Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

MY CLASSMATE - 3

 






Simulizi : My Classmate

Sehemu Ya Tatu (3)





Alijua atakufa, ndomana alianza kulia kabla. Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti..!



Daniel alinisogelea taratibu na kuniuliza kwa upole.



"Kuna kitu wanahisi unacho.wanataka kukuua ili kisitoke nje.Ni kitu gani unahisi Abdul ?"

"Mimi sina kitu kaka Daniel. Sijui hata wananitakia nini ?"

"Kipo kitu Abdul"

"Kitu gani sasa kaka ?"

"Mayasa alishawahi kukupa kitu chochote enzi za uhai wake ?"

"Amewahi kunipa vingi lakini siyo vya kudumu"

"Raiya alikupa nini cha kudumu ?"

"Hamna zaidi ya hii simu"

"Hebu ilete"

Nikampa

Daniel aliiangalia ile simu kwa makini.Aliigeuza nyuma.Aliifungua ile simu kule nyuma.Kule inakokaa betri ilidondoka chini karatasi ndogo.



Mimi nilishangaa sana.Sikuwa nimeweka karatasi yoyote kwa kuwa sikuwahi kuifungua simu ile tangu alivyonipa Raiya.

Daniel akaisoma kwa sauti ile karatasi.



"Kwenye laptop ya mmewangu kuna faili la siri.Linahusu mpango wa kuangamiza watoto wa viongozi nchi hii na mambo mengi ya siri sana .Abdul jaribu kulifikisha suala hili kunapohusika ili kuliokoa Taifa hili"



Nilishangaa sana. Sasa nilimuhusudu sana Raiya.Nilimuona ni mtu mwenye akili kuliko mtu yeyote duniani.Raiya kumbe alikufa na siri kubwa sana.Ambayo aliifikisha kwangu kwa siri pia.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nilimuhusudu zaidi Daniel.Aligundua kitu nilichokaa nacho miaka miwili bila kutambua .Nilikiri Daniel hakuwa mtu wa karne hii.Alikuwa na akili za ziada.



Daniel alitoka nje na kile kikaratasi.

Baada ya dakika kumi na tano walikuja askari wawili kuja kuutoa mwili wa yule jamaa.



Daniel alitoka nje kwa nia moja tu.Kumtafuta mume wa Raiya popote alipo.Ilikuwa lazima ampate popote atakapokuwa!



Upande wa kina Avast ilikiwa ni patashika na taharuki.Ilikuwa saa saba ya mchana sasa avira hajarudi.Ilikuwa ajabu.Avira hakuwahi kufanya kazi muda mrefu namna hii.



Hufanya mambo kwa haraka na uhakika.Hiyo ndio sifa kuu ya Avira.Alitekeleza kazi ya kumuua Raiya robo saa tu alivyoenda magereza.

Leo masaa zaidi ya matano alikuwa hajarudi.

Walimsubiri.

Walimsubiri sana.

Hakurudi.

Na hajarudi mpaka leo !.



Daniel alivyotoka palepale moja kwa moja alienda kwa dada yake Raiya.Alienda na kumuulizia mtaa na namba ya nyumba akiyokaa Raiya huko dar es salaam ilipo.

Baada ya kuelekezwa Daniel aliweka booking ya ndege ya kwenda Dar es salaam kesho yake asubuhi.

Aliipata.



Usiku ule ulikuwa mgumu sana kwa avast na Salehe.Wakaanza kuhisi huenda Avira amekamatwa.Wakawa wanahofia endapo Avira atakuwa kakamatwa anaweza kutoa siri.Siri pekee ambayo hawakutaka itoke ilikuwa kwenye laptop, nyumbani kwa Salehe, Dar es salaam.



Wakapanga kesho Avast aende Dar es salaam kuichukua ile laptop.Ili siri isifike mikononi kwa adui !



Hawakujua.Watakutana na nini huko Dar es salaam ?



Avast anaenda Dar es salaam kesho kuifata laptop yenye siri mzito.

Daniel anaenda Dar es salam kesho kuifata laptop yenye siri mzito !



Wasakana !

Watakutana Dar es salaam ?



Avast kesho anaenda Dar es salaam kuifata laptop yenye siri nzito !

Kesho Daniel anaenda Dar es salaam kuifata laptop yenye siri nzito!

Wasakana !

Watakutana Dar es salaam !



Daniel Mwaseba ndiye alikuwa wa kwanza kufika nyumbani Kwa Salehe Mikocheni.

Hakupata shida sana kuingia ndani ya nyumba ya Salehe.Hakukuwa na ulinzi wowote kwenye nyumba ile.



Aliruka ukuta na kuingia ndani. Aliitafuta laptop ndani ya chumba cha Daniel.

Chumba hakikuwa na vitu vingi sana.

Kulikuwa na kitanda kikubwa,meza ya kujirembea na kabati kubwa la nguo.

Robo saa ilitosha kukipata alichokuwa anakitaka ndani ya nyumba ile kubwa.Aliikuta laptop ndani ya kabati la nguo chumbani katika chumba cha kulala cha Salehe.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Aliiweka laptop yenye siri nzito kwenye begi na kuanza kutoka.Hakutaka kuifungua mle ndani.Aliona siyo sehemu salama.

Alipita sebuleni akafungua mlango wa sebule wa kutokea nje.

Sasa akawa anatembea katika uwanja mpana kulielekea geti la nyumba ile.Alilikaribia kabisa geti.Zilibaki hatua kama tano ndipo geti ili Daniel atoke nje ya nyumba ile.Ghafla geti lilianza kufunguka lenyewe !



Aliingia mtu mrefu, mweusi, mkakamavu.

Alikuwa ni Mmrekani mweusi.

Kwa jina alikuwa anaitwa Avast !

Pacha wa Avira aliyemuuwa kwa mateso makubwa jana kule Arusha.



Sasa Daniel Alikuwa anatazamana macho kwa macho na Avast. Wote wakiwa Na bastola mkononi !

Avast alikuwa anauangalia sana mfuko alioubeba Daniel.

Akajua ndani ya mfuko ule kipo alichokifuata.Laptop yenye siri nzito !



"Wanaume wanaojiamini hawapambani kwa silaha.Tuweke silaha chini na tuoneshane ubabe" Avast aliongea kwa sauti yake mzito na ya kujiamini yenye lafudhi ya kimarekani.Aliongea kwa majigambo.



Daniel alitii, kwa sababu alijiamini.Alitaka kumuonesha Avast jinsi Wanaume wa kweli wanavyopigana!

Waliweka bastola chini.

Sasa Ulikuwa mpambano wa haja.Mshindi alitakiwa kuondoka na laptop ile yenye siri nzito.



Ndani ya sekunde thelathini walikuwa wanaangaliana tu .Kila mmoja akifikiria jinsi ya kumuingilia mwenzie. Avast ndiye alitangulia kushambulia.

Avast aliruka juu na kumuelekezea Daniel mateke mawili ya nguvu kuelekea kifuani mwa Daniel. Daniel hakujiandaa vizuri .Mateke yale yalitua sawia Kwenye kifua chake.Nguvu ya mateke yale yalimfanya Daniel adondoke chini. Huku mfuko wenye laptop nao ukidondoka chini!.



Daniel alinyanyuka kivivu.Avast alirusha teke la kulia lililokuwa linaenda mbavuni kwa Daniel.Alijaribu kulipangua lakini alizidiwa nguvu na uzito wa teke lile.Lilimpata kidogo Kwenye mbavu.Aligumia kwa maumivu !



Avast alirusha ngumi na wakati uleule Daniel alirusha ngumi.Ngumi zile zilikutana katikati.Ila Daniel ndiye aliyepata madhara.Ngumi ya Avast ilikuwa na nguvu zaidi.Daniel aliumia mkono.



Sasa Daniel akajua akitumia nguvu atapigwa.Yule jamaa alikuwa hatari sana.

Sasa aliona ulikuwa wakati wa kutumia zaidi akili .

Avast alirusha mateke mawili kwa mpigo.Kwa miguu miwili tofauti.

Moja lilimpata Daniel kwenye mbavu ya kushoto na lengine mbavu za kulia.Daniel alidondoka chini kwa nguvu.Alikuwa ameumia mbavu vibaya sana.

Avast hakuwa mtu wa mchezo kabisa!



Avast alitoa kichupa kidogo cha dawa ya proxine ,akapaka kwenye kiganja chake na kwenda kumpaka Daniel pale chini alipokuwa amelala...!





Avast alikuwa anamfata Daniel. Akiwa amedhamiria kumpaka sumu ya Proxine pale chini. Ile anataka kumgusa Daniel alijisogeza kwa nguvu na kwa haraka.Avast aligusa sakafu !



Daniel alinyanyuka sasa.Akawa makini zaidi.Akijua kosa moja tu linaondoka na maisha yake.Alisimama imara sasa!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Avast nae alikuwa anataka kufanya haraka ili ile sumu ya Proxine isimdhuru.Ilikuwa na uwezo wa kukaa kiganjani kwa dakika kumi na tano.Baada ya hapo ingemdhuru yeye mwenyewe.



Daniel akajua hiyo ni nafasi pekee ya kumshinda Avast. Avast alirusha teke lililompata Daniel kwenye shingo. Teke lile lilimpeleka Daniel chini bila kutaka.Avast akawa anamsogelea tena ampake Proxine.Hakumgusa, alikutana na ngumi takatifu ya pua damu, zikaanza kumtoka.Avast hakujigusa pua.Kujigusa Ilikuwa inamaanisha kujivua ngozi.Kujiua mwenyewe kwa sumu kali ya Proxine.



Wote walikuwa wamesimama,wanaangaliana kama majogoo.Avast alirusha kofi kwa kutumia ule mkono wake wa kulia wenye sumu ya Proxine .Daniel aliliona Kofi lile.Alinesa kidogo likapita jumla.Daniel alipata nafasi. Kwa kutumia mkono wake wa kushoto alipiga ngumi ya nguvu kwenye mbavu za Avast.Avast Aligumia kwa maumivu.Alitamani kujishika mbavu lakini hakuruhusiwa na Proxine.Proxine sasa ikawa zuio kwake mwenyewe!



Sasa Avast mbavu zilikuwa zinamuuma huku damu zinachuruzika puani.Alikosa umakini, hakuweka kinga usoni.Daniel aliitumia vizuri hiyo nafasi.Alipiga ngumi mbili za haraka usoni kwa Avast.Avast Akawa anaona nyotanyota !



Avast aliyumba kutokana na uzito wa zile ngumi, lakini hakuanguka.Daniel alirusha teke kali lililompata Avast kwenye goti lake.Alienda chini taratibu.

Kama Avira, Avast alikuwa analia naye.Alikiona kifo.Kwa mbali kikimsogelea Proxine ilianza kuleta mrejesho.

Alijaribu kutoa dawa ya kuiondoa ile sumu ya Proxine, akaishika mkononi.Akitaka kufungua kile kichupa ili aondoe ile sumu hatari.Alichelewa.

Teke kali la Daniel liliupiga ule mkono ulioishika ile dawa.Chupa ilidondoka sakafuni na kuvunjika !



Avast sasa alilia kwa sauti kama mtoto mdogo. Alilia Kwa sauti kali! Daniel alikuwa anacheka kimoyomoyo.

Auwae kwa upanga siku zote huuwawa kwa upanga !



Daniel aliruka "double kick".Miguu yake yote miwili ilitua kwenye kifua cha Avast.Avast alitapika damu.

Huku akitapika damu ngozi yake ilianza kuvuka taratibu.

Daniel hakusubiri.Alichukua lile begi lenye laptop na kutoka nalo nje akiwa anakimbia.



Akitafuta hotel salama na kujifungia ndani peke yake.Tayari kuifungua ile laptop yenye siri nzito.Moyo wake ulikuwa unamwenda kasi alipoliona faili lililiandikwa siri ! Akabofyabofya kidogo. Sasa akatulia na kuanza kulisoma.



Ghafla mlango ulifunguka kwa kasi!Ulikuwa umevunjwa kwa teke zito !.Waliingia wazee wawili wakiwa wamevaa suti nzuri nyeupe.



"Hatujaja kuua.Tumefata laptop tu !" Mzee mmoja alisema.

"Hamuwezi kuipata laptop mpaka mniuwe kwanza"Daniel nae alijibu.

Wale wazee walicheka kwa sauti kwa pamoja.Walijiamini sana !



Walitoa bastola .Midomo miwili ya bastola ilikuwa inamuangalia Daniel ! Hakuihofia.

Yeye alitabasamu tu.



Wale wazee wawili Walikuwa wamenuna hasa.Tabasamu lile la Daniel waliliona kama dhihaka toka kwa Daniel. Wakawa wanamsogelea taratibu pale kitandani alipokaa.Daniel aliacha kuwaangaalia.Akawa anaitazama ile laptop.Ikifanya alichoiagiza.Ilikubali !



Kichwani alifikiria cha kufanya.

Jamaa walimkaribia sasa.Zilibaki hatua kama tano wamfikie kabisa.

walikuwa makini.Walikuwa wanamtambua Daniel.Walijua kosa moja tu lingewagharimu maisha yao yote !



"Simama juu !" Mmoja aliamrisha.

Daniel alisimama taratibu.

"Mikono juu!" Yule yule wa mwanzo alitoa amri nyingine

Daniel alinyoosha mikono yake juu.

Yule aliyetoa amri alimsogelea huku yule mwengine akiwa amebaki palepale.Akimnyooshea bastola yake.

Jamaa alimpekua Daniel harakaharaka.Alipata visu viwili na bastola moja.Hivyo viliwekwa sehemu ya kawaida.

Silaha alizoweka sirini hakuzipata.Zilihitaji mtu anayejua kupekua hasa.

Akaishika ile laptop.Bila kuitazama akaifunga.Wakawa wanarudi kinyumenyume sasa.



"Naitwa kaspersky " yule aliyemsachi Daniel alisema.

"Naitwa Zwangendaba" Na yule aliyekuwa kimya muda wote alisema.

Wakatokomea na laptop mbio!



"Tutakutana tu " Daniel alisema kimoyomoyo, huku akitabasamu.

Akatoka nje taratibu.Kwa utulivu mkubwa.

Kama hajatizamwa na midomo miwili ya bastola dakika chache zilizopita.



Alitembea kwa madaha.Kwa mwendo wa kujiamini.Huku akijiuliza kwanini wale jamaa walimwacha akipumua.

Akawacheka ujinga.Hawakujua kuwa walifanya kosa la karne.Daniel Mwaseba alikuwa zaidi ya wanavyomfahamu !



Akarandaranda mitaa ya Mikocheni bila uelekeo maalum.Aliranda makusudi.Alikuwa anachunguza kama kuna mtu anamfatilia.Hakumwona mtu !



Akaingia kwenye internet cafe moja.Akalipia masaa mawili.Akaifungua email yake.Aliikuta akichokitaka !



Daniel aliikuta email iliyotumwa muda mfupi uliopita.

Aliwapongeza wamiliki wa hoteli ile aliyokuwa mwanzo kwa kuweka wireless internet. Aliikuta email aliyojitumia yeye mwenyewe muda mfupi uliopita alivyokuwa kule hotelini.Kabla ya wale jamaa hawajamvamia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kichwa cha email kilisomeka "Siri".Daniel akatabasamu tena !

Sasa alianza kuisoma..!



Aliikuta email aliyojitumia yeye mwenyewe muda mfupi uliopita alivyokuwa kule hotelini.Kabla ya wale jamaa hawajamvamia. Kichwa cha email kilisomeka "Siri".Daniel akatabasamu tena.Alianza kuisoma ile email ya siri !



"Hili ni Angamizo !. Macho yasiyohusika hayapaswi kabisa kuona maandishi haya.... !



Ghafla Daniel alihisi anapapaswa bega.Daniel aligeuka.Alikuwa anatazamana uso kwa uso na Zwangendaba !.



" Sasa nimekuja kuichukua roho yako rafiki yangu " Alimnong'oneza Kwa sauti ndogo iliyopenya vizuri katika sikio la kushoto la Daniel.



Kwa mara ya kwanza mapigo ya moyo yalimpiga Daniel !.

Hakutegemea kabisa watu wale kuwa mahali pale muda ule.Hakutegemea kabisa kukamatwa kirahisi namna ile.

Alihisi

Kutekenywa na kitu kigumu mbavuni.Akaelewa. Alikuwa ameguswa na bastola kwenye mbavu zake !



"Simama juu" Zwangendaba alinong'ona tena.Daniel alisimama.



Watu wote ndani ya internet cafe hawakuelewa nini kinaendelea.Kila mtu alikuwa anatazamana na kompyuta yake.Daniel alikuwa anatekwa kimya kimya !



Kaspersky naye aliingia ndani ya internet cafe.Akaisogelea ile kompyuta akiyoitumia Daniel.Akaifuta ile email ya siri.Akarudi nje wakapanda kwenye Noah yao nyeusi.

Safari ya kwenda kusikojulikana iliaanza !



Ndani ya gari ilikuwa kimya.Hakuna aliyeongea.Wale majamaa wawili walikuwa wanavuta bangi kwa fujo.

Gari yote ilitapakaa moshi wa bangi.

Yalikuwa mateso kwa Daniel. Hakuwa mvutaji hata wa sigara.Lakini hakuruhusu hata kukohoa.Alijua kukohoa tu ataonekana dhaifu mbele ya watu wale.



Safari isiyojulikana ilifika mwisho.Ilikuwa nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.Kulikuwa na kibanda kidogo porini.Kibanda kilichojitenga na nyumba za watu. Walimuweka kwenye kibanda hicho.

Daniel alishuhudia migongo ya Kerspersky na Zwangendaba ikitokomea. Daniel walimfungia kwenye kibanda hicho !



Kilikuwa kibanda kidogo chenye mlango mmoja tu.Hakukuwa na madirisha wala sehemu yoyote ya kutolea au kuingiza hewa.

Walimfungia kinjenje.Alisikia muungurumo wa gari, jamaa walitoweka kwa kasi kwa gari yao.Kwenda kumalizia mpango wao hatari wa Angamizo !.



Hawakutaka kumuua Daniel. Nia yao Daniel ashuhudie Angamizo litakaloikumba Serikali yake.Walimuacha hai ili ateseke kwa kuona Angamizo hilo !

**************



"Mimi niliendelea kukaa kule kwenye chumba cha siri cha Polisi Arusha.Nikiwa nishachoka sasa.Nilikuwa nautamani sana uhuru wangu.Sikumuona Daniel ndani ya siku tatu.Nilikuwa natamani kumuona Daniel. Maana yeye ndio alikuwa tumaini langu pekee la kuurudisha Uhuru wangu tena.Nilianza kukonda kwa mawazo."



Upande wa Polisi nao ulichanganyikiwa sana.Kutoonekana kwa Daniel kwa siku tatu bila mawasiliano lilikuwa jambo la kushangaza sana.Wakahisi huenda Daniel yuko katika matatizo makubwa.Walimtafuta kila sehemu waliyoifikiria bila mafanikio yoyote.



Ndani ya kibanda kile Daniel aliteseka sana.Kulikuwa na joto kupita kiasi. Ukijumlisha na njaa pamoja na kiu kikali alichokuwa nayo, yalikuwa mateso makubwa sana!



Alivyoachwa tu Daniel siku ileile alitafuta njia ya kujiokoa bila mafanikio.

Mlango ulikuwa ni geti gumu la chuma.Ukuta wa tofali ulikuwa mrefu wa kunyooka mgumu kuupanda.Kwa juu ziliezekwa bati za udongo.

Ndani kulikuwa na giza kiasi cha kutotambua usiku au mchana. Hakukuwa na madirisha kabisa katika kibanda kile.



Dakika ya kwanza tu aliyowekwa Daniel alianza kutafuta namna ya kujiokoa.

Hadi leo siku ya tatu hakuipata.Na wala hakuwa na dalili ya kuipata.Alidhohofika sana kwa mawazo.Alidhohofika sana kwa njaa.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sasa alilala chini akiwa amekata tamaa.Alikuwa anakisubiri kifo .

Huku akisikitika siyo tu kwa kutozitimiza harakati alizozianzisha duniani.Hapana,alisikitika kwa kutofanikiwa angalau kujua watu wale walikuwa na siri gani wakiyoilinda namna ile.



Alikuwa amelala chini huku akikoroma sasa.Hakuwa na nguvu sasa.

Ndipo likamjia tumaini.Akakumbuka kitu pekee kinachoweza kumuokoa mahali pale. Mungu !. Daniel alipiga magoti kwa shida na kuanza kumuomba Mungu.



Hakuwa mhudhuriaji kabisa wa nyumba za ibada.Lakini leo alikwama kweli.Alimuomba Mungu kitu kimoja tu.



Amuokoe katika mdomo wa mauti ili akaitetee nchi yake !





Amuokoe katika mdomo wa mauti ili akaitetee nchi yake..!



Aliomba ndani ya nusu saa.Hakikutokea kitu.

Sasa aliamua kulala akiwa amekosa matumaini kabisa.Daniel alimuona malaika mtoa roho akimsogelea !

Alikata mawasiliano na dunia.

Alizimia !

*************



Ni siku ya pili leo mke wazee Washiro hakwenda kuchuuza samaki mtaani.Alikuwa anamhudumia mtu aliyemuokota mumewe,Mzee Washiro.



Katika mizunguko yale ya kutafuta matunda ya mabungo porini ili akayauze sokoni Bagamoyo apate pesa ya nauli ili aende Arusha kumwangalia mwanae aliyekuwa mikononi mwa Polisi.Mzee Washiro alikutana na kitu cha ajabu.



Ni mwezi sasa tangu mwanae Abdul alipompigia simu na kumueleza kuwa amepatwa na matatizo Arusha.

Mwanawe alikamatwa Kwa kosa la kumuua mtoto wa makamu wa Raisi wa Zanzibar,Mayasa Ally.



Siku ya tatu baada ya kuacha kazi yake ya uvuvi ambayo aliona inamuingizia pesa pole pole aliamua kuingia msituni kutafuta matunda hayo pori na kwenda kuyauza sokoni.Sasa alikuwa na akiba ya elfu kumi na tano ndani.



Siku ya nne aliyoenda msituni kutafuta mabungo, hakurudi na mabungo.Alirudi na mwili wa mtu aliyepoteza fahamu !



Siku hiyo alikiona kibanda kidogo kilichokuwepo katikati ya msitu.Mzee Washiro alikisogelea kwa tahadhari.Alisikia mtu akikoroma ndani ya kibanda hiko. Bila shaka alikuwa katika matatizo makubwa.Alivunja kufuli ya kibanda kile kwa kutumia jiwe kubwa , alimkuta mtu aliyekuwa kapoteza fahamu ndani yake.Alimchukua na kumpeleka nyumbani kwake.



Tangu siki hiyo Daniel alikuwa anahudumiwa na mama Washiro. Mama yake mzazi na Abdul.

Hawakuwa na uwezo wa kumpeleka hospital.Daniel alihudumiwa kwa dawa za kienyeji.Siku ya pili leo fahamu za Daniel hazikuwa zimerejea.



Siku ya tatu alfajiri walisikia makelele katika chumba cha mgonjwa wao.Daniel alikuwa analia usingizini.

Mzee Washiro alienda chumbani na kumkuta Daniel akigaragara kitandani.Alikuwa anataja neno moja tu.

Angamizo.

Angamizo.

Angamizo.

Mzee Washiro hakuelewa Maana ya maneno hayo.Lakini alijawa na furaha moyoni kuona mgonjwa wao amepata nafuu.



Siku hiyo ndio ilikuwa mwanzo wa Daniel kurejea duniani.Ilihitajika lishe bora tu ili Daniel arudi katika hali yake ya kwaida .Maana hakuwa na jeraha lolote mwilini.



"Nashukuru sana mzee kwa msaada wako"Daniel alisema siku moja.

"Usijari kijana"

"Umenisaidia sana.Umenitoa kwenye ufu na kunirudisha duniani.Mungu akubariki sana!

" Amina"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Sasa mzee naomba uniazime simu yako niwajulishe ndugu zangu hali yangu"



Mzee Washiro alimpa simu Daniel Mwaseba.



Simu aliyopiga Daniel ilizua chereko upande wa pili.

Daniel alipiga simu kwa Inspekta Jenerali wa Polisi,IJP John Rondo alifurahi sana.Kwani alihisi Daniel ameuwawa.Nusu saa baadae helkopta ya kijeshi ilitua ndani ya mji wa Bagamoyo na kumbeba Daniel na kumpeleka Dar es salam kwa uangalizi maalum.Alimuahidi Mzee Washiro ipo siku atarudi tena kulipa fadhila kwa aliyomfanyia..!









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog