IMEANDIKWA NA : FRANK MUSHI
*********************************************************************************
Simulizi : The Worst Valentine's Day
Sehemu Ya Kwanza (1)
“….kwa,kwa,kwa” ile sauti ya viatu bado ilisikika ikitembea katika korido ya nyumbani kwangu na hali ya hewa ilikuwa ya upepo mkubwa..hofu ilitaka kunikamata lakini nilihisi kuwa naota na hivyo nilitoka tena kwa mara nyingine taratibu nikichungulia ni nani aliyekuwa akija lakini sikuona kitu,,,nilifungua dirisha nakutazama nje niliona giza nene na sauti na mwanga wa radi ukipiga hapo mvua ikafata na ile sauti sikuisikia tena,,,bado shauku yangu ilikuwa ni kukutana na JAMSHID JABIR ambaye ni mwaka wa tatu sasa toka nimekutana nae kwenye mtandao wa kijamii wa FACEBOOK,,,alikuwa mwanaume mtanashati kwa kumwangalia kwenye picha nakumbuka ni wakati natoka Finland kuja Tanzania ndiyo siku niliamua kuwa nitakuwa na yeye, hapo ikiwa ni miaka miwili toka anitongeze na mimi kukubali kuwa na yeye,,ingawaje nilikuwa mkristu lakini niliamini kabisa kwa Jamshidi nitabadilisha dini,,wengi wangeona uamuzi wangu huu ni wa kishenzi lakini sikujali kwa kuwa mapenzi hayana kanuni maalumu wala hakuna sehemu ya kuweza kuonana na mtu ambaye angeweza kuyafanya maisha yako yawe ya furaha,,niliamini hivyo.
Nakumbuka mara baada ya Jamshid na mimi kukubaliana kuwa wapenzi alifunga safari na kuja Finland kunifata kipindi icho nikisoma chuo kikuu cha Helsinki kule Finland,,alinieleza mengi kuhusu yeye lakini kikubwa ni kwamba baba yake alikuwa ni mfanya biashara wa mafuta huko Mascat nchini Oman na kwamba asilia yao ni visiwa vya karafuu Zanzibar na kwa wakati huo anaishi Zanzibar na wazazi wake,,nilimpenda sana si kwa sababu kwao walikuwa na uwezo hapana nilimpenda kwakuwa yeye alikuwa mwanaume wa kwanza kunivutia,,historia ya maisha yangu haikunipa kabisa mwanya wa kuyatamani mapenzi licha tu ya kuyasogelea na hii ndiyo sababu kubwa iliyonifanya niamini kwa hakika kabisa nilikuwa nikimpenda Jamshid,,,katika maisha na Jamshid nilijitahidi sana kukusanya taarifa zinazomuhusu na kuchunguza kwa kadiri nilivyoweza na nilijiridhisha kabisa kuwa Jamshid ndiye mwanaume wa maisha yangu, nilitunza usichana wangu ili kumuhifadhia Jamshid kwa kipindi chote toka nijuane naye na LEO HII ikiwa ni siku ya wapendanao nilijiandaa kabisa KUUTOA USICHANA WANGU kwa Jamshid,,nakumbuka wakati narudi kutoka masomoni nilitamani sana kuwaarifu marafiki zangu kuhusu Jamshid lakini nililiweka hilo kuwa siri kwa muda mpaka nikatambulishwe nyumbani kwa kina Jamshid,,,kwakuwa wazazi wangu walifariki siku nyingi na sikuwa na ndugu nchini Tanzania niliishi peke yangu na Magret ambaye ni mfanyakazi wa ndani kwenye lile jumba kubwa nililoachiwa na Mzee Herman Obieng ambaye ndiye baba yangu aliyefariki dunia miaka mingi iliyopita baada ya mama yangu kubakwa na majambazi nane waliovamia nyumba yetu siku mbili kabla ya kifo cha baba yangu,,,unyama ule uliotendeka mbele yangu ndio uliofanya niwachukie wanaume kuliko kitu chochote lakini kwa Jamshid siku na la kusema…
*******
Jana yake asubuhi nilipokea simu kutoka kwa Jamshid akinitaarifu kuwa angekuja kwangu siku iliyofuata mabayo ilikuwa ni siku ya wapenda nao maarufu kama Valentine’s day,,hii kwangu ilikuwa taarifa ya furaha sana,,,siku iyo nilikaa nikiwasiliana na Jamshid na maongezi yetu yote yalilenga katika kufanya mapenzi tu,,kwa hakika na dhati ya moyo wangu nilitamani sana kulala kitanda kimoja na Jamshid,,nilitamani sana Jamshid aweke historia katika maisha yangu..
*****
Niliamka mapema siku hiyo na nilianza kufanya usafi kila kona ya nyumba hiyo,,furaha niliyokuwa nayo siku hiyo ilikuwa ni kubwa kuliko furaha yangu niliyowahi kuwa nayo siku nilipofika nchini Finland,,ni kubwa sawa na furaha ambayo ningekuwa nayo kama wazazi wangu wangerudishwa katika maisha yangu,,,majira ya saa 8 mchana ya siku iyo niliwasiliana na Jamshid na alinitaarifu kuwa yuko bandarini huko Zanzibar akisubiri boti ya kuja Dar na majira ya saa 12 jioni nilimtuma Magret kwa rafiki yangu akalale ili kunipa uhuru wa kula raha na Jamshid,,,nilifahamu fika nyumba ile ilikuwa kubwa kwa yeye kukaa lakini nilitaka kuwa huru zaidi kama ni kulia na kucheka nilitaka nilie na kucheka mpka mwisho wa uwezo wangu,,,kwa hakika hii ilikuwa siku kubwa kwangu ukizingatia ilikuwa ni siku ya kwanza ya wapendanao mimi kuwa na mpenzi, kwaiyo niliichukulia kwa uzito wa peke yake..
“kwa,,kwa,,kwa”nilisikia tena ile sauti ya viatu ikitembea kwenye korido kuelekea jikoni,,hapo ilikuwa inaelekea saa 3 ya usiku na simu ya Jamshid haikua inapatikana tena,,,taratibu upepo na radi zilizidi na hatimaye sasa umeme ukakatika na mwanga wa mishumaa ulianza kuiangaza nyumba ile toka pale sebuleni mpaka chumbani,,hofu na woga ulianza kunijia nikanyanyua simu yangu ya mkononi kutaka kupiga kwa Jamshid lakini nilichoka baada ya kukutana na ujumbe unaoonyesha kuwa hakukuwa na mtandao “NO SERVICE”,,,hapo ilizidi na taratibu furaha yangu ilianza kupotea zile ngurumo za radi na sauti za kutisha ziliusumbua ubongo wangu nisijue cha kufanya na ghafla nilitazama ile nguo niliyokuwa nimevaa nikashtuka kuona si nyeupe tena bali nyekundu taratibu nilianza kusikia milango ikifunguliwa na upepo mkali ukiingia ndani lakini ile mishumaa haikuzimika nilianza kulia kwa nguvu lakini sauti haikutoka, nilianza kusikia sauti za ajabu kama wanyama wa mwituni na ghafla madirisha yalifunguka na kwambali kulikuwa na mwanga mkubwa na kundi kubwa la watu wakija usawa wa nyumbani kwangu sikuelewa chochote na hapo mkojo mwembamba machozi na kamasi vilinitoka,,mawazo ya Jamshid hayakuwepo tena na hapa sikuwaza kitu chochote,,nilitamani iwe ni ndoto lakini haikuwa,,,wakati nataka kukimbia nilishtuka kuona siwezi kutoa mguu pale nilipo,,,na mpaka hapo lile kundi kubwa la watu lilikuwa limekaribia kabisa na niliona ukuta wa nyumba ukifunguka kama geti la uwanja wa taifa na wale watu waliingia na kusimama mbele yangu walikuwa wamevaa nguo nyekundu na wamejifunika vitambaa vyeusi,,nilipatwa na haja ndogo kwa mara nyingine tena na hapo mmoja aliyekuwa mbele alivua kile kitambaa na hapo ndipo nilipogundua ni Jamshid……
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
na ndipo nilipoona macho yake yakiwa mekundi na miale ya moto ilioneka na kwenye macho yake,,meno miwili marefu yalichomoza mdomoni kwake na ile hali ilizidi kunitisha na nilitamani nife ili nisione yaliyokuwa yanatokea,,alinisogelea na kunishika na kisha akanisemesha kwa lugha ya kiarabu lakini sikuelewa aliirudia tena ile lugha na wakati huu akinisogelea kwa karibu,,nilitetemeka sana na kwa muda mfupi nilikuwa tayari nimekonda lakini sikuweza kusogea wala kupiga kelele, wakati huo wale wengine walikuwa bado wamejifunika usoni na vitambaa vyeusi na walikuwa wameinama kama wanasujudu,,,haya yote yalikuwa maajabu kwangu,,,taratibu nilianza kuona ule ukuta wa nyumba ukirudi kama mwanzo na umeme ukarudi nilitazama pale sebuleni palikuwa pakubwa na idadi ya watu waliokuwa pale walikuwa ni zaidi ya hamsini na kulikuwa na boksi kubwa nyuma yao kama vile la friji,,hapo Jamshid aliendelea kunitazama na kuniongelesha kwa ile lugha ya kiarabu hata ivyo sikujibu kwakuwa sikuielewa na hapo alibadili lugha na kuanza kuongea Kiswahili;
“Asalam aleyku”alinisalim mara hii kwa salam ambayo nayo sikuweza kuijibu,,
“Jina langu naitwa jini Shamsu, naishi katika kilindi cha maji ndani ya bahani ya hindi nyumbani kwetu ni Nungwi, mbele yako kuna majini tofauti zaidi ya 50 ila niwatambulishe kwa majina wakuu wangu,,ATHA huyu ni mkuu wangu, ndiye mungu wa kiarabu wa kuabudu sanamu,,yupo TARAKADHURU jini lililompa baba yako mali kwa masharti akakiuka,,yupo jini AL-RAHAB aliyekukatia umeme wakati tunakuja,,yupo jini ABADI ambaye ndio yeye na kundi lake waliohusika kuvamia nyumba yenu na kumbaka mama yako mpaka kufa,,yupo jini FARK na majani mengine”. Ilikuwa sauti ya Jamshid ikiongea hayo yote ambayo kwangu mimi sikuyaelewa na hapo akili yangu ilihama na kurudi miaka mingi nyuma wakati wale majambazi wameivamia nyumba yetu,,,ilikuwa ni majira ya saa nane usiku ambapo nilikia sauti ya baba na mama wakipiga kelele nikashtuka na muda mfupi mbele nikatoka mpaka kwenye korido na ndipo nilipokamatwa na kupelekwa moja kwamoja mpaka pale walipowekwa wazazi wangu na mimi nikafungwa pamoja nao,,mama yangu alichukuliwa na kuvuliwa nguo mbele yangu na baba na kisha walianza kumuingilia mmoja baada ya mwingine,,,alilia kwa uchungu sana lakini hakuna ambalo tungeweza kufanya nakumbuka yale majambazi yalimgeukia baba na kuanza kumsemesha kwa lugha ambayo hata ivyo sikuielewa na baba aliwajibu huku akionekana kuzidi kuomba msamaha,,kwakuwa akili yangu ilikuwa ndogo sikuwaza ile ni lugha gani na kwanini mambo yote yalitokea kwa haraka,,,nakumbuka kesho yake asubuhi mama alifariki lakini usiku ule baada ya wale majambazi kuondoka nilimsihi baba tumpeleke hospitali lakini alikataa na badala yake alimpigia simu mtu nisiyemfahamu na kuongea nae kwa lugha ileile ile ambayo wale watu waliongea nae na sasa ndo napata akili kuwa lugha ile ilikuwa ni kiarab,,siku moja baada ya mazishi ya mama nakumbuka vizuri kuwa baba aliniita na kuni na kunikalisha chini na maongezi yetu yalianza kwa yeye kunipa mlolongo mrefu wa mambo ambayo hata hivyo sikuelewa maana hakuwa wazi;http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Binti yangu mama yako amefariki na hatuna la kufanya juu ya hilo,,wewe una umri mdogo lakini kuanzia hivi sasa unatakiwa ujifunze kujitegemea na kuongoza biashara zangu na miradi mingine” hiyo ilikuwa sauti ya baba yangu ikinipa taarifa na hapo ilikuwa ni siku moja kabla ya kifo chake
“baba tupo wote mimi sidhani kama nitaweza kufanya hayo”nilimuambia kwa sauti ya upole lakini nilishangaa baba alivyoamka na sauti ya ukali
“utaweza na ni lazima uweze,,usiseme tupo wote,,” hiyo ilikuwa sauti ya baba yangu ikinipa taarifa na hapo ilikuwa ni siku moja kabla ya kifo chake
“baba tupo wote mimi sidhani kama nitaweza kufanya hayo”nilimuambia kwa sauti ya upole lakini nilishangaa baba alivyoamka na sauti ya ukali
“utaweza na ni lazima uweze,,usiseme tupo wote,,you are only you,,am dead already (uko peke yako, mimi nimeshakufa tayari)”..Nilishangazwa na taarifa hii lakini zaidi sikutilia maanani maneno ya baba kwakuwa nilijua ni msongo wa mawazo kwa kifo cha mke wake, lakini alinyanyuka pale na kusimama pembeni akachukua simu yake ya mkononi na kuanza kupiga simu na hapo nilimsikia akiongea na mtu kwa lugha ya kifaransa;
“la cargaison est arriv???” (Mzigo uliwasili?) Ilikuwa sauti kavu ya mzee ikiuliza na baada ya upande wa pili kujibu nilisikia tena akimsemesha kuashirika kuwa tayari walishakubaliana.
“Venez chez moi maintenant” (Njoo nyumbani kwangu sasa hivi),,baada ya hapo baba alibonyeza teza vitufe vya simu yake na akaiweka tena sikioni na sasa alikuwa akiongea na Rorbahcho rafiki yake wakijerumani aliyekuwa akiishi Tanzania ambaye ndiye niliyekuwa nikimchukulia kama baba yangu mdogo kwakuwa sikuwahi kumuona ndugu ya baba yangu,,,waliongea kwa sauti ya chini lakini niliweza kumsikia baba akimueleza jambo na kwakuwa nilielewa japo ni kidogo nilimuelewa;
“Ich konnte jeden Tag ab heute sterben” (ninaweza kufa siku yoyote kuanzia leo) hili lilikuwa kati ya maneno machache sana ambayo niliyasikia katika yale maongezi ambayo baba aliongea na Mzee Rorbahcho lilinishtua na kuniumiza ila sikuelewa chochote kilichokuwa kikiendelea pale niliendelea kumsikiliza akiongea na nilibahatika kusikia maneno mengine na kiasi cha pesa kilichonishtua;
“make 200,000/= pfund auf meiner tochter-konto übertragen”(hamisha paundi 200,000 taslim kwenda kwenye akaunti ya binti yangu),,fedha hii ilikuwa ni sawa na shilingi za kitanzania milioni mia tano,,nilitaka kumuuliza baba nini kilikuwa kinaendelea lakini sikupata mda wa kufanya ivyo kwani baada ya yeye kumaliza kuongea na simu hiyo alimpigia simu Samah ambaye ni binti mwenye asili ya kiarab na mda si mrefu niliona akiingia na gari yake nyeusi aina ya Cadillac,,Samah alikuwa ni mwanasheria wa familia yetu na baada ya yeye kufika kwa haraka niliitwa ndani na makabidhiano ya mali yalianza,,mambo yalikwenda haraka sana na sikuweza kuuliza chochote zaidi ya kuweka sahihi kwenye lundo la makaratasi yaliyokuwa pale mezani,,na baada ya muda mfupi tulimaliza na Samah aliambiwa anipeleke kwenye kila sehemu ambayo tumeweka sahihi makatasi yake,,,niliingia kwenye gari ya Samah na muda mfupi mbeleni tuliingia kiwanda cha Maji ya kunywa cha MORIS FOOD INDUSTRIES na hapo alikusanya wafanyakazi wote na kunitangaza kama mmiliki wa kiwanda hicho,,,hakuna aliyehoji na sikuwa naelewa nini kinaendelea bado,,,niliingia kwenye gari na moja kwa moja nilipelekwa maeneo mengine mengi na mida ya saa saba tuliingia kwenye nyumba kubwa ambapo ndani nilikutana na mwanamke mrembo aliyevaa baibui ya rangi ya dhahabu na Samah alinitambulisha kuwa yule aliitwa Maysa ndiye aliyemsaidia baba yangu kupata uraia wa Tanzania kipindi alipoingia nchini akitokea Rwanda enzi izo akiwa kijana,,alinifahamisha kuwa Maysa alikuwa ni Msaidizi wa balozi wa Oman nchini Tanzania lakini hata hivyo sikuelewa kwanini tuko pale,,,waliniingiza ndania na mara hiyo Maysa aliniambia nisiogope chochote na akaja mbele yangu na chupa ya juice na kuniwekea nilipoinywa nilitapika lakini alichoniambia ni kuwa sasa naweza kujitegemea yote yalitokea haraka na hakuna muda wa kuuliza swali nilikuwa kama nimepigwa na butwaa lakini baada ya kunywa ile juice nilipata nguvu za ghafla na woga uliniishia.
*****
“Faith” nilishtuka toka kwenye dimbwi la mawazo lililonifanya nisahau kilichokua mbele yangu.
“Abee” niliitika kwa sauti ya mshtuko iliyojaa woga na kilio,,Jamshid alinyanya mikono yake kama aliyekuwa akiagiza kitu na hapo wale watu wote walikaa pande mbili na katikati yao kukatokea sufuria kubwa lenye maji ya moto yanayochemka.
“Leo ni siku ya wapendanao na ni siku ya kutimiza maagano,,ni siku ya malipizi ni siku ya adhabu kwa wote waliosaliti ufalme wa majani,,leo ni siku ya sherehe na leo ni siku ya kunywa damu,,leo ni siku ya kufunuliwa kwako na siku ya kujua ukweli unaouma” aliongea Jamshid na hapo aligeuka na kuongea na wale waliokuwa wameketi pale ambapo ukuta ulichanika na wao kuingia,,,aliwasemesha kwa lugha ya kidachi ambayo na mimi ghafla nilijikuta nikiifahamu;
“Brengen dat verrader hier” (mleteni yule msaliti hapa) hapo waliondoka wale jamaa kupitia ile kona ya ukuta na hapo walirudi na mtu kwenye kiti chenye matairi kupitia pale kwenye ule ukuta na alikuwa amefunikwa,,baada ya kumfikisha pale aliwanyanyua wengine na kuwaambia tena kwa lugha ile ile ila muda huu alisema kamleteni yule Malaya,,,baada ya hawa kutoka aliingizwa mtu mwingine akiwa na hali kama ile ya yule wa kwanza na hapo walifunuliwa vile vitambaa,sikuamini nilichokiona,,,alikuwa ni baba yangu na mama yangu wote wakiwa hai,,walikuwa wamekonda na walionekana wadhoofu kupita maelezo nililia kwa uchungu mkubwa na kutaka kuwafata lakini sikuweza kunyanyua mguu pale nilipokuwa,,nililia nikimuita mama na baba lakini haikusaidia mana wao pia machozi yaliwatoka na walionekana wakitaka kuongea lakini hali waliyokuwa nayo sauti haikuweza kutoka,,,hapo niliisikia tena sauti ya Jamshid ikiita na hapo wasichana wawili waembo waliamka na kutoa vitambaa vyao na mikononi walikuwa na mapanga mawili marefu yaliyokuwa yaking’aa kuonyesha kuwa yanilikuwa makali kama wembe,,,nilifuta machozi na kuwatazama usoni sikuamini kuwa wale walikuwa MAYSA NA SAMAH…
Maysa alinitazama kwa macho makali yenye miale ya moto,,alisogea mpaka pale alipokuwa Jamshid na kuinama akionyesha ishara ya kusujudu au kama vile kumpa heshima,,hapo niligundua kabisa kuwa Jamshid alikuwa mkubwa pale na wengine wote walikuwa wakitekeleza maagizo yake,,,Jamshid alimtazama Maysa na kumuambia;http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tulikukabidhi huyu msichana toka siku ya kwanza baba yake alipousaliti ulimwengu wa majini lakini ulimuweka huru kwa muda mrefu karibu achukuliwe na walimwengu na siku ya leo tukitekeleza Hukumu ya wazazi wake wewe utasimamia uhai au ufu wake” aliongea Jamshid huku akinitazama machoni,,,na Maysa aliinama kuonyesha ishara ya utii,,,hapo Samah alinyanyuka na taratibu akamsogelea Jamshid na kumkabidhi lilile panga moja,,wote waliokuwamo pale ndani walianza kuimba wimbo wa kuhamasisha wasaliti wachinjwe na damu inywewe pale,,,sauti zile zilikuwa kubwa na mda huu baba yangu alitolewa pale kwenye kile kiti na kuning’inizwa juu kisha nilishuhudia panga lile kali likipita mguuni mwa baba yangu na palepale mguu ulidondoka,,japokuwa hakuwa na sauti toka alipoingia pale ndani lakini maumivu ya panga lile lilipopita katika mguu yake yalimfanya atoe sauti kubwa iliyoujaza ukumbi wa pale tulipokuwa,,damu ilianza kuchuruzika katika mguu ule na chombo kama birika kililetwa pale na ilikingwa kisha walianza kugawana wote wakinywa na kufurahi,,mtu pekee ambaye hakunywa alikuwa ni Jamshid na Samah,,ila wengine wote walikunywa kwa furahanililia sana hasa baada ya kumuangali baba yangu yangu akilia na kuteseka pale juu,,,nilitamani kupata nguvu na uwezo ili niweze kumsaidia lakini sikuweza kwakuwa bado hata kama ningeweza kunyanyua mguu pale lakini nisingeweza kushindana na nguvu ya majini, muda huo ilikuwa inaelekea saa tano kamili usiku,,,nilimtazama Jamshid usoni na kukumbuka siku aliyokuja Finland kunitembelea,,,alikuwa kijana mtanashati sana ambaye msichana yeyote mwenye akili timamu asingeweza kumpita bila kujisemea moyoni kuwa huyu kijana anabamba,,,nakumbuka alipokuja tulienda nae chuoni Helsinki katika mgahawa wa SUNSET uliopo njekaribu kabisa na darasa wanalosoma wanafunzi wa shahada ya Utawala na Usuluhishi wa migogoro,,darasa ambalo limejaa wanafunzi wengi warembo na wengi wao walikuwa ni Wavenezuela na Wafilipino na Wabrazil ambao ni maarufu sana kwa urembo duniani,,,nakumbuka sikuiyo baada ya wanafunzi wa darasa hilo hawakusita kusimama na kumuangalia Jamshid akiwa ndani ya T-shirt nyeusi iliyoandikwa WELCOME TO AFRICA na jeans nyeusi,,,katika kipindi chote alichokaa na mimi pale Finland Jamshid hajawahi kuvaa nguo tofauti na yenye rangi nyeusi hiyo haikunishtua kwakuwa alishanambia anapenda nguo za rangi nyeusi,,,hayo yote yalikuwa maisha ya siku tatu nchini Finland!
“Faith” nilishtuliwa na sauti ya Samah aliyekuwa akiniita na mkononi alishikilia kikombe kilichokuwa na damu,,,akili yangu ilirudi nyuma na kukumbuka siku niliyoenda kwa Maysa kikombe nilichopewa nacho ile juice siku ile kilikuwa hikihiki cha leo nilikataa kuinywa na kulazimisha kufungwa mdomo lakini Samah alicheka sana kwa sauti kubwa na kusababisha wengine kucheka sauti ile ya mwangu iliufanya mdomo wangu kufunguka taratibu na sasa Samah alikiweka kile kikombe na nikajikuta nakipokea na kuanza kunywa ile damu,,sikujua ni nini kinatokea katika maisha yangu lakini sikuwa na woga tena,,nilipata nguvu za ghafla na hapo niliweza kunyanya miguu yangu na ndipo sasa nilipokabidhiwa panga kali alilokuwa ameshikilia Maysa baba yangu alishushwa chini na wakati huu bado akilia kwa uchungu,,,nilimtazama usoni na hapo nilimsikia akisema;
“Faith don’t do this, you will enter in a covenant that will make u more than them”( Faith usifanye hivyo,,utaingia kwenye agano ambalo litakufanya uwe zaidi ya wao),,,ilikuwa sauti iliyojaa majonzi na simanzi tele toka kwa baba yangu,,,sikutaka kumsikiliza zaidi,,nilinyanyua lile panga juu na kulishusha kwenye mguu wa pili wa baba yangu na sauti kali ya uchungu ilimtoka,,baba yangu hakulia kwakuwa nilimkata lakini ninauhakika aliliakwakuwa pengine alijua ninini kitanitokea,,,nilimaliza kumkata ule mguu na kuendelea kumkatakata vipande vipande mpaka nilipofika kiunoni,,,cha ajabu baba alikuwa bado hai walikuwa wakimnywesha nyongo kila ambapo damu ilikuwa ikimtoka,,,baada ya mimi kutenda hayo katika hali isiyoyakawaida walinipa tena kile kikombe na mara hii nilipokunywa nilijikuta nimerudi kama mwanzo na hapa niligundua nilichokitenda kuwa ni kuondoa uhai wa baba yangu,,,nililia tena kwa uchungu kwa kuwa sasa niliona kile baba alichokisema,,,wakati huu wote Jamshid alinitazama kwa makini sana na kwa macho makavu lakini alionekana kunionea huruma,,nilipata ujasiri wa kumtazama na ndipo maneno yaliponitoka mdomoni mwangu;
“kwanini ulikuja katika maisha yangu Jamshid,,kwanini umekuja kuharibu kila kitu katika maisha yangu,,kwanini Jamshid?”,,Machozi na kwikwi ziliniandama lakini mpaka hapo Jamshid hakunijibu chochote alinitazama kama mtu aliyekuwa akiisoma nafsi yangu na ndipo aliponyanyuka na kunisogelea wakati huo wote wengine walikuwa wakiendelea na kula vipange kwa zile nyama nilizokata toka kwenye mwili wa baba yangu;
“Faith,nilikuwa kama wewe,,nilitendewa ulichotendewa wewe,,yalinitokea haya kama yanavyokutokea wewe na kama yatakavyokutokea leo na muda wote,,nakupenda kweli lakini ni lazima uwe kama mimi kwakuwa wote lazima tutumikie adhabu kwa makosa ya wazazi wetu” aliongea huku akinitazama.
“lakini mimi sitaki haya,,kama unanipenda niokoe na hili”,,,nilimuongelesha Jamshid kwasauti ambayo nina uhakika kabisa ilimshawishi na kumuonyesha fika kuwa nilihitaji kuwa sehemu ya ulimwengu na si sehemu ya kuzimu,,,mara hii alinitazama katika macho ya kibinadamu yaliyoonyesha shauku ya kutaka kunisaidia,,,macho yake yalinikumbusha siku ya kwanza kabisa namuona pale Vantaa Airport aliponikumbatia na kuibusu midomo yangu,,nilipata msisimko wa ajabu na kila nilipomtazama machoni sikuhitaji aniambie kuwa ananipenda kwakuwa macho yake yanieleza wazi,,kwa mda huu na nikionacho ndo napata akili kuwa ule ulikuwa mvuto wa kijini,,;
“ni lazima upitie mateso haya,,,ni lazima ushuhudie kila kitu kinachotokea hapa na kitakachotokea katika maisha yako yote,,,huu ni mwanzo wa anga la giza,,ni mwanzo wa sala za wafu na ufalme wa kuzimu,,huo ndo mfumo mpya wa maisha yako”,,,aliniambia na kugeuka kuelekea kwa wenzake pale pembeni yangu,,,kisha Samah alinifata na kuniletea tena kile kikombe lakini mda huu sikunyanyua tena mdomo,,alifanya kama mara ya kwanza lakini ilishindikana,,,hasira ziliwajaa wote na ndipo walipofungua lile boksi kubwa lilikuwa nyuma pale wakati wanaingia,,ghafla nilisikia tumbo likinikata baada ya kuona ni Magret ambaye ni mfanyakazi wa ndani wa nyumbani kwetu na ambaye leo hii tu nilimtuma kwa rafiki yangu ili anipe nafasi na Jamshid,,,lakini sasa nilishangaa kwanini walimleta pale,,bila kupoteza muda walimvua nguo zote na kumuacha uchi,,,alikuwa akilia lakini sauti haikutoka,,kilio chake kilinikumbusha kuwa Magret na yeye alikuwa ni yatima,,wazazi wake waliuawa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya nchini Rwanda na yeye alikuja Tanzania kama mkimbizi na kufanikiwa kupata kazi pale nyumbani,,mara nyingi hakupenda kuongelea kuhusu maisha yake wala ya wazazi wake lakini siku zote kila nilipoonyesha kusikitishwa na namna majambazi yalivyovamia nyumbani kwetu na kumbaka mama yangu alinipa moyo na kuniambia yeye alipatwa na makubwa zaidi ya yale lakini bado hataki kumlaumu mungu kwa kilichotokea,,katika maisha yangu baada ya kifo cha wazazi wangu Magret ndiye aliyekuwa maisha yangu tena,,alikuwa zaidi ya rafiki,,hata kipindi nikiwa finland yeye alikaa na nyumba na kila kitu nilikikuta salama japo nilikuwa na kawaida ya kurudi kila baada ya miezi miwili ila yeye alikuwa mtu wangu wa karibu,,mar azote pamoja na kupata msaada wa usimamizi wa makampuni ya wazazi wangu toka kwa Maysa na Samaha kazi iyo ilinishinda na kuamua kuuza hisa zote na kujitoa umiliki wa kampuni nikiwa nimebakiwa na saluni tatu kubwa katikati ya jiji la Dar es salaam na nyingine Mwanza na Arusha mali zote hizi Magret alizisimamia kwa ustadi na uaminifu mkubwa na hakuwahi kuiba hata shilingi tano,,,yeye alikuwa kila kitu kwangu na sasa nilikuwa nikishuhudia akidhalilishwa mbele yangu na sikuwa na lakufanya zaidi ya kulia nae;
“Jamshid niueni mimi,,nifanyeni mtakalo lakini waacheni wengine wote”,, nilimsemesha Jamshid huku nikilia na yeye alimgeukia tena Samah na hapo Samah alinifata akinionyesha ishara ya kwamba nifungue mdomo ili ninywe ile damu ndani ya kikombe lakini nilizidi kufunga mdomo,,,nilifahamu nikinywa tena ile damu ningebadilika na kuwa kama wao na kumkatakata tena baba yangu au mama yangu au Magret na sikuwa tayari kufanya hivyo.
“Siwezi kufanya ivyo,, siwezi Samah tafadhali,,waache wote niueni mimi nifanyeni mtakavyo”,,,nilimwambia Samah lakini nilikuwa kama nimemuambia waueni,,,Maysa alimsogelea Magret na bila kusita alimshika ziwa lake la kushoto na kupitisha lile panga kali lililopita bila kugoma popote,,,nilimsikia akipiga kelele kubwa na hapohapo alipoteza fahamu,,,gauni lile jekundu la Maysa lilikuwa limeloa damu na mkononi alikuwa amebeba lile titi la Magret ambalo aliliingiza kwenye lile sufuria lenye maji yaliyokuwa yanachemka,,,wakati huu nilikuwa silii tena ila nilikuwa ninafikiria namna ya kufanya mambo yasiendelee tena kutokea pale,,akili yangu sasa hayakuwaza tena juu ya jambo jingine lolote zaidi ya kuwakomboa wale waliokuwa wananihusu pale,,,niliamua sasa kuwa huu ndo wakati wakuonyesha mimi ni nani na nini uwezo wa nguvu za watu walionipigania,,,pengine leo katika maisha yangu yote ndio nakwenda kuonyesha uhalisia wangu na utambulisho wangu,,,pengine hata wazazi wangu baada ya kifo chao hawajawahi kujua binti yao nilikuwa mtu wa aina gani,,,macho yangu yalianza kujaa ngumu na mwili wangu ulipata nguvu zaidi na zaidi kila nilipowaza juu ya asili yangu,,taratibu kama vile waliokuwepo pale walianza kushtuka juu ya ujio wa jambo jipya,,nilimtazama baba yangu akiteseka pale chini na kumwangalia Magret aliyekuwa bado amepoteza fahamu nikaona ipo haja ya kurudi nilikokuwa,,,nilimtazama mama yangu aliyekuwa amekonda kupita kiasi na ndipo nilipopaza sauti;
“COOOMEEEE THE ANGEEELLLLS OFFFF LIIIGGHHT”(njooni malaika wa nuru),,,nilipaza sauti mara tatu na ngurumo kubwa za radi ziliitikisa ile nyumba moto mkubwa ukawaka na mvua kubwa ikaanza kushuka,,,Jamshid alinisogelea na lile panga kwa karibu na kuniuliza mimi ni nani na nina nguvu gani,,,na mimi nilimjibu kwa sauti kuu…
“Am a FREEMASON”
“unasema nini” nilisikia sauti ya Jamshid ikiuliza kwa shauku ya kutaka kujua nilichokisema,,mda huo wale wengine wote waliyeyuka na sikujua walitokaje pale,nilipotazama pale ndani hata hivyo nilimwona Magret tu ambaye alikuwa bado pale chini.
“kama ulivyosikia”nilimjibu Jamshid na kukimbia pale alipokuwa Magret nikamnyanyua na ghafla nilishangaa kuona lile ziwa likiwa halijakatwa,,hapo bado ngurumo za radi na ule moto uliendelea kuwaka na ndipo niliponyoosha ishara ya vidole viwili na pale kila kitu kilitulia,,,sikumwona baba yangu wala mama yangu na pale ndani palikuwa shwari kabisa,,niligeuka tena na sasa nilimuona Jamshiod aliyekuwa amesimama huku akitetemeka na mda huu alikuwa katika hali ya kibinadamu..nilimsogelea na hapo nilipata ujasiri mkubwa wa kumpiga kofi shavuni;
“nakuchukia kuliko kitu chochote katika maisha yangu,,ondoka hapa”,,nilimwambia Jamshid na hapo nilishuhudia machozi yakimtoka na sauti yake ilisikika ikiniambia;
“sina hatia,,ipo siku utaujua ukweli Faith” aliniambia na muda huohuo sikumuoana tena,,nilikaa pale chini nikalia kwa uchungu sana na ndipo nilipomwona Magret akifungua macho taratibu,,nilimkimbilia pale chini na ndipo nilipogundua Magret hakufahamu lolote lililokuwa likiendelea;
“kwanini unalia dada Faith” ndilo swali la kwanza alilonihoji na nilijitahidi kumficha ukweli wa mambo ili kama ni kweli hatokumbuka basi katika maisha asikae akumbuke lile tukio lililotokea pale,,sikutamani kabisa mtu yoyote afahamu kilichotokea kwakuwa hata mimi nilitamani kuusahau ukweli niliouona,,,maswali mengi yalikijaza kichwa changu lakini kikubwa ni wapi wamepelekwa wazazi wangu na ni kwanini Jamshid alibaki nyuma,,mapenzi na Jamshid sikuyawaza tena na sasa nilihisi maisha yangu yameshaharibika kabisa siri zangu zimeshabainika na sasa kila mtu atajua kuwa najihusisha na kundi ambalo wengi wanaliogopa;http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“dada Faith”,,ilikuwa sauti ya Magret ambaye alikuwa tayari ameshaamka pale chini na nilimuona akiwa amesimama dirishani,,hapo woga ukanijia tena upya.
“unasemaje”nilimuuliza kwa shauku maana alionekana na yeye alikuwa akitazama nje.
“kuna magari matatu yameingia kwetu meusi,njoo uyaone”nilinyanyuka pale nilipokuwa na moja kwa moja nilienda mpaka dirishani nakutazama nje, ndipo nilipogundua kuwa walikuwa ni wakuu wa kundi la freemason nchini Tanzania,,hofu ilinijaa na hapohapo nilisikia tumbo likikata,,nilimwambia Magret kuwa wale walikuwa wageni wangu na nilimuomba aende chumbani,,,na mimi nilitoka taratibu nikaingia chumbani nikavaa gauni langu refu na kisha nilitoka mpaka pale nje ambapo moja kwa moja nilikutana na mzee Vladimir ambaye ndiye mwenye cheo kikubwa kwa hapa Tanzania;
“vi salute nel nome di angeli della luce”(nakusalimu katika jina la malaika wa nuru) nilimsalimu kwa lugha ya kiitaliano kwakuwa ndiyo lugha niliyoambiwa kuitumia wakati nikisalimiana na mkubwa wangu,,,alininyanyua pale nilipopiga magoti na kuniangalia machoni kisha kunipa mkono kama tulivyozoea kupeana kwa ishara zetu,,,mawazo yangu yote hayakuwa pale, nilikuwa nikiwaza ni nini kitatokea kwakuwa kwa mara ya kwanza sasa toka nijiunge na kundi hili kwa ushawishi wa Mzee Rorbahcho aliyekuwa rafiki mkubwa wa baba yangu mpaka leo hii sijawahi kufatwa na viongozi wangu na leo ikiwa ndo nimetumia nguvu za wakuu wa nuru nimekuja kufatwa nyumbani,,hii kwangu ilikuwa ni hofu nyingine tena,,,akili yangu ilivurugika na sasa nilianza kujuta kila kilichotokea kwenye maisha yangu,,,saa yangu ya mkononi ilionyesha mda huo ulikuwa ni saa 5 na dakika 33,,ikimaanisha siku ya wapendanao ilikuwa bado haijaisha; nilipotazama vizuri alioongozana nao niligundua kuwa alikuwamo Mzee Rorbahcho nae alikuja na kunishika mkono..mpaka hapo ile hofu ikaondoka na ndipo niliposikia sauti ya yule kiongozi ikiniambia tena;
“Noi vi proteggera ma si fara presto il tuo sacrifice”(tutakulinda ila utatoa sadaka yako muda sio mrefu)..milishtushwa na neno sadaka lakini sikupata muda wa kuuliza kwani wale waliingia kwenye gari na kuondoka,,,bado akili yangu ahaikuwa sawa na sasa nilikaa pale chini tena nikilia,,,ila ghafla machozi yalinikauka baada ya kunyanyua uso wangu na kumuona Jamshid akiwa amesimama mbele yangu na kunipatia kitambaa ili nijifute machozi,,hasira zilinirudia tena na sasa nilitoka pale kwa kasi na kukimbilia ndani nikachukua bastola yangu na kutoka nje ambapo nilimkuta Jamshid akiwa amesimama palepale,,,niliikoki na kunyoosha kuelekea kwake na bila kuhoji mara mbili niliifyatua risasa mara tano mfululizo lakini hakuna hata moja iliyopenyeza mwili wake,,nilizidi kulia na kufyatua risasi ovyo huku nikimulekea yeye lakini niliishiwa tena na machozi nilipoona na yeye alikuwa akili,,katika hali isiyokuwa ya kawaida nilimtazama Jamshid na kumuonea huruma,,mara hii na mimi machozi yalinitoka si kwasababu nyingine ila nahisi ni kwasababu ya mapenzi niliyokuwa nayo kwa Jamshid,,nilijaribu kuidanganya nafsi yangu kuwa namchukia Jamshid lakini haikuwa hivyo katika uhalisia wake,,nilimpenda Jamshid kwa kila hali na kikuwa nilikuwa nikikumbuka aliponambia pale ndani kuwa alikuwa kama mimi lakini alikuwa alivyo kwa makosa ya wazazi wake..nilimsogelea pale alipokuwa amesimama na kwa sauti ya ukali iliyojaa mahaba nilimuuliza;
“unataka nini katika maisha yangu ewe jini usiye na haya”nilijitahidi kumkazia macho ili asione udhaifu wa kihisia ulioanza kutanda ndani ya uso wangu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Faith,,nililazimishwa kuwa hivi baada ya wazazi wangu kukiuka masharti ya jini lililompa utajiri baba yangu,,,baba yangu alikuwa ni mmiliki wa kisima kimoja cha mafuta huko uarabun,,kuna kipindi mafuta hayakuwa yanapatikana kabisa na ndipo alipoamua kwenda kutafuta namna ya kuhakikisha kisima chake kinatoa mafuta kama kawaida,,,alifanikiwa na kupewa kaya ya majini ili kufanya usimamizi wa shughuli zake kwa ahadi kuwa angenitoa sadaka lakini baadaye aliwakatalia na ndipo walipoanza kumuandama na kisha kumfilisi na mwishowe walikuja kumuua na nililazimishwa kunywa damu yake na toka pale niligeuka kuwa kama wao,,niliamia kisiwani nungwi chini kabisa ya bahari na kuishi huko nikinywa damu za watu waliopotelea baharini kwa muda wa miaka 7 na ndipo nilipopandishwa cheo na kuachiwa,,siipendi hali niliyopo na kwasasa nimefukuzwa na hawataniacha mzima mpaka niende na wewe,,,naamini unaweza ni saidia kwakuwa uwezo wako na wa watu wako ni mkubwa kuliko uwezo”,,,aliongea hayo Jamshid huku machozi yakimtoka,,,nilisikia uchungu kwa yale machache aliyoyaongea na hapo nilimfata na kumkumbatia,,,sikuamini kwa ulo msisimko niliousikia wakati namkumbatia Jamshid pale nje,,nilimkumbatia kwa takribani dakika tatu bila kumuachia na wala sikutamani kumuachia pia,,,alikuwa na mvuto wa aina yake kwa hakika ya moyo wangu huyu ndo alikuwa chaguo langu.
****
Nilimvuta mpaka ndani na ndipo niliponyanyua simu yangu ya mkononi nikampigia mzee Rorbahcho nikimuomba kuonana nae,,na yeye alinambia tukutane mda ule ule,,Lapodiz café iliyokuwa mita mia tano toka pale kwangu,,nilimuingiza Jamshid kwenye gari na kuondoa gari kwa kasi ya ajabu na ndani ya dakika tatutulishafika,,nilishukla na kumueleza mzee Rorbahcho kila kitu na yeye aliniambia tunaweza kumsaidia Jamshid akarudi katika hali ya kawaida kwakuwa katika ulimwengu wa nuru mengi yanawezekana,,,hapo tulipanda gari yake na moja kwa moja tulielekea mpaka eneo letu la kukutania maarufu kama MASONIC LODGE,,na pale aliniacha nje na yeye na Jamshid waliingia ndani ambapo wakubwa wa kundi hili walikutana,,nilisubiri nje kwa masaa matatu na hapo sikupata usingizi hata kidogo,,baadaye walitoka na sasa Jamshid alionekana ni mzima kabisa,,nilielezwa kuwa watamlinda na hakuna nguvu inaweza kushindana nao.
****
WIKI MBILI MBELE
Haikuwa rahisi kumuonyesha Jamshid hisia zangu tena kwa siku zilizofuata japo aliishi nyumbani kwangu kwa takribani wiki mbili sasa mar azote alikuwa akijitahidi kuomba msamaha na kunieleza yale yaliyotokea hayakuwa katika mipango yake na sasa niliamua kumsamehe na sasa mapenzi yetu yalianza upya,,,Jamshid alifanikiwa kuuingia mwili wangu na kuweka historia ya kuwa mwanaume wa kwanza katika maisha yangu kushika mwili wangu na hata kuvua nguo yangu ya ndani,,nilisikia maumivu makali siku ile lakini raha niliyoipata iliziba maumivu yale niliyoyasikia,,na sasa maisha yalikuwa ni kati ya mimi na yeye na Magret ndani ya jumba letu kubwa lililojitenga na maeneo ya watu wengine,,,bado nilikuwa na hofu ya pengine labda hali ya hatari ingeweza kujitokeza tena lakini kwa maisha niliyoyaanza na Jamshid niliamini ningekuwa salama kabisa..nilimpenda Jamshid kuliko kitu kingine chochote,,upendo wangu kwa Jamshid ulikuwa sawa na nilivyompenda Magret japo kwa Magret ulizidi kiasi kwakuwa yeye alikuwa ni sehemu ya maisha yangu,,Jamshid na Magret kwasasa ndio walikuwa baba yangu na mama yangu, niliwapenda sana na kila muda niliwafikiria wao.
“pipiiiiii,,,,,pipiii” ilikuwa ni honi ya gari iliyokuwa ikiashiria kuwa kuna gari nje lililotaka kuingia ndani,,nilichungulia nje nikaona Juma ambaye ndiye milinzi mpya wa geti akiende kufungua geti ilikuruhusu gari kuingia, nilibaki palepale dirishani kutazama ni nani aliyekuwa akiingia na ndipo nilipogundua kuwa alikuwa mzee Rorbahcho,,nilipomuona nilikumbuka siku ya kwanza mzee Rorbahcho alipokuja kikazi nchini finland na kunichukua mpaka Uingereza, mzee huyu alikuwa kama baba yangu kwakuwa kila nilipomuona alikuwa akinikumbusha juu ya baba yangu,,alikuwa rafiki mkubwa sana wa kibiashara wa baba yangu hivyo mara nyingi nilimsikiliza kwa yale aliyoniambia,,siku hiyo tulipoenda Uingereza alinielezea juu ya kundi la freemasons,,ni yeye ndiye aliyenishawishi kuingia kwenye kundi hilo na baada ya kunikutanisha na mzee Richardson White mkuu wa kundi hilo nchini Uingereza basi nilikubali kwa moyo mmoja kujiunga na kundi hilo,,niliandikishwa kama mwanachama wa kundi hilo nikiwa ndani ya SURREY PROVINCIAL GRAND LODGE iliyopo kusini magharibi mwa Uingereza inayojumuisha maeneo ya Hampshire na Berkshire na mengine,,yeye ndiye aliyenitolea kiingilio na kuhakikishwa nawekwa kwenye Masoni lodge itakayoniwezesha kufanikisha kuhudhuria kila mkutano utakaofanyika,,Surrey Lodge ilikuwa inawanachama zaidi ya mia 300 na Uingereza yote katika Lodge zote zaidi ya 8000 ilikuwa inawanachama 300,000,,hivyo kuingia kwangu ndani ya kundi la freemasons kulitengeneza upya sehemu ya maisha yangu na uamini wangu,,nilidhani ningeiacha dini yangu lakini haikuwa hivyo bali niliingia katika jumuiya kubwa iliyokuwa na msaada kwangu;
*****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilitoka nje baada ya kuhakikisha kuwa mzee Rorbahcho alikuwa ndani ya geti langu na kwa haraka nilimfata pale alipokuwa na kusalimu na yeye aliitika,,nilimkaribisha ndani lakini hakuingia badala yake alinipa taarifa ambayo ilinifanya nilie na nianze kujuta tena;
“the angels of the light requires you to give your sacrifice today night before 00:00”(malaika wa nuru wanataka utoe sadaka yak oleo usiku kabla ya saa 6:00) aliniambia kwa sauti kavu isiyokuwa na mtikisiko wala mawimbi.
“and what’s that sacrifice”(na ni sadaka gani) nilimuuliza huku nikitetemeka,,nilitamani anijibu kuwa ilikuwa kiasi chochote cha pesa lakini si anambie ilikuwa ni mtu tena.
“you choose between Jamshid or Magret”(utachagua kati ya Jamshid au Magret),,
“hapana haiwezi kuwa hivyo”..nilianza kulia na kumfuata mzee Rorbahcho huku nimepiga magoti,,sikutaka kusikia yale maneno na sikuwa tayari kumtoa yoyote kati ya hao wawili,,pengine ingeonekana huu ndo muda wa mimi kumtoa Jamshid lakini hapana,,Jamshid alinipenda kweli na mimi nilimpenda kuliko kitu chochote kwenye maisha yangu na sikuwa tayari kumpoteza kwa siku za karibuni, maana kumpoteza Jamshid kwa sasa ilimaanisha kupotea mimi mwenyewe,,nampenda Jamshid achilia mbali yaliyotokea baina yangu na yeye ambayo hata hivyo kwasasa sijali kitu chochote,,ninachokiangalia mbele yangu ni maisha yangu na Jamshid,,nilikuwa tayari kutoa uhai wangu kwa ajili ya Jamshid…nilimgeukia tena mzee Rorbahcho na kumsihi tena;
“tafadhali nisaidie baba, sina namna ya kumtoa yeyote kati yao,,nichukueni mimi lakini hawa waacheni” nilizidi kulia na muda huu jasho na machozi yaliujaza uso wangu,,nilitamani aniambie nitoe hata mali zangu zote kuliko kumtoa yoyote kati yao,,sikuwa tayari;;
“you have no any other option Faith,,once they say,,there is no rebuting nor denial”(hauna njia nyingine Faith,wanaposema hakuna kufuta kauli wala kukataa)..hii ndiyo kauli aliyoniambia mzee Rorbahcho na kuniacha pale chini nikilia,
****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilinyanyuka pale chini na kuangalia huku na huku sikuona kama kuna aliyeniona,,nilisogea mpaka mbele palipokuwa na bomba la maji na kulifungua kisha nikanawa uso na kujifuta lile vumbi kisha nikaondoka pale huku nikionyesha uso wa furaha na kuingia ndani kimyakimya huku nikinyata nia yangu ikiwa ni kwenda kubadilisha nguo na kuondoka niende mbali na nyumbani pale kwa muda, sikuona mtu yoyote pale sebuleni na hivyo niliharakisha na kuingia chumbani nako pia sikumkuta Jamshid,,niliingia bafuni na kuoga haraka na nilipotoka nilimkuta Jamshid ameketi kitandani.
“vipi mbona kama unatoka” lilikuwa la swali la kwanza kuulizwa na Jamshid, sikutaka kumuonyesha kabisa kuwa siko sawa au kulikuwa na tatizo kwakuwa jambo la kwanza kabisa nililokuwa silitaki katika dunia ni kumuona Jamshid anakuwa nahuzuni,,hivyo nilimtazama kwa tabasamu pana lililojaa majonzi yaliyojificha na sikumjibu kitu bali nilimfata mpaka pale kitandani na kumkumbatia,,nililia sana moyoni japo machoni bado lile tabasamu lilikuwa likiificha huzuni na mtihani mkubwa niliokuwa nao,,pamoja na mambo mengine Jamshid alijua nilichokuwa na kihitaji kila mara nilipohitaji chochote,,alijua namna ya kunifanya nisahau kila kitu kilichowahi kutokea usiku wa siku ya wapendanao,,Jamshid hakufurahishwa na ukweli kuwa nilikuwa ni freemason lakini kwakuwa haikuwa na athari kwenye mapenzi yetu hakutaka kujihangaisha kuniambia lolote juu ya hilo,,nikiwa bado nimemkumbatia huku nikiwaza juu ya sadaka niliyotakiwa kuitoa kabla ya usiku wa saa sita ya leo nilihisi mikono ya Jamshid ikipita mgongoni mwangu na hapo hisia zangu ziliama na hamu ya kujiunga kwenye ulimwengu mwingine na Jamshid ziliukabili mwili na fikra zangu,,nilizidi kujihisi kama vile namwagiwa maji huku macho nikiwa nimeyafumba kuruhusu ulimwengu wa mapenzi kuzama ndani ya ubongo wangu,,nilishtuka nikiwa nimelala kitandani na muda huu Jamshid aliendelea na utundu wake wa kucheza sera na mwili wangu,,ulimi wake ndio ulionifanya nisikie usingize wenye mchanganyiko na upepo wa mawaridi ulioufanya moyo wangu unukie tena,,nilifungua macho nikamuona Jamshid akizidisha utoto wake kwa kuyanyonya maziwa yangu ambayo bila kificho yalimpa raha,,na mimi bila kujizuia nilinyanyuka na kutupa ile taulo chini kisha nilianza kujibu mashambulizi,,nilitamani sana raha niliyokuwa nikiisikia hapa iwe sehemu ya maisha yangu ya kila siku lakini haikuwa hivyo,,nilikuwa na fedha nyingi sana kwenye akaunti yangu,,nilikuwa na elimu nzuri na maisha mazuri na nyumba nzuri,,,nilikuwa ni moja kati ya wasichana warembo wa jijini Dar es Salaam hivi vyote nilikuwa tayari kuvitoa ilimradi tu nibakiwe na Jamshid na Magret kwenye maisha yangu lakini hakuna aliyevihitaji,,nilizidi kuweka akili yangu kwenye kile tulichokuwa tukikifanya na Jamshid na sasa akili yangu ilizama kabisa kwenye dimbwi kubwa la mapenzi baada ya Jamshid kuupitisha ulimi wake palipo na hisia zangu,,sikujielewa au kujiona vizuri lakini kwa hakika nilitoa sauti iliyodhihirisha kuwa Jamshid alikuwa akitenda vyema kazi yake na sikuwa na jingine la kufanya zaidi ya kumuonyesha kuwa nilikuwa niitambua kazi yake nzuri juu ya mwili wangu,,,tulipeana raha ile kwa muda wa masaa matatu na mpaka hapo nilikuwa nimechoka vya kutosha na usingizi ulitupitia kwa pamoja pale kitandani.
***
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment