Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

MIMI NI MUAFRIKA (I'M AFRICAN) - 4

 








Simulizi : Mimi Ni Muafrika (I'm African)

Sehemu Ya Nne (4)





Msitu wa mikoko.

Waafrika wakaacha marumbano,wakakaa tayali kwa ajili ya vita, Angel alikuwa tayali kuwasaidia,watakapohitaji msaada wake, Angel alikuwa binti mdogo lakini alijitambua,muda wote tabasamu lilionekana katika macho yake, aliwaheshimu na kuwapenda watu wote, rangi zote, japo mwanzoni aliichukia Afrika kwa umaskini wake, lakini baada ya muda mfupi akatambua kwa nini Afrika ilikuwa maskini, mali zake zilinyonywa na wazungu, wakatawaliwa kwa nguvu, wakauawa kikatili, akaapa kuhakikisha anashirikiana nao kupigania uhuru.



“,Sikilizeni, wote tuko hapa,kila mtu atege masikio yake vizuri …”,mzee Nyamigo aliongea,Waafrika wote wakatega masikio kumsikiliza, walimfahamu kwa uwezo wake mkubwa wa kutega mitego sehemu mbalimbali, mitego ya kuwinda wanyama, lakini leo alitoa ushirikiano kutega mitego kuwanasa wazungu.



“,sema mzee, muda wowote watakuja msituni kututafuta! “,kijana mwingine aliitikia.



“,kweli kabisa, muda ndo huu, vita imefika “,Mpuzu na Ishimwe wakaongea.



“,jambo la kwanza, mahali pazuri na salama kwa ajili ya kujificha, ni juu ya miti ya ubuyu, miti yenye majani mengi, sio rahisi sisi kuonekana, lakini ni rahisi kwetu sisi kumuona na kumshambulia adui …”,mzee Nyamigo aliongea.



“,Kweli kabisa, kweli kabisa …”,Waafrika wakaitikia, walikubaliana na maneno aliyo yaongea mzee Nyamigo, wakaa kimya, ili wasikilize maneno aliyotaka kuongea kwa mara nyingine tena.



“,Hakikisha unapoua, unachukua bunduki,mtoto wa gavana atatufundisha namna ya kuzitumia. “,mzee Nyamigo aliendelea kuongea, watu wakatikisa vichwa, bila shaka walikuwa pamoja naye, walimuelewa vizuri sana.



“,Tunaanza sasa kutega mitego, wazee na wamama mnatengenezewa ngazi, mtapandishwa juu ya miti, huko pia mtawekwa mahali salama, msiweze kuanguka na kudondoka chini …”,Mzee Nyamigo akamalizia kuongea,wazee na vijana wenye nguvu wakagawana makundi,therathini kupandisha wanawake na wazee juu ya miti kujificha na kuhakikisha usalama wao, huku kundi lingine la watu therathini wakitega mitego kila kona, pembe zote ndani ya msitu,purukushani zikaanza mara moja, mara baada ya mzee Nyamigo kumaliza kuongea.



Mzee Nyamigo, Mpuzu na Ishimwe,wakaongoza kundi la kutega mitego, miti mithili ya visu ikachongwa,wakakata fito zilizokuwa na uwezo wa kujikunja na kufyatuka, mwisho wa fito wakaweka kipande cha mti mdogo kilichochongoka mithili ya kisu, kisha wakaikunja fito, wakaunganisha na kamba, kamba ikafukiwa vizuri na majani ya miti, mtu yoyote akigusa kamba bila kutambua, basi angeufyatua mtego ukamjeruhi vibaya sana.



Wakasogea karibu kabisa na mti mwingine, mti mkubwa wa ubuyu tofauti na ule ambao Mpuzu alikuwa amejificha mwanzoni, “hapa tunatega mtego, tuchimbe shimo kwenda chini, wakija, askari waliotangulia watadumbukia, wengine watapigwa na butwaa kumshangaa mwenzao aliyechukuliwa na mtego, wakizubaa, sisi tutawashambulia tukiwa juu ya miti, “mzee Nyamigo, mtaalamu wa mitego aliongea, akaungwa mkono.



Wakachukua mapanga yao makubwa, Mpuzu akahesabu panga tano upana, panga tano urefu, “,Shimo dogo sana, askari huwa wanatembea kwa msururu, inatakiwa askari kumi wote wadumbukie kwa pamoja “,Ishimwe alitoa wazo, wote waka muunga mkono.



Mpuzu akaongeza shimo, akahesabu panga kumi urefu, panga kumi upana, kisha wakaanza kuchimba shimo hilo katikati ya barabara, barabara iliyokuwa inaelekea katikati ya msitu. Kwakuwa kundi lote la watu therathini walikuwa na mapanga yao, isitoshe ardhi haikuwa ngumu, wakachimba futi saba kwenda chini, udongo wakaubeba na kuutupilia mbali, kwa saa moja tu, shimo lilikamilika,wakaweka mapanga ishirini ndani ya shimo kwa kuyasimamisha, tayali kwa kumjeruhi adui, wakachukua fito dhaifu wakazipanga juu ya shimo, wakapanga matawi ya miti madogomadogo, kisha wakaweka udongo juu yake, pamoja na majani,mtego ukawa umekamilika.



“,Ewalaaa, lazima tuwakamate …”,walifurahi na kujipongeza kwa mtego wao huo, mtego ambao walitegemea utaua wakoloni wengi, kisha wakasogea umbali wa mita hamsini na mahali walipotega shimo.



Waka angaza huku na kule, wakaliona gogo ambalo lilikatwa na kutelekezwa barabarani, wakalichukua, wakalipandisha juu ya mti pembeni ya barabara, kisha wakalifunga na kamba ngumu, kisha kamba iliyoshika gogo hilo ikapitishwa na kutegeshwa barabarani,ikafukiwa na majani ya miti, kamba hiyo ikafungwa kizembe upande wa pili wa barabara, yoyote yule atakaye jikwaa katika kamba, basi gogo lingemwangukia.Nusu saa ilitimia, mitego yote ilikamilika, wakarudi katika maficho yao, kuwasubili wakoloni waingie msituni, wawashambulie na kuwaua bila huruma.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

…………………………………

“Mikoko forest “kibao kilisomeka, dereva wa gari la Richald Robeni akasimamisha gari, gavana akashuka, mke wake na yeye akashuka. Gari zote zikasimama, tayali walifika mwisho wa safari yao.



“,Kundi moja pita huku, itakua na mimi pamoja na mke yangu, kundi ya pili pita kule mkono yangu ya kulia, right hand, itaongozwa na makamanda wa jeshi …”,Richald Robeni aliongea kwa kiswahili kibovu, akachomoa bastola yake, akapita upande wa kushoto wa msitu, njia ambayo Waafrika hawakujificha kabisa, askari wengine wakamfuata,kundi la pili likapita upande wa kulia, mahali ambapo Waafrika walijificha na kutega mitego yao, kundi la pili liliongozwa na kiongozi mkuu wa jeshi Agustino Darwini, jenerali mkatili asiye na huruma hata kidogo, aliwachukia Waafrika, huku akiwa na historia ya kutoa adhabu za kunyongwa kwa Waafrika waliogoma kulipa kodi ya kichwa, leo hii aliingia vitani, kukutana na maadui wake uso kwa uso …



Msitu wa mikoko;

Mlio ya magari ulisikika, mwangwi ukasikika na kupenya sehemu zote za msitu wa Mikoko, Mpuzu akapanda juu kabisa ya mti wa ubuyu, alitaka kudhibitisha kama sauti zilizosikika zilikua za magari ya kikoloni,akiwa juu ya mti wa ubuyu, aliona msafara wa magari ya wazungu mia moja, kilomita takribani tano kutoka msituni, akashuka haraka juu ya mti, kuwapatia taarifa Waafrika wenzake.



“,Wanakuja, sio muda mrefu watakua mahali hapa,nazani wanawake na wazee wako mahali salama kwa sasa, lakini wanapaswa kutulia kimya, wasipige kelele, vijana kumi wenye silaha pandeni juu ya mti huu wa ubuyu, wengine pandeni kwenye miti mingine karibu na mitego ilipotegwa ……”,Mpuzu Yahimana aliongea, Angel alikuwa pembeni yake,vijana kumi wakapanda juu ya mti mkubwa wenye urefu wa futi mia moja kwenda juu, mti uliojaa matawi na kuficha Waafrika, wanawake, wazee pamoja na watoto.



Vijana na wanaume wa kiafrika wenye nguvu, wakapanda kwenye miti karibu kabisa na mitego waliyotega, kwa ajili ya mashambulizi. “,Unaenda wapi? baki utakufa, si salama tunapoelekea, “Mpuzu alimfokea dada yake Mwamvua, aliyetaka kuongozana nao, kwenda kupambana, mkononi hakuwa na silaha nyingi zaidi ya panga kubwa katika mkono wake wa kulia.



“,Siwezi kufa kirahisi,hata nikifa,nitakuwa nimekufa kishujaa,naenda kupigania uhuru wa nchi yangu…”,Mwamvua akiwa na nyuso isiyo na tabasamu wala furaha aliongea,alidhamiria kupambana kufa na kupona kupata uhuru wa nchi yake, haijalishi alikuwa na umri kiasi gani.

“,Let her go with us, she know how to fight, anajua kupigana, alipiga white people kule kwa great fort ,muache aende na sisi…”,Angel alimtetea wifi yake mtarajiwa, alishuhudia kwa mara ya kwanza Mwamvua alivyowatia adabu askari wa kizungu katika ngome ya wakoloni,siku mbili zilizopita,tangu siku hiyo alimuheshimu Mwamvua, msichana mdogo mwenye umri wa miaka kumi na tatu tu.



“,Sawa, twende, lakini kuwa makini, maana hujapona vizuri majeraha yako……”,Mpuzu aliongea, akamruhusu mdogo wake kuongozana naye, wote wakakwea miti,wakiwa na silaha za jadi isipokuwa Angel peke yake aliyekuwa na bastola mkononi, bastola aliyotoka nayo katika ngome ya wakoloni.



…………………………………

Jenerali Agustino Darwini aliongoza msafara, kundi la pili la askari mia tatu wa kikoloni,wakafuata njia ndogo iliyopita mkono wa kulia wa kibao chenye jina la msitu,wakaanza kuingia katikati ya msitu.Wakijiamini kwani silaha za Waafrika,silaha za jadi, hazikuwa na uwezo wa kufua dafu mbele ya silaha za wazungu, bunduki pamoja na miripuko ya mabomu.



“,Chochote kitakachotokea mbele ya macho yako,just kill, ua kuyakomboa maisha yako, bila hivyo jeshi lote litapata adhabu kutoka kwa gavana, hakikisha unarudi na kichwa cha Muafrika katika ngome kubwa……”,jenerali wa kikoloni, Agustino Darwin aliongea kwa kiswahili safi kabisa, akiwa mbele kabisa ya askari mia tatu wa kundi lake, macho yake yaliangaza mbele pamoja na msituni, akasahau kuangalia chini pamoja na juu ya miti, mahali walipojificha Waafrika.



Safari ilipamba moto,kundi la jenerali Agustino likaingia katikati ya msitu, macho yao yaliangaza mbele, pamoja na kona zote za msitu, wakapuuzia kuangalia juu ya miti, waliamini Waafrika wangejificha vichakani, mahali salama na vigumu kuonekana, kinyume kabisa na fikra zao, vijana hodari wa Kiafrika walikua juu ya miti ,wakiwaona vizuri askari wa kikoloni,wakijipanga namna ya kuwashambulia, wakawasubili wasogelee mitego yao, ili wawashambulie vizuri.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“,ooooh, help me!, help me!, nisaidieni ,…”,



“,Paaaa, paaaa, paaa …”,



“,Hel…p…me. …,nak…ufa ” ,



kelele zilisikika, jenerali Agustino alipiga kelele kuomba msaada,alijikwaa kwenye mtego wa kamba bila kutegemea, mguu wake ukaburuzwa na kamba mita kadhaa, askari wake wakashambulia bila mafanikio, gogo kubwa lilitoka juu ya mti na kutua katika tumbo la jenerali Agustino Darwin, damu nzito ikatoka mdomoni, mapuani na masikioni, jenerali wa askari wa kikoloni akafa palepale. Askari wake wakabaki wamepigwa na butwaa, kundi lote la askari wa kizungu wakashusha silaha zao mikononi mwao, wakausogelea mwili wa kamanda wao kuuchunguza. Wakiwa hawa amini kile kilichotokea.



“,Amekufa …”,



“,Yes, tayali amekufa, bastard Africans! “,



“,What this, wametuua sana,hii ni dharau, we must show them respect …”,



“,Foolish Africans, wapumbavu kabisa,tukiwakamata,there is no mercy…”,



Kundi la pili la askari wa kikoloni,kundi ambalo liliongozwa na jenerali Agustino Darwin,waliuzunguka mwili wa kiongozi wao,bila tahadhari yoyote,huyu alisema hili,yule akasema lile,bila kutambua uwepo wa maadui zao juu ya miti.



“,Pyuuu,pyuuu,pyuuu…”,



“,Yalaaa,am dying,nakufaa…”,



“,Pyuuu,pyuuu…”,



“,Aaaaaaah…”,



“,Run,run,kimbia,take your guns,shoot them,washambulie……”,



Ghafla kundi la askari wa kikoloni wakashambuliwa,zaidi ya askari kumi wakafa papo hapo,wengine wakafarakana,wakakimbilia msituni,kila mtu njia yake,hawakutambua mahali mishale iliweza kutokea,hawakufahamu mahali walipojificha maadui zao,ghafla mashambulizi yakasimama ,msitu ukawa kimya,kelele na vilio vya wakoloni ndivyo viliutawala msitu.



Askari wa kikoloni takribani ishirini walikimbilia mbele baada ya kushambuliwa, huku macho yao yakiwa bize kuangaza mbele yao, bunduki zao zilikuwa mikononi tayali kwa ajili ya kushambulia adui yoyote yule, hawakujua mahali walipokuwa wanakimbilia kama kulitegwa mitego, pia kulikuwa na askari wa Kiafrika wakiwa wamejiandaa kwa ajili ya kufanya mashambulizi.



“,Go, go, songa mbele, usiogope,be strong …”,



“,don’t worry boss, tutakamata watu nyeusi yote …”,



“„Let’s move, kimbia, songa mbele …”,



Kundi la askari ishirini lilitangulia mbele, likawaacha wenzao nyuma, baada ya kushambuliwa, wengine wakauawa na wengine kutokomea msituni kuyaokoa maisha yao, baada ya kushikwa na taharuki mara tu baada ya kushambuliwa. Kundi likasonga mbele, kila mmoja akimtia moyo mwenzake, walijiamini, waliiamini rangi yao, wakawadharau Waafrika, waliamini lazima watalipiza kisasi na kuwakamata Waafrika,na kuwapatia adhabu kali ikiwemo kunyongwa na kazi ngumu za shambani bila chakula wala maji.



“,yalaaaa, fu…ck…you, foolish Afric…ans,naku…faa …”,



“,don’t move, msije, sima…m…a …”,



“,Puuuu …”,



“,Yalaa…aa, you ki…lled

us (mmetuua) “,



Ghafla askari mmoja aliyekuwa mbele akatumbukia ndani ya shimo, baada ya kukanyaga mtego, akapiga kelele huku akitukana matusi ya kila aina,mwingine tena akatumbukia shimoni, akapiga kelele, akawaonya wenzake wasimame mahali walipo, hawakusikia, wakasogea mbele bunduki zao zikiwa mikononi, walitaka kuwakomboa wenzao waliotumbukia shimoni, wakajikuta wanakanyaga mahali pasipo stahili, kundi lote la watu kumi na nane waliokuwa wamebakia wakatumbukia shimoni, wakapiga kelele za maumivu, visu vilivyokuwa vimetegwa shimoni vikawachoma choma,mwingine kifuani, mwingine tumboni, wakafa palepale, ukimya ukatawala tena ndani ya msitu.



…………………………………

Gavana Richald Robeni, mke wake malikia Magreth, askari mia tatu pamoja na baadhi ya viongozi wa kikoloni walipita upande mwingine wa msitu, upande wa kushoto ambao haukuwa na mitego yoyote iliyotegwa, isitoshe Waafrika hawakujificha katika upande huo wa msitu.



Gavana na kundi lake walisonga mbele, walikuwa makini sana, waliangaza pembe zote za msitu kwa umakini wa hali ya juu, silaha zilikua mikononi mwao, macho yao yaliangaza mita mia moja mbele, juu na chini, kushoto na kulia. Laiti kama wangepita upande wa kulia, mahali walipo jificha Waafrika,kwa umakini walio nao,bila shaka wasingepata madhara makubwa, pengine wangetambua mahali walipo jificha maadui zao.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“,Yala…aa, nakuf…aa, fuck you,……”,



“,paaa, paaa, paaa! “,



Ghafla gavana alisimamisha msafara, alisikia kelele na milio ya risasi upande wa pili wa msitu, hakuona haja ya kuendelea kusonga mbele.

“,let’s go back!,twendeni upande wa pili wa msitu, huko ndiko kuna maadui,”



“,listen, listen, they are shouting, wanapiga kelele mingi huko, wanashambuliana …”,



“,My daughter jamani,let them not kill my daughter, wasimuue mwanangu ……”,



Kundi lote liligeuka nyuma, kila mmoja alisema neno lake, baba yake Angel Richald Robeni aliwahofia askari wake kuuawa, mama yake Angel alihofu mwanae kuuawa, baada ya kusikia milio ya risasi na kelele za vilio, wote wakaanza kurudi nyuma wakikimbia, upande wa pili wa msitu.



Msitu wa mikoko;

Mpuzu Yahimana aliongoza mashambulizi,waliwashambulia kwa mishale askari wa kikoloni, walipojaribu kuwasaidia wenzao waliojeruhiwa na mitego iliyotegwa na Waafrika, askari wa kikoloni hawakutambua mahali adui zao walipojificha, ilibidi wakimbilie vichakani, kila mtu njia yake, kuziokoa nafsi zao …



“,Tushukeni chini, tuwafuate porini, wengine wakusanye bunduki za maadui tuliowaua,tuzihifadhi mahali salama,maana vita haiishi leo wala kesho……”,Mpuzu aliongea, wote wakakubaliana naye,wakateremka juu ya miti, askari takribani therathini, akiwemo Angel Richald pamoja na Mwamvua.



“,Tufanye haraka, maadui bila Shaka na wao wanatutafuta, “Mwamvua aliongea.



“,Kweli kabisa, kweli kabisa, tufanye haraka! “,mzee Nyamigo aliongea kwa mkazo, akitikisa kichwa,akashika tawi la mti, akaning’inia kama nyani, akaruka chini…



dakika tatu zilitumika,kundi moja la askari lilikuwa chini, wakaanza kuokota silaha,kutoka kwa Wazungu waliouawa baada ya kutumbukia shimoni, huku wengine wakishambuliwa na mishale,waliendelea kukusanya bunduki, wakawasachi mifukoni, wakawanyanganya mabomu waliyokuwa wameweka katika mifuko yao, Mpuzu alikuwa bize akiangalia kila kona ya msitu, akichunguza usalama, wenzake wakiwa wanakusanya silaha kutoka kwa wazungu waliopoteza maisha.



…………………………………

Kundi la pili la Waafrika, kundi ambalo liliongozwa na Ishimwe, walimaliza kushambulia, waliua askari wa kizungu wengi sana, zaidi ya hamsini, huku kiongozi wao wa kizungu, jenerali Agustino Darwin akiuawa vibaya na gogo ambalo lilitegwa na kumpiga tumboni.



“,Leo kapatikana, roho yake mbaya, imesababisha afe kifo kibaya, ona sasa …!”,Ishimwe aliongea,akiwa pamoja na kundi lake la askari therathini, wakiutazama mwili wa kamanda wa kikoloni, jenerali mkatili ambaye aliwachukia sana Waafrika.



“,Puuuu, puuuu … “,..

“,Muache,ameshakufa! “,

“,Wacha nimtie adabu! “,

“,Achana naye,tayali ameshakua mzoga ……”,.

“,Pumbafu sanaa, ngozi nyekundu kama nyanya, harafu unajifanya mjanja, leo umepatikana! “,



Mpuzu alimshika kijana mwenzake, aliyekuwa na hasira kupita kiasi, licha ya Agustino Darwin kupigwa na gogo tumboni,akakata roho, lakini kijana huyu alikuwa bado ana hasira naye, alimpiga ngumi tumboni, akimtukana matusi ya kila aina, alichoshwa na ukatili wa jenerali huyu aliokuwa akiwafanyia.



“,Wengine okoteni silaha tuondoke, watatushambulia,wameingia vichakani,…”,

“,tushamaliza, ”

“,kama mmemaliza, turudini nyuma tukaonane na wenzetu! “,

“,Sawa, sawa …”,



Walimaliza kuokota bunduki za wazungu, wakarudi nyuma,kuonana na wenzao, kundi la Mpuzu.Macho yao yaliangaza mita hamsini mbele, hamsini nyuma, kulia na kushoto, walikuwa makini wasije wakashambuliwa na askari wa kikoloni waliokimbilia vichakani, walipo washambulia awali na kuwazidi nguvu.



…………………………………

Makundi yote mawili, makundi ya askari wa Kiafrika, yalikutana pamoja, wakiwa na machale, walijadiriana namna ya kuendeleza mapambano dhidi ya wazungu,ili kupigania uhuru wao …

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“,Wameingia vichakani, tuwafuate! “,

“,Hapana, huko sio salama, tutakufa! “,

“,Kweli, mahali salama kwa mashambulizi, ni juu ya miti, turudini huko, wakija maeneo haya tuwashambulie !”,

“,Wazo zuri, tufanye hivyo! “!

“,Jamani, sikieni, hamsikii sauti za miguu, kuna watu wanakuja …”,

“,Harry up, let’s go back, tupande juu ya miti …”,

“,Hata mimi nasikia,wanakuja! “,



Kundi lote la takribani askari sabini, walipanda tena juu ya miti,baada ya kijana mmoja wa Kiafrika kusogeza sikio lake juu ya ardhi, karibu na udongo, akasikia ardhi ikitetemeka kwa mbali, bila shaka kuna watu walikuwa njiani wanakuja, tena wakikimbia, Angel Richald, mpenzi wake Mpuzu, mtoto wa gavana Richald Robeni, hata yeye alikuwa akichezwa na machale, akawahimiza wenzake, wakapanda juu ya miti haraka sana, ndani ya sekunde kumi, wote walikuwa juu ya miti, mikononi walishika upinde na mishale, huku bunduki walizowanyanganya wazungu wakiwa wamezikusanya pamoja, na kuziweka mahali salama juu ya mti, Angel alichukua bunduki moja aina ya smg, pamoja na baadhi ya mabomu madogo takribani matano, silaha zote za kizungu alijua namna ya kuzitumia, mafunzo aliyoyapata katika jeshi la Uingereza, aje kurithi mikoba ya baba yake, miaka kumi ijayo.



“,Shiii, silence please, they are coming, wanakuja! “,



“,Yeah wanakuja,kaeni tayali kwa ajili ya kushambulia,”



“,Sawa, sawa. …”,



Angel Richald, aliwasisitiza wenzake kuwa makini, kujiandaa kwa ajili ya mashambulizi, bunduki yake aliishikilia ipasavyo, jicho lake la kushoto alikuwa amelifumba, jicho lake la kulia lilitazama darubini, na kumuweka adui kwenye targeti, huku kidole kimoja cha mkono wake, kikijiandaa kwa ajili ya kuvuta taiga ili kuruhusu risasi kumiminika na kuteketeza maadui.



…………………………………

Malikia Magreth alikuwa mbele, mume wake, gavana Richald Robeni alifuatia, kisha kundi la askari wa kikoloni wakafuata, nyuma ya gavana Richald Robeni.Msururu ulikuwa mrefu, kutokana na wingi wao, wote walikimbia kwa kufuata njia ndogo, nyembamba, iliyokuwa ikiingia katikati mwa msitu, upande wa kulia.



“,What!, they have killed him, wamemuua Darwin! “,

“,Wamemuua kwa mtego,shit! Africans are bastard, we will kill you too, tutawaua ……”,



Wakiwa wanakimbia, ghafla mama yake Angel, malikia Magreth alifunga breki, alikutana na mwili wa kiongozi wao wa jeshi, walipoangaza upande wa pili, askari wengi wa kikoloni walikuwa wamepoteza maisha, wakavua kofia zao, jasho jembamba likawatoka, walichoka,



“,Who are you, wewe ni nani? “,

“,Colonial soldiers, askari wa kikoloni, don’t shoot us, msitushambulie …”,



Ghafla, malikia Magreth machale yalimcheza, alihisi majani ya vichaka yakicheza cheza, akanyosha bastola yake vichakani, kundi lote la askari wa kikoloni wakanyosha silaha zao kuelekea sehemu hiyo ya vichaka, askari takribani ishirini, askari wenzao wakajitokeza, huku wakionekana kuchoka sana.



“,Tulishambuliwa, wengine wakauawa, hatujui maadui walitokea upande gani, tumetoka vichakani kuwatafuta hatujawaona, ”

“,Tuondokeni, tusonge mbele …”,

“,But why this!, kwanini silaha zao hazipo mahali hapa?…”,

“,Enemies have taken them, maadui watakua wamechukua silaha zao, they want to fight us with guns, wanataka watuue kwa bunduki, they can’t kill us , tuondoke …”,



Walimaliza kujibizana wakiwa na huzuni, wakavaa kofia zao, wakakamata bunduki zao, wakaanza kusonga mbele, kufuata barabara.Macho yao yalikuwa makini, kuangaza kila kona wasije wakashambuliwa, mioyo yao ilianza kujawa na uoga, tofauti na awali, kwa sasa Waafrika walikua hatari sana, wenye mioyo ya ukatili kwa askari yoyote yule wa kikoloni, walikuwa hawana budi kuwa makini, kuepuka kifo.Walikimbia mita chache tu, baada ya dakika tano tu, wakashtuka tena ghafla, walikutana na maiti nyingine za wenzao waliouawa kikatili, ishirini ndani ya shimo, wakiwa wamechomwa na mapanga sehemu mbalimbali, baada kunaswa na mtego wa shimo, wengine walipigwa na mishale …



“,Shit! We are finished, wametega mitego kila kona, we have to be careful …”,

“,Why,hizi people nyeusi imekuwa katili sana, kama pata him or her, we are going to eat them, lazima kula nyama zao! “,



Walifoka, kila mmoja aliongea neno lake, gavana Richald Robeni pamoja na mke wake walishika vichwa vyao kwa huzuni, askari wao walikuwa wameuawa kikatili, wakaanza kuondoka tena, malikia Magreth, mke wake gavana, aliwaza tu kuhusu usalama wa mwanae, alitaka kufanya kila njia, asije akauawa na jeshi la kikoloni, kwani walikuwa na hasira sana baada ya wenzao kuuawa.



“,Lets move on, tusonge mbele …”,

“,Yes boss, let’s go to look for this stupid race, …”,



Gavana Richald Robeni alilihimiza jeshi lake kutokukata tamaa, mke wake akasimama, akaanza kusonga mbele, gavana akafuatia, kisha kundi lote la askari wa kikoloni wakafuata kwa nyuma,dakika mbili zilipita, dakika tatu zikapita,walikuwa njiani wakikimbia kusonga mbele



“,Paaaaa! “,



“,I’ m…dying, nakufa…aa ……”,



“,My mother!, mamaaa!, don’t die,aim sorry mom…”,

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ghafla risasi ilisikika, ikapenya katika kichwa cha malikia Magreth, ubongo wake ukasambaratika, Angel Richald ndiye aliyekuwa ameshika bunduki, akiwa juu ya mti, alifyatua risasi bila kujua kuwa kiongozi wa kundi, alikuwa ni mwanamke, tena mama yake mzazi, ukelele wa uchungu ukasikika, akakata roho palepale, Angel alipiga kelele za huzuni bila kutegemea,hakutegemea kumuua mama yake,mikono yake ilikufa ganzi, mwili ukakosa nguvu, akaachia bunduki yake aina ya smg, ikadondoka chini, askari wa kikoloni walipandwa na hasira, akiwemo baba yake mzazi na Angel, gavana Richald Robeni, hakutegemea kama mwanae alikuwa msaliti kiasi kile, akamuua mpaka mama yake mzazi, jeshi lote la kikoloni walisikia kelele za Angel, wakatambua mahali risasi ilipotekea ,waliinua silaha zao juu kwa pamoja, kushambulia mti mkubwa ambao Angel pamoja na askari wengine wa Kiafrika walikuwa wamejificha …



Msitu wa mikoko

Angel Richald alikuwa hana silaha yoyote ile,moyo wake ulikuwa na maumivu makali baada ya kumuua mama yake mzazi kwa mikono yake mwenyewe,nguvu zikamuishia, akajikuta ameiachia bunduki yake bila kupenda.Mpuzu Yahimana, mpenzi wake Angel, alihuzunika kwa kile kilichotokea, japo alikuwa vitani kupigania uhuru wa Mwaafrika, lakini hakuwahi kufikiria kuwaua wazazi wa Angel, viongozi wa serikali ya kikoloni, gavana Richald Robeni, pamoja na mke wake malikia Magreth hata siku moja, jeshi la kikoloni walizinyosha silaha zao juu ya mti, mahali risasi ilipotokea na kumuua malikia Magreth, mahali kilio cha Angel kilikuwa kinasikika…



“,Shoot them, kill all of them including my daughter, she has killed her mother, she has killed my wife ……”,( wapigeni na risasi, waueni wote akiwemo binti yangu, amemuua mama yake, amemuua mke wangu …)



Gavana Richald Robeni alitoa amri, akiwa amenyoosha silaha yake, akijiandaa kuvuta taiga ya bunduki yake, kuruhusu risasi,vijana wake, askari takribani mia moja hamsini waliosalia, wakajiandaa kuvuta taiga,kulishambulia jeshi la watu weusi waliokuwa wakidai uhuru wao kwa kuingia vitani.



“,Papaaa!paaa!paaa paaaa……”,jeshi la askari wa kikoloni walishambulia.



“,wafyatueni na mishale,lukeni,tokeni juu ya miti,tukimbilie vichakani……”,Mpuzu Yahimana aliwahimiza vijana wake,washuke juu ya mti kuzikoa nafsi zao,silaha zao za jadi zisingefua dafu mbele ya risasi za moto za askari wa kikoloni.



“,papaaa,paapaa…”,askari wa kikoloni waliendelea kushambulia,wakiutekeza mti mkubwa wa ubuyu,matawi na majani ya miti yakateketezwa,yakadondoka chini na kuwalaani wazungu.



“,Yalaaa,nakufaaa,uwiiii!,Mrungu turongole(Mungu tusaidie),tunakufaa……”Kelele za machungu zilisikika,mashujaa wa Kiafrika walipiga kelele za maumivu, risasi zilipenya katika miili yao,wengine tumboni,wengine kichwani,Ishimwe alimanusura apigwe risasi,lakini alimuona mlengaji aliyekuwa amemuweka kwenye tageti,akaruka upande wa pili wa mti,risasi ikamkosa,askari wa kikoloni akaikoki tena amshambulie Ishimwe,alichelewa sana,Ishimwe aliuvuta upinde wake mpaka mwisho,akaufyatua,mshale ukatoboa jicho la askari yule wa kikoloni,ukatokea upande wa pili wa kichwa chake,akafa palepale.Ishimwe akadaka tawi la mti,akaruka chini,akatokomea vuchakani,mahali walipoelekea wenzake walioruka juu ya mti kabla yake…



Angel aliiona bunduki ya baba yake ikielekea upande wake,bila shaka baba yake alitaka kumuua,akaangalia upande wa pili,askari wa kikoloni takribani kumi walijiandaa kumshambulia,hakuwa na hofu yoyote ile,aliona bora afe kuliko kubaki duniani,moyo wake ulimsuta,alijiona ana hatia kubwa kwa kumuua mama yake,hakuona haja ya kukimbia kama walivyofanya Waafrika,walioruka huku na kule,kuelekea mafichoni,katika vichaka virefu msituni.Mpuzu aliwashambulia askari wa kikoloni kwa mishale,yote ikaenda pembeni,hakuua askari hata mmoja,alipogeuka upande wa pili,akamuona mpenzi wake anataka kushambuliwa,alikuwa hajielewi kabisa,akamvuta,Angel akadondokea kifuani kwake,akamkumbatia,mkono wake wa kushoto ulimshika Angel kwa nguvu,mkono wake wa pili ukakamata tawi la mti,huku risasi zikiwakosa kosa,zikipita juu ya vichwa vyao kwa fujo,Mpuzu Yahimana akaruka chini,wakakimbila msituni,huku Angel akilia kilio cha kwikwi,walipogeuka nyuma,walishuhudia maiti nyingi za Waafrika,zikidondoka juu ya mti,wakahuzunika,wakapiga moyo konde,wakasonga mbele na kutokomea vichakani…



“,Kufa,kufa,poor race,i hate you,……”,askari mmoja wa kikoloni,alifoka kwa hasira,akipiga mateke maiti za askari wa Kiafrika,ambao walikuwa bado wakihangaika kukata roho,alizungusha vichwa vyao,akawamalizia,aliwachukia sana Waafrika.



“,Lets follow them,tuingie kwa vichaka kuwatafuta…”,askari mmoja aliongea,akawahimiza wenzake kusonga mbele,kuwafuata Waafrika mahali walipokimbilia.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“,Stop!,don’t follow them,wacha fuata jinga hizi,let’s go back,turudi kwa great fort,we have to add more soldiers,askari yangu kufa nyingi sana……”,gavana Richald Robeni aliwazuia vijana wake kusonga mbele, askari wake wengi sana walikuwa wamepoteza maisha, jeshi lake lilikuwa limepungua, alitaka kurudi katika ngome yao kuongeza nguvu, askari wake wakatii amri yake, wakanyenyua mwili wa malikia wao kwa heshima, wakaupigia saluti, wakaanza safari ya kurudi katika ngome yao, wakiwa na majonzi makubwa …



…………………………………





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog