivipi?”“Yule kaka nimetoka nae mbali kidogo, kaniambia kuwa yeye huwa anawasaidia watu kuongeza kipato chao, basi aliniambia vitu vingi sana hadi tumefika hapa akaniambia nimpe mkoba wangu na simu yangu nami sijui vipi nikampatia ila alipoondoka ndio nimegundua kuwa nimetapeliwa hapa sijui hata nyumbani narudi vipi”“Duh pole sana”Kisha mama Angel akampa yule mdada elfu tano ili iweze kumsaidia kama nauli ya kurudi, basi alirudi kwenye gari ya mume wake na safari iliendelea.Usiku huu baba Angel aliona vyema kuuliza kuhusu mkewe kwenda kuongea na yule mwanamke, kuwa ni kitu gani kilimfanya aende kuongea na yule mwanamke, basi alimwambia tu kuwa yule mwanamke alikuwa katepeliwa ila hakusema kama tapeli mwenyewe ni Derrick kwani aliamini kuwa aliyemuona Derrick alikuwa ni yeye mwenyewe, basi alimulezea mumewe tu lile tukio la yule mwanamke, basi baba Angel akasema,“Ila tamaa ya kupata hela kwa haraka haraka ndio inayofanya wengi watapeliwe, ukianza kufatilia utaona wengi kweli walitamani hela za haraka. Ila mke wangu kuna tatizo lingine”“Lipi hilo”“Sikukwambia sijui, ila ni hivi Steve hajaenda ofisini kabisa, nilimpigia simu akapokea madam Oliva, kwahiyo Steve yupo kwa madam Oliva”“Kheee jamani huyu mwanamke ni nyoka, kwahiyo ndio alitaka akuweke wewe hivyo jamani!! Si ningekuwa chizi mimi loh!! Ila pale dukani itabidi tumpe mtu mwingine, la sivyo huyo Steve atahonga duka letu kwa huyo madam wake”“Mmmh sijui, ila tutafanya hivyo”Basi waliaongea ongea pale na kuamua tu kulala kwa muda huo.Angel kama kawaida alimuomba bibi yake simu na kuanza kuwasiliana na wale watu wake aliokuwa akiwasiliana nao sana, yani kitu pekee ambacho huwa kinamfanya kuomba simu kwa bibi yake ni kuwasiliana na Samir, na huwa akiipata hiyo simu anaanza kumtumia ujumbe Samir,“Samir”“Oooh niambie malaika wangu, unajua Angel nakupenda sana”“Jamani Samir unafanya nihisi hakuna mwanaume tena katika ulimwengu huu mwenye mapenzi kama wewe, ukimtoa baba yangu”“Ni kweli kwa waliobaki hakuna kweli, tumebaki wachache sana. Ila Angel siku za mbeleni huko tutaishi pamoja na kuwa mke na mume”“Nitafurahi sana Samir”“Vipi na shule bado hujatajiwa”“Sijatajiwa ila baba alisema kuwa naweza leo kwenda kufanya usahili”“Basi ukienda kuwa makini sana Angel ili unitajie hiyo shule maana nataka tusome pamoja ili niwe nakulinda kipenzi changu”“Mmmh Samir una vituko sana”Mara simu ya Angel ilianza kuita, alipoangalia ni Mussa aliyekuwa anapiga, ila kwavile alipenda zaidi kuwasiliana na Samir, kwahiyo hakupokea ile simu ya Mussa na kuendelea kuwasilina na Samir.Kesho yake mapema kabisa, baba Angel alijiandaa na kwenda ofisini kwake, kisha alienda kwenye ujenzi wake ambapo alitaka kufanya sherehe kidogo ya ufunguzi wa jingo lake hilo ila alitaka kumshtukiza tu mke wake kwahiyo hakutaka kumwambia ni kitu gani kitaendelea.Basi alipomaliza hapo, kuna mwalimu aliwasiliana nae kuhusu Angel kwenda kufanya usahili basi alipoondoka hapo alienda kumfata Angel ambaye alifanya ule usahili na kumrudisha nyumbani, ila wakati wa kurudi simu ya Angel ilianza kuita maana siku hiyo alisahau kumrudishia bibi yake, basi baba yake alisimamisha gari pembeni na kuanza kumuuliza Angel,“Nasikia simu inaita?”Angel hakuwa na jibu, basi baba yake akamwambia,“Hebu nipe hiyo simu niione”Angel hakuwa na namna zaidi ya kutoa ile simu ili baba yake aweze kuiona, basi baba Angel alichukua ile simu na kuiangalia kwakweli ilikuwa ni simu ya gharama sana, akamuuliza,“Hii simu umepewa na nani Angel?”“Samahani baba, nilipewa na babu”“Na babu? Babu yupi huyo?”“Nilimfahamu kwa bibi kule nilipokuwa, ndio akaniletea hii simu”Kwakweli baba Angel aliiangalia sana ile simu ila hakuongea jambo lingine lolote na kurudisha ile simu kwa Angel, kisha safari iliendelea ambapo alimfikisha Angel kwa bibi yake halafu yeye akarudi katika ujenzi wake ili kupanga na baadhi ya vijana kuwa mahali hapo atafanikisha vipi kwaajili ya sherehe yake fupi ya ufunguzi wa kiwanda chake, basi alipanga nao pale na kisha kuondoka zake kurudi nyumbani, kiukweli alikuwa amechoka sana siku hiyo kutokana na matembezi aliyokuwa nayo.Kulipokucha leo kabla baba Angek hajaondoka aliona ni vyema kwanza akiongea na mke wake, basi alianza kuongea nae pale kuhusu Angel,“Halafu mama Angel unajua mwanao anamiliki simu ya aina gani?”“Eeeh ya aina gani?”“Mwanao anamiliki simu ya gharama sana, niliwahi kuulizia zile simu wanauza milioni, mbili nimemuuliza tu nani kampatia ile simu kasema baba yake kule kwa bi I yake alipokuwa yani kwa mama yangu, kwakweli nimesikitika na kushindwa hata kuongea lolote”“Kheee na mama yangu nae kamuachia simu jamani wakati niliongea nae!”“Kuongea na mama hakusaidii kitu ila hapa naona cha muhimu ni wewe kuongea na Angel”“Niongee nae nini sasa?”“Yule ni mtoto wa kike na wewe ndio mama, tafuta siku na uongee na mtoto ukweli”“Unamaana nimuelezee kuhusu uhalisia wake”“Aaaah sijasema hivyo maana hayo ni maamuzi yako, ila ninachoongelea hapa ni ile hali ya mama kuongea na mtoto wake wa kike”“Unajua sikuelewi mume wangu, niongee nae kuhusu nini?”“Sikia nikwambie, kaa chini na Angel mueleze ukweli wote kuhusu mahusiano, najua umepitia changamoto nyingi pia kwahiyo unaweza kumueleza mtoto wako hata kwa kuto kusema ni wewe yani ukasema kuna rafiki yako yalimpata haya na haya na haya, mueleze ukweli mtoto ajue kuhusu mahusiano kwanza, hata ukimueleza ukweli kuhusu uhalisia wake na bila kumueleza ukweli kuhusu mahusiano basi atatembea na hao unaosema ndugu zake maana ataona ni kawaida, sasa kaa na echini mwambieukweli jinsi mahusinao yalivyo hata yakimtokea puani bado atakumbuka kuwa lakini mama alisema, kwani tukiendelea kumthibiti kuhusu simu bila kumwambia ukweli napo ni kazi bure, utamzuia na simu hii kuna jamaa atamnunulia simu nyingine. Angel ni bvinti mzuri tena mzuri sana ila akiharibikiwa basi ule uzuri wake hautoonekana kwani kila sehemu atakuwa akielezewa kuhusu sifa mbaya, mama Angel kaa chini na mtoto”“Nitajitahidi mume wangu, kwani sitaki mtoto aharibikiwe”“Maana naona kuna wanaume wameanza kuichanganya akili yake kiasi kwamba nahisi ana mawazo yupi ni yupi katika maisha yake, na ikiwa tukiona kuna mwanaume anamfatilia sana mtoto wetu basi hatuna budi kufatilia uhalisia wa huyo mwanaume ingawa ni ngumu sana kuchunga kila mwanaume anayemfatilia mtoto wetu. Ila mueleze mtoto ukweli ili aweze kujilinda na kujichunga”Mama Angel alimuelewa vyema kabisa mume wake, kwahiyo alikubaliana nae na kile alichokuwa akikisema na kusema kuwa atakitekeleza.Usiku wa leo, Vaileth bado aliamua kuwa mbali kabisa na Junior kwani kila akifikiria kuhusu laki tano ambayo Junior aliichukua kwake na kukumbuka aliyoyasikia kuwa alipeleka hela hiyo kwa mwanamke, alijikuta akiwa hana furaha tena na Junior kiasi cha kufanya amchukie sana, ila kabla hajalala alitumiwa ujumbe na Junior,“Vaileth mpenzi wangu, nifanye nini ili uweze kunielewa, sijui hata nikuelezeje ila mama yangu si mkweli”“Oooh mama yako si mkweli, kwahiyo mama yako kapanga na Samia au? Halafu usiniongezee hasira Junior”“Basi, ila niambie nifanye kitu gani kwasasa uweze kunisamehe”“Nirudishie laki tano yangu, sitaki maneno mengine”“Sawa hakuna tatizo, hiyo hela nitakupatia tu hakuna tatizo”Vaileth hata hakuendelea kuwasiliana nae zaidi ya kutafuta usingizi tu muda huo ila akapigiwa simu na ndugu yake Prisca na kuipokea,“Unajua nini Vai, natamani kuja kwenye hiyo nyumba kukuona ila naogopa na ninaona aibu”“Pole sana, kwa yale mambo lazima uone aibu”“Kwanza hongera sana, nasikia matusi uliyofanya kijijini huko”“Matusi gani tena?”“Si umerekebisha nyumba ya wazazi, nasikia wameweka bati na wamerekebisha kote yani nasikia pamependeza nyumbani kweli, halafu mjomba kawasaidia kuvuta umeme kwa ile hela”“Oooh swala zuri sana, kwahiyo nyumbani kuna umeme kwasasa?”“Ndio, unajua nguzo za umeme zilipita pale pale ila sababu ya pesa ndiomana hawakuvuta, halafu nyumba ya bati zilizooza na umeme wa kazi gani? Ila Vai umefanya kazi kubwa sana, hongera mdogo wangu umefanya jambo la akili. Ila ngoja nikuulize, zile pesa ndio mshahara au kitu gani? Na mimi natamani kupata kazi za ndani jamani, kwa miezi michache tu umeweza kufanya kitu cha namna ile nyumbani!! Oooh na mimi nitafute kazi za ndani sasa”“Sikia kwanza, ile pesa sio mshahara ila ile pesa nimepewa na wazazi hapa, nilipowaambia tu kuhusu nyumbani basi wakanipatia ile pesa, tena mama aliituma mwenyewe kwa mama nyumbani kupitia simu ya mjomba, tuliwasiliana nao na kutuma ile pesa, kwakweli hii familia wananipenda sana na wananilea sana, kwakweli nawapenda”“Haya, ila nasikia kule kijijini kuna mkaka mwalimu anafundisha shule ya jirani, toka kaambiwa kuhusu wewe basi anasema ukirudi tu anakuoa, kwahiyo jiandae na ndoa”“Jamani ndugu yangu, usinichekeshe mie, ngoja nilale halafu tutaongea vizuri siku nyingine unajua ni usiku huu!”“Najua ndio, ila huu ni muda mzuri wa kukupata hewani ila hakuna tatizo usiku mwema”Basi Vaileth alikata ile simu ila hakutaka kutilia maanani kuhusu huyo kijana mwalimu wala nini zaidi ya kufikiria mambo mengine na kulala tu.Leo baba Angel kabla ya kwenda ofisini, alipitia kwanza kwenye ujenzi wake kuangalia maandalizi ya ufunguzi yatakavyokuwa maana alishaongea nao, kwahiyo alienda tu kuangalia na kupanga zaidi,“Ila bosi, kukipambwa kidogo hapa nje basi shughuli itapendeza zaidi”“Kwahiyo kuna umuhimu wa kutafuta mpambaji?”“Ndio, kuna umuhimu wa kufanya hivyo”“Mimi sijuani sana na watu wengi, basi mtanitafutia mtu mnayeona anafaa na kumpa hii kazi”“Oooh kuna baba mmoja hivi anaitwa Babuu ni hatari kwa mapambo, yani akikupambia mahali lazima ubaki mdomo wazi”“Basi nitafutieni huyo Babuu na muelekezeni tunachotaka halafu mtaniambia gharama zake”“Sawa, hakuna tatizo juu ya hilo”“Nataka ile siku ikifika mimi na familia yangu yote tuwe hapa na nitaongea machache kidogo kwani hiki ni kiwanda changu cha kwanza kufungua na ninahitaji kifanye vizuri”“Usijali bosi, kwanza eneo umepata zuri na kubwa, lazima kiwanda kitafanya vizuri sana”Basi alikubaliana na huyu kijana na kutembelea tembelea baadhi ya vifaa alivyoviweka kwani kuna watu aliwaweka watengeneze bidhaa ambazo zitakuwepo siku ya ufunguzi na kufanya watu wafahamu bidhaa zake, basi alipomaliza aliondoka zake na kuelekea kazini kwake.Ila leo alipoingia ofisini tu kuna mgeni alikuja ofisini kwake, mgeni huyo alikuwa ni Sia, basi akamuuliza,“Kheee Sia, umefata nini kwani?”“Sijaja kwa nia mbaya ila nimekuja kukupa habari flani hivi”“Habari gani?”“Shemeji yako Derrick ni tapeli”“Kivipi?”“Ni hivi, Derrick ana michezo ya kitapeli na wengi sana kawatapeli na kuwaliza, mimi mwenyewe alitaka kunitapeli, nikamuangalia na kumuuliza Derrick mbona mimi nakufahamu vizuri sana, yani unataka kunitapeli kweli! Basi akaona aibu na kuondoka, kwakweli Derrick sio mtu mzuri kwasasa”“Duh!! Ila kwanini umekuja kuniambia hayo?”“Nimekuja kukwambia ili nyie mjue cha kufanya na huyu ndugu yenu, unajua utapeli sio sifa nzuri eeeh!! Tapeli hana tofauti na mwizi, ila tofauti yake ni kuwa yeye hapori bali unampa mwenyewe na mwizi anaphora ila tapeli ni kama mwizi tu kwani anakuumiza kimaisha na kisaikolojia, kwahiyo mnatakiwa mjue cha kufanya”“Sasa cha kufanya ni kipi hapo?”“Sikia nikwambia, kwasasa unaona hakuna cha kufanya ila hii ni sifa mbaya ambayo haitaishia kwa Derrick tu bali itasambaa hadi kwenye familia yenu, hebu angalia ulivyo na pesa na jina zuri mjini halafu Derrick anamtapeli mtu na kusikika kuwa yule ni shemeji wa Erick, unajua sio sifa nzuri kabisa hiyo. Hebu kuweni makini na ndugu yenu, yule Derrick ni msomi, na mpaka kawa vile lazima kuna kitu kimemfanya awe vile, msikubaliane na ile hali kabisa, nyie mnasali siku hizi na uzuri ni kuwa mnatambua jinsi gani nguvu za giza zinafanya kazi, mkomboeni ndugu yenu”“Kheee ulivyoongea kwa uchungu, sawa mama nimekuelewa”“Jamani, leo mbona nitalala huku nikitabasamu, Erick umeniita mama!! Asante sana”Baba Angel alicheka tu huku akitikisa kichwa, basi Sia aliinuka na kumuaga baba Angel huku akimwambia,“Naomba ufanyie kazi hilo nililokwambia, msimuache Derrick aendelee kupotea, ha[endi kuwa vile, msaidieni”Sia akaondoka zake, ila kuna muda kama aliona kuwa Sia anazungumza ukweli kuwa wanapaswa kumsaidia Derrick, ila kwavile siku ile alikuwa na mambo mengi ya ufunguzi wa kampuni yake ambao karibia unafanyika basi ndio kitu alichofikiria zaidi.Leo, mama Angel alikuwa amekaa sebleni na Erick wakiangalia Tv, kidogo ilikuwa ni tofauti kidogo kwani mara nyingi Erick sio mpenzi wa kuangalia Tv, basi kulikuwa na kipindi cha mahusiano na kuna mtu alipiga simu kuwa ameachwa na mpenzi wake, alipomaliza kuongea kwenye simu, wale watangazaji wakaanza kudadavua sasa ambapo mmoja akasema,“Jamani kuachw akunauma tena sana”Mwingine akadakia,“Ni kweli kunauma ila inatakiwa ifikie hatua watu waone kuachwa au kuachana ni kawaida tu, sasa mtu mmekutana kimjini mjini asikuache kwasababu gani? Akipata mpya anayefaa anakuacha tu, mtu mwenyewe mmekutana na meno yote mdomoni, asikuache umezaliwa nae tumbo moja huyo? Ni pacha wako hadi asikuache”Wale watangazaji walikuwa wakicheka sana huku wakiongea kwa furaha, basi Erick alimuangalia mama yake na kumuuliza,“Kwani kuna mahusiano ya kimapenzi kwa watu waliozaliwa tumbo moja au mapacha?”“Mmmh mahusiano ya kimapenzi? Haiwezekani maana ni ndugu”“Sasa hawa mbona wanasema kuwa mtu ambaye hujazaliwa na tumbo moja au mtu ambaye sio pacha wako ni lazima akuache, sasa kuna umuhimu gani wa kuwa na mahusiano”“Hujaelewa hapo mwanangu, ni hivi katika mahusiano kuacha na kuachwa ni kawaida kwani mtu anahitaji apate mtu wa kuridhika nae, anaweza kuona tabia ambazo hazifai kwake na akakuacha, ila ndugu kuachana ni ngumu, sio kimahuano ya kimapenzi bali kimahusiano ya kindugu, kuachana ni vigumu sana kwani ni ndugu wanajuana toka watoto na damu zao zimewaunganisha, kwa undugu wa mapacha ndio ngumu kabisa kuutenganisha. Ila kuna usemi usemao ndugu wakigombana chukua jembe ukalime kwahiyo mambo ya ndugu kidogo ni mambo ambayo yana gusa sana”“Kwahiyo mama ndugu hawawezi kuwa wapenzi”“Jamani Erick, uliona wapi ndugu wakawa wapenzi jamani! Kuna baadhi ya kabila tu ndio zinaruhusu mabinamu kuoana ila ndugu kuwa wapenzi ni kinyume kabisa”“Ila mama, ukisoma kwenye Biblia unaona kuwa mtu wa kwanza kuumbwa ni Adam halafu akafatia Eva, hiyo inamaanisha kuwa duniani wote ni ndugu hivi ni kweli ndugu hawaoani? Au Mungu aliumba watu wengine tofauti na hao kwanza?”“Kheee wewe mtoto usinitie kiungulia mie, mambo ya uumbaji nitayajulia wapi jamani, kwanza nenda kaoshe ile gari pale nje maana unaongea sababu huna kazi za kufanya kwasasa”Basi Erick aliinuka na kwenda kuosha gari ambalo mama yake alimwambia ila bado alikuwa na maswali yake ambayo mama yake hakuwa na majibu na hayo maswali.Wakati akiosha gari lile, alienda Erica kule ambapo kaka yake alikuwa akiosha gari, alimnyatia kwa nyuma na kumwagia maji na kufanya Erick ashtuke sana, kisha walianza kukimbizana na kusahau hata kile alichokuwa akifanya.Walikuwa wakikimbizana huku kila mmoja akipata maji anamvizia mwenzie na kummwagia, kitendo hiko kilifanya kummwagia maji baba yao ambae alikuwa ndio amerudi,“Nyie watoto vipi kwani?”“Samahani baba”‘Hebu njooni hapa”Erica na Erick walisogea kwa baba yao ambaye alianza kuongea nao,“Haya, huo mchezo wa kumwagiana maji mmeutoa wapi?”“Baba, nilikuwa naosha gari ila Erica akaja nyuma yangu na kunimwagia maji”“Eeeh Erica kwanini umefanya hivyo?”“Baba, zamani tulipokuwa watoto basi mimi na Erick tulikuwa tukicheza michezo mingi sana ila siku hizi huwa simuelewi Erick maana muda mwingi kama ananikwepa basi ndio nikaamua kuja kuanzisha mchezo wa kummwagia maji”Baba Angel alitikisa kichw akama kusikitika kidogo halafu akacheka na kusema,“Yani nyie watoto mnaakili mbovu sana, hebu cheki mlivyolowa chapachapa jamani. Haya Erick acha tabia ya kumkwepa mdogo wako, uwe unaongea nae na kucheza nae”Basi Erica akasema,“Tena ni vyema baba kama mimi na Erick tukisoma shule moja kama zamani”“Hilo tutaliongelea pia, Erick wewe ndio mlinzi wa dada yako na sio mtu wa kumkwepa. Haya nendeni mkabadilishe nguo”Basi waliingia ndani na baba yao nae aliingia ndani na moja kwa moja kwenda chumbani kwa mke wake na kuongea nae,“Kesho, naomba uwaandae vijana wetu wote maana kuna mahali tunaenda halafu tutaenda kumpitia na Angel, na mama kwenda nae hiyo sehemu”“Ni wapi huko?”“Aaaah utajua tu mke wangu, ni surplise”Basi mama Angel hakuongea zaidi, aliwafata tu watoto na kuwaambia kuwa wajiandae kuna mahali wataenda siku ya kesho.Kulipokucha, kila mtu alijiandaa kama walivyoambiwa kisha safari ikafanyika ya kwenda kumfata Angel ila kwa bahati mbaya hawakumpata Angel maana alikuwa kaondoka na bibi yake, kuna mahali walienda basi mama Angel akamwambia mumewe,“Unaona sasa mambo yako ya kushtukiza, hatujawapata wala nini ni bora watu kuwaandaa kwanza”“Sawa, hakuna tatizo nitawapeleka wao siku nyingine”Kisha waliondoka pale na kuelekea kwenye safari yao.Moja kwa moja walifika kwenye kile kiwanda ambacho baba Angel alikuwa amejenga, na palikuwa pamepambwa sana na kumfanya mama Angel afurahi kwani ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kuwa yeye na mume wake siku moja wamiliki kiwanda chao, na akajua kuwa kiwanda kile ndio ufunguzi wa wao kuwa na viwanda mbalimbali.Basi baba Angel aliwatembeza kwenye kile kiwanda huku akiwaelekeza mambo mbalimbali, basi mama Angel akamwambia,“Ila umekosea sana kutokutushirikisha, unajua ungetushirikisha basi ingekuwa rahisi kwa ndugu zetu wote kuwepo mahali hapa”“Hakuna tatizo, kuna siku nitafanya sherehe mahali hapa, na ndugu wote nitawaalika”Basi mama Angel na familia nzima walifurahi na kukaa pamoja huku wakiongea mambo mbalimbali, muda huu baba Angel aliingia tena kiwandani ili kuelekezana kidogo na aliamua kumchukua Erick kwani kuna kitu aliwahi kuambiwa kuhusu Erick kwahiyo alitaka kusikia kwanza mawazo yake.Muda huu Erica alikuwa akizunguka maeneo ya nje ya kiwanda kile, huku mama yao akiwa amekaa na mtoto mara mama Angel alishangaa Erica kufika na mtu pale kwake huku akimwambia mama yake,“Mama mtu huyu nimekutana nae njiani, kaniuliza jina nikamwambia naitwa Erica, akasema anahitaji kumuona mama yangu ndio nimemleta”Mama Angel alikuwa kimya tu akimuangalia mtu huyu kwani mtu huyu alikuwa ni Rahim, yani baba mzazi wa Angel. Muda huu Erica alikuwa akizunguka maeneo ya nje ya kiwanda kile, huku mama yao akiwa amekaa na mtoto mara mama Angel alishangaa Erica kufika na mtu pale kwake huku akimwambia mama yake,“Mama mtu huyu nimekutana nae njiani, kaniuliza jina nikamwambia naitwa Erica, akasema anahitaji kumuona mama yangu ndio nimemleta”Mama Angel alikuwa kimya tu akimuangalia mtu huyu kwani mtu huyu alikuwa ni Rahim, yani baba mzazi wa Angel.Kwanza kabisa mama Angel alijikuta akikosa ujasiri kabisa, kisha akamwambia Erica aende mbali ili yeye aweze kumwambia yule mwanaume aondoke, ila Erica akasita na kumwambia mama yake,“Mama, kuna kitu nataka nikwambie”“Uniambie nini? Ondoka nimekwambia ondoka upesi”Mama Angel aliongea kwa ukali na kufanya mtoto wake aondoke kwa unyonge sana kwani hata alichokuwa anataka kusema kwa mama yake hakuweza kusema tena, kisha Rahim akamwambia mama Angel,“Mtoto hafai kufanyiwa ukali namna hiyo, hebu angalia ulivyomfananisha sura na alivyoondoka kwa unyonge, hivi roho haikusuti kumfokea hivyo!!”“Na wewe ondoka, mambo ya familia yangu hayakuhusu”“Yananihusu maana hata mimi ni baba yao pia”“Mjinga wewe, hebu ondoka zako huko”Rahim hakuondoka ila alivuta kiti na kukaa karibu na mama Angel kisha akasema,“Nilimuangalia sana huyu mtoto kafanana na wewe jamani, yani kafanana na wewe sana. Nikajikuta nikimuuliza jina lake, aliponiambia Erica moyo wangu ulidunda na kumuuliza mama yako yuko wapi akasema yupo mahali hapa, nikamuomba anilete kwa mama yake”“Naomba uende Rahim”“Niende kivipi Erica, kwani mimi nina ugomvi na wewe jamani!! Inakuwaje utake kunifukuza hivyo!!”“Naomba tu uende, sina matatizo na wewe. Kwanza hapa nipo na familia yangu”“Una hofu na Erick, kwani Erick hanifahamu? Angekuwa hanifahamu ni vizuri sana ila ananifahamu kwa uzuri tu, sasa nakushangaa wewe Erica kutaka kuwa na hasira kiasi hiko jamani. Huna sababu ya kunichukia wala sababu ya kunifukuza, mtoto wangu Angel yuko wapi nimemkumbuka sana, natumai kakua sana”“Sahau kama kuna mtoto ulizaa na mimi”“Kwamaana hiyo Angel alikufa!!”“Kheee usinichulie Rahim, naomba uniache na watoto wangu kwa amani”“Oooh nilijua Angel amekufa, ngoja nikwambie jambo ambalo sikuwahi kukwambia na wala hukuwahi kulijua nadhani, ingawa mimi nina watoto wengi sana kwasasa, ila mtoto pekee aliyekaa katika akili yangu ni Angel unajua kwanini?”Mama Angel alikaa kimya tu, basi Rahim aliendelea kuongea,“Unajua mwanaume unaweza ukawa na wanawake wengi sana ila katika maisha yako kuna mwanamke unaona kabisa kagusa maisha yako, basi katika maisha yangu si wake niliooa na kuacha, si wanawake nilioishi nao ila bado huwa nakufikiria wewe kwani uliyagusa maisha yangu Erica, ulikuwa ni mwanamke ambaye ulifaa kuwa na mimi nadhani ningekuwa nawe kwasasa ningekuwa zaidi ya hapa, na wala pengine nisingezaa hovyo kama hivi.Erica, nina kila sababu ya kumfikiria Angel na kumpenda Angel sababu nilimpenda mama yake ambaye ndio wewe. Erica wewe ni mwanamke wa tofauti sana, umeumbiwa upendo tena upendo wa dhati, kwakweli huwa siachi kukufikiria katika maisha yangu….”“Naomba unyamaze Rahim, sitaki kukusikia unachotaka kuongea, naomba uende”“Hivi unafikiri namuogopa Erick? Kwani hajui ni jinsi gani nakupenda? Anajua vizuri sana, naelewa ni kwanini kakung’ang’ania hadi leo hataki kukuacha, una mapungufu yako ila wewe una sifa bora za mwanamke ambazo mtu yoyote atapenda mkewe awe hivi, kwanza wewe ni mzuri kiasi kwamba hata kukutambulisha kwa watu kuwa huyu ni mke wangu unaonekana umefanya jambo la maana, wewe ni mtafutaji, una upendo, una huruma, unajali, huchepuki, ukiwa na mwanaume unampenda kweli. Aliyenivuruga hadi nikaachana na wewe namlaani hadi kesho ni yule mwanamke waliyenitafutia kuoa ndio chanzo yule, ila mimi nakupenda Erica hadi kesho na imani yangu inaniambia kuwa ipo siku mimi na wewe tutaungana na kuwa kitu kimoja, tutaishi pamoja tukilea mtoto wetu katika maadili mema”Mama Angel alikuwa na hasira akasimama ili aondoke, ila mumewe muda huo huo akasogea eneo lile ila na yeye alipomuona Rahim alijikuta akichukia sana kiasi kwamba hata hakumsalimia zaidi ya kumwambia mke wake aende kwenye gari na aliwafata watoto wake nao kuingia kwenye gari kisha alimwambia Erick awapeleke nyumbani ambapo alifanya hivyo kwahiyo alibaki yeye tu na watu pale kiwandani hakutaka watoto wake wahisi kitu chochote kile.Baba Angel alipomaliza ndipo alipomfata Rahim na kumtaka kuondoka,“Naomba uondoke sehemu yangu”“Kwakweli Erick unasikitisha sana, mwanaume gani wewe ambaye muda wote una mashaka na mkeo? Kumbuka huyo unayemuona mkeo nimezaa nae mimi”“Hiyo ya kuzaa nae sio sababu Rahim, sikia nikwambie unajua mimi nilikuwa nawe vizuri tu na nikakwambia uwe unakuja kwangu kwaajili ya wewe kucheza na mtoto ili akuzoee halafu ukataka kufanya nini nyumbani kwangu?”“Najua nilitaka kufanya makosa, ila Erick wewe ni mwanaume una wasiwasi gani lakini? Unampenda Erica na anakupenda, unajua hawezi kushawishika kijinga, tatizo lako ni nini lakini?”“Unajua wewe akili yako naona imeliwa na hivyo virusi vya ukimwi kichwani!”“Nani kakwambia kuwa mimi nina virusi, unajua usiongee kitu ambacho huna ushahidi nacho. Kwani virusi ni kitu gani katika maisha, watu wanaishi navyo na wanadundika tu hapa tunayemuongelea ni Erica. Hebu sikia Erick, wewe ulikuwa rafiki yangu na matendo yetu yaliendana kwa asilimia mia moja, kwahiyo kubadilika kwako kwasasa hakukubadilishi wewe unabaki kuwa Erick siku zote, ni kweli umemuoa Erica, mmelea mtoto wangu, umezaa nae watoto wengine, ila tambua kuwa hata mimi bado nampenda Erica, ungeelewa hilo basi ungekaa na mimi na kunishauri kisaikolojia na sio kunikwepesha na familia yako”“Hivi utake kumbaka mke wangu halafu nikuache karibu na familia yangu nina wazimu au ni kitu gani! Kwanza Rahim naomba uende”“Yuko wapi mwanangu Angel?”“Laiti kama nikikaa na huyo Angel nikamueleza yale maovu yako basi hatokaa kukutaka uwe baba yake kamwe, hivi si wewe mwenyewe uliyesema Angel angekuwa sio mtoto wako basi ungemtamani kimapenzi kisa ni mzuri sana, hivi Rahim kwanini hukui jamani!! Kwasasa wewe ni baba tena una watoto lukuki, hivi nikae chini na kumueleza Angel maovu yako moja mbili tatu atakutamani wewe uwe baba yake!!”“Nadhani hukunielewa, kwani nilivyosema vile ndio nilimaanisha kuwa namtamani, hivi naweza kutembea na mtoto wangu mimi!! Sio mtoto wangu tu, hivi hata mtoto wa rafiki yangu na jamii yangu naweza tembea nae wakati na mimi nina watoto wadogo! Mambo mengine uwe unayatafakari kwanza, sawa tuseme nilisema hivyo, au hata ningembaka mtoto wangu mwenyewe je hilo lingebadilisha chochote kuwa mimi ndiye baba yake mzazi? Na siwezi kufanya hivyo mimi, Erick una watoto wako sasa, nahitaji mtoto wangu hilo tu basi”“Naomba uende”“Naenda ila weka akilini kuwa nahitaji mtoto wangu, siku nikiamua kutumia nguvu basi familia yako nzima nitaitikisa”halafu Rahim akaondoka zake, kiukweli baba Angel hakuwa na furaha kabisa na moyo wake uliingia simanzi gafla na muda huo huo akaacha tu maagizo kwa mtu halafu yeye akaondoka zake.Siku hii baba Angel aliamua kuita bodaboda na kuondoka nayo kuelekea nyumbani kwake, alipofika tu alioga na moja kwa moja kujilaza, hakuongea kitu chochote na mkewe na kumfanya hata mama Angel kujihisi vinaya maana lile tukio la kufatwa na Rahim hakulipenda pia, basi alikaa karibu na mumewe pale alipokuwa amelala na kufikiria mambo kadhaa ambayo aliwahi kufanyiwa nyuma na Rahim,“Alinidanganya ananipenda, nikampa moyo wangu nami nikampenda, nikampa mapenzi yangu, nikapata mimba yake na akakubali kila kitu kuwa atanitunz na kunihudumia na kuahidi kunioa, nilijificha na mimba ile maana alisema nitakuja nitakuja ila hakutokea, baadae nyumbani wakajua, nikabahatika kujifungua na ahadi yake kwangu iliendelea nitakuja ila hakuonekana, akanipa sharti gumu ambalo sikuwahi kufikiria kuwa kuna siku ataniambia vile maana tulikubaliana kuoana hata bomani sababu ya utofauti wa dini zetu, akaniambia nibadili dini, nikamfikiria mwanangu, nikafikiria aibu niipataye kwa kuzaa nje ya ndoa, nikafikiria jinsi ninavyojificha ili ndugu wasijue, nikaona ni bora nikubali ili anioe niepukane na aibu, nikakubali na kumwambia kuwa nipo tayari kubadili dini unioe ili tuishi na kulea mtoto ila alinibadilikia, ndio kwanza hakutaka tena mawasiliano na mimi, hakutaka tena kumuhudumia mtoto hakutaka tena kusikia chochote kuhusu mimi, maisha yakawa magumu sana kwa upande wangu maana kila mahali nanyooshewa kidole, nimemaliza chuo na zawadi ya mtoto, nikashindwa kwenda kutafuta kazi maana mtoto alikuwa bado mdogo na mimi sina mbela wala nyuma yani sikuwa na msingi wowote wa maisha, niliona dunia inanicheka, niliona dunia inanitenga, niliwaza kwanini nastahili adhabu hii wakati hakuna baya nililowahi kuliwaza kwa huyu mwanaume, anizalishe na bado anidhalilishe na kunifanya nioenekane sina thamani yoyote katika maisha, muda wote macho yangu yalijaa machozi, nilimshika mwanangu na kulia nae sana, kuna muda nilijiona kuwa mimi ni mwanamke mpumbavu sana kwa kumuamini mwanaume, ila alinionyesha mapenzi na nikaamini kuwa ananipenda. Katika kukata kwangu tamaa, alirudi kwangu Erick na sasa alirudi akiwa mpya kabisa na kunipa mapenzi yote na kuchukua jukumu la ubaba kwa mtoto wangu Angel, ananipenda na anampenda mtoto wangu ila bado aliona kuna umuhimu wa Angel kumtambua baba yake halisi, ni kitu gani tena Rahim alitaka kunitenda kwenye nyumba ya mume wangu?? Na bado aliweka na vitisho kuwa kama atashindwa kwangu basi atafanya kwa mwanangu, ambaye ni mtoto wake mwenyewe, Rahim kawa ni mwanaume wa ajabu sana katika maisha yangu. Najuta kumfahamu, sijui ni kwanini nilikutana nae. Moyo wangu unajawa na machozi tena, ameivunja furaha ya mume wangu ambaye ananipenda sana, nitakuwa mgeni wa nani mimi, sijapanga haya katika maisha yangu ila sijui kwanini yananifata jamani!!”Alikuwa akilia huku akiongea hayo, na muda huu alilia hadi mumewe alisikia na kumfanya baba Angel aamke na kukaa na mkewe kisha alimkumbatia na kumwambia,“Usijali mke wangu, mimi na wewe tunapendana na hilo ndio la msingi kwetu, watoto ni ziada yetu ili kukamilisha furaha ya nyumba yetu. Usijali mke wangu, hata mimi nafikiria vingi pia, usidhani nimechukia kwani siwezi kuchukia sababu ya hili ila tu sijafurahishwa nalo ila Mungu ni mwaminifu atatusaidia na kujua ni jinsi gani tutaweza kushinda na kuvuka hapa tulipo”Basi alikumbatiana pale na mume wake na kuona kidogo moyo wake ukirudisha tabasamu na furaha basi mumewe akamuomba kuwa apumzike kidogo naye alifanya hivyo.Kulipokucha, wakati baba Angel akijiandaa kwenda ofisini akapata ukumbe kutoka kwa madam Oliva,“Kuna jambo nahitaji ushauri kutoka kwako”Baba Angel alishangaa tu ila hakujibu kitu kwenye ule ujumbe bali alimaliza kujiandaa kisha kumuaga mkewe pale na kwenda kazini.Mama Angel alibaki nyumbani na familia yake, ila muda kidogo Erica alienda kukaa na mama yake na kumuuliza mama yake,“Kwani mama, yule baba wa jana ni nani?”“Aaaah ya jana si yalishapita mwanangu, sidhani kama ni vyema kuyazungumzia”“Yalipita ndio, ila sikuelewa mama hebu ona jinsi tulivyorudi nyumbani inaonyesha hata haikupangwa iwe vile, baba karudi badae na pikipiki, sijaelewa vitu vingi vya jana. Halafu yule baba alivyokuwa akiongea na mimi mmmh!”Mama Angel alishtuka kidogo na kumuuliza,“Aliongea nini na wewe?”“Kwanza, aliponiona alishtuka halafu akaniita, akaniambia unafanana sana na mwanamke mmoja ambaye nampenda sana, nikamshangaa”“Mmmh! Akasemaje tena?”“Ndio akasema unaitwa nani, nikamwambia naitwa Erica, akasema mimi ni mzuri sana, halafu akauliza mama yako yuko wapi, nikasema ulipo ndio akasema nimlete ulipo. Ni nani yule mama?”“Mmmh Erica, achana na hizo habari ila ukikutana tena na yule mtu akikuita usiende tafadhari”“Halafu mama, nisamehe jana sikukwambia alinipa na hii hapa hela”“Kheee alikupa na hela? Wewe ulianza kuongea nae muda gani na alikuwa hela ya nini?”“Aliniambia kuwa mimi ni mzuri sana, ananipongeza kwa kuzaliwa mzuri ndio akanipa na hii hela”“Mbona hukusema?”“Niliogopa mama kukwambia pale wakati ulishaniambia niondoke”Kisha Erica akatoa zile pesa na kumfanya mama yake ashangae sana kwani zilikuwa ni nyingi tu, akachukua zile pesa kwa mwanae na kwenda chumbani kwake bila kuongea kingine na mtoto wake, hata Erica alibaki sebleni akishangaa tu.Mama Angel aliingia chumbani huku machozi yakimtoka, akakumbuka mara ya kwanza kutekwa akili yake na Rahim ilikuwa ni katika pesa, yani Rahim alikuwa ni mwanaume ambaye alimpa sana pesa, kwahiyo alipoona Rahim kumbe kampa mwanae pesa, aliumia sana moyoni mwake na kujisemea,“Hivi Rahim ana nini lakini jamani, kwanini ampatie mwanangu pesa? Tena pesa nyingi namna hii jamani!!”Mama Angel aliihesabu hela ile aliona kuwa ilikuwa ni laki mbili halafu kwenye zile hela kulikuwa na kadi yenye namba za simu za Rahim,“Sasa kamuwekea namba huyu mtoto wangu ili amtafute au nini jamani? Mbona kuna wanaume wana laana jamani loh!!”Kwakweli mama Angel alisikitika sana kwa alichokifanya Rahim.Baba Angel akiwa ofisini kwake akiendelea na kazi zake za hapa na pale, mara alifika madam Oliva ila kiukweli baba Angel kwa kipindi hiki alikuwa akimuogopa sana madam Oliva maana hakumuamini tena, ila alimkaribisha tu na kuongea nae,“Jamani baba Erick, kama unanikwepa vile, hebu sahau yote yaliyopita”“Haya, niambie”“Ningependa tupate mahali tuzungumze maana kuongelea ofisini swala hili kidogo sio vizuri, naomba chagua mahali gani ambapo patatufaa ili tuzungumze, sina nia mbaya na wewe baba Erick, usinifikirie vibaya tena. Ni wapi sasa tutakaa na kuzungumza”“Basi nitakwambia”“Mmmh jamani, hukawii kusema kuwa umesahau wewe”“Hapana, sisahau wala nini au utanikumbusha muda nikiwa natoka kazini. Leo nitatoka kwenye saa kumi”“Sawa nitakukumbusha basi”Kisha madam Oliva akaondoka zake, na baba Angel akaendelea na shughuli zake zingine.Muda wa kutoka ni kweli madam Oliva alimkumbusha tena, basi akamwambia mahali pa kukutaniana ambapo kweli alivyotoka ofisini alienda mahali hapo na kukutana na madam Oliva kisha kuanza kuongea,“Haya, niambie ni kitu gani ulikuwa unataka kunieleza?”“Kwanza kabisa, ni kweli nilikuwa nakutaka yani nisikatae, mimi ni mtu mmoja ambaye huwa napenda kusimamia ukweli hata kama ukichukia au vipi ila ni vyema nimeongea ukweli. Sababu ya kukutaka unajua ni nini?”“Eeeh ni nini?”“Nilikuwa naona fahari sana ukimsifia mke wako mbele yangu, yani wewe ni mwanaume unayejiamini na ni wanaume wachache sana wenye uwezo wa kufanya hivyo, kingine ni yule mwanamke Sia, yani jinsi alikuwa anakuhitaji ndio kitu pekee kilichofanya nikutake pia ili na mimi nipate hicho ambacho wanawake wenzangu wanang’ang’ania kutoka kwako. Na nimetumia madawa mengi sana kukupata ila imeshindikana, kiukweli nguvu iliyokuwepo kati yako na mke wako ni kubwa sana. Kitu kingine mimi nilikuwa simjui Steve wala sikuwa namfatilia habari zake kumbe ni rafiki yangu wa facebook kwa miaka mingi sana na siku zote huwa ananitumia ujumbe lakini simjibu sababu mimi nilikuwa naangalia maisha yangu tu. Kumbe huyu Steve alikuwa akinipenda kwa muda mrefu sana ila hakujua ni jinsi gani anaweza kunipata, kwa kupitia vile viatu ambavyo nilikutegeshea wewe basi Steve akaanza kuhaha kunitafuta, na sasa mimi na yeye tupo pamoja. Naweza sema ni nguvu ya dawa imetumika ila na nguvu ya mapenzi imetumika pia, sababu kwanini vile viatu asingevaa mtu mwingine zaidi ya Steve?”Baba Angel alicheka kwanza kwani akiifikiria historia ya Steve hakudhani kama kuna nguvu ya mapenzi hapo, kwani Steve alishawahi kula tunda ambalo Sia aliliweka dawa ili apendwe na yeye ila akala Steve na Steve kuanza kuishi na Sia, kwahiyo yeye aliona ni mauzauza ya Steve tu, madam Oliva akamuuliza,“Mbona unacheka?”“Hapana, nafurahia tu mapenzi yako na Steve”“Sasa ushauri niliokuita kukuomba ni huu, nahitaji kufunga ndoa na Steve, nahitaji wewe na mke wako ndio muwe wasimamizi wetu”Baba Angel akashtuka kwanza na kumwambia madam Oliva,“Swala la nyie kufunga ndoa ni jema, ila swala la mimi na mke wangu kuwa wasimamizi wenu naomba unisamehe tu kwa hilo maana halitawezekana”Madam Oliva alijaribu kumshawishi pale baba Angel ila alikataa kabisa kwa wao kuwasimamia ndoa yao.Mama Angel akiwa chumbani kwake muda huu huku akipanga namna ya kumueleza mumewe kuhusu Erica kupewa hizo pesa, alishangaa tu kupokea simu kutoka namba ngeni akaanza kuongea nayo,“Mimi ni Sia, usinikatie simu ni jambo nataka kuongea na wewe”“Jambo gani hilo?”“Mumeo, muda huu yupo hotelini na madam Oliva, kuwa makini sana la sivyo unampoteza. Ni kheri umpoteze kwangu kuliko kwenye mikono ya mamba ya yule mwanamke”Kisha Sia akakata simu, kwakweli mama Angel kama akili yake ikagoma hivi kwani hakujua ni kwanini mumewe aweze kwenda hotelini na Oliva baada ya kujua mambo mengi sana kuhusu madam Oliva, kisha akaamua kumpigia mumewe simu kwa muda huo, na mumewe alipokea,“Upo wapi baba?”“Samahani mke wangu sikukwambia, kuna hoteli hapa nimepita mara moja”“Umepita kufanya nini? Nakuomba nyumbani mume wangu”“Sawa, narudi muda sio mrefu. Nakupenda sana mke wangu”Basi mama Angel alikata ile simu huku akitafakari mambo kadhaa.Muda huu Erick alikuwa amekaa kwenye bustani basi Erica alienda kuongea nae na kumwambia kuhusu mbaba aliyempatia pesa,“Yule baba wa jana mliyemuona amekaa pale na mama, alinipa hela jana laki mbili pamoja na kadi yenye namba zake za simu”“Kheee ili iweje? Viko wapi hivyo vitu?”“Nimempa mama leo, unajua nilishangaa sana alivyonipa”“Alisema anakupa ili iweje?”“Kwanza alinisifia huyo balaa, akasema kuwa mimi ni mzuri sana, akasema nina sura nzuri ya upole, na macho ya kuvutia kisha akanipa hela ya kusema kuwa ni hela ya kunipongeza kwa uzuri niliokuwa nao”“Hao ndio wababa wasiofaa, ndio mafataki hao mdogo wangu ila nakupongeza swala moja la kwenda kumkabidhi hiyo hela mama, nakupongeza sana na siku nyingine mtu kama huyo akikupa hela kata kabisa”“Sawa sawa, halafu baba alisema usiwe unanitenga jamani Erick!!”“Sikutengi na nitaongea na baba ili tusome pamoja kama zamani, najua baba atanielewa tu”“Oooh hapo nimefurahi sasa, ila kama baba alisita siku ile”“Sikumsisitiza tu, ila subiri nimwambie vizuri basi baba atakuleta tu shuleni kwetu”Hili swala Erica alionekana kulifurahia sana.Baba Angel alifika nyumbani, ila wakati anaongea na mama Angel wala hakumuuliza sababu ya kupitia hotelini ila alimweleza tu vile ambavyo Erica amepewa hela na Rahim, kwakweli baba Angel alisikitika sana na kusema,“Katika watu wapuuzi namba moja duniani basi ni Rahim, sijui lini akili yake itakaa vizuri na kuwaza kutenda matendo mema. Hebu ona mimi naishi vizuri na Angel nampenda na kumuhudumia, ila yeye bila aibu ameanza swala la kumuhonga mwanangu kweli!! Hebu naomba hiyo kadi yake nimuulize vizuri alipo ili nikaongee nae, sitaki ujinga kwa watoto wangu”Basi baba Angel alichukua ile kadi na kuwasiliana na Rahim ambaye alimtajia alipo na muda huo huo baba Angel aliamua kuondoka nyumbani kwake ila hakupanda gari bali alikodi pikipiki tu na kuondoka nayo, hata mama Angel aliona ni vyema asingemwambia mume wake kwani alimuona hasira aliyokuwa nayo baada ya kuambiwa hayo.Alifika mahali alipo Rahim, na kumkuta akicheka tu na kutikisa kichwa,“Hivi Rahim jamani mbona una akili mbovu wewe!! Kwahiyo umeona vyema kabisa kumuhonga binti yangu na kumpa namba zako za simu?”“Kwani tatizo liko wapi Erick? Nimempa binti yako pesa, laki mbili tu? Nimempa na namba zangu za simu ili niwe nawasiliana nae hata mara moja moja, wewe je? Unamuhonga binti yangu kila siku zaidi ya kila kitu maana nasikia hadi kuna baadhi ya biashara zako zinasimama kwa jina la binti yangu, na kila siku unampigia simu binti yangu, kati ya mimi na wewe nani mwenye nia mbaya na mtoto wa mwenzie”“Hivi una akili kweli wewe!!”“Nina akili ndiomana nafanya haya”“Sitaki uwe karibu na binti yangu, tena hata Angel sitaki uwe karibu nae”Rahim akacheka na kusema,“Unajua Erick utawadanganya wengine tu ambao hawakujui vizuri ila sio mimi ninayekujua ndani na nje, utamdanganya huyo huyo Erica wako ndani, unajua kabisa Angel sio mwanao ila unajifanya unampenda kufa, hadi mali zako umemuandikisha, lengo lako ni nini? Nikikwambia unatembea na Angel utawezaje kukataa wewe?”Kiukweli baba Angel alichukia zaidi na kujikuta akishindwa hata kumjibu na zile hela hakumrudishia na muda huo huo akaondoka huku Rahim akiwa anacheka sana.Baba Angel alienda moja kwa moja stendi na kupanda kwenye daladala huku akiwa na mawazo sana. Alikuwa akiwaza moyoni mwake,“Hivi wanaume wote wanaolea watoto ambao sio wao huwa wanapatwa na adhma hii ambayo naipata mimi? Kwanini inakuwa hivi lakini, kila nikutanapo na huyu mtu kwasasa ni kuichosha tu akili yangu”Alikuwa akiwaza hadi alijikuta akisema,“Dah!!”Kwa sauti ambayo jirani yake aliisikia, basi yule jirani yake alimsalimia,“Habari baba”Alitazamana na yule jirani yake ambaye alikuwa ni mwanamke, na kubaki wakishangaana kwa muda, kwani ni mtu ambaye walikuwa wakifahamiana.Muda huu Erica alikuwa akizunguka maeneo ya nje ya kiwanda kile, huku mama yao akiwa amekaa na mtoto mara mama Angel alishangaa Erica kufika na mtu pale kwake huku akimwambia mama yake,“Mama mtu huyu nimekutana nae njiani, kaniuliza jina nikamwambia naitwa Erica, akasema anahitaji kumuona mama yangu ndio nimemleta”Mama Angel alikuwa kimya tu akimuangalia mtu huyu kwani mtu huyu alikuwa ni Rahim, yani baba mzazi wa Angel.Kwanza kabisa mama Angel alijikuta akikosa ujasiri kabisa, kisha akamwambia Erica aende mbali ili yeye aweze kumwambia yule mwanaume aondoke, ila Erica akasita na kumwambia mama yake,“Mama, kuna kitu nataka nikwambie”“Uniambie nini? Ondoka nimekwambia ondoka upesi”Mama Angel aliongea kwa ukali na kufanya mtoto wake aondoke kwa unyonge sana kwani hata alichokuwa anataka kusema kwa mama yake hakuweza kusema tena, kisha Rahim akamwambia mama Angel,“Mtoto hafai kufanyiwa ukali namna hiyo, hebu angalia ulivyomfananisha sura na alivyoondoka kwa unyonge, hivi roho haikusuti kumfokea hivyo!!”“Na wewe ondoka, mambo ya familia yangu hayakuhusu”“Yananihusu maana hata mimi ni baba yao pia”“Mjinga wewe, hebu ondoka zako huko”Rahim hakuondoka ila alivuta kiti na kukaa karibu na mama Angel kisha akasema,“Nilimuangalia sana huyu mtoto kafanana na wewe jamani, yani kafanana na wewe sana. Nikajikuta nikimuuliza jina lake, aliponiambia Erica moyo wangu ulidunda na kumuuliza mama yako yuko wapi akasema yupo mahali hapa, nikamuomba anilete kwa mama yake”“Naomba uende Rahim”“Niende kivipi Erica, kwani mimi nina ugomvi na wewe jamani!! Inakuwaje utake kunifukuza hivyo!!”“Naomba tu uende, sina matatizo na wewe. Kwanza hapa nipo na familia yangu”“Una hofu na Erick, kwani Erick hanifahamu? Angekuwa hanifahamu ni vizuri sana ila ananifahamu kwa uzuri tu, sasa nakushangaa wewe Erica kutaka kuwa na hasira kiasi hiko jamani. Huna sababu ya kunichukia wala sababu ya kunifukuza, mtoto wangu Angel yuko wapi nimemkumbuka sana, natumai kakua sana”“Sahau kama kuna mtoto ulizaa na mimi”“Kwamaana hiyo Angel alikufa!!”“Kheee usinichulie Rahim, naomba uniache na watoto wangu kwa amani”“Oooh nilijua Angel amekufa, ngoja nikwambie jambo ambalo sikuwahi kukwambia na wala hukuwahi kulijua nadhani, ingawa mimi nina watoto wengi sana kwasasa, ila mtoto pekee aliyekaa katika akili yangu ni Angel unajua kwanini?”Mama Angel alikaa kimya tu, basi Rahim aliendelea kuongea,“Unajua mwanaume unaweza ukawa na wanawake wengi sana ila katika maisha yako kuna mwanamke unaona kabisa kagusa maisha yako, basi katika maisha yangu si wake niliooa na kuacha, si wanawake nilioishi nao ila bado huwa nakufikiria wewe kwani uliyagusa maisha yangu Erica, ulikuwa ni mwanamke ambaye ulifaa kuwa na mimi nadhani ningekuwa nawe kwasasa ningekuwa zaidi ya hapa, na wala pengine nisingezaa hovyo kama hivi.Erica, nina kila sababu ya kumfikiria Angel na kumpenda Angel sababu nilimpenda mama yake ambaye ndio wewe. Erica wewe ni mwanamke wa tofauti sana, umeumbiwa upendo tena upendo wa dhati, kwakweli huwa siachi kukufikiria katika maisha yangu….”“Naomba unyamaze Rahim, sitaki kukusikia unachotaka kuongea, naomba uende”“Hivi unafikiri namuogopa Erick? Kwani hajui ni jinsi gani nakupenda? Anajua vizuri sana, naelewa ni kwanini kakung’ang’ania hadi leo hataki kukuacha, una mapungufu yako ila wewe una sifa bora za mwanamke ambazo mtu yoyote atapenda mkewe awe hivi, kwanza wewe ni mzuri kiasi kwamba hata kukutambulisha kwa watu kuwa huyu ni mke wangu unaonekana umefanya jambo la maana, wewe ni mtafutaji, una upendo, una huruma, unajali, huchepuki, ukiwa na mwanaume unampenda kweli. Aliyenivuruga hadi nikaachana na wewe namlaani hadi kesho ni yule mwanamke waliyenitafutia kuoa ndio chanzo yule, ila mimi nakupenda Erica hadi kesho na imani yangu inaniambia kuwa ipo siku mimi na wewe tutaungana na kuwa kitu kimoja, tutaishi pamoja tukilea mtoto wetu katika maadili mema”Mama Angel alikuwa na hasira akasimama ili aondoke, ila mumewe muda huo huo akasogea eneo lile ila na yeye alipomuona Rahim alijikuta akichukia sana kiasi kwamba hata hakumsalimia zaidi ya kumwambia mke wake aende kwenye gari na aliwafata watoto wake nao kuingia kwenye gari kisha alimwambia Erick awapeleke nyumbani ambapo alifanya hivyo kwahiyo alibaki yeye tu na watu pale kiwandani hakutaka watoto wake wahisi kitu chochote kile.Baba Angel alipomaliza ndipo alipomfata Rahim na kumtaka kuondoka,“Naomba uondoke sehemu yangu”“Kwakweli Erick unasikitisha sana, mwanaume gani wewe ambaye muda wote una mashaka na mkeo? Kumbuka huyo unayemuona mkeo nimezaa nae mimi”“Hiyo ya kuzaa nae sio sababu Rahim, sikia nikwambie unajua mimi nilikuwa nawe vizuri tu na nikakwambia uwe unakuja kwangu kwaajili ya wewe kucheza na mtoto ili akuzoee halafu ukataka kufanya nini nyumbani kwangu?”“Najua nilitaka kufanya makosa, ila Erick wewe ni mwanaume una wasiwasi gani lakini? Unampenda Erica na anakupenda, unajua hawezi kushawishika kijinga, tatizo lako ni nini lakini?”“Unajua wewe akili yako naona imeliwa na hivyo virusi vya ukimwi kichwani!”“Nani kakwambia kuwa mimi nina virusi, unajua usiongee kitu ambacho huna ushahidi nacho. Kwani virusi ni kitu gani katika maisha, watu wanaishi navyo na wanadundika tu hapa tunayemuongelea ni Erica. Hebu sikia Erick, wewe ulikuwa rafiki yangu na matendo yetu yaliendana kwa asilimia mia moja, kwahiyo kubadilika kwako kwasasa hakukubadilishi wewe unabaki kuwa Erick siku zote, ni kweli umemuoa Erica, mmelea mtoto wangu, umezaa nae watoto wengine, ila tambua kuwa hata mimi bado nampenda Erica, ungeelewa hilo basi ungekaa na mimi na kunishauri kisaikolojia na sio kunikwepesha na familia yako”“Hivi utake kumbaka mke wangu halafu nikuache karibu na familia yangu nina wazimu au ni kitu gani! Kwanza Rahim naomba uende”“Yuko wapi mwanangu Angel?”“Laiti kama nikikaa na huyo Angel nikamueleza yale maovu yako basi hatokaa kukutaka uwe baba yake kamwe, hivi si wewe mwenyewe uliyesema Angel angekuwa sio mtoto wako basi ungemtamani kimapenzi kisa ni mzuri sana, hivi Rahim kwanini hukui jamani!! Kwasasa wewe ni baba tena una watoto lukuki, hivi nikae chini na kumueleza Angel maovu yako moja mbili tatu atakutamani wewe uwe baba yake!!”“Nadhani hukunielewa, kwani nilivyosema vile ndio nilimaanisha kuwa namtamani, hivi naweza kutembea na mtoto wangu mimi!! Sio mtoto wangu tu, hivi hata mtoto wa rafiki yangu na jamii yangu naweza tembea nae wakati na mimi nina watoto wadogo! Mambo mengine uwe unayatafakari kwanza, sawa tuseme nilisema hivyo, au hata ningembaka mtoto wangu mwenyewe je hilo lingebadilisha chochote kuwa mimi ndiye baba yake mzazi? Na siwezi kufanya hivyo mimi, Erick una watoto wako sasa, nahitaji mtoto wangu hilo tu basi”“Naomba uende”“Naenda ila weka akilini kuwa nahitaji mtoto wangu, siku nikiamua kutumia nguvu basi familia yako nzima nitaitikisa”halafu Rahim akaondoka zake, kiukweli baba Angel hakuwa na furaha kabisa na moyo wake uliingia simanzi gafla na muda huo huo akaacha tu maagizo kwa mtu halafu yeye akaondoka zake.Siku hii baba Angel aliamua kuita bodaboda na kuondoka nayo kuelekea nyumbani kwake, alipofika tu alioga na moja kwa moja kujilaza, hakuongea kitu chochote na mkewe na kumfanya hata mama Angel kujihisi vinaya maana lile tukio la kufatwa na Rahim hakulipenda pia, basi alikaa karibu na mumewe pale alipokuwa amelala na kufikiria mambo kadhaa ambayo aliwahi kufanyiwa nyuma na Rahim,“Alinidanganya ananipenda, nikampa moyo wangu nami nikampenda, nikampa mapenzi yangu, nikapata mimba yake na akakubali kila kitu kuwa atanitunz na kunihudumia na kuahidi kunioa, nilijificha na mimba ile maana alisema nitakuja nitakuja ila hakutokea, baadae nyumbani wakajua, nikabahatika kujifungua na ahadi yake kwangu iliendelea nitakuja ila hakuonekana, akanipa sharti gumu ambalo sikuwahi kufikiria kuwa kuna siku ataniambia vile maana tulikubaliana kuoana hata bomani sababu ya utofauti wa dini zetu, akaniambia nibadili dini, nikamfikiria mwanangu, nikafikiria aibu niipataye kwa kuzaa nje ya ndoa, nikafikiria jinsi ninavyojificha ili ndugu wasijue, nikaona ni bora nikubali ili anioe niepukane na aibu, nikakubali na kumwambia kuwa nipo tayari kubadili dini unioe ili tuishi na kulea mtoto ila alinibadilikia, ndio kwanza hakutaka tena mawasiliano na mimi, hakutaka tena kumuhudumia mtoto hakutaka tena kusikia chochote kuhusu mimi, maisha yakawa magumu sana kwa upande wangu maana kila mahali nanyooshewa kidole, nimemaliza chuo na zawadi ya mtoto, nikashindwa kwenda kutafuta kazi maana mtoto alikuwa bado mdogo na mimi sina mbela wala nyuma yani sikuwa na msingi wowote wa maisha, niliona dunia inanicheka, niliona dunia inanitenga, niliwaza kwanini nastahili adhabu hii wakati hakuna baya nililowahi kuliwaza kwa huyu mwanaume, anizalishe na bado anidhalilishe na kunifanya nioenekane sina thamani yoyote katika maisha, muda wote macho yangu yalijaa machozi, nilimshika mwanangu na kulia nae sana, kuna muda nilijiona kuwa mimi ni mwanamke mpumbavu sana kwa kumuamini mwanaume, ila alinionyesha mapenzi na nikaamini kuwa ananipenda. Katika kukata kwangu tamaa, alirudi kwangu Erick na sasa alirudi akiwa mpya kabisa na kunipa mapenzi yote na kuchukua jukumu la ubaba kwa mtoto wangu Angel, ananipenda na anampenda mtoto wangu ila bado aliona kuna umuhimu wa Angel kumtambua baba yake halisi, ni kitu gani tena Rahim alitaka kunitenda kwenye nyumba ya mume wangu?? Na bado aliweka na vitisho kuwa kama atashindwa kwangu basi atafanya kwa mwanangu, ambaye ni mtoto wake mwenyewe, Rahim kawa ni mwanaume wa ajabu sana katika maisha yangu. Najuta kumfahamu, sijui ni kwanini nilikutana nae. Moyo wangu unajawa na machozi tena, ameivunja furaha ya mume wangu ambaye ananipenda sana, nitakuwa mgeni wa nani mimi, sijapanga haya katika maisha yangu ila sijui kwanini yananifata jamani!!”Alikuwa akilia huku akiongea hayo, na muda huu alilia hadi mumewe alisikia na kumfanya baba Angel aamke na kukaa na mkewe kisha alimkumbatia na kumwambia,“Usijali mke wangu, mimi na wewe tunapendana na hilo ndio la msingi kwetu, watoto ni ziada yetu ili kukamilisha furaha ya nyumba yetu. Usijali mke wangu, hata mimi nafikiria vingi pia, usidhani nimechukia kwani siwezi kuchukia sababu ya hili ila tu sijafurahishwa nalo ila Mungu ni mwaminifu atatusaidia na kujua ni jinsi gani tutaweza kushinda na kuvuka hapa tulipo”Basi alikumbatiana pale na mume wake na kuona kidogo moyo wake ukirudisha tabasamu na furaha basi mumewe akamuomba kuwa apumzike kidogo naye alifanya hivyo.Kulipokucha, wakati baba Angel akijiandaa kwenda ofisini akapata ukumbe kutoka kwa madam Oliva,“Kuna jambo nahitaji ushauri kutoka kwako”Baba Angel alishangaa tu ila hakujibu kitu kwenye ule ujumbe bali alimaliza kujiandaa kisha kumuaga mkewe pale na kwenda kazini.Mama Angel alibaki nyumbani na familia yake, ila muda kidogo Erica alienda kukaa na mama yake na kumuuliza mama yake,“Kwani mama, yule baba wa jana ni nani?”“Aaaah ya jana si yalishapita mwanangu, sidhani kama ni vyema kuyazungumzia”“Yalipita ndio, ila sikuelewa mama hebu ona jinsi tulivyorudi nyumbani inaonyesha hata haikupangwa iwe vile, baba karudi badae na pikipiki, sijaelewa vitu vingi vya jana. Halafu yule baba alivyokuwa akiongea na mimi mmmh!”Mama Angel alishtuka kidogo na kumuuliza,“Aliongea nini na wewe?”“Kwanza, aliponiona alishtuka halafu akaniita, akaniambia unafanana sana na mwanamke mmoja ambaye nampenda sana, nikamshangaa”“Mmmh! Akasemaje tena?”“Ndio akasema unaitwa nani, nikamwambia naitwa Erica, akasema mimi ni mzuri sana, halafu akauliza mama yako yuko wapi, nikasema ulipo ndio akasema nimlete ulipo. Ni nani yule mama?”“Mmmh Erica, achana na hizo habari ila ukikutana tena na yule mtu akikuita usiende tafadhari”“Halafu mama, nisamehe jana sikukwambia alinipa na hii hapa hela”“Kheee alikupa na hela? Wewe ulianza kuongea nae muda gani na alikuwa hela ya nini?”“Aliniambia kuwa mimi ni mzuri sana, ananipongeza kwa kuzaliwa mzuri ndio akanipa na hii hela”“Mbona hukusema?”“Niliogopa mama kukwambia pale wakati ulishaniambia niondoke”Kisha Erica akatoa zile pesa na kumfanya mama yake ashangae sana kwani zilikuwa ni nyingi tu, akachukua zile pesa kwa mwanae na kwenda chumbani kwake bila kuongea kingine na mtoto wake, hata Erica alibaki sebleni akishangaa tu.Mama Angel aliingia chumbani huku machozi yakimtoka, akakumbuka mara ya kwanza kutekwa akili yake na Rahim ilikuwa ni katika pesa, yani Rahim alikuwa ni mwanaume ambaye alimpa sana pesa, kwahiyo alipoona Rahim kumbe kampa mwanae pesa, aliumia sana moyoni mwake na kujisemea,“Hivi Rahim ana nini lakini jamani, kwanini ampatie mwanangu pesa? Tena pesa nyingi namna hii jamani!!”Mama Angel aliihesabu hela ile aliona kuwa ilikuwa ni laki mbili halafu kwenye zile hela kulikuwa na kadi yenye namba za simu za Rahim,“Sasa kamuwekea namba huyu mtoto wangu ili amtafute au nini jamani? Mbona kuna wanaume wana laana jamani loh!!”Kwakweli mama Angel alisikitika sana kwa alichokifanya Rahim.Baba Angel akiwa ofisini kwake akiendelea na kazi zake za hapa na pale, mara alifika madam Oliva ila kiukweli baba Angel kwa kipindi hiki alikuwa akimuogopa sana madam Oliva maana hakumuamini tena, ila alimkaribisha tu na kuongea nae,“Jamani baba Erick, kama unanikwepa vile, hebu sahau yote yaliyopita”“Haya, niambie”“Ningependa tupate mahali tuzungumze maana kuongelea ofisini swala hili kidogo sio vizuri, naomba chagua mahali gani ambapo patatufaa ili tuzungumze, sina nia mbaya na wewe baba Erick, usinifikirie vibaya tena. Ni wapi sasa tutakaa na kuzungumza”“Basi nitakwambia”“Mmmh jamani, hukawii kusema kuwa umesahau wewe”“Hapana, sisahau wala nini au utanikumbusha muda nikiwa natoka kazini. Leo nitatoka kwenye saa kumi”“Sawa nitakukumbusha basi”Kisha madam Oliva akaondoka zake, na baba Angel akaendelea na shughuli zake zingine.Muda wa kutoka ni kweli madam Oliva alimkumbusha tena, basi akamwambia mahali pa kukutaniana ambapo kweli alivyotoka ofisini alienda mahali hapo na kukutana na madam Oliva kisha kuanza kuongea,“Haya, niambie ni kitu gani ulikuwa unataka kunieleza?”“Kwanza kabisa, ni kweli nilikuwa nakutaka yani nisikatae, mimi ni mtu mmoja ambaye huwa napenda kusimamia ukweli hata kama ukichukia au vipi ila ni vyema nimeongea ukweli. Sababu ya kukutaka unajua ni nini?”“Eeeh ni nini?”“Nilikuwa naona fahari sana ukimsifia mke wako mbele yangu, yani wewe ni mwanaume unayejiamini na ni wanaume wachache sana wenye uwezo wa kufanya hivyo, kingine ni yule mwanamke Sia, yani jinsi alikuwa anakuhitaji ndio kitu pekee kilichofanya nikutake pia ili na mimi nipate hicho ambacho wanawake wenzangu wanang’ang’ania kutoka kwako. Na nimetumia madawa mengi sana kukupata ila imeshindikana, kiukweli nguvu iliyokuwepo kati yako na mke wako ni kubwa sana. Kitu kingine mimi nilikuwa simjui Steve wala sikuwa namfatilia habari zake kumbe ni rafiki yangu wa facebook kwa miaka mingi sana na siku zote huwa ananitumia ujumbe lakini simjibu sababu mimi nilikuwa naangalia maisha yangu tu. Kumbe huyu Steve alikuwa akinipenda kwa muda mrefu sana ila hakujua ni jinsi gani anaweza kunipata, kwa kupitia vile viatu ambavyo nilikutegeshea wewe basi Steve akaanza kuhaha kunitafuta, na sasa mimi na yeye tupo pamoja. Naweza sema ni nguvu ya dawa imetumika ila na nguvu ya mapenzi imetumika pia, sababu kwanini vile viatu asingevaa mtu mwingine zaidi ya Steve?”Baba Angel alicheka kwanza kwani akiifikiria historia ya Steve hakudhani kama kuna nguvu ya mapenzi hapo, kwani Steve alishawahi kula tunda ambalo Sia aliliweka dawa ili apendwe na yeye ila akala Steve na Steve kuanza kuishi na Sia, kwahiyo yeye aliona ni mauzauza ya Steve tu, madam Oliva akamuuliza,“Mbona unacheka?”“Hapana, nafurahia tu mapenzi yako na Steve”“Sasa ushauri niliokuita kukuomba ni huu, nahitaji kufunga ndoa na Steve, nahitaji wewe na mke wako ndio muwe wasimamizi wetu”Baba Angel akashtuka kwanza na kumwambia madam Oliva,“Swala la nyie kufunga ndoa ni jema, ila swala la mimi na mke wangu kuwa wasimamizi wenu naomba unisamehe tu kwa hilo maana halitawezekana”Madam Oliva alijaribu kumshawishi pale baba Angel ila alikataa kabisa kwa wao kuwasimamia ndoa yao.Mama Angel akiwa chumbani kwake muda huu huku akipanga namna ya kumueleza mumewe kuhusu Erica kupewa hizo pesa, alishangaa tu kupokea simu kutoka namba ngeni akaanza kuongea nayo,“Mimi ni Sia, usinikatie simu ni jambo nataka kuongea na wewe”“Jambo gani hilo?”“Mumeo, muda huu yupo hotelini na madam Oliva, kuwa makini sana la sivyo unampoteza. Ni kheri umpoteze kwangu kuliko kwenye mikono ya mamba ya yule mwanamke”Kisha Sia akakata simu, kwakweli mama Angel kama akili yake ikagoma hivi kwani hakujua ni kwanini mumewe aweze kwenda hotelini na Oliva baada ya kujua mambo mengi sana kuhusu madam Oliva, kisha akaamua kumpigia mumewe simu kwa muda huo, na mumewe alipokea,“Upo wapi baba?”“Samahani mke wangu sikukwambia, kuna hoteli hapa nimepita mara moja”“Umepita kufanya nini? Nakuomba nyumbani mume wangu”“Sawa, narudi muda sio mrefu. Nakupenda sana mke wangu”Basi mama Angel alikata ile simu huku akitafakari mambo kadhaa.Muda huu Erick alikuwa amekaa kwenye bustani basi Erica alienda kuongea nae na kumwambia kuhusu mbaba aliyempatia pesa,“Yule baba wa jana mliyemuona amekaa pale na mama, alinipa hela jana laki mbili pamoja na kadi yenye namba zake za simu”“Kheee ili iweje? Viko wapi hivyo vitu?”“Nimempa mama leo, unajua nilishangaa sana alivyonipa”“Alisema anakupa ili iweje?”“Kwanza alinisifia huyo balaa, akasema kuwa mimi ni mzuri sana, akasema nina sura nzuri ya upole, na macho ya kuvutia kisha akanipa hela ya kusema kuwa ni hela ya kunipongeza kwa uzuri niliokuwa nao”“Hao ndio wababa wasiofaa, ndio mafataki hao mdogo wangu ila nakupongeza swala moja la kwenda kumkabidhi hiyo hela mama, nakupongeza sana na siku nyingine mtu kama huyo akikupa hela kata kabisa”“Sawa sawa, halafu baba alisema usiwe unanitenga jamani Erick!!”“Sikutengi na nitaongea na baba ili tusome pamoja kama zamani, najua baba atanielewa tu”“Oooh hapo nimefurahi sasa, ila kama baba alisita siku ile”“Sikumsisitiza tu, ila subiri nimwambie vizuri basi baba atakuleta tu shuleni kwetu”Hili swala Erica alionekana kulifurahia sana.Baba Angel alifika nyumbani, ila wakati anaongea na mama Angel wala hakumuuliza sababu ya kupitia hotelini ila alimweleza tu vile ambavyo Erica amepewa hela na Rahim, kwakweli baba Angel alisikitika sana na kusema,“Katika watu wapuuzi namba moja duniani basi ni Rahim, sijui lini akili yake itakaa vizuri na kuwaza kutenda matendo mema. Hebu ona mimi naishi vizuri na Angel nampenda na kumuhudumia, ila yeye bila aibu ameanza swala la kumuhonga mwanangu kweli!! Hebu naomba hiyo kadi yake nimuulize vizuri alipo ili nikaongee nae, sitaki ujinga kwa watoto wangu”Basi baba Angel alichukua ile kadi na kuwasiliana na Rahim ambaye alimtajia alipo na muda huo huo baba Angel aliamua kuondoka nyumbani kwake ila hakupanda gari bali alikodi pikipiki tu na kuondoka nayo, hata mama Angel aliona ni vyema asingemwambia mume wake kwani alimuona hasira aliyokuwa nayo baada ya kuambiwa hayo.Alifika mahali alipo Rahim, na kumkuta akicheka tu na kutikisa kichwa,“Hivi Rahim jamani mbona una akili mbovu wewe!! Kwahiyo umeona vyema kabisa kumuhonga binti yangu na kumpa namba zako za simu?”“Kwani tatizo liko wapi Erick? Nimempa binti yako pesa, laki mbili tu? Nimempa na namba zangu za simu ili niwe nawasiliana nae hata mara moja moja, wewe je? Unamuhonga binti yangu kila siku zaidi ya kila kitu maana nasikia hadi kuna baadhi ya biashara zako zinasimama kwa jina la binti yangu, na kila siku unampigia simu binti yangu, kati ya mimi na wewe nani mwenye nia mbaya na mtoto wa mwenzie”“Hivi una akili kweli wewe!!”“Nina akili ndiomana nafanya haya”“Sitaki uwe karibu na binti yangu, tena hata Angel sitaki uwe karibu nae”Rahim akacheka na kusema,“Unajua Erick utawadanganya wengine tu ambao hawakujui vizuri ila sio mimi ninayekujua ndani na nje, utamdanganya huyo huyo Erica wako ndani, unajua kabisa Angel sio mwanao ila unajifanya unampenda kufa, hadi mali zako umemuandikisha, lengo lako ni nini? Nikikwambia unatembea na Angel utawezaje kukataa wewe?”Kiukweli baba Angel alichukia zaidi na kujikuta akishindwa hata kumjibu na zile hela hakumrudishia na muda huo huo akaondoka huku Rahim akiwa anacheka sana.Baba Angel alienda moja kwa moja stendi na kupanda kwenye daladala huku akiwa na mawazo sana. Alikuwa akiwaza moyoni mwake,“Hivi wanaume wote wanaolea watoto ambao sio wao huwa wanapatwa na adhma hii ambayo naipata mimi? Kwanini inakuwa hivi lakini, kila nikutanapo na huyu mtu kwasasa ni kuichosha tu akili yangu”Alikuwa akiwaza hadi alijikuta akisema,“Dah!!”Kwa sauti ambayo jirani yake aliisikia, basi yule jirani yake alimsalimia,“Habari baba”Alitazamana na yule jirani yake ambaye alikuwa ni mwanamke, na kubaki wakishangaana kwa muda, kwani ni mtu ambaye walikuwa wakifahamiana. Alikuwa akiwaza hadi alijikuta akisema,“Dah!!”Kwa sauti ambayo jirani yake aliisikia, basi yule jirani yake alimsalimia,“Habari baba”Alitazamana na yule jirani yake ambaye alikuwa ni mwanamke, na kubaki wakishangaana kwa muda, kwani ni mtu ambaye walikuwa wakifahamiana.Basi alimuitikia salamu yake,“Salama MAnka, umekuwa mmama siku hizi”“Hata wewe umekuwa mbaba, unajua sikutegemea kama ningekutana na wewe jamani”“Mungu ni mwema wakati wote”“Unaenda wapi? Yani sikutegemea kukutana nawe kwenye daladala, vipi gari iko wapi? Najua wewe upo vizuri kitambo sana”“Aaaah nimeamua tu”“Nilienda kumuona mtoto wetu yupo kwa bibi yake”Baba Angel alishtuka kiasi kwani alishangaa kuwa hakumuuliza chochote kuhusu mtoto ila huyu mwanamke alisema mhivi, ila baba Angel hakuongeza neno lingine lolote, basi kituo kilichofuta baba Angel alikuwa anashuka na kumuaga yule mwanamke ila yule mwanamke alishuka pia, kwahiyo pale kituoni walikuwa pamoja, kisha baba Angel alisogea nae pembeni na kumwambia maana alihisi pengine mwanamke huyu ana neno na yeye,“Niambie Manka”Huyu mama alianza kulia na alimsogelea baba Angel na kumkumbatia tena alilia kwa muda mrefu, basi baba Angel akamwambia,“Unajua tupo njiani?”“Najua ndio, ila ni wapi nitakupata mimi na kukueleza uchungu nilionao juu yako”Baba Angel akashtuka na kumuangalia vizuri huyu mwanamke, ila ilikuwa kwenye mida ya saa tatu usiku kwahiyo kulikuwa na giza kiasi kwamba sio rahisi kuangaliana labda iwe kwenye mwanga ila baba Angel alimuangalia na kumuuliza,“Kwani tatizo ni nini? Una shida gani?”“Natamani siku moja uje nyumbani kwangu, uje kumuona mtoto wako”Baba Angel akashtuka sana na kuuliza,“Mtoto wangu!!”“Ndio, mtoto wako. Najua ni mimi ndiye nilitaka kuwa na wewe ila sababu nilikuwa nakupenda, uliposema upo kujipooza kwangu sikukataa ila nilipopata mimba niliogopa kukwambia kwani ulikuwa na mtindo wa kupeleka mwanamke hospitali akachomolewe mimba yake na mimi sikutaka hilo kwani nilitaka mwanangu adumu na mimi”“Unajua unanichanganya Manka?”“Sikuchanganyi ila nakwambia ukweli, nina mtoto wako. Roho inaniuma kwa mwanangu kujua kwamba hana baba halafu anae roho inaniuma sana”“Sikuelewi, yani sielewi chochote”“Huwezi kunielewa hadi siku ukate shauri na kuja nyumbani kwangu kumuona mtoto wako”Mara simu ya baba Angel ilikuwa inaita, kuangalia ni mkewe alikuwa akipiga basi akaipokea na kuanza kuongea nayo,“Uko wapi mume wangu? Usiku huu ujue!”“Nakuja, nipo stendi tu hapa usijali”Basi baba Angel alikata simu na kuamuangalia Manka, kisha akamwambia“Inatakiwa tupate siku ili tuweze kuzungumza kuhusu hilo swala”“Hilo ndio jambo jema Erick, nitafurahi sana. Nimekuwa na uchungu, na majonzi na kulia siku zote. Roho inaniuma sana, sio kosa langu kwa mwanangu kukosa baba ila ni kosa la mapenzi yangu kwako, nilikupenda, nilikuthamini na ndiomana mtoto wetu namlea kwa upendo wa hali ya juu kiasi kwamba sitaki hata kumgusa mtoto huyu, nampenda sana ndio kila kitu katika maisha yangu”Basi baba Angel alimpa tu kadi yenye namba zake ili waweze kuwasiliana, basi Manka aliichukua ile kadi na kumkumbatia baba Angel tena hakutaka kumuachia kabisa huku akimwambia,“Nakupenda sana Erick, katika maisha yangu sijawahi kumpenda mwanaume yoyote kama wewe. Nakupenda na daima nitakupenda”Baba Angel alijitoa kwenye mikono ya yule mwanamke ila bado yule mwanamke alikuwa kamshikiria basi baba Angel akamwambia,“Samahani Manka, natakiwa niwahi kurudi nyumbani unajua nina familia yangu, kwasasa mimi ni mume wa mtu na nina watoto, natakiwa kurudi kwangu, tutaongea tena”Manka alionekana kulia sana tena alilia kwa muda mrefu halafu ndio alimuachia baba Angel na kumuaga, basi baba Angel aliondoka zake na moja kwa moja alichukua pikipiki na kwenda nyumbani kwake huku kichwa chake kikiwa kimebeba mawazo ya kutosha.Baba Angel alipofika nyumbani kwake na kuingia chumbani aliona ni vyema akaoge ili apumzishe akili yake na mawazo kwani alijiona kuwa na mawazo mengi sana, kwahiyo alihisi akioga basi atapata nguvu na kuweza kuichanganya vyema akili yake.Basi alitoa nguo zake na kuzitundika halafu yeye akaenda kuoga, muda ule mama Angel nae akaingia chumbani ila alihisi kusikia harufu ya manukato mengine katika shati la mume wake, basi alilichukua karibu na kulinusa na kugundua kuwa lazima kuna mtu mumewe alikuwa nae, alianza kuwaza huenda akawa madam Oliva, ila akakumbuka kuwa mwanzoni ndio alitoka kwa madam Oliva na alibadili nguo wakati akienda tena kuonana na Rahim, akajiuliza tena labda hakwenda kuonana na Rahim bali alikutana tena na madam Oliva, wakati akiangalia lile shati la mume wake, kuna kitu kilimstaajabisha sana, kwani aliona midomo ya mwanamke yenye rangi kwenye hilo shati kwahiyo rangi ya midomo ilibaki kwenye shati la mume wake, hapo mama Angel ilimuuma sana na kujikuta akitoa machozi huku akikumbuka maneno ya dada yake kuwa unajifanya unamuamini sana huyo mwanaume eeeh! Ila alijifuta yale machozi kwani bado hakuona kama ni vyema kumuhisia vibaya mume wake ingawa kuna vitu vimejionyesha wazi kabisa, aliwaza kuwa mumewe akitoka amuulize vizuri maana hakuelewa, moyo mwingine ukamtaka asimuulize ila amchunguze, ila aliona kufanya vile ni kuzidi kuumia kwenye moyo wake, wakati anawaza hayo mumewe nae alitoka bafuni na kumkuta mke wake na lile shati mikononi mwake, akamfata karibu na kumkumbatia ila mke wake akajisogeza na kufanya amuulize,“Tatizo ni nini mke wangu?”“Nieleze kuhusu shati lako, nasikia harufu ya manukato mengine na kuna rangi ya mdomo kwenye shati lako. Je umeanza kunisaliti mume wangu?”“Hapana, na sina sababu ya kufanya hivyo. Ngoja nikwambie ukweli, kuna mwanamke nilikutana nae njiani ila tunafahamiana hata na wewe unamfahamu sababu tumesoma nae, basi aliponiona ndio alinikumbatia nadhani rangi ya midomo yake ikashika shati langu”“Kwahiyo alijilaza kifuani kwako?”“Hata sijui nikueleze vipi mke wangu unielewe ila ndio kama nilivyokwambia”“Huyo mwanamke ni nani?”“Ni yule Manka, ambaye tulisoma nae”“Aaaah yule alikuwa binti mzuri sana darasani”“Hapana, wewe ndio ulikuwa mzuri darasani”Mama Angel akatabasamu kwani aliona raha kusifiwa na mume wake, na kujikuta akimsamehe tu kwa kosa lile kisha akamuuliza mambo ya alipotoka,“Kwahiyo ulionana na Rahim?”“Dah! Nimeonana nae, ila ni pasua kichwa hatari nikikwambia alichoniambia kwa hakika utanionea huruma mke wangu”“Pole jamani, kakwambiaje kwani?”Baba Angel alimueleza maneno ambayo aliongea na Rahim, kiukweli hata mama Angel alijihisi vibaya sana, roho yake iliumia mno na kujikuta akisema,“Katika maisha kuna makosa ambayo mtu uliwahi kuyatenda, basi ukifika kwenye maisha mengine unatamani upate ufutio wa kufuta makosa yako, jamani mimi hii dhambi ya kuwa na Rahim naona inanitesa maisha yote, hadi sijielewi. Mara nyingine sielewi kwanini Angel alikuja kwenye maisha yangu”Mumewe akamziba mdomo na kumwambia,“Shiiiii usiseme hivyo mke wangu tafadhari, Angel ni baraka kwetu. Usiwaze hayo kabisa, hapa tunayemuongelea ni chizi mmoja anayeitwa Rahim ambaye amekosa akili ya kutafakari na kujifikiria na sio Angel ambaye ni malaika asiyetambua lolote maana yeye sio kosa lake kuwepo katika maisha yetu”“Ila jamani, Rahim ana mambo ya karaha sana. Hivi ndio wananikazania kweli nimwambie Angel huu ujinga wa baba yake mzazi?? Bado kwakweli, ngoja nijipange ndio nitamwambia. Na vipi ile hela yake ulimrudishia?”“Oooh hata sijamrudishia chochote”Baba Angel alichukua suruali yake na kukuta ile hela ya Rahim ipo tu ila ile kadi ya Rahim haikuwepo ndipo alipogundua kuwa Manka badala ya kumpa kadi ya namba zake yeye za simu ila alimpa kadi yenye namba za Rahim za simu, hapo aliwaza kiasi ila hakumwambia ukweli wa hilo mke wake kwani hata alichoongea na Manka hakumwambia wala nini, basi mama Angel akasema,“Basi hizi pesa tuziache tu maana hata sio wa kuonana nae tena yule mtu atatufanya tusiwe na raha ya maisha bure kwa ujinga wake”Basi wakakubaliana vile kuwa wasimfatilie tena Rahim wala nini atazidi kuwaumiza kichwa, kisha walienda kula na kuamua kulala tu kwani muda nao ulikuwa umeenda.Junior alikuwa chumbani kwake ila hakuwa na raha kabisa, kitendo cha yeye kukosa ukaribu tena na Vaileth kilimuumiza sana, aliwaza ni jinsi gani anaweza kuipata tena hiyo laki tano ili aweze kumpa Vaileth na aweze kusamehewa. Kuna jambo lilimjia kichwani mwake, aliona kesho yake alifanyie kazi jambo hilo, kwahiyo alilala akiwa na mawazo sana kichwani mwake siku hiyo.Basi kesho yake palipokucha kabisa alijiandaa na kutoka huku akisema kuwa anaenda matembezi tu, akaenda sehemu mbali mbali kuangalia uwezekano wa kupata pesa ila ikawa ni ngumu sana sema kuna kitu alikumbuka kwani alikumbuka kuwa kuna ofisi mamake mdogo aliwahi kumtuma na kule ofisini walionekana kumsifia sana, basi akafikiria na moja kwa moja kwenda kwenye ile ofisi, kisha akaomba kuonana na yule bosi ambaye alionekana kumsifia sana ingawa yule bosi alichukua namba za Junior ila hakumtafuta Junior, basi Junior aliingia pale kwenye ile ofisi na kukutana na yule bosi, basi akamsalimia pale na kuanza kuongea nae,“Samahani, mama yangu ni mgonjwa sana yani inatakiwa milioni moja kwa tatizo lake ila nimejikakamua kutafuta laki nne bado laki sita sijui utanisaidiaje baba yangu”“Aaaah jamani, kalazwa wapi mama yako?”“Kalazwa Muhimbili”“Anaumwa nini kwani?”“Ana uvimbe umeota kwenye kizazi ndio wanataka kumfanyia upasuaji”“Aaaah mbaya sana hiyo, kwakweli inasikitisha sana. Sikia una simu hapo?”“Ndio ninayo”“Ngoja nikurushie basi pesa kwenye simu yako, naitoa benki na kukurushia moja kwa moja halafu wewe utaenda kuitoa, dah nimesikitika sana. Utaniambia hali ya mama yako basi, nikipata muda tutawasiliana ili nije kumuona”Basi yule baba alimuuliza Junior namba zake za simu na wakati huo huo alimrushia fedha kwenye simu yake na pia akatoa laki moja na kumkabidhi Junior, kisha akamwambia“Hii itakusaidia saidia nauli na mambo mengine madogo madogo, na hiyo itakayo baki huko itakusaidia katika mahitaji mengine madogo madogo ya mgonjwa, usisite kuja kuniambia lolote litakaloendelea. Mpe pole sana mama yako, dah nimeumia sana”Junior alimshukuru yule baba na kuondoka zake pale ofisini.Yule baba kwakweli alisikitika, alimuita mwenzie ambaye alikuja na kuongea nae,“Unajua huyu mtoto wa James kaja leo sababu mama yake kalazwa hospitali yani walikosa laki sita tu za kuweza kumsaidia mama yake”“Jamani dah!! Mtoto wa James wa kuteseka hivi jamani!!”“Ndio hivyo, kwakweli nimetoa hela yangu bila kujielewa na kumpa kijana huyu, nikikumbuka baba yake alivyokuwa jamani!! Roho imeniuma sana”“Basi utamuulizia vizuri alipolazwa mama yake ili twende tukamuone, ila si ulisema huyu mtoto anaishi na Erica, unajua maisha anayoishi Erica siku hizi sio ya kukosa laki sita jamani”“Familia zinaficha mengi hizi huwezi jua kinachoendelea kwakweli, ila nimeumia sana”“Kwakweli pole yake, jinsi James alivyokuwa akijitoa kwenye matatizo ya watu dah!! Ukiachana na ulevi na uhuni wa James ila alikuwa akijitoa sana”“Nakumbuka wakati mama yangu anaumwa moyo, sina mbele wala nyuma, James alitoa hela ya mfukoni kwake na kulipia gharama zote za mama kwenda kutibiwa India, kiasi kwamba mama alipokuja kusikia kifo cha James alilia sana kama kafiwa na mwanae wa kumzaa, kwakweli James ni mfano wa kuigwa alikuwa na roho nzuri sana”Basi walikazana kumsifia tu James huku wakiumia sana kwa swala la kusikia kuwa mama Junior anaumwa.Junior alienda kutoa pesa huku akiangalia katumiwa na yule baba kwenye simu yake, alichekelea sana na kufurahi sana,“Wow, kumbe kanitumia milioni moja!! Jamani sikujua kama naweza kupata fedha kirahisi namna hii dah!!”Alifurahi sana na kuitoa ile pesa, yani alikuwa akitabasamu tu njia nzima ila aliwaza jambo moja kuwa yule bosi akimpigia je kutaka kujua hali ya mama yake? Akaona kitu chema ni kuzima simu hata kwa siku tatu ili asiwasiliane kabisa na huyo bosi kwani hakuwa tena na jibu la kumpa, basi alikuwa akirudi kwao huku akijisemea,“Yani nafanya yote haya sababu ya mapenzi tu dah!! Nampa mama yangu ugonjwa, ili tu kumridhisha mwanamke! Aliyeleta mapenzi aiseee katuweza, tena kaniweza kweli mtu kama mimi, Vaileth ananipa kila kitu lakini sijui ni kitu gani kinanitamanisha kwingine jamani!! Ila nitatulia kwasasa, maana huu uongo jamani umezidi, eti mama ana uvimbe sijui nilipanga saa ngapi kuongea vile! Kweli mimi nina akili sana”Alikuwa akitabasamu huku akirudi kwao, na alipofika ni moja kwa moja alienda chumbani kwake kwanza kuweka zile pesa.Halafu alitoka na kwenda kwenye bustani ambako alimkuta Erick amekaa na kuanza kuongea nae,“Siku hizi unapenda sana maeneo haya eeeh!!”“Huwa napenda sababu Napata muda mzuri wa kutafakari mambo mbalimbali”“Hivi ni mambo gani zaidi huwa unatafakari Erick ikiwa hapo huna mwanamke wala huwazi kuhusu mwanamke, maana huwazi kuhusu Samia wala Sarah yani sijui ukoje wewe ndugu yangu”“Mimi huwa nawaza kuhusu maisha tu”“Sasa maisha yamefanyeje ikiwa huwazi vyema kuhusu kupata mwanamke au kuwa na mwanamke?”“Sasa mwanamke wa nini katika maisha yangu? Mama yangu na dada zangu wananitosha”“Hivi wewe mzima kweli, huyo mama yako na dada zako ndio watakupa utamu”“Halafu Junior naomba ukiwa unaongea na mimi kwanza jua kabisa unaongea na mdogp wako, ongea na mimi mambo ya kunijenga sio mambo ya kijinga kama hayo ya wanawake”“Sasa mambo ya kukujenga kama yapi?”“Hivi unajua kama wewe ni mwanaume, na sisi wanaume ndio tunaotegemewa katika maisha, yani hapo uniambie mdogo wangu, biashara Fulani inalipa, au kuna biashara nimefikiria ambayo ikifanywa hivi na hivi inaleta faida kubwa, au mdogo wangu kuna mtu nimesikia anauza kiwanja”“Kwahiyo sisi tunaweza kununua kiwanja? Tunaweza kufanya biashara?”“Hakuna kitu kinachoshindikana, halafu kitu kama hatuwezi na wazo letu ni zuri si tunamshirikisha baba hapo, kama anaona inawezekana kufanywa na sisi basi atatushika mkono tu kutusapoti ili tufanikishe na kama tukishindwa kabisa na akiona wazo la maana basi analishikiria yeye. Unajua ni nani alimwambia baba kuhusu swala la kujenga kiwanda? Ni mimi mwenyewe nilimwambia baba jinsi ninavyofikiria kichwani na mwisho wa siku baba kafanya kweli ingawa wazo hili nilimwambia miaka mitatu iliyopita, kwahiyo kujitoa na kuwaza ya maana ni muhimu sana”“Mmmh dogo una mambo sana, ngoja niendelee kukaa nawe ili kuikomaza akili yangu maana naona una mawazo mapana sana kushinda hata mimi kaka yako”Basi alianza kuongea nae kuhusu mambo ya shule maana hakutaka kuambiwa kuhusu vitu vingine asivyoweza kuelezea.Baba Angel leo akiwa kazini kwake, alitulia ila alikuwa na mawazo kiasi huku akifanya kazi zake, basi yule rafiki yake Juma alienda kumtembelea na kuongea nae mawili matatu pale,“Hivi swala nililokwambia umelifanyia kazi?”“Swala gani?”“Nimekwambia kuwa mchukue yule kijana wako, weka pale kiwandani hata kwa mwezi mmoja halafu uangalie kiwanda chako kitafanyaje”“Dah!! Sijalifanyia kazi ujue”“Yani Erick unakaa na fursa halafu unashindwa kuitumia kweli! Unajua kijana wako ni fursa yule, tena karibia anafungua shule inatakiwa uwe nae makini kwasasa ili hata akiwa anaenda shule basi kipindi cha mwisho wa wiki unamchukua na kumtumia, yule kijana ana akili sana, yupo vizuri sana kichwani”“Nashukuru kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi hakuna tatizo”“Nitakuja tena nadhani kesho alasiri ili kuangalia ulipofikia”“Sawa hakuna tatizo”Basi aliagana nae na yeye kuondoka zake, baba Angel alifikiria kwa makini na kuona ni vyema kumtumia mtoto wake huyo katika maendeleo yake, alijisemea,“Ila ni kweli, Erick ana akili sana, halafu anajitambua sijui kapata wapi ufahamu aliokuwa nao ila nadhani ni malezi ambayo tumempa. Siku zote huyu mtoto amekuwa akinishauri vitu vya maana sana, natakiwa kufanyia kazi swala hili na kesho nitaenda nae kiwandani na kumuacha huko, nitaanza kumjaribisha tu hadi azoee kwanza ndio nadhani itakuwa rahisi kwake kutoa mawazo yake, ila namuhurumia mwanangu bado mdogo, awaze biashara na masomo dah!!”Ila aliona ni vyema kufanya hivyo kwani itakuwa ni bora kwa maisha yao na maisha ya kijana wao.Alipomaliza kazi zake baba Angel aliamua kwenda nyumbani kwake mapema, ila alipokuwa njiani alifikiria kuhusu mke wake, akafikiria kwa yale yote yaliyopita ni vyema akamchukulia zawadi mke wake na iwe rahisi kwa yeye kuanza kumpeleka Erick kiwandani na hata mkewe asikatae kuhusu hilo, basi moja kwa moja alienda kwenye lile duka la baba Emma na mama Emma na kuongea nao,“Nimekuja leo tena kuchukua zawadi ya mke wangu”Mama Emma akawahi na kusema,“Leo zamu yangu kumchagulia mkeo zawadi”Ila baba Emma akasema,“Mke wangu, wewe tulia tu. Ngoja kwanza tumuulize muhusika. Eti zile zawadi ambazo huwa nakuchagulia huwa mkeo hazipendi?”“Oooh huwa anafurahia sana, na azisifia kuwa ni nzuri”“Basi na leo nikuchagulie au unasemaje?”“Ndio, hakuna tatizo”Basi baba Emma alimuangalia mkewe na kusema,“Eeeh umeona sasa, mimi ndio noma kwenye kuchagua zawadi”Basi baba Emma alimchagulia baba Angel kiatu na kumpatia kisha akamwambia,“Leo mpelekee zawadi ya hiki kiatu au unaonaje?”Baba Angel alikiangalia kile kiatu na kumuuliza baba Emma,“Kheee umejuaje kama mke wangu anavaa namba hii ya kiatu? Maana umeniachagulia kiatu kizuri na cha kumtosha kabisa”“Nimekisia tu, hata sikujua kama kitamtosha”Basi baba Angel alilipia ile pea ya viatu na kuondoka nayo kwenda nyumbani kwake.Alipofika tu alipokelewa na mke wake kama kawaida na waliingia ndani huku wakiongea mambo mbalimbali na alimpa mkewe ile zawadi aliyomtafutia, kwakweli mama Angel alijaribisha na kufurahi sana kwani kiatu kile kilimpendeza na kilimkaa vizuri sana mguuni hata mumewe aliona ni namna gani kile kiatu kilivyompendeza mkewe, basi mama Angel alimshukuru sana mumewe ila leo hakusita kumuuliza,“Samahani mume wangu, unajua sijawahi kukuuliza hivi. Mbona siku hizi umekuwa noma sana kwenye kuchagua zawadi yani kila zawadi unayoniletea ni balaa jamani!!”“Nitakupa siri ya kunifanya niwe hivi mke wangu, nitakupeleka duka ambalo linauza vitu hivi vya kijanja”“Yani kila unachoniletea nikivaa kinanipendeza hatari, ona hiki kiatu sasa, dah yani mume wangu ni noma. Asante sana”Baba Angel alifurahia sana kuona mkewe anafurahia zawadi ambazo yeye anampelekea.Usiku wa leo Junior alimtumia ujumbe Vaileth akimwambia,“Vai, mke wangu naomba leo uje chumbani kwangu”“Nikome kabisa, tena unikome nani mke wako? Mkeo ni huyo ambaye ulichukua laki tano kwangu na kumpelekea, nimekaa kimya usifikiri siumii mtu mzima mie, naumia vizuri sana”“Samahani mke wangu, naomba unisamehe, ila nataka nikukabidhi ile laki tano”“Niletee ila siji chumbani kwako”“Basi nifungulie mlango, nije”“Junior, usifikiri utanidanganya kama siku zote, kwakweli nikiona unanidanganya nipo radhi kwenda kulala sebleni kama ukigoma kutoka”Basi Junior aliinuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Vaileth, kikuweli alitamani sana kuwa nae pamoja, basi alifika pale na kuingia mule chumbani kwa Vaileth na kuanza kumwambia,“Nisamehe Vai jamani mpenzi wangu”“Junior, mimi sio mtoto ujue. Yani mimi ni mtu mzima na nina mtoto tayari, kwahiyo maswala ya kukaa na kudanganywa na mwanaume kila leo siwezi tena, usinidanganye wala kunitania naomba kila mmoja awe na maisha yake. Naomba kama huna cha maana nenda zako tu”Junior akatoa zile hela na kukaa kitandani, ila muda huu hata Vaileth alipunguza ule ukali wake na kuanza kuongea taratibu na Junior, alimwambia,“Kumbe umezileta kweli!”“Sikia Vaileth, nakupenda na wala sikudanganyi, unasikiliza watu wanachosema ila hakuna ukweli wowote, mimi sijaenda kumuhonga mtu yoyote hiyo hela jamani”“Kwahiyo mama yako nae ni muongo!”“Ndio ni muongo, humjui mama yangu wewe. Mimi ndio namjua mama kuwa anaweza kufanya kitu gani, yani yale mambo kayatengeneza tu kwani anahisi kuna kitu kinaendelea baina yangu na yako kwahiyo lazima aniharibie, mimi kweli kuna biashara nilienda kufanya na hii hela ndiomana imekuwa hivi Vaileth. Na kukuhakikishia haya, ni kwamba ile biashara niliyofanya nimepata na faida kwahiyo nimekuletea mtaji na faida”“Kheee kumbe!!”“Hesabu hizo hela”Vaileth alizihesabu na kukuta ni laki nane, alifurahi sana hata aliamini maneno ya Junior kuwa alikuwa akifanyia biashara ile pesa, yani siku hii alisahau kama hata aligombana nae maana aliongea nae vizuri sana na kuendelea kuhadiana nae mambo mbalimbali.Kulipokucha tu, baba Angel alienda kumuamsha Erick ambaye alijiandaa halafu moja kwa moja alienda nae kwenye kiwanda chake na kumwambia,“Mwanangu, wewe ndio mtoto wa kiume kwenye familia, na wewe ndio wa kuwashikiria dada zako. Leo nimekuleta huku kiwandani ili nikuache na hawa wafanyakazi halafu utembelee kila kitu na uangalie ni kipi kipunguzwe na kipi kiongezwe, kumbuka hii ni biashara ya familia kwahiyo lazima tuiendeleze. Badae nitakuja kukuchukua mwanangu, natumai umenielewa”“Nimekuelewa baba”Basi baba Angel alimuacha Erick hapo halafu yeye alienda ofisini kuendelea na shughuli zake kama kawaida.Kwenye mida ya saa tisa, alifika yule rafiki yake Juma na kuanza kuongea nae,“Umefata wazo langu?”“Ndio, nimempeleka leo mwanangu na kumuacha pale kiwandani nitamfata muda sio mrefu”“Basi, twende wote ili na mimi nikaangalie kidogo”“Sawa, hakuna tatizo”Basi baba Angel aliweka vitu vyake vizuri halafu akatoka akiwa ameambatana na Juma, ila walipofika nje ya ofisi kuna jambo liliwashangaza sana, kwani alimuona Sia ambaye anaonekana alitaka kwenda pale ofisini ila alipowaona alikimbia sana utafikiri kaona kitu cha ajabu. Basi baba Angel aliweka vitu vyake vizuri halafu akatoka akiwa ameambatana na Juma, ila walipofika nje ya ofisi kuna jambo liliwashangaza sana, kwani alimuona Sia ambaye anaonekana alitaka kwenda pale ofisini ila alipowaona alikimbia sana utafikiri kaona kitu cha ajabu.Baba Angel aliona kuwa ile sio hali ya kawaida, kwani siku ya kwanza alifikiria ni sababu ya yeye, alihisi pengine Sia alimuogopa yeye ila leo alihisi kuna jambo ambalo Sia analikimbia kwa Juma, basi alimuangalia Juma na kumuuliza,“Unamfahamu yule mwanamke?”“Aliyekimbia?”“Ndio, unamfahamu?”“Unajua sijamuona vizuri kwahiyo siwezi kusema kama namfahamu au la sema alivyokuwa akikimbia kuna mtu nimemfananisha nae, kwani anaitwa nani?”“Anaitwa Sia, na wewe unamfananisha na nani?”Waliingia kwenye gari huku Juma akiwa hajajibu swali lolote aliloulizwa hapo na baba Angel, ambapo aliamua kumuuliza tena,“Unamfahamu huyo Sia?”“Hapana, simfahamu Sia, sina kumbukumbu ya jina hilo katika maisha yangu”Basi baba Angel alianza kuendesha gari huku akimuuliza,“Ila umemfananisha na nani sasa?”“Dah!! Niliyemfananisha nae hata sipendi kumuongelea, unajua katika maisha tunapitia mambo mengi sana na vikwazo vingi sana kuna wakati mtu hadi unasema sijui ilikuwaje”Alionekana kusikitika sana, swala la kumfanya baba Angel apende kufahamu kwa undani zaidi, basi alimuuliza tena,“Jamani Juma, unajua wewe ni rafiki yangu mkubwa sana, naomba niambie unamfananisha na nani? Alikuwa akiitwa nani huyo mtu?”“Alikuwa akiitwa Baby”“Baby? Kuna mtu anakuwa na jina hilo jamani!!”“Yani yeye alisema kuwa alipozaliwa kwao walizoea kumuita Baby, Baby na mwisho wa siku hilo ndio likawa jina lake”“Kwahiyo na shuleni alitumia jina hilo hilo?”“Ndio, hata rafiki zake aliowahi kunitambulisha kipindi hiko walikuwa wakimuita Baby”“Duh!! Unajua ndio nasikia kwako!”“Ndio lilikuwa jina lake hilo”“Haya niambie basi alikufanya nini?”“Kwakweli sipo tayari kuongelea hilo kwasasa, nisamehe rafiki yangu nitafute tu siku nyingine”“Basi kesho nitakutafuta, unajua mtu unapopata habari mbalimbali unaweza kujifunza na vitu mbalimbali. Inawezekana nisijifunze mimi ila wakajifunza watoto wangu”“Ila Erick jamani, unapenda kupata habari. Basi kesho nitakuelezea, kwasasa tumuongelee Erick mdogo tu”Na kwa bahati walikuwa wamefika kiwandani na kushuka, moja kwa moja walimfata Erick ofisini ila hakuwepo, basi walimuulizia alipo na kumkuta yupo kiwandani pia akiwajibika, basi baba yake alimuita ofisini na kuanza kuongea nae.Ni Juma ndio alianza kumuuliza maswali Erick mdogo,“Umeionaje kazi mwanetu, unaonaje kiwanda?”“Kipo vizuri na kazi inaenda vizuri”“Na vipi mbona usiwe ofisini mpaka tukakukuta kule kwenye mashine?”“Ni hivi, muhusika yani mwenye mali lazima uonyeshe kuwa kazi yako unataka ifanywe vipi, kwahiyo nahitaji kuwa mfano bora kwa wafanyakazi wote wa hapa kiwandani, pia sijataka wajihisi vibaya kwa kusimamiwa na kijana mdogo”Baba Angel na Juma waliangaliana kisha baba Angel akamwambia mwanae,“Muda umeenda sasa, kesho nitakuleta tena na kila siku atakuwa dereva anakuleta huku kwani kuanzia sasa hiki kiwanda kipo chini ya usimamizi wako”Erick alitabasamu na kufurahi sana, kisha alienda kuweka sawa na kuondoka na baba yake pamoja na Juma.Moja kwa moja waliondoka pale na njiani Juma alishuka na kuwaacha ndani ya gari kisha Erick na baba yake wakiendelea na safari huku baba yake akimuuliza baadhi ya maswali ya kiwandani na alifurahishwa na majibu ya mtoto wake,“Oooh najivunia sana kuwa na mtoto mwenye akili”“Nami najivunia sana kuwa na baba mwerevu”Basi walikuwa wakitabasamu tu na safari ikiendelea hadi walipofika nyumbani ambapo baba Angel alienda chumbani na kuanza kuongea na mke wake,“Eeeeh vipi Erick huko kiwandani”“Kwakweli mke wangu tuache masikhara ila huyu mtoto ni jembe kweli tumepata, mtoto wetu ana akili sana”“Itakuwa karithi kwangu huyu”“Mmmh!!”“Sasa unaguna nini jamani, mume wangu?”“Inamaana mimi sina akili?”“Hapana sina maana hiyo, ila Erick atakuwa karithi kwangu akili”“Hukawii kusema na Erica karithi kwangu umbea”Wakacheka tu, kisha baba Angel aliongea tena,“Vyovyote vile ila Erick ni zawadi tuliyopewa na Mungu, na huyu atawalinda na kuwalea dada zake”“Kweli kabisa mume wangu”Mara simu ya baba Angel ilianza kuita, basi akaichukua kuangalia na kuona aliyekuwa anampigia ni madam Oliva, basi akamtazama kwanza mkewe na kupokea ile simu,“Halafu unajua kama watoto washachaguliwa shule nzuri tu za sekondari”“Nishawatafutia shule mbona”“Aaaah kumbe! Nilijua bado”“Mmmh umesahau kuwa ni wewe ndio ulikuwa ukinielekeza shule ya kuwapeleka watoto!!”“Ooooh nilisahau, yani mapenzi anayonipa Steve hadi sikumbuki jamani, yani Steve ananipenda hadi najiogopa. Hivi ni kweli mtu anaweza kukupenda hivi maishani?”“Usiku mwema”Baba Angel akakata ile simu na kuamuangalia mkewe ambaye alikuwa akingoja kwa hamu kusikia kutoka kwa mumewe kuwa ni kitu gani alikuwa akizungumzia,“Alikuwa ananiambia tu shule walizochaguliwa Angel na Junior, ila kwavile nishawatafutia shule zingine basi tena”“Ila mbona kama nahisi kuna mazungumzo mengine?”Baba Angel akakumbuka kitu na kusema,“Oooh nimekumbuka, hivi biashara yetu kule itafungwa hadi lini? Itabidi tutafute mtu wa kukaa kwenye ile biashara”“MMmmh nani sasa?”“Ngoja mke wangu, kuna mtu namfikiria ngoja nitamtafuta kuongea nae”“Nani huyo?”“Nitakwambia tu, ila nadhani atafaa katika kuendeleza gurudumu la biashara yetu”“Sasa si umtaje?”“Nikimtaja lazima utakataa”“Mmmh usiniambie kuwa mtu huyo ni Derrick, tafadhari usimfikirie Derrick kabisa yani”“Jamani mke wangu!!”Baba Angel hakutaka kuendelea kuongelea mambo yale zaidi zaidi aliamua tu waendelee na mambo mengine na kwenda kulala tu.Kulipokucha, baba Angel aliondoka na Erick kama kawaida na kwenda kumuacha kiwandani ila leo alimuomba dereva akamfate Erick muda wowote ambao Erick atamwambia kuwa aende kumfata, kisha baba Angel akaenda zake ofisini kwake.Ila alivyofika ofisini alikumbuka tukio la jana yake la Sia kumkimbia Juma, akajiambia,“Nahitaji kujua ukweli, ila inaweza kuwa ukweli ninachohitaji kujua? Nahitaji kujua huyo Baby alimtenda nini Juma, na je Sia ndio anaweza kuwa huyo Baby? Mmmh sidhani lakini”Akampigia simu Juma na kuongea nae,“Vipi tutaonana leo tuongee kidogo”“Labda uje huku karibia na kwangu”“Sawa nitafika huko kwenye saa nane au saa tisa alasiri”Basi wakakubaliana, kisha akaendelea na kazi zake ila muda kidogo madam Oliva alifika ofisini kwa baba Angel na kuanza kuongea nae,“Mbona jana ulinikatia simu? Ulihisi wivu?”“Sasa wivu wa nini?”“Wivu wa kusikia kuwa Steve ana mapenzi hadi shetani anaogopa?”Baba Angel alitikisa kichwa na kumwambia madam Oliva,“Unajua unataka kunichekesha tu, sasa mapenzi ya Steve kwako yanitie wivu kwasababu ipi? Mimi nina mke wangu na ninampenda sana sasa tatizo liko wapi?”“Basi huo upendo wako kwa mke wako ni cha mtoto maana Steve ni ananipenda zaidi ya neno lenyewe kupenda, sijawahi kupendwa hivi katika maisha yangu yote”“Ila upendo wa uhalisia ni mzuri sana kuliko upendo wa dawa, umemchanganya kijana wa watu akili zote pale alipo hazifanyi kazi halafu upo hapa kunieleza na kujitapa kuwa Steve anakupenda sana, kweli akili zako zipo sawa mwalimu?”“Kheee kweli nimeichanganya akili yako hadi leo umeniita mwalimu! Ni kweli mimi ni mwalimu tena mwalimu ninayeijua taaluma yangu vizuri kabisa, ndiomana sipendi kukaa ndani ya uongo na kuwa mwalimu sio shida kwani wote sisi ni binadamu tuna hisia na mawazo tofauti tofauti”“Sijui unazungumzia nini?”“Huwezi kujua hadi mwalimu nikae chini na kukuelewesha ni kitu gani namaanisha, ngoja nikamuwahi mume wangu muda huu. Nitakuja kwaajili ya mipango ya harusi”Kisha madam Oliva akainuka na kuondoka, basi baba Angel alitikisa kichwa na kusema,“Sasa hili ni tatizo lingine nimezua nikitoa Sia jamani mmmh!! Yani hili ni tatizo kabisa kabisa”Baba Angel akaamua tu kuendelea na kazi zake, muda wake ulipofika alifunga kazi na kuwasiliana na rafiki yake Juma na kwenda kuonana nae.Baba Angel alifika walikopanga kuonana na Juma, kwahiyo walikaa katika moja ya migahawa huku wakiongea ongea ambapo bado baba Angel alikuwa kisisitiza kujua hizo habari za Baby,“Kwanini umekazana hivyo? Unazani yule mwanamke aliyekimbia ndio atakuwa Baby?”“Hapana sijui, hata hivyo yule mwanamke haitwi Baby, bali anaitwa Sia. Yani natamani tu kujua kuhusu huyo Baby sijui kwanini ila natamani kujua”“Ipo hivi, Baby alikuwa ni mwanamke ambaye nilimpenda sana, nilimthamini sana huwezi amini nilimpeleka kwa ndugu zangu wote, yani hakuna mtu kwetu ambaye hakumfahamu Baby, lakini yeye alinitambulisha tu kwa rafiki zake na kuogopa kunipeleka kw awazazi wake wala ndugu zake akisema kuwa yeye bado mdogo. Ila nilikuwa nae sababu sikutaka kumkosa kabisa, nakumbuka nilihitaji kumuoa ila Baby alisema haiwezekani kwani mimi na yeye tupo na dini tofauti, nisikudanganye Erick sababu ya Baby mimi nikabadili dini na kumuomba akanitambulishe kwa wazazi wake ili tuoane, akadai kuwabado hajafikia wazo la kuolewa ni mapema mno kwake, tukaendelea tu na mahusiano, kitendo alichonifanyia Baby ni kupata mimba yangu na kwenda kuitoa huku akisema hajajiandaa kuzaa na mimi, kwakweli niliumia sana, nikaona kuwa Baby ni mwanamke asiyenifaa alianza kukata mawasiliano na mimi, na mwishowe alikuja kuniambia kuwa kuna mpenzi wake kampata na wanapenda sana, mimi nimsahau kabisa, niliumia sana moyo na hapo Baby aliondoka katika maisha yangu sikuwa nae tena. Ilipita kama miaka mitatu au minne nikakutana na Baby akiwa amejawa na machozi usoni, nilimuuliza tatizo ni nini? Aliniambia katendwa sana na mapenzi, kiukweli nilimuhurumia. Nisikudanganye, kipindi hiko nilikuwa nipo kwenye harakati za kuoa huyu mke niliyemuoa sasa, ila nilikuwa radhi kuahirisha ndoa kwaajili ya Baby, na niliondoka nae na kwenda nae nyumbani kwangu tulikaa huko kwa siku mbili huku tukiwa na furaha sana na kufurahia maisha, nilimwambia Baby kuwa nitamuoa na alikubali kubadili dini yeye na kusema kuwa ataitwa Johari, nilifurahi sana alipotaja jina hilo. Ila alipoondoka kwangu akabadilika kabisa, hakutaka tena mawasiliano na mimi, akasema nisimtafute tena, niliumia sana na kufanya maamuzi ya haraka kumuoa Johari tena bila ya sherehe wala nini. Baada ya miezi michache, Baby aliniletea picha za harusi yake, niliumia sana, kiukweli alipendeza sana, nikatamani yule mwanaume aliyemuoa Baby ningekuwa mimi. Ila kuna kitendo kimoja alinifanyia Baby cha kuniumiza zaidi ya nilivyoumia mwanzo, yani huyu Baby huyu ni zaidi ya nilivyomjua. Ila sitasema ni kitu gani alinitenda”“Mmmh alikufanyeje jamani, kitu hiko kinaweza kuwa msaada baina yangu na yako”“Kwani unamfahamu huyo Baby?”Baba Angel akafikiria kidogo, ni kweli hakumfahamu huyo Baby, ila alishangaa kwanini alitaka kujua habari zake, alimuwaza Sia kuwa amfikirie kuwa ni Baby kidogo alikuwa na mashaka na kumwambia Juma,“Unajua nini nilikuwa nataka niangalia kama yule Sia ndio anaweza kuwa Baby, ila naona wazo langu linagoma. Unajua yule Sia nimewahi kuwa nae kwenye mahusiano, ila ana maisha halisia sana, na katika maisha yake kitu pekee anachokitaka ni kupendwa yani yeye analilia kupendwa usiku na mchana hadi anaenda kwa waganga”“Mmmh basi hawezi kuwa Baby huyo, kwani Baby alikuwa hayo mambo ya waganga anayapinga kabisa. Nishawahi kumshawishi kufanya hivyo wakati kuna mambo yangu yamekwama ila Baby alikataa kabisa”“Kumbe na wewe unaendaga kwa waganga?”“Jamani Erick, tumekuja kuongelea nini na wewe unasema nini tena!! Unajua kuna baadhi ya mambo unaona hayaendi, ukiangalia kushoto hola, kulia hola unaona ni vyema nikatafute kinga kidogo, hatuendi kuroga ila kutafuta vya kutusaidia”“Mmmh!”“Tuachane na hizo stori jamani Erick, mimi nitaanza kukueleza bure mambo usiyopaswa kuyajua. Niambie kuhusu Erick”Basi waliongea pale na kuagana halafu baba Angel alienda kumfata mwanae maana dereva alisema kuwa hakupigiwa simu na Erick.Akiwa njiani baba Angel kuna mambo alikuwa akiyafikiria kichwani mwake, kwa muda huo mambo ya Sia na Baby hakuyaweka akilini ila alichoweka akilini ni kuhusu rafiki yake Juma kusema kuwa huwa ana tabia ya kwenda kwa waganga basi akajisema,“Mmmmh ni kweli Juma amenipa wazo zuri sana ila sio wa kumuamini sana na yeye, akinigueka na kwenda kumroga mwanangu je!! Natakiwa kuwa na mipaka na huyu mtu sasa”Basi moja kwa moja alienda kiwandani na kumkuta Erick akiwa hana habari kabisa kama anatakiwa kurudi nyumbani, basi baba yake alimwambia akamilishe na kuondoka.Wakiwa kwenye gari alimsema kwanza,“Unatakiwa kuwa na kiasi cha kazi Erick, sio muda wote ufanye kazi. Nimejaribu kuongea na mmoja hapo nasikia chai hunywi wala chakula cha mchana huli, sasa utaishi maisha gani jamani mwanangu Erick eeeh!! Na leo nimeona hata muda wa kuondoka huna habari nao, mwanangu kazi ipo tu ila mwili nao unatakiwa kupumzika ndiomana kuna muda wa kulala ila kufanya miili yetu ipumzike, mwanangu usifanye nijute kukuweka kiwandani, niahidi kuwa utabadilika”“Nitabadilika baba, samahani”“Yani usirudie tena kitu hiko, hebu angalia kumbe hujala tangia asubuhi jamani. Hapana Erick sitaki hii kitu tena”“Sawa baba nimekuelewa”Basi walifika nyumbani na kama kawaida baba Angel alienda chumbani ila muda huu Erick alienda chumbani kwake na kumkuta Erica ndio yupo mule kweye chumba chake, basi alikaa kitandani na kumuuliza,“Vipi leo Erica mbona upo chumbani kwangu?”“Unajua kukumiss! Nimekumiss sana Erick, ila umechoka na umenyong’onyea sana inaonyesha una njaa wewe”“Ni kweli nina njaa sana”“Kheee halafu leo tumepika chapati na rosti ya maini, sasa itakuwaje?”“Duh!! Sitashiba, sijala toka asubuhi halafu mnipe chapati sijui na rosti la maini jamani mtafanya nile chambati hizo kama mbuzi na mimi kutafuna sana siwezi. Nikuombe kitu Erica?”“Niombe tu”“Naomba kanisongee ugali, nakuomba tafadhari”Basi muda huo huo Erica alienda jikoni na kubandika sufuria na kwaajili ya kusonga ugali, basi Vaileth nae alienda jikoni na kumkuta Erica ndio anakorogea uji na kumuuliza,“Kheee nini unapika?”“Nataka kusonga ugali kwaajili ya Erick, njaa inamuuma sana”“Oooh nyie mapacha mnajaliana hadi raha jamani”Erica alitabasamu na kumwambia Vaileth,“Dada, niangalizie samaki humo kwenye friji unipakie na viungo nimkaangie”Basi Vaileth alifanya vile na Erica alipomaliza alimuweke kile chakula Erick na zile mboga yani samaki wa kukaanga na rosti ya maini, basi Erick alitoka tu chumbani na kuanza kula kile chakula, kwakweli alikuwa na njaa kiasi kwamba alikula chakula chote huku akifurahi na kumsifia sana dada yake kwa upishi wake,“Ndiomana baba huwa anasema, kwakweli Erica kwenye mapishi wewe ni kiboko”“Mmmh njaa hiyo, kwani ugali nao una utaalamu?”“Ndio una utaalamu, kuna watu hawajui kusonga ugali, sio niseme watu tu hata mimi mwenyewe siwezi kusonga vizuri hivi kama ulivyosonga wewe, yani mtu unakula ugali unaona kabisa umeiva, ugali laini na mzuri, mwingine sasa anasonga ugali mgumu kama jiwe”Erica alicheka, ila muda huo kuna mgeni alikuwa amefika ndani kwao ila hawakumuona mpaka alipowasogelea pale mezani na kumuuliza Erick,“Ushawahi kuona mtu kasonga ugali mgumu kama jiwe?”Wakamuangalia na kumsalimia kwa pamoja,“Shikamoo shangazi”Alikuwa ni shangazi yao Tumaini, aliitikia ila alionyesha kuwa hakuwa na furaha kabisa, kisha akamwambia Erica,“Kaniitie mama yako, maana nimefika muda sana tu”Basi Erica alienda kumuita mama yao ambaye kwa muda mfupi tu alifika ila alishangaa kwa muda ule kumuona wifi yake akamkaribisha,“Karibu wifi ila mbona muda huu!! Kwema kweli huko?”“Kwema ndio, kuna mahali nilikuwepo sio mbali na hapa kwahiyo wakati naondoka nikasema ni vyema nije kuwasalimia kidogo”“Oooh karibu sana na umefanya vizuri”“Ila ndio nataka kuondoka”“Jamani, ngoja nimuita basi kaka yako”“Aaaah usimuite, twende nje mara moja”Basi mama Angel alitoka na wifi yake ila kufika kule nje wifi yake alimwambia,“Unajua sikupanga kabisa kuja huku, ila nilipokuwa sio mbali na hapa kiasi kwamba sikujihisi vizuri kuondoka bila kuja kuwasalimia, ila kumbe Mungu alikuwa na maana halisi ya kunileta mimi huku”“Unamaanisha nini?”“Hivi Erica, kweli kabisa wewe wa kuwaletea watoto mambo ambayo yalifanyika miaka ya nyuma kabisa kabla hawajazaliwa? Watanionaje mimi kuwa shangazi yao sijui kupika au?”“Unajua sikuelewi”“Hunielewi kitu gani, umewaambia watoto wako kuwa mimi sijui kupika. Umewaambia kuwa niliwahi kusonga ugali mgumu kama jiwe, kwakweli sijapenda na sijapenda kabisa, Halafu alimtia singi yani alimsukuma kichwa kwa mkono, kisha akapanda gari lake na kuondoka zake.Mama Angel hakuelewa chochote kwani hakuwepo sebleni wakati watoto wakiongea hayo, kumbe naye Tumaini kajihisi tu bila hata ya kusemwa wala nini.Usiku huu, Angel alikuwa na simu yake ambapo kwa muda huu alinyata tu na kuichukua chumbani kwa bibi yake ambaye alikuwa amelala na yeye wazo lake lilikuwa ni kuwasiliana na Samir, basi aliwasha simu yake na kujaribu kumpigia Samir ambaye alimpigia yeye, basi alianza kuongea nae,“Unajua nimekumbuka hata sauti yako, jamani Samir karibu hata uje unione tu”“Basi kesho kutwa yani Jumamosi nitajitoa muhanga na kuja huko hata usijali kipenzi changu”Wakati akiendelea kuongea nayo mara alisikia kama mlango wa bibi yake ukilia, kwahiyo alishtuka sana na kufanya simu ianguke chini na ilianguka vibaya sana kiasi kwamba ilipasuka kwenye kioo, yani roho ilimuuma sana, alipoona pametulia aliiokota simu yake na kujaribi kuiwasha iliwaka ila ilikuwa kama na ukungu kwa mbali sababu ya kioo kupasuka, alikosa raha kabisa, ujumbe wa Samir uliingia kwenye simu yake,“Tatizo ni ni mpenzi?”“Yani nilisikia kama bibi basi simu si ikanianguka, imepasuka kioo yani simu yangu imeondoka shoo yote”“Oooh pole, utanitajia basi aina ya simu ili niangalie uwezekano wa kuitengeneza”Basi Angel akamwambia kuhusu simu yake na Samir alimuahidi kuitengeneza, alimwambia kuwa hiyo kesho kutwa ataenda kuitengeneza.Basi Angel aliirudisha ile simu kwa bibi yake na kumkuta amelala hana hata habari, basi na yeye alirudi chumbani kwake na kulala sasa, aliwaza kiasi kuhusu simu yake ila aliamini kuwa Samir atafanikisha hilo la kumtengenezea simu yake.Leo jioni wakati Samir yupo kwao, alikuwa na mawazo kiasi basi mdogo wake alianda karibu na kumuuliza,“Kwani kaka unawaza nini?”“Unajua nini nina hitaji laki mbili ya haraka, sijui naipata vipi”“Oooh kaka, unaahidi kunipa nini nikikupatia hiyo laki mbili”“Halafu wewe jamani, hiyo laki mbili utaitoa wapi sasa eeeh!!”Kisha Samir aliachana na mdogo wake na kuondoka zake, kwenda kwenye matembezi yake, ila siku jioni hii alikutana na Hanifa, na kumshangaa pale,“Kheee Hanifa una mimba?”“Sasa unashangaa kitu gani kwani ni jambo la ajabu kwa mwanamke kubeba mimba?”“Hapana sio jambo la ajabu ila wewe bado mdogo”“Usitake nicheke mie, mdogo!! Kwani mimba nimejipa au? Si ndio nyie nyie wanaume mmenipa!”“Kwahiyo kumbe ulifanya mtihani wa mwisho ukiwa na mimba!!”“Ndio, nilikuwa najibana ila kipindi kile ilikuwa bado ni ndogo, yani Samir unavyoshangaa utafikiri huajwahi kumpa mwanamke mimba!! Unafikri habari zako na Warda hatuzijui? Wewe si ulimpa mimba Warda na umeenda kumtoa”“Kheee jamani, watu mnayatafutaga maneno hata sijui huwa mnayatafuta wapi jamani, nani kakwambia maneno hayo?”“Unadhani ni siri hiyo? Sio siri kabisa, bora mimi ninayeenda kuzaa kuliko huyo aliyetoa. Najua na huyo Angel nae atapata mimba yako tu na utamtoa kama kawaida sababu unaogopa aibu na kwenu huna cha kumjibu yule baba yako mshika dini lakini ana watoto wengi”Samir hakutaka kuongea sana na huyu Hanifa, kwanza alimuona wazi maisha yamempiga kwa kubeba mimba, kwahiyo aliachana nae na kuondoka zake.Usiku wa leo, Junior akiwa chumbani kwa Vaileth walijikuta wakiongea mambo mengi sana ya maisha yao basi Vaileth alimdadisi pia,“Kwanini simu yako unaizima Junior? Kuna wanawake zako eeeh unaogopa watakupigia?”“Hapana, ila kuna watu sitaki wanipate hewani”“Mmmh mimi nina hisia mbaya, maana wewe Junior hata huaminiki”“Haya, iwashe hapo iache hewani hadi asubuhi uone kama kuna mwanamke wa kunitafuta”Basi Vaileth aliiwasha ile simu ya Junior, ila muda ule ule kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Junior, jina la mtu ujumbe lilitokea Samia, basi Vaileth alifungua ule ujumbe na kuusoma,“Junior, nimekumiss. Kesho nitakupa kweli ila naomba uniletee laki mbili halafu ndio nitakupa”Vaileth alimtazama Junior kwa gadhabu kubwa sana. Basi Vaileth aliiwasha ile simu ya Junior, ila muda ule ule kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Junior, jina la mtu ujumbe lilitokea Samia, basi Vaileth alifungua ule ujumbe na kuusoma,“Junior, nimekumiss. Kesho nitakupa kweli ila naomba uniletee laki mbili halafu ndio nitakupa”Vaileth alimtazama Junior kwa gadhabu kubwa sana.Kisha alimtingisha na kumwambia,“Sikumpa Samia hela yoyote, nilienda kufanyia biashara, utumbo gani huu kaandika huyo Samia wako!”Junior alichukua ile simu na kusoma ujumbe wa Samia, kwanza moyo wake ulidunda kiasi kisha akamuangalia Vaileth na kumwambia,Vai mpenzi wangu, sijui nikuelezeje ili upate kunielewa, haka katoto kametumwa na mama lazima mama yangu ndio kakatuma kufanya ujinga kama huu. Hakuna kinachoendelea baina yangu na Samia”“Unanifanya mimi mjinga eeeh!! Narudia, mimi sio mtoto Junior wa kunidanganya kila siku kwanini lakini Junior? Naomba uwe mkweli ili angalau nikuelewe maana naona unanichanganya tu”“Jamani Vai mpenzi, huo ndio ukweli”“Junior, hivi unajua umri wangu kwasasa? Unajua mimi na wewe tumepishana miaka mingapi? Unajua ni mangapi nimepitia hadi leo? Junior sio mdogo mimi, naelewa mengi tu, niambie ukweli sio unafanya kazi ya kunificha ficha na kunidanganya”“Vaileth, sina cha kukwambia zaidi ya niliyokwambia”“Sasa basi, kwa siku ya kesho sitaki kukuona ukitoka hata kwenda dukani, nataka ukae hapa hapa nyumbani, nimechoka na uongo wako Junior”“Nimekubali, sitatoka wala sitaenda popote mpenzi wangu”Junior alijua ni jinsi gani Vaileth amechukia, kwahiyo alikuwa akimbembeleza tu.Baba Angel leo kabla hajaondoka nyumbani kwake, mkewe alimuagiza,“Leo naomba uniletee hereni”“Kheee hereni!!”“Ndio, hereni nataka kuvaa hereni”“Mbona unazo nyingi tu mke wangu”“Ndio ninazo nyingi ila nahitaji mpya”“Ooooh sawa, hakuna tatizo nitakuletea”Kisha baba Angel akambusu mkewe pale na kumuaga ambapo aliondoka ila siku hii Erick mdogo alipelekwa kiwandani na dereva kwahiyo yeye hakuwa na kibarua cha kumpeleka Erick kiwandani.Baba Angel alifika ofisini kwake na kuanza kazi zake mbalimbali, baada ya muda kidogo tu alipigiwa simu na rafiki yake Juma, na kuanza kuongea nayo,“Vipi maendeleo ya Erick?”“Yupo vizuri tu”“Kesho nitakuja kumuona”“Ila Kesho, atakuwa nyumbani tu hatienda kiwandani”“Kwanini tena?”“Kesho ni Jumamosi, nahitaji mwanangu apate angalau muda wa kupumzika, sio mashine ile”“Oooh sawa, basi nitakuja nyumbani kwako kumuona”Baba Angel alimuitikia tu ila hakupenda wala nini, basi alivyokata simu akaanza kujifikiria tena,“Lazima nijue ni kwanini anahitaji kujua maendeleo ya mtoto wangu, kuna kitu gani kaona kwa mwanangu!! Ni rafiki yangu ndio ila siwezi kumuamini kwa asilimia mia moja”Akatikisa kichwa na kuamua kuendelea tu na kazi zake.Junior alikuwa tu nyumbani kutimiza swala la Vaileth kuwa asitoke siku hiyo yani asiende popote, hiyo laki mbili ya kumpatia Samia ni kweli alikuwa nayo ila kwavile Vaileth kamkataza kutoka akaona kuwa anaweza kukosa kotekote, basi akamtumia ujumbe kwanza Samia,“Una uhakika Samia kuwa utanipa kweli?”“Sasa nawezaje kusema uongo jamani Junior!”“Kumbuka na leo Ijumaa, utasema unaenda kuswali wewe”“Kwani kuswali muda wote!! Hebu tuma kwanza hiyo hela uje nikupe mambo”Tamaa ya mwili ikaanza kumshika Junior, alijikuta akitamani sana, akamtumia Samia ujumbe mwingine,“Mimi sitaki kukutumia ila nataka nikuletee mwenyewe ili unipe kweli”“Haya niletee, kwani unafikiri nakudanganya!”Basi Junior akainuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwake kujiandaa kwani hapo alihisi kama mihemko ikimpanda vizuri kichwani, alijiandaa na kuchukua ile pesa vizuri akaiweka mfukoni, alikuwa na laki mbili na elfu hamsini, kwa mawazo yake ilikuwa laki mbili ampe Samia halafu elfu hamsini ndio imfae kwa matumizi mengine ila wakati anataka kutoka tu chumbani kwake, alipofungua mlango alibambana na Vaileth ambaye aliingia nae chumbani kisha Vaileth akamwambia,“Umejiandaa unaenda wapi mpenzi wangu Junior?”“Aaaah naenda kwa mama, nimeitwa mara moja”“Mbona hukuja kuniambia? Wakati tumekubaliana kuwa leo usitoke!”“Samahani mpenzi wangu”“Kama kweli unanipenda naomba uniruhusu jambo moja”“Jambo gani?”“Naomba nikukague”Junior akaona huo ni msala, kuanza kukaguliwa na Vaileth tena alikuwa akikataa ila mwisho wa siku alikubali na Vaileth alimkagua na kukuta zile pesa ambapo alizichukua halafu akamuuliza,“Junior kweli unanipenda mimi? Unanithamini? Unaniamini?”“Ndio”“Kwanini unamtamani Samia? Kubali jambo hili, kukaa hapa nyumbani bila kwenda popote au kwenda kwa huyo Samia ila sahau kila kitu kuhusu mimi, chagua moja hapo kama unaenda kwa huyo Samia nikurudishie hizi hela, kama unabaki nikae nazo kwanza”Junior akafikiria na kusema,“Siendi kwa Samia, ila sitaenda popote kwaajili yako”Basi Vaileth alichukua zile hela na kwenda nazo chumbani kwake, yani Junior aliona kawezwa kweli siku hiyo na Vaileth ilibidi tu akajilaze ila akasema,“Huyu Samia alinikomesha sana siku ile, ngoja nami nimkomeshe kuwa naende halafu mwisho wa siku siendi kumbe nimezuiliwa huku”Akaanza tena kuwasiliana na Samia ila muda huu alikuwa kajilaza tu kitandani.Muda huu baba Angel alifikiria kitu, akataka kujua kama huyo Baby na Sia ni mtu mmoja, basi aliamua kwenda nyumbani kwa Sia kwa muda huo.Ni kweli alifika kwa Sia na kumkuta akifagia uwanja wake, basi akasimama nyuma yake kidogo na kumuita,“Baby”Ila Sia hakuitika, basi baba Angel akaita tena,“Baby, Baby”Sia akageuka na kuonekana kutokuamini kabisa, kwani alienda kwa haraka na kumkumbatia baba Angel ambaye alimtoa mwilini mwake na kusema,“Kumbe unaitwa Baby?”“Ooooh Mungu ni mwema sana, nilijua tu kuna siku Erick utarudi kwangu, yani leo umeniita kimahaba hadi raha, nimependa sana ulivyoniita baby”“Kimahaba!! Nimekuita kimahaba kivipi wakati ndio jina lako hilo”“Lipi hilo?”“Si unaitwa Baby wewe!!”“Ndio, kwa wewe lakini yani wewe uwe unaniita hivyo hivyo na kufanya moyo wangu uburudike sana, nilitamani kweli mtu atokee na kuniita kimahaba hivi”“Unajua Sia usinichanganye eeeh!! Sijakuita kimahaba mimi, yule mtu uliyemkimbia ndio kasema wewe unaitwa Baby?”“Mtu gani niliyemkimbia?”“Unajifanya akili inarudi na kutoka eeeh! Wewe mwanamke ni mwehu nini, yule mwanaume wa siku ile si alikuwa mwanaume wako wewe au?”“Unajua hata sijui unazungumzia kitu gani?”“Kwani wewe ni kipi kilikukimbiza siku ile nyumbani kwangu? Na kipi kilikukimbiza siku ile ofisini kwangu”“Ooooh ni yule mwanaume uliyekuwa nae”“Ni nani yako yule?”“Dah historia ndefu, kumbe una wivu Erick eeeh!! Sijui nikuelezeje, nipo tayari kukwambia ukweli ila naomba unipatie laki mbili nina shida sana”Baba Angel alienda kwenye gari yake na kutoa laki tatu na kumkabidhi Sia kisha akamwambia,“Haya nieleze kuhusu yule mtu”“Kwanza anaitwa nani yule?”“Inamaana unamkimbia mtu usiyemjua jina lake? Anaitwa Juma”“Ooooh Juma, basi mimi namfahamu kwa jina lingine la Brian, ni hivi yule kaka alikuwa na mahusiano na dada yangu ila dada yangu hakumpenda hata kidogo ila yeye alimpenda sana dada yangu na alikuwa akimlazimisha kuwa kwenye mahusiano nae, kuna kipindi dada yangu akapata ujauzito basi yeye aliung’ang’ania kuwa ule ujauzito ni wake, siwezi jua ukweli uko wapi maana siri ya mtoto anayo mama, ila dada yangu alisema kuwa mtoto ni wa mwanaume mwingine ila yeye alikuwa akimng’ang’ania mtoto kuwa ni wake, basi kuna kipindi dada yangu aliumwa sana, wakati anakufa aliniachia mtoto wake na kusema kuwa nimlee mimi na nisimpe mtu yoyote yule, basi ndio nimechiwa huyo mtoto kumlea, yule baba kila mahali anaponikuta ni kunipa kichapo tu kuwa nimpe mtoto wake, na mimi siwezi kufanya hivyo kwani mtoto huyu niliambiwa nisimtoe”“Mmmh Sia jamani, mbona kama uongo. Huyo dada yako aliitwa nani?”“Aliitwa Anna”“Mmmmh!! Mbona kaniambia kuwa huyo mwanamke aliitwa Baby?”“Hapana, anaitwa Anna, yani huyo Andrew na huyo Anna walikuwa wakiitana kwa majina yao wenyewe ndiomana mimi nakwambia kuwa simjui huyo mtu kwa jina la Juma”“Mmmh unajua sikuamini kabisa”“Kwahiyo unahisi ni mimi ndio huyo Anna? Ukitaka nitakupeleka hadi kaburini kwa huyo dada yangu”“Naomba nimuone mtoto wa huyo Anna”Basi Sia akaita,“Amina, njoo”Muda kidogo huyo Amina alifika, na Sia alimwambia,“Msalimie babako mdogo, huyu ndio baba mzazi wa Elly”Baba Angel alimuangalia Sia, ila alishindwa kuikataa salamu ya huyu Amina ambaye umri wake ulikuwa sambamba na umri wakina Erica, Erick, na huyo Elly. Basi Amina alivyoondoka, baba Angel akauliza kwa Sia tena,“Kwani hawa watoto wamezaliwa mwaka mmoja? Maana naona huyu mtoto umri wake kama wanangu na kama mwanao”“Sio mwaka mmoja tu, bali hawa watoto wote wamezaliwa siku moja, yani wakati mimi najifungua, basi dada yangu nae alikuwa akijifungua, na mkeo nae halikadharika, kuna mambo mengine huwa Mungu anayaweka kwa makusudi yake tu”“Itawezekana vipi wakati wewe na Erica mlibeba mimba kwa wakati tofauti?”“Kama wewe sio baba wa mwanangu una uhakika gani kuwa mimi na Erica tulibeba mimba kwa siku tofauti! Yani unajikanyaga mwenyewe Erick, ila juwa kuwa Elly ni mtoto wako uliyezaa na mimi. Ukatae ukubali huo ndio ukweli”“Aaaah kwaheri bhana”Baba Angel akaenda kwenye gari yake na kupanda na kuondoka zake, ila njiani akakumbuka zawadi ya hereni aliyoagizwa na mke wake basi akaamua kupitia kwanza kwenye lile duka halafu ndio aende kiwandani kumchukua Erick maana alimuuliza dereva wala hakuwasiliana na Erick, ila badae akaona ni vyema aende kumchukua Erick kwanza halafu ndio aende nae dukani.Moja kwa moja baba Angel alienda kiwandani kumchukua mtoto wake, ila alimkuta yupo tena makini na kazi zake, akamfata na kumwambia kuwa waondoke, kisha Erick alimtii baba yake na kuondoka nae, halafu alianza kuongea nae,“Erick jamani, sijakuleta kiwandani kuja kujiumiza na kuhenyeka na kazi, nilikuleta ili uje kusoma mazingira, hebu jione ulivyochoka jamani!! Kwakweli utaniudhi, bora nitafute watu wengine wa kusimamia kuliko kumtesa mwanangu. Kwanza umekula leo?”Erick aliitikia tu kwa kichwa, basi baba Angel akamwambia“Unanidanganya Erick, halafu ukifika nyumbani upikiwe ugali na samaki, kwanini lakini mwanangu!! Dah unanikwaza sana, itabidi tupitie mahali uende kula”“Hapana, baba nitaenda kula nyumbani”“Hapana, nyumbani utakula kidogo ila lazima tupitie mahali ukale”“Baba, jana Erica aliniahidi kuwa leo atapika chakula kizuri sana kwaajili yangu, naomba nikale nyumbani”“Kheee!! Kumbe umeshinda na njaa sababu ya chakula atakachopika Erica!! Haya, ngoja nami nijiandae kwa chakula atakachopika Erica”Kisha akaenda na Erick kwenye lile duka kwaajili ya kumnunulia mke wake hereni, alivyofika pale tu aliwaambia kuwa siku hii anataka hereni, basi Erick nae aliwasalimia pale kisha baba Emma kama kawaida alienda kuchagua hereni za kumpa baba Angel ampelekee mkewe,“Naamini hizi atazipenda sana, si unaona zilivyo nzuri eeeh!!”Mama Emma nae akachagua zingine,“Mimi ni mwanamke, ni rahisi kujua mwanamke anapenda nini, hizi hereni atazipenda zaidi kuliko hizo ulizochagua baba Emma”Yani wakabishana hadi Erick na baba yake walikuwa wakicheka basi Erick akamwambia baba yake,“Baba, chukua zote halafu utaona mama atapenda hereni zipi zaidi”Baba Emma akasema,“Eeeeh wewe ndio umesema vizuri ila nina uhakika, atapenda zaidi hereni hizi”“Basi kweli baba Emma hujui, zote atazipenda ila zaidi ni hizi nilizomchagulia mimi”Baba Angel alicheka na kufata ushauri wa Erick kuwa achukue zote kwa pamoja, basi walichukua na kuondoka.Wakiwa kwenye gari alimwambia baba yake,“Baba, utampelekea mama achague hereni azitakazo halafu atakazoziacha tutampa Erica”“Oooh hapo sawa mwanangu, nitafanya hivyo basi”Waliondoka sasa na kuelekea nyumbani kwao.Samir alimfata mdogo wake ambaye alikuwa amekaa sebleni huku ameshikilia simu yake, alimuuliza,“Haya mpango wako wa kupata laki mbili umeishia wapi?”“Aaaah tatizo kaka huniamini, halafu huyu mjinga nae sijui kakwama wapi, kila muda anasema anakuja anakuja”“Ni nani huyo? Unajua mdogo wangu una vituko sana wewe!!”“Ngoja kaka nikwambie, kuna huyu mtu ananifatilia kweli yani ananitongoza, mara ya kwanza nilimwambia niletee laki tano akaniletea, na sasa nimemwambia laki mbili”“Mmmmh hiyo tabia umeipata wapi Samia? Mtoto mdogo hivyo umeanza kupenda hela, unajua sikukuelewa kabisa, lakini kama ni ujinga huo hapana kwakweli”“Sio ujinga kaka, kwani kuna chochote nafanya nae jamani!! Mimi nachukua hela yake tu, nafanya kamavile baba alivyonifundisha”“Aaaah yani baba ndio anakufundisha na wewe ujinga wake jamani!! Ila amakweli baba tunae loh!! Haya na huyo anayekufatilia ni nani?”“Anaitwa Junior, ni ndugu yake na Erica”“Wewe mjinga wewe, kaone vile. Junior atakubaka wewe, hakuna mtu mwenye akili mbovu kama Junior, wewe mtoto ukoje lakini. Hebu acha kuwaza ujinga, kaone vile, ndiomana watoto huwa mnakatazwa simu maana naona simu inakupa kichaa hiyo. Mjinga wewe”Kisha Samir akaondoka zake, maana hakupenda kile kitu kilichosemwa na mdogo wake, ni kweli hakuwa na pesa ila hakutaka ipatikane kwa njia hiyo.Angel akiwa ametulia kwa bibi yake, muda huu alikuwa akiangalia simu yake huku akiwaza kama kuna uwezekano wa kupona kioo cha simu yake, yani akawaza sana basi akaamua kumtumia ujumbe Samir maana alimuahidi kutengeneza ile simu,“Sasa Samir vipi mbona hujanipa jibu?”“Dah samahani, yani nimeulizia matengenezo ya kioo kwa hiyo simu ni laki mbili, ila samahani kwasasa nimepungukiwa kidogo na hela ila nitaitengeneza tu”Angel alimuitikia ila alionekana kukosa furaha kabisa kwani aliona wazi ile simu ikiendelea inazimika kabisa, ila akakumbuka kuwa jana yake alimtafuta na Ally na alimwambia swala lile, basi akataka kumtafuta tena ila muda ule ule ujumbe wa Ally uliingia kwenye simu yake,“Angel nimeulizia matengenezo ya hiyo simu nimeambiwa ni laki mbili, nikutumie ukaitengeneze au nije niifate niipeleke kwa fundi akaitengeneze”“Njoo uifate tu, maana mimi sitaweza kwenda popote”“Kwanini usimwambie bibi yako kuwa unaenda kuitengeneza simu halafu kesho nije nikuchukue twende kwa fundi”“Ngoja nitajaribu”Basi Angel akakubaliana hivyo na Ally, na kuinuka ili akaongee na bibi yake kuhusu swala hilo, ila alipofika tu kwa bibi yake ni bibi yake ndio alianza kuongea,“Yani hawa wamenishtukiza tu, inabidi kesho nikakutane na wenzangu kwenye kikoba, yani kuna watu wa mikopo ndio inabidi tukawajadili kesho”“Sawa bibi hakuna tatizo”“Na wewe utakuwa unafanya nini?”“Mimi natabaki nimelala tu bibi”Basi Angel hakuona haja ya kuomba ruhusa kwa bibi yake kwani aliona ni nafasi iko wazi kabisa ya yeye kuweza kutoka.Baba Angel na Erick muda huu waliungana na wengine mezani kupata chakula cha usiku kwanza, kwani Erica alipika chakula cha kuweza kuliwa na familia nzima, na siku hiyo alipika pilau, basi baba Angel alikula huku akisifia,“Kheee kweli tumekuza, yani binti yangu umekuwa hadi unaweza kupika pilau tamu namna hii!! Ndiomana Erick kagoma kula pote hadi tufike nyumbani”Basi Erica alikuwa kitabasamu tu huku akimshukuru baba yake kwa zile sifa alizompa, wote ndani walikula na kusifia kile chakula, basi kila mmoja aliposhiba siku hiyo walimshukuru sana kisha kila mmoja alielekea kwenye mambo yake.Baba Angel na mama Angel waliingia chumbani ambapo mama Angel cha kwanza aliuliza,“Hereni nilizokuagiza mume wangu ziko wapi?”“Aaaah nimekuja nazo pea mbili, ila unatakiwa kuchagua moja maana nyingine itakuwa ya Erica”“Mmmh umemkumbuka mwanao eeeh!! Anajua nini ndiomana kawapikia pilau leo!!”Baba Angel alicheka tu na kutoa zile hereni, basi mama Angel alizishika na kusema,“Zote ni nzuri na zinapendeza sana”“Kwahiyo umechagua hereni zipi mpenzi?”“Aaaah nimezipenda zaidi hizi hapa, nimezipenda sana”Basi alichukua na kuzijaribu kisha akajiangalia kwenye kioo na kujiona kuwa kapendeza sana, basi alimshukuru mume wake na kumwambia,“Yani asante sana, ila siku hizi umekuwa noma katika kuchagua zawadi mume wangu, dah nimezipenda hizi hereni sana”“Ooooh nimefurahi kusikia hivyo mpenzi, basi lete hizo nimpelekee Erica sasa”Basi mama Angel alimkabidhi zile hereni na moja kwa moja baba Angel alienda nazo kwa Erick kwanza kwani alitaka kumuuliza jambo kwakuwa yeye alisahau,“Eti Erick, hizi hereni ndio alichagua yule mama au yule baba?”“Ni yule mama ndio alichagua hizi, kumbe mama kapenda zile alizochagua yule baba eeeh!!”“Ndio, kazipenda zile mama yenu. Chukua mpelekee Erica”Basi baba Angel alitoka ila alikuwa akishangaa sana kwanini vitu akichagua yule baba Emma basi hutokea mkewe akavipenda sana vitu hivyo kama hizo hereni, basi alirudi ndani na kuongea na mke kidogo,“Mke wangu, hivi wewe unapenda nini?”“Mmmh mimi napenda vitu vingi sana ila cha kwanza kabisa ni wewe”“Aaaah jamani, asante mke wangu. Yani nilikuwa namaanisha kwenye zawadi unapenda nini?”“Napenda kila zawadi unayoniletea haswaa zawadi unazoniletea siku hizi, nazipenda sana. Kama hizi hereni uwiiii jamani sijui mume wangu umejuaje kuwa nitafurahi namna hii kwa hereni hizi!”Basi baba Angel alitabasamu tu,ila kwa muda huo waliamua tu kulala.Kulipokucha, baba Angel alikumbuka jambo kuhusu Juma kutaka kuja kuonana na mtoto wake basi akaita familia yake na kuongea nao,“Jamani, leo ni Jumamosi. Wiki ijayo shule zinafunguliwa, kwahiyo nisipofurahi kwasasa nanyi watoto wangu basi itakuwa ngumu sana kufurahi tena, kwahiyo naomba mjiandae leo tutaenda ufukweni kutembea”Wote walifurahia tena walifurahi sana, mama Angel aliuliza,“Mimi na Ester je?”“Naye tunaenda nae, kwani tatizo liko wapi mke wangu? Tunaenda na Ester wetu kufurahi”Baada ya hapo kila mmoja alijiandaa kwaajili ya hiyo safari ambayo baba yao ameipanga.Walipomaliza walipanda kwenye gari, basi wakati baba Angel akijiandaa kutoa ile gari kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake, alipoangalia ulikuwa unatoka kwa Juma,“Ndio nipo njiani nakuja, leo nakuja na mke wangu”Baba Angel hakutaka kuongea chochote wala hakutaka kumwambia mke wake kwani anajua wazi mkewe akijua atakazana wabaki ili wawapokee hao wageni, kwahiyo moja kwa moja aliondoa gari na kuelekea ufukweni.Angel aliwasiliana na Ally na kujiandaa kabisa, basi Ally alifika muda ambao bibi Angel hakuwepo nyumbani kwahiyo Angel alitoka na moja kwa moja alipanda kwenye bajaji ya Ally na kuanza kuelekea kwa fundi ili Angel akatengenezewe simu yake, basi alikuwa akiongea nae,“Yani Angel mimi nakupenda sana, nipo tayari kufanya chochote kwaajili yako ili tu wewe ufurahi”“Ila ile kauli ya mamangu mkubwa kuwa sisi ni ndugu uliichukuliaje?”“Aaaah mimi nimechukulia tu kama mtu kaongea kama kuongea kwani huo undugu mimi na wewe utatokea wapi? Tupo tofauti kabisa yani, mimi ninachojua nakupenda basi”“Ila mimi nina mpenzi”“Huyo mpenzi wako angekuwa wa maana basi yeye ndio angeingia dhamana ya kutengeneza simu yako, ila mimi ndiye ninayekupenda kwa dhati”Angel hakujibu kitu kwani lengo lake ni ile simu ipone tu ili isizimike maana alijua ikizimika basi ndio mawasiliano hakuna tena.Walifika kwa fundi na moja kwa moja kumkabidhi ile simu kwaajili ya matengenezo, ila Ally alimuomba kitu Angel,“Wakati simu inatengenezwa hapa, twende pale tukapate vinywaji kidogo”Angel alikubali na walitoka kwa yule fundi huku Ally akiwa amemshika mkono Angel ila pale nje Angel alishtuka kidogo kwani alimuona Samir ambaye inaonyesha alikuwa akienda kwa fundi yule yule, ila Samir aliwakaribia na kumuuliza Ally,“Nani yako huyu?”Ally nae alijibu kwa kujiamini,“Huyu ni mpenzi wangu, kwani vipi?”Samir alionekana kuwa na hasira sana, kwani muda ule ule alikunja ngumi na kumshindilia Ally puani. Walifika kwa fundi na moja kwa moja kumkabidhi ile simu kwaajili ya matengenezo, ila Ally alimuomba kitu Angel,“Wakati simu inatengenezwa hapa, twende pale tukapate vinywaji kidogo”Angel alikubali na walitoka kwa yule fundi huku Ally akiwa amemshika mkono Angel ila pale nje Angel alishtuka kidogo kwani alimuona Samir ambaye inaonyesha alikuwa akienda kwa fundi yule yule, ila Samir aliwakaribia na kumuuliza Ally,“Nani yako huyu?”Ally nae alijibu kwa kujiamini,“Huyu ni mpenzi wangu, kwani vipi?”Samir alionekana kuwa na hasira sana, kwani muda ule ule alikunja ngumi na kumshindilia Ally puani.Ally alionekana kuchukia na yeye ila kabla hajafanya lolote, alishtukia akipigwa teke na Samir hadi akaanguka chini, yani ni Angel ndio alienda kumsaidia kuinuka pale chini, Samir alitaka kumshindilia teke lingine pale chini ila Angel akamzuia,“Wewe Samir ukoje wewe yani hata huulizi jamani eeeh!!”“Niulize mara ngapi? Si amejibu kuwa ni mpenzi wako!”“Kumbe Samir hujui akili zangu eeeh!! Yani umeshindwa kuniuliza mimi mwenyewe!! Sasa kuanzia leo sikutaki”Kisha Angel alimsaidia Ally pale chini kuinuka, ila Samir alikuwa kama katengenezewa kidonda vile basi akamsogelea Angel na kuanza kumuomba msamaha,“Samahani Angel mpenzi hii hali haitajirudia”“Mjinga wewe, siwezi kuwa na mahusiano na mwanaume bondia, hebu nipishe huko sikutaki na usinitafute tena”Bado Samir hakuelewa kabisa, na kuamua kumpigia magoti Angel ili aweze kusamehewa na Angel ila bado Angel alikuwa mgumu kufanya hivyo na alimwambia Samir aachane nae kabisa, yani Angel aliona kamavile siku yake imeharibika kwani aliingia kwa yule fundi na kumuomba simu yake ambayo bado hakuanza kuitengeneza ila Angel alitoka nayo na kuanza kuondoka, ikabidi Ally amfate na kuingia nae kwenye bajaji halafu wakaondoka huku akimuuliza,“Sasa Angel mbona umetoa simu kwa fundi kabla ya kutengenezewa”“Nimeghairi sitaki tena itengenezwe”“Oooh jamani Angel, nakuomba jambo moja basi tupitie hapo upate japo simu ya mawasiliano kwa hii laki mbili maana nipo nayo kwaajili yako”Angel hakujibu kitu ila Ally alipita nae dukani na kununua nae simu nyingine ambayo walinunua kwa laki mbili na elfu ishirini kwani ndio simu angalau ambayo Angel alionyesha kuipenda na kuvutiwa nayo.Wakati wanatoka kwenye duka lile, Angel alimuona mama mmoja ambaye yule mama ashawahi kumuona mara kadhaa ila yule mama alionekana kuongea jambo na Ally na kumpatia Ally pesa kidogo.Basi wakati wanaondoka, Angel alimuuliza Ally,“Kwani yule mama ni nani?”“Ni mama yangu mdogo yule, huwa kuna kazi zake ananipa ndio katoka kunipatia pesa. Sasa Angel mimi ndio nitakuwa mpenzi wako eeeh!! Usikatae Angel tafadhari, nakupenda sana”“Ndio utakuwa mpenzi wangu, ila sharti langu ni moja usiniletee habari za kufanya ngono”“Mmmmh!!”Kuna jambo Ally aliwaza kichwani,“Mapenzi bila ngono inawezekana kweli!!”Ila hakusema ili Angel asifikirie vingine, bali alimjibu,“Hakuna tatizo ila tu ni vyema tuwe tunapata muda mzuri wa kubadilishana mawazo na kuambiana mambo mbalimbali”“Sawa hakuna tatizo juu ya hilo”“Nakupenda sana Angel”“Asante, wewe ni kijana mstaarabu nimependa ulichofanya leo, hukuonekana kumjibu vibaya yule aliyekupiga, hukuonekana kutaka kumrudishia wala nini, nakuona kuwa ni kijana mwema. Ila kuhusu mapenzi inabidi unisubiri maana mimi ninasoma,subiri nimalize masomo yangu”“Sawa sawa, hakuna tatizo Angel.”Basi walifika hadi kwa bibi yake Angel na Ally alimuaga hapo Angel na kuondoka zake.Tumaini, kuna mahali alikuwa ametoka muda huu ila njiani alimuona Sia na kuamua kusimamisha gari ili kuongea nae, alifanya hivyo mara kwa mara sababu ni mtu ambaye alikuwa rafiki yake kabla,“Sia, Sia”Sia akasogea karibu na kusalimiana nae,“Unajua kuna wakati huwa najiuliza kuwa Tumaini huwa ananikumbuka kweli”“Kwanini nisikukumbuke sasa?”“Sijui basi tu, umetoka wapi kwani muda huu?”“Kuna mahali nimetoka nikataka kwenda kwakina Erica nikawasalimie kidogo maana kuna ujumbe nilikuwa nao kwaajili ya Erica ila njiani kabla sijafika nikakutana na Derrick akaniambia katoka huko, kuwa wenyewe hawapo”“Kheee wameenda wapi?”“Nasikia wameenda kutembea, Derrick alisema kuwa alienda huko alikuwa na maongezi na Erick sijui ila hajawakuta, basi nikaamua kuondoka, nimemwambia Derrick tuondoke wote kagoma, kasema kuwa ana safari zake”“Mmmh huyo Derrick na huo utapeli wake sijui kama hajaliza mtu huko kwa Erick!!”Sia akacheka, kisha Tumaini akamuuliza,“Na wewe umetoka wapi?”“Nimetoka huko kufanya maovu”Tumaini akatikisa kichwa kidogo na kusema,“Kweli umetoka kufanya maovu maana mambo yako siku hizi ni zaidi hata ya neno lenyewe maovu, hivi kwanini Sia umekuwa hivyo unajua sio Sia yule niliyemfahamu miaka kadhaa iliyopita, niliyekuwa namsaidia katika mambo mbalimbali hadi nikajiingiza kugombana na Erica kama nami namgombea Erick kumbe kwaajili ya kukuonea huruma wewe, yuko wapi yule Sia wa siku zote?”“Siku mtakayokubali kuniweka mimi kama mmoja wa familia yenu basi nitaonekana kwenu kiundugu na nitakuwa nanyi bega kwa bega tukisaidiana mambo mbalimbali ila mkiendelea na kunitenga basi na mimi nitawatenga”“Ila unajua wewe ni mwezi mchanga yani huwa sikuelewi kabisa, nilikuwa nakusalimia tu kaendelee na maovu yako”Kisha Tumaini akarudi kwenye gari yake na kuendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwake.Angel alitulia ndani, ila kwa upande mwingine aliona ni vyema kwa yeye kupata simu mpya, maana atamficha bibi yake na kumuacha abaki na ile nyingine, na alishukuru muda huo bibi yake hakuwepo nyumbani wala nini, kwahiyo alirudisha ile simu kwa bibi yake na kuijaza chaji hii nyingine na kuweka laini yake, ambapo muda mfupi tu alipokea ujumbe toka kwa Samir,“Angel umenikataa sababu ya kumpiga ngumi yule kijana au sababu ya kukosa laki mbili?”“Aaaargh umeniudhi bhana, sitaki ujinga mie”“Ila kumbuka Angel tunapendana sana”“Sijali kitu, ninachojali ni kumpata mwanaume wa kawaida na sio bondia”“Mmmmh Angel jamani, usinifanyie hivyo”Ila Angel hakumjibu chochote kwani yeye alikuwa akifikiria vitu vingine kabisa, aliona kuwa ile itakuwa ni adhabu kwa Samir na kumfanya asije kurudia siku nyingine kufanya alichokifanya.Basi akamtumia ujumbe Ally,“Yani hii simu ni nzuri hiyo hadi raha, haina vitu vigumu kama ile niliyokuwa naitumia”“Oooh, ndio simu za gharama zina mambo mengi zile ndiomana wanaziuza bei sana. Ila hiyo ni nzuri na rahisi kutumia, sasa jiunge whatsapp uwe unanitumia picha zako”“Mmmmh!! Ngoja nitafanya hivyo basi hakuna tatizo”Muda kidogo bibi yake alirudi na kumuita Angel, ambapo Angel alienda kwa bibi yake,“Mjukuu wangu ulikuwa umelala?”“Ndio bibi, si unajua nipo mwenyewe maana hata Maria hayupo”“Kheee kumbe bado hajarudi toka jana!! Mmmh kashapata mwanaume wa kumdanganya yule, haya nimeleta chakula kwahiyo hakuna kazi ya kupika”Angel alitabasamu kwani hata wazo la kupika hakuwa nalo, basi bibi yake alitoa chakula na kumfanya Angel aulize,“Umetoa wapi hiki chakula bibi?”“Kule tulipofanya kikao leo tuliandaliwa chakula, kimebaki sasa kila mtu kabeba nikaona kwanini nisibebe mie! Nikajibebea zangu tuepuke bajeti”“Jamani bibi, umenikumbusha mama tulienda hotelini akabakisha chakula weeee akaomba mfuko na kufunga chakula chake”“Kheee mama yako nae, kwa hela zote zile bado anakumbuka chakula chake. Ila ni vizuri, hata wewe uwe hivyo sio unaacha acha chakula kizembe”Walikula pale na walipomaliza, Angel alienda chumbani kwake sasa ila akajikuta akikumbuka kitu, alimkumbuka yule mama aliyekuwa akiongea na Ally, akakumbuka kuwa kuna siku yule mama aliwahi kupigwa kibao na Samir, halafu Erick alikuwa hampendi kabisa yule mama, basi akajiuliza,“Yule mama ni nani? Mmmh!”Ikabidi aachane na hayo na kuamua kulala tu.Muda huu baba Angel na familia yake walikuwa wamerudi nyumbani na walikuwa wamechoka sana kutokana na mambo yote yaliyofanyika siku hii.Basi walijiandaa kulala ndipo baba Angel aliposhika simu yake na kukutana na jumbe mbalimbali moja ya jumbe zilizokuwepo ilikuwa ni ujumbe toka kwa Juma, ujumbe huu ulimshtua kidogo hadi alimsomea mkewe,“Kuna ujumbe kanitumia Juma, kiukweli umenishtua hapa”“Ujumbe gani?”“Ngoja nikusomee, umetoka kwa yule rafiki yangu Juma”Basi baba Angel alianza kumsomea mkewe ule ujumbe,“Mmmh kiukweli kilichonipata leo hapo nyumbani kwako hadi najuta, ungeniambia mapema kuwa hutokuwepo kuliko hivi ndugu yangu, nimekuja na mke wangu leo ila sijakukuta wewe wala familia yako, halafu nakupigia simu hupokei. Ila hilo sio swala la muhimu, kinachoniuma ni mtu ambaye nimekutana nae hapo na akajitambulisha kuwa yeye ni mnajimu, huwezi amini katutapeli mimi na mke wangu milioni tatu hivi hivi jamani. Yani tumerudi nyumbani ndio tumegundua utapeli wa huyu jamaa!! Kwakweli sijafurahishwa kabisa na hiki kitendo cha huyu mtu tena kwenye geti lako, nasikitika sana”Baba Angel akamuangalia mkewe na kumuuliza,“Inawezekana akawa Derrick kweli!!”“Mmmh, ngoja nikamuulize mlinzi, ila nahisi ni Derrick tu. Kwanini anafanya hivi lakini jamani!! Aaarggh!”Basi mama Angel akataka kutoka ili akamuulize mlinzi, ila mumewe alimrudisha na kwenda yeye mwenyewe kuuliza kwa mlinzi.Alimkuta mlinzi getini na kumuuliza,“Ni watu gani walikuja leo?”“Mmmh walikuja yule baba wa siku ile na mama mmoja hivi waliwaulizia niliposema hampo waliamua kuondoka”“Ni nani walikutana nae nje ya geti? Au ni nani mwingine alikuja?”“Mmmh sijui kwakweli maana mimi nilikuwa ndani ya geti wakati wanaondoka”“oooh sawa, usiku mwema”Baba Angel alirudi kwa mkewe na kumwambia alichosema mlinzi, halafu akasoma tena ule ujumbe wa Juma na kumuuliza mke wake,“Kwani mnajimu ndio mtu gani?”“Ni mtu mwenye elimu ya nyota, haya sasa hadi rafiki yako katapeliwa si huwa unasema wanaotapeliwa si wenye tamaa ya mali!!”“Sasa unadhani ni kitu gani kilichomfanya Juma na mkewe watapeliwe? Nadhani huyo mtu kawadanganya kuwa yeye ni mtaalamu wa nyota na kawadanganya kuhusu nyota zao maana matapeli wengi sana huwa wanatumia hiyo. Ila najiuliza, hiyo milioni tatu wameitoa vipi nao!!”“Dah!! Ila matapeli ni wabaya sana, natamani kumjua tapeli mwenyewe. Kama sio Derrick sijui yani”Basi waliamua tu kwa muda huo kulala kwani muda nao ulikuwa umeenda sana.Kulipokucha familia nzima ilijiandaa na leo na kwenda Kanisani kwahiyo hapo nyumbani hakuna mtu ambaye alibaki zaidi ya mlinzi wao tu.Muda huu bibi Angel alitoka na mjukuu wake Kanisani, wakati wapo njiani kuna mama mmoja walikutana nae ambaye alionekana kumfahamu bibi yake Angel basi aliwasalimia pale na kuuliza,“Kheee huyu ndio mtoto wa Erica, yule aliyekuwaga anamficha ndani!”Bibi Angel akaona huyu anamletea mada zisizoeleweka, basi akambadilishia mada na muda huo huo wakaondoka zao.Walipofika tu nyumbani, wakaandaa chakula na kuanza kula basi Angel akamuuliza bibi yake,“Kwani bibi, mama alikuwa ananificha mimi?”“Aaaah achana na yule mwanamke aliyeuliza pale ni chizi”“Mmmh bibi!!”Mara alifika Mage na kuwakuta wanakula pale, walimkaribisha naye alikaribia huku akisifia,“Nina mguu mzuri sana, mimi ni mkulima halisi. Hebu Angel kanipakulie na mimi chakula”Angel akaenda kumpakulia na kumletea, ambapo Mage alianza kula na kusema,“Mmmh hiki chakula kapika nani?”“Angel huyo”“Mmmh Angel nawe hata sio mpishi hodari kama mama yako, ila kitamu kiasi chake ila mama yako ni noma”“Ukitaka pishi la Erica basi upikiwe na Erica mdogo mbona utajing’ata vidole, mtoto mdogo ila anajua kupika balaa”Angel hakupenda ile sifa ambayo alipewa Erica na kuachwa yeye dada mtu, kwahiyo alivyomaliza kula tu aliamua kwenda zake chumbani kwake, halafu pale sebleni bibi yake na mamake mkubwa walikuwa wakiongea,“Kwanza mama samahani, najua swala hili hulipendi hata kidogo ila sina budi kukuletea tena naomba msaada wako”“Swala gani tena?”“Mama, mimi ni dada. Mimi ndiye mkubwa wa hii familia na ndiye muhimili, natakiwa kusimama imara kwaajili ya wadogo zangu. Ni kweli Derrick kazaliwa nje ya ndoa ila bado ni mtoto wa baba yetu yani bado ni ndugu yetu, mama nahitaji msaada wako kama mzazi wetu”“Sasa msaada gani unataka kutoka kwangu”“Itakuwa vyema sana ukituita watoto wako wote hapa na kutufanyia kikao na sisi tuweze kuzungumza, nahitaji sana mimi na familia tushirikiane kumuokoa Derrick anahangamia mama. Yani Derrick ni tapeli haswaa na wala sio wa kusingiziwa”“Sasa, Mage jamani unaniingiza kwenye mambo yasiyonihusu kabisa. Hivi mimi ni mtoto wa baba yenu au kitu gani?”“Hapana mama ila wewe ni mama yetu, tafadhari mama nakuomba sana fanya hivi kwaajili yetu mama yengu jamani nakuomba sana”“Naomba nisikujibu kwa leo, nitakujibu siku nyingine ngoja nifikirie kwanza”Muda kidogo simu ya bibi Angel iliita basi aliipokea na kuongea nayo kw amuda kidogo, alivyokata alimuangalia mwanae na kusema,“Jamani, watu wengine wana majaribu sana. Eti wananipigia leo kuwa kesho kuna kitchen party na mimi natakiwa nikaongee jamani, sasa nitaenda kuongea nini? Na nitajiandaa muda gani? Haya ni makwazo sasa”“Mmmh mama jamani, hebu nenda tu. Itakuwa katika kufikiria huko wametambua kuwa kuna mama wa maadili hapa ndiomana wamekuita, wasamehe kw akukushtukiza tu ila nenda mama”“Aaaah washanichanganya tayari, ukiwa unaondoka naomba mwambie yule dada msusi wa barabarani aje anisuke kama hana mteja leo”“Mmmh utapendeza mama, hadi na kusukwa, sipati picha. Upige picha tu huko nije kuziona mie”Basi Mage alimuaga mama yake na kuondoka zake, na bibi Angel alienda kumpa Angel taarifa hiyo ila ilikuwa ni furaha kwa Angel kwani hakupenda vile bibi yake anavyomchunga sana.Familia ya mama Angel waliporudi nyumbani, moja kwa moja walifikia kula chakula na kukaa huku wakitafakari mambo mbalimbali wakati huo Erick na Erica walienda kuandaa vitu vyao vizuri maana kesho yake ilikuwa ni shule zinafunguliwa.Basi mama Angel alikuwa katulia tu na mgeni akafika pale kwao alikuwa ni Tumaini ambaye walianza kuongea nae,“Naona leo hakuna umbea uliowaambia watoto”“Mmmh wifi jamani, umbea gani mimi niliusema jamani!!”“Haya, tuachane na hayo, jana nilikuwa nakuja hapa ila nikaambiwa hampo, nilikuwa na ujumbe wako”“Ujumbe gani?”“Kuna mwalimu mmoja hivi alikuwa akimfundisha Angel pale nyumbani kwangu anaitwa mama Sarah, sasa juzi nimekutana nae, sijui ikawaje nikakuongelea akasema anakufahamu sijui mlisoma wote”“Mmmmh nani huyo?”“Mimi simjui jina lake ila najua tu jina la mama Sarah, ila namba zake zile zingine kabadili ndio kanipa kadi yake nikuletee ili awasiliane na wewe, anasema kuwa ana mengi sana ya kuongea na wewe”Basi Tumaini akatoa pochi yake ili aweze kutoa hiyo kadi ili amkabidhi mama Angel, ila alipekua na kushtuka kisha akajiuliza,“Mbona hiyo kadi siioni tena”“Kwani uliiweka wapi?”Tumaini akatafakari kwa muda na kusema,“Ooooh nimekumbuka, jana nilipokutana na Derrick aliniomba chenchi ya elfu kumi, nadhani wakati nampa ndio nikampa na kadi. Ila mmmh mbona na hela za kwenye hii pochi sizioni”“Kwani ulikuwa na pesa ngapi?”“Nilikuwa na laki moja kwenye pochi, naona hii elfu ishirini tu. Tatizo ni nini jamani!!”“Kwani Derrick ulikutana nae wapi?”“Nilikutana nae njiani wakati nakuja huku na ndiye aliyeniambia kuwa katoka huku pia ila hajawakuta”Kengele ikalia kwenye kichwa cha mama Angel kuwa Derrick lazima kamtapeli hadi Tumaini, yani alishangaa sana kwa Derrick kumtapeli Tumaini wakati alikuwa ni mtu wake wa karibu sana, ila alisikitika na kushindwa kusema chochote kwa wakati ule ambapo Tumaini nae akaendelea kuongea,“Jamani, jana sijafungua hii pochi muda mwingine wowote zaidi ya muda wa kumpa Derrick chenchi Derrick tu, inamaana nimekutana na chumaulete au?”“Pole sana”“Unajua sielewi, ngoja niende nyumbani kwangu”Yani Tumaini akaondoka muda huo huo.Basi mama Angel alienda kumueleza mumewe kuhusu tukio la Tumaini,“Yani nahisi aliyewatapeli wakina Juma ni huyo huyo Derrick tu”“Dah!! Huyo Derrick sasa ni tishio, bila kufanya kitu mapema itakuwa balaa, yani katoka kutapeli milioni tatu, halafu akaenda kutapeli elfu themanini dah!! Huyu Derrick amezidi sasa”Baba Angel alitulia kimya kwa muda kwanza akifikiria ni kitu gani anweza kufanya ili kumuokoa Derrick kutokana na ile tabia aliyojiingiza nayo.Usiku wa leo, Angel alikuwa akiwasiliana na Ally na kumwambia kuwa bibi yake kesho anaenda kwenye sherehe,“Oooh hilo ni swala zuri sana kwangu, basi kesho nitakuja kukuona ili tuongee mawili matatu”“Ila kama nilivyokwambia kuwa na mimi tutaongea kawaida tu, hakuna cha ngono”“Mbona nimekubali hilo Angel, mimi nakupenda na nipo tayari kukusubiri hadi umalize shule. Shida yangu ni kuongea na wewe tu”Angel alikubali, ila muda huo kulikuwa na jumbe kadhaa za kutoka kwa Samir, sema Angel hakujibu kabisa, basi Samir akatuma ujumbe mwingine,“Angel umenichunia ila sijui kosa langu kwako, sema siwezi kuacha kukupenda, nitakulinda siku zote, siwezi kuacha huyo fedhuli aharibu maisha yako. Mtu mwenyewe dereva wa bajaji, hana hadhi yako Angel jamani. Mimi ndiye mwanaume ninayekuafaa, nakupenda sana”Angel hakumjibu, ndio kwanza aliaendelea kuwasiliana na Ally kwani aliona Ally ni mwanaume mstaarabu sana na ni mwanaume anayesikiliza kwahiyo kwake ilikuwa ni vyema zaidi kuwasiliana na Ally.Basi muda wa kulala ulipofika aliona ni vyema kulala tu, kuhusu hii simu mpya ya Angel aliyokuwa nayo, bibi yake hakujua kabisa swala hili maana ile nyingine alikuwa akiiona tu chumbani kama kawaida.Kulipokucha, Erick na Erica walienda shuleni kama kawaida kwenye zile shule ambazo wanasoma, ila Erick alivyofika shuleni alipokelewa kwa shangwe kubwa sana na Sarah, yani Sarah alionekana kumfurahia sana Erick,“Halafu nina zawadi yako”“Mmmh zawadi gani?”“Nitakupa tu hata usijali ila nitakupa kesho, sema nilikukumbuka sana Erick jamani!”Erick alikuwa akicheka tu, na moja kwa moja alienda darasani ila Sarah nae alienda kwenye darasa lile lile alilosoma Erick na kumfanya Erick amuulize,“Jamani Sarah, wewe si unaingia kidato cha tatu?”“Unajua nini kilichotokea? Nitakwambia tu ila kwasasa jua kuwa tunasoma wote”“Ulifeli?”“Hapana, sijafeli na siwezi kufeli”“Sasa kwanini imekuwa hivi!!”“Siwezi kukaa mbali na wewe Erick, nipo tayari kurudia kidato”“Kheee mambo gani haya, sijawahi kusikia katika maisha yangu jamani!!”“Erick nawe jamani, mimi naweza kuendelea au kurudia ila ni wewe ndiye unayeweza fanya niendelee au nirudie”“Kwahiyo unataka nifanye kitu gani?”“Nitakwambia, usijali”Kiukweli Erick alikuwa akimshangaa sana Sarah, alimuangalia tu bila kummaliza.Bibi Angel alijiandaa na kuondoka zake, muda huu Angel alibaki nyumbani mwenyewe na muda kidogo tu akafika Ally kanakwamba alikuwa mahali akisubiri bibi Angel atoke tu, basi alifika ndani na kugonga kisha Angel akamkaribisha.“Kheee umejuaje kuwa bibi kashaondoka?”“Nimehisi tu Angel”Basi aliingia ndani kwakina Angel na kumkumbatia Angel ila Angel alijitoa na kumwambia,“Sio wakati sahihi wa kunikumbatia”“Wakati sahihi ni upi mpenzi wangu?”“Mmmh sipendi kukumbatiwa”“Haya yaishe, nimekuletea tunda kama ishara ya upendo wangu kwako, naomba ung’ate kidogo tunda hili”Basi angel alichukua lile tunda na kung’ata kidogo ila gafla alikuwa kama mtu aliyekunywa kilevi na kuanguka, basi Ally akamnyanyua ila wakati anataka kutoka naye tu alitokea Samir. Basi angel alichukua lile tunda na kung’ata kidogo ila gafla alikuwa kama mtu aliyekunywa kilevi na kuanguka, basi Ally akamnyanyua ila wakati anataka kutoka naye tu alitokea Samir.Ambaye hata hakuuliza na wakati huo huo kuanza kumshambulia Ally, ni alimpiga siku hii hadi Ally alianguka chini na kuanza kutoa damu puani, kisha Ally alijitahidi kuinuka na kumuacha Samir akimshughulikia Angel halafu yeye alitoka nje na kuondoka zake ingawa alikuwa kaumia vibaya sana maana Samir alimpiga hovyo hovyo bila kujali kitu chochote.Kisha Samir, akamlaza Angel vizuri kwenye kiti huku akijaribu kumpa huduma ya kwanza,“Umepatwa na nini Angel, amka mpenzi wangu.”Samir alijitahidi pale huku akiwaza moyoni mwake,“Kwani huyu kijana alitaka kumfanya nini Angel? Bibi yake Angel yuko wapi? Kwanini imekuwa hivi? Inamaana nisingetokea basi huyu kijana angekuwa kambaka Angel au? Kwanini Angel unaruhusu jambo kama hili katika maisha yako!”Basi Samir alikaa pale na Angel huku akimsikilizia Angel aweze kuamka maana alikuwa kama mtu aliyelewa sana kiasi kwamba haelewi kinachoendelea na hata akishtuka anaongea kilevi na kuendelea kulala yani hapo ndio palimchanganya zaidi Samir.Ukapita muda mrefu sana huku Samir akiwa amekaa huku kichwa cha Angel amekiegamizia kwenye miguu yake na kuwa kama akimbembeleza Angel aamke.Muda huu mlango ukafunguliwa, na kuingia bibi yake Angel, kulikuwa na zile damu zilizoanguka toka kwa Ally chini, na kumfanya bibi yake Angel asielewe kitu kabisa, pale sebleni alivyomkuta Samir kamlaza Angel vile halafu kuna damu damu pembeni yao hakuelewa, alimuangalia Samir kwa gadhabu sana,“Wewe mjinga, umebaka mjukuu wangu!”“Hapana bibi”Bibi alimuinua Samir na Angel kuachwa pale chini, yani bibi alikuwa na khasira sana kiasi kwamba alijikuta akichukua mwiko na banio jikoni kwake na vyote viliishia katika mwili wa Samir, ni alimpiga tena alimpiga sana na hakutaka hata kumuachia, kila Samir alipotaka kujitetea wala bibi hakuelewa jambo kwani yeye alipiga tu tena popote, na kumfanya Samir aanguke kisha akaenda kukanyaga mguu wa Samir na kufanya mguu ule uteguke, yani Samir akaona kuendelea kujitetea kwa huyo bibi ni kujitafutia balaa, basi akajikongoja na kufanikiwa kujiengua toka mikononi mwa yule bibi, yani bibi Angel alikuwa na hasira sana.“Kambaka mjukuu wangu hadi kazimia!! Hivi Angel akipata mimba hapa nitasemaje mimi?”Bibi akambeba Angel hadi chumbani kwake, akamvua nguo zote na kumkagua, akakuta mjukuu wake hakuingiliwa kimwili ni hiasia zake tu sababu aliona zile damu pale chini kwenye sebule yake na hakujua kuwa zile damu ni za kitu gani.Basi akamchukua mjukuu wake na kwenda kumuogesha, alipofanya vile tu ikawa Angel karudiwa na ufahamu wake huku akishangaa kuwa ni kitu gani kimetokea, alishangaa kwa muda na kumuuliza bibi yake,“Kwani nini bibi?”“Aaaah sielewi, pia, wewe mtoto utaniua kwa presha. Hizo shule na zianze tu maana siwezi kwakweli”Kisha bibi alimuacha Angel apumzike maana hata alipokuwa akimuuliza naye Angel alikuwa haelewi, basi bibi alimuacha na kwenda kufunga milango yake vizuri na kwenda kulala huku akitafakari kuwa ile hali sio hali ya kawaida kabisa kwake, yani kuna kitu kingine aliwaza, na kumfanya akose raha kabisa.Kulipokucha, Angel anajifikiria pia kuwa ni kitu gani ambacho kimetokea ila hapati jibu yani kama kumbukumbu zake, zimefutika hivi. Mara akapokea ujumbe toka kwa Samir,“Unaendeleaje Angel? Mimi naumwa sana mguu, unanivuta sana kutokana na kile kipigo nilichopata jana toka kwa bibi yako, ila bado nakupenda sana Angel”Pale ndio Angel akashtuka kusikia kuwa Samir kapigwa sana, basi akamuuliza,“Unajua Samir sielewi kitu, naomba nieleweshe kwani imekuwaje? Ulikuja muda gani huku kwetu hadi bibi akakupiga?”“Ipo hivi Angel, mimi nilikaa nyumbani ila nilijiona nikikosa amani kabisa katika moyo wangu, nikasema lazima nije nikuone bila kuhofia uwepo wa bibi yako wala nini. Nimefika hapo kwenu na kukuta ni kimya sana, sijui ni kitu gani kilichoniambia kuwa niingie ndani kwenu bila kugonga sehemu yoyote, nikamkuta yule mwanaume wa siku ile ambaye alisema ni mpenzi wako kakubeba halafu hujitambui kabisa, sijui alitaka kukupeleka wapi ila mimi niliingiwa na hisia mbaya sana jumlisha na wivu, nilihisi alitaka kukubaka kwani alionekana kuwa na uchu sana na wewe, basi nilipata hasira sana na kuanza kumpiga hadi mwisho alikimbia, ukabaki wewe na mimi, nikajaribu kukuamsha wapi hukuamka wala nini kwahiyo nilikaa na wewe hapo sebleni kwenu. Nikijaribu kukubembeleza na kufanya kila ninachojua ili uamke, ndio akatokea bibi yako ambaye naye alinihisi vibaya, kwakweli kanipiga vibaya mno sijategemea kuwa huyu bibi ndio angenipiga kiasi hiki jamani!!”“Kheee pole jamani Samir, pole sana”“Asante, ila na wewe unaendeleaje?”“Mimi naendelea vizuri kabisa, pole Samir na asante kwa kuniokoa”Basi Angel aliwasiliana na Samir na kuonyesha kuwa anamuhurumia sana, ila kuna tukio la mwisho alilikumbuka, akakumbuka kuwa Ally alimpa tunda ambapo alipoling’ata tu alipatwa na usingizi wa ajabu, basi hapo akawaza kuwa huenda Ally kuna kitu aliweka kwenye lile tunda ndiomana lilimfanya vile, hakutaka kumtafuta Ally wala kuongea nae kuhusu kitu chochote kile.Leo, wakati Erick yupo darasani, Sarah nae alikuwa katika darasa lile kama jana yake tena alikuwa karibu kabisa na Erick, kwakweli Erick hakupenda kwani alijua wazi hata itakapofikia kwa dada yake yani Erica kuhamishiwa hapo basi hatopenda ule ukaribu wake na Sarah, kwahiyo akajaribu kuongea nae ili aende kwenye darasa lao kama kawaida,“Sarah, niambie ni kitu gani unataka nifanye ili uweze kuendelea na kidato unachosoma?”“Nahitaji uniambie kuwa unanipenda, basi nitaweza kusonga mbele maana mimi ninakupenda sana”“Lakini Sarah, hivi unajijua kuwa wewe nib ado mdogo na hutakiwi kuwa na mawazo ya namna hiyo kabisa”“Mimi sio mdogo, naweza kuwa mdogo wa umri ila sio mdogo wa mawazo na akili. Mama yangu ananifundisha kuwa halisi na kuishi maisha yenye uhalisia, kwahiyo siwezi kuwa kinyume na uhalisia, nakupenda tena sana na ninahitaji na wewe unipende vile vile.”“Kwahiyo nikikwambia nakupenda ndio utaweza kuendelea na kidato cha tatu?”“Ndio, naomba unipende Erick”“Basi nakupenda, naomba uendelee na masomo yako, usifanye makosa ukaja kujutia milele”Yani Sarah alihisi raha sana kuambiwa na Erick kuwa anapendwa, basi alimkumbatia kwafuraha na hapo akakubali kuondoka kwenda kwenye darasa lingine, ila Erick alikuwa akimshangaa sana, alishangaa mno kuwa Sarah anatoa wapi kiburi cha kufanya kile alichokuwa anakifanya, basi kuna mwanafunzi mmoja alimfata Erick na kumwambia,“Unabahati sana ya kuongea na huyu binti?”“Kwani huwa haongei?”“Hapana, ila anachagua sana watu wa kuongea nao kutokana na kwao kuwa na hadhi”“Kivipi?”“Hii shule ni ya babu yake Sarah, halafu mama yake Sarah ni mtoto wa kipekee sana kwao na hivyo kuishi maisha Fulani na huyu Sarah ya kumdekeza sana, unavyomuona huyu Sarah hakuna mwalimu hata mmmoja anayemfokea wala kumpiga wala kumpa adhabu na ndio hivyo hivyo anavyoishi kwao, kwakweli unabahati sana. Nilikuwa nasikia maongezi yenu, una bahati sana ya kupendwa na huyu binti, kwanza ni mzuri, kwao wana hela, ana umbo zuri na mcheshi. Ukimuacha binti kama huyu basi kutakuwa na kitu unakitafuta”Erick alimuangalia huyu mwanafunzi na kutokumjibu kwa muda huu kwani angeyajua mawazo ya Erick wala asingejisumbua kuongea maneno mengi vile kuhusu Sarah.Baba Angel wakati anakamilisha kazi zake, akafuatwa ofisini na rafiki yake juma na kumkaribisha vizuri tu kisha akaanza kuongea nae,“Karibu, na pole sana kwa yaliyokupata nyumbani kwangu”“Dah!! Erick umenifanyia dhambi sana ni bora ungeniambia mapema kuwa haiwezekani kuliko kwa nililolipata nyumbani kwako. Ila cha kwanza kabisa, Erick mdogo anaendeleaje?”“Anaendelea vizuri tu”“Kwahiyo yupo kiwandani kwasasa?”“Hapana, unajua shule zimefunguliwa nimeacha mwanangu aende shule, kiwandani atakuwa anaenda mara moja moja”“Unajua kuna wakati unachekesha sana Erick, hivi unashindwa nini kufikiria lasilimali ambayo Mungu amekupatia? Ndio kwanza wiki hii wamefungua shule, mara nyingi huwa wiki hii haichanganyi sana na masomo, mimi nilijua utamuachia wiki hii kiwandani halafu wiki ijayo ndio aanze shule, ila hata angeanza shule bado kungekuwa na nafasi nzuri tu ya yeye kwenda kiwandani hata kukaa kwa nusu saa kiwandani ni jambo jema kwake. Usipoteze hiyo bahati”“Juma sikia, mimi nawapenda sana wanangu. Najua mali zote nilizokuwa nazo bila elimu ni kazi bure, kwahiyo ni bora mwanangu apate elimu kwanza”“Yani mimi ndio ningepata hazina hii basi Mungu anajua ni jinsi gani ningeitumia, haya elimu ni muhimu ngoja nikuulize ni kwanini watu wanasoma?”“Ili kuondokana na ujinga”Juma akacheka kwa muda na kusema,“Ngoja nikwambie, nenda chuo chochote uliza hata watu kumi kwanini wanasoma. Asilimia kubwa watakwambia ili wapate kazi nzuri na walipwe vizuri badae, wengine watakwambia ilia pate heshima kuwa ni msomi. Hakuna anayesoma na kusubiri kukaa kukaa tu bila kazi, nenda kwa wasomi wasiokuwa na kazi utawakuta wapo kuilalamikia serikali, nimesoma lakini hakuna ajira, bora hata nisingesoma. Hakuna mtu anayepoteza muda wake shuleni halafu asipate kitu, kwahiyo tunasoma ili tupate kazi nzuri na kupata hela. Sasa Erick yupo vizuri kichwani, ana mawazo mazuri, kwanini bado unamng’ang’aniza na shule? Muache afanye maujuzi yake uingize kipato”“Juma, nisikie kwanza, unajua mimi nilipoanza na mke wangu kipindi yeye kamaliza chuo na mimi nilikuwa na pesa sana, kiukweli niliumia sana moyo ni kweli nina pesa lakini mke wangu kanizidi elimu, sitaki jambo kama hili lijirudie kwa watoto wangu. Kuna kipindi mimi nilikuwa naendelea na biashara zangu huku najiendeleza kielimu, yani ukisoma akili inapevuka na unawaza mambo makubwa zaidi, ni kweli unaweza kuwa na mawazo mazuri ila yale mawazo yako yaongezee na elimu kwa hakika utayafurahia sana. Kwa upande wangu mimi bado elimu ni bora sana”“Amakweli upele hukuota asiye na kucha”“Hebu tuachane na hayo, haya niambie ulitapeliwa vipi milioni tatu?”“Dah!! Yani hadi aibu, yule mtu alisema yeye ni mnajimu anashghulika na maswala ya nyota na kusema kuwa kwa siku ile nyota kwa upande wetu imekaa kimafanikio, na chochote nitakachotoa kwa nyota basi nitapata mara kumi sababu nyota ya siku hiyo kwa upande wangu ilikuwa katika asilimia kumi. Unajua mwanzoni nilikuwa na mashaka naye, ila akasema kama una elfu kumi hapo lete nikuonyeshe jinsi nyota itakachokujibu leo. Basi tukampa elfu kumi na akaiinua juu na kusema naomba nyota mtu huyu mjibu muda huu ya kuwa unatoa asilimia kumi, cha kushangaza kabisa kwenye mfuko wangu ikapatikana laki moja, kwenye mfuko ule niliotoa elfu kumi,kiukweli nilitamani sana. Ndipo tulipoamua kutoa ile milioni tatu ndani ya gari tukitarajia kupata milioni thelathini, aliuliza tunakaa wapi tukamtajia, basi akaichukua ile milioni tatu na kuipandisha juu akasema ewi milioni tatu sikia kwa nyota ya leo inayozalisha asilimia kumi basi naomba ukamzalishie huyu mtu aliyetoa kwa moyo wake. Wakifika tu nyumbani kwao basi hiyo milioni tehalathini ipatikane kwao, tulifurahi sana na pale alituambia tukae kama dakika tano ndio tuondoke, basi tulikaa pale dakika tano wakati yeye kaondoka ndipo na sisi tulipoondoka, tuliporudi nyumbani ndio tulijua kuwa tumetapeliwa maana haikuwepo milioni thelathini wala ile laki moja nayo haikuwepo”“Dah!! Pole sana, huyo jamaa nadhani anatumia mazingaombwe. Nakumbuka kipindi kile shule ya msingi kuna majamaa walikuwa wanakuja shule mnachanga kiingilio kwenda kuwaangalia, basi mara wanaonyesha mtu kala ndizi moja halafu anaanza kujisaidia ndizi, au karatasi zinachanwa chanwa kwenye kopo halafu zinageuka na kuwa hela. Dah pole sana ndugu yangu jamani”“Asante nashukuru, basi hayo ndio yaliyonipata hapo nyumbani kwako, ila ngoja niondoke kwa muda huu kuna mahari nataka kuwahi. Ila ndugu yangu itabidi unichangie nusu hasara”“Ngoja nikajadiliane na mke wangu kuhusu hilo”“Duh wewe jamaa yani, kila kitu nikajadiliane na mke wangu, ila hata mimi ningemuoa Baby nadhani ningekuwa hivyo hivyo. Kwaheri”Basi Juma akaondoka zake na kumuacha baba Angel akiendelea na kazi zake zingine.Baba Angel aliporudi nyumbani kwake anaamua kumueleza mkewe kuhusu kisa kilichompata Juma na mke wake hapo nyumbani kwao, kwakweli hata mama Angel anasikitika sana na kusema,“Inamaana Derrick kafikia hiyo hali ya kutapeli kwa mazingaombo?”“Ndio, unadhani bila mazingaombo atawapata wangapi wa kuwatapeli, lazima awadanganye kidogo ili wamuamini halafu awatapeli. Ila mke wangu huwa siku zote ndio inavyokuwaga ukitaka kupata pesa ya bure bila kuifanyia kazi ndio mambo kama haya unatapeliwa, yani wapi hapo unaweka milioni tatu unapata milioni thelatini jamani!! Tena ndani ya wiku moja, tamaa ndio inayofanywa tutapeliwe. Nadhani sasa utakubaliana na mimi”“Ni kweli tamaa ila tamaa imeletwa na hali ngumu ya maisha”“Hata kama, inatakiwa mtu ujiulize kwanza, yani naweka milioni tatu Napata milioni thelathini? Ipo siku atakutana nao tena na kuwaambia kuwa siku hiyo nyota inazalisha kwa asilimia mia moja, ukiweka milioni tatu unapata milioni mia tatu, na bado kuna watakaomuamini na kuwekeza kwake kwenye mazingaombwe. Kwakweli Mungu atusaidie tu. Watoto wanaendeleaje mke wangu?”“Wapo salama, walienda shule vizuri na wamerudi vizuri”“Erick alisema kwasasa yupo tayari kusoma na Erica, nimekosa tu muda wa kuwahamisha”“Aaaah waaache hivi hivi hata usisumbuke, kama kusoma wanasoma tu vizuri hakuna tatizo, mimi naona ni vyema sana wanavyosoma hizi shule tofauti kumbuka Erica ni mbea sana anaweza akamkwaza kaka yake bure”“Ngoja wakisema tena basi ndio nitalifanyia kazi ila kwasasa wacha niwaache tu wasomo walivyozoea.”Kwa muda huo waliamua tu kulala kwani ilikuwa ni usiku tayari.Kulipokucha tu, baba Angel anajiandaa zake kama kawaida mapema kabisa na kumuaga mke wake ila leo anamuuliza,“Nikuletee zawadi gani?”“Mmmh!! Niletee gauni”“Ooooh umechagua gauni, basi hakuna tatizo nitakuletea mke wangu”Basi anambusu na kuondoka zake, ila muda huu watoto nao ndio waliondoka kwenda shuleni, basi baba Angel alipotoa gari lake nje ya geti kuna mtu alimuona kajibanza pembezoni mwa ukuta wake, basi akatoka kwenye gari na kumfata mtu huyo akamkuta ni Sia,“Una nini lakini wewe mwanamke? Ni kitu gani kinakuleta kuja kuchungulia nyumbani kwangu?”“Naomba unisamehe bure tu”Halafu leo Sia hakuongea maneno mengi kwani muda huo huo aliondoka zake na kuamuacha baba Angel akimuangalia tu huku akimsikitikia.Leo madam Oliva, anaamua kwenda na Steve madukani ili kumfanyia manunuzi ya baadhi ya vitu kama nguo, na kweli walibahatika kupata walichokuwa wanakitaka, ila wakati wanaondoka walikutana na Dora ambaye alichukia sana na kuanza kusema,“Hivi wewe Steve mdogo wangu akili yako lini itakuwa jamani!! Kwanini wanawake wanakuvuta na madawa kila siku, yani wewe umekuwa ni mtu wa kuvutwa na madawa tu kwanini lakini?”“Sijavutwa na madawa mimi ila nimempenda mwenyewe, ni mimi ndiye niliyeanza kumpenda Oliva kwahiyo hayo madawa unayasema wewe”“Kwahiyo unaona raha mwenyewe kwa hayo maisha ya kwenda kufanyiwa shopping na mwanamke wakati wewe ndio unatakiwa kufanya hivyo. Hivi unajiita mwanaume kweli kwa hali hiyo!”Madam Oliva naye akaongea,“Wifi jamani usiwe na jazba kiasi hiko, kaka yako akimpenda mtu unatakiwa na wewe kukubali sio kupinga tu muda wote, haya unapinga umemtafutia kaka yako mwanamke wa kuwa nae? Unajua mara nyingine unapinga ila fikiria maisha ya hao watu. Steve ananipenda na mimi nampenda kwani tagtizo liko wapi tukiwa pamoja? Tatizo liko wapi tukiamua kuoana? Yani unataka tu kukuza mambo ila haya ni mambo ya kawaida kabisa, acha kuwa na mawazo mgando ndugu yangu, wivu kidonda ukizidisha utakonda”“Kwahiyo mimi nina wivu?”“Acha hizo jamani wifi”Kisha madam Oliva aliondoka na Steve na kwenda kupanda gari yao na kuondoka zao, kwakweli Dora alibaki akiwaangalia kwa gadhabu tu ila kuna kitu alifikiria na kusema,“Sikumpenda James, ila niliamua kumkomesha sababu yeye alinikomesha kwa kunilewesha na kunibaka na kunikana kwa watu kuwa hawezi kuwa na mwanamke kama mimi. Nikaamua kumkomesha na kumuendea kwa mganga ambapo nilichukua dawa na kumuwekea, alipoitumia akanipenda sana kiasi hata mkewe alipotaka talaka ilikuwa jambo rahisi tu, na hadi mimi na yeye tuakaamua kuoana na hadi sasa nina mtoto naye, kwakweli haya mambo ni makubwa ila yanawezekana. Kiukweli nimeumia ila nadhani hata ndugu wa James kwa kipindi kile waliumia sana tu, inatakiwa sijui nifanyeje jamani. “Aliongea kwa muda na kauamua kuondoka eneo lile.Baba Angel alipotoka ofisini tu ikawa kama ambavyo alipanga kuwa anaenda kumtafutia mkewe zawadi, basi akaenda kwenye duka lile na aliposema anahitaji gauni kwaajili ya mke wake ikawa kama kawaida baba Emma alimchagulia gauni na kufurahi akalilipia pale kisha akaondoka, ila leo baba Angel akatafuta duka lingine linalosifika kuuza nguo nzuri sana za wanawake, basi alienda huko na kuchagua gauni zuri sana na lenye rangi nzuri na kila mmoja pale dukani alisifia kuwa ile nguo ni nzuri sana, akailipia na kuondoaka nazo, alitaka na siku hii mkewe aende kuchagua ilia one mkewe atachagua nguo ya aina gani.Baba Angel alifika nyumbani na kumkuta mkewe katulia tu kama kawaida na kuanza kuongea nae,“Za hapa mke wangu?”“Ni nzuri tu, ila leo alikuja Derrick”“Mmmh umemwambia mambo anayoyafanya”“Siwezi ujue, yani mimi huwa siwezi hata kuongea na yule mtu, huwa najionea kichefuchefu tu. Ila mbona Derrick anakutafuta sana kuna ajenda gani kati yako na yake au unataka kumpeleka auze duka kule?”“Aaaah hapana mke wangu, ila niliwahi kumwambia kuwa nina maongezi nae, sasa kwa tabia zake hizo za kitapeli sitaki hata afike ofisini kwangu asije akatapeli wafanyakazi wangu bure”Mama Angel alicheka kiasi na kumuuliza mume wake,“Eeeeh zawadi yangu iko wapi?”“Nimeleta magauni mawili, ila nahitaji uchague moja uvae halafu usiku wa leo twende matembezi”“Jamani na mtoto atabaki na nani?”“Kwani wakina Vai wanafanya nini? Watabaki na mtoto kwa muda wakati wazazi tumeenda kutembea”Basi mama Angel alicheka tu, na muda huo baba Angel alitoa zile gauni, ila macho ya mama Angel yalikuwa kwenye lile lile gauni ambalo mumewe kalinunua toka kwenye duka la baba Emma, akasema,“Nitavaa hili gauni, nina uhakika litanipendeza sana”“Oooh, kwanini usivae hili lingine basi. Hujalipenda au?”“Hapana, nimependa zote mbili ila mtindo huu umenivutia zaidi”Mama Angel alijaribu lile gauni na kweli lilimpendeza sana kama alivyotarajia, basi mumewe alimwambia kuwa ajiandae ili siku hiyo watoke hapo nyumbani na kwenda mahali kupata chakula cha usiku.Mama Angel na baba Angel walijiandaa kisha wakatoka zao na kwenda kupata chakula cha usiku hotelini kwa siku hiyo, huko baba Angel alimuuliza baadhi ya maswali mke wake kwani kuna vitu vingi alikuwa akijiuliza kuwa kwanini mkewe alipenda sana zawadi alizotoka nazo kwa baba Emma? Basi alimuuliza,“Hivi kuna kitu unapenda mke wangu halafu mimi sijui?”“Mmmh sidhani sababu vyote ninavyovipenda unavijua mume wangu, ona kama gauni hili lilivyonipendeza”Baba Angel alitabasamu tu ila kiukweli hakuwa yeye ambaye anamchagulia mkewe zile zawadi za kuvutia ila alikuwa ni baba Emma.Basi alizidi kumwambia pale ni jinsi gani anampenda,“Unajua nakupenda sana mke wangu, nahitaji kuwa nawe siku zote za maisha yangu”“Hunifikii mimi kwa jinsi nikupendavyo Erick”Mara pembeni yao kuna mtu alienda akakaa, wakashtuka kidogo, na kuamuangalia yule mtu alikuwa ni Rahim ambaye alitabasamu na kuwaambia,“Nawaona wapendanao, hivi huwa hamchoki kupeana ahadi za mapenzi kila siku? Najua ipo hivi watu mkiwa katika ndoa mnachokana kwa haraka sana ila mnaishi kwa mazoea tu, ila nyie hamchoki jamani, halafu wewe Erica si una mtoto mdogo wewe ila umefanikiwa kumuacha nyumbani na kuja hotelini na mumeo kuendelea kupeana ahadi zisizoisha za mapenzi, nadhani na mwanangu naye wakati mdogo ulikuwa ukimfanyia kama hivi, yani wewe mwanamke una laana”Ila leo sio baba Angel wala mama Angel ambao walimjibu kwani baba Angel aliinuka na kumshika mkono mkewe kisha akaondoka nae hadi nje na kupanda kwenye gari wakianza safari ya kurudi nyumbai kwao.“Bora turudi tu mke wangu, siku yetu isiharibiwe na mwehu mmoja”Basi moja kwa moja waliamua kwa muda huo kurudi nyumbani tu.Usiku wa leo, Angel aliamua kumtumia ujumbe Samir ili kujua hali yake kutokana na kile kipigo alichopewa na bibi yake,“Unaendeleaje Samir?”“Naendelea vizuri ila mguu unaniuma sana yani sina hata amani sababu ya mguu”“Dah!! Itabidi uende hospitali basi”“Nitaenda tu, ngoja nijisikilizie”“Hapana usiniambie hivyo, nataka kesho nikikupigia unipe majibu kuwa umeenda hospitali, sawa”“Haya nimekuelewa mama, una amri kama mjeda vile”Angel akacheka na kumwambia,“Hahahah, mjeda tena bila amri utatekeleza kweli wewe!! Nataka kesho uende hospitali Samir tafadhari”Basi Samir akapiga simu na wakaanza kuongea kwenye simu sasa,“Unaona hata sauti yako inaonyesha kuwa unaumwa?”“Hapana bhana, hii ni sauti ya usingizi tu. Nilitaka kusikia na sauti yako wewe ya usingizi tu”“Ila kesho nenda hospitali”Basi akaagana nae na kukata simu, muda huu bibi Angel alikuwa kwenye mlango wa Angel kwahiyo alisikia akiongea na ile simu kwakweli alisikitika sana kiasi kwamba hakujua ni kitu gani afanye na Angel, kwani simu ile ipo chumbani kumbe mwenzie ana simu nyingine.Samir leo, aliamua kwenda hospitali kama alivyoongea na Angel, na kweli alienda na kupatiwa matibabu ila wakati anatoka pale hospitali kuna mwanamke alimuona, huwa hampendi huyu mwanamke kabisa kwani anaona kuwa anafatilia sana maisha yao, basi akaamua kumfata kwa nyuma kuona kama ndio mwenyewe.Na kweli alimuona kuwa ndio yule yule mama asiyempenda, basi akamfatilia nyuma akamuona kaingia wodini kuona wagonjwa, basi akamfatilia na kukuta yule mwanamke kaenda kumuona Ally ambaye alikuwa amelazwa. Na kweli alimuona kuwa ndio yule yule mama asiyempenda, basi akamfatilia nyuma akamuona kaingia wodini kuona wagonjwa, basi akamfatilia na kukuta yule mwanamke kaenda kumuona Ally ambaye alikuwa amelazwa.Moja kwa moja Samir alijua kipigo alichompa yule Ally ndio kimemfanya alazwe, basi alikaa mahali akimsubiri yule mama atoke kumuona Ally kwanza, na alipotoka tu akamfata nyuma na kumsimamisha,“Wewe mmama wewe, una nini lakini?”“Kuna na adabu wewe mtoto, mimi ni sawa sawa na mama yako”“Kumbe wewe ndio umemtuma huyo Ally kwa Angel!! Kwani una matatizo gani wewe mama jamani!”“Inamaana wewe ndiye uliyempiga Ally!! Hivi unajua wewe huna akili kabisa, unapigana na Ally kumgombea dada yako, mimi nataka nikusaidie wewe ili usitembee na dada yako ila akili zako ni mbovu kabisa”“Nani dada yangu sasa?”“Huyo Angel ni dada yako kama hujui, wewe na Angel baba yenu ni mmoja”“Kheee wewe mama vipi una wazimu nini? Angel ana baba yake na mimi nina baba yangu, hatuwezi kuwa ndugu”“Nikatalie ila huo ndio ukweli, baba yako wewe ndiye baba mzazi wa Angel, usione Angel anaishi vile ukadhani yule anayeishi nae ni baba yake mzazi, hapana, yule ni baba mlezi tu”“Wewe umejuaje?”“Mimi ni mtu mzima, mambo mengi sana nayajua sababu umri wangu unaniruhusu kujua mengi. Nakwambia lile lililokuwa kweli, siku zote Angel kafichwa ukweli huu sababu wazazi wake hawataki wajue kuwa yule anayeishi nae sio baba yake mzazi, kwa kifupi baba yako wewe ndiye baba mzazi wa Angel”“Ila kuna kitu hukijui pia kuhusu mimi”“Kitu gani?”“Sitakwambia ili uendelee kutokukijua, ni mimi peke yangu ninayekijua. Kwa kifupi ni kuwa Angel sio dada yangu na nitaendelea kumpenda siku zote za maisha yangu, na wewe utakuwa shahidi wa ndoa yetu!”“Unajua una kichaa wewe, kwahiyo huamini kama Angel ni mtoto wa baba yako?”“Awe mtoto wa baba, asiwe mtoto wa baba sijali kitu ninachojali ni kimoja tu kuwa nampenda sana. Kwahiyo hiyo habari yako achana nayo kabisa, kwahiyo unamfatilia Angel pia ili kumueleza kuwa yeye na mimi ni ndugu? Unachekesha sana wewe kimama ndiomana umeshupaa kama unakula saruji, kione vile”Halafu Samir akaondoka zake, alipofika kwao tu akampigia simu Angel ambaye alipokea muda ule ule,“Angel, unamkumbuka yule mama ambaye nilimzaba kibao nje ya geti lenu?”“Namkumbuka ndio”“Basi yule mama ndio yupo shirika moja na huyo Ally, kwa kifupi ni kuwa yule mama sio mgtu mzuri. Yeye kawaida yake ni kugombanisha watu tu, nyumbani kwetu mama yangu hataki hata kumuona yule mwanamke, yani yeye kugombanisha watu ndio anaona fahari yake. Kwahiyo ndio inaonekana kamtuma Ally kukuwekea dawa kwenye tunda, na lengo la Ally lilikuwa ni kukubaka”“Kheee jamani!! Asante Samir kwa kuniokoa sijui ningekuwa katika hali gani mimi baada ya kubakwa”“Pole sana, ila bibi yako hajanielewa kuwa mimi sikuwa na nia mbaya na wewe. Kwanza siwezi kufanya chochote na wewe bila ridhaa yako, yani bibi hakunielewa tu, sipo hivyo alivyodhani”“Masamehe bure bibi yangu, hakujua kama umenisaidia maana sijui ingekuwaje jamani!!”Basi aliongea nae na kukata ile simu.Mara mlango wa chumbani kwa Angel ulifunguliwa na bibi yake ndio aliingia mule ndani, kiukweli Angel aliogopa sana ukizingatia ni muda mfupi tu ametoka kuongea na simu, ila bibi yake alifika na kukaa pembeni yake kisha kuanza kuongea nae,“Angel mjukuu wangu, najua kama kusema nishasema sana, kama kukuchunga nishakuchunga sana na kama kukupiga nishafanya hivyo. Ila kwa muda huu naomba uniambie ukweli wa hiyo simu nyingine, usinifiche jambo tafadhari”“Bibi samahani, nitakwambia ukweli wote. Nilichukua ile simu nyingine chumbani kwako bila ruhusa yako, ila simu ile ilianguka na kupasuka kioo, basi nikamwambia Samir na akaahidi kunitengenezea na nikamwambia Ally pia nae akaahidi kunitengenezea”“Kwahiyo ukategesha huku na huku?”“Hapana bibi, mimi nilisema tu ila mwisho wa siku ni Ally ndio alipata hela ya kunitengenezea”“Ikawaje?”Yani leo Angel alimueleza bibi yake kwa ukweli wote, hadi alivyoondoka na Ally kwenda kwa fundi na jinsi Samir alivyompiga Ally, na jinsi yeye alivyochukizwa na kitendo kile, na jinsi alivyoahidiana na Ally kutembelewa na yale yaliyotokea.“Oooh naona umekuwa sasa mjukuu wangu, hadi umeacha uongo!! Sifa kwa Mungu, haya sasa ngoja nikuulize swali lingine, kati ya Ally na Samir unampenda nani?”“Kiukweli bibi mimi nampenda Samir maana kasema yupo tayari kunisubiri hadi nimalize shule”“Ila unajua kama hayo ni maneno ya kawaida kwa wanaume? Ila sina shida sana na huyo Samir kwani bibi yake namfahamu hata mama yake namfahamu ila huyo Ally naomba uwe nae mbali kabisa”“Kwahiyo bibi umeniruhusu niwe na Samir?”“Mjinga wewe, siwezi kukuruhusu huo ujinga hata mara moja, hapa nilipo nawaza tu cha kufanya na wewe kuhusu hizo simu maana ndio zinazochanganya akili yako”Basi Angel akamueleza pia kuhusu mwanamke ambaye Samir kamuona hospitali na kusema yupo shirika moja na Ally,“Huyo mwanamke ni nani?”“Simjui ila hata nyumbani huwa hawampendi kabisa, Samir anasema huyo mwanamke ni mbea sana na anapenda kufatilia mambo ya watu”“Basi nitamjua tu hakuna tatizo, ila bado nafikiria cha kukufanya na hizo simu. Ila bora tu urudi shule wewe maana naona utanitia kichaa bure jamani”Angel alikaa kimya tu, ila hakuamini siku hiyo kwamba hakufokewa na bibi yake wala hakupigwa licha ya simu aliyomkuta nayo.Erica alikuwa anakaribia kutoka shule, alifika rafiki yake Samia na kumsisitiza kuhusu Junior kumpatia yeye pesa,“Mmmh Junior nae, ana tamaa sana yule halafu muhuni sana”“Namjua vizuri yule kaka yako halafu mimi simpendi wala nini, yani simpendi kabisa”“Tena uwe unamshushua kabisa”“Ila nina ujumbe wangu huu naomba ukamkabidhi Erick”Samia alimpa Erica ule ujumbe ambapo ulikuwa ndani ya bahasha, na juu ya bahasha hiyo iliandikwa Erick, basi Erica alikubali kuwa barua hiyo ataifikisha,“Nitafurahi sana ukimpatia ujumbe wangu huo, halafu mwambie kuwa nasubiria barua kesho toka kwake kwahiyo atakuagiza wewe”“Sawa, hakuna tatizo”Erica aliiweka ile barua ila kiukweli alitamani sana kujua ni kitu gani kilikuwa kimeandikwa kwenye ile barua, alitamani sana afike nyumbani mapema ili aangalie kuna ujumbe gani.Erica alipofika nyumbani tu, cha kwanza alienda chumbani kwake na kabla hata hajavua zile sare za shule alifungua kwanza ile barua na kuanza kuisoma,“Kwako Erick, najua utastaajabu sana kwa hii barua yangu fupi, inawezekana si kawaida kwako kuambiwa na mwanamke neno nakupenda, kwakweli nimevumilia sana ila nimeshindwa, nakupenda sana Erick, nahitaji uwe mpenzi wangu. Tafadhari naomba unijibu”Basi Erica alisoma mara mbilimbili na kusema,“Kheee hivi huyu Samia ana wazimu au kitu gani? Yani kabisa kaka chini na kuandika barua kama hii kwa Erick jamani!! Sasa ngoja nimjibu, mjinga kabisa huyu msichana”Akachukua peni na karatasi na kuanza kuandika jibu kwa Samia, ila alijifikiria na kusema,“Ila Samia atasema mbona muandiko sio wangu?”“Ngoja nikampelekee Erick mwenyewe aamue mwenyewe, akikubali tu basi nauvunja undugu leo”Akatoka chumbani kwake na moja kwa moja akaingia chumbani kwa Erick ambapo alikuwa akibadilisha nguo, yeye mwenyewe Erica alipoingia alishtuka na kumwambia“Jifunike jamani Erick”“Na wewe kwanini unapenda kuingia chumbani kwangu bila hodi!”“Mmmh yani hadi mimi nigonge hodi jamani!! Sijazoea hayo”Basi Erick alijifunga taulo na kukaa ili kusikiliza ujumbe ambao umeletwa na Erica,“Samahani, Samia kanipa barua yako ila sijaweza kuvumilia nimeifungua na kuisoma ndio nimekuletea, naomba nisamehe”“Ingekuwa siijui tabia yako ya umbea sawa, ila naijua fika tabia yako”“Jamani Erick, ndio maneno gani hayo!!”Erick alichukua ile barua na kusoma ule ujumbe, alisikitika sana na kumuangalia Erica kisha akamuuliza,“Nishauri nimuandikie jibu gani?”“Sina ushauri ila usirogwe kukubali maana leo nitavunja undugu baina yetu”“Kwanini sasa?”“Kwanini!! Inamaana umesahau ahadi yetu au!!”“Ahadi yetu naikumbuka, ni kuwa nisiwe na rafiki wa kike na wewe usiwe na rafiki wa kiume, haya huyu sio rafiki anaomba kuwa mpenzi. Kwani wewe unaweza kuwa mpenzi wangu?”Erica alichukia kwa swali hilo, aliinuka na kuondoka zake na kumfanya Erick ajue kuwa amemkera kwa swali alilomuuliza.Baba Angel leo wakati anarudi nyumbani kwake, alimuona Derrick njiani, tena akiwa amesimama na mtu yani hapo akili ikamcheza kuwa Derrick anataka kumliza mtu huyo, basi akasimamisha gari, akashuka na kumfata karibu halafu akamuita yani Derrick alishtuka kama mtu aliyeshtuliwa toka usingizini kiasi kwamba hata hakuweza kuongea tena na yule mtu ila Erick alimvuta mkono pembeni na kuongea nae,“Derrick, hiki unachokifanya sio kabisa na kitakupeleka pabaya”“Najua ushasikia vingi kuhusu mimi, hata wewe unaweza kuwa mmoja kati ya watu wanaonichukia”“Sikuchukii kabisa, na nikuchukie kwasababu ipi? Naomba twende mahali tuongee kidogo”Basi wakapanda kwenye gari, na kweli walishuka mahali na kupata sehemu nzuri na kukaa kisha kuanza mazungumzo ya hapa na pale,“Kwanza kabisa Derrick ni kitu gani kikubwa kinakusumbua?”“Sijui nikuelezeje upate kunielewa, ni hivi katika dunia mimi ni kiumbe nisiyekuwa na bahati kabisa”“Huna bahati kivipi?”“Kwanza kabisa, mimi nimeanza kukataliwa toka nipo tumboni mwa mama yangu, nimezaliwa sijapata mapenzi ya baba kabisa, nimepelekwa nyumbani kwa baba nasikia tukatimuliwa, toka hapo ndugu wa baba hawanipendi ni wachache tu wanaonaoniona kama mmoja wa familia yao. Nimekazana nitoke kimaisha, mama yangu kapata tabu ya kunisomesha na kweli nimefika chuo, nimehangaika kupata kazi, nikapata kazi ila hiyo kazi nimefukuzwa, hivi ni maisha gani nitakayoishi mimi? Kwanini dunia inanifanya hivi!! Ndiomana nikaamua nichague aina nyingine ya maisha kwani hata mimi natamani nimuhudumie mama yangu, nae aishi vizuri na ashukuru kunizaa”“Unajua Derrick umekata tamaa mapema sana, yani elimu yako hupendezi kabisa kufanya kazi ya kitapeli, hivi kweli umetafuta kazi kote imeshindikana? Kuna siku hata umewahi kuja kwangu na kusema shemeji nisaidie angalau nipate kazi?”“Hivi nakuja vipi kwako ikiwa mkeo ambaye nina undugu nae, hataki hata kuniona. Yani mimi sijui ni gundu sijui ni kitu gani. Katika maisha yangu ni kweli nilikuwa muhuni sana ila hakuna kitu ambacho sikupenda kama kutoa mimba, ila kuna mwanamke aliivuruga akili yangu kwa kutoa mimba yangu, huyu alikuwa ni mwanamke wa kwanza kumpa mimba na alikuwa wa kwanza kuitoa mimba yangu, kiukweli aliivuruga sana akili yangu, toka hapo huwa nahisi akili ikiwehuka tu. Kuna mwanamke nimezaa nae, na siku zote najua mtoto ni wangu kumbe mtoto mwenyewe katupa mababa wawili, yani wanawake jamani dah!! Ameona sieleweki ndio anasema yule mtoto sio wako, nimeumia sana, ila najua yule ni mwanangu ila tu sababu wanawake wanaangalia sehemu yenye maslahi zaidi”“Kwahiyo huyo mtoto yuko wapi?”“Najua basi, yule mwanamke alihama na watoto wake, roho iliniuma sana kila siku naenda kumlilia mwanangu, nilimpa jina la mama yangu ila yeye kampa jina lake analolijua mwenyewe. Yote hii sababu sijapata maslahi tu”“Toka uanze kutapeli hujapata maslahi tu!!”“Sijui ni kitu gani, sijui ni laana sijui ni nini. Yani mimi huwa natapeli hela za maana ila hakuna kitu cha maana ninachofanya”“Unapotea ndugu yangu, yani unapotea kabisa. Kiukweli Erica kanibadilisha mimi ila ilikuwa rahisi sababu na mimi niliona ile njia niliyokuwa napita haikuwa njia sahihi kwa mimi kuendelea nayo, unajua kuna vitu vingine badala vikuendeleze vinakutia umasikini tu, unapata pesa ya laana kwa uongo ila pesa hiyo hiyo unayopata unaenda kumalizia kwa wanawake, haya hayo maendeleo utayatoa wapi?”“Ni kweli kabisa, ila hii laana imeletwa na yule mwanamke aliyetoa mimba yangu”“Basi achana na hayo, kama upo tayari naomba kesho niache mambo yangu nikupeleke kwenye maombia. Upo tayari?”“Mmmmh!!”“Nini sasa Derrick?”“Utanipeleka kwenye maombi, utanipa na kazi? Maana hata niombewe na wachungaji wote duniani, na mshekhe nao waungane wote, ila kama sina kazi mwendo utakuwa ni huu huu wa kutapeli tu”“Dah!! Yani wewe jamani!! Nitakupatia na kazi, ila sasa huwezi kufanya kazi vizuri kama hujaamua kuacha kabisa haya unayoyafanya”Basi wakakubaliana pale kuwa wataonana kesho yake ili kuweza kuzungumza na kwenda huko kwenye maombi.Baba Angel leo aliporudi nyumbani kwake hakumwambia mkewe swala la yeye kuonana na Derrick kwani alijua wazi kuwa mkewe hawezi kukubali swala la kuongozana na Derrick kutokana na mambo ambayo Derrick huwa anayafanya.Basi baba Angel alienda kuoga, muda huu mama Angel alipigiwa simu na dada yake Bite na kupokea,“Erica, nipigie”Simu ikakatika, mama Angel alipotaka kupiga akagundua kuwa simu yake haina salio, basi akachukua simu ya mume wake ili kupigia dada yake, ila alipoichukua tu simu ya mumewe kuna ujumbe uliingia katia simu ile,“Erick, asante sana kwa hii pesa uliyonipa. Mtoto wetu Elly hajambo na muda huu ameshalala, anawaza masomo yake tu. Kumbuka nakupenda sana, by Sia”Mama Angel alisoma ule ujumbe mara mbilimbili na aliona ukimuumiza tu, basi aliufuta na hata kumpigia simu dada yake hakumpigia tena kwani alishakuwa na hasira kwa muda huo.Basi mumewe alivyotoka bafuni wala hakumwambia kitu chochote zaidi ya kuendelea na mambo mengine ila moyo ulikuwa ukimuuma sana ikabidi aulize tu maana alishindwa kuvumilia,“Mara ya mwisho kuonana na Sia ilikuwa ni lini?”Baba Angel akahisi tu kuna kitu ambacho mkewe lazima kawa na mashaka nacho, basi akaamua kumueleza vile ilivyokuwa jinsi Sia alivyomkimbia Juma na jinsi Juma alivyomueleza, na jinsi yeye alivyoenda kutafuta ukweli kwa Sia,“Ni hivyo mke wangu, hakuna lingine zaidi ya hayo”“Sawa, nimekuelewa, napenda sana vile unavyokuwa muwazi kwangu”“Nisipokuwa muwazi kwako nitakuwa muwazi kwa mtu gani sasa? Mimi nakupenda mke wangu na daima itabaki hivyo”Mama Angel alifurahi sana na kwa muda huo hakulala na kinyongo tena.Asubuhi wakati wamejiandaa kwenda shuleni, ndipo Erick alipompa Erica karatasi na kusema ni jibu la Samia, basi Erica alilichukua na kuliweka kwenye begi, basi alipoingia kwenye gari la shule tu akaifunua ile karatasi ndani ya begi na kusoma, iliandikwa kwa maneno machache sana,“SIKUTAKI, by Erick”Erica alitabasamu na kuchekelea sana jibu lile kisha akafunga vizuri ile karatasi na alipofika shuleni tu alimkabidhi Samia, ambaye alimuuliza kwanza,“Ila Erick alikuwaje baada ya kuona ile barua yangu?”“Sijui, maana mimi huwa sifatilii mambo yasiyonihusu”“Mmmmh hata huu ujumbe hujasoma?”“Kwanza kanipa asubuhi hii, niliweka kwenye begi moja kwa moja, sijui hata kaandika nini na yeye”Samia hakusoma kwani na yeye moja kwa moja akaweka kwenye begi lake na kumtaka Erica waende darasani,“Kheee mbona hujasoma?”“Nitasoma mwenyewe tu”Basi wakaenda darasani ila ukweli wa ile barua alikuwa anafahamu kila kitu kilichoandikwa humo ila akajifanya tu hafahamu chochote kile.Baada ya vipindi kuisha, Erica na Samia waliagana halafu kila mmoja aliondoka kwani walikuwa wakipanda gari tofauti za shule.Erick wakati wamepanda gari ya kuelekea nyumbani, kama kawaida Sarah alienda na kukaa karibu yake huku akiongea nae mambo mbalimbali,“Kwahiyo kwasasa Erick wewe ni mpenzi wangu”Erick alikaa kimya tu, kisha Sarah akaendelea kusema,“Kuna zawadi nimekuletea Erick”“Zawadi gani?”“Ila nataka umpelekee mama yako”“Mmmmh!! Nini tena?”Basi Sarah alitoa mfuko kwenye begi lake na kumkabidhi Erick ambaye aliuweka vizuri tu, kisha Erick alimuuliza Sarah,“Kwani ni kitu gani hiki?”“Ni zawadi tu lakini ya mama yako, yani mama mkwe wangu”“Mmmh!!”“Unaguna nini jamani Erick, mimi nakupenda tena nakupenda sana. Nahitaji kuwa pamoja na wewe hadi mwisho wa maisha yani wewe pekee ndio uje kuwa mume wangu, nipo tayari kufanya chochote na wewe”Kwakweli Erick hakuwa na kitu cha kusema, na kwa wakati huo alifika kwao na kushuka.Moja kwa moja Erick alipoingia ndani tu alimkuta mama yake yupo sebleni akamsalimia na kumwambia,“Mama, kuna zawadi yako nimepewa na Sarah nikuletee”“Oooh jamani Sarah, nimemkumbuka sana sijui lini atakuja tena kuniona jamani, dah binti ana roho ya upendo sana”Kisha Erick alitoa ule mfuko na kumkabidhi mama yake, ambaye alishukuru sana halafu Erick alienda zake chumbani kwake kubadilisha sare zake za shule na kuoga.Baba Angel alitoka kwenye kazi yake na kupitia kiwandani, sababu aliwasiliana na Derrick ila hakuweza kumpata hewani kwahiyo aliamua tu kwenda kwenye kiwanda chake ili aangalie maendeleo ya kile kiwanda, alikuta kipo kawaida tu basi akamuita ambaye huwa anasimamia pale na kumuuliza,“Eeeh shughuli zinakwendaje hapa”“Ziko vizuri tu, ila yule kijana wako alikuwa hatari sana”“Hebu niambie kwanza”“Yule kijana wako akija hapa kiwandani kama mwezi hivi basi tena!! Yani mambo yatanyooka hatari, ila tatizo lake hali chakula cha hapa sijui kwanini”“Aaaah yule hajazoea kula mbali na nyumbani”“Basi kama utaweza, kuna kuwa na mtu maalum wa kumletea chakula, nakwambia baada ya mwezi utafurahi na roho yako”“Dah!! Hapo ni mpaka shule zifungwe, mwanangu anasoma siwezi kumkatishia masomo sababu ya biashara zangu, ngoja nitavumilia tu. Ila siku hizi nitakuwa nakuja kila siku mimi mwenyewe”Wakaongea pale, kisha baba Angel akatembelea biashara yake kwa uzuri kabisa na kuondoka zake kuelekea nyumbani kwake, ila njiani gari lake lilisimamishwa na aliyesimamisha alikuwa ni Juma basi akasimama halafu Juma akapanda na kumwambia,“Bila shaka unaelekea nyumbani kwako!!”“Ndio, naelekea nyumbani kwangu”“Basi twende wote, yani nilipoona gari lako linapita nimejikuta tu namkumbuka kijana wako Erick natamani sana kumuona”Kiukweli baba Angel alianza kuwa na mashaka na rafiki yake Juma kwahiyo hakutaka huyu Juma kuwa na ukaribu na mtoto wake yoyote yule, basi akaamua kumdanganya tu kwa muda huo,“Aaaah unajua watoto wangu hii wiki ya kufungua shule wanatokea kwa bibi yao”“Kheee bibi yao yupi?”“Yule mama wa mama yao yani mama mkwe wangu, kwahiyo watoto wote wapo huko sie tunalea tu kichanga chetu”“Dah!! Nilitaka kwenda kumuona Erick ila basi tena, utaniambia siku watakayorudi. Utanishusha mbele tu hapo”Basi waliendelea na maongezi mengine hadi alipofika anaposhuka, yani baba Angel alipumua kidogo ila bado hakumuelewa rafiki yake kwanini anataka ukaribu ule na mtoto wake!! Alikosa jibu kabisa yani.Mama Angel alikuwa ndani akiitathimini zawadi ambayo amepewa na Sarah, basi aliangalia na kusema,“Yani huyu mtoto kama alikaa katika akili yangu, sijui kafikiria nini kunipa zawadi kama hii jamani maana nilikuwa nafikiria sana kwenda kununua hiki kitu na mimi nitamshtukiza mume wangu kwa zawadi pia itakayotokana na hii”Kisha akaweka ile zawadi yake vizuri na kwenda chumbani kwa Erick ambapo alimkuta amekaa tu akiandika kwa muda huo,“Oooh mwanangu unajisomea, vizuri sana. Ila mwambie Sarah nimefurahia sana zawadi yake, yani ni binti mwenye upeo wa hali ya juu”“Sawa mama nitamwambia”“Unajua ni zawadi gani amenipa?”“Sijui!”“Sasa mbona hujaniuliza? Yani wewe!! Angekuwa Erica basi kitambo tu kashajua ni zawadi gani nimepewa mama yake. Amenipa zawadi ya kitenge, ni kitenge kizuri hicho, kina rangi nzuri sana, nitakuosha nikiwa naenda kukishona”Erick alitabasamu tu kisha mama yake alimtakia kujisomea kwema halafu yeye aliondoka na kwenda chumbani kwake.Muda huu baba Angel nae alikuwa amewasili basi waliongea mengi ambapo alimueleza pia kuhusu rafiki yake Juma kuulizia kuhusu mtoto wao,“Mmmh usimuamini sana huyo mtu mume wangu, kwanza ameweza kuishi na Johari jua kuna tabia kafanana na Johari, kumbuka Johari ni rafiki yangu ila alikuwa ni chanzo kikubwa cha mimi na wewe kuwa mbalimbali na kuchukiana”“Nakumbuka”“Kwahiyo Juma, inawezekana hata akatumwa na mke wake, sio wa kuwaamini sana wale”“Ni kweli, sitaki kuwaamini sana, ni vile vile kama ambavyo huwa simuamini Dora ingawa anadai kabadilika kwa asilimia kubwa ila bado huwa nashindwa kumuamini moja kwa moja”Wakaongea ongea na muda huo waliamua tu kulala maana hapakuwa na jambo lingine la kufanya ila bado baba Angel hakumwambia mkewe kile alichoongea na Derrick.Nyumbani kwakina Samia, siku hii Samia hakwenda shuleni alikuwa kajikalia nje huku akilia, basi mama yake alimuona na kwenda kumuuliza,“Tatizo nini Samia?”“Mama, kuna mwanaume nampenda sana halafu yeye kaniambia hanitaki”Huyu mama alikaa chini kwani alijua mwanae atakuwa na matatizo ya kisaikolojia, kwahiyo aliamua kuongea nae kwa utaratibu,“Samia, umeanza lini hayo mambo ya kupenda wanaume jamani!!”“Mama, sio kosa langu nimejaribu kuvumilia ila nimeshindwa, nampenda sana”“Kwahiyo leo hujaenda shule kwasababu hiyo?”“Ndio mama, nampenda sana sijui nifanyeje”“Pole mwanangu, ila inabidi nikupe darasa la kutosha kuhusu mapenzi na akili yako ikae sawa.”Samia akampa mama yake na lile karatasi ambalo kaandikiwa na Erick kuwa hatakiwi, basi mama yake akalichukua na kulisoma, kisha akainuka kwa gadhabu kubwa sana na kumuuliza Samia kwa ukali,“Kwahiyo huyo mwanaume anaitwa Erick?”“Ndio mama, anaitwa Erick”Mama Samia alizidi kupandwa na hasira kiasi kwamba, alianza kumpiga mwanae tena alimpiga hovyo hovyo hadi Samia akazimia. Samia akampa mama yake na lile karatasi ambalo kaandikiwa na Erick kuwa hatakiwi, basi mama yake akalichukua na kulisoma, kisha akainuka kwa gadhabu kubwa sana na kumuuliza Samia kwa ukali,“Kwahiyo huyo mwanaume anaitwa Erick?”“Ndio mama, anaitwa Erick”Mama Samia alizidi kupandwa na hasira kiasi kwamba, alianza kumpiga mwanae tena alimpiga hovyo hovyo hadi Samia akazimia.Ila huyu mama hakuonyesha kujali wala nini ila alionekana kuwa na hasira zilizopitiliza, basi alitokea Samir na kumuuliza mama yake kinachomfanya kuwa na hasira kiasi kile,“Kwani kuna nini mama?”Kisha Samir akainama kama kumuamsha mdogo wake, ila mama yake akasema,“Achana nae huyo ataamka mwenyewe”“Khee mama, kamavile hujatuzaa wewe!! Kama vile hukutuzaa wawili tu kama mboni za macho yako!! Siku zote mama ndio mwenye uchungu na watoto wake tofauti na baba, hivi usipotujali wewe unadhani ni nani atatujali? Usipotupenda wewe ni nani atatupenda? Angalia baba ana watoto kibao, na kiukweli hakuna anayempenda sababu ni wengi mno kwahiyo wote anatuona kawaida, ila wewe ndiye mama yetu, ndiye pekee tuliyebakiwa nae, na wewe hutupendi tena kweli!! Tutakuwa wageni wa nani sisi?”Haya maneno yalionekana kumuingia sana mama yao, ambaye alikaa chini na kujikuta akianza kulia tena akilia kwa uchungu mpaka Samir ikabidi amfate sasa mama yake, muda huu hata Samia alikuwa kazinduka, kwahiyo Samir alimuingiza Samia ndani na mama yao aliingia ndani kisha alianza kuongea nae,“Kwani mama tatizo ni nini?”“Unajua mdogo wako kaanza tabia mbaya, kaanza tabia ya kupenda wanaume, unajua ni mdogo sana huyu kufanya huo ujinga!! Nilitaka kukaa na echini ili nianze kumueleimisha, ila kilichonichefua zaidi ni hilo jina la mwanaume anayemtaka”“Kheee jina gani mama?”“Muulize mwenyewe, si huyo hapo”Samia alijibu huku kajiinamia chini,“Anaitwa Erick”“Kheee kwahiyo mama, tatizo sio Samia kuanza tabia ya wanaume ila tatizo ni hilo jina la Erick!!”“Ndio, sitaki kulisikia hilo jina katika nyumba yangu hii, halafu wewe Samia hayo mambo ya kupenda wanaume umeanza lini? Mbona hukuwa hivyo wewe!!”Samir akajibu,“Huyu naona kichwa chake kinaharibiwa na mawazo anayopewa na baba, maana baba ndio anamwambia aombe hela kwa wanaume”“Oooh jamani, huyu mwanaume huyu loh anataka kuniharibia watoto tu kama yeye alivyoharibika, haya nipeni presha kwahiyo na wewe Samir unampenda nani?”“Kuna mdada nampenda sana anaitwa Angel”“Kheee kumbe na wewe tayari, jamani nyie watoto vipi jamani. Haya hiyo Angel na wewe ni vipi? Mnajua msinichanganye kabisa akili yangu, hebu watoto nyie mkue katika misingi imara, nawafundisha mambo mbalimbali halafu mnafanya ujinga, haya wewe Samia unampenda mtu anaitwa Erick unataka nini katika maisha yako? Unaakili kuwa kuna ndoa hapo kati yako na huyo kiumbe? Na wewe Samir huna hata aibu unampenda mwanamke anaitwa Angel, aaah jamani nyie watoto msifanye nijute kuwazaa jamani.”“Ila mama kwani mimi kuwa na Angel kuna ubaya gani jamani, nampenda na yeye ananipenda”“Haya, ubini wa huyo Angel ni nani?”“Anaitwa Angel Erick”“Ptuuuu nishasema sitaki kusikia hilo jina hapa nyumbani kwanfu, nyie watoto nadhani hamnijui vizuri mie mama yenu ila dawa tenu inachemka jikoni”Basi mama yao aliinuka na kuondoka zake ilionyesha ni jinsi gani hilo jina la Erick lilimtia hasira sana.Ila muda huo huo baba yao nae alirudi na kuwakuta watoto wake sebleni wakiwa wamejikunyata, ila huyu baba huwa anampenda sana Samia, kwahiyo alisogea karibu na kumuuliza,“Tatizo nini mwanangu?”Samir alijibu,“Tatizo Erick”Baba yao akashtuka sana,“Erick!! Hilo jina limekuja vipi nyumbani kwangu humu?”“Mama kampiga Samia sababu Samia anampenda kijana mmoja aitwae Erick, mama kasema hataki kusikia hilo jina humu ndani”“Ila jamani watoto wangu hata mimi msije kunitajia hilo jina tafadhari, yani watu wenye majina hayo huwa hawana ubinadamu kabisa, wana roho mbaya kama za wanyama. Sikieni watoto wangu, mimi huwa nawafundisha yaliyomema na mazuri, hebu achaneni na hao vichwa panzi. Haya msisononeke wala msihuzuke sababu ya mama yenu kuwapiga sijui kuwafanya nini badala yake nendeni mkajiandae halafu twende tukatembee maeneo huko”Basi baba yao akaenda zake ndani ila hakuongea chochote wala kumuuliza chochote mke wake kwani ndio walikuwa na utaratibu huo kwa siku zote.Baba Angel alikuwa akiendelea na kazi zake mbalimbali ila leo alifatwa ofisini na madam Oliva, akahisi ndio mambo yale yale anataka kuyaanza tena madam Oliva, ila leo alikuja na ujumbe mpya, baada tu ya salamu alianza kuongea na baba Angel,“Hivi mtoto wenu Angel mmemlea vipi?”“Kivipi?”“Unajua binti yule bado mdogo sana, kwa mila zetu za kiafrika yule binti bado mdogo jamani. Sio wa kuanza kugombewa na wanaume”“Kugombewa na wanaume!! Kivipi? Sikuelewi”“Sikia nikwambie, kuna siku nilikuwa naende kwenye mizunguko yangu, nikamuona Angel mahali akiwa amesimama na mwanaume, ile sehemu ilikuwa ni kwa fundi simu, mara alitokea kijana mwingine na gafla alianza kumpiga yule kijana hadi chini sikuelewa kitu pale ila Angel aliongea ongea na yule kijana alionekana kumpigia magoti kama kumuomba msamaha ila gafla yule kijana mwingine na Angel wakaondoka, wakapanda bajaji wakaenda zao. Nilienda kuuliza imekuwaje ndio nikasikia kuwa wale vijana walikuwa wakimgombea Angel, kwakweli kama mzazi nimeumia sana sijajisikia vizuri kabisa yani. Angel katika lile rika lake sio sawa kuanza kugombewa na wanaume”“Unajua sikuyajua hayo kwakweli, Angel yupo kwa bibi yake, amewezaje kutoka na kwenda kukutana na mwanaume!! Ni kweli haya mambo yanasikitisha sana, hata mimi kama mzazi wake sijapenda kwakweli ila madam una uhakika ni Angel?”“Hivi mimi nije kumsingizia Angel ili nipate faida gani? Au nije niseme wakati sio Angel niliyemuona ili iweje sasa? Siwezi kufanya kitu cha namna hjiyo, nimekuja kukwambia kuhusu Angel sababu ni Angel niliyemuona, na mimi kama mzazi nimeumia ndiomana nimekuja kukwambia”“Haya mwalimu, unashauri nini kifanyike sasa?”“Cha kuwashauri, shule ambaye utampeleka Angel kidato cha tano mpeleke shule ya misheni yani zile shule zenye muongozo wa kidini halafu umuache chini ya uangalizi wa masister, muokoe mwanao, msaidie kwasasa maana ni wengi watamsifia kuwa mzuri ila hawana lengo zuri na maisha yake, kwahiyo ni bora kumuweka makini mapema sana”“Nashukuru kwa ushauri wako madam, una ushauri mzuri ila na mimi ngoja nikuambie jambo. Naomba mpe uhuru Steve, imezidi sasa, yani hadi namuhurumia, mpe uhuru wake, ebu muache akupende mwenyewe ndio upendo wenye raha ila sio huo upendo wa kufugana ndani, mpe uhuru wake”“Nimekusikia”“Nawaza, ingekuwaje ndio ungenipata mimi, wewe mwanamke sio mzuri ujue, yani familia yangu sijui ingekuwa kwenye wakati gani. Samahani nimewaza kwa sauti”Madam Oliva aliinuka na kuondoka zake, tena siku hii hakuaga inaonyesha maneno ya mwisho ya baba Angel yalimuingia vizuri kwenye akili yake.Mama Angel akiwa nyumbani leo huku akiendelea na mambo mengine alipata ugeni ambao hakuutarajia kabisa, alikuwa ni rafiki yake wa muda mrefu sana aliyeitwa Johari, basi alimkaribisha sana na kuanza kuongea nae,“Kheee Johari jamani, leo umekuja kwangu!”“Ndio, unajua nimekukumbuka sana shoga yangu, ni kweli mengi sana yamepita baina yetu kiasi cha kufanya tusiwe na ukaribu vizuri ila kiukweli nimekukumbuka sana”“Karibu sana”“Na wewe karibu sana nyumbani kwangu, mumeo anapajua ni wapi naishi na mume wangu. Siku ile tumekuja hatujawakuta mimi nikasema hakuna tatizo cha msingi nimepajua nikaona basi nitafunga safari tu mwenyewe na kuja kukutembelea”“Karibu sana, kuwa huru rafiki yangu”“Eeeh saivi una watoto wangapi mwenzangu?”“Wanne, yule wakwanza Angel, wapili ni mapacha kuna Erick na Erica na wa tatu ni huyu wa mikononi”“Oooh, mimi ninao watano kwasasa, nimekuzidi mmoja”Wote wakacheka na kuendelea na mazungumzo mengine,“Kwahiyo watoto wako wote upo nao?”“Mmmmh mwenzangu unafikiri maisha ya kutangatanga nayo ni maisha!! Wanawake tuna siri nyingi sana ni Mungu tu anatufichia hizi siri tulizokuwa nazo na vifua vyetu, kwa kifupi nina watoto sita ila yule mkubwa alichukuliwa na baba yake yule mwalimu kwahiyo anaishi na baba yake”“Inamaanisha huyo mtoto mumeo hamjui?”“Anamjua ila kuna siri nyingi tu wee acha tu”“Mmmh Johari jamani hujaacha kwani kuhangaika jamani! Si ulisema umeridhika na mumeo wewe?”“Nadhani Erica hunielewi, ni kwamba wanawake tuna siri nyingi sana, nina ndugu yangu kaolewa na ana watoto ila wale watoto hata sio wa mume wake, tena kila mtoto ana baba yake, ila mumewe hajui kitu yani anajua watoto ni wake, huwa ananiambia Johari naomba nisife mapema maana kufa na siri hizi naona nitaenda kuchomwa moto”Johari akacheka, kisha mama Angel akamwambia,“Ila sio vizuri hivyo, hajamfanyia sawa mume wake, angemwambia ukweli tu”“Wewe unaweza kumwambia ukweli mumeo kuhusu kila kitu! Kuna vitu mtu huna namna ni lazima umdanganye tu mumeo, unadhani aseme ukweli halafu aende wapi na watoto? Atawaeleza nini wakati wamekuwa wakijua yule ni baba yao? Yani unakufa na tai shingoni shoga yangu”“Mmmh jamani siwezi kumficha mume wangu kitu cha namna hiyo, kwahiyo wewe unaweza mficha mumeo kitu cha namna hiyo?”“Erica hujui tu wanaume nao wana siri hao halafu wanamaudhi hatari kwahiyo huwa tunavumiliana tu maana ndio misingi ya ndoa ilivyo ni kuvumiliana”“Ni kweli kuna kuvumiliana ila usiwe tena na mambo ya kusaliti ndoa yako, ujinga ni zamani, mtu ukiamua kutulia unatulia moja kwa moja”“Haya, kilichonileta kwako ni wewe unipatie mawazo mbalimbali ya biashara, nahitaji kufanya biashara ila mtu wa kunishika mkono ndio sijampata”“Sawa hakuna tatizo, kama una muda kesho kutwa nitafute ili nikupeleke mahali, utafurahi kwa wazo utakalolipata huko”“Ila usimwambie mume wangu, nataka nifanye mwenyewe yani mume wangu asielewe kitu chochote”“Kheee Johari hadi kuhusu biashara unamficha mumeo!”“Shauri yako wewe, kuwa mjinga tu mwambie mwanaume kila kitu ila atakapokugeuka atakuacha mtupu kabisa, mwanaume sio ndugu yako, sio baba yako wala mama yako, usijifanye kumuamini mwanaume kwa asilimia mia moja, unatakiwa kumuamini nusu nusu”“Duh!!”“Shangaa tu, habari ndio hiyo, utaona anakupenda, anakujali, anakuthamini ila anachofanya nyuma ya pazia ukikijua unaweza ukafa kwa presha, hebu usimuamini hivyo mwanaume. Ila sijaja kukuvunjia ndoa, sema tu nakufundisha misingi ya ndoa na vile wanawake tunavyotakiwa kuishi, wanaume wenyewe wanasiri kibao, wacha na sisi tufiche siri zetu”Basi wakaongea mengi na kukumbushana mambo mengi sana, mwisho wa siku Johari aliaga kuwa anaondoka, ila mama Angel alishindwa kumsindikiza mbali sababu muda huo mtoto alikuwa akilia sana na hakuweza kutembea na mtoto wake, kwahiyo ilibidi aagane nae tu.Wakati Johari anatoka nje ya geti la mama Angel, yani baada ya hatua kama mbili hivi alishikwa bega, akageuka na kumuona mwanamke kasimama nyuma yake basi akasimama pia na kuanza kusalimiana na yule mwanamke kisha wakaanza kuongozana nae, ndipo yule mwanamke akajitambulisha kwa Johari,“Samahani, ngoja nijitambulishe kwako, mimi naitwa Sia”“Oooh sawa sawa, na mimi naitwa Johari”“Naona umetoka kuonana na Erica, ni rafiki yako eeeh!”“Ndio ni rafiki yangu tena sana, toka utotoni. Umejuaje kama nimetoka kumuona yeye”“Nilivyokuona umetoka tu hapo getini basi nikahisi hivyo, hivi Angel yupo kwani?”“Mmmh halafu sijamuuliza ila nasikia watoto wake wapo kwa bibi yao”“Hivi unajua kama yule Angel sio mtoto wa mume wake huyu rafiki yako!”“Mmmh kivipi?”“Mwenzangu, mwanadamu mnyime chakula lakini sio maneno, unaweza ukatunza siri miaka nenda miaka rudi ila kuna siku ukweli unabumburuka wazi kabisa, mtoto sio wa Erick wala nini natumai Erick unamjua yani mume wake na Erica”“Namjua ndio, nimesoma nao wote wawili”“Oooh kweli nyie ni marafiki sana, ila duh Erica msiri jamani hadi wewe rafiki yake hujui loh!! Yule Angel sio mtoto wa Erick, yule Angel ana baba yake anaitwa Rahim, tena baba yake ana asili ya kipemba sijui kiarabu yani ni mshombeshombe hivi, ni mzuri sana ndiomana hata huyo mtoto ni mzuri sana”“Mmmmh yani sikuelewi”“Ndio hivyo, hata mtoto mwenyewe hajui kama kafichwa”“Erick je!”“Erick anajua ukweli sijui hajui maana huwa anajipumbaza, mtoto hafanani nae hata ukucha ila anasema mtoto wangu wa kwanza, hadi kote wanamuita baba Angel wakati sio mtoto wake yule, maana mtoto yule ana baba yake yupo tu”“Unajua nashangaa kitu gani, Erica ni rafiki yangu mkubwa tu. Nilipozaa mara ya kwanza sieleweki sina mwanaume wa kunioa, alibaki ananishangaa na kusema bora kusoma, haya sasa kasoma kiko wapi? Kaenda kuzaa mtoto wa kwanza na mwanaume mwingine, je mimi na yeye tuna tofauti gani? Yani mimi na yeye tupo sawa sawa kasoro majina tu. Ila wanawake sisi loh!! Tena usikute ananisisitiza kutulia halafu labda hata huyu mtoto wa mwisho sio wa mume wake”“Mmmh hilo sijui, atakuwa wa nani sasa?”“Chunguza tu, mbona na huyu mtoto nimejaribu kumshika pale hafanani na Erick wala Erica”“Mmmh ngoja nichunguze na hilo, nikipata ukweli nitafurahi sana”“Kwani wewe kitu gani kinakufanya umfatilie?”“Humjui tu rafiki yako, ana majivuno sana yani anajiona kuwa yeye ndio mwanamke wa pekee katika ulimwengu huu. Yani yeye haoni kitu chochote zaidi ya kujiona yeye yupo juu, sijui anapendwa, sijui anapesa, anaringa sana yule mwanamke”Muda huu walifika kwenye stendi ya daladala na kupeana namba za simu ili wawe wanawasiliana, kwakweli Johari alishangaa sana baada ya kufikiria ile siri ya rafiki yake.Kweli leo, wakina Samir walienda kutembea na baba yao, na kweli kwao ilikuwa ni ajabu sana siku hii maana sio kawaida kwa familia hii kabisa, kwahiyo alienda na watoto wake kwenye hoteli moja kula na kunywa, wakaagiza chakula pale na kuanza kula na vinywaji wakinywa huku baba yao akiwaambia watoto wake ni kiasi gani anawapenda,Basi Samir alimuuliza baba yao,“Mmmh baba kwahiyo unatupenda sisi kuliko watoto wako wote?”“Kuna mwaka ambao watoto wangu wote nitawaweka pamoja, unajua mkubwa ana umri gani?”“Hatujui baba?”“Ana miaka ishirini na nne, yani mimi nina binti mkubwa kabisa wa kumuozesha, siku ya harusi yake nitachukua watoto wangu wote hadi wale ninaokataliwa kuwa nao”“Kheee kuna watoto wengine unakataliwa kuwa nao!!”“Yani mwanangu Samir, ngoja nikwambie haya, katika maisha yako usije ukarogwa kuwa na mwanamke asiyekuwa na akili, atakusumbua sana, asilimia kubwa ya wanawake niliozaa nao hawana akili, mwanamke msomi alikuwa ni mama yenu na mwanamke mmoja hivi ila yule dada alikuwa msomi halafu kumbe ni kichaa, nimezaa nae mtoto nimemuhudumia vizuri mtoto kaenda kumpa jina analolitaka yeye, kampeleka mwanangu Kanisani na kibaya zaidi kampa mwanangu baba mwingine”“Kheee baba!!”“Ila huwa nawaambia kuwa siku zote mtu hukumbuka asiliyake tu, waache wamlee malaika wangu ila ipo siku atarudi kwenye himaya yangu, na kipindi hiko watajiona wajinga sana sababu wamenisaidia kulea na hawatopata kitu toka kwa mwanangu. Kuna wanawake vichaa sana, ndiomana mwisho wa siku nikaamua tu kutulia na kumuoa mama yenu”“Ila baba kwanini ukawa na wanawake wengi hivyo!!”Ila baba yao kuna watu aliwaona na kuwafahamu basi akaaga watoto wake kwa muda na kwenda kuwasalimia watu hao.Alienda kwenye ile meza na kukaa na kuanza kuongea nao kwa kuwasalimia,Unanikumbuka ndugu Bahati”“Nakukumbuka vizuri sana, wewe tena”“Naona upo na mkeo”“Ndio, nipo na mke wangu si unajua mara moja moja lazima nifurahi na familia yangu”“Siku hizi umeacha mawazo ya yule kivuruge wako?”“Aaaah sio habari za kuongelea hapa jamani, hebu karibu tuongee mambo mengine”Basi baba Samir alimuangalia huyu Bahati halafu akamuangalia mke wa Bahati na kumwambia,“Naona shemeji umefanya jitihada kubwa sana za kumbadilisha mumeo, hongera kwa hilo”“Asante”Kisha alimuangalia mumewe na kumwambia,“Inatakiwa tuondoke sasa maana muda wetu wa kukaa hapa umeisha”Basi walimuaga baba Samir pale na kuondoka zao, kwahiyo ilibidi arudi kwa watoto wake tu ambapo alikaa nao kidogo na kuondoka nao.Baba Angel leo aliporudi nyumbani kwake, aliamua kuongea na mke wake kile alichoambiwa kuhusu Angel, kwakweli mama Angel alishtuka sana,“Nani kakuletea hayo maneno baba Angel?”“Hapana sitasema ni nani ila ni mtu ambaye anamfahamu vizuri sana Angel, mke wangu inatakiwa tuwe makini sana na mtoto”Basi muda ule ule mama Angel aliamua kumpigia simu mama yake ili kujua ni kitu gani kinaendelea kuhusu mtoto wake, muda ule ule mama yake nae alipokea simu na kuanza kuongea nayo,“Tena afadhari umenipigia mwanangu, nilikuwa nataka kukupigia muda tu ni kuhusu huyu Angel”“Kafanyaje mama?”“Unajua hadi kuna muda sielewi cha kufanya, hivi unajua huyu ni binti mkubwa sio sawa nimfunge kamba au nitembee nae kila mahali kwa kuhofia kuwa atafanya ujinga”“Vipi tena mama?”“Ni hivi, kuna siku hapa ilikuwa patashika, nilitoka kidogo tu kwenda kwenye shughuli huko, narudi namkuta Angel kazimia huku yule kijana asiyejielewa yule Samir yuko pembeni yake, kwakweli nilichukia sana nilimpiga mno kijana wa watu. Mungu anisamehe tu, huyu mtoto wenu ananitia dhambi haswaaa, kumbe sijui kuna kijana mwingine alifika nae kampa Angel tunda lenye madawa ili ambake, jamani huyu mtoto huyu anataka kunitia dhambi unajua nimepatwa na mawazo hadi nikajikuta sijawapigia simu kwa wakati”“Duh!!”“Tena hiyo haitoshi maana, ile simu Angel nilimpokonya kumbe kanunuliwa simu nyingine na mwanaume mwingine. Yani Erica huyu mtoto wako kwakweli kanishinda tabia, nitapiga nimuumize jamani”“Oooh asante mama kwa kuniambia, ngoja nijadiliane na baba yake hapa tujue cha kufanya”“Yupo ila nikampe simu uongee nae”“Hapa mama hata sitaki kuongea nae, ataniumiza kichwa tu, ngoja baba yake niongee nae. Asante mama, usiku mwema”Mama Angel aliagana na mama yake kisha akamuangalia mumewe na kumwambia,“Yani uliyoambiwa kuhusu Angel ni ukweli mtupu hadi nahisi kichwa kuvurugika hapa, hivi tufanyeje sasa?”“Nimeshauriwa kuwa tumpeleke kwenye shule za misheni na tumuache chini ya uangalizi wa masister”“Naona hiyo ni nzuri, na akitoka shule nitakaa nae na kumueleza maana huyu mtoto anajitia kichwa rungu jamani khaaa sijapata kufikiria kama angekuwa anawaza ujinga kiasi hiki jamani Angel, kwahiyo sasa tutaenda lini kumchukua?”“Nadhani keshokutwa twende kumchukua, au nitaenda mimi mwenyewe hakuna tatizo”“Sawa nimekuelewa, ila kule kwa Tumaini alishika adabu yule, kweli mama saivi kazeeka jamani, kweli Angel wa kumshinda bibi yake kweli!! Kweli mama kaanza kuchoka loh!”“Miaka inaenda, mama yangu ndio kabisa nadhani hata muda wa kumfokea mjukuu hana kabisa, yani huyu Angel akikaa kwa mama yangu hata mwezi kwa tabia zake hizi basi angerudi na mimba maana mama hana muda wa kufatilia kabisa”Wakajadiliana pale na kuamua kufanya mambo mengine tu kwa muda huo.Usiku wa leo, Erica alienda chumbani kwa kaka yake na kumuuliza,“Kwani Samia ulimjibu nini?”“Mmmh Erica hujaona nilichomjibu Samia kweli!”“Sijaona ndio, maana mimi niliweka tu ile barua kwenye mkoba na kumpelekea”“Nilimwandikia kuwa hata na mimi nampenda”“Mmmh mbona leo hajaja shule basi!”“Sasa asipokuja shule nahusika vipi hapo?”“Inaonyesha ulimjibu vibaya kwahiyo kaumia moyo ndiomana hajaja shule”“Hayo ni mawazo yako Erica, ila mimi nimemwambia kuwa nampenda”“Kwahiyo upo tayari kuwa mpenzi wake?”“Erica, mimi bado ni kijana mdogo, je huwa husikii mafundisho ambayo mama huwa anatufundisha? Mama katufundisha nini kuhusu mapenzi? Mapenzi yapo, na muda muafaka ukifika basi yatakuja yenyewe tu bila kulazimishwa, kwasasa mimi bado ni kijana mdogo na wewe bado ni binti mdogo, hapa maana yangu ni hii hata wewe usiingie vishawishi vyovyote vile vya kujiingiza kimapenzi na mtu yoyote yule maana bado ni binti mdogo, mapenzi yapo, yalikuwepo na yataendelea kuwepo. Tukae na msemo huo wa mama”“Ila mimi nishawishike kivipi, yani kitu gani kitanishawishi?”“Ni kweli hakuna cha kukushawishi na ndio usishawishike, mabinti wengi hudanganywa na pesa, sasa wewe ni nani wa kukudanganya na pesa ikiwa baba yetu anahenyeka kwaajili yetu hakuna kitu ambacho tuakosa hapa nyumbani, haya kuhusu upendo familia nzima tunakupenda, kama mimi nakupenda sana mdogo wangu sasa kitu gani kitakushawishi?”“Ila kwani imekuwaje mpaka Samia akuandikie wewe kuwa anakupenda sana?”“Achana na Samia, hajafunzwa maadili yule maana angekuwa amefunzwa maadili basi asingeweza kufanya alichokifanya, ila Erica wewe uishi hivyo hivyo maana siku nikute sijui kuna mkaka anakufatilia sijui yani nitamfanya kitu gani, kwahiyo kuwa makini sana mdogo wangu”“Sawa, nimekuelewa”Kisha Erica aliinuka na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake kwenda kulala.Leo Erick akiwa darasani, muda wa mapumziko alifatwa na Sarah na kuanza kuongea nae,“Ila Erick mbona muda mwingi unaonekana kama una mawazo sana?”“Aaaah ni kawaida, binadamu lazima uwaze mambop mbalimbali”“Lakini wewe umezidi jamani, sikia mama yangu kakukumbuka kweli, vipi kesho njoo basi nyumbani kwetu”“Mmmh siwezi”“Jamani!! Au nije mimi kukuchukua, najua mama yako hawezi kukataa kuhusu swala hili, najua lazima atakubali, kwani kuna ubaya gani Erick kuja kwetu!”“Ngoja nikuulize Sarah, hivi ni malezi gani ambayo mama yako amekupatia wewe? Kwa kifupi yani unaishije na mama yako nyumbani?”“Sijui nikwambie vipi ila mama yangu ananipenda sana, huwa anasema mimi ni mtoto ambaye kazaa na mwanaume aliyempenda sana, ndiomana mara kwa mara huwa tunaenda kwenye kaburi la baba na kulipalilia na kukaa kidogo huko, kwakweli mama yangu ananipenda sana”“Unajua kupika wewe?”“Kwanini umeniuliza hivyo?”“Kufua je? Unajua kuosha vyombo?”“Mmmh ndio unanipima ili ujue kama nafaa kuolewa au sifai au ni kitu gani?”“Hapana, mikono yako Sarah ni laini sana kiasi kwamba sidhani kama kuna kazi yoyote huwa unafanya nyumbani kwenu”“Mmmh tusijadili hayo, ila nitakueleza vizuri kuhusu mimi”Kengele ya kurudi darasani ililia ilibidi waachane na kila mmoja kuelekea kwenye darasa lake.Leo Johari akiwa nyumbani kwake, mumewe akamuomba jambo moja,“Hivi yule mke wa Erick si unapafahamu kwao?”“Ndio napafahamu”“Naomba unipeleke”“Kwani unataka kwenda kufanya nini?”“Nataka kwenda kumuona mtoto wa Erick aitwaye Erick, kuna jambo la muhimu sana mke wangu juu ya huyu mtoto tunatakiwa kuwa nae karibu mtoto huyu ni mali kubwa sana”“Mmmh uwe nae karibu anakuhusu?”“Hata kama, mtoto wa mwenzio ni mtoto wako, kuna vitu ukiviona kwa mtoto unatakiwa kuwa makini sana lkwani leo na kesho utafaidika pia”“Mmmh, haya twende lini?”“Nahitaji twende leo”Ilibidi Johari ajiandae kisha yeye na mumewe waliondoka na kwenda moja kwa moja hadi kwa bibi Angel na hapo walimkuta Angel na bibi yake, basi waliwasalimia na kuanza kuongea nao mawili matatu, ambapo Juma aliulizia pia kuhusu watoto wa Erick,“Eti Erick mdogo yupo?”“Mmmh hayupo”“Ila si washatoka shule!! Maana leo ni Ijumaa”“Hawaishi mahali hapa, wapo kwao”“Mmmh kumbe! Lakini mbona baba yao aliniambia kuwa wapo huku”Mara alifika mgeni kwenye nyumba ile, na huyo mgeni alikuwa ni mama Junior, ila cha kushangaza yani kila mtu pale alibaki kustaajabu kwani mama Junior alisogea karibu na Juma na kumkunja kama anataka kupigana nae. Mara alifika mgeni kwenye nyumba ile, na huyo mgeni alikuwa ni mama Junior, ila cha kushangaza yani kila mtu pale alibaki kustaajabu kwani mama Junior alisogea karibu na Juma na kumkunja kama anataka kupigana nae.Basi bibi Angel alisogea pale na kumuweka mama Junior pembeni huku akimuuliza,“Kwani tatizo kitu gani Bite?”Mama Junior alimuangalia Juma kwa gadhabu sana na kumwambia,“Ulidhani hatutakutana?”Mama yake akamuuliza tena,“Kwani amekufanyeje? Hebu shusha presha kwanza mwanangu”Mama Junior alikaa chini na kusema,“Huyu baba amenifanyia roho mbaya sana, sikia mama nadhani kila mara huwa unaniuliza ni kwanini sifatilii mali za marehemu James wakati nilizaa nae, basi chanzo ni huyu hapa”“Yani yeye kafanya nini?”“Hivi mama unajua kuwa huyu ni rafiki mkubwa sana wa marehemu James, alinipa maneno machafu sana huyu. Namchukia simpendi kabisa na sitaki hata kumuona”Juma akasema,“Naomba unisamehe, sikujua haya”“Mjinga wewe, ambacho hukujua ni kitu gani?”Mama Junior alikuwa na hasira sana, basi Johari akaanza kumtuliza pale,“Lakini dada Bite, ongea vizuri ili tukuelewe”“Mjinga nini wewe, si umuulize vizuri mumeo ndio umuelewe”Basi kwasababu ya hasira alizokuwa nazo mama Junior ilibidi wakina Johari waage tu na kuondoka zao.Pale ndani, mama Junior alibaki na mama yake, na hapo bibi Angel akamwambia Angel akalete maji ili mama Junior ashushe hasira zake, basi alimletea maji na kuyanywa kwanza, ila hakutaka kuongea kwa muda huo na kuomba muda kidogo apumzike kwahiyo alienda kulala kidogo.Basi Johari na mumewe wakati wanaondoka, waliulizana,“Kwani wewe umemfanya nini huyu dada?”“Unajua sikuweza kuunganisha matukio, kumbe huyu ni dada yake Erica?”“Ndio, tena kutoka huyu basi ndio akafatia Erica, tena kwenye familia yao basi Erica na huyu ndio wanapendana sana”“Dah!! Mimi sikujua kabisa”“Kwani mambo gani ulimfanyia?”“Sikia nikwambie kwa kifupi, huyu mwanamke alimuomba mumewe talaka kwa madai kuwa mumewe kaathirika, na aliomba ile talaka kwa madaha kabisa, nakumbuka ile kesi ya talaka ni mimi ndio nilikuwa nampeleka James mhakamani, ikaendeshwa ile kesi hadi ikabidi waachane kwa talaka sasa, ila kiukweli James alimpenda sana huyu mke wake, sema mimi niliumia mno kwa jinsi huyu mwanamke alivyoamua kumfanyia mumewe, alikosa hata utu kitu kidogo tu mwanaume mwenyewe umeathirika, kiukweli James alioa yule mwanamke mwingine sio kwasababu alimpenda ila ni sababu ilimbidi tu kufanya vile ndiomana aliamua kuoa. Cha kushangaza, yule yule mwanasheria aliyekuwa anashadadia ishu ya talaka ndio mwanaume aliyemuoa huyu mwanamke, si inamaana kwamba ni kitu ambacho walipanga? Yani huyu hakuona njia nyingine yoyote kwa mumewe zaidi ya kuomba talaka? Kwakweli alinikera sana, ilitakiwa agaiwe na yeye sijui urithi sijui nini na nini, basi na mimi nikatafuta wanasheria wangu wenye figusu hadi hakupata kitu hata baada ya msiba wa James, yani hakuna kitu alichoambulia ila kosa ni langu mimi, ila nilifanya sababu huyu mwanamke alinikera sana, hakuwa wa kumfanyia vile rafiki yangu. Sema sikujua kama nitakuwa nafahamiana nae”“Hujamfanyia vizuri hata kidogo, kwanza yeye na huyo mumewe ndio wanajua ndani walikuwa wanaishije? Na iweje mwanaume akaathirika wakati mwanamke hana, ni wazi kuwa mwanaume huyo hakutulia, unaweza kumlaumu sana huyu lakini nadhani ni kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao ndiomana ikawa hivyo ilivyokuwa. Huyu dada ninamjua kitambo sana, hana hayo mambo kabisa, kwa kifupi huyu dada sio muhangaikaji, itakuwa huyo mwanasheria alionyesha nia ya dhati na yeye akaona nisihangaike sana bora nipate wa kutulia nae, unamlaumu bure tu. Halafu ulikazania hivyo mali za rafiki yako ulitaka azipate nani sasa? Ulikuwa na malengo gani? Huyu dada na huyo mumewe si wana mtoto lakini?”“Unajua badae nilitambua kosa langu ila sikuwa na la kufanya wala nini labda turudie tena kesi, ni hivi yule mwanamke aliyekuwa anaishi na James kwa kipindi hiko, walikuwa katika ndoa na wana mtoto pia, aliongea na mimi nimsaidie ili aweze kumiliki mali za mume wake maana ni haki yake, alikuwa anahofia kwa watu kutokea na kuzitaka zile mali”“Na yeye ana roho mbaya, utafikiri yeye ndio alikuwa wa kwanza kuolewa? Tena wewe mwenyewe ndio ufanye jitihada ili mtoto wa huyu dada nae apate haki yake”Muda huu walikuwa wakiendelea tu na safari yao ya kurudi nyumbani kwao.Baba Angel leo alirudi mapema nyumbani kwake, maana kuna jambo alikuwa amelipanga kwenye kichwa chake na kuna safari alikuwa ameipata, kwahiyo aliona ni vyema kwenda kuzungumza na mkewe kwanza,“Natakiwa kusafiri, nitakaa huko kwa muda wa mwezi mmoja”“Mmmmh mwezi mmoja!! Jamani, itakuwaje hapa sasa?”“Mama Angel, kwani ni mara ya kwanza kwa mimi kusafiri? Si huwa nasafiri mara kwa mara? Ila kuna kitu nataka kukiweka sawa kwanza”“Kitu gani hiko?”“Nitahakikisha Angel nishampeleka kwenye ile shule maana nasikia masomo yameshaanza, halafu Junior nae aende shule ingawa sio mbali sana na hapa ila ni bweni, akasome huko aache ujinga wa hapa nyumbani. Nitaacha maelekezo ya kutosha kwa Erick ili angalau mwisho wa wiki hata mara moja au mbili aende kiwandani”“Kwani hiyo safari ni ya muhimu sana eeeh!”“Ndio ni ya muhimu na itatuingizia hela nyingi, kwanza kesho naenda kumchukua Angel halafu napitia nae kununua baadhi ya vifaa yani asifikiri atakaa nyumbani maana ni shule moja kwa moja, uzuri ndio shule aliyofanya usahili, nikifika namkabidhi kwa sister ambaye atafatilia nyendo zake zote”“Kheee kwahiyo Angel shule lini?”“Kesho kutwa, naenda kumkabidhi shuleni, kwahiyo Jumatatu ataanza kuingia darasani”“Sijui atafurahi, sijui atachukia!”“Tusifikirie hilo kwasasa, ila tufikirie elimu ya Angel”“Sawa, nimekuelewa ila safari yako imekuwa gafla sana nitakukumbuka mno jamani mume wangu”“Wasiwasi wako nini, bado sijasafiri”Mama Angel alionea tu kwa huruma kwani aliona wazi kuwa atamkumbuka sana mume wake kwani ameshamzoea na muda mwingi wanakuwa wapo wote.Usiku wa leo Erica alimfata Erick na kuanza kumwambia habari za Samia maana alikutana nae shuleni,“Nasikia Samia alipigwa na mama yake hadi akazimia”“Mmmh kwanini sasa?”“Si alimwambia mama yake ukweli kuwa anakupenda wewe, basi mama yake kamwambia hataki kabisa kusikia jina lako likitajwa katika masikio yake”“Kwahiyo Samia amekoma eeeh!!”“Sasa umefurahia jamani! Kumbuka Samia anakupenda”“Tena mama yake kafanya vizuri sana kumpiga, ni utaratibu wa wapi huo kwa binti mdogo kama Samia kumtaka kimapenzi kijana mdogo kama mimi! Yani bora kapigwa ili akili imkae sawa”“Ila cha kushangaza sasa, anasema ingawa amepigwa ila hatoacha kukupenda wewe”Erick alitabasamu kisha Erica akamwambia,“Hatujacheza siku nyingi karata, basi leo tucheze karata”“Ila leo nimechoka sana”“Ndio najua kama umechoka, basi tucheze japo mchezo mmoja tu”Erick akakubali na kuanza kucheza karata, walipokuwa wakicheza zile karata ziliwanogea na kujikuta wakilala humo humo chumbani tena wakiwa hawana habari kabisa.Leo mama Angel alienda chumbani kwa Erick maana alikuwa akitaka kuongea nae kuhusu baba yake, aliwakuta wakiwa wamelala tena hawana habari huku karata zile zikiwa pembeni, yani mama yao alitikisa kichwa na kuwaamsha,“Nyie, hebu amkeni yani nyie mbona mna akili mbovu kiasi hiko!! Erica huna chumbani kwako wewe hadi unakuja kujilaza kwenye chumba cha kaka yako?”“Nisamehe mama”“Halafu mambo ya karata si niliwakataza mimi, kwanini hamsikii kitu nyie watoto mna matatizo gani kwani?”“Tusamehe mama”“Haya inukeni hapo, wajinga nyie”Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake ila kwavile mama yake alizichukua karata alijua wazi hawezi kuzipata tena, na ukizingatia mtu ambaye alikuwa akimletea karata ni Abdi ambaye hawasomi pamoja tena, basi alisononeka sana na kumuacha mama yao akizungumza na Erick mule chumbani.Siku hii Johari alipigiwa simu na Sia na kwenda kukutana nae na kuongea nae mambo mengi,“Sikia nikwambie, nataka nikuonyeshe mwanaume ambaye amezaa na Erica yule Angel”“Mmmmh! Ila wewe nawe una mambo lakini!”“Hapana, unajua kuna umuhimu wa huyu mwanaume kupata haki yake, kuna umuhimu wa huyu kumtambua mtoto wake”“Ila duh wewe una mambo zaidi, kuna mambo mimi huwa najua ila mengine huwa sijui, ila wewe unamjua hadi mwanaume aliyezaa na Erica!”“Namjua ndio nataka nikakuonyeshe, tena twende leo leo”“Ila unataka kunionyesha ili iweje?”“Umjue, ili hata pengine utaweza kumwambia ukweli huyo mwanaume”“Aaaah mtihani mzito huo, haya nipeleke”Mara simu ya Johari ikaanza kuita, kuangalia ni mama Angel basi akapokea na kuanza kuongea nayo,“Unakumbuka lakini Johari, ni leo njoo mara moja nikupeleke mapema si unajua kuwa nina mtoto mdogo”“Oooh naelewa ndio, nakuja muda sio mrefu”Basi Johari aliamua tu kumuaga Sia na kuachana nae kwa muda huo, kiukweli Sia hakupenda kwani alitaka Johari amtambue mwanaume aliyezaa na mama Angel.Basi Johari alienda kwa mama Angel na kufanikiwa kwa muda ule ule kuondoka pale nyumbani kwani mama Angel hakutaka kuchelewa ukizingatia alikuwa na mtoto mdogo, basi walipokuwa kwenye gari kuna swali Johari alimuuliza mama Angel,“Hivi Erica unajua kuwa sisi tulikuwa marafiki wakubwa sana, tulipendana na kufanya mambo mengi sana, ila imekuwaje siku hizi tupo mbalimbali au kisomo ndio kimetutenganisha? Huniambii siri zako, haupo karibu na mimi hata sijui tatizo ni nini?”“Ni kweli Johari ulikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana, ulinifanyia mambo mengi ila nilisamehe. Sema kitu kimoja ambacho sikipendi katika maisha yangu ni kuwa sipendi rafiki mnafki yani wewe Johari ni rafiki yangu ila ni mnafki yani hushindwi kunizunguka wewe, halafu mwenyewe unajionea sawa kabisa, sijui ni urafiki wa aina gani huo”“Hayo yalikuwa ni mambo ya zamani Erica, kwasasa tumekuwa watu wazima na tuna familia, tunahitaji watoto wetu waishi vizuri na wapatane kama ndugu ila mama zao tukiwa mbalimbali hivi sio picha nzuri ujue! Ila wewe Erica kuna rafiki yako ambaye unamuona sio mnafki kweli!”“Yupo ndio, nina rafiki anaitwa Fetty yani yeye maisha yake ni uhalisia, halafu sio mnafki kwangu, huwa ananifundisha na kunielekeza mambo mengi sana, nikifanya vizuri atanipongeza, nikikosea ataniambia tena kwa utaratibu ila mnafki, ukikosea anaenda kukusema kwa watu ili akuharibie zaidi sasa unapata faida gani? Yani mimi huwa sipendi unafki”“Mmmh nimeacha mambo ya unafki jamani Erica, eeeh unanipeleka wapi?”“Tena nimekumbuka, ngoja tupitie hapo stationary nikununulie daftari na peni, nakupeleka huko kuna semina ya ujasiliamali, nikikuelekeza mimi naweza nikakupoteza ila ukienda kwenye semina afadhari utapata mwanaga wa mambo mbalimbali, ndiomana nimekuharakisha leo sababu tangazo lao nililisikia”Basi walifika kwenye duka na kusimama, kisha wakashuka na kwenda kununua hivyo vitu, wakati wanaondoka kuna mwanamke ambaye mama Angel alifahamiana nae, alifika na kumsalimia mama Angel, na yeye alimsalimia halafu akaondoka na Johari, wakapanda kwenye gari ila Johari akamuuliza,“Nani huyo?”“Ni mwalimu wa shule wanayosoma watoto wangu, ila ni mnafki sana yani sikujua kama anaweza kujivika moyo wa kijasiri namna hiyo na kunisalimia”“Mmmmh kwanini?”“Nikikueleza mambo yake utashangaa, kwa kifupi alitafuta dawa sijui kwa mganga wa kienyeji huko na kumuwekea mume wangu ili amtege yani amchukue kimoja, ila Mungu sio Athumani, ile dawa akaitumia mwanaume mwingine basi ndio kamganda hatari, namshangaa hata anapata moyo wa kunisalimia”“Duh! Ila wanadamu wabaya sana, hata mimi kuna mwanamke huyo aliachwa na mumewe, hana mbele wala nyuma ila nashangaa sana eti naye alitaka kumuwekea dawa mume wangu ili ampate, yani katika maisha tunakutana na watu wa ajabu jamani”Basi walifika kwenye hiyo semina, mama Angel alilipa kiingilio kwaajili ya rafiki yake na kumuacha hapo kwani kuna mahali alitaka kupitia halafu ndio arudi nyumbani kwake kwaajili ya mtoto wake.Moja kwa moja mama Angel alipitia sehemu aliyotaka kwenda, ilikuwa ni kwa fundi ambaye alimpelekea kitenge amshonee maana alikuwa akitaka kupata sare ya kitenge kile, yani alishona nguo yake na shati la mumewe, kilikuwa ni kitenge ambacho alipelekewa zawadi na Sarah.Basi wakati yupo kwa yule fundi ndipo alikutana na mtu ambaye wanafahamiana kwa zamani, wakasamiana pale alichukua bidhaa zake na walitoka nje wakiongea kiasi,“Unajua mara ya mwisho tumekutana ni pale hospitali yani wewe Erica jamani, bado tu unatuchukia sababu ya mjinga mmoja”“Sio hivyo Babuu ila siku ile nilikuwa na mambo mengi sana, unafanya nini siku hizi?”“Najishughulisha na mapamba, napamba vizuri sana, sijisifii ila ukitaka utaona kazi zangu”Basi Babuu alichukua simu yake na kuanza kumuonyesha mama Angel baadhi ya picha za mapambo ambayo huwa anafanya, kwakweli yalikuwa mazuri sana, ila kuna picha ilimshtua kidogo na kumuuliza Babuu huku akimuonyesha ile picha,“Inamaana ni wewe ndio ulipamba mahali hapa?”“Ndio ni mimi”“Khaaa unajua hiki ni kiwanda changu na mume wangu, yani kumbe mpambaji ulikuwa ni wewe, kwakweli palipendeza sana. Mbona sikukuona?”“Aaaah kumbe!! Mimi huwa nikimaliza shughuli zangu naondoka, naacha vijana tu ambao ndio hutandua mapambo, ila ningejua kabla basi ningesubiri hata nikusalimie”Mama Angel akatabasamu tu, kisha Babuu aliendelea kuongea,“Unajua nini, katika maisha mtu unapitia katika mambo mbalimbali, ila yote huwa yapo kwaajili ya kujifunza. Ila huwa sisahau kamwe, siku ambayo nililala rumande sababu ya uzurulaji tena uzurulaji wenyewe nilikamatwa baada ya kutoka kukuona wewe, nilikuomba nikalale guest ukakataa na kutaka nirudi nyumbani basi nikarudi na kukamatwa na askari usiku ila wewe ulihisi nimeenda kwa wanawake zangu, natoka na uchafu wangu rumande, moja kwa moja chuoni kwenu nakutana na rafiki yako yule Dora ananipa maneno ya kejeli na karaha, huwa sisahau hii siku katika maisha yangu jamani”“Yamepita jamani, nisamehe”“Ila ni funzo kwangu na kwako pia, tena kwako ndio ujifunze vizuri hata mumeo ndani usije ukamfanyia vile kama ulivyonifanyia mimi, yani wewe hisia zako zinapokupeleka basi ndio huko huko, hujali kuwa hiki kitu ni cha kweli au cha uongo ila wewe upo tu kukazana na misimamo yako, kwakweli hapo ujirekebishe”“Mmmmh yameisha na maisha yameendelea, ila nashukuru hujakaa na kinyongo kwangu”“Ni kweli sina kinyongo ila mimi ni tofauti na ulivyonifikiria, nilikuwa mkweli kwako, nilikupenda na kukujalia na leo pengine ndio ungekuwa mke wangu, ila naona Mungu alipanga iwe hivi”Mama Angel aliona kuendelea kuongea na Babuu pale basin i kuanza kukumbusha mambo yaliyopita kwa sana, ikabidi tu amuage kwani alimwambia kuwa ana mtoto mdogo, basi Babuu nae akaagana nae ila akampa kadi ya namba zake ili wawe wanawasiliana, kisha mama Angel aliingia kwenye gari yake na kuondoka.Basi baba Angel alifanikiwa kwenda kumfata Angel na kumueleza lengo mama yao kuwa ni kumpeleka Angel shule, basi akaondoka nae na kupanda nae kwenye gari kisha akampa barua ya kukaribishwa shuleni na kumwambia,“Sasa tunaenda dukani kununua vyote vilivyoandikwa hapo, kwaajili ya wewe kwenda shule’“Kwani shule naenda lini baba?”“Kesho nakupeleka shule”“Duh baba!!”Baba Angel wala hakuongea zaidi, na moja kwa moja walianza kuingia madukani na kununua vitu mbalimbali kama vifaa vya shule.Walipomaliza, wakati wanaondoka walikutana na madam Oliva ambapo aliwasalimia na kutaka kuongea kidogo na baba Angel, basi Angel aliingia kwenye gari na wao kubaki pale nje,“Mmmh Erick, sio muda wote nikitaka kuongea na wewe basi naongea ujinga! Hapana, kuna muda nataka kuongea na wewe mambo ya maana”“Mambo gani hayo?”“Ni hivi, hili jambo ni leo leo nimeliona kwa nyakati tofauti, kwanza nimemuona yule Sia akiwa na mwanamke mmoja hivi wakionekana kama wakijadili kitu halafu kuna mahali tena nimemuona mkeo na huyo mwanamke wakiongea na kufurahi inaonyesha ni marafiki, yani hili ni swala la leo leo. Mimi ni mwalimu na kwa bahati naweza kumsoma mtu hata kama simfahamu, naweza kuongea nae kidogo tu nikamsoma. Kwanza ni hivi Sia sio mtu mzuri katika familia yako, yani yule yupo kwa lengo la kuiangusha familia yako, kwanza kumbuka anakupenda sana na inamuuma sana kuona kuwa unafuraha na mke wako, kwahiyo anafanya juu chini ili furaha hiyo isiwepo, kuna muda utaona kama anaongea nawe vizuri ila sio mtu mzuri na kama ni mtu mzuri basi hayo anayosema kayaficha angewaweka wazi. Halafu kitu kingine huyu mwanamke niliyemuona na Sia anaonekana macho juu juu sana, nilipomuona na mkeo nimeshtuka, hadi nilienda kumsalimia mkeo, nadhani hajaelewa ni kwanini nimeenda kumsalimia ila ni sababu ya yule mwanamke, mwambie mkeo awe nae makini sana asije akalia badae. Hata kama ni rafiki yake ila awe nae makini sana, asimuamini kwa asilimia zoyte ataumia moyo wake bure”“Oooh nimekusikia, ila sijui huyo mwanamke ni nani?”“Ukimuuliza mkeo, atamjua ni nani. Muulize mwanamke ambaye mlikutana na madam Oliva ukiwa nae, alivaa gauni rangi ya nyeusi lenye maua ya njano, na kichwani kasuka yeboyebo halafu kajitanda ushungi kiasi atamkumbuka tu”“Sawa, hakuna tatizo. Nashukuru kwa hilo.”“Utaniambia shule unayompeleka Angel, niwe namtembelea”“Sawa, nitakwambia”Kisha akaagana nae na akaenda kumuaga Angel pia na kuondoka zake.Baba Angel na mwanae walirudi nyumbani sasa, ila muda huu walimkuta mama Angel tayari yupo nyumbani huku akishughulika na mapishi maana alijua wazi mwanae anakuja halafu kesho yake mwanae ataenda shuleni kwahiyo hatokuwa hapo nyumbani, licha ya hasira alizokuwa nazo dhidi ya mwanae ila akaona vyema kumpikia mwanae chakula ambacho huwa anakipenda sana.Kwahiyo walivyofika tu, waliwapokea na kuongea kidogo kisha Vaileth na Erica walienda kuandaa chakula ili waweze kula kwa pamoja, na kweli walikaa siku hiyo kama familia wakila na kufurahi.Baada ya hapo, mama Angel alienda na Angel chumbani kwa Angel ili kumsaidia kuweka vitu vyake vizuri kisha alianza kuongea nae,“Sikia Angel, nilitamani tupate wasaa wa kuzungumza hata kwa wiki moja ila nahitaji zaidi usome, nenda shule ujifunze vitu vingi uweze kupanua akili yako na fikra zako”“Asante sana mama”“Haya, na hizo simu ulizokuwa unatumia kwa bibi yako ziko wapi?”Angel hakujua kama mama yake angekumbuka hizo simu, kwani kwa mawazo yake aliona vyema kama usiku wa siku hiyo aweze kuwasiliana na Samir na kumueleza kuhusu yeye kupelekwa shule maana hakumwambia chochote kwahiyo hata kwa upande wake ilikuwa gafla kidogo, na muda mama yake anamuuliza aliogopa kukataa na kuamua kutoa zile simu kumkabidhi mama yake, yani mama Angel alisikitika na kumuangalia mwanae huku akipokea zile simu, aliziweka pembeni na kuzungumza nae,“Hivi Angel mfano ndio ungebakwa siku hiyo? Ungepata mimba ingekuwaje?”Angel alikaa kimya tu, kisha mama yake akaongea,“Sijui sijawahi kuongea na wewe, ila hata kama sijawahi nina uhakika bibi yako ameshakufundisha haya mara nyingi tu, Angel ukimaliza kidato cha sita naomba uje uniambie kuwa mama nimekuwa mkubwa sasa naomba unipe simulizi ya maisha, basi nitakupa simulizi inayohusu maisha yangu mwenyewe na wala sio ya mtu mwingine. Mwanangu sio kila anayekwambia anakupenda ukahisi anamaanisha, katika maisha tumezingirwa na maadui kila kona, kwahiyo mwingine ana lengo la kukuangamiza. Haya, huyo kijana unamfahamu vizuri? Angekubaka ingekuwaje? Niambie kwanza umefahamiana vipi na huyo kijana aliyetaka kukubaka?”“Mama, kwanza naomba unisamehe ila yule kijana ni dereva bajaji, siku moja niliamua kurudi kwa shangazi kwa miguu ndio nilikutana nae akanipa lifti basi ndio nikazoeana nae hapo. Halafu ni kijana ambaye aliwahi kukuleta wewe hapa nyumbani, nikaja kumpa hela kama unakumbuka”“Mmmh sikumbuki, kwahiyo ulimfahamu kwa njia hiyo, je hukuona kama kuna kitu kibaya anaweza kukufanyia ukizingatia humfahamu vizuri?”“Sikujua mama, alikuwa anaongea vizuri sana. Ila siku aliyogombana na Samir, nilimuona na yule mama ambaye mara nyingi anakuja hapa nyumbani, hata Erick hampendi yule mama, nilimuona akimpa pesa, halafu Samir nae aliniambia kuwa alipoenda hospitali alimuona yule mama akienda kumuona, Samir pia huwa hampendi yule mama sijui tatizo ni nini ila huwa anasema kuwa yule mama ni mbea sana, na akasema kuwa Ally atakuwa katumwa na yule mama”“Mmmh anaitwa nani huyo mama?”“Simjui, ila muulize Erick atakwambia jina la huyo mama”Ila mama Angel alihisia kitu, sema tu aliendelea kumpa nasaha mtoto wake na kumsaidia kupanga vitu pale na mwisho wa siku aliondoka na zile simu kwenda nazo chumbani kwake kwahiyo Angel hakuweza kuwasiliana na Samir kuhusu kwenda kwake shuleni.Kulipokucha, wote kwa pamoja waliakaa sebleni na kula chakula cha asubuhi kwa pamoja kumuaga Angel na kumtakia masomo mema, kisha Angel na baba yake wakaondoka na kuanza safari yao.Wakati Angel anaondoka na baba yake, wakiwa kwenye gari ndipo Angel alipomwambia baba yake kuwa kuna kitu kasahau kununua jana,“Tafadhari baba, naomba ninunue leo”“Jamani Angel unataka kwenda na vingapi shuleni mwanangu?”“Hiko kimoja tu baba, ni cha muhimu sana”“Haya tumesahau kitu gani?”“Nahitaji poda baba”“Khaaa ila watoto wakike jamani!! Haya ngoja tupitie dukani hapo”Basi walifika kwenye duka na kushuka kisha Angel alienda kuchagua poda aitakayo halafu baba yake akawa anailipia, wakati huo kuna mbaba alisikika akimuongelesha Angel,“Umekuwa mkubwa Angel”Baba Angel pia alisikia na kuamua kugeuka nyuma ili kuangalia ni nani aliyekuwa akiongea na Angel.  Basi walifika kwenye duka na kushuka kisha Angel alienda kuchagua poda aitakayo halafu baba yake akawa anailipia, wakati huo kuna mbaba alisikika akimuongelesha Angel,“Umekuwa mkubwa Angel”Baba Angel pia alisikia na kuamua kugeuka nyuma ili kuangalia ni nani aliyekuwa akiongea na Angel.Aliomuona aliyekuwa akiongea na Angel alipumua kidogo, kisha aliwafata pale karibu na yule baba alimsalimia pale baba Angel kisha baba Angel hakutaka maneno mengi sana na kuondoka na Angel ila yule baba alimsimamisha na kumuuliza,“Samahani, kwani muda huu unampeleka wapi?”“Anaenda shule huyu”“Hongera sana, wewe ni mwanaume wa pekee. Mwanzoni sikufikiria kama ungefanya hivi kwa huyu mtoto, nilijua ni mimi tu mwenye uwezo wa kuwa na mapenzi nae, hongera sana”Baba Angel alimuangalia tu na hakujibu kitu ila alipanda kwenye gari na mwanae na kuondoka zao.Wakiwa kwenye gari, Angel alimuuliza baba yake,“Kwani baba huyu tuliyekutana nae ni nani?”“Anaitwa Bahati, ni rafiki wa zamani kidogo. Alikuona zamani ndiomana ameshangaa kuwa umekuwa mkubwa”“Mbona anasema kuwa hakufikiria kama ungefanya hivi kwangu?”“Angel mwanangu, kuna vitu katika maisha havitakusaidia kwa wakati huu, kwahiyo sio lazima kuvijua, nimekutajia tu anaitwa nani ili umtambue. Na siku nyingine ukimuona basi umjue”“Sawa baba”Safari ikaendelea, ila kuna mahali kidogo gari ilisimama katika foleni, na Angel alimuona mtu akivuka barabara, basi alimuuliza baba yake,“Baba, samahani, yule anaitwa nani?”“Kwani unamfahamu?”“Namfahamu kidogo”“Yule, anaitwa Sia, unamfahamu vipi?”“Kuna stori nimemsimulia mama, basi ukirudi mwamabie huyo mtu aliyekwambia Angel anaitwa Sia”Baba Angel kidogo alishtuka na kumuuliza mwanae,“Ni stori gani?”Kwani alimfahamu vizuri sana Sia, ila kwavile Angel alikuwa huru kuongea kila kitu na baba yake, basi alimsimulia baba yake kila kitu toka alipokutana na Ally na jinsi alivyotaka kumtengenezea simu na jinsi Ally alivyopigwa na Samir, kwahiyo alimsimulia baba yake kila kitu ambaye alisikitika tu kwa kusikia yale,“Nilimuuliza Ally, akasema kuwa huyu mwanamke ni mamake mdogo ila nimekuwa nina mashaka sana na huyu mwanamke, na vile alivyoniambia Samir ndio kabisa baba, nimekuwa na mashaka nae.”“Ila mwanangu, cha kujifunza hapo ni kuwa usimuamini mtu kupitiliza, yani wewe fanya mambo yako mengine na usiwe na imani na mtu kupitiliza kwani huwezi jua kuwa huyo mtu anakuwazia vitu gani”Baba Angel aliongea na mwanae kule na kujaribu kumuelekeza vitu na mambo mbalimbali ya maisha huku akiendelea kumpeleka shuleni.Muda huu, mama Angel alikuwa akimpangia vizuri mumewe nguo za safari kwani alijua wazi kuwa, mumewe akitoka huko basi atamalizana na Junior na kuondoka kwenye hiyo safari yake.Wakati akipanga nguo, aliambiwa kuwa kuna ugeni, basi aliamua kuacha na kuongea kwanza na mgeni huyo, alipofika alikuta ni rafiki yake Fetty amefika kumsalimia, basi alimkaribisha na kwenda kukaa nae bustanini kwani alikuwa na mazungumzo nae,“Kwanza Erica za siku?”“Nzuri tu, vipi wewe na familia yako na ndoa yako?”“Kwakweli namshukuru Mungu maana naendelea vizuri, unajua nilikata tamaa yani sikuwa na raha kabisa jinsi mume wangu alivyobadilika na kuanza tena kukutaja wewe. Ingawa najua wazi hawezi kuwa na wewe ila nilikuwa naumia sana kwa alichokuwa anakifanya”“Pole sana ndugu yangu, kwakweli hata mimi mwenyewe nilikuwa sielewi wakati maisha yamebadilika na kila mtu na maisha yake. Ila hongera kwa kufanikiwa kumuweka katika mstari”“Unajua nini, na mimi bado kidogo tu nianze kuhangaika maana nilichoka. Mwanaume haeleweki hata kidogo, ndiomana nilikuwa natoka kwangu bila kuaga na kwenda kufanya mambo yangu, ila kuna mama nimekutana nae, kiukweli amenifundisha mambo mazuri sana na amenifungua akili yangu. Nikajiuliza ni wapi nakosea? Kwanini mume wangu akakumbuke alipotoka na kuacha kunikumbuka mimi? Nikaona kuwa lazima kuna kitu nakosea, na sikuona kama ni vizuri kumchukia mume wangu, basi nilianza kujirekebisha, cha kwanza sikutaka tena kuanza mabishano na mume wangu maana mimi nilikuwa na hiyo tabia, akipanda basi na mimi napanda, ila yule mama alinishauri vyema sana, nikaanza kujishusha na kuwa mpole, kiasi kwamba hata siku moja mume wangu aliniuliza, hivi ni wewe Fetty niliyekuzoea au kaja Fetty mwingine? Sikuwa namjibu vibaya mume wangu na nimefanya upendo wake kwangu unawili sasa. Huwezi amini kwasasa tunaishi kwa maelewano sana, yani hakuna tatizo kati yetu. Ila kilichonileta leo sasa unajua ni nini?”“Niambie”“Ni hivi, kwanza nilitaka kukushudia hayo kuhusu mimi na mume wangu ila pili, nataka kukwambia kuhusu yule mwanamke aliyekuwa anakusumbua sana wewe akili kipindi unakaribia kwenye ndoa yako na Erick”“Mmmh unamsema Sia huyo!”“Ndio huyo huyo, kwanza Sia anaonekana kuwa na matatizo ya kisaikolojia, halafu kila anayetambua yupo karibu na wewe anaanza kumwambia kuhusu Angel. Hebu fikiria, kakutana na mimi siku hiyo akaanza kuniambia sijui Angel sio mtoto wa Erick, yani nilimuangalia na kutamani kumzaba vibao, hata kama sio mtoto wa Erick basi yeye inamuhusu nini? Kwanza siri ya mtoto aijuaye ni mama. Akaanza kuniambia, naomba nikupeleke kwa baba mzazi wa Angel, yani kiukweli yule mwanamke sio mtu mzuri na mambo yako wewe yanamuhusu nini na anayajuaje?”“Kwahiyo na wewe unaamini kuwa Angel sio mtoto wa Erick?”“Mmmh sio naamini, bali mimi ukweli naujua vizuri, halafu huwezi amini hii kitu ni leo mume wangu ndio kaniambia sijui alikutana na Angel pamoja na Erick, basi alivyorudi nyumbani akasema, ana furaha sana. Nikamuuliza kwanini, akasema kuwa sikudhani kama Erick angeweza kumpenda vile Angel ukizingatia sio mtoto wake kabisa, siku zote nilikuwa nataka kumlea Angel ila kwa upendo niliomuona nao Erick basi naamini Erica ana furaha sana kuwa nae”“Kumbe ulikuwa hujui!”“Ndio nilikuwa sijui, ila mimi siku zote nakwambia ni mbea sana sema sifatilii mambo yasiyonihusu, sasa yeye kumwambia kila aliyekuwa karibu yako ni nini? Tumaini anaujua ukweli?”“Mmmh! Nadhani anajua, familia ya wakina Erick ipo tofauti sana, wana upendo wale. Yani Tumaini licha ya ukorofi wake ila ana upendo mkubwa sana kwa watoto, na ukimpelekea mtoto wako usifikiri atamtenga na watoto wake, anajua sana kulea. Hata Angel aliishi nae kipindi akisubiria mitihani ya mwisho”“Basi tulia, nitajua cha kufanya na huyu Sia. Nataka kujua ni kwanini anapenda kufatilia mambo yako na anapata faida gani, najua Tumaini hawezi kumfokea sababu ni shoga yake, il hilo jambo la Sia limeniuma na kufanya nije siku ya leo kukueleza hayo”“Nashukuru sana, nami nimeelewa vizuri tu, hakuna tatizo”Waliongea na mambo mengine mbalimbali na kisha kuagana ambapo Fetty aliondoka zake kuelekea nyumbani kwake.Jioni ya leo wakati baba Angel anarudi toka kumpeleka mwanae shuleni, moja kwa moja alipitia nyumbani kwa Sia, ambapo alimkuta, kama kawaida Sia alikuwa akitabasamu alipomuona na kutaka kwenda kumkumbatia ila alipomsogelea baba Angel alimdaka Sia kwa kibao kwenye shavu, ambacho kilimfanya Sia hadi aanguke chini na kuanza kujiliza,“Jamani, kwani nimefanya nini?”Alikuwa akilia huku akishikilia shavu lake, baba Angel aliinama pale chini na kumwambia,“Wewe mjinga si nilishakwambia achana na familia yangu”Kisha baba Angel aliinuka na kumpiga teke Sia, teke lile lilimsukuma Sia kidogo na kumfanya ahisi hata maumivu ya lile teke, basi akainuka taratibu,“Kumbe una hamu Erick ya mimi kuanza tena kuifatilia familia yako, yani kuja kunipiga hivi kweli!!”“Hivi unafikiri mambo yako uliyoyafanya siyajui, hivi wewe wa kwenda kupanga na mtu ili ambake mtoto wangu! Una akili kweli wewe!! Tena nadhani hela zangu mwenyewe nilizokuwa nakupa ndio ulikuwa unaenda kufanyia huo uovu wako, unaniletea ukichaa wako mimi!!”“Nisamehe bure tu, ila mimi sijafanya hivyo kwa kutaka kumuharibia mwanao ila mimi namuokoa yule mtoto asije kutembea na kaka yake, unajua Samir ni kaka yake?”“Kaka yake kivipi?”“Samir ni mtoto wa Rahim, ndiomana nilikuwa nafanya Angel awe mbali na Samir”“Halafu abakwe na kijana uliyemuandaa wewe!!”“Hapana, yule kijana asingembaka kihivyo”“Unajua wewe mwanamke ni kichaa eeeh!! Sikia nikwambie, Angel ni mtoto wangu na kama huyo Samir ni mtoto wa Rahim basi ndio vizuri atakuwa na Angel maana Angel ni mtoto wangu, unajifanya hamnazo, basi mimi ndio hamnazo zaidi yako”“Usiwe hivyo Erick, hebu fikiria wewe watoto wako usikie wameoana utajisikiaje? Kumbuka Rahim hajapenda kuwa na watoto kila mahali imetokea tu, na kuhusu huyo Angel ni nyie ndio mmemfuga ili asimjue baba yake, sio vizuri hivyo. Na mimi nitamwambia ukweli Rahim”Baba Angel alimuangalia Sia kwa gadhabu zaidi, kisha akamsogelea na kumzaba vibao visivyokuwa na idadi halafu akamkunja na kumwambia,“Ole wako, mjinga wewe nitakutia ngeu. Jitie tu akili zimekuruka”Halafu baba Angel akaondoka zake na kumuacha tu Sia pale akilia huku akishika mashavu yake.Baba Angel alifika nyumbani kwake usiku, na akamuita Junior na kumwambia kuwa kesho yake ataenda kununua nae vitu na kwenda kumkabidhi shuleni, hapakuwa mbali ila ilikuwa ni shule ya bweni.Kisha alipomaliza ndio alienda kuongea na mke wake, kwa wakati huo hata hakuwa na ya kuongea mengi kwani alikuwa na uchovu mwingi alimwambia tu mkewe kuwa siku ya kesho kutwa ndio angesafiri sababu sehemu yenyewe anatakiwa Jumatano, mkewe alimuelewa na hakuwa na tatizo nae juu ya hilo,“Kwahiyo utasafiri na ndege au basi?”“Nitasafiri na basi tu”“Sawa, hakuna tatizo basi”Muda huu waliamua tu kulala kutokana na uchovu.Basi kulipokucha, baba Angel alijiandaa na moja kwa moja kuondoka na Junior kwenda kununua nae mahitaji yani Junior hakudhani kama ingewezekana kweli kwa siku hiyo kupelekwa shuleni ila hakujua vizuri baba Angel huwa akiamua lake basi ameamua tu.Leo, Elly hakwenda shule sababu aliona kama mama yake hana hali nzuri, alimua kukaa nae nyumbani tu,“Elly jamani kwanini hukwenda shule?”“Mama unanificha tu ila nakuona kuwa haupo sawa kabisa, angalia mashavu yako yalivyovimba hivyo, toka jana huniambii ukweli ila mama haupo sawa”Mama Elly aliinama chini na kulia ambapo mtoto wake alimsogelea karibu ili kujua kinachomliza mama yake,“Kwani tatizo nini mama?”“Unajua sikufikiria kumpata mtoto mwenye kujali na mwenye upendo kama wewe Elly, kwakweli mwanangu upo tofauti sana. Ni kweli sipo sawa ila hii sio sababu ya kukufanya wewe usiende shuleni jamani!!”Mara simu ya mama Elly iliita na kuongea nayo pale, na baada ya kuikata alimuangalia mwanae na kuinuka,“Sasa nimepata nguvu, unajua nini sina hela mwanangu halafu Amina nae si unaona kuwa anahitaji matibabu kwasasa, sema kuna jambo limetokea”“Jambo gani mama?”“Yule dada yangu wa mkoani, amesema kesho nimsafirishe Amina, na yeye atampokea kwahiyo sasa ngoja nimuandae Amina kwaajili ya safari”Alienda kujiandaa kwa muda huo bila ya kujali kuwa kavimba mashavu au la ila alijiandaa haraka haraka na kwenda kumtafutia mkoba Amina wa kuwekea nguo zake ili aweze kumsafirisha vizuri.Muda huu Tumaini alienda nyumbani kwa mama Angel kuongea nae mawili matatu maana kuna ujumbe aliupata ndio alikuwa amemletea ujumbe huo,“Niambie wifi yangu”“Kheee leo naona umekuja na furaha hadi kuniita wifi!!”“Aaaah jamani, kawaida tu ila nina maongezi na wewe. Tupate mahali tuzungumze maana humu ndani kwako siku hizi naogopa, hivi Erica yupo?”Mama Angel alicheka na kumjibu wifi yake,“Erica yupo shuleni, anaogopewa eeeh! Ila twende sebule ya juu kule”Basi wakaenda zao hadi sebule ya juu na kuanza kuzungumza,“Kwanza kabisa yule mama Sarah ulimtafuta?”“Kheee umesahau wewe kuwa ulitapeliwa na Derrick sijui hela pamoja na namba ya huyo mama Sarah!”“Dah eti nilisahau jamani loh! Basi nimepata habari za mama Sarah, unajua mimi sio mbea ila huwa naletewa habari tu usije sema Erica karithi kwangu, akuuu Erica karithi kutoka kwenye ukoo wako”“Aaaah jamani, haya habari gani hizo?”“Ni hivi, nasikia mama Sarah alikuwa akiishi na mwanaume ila huyo mwanaume alikufa, toka hapo yule mama Sarah nasikia kazi yake ni kuiba waume za watu tu”“Mmmh!!”“Sasa nina mashaka, kama anakufahamu basi kuwa makini sana na mumeo maana kwa niliyoyasikia kumuhusu nikanyoosha mikono juu”“Ila hivi nafahamiana nae kweli!!”“Anadai anafahamiana na wewe, kingine kilichonileta sasa”“Eeeh kipi hiko?”“Kuna kijana mmoja ni dereva bajaji, alikuja nyumbani kwangu jana, akisema kuwa alikuwa na mahusiano na Angel, halafu kuna siku sijui Angel alipoteza fahamu basi akambeba ili kumsaidia ila akatokea kijana ambaye alidai kuwa na mahusiano na Angel pia, yule kijana akampiga sana hadi alikuwa amelazwa, ndio ametoka, kaja jana nyumbani kwangu akiwa anachechemea. Unajua sijaelewa kabisa ndiomana leo nimekuja huku”“Kheee, ngoja nikusimulie yaliyotokea yani hadi tumeamua kumpeleka Angel shule mapema kabisa”Basi mama Angel alianza kumsimulia toka alipowasiliana na mama yake na jinsi Angel alivyomsimulia, kisha akamwambia,“Ila nahitaji kuonana na huyo kijana ili niongee nae vizuri maana kuna mambo nataka kumuuliza”“Yupo tu, na uzuri napafahamu hadi nyumbani kwao, anaishi na bibi yake. Hata sielewi alianza lini mahusiano na Angel jamani, mambo haya loh!!”Walizungumza tena, ila Tumaini alipigiwa simu kwahiyo muda huo huo akaaga na kuondoka zake.Tumaini, leo hakutembea na gari kwahiyo akiwa njiani kuna mtu alimsimamisha na alipomuangalia mtu huyo alikuwa ni Sia, basi alianza kumsalimia pale na kumuuliza,“Mbona umejitanda hivyo? Unajua hadi sikukufahamu!”Sia akajifunua kagha alizokuwa kajifunikiza kiasi,“Kheee mbona umevimba mashavu hivyo!”“Mambo ya mdogo wako hayo?”“Ni Erick ndio kakufanya hivyo jamani!Imekuwaje tena? Hayo mambo yalikuwa zamani, imekuwaje kwani?”“Yani hata mimi simuelewi, nilikuwa nyumbani kwangu ila kuna kijana mmoja hivi huwa anakuja kunisaidia baadhi ya kazi nyumbani kwangu, mara akaja Erick, sijui akafikiria nini kuhusu mimi na yule kijana, jamani alianza kunipiga vibao visivyokuwa na idadi. Sijui kwanini Erick ananifanyia hivi! Ana maisha yake kwasasa, ana mke na watoto ila kwanini ananionea wivu mimi!!”“Unajua sikuelewi Sia, yani Erick akuonee wivu wewe?”“Kama huamini mpigie hapo simu muulize kama jana hajaja kwangu na kunipiga?”Kwakweli Tumaini hakuyaamini maneno ya Sia kabisa, basi alichukua simu yake na kumpigia kaka yake, alivyosalimiana nae tu alimuuliza,“Eti, Erick, nasikia jana ulienda nyumbani kwa Sia na kumpiga sana”“Huyo mwanamke ni kichaa, najua lazima kakuletea hayo maneno akifikiri kuwa wewe ni mtetezi wake, tena mwambie akiendelea nitamkata miguu yake kabisa”Simu ikakatika, kisha Tumaini alimuangalia Sia na kumuuliza,“Kwani ulimfanya nini?”“Nimfanye nini unadhani? Ni ile tu mimi kumtetea yule mkaka basi ndio imekuwa tatizo, yani kama kaka yako ananipenda si anioe tu nijue moja kuliko kunifanyia hivi mtoto wa watu mie, na mimi nastahili kupendwa, nastahili kudekezwa kama anavyomdekeza Erica”“Mmmh pole sana”“Asante, ila naomba unisaidie namba ya mama Erick tena”“Unataka kumueleza huu ujinga?”“Hapana, ni vitu vingine kabisa. Aliniambia niwe namwambia maendeleo ya Elly shuleni, naomba namba yake tena maana mimi nimebadili simu ile nyingine iliharibika”“Mmmh!”Tumaini aliguna ila alimpa namba na kuagana nae, kisha kila mmoja kuelekea kwenye safari yake aliyokuwa akienda.Ila Tumaini aliondoka hapo huku akijiuliza maswali mengi sana,“Yani sielewi, kweli kabisa Erick ampige huyu mwanamke sababu ya wivu! Hapana kuna kitu kingine huyu mwanamke kakifanya, lazima ni hivyo”Wakati Tumaini akiendelea mbele, kuna mahali alimuona kaka yake akiwa kasimama na mwanamke, basi hakusita kumfata na kumsalimia, kidogo kaka yake akajiuma uma midomo na kumtambulisha Tumaini,“Aaaah huyu ni mdogo wangu anaitwa Tumaini, halafu mdogo wangu huyu ni wifi yako anaitwa Mariam”Tumaini akaitikia pale na kumvuta kidogo kaka yake pembeni huku akidai anataka kuongea nae kidogo,“Kaka Deo jamani hapana kwakweli, kwanini kutufanyia hivi wanawake? Unajua na mimi ni mwanamke tena nimeolewa na ninaumia sana kuona mwanamke mwenzangu anafanyiwa kinyume. Kweli unapata ujasiri gani wa kunitambulisha kuwa yule ni wifi wakati mimi namjua mama Junior?”“Sikia nikwambie kitu, siku zote hutakiwi kuwa upande wa wifi yako ila unatakiwa kuwa upande wa kaka yako. Hiko ndio kitu ambacho ulikuwa ukigombana na Erick kipindi kile, sababu ukiwa tayari na uelewano na wifi Fulani basi unaona ndio maisha ya uwifi yameishia hapo ila hapana, mwache kaka yako awe huru na afanye anachojisikia”“Sio kwa stahili hii, kumbuka umeoa, na licha ya kuoa yule mwanamke anavumilia sana kukulelea mitoto uliyozaa huko, badala na wewe utulie ndio kwanza unafanya mambo ya ajabu. Tena hata Junior humlei wewe maana alikuwa akimlea mwenyewe na sasa analelewa na Erick ila mitoto yako anailea pale kwa upendo kabisa, unawezaje kumsaliti mwanamke kama yule?”“Mambo ya ndani huwezi kuyajua wewe, fanya yako niache na maisha yangu”Tumaini alimuangalia kaka yake kwa gadhabu sana kiasi kwamba aliondoka hapo bila hata kumuaga huyo wifi mpya aliyetambulishwa na kaka yake, yani alijikuta tu akisikitika kuhusu wifi yake aliyemzoea.Baba Angel alipomaliza kumkabidhi Junior shuleni, alitoka pale na moja kwa moja kwenda shuleni kwakina Erick ili kumchukua Erick na hapo ilibidi apate ruhusa toka kwa madam Oliva, maana alikuwa ni mwalimu wa nidhamu na ilikuwa ni zamu yake kwa wiki hiyo, basi baba Angel alienda ofisini kwake na kuongea nae,“Ila swala langu umelifanyia kazi?”“Swala gani tena?”“Si lile la mkeo na yule shoga yake?”“Dah ndio unanikumbusha ujue, yani mimi mambo ya wanawake huwa sifatilii sana wala nini. Kwahiyo nipe ruhusa mwalimu, halafu nikuombe kitu kama siku kukiwa hakuna masomo jioni naomba umpe ruhusa Erick ili dereva aweze kumchukua”“Kwani atakuwa anaenda wapi?”“Ni kwenye kiwanda changu, nahitaji Erick awe anasimamia japo kwa ufupi tu, najua kuwa anasoma na masomo yanambana sana ila nahitaji awe anapata muda angalau hata dakika kumi na tano kuwepo kiwandani kwaajili ya kufunga mahesabu”“Oooh hayo ni mambo ya maendeleo na ni mazuri sana, ila kuna kitu naomba nikusaidie”“Kitu gani?”“Mara moja moja niwe nampeleka Erick huko kiwandani na nimsubiri amalize na kumrudisha nyumbani ili pia kutunza muda wake vizuri wa kimasomo na kutokupoteza uelekeo”“Mmmh haya hakuna tatizo”“Kwahiyo tunaanzia leo, yani hapa naacha mtu ili na mimi nikaone kidogo huko kiwandani”Basi baba Angel hakuona kama ni tatizo, akaamua kuondoka na madam Oliva huku akiambatana na Erick hadi kiwandani ambapo walionyeshana pale, na baba Angel alimuelekeza Erick cha kufanya kipi akiwa hayupo, na mambo mbalimbali kisha wakaondoka na hivyo ikambidi baba Angel kumpitisha kwanza madam Oliva nyumbani kwake.Walifika hadi kwa madam Oliva ambaye aliwakaribisha vizuri kabisa,“Karibuni jamani, sio vizuri kuishia nje, karibuni hata ndani kwangu mnywe japo maji”Baba Angel alikumbuka siku ambayo yule madam alimwekea dawa, na kujikuta akigoma tu na kudai kuwa wanaharaka sana, muda huo huo Steve nae aliyeonekana kuwa alitoka ndio alikuwa akirudi tu taratibu akitembea, kwahiyo alipoona gari pale getini alisogelea ili kuangalia ni nani, akakutana na baba Angel sasa ambapo baba Angel alimsikitia Steve tu alipomuona ila hakuongea kitu zaidi ya kuaga na kuondoka zake.Wakiwa njiani Erick alimuuliza baba yake,“Ila baba, sijakuuliza swali hili hivi duka letu kule limeishia wapi? Halafu huyu si ndio alikuwa akiuza duka letu?”‘Ndio, ila huyu hauzi tena, natafuta mtu mwingine ila muaminifu wa kufanya hivyo, sema bado sijampata kwahiyo duka limefungwa tu”“Niruhusu mimi nitafute mtu”“Kheee utampatia wapi wewe?”“Niruhusu tu baba, utaona na duka litafanya vizuri”“Nakuamini mwanangu, basi muda huu twende kwanza tukatembelee pale dukani ingawa muda umeenda ila nitakuelekeza vichache pale na utaweza kujua cha kufanya”Kisha safari kwa muda huo ikawa ni moja kwa moja hadi dukani ambako alikuwa akiuza Steve na kumfanya baba Angel amuelekeze vizuri mwanae pale, kwahiyo muda walioondoka kurudi nyumbani ilikuwa ni muda umeenda sana na kulikuwa na uchovu haswaa kwa baba Angel ambaye alikuwa na mizunguko sana kwa siku hiyo.Walipofika nyumbani, ni moja kwa moja kujindaa tu kulala kwahiyo vitu vingi baba Angel hakuongea na mke wake hadi palipokucha, ni mama Angel aliyemuamsha mumewe mapema maana walishaongea kuhusu hiyo safari, basi aliamka na kwenda kuoga na kujiandaa kisha walikaa kidogo na kuongea,“Hivi unajua mume wangu hatujaongea mambo mengi sana?”“Ni kweli ila hii safari nayo ni ya gafla sana”“Ila kwanini umechagua kupanda basi na sio ndege?”“Nikirudi kutoka hiyo safari utajua vizuri mke wangu ni kwanini sijapanda ndege, wenyeji watanipokea kutoka kwenye basi na sio ndege”“Sawa nimekuelewa”Muda ulifika na baba Angel kutaka kuondoka, kwani tayari alishaongea na dereva ila mkewe alimwambia,“Subiri kidogo tuondoke wote, maana nitakusindikiza hadi stendi kuu”“Mke wangu jamani, baki tu na mtoto”“Hapana, siwezi kubaki na kuacha bila kukusindikiza”Ilibidi baba Angel akubali tu ingawa hakutaka kumchosha mke wake, kwahiyo waliondoka pale kuelekea stendi, walipofika moja kwa moja mama Angel alimsindikiza mumewe kwenye basi alilotakiwa kupanda ila kwa bahati nzuri au mbaya, lile basi lilikuwa ndio basi ambalo Sia alimpakiza yule mtoto Amina, kwahiyo wakati Sia anashuka kutoka kumuweka Amina kwenye siti ndio akakutana na baba Angel na mama Angel mlangoni, basi Sia akasema,“Jamani Erick kama ulikuwa unakuja kusindikizwa na mkeo si ungeniambia tu ili nisihangaike kuja kukusindikiza?” Ilibidi baba Angel akubali tu ingawa hakutaka kumchosha mke wake, kwahiyo waliondoka pale kuelekea stendi, walipofika moja kwa moja mama Angel alimsindikiza mumewe kwenye basi alilotakiwa kupanda ila kwa bahati nzuri au mbaya, lile basi lilikuwa ndio basi ambalo Sia alimpakiza yule mtoto Amina, kwahiyo wakati Sia anashuka kutoka kumuweka Amina kwenye siti ndio akakutana na baba Angel na mama Angel mlangoni, basi Sia akasema,“Jamani Erick kama ulikuwa unakuja kusindikizwa na mkeo si ungeniambia tu ili nisihangaike kuja kukusindikiza?”Wote walijikuta wakimshangaa Sia, ni pale baba Angel aligundua kuwa huyu mwanamke ana matatizo ya akili, ila gari nalo lilikuwa linataka kuondoka, basi baba Angel akasogea karibu na mkewe na kumwambia,“Tafadhari mke wangu usimsikilize huyo mwanamke, ona kama mgonjwa wa akili anaongea peke yake, nakuomba kwa muda huu urudi tu nyumbani”Akambusu na yeye kupanda ndani ya lile basi halafu likaondoka maana ilikuwa kama linamsubiria yeye, basi mama Angel nae alikuwa akirudi kwenye gari yao ila Sia alimfata kwa nyuma na kuongea nae tena,“Unajua kuna muda huwa unahisi mimi ni kama chizi ila kuna muda huwa unahisi naweza kuwa naongea ukweli, pole sana sababu hunielewi ila ukitafakari utanielewa vizuri sana”Mama Angel hakumjibu na kwenda hadi walipoacha gari lao, na kutaka kufungua mlango ili apande ila kabla hajafungua ule mlango, Sia alienda mbele yake, hadi ikabidi aongee,“Kwani una matatizo gani wewe?”“Matatizo unayo wewe ambaye hujiamini”“Unajua wewe, kweli una kichaa. Sasa mimi nisijiamini kwa lipi? Hebu sogea hapo nipande”Sia alisogea ila mama Angel alipofungua tu mlango na yeye alifungua wa nyuma na kupanda pia, mama Angel hakutaka kuongea sana na kuondoa gari lile mahali pale, maana yeye alivyoamua kumsindikiza mumewe aliondoka na mumewe tu kwahiyo hawakuondoka na dereva.Basi alifika mahali akasimamisha akapaki gari pembeni sasa na kumuuliza Sia,“Kwani tatizo lako ni nini? Kitu gani unahitaji toka kwangu?”“Kwani hujui? Ninahitaji kuwa mke mwenzio, ni hivi Erick hataki kunioa sababu anajua kuwa wewe utachukia na kudai talaka ndiomana anaogopa kufanya hivyo, ila wanawake tuwe na huruma jamani hebu tuhurumiane, kubali Erick anioe na mimi ili nami niwe na mume”Mama Angel akacheka kidogo na kumuuliza,“Kwani huyo wa kukuoa ni mimi au Erick?”“Ni Erick”“Sasa mbona unakuja kuniomba mimi? Unajua una wazimu wewe eeeh! Ngoja nikwambie, nahisi hujui kuhusu mimi vizuri, kwenye ukoo wetu hakuna mambo ya uke mwenza, yani sahau kabisa kuwa utaolewa ikiwa mimi nipo ndani yani sahau kuhusu hilo. Halafu jambo lingine, wewe ni mwanamke wa aina gani ambaye huelewi neno sikutaki? Huyo Erick ulikuwa nae na alikufanyia vituko vyote vya dunia ila ukajifanya unapenda sana, saivi unaaanza kuhangaika kama paka shume. Hivi unadhani ujinga uliokuwa ukifanyiwa na Erick anaweza kunifanyia mimi? Sikia nikwambia, kama mwanamke unatakiwa uishi kwa kujitambua sio kuendeshwa kama toy, wewe unaona kabisa kwa matendo ya huyu mwanaume hakuna upendo hapa bado unakomaa tu kumfatilia, na mpaka leo hujakata tamaa, hivi ni mwanamke wa aina gani wewe?”“Mimi ni mwanamke wa kawaida tu kama wanawake wengine, sikia nikwambie Erica, nimejua kuteseka kipindi nikiwa kwenye mahusiano na huyo Erick, muulize kanitoa mimba ngapi? Muulize mara ngapi nimemfumania na nikamsamehe tu, muulize ni mara ngapi alikuwa akinikosea ila nikimuuliza ananipiga mimi, ila sababu nilimpenda basi nilivumilia kila kitu, nilikuwa naenda kwao mimi, nasafisha chumba chake, nafua kila kitu chake, nikiamini kuwa kuna siku nitaishi nae kama mke na mume, usinilaumua wala usinione mjinga. Mbona wewe umezaa na Rahim? Si uliamini atakuoa pia, yani maisha ndivyo yalivyo kwahiyo usinishangae mimi”“Kwahiyo kama nilizaa na Rahim ndio unataka nimkazanie huyo Rahim anioe? Akili zako ziko wapi Sia? Mtu ukishafanya kosa moja basi usitake kulirudia kosa hilo, ukianguka unainuka na kujikung’uta kisha maisha yanaendelea”“Ungetambua hayo basi ungemuonyesha Angel baba yake”“Baba yake gani sasa? Angel ni mtoto wa Erick, hutaki nenda kachote maji uoge ili upate nguvu za kuendelea kubisha”“Kwahiyo Rahim?”“Huyo unamjua wewe, ila mama wa Angel ni mimi na baba wa Angel ninayemtambua ni Erick. Kama Angel ulimzaa wewe basi itakuwa baba yake ni Rahim ila kwa niliyemzaa mimi ni mtoto wa Erick”“Yani unajibu kwa madaha kiasi hiko!”“Ndio, naomba ushuke tu kwenye gari yangu kiroho safi wala sitaki kugombana na wewe”Na kweli leo Sia hakubisha wala nini kwani moja kwa moja alishuka kwenye lile gari na mama Angel aliendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwake.Vaileth hakufanya kazi yoyote siku hiyo maana alikuwa na kibarua cha kumbembeleza mtoto Ester tu, ukizingatia mama yake alijua kuwa atawahi kurudi ila haikuwa hivyo, alichelewa kurudi, basi wakati akimbembeleza ndipo alikuja shangazi yao na wakina Erica yani Tumaini, kwahiyo alimkuta Vaileth akimbembeleza mtoto,“Kheee mama yake yuko wapi?”“Alitoka asubuhi kwenda kumsindikiza baba, maana baba leo kasafiri”“Loh! Hawa nao jamani, halafu mbona safari za kimya kimya hizo hata hawasemi loh!”Basi alikaa kimya na kumtaka mtoto na yeye akimbembeleza mtoto yule, basi akamwambia Vaileth akalete vitu vitu vya kuchezea mtoto ili amzubaishe navyo, ambapo Vaileth alifanya vile, na kati ya vile vitu alikuwepo na mdori ambaye aliwahi kuletwa na Sarah, basi Tumaini alipomshika yule mdori alijikuta akikumbuka kitu,“Mbona kama namjua huyo mdori, au nilikuwepo wakati wakinunua!”Vaileth alisikia na kujibu,“Hapana, huyo mdori aliletwa na binti mmoja hivi anaitwa Sarah ni rafiki mkubwa sana wa Erick”“Oooh sawa, nashukuru kufahamu”Basi akawa anambembeleza mtoto kwa kumchezeshea yule mdori ni kweli mtoto alinyamaza huku akiangalia jinsi yule mdori alivyo, alicheza cheza nae pale yule mtoto hadi mwisho akalala pale pale na hata Tumaini nae alijihisi uchovu na kulala pia kwenye kochi.Mama Angel aliporudi aliwakuta pale sebleni na kumshtua wifi yake, wakasalimiana pale,“Ila wewe, unawezaje kwenda kumsindikiza mumeo na kuacha mtoto mdogo hivi nyumbani!”“Jamani, kwahiyo hakuna nitakachoweza kumfanyia mume wangu sababu nina mtoto mdogo!!”“Hapana sina maana hiyo, ila kwanini usingeenda nae tu! Mtoto Amelia sana huyu”Basi mama Angel alimchukua mwanae ambaye alimka pia kwa muda huo na kwenda nae chumbani ili kumnyonyesha mwanae, na kweli alienda na kumnyonyesha huko halafu mwanae akalala na kumuacha chumbani amelala kisha akatoka tena sebleni ambapo wifi yake akamuuliza,“Kwani ulipotoka kumsindikiza mumeo ulipitia wapi?”“Sijapitia popote, ila kuna chizi mmoja kanichelewesha sana”“Chizi gani huyo?”“Si huyo Sia, jamani kwa kifupi ni kwamba nimemchoka Sia, yani nimemchoka kabisa, ana mambo ya ajabu sana tena hajifikirii wala nini”“Hata mimi alikuwa rafiki yangu ila kwasasa nimemchoka pia, natumai hajakuharibia siku yako. Naomba Mungu akusaidie uweze kupambana na huyu adui maana naona Sia kawa adui yako kabisa”“Amen, Mungu anisaidie tu kwakweli. Ananiandama na watoto wangu balaa, akianza balaa zake unaanza kuwaza ni kwanini nimemfahamu huyu kiumbe jamani.”“Pole sana, tuachane na huyo mtu kwasasa. Ngoja nikuulize tu, hivi huwa unaongea na dada yako Bite”“Kuongea kuhusu nini?”“Naomba umshauri dada yako atafute mwanasheria kwaajili ya kusimamia mali za Junior, unajua Junior nae anastahili kupata urithi wake. Nimefikiria sana juu ya hilo nikaona nije kuongea nawe hivyo, ukizingatia kwa niliyoyaona jana”“Yapi hayo?”“Sikwambii kwa ubaya, ila jana nimekutana na kaka Deo akiwa kasimama na mwanamke mwingine, halafu bila aibu amanitambulisha kwa huyo mwanamke kuwa ndio wifi yangu, kwakweli nimeumia sana, maana mimi ni mwanamke, na dada Bite namfahamu vizuri sana, ni mwanamke mwenye roho nzuri na asiye na makuu ni kwanini amfanyie hivi basi! Nimeumia, naona pale hakuna chochote atakachoambulia Junior maana kaka yangu siku zote hajamuhesabia Junior kama mwanae, ni tatizo pia kwa wifi yangu ukizingatia hajazaa na kaka Deo, kiukweli nimemuonea huruma sana mama Junior, msaidie kwa hili”“Nashukuru sana, ila kwanini baadhi ya wanaume wapo hivi jamani!! Hivi mtu kama dadabyangu ndio wa kumfanyia ujinga kiasi hiko kweli!! Masikini, mwanamke wa watu ni mpole na asiye na makuu ila hana bahati na mapenzi kabisa, sijui kwanini yani”“halafu kitu kingine ambacho naona wazi kaka Deo hajamfanyia sawa mama Junior, ni ile hali ya kumkataza kufanya kazi, ili tu amlelee watoto wake, masikini dada yako ni mpole na ana utu, akakubali hiyo hali na kukaa tu bila kazi. Naona cha muhimu pia ni kumsaidia apate kazi, kumsaidia pia apate urithi wa mumewe maana yule alikuwa ni mke halali wa ndoa licha ya talaka ile”“Unajua katika maisha kuna mambo tunayafanya halafu badae tunakuja kujutia sana na kujiuliza kuwa tumeanzaje kufanya mambo ya namna hii. Ila kabla ya kwenda kufungua nae kesi, nitamtafuta kwanza Dora na kuongea nae ili nisikia anasemaje juu ya hatma ya mali za watoto”“Hapo sawa kabisa, ila Dora atakubali kurudisha kwa amani kweli?”“Kumbuka Dora kaokoka kwasasa, natumaini atakubali tu, tukiona anabisha basi tutatumia hata viongozi wa kanisa lake kumshauri. Ila kaka yako anachofanya sio sawa kabisa, ndiomana dada yangu hakutaka kuolewa tena, bora angeishi kwa maisha aliyojiamulia kuliko hiko alichofanywa na kaka yako”“Ila sio ndio mtuchukie ukoo mzima, halafu usimwambie ukweli kuhusu hayo, yani mwambie tu unashughulika kwaajili ya Junior”“Siwezi kumwambia kuhusu hayo, mambo ya mapenzi, unaweza sema hapa halafu ugeukwe na uonekane ni mnafki na una lengo la kubomoa ndoa yao. Ila nitashughulika na hayo maana roho inaniuma pia”Waliongea pale na Tumaini aliamua kuaga na kuondoka zake.Jioni ya siku hii wakati Erica amerudi tu kutoka shuleni, muda mfupi Junior nae alirudi na kumfanya mama Angel amshangae,“Wewe Junior jamani, si jana ndio umepelekwa shule wewe!!”“Ni kweli mamdogo ila kiukweli bamdogo kanichukua haraka haraka sana, kuna vitu nilisahau. Kwahiyo kesho nitatokea hapa kwenda shuleni”“Kheee Junior jamani”Basi Junior alienda chumbani kwake, muda kidogo Erick nae alirudi basi mama yake alimuita na kuongea nae,“Kwahiyo Erick ulipitia kiwandani?”“Ndio mama”“Ngoja nikwambie kitu mwanangu, sio kila siku ndio uwe unapitia kiwandani. Kumbuka una masomo na pia unahitaji muda wa kupumzika, sijui unanielewa”“Nakuelewa mama”“Vipi Sarah hajambo!”“Leo sijaonana nae, hajafika shule leo”“Oooh labda anaumwa jamani, basi na kesho asipokuja utaniambia Erick. Sawa mwanangu”“Sawa mama”Kisha Erick akaenda chumbani kwake kubadilisha sare za shule, muda huo huo akafatwa na dada yake ambaye alipoingia tu alimuuliza,“Kwanini mama anapenda sana kumuulizia Sarah?”“Sijui ila nadhani ni kwavile Sarah ni mcheshi na ana upendo ndiomana mama anamuulizia”“Mama kajuaje kama Sarah ana upendo?”“Si kwa zile zawadi ambazo Sarah huwa anampa mama”“Mmmmh zawadi gani hizo?”“Umeona kitenge alichovaa mama Juzi! Basi alipewa zawadi na Sarah”“Mmmh!”“Ndio hivyo, hutaki!! Unadhani sisi ambavyo hatumkumbuki mama kwa zawadi ndio watu wan je nao wapo hivyo? Wenzetu wanamkumbuka mama yetu, kwahiyo tujirekebishe”“Haya nimekusikia, ila mimi sina hela za kumnunulia mama zawadi, nitafanyeje sasa? Naona Sarah atakuwa akiishi maisha ya kujiachia sana kama anayoishi Samia, ila mimi nafugwa sana hadi sina raha kabisa”“Jamani Erica, raha gani unayoita wewe lakini eeeh!”“Sikia nikwambie, Samia ana simu na anawasiliana na mtu amtakaye, akitaka mahitaji yake anapewa hela na anaenda kununua mwenyewe, kwahiyo anazunguka mwenyewe madukani na kununua atakacho ni tofauti na mimi. Nipo shuleni ila utakuta sina hata mia, kisa tu kila kitu nakula cha shule, yani siwezi kununua hata pipi, ni Samia tu huwa ananiletea zawadi mara za pipi, biskuti na keki ila mimi sina hela ya kumnunulia hata maji, mama ananipa maisha ya manyanyaso sana”“Utaona ni manyanyaso kwasasa, ila ukikua utaona kuwa mama alikuwa akikuweka katika misingi imara, ni kweli huna hela ila huwa hutamani hela hata ukute mtu kaianhgusha ndiomana ile laki mbili ulikuja kumkabidhi mama, ni kitu gani utake mama asikununulie? Ila usijali, nitaongea na mama ili awe anakupa hata mia tano ya kulinda begi lako la shule”“Oooh hilo swala zuri sasa, na mimi nitaweza kumnunulia mama zawadi kama huyo Sarah”Kisha Erica alitoka, ila ilionekana wazi hakupenda kabisa mama yake kuonekana kumsifia sana Sarah, kwahiyo aliona kama Sarah anapendwa zaidi na mama yake.Usiku wa leo, Junior alienda kulala chumbani kwa Vaileth huku akilalamika kuhusu shule,“Sijui ni kwanini wamenipeleka shule ya kulala huko huko, mimi siwezi sijui wana mpango nifeli hawa!”“Hamna Junior, wanakuandalia mazingira mazuri sana, ila kwasasa unaona kama wanajisumbua ila wanakuandalia mazingira mazuri sana kwa wewe kuweza kusoma na kufika mbali. Usiwe kama wakina sisi”“Ila mimi sitaweza kusoma nikiwa nalala shule, yani nalala mbali na wewe ndio kusoma gani huko? Nataka niwe nalala karibu na wewe ndio nitasoma vizuri zaidi”“Mmmh sijui wewe na mamako mdogo, mtaelewana wenyewe ila asitufumanie tu maana nadhani iatakuwa ni balaa sijui nitarudishwa kijijini mweeeh!”“Usijali, muone hivihivi huyu mamdogo na ukali wake, ila ni mpole sana hakuna mfano kwahiyo hata akitufuma atatusamehe tu”Basi kwa siku hiyo walilala vizuri kabisa, na kulipokucha, Junior alienda kujiandaa na kuondoka zake kwenda shuleni, hakupita kumuaga mama Angel wala nini, ni moja kwa moja alienda shuleni tu.Mama Angel alitulia nyumbani kwake na kuwasiliana na mume wake kumuuliza kuhusu huko alipoenda, na alipompigia simu tu alipokea na kuanza kuongea nae,“Nisamehe mke wangu kwa kutokukwambia kuwa nimefika, huku mtandao unasumbua sana”“Dah pole jamani”“Halafu kuna baridi sana, kitu kingine sikukwambia asante sana kwa hizi shati ulizoniwekea yani leo nimevaa hii ya kitenge kila mtu ananisifia kuwa nimependeza sana, asante mke wangu”“Asante pia mume wangu, ila kuwa muangalifu huko. Nakupenda sana”Basi akaagana nae, na kuweka simu pembeni, muda huu alisogea Vaileth karibu na kumwambia mama Angel,“Mama, hongera sana.”“Hongera ya nini?”“Huwa siku zote natamani kusema ila nashindwa, kwakweli maisha yenu yapo vizuri sana yani nyie mnapendana hadi shetani mwenyewe anaogopa”Mama Angel akacheka na kumwambia Vaileth,“Usijali na wewe siku moja utampata mwanaume wa ndoto zako, ambaye atakupenda na kukujali kwa kila hali”“Asante mama”Ila kabla hajakaa sawa, alifika mgeni na mgeni huyo alikuwa ni Dora yani kabla mama Angel hajachukua hatua ya kumfata Dora tayari Dora alishafika nyumbani kwake.Basi akaamua kwenda nae kwenye bustani ili kufanya nae mazungumzo,“Bora leo umenikumbuka Dora”“Mmmh kilichonileta hapa sasa mmmh!”“Nini tena?”“Unajua nahitaji kukaa na dada yako ili tujue cha kufanya na watoto wa marehemu wote wapate haki zao, maana kuna wangu Jesca, kuna wa dada yako, Junior na kuna yule James. Nahitaji wapate haki zao”“Kwakweli Dora umebadilika ndugu yangu, tena umebadilika sana tu.”“Unajua kitu gani? Kama kawaida yangu ya kutaka kuanza shari na mwanamke anayeishi nae Steve, ila nilivyofika mlangoni kwa yule mwanamke shari yote iliniisha maana nilimuona mtoto wa James ndio kawa mlinzi, kweli baba yao atakuwa anafurahi huko alipo? Hata kama wafu hawasikii chochote ila hiki nilichofanya naona sio kizuri kabisa mbele za Mungu hata mbele za wanadamu”“Ila ni vizuri kama umeamua hivyo, kwa tupange sasa itakavyokuwa ili wote kupata haki yao na kama kusimamiwa basi wasimamiwe na mama zao”“Naona wanaweza kujisimamia labda Junior sababu anasoma ila huyo James kwakweli, roho imeniuma sana kumkuta ni mlinzi”Wakajaribu kuongea cha kufanya pale na kufikia muafaka wa kuona kuwa kipi bora na kipi kifanyike.Siku hii Erica aliporudi kutoka shule, alimfata mama yake na kumwambia,“Mama, kwani Erick hajakwambia?”“Kuniambia kuhusu nini?”“Jana nilikuwa naongea nae, wenzangu shule mama wanakujaga na hela ila mimi utakuta sina hata mia ya maji. Pale shule mbona duka lipo ila siwezi kununua hata pipi, basi Erick akasema atakwambia ili uwe unanipa angalau mia tano”Mama Angel alicheka na kusema,“Kweli umejanjaruka, naona ile laki mbili imekutoa ufahamu mwanangu. Toka lini ukadai hela wewe! Shule unayosoma, maji ya kunywa yapo, chai mnapewa, chakula cha mchana mnapewa tena kizuri tu haya unataka hela ya nini? Ule pipi umekuwa mtoto?”“Sio hivyo mama, wenzangu wote wanakuja na hela shuleni na wanaweza kununua chochote kile. Ni kweli tunakunywa chai ila muda mwingine mtu unatamani soda”“Sasa kama unatamani soda si uwe na kopo lako unamimina juisi unaenda nayo shule”“Ila mama jamani! Haya basi”Erica aliondoka zake na kwenda chumbani kwake, ila Vaileth alimsogelea mama Angel na kumwambia,“Mama, ila ni vizuri ungekuwa unampa hela hata kidogo”“Hela ya nini sasa huyu? Kwanza bado mdogo halafu kila kitu shule anakipata”“Ni kweli ila shuleni kuna vishawishi mama, mbona Angel mlikuwa mkimpa hela?”“Kheee muulize Angel kama kuna hela huwa anapewa hapa nyumbani! Labda apewe na baba yake”“Ila mama, ukitaka mtoto wa kike asiwe katika vishawishi basi jaribu kumfanya asiwe na uhitaji wa lazima nje, mfano kitu kidogo kinaweza kumtia kwenye vishawishi Erica, ndiomana kipindi kile mnalalamika kuhusu ile shule na kusema kuwa Erica anaongea sana na vijana sababu wanampa mahitaji ayatakayo, haya niliongea na Angel kidogo tu akanielezea kuwa yule mwanaume alienda kutengenezewa simu sababu yule mwanaume alisema laki mbili anayo na mwisho wa siku akataka kumbaka Angel, ila mambo kama hayo si Angel angekuwa wazi tu kwenu! Naomba usinifikirie vibaya mama ila nasema sababu naelewa wazi inavyokuwa. Hivi huyo Sarah ambaye huwa unamsifia kuwa mtoto anajiongeza, ni nani huwa anampa pesa ya kufanya ayafanyayo?”“Mmmmh!! Ila sipendi kumzoesha mwanangu hela, ila basi nitakuwa nampa japo mia tano aliyosema. Ila huyu Erica lengo lake ni kuagiza karata tu, yani akishakuwa na hela atanunua karata lazima maana anapenda sana kucheza karata”Basi muda huo Erick nae aliwasili kutoka kiwandani sababu alikuwa anatoka shule na kupitia kiwandani kwanza halafu ndio anarudi nyumbani, baada ya salamu mama Angel alimuuliza kuhusu Sarah,“Vipi leo Sarah amekuja?”“Hajaja mama, nahisi labda atakuwa anaumwa”“Jamani masikini, unapafahamu kwao?”“Napafahamu ndio, si nishawahi kumrudisha kwao”“Basi tufanye hivi, kama hadi kesho hajaja shule itabidi usiende kiwandani kesho, ukitoka tu njoo nyumbani ili twende kumuona Sarah nyumbani kwao”“Mmmh mama!”“Ndio, hakuna cha kuguna. Kwahiyo itakuwa hivyo, jitahidi kesho tufanye hivyo”“Sawa mama”Basi Erick akaenda kuendalea na mambo yake mengine kwani alikuwa amechoka.Siku ya leo Erick alipokuwa yupo shuleni, wakati muda unakaribia kutoka aliitwa na madam Oliva ambaye alimtaka waende kiwandani,“Aaaah leo siendi madam”“Kwanini?”“Nataka kuwahi nyumbani”“Sio nilivyokubaliana hivi na baba yako, basi twende leo halafu kesho ndio usiende, sawa”Erick hakuweza kumkatalia madam hata hivyo kule kiwandani hakuwaambia kuwa siku hiyo hatoenda kwahiyo aliondoka tu na madam kuelekea huko kiwandani.Basi walivyofika, Erick aliingia kiwandani wakati huo madam Oliva alikuwa amekaa nje ya gari lake huku akiangalia angalia mazingira ya pale, mara kuna mtu alisogea na kumsalimia,“Habari”“Nzuri tu, sijui tunafahamiana?”“Hapana hatufahamiani, mimi naitwa Rahim na wewe unaitwa nani mwenzangu?”“Mimi naitwa madam Oliva, ni mwalimu wa sekondari”“Oooh, katika maisha yangu nilitamani sana kuoa mwalimu ila sikupata bahati hiyo unajua kwanini nilitamani kuoa mwalimu?”“Kwanini?”“Kwasababu mwalimu ni mtu ambaye ana maadili na huwa anafundisha vyema watoto, ana muda wa kutosha wa kuangalia watoto na pia muda wa kutosha wa kuela mume na familia sababu mwalimu habanwi sana kwenye kazi yake, tofauti na kuoa mke nesi au daktari kwani kidogo tu mara nipo shifti ya usiku, mara natakiwa siku mbili kazini yani mimi ningepata bahati ya kukutana na mwanamke mwalimu kwa hakika ningeoa upesi sana”Basi madam Oliva alitabasamu tu, na kumuangalia vizuri Rahim aliyekuwa akiendelea kumpa sifa,“Kwanza wewe licha ya kuwa mwalimu maana kuwa mwalimu ni sifa toshelezi ya kumfanya mwanaume apate hamu ya kukuoa, sasa nikitoa swala la kuwa mwalimu, pia wewe ni mwanamke mrembo sipati picha enzi za udogo wako, kwakweli madam wewe ni mrembo sana, una sura nzuri na umbo zuri la kuvutia, umevaa kiheshima na una vutia kwakweli”“Dah! Hizo sifa zote kwema?”“Kwema tu, najua ushanisoma tayari, maana mnaupeo wa kuelewa vitu zaidi ndiomana mkapendelewa na kuwa walimu wetu”“Jamani leo kweli nimekutana na mtu maana sio kwa sifa hizi, nimekuwa mwalimu kwa kipindi chote hiki ila sijawahi pata mtu wa kunisifia kiasi hiki na kufanya nijivunie kwa kazi yangu”“Kwanza kuna mwalimu kweli anaweza kukaa bila kuolewa? Yani akose mume wa kumuoa? Labda aamue tu, kila mwanaume anapambana apate mwanamke mwalimu na aoe mwanamke huyo, vipi madam umeolewa?”“Khaaa jamani, mimi sijaolewa ila naishi na mwanaume”“Oooh sifa nyingine ya mwalimu ni hiyo hapo, kuwa mkweli katika maisha. Hongereni sana walimu, Mungu kawabariki kwa kila idara. Chukua hii kadi yangu ili tuwe tunawasiliana kwa mambo mengi tu, mfano biashara na kushauriana kwani ushauri wa mwalimu huwa ni ushauri bora zaidi ndiomana mnafanya watoto wapanuke akili na kuwa viongozi wakubwa. Sifa zote zipo kwenu walimu, kwaheri”Madam Oliva alichukua zile namba huku akitabasamu tu maana alipewa sifa zilizopitiliza kabisa.Rahia alipoondoka tu, Erick nae alitoka kisha madam Oliva alimrudisha Erick kwao halafu yeye kwenda nyumbani kwake.Erick alipoingia alimkuta mama yake ameshajiandaa na swali aliloulizwa kwanza lilikuwa,“Sarah amekuja shule leo?”“Hajaja”“Na mbona umechelewa?”“Nilipita kiwandani mama”“Ila wewe dah! Haya hata usiende kubadili nguo, tutoke sasa hivi twende kumuona Sarah”Erick hakubisha kitu chochote ila aliacha tu begi lake la shule pale sebleni na kuondoka na mama yake ambaye alimuachia Vaileth maagizo ya mtoto ambaye alikuwa amelala kwa muda huo.Basi waliondoka na moja kwa moja walienda mpaka kwakina Sarah, na kushuka. Waligonga mlango kuna mdada alienda kufungua mlango na kuwakaribisha, Sarah walimkuta amekaa sebleni huku kajifunika na blanket halafu kuna picha alikuwa akiangalia, ila alipomuona Erick aliinuka na kwenda kumkumbatia kwa furaha yani alifurahi sana kwa Erick kwenda kumtembelea. Basi walimsalimia pale, na kumuuliza hali yake,“Yani naumwa halafu mama nae hayupo”“Sasa ulienda hospitali?”“Sijaenda, sababu mama hayupo”“Khaaa jamani, itabidi twende muda huu huu”Mama Angel akataka muda huo huo wampeleke Sarah hospitali ila Sarah akasema,“Dada alinipa dawa, ila nilikaa hapo nikiangalia picha ya marehemu baba yangu na nilivyomuona Erick ndio nimejihisi kupona kabisa”Sara alijikuta akimpa tu mama Angel ile picha ya marehemu baba yake, ila mama Angel alipoiangalia ile picha alionekana kushangaa sana kwani ni mtu aliyemfahamu vizuri kabisa.

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog