Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

SIPASWI KUSAMEHEWA - 2

 








Simulizi : Sipaswi Kusamehe

Sehemu Ya Pili (2)





Baada ya hatua kama mbili hivi, ndio Esmile akakumbuka na kugeuka, akamsimamisha Mam ma kumuuliza

“Una simu Mam?’’

“Aaah Esmile, mi bado mwanafunzi, simu ya nini?” alisema Mam na kucheka.

“Haa, kumbe bado unaendelea kusoma?’’ Esmile alijikuta ameuliza swali la kijinga kabisa.

“Ha!...’’ alishangaa Mam na kisha..

“Ajabu nini Esmile kwa mimi kusoma? Ama sifanani na elimu?” swali la Mam lilimfanya Esmile ajione mjinga, ikamlazimu alimalize suala lile kimya kimya

“Hapana Mam, usinielewe vibaya, kwa sasa unasoma wapi?’’

“Benjamin Mkapa kidato cha 6’’

“Bado maskani ni kule kule Kigogo?”

“Yah! Pia nilikuwa nakutania, nina simu ila tu sikutoka nayo kwa sababu fulani, ila tu kama hutajali nikupa namba,”

“Haswaa, hilo ndio la maana!” Esmile akampa simu yake Mam, nae akaandika namba yake na kuendelea kuishika simu ya Esmile, kisha akasema

“Esmile nimefurahi sana leo kukutana nawe, ninaamini leo nitalala usingizi mnono sana”Esmile akacheka huku akisema furaha yake yeye itasababisha asilale kabisa

“Ninaamini picha hii ya ‘Ecotite’ usiku wa leo itapata shida, maana ni zaidi ya mshangao jinsi tulivyokutana”

“Hahahaa! Halafu tuliagana tukisema tutawasiliana lakini wakati huohuo wala hatukupeana namba za simu, Sijui ingekuwaje?” Esmile nae akacheka na kujishangaa hata nae, leo amekuwaje?

“Hapo tena… nawe jiulize! Huenda ilitokana na furaha kupitiliza,” sasa ndio wakaagana huku Mam akimrudishia simu yake Esmile na kila mmoja akatabasamu na kuanza safari yake.

Esmile sasa akaitazama namba kidogo, aliitazama vizuri na kuridhika, sasa ndio akaanza kuisave.

Hata kabla hajaisave namba ile simu yake ikaita tena, akapokea na kuanza kuongea tena na mtu yule yule aliekuwa akiongea nae awali. Sasa alikuwa akimpa maelezo fulani marefu.

Esmile kwa taratibu akaanza kuelekea Kitega uchumi ilipo ofisi yao, hakupata nafasi ya kukata simu ile hadi anaingia ofisini. Alielekea moja kwa moja kama alivyoelekezwa, maana alikuwa akisubiriwa yeye tu.

Alipowasili ndani akazima simu na kuketi kwenye mkutano. Alikuta kikao kikiwa kinaendelea na akajulishwa ajenda juu ya kupata habari ya kuletewa barua kutoka kwenye kampuni moja ya binafsi ikitishia kuwaburuza mahakamani iwapo tu watawacheleweshea mzigo wao ambao tayari wameulipia.

Sasa nae akajiuliza kuna umuhimu gani way eye kuitwa pale ikiwa yeye si mmoja kati ya watu wanaopaswa kuwemo mle kwani waliokuwepo mle karibu wote ni wakurugenzi wa idara mbalimbali, akatulia asikilize dhumuni la kuitwa kwake.

Wakati kikao kinaendelea ndio akakumbuka kitu, kilikuwa ni kitu muhimu pia, alikumbuka kuwa hajasave namba ile aliyopewa na Mam, akishangaa kwa nguvu hadi watu wote wakamtazama na kumuuliza kulikoni? Akawaomba radhi na kutoka nje kidogo.

Akawasha simu lakini hakuna kitu alichoambulia, kwani tayari ilikuwa imefutika, akahisi huenda aliibeep, alipoangalia vizuri hakuikuta, alijikuna kichwani na kupiga ngumi ukutani, akajilazimisha kuikumbuka, lakini hakufanikiwa aliweza kukumbuka namba 4 za mwisho, lakini Code namba ya Mtandao na namba mbili za mwanzo, hakuzikumbuka kabisa.

Alitamani mno kulia, lakini aliona hata kama atalia, nini kitamsaidia kuirejesha namba ile iliopotea? Kilichopotea huwezi kukirudisha kwa masikitiko ama kwa kilio, akazima simu yake na kurejea tena mkutanoni. Alivyovuta kiti na kukaa akishangaa kuona watu wote wakimtazama yeye, akahisi huenda ameharibu, akajitazama, hakuona kasoro yoyote.

Alikuwa nje kwa dakika zisizozidi 3, lakini inaonesha kuna mengi yalizungumzwa kwa muda ule mchache, maana akamsikia Mkurugenzi wake akikohoa kidogo kutengeneza sauti kisha Mkurugenzi akamuita na kusema;

“Kampuni imekuteua wewe uende Mombasa kushughulikia suala lile la container zile tatu za pikipiki mali ya Athuki General ya Tabora, ili ziweze kufika hapa haraka iwezekanavyo na ikiwezekana zitumwe huko ndani ya wiki mbili tu tangu sasa, sawa Esmile?’’

Hakuwa na sifa ya kubisha, uongo, fitna wala ugombanishi, mitaani hata ofisini, daima alikuwa mtiifu. Akakubali na kutakiwa kuondoka siku iliyofuata kwa ndege, kila kitu atakikuta pale siku hiyo ya safari asubuhi kabla ya kwenda Airport.

Akarejea nyumbani akiwa mwenye masikitiko makubwa sana na kujiona yeye ni mtu mwenye bahati mbaya iliyoje, kwani alimpoteza Mam siku ile ya kwanza tu alipomuona, leo tena kapoteza namba ya simu mara tu baada ya kuichukua, basi ikambidi awe mpole hasa baada ya kujua kuwa ni wapi atampata baada ya kurejea kwenye safari yake.

Aliwasili nyumbani kwao saa nne usiku, baada ya kuwasalimia wazazi wake akaingia chumbani, baada ya muda akatoka akiwa amebadili mavazi na kuungana na wazazi wake waliokuwa wakiangalia TV, akatumia muda ule kuwaaga kwa safari ile ya dharula, hawajashangaa, kwani ile haikuwa safari yake ya kwanza, ila wakamtakia safari njema huko aendako.

Akaingia ndani na kujilaza kitandani huku akitazama picha kadhaa alizopiga na Mam huku akitabasamu na kutikisa kichwa, akaiambia nafsi yake

“Hatimae ndoto ya kuwa nawe tena Mam imeanza kurejea taratibu, naomba Mungu usije kutoweka na kunipotea tena katika maisha yangu, kwani sasa nina hakika nitakutia mikononi mwangu,” alijipa moyo na hatimae usingizi ukampitia na kujikuta kalala bila kuwa amejitayarisha kulala.

Usiku mnene ndio ukamshiyua na kuamka, akaenda maliwatoni kuoga na kurejea tena kulala hadi asubuhi ilipowadia, ndio akaamka na kuanza kufanya mazoezi mepesi ya kuchangamsha mwili wakati akisubiri jua lichomoze.

Wakati jua likichomoza asubuhi ile, gari la ofisini nalo lilipaki nje ya nyumba ya kina Esmile, akaisikia na kutoka kukutana na dereva, maana haikuwa kawaida. Dereva akamwambia amemletea kila kitu kinahohusiana na safari yake kutoka ofisini na pia yupo tayari kumuwahisha Airport…



Mambo ya kuoga na kufungua kinywa alikuwa ameisha yafanya, hivyo kwa kuwa yeye alikuwa tayari tayari, alirudi ndani na kuelekea kilipo chumba cha wazazi wake na kuwaaga huku nao wakimtakia safari njema.

Akanyanyua kibegi chake kidogo na kuchomoka hadi garini akimuacha baba yake akimtazama kwa tabasamu huku akimwambia mkewe kuwa anajivunia kuwa na motto wake Yule, akamuaga tena kwa mkono na kuingia garini kuelekea Airport.

Upande wa Mam alisubiri simu ya Esmile kwa usiku mzima, hakuisikia, hadi asubuhi ile ya siku ya pili kimya. Nae akajuta kwa nini hakuchukua tena namba yake kwa mara nyingine.

Japokuwa hakuwa na chochote kwa Esmile lakini alipenda tu kuendelea kumshukuru kutokana na kumuokoa na kifo. Alipotafakari sana na kushindwa kupata jibu kwanini Esmile hajampigia, akaamua kutulia.

Siku ya Jumamosi alipofika Mombasa ilikuwa ni siku fupi kikazi, na siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya mapumziko, hivyo Jumatatu alijidamka na kufanikiwa kuzipata Kontena zote tatu ikiwa ni jioni kabisa. Akapiga simu na kuongea na Mkurugenzi na kumpa habari ya hatua aliyofikia kwa siku ile ya kwanza kule Mombasa.

Alishindwa kuamini alijua Esmile anamdanganya, ila kutokana na msisitizo wake kuwa kesho kuna Meli itapakia mzigo, je apakie na hizo Kontena? Ila meli inashushia Tanga, mkuu wake akakataa na kumwambia asubiri yeye atampigia kumpa maelekezo mara baada ya kuwasiliana na watu wa bandari ya Dar es Salaam.

Muda mchache baadae, akapigiwa simu na kuambiwa kuwa pale Dar mambo si shwari, bandari imefurika na hakuna parking meli bado ni nyingi mno na zina mzigo, sasa wafanyeje?

Esmile akamwambia bosi wake kuwa hilo ni suala dogo sana. Wangemsikiliza nae atoe ushauri. Lakini hata kabla hajatoa ushauri autakao, bosi wake akamkatiza kwa kumwambia kuwa kule Tanga atakapo yeye kuna usumbufu sana ni heri wasubiri.





“Lakini bosi we ungenisikiliza tu name ushauri wangu ni upi, hilo la Tanga nafikiri umelisema name nimekuelewa,” aliongea Esmile na kumfanya bosi wake atulie na kumsikiliza ana ushauri gani kijana Yule ambae wote ofisini walimuamini sana kuwa ni kichwa cha ofisi.

“Tukiachana na bandari ya Tanga, bandari sisi nchini kwetu tumejaaliwa kuwa nazo nyingi, ni suala la kuchagua nyingine,”

“Kama ipi vile kwa mfano?”

“Naona bandari ya Bagamoyo inafaa zaidi mkuu, kwani ni karibu hata na Dar Es Salaam…”

“Ah! Ah! Ah… hiyo ndio hakuna kitu kabisa kijana wangu,”

“Kwanini mkuu?” aliuliza Esmile kwa mshangao.

“Huko kuna matatizo mengi na pia ni wasumbufu sana Esmile.” Bado Esmile hakuafiki juu ya hilo na kutaka kujua huo usumbufu wa Bagamoyo ni upi. Akajibiwa kwamba hata ofisi ya mapato kule ni ndogo, si kubwa na ndio maana inalazimu hata wafanyakazi wake wanapaswa kutoka huku Dar.

“Na kwa vile Dar pia kuna mzigo tena umefurika, wafanyakazi hawawezi kuondoka huku Dar kwenye mizigo mingi, wakaelekea Bagamoyo kwa ajili ya mizigo michache tu iliopo huko..,” hata Esmile nae sasa aliweza kuona kuwa wakifanya hivyo, yaani kupakia hadi Bagamoyo, watakuwa hawajakwepa tatizo lolote.

Vichwa vikawauma wote, hakuna aliepata kuongea, wakaomba muda kidogo wa kufikiri na pia Mkurugenzi akamwambia ampe dakika kama tano tu ili awasiliane na wenzie na kasha atamjulisha.

Walikata simu huku Esmile akijuta kuja huku bila kujipanga, aliamini kabisa kama wangekuwa wamejipanga mapema, leo wasingekwama kabisa kufikia muafaka, lakini lawama zote alizielekeza kwa bodi ya kampuni yao kwa kuona ule ni uzembe wa kwao wao, akajiona yeye hahusiki kabisa.

Baada ya dakika zisizozidi 10 hivi, simu ya Esmile ikaita, akaipokea haraka haraka na kuongea na mpigaji ambae alikuwa ni bosi wake, akamwambia wameshauriana na bodi ya Wagurugenzi na sasa wamekubaliana na shauri wake wa kupitisha mzigo ule kwenye bandari ya Tanga.

Esmile akapumua kwa nguvu na kumwambia bosi wake kuwa nae sasa suala la kuteremshia mzigo ule Tanga analipinga hilo, Mkuu akashangaa na kumuuliza kuwa ule si ulikuwa ni ushauri wake yeye?

Alikubali Esmile na kusema baada ya tathmini ndogo aliyofanya, amegundua kuwa itakuwa ni ngumu sana kuitekeleza ahadi waliyo kubaliana na Athuki, pia kuna sababu nyingine. Mkurugenzi alipotaka kujua sababu, akajibiwa kwamba;

“Gharama za kusafirisha mzigo toka hapa Mombasa hadi Tanga, kweli ni ndogo sana, hilo ni kweli, tatizo lipo kutoka Tanga hadi Tabora, hizo gharama ni za nani? Ofisi yetu ama Athuki?”

Bosi akamjibu kuwa Athuki amelipia gharama zote za kupelekewa mzigo hadi Tabora, hivyo kama kuna faida katika biashara ile, itaingia kwenye ofisi yao, na kama kuna hasara, pia ni hivyo hivyo. Esmile akamuhakikishia kuwa hakuna hasara watakayopata, kama kweli jamaa anataka mzigo umfikie akiwa Tabora, yeye aondoe shaka.

Ili kumtia mori, bosi akamuahidi Esmile 10% ya faida itakayopatikana itakuwa ni yake ila hatohusika na hasara yoyote. Esmile hakuamini akauliza kama ni kweli, akahakikishiwa kuwa ni kweli, kisha wakaagana na kukata simu.

Akili ikaanza kumzunguka sasa, ni kipi afanye ili kuilinda heshima ya kampuni na vilevile kumfurahisha mteja wao bila kuiathiri kampuni yao? Akashika simu yake kwa nia ya kuingia WhatsApp ili apoteze muda katika kuuvuta muda wa kula na kulala.

Baada tu ya kuishika na kutoa Lock, ghafla kama mtu aliepigwa na shoti ya umeme, tena umeme ule wa radi, akatoa ukelele wa kushangilia…http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Jumanne asubuhi Esmile akaomba aingiziwe shilingi milioni 8 kwenye akaunti yake. Pesa ikaingizwa nakufanya Esmile kuanza kuhangaika huku na kule, akipita pande hizi na zile, hadi kufikia mchana akawa amepata magari ya kusafirisha mzigo kwenda Kisumu, na Esmile aliona ni bora afanye hivyo ili kuufikisha mzigo Kisumu kisha kuupeleka Mwanza kupitia Ziwa Victoria.

Mambo ya Mtandao, kabla ya kuongea na boss wake Esmile, alikuwa anatalii mji wa Mombasa kupitia Kenya Map, hivyo hata wakati ule alivyoishika simu, akakuta Map ikiwaimeganda palepale alipokuwa ameiacha kabla hajamaliza kuongea.

Hapo sasa ndio alipata wazo hilo na kuingia kwenye Google map, akaona kuna uwezekano wa kuhamisha mzigo toka baharini hadi ziwani kupitia nchi kavu.

Alichokifanya mwanzo ni kuangalia ni bandari gani upande wa Ziwa Victoria inamfaa, kasha akatazama umbali kutoka Mombasa hadi ilipo bandari husika.

Umbali wa kutoka Mombasa ilipo bandari kwenye fukwe za bahari ya Hindi, hadi Kisumu ambapo kulikuwa na bandari ya Ziwa Victoria, ulikua ni mkubwa mno, lakini ilikuwa ndio njia pekee ambayo ilikua ni muafaka kwa yeye ili kuendana na muda.

Safari ilianza saa 10 jioni ya siku ileile na walitembea usiku mzima hadi alfajiri ya siku ya pili walikuwa wapo Thika, pale wakapumzika kidogo na safari ya kuelekea Kisumu ikianza tena baada ya muda.

Huku Kisumu tayari aliwasiliana na jamaa, jamaa huyo alimjua kupitia mitandao, alikuwa ni mmoja kati ya wafanyakazi wa Mtandao wa Hyper Link, kampuni ambayo aliipa azi ya kusafirisha mzigo wake, ila yeye Esmile alikuwa bado yupo Mombasa akisubiri ndege ya kumfikisha huko. Mara mchana watu waliobeba mzigo ule wakampigia simu kuwa wanataka kushusha mzigo na walimuuliza wateremshie wapi.

Akawaambia waende moja kwa moja bandarini kuna mtu watamkuta na atawapa malekezo.

Saa 10 jioni nae akawa amewasili Kisumu, kwa kuwa kila kitu kilikuwa kimeandaliwa kwa kushirikiana na jamaa wa kwenye meli ile ya mizigo, mzigo ukaingia melini na ilikuwa ni bahati kuwa huo ndio mzigo pekee uliokuwa ukisubiriwa, saa 1 usiku safari ya kutoka bandari ya Kisumu nchini Kenya, kuelekea jijini Mwanza Tanzania ikaanza.

Alipohakikisha meli imeondoka, akatuma Fax ofisini akitaka yaandaliwe malipo kwa ajili ya kampuni ya Hyper Link iliyosafirisha mzigo ule toka Kisumu hadi Mwanza, malipo yaliyobaki ambayo ni shilingi za kitanzania milioni tatu tu. Haikupingwa, malipo yakafanyika.

Nae hakulala pale, ndege ya mwisho kuelekea Tanzania, ilikuwa inaondoka saa 3 usiku na kutua Mwanza saa 5, humo ndio nae akaingia. Mwanza akafikia hotel moja iitwayo ya kifahari iliyopo maeneo ya Nyegezi.

Kabla hajalala akawasiliana na ofisa wa meli ile inayosafirisha zile kontena, kumuuliza utaratibu wa usafiri wa meli zao na hutumia muda gani kufika Mwanza.

Akajibiwa kuwa hutumia saa 15 hadi 18, hivyo hadi kesho yake mchana mzigo wake utakuwa tayari bandarini, akawashukuru na kulala.

Alhamis saa nane mchana, tayari Esmile alikuwa bandarini na aliweza kuiona meli ile ikiwa imepaki na shehena ya mizigo, alifurahi moyoni na kuanza utaratibu wa kutoa mzigo ule.

Alikuwa na karatasi zake zote za kutolea mzigo bandarini, huitwa BOL (Bill of Lading) ilimchukua muda mrefu kidogo, lakini kwa kuwa maandalizi alikuwa ameyaanza tangu wakati ameamka asubuhi, alienda kila sehemu na ilipokuwa imebaki ni kuthibitisha tu, je mzigo uliomo kwenye Container ndio halisi unao onekana kwenye BOL, makabrasha ya usafirishaji?

Hivyo ukaguzi ulifanyika kuanzia jioni na kwa kuwa na uwepo wa vifaa vya kisasa vya ukaguzi, walimalizia ile siku pale hadi jioni, lakini bado hakufanikiwa hadi ijumaa mchana ndio alikamilisha taratibu zote na kuutoa mzigo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kazi ya kutafuta gari za kutoa kontena zile haikuwa nzito, maana palepale palikuwa na madalali, akawapa kazi ya kumtafutia gari ya kusafirisha kontena zile hadi mjini Tabora kwa wenyewe Hata haikushukua muda, kufika saa 11 jioni jamaa wakaanza safari kuelekea Tabora wakiahidi kulala Nzega ili kesho mchana wawe wameingia Tabora.

Aliwapa advance na kuwaahidi pesa nyingine atawapa wakifika mwisho wa safari ambapo ni Tabora, hawakukataa, maana huo ndio utaratibu uliopo na ndio uliozoeleka pia.

Esmile akazima simu yake kukwepa usumbufu maana alitaka awe huru wakati huu akijipanga kwa safari ya Tabora siku ifuatayo. Alikata mitaa ya jiji la Mwanza na kufurahia mandhari nzuri ya milima kwenye jiji lile, jiji la miamba, ‘The Rock City’

Usiku uleule alikwenda hadi nyegezi kituo cha mabasi na kukata tiketi ya kuelekea Tabora alikata basi ambalo alihakikishiwa kuwa ni salama na kuendelea kukata mitaa, alimchukua jamaa wa boda boda na kumtaka ampeleke sehemu mbalimbali ambazo alimwambia.

Kwa hakika alitembea mno hadi kufikia saa tano usiku ndio akarudi hotelini kulala akiwa amechoka lakini ameridhika kutokana na burudani aliyoipata.

Saa 11 alfajiri alarm aliyotegesha ilimuamsha na kujitayarisha na kujiswafi kasha akaelekea kituoni na kupanda basi ambalo liliondoka Jijini Mwanza saa 12 asubuhi kuelekea mkoani Tabora kwa kupitia Shinyanga.

Jumamosi mkoani Tabora huwa kuna mnada mkubwa sana sehemu iitwayo Ipuli hapo huitwa Mnadani watu wengi kama si wote huenda huko kwa nia ya kuburudika kwa nyama choma na burudani mbalimbali zinazopatikana kule.

Basi liliondoka Mwanza saa 12 asubuhi na hadi inafika saa tatu na nusu pale Nzega, hawakuweza kuziona zile Semi, japo Esmile aliamini watazikuta njiani, pale Nzega hawakukaa sana safari ikaendelea sasa wakaingia kwenye kipande kidogo cha barabara ya vumbi kuelekea Tabora mjini.





Saa 6 kasoro walifika eneo fulani ambapo hapakuwa mbali na mji, aliona watu wengi mno, alipouliza kwa mtu aliekuwa jirani yake, akaambiwa pale ndio mnadani. Alipogeuza shingo upande wa pili aliziona semi zote tatu zikiwa zimepaki, akafurahi moyoni na wastani wa dakika kadhaa hivi wakawa wameingia mjini.

Kutoka stand mpya, kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani, umbali mdogo pana hotel nzuri na maarufu, hapo ndio Esmile alipelekwa na jamaa wa bodaboda, lakini kabla jamaa hajaondoka, akamuuliza kama anapajua Athuki General Traders, jamaa akacheka kwanza.

Kisha akamjibu, hakuna mtu Tabora hii asiemjua, ni mtu mwenye uwezo na ana duka kubwa sana la pikipiki na spare zake, na wakiwa palepale akamuonyesha kwa kidole lilipo duka lile. Akaridhika na kumlipa jamaa chake kisha akaingia hotelini kwa ajili ya kutafuta malazi.

Vyumba vilikuwa vizuri na hata mji aliweza kuuona vizuri akiwa kwenye dirisha la chumba chake ghorofa ya nne, akaridhika na kwenda kuoga na huku akiwa ameacha order ya chakula, baada ya kumaliza mipango yake pale hotelini kama kula na kuoga, akatoka.

Safari ilikuwa ni kwenda kwa tajiri sasa moja kwa moja ili akamueleze ujio wake pale mjini. Akawasha simu na kumpigia dereva mmoja wa magari na kumwambia wasiondoke hadi atakapowajulisha wapi pa kwenda.

Kasha akawapigia wazazi wake na kuwajulisha kuwa yupo mkoani Tabora katika kukamilisha kazi aliyotumwa, walishukuru kwa taarifa na kumtakia mafanikio katika ile hatua yake ya mwisho.

Akiwa kwenye mlango wa duka la Athuki, simu yake ikaita, ilikuwa imetoka ofisini, alikuwa ni Badria, Sekretari wa ofisini kwao ambae huwa wanataniana sana, lakini kabla hajamtania, Badria akatoa maelezo ambayo yaliashiria jambo muhimu.

Alimwambia afanye kila awezalo atafute sehemu nzuri akae tulivu na waweze kuongea, akamwambia pale alipo yeye Esmile, ni sehemu tulivu kuliko alipo yeye Badria, kauli ambayo aliamini Badria atacheka, lakini wala haikuwa hivyo.

Badria alichokisema ni kumtaka Esmile abaki hewani vile vile kwa kusubiri kuunganishwa na namba nyingine, kitu ambacho Esmile nae akapata taswira nyingine na kutulia kweli akisubiri hiyo simu muhimu.

Kumbe ni bosi alikuwa akitaka kuongea nae, akamuunganisha, swali la kwanza bosi alimuuliza alipo, Esmile akamjibu kuwa yeye yupo Tabora dukani kwa Athuki, bosi alionekana kama amechanganyikiwa, akamwambia kampuni ya Athuki imewapa masaa 24 tu wawe wamefikisha mzigo, lah sivyo watawaburuza kortini.

‘‘Ha ha haaa… Unasikia bosi, waambie hiyo ni siku nzima, sisi wala hatuhitaji, waambie watupe saa moja tu, mzigo wao utakuwa mlangoni kwao,” akacheka Esmile cheko ya kumshawishi mtu wa upande wa pili nae acheke.

Lakini wala hakuonesha dalili ya kucheka bali alijidhihirisha kuwa ana jazba kutokana na sababu anazo zijua mwenyewe.

“We Esmile mi sitanii, ebo? Hivi unafikiri wakati wote ni wa utani eti? Huu ni wakati wa kazi…”

“Sasa mkuu mbona hatuaminiani? Mi nipo hapa dukani kwa Athuki, lengo ni kumkabidhi mzigo wake kama inavyotakiwa, hayo masuala ya utani yametoka wapi na yameanza lini?”

Esmile nae sasa akapandwa na jazba na kukata simu, hata mkuu aliliewa hilo, akampigia hakupokea, aliiacha ikaita hadi ilipokata akaizima kabisa, sasa bosi akabaki njia panda. Esmile akaingia ndani na alijitambulisha pale na kukaribishwa ofisini alimkuta muhusika wa uingizaji mizigo.

Alimkaribisha kwenye ofisi yake nadhifu, huko alimkuta jamaa akiongea na simu, alimsubiri na alipomaliza, pia akajitambulisha na kukaribishwa kiti ambacho kilikuwa kwa ajili ya wageni kama yeye. Hakika alishangaa mara baada ya Esmile kumueleza hatua waliofikia.

Ofisa yule naye akajitambulisha kwa jina la Hassan Ubaya, alitabasamu tu baada ya kukumbuka kuwa ni muda mchache tu uliopita alipiga simu ofisini kwao na kuongea na Mkurugenzi wa RCCF akitishia kuwaburuza Mahakamani iwapo hawatofikisha mzigo kwa wakati waliokubaliana.

Esmile alitabasamu baada ya kusikia hivyo,

“Unajua bwana Esmile, kampuni yenu tuliipa kazi hii, tukiamini kabisa kuwa inaweza kutufikishia mzigo wetu kwa wakati, lakini ikiwa imebaki wiki mbili, kila tunapopiga simu, majibu yanakuwa hayaeleweki…” aliongea bwana Hassan.

“Eenh ni kweli kaka, lakini ujue kwa sasa mambo ni magumu sana hasa haya yanayohusu bandari, process zimekuwa ni ndefu kidogo katika kudhibiti mapato, lakini kwa kuwa tumelikamilisha, nafikiri mtaendelea kutuamini…” alimaliza huku akicheka.

Hassan akatikisa kichwa kukubali na kumuuliza ni wapi ulipo mzigo. Akamuelekeza yalipo magari na mzigo, wakatoka pamoja na gari ndogo hadi Mnadani. Hiyo ilikuwa ni saa10 jioni, wakawachukua madereva na gari zao hadi ilipo Yard ya Athuki, wakati wakishusha kontena zile, Esmile alikuwa akimalizana na madereva.

Baada ya hilo zoezi nalo kukamilika, akakabidhi makabrasha yote yanayomstahili Athuki General Trader kwa Hassan kisha wakaagana na akaondoka. Hassan akimuahidi kuingiza cheki ya malipo hayo ndani ya siku tatu.

Wakashikana mikono kuagana na kila mmoja akashika hamsini zake, ila Esmile Hakuwa na mwelekeo sahihi ila tu ikawa ni kukata mitaa hadi usiku aliporejea hotelini.

Usiku ule wa kwanza kuwepo pale mkoani Tabora alikua yupo mpweke sana, akatoa simu yake na kuitafuta picha ya Mam ambayo aliamini itamfariji kwa namna moja ama nyingine.

Kweli aliitoa simu na kuanza kuangalia huku akitabasamu na kupata hamu ya kutaka kuongea nae, lakini picha dumu daima dawamu huwa haina herufi hata moja kinywani japo taswira yaonesha uwepo wa mdomo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Siku iliofuata saa 5 asubuhi alikwenda ofisi za shirika la Ndege na kubahatika kupata tiketi ya Dar, alipanda ndege iliyokuwa ikitoka Mwanza kuelekea Dar kupitia Kigoma, ambayo aliambiwa itaondoka pale saa saba na robo adhuhuri ile.

Hadi saa 1 usiku ndio aliwasili Dar akiwa ni mwenye furaha tele kwa kufanikisha zoezi lile aliloagizwa kwa asilimia 100…

********

Kazi imekamilika kwa 100%, mkwaruzano na bosi wake utapokelewa vipi kazini atakapokwenda? Mam bado hajaeleweka, je atapatikana?



Siku takriban 9 sasa bila ya Esmile kuonana na Mam, lakini pia wala hajawasiliana kwani namba aliipoteza mara tu baada ya kuipata. Mam aliisha subiri sana simu kutoka kwa Esmile lakini wala haikutokea, akabaki akisubiri tu.

Kibaya zaidi yeye hata hakuuliza ni wapi anaweza kumpata, maana kwa jinsi alivyo na hamu ya kutoa shukrani zake za dhati, alitamani kumuona, lakini sasa angemtafutia wapi? Ndio hapo sasa akakiri kuwa anapaswa kusubiri tu sikuambayo Esmile atamtafuta mwenyewe.

Jumatatu ya leo Esmile nae alipanga kumtafuta Mam mara tu baada ya kutoka kazini. Alianzia kazini na kupokelewa kwa shangwe na wafanyakazi wenzake hadi akashangaa. Alipouliza sababu akaambiwa kuwa ameokoa mamilioni ya shilingi, pesa za kampuni.

Akawauliza kivipi? Akajibiwa kwamba asubiri kwani ameandaliwa kijisherehe kifupi mchana wakati wa lunch. Hakujali kwa kuamini wanamtania tu. Akamuulizia Mkurugenzi akaambiwa bado hajafika. Akawaaga wenzie kuwa anatoka kidogo ila hatochelewa.

Sekretari alimkatalia kabisa na kumwambia kuwa bosi amesema asitoke pale atakapofika hadi watakapo wasiliana nae. Esmile akasonya tu na kusema anatoka na atakavyo amua yeye bosi, afanye tu, atapokea uamuzi wake wowote kwa mikono miwili.

Alishangaa sana katibu muhtasi wa Mkurugenzi, akamuuliza Esmile amekuwaje? Hiyo haikuwa tabia ya Esmile, akamtazama na kumuona akiwa ni kama mtu mwenye mawazo mengi, kauli ile iliyomkera, ilimkumbusha Tabora, dukani kwa Athuki General.

“Dada yangu ungejua alichonijibu mkuu, usingeniambia kauli yake, aliniudhi sana na sitamani hata kumuona,” aliongea huku akitengeneza miwani yake na kumuaga tena kwa mara nyingine, hakuwa na uwezo wa kumzuia, akamuitikia na Esmile akatoka.

Safari yake iliishia kwenye geti la shule ya Benjamin Mkapa, akapaki gari yake na kuingia ndani hadi ilipo ofisi ya taaluma, alikaribishwa na kuoneshwa mahala pa kukaa ndio akaulizwa shida yake baada ya salamu.

Akamuulizia Maryam Mahmoud kama yupo shule wakati huo, mkuu wa taaluma akamuuliza anasoma kidato gani? Esmile akamwambia kuwa anajua yupo kidato cha sita na hajui chochote zaidi ya hapo.

“Mam ni nani wako na una shida gani?” Mwalimu alimuuliza huku akifunuafunua file moja na kumuangalia Esmile kwa jicho la kumuambia Usinidanganye.

“Mam ni jirani yangu lakini ni zaidi ya ndugu, maana ninahusika kwa kiasi kikubwa na hata sasa nimekuja kwa sababu ya tatizo dogo lililotokea nyumbani,”

“Huoni kuwa utamchanganya na kusababisha ashindwe kusoma na kuimalizia siku ya leo?”

“Hapana mkuu, sitamwambia habari za matatizo yaliyopo nyumbani,” alijitetea Esmile na kusababisha mwalimu ashike mkono wa simu ya mezani na kubofya namba Fulani.

Mwalimu wa Taaluma akapiga simu kwa mwalimu wa darasa na kumuulizia kama Maryam yupo, jibu halikusikika ila Esmile akamsikia mwalimu akamuagiza anaeongea nae amwambie Mam afike ofisini kwake mara moja.

Akiwa ni mwenye wasiwasi mkubwa, aliteremka ngazi akiwaza ni nini kilichotokea, alifikiri labda ni ule mgomo baridi waliouanzisha ndio umeshitukiwa na kusababisha aitwe huko, ama huenda nyumbani kuna tatizo? Hakuona haja ya kujiumiza kichwa zaidi, liwalo na liwe, ngoja aende tu, lililopo atalijua hukohuko.

Ile kuingia ndani akakutana na sura ya mtu anayemjua vizuri, alionekana kuwa na tabasamu kubwa usoni mtu huyo, wakati Mam alikuwa na sura ya wasiwasi na hofu tele, akamsalimia mwalimu wake kwanza, kisha akamgeukia Esmile, na wote wakamjibu kwa pamoja, kisha mwalimu akamuuliza Mam;

“Do you know this boy? (unamjua huyu kijana)?” moyo wa Esmile ukapiga mshindo, hakutegemea kama swali kama hilo ataulizwa Mam na mwalimu wake.







“Yes madam, he is our neighbor (ndio bimkubwa, ni jirani yetu)” jibu hilo likampoza kidogo

“Sawa ameleta ujumbe toka kwenu, nendeni chumba cha maongezi, nawapa dakika 5 tu, umenielewa?’’

‘‘Yes madam’’

Mam akatangulia na kufungua mlango wa kioo, sitting room hii ya shule ilikuwa kwenye varanda pana, imejengwa kwa vioo kila upande, ila upande mmoja ambao wenyewe ni ukuta wenye dirisha la kioo, kubwa sana, kwa hiyo kila apitae pale huweza kuona kila kinachoendelea mule ngani.

Alimkaribisha kwenye sofa la mtu mmoja kisha na akakaa kwenye sofa la watu wawili. Wakati anaketi akaweka kidole chake cha shahada kwenye midomo yake, kisha akatoa kalamu toka kwenye sketi yake na kufanya ishara ya kuandika, akimaanisha kuomba karatasi.

Esmile akamuelewa na kutoa notebook mfukoni, akafunua karatasi kadhaa na alipoona sehemu inayofaa kwa kuandika, akampatia Mam. Alichokiandika kwenye ile karatasi ile kilikuwa ni hiki; ‘Usiongelee mapenzi hapa, please...’ akapokea na kusoma kisha akamwambia kwa sauti

“Ok Mam kilichonileta hapa nafikiri unakijua, hali ulivyoiacha nyumbani asubuhi imebadilika na kuwa ni mbaya zaidi, hivyo tumeamua kumpeleka Ocean road, that’s why mi nimekuja hapa kukujulisha, ukitoka hapa upite kule kwanza,” huu ulikuwa uzushi mtupu maana hawa watu hawakuwa majirani na hakuna hata mmoja anayepafahamu nyumbani kwa mwenzake….

Katika chumba kile cha wageni kwenye shule hiyo walimu waliweka uamuzi wa kutegesha microphone ili kunasa sauti kutokana na tabia ya baadhi ya wanafunzi kuwaleta wapenzi wao na kuja kuzungumza habari za mapenzi badala ya mambo muhimu.

Hivyo mazungumzo yote kwenye chumba kile yalikuwa yakisikilizwa na walimu wa nidhamu hivyo Man alishawahi kuambiwa juu ya hilo naye alichukua tahadhari kubwa…

“Unajua Esmile usingekuja hapa kwani sasa masomo yananipita, mi nilitaka nisije shule ila yeye mwenyewe akanilazimisha, sasa sijui nifanyeje?’’

“Wala usihofu Mam, mi ninachotaka tu ni wewe kufahamu...” huku akimpa kile kikaratasi kilicho andikwa ‘Nina shida muhimu ya kuongea nawe, tutaonana wapi na saa ngapi?”

Wakati ule nae akijibu kwa mtindo wa maandishi, pia kwa sauti akasema;

“Cha muhimu hapa mimi nikitoka shule...” kabla hajamaliza Mam akampa notebook Esmile



“Cha muhimu hapa mimi nikitoka shule…”

Kabla hajamaliza akampa notebook Esmile na kuendelea…

“..nitapitia kwanza nyumbani then nitaelekea Ocean road” Ujumbe kwenye karatasi ulisema.. ‘Nisubiri kituo cha Karume kati ya saa 8 na robo na saa 8 na nusu’ na Esmile akaandika ‘Funguo hizi ni za Rav 4 nyeusi namba T 009 XVZ nitaipaki Karume, nisubiri ndani,’ akachomoa funguo moja na kumkabidhi nyingine kisha akasema kwa sauti huku akimpa kikaratasi na funguo

“Na funguo hizi hapa si umesema utaanzia nyumbani?’’ Mam akatabasamu na kujibu;

‘‘Ndio, ni lazima nianzie nyumbani kwanza ili kubadili nguo na kuandaa chakula ndio name nijue mipango mingine,”

‘‘Haya basi tutaonana hukohuko,” Esmile aliongea bila kubainisha watakutana wapi, maana alisema wataonana hukohuko.

Kisha akatoka na kuelekea zilipo ofizi za waalimu ili kwenda kumshukuru mwalimu, kwa kutumia funguo yake ile moja aliyobaki nayo, akatoa gari hadi Karume na kuipaki, nyuma ya kituo cha daladala cha Karume, kisha akadandia daladala hadi Samora akaingia ofisini mwake pale Kitega Uchumi.

Kila alipokuwa akipita alikuwa akipewa hongera, akawa akiendelea kushangaa, sasa akamshika mkono mmoja wa rafiki zake pale ofisini na kukaa nae kwenye ngazi akitaka amuulize ni vipi kila mtu anampa hongera na wakati issue ilikuwa ni Jumamosi ambayo si siku ya kazi ndio walifanikisha zoezi lile?

“Ni kweli Esmile, ile ilikuwa ni siku ya mapumziko, lakini Katibu Muhtasi alikuwepo ofisini na akatupia kila kitu mtandaoni kwenye group yetu ya WhatsApp ambayo wewe uliikataa,”

“Ahaa! kwa hiyo ndio mkajua wote?”

“Uliza swali Esmile, kwanza kwanini ulilikwepa group letu la ofisi?”

“Ujue nina magroup mengi sana ndio sababu, lakini soon nitajiunga uckonde boss,” akataniana nae kidogo kisha wakanyanyuka na kuelekea ofisini.

Kufika kwa katibu muhtasi akakuta ujumbe kuwa anatakiwa haraka ofisini kwa bosi, akapanda hadi ghorofa ya 7 ilipo ofisi ya Mkurugenzi wake na kuingia akiwa amebadilika.

Sura yake haikuonesha furaha kabisa, hata mkuu wake alipomuona akatambua hilo, lakini yeye akajifanya kama amesahau, akamuuliza ni nini tatizo? Esmile akamjibu

“Katika maisha yangu sitajaribu kumfurahisha mtu kwa kile nifanyacho kwa maslahi ya wengi, na katu sitaeleza ugumu niupatao wala mafanikio yangu bali yataonekana kutokana na mabadiliko kwa mwenye akili,” akanyamaza.

“Unamaanisha nini kijana?”

“Kama ni shida mzee wangu, watu wengi wamepitia mazingira kama haya ninayopitia mimi au zaidi ya haya,mzee wangu umenidhalilisha sana nikiwa Tabora,” hivyo Mkurugenzi alitumia muda ule kumuomba radhi kwa mgongano wao alipokuwa Tabora.

Hakuwa na budi ila kukubali na kumsamehe, kisha Mkurugenzi akampongeza kwa kazi mzuri alioifanya tangu ameondoka jijini mpaka amerejea, alishukuru Esmile na kutabasamu kwa mara ya kwanza tangu aingie mle ndani.

Mwisho akamwambia walikuwa wamemuandalia sherehe ndogo hapa hapa ofisini.

Alishukuru na kumtaka radhi bosi wake kwa kutaka ile sherehe iahirishwe, alipoulizwa ni kwanini? Akajibu kuwa mchumba wake ni mgonjwa na muda huu yupo njiani kuletwa Jijini kutoka Arusha, anategemea kuwasili muda wowot

Akampa pole sana ila hakuridhia suala la kuahirisha mpango wa sherehe ile ya kumpongeza, bali akaamuru waitwe wafanyakazi wote mara moja kwenye ukumbi wa mikutano. Ndani ya dakika 7 hivi wafanyakazi wote wakawa wamewasili na dakika 2 mbele, mkurugenzi nae akawa amewasili na kuanza kuongea na wafanyakazi wake.

Aliwaambia sababu kubwa ya kikao kile cha dharula ni kutaka kumpongeza mfanya kazi mwenzao, Esmile Hanson

‘‘Ninapenda kuwajulisha kuwa Esmile ameweza kuokoa pesa nyingi sana mali ya kampuni, zaidi ya shilingi Milioni 25 ambazo zingeweza kuangamia,” wakapiga makofi na kuendelea kumwaga sifa na kusemahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

‘‘Aliahidiwa 10% na bodi ya Kampuni kama atafikisha mzigo ule Dar kabla ya siku 14 lakini ndani ya siku 8 kontena ikawa imefika Tabora, hivyo bodi imeamua kutoa ile 10% kwenu wafanyakazi wote kama changamoto kwenu...’’ wafanyakazi wakishangaa, kisha wakapiga mbinja, bosi akatabasamu na kuendelea

‘‘Baada ya kuamua hivyo, bodi ikaamua kumpa 20% badala ya 10% iliokuwa imemuahidi awali’’ Hakuamini Esmile, wenzie wakampongeza kwa makofi, kisha Mkurugenzi akaendelea;

“Hivyo Esmile, pesa hiyo itaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti zenu leo hii hii na tumeamua kufanya hivi ili iwe ni fundisho na mfano kwa wengine waweze kujituma zaidi ya Esmile, ahsanteni’’ wakasimama na kupeana mikono na kusambaa kila mmoja akichukua vinywaji na kuelekea ofisini mwake.

Baadhi walikuwa wakiendelea kumpa hongera wakitaka kujua ni njia zipi alizotumia hadi kufanikiwa vile? Aliwaambia kwa kifupi tu huku wengine wakishangaa alipata wapi akili ile ya kufanya hivyo.

“Wewe ni kiumbe mwenye akili nyingine duh!” aliongea mfanyakazi mwenzie huku Esmile akigonga nae kisha akawaaga kuwa anaenda ofisini kwa bosi mara moja.

Wakasambaa wote kila mmoja akishika hamsini zake na Esmile yeye alielekea moja kwa moja kwa mkurugenzi akitaka kujua ni vipi ameokoa pesa zile, kwani hakuelezwa ni vipi ameziokoa, lakini alimwambia ana muda mfupi wa kuwepo pale kwani mchumba wake ni mgonjwa na yupo njiani anakuja, akaomba aelezwe kifupi tu.

Akatikisa kichwa Mkurugenzi, kisha akaanza kumwambia kuwa kampuni ya ATHUKI GENERAL TRADERS ilitoa jumla ya shilingi million 50 kwa ajili ya kufikishiwa kontena zake Tabora kutoka China, ofisi ikitegemea kupata faida ya shilingi Milioni 10 pekee, hivyo hadi mzigo unawasili Mombasa tayari tulikuwa tumeisha tumia shilingi Milioni 10.

“Kwa maana hiyo baada ya gharama zote, hadi kontena zinafika Tabora, ilitumika Milioni 25 tu na tena zilifika kabla ya wakati na makubaliano yalikuwa kama zitachelewa kufika kwa wakati tuliokubaliana, tutalazimika kuwalipa kiasi cha 50% ya gharama za usafirishaji, na wakati huo huo kama tutawahisha wao watatulipa zaidi 20% ya gharama ya usafiri,” akatulia na kunywa maji kisha akaendelea;

Je ataendelea kumwambia nini? Vipi upande wa Mam?



“Kwa maana hiyo baada ya gharama zote, hadi kontena zinafika Tabora, ilitumika Milioni 25 tu na tena zilifika kabla ya wakati na makubaliano yalikuwa kama zitachelewa kufika kwa wakati tuliokubaliana, tutalazimika kuwalipa kiasi cha 50% ya gharama za usafirishaji, na wakati huo huo kama tutawahisha wao watatulipa zaidi 20% ya gharama ya usafiri,” akatulia na kunywa maji kisha akaendelea;



Bosi akaendelea na mazungumzo…

“Kwa kuwa uliwahisha kabla ya muda, mteja wetu ametuongeza 20% pesa ambayo ofisi ilikuwa imekadiria kama faida. Na baada ya juzi wewe kuwakabidhi mzigo wao, alitushukuru na kutuwekea fungu letu, nami nikaiita bodi na kuieleza hali halisi tangu makubaliano yetu ya awali, basi nao wakaridhika na kuamua kukuongeza kama hiyo ili kukupa morali, je una swali lingine?”

Esmile hakuwa na swali tena, alimshukuru tu bosi wake maana hakutaka mazungumzo yawe marefu sana hasa kutokana na ukweli kwamba ilikuwa imeshafika saa 7 mchana, muda ambao aliona ni muafaka kwake kuelekea kituoni Karume alipopanga kukutana na Mam.

Bosi akasema sawa kama hana swali linguine, ila akamwambia anataka ampe kazi moja ndogo aifanye

“Najua kwa kasi yako wewe utaweza kuimaliza maana naihitaji kabla sijaondoka ofisini mchana huu Esmile.”

Hapo Esmile akabadilika kabisa, akili ikaenda mbali mno, maana aliona akizembea kidogo tu hapa, atapoteza nafasi nyingine ya kukutana na Mam ilimbidi kumkumbusha bosi ule uongo wake kwamba mchumba wake anakuja kwa matatizo na inabidi awahi kutoka.

“Pia Mkuu akili yangu naona kama vile haijakaa sawa, hakika akili yangu haijatulia, kwa leo ungeniacha tu nikaenda kumpokea mtu huyu, huenda nikapata nafuu na akili yangu ikatulia.” Alijitetea sana na Bosi alimuelewa

“Mapenzi ya ujana matamu sana Esmile, (akasema huku akitabasamu na kumuangalia Esmile ambae nae sasa akatabasamu) kasha Boss akaendelea

“Sawa mi nakuruhusu uende, jitahidi kesho mapema ukifika tuonane…”

“Ahsante Booss, kazi njema,” wakapeana mikono na kasha Esmile akatoka na kuwaaga wenzie KWa kuahidi kuonana nao siku ifuatayo panapo Majaaliwa yake Mola.

Alipotoka nje alikuta kuna hali ya mvua mvua, kama ujuavyo jiji la Dar es Salaam, kwa wanaolijua vema jiji hili, wanatambua vizuri kwamba mvua ikinyesha hasa katikati ya Jiji, basi kila kitu kinaharibika.

Hali ile ikamtisha, akamuomba dereva amuwahishe maeneo ya Karume kupitia gari la ofisi, jamaa akamuuliza ilipo gari yake akamjuza kuwa gari ile ipo huko Karume ambapo anataka amuwahishe.

Jamaa akamrushia funguo za gari na kasha yeye akazunguka upande wa pili na kusubiri Esmile aingie ndani ya gari na kumfungulia mlango. Baada ya sekunde kadhaa, aliwasha gari haraka na tayari zilishapita dakika 15 yangu saa saba kamili ilipotimia.

Mvua ikaongeza kasi na foleni ikaanza, ikamlazimu sasa kufanya faulo za hapa na pale barabarani ili kuhakikisha anawahi miadi yake na jambo la kushukuru ni kuwa alikuwa anajua njia za mchepuko.

Saa nane kasoro dakika tano alikuwa usawa wa geti la shule ya Benjamini Mkapa, alipaki gari na kushuka, dereva wao akahamia upande wa pili na kuondoa gari. Yeye alikuwa upande wa Barabara ya mtaa wa Lindi akawa na imani kubwa kwamba anawahi na wakati huo mvua ilishapunguza kasi yalibaki manyuyu madogo madogo sana.

Wakati huo wanafunzi walikuwa ameanza kutoka kwa makundi usawa wa geti. Alifika sehemu aliyoahidi na kubaki gari lake ikiwa ni dakika tano zilishapita tangu saa nane kamili. Aliona wanafunzi wakipita na kisha akamuona Mam akiwa ameongozana na binti ambae alionekana kama ni rafiki yake wakilisogelea gari. Esmile muda huo alikuwa ameketi ndani ya gari ili kuyakwepa matone madogo madogo ya mvua, walipokaribia akashuka…

“Mambo Esmile?”

“Poa tu Mam, za masomo?”

“Fresh,” alijibu Mam akisuasua

“Naona upo na mrembo?”

“Ooh, ni kweli, nilitaka nikufahamishe baadae, ila tu ngoja nikutambulishe sasa..” huku akimshika bega rafiki yake, akamtambulisha huku akimtazama Esmile.

“Huyu ni rafiki yangu kipenzi anaitwa Rahel au unaweza kumuita Pacha wangu, anaishi maeneo ya Jangwani, huandamana nae kila nitokapo hapa shule,” baada ya kusema hivyo, Mam akageuka na kumtazama Rahel

“Huyu ni Esmile, nafikiri taarifa zake unazijua ndio mwokozi wangu huyu Rahel,”

Esmile na Rahel wakasogeleana na kusalimiana kwa furaha na kila mmoja akishukuru kumuona mwenzie.

“Samahani warembo hapa nimebaki na soda moja ambayo itapendeza zaidi kama nitampa mgeni wetu wa leo, yaani Rahel, we Mam utakunywa baadaye...” wenyewe walijidai wamezoeana sana kumbe uongo mtupu, wakacheka huku Esmile akimkabidhi Rahel ile soda.

Baada tu ya kuipokea Esmile akawaaga kwenda kwa muuza vinywaji baridi kibanda ambacho wala hakikuwa mbali sana ili amchukulie kinywaji Mam

“Mam ngoja nikuchukulie soda moja hapo yenye ujumbe maalum kwako,”

“No! Hapana, nitakunywa siku nyingine, acha sisi tuwahi nyumbani’’ Mam alisema maneno hayo huku akimkabidhi ile funguo Esmile

“Ingieni basi garini, sasa mtawahi vipi?” aliwauliza Esmile wakati akifungua mlango wa gari yake na kuanza kuingia yeye kwanza.

Akafungua milango mingine na kuwakaribisha, Rahel alikuwa ni mapepe mno akaingia mbele, sehemu ambayo Esmile alitegemea atakaa Mam, na ili kuonyesha kuwa yeye anaijua sana gari ile Rahel akalaza kiti, Mam akakaa nyuma yao.

Esmile akageuza gari na kuingia barabara ya Uhuru na kuelekea Kawawa, kwanza akiwa na nia ya kuelekea Jangwani ili kumuacha Rahel angalau karibu na kwao, kasha waende Kigogo nyumbani kwa kina Mam.

Wakiwa njiani, wote walikuwa kimya kabisa kila mmoja ana wazo lake, wakati Esmile akiwaza ni vipi amuanze Mam, Rahel alikuwa na mawazo mengine kabisa alishampenda Esmile hivyo naye alijiwazia namna anavyoweza japo kuwa na wasaa wa mawasilinao ya pembeni na Esmile.

Mam nae alikuwa akifikiri kichwani mwake ni kipi ambacho Esmile anataka kukisema, japo nae alikuwa na yake anataka kuyasema, lakini alihisi ya Esmile yatakuwa ni mazito zaidi.

Rahel anawaza kumtia mikononi Esmile, Mam Mam nae anawaza ni nini Esmile anataka kuongea nae.. nini kitatokea hapa? Kati ya Mam na Esmile nani ataanza kusema kinachomsumbua? Nani atavunja ukimya kati yao? Na atakuja na mada gani?









Esmile akiwaza ni vipi amuanze Mam, Rahel alikuwa na mawazo mengine kabisa alishampenda Esmile hivyo naye alijiwazia namna anavyoweza japo kuwa na wasaa wa mawasilinao ya pembeni na Esmile na Mam



Mam nae alikuwa akifikiri kichwani mwake ni kipi ambacho Esmile anataka kukisema, japo nae alikuwa na yake anataka kuyasema, lakini alihisi ya Esmile yatakuwa ni mazito zaidi.



Walipoingia barabara ya Kawawa, bado ukimya ulitawala, Rahel ndi akauvunja kwa kuuliza



“Esmile mimi huwa karibu sana na Mam, mbona sijawahi kukuona hata mara moja?’’



“Ni kweli Rahel, mi kidogo kwa kweli nimebanwa, wakati mwingine hufika hata wiki mbili bila kuonana na Mam’’



“Anhaa! Kwani unafanya kazi gani?”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nipo kwenye kampuni moja ya kutoa mizigo bandarini, ofisi zetu zipo Mtaa wa Samora, jengo la kitega uchumi,”



‘‘Ok ila mi si mwenyeji pande za huko’’



‘‘Utamwambia Mam akulete yeye ni mwenyeji” kisha akampachikia Mam akimtazama kwenye kioo cha ndani ‘‘Uongo Mam?” Mam alicheka na kukubali kwa kichwa.



Akiwa na tabasamu usoni, aliendelea kumtazama Mam kupitia kwenye kioo cha ndani na macho yao yalipokutana kila mmoja alielekea upande wake, lakini wote walitazama nje walipofika njia panda ya Kigogo na Jangwani, Esmile alisimamisha gari na kumuuliza Rahel amuache wapi. Rahel aligoma kuachwa njiani akalazimisha wampeleke hadi kwao.



Esmile akajitetea tena



“Sina nia ya kukuacha njiani, bali muda ndio unakataa, siku nikiwa huru nitakuja na Mam si anapajua?’’ bado Rahel hakukubali na kuwataka wampeleke,



“Mi najua vizuri sana kuwa Mam anapajua nyumbani, lakini wewe hupajui, name nataka wewe ndio upajue,” aliongeza Rahel.



“Yaani nitapajua na kuja kwenu kila mara hadi utaniona kero, ila kwa leo niache kwa kuwa muda unabana sana Rahel,”



“Acha nyodo motto wa kiume, kwani tunaenda Kigoma kwa miguu?” aliongea Rahel kwa sauti ya kuonyesha amekasirishwa, Esmile akamtazama Mam na kumuuliza kwa upole, sauti ambayo ilionesha kuwa, amekubali yaishe.



‘‘Mam una haraka sana au twende kwanza kwa kina Rahel?”



‘‘Sina haraka kivile, ila Rahel kwani ni lazima tufike kwenu leo?’’



‘‘Ndio Mam, angalau Esmile anywe maji tu’’



“Ah! we nae Rahel una king’ang’anizi sana, haya Esmile twende’’



Kwa kufuata maelekezo ya Rahel, wakawasili hadi nje ya nyumba yao na kusimama, Rahel akashuka na kuwataka nao washuke, hapo ndio pakawa hapatoshi, wakagoma kabisa na kumuahidi watakuja siku nyingine.



Wakamuaga na Esmile wakati anageuza gari, Rahel akamuita Mam na kumwambia ampe namba yake ili wawasiliane, wakaitika wote garini na kuondoka.



Mbele kidogo kabla ya kukatisha kona ya kigogo, Esmile akamuomba Mam ahamie mbele ili waweze kuongea, Mam akamwambia wanaweza kuongea bila hata ya kuwa karibu, maana wapo wawili tu ndani ya gari.



Esmile akapaki gari pembeni na kumuonba Mam dakika 5 za maongezi. Mam akakubali na kumtaka waongee kwa haraka maana muda huu anapaswa kuwa nyumbani akiwasaidia wazee wake.



Akamuomba Mam asogee upande mmoja wa siti yake, kasha nae akailaza siti yake pakawa hakuna kipingamizi chochote kati yao, Esmile akiwa amelaza kiti na kuwa karibu zaidi na Mam, akanza kuongea nae huku akimtazama usoni na Mam akiwa anachezea vidole vyake huku akivitazama, akafunguka;



‘‘Mam ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu tulipoonana kwa mara ya kwanza, nafikiri unaikumbuka siku hiyo ambayo ilitukutanisha mimi nawe? Ni kama jana tu vile…” Mam akatikisa kichwa kukubali na kutokana na kauli ile akapata ujasiri wa kunyanyua sura yake na kumtazama, Esmile akaendelea



“Sikuona umuhimu wowote na siku ile nilikuchukulia kama mtu wa kawaida tu sana, hivyo nilitoa msaada ule kwako kwa kuchukulia wewe ni binadamu mwenzangu tu ambae unastahili kuishi, ndio sababu nikafanya vile pasina kutegemea malipo yeyote toka kwako ama kwa mtu mwingine yeyote, tupo pamoja Mam?” alimuuliza ili tu kumjenga kisaikolojia, Mam akasema

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nakumbuka sana siku ile, naikumbuka vizuri mno na ni siku ambayo sitaisahau katika maisha yangu, na kwa kuwa siku hiyo siwezi kuisahau, ina maana kuwa hata wewe Esmile katu sitakusahau milele, nina mengi sana ya kukwambia tangu tulipo achana…”



“Ok! Ok!japo unasema una mengi ya kuniambia tangu tulipo potezana, hakika nina hamu kubwa mno ya kusikia toka kwako lakini leo naomba unisikilize mie kwanza Mam nifikishe kile ambacho nimeshindwa kukifikisha kwa zaidi ya miaka miwili sasa, Sijui unaniruhusu niendelee?” aliuliza huku akimtazama kwa umakini zaidi a awali



“Yap! Unaweza tu kuendelea Esmile,”







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog