Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

MIMI NI MUAFRIKA (I'M AFRICAN) - 3

 








Simulizi : Mimi Ni Muafrika (I'm African)

Sehemu Ya Tatu (3)







Msitu wa mikoko; 7;00am

Vijana kumi wa kiafrika, mikononi walishika silaha zao za jadi, upinde na mishale pamoja mapanga, nyuma yao msururu mkubwa uliwafuata, msururu wa wanawake, wazee pamoja na watoto, wote walikuwa vifua wazi,licha ya baridi ya asubuhi hawakuweza kuhisi baridi ile,miili yao ilizoea hali ile kwa miaka nenda rudi, watoto walizaliwa na kukuta wazazi wao wakivaa magome ya miti huku matumbo yao yakiachwa wazi, wakakua wakifundishwa kuvaa magome ya miti kama mavazi yao, huku ngozi za wanyama wakizitumia kulalia.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“,piiiiiiiii, piiiiiiiii”,Mwatope, mmoja wa vijana shujaa wa Kiafrika, alikuwa miongoni mwa vijana kumi waliochaguliwa na Ishimwe kuwalinda na kuwaongoza wanawake na wazee mpaka mafichoni msitu wa mikoko, baada ya kuukanyaga msitu, msitu wa mikoko, akakumbuka maelekezo aliyokuwa amepewa, akaingiza vidole viwili mdomoni mwake, akaukunja ulimi wake, akapuliza kwa nguvu, mlio mithili ya filimbi ukasikika, wananchi wa Goshani huita filimbi ya Kiafrika, hutumika wakati wa kujulisha hatari pamoja na kuchungia mifugo, mwangwi ukasikika kila kona ya msitu.



“,Piiiiiiii, piiiiii …”,Mwatope akaingiza tena vidole viwili vya mkono wake wa kulia, akaukunja ulimi wake, akapuliza tena kwa nguvu, mlio wa filimbi ya kiafrika ukapenya na kusikika kila kona ya msitu, huku Mwatope pamoja na msafara wake wakiwa wamesimama, wakisubili waweze kujibiwa, watambue mahali ambapo waafrika wenzao walikuwa wamejificha …



“,Fwiiiiii, fwiiiii ……”,mlio wa filimbi ya Kiafrika ukasikika upande wa pili katikati ya msitu, ulipulizwa kwa staili nyingine, walikadiria mahali mlio uliposikika,wakafuata kinjia kidogo kilichoelekea katikati ya msitu,huku wakiwa makini wasishambuliwe na wanyama wakali …



………… ….……………………

Great fort (ngome kubwa) 7;50

Magari takribani hamsini yalitoka katika ngome ya wakoloni, nyuso zao zilikunjamana kwa hasira,askari wa kikoloni walikuwa na mijeledi pamoja na bunduki zilizojaa risasi, siku mbili mfululizo shughuli za shambani hazikufanyika kwa ufanisi katika mashamba yao ya mkonge,manamba wa Kiafrika hawakutokea,wakazidi kujawa na hasira, kichwani walifikilia kisasi, walikuwa na shauku ya kuua Waafrika kama wenzao walivyouawa usiku uliopita.



“,Atakaye kataa, atakayegoma kufungwa, atakaye leta jeuri, kill him or her ……”,gavana Richard Robeni akiwa amevalia singrendi tu majira ya asubuhi, alitoa amri kwa askari wake ambao waliendelea kutoka na magari katika ngome yake, hakutaka kuongozana nao, hakutaka kuombwa msamaha na Waafrika,alikataa kuongozana na majeshi yake, akarejea ndani ya nyumba yake, huku sigara kubwa ya kizungu ikiwa mdomoni mwake …



………………………………

Makazi duni; 8;40

Askari wa kikoloni hawakutaka kuuliza, walisimamisha magari yao, walishuka na mijeledi yao, wakaanza kusogelea mabanda ya Waafrika yaliyoezekwa kwa nyasi, walitaka kuwakurupusha na bakola wakiwa usingizini, hawakutumia akili hata kidogo.



“,Yalaaa, fuck yo…u, fuc…k u ……”,askari mmoja alipiga kelelee, akatukana kwa kizungu, akafia palepale mlangoni katika kibanda cha Waafrika,mshale ulipenya katika jicho lake moja na kutokea upande wa pili wa kisogo chake, alifyatua kamba mlangoni bila kujua.



“,Kill all of them, shambulia na risasi nyumba yao wauaji wakubwa, ……”,amri ilisikika kutoka kwa askari aliyevaa mikanda mingi begani na kiunoni,alikuwa na cheo kikubwa kuliko wenzake.



“,Uwiiiii! nak…ufaa…aa”,askari mwingine alilalamika,mshale ulipenya katika tumbo lake alipoingia kwa pupa na mjeledi mkononi katika kibanda cha pili cha Waafrika.



“,Paaaaa, paaaaa, paaaa …”,Askari wa kikoloni wakafyatua risasi kwa fujo vibanda vile.



“,puuuuuu, puuuu, puuuu …”,mripuko ukasikika, vibanda vile viliripuka, askari waliokuwa karibu nguo zao zikashikwa na moto, wakakimbia huku na kule, wakipiga kelele kama wenda wazimu.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“,Puuuuuu, puuuu! “,gari iliyokuwa karibu na kibanda kimoja ikachemka, ikashika moto, ikaripuka, askari wote wakatoka kwenye magari yao na kuanza kukimbia kimbia, wengine walikuwa bize kuokoa wenzao, huku wengine wakikimbia kuziokoa nafsi zao.



Msitu wa mikoko;

Angel alishtuka kutoka usingizini, baridi kali majira ya asubuhi, baridi kali kutoka bahari ya hindi,mita elfu mbili kutoka msitu wa mikoko, ilipenya katika ngozi raini ya msichana mrembo wa kizungu, licha ya kuvaa nguo mwilini mwake, brauzi yake haikumsaidia kumkinga na baridi.



Japo alihisi baridi na kuamka usingizini mapema sana,mpenzi wake Mpuzu alikuwa bado amelala, Angel alipotazama upande wa pili wa matawi ya mti, wazazi wake Mpuzu pamoja na Mwamvua, na wenyewe walikuwa bado wamelala.



“,I have to get clothes for them, lazima nipate nguo kwa ajili yao, they can get sick,baridi not good for their health “,Angel aliongea, macho yake yakimtazama Mpuzu Yahimana pamoja na ndugu zake kwa huruma, aliwahurumia kwa baridi kali ya msituni,wakiwa kifua wazi, alisahau kujihurumia yeye.



“„Piiiii piiiii, “Angel alishtuka,mlio mithili ya filimbi ulipenya katika misikio yake, akaangaza huku na kule,hakuona kitu chochote kile, “Mpuzu, Mpuzu, work up, Mpuzu work up ” ,aliita huku akimpiga biga Mpuzu begani, Mpuzu akashtuka, akayafumbua macho yake.



“,Piiii, piiiiiii …”,mlio ukasikika tena, Mpuzu akiwa bado amepigwa na butwaa baada ya kukurupushwa usingizini, akaitambua vizuri sauti ile, akaingiza vidole viwili kinywani mwake, akaukunja ulimi wake, akapuliza kwa nguvu. “Fliiii, fliiii “,mlio wa kipekee ukasikika, aliwajibu Waafrika wenzao waliokuwa wanawatafuta msituni.



“,Usjali, hakuna hatari yoyote ile, ndugu zetu wanakuja, “Mpuzu alimuondoa shaka Angel, upande wa pili wazazi wa Mpuzu, dada yake Mwamvua walikuwa macho, kelele za Angel kumuamsha Mpuzu ndizo zilizowakurupusha usingizini,walitabasamu, walitambua mlio wa filimbi ya kiafrika, ndugu zao walikuwa wanakuja kuungana nao.



…………………………………

Ngome kubwa;

Gavana Richald Robeni alikosa furaha, mke wake malikia Magreth na yeye pia hakuwa na furaha, furaha yao ni Angel, mtoto wao wa kipekee,lakini aliwakimbia na kuitoroka ngome yao, jambo ambalo liliwafanya wawachukie zaidi Waafrika, kwani ndio chanzo cha binti yao kutoroka, waliamini walimlaghai akakubali kuungana nao, waliapa kumrudisha mikononi mwao kwa gharama yoyote ile …



“,Lakini tusimlaumu sana mtoto, pengine ameshindwa kuvumilia manyanyaso tunayowafanyia watu weusi, tujilaumu sisi wenyewe kwa kuwa wakatili ,we have to blame our self……”,mama yake Angel, malikia Magreth aliongea,kauli ambayo ilimfanya aondoke mbele ya mume wake, kabla hajachapwa kibao, kwani mume wake, gavana Richald Robeni alimuangalia kwa macho makali yaliyojaa hasira, yakimtaka atengue kauli yake iliyojaa ukweli ndani yake.



“,Women are foolish, jinga kabisa wewe! ” ,gavana Richald Robeni alifoka,mke wake akitokomea mbele ya macho yake, tangu Angel atoroke nyumbani kwao, kila mmoja alimlaumu mwenzake kuwa chanzo cha matatizo, upendo ukatoweka ghafla, hawakusemeshana kama awali.



…………………………………

Slum area(makazi duni)

Askari wa kikoloni walikimbia huku na kule,wengine waliwasaidia wenzao waliojeruhiwa, wengine wakaendelea kuwatafuta Waafrika katika makazi yao bila mafanikio.



“,Puuuu, puuu “,mripuko mwingine ukasikika, kibanda cha tatu kiliwaka moto, askari wa kikoloni wakarudi nyuma, fikra zao zikafunguka.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“,Don’t get in,tumetegwa, tutakufa,tunapaswa kuwa makini,msiingie katika vibanda vyao,kuna miripuko …”,kamanda wa kikoloni aliongea, aligundua mtego uliotegwa kwa ajili yao,wakatii amri, askari wote wakarudi nyuma.



“,We want our freedom, tunataka uhuru wetu “,maneno yalisomeka katika milango, baadhi ya mabanda,bila shaka maandishi yaliandikwa na Waafrika wachache waliobahatika kufundishwa kusoma na kuandika,katika shule za wakoloni, na kuajiriwa kama wasimamizi wa manamba katika mashamba ya Wakoloni.



“,the literate ones, they need to fight us and get their freedom, Africans were born to be slaves,(Wasomi wanataka kupigana na sisi wapate uhuru wao, Waafrika walizaliwa kuwa watumwa),turudi tukatoe taarifa, Waafrika wameingia msituni ……”,kamanda wa kikoloni, akiwa amevalia kaptula nyeupe, viatu pamoja na soksi nyeusi, huku mikanda ya kijeshi ikizunguka begani mpaka kiunoni, aliongea na kuwapatia maelekezo vijana wake,askari wote wakapanda kwenye magari yao, maiti zikapakiwa kwenye magari, pamoja na waliojeruhiwa,wakayaondoa magari yao, walipofika kilomita tatu, wakashambulia kwa risasi mabanda ya Waafrika, mripoko mzito ukasikika kila kona, makazi duni yakateketezwa.



“,Do you see, tulikuwa tumetegwa, tungekufa wote! “,kamanda yule akiwa ndani ya gari lake aliongea kwa mara nyingine tena.



“,Stupid Africans, we will kill them, hatapona hata mmoja, “askari wa kikoloni wakiwa wamejawa na hasira walifoka kwa hasira, siku ya pili waliuawa bila kulipiza kisasi,wakaendelea na safari yao, kurudi katika ngome yao, wakiutazama moshi mkubwa wa mripuko ukitanda hewani …



…………………………………

Ishimwe akiwa na wenzake, waligeuka nyuma kilomita tano, karibu na msitu wa mikoko.Waliona makazi yao yaliteketea kwa moto, japo walizipenda nyumba zao, hawakuwa na budi kuziacha na kupigania uhuru wao …



“,Lazima wafe,kwa moto huo, watakuwa wamerudi na maiti nyingi katika ngome yao, tunawakaribisha msituni, watakufa na wote wataisha,tutaenda kuishi katika ngome yao kama mashujaa ……”,mzee Nyamigo aliongea, wote wakashangalia, silaha zao wakazinyoosha juu kwa mikono yao ya kulia,ishara ya umoja na ushindi, kisha wakaingia msituni, kuungana na wenzao.



…………………………………

Mwatope alikuwa ametangulia mbele, mkononi alishika upanga kwa ajili ya kukata matawi ya miti kusafisha njia,upinde na mishale ilifungwa vizuri katika mgongo wake, nyuma msafara mrefu ulimfuata, huku nyuma kabisa vijana wenzake wakidumisha ulinzi.



Walifika katikati ya msitu, wakasimama ghafla, walihisi uwepo wa hatari juu ya mti mkubwa,kwani majani kadhaa yalimuangukia Mwatope, akasimamisha msafara kwa kutumia ishara ya mkono, kisha akatazama juu kwa umakini.



“,Pomweee Mwatope, (Habari Mwatope) ,tuko huku juu ya mti “,Mpuzu aliongea, kumbe ndiye aliyedondosha majani ya mti chini, alitaka wenzake wamuone.



“,Pomweee Mpuzu, “Mwatope, pamoja na msafara wake wote wakatazama juu, walimuona Mpuzu juu ya mti wa ubuyu akishuka, wakamsalimu.



“,Karibuni sana, karibuni tuupiganie uhuru wetu,juu ya miti ni sehemu nzuri ya kujificha kwa ajili ya mapambano, “Mpuzu aliongea.



“,Ndugu zako wako wapi?, “Mwatope alimuuliza Mpuzu, huku Mpuzu akiteremka chini kwa kutumia kamba, dakika tatu alitumia, tayali alifika chini.



“,Mtoto wa gavana yuko wapi?, kama ni msaliti na anaroho mbaya, tutamuua “,kundi kubwa la wanawake waliosindikizwa msituni waliuliza,wakaongea maneno makali, yakapenya vizuri katika moyo wa Mpuzu.



“,Ndugu zangu wako juu ya mti, mtoto wa gavana na yeye yuko juu ya mti, hana shida yoyote, sio mbaguzi na hana roho mbaya …”,Mpuzu aliongea,akamtetea mpenzi wake Angel, mtoto wa gavana Richald Robeni.



Angel alisikia mazungumzo ya Mpuzu pamoja na Waafrika wenzake chini ya mti,alishuka juu ya mti, akateremka kwa kamba, akafika chini, alikuwa mwepesi, alizimudu purukushani za mapambano.



“,Good morning, i don’t hate you, i love you …”,Angel aliongea kwa kingereza,waafrika wengi hawakuelewa, wachache tu ndiyo waliweza kuelewa maneno ya Angel.



“,Pyuuuu, “mshale ulisikika, Angel akakwepa, ukachoma na kupenya katika mti wa ubuyu, Angel akaruka serekasi kwenye mti, akauchomoa, akaruka tena, akajitupa kwa ufundi, akafika chini akiwa amesimama, akauvunja mshale kwa goti lake, Mpuzu akasimama mbele yake kumlinda.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“,Magope, kwanini unataka kumuua mtoto wa gavana, ukimuua na mimi nitakuua “,Mpuzu aliongea, huku akiwa amesimama kumkinga Angel asijeruhiwe, japo Angel hakuwa na wasiwasi, muda wote alitabasamu.



“,Ametutukana, hawezi kututukana Waafrika mbele yetu…”,Magope akiwa nyuma kabisa ya msafara aliongea, huku akitetemeka, alitambua msichana aliyetaka kumjeruhi hakuwa wa mchezo mchezo hata kidogo, wanawake wote waliokuwa katika msafara ule walishangazwa na kitendo cha Angel kukwepa mshale, tangu wazaliwe hawakuwahi kuona mtu hodari kama Angel anayeweza kuukwepa mshale wa kiafrika.



“,Alitusalimia, akasema hatuchukii, anatupenda “,mwanamke wa umri takribani miaka sabini aliongea, alibahatika kufanya kazi katika nyumba za wakoloni wazungu,miaka mingi iliyopita, wakampenda, wakampeleka katika shule za wakoloni kupata elimu, akasoma mpaka darasa la nne, akafundisha shule zao mpaka mnvi zikamjia, akakosa nguvu za kumudu kazi ya ualimu, wakamfukuza, akarudi katika makazi duni, aliongea na kumtetea Angel.



“,Usirudie tena,”bibi yule alimpatia onyo Magope,huku mzee Yahimana, mke wake, pamoja na Mwanvua wakiteremka juu ya mti, baada ya kusikia marumbano chini ya mti.



“,Kuna nini hapa?, mbona fujo na kelele za marumbano, mbona mmeshikiana silaha? “,Ishimwe alifika na kundi lake, akamtwika swali Magope aliyekuwa amejiaandaa kwa mapambano, Magope akarudisha upinde chini huku uso wake ukiwa umejaa nsoni.



“,Hakuna kitu, msiwe na wasiwasi “,,bibi yule aliyetafsiri maneno ya Angel, alitumia busara, akaficha ukweli, hakutaka waendelee kurumbana, Ishimwe na kundi lake wakakubaliana naye, siku zote walimuheshimu kutokana na elimu yake pamoja na umri wake aliokuwa nao.



…………………………………

Ngome kubwa;

Magari ya askari wa kikoloni yaliingia kwa fujo, gavana na mke wake walitoka nje, walikuwa na shauku ya kujua kilichotokea makazi duni,viongozi wengine wa vyeo vya juu katika serikali ya kikoloni hawakutaka kupitwa, na wenyewe walitoka katika majumba yao, kushuhudia kilichotokea.



Walipigwa na butwaa, hofu na woga ukawajaa,hawakuamini walichokiona mbele ya macho yao, maiti za askari wa kizungu takribani hamsini zilishushwa kwenye magari, majeruhi takribani mia moja wakishushwa kwenye magari yao, wakiwa wamejeruhiwa vibaya na moto.



“,I told you mr Richald, nilikwambia baba Angel, wewe ndiyo chanzo cha yote, kitendo cha wewe kukubali Angel atoke Uingereza na kuja huku kuona ukatili wako, ndicho kilichombadirisha moyo wake, ona sasa, bila shaka yeye amechangia kwa namna moja kuua wazungu wenzake, kila silaha anajua kuitumia, umemfundisha mwenyewe vita, atakupiga na kukuua kwa mikono yake mwenyewe, pumbavu kabisa! “,malikia Magreth alifoka, akashindwa kuvumilia kushuhudia maiti zikishushwa, akarejea ndani, akamuacha mume wake akiwa hana cha kumjibu.



Mume wake,gavana Richald Robeni akasogea taratibu, alitaka kuwauliza askari wake kilichotokea, huku viongozi wengine pamoja na askari ambao hawakwenda makazi duni, na wenyewe wakisogea karibu na magari yao ya kikoloni,huku majeruhi wakibebwa kwa machela kupelekwa hospitalini



Ngome kubwa (the great fort)

“,They want freedom, hawako katika nyumba yao,wametega explosives kwa majumba yao,wakaenda kujificha kwa forest “,kamanda na kiongozi wa askari alivua kofia, akapiga saluti mbele ya gavana Richald Robeni, kisha akatoa maelezo, kila kitu kilichotokea katika makazi duni.



“,What?,so it means hamjakamata hata Muafrika moja,you are killed,and then mnakuja hapa bila kamata hata moja,you tell me nonsense!”,gavana Richald Robeni alibwatuka,cheche za mate zitoka modomoni mwake,zikamrukia askari yule aliyesamama mbele yake,maneno yalipenya katika nafsi yake,akajiona hafai mbele ya bosi wake,akakosa majibu ya kujitetea.



“,Mimi ona nyie iko seriuous,taka toa freedom kwa foolish Africans,never! don’t expect that to hapen,haitatokea hata kwa siku moja!”,gavana Richald Robeni aliendelea kufoka,askari wote walio sikiliza maneno yake,waliinamisha chini nyuso zao kwa aibu, walisubili amri ya mwisho kutoka kwa gavana.



“,Genaral Agustino!”,gavana Richald Robeni aliita.



“,Yes boss (ndio mkubwa) “,jenerali Agustino Darwin,mkuu wa jeshi la kikoloni, aliitika.



“Come here, (njoo hapa)”,gavana Richald akaita kwa kizungu.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Jenerali Agustino Darwin

akasogea karibu kabisa na mkuu wake wa kazi, gavana Richald Robeni.Akapiga saluti,akasimama wima kwa heshima, tayali kwa ajili ya kupokea maagizo.



“,Arrest them, take them to European prisons, sitaki upuuzi mimi, wote wakae gerezani ……”,gavana Richald Robeni aliongea, askari wote waliopewa kazi ya kuelekea makazi duni, kuwakamata Waafrika wote, wakawekwa chini ya ulinzi,kiongozi wao na yeye akakamatwa, wakapelekwa katika magereza ya wazungu, wakafungiwa ndani yake.

Dakika kumi na tano baadae,tarumbeta likapulizwa, mlio wake ukasikika pembe zote za ngome ya kikoloni. Wazungu wa kiingereza, waarabu, wahindi pamoja na askari wote wa kikoloni wakaitikia wito, wakatii mlio wa ngoma uliyopigwa kwa kusogea mbele ya kasri kubwa la gavana Richald Robeni.



“,My daughter is not here,she is not my daughter anymore, now and onwards! ,(mwanangu hayuko hapa, sio mtoto wangu tena, sasa na kuendelea) “,pembeni yake akiwa amesimama mke wake, malikia Magreth, wote walijawa na huzuni kubwa,japo hakukubaliana na maamuzi ya mume wake, hakuwa na jinsi, mwanaume atabaki mwanaume siku zote, akakubali shingo upande, gavana Richald Robeni akatangazia uma, kutomtambua Angel kama mtoto wake tena.



“,Whenever you see her, popote mtakapo ona sura yake,muueni, kill her, she is killing our people, she has joined Africans, anatoa siri zetu kwa watu weusi,jiandaeni kwa vita, take your weapons, chukueni silaha tuondoke msituni, ……”,gavana Richald aliongea kwa hasira, akachanganya kiswahili na kiingereza, akatoa maelekezo kisha akaelekea ndani ya nyumba yake,akavaa kombati zake za vita, mke wake naye hakutaka mwanae auwawe na wazungu wenzake, akavaa suruali, akachukua bastola yake, akaungana na jeshi la wakoloni akiwa na nia ya kuhakikisha mtoto wake anakuwa salama.



“,let’s go, tuondoke, twendeni tukarudishe heshima ya rangi yetu …”,Richald Robeni aliongea, akaingia kwenye gari lake la kifahari, gari aina ya the Roll Royce,mke wake na yeye akajipakia ndani ya gari hilo,wakaanza safari, wakiongoza msafara wa askari pamoja na viongozi wengine kuelekea msituni.

“,twendeni, hakuna hata people moja baki kwenye great fort, wote tunaenda msituni, Harry up, Harry up! “,kamanda mwingine, kiongozi wa kundi la pili la jeshi la kikoloni, aliwaongoza askari wake, kuchukua silaha zao, bunduki na mabomu, wakajipakia kwenye magari yao na kuufuata msafara wa magari ulio ongozwa na gavana wao.



…………………………………



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog