Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

NAUZA BIKIRA YANGU - 5

 





    Simulizi : Nauza Bikira Yangu
    Sehemu Ya Tano (5)




    “Oroo ondokeni hapo, Nendeni Guest”

    Sauti ya askari iliwashtua Tusmo na Rajiv na kuachiana kwa woga kisha wakaingia katika Gari na kurudi nyumbani huku Rajiv akitumia muda mrefu kumshukuru Jose B wa ukweli.Mpaka wanafika

    nje ya nyumba yao walikua wamezungumza mambo mengi huku Jose B akimuahidi Rajiv kumtafutia Fremu ya kufungua Sehemu ya kutengenezea simu na kompyuta kazi ambayo angeingiza kiasi kikubwa cha fedha. Ndani ya wiki moja Jose B na Rajiv walikua marafiki wakubwa sana huku Rjiv akiwa tayari anamiliki ofisi yake ya utengenezaji wa Simu na Compyuta iitwayo COMPUTER MASTER. Wingi wa wateja waliokuwa wakija kupata huduma katika ofisi hiyo ulimfanya Rajiv kufanya kazi mpaka usiku kitendo kilichopelekea Rajiv aamue kumuajiri Jose B ili amsaidie kazi ndogondogo kama ya kufungua na kuhifadhi vifaa vya wateja wake. Hakuna mtu ambaye aliharibikiwa na simu ndani ya Mwanza nzima asiipeleke Dukani kwa Rajiv au Muhindii. Ofisi mbalimbali zilipeleka Kompyuta katika ofisi ya Rajiv na kujikuta akijijengea jina kubwa na kupata kipato kikubwa sana ambacho kilimpelekea kuhama eneo la mabatini na kuhamia Kapripoint eneo la watu wa hai ya juu zaidi. Mapenzi ya Rajiv kwa Tusmo yalikua mara Dufu baada ya kukuta tusmo akiwa bado ni bikira na Upendo ukakomazwa na Kitumbo cha Tusmo kilichoanza kuchomoza Taratibu huku usimbufu wa hapa na pale wa kutaka vitu vichachu ukimkabili rajiv kila mara hali iliypelekea kuamua kum tafutia msaidizi wa ndani kwa ajili ya kumsaidi kazi ndogondogo za pale nyumbani. Miezi ilizidi yoyoma huku hali ya Tusmo ikizidi kunawiri. Tumbo lilizungumza lenyewe hakuna mtu ambaye alitaka kuuliza kuhusu hali ya Tusmo kila aliyekutana nae hakusita kumuita mama kijacho. Rajiv alifurahishwa na maendeleo mazuri ya Mke wake na kila mara muda wa kwenda kliniki ilibidi amuache Jose B ofisini na yeye kwenda na mkewe kliniki.

    ****

    Faida ailiyopata ndani ya miezi minne ilimuweka kileleni na kumuongezea heshima Dunia nzima, Aliheshimika huku akihesabika kuwa Tajiri wa Kwanza Duniani aliye na Fedha zinazoingia bila kutolewa katika Benki. Alkuwa ndiye muhimili mkuu katika benki mbalimbalizilizo Afrika na nchi za kusini mwa Amerika. Kampuni ya Taylor Kurt ilikua busy huku akiongeza wafanyakazi kwa kazi kubwa iliyokuwa ikiendelea. Wakati Taylor Kurt akifurahia Mafanikio muda huo ndio muda ambao Martine Cruez alikua akiumizwa kichwa na utajiri wa Taylor Kurt.

    “Karma sasa inatosha huyu mtu anazidi kuwa Tajiri”

    Martine Cruez alikua akiongea na Karma ndani ya chumba cha siri kilicho ndani ya ofisi yake.

    “Usijali huo utajiri wake tumeujengea juu ya Bonge la Barafu kangazi kinafika muda si mrefu na Barafu itayeyuka na hato uwa yeye tena”

    Karma alitoa jibu huku akiweka pochi yake kwapani na kuinuka kutaka kuondoka.

    “Karma nimekuita hapa tuungumze wewe unaondoka, Nahitaji kujua nini kinaendelea maana sikuelewi”

    Martine Cruez aliongea kwa ukali huku akimtolea macho Karma. Karma alimuangalia Martine Cruez na kuachia Tabasamu, Tabasamu la hasira, Tabasamu lililojaa maswali mengi katika ubongo wa Martine Cruez. Karma alidondosha pochi yake chini. Kisha akavua miwani na kuidondosha chini. Taratibu akavua Saa yake ya mkononi na kuidondosha chini. Akainama na kuvua viatu. Martne Cruez alizidi kumtazama Karma kwa mshangao bila kujua anachofanya. Karma akaanza kuvua nguo yake ya juu na kuacha maziwa yakiwa nje. Akamsogelea Martine Cruez kwa mwendo wa Taratibu alipomfikia Akavua sketi na kubakiwa na chupi pekee. Akapiga hatua akawa karibu kabisa na Martine Cruez kisha akavua na Chupi akabaki kama alivyozaliwa.

    “Unauonaje Mwili wangu?”

    Ni swali toka kwa Karma lililomlemea Martine Cruez na kujikuta akipepesa macho kwa woga.

    “Si nakuuliza unauonaje Mwili wangu”

    Ni swali lililoulizwa kwa mara nyingine tena kwenda kwa kiumbe tajiri na mwenye msimamo Martine Cruez, Swali ambalo alishindwa kulijibu kwa haraka.

    “Ok, ni swali gumu, Unaweza lala nami nikaridhika pasipo kuniandaa?”

    Swali hili lilimfunga mdomo Martine Cruez na kumfanya kuwa bubu akajikuta analijibu kwa kichwa kuashiria kuwa haiwezekani.

    “Ok kwa hiyo unakubali kuwa hata mwanamke awe mzuri vipi hawezi kuridhika pasipo kumuandaa”

    “Yes”

    Martine Cruez alijibu kwa kifupi huku akiangalia chini.

    “Unajua ndio maana mnasalitiwa na wanawake zenu sababu ya haraka zenu, Mnataka kila kitu kifanywe harakaharaka pasipo kuandaa mazingira mazuri ya kufanya mnachohitaji, Taylor Kurt anahitaji kuandaliwa kama mwanamke anavyoandaliwa ili afike kileleni, Niachie nimalize kazi yangu.”

    Karma aliongea kwa upole kisha akarudi alipoacha nguo zake na kuanza kuvaa akaokota pochi yake na saa akaondoka huku akibamiza mlango kwa nguvu na kumuacha Martine Cruez akiwa hoi.

    ****

    Siku zote hakutaka kutoka ndani ya nyumba yakepasipo kwenda moja kwa moja katika chumba cha binti yake wa pekee kumjulia hali, Ni binti ambaye aliyekuwa kabeba Eneo kubwa la furaha yake katika maisha yake. Mke wake aliyekuwa hoi kitandani kwa tatizo la kansa ya kizazi iliyosababisha kuondolewa kwa kizazi chake na kupelekea kushindwa kuwa na uwezo wa kupata mtoto katika maisha yake. Hakuna kitu alichokuwa akikitegemea katika maisha yake kama mtot wake wa pekee. Alifanya kazi kwa bidii huku akihakikisha anasimamia vyema biashara zake ili mwanae aje arithi utajiri wake. Wafanyakazi wapatao ishirini walioajiriwa kwa ajili ya kumuhudumia binti yake. Hakuna mtu aliyeruhusiwa kuwa karibu na binti yake zaidi ya mama yake na yeye pekee. Hata wafanyakazi walikua wakimuhudumia kwa muda maalumu na ni chini ya uangalizi wa kamera za cctv. Huyo alikua ni Angelica binti wa Tajiri mkubwa nchini marekani. Binti ambaye alikua akidekezwa kupita kitu chochote na kila alichohitaji kutoka kwa baba yake kilifanywa kwa usahihi na kwa haraka zaidi. Akwa ni muhitimu wa chuo kikuu cha Havard cha Marekani akiwa na Digrii ya Biashara. Baba yake hakutaka aanze kazi mapema alitaka kumuandalia mazingira mazuri zaidi ya kazi kabla ya kumkabidhi ofisi rasmi. Alitaka kustaafu kwanza na kubaki kama mshauri wa kampuni akimuachia binti yake usukani katika kuendeleza kampuni yake. Taylor Kurt akiwa kabeba ua ridi jekundu ni moja kati ya vitu ambavyo vilikua vikipendwa na Angelica.

    “Good Morning Mrembo wangu”

    Taylor Kurt alimpa binti yake lile ua huku akimbusu, wakati Angelica akiwa kalala kitandani kwake.

    “Thank you Dad, I love you everyday” (Ahasnte baba, Nakupenda sana kila siku”

    Angelica alijibu kwa furaha huku akirudisha busu katika paji la uso la baba yake.

    “Unakumbukakuhusu Tarehe 5 jumatatu ya mwezi ujao.”

    “Yes dad, Nakumbuka”

    “Unakumbuka nini?”

    “Si ndio siku ambayo utanikabidhi kampuni?”

    “Yes nachokupenda kumbukumbu zako ziko vizuri sana, Sawa siku njema wachaniwahi ofisini”

    “Thank you Dad” {Ahasnte Baba}

    Taylor Kurt alitoka na kuelekea katika Gari yake taratibu na kuingia ghafla simu yake ikaanza kuita alipoitazama akakutana na Jina KARMA katika simu yake.

    “Mh kuna tatizo gani tena mbona asubuhi sana”

    Taylor Kurt alizungumza mwenyewe huku akibonyeza kitufe cha kupokelea simu.

    ****

    Siku zote Rajiv alikua akiumiza kichwa jinsi software ya mtandao wa Google inavyofanya kazi, Uwezo wake wa kutafuta kitu kwa haraka na kukileta katika uso wa kompyuta ulizidi kumchanganya akili. Kila siku baada ya muda wa kazi kwisha Rajiv alijifungia ndani ya ofisi yake huku akitumia saa moja kuchunguza uwezo wa vitu mbalimbali vinavyotumia software na kufanya kazi. Kwa kutumia Kapasta za simu mbovu aliweza kuunda kitu ambacho hakujua ni kitu gani kitafuata mwishoni. Kila kifaa alichokua akikiweka katika kifaa kile alikua akikiandika pembeni ili asisahau vifaa alivyotumia kutengenezea. Kila jioni baada ya kazi Rajiv alikua akipenda kupita katika Supermarket kubwa ya mwanadada mjasiria mali aitwae Mwana eid el abri na kununua Aple la kijani kwa ajili ya mkewe.

    “Mke wangu unapenda ma aple”

    Rajiv alikua akimwambia mkewe wakati akimpokea Aple kabla ya chochote wakati anaingia nyumbani.

    “Sio mimi ni mtoto”

    Tusmo alijitetea huku akimbusu mume wake shavuni. Upendo wao ndani ya nyumba ulikua ni wa kupitiliza uliopelekea mpaka mfanyakazi wao wa ndani kuvutiwa nao kwa jinsi walivyokuwa wakipendana.

    “Sasa mume wangu utanipa zawadi gani nikikuzalia mtoto”

    “nitakupa zawadi ya Tofaa la kipekee, Dunia nzima itakua ikitamani kumiliki tofaa hilo na litabadili mfumo wa ukaribu wa dunia kuwa karibu zaidi”

    Rajiv alisimama na kuelekea katika jokofu ndogo pale sebuleni na kutoa maji katika jagi na kumimina kwenye glas akanywa kidogo.

    “Honey naomba maji na mimi”

    “Naona mtoto anataka maji”

    Rajiv alimtania mkewe huku akiwa anampelekea maji pale alipo.

    “Haya kunywa maji mke wangu mpendwa, Si unajua maji ni Afya”

    “Ndio nafahamu Mpenzi”

    “Baba nikuandalie chakula”

    Sauti ya mfanya kazi wao wa ndani iliwashtua na Rajiv akageuka kumuangalia.

    “Oh dada usijali, nitajiwekea mwenyewe wewe nenda kapumzike najua umechoka kwa kazi”

    “Nashukuru Baba usiku mwema”

    Yule mfanyakazi akaondoka na kuwaacha wakiongea wakiendelea na maongezi yao kwa furaha.

    “Baby kesho tutaenda wote clinic?”

    “Mpenzi naomba kesho nisiende ili niweze kwenda kumalizia matayarisho ya zawadi yako si unajua mwezi ujao tu tunategemea mgeni hapa nyumbani”

    “Mh baby hutaki kumsindikiza mgeni stand, kwa hiyo hutompokea”

    “Mpenzi ni kesho tu ila siku nyingine lazima niwe katika mapokezi ya mgeni huyu”

    “nibusu kwanza ndio nikubali”

    “Mmmh mwah”

    “Sawa nimekubali ila usije ukaomba ruhusa nyingine mpaka mgeni aje”

    “Sawa usijali mpenzi wangu”

    ****

    Kwa haraka ya kupokea simu aliyokuwa nayo Taylor Kurt alijikuta akibonyeza kitufe cha kukatia simu badala ya kile cha kupokea simu. Kwa wasiwasi aliokuwa nao kutokana na simu ile alijikuta akijaribu kupiga namba ya Karma na kujikuta akitoa simu sikioni kwa upole, ni jibu alilokutana nalo akifahamishwa kuwa mtumiaji wa namba ile anaongea na simu nyingine. Wakati akitafakari huku macho yake yote mawili yakiwa juu ya simu ile na akili yake ikiwa kwa Karma mara simu inaingia. Ni namba mpya ambayo hakuwahi kuiona katika simu yake, Wazo la kuikata simu ile ili kuruhusu simu ya Karma kuingia kwa urahisi likamjia. Wakati akijiandaa kukata alijikuta akisitisha zoezi la kukata simu na kuamua kupokea simu ile.

    “Karma anaongea tunaweza onana muda huu”

    “Ndio bila shaka”

    “Basi tukutane Breakfast point mmuda huu”

    Karma aliongea kwa haraka kasha simu ikakatwa, Kwa mwendo wa kasi Taylor Kurt alikua akiendesha gari lake aina ya Cahaverlote kuelekea kwenye mgahawa maarufu kwa ajili ya kifungua kinywa wa Breakfast point. Akitafuta eneo zuri la kupaki gari Taylor Kurt aliweka gari lake katika maegesho kwa upande wa nyuma na kuingilia katika mlango wa watu maarufu wa mgahawa huo na kutokea eneo maalumu la hadhi ya juu na kukaa. Muhudumu aliyevalia mavazi meupe na kuonyesha usafi wake alikua mbele ya Taylor Kurt kwa unyenyekevu akimpa menu ili achague kifungua kinywa. Taylor Kurt hakuna alichokua akihitaji kwa wakati huo zaidi ya kumuona Karma na kujua ni kitu gani cha muhimu kiasi hicho kilichopelekea wao kukutana haraka zaidi.

    “Coffee please” {Kahawa tafadhali}

    Taylor Kurt aliagiza kahawa pasipo kuangalia kitabu cha mpangilio wa vinavyopatikana ndani ya eneo hilo. Muhudumu akaondoka na kwenda kumuandalia Taylor Kurt Kahawa. Karma akiingia kwa mwendo wa haraka huku akiwa kashika karatasi nyeupe mkononi bila kupoteza muda akakaa katika kiti na kuanza mazungumzo.

    “mzigo unaokwenda Japani umekamilika ila Fomu ya kumiliki mzigo haukuweka sahihi yako na inapaswa mzigo kuondoka leo au kesho”

    Karma aliongea huku akiweka karatasi vizuri ili Taylor Kurt aweze kuweka sahihi yake . Taylor Kurt akaweka sahihi na kumakbidhi Karma ile karatasi Karma akaamka na kutaka kuondoka.

    “Samahani naweza pata dakika tano ya kuzungumza na wewe?”

    Taylor Kurt alimwambia Karma aliyekuwa tayari amekwisha amka na kuanza safari ya kutoka ndani ya eneo lile.

    “Ok usijali waweza ongea nami kwa muda wowote unaohitaji”

    Karma alijibu na kuketi katika kiti huku akimuangalia muhudumu aliyekua akiandaa kahawa juu ya ile meza.

    “Karma nina binti yangu ningependa awe na uwezo kama wewe maana nategemea kumkabidhi kampuni jumatatu ya kwanza ya mwezi ujao mimi nistaafu nibaki kuwa mshauri tu”

    Karma alikaa vizuri baada ya kusikia kile alichoambiwa toka kwa Taylor Kurt

    “Je alishawahi kufanya biashara awali”

    “Hapana ndio kamaliza chuo miezi sita iliyopita”

    “njia ngumu ndiyo ifikapo katika mafanikio ni vyema ukampa mtihani kwanza”

    “Mtihani gani?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Karma alifikiria kwa sekunde kadhaa kasha akaangalia kikombe chenye kahawa kilicho juu ya meza alichowekewa Taylor Kurt

    “Mbona hunywi kahawa”

    “Sijisikii kunywa”

    “Je unafahamu kahawa hiyo imetoka wapi”

    “Ndio hii ni kahawa Toka Tanzania eneo moja nasikia linaitwa Meru”

    “Ooh je unajua imefikaje hapa?”

    “sifahamu ila itakua kuna kampuni ndio inaleta hapa”

    “Mmh laiti ungejua wakulima wanaolima kahawa hiyo hutumia jembe la mkono, Hufanya palizi katika mazingira magumu, Uvunwaji wake hufanywa kwa mikono kwa kuchuma mojamoja na hata soko lake halilingani na kazi wanayofanya katika kuhakikisha inakuwa bora na wewe leo imekufikia wanaamini wamepanda kilicho bora na wewe unakifurahia ila cha kushangaza hufikirii hata kuinywa, hivyo ndivyo siku zote huwa. Ukijua ugumu wa upatikanaji wa kitu ulichonacho utakitunza”

    Taylor Kurt alijikuta akinyanyua kile kikombe chenye kahawa na kunywa taratibu.

    “Sasa nitafanyaje ili ajue thamani ya kampuni”

    “Mpeleke akaone mazingira ya soko, milima na mabonde ya soko letu lilipo akirudi atathamini kila shilingi itakayoingia.”

    “Unamaanisha aende Japan na mzigo”

    “Haswaa”

    “hiyo itakua ngumu, Angelica hawezi safari katika mfumo huo”

    “Usijali huo ulikua ni ushauri usio na malipo japo ulipaswa ulipie, Mapenzi ya kuku kwa yai ndio yamesababisha yai kupasuka kwa urahisi. Dunia ni duara wewe utapita na utamuacha fikiri utamuacha katika mazingira gani”

    Kauli ya Karma ilimlainisha Taylor Kurt na kukubali Angelica kwenda na mzigo Japan kwa ajili ya kwenda kujifunza biashara inavyofanyika huko sokoni.

    ****

    Feb 1989. Kilikua ni kipindi kigumu sana kwa Rais wa Marekan Russ Pickett

    , Tuhuma zilizokuwa zikipelekwa moja kwa moja nan chi mbalimbali juu ya marekani kuhusika katika usambazaji wa dawa za kulevya katika nchi zao. Suala hilo liliamsha hisia za wananchi wa marekani kutokana na unyanyasaji wanaokabiliana nao wanaposafiri kwenda nchi nyingine. Upekuzi wa hali ya juu unaofanywa dhidi yao katika viwanja vya ndege mbalimbali waliona kama ni udhalilishaji huku lawama nyinig zikipelekwa kwa Rais wao. Tuhuma za Rais kushirikiana na matajiri wan chi hiyo katika mpango wad aw haramu hizo zilizidi kuchafua ikulu ya marekani na Rais wao pia. Kila kukicha vikao vya vitengo mbalimbali vya usalama wa marekani vilikua vikihangaika kuweza kutatua tatizo. Misaada iliyokua ikitolewa na shirika la watu wa marekani liitwalo American Aid ilikua ikikataliwa nan chi mbalimbali katika kuonyesha msimamo wao katika lile wanalolizungumzia. Zawadi nono ikawa imetangazwa kwa yeyote atakayepata taarifa juu ya Raia yeyote wa Marekani anayejihusisha na uuzwaji wa Dawa za kulevya katika nchi yeyote nje ya amerika. Mpango wa kurudisha heshima na imani ya Marekani kwa nchi mbalimbali ulikua ukipangwa kila kukicha huku shughuli ya kutafuta pa kujifutia madoa ikifanyika kwa umakini mkubwa sana.

    “Napendekeza Kazi ya ukaguzi ifanyike katika nchi zenye malalamiko, Naona FBI wafanye kazi hiyo”

    Alitoa maelekezo Mkuu wa kitengo cha usalama wa Marekani ndugu Berno mckath wakati wa kikao cha viongozi wa ngazi ya juu wa usalama Marekani.

    “mimi napendekeza tuipe kazi na kampuni nyingine binafsi kwa ajili ya kazi hii”

    Rodric vidic Afisa usalama wa jimbo la Texas alitoa wazo lake lililopita moja kwa moja na Karata ikadondokea katika kampuni ya Left Eyes investigative ya nchini urusi. Baada ya siku mbili mkataba wa kazi ulikua umekwisha sainiwa na Mpelelezi wa kimataifa Modach Vox alikua kakabidhiwa kazi hiyo na Marekani ilihitaji ripoti haraka iwezekanavyo.

    Modach akiwa katika ndege ya Gulf Air akitokea urusi kuelekea Amerika huko ndipo alipoona akaanzie kazi yake. Safari yake iliishia katika uwanja wa kimataifa wa J.F Kenedy na kupokelewa na hali ya hewa yenye utulivu ndani ya nchi ya marekani. Haraka akaingia katika Tax na safari ikaishia ndani ya Hotel ya Hilton Palace ndani ya chumba namba 1234Qb,. Mo kwa tahadhari alianza kukagua chumba kila mahali kwa ajili ya usalama wake. Camera maalumu ya Stv inayorekodi matukio yote ndani ya chumba kile ilikua imefungwa kwa juu, Kwa kutumia simu yake alipiga picha kile chumba, Haraka haraka akawasha kompyuta yake na kutoa printa ndogo kwenye begi lake na kuprint ile picha akaigundisha mbele ya kamera ile ikiitazama ile picha. Tayari alikua keshamdanganya mtu anayetazama usalama wa hoteli ile kupitia ile kamera. Alikaa juu ya kitanda na kuanza kupanga mipango yake. Ghafla mlango ukaanza kugongwa kwa fujo huku mgongaji akiwa na haraka ya kufunguliwa mlango ule. Kama umeme bastola yake ikiwa mkonnoni akinyatia mlango taratibu ili kukabiliana na yeyote atakayejaribu kufanya chochote dhidi yake. Kasi ya kugongwa kwa mlango ilizidi na kufanya Rodric kukaa sawa huku akitumia mkono mmoja kwa tahadhari kufungua mlango.

    ****

    Hakuna kitu ambacho hakutaka kukisikia katika maisha yake kama mpango wake wa kuimaliza afrika kukwama. Kitendo cha kukamatwa kwa kontena la pombe kali zilizo katika paketi kilimchanganya sana. Hakutaka pombe zile zifike katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali ya Tanzania kwani kitendo hicho kinaweza kukwamisha kila kitu katika mipango yake. Ndege yake kubwa aina ya Boeng C 456DD ilikua ikikata mawingu kuutafuta ukanda wa anga la Afrika Mashariki. Ndani ya Masaa matatu tayari Camillah alikua akiikanyaga Ardhi ya uwanja wa kimataifa wa Jk Nyerere. Vijana wane waliokua wamevalia suti nyeusi na miwani za kuzuia Jua zikiwa zimeyaziba macho yao vyema. Kibao kilichoandikwa jina la Camillah kilitosha kumuelekeza Camillah na kuwafuata safari ikakomea ndani ya Benzi ya Rangi ya Njano na Safari ikaanza kwa mwendo wa taratibu. Kila sekunde iliyokua ikisogea kuikaribia Dakika ndivyo Tairi za Gari zilikua zikiongeza kasi na kufanya gari kuyapita magari kama yamesimama. Safari ikaishia ndani ya ukuta mrefu wa Godown la American Bussiness na kuongozwa moja kwa moja mpak kwenye chumba kilichojengwa chini ya Jengo dogo ambalo hutumika kama ofisi ya Jengo hilo. Wazee wawili waliokua wamekaa katika meza ya Duara macho yao yalikua yakimtizama Bibi Camillah ambaye alikua akiingia kwa mwendo wa haraka huku akiwa kafuatana na vijana wawili waliotoka kumpokea uwanja wa ndege. Bi. Camillah akiwa na haraka akakaa katika kiti huku akihitaji kusikia kitu mipango ya kuzuia hatari yeyote isije tokea dhiid ya mpango wake. Mzee mmoja akiwaashiria wale vijana watoke nje ndani ya Chumba wakabaki watatu tu. Kimya kilitawala kila mmmoja akisubiri mwenzake aanze kuzungumza.

    “Mmefikia wapi”

    Bi. Camillah aliuliza swali huku akimtazama kila mmoja kwa zamu, Swali ambalo halikujibiwa kwa haraka kitendo kilichofanya Bi. Camillah kupandwa na jazba.

    “Coren wewe nakuamini sana mbona leo unanishangaza”

    Bi. Camillah alimsemesha Coren mzee mmoja kati ya wazee wale wawili pale ndani.

    “Yes Madam suala liko pabaya sana sample ya pombe inatarajiwa kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Jumatatu na leo ni jumamosi. Tumejaribu kumshawishi mkemia mkuu wala hataki kutusikiliza”

    Coren aliongea kwa masikitiko huku kainamisha kichwa chini.

    “Mmh Kwani huyo Mkemia analipwa pesa ngapi kama mshahara wake”

    “Haizidi Dola elfu mbili kwa pesa ya Tanzania”

    Mzee Kanote alijibu huku akibonyeza bonyeza simu yake.

    “Anaishi wapi”

    “Anaishi eneo moja la viongozi linaitwa masaki”

    “Kaoa”

    “Ndio na ana mtoto mmoja tu”

    “Anaishi na Mkewe”

    “Hapana, Tumesikia walishaachana miaka mingi iliyopita”

    “Naweza pata picha yake”

    “Ndio bila shaka”

    “Nahitaji haraka, Sasa hivi”

    Coren aliinuka na kuingia chumba cha pili ndani ya ile ofisi na kutoka na Picha kubwa na kumkabidhi Bi. Camillah, Akaitazama na kutabasamu.



    **** http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    FBI walikua wakihangaika usiku na mchana kutafuta chanzo cha usambazwaji wa dawa za kulivya aina ya HD ambazo nchi za nje ya Marekani . Msukumo wa Russ Pickett Rais wa marekani kuhimiza Vyombo vya usalama vya nchi hiyo kuhakikisha wanaidhihirisha dunia kuwa Serikali haihusiki na usambazwaji wa Dawa za kulevya katika nchi nyingine ulisababisha maofisa wa usalama wa nchi hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kuitoa nchi yao katika fikra hizo. Maafisa watatu wa FBI Solomon, Abra na Coso walikua wamekaa katika Chumba namba 89 ndani ya Hoteli ya Crane view. Juu ya meza kukiwa na Ramani kubwa ya Dunia huku wakiitazama kwa makini zaidi.

    “Mimi napendekeza Tuanzie na Pakistan maana hii nchi ndiyo inasambaza dawa za kulevya sana”

    Abra alitoa wazo ambalo halikupata sapoti lililosababisha kimya kuchukua nafasi huku macho yakiwa bado juu ya Ramani ile

    “Mnaonaje Tukaenda China maana China wanasafirisha mizigo mingi kwenda Afrika na Nchi zinazoathiriwa na Dawa za Kulevya zaidi ni Afrika hapo tutapata pa kuanzia na pia tutaweza kujua mtandao mzima wa Genge la wauza dawa za kulevya”

    Coso akatoa wazo lake ambalo nalo lilipokewa na ukimya, ukimya ambao uliashiria wazo hilo halikuwa na mshiko katika eneo hilo kwa wakati huo.

    “Sikilizeni mimi akili yangu inanituma niende korea japo sijui nini kinanifanya niamini huko ndipo kuna suluhisho, Sasa mapendekezo yangu kila mmoja wetu aende kule alipopendekeza na atakayeona njia tujulishane tumpe nguvu. Cha msingi ni mafanikio haraka iwezekanavyo.”

    Solomon alizungumza huku akikunja ile Ramani na kuiweka katika Begi. Akabeba Begi lake mgongoni na kuondoka bila kuaga. Coso kwa Tabasamu akampiga kibao kidogo Abra na kumvuta mkono kumuamsha pale alipokaa wakaanza kukusanya vifaa vyao kasha wakatoka kwa pamoja mpaka nje ya Jengo lile. Huku wakiwa wamekubaliana na Solomon kuwa Coso aende China, Abra aende Pakistan na yeye ataenda Korea. Yote ikiwa kwa Lengo moja kuitoa nchi ya marekani katika hatia ya usambazaji wa Dawa za kulevya.

    ****

    Jose B wa Ukweli hakuamini kile ambacho alikua akikiona mbele ya macho yake. Hakuamini kama kifaa kile kilitengenezwa na Rafiki yake wa kihindi, kitu alichoamini ni wazungu pekee ndio wenye akili ya kuunda kitu na kufanya kazi. Katika kumbukumbu yake hakuweza kukumbuka kama alishawahi kuona kifaa kama kile katika maisha yake mpaka wakati ule. Ni simu ambayo ilikua na uwezo wa ajabu iliyoundwa na Rajiv. Ni simu yenye Sensa zaidi ya tisa ambayo inaweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Kitendo cha simu ile kuzima tv kuwasha AC, kuandika ujumbe mfupi kwa njia ya sauti kilimchanganya akili zaidi. Kifaa hicho ndicho kilimchanganya Jose B wa Ukweli na kumuona Rajiv kama mtu ambaye hakustahili kuishi katika nchi ya Kiafrika.

    “Sasa hiyo simu unaifanyia nini”

    Jose B alimuuliza Rajiv swali ambalo alikua na shauku ya kupata jibu haraka zaidi.

    “Nina plan ya kutafuta kampuni inayotengeneza simu na kuuza wazo hili ndio maana kila kifaa nilichotumia nimekiandika ili waweze kuunda simu nyingi zaidi”

    “Mh hiyo simu itaitwa nini sasa”

    “Hii ni zawadi, Zawadi kwa ajili ya mke wangu mpendwa, hii simu itaitwa Tunda, Tunda ambalo Mke wangu analipenda sana, Na naamini hata motto wangu aliye ndani ya Tumbo la mke wangu atakua analipenda Tunda hilo”

    Rajiv aliongea huku akimuangalia Jose B

    “Tunda Ga ni hilo?”

    “Hii simju itaitwa Apple na kampuni itakayonunua itabidi isibadili jina la simu hii naamini italeta mapinduzi makubwa ya kitekinolojia katika miaka ijayo. Nataka nikumbukwe na Vizazi vijavyo.



    ****

    Akili yake ikifanya kazi kwa haraka mkono mmoja ukiwa umekamatia vyema bastola yake, Alitanguliza kiatu cha mguu wa kushoto kutoka nje huku mwili ukiwa bado ndani ili kusikilizia shambulio lolote hakuhisi hatari zaidi ya kusikia sauti ya kilevi ikizungumza. Macho yake yakakutana na kijana mwenye sura ya upole japo kwa wakati huo alikua kazidiwa na kilevi huku pembeni yake akiwa kamkamata vyema mwanamke aliyeonekana kama ni mpenzi wake.

    “We nani mbona upo kwenye Room yetu”

    ******

    Modach alijibu kwa upole kitendo kilichopokelewa na Yule kijana kwa upole na kupepesa macho na kujikuta akinyoosha mkono kugusa jicho ishara ya utukufu kwa watu Fulani kitendo ambacho kilimshtua zaidi Modach na kujikuta akimuangalia Yule kijana kwa wasiwasi, Akimtizama Yule kijana mpaka alipotokomea ndani ya chumba cha tatu toka katika chumba chake, Modach alirudi ndani haraka na kuwasha kompyuta mpakato yake na kuanza kufungua kitu haraka haraka na kuandika vitu Fulani. Picha nyingi zikatokea mbele ya ie kompyuta za watu ambao wameshika jicho ishara aliyoonyeshwa na Yule kijana. Macho ya Modach yakatembea taratibu katika picha moja baada ya nyingine ndipo yalipokomea katika picha moja na kuitizama kwa umakini zaidi. Akitumia eneo la kuvutia picha kwa ukaribu na kuivuta picha ndipo alipopatwa na mshtuko zaidi. DON LEWIC jina lililopandisha joto kali katika mwili wake. Gaidi anayetafutwa kwa udi na uvumba na serikali ya Marekani. Picha iliyo mbele yake ilikua sawasawa na mtu aliyemuona muda mfupi uliopita. Hakuamini kama gaidi kama Yule atakua ndani ya marekani akila maisha kiasi kile pasipo kugundulika na mtu yeyote. Mawazo ya wasambazaji wa dawa za kulevya kuwa magaidi yalimsonga na kujikuta akifikiri tayari amegundulika ameingia marekani kuwapeleleza.

    Mawazo ya kuhama hotel ndiyo yalimjia na kuanza kukusanya kilicho chake. Maamuzi ya kuwasiliana na mkuu wake wa kazi ili kumpa taarifa ya kufika kwake na alichokutana nacho ilia pate ushauri. Kwa kutumia tablet yake akaanza kubonyeza namba Fulani kupitia mtandao wa viber na tayari Colins Hawk alikua hewani akizungumza na modach.

    “Nini kipya huko?”

    “Boss nimekutana na kesi nyingine huku tofauti na nilichokifuata”

    Modach aliongea kwa sauti ya chini kama vile hataki mtu mwingine amsikie.

    “Kesi gani hiyo?”

    “Unakumbuka kundi la Gang Mafia”

    “Ndio nakumbuka si wale waliomuua Ronald kwa kumkata kiungo kimoja kimoja na wakawatumia America cd ya video”

    “Yes hao hao”

    “Wamefanyaje sasa?”

    “Unamkumbuka Yule aliyekua akifanya ule unyama kwenye ile video”

    “Yes si marehemu Don lewic”

    “Yes sasa huyo Gaidi hajafa yupo hai”

    “Wacha maneno wewe Don alikufa katika ajali ya ndege na Dunia nzima inatambua hilo”

    “Boss huwezi amini nimemuona dakika saba zilizopita na kalala chumba cha tatu toka nilipo mimi”

    “My God, Sasa ngoja niwasiliane na FBI ili aweze kukamatwa huyo ni Gaidi namba mbili anayetafutwa na America”

    “Ah boss niachie hiyo kazzi utaharibu kazi yangu inavyoonekana amekuja kunifuatilia tu”

    “Sawa ila kuwa muangalifu na nijulishe kwa kila kitu asije akakuzidi ujanja kumbuka huyo ni mtu hatari sana si wa kucheza nae”

    “Sawa Mkuu”

    Modach akakata simu na kujilaza kitandani mipango ya kuondoka katika ile hoteli ikatoweka na sasa akawa na mikakati mipya. Kuhakikisha anamkamata Don na kumkabidhi kwa serikali ya Amerika ndipo aendelee na kazi aliyotumwa nan chi yake.

    **** http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kucha zikiwa zimetengenezwa vizuri sana na kufanya miguu yake kuongezeka thamani kwa kupambwa kwa kucha zenye rangi ya kuvutia. Huku viatu vilivyo wazi vikiwa na kamba iliyoshikilia miguu yenye weupe wa kizungu, Gauni fupi lililoishia juu ya magoti liliruhusu mapaja malaini nay a kuvutia yaweze kuonekana vyema huku gauni likiwa limemshika vizuri na kuruhusu chuchu zake kuchomoza vyema kama mbalamwezi ya magharibi. Nywele ndefu zilizolala mgongoni zinazoashiria matunzo mazuri zilizobebwa na kichwa kidogo cha mviringo chenye sura ya kuvutia na macho ya rangi ya paka huku midomo ikiwa imepakwa rangi nyekundu yam domo yenye kung’aa. Akiwa mwenye Furaha nje ya Uwanja mdogo wa ndege wa Oklahom tayari kwa safari ya kuelekea Japan. Akipokea maelekezo toka kwa Karma Angelica alisikiliza kwa makini kila alichokua akiambiwa na Karma. Bahasha ya Khaki ndiyo ilikua ya mwisho kupokea toka kwa Karma na kumruhusu kuondoka Angelica akimpungia mkono baba yake alielekea katika ndege tayari kwa kuanza safari ya kuelekea Japan kwa ajili ya kusindikiza mzigo na kuukabidhi kwa mteja huku akitegemea kukutana na kontena la mzigo atakapofika japan. Rubani wa ndege aliruhusu tairi za ndege kutembea na kutafuta kasi ya kuuacha uwanja baada ya dakika kadhaa tayari tairi zilikua zikiingia ndani na ndege ilikua ikitafuta usawa wa anga na kutulia safari ilikua imekwisha changanya. Huduma ndani ya ndege ilikua ya hali ya juu sana kwa Angelica wahudumu waliokuwa wakimsikiliza kwa kila kitu walikua wakimuhudumia kwa hadhi ya juu kulingana na heshima na utajiri wa baba yake nchini Marekani. Saa nne zilikua zimekwisha pita Angelica alikua kalala kwenye siti yake iliyokua imekunjuliwa na kuwa kama kitanda. Kengele ya hatari ilianza kulia katika kichwa cha Rubani taa ya hatari ilikua inawaka katika dashboard ya ndege, Ishara ya tatizo katika ndege ile ilionekana muungurumo wa ndege ukabadilika ukiambatana na mtingishiko mkubwa wa ndege ile. Abiria walishtushwa na mtingisiko wa ndege ile na kushtuka. Angelica aliamka na kushangazwa na hali aliyoiona katika ndege ile. Abiria walikua wakipiga kelele hovyo huku wengine wakivaa parachute kwa kusubiri lolote litakalotokea. Hofu ikamtanda huku harufu ya kifo ikipuliza katika pua ya kila abiria ndani ya ndege ile. Marubani wa ndege ile walikua busy kuwasiliana na viwanja vya ndege vilivyo karibu ili kuweza kuruhusiwa kutua huku ndege ikipoteza muelekeo na mwishowe mawasiliano yakakatika. Sauti ya muhudumu wa ndege ile kuwataka abiria kuvaa parachute ndiyo iliwakatisha tama abiria wote huku Angelica akilia kwa uchungu, Hakuamini kama anauacha utajiri wa baba yake na hakuamini kama mtihani wa biashara aliopewa na baba yake anaufeli kabla ya kukamilisha kuufanya tena anafeli akiwa ndani ya ndege huku akifikiri mwili wake utatolewa ukiwa katika hali gani ndani ya ndege ile, ukiwa majivu au ukiwa umepondwa pondwa na vyuma vya ndege ile. Mwili kukosa nguvu na miguu kulegea ndicho kilifuata na usingizi usio na fahamu ya chochote ukamkumba, Angelica alikua keshazimia siku nyingi.

    ****

    Rajiv alikua keshakamilisha kuunda simu aliyoipa jina la Aple na sasa alikua akifikiri ni njia gani ya kuweza kuuza wazo la simu hiyo na kuweza kufanyiwa kazi haraka. Kampuni pekee ya kukuza bidhaa zilizobuniwa na wabunifu wadogo na kuwakutanisha na makampuni makubwa kampuni ya Ajax tecn ndiyo aliyokua akiifikiria wakati wote. Kikwazo alichokua akikutana nacho katika kampuni hiyo ni kuwa mmiliki wa kampuni hiyo ni muhindi wa dini ya Wa hindu. Taarifa yake kuasi dini hiyo ilikua ipo katika kampuni hiyo hicho ndicho kitu ambacho kilimkosesha nguvu Rajiv na kujikuta akiweka simu ile ndani pasipo kufanya lolote.

    “Mume wangu mbona siku hizi mbili umekua mpole sana, Kama una mawazo hivi nini tatizo”

    Tusmo alimuuliza Rajiv swali ambalo lilimvunja nguvu Rajiv

    “Mke wangu nafikiria mahali pa kuuzia ile Apple niliyounda na kampuni ambayo nilifikiri inaweza nisaidia kukutana na kampuni kubwa duniani haiwezi nisaidia sababu mmiliki ni muhindi”

    “Usijali mume wangu nakushauri we tulia utapata mteja tu”

    “Sawa ila kama ikitokea sijaiuza basi atauza mtoto wetu na password ni Tufaa, Anaweza kuzima system ya simu hii kwa password hiyo na iwapo akiiweka katika engine yake ya software inazima simu zote zitakazotengenezwa kwa mfumo huu kwa hiyo hakuna anayeweza kumdhulumu”

    “Lakini mume wangu kwanini usimtumie Jose B maana yeye anajuana na watu wengi sana.”

    “Yes wazo zuri sana, Tena ngoja nimpigie simu aje hapa tuzungumze hilo suala”

    Rajiv akampigia Jose B, Baada ya muda Jose B wa ukweli alikua pale na wakaanza mazungumzo.

    “Jose unakumbuka ile simu niliyoiunda?”

    “Ndio naikumbuka”

    “Ok nataka unisaidie kutafuta mteja atakayeweza kununua mchoro wa simu hiyo ili waunde nyingi”

    “Kwani wewe unataka kuuza kwa nani sasa”

    “Sina pa kuuzia ndio maana nimekushirikisha sababu wewe ni mwenyeji sana”

    “Ah hapa Mwanza hiyo dili haiwezi faa hapa labda dili ya sangara mimi napendekeza tuipeleke Dar hii Dili”

    “Wazo lako ni zuri sasa mimi siwezi kwenda Dar si unaona hali ya shemeji yako unaonaje nikakupatia nauli ukaenda kutafuta kampuni ya kuwauzia”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sawa mimi niko tayari maana jiji la Dar nalijua juu chini nitaingia kila kampuni”

    Jose B alijinadi kwa Rajiv, Wakakubaliana Rajiv akampatia pesa ya kutosha pamoja na mswada wa maelezo ya mchoro wa simu hiyo pamoja jinsi inavyofanya kazi, Siku ya pili Jose B alikua ndani ya basi la BM Safari tayari safari ya kwenda jijini Dar ilikua imeanza.

    ****

    Hali ilikua ya baridi sana, kila mtu alikua kavaa koti la kuzuia baridi, Barafu zilikua zimetanda kila sehemu, Ulikua ni msimu wa baridi katika nchi ya Sweden. Ni ndani ya Uwanja wa ndege wa Stockholm wafanyakazi wa uwanja huo walikua wamezunguka ndege iliyokua imetua muda mfupi uliopita. Wafanyakazi wa jeshi la zima moto la nchi hiyo walikua karibu kabisa na ndege hiyo huku wakiwa na vifaa vyao tayari kwa lolote litakalotokea, Abiria waliokuwa wakibadili ndege hawakua mbali na tukio hilo walikua karibu wakijaribu kuangalia kilichotokea eneo hilo. Ni ndege ndogo iliyokua ikitokea marekani na kupoteza muelekeo ilikua imefanikiwa kutua katika uwanja huo kwa mafanikio pasipo kuleta athari yeyote. Waokoaji walikua watoa abiria katika ndege ile na kuwapatia huduma ya kwanza. Solomon mpelelezi maarufu wa kimarekani kutoka FBI alikua ameshuka katika ndege na alikua akisubiri kubadili ndege inayoelekea Korea alipokua akienda kufanya kazi ya kutafuta wasambazaji wa dawa za kulevya ili kuitoa hatiani nchi yake ya Marekani. Tukio alilokutana nalo pale uwanja wa ndege lilimvutia na kujikuta akisogea karibu na kutaka kujua ni kitu gani kimetokea. Taarifa ya ndege ile kutokea Marekani na ilikua ikielekea Japan zilimvutia na kutaka kujua Kila abiria aliyekua ndani ya ndege ile. Uhusiano mbaya wa Marekani na japan kwa kipindi hicho ndio ulimfanya Solomon kushangazwa na safari ya ndege ile kwenda japan tena ndege ya moja kwa moja toka Amerika pasipo kutua uwanja wowote wa ndege. Angelica Taylor Kurt ndilo jina lililomshtua Solomon na kujikuta akitaka kujua mengi zaidi kuhusiana na abiria huyo ambaye kwa wakati huo alikua akipatiwa huduma ya kwanza.

    “Samahani naweza ongea na huyo binti?”

    Solomon alikua akiongea na muhudumu aliyekua akimpa Angelica huduma ya kwanza

    “Sory haiwezekani, Kwanza haturuhusu watu kuja eneo hili wewe ni nani”

    Yule muhudumu alimjibu Solomon kwa ukali na kuendelea kutoa huduma kwa Angelica huku akiwa kimya akimshangaa Solomon. Solomon akatoa kitambulisho kilichomtambulisha kama FBI toka America Yule muhudumu akatoa ushirikiano wa kutosha.

    “Ok ongea nae, Samahani kwa usumbufu”

    Solomon alimuangalia Angelica aliyevimba macho kwa kulia, Kisha akatabasamu kumuandaa Angelica vizuri kisaikolojia.

    “Hujambo Angelica”

    “Sijambo, Umenijuaje?”

    Angelica Aliuliza kwa Mshangao

    “Usijali, Baba yako ni mtu maarufu sana America kwahiyo usishangae wewe kufahamika katika nchi yeyote”

    Kauli ile ilimfurahisha Angelica na kumfanya akae vizuri huku akimuangalia Solomon machoni.

    “Ulikua unaelekea Japan kufanya nini?”

    “Umejuaje nilikua naenda Japan”

    Angelica hakupenda maswali, Alishangazwa na mtu aliyekua akimuuliza maswali alionekana kumjua zaidi.

    “Oh, umependeza sana Angelica, Wewe ni mrembo sana”

    Solomon alimchombeza Angelica kwa kumsifia alishagundua Angelica anapenda sana sifa kitendo kilichojenga tabasamu katika sura ya Angelica.

    “Nashukuru sana”

    “Unaonekana kama Malkia vile”

    Solomon aliendelea kumchombeza ili kumuweka sawa aweze kujibu maswali yake

    “Nashukuru sana kwa kugundua kupendeza kwangu”

    “Ulikua unaenda Japan kufanya nini maana waandishi wa habari wangekusumbua sana kwa uzuri wako”

    “Mmh ninaenda kusindikiza mzigo wa kampuni ya baba”

    “Oh sawa, kwani huo mzigo unakutana nao wapi ili nikufundishe njia za kuwakwepa waandishi wa habari wasikusimbue mrembo wewe”

    “Nakutana nao TOKYO tayari utakua umepakiwa katika gari kwa ajili ya kuelekea kwa mteja”

    “Aah Tokyo si shida sana kama KAWASAKI kwani mzigo unaelekea katika kampuni gani?”

    “Ni kampuni ya ZATRA, mmiliki anaitwa INAMOTO YANG”

    “Kwani ulishawahi kufika Japani hapo awali?”

    Kabla Angelica hajajibu muhudumu wa uwanja ule alifika na kumchukua Angelica na kumpeleka kwenye ndege nyingine ambayo alipaswa kupanda na kuendelea na safari yake, Solomon alibaki na swali lake lisilokuwa na jibu na Safari ya kuelekea Korea akaona haina maana tayari alikua na walakini juu ya mtoto wa Taylor Kurt anachofuata Japan. Wasiwasi wa mmiliki wa Kampuni ya ZATRA Mr. Inamoto Yang kushirikiana na Taylor Kurt katika biashara haramu ulimfanya kuhairisha safari ya Korea na uelekeo wake ukaelekea Japan kwenda kumpeleleza Angelica na kuangalia ni mzigo gani alikua akiupokea na kuupeleka kampuni ya Zatra.

    ****

    Wakati ndege iliyombeba Angelica ikiwa inaacha Ardhi ya Oklahom tayari Karma alikua akielekea upande wa pili kwa ajili ya kupanda ndege kuelekea Japan kwa ndege nyingine. Lengo likiwa ni kumfuatilia Angelica ili asikwame sehemu yeyote. Kitendo cha Ndege iliyombeba Angelica kutua Stockholm kilimshtua sana Karma na kujikuta akifikiri tatizo litakua limetokea. Hapo ndipo aliposogea na macho yake yakagongana na Angelica akiwa anazungumza na Solomon. Tukio la Solomon kumuonyesha Yule Muhudumu kitambulisho cha FBI kilishuhudiwa na Karma na kujikuta akiishiwa na nguvu na kuona mipango yake inaelekea kufeli muda si mrefu. Wazo la kutaka kumpigia simu Martin Cruez na kumueleza tatizo liligonga kuta za ubongo wake. Simu ikiwa mkononi huku akibonyeza namba fulamni mara akashuhudia Angelica akichukuliwa na Muhudumu wa ule uwanja na kupelekwa katika ndege tena ndege ileile ambayo alitarajia kusafiri nayo kuelekea Japan. Karma alishusha pumzi na kuondoka kwa mwendo wa Taratibu na kupotelea katikati ya watu huku akielekea sehemu ya kukagulia tiketi kwa mara ya pili kabla ya kuelekea katika ile ndege. Akiwa katika foleni macho yake yakakutana na sura ya Solomon alikua akibadili tiketi ili aweze kusafiri na ndege ile aliyopanda Angelica.

    “Shit huyu hanijui mimi ni nani?”

    Karma aliongea nwenyewe na kutoka katika mstari na kuelekea upande wa pili wenye ofisi nyingi zilizopangana na kuingia ofisi moja.

    “Habari”

    Karmaalimsalimia mwanamama wa makamo aliyekua amekaa kwenye kiti mbele yake kukiwa na kompyuta

    “Salama naweza kukuhudumia kama hutojali”

    “Nashukuru, Naweza pata ndege ya kukodi inayokwenda kasi zaidi”

    “Ndio inapatikana ila ni gharama kidogo”

    “Usijali kuhusu fedha nataka niende Japan haraka”

    “Sawa unaweza kulipia ukaondoka baada ya dakika ishirini”

    “Sawa naweza lipia kwa hundi”

    “Inawezekana”

    Karma akatoa kitabu cha hundi na kuandika kiasi cha fedha kilichohitajika, baada ya kukamilisha taratibu ndani ya dakika ishirini alikua ndani ya ndege na safari ilikua imekwisha anza



    ****

    ****



    Kwa ujira wa Dola elfu kumi Mzee kamba ndefu alikua kakubaliana na dili la kubadilishwa sura kwa ajili ya kufanya kazi atakayoelekezwa kufanya. Uhakika wa maisha yake kulindwa ndio ulimpelekea kukubaliana na dili aliyopatiwa ni dili ya kujifanya kama Mkemia mkuu wa Serikali. Umbo la Mzee Kamba ndefu lilikua limeshahabiana sana na la Mzee Deus Lyimo mkemia mkuu wa serikali anayeaminika kwa kufanya kazi kwa uaminifu katika serikali. Akiwa anaishi katika eneo la Masaki eneo maarufu wanaloishi viongozi wa serikali. Mzee Deus hakua na mazoea na watu muda wote alikua mkimya kabisa hakuwa na mazoea hata ya kuongea na familia yake muda wote alikua siriazi. Mke wake mara ya kwanza alikua akichukizwa na aina ile ya maisha ya mumewe lakini ilibidi akubaliane nayo. Walikua wakiishi peke yao na mfanyakazi wa ndani huku watoto wao wawili wakiwa wanaishi nje ya nchi wanaposoma. Kila jioni Mzee Deus alipenda kupitia katika hoteli ya Sheratoni na kunywa kahawa kila jioni baada ya kazi na kisha kuelekea nyumbani kwake alipokua akipelekwa na Ally Dadu Dereva Tax maarufu hapo hotelini. Ni jumapili siku ambayo huwa anatumia kupumzika nyumbani lakini siku hiyo alikua akitoka katika maabara kwa kazi moja tu ya kupima pombe iliyosadikiwa kuwa na kemikali hatari kwa mwili wa binadamu. Baada ya kazi alijaza ripoti ambayo alitakiwa kuiwasilisha kwa waziri wa Afya kesho yake asubuhi. Mkoba wake ukiwa kwapani kama kawaida safari yake ikaishia Sheratoni na kunywa Kahawa kisha akatoka nje na kumuangalia Ally Dadu na kumtafuta bila mafanikio. Ni Tax moja tu ndiyo ilikua imepaki pale ndipo alipoifuatilia na kuingia.

    “Nipeleke Masaki”

    “Sawa Boss”

    Dereva Tax alijibu na kuwasha gari, Baada ya mwendo wa dakika tano Deus Lyimo alisikia kitu cha baridi kikimgusa kichogoni kasha Dereva akaamriwa kugeuza gari na Safari ikaishia ndani ya Godown la American Bussiness. Na kutolewa katika ile gari akiwa na Yule dereva wakapelekwa katika chumba kimoja wakakutana na mwanamke wa kizungu. Bibi Camillah.

    “Karibu Muheshimiwa”

    Deus alimshangaa Yule mama huku akiangalia mazingira ya kile chumba kilichopakwa rangi nyeupe hakikua na doa la aina yeyote.

    “Nahitaji kuongea na wewe Muheshimiwa”

    “uongee na mimi kuhusu nini?”

    Mzee Deus alijibu huku akishikilia mkoba wake vizuri.

    “Nachotaka kukwambia sitaki mtu mwingine asikie”

    Bi. Camillah akachomo bastola na kumpiga Yule dereva risasi ya kichwa iliyokatisha uhai wake kitendo kilichomshtua Mzee Deus na kutetemeka.

    “Usiogope wewe nitakuua polepole, Naomba huo mkoba”

    “Hapana, Una nyaraka za serikali”

    “Ok hutaki?”

    Bi. Camillah akaangalia upande wa pili wenye mlango.

    “Ingia”

    Akaingia mzee aliyefanana na Mzee Deus kwa kila kitu mpaka mavazi mpaka mkoba alioubana kwapani, Mzee Deus akashangaa kabla hajaongea chochote Bi. Camillah alikua karibu yake akampulizia Death Perfume ni marashi yaliyokatiza uhai wa Deus taratibu na kupelekea Deus kuanguka kama gunia la chumvi.

    Mzee kamba ndefu aliyebadilishwa sura na kufanana na Mzee Deus kwa kila kitu aliondolewa na kuingizwa katika tax na kupelekwa nyumbani kwa mzee Deus, Mke wa Mzee Deus Mkemia mkuu wa Serikali akampokea kama mumewe, Mzee kamba ndefu akaingia moja kwa moja chumbani na kulala bila kuongea na mke wa Deus. Mke wa Deus hakushangaa sababu ni maisha aliyozoea alipanda kitandani na kulala pembeni ya mzee Kamba ndefu huku akijua ni mumewe. Mpaka asubuhi Mzee kamba ndefu alipoamka na kuandaliwa kifungua kinywa na mavazi akabadili saa nne gari la wizara lilikua limemekuja kumchukua kwa ajili ya kupeleka ripoti kwa waziri. Jioni ya siku hiyo magazeti yalikua yakiandika Ripoti ya mkemia mkuu ikikanusha hofu ya pombe zile kitendo kilichopelekea vijana kusherehekea kwa kuinywa pombe ile kwa fujo. Bi Camillah alifurahishwa na mfanikio ya kuzuia kikwazo kile kilichotaka kuharibu mipango ile huku akimpatia Mzee kamba ndefu ujira mnono. Ujira wa kutumbukizwa katika acid na kupotea mpaka mifupa.

    ****

    Hakuamini kile alichokiona kupitia kompyuta iliyo mbele ya ofisi yake, Katika utendaji wake wa kazi hakuwahi kufikiri kama kuna siku atapokea taarifa ambayo itapokelewa na Rais wanchi yake kama taarifa aliyokutana nayo kwa wakati huo, Ni taarifa ambayo itamuongezea nafasi nzuri sana katika serikali ya Marekani. Hakuamini kama mtu ambaye aliwahi kusababisha Viongozi wane wa ngazi ya juu ya serikali wajiuzulu kutokana na kushindwa kumdhibiti mtu huyo na kwa wakati huo ni miaka nane zaidi ilikua imekwishamalizika tokea kutangazwe kutafutwa kwa mtu huyo. Hakutaka kuwa na papara alitamani yeye akabidhiwe mtu huyo peke yake kabla ya kutoa taarifa sehemu yeyote. Bastola yake ikiwa imekaa vyema katika mkanda wa silaha uliozunguka kupitia kifuani kwake. Kifaa maalumu cha GPS kilikua kiko on na kwa mwendo wa Haraka akakimbilia katika Gari la kijeshi aina ya Hummer II akatoka eneo la ofisi kwa mwendo wa kasi kuelekea barabara ya Newvile park huku macho yake yakiangalia GPS kila dakika. Ndani ya dakika kumi gari ilikua imepaki nje ya Hotel ya Hilton Palace, Pasipo kusubiri akaingia na kupanda ngazi haraka kuelekea juu. Kwa mwendo wa Tahadhari alianza kuhesabu vyumba vya hotel ile huku akiwa makini kama anatafuta kitu. namba 1230Qb, 1232Qb…, Baada ya hatua tatu akapishana na kijana mtanashati aliyekamatia vyema sigara yake katika vidole. Akiwa hana muda nae aliendelea kutafuta chumba alichokitaraji ghafla akasikia muunguzo katika mkono wake ni muunguzo wa moto ni sigara ya Yule kijana iligusana na ngozi ya mkono wake, Kwa Ghadhabu aligeuka na kumtazama Yule kijana kwa chuki.

    “Im sory Sir” {Samahani bwana mkubwa}

    Yule kijana alijibu kwa unyenyekevu

    “Fuck you”

    Alimjibu Yule kijana kwa hasira na kugeuka kuendelea na kazi yake, Kama umeme bila kutarajia mkono wa Yule kijana ulizama na kuchomoa bastola iliyowekwa katika mkanda alipogeuka akajikuta bastola yake imemuelekea yeye.

    “Folowing my instruction” {Fuata maelekezo yangu}

    Ni mpelelezi wa kirusi Modach alikua katika sura isiyo ya kawaida, Alikua akimpa amri kwa sauti ya chini sana Afisa usalama wa jimbo la Texas Rodric Vidic. Akifuata maelekezo huku mikono yake ikiwa kichwani kama alivyoelekezwa na Modach, Rodric alijiona ni mpumbavu sana kutoka ofisini bila Taarifa. Na sasa alikua mikononi mwa mtu asiyemfahamu, Aliamini fika huo ulikua mwisho wake na hakuna mtu ambaye angefahamu kutekwa kwake. Modach akirudi nyuma hatua mbili alimuamuru kwa sauti ya Chini rodric.

    “Toa black key fungua chumba namba namba 1237Qb kwa tahadhari”

    Rodric alitoa fungua, ni funguo mweusi ni funguo ambao majasusi na Maafisa usalama wa nchi huwa nazo. Ni funguo yenye uwezo wa kufungua kitasa chochote kile. Rodric aliingiza funguo katika kitasa kwa tahadhari na mlango ukafunguka.

    “Attack”

    Aliamriwaa avamie, Rodric akaingia kwa haraka huku nyuma Modach akiingia kwa haraka huku bastola ikiwa tayari kwa chochote. Katika kitanda mwanaume akiwa chini juu yake akiwa mwanamke wakifsnys mspenzi. Mshtuko alioupata Yule mwanaume alijaribu kuinuka akakutana na pigo takatifu toka kwa Modach lililompeleka chini kabla hajaamua cha kufanya tayari pingu ilikua katika mkono wake na kuunganishwa na mkono wa Rodrick huku bastola ikiwa nyuma yao amri ya kutangulia kutoka nje ilisikika toka kwa Modach Rodrick alitii huku akimvuta Yule kijana wakatembea kwa woga huku Yule kijana akiwa uchi. Modach aliwaongoza mpaka kwenye gari la Rodric huku wakipishana na watu waliokuwa wakiwashangaa. Modach akatoa amri Rodric aendeshe gari kuelekea ofisini kwake Makao makuu ya FBI hapo Texas. Gari lilitembea kwa dakika kumi na tano tofauti na muda aliotumia kufika katika hotel ile huku kichwani akiwa na mawazo kitu kinachoenda kutokea toka kwa mtu aliyemteka. Hakujua mtu aliyefungwa nae pingu ni nani. Gari lilifika nje ya ofisi yake wakaamriwa washuke na kuingia ndani ya Ofisi huku Modach akibaki ndani ya lile gari bastola ikiwa imewaelekea wao. Rodric aliingia ndani huku akimvuta Yule kijana. Maafisa waliokuwa bize asubuhi hiyo walipigwa na butwaa bastola zao zikatoka kiunoni kwa tahadhari kunyoosha Rodric alipotokea.

    “My God Terorist Don?” {Mungu wangu Gaidi Don}

    Ni sauti ya Afisa mmoja wa FBI iliyomshtua Rodric na kugeuka kumtzama mtu aliyefungwa nae pingu hakuamini kama ni Don gaidi aliyekua anatafuta na marekani, Hakuamini kama Yule ndiye mtu ambaye alitumiwa Email kuwa amekamatwa katika Hotel ya Hilton aende akamchukue. Mchezo aliochezewa na mtu asiyemfahamu ulimshangaza. Maafisa wenzake wakimzunguka huku bastola zao zikimuelekea Don, Pingu ilifunguliwa Don akawekwa chini ya ulinzi mkali huku taarifa ikisambazwa kupitia mtandao katika vitengo vyote vya usalama America nzima. Rodric alipotoka nje hakukuta gari wala mtu aliyemteka na kumleta pale.

    ****

    Saa tano asubuhi katika Ofisi za Balozi wa marekani ndani ya jiji la Tokyo, Mgeni aliyevalia Tisheti nyeupe yenye maandishi yanayosomeka “I LOVE AMERICA” alikua mbele ya meza ya katibu muhtasi wa Balozi huyo huku mkononi kashika Boksi kubwa lililofungwa vizuri kwa karatasi la zawadi.

    “Samahani nahitaji kuonana na Balozi”

    Yule mgeni alimwambia katibu muhtasi na kujibiwa Balozi yupo busy aache ujumbe, Yule mgeni akaacha lile Boksi pale na kuondoka akiacha maagizo ni mzigo wa Balozi. Katibu muhtasi hakutaka kuhoji sababu ni kawaida wageni mbalimbali kutoka marekani kumletea zawadi balozi huyo pindi wanapokuja Japan. Balozi akiwa mwenye furaha kwa siku hiyo baada ya kupokea taarifa toka kwenye vyanzo vya Taarifa kutoka ikulu ya Marekani kuhusu kukamatwa kwa Don alijibu kwa furaha sauti ya mlango kugongwa akakutana na katibu Muhtasi akiingia na box kubwa.

    “Mzigo wako umeletwa na Raia wa America”

    Balozi alipokea na kuuweka pembeni kasha akaufungua kwa shauku. Mshtuko alioupata hakuutegemea kabisa, Hakutegemea kama kuna siku angeweza kufungua zawadi mbaya kama zawadi aliyoifungua muda huo. Ni muda ambao alikua na furaha lakini Furaha yake iliyeyuka Ghafla. Ni kichwa cha Solomon kilikua kimewekwa katika Box huku kukiwa na ujumbe mfupi ulioandikwa katika karatasi. “AMERICA FANYENI MAMBO YA MSINGI WACHENI KUFUATILIA MAMBO YA WATU” Balozi alichanganywa na ujumbe ule huku akiwa haamini kama mpelelezi machachari aliyetegemewa na America SOLOMON alikua kauawa kinyama na kichwa chake ndio kile kilikua mbele yake.

    “Unamjua aliyeleta huu mzigo”

    Ni swali lililotupwa kwa Katibu Muhtasi

    “Simjui”

    “Shiit”

    Taarifa ya kifo cha Solomon ilisambaa kama moto katika nyasi kavu na kuenea America nzima kupitia Tv na mitandao ya kijamii, Mmoja kati ya watu waliopata taarifa hiyo ni Modach taarifa iliyomsafirisha mpaka Japan kwenda kujua ni kwanini Solomon kauawa ndani ya nchi hiyo huku akiamini kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia.

    ****

    Jose B akiwa ndani ya jiji la Dar Es Salaam kwa mara nyingine tena akiishangaa wingi wa magari ndani ya jiji hilo tofauti na mara ya mwisho alipolikimbia jiji hilo baada ya kunusurika na kifo. Kifo cha tama ya kuuza siri ya kizuizi, Sasa alikua ndani ya jiji hilo kwa biashara halali, Biashara ya kuuza mchoro wa simu, Simu aina ya Aple ambayo imetengenezwa na kijana wa kihindi aishie ndani ya jiji la mwanza. Fikra za Jose B ni kuzunguka katika makampuni ya mitandao ya simu lakini mpaka wiki kwisha hakuna mafanikio aliyopata. Hofu ya kuishiwa na fedha ilimfanya Jose B kupanga safari ya kurudi jijini mwanza baabda ya kushindwa kufanya biashara iliyomleta Jijini Dar. Akiwa katika kijiwe cha mama muuza mihogo nje ya Godown la American Bussiness Solution akila mihogo huku akipiga story na wafanyakazi wa Godown hilo alipata faraja baada ya kusikia kampuni hiyo ni ya kimarekani na inahusika na kusambaza simu katika nchi mbalimbali. Shauku ya kujipenyeza ndani ya jingo hilo ilimkamata huku akifikiri njia gani itamuingiza humo ndani ukizingatia ulinzi mkali uliotanda katika jingo hilo. Maelekezo aliyopata toka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Godown hilo kuwa kila asubuhi vibarua wapya huandikwa hapo ndio yaliyomfanya Jose B kuwa asubuhi sana nje ya Godown na kukaguliwa kasha akaingia ndani ya jingo hilo. Muda mwingi Jose B alikua akichunguza kila mtu aliye ndani ya jingo hilo nia yake ikiwa ni kujua kiongozi mkuu wa Godown hilo ambaye ataweza kuzungumza nae kuhusu biashara yake.

    Ni siku ya tatu Jose B hakupata mafanikio yoyote ya kuongea na kiongozi yeyote kutokana na kila mtu kuwa busy na kazi huku muda mwingi wakitumia kufanya kazi chini ya ulinzi mkali.

    “We kijana nifuate”

    Ni sauti ya mzee mmoja ikimtaarifu Jose B amfuate, Jose B kwa wasiwasi akamfuata wakaingia katika chumba kimoja chenye kompyuta kyingi ukutani. Yule mzee akakaa kwenye kiti akimuangalia Jose B kwa makini.

    “Unaitwa Nani?”

    “Naitwa Joseph”

    “Umetumwa na nani kutuchunguza”

    “Sijatumwa na yeyote kuwachunguza”

    “Mbona tokea ufike hapa umekua ukifuatilia kitu Fulani huku na wala si kazi”

    “Unajua mzee wangu mimi kilichonileta hapa nina biashara nafanya sasa nilitegemea nitapata mtu wa kufanya nae hii biashara”

    “Biashara Gani”

    “Nina mchoro wa simu ambao nataka niuuze ni simu ambayo ina uwezo wa hali ya juu”

    “Mchoro wa simu?Umeupata wapi?”

    Yule mzee aliuliza kwa mshangao huku akimuangalia Jose B kwa mshangao

    “Kuna rafiki yangu yupo mwanza ndiye aliyeunda hiyo simu na ana sample yake ni simu ya ajabu sana.”

    Jose B alijieleza maelezo ambayo yalimvutia Yule mzee

    “Sasa sikia wewe kamlete huyo mtu aje akutane na Bosswetu mkubwa anaitwa Karma atakuja wiki ijayo mimi nitawakutanisha nae na mtazungumza ila kama una ujanja ujanja wako hautopona maana utapotea hii si sehemu ya mchezo. “

    Yule mzee alimtahadharisha Jose B. Jose B alifurahi kwa hatua aliyofikia kwa kutumia fedha aliyoingiza wakati anafanya kazi pale aliweza kukata tiketi ya ndege na kurudi mwanza haraka kwenda kupeleka taarifa ya Mafanikio kwa Rajiv.

    *** http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitabu kidogo cha Taarifa alichokikuta katika nguo za Solomon zilizotelekezwa katika nyumba ya kulala wageni ndani ya jiji la Tokyo kilikua katika mikono yake, Neno pekee Bandari ya Tokyo ndilo lilikua likimchanganya. Akiwa katika Bandari ya Tokyo nguo kuu kuu alizovaa zilidhihirisha kuwa yeye ni kijana masikini aliyekua katika eneo lile kwa kazi ya kubeba mizigo pekee. Akiwa anashangaa shangaa ukubwa wa bandari ya Tokyo moja ya bandari kubwa katika ukanda wa bahari ya pacific nay eye kuingiza kontena nyingi kuoka nchi nyingi duniani na kua mizig mingi zaidi. Akiwa anazidi kushangaa alishtushwa na kijana mmoja mwenye mwili mnene akimgusa makalio akageuka na kumuangalia

    “Unatafuta nini? Kama kazi nenda kule”

    Akamuonyesha eneo ambalo kulikua na vijana wengi waliokua wameunga mstari wakiandikwa majina na kupewa ovaroli za kibuluu na mabuti. Modach alikimbia na kuunga mstari akawa mmoja kati ya watu waliopata kibarua katika bandari ile. Kazi ya kuhesabu kontena zilizokua zikitoka ndani ya Bandari hiyo ndiyo aliyokua amepewa Modach. Alifanya kazi kwa makini huku mkononi akiwa na kitabu kidogo cha kumbukumbu akiandika kila kontena lililotoka. Mpaka kufika saa kumi na mbili jioni muda wa kutoka kazini hakuna kitu alichogundua pale katika bandari. Bado kichwani alikua anawaza sababu ya Solomon kuandika neon Bandari ya Tokyo. Alirudi hotelini akiwa amechoka ikiwa ni siku ya jumamosi huku akipanga kwenda tena pale bandarini siku ya jumapili, Siku ambayo kunakua hakuna pilika nyingi, Kwa kuwa aliambiwa yeye anaweza kuja kufanya kazi siku hiyo kutokana na sehemu aliyokua kafanya siku hiyo ilimbidi kwenda kujaribu tena kufuatilia bandari hiyo kama atagundua kitu chochote. Saa moja na nusu alikua keshafika ndani ya Bandari ya Tokyo na kuanza kazi aliyofanya jana yake. Akili yake ilikumbwa na kiharusi cha kuuwaza, ni macho yake yalipopeleka taarifa katika ubongo wake juu ya kiumbe cha ajabu alichokiona, Aliwahi kupita katika nchi nyingi zinazosifika kuwa na viumbe wa ajabu zaidi kama Venezuela, Brazili, Spain nan chi kadhaa lakini mboni za macho yake hazikuwahi ,ufaidi kama muda huo kilichokuwa mbele ya macho yake. Kundi la vijana waliojazia miili yao wakiwa kila upande kuhakikisha hakuna anayeweza kukisogelea kiumbe hicho. Akili ya Modach ilishindwa kufanya kazi kama kawaida yake aliduwaa kwa muda huku miguu yake ikipoteza uelekeo. Ujasiri wa kiume ukamvaa na kuamua kumfuata Yule kiumbe akitembea kwa hatua za haraka. Akiwa amebakiza hatua chache kumfikia alijikuta akikabiliana na pigo la kushtukiza kutoka kwa mmoja wa vijana waliomzunguka Yule kiumbe na kudondoka mbele ya kile kiumbe. Kama vile hajamuona kile kiumbe kikaruka mwili wa Modach uliolala pale chini kwa maumivu na kuendelea na safari. Modach akijikongoja huku akikiangalia kile kiumbe. Kitabu chake cha kumbukumbu kikiwa pembeni alikiokota haraka na kusimama kama hakuna chochote kilichotokea. Kile kiumbe kilisimama pembeni ya Crane inayopakia kontena katika magari na kuletewa karatasi ya kuweka sahihi akaweka na kontena nne zikapakiwa katika gari tofauti. Wakati Modach anajiandaa kuandika idadi ya kontena zinazopakiwa akapokea maagizo kutoka kwa msimamizi wake wa kazi kuwa asiandikie zile kontena ni mzigo wa tajiri wa kimarekani huwa unapita bila kufanyiwa ukaguzi. Modach aliguna na kusoma namba za magari yaliyopakia mzigo na kuziandika pembeni akaenda upande wa pili kuendelea na kazi. Kisu kidogo kilipita katika mkono wa Modach na damu nyingi zikanza kumwagika. Kelele ya maumivu ndiyo ilimvuta msimamizi wa kazi wa Modach na kumkuta Modach akilia kwa mumivu. Haikuhitaji kuuliza kuwa Modach alihitaji kwenda Hospitali. Alipatiwa pesa na kuruhusiwa kwenda hospitalini kupata matibabu. Hiyo ndiyo ilikua njia sahihi ya Modach kuweza kutoka eneo lile kirahisi kwa kujikata kwa kisu kwa mkono wake mwenyewe kulitosha kupata ruhusa tena ruhusa ambayo hata asingerudi kabisa kusingekuwa na shaka juu yake. Kwa mwendo wa haraka akaingia kwenye tax na kumuamuru dereva afuatilie magari manne yaliyobeba kontena yaliyokuwa yakitoka nje ya Jiji la Tokyo gari ilikua ikielekea katika mtaa wa Takeshita Dori mtaa wenye duka mengi ndani ya Jiji la Tokyo. Yale magari yalikua yakielekea barabara ya mtaa wa Showa Dori mtaa wenye Ma godown mengi ndani ya jiji la Tokyo. Modach alifuatilia kwa umakini mpaka alipokutana macho yake yalipogongana na maandishi makubwa American business Solution. Yale magari yakasimama nje ya jingo hilo. Uamuzi wa kuwasiliana na kikosi cha usalama cha nchi hiyo baada ya kutilia mashaka mzigo ule ulikua sahihi kwake. Tayari taarifa ilikua imekwishafika katika chumba cha mawasiliano cha wanausalama wa Japani n a magari yapatayo ishirini ya polisi yalikua yakielekea eneo hilo. Kile kiumbe cha ajabu kilishuka katika gari lililokua likifuata yale magari kwa nyuma na kutoa simu akaanza kupiga. Si mwingine alikua ni Angelica Taylor Kurt binti mrembo mtoto wa Tajiri mkubwa America aitwaye taylor Kurt.

    ***

    Kitendo cha kutoka nje ya uwanja wa ndege wa Narita International Airport (NRT) wa jiji la Tokyo alipokelewa na Kundi kubwa la dereva Tax kila mmoja akivutia biashara kwake. Macho yake yakachagua tax ya Mzee wa makamo aliyesimama pembeni akiwa kaka juu ya boneti ya gari yake.

    “Nipeleke Hotelini Tafadhali”

    Solomon alitoa maelekezo na kuingia kwenye gari safari ikaanza. Gari ilikua ikitembea kwa mwendo wa taratibu sana kuelekea nje ya uwanja huo wa ndege. Baada ya kukamata barabara kubwa Solomon hakuamini mwendo wa gari ile ni kama inaendeshwa na kijana mdogo huku sauti ya muziki ikiwa juu na dereva akichezesha kichwa kufurahia muziki wa kijapani uliokua ukipigwa. Alikua akicheza kama wafanyavyo wamarekani weusi wanaopenda muziki wa hiphop. Solomon akiwa anatabasamu bila wasiwasi huku akifurahishwa na umahiri wa mze Yule na uchangamfu wake alishtushwa na beki kali iliyofungwa na kusababisha gari kugeuka kule lilipotokea na gari kubwa aina ya scania lenye bodi kubwa lililo wazi likiwa limepaki Yule mzee akaingiza ile gari ndani ya bodi la lile gari na bodi ikajifunga. Solomon kwa taharuki akatoa bastola yake mara akakumbana na kicheko kutoka kwa Yule mzee kasha Yule mzee akachomoa bastola na kujipiga ya kichwa akatulia kimya milele akiwa kaangukia kwenye usukani. Solomon hakujua kinachoendelea gari lilitembea kwa mwendo mkali na kuishia katikati ya msitu. Mlango ukafunguliwa.Kundi la wanawake wengi wapatao thelathini walioshikilia bunduki za kivita walikua wamesimama kuzunguka gari lile wakati Solomon akishuka kutoka katika gari lile. Hakuamini kile anachokiona kosa alilofanya ni kumuamini Yule mzee tena imani iliyo nje ya taaluma yake. Alijilaumu huku akiwa mnyonge sana, Amri ya kuweka silaha yake chini aliitii bila ubishi na kutoka mikono ikiwa kichwani mpaka nje wale wanawake wenye silaha wakamzunguka huku wakiwa wamenyoosha midomo ya bunguki zao kwa Solomon

    Helcopta ilitua wakati Solomon kasimama katikati bila kusemeshwa kitu, kutoka katika ile helcopta alishuka mwanadada machachari, Karma akiwa kashika upanga mkononi.

    “Good Evening American” {Habari za jioni mmarekani}

    Karma alimsalimia Solomon kwa Dhihaki. Huku akimsogelea karibu na kumpapasa kifua kwa kutumia ule upanga.

    “Kushoto”

    Karma aliongea neno hilo pekee wanawake wanne wenye miili mikubwa wasio na mzaha wakatoka na kumkamata Solomon na kumlaza juu ya Gogo kubwa lililolaazwa pembeni. Karma akasogea kwa Maringo na kunyanyua upanga kilio cha maumivu ndio sauti pekee ya mwisho iliyotoka kwa Solomon.

    “Mmoja wenu atapeleka kichwa chake kwa balozi wa Amerika hapa Tokyo”

    Karma akatoa karatasi yenye ujumbe akawakabidhi na kurudi katika helcopta na safari ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa Haneda Airport na kuingia katika ndege ya kukodi safari ya kuelekea Tanzania kwa mapumziko ikaanza baada ya kukamilisha kazi ngumu kazi ya kumlaza kimya milele Solomon jasusi wa FBI aliyeponzwa na uaminifu wake kwa mzee asiyemjua..

    ****

    Mapenzi mazito kwa mkewe ndiyo yalikua kitu kikubwa katika maisha yake, hakutaka kukaa mbali na mkewe hicho ndicho kitu ambacho alipingana nacho wakati wote. Suala la yeye kusafiri kuelekea Dar huku nyuma akimuacha mkewe halikumuingia akilini, mabishano makubwa kati yake na Jose B yalifikia muafaka wote watatu wasafiri kuelekea Dar es Salaam katika kufanya biashara ya mchoro mpya wa simu. Tiketi zilikatwa siku inayofuata ambapo asubuhi ya siku hiyo ilikua ni asubuhi iliyogubikwa na wingu zito huku dalili za mvua zikiwa zinaonyesha wakati wowote mvua italikumba jiji la mwanza. Akiwa kamshika mkono mke wake pembeni kuna mabegi yao ni mtu mmoja tu alikua akisubiriwa ili waingie kwenye gari. Ni Jose B wa ukweli. Kwa mbali Jose B alionekana akiwa na begi lake mgongoni na kufika aliposimama Rajiv na Tusmo.

    “Vipi mmesubiri sana?”

    Jose B aliongea huku akibeba begi kubwa la Rajiv lililokua pale chini na kuelekea kwenye gari la Raqeeb lililokua limesimama ndani ya kituo kikuu cha mabasi cha Mwanza. Tusmo na Rajiv wakafuata nyuma wakiwa wamebeba begi dogo mkononi na kuingia kwenye gari na kwenda kukaa kwenye kiti pamoja. Ni siti ya watu watatu waliyokaa Rajiv, Tusmoo na Jose B wa ukweli na safari ya kuelekea Jijini Dar es Salaam ikaanza.

    “Hivi hao watu ni wakweli kweli”

    Rajiv alimuuliza Jose B swali ambalo jose B alilijibu kwa uhakika zaidi.

    “Yaani ni uhakika kwanza huyo mtu anayetukutanisha nao kanipa uhakika wa asilimia tisini kuwa biashara itafanyika lazima”

    “Nitafurahi kama nikitimiza ndoto yangu na kuudhihirishia ulimwengu kuwa Tanzania ni moja ya nchi duniani yenye uwezo wa kushindana na chi nyingine katika teknolojia ya mawasiliano”

    Rajiv aliongea kwa kujiamini huku Tusmo akiwa amejilaza kwenye kiti na kuonekana kama anapitiwa na usingizi wakati huo gari lilikua linaanza kuacha jiji la mwanza na kuanza kukutana na miji midogo ya jiji hilo.



    ****

    Kichwa chakekilikua kikifikiria shemu ambayo anaweza kupumzika bila kupata bugudhi yeyote. Serikali ya akili yake ilikua ikikagua ukanda wa afrika ni nchi gani inayoweza kuwa tulivu kwa wakati ule. Akili yake ilikuaikishindana kati ya visiwa vya komoro na Nchi ya Tanzania iliyoko katika ukanda wa Afrika mashariki. Jarida la biashara liitwalo DAR lilikua mkononi mwake huku akitazama maeneo ya kuvutia ya nchi ya Tanania na kujikuta akiamua kuelekeanchini Tanzania. Alizima simu yake ya mkononi na kukaa vyema katiiri ka kiti cha ndege huku akiwa kajilaza kwenye kiti akisubiri muda wa ndege kuiacha Ardhi ya Japani uweze kutimia. Sauti ya Msichana ilisikika kupitia katika vikuza sauti vilivyo ndani ya ndege ile ikiwataarifu abiria kufunga Mikanda ndipo Aliposhtuka na kufunga Mkanda vyema na Sauti ya pili ikawaarifu kuwa ndege inapaa. Ndipo baada y dakika tatu ndege ilitembea kwa umbali mfupi na kuanza kuiacha Ardhi ya Japani Taratibu. Abiria wakiwa wenye furaha huku kila mmoja akiwa na fikra za kule aendako. Mazungumzo tofauti tofauti ya abiria yalikutana na kutengeneza sauti ya kelele ndani ya ndege hiyo. Kelele ambazo hazikua na athari yeyote kwa abiria wengine ila kelele hizo zilikua kama kero kwa Karma ambaye kila dakika alikua akisonya. Baada ya Saa moja ukimya ulitawala ndani ya ndege hiyo. Ni ukmya ulliosababishwa na abiria kunyamaza na kupotelea katika usingizi huku wakiacha Sauti ya Tv kusikika tu. Muda huo ndio muda ambao ulikua sawa kwa Karma kuweza kuuchapa usingizi kwa uchovu aliokua nao kwa safari ndefu alizounganisha na kazi nzito aliyotoka kuifanya ndani ya jiji la Tokyo. Safari ya muda mrefu angani na usingizi mzito ulishtushwa na sauti ya Muhudumu wa ndege ile kupitia vipaza sauti kuwatarifu abiria kufunga mkanda kwani ndege ilikua katika hatua za kutua katika uwanja wa ndege wa Amsterdam Uholanzi kwa ajili ya Abiria kuweza kubadilisha ndege nyingine. Karma akashtuka na kuvuta mdomo huku akionekana dhahiri amechukizwa na sauti ile iliyomuamsha kutoka aktika usingizi mzito. Akichukua mkoba wake na kuangalia kama vitu vyake viko sawa. Akajifunga mkanda vyema na kusubiri ndege kutua. Ndege ilianza kutua taratibu na kutembea kwa mwendo mfupi ikizunguka uwanja na kusimama . Karma kwa mwendo wa haraka pochi ikiwa kwapani alielekea ulipo mlango wa ngege huku akipita katikati ya abiria wenzake na kushuka haraka mpaka chini na kuelekea moja kwa moja katika mlango wa kuelekea upande wa pili wa uwanja ule na kusimama mbele ya dawati la mkaguzi wa tiketi kabla ya kuingia upande ule.

    “Your Ticket Please” {Tiketi yako Tafadhali}

    Msichana aliyeonekana yuko bize huku akibonyeza bonyeza kompyuta alimwambia Karma kwa Upole. Karma aliingiza mkono katika Pochina kutoa Tiketi na kumkabidhi yule dada akairekodi katika kompyuta yake na kumkabidhi huku akimuelekeza eneo la kwenda kusubiri ndege atakayoondoka nayo. Karma alienda mpaka eneo maalumu la kusubiria ndege na kukaa katika kochi huku akijiegamiza kichwa na macho yake kuelekeza katika Tv kubwa iliyo mbele yake. Uso wake ulipambwa na tabasamu baada ya kukutana na Habari ambayo ilikua ni yenye kumfurahisha. Ni habari juu ya kifo cha mpelelezi wa Marekani ambaye alikatwa kichwa na kichwa chake kupelekwa kwa Balozi wa Marekani nchini Japani.

    ****

    Hali ilikua ya joto sana katika Jiji la Texas, Ni siku ya jumapili ndani ya kanisa la St. Peres lililoko katika mji wa Arkansas moja ya miji maarufu ndani ya Jiji la Texas nchini Marekani. Waumini wakiwa kimya wakisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na Padri Valence kwa umakini. Huku upande wa kushoto katika benchi la pili alikua kakaa Taylor Kurt tajiri mkubwa nchini marekani anayemiliki kampuni kubwa ya Mawasiliano Duniani iitwayo Micronet. Smu aina ya Micphone ilinayotengenezwa na kampuni yake ilikua ikitesa katika soko la dunia huku akiongoza kwa mauzo katika nchi nyingi duniani hasa hasa Africa, Misaada aliyokua akiitoa katika nchi nyingi masikini zilizopo kusini mwa jangwa la sahara kupitia shirika lake la Kurt Foundation ndiyo iliyomfanya kupata heshima kubwa Duniani na kuwa mmoja kati ya watu wanaoheshimika zaidi Duniani. Akiwa kakaa kimya huku akipitia vifungu kadhaa katika biblia yake yenye kava la Dhahabu, Mara Simu yake ya mkononi inamtingisha ikiwa mfukoni. Kwa tahadhari anaitoa na kutembea kwa mwendo wa taratibu mpaka nje ya kanisa hilo, Mpaka anafika nje Tayari simu ilikua imekatika.Huku akivaa miwani yake na kutazama namba ya mpigaji wa simu.

    Taylor Kurt akabonyeza kitufe cha kuzima simu na kuirudisha simu mfukoni kisha akarudi kanisani kuendelea na Ibada. Muda wa kwenda kushiriki chakula cha bwana ulipowadia Taylor Kurt akijiandaa kusimama na kuingi katika mstari wa kushiriki mara anaguswa bega, Anageuka na kukutana na Sura ya Mkurugenzi wa kampuni yake akiwa anatokwa na jasho akamshika mkono na kutoka nae nje huku akiwa mwenye wasiwasi.

    “What Happening Mark?” {Mark, Kuna tatizo Gani}

    Taylor Kurt alimuuliza Mark huku akiwa mwenye wasiwasi.

    “She is Arrested” {Amekamatwa}

    Mark alitoa jibu ambalo lilimlegeza Taylor Kurt magoti na kumdondosha chini kama kiroba.



    *****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haya Sasa Mzigo unasonga Mbelee, Rajiv akiwa na mkewe Tusmo pamoja na Jose B wa ukweli wapo katika Bus wanatoka Mwanza wanaelekea Dar es salaam kufanya biashara je watafanikiwa? Karma kashafanya kazi yake na yupo safarini kuelekea Tanzania je safari yake itafanikiwa? Tajiri Taylor Kurt kapokea Taarifa ya kukamatwa kwa Mwanamke je ni nani? Na je itakuaje? Je ni nani anauza Bikira. Tuendelee na Utabiri kwa anayweza. Coment na like za kutosha.



    NB: Nashindwa kuendelea kwa wakati sababu nakatishwa tamaa na like zenu naona kama hadithi si nzuri. Like hazitoshi kabisaa —



    MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog